Search This Blog

Sunday, 22 May 2022

HUJUMA - 3

 







    Simulizi : Hujuma

    Sehemu Ya Tatu (3)



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mkononi mwa Kamanda Amata kulikuwa na bahasha iliyowekwa kitu fulani ndani yake.

    “Hapo hapo Fasendy, shoot... shoot Fasendy,” yule kijana alimwambia Fasendy, alipomgeukia alikutana na jicho kali la Fasendy.

    “Kwani mi sijui kazi yangu?” Fasendy akamuuliza, kisha akarudisha jicho kwenye kile chombo na kupachika dole la shahada la mkono wa kulia katika kifyatulio, akavuta taratibu na kumwacha Kamanda Amata asogee pasipo na watu.

    Kamanda Amata aliteremka ngazi na kutembea kwa hadhari pale upenuni kwenye maegesho ya hotele akiiendea gari yake, lakini ghafla alisikia mlio wa risasi nzito na bahasha aliyoishika mkononi mwake ikipigwa na kutoka mkononi mwake.

    “Shabash,” alitamka, huku akiruka kiustadi kuliacha eneo lile na kufikia kwenye maua ambayo yalimkinga asionekane.

    Kutoka juu ya ghorofa lile, Fasendy alitazama kwa mashine yake lakini hakumuona Amata zaidi ya watu wachache waliokuwa wametawanyika eneo lile.

    “Uemuona alivyokuwa mwepesi?” Fasendy akamuuliza yule kijana ambaye alibaki katoa macho na darubini yake ikiwa inaning’inia kifuani mwake.

    “Sasa kwa nini hukumuua, hivi unafikiri Sharon na Shalabah watatuelewa!” alilalamika yule kijana.

    Fasendy hakujibu neno, alimtazama na kisha akainuka na kunyanyua bunduki yake, akasimama na kumtazama yule kijana, “Muda bado.”



    JIDKA SODONKA



    Kamanda Amata aliegesha gari kwenye moja ya majengo makubwa katika barabara hiyo kubwa, Jidka Sodonka. Moja kwa moja akaingia ndani ya jengo hilo na kukuta watu waliokuwa wakifanya usafi na katika vijia vya jengo hilo kulikuwa na makasha ya takataka mengi. Akaliendea mojawapo na akatumbukiza kitu kilicho kwenye mfuko wa plastiki kwenye moja ya kasha hizo, yeye mwenyewe akapita moja kwa moja na kuingia katika moja ya duka la nguo, aksimama katika mlingoti mmoja ulioning’inizwa nguo za kike, lakini jicho lake likawa makini kutazama katika kasha lile. Sekunde chache alimuona mzee wa makamo akipita karibu na lile kasha akiwa kavalia mavazi kama ya wale wanaofanya usafi, akachukua lile kasha na kuondoka nalo kuelekea mahali wanakomwaga taka hizo. Kamanda Amata akatoka mle dukani mara baada ya kuona lile kasha limerudishwa pale, alipolipita lilikuwa tupu, akaelekea nje ya jumba hilo lenye maduka mengi ndani yake. Akiwa ameketi katika gari yake, simu yake ikaingia ujumbe, akaitazama, akausoma na alipomaliza akawasha gari na kuondoka.



    §§§§§



    Kituo cha basi cha W Sheikh Abaadir, kilicho nje kidogo ya mji wa Mogadishu kilikuwa na watu wengi wakisubiri usafiri wakwenda sehemu mbalimbali. Kamanda Amata aliweka gari yake mbali kidogo na kituo hicho na kusogea kwa mwendo wa miguu. Katikati ya wasafiri kulikuwa na benchi lililokaliwa na watu kadhaa huku wengine wakiwa wamesimama kutokana na ufinyu wa eneo hilo. Alipokuwa akiliendea benchi hilo alitoa sigara mfukoni na kuiweka kinywani kisha akaibana sawia na midomo yake, akaanza kujipapasa kutafuta kiberiti asikione. Kati ya watu waliokaa katika benchi lile mmoja akawasaha kiberiti cha gesi na kunyanyuka, Kamanda Amata akamfuata mtu huyo mpaka katika moja ya gari nyingi zilizoegeshwa kituoni hapo.



    “Kamanda Amata,” yule mtu akaita kwa sauti tulivu.

    “The Chamelleone,” Kamanda naye akajibu, kisha ile gari ikaondoka, na kutoka nje ya mji kabisa ikipita katikati ya jangwa nene lenye jua kali na vumbi.

    Baada ya mwendo wa takribani saa moja ile gari iliegeshwa kwenye nyumba kuukuu iliyozungukwa na miti michache. Kamanda akatelemka na kuongozwa na yule mtu mpaka ndani ya sebule kubwa, hapo alimkuta mtu anayemfahamu fika, The Chamelleone alikuwa ameketi katika sura ileile aliyokuwa ameizoea tangu zamanai.

    “Karibu Kamanda,” akamkaribisha.

    “Asante sana, kila linalopita kwangu ni kama ndoto za alinacha,” Kamanda akasema.

    “Inabidi iwe hivyo, maana leo hii asubuhi ulikuwa unauawa, na usingekikwepa kifo hicho, lakini umepona, una bahati,” Chamelleone akamwambia Amata. Kamanda Amata akamweleza juu ya tukio la asubuhi la kupigwa risasi bahasha iliyokuwa mkononi mwake.



    “Kamanda Amata, hawa jamaa hawatanii kabisa katika kuua, na sasa wamecharuka maana wamegundua ulilolifanya hivyo pale hotelini kwako sio salama tena na ningekushauri uhamie huku shamba,” Chamelleone alimwambia Amata.

    “Nakubaliana na hilo, lakini huku ni mbali sana, na mi nataka nikamilishe kazi hii mapema iwezekanavyo,” Kamanda akajibu.

    “Usijali, kwanza kabla ya kuendelea kufanya kazi hii unatakiwa ufanye kazi moj ya ziada, umpate Jamir, kutoka kwake utapata jinsi ya kuimaliza hii kazi ndani ya dakika chache,” Chamelleon akamwambia Amata.

    “Jamir! Bado yupo hai?” Kamanda akauliza.

    “Jamir yupo hai, nitakuelekeza alipofichwa, ukiweza ukamtoe ili pamoja au vyovyote vile umalize sakata hili, nitafurahi sana kama utaimaliza hujuma hii na wahujumu wajulikane,” Chamelleone akamweleza Amata.

    Kabla ya kuanza mazungumzo yale na Amata kwanza akawataka wale watu wake kutoka mle ndani ili abaki yeye na kijana wake tu. Hali ilipotulia alimtazama Kamanda usoni kisha akashusha uso wake mahala pake.



    “Unahitaji kupumzika, macho yako yanaonesha wazi umechoka na una usingizi,” The Chamelleone akamwambia Amata, “…Utakapoamka ndipo utaianza kazi hii kwa umakini zaidi kwa sasa kutokana na uchovu wako hutokuwa makini, watakukamata,” almalizia.

    Kamanda Amata akaitikia kwa kichwa na kutulia kochini, “Umepata mzigo?” akamwuliza.

    “Ndiyo, nimeupata na baadaye nitauchunguza kuona kama ni sahihi au kuna mchezo mwingine uliochezwa katika hili, nakusubiri uamke ili tuone pamoja, (akamtazama Kamanda kwa makini) naona bado una maswali uliza tu,” Chamlleone alimwambia.

    “Hapana sina swali, nahitaji kupumzika,”

    “Ok, Kamanda.”

    Yule mzee mtu mzima akanyanyuka kitini na kuiendea simu iliyopachikwa ukutani, akaipachua na kuminya tarakimu Fulani kisha akaiweka sikioni; akaongea maneno machache kwa lugha ya kiarabu na kisha kurejea kitini. Haikupita sekunde kumi mwanadada mrembo alitokea katika mlango mmoja kati ya mingi ya jumba lile, akiwa amevalia siketi ndefu iliyonyima nafasi japo vidole vya mguu kuonekana, kuyoka kiunoni kwenda juu alivalia sidiri inayowakawaka kwa vingaro vyake vya kupendeza huku akiwa na kiblauzi cha mtindo huohuo kisicho na vifungo mbele na nikifupi kiasi kwamba hakijafika kiunoni, kwa jinsi hiyo tumbo lake mwororo lilikuwa wazi na kuruhusu kitovu mbonyeo kuonekana wazi.



    Moja kwa moja alikuja kwa Kamanda Amata na kumsalimu kwa adabu.

    “Mfuate,” ilikuwa sauti nzito ya Chamelleone ikimwambia Kamanda, naye akanyanyuka na kumfuata yule mrembo aliyekuwa akitembea mwendo wa ki-paka ulioyafanya makalio yake madogo kuyumba huku na kule, bila shaka alikuwa miss, Kamanda alijiwazia kichwani mwake huku macho yake yakiburudika kwalo.





    §§§§§§

    Chumba kikubwa kilimlaki Kamanda Amata, kitanda kikubwa chenye miguu mirefu, kitanda cha kisultani, aliendelea kuwaza.

    “Utapumzika hapa na kwa shida yoyote utapiga simu, namba zote zipo hapo, asante,” yule mrembo alimwambia Kamanda Amata.

    “We unaenda wapi, mi nilijua unabaki na mimi,” Kamanda akaanza uchokozi. Yule mwanadada akacheka na kutoka nje, lakini kabla hajaufunga mlango alimtazama Amata, “Namba za simu hizo hapo…” akamwambia kisha akaufunga mlango nyuma yake. Kamanda Amata akakitazama kile chumba kwa haraka haraka, akabonyeza itufe Fulani kwenye saa yake na kuigeuzia huku na kule aone kama kuna chochote kilichotegeshwa ndani humo hasa vinaa sauti na vitu vyenye madini ya milipuko. Usalama ulikuwa kwa 100%, akaufunga mlango na ufunguo kisha akajiandaa kujiswafi kabla ya mapumziko.



    §§§§CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Fasendy, umefanya nini? Tangu nimeanza kukupa kazi leo umenivuruga akili yangu,” aliongea kwa wahka bwana Shabalah, huku akimtazama mwanamke huyo aliyesimama kando kidogo ya mlango wa kijiofisi hicho ambacho daima hupenda kukutania kwa mipango yao.

    “Shalabah, sikufanya makusudi, wakati mimi nimemuweka kwenye shabaha mtu wangu, huyu Jeslaim akanigonga begani kuniambi kitu hivyo bunduki ikacheza nyuzi chache sana lakini kutokana na umbali wa mlengwa tayari ilikuwa ni Off-Target,” akajitetea. Jeslaim aliyekuwa pembeni kidogo akisikiliza juu ya matokeo ya umbea aliouleta, sasa alipambana na jicho kali la Shalabah, macho yakamtoka pima kwa woga, akajua wazi kuwa amekwishaingia matatizoni kwa swala ambalo si la kweli.

    “Msilete mchezo katika hi…” kabla hajamaliza kutoa onyo lake simu yake ya kiganjani ikaita kwa fujo, akainyakua na kuweka sikioni.

    “Hello…” akaita na kuisubiri sauti ua uapnde wa pili kujibu.

    “…aonekani pande zote za jiji? (…) ok, sasa hakikisheni mpo karibu na hiyo gari kwa maana lazima atarudi tu hata kama ni wiki ijayo.”

    Shalabah akakata simu na kuipachika kwenye kibweta chake. Akawatazama wale watu wawili, mmoja baada ya mwingine. Kisha hakuwa na la kusema aliwataka kuondoka mara moja.

    Na dakika ileile Sharon aliingia mle ndani na kulete habari nyingine kwa Shalabah.



    “Sikia, weka watu wawili chumbani mwake, kule kwenye gari weka kama wane hivi kisha wengine wawe tayari-tayari kwa amri yoyote ile, mkiona tu jicho lake mulitungue, Fasendy atasubiri tayari kwa amri utakayompa, mi naandaa kikao cha biashara kesho, jamaa wanakuja kununua yale makombora kesho na wataingia na meli yao hapa usiku wa manane wa kesho hiyohiyo, hakikisha pia ulinzi unaimarishwa baharini, weka doria kali yule majinuni asituharibie,” Shalabah akamaliza na kuketi kitini huku akifungua kile kitambaa cha kichwani na kukiweka juu ya meza, akashusha pumzi ndefu na kubaki akitazama ukuta usiyo na picha wala pambo lolote kama zezeta.



    Dar es salaam

    Gina binti Komba Zingazinga aliishusha miwani yake myeusi, bado alikuwa ameegemea gari yake upande wa mbele wa boneti, akihakikisha hampotezi mtu huyo ambaye ni windo analolifuatilia siku ya pili sasa. Alimtazama akiwa ametoka katika hoteli ya Kilimanjaro na kuingia kwenye gari maalumu la kupelekea wageni uwanja wa ndege. Naye bila ajizi akajitoma ndani ya gari yake na kuiwasha kisha akaitoa kuifuata ile gari ya hoteli iliyombeba yule bwana.

    Kama kawaida ya jiji la Dar es salaam, jumapili hiyo barabara zilikuwa nyeupe kabisa, gari zilikuwa ni chache sana, hivyo haikuwapa taabu kuufikia uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere kule pande za Ukonga. Kati ya gari yake na ile ya hoteli kulikuwa na kama gari nne katikati lakini walipofika pale kwenye kona ya kuingia uwanjani ni yeye alikuwa wa kwanza kuitoa kushoto kidogo gari yake na kuwasha indiketa, hivyo hivyo sekunde chache baadaye na ile gari ya hoteli ikafanya hivyo na kuanza kukunja kona kuingia uwanja wa ndege.

    Alishuka na kuufunga mlango wa gari yake, akaipachika tena ile miwani usoni pake na kuvuata hatua za madaha, hatua za mwanamke mrembo kuelekea katika jengo kubwa la uwanja ule, hakuonesha dalili za kumfuatilia mtu wala lolote lile, alionekana kuwa kivyake, moja kwa moja akaufuata mlango wa kuingilia abiria, mlango ambao yule bwana alipita pale muda si mrefu, Gina akasimama mbele ya mwanadada mmoja mrembo aliyejipaka rangi yam domo kama kachinja njiwa kwa meno. Akamsalimi na kumtupia swal, “Umemuona yule bwana mwenye suti ya kijivu?” akamwuliza yule mhudumu. Yule mhudumu akajibu kwa kutikisa kichwa, “Niambie anakwenda wapi sasa hivi?”



    “Kwa nini unauliza, mi sio kazi yangu kutoa habari za wasafiri nenda paleeeee ofisi ya Maelezo,” yule mhudumu alijibu huku akimuonesha kwa kidole ofisi ndogo ilioandikwa kwa Kimombo na Kiswahili, Information/Maelezo.

    “Sikiliza mrembo,” Gina alianza lugha ya ulaghai, “Nisaidie mwanamke mwenzio, yule mzee ni m’me wangu, kaniaga anaenda Nairobi kikazi sasa mi nataka nijue maana kila wakati ananidanganya”. Gina alisema hayo huku mezani kwa mhudumu huyo kukiwa na noti ya shilingi elfu kumi, yule mhudumu alimtazama na kucheka, ndoa zina mambo, ndo maana sitaki kuolewa, yule mhudumu alijisemea kwa sauti ya kujisikia mwenyewe.

    “Anakwenda Mtwara na ndege ya saa 4.30 asubuhi hii,” akajibiwa. Gina akatikisa kichwa juu-chini kuashiri kaelewa.

    “Na kurudi lini?” akaongeza swali.

    “Leo hii hii jioni, ndege ya saa 12.00,” akajibiwa Gina akafurah9i moyoni, akaaga na kutoka nje, moja kwa moja akaenda na kusimama mbele ya luninga kubwa iliyokuwa ikionesha ratiba ya ndege zinazoondoka. Air Tanzania - TC 206 saa 4.30 as- Dar – Mtr, aliisoma ile ratiba na kuitazama saa yake ilikuwa imebaki dakika sabini na tano hivi ile ndege iondoke, akasogea mahali ambapo hakuna watu akaiinua saa yake ya mkononi na kubofya kitufe fulani, “Mission Mtwara,” akatamka maneno hayo huku akitazama ile saa.



    Sekunde chache baadaye saa yake ikamfinya kwa upande wa chini, akaitazama ilikuwa ikiwaka-waka kijimwanga cha kijani, aliitazama na kubofya mahala fulani, ile saa ikatoa kijimkanda chenye maandishi katika moja upande wake, Gina akakavuta na kukasoma. Bon Voyage aliyasoma maneno hayo ya Kifaransa yaliyomtakia safari njema, tayari alielewa kuwa anatakiwa aende Mtwara muda huo bila kuchelewa.

    Kwa hatua za haraka, alikimbilia kwenye ofisi moja ya Air Tanzania na kuingia ndani.

    “Samahani dada, ninahitaji tiketi ya sasa hivi nakwenda Mtwara,” Gina alieleza.

    “Ndege imejaa,” akajibiwa.

    “Hata kama, ni bora abaki rubani mimi niondoke,” Giana akasisitiza. Yule mwanadada aliyevalia nguo nadhifu, sketi nyeusi na blauzi ya rangi ya machungwa ilipachikwa na kitambaa shingoni mwake kikining’inia kwa nyuma, aliinua uso wake wa duara na kumtazama Gina, Mtazame vile, ka’ katumwa, alijiwazia na kisha akasimama mbele ya Gina kati yao wakitengwa na meza kubwa yenye fomeka safi juu yake, akamsogezea sura yake Gina kama anamshushua kitu, “Ndege imejaa mdada, umeelewa?”



    “Hata kama imejaa, lazima niende, uwe na lugha ya kistaarabu kwa wateja,” Gina alaing’aka na kufungua pochi yake, akatoa kikadi maalum na kumpa, yule mwanadada alikipokea na kukigeuza-geuza, hakuamini. Ilikuwa kadi maalumu inayomtaka ampa usafiri wakati wowote bila gaharama ya yoyote bila swali lolote, usafiri wa kwenda popote ndani ya ardhi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Yule dada akagwaya, akajirudisha kitini kama aliyesukumwa na mtu, akabonya kompyuta yake na kuingiza tarakimu Fulani ndani yake, kisha akampa ile kadi Gina.

    “Na ya kurudi mrembo, ndege ya saa kumi na mbili jioni,” Gina akaongezea kumwambia kwa nyodo ilhali akijua wazi kuwa anamkera mwanadada huyo. Dakika mbili alikuwa na tiketi mkononi, akaondoka zake.

     



    UWANJA WA NDEGE – MTWARA

    SAA 5.15 asubuhi walishuka katika uwanja wa ndege wa Mwara, jua lilikuwa likiwaka kwelikweli, joto la mvuke wa bahari lilikuwa likihisika bila kificho. gina alimtazama yule bwana ambaye alitoka na mkoba wake na kuiendea meza ya ukaguzi na wakati huohuo Gina aliifikia meza hiyo. Kabla hajauliza chochote alijifanya kuinama kuweka vizuri kiatu chake na wakati huohuo akabandika kidubwasha kidogo kwenye mkoba wa bwana huyo ambao ulikuwa chini sakafuni.

    “Samahani dada, naweza pata tax hapo nje?” Gina aliuliza na kupewa jibu. Akatoka nje na kutazama, kweli, tax kadhaa zilikuwa eneo lile, akaichagua moja na kuingia kiti cha nyuma.

    “Wapi uelekeo dada?” akauliza dereva tax kwa lafudhi ya Kimakonde ambayo haikujificha kabisa ukijumlisha na chale alizokuwa nazo usoni mwake, hivi hawa watu bado wapo! Alishangaa peke yake, “Tulia nitakwambia,” akamjibu.

    Dakika kama tano baadae yule bwana alitoka na kuingia kwenye Range Rover moja iliyokuwa ikimsubiri. Muda huohuo Gina akachomoa kidubwasha kidogo cha kupachika sikioni chenye mfano wa kile kifaa atumiacho Kiziwi katika kunasa mawimbi ya sauti (shine sikio au audiometer) na kukipachika sikioni mwake. Kila mtu aliyemuona alijua binti huyo mrembo ni kiziwi kumbe la, kutoka katika kile kifaa aliweza kusikia mazungumzo yote ya ndani ya gari alilopanda yule bwana.

    “Ok, twende, nipeleke Makonde Hotel,” Gina alimwambia yule dereva na kisha wakaondoka eneo lile, “Usikimbie sana kuna ndugu zangu kwenye gari ile sasa usikae mbali nao,” alimwambia yule dereva na safari ikaendelea.



    §§§§CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    HOTELI Makonde, ni hoteli safi nay a kisasa iliyojengwa pembezoni kabisa mwa fukwe ya Shangani. Watu wengi walipenda kwenda kupumzika katika hoteli hiyo iliyokuwa ikisifiwa kwa utulivu, huduma na usafi wa hali ya juu. Hoteli hiyo iliyokuiwa ikimilikiwa na kijana wa Kimakonde kutoka Mtwara ilikuwa ni hoteli inayovuma sana katika ukanda wa pwani ya Afika Mashariki. Vigogo na matajiri mbalimbali hupenda kwenda kupumzika katika hoteli hiyo kila mwisho wa juma.

    Bw. Goloko Mikidadi, mtu wa makamo aliyewahi kuwa kigogo wa serikali ya awamu ya kwanza alikuwa ameketi katika moja ya viti vya kiutamaduni vilivyokuwapo katika ukumbi mkubwa wa hoteli hiyo. Meza iliyotakiwa kuwa mbele yake ambayo kwa sasa ilikuwa kushoto kwake ilibeba chupa kubwa la John Walker na kibweta kilichojaa vibonge vya barafu. Bilauri yenye kiuno ilitulia na kinywaji hicho ndani yake kikisubiriwa kumiminiwa katika tumbo la binadamu huyo. Ni siku nyingi sana alikuwa hajafika katika mkoa ule wa Mtwara, mkoa ulio katika miisho ya nchi, upande wa Mashariki ya Kusini. Alikuwa akiingalia saa yake iliyokuwa ikimuonesha kuwa ni saa tano ikikimbilia kuwa na dakika kumi na tano hivi. Gari iliyokuwa imemleta pale ilikwishaondoka kitambo kuendelea na shughuli nyingine. Aliinua ile bilauri na kuipachika kati ya midomo yake na kuibinua kwa mkono wake wa kuume kwa madaa mazito, maisha si ndiyo haya, alijiwazia pindi akiiteremsha mezani ikiwa tupu.



    Kutoka mbali, aliiona boti iliyokuwa ikija kasi sana, kwa kuwa yeye alikuwa amegeukia upande wa bahari; aliweza kuiona bila tabu boti ile iliyokuwa ikija kwenye fukwe ya Shangani. Yule bwana alikenua kidogo kisha akafunga kinywa chake, kama ungekuwa jirani naye basi ungejua kuwa ana tatizo la kiakili, lakini haikuwa hivyo bali alikuwa akimfurahia mtu aliyetakiwa kukutana naye siku hiyo.

    Ile boti ilifika mpaka katika gati ndogo pale Shangani ambayo hutumika na watu wa michezo ya yacht, nahodha wake akaifunga kamba na kupeana mikono ya asante na yule bwana aliyemteremsha katika boti ile. Alikuwa mnene kiasi, mwenye ngozi ya kizungu iliyopigwa jua la kutosha lililoifanya sasa ionekane kama Mhindi mwekundu, alivaa jeans aina ya Lee na raba matata sana huku kichwani akijifunika kwa pama kubwa lililopambwa na picha ya wanyama wakubwa watano wanaopatikana Tanzania. Alivuta hatua na kuvuka kwa hadhari sana ile barabara iliyokuwa ikikatisha mbele yake. Akazikwea ngazi na kufika ghorofa ya kwanza, ghorofa iliyotengenezwa kwa miti na mbao ngumu.

    “Karibu Komredi, nimekuwa nikikusubiri kwa hamu sana,” Bwana Goloko Mikidadi alisimama na kumpa mkono wa karibu yule mwenyeji wake.



    “Naitwa Mr. Reubellen Vinchinsk,” akajitambulisha.

    “Naitwa Bwana Goloko Mikidadi,” naye akajitambulisha.

    Kisha wawili hao wakaketi chini kwa mtindo wa kutazamana. Bwana Goloko akavuta mkoba wake na kuufungua kisha akatoa, akatoa kabrasha moja jembamba na kuliweka mezani. Reubellen Vinchinsk akavuta lile kabrasha na kupitisha macho kisha akaingiza mkono katika mfuko wake wa shati na kuchukua peni, akaweka saini mahala Fulani kisha akamrudishia yule bwana naye akaweka saini mahala pengine, wakagawana kila mmoja nakala yake, kisha wakapeana mikono.







    Nukta hiyohiyo mhudumu alifika na kuleta vibonge vya barafu vingine pamoja na bilauri ya pili kisha akammininia kinywaji na kuondoka. Wale mabwana wawili waliinua bilauri zao na kugonga cheers, kisha wote wakajimiminia vinywaji hivyo matumboni mwao mpaka vikaisha ndipo wakashusha chini zile bilauri.

    “Bwana Goloko, siamini kabisa kama huu mpango umekuwa sawa, kwa jinsi nilivyokuwa napewa taarifa za mambo mengi yaliyotukia huko nyuma juu ya hili, lakini sasa ndiyo naamini kwamba limewezekana,”  Reubellen Vinchinsk alimwambia Bw. Goloko.

    “Ni kweli, ni mambo mengi sana yametukia, watu wamepoteza maisha katika mkataba ishu hii, watu wameuana hapa kaka, fikiria mkakati ulianza tangu mwaka 1975, ukaleta tabu na katikati ukasimamishwa kwanza, Mwalimu Nyerere alikuwa mkali sana, kila aliyejaribu kufanya blaa blaa ama alitimuliwa kazi, alifungwa maisha na wapo walionyongwa. Kipindi kile mimi nilikuwa katibu wa wizara nyeti ya Maji Nishati na Madini, nilitimuliwa ofisini kama mbwa, ikabidi tukae chini na wadau kuona mbaya wetu ni nani, tulipomgundua, tukamfutilia mbali,” Bwana Goloko akamwambia yule Mzungu koko.

    “Aisee, (akamwinamia) mlimuua?” akauliza yule mzungu

    “Sasa tufanye nini komredi? Tulimuua ni muda mrefu sasa hata tumemsahau.”



    “Alikuwa kitengo gani hapa au serikalini?”

    “Yule bwana alikuwa idara ya uchunguzi, lakini kumbe tuligundua kuwa ni afisa wa ngazi ya juu wa usalama wa Taifa hapa Tanzania, na ndiye alikuwa akitoa taarifa Ikulu moja kwa moja, hatukuona haja ya kumuacha, tulimuua dakika chache akitoka kwenye mkutano wake na Mwalimu Nyerere pale Chamwino njia panda,” Goloko alibwabwaja.

    “Mlifanya la maana sana komredi, watu kama hao ni kuwafanyia hivyohivyo tu,” yule mzungu akamwambia kisha wakaendelea kunywa.

    “Ok, tuyaache hayo, sasa mkakati wa leo unakuwaje?” yule mzungu aliuliza.

    “Usiku wa leo naondoka, naelekea Mogadishu, pale tutakuwa na kikao cha mauziano ya ule mzigo kisha kamisheni za kila mmoja zitafanyika baada ya kikao hicho,” Goloko alisema.

    “Nategemea akaunti zitacheka soon.”

    “Masaa ishirini na nne tu komredi utatajirika kwa kazi uliyoifanya…” kabla hajamaliza kusema wote wakaangua kucheka.

    Bw. Goloko Mikidadi akaitazama saa yake tayari ilikuwa imetimu saa nane za mchana, akaagana na mwenyeji wake kisha kila mtu akachukua hamsini zake.



    §§§§§

    Wakati wawili hao wakiongelea juu ya ule mkakati mzito na ulipofikia, Gina alikuwa ndani ya chumba kidogo alichopanga katika lodge moja iliyokuwa mkabala na hoteli hiyo, aliweza kusikiliza mazungumzo yote huku akirekodi katika kimashine chake kidogo. Alipojiridhisha na alichokipata, alifunga vifaa vyake na kutia mkobani, hakuona haja ya kupoteza pale, alichokitaka sasa ni kumfuatilia yule mzungu ili amjue ni nani na anatoka wapi, alifunga mlango nyuma yake na kuteremka ngazi kumuwahi yule mtu. Alipofika chini alipita kwenye ujuia mdogo na kutokea nyuma ya lodge ile, eneo ambalo lilionekana kuwa ni sehemu ya kufulia nguo, aliruka ukuta mfupi na kutua kwa nje ambako moja kwa moja unaelekea baharini, akavuta hatua ndogondogo na kutokea upande wa kushoto wa lodge hiyo; akachukua ujia na kuufuata taratibu kisha akateremka na barabar ya vumbi iliyokuwa ikielekea baharini. Alipofika jirani kabisa na ile yacht club, akatulia na kumtazama yule bwana mzungu akiwa analipia ile boti yake kisha akaingia na wale viajana wake wakaliwasha na kuliingiza majini, Gina aliinua camera yake ndogo lakini yenya nguvu sana na kupiga picha boti ile. Hakuona haja ya kumfuatilia kwani alichokitaka alikwishakipata.



    §§§

    MADAM S alimtazama Gina pale alipoketi usiku wa siku ile, “Una uhakika?” akamwuliza.

    Asilimia 100, mimi ndiye nilikwenda Mtwara, yule ni Bw. Goloko mwenyewe na mazungumzo yao ninayo kwenye mashine.

    “Unasema?” Madama aliuliza kama mtu aliyeshtuliwa.

    “Mazungumzo yao ninayo katika masine yangu,” Gina akajibu tena. Kisha akaufungua mkoba wake na kutoa ile mashine akampa Madam S.  Madam S akasikiliza mazungumzo yote ya wawili wale, akitazama sss yake ilikuwa tayari ni saa tatu usiku.

    “Kama vipi mi’ naona tu n’naona tungemkamata usiku huu,” Gina alishauri.

    “Hapana, muache aende ili tumkamate na kidhibiti,” Madam S alijibu, “Asante Gina, naona sasa umeanza kukomaa taratibu, kaa tayari ukihitajika msaada huko Somalia ujue hiyo ni nafasi yako na hakuna mwingine.”

    Gina aliitikia kwa kichwa alipokuwa akiinuka tayari kwa kuaga na kuondoka, kabla hajaufikia mlango alisikia Madam akiita, “Gina!” akageuka na kuitika “Yes Madam,”… “uwe muangalifu sasa.”



    §§§§§

    Kamanda Amata alifumbua macho na kurudiwa na fahamu zake, aliliendea dirisha na kuvuta pazia kando, kigiza kilikuwa tayari kimelivamia anga na kuruhusu nyota nzuri kulipamba anga lile, akameza funda la mate na kuliachia lile pazia kurudi mahala pake. Kwa hatua fupi fupi akakifikia kitanda na kujitupa juu yake, mawazo yalifudikiza fikra zake, aliwaza na kuwazua akapanga na kupangua. Akajaribu kutathmini mpaka hapo alipofikia amefikia wapi, akajisifu kwa ushujaa wake mwenyewe lakini bado aliumiza kichwa jinsi ya bkumaliza na kupata kile alichotumwa na serikali yake, akajiinua tena na kulivamia bafu, akaoga kwa muda mrefu huku akifikiri la kufanya.

    Alipohakikisha kuwa yupo tayari kwa kazi usiku ule ambao kichwa chake kiliupa jina usiku wa kazi aliinua simu na kupiga namba Fulani na haikuchukua muda mlango ule ukafunguliwa na binti yuleyule akaingian na kuufunga nyuma yake. Alimkuta Kamanda Amata amekwishajiweka tayari ndani ya kadeti nyeusi, viatu vyeusi vyenye soli ya mpira isiyofanya kelele, fulana nyeusi iliyomshika mpaka kwenye koo, kaba shingo yenye mikono mirefu. Tayari alikuwa amekwishapanga kila kinachohitajika mwilini mwake kama silaha na bastola yake aliyopewa na Chiba ilikuwa tayari upande wake wa kuume wa kiuno.



    “Waaaaooohhh!” yule binti alihamaki huku akimsogelea Kamanda Amata pale aliposimama, kwa kutumia vidole vyake laini alitomasatomasa kifua cha Amata kilichoonekana kujaa vizuri kimazoezi, Amata akaushika mkono wake na kuushusha chini.

    “Nipeleke sebuleni,” alimwamuru yule mrembo naye akatii, akaongoza na kumtoa Amata mpaka sebuleni ambako alimkuta Chamelleone akiwa ameketi akitazama luninga kubwa iliyo mbele yake.

    “Naona Kamanda wangu uko tayari,” Chamelleone alimwambia Kamanda Amata huku akijiweka vizuri kitini, “Pata kinywaji kidogo kikuchangamshe mwili, najua mpiganaji hatakiwi kulakula ovyo,” wote wakacheka. Kamanda Amata akainua glass na kugonga cheers, na mzee yule kisha akabugia pombe yote kwa funda moja tu.

    “Asante sana mzee, mimi naona niingie town nina mambo ya kukamilisha na kisha nitakujuza kinachoendelea, kuhusu hilo linguine tufanye wakati mwingine,” kamanda alitoa shukrani nna wakati huo alikuwa akiuendea mlango wa mbele wa nyumba hiyo. Gari ile ile iliyomleta ilikuwa ikimsubiri nje, akaingia na kurudi mjini.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    §§§§§

    Vijana watatu waliokuwa jirani kabisa na gari ya Amata pale katika kituo cha mabasi cha W Sheikh Abaadir walikuwa wameanza kukata tama ya kumnasa mmiliki wa gari hilo. Walikuwa wakibadilisha aina za mikao au misimamo wakingoja na kungoja tangu mchana wa siku hiyo.

    Kule hotelini nako vijana waliowekwa kuizingira hoteli ile, walingoja bila mafanikio, kila walipojaribu kufanya mawasiliano huku na kule mtu nhuyo hakuonekana kabisa katika viunga vya jiji la Mogadishu, iliwasumbua akili, walihaha.

    “Sasa atakuwa kajificha wapi hayawani huyu?” Sharon alijiuliza kwa sauti ya chini huku akiyupa nje ya gari kichungi cha sigara iliyokwisha, akasonya kwa hasira. Fasendy mwanamke pekee aliyekuwa juu ya landcruiser hiyo yenye mtutu mkubwa wenye nguvu alitulia palepale akicheza gemu katika simu yake. Mpaka giza lilipokuwa likiingia hawakumuona Kamanda Amata wanayemsubiri wala kivuli chake, kila mmoja akakata tamaa. Mara redio iliyokuwa mkononi mwa Sharon ikakoroma kuashiria kuna taarifa mpya inayotaka kuingia muda huo.

    “Sharon, usiku wa leo tuna wageni wengi uwanja wa ndege, naomba uchague vijana watano wazuri katika usalama uwaweke pale, wakiongozwa na wewe mwenyewe, msako wa huyo Hayawani muachie Fasendy, na vijana wengine wanakuja kushika nafasi za hao watano,” ilimaliza sauti ya Shalaba.



    §§§§§§

    Baada ya kuliacha gari alilokuwa amepanda kama mita mia tano hivi mtaa wa pili nyuma ya kile kituo cha mabasi, Amata alipita kwenye vibaraza vya maduka na kutokea nkwenye barabara kubwa inayoelekea katika kituo kile. Alisimama mbele ya duka kubwa la vyombo akitazama huku na kule, alijua kwa vyovyote vile lazima wamuwekee mtego katika gari lake, hivyuo aliamua kuwacheza shere, alikodi tax na moja kwa moja akaelekea hotelini kwake.

    Mbele ya hoteli ile alijaribu kusoma sura za watu na akagundua kuwa kuna sura ambazo hawezi kuziamini hata kidogo, aliamua kuwabadilishia mchezo. Ilikuwa lzima afike katika chumba chake kwani kuna dokumenti alizokuwa akizihitaji kwa usiku huo. Akazunguka nyuma ya hoteli na kuichunguza akagundua kuna mlango wa kutokea upande huo wa nyuma, akajaribu kuutikisa akakuta umefungwa, akatulia kimya kufikiri mara mbili la kufanya. Nukta hiyohiyo akasikia sauti za watu wanaoongea wakija upande wa nyuma wa hoteli ile, akajibana katikati ya mabomba mawili ya uchafu, yanayotiririsha majitaka toka juu kuleta chini. Walikuwa ni walinzi wa hoteli hiyo, walipompita aliamua kukwea kupitia yale mabomba. Chumba chake hakikuwa juu sana ilikuwa ni ghorofa ya tatu tu, hivyo haikumchukua muda kwa mtu kama yeye kufika usawa wa chumba chake, pale kulikuwa na kaukuta kalikojitokeza ambako kalikuwa kamebeba ndoo kadhaa za maua, akakanyaga kwa uangalifu kabisa asije kudondosha hata moja, alipohakikisha kuwa yuko usawa wa dirisha la chumba chake akalitikisa kidogo na lenyewe likatii amri, taratibu akaingia kupitia dirisha hilo kubwa lililoundwa kwa aluminiam safi, akatua ndani ya chumba hicho kwa madaha bila kufanya kelele yoyote kwani alijua kuwa lazima wapo wengine walio ndani.



    Akakiendea kitanda chake na kukibonyezabonyeza, kilikuwa kimetulia kama kilivyo. Kamanda Amata akalisogelea kabati kubwa la nguo. Akashika kitasa cha mlango huo tayari kuuvuta lakini kengele za hatari kichwani mwake ziligonga, akajiandaa, kisha akavuta kwa nguvu ule mlango. Hakuwa tofauti na hisia zake, alipofuangua mlango tu, mtu mmoja aliyekuwa amejificha ndani ya kabati hilo alijitokeza kwa minajiri ya kumpamia Kamanda Amata, lo, Kamanda alipoufungua ule mlango tayari alikuwa kajiweka kando hivyo yule mtu akapitiliza peke yake na kumpita Amata ambaye alinyanyua mguu na kumpiga ngwala maridadi iliyomfanya mtu yule atue kwa uso katika sakafu na kuvunja mwamba wa pua. Kabla hajajigeuza, mguu mzito ulitua nyuma ya shingo yake na kumfanya mtu huyo kugugumia kwa maumivu. Amata akamwinamia palepale alipo na kumtazama mtu yule ambaye alikuwa chini, damu zikimvuja puani huku akilia kwa uchungu, lakini hakuweza hata kujigeuza kutokana na uzito wa guu la Amata.



    “Wenzako wako wapi?” Kamanda alimuuliza.

    “Niko pe-pe-ke ya-ngu,” alijibu kwa shida huku akijaribu kujiinua, lakini hakuweza kufanya hivyo.

    “Unanitania sio?” Kamanda aliuliza na kumkanyaga kwa nguvu, yule mjinga pale chini alianza kutupatupa miguu na mikono kwa kutafuta pumzi.

    “Ni-niiii-takwa-mbi-i-a,” alijibu. Kamanda Amata akalegeza mguu kidogo.

    “Haya sema,”

    “Wa-po nje,” akajibu.

    “Wangapi?” Kamanada akahoji.

    “Si- si… unaniumiza bwana,” yule mtu akashindwa kutoa jibu na badala yake akamtamkia maneno hayo Kamanda.

    “Niambie, yule komandoo na wale wengine mmewaweka wapi?” akauliza tena.

    “Si si – sijui mi-mi,” akajibu.

     Muda huohuo saa ya Kamanda Amatav ikaanza kumfinya kwa fujo kuashiria kuna ujumbe ulikuwa ukiingi. Ni nafasi hiyohiyo ambayo yule mjinga pale chini aliitumia, alijigeuza kwa nguvu na kuwa chali akitaka sasa kusimama, teke moja kali nla Amata lilikuwa likienda kupiga korodani, yule bwana akaipanga mikono yake kwa mtindo wa x na kuchanua viganja vyake chini kidogo ya kiuno chake kusha akabonyea kufanya kama anachuchumaa, teka la Amata halikuwa pata lilipokusudiwa bali lilikingwa kwa hiyo mikono kwa usatdi kabisa.



    Kamanda Amata akaona akile ta mchezo hapo kazi itakuwa ngumu, wakati yule jamaa akiushusha mguu wa Amata chini mara tu baada ya kulipangua lile pigo kwa akili zote, kamanda Amata alishusha kichwa cha nguvu na katika paji ola uso la yule mjinga. Nyota zilimzunguka maana aliona kama kadondoshewa tofali, alipepesuka na kujibwaga kitandani, akajisjika pale alipopigwa kama kumepasuka lakini alishuhudia nundu lililojitokeza bila hata kushauriwa. Yule mjinga kutoka pale kitandani alijirusha kinyumenyume sarakasi inayoitwa ‘back’, akatua upande wa pili na wakati huohuo alichomoa visu viwili na kuvirusha kwa umahiri kumwelekea Amata ambaye aliviona na kujitupa chini sakafuni na kuruhusu visu vile kukutana na ukuta. Kama ni kosa yule mjinga alilifanya hapo, alirukia kitandani ili atue upande wa pili ambapo alijua Kamanda Amata yuko chini, na Kamanda Amata alikwishajua nini yule bwana atafanya baada ya yeye kujitupa chini, na ndivyo ilivyokua, yule bwana alikanyaga kitanda na kujirusha upande wa pili, kabla hajafika chini, Kamanda Amata alirusha teke kali la na kiatu chake upande wa mbele kikapiga kwenye pingili za mwisho za uti wa mgongo ‘sacrum’ karibu na nyonga, yule bwana akajikuta kama anaishiwa nguvu za miguu, alijibamiza ukutani na kujibwaga chini kiama gunia, marehemu.







    Kamanda Amata akasonya na kuiweka saa yake vizuri, kisha katika lile kabati akachukua kijitabu kidogo kutoka katika vitu vya Marehemu Gwamaka, akatia mfukoni, akajiongezea na vikolokolo vichache katika mifuko yake ya akiba, kisha akatoka kwa jinsi ileile aliyoingilia.

    Walinzi waliowekwa doria upande wa chini, walikuwa bado wakizungukazunguka kutafuta wapi windo lao litatokea, labda hapa au pale lakini walikuta usiku unazidi kuwa mwingi na hakuna dalili za windo hilo kurudi.

    Kiongozi wa kundi lile lililokuwa likiweka doria chini ya hoteli hiyo aliinua simu yake ya upepo na kupiga kwa mtu ambaye alimuweka ndani ya chumba cha hoteli ili kutoa taarifa pindi tu windo lao litakapofika. Simu iliita na kuita lakini hakuna jibu lolote.

    “Hamsud, huyu jamaa mbona hapokei simu, hebu panda juu umwangalie,” akatoa maagizo kwa kijana mwingine. Yule aliyeagizwa akaweka pembeni bunduki yake na kutwaa bastola moja na kuipachika kiunoni, akashuka garini na kuzijongea ngazi za jengo hilo. Sekunde chache tu aliufikia mlango wa chumba kile, akagonga na kugonga lakini hakuna jibu lolote. Akatoa funguo Malaya, akajaribu kuufungua ule mlango, ukafunguka, lo, hakuamini alichokiona, alitazama mwili wa swahibaye uliokuwa umelala bila uhai.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Shiiiiiiittttt!!!!” akang’aka kwa hasira, akarudisha mlango na kuufunga kama ulivyokuwa. Kisha kwa hatua fupifupi kama za mtu aliyelewa, Hamsud alijivuta na kuteremka chini.

    “Vipi?” yule kiongozi alimuuliza.

    “Hakuna mtu, amekufa,” Hamsud akajibu.

    “What?” yule kiongozi alijishika kichwa kwa mshangao, akawa anazungukazunguka huku na kule. Akampiga kijikofi Hamsud na kuelekea naye ndani, walifika katika chumba na kutazama maafa waliyoyakuta. Yule kiongozi akaugeuza ule mwili wa yule marehemu. Akatikisa kichwa, na mikono yake akaiweka kiunoni mwake. Ametuzidi kete mwanaharamu huyu, yule kiongozi alijiwazia. Wakapekua makabati na kukuta peupe, Kamanda Amata aliondoka na kila kitu chake mle chumbani, kwa ujumla alihama, lakini hakuna aliyemuona kutoka nje.



    §§§§§

    Shabalah alishusha simu masikioni mwake akiwa amefura kwa hasira, alitamani amuone huyo mtu anyeitwa Amata ili amtafune kama ikibidi. Kama kuna kitu kilichomuuzi sana ni kitendo cha mtu wake kuuawa ndani ya hoteli pasina muuaji kuonekana. Shalabah alichanganyikiwa, akainua simu yake na kuwapa taarifa wengine wote ili kukomaza doria usiku huo, wakiwa wamepewa amri ya kuhakikisha Amata anapatikana ama mfu au hai.

    Kituo cha mabasi cha W Sheikh Abaadir

    KAMANDA Amata akatulia kwenye kona moja ya jengo lililokuwa na watu wengi, kila akitazama saa yake alikuwa akiona muda unamkimbia na wakati huo alikuwa akilitaka gari lake, alijua wazi kuwa kwa vyovyote wapo wanaomtega katika eneo hilo. Kamanda Amata aliamua la kuamua, akajivuta taratibu mpaka kwenye gari yake akainua mkono na kuitazama saa yake, akaizungusha kwa namna ya pekee kidogo, lengo ilikuwa ni kutazama kama kuna kitu chochote cha hatari ambacho kimetegwa katika gari hilo, alipoona kuna usalama, akafungua buti ili kuweka mabegi yake, lo, alijikuta akitazamana na mtutu wa shot gun, uso kwa uso, Kamanda Amata akamtazama mtu huyo aliyekuwa amelala ndani ya buti lile.

    “Tumekukamata sasa, mshenzi wewe, umeshatuulia wenzetu wengi tu lakini leo hii ni zamu yako,” sauti ilitoka nyuma yake, alipogeuka tu alijikuta akikutana na konde zito lililotua shavuni mwake, hakuyumba, alisimama kidete akimtazama huyo aliyepiga konde hilo, Amata akajifuta pale lilipotua konde hilo. Wale waliofuatana na mtu huyo wakacheka kwa kitendo kile, Amata alichukizwa sana kwa hilo aliona kama anazihakiwa.



    “Mpekue…” amri ilitoka.

    Kamanda akapekuliwa na wakatoa bastola yake iliyokuwa kwenye kikoba maalumu.

    “Yuko safi,” akajibu yule aliyekuwa akimpekua huku akimkabidhi yule kiongozi wao ile bastola. Kisha Kamanda Amata akafungwa pingu na kuingizwa kwenye land cruiser iliyofika wakati huo, kisha mmoja wale maharamia akatakiwa kuiendesha ile gari ya Amata. Kamanda Amata akawapatia rimoti kwa ajili ya kuendeshea gari ile, gari iliyokuwa ikitumia rimoti tu.

    “Lala chini, unaangalia nini?” mtu mwingine alimuamuru Amata huku akimpiga na teke moja kali la usoni ambalo lilimpeleka chini, kisha wale jamaa wakasimama juu yake. Ile land cruiser ikawashwa.

    Mbala mwezi ilizidi kung’aa katika anga la Mogadishu, wakati ile land cruiser ikiondoka na kutimua vumbi ikiwaacha yule kiongozi wa kikosi na yule jamaa aliyetakiwa kuiendesha ile gari ya Kamnda Amata. Wakiwa njiani kuelea chimbo, simu ya upepo ya mmoja wa askari aliyekuwa katika ile landcruiser iliita, akaichomoa na kubofya kitu Fulani kisha akajiruhusu kuongea.

    “Sierra 1, Sierra 1,” aliitikia ile simu.

    “Geuza gari mrudi hapa mara moja,” ilikuwa sauti ya kiongozi wa kikosi aliyebaki kwenye gari ya Kamanda. Ile Cruiser ilipiga norinda na kurudi ilikotoka.

    Kamanda Amata akiwa ndani ya ile cruiser huku watu watatu wamesimama kwa kumnyaga mgongoni, alijua wazi kuwa tayari gari imewashinda kuwasha, alipiga akili kujua nini anatakiwa afanye ili aweze kutoroka katika mikono ya hao maharamia.

    “We mbwa! Usitufanye sisi mabwege unasikia wewe!” alikoroma kwa hasira yule kiongozi, “Haya utuambie hii rimoti yako unaitumiaje?” akauliza. Kamanda Amata alimwangalia tu hakumjibu, akatema mate chini yaliyochanganyika na damu, akajiinua kwa tabu kutoka pale alipolala na kukaa kitako, akawapa ishara ya kuomba apewe ile rimoti. Yule kiongozi alikataa na kumtaka amwelekeze kutoka pale alipo, Kamanda Amata kakohoa kidogo.



    “Nobu nyekundu mara mbili kisha ya kijani mara tu, tofauti ya mbonyezo ni sekunde mbili kwa kila kibonyezo,” akatoa maelekezo na kutulia akiangalia kitakachoendelea.

    “N-n-nobu nyekundu,” akawa akibonyeza huku akirudia maneno ya Kamanda jinsi ya kuitumia rimoti ile, alipofika kwenye nobu ya kijani na kukibonya kisha akasubiri sekunde mbili ili akamilishe muamala.

    Na hapo ndipo alipoikuwa akisubiri Kamanda Amata. Mara tu alipobonyeza, sauti kali za bunduki kubwa, nzito ilisikika katika mtindo wa burst, zile kelele zikawafanya wale jamaa wachanganyikiwe wakijua wazi kuwa wamevamiwa.

    Wakiwa katika kushangaa kwa taharuki wengine wakilala chini kujikinga na adha hiyo, kamnada Amata aliinuka kutoka pale alipokuwa amelala ndani ya ile gari. Mjinga mmoja akamuona na kumrushia teke kali akimuamuru kulala chini, Kamanda Amata akiwa tayari kajigeuza na kuwa chali alidaka kanayagio la mtu yule na kuzungusha kwa nguvu ule mguu, yule jamaa akapiga kelele za uchungu kisha Kamanda Amata akamsukumia nje na kumbwaga. Alijinyanyua kwa ustadi kabisa bila kugusa popote pale, akasimama wima na kukutana na mtu mwingine aliyekuwa bado juu ya ile gari.

    “Simama!!!” yule mtu alibwata, kabla hajajiweka sawa na bunduki yake, alijikuta akipata kichwa kikali cha nguvu kilichopmpeleka nyuma, Kamanda Amata alimuwahi na kuichomoa bastola kiunoni mwa yule jamaa, kwa mikono yake miwili iliyofungwa kwa pingu, alfyatua risasi na kumpiga kifuani yule mjinga akambwaga nje ya gari. Aligeuka na kumkuta yule kiongozi wao badoa hajajiweka sawa.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Anatorok…” zilikuwa ni kelele za mtu mwingine aliyekuwa kalala chini barabarani lakini kabla hajamaliza kauli yake alizimishwa kwa risasi ya kichwa. Kamanda Amata aliruka na kutua ardhini, kisha akajitupa kwa sarakasi maridadi kabisa. akiwa kapiga goti moja chini, alimtwanga risasi mtu mwingine na alipotaka kumgeukia yule kiongozi wao alijikuta kila akifyatua risasi zinagoma, chemba imeishiwa, akaitupa pembeni ile bastola. Wakati huo huo yule kiongozi wa wale jamaa akawa anakuja akikimbia pale alipo Amata huku akitoa matusi ya ajabu, Amata hakumsubiri amfikie, alisimama kwa haraka na kuruka kwa akilina kumchapa teke moja la shavu lililompeleka chini huku bunduki yake ikilalama kwa uchungu na kutawanya risasi huku na kule, kizaazaa. Kamanda Amata alikimbia akawahi kwenye gari yake, akafungua na kuketi kitini huku nje bado kukiwa na kile kizaazaa, bado mikono yake ilikuwa na pingu, akawasha gari kwa kutumia swichi maalum, akaliseti liwe katika automatiki, kisha akaliruhusu liondoke huku akiwa kakamata usukani kwa mikono yote miwili.

    Aliizungusha ile gari kwa ustadi wa hali ya juu, wale maharamia waliobaki walifyatua yisasi  kupiga matairi na wengine wenye vioo lakini gari ya Kamanda iliyotengenezwa na wanasayansi wa Kitanzania haikupata dhara lolote, iliingia barabarni na kuondoka kwa kasi.



    Wale jamaa nao wakaamka na kuingia kwenye ile landcruiser na kumkimbiza Kamanda.

    “Tulikwishamkamata lakini ametutoroka, ova,” ilikuwa sauti ya yule kiongozi akiwasiliana na kamanda wao, Sharon.

    “Hakikisha hamumpotezi tunakuja na nguvu kubwa zaidi, ova,” Sharoni alimjibu.

    “copy,” alimaliza kwa kujibu namna hiyo akaiweka ile redio kitini kisha wakaingia barabarani na kuanza kufuata uelekeo wa kule alikokwenda Amata.

    Kupitia kamera maalumu iliyokuwa nyuma ya gari ya Amata aliweza kuwaona wale jamaa wakija na ile cruiser yao kwa kasi ya hatari, akatazama vizuri na kuona kuna jamaa tayari juu ya lile bunduki kubwa la kudungulia akijaribu kulenga shabaha. Kamanda Amata akakunja kona kwa ustadi mkubwa na ufundi wa hali ya juu, ile gari ikasota na kuzunguka barabarani ikatazama ilikotoka, nukta hiyohiyo mikono yake miwili yenye pingu lakini liikamata bastola yake kwa umakini wa hali ya juu sana alifinywa jicho moja huku akiwa kauacha usukani peke yake, alifyatua risasi iliyopiga na kuchana sehemu ya mkono wa mtu yule aliye juu ya gari.

    Yule bwana akapiga yowe na kuachia lile bunduki huku akivuja damu katika kiganja cha mkono.

    Kamanda Amata akajaribu kulenga tena lakini mara hii alijikuta anashindwa, akakamata usukani na kuiweka gari sawa na kukanyaga mwendo. Mfukuzano uliendelea kwa kasi ya hatari, huku wale jamaa wakimwaga njugu lakini bado walishin dwa kuidhibiti gari ya Amata iliyopewa jina la Kilimanjaro kutokana na uzuri wake ilivyo na matata yake yaliyowekwa kwenye mfumo huo. Kamanda Amata alijitahidi kuendesha huku akifungua pingu kwa kutumia kipini maalumu kwa kazi hiyo kilichokuwa katika saa yake, alikichomoa kwa vidole viwili na kukibana kwa meno; punde si punde ile pingu ilifyatuka mkono mmoja. Kamanda Amata alikuw akishusha mteremko mrefu, tayari alikuwa ameyaacha makazi ya watu na kulifikia jangwa, mara nyuma yake juu kukatokea chopa kubwa. Mvumo wa mapangaboi yake ukamfanya Kamanda Amata ajue kuwa sasa kazi imeamka.



    Washenzi wamenipania, aliwaza huku akiendelea kukanyaga mafuta na kuongeza kasi ya ile gari. Sasa alikuwa akifukuzwa juu na chini. Hakujua la kufanya, hakujua jinsi ya kujiokoa katika domo la mamba. Kamera  katika gari yake zikawa zinafanya kazi sawasawa, nyuma aliiona ile cruiser na juu aliiona ile chopa. Alipotazama vizuri alimuona yule aliyekuwa kwenye chopa mlango akilifutia bunduki lake kubwa lenye risasi za kulipuka upande mmoja. Akajiweka tayari, akafunga mkanda wa kiti sawasawa. Akafungua kijikasha kilicho karibu kabisa na mkono wa gia, akapapasa vinobu kadhaa. Alipogeuka tena kutazama ile kamera yake aliona kitu kama moto kikitokezea pale kwenye domo la ile bunduki, mara moja akajua amedunguliwa. Alam katika gari ikaanza kupiga kelele, Kamanda bila kuchelewa alibinya vitufe Fulani kwenye kile kiboksi mara paa la gari likafunuka na kile kiti cha dereva kikafyatuliwa kwa nguvu na kurushwa juu kama mita 150 hivi. Lile bomu lililopigwa likaifumua gari ya Kamnda nukta ileile na kuichakaza vibaya.

    “Iiiiiiiiiiihaaaaaaaaaaa,” ilikuwa ni kelele ya shangilio la yule jamaa kwenye ile chopa akishangilia shabaha yake. Kila mtu alikuwa akishangilia mpaka wale wapio katika ile cruiser. Ile chopa ikageuka na kwenda kutua mbele kidogo, na ile gari nayo ikasimama.

    “Bora tumemuua, mshenzi huyu,” aliongea Sharon huku akikimbia kuwahi kule inakoungua ile gari akifuataiwa na wenzake kutoka katika gari na ile chopa kila mmoja akiwa na furaha.

    “Tumemlipua nina uhakika hapa haponyoki,” Sharon alikuwa akionmgea kwa simu ya upepo.

    “Oh, hongereni sana, kumuua huyo jamaa ni sawa na kufanikisha mipango yetu yote,” Shalabah alijibu huku akionesha tabasamu lake bila kuficha, akiwa anaelekea uwanja wa ndege kwa ajili ya kupokea wageni wanaoingia usiku huo kwa minajiri ya kumaliza biashara yao.

    Sharon na wale maharamia wengine walilisogelea gari la Amata lililokuwa likiteketea kwa moto mkali wa ule mlipuko, hakuna aliyesogea kariobu, wote waisimama mbali kidogo wakilitazama likiisha.



    DAR ES SALAAM – TANZANIA

    CHIBA alishtuka kukuta kompyuta iliyokuwa imeunganishwa na gari ya Amata kwa mtambo wa satellite ikiwa inaonesha mchelemchele kwamba hakuna mawasiliano. Alihamaki kaidogo hakuelewa nini kimetokea, kwa tokeo hilo alijuwa wazi kuwa lazima Kamanda Amata amepatwa na shida kubwa au gari peke yake imepatwa na shida, hakujua kipi ni sahihi. Aliinua simu na kumwita Madam S aliyekuwa kwenye mazungumzo na Dr. Jasmin pamoja na Gina, wote watatu wakakimbilia kwenye chumba cha mawasiliano.

    “Vipi Chiba?” akauliza.

    Akamuonesha ile kompyuta, Madam S akakodoa macho, “What?”

    “Mawili, ama Kamanda na gari lake au gari peke yake imelipuka,” Ciba alijibu.

    “Lo, hebu mtafute kwa mawasiliano yake binafsi,” Madam S alitoa amri. Gina na Dr. Jasmin walibaki midomo wazi hawajui kipi ni kipi.

    “Hapatikani!” Chiba alishusha simu chini.

    Madam S akashusha pumzi ndefu, akajishika kiuno, “No; yuko salama, hawezi kufa kikuku hivyo, we jaribu kumtafuta.”

    “Kama alikumbuka kuminya nobu ya dharula, bila shaka atakuwa hai,” alijibu Chiba.

    “Nobu ya dharula?” Gina na Jasmin wakauliza pamoja kisha wakatazamana.

    “Yeah, kweye ile gari kuna nobu ya dharula ukiibonyeza, inakutoa nje wewe dereva pamoja na kiti chako na kama ni ajali basi gari hupata peke yake,” Chiba akawaelewesha.

    “Lakini si ulimuonesha?” Gina akahoji.

    “Yap, nilimuonesha.”

    “Basi, kabonyeza, hajafa huyo, tusubiri taarifa nyingine,” Madam S akajiaminisha.





    Chiba aliendelea kufanya kila analoweza kumtafuta Kamanda Amata, kila simu aliyopiga haikupatikana, alijaribu huku na huku wapi, alipoona kila kitu kimeshindikana, akanyanyuka na kwenda kupata kikombe cha kahawa.



    PUUUU! Kamanda Amata alidondoka na kiti chake umbali wa takribani mita 200 kutoka pale kwenye tukio, akaguna kwa mtuo huo, kisha akafungua mkanda wa kiti hicho na kufyatua ule mwamvuli uliomteremsha hapo, akajitoa eneo lile na kutulia kimya nyuma ya kichaka cha mmea wa mkakati, mmea unaostawi jangwani. Alitazama kule barabarni na kuona ile chopa ikiwa chini na ule moto sasa ulikuwa ukipungua taratibu.

    Hapa sasa ni kurudi mjini, alijiwazia huku akijipekuwa kuona kama ana kila kitu, bastola hakuna, akakumbuka kuwa amechukua yule kiongozi wa lile kundi, alibakiwa na silaha za baridi tu, kama visu vidogodogo na vikolokolo vingine. Kwa kuwa eneo lile lilikuwa jangwa, na hakukuwa na mbala mwezi alitulia kusubiri watu wale waondoke. Haikupita muda aliona wakiingia kwenye gari na ile chopa kisha kuondoka na kuliacha lile eneo pweke kama awali. Kamanda Amata akavuta hatua kuelekea barabarani.

    Alijishika kiuno kulitazama gari lile ambalo sasa lilikuwa haliwaki tena, ila lilikuwa limebaki gofu tu.



    Akainua mkono wake na kutazama saa, ilikuwa ikikaribia saa sita tano nne za usiku. Akaliendea jiwe kubwa lililokuwa mahala pale na kuketi.

    Haukupita muda, aliona mwanga wa gari ikitokea mbali kidogo, akasogea barabarani na kusubiri, macho hayakumdanganya, alipunga mkono kuashiria gari hiyo kusimama, na ile gari ikampita kidogo kisha ikasimama mbele kama umbali wa kutupa jiwe. Kamanda Amata akaiendea, ilikuwa ikiendeshwa na mwanamke aliyekuwa na watoto wawili ndani ya gari. Kamanda Amata akaomba msaada wa usafiri mpaka mwanzo wa mji tu, yule mama alikuwa ni mtyu wa dini sana, akamwambia aingie huku akimpa pole kwa kuunguliwa na gari yake.

    “Kwa hiyo ulikuwa unatoka uwanja wa ndege?” akauliza.

    “Ndiyo, nimeingia hapa Mogadishu kama masaa manne yalopita,” Kamanda akajibu kwa kuongopa.

    “Sasa utafanyaje usiku huu na ulikuwa waelekea wapi wewe?” akauliza yule mama.

    “Nilikuwa naenda Kismayu, lakini sasa itabidi kubadili ratiba, kwani sina chochote.”



    “Yaani uko kama ulivyo hivyo? Tena umechafuka vumbi la jangwa kwelikweli, basi hata ufike nyumbani uoge,” yule mama alionesha ukarimu wa hali ya juu sana.

    “Hapana asante sana,” Kamanda alishukuru huku akijua kuwa akijilegeza kwa huyo mama ataharibu kazi.

    “Hapana bwana usiogope, mimi sina mume, mume wangu aliuawa kitambo yeye alikuwa mwanajeshi,” yule mama akaeleza.

    “Usijali mama, nitakuja, lakini ngoja kwanza nifike uwanja wa ndege nikapate kibali kingine japo cha muda wa kuwa hapa,” Kamanda aliomba.

    Baada ya mvutano mkubwa na mwanamama yule, mwisho Kamanda alishinda, yule mama akampa kadi ya kibiashara na kumwambia akimaliza kazi yake tu huko uwanja wandege basi amtaarifu ili amkaribishe kwake kabla ya kuendelea na hiyo safari yake ya Kismayu.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    §§§§§



    Wanawake bwana! Akajiwazia na kutikisa kichwa wakati akivuka barabara na kuelekea upande wa kituo cha tax, akajificha sehemu na kujikung’uta vumbi kisha akachukua tax moja wapo.

    “Uwanja wa ndege tafadhali,” akamwambia dereva wa tax.

    Kamanda Amata ilimbidi abadili ratiba ya kazi usiku huo, kwani kwanza alipanga kwenda kule kuliko na ghala la hao jamaa lakini kutokana na vitu vyake vyote kuungua katika ile gari hivyo hakuwa na kumbukumbu nyingine ya kumuongoza kwenda kule, maadam alisiki katika mawasiliano ya watu wale kuwa kuna wageni wanaokuja uwanja wandege basi aliamua kwenda kuona kwanza ni nani na nani wanakuja usiku huo.

    “Tayari boss,” yule dereva tax alimshtua Amata aliyekuwa kapitiwa na usingizi, akaamka na kumpa noti ya dola ya kimarekani kisha yeye akavuka barabara moja na kuwasili katika maegesho ya magari. Akachomoa simu yake na kubonyeza namba fulani.

    Akaweka simu sikioni na kusubiri majibu ya upendo wa pili.

    “Yeah, Ahab!” akaita.

    “Ndiyo, unaongea na Ahab hapa, nani mwenzangu?” Ahab akauliza.



    “Mimi ni rafiki yako tulikutana siku chache zilizopita hapo Uwanja wa ndege nikakuahidi kukupigia pindi tu nikitulia,” kamanda alimkumbusha.

    “Yeaaaaah, uuuuuu n’mekukumbuka asee,” akajibu.

    “Niko hapa Uwanja wa ndege, ninahitaji msaada wako wa haraka,” akamwambia.

    “Bila shaka braza, uko wapi?” Ahab akauliza.

    “Niko nje hapa, njoo nyuma ya hili jengo la matangazo,” akamwambia.

    “Sawa, sawa niko njiani.”

    Kamanda Amata akarudisha simu mahala pake na kuendelea kujibana pale pale alipo, kila alipokuwa akiangaza macho hakumuona yeyote aliyekuwa akimuhitaji. Mara akamuona Ahab, yule kijana anayefanya kazi za kubebea wasafiri mizigo yao akiwa anashangaa shangaa.

    “Ahab,” akaita, na yule kijana akashtuka kutazama pale mahali akamuona Kamanda akiwa pale.

    “Eee braza! Sema,” Ahab akamuendea.

    “Sikia nahitaji msaada wako rafiki, naweza kupata vazi la wafanyakazi wa hapa uwanja wa ndege?” akamwambia. Ahab akashtuka kidogo na kumtazama Kamanda, alikuwa kama hajasikia vizuri kile alichomwambia. Akatahayari kwa ombi hilo na baadae akawa kama mtu aliyekurupuka, “Sawa, sawa inawezekana, nilikuwa nafikiri jinsi ya kupata.”

    “Nahitaji sasa hivi, nikimalizia kazi tu nitakupa urudishe, ila usimwambie mtu,” Kamanda akamuasa.



    “Ok, nifuate,” sauti ya Ahab ilitoka kinywani mwake huku akiliacha eneo lile na Kamanda Amata akamfuata nyuma. Ahab akamwongoza Kamanda mpaka pembezni mwa jengo lile la uwanja wandege sehemu ambayo haruhusiwi mtu kupita kirahisi, akaingia nae kwenye kijimlango kidogo na wakatokea kwenye chumba kilichojaa maboksi tupu mengi sana yaliyovurugwa vurugwa.

    “Subiri hapa, ila braza ni hatari wakinikamata,” Ahab alisema kwa woga, Kamanda Amata akampa ishara ya kutokuwa na wasiwasi akimtaka aendelee mbele.

    Dakika mbili baadae, alirudi pale akiwa na mfuko wa plastiki, akamtupia Amata. Ndani ya mfuko huo kulikuwa na nguo ndefu iliyounganishwa kutoka juu hadi chini. Akalivaa haraka haraka na sasa kuonekana kama mmoja wa wafanyakazi wa hapo. Akamwambia Ahab wataonana punde tu akimaliza kazi yake. Akamsisitizia kutosema au kutamka lolote juu ya hilo.

    Kamanda Amata akatokea kwenye kile kimlango na kuzunguka mbele ya uwanja ule ambako watu huingia na kutoka, magari hushusha na kupakia, akaenda moja kwa moja hadi sehemu iliyoonekana kuna vikokoteni vingi vimezagaa na wachache wa wafanyakazi waikuwa wakivikusanya kurudisha ndani, naye alijiunga nao akapata nafasi ya kuingia ndani ya uwanja huo. Bado alikumbuka kuwa ndege zinazosubiriwa ni moja ya Ethiopia ambayo wageni hao wote watashuka pamoja pasina wao kujuana. Aliitazama saa yake, ilimuonesha saa saa saba za usiku, bado ilibaki muda kidogo tu ndege hiyo ifikie. Kamanda Amata alifanya kila analoweza kujaribu kuona sura zilizopo eneo lile ndani na nje ili kubaini kati ya maharamia waliopo hapo basi ni nani yupo, lakini hakuweza, lakini alimini kuwa ama walikuwa nje au kuna sehemu ambayo walikuwa wamejibana, wanaogopa nini sasa? Akajiuliza.



    §§§§§



    Bw. Goloko alifyatua kitufe cha mkanda na kushusha pumzi ndefu, kisha akatazama abiria waliokuwa wakiteremka kwenye ndege hiyo. Alizitazama tiketi zake na kisha akazihifadhi vizuri, akasimama mara baada ya wale watatu waliokuwa pembeni yake kufanya hivyo.

    Alikuwa ni mzee wa makamo, kichwa chake kilikuwa na mvi za kuhesabika, shati lake la kitenge cha Urafiki lilikuwa limemka sawia. Weusi wake ulikuwa tofauti na abiri wengine waliokuwamo ndegeni ambao waling’aa kidogo ama kwa asili yao au kwa kutakata kwa wema. Kwa hatua za uhakika alishusha mguu mmoja baada ya mwingine huku macho yake yakitazama vizuri ngazi ile labda miguu isije kukosea na kufanya ajali isiyo lazima.

    Aliwahi kuwa katibu wa wizara nyeti ya Maji, Nishati na Madini, kigogo katika serikali ya sera za ujamaa na kujitegemea, serikali iliyopambana vikali na wahujumu uchumi, iliyowasaka mpaka mapangoni na mashimoni baada ya kuifanya nchi kupitia katika kipindi kigumu kiuchumi, serikali ya Mwl. Nyerere. Mzee huyu aliyefukuzwa kazi katika wizara hiyo mara tu alipobainika kupokea hela ndefu kutoka kwa tajiri mmoja mkubwa huko duniani ambaye wengi hawakuwahi kumuona kwa macho, alifukuzwa kazi kama mbwa na serikali ya awamu hiyo, na hiyo ilikuwa ni bahati kwani wengine walifungwa kabisa.



    Hata akiwa nje ya kifungo bado aliweza kufanya kazi hiyo ya kuhakikisha hujuma hiyo inawezekana, na hakika iliwezekana, na usiku huu alikuwa akija kukamilisha mazungumzo na wadau wengine ili kufanya malipo ya mabilioni ya pesa na kuwagawia washikaji zake.

    Nyuma yake kulikuwa na watu wengine wawili waliojaa katika suti kali za bei mbaya ambazo hapa zingeweza kuvaliwa na kiongozi wa juu wa serikali. Nao walikuwa wkishuka ngazi hizo kwa madaha kabisa wakijitabiria utajiri unaowafikia dakika chache zijazo.

    Kamanda Amata kutoka pale alipokuwapo moyo wake ulipiga chogo chemba kumuona mzee yule, hakukosea, ni yeye, aliyewahi kuitwa Mheshimiwa, alimtazama kwa makini sana huku akiendelea kujifanya anasafisha kwa mashine katika sakafu hiyo ng’avu. Alipomuona tu mzee huyo na kuhisi jambo, aliirudisha ile mashine mahala pake na kujongea karibu na eneo la wageni hao kusubiri mizigo yao, akapita mpaka kwenye tundu ambako mizigo hiyo hutokea, na kuikodolea macho akijifanya kuiweka vizuri pindi inapotaka kudondoka, lakini jicho lake lilikuwa likitazama nyendo za yule mzee. Akamuona akipokelewa kwa bashasha na wenyeji wake, akatzama sura za wenyeji wake hakuna aliyemtambuwa, inaonekana hawa ndio matop wao, alijiwazia kisha akatazama mizigo mingi inayochukuliwa, akabaini watui hao wana wageni zaidi ya mmoja na kweli alishuhudia wageni wane waliokusanywa nao na kisha kupakiwa mizigo yao katika kitoroli, Amata akawahi kuwasaidia nao wakaridhia bila kumjua kutokana na vazi alilovaa na kofia aliyojitwika kichwani, miwani aliyoichukua kwa Ahab iliupoateza kabisa uso wa kijana huyo, akakokota kile kitoroli mpaka sehemu inayotakiwa.



    Cadillac Escalade/ESV, gari ya bei mbaya ya kutisha, ilisimama miguuni mwa Amata na mlango wa nyuma ukafunguka wenyewe bila kuguswa na mtu. Akapakia mizigo yote ndani ya gari hiyo huku akikariri sura za wageni hao, akilini mwake alijuwa wazi kuwa watachukuliwa na gari yenye buti la kufunika ili atumbukiemo, lakini walileta gari hiyo ya gharama yenye umbo asilolitarajia. Akapakia mizigo na kuliona gari hilo likiondoka taratibu. Akaikariri namba ya gari hiyo ya kifahari SOM kisha ikafuatiwa na maandishi ya kikwao na chini ikamalizia AC528B, akachomoa peni kutoka mfuko wake wa siri na kuiandika pembeni, akaitazama ile gari ikiondoka taratibu na kuacha eneo lile na nyuma yake ikafuatia nyingine iliyokuwa wazi juu na aliona wazi kuwa waliokaa mle ndani walikuwa na bunduki kubwa walizozifutika kwenye miguu yao ila mitutu yake ilionekana wazi. Aliinua simu yake na kubofya namba Fulani kisha akatega sikioni.



    §§§§§



    Kelele ya simu ilimshtua Chiba aliyekuwa bado akifanya kazi ya kumtafuta Amata, akainyakuwa na kuiweka sikioni.

    “Hello!” akaita.

    “TSA 1,” akajibu upande wa pili. Chiba akarukwa na furaha, akamuunganisha Madam S kutoka chumbani kwake.

    “Ndiyo Amata, vipi wewe maswahibu gani yamekukuta huko?” Madam aliuliza kwa sauti ya usingizi.

    “Niko poa, ila gari yangu imelipuliwa vibaya sina usafiri kwa sasa na vifaa vyangu vingi vimeharibika, lakini hilo si tatizo, niko uwanja wa ndege nimemuona mzee Goloko kafika usiku huu, mna taarifa yoyote juu yake?”

    “Yeah, ndio maana tulikuwa tukikutafuta sana kukupa taarifa hiyo kuwa umfuatilie amekuja nkufanya nini huko? Leo TSA 4 alifuatilia nyayo zake na kupata mengi, kwa vyovyote anahusika na hujuma hii, tumeshamkabrasha pamoja na raia mmoja wa Kirusi ambaye yupo kule Mtwala ‘kisimani’ anaitwa Mr.  Reubellen Vinchinsk, naye tunamuangaza pia, tutawapata tu mmoja mmoja, pole kwa matatizo, sasa unasemaje?” Madam S alimweleza kwa kifupi.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nimeng’amua samaki alipo, mayai yake kumi na mbili yamebaki kumi tu, na yai moja nimelinyofoa kiini ninacho, sasa natafuta wadogo zangu nikishajua walipo ndiyo niliamshe rasmi hapa jangwani,” Kamanda aliongea kwa lugha ya mafumbo ambayo walielewa wao wenyewe tu. Walipomaliza, kamanda akakata simu na kuiweka mahala pake, akavua lile gwanda alilovaa na kulikunja vizuri, akampigia rafiki yake Ahab na kumpatia pamoja na hela kidogo. Ahab akashukuru sana na kumwambia Amata kama ana shida yoyote amtafute muda wowote.

    Swala gumu lililofuatia hapo ni jinsi ya kurudi mjini, akili yake ilizunguka sasa akaanzie wapi, mara simu yake nyingine ikaita akaichomoa na kuitazama, lo, ni yule mwanamama wa kiarabu aliyempa lift akaipokea, simu ilitaka kujua ni wapi alipo kwa wakati ule, Kamanda akagwaya.







    “Ni usiku sasa, nikuchukue upumzike nyumbani na kesho utaendelea na shughuli yako,” Kamanda aliisikiliza sauti hiyo akashindwa ajibu nini, aliitafakari mara mbilimbili. Huwezi kujua labda ananiepusha na balaa kubwa zaidi, lakini pi itakuwaje kama ni mtego? Akabanwa na maswali hayo mazwili yasiyo na majibu.

    “Nipo Uwanja wa ndege,” akajibu Kamanda.



    §§§§§§

    Ndani ya jumba kubwa la kifahari, jopo la watu sita liliketi katika meza ndefu iliyokaa kwa umbo la ovali, mbele yao kulikuwa na luninga kubwa iliyoonesha taswira ya mtu, Mr. Lonely.

    “Nawakaribisha sana wageni wangu kwa moyo mkunjufu,” Mr Lonely alikaribisha, sauti yake ilisikika kutoka katika luninga ile kubwa. Na kila mjumbe aliketi sawia kwenye kiti chake, huku vinywaji mbalimbali vikipitishwa na akina dada warembo kabisa waliokuwapo hapo kwa idadi ya wageni, ikiwa na maana kuwa kila mgeni alikuwa na mahudumu wake kwa kila kitu. Baada ya kula na kunywa na kutambulishana, kufahamiana vyema, ilipangwa siku ya pili asubuhi ndipo biashara hiyo ifanyike rasmi. Usiku huo kila mmoja alipewa mahala pa kulala katika jumba hilo kubwa na pweke, wakisubiri siku jua la siku inayofuata ili wakamilishe.

    Asubuhi iliyofuata



    Kila mmoja akiwa ndani ya suti nadhifu, baada ya kupata kifungua kinywa na huduma zingine za kibinaadamu ndani ya jumba hilo la kifahari walikutana tena kwenye sebule ileile na kuketi katika meza ileile kwa mtindo uleule. Kati ya watu hao alikuwepo Bwana Shalabah pamoja na yule bwana mnene asiye na shingo ila kiwiliwili kilichoungana na kichwa tu, alijulikana kama kwa jina moja tu la Hussein.

    “Ndugu wadau natumaini hakuna la kutuchelewesha, leo ni siku tuliyoingoje kwa muda mrefu sana ili kukamilisha zoezi letu la kuuziana zile silaha za maangamizi,” Bwana Hussein akaanzisha mazungumzo. Kila mtu akaitikia kwa kichwa kuashiria ni sawa, kisha akaendelea kusema, “Na ninapenda kumshukuru sana komredi Goloko Mikidadi kwa kazi ngumu ambayo ilitaka hata kuyagharimu maisha yake, lakini Mungu mkubwa leo tuko naye hapa, bila huyu jambo hili lisingefanikiwa kani tangu miaka kumi iliyopita alikuwa akihakikisha mambo yanakwenda na leo msemo wa kwao Tanzania umetimia Mvumilivu hula mbivu,” akajikohoza kidogo kisha akavuta faili lake lililofingwa kwa tepe za dhahabu, “Kama mnavyojua, kazi hii haikua ndogo mpaka hapa tulipoifikisha…”



    Baada ya mazungumzo marefu kati yao, na kukubaliana namna ya kununua silaha hizo za maangamizi, kwanza ikabidi wakaangalie ghalani aina yenyewe ya silaha na wakati huo zilitakiwa kupakiwa na kuondoka katika eneo hilo. Wajumbe waliafiki na kuanza kujipanga kutoka kuelekea huko ziliko.

    Shalabha aliwaongoza mpaka katika mlango Fulani akabonyeza kitufe na mlango ule ukafunguka kisha wote wakaingia na kujifungia ndani. Ilikuwa ni lifti iliyowateremsha chini kabisa kama mita hamsini hivi, ikasimama wote wakatoka na kufuata ujia mrefu mpaka kwenye sehemu kama kijisebule hivi, Shalabah akabonya sehemu na sekunde chache tu kilikuja chombo kama gari kilichokuwa kikipita kwenye mkondo wa maji, kikasimama mbele yao na wote wakaingia na chombo kile kikaondoka.



    §§§§§

    Mwali wa jua la asubuhi ulipenya kati ya vioo vya dirisha lililopendezeshwa kwa mapazia mazuri ya kupendeza, akavuta moja kulisogeza pembeni na kupepesa jicho, anga samawati lisilokuwa na wingu lilimlaki, akainua mkono na kutazama saa yake, ilikuwa ikikimbilia saa tatu asubuhi, lo, nimelala kama mtoto mdogo, alijiwazia na kuamka, akaketi ukingoni mwa kitanda, kilikuwa chumba kikubwa kizuri chenye kila kitu kilionekana wazi hakikutumika kwa muda mrefu, lakini harufu nzuri ya ‘air freshner’ ilikifanya kionekane kizuri maradufu. Kamanda Amata aliingia maliwato kujiweka sawa, hakuwa na nguo za kubadilisha baada ya mizigo yake kuungua pamoja na gari usiku uliotangulia. Lakini ulikuwa ni ukarimu wa ajabu kwani pembeni yake kulikuwa na suti maridadi iliyoning’inizwa, suti mchanganyiko, suruali nyeusi na juu koti la kijivu, shati safi la bluu bahari lililowekwa tai ndefu mpya kabisa ikiwa hata haijafungwa bado. Amejuaje? Akijuliza huku akijifuta maji kwa taulo safi jeupe, mara mlango ukagongwa, akatulia kidogo, ukagongwa tena. Kamanda Amata akajifunga taulo na kuuendea, akaufungua kidogo na kukutana uso kwa uso na yule mama.



    “Habari za asubuhi,” akamsalimu.

    “Salama, umemakaje wewe?” yule mama akauliza.

    “Nimeamka salama, asante kwa ukarimu wako, wewe ni mwanamke wa pekee sana,” Amata alimshukuru. Yule mama alimtazama Amata usoni kwa jicho lililoongea, akarudisha macho yake kifuani mwa kijana huyo, kifua kilichojaa kimazoezi.

    “Pole sana,” akamwambia Amata. Pole hiyo ilimshtua kidogo akamkazia macho na kumtupia swali, “Pole ya nini?”

    Badala ya kujibu, alipitisha kiganja cha mkono wake kwenye ubavu wa Kamnda Amata na kuumgusa kwa mguso laini uliomfanya Amata kutulia kwa nukta kadhaa.

    “Umeumia sana hapa,” alimwambia.

    “Ni kweli nilipata ajali mbaya sana,” Kamanda akajibu huku kiganja cha mkono wake kikiwa kimekifumbata kile cha yule mwanamama bado kikiwa kimeugusa ubavu wa Amata, yule mama akaingia ndani ya chumba kutoka pale mlangoni alipokuwapo, na kuurudisha mlango kwa kuugonga na makalio yake.



    Hakuwa mtu mzima sana, alikuwa wa wastani labda miaka thelathini na mitano au arobaini, alikuwa mfupi kiasi mwenye mwili ulioshiba. Kamanda Amata hakuamini alipomtazama kwa ukaribu, alivaa jeans iliyombana sawia na kufanya shepu yake ilitengenezeka vyema kwa unene ule kuonekana sawia, wakatazamana kwa nukta kadhaa mara pepo likafanya kazi yake, ndimi za wawili hao zikabadilishana mawazo vinywani mwao, wakapapasana hapa na pale na taulo la Kamnda Amata likadondoka chini baada ya kuondolewa kiufundi na mwanamama huyo. Alionekana kuwa na moto wa hali ya juu wa kuibanjua amri ya sita kwa jinsi alivyokuwa akimng’ang’ania mwili wa Amata.

    Kamanda Amata akameza mate pindi alipouona mwili ule mwororo ukiondolewa mavazi ya juu, alikuwa kajitunza, matiti mawili hayakuanguka abadani, yalisimama kama msichana asiyevunja ungo.



    §§§§§

    Fasendy alishindwa kuiamini taarifa aliyopewa usiku uliopita kuwa yumkini Kamnada Amata atakuwa amekufa kwenye ule mlipuko. Alikuwa akiwasikiliza vijana watatu waliokuwa wakiongea wakati wakiwa katika lindo la nje karibu kabisa na bandari ya zamanai ya Mogandishu, wakiongea na kucheka sana huku wakiendelea kula mirungi na kuwa kama mbuzi.

    Fasendy alitikisa kichwa kwa dharau na kuwaona kama watu wasiojua wasemalo kwa kuwa hawakuwa wakimjua Kamanda Amata na mambo yake. Mara redio aliyokuwa ameishika mkononi mwake ikaanza kukoroma kuashirian kuwa kuna mwito utakaoingia muda si mrefu.

    “Sierra 5, Sierra 5,” ile sauti ikaita. Yule kijana mmoja kati ya wale waliokuiwa wakiongea akiinua ile redio na kujibu, “Sierra 1 umesomeka,” alipomalisa aliminya kidubwasha Fulani.

    “Sierra 5 hali usalama ikoje?”

    “Sierra 1 usalama huku upo sawa hakuna tabu yoyote,” akajibu.

    “Sierra 5 hakikisha umakini wako unakuwa makini muda wote, tuna hakika yule shetani anaweza kuibuka muda wowote,” ile sauti ikajibu.

    “Read and clear!”



    Baada ya kuongea na watu wa upande wa pili, yule bwana akamgeukia mwenzake, “Habib, unajua mi simuelewi huyu mwanamke sasa hivi.”

    “Kwa nini?” akahoji Habib

    “Jana asubuhi badala ya kumlenga yule shetani, kafanya off target,” Habib akaeleza. Kisha wote wawili wakageuka kumtazama Fasendy aliyekuwa kasimama mbali na wao akiendelea kuvuta sigara yake, akipanga na kupangua.

    “Oya, mi nawaacha kidogo narudi baadae,” Fasendy aliwaaga wale jamaa wawili kisha akaondoka eneo lile.

    Wale jamaa wakatazamana, “Unaona?” akamuuliza Habib.

    “Si amesema atarudi!” Habib akajibu, yule bwana akainua redio yake na kubofya tufe moja wapo, akaiweka tayari.

    “Sierra Sierra,”

    “Unasikiwa Sierra,” akajibiwa.

    “Sierra 5, lindo limepungua, mwanmke kaondoka,” akatoa taarifa.

    “Sierra 1, ujumbe umefika unafanyiwa kazi,” ile sauti ikamjibu na mawasiliano yakakatika.



    §§§§§CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Fasendy alivuta hatu mpaka barabarni akasimamisha tax iliyokuwa ikikatiza hapo, akingia na kujitupa katika kiti cha nyuma.

    “Jazeera Palace,” alimwambia yule dereva.

    Alipofika akamlipa yule dereva na yeye moja kwa moja akakatisha kwenye maegesho ya magari na kuingia mpaka mapokezi, akamsalimu mwanadada aliyemkuta hapo na kumpa bahasha moja ndogo iliyoandikwa juu jina la mlengwa. Mara hiyo hiyo simu yake ya mkononi ikaanza kufurukuta kwa fujo kutoka katika nguo yake, akaito na kuiweka sikioni.

    “Fasendy, kwa nini umeondoka kwenye point yako na unajua tunaihitaji shabaha yako,” sauti ya Sharon ilisikika.

    “Sijaondoka, nipo katika kutekeleza majukumu yangu kama tulivyokubaliana,” akajibu huku akiwa anatoka katika hoteli ile kurudi barabarani. Akapita kwenye maegesho na kuakatiza kijibustani cha maua marefu mpaka barabarni kwenye maegesho ya tax, akaingia katika noja wapo na kuagiza kurudishwa kule alikotoka. Kichwani mwake gadhabu ilimshika hasa alipopata ile simu kwani alijua kwa vyovyote ni walewale waliotoa taarifa.



    §§§§§

    “Aaaaa usiende Amata,” mwanamke wa Kiarabu alilalama kitandani wakati Kamnda Amata akikiacha kitanda na kuoliendea bafu kwa mara ya pili.

    Akiwa mbele ya kioo kikubwa alijiweka sawa tai yake na kutazama kama koti lile limemkaa sawa au la.

    “Unaenda Kismayu?” yule mwanamama aliuliza.

    “Hapana, naenda mjini kuna kazi ya kufanya,” akajibu.

    “Twende wote,” yule mwanamama akaasisitiza hiloo kwa Amata.

    “No. we baki hapa na watoto, nitarudi, lakini kama hutojali uniazime gari,” akamwambia. Yule mwanamama aliyejulikana kwa jina la Hassna alitoka kitandani na kuliendea bafu, dakika mbili tatu tu akatoka na kujitupi mavazi yake akionesha wazi kutoridhika na jibu la Amata. Akatoka na kumpa ishara ya kumfuata, moja kwa moja mpaka sebuleni.

    “Pata kifuangua kinywa kwanza kisha utaenda,” akamwambia Amata huku dada wa kazi akiandaa hiki na kile. Kamanda Amata akatazama saa yake, ilikuwa inakimbilia saa nne za asubuhi, penzi kitovu cha uzembe alisema Ngoswe, Kamanada akawa akijiwazia.

    Wakiwa ghorofa ya chini, Hassna alimwongoza Amata mpaka banda la uani, “Hii hapa utatumia,” akamwambia huku akivuta tambala kubwa lililojaa vumbi, akalifunua gari lililofichwa katika tambala hilo. Kila mtu alibana pua kwa kuogopa vumbi hilo.

    Gari moja matata, iliyoweka ufito wa alluminium juu ya bonet lake, “Sawa, ina mafuta?” akauliza Amata.



    Yule mwanadada akawa akining’iniza funguo za gari hiyo, akamrushia Kamanda naye akazidaka kwa umahiri, “Mafuta?” akarusha swali kwa yule Hassna.

    “Jamani mafuta si umeshatia au unataka kutia tena?” Hassna aliuliza huku anacheka kwa utani. Kamanda Amata akabana jicho moja na kuzama ndani ya gari hiyo, 504. Akaitekenya kwa funguo ile nayo ikawaka, Kamanda Amata akaitoa ile gari kwa kasi na kuingia barabarani. Nimechelewa sana kuanza kazi, alijisemea huku kauma meno, akikunja kona moja baada ya nyingine, akaegesha gari hiyo mbele ya benki moja kubwa mara tu alipoona ibao cha ATM. Akashuka na kuilekea mashine hiyo, akatoa kiasi cha pesa anachokihitaji na kurudi ndani ya gari. Kwanza nahitaji silaha, aliongea na nafsi yake huku akiingia barabarani.

    MOQDISHU ARM MARKET ni maandishi yaliyokuwa yakisomeka juu ya mlango mkubwa wa duka hilo, halikuwa na watu wengi bali ni wachache sana, zaidi zaidi palionekana pamefungwa muda wote.

    “Tukusaidie nini?” akauliza mlinzi mlangoni.

    “Nahitaji huduma,”nakajibu Kamanda.

    Yule mlinzi akamchukua na kumuingiza ndani ya duka hilo kubwa, ndani yake hamkuwa na bidhaa nyingine zaidi ya silaha za kila aina. Kamanda Amata alifikishwa kaunta na kuonana na mhusika.

    “Ee nahitaji bastola mbili zenye nguvu na risasi zake,” kamanda aliagiza.



    “Ok, bahati mbaya zile zenye nguvu kabisa zimekwisha nab ado hatujapata mzigo, ila nitapendekeza kwako, Smith and Wesson double barell na Nagnum 22 au ukipenda kuna hii Revovler,” mzee wa makamo alimwambia Amata naye akaitika kwa kichwa. Dakika kadhaa tu.zile zana zilikuwa tayari mezani, “Huu hapa mzigo kaka,” yule babu alimgutusha Kamanda aliyezama katika mawazo, akachukua Magnum 22 na kuijaribu kidogo kwa kuitekenya hapa na pale, alipojiridhisha akaiweka mezani, kisha akajaribu na nyingine zote.

    Alipohakikisha zinamfaa, akazilipia na kuchukua risasi za kutosha.

    “Sasa kijana kuna utaratibu wa kiserikali wa kumiliki silaha huwezi kununua kama machungwa,” yule babu akawa mkali kidogo, alipoinua macho akakutana na macho makali yasiyo na masihara, macho ya mpiganaji, Amata Ric au Kamanda Amata.

    “Sikujua kama hata Somalia mnahitaji vibali kumiliki silaha,” Kamanda Amata alimwambia, akatoa noti ya dola hamsini na kumuwekea mezani, “ Nenda ukanijazie fomu zote, mi sina muda,” yule mzee akakenua kwa fuaraha, chezea noti wewe. Kamanda akarudi katika gari yake.







    JAZEERA PALACE



    Peugeot 504 iliingia maegeshoni taratibu na kuwekwa mahala salama. Kamanda Amata akashuka akiwa na balaghashia kichwani na moja kwa moja akaenda kaunta ya hoteli hiyo.

    “Oh, karibu, umenishtua sana,” alisema mhudumu wa mapokezi huku akimpa kijibahasha kidogo, na wakati huohuo akampa ishara ya kuzunguka upande wa pili, Kamanda Amata alifanya hivyo, akamfuata yule mhudumu wa kike katika kiujia kilichotenganisha ofisi mbalimbali.

    “Jaffer, nakwambia hili kwa kuwa nakupenda,” yule mhudumu alianza namna hiyo na Amata akahisi kama hajasikia vizuri, akamkazia macho, “Unatafutwa na polisi kwa kuwa wana mashaka na wewe kwa nini chumba chako kinatokea mauaji mara kwa mara, nakuomba uondoke hapa haraka usirudi,” yuele mhudumu alikuwa akiongea huku akitazama huku na huku kama anayehofia jambo Fulani, akaingiza mkono katika nguo yake na kutoa kadi ya kibiashara akampatia, “Kama unataka kujua lolote nipigie.”

    Kamanda Amata akaitazama ile kadi, “Ok, nitahitaji maelezo juu ya chochote kinachoendelea sawa? Nitakuta baadaye.”



    “Haya, nenda, pita huku nyuma haraka,” mhudumu akamwonesha njia Amata na ye akaifuata. Akazunguka nyuma ya jengo la hotel hiyo na kuruka uzio mdogo wa michongoma kisha akatokea katika maegesho ya magari, akatazama usalama huku na kule kama kuna anayemhofia, usalama ulikuwepo, akavuta hatua na kuingia katika ile gari, akatoka taratibu eneo hilo na kuchukua barabara kuu inayoelekea nje ya mji lakini inapita mbele ya bandari ya Mogadishu ikianzi ile mpya na kumalizia ile ya zamani. Akiwa anakaribia kuiacha ile barabara kuu ili kuchuku barabara ndogo, alikuta kuna foleni kubwa, hakujua mbele kuna nini, hakuona haja ya kupoteza muda kwani alijua wazi jinsi anavyowindwa, akaigeuza gari na kurudi alikotoka, mara akasikia ving’ora vya polisi nyuma yake, “Polisi, weka gari pembeni,” akaamriwa.

    “Shiiit,” akang’aka na kupiga ngumi usukani huku akiitoa ile gari na kuiweka sehemu salama nje ya barabara. Afisa wa polisi akasogea mpaka pale dirishani, akamwamurtu kuteremka.

    “Lete vitambulisho!”

    Kamanda Amata akawapa hati ya kusaifiria ya serikali ya Congo iliyomtambulisha kwa jina la Zubi Mathuren.

    “We ni raia wa Congo?” akaulizwa lakini hakujibu, “Mpekue!”

    Askari mmoja alimpekua na kumkuta akiwa na bastola hizo tatu mwilini mwake, “Nyie ndiyo tunaowatafuta, mnatoka kwenu mnakuja kupoteza amanai hapa halafu jumuia ya Kimataifa inasema Somalia hakuna amani, tia pingu huyo,” yule afisa wa polisi akatoa amri.



    Kamanda Amata akatiwa pingu, kisha gari yake ikapekuliwa na walipofungua buti la gari hiyo, wale polisi wakabaki midomo wazi, hawakuamini wanachokiona.

    “Nini hiki kwenye buti?” yule afisa aliyekuwa akipekua aliuliza. Kamanda Amata alibaki kumtazama kwa kuwa alikuwa hajui ni nini ,kipo ndani yake. Yule polisi mwingine akamshika kwenye kiwiko na kumvuta upande wa nyuma wa gari hiyo. Hakuamini anachokiona, mwili wa binadamu ulikuwa ndani ya buti la gari, ukivuja damu mbichi. Kamanda Amata akautazama mwili ule kwa makini moyo wake ukapiga tik – tak, Hassna, mwanamke aliyelala nyumbani kwake, na kufanya naye mapenzi asubuhi tu ya siku hiyo, aliyempa gari hiyo atumie. Amewekwa saa ngapi humu na mi nilimuacha nyumbani? Akili ya Kamanda Amata ilifanya kazi haraka haraka, akamuinamia yule marehemu, kwa mikono yake iliyofungwa pingu mbele akakamata nguo ya Hassna, akamuinua, chozi likamdondoka. Amewakosea nini mwanamke huyu, mbina watu ni wakatili hivi?. Kamanda Amata akaurudisha chini ule mwili wa Hassna na kuulaza tena katika buti lile.

    “Wewe ni muuaji, jamb…!” aliongea kwa kelele yule askari, kabla hajamaliza kusema hayo, taa ya kimulimuli kwenye gari ya polisi ilitawanyika vipande vipande, kioo cha mbele cha gari ya Kamanda kikamwagika na kuwa kama chumvi barabarani, jicho la Amata lilishuhudi land cruiser pick up juu yake ikiwa na watu kama watano wenye silaha.



    “Ambusssshhhhh!!!!” polisi mwingine alipiga kelele wakati huohu Kamnda Amata alijitupa chini na kumshuhudia yule polisi aliyepiga kelele kutoka nyuma yake akipaishwa juu na kutupwa kando akiwa marehemu. Amata alijibiringisha uvungu wa gari na kutokea upande wa pili, pingu alizovalishwa zilimnyima uhuru wa kufanya makeke yake. Hali ya pale mahala ikavurugika, kelele la marushiano ya risasi na harufu ya baruti zilitawala. Kutoka uvungu wa gari ile aliona tairi za ile land cruiser zikisugua lami na kufanya kelele nyingi, alitazama hapa na pale hakuna pa kutorokea. Akajua wqazi kuwa akijitokeza tu atakuwa chakula cha risasi hizo zenye hasira. Kando mwa barabara, kulikuwa na mtaro mkubwa sana uliounganishwa na bomba kubwa la maji machafu linaloelekea baharini, akazungusha akili haraka haraka akajibiringisha kwa haraka na kujidondosha mtaroni, kutokana na wingi wa maji yanayopita katika mtaro huo, nay eye hali kafungwa mikono, hakuweza kupingana nayo yalimbeba.

    Wale jamaa walishuka kwenye gari yao na silaha kali mkononi, wakiwa wamekwisha wacharaza askari wote risasi na wote kuwa marehemu.



    “Katoroka?” mmoja aliuliza.

    “Yule sio binadamu asee, alikuwa hapa chini ya gari,” mwingine alijibu huku akiwa ameshika silaha yake ikiangalia juu kwa usalama zaidi.

    “Tawanyika mumtafute!” yule kiongozi alitoa amri; wale jamaa waliotafuna mirungi walizagaa kama vichaa wakipiga makelele ya kuonesha munkari wa hali ya juu, “Angalieni kwenye mtaro,” alitoa amri nyingine na wawili kati yao walijitosa kwenye mtaro kumsaka Amata.

    Mkondo wa maji ulikuwa ni wa kasi sana ndani ya bomba kubwa la maji machafu, harufu mbaya ilitawala ndani humo, Kamanda Amata aliwaona wale watu waliokuwa wakija kumtafuta wakiwa na silaha mikononi mwao, Amata alijificha kwenye maungio ya bomba akajibana akisubiri.

    “Songa mbele!” ilikuwa sauti ya yule wa nyuma ikimuamuru wa mbele, huku wakipiga risasi ili mradi walikuwa wamerukwa akili. Mmoja alipofika pale kwenye maungio tu, Kamanda Amata alimkamata kwa mikono yake miwili na kumvuta kwake, akampa ndosi moja matata yule bwana akapepesuka na nguvu ya yale maji ikaanza kumshinda, Amata alimpachika mikono yake shingoni na kumbana kabala ya nguvu mpaka alipohakikisha yule bwana kalegea akamuachia akajibwaga chini.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Yuko hukuuuuu!” yule wa pili akapiga kelele baada ya kuona mwili wa mwenzake ukijibwaga majini na kubebwa na maji hayo. Mara Amata akasikile ukelele wa maumivu alipotokeza kichwa kuangalia kulikoni alimshuhudia yule jamaa akijibamiza katika moja ya kingo za bomba lile ambalo liliungana na mtaro mkubwa, akajibwaga na kutulia. Akiwa katika kutaharuki nani aliyefanya shambulizi hilo, akashikwa mkono na kuvutwa upande wa pili, akikimbizwa kupita ndani ya maji mpaka eneo Fulani. Yule mtu akamuachia na kunyanyua mikono yake akafungua mfuniko mkubwa wa chuma kwa mikono yake, mwanga wa jua ukaingia ndani ya bomba hilo yule mtu akapanda kwa ufundi wa ajabu sana kiasi kwamba Kamanda Amata alijua wazi kuwa kama mtu huyo si mwanajeshi basi ni mtu aliyepitia jeshi, yule mtu aliyekuwa kava sox mpaka usoni na kuonekana macho tu alimpa ishara Kamanda Amata kupita pale kwenye tundu; naye bila kusita akajirusha kwa namna ileile na kupenya wote wakatokea juu ya bomba lile, yule mtu akalivuta lile funiko na kulirudisha mahala pake kisha akaanza kutimua mbio na Kamanda Amata akiwa anamfuata. Walikuwa mbani na ile barabara, walikimbia kufuata fukwe ya bahari iliyopo eneo hilo kwa mwendo kama wa dakika tano, kisha yule mtu akasimama, akaingiza mkono mfukoni na kutoa kitu kama funguo ndogo akaipachua ile pingu nayo ikafunguka, akaitupa mbali na kuendelea na safari na Kamnda Amata bila kuongea, walipita katika majumba jirani na eneo hilo. Na mbele ya eneo hilo walisimama, yule mtu akatoka ile sox yake usoni, Kamanda Amata hakuamini anyemuona mbele yake.

    “Umeokoa maisha yangu?” akamwuliza kwa mshangao mkuu.



    §§§§§§

    KATIKA ghala kubwa lililojengwa chini ya maji, wale wafanya biashara waliokuja kufanya biashara ile haramu waliketi kwenye moja meza kubwa kwa mtindo wa nusu duara, wakiwa wamefungua mnakabrasha Fulani mezani hapo, pembeni yao kulikuwa na vijana wasiocheka, walioweka ‘uso wa mbuzi’ waliojazia kimazoezi, mmoja upande huu na mwingine upande ule, wakifuatilia kila hatua ya mazungumzo ya wanene hao.

    Ilionekana kuna kitu kama kutokukubaliana katika biashara hiyo, kwani ubishani kati ya watu wale ulikuwa mkubwa sana.

    Yule mtu mnenen ambaye alikuwa na Shalabah wakifanya mazungumzo hayo kwa niaba ya Mr. Lonely aliinuka na kuelekea ukutani, kisha ile meza ikazunguka na kumtazama yeye, pale ukutani likashuka pande la kitambaa na mara nuru kutoka kwenye chombo maalumu ikang’aza kitambaa kile.

    “Wote tutazame hapa,” alisema yule mtu huku akiwa ameshika kijifimbo kirefu akinyooshea kule kwenye ule mwanga, “Hii ndiyo aina ya makombora yaliyopo kama mlivyoomba, nawahakikishieni mtaadabisha ile serikali mnayotaka kuiangusha na washirika wake wote, makombora haya yanaitwa R-36 au unaweza kuyaita kitaalamu Intercontinental Ballistic Missile (ICBM) wengine huliita Shetani, ni kombora ambalo liligunduliwa na watu wa Russia miaka ya nyuma lakini likarekebishwa na kuongezwa madoido na nguvu na wanasayansi wa kijeshi kutoka Tanzania kule Mtwara na kuliweka tena kombola hili kama silaha tishio au silaha ya maangamizi.



    Lina urefu wa mita 32.2 yaani ni sawa na futi 106,  kipenyo chake ni mita 3.5 au futi 10. Limeiwa pia Shetani kwa sababu lina uwezo wa kwenda kasi ya mita 7.9 na mlipuko wake linapofika lilipokusudiwa ni mkubwa na wa kutisha,” kisha akawaonesha jinsi lilivyoundwa na, akawaonesha na mfano wa mlipuo wake kwa kutumia video ya kutengenezwa kwa kompyuta, ukumbi wote ulibaki kimya wakati kile kitambaa kikirudi juu mahala kilipotoka. Kila mtu alishusha pumzi ndefu na kujiweka sawia kitini kwake. Hakuna aliyekuwa na shaka katika hilo.

    Yule bwana naye akarudika katika siti yake na mazungumzoy akirndelea, mwisho waliafikiana jinsi ya kusafirisha kwa ujumla.

    “Sawa?” akauliza yule mtu.

    “Sawa”

    Haya anza kuhamisha pesa. Mmoja kati ya wale wageni aliyeonekana kuwa ndyiye mkubwa wa lile jopo lote akachukua kompyuta na kuwasha kisha akaingiza vijinamba Fulani na kusubiri, ilipofunguka akaunganisha na mtandao moja huko Ulaya wa benki na kushuhudia muamala unafanyika katika nia ya kielektroniki kutuma mabilioni ya pesa katika namba za akauti kama ilivyoelekezwa.

    Bwana Goloko Mikidadi alikuwa ameketi kwa utulivu juu ya kiti chake, mawazo yalikuwa yamegubika akili yake, alitazama kwa makini malekezo yaliyotolewa na yule bwana pale katika kile kitambaa na hapo ndipo alipogundua ni nini alikuwa amefanya na wenzi wake, mauaji ya kikatili, mauaji yasiyo na huruma kwa kila aliye karibu ama ana hatia au hana, silaha haina macho.



    Aliwatazama wenzake wote waliokuwa katika kikao na kuwaona jinsi nyuso zao zilivyo na furaha lakini ni yeye tu aliyeonekana hana furaha. Alitamani ajitoe katika biashara hiyo lakini alijikuta hawezi kwani yeye ndiye kinara na alichofuata hapa ni mgao wake na washirika wake wengine walio Tanzania ambao walikuwa wakisubiri kwa hamu wauage umasikini kwa biashara hiyo. Nafsi yake ilimsuta, roho yake ikamzomea, akakosa amani.

    “Kijana, naweza kuonana na Mr. Lonely?” alimuuliza Shalabah.

    “Mr. Lonely!” akatulia kidogo, “Ni mtu ambaye huwezi kumuona kwa macho, na ukimuona, hakika utakufa,” Shalabah akajibu kwa nyodo.

    “Nahitaji kumuona,” alisisitiza Bwana Goloko.

    “Mzee, huwezi kumuona, kama una ujumbe nipe nitamfikishia,” Shalabah akajibu. Ulikuwa ni mvutano mkubwa kati ya Shalabah na Goloko katika swala la kumuona Mr. Lonely. Bwana Goloko alikuwa ameamua kumuona Mr Lonely kwa minajiri ya kujitoa katika biashara hiyo aliyoiona kwa wakai ule kuwa ni haramu, akiwa amesahau tangu huko walikotoka wakiwa wanatengeneza zengwe la kuitia mkononi ile hela chafu kutoka katika mikono ya vikundi vya waasi huko Pakistani, Khazakistani na Huzbekhstani. Mr. Lonely ambaye daima alikuwa akifadhili na kuwauzia silaha kalikali waasi karibu wengi duniani, sasa alimua kufanya kufuru hiyo kwa kuwauzia makombora hayo hatari kabisa yenye uzito mkubwa katika malipuzi. Ilikuwa ni pesa ndefu ambayo ingeyajaza mabenki ya wenye uchu hao kupita kawaida. Kwao methali isemayo subira huvuta heri ilichukua maana yake halisi, walionyongwa wangekula watoto wao, waliofungwa wangezikuta wakitoka, waliopon uraiani kama akina Goloko wangeszifaidi kwa nafasi yao, kwa kula kuku kwa mrija.







    §§§§§

    “Rafiki yangu Bwana Goloko, tumekuwa tukiwasiliana sana kwa njia ya wajumbe tu, miaka mingi sana sasa, leo tumeonana uso kwa uso, una bahati ya pekee kati ya viumbe vya ulimwengu,” Mr Lonely aliongea kwa tuo, aliongea kwa madaha sana. Bwana Goloko alikuwa akitumbua macho tu alipojikuta amekal;ia kiti chenye kingo za ndhahabu, alikanyaga sakafu ya kioo ambayo chini yake aliweza kuona viumbe vya baharini vikitalii na kuvinjari.

    “Mr. Lonely, kweli kabisa nimeona nilichofanya si sahihi, nilikuwa na ombi moja tu kwako, kunitoa katika mchakato huu, katika orodha ya wale washirika wako wa kibiashara, sihitaji pesa zako,” Goloko alisema.



    “Goloko Mikidadi, umekuwa  swahiba wangu wa kalamu kwaa muda mrefu sana, ukaongea na mjumbe wangu ukijua ni mimi kwa miaka yote, nikakupa pesa nyingi ili ufanikishe wewe na wenzako kuhujumu nchi yenu na kunipa siri hii nzito, sasa tumemaliza, nukta ya mwisho unasema hutaki kuwepo? Magari ya kifahari, watoto wako wanasoma Ulaya, jumba la ghorofa, hoteli kubwa unayomiliki, je utanirudishia vyote hiyo na we urudi kwenu Mafia, kisiwani ukavue samaki kwa ngalawa ya miti? Kumbuka huna nyumba wewe, nilikukuta katika nyumba ya serikali, nyumba ya Nyerere, lakini sasa upo kwenye ghorofa kubwa unadai unataka kujitoa, hainiiingii akilini ukizingatia tayari tumefika mwisho,” Mr Lonely aliongea kwa utaratibu sana. Bwana Goloko alijikuta akikumbuka kweli hakuwahi kujenga hata nyumba katika utumishi wake wa umma katika serikali ya awamu ya kwanza, alipokuwa katika mchakato wa kuhujumu taifa lake, utajiri wake ulikuwa ukiongezeka kwan kasi pasina kujua ni ni wapi ilikuwa ikitoka, kazin yake ilikuwa ni kutoa siri tu na mipango kwa mtu asiye mjua, kusaini mikataba na makabrasha yaliyo na tija kwake na wenzake. Alijikuta hana jibu, hana la kufanya. Utajiri ule wote auche arudi kwao Kilindoni kuvua samaki.



    “Nimeamua,” aliropoka.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ok, nimekuelewa, sasa wewe nenda na mi nitakutoa kwenye orodha yangu, sipendi watu vigeugeu, lakini shukrani yangu kwako ni hii,” akaita kwa ishara ya mkono wake, mwanadada mrembo kama malaika aliingia katika kasri ile pweke akiwa na kijibegi kidogo mikononi mwake, akampa Goloko.

    “Safari njema sana, wasalimie uendako, hakikisha humwambii mtu yeyote juu yah ii biashara, sawa?” Mr Lonely akampa onyo. Goloko akaondoka kwenye lile kasri la ajabu, akaingizwa kwenye chombo maalumu cha kumtoa mle ndani. Alipofungiwa milango alitabasamu, akafungua kile kibegi, kulikuwa na pesa maburungutu kadhaa, akaona hayo yangemtosha na si yale ya udhalimu.

    “Hakuna mtu aliye muaminifu duniani,” Mr. Lonely akasema kwa sauti ya chini na kubofya kitufe Fulani kwenye meza yake. Vyuma vikali vikachomoka kwenye kila chombo alichopanda Goloko, vilikuwa vyuma kama kumi hivi vikamchoma huku na huku, mbele na nyuma, hakukuna na muda wa kupiga kelele wala muda was ala ya mwisho, alibaki kutumbua macho tu, roho ikamwacha kwa taabu.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog