Simulizi : Shujaa Wa Taifa
Sehemu Ya Pili (2)
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alichukua taxi na baada tu ya kumuelekeza dereva wa taxi huyo kuwa anaelekea kwa waziri wa mambo ya ndani yaani nyumbani kwake na si ofisini kwake basi hakuitajia kutoa maelezo mengine Zaidi ya kupelekwa.
“dada mbona usiku waziri atakupokea kweli maana ana walinzi hata rais hana” dereva wa taxi hiyo alichombeza wakiwa wanaendelea na safari.
Zarish akacheka kabla ya kujibu, “ hao walinzi watu maarufu kama sisi hawatujui kwani mpaka washindwe kuniruhusu”
“aah kweli hata mimi naona maana yule jamaa mi namuogopa kweli huwa yupo serious kweli kweli , hata kuzoeleka sijui kama anazoeleka , sasa nashangaa na wewe umemzoea hivi aaah tuambiane umemzoeaje au ndo uchawi wa babu unafanya kazi” dereva wa taxi huyo akatania na kumfanya Zarish acheke kwa nguvu.
“hamna bwana mbona yupo poa sana yule jamaa, sema tu wazambe hamumjui tu ipo siku mtamjua na mtakuwa mmeshachelewa, tumempata waziri mwenye akili sana tujivunie kwa hilo kwakweli” Zarish akaongea huku akiendeleza tabasamu lake lililomzidisha sifa ya urembo.
“mmmh mmmmh sidhani kama kila mtu anamtamani, jamaa watu wengi wana mchukia yaani anaingilia majukumu hadi ya wizara za wenzake ndo anachokera”
Baada ya kauli hiyo kutoka katika kinywa cha dereva huyo wa taxi kicheko tu ndicho kilichokuwa kikitawala kwa mwanadada Zarish
“sasa huo ndio uchapakazi ambao rais Stanford amesisitizia kwenye sera zake kwahiyo mwache afanye kazi pale wenzake wanapojisahau” Zarish akaongea
“mmmh sasa ndio awawajibishe watu ambao hana mamlaka nao?”
“aaah bwana eeee tuachane nazo hizo zingine siasa tu”
“na kweli ngoja niachane nayo nisije nikaletewa noah nyeusi bure” dereva wa taxi aliongea kwa utani na kumfanya Zarish acheke kicheko kikubwa huku akijiziba mdomo wake.
Basi safari ilizidi kuendelea na mijadala ya hapa na pale ikiendelea hadi pale walipofika nje ya nyumba ya nyumba ya muheshimiwa huyo.
Gari ikapaki nje ya jengo hilo na Zarish akashuka baada ya kumlipa dereva taxi huyo.
Dereva akageuza na kuondoka.
Zarish alianza hatua za taratibu kuelekea lango kuu la mlango huo.
Mara
“stop tulia hivyo hivyo!” ilisikika sauti ya askari kutokea nyuma ya Zarish.
Zarish akasimama huku akitetemeka.
Askari huyo aliyevalia sare ya kazi akamsogelea.
“mikono juu”
Zarish akatii!
Askari huyo akaanza kumpekua Zarish. Alipohakikisha hana kitu akaanza kumuhoji maswali, “enheee una shida gani usiku huu kwa muheshimiwa?”
“ameniita muheshimiwa!” Zarish akaongea akitetemeka.
“unaitwa nani?”
“Zarish”
“anhaaa ndo wewe”
Neno hilo lilimuondoa hofu ambayo awali ilipotea kila alipoitazama silaha ya moto ya askari huyo.
“aya twende!” askari huyo akaongea huku akimwelekezea ndani Zarish. Wakaingia getini wote na kumnkabidhisha kwa walinzi wa ndani ambao ni wa kike.
Hakika waziri huyo alikuwa na ulinzi kamilifu maana kila kona kulikuwa na walinzi wa aina mbali mbali, yaani nyumba hiyo ililindwa utasema ni ikulu vile.
Alikaribishwa ndani na kukaa sebuleni ambapo aliambiwa mheshimiwa hayupo kwahiyo amsubiri.
Alipoangalia saa aligundua ni saa mbili usiku hivyo hakuwa na haraka sana ya kuondoka kutokana na muda haukuwa umeenda sana, na kwanini awe na hofu ya muda wakati yupo sehemu yenye ulinzi usio na shaka? Akabaki akimsubiri!
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alberto banguli baada ya msafara wake wa magari lukuki kuelekea ofisi ya rais hatimaye wakafika.
Waliposhuka kwenye magari yao kuingia ndani ya jengo hilo la ikulu, saluti tu peke yake ndizo zilizokuwa zikiwalaki kuelekezewa waziri banguli.
Safari iliwapeleka moja kwa moja hadi katika chumba apatiwacho huduma za kitabibu mhe. Dkt Stanford,rais.
Walinzi wake anawaamuru wabaki nje, na kuingia mwenyewe.
Anamkuta rais akiwa amelala huku akionesha hali yake si nzuri.
Akamsogelea!
Akaachia tabasamu la kikatili!
“mr Stanford ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha haaa” banguli aliongea na kujichekesha kikebehi.
Rais akabaki akimtazama tu kwa huzuni.
“nilikuambia mimi ndiye rais wa n chi hii kwanini lakini unakuwa sio mwelewa?” banguli akaongea kiupole huku akimtazama rais.
“kama unataka mema ya nchi hii inabidi utilize kihere here, kwahiyo unataka useme wewe ndo mwenye huruma sana nah ii nchi kushinda watu wote? Sasa nakupa last warning usipofanya yale nayotaka na kukubaliana nayo kwa asilimia zote itakuwa ndio mwisho wa wewe kuishi zambe, vinginevyo chumba chenye giza kitakuwa ndio makazi yako ambapo hakuna yeyeote atakayejua kuwa upo huko”
Banguli alitoa onyo lililompa wasiwasi rais aliyepo kitandani akiwa amelala.
Mhe. Dkt Stanford akabaki ameduwaa huku akijilaumu kwanini alimwamini kijana huyo na kumpa kila kitu n ahata pale taifa zima lilipogundua mabaya yake yeye aliendelea kumkingia kifua, inamaana hayo ndio malipo ya hayo yote? Swali hilo lilipita kichwani mwa rais lakini hakukuwa na jibu la wazi Zaidi tu ya kudondosha machozi, machozi ya mtu mzima kwa mtoto ni kama vile baba alie mbele ya mtoto, ni kweli laana itapingika?
‘masikini wananchi wangu wa zambe mnisamehe sana sina tena chaguzi, sikujua kuwa huyu mtu atakuwa nyoka kuliko ndongoro yule nyoka mwenye sumu kali’ alijisemea kimoyoni rais huku akimtazama banguli ambaye muda huo alikuwa akitamba tu.
“kwahiyo ndio hivyo mzee kama bado unatamani Maisha naomba kihere here chako kiishe wewe utabaki kuwa kibaraka tu utafanya kazi vile ntakavyotaka, full stop” banguli aliongea kauli za majigambo huku akigeuka na kutaka kuondoka.
“alberto!” rais akaita kwa tabu sana
Alberto banguli akageuka!
“unasemaje mzee rais aliyejiudhuru?” banguli akaongea huku akimtazama rais kwa kiburi.
“kumbuka siku zote hakuna mwanzo lililokosa mwisho, kumbuka ubaya ulipwa kwa ubaya. Mateso yote ya wana zambe wewe ndo chanzo na mungu anakuona, ipo siku isiyo na jina utakuja kulipia. Yupo wapi mfalme farao aliyekuwa kiburi na mwenye nguvu eee, yupo wapi mabutu seseko ee, sasa badilika kwani nani atakayekusema ukiwa unakula vya wananchi lakini unawatendea haki ee” rais aliongea kwa masikitiko makubwa.
Banguli akaanza kucheka kwa dharau.
Baada ya kicheko hiko akaanza kuongea,”nilikuwa sijui jinsi ya kuiba mali za wananchi ukanifundisha, nilikuwa ni kiongozi mwadilifu ukanifundisha nifanye mambo yasiyo na uadilifu ili tu kutimiza mahitaji yako binafsi, sasa leo nimekomaa siogopi lolot endo unanipa mifano ya watu waliokuwa wakitumia nguvu kuliko akili? Kweli mimi wa kunifananisha na mabutu au farao? Nadhani uwezo wangu katika kutoa maamuzi upo juu kuliko yeyote katika nchi hii, sasa ni nani atakayekuja kunipindua? Jibu hakuna ha ha ha ha ha ha haaaaa” banguli aliongea na kumalizia kicheko cha kidharau.
Akageuka na kuanza safari ya kuondoka lakini alipofika mlangoni akageuka nyuma na kuongea,” sikia mambo niliyokueleza ni kuzingatia sana kama bado uhai wako una thamani, nadhani unafahamu vizuri uwezo wangu hasa linapokuja swala la kuua, maana mipango yako yote ya mauaji mimi ndio mratibu wako, sasa kama na hilo bado unakumbuka kuwa makini sana na lolote utalotaka kufanya au kuongea pasipo kunishirikisha mimi, shubamiiiiiiiiit!!!” akamaliza maongezi hayo na kuondoka.
Rais akabaki ametaharuki huku shuka lote alojifunika likiwa limelowa jasho.
Banguli akachukua msafara wake na kurudi zao nyumbani kwake.
Msafara ule uliishia katika nyumba yake waziri banguli. Na alipofika tu alipokelewa na wafanyakazi walio mpokea kwa kumbeba na kumpeleka sebuleni kama alivyowapangia kila afikapo nyumbani kwake.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakamvua viatu na kumuacha sebuleni pale ambapo baada ya kuangaza macho yake pembeni akakutana na mrembo Zarish aliyechoka kwa usingizi.
“oooh mrembo kumbe umetii amri yangu!” banguli akaongea huku akitabasamu. Yaani nje ya shughuli ya ugaidi unaweza sema banguli ni moja ya viongozi anayesikiliza sana raia wake na mwenye huruma na upendo, kumbe vyote hivyo vilibaki kama kava la movie za ngono ambapo linanogeshwa kwa picha ambayo haiendani na kusudi la muvi hiyo.
“ndio mkuu!” Zarish akaongea huku akijaribu kulazimisha usingizi uondoke usoni mwake.
Banguli mbali na waziri ni mume mwenye mke mmoja lakini kutokana na matatizo ya mkewe ya kusumbuliwa na tumbo kwa muda mrefu hivyo amemsafirisha na kumpeleka india kwa ajili ya matibabu akiwa pamoja na mama yake mzazi ambaye ndiye msaada mkubwa wa mke huyo nchini india kwa tatizo lolote kama ndugu. Pamoja na udikteta na ujahili alio nao banguli lakini alimpenda mno mkewe na hakutaka mke huyo apate tatizo lolote.
Hivyo ndani humo alibaki yeye na wafanyakazi tu, kwani hawakubahatika kupata mtoto.
“twende chumbani” banguli akaongea.
Zarish akashtuka kidogo lakini hakutaka kuonesha hofu hiyo wazi wazi.
Wakaanza safari ya kuelekea chumbani huko huku banguli akiwa ameushika mkono mmoja wa Zarish na kumuongozea chumbani kwake.
Baada ya kona za hapa na pale kuzipita kordo kadhaa wakaingia ndani ya chumba cha banguli.
Zarish akaanza kupepesa macho kuangalia huku na kule ndani ya chumba hicho, hakuamini kama kuna siku moja angeweza kuingia ndani ya chumba cha waziri hata kwa kufagia tu.
Chumba hicho kilipambwa vizuri ambapo mapazia mbali mbali yenye rangi za kupendeza yalizunguka pembezoni mwa chumba hicho na kufanya kutenganisha sehemu ya maliwato pamoja na kitanda.
Kitanda chenyewe hakikuwa cha mchezo, si unajua vile vitanda vyenye maji chini, basi ndio kilikuwa chumbani kwa waziri huyo. Ushafikiria kuhusu bei yake? Ni kubwa mno, ila kwake ilikuwa ni pesa ndogo sana kwakuwa kodi za wananchi zilikuwa zikikusanywa ipasavyo kwa vyanzo mbalimbali. Sasa kwa nini asinunue kitanda cha hivyo ili hali pesa zipo.
Zarish akabaki ameshangaa akisubiri amri ya kufanya lolote kutoka kwa mkuu wake huyo wa n chi.
“karibu mrembo” sauti kavu kutoka katika kinywa cha mr alberto banguli ndiyo pekee iliyomshtua mwanadada huyo aliyekuwa katika mduwao baada ya kuona mazingira ya chumba hicho.
Banguli aliongea hayo huku akichojoa shati lake na kubaki tumbo wazi, baadae ikafuata suruali ambapo alibaki na bukta laini.
“asante” Zarish akaitikia huku akionesha wasiwasi mkubwa.
Banguli akaelekea kitandani na kuketi huku akiegemea mto na kufanya kukaa sawasawa.
Muda huo huo kupitia rimoti ya radio aliyoishika banguli mkononi mwake akabofya vitufe kadhaa na hatimaye mziki laini ukaanza kuchombeza ndani humo.
Kisha akampa ishara Zarish aanze kazi.
Taratibu mwanadada huyo akaanza kujishika shika sehemu zake za mwili huku akijibiringita kama vile nyoka aliyemwagiwa mafuta ya taa, hiyo ndio ilikuwa staili ya mwanadada huyo aanzapo kucheza.
Mara akaanza kukiviringita kiuno chake kuendana na ala za mziki huo uliokuwa ukichombeza.
Mr banguli akabaki ameduwaa akimtazama mwanadada huyo kwa uchu.
Zarish akawa anazipunguza nguo zake kadri mziki huo ulivyokuwa ukizidi kukolea kama vile afanyavyo awapo stejini katika bar ya kismart. Yaani linapokuja swala la kucheza Zarish huwa hajivungi wala kuona aibu, anajiacha kweli kweli.
Kadri mziki huo ulivyokuwa ukizidi kukolea ndipo na Zarish nguo zake zilizidi kupungua na hatimaye kubaki na nguo ya ndani ambayo iliunganishwa kutokea kwenye matiti hadi kwenye maungo yake ya siri kwa maana rahisi lilikuwa ni vazi watumialo wasanii wakike wawapo stejini ili kujizuia kuanika sehemu zao za ughaibuni. Hapo ndipo wepesi wa Zarish ukajidhihirisha, alijiachia kwa kucheza huku akipambwa na tabasamu na kwa uchokozi alikuwa akijipitisha karibu na waziri huyo yaani alijipandisha kitandani kabisa.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Banguli alionesha kuinjoi wazi wazi kwani muda wote alijengwa na tabasamu pana huku na yeye akiitumbuiza mikono yake kushika sehemu mbalimbali za mwanadada huyo hasa hasa kiuno pale anapopata nafasi hiyo.
Uvumilivu ukamshinda waziri huyo pale alipogeuziwa makalio yaliyokuwa yakichezeshwa ya mwanadada Zarish huku akiwa katika staili ya kuinama, kwa lugha nyepesi tunaita kubong’oa, akakikamatia kiuno chembamba cha mwanadada huyo na kumvuta kwa kasi kuelekea upande wake.
“aaaaah” Zarish akatoa mguno kuonesha kushangazwa na tukio lile. Ila Zarish bwana nadhani hili ndilo alilokuwa akilitaka maana kucheza akiwa katika hali hiyo mbele ya kidume rijali ulitegemea nini, sasa mshangao unakujaje? Basi banguli akafanikiwa kumdondoshea Zarish kwenye mwili wake na kubaki wakitazamana uso kwa uso.
Wakaganda wakitazamana huku kila mmoja akiwa na uchu wa kumlarua mwenzake. Ile hofu ya Zarish kuona yupo na waziri tena mume wa mtu ikampotea na kujiona kama yupo na mtu wa kawaida tena sehemu isiyo na ulinzi, akajikuta akikisogeza kinywa chake na kukikutanisha na kinywa cha waziri huyo.
Banguli akaunyoosha mkono wake hadi kuifikia switch ya taa iliyopo maeneo ya karibu na kitanda hicho, kilichofuata ni giza tu baada ya kuzizima taa za chumba hicho.
Kilichoendelea hapo basi ilibaki ni siri ya wawili hao.
*****
Asubuhi na mapema wa kwanza kuamka alikuwa ni Zarish, alipoangaza macho yake kitandani alimuona waziri akiwa bado yupo katika usingizi tena akikoroma na mate yakimchuruzika mdomoni.
Zarish akatabasamu!
‘yaani ujanja wote ule kumbe kwenye usingizi ni boya hivi’ Zarish aliongea huku akijinyanyua kitandani hapo.
Alichukua shuka na kujifunga kuustiri mwili wake mara baada ya kujiona akiwa mtupu.
Akaelekea bafu iliyopo ndani ya chumba hicho ambapo alisafisha mwili wake kwa kuoga. Akiwa anarejea kitandani mara akasikia sauti ya mtu akilalamika.
“aaaaaaah mnaniuaa naombeni mniache”
Sauti hiyo ilimchanganya. Ndipo shauku ya kutaka kujua mtu huyo kulikoni ikamjaa moyoni mwake. Akiwa na shuka lake alilojitanda akausogelea mlango wake taratibu
Akaufikia na kubinya kitasa taratibu.
Akaufungua!
Akaupeleka uso wake taratibu kuchungulia kwa nje. Akaanza upande wa kushoto na alipoupeleka uso wake upande wa kushoto akaona watu waliovalia mavazi ya jeshi la polisi la nchi hiyo wakimburuza mtu aliyeonekana kuwa na damu mwili mzima huku akilalamika.
Zarish akashtuka na mshtuko wake haukuishia ndani tu akautoa nje nah apo ndipo akajishtukia akipiga kelele bila kujua alikuwa katika mikono isiyo salama.
“mamaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa” akatoa ukunga.
Ukunga huo uliwashtua askari wale, si askari tu peke yao hata banguli aliyepo chumbani naye akashtushwa na sauti hiyo.
Zarish akaubamiza mlango huo kwa wepesi na kuuegemea huku akihema kwa jazba, banguli alishangazwa na hali hiyo ndipo kwa wepesi akamsogelea.
“umepatwa na nini mrembo?” akamhoji
Zarish akabaki kama aliyepagawa akihema juu juu, ni wazi kwake jambo lile lilikuwa ni geni.
Banguli akamsogeza Zarish pembeni kisha akaufungua mlango ule kuangalia mrembo huyo amaeona nini. Hakuona kitu lakini sauti za mtu akilalamika ziliendelea kusikika. Ndipo akajivuta kuelekea katika chumba kimoja ambacho chenyewe huwa ndio maalum katika jumba hilo kwa shughuli hiyo ya kuadhibu watu waendao kinyume na matakwa yake.
Alipofika huko akakuta askari wakimpa suruba kijana mmoja ambaye kutokana na damu nyingi kujaa mwilini mwake kote hakuweza kutambulika hat asura yake.
Wakaacha walipomuona mkubwa wao huyo na kuto saluti kwa pamoja.
“enheee na huyu nae amefanyaje?” akahoji akikinyanyua kichwa cha kijana huyo kwa kutumia nywele zake.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“huyu ni mwandishi aliyejaribu kupindisha matakwa yako mkuu, aliyeandika Makala ya kusema nchi imepoteza mwelekeo katika Makala ya gaazeti la kimataifa” mmoja wa askari akatoa maelezo hayo.
Ni kama vile maneno hayo yalimwongeza hasira mr. banguli ndipo aliomba kirungu kutoka katika moja ya askari wale. Alipopewa tu miguu ya kijana huyo ilikuwa ni halali yake kwani aliisurubu kwa kuigonga kwenye magoti, na kugonga kwenye sio kwa mchezo ni kugonga haswa.
Kelele tu ndizo zilizokuwa zikitoka kinywani kwa kijana huyo.
Alipohakikisha ameridhika akakirudisha kirungu kile kwa askari wale .
“hakikisheni na yule dada hatoki, atabaki humu milele lakini msimpe adhabu yeyote ila hasitoke tu humu ndani” aliongea huku akiondoka.
“sawa mkuu” askari wale wakaitikia huku wakimpigia saluti.
Akatoka katika chumba hicho.
Aliporejea chumbani kwake akamkuta Zarish akiwa kajikunyata huku akionesha hofu pima kwa kukumbatia magoti yake baada ya kuikusanya miguu yake.
Akamfuata!
“vipi mbona upo hivyo?” akamuhoji Zarish akiwa kaukunja uso wake.
Zarish akatikisa kichwa kuonesha kukataa hakuna lolote.
“sasa nisikilize kwa makini” banguli akaanza kuongea huku akimshika mgongoni Zarish aliyekuwa akitazama kwa hofu kubwa. Akaendelea,” haya uliyoyaona ni baadhi tu ya machache yanayotendeka ndani ya nyumba hii, kuna mengine mengi makubwa Zaidi ya lile uliloliona”
Zarish alishtushwa na kauli hiyo, kupigwa mtu hadi kuvuja damu ni tukio dogo je hilo kubwa lipoje? Mawazo hayo yakapita katika kichwa cha Zarish nah apo ndipo hofu ikazidi kumtanda na kufanya amuogope Dhahiri waziri huyo ambapo hakutegemea kuwa atakuwa na matendo hayo aliyoyaona nyumbani mwake tena akishirikiana na jeshi lenye dhamana ya kulinda uhai wa raia na si kutoa uhai huo.
“sasa wewe ndiye utakayetumika kunisafisha mimi na kuwaaminishia raia kuwa mimi ni mtu mzuri ili kufuta fikra za watu wanaonidhani dhani kuwa ni mbaya, sasa kwahabari rahisi tu wewe humu hautotoka utabaki kuwa kibaraka wa humu hadi pale nitakapochoka kukutumia”
Zarish akashtuka kutokana na kauli hiyo ya waziri huyo ambaye hakuonesha hata chembe la masihara.
“na kingine nitakupandisha chati kila siku kwa kuzidi kuling’arisha jina lako na ntakutengenezea show za kimataifa ambazo zitasimamiwa na ofisi yangu, lengo ni nini? Nahitaji nikuweke maarufu na watu wakukubali ambapo itaingiwa urahisi kukuamini utapoongelea mazuri kuhusu mimi” aliongea mheshimiwa huyo huku akichezea chezea mwili wa mwanadada huyo ambaye bado alionesha kuwa na hofu.
“siri ya mabaya yangu ibaki kuwa hapa hapa, endapo utakubali kufanya kazi nami kwa jinsi vile navyotaka basi tutaenda vizuri sana na utafurahia Maisha haya ya duniani hadi mwisho wa uhai wako, lakini kinyume chake sitaki nikueleze saa hivi lakini naona mfano kwa yule mtu umeuona. Kumbuka mimi nina nguvu kuliko rais wenu kwahiyo nitakapotamka lolote lile lazime litekelezwe” banguli akamaliza kutoa maelezo hayo huku akichukua taulo na kuelekea bafuni.
Zarish akabaki kama aliye ndotoni asijue kuwa yale ayasikiayo ni ya kweli au yu kwa ndoto! Hakupata jibu!
Bwana banguli baada ya kurejea kutoka bafuni akavalia pajama lake la kulalia na kumchukua Zarish kwa ajili ya kuelekea chumba maalum cha chakula kwa ajili ya kupata kifungua kinywa cha asubuhi hiyo.
Zarish alibaki mtu asiye na Amani hata chembe,muda wote aliwaza kuwa anaweza kufanyiwa lolote lile la kumdhuru.
******
Makamanda tisa wa jeshi la wananchi wa zambe waliovalia mavazi ya kiraia wanafanikiwa kuwasili katika ardhi ya nchi ya zambe katika airport ya jiji la ntovo baada ya wote kufuzu mafunzo yao ya ukomandoo salama salmin.
Kati ya makamanda hao alikuwepo na kijana D’oen.
Walipokelewa kwa mapokezi mazuri kutoka kwa wanajeshi wenzao wa kikosi kimoja. Na hata mkubwa majeshi bwana HAMBABE aliwapokea mapokezi mazuri mno.
Vile vile mapokezi ya makomandoo hao kwa Rais yalipangwa baada ya rais kuwaalika katika ikulu yake.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Basi siku hiyo ilivyofika makomandoo hao walialikwa ikulu na ndipo ikafanywa hafla fupi kwa ajili ya kuwapongeza makomandoo hao.
Kama ilivyo siku zote mwaliko tena mwaliko kutoka kwa mkuu wan chi huwa ni wa kipekee sana na hauwezi kukataliwa, D’oen pamoja na makomandoo wenzake waliitikia wito huo.
Hafla hiyo iliudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kisiasa, viongozi wa kijeshi na mkuu wao na hata captain Ashey-tiffa pamoja na hance pia walihudhuria hafla hiyo.
Bendi ya jeshi pia nayo ilikuwepo kunogesha sherehe hiyo.
Rais mwenyewe mhe. Dkt Stanford alikuwepo. Vilevile bwana mkubwa banguli ambaye aliekti mtu mwenye heshima kwa rais na kujifanya kama sio gaidi aliyempindua rais huyo pia alikuwepo. Na hata ilipofika nafasi yake ya kuongea kama kiongozi wa mambo ya ndani ya nchi, alikuwa akimsifia mno rais Stanford na kumpa sifa kuwa hajawahi kuona rais bora nchini hapo kama bwana Stanford.
Kama kawaida alipigiwa makofi kwa maneno hayo.
Na hata rais naye hakutaka kujionesha kuwa yeye sio muongozaji wan chi hiyo, hivyo alijionesha kama mtu mwenye furaha muda wote ambapo ni tofauti na uhalisia.
Walizungumza viongozi wengi mno akiwemo waziri wa mambo ya nje ya nchi na hadi pale aliposimamishwa mkuu wa majeshi kwa ajili ya kumkaribisha rais kwa ajili ya kuja kuwatunukia shahada za pongezi makomandoo hao.
Bwana HAMBABE kiongozi wa majeshi aliyekosa mvuta kwa wanajeshi wavyeo vya chini kutokana na uongozaji wake mbovu, akasimama na kuelekea mbele kwa ajili ya kutoa hotuba ya kumakaribisha rais.
Makofi hafifu yalipigwa kumsindikiza kiongozi huyo.
Ashey-tiffa mwenye uchungu wa kulipiza kisasi kwa kiongozi huyo ambaye aligharimu uhai wa baba yake hasira zilimpanda baada ya kumuona kiongozi huyo akisimama katika jukwaa la mahali hapo kwa mbwembwe huku akifurahi.
Ghafla mawazo yakampeleka mbali
“mwanangu usikubali hata siku moja kuuza utu wako kwa sababu ya uongozi, hakika hata kama upo kwenye mfumo wa utawala unaoongozwa na mtu asiye mwadilifu kuwa wa kwanza kuleta mabadiliko hayo” tiffa alikumbuka kauli hiyo ya baba yake siku moja alipokuwa akiongea nae.
Ghafla machozi yakaanza kumiminika kutokea kwenye vishimo vya macho yake.
Akafikiria kuhusu kumshuti kiongozi huyo hapo hapo lakini akaghairisha, aliwaza ingekuwaje endapo shabaha yake isingefanikiwa? Si angekamatwa n ahata kuuliwa kabla hajakamilisha matakwa yake. Akabaki akivuta subira kama hapo awali alipokubaliana na D’oen kuhusu subira ya swala hilo.
Baada ya kiongozi huyo kuongea alimpa ruhusa rais kuja kutoa pongezi kwa vijana hao.
Rais alisimama na kutoa hotuba fupi ambayo ilifuatia kuwatunukia shahada makomandoo hao. Baada ya hayo yote walielekea kwenye meza ya chakula wote waliohudhuria hafla hiyo.
Baada ya kukamilika kwa hafla hiyo kila mmoja alitawanyika.
Habari iliyobaki baadae kwenye vyombo vya habari ni kuionesha hafla hiyo. Hakika ilikuwa ni habari ya taifa zima.
****
Mipango ya D’oen ya kuikomboa nchi katika ubinywaji na mpango wa tiffa wa kumuondoa duniani kiongozi wao bwana HAMBABE ilipangwa kwa kasi.
Mipango hiyo iliwiana sana maana bila kumuondoa mkuu huyo wa majeshi na kulipindua jeshi basi swala la kulikomboa taifa linakuwa ni ndoto, kwasababu mkuu wa majeshi ndio mwenye amri na nguvu kuliko hata rais, lakini kibaya Zaidi mkuu huyo wa majeshi ni kibaraka wa banguli kwahiyo ni ngumu kutoa maamuzi magumu. Suluhisho pekee lilibaki ni kupinduliwa kwa kiongozi huyo.
D’oen kwakuwa kipindi wapo nje na makamanda wenzake alishawahi kulizungumzia swala la kumpindua mkubwa wao na aliungwa mkono kwa asilimia zote na makamanda wale kwani nao walishachoshwa na uongozi wake mbovu, hivyo akaanza mipango ya kumteka mkubwa huyo wa majeshi kimya kimya bila yeyote kujua.
Hivyo katika misheni hiyo ya hatari wakawa watu kumi na moja ukiongeza makamanda hao nane pamoja na tiffa, hance na D mwenyewe.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Plan ya kwanza ya kumtia mbaroni kiongozi huyo ikapangwa.
Ilikuwa ni plan iliyotumia akili sana kuliko nguvu.
Ilikuwa ni plan ya kuuteka msafara wa kiongozi huyo baada ya kupata taarifa za kiongozi huyo kwenda kufungua mafunzo ya kijeshi katika kituo cha mpodo nje kidogo ya jiji la ntovo.
Makomandoo hao nane wakiongozwa na D’oen pamoja na mwanadada tiffa na hance wakaanza mchakato wa kuuteka msafara huo bila kujulikana.
Walianza na dereva wa kiongozi huyo, kwakuwa alikuwa akipenda sana warembo, hivyo usiku mmoja kabla safari ya kiongozi huyo wakamtumia Mwanadada mrembo waliyemlipa kwa ajili ya kumuadaa dereva huyo. Kama walivyopanga sekunde chache baadae dereva huyo ambaye alikuwa na cheo cha ustaff sajent alikuwa hoi kindatani akiwa hajitambui baada ya kuchanganyiwa madawa ya usingizi kwenye kinywaji chake.
Sekunde hiyo hiyo mwanadada huyo akairuhusu simu yake izitafute namba za D, akazibofya kuzipiga baada ya kuzipata.
Simu ikapokelewa baada ya kuita kwa muda mrefu
“huku mambo yashakuwa tayari” akatoa taarifa na kukata simu hiyo.
Muda mchache ndani ya chumba hicho cha hotel iliyoenda kwa jina mahaki wakaingia makomandoo wawili, alikuwa ni D pamoja na mwenzio mmoja.
“good job lady” aliongea D huku akimpa busu la shavuni dada yule.
Ndipo walichukua simu zao na kuipiga kamera sura ya dereva yule pande zote.
Baada yah apo D akachomoa chupa ya dawa mfukoni mwake pamoja na bomba jipya la sindano. Akalifungua bomba lile la sindano na kuanza kuifuta dawa kutokea kwenye kichupa kile. Baada ya kuhakikasha amefanya yote hayo kwa makini akaishindilia sindano hiyo katika mwili wa dereva yule na kuumiminia dawa kutoka ndani ya bomba la sindano lile.
“kwisha kazi yako MR.HAMBABE, dereva wako kwa masaa 25 ndio atazinduka toka usingizini” aliongea D huku wakifanya wote wacheke.
Wakaichukua simu yake ya mkononi na kutokomea nayo baada ya kukifunga chumba kile ndani yake walipomuacha dereva yule mwenyewe, kisha funguo wakampenyezea kwa chini.
Wakamlipa dada yule kiasi walichokubaliana na kuachana nae.
Safari iliwapeleka moja kwa moja hadi katika hoteli moja iliyo mafichoni kidogo ya nje ya jiji la ntovo ambapo walieka kambi kwa muda.
Huko walipokelewa na wenzao. Utaratibu wa kusafisha picha zile walizochukua kutoka kwa dereva ukaanza na muda mchache baadae tayari picha za sura ya dereva yule zikawa zimeshatengenezwa.
Ndipo akapewa kijana mmoja kati ya makomandoo wale picha zile na kuingia nazo mjini kwa ajili ya kutafuta sehemu wanayotengeneza mask kwa ajili ya kutengeneza mask y asura ile.
Hakutumia muda mwingi sana, ndani ya muda mchache akawa amesharudi akiwa na mask ya dereva yule. Na alipopewa hance ambaye ndiye alikuwa na mwonekano pamoja na urefu sawa na dereva yule basi ilimfiti kabisa na pengine ungeambiwa huyo ni hance na si dereva unaweza ukakataa.
Walifurahi mno na kuahidi kumtia mbaroni mkubwa huyo wa majeshi.
Furaha iridhihirika wazi kwa mwanadada tiffa n ahata kujikuta akitokwa na machozi.
Akamkumbatia D’oen kwa furaha
“nashukuru sana D” aliongea huku akililia kwenye bega la D’oen.
“usijali hii ni kwa ajili ya baba yako na nan chi yetu wote”
“nakuahidi kukupa zawad nzuri tukifanikisha kumtia mbaroni jasusi huyu” aliongea tiffa akiwa bado yupo katika bega la D’oen. Baadae wakaachiana.
Wakakaa tayari kusikilizia kukuche huku muda wote masikio yao yakiwa kwenye simu ile ya dereva.
“ila mimi nina swali” hance akaanza kuongea huku akifanya kila mmoja awe makini kumsikiliza.
Akaendelea,”funguo za gari ntazipata wapi? Na kingine hiyo gari inapark wapi?”
“mmmh hilo nalo neno” komandoo mmoja alisadiki kauli ile.
“mmmh afu hilo hatujarifikiria kweli!”
“mmg tumebugi”
Makomando mbalimbali waliongea kuiunga mkono hoja ile ya hance na kujiona watu walio na mipango dhaifu.
D’oen ambaye ndie kodineta wa mpango ule mzima akacheka kabla ya kukatisha mjadala ule.
“sikilizeni nyinyi”CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Aliongea D’oen akiwa mwingi wa tabasamu ambapo hata tiffa aliye karibu yake ambaye mwanzo aliingiwa na wasiwasi kwa kuona mpango wake unaenda kufeli alianza kupata matumaini huku akisikiliza jibu kutoka kwa komandoo huyo aliyemuamini mno na kumzoea.
“maswali ya majibu yenu yote ni marahisi mno, nashangaa tu mnavyojipa wasiwasi” akatoa kauli iliyowaacha wenzake wakijiuliza kwa kutaka ufafanuzi Zaidi.
“una maanisha nini kiongozi?” hance akahoji akiwa tayari kupata jibu la swali hilo.
“ha ha ha ha ha ha ha ha haaaaaa” D’oen akacheka kabla ya kutoa jibu.
“nitawaambia” D’oen aliongea huku akinyanyuka na kuliendea friji dogo lililo ndani ya chumba hicho cha hotel. Akalifungua na kutoa vinywaji kisha kuwarushia wenzake. Ambapo alihakikisha kila mmoja amepata.
Akarudi na kuketi.
Ili kuwaondoa wasiwasi wahudumu wa hotel hiyo makamanda hao walikodi kila mmoja chumba chake lakini hawakuvitumia badala yake wote walikutana kwenye chumba kimoja kwa ajili ya mazungumzo hayo ya mikakati ya kumteka kiongozi huyo.
“mnakumbuka siku ile tulipoitwa ikulu?” akaongea kwa staili ya kuhoji D’oen
Kila mmoja alitikisa kichwa kuitikia
Akaendelea,”nilifanikiwa kuwa na ukaribu wa muda mchache na dereva wa HAMBABE nah apo ndipo nilianza kumchunguza kwa kujua hii plan itakuja tokea siku moja”
Kila mmoja alipata matumaini na kuwa tayari kusikiliza maneno yale.
“alinieleza funguo huwa anakaa nayo mkuu, yeye ni kupigiwa sim utu na kumfuata hata gari pia huwa inalala kwa mkuu, kwahiyo hapo bado mna wasiwasi plan yetu imefeli?”
Wote wakacheka na matumaini mapya yakawajia.
“wewe ni kichwa hasa D” tiffa akasifia huku akimtwanga busu la shavu kijana D’oen. Busu lile lilipenya mpaka moyoni, ghafla D’oen akajikuta ameduwaa kumtazama mwanadada yule kwa hisia kali za kimahaba.
Wakabaki wakiangaliana wakikodoleana macho.
Makomandoo wengine wakiwemo na hance wakakonyezana baada ya kuona tukio hilo.
Makomandoo wakajikooza hapo ndipo wawili hao wakarudisha fikra zao kwenye kikao kile cha kusubiria kukuche.
“kwahiyo wewe hance, asubuhi utaenda nyumbani kwa mkuu then kulingana na ratba mkianza safari utatuambia, kisha ukifika njia panda ya tini karibia na pale kwenye kichaka kirefu utakuta tuta, hilo si tuta la kawaida ila ni bomu kwahiyo utapita kwa kasi kisha utabonyeza kidude hiki ambapo bomu lile litasambaratika, na hapo ndipo utawapoteza kwa kuingia njia isiyo yao. Mbele utakutana na sisi ambapo tutaitelekeza gari hiyo na kuondoka nay a kwetu ya kazi” alizungumza D’oen huku akimkabidhi kidude mithiri ya rimoti chenye kitufe kimoja.
Hance akakipokea!
Mara kutoka katika ile simu ya dereva ikaanza kusikika mlio wa kuita.
Walipoiangalia walikutana na jina MAJOR GENERAL HAMBABE.
Hance aliyevaa uhusika wa dereva akajikooza kabla ya kuipokea simu hiyo na kuweka spika ya nje.
“jambo afande!” akasalimia kwa sauti aliyoiigizia kabisa na ya dereva yule, kwakweli hance mbali na taaruma yake ya ujeshi vile vile alikuwa vizuri sana katika kuiga sauti za watu, hivyo kwa muda mfupi aliimasta sauti ya dereva yule ambaye alikuwa hajitambui muda huo.
Wote wakacheka kimya kimya kwa kuziba vinywa vyao wasisikike!
“jambo..sasa kesho alfajiri uje uchukue gari ukaweke mafuta kwa ajili ya maandalizi ya safari itakayoanza saa nne asubuhi,sawa?” sauti kutoka upande wa pili wa simu ikasikika.
“sawa mkuu!”
“aya usiku mwema, usisahau na ile faili!” mkuu akaongezea na neno lililomwacha asijue hajibu nini lakini D’oen akampa ishara ya aseme sawa.
“sawa mkuu, nawe pia!” akaitikia na simu ikakatwa.
“mmh sasa hilo faili ndio mtihani!” hance akaongea
“hakuna cha mtiani wowote we kesho nenda kwake mengine yatajulikana kesho hiyo hiyo!”D’oen akaongea.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Basi baada ya kukamilisha mpango huo kila mmoja akarejea chumbani kwake kwa ajili ya kuisubiri kwa hamu kesho ya tukio la hatari yaani kumteka mkubwa wa majeshi ya nchi, hakika ulikuwa ni mpango hatari ambao haujawahi kutokea tangu dunia iumbwe.
D’oen hakupata usingzi kabisa hadi pale kulipokucha na kuwaamsha makamanda wake. Wakajiandaa na hapo ndipo safari ya hance kwenda kwa mkuu yule ikaanza.
Wenzake wakamtoa hofu na kumweleza asijali ushindi u kwao.
Akawaaga wenzake na kuishia zake kuelekea nyumbani kwa kiongozi yule.
*****
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment