Simulizi : Nyuma Ya Pazia
Sehemu Ya Pili (2)
Aliondoka na kuelekea Le Grand Casino mara baada ya kuongea na dereva taxi yule. Ilipopita muda wa masaa matatu aliona namba mpya hivyo aliuona urahisi wa kazi na kuelewa yule alikuwa dereva taxi aliyemuagiza hivyo Aliamua kumuita ndani.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Bill nenda kamlete mgeni wangu pale nje" Aliagiza Jack Loyce.
"Sawa"
* * *
Mara baada ya kumlipa ujira wake yule dereva pikipiki, aliamua kukaa kusubiria huyo mtu atakae muijia ili akaonane na adui yake wamalizane. Aliamua kuongea na Opareta:
"Namsubiri mtu ametumwa aniijie hapa nje"aliongea Joachim.
"Sawa ila kuwa makini nao"Alionya Opareta wake.
Alikaa huku akitafakali jinsi ya kufanya na ndipo alipofikilia kwa nini mtu yule ampokee wakati hamfahamu na akamchangamkia kama vile anamfahamu. Hapo ndipo wazo lilimjia kuwa atakuwa alikuwa na miadi na mtu na walikubaliana kukutana.
"Hii ndio nafasi nzuri ya kutumia kumnasa"Alijisemea moyoni Joachim.
Akiwa bado na mawazo huku akiangalia angemnasaje Jack Loyce ghafla alishangaa kuonawatu wanne wenye suti safi nyeusi huku wakiwa na miili iliyojengeka vizuri.
"Wewe mpuuzi ukumbuke kuwa uko kwenye mikono yangu sasa basi chagua unanipa faili au nikufanyie yale ya yule mzee wako."Aliongea kwa jeuli na kiburi cha hali ya juu.
"Na ukumbuke kuwa hujui unaecheza nae..."Alijinadi Joachim.
"Haaaa.....masikini yani unajipa moyo wakati uko mikononi pangu.......... nimemuua Mwenyekiti wa TAU na Kiongozi mkuu wa Majeshi ije uwe wewe...."
"Ko wewe ndo Jeshi Jeusi au Rising Mafias......????."Aliuliza kwa dharau Joachim.
"Haa...ko unafuatilia watu usiowafahamu."
"Sijaona mtu kati yenu"Alijinadi tena Joachim.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mkamateni akatu............."Alikatishwa kauli kwa teke aliloruka Joachim na kumpata Jack Loyce hadi akaanguka chini. Wale vijana wanne haraka walimsogelea lakini hakuna walichoangulia zaidi ya ngumi na mateke. Kama ulivyokuwa wasifu wake kuwa vizuri katika suala la mapambano ya ana kwa ana kwa Joachim Bartazar na kwa Jack Loyce ilikuwa hivyo hivyo, na mara baada ya kuamka pale chini haraka haraka aliruka aina fulani ya mateke na kumpata vilivyo Joachim. Si kazi rahisi kwa komando kama yeye kukubali kuwa chini ya ulinzi hivyo alizungusha . Mateke kwa wale vijana hadi wakawa hoi kisha akahamia kwa Jack Loyce ambae aliamua kujipanga mara baada ya kuona moto anaocheza nao utamgharimu maisha. Alianza na karate kisha akarudi hadi judo ilimradi aweze kuishinda vita iliyokuwa mbele yake. Joachim hakuwa na papara ila alikuwa akitoa mapigo ambayo yalimuingia Jack vizuri. Mara baada ya kuona vita yake inaelekea kuisha na mshindi kutokuwa yeye aliamua kuchupa hewani kisha akachomoa kisu kitoka kiunoni pake na kumchoma nacho Joachim begani. Hakuishia hapo alikichomoa na kukielekezea tumboni ila alitulizwa vizuri na mkono mkakamavu uliozoea shida na kazi ngumu za kijeshi nao ni wa Joachim. Hakupoteza muda alivuta ngumi na kuiachia kama risasi iliyotoka kwenye bastola yeye uchu wa kuitoa roho ya kiumbe chochote mbele yake. Ilkuwa ngumi safi iliyotua vizuri katika uso waJack nakumfanya arudi nyuma ila alizuiwa asidondoke kwa mkono wa Joachim uliokuwa uumemshika vizuri na kumvuta. Alimpatia ngumi nyingine iliyompoteza kabisa Jack Loyce katika ushindani ule. Alimuachia huku akigumia kwa maumivu huku na yeye akiugulia maumivu ya kisu alichochomwa bega la kushoto. Alimuangalia Jack Loyce ambae hakuwa na muda wa kuamka huku akiwa na uvimbe usoni na jicho lake moja kuwa jekundu. Joachim alitoa koti la suti alilokuwa amevaa huku akigumia kwa maumivu.
"Shenz.....mchezo kwisha...."Aliongea Joachim. Wakati akiangalia jinsi alivyoumia alishangaa kumuona Jack Loyce akifyatuka na kupotelea kwenye watu wengi waliokuwa casino. Joachim alibaki akishangaa kwani alikuwa na kazi ya kumuhoji Jack Loyce aliyekimbia sasa hivi....
Wakati akiangalia jinsi alivyoumia alishangaa kumuona Jack Loyce akifyatuka na kupotelea kwenye watu wengi waliokuwa casino. Joachim alibaki akishangaa kwani alikuwa na kazi ya kumuhoji Jack Loyce aliyekimbia sasa hivi.
Hakutaka kimlegezea ila nae alitoka nduki huku akieaacha wale wengine pale chini waki gaagaa. Mara tu baada ya kutoka alikutana na kundi kubwa la wale watu huku wakiea na bastola zao mikononi. Alirudi ndani ya chumba kile spidi na kujirusha nyuma ya makochi huku risasi zikimfuata kwa nyuma. Alitulia hadi risasi zile zilizokuwa zikirushwa mfululizo zilipokoma ndipo lilipomjia wazo kuwa hakuwa na silaha yoyote. alitambaa na kuchukua bastola mbili kutoka kwa wale jamaa aliowapatia mkon'goto. Alirudi sehemu yake na kutulia.
"Bill na Dickie ingieni mkauangilie huo mzoga.."ilisikika sauti ikiamrisha.
"Sawa...."ilisikika sauti ikijibu huku kukifuatiwa na vishindo vya minyato kuelekea ndani. Joachim alitulia tuli huku akiwa tayari kwa lolote lile. Maumivu ya kisu alichochomwa na Jack Loyce yaliendelea kumtesa.
"Au na wewe George nenda...."aliisikia sauti hiyo tena Joacbim. Wakati huo wengine waliendelea na msako kwani hawaku uona mzoga wao kama walivyotaraji. Hakuwapa muda aliinuka kutoka alipokuwa amejibana na kuacbilia risasi mfululizo kuelekea kwa yule aliyeingia mlangoni na kukifumua kichwa chake huku kwa haraka ya hali ya juu aliwamiminia risasi za kifuani wale wengine. Kitendo kile alikifanya ndani ya sekunde sita tu. Alia.ua kutoma spidi mle chumbani huku akipiga risasi mlangoni zilizompata mmoja kati ya wale waliobaki nje ya chumba kile. Aliwaacha wakiduwaa na kujichanganya na watu waliokuwa mle Casino. Alinyooka moja kwa moja nje huku akiwaacha wakiwasiliana wao kwa wao ili wamtie mbaroni. Alipofika nje aliifuata barabara ya kuelekea Posta huku akitembea kwa haraka sana. Aliangalia saa yake na kugundua ilikuwa saa tano na nusu usiku. Kabla hajafika mbali aliwaona wakiyoka nje spidi na kujigawa ili wamtafute. Hakuloteza muda alijibana katika moja kati ya nguzo za majengi ya maeneo yale.
"Unafanya nini hapa...."Lilikuwa swali lililomsitua Joachim.
"Shiiiiii.....tulia mzee lasi hivyo utawawa"Aliongea Joacbim kwa tahadhari na kumfanya mzee yule wa kimasai ataharuki na kumuangalia Joachim ambae alikuwa akiwaangalia wale watu waliokuwa wakimtafuta kwa udi na uvumba.
"Sijakuelewa kijana nieleweshe haraka la sivyo napiga filimbi....."aliogea mzee yule kwa msisitizo wa hali ya juu na kumfanya Joachim ageuke kumuangalia.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mzee wale unaowaona ni majambazi na wananitafta mimi namimi ni polisi wanataka wafute ushahidi wa jambo fulani na wana silaha nzito pale...."Aliongea Joachim kwa kumuelewesha mzee yule kwa maneno ya uongo. Mzee alishikwa na hofu na kubaki akitetemeka asijue la kufanya.
"LAkini usijali upo mikono salama hata kama nikifa huta dhurika...."Alimtoa wasiwasi Mzee yule aliyekuwa akilinda jengo lile tena kwa rungu, fimbo na sime ya ulanga wa kimasai. Joacbim alitoa bastola zake mbili na kuzishika mkononi hiyo kumuoyesha mzee yule yeye amekamilika. haukupita muda mmoja kati ya wale alijitokeza na kuelekea uelekeo wa jengo alilojificha Joachim. Joachim alitoka eneo lile huku akimshauri mzee yule ajifiche na asionekane. Mzee yule kwa kitete alitoka mbio kuelekea upande wa nyuma jengo lile lakini kabla hajafika alikokuwa akienda alishituliwa na kauli nzito;
"We simama hapo hapo...."
Alisimana huku akiwa na woga mara baada ya kuona bastola ikimuangalia usoni.
"We ni nani?"Aliuliza gaidi yule huku akiwa amemnyooshea bastola.
"Nani mimi?"
"Kwani nani mwingine?"
"Mie ni mlinzi wa hapa.............."Kala hata hajamaliza kumjibu alimuona mtu yule akivuja damu kichwani pake na kuanguka chii kama mzigo.
"Kila la heri mzee..." Joachim alimzinduaaa mzed yule aliyekuwa akiiangalia maiti ya mtu yule na kuondoka zake.
Alivuka barabara na kutokea upande mwingine kisha akavuka katikati ya majengo mawili marefu ya ghorofa na kutokea Halmashauri ya Wilaya ya Ilala. alipofika pale aliamua kuelekea Posta mpya. Aliamua kwenda mwendo wa polepole kwani alikuwa maumivu mwili mzima huku jeraha la kisu likiwa linaongoza kwa kummaliza nguvu. Lakini akiwa hana hili wala lile aliona kundi kubwa la wale maadui zake wakija mbio nyuma yake. Hakuwa na uamuzi mwingine zaidi ya kuanza kukimbia ili kuinusuru roho yake. Alikuwa hajakimbia umbali mrefu ghafla alishangaa gari ainaa ya TOYOTA LAndcruiser VX na kufunguliwa mlango huku sauti ya kike Ikifuatiaa;
"Ingia twende......."
Hakutaka kupoteza muda aliingia na kufunga mlango huku akimuachia nafasi dereva afanye yake.
Hakutaka kupoteza muda aliingia na kufunga mlango huku akimuachia nafasi dereva afanye yake.
* * *
Sauda Mansoor ndio kama alivyofahamika kutokana na kufahamika sana kwa watu. Hiyo ilitokana na urembo aliokuwa nao bibie huyo. Sio tu urembo uliochanganyika na uarabu aliourithi kutoka kwa baba yake ila hata umbo zuri lililoumbika ndio zilikuwa moja kati ya silaha zilizomlinda na kumletea umaarufu popote aendako. Alikuwa ni zao la bibie Asia Binti Ringo moja kati ya watoto wa mzee Ringo, Mzee wa kisambaa mwenyeji wa Tanga. Kutokana na hali ngumu ya mzee wake Asia akaamua kutoka Tanga na kuja Jijini Dar es Salaam ili aanze maisha yake mwenyewe. Alijua mjini maisha ni rahisi kweli ila alikumbana nayo na kutamani kurudi kwa Mzee Ringo akakae asubiri kuolewa. Alikuwa na miaka kumi na nane tu. Ndipo alipokumbana na Tausi Mtoto wa mjini na kumfunza jinsi ya kuishi mjini. Usiku wa manane alikuwa halali akitafuta mteja wa biashara yake ili tu mkono uende kinywani.
Tangu aanze biashara yake hakuwahi kukosa mteja huku wengine wakimrudia tena na tena. Alikuwa akiuza mwili wake kwa ajili ya kuwafurahisha wateja. Akiwa katika hekaheka zake ndipo aliposhangaa gari zuri la kifahari la nyakati hizo TOYOTA MARK II ikisimama karibu yake na mwarabu mmoja mzuri akitoka na kumfuata Asia. Na huo ndio ukawa mwanzo wa Asia kufahamiana na Mansoor Salim mwarabu kutoka Oman. Asia alihama katika chumba alichokuwa akikaa na shoga yake Tausi aliyemfunza Jiji na kuishi na Mansoor hotelini huku wakila starehe za kila aina na kwenda sehemu tofauti tofauti nchini na nje ya nchi. Haikuwa tatizo kwake pale alipoamua kubeba mimba ya Mansoor huku akifurahia maisha yale. Haikuwa kama alivyopanga kwani mara baada ya kumwambia Mansoor mambo yalibadilika,
"Nini mimba yangu?"Aliuliza kwa mshangao.
"Ndio mpenzi"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"kama ni yangu itoe."
"khaa...ki vipi tena?"Aliuliza Asia kwa mshangao.
"Siko tayari kuzaa na mwanamke mweusi!!"Ndio lilikuwa jibu la Mansoor huku akibinua midomo kwa dharau.
"Sitoi hu ujauzito."
"Acha wewe utakuwa baba na mama basi"Alimaliza na kuondoka pale sebuleni.
"Sawa."Aliitikia Asia.
"Na naomba uindoke hapa hotelini mimi naondoka kesho katafute unakokujua wewe."Alimalizia Mansoor.
Hakuwa na jinsi aliamua kurudi kwa shoga yake kule Mburahati. Alipokelewa na kukaa pale ila baada ya wiki tatu alipata mzigo kutoka kwa Mansoor Salim ambao ni pesa na barua fupi iliyosema;
Kwako Kipenzi,
Natumaini uko tayari kunisamehe kwa yale yaliyotokea. Naomba unitunzie siri hiyo kwani siyo desturi yetu huku Oman kuwa na mtoto nje ya ndoa na ndio maana nikafanya hivo. Ukijifungua mtotomwambie baba yake nipo na nampenda sana kama nilivyokupenda wewe. Mwambie hata kama akinihitaji nitakuja kumuona. Tafadhali Asia nisamehe kwa sasa nimesharudi Oman na biashara zangu zote nimezifunga na kuondoa makazi Tanzania kabisa. Nakuoenda sana pokea mzigo huo na kuwa tayari kuniambia matatizo yoyote yale yatakayotokea.
Wako kipenzi,
Mansoor Salim
Rd #168 ,House no 1057 Oman,
Saudia Arabia.
Aliimaliza barua ile ya machungu ambayo ili mfanya kidogo awe na matumaini na maisha yake ya baadae. Alifungua begi alilotumiwa na kukuta rundo la hela zilizopangwa vizuri.
Mara baada yakujifungua mtoto wa kike alimpatia jina la Sauda jina alilochagua baba yake mtoto na kumpeleka kwao Tanga wakamuone mwanae na kuwekewa tambiko la kikwao.
Na huyo ndio Sauda Bint Mansoor aliyekuwa akiendesha gari kwa spidi iliamfikishe Jiachim nyumbani na kumpatia matibabu kutokana na majeraha aliyopata.
Alikuwa akiendesha kwa spidi kali huku akimuangalia joachim aliyukuwa ameegemea siti yake na kugugumua kwa maumivu alikuwa akiyapata mara baada ya kuchomwa kisu na baadhi ya risasi kumchuna wakati akijirusha nyuma ya makochi ili kujnusuru. Alikuwa akimuangalia Sauda jinsi alivyokuwa mtaaramu wa kuendesha gari tena kwa spidi.
"Hivi ulijuaje niko pale?"Aliuliza Joachim.
"Opareta alinipigia na kuniambia".Alijibu huku akiwa bize na usukani wakati akikata kona na kusimama mbele ya geti kubwa jeusi.
"Mh....."Aliguna Joachim wakati Sauda akishuka ndani ya gari na kuenda kufungua geti lie huku akiwa amezima taa za gari. Joachim alimuangalia mwanadada yule akihangaika na geti kisha akatikisa kichwa na kujiangalia. Mara baada y kufanikiwa kufungua alirudi na kuliinguza gari ndani. Alirudi na kuchungulia nje kisha akafunga geti na kurudi kwa Joachim.
"Tumefika"Aliongea huku akitoa tabasamu pana usoni pake.
"Oke.."Alijibu huku akijikongoja kushuka kwenye gari.
Waliingia ndani na kuelekea chumba maalum kwa ajili ya wageni na kumuweka Joachim mle ndani.
"Feel like home ( jisikie kama nyumbani)"Aliongea Sauda huku akitoka.
"Subiri mama unaenda wapi wakati mgeni sijui wapi chooni na wapi bafuni"Aliongea Joachim.
"Subiri nakuja"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mh...haya"
Aliondoka na kuelekea katika chumba chake kisha baada ya dakika tano alirudi na kibegi kidogo chenye msalaba mwekundu.
"Jiandae.."
"Na nini?"Aliuliza kama vile hajui huku akilitoa koti na shati alivyokuwa amevaa. Alibaki kifua wazi na mwili wake uliojazia na kujichonga kimazoezi ukibaki wazi. Alikuwa na kifua kilichojichonga na kumuwekea umbo zuri kama la mbeba vitu vizito.
"Safi."Alisema Sauda mara baada ya kukiona kifua cha Joachim.
"Vipi?"Aiuliza kwa mshangao mkubwa Joachim.
"Nimekipenda sana kifua chako"Aliongea huku akivaa glovu ili ampatie matibabu.
"Mi mwenyewe nimependa umbo lako" Alitania Joachim.
"Muone....."
"Nani?"
"Si wewe"Waliendelea kutaniana huku akimpatia matibabu ya majeraha Joachim. Mara baada ya pale walipata chakula kilichoandaliwa na Sauda kisha walienda kumalizia usiku ule.
"Usiku mwema"Waliagana kisha kila mmoja na chumba chake.
* * *
Asubuhi sana Saudi alikuwa amekwisha damka na kuelekea chumbani kwa mgeni wake ili amsalimie. Mara baada ya kugonga mlango mara kadhaa bila kufunguliwa aliamua kuingia huku ukiwa na hofu. kilichomshangaza ni kutokuwepo kwa Joachim.
Mara tu baada ya kujiona yuko sawa alitoka chumbani alimokuwa na taratibu aliufuata mlango mkubwa huku akiangalia saa yake iliyokuwa ikionyesha ni saa 10:24 usiku. Alifanikiwa kuufungua na taratibu akaurudishia na akaanza akajikongoja huku akilifuata geti la nyumba hiyo kubwa na nzuri. Akilini aliwaza kuhusu gari lake hivo mara tu baada ya kutika ndani ya geti alianza kutafuta usafiri hadi pale alipoliacha gati lake.
"Duh!mbona hamna usafiri wowote hadi saa hii." alikuwa akitoa lawama mara baada ya kutembea muda mrefu bila mafanikio ya usafiri njiani. Bastola yake kiunoni, ndio ilikuwa ngao yake hivyo alijiamini huku mkono akiwa ameuweka katika bega la kushoto ambalo ndio lilikuwa jeraha kubwa zaidi ya lile la mchubuko wa risasi. Aliendelea kujikonhoja huku akijiuliza pale ni wapi na kwa nini Sauda aliamua kukaa huko. Alikuwa tayari katembea mwendo mrefu wa kama Kilomita 5 hivi. Ndipo alipotokea barabara ya lami na safari yake kupamba moto hivyo aliendelea kuupiga mguu hadi majira ya saa 11 hivi ndipo alipopata usafiri ili arudi kwake.
"Wapi mkubwa?" Aliuliza dereva wa pikipiki.
"Magomeni kwanza"
"Dah!sina uhakika na mafuta yangu ila twende buku 10 tu" Aliongea kwa kutokujiamini dereva yule huku akimuachia nafasi ya kukaa abiria wake yule.
Safari ilianza na kuelekea Magomeni alipoacha gari kwa mlinzi mmoja hivi wa majengo pale Mapipa. Mara baada ya kufika alimlipa ujira wake yule dereva wa pikipiki kisha akampatia na mlinzi yule pesa kiasi cha Elfu Ishirini (20,000) a kuondoka kuelekea kwake. Alipaki gari na kushuka kisha akaelekea ndani moja kwa moja chumbani kwake ambako alifika kuvua koti huku maumivu yakimpata vilivyo kwani majeraha yake yalikuwa bado hayajapona. Alivua nguo zoke kwa ujumla na kuingia bafuni ambako alioga na kisha kujifuta jasho. Hakuwa na la kufanya wakati ule kwani alisumbuliwa na uchovu sana hivyo aliamua kujipumzisha.
---------------------------------------
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mwanga angavu ndio uliomuamsha na kumfanya asione vizuri vivuli vya watu wanne waliokuwa wakimtazama na kumpigapiga ili aamke. Alikuwa katikati ya pori na hakuna anayefahamu alifikaje pembeni aliiona sura fulani aliyowahi kuiona kabla lakini hakukumbuka ni nani mtu huyo. Hakuwa peke yake bali alikuwa na mtu mmoja hivi aliyeonekana kama ndio bossi wao kwani alikuwa kavaa suti safi nyeusi na iliyoonyesha ni ya gharama kubwa huku mdomoni akiwa na sigara kubwa. Alikuwa na saa ya dhahabu na viatu vizuri vilivyochangia muonekano wake uwe wa kipapaa au mtu fulani mkubwa Serikalini. Kichwani alivalia kofia kubwa aina ya Pama hivyo ilimficha sura na kumfanya asionekane vizuri.
"Kama anafahamu chochote kuhusu mimi ’UA’ tu hana faida kwangu" Alitoa kauli hiyo yule mtu hivo kuonyesha alikuwa mnyama kiasi gani. Hakukuwa na jinsi alisikia mlio wa Risasi na kufuatia yeye kuanguka chini.
ALISHTUKA! Ghafla pale kitandani huku ndoto ile ikikatika na bila ya muendelezo wowote.
"Ah!ndoto gani hizi" Alijiongelea wakati akiamka kitandani hadi wakwti huo ilikuwa saa 5 kasoro dakika 7 tu. Alijikongoja na kukiacha kitanda kisha akaelekea sebuleni. Alifungua friji na kutoa chupa ya pombe kali aina Teacher kisha akaanza kunywa huku akielekea jikoni. Aliangalia apike nini ila akaona atachelewa hivyo alirudi chumbani huku akiwa na chupa yake mkononi na kubadili nguo huku akivaa shati lake jeusi na suruali nyeusi kisha akavaa na viatu. Aliingia ndani ya gari na kulitia moto kurudi mjini. Hakusahau bastola yake wala kitambulisho chake cha kazi.
Moja kwa moja hadi kazini kwake na kuanza kazi kama kawaida yake.
"Joachim mbona leo umechelewa sana na si kawaida yako."Aliongea mmoja wa wafanyakazi wenzake ajulikanae kama Dorice na rafiki mkubwa wa Joachim.
"Ah..!majukumu mama" Alitana Joachim.
"Ila Mkurugenzi anakuhitaji"
"Ooh!alikuja humu ndani kwani?" Aliuliza kwa mshangao.
"Yah!"
"Okay" Alitoka katika kiti chake na kuifuata Ofisi ya Bosi wake huyo wa kihaya Dr. Josephat Kamugisha ambae ndie alikuwa akiiongoza kampuni ile. Alifungua mlango na kuingia moja kwa moja kisha akaketi na kumsalimu Bosi wake huyo.
"Leo mbona umechelewa sana na hii tabia umeanza lini eh!" Alianza kofoka Mzee Yule. Joachim hakutaka kuongea chochote wala kujitetea kwani kufanya vile kungemuongezea hasira Bosi wake yule.
"Sipendi hii tabia ijirudie nenda na kuna makontena yameingia yashughulikie" Alimalizia.
"Sawa" Alitoka na kuelekea ofisini kwake ambako alitoka jioni ya saa 10 mara baada ya kumaliza kushughulikia kazi aliyopatiwa na Bosi. Mara tu baada ya kutoka alikutana na Dorice ambaye alikuwa akimsubiri mapokezi.
"Haaa!bado upo hadi saa hizi" Alishangaa Joachim huku akiangalia saa yake.
"Ndio nilikuwa nakusubiri wewe"
"Naam!?" Aliitika kwa mshangao.
"Kwani vibaya bwana hebu twende" Walienda hadi alipopaki gari Joachim na kuingia garini kisha wakaondoka pamoja.
"Leo wikiendi kwa hiyo utakuwa wapi?"Aliuliza Dorice binti mrembo wa kichaga.
"Nyumbani kwangu" alijibu huku akiwa na usukani.
"Kwa nini sasa?"
"Napenda leo iwe hivo basi"
"Ok nitakuja kujumuika nawe"
"Haina shida"
"Wow !nilikuwa nasubiria hicho tu kwa hiyo andaa vinywaji" Aliongea kwa furaha huku akitabasamu na kuyafanya meno yake meupe yaonekane.
Ghafla simu ya Joachim iliita. Tiii Tiii mara baada ya kupokea tu alisikia;
"Ajenti 79 onlaini"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Yes Sir"
"Mr. Maebo anazikwa kesho kutwa saa 5:00 asubuhi hivyo utahitajika" sauti ile iltoa amri.
"Sawa mkuu" Aliitikia kisha akakata simu.
"Bosi ?"Haraka haraka Dorice alidakia.
"Yap!"
Alimpitisha hadi kwao na Dorice kisha yeye akaelekea kwake huku akiendelea kuitafakali safari ya maisha yake na mbeleni.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment