Search This Blog

Sunday 22 May 2022

RISASI NNE - 2

 







    Simulizi : Risasi Nne

    Sehemu Ya Pili (2)



    Joseph Rutashobya alianza maisha mapya, maisha pa sin a baba wala mama, hakumuamini mtu, kila aliyemuona kwake alimuona kama mnyama, kitendo walichofanyiwa wazazi wake kilimuuma sana na kilimuachia kumbukumbu mbaya moyoni mwake. Aliamua kuishi peke yake, kila kukicha alikuwa akitembea mwendo mrefu kwenda asikokujua, matunda ya mwitu na vyakula vya kuomba, wakati mwingine vyakula vya jalalani vilimsitiri na adha ya njaa. Kutokana na umri wa Joseph ilikuwa vigumu kutafuta ndugu aliamini kama wazazi wake wameuawa basi kila binadamu mwenye uhusiano na yeye ameuawa, hali hii ilimfanya mara akimbie mara atembee kwenye barabara ndefu za vumbi na machaka ya kutisha.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Baada ya mwendo wa siku nyingi wa mvua na jua hatimaye Joseph alifika Bukoba Mjini, kwa jinsi alivyokuwa alihitaji kitu japo cha kula au kunywa ili aweze kupoza njaa kali iliyokuwa imemletea udhoofu. Kila duka aliloingia na kujaribu kuomba chochote alifukuzwa kama mbwa, Joseph akaona maisha hayo hayawezi bora kama angekufa pamoja na wazazi wake, akaamua kwenda kwenye magari mabovu ili kujistiri kwa siku hiyo akiwa amekata tama kabisa ya kupata hata chakula, kichwani mwake mawazo mengi yalikuwa yakipita ‘Au nikaibe tu?’ alijiuliza, lakini kila alipotaka kupitisha uamuzi huo alikumbuka maneno ya mama yake siku nyingi nyuma yaliyokuwa yakimwambia ‘Mwanangu hakuna kitu kibaya kama wizi, ni bora ukaomba kama unahitaji kitu, lakini si kuiba, ukiiba watakupiga na kukuua,’ maneno hayo yalimjengea ukuta katika maamuzi yake, ‘Nikiiba nitapigwa na kuuawa,’ aliyaelewa maneno hayo lakini alibaki njia panda kwa sababu hata akiomba alikuwa hapewi wala hapati.

    Akiwa njiani kutafuta maeneo ya kujitiri alikutana na watoto ‘wakora’ waliokuwa wakigombana, Joseph akasimama kuwatazama, akagundua kulikuwa na makundi mawili yasiyopatana na kila kundi lilikuwa na kiongozi wake, hakujua ni nini wanachogombea, aliwatazama kwa dakika kadhaa na alipoona sasa wameanza kupigana, Joseph hakuifurahia hali ile, kwa nini wapigane, akawaendea na kusimama katikati yao.



    “Kwa nini mnapina nanyi ni marafiki?” akawauliza.

    “Toka hapa kwanza we nani hata uingilie ugomvi wetu, nenda zako ukalelewe na mama yako huko, hapa tunaishi nmanunda tupu, tutakumaliza sisi!” walipiga kelele zilizopishana na haikueleweka nani kasema lipi na lipi kasema nani. Joseph akaamua kuondoka na kuwaacha watoto hao, mmoja kati yao akatukana tusi lililomtaja mama, Joseph akashikwa na hasira, akageuka na kurudi akamkamata Yule aliyetukana, ngumi vichwa na mateke vilitawala, mara wenzake wakaingia kumsaidia Joseph hakujali kwani hasira zilimfanya kama kichaa, akawapiga vibaya wote watano, wakakimbia na kumuacha peke yake. ‘Kumbe na mi najua kupigana!’ alijisemea moyoni kisha akavuta hatua fupifupi na kwenda kuketi karibu na jumba bovu moja ambalo lilikuwa hapo jirani na barabara. Usingizi ukampitia, akalala. Aliposhtuka usingizini, akajikuta hayupo peke yake, kuna watoto wa rika lake, wako watatu. Akawatazama kwa zamu.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mnataka nini?” akawauliza.

    “Sisi tunataka ujiunge kwenye chama chetu,” wakajibu. Jose aliielewa kauli hiyo kwani hata shuleni alikotoka alisikia mara nyingi watoto wenye mtazamo mmoja kujisema kuwa wana chama chao. Akakubaliana nao, wakafurahi sana. Mmoja wao akajitolea kwenda kuleta chakula, Jose hakujua ni vipi na ni wapi, baada ya nusu saa wote walikuwa wamesinzia tena kwa shibe ya chakula hicho mchanganyiko kilichokuja kwenye mfuko wa plastiki.



    Joseph Rutashobya akajitambulisha kwa vijana hao kama ‘Joru’ akaingia rasmi kwenye maisha ya ukora, akawa hakamatiki, mhindi gani asiyemjua Joru, kila uchwao watoto wa Kihindi wanarudi nyumbani wakilia, Joru kawapora, hela, chakula chao cha shule na wakileta ukaidi wanapigwa makwenzi. Akimaliza kupora vitu hivyo moja kwa moja alikuwa anavileta maskani na kula na wenzake, lakini pesa alikuwa akificha daima. Hakuna chama chochote cha watoto wa mtaani kilichokuwa hakimjui Joru, kila wanachama wake wakipigwa yeye ndiye anaenda kama mtetezi na kupiga wote atakaowakuta huko. Maisha hayo yalimjenga usugu Joru akawa haogopi mtu wala watu, mara kadhaa alikurupushwa na polisi lakini alikuwa mjanja sana kwani alikuwa akihamisha chama chake kila baada ya siku mbili na kuwaficha mahali pengine, hiyo iliwafanya polisi au wanaomtafuta washindwe kujua yuko wapi.



    Siku moja jioni kama kawaida alikuwa katika harakati zake za kutafuta windo, ndipo alipopambana na mtoto wa mwarabu maarufu sana hapo Bukoba mjini. Wakati Joru na wenzake hawana kitu, wameteseka kwa njaa mchana kutwa yeye alikuwa akirusha maandazi kuwapiga njiwa. Hali hiyo Joru ilimuumiza sana, alimtazama sana Yule motto na kisha akawaambia wenzake wamsubiri akamwende, makofi matatu ya mashavuni yalimtia akili Yule motto akampa joru mfuko wa maandazi yaliyobaki na pesa kidogo alizokuwa nazo mfukoni, bahati mbaya alipofanya hayo kulikuwa na polisi aliyekuwa akimuona. Joru na wenzake wakaondoka kwenda maskani kama kawaida.

    Usiku wa siku hiyo Josru akiwa na watu wake ndani ya magari mabovu walikuwa wakisikiliza redio, redio ndogo ambayo Josu alimpora mmoja wa watoto wa kihindi hapo mjini. Ilikuwa kipindi cha majira, saa tatu usiku, hotuba ya kihistoria ya Mwalimu Nyerere ilikuwa ikirudiwa redioni, hotuba hii ilimkuna sana akajikuta akishangilia na kupiga makelele ovyo mpaka wenzake wakaamka.

    “Joru vipi una kichaa wewe?” wakamuuliza, lakini Joru aliendelea kushangilia na kupiga mbinja, hii haikuwa tabia ya Joru hata kidogo. Lakini siku hiyo alikuwa kama mtu aliyewehuka akili.

    “Sikilizeni, Rais Nyerere anaongea,” akawaweke kale karedio katikati yao.



    “….nia ya kumpiga tunayo, uwezo wa kumpiga tunao, nguvu za kumpiga tunazo…” maneno hayo wenzake hawakuyaelewa ila Joru alielewa kwa sababu alikuwa akisikiliza mara kwa m,ara redio, akawaeleza wenzake.

    “Rais Nyerere anaenda kumpiga Idd Amin,” aliwaambia na wote wakaungana katika furaha yake. Wakiwa katikati ya furaha yao, mara wakavamiwa na kundi la watu, wakakamatwa na kufungwa kamba wakapelekwa kituo cha polisi. Joru alikuwa akilia njia nzima kwa kitendo hicho mpaka alipofikishwa polisi, pale alimkuta Yule mtoto wa kiarabu akiwa na baba yake, Joru alitokwa na macho kukutana na motto Yule….



    “Huyu ndiye aliyeninyang’anya maandazi yangu,” Yule motto wa Kiaarabu alizungumza huku machozi yakimtoka. Joru alimkazia macho ya hasira. Wale polisi wakamwambia Joru lazima apate adhabu kwa lile alilolifanya. Joru akagoma, akakataa katakata kwamba yeye hakumnyang’anya maandazi. Lakini mabishano kati ya watoto hawa yalikuwa makali mpaka mmoja wa polisi alipoingilia kati. Joru akachapwa viboko nane na wale askari na wenzake wakachapwa viboko vine vine kila mmoja kisha wakaambiwa wasionekane kabisa mtaani.

    Tangu hapo Joru akaona maisha hayo si mazuri maana siku nyingine anaweza hata kuuawa. Mchana wa siku iliyofuata, mji ulikuwa na hekaheka sana, kila kona kulikuwa na askari na wanajeshi, ndegevita nazo zilikuwa zikipita huku na kule na kufanya kelele zisizo na mwisho. Joru aliutazama mji wa Bukoba na kuona haumfai hivyo aliamua kutafuta mahali pengine ambapo angeweza kuendesha maisha yake. Jioni ya siku hiyo hakuwaaga wenzake, wote walijua tu kuwa amekwenda kutafuta chochoite kama kawaida lakini sivyo, mguu na njia, malazi yakawa porini. Baada ya kupata vibarua hapa na pale akapata nauli kidogo akapanda basi na kushukia Bihalamuro, huko hakuwa na mtu anayemjua, kama kawaida yake alijikuta mitaani tu akizurula hapa na pale na kuangalia hiki na kile, siku ya kwanza ilimuishia katika mgahawa fualani ambapo kwa kuwa hakuwa na chochote aliomba mmiliki wa mgahawa huo ampe japo kazi ya kusafisha vyombo ili apate kula, ikawa hivyo. Siku zikaenda na miaka ikapita, Joru akaanza kuwa kijana mkubwa, kifua kilianza kutanuka, sauti ikawa nzito ya kutosha, Joru alibalehe na kuwa rijali, hakuona tena umaana wa kufanya kazi ya ile ya kuosha mabakuli kila siku, maana tangu alipoianza mpaka siku hiyo ilikuwa ni tabu tu, pa kulala ilikuwa tabu, aliwekewa kilago katika banda la kuku hivyo yeye na kuku waliishi pamoja.

    Hali ya utulivu ilirudi nchini ijapokuwa kiuchumi maisha yalikuwa magumu sana, Joru alikaa mpaka miezi mine hajalipwa chochote kila akimwambia tajiri wake alicojibiwa hakikumridhisha. Majibu mabovu ya dharau yalikuwa ndiyo apewayo kila uchwao. ‘Nitamvumilia mpaka lini?’ alijiuliza mara nyingi, pale anapomuona akiwanunulia watoto wake vitu mbalimbali vingine ikiwa ni vya kuchezea tu wakati yeye hana chochote hana hata hela ya kununua dawa ya mswaki. Joru aliwakwa na hasira, akaamua kumfanyizia bosi huyo kitu ambacho hatokisahau maishani mwake.

    Siku moja ilikuwa jioni ya jumamosi, Joru alijifanya anaumwa sana, Yule bosi wake hakumjali sanasana alimpangia kazi nyingi za kufanya siku yote. Ilipotimu mida ya saa kumi jioni yeye na watoto wake wakatoka lakini walimuacha binti mkubwa wa yapata miaka 20 hivi ili aangalie kinachoendelea katika mgahawa huo. Joru alianza kulaghai binti huyu kwa neno hili na lile, ijapokuwa binti Yule alikuwa hataki kusikioliza maneno matamu ya mapenzi aliyokuwa akiambiwa na Joru, kijana huyo hakukata tama, kila alipomkuta kasimama alimshika maziwa, mara kumtomasa kiunoni ilimradi tu amuamshe nyege lakini Yule binti alikuwa akikasirika sana hata wakati Fulani alimpiga Joru kwa chupa ya chai. Joru alitafakari sana, ijapokuwa pamoja na umri wake huo yeye kama kijana hakuwahi kufanya mapenzi na mwanamke ila katika mazunguzmo yao ya vijiweni alipata raha ya tendo hilo kihisia zaidi.

    Akaachana na msichana huyo na kwenda zake bandani anakolala, alikusanya kila kilicho chake na kutia katika kijibegi chake cha mgongoni alichojinunulia siku za karibuni, ‘Sasa naondoa nyodo za huyu binti na hilo litakuwa pigo kwa baba yake, mi ndio Joru motto wa kikopo, motto asiye na wazazi, baba yake Jua mama yake mwezi kaka na dada zake nyota, maadu zake Mvua na jua,’ alijisemea huku akijipigapiga kifuani.

    Jioni hiyo kabla bosi wake hajarudi, akiwa bado yupo yeye na binti huyo Kokusima, Joru alijibanza katika mlango wa banda alilokuwa akilala, akimwangalia binti huyo akienda kuoga, Joru aliifurahia bahati hiyo kwa kuwa binti huyo alivaa kanga ya Mombasa kwa mtindo wa lubega na nyingine akajifunga kiunoni, alipoingia tu Joru alimpa kama sekunde 25 nhivi akijua tayari kwa kuda huo atakuwa kabaki kama alivyozaliwa, akanyata taratibu kwa mwendo wa kinyonga mpaka pale mlango wa bafuni, mlango wa bati ulioshikizwa kwa kamba tu kwa upande wa ndani. Joru kwa mara ya kwanza aliliona umbo la mwanamke asiye na nguo, kwa kuchungulia katika pachipachi za mlango ule, mara akaona damu inachemka, moyo unamuenda mbio, akasukuma mlango na kuingia baada ya ile kamba kukatika kisha akaurudishia.

    “Jamani nani huyo?” Kokusima aliuliza huku sabuni ikiwa imemtapakaa mwilini hakuweza kufumbua macho.

    “Utamjua baadae,” Joru akajibu.

    “Ha! Joru, yaani unanifuata bafu…” kabla haja maliza, Joru akamkamata na kumbana mdomo asitoa sauti, kisha kukuru kakara zikaanza, kutokana na nguvu za Joru alifanikiwa kumdhibiti Koku, kofi moja kali, Koku akawa mpole.

    “Ukipiga kelele nakumaliza,” Joru alimuonesha kisu ambacho Koku alikiona kwa tabu sana kutokana na sabuni iliyokuwa ikimuwasha machoni, Joru akaanza shughuli yake mara baada ya kuitoa dhana yake iliyosimama vyema, japokuwa Koku alileta upinzani wa kimyakimya lakini nay eye hakuwahi kujaribu mchezo huo, hivyo mambo yakaenda japo kwa shida, huku Koku akilia, Joru hakujari yeye aliendelea na shughuli yake mpaka alipoona inatosha, akamuwacha Koku bafuni akiwa anajililia yeye akatoka na kubeba kibegi chake na kuondoka zake, akapita kwenye mgahawa, akakuta wafanyakazi wakiendelea na kazi zao, akapita kaunta kwa sababu walikuwa wakimjua hawakuwa na shida naye, Joru akavuta droo na kubeba mauzo yote kisha akaondoka zake. Mlangoni alikutana na bosi wake akirudi na familia wakirudi. Ilikuwa kama saa mbili usiku hivi wakasalimiana kama kawaida, Joru akaficha kibegi chake, ile gari ya bosi wake ilipoingia tu katika uwanja wa ile nyumba, Joru akapotelea mitaani, moyoni mwake roho yake kwatu, pesa kapata na binti wa bosi kamnanihii.

    §§§§§CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baba wa Koku alikaribishwa na kilio cha binti yake, alichokisikia kutoka bafuni.

    “Mama Koku, huyo si Koku anayelia, hebu nenda kamwangalie,” akamwagiza mkewe akamwangalie binti yao kule bafuni. Lo, mama alimkuta bintiye akiwa chini sakafuni, hana nguo, mwili bado umejaa povu la sabuni, kilio kinatawala, hapa na pale palikuwa na damu zilizochanganyika na damu.

    “Nini mwanangu?” mama akauliza.

    “Joru, Joru kanibaka!” alijibu Koku. Mama Koku akatoka na kumpa taarifa mumewe, hasira ikawaka, ‘Namuua Joru,’ alijiwazia, akaingia ndani akachukua kisu chake kikubwa na kupotelea mtaani kumsaka Joru, aliposhindwa, akaripoti polisi, polisi wakaingia kumsaka Joru kila kona, Joru hakuonekana, kila walipouliza, vijiweni kote Joru hakuonekana.

    Ilikuwa ni fadhaha kwa familia, aibu kwa Koku, Mama wa Koku alibaki hana la kusema, alikwenda bandani alikokuwa akilala Joru na kukuta kijikaratasi juu ya godoro, akakiokota. Ilikuwa ni ngumu kusoma maandishi hayo yaliyoandikwa kwa mwandiko mbaya kama kapita bata, na hii ilichangia kwa Joru kuwa na kisomo cha madarasa matatu tu.

    “…Nimefanya kazi sana, hamtaki kunilipa mshahara, nilichokifanya ndicho shukrani na malipo yangu, asanteni kwa kila kitu. Mimi ni mtoto wa mtaa, na mtaa utaendelea kunilea mpaka siku utakaponichoka wenyewe…”

    Baada ya kusoma kijikaratasi kile Mama Koku akaangusha chozi, akalia sana lakini hana la kufanya. Alimpenda sana Joru lakini hakuamini alichokifanya na hakuamini alichofanyiwa. Baada ya Joru kukosekana kila mahali, hasira za mzee huyo zilipungua ijapokua alihapa kuwa popote atakapokutana naye lazima amtoe uhai kijana huyo asiye na faida.

    §§§§§

    Joru pamoja na upole wake, sasa aliingia katika magenge ya kihuni, wavuta bangi na wacheza kamali katika viunga vya mji mdogo wa Biharamulo, kwa kuwa alihofia siku yoyote kukamatwa na polisi, Joru alikuwa kila usiku akilala porini, akikwea juu ya mti na kujipumzisha, hayo ndiyo yalikuwa maisha ya Joru.

    Siku moja akiwa katika malalo yake huko porini alijikuta akiota ndoto mbaya sana, watu wakimchoma moto na kumpiga kwa magongo na mawe, alishtuka kutoka usingizini na kudondoka kutoka katika lile tawi mpaka chini, akaumia kiuno, Joru akawa hawezi kutembea isipokuwa ni kutambaa tu, hakuwa na ujanja, alijikaza na kutambaa kwa mwendo wa kitambo mpaka barabarani, hapo alipata msaada wa kijana mmoja ambaye alimfikisha katika hospitali ya jeshi la wananchi, pale akapata matibabu na kupumzishwa kwa wiki kadhaa.

    “…Joseph mwanangu…. Najua unateseka sana, lakini maisha unayoyaishi hayakustahili, achana na tabia za uhuni, rudi uwe Joseph yuleyule niliyemuacha, roho ya Rutashobya haitakuacha mpaka utimize lile inalotaka,…”

    Sauti hiyo ya mama yake ilimjia katika mawazo kama radi kali, Joru alianza kutetemeka kwa hofu, akiwa pale kitandani, akazama katika wimbi la mawazo, akamkumbuka mama yake na baba yake, akayakumbuka mateso makali waliyoyapata mpaka kifo chao, akakumbuka kauli ya baba yake ya mwisho ambayo haikuisha iliyomwambia ‘nyuma ya choo’, Joru akajiuliza mara kadhaa, nyuma ya choo, hakujua baba yake alitaka kumwambia nini, akatulia na kuruhusu machozi yamtiririke. Mara pembeni yake akasimama daktari mwanamke, aliyevalia kijeshi na juu yake alikuwa na koti jeupe, Joru akamtazama kwa kumhusudu mwanadada huyu aliyependeza katika nguo zake hizo.

    “Samahani daktari,” Joru aliuliomba. Yule daktari mwanadada akageuka na kumtazama Joru kwa jicho kali, kisha akavuta hatua kumfuata pale alipolala.

    “Naomba kukuuliza, hivi Idd Amin alishakamatwa?” Joru aliuliza. Swali hilo kwa askari huyu lilikuwa swali la kipumbavu sana, akacheka kwa dharau.

    “Hakukamatwa, alitoroka,” Yule daktari akajibu huku akiondoka. Joru alikaza macho kumwangalia daktari Yule mpaka alipopotelea katika vyumba vingine vya wodi hiyo. Joru akakumbwa na usingizi na kulala fofofo, ndoto nyingi nzuri na mbaya zilimjia kichwani mwake, aliweweseka sana, “Nitalipa kisasi, baba usihofu nitalipa kisasi,” alikuwa akisema kwa sauti ya chini ambayo ilisikiwa na mtu aliye jirani yake tu. Joru alihisi anaguswa na kutikiswa mguu wake kuwa aamke, akapambana na hali hiyo mpaka mwisho akaamka na kufumbua macho yake. Pembeni yake alisimama mwanaume mmoja, si kijana sana wala si mzee sana, walitazamana macho …





    “Nimekusikia ulipokuwa ukujitambulisha kwa daktari mara ile ya kwanza,” Yule mwanaume alimsemesha Joru, akakohoa kidogo akavuta kiti na kuketi karibu na kitanda alicholala Joru, akaendelea kumtazama kijana huyo, “Joseph Rutashobya, nimekuwa nikilisikia jina hili kwa muda mrefu sana, mpaka nikawa na hamu ya kukuona,” akaendelea kusema.

    “Wewe ni nani?” Joru aliuliza.

    “Usiogope, kwanza kwa nini umemuuliza daktari kama Idd Amin amekamatwa?” akamuuliza.

    “Nimeuliza kwa sababu nataka kujua,” Joru akajibu.

    “Ina maana wewe hujui lolote juu ya Idd Amin?” Yule mtu akmuuliza tena.



    “Aaah! Ndio sijui lolote, mi naishi nje ya ulimwengu, siwezi kujua ya ulimwengu, nilitoka zamani sana,” Joru alijibu. Maneno haya yalimuweka Yule mtu njia panda, hakuelewa Joru alikuwa akimaanisha nini kwa kauli yake hiyo, akabaki akimtazama tu.

    “Mbona unaniangalia?” Joru alimuuliza Yule mwanaume.

    “Nakushangaa kwa kile unachoniambia, unaishi wapi?” Yule mwanaume alimwuliza tena.

    “Sijui nikujibu nini, ninapoonekana ndipo ninapoishi, linaponikuta giza ndipo ninapolala,” akajibu Joru.

    “Ok, nimekuelewa, nitahitaji tuonane mara ukitoka hospitali,” Yule mwanaume akamwambia. Joru alimtazama kwa kitambo, hakummaliza yule mtu, kisha akafungua kinywa chake na kumuuliza.

    “Nitakupataje, nikuulizie wapi na kwa jina gani?”

    “Captain Shibagenda, ukitoka tu hapa ulizia hata hapo getini watakuleta kwangu,” Yule mwanaume akajibu na kuondoka kutoka nje ya wodi ile.

    “Captain Shibagenda,” Joru alijisemea kwa sauti ya chini na kuvuta shuka kujifunika gubigubi.



    Joseph Rutashobya, aliendelea kulala palepale, ilikuwa wiki kadhaa zimepita tangu afike katika hospitali ile ya jeshi. Bila kutegemea jioni ya siku hiyo aliruhusiwa kutoka hospitali. Joru alitoka katika jengo la wodi ile na polepole alikuwa akivuta hatua ndogondogo kuelekea getini mwa kambi hiyo, alifikiria kumuulizia Yule mtu lakini moyo wake ulisita, akaamua kutoka na kuondoka. Joru alikuwa hajui hata ni wapi akielekea, akafuata njia iliyokuwa ikielekea madukani.

    “Joseph!” mara alisikia sauti ya kike ikiita. Joru akasimama kwa mshtuko na kugeuka, ilikuwa ni giza kidogo hakuweza kumuona vyema Yule anayemwita, alipomsogelea akamfahamu, dakatari wa kike aliyekuwa akimtibia pale hospitali, “Unaenda wapi?” akamuuliza.

    “Nimeruhusiwa, naenda kulala,” akajibu Joru, huku akimtazama daktari Yule.

    “Unaenda kulala wapi? Mbona mi nimeambiwa kuwa wewe umeokotwa tu barabarani? Joru hebu nambie ukweli,” Yule dada akamwambia Joru. Joru akainama chini kwa aibu kidogo, kisha akamtazama mwanadada Yule ambaye ukimtazama huwezi kufikiri kama ni ‘binti jeshi’. Joru akashikwa mkono, akashtuka na kumtazama Yule daktari, “Twende ukale, kisha nitakuruhusu uende kutafuta pa kulala.”



    Joru akaongozana na yule dada ‘binti jeshi’ wakarudi tena jeshini katika kota za wafanyakazi. Joru aliona watoto wengi waliokuwa wakicheza michezo mbalimbali kwa furaha sana huku mama na baba zao wakiwa vibarazani wameketi wakibadilishana mawazo. Hali hiyo ilimhzunisha sana Joru alikumbuka miaka kadhaa nyuma kijijini kwao, alimkumbuka Kemilembe wake kwa mara yakwanza, lakini mpaka muda huo hakujua binti huyo yuko wapi, sanasana alijua atakua amekufa kama walivyokufa wengine, Joru aliamini kuwa ni yeye tu aliyepona kutoka katika kijiji kile.

    Mwenyeji wa Joru aliandaa chakula na kuweka mezani, akamkaribisha Joru nao wote pamoja wakaanza kula huku mazungumzo ya hapa na pale yakiendelea.

    “Hebu nambie Joru, kwa nini siku ile uliniuliza juu ya Idd Amin? Kiukweli mtu huyo hakukamatwa na wala hajafa, alitoroka baada ya majeshi ya Tanzania kufika kabisa jirani na pale alipo,” alimwambia kwa kifupi.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Na Mali ya Mungu, alikufa au amekamatwa?” Joru akamuuliza tena swali geni kabisa. Yule daktari akanyamaza kimya kwa sekunde kadhaa, akamtazama Joru usoni.

    “We unamjua Mali ya Mungu?” akamwuliza Joru.

    “Ndiyo namjua sana, sana tu, na kama yuko hai nina shida naye,” Joru alimwambia Yule dada.



    “Yupo, katika vita ile hakufa, lakini sijui sasa atakua wapi, we umemjuaje na una shida gani naye?” Joru alipokea swali linguine.

    “Kiukweli, siwezi kukwambia ni nina shida naye gani, lakini siwezi kumpata, basi,” Joru akajibu na kuinua kikombe chake cha chai, akapiga funda kadhaa kwa mtindo wa mruzi.

    “Ulale hapa Joru,” Yule dada alimuomba Joru alale pale.

    “Hapa, kwangu si mahali salama, sijazoea kuishi na binadamu,” Joru akajibu. Baada ya muda mfupi Joru aliandaliwa maji ya kuoga katika bafu la nje na kutakiwa kwenda kuoga. Joru akashukuru akanyanyuka na kuonesha chumba atakachotumia kulala, akakitazama na kwenda zake bafuni kuoga.

    Joru, kutokana na aina ya maisha aliyokuiwa anaishi hakuona usalama wowote wa kuishi na watu kama hawa, baadae aligundua kuwa unaweza kuwa ni mtego ili akamatwe na wabaya wake, hakuwa tayari, aliliacha taulo juu katika msumari nay eye kupotelea nje akimuacha Yule dada bintijeshi akimsubiri, Joru alitoka nje ya kambi ya jeshi na kupotelea anakokujua yeye.



    4 rejea MTUKULA JESHINI



    Mkuu wa majeshi Shibagenda aliondoka eneo lile na mgeni rasmi na kuendelea kukagua gwaride hilo. Walipomaliza ukaguzi huo wakarudi jukwaani kuungana na wageni wengine ili kupisha gwaride hilo kufanya utaratibu mwingine wa maadhimisho hayo.

    “Gwarideeeee!!!! Kulia geuka!” amri ilitolewa wanajeshi wote wakageuka kulia na kupiga mguu chini, kisha viongozi wa gadi mbalimbali wakaondoka katika maeneo yao kwa mwendo wa haraka na aina yake na kusimama mmbele ya vikosi vyao wakisubiri amri nyingine ya kiongozi wao.



    “Gwaride litapita mbele ya mgeni kwa mwendo wa pole, na kisha mwendo wa haraka, mbeleeeeeeee tembea!” amri ikatoka, na ngoma laini kutoka kwa kikosi cha bendi ya tarumbeta cha jeshi ikaanzisha wimbo mtamu na kuwafanya vijana hao waanze kutembea kwa madaha na maringo, kila aliyekuwa hapo alitazama miguu ya vijana hao iliyokuwa ikienda kwa ufundi mkubwa, hakika walipendeza, hakika walivutia, hakika waliipamba sherehe hiyo.

    “…Wazazi wangu wangekuwepo, siku hii wangeifurahia sana, mama angenikumbnatia na kunibeba kama nilivyokuwa mchanga, angenitemea mate kwenye paji la uso ili safari hii iwe ya Baraka na mafanikio….”



    Joru alikuwa akisema moyoni maneno hayo, akiwa anapita mbele ya jukwaa la mgeni rasmi akiwa amegeukia kulia kama ishara ya heshima kwa mgeni rasmi gwaride linapokuwa katika mwendo wa pole. Mawazo ya Joru yalikuwa ni juu ya wazazi wake siku nzima ya sherehe hiyo. Baada ya dakika thelathini gwaride lilikuwa limejipanga tena mbele ya wageni baada ya kumaliza sehemu hiyo ya kutoa heshima.

    Watu walikuwa wamefurika katika uwanja huo wakishangilia na kupiga makofi kila vijana hao wanapoonekana kufanya jambo Fulani la ukakamavu, Joru alikuwa akisumbuliwa na kelele za mashangilio hayo kwa maana alijua wazi kuwa hazimhusu yeye.

    Gwaride lilikwisha, tayari ilikuwa ni saa saba mchana, mawingu yalilifunika jua na kufanya hali ya hewa kuwa ya kaupepo kidogo uwanja ulibaki kimya na hakukuwa na mtu katikati isipokuwa wageni na raia waliokuja kuwapongeza ndugu zao kwa kuhitimu mafunzo.



    Muongoza sherehe alitangaza kuwa sasa ni wakati wa vijana hao kuonesha umahiri wa mafunzo waliyoyapata. Walianza kuonesha aina mbalimbali za mapigano ya silaha baada ya kumaliza hapo yalifuata mapigano ya mikono, umahiri uliooneshwa wa kucheza mitindo ya kungfu na karate iliwakosha watazamaji, muda wote walikuwa wakiwashangilia vijana hao waliokuwa ndani ya mavazi rasmi ya kijeshi. Baada ya hapo lilifuata onesho la mtu mmoja jinsi anavyoweza kuwakabili watu zaidi ya watano, Joru alikuwa ni huyo mtu mmoja, kazi ikaanza, akavamiwa na wenzake wasiopungua watano, Jorun akaonesha umahiri wa kuwapa kipigo kwa mtindo wa Karate, akipangua na kupiga, akijijengea umakini ili asipatwe na shambulizi lolote, mara kwa mara alionekana jinsi anavyobadili miondoko ya mikono na miguu yake na kutoa aina ya ukelele iliyokuwa ikipendezewsha mchezo huo, dakika tatu alikuwa tayari kawalaza wote chini, makofi na nderemo vikatawala. Likaja onesho la tatu, kijana yuleyule, sasa alitakiwa kupambana na watu wane wenye visu na mapanga hali yeye hana chochote, Joru alitunisha misuli yake kuonesha jinsi mwili wake sasa ulivyokakamaa kimazoezi, akaonesha umahiri wa kukwepa na kupiga kiufundi kisha akawashinda wote wane na kuwalaza chini, akakusanya mikono yake kifuani na kuinama kwa heshima, makofi yalisikika kila kona. Brigedia Shibagenda hakuamini anachokiona kutoka kwa huyui motto wa mtaani, mtoto aliyesumbua mitaa ya Bukoba mpaka Biharamulo, aliyeonekena takataka, aliyelazwa kwenye mabanda ya kuku lakini leo hii alionekana wazi kuwa ni hazina ya JW, Shibagenda aling’amua wazi kuwa mitaani kuna hazina nyingi zinazozurula ovyo bila kuwekewa mkakati, alijikuta akisimama na kupiga makofi ya kumpongeza.



    Joru alirudi nyuma na kupisha onesho linguine ambalo liliwasilishwa na wengine kwa umahiri mkubwa na wa kisasa. Baada ya maonesho kadhaa kupita, pale mbele pakawekwa tofali na ilitakiwa mtu mmoja aje kulivunja kwa mikono pia kulikuwa na miti iliyowekwa kma magoli ya mpira yote hayo ilitakiwa mtu ayavunje kwa umahiri, mbele ya wote akasimama Joseph Rutashobya, alipoonekana tu mbele ya watu, wote wakaanza kushangilia huku vijana wakipiga mbinja na kutamka Joru, Joru, Joru Joru. Joru akasimama katika msimamo wa mashambulizi huku akibadilisha mwendo wa mikono yake katika mtindo wa kupendeza, akavuta hatua na kuruka hewani kwa mtindo wa aina yake akapiga kile kigogo kwa mguu wake kikapaa juu, Joru alipotua chini akajirusha tena kwa ufundi na kukizabu kwa mguu wake mwingine na kukipasua vipande viwili, alipotua chini moja kwa moja mkono wake wa kulia ulipiga pigo moja juu ya tofali na kulitawanya vipande vipande, Joru aliuma meno mkono wake ukatetemeka, “Yuko wapi Mali ya Mungu?” aliongea kwa sauti ya chini huku chozi likimtoka kwa hasira. Makofi, vigelegele, nderemo na vifijo vilimfanya Joru ajue kuwa wapo wanaompenda, wapo wanaomhitaji, wapo wanaomthamini katika jamii, alitikisa kichwa kwa masikitiko, akamuomboleza baba na mama yake, akasimama na kutoa ishara ile ile ya heshima na kurudi kukaa walipokuwa wamekaa wenzake.

    Ilipotimu saa nane na nusu sherehe ile ilikuwa ikifika ukingoni, ilikuwa ni wakati wa kutoa zawadi maalum kwa wahitimu.



    Miongoni mwa wageni waliohudhuri alikuwepo Dr Janeth Ishengoma, huyu aliposikia jina la Joseph Rutashobya likitamkwa kuwa amepata zawadi ya utii, mlenga shabaha mahiri na ukakamavu, alijikuta anashidwa kujizuia, alikuwa akimfananisha kijana huyu na Yule aliyemtoroka nyumbani kwake siku ile alipomkaribisha na kumuwekea maji bafuni maji ya kuoga na aliporudi hakumkuta, Dr. Janeth alimtafakari Joru hakummaliza alimtazama jinsi anavyotembea kwa ukakamavu akipewa zawadi yake huku mashangilio yakiongezeka, Joru, Joru, Joru, Joru…



    §§§§§



    Turudi nyuma, nyumbani kwa Dr Janeth…



    Joru alitazama huku na kule hakuona mtu maana usiku ulikuwa mwingi, akaingia mitaani na kutafuta sehemu yenye kichaka na kujipatia usingizi wake hapo huku bado mguu wake ukiwa haujakaa sawa kwa shuruba nyingine.

    Joru alitamani kurudi kuishi na watu lakini aliona wazi kuwa siku akipambana na polisi lazima atafungwa kwa maana alikumbuka madhambi mengi aliyoyafanya na zaidi kumbaka binti wa bosi wake hili lilimuumiza kichwa. Alitamani kurudio kwao kijijini lakini bado alipata kumbukumbu mbaya ya matukio yaliyopita, hakutaka kurudi kule kwanza aliamini kuwa kila mtu atakuwa amekwishakufa kama ilivokuwa kwa wazazi wake, ilimpa shida.



    Kulipopambazuka hakutaka kuonekana mitaa ile kabisa, alijivuta taratibu huku mguu mmoja bado ukionekana wazi kuwa kuwa haukuwa sawasawa. Alipokuwa akiifuata barabara kubwa pembezoni tu mwa ile kambi ya jeshi ambako alikuwa akitibwa, akaona gari moja ambayo anaijua fika ikipita kwa kasi na mbele yake ikapunguza mwendo, Joru akasimama kuitazama, akaikumbuka, gari ya bosi wake aliyekuwa akimlaza katika banda la kuku, Joru akatabasamu, ‘Watakoma mama zao,’ akajisemea neno hilo la kashfa, kisha akatoa sonyo refu. Akaendelea kuitazama ile gari ikikata kona kuingia mle jeshini, Joru akashtuka, ‘lo, ningelala kwa Yule mwanamke ningekamatika leo, asante Mungu,’ akajisemea kisha akingia zake mtaani kwa upande mwingine, alipokuwa katika kutembeatembea akitafuta wapi anaweza kupata kifungua kinywa, akahisi mtu akimshika bega, Joru akashtuka, moyo wake ukafanya paaaa!CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Joru,” sauti nzito ya kiume ikayafikia masikio yake. Alipogeuka hakuamini macho yake, Kalokola, rafiki yake wa siku nyingi, aliyekuwa naye katika chama kimoja cha mitaani, sasa walikutana baada ya muda mrefu sana kupita, kila mmoja alikuwa baba tosha kwa kupevuka.



    “Kalo, upo? Leo imekuwa bahati sana aisee, tangu tuachane sijaonana na mtu yeyote katika chama chetu, vipi jamaa wanaendeleaje?” Joru aliuliza kwa furaha sana.

    “Aaaaa siku ile wewe ulipoondoka, na chama kikaishia palepale, mimi siku hizi sipo kule kaka, nafanya kazi ya ufundi magari,” Kalokola akamwambia Joru.

    “Aaaaa mwenzangu umeula! Mimi bado natangatanga na mtaa maisha yananisukuma huku na kule lakini naendelea vyema, nilipowaacha nikaja huku Biharamulo na kufanya vibarua lakini waliniuzi nikawafanyia mbaya, yaani hapa mda wowote nitakuwa mikononi mwa polisi,” Joru alimweleza rafikiye kwa kifupi.

    “Aaaa Joru, haujaacha tu fujo zako? Nyoka wa kijani, Joru,” Kalokola aliongea huku akimpigapiga mgongoni kisha wote wakaangua kicheko.



    “Sasa Kalo, mwenzio hapa hata chai sijapata halafu naumwa si unaona nachechemea mguu huu,” Joru akajieleza.

    “Joru, hilo lisikuumize kichwa, wewe ni rafiki yangu sana, unakumbuka uliniokoa kwenye yale mapigano pale Bukoba na wale watoto wakora, siku yetu ya kwanza kukutana na tukakutawaza kuwa mkubwa wetu,” wakacheka tena na kugonganisha viganja vyao.

    Kalokola na Joru wakajivuta mpaka kwenye mgahawa wa jirani na kuingia kisha wakaagiza chain a maandazi kila mmoja, wakanywa huku wakiongea mambo mengi yaliyopita, wakibadilishana mawazo ya kila mmoja alivyofika hapo. Joru alivutiwa sana na mapambano aliyopambana Kalokola katika safari yake.

    “Yaani Joru, bora uliondoka, haikupita siku mbili, lilitokea vurugu pale mjini tukakusanywa wote, mi nilifungwa miaka miwili ndipo nilipojifunzia ufundi magari huko magereza, nimetoka jela hata miezi saita sijamaliza bado, nimejishikiza ufundi kwenye gereji ya mwarabu mmoja hivi,” Kalokola alimweleza Joru.

    “Safi sana Kalo, umefanya jambo jema sana, sasa utafute pesa, upange au ujenge uoe mke uzae watoto na ujenge familia yako,” Joru alimwambia Kalokola maneno hayo mazito huku mkono wake ukiwa umetua juu ya bega la rafikiye nay eye machozi yakimdondoka taratibu.



    “Joru, kwa nini unalia rafiki?” Kalokola akamuuliza.

    “Siijui kesho yangu, nasubiri kufa kwangu, sidhani kama nina thamani duniani tena, hata nikifa ni manispaa itakayonizika endapo itagundua maiti yangu, kama la, basi nitabaki niliko na mwili wangu kuliwa na fisi au tumbusi,” Joru aliyasema hayo huku machozi yakimtiririka.

    “Joru, acha kulia, umesema vyema kuwa kesho yako huijui name nakuhakikishia kesho yako anaijua Mungu, we tulia, sasa una mpango gani?” kalokola alimtuliza Joru na kisha kumtupia swali.

    “Nafikiri kwenda kufia Uganda, nataka nikalipize kisasi cha mauaji ya wazazi wangu,” Joru alijibu.

    “Joru, unamjua aliyeuwa wazazi wako?” Kalo aktupa swali linguine.

    “Namjua na nimemuona, anaitwa Mali ya Mungu, kama yuko hai lazima nikamuue kama amekufa basi nikalikojolee kaburi lake,” Joru alijibu kisha akatikisa kichwa chake, akata andazi na kujimiminia chai yote iliyobaki kikombeni, “Aaaaaaaaaggghhhhh! Tanzania Tea Blenders, aisee asante sana kwa kifungua kinywa, sasa mi nafikiri tuagane, nahitaji kupumzika,” Joru akamalizia kusema.

    “Joru huna pa kupumzika, nifuate, pale gereji kuna magari mengi mabovu nitakutafutia mojwapo upumzike na hatokusumbua mtu,” Joru alikubaliana na nrafiki yake, wakatoka nje ya mgahawa huo.

    “Una shilingi mia tano hapo?” Joru akauliza.

    “Ipo, vipi?”



    “Ninunulie kofia, nijisitiri pia sura yangu isionekane na wabaya wangu,” Joru akamjibu Kalo.

    “Ok, kofia gani inakufaa, balaghashia, pama, kapelo, balleti au ipi?” Kalo akauliza kwa kutaja mlolongo wa kofia.

    “Haujaitaja kati ya zote, ninunulie ‘Mungu usinione,’ cap,” Joru akajibu.

    Joru na Kalokola waliwasili kaytika gereji anayofanyia kazi kalokola, na kama alivyomuahidi akamfungulia mlango wa hiace moja iliyokuwa hapo muda mrefu na kumuweke kiti kwa kulala, Joru akashukuru na kujipumzisha hapo. Joru alibebwa na usingizi mzito ambao hakupata kwa siku nyingi.

    “…Umekuwa sasa Joseph, ni wakati wako wa kuanza kile niichokwambia, usione unafanikiwa kukwepa hatari nyingi, ni baba na babu zako wanaofanya hio kwa kuwa wanakulinda ili uilipie damu yao iliyomwagika…”

    Joru alikuwa akiota na kuyasikia maneno hayo aliyokuwa akiambia na baba yake katika ndoto hiyo.

    “Sawa baba, nitatimiza,” naye alijibu akiwa usingizini.



    “….Usikate tamaa Joseph, usiyachukie maisha, njia yako itafunguka muda si mrefu nawe utaliona jua katikati ya giza, latakaloondosha kwako nuru hafifu ya mbala mwezi na kukuangazia kwa mwanga mpya….”



    Joru aliitikia tena lakini bado alikuwa katika usingizi mzito sana, akaendelea kuota ndoto mbayambaya na nzuri nzuri, Joru aliota akitembea juu ya daraja kubwa sana mara akawa anasikia mtoto analia, sauti ya kuomba msaada, sauti ya mtoto mchanga, Joru akasimama na na kutafuta wapi mtoto huyo, mara akamuona motto akilia akiwa amelazwa pembeni tu mwa barabara aliyokuwa akipita, karibu kabisa na daraja lile, alimtazama na kutetemeka sana. Akavuta hatua kumsogelea maana huruma iliukamata moyo wake akamfuata motto Yule taratibu na kumyanyua akamkumbatia kifuani mwake, mara akasikia sauti za vicheko zenye mwangwi wa kutisha zikafuatiwa na makofi ya pongezi.



    “….Umekuwa mkubwa Joru, sasa una motto mchanga aliyezaliwa muda huu, hakikisha unamtafutana kumpata huyo ndiye atakuwa faraja yako maishani….”



    Joru alikurupuka kama mtu aliyegutushwa ghafla akawa anahema kwa nguvu zote kama mbwa aliyekimbia mwendo mrefu. Akashuka kutoka katika ile gari aliyokuwa amelala, akaliendea bomba na kunawa maji na mengine akanywa kisha akajishika kiuno na kutafakari jambo. Alitazama huku na kule hakumuona Kalokola akauliza kwa jamaa waliokuwa pale wakamwambia Kalokola ametoka kuna gari wamekwenda kulichukua lakini hawakujua atarudi saa ngapi. Joru akaamua kuondoka akawaachia ujumbe kuwa atarudi siku ya pili yake.



    §§§§§

    Mapinduzi ya Rwanda na Burundi 1994



    Taarifa ya kudunguliwa kwa Rais wa Burundi na Rwanda mwaka 1994 zilimfikia Joru akiwa kajipumzisha kwenye makazi yake ya muda ambayo hakuna aliyekuwa akiyajua. Alikuwa akionekana mjini mara tu akiwa na mahitaji ya muhimu lakini wakati mwingine hakuwa na muda wala haja ya kuja mjini. Mjini kwake aliona hakumfai kabisa kabisa kwa maana kila akitua huko lazima kutokee janga ambalo kama si kuhusishwa basi mara kadhaa lilala katika votuo vya polisi, akaona haina haja, akaamua kuhamia porini kabisa huko Biharamulo. Daima aliowaona huko ni majambazi tu kutoka nchi za jirani.



    Baada ya vita vya Rwanda na Burundi, wananchi wengi walikuwa wakijimilikia silaha bila ya mpango maalumu, na baadhi ya wanajeshi kutoka nchi hizo walikimbili katika mpaka wa Tanzania na kufanikiwa kupenya na kuingia na silaha nzito za kivita. Polisi wa Tanzania ilikuwa ni kazi kubwa sana kwao kuwakabili majahili hao kwani walikuwa wamekwishachoka maisha. Joru alikuwa akiwaona mara nyingi walivyokuwa wakijificha huko maporini na kuteka magari makubwa au yale ya abiria ilitegemea, walikuwa hawana mzaha ukiwasogelea kwenye 18 zao wanakumaliza, wao kuua ilikuwa ni kama kukanyaga mende tu. Mwanzoni Joru alikuwa akiogopa sana, hasa pale aliposhuhudia wakimuua mmoja wao waliedai kuwa amewasaliti na kuwachongea kwa polisi. Lakini basi, Joru aliamini kuwa huo ndiyo ulimwengu wao.



    Wizi wa utekaji mabasi na malori ukashamili, na hapo alipokuwa Joru kapafanya kama makazi yake ndio haswa palikuwa njia yao ya kupitisha mali kuzikimbizia porini, hapakuwa mbali na barabarani ni kama kilomita moja hivi. Siku moja walipokuwa wakipita hapo Joru alikuwa kapumzika juu ya mti mkubwa ambao matawi yake yalimfanya hasionekane na yeyote anayepita chini. Siku hiyo ilikuwa tofauti kabisa, wale majambazi walikuja wakaketi chini ya ule mti wakivuta bangi zao na wengine kubwia unga, vifaa vyao walikuwa wameviweka chini mara akasikia mruzi toka mbali na wale jamaa wakakurupuka na kuondoka eneo lile kwa kasi, wakabeba vifaa vyao lakini walisahau pale chini darubini, Joru alipohakikisha wameondoka, akashuka mpaka chini na kuichukua ile darubini kisha akapanda nayo tena juu ya mti. Mara akaona polisi wakija pamoja na wanajeshi wakikagua kila chaka wkapita mpaka pale alipo alikuwa akiwa tazama tu, wakasaka huku na kule lakini hawakuona mtu wakaondoka zao.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Mara nyingine tena, Joru alishuhudia wale jamaa wakiteka malori na mabasi kwa wakati mmoja wakiwavua nguo wasafiri na kuwapora kila kitu mwisho wakawaacha wakiwa uchi wa mnyama. Koru alikuwa akiumia sana juu ya jamaa hawa na alikuwa akipata uchungu sana lakini alikuwa hajui nini atafanya. Usiku wa siku hiyo alikuwa ameshuka chini ya ule mti ili apate matunda mwitu, alipokuwa ameketi chini usiku ule akapitiwa na usingizi palepale. Na siku hiyo ndiyo ilikuwa siku ya msakao mkali wa usiku kwa usiku ndipo walipomkamata joru pamoja na majambazi wengine na kuja nao mpaka barabarani.



    5 rejea JORU NA MAJAMBAZI



    Joru alipomaliza kumsimuliamkisa hicho Captain Shibagenda, akaanza kulia. Shibagenda akamtazama kwa jicho la huruma, akawauliza wote majina yao, akagundua kuwa ni Joru peke yake ambaye ni Mtanzania. Joru hakumkumbuka mtu huyu lakini Shibagenda alimkubuka Joru ndiyo maana akamuulia ‘Hata wewe jambazi? Alijua ugumu wa maisha ya Joru, mara ya kwanza alimuona Joru wakati alipokwenda na kikosi kutoka Mtukula katika kijiji cha akina Joru mara baada ya yel mauaji. Wakati Joru anarudi kijijini asubuhi ile, wanajeshi hao walikuwa wamejificha katika machaka ya migomba wakitaka kuona kama kuna mwanajeshi wa Uganda atakayekuja hapo ili wamshughulikie lakini alikuja Joru tena kwa kunyata na kwa hadhari ya hali ya juu. Alipokuwa akisikiliza hiyo simulizi kutoka kwa Joru akamkumbuka kijana huyu na tukio lile.

    Mara ya pili alimuona kijana huyu katika hospitali ya jeshi hapo Shibagenda aakiwa na cheo cha Captain, alizungumza machache na Joru, akamtaka kumtafuta lakini Joru alipotea katika mazingira ya kutatanisha. Sasa wanakutana katika mazingira yasiyo rafiki hata kidogo.

    Shubagenda akamtazama Joru, akamwita kwa ukali.

    “Njoo hapa!”….



    Joru akamsogelea mwanajeshi huyu kwa utulivu sana, hakumtazama usoni kwa woga aliokuwa nao maana alijua ukishaingia mikononi mwa mjeshi basi ujue kinachofuata kama si kifo basi ni kipigo cha mbwa mwizi. Joru alisimama mbele ya kapteni Shibagenda.

    “Nitazame usoni!” Shibagenda alimuamuru joru, Joru akafanya hivyo, “Sasa nakuamuru uondoke, ukimbie kutoka eneo hili bila kusimama wala kugeuka nyuma, sawa?!”

    “Sawa afande,” Joru akajibu kwa utii huku akiwa anatetemeka. Shibagenda akamnong’oneza Joru, “Kesho uje kambini na unione mimi,” Joru akajibu kwa kutikisa kichwa na kisha akaanza kutimua mbio. Joru alikimbia kama mtu aliyepatwa na kichaa, hakutazama nyuma bali alikimbia bila kusimama kimbio kama la saa moja hivi.

    Kitu kama radi kilipiga kwa nguvu, Joru aliusikia ukelele huo wa nguvu na kuhisi vumbi likitimka mbele yake,



    “…..Kimbia mwanangu, kimbia bila kuchoka….”



    Joru aliisikia sauti ya baba yake ikimwambia kwa mwangwi mwingi uliotoka huku na huko. Kila aliyemuona Joru katika mbio hizo alifikiri kuwa nkijana huyu kwa vyovyote kachanganyikiwa, walimtazama wakamuacha. Joru akasimama katika duka moja dogo, akatazama alikotoka, hakika ni mbali, alikuwa akihema kama aliyekuwa anakimbizwa, akainama na kufuta jasho, kisha akaliendea bomba la karibu, kulikuwa na akinamama waliokuwa wakichota maji, walipomuona Joru akija hapo bombani walimpisha maana walimjua kijana huyo mtukutu, Joru akanywa maji na mengine akajimwagia kichwani kisha akapotelea mitaani.



    Baada ya mwaka mmoja…



    JORU baada ya misukosuko mingi ya maisha akipambana na hili na lile, alikumbuka kauli ya Shibagenda kuwa amtafute, ingawa Joru hakupenda kukutana na mtu huyu akijuwa kuwa kwa vyovyote atakuwa kawekewa mtego wa kukamtwa, alikaa akatafakari, “Kama kunikamata si siku ile ile angenikamata, kwa nini aliniachia?” alijisemea moyoni, akakta shauri akaamua kwenda kuonana na mtu huyo ili ajue kile alichokua akimuitia ni kipi, akaanza safari.



    §§§§§



    Joru alikuwa ameketi katika nyumba ya Shibagenda, akifungua gazeti kurasa hii na ile, akijaribu kusoma hapa na pale.

    “Joru!” alistuliwa na sauti ya Shibagenda aliyekuwa ndio kwanza ameingia nyumbani kwake, akiiweka kofia yake juu ya meza. Alipewa taarifa ya ugeni huo akiwa ofisini, Shibagenda alikuwa mkuu wa kambi hiyo baada ya kupandishwa cheo. Joru alimuona jinsi alivyobadilika kwa kuchafuka kwa tepe za kung’aa na vitu vingine visivyoeleweka.



    “Ulikuwa wapi siku zote Joru, nilijua hutoweza kuja kama ulivyofanya awali, hata hivyo ni mwka sasa,” Shibagenda alimwambia Joru.

    “Ni kweli, nimekuwa nikiogopa sana kukutana na watu wanaofanya kazi za usalama nikihofia kuwa nitakamatwa na wabaya wangu,” Joru alieleza, kisha akamsimulia mabaya yote ambayo kayafanya na watu wanamtafuta. Shibagenda alisikitika sana lakini aliipenda hiyo simulizi kwa kuwa aliona jinsi gani kijana huyu alivyokuwa si mtu wa kukata tamaa na kuiacha haki yake iende, mtu wa kutimiza alilolipanga kwa njia yoyote. Shibagenda hakuwa na kitu cha kufanya Na Joru kwa wakati huo lakini hakupenda kumuacha kijana huyu aendelee kuzagaa mitaani ilhali alimuaona akiwa tangu na miaka kumi mpaka sasa mbaba wa kutosha. Alifikiri kitu kisha akamtazama tena kijana huyu.

    “Sikia Joru, nilikuwa nakutafuta sana, wewe hunijui mimi ila mimi nakujua wewe,” Shibagenda alianza kumueleza jinsi alivyomjua. Simulizi hiyo ilimrudishia uchungu Joru, akaanza kulia kiume bila kutoa machozi.



    “Nikuulize swali Joru, unamjua aliyemuua baba yako au unamkumbuka?” Shibagenda aliuliza.

    “Anaitwa Mali ya Mungu,” Joru akajibu mara moja, jina hilo lilionesha wazi mshtuko wake. Shibagenda alimkumbuka vizuri Mali ya Mungu, alimkumbuka jinsi walivyopambana huko Masaka wakati wa vita vya kumng’oa Nduli, Mali ya Mungu alikuwa ndio kiongozi wa kikosi cha mwisho kabla hujamfikia Idd Amin, aliyeaminika na mtu huyo kwa asilimia zaidi ya mia. Alikumbuka jinsi walivyopambana kwa takribani dakika arobaini na tano, Mali ya Mungu alionesha umahiri mkubwa sana wa kupanga vijana wake katika pambano hilo ambalo almanusura liwamalize Watanzania, lakini vijana wa JW nao walikuwa ngangari, wakijua wanachokifanya, waliweza kuwadhibiti lakini Mali ya Mungu alitoroka na hakuonekana tena.

    “Ni mtu hatari sana,” Shibagenda akasema.

    “Lazima nimuue kama bado yuko hai,” Joru alijikuta akiropoka.

    Shibagenda alimtazama Joru kwa jicho kali, “Hivi huyu haelewi maana ya ‘mtu hatari’?” Shibagenda alijiwazie kisha akatikisa kichwa na kujiweka vizuri kitini, akashusha pumzi na kumwambia Joru, “Vipi, bado unataka kuishi mtaani kufukuzana na polisi na kuwakimbia wabaya wako?”

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sina jinsi, sina maisha mengine, hapa nataka kutafuta pesa kwa njia yoyote ile niende Uganda, nina shida huko,” Joru alijibu. Shibagenda alielewa kile anachokimaanisha Joru.

    “Sawa, sasa kama upo tayari, mimi nina nyumba kule Mtukula, shambani kwangu, kama unaweza kuishi na kunitunzia nyumba ile, nitakuwa nakulipa kila mwezi, ili ukae mbali na mji, utulize akili na kupanga mipango yako mpaka utakapoona upo tayari kwa jambo lingine,” Shibagenda akamwambia Joru. Joru aliitika na kukubali jambo hilo.

    Jioni ya siku hiyo waliondoka na gari ya jeshi kuelekea Mtukula, huko Joru alianza maisha mapya, alikuwa akikaa kwenye nyumba kubwa ya Shibagenda, pamoja nae alikuwa akiishi na mke wa Shibagenda na watoto wake wawili. Yeye alipewa nyumba ya uani yenye kila kitu, kitanda, seti ya makochi, jiko na kadhalika wa kadhalika. Joru hakuamini, alitazama nyumba hiyo iliyoonekana haikukaliwa na watu kwa kipindi kirefu, alijitupa kitini na kufungua redio ndogo iliyokuwa hapo, imeunganishwa na umeme. Akasikiliza kipindi cha michezo kupitia RTD.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog