Search This Blog

Sunday, 22 May 2022

JULAI SABA - 1

 







    IMEANDIKWA NA : RICHARD MWAMBE



    *********************************************************************************



    Simulizi : Julai Saba

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Dunia inakumbwa na wimbi la ugaidi, matukio ya kutisha yanayopoteza maisha ya walio wengi katika pande mbalimbali za dunia ikiwemo Afrika hususan Tanzania. Nchi zinazoendelea zinajumuishwa kuwa na mahusiano na mataifa beberu ya Maghalibi. hivyo zinashambuliwa na makundi hayo.

    Idara za usalama za Tanzania zinafanikiwa kumtia mkononi Jegan Grashan akihusishishwa na mlipuko wa ubalozi wa USA, Dar es salaam mwaka 1998. Swahiba zake wanaishinikiza serikali imuache huru kwa kutekeleza milipuko kadhaa, wanaipa siku saba iwe imekamilisha hilo. Je litawezekana?

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tiririka na mkasa huu mwingine unaomhusisha Kamanda Amata. Mkasa wa kusisimua. Mkasa wa Kigaidi.



    CHAPISHO LA 01



    1

    MVUA KUBWA ilikuwa ikinyesha katika jiji la Dar es salaam, jiji linalosifika kwa joto kali linalowafanya watu wake kujutia kila siku kwa nini wanaishi hapo, lakini bado kuhama hawataki. Radi za hapa na pale ziliendelea kumulikan ardhi yote ya eneo la Tazara katika makutano ya barabara zenye majina ya viongozi wakubwa Africa, barabara ya Nyerere na ile ya Mandela, umeme ulikuwa umekatika na giza lilitawala kila mahali jioni hiyo, haikuwa usiku sana kwani ndiyo kwanza kipindi cha majira kutoka RTD kilikuwa kikianza, hakuna aliyeweza kuvuka katika makutano hayo, magari yalijaa kila upande mpaka kule kwenye service road, kelele za honi zilitawala na matusi ya hapa na pale, wengine wakijifanya ndiyo askari kuongoza magari lakini bado hali ilikuwa tete, si wakwenda Buguruni, wala Ukonga wote walitua pale, mvua iliendelea kunyesha kwa fujo na ngurumo zikitawala.



    Katikati ya makutano yale kulikuwa na gari aina ya Peugeot imesimama hali inaunguruma, dereva wake alishuka na kupiga kelele za hapa na pale akiwaomba wengine wampishe lakini hakuwapo wa kumpisha, kwa hasira yule bwana aliubamiza mlango wa gari na kujichanganya na vijana waliojaa eneo lile, haikupita dakika mbili mlipuko mkubwa ulitokea katika gari ile, anga lote lilifunikwa na rangi nyekundu iliyochanganyika na moshi mweusi, watu walitawanyika huku na kule wengine wakitokea katika madirisha ya daladala, ilimradi tu kujiokoa. Vilio vilisikika huku na kule watu waliumia sana na wengine kupoteza maisha, gari zaidi ya ishirini zilidaka moto eneo lile.



    Gari za zimamoto kutoka kampuni binafsi na lile la jiji yalifika huku polisi wa kutuliza ghasia wakiwa tayari kusaidia majeruhi kuwakimbiza hospitali ya Dar Group, Temeke na wengine Muhimbili moja kwa moja, kazi ilikuwa ngumu kwa kila mtu aliyekuwa pale, wananchi wote walisogezwa mbali na eneo la tukio ili kupisha shughuli za uokoaji. Baada ya takribani dakika arobaini na tano gari ya jeshi ilisimama karibu kabisa na jengo la S.S Bakhresa, wakashuka na vifaa vyao kuelekea pale palipotokea mlipuko walilizungushia gari lile utepe maalum na kukusanya kila kilichoonekana na uhusiano na mlipuko ule kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Hali iliendelea kuwa tete eneo lile kila mtu alilia kivyake.



    ??????



    “Ingia kaka, umemaliza kazi” bwana mmoja alisema huku akiufungua mlango wa Toyota prado na kumruhusu huyo aliyemwita kaka kuingia kwenye gari hiyo, kasha ikageuza na kuchukua barabara ya Mandela kuelekea Buguruni.

    “Bado, kazi ndiyo kwa nza inaanza” yule bwana aliwaeleza wenzake huku gari ile ikitokomea kwa kasi maeneo ya Sukita kuielekea Ubungo.

    “Hii ni vita ya tatu ya dunia, na tunaiendelezea hapa Tanzania, kwa kuwa ulinzi wan chi hii hauko makini” aliongea bwana mmoja aliyeonekana kama ndiyo kiongozi wao.



    ??????



    Mlio mkali wa simu ulimshtua madam S usingizini, alisonya na kuiinua simu ile huku akiwa bado kitandani mapema namna hiyo.

    “Hey, nani?” aliuliza kwa hasira.

    “Madam S, washa runinga yako TBC kasha nitakupia baadaye kidogo” sauti ya upande wa pili ilitoa ombi, madam S bila kuchelewa aliichukua rimoti na kuiamuru runinga ile kufanya kazi. Alipigwa na butwaa na moyo ukaanza kumuenda mbio, ukizingatia na umri nao ulikuwa umekwenda, aliifutailia habari ile, na kwa mbali macho yake yalianza kujaa machozi. ‘Oh my God’ alijisemea moyoni, ‘Nini tena hii?’ alijiuliza mwenyewe wakati akimfuatilia Grace Kingalame akitoa maelezo ya moja kwa moja kutoka eneo la tukio. Madam S alinyanyuka kitandani na kuutafuta mlango wa bafu, baada ya kujiweka sawa alivalia suruali yake nadhifu na fulana yake nyeupe iliyoandikwa Naipenda Tanzania, na juu yake alijitupi kijikoti cheusi, bastola yake aliipachika sawia katika mkanda wa suruali aliyovaa na kutoka moja kwa moja aliiendea gari yake aina ya Toyota Spacio na kuondoka akiiacha nyumba yake ikibaki na mlinzi tu. Njia nzima madam S alikuwa akilaani kilichotokea hapo Tazara, kama kawaida yake alitamani huyo mtu amkamate mara moja ili amuoneshe shughuli nene kwa kufanya jambo kama hilo. Alifika eneo la tukio na kukuta shughuli zikiendelea hasa zile za uchunguzi, pale alikutana na wakuu wa polisi na vyombo vingine vya usalama kila mmoja akiwa hana la kusema juu ya tukio hilo, laana za kumlaani aliyetenda hilo na vizazi vyake vyote ndizo zilikuwa midomoni mwao.

    “Atakamatika tu” Madam S alimwambia IGP walipokuwa katika mazungumzo huku wakiangalia shughuli ile ikikaribia kufika ukingoni.

    Madam S aliinua simu yake na kuitazama, ilikuwa yapata saa tano usiku, aliwaaga wenzake na kuondoka eneo lile mara moja huku akiwa na mawazo lukuki kichwani mwake.



    Siku iliyofuata



    “Miranda!” sauti nzito iliita kutoka mlango wa pili, ilikuwa ni sauti ya waziri wa ulinzi ambaye ndiyo kwanza alikuwa akiingia ofisini kwake asubuhi hiyo. Miranda alitii wito huo mara moja alikiacha kiti chake na kuufuata mkango mkubwa wa kioo uliokuwa kushoto kwake na kuufungua.

    “Nimefika mzee!” aliitikia. Bwana Sixtus Maige, waziri mwenye dhamana ya ulinzi katika serikali ya Tanzania aliinua sura yake iliyoonekana usawajika kwa mawazo na kujawa mikunjo ya hasira na uchungu.

    “Naomba uniitie Madam S, kitengo maalum usalama wa Taifa tafadhali, fanya hilo sasa hivi” aliamuru na Miranda mara moja alitii agizo alilopewa. Ndani ya ofisi yake aliandika fax ya haraka na kuituma kunakohusika, kisha akatulia akiendelea na majukumu yake mengine.



    Dakika kumi na tano zilikuwa nyingi, mlango wa katibu muhtasi wa waziri wa ulinzi miss Miranda ulifunguliwa na mwanamama wa makamo aliingia ndani na kumtazama binti yule aliyekuwa anajitazama kwenye kioo huku akipaka rangi ya mdomo. Miranda alistuka aliposikia mlango ukifunguliwa na kugeuka haraka.

    “Nimepata ujumbe msichana, mzee yupo?” madam S aliuliza na Miranda bila kujibu alimuonesha ishara ya kuingia katika ofisi ya mheshimiwa.

    “Karibu sana madam S, nilikuwa nakusubiri kwa hamu kubwa, kwa kukuona tu nahisi kazi imekwisha” waziri wa ulinzi mheshimiwa Maige alimkaribisha mgeni wake na kumuonesha kiti cha kukaa naye bila kusita akafanya hivyo, kasha mheshimiwa akaendelea, “Madam S najua wazi kuwa unafahamu lile nililokuitia, sina haja ya kulieleza maana jana sote tulikuwa kule Tazara kwenye lile tukio. Wito wangu hapa ni kutaka kuona pamoja nawe jinsi ya kulimaliza hili swala na kuwakamata wahusika, mheshimiwa Rais amesema lifanyike mara moja, na mi nikaona kuwa wewe ndiye unaejua jinsi ya kuifanya kazi hii kwa utaalam”

    “Ooh mheshimiwa, nimekusikia, nimetafakari sana juu ya hili swala tangu jana, lakini akili yangu haisomi”

    “Kwa nini?”

    “Sasa hivi sina watu, TSA 1 tumetuma huko China kwa ajili ya ile issue ya madawa ya kulevya, TSA 2 naye yupo kule Malawi kwa ajili ya kuweka mazingira tayari kwa ile kazi yetu, tufanyeje mheshimiwa, serikalai itakalosema sisi tutatii” madam S aliongea kwa msisitizo mkubwa.



    “Ok! Nimekuelewa vizuri, sasa naomba TSA 1, kamanda Amata arudi mara moja kwa ajili ya kazi hii” waziri maige alitoa oda.

    “Sawa mheshimiwa, litatekelezwa mara moja” madam S alijibu kwa heshima.

    “Akifika nchini naomba moja kwamoja uje nae hapa” mheshimiwa aliongeza. Madam S aliinua mkono wake na kuitazama saa yake kasha akabonyeza kitufe Fulani na kuendelea kubonyeza vijitufe vingine juu ya saa hiyo aina ya casio, kasha akatulia na uendelea na mazungumzo na waziri Maige wakijadili hali halisi ya tukio zima lililotukia usiku wa jana.



    Hong Kong – ChinaCHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Cheung Sha beach, Lantau



    Kamanda Amata alikuwa juu ya kitanda safi kilichotengenezwa kwa plastick huku akiwa amejilaza kifua chake alikiruhusu kipigwe na upepo wa pwani, akiitazama bahari tulivu iliyokuwa na mawimbi kiasi, pembeni yake mwanadada mrembo alikuwa amejilaza pamoja nae wakiongea mawili matatu.

    Baada ya mazungumzo yao yaliyokuwa marefu kiasi na kujawa na vicheko vya mahaba, walinyanyuka kutoka kwenye vitanda hivyo na kuelekea hotelini alikofikia kamanda Amata kwa ajili ya kuendeleza mazungumzo yao kwa vitendo. Akiwa anakaribia katika ngazi za kuingilia mapokezi ya hotel hiyo alipishana na mtu mmoja aliyekuwa akimtazama sana, Amata hakumtilia maanani mtu huyo, mkono wake wa kuume ukiwa kiunoni mwa mwanadada akili yake isingeweza kuwa makini tena katika jambo lingine.



    Walipanda ngazi kadhaa na kuufikia mlango wa chumba chake, Amata alikitazama kitasa cha mlango ule na kumrudisha kwa nyuma yule mwanadada kisha akatumbukiza ufunguo wake na kuufungua ule mlango, kwa hatua za hadhari aliingia ndani ya chumba ile, aliangaza huku na huku lakini hakuona dalili ya mtu ndani mle, lakini kila alipopiga hatua kwenda ndani alihisi damu ikikimbia na nywele kumsimama, alisogea kwa ndani ili kwenda kuichukua bastola yake aliyoificha chini yam to, hamad! Teke la nguvu lilitua tumboni mwake, kwa wepesi wa hali ya juu, Amata aliudaka ule mguu upande wa kanyagio na kuuzungusha kwa nguvu mpaka akauvunja, yowe la uchungu lilimtoka yule mtu, Amata alimsukuma na kumbamizia ukutani, akageuka nyuma haraka kumtazama yule mwanadada ndipo alipokutana na bastola iliyokwishatolewa usalama ikiwa mikononi mwa yule mwanadada ikimlenga yeye, Amata alijirusha kwa haraka na risasi iliyotoka ilichimba ukuta, kwa haraka aliuzungusha mguu wake na kumpiga ngawala safi yule mwanadada ambaye alipaa juu na kutua katika meza kubwa ya kioo huku bastola ikimtoka mkononi, iliokotwa na kamanda Amata na kushikwa barabara mikononi mwake. ‘Sina muda wa kupoteza,’ alijiwazia na kuifyatua ile bastola, risasi moja alifumua kichwa cha yule jamaa na nyingine ilizama moyoni mwa yule mwanadada, ‘Wanaharamu’, mara akasikia kamlio kadogo kama ka mashine ya typewriter kakilia kutoka katika kitu kama kitabu juu ya droo ya kitanda, alikawahi na kutoa kijikaratasi kirefu kilichokuwa na maandishi machache.



    “Hali siyo nzuri, rudi haraka mgonjwa anahitaji msaada wako, Tena Sana Aisee” alikirudisha kile kikaratasi katika ile notebook bandia kumbe ilikuwa ni fax mashine akaifungua tena ile fax machine yake na kurudia kusoma kile kikaratasi, akabaki akishangaa ‘Nini kimetokea?’ alijiuliza kwa kuwa kazi aliyotumwa huko ilikuwa ndiyo kwanza imepamba moto, alinyanyauka na kufungua kabati la nguo kasha akapaki kila kitu begini, alipokamilisha akaitazama ile miili ya wale viumbe wawili waliotaka kuiondoa roho yake, akatoka taratibu katika chumba hicho na kujipanga kwenda uwanja wa ndege tayari kwa safari.



    Dar es salaam



    Kamanda Amata alikaribishwa na vichwa vya habari vya kutisha katika magazeti siku hiyo, ‘Mlipuko mkubwa waitikisa Dar es salaam’ na lingine likaandika, ‘Ugaidi waigubika Dar’, na mengine mengi yaliandika kila moja kwa jinsi zake.

    Kamanda Amata aliinua uso wake na kumtazama waziri wa ulinzi kasha akamtazama madam S na kushusha pumzi ndefu.

    “Yes, Kamanda, hiyo ndiyo hali halisi iliyoukumba mji wetu, taifa lipo kwenye maombolezo ya siku tatu, bendera nusu mlingoti. Serikali inaiomba ofisi yenu wewe pamoja na madam S kuikamilisha kazi hii kwa haraka na ufanisi mkubwa, tuko tayari kuto msaada wowote pale utakapoitajika, nawatakia mafanikio mema katika hili na Mungu awatangulie” waziri wa ulinzi mh Maige alimaliza rai yake

    “Amin!” kamanda Amata alijibu na kumtazama madam S. akiwa ndani ya suti yake nyeusi Amata alinyanyuka kitini na kuongozana na madam S kutoka katika ofisi hiyo, walipita pale alipo Miranda na kugana nae, jicho la kamanda Amata lilimtazama kwa tuo mwanadaa huyo ambaye daima utamkuta akitengeneza kama siyo nywele basi rangi ya midomo kupitia kijikioo kidogo alichokihifadhi katika motto wa meza.



    “Hata usipojiremba, we bado ni mrembo tu” Amata alianza uchokozi wa maneno kwa mwanadada Yule.

    “Mmmmm kamanda, kuna warembo nitakuwa mimi?” alimjibu huku akiyarembua yale macho yake makubwa, “Nitoe lunch leo,” alitupa ombi huku akiendelea kujitazama kiooni.

    “Usijali, mrembo kama wewe hakuna mwanaume atakayekunyima lunch, hata dinner kabisa” Amata alijibu huku akiwa ameushika mlango tayari kutoka.

    Piipiiii, honi za gari ya madam S zilimshtua kamanda kwenye maongezi yale.

    “Unaitwa na mama yako huko uende,” Miranda alimwambia Amata

    “Ok Beibi, nitakucheki mida” alijibu na kutoka nje.

    Aliingia garini na kuketi, kasha akajifunga mkanda wa usalama.

    “Hivi hii tabia yako utaiacha lini? Wengine wake za watu hao!” madam S alimueleza Amata.

    “Aaa bibi, hata mimi mtu jamani” alijibu kwa utani.

    “Shauri yako hivi vingine vitakugharimu sana”

    “Shaka ondoa”



    ??????



    “Hili bomu lilikuwa ni bomu la masaa, bomu ambalo hutegwa makusudi kwa malengo maalum, kwa hiyo siyo mlipuko wa kawaida ni wa kukusudiwa” kapteni Savana alikuwa akimpa ripoti ya kwanza ya uchunguzi kamanda Amata walipokutana pale makao makuu ya jeshi Upanga.

    “Kwa hiyo unataka kuniambia mlipuaji alitega kwa malengo maalum?”

    “Ndiyo”

    Kamanda Amata alitazama lile faili lililo mbele yake na kuligeuzageuza. Baada ya mazungumzo ya kina waliagana na Amata akaenda mahali pengine kwa uchunguzi....



    BREKI ilikuwa katika kituo cha polisi cha Tazara kuitazama gari ile iliyotumika kwa mlipuko ule. Mezani mbele yake alikutana na ASP Majegero.

    “Kuna lolote mmepata kuhusu hii gari iliyobeba mlipuko?” lilikuwa ni swali la Amata kwa ASP majegero.

    “Aaa hapana ila bado tunaendelea na uchunguzi ukizingatia gari yenyewe imeungua vibaya inakuwa ni ngumu kutekeleza hilo kwa wakati”

    “Ok, hebu nilione.” Wote wawili walitoka na kuzunguka uani kuiona gari ile, Amata aliitazama jinsi ilivyochakaa, aliizunguka na mara akakutana na kile alichokuwa akikitafuta.



    Plate namba ya gari hiyo iliyoungua vibaya kwa moto, Amata aliing’oa na kuitazama kisha bahati nzuri namba zake zilikuwa za kugongwa siyo zile za kupuliza, Amata alisoma namba zile kiurahisi na kuziandika kwenye kijitabu chake kidogo kasha akaagana na Yule askari polisi na kuondoka zake. Breki ya kwanza ilikuwa katika jingo la TRA pale Samora evenue, alishuka na kufika mapokezi ambapo aliomba kuonana na ya kuperuzi katika mtandao wao.

    “Kadiri ya namba hii hiyo ni gari inayomilikiwa na mama mmoja anaitwa Miss Jesca Mdachi” Yule dada alimjibu Amata.

    “Ok, maelezo yake mengine tafadhali” Kamanda Amata aliomba

    Yule mwanadada aligeuka kwenye kompyuta na kuprint karatasi Fulani akarudi na kumpatia Amata.



    “Kila kitu kimeandikwa hapa” alimwambia Amata

    “Ok asante sana mrembo” Amata alishukuru.

    “Kuna linguine tafadhali?” Yule dada alihoji kama kuna lingine anahitaji msaada nalo. Amata alimtazama Yule dada kwa uchu alivutiwa na kifua chake kilichobeba matiti yaliyojaa vizuri.

    “Hapana kingine zaidi ya namba yako ya simu, kama upo radhi” Amata alitoa ombi lingine la binafsi, Yule mwanadada alimtabasamia Amata kisha akauvuta mkoba wake na kutoa business card na kumpatia, kisha Amata akaondoka zake.



    ??????



    “Hatutawaacha hai hata mara moja, kila tutakapoamua kulipua tutahakikisha tunaua watu zaidi ya hamsini. Kosa lenu mnalijua, kuingilia mambo yasiyowahusu, vita ya watu wa Maghalibi na sisi, ninyi haviwahusu, kwa nini mnaingilia. Sasa tunasema kwa sauti moja, tutawaua na tutawaua mpaka mtakapomuachia huru ndugu yetu Jegan Brashan mliyemfunga katika magereza yenu huko Tanzania. Tunawapa siku saba mumuwache huru zikipita bila kutekeleza mlipuko mwingine utatokea karibu kabisa na pua zenu…”



    Waziri wa ulinzi bwana Maige aliizima cd ile iliyokuwa ikitoa ujumbe huo katika luninga kubwa iliyofungwa ofisini hapo, kisha aligeuka kuwatazama Amata na madam S pamoja na watu wachache waliokusanyika ofisini hapo baada ya wito wa dharula kutoka kwa waziri huyo.

    “Hii cd imeletwa na Miranda ameikuta katika sanduku letu la posta asubuhi hii,” waziri Maige alilieleza lile jopo. Madam S alitoa kitambaa chake na kujifuta jasho ilhali hakuwa na jasho ilimradi tu akili yake ilikosa utulivu.



    “Kazi tunayo, tena siyo ndogo” madam S alisema kwa utulivu.

    “Sasa wewe mama ukisema hivyo sisi tutasemaje?” aliuliza mjumbe mwingine aliyekuwa katika kikao hicho. Wote wakabaki kimya kwa muda wakitafakari hili na lile.

    “Lakini hawa ni nani? Al Qaeda, Al-Shabab, Boko Haram au ni nani?” alitupa swali mtu mwingine.

    “Mimi na wewe hatujui, ndiyo maana niliwaita ili ninyi kama watu wa juu wa usalama wa nchi hii mlipatie ufumbuzi” waziri Maige alijibu.

    “Ina maana baada ya siku saba tutegemee mlipuko mwingine sivyo?” aliuliza mjumbe mwingine.

    “Ndiyo maana yake, hapa hatujui tunapigana na nani na wangapi na wako wapi, katika medani za ijeshi tunasema, adui mbaya ni yule aliye ndani yako. Sasa adui huyu tayari yuko nchini mwetu, tufanye juu chini kabla ya wiki tuwe tumefanikisha hilo” Madam S alizungumza kwa jazba.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Wanataka tumuachie huru Jegan Brashan na wao wasitishe malipuzi yao, ninyi mnasemaje?” waziri aliuliza.

    “Dunia itatushangaa sana kwa kufanya hilo, kumuachia Jegan! Hilo sijahafiki hata kidogo, tuone kwanza hii wiki moja tunafikia wapi,” madam S alijibu.

    “Kamanda Amata mbona uko kimya sana? Huna la kuzungumza?” waziri alimuuliza Amata

    “Jegan Brashan, hawezi kuwa huru hata iweje, hata iwe vita ya tatu ya dunia, mimi Amata TSA namba 1 sitalikubali, labda itoke maiti yake lakini si yeye kamili” alimaliza kwa kauli tata.

    “Amata, unazungumza nini? Tunataka tupate muafaka wa hili,” waziri Maige alimkaripia kidogo Amata.

    “Kwanza hiyo cd imenipa mwanga, nataka nianze na Jegan Brashan kisha hapo nitajua wapi pa kuendelea, naomba mnipe muda wa siku tano kisha tuone tena pamoja” Amata alimaliza kusema. Wote waliafikiana nae na kupeana kazi mbili tatu kisha wakatawanyika.



    Gereza la Ukonga



    “Jambo afande!” Amata alisalimu

    “Jambo!” alijibu askari mmoja liyekuwa getini akiangalia usalama wa eneo hilo ambalo limehifadhi watu hatari kwa usalama wa taifa hili. Aliliendea gari la Amata na kuzungumza nae machache kisha akafunguliwa geti na kuingia, aliiacha ile njia inayoelekea chuo cha maafisa na kukunja kushoto kuufuata mlango amkubwa wa gereza hilo, baada ya mwendo wa kama mita mia mbili hivi aliegesha gari yake na kuteremka, alirekebisha tai yake na kujiweka koti lake vizuri kisha akauendea mlango ule na kutikisa kichuma Fulani, mara kajimlango kalikokuwa katikati ya ule mlango mkubwa kakafunguliwa naye akajitoma ndani.

    “Naweza kuonana na bwana jela?” aliwauliza wale maafisa aliyowakuta pale.

    “Bila shaka, nifuate…”

    Kamanda Amata alimfuata yule askari na mara wakafika kwa bwana jela, yule askari akarudi na Amata akabaki pale.

    “Naitwa Amata,” akajitambulisha na kutoa kitabulisho chake na kumkabidhi.



    “Ndiyo bwana Amata, karibu sana chuo cha mafunzo, nikusaidie nini tafadhali?”

    “Yah nahitaji kumuona mfungwa wa kigaidi bwana Jegan Grashan, nina mazungumzo nae”

    “Bila shaka, je una kibali maalum? Maana huyu mfungwa hatakiwi kuonana na mtu yeyote wala kuona mtu yeyote”

    “Nimetumwa na serikali, na kitambulisho changu ndiyo kibali” Amata alijibu kwa tindo huo.

    “Ok, ngoja nikupe vijana wakupeleke, ila uwe makini sana tusije kupata lawama”

    Baada ya dakika tatu hivi vijana wanne waliovalia sare nadhifu ya magereza, wenye maumbo ya kipiganaji hasa, mabegani mwao walikuwa na vile vibaka vya kijani, Amata mara moja alijua wale ni vijana wa kazi KMKGM.



    Jegan Grashan, kijana anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka thelathini hivi, alitokea kuwa gaidi tishio katika ukanda wa Africa Mashariki, akiwa anafanya kazi na kundi kubwa linaloendesha shughuli hizo sehemu mbalimbali za dunia. Alipitia mafunzo ya kijeshi huko Pakistan na kuwa mpiganaji hodari, lakini baada ya muda Fulani aliai jeshi na kujiunga na vikundi vinavyoendesha mapinduzi kwa njia za kigaidi ndani na nje ya Pakistani mapaka alipojikuta kwenye mtandao mkubwa na wa kimataifa na kutekeleza mauaji mengi sehemu mbalimbali, japokuwa dunia ilikuwa ikimsaka kwa udi na uvumba huko Mashariki ya kati, kumbe kijana huyu hatari alikuwa ameweka makazi yake Africa ya Mashariki katika mji wa Mombasa, Kenya, wakati dunia imeanza kumsahau kwa unyama wake, Jegan aliibuka tena mwaka 1998 Tanzania na Kenya, alipopanga milipuko iliyopishana dakika kumi tu, ule wa Dar es salaam ulitokea saa 4” na ndipo dunia ilipostuka na kutambua kuwa mtu huyu bado yupo asakwe mpaka apatikane. Ilipita miaka kadhaa serikali ya Tanzania ilipomtia mkononi Jegan katika viunga vya mji wa Tanga akiwa mbioni kutorokea ughaibuni. Ndipo ilimchukua na kumuweka jela katika gereza kuu la Ukonga akiwa anasubiri hatima yake isiyojulikana ni lini ingetimia.



    ??????



    Jegan Grashan aliketishwa katika kiti cha chuma huku akiwa amefungwa minyororo madhubuti katika kiti kile, wale vijana wa KM wa magereza walitakiwa kusubiri nje ya chumba cha mahojiano, ndani alibaki Kamanda Amata na Jegan, wawili tu walioketi kwa kutazamana. Jegan alimtazama Amata kwa jicho la chuki na hasira, lakini Amata alikuwa akimtazama kwa jicho la upendo na ukarimu.

    “Jegan, rafiki zako wametuomba tukuachie huru, upo tayari?” Amata alianza kumuuliza swali la kizushi.

    “Usinifanye mimi mtoto, ninajua leo ni tarehe ngapi na ni nini kimetukia juzi” Jegan alijibu kwa sauti ya kukwaruza.

    “Ok, je hiyo ndiyo njia ya wao kuomba uwachiwe huru?” Amata aliendelea

    “Naam, na mtakwisha ninyi vibaraka wa Maghalibi, hii vita hamuiwezi kamwe, wao wanataka mimi niachiwe huru lakini mimi nimetumwa kwa Wamarekani nina ujumbe wao na wao wanaufahamu” Jegan alijibu huku akimwangalia Amata kwa gadhabu.

    “Kwa hiyo ujumbe wao uliusafirisha kwa milipuko ya mabomu?”

    “Ha ha ha ha Kamanda Amata, we ni mtoto mdogo sana na jina lako tunalo kati ya watu wanaotakiwa wachinjwe” Amata aliingiwa na hofu kidogo aliposikia mtu huyu akilitaja jina lake tena kwa ufasaha.

    “Niambie ninyi ni nani na mna uhusiano gani na vitendo vya kigaidi vinavyosambaa duniani kote hivi sasa?”



    “Usiniambie hujui kitu wewe mwana Intelijensia, hii ni vita kaka, tunapiga kila walipo adui zetu, 1998 tumepiga pale Dar, ile ilikuwa ni onyo na ile ilikuwa ni opereshen al – aqsa, ilipangwa kaka, na ile ya Nairobi ilikuwa ni opereshen kama hiyo, nakwambia haya yote nikijua wazi hutoyafikisha popote kaka. Kama wewe ni mwana historia kumbuka mlipuko wa bomu ulikuwa tarehe 7 august 1998 ambao ilikuwa ni miaka nane kamili tangu majeshi ya Marekani yaikalie Saudi Arabia. Una swali lingine?”

    Amata alijikuta ameduwaa kwa kuwa mambo yale hakuwahi kuyaunganisha namna hiyo katika kazi zake na wala hakujua kama yana uhusiano mkubwa namna hiyo.

    “Swali langu la msingi ni kuwa nani anayewatuma na kuwafadhili?”

    “Kamwe sintokwambia, kwa kuwa haitakusaidia, lakini kwa kifupi mabosi wenu walioko Maghalibi ndiyo wanaotutuma”

    Ilipita takribani saa nzima ya mahojiano kati ya wawili hawa, kamanda Amata alipata majibu mengi sana ya maswali ambayo labda angeyauliza miaka kumi liyopita ila yale aliyoyataka leo hakuyapata kabisa kwa wepesi.



    MIAKA KADHAA ILIYOPITA

    7 august, 1998



    Gari aina ya Nissan Atlas iliyokuwa imepakiwa mlipuko wenye uzito wa kilogram 900 ambapo madini aina ya TNT yaliunganishwa na mitungi kumi na tano ya hewa ya Oxygen na kuzungukwa na mifuko minne ya amonium nitrate, waya uliounganishwa kutoka katika bomu hilo mpaka katika betri zilizokuwa upande wa nyuma wa gari hiyo na switch yake kuunganishwa chini ya dashboard. Gari hiyo iliegeshwa nje ya jengo la ubalozi pale katika barabara ya Bagamoyo, mlipuko wake haukuleta maafa sana kwa kuwa eneo lile hakukuwa na makazi ya watu jirani yake tofauti na Nairobi kule Kenya.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilikuwa ni kizaazaa katika eneo hilo watu walitawanyika ovyo, vioo vya madirisha vilivunjika, gari za zima moto na uokoaji hazikuchelewa kufika, taharuki iliukumba jiji lote la Dar es salaam.

    Jegan Grashan alimaliza kazi yake aliyoikusudia na bila kuchelewa alipanda boti inayoelekea Pemba na kutokomea uko akisikilizia ni nini kitaendelea.

    Vyombo vya dola vilianza uchunguzi wake mara moja kutafuta chanzo cha mlipuko huo, FBI kutoka Marekani nao walifika haraka sana kusaidia, na baada ya miezi kadhaa Jegan Grashan alikamatwa na kuhusishwa moja kwa moja na uandaaji wa milipuko hiyo (masterminds), baada ya kesi yake kuunguruma kwa kipindi kirefu alihukumiwa na kuwekwa katika gereza kuu la Ukonga.



    ??????



    Kamanda Amata akaondoka eneo la gereza kurudi mjini, aliitazama saa yake ya mkononi, ilimuashiria kuwa ni saa saba mchana, alikanyaga mafuta kuwahi mjini kwani alikuwa na miadi na kimwana Miranda kwa chakula cha mchana, alipoanza kuteremka kilima kidogo cha kushukia Banana kuelekea alisikia kishindo kikubwa na gari yake ilianza kuyumba kushoto kulia, alijaribu kuiongoza vema lakini bado ilikuwa ikiyumba, kutokana na mafunzo aliyoyapitia ya uendeshaji gari wa kujihami ‘defensive driving’ aliyopewa alipkuwa ughaibuni aliiendesha gari hiyo kwa umakini mkubwa na alipoweza kuweka sawa alikutana uso kwa uso na lori la mchanga kishindo kikubwa kilisikika, gari ya Amata iligongwa na kukanyagwa vibaya...



    KITENDO bila kuchelewa, Subaru moja nyeusi ilifika eneo hilo na kusimama jirani, watu wanne walishuka haraka na kuelekea kunako gari ya Amata, walichungulia huku na huku lakini hawakuona kitu wala mtu, mara ghafla kutoka upande wa pili wa gari ile ya mchanga kamanda Amata alijirusha na kumpiga double kick mmoja wao ambaye alidondokea katika michongoma iliyo jirani tu na barabara, kabla hajakaa sawa; tayari Beretta 92, bastola ya kiitaliano ilishafanya yake na yule mtu kuitwa marehemu, yule wa pili alijikuta ana kwa ana na kamanda Amata alijaribu kujitetea lakini haikuwezekana, mateke ya kuzunguka ya Amata yalimfanya ashindwe kujielewa na kuyumba vibaya alisimama na kujipanga kimapigano huku wale wenzake wakitafuta upenyo wa kuiondoa gari yao maana tayari gari zilikuwa zimejaa eneo lile, alirusha ngumi ambayo iliepwa na Amata, kisha Amata alijibu mapigo kwa makonde kadhaa ya mbavuni na kummaliza pumzi, wakati Amata anataka kupeleka mashambulizi mengine jicho moja liliwaona wale wanaotaka kutoroka mmoja akiwa na bastola tayari akimlenga na alipoifyatua tayari Amata alitoka eneo lile kwa kujiviringa chini na kupita uvungu wa lori na kuacha risasi ile ikipita kifuani kwa yule mwenza wao akipaishwa nakudondoka kama mzigo.



    Amata alitokea upande wa pili, tayari hima hima bastola yake mkononi tena, alisikia kelele za tairi ya gari ikijigeuza barabarani lakini walichelewa bastola ya Amata alipasua kioo cha nyuma cha gari hiyo na kumjeruhi vibaya mmoja wao lakini dereva aliendelea kuiondoa gari ile kurudi uelekeo wa Pugu, kamanda Amata alitazama huku na huku akamfuata mwanamama mmoja aliyekuwa hapo na gari yake aina ya Toyota Harrier na kumtoa kwenye usukani kisha kukaa na kuiondoa kwa kasi kuifuata ile Subaru. Mwendo ulikuwa si wa kawaida, walipita mbele ya gereza la Ukonga na kuelekea pande za Gongo la Mboto, Amata alifanya juu chini asiipoteze ile Subaru ambayo ilikuwa ikienda kasi sana huku ikifanya ovateki za hatari, Amata naye alihakikisha anakwenda sambamba nalo, walipoimaliza Gongo la mboto na kuianza Pugu, tayari magari mengi yalipungua, Amata alikaza mguu na ile Harrier ilitii, dakika chache tu alikuwa anaikaribia ile Subaru. Kwa kasi ileile walipandisha mlima wa Pugu tayari Amata alishaanza kuipita ile Subaru mara ghafla akanyonga usukani upande wa kushoto na kuigonga ile gari kwa nyuma kidogo ya ubavu wake na kuifanya ile gari kuyumba upande wa kushoto na kupoteza muelekeo mara ikatumbukia na kubingirika katika bonde la mlima huo.



    Amata alishuka katika gari yake bastola mkononi na kuifuata kule chini mpaka ilipokwama, alitazama ndani na kumuona yule dereva akiwa hoi pale kwenye usukani, akauvuta mlango kwa nguvu na kumtazama kwa makini yule bwana aliyejiinamia huku usukani ule ukiwa umembana kifuani, damu zilimtoka kinywani na puani, hakuna msaada, yule mwingine tayari alikwishakufa maana alionekana kuvurugwa kichwa chote kwa risasi ya kamanda Amata iliyofumua ubongo wake na kusambaratisha kichwa chake, alimsogelea yule aliyekuwa dereva wa gari ile na kumtazama vizuri, akamzaba kofi la shavu lililomfanya pamoja na maumivu yake kugeuka.

    “Ninyi ni nani?” alimuuliza huku akimuwekea bastola kichwani, yule jamaa alionekana kutetemeka, “Sema, usipoteze muda!” aling’aka kamanda Amata huku akivuja damu sehemu ya paji la uso ambapo palichanika kwa vioo katika ajali ile. Yule jamaa alikuwa akihema kwa tabu sana, mara simu ya Amata ikaita, akaingiza mkono mfukoni na kuitoa alipotazama kwenye kioo aliona jina la ‘Miranda’ likiwakawaka, akabonyeza kitufe chekundu na kuirudisha mfukoni, alipogeuka kwa yule jamaa alimkuta tayari ameshakufa akiwa anamwagika povu na damu kinywani. Kamanda Amata aliirudisha bastola yake mahali pake na kumpekuwa yule jamaa, bahasha ya khaki ilikuwa katika mfuko wake, vitambulisho kadhaa na kadi za kibiashara, alipoona vinatosha alivihifadhi mfukoni mwake na kupanda kile kilima kuifuata ile gari aliyoiacha pale juu. Akajikung’uta vumbi na kujihifadhi ndani yake, aliiwasha na kuigeuza kisha taratibu kuifuata barabara ya Nyerere kurudi mjini, mbele kidogo alikutana na gari za polisi wakamuwashia taa kwa ishara ya kusimama nae akatii.



    Amata alimuona yule mama aliyemnyang’anya gari akiwa na wale polisi wakimfuata, akashuka na kuwasubiri.

    “Kijana tunakuweka chini ya ulinzi kwa kuwa umepora gari ya watu na kufanya mauaji” polisi mmoja alimwambia Amata huku akitoa pingu zake mfukoni mwake, Amata alinyoosha mikono yake na kufungwa zile pingu huku shati lake likiendelea kulowa kwa damu tiririka zilizokuwa bado zinadondoka kwenye jeraha lake. Akaingizwa kwenye gari Land Cruiser ya polisi na kuamuriwa alale chini kisha wale polisi wakasimama juu yake na ile gari ikageuzwa kurudi mjini huku polisi mmoja na yule mama wakiingia katika ile harrier na kuwafuata nyuma.

    Mabatini polisi, Stakishari

    “Weka ndani jambazi hili, linapora magari ya watu tu,” yule polisi alimwambia mwenzake huku akimsukumia Amata nyuma ya kaunta.

    “Vua mkanda, vua viatu uingie pale kwa wakora wenzio” aliamuru polisi aliyekuwa nyuma ya kaunta karibu kabisa na WP mmoja aliyekuwa akiandikaandika katika daftari kubwa, aligeuka na kumuangalia Amata kwa makini juu mpaka chini, kisha akasonya.

    “Unashangaa nini si umeambiwa uingie huko ndani” yule WP naye aliongea huku akibetua midomo yake.



    “Tafadhali afande nakubali, ila naomba nimpe taarifa mke wangu ili ajue niko wapi” Amata aliomba

    “Haya we afande Mary, msaidie ombi lake kisha aende huko ndani” amri ilitolewa na yule polisi aliyemleta Amata pale kaunta.

    WP Mary alimtazama Amata kwa mara ya pili na kubetua midomo yake kinafiki.

    “Unaomba tu upige simu unajua anayezilipia ni nani? Haya taja namba haraka watu tuna mambo mengi,” WP Maria alimueleza Amata kwa sauti kali, Amata alimtajia namba ile yenye takribani tarakimu saba, WP Maria alizungusha tarakimu zile kisha akaweka kile chombo sikioni.

    “Haya inaita, ongea haraka,” WP Maria alimwambia Amata.

    “Hello mama, mimi kijana wako, nakupa taarifa kuwa nimekamatwa na polisi nipo hapa kituo cha Mabatini Stakishari Ukonga, msaada wako tafadhari” Amata alirudisha simu kwa WP.

    “Ongea na mama tafadhali” alimwambia

    “ (…) Ee tumemkamata mwanao we njoo ndiyo utajua kosa lake, hatuna muda wa kuongea kwenye simu” WP Maria alimaliza na kukata simu.

    “Haya ingia huko ndani,” alimwambia Amata, naye bila shida aliingia na kufungiwa selo pamoja na vijana wa kihuni wa kila aina ndani humo.



    ??????

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Jambo afande!” OCD Masoketi aliwasabahi polisi waliokuwa katika kaunta ya kituo hicho na wote wakakauka kwa kusalute kwa mkuu wao wa kazi, walionbekana wazi kujiweka sawa hapa na pale maana hawakutegemea ujio huo kwa muda wa adhuhuri kama ilivyotoke. OCD Masoketi alisimama karibu na ile kaunta na kuwaangalia wale vijana walioonekana busy na kazi mbalimbali.

    “Afande, kuna mtu mmemkamata na kumuweka ndani hapa mida hii?” OCD akauliza

    “Ndiyo mkuu, ni jambazi aliyepora gari ya huyu mama tunayemchukua maelezo sasa,” alijibu WP Maria

    “Mna uhakika gani kama ni jambazi?”

    “Kwa maelezo ya huyu mama, ni kuwa gari yake alinyang’anywa katika eneo la ajali pale karibu na Banana na kabla ya hapo anasema huyu mtuhumiwa alikuwa anarushiana risasi na watu wengine. Na hapa tumemkuta na bastola aina ya Berreta 92 vyote vimehifadhiwa mkuu” alijibu polisi mwingine aliyemleta Amata pale kituoni.



    “Muwe makini na kazi yenu nyie vijana, nimeshawaambia mara nyingi jinsi ya kumhiji na kumchunguza mtuhumiwa, au hamjajifunza CCP? Haya nifungulieni huyo mtu haraka mniletee ofisini kwangu” OCD Masoketi aliongea huku akiwanyooshea mkono uliokuwa na redio call mkononi. Kamanda Amata alifunguliwa kutoka selo na kuongozwa na WP Maria mpaka ofisini kwa OCD.

    “Karibu kamanda, keti kitini, WP mletee kinywaji baridi tafadhali” OCD alitoa oda na kutekelezwa na WP kwa haraka, huku kichwani mwake akitafakari ni nani huyu anayeitwa kamanda. Mazungumzo yalifanyika ofisini mle kwa dakika chache tu na yule mama alipewa maelekezo ya kufuata ili kesho yake apewe gari ingine kwa kuwa ile ilikuwa imeharibika sana upande wa mbele, baada ya kumaliza kila kitu alirudi kaunta na kurejeshewa vitu vyake vyote alipovikagua viko salama, akachomoa kadi yake moja ya biashara na kumtupia WP Maria.

    “Baadae unitafute,” alisema huku akiteremka ngazi na kusimama kwa muda. Yule mama aliondoka na tax aliyolipiwa na Amata na kuiacha ile gari yake pale kituoni, akiwa bado na mazungumzo na OCD mara freelander ya kijivu ilisimama kando kidogo ya mti mkubwa uliokuwa hapo, wakaagana na OCD kisha akaiendea ie gari na kuingia ndani.



    “Amata nini tena? Mbona una majanga kijana?” ilikuwa sauti nyororo ya Gina, katibu wake muhtasi katika ofisi yao ya AGI International-clearing and forwading.

    “Ah Gina we acha tu, hebu nipeleke hospitali kwanza kisha tukapate lunch mahali”

    “Kwanza nashangaa kukuona hapa, we si ulikuwa China!?”

    “Nimerudi jana ila sikukwambia makusudi ilikuwa surpries tu,” kisha wote wakacheka na kugonga viganja vya mikono yao.

    “Haya bwana nimefurahi kukuona tena nilikuwa mpweke kweli bora umerudi mtu wa kunipa faraja” Gina aliongea huku akiingiza gari barabara ya Nyerere na kuiacja ile ya Segerea.

    “Mmm unataka nipigwe na Malick?” Amata akamtania Gina huku wakipotelea mjini.



    ??????



    Betram aliinua mkono wake na kutazama saa yake ilikuwa tayari saa tisa na dakika kadhaa, akiwa bado amesimama katika dirisha la ghorofa ya tano akiangalia chini getini labda atawaona vijana wake wakirudi haikuwa hivyo, moyo wake ulianza kukumbwa na wasiwasi, alitoka pale dirishani na kuindea meza kubwa yenye kompyuta na vitu vingine vya mawasiliano ambapo kulikuwa na mtu mmoja wa makamo.

    “Kaka! Hawa jamaa sidhani kama wamefanikiwa misson tuliyowatuma naona muda unakwenda, vipi unawapata kwenye GPS?” Betram alimuuliza Shakrum mtaalamu wao wa mawasiliano.

    “Hapana hata huku siwaoni kabisa nafikiri kwa vyovyote watakuwa wamepata tatizo maana hata simu zao hazipatikani kabisa” Shakrum alijibu, huku akijaribu kubofyabofya tena simu iliyopo pale mezani akijaribu kuwatafuta swahiba zao hao. Alipojaribu kupiga ile simu kwa mara nyingine iliita kwa muda mopaka ikakatika, moyo ukaanza kumuenda mbio, kabla hajasema lolote simu ya mezani iliita akainyakuwa kwa shauku.



    “Fungua TV yako utazame TBC” sauti ya upande wapili ilimwambia kisha simu ikakatika. Shakrum alinyanyuka haraka na kuindea TV kubwa iliyopo hapo sebuleni na kuiwasha kisha kuchagua ile channel aliyoambiwa.

    “Mama yangu mzazi!” Betram alitamka kwa sauti huku mikono yake ikiwa kichwani kwa mshangao, walitazama ile habari ya wakati huo ikionesha ajali iliyotokea mchana ule na nini kiliendelea, kisha gari iliyokutwa katika bonde la mlima wa Pugu na maiti za watu wawili ambazo hazikutambulika kwa mujibu wa polisi.

    “Shakrum, fanya haraka funga vitu vyako tuondoke hapa siyo pa kukaa tena, twende Mombasa tukajipange upya tuendeleze kazi yetu, hatukati tamaa” Betram alimweleza Shakrum kwa kumsisitizia huku akiingia chumbani kwake na kukusanya kila kinachomhusu, ndani ya nusu saa walikuwa tayari kwenye gari yao aina ya Toyota Prado tayari kwa kuondoka. Mara simu ya Betram ikaita

    “Ee ndiyo tunaondoka sasa na jamaa zetu wane wameuawa katika sakata hilo wameshindwa kufanikisha mission yetu (…) yeah nimekusikia boss, tutakuwa hapo alfajiri ya kesho.”



    ??????



    Usiku huo Kamanda Amata aliegesha gari yake karibu na barabara ya kuingia hosteli za chuo kikuu zilizopo Mabibo, kisha akateremka na kutembea kwa tahadhari akiufuata ukuta unaotenganisha kiwanda kimoja na magenge ya wauza mboga, ilikuwa kama saa nane hivi eneo lote lilitawaliwa na ukimya wa hali ya huu, watu walishalala zamani waliobaki nje ni makahaba, wezi, wachawi na wale tu wenye kazi maalum. Aliendelea kuambaa ambaa na ule ukuta mpaka upande wa nyuma na hapo alijikuta karibu na jingo refu la ghorofa kama saba hivi lililojengwa ndani ya wigo ule, sauti za watu zilisikika zikitoka upande wa ukuta ule kule alikotoka, kwa utulivu mkubwa alijibana kati ya ukuta na nguzo kubwa ya umeme, hakuweza kuonekana na mtu hasa kutokana na mavazi yake meusi yaliyomfanya afanane na kiza cha usiku huo. Vijana kama watatu walipita eneo lile wakiwa na vitu mbalimbali wamevibeba huku wakionekana kulaumiana kwa jambo Fulani, vibaka. Walipopita tu, taratibu Amata alikwea ile nguzo ya umeme na kujikuta juu ya ukuta, kisha akatua ndani taratibu na kuchuchumaa kwa ustadi uliowafanya walinzi wa eneo lile wasistuke kama kuna kiumbe kimeingia. Kisha akatazama huku na huku ili aone wapi pa kuelekea, mlinzi mmoja alipoenda upande wa pili Amata alikimbia kwa tahadhari na kujificha nyuma ya matank ya maji yaliyowekwa pembezoni mwa jengo lile, alitazama mlango wake wa kuingilia ndani kisha akauendea na kupachika ile funguo yake maalum kisha akaingia na kuufunga nyuma yake, ngazi ndefu zilikuwa zikimsubiri, akapanda ya kwanza na ya pili akakutana na milango kadhaa, hakujua hasa mlango gani anaoukusudia, alisimama kidogo kisha akatoa simu yake na kuipiga namba Fulani, akasikia mlio wa simu inaita ghrofa ya juu, akaikata na kutulia kidogo kisha akaendelea kupanda ngazi hadi gorofa mbili zinazofuata na kukuta mlango mmoja tu, akatoa funguo zake na kupachika tunduni alipozungusha tu mlango ulilegea na kufunguka.



    Sebule kubwa lilimkaribisha lililojazwa vitu vya thamani vya kisasa aliichunguza ile sebule kwa macho kisha akaenda kwenye meza kubwa iliyokuwa na kompyuta juu yake akaiwasha na kujaribu kupekuwa hapa na pale lakini hakuna cha maana alichokiona, akaiacha na kuingia chumbani hakuna mtu, akafikiri kwa muda akaona windo lake alilolitegemea amelikosa akageuka kuondoka, lakini macho yake yakavutwa na karatasi moja iliyo chini ya kabati, akaiendea na kuiokota akaifungua harakaraka ilikuwa ni tiketi ya ndege ya iliyobeba jina la Shakrum Shakran, raia wa Khazakistan, aliyeingia nchini siku nne nyuma kwa ndege ya shirika la ndege la Qatar, kamanda Amata aliitia mfukoni tiketi ile na kutoka katika jengo lile kwa mtindo uleule.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kenya Bay Beach Hotel – MOMBASA



    Ukimya ulitawala katika meza moja ya duara iliyozungukwa na watu takribani saba waliokaa kwa kutazamana, hakuna aliyeongea kabisa ilionekana kama wote wamepatwa na mshangao. Aliyeonakana kama kiongozi wao alikohoa kidogo na kuwatazama wenzake walioonekana kama wamegutushwa kwa kukohoa huko.

    “Leo ni siku ya tatu tangu tutekeleze ule mlipuko pale Dar, tunawasikiliza kama watatimiza takwa letu la kumuacha huru Jegan Grashan, lazima tumkomboe mwanamapinduzi wetu kwa damu iwayo yote. Tanzania wametuchokoza, kuwaua vijana wetu wane kwa siku moja ni dharau kubwa sana, tutahakikisha tunalipiza kwa mamia ya damu. Sasa tusuke mpango mwingine wa kuwamaliza mpaka aikulu yao itikisike kwa hofu” aliongea kwa jazba na kupiga meza kwa ngumi. Kila mmoja lionekana kushusha pumzi nzito.

    “Mbaya zaidi yaani mtu mmoja awamalize watu wanne, watu waliofuzu mafunzo ya kijeshi, ya upiganaji wa silaha na ana kwa ana, bado sijaamini, Betram, inawezekanaje?”

    Betram alitulia tuli hakuwa na jibu la uhakika kwa maana kama ni taarifa alikwishaifikisha jinsi ilivyo.



    “Aah inaonekana walifanya makosa kidogo, kwa sababu tulipofika Tanzania kwanza tulianza kufanya uchunguzi wetu wa wapi pa kuanzia, tukagundua kwamba kuna mtu wao mmoja ambaye ni matat sana katika kugundua hujuma kama hizi, kwa hiyo nikawapanga kumshambulia na kumpoteza mara moja, lakini ndiyo hivyo badala yake ni yeye pekee aliyewamaliza wote wanne.” Betram alijibu.

    “Ok, sasa tunabadilisha mbinu, nitakuongezea wtu wawili wa juu, ambao wao wanaijua kazi yao sawasawa na hawaweai kufanya makosa kama hayo. Sasa hebu Shakrum, weka hiyo DV cam niwape onyo kali” yule kiongozi wao aliyejulikana kwa jina la Beishal alitoa amri na mara moja ile mashine ya kurekodia ikategwa tayari kwa kumrekodi, kama kawaida akavaa ile sox yake usoni.



    “…Imebidi kuwapa onyo hili mapema kwa kuwa mmetupotezea wapiganaji wetu wane ambao mtawalipia kwa damy nyingi kutoka kwa wananchi wenu wasio na hatia, tunakuja tena kwa nguvu mpya badala ya zile siku saba sasa mlipuko mkubwa muutegemee ndani ya saa 48 tu. Vijana wetu wane thamani yao ni sawa na wananchi wenu mia moja, kaeni tayari, hatutawaacha kwa kuwa mmejiingiza kwenye vita isiyowahusu, na kwa tukio la jana mmechokoza nyuki, tutawauwa mpaka mumuachie huru kaka yetu Jegan Grashan mpigania haki asiyechoka…”



    Kama kawaida yao wakaituma ile DVD kwa njia ya DHL ili ifike kwa haraka zaidi.

    “Betram, nakubadilisha nafasi yako, wewe utakwenda Somalia na Shailan wa Somalia ataongoza vita baridi huko Tanzania na vijana wengine watatu nitawaongeza, mmoja nitamtoa Mali mwingine Afghan na Pakistan nina uhakika watamaliza kazi ndani ya wakati kwa mbinu yoyote ile” Beishal alimaliza na kuwtaka kila mtu kurejea katika kazi yake na mapinduzi yaendelee kama yalivyopangwa.



    Dar es salaam



    Waziri wa ulinzi alionekana wazi akitetemeka baada ya kuitazama DVD ile iliyowafikia mchana wa jua kali la saa saba, alishika remote na kuitoa katika ile mashine maalumu kwa kazi hiyo, aliirudisha kwenye kasha lake na kuiweka mezani kisha akamtazama IGP aliyekuwa ameketi hapo.

    “Unafikiri wapi hawa jamaa watalenga kwa sasa?” sauti ya kitetemeshi kutoka kwa waziri Maige.

    “Aaa hapa nikujipanga kila kona yenye mikusanyiko ya watu, inabidi CID wetu wafanye kazi ngumu ya kujichanganya na watu, na sasa hatuwezi kuilinda Dar peke yake wanaweza kwenda kulipua Kigoma, hawa jamaa hawana mana kabisa” IGP alimueleza waziri.

    “Mwisho wa yote ni nini?” alitupa swali na waziri wa mambo ya ndani akajibu.

    “Hawa jamaa wana mtandao mkubwa sana, kwa hiyo kupambana nao inabidi kutumia vyombo vyetu vyote vya usalama nchini kwa sababu hujui watatokea wapi.”

    Maazimio ya kikao hicho yalipitishwa na kila kona kulimwagwa polisi wa kutosha na ukaguzi kila sehemu zenye mikusanyiko ya watu, hakika hali ilikuwa tete, ilikuwa ni sawa na kupigana na gizani maana humuoni unayemshambulia, ilmradi tu kila sehemu kulikuwa na ulinzi wa kutosha.



    ??????



    Amata alishusha simu yake kutoka sikioni na kuiweka mezani kwake kisha akainua kikombe cha kahawa na kupiga funda moja. Akavuta gazeti mojawapo lililokuwa hapo mezani na kusoma habari nzito iliyobeba kurasa ya kwanza (good copy) iliyosomeka

    ‘Magaidi watoa kitisho kingine, kuishambulia Dar es salaam muda wowote’

    aliisoma habari ile kwa kina sana na kuielewa vizuri, kichwani mwake mawazo mengi yalimzunguka akifikiri nini cha kufanya kwenye sakata hilo wakati wakiwa wamebakiwa na siku nne tu walizopewa na magaidi wale. Alivuta kitabu chake cha kumbukumbu na kufungua karatasi kadhaa alizokuwa akiandika andika na kusoma mambo Fulani, mara simu yake ikaita, akainyanyu kwa haraka.

    “Yes hello! (…) Ok asante (…) sasa hivi natuma mtu” aliishusha simu yake na kumuita Gina ambaye muda huo alikuwa akichapa kazi Fulani katika computer yake ndogo.



    “Niambie kaka” aliitika wito

    “Kuna kazi kidogo, nenda pale ofisi za Qatar airways kuna mzigo watakupatia uniletee haraka” alitoa maagizo. Gina bila kuchelewa aliiacha ofisi na kukodi bajaji ili aweze kuwahi kazi aliyotumwa.

    Ofisini alibaki Amata peke yake akiumiza kichwa kujua jinsi ya kulimaliza swala hilo mara kengele ya mlango ikalia, akafikiri kidogo na kuivuta droo yake, akatoa bastola yake aina ya Beretta 92 na kuitia katika mfuko wa koti huku ameishikilia tayari tayari maana hakuna kuaminiana nyakati hizo, aliuendea mlango na kuufungua kwa tahadhari ya hali ya juu, hakuyaamini macho yake, mwanadada mrembo alisimama mbele yake akiwa amevalia vazi refu kutoka juu mpaka chini, alimtazama Amata kwa jicho la mahaba na kutaka kuingi ofisini mle, Amata alibaki tu kumtazama msichana yule aliyekadiriwa kuwa na umri kama wa miaka 28 hivi.

    “Karibu sana, wewe ni nani?” kamanda Amata aliuliza

    “Nimeagizwa kuleta mzigo ofisini kwako, bila shaka wewe ni kamanda Amata” alijibu yule msichana. Kengele za hatari kichwani mwa Amata zikagonga.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nipe tafadhali na uniambie ni nani aliyekutuma” Amata alimwambia.

    “Sawa twende ndani,” akisema yule msichana huku akivuta hatua kuingia ofisini kwa Amata, Amata alijikuta akimruhusu kupita ofisini kwake na moja kwa moja akaketi katika kiti kinachotazamana na kile alichoketi Amata, mara akasikia mlio wa alarm ukitoka kwenye saa yake ambayo alikuwa ameivua na kuiweka mezani hapo kwa muda mrefu. Mlio ule ulizidi kuwa mkali, Amata akachomoa bastola yake na kumuelekezewa yule msichana.

    “Simama haraka, haraka” alimuamuru. Yule msichana akataka kuwa mbishi.

    “Nitakufumua kichwa chako sasa hivi, shetani wewe simama” alimuamuru tena na ile saa ilizidi kupiga kelele kuashiri imeditect aina ya mlipuko ulio jirani sana na eneo ilipo. Amata aliona anapoteza muda na kifo kilikuwa dhahiri mbele yake, hakupenda kumpoteza kwa risasi kiumbe yule mrembo mwenye sura ya kuvutia, alirudisha bastola yake kiunoni na kumtandika makofi mawili ya haja mpaka yule msichana akasimama.



    “Vua hilo nguo lako haraka?” alimuamuru, yule msichana alichomoa bastola kutoka kwenye ile nguo yake na bila kusita aliiondoa usalama tayari kufyatua, lakini alichelewa, ticktack iliyopigwa na Amata iliitoa ile bastola mkononi mwake na kufyatuka ikiwa hewani, ngumi moja ya usoni ilimchanganya yule msichana kabla hajakaa sawa, teke moja lililopigwa nyuma ya magoti yake lilimfanya apige magoti, Amata kwa wepesi alimvua lile gauni lake refu kwa kulivuta juu na kumuacha msichana yule chuchu nje akibaki na chupi tu. La haula la kwata bomu lilitegwa kwa saa lilikuwa limefungwa kuzunguka tumbo lake dogo, likiwa na milipuko kadhaa, na saa ya kidigitali ilikuwa ikiwakawaka kuonesha ni dakika mbili tu zilibakia. Kwa wepesi wa ajabu alichukua kiberiti chake na gazeti alilokuwa akisoma akaliwasha na ule moshi wake akauruhusu uwende kwenye sensa maalum ya kusensi moshi, punde tu kengele kali zikalia jengo zima na na vifaa maalum vya kumwaga maji kusaidia uzimaji moto vikafunguka kila kona maji yalimwagika tayari kuzima moto wowote ambao upo eneo lile, watu walitawanayika milango ilibamizwa wote wakitaka kutoka nje kuokoa maisha yao. Kwa kisu chake cha kukunja alikata ule mkanda maalum uliofungiwa lile bomu na kufanikiwa kulitoa tumboni mwa yule msichana, kwa haraka akatoka nalo likiwa mkononi kuelekea nje huku akiwapiga vikumbo watu waliokuwa koridoni wakikimbia kuokoa maisha yao. Alifanikiwa kufika katika ngazi za kushuka chini au kupanda juu, aliitazama saa ya lile bomu ilisoma bado sekude 55 tu, aliingia kwenye lifti na kuiamuru ipande ghorofa ya juu kabisa nayo ikatii. Sekunde 40 alikuwa juu kabisa ya jengo la JM MALL, aliisoma ile saa hakuwa na ujanja, alijaribu kufanya anachoweza ilipotimu bado sekunde 2 alilirusha juu lile bomu na kisha kulala chini, mlipuko mkubwa ulitokea angani watu waliochini walishtuka hawakujua nini kimetokea, moshi mzito ulitawanyika juu na mtikisiko wake ulifanya baadhi ya vyoo vya madirisha ya majengo mengine kupasuka na kutawanyika barabarani, watu walikuwa wakikimbia ovyo huku na kule. Kamanda Amata aliinuka kutoka pale alipolala na kushuhudia mshikemshike uliokuwa huko chini, alirudi haraka kwenye lifti na kuingia kisha kuimauru iteremke mpaka pale pale alipopandia.



    Aliusukuma mlango wa ofisini kwa nguvu na kuingia kwa minajiri ya kumuwahi yule msichana, peupe, hakuna msichana wala nguo yake, altazama huku na huku hamna mtu, aliichomoa bastola yake na kuwahi chini ya jingo lile ambapo vurugu kubwa ilikuwa pale katika korido kubwa karibu na supermarket ya Shopprite, ailisimama na kutazama huku na kule asimuone, akasogea karibu na barabara kubwa, barabara ya Samora, huku na huko alimuona mtu aliyevaa vilevile akamkimbilia na kumkamata, sio yeye, Amata alichanganyikiwa, akendelea kusaka huku na huko, hakuna mtu, kila mtu alimuona kama amechnganyikiwa.

    Gari za polisi zilianza kuingia eneo lile kwa mbwembwe zikifuatiwa na zile za zimamoto, tayari askari wa usalama barabarani walishaifunga barabara ya Samora kuanzia mnara wa sasa mpaka makutano na barabara ya Morogoro ili kuruhusu shughuli za uokoaji kuendelea kama inabidi. Kamanda Amata akiwa na bastola yake mkononi aliteremka ngazi na kufika barabarani ambako kulikuwa na vurugu za watu tu wakikimbia na kukanyagana kelele za ‘bomu, bomu’ zikitawala eneo lote hilo.



    Watu wa zimamoto waliingia ndani ya jengo hilo tayari kwa kazi yao ya uokoaji, watu waliobakia ndani walikuwa wakitolewa na kupakiwa kwenye gari za wagonjwa kwa kukimbizwa hospitalia. Amata alirudisha bastola yake kiunoni na kusimama sehemu akitazama pilikapilika zilizokuwa zikiendela huku macho yake yakipepes kiufundi kuangalia kila anayeingia au kupita eneo hilo. Moyo ulimpiga kwa nguvu alipoona wafanyakazi wawili wa zimamoto wakiwa wamemshika msichana mmoja wakitoka naye nje katika harakati za kuuokoa lakini cha kushangaza msichana yule hakupakiwa kwenye gari la wagonjwa bali walimpakia kwenye gari ya zimamoto kisha wale jamaa nao wakapanda, ile gari aina ya Dennis iligeuzwa na kuanza kuondoka eneo lile ikichukua barabara ya Samora kuelekea picha ya askari kisha kuifuata barabara ya Maktaba.

    Kamanda Amata aliijua ile ni trick na alijua kuwa kwa vyovyote ilikuwa ni mbinu ya kumuokoa binti huyu, hakuwa na muda wa kujiuliza maswali mara mbili, alitazama huku na huko na kumuona askari mmoja aliyekuwa na Honda ya kipolisi 350 CC, alimfata na kumuamuru ashuke mara moja, kisha akakaa juu ya lile pikipiki na kuingiza gia ya kwanza, alilizungusha kwa ufundi mkubwa na kuiacha barabara ya Samora na kuichukua ile ya Morogoro, alipofika barabara ya Bibi Titi alikunja kulia kwa kutumia upande usio sahihi ili kuikabili ile gari ya zimamoto, hakukosea kwani aliiona ikija upande huo mara moja akaitoa ile bastola yake ya kiitaliano na kulenga tairi ya ile gari, shabaha ya kwanza haikuwa sahihi, dereva wa gari ile aliliona hilo akayumbisha gari na kufanikiwa kuiepa ile risasi, Amata aliuma meno, wakiwa jirani kabisa kabla hajafanya lolote, kishindo kiliskika , pikipiki ya kamanda Amata ilikanywagwa na kupondwapondwa kabisa.



    Amata alijirusha pembeni upande wa jingo la wizara ya Vijana na kutua sawia kwa goti moja bastola mkononi, shabaha ya pili ilipiga tairi ya nyuma na kuifumua vibaya, ile gari iliyumba barabarani na kusababisha ajali kadhaa lakini hakuna aliyefuatilia, jamaa waliijua vyema kazi yao, ile gari ikaacha barabara ya Bibi Titi pale kwenye mataa ya DIT na kukunja kulia kuelekea Faya, kamanda Amata alibaki chini barabarani hana la kufanya ile lori imeshaondoka, ‘Hayawani wakubwa hawa’ aliwatukana kimoyomoyo na kujinyanyua lakini alijikuta akirudi chini na maumivu makali kwenye bega lake la kulia, aliiokota bastola yake na kuiweka mahali salama, watu walianza kujaa wakijuwa kuwa hilo ni jambazi wengine walitwaa mawe tayari kumpiga, kamanda Amata aliona hiyo ni hatari, aliichomoa bastola yake na kufyatua risasi kadhaa hewani na kuwafanya watu wale kutawanyika, kwa haraka alinyanyuka pale alipo licha yakuwa alikuwa na maumivu alijikokota na kuifikia tax ya jirani na kuomba apelekwe eneo la tukio na mara yule dereva akfanya hivyo.



    Madam S, alitulia tuli kama maji ya mtungini huku akili yake ikizunguka kwa kasi, akitafakari jaribio lile ambalo kama si Amata basi jengo la JM MALL lingekuwa likiteketea na kusababisha vifo vingi hasa cha kamanda Amata ambaye ofisi yake ya siri iko hapo katika jengo hilo. Hakuwa anajielewa sawasawa, mbele yake mezani kulikuwa na mafaili kadhaa ambayo labda alitaka kuyafanyia kazi au sijui alitaka afanye nini nayo. Aliinuka na kupekua faili moja baada ya jingine kisha akachukua moja na na kulitia katika begi maalum na kufunga ofisi, alijipakia katika gari yake na kuondoka eneo lile.

    Breki yake ilikuwa mbele ya ofisi ya wizara ya ulinzi, moja kwa moja aliingia ofisini kwa mheshimiwa Maige na kulitoa lile faili kisha kulitupia mezani kwa waziri huyo.

    “Mheshimiwa, mi naona ili tuifanye kazi yetu vizuri, muachilie huyu mtu huru” madam S aliongea kwa jazba.

    “Oh! Madam, vipi tena? Mbona hasira mchana huu?” waziri Maige aliongea huku akiwa amesimama.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hivi leo wangekufa watu mamia, kama si Amata kufanya aliloweza, msichana yule alitaka kujitoa mhanga kwenye ghorofa ya ngapi sijui, hapana mheshimiwa, mpe removal order huyo mtu atoke arudi kwao”

    Juu ya meza ya waziri Maige faili lililoandikwa ‘JEGAN GRASHAN’ lilikuwa limetulia likisubiri amri ya waziri ili lifanyiwe kazi. Waziri Maige aliliangalia faili lile na kutikisa kichwa chake kuonesha kama hajakubaliana na kitu Fulani.

    “Madam!” hili swala lipo juu ya uwezo wangu, inabidi mheshimiwa Rais ndiye aamue juu ya huyu mtu kama kutoka au la”

    “Mheshimiwa waziri, naomba ulishughulikie hili haraka iwezekanavyo. Mi nafikiri tukimuachia huyu, tutakuwa katika hali ya utulivu sana hapo tunaweza kuwasaka hawa jamaa kwa taratibu tu mpaka tuwakamate”



    Gereza la Ukonga



    “Kwa nini watu wako wanafanya milipuko ya namna hii? Wanafikiri kwa kufanya hivyo ndiyo tutakuwacha huru?” kamishna wa Magereza Tanzania alikuwa akimuuliza Jegran, huku akiwa na jopo la watu wengine, waziri Maige na madam S walikuwa miongoni mwao.

    “Kwa nini mnaniuliza swali kama hili? Ninyi wenyewe mnajua na wamekwishawaambia wanataka nini, mkitekeleza wanalotaka mtakuwa huru dhidi ya mashambulizi haya, msipotekeleza mtaendelea kuangamia,” Jegran alijibu kwa sauti yake kavu nay a upole.

    “Serikali ya Tanzania inataka kukuacha huru! Uko tayari?” waziri wa ulinzi bwana Maige alimuuliza.

    “Hata mi nashangaa kwa nini mmenifunga bila kosa, sina kosa mimi” Jegran alijibu.

    “Huna kosa!? Kuulipua ubalozi wa Marekani hapa nchini si kosa?” Madam S aliuliza kwa jazba

    “Nililipua ubalozi wa Marekani, wangenikamata Wamarekani, sasa ninyi mmenikamata kwa kosa gani? Ndiyo maana mnapata misukosuko, na sasa jiandaeni kwa maangamizi”

    Madam S alishikwa na hasira na kuuma meno. Baada ya mazungumzo hayo na tayari wakikubaliana kumuachia huru gaidi huyo, jopo hilo lilitoka katika eneo hilo na kuondoka zao.



    ??????



    Akiwa na bandage yake mkononi, kamanda Amata alitembea taratibu pembezoni mwa barabara ya Morogoro katika eneo la Jangwani ambapo ile gari ya zimamoto ilikuwa imetelekezwa hapo na jeshi la polisi lilikuwa likifanya jitihada za kuiondoa katika eneo hilo.

    FK Security Group, ilikuwa ni nembo iliyong’aa sana katika ubavu wa gari ile, kamanada Amata aliitazama nembo ile na kuipiga picha kwa sababu mbalimbali za kazi yake, kisha bila kuongea na mtu yeyote aliingia kwenye tax na kuomba kupelekwa eneo la Mikocheni.



    FK Security Group



    Taratibu aliuendea mlango ulioandikwa FK Security na kubofya kitufe cha kengele, alipoitikiwa aliufungua na kuingia ndani. Msichana mrembo alikuwa nyuma ya kompyuta kubwa akiendelea na kazi.

    “Karibu kiti kaka, nikusaidie nini?” alimuuliza Amata.

    “Naitwa Stephen Amalutwa, muandishi wa gazeti la Dar es salaam leo, nimekuja hapa kuulizia juu ya sakata la gari lenu la zima moto kutumika katika jaribio la kigaidi pale JM MALL ghorofa ya saba” alijitambulisha huku akiweka kitambulisho chake mezani, kitambulisho cha uandishi wa habari.

    “Gari yetu sisi, imetumika? Ipi hiyo, mbona mi sina taarifa na nadiye ninaeratibu shughuli zote za ofisi hii?” aliuliza yuke dada.

    “Inawezekana, lakini gari ile ni ya kwenu,” Amata, muandishi bandia akatoa simu yake na kumuonesha ile picha ya gari hiyo na namba zake za usajiri, yule dada alipatwa na mshtuko na akanyanyuka na kumwambia Amata asubiri, kisha akaenda na kuingia katika ofisi Fulani, na baada ya dakika kadhaa alitoka na kurudi pale alipokuwa mwanzo.

    “Bwana Amalutwa, haya ingia ofisi namba tatu pale utapata majibu yako yote” aliambiwa.

    Kamanda Amata aliinuka na vifaa vyake, na kuelekea katika ofisi aliyoelekezwa.



    Mbele yake aliketi bwana mmoja mnene kidogo ambaye alikuwa na ndevu nyingi zilizouzunguka uso wake kwa upande wa mashavuni, walitazamana na Amata kisha wakasabahiana na kuanza mazungumzo yao.

    “Kutokana na maelezo yako bwana Amalutwa, sisi hatuna gari ya uokoaji yenye namba hizo, gari zetu zote ni hizi hapa” aliongea yule bwana aliejitambulisha kwa jina moja tu, Scoletti. Alitoa faili kubwa na kufungua kadi original za usajiri wa magari yale, Amata alitazama na kweli hakuona gari iliyosajiriwa kwa namba hizo.

    “Na unasemaje kuhusu hii nembo yenu ya kampuni katika gari ile?” alimuuliza

    “Aaaa itakuwa ni wahuni tu wameamua kutumia jina letu tu ili kutuharibia biashara, kama unavyojua sisi ndiyo kampuni ya kwanza ya binafsi kuanza kutoa huduma hii” Scoletti alijibu huku akirudisha lile faili. Kwenye shelf maalum lililo katika kabati moja kubwa pembezoni mwa ukuta. Amata aliandika vitu Fulani katika kijitabu chake, kwa macho ya kipelelezi aliiangalia ofisi ile na kuona sehemu zote zenye ulinzi na vifaa vya ulinzi moyoni mwake aliahidi kurudi usiku huo kwa upekuzi zaidi. Waliagana na kuondoka katika ofisi hiyo.



    Scoletti alitoka ofisini kwake akiwa amefura kwa hasira mapaka kwa secretary wake.

    “Wewe, nikwambie mara ngapi unielewe? Nimeshakwambia sitaki umruhusu mtu au uongee na mtu kitu usichokijua, wengine hawa wanatupeleleza, utasababisha kampuni hii kufungwa wewe. Sasa nakupa likizo ya mwezi mmoja na malipo yote yanayokustahili, utarudi kazini baada ya mwezi mmoja” alimkemea yule dada.

    “Lakini Boss, yule si ni mwandishi wa habari nae alikuwa katika majukumu yake ya kazi?” aliuliza yule dada.

    “Nani aliyekwambia? Yule ni mpelelezi wa serikali, mpelelezi anayetegemewa hapa Tanzania. We unaruhusu watu tu waingie, tunaweza kuuawa humu ndani na we usijue” kisha akampa sonyo refu. Baada ya dakika mbili akaja na hawala ya fedha mkononi na kumkabidhi yule dada.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Yule secretary hakuwa na la kufanya, likizo ya dharula ilikuwa mezani kwake, hawala ya fedha kwa likizo ilikuwa mkononi mwake, milioni mbili zilisainiwa, machozi yalikuwa yakimlenga yule dada kwa kosa alilolifanya, aliichukuwa ile barua na ile hawala kisha akaagana na boss wake na kuondoka. Alisimama nje katika barabara ya Bagamoyo, akaangalia kushoto kulia hakuona anachokitafuta. Mara akatoa kadi ya kibiashara na kuitazama juu yake iliandika kwa wino mweusi na maandishi ya kuremba Mr Stephen Amalutwa, ikifuatiwa na namba kadhaa za mtu huyo, aliinua simu yake na kupiga namba Fulani kisha akaweka sikioni.

    “Halo, yeah mimi ni secretary wa FK Security, sijui naweza kukuona kaka yangu (…), hapana we nambie nikuone wapi mi nitakuja” aliongea na simu ile na miadi ya kukutana saa kumi nambili jiono ilikuwa dhahiri kwake, kukutana na mwandishi bandia Mr Amalutwa. Moyoni mwake yule dada alikuwa na uchungu wa kupewa likizo ile maana alijua anaweza kufuatiwa na barua ya kuachishwa kazi muda wowote, lakini milioni mbili alizopewa zilikuwa zikimfariji na kumfuta machozi katika hilo.



    ??????



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog