Simulizi : Nyuma Ya Pazia
Sehemu Ya Tano (5)
ILIPOISHIA...CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kabla ya kupewa mission hii nilikuwa Senior Secretary Servise kwenye kitengo cha RMG yaani Rising Mafia Goals na mie ndie niliyekuwa nikipanga vikosi vya uvamizi na hata taarifa za wapelelezi wote wanaotufatilia kisha kuuawa na ndipo alipokuja jamaa anaeyetambulika kama Luteni Albert Lao, Katibu Kiongozi wa Masuala ya Kigaidi ndani ya National Defence Agency na kuleta taarifa zenu wewe na Bwana Harold Maebo, Mkurugenzi wa National Defence Agency. RM Paul ndie aliyeagiza muuawe mapema na faili la taarifa zao liletwe ndipo akakabidhiwa hiyo kazi RM Jack Loyce kwa kazi hiyo ila ulinishangaza ulivyomuua kwani ulifanya nitamani kukuona ukoje au wa aina gani kwani RM Jack Loyce alikuwa tishio kambini na alipewa kazi za hatari tu." Alimaliza na kumduwaza Joachim kwa jina la Luteni Albert Lao.
"Sasa nimegundua kuna mengi NYUMA YA PAZIA. Na kuna wengi NYUMA YA PAZIA la amani." Aliongea huku akitoka nje ya geti la boma la nyumba ya Sauda.
Waliongoza huku wakifuata barabara kurudi barabara kuu. Walipofika barabarani ilikuwa imetimia saa 5 kamili usiku.
ENDELEA....
Hapakuwa na usafiri wowote maeneo yale hivyo waliendelea kutembea huku Davis akijikokota polepole kwani mwili wake wote ulikuwa unauma kutokana na maumivu ya kipigo alichokipata kutoka kwa Joachim. Wakati wakitembea kwa nyuma waliona mwanga wa gari iliyokuwa ikija usawa wao. Bila kupoteza muda Joachim alinyoosha mkono wa kuonyesha anaomba lifti hivyo dereva wa gari ile alipunguza mwendo na kuwapakiza nyuma kwenye bodi kwani ilikuwa ni Suzuki Carry. Walienda hadi mjini na kushukia kwenye kituo cha daladala na kupanda kuelekea Mwananyamala. Walishuka pale na kuelekea Hospitali kama ambavyo Davis alimuelekeza huku wakiwa wote. Muda wote huo walikuwa wakiongea mambo tofauti tofauti huku Davis akitamani kumuona mke wake.
*******************************
Davis Lenard alikuwa moja kati ya wanajeshi wa Kikosi cha Rising Mafia kama walivyofahamika au Jeshi Jeusi tena akiwa kama Senior Secretary wa Rising Mafias katika upande wa Malengo ya Jeshi. Alijiunga nao miaka mitatu nyuma mara baada ya kumaliza mafunzo ya kijeshi ya awali ya Jeshi la Kujenga Taifa na kukosa ajira. Mawazo ya kujiunga na Rising Mafia yalimjia mara baada ya Maisha kumuelemea huku elimu ya kidato sita aliyokuwa nayo kutokuwa na lolote wala chochote.
Alipelekwa nchini Ethiopia na kupewa mafunzo ya kijeshi huku wakipewa sumu kwa maneno juu ya nchi yake jambo lililoupoteza uzalendo wake kwa nchi yake na kuwa adui mkubwa huku akijiandaa kuwa moja kati ya Askari wa Mapinduzi watakao itoa serikali madarakani. Alikuwa kama askari wa kijeshi tena aliyekamilika. Wao walikatazwa kujihusisha na mapenzi ila waliruhusiwa kumtumia mwanamke yeyote watakavyo na sio kuoa wala uchumba hadi watakapo maliza kazi. Lakini kwa Davis ilikuwa tofauti kwani wakati anaenda mafunzoni aliacha mpenzi hivyo aliporudi aliendelea naye tena kwa siri kubwa sana. Hakuna aliyejua kuwa yeyd alikuwa na mpenzi tena aliyempangia nyumba nzuri ya vyumba viwili na sebure, choo cha ndani, jiko na stoo. Alikuwa akienda nyakati za usiku tu pale anakuwa hayupo zamu ya kulinda. Hakuwahi kumwambia mwanamke yule kazi yake ila alimfungulia miradi kisha yeye akawa anaonana naye usiku tu na sio siku zote. Hata pale alipompa mimba hakuwa na wasiwasi tena alifurahi kwani hakutegemea kama angefanikiwa kuacha alama katika maisha yake ambayo ni mtoto. Lakini jambo moja lilimsumbua nalo ni siku atakayo fahamika kama ana familia na huwa anaihudumia mwenyewe. Hapo akaihisi hayuko huru kama uhuru alioutaka. Ndipo maneno ya kizalendo yakaanza kumrudia tena.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Lakini kila alifikiria kuhusu ajira ndivyo alivyozidi kung'ang'ania Rising Mafia.
Wakati alipokuwa akifikiria hayo yote ndipo alipopata taarifa juu ya mpenzi wake kutaka kujifungua na siku hiyohiyo nae akapangiwa MISSION ya kwenda kumkomboa RM Paul Addas na kwenda kumsaka mtu yeyote wa karibu na Joachim. Wakamchagua Sauda Mansoor mara baada ya kupewa taarifa vizuri na Luteni Albert Lao ambaye alikuwa ni pandikizi wa jeshi lile katika Kitengo cha Ulinzi cha siri cha Nchi yaani NDA. Walimvamia Sauda kwa umakini kwani walipewa onyo kuwa mrembo yule hakuwa wa mchezo na ndio maana akawekwa katika kitengo kile. Walifanikiwa kuvamia ingawa hawakujua kama Joachim Bartazar nae alikuwa pale hivyo walijikuta katika wakati mgumu ingawa walifanikiwa kumpata Sauda Mansoor kama mateka wao huku nae akijikuta ni mateka wa Joachim.
*******************************
"Karibuni niwasaidie nini?" Aliuliza Nesi aliyekuwa zamu usiku ule pale Mapokezi.
"Naitwa Inspekta Dennis Mussa." Aliongea Joachim huku akitoa kitambulisho chake cha bandia na kumuonesha yule Nesi ambae alibadilika ghafla na kujawa na uoga mara baada ya kujua yule ni Askari Polisi.
"Naam, naomba nikusaidie Inspekta." Aliongea kwa heshima wakati ule.
"Kuna mgonjwa ameletwa hapa kujifungua nna shida naye ya kuchukua maelezo fulani." Aliongea Joachim huku akimuangalia Davis aliyekuwa ameinamisha kichwa chini.
"Anaitwa nani?"
"Hellen Michael" Alidakia Davis.
"Ngoja niangalie yuko wodi gani?" Aliongea yule Nesi huku akifanya haraka haraka kuangalia daftari la wagonjwa waliolazwa. Hakuchukua muda aliliona jina la mgonjwa waliyemtaja kisha akawaelekeza sehemu ilipo wodi hiyo. Aliwaandikia kikaratasi kitakacho waruhusu waingie wodini bila kusumbuliwa na mtu.
Taratibu walichapa mwendo kuelekea kwenye wodi hiyo. Walipofika walimkuta Nesi mwingine aliyewapokea mara baada ya Joachim kujitambulisha kama mwanzo kisha akampatia na kile kikaratasi. Aliwapeleka hadi kwa mgonjwa wao kisha akatoka. Davis alishindwa kuificha furaha yake pale alipomuona Hellen akiwa amelala na pembeni akiwepo mtoto mdogo nae amelala. Taratibu alijisogeza hadi pale kitandani na kumbusu kichwani jambo lililomfanya mwanadada yule aamke na kukutana na sura ya mpenziwe. Alitabasamu huku akimuangalia Davis ambae wakati huo furaha yake ilikuwa imezidi.
Joachim alikuwa mtazamaji tu huku nae mawazo ya kujenga familia yakimjia. Alikuwa akitoa tabasamu tu huku akiangalia huku na huko.
"Wa kiume au?" Aliuliza Joachim aliyekuwa akiwaangalia.
"Wa kiume" Alijibu mama wa mtoto na kumfanya Joachim na Davis kufurahi. Davis ndo alizidi kuwa kama chizi kwani furaha yake ilizidi kifani.
"Nakupenda mke wangu." Aliongea huku akiruhusu machozi kumtoka kwani aliona tayari ametimiza malengo yake. Wakati Davis akiendelea kuongea kuongea na mpenziwe au mama mtoto wake, Simu ya Joachim iliita kwa muito wa kutetema au Vibration. Aliisikia mwenyewe akatoka nje kisha kwani hakumjdua mpigaji na ilikuwa namba mpya.
"Hallow, nani mwenzangu?" Aliuliza.
"Hupaswi kunifahamu sana ila mimi ni mtu mwema sana ambaye nakupa taarifa hii, chagua ulete mafaili mawili yanayohusu Rising Mafias au tukutumie kichwa cha huyu kahaba wako? Oh! samahani huyu mpenzio." Aliongea kwa dharau mpigaji.
"Unamjua unayempigia?" Aliuliza Joachim kwa dharau.
"Sana tu ila kama utaona taarifa zangu hakufai sawa pia" Aliongea mpigaji.
"Taarifa zako...."Alikatishwa.
"Sina haja ya kubishana na wewe ongea na malaya wako....."
"Joachim usitoe chochote acha nife nchi iwe huru...." Aliongea Sauda kisha akanaswa kibao hadi akapiga kelele na kumfanya Joachim kuwa mpole.
"Nahisi umenisikia una masaa 48 kuanza sasa basi au uje mwenzio atoke.?"Aliongea yule mtu na kukata simu.
Aliiangalia simu yake huku akijaribu kumfikilia yule aliyempigia. Mawazo ya Sauda kuumia yakamjia na hapo bila kuchelewa alipiga hatua kadhaa kuelekea ndani ambako alimkuta Davis akiendelea kuongea na mama mtoto wake.
"Bado sana." Aliuliza Joachim huku akiwaangalia.
"Nipe dakika 5 za mwisho kaka." Aliongea Davis. Joachim aliangalia simu yake huku akikadiria muda kwani wakati ule ilikuwa ni saa 8 na dakika 20 Usiku. Mawazo yake yote yalihamia kwa Sauda wakati ule ambae ilionesha yuko kwenye mateso mazito. Alikuwa akiangalia muda kila mara na hapo ndipo alipomsitua Davis.
"Hey, Davis tayari inatosha..... Twende." Davis aliinuka huku akimuangalia Hellen na mwanae na hapo ndipo akakumbuka kuwa hakumpatia jina mwanae.
"Kaka... sijampatia jina."CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Muite... Joachim." Alilopoka Joachim huku akiufuata mlango wa kutokea wodini.
"Umelisikia jina la mwanetu..... Joachim."Aliongea Davis huku nae akiwa katika harakati za kuondoka.
"Ndio halafu zuri." Alikazia Hellen.
"Asubuhi, nitakuja." Aliongea Davis huku akiondoka kumfuata Joachim.
Walipotoka nje walitoka moja kwa moja hadi mapokezi na kumuaga yule dada kisha wakapotelea mjini.
*******************************
"Luteni Frank Mapungo."
"Sir." Aliitikia Joachim.
"Simama juu. Hatua kumi mbele songa." Aliongea Kiongozi wa Kombania aliyokuwa Joachim na kumfanya asimame kisha akaanza kupiga hatua kwenda mbele huku akiwa na bunduki yake aina SMG-56 mkononi iliyotengenezwa na Mchina mwaka 1956. Alikuwa kaishikilia sawa sawa huku kwa nyuma kukiwa na Askari wawili wa shabaha yaani Snipers wakimlinda. Peki (Begi la kijeshi) mgongoni ndio lililomfanya asikie uzito kwani lilijaa magazine zilizoshiba risasi 30 kila moja, maji, chakula na dawa kadhaa. Alipopiga hatua kumi ndipo alipoona risasi ikimpita na kupiga mti. Hakufikilia mara mbili alijitupa chini kisha akaachia risasi tatu kuelekea upande ilipotokea sauti ya bunduki. Wenzake nao walifanya vile alivyofanya. Walifanikiwa kumshusha mdunguaji wa adui yao kisha yeye akaendelea mbele kwa kutambaa. Muda wote alihakikisha kaiweka bunduki yake tayari kwa mashambulizi. Wakati akiendelea kujivuta ndipo alipojikuta akivuta kamba nyembamba iliyoashiria kulikuwa na bomu limetegwa. Hapo aliwahi kuibana kamba ile ili kuzuia mlipuko kisha taratibu aliiangalia kamba ile na kwa mbele alikutana na bomu lililokuwa likiisubiria roho yake.
Wenzake wote walikaa kimya kumuangalia huku wakiwa wametulia. Walibaki sita tu katika Platoon yao huku Joachim akikamilisha idadi ya Wanajeshi saba waliokuwa katika kikosi kile kilichopelekwa katika misitu ya D.R.C. iliyokuwa na wavamizi ambao walikuwa na harakati ya Kupindua nchi ile huku Joachim au Luteni Frank Mapungo akiwa moja kati ya wanajeshi wa Tanzania waliochaguliwa katika oparesheni ile. Alituliza akili kabisa huku akiibana ile kamba ya bomu aina ya ya Mine Bomb yaani mabomu ya kutega ardhini.
Wenzake wote waliendelea kujilinda na mlipuko ule kwa kuendelea kulala chini huku wakiendelea kuweka ulinzi kwa Luteni Mapungo aliyekuwa akiendelea kutegea bomu.
"BOOOM!!!"
Ulikuwa mlio uliomfanya akurupuke katika njozi ya ajabu iliousindikiza usingizi wake kama vile alikuwa Sinema. Alivyoshtuka alimfanya na Davis pia aamke na kumuangalia kwani alijiuliza Jamaa kwa nini alikurupuka.
"Vipi?" Aliuliza Davis.
"Ah! nimeota tu ila hamna shida." Alijibu huku akitoka kuelekea msalani kwani walichukua chumba katika Lodge moja hivi mitaa ya Kinondoni. Alinawa uso huku akikiangalia kioo kilichouonesha uso wake na mwili wake pale alipotoa tisheti aliyoitia mwilini tangu siku moja iliyopita. Alijiangalia alivyojazia kwa mazoezi anayofanya. Pia kidonda chake kinachoelekea kupona pia. Wakati akiendelea na zoezi lile simu yake iliita huku namba ambayo hajahi kuwa nayo katika simu yake yaani hakuwahi kuisave ilionekana.
"Hallow"
"Yes, nani mwenzangu?" Aliuliza Joachim.
"Oh! kumbe namba yangu hukusave?" Alijibu mtu yule.
"Naam, nahisi nilisahau!"
"Okay, ni mimi mtu mwema sana ninae mlinda malikia wako."
"Shit!" Alijibu Joachim.
"Sasa... ni saa 2 umebakisha masaa 40 tu mimi mwenyewe ndie nitakae leta hicho kichwa cha huyu malaya wako na kisha nikumalizie wewe... hivyo basi fanya uwezavyo ulete. Basi sina mengi." Alimaliza kuongea akakata simu kukwepa mijadala mingi. Joachim alibaki ameganda huku akifikiria cha kufanya.
Alitoka huku akiwa na wasiwasi hadi Davis akaelewa kuwa Joachim hakuwa sawa kwani walijuana jana tu lakini alimtambua yukoje.
"Kambi yenu ulinambia iko wapi?" Ndio swali alilolitoa Joachim.
"Kwani vipi kaka?" Aliuliza Davis huku akimshangaa Joachim.
Kabla hajamjibu simu yake iliita tena huku ile namba ya mtu asiyemjua ikionekana kwenye kioo cha simu yake. Aliipokea huku akikaa kimya bila kuongea chochote.
"Oh! rafiki nilisahau kukwambia mahala pa kukutania." Aliongea yule jamaa kwenye simu.
"Enhe"
"Kama ukiwa tayari nitakupigia na kila baada ya masaa mawili mi nitakupigia hadi muda utakapoisha." Kisha akakata simu kama ilivyokawaida yake. Joachim alielewa kwani mtu yule alikuwa akizima simu papo hapo na hata alipojaribu kumtafuta Opareta wao ili amtambue mpigaji jibu lilikuwa..
"Hiyo sio simu mkuu ni kompyuta na amefunga mtandao wakd wa location hivyo hauwezi kufahamu wapi alipo"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Dah! poa" Alijibu Joachim.
Waliamua kutoka ili waangalie watafanyaje.
"Nahitaji msaada wako." Ndio neno aliloongea Joachim huku akichapa hatua kadhaa na Davis mara baada ya kuiacha Lodge ile waliyojipumzisha usiku ule.
"Niko tayari kaka" Alijibu Davis huku nae akiendelea kupiga hatua.
Walipofika barabarani walinyooka hadi kituo cha daladala na kupanda gari kuelekea Posta.
*************************************
NATIONAL DEFENCE AGENCY (NDA).
Viongozi wote walikuwa na pilikapilika mara baada ya Luteni Sauda Mansoor kutekwa tena na Kundi kubwa kabisa hivyo walikuwa wakitafta njia za kufanya kumnasua huku wakiendelea kupata taarifa za Joachim nae kutaftwa na watu wale.
"Kwa hiyo tunafanyaje kuhusu huyu bibieh." Aliuliza Luteni Albert Lao ambae alikuwa Katibu Kiongozi wa Masuala ya Kigaidi ndani ya NDA.
"Kwani Luteni Lao haiwezekani kutoa watu saba wa kuifanya hiyo kazi ipasavyo." Aliongea Kapteni Marwa aliyekuwa Mwakilishi Mkuu wa Jeshi la Wananchi ndani ya NDA.
"Anachoongea Kapteni kiko sahihi kabisa." Alidakia Kapteni Sanga ambae alikuwa Kiongozi wa Masuala ya Mawasiliano na Teknolojia.
"Hapana inabidi tumpate Joachim ili tujue nae ana nini cha kuchangia Viongozi wangu". Alijibu Luteni Albert Lao.
"Haina haja cha kufanya ni kuagiza vijana kumi mapema wafanye hii kazi ikiwemo kukisambaratisha hicho kikosi." Kapteni Sanga alidakia mara baada ya kuona Luteni Lao anaweka mkazo.
Wakati huo hakuna aliyeuelewa mpango wa Luteni Lao kung'ang'ania Joachim ahusishwe kwani kila kitu yeye alikifahamu na hata mipango ya kumteketeza yeye ndie alikuwa akiipanga yaani Master plan. Waliendelea na kikao chao cha takribani masaa mawili huku Luteni Lao aking'ang'ania Joachim ahusishwe kama mhusika mkuu na muhafaka ukawa na hao vijana kumi kuandaliwa.
Alitoka katika chumba cha mikutano huku akiweka tabasamu la kuchonga ili mradi asionyeshe chuki aliyokuwa nayo baada ya kushindana na wakubwa wake lakini pia kupingwa kwa mawazo yake.
Taarifa zilitumwa makao makuu ya Jeshi la Wananchi kuwa Ikulu inahitaji vijana kumi hatari kabisa katika masuala ya kivita na uvamizi. Walitumia njia ya Ikulu kwa ajili ya kujiziba NDA isifahamike ni nini na wapi ipo.
Taarifa zilipofika ndipo wakateuliwa Vijana hao wengine wakiwa na vyeo vidogo tu lakini hatari kuotea mbali. Walituma taarifa zilizowafikia wao moja kwa moja na kuagiza Gari likawachukue pale Lugalo. Lilikuwa ni Zoezi la masaa matano tu tangu watume taarifa na vijana walikuwa wamepelekwa hadi Katika majengo ya Posta na Kuingia katika moja ya Jengo na kisha wote waliingia kwenye Lifti huku wakiwa na yule dereva aliyewafuata na kisha akabonyeza namba fulani katika ile lifti nayo ikaanza kushuka chini kwa haraka. Ilipofika sehemu ilipotakiwa walishuka na kuiacha irudi juu kuendelea na shughuli zake katika jengo lile.
"Private Anold Erick Mlangwa." Aliita Luteni Lao.
"Sir." Mwenye jina akaitikia na kuingia katika chumba cha mikutano.
"Private Kulwa Labani Mlangwa"
"Sir" Nae alifanya vile kama mwenzake huku zoezi lile likiendelea vyema na wote kuingia ndani.
"Karibuni sana. Naitwa Meja John Kibwa Mambo." Alijitambulisha Mwenyekiti wa kitengo cha masuala ya kigaidi ambae hakuwepo muda kidogo na alirudi kwa ajili ya kuendeleza majukumu yake yaliyokamatwa na Luteni Lao kwa kipindi alichokuwa hayupo.
"Hapa ni NDA yaani NATIONAL DEFENCE AGENCY na mmepata nafasi ya kuungana nasi." Wote wakapiga makofi kisha wakaendelea kusikiliza.
"Mbele yenu kuna Mission tena hatari sana ambayo itaingiza mamilioni fedha mifuko mwenu pia kuokoa Tanzania yetu iliyodondokewa na tone la damu ya adui mwenye uchu na nchi yetu. Sasa basi tuliapa kuilinda na kuitumikia Tanzania hivyo huu ndio wakati." Alimalizia Meja Mambo aliyekuwa kavaa gwanda zake ya Kijeshi au Bakabaka kwa lugha ya mtaani iliyokuwa na alama ya Nembo ya Taifa au bibi na bwana kuonyesha Cheo chake. Alitoa ishara na Luteni Lao akatoa mafaili kumi na kumpatia kila mmoja la kwake.
"Mission nzima imo humo. Kuna kikosi kinaisumbua nchi kinajiita Rising Mafias au Jeshi Jeusi ambao makao yao hayafahamiki....."
"No. Yanafahamika." Alidakia Joachim aliyekuwa na Davis mara baada ya kuingia kwa kasi mle ndani.
"Joachim???" Alishangaa Luteni Albert Lao.
"Sio Joachim tu baki ni Luteni Kanali Frank Joachim Mapungo." Mara baaba ya kusema hivyo Meja Mambo alijibana kuwainua waliokaa na kupiga saluti kwani yeye peke yake alikuwa na cheo kikubwa pale. Luteni Lao alibaki kaduwaa tena alipomuona Davis Leonard ambae alikuwa akimkata jicho la husuda na umeumbuka.
Taratibu alitoka nje ya chumba lakini Davis alimuwahi.
"Subiri braza."CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Aligeuka nyuma na kumkata jicho kali huku akimuuliza.
"Umeniharibia sio?"
"Sio kukuharibia bali ni Uzalendo tu wa kuipenda nchi yangu." Alijibu kwa kebehi.
"Shenzi sana." Aliongea Luteni Lao huku akielekea ofisi mwake na kupiga simu kuwa tayari wamepata doa katika kazi yao.
Alikuwa amesahau kuwa hakuna simu inayotoka mle ndani bila ruksa maalum wala inayoingia bila kurekodiwa.
"National Defence Agent your call will be recorded by NDA press 1 to Allow or hang up.(Ajenti wa Usalama wa nchi simu itarekodiwa na NDA bonyeza 1 kuruhusu au kata.!" Ndio maneno yaliyopenya katika masikio yake. Kwa hasira aliiweka simu mezani na kushika kichwa na hapo hapo mlango wake ukafunguka.
"Albert Alban Lao... uko chini ya Ulinzi tena wetu sisi." Aliongea Luteni Kanali Frank Mapungo huku akiwa na Meja Mambo pamoja na Wale vijana kumi ambapo mmoja wao alifika na kumvua vyeo vyake vyote kisha akamuinua juu tayari kwa mateso.
Alikuwa katulia tuli kama vile kamwagiwa maji ya baridi. Aliinuliwa juu huku akiongozwa kuelekea chumba maalum cha mahojiano huku wakimtoa wasiwasi wa kuipoteza roho yake kwani wakati alipokuwa akichukua mafunzo ya Uafisa kadeti aliambiwa juu ya sheria za mamruki anapokamatwa hukumu yake huwa kifo ni tu.
"Albert Alban Lao isitoshe sio jina lako kamili?" Aliongea Frank huku akizunguka kiti na meza alipokuwa Luteni Albert Lao ambaye hakujibu chochote zaidi ya kukaa kimya.
"Najua mafunzo ya uafisa bado yako ndani yako na ndio maana huwezi kunijibu." Aliongea Frank huku akivuta kiti na kukaa.
"Hata ufanyeje tayari nchi imeshatwaliwa subiri uone." Aliongea Albert Lao.
"Mmechelewa na sijaja kubishana na wewe mimi nataka nimpate Sauda tu."Aliongea Frank.
"Sifahamu alipo...." Kofi zito ndilo lililomfanya anyamaze huku damu zikimtoka puani kumaanisha kofi lililotoka mkononi kwa Frank lilimfana kweli kweli na kumfanya asiendelee kuongea.
"Huo ni mwanzo tu wapi alipo Sauda?"
"Sifahamu."
Hakuongea tena bali aliinuka na kumpiga ngumi iliyompeleka chini na kiti chake alichokuwa amefungiwa pingu kwa nyuma. Alitoka na kumuacha pale chini huku akitoa amri ya Albert Lao apelekwe chumba cha mateso na yeye ndie atakaye husika na kumuhoji.
Mara baada ya kutoka nje ya chumba kile simu yake iliita na alipoiangalia ndipo akagundua ni yule mtu wa Rising Mafia.
"Hallow... " Aliongea Frank huku akitoa ishara ya kurekodiwa kwa maongezi yake.
"Oh! yamebaki masaa 36 ndugu yangu, kazi yangu vipi.?" Aliuliza Yule mtu.
"Tayari mafaili ninayo." Alidanganya Frank au Joachim kama alivyofahamika.
"Naam, tukutane Benjamin Tower kuna gari inakusubiri hapo aina ya Toyota VX wewe ni mheshimiwa ujue.?" Aliongea huyo mtu.
"Saa ngapi?"
"Sasa hivi si uko karibu na maeneo hayo." Aliongea huyo mtu huku akimfanya Frank ashangae na hapo ndipo akakumbuka kuwa mtu huyo anatumia Kompyuta kuzungumza nae hivyo anamuangalia kupitia Location lakini hakujua wapi yeye yupo, bali alidhani yuko katika moja ya majengo pale Posta kumbe alikuwa Chini ya Majengo yale. Baada ya kumbuka vile alitabasamu na kuitikia.
"Sawa."
Alikata simu kuangalia simu yake kisha akamuonesha ishara Opareta kuwa vipi.
"Nimepapata wapi alipo ingawa alikuwa ameficha Location ila nimecheza na IP Adress yake, yuko Maeneo ya Kinyerezi." Aliongea Opareta yule huku akionyesha jinsi alivyokuwa mtundu wa mtandao na kuweka sawa miwani yake na kukiegemea kiti chake kudhirisha kazi kwisha.
"Vijana mko tayari kwa kazi?" Ndicho alichouliza Frank mara baada ya maelezo ya Opareta.
"Ndio mkuu!!" Walimjibu huku wakibana mikono yao kama kujiweka miguu sawa.
"Meja Mambo waandae vijana mimi naondoka naenda kuanza hivyo." Aliongea Frank huku akitoka kuelekea usawa wa lifti.
"Mkuu mesahau kitu." Aliongea Mzee yule wa makamo alijikuta akimhusudu Joachim au Luteni Kanali Frank Mapungo.
"Kipi Meja?"
"Opareta muwekee chip ili tuweze kufahamu wapi ulipo." Aliongea mzee yule na kumfanya Frank akubali na kuona kweli alisahau icho kitu. Opareta alikuwa shapu hivyo aliwahi na kumbandika kifaa fulani kidogo sana kama punge ya mchele katika upande wa mguu wa Frank.
"Nipe na nyingine nimeze." Aliongea Frank na Opareta akafanya hivyo.
"Mkifahamu nilipo bonyezeni alam na mimi nitaona kwenye saa kisha muje na mkifika pia bonyezeni." Aliongea Frank wote wakaitikia.
Alitoka huku akimuacha Davis mahala pale katika chumba maalum huku akitoa oda ya asiguswe na mtu yeyote yule na kuondoka.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mara baada ya kufika eneo aliloelekezwa aliona gari aliyoelekezwa huku ikiwa na namba za Serikali T 501 STK. Alielekea katika gari ile na alipokaribia alifunguliwa mlango na mtu aliyekuwa ndani na hapo ndipo alijuwa kuwa hajakosea na alikuwa akisubiriwa.
"Karibu Bwana Joachim Bartazar." Ilikuwa sauti ya njemba iliyokaa upande wa kulia kwake huku ikiwa imevaa suti nadhifu nyeusi huku akisindikizi na miwani ya giza yaani myeusi.
"Mkague kama ana chochote zaidi ya mafaili yetu." Aliongea mtu mwingind aliyekaa siti ya mbele pembeni ya dereva huku naye akiwa na mavazi sawa na ya yule aliyeko pembeni ya Frank pamoja na dereva pia. Alipitishiwa kifaa fulani kilichokuwa na Alam kama kuna tatizo nacho hakikusita kulia pale kilipofika kiunoni mwake.
"Tiiii!! ti! ti! ti!" Ndio mlio kilioutoa kilipofika kiunoni mwake.
"Nipe hiyo chuma kaka." Aliongea kwa kumkebehi Joachim nae akaitoa bastola yake na kumpatia. Walipomaliza ukaguzi alivikwa kitambaa cheusi kama foronya kilichomfanya asione popote kisha safari ikaanza.
**************************************
RISING MAFIAS, HEAD QUATER.
Mara baada ya Toyota VX nyeusi kuwasili maeneo yale katika moja ya Godauni kubwa lililokuwa pembeni kidogo ya Jiji maeneo ya Kinyerezi, Frank Mapungo alishushwa huku akitolewa kile kitambaa na hapo akaamini yupo sehemu sahihi.
"Naitwa Profesa Jackson Mataba namuwakilisha kaka yangu, Waziri wa Ulinzi aliyetoroka nchini." Alianza kuongea yule mtu aliyekuwa kavalia gwanda nyeusi huku akiiweka ikae sawa mwilini pake na kupambwa na vyeo mbalimbali kuonyesha alikuwa mkubwa maeneo yale.
"Nashukuru kukufahamu." Alijibu Frank.
"Nipatie kazi yangu niliyokupa."
"Nipatie mtu wangu kwanza."
"Usijitie kiburi kijana, lete kazi au msitoke hapa." Aliongea mzee yule huku akimkazia macho Frank ambaye yeye alimfahamu kwa jina la Joachim.
"Okey, Haya hapa." Aliongea Frank huku akimkabidhi.
"Whaoh! kazi nzuri, ndio yenyewe mleteni huyo binti walau amuone." Aliamrisha yule mzee na muda si mrefu Sauda aliletwa akiwa katweta kwa vipigo na mateso ya wale washenzi.
"Mbona mmemuumiza hivi?" Aliuliza Frank.
"Sababu hakuwa na haki mbele yetu." Alijibu huku akiendelea kupekua mafaili aliyopewa na kukenua meno.
"Joachim? umemletea huyu mshenzi haya mafaili....?" Aliuliza Sauda huku akipigwa kofi zito hadi akadoka chini na kuinuliwa tena na njemba iliyokuwa imemkamata vilivyo.
Saa ya Frank ilionesha mwanga uliomfanya aelewe ishara nayo ilimaanisha wanakuja huku yeye akijifanya mvumilivu lakini alipokuwa akimuangalia Sauda alikasirika. Hata pale mwanga wa pili ulipowaka alionyesha tabasamu lililomfanya Sauda ashangae.
"Kwa hiyo mie namchukua mtu wangu?" Aliongea Frank huku akiinuka katika kiti lakini kabla hajakaa sawa alijikuta chini huku akiwa haelewi nani mrushaji wa teke bora kama lile huku akielewa dhamira ya mchezo ule.
"Sio rahisi kama unavyodhani Shenzi wewe!" Aliongea Simon Jacob huku akimkanyaga kifuani Frank.
"Unajua haya mambo unayachukulia wepesi sana eh!" Aliongea Professa Jackson Mataba ambae ni Mpwa wa Professa Alphonce Kaigimo, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi.
"Unaenda tofauti na makubaliano Professa." Aliongea kwa hasira huku akijaribu kuinuka lakini mguu mzito wa Simon Jacob ukimzuia.
"Hakuna makubaliano yoyote baina yetu labda ukubaliane na zoezi dogo tulilonalo." Aliongea Papaa Paul aliyeingia ofisi na kuingilia maongezi baina ya watu wale.
"Hakuna zoezi lingine hapa zaidi ya kumfyatua huyu." Aliongea Simon huku akimuinua Frank ambalo lilikuwa kosa kwani kwa wepesi wa hali ya juu aliivuta bastola iliyokuwa kiunoni mwa Simon Jacob huku akiyaziba makosa kwa kufyatua risasi mbili kuelekea kwa walinzi wa mlango wa kuingilia katika ofisi ile. Kisha alijichomoa haraka mikononi mwa Simon huku akimuacha ameduwaa.
"Mmenikosea sana." Aliwaambia huku akimuinua Sauda na kumuweka begani na bastola yake ikiwa imemuelekea Professa Mataba ambae macho yalikuwa yamemtoka.
"Na asijiguse mtu wote mikono juu."
Wakati akiendelea kuwaweka watu wale watatu chini ya ulinzi wake. Bastola iliyokuwa mkononi mwake ilikuwa tayari imewekwa tayari hivyo alianza kutoka huku amewaelekezea silaha ile.
"Atakae jigusa ndio atanifahamu" Ndio lilikuwa neno nilililomtoka mdomoni wakati ule.
**************************************
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Taratibu kikosi maalum yaani "NDA Special Force" walianza kuingia katika kambi ile huku Davis akiwaongoza kupita njia za Panya. Walikuwa wako kikamilifu na idadi ya watu kumi na mbili pamoja na Davis Leonard. M 16 ndio silaha walizokuwa nazo, aina hatari ya rifle iliyotengenezwa na Mmarekani kwa ajili ya Vita miaka ya 1960 hadi 1978. Taratibu wadunguaji walianza kukaa maeneo yao maalum ili waifanyie kazi yao.
Walibaki wengine tisa wao wakaendelea kuingia huku M 16 ziliyofungwa kifaa cha kuzuia sauti zikiwashusha mmoja mmoja. Ishara za vidole ndio zilizowatawanya mara baada ya kuamrishwa na kiongozi wao.
Kila walipopita walitega bomu huku wakiendelea kuingia ndani zaidi mwa kambi ile ya Mamafia.
**************************************
"Usijidanganye kama utatoka humu salama au ukiwa hai Joachim." Aliongea Professa Mataba huku akitoa tabasamu la kinafiki. Hakutaka kuongea sana bali alivuta trigga iliyoruhusu risasi moja kutoka na kulivunja goti la bwana mkubwa yule.
"Aaaagh!! nakufa." Alipiga ukelele Professa Mataba huku akianguka chini.
"Sitaki kelele." Aliongea Frank huku akiufungua mlango na kutoka nje huku akiwa amemuweka Chambo Papaa Paul ili awe salama.
" Naomba nitembee." Aliongea Sauda na kumfanya Frank amshushe na kumpatia bastola moja.
"BOOOM!!......... BOOOM!!" zilikuwa sauti za milipuko pamoja na mtetemo mkubwa.
"Tumevamiwaaa!!" Ndio maneno yaliyoropokwa na Wanajeshi wa Rising Mafias huku wakikimbia kuelekea Amala wanapohifadhi silaha zao. Lakini walikuwa wamechelewa kwani 'NDA Special Force' walikuwa tayari wameliteka kwani walijua kutakuwa vile.
Baada ya mlipuko ule Papaa Paul aliwachoropoka Frank na Sauda na kuwakimbia.
"Sauda wako huyo." Aliongea Frank akimwambia Sauda amfatilie Papaa Paul na yeye akaelekea upande mwingine. Kwa hasira zote Sauda alitoka mbio huku akiwa na maumivu kutokana na kuteswa sana. Kwa mbali alimuona Papaa Paul akiwasha gari aina ya Range Rover Evoque na kutoka mbio. Hakumuacha nae aliingia katika Jeep iliyokuwa ipakiwa pale na kwa mwendo wa kasi akamfuata kwa nyuma. Hawakutaniana kwani Sauda alifanya juu chini amkamate Mr. Paul au Papaa Paul jina alilopewa na Waimba dansi wa Kikongo. Nae hakutaka hilo litokee hivyo aliichochea gari vilivyo.
Utaalamu wa Sauda na kuendesha gari ndio uliomfanya awe sambamba nae na kuanza kumgonga kwa upande ilimradi atoke njiani. Waliendelea kugongana lakini Sauda alimzidi uwezo Papaa na kumfanya ahame barabarani na kujigonga katika daraja. Kwa kasi nae Sauda alisimama kwa mbele huku akiwa shapu kushuka akiwa na bastola yake mkononi.
"Nisaidie kunitoa nisaidie tafadhari." Aliongea Papaa ambae alikuwa amelowa damu huku amebanwa na usukani wa gari mara baada ya kujigonga darajani.
"Nani akusaidie Mr. Paul...... ni bora ukafa kuliko shida unazotuletea." Aliongea Sauda. Wakati waliendelea kubishana Sauda alisikia kitu kama cheche zikilia katika boneti ya gari ile huku moyo ukifuatia. Hakupoteza muda alitoka nduki na muda ule ule kulitokea mlipuko mkubwa ukifuatiwa na gari ile kuruka juu. Kwa haraka alilala chini na kuuruhusu moto mkubwa upite juu yake.
**************************************
Mara baada ya kumuacha Sauda amfuate Papaa Paul yeye aliingia katika Oparesheni ile hiku akikamata SMG 56 aliyoiokota kwenye moja ya maiti za Wanajeshi wa Rising Mafia. Aliendelea kuwashusha huku akimtafuta Professa Mataba. Alipoingia ndani ya jengo lile ndipo alipokutana na Simon Jacob akiwa bunduki yake mkononi na nyuma yake akiwepo Professa Mataba.
"Hatimaye tumekutana tena." Aliongea Simon Jacob huku akiikoki bunduki yake na upesi kuvuta trigger au kifyatulio cha risasi ili kuruhusu risasi lakini hazikutoka na kuashiria zilikwisha. Nae Frank (Joachim) alitabasamu na kuruhusu risasi kadhaa ambazo nae hazikutoka kuashiria hakuna kitu katika magazini yake.
"Ha! ha! ha! safi na leo ndio utanifahamu." Alionge Simon Jacob huku akimfuata Frank polepole.
Walipokaribiana alimtishia Frank kumrushia ngumi ambayo Frank aliiona na kuikwepa huku akiruhu ngumi halali iingie vilivyo katika upande wa kushoto wa tumbo lake ambayo ilirushwa kwa ustadi na Simon. Alipougundua mchezo ule ndipo akajipanga kwani Simon alionekana ni hatari kuliko yeye. Simon alitoa kisu chake na kukiweka sawa ili amuue Frank kwa kifo cha ajabu na hapo ndipo akaanza kumtishia kumchoma huku akimchapa mateke yaliyomuingia vizuri Frank ambae alikuwa akiwaza kukwepa kisu.
Professa Mataba alikuwa akiangalia tu kwani kazi utazamaji ilimfaa zaidi huku akifurahi pale Frank alipopigwa.
'France kick' au teke la Kifaransa ndilo lililomzindua na kumrudisha kwenye hali ya kupambana kwani lilimtupa mbali na kumuumiza. Aliinuka na kujipanga vilivyo huku akimaubiria Simon, chotara wa kizungu. Mara baada ya Simon kumkaribia alirusha ngumi nzito ya mkono wa kishoto nae Frank akaiona na kuikwepa kisha akaachia yake kwa spidi zote iliyoelekea katika kwapa la kushoto la Simon na kuuruhusu mkono uteguke.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Aoooghh.." Alilalamika Simon baada ya kuteguka kwa mkono wake wa kushoto. Frank hakutaka kuongea sana hivyo aliruka juu na kuachia tekw lililompata Simon usoni na kumfanya apepesuke. Alipoona haendi.chini ndipo akaanza kumpelekea ngumi za haraka haraka na kumfanya Simon ashindwe kuziona zote. Alipoona amefanikiwa kumchanganya alimkanyaga mguu mmoja kisha akamsukuma huku akiutengua mguu wake na kumfanya Simon apige kelele.
"Aaaah!!"
Hakumpa nafasi alimtupia na 'Double kick' kumsindikiza nalo. Alianguka chini nae hakuwa mbali alimkanyaga kifua na kumfanya ateme damu. Kisha alimkanyaga shingo na kuivunja kabisa huku Professa Mataba akiangalia na macho yamemtoka. Alianza kumfuata Professa Mataba huku akimuandalia ngumi nzito. Lakini kabla hajamfikia Professa alitoa bastola yake ambayo alikuwa ameisahau kutokana na uoga na kumnyooshea Frank. Hapo kidogo tabasamu la kunusurika lilimjia kwani alivuta kifyatulio na kuruhusu risasi mbili zilizompiga Frank begani na kumrusha hadi chini.
"Ha! ha! ha! ha!! nilikwambia kijana." Alijitapa Professa Mataba huku akiikoki tena bastola yake ili kuweka risasi chemba na kuilengesha kichwani mwa Frank.
"Paah!! paaah!! paah!!" Ulikuwa mlio wa risasi tatu zilizomfanya Frank afumbe macho kwani alijua ule ndo mwisho wake. Lakini wakati amefumba macho alisikia kishindo cha mtu akidondondoka chini. Alipofumbua aliuona mwili wa Professa ukiwa pembeni yake huku Davis Leonard akiingia na kuugusa mwili wa Professa kama yuko hai. Alikuwa amempiga risasi ya kichwa na kuuta uhai wake palepale. Kisha alimfuata Frank ambaye alikuwa pale chini ametulia.
"Kazi imekisha sio". Aliuliza Frank.
"Naam kaka..." Alijibu Davis huku akiwa ameishikilia bunduki yake.
"Safi......" Alimalizia na kuzimia kwani alivuja damu nyingi pale chini.
MIEZI MITATU.... Baadae.
Mara baada ya kutoka hospitalini ndipo alikafanyiwa sherehe kubwa huku Mheshimiwa Rais akiwepo katika kumpongeza Luteni Kanali Frank Mapungo na hapo ndipo watu wengine wakamfahamu vyema Joachim Bartazar kuwa alikuwa na cheo kikubwa Jeshini.
Luteni Kanali Frank Mapungo akapandishwa cheo na kuwa Kanali Frank Mapungo huku Sauda Mansoor nae akiwa kama Kapteni. Alipatiwa nyumba yeye pamoja na Sauda huku nae Davis akipatiwa nafasi ya kufanya mafunzo ya Uluteni.
Hakutaka kumsahau Doris alipanda ndani ya gari yake mara baada ya kupita siku kadhaa. Alipofika alishuka na kugonga getini. Hazikupita dakika nyingi mlango ulifunguliwa na mlinzi akatoka na kukutana na Frank aliyevaa nguo za kazi huku akiwa amechafuka kwa vyeo na nishani mbalimbali.
"Karibu mzee, sijui nikusaidie nini?" Aliongea yule mlinzi kwa uwoga kutokana na kuogopa gwanda za kijeshi tena huyu alionekana ana cheo kikubwa.
"Tafadhari naomba kuonana na Doris." Aliongea Frank.
"Ngoja nimuite."
"Nahitaji kuingia ndani."
"Ah!! karibu ndani." Alidakia huku akiogopa.
Frank aliingia ndani huku akimsubiria Doris sebuleni mara baada ya kuingia ndani kabisa. Doris alipotokea ndani alikutana na Frank ambaye yeye alimfahamu kama Joachim. Lakini sasa alikuwa mtu tofauti kwani alikuwa kavaa nguo za kijeshi tena mwenye cheo huku kifuani pake akiwa na beji yenye jina tofauti na analolifahamu 'F.J.Mapungo'.
"Joachim!!" Aliduwaa Doris.
"Naam." Aliitikia Frank.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ulikuwa wapi muda wote... na hizi nguo?" Alitupia swali juu ya swali.
"Naitwa Frank Mapungo.... Joachim lilikuwa jina la kazi."Aliongea Frank na kumfanya Doris ashangae.
Hapo ndipo alipoelewa nini maana ya yale yote yaliyotokea. Waliongea mengi kisha akaaga na kuondoka. Alirudi na kukutana na Sauda ambaye tayari walikuwa wameanza mahusiano na kuelekea katika nyumba ambayo walikuwa wamechagua kuishi pamoja.
*MWISHO*
0 comments:
Post a Comment