Search This Blog

Sunday, 22 May 2022

SHUJAA WA TAIFA - 3

 







    Simulizi : Shujaa Wa Taifa

    Sehemu Ya Tatu (3)





    Muda si mrefu hance akawa ameshaingia katikati ya jiji la ntovo baada ya kukodisha taxi, na hatua si nyingi akawa ameshawasiri katika nyumba ya mkuu wa majeshi.

    Akapokelewa na walinzi lufufu wa nyumba hiyo. Ila kwakuwa alikuwa akifahamika kama dereva wa bosi wa nyumba hiyo akaruhusiwa kuingia.

    “we bwana mbwembwe wewe kila siku unabadilisha mwendo wewe tu aaaai” askari mmoja wa getini hapo aliongea huku akimruhusu hance apite bila kujua kuwa huyo si dereva waliomzoea siku zote, ni dereva mtoa roho.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akajichekesha huku akipita, hapo hofu ilimtoka baada ya kuthibitishiwa na walinzi kuwa amefanana kabisa na dereva mara baada ya kutougundua utofauti uliowatilia mashaka.

    Muda mchache baadae akawa ameshafika katika sebule ya nyumba hiyo.

    Akatoa simu na kumtext mkuu kumtaarifu kuwa yupo mahali hapo.

    Muda mchache baadae jenerali huyo akatoka akiwa na mavazi ya kulalia.

    Hance akajikakamaza na kutoa salamu akiwa amesimama.

    Mkuu huyo akaipokea salamu hiyo.

    Mara katika hali isiyotegemewa jenerali Hambabe akachomoa pistol kwenye nguo yake hiyo ya kulalia na kuuelekeza mdomo wa pistol hiyo kwa hance.

    Hance akabaki ameduwaa!



    Maswali kibao yakabaki kichwani kwa hance yasiyo na majibu

    ‘ina maana amenitambua mimi ni nani?’ swali hilo likapita katika kichwa chake,’sasa mbona walinzi hawakunitambua?’ akazidi kujiuliza maswali lukuki pasipo na jibu la ana kwa ana.

    Bado mdomo wa pistol yenye hasira ukabaki ukielekezwa kwake.

    Hapo ndipo mlango wa kuelekea kuzimu aliuona waziwazi.

    Mara nyuma ya jenerali kuna mtu alionekana akija kwa mwendo wa polepole, hance akabaki kumwangalia huyo anayekuja. Hakuyaamini macho yake baada ya kumuoana na kijana ambaye sura yake ndio ameivaa yeye. Alikuwa ni dereva Dickson au dick kama wapendavyo kumuita watu wengi,dereva wa mkuu huyo wa majeshi kwa muda mrefu sana.

    Na si yeye tu bali aliwaendesha takribani wakuu wa majeshi sita kabla ya HAMBABE.

    Alisimama nyuma ya mkuu wake na Dhahiri alionesha kudhoofika kwa hali.

    “umeshangaa ee? Vipi hukutegemea?” Hambabe alihoji kidharau kumwelekea Hance aliyeonesha kuduwaa na hasiamini akionacho mbele yake. Aliambiwa kuwa kijana huyo kaachwa hotelini tena kwa kuchomwa sindano yenye kudumu masaa 25 iweje amuone mahali hapo? Hakika ikabaki sintofahamu kubwa ndani ya kichwa cha hance.

    ‘ina maana nimeuzwa? Au kuna mtu katuchezea denge?’ alizidi kujipa maswali ambayo ni sawa na kujiuliza kwanini jicho halikuitwa mguu na kuamua kupewa jina hilo? Hakika maswali yake hayakupata majibu.

    Dick akakohoa na taratibu akalisogelea kochi lililo pembeni yake na kuketi,muda mfupi usingizi ulimvaa.

    Hance akabaki akiduwaa akigeuza kichwa kumtazama Dick. Kabla hajapata fahamu za kutambua ni nini kile kinachoendelea alishtukia risasi ya bega, na alipogeuka kumuangalia kamanda huyo asiye na chembe hata ya huruma akaongezwa nyingine ya moyo. Akaanza kupepesuka na kabla hajadondoka akapigwa nyingine ya koromeo.

    Hance hakuwa na ujanja tena, hivyo taratibu akaanza kudondoka kuelekea chini.

    “tukimaliza mission hii hakika nchi itakuwa ni yetu” mawazo kutoka katika kauli ya D’oen aliyeongea kipindi wanapanga mpango huo yakamjia na hapo akajikuta akiionea huruma nchi yake iliyoingia katika mikono ya viongozi wanaojali matumbo yao, hakuona tena matumaini ya wananchi aliyejitoa kuwapigania kwa kumuondoa kiongozi huyo madarakani.

    Aliona dunia nzima ni kama vile inamsaliti.

    Kama gunia la mahindi akadondoka chini.

    Kipindi akiwa chini kwenye sakatul mauti roho ilikuwa ikimuuma sana kuiacha nchi ikiwa bado haijapata lile alilopania kulifanya, nah apo tayari roho ikawa imekwisha achia kiwili wili.

    Hance ukawa mwisho wake umeishia hivyo, akiwa ameondoka na deni la nchi yake kwa lile alilolikusudia.

    Hambabe akamsogelea hance na kumvua kile kinyambolelo cha dick alichokivaa usoni mwake. Hapo ndipo uso wake ule wenye bashasha na mapenzi kwa watu ukaonekana akiwa hana tena uhai.

    “pumbavu sana, hawa ndio makamanda feki! Sasa wenzake lazima wapatikane kabla sijaenda kufungua kikao” akaongea mkuu huyo huku akiitoa simu ya hance mfukoni na kuichukua. Alisahau kuwa simu aliyokuwa akitumia hance si yake bali ni ya dick. Alijua kwa kukaa na simu ile basi angeweza kuwapata makomandoo wale wakiwa na mwanadada tiffa. Alijidanganya!



    ****

    Hance kipindi anaondoka aliifunga kamera kwenye sole ya kiatu chake cha travota ambayo ilikuwa ikimuonesha kila anapopita na mazingira ya mahali apitapo.

    Wire-less Kamera hiyo iliunganishwa moja kwa moja hadi kwenye laptop ndogo waliokuwa wakitumia makamanda waliobaki katika kambi ile yaani D’oen na wenzie. Hivyo walikuwa wakiona mandhari yote aliyokuwa akipita hance isipokuwa yeye halikuwa haonekani kwa sababu kamera hiyo haikuwa inammulika yeye maana yeye ndiye aliyekuwa ameifunga mguuni mwake kwenye sole sehemu ya uwazi.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hivyo hadi tukio la hance kushtukiwa na maongezi yaliyokuwa yakiendelea baina yao waliweza kuyashuhudia moja kwa moja kutokea kwenye laptop waliyoikodolea macho.

    Hadi hance kufikia hatua ya kuuliwa hilo nalo waliliona.

    D’oen alipiga yowe la uchungu baada ya risasi zile zilizotua katika mwili wa hance.

    “haaaaaaaaaaaaa noooooooooooooo haiwezekani kuna kuna mtu ametuuuuuuza” D’oen akaongea kwa jazba huku akitaka kuondoka eneo hilo na kwenda kumsaidia hance lakini makomandoo wenzake wakamzuia. Ilikuwa ni mshike mshike hadi pale alipokubali kutulia.

    Mara pembeni simu ya mmoja wao ikaita ilikuwa ni namba ngeni..

    Ilikuwa ni sakafuni na mwenyewe hakuwepo, inawezekana alikwa bafuni!wakaiangalia pasipo na kuipokea! Ikakata! Baadae ikaanza kuita tena, ikaita bila kupokelewa ikakata! Baadae ujumbe mfupi wa maneno ukatua ndani ya simu hiyo. D’oen hakuvumilia akaamua aichukue na kuufungua ujube huo.

    Hakuyaamini macho yake baada ya kukutana na ujumbe ulioingia ndani ya simu hiyo.

    Ulikuwa ni ujumbe uliosomeka hivi,

    “sasa tuambie wanapatikana wapi ili tuwacontrol kabla hawajaleta effect kwenye taifa,lakini ulisema ni wakina nan hao mbona sijawafahamu?unaweza kunitajia tag namba zao?”

    “haaaaaaaaaaaa nooooooooooooo izzy anauzaaaaaaaaaaa” D’oen kwa jazba akaongea huku akiibamiza chini ya sakafu simu ile.

    Wenzake wakabaki wakishangaa!

    “vipi master!” mmoja akauliza

    “izzy yupo wapi? “ akahoji

    “itakuwa yupo bafuni!”

    “kamlete hapa!”

    Akainuka komandoo mmoja na kwenda kumtafuta, baadae alirudi akitoa jibu la hayupo.

    “izzy ametuuza huyu ndio adui yetu sasa ndo amesababisha kifo cha hance,ametuchoma ila mungu alivyo mkubwa amesahau simu yake! Atakuwa ameondoka saa ngapi? Hivi kipindi hance anaondoka alikuwepo?”

    Kila mmoja akafikiria kidogo kuvuta kumbu kumbu za nyuma kabla ya kujibu swali lile. Wote hawakuwa na uhakika muda gani ametoka eneo lile.

    Hivyo uamuzi wa kutoka eneo hilo haraka vile iwezekanavyo ukatoka.

    Wakajinyanyua na tayari makomandoo nane wakiwa na mwanadada tiffa wenye uchungu wa kumpoteza mwenzao wakaanza safari kupotea eneo lile huku wakihakikisha awaachi ushahidi wowote.

    Sasa wakawa ni mfano wa wanajeshi waasi katika taifa lao, hawakuwa na mahali pa kuishi Zaidi ya kuwa wakimbizi kwani kila kona makomandoo nane picha zao zilitangazwa kuwa wanatafutwa kwa kupewa kesi ya watu wasiopenda Amani ya nchi.

    Hawakujuta kwasababu lengo lao lilikuwa ni kukomboa nchi na kwenye ukombozi yote hayo hutokea.

    Hivyo kwa kujificha vivyo hivyo waliendeleza plan zingine.

    JINSI ILIVYOKUWA.

    Baada ya D’oen na komandoo mmoja aliyetambulika kwa jina la izzy kuhakikisha wamechukua simu ya dereva pamoja na kuchukua picha zake, walifanya uamuzi wa kurejea kambini kwao baada ya kumfungia dereva yule ndani. Wakaagana na yule mdada kisha kurejea kambini kwao, kambi ya kazi nje ya jeshi la zambe.

    Kumbe kichwani wazo la usaliti lilimjenga kijana izzy kwa tamaa ya kupandishwa cheo kizembe bila kuenyea. Ndipo uamuzi wa kuwachomesha wenzake kwa jenerali ukamjia.



    Kipindi chote wakipanga mikakati na wenzake ya kumteka jenerali tayari yeye hakuwa upande wao.

    Aliwasubiri kipindi wanaenda kulala baada ya kuwarekodi mambo yote waliokuwa wakiongea, nah apo ndipo aliwasiliana na jenerali mwenyewe ana kwa ana usiku huo huo.

    Alipopokea simu alimweleza kila kitu nah apo ndipo alimwahidi jenerali huyo kumpelekea kijana wake yaani dereva usiku huo huo na ushahidi wa mipango kutoka kwa makomandoo wale.

    Basi alikubaliana na jenerali kukutana usiku huo huo katika hotel ile alofungiwa dereva wake baada ya masaa machache kutoka muda huo.

    Alichokosea kipindi anaondoka usiku huo aliisahau simu yake katika chumba kile walichofanyia kikao ambacho ndicho alikuwa akikitumia yeye.

    Alikuja kuligundua hilo alishafika mbali na eneo hilo, alihofia kurudi inawezekana ikawa simu ya jenerali kuwa imeingia na wenzake kuinasa, hivyo aliamua kuondoka bila kurudi nyuma.

    Alifika kwenye hoteli ile ikiwa muda umekwenda sana, na baadae wawakilishi wa jenerali wakawasiri akawapokea na kuwapeleka hadi kwenye chumba hicho ambapo aliingiza mkono chini kutafuta ufunguo wa mlango huo.

    Akaupata na kufungua!CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kweli walimkuta dereva dick akiwa hoi kwa usingizi.

    Wakambeba na kumpeleka kwa jenerali.

    Wakafika!

    Mkuu alitoka chumbani baada ya kupewa taarifa kuwa watu wake washafika.

    Alisikitika sana hali ile alofanyiwa dereva wake.

    Hivyo akaamuru apewe dawa za kuamshwa mapema.

    “hao vijana itabidi utupeleke, ni watu wabaya sana” akaongea mkuu akimwangalia izzy kwa makini.

    “ndo hivyo mkuu, ni makomandoo tena ushahidi wa mipango yao ninayo” izzy akaongea huku akimsikilizisha mkuu sauti za makomandoo wenzake wakipanga mipango ile.

    “nahitaji vijana hawa wakamatwe mara moja, na huyo atakayekuja mwache tu mamaeee atajuta anadhani mimi ni mtu wa mchezo ee?” aliongea Hambabe kwa dharau huku akielekea chumbani kwake.

    Dick mara moja alipewa dawa za kupambana na dawa ile aliyodungwa mwanzo ,kisha akapumzishwa ndani humo.

    Izzy akabaki sebuleni akisubiri amri ya mkuu. Baadae akapewa amri ya kurudi kule kambini aendelee kuwa na wenzake kwa ajili ya kuwasoma.

    Akaondoka lakini alipokumbuka kuwa kule aliacha simu na uwezekano wa kushtukiwa kupitia simu ile ulikuwa mkubwa, hivyo akaghairi kurudi hoteni kule kwa makomandoo wenzake.

    Hata baada ya mauaji ya hance alipochukua kundi la wanajeshi kwenda kuvamia hoteli ile walikuta patupu ikiwa tayari makomandoo wale wameshaondoka.

    ******

    Zarish alizidi kukosa mvuto siku hadi siku, ile nyota yake ya awali ikaanza kupotea n ahata muda mwingine kwenye show aliishia kutupiwa mawe n ahata muda mwingine kukosa mashabiki, hiyo yote ilitokana na kuisifia serikali ambayo ilikuwa ikionea wananchi kwa kuminya haki zote za msingi.

    Hakuona hata ile thamani aliyokuwa akiipata mwanzo.

    Hapo awali japo alikuwa na kipato cha kati lakini alipata furaha kwa kukubalika na watu wengi, nani alikosa kuhudhuria pale aliposikia mwanadada huyo ana show? Hasa ule uwezo wake wa kutumia kiuno kwenye kusakata nyonga ndio ilikuwa kivutio kikubwa mno. Na hata baadhi ya wasanii wa kuimba mziki walimtumia kwa ajili ya kupata mashabiki.

    Lakini hali imebadilika kabisa kila mtu alimuona kama kituko. Mwanadada huyo alitamani ajitoe kwenye kifungo hicho kilichompa kila aina ya starehe isipokuwa furaha ya uhuru. Angewezaje kumtoka bwana banguli wakati alishapewa masharti? Hivyo ikabidi abaki kuwa jeuri na kuwaoneshea wananchi wao si kitu kwake, akipendwa na banguli inatosha.

    Maisha yalizidi kusonga!

    Chuki na hofu kutoka kwa wananchi zilizidi kukithiri hasa baada ya mauaji ya watu mbalimbali ambao walionesha hawakuwa upande wa serikali n ahata watoto na wamama wajawazito wasio na hatia wakawa mashakani kwa kukosa huduma safi na salama kutoka hospitalini.

    Hali ikawa tafrani.

    Ule uvumilivu ukazaa kikomo na hapo ndipo wananchi wakaingiwa na uamuzi magumu. Yea ndio ni uamuzi magumu kweli kweli, uamuzi kuamua kuipigania haki kwa kuamua kuandamana kudai haki , ikawa liwalo na liwe.

    Mabango mbalimbali ya kumshinikiza rais ELIAS STANFORD na waziri wake wa Mambo ya ndani ALBERTO BANGULI wajiudhuru yalipambwa kwenye maandamano hayo.

    Wananchi lufufu wa jiji la ntovo wakaungana wakipaza sauti zao

    “rais jihudhuru tumekuchoka!!! Rais jihudhuru tumekuchoka!! Wazir wa mambo ya ndani jihudhuru tumekuchoka!!”

    Sauti zilipazwa kila kona ya jiji hilo.

    Jeshi la polisi lililopokea oda kutoka makao makuu halikuvumila swala hilo. Waliingilia kati na kuanza kutawanyisha watu kwa kutumia mabomu ya machozi.

    Ni kama vile walikuwa wakiongeza spidi ya waandamanaji hao wenye hasira kali ambao walikuwa wakiyafuta mabomu hayo nyusoni mwao kwa kujisafisha na maji.

    Baada ya technique hiyo ya mabomu ya machozi kutofua dafu hapo ndipo walianza kupiga risasi baridi angani lakini haikusaidia ni kama vile masikio ya wananchi yalikuwa yameziba.

    Bado wimbo wao wa kushinikiza rais na wazir wake wa mambo ya ndani wajiudhuru uliendelea.

    “rais jihudhuru tumekuchoka!!! Rais jihudhuru tumekuchoka!! Wazir wa mambo ya ndani jihudhuru tumekuchoka!!”

    Ndipo polisi hao wakaanza kutembeza virungu kwa kila mwananchi wanayemkamata na kumtupia ndani ya gari yao kubwa.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wananchi nao walikuwa wakirusha mawe kuwashambulia polisi hao.

    Hapo ndipo uamuzi wa kutumia silaha za moto ukawaingia polisi hao, ndipo kupitia mdunguaji wao (sniper) akaanza kutungua wananchi walioonekana kimbelembele yaani mmoja mmoja.

    Hapo ndipo lilitokea tukio la kushangaza.

    Ndio ni tukio la kushangazwa haswaa. Sniper yule kutokea katika kikosi kile cha askari waliokuwa wakituliza ghasia akaonekana akiiachia silaha yake kwa ghafla na kudondoka chini. Alipigwa risasi katika paji lake la uso, kama askari wale hawajakielewa vizuri kilichotokea. Mara tena askari wawili kutoka upande wa kulia na kushoto mwa sniper yule nao wakaachia silaha zao na kudondoka chini.

    Ni wazi aliyefanya matukio yote hayo alikuwa ni mdunguaji haswaa maana wote walilengwa sehemu ile ile yaani kwenye mapaji ya nyuso zao.

    Hakika lilikuwa ni pigo la kushtukiza ambalo hata askari wenyewe hawakujiandaa kupata pigo lile.



    Wananchi hapo ndipo wakapata nguvu ya kupambana na polisi hao.

    Askari mmoja alimshuhudia kijana mmoja akitokomea kutoka katika kundi la wananchi wale wenye hasira kali. Alishangazwa kumuona kijana yule akiwa na silaha aina ya SMG huku akiwa amevalia mavazi ya kiraia ambapo miwani meusi ilimnogesha usoni mwake.

    Alipata shauku ya kumfuatilia kijana yule.

    Alitoka katika kundi la askari wenzake wanaopambana na wananchi na kuanza kumfuatilia kijana yule.

    Alimuona akiingia katika gari na kuanza kuelekea upande wa magharibi wa jiji hilo upande wa baharini.

    Hapo hapo akatoa radio call yake na kutoa taarifa makao makuu juu ya mtu yule aliyeelekea upande wa baharini

    Alipotoa taarifa ile muda si mrefu ikafika maeneo hayo defender ya polis na askari yule akaidandia huku akielekeza ilipoelekea gari ile.

    Wakaanza kuifukuzia.

    Baada ya mwendo mrefu hatimaye wakafanikiwa kulifikia daraja refu lilikuwa likipita juu ya bahari. Na muda si mrefu waliiona gari ile ikiwa imesimama pembezoni mwa kingo za daraja hilo.wakapaki kwa mbali kuisikilizia huku wakiwa wameielekezea bastola zao.

    Kijana D’oen kutokea ndani ya gari ile ndogo iliyopaki pembezoni mwa daraja akatoka na kutoa simu yake mfukoni kwa ajili ya kuwasiliana na wenzake.

    “hey stop!” sauti kutoka kwenye defender ikapaza kumzuia D’oen ambaye hapo awali hakujua kuwa alikuwa akifuatiliwa.

    “ukijaribu kusogeza hata hatua moja tunafumua kichwa chako”

    Cha kushangaza ndani ya defender hiyo ya askari akashuka waziri wa mambo ya ndani ya nchi ndugu Alberto Banguli huku akiwa na silaha ya SMG mkononi mwake.

    D’oen kabla hajafanya lolote banguli tayari alisharuhusu trigger ya silaha yake kuweza kumimina risasi baada ya kuikoki.

    Alifungulia usalama hadi mwisho hivyo alivyominya trigger hiyo risasi kadhaa zikamiminika na kutua katika sehemu mbali mbali za mwili wa D’oen.

    D’oen hakutaka kupoteza muda baada ya kuona waziri huyo mwenye dhamana ya usalama wa raia akikiuka maadaili ya kazi yake hana utani hata wa kusingiziwa, hivyo ili kuokoa Maisha yake akafanya uamuzi wa kujirusha kuelekea baharini kwa kupita juu ya kingo za daraja hilo.

    Makomandoo wenzake wakiwa na mwanadada tiffa kwa mbali wanalishuhudia tukio hilo wakiwa wanawasili eneo hilo. Tiffa anajaribu kupiga kelele huku akihitaji kumkimbilia D’oen kwa ajili ya kutoa msaada lakini aliishia kuzuiwa na wenzake, kwani kitendo cha wao kuonekana tu na maaskari hao ni hatari achilia mbali kwenda eneo hilo.

    Hivyo wakamkokota tiffa na kuishia eneo hilo kwa upesi sana wasije wakashtukiwa.

    Askari wakasogea karibu na kingo za daraja hilo na kuanza kuzimimina risasi ndani ya maji.

    Wakaacha kurusha risasi hizo ili kusikilizia, lakini haukuweza kuibuka mwili wa kijana huyo.

    Damu tu ndizo zilikuwa zikielea eneo hilo alilozamia.

    Walisubiri mwili huo uibuke lakini wapi!

    Waziri akaamuru jeshi la maji lije upande huo na kuzama kumtafuta.

    Lakini pia walivyotoka walikuwa ni wenyewe tu pasipo na D’oen. Wakaleta na nyavu ili kumvua kama alinasa huko chini basi aweze kuvuliwa kama samaki lakini wapi hakuonekana!

    Wakakata tamaa na kujihakikishia kuwa mtu huyo atakuwa amekufa tu.

    Wakaondoka kwenda kupambana na wananchi wengine ambao bado walionesha vurugu.



    ******

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hakika jiji zima la ntovo likazima, maiti tu na damu ndizo zilizokuwa zikiupamba mji huo. Hakika ilikuwa ni zaid ya huzuni pale watoto wadogo walipokuwa wakilia kulilia wazazi wao waliopoteza Maisha katika vita na askari.

    Na upande wa askari nao waliuwawa kwa kiasi chao nah apo ndipo hasira zikawapanda wakatoa oda kwa yeyote anayefanya kazi basi saa kumi asionekane barabarani.

    Basi nchi ikabaki mikononi mwa amri za vitisho na wale waliokaidi amri za kipolisi walikiona cha ntemakuni.

    Rais alitamani sana aongee na vyombo vya habari kuhusu hali hiyo lakini aliogopa kuuawa hivyo akabaki mliaji tu ofisini kwake bila hata kutekeleza. Na hata viongozi wenzake aliowaamini kama makamo wake walimgeuka na kuwa upande wa dicteta banguli, unafikiri wangefanyaje kama si hivyo kwani wao hawakuogopa kufa? Hawakuijua power aliyo nayo bwana huyo kwani hadi wamkatalie? Wakabaki wakimuunga mkono kwa kuogopa kuuliwa.

    Taifa la zambe likabaki kama tanuru la mkaa tu, mambo yote hayo yliyokuwa yakiendelea yalifichwa yasisikike duniani kokote Zaidi ya kuishia ndani humo kwakuwa hakukuwa na wa kuzifikisha.

    Na mara kibao viongozi mbali mbali wa nchi za nje walipoitembelea nchi hiyo walipokelewa kwa furaha kuu bila kuwajulisha kuwa nchi hiyo ilikuwa si ya kidemokrasia na Amani tena.

    Na hata mabalozi wan chi mbali mbali katika nchi hiyo walifichwa mambo hayo n ahata wengine kuongwa donge nono pindi wayagunduapo hayo.

    Yote hayo yalifanywa ili kulinda siri ya nchi hiyo ili asitokee wa kutolea msaada. Basi nchi hiyo bado thamani yake ya nchi za Amani ikaendelea kutukuzwa kidemokrasia.

    Hivyo msaada wote wa nchi hiyo ulitegemea sana mashujaa wa ndani ya nchi kuliko kokote.

    Wananchi walibaki kama wakiwa wakifuata sheria za kigaidi za nchi hiyo. Wakina Zarish na watawala pamoja na watu maarufu walikuwa wakimuunga mkono banguli ndio pekee waliifurahia nchi hiyo.

    Waliitumbua vile watakavyo!

    Zarish baadae akafanikiwa kupachikwa mimba na waziri banguli na h apo ndipo waziri huyo akaamua kuishi kabisa na dada huyo kama vile mke wake. Waziri huyo hakujali vile ana mke.

    Hapo ndipo wananchi wakaamini kabisa huyo ni kibaraka wake na heshima yake ya uwaziri ikaisha kwa wananchi.

    Mke wa banguli alizisikia taarifa hizo na kushuhudia mara baada ya kurudi nchini mwake kutokea kwenye matibabu lakini hakuwa na la kufanya Zaidi ya kukubaliana na hayo yote huku akilia na moyo.



    Kwani na yeye hakuogopa kufa wakati alikuwa akishuhudia watu kibao wakiteswa ndani ya nyumba ile kisa ni kupingana na bwana mkubwa huyo, sasa yeye ni nani hadi asiogope hilo? Kufa kisa kupanua mdomo wake kumuhoji mumewe ilihali kunyamaza lilikuwa ni zoezi rahis kwake, akaamua kuwa mpole.

    Upande wa tiffa pamoja na makomandoo saba waliobaki walikuwa ni watu wenye huzuni tele, huzuni yao ilitokana na kumpoteza mtu muhimu sana katika kuleta ukombozi wa nchi yao.

    Wakiwa katika maficho hayo ndani ya msitu maarufu wa tini, mwanadada tiffa ndiye aliyeonekana kuchanganyikiwa kuliko hata wenzake na zimwi la kukata tamaa liliusakama moyo wake. Hakuamini kutimia kwa mipango yake bila ya D’oen.

    Kulia kwake ndilo likawa hitimisho la mwisho kwake.

    “kukata tamaa kwa mwanajeshi ni sumu kubwa tiffa, hata iweje lazima nchi hii irudi katika Amani yake ya awali, iwe isiwe nakuhakikishia lazima mkuu tumkamate na nchi hii irudi katika umiliki wa wananchi kama hapo awali. Hakuna kukata tamaa!”

    Aliyakumbuka vizuri maneno ya D’oen ambayo aliyaongea usiku mmoja kabla ya kumtuma hance kwenda kuvamia nyumba ya mkuu wa majeshi.

    “komandoo siku zote hafi, hata akifa bado damu yake itaendelea kuishi katika Maisha na kulipa kisasi kwa wale waliosababisha kifo chake”

    Bado mwanadada tiffa aliendelea kuyakumbuka maneno ya mwanakaka huyo kipindi akiwa ameketi chini kwenye vichaka porini walipoeka kambi yao.

    Komandoo mmoja akamsogelea.

    “captain!” komandoo huyo akamwita tiffa kwa cheo chake cha jeshini.

    Tiffa alimgeukia komandoo huyo huku akiwa na macho yaliyovimba kwa kilio.

    “captain utalia hadi lini?”CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ni kama kauli hiyo ilinyanyua kilio upya cha mwanadada huyo, akaanza kulia.

    Komandoo huyo akatumia muda huo kumbembeleza, akakichukua kichwa cha mwanadada huyo na kukiegemezea kwenye mapaja yake huku akimbembeleza.

    “hakika nakuhakikishia lazima yule mshenzi tumtie mbaroni, ukiona shida zinazidi ujue neema inakaribia. Niamini lazima tufanikishe mission hii” komandoo huyo akaongea huku akichezea nywele za tiffa.

    Ni kama maneno yale yalikuwa yakitoka katika kinywa cha D’oen na hivyo ndivyo tiffa alikuwa akiisikia sauti ile ya komandoo yule na kuifananisha na kabisa na D’oen ambaye alitokea kumzoea kupita maelezo.

    ‘pumzika kwa Amani D’oen,nakupenda sana D na najilaumu kwanini sikukuambia mapema hadi umetutoka, lazima nilipe kisasi kwa washenzi wote waliosababisha kifo chako, pumzika kwa Amani D wangu’ akajisemea kimoyoni akiwa kakilaza kichwa chake katika mapaja ya komandoo yule amchezeaye nywele.

    “oya msosi wetu unakaribia kuisha tunafanyaje sasa wana?” komandoo mmoja alipaza sauti akiwashtua wenzake walio bize kila mmoja na kazi yake. Kuna waliokuwa wakisafisha silaha kwa kutumia mdeki, na kuna wengine waliokuwa wakiweka mazingira ya kambi hiyo vizuri.

    “twende mjini, tukatafute chichote kitu” komandoo aliyekuwa akimbembeleza tiffa akaongea.

    “tena tukavamie taasisi za serikali” komandoo mwingine aliongea huku akimalizia na tusi kavu baada ya kauli hiyo.

    Wazo hilo liliungwa mkono na makomandoo wote.

    Hawakuwa na namna ya kuishi Zaidi ya kukwapua ndio wapate mahitaji yao, kwakuwa hawakuwa na kazi yeyote ya kuwaingizia kipato. Hivyo walipanga wakavamie taasisi za kiserikali, waliamini kabisa kufanya hivyo licha ya kujipatia mahitaji yao vilevile ilikuwa ni moja ya kisasi kwa serikali.



    *****

    Upande wa waziri banguli, Zarish akafanikiwa kujifungua salama mtoto wa kiume. Hapo ndipo furaha ya muda mrefu ya waziri huyo ya kupata mtoto ikajidhihirisha waziwazi.

    “nakupenda sana mke wangu” aliongea akimbusu Zarish aliyelala kitandani baada ya muda mfupi kujifungua katika moja ya hospitali kubwa jijini ntovo.

    “nashukuru sana!” Zarish aliongea huku akitabasamu.

    Baada ya muda si mrefu mwanadada huyo akaruhusiwa arudi nyumbani kwakuwa alijifungua bila matatizo yeyote.

    Msafara wa waziri banguli ukatoka ndani ya hospitali hiyo wakiwa na mwanadada Zarish na mwanae.

    Basi Maisha yalizidi songa na miezi kadhaa ikikatika. Zarish japokuwa alikuwa akipata kila kitu lakini kitendo cha kushuhudia roho za watu zisizo na hatia zikitolewa bila huruma katika jumba hilo lilimuumiza mno kama binadamu mwenye moyo wenye nyama.

    Roho ilizidi kumuuma Zaidi baada ya siku moja kuingia katika chumba kile cha mateso na kufanikiwa kumuona kijana ambaye taifa zima lilijua amefariki, kumbe haikuwa hivyo! Alikuwa akiendelea kujipatia mateso katika chumba hicho kwa kile kinachoitwa kukiuka amri za mheshimiwa huyo.

    Macho aliyatoa pima baada ya kumuona kijana huyo akiwa amedhoofika mno. Machozi yalianza kummiminika Zarish bila kuyaruhusu baada ya kugandisha macho akimwangalia afordias

    .



    Afordias miaka ya nyuma kipindi nchi ya zambe ikiwa na Amani na utulivu aliwahi kuwa maarufu mara kibao pale alipoudhihirisha umahili wake wa kuichambua siasa na demokrasia ya nchi hiyo pamoja na kuikosoa serikali. Na Makala zake kila siku zilikuwa zikiwekwa katika gaazeti binafsi la taifa hilo liendalo kwa jina UPENDO.

    Alizidi kujipatia umaarufu mno pale alipomchambua rais ELIAS STANFORD kipindi cha kampeni za rais huyo akiuwania urais huo.

    Alizidi kushika hatamu katika kazi hiyo hadi pale alipokuja kutekwa na Banguli baada ya kuandika Makala yake iliyoenda kwa kichwa kilichosomeka kwa maandishi makubwa UTII AMA UOGA? Ndani yake aliizungumzia serikali ya ELIAS pamoja na madudu yake mengi na kibaya Zaidi hakuandika hata moja lililosifia uongozi huo wa ELIAS STANFORD.

    Hilo likawa ni kosa kubwa!CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ni vipi gaazeti hilo lingetoka nje ya nchi? Si angelipaka matope taifa? Basi amri kutoka wizara husika ikatoka kuwa gaazeti hilo lifungiwe, na kwa siri Afordias akatekwa!

    Ndugu zake walitoa taarifa katika vyombo husika za kupotea kwa ndugu yao huyo lakini ikaishia hewani kwa kutolewa ahadi ya kutafutwa, na hata wanasiasa walilifikisha swala la kupotea kwa kijana huyo bungeni lakini ikawa ni patupu hakuna mwanga wala nuru ya kupatikana kwa kijana huyo.

    Ikabaki tu kuanika matanga kwa ndugu zake na kuomboleza msiba. Na wananchi walijua kijana huyo mahiri amefariki, na taifa likaandika barua kuonesha limesikitishwa na taarifa za kupotea kwa kijana huyo na ndipo habari za kijana Afordias zikawa zimekwisha hapo!

    Kitendo cha Zarish kumuona kijana huyo mahali hapo roho ilimuuma mno.

    “afordias!” Zarish akajishtukia akiita.

    Kuita kwa Zarish jina lile la kijana yule, wakati huo huo upande mwingine wa kijijini, mama mzazi wa Afordias akiwa anatafuna tonge la ugali akajing’ata.

    Mama huyo akaugulia vijimaumivu kidogo vya kujing’ata lakini baadae maumivu hayo yalikolea hadi moyoni pale alipomkumbuka mwanaye pekee kipenzi, Afordias. Na bila kuvunga akajikuta akilia. Mumewe aliyekuwa pembeni na yeye akikata matonge kwenye sahani hiyo hiyo ya msosi akamwangalia mkewe kwa huzuni.

    “unalia nini mke wangu?”

    “nimemkumbuka mwanangu, na kama nilivyokuambia nimeota ananiambia hajafa!” mama akaongea kwa huzuni.

    “achana na ndoto hizo sahau mama Ford” baba huyo akambembeleza mkewe.

    Basi upande wa Zarish baada ya kuita neno lile, afordias akiwa anamshangaa ambaye kutokana na mateso alikuwa akiangalia kwa shida mara kijakazi mmoja wa banguli akaiskia sauti ile ya Zarish, ndipo hisia za kana kwamba kuna mtu yumo katika chumba kile cha siri zikamjia.

    Huku akinyata akaufikia mlango wa chumba kile, kwa wepesi akaufungua na kuielekezea bastola aliyoishika kwa mwanadada Zarish ambaye alikuwa tayari alishaanza zoezi la kumfungua Afordias Kamba zilizomfunga mikono, miguu na hata mdomo.

    “hey hands up!”

    Zarish akashtuka baada ya kauli hiyo na alipogeuka alikuta amenyooshewa mdomo wa bunduki.

    ‘nimekwisha’ kwa jinsi alivyokuwa akimjua vizuri banguli akajisemea kimoyoni huku akiona hana tena muda mrefu wa kuishi kwake.

    “toka nje!” kibaraka huyo akaongea huku akimwelekeza Zarish kwa ishara.

    Zarish akiwa na hofu huku mikono kanyoosha juu akanza kuelekea nje ya chumba hicho.

    Akiwa bado kawekewa telo wakafanikiwa kutokea sebuleni ambapo walikutana na walinzi wengine wakionesha uso wa mshangao.

    “vipi imekuwaje?” askari mmoja aliyeonekana kuwa ndio mkuu wa maaskari wa jengo hilo akaongea akimwangalia Zarish na kibaraka kwa zamu.

    “nimemkuta kwenye chumba cha adhabu akitaka kumsaidia yule kibaraka”

    Mara muda huo huo bwana Banguli akasogea eneo hilo kutokea chumbani kwake.

    Ndipo Zarish akakimbia na kujikumbatisha katika mwili wa banguli huku akijiliza kinafiki. Dah wacheza sinema ni hatari sana.

    “baby mfanyakazi wako alikuwa anataka kunibaka nimemkatalia ndo kaniwekea telo” Zarish akaongopa.

    Banguli akamgandua dada huyo kutoka katika mwili wake na kwa ghafla akamtandika kibao cha shavuni. Zarish akabaki akiugulia kofi hilo huku akiwa bado kashikilia shavu lake alilopigwa kofi.

    Akabaki ameduwaa!

    Ndipo banguli akaamrisha tv za sebuleni hapo ziwashwe!

    Zikawashwa!

    Muda mfupi baadae Zarish akaanza kuonekana akiingia katika kile chumba na hata alipokuwa akitaka kumfungua Kamba Afordias na hadi alipofumaniwa na kibaraka yule yote hayo yalioneshwa kwenye tv zile. Zarish alisahau kuwa nyumba hiyo ilikuwa na cctv camera kila mahali.

    “aya sasa hiyo ndio kutongozwa au labda sisi kutongozwa hatujui eti?” banguli akaongea huku macho yake yakiwa yamejaa hasira kumuelekea Zarish.

    Zarish akabaki akilia.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Banguli akaomba apewe bastola! Akapewa, na bila kuchelewa akaielekeza kwa Zarish!

    “mwanamke fedhuli wewe, yaani unadiliki kukengeuka maagizo yangu, lengo lako lilikuwa nini hasa au unajiona wewe ni bora kuliko yeyote kwa kujaribu kufanya yasiyokuhusu? Sasa Sali sala zako za mwisho kabla sijakuua kwasababu uhai wako upo mikononi mwangu, shaaabash!” banguli akaongea huku akiielekeza bastola hiyo kwa Zarish.

    Banguli hakuonesha mchezo hata mara moja.

    “mume wangu nisamehe, mtoto tutamuacha yatima” Zarish akaongea akilia na jasho nalo likimtoka.

    “haha ha ha ha haaaa kwahiyo unataka kuleta ushenzi wako alafu nikusamehe kwa kivuli cha mtoto, hapana sijawahi kusaliti msimamo wangu na kamwe sitosaliti, wacha uende tu kwa mola wako” banguli aliongea huku akimaanisha hana masihara na aliloliamua.

    Akakoki vizuri silaha yake.

    Zarish akafumba macho akisubiria mauti yale.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog