Search This Blog

Sunday, 22 May 2022

FUTA MACHOZI MPENZI - 4

 





    Simulizi : Futa Machozi Mpenzi

    Sehemu Ya  Nne (4)



    CIA walichanganyikiwa, hawakujua ni kitu gani kilitokea mpaka kumkosa William ambaye mpaka muda huo hawakujua alikuwa mahali gani. Walichokifanya ni kuziweka picha zake nyingi na kusema kwamba kwa mtu yeyote ambaye angefanikisha kupatikana kwake basi angeweza kupewa kiasi cha dola milioni moja.

    Tangazo hilo lilikaa hewani kwa saa moja tu ndipo walipoamua kulibadilisha, walijua kwamba William alikuwa amebadilishwa sura hivyo ingekuwa vigumu sana kumpata kwa sura yake, wakachukua picha zilizopigwa uwanja wa ndege ambazo zilionyesha akiwa na sura ya Kirusi na kuziweka kwenye mitandao ya kijamii, kuwapa waandishi wa habari na kuzibandika kila kona.

    “Sasa William si mtu mweusi, imekuwaje tena?” aliuliza jamaa mmoja huku akionekana kuchanganyikiwa.

    “Hata mimi nashangaa! Labda alibadilishwa sura. Cha msingi sisi tumtafute huyu Mrusi mwenye sura hii,” alisema jamaa mwingine.

    Kila mtu akawa makini barabarani, huyo William aliyekuwa akitafutwa hakuwa mtu mweusi tena, alibadilika na kuwa Mzungu. Kila kona, wale watu waliokuwa wakifanana naye, walichukuliwa na kupelekwa polisi ambapo baada ya kuambiwa kwamba hakuwa yeye, wakarudishwa walipotolewa.

    Hali ilikuwa ngumu mitaani, kila mtu alizitolea macho picha zile zilizokuwa zimebandikwa na kuwakamata watu waliofanana naye lakini hawakuweza kumpata mtu sahihi.

    Wakati hayo yote yakiendelea, nchini Urusi hali ilikuwa mbaya, KGB walichanganyikiwa, hawakuamini kama kweli William aliwatoroka kwenye ndege na kuwaua watu wao. Walichokiamini ni kwamba William alitumia ujanja kuilipua ndege na si kwamba ndege ilipata hitilafu angani.

    Walijua kwa namna moja au nyingine ilikuwa ni lazima kwa CIA kufanya juu chini kumpata mtu huyo, pia walijua kwamba kwa jinsi utandawazi ulivyokuwa mkubwa ilikuwa ni lazima watu wamuone William na hivyo kupiga simu huko, hivyo kitu cha kwanza kabisa kukifanya kilikuwa ni kuzitraki simu zao.

    Ilikuwa kazi kubwa na ngumu lakini kutokana na uwezo wao mkubwa, wataalamu waliokuwa nao, walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuzitraki simu hizo na ndiyo maana hata mwindaji alipopiga simu, waliipata simu hiyo na wao kusikiliza, kwa kuwa wengine walikuwa nchini Canada, ilikuwa ni lazima wafike kule alipokuwa haraka sana.

    CIA wakajiamini, wakajua kwamba simu hiyo waliisikia wao tu hivyo hata kujipanga kwao hakukuwa na uharaka kama uliotakiwa. Wakawapigia simu maofisa wa CIA waliokuwa Canada na kuwaambia kile kilichotokea na hivyo kuelekea huko kwa ajili ya kuonana na mtu huyo.

    Baada ya dakika ishirini na tano walikuwa mahali hapo, kwanza kabisa, kabla ya kushuka ndani ya gari wakaanza kumtafuta mzee huyo kwa kumwangalia huku na kule. Kila walipomtafuta, hawakumuona kitu kilichowapelekea kuteremka na kwenda kuulizia.

    “Nani?” aliuliza mhudumu wa mgahawa.

    “Kuna mtu alitumia simu hii! Yupo wapi?” aliuliza jamaa wa CIA.

    “Eeh! Mbona aliondoka dakika kumi zilizopita.”

    “Aliondoka?”

    “Ndiyo! Kuna watu walifika mahali hapa na kumchukua. Walikuwa Warusi,” alisema mhudumu yule.

    “Ulisikika neno lolote kutoka kwao?”

    “Ndiyo! Waliuliza yupo wapi? Mzee akasema nyumbani kwake, wakaingia garini na kuondoka,” alisema mhudumu yule.

    “Walielekea njia gani?”

    “Ile kule!”

    “Tutapajuaje kwake?”

    “Nyie nendeni, kule kuna nyumba moja tu, nahisi ndiyo yake,” alisema mhudumu huyo.

    Hakukuwa na muda wa kupoteza mahali hapo, walikwishajua kwamba mbali na wao pia kulikuwa na Warusi waliokuja kumchukua mzee huyo na bila shaka walikuwa njiani kwa ajili ya kumchukua William.

    Hawakutaka kuona hilo likitokea, William alikuwa mali yao na si ya mtu mwingine. Safari ya kuelekea huko ikaanza, njiani, kila mmoja alikuwa makini. Japokuwa theluji iliondolewa barabarani kwa ajili ya magari kupita lakini tayari theluji nyingine ilirudi na kuanza kutapakaa barabarani.

    “Guys! Get your guns ready!” (Andaeni silaha zenu) alisema mkuu wao, kila mmoja akaandaa bunduki yake kwani tayari walikuwa wamekaribia karibu na mahali ilipokuwa nyumba hiyo.

    ****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mzee yule mwindaji na wale maofisa wa KGB wakafika mahali pale palipokuwa na nyumba kisha mzee huyo kuufungua mlango wa kuingilia katika handaki lile. Kwa jinsi lilivyokuwa limejengwa, hata hao KGB walishangaa kwani haikuwa rahisi kwa handaki kama hilo kujengwa kama lilivyokuwa, ilionyesha dhahiri kwamba mzee huyo alikuwa mtu mwenye mafunzo fulani ya kijeshi.

    Wakaingia chini, pale alipokuwa amemuacha William, hakuwepo, alijaribu kuangalia huku na kule, hakumuona. Alichanganyikiwa, hakujua ni kitu gani kilikuwa kimetokea. Kipindi kifupi kilichopita alimwacha mtu huyo ndani ya handaki hilo, tena akiwa hoi lakini cha ajabu alipokuwa amerudi na watu hao waliokuwa wakimuhitaji, hakumkuta.

    “Yupo wapi?” aliuliza jamaa mmoja.

    “Sijui! Alikuwa hapa, nilimuacha hapa,” alijibu mzee huyo huku akionekana kuwa na hofu kubwa.

    “Kama ulimwacha hapa, yupo wapi?” aliuliza mwingine.

    “Hata sijui! Nilimuacha hapa,” alijibu mzee huyo huku akionekana kuwa na uhakika na alichokuwa akikisema mahali hapo.

    Wote wakamuona mzee huyo kuwa muongo, walijua kwamba alikuwepo sehemu, aliamua kumficha kwa kuwa aligundua kwamba hao hawakuwa Wamarekani bali ni Warusi, alichokifanya jamaa mmoja ni kumsogelea, akatoa bunduki yake na kumnyooshea.

    “Tunakupa dakika moja kutuambia ukweli! Yupo wapi?” aliuliza jamaa huyo.

    “Jamani! Hiyo michezo na bunduki sipendi, huwa nimeiacha kitambo sana. Ni michezo hatari mno, toa bunduki yako mbele yangu, huwa nachukia mtu akinionyeshea bunduki,” alisema mzee huyo, alizungumza kwa kujiamini.

    “Sekunde arobaini zimebaki!”

    “Naomba utoe hiyo bunduki mbele yangu!”

    “Sekunde ishirini!”

    “Toa bunduki!”

    “Sekunde kumi!” alisema jamaa huyo huku kila mmoja akiwa na uhakika wa William kufichwa ndani ya nyumba hiyo.

    “Sekunde tano...”

    Hata kabla hazijamalizika, mzee huyo akaruka sarakasi kwenda juu, aliporudi chini, alitua kwa nguvu na kuupiga mkono wa jamaa yule aliyeshika bastola, huku wengine wakiwa hawajachukua hata tahadhari, wakajikuta wakivamiwa na kuanza kupigwa.

    Hata kabla hawajachukua uamuzi, mzee yule akaipata bastola ile iliyokuwa imeanguka kutoka mkononi mwa jamaa aliyempiga kwanza, alipoipata tu, akaanza kuwamiminia risasi mfululizo, ni ndani ya dakika moja tu, wote walikuwa chini huku miili yao ikitapakaa damu.

    “Huyu dogo yupo wapi?” alijiuliza, alichokifanya ni kutoka ndani ya handaki lile, alipofika nje tu, macho yake yakatua katika gari lililokuwa likija kwa kasi, kitu alichohisi ni kwamba watu hao walikuwa Warusi wengine, hivyo akaanza kuwamiminia risasi huku akirudi ndani ya handaki lile.

    “Piga risasi...” alisema jamaa mmoja wa CIA na hivyo kufanya hivyo lakini hakukuwa na risasi iliyompata, akaingia ndani ya handaki.

    Wakaelekea kule kulipokuwa na nyumba ile iliyoteketea, walitembea kwa umakini mkubwa kwani mtu waliyekuwa wakipambana naye alionekana kuwa si mtu wa mchezomchezo. Walipofika, wakaufungua mlango wa kuingia ndani ya handaki lile.

    Humo, walipigwa na mshangao mara baada ya kuona maiti za watu wanne zikiwa chini huku damu zikiwatoka. Walipowaangalia vizuri watu hao, walikuwa Warusi. Wakawapekua mifukoni mwao, wakawakuta wakiwa na vitambulisho vilivyowatambulisha kwamba walikuwa majasusi kutoka katika Shirika la Kijasusi nchini Urusi, KGB.

    “Hawa ndiyo wabaya wetu.”

    Hawakujua mtu waliyekuwa wakimtafuta alikuwa mahali gani, lakini walipokuwa wakiangalia huku na kule kumtafuta, wakafanikiwa kuliona bomba kubwa kwa chini, lilikuwa kubwa kiasi cha kuingia mtu na kuanza kutambaa ndani yake.

    Wakajua dhahiri hilo ndilo lilikuwa bomba alilolitumia mzee huyo, walichokifanya na wao kuingia ndani huku wakiamini kwamba mtu huyo alikuwa humo, kwa kile alichokifanya, kilikuwa kitu hatari kilichomtambulisha kama mwanajeshi au jasusi mmoja mkubwa, kwani kupambana na watu hao haikuwa kazi rahisi kwa mtu wa kawaida.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Saa kadhaa zilikatika, William alikuwa kwenye hali mbaya, muda wote alikuwa kimya, alionekana kama tayari alikuwa mfu. Pale alipokuwa, hakuweza kusogeza kiungo chake chochote kile na hata kuufumbua mdomo wake alishindwa kabisa.

    Ilipofika saa 7:26 usiku, hali yake ikaanza kurudi kama ilivyokuwa, akaanza kupata nafuu na kitu cha kwanza kabisa alichokihisi ni kuona vidole vyake vikianza kusogea huku na kule. Akajitahidi kuinuka pale alipokuwa, akashindwa kabisa lakini kidogo viungo vyake vilianza kupata nafuu.

    Hakusimama pale alipotoka, alitulia na kadiri muda ulivyokuwa ukizidi kwenda mbele na ndivyo alivyokuwa akipata nafuu. Ilipofika asubuhi, mwili ukawa na nguvu tena lakini hakutaka kujionyesha, hakutaka kumuonyeshea mzee yule kwamba alikuwa amerudi katika hali ya kawaida.

    Mwindaji yule hakujua kama William alirudi kwenye hali yake ya kawaida, akamnywesha uji kama kawaida na alipoona mwanaume huyo akitangazwa kwenye televisheni kwa kutumia sura ile ya bandia aliyokuwa nayo, akaondoka kwa ajili ya kuwasiliana na CIA.

    Huku nyuma William hakutaka kukaa, akasimama, akajaribu kutoka ndani ya handaki lile kwani mpaka hapo alipofikia, hakutakiwa kumwamini mtu yeyote yule.

    Akasimama na kujaribu kwenda nje, kulikuwa na baridi kali mno, hakutaka kwenda huko, alichokifanya ni kurudi ndani, akaangalia huku na kule ndipo akakutana na bomba kubwa likiwa limeelekea upande mwingine kabisa.

    Hakutaka kusubiri, alijua kwa namna moja au nyingine ilikuwa ni lazima bomba hilo lielekee sehemu ambayo aliamini ingekuwa salama kwa maisha yake. Akaingia ndani ya bomba lile na kuanza kutambaa kuelekea upande wa pili kabisa ambao hakujua ni upande gani.

    Japokuwa mule kulitakiwa kuwa na joto lakini kwa kipindi cha baridi kali kama kipindi hicho, hakukuwa na joto lolote lile, kulikuwa na baridi kali na muda wote meno yake yalikuwa yakigonganagongana tu.

    Alitambaa kwa dakika kumi na tano ndipo akafika mwisho wa bomba lile ambalo lilionyesha kwamba kila kitu kilichokuwa kikipitishwa mule, kilikwenda katika mto mkubwa ambao nao kipindi hicho maji yake yote yaliganda na kuwa barafu.

    “Mungu wangu! Nifanye nini?” alijiuliza.

    Kwa kuwa aliamini kwamba alikimbia hatari, hakutaka kusubiri mahali hapo, akajitokeza kuanzia kichwani mpaka kifuani kwa staili ya kulala chali, akalishikilia bomba lile na kupanda juu yake.

    Ilikuwa kazi kubwa kwa mtu kama yeye ambaye mwili wake haukuwa na nguvu za kutosha lakini hakuwa na jinsi, alipopanda, kilichofuata ni kuondoka mahali hapo. Alishindwa kujua sehemu alipokuwa akielekea, kulikuwa ni porini, pori ambalo miti yake yote ilikuwa imetawaliwa na theluji nyingi, hakutaka kusimama sehemu, aliendelea kusonga mbele huku akisikia baridi kali japokuwa mwilini mwake alikuwa na sweta zito lililokuwa na skafu shingoni mwake.

    Safari yake hiyo ikaishia sehemu ambayo kulikuwa na mgahawa huku kukiwa na magari manne ambayo yalikuwa yakitumika kusafishia njia kwa ajili ya wakazi wa eneo hilo kupitisha magari yao, akaelekea kule kulipokuwa na magari yale, kwa bahati nzuri kwake akakutana na msichana mmoja mrembo ambaye kwa kumkadiria tu hakuwa na miaka zaidi ya kumi na tano.

    “Do you speak English?” (unazungumza Kiingereza?) alimuuliza.

    “Yes! I do! What can I help you si?” (ndiyo! Ninazungumza! Nikusaidie nini bwana mkubwa?) aliuliza msichana huyo aliyekuwa na mbwa wake pembeni.

    “Where am I?” (nipo wapi?)

    “What do you mean?” (unamaanisha nini?)

    “I mean where am I right now?” (namaanisha nipo wapi sasa hivi?)

    “Winkler...”

    “What the hell is Winkler?” (ndiyo wapi huko)

    “Southern Winnipeg, Canada,” Kusini mwa Winnipeg, nchini Canada) alijibu msichana yule.

    “Is there any phone booth around?” (kuna kibanda cha simu karibu?) aliuliza William.

    “Yeah!”

    Akaonyeshewa sehemu kulipokuwa na kibanda cha simu, hakikuwa mbali sana na mahali alipokuwa. Akaanza kuelekea huko, hakuacha kutetemeka, japokuwa mwilini mwake kulikuwa na sweta, jaketi kubwa lakini alihisi baridi ikiingia mpaka kwenye mifupa yake.

    Akafika katika kibanda hicho, akajipekua mfukoni na kutoa senti hamsini aliyokuwa nayo na kuiweka kwenye simu kisha kumpigia mpenzi wake Linda. Simu iliita, iliita na kuita lakini haikuwa ikikpokelewa na mwisho wa siku kuambiwa kuacha ujumbe mfupi.

    “Linda! Naomba unisaidie, nipo Canada sehemu inayoitwa Winkler. Nipo hai, sikufa, naomba uwaambie FBI kwamba nipo hai ila wakichelewa watakuta nimekufa,” alisema William na kisha kukata simu.

    Alitamani kubaki kibandani kwa kuamini kwamba Linda atakapowaambia FBI basi ingekuwa rahisi kwao kumfuata mahali pale ila tatizo lilikuwa ni baridi lililokuwa likipiga.

    Hakuvumilia kubaki mahali hapo, alichokifanya ni kuondoka na kuelekea sehemu iliyokuwa na baa na kuingia ndani ambapo kulikuwa na watu wengi waliokuwa wakilewa pombe kali.

    Kila mtu aliyemuona William akiingia, alibaki akimshangaa, ilikuwa vigumu sana kwa kumuona Mrusi akiingia ndani ya baa zilizokuwa zikimilikiwa na Canada kutokana na ugomvi uliokuwepo baina yao.

    Walimshangaa, hawakujua mwanaume huyo alijiamini nini na wakati wao walikuwa wengi ndani ya baa hiyo. Muziki uliokuwa ukipigwa kwa sauti ya chini, ukazimwa kabisa, wale waliokuwa na silaha pembeni, wakazishikilia kisiri kwani ilikuwa ni lazima kumpiga mwanaume huyo ambaye aliingia kwenye anga zao kwa kuwa hata Wacanada waliokuwa wakielekea nchini Urusi, nao walikuwa wakipigwa sana na wengine kuuawa.

    William hakujua kitu chochote kile, hakujua kwamba ile sura ya bandia aliyokuwa amevishwa ndiyo iliyokuwa ikimuharibia. Hakuzungumza na kitu, alikwenda katika meza moja na kutulia chini.

    “Nikusaidie nini?” aliuliza mhudumu mmoja, japokuwa uso wake ulikuwa kwenye tabasamu lakini William aligundua kwamba tabasamu hilo halikutoka moyoni.

    “John Walker!”

    Mhudumu huyo akaondoka, hata kabla hajarudi, wanaume wawili wakasimama na kuanza kumfuata kule alipokuwa. Walipofika katika meza ile, nao wakachukua viti na kukalia katika meza ile.

    William alibaki akishangaa, hakujua sababu iliyowafanya watu hao watoke kule walipokuwa mpaka katika meza yake, akagundua kwamba kulikuwa na kitu. Hakuwasalimia, alinyamaza, mwanaume mmoja akaegemea kiti makusudi na kuifanya bastola yake kuonekana kiunoni.

    “Umekuja kufanya nini humu Mrusi?” aliuliza jamaa mmoja, sura yake ilionyesha dhahiri kwamba kuua halikuwa jambo gumu kwake.

    “Nani? Mimi? Mimi siyo Mrusi.”

    “Sikiliza, kaka yangu aliuawa nchini Urusi mwaka jana, baba yangu aliuawa hukohuko pia kwa vitu visivyoeleweka kwamba ni chuki binafsi. Kila unayemuona humu ndani, ndugu yake aliuawa nchini Urusi. Tulijiapiza kulipiza kisasi, wakati tukiwa na hasira sana juu yenu, hatimaye umeingia kwenye kumi na nane zetu,” alisema jamaa mwingine, wale waliokuwa pembeni wakaanza kusogea kule walipokuwa.

    “Francis...” aliita jamaa mmoja aliyekuwa mbali.

    “Unasemaje!”

    “Unamchelewesha, unamuhoji kwani wewe mwandishi wa habari?” alisema jamaa mmoja aliyekuwa kaunta, alichokifanya ni kusogea kule walipokuwa, alipofika kwenye meza ile, akachomoa bastola yake, akampiga risasi mbili William, moja ikaenda kwenye bega la kushoto na nyingine kuzama kwenye mbavu zake, hapohapo akaanguka chini, damu nyingi zikaanza kumtoka.

    “Mmalizie kabisa,” alisema jamaa mwingine, jamaa yule akaichukua bastola yake, akamnyooshea tena William, alidhamiria kuua, mlio wa risasi ukasikika, damu zilizokuwa zikimtoka William, zikaongezeka pale sakafuni alipokuwa amelala.

    “Aagghh...” alipiga kelele William sakafuni pale huku akiwa kwenye maumivu makali, akaona kabisa mtoa roho alimkaribia na alitaka kuitoa roho yake

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Dokta...dokta...” aliita msichana mmoja, alikuwa nesi aliyekuwa akikimbia kuelekea katika ofisi ya dokta mkuu, watu wote waliomsikia, walimshangaa, alikuwa akikimbia huku akionekana kuwa na haraka sana, kama alikuwa na jambo fulani alilotaka kumwambia daktari aliyekuwa akimfuata, alipoufikia mlango, akaufungua na kuingia ndani.

    Dokta Sam aliyekuwa ndani ya ofisi hiyo akamwangalia nesi huyo huku amimshangaa, alitaka kusikia kile alichokuwa amemfuata ndani ya ofisi yake. Nesi huyo akamwambia kwamba mgonjwa aliyekuwa ameletwa ndani ya hospitali hiyo na kupoteza fahamu kwa wiki mbili, hatimaye aliyafumbua macho yake pale kitandani alipokuwa.

    “Unasemaje?”

    “Godson amefumbua macho,” alisema nesi huyo.

    Dk. Sam hakutaka kubaki ofisini kwake, naye akachomoka na kuelekea kule kulipokuwa na chumba alicholazwa Godson, alipofika, akamwangalia kitandani pale, kweli, baada ya kulala kitandani kwa wiki mbili mfululizo huku akiwa hajitambui, hatimaye mgonjwa huyo aliyafumbua macho yake na kuangalia huku na kule.

    Godson hakukumbuka kitu, hakujua mahali alipokuwa palikuwa wapi. Aliangalia huku na kule kwa mshangao mkubwa, alipoiona dripu iliyokuwa ikining’inia juu yake ndipo akagundua kwamba mahali hapo palikuwa ni hospitalini.

    “Nimefikaje?” alijiuliza.

    Hapo ndipo akajaribu kukumbuka tukio la mwisho kabisa alilokuwa amelifanya. Alimbuka kwamba alikuwa ndani ya gari, alipofika Sinza Makaburini kwenye kona ya kuelekea Barabara ya Sam Nujoma, kuna gari lilikuja mbele yake na kuligonga gari alilokuwepo, baada ya hapo, hakukumbuka kitu gani kiliendelea.

    “Nilipata ajali?” alijiuliza kitandani pale.

    Muda wote huo Dk. Sam alisimama pembeni na kumwangalia mwanaume huyo, kwake, kile kilichokuwa kikionekana kilikuwa muujiza mkubwa, hakuamini alichokuwa akikiona mahali hapo.

    Ni kweli walikuwa wakipokea wagonjwa kila siku lakini kwa jinsi Godson alivyokuwa ameumia na kupoteza fahamu, moyo wake ulimwambia wazi kwamba mwanaume huyo asingerudiwa na fahamu na ni lazima angekufa palepale kitandani.

    “Dok..ta...mp..en..zi wan..gu..yup..o wap..i..?” aliuliza Godson kwa tabu kabisa huku akisikia maumivu makali.

    “Subiri! Pata muda wa kupumzika kwanza,” alisema Dk Sam huku akimuweka vizuri kitandani pale.

    Alishindwa kuwataarifu wazazi wake kutokana na muda kwenda sana. Ilikuwa ni saa nane usiku, hakuona kama lingekuwa jambo muhimu kuwapigia simu na wakati asubuhi inayofuata tu watu hao wangekuwa hospitalini hapo.

    Godson hakuacha kumuulizia mpenzi wake, alikuwa hoi lakini hakuona kama hiyo ilikuwa sababu ya kutokuwa na mpenzi wake mahali hapo. Muda ulizidi kusogea huku Godson akitamani kumuona mpenzi wake, Melania.

    Ilipofika saa 1:30 asubuhi, akapewa taarifa kwamba mpenzi wake na wazazi wake walikuwa hospitalini hapo kwa ajili ya kumuona. Akatamani kuonana nao na hivyo muda wa kuona wagonjwa ulipofika, watu hao wakaingia humo ndani.

    Kitendo cha Melania kumuona mpenzi wake akiwa amefumbua macho, akamsogelea, alipomfikia, akamkumbatia huku akitiririkwa na machozi mashavuni mwake. Kilipita kipindi kirefu, alikata tamaa, aliona kama Mungu asingeweza kumrudishia fahamu mpenzi wake, kila alipokuwa akimwangalia, alikuwa akilia tu lakini siku hiyo, machozi yake ya majonzi yakabadilika na kuwa machozi yenye furaha.

    “Umerudiwa na fahamu mpenzi...umerudiwa na fahamu mpenzi...” alisema Melania huku akimwangalia mpenzi wake ambaye kila alipokuwa akijibu, mwili wake ulikuwa ukiuma.

    Furaha ikarudi moyoni mwake, Melania hakutaka kuondoka hospitalini hapo, muda wa kuona wagonjwa ulipokwisha, alitoka ndani na kukaa kwenye mabenchi yaliyokuwepo mahali hapo. Huyo ndiye alikuwa mtu muhimu katika maisha yake, moyo wake ulikosa tumaini, alikataliwa na William, mtu pekee ambaye aliamini kwamba angempa furaha katika maisha yake yaliyobaki alikuwa Godson tu.

    “Mungu! Naomba umponye kabisa mpenzi wangu! Sina furaha, sina amani moyoni. Mungu, unajua kwamba nimeumia sana, naomba unifariji, naomba umponye mpenzi wangu,” alisema Melania huku akiyafuta machozi yake pale kwenye benchi alipokaa.

    ****

    “Inakuwaje washikaji? Niliwaambia mkamuue yule mbweha, mbona hamjakamilisha kazi yangu?” aliuliza Nicholaus huku akiwa ameshika simu.

    “Kazi ipi?”

    “Ya yule mshikaji!”

    “Yule aliyepata ajali Sinza?”

    “Ndiyo!”

    “Mbona alikufa kitambo tu! Nahisi hata kuzika washazika!”

    “Acheni masihara! Huyo mtu hakufa!”

    “Hakufa? Kivipi? Kaka uliuona ule mzinga wenyewe lakini?” aliuliza jamaa aliyekuwa upande wa pili ambaye alikuwa akizungumza na Nicholaus.

    Nicholaus akawaambia kwamba mtu huyo hakufa bali alikuwa hoi hospitalini. Katika kila hatua ambayo Godson alikuwa akipitia, Nicholaus alifuatilia. Kila siku ilikuwa ni lazima kwenda hospitalini na kufuatilia. Alipoambiwa kwamba Godson alikuwa akipata nafuu, moyo wake ulimuuma sana.

    Siku zikakatika na ndipo alipoamua kuwaambia watu hao ukweli kwamba mtu aliyewaambia wamuue alikuwa mzima wa afya na mbaya zaidi hali yake iliendelea kutengemaa mpaka kurudiwa na fahamu.

    Vijana hao wakamwambia kwamba wangekamilisha kazi hiyo haraka iwezekanavyo. Hawakutaka kukaa makao makuu tu bali walichokifanya ni kupanga mikakati ya kumuua Godson palepale kitandani alipokuwa.

    “Huyu tutamuua! Tutajifanya madaktari,” alisema jamaa mmoja.

    “Basi haina shida! Tufanyeni juu chini mpaka tufanikiwe,” alisema kijana mwingine.

    ****

    Mzee yule mwindaji, Caspean Hill aliendelea kupita kwenye bomba lile kubwa kuelekea upande wa pili. Alikuwa akitambaa kwa kasi sana kwa kuamini kwamba wale watu waliokuwa nyuma yake ambao aliwaacha kwenye handaki lile wangeweza kumfuata kule alipokuwa na kumuua.

    Hakutaka kukubali, hakutaka kuona akiuawa kizembe namna ile, aliendelea kwenda mbele mpaka alipofika mwisho wa bomba lile ambapo kwa chini kulikuwa na mto ulioonekana kuganda na barafu kutanda juu yake, alichokifanya ni kupanda kwa juu na kuelekea njia ileile aliyoelekea William.

    Alipiga hatua huku bunduki ikiwa mikononi mwake, tayari alijua kwamba William alikuwa mtu muhimu sana, mwanaume huyo alikuwa fedha, alikuwa utajiri wake ambao piga ua ilikuwa ni lazima ampate na kuwakabidhi CIA ambao walikumtafuta kwa udi na uvumba.

    Alipiga hatua mpaka alipofika katika baada ile aliyokuwa William. Hakuhisi kama mtu huyo alikuwa mahali hapo kwani kwa jinsi alivyoonekana, ilikuwa ni lazima kutoka nje kabisa ya eneo hilo, hivyo akapuuza.

    Alipopiga hatua kadhaa, ghafla akasikia mlio mkubwa wa risasi kutoka ndani ya baa ile. Machale yakamcheza, kitu kilichokuja akilini mwake ni jina la William tu, hivyo kwa haraka sana akaanza kuelekea kule kulipokuwa na baa ile, tena kwa mwendo wa kasi.

    Alipofika kwenye kidirisha kidogo cha kioo, akachungulia ndani, macho yake yakatua kwa watu watano waliomzunguka mtu mmoja mahali hapo. Akapeleka macho yake kwa mtu aliyezungukwa na kugundua kwamba alikuwa William, tena mwanaume mmoja alimnyooshea bastola na kutaka kumpiga risasi nyingine.

    Mzee Caspean hakutaka kuchelewa, hapohapo akanyoonesha bastola yake kwa watu wale na kuachia risasi mbili, moja ikapiga bega la jamaa aliyetaka kumuua William na nyingine ikampata jamaa mwingine maeneo ya ubavuni akaanguka chini na damu kuanza kuwatoka.

    Wale wengine walipoona hivyo, wakaanza kukimbia kwa kupitia mlango wa nyuma. Walichanganyikiwa, walishambuliwa na mtu ambaye hawakujua alikuwa wapi. Si wao tu bali hata wauzaji na wahudumu ndani ya baa ile wote wakakimbia kuelekea nje kwa kupitia mlango wa nyuma.

    Mzee yule akachomoka dirishani na kuelekea kule alipokuwa William, alipomfikia, akamuinamia na kumuweka juu ya kiti na kumtaka kutulia kwani alikuwa kwenye mikono salama, akaanza kumpa huduma ya kwanza.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Wewe ni nani?” aliuliza Mzee Caspean, alijifanya hajui, alitaka kumsikia mwenyewe akilitaja jina lake.

    “William,” alijibu William kwa sauti ndogo.

    “Unafanya nini huku? Na kwa nini unatafutwa?”

    “Nilitekwa!”

    “Ulitekwa? Na nani? Warusi huwa hawatekwi kirahisi!” alisema mzee huyo.

    “Mimi siyo Mrusi!”

    “Siyo Mrusi! Ni nani sasa?”

    “Mwafrika!”

    “Mwafrika? Kivipi?”

    William akaanza kumwambia kila kitu kilichotokea, Mzee Caspean hakuamini, alimwangalia vizuri mtu huyo, ilikuwa vigumu kugundua kama alikuwa Mwafrika. Akamnyanyua na kumpeleka bafuni, huko, akachukua maji ya moto kidogo na kumwagia na kuanza kumtoa sura ambayo aliambiwa kwamba alikuwa nayo.

    Kweli, alipoanza kumtoa sura ile ya bandia ndipo akaamini kwamba mtu huyo alikuwa Mwafrika kama alivyosema. Hakuishia hapo, mwili mzima alikuwa amebandikwa vitu vilivyoonyesha kwamba alikuwa Mrusi hivyo kutolewa vyote na kubaki kama alivyozaliwa.

    Mzee Caspean alishangaa, hakuamini kile alichokiona. Mwanaume aliyesimama mbele yake alikuwa mbaya mno, alifanana na sokwe, yeye mwenye alitamani kukimbia kwani alihisi kwamba mtu huyo hakuwa binadamu, bali alikuwa mfano wa sokwe mtu.

    “Nahitaji laptop,” alisema William huku akionekana kuwa na maumivu makali.

    “Laptop tu au kompyuta yoyote?” aliuliza mzee huyo.

    “Yoyote ile.”

    “Sidhani kama tunaweza kuipata. Hebu tutoke hapa.”

    Wakatoka na kuelekea nje huku Mzee Caspean akiwa amemshika kwa kuupitisha mkono wa William begani mwake, huko, wakaanza kuangalia huku na kule, kwa bahati nzuri kwao wakafanikiwa kuziona nyumba kadhaa na hivyo kuifuata nyumba moja ambayo nje kulikuwa na theluji kila kona, tena nyingine zikiendelea kudondoka.

    Walipoifikia, wakagonga mlango ambapo baada ya sekunde kadhaa, ukafunguliwa na msichana mmoja aliyeonekana kuwa mrembo wa sura. Alipomuona William, ilikuwa bado kidogo aufunge mlango kwani alimuogopa mno, hakuamini kama huyo alikuwa binadamu, alihisi Mzee Caspean alikwenda hapo na sokwe.

    “Tunahitaji msaada wako!” alisema Mzee Caspean, wakati akiyazungumza maneno hayo, alikuwa akiusukuma mlango na kuingia ndani.

    “Msaada gani?”

    “Kompyuta!”

    Kwanza msichana huyo aliogopa, hakujua watu hao walikuwa wakina nani na kwa nini walihitaji kompyuta. Walimwambia kwamba walikuwa watu wazuri ambao hawakuwa na tatizo lolote lile, msichana huyo hakuridhika, William akamwambia kwamba yeye ndiye alikuwa William, mwanaume aliyeanzisha Mtandao wa MeChat.

    “Wewe ndiye William wa MeChat?” aliuliza msichana huyo huku akionekana kushtuka.

    “Ndiyo!”

    Kitu cha kwanza alichokifanya msichana huyo ni kuchukua boksi kubwa la chumba lililoandikwa Fist Aid Kit ambalo lilikuwa na dawa kadhaa kisha kuanza kumuhudumia William aliyeonekana kuwa kwenye maumivu makali.

    Baada ya msichana huyo kumaliza kumuhudumia William, akasimama na kuelekea ndani, baada ya sekunde kadhaa akarudi huku akiwa ameongozana na kaka yake ambaye sura yake ilionyesha tabasamu pana, hakuamini kama siku hiyo William alikuwa ndani ya nyumba yao.

    Mtandao wake ulikuwa umekimbiliwa kwa kasi, watu walikuwa wakiutumia, ndani ya muda mchache ulikuwa na watu wengi kupita kawaida. Kaka wa msichana huyo alipomuona William, hakuamini, alimfahamu kwa kuwa mara ya kwanza alimuona kwenye televisheni.

    Alichokifanya ni kupiga naye picha kwa staili ya selfie huku akionekana kuwa na furaha kupita kawaida. Alipomaliza, akamgawia laptop kama alivyoomba, William akaifungua na kuanza kubadilisha baadhi ya vitu katika mtandao wake.

    “Unaweka nini?”

    “Subiri. Utaona,” alisema William huku akiendelea kuchezea kompyuta yake, alichokifanya kaka wa msichana yule ni kuzichukue zile picha alizopiga na William kisha kuzituma kwenye akaunti yake kama lengo la kuwaambia marafiki zake kwamba alikuwa mtu wa kwanza kupiga picha na mwanzilishi wa mtandao huo.

    “I make them feel jealous on me,” (nataka wasikie wivu juu yangu) alisema kijana huyo huku akitabasamu.

    ****

    Maofisa wa CIA na FBI walichanganyikiwa, waliwasiliana na wenzao waliokuwa nchini Canada na kuwauliza kuhusu William lakini watu hao waliwaambia kwamba hawakufanikiwa kumpata William. Hawakujua tatizo lilikuwa nini kwani Mzee Caspean aliwapigia simu na kuwaambia kwamba alikuwa na William nyumbani kwake, sasa kwa nini wasimpate?

    Waliwauliza kama walikutana na huyo mzee, maofisa hao wakawaambia kwamba walikutana na ugumu kwani dalili zinaonyesha kwamba simu zao walizitraki, kwani walipofika hapo, tayari Warusi walikuwa mahali hapo na walimchukua mzee huyo na kwenda naye huko.

    “Mmh! Warusi? Inakuwaje?”

    Maofisa hawakuishia hapo, waliwaambia kila kitu kwamba hata baada ya kwenda kwa mzee huyo, walikuta Warusi wale wakiwa wameuawa kwa risasi na moja kwa moja kumuhusisha mzee huyo ambaye aliwakimbia kwa kupitia kwenye bomba ambalo hawakujua lilipokuwa likiishia.

    “Kwa hiyo William hamkumkuta?”

    “Ndiyo mkuu!”

    “Ooh!”

    Kilikuwa ni kitendo kidogo cha kumfuata William nchini Canada na kumchukua lakini ilionekana kuwa na ugumu sana. Maofisa hao wakachanganyikiwa, hawakuelewa sababu zilizozifanya harakati zao za kumpata William kuwa ngumu kiasi hicho.

    Wakati wakiendelea kutafakari ni kitu gani walitakiwa kufanya, msichana mmoja akaingia humo huku akionekana kuwa na haraka sana, alipofika, akachukua simu yake na kuwaonyeshea kitu maofisa hao.

    Ilikuwa ni picha ya William ambapo alikuwa amepiga na jamaa fulani ambaye kwenye Mtandao wa MeChat alikuwa akitumia jina la O’Brein Cook. Waliiangalia picha ile, William alionekana kuwa kwenye maumivu makali, kwa begani alikuwa akitokwa na damu, japokuwa alifungwa bandeji lakini damu hazikuzuilika kumtoka.

    “Track the location,” (Lichunguzeni eneo husika) alisema mkuu wa CIA.

    Hilo ndilo lilofanyika, wakaichukua picha ile na kuiingiza kwenye kompyuta zao na kuangalia mahali ilipokuwa imepigwa. Hiyo haikuwa kazi kubwa, ndani ya dakika tano tu majibu yakasoma kwamba picha ile ilikuwa imepigwa nchini Canada katika eneo lililoitwa Winnipeg nchini Canada.

    “It’s not far away from where they are,” (si mbali kutoka pale walipo)

    “Yeah!”

    Hapohapo wakawapigia simu wenzao na kuwaambia mahali William alipokuwa, ilikuwa ni lazima kwenda huko tena haraka iwezekanavyo kwani dalili zilionyesha kwamba kama wangeshindwa kumpata basi Warusi wangeweza kufanya lolote liwezekanalo kumpata.

    “Si mbali sana na hapa! Tunakwenda!” alisema jamaa aliyekuwa Canada na hivyo kuanza kwenda huko.

    ****

    “Kwanza ilikuwaje?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nilikuwa nikiishi na baba yangu! Alikuwa akinipenda sana. Maisha yalikuwa mazuri mno, mpaka kufikia kipindi hicho sikuwa nimemfahamu mama yangu. Baada ya kufikisha miaka kumi na nane, baba akanionyeshea mama yangu! Alikuwa mwanamke mzuri sana, alipendeza mno, sura yake ilifanana na sura yangu, aninivutia mpaka mimi mwenyewe.

    “Kilio changu siku zote kilikuwa ni kuuwataka warudiane, sikuwa na furaha kuwaona wakiishi mbali mbali hivyo ili kunifanya binti yao nifurahi, wakakubali kuishi pamoja. Maisha yalikuwa mazuri, nilijiona mtu mwenye furaha kuliko watu wote duniani. Baada ya mwaka mmoja, baba yangu akafariki kwenye ajali ya gari iliyotokea Manhattan hivyo kuishi na mama yangu ambaye baadaye aliolewa na mwanaume katili, aliyenitesa na kunipa msongo wa mawazo,” alisema msichana mmoja aliyeitwa Cassey Mike.

    Kwa kumwangalia, alikuwa msichana mrembo, alivutia, sauti yake nyororo aliyokuwa akiitumia kuongelea iliwapagawisha wanaume wengi. Alikuwa katika kipindi cha Jerry Springer, alikuwa akiyahadithia maisha yake aliyopitia kipindi cha nyuma.

    Japokuwa ilikuwa ni historia tu lakini kila mtu aliyekuwa akiisikiliza aliumia moyoni mwake. Alikuwa msichana mdogo, mwenye utajiri mkubwa lakini hakukuwa na aliyeamini kama kweli alipitia maisha hayo yenye kumsisimua kila mtu aliyekuwa akimsiliza.

    “Ikawaje?” aliuliza Jerry, watu wote waliokuwa wakikifuatilia kipindi hicho walikuwa kimya, Casey ndiye aliyeutawala ukumbi huo huku kituo cha televesheni cha CNN kikionyesha moja kwa moja kilichokuwa kikiendelea huku kila mtu akitaka kusikia kwa kifupi maisha aliyopitia msichana huyo bilionea na mwanamitindo maarufu duniani.



    Msichana Cassey aliendelea kusimulia historia ya maisha yake, kila mtu aliyekuwa akimsikiliza aliumia moyoni mwake, matukio aliyokuwa amepitia, jinsi baba wa kambo alivyomtesa, wanawake waliomsikiliza walikuwa wakitiririkwa na machozi tu.

    Hiyo ilikuwa historia ya maisha yake. Iliisha, ilipita na katika kipindi hicho alikuwa na maisha mengine kabisa, maisha ya kuogelea katika ulimwengu wa pesa. Alikuwa na kiasi kikubwa cha pesa, alimiliki kampuni, magari ya kifahari na nyumba za bei mbaya zilizokuwa Las Vegas. Calfornia na sehemu nyingine nyingi nchini humo.

    Kila alipokuwa, watu walimuheshimu Cassey, japokuwa alikuwa binti mdogo lakini alipendwa mpaka na mabilionea wengi ambao kila siku walitamani hata kulala naye kitandani.

    Cassey hakuwa mwepesi, aliwachukia wanaume kwa ajili ya baba wa kambo. Mambo aliyofanyiwa katika maisha yake, kwake, kila mwanaume aliyekuwa akikutana naye alionekana kama shetani. Hakuwa mwepesi, hakujirahisisha hata kidogo, kwake, ilikuwa ni bora kufanya mapenzi na midoli ya kiume kuliko mwanaume.

    “Na vipi kuhusu wanaume?” aliuliza Jerry Springer.

    “Ninawachukia wanaume, sipendi hata kuwaona,” alisema Cassey huku akimwangalia Jerry.

    “Kwa hiyo hata mimi unanichukia?”

    “Hahah! Jerry bhana! Kwani wewe unanitaka?” aliuliza Cassey na kuanza kucheka.

    Alichokizungumza ndiyo ukweli wenyewe. Kulikuwa na wanaume wengi waliomfuata na kumwambia walimpenda lakini aliwakatalia. Walikwenda mabilionea, wacheza filamu, tenisi, waendesha magari ya Formula One, wachezaji wa kikapu na baseball lakini wote hao aliwakatalia kwa kuwaambia kwamba aliwachukia wanaume mno.

    Tangu alipokuwa akibakwa na baba wa kambo, hakutaka tena kuwa na mpenzi, kwa kuwa aliwachukia wanaume, alichokifanya ni kununua mdoli wa kiume nchini China na kuupeleka nyumbani kwake, California, na ndiyo mdoli ambao ulimaliza shida zake kitandani.

    Hayo yalikuwa maisha yake, hakutaka kuficha, aliwaambia watu wengi kwamba alishiriki mapenzi na mdoli uliokuwa nyumbani kwake. Wengi walimshangaa, walimuona mtu wa ajabu lakini hakutaka kujali, bado msisitizo wake ulikuwa uleule kwamba aliwachukia wanaume.

    Baada ya kuzungumza sana, akamwambia Jerry kwamba alitaka kutengeneza kitabu cha maisha yake, alitaka kuwaandikia wale waliokuwa wakilelewa maisha ya hovyo kwamba bado walikuwa na nafasi ya kupata mafanikio, haikujalisha walipitia matatizo gani, kama Mungu alitaka kuwanyooshea katika maisha yao basi wangefanikiwa na kuwa matajiri wakubwa huko mbele.

    Alipoondoka katika ukumbi huo alipokuwa akifanyiwa mahojiano, akaelekea nyumbani kwake. Kichwani mwake alikuwa na mawazo tele, alitaka kuandika kitabu cha historia ya maisha yake, alitaka kuyaweka maisha hayo kwenye kitabu, akutane na mwandishi wa vitabu na kumuandikia lakini hakujua ni nani alistahili kukiandika kitabu hicho.

    “Labda Chilongani,” alijisemea ndani ya gari.

    Monye Chilongani Mtanzania aliyekuwa akiishi Philadelphia nchini Marekani, alikuwa mmoja wa waandishi wakubwa duniani. Alikuwa miongoni mwa waandishi walioandika vitabu vya watu wengi akiwemo Barack Obama, Celine Dion, Tiger Woods na wengine wengine. Kwake, mwandishi huyo alionkana kuwa bora hivyo alichokifanya ni kutafuta mawasiliano naye na kumpigia simu.

    “I can’t do that right now,” (siwezi kufanya hivyo kwa sasa?) alisema mwandishi huyo alipopigiwa simu.

    “Why?” (kwa nini?)

    “I got something to do Cassey, but thank you,” (nina kitu cha kufanya, ila nashukuru)

    “What is it?” (kitu gani?)

    “I do write Trump’s book, so I’ve to travel here and there. Maybe, let’s do it next year,” (ninaandika kitabu cha maisha ya Trump kwa hiyo natakiwa kusafikiri huku na kule. Labda tufanye mwaka ujao) alisema Monye kwenye simu.

    “Next year? I can’t wait.” (mwaka ujao? Siwezi kusubiri)

    Hakuwa na jinsi, alitamani sana kitabu chake kiandikwe na mwandishi huyo lakini iliposhindikana, akaamua kuwatafuta waandishi wengine na kufanikiwa kumpata mwandishi wa Kifaransa aliyeitwa Babi D’e Consious ambaye ndiye alitakiwa kukiandika kitabu hicho.

    “Hakuna shida. Dola milioni 1.5,” alisema Babi.

    “Hakuna tatizo!”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hilo likamalizika na kilichokuwa kimebaki ni kuendelea kuwasiliana na mwandishi huyo ambaye alifika nchini Marekani na kuanza kukiandika kitabu hicho. Muda mwingi aliokuwa akisimulia matukio yaliyokuwa yakitokea, Cassey alikuwa akilia, hakuamini kama kulikuwa na binadamu ambaye aliwahi kupitia maisha kama aliyokuwa amepitia kipindi cha nyuma.

    Siku zikakatika, baada ya kukatika miezi miwili, kitabu kikakamilika, kikachapishwa na kitu kilichokuwa kimebaki ni kukitangaza kwa ajili ya kuingia sokoni. Akawatafuta watu wengi ambao walimsaidia kumfanyia matangazo mbalimbali, alipomaliza, kuna sehemu moja tu ambayo alitakiwa kufanya matangazo hayo, sehemu yenye nguvu ambayo aliamini kwamba ingemsaidia kuuza.

    “Ni lazima nikitangaze kwenye Mtandao wa MeChat kwa ajili ya kuwafikia watu wengi zaidi,” alisema msichana huyo, alichotakiwa kufanya ni kuwasiliana na William, mmiliki wa mtandao huo kwa ajili ya kumfanyia kazi yake.

    ****

    Linda hakuwa na furaha, moyo wake ulikuwa na mawazo mno. Muda mwingi alikuwa akilia akimtaka Mungu amrudishe mpenzi wake salama nyumbani. Hakuacha kuwasiliana na maofisa wa FBI na CIA ambao pia walitumia muda wao mwingi kuwaweka walinzi wao alipokuwa akiishi kwa kuamini kwamba Warusi wangeweza kumteka ili William awafanyie kazi yao.

    Tangu mpenzi wake atekwe, zilipita siku mbili hakuwa amelala, kitanda kilionekana kuwa na miba kila sehemu, asingeweza kulala na wakati mpaka muda huo hakujua mahali alipokuwa mpenzi wake.

    Maofisa wa FBI walimpa moyo kwamba mpenzi wake angeweza kupatikana, hakutaka kuliamini hilo kwa asilimia mia moja, alitaka kuona likifanyika na kuletewa nyumbani kwake, hapo ndipo angeamini kwamba kazi ilifanyika na kuwa na amani moyoni mwake.

    Siku ya tatu ilipoingia, akapigiwa simu na kuambiwa kwamba William alipatikana nchini Canada katika Mji wa Winnipeg. Hakuamini, akataka kumuona au kuwasiliana naye. Hilo halikuwezekana kwani kwa kipindi hicho William alikuwa kwenye hali mbaya kutokana na risasi alizokuwa amepigwa.

    “Ila ninataka kuzungumza naye!”

    “Utazungumza naye akifika. Kwa sasa yupo kwenye hali mbaya,” alisikika mwanaume kwenye simu.

    “Atakufa?” aliuliza huku akilia.

    “Hapana! Hawezi kufa,” alijibu mwanaume huyo na kukata simu. Japokuwa aliambiwa kwamba mpenzi wake asingekufa, moyo wake ulikuwa na hofu kupita kawaida.

    ****

    Maofisa wa CIA hawakuchelewa, kwa haraka wakafika mahali ambapo waliambiwa kwamba William alikuwepo. Walipofika hapo, wakaizunguka nyumba na kuingia ndani huku wakipiga kelele kwamba wao walikuwa CIA.

    Mzee Caspean baada ya kusikia hivyo, akatupa bastola yake chini, wanaume wanne wakaingia na kumuweka chini ya ulinzi na kumbeba William aliyekuwa kwenye kochi huku akiwa hoi. Hawakuzungumza kitu, yeye na mzee huyo wakapakiwa kwenye gari na kuondoka mahali hapo.

    William alikuwa akilia kwa maumivu makali. Alipoteza kiasi kikubwa cha damu na kadiri dakika zilivyokuwa zikisonga mbele zilionyesha kwamba angeweza kufariki akiwa njiani. Wakafika salama mjini Winnipeg ambapo akapelekwa katika Hospitali ya St. Carthbert ambapo akalazwa kitandani huku akiwa hoi.

    Madaktari wakaanza kuifanya kazi yao, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kutoa risasi zilizokuwa mwilini mwake. Kila mmoja alishangaa, kwa jinsi alivyokuwa amejeruhiwa ilikuwa vigumu sana kwa mtu kukaa kwa kipindi kirefu huku akiwa hai kwani alikuwa na majeraha makubwa katika sehemu zile alizokuwa amepigwa risasi.

    Simu zikapigwa mpaka nchini Marekani, wakawaambia kwamba William alipatikana akiwa hoi na katika kipindi hicho alikuwa akitibiwa hospitalini. Kila mmoja akaonekana kuwa na furaha tele, hawakuamini kama maofisa wa CIA wangefanya kazi hiyo kwa haraka sana mara baada ya kupewa taarifa juu ya mahali alipokuwa mtu huyo.

    Baada ya kukaa kwa saa moja na kutibiwa huku akiandaliwa kwa ajili ya safari, William na Mzee Caspean ambaye kichwa chake kiliendelea kufikiria pesa, wakachukuliwa na kupelekwa ndani ya ndege kwa ajili ya kupelekwa nchini Marekani.

    Kutoka Winnipeg mpaka Marekani haikuwa mbali, walichukua dakika arobaini na tano tu, ndege ikaanza kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JFK jijini New York ambapo hapo kulikuwa na magari zaidi ya kumi yakiwasubiri watu hao.

    “How is he?” (anaendeleaje?) aliuliza jamaa mmoja.

    “He is just fine,” (anaendelea vizuri tu)

    Wote wakachukuliwa na kupakizwa ndani ya gari ambalo lilianza safari ya kuelekea katika Hospitali ya Main View Medical Center iliyokuwa hapohapo New York. Msafara wake ulikuwa mkubwa, zaidi ya magari kumi yalikuwa yakiongoza huku kila mtu aliyekuwepo katika msafara huo akiwa na silaha nzito kwani mtu waliyekuwa wakimlinda alikuwa na heshima kubwa, mtu ambaye alionekana kuwa na thamani kuliko hata waziri mkuu wa nchi hiyo.

    Hawakuchukua muda mrefu wakafika hospitalini hapo ambapo William akaanza kupatiwa matibabu huku chumba alichokuwepo kikilindwa kwa ulinzi mkali kwa kuepuka kutekwa tena na Warusi, ulinzi huo haukuwa ndani tu, hata nje ya jengo hilo bado kulikuwa na watu waliokuwa na silaha, kwa muonekano tu, ilionyesha kama rais wa nchi hiyo alikuwa humo kupata matibabu.

    Siku hiyohiyo baada ya Linda kupigiwa simu, akaondoka jijini Massachuesetts na kuelekea New York huku akiwa kwenye hali ya ujazito aliyokuwa nayo. Ndani ya ndege, kichwa chake kilikuwa kikimfikiria mpenzi wake, alimuomba Mungu kwa hali aliyokuwa nayo, hakutaka kumuona mwanaume huyo akiondoka mikononi mwake kwani ndiye mtu pekee ambaye aliamini kwamba angeweza kumfariji katika maisha yake.

    Alipofika, akapokelewa na kupelekwa huko hospitali. Kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kuelekea hospitalini huku maofisa wa CIA wakiwa wanamlinda kila hatua kwa kuepuka utekaji, akachukuliwa mpaka hospitalini huko.

    Kitendo cha kumuona mpenzi wake kitandani, akatabasamu, naye William akarudisha tabasamu pana. Akamsogelea pale alipokuwa na kumjulia hali. William akafurahi mno, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kulishika tumbo la Linda.

    “Anaendeleaje?” alimuuliza Linda.

    “Ni mzima! Anaendelea vizuri na amekukumbuka pia,” alisema Linda huku akiachia tabasamu pana.

    Rais akapigiwa simu na kuambiwa kwamba William alipatikana na walikuwa naye mikononi mwao. Japokuwa kulikuwa na ulinzi mkubwa lakini rais huyo akaagiza ulinzi uongezeke kwani mtu waliyekuwa naye alikuwa muhimu kuliko katiba ya nchi hiyo kipindi hicho.

    Hilo likafanyika, polisi wakawekwa, ndani ya hospitali hiyo, wakawekwa maofisa wengine wa CIA waliojifanya kuwa madaktari kumbe nyuma ya pazia bado waliendelea kuhakikisha ulinzi unafanyika vya kutosha humo ndani.

    Watu walipotangaziwa kwamba William amepatikana, kila mmoja akashusha pumzi, wakafurahi kwani wengi wakaona kwamba huo ndiyo ulikuwa muda wa kuutumia Mtandao wa MeCat uliokuwa ukijiendesha wenyewe, tena kwa kasi kubwa huku mamilioni ya watu wakiendelea kujiunga kila siku.

    Mzee Caspean hakutaka kuondoka, moyo wake ulikuwa na furaha, hakuamini kama kweli William yule aliyekuwa amemsikia kwa kipindi kifupi, genius aliyekuwa ametikisa dunia ndiye yule ambaye alimsaidia, moyoni mwake akajiona mkombozi ambaye alitakiwa kuheshimiwa na kila mtu kwani bila yeye, mtu huyo angeweza kuuawa kitambo tu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    William alikaa hospitalini kwa muda wa mwezi mzima ndipo aliporudi nyumbani kwake. Akaendelea kuingiza fedha kupitia mtandao wake ambao ulionekana kuwa bora kuliko mitandao yote duniani.

    Makampuni hayakuacha kujiunga na kujitangaza huko, kila siku ilikuwa ni lazima kampuni mpya kujiunga na kumpa kiasi kikubwa William. Akaanza kuwa bilionea, kwake, hakuangalia pesa, hakuangalia heshima, kitu pekee alichokiangalia ni kuwapa watu kile walichokuwa wakikihitaji.

    Hakutaka kumuacha Mzee Caspean, aliyaokoa maisha yake, aliuthamini mchango wake hivyo baada ya kulipwa dola milioni moja, William akamuongezea nyingine na kumnunulia jumba kubwa la kifahari pembezoni mwa Jiji la Ottawa nchini Canada, karibu na bahari.

    “Hii ni yangu?” aliuliza Mzee Caspean mara baada ya kutumiwa picha ya jumba alilonunuliwa.

    “Ndiyo! Hiyo ni nyumba yako!”

    “Siamini!”

    “Ishi katika imani! Hii ni nyumba yako!” alisema William huku akiachia tabasamu pana.

    Siku ziliendelea kukatika, baada ya mwezi mwingine kuingia, akapokea ujumbe mfupi wa maneno kutoka kwa msichana mrembo, Cassey aliyetaka kuonana naye kwa kuwa alikuwa na kazi kubwa aliyotaka kufanya naye.

    Alishangaa, alizoea kumsoma msichana huyo kwenye majarida, umaarufu wake, utajiri wake ulitisha sana na hakuamini kama kipindi hicho msichana huyo alitaka kuonana naye. Hilo halikuwa tatizo, akawasiliana naye na kumwambia amfuate ofisini kwake, ndani ya saa mbili, msichana huyo alikuwa amekwishafika.

    “Ninataka kumuona William,” alisema Cassey.

    Dada wa mapokezi aliambiwa kuhusu yeye, hakukuwa na tatizo, akamchukua na kumpeleka katika ofisi ya bosi wake. Alipofika, wakasalimiana na msichana huyo kukaa kwenye kochi, akakunja nne, upaja wake mweupe, ulionona, uliofunikwa na sketi yake fupi ukaonekana, William akaukodolea macho kama vile aliona kitu kigeni.

    “Unashangaa nini?” aliuliza Cassey huku akiachia tabasamu, na kwa mbali alijiweka vizuri ili upaja uendelee kumtoa udenda mwanaume huyo.

    “Jinsi Mungu anavyojua kuumba. Mungu fundi sana aisee,” alisema William huku akimwangalia Cassey kwa jicho lililomaanisha kitu cha tofauti kabisa.

    Japokuwa msichana huyo alicheka kwa kuhisi kwamba ni masihara, lakini kwa William, kile alichokizungumza alimaanisha, alitokea kuvutiwa na msichana huyo lakini kabla hajasema kitu chochote juu ya uzuri aliokuwa nao Cassey, picha ya Linda akiwa kitandani ikamjia kichwani mwake. Akachanganyikiwa.



    Vijana watatu walikuwa wamejipanga kwa ajili ya kukamilisha kazi waliyokuwa wamepewa na Nicholaus ya kumuua Godson aliyekuwa kitandani. Kwao, haikuwa kazi ngumu hata kidogo kwani kila walipofikiria namna ulinzi wa hospitali nyingi za Kitanzania kuwa hafifu, walijua kabisa wangefanikiwa kile walichotaka kukifanya.

    Wakaingia dukani, ilikuwa ni lazima kujifanya madaktari ili iwe rahisi kwao kufanya mauaji ya mgonjwa Godson aliyekuwa kitandani. Huko, walipata makoti meupeya kidaktari waliyotaka kuwa nayo, wakanunua mashine za stethoscopes zilizokuwa zikitumika kusikilizia mapigo ya moyo kwa mgonjwa.

    Hawakuishia hapo bali walinunua mpaka miwani, walihitaji kuwa na muonekano kama madaktari, hawakutaka watu wafahamu kwamba hawakuwa madaktari katika hospitali hiyo.

    Walipohakikisha wamepata kila kitu, wakaanza safari ya kuelekea katika hospitali hiyo kwa ajili kufanya kazi hiyo waliyotakiwa kufanya. Siku ya kwanza haikuwa ya kumuua Godson bali walikwenda kuangalia usalama wa hospitali hiyo kubwa, kama je, wangeamua kwenda kufanya mauaji, kulikuwa na ulinzi wa kutosha?

    Walipofika, wakajigawa na kuanza kufanya mambo yao. Walitembea katika wodi mbalimbali, walizungumza na wagonjwa. Hakukuwa na daktari yeyote aliyeonekana kuwashtukia, kutokana na wingi wa madaktari hospitalini hapo, ilikuwa ni vigumu kuwatambua.

    Walifanya uchunguzi wao na kugundua chumba alichokuwa Godson, hakukuwa na ulinzi wowote, waliangalia kisiri jinsi madaktari na manesi walivyokuwa wakiingia ndani ya chumba hicho ambacho kwa nyuma kilikuwa na mlango mwingine.

    “Ni kazi nyepesi mno kufanyika, hebu turudini,” alisema jamaa mmoja aliyeitwa Kibra ambaye alikuwa na muonekano halisi wa kidaktari.

    Wakaondoka na kurudi kujipanga. Mwanzoni waliiona kazi hiyo kuwa kubwa na ya hatari kiasi kwamba walihofia hata kuifanya lakini baada ya kwenda kwa ajili ya uchunguzi, waliona kuwa haikuwa kazi ngumu hata kidogo.

    Walipofika kambini wakawasiliana na Nicholaus, wakamwambia kwamba kazi aliyokuwa amewapa kwa mara hiyo ya pili ingefanyika kwa urahisi zaidi kwani mtu waliyetakiwa kumuua, mpaka kumfikia hakukuwa na ugumu wowote ule.

    “Yaani hakuna ugumu kabisa!”

    “Kweli?”

    “Yeah! Yaani ni kama kumsukuma mlevi kwenye mteremko wa mlima,” alisema Kibra.

    “Basi sawa! Naomba mfanye hivyo haraka sana!”

    Nicholaus akawa na matumaini makubwa kwamba kazi yake ingefanyika kwa haraka zaidi. Hakumpenda Godson, hakufanya hivyo kwa kuwa alimfahamu vizuri, hakumfahamu sana lakini kwa kitendo cha kumchukua Melania ndicho kilichomkasirisha zaidi.

    Hakutaka kumuona Melania akiwa na furaha, alijitahidi kumuwekea maumivu makubwa moyoni mwake na ndiyo maana alijitahidi kufanya kila liwezekanalo ili alie, abubujikwe na machozi katika maisha yake yote.

    Aliwaamini vijana hao, aliwaona wakiwa na umakini mkubwa kwani hata walipomwambia mbinu waliyokuwa wameitumia, aliwasifia kwamba walifanya kazi kubwa sana na walihitaji pongezi.

    Siku mbili mbele, Kibra na wenzake wawili, Ibra na Badi wakarudi katika hospitali ile. Muonekano wao ulikuwa uleule, ilikuwa vigumu sana kugundua kwamba watu hao hawakuwa madaktari bali walikuwa wauaji ambao walitumwa hospitalini hapo kwa ajili ya kufanya kazi yao tu.

    Waliwaangalia wagonjwa, wakawafariji na wakati mwingine wakiwaandikia vidonge ambavyo walitakiwa kuvichukua. Kutokana na ukubwa wa hospitali hiyo, ilikuwa ni vigumu kwa madaktari kujuana, hivyo kila mtu aliyeonekana kuvaa koti kubwa walihisi kwamba ni daktari wa kweli, na mbaya zaidi katika kipindi hicho kulikuwa na wanafunzi wengi waliofika kwa ajili ya kufanya ‘field’.

    Wakati wanaendelea na mambo yao humo, wakaugundua ule mlango uliokuwa nyuma katika chumba alicholazwa Godson, hivyo Ibra na Badi wakaelekea kule nyuma huku wakimwacha Kibra ambaye alijiandaa kwa kwenda ndani ya chumba kile, afanye mauaji na apite mlango wa nyuma.

    Ndani ya mfuko wa kulia wa koti lake alikuwa na kisu kidogo huku katika mfuko wa kushoto akiwa na kitambaa kizito, alitaka kuingia ndani ya chumba hicho na kisha kumziba pua na mdomo kwa kitambaa kile kisha kumuua kitandani hapohapo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kuona hali ni ya amani kabisa, dakika ishirini kabla ya muda wa kuwaona wagonjwa kuwadia, harakaharaka Kibra akaanza kwenda katika chumba kile. Alipofika kwenye korido, macho yake yakatua kwa wazazi wa Godson waliokuwa na Melania kwenye mabenchi, akasogea mpaka kule walipokuwa, walipomuona, hakukuwa na aliyejua kama mtu huyo hakuwa daktari kama madaktari wengine.

    Uso wake ulionyesha tabasamu pana lililoficha ukatili wake, kwa kumwangalia harakaharaka alionekana kama daktari mzoefu, aliyekuwa na digrii yake kichwani kumbe upande wa pili alikuwa muuaji mkubwa tu.

    “Za hizi?” aliwasalimia huku akiachia tabasamu lillowadanganya watu hao.

    “Safi tu daktari!”

    “Poleni kwa kuuguliwa!”

    “Tunashukuru!”

    Walipojibu, hakutaka kupoteza muda wake mahali hapo bali akaufungua mlango na kuingia ndani. Alipofika, macho yake yakatua kwa Godson aliyekuwa amelala kitandani. Kwa mwendo wa taratibu, wa madaha kabisa akaanza kumsogelea ambapo baada ya kumfikia, akatoa kitambaa chake mfukoni tayari kwa kuziba pua na mdomo kisha kumchoma visu mfululizo na kukimbia kupitia mlango wa nyuma.

    “Pumzika kwa amani mshikaji wangu,” alisema Kibra, hapohapo akatoa kitambaa chake na kumziba Godson aliyeanza kukukuruka kukiondoa kitambaa hicho kilichomziba vilivyo.

    ****

    Hakutaka kujificha, alijitahidi kujizuia kumpenda msichana Cassey lakini ilishindikana kabisa. Kila alipomuweka Linda kichwani mwake, msichana huyo alitoka na moyo wake kuanza kumtamani mrembo aliyekuwa ofisini huko.

    Upaja wake ukazidi kumdatisha, kila alipozungumza naye hakuacha kumsifia, alimpa sifa kemkem mpaka nyingine hakustahili kuwa nazo. Naye Cassey ni kama alijua, akajitanua zaidi na kumfanya William kuwa hoi, kila alipoendelea kuuangalia upaja ule, udenda ulimtoka kama fisi aliyeuona mfupa.

    “Unanitania sana William,” alisema Cassey huku akimwangalia mwanaume huyo.

    “Siwezi kukutani! U msichana mrembo sana aisee! Utadhani hukuzaliwa, ni kama umeshushwa kutoka mbinguni,” alisema William hakuona kama hiyo ilitosha, akasimama na kuanza kumsogelea msichana huyo.

    “Nashukuru sana!”

    “Labda Mungu alikupendelea, udongo aliokuumbia wewe ni tofauti kabisa na wetu,” aliendelea kumsifia.

    “Mmh!”

    “Kweli tena! Hebu jiangalia hata wewe mwenyewe, angalia jinsi tabasamu lako lilivyokuwa tamu, angalia jinsi unavyocheka, meno yako meupe yaliyopangiliwa vizuri yanavyoonekana. Cassey, nimewahi kuwaona wanawake wengi ila sijawahi kumuona malaika kama wewe,” alisema William.

    Moyo wake ukafa na kuoza, alisahau kabisa kama kulikuwa na mtu aliyeitwa Linda. Moyo wake ukaangukia katika penzi la msichana huyo. Akaendelea kupiga hatua kumsogelea msichana huyo, alipomfikia, akamshika shingoni.

    Yeye mwenyewe hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea, siku hiyo alionekana kama mtu aliyeingiwa na pepo la ngono. Kwa sababu alisifiwa sana, kichwa cha Cassey kikavimba na kuachia tabasamu pana, akajiona kuwa mrembo zaidi ya wanawake wote.

    “Ninajaribu kumfikiria Mungu, alitumia muda gani kukutengeneza wewe, manake sisi wengine wabaya alitumia dakika kumi ila naamini kwako alitumia zaidi ya saa mbili, ili uje kutuchanganya wanaume marijali kama sisi,” alisema William.

    Hakutaka kuzungumza maneno mengine zaidi ya hayo. Ingawa msichana Cassey aliwachukia sana wanaume lakini kwa William, kwa jinsi alivyokuwa akimsifia, ubaya wake haukuonekana kabisa, alijiona akiwa amekaa karibu na mwanaume mwenye sura nzuri sana.

    William alimsifia kwa zaidi ya dakika kumi ndipo walipoanza kuzungumza kile kilichomleta msichana huyo ofisini humo. Kwake, halikuwa tatizo kabisa, msaada aliouhitaji Cassey haukuwa na tatizo kabisa na kwa sababu alitaka kumvuta zaidi mikononi mwake, hata kiasi cha fedha alichotakiwa kulipia kwa ajili ya matangazo juu ya kitabu hicho hazikuhitaji, aliambiwa kwamba kila kitu kingefanyika bure kabisa.

    “Kweli?”

    “Ndiyo! Nikutoze hela ili iweje.”

    Muda wote William aliongea kiutani lakini alikuwa akimaanisha moyoni mwake. Mbele yake alimuona amekaa msichana mrembo sana, hakutaka kumtoza kiasi chochote cha fedha kwani hilo lingemfanya kumkosa na yeye hakutaka kabisa hilo litokee maishani mwake.

    Wakakubaliana, wakapeana namba za simu kwa ajili ya mawasiliano. William hakutulia, kila siku ilikuwa ni lazima kuwasiliana na msichana huyo mrembo, aliendelea kumsifia kwa kumwambia kwamba alikuwa mrembo hata zaidi ya huyo Cleopatra, alikuwa mrembo zaidi ya Alicia Keys, Megan Fox na wanawake wote duniani.

    Mawasiliano hayo yalikuwa yakifanyika kwa siri sana, Linda hakuwa akifahamu kama mpenzi wake alikuwa kwenye harakati za kumpata msichana bilionea ambaye alikuwa akisifika kwa kipindi hicho, Cassiy aliyejitangaza kuwachukia sana wanaume.

    Siku zikakatika, Cassey hakutaka kuonekana kuwa msichana mwepesi, msimamo wake ulikuwa uleule kwamba aliwachukia wanaume na kamwe asingeweza kuwa nao. Kwa William alionekana kama kushindwa kwani meseji alizokuwa akitumiwa na mwanaume huyo zilikuwa kali na zilizomfanya azidi kujisikia mzuri kuliko wanawake wote.

    “Wakati mwingine tunahitajika kumshukuru sana Mungu,” alimwandikia msichana huyo.

    “Yeah! Ni kweli kabisa...”

    “Hasa kumshukuru kwa kutukutanisha na vitu vizuri. Kama kuna wengine wanashukuru Mungu kununua vitu vizuri kama magari, nyumba, hivi na mimi sitakiwi kumshukuru Mungu pia?” aliuliza William, walikuwa wakiendelea kuchati tu.

    “Kwa lipi?”

    “Kunikutanisha na msichana mrembo kama wewe!”

    “Jamani! Nasikia aibu mwenzako ukiniambia hivyo!”

    “Kweli tena! Kila nikikaa hapa sebuleni, picha yako inanijia kichwani mwangu, umenikaa kwenye kichwa changu na mbaya zaidi umeniganda na kuning’ang’ania

    . Hivi una nini wewe mrembo?”

    “Jamaniiiiiii!”

    “Au wewe jini?”

    “Eeh! Jini tena?”

    “Ndiyo! Huwa sipendi kuwa na msichana yeyote yule zaidi ya yule ninayeishi naye, ila kwako, nahisi umeniendelea Thailand kuniroga! Hakika umekuwa mtu muhimu sana kwangu! Kila ninapokaa, ninamwambia Mungu asante kwa wema wako, ila zaidi, asante kwa kunikutanisha na Cassey,” aliandika William.

    Aliwajua wasichana, alijua jinsi ya kuwasifia, usomaji wake wa vitabu mbalimbali ulimpa ujuzi mkubwa wa kuzungumza nao kupitia maandishi. Waliendelea kuwasiliana kila siku huku akimuonyeshea kwamba yeye ni msichana mrembo ambaye alistahili kupendwa na mwanaume maisha yake yote.

    Wakati hayo yote yakiendelea, Linda hakuwa akijua, mapenzi yake kwa mpenzi wake huyo yalikuwa kama kawaida. Kila siku usiku alilala pembeni yake, alikilalia kifua chake kwani hakukuwa na mwanaume mwingine ambaye alitakiwa kumfariji kwenye kipindi alichokuwa nacho.

    Ubaya wote aliokuwa akiufanya William hakuufanyia nyumbani, alijua jinsi ya kucheza na simu yake, aliifunga vilivyo kiasi kwamba ilikuwa vigumu kugundua kama alikuwa akipigiwa na mtu yeyote,

    “Hivi Linda akijua itakuwaje?” alijiuliza.

    Alijiamini kwamba Linda asingeweza kufahamu kitu chochote kile kwani hata kuwasiliana naye alifanya hivyo akiwa ofisini kwake na si nyumbani. Siku zikakatika, akaendelea kutengeneza pesa ndefu kupitia mtandao wake wa kijamii.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Makampuni yaliendelea kumiminika kila siku, aliyabadilisha maisha yake, akaanza kuukimbilia ubilionea. Alikuwa na kampuni kubwa, jengo kubwa ambalo ndani yake lilikuwa na wafanyakazi zaidi ya mia moja huku akimuhamisha mama yake Tanzania na kumnunulia jumba la kifahari Chicago.

    Aliyaendesha maisha yake kupitia kampuni hiyo lakini nyuma ya pazia bado alikuwa akifanya kazi chini ya serikali, kila kitu walichohitaji kujua kuhusu maadui zao, hasa mambo ya mawasiliano, alipelekewa kazi hiyo William ambaye aliifanya kwa moyo mmoja.

    Yeye ndiye alikuwa adui mkubwa wa maadui wa Marekani kwani kila walipokuwa wakiwasiliana kwa njia ya simu au aina yoyote ya mawasiliano yalidakwa na CIA na hivyo kufuatilia.

    ISIS hawakuwa na furaha naye, waliumia sana kwani kila walipokuwa wakipanga mipango yao wakalipue wapi, kitendo cha kuwasiliana tu, walijikuta wakidakwa na kulipuliwa wao.

    “Cassey! Ninahitaji nikuone leo,” alisema William, alihakikisha anabaki ndani ya gari ndipo akaanza kuzungumza naye.

    “Wapi na muda gani?”

    “Muda wowote ule na sehemu ambayo kidogo itakuwa na kificho,” alisema William.

    “Basi sawa! Labda tuonane kule kwenye mgahawa wa Mc Donald!” alisema Cassey.

    “Hapana! Huko ni noma. Tutafute sehemu ambayo hakuna watu, tuwe wawili, si unajua waandishi wengi, ninataka nikuone, niuangalie uumbaji wa Mungu kwa karibu zaidi,” alisema William.

    “Mmh! Sawa! Basi kwenye Hoteli ya Meladiva, unaonaje?”

    “Hakuna tatizo!”

    “Muda gani?”

    “Saa moja usiku!”

    “Na mkeo akikuulizia?”

    “Nitamwambia nipo na wewe hotelini!”

    “Weeee...unasemaje?”

    “Nakutania, nitamwambia chochote kile,” alisema William na kutoa kicheko.

    Walipanga kuonana, waliwasiliana kwenye simu kwa siku kumi mfululizo na mara zote hizo William alikuwa akimsifia Cassey na kujiona kama alizaliwa kwenye dunia ya peke yake.

    Siku hiyo kazi hazikuenda kama ilivyotakiwa, kila alichokuwa akikifanya, kichwa chake kilimfikiria Cassey, jinsi alivyoumbika, umbo namba nane na kikubwa zaidi kilichokuwa kikikumbukwa kichwani mwake kilikuwa ni mapaja manene aliyokuwa nayo.

    Alifanya kazi pasipo kuwa na umakini mkubwa mpaka pale alipokuwa tayari na kumpigia simu. Walipokubaliana, wakaelekea huko ambapo msichana Cassey alifika na aliyekuwa akimsubiri alikuwa William tu.

    Kwa kipindi hicho alihitaji ukaribu na jamaa huyo. Alihitaji kitu ambacho kwake kingekuwa muhimu sana, aliamini kwamba kama angekubaliana na William na kuwa wote kimapenzi basi kile alichokuwa akikihitaji kingekwenda kama kilivyotakiwa.

    Hakufikiria mapenzi kichwani mwake, alifikiria pesa, namna ya kupata fedha zaidi ya alizokuwa nazo. Kwa kumtumia mwanaume huyo, biadhaa zake zingetangazwa kwenye Mtandao wa MeChat bure kabisa kitu ambacho kingeendelea kumpa fedha kila siku.

    “Yaani kumpa pesa kwa ajili ya kuingiza fedha baadaye, sidhani kama kuna tatizo,” alisema Cassey huku akiachia tabasamu pana.

    Hicho ndicho alichokifanya. Wakati akiwaza hayo huku akiwa chumbani, tayari William alifika hotelini hapo, alivalia kofia kubwa na miwani, ilikuwa vigumu kumgundua na alipofika mapokezi, alimpigia simu Cassey na kumwambia kwamba alifika hivyo msichana huyo kuzungumza na mapokezi, akawaambia kuhusu mtu huyo, kwa jina la uongo, jinsi alivyovaa na hata alipokuwa akipandisha, hakukuwa na mtu aliyekuwa na hofu naye.

    Akafika mpaka katika chumba husika, akagonga hodi na Cassey alipoufungua mlango, wakakumbatiana na kuingia ndani. Hawakuongea kitu chochote kile, walikuwa wakiwasiliana kupitia vitendo tu.

    Walibusiana, walishikana hapa na pale na hawakujua kitu gani kilitokea, ghafla wakajikuta wakiwa watupu kabisa na hivyo kukisogelea kitanda. Wakajilaza kitandani, kikaanza kulalamika sana lakini hakukuwa na aliyejali, hakukuwa na aliyegundua kwamba walikuwa wakikiumiza kitanda hicho mpaka kulalamika kiasi hicho.

    Kwa uzuri wa uzuri wa Cassey, William alihisi kama anafanya mapenzi na malaika kwani alikuwa na uzuri wa ajabu. Wakati shughuli hiyo ikiendelea, simu yake ikaanza kuita, akaichukua na kuangalia mpigaji, alikuwa mpenzi wake, Linda, hakuipokea, akasonya kisha kuiweka pembeni.

    Aligalagazwa sana, mwili wake ulimsisimka na kuhisi kama alikuwa kwenye pepo ndogo. Kwa sababu Cassey alitamani sana mwanaume huyo apagawe naye, akaanza kumfanyia vitu ambavyo aliamini hakukuwa na mwanaume yeyote duniani aliyewahi kufanyiwa.

    Walichukua saa moja tu, William alikuwa hoi, aliangalia huku na kule, viungo vyote vikawa vinauma, mwili ulikosa nguvu kabisa. Aliyatupa macho yake pembeni, Cassey alikuwa akimwangalia tu, hapohapo akamlalia kifuani.

    “Unajisikiaje?” aliuliza msichana huyo.

    “Safi tu! Kuna kipindi nilihisi kama nafanya mapenzi na roboti, hivi huchoki?” aliuliza William.

    “Huwa sichoki hasa ninapokutana na mwanaume kama wewe. Naomba tena!” alisema msichana huyo.

    “Utaniua!”

    “Jamani naomba tena!” alisema Cassey!

    Hakutaka kuchelewa, akamfuata William kwa juu na kujilaza, akaanza kumfanyia utundu wa kila aina wa kumrudisha mwanaume huyo kwenye mchezo na kweli ndani ya dakika tano, akarudi tena mchezoni na kuanza kufanya naye.

    Walichukua saa moja jingine, kila mtu akawa hoi. William akainuka kitandani na kwenda bafuni, akaoga, alipoangalia saa yake, ilikuwa saa nne usiku. Akachukua simu na kuangalia, akakutana na meseji nne zikiwa zimeingia, akaanza kuzisoma.

    ‘Pole na kazi mpenzi. Nimekumisi, nahitaji kukuona, punguza kazi na uje kuwa karibu nami kwani si unajua hali yangu si nzuri,’ ilikuwa ni meseji ya kwanza.

    ‘Mpenzi upo wapi? Mtoto wako amekukumbuka, ananisumbua sana tumboni. Njoo uonane naye, kila wakati ananiulizia wewe upo wapi,’ ilikuwa meseji ya pili.

    ‘Mpenzi! Leo nitahitaji unikumbatie usiku mzima, nilisikie jasho lako mpenzi wangu, naomba usichelewe kurudi,’ ilikuwa ni meseji ya tatu.

    ‘Nimekuandalia chakula, sitotaka nile peke yangu, nakusubiri tule wote, hata kama utarudi alfajiri, nitataka nile nawe, si unajua kwamba leo ni siku yako ya kuzaliwa? Nilitaka tusherehekee wote ila umeondoka na bado hujarudi. Mpenzi! Naendelea kukusubiri kochini,’ ilimalizia meseji ya nne.

    Alipozisoma, moyo wake ukanyong’onyea, akahisi huruma nzito ikimuingia moyoni mwake, hakuamini kama siku hiyo ilikuwa siku ya kuzaliwa yake ya kuzaliwa na hivyo alitakiwa kuwa pamoja naye.

    Alimwangalia Cassey, hakummaliza, alikuwa msichana mrembo lakini kwa kipindi hicho alitakiwa kuwa pembeni ya mpenzi wake ambaye alikuwa na ujauzito wa miezi sita. Hakutaka kuendelea kubaki hotelini, alimuaga Cassey na kurudi nyumbani.

    Njiani, alikuwa na mawazo tele, moyo wake ulijuta, hakuamini kama kweli siku hiyo alimsaliti mpenzi wake kwa msichana Cassey. Alijilaumu lakini kila uzuri wa Cassey ulipomjia kichwani mwake, wakati mwingine alijisikia fahari kwa kufanya mapenzi na msichana kama huyo.

    Hakuchukua muda mrefu, akafika nyumbani na kuliingiza gari. Akaelekea mpaka ndani, alipofika sebuleni, macho yake yakatua kwa Cassey aliyekuwa amelala kwenye kochi huku tumbo lake likiwa kwa juu.

    Kwanza kabla ya kumsogelea akasimama, akahisi kitu chenye ncha kali kikiuchoma moyo wake kiasi cha macho yake kubadilika na kuwa mekundu na ndani ya dakika moja tangu asimame pale alipokuwa, machozi yakaanza kutiririka mashavuni mwake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nimemsaliti Linda? Hivi nina akili kweli?” alijiuliza huku akimwangalia msichana huyo.

    Akamsogelea pale kochini alipokuwa amelala, hata kabla hajamfikia, macho yake yakatua kwenye keki kubwa iliyokuwa mezani huku kukiwa na whiskey kubwa. Akaisogelea meza ile, alipoitazama keki ile, iliandika ‘Happy Birthday my hubby’.

    Ulikuwa ni ujumbe mzuri lakini uliuchoma moyo wake vilivyo, akamwangalia tena Linda aliyekuwa amelala kochini kwa kuwa alichoka kumsubiria, alipomfikia, akakaa karibu yake na kumwamsha. Linda alipoamka na kumwangalia mpenzi wake, tabasamu pana likamjia, hakuamini kama alirudi salama nyumbani.

    “Nimekukumbuka mpenzi wangu,” alisema Linda huku akimkumbatia William.

    “Nimekukumbuka pia mpenzi! Pole kwa kunisubiri, nilikuwa na kazi nyingi za kuunganisha mawasiliano ya MeChat na Mtandao wa Yahoo. Samahani kwa kutokukutaarifu mpenzi,” alisema William, alidanganya mpenzi wake, aliumia moyoni mwake kufanya hivyo lakini hakuwa na jinsi, ili kumfurahisha ilibidi amdanganye kama alivyokuwa akifanya.

    Hiyo ilikuwa ni siku ya kwanza kufanya mapenzi, haukuwa mwisho, penzi la Cassey lilimchanganya mno kiasi kwamba kuna wakati alikuwa akichelewa kurudi nyumbani kwa kisingizio cha ubize na wakati mwingine akilala hukohuko nje.

    Penzi la Cassey likamchanganya mno. Kuna wakati Linda alipokuwa akimpigia simu, hakuwa akiipokea kabisa, alijua vilivyo jinsi msichana huyo aliyokuwa akiumia lakini hakutaka kujali sana, kwake, kwa kipindi hicho Cassey alikuwa kila kitu.

    “Leo sitoweza kurudi tena mpenzi,” alisema William.

    “Kwa nini? Siku ya tatu hii!” aliuliza Linda huku akionekana kushtuka.

    “Nimepata safari ya kwenda Nevada.”

    “Jamani! Sasa si nitakufa kwa mawazo?”

    “Usijali mpenzi! Ni lazima tutafute hela popote pale zilipo,” alisema William, akamzugazuga na maneno mengine na kukata simu.

    Ni kweli alikuwa na safari ya kwenda Las Vegas huko Nevada lakini hakujua ni kwa jinsi gani angemdanganya mpenzi wake. Alimwambia kwamba alikuwa na kazi kubwa alikuwa akienda kufanya huko, kwa Linda, hakukuwa na tatizo, ilikuwa ni siku ya tatu hakuwa ameonana naye lakini hakuwa na jinsi.

    Hakwenda huko kikazi bali alikwenda huko kula maisha na msichana Cassey. Mpaka kipindi hicho hakukuwa na mtu aliyegundua kama wawili hao walikuwa wakitoka kimapenzi.

    Kwenye Mtandao wa MeChat matangazo yake yalijaa, watu wengi walinunua kitabu chake pasipo kulipia kiasi chochote cha pesa. Walipofika Las Vegas, wakaenda kupanga kwenye hoteli kubwa na ya kifahari.

    Hakukuwa na mtu aliyegundua kwamba mteja aliyekuwa na msichana Cassey alikuwa William ambaye alikuwa maarufu sana kwa kipindi hicho. Japokuwa alimwambia Linda kwamba angekaa huko siku mbili lakini zikaongezeka na kuwa wiki nzima.

    Walicheza michezo yote ya kitandani huku kila mmoja akionekana kuwa na furaha. Siku ya kwanza ikapita, ya pili ikaingia, ya tatu na ya nne, bado hawakuondoka Las Vegas, waliendelea kula bata kama kawaida.

    “Twende kwenye mgahawa tukanywe kahawa,” alisema Cassey.

    “Kwa nini tusinywe humuhumu kama kawaida?”

    “Tunakaa sana ndani mpenzi! Naomba twende,” alisema Cassey.

    Ilikuwa ni saa tano ya usiku, hawakutaka kubaki ndani, William hakutaka kwenda huko lakini hakuwa na jinsi, akamshika mkono Cassey na kisha kuondoka ndani kuelekea huko. Alivalia kofia, alijua kwamba kusingekuwa na mtu ambaye angemuona na kumgundua.

    Walipofika chini kwenye mgahawa, wakatulia na kuagiza kahawa. Humo ndani kulikuwa na watu wachache, walijua kabisa hakukuwa na mtu aliyekuwa akiwaona pale walipokaa, walijiachia, walikaa kimahaba kama wapendanao. Wakati mwingine walikuwa wakibusiana, walijisahau kabisa.

    “Ninakupenda Cassey...” alisema William huku akimwangalia msichana huyo.

    “Nakupenda pia,” alisema Cassey. Hapohapo akamsogelea usoni na kisha kuanza kubadilishana mate, wakati tukio hilo likiendelea, wakashtukia wakipigwa picha tano mfululilizo.

    “Kwacha...kwacha...kwacha...” ilisikika milio ya kamera, walipomwangalia nani aliwapiga picha, wakamuona jamaa aliyevalia koti kubwa lililoandikwa kwa nyuma New York Times akiondoka, akaingia ndani ya teksi na kupotea. Alikuwa mwandishi wa habari wa gazeti hilo kubwa Marekani.



    William alichanganyikiwa, hakujua ni mwandishi gani aliyempiga picha. Hakutaka kubaki mahali hapo, akatoka nje ya mgahawa ule kwa ajili ya kumfuata mwandishi huyo ila bahati mbaya sana teksi aliyokuwa amepanda ikapotea machoni mwake.

    Moyo wake ukaanza kumfikiria mpenzi wake, Linda kwani alihisi kwamba iwe isiwe ilikuwa ni lazima habari ile kuchapishwa gazetini na hatimaye kumfikia Linda. Aliumia sana, hakutaka kuona hilo likitokea, hapo ndipo akaanza kujuta kwa kile alichokifanya, akatamani kuondoka haraka sana kurudi New York na kumuomba msamaha Linda ili hata kama habari ile itatoka basi kusiwe na maumivu makubwa kwa msichana huyo.

    Akarudi ndani ya mgahawa, hakutaka kubaki mahali hapo, hakuwa sawa, na kila alipokaa, ni mawazo ya Linda ndiyo yaliyokuwa yakimjia kichwani mwake. Hakumwambia Cassey warudi ndani, alichokifanya ni kuchukua koti lake na kurudi ndani peke yake.

    Akaingia ndani ya lifti, wakati ikijifunga tu, Cassey akatokea, akazuia na yeye kuingia ndani. Hawakuzungumza kitu chochote kile, Cassey hakuona kama huo ulikuwa muda muafaka wa kuzungumza na William ambaye alionekana kutokuwa sawa kabisa.

    Walipofika katika ghorofa ya juu kulipokuwa na chumba walichochukua, wakateremka na kuelekea chumbani humo. Walipofika, William akajilaza kitandani huku akionekana kuwa na mawazo lukuki, kilichomuumiza kichwa ni kwamba Linda angechukuliaje kama angeona habari kuhusu yeye kuwa na mwanamke huko Las Vegas?

    “William mpenzi....”

    “Naomba uniache kwanza.”

    “Nikuache kwa nini? Kwanza niambie ni kwa nini unakuwa na mawazo hivyo? Kisa picha?” aliuliza Cassey, alijifanya kushangaa.

    “Kisa si picha, kisa ni Linda. Atajisikiaje akiziona hizo picha!” alisema William huku akionekana kuumia sana moyoni mwake.

    “Basi itabidi tuwasiliane na waandishi, tuwahonge wasitoe habari hiyo,” alisema Cassey.

    “Unawajua waandishi?”

    “Ndiyo! Yule aliyetupiga picha anaitwa Shawn Gill, ni mwandishi wa kujitegemea ambaye anapenda sana kujifanya mwandishi wa New York Times,” alisema Cassey.

    “Yule wa habari za kidaku?” aliuliza William kwani mwandishi huyo alikuwa maarufu sana kwa habari za kiaku hapo Marekani.

    “Ndiyo huyohuyo!” alisema Cassey.

    Hakukuwa na kingine alichokitaka zaidi ya kumwambia Cassey ampatie namba yake ili azungumze naye. Hilo halikuwa tatizo, akapewa namba ya Gill na kumpigia, simu iliita kwa sekunde chache na sauti ya mwanaume kusikika upande wa pili.

    William akajitambulisha na kumwambia kwamba alitaka kuonana naye. Hilo lilikuwa gumu sana kwa Gill kwani aliamini kwamba habari aliyokuwa nayo ilikuwa kubwa ambayo kama angewauzia kampuni za magazeti basi angeweza kupata pesa nzuri sana.

    “Kuonana haiwezekani!” alisema Gill.

    “Gill! Wewe ni mwanaume kama mimi! Hivi utajisikiaje kama utaona mwanaume mwenzako nimeadhirika katika jamii? Utajisikiaje kusikia mpenzi wangu mjauzito kajiua kwa ajili ya habari uliyoichapisha! Unahisi ni kitu kizuri?” aliuliza William.

    “Basi sawa. Tuonane! Ila utatakiwa kuzilipia!”

    “Haina shida. Nitafanya hivyo ila ni lazima uje na kompyuta yako nihakikishe kwamba unazifuta baada ya kukulipa,” alisema William.

    “Hakuna shida.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hakutaka kukaa sana, usiku huohuo alionana na Gill na kumwambia kwamba alihitaji kumlipa kisa cha dola elfu ishirini zaidi ya shilingi milioni arobaini kwa ajili ya kuizima habari hiyo. Kiasi hicho kilikuwa kidogo kwa Gill kwani aliamini kwamba kwa jinsi picha zile zilivyokuwa, maisha ya William yalivyokuwa ni lazima angelipwa kiasi kikubwa cha fedha.

    “Hicho ni kidogo sana. Ongeza dau,” alisema Gill.

    ****

    Mwandishi Gill alikuwa kwenye furaha kubwa, hakuamini kama alifanikiwa kupata picha za William akiwa na msichana bilionea, Cassey. Alisikia kwa kipindi kirefu kwamba watu hao wawili walikuwa kwenye uhusiano wa siri, alitaka kufuatilia kwani aliamini kwamba kama angekamilisha stori hiyo basi angepata pesa nyingi sana.

    Aliposikia kwamba William alikuwa akielekea Las Vegas, Nevada aliamini kwamba kwa namna moja ama nyingine ilikuwa ni lazima kuwa na msichana huyo, hivyo akajilipia usafiri na kuelekea huko.

    Alipofika, kwa kutumia watu wake waliokuwa hotelini wakampa taarifa hoteli aliyokuwa amefikia Cassey na kuamini kwamba naye William alikuwa hukohuko. Alichokifanya ni kwenda na kuchukua chumba katika hoteli nyingine ya jirani.

    Alifanikiwa. Akaendelea kufuatilia kila siku kwenye hoteli ile mpaka kufanikiwa kuzipata picha hizo ambazo aliamini kwamba zingekuwa dili sana. Alipofika hotelini, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kuwapigia simu wahariri wa magazeti ya Independent na New York Times na kuwaambia kwamba alikuwa na habari ya William hivyo alihitaji kuambiwa ni kiasi gani angelipwa.

    “Una picha zao?”

    “Zipo! Tena nilizipiga kama mvua!”

    “Daah! Njoo nazo. Tutakupa dola elfu tano!” alisema mhariri wa Gazeti la Independent.

    “Dola Elfu tano tu?”

    “Ndiyo! Tunatakiwa kuziona picha zenyewe kwanza. Zikiwa nzuri, dau linaongezeka.”

    “Basi subiri.”

    Akakata simu na kumpigia mhariri wa Gazeti la New York Times na kumwambia kuhusu habari hiyo na picha za kumwaga alizokuwa nazo. Ilikuwa habari nzuri ambayo kusingekuwa na mhariri yeyote yule ambaye angekataa kuzitumia picha na habari hiyo kwani kwa kipindi hicho huyo William ndiye alikuwa habari ya mjini.

    Wakakubaliana malipo yawe dola elfu kumi. Kwanza haikuwa tatizo, alikubaliana naye na kumwambia kwamba angemtumia kwenye barua pepe yake kwa ajili ya kuzitoa. Wakati akiwa anasubiri, akapokea simu kutoka kwa William na kumwambia kuhusu hizo picha, alimuomba sana asizitoe kwani kama angefanya hivyo ingekuwa balaa.

    Alichokifanya ni kupanga kuonana naye usiku wa siku hiyo. Alijua kwamba inawezekana William angemfanyia ubaya wa kumpokonya kompyuta yale ya mapajani na kuzifuta picha hizo huku akiwa na watu wake.

    Alipolifikiria hilo, akaogopa hivyo kuzihamisha picha hizo na kuziweka katika barua pepe yake kama ulinzi zisiweze kupotea. Alipomaliza na kuhakikisha kwamba kwenye kompyuta yake, kadi ya kamera hakukuwa na hizo picha zaidi ya kwenye barua pepe yake tu, akawa huru kwenda huko.

    Alipofika, akazungumza naye, japokuwa aliahidiwa kupewa malipo makubwa kwa ajili ya picha hizo lakini akakataa, akataka kiasi cha dola elfu hamsini ambazo zilikuwa ni zaidi ya shilingi milioni arobaini.

    Kiasi hicho kilikuwa kikubwa hata zaidi ya alichoahidiwa na wahariri wa magazeti lakini hakutaka kuridhika, akahitaji kiasi kikubwa zaidi na hivyo kuanza kupanga tena malipo.

    “Nitakupa dola elfu arobaini!”

    “Naomba hamsini!”

    “Gill! Mbona kiasi kikubwa hicho?”

    “Hivi dola elfu hamsini na uhai wa mpenzi wako, kipi kitu muhimu?” aliuliza Gill.

    “Gill! Nisaidie mimi mwanaume mwenzako!” aliomba sana William.

    Wakati wakizungumza hayo mara kwa mara simu ya Gill ilikuwa ikiita, alikuwa akipigiwa na waandishi wa habari ambao waliihitaji sana hiyo habari kwani kwao, kama wangepewa picha basi ingekuwa nafuu kwao.

    Gill akamuonyeshea William simu zile zilizokuwa zikiingia kutoka kwa waandishi mbalimbali, akaogopa na kuhisi kwamba kama asingempa kiasi cha pesa alichokuwa akikihitaji basi angekwena kuwauzia watu hao.

    “Kwa hiyo hizo picha unazo hapo?” aliuliza William.

    “Ndiyo! Nimeziweka kwenye barua pepe yangu! Huko ni sehemu salama kabisa,” alisema Gill.

    “Umeziweka kwenye barua pepe?”

    “Ndiyo!”

    “Kwenye kompyuta yako hazijabaki?”

    “Hakuna! Na kwenye kadi hakuna.”

    “Kwa hiyo ulihisi ningekuvamia na kukuibia kamera au kompyuta yako?” aliuliza William huku akimwangalia Gill machoni, kidogo uso wa William ukaanza kutoa tabasamu kwani kitendo cha kuambiwa kwamba picha zile zilihamishwa kwenye kadi ya kamera na kompyuta na kuwekwa kwenye barua pepe ilimpa urahisi wa kuona kwamba iwe isiwe ilikuwa ni lazima kuingia kwenye barua pepe ya Gill na kuzifuta, kama alivyomfanyia Nicholaus.

    “Nilihisi ningefanyiwa mabaya.”

    “Basi wewe ni mpumbavu sana,” alisema William huku akimwangalia Gill.

    “Mpumbavu?”

    “Ndiyo! Tena yule wa kwanza kabisa.”

    “Unamaanisha nini?”

    “Wewe ni mpubavu Gill! Sizitaki tena picha hizo. Ukitaka kuwauzia waandishi wa habari kawauzie mpumbavu wewe,” alisema William.

    “Unasemaje?”

    “Kwani hujanisikia? Wewe ni mpumbavu sana. Umekalia kufuatilia maisha ya watu. Aya kazitoe hizo picha mjinga wewe. Hata ukiwapa waandishi wa habari, siogopi ng’oo,” alisema William kwa kiburi sana.

    Gill hakuzungumza kitu, moyoni mwake aliumia sana, alikasirika kwani kitendo cha kutukanwa kilimkasirisha kupita kawaida. Akasimama na kuondoka, hakutaka kwenda hotelini, alikuwa na hasira lakini akahisi kama hasira hizo zilikuwa ndogo sana hivyo alichokifanya ni kupitia baa, akanywa pombe, hasira zikazidi na kuanza kurudi hotelini.

    Njiani alizungumza na mhariri wa Gazeti la New York Times na kumwambia kwamba ndani ya dakika chache angemtumia picha za William zilizoonyesha kwamba alikuwa akitanua na msichana Cassey.

    Alipofika chumbani, akaweka pombe alizozibakisha mezani kisha kuchukua kompyuta yake. Moyo wake ulikuwa na hasira kali mno, alitetemeka sana kwani maneno aliyoambiwa na William kwamba alikuwa mpumbavu yalimkasirisha pasipo kujua sababu iliyomfanya mwanaume huyo kumtukana namna hiyo.

    Akaifungua kompyuta yake na kuiunganisha na huduma ya internet na kuanza kuifungua barua pepe yake ili azitume picha zile. Akaiingiza anuani na alipoingia neno la siri, ilikataa kufunguka kwa kuambiwa kwamba aliingiza neno la siri lisilokuwa lenyewe.

    Hakuacha, alijua kwamba hilo hutokea mara kwa mara, alijaribu zaidi na zaidi, zaidi ya mara ishirini lakini barua pepe haikuweza kufunguka kitu kilichomuumiza sana moyoni mwake.

    “Tatizo nini?” alijiuliza, ila kabla hajapata jibu, maneno ya William yaliyomwambia kwamba ni mpumbavu yakaanza kujirudia kichwani mwake, bahati nzuri zaidi, akatambua kwamba William aliyasema yale baada ya kusikia kwamba alizihifadhi picha zile kwenye barua pepe tu.

    “Atakuwa amehacki barua pepe yangu!” alisema Gill huku macho yakianza kuwa mekundu na baada ya sekunde kadhaa yakaanza kutiririka mashavuni mwake.

    Alijuta moyoni mwake kwa kumwambia William ukweli, alijilaumu na kujiona mpumbavu sana kwani hakutakiwa kuziweka picha zile kwenye barua pepe tu, tena hasa akipambana na mtu aliyeonekana kuwa hatari kwenye masuala ya kompyuta.

    Baada ya saa moja kupita tena huku akijaribu kila wakati, barua pepe yake ikakubali kufunguka, alipokwenda katika faili alilohifadhia picha zile, hakuikuta picha hata moja. Hapohapo akayafumba macho yake na kuanza kulia, kiasi cha fedha alichokuwa ameahidiwa kikaota mbawa, na mbaya zaidi wahariri wakubwa wa magazeti waliotaka kununua habari ile na picha waliendelea kumpigia kama kumsisitiza kwamba walizihitaji picha hizo kuliko kitu chochote kile.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Habari zenu jamani!” ilisikika sauti ya Dk. Sam kutoka nje ya chumba alicholazwa Godson.

    Kibra aliyekuwa ndani ya chumba alicholazwa Godson akashtuka baada ya kusikia sauti kutoka nje ya chumba kile, tena baada ya hapo, kilichofuata kilikuwa ni sauti ya miguu iliyokuwa ikielekea kule chumba kilipokuwa.

    Hakuwa amemchoma sindano Godson, alikuwa nayo kwenye koti, alichokitaka kwanza kilikuwa ni kumuua kitandani pale na kisha kumchoma sindano ionekane kama madaktari wa hospitali hiyo walikuwa wamehusika katika mauaji ya mwanaume huyo.

    Hakutaka kubaki mahali hapo, aliogopa kwa kuhisi kwamba angekamatwa hivyo alichokifanya ni kukimbia kwa kupitia mlango wa nyuma na kumwacha Godson akiwa hoi huku akikohoa mfululizo kitu kilichompa maumivu makali.

    “Vipi?” aliuliza jamaa mmoja baada ya kumuona Kibra akitoka mbio ndani ya chumba kile.

    “Tusepeni! Kimenuka!” alisema Kibra.

    “Kimenuka? Kivipi?”

    “Twendeni!”

    Hawakutaka kubaki mahali hapo, wakaondoka huku kila mmoja akionekana kuchanganyikiwa, walipoingia ndani ya gari, Kibra akawahadithia wenzake kile kilichotokea na ugumu aliokutana nao ndani ya chumba kile hata kabla ya kumuua Godson.

    “Dah! Ndiyo tushashindwa aiseee,” alisema mwenzake huku akikishika kichwa chake kuonyesha kushindwa.

    Mule ndani, Dk. Sam akaingia, alishangaa kumkuta Godson akikohoa mfululizo, alishangaa, ilikuwaje mpaka awe katika hali hiyo na wakati hakuwa akiumwa kikohozi. Kwa kutumia sauti yake yenye maumivu Godson akamwambia daktari kwamba kulikuwa na daktari mwingine aliyeingia ndani ya chumba hicho ambaye alitaka kumuua.

    “Kuna daktari alitaka kukuua?”

    “Ndiyo!”

    “Daktari gani?”

    “Simjui! Amekimbia kuelekea mlango wa nyuma,” alisema Godson na Dk. Sam kuelekea nje kwa kupitia mlango wa nyuma lakini hakuona mtu.

    Dk. Sam akatoka ndani ya chumba kile, akaelekea nje na kuwauliza wakina Melania kama walimuona daktari yeyote akiingia ndani ya chumba kile. Walisema kwamba walimuona lakini hawakujua kama alikuwa daktari wa kweli au la.

    Walimuelezea jinsi alivyokuja na kuingia ndani. Muonekano wake ulifanana na daktari na hivyo wote kuhisi kwamba alikuwa daktari. Hakutaka kuwaficha, aliwaambia ukweli kwamba mtu aliyekuwa ameingia ndani ya chumba hicho hakuwa daktari kama walivyohisi bali alikuwa mtu aliyetumwa kwa ajili ya kumuua Godson.

    “Unasemaje?” aliuliza baba yake Godson.

    “Kuna mtu alitaka kumuua ndani!”

    “Nani? Kijana wangu?”

    “Ndiyo mzee!”

    Wakaingia ndani na kumkuta Godson akiendelea kukohoa. Walimuuliza kilichotokea na yeye akawaambia ukweli kwamba kulikuwa na daktari aliyekuwa ameingia ndani ya chumba kile kwa lengo la kumuua, aliwahadithia kila kitu kilichotokea.

    Hapo wakapata majibu juu ya ajali iliyotokea kwamba kulikuwa na mkono wa mtu. Mazingira ya ajali kwa jinsi walivyohadithiwa wakaamini kuwa kulikuwa na mtu aliyeipanga ila hawakujua alikuwa nani.

    “Hii ajali ilipangwa,” alisema baba yake Godson.

    “Kwa nini?”

    “Kutokana na mazingira ya ajali. Halafu hili lililotokea inaonyesha kabisa kuna mtu anataka kumuua mtoto wangu,” alisema baba yake Godson.

    Kila mmoja alikuwa na uhakika kwamba inawezekana kulikuwa na mtu aliyetaka kumuua Godson hivyo ilikuwa ni lazima kuwasiliana na polisi na kuwaambia kwamba walihitaji ulinzi nje ya wodi hiyo kwani vinginevyo Godson angeweza kuuawa.

    “Una chembechembe za ugomvi na mtu yeyote?” aliuliza polisi mmoja.

    “Hapana!” alijibu daktari.

    “Kweli?”

    “Ndiyo! Sikuwahi kugombana na mtu, kuanzia kazini mpaka mtaani!” alijibu Godson.

    “Mzee?”

    “Hata mimi sijawahi! Sina ugomvi na mtu!”

    Hawakujua kwamba mtu aliyekuwa akisababisha hayo alikuwa Melania, hawakuwahi kuhisi kwamba kulikuwa na mwanaume aliyekuwa na hasira kali za kutaka kuuchoma moyo wa Melania na kumfanya kulia kila siku.

    Ulinzi ukaimarishwa mahali hapo, polisi mmoja akawekwa kwa ajili ya kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa mahali hapo. Hawakutakiwa kuogopa kitu chochote kile. Polisi yule aliyepewa jukumu la kulinda mahali hapo, alipewa nafasi ya kutembea hata ndani ya chumba kile kuhakikisha kwamba kila kitu kinakwenda kama kinavyotakiwa kwenda.

    “Kidogo moyo wangu una amani,” alisema Melania kila walipokuwa wakimwangalia polisi ambaye alionekana kuwa makini hasa.

    ***

    “Picha zisioni!” alisema Gill kwenye simu.

    “Unasemaje?” aliuliza Mhariri wa Independent.

    “Picha sizioni!”

    “Wewe uliziwekea wapi?”

    “Kwenye barua pepe yangu!”

    “Sasa si uchukue kwenye kadi na uzitume tena.”

    “Mkuu! Yaani nilizifuta kule kwani William alitaka kuzungumza nami.

    “Kwa hiyo ukazitoa kwenye kadi moja kwa moja?”

    “Ndiyo!”

    “Wewe ni mpumbavu sana Gill.”

    Gill alichanganyikiwa, alipoambiwa kwamba alikuwa mpumbavu, akakubaliana naye kwani kile alichokuwa amekifanya, hakuwahi kukifanya hata mara moja. Alikuwa na habari kubwa ambayo ingeifanya dunia kutetemeka lakini kwa upumbavu wake, hofu ya kutekwa na kupokonywa kamera ikamfanya kuzipoteza picha hizo.

    Wakati yeye akijiona mpumbavu, William alijiona mjanja, moyo wake ulikuwa na furaha tele kwani aliamini kwamba kwa kupitia zile picha, kama kweli zingetolewa katika magazeti na mitandao ya kijamii hakika uhusiano wake ingevurugika sana.

    Hakutaka kubaki Las Vegas, alichokifanya ni kurudi New York ambapo baada ya kukutana na mpenzi wake, Linda, akamkumbatia na kumuonyeshea ni jinsi gani alikuwa amemkumbuka katika kipindi alichokuwa mbali naye.

    Ilikuwa ni vigumu kwa Linda kugundua kwamba mpenzi wake huyo alikuwa akimdanganya, alimuonyeshea mapenzi ya dhati, alimjali na hata namna alivyokuwa amemkumbatia, alionyesha ni jinsi gani alimkumbuka, alimg’ang’ania kama mtu asiyetaka kumwachia tena.

    “Nimewakumbuka mpenzi wangu!” alisema William huku akiwa amemkumbatia Linda, tena kwa kumng’ang’ania kabisa.

    “Tumekumbuka pia.”

    William hakutaka kuchelewa, hapohapo akambeba juujuu na kumpeleka chumbani, walipofika, wakajitupa kitandani na kuanza kucheza michezo ya kiutu uzima. Sauti za mahaba zilisikika chumbani humo, Linda alimng’ang’ania William kitandani, hakutaka kumwachia kwani aliukumbuka utundu wake kitandani hapo.

    Walichukua dakika arobaini, wakaachiana, wakalaliana tu na kupigana mabusu mfululizo huku William akimwambia Linda jinsi alivyokuwa akiichukia kazi yake kwani ilimfanya kuwa mbali naye na wakati hakutaka kuona hilo likitokea.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hayo ndiyo maisha waliyokuwa wakiishi, mpaka mimba ya Linda inafikisha miezi nane, uhusiano wa siri kati ya William na Cassey ulikuwa ukiendelea kama kawaida. Walikuwa wakiwasiliana huku wakionana kwa siri sana kiasi kwamba hata waandishi wa habari waliokuwa bize kuwafuatilia na kuwanasa ilikuwa vigumu kuwaona wakiwa pamoja.

    “Mpenzi! Kuna kitu nataka kuzungumza nawe,” alisema Cassey wakati akizungumza na William kwenye simu.

    “Kitu gani?”

    “Siwezi kukwambia kwenye simu. Naomba tuonane!” alisema Cassey.

    Kuonana naye halikuwa tatizo, alichokifanya William ni kukodisha gari ya kawaida ambayo kama mtu mwingine angeiona asingeweza kugundua kama tajiri kama yeye angekuwa akiendesha gari hilo.

    Akampigia simu Cassey na kumwambia kwamba alitakiwa kwenda katika Kituo cha Televisheni cha CBC kilichokuwa hapo New York, atakapofika huko, ajifanye anakwenda kumsalimia mtu humo na akitoka basi aingie kwenye gari lake atakalokwenda nalo.

    Hilo halikuwa tatizo na ndiyo zilikuwa njia walizokuwa wakizitumia ili wasiweze kugundulika. Msichana huyo akaenda huko na alipokuwa akitoka, akaliacha gari lake na kulifuata gari alilokuwa William na kuingia ndani.

    Kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kupigana mabusu mfululizo, kila mmoja alimkumbuka mwenzake, walishikana hapa na pale, waliporidhika, wakatulia, William akaliondoa gari hilo mpaka katika sehemu iliyokuwa na bustani ya Riverside iliyokuwa Manhattan, hawakuteremka bali walitulia humohumo kwenye gari sehemu ya kuegesha magari.

    “Aya! Niambie sasa,” alisema William.

    “Shika hii!” alisema Cassey huku akimpa bahasha ya kaki William.

    “Kuna nini mbona unanitisha?”

    “Usiogope bwana.”

    William akaichukua bahasha hiyo na kisha kuifungua, alichokiona hakukielewa, kilikuwa ni picha iliyopigwa kwa kutumia Utra-Sound. Alijaribu kuiangalia karatasi hiyo ya ‘magnetic film plate’ na kuona kitu ambacho hakukielewa.

    “Ndiyo nini hii? Mimi sijasomea utabibu,” alisema William huku akiiangalia vizuri.

    “Nilikwenda hospitali!”

    “Ndiyo!”

    “Nikapimwa na kuonekana kwamba nina ujauzito wako,” alisema Cassey.

    “Unasemaje?”

    “Nina mimba yako!”

    “Mimba yangu?”

    “Ndiyo!” alijibu Cassey huku akiachia tabasamu pana.

    William hakuamini alichokisikia, hakujua kama kile kilichokuwa kikiendelea kilikuwa ndoto au kitu kilichokuwa kikitokea katika maisha yake halisi. Alimwangalia Cassey, alionekana kumaanisha kwamba alikuwa na mimba.

    Msichana huyo alikuwa akionyesha tabasamu pana lakini kwa William hali ilikuwa tofauti kabisa. Hofu ikamjaa, mapigo ya moyo yakaongezeka kasi, mwili ukamtetemeka, japokuwa ndani ya gari lile kiyoyozi kilikuwa kikipuliza lakini kijasho chembamba hakikuacha kumtoka William.

    “Unasema una mimba?”

    “Ndiyo mpenzi! Bado daktari hawajajua ni jinsia gani lakini nitafurahi nikimpata wa kike,” alisema Cassey maneno ambayo yalionekana kama msumari wa moto moyoni mwa William.

    William hakuwa na furaha hata kidogo, hakuwahi kutarajia kama angeweza kumpa mimba msichana huyo. Kichwa chake kilimfikiria mpenzi wake, Linda ambaye alikuwa naye mjauzito na baada ya mwezi mmoja walitarajia kupata mtoto wa kwanza.

    Hakuwa na ndoto za kuzaa na mwanamke mwingine zaidi ya Linda. Akaegemea kiti chake na kuangalia juu, kadiri alivyoendelea kukaa ndani ya gari lile ndivyo alivyokuwa akiingiwa na hofu zaidi.

    “Cassey!”

    “Unasemaje mpenzi? Mbona unaonekana huna raha? Hutaki mtoto?” aliuliza Cassey.

    “Nataka ila....”

    “Ila nini?”

    “Naomba ukaitoe mimba hiyo!”

    “Unasemaje?”

    “Naomba ukaitoe mimba hiyo!” alisema William huku akimwangalia Cassey.

    “Nikatoe mimba?”

    “Ndiyo!”

    “Yaani nimuue mtoto wangu?”

    “Bado hajawa mtoto!”

    “Hicho ni kitu kisichowezekana hata kidogo!”

    “Cassey.”

    “Nimesema hivi! Nilikuwa nahitaji sana kuzaa na wewe, nimefanikiwa kubeba mimba yako! Kuitoa, sahau kabisa maishani mwako. Sitoweza kuitoa na sitofikiria kuitoa hata mara moja,” alisema Cassey huku akionekana kuwa na hasira kwani hakutegemea kama William angemwambia maneno kama hayo. Alichokifanya ni kufungua mlango wa gari na kutoka huku akionekana kuwa na hasira kupita kawaida.

    “I am fuckin dead..” (nimekwisha...) alisema William huku akilalia usukani wa gari lile.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog