Search This Blog

Sunday, 22 May 2022

TAHARUKI - 2

 







    Simulizi : Taharuki

    Sehemu Ya Pili (2)



    Lakini mbali ya kuwa na biashara halali, Mokili na Wibo walikuwa na siri nzito iliyowaunganisha pamoja kiasi cha kuwafanya marafiki wakubwa wasioweza kutenganishwa.



    Ukweli ni kwamba wote walikuwa wahalifu wa kimataifa, wakijihusisha na hujuma nzito ambazo baada ya kufanikisha walilipwa donge nono la fedha kutoka katika magenge makubwa ya wahalifu wa kimataifa duniani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Basi, ndiyo safari hii walipopata kibarua ambacho kingewalipa donge nono kupita yote waliyowahi kulipwa katika shughuli zao za uhalifu wa kimataifa. Kilikuwa kibarua cha kusugua kichwa hasa mpaka waweze kufanikiwa, na kwa vile ni watu ambao hawakupenda kushindwa, au kukata tama, wakaamua kujaribu! Ni kuiba mkufu wa thamani uliohifadhiwa miaka mingi, ulioko ndani ya kasri ya Malkia wa Uingereza!



    Sababu za kuutafuta mkufu ule wathamani, uliotengenezwa kwa madini ya almasi, ni kwamba ulitakiwa na mfanyabiashara, bilionea wa Kireno, Miguel da Silva, aliyekuwa akijishughulisha kazi za uchimbaji wa madini ya almasi nchini Angola . Yeye alikuwa ameugundua mgodi mpya wa almasi, ambao ulikuwa bado haujaguswa kabisa na wachimbaji wengine, kwani kila mchimbaji akiyejaribu kuanzisha machimbo katika mgodi huo, alikufa katika mazingira ya kutatanisha kabla ya kutimiza azma yake.



    Inasemekana kwamba, kulikuwa na mzimu wa hatari, ulioogopwa sana na wachimbaji waliokuwa wakijishughulisha na uchimbaji wa madini. Hivyo, hakuna mtu aliyethubutu kuchimba kwa kuhofia hasira na ghadhabu za mzimu, ambayo ingeweza kuwadhuru na hata kuwasababishia vifo!



    Ndipo mtu yule, bilionea wa Kireno, Miguel da Silva, aliyekuwa anaumezea mate mgodi ule mpya, na ambao ulikuwa haujaguswa, alipoamua kufanya jambo moja la kuweza kumfanikisha azma yake. Aliamua kusafiri kwa ndege yake aliyokuwa anaimiliki, hadi nchini Senegel, katika jiji la Dakar .



    Aliamua kwenda huko kwa lengo maalum, ambalo ni kumtembelea mganga mmoja maarufu sana wa kienyeji, aliyejulikana kwa jina la Ndiru Kobbe, ambaye sifa zake zilitapakaa sana ndani na nje ya Afrika, kwa jinsi alivyokuwa akisaidia watu waliokuwa na matatizo ya aina yoyote yaliyoshindikana!



    Miguel da Silver alifika salana jijini, Dakar , na kumtafuta mganga yule, ambaye alikuwa amejichimbia katika viunga vya nje ya jiji, umbali wa kilometa ishirini hivi. Akiwa ni mtu mwenye fedha, Miguel alikodi gari maalum, akiwa na wapambe wake, ambalo lilimfikisha kwa mganga yule, na kukaribishwa vizuri. Akaeleza shida yake iliyokuwa imempeleka kule, ikiwa ni kuhitaji dawa za kuweza kufanikisha kuchimba madini ya almasi katika ule mgodi mpaya, ulioogopewa na watu wengi.



    Baada ya kupiga ramli, Ndiru Kobbe alimpa masharti ambayo kama angeyatimiza, basi, angeweza kuchimba madini katika mgodi ule usioguswa na mtu, pia mizimu iliyokuwa na ghadhabu isingemdhuru. Mganga Kobbe alimweleza Miguel kwamba, mizimu ya mababu ilikuwa inataka ‘Mkufu’ wa thamani kubwa, uliotengenezwa kwa madini ya almasi, ambao ulikuwa umeibwa na wazungu kutoka kwa Malkia, Nzinga Mbadi, urejeshwe kwa chifu wa utawala wa jadi, kule eneo la Bihe, nchini Angola . Pale ndipo mizimu ingetulia na kuruhusu machimbo kuendeshwa kwenye mgodi huo uliojaa almasi kuliko migodi mingine yote katika nchi ya Angola .



    Mganga, Ndiru Kobbe aliendelea kufafanua kwamba mizimu ya mababu ilikasirika kwa sababu mkufu ule ulikuwa maalum kwa utawala wa kijadi barani Afrika. Na almasi zilizotumika kuutengeneza, zilitoka katika mgodi huo, ambao sasa mizimu tele ilikuwa ikiishi ndani yake. Ndiru aliendelea kumweleza Miguel, kuwa mizimu ya mababu wa Afrika, haikutaka Wazungu wauguse mkufu ule wa almasi kwa mikono yao , hivyo ukirejeshwa mikononi mwa Mzungu, kamwe wasingeupokea!



    Hapo ndipo, Bilionea, Miguel, alipochekecha akili baada ya kuambia masharti yale na mganga yule mashuhuri. Alimlipa gharama zote za ramli, na gharama nyinginezo, kisha akaamua kuondoka nchini Senegel, na kurudi nchini Angola, ili aweze kujipanga katika kutekeleza mpango ule alioudhamiria, kwa kuumiliki ule mgodi wa almasi. Ili bilionea yule apate faida ya almasi zilizomo ndani ya mgodi ule, aliamua kugharamikia fedha nyingi kwa kuwatumia waafrika wanaoishi Ulaya, na wanaovuma kwa uhalifu wa kimataifa.



    Ndiyo, baada ya kuhangaika sana , aliwapata watu hao. Walikuwa ni Mokili wa Ngenge na Wibo Eze, ambao walitakiwa watumie akili na uzoefu wao wa kijamabazi, ili kujua ule mkufu uliotapeliwa na wazungu kwenye karne ya 17, kutoka kwa Malkia, Nzinga Mbadi, kule Bihe, nchini Angola , ulikuwa wapi. Na kisha wafanye juhudi kuurejesha Angola kwa mizimu ya mababu wa Waafrika. Baada ya kuitekeleza kazi ile, basi, Bilionea Miguel da Silver angewalipa fedha nyingi!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ndipo wanaume wale walipoichangamkia kazi ile!



    *******

    Hakupenda kushindwa kitu. Mokili wa Ngenge, akiwa ni mtu anayejuana na watu wengi sana , wema na wabaya, haraka sana , aliwasiliana na kinara, Wibo Eze, aliyeko nchini Uingereza. Wakakutana faragha na kupanga la kufanya juu ya kupata watu maalum wa kuifanya kazi ile ya kwenda kuuiba ule mkufu uliokuwa ndani ya Kasri la Mali kia, ingawa walijua kuwa ni kazi ngumu sana .



    Baada ya wiki mbili hivi, Mokili na Wibo, walikutana nyumbani kwa Mokili, jijini Paris , kupanga cha kufanya. Walijichimbia ndani ya kile chumba cha faragha ambacho hakuna mtu yeyote ambaye angejua kilichokuwa kinaendelea.



    “Mshirika wangu, Wibo,” Mokili akasema kwa sauti ndogo, laikini iliyosikika.



    “Nakusikiliza mshirika...” Wibo Eze akaitikia.



    “Nimekuita tuonane na kupanga cha kufanya, kwani tenda nzito ndiyo hiyo imeangukia mikononi mwetu. Mkufu unatakiwa upatikane, unasemaje?”



    “Ni kweli, ni tenda nzito. Lakini ni kazi ngumu sana , hasa uk izingatia kuwapata watu wa kuweza kwenda kuingia ndani ya Kasri la Mali kia? Uk weli ni kwamba nimechanganyikiwa!” Wibo alimwambia Mokili.



    “Usichanganyikiwe mapema Wibo. Wewe ni mtu wa kazi, tukae chini na kupanga la kufanya, na kumbuka kuwa tumewahi kufanya kazi nyiongi sana , na nyingi tumefanikiwa!”



    “ Hilo ni kweli, hebu anza kuchanganua akili yako, halafu na mimi nitakusaidia kuchangia...”



    “Vizuri sana Wi bo, mimi nina mtu wangu, ambaye ni raia wa Kongo, aitwaye, Hamisi Kengwa, natumaini nikimpata huyo, tunaweza kukubaliana naye, kwani amefanikisha kazi nyingi sana ...” Mokili alimwambia Wibo.



    “Mtu huyo anaishi hapahapa Ufa ransa?”



    “Ndiyo, anaishi hapahapa jijini Paris , ambapo anajishughulisha na kazi za muziki, akijifanya mwanamuziki, kumbe ni kivuli tu.”



    “Aisee, basi mtu huyo atatufaa,” Wibo akasema na kuongeza. “Na mimi pia, nina jamaa yangu, Mnigeria, anayeitwa Edmond Balle, ambaye ni mtu wa kazi, na mara nyingi hujishughulisha na kazi za utapeli wa kimataifa. Nafikiri tukimpata, tunaweza kuwakutanisha na kupanga cha kufanya.”



    “Mtu huyo anaweza kutufaa kwa jinsi ulivyoniambia ni tapeli, je, anaishi wapi mtu huyo?”



    “Anaishi hapahapa Paris ...”



    “Basi, ni kazi ndogo tu, tuwasiliane nao na tukutane. Nina hakika tutafanikiwa.”



    “Hakuna tatizo nitafanya hivyo, ninampigia simu muda huu...”



    Wibo akasema huku akichukuwa simu yake na kuanza kumpigia Edmond Balle.



    “Na mimi ngoja nimpigie Hamis Kengwa,” Mokili naye akasema huku akimpigia simu Hamisi Kengwa.



    Baada ya saa tatu hivi, wanaume wale wanne, walikutana pale nyumbani kwa Mokili, mtaa wa Mtakatifu Dennis. Wakajichimbia ndani na kuanza kupanga mpango wao ule kabambe, ambao uliweza kuwashtua hata watu wale waliotakiwa kwenda kuifanya kazi ile. Hata hivyo baada ya kujadiliana sana , walifikia uamuzi wa kutumia uchawi wa kuweza kuingia ndani ya Kasri lile la

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Malkia!



    Ulikuwa ni uchawi wa aina yake!



    Walisafiri kwa ndege maalum inayomilikiwa na Mokili wa Ngenge, hadi nchini, Demokrasi ya Watu wa Kongo, ambapo walifikia katika mji wa Goma, ulioko Mashariki mwa nchi ile. Kule kulikuwa na mganga maarufu, aliejulikana kwa jina la Profesa Litumbo Embako, ambaye aliweza kuwapatia dawa maalum. Ilikuwa ni dawa ya kupaka mwilini, inayofanya mtu asiweze kuonekana na binadamu wa kawaida, wakati akita ka kutenda jambo fulani la madhara na hata wizi.



    Mara nyingi, dawa kama ile, huwa inatumiwa na wachawi wa usiku, wakati wanapokuwa katika shughuli zao za kuwanga usiku, kiasi cha kufanya wasionekane. Ukweli ni kwamba, walipopatiwa dawa ile kwa kiasi kikubwa cha fedha, ambacho Mokili qwa Ngenge alikitoa bila kipingamizi chochote, halafu wakafunga safari kurudi nchini Ufa ransa kwa kutumia usa firi ule wa ndege. Hakika walikuwa na matumaini makubwa ya kuupata mkufu ule wa alma s i uliokuwa unahitajiwa kwa udi na uvumba!



    Baada ya mwezi mmoja hivi, mpango wote ulikuwa umesharatibiwa na Mokili wa Ngenge, ambapo aliwasafirisha, Hamisi Kengwa na Edmond Balle, na kufikia nyumbani kwa Wibo Eze, jijini London . Pale walikaa kwa muda huku wakichorewa ramani nzima jinsi ya kuingia ndani ya lile Kasri la Malkia, na sehemu ulipohifadhiwa ule mkufu wa thamani kubwa!



    Hawakupata shida ya kuigundua sehemu ile ulipowekwa mkufu ule. Ulikuwa katika sehemu ya wazi tu, iliyokuwa katika njia panda kati ya njia inayoelekea katika jumba lile la mikutano, ofisi ya Malkia, bwawa, na bustani kubwa iliyoko mbele ya Kasri. Ulikuwa umehifadhiwa ndani ya sanduku kubwa la kioo, lililokuwa juu ya mnara mdogo uliotengenezwa kwa marumaru. Tuseme ulikuwa katika sehemu ya wazi kabisa, lakini kuusogelea ndiyo ilikuwa kazi kubwa sana , kwani kulikuwa na ulinzi wa hali ya juu, askari polisi maalum wanaomlinda Malkia, walikuwa wamejipanga eneo lote, usiku na mchana!



    Ndipo usiku huo awalipoamua kuitekeleza kazi ile, wanaume, Hamisi Kengwa na Edmond Balle, walipoelekea katika Kasri la Malkia, wakiwa na gari aina ya Rolls Royse, lililokuwa linaendeshwa na Wibo Eze. Walikuwa kama watu waliokuwa katika matembezi yao , na walipofika katika mtaa mmoja, umbali wa mita mia moja kutoka katika Kasri lile, ndipo walipojipaka ile dawa maalum ya kuwafanya wasionekane, halafu wakashuka garini na kutembea kwa miguu. Kwa muda wote, Wibo alikuwa akiwaona walipokuwa garini, wakijipaka dawa ile ya maji maji.

    Lakini Hamisi na Balle waliposhuka, walionekana kama kivuli tu, kwani hakuweza kuwaona zaidi ya kuambulia giza !



    Ndiyo walikuwa wameishia kwenda kuuiba mkufu ule, ambapo waliingia kwa ur ahisi, bila kuonekana na walinzi waliokuwepo pale. Wakaliendea lile sanduku la kioo, lililokuwa limeuhifadhi ule mkufu ndani yake, wakalifungua kichawi na hatimaye kuuchukuwa bila kipingamizi chochote.



    Ulikuwa ni mkufu uliokuwa uk imeremeta kwa usiku ule na kufanya upendeze sana . Na baada ya kuuchukuwa, wakauhifadhi ndanmi ya mfuko maalum na kuondoka katika eneo lile haraka sana kama walivyofika. Wakamkuta Wi bo Eze akiwasubiri katika eneo lile alilokuwa anawasubiri.



    Saa saba za usiku wa siku ile, tayari mkufu ule wa thamani kubwa, ulikuwa mikononi mwa Wibo Eze! Mungu ampe nini?

    Basi, ndiyo hali halisi ilivyokuwa, jinsi mkufu ule ulivyoibwa na kuutikisa ulimwengu mzima!



    ********

    Frank Mumba, mpelelezi wa kimataifa, alijiandaa vya kutosha, punde baada ya kutakiwa kwenda, jijini London , nchini Uingereza, kwa kazi ile maalum. Alikuwa ameshakata tiketi ya ndege, na siku ya tatu yake ndipo alipoamua kuondoka. Saa mbili na nusu za asubuhi aliondoka pale nyumbani kwake, Survey, na kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, akisindikizwa na mdogo wake, John, aliyekuwa anaishi naye. Ile ndege aliyokuwa anaondoka nayo, ilikuwa iondoke majira ya saa nne za asubuhi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kutoka pale nyumbani kwake, walitumia usafiri wa lile gari lake dogo , Nissan March, ambalo mdogo wake ndiye alikuwa akiendesha, ukizingatia alitegemea ndiye atakayerudi nalo baada ya Frank kuondoka. Baada ya kufika uwanja wa ndege, Frank akafanya taratibu zote za pale, na mwishowe akapanda ndani ya ndege, kubwa ya Shirika la Ndege la Uingereza, British Airways.

    Saa nne kamili za Afrika mashariki, ndege kubwa aina ya Air Bus 380 ya Shirika la Ndege la Uingereza, ilipaa kutoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es salaam .



    Ndani ya ndege hiyo, alikuwepo mpelelezi mashuhuri, Frank Mumba. Akiwa ndani ya ndege, Frank alichungulia nje dirishani, ambapo aliweza kuiona mandhari ya jiji la Dar es Salaam kwa mbali kwa jinsi ndege ilivyokuwa inachukua uelekeo. Ni jiji ambalo hakujua kama angerejea hai kutoka huko anakoelekea na kufurahia kulitazama tena.



    Ndege ilipopaa angani na kukaa sawa, ndipo Frank Mumba alipogeuka upande wake wa kushoto na kumwangalia abiria mwenzake aliyekuwa amekaa naye. Alikuwa ni abiria mwenye jinsia ya kike, mwanadada mrembo, ambaye kwa muda wote alikuwa akimtupia jicho la wizi tokea walipopanda ndege hiyo. Frank akiwa ni mtu mcheshi na anayependa kufahamiana na watu, hasa wototo wa kike, aliona ni muda muafaka wa kuuvunja ukimya uliokuwa umetawala baina yao wawili.



    “Hujambo bibie?” Frank akamsalimia kwa sauti ndogo lakini iliyosikia.



    “Mimi sijambo…” mwanadada yule akaitikia kwa lafudhi ambayo ilionyesha si ya Kitanzania.



    “Mimi naitwa Frank Mumba, sjui wewe mwenzangu?” Frank akaendelea kusema.



    “Nashukuru kukufahamu. Na mimi naitwa Scola…” mwadada yule mrembo akasema.



    Frank akaendelea kumwangalia akitegemea jibu lenye maelezo ya kina zaidi kutoka kwake. Na mwanadada yule alikuwa ameshang’amua hilo , hivyo akaendelea kulifafanua jina lake ipasavyo , “Jina langu kamili ni Scola Eze…natumaini umeridhika kaka…” Scola akamaliza huku akitoa tabasamu la kukata na shoka, kiasi cha uzuri wake kuonekana!



    “Nashukuru sana Scola. Naona unatokea nchini Nigeria sivyo?” Frank akaendelea kumwuliza.“Ndiyo, wala hujakosea,” Scola akasema na kuongeza. “Umejuaje kwamba mimi ni Mnigeria?”



    “Ah, nimewahi kuishi Nigeria …na baadhi ya masomo ya chuo, nimesomea kule. Hivyo ni rahisi sana kumfahamu raia wa nchi ile…”



    “Aisee, ulisomea wapi, na ukaishi sehemu gani?” Scola akaendelea kumuuliza Frank.



    “Nimesomea katika Chuo Kiuu cha Ibadan . Lakini nilipokuwa naishi huko, nilikaa katika miji ya Abuja , Lagos , Port Harcourt na Jimbo la Kano …” Frank akamwambia.



    “Kwa hivyo inaonyesha wewe ni mwenyeji sana Nigeria hata kuliko mimi?”



    “Tena sana Scola. Kwa sababu hata wewe kwa majina yako nimeshagundua kwamba unatoka katika kabila la Yoruba…”



    “Ni kweli, nimekubaliana na wewe kuwa unaifahamu Nigeria ,



    “Scola akasema huku wakigonganisha viganja vyao vya mkono.



    “Je, unaishi Dar es Salaam ?” Frank akaendelea kumuuliza.



    “Hapana, mimi naishi London , nchini Uingereza. Nilifika Dar es Salaam kusalimia shangazi yangu anayefanya kazi katika Ubalozi wa Nigeria .”



    “Mimi pia nasafiri kuelekea London . Hivyo nisitie shaka kwa kuwa nimeshapata mwenyeji?”



    “Usihodu Frank, Scola yuko tayari kukupokea London ...”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nashukuru sana …” Frank akamwambia na kuona kuwa alikuwa amekutana na mwanadada mcheshi anayependa utani.



    “Lakini jijini London unaishi wapi?” Frank alioendelea kumwuliza Scola.



    “Kwani wewe ni mwenyeji London ?”



    “Ndiyo, London kwangu ni kama Dar, hakuna nisipopafahamu…”



    “Basi, mimi naishi mtaa wa Porchester Terrace, eneo la Bayaswater, nyumba namba 50 A…” Scola akamwambia Frank.

    Aliamua kuwa muwazi kwa mwanaume yule, ambaye alikuwa ameshamwamini kwa kipindi kile kifupi.



    “Je, umeolewa?” Frank akaendelea kumchunguza!



    “Bado sijaolewa…” Scola alijibu huku akitabasamu.



    “Urembo wote huu?” Frank alisema huku akimwangalia Scola, kisha akaendelea. “Mijibaba ya kizungu, London haijang’ang’ania?”



    “Mapenzi ni mioyo ya watu wawili wapendanao kuridhiana; wala siyo urembo na uzuri wa mwanaume au mwanamke…” Scola akasema.



    “Nimevutiwa na hekima yako ya kujibu maswali.”



    “Kivipi?”



    “Unaonyesha ni mwanamke mwenye hekima sana kwa mtazamo wangu…hivyo nakupongeza sana .”



    “Nashukuru sana …” Scola alisema na kuongeza. “Lakini wewe unashughulika na kazi gani?”



    “Mimi ni mwandishi wa habari wa kujitegemea,” Frank akamdanganya. Hakupaswa kumwambia ukweli juu ya kazi yake ya upelelezi aliyokuwa anafanya!



    “Unafanyia shirika gani la habari?”



    “Nafanyia Shirika la Reuters, shirika kongwe la habari duniani. Natumaini umenipata Scola.”



    “Nimekupata…” Scola akasema huku akionyesha kama vile alikuwa hamuamini, akijua alimdanganya. Ni kwa jinsi Frank alivyoweza kumsoma mawazoni mwake!



    “Vipi na wewe kazi yako?”



    “Mimi ni msanii.”



    “Msanii wa nini? Mwanamuziki, mchoraji, mcheza filamu au…”



    “Vyote…mimi ni msanii wa vihusika vyote ulivyotaja.”



    “Basi nashukuru…”



    Baada ya kumaliza mazungumzo yao , wote wakanyamaza huku ndege ikiendelea kukata mawingu. Na pengine wakapitiwa na usingizi, ukizingatia uilikuwa ni safari ndefu na ya kuchosha kutoka Dar es Salaam, Tanzania , hadi London , nchini Uingereza…



    ******* CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa muda wote waliokuwa safarini ndani ya ndege, Frank Mumba na Scola Eze, walikuwa wamezoeana sana . Walishirikiana kwa kila kitu, kiasi kwamba Scola alikuwa akimsikitikia sana Frank, kwani huko alipokuwa anakwenda, alikuwa ameshawekewa mtego wa kushughulikia ili asiweze kuifanya ile kazi iliyokuwa inampeleka London , ya kuutafuta ule mkufu wa thamani uliotoweka.



    Ukweli ni kwamba, Scola Eze hakuwa msanii kama alivyojitambulisha kwa Frank Mumba, na wala hakuwa ametokea nchini Tanzania kwa shangazi yake anayefanya kazi kwenye ubalozi wa Nigeria . Ule ulikuwa ni uongo uliotukuka, akiwa katika kazi yake maalum aliyokuwa amepewa na watu maalum!



    Ni kweli kwamba, Scola alikuwa anaishi nchini, kwa rafiki yake, Jenniffer Okenyi, ambaye ndiye aliyekuwa anafanya kazi kwenye Ubalozi wao, jijini Dar es Salaam. Ni mara nyingi sana alikuwa akifanya safari zake na kufikia kwa rafiki yake huyo, kiasi kwamba akawa ni mwenyeji tosha. Kwa vile alishakuwa mwenyeji, ndipo wahalifu wa kimataifa, waliokuwa na mtandao mkubwa, walipoamua kumtumia kufuatilia nyendo za Frank Mumba!



    Scola alikuwa ametumwa kumfuatilia mpelelezi yule mahiri, ambaye kwa vyovyote walijua ni lazima atakuwa mmoja wa wapelelezi wa kimataifa watakaojitokeza kupeleleza, akisaidiana na swahiba wake, Bw. Brown Lambert. Ukweli ni kwamba, wahalifu wale wa kimataifa, walikuwa na orodha ya wapelelezi wote hatari ulimwenguni, ambapo hata Frank Mumba alikuwepo!

    Basi, watu wale waliouiba mkufu ule, ndiyo waliomtuma, akiwemo kaka yake wa damu, Wibo Eze.



    Alimtumia Scola, ambaye alianza tangu mwanzo kufuatilia nyendo za mpelelezi Frank, atafanya nini tokea apate taarifa za kuibwa kwa mkufu ule. Frank hakuweza kugundua chochote, hadi siku ile alipokata tiketi ya ndege, ambapo na yeye Scola akakata tiketi ya kukaa sehemu moja ili aweze kumfuatili nyendo zake,

    na aweze kuwasiliana na kaka yake, Wibo Eze!

    Ndivyo ilivyokuwa!



    Ndege ile ya Shirika la Ndege la Uingereza, ilitua salama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Heathrow, jijini London .



    Frank Mumba alikuwa na matumaini makubwa ya kumkuta mwenyeji wake, mpelelezi, Brown Lambert, akiwa amefika pale uwanjani kumpokea. Baada ya kumaliza shughuli zote za pale uwanjani, Frank na Scola waliongozana na kutoka ndani ya jumba lile uwanja, sehemu ambapo hukaa watu wanaosubiri kupokea wageni wao wanaowasili kutoka sehemu mbalimbali. Wote walikuwa wamebeba mizigo yao katika vitoroli, ambavyo walikuwa wakivisukuma taratibu.



    “Karibu London Frank…” Scola alimwambia Frank.



    “Ahsante sana …nimekaribia…” Frank alimjibu.



    “Sasa tutaonana lini baada ya kuachana hapa leo?”



    “Utanipigia simu, kwa vile sijaifahamu ratiba ya mwenyeji wangu...” Frank alumwambia huku akimminya mkono wake laini.



    “Hakuna tatizo Frank…nitakupigia simu, siwezi kukutosa,” Scola akamwambia Frank.



    “Basi, nitaisubiri kwa hamu…” Frank akamwambia na huku akiyaangaza macho yake sehemu ile walipokuwa wamejaa watu waliofika kuwapokea wageni wao.



    Kwa mbali kidogo, Frank akamwona Brown Lambert akimpungia mkono. Lakini kwa sababu za kiusalama zaidi, Frank alimwonyesha ishara kwamba alikuwa ameshamwona, hivyo amsubiri ndani ya gari. Bw. Brown alifanya kama alivyoambiwa. Akamwacha Frank akiagana na Scola.



    Wakati Frank Mumba na Scola Eze walipokuwa wanaongea katika kuagana, alitokea mwanaume mmoja mrefu, mweusi na mwenye mwili uliojengeka. Alikuwa amevalia mavazi ya gharama na kuonekana mtu mwenye uwezo wa kifedha, ukizingatia gari alilofika nalo pale lilikuwa la kifahari aina ya Rolls Royce ya rangi nyeusi. Akawajongelea pale walipokuwa wamesimama, na wakati huo Scola alikuwa akitoa tabasamu pana baada ya kumwona mtu yule.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Oh, kaka…” Scola akasema, kasha akamkumbatia kwa ishara ya kusalimiana.



    “Oh, Scola dada’ngu…pole na safari…” mtu yule akamwambia kwam sauti ya kijivumi.



    “Ahsante kaka yangu...” Scola akasema huku akijiondoa kifuani mwa mwanaume yule.



    “Karibu sana ...” akaendelea kusema mwanaume yule. Baada ya kusalimiana na Scola, mwanaume yule akamgeukia Frank na kumwambia:



    “Hujambo bwana?”



    “Mimi sijambo…” Frank akaitikia huku akimwangalia kwa makini mtu yule. Alikuwa ni Wibo Eze, kaka yake na Scola, anayeishi pale jijini London .



    “Karibuni London,” Wibo Eze akawaambia huku naye akimwangalia kwa makini Frank.



    “Kaka, huyu ni abiria mwenzangu tuliyekutana naye ndani ya ndege, tokea Dar es Salaam , Tanzania .”



    “Oh, nashukuru kumfahamu…karibu sana . Mimi naitwa Wibo Eze…ni kaka yake na Scola…” Wibo alimfahamisha Frank.



    “Nashukuru kukufahamu,” Frank akamwambia Wibo Eze.

    “Je, una mwenyeji wako?” Wibo akamuuliza.



    “Ndiyo, ninaye mwenyeji wa kuja kunipokea…hakuna wasiwasi.”



    “Ok, kama unaye mwenyeji, sisi tunaondoka...” Wibo akamwambia huku akiendelea kumwangalia kwa makini.



    “Hakuna shaka...” Frank naye akasema huku akimwangalia Wibbo Eze! Mwili wake ukasisimka bila kujua ni kwa sababu gani!

    Baada ya kutambulishana, Scola na kaka yake, Wibo Eze, walipanda ndani ya gari, Rolls Royce, na kuondoka pale uwanjani kwa mwendo wa wastani.



    Frank akasimama kwa muda huku akiliangalia gari hilo hadi lilipopotea. Ndipo aliponyanyua hatua kuliendea gari la Brown Lambert, lililokuwa limepaki katika sehemu ya maegesho.



    Frank Mumba alilikariri jina la Wibo Eze, aliyejiita kaka yake Scola Eze. Kwa sababu mara tu alipomtupia jicho, kwa ujuzi wake na uzoefu wa kazi ya upelelezi, alimgundua kuwa hakuwa mtu wa kawaida. Alikuwa amehifadhi siri nzito, na pia, aligundua kuwa na Wibo Eze alikuwa amemshtukia kama alikuwa ni mpelelezi wa kimataifa anayefuatilia kuibwa kwa mkufu ule wa thamani, ndani ya kasri ya Malkia, jijini London .

    Wibo Eze, alikuwa ni raia wa Nigeria , aliyekuwa anaishi maisha ya kifahari katika mtaa wa Porchester Terrace, eneo la Bayswater, nyumba namba 150 A, katikati ya jiji la London . Alikuwa ni mtu mwenye fedha, alizokuwa akizitumia katika starehe, na kutembelea magari ya kifahari. Ni kwa nini apelekee kengele ya mashaka na wasiwasi katika fikara za mpelelezi mahiri, Frank Mumba?

    Ni siri gani nzito aliyokuwa ameficha Wibo Eze? Hata hivyo akamweka kiporo!

    Frank Mumba akatembea hadi alipolifikia gari la Brown Lambert, aina ya Opel Manta, lililokuwa katika sehemu ya maegesho. Bila kupoteza muda, Frank akaufungua mlango na kuingia ndani. Brown akalitia gari moto na kuliondoa kwa mwendo wa taratibu, na kuliingiza barabarani. Wakati huo, Brown alikuwa amevalia miwani mieusi, ambayo haikuwa ya kawaida, bali ni maalum katika shughuli za kipelelezi.

    “Karibu London Frank…” Brown akamwambia.

    “Nimekaribia Brown,” Frank akasema.

    “Nashukuru kwa kuzingatia muda. Umekuja wakati muafaka…”

    “Ni muhimu kuzingatia muda.”

    “Naona pia, umeongozana na kimwana wa Kiafrika…”

    “Ndiyo, nimekutana naye ndani ya ndege ile niliyokuja nayo.”

    “Aisee?” Bw. Brown akasema huku akipangua gea na kuongeza mwendo.

    “Mbona unauliza hivyo?” Frank akamwuliza. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nimeuliza tu, lakini ni bomba. Lakini cha muhimu ni kuwa macho na vimwana wa namna ile, kwani wanawake warembo wakati mwingine ni hatari sana .”

    “Hata mimi naelewa hilo , lakini vilevile wanaweza kukusaidia katika upelelezi.”

    “ Hilo ni kweli,” Brown akaunga mkono. “Lakini tuyaache hayo. Mimi nimekutafutia sehemu nzuri ya kufikia. Ni katika hoteli ya kimataifa ya London Hilton, au unasemaje?”

    “Hakuna shaka, ninashukuru sana . Nitakuwa sina fadhila kama nitasema hainifai…” Frank akamwambia. Na wakati huo gari lilikuwa likiendelea na safari hadi walipofika kwenye hoteli ile.

    London Hilton Hotel, ni hoteli ya Kimataifa, iliyoko katika mtaa wa Oxford Street , kwenye eneo moja wapo lenye mandhari ya kuvutia jijini London . Hoteli ile inatazamana na bustani ya kuvutia, ambapo vyumba vyake vimejengwa kumruhusu mteje kuitazama mandhari nzuri ya jiji lile, akiwa yuko ndani ya hoteli. Ilikuwa na vyumba 446, migahawa mitatu, baa mbili, saluni, duka la zawadi na sehemu ya kufanyia mazoezi. Ni hoteli yenye huduma zote zinazotolewa katika mahoteli ya kimataifa.

    Basi, ndani ya hoteli ile, ndipo Brown alipomchukulia chumba, mpelelezi mwenzake, Frank Mumba, ambapo alimpangishia chumba namba 222 miongoni mwa vyumba 446 vya hoteli ile ya kimataifa. Ni chumba kizuri kilichokuiwa na huduma zote muhimu, ambapo Frank asingepata shida kamwe. Baada ya kupatiwa chumba, Frank Mumba aliongea machache na Brown, kuhusu ile kazi iliyokuwa inawakabili mbele yao . Hata hivyo walipanga kuwa waianze siku ya pili inayofuata, kwani Frank alijisikia kupumzika ili kuuondoa uchovu wa safari.

    Baada ya kuhakikisha kila kitu kilikuwa safi , Brown akaondoka huku akiwa na matumaini makubwa kwa vile mshirika wake wa karibu, Frank Mumba, alikuwa amefika. Ari na nguvu ilimwingia tayari kwa kuanza msako dhidi ta wakora waliokwapua ule mkufu wa thamani kubwa. Hata hivyo, baada ya kupumzika kidogo, Frank Mumba alijihisi mpweke, kwani alikuwa akimuwazia kimwana, Scola Eze, aliyekutana naye ndani ya ndege. Kwa muda ule alimhitaji sana , hiyo aliamua kumpigia simu na kumjulisha sehemu aliyokuwa amefikia, katika hoteli ya London Hilton.

    Scola akamkubalia na kumwambia kuwa angemtembelea pale hotelini kesho yake, kwani kwa muda ule alikuwa na maongezi muhimu na kaka yake, Wibo Eze. Na pia, yeye alikuwa na hamu na kampani yake tokea walivyoachana muda ule walipowasili kwa ndege, wakitokea Dar es Salaam , Tanzania . Lakini ukweli ni kwamba huku nyuma ya mapazia, kulikuwa na siri kubwa, ambayo kamwe Frank Mumba hakuijua!

    Ni siri nzito!

    ********

    Majira ya saa tano za mchana, Wibo Eze na dada yake, Scola Eze, walikuwa wamekaa ndani ya ile sebule nadhifu, wakiwa katika maongezi, punde tu baada ya kufika nyumbani kwa kaka yake, mtaa wa Porchester Terrace. Na ile ni siku ya pili yak, baada ya kupumzika vya kutosha na kuuondoa uchovu wa ile safari ndefu ya ndege, kutoka Dar es Salaam , nchini Tanzania .

    Hakika Wibo alifurahi sana baada ya kuona dada yake, Scola, ameweza kuongozana na mtu yule muhimu, mpelelezi hatari, Frank Mumba kutoka nchini Tanzania hadi pale London . Ni kwamba walitegemea angekwenda kufuatilia wizi ule wa mkufu baada ya kutaarifiwa na Brown Lambert, miongoni mwa wapelelezi mashuhuri wa kimataifa, wanaofahamika.

    “Nakupa hongera ndugu yangu kwa kuweza kuja na mtu wetu...” Wibo akamwambia kwa sauti ndogo.

    “Nashukuru sana kaka yangu,” Scola akasema na kuongeza. “Hiyo ni moja ya kazi yangu.”

    “Pamoja na hayo, inakubidi uwe jirani naye ili sisi tuweze kumnasa tunduni. Je, unaweza kujua amefikia wapi?”

    “Ndiyo, najua. Amefikia London Hilton Hotel, chumba namba 222.”

    “Vizuri sana , je utamtembelea?”

    “Bado hatujawasiliana kuwa nimtembelee muda gani.”

    “Jaribu kuwasiliana naye mara kwa mara.”

    Wakati Wibo na Scola walipokuwa wakiongea pale sebuleni, ndipo simu ya Scola ilipoita, na alipoangalia namba za mpigaji, aliona ni Frank Mumba!

    “Mh, imekuwa bahati!” Scola akamwambia kaka yake Wibo.

    “Ni mtu wetu?” Wibo akauliza.

    “Ndiye yeye...”

    “Basi, ongea naye...”

    Scola akaipokea simu ile, na kuongea na Frank Mumba.

    “Haloo...Frank...” Scola akasema.

    “Haloo...Scola...hali yako...” upande wa pili ukasema, akiwa ni Frank Mumba aliyekuwa ndani ya chumba namba 222 alichokuwa amefikia.

    “Ni nzuri...sijui wewe...” akasema Scola.

    “Naona umeshapumzika vya kutosha, je, unaonaje ukinitembelea hapa hotelini?”

    “Hakuna wasiwasi, mimi najiandaa, nitakuwa hapo hotelini muda siyo mrefu...”

    “Haya, nakusubiri...” CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kumaliza kuongea na Frank, Scola akamjulisha Wibo kuhusu ujumbe ule wa simu, ambapo alifurahi sana , hivyo akamruhusu amtembelee kule hotelini.

    “Hakuna wasiwasi dada, unaweza kwenda kumtembelea,” Wibo akamwambia.

    Wibo akamkabidhi Scola gari dogo la kifahari, aina ya Ford Munstang, lenye milango miwili, na kumwambia aende nalo. Na kweli baada ya kujiswafi na kuvalia vizuri, mrembo Scola alipanda lie gari na kuutoka mtaa ule, kuelekea London Hilton Hotel, ambayo ilikuwa mbali na pale alipokuwa anaishi Wibo Eze. Scola alikuwa mwenyeji sana ndani ya jiji la London , hivyo barabara zake hazikumsumbua. Akaendesha gari hadi alipofika kwenye hoteli ile, ambapo akalipaki gari katika eneo la maegesho, halafu akashuka na kelekea ndani ya hoteli ile. Akapanda lifti iliyomfikisha juu alikopanga chumba Frank Mumba, na baada ya kuufikia mlango wa chumba kile, akaugoga na kuingia ndani, ambako alimkuta Frank akimsubiri kwa hamu ndani ya chumba hicho, kiasi kwamba alipoingia tu, Frank alimpokea kwa mabusu mazito kana kwamba walikuwa wamezoeana kwa muda mrefu sana .





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog