Simulizi : Balaa
Sehemu Ya Pili (2)
Usiku
uleule Tano alirudi Kilwa Kivinje. Kuendelea na kazi yake ya ulinzi pamoja
kumuwinda Dr Yusha. Maana usiku wa siku hiyo pia, ilikuwa lazima waipata mioyo
kumi na tano katika chumba cha kuhifadhia maiti. Alifika Kivinje mishale ya saa
tano usiku. Na kuikuta kazi ya kutoa mioyo
imeshaanza.
Asubuhi mji wa Kilwa Masoko uliamka na
taarifa mbaya tena. Taarifa ya kifo cha Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya
Kilwa, Ndugu Alex Mwasola. Mwasola alikutwa ameuwawa nyumbani kwake. Muuza
maziwa ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kushuhudia maiti ya Mwasola. Alikuwa na
ratiba ya kumpelekea maziwa kila siku. Siku hiyo aligonga sana mlango nje,
aliposukuma mlango ulifunguka na alipoingia ndani, alilakiwa na maiti ya bosi
wake. Mwili wa Mwanasheria Mwasola, umelala juu ya sofa huku ukiwa umetapakaa
damu kifuani. Alirudi nyuma na kuondoka bila kuaga. Hakumsimulia mtu kuhusu
tukio lile, muuza maziwa aligeuka bubu.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Halmashauri ya
wilaya ya Kilwa, katika ofisi ya Mwanasheria watu walikuwa wamejaa. Ilikuwa siku
ya kazi kwahiyo watu walijaa kufata huduma katika ofisi hiyo, watu wengi
walikuwa wamekaa nje ya ofisi hiyo kwa kadri ya saa tano, bila Mwanasheria
kutokea. Walijaribu kumpigia simu lakini simu yake iliita bila kupokelewa.
Bahati mbaya Mwasola alikuwa hajaoa na wala hakai na mtu yeyote nyumbani kwake.
Ilibidi atumwe mlinzi kwenda kwa Mwanasheria kumwangalia. Ilipo ofisi ya
mwanasheria na mtaa wa National hakukuwa mbali sana. Yule mlinzi aliyetumwa kwa
Mwanasheria alikutana na balaa.
Picha mbaya kama aliyokutana nayo
Muuza maziwa. Mwili wa Mwanasheria ukiwa umelala sofani huku kisu kikiwa
kinaning'inia kifuani mwake, na damu zilizoanza kukauka kifuani. Yule mlinzi
alishindwa kuvumilia, alipiga makelele, makelele yaliyowajaza kwa kasi
majirani.
Walimkuta Mwanasheria
ameuwawa!
Illikuwa majonzi na kilio kikubwa sana kwa
majirani.
Baada ya muda mfupi, askari Polisi waliwasiri.
Haikujulikana hata ni nani aliyewapigia simu Polisi hao.
Walianza
kufanya uchunguzi mle ndani, baadae wakauchukua mwili wa Mwanasheria na
kuupeleka hospitali kwa ajili ya uchunguzi
zaidi.
Muda mfupi tu habari za kifo cha
Mwanasheria zikasambaa Kilwa nzima. Zilisambaa mpaka kilabuni na kumfikia
Mwanasheria mlevi.
Taarifa za kuuwawa kwa
Mwanasheria zilimstua sana Mwanasheria mlevi. Alilala kilabuni siku ile
Mwanasheria. Na aliyemletea taarifa za mauaji hayo ni rafiki yake kipenzi katika
ulevi, mama Kindumba.
"Mwanaaa" Mama kindumba
aliita kilevi huku akifupisha jina la Mwanasheria.
"Nambie mama
kindumba" Mwanasheria nae aliitikia kwa sauti ya kilevi pia.
"Umesikia
wajina wako kauwawa!"
"Nani
tena?"
"Mwanasheria"
"Mama kindumba unaumwa nini,
Mwanasheria si mimi hapa" "Mwanasheria wa ukweli bana"
"Unaamaanisha
Bwana Mwasola?"
"Ndiyo huyo huyo"
"Haaaa!"
"Ndo
hivyo wamemkuta kapigwa bonge la kisu nyumbani kwake"
"Aisee, lakini
poa bora nibaki Mwanasheria peke
yangu"
Mwanasheria mlevi alitia mzaha
uliomchekesha kila mtu pale kilabuni. Bila kujua balaa iliyoko ndani
yake..
"Ngoja nimpigie Dokta Yusha alikuwa rafiki yake
sana"
Simu hiyo ya Mwanasheria kwenda kwa Dokta
Yusha ilizua kizaazaa kipya..
Walimkuta
Mwanasheria ameuwawa!
Illikuwa majonzi na kilio kikubwa sana kwa
majirani.
Baada ya muda mfupi, askari Polisi waliwasiri.
Haikujulikana hata ni nani aliyewapigia simu Polisi hao.
Walianza
kufanya uchunguzi mle ndani, baadae wakauchukua mwili wa Mwanasheria na
kuupeleka hospitali kwa ajili ya uchunguzi
zaidi.
Muda mfupi tu habari za kifo cha
Mwanasheria zikasambaa Kilwa nzima. Zilisambaa mpaka kilabuni na kumfikia
Mwanasheria mlevi.
Taarifa za kuuwawa kwa
Mwanasheria zilimstua sana Mwanasheria mlevi. Alilala kilabuni siku ile
Mwanasheria. Na aliyemletea taarifa za mauaji hayo ni rafiki yake kipenzi katika
ulevi, mama Kindumba.
"Mwanaaa" Mama kindumba
aliita kilevi huku akifupisha jina la Mwanasheria.
"Nambie mama
kindumba" Mwanasheria nae aliitikia kwa sauti ya kilevi pia.
"Umesikia
wajina wako kauwawa!"
"Nani
tena?"
"Mwanasheria"
"Mama kindumba unaumwa nini,
Mwanasheria si mimi hapa" "Mwanasheria wa ukweli bana"
"Unaamaanisha
Bwana Mwasola?"
"Ndiyo huyo huyo"
"Haaaa!"
"Ndo
hivyo wamemkuta kapigwa bonge la kisu nyumbani kwake"
"Aisee, lakini
poa bora nibaki Mwanasheria peke
yangu"
Mwanasheria mlevi alitia mzaha
uliomchekesha kila mtu pale kilabuni. Bila kujua balaa iliyoko ndani
yake..
"Ngoja nimpigie Dokta Yusha alikuwa rafiki yake
sana"
Simu hiyo ya Mwanasheria kwenda kwa Dokta
Yusha ilizua kizaazaa kipya.
"Hallo Dokta Yusha
"
"Nambie Mwanasheria"
"Una taarifa za msiba
Dokta"
"Nani tena amefariki Mwanasheria?"
"Mwanasheria
Mwasola ameuwawa!
" Acha utani Mwanasheria, Mwasola ameuwawa!
"
"Kachomwa kisu Dokta"
"Etiiiii"
"Ndiyo hivyo
Dokta"
"Nakuja Masoko sasa hivi, ahsante sana kwa taarifa
Mwanasheria"
Simu ikakatwa.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Dokta Yusha
aliipokea simu ile akiwa katika benchi la wagonjwa. Lakini mtu wa pembeni yake
hakuwa mgonjwa, alikuwa ni Tano wa Six killers, katika harakati zake za
kumuwinda Dokta Yusha. Alisikia kila kitu alichoongea Dokta Yusha, huku
akishangazwa na taarifa kwamba Mwanasheria kauwawa ilhali Dokta alikuwa anaongea
na Mwanasheria.
Dokta Yusha alinyanyuka pale
kwenye benchi, akiwa na Lengo la kwenda Kilwa Masoko kwenye msiba. Alipanda gari
yake na kuondoka bila ya kujua kama kuna mtu alikuwa anamfata nyuma kwa kutumia
pikipiki. Sasa Tano aliamua kuumaliza mchezo, kumuua Dokta Yusha kisha kwenda
Kilwa Masoko kumuua huyo Mwanasheria mpya!
Hii inaitwa LIWALO NA LIWE!
Tano aliona mchezo unaelekea kubaya, aliamua kuumaliza
leo!
Walipofika karibu na kijiji cha Mpara gari la
Dokta Yusha lilipata tatizo la kiufundi, lilizima ghafla na kusimama. Ilikuwa
bahati mbaya kwa Dokta Yusha..na bahati nzuri sana kwa Tano wa Six
killers
Dokta Yusha alisimamisha gari. Na kuanza
kulikagua, Tano nae alisimama pale na pikipiki yake.
Hatari ilikuwa
inamkaribia Dokta Yusha!
"Vipi tena kaka" Tano
aliuliza huku alimsogelea Dokta Yusha.
"Gari linanisumbua kidogo"
Dokta alijibu huku akilichungulia gari lake kwa chini,
uvunguni.
"Ngoja nikusaidie
kidogo"
"Sawa"
Dokta Yusha alifanya
kosa, kukaribiana na Tano, tena wakiwa wawili porini lilikuwa ni kosa kubwa
sana. Tano hakuelekea kwenye gari, Tano alimfata Dokta Yusha pale chini. Dokta
Yusha alimtazama yule jamaa na kuingiwa na woga kidogo, alishangaa jinsi ya yule
dereva pikipiki alivyokuwa anamfata kwa kasi, tena kishari!
Dokta
Yusha nae alisimama, alijipanga kwa shari
yoyote.
Tano alitoa kitu kwenye mfuko wa ndani wa
koti, ilikuwa bastola!
Sasa Dokta Yusha hakuwa na mshangao tena,
alikuwa makini. Kitu ambacha Tano alikuwa hajui, Dokta Yusha alikuwa amepitia
mafunzo ya uaskari kabla ya kuwa dokta, mafunzo ya uaskari magereza huko Kiwira,
Mbeya. Na kufanya kazi kama askari magereza mkoani Mtwara. Dokta Yusha hakuwa
mgeni kuitumia bunduki, hakuwa mgeni wa kutazamana na bastola. Ndio maana
bastola aliyooneshwa na Tano haikumtisha kabisa, zaidi ilimuongezea
umakini.
Tano yeye alimchukulia Dokta Yusha kama
raia wa kawaida, raia ambaye atatetemeka baada ya kuoneshwa bastola, au labda
atajikojolea baada ya kuona bastola ikimuelekea usoni mwake.
Lakini
haikuwa hivyo kwa Dokta Yusha!
Tano na Dokta Yusha
walikaribiana sana, Tano alifanya kosa la kiufundi, alimkaribia sana Dokta Yusha
na ukaribu ule ulizua jambo!
Dokta Yusha
alirudisha nyuma mguu wake wa kulia, na kuuleta mbele kwa kasi na nguvu kubwa
sana!
Mtindo wa kuupeleka mguu namna ile huitwa teke!
Teke
lile la Dokta Yusha lilifika ulipokuwa mkono wa Tano ambao ulikuwa umeshika
bastola, bastola ilisukumwa kwa kasi na kujisweka pembeni ya barabara. Sasa
Dokta Yusha na Tano walibaki mikono mitupu, wakitazamana kama
majogoo.
Tano alitabasamu, alifurahi sana na
ujanja aliouonesha Dokta Yusha, alimuona kama amejipalia mkaa wa moto, Tano
alijiweka vizuri kimapambano!
Dokta Yusha naye
hakutetereka, hakutetemeka, alimwangalia jinsi Tano alivyosimama na kupanga
ngumi, yeye alikuwa amesimama tu kawaida.
Tano alimfata Dokta Yusha
kwa kasi kwa teke lilikuwa linaelekea tumboni kwa Dokta Yusha, kwa kasi ya ajabu
Dokta Yusha alijisogeza pembeni kidogo, kukwepa lile teke. Tano akapita kwa kasi
na lile teke lake hadi pembeni mwa barabara kwenye nyasi fupi. Tano alisimama
tena huku akiwa amefura kwa hasira, kukwepa vile na Dokta Yusha ilikuwa ni
dharau kubwa sana kwake, akajipanga tena upya, kwa bahati mbaya alikuwa
anaongozwa na hasira. Ni kosa kubwa sana katika mapambano kuongozwa na
hasira.
Dokta Yusha alicheka kwa sauti kubwa kwa
dharau, alicheka kwa lengo la kuzidi kumtoa Tano wa Six killers mchezoni, na
kweli kicheko kile kilipokelewa tofauti kabisa na Tano muuaji, kicheko
kiliibadirisha ile hasira ya Tano na kuigeuza kuwa jazba!
Dokta Yusha
alifanya vile makusudi, kwa jinsi alivyomuona amesimama Tano na jinsi
alivyopanga ngumi, alijua Tano siyo wa kiwango chake. Tano alikuwa mahiri zaidi
yake. Sasa alikuwa anatumia mbinu ya kumpandisha hasira Tano ili apoteze
umakini, huku yeye akifikiria namna ya kujiokoa na alifanikiwa tena kwa
hilo!
Tano alifura kwa hasira na jazba ya hali ya
juu. Moyoni mwake kulikuwa kunafukuta!
Alirusha
ngumi kwa mkono wake wa kulia, ngumi ya nguvu iliyorushwa na mtu mwenye nguvu,
Dokta Yusha alijaribu kuikwepa, lakini hakufanikiwa kuikwepa yote, mkwaruzo wa
ngumi ile ulimpata kidogo katika sehemu ndogo ya mbavu ya kushoto, alisikia
maumivu kidogo, lakini hakutaka kuonesha kama alisikia maumivu, Tano hakusubiri,
ngumi ya kushoto sasa ilikuwa inaelekea katika mwamba wa pua wa Dokta Yusha, kwa
kasi na umakini Dokta Yusha alifanya mambo mawili ya kustaajabisha
sana...
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Dokta Yusha,
aliikwepa ile ngumi, huku nae akipiga ngumi yake kwa nguvu iliyotua barabara
katika mbavu za Tano!
Tano hakuamini kasi aliyoitumia Dokta Yusha
kukwepa ngumi ile, pia hakuamini uzito wa ngumi wa Dokta Yusha, sasa tano akajua
anapambana na mtu anayejua anachokifanya. Hakujiuliza tena, sasa aliamua kupiga
mapigo ya kifo, mapigo ambayo yakimgusa mpigwaji yanaondoka na roho
yake....Balaa!
Tano alianza na teke lilikwenda kwa kasi kama umeme,
teke liliombatana na uzito wa kilo kadhaa. Dokta Yusha aliliona teke lile, teke
liliolekezwa shingoni kwa lengo ya kuondoka na shingo yake, aliinama kidogo,
teke likapita, ila upepo wa teke lile ulimyumbisha Dokta Yusha na kumdondosha
chini, akiwa amelala pale chali, tano aliruka juu na kushuka chini huku akiwa
amekitanguliza kifuti cha mguu wake wa kushoto, kifuto kilichoelekezwa katika
upande wa kushoto wa kifua dokta Yusha, pale unapokaa moyo!
Dokta
Yusha alijisogeza kidogo pale chini akiwa amelala vile vile, na kifuti cha dokta
Yusha kutua katika lami, nguvu iliyoambatana na kifuti kile, na kutua kwenye
lami ngumu, goti la Tano liligeuka palepale!
Tano alitoa ukelele
mkubwa sana. Dokta Yusha alisimama na kwenda pale alipolala Tano huku akiwa
amelishikia goti lake.
Dokta Yusha alijisachi mfukoni, na kutoa simu
yake ya mkononi. Aliitafuta namba ya OCD ya kilwa, na kumpigia. Alimuelekeza
kila kitu kilichotokea pale barabarani, na OCD alimwambia kwamba watafika askari
pale baada ya muda mfupi.
Tano hakuwa na ujanja
wowote, alikaa pake huku akilia, akisubiri hatma yake, mambo yalikuwa
yameshaharibika.
Baada ya muda mfupi gari la
polisi lilifika, likiwa na askari polisi sita waliovaa sare zao safi za jeshi la
Polisi, wakiwa imara na bunduki mkononi kila mmoja. Walimbeba Tano na kumpakia
nyuma ya gari ile ya Polisi. Dokta Yusha alipanda mbele ya gari ile, na safari
ya kuelekea kituo cha polisi Masoko
ilianza.
Dakika kumi zilitosha kuwafikisha askari
wale wakiwa na Tano wa Six Killers katika kituo cha Polisi cha Masoko. Askari
wawili walimshusha Tano msobemsobe, hawakujari kabisa makelele yake aliyokuwa
anayapiga kutokana na maumivu akiyoyapata kutoka na maumivu ya kwenye goti. Kwa
bahati mbaya askari wale hawakuwa na huruma kwa Tano, kwa kuwa hawakuwahi
kufundishwa kumuonea huruma Mhalifu katika mafunzo huko chuoni
Moshi.
Tano aliingizwa ndani ya kituo cha Polisi tayari kwa kuanza
kuhojiwa.
Na alivyowekwa tu katika sakafu ya
Polisi alikumbana na maswali mfululizo toka kwa askari wale. Kila askari alikuwa
anauliza swali lake kwa sauti kubwa na ukali.
Tano alihisi kama
wanampigia kelele, hakujibu kitu, alinyamaza
kimya!
Dokta Yusha yeye aliitwa ofisini kwa mkuu
wa upepelezi Wilaya. Alieleza kila kitu kilichotokea tangu alipopokea ile simu
ya Mwanasheria mlevi. Simu iliyomtaarifu juu ya msiba wa Mwanasheria wa
Halmashauri ya wilaya ya Kilwa, nae kuamua kwenda kilwa Masoko kwenye
msiba.
Dokta Yusha alivyomaliza maelezo yake tu
hapohapo wakatumwa askari kwenda kumkamata Mwanasheria. Mkuu wa upelelezi wa
wilaya alihisi Mwanasheria mlevi anahusika na mbinu zile chafu!
Askari
walewale waliomleta Tano waliingia tena kazini kumtafuta Mwanasheria mlevi
popote alipo
Mwanasheria bado alikuwa kilabuni,
hana hili wala lile. Alikuwa anakunywa pombe huku akiongea neno kila linalomjia
kichwani mwake. Bila kujua kama askari sita wenye silaha walikuwa njiani
wanaelekea pale kilabuni kumkamata yeye, akituhumiwa kupanga mauaji ya Dokta
Yusha! Ghafla! Vumbi lilitimka pale kilabuni, gari ya Polisi lilifunga breki
kali sana! Askari walikuwa wameshuka kabla hata ya breki ile. Walishuka kwa
mbwembwe na bunduki zao mikononi. Walevi walitimka mbio, pombe zote ziliwatoka
vichwani. Mwanasheria mlevi hakusogea hata hatua moja, alikuwa ameshazungukwa na
askari polisi watatu. Midomo ya bunduki ikielekezwa kichwani kwake! Mwanasheria
hakuwa jasiri kama Dokta Yusha, yeye alikuwa anatetemeka, hakuweza kuuzuia
kabisa mkojo usimtoke. Kuelekezwa bunduki kichwani kwake ? Alikosa la kusema,
askari walimuamuru asimame, na kumuelekeza pa kuelekea, ndani ya gari ya Polisi.
Alifika ndani ya gari, na kukaa chini bila kuambiwa..machozi yalimtoka na
kudondoka katika sakafu ya bodi ya gari ile. Askari hawakulijari lile chozi,
hawakuwa na muda wa kulijari chozi la Mhalifu, walidandia gari na kuondoka kwa
kasi kubwa sana, safari kituo cha Polisi Masoko. Laiti wangemjua Mwanasheria
mlevi... Walipofika kituo cha Polisi, Polisi hawakuuliza, ilikuwa ni mateke,
ngumi na vifuti kwa Mwanasheria mlevi. Polisi walikuwa wanampiga Mwanasheria
bila kujua kwanini wanampiga, na Mwanasheria nae hakujua kwanini anapigwa!
Mwanasheria alipoteza fahamu kituo cha Polisi. Wote wawili Tano na Mwanasheria
walipelekwa kituo cha afya Masoko, chini ya ulinzi mkali sana wa askari Polisi.
Kama ilivyo kawaida katika hospitali nyingi Tanzania, wahalifu huwa hawapati
huduma nzuri pindi wanapoumwa. Labda kwa kuwa wanakuwa hawana wauguzi wa kuwapa
pesa wagonjwa( hongo). Hali hiyo iliwakuta Tano na Mwanasheria pale kituo cha
afya Masoko. Waliachwa wamelala katika vitanda vyao wakiwa na pingu zao
mikononi. Saa kumi na mbili jioni, Mwanasheria alizinduka, ni kudra za Mungu tu
ndizo zilimuasha. Mwanasheria hakupata huduma yoyote ile pale kituo cha afya.
Mwanasheria aliamka na maneno yake, Mwanasheria aliamka na lawama za kutosha,
lawama kwa Polisi, lawama kwa Serikali, lawama kwa mfumo mzima wa nchi, lakini
lawama hazikusaidia, ukweli ulibaki palepale, Mwanasheria alikuwa amelala
kitandani akiwa hoi bin taaban na pingu zake kitandani ! Tano wa Six killers
naye alikuwa katika wakati mgumu sana, mguu wake ulikuwa umeumia vibaya sana,
alikuwa anagugumia kwa maumivu. Lakini hakuwa na jinsi, alikuwa amelala katika
kitanda kidogo cha kituo cha afya akiwa dhooful hali, huku akiwa hana namna ya
kuwapigia wenzie ili awataarifu kwamba alikuwa mahali pale, kwa kuwa simu yake
ilikuwa katika kituo cha Polisi.
***** CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kundi la Six
Killers walikutana kwa kikao cha dharura. Kikao kilichokuwa kinaongozwa na Don
Genge mwenyewe, kikiwa na ajenda kuu mbili. Ajenda ya kwanza ilikuwa ni
makabidhiano ya mioyo kumi na tano iliyopatikana kwa siku ile ya pili. Mambo
yalienda sawa, na Dokta Sharifa alikabidhi deli kubwa jekundu lenye mioyo kumi
na tano. Ajenda ya pili, ilikuwa inahusu kutoonekana kwa Tano. Masaa zaidi ya
sita, Tano alikuwa hajaonekana, na simu yake ilikuwa haipatikani! "Hii ni siku
ya tatu ya Mpango huu, kwa asilimia 90 mpango wetu umeenda sawa, lakini Kwa
bahati mbaya sisi hatufanyi kazi kwa asilimia 90. Huwa tunafanya kazi kwa
asilimia 100, au zaidi ya hizo ikiwezekana. Tano hajulikani alipo, na hizo ndio
asilimia 10 tulizozipoteza. Natoa masaa mawili, Tano akiwa hai au amekufa mwili
wake uwe hapa!. Baada ya masaa hayo mawili, tutaenda kutoa mioyo tukiwa na Tano
kama atabahatika kuwa hai, mmebaki wa tano, hakikisheni mnarudi na Tano! Mnaweza
kwenda..." Six killers walitoka mle ndani kwa lengo kuu moja, kwenda kumtafuta
muuaji aliyepewa namba Tano.
Mbili alitoka nje, na
kukutana na Sita. Walijipanga vizuri kwenda kumtoa Tano katikati ya maaskari
wawili wenye bunduki!
Askari hawakuwa kizuizi
kabisa kwa Mbili, bunduki hazikuwa tishio kabisa kwa Mbili. Alipewa namba mbili
katika kundi la Six killer's kwa kuwa alikuwa mahiri kuliko wanakikundi wanne
waliobakia. Wakiwa na Sita, walijiandaa kwa
uvamizi.
Kule ndani Mwanasheria alikuwa anaendelea
kuongea kama ilivyo ada yake. Askari Polisi walijaribu kumnyamazisha bila
mafanikio yoyote. Kilabu sasa kilihamia katika kituo cha afya. Makelele yale
yale ya Mwanasheria yalichangia kwa kiasi kikubwa kupunguza umakini kwa askari
wale wawili. Wote walikuwa wanajitahidi kumnyamazisha Mwanasheria na kusahau
kabisa suala la ulinzi.
Mbili na Sita walikuwa
nje ya wodi ile. Walisikia kila kitu kilichokuwa kinaendelea kule ndani.
Walijipanga vizuri.
Moja, mbili taaaaa.....wote
kwa pamoja waliukumba ule mlango wa wodi kwa kutumia miili yao ya kimazoezi na
wote kujikuta wako ndani. Kila mmoja kwa namna yake na bastola zao
mkononi.
E bwana
weee!
Mbili alijiviringisha kwa mtindo wa sarakasi
na kujificha nyuma ya kitanda alicholala Tano huku akibonyea kidogo ili kile
kitanda kimfiche, Sita nae alijiviringisha kwa kasi na kumfikia moja kwa moja
askari mmoja na kumkaba shingoni, huku akimtumia kama ngao!
Huku
bastola yake ikimtazama yule askari mwengine. Askari wote wawili waliwahiwa
vizuri sana. Yule askari aliyepigwa kabali ilinasa kisawasawa, alijaribu kujitoa
bila kutegemea, huku yule askari mwengine aliyeoneshwa bastola hakuwa na lolote
la kufanya, alibaki ameganda kama sanamu. Six Killers walihamishia balaa
wodini.
Ghafla! Yule askari aliyesimama alijishika
kifuani, kulikuwa na majimaji mekundu, damu! Bastola ya Mbili yenye kiwambo cha
kuzuia sauti ilikuwa imefanya kazi iliyotumwa. Yule askari aliyesimama alikuwa
amepigwa risasi takatifu ya kifua. Aliyumba kidogo huku akipiga kelele, na
kudondoka chini mzimamzima kisogo kikitangulia kufika chini !
Askari
alikuwa mfu zamani sana kabla hata hajaigusa sakafu ya
hospitali.
Sita naye aliongeza nguvu katika ile
kabari, yule askari alikosa pumzi, nguvu zikamuishia, alilegea. Sita alimuachia
yule askari, akadondoka chini. Vitendo vyote vilivyokuwa vinatokea Mwanasheria
mlevi na Tano walikuwa wanashuhudia kila kitu,
kimyakimya.
Wakati Tano akiufurahia ujio wa watu
wale wawili aliokuwa anawafahamu vizuri sana, Mwanasheria mlevi alikuwa katika
mshangao mkuu, hakutegemea wala kuelewa kinachotokea mle ndani
wodini.
Mbili na Sita walikisogelea kitanda
alicholala Tano. Waliliangalia lile jeraha kubwa la Tano pale mguuni, wote
walimuonea huruma. Walimbeba na kutokomea nae
kusikojulikana!
Baada ya robo saa kutokea kwa
tukio lile, mganga wa kituo cha afya Masoko aliingia katika wodi
ile.
Mganga alikutana na Balaa !
Miili ya askari wawili
ilikuwa imelala chini, ikiwa haina uhai. Na mwili wa mgonjwa mmoja ukiwa haupo
huku mwili wa Mwanasheria mlevi ukiwa juu ya kitanda, ukiwa umeloa jasho, hakika
Mwanasheria aliyaona matukio ambayo hakutegemea kuyaona katika maisha yake.
Alikuwa anatetemeka huku anatoa jasho!
Daktari
hakuamini kabisa madhara yaliyotokea mle wodini. Alijishika kichwa huku akipiga
kelele za kuomba msaada. Ndani ya dakika chache manesi na baadhi ya watu
waliokuja pale hospitali walijaa katika wodi ile. Kila mmoja alistaajabu
kilichotokea mle ndani, ilikuwa ni balaa !
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nesi mmoja alipiga
simu kituo cha Polisi kuwataarifu juu ya mauaji yale. Askari waliwasili baada ya
muda mfupi sana, na kushuhudia unyama mkubwa waliofanyiwa askari wenzao. Huku
Mwanasheria mlevi akiwa ni shuhuda pekee aliyeshuhudia kila kitu. Nusu saa
baadae, kundi hatari la Six Killers walikutana tena na bosi wao. Ilikuwa ni
furaha kubwa sana kwao, kuitekeleza kazi ile ya masaa mawili kwa nusu saa tu.
"Hongereni sana vijana wangu, mmefanya kazi kwa haraka sana, ila sina uhakika
kama mmeifanya kwa umakini ninaouhitaji" Don Genge alikuwa anaongea huku
akiwaangalia Mbili na Sita usoni. "Hakika tumefanya kazi kwa umakini mkubwa mno
Bosi" Mbili alijibu kwa kujiamini. "Mmeua watu wote waliowashuhudia? Kuanzia
huyo askari aliyekupeni siri mahali alipo Tano, Mganga mkuu pamoja na huyo
mgonjwa aliyelazwa pamoja na Tano?" Mbili na Sita waliangaliana usoni,
waligundua kuwa walikuwa wamefanya kosa! "Tumefanya kosa, dakika kumi" Mbili
alijibu kibabe. "Naongeza kumi na tano" "Sawa mkuu" Waliondoka. Walikuwa
wamepewa dakika kumi na tano kuhakikisha yule askari aliyewapa siri, Mganga mkuu
na Mwanasheria mlevi wanauwawa! Kundi zima sasa kasoro Tano tu walinyanyuka na
kuingia tena kazini. Dakika kumi baadae kundi zima la Six Killers lilikuwa
limerejea tena. Wakiwa wamefanikisha kuwauwa watu wawili kati ya wale watatu.
Askari na mganga mkuu walikuwa wameelekea kuzimu kwa mtindo tofauti, wakati yule
askari aliuwawa kwa bastola nyumbani kwake, Mganga mkuu wa hospitali aliuwawa
kwa kisu ofisini kwake. Wote wakiwa hawajawahi kutumia hata senti tano katika
zile laki moja walizokuwa wamepewa. Tatizo lilikuwa kwa Mwanasheria mlevi,
walienda mle wodini hawakumkuta yule mgonjwa, na kwa bahati mbaya hawakuwa
wameishika kabisa sura yake. Lilikuwa kosa la kubwa sana walilolifanya wauaji
wale wazoefu. Askari Polisi sasa walikuwa wanamlinda Mwanasheria mlevi kupita
kiasi. Jeshi la Polisi hawakuwa wanajua kabisa kama kuna watumishi walihusika
katika kutoa siri, na kupokea hongo kutoka kundi la Six Killers. Nusu saa baadae
taarifa mbaya zikalifikia jeshi la Polisi. Taarifa mbaya za vifo ! Kifo cha
Sajenti Alex Omolo wa kituo cha Polisi Masoko, na kifo cha daktari Mosha
Gabriel, Mganga mkuu wa kituo cha afya Masoko. Askari walitapakaa mtaani
kuwasaka watu waliowauwa Afande Alex Omolo na Dokta Mosha Gabriel. Askari
walifanya msako kimyakimya. Lakini ilikuwa kama wanawatafuta watu ambao
hawakuwahi kuwepo duniani. Msako wao haukuwasogeza kabisa karibu ya Muuaji!
Wakati askari wakimwagika kama njugu huko Kilwa Masoko kuwatafuta watu
waliowauwa Afande Alex na Dokta Mosha, Kundi hatari la Six Killers walikuwa wapo
njiani kwenye gari wakielekea hospitali ya wilaya Kilwa Kivinje huku wakilaumiwa
vibaya mno na Don Genge kushindwa kumuua mgonjwa aliyewashuhudia wakati
wanafanya mauaji. Ilikuwa ni lawama nyingi sana, kundi zima walikuwa kimya
wakati Don Genge akifoka! "Six killers huwa hatufanyi makosa. Kosa lolote
inamaanisha kujiweka katika hali ya hatari, na mipango yetu kukwama. Ona sasa,
yule Dokta mpumbavu bado anaishi, yule mgonjwa mpumbavu bado anaishi. Ni makosa
haya, Dokta mpumbavu anamfahamu Tano, Mgonjwa mpumbavu anawajua Mbili na Sita.
Ni makosa makubwa sana, lazima wafe!" Kundi la Six Killers walimwacha Tano
katika nyumba yao iliyokuwa kama kambi ya muda mfupi huko Ngome, akipatiwa
matibabu na daktari waliyemkodi. Wao walikuwa wanaenda Kilwa Kivinje kufanya
kazi yao hatari! Ya kutoa mioyo ya wagonjwa kumi na tano kama ilivyo
ada.
Ingawa askari Polisi walimtaka Dokta Yusha
akae pale kituo cha Polisi kwa usalama wake. Lakini Dokta Yusha hakukubali
kabisa, Dokta Yusha alipinga katakata. Alikuwa anataka kutoka ili akamzike
rafiki yake Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa, pia alikuwa anataka
arudi hospitali Kilwa Kivinje kuwaona wagonjwa wake. Polisi hawakuwa na jinsi,
walimruhusu Dokta Yusha atoke pale kituo cha Polisi. Katika mtaa wa National,
katika nyumba aliyokuwa anaishi Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa
kulikuwa na umati wa watu mkubwa sana. Watu wengi wakilia kwa uchungu mkubwa
mno, msiba huu ulikuwa msiba mkubwa sana ndani ya Kilwa Masoko. Alivyotoka kituo
cha Polisi, Dokta Yusha alienda moja kwa moja msibani. Alishiriki vizuri kwenye
shughuli za mazishi. Hadi Mwanasheria alivyopumzishwa katika makazi yake ya
milele katika makaburi ya Sanga. Baada ya mazishi, Dokta Yusha alielekea
hospitali Kilwa Kivinje ambako kundi la Six killers Don Genge nao walielekea
huko. Huko wakiwa na mikakati ya kumuua yeye na Mwanasheria mlevi. Kundi la Six
killers walikuwa wamejipanga vizuri sana huko Kilwa Kivinje. Kutokana na
kutokuwepo kwa Tano, ratiba zao zilibadirika kidogo. Kazi ya kumuwinda Dokta
Yusha sasa alipewa Sita. Huku waliobaki walikuwa wanalinda eneo la chumba cha
kuhifadhia maiti ili operesheni yao ya kutoa mioyo iliyotarajia kufanyika usiku
wa siku hiyo iende vizuri. Kwa bahati nzuri siku hiyo ilitokea ajari ya basi
katika kijiji cha Somanga. Ajari ilioua watu thelathini na kujeruhi saba, Six
killers walikuwa na uhakika wa kupata mioyo thelathini ambayo, mara mbili ya oda
yao, bahati ilioje? Saa moja usiku Dokta Yusha alikuwa anaelekea Kilwa Kivinje.
Kwenda kuwaangalia watu aliowapenda sana. Ambao sasa walikuwa wagonjwa, Mkewe
kipenzi Nasra, rafiki wa mkewe, Hasina na mkwe wake. Njiani roho ilikuwa
inamdunda sana, bila kujua kwanini hali ile ilimtokea. Laiti Dokta Yusha angejua
anayoenda kukutana nayo huko basi angeusikiliza moyo wake, Dokta Yusha alikuwa
anaenda kwenye balaa kubwa sana! Na moyo wake uliligundua hilo mapema sana.
Lakini hakuusiliza moyo wake, au labda hakuuelewa moyo wake unamaanisha nini?
Nusu saa ilitosha kumfikisha Dokta Yusha Kilwa Kivinje. Na moja kwa moja alienda
katika wodi waliolazwa wakina Nasra. Hali ya wagonjwa wale wawili ilikuwa
vilevile. Mkewe kipenzi Nasra na rafiki wa mkewe Hasina walikuwa wamelala katika
usingizi ule mbaya, usingizi nzito usiojulikana mwisho wake. Huku Mzee Mpaukha
naye akiwa kalala kwa kujifunika nusu shuka safi ya hospitali, shuka
iliiyoiashia kifuani, uso ukiwa wazi. Dereva alikuwa amejifunika shuka la
hospitali gubigubi sawa na mgonjwa mwengine aliyelala kitanda cha pili toka pale
alikolala dereva. Kumbe jirani yule alikuwa ni Sita wa Six killers, akiwa
amejificha kwa kujifunika gubigubi katika kitanda kimoja katika wodi ile. akiwa
amepania kummaliza Dokta Yusha kabla hajaenda katika jukumu lake lengine la
usiku ule. Dokta Yusha kama kawaida yake alienda kwenye kitanda alicholala mkewe
kipenzi, Nasra, alimwangalia kwa muda mkewe, bado alikuwa katika hali ya kutia
shaka. Alipiga hatua chache na kukisogelea kitanda cha Hasina, nae alikuwa
taabani kwa ajari ile. Alisogea tena hadi kitanda alicholazwa Mzee Mpaukha, Mzee
Mpaukha alikuwa amelala, hakutaka kumsumbua, alimshuhudia akipumua vizuri.
Alikiangalia kitanda alicholazwa dereva wa Mzee Mpaukha, alimwona amejifunika
gubigubi. Alikisogelea taratibu kile kitanda, alikuwa anasogea Huku akiiona kuwa
kitanda cha pili kutoka kitanda cha dereva Musa nacho kulikuwa na mgonjwa
aliyejifunika gubigubi kama Musa, alipanga kwenda kumwangalia nae, bila kujua
dhamira mbaya ya mgonjwa aliyelala kitanda kile. Kitanda kililaliwa na Sita wa
Six killers. Na lengo lake kuu ni kumuuangamiza Dokta Yusha. Dokta Yusha alifika
kitanda alicholazwa dereva Musa. Aliifunua lile shuka na kumwangalia Musa usoni.
Alistuka sana! Alikuwa daktari, na hakuhitaji kifaa chochote kile kutumia ili
kumpima dereva Musa, macho ya kidaktari yalitosha kumwambia kwamba alikuwa
anatazamana na mtu ambaye ameshafariki ! Nguvu zilimuisha Dokta Yusha. Kwa hali
aliyomuacha nayo dereva Musa, haikumuingia akilini hata kidogo kama Musa
angefariki, moja kwa moja alijua kwamba ameuliwa! Kwa jinsi hali aliyoiacha,
angeamini kama mkewe Nasra ama Hasina wangekuwa wamefariki, maana ndio ambao
walikuwa katika hali ngumu, lakini siyo dereva Musa. Dokta Yusha Alijua kwa
vyovyote vile kuna mchezo mbaya ulikuwa unaendelea mle wodini. Kwa mwendo wake
uleule wa taratibu alikuwa anakisogelea kile kitanda alicholazwa mgonjwa
mwengine, ambaye nae alijifunika gubigubi, au pengine alifunikwa gubigubi baada
ya kuuwawa kama dereva Musa. Bila kujua kitanda alichokuwa anakisogelea ndio
kitanda alicholala Sita. Muuaji hatari toka kundi la Six killers, ambaye ndiye
alimuua dereva Musa kwa kumnyonga shingo muda mfupi uliopita. Dokta Yusha
alikifia kile kitanda ambacho alilala mtu hatari sana. Aliishika ile ncha ya
shuka taratibu na kuanza kumfunua yule mgonjwa. Hamadi! Dokta Yusha alikuwa
anatazamana na mdomo wa bastola. Moyo wa Dokta Yusha ulipiga kwa kasi sana.
Kilikuwa ni kitendo cha ghafla ambacho hakukitegemea kabisa. Sita wa Six killers
alinyanyuka pale kitandani na kukaa kitako. "Hongera sana Dokta Yusha, uko
vizuri sana, tumeona ulichomfanyia Tano,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
hongera Dokta Yusha" Sita alikuwa anaongea huku akiipangusa vumbi bastola yake kwa kutumia shuka la hospitali. "Mwisho wako umefika Dokta Yusha, nakuuwa! Ndio nitakuuwa baada ya mateso kidogo lakini" Sita aliongea kwa kujiamini sana. Dokta Yusha aliamua kutulia, alijua kuwa na wasiwasi hakutomsaidia, aliamua kuwa makini ili ajue anatoka vipi katika kisanga kile kipya. "Unaona wagonjwa wako wote wamelala, sipendi tuwasumbue, tutoke humu ndani kimyakimya nikakusulubu huko nje, sitaki niwamalize hawa kwa ujinga wako" Sita alimtahadharisha Dokta Yusha. Dokta Yusha hakuwa na jinsi, aliongoza mwenyewe mlangoni, huku akifuatwa na Sita wa Six killers na bastola yake. Wakiwa wameongozana walifika nje, Dokta Yusha alisimama akisubiri maelekezo toka kwa Sita. "Elekea chumba cha kuhifadhia maiti" Sita alitoa maelekezo kwa sauti ya chini. Bila kujishauri Dokta Yusha alielekea katika chumba cha kuhifadhia maiti, huku akifuatwa nyuma na Sita. Dokta Yusha hakuwa anajua balaa alilokuwa anaenda kulishuhudia katika chumba cha kuhifadhia maiti. Waulikuta mlango wa chumba cha kuhifadhia maiti upo wazi. Waliingia ndani. Hali aliyoikuta Dokta Yusha mle ndani ilimstua sana! Aliona maiti zimelazwa bila mpangilio mle ndani, tena sakafuni. Maiti zenye majeraha ya kutisha sana, ambayo ni ngumu kutazamwa na macho ya kawaida. Aliangalia watu aliowakuta mle ndani, wote wakiwa makini na shughuli zao za kinyama, walikuwa hawamwangalii kabisa yeye. Macho ya Dokta Yusha yalitua kwa Dokta Sharifa, daktari wa kike alikuwa makini bila wasiwasi wowote, akiishughulikia maiti iliyolazwa juu ya meza mbele yake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
hongera Dokta Yusha" Sita alikuwa anaongea huku akiipangusa vumbi bastola yake kwa kutumia shuka la hospitali. "Mwisho wako umefika Dokta Yusha, nakuuwa! Ndio nitakuuwa baada ya mateso kidogo lakini" Sita aliongea kwa kujiamini sana. Dokta Yusha aliamua kutulia, alijua kuwa na wasiwasi hakutomsaidia, aliamua kuwa makini ili ajue anatoka vipi katika kisanga kile kipya. "Unaona wagonjwa wako wote wamelala, sipendi tuwasumbue, tutoke humu ndani kimyakimya nikakusulubu huko nje, sitaki niwamalize hawa kwa ujinga wako" Sita alimtahadharisha Dokta Yusha. Dokta Yusha hakuwa na jinsi, aliongoza mwenyewe mlangoni, huku akifuatwa na Sita wa Six killers na bastola yake. Wakiwa wameongozana walifika nje, Dokta Yusha alisimama akisubiri maelekezo toka kwa Sita. "Elekea chumba cha kuhifadhia maiti" Sita alitoa maelekezo kwa sauti ya chini. Bila kujishauri Dokta Yusha alielekea katika chumba cha kuhifadhia maiti, huku akifuatwa nyuma na Sita. Dokta Yusha hakuwa anajua balaa alilokuwa anaenda kulishuhudia katika chumba cha kuhifadhia maiti. Waulikuta mlango wa chumba cha kuhifadhia maiti upo wazi. Waliingia ndani. Hali aliyoikuta Dokta Yusha mle ndani ilimstua sana! Aliona maiti zimelazwa bila mpangilio mle ndani, tena sakafuni. Maiti zenye majeraha ya kutisha sana, ambayo ni ngumu kutazamwa na macho ya kawaida. Aliangalia watu aliowakuta mle ndani, wote wakiwa makini na shughuli zao za kinyama, walikuwa hawamwangalii kabisa yeye. Macho ya Dokta Yusha yalitua kwa Dokta Sharifa, daktari wa kike alikuwa makini bila wasiwasi wowote, akiishughulikia maiti iliyolazwa juu ya meza mbele yake.
Macho ya Dokta
Yusha yalitua kwa Dokta Sharifa, daktari wa kike alikuwa makini bila wasiwasi
wowote, akiishughulikia maiti iliyolazwa juu ya meza mbele yake. Dokta Yusha
aliitazama kwa makini ile maiti akitaka kujua Dokta Sharifa alikuwa anaifanyia
kitu gani. Bila wasiwasi wowote Dokta Sharifa alichomeka kisu kwa nguvu kidogo
kifuani kwa yule maiti aliyekuwa amelazwa katika kitanda kilichokuwa mbele yake.
Mwili wa Dokta Yusha ulimsisimka kwa hofu na woga, alifumba macho ili
asiushuhudie unyama ule. Alipofumbua macho aliona moyo wa yule maiti ukiwa
mkononi mwa Dokta Sharifa ! E bwana eee! Nesi mmoja alienda pale kwenye meza
iliyolazwa maiti akiwa na deli jekundu, ule moyo ukawekwa humo. Na Dokta Sharifa
alianza kuushona ule mwili. Dokta Yusha sasa alikumbuka, alikumbuka kuhusu kile
kidonda alichokutwa nacho mama Mpaukha kifuani. Kumbe mama Mpaukha alifanyiwa
mchezo huu mbaya, mama Mpaukha naye alitolewa Moyo! Hasira zilimpanda Dokta
Yusha, mishipa ya kichwa ilimsimama huku machozi yalikuwa yanamtiririka bila
kupenda. Alitamani awauwe watu wote waliokuwemo mle ndani, lakini hakuweza,
atawauwa vipi ilhali yeye ndiye aliyekuwa katika hatari zaidi ya kuuwawa! Chozi
la Dokta Yusha lilimsha shangwe mle ndani. Watu wote walikuwa wanamcheka Dokta
Yusha alivyokuwa analia. Dokta Yusha alijiona kama yupo katikati ya mashetani
wenye roho mbaya. Alipangusa machozi kwa kutumia kiganja chake cha mkono wa
kushoto. Aliwaona manesi wawili wakichagua maiti nyingine pale chini, ilikuwa
mithili ya wanunuzi wakichagua nguo katika soko la Tandika. Wakaipata maiti
wakiyoitaka. Wakaibeba na kuipeleka kwenye ile meza iliyokuwa mbele ya Dokta
Sharifa. Dokta Sharifa aliendelea na kazi yake huku akitabasamu. Kwa mara
nyingine tena, daktari katili wa kike Sharifa Juma alichomeka kile kisu chake
kifuani mwa ile maiti mwengine. Aliifanyia kama alivyoifanyia ile maiti ya
awali. Safari hii Dokta Yusha alithubutu kuangalia, aliangalia kila hatua ya
kikatili iliyofanywa na mabaradhuli wale. Alibaki anatikisa kichwa tu kwa
masikitiko. Hakutegemea kabisa kama kitendo kile cha kikatili kinafanywa na
daktari wa kike anayeheshimika zaidi wilayani Kilwa, Dokta Sharifa. Ama hakika
hali ilikuwa ya kusikitisha sana. Dokta Yusha aliangalia upande wake wa kulia,
alimwona Dokta Zaidi Kilumba akiwa ametulia tuli kitini. Akitabasamu huku
akimwangalia Dokta Yusha kwa dharau. "Una dhamana kubwa sana Dokta Kilumba,
umeaminiwa na Taifa kuiongoza hospitali hii, kuwahudumia wananchi maskini, tena
wagonjwa. Kinachofanyika hapa siyo haki Dokta Kilumba. Ndio! Hii siyo haki
kabisa Dokta, kwanini unafanya hivi vitu ? Kumbuka maadili ya kazi ya udaktari,
Kumbuka kiapo ulichoapa Dokta, kinafanana na kinachofanyika hapa Dokta?" Dokta
Yusha alisema kwa hisia na uchungu mkubwa sana. "Hahaha eti maadili ya kazi,
hahaha eti kiapo cha udaktari, kiapo cha udaktari nd'o nini, kwa taarifa yako
hii kazi tumelipwa hela nyingi sana! Tofauti na hizo zinazowafanya madaktari
wagome kila siku. Unazungumzia maadili ya kazi, hivi kuna maadili mbele ya
pesa?" Dokta Kilumba alikuwa anaongea akiwa amekaa palepale katika kiti,
anaongea bila wasiwasi wowote. "Mtalipa Dokta kwa huu unyama mnaofanya hapa,
naapa mtalipa!. Hata mkiniua mimi kizazi kijacho kitakuja kulipa damu za watu
hawa wasio na hatia!" Dokta Yusha munkari ulianza kumpanda. "Tulipe damu gani
Dokta Yusha wakati hawa wameshakufa, hizi ni maiti Dokta?" "Usibishane nae, yeye
tunamtoa moyo leo akiwa anajiona. Ili tulipe vizuri hizo damu anaozisema huko
mbinguni kama kupo!" "Mletee hapa!" Sita akamshika mkono na kumvuta. Kumpeleka
pale alipo Dokta Kilumba. Alipofikishwa pale ndipo Dokta Yusha alimuona mtu
mwengine kabisa, ambaye hakuwa amemuona pindi alipoingizwa mle ndani. Na hakuwa
amemuona kabisa katika maisha yake. Mzee mwenye sura ya kikorofi, alikuwa na
sharubu mithili ya Karl Peter's 'mkono wa damu'. Mzee mwenye mwili uliojengeka
kimazoezi, mrefu sana, kwa majina alikuwa anaitwa Don Genge. Dokta Yusha
alidhani ile sauti ya kuitwa imetoka kwa Dokta Kilumba, la hasha. Haikuwa hivyo,
kumbe alikuwa ni jasusi Don Genge mwenyewe. "Hahaha hiki ndio kifaranga
kinachowasumbua?" Don Genge aliuliza kwa kejeli huku akiubinua kwa juu mdomo
wake mpana. "Ama kweli maajabu hayana mwisho duniani. Wewe ndio umemvunja goti
komando Tano? Kwa nguvu gani ulizonazo mpumbavu wewe, kwa akili gani ulizonazo
mjinga wewe? Don Genge alikuwa anauliza maswali bila ya kusubiri majibu toka kwa
Dokta Yusha. Kamtie kwenye gari tuondoke nae kambini tukaone uwezo wake mpaka
Komando Tano ashindwe kumkamata na kuambulia kuvunjwa goti." Kwa haraka Sita
alimsukasuka Dokta Yusha na kumpeleka kwenye gari. Gari aliloingizwa dokta Yusha
ni yale magari yenye bodi zenye visanduku nyuma. Mara nyingi hutumika katika
mahospitali kusafirishia dawa. Kundi la Six killers nao walikuwa wanautumia gari
aina hiyo kusafirishia mioyo. Na leo hii gari hiyohiyo ilitumika kama mahabusu
inayotembea kwa Dokta Yusha. Ndani ya kile kisanduku kulikuwa na giza totoro,
pia kulikuwa na joto sana, maana hakukuwa na uwazi wa kupitisha mwanga wowote
katika kisanduku hiko. Kilikuwa kisanduku kidogo sana kilichompa shida sana
Dokta Yusha. Ilimbidi ajikunje sana ili akae vizuri mle ndani ya gari. Hakukaa
vizuri lakini alikaa. Baada ya nusu saa alisikia kelele za miguu ya watu
ikielekea pale kwenye gari aliyokuwa ndani yake. Mara alisikia mlango wa ile
bodi ukifunguliwa. Ulifunguka. Yule jamaa aliyetambulika kwa jina la komando
Sita aliingia na kuweka deli, deli la kuhifadhia mioyo ya maiti. Baada ya kuweka
lile deli jekundu yule jamaa alitoka nje. Kile kisanduku kikafungwa tena. Giza
likarejea kwa kasi! Akiwa kule nyuma ya gari alisikia gari likiwashwa. Na safari
ya kuelekea kusikojulikana ilianza. Gari lilitembea sana, takribani saa sita
lilikuwa halijafika lilikokuwa linaenda. Dokta Yusha aliamini safari ile ilikuwa
ni nje ya wilaya ya kilwa, au nje ya mkoa kabisa. Maana hakukuwa na sehemu ndani
ya kilwa ya kutembea saa nyingi namna
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ile. Sasa alianza kulizoea giza, na kuyaona vizuri mandhari ya kule nyuma kwenye kisanduku. Kwenye sakafu ya gari ile, aliyaona madeli matatu yakiwa yamewekwa pamoja. Hakujua ni madeli ya nini, ingawa alihisi yatakuwa ya mioyo. Dokta Yusha hakutamani hata kuhangaika kuyafungua. Aliangazaangaza mle ndani ya gari, hakuona kitu kingine zaidi ya yale madeli mekundu. Mara gari lilisimama, ishara kuwa lilikuwa limefika ilikokuwa inaelekea. Saa zaidi ya nane walizitumia barabarani. Ilichukua kama robo saa ndipo akaja kufunguliwa kule nyuma. Dokta Yusha akaona tena mwanga halisi wa dunia. Alishuka mwenyewe bila kuambiwa. Alikuwa amechoka sana kukaa mle ndani ya kisanduku. Joto kali ndani ya kisanduku na kukosa hewa kulimuadhibu barabara Dokta Yusha. Alishuka chini, alikutana na nyumba ndogo ya kisasa. Nyumba iliyonakshiwa kwa rangi ya bluu. Huku chini kukiwa na michirizi ya rangi nyeusi. Juu iliezekwa na bati za vigae toka Afrika ya Kusini. Nyumba hiyo ilikuwa imezungukwa na ukuta mkubwa sana wenye rangi ya bluu pia. Ulikuwa ukuta mrefu ulioipita hadi nyumba yenyewe. Yaani kama mtu akiwa kwa nje ataishia kuuona ukuta tu. Hatuiona nyumba ile. Dokta Yusha aliingalia kwa makini nyumba ile huku akiangalia mandhari ya sehemu ile. Alikiri kuwa hakuwahi kufika hata siku moja mahali pale. Hakujua kabisa nyumba ile ilikuwa mahali gani ndani ya nchi ya Tanzania?
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ile. Sasa alianza kulizoea giza, na kuyaona vizuri mandhari ya kule nyuma kwenye kisanduku. Kwenye sakafu ya gari ile, aliyaona madeli matatu yakiwa yamewekwa pamoja. Hakujua ni madeli ya nini, ingawa alihisi yatakuwa ya mioyo. Dokta Yusha hakutamani hata kuhangaika kuyafungua. Aliangazaangaza mle ndani ya gari, hakuona kitu kingine zaidi ya yale madeli mekundu. Mara gari lilisimama, ishara kuwa lilikuwa limefika ilikokuwa inaelekea. Saa zaidi ya nane walizitumia barabarani. Ilichukua kama robo saa ndipo akaja kufunguliwa kule nyuma. Dokta Yusha akaona tena mwanga halisi wa dunia. Alishuka mwenyewe bila kuambiwa. Alikuwa amechoka sana kukaa mle ndani ya kisanduku. Joto kali ndani ya kisanduku na kukosa hewa kulimuadhibu barabara Dokta Yusha. Alishuka chini, alikutana na nyumba ndogo ya kisasa. Nyumba iliyonakshiwa kwa rangi ya bluu. Huku chini kukiwa na michirizi ya rangi nyeusi. Juu iliezekwa na bati za vigae toka Afrika ya Kusini. Nyumba hiyo ilikuwa imezungukwa na ukuta mkubwa sana wenye rangi ya bluu pia. Ulikuwa ukuta mrefu ulioipita hadi nyumba yenyewe. Yaani kama mtu akiwa kwa nje ataishia kuuona ukuta tu. Hatuiona nyumba ile. Dokta Yusha aliingalia kwa makini nyumba ile huku akiangalia mandhari ya sehemu ile. Alikiri kuwa hakuwahi kufika hata siku moja mahali pale. Hakujua kabisa nyumba ile ilikuwa mahali gani ndani ya nchi ya Tanzania?
Sita wa Six killers alimshika
mkono Dokta Yusha na kuizunguka nyumba ile kuelekea nyuma kwa kupitia mkono wa
kushoto. Walipofika uwani Dokta Yusha macho yake yalitazamana na kibanda kidogo
mithili ya stoo. Sita alifungua kile kibanda kwa funguo na kumsukumia Dokta
Yusha mle ndani.
Kilikuwa ni kibanda kidogo kwa
nje, na ndani pia. Dokta Yusha alisimama hatua kama mbili toka katika mlango wa
kile chumba na kuanza kukiangalia. Kilikuwa ni chumba ambacho hakukuwa na kitu
chochote zaidi ya kiti kimoja tu cha chuma. Kuta yake ilipakwa rangi nyekundu
ambayo ilikuwa inaumiza macho ukiitazama muda mrefu.
Dokta Yusha
alipiga hatua za taratibu kuelekea katika kile kiti. Alikuwa na lengo la kwenda
kukikalia kiti kile. Maana hakukuwa na sehemu nyingine ya kukaa zaidi ya kwenye
kile kiti. Alikikaribia kabisa kile kiti, alitaka kukaa lakini aligairi.
Alikitilia mashaka kile kiti. Kwanini kile kiti cha bati kiwekwe katika chumba
kile, ni kweli kimewekwa kwa lengo la kukalia tu? Au kuna lengo lengine, siku
zote wasiwasi akili. Dokta Yusha hakukaa, alirudi kinyumenyume hadi ukutani.
Akakaa chini taratibu huku akikiangalia kwa makini kile kiti cha
chuma.
Dokta Yusha alikaa pale chini sakafuni huku
akitafakari mustakabari wa maisha yake. Aliona mambo yamebadirika kwa kasi sana,
tena yakianzia siku ya sherehe ya ndoa yake.
Aliwakumbuka wagonjwa
aliowaacha hospitali. Mkewe kipenzi Nasra, rafiki wa mkewe, Hasina na mzee
Mpaukha, alijua watakuwa katika hali ngumu sana kwa kutokuwepo yeye, pia alijua
jinsi walivyoikaribia hatari ya kutolewa mioyo na wale mabaradhuli. Alimfikiria
dereva wa Mzee Mpaukha, Musa akijua kwa vyovyote kwa sasa atakuwa katika chumba
cha kuhifadhia maiti, akisubiri kutolewa moyo .
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kwanini moyo?
Itakuwa wanafanyia nini hiyo mioyo? Tena bila shaka mioyo ya maiti ndiyo
inayohitajika ndio maana wameweka kambi hospitali tena katika chumba cha
kuhifadhia maiti. Lazima nijue undani wa sakata lile, na Lazima nihakikishe watu
hawa wenye nia mbaya wanafikishwa katika vyombo vya sheria" Dokta Yusha aliwaza
hayo bila ya kujua yupo sehemu hatari kiasi gani, bila kujua atatoka vipi ili
akawafikishe katika vyombo vya sheria ilihal alikuwa tunduni akisubiri adhabu
yake, bila shaka adhabu ya kifo!
Wakati akiwaza
hayo alisikia mlango ukifunguliwa kwa nje. Ukafunguka kidogo na mtu mpya
alisukumwa kwa nguvu kuingizwa mle ndani. Dokta Yusha alimwangalia vizuri mtu
yule walitambuana.
"Wamekuleta huku
Dokta"
"Nawe wamekuleta huku"
Ilikuwa
ni kushangaana tu. Mtu yule alikuwa ni mmoja wa askari wa kituo cha Polisi
Masoko. Tena ndiye askari aliyemhoji dokta Yusha alipoenda Polisi
.....
"Eeh imekuwaje ukafika huku" Dokta Yusha
aliuliza kwa wahka mkubwa.
Huku akiwa amesimama yule askari alianza
kuelezea.
"Ulivyoomba kutoka pale Polisi ili kwenda kwenye mazishi ya
Mwanasheria tulikukubalia, lakini ulivyotoka tu tulikubaliana tukufuate kwa
nyuma, na ni mimi ndiye niliyepewa jukumu hilo. Nilikufuata kwa nyuma kila
ulikoenda. Mpaka wanakuingiza kwenye gari mimi nilikuwa nashuhudia. Lakini
nikiwa nimejibanza nyuma ya wodi moja nikisubiri muda muafaka wa kuja kukuokoa,
nikiwa pale nyuma ya wodi nilipojificha nilistukia nimepigwa na kitu kizito
kisogoni. Toka hapo sikujua nini kiliendelea. Nimeamka toka ndani ya gari dakika
kama sita zilizopita na wakanileta moja kwa moja humu"
"Hivi tuko wapi
hapa Afande?"
"Hata sifahamu, maana nilizimia kabisa, nimezinduka
nimejikuta nipo humu"
"Itakuwa tuko mbali sana Afande, saa nane
tumetumia mpaka kufika hapa"
"Saa nane?"
"Ndio,
Afande"
"Mh itakuwa wametuleta wapi washenzi hawa" Yule askari alikuwa
anaongea huku anapiga hatua kuelekea kukaa katika kile kiti pekee cha chuma mle
ndani. Alikikaribia kile kiti na kusema.
"Sijui
watakuwa wana mpango gani hawa wanaharamu"
"Nooooo afande usikae
hapooooo!" Dokta Yusha alipiga kelele kali kumuonya yule askari asikalie kile
kiti chuma, lakini alikuwa amechelewa sana.
Jamaa
alikaa kwenye kiti kilichotokea...........Dokta Yusha alifumba
macho!
Kiti kilibadirika rangi na kuwa chekundu sana, askari hakutoa
hata ukelele mdogo, rangi nyekundu ya kiti ilienda sambamba na rangi ya askari
yule. Kumbe kiti kile kilikuwa na shoti ajabu ya umeme!
Dokta Yusha
alithubutu kufumbua macho, macho yalimtoka pima! hakutegemea kabisa kitendo
kile. Ingawa alikuwa anahisi kiti kile sio kizuri tangu alivyoingia katika
chumba kile, lakini hakudhani wala kufikiria kwamba kina madhara namna ile. Yule
askari alianza kubadirika rangi tena, akawa mweusi tii huku akikakamaa ilhali
kiti kilibaki na rangi yake ileile nyekundu. Dokta Yusha aliyaangalia yote huku
huku akitetemeka, mikono yake ikiwa kauziba mdomo wake. Alikuwa anaangalia picha
mbaya sana!
Huku akitetemeka dokta Yusha alisimama, kwa kiasi kikubwa
akisaidiwa na ukuta katika kumsaidia kunyanyuka pale chini. Alivyosimama tu
alikaribishwa na kitu kingine, harufu, ule mwili uliokakamaa pale chini ulianza
kutoa harufu kali sana!
Dokta Yusha alijitahidi kubana pumzi ili
harufu ile isiyoeleweka isiingie puani mwake, ilikuwa ngumu sana, maana
kuendelea kubana pumzi kulimaanisha anakiita kifo chake mwenyewe. Hata hivyo
hakutaka kabisa kuvuta harufu ile, aliendea kuziba pumzi huku anaachia mara
chache chache, akiwa katika hali hiyo ngumu sana katika maisha yake, mara
alisikia kelele za mlango, ishara kuwa mlango ulikuwa unafunguliwa. Mlango
ukafunguliwa, aliingia Sita wa Six killers kwa majigambo makubwa sana. Alienda
hadi pale ukutani ambako Dokta Yusha alikuwa
amesimama.
"Hahaha Dokta nawe unahisi harufu,
siamini. Wewe ni daktari bwana unakutana na harufu mbaya zaidi ya hii. Hebu
simama" Sita alisema kwa urafiki zaidi.
Dokta
Yusha alimwangalia Sita huku akionesha sura ya upole sana. Lakini sura yake ya
upole haikusaidia kitu. 'Maji aliyavulia nguo..............'
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Haya toka nje"
Sita wa Six killers alimwambia huku akionesha kwa kidole cha shahada mahali
mlango ulipo.
Dokta Yusha alitoka nje ya chumba
kile huku akifuatiwa na Sita. Alipotoka tu nje, alikutana na jamaa mmoja akiwa
amekaa katika kiti cha plastiki huku anavuta kiko. Jamaa yuleyule aliyekuwa
anaongea kwa majivuno na kujiamini kule katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Alikuwa anaitwa Don Genge.
Dokta Yusha alisimamishwa mbele ya Don
Genge huku nyuma yake akiwa amesimama imara Sita. Pembeni ya Don Genge upande wa
kushoto walikuwa wamesimama watu wawili, na upande wa kushoto walikuwa
wamesimama watu wawili. Don Genge alikuwa kati mithili ya
Mfalme.
"Naitwa Don Genge, umeshawahi kulisikia
hilo jina" Don Genge aliuliza punde tu Dokta Yusha alivyowasiri
pale.
Dokta Yusha alikataa kwa kutingisha kichwa.
"Wewe ni
bubu?"
"Hapana"
"Kwanini unapenda sana kufatilia mambo ya
watu?" Don Genge aliachana na mwendelezo wa swali la awali na kuuliza swali
jipya.
Dokta Yusha alikaa kimya, kimya ambacho kilimkasirisha sana Don
Genge.
Don Genge alinyanyuka, akamsogelea Dokta Yusha huku
akitabasamu. Ghafla, Don Genge alirusha kibao kilichotua sawia katika shavu la
kushoto la Dokta Yusha. Dokta Yusha aliyumba kidogo, kisha akasimama tena wima.
Alijishika shavu lake la kushoto kwa mkono wake wa
kulia.
"Kwanini unapenda kufatilia mambo ya
watu?" Sasa Don Genge aliuuliza uso wake ukiwa karibu sana na uso wa Dokta
Yusha.
"Nisamehee sirudii tena" Dokta Yusha aliamua kuomba msamaha
bila ya kujielewa.
"Hakuna mtu aliyewahi kuingia katika nyumba hii,
akatoka hai, wote wameuwawa, tena kikatili sana! Ila wewe utakufa kifo cha
tofauti....." Don Genge aliacha kuongea, aliacha maneno yale yamuuingie vizuri
Dokta Yusha. Akavuta kiko kidogo, halafu akampulizia moshi Dokta Yusha. Dokta
Yusha alikohoa kutokana na ule moshi.
".........Utakufa kifo cha
tofauti sana, utakufa kwa njaa!
Siku nyingi nilikuwa najiuliza hivi
binadamu anaweza kukaa siku ngapi bila kula? Lakini nitapata jibu la hilo swali
kupitia wewe" Don Genge alikuwa anaongea wakati Dokta Yusha alikuwa anaendelea
kukohoa kutokana na ule moshi. Lakini Don Genge hakujari kama kasikia ama
hajasikia.
"Hebu mrudishe ndani kule"
"Hapana, musinipeleke
katika kile chumba" Dokta Yusha alikuwa anakataa kurudi tena katika chumba kile
chenye harufu ya mbaya na ya kuchukiza.
"Kile ndio chumba chako, lile
ndio kaburi lako, usilikatae, ulipende Dokta, peleka
huyo!"
Sita alimshika suruali kwa nyuma Dokta
Yusha mithili ya kibaka ashikwavo na askari na kumrudisha katika kile chumba
chenye harufu kali sana...
Hali ilikuwa ngumu sana
katika chumba kile, ambacho nd'o ilikuwa selo ya Dokta Yusha, au kubali la Dokta
Yusha kama alivyosema Don Genge. Lakini Dokta Yusha ilimbidi akae katika selo
ile, hakuwa na jinsi. Aliishi mule kwa hofu kubwa sana, kila kitu alichoongea
Don Genge bado kilikuwa kinarindima katika kichwa chake, kwamba kile kitakuwa
chumba chake, pia litakuwa nd'o kaburi
lake.
"Nakubari kitakuwa chumba changu, tena kwa
muda bila shaka, lakini haliwezi kuwa kaburi langu kamwe" Dokta Yusha alijisemea
mwenyewe kwa ujasiri.
Sasa alikuwa anaivuta harufu yote ya chumbani,
hakuwa anaziba tena pua, aliamua liwalo na liwe, harufu yoyote iingie puani
mwake, lakini lazima atoke mle ndani.
Usiku
uliingia, usiku ambao Dokta Yusha alipanga nd'o uwe kilele cha yeye kuishi
katika selo ile, lazima atoke mle ndani. Ndani ya chumba kile kulikuwa na giza
kubwa sana. Dokta Yusha alinyanyuka kwenye sakafu alipokaa na kuusogelea mlango.
Alishika komea la mlango na kujaribu kulizungusha taratibu.
Mlango
ulikuwa umefungwa!
Dokta Yusha ilimpasa kutafuta
njia nyingine mbadala ya kumuwezesha kutoka katika chumba kile cha kifo.
Ilimpasa kutumia akili za ziada kutoka katika chumba kile cha
mauti.
'Lazima nitoke humu, siwezi kufa kikondoo
humu'
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Dokta Yusha
aliangalia juu ya kile chumba, alikutana na vigae vilivyowezekwa vizuri sana
kule juu. Hakuna mjanja atakayeweza kufanya chochote ili kupita katika vigae
vile. Ilikuwa ngumu sana!
Dokta Yusha alirudi nyuma, akarejea tena
ukutani, akauangalia ukuta, akautomasa ule ukuta kwa kidole, ulikuwa ukuta mgumu
sana!
Mlango, ukuta, bati vyote havikumruhusu
kabisa Dokta Yusha kutoka katika chumba kile cha
hatari.
Dokta Yusha alichoka, alikaa chini ili
kusubiri kukiona kifo cha njaa jinsi
kinavyokuwa.
Saa kumi kamili alfajiri ilimkuta
Dokta Yusha akiwa macho. Alikuwa hajasinzia hata kidogo, muda wote alikuwa
anafikiria namna ya kutoka katika chumba kile lakini hakupata namna ya
kutoka.
Mara, alisikia tena kelele za mlango kwa nje, ishara kama ya
mwanzo kuwa mlango ulikuwa unafunguliwa.
'Ama
zake, ama zangu!'
Aliingia tena Sita, akiwa
kashika bunduki aina ya SMG mkononi. Alisimama pale mlangoni na kumwangalia
Dokta Yusha. Sita wa Six killers alikuwa ameenda kuhakikisha tu kama Dokta Yusha
hajafanya ujanja wowote wa kujaribu kutaka kutoroka. Sita alimshuhudia Dokta
Yusha akiwa amekaa palepale alipomwacha awali. Akadanganyika kwamba Dokta Yusha
hajafanya kitu chochote kile cha kujaribu kutoroka.
Alijidanganya.
Dokta Yusha alitafuta sana njia ya kutoka mle ndani lakini
hakuipata.
Sita aligeuka nyuma ili arudi nje kuendelea na lindo
lake.
Kwa kasi ya haraka Dokta Yusha alinyanyuka pale chini na kupiga
hatua mbili kubwa sana, hatua zilizomfikisha mpaka pale mlangoni. Alipokuwa Sita
wa Six killers.
Wakati Sita anataka kugeuka nyuma kujua sababu ya
vishindo viwili alivyovisikia, alichelewa sana!
Alikuwa kakabwa vizuri
sana na Dokta Yusha. Kabali maridadi iliyomtetemesha Sita na kuidondosha bunduki
chini.
Dokta Yusha hakujari, alimvuta Sita kwa nyuma kwa nguvu.
Mwanzoni Sita alijikomaza lakini baadae Ilibidi ajilegeze, maana kukomaa
ilimaanisha kuumizwa zaidi na ile kabali.
Kujilegeza nako lilikuwa
kosa kubwa sana alilolifanya Sita. Kosa ambalo atalijutia mpaka kesho, kama kuna
maisha baada ya kilichomtokea pale. Dokta Yusha alimvuta Sita kwa nguvu na
kujikuta akimsukumia pale katika kiti cha kifo!
Balaa!
Sita
alibadirika naye, mwili ulibadirika sambamba na kiti, Ilikuwa ni rangi nyekundu
mithili ya tanuru la moto!
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment