Search This Blog

Sunday, 22 May 2022

RISASI NNE - 4

 







    Simulizi : Risasi Nne

    Sehemu Ya Nne (4)



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Joru siamini kama ni wewe, siamini kabisa, sikujua kama mtoto Yule ni wako, lakini jina lake lilinifanya nimpende kama mwanangu, kwangu nilimuona kama mume, hata nilipolala naye kitandani nilihisi niko na Joru wangu, nakupenda sana Joru,” Kemi alimweleza Joru kisha machozi yakafuata na kutiririka juu ya mashavu yake meusi, yanayopendeza kwa rangi hiyo aliyojaliwa na Mungu, akamtazama Joru usoni, huku akiwa amejawa na uchungu, “Joru, nimekutunzia usichana wangu mpaka sasa ingawaje sikujua kama upo hai au umekufa, niliapa sintompa mwanaume yoyote penzi langu isipokuwa wewe, nilitaka kubkwa lakini nikapigania mwili wangu mpaka nikajinasua mikononi mwa nunda, ijapokuwa nilimuua bila kukusudia na kufungwa jela miaka miwili, bado nilikukumbuka Joru, sasa moyo wangu unauma sana kuona kuwa mtoto Yule ni wako, najua huwezi kupata mtoto bila mwanamke, ijapokuwa hautakuwa tayari kunioa lakini kabla sijampa penzi mwanaume mwingine nilitaka wewe uwe wa kwanza, wewe uondoe kizinda cha uke wangu, niko tayari hata kama umepata ugonjwa huko ulikopita,” Kemi akaangusha chozi.

    Joru akamsika mbega na kumvutia kwake, akamkumbatia katika kifua chake kipana, akamsaidia kulia kwa sekunde kadhaa, kisha akamtoa, mikono yake ikiwa katika mabega ya Kemi alimtazama usoni.



    “Kemilembe, daima umekuwa ndani ya moyo wangu, kiukweli kabisa siwezi kubishana na moyo, ninakupenda kipepeo, nimekuwa nikikulilia daima, nikikuomboleza kama umekufa lakini bado Mungu alikuwa na mpango na sisi. Nimeishi kwa taabu sana Kemi, porini na katika maeneo hatarishi, nimefanya kazi kwa bwana mmoja nikidhulumiwa ujira karibu mwaka mzima, kwa hasira ili kulipiza kisasi kwa bwana huyo aliyekuwa akinilaza pamoja na kuku ndani ya banda lililojaa utitiri, nikaamua kumbaka binti yake, Koku, kumbe siku hiyo inaoneka alikuwa katika siku za uzazi, akashika mimba pa si mi kujua, siku ya mwisho ya kuhitimu kozi yangu ya jeshi ndipo aliponilete mtoto huyu, akanambia kuwa yeye amechumbiwa na bwana mwingine hivyo mimi nilee mwanangu, nikamchukua.” Joru akaeleza, akameza mate kisha akaendelea, “Hakuna mwanamke nampenda kama Kemi, daima sikuona thamani ya maisha bila wewe, daima nilikuwa naomba Mungu kama upo hai tukutane tena na sasa limetimia, nisamehe mpenzi, nisamehe sana, lakini elewa kuwa wewe si ubavu wangu bali ni moyo wangu, nakupenda Kemi, uwe mama wa watoto wangu, tuishi, tutulie, tujenge familia,” Joru akamaliza na kumtaza Kemi usoni. Machozi ya Kemi yalikauka, tabasamu likachanua kama ua la yugiyugi. Kemi akamsogelea Joru, akashika kifungo cha gwanda lake na kukifungua, kisha cha pili, mara cha tatu mpaka vyote vikaisha, akamvua gwanda lile na kuliweka kochini, Kemi hakuishia hapo, akaufyatua mkanda mnene wa suruari ya Joru, akalegeza zipu, jicho lake likapenya ndani ya eneo nyeti la Joru, akaona jinsi gani kijana huyo alikuwa kwenye hari, kwani alituna kiukweli.



    Kemi akamkalisha Joru kochini, akamvua buti zake na kuziweka kando akamtoa na suruali akaiweka kando na kumuacha akiwa na vesti na boxer pekee, kifua chake kilichokuwa kikipanda na kushuka kilimhamasisha Kemi, akawa akikaukiwa mate kila sekunde, akasimama. Joru akaelewa nini maana ya Kemi kusimama, naye akasimama na kumkumbatia akambusu kwa bashasha, kama alivyokuwa akiona kwenye sinema, akaupitisha ulimi wake kinywani mwa binti huyo, Kemi nae hakuwa nyuma akakubaliana na hilo, ndimi zao zikaogelea katika kinywa cha kila mmoja. Joru akaishusha zipu ya blauzi ya Kemi kabla hajaitupa pembeani na kukutana na kifua mororo cha binti huyo, matiti mawili ya ukubwa wa wastani yalikipamba kifua hicho kilichopendeza, kilikuwa kikipanda na kushuka kikionesha ni jinsi gani kilitamani. Joru akacheza na mtiti hayo, akiyaminya kwa ustadi na kuyanyonyanyonya, akaona Kemi akilalamika kwa raha, akamnyanyua na kuingia naye chumbani, akambwaga kitandani kisha akamalizia kuitoa sketi ya binti huyo. Baada ya dakika kama kumi na tano za kuliwazana kwa kushikana hapa na pale kimya bila yeyote kuongea, sasa kila mtu akawa kama alivyozaliwa akishuhudia umbo la mwenzie, wawili hao wakazama katika mapenzi mazito, Kemi alikuwa akilalamika hasa kwa kusikia maumivu kwa kuwa ilikuwa ni mara yake ya kwanza, shughuli ilikuwa pevu, Joru akiwa ni mara moja katika maisha yake kufanya tendo hilo, hapo kwa Kemi alifurahia, kila mtu akawa anaongea lugha yake, lugha iliyojulikana maana na wao wenyewe.



    Baada ya saa nzima ya mapenzi mazito, tayari Joru alikuwa ameshafungua njia kama Kemi alivyomuahidi, usingizi ukawapitia wote wawili, waliposhtuka ilikuwa saa nane mchana, kila mmoja akakimbilia bafuni kujiswafi, lakini bado kila mmoja alikuwa na hamu na mwenzake, hivyo wakatumia muda mwingine kujuliana hali ndani ya bafu hilo lililojengwa kwa ndani ya nyumba hiyo. Ilikuwa ni furaha ya watu wawili kukutana tena.

    Baada ya wiki moja

    “Joru mpenzi, ijapokuwa tumeonana baada ya miaka mingi, lakini unaonekana huna furaha” Kemi alimwuliza Joru, wakiwa wameketi kwenye jiwe nje ya nyumba ya Shibagenda pamoja na mtoto wao.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ni kweli usemalo mpenzi, sina raha hata kidogo, kuna jambo natakiwa kulifanya lakini sijajua ni wapi pa kuanzia,” Joru akajibu.

    “Niambie nitakusaidia, kama tumekutana tena na jambo hilo hujaweza kulitatua basi amini kwamba ni mimi wa kukusaidia ili ulitatue sasa,” Kemi aliongea kwa lugha ya ushawishi.

    “Kemi, kabla baba yangu hajafa aliniambia maneno machache lakini pia hakuyamaliza, akakata roho,” Joru akamwambia Kemi.

    “Maneno gani?” Kemi akahoji.



    “Aliniambia nilipize kisasi kwa mtu aliyemwaga damu ya wanakijiji na damu ya Rutashobya, sasa hili ni deni ambnalo liko moyoni mwangu kwa miongo miwili sasa, nitaaniza wapi, sijajua, kabla hajafa ilionekana kuna kitu anataka kuniambia, aliishia tu kusema neno ‘nyuma ya choo’ lakini hakunambia nini alimaanisha,” Joru akamueleza Kemi kile kinachomsumbua akilini mwake.

    “Nyuma ya choo?” Kemi akauliza.

    “Ndiyo, nyuma ya choo,” Joru akajibu. Kemi akatulia kimya akitafakari jambo, kisha akamtazama Joru aliyekuwa akicheza na mwanawe, akatabasamu kuwaona hao Joru wawili wakicheza kwa furaha.

    “Joru, huna budi kufanya uloambiwa, kuna kitu nakumbuka sasa, nafikiri kitakuwa na maana kwako, nafikiri, labda ni jibu la swala lako,” Kemi alimweleza Joru, akaketi vizuri na kumtazama.



    1977

    kijijini kwa JORU na KEMI



    JIONI ya siku moja, mzee Rutashobya, aliingia chumbani mwake na kufungua mkoba ambao una kitu alichokihifadhi kwa miaka mingi sana, akakitoa na kukitia katika mfuko wa plastiki kisha akatoka nacho nje, nyuma ya nyumba akihakikisha hakuna anayemwona katika kufanya hilo. Akachukua jembe na kuzunguka nyuma ya choo, akachimba shimo la kina cha nusu mita na kutumbukiza ule mfuko, kisha akafukia vizuri na kutandaza nyasi juu yake. Akaangalia sana kama kuna mtu aliyemuona hakuona kitu.



    Wakati huo mzee Rutashobya akafanya hayo, Kemilembe alikuwa akitoka kuteka maji, akamuona baba wa Joseph akifukia kitu chini. Kemi akasimama kwenye nyasi ndefu ili kuona nini kinatukia, alishuhudia kila kitu mpaka Yule mzee alipomaliza. Kwa kuwa Kemi alijuwa kuwa hayamhusu, alaiendelea na safari ya kuingia nyumbani. Mzee Rutashobwa akamuona Kemi, akajiuliza kama atakuwa amemuona wakati akilifanya hilo, akamwita Kemi, akimtaka kwanza aweke ndoo ya maji nyumbani kwao. Baada ya hapoi Kemi alikuja mpaka pale nyuma ya choo.

    “Kemi, ulikuwa unatoka wapi?” akauliza Rutashobya.

    “Kuteka maji,” Kemi akajibu kwa lafudhi ya Kihaya.

    “Umeniona hapa nilikuwa nafanya nini?” akauliza tena.

    “Ndiyo babu nimekuona, umefukia mufuko,” akamjibu kwa ustadi sana.

    “Sasa sikiliza, hapa nimefukia sumu, sumu mbaya kabisa ambayo ukiishika lazima ufe, usije kucheza hapa na wenzako, sawa?” Rutashobya akatoa onyo.



    “Sawa babu!” Kemi akajibu. Watoto wa kijiji hicho walizoea kumwita mzee Rutashobya ‘babu’ kutokana na uchezhi wake kwa watoto, akiwatania kila kukicha, hivyo daima walimpenda sana mzee huyu.

    “Usimwambie mchumba wako Jose, sawa?” akamsisitizia. Kemi akaitikia na kukiri kuwa hatomwambia mtu. Kemi alipoondoka mzee Rutashobya nae akatoka eneo lile, alijua wazi kuwa baada ya siku chache tu Kemi atasahau juu ya tukio lile na ndivyo ilivyokuwa.

    Kemi hakukumbuka tena hata kama alimuona mzee huyo akiwa pale, siku, miezi ikapita. Lakini yeye tu Rutashobya aliyejua kuwa amefukia kitu gani, malengo yake si kumpa mtu yeyote kitu hicho bali aliamua kukitupa kwa kuwa ni sumu mbaya kabisa, alikitupa kwa mtindo huo kwani aliona wazi kama akitupa kwa njia ya kawaida, watoto na watu wengine wangezurika nacho.



    Siku alipokuwa anakufa baada ya mateso makali ya vibaraka wa nduli Idd Amin, aliona kuwa ni wakati wa kumwambia mwanawe, japokuwa haikuwa dhamira yake tangu kwanza, kabla hajamwambia ni nini kipo mzee Rutashobya akakata roho, Joru akabaki gizani, hakujua ni nini baba yake alitaka kumwambia.



    Rejea Joru na KEMI

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    JORU alisisimkwa mwili kwa habari hiyo ya Kemi, hakuwahi kuisikia hata mara moja katika maisha yake, alimkumbatia Kemi kwa nguvu.

    “Kemi, twende kijijini, nikachimbe hapo nione kuna nini!” joru alisisitiza. Kemi akamtazama Joru, akatikisa kichwa.

    “Joru, hakuna kijiji kule ni mapori na machaka ya kutisha!” Kemi akamwambia Joru….





    Siku mbili baadae…



    JOSEPH Rutashobya alisimama juu ya kilima kidogo, akatazama eneo lote lililokuwa na kijiji walichokiishi zamani, mahame, hakukuwa na nyumba hata moja, hakukuwa na binadamu aliyeishi, migomba na mibuni vilifanya machaka ya kutisha. Joru akainama kichwa kwa muda na kuwaomboleza wapendwa marehemu wote waliouawa siku hiyo, aliwaombea na wale wote walijaribu kukipigania kijiji chao. Akamtazama Kemi aliyekuwa kajifunga lubega, wakaanza kutelemka kilima kuelekea bondeni. Mkononi akiwa na upanga na jembe dogo, Kemi alikuwa na akimfuata kwa nyuma wakati Joru akikatakata vichaka na kufanya njia. Haikuchukua muda walikuwa chini kabisa, kwenye tambarare ya vichaka. Joru alitazama eneo lile, akakumbuka vipindi vingi sana vya utoto wake, akamtazama Kemilembe, aktazama tena eneo lile walilokuwa wakiishi.



    ‘Joseeeeee, twende tukacheze !!!!’



    Aliihisi sauti ya kitoto ya Kemi ikipita masikioni mwake miaka zaidi ya ishirini iliyopita, hisia kali zikauteka moyo wake, kumbukumbu ya matukio mengi ya maisha ikajaa kichwani mwake, aliwaona mtu mmoja mmoja aliyemkumbuka, rafiki zake, wazazi wake na memngine mengi. Machozi ya uchungu yakamtiririka, akamkumbatia Kemi kwa uchungu.

    “Kemi, kijiji kilichotulea, kijiji kilichotukutanisha duniani, kijiji kilichotujengea mapenzi yetu, kijiji tulichokipenda sana, leo hii si kijiji tena, mahame na ukiwa…” Joru alimwambia Kemi. Kemi akaegama kifuani mwa Joru.



    “…Wewe ni mali ya Mungu na mimi ni Mali ya Mungu…”



    Sauti iliyofuatiwa na mwangwi, sauti mbaya iliyomchukiza Joru, na kutia hasira mpya katika moyo wake, donge lilimshika, Joru alianza kutetemeka na kupumua kwa nguvu. Kemi aliyaona mabadiliko hayo ya Joru, akamtazama kwa woga kijana huyo aliyekuwa na mwili unaotisha pindi awapo hasirani.

    “Nini Joru?” Kemi aliuliza.

    “Lazima nilipe kisasi, lazima nimuue kwa mkono wangu, damu ya Rutashobya na Watanzania haiwezi kupotea hivi hivi,” Joru alimjibu Kemi, kisha akasogea taratibu kwenye eneo ambalo alihisi kabisa ndipo alipouawa baba na mama yake



    “………Aaaaaaaaiiiigghhh!!!!.........”



    Sauti ya mama wa Joru ilirudi kwa kishindo moyoni mwa Joru, akashtuka, moyo ukawa unamwenda mbio, akasimama na kutazama chini taratibu, akaondoa mguu wake uliokuwa umevikwa buti la kijeshi, buti la Muamerika, akaona kitu kinachong’aa kwa jua lile la saa nane mchana, akainama na kufukua udongo ule kidogo tu, kidani, akakivuta, kikajifukua kutoka udongoni. Joru alikikumbuka kidani kile, akakigeuzageauza, kidani cha mama yake. Alikisafisha kwa nguo yake, kilikuwa na kutu lakini hazikuwa za kutisha, Joru akamtazama Kemi, akaitazama shingo ile ya upanga, akampa ishara ya kuwa asogee, naye akafanya hivyo aliposogea akamvisha kidani kile shingoni mwake.



    “Sasa wewe ndiye mama Rutashobya!” Joru akamwambia, kisha wakaendelea kuelekea eneo husika.

    “Asante Joru,” Kemi alijibu huku akiendelea kumfuata nyuma Joru mpaka walipofika eneo walilohisi ni lenyewe ambalo lilikuwa na choo.

    Kemi akavuta hatua chahe, akasimama mbele kidogo ya Joru, palikuwa na udongo uliodidimia kiasi na nyasi kavu zilizokuwa eneo hilo. Akasimama na kutazama mbele, akauona mti ambao alijificha akimtazama mzee Rutashobya alipokuwa akifukia mfuko ule, kisha akarudisha macho yak echini tena na kuonesha kidole.

    “Joru, ni hapa bila shaka, siku ile mimi nilijificha pale kwenye ule mti na ndoo yangu kichwani,” Kemi akamwambia Joru. Macho ya joru yalimtazama Kemi kwa upendo mkubwa.

    “Wewe ni mtu wa pekee sana kwangu,” Joru akasema, kisha akainua kijembe chake na kuchimba taratibu. Joru alichimba huku Kemi akiwa pembeni kuangalia kinachotokea. Haikuchukua muda, Joru aliunasa mfuko wa plastiki, akatupa kijembe pembeni, akaushika ule mfuko mchafu na kuuvuta taratibu kuja nje,

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Kesho na keshokutwa utakua kijana mwanangu, hakikisha unalipa kisasi kwa damu hii inayomwagika, damu ya familia yako, damu ya wazazi wako,’



    Sauti ya baba wa Joru ilimrudia mwanawe alipokuwa akivuta mfuko ule, wakati mfuko ule ukichomoka taratibu ardhini, Joru aliukumbuka, aliukumbuka bila shaka.

    ‘Jose, usiutupe mfuko huo una kazi kubwa baadae,’

    Maneno hayo yalipata maana siku hiyo kwa Joru, mawazo yalikuwa lukuki, hakuna aliyeongea wala kumuuliza mwenzake, kila mmoja alitaka kuona tu nini kilikuwa kwenye mfuko huo.

    “Joru, kuna sumu humo ndani” Kemi alimwambia Joru.

    “Hakuna sumu, baba alikuwa anakutisha tu, hakutaka uje uchezee, ngoja uone,” joru akajibu na kumalizia kuuvuta ule mfuko nje kabisa ya shimo lile, ulikuwa umefungwa vizuri, umefungwa kifundo. Joru akaupapasa, sasa alikuwa mtu mzima alielewa nini kilikuwa katika mfuko huo, akaufungua na kukitoa, bastola ya kizamani na risasi nne. Tabasamu pana likaupamba uso wa Joru. Akaigeuzageuza bastola ile, ilikuwa ya kizamanai kwelikweli, na risasi zake nne ambazo hazikuwamo katika magazine, ila pembeni katika kikasha cha chuma. Kemi alishangaa sana aliijua bastola kwa kuwa aliwahi kuiona katika senema za kizungu, na aliiona kwa askari wakati alipokuwa gerezani.



    Joru akaitazama ile bastola iliyokula kutu za kutosha, hakika ilikuwa ya kizamani. Alipokuwa mtoto alikiona kitu hiki mara kadhaa ndani kwako lakini hakuwahi kujua kazi au matumizi yake, lakini sasa anajua hata kwamba ilitumika katika vita kuu ya pili ya dunia ambayo kwa simulizi, baba yake mzee Rutashobya alishiriki, babaambaye hata yeye alizoea kumwita babu. Akachomoa risasi zile nne ailizokuwa ndani ya kibweta kile cha chuma, ni nne tu na si zaidi, alizitazama kwa makini, hakujua lengo la baba yeke kuzifukia, labda hakutaka mtu azione au hakutaka watu wabaya kama Mali ya Mungu kuzipata kwa maana wangetumia kwa matumizi mabaya vilevile.

    “Kemi, turudi, hakuna la zaidi,” Joru akamwambia Kemi kisha wakageuza na kurudi walikotoka wakiwa wameshikana mikono.

    Joru alifika nyumbani, kazi ya kwanza aliyoanza nayo ni kuisafisha ile bastola kwa kutumia mafuta maalumu ili iweze kufanya kazi upya. Alikuwa kaka peke yake nyumba ya nyumba wakati Kemi akiendelea na kazi nyingine kwa mama Shibagenda ikiwamo kumlea Joru mtoto.

    Masaa matatu, yaliirudisha ile bastola katika uhai mpya, ilikuwa iking’aa, iking’aa mpaka inaumiza macho. Mtutu wake wa chuma king’avu ulirudi katika uhai, kitako chake cha mbao ya mpingo kiling’azwa kwa mafuta, kila kitu kilirudi kati uhai.



    Joru aliziweka sawa risasui na akahakikisha kuwa zipo sawa kwa kazi zitakayotumwa, akavuta kikasha kingine ambacho risasi zake zinaingiliana na ile bastola, akajaribu kuipachika katika magazine ikakaa sawa akapachika nay a pili nayo ikawa sawa, akaichukua ile magazine na kupichika mahala pake, akajaribu hiki na kile. Joru aliziheshimu zile risasi nne, hakutaka kuziharibu kwani alijua sasa kuwa zina kazi maalumu, kazi ngumu ya kisasi. Akaishika bastola, akafanya kama analenga, akabana jicho moja, bahati nzuri kulikuwa na mwewe aliyekuwa anapita, akaondoa usalama na kufyatua bastola hiyo. Kwa mara ya kwanzaq alipata ladha ya mlio wa bastola ya kale, Yule mwewe alijilaumu kwa nini alipita eneo hilo, kwani ni manyoya tu yaliyoonekana angani, alipotua chini hakujulikana ndani ni wapi na nje ni wapi. Joru akatikisa kichwa kuonesha haamini kinachotokea.



    “Asante Rutashobya, risasi hizi nne zitaishia kichwani mwa Mali ya Mungu kama amekufa basi nitazifyatua juu ya kaburi lake,” Joru alijiseme kwa sauti ya utulivu, akachukua zile risasi nne na kuzisweka katika kibweta chake kama kwanza, akakiweka katika mkoba wake mdogo wa kijeshi kisha akaiweka ile bastola na kunyanyuka kutoka pale alipoketi kwa muda mrefu. Alipogeuka akakutana uso kwa uso na mama Shibangeda.

    “Vipi Joru mbona watushtua?” Mama Shibagenda akauliza.

    “Pole na samahani mama, nilikuwa nafanyia mazoezi kifaa change maalumu, maana natakiwa kwenda Uganda siku nne zijazo,” Joru akajibu.

    “Kikazi au binafsi?” mamaShibagenda akauliza.

    “Kikazi mama, na ni kazi ya hatari sana kuliko unavyofikiria,” Joru akajibu kwa kirefu.

    “Kazi gani mwanangu?” mama Shibagenda akazidi kuhoji.

    “Mama, wakati wa vita vya Uganda. Jeshi la Tanzania lilifanya kazi kubwa sana ya kumfurusha nduli Idd Amin, lakini kuna kitu walikuwa hawajamaliza, nimetumwa kwenda kumaliza hicho kimoja, ila ni hatari, kuna mawili, kurudi au kuzikiwa huko huko,” Joru alimwambia mama Shibagenda.



    “Joru!” Mama Shibagenda aliita kwa mshangao, akajishika kiuno na kumtazama mwanajeshi huyo kijana.

    “Mbona unashtuka mama?” Joru akauliza na kusimama kutoka pale alipokuwa.

    “Mimi hiyo kazi yenu inaniuzi, yaani baba yako angejua unataka kwenda huko angeshakukataza, bora ulienda kwa kutoroka, ila we Joru ni dume huogopi,” Mama Shibagenda akamwambia Joru. Kisha wote wawili wakafuatana kurudi upande wa pili wa nyuma, mwendo wa hatua ishirini, mama Shibagenda akasimama na kumzuia Joru.

    “Enhe, nambie, kuhusu Kemi, nimependa sana stori yenu, sasa unaoa au unaenda kumtafuta Yule uliyezaa naye?” Mama shibagenda akauliza.

    “Mama, mimi sijazaa na mtu, Yule kazaa mwenyewe, kwanza kaniuzi sana, mwanamke gani mwenye roho mbaya ya kuniletea mtoto na lkisha yeye kuondoka, je kama asingeniona, si angeweza hata kumtumbukiza chooni? Wanawake wa mtindo huu hawafai katika jamii, wajirekebishe. Lakini nakushukuru mama kwa kunilelea mtoto, na Mungu alikuongoza ukampata mpenzi wangu kipenzi, Kemilembe, huyo ndiye mama wa Joru, nampenda sana Kemi,” Joru aliongea kwa hisia na masikitiko.



    Joru akamuona mwanawe akicheza kibarazani pamoja na mtoto wa Shibagenda.

    “Kuna watu wamezaliwa na wema wa ajabu na upendo wa kupindukia, nah ii ni familia ya Shibagenda, asanteni sana kwa ukarimu wenu mmenilea, mkatulea mpaka sasa, muendelee kutulea mpaka tutakaposimama kwa miguu yetu wenyewe, nitamuoa Kemi pindi nikitoka kwenye Operesheni Mali ya Mungu huko Uganda,” Joru akamwambia mama Shibagenda na kumnyanyua mwanawe.

    “Yalivyofanana basi!!!” Kemi akazungumza kutokea mlangoni alikokuwa amejificha.

    Joseph Rutashobya aliitazama kalenda ya ukutani kwenye ukuta wa nyumba ya Shibagenda, akahesabu siku zilizobaki kwa mapumziko yake, hazikuwa haba, zilikuwa saba, akatikisa kichwa, akaamua moyoni kesho naanza oparesheni yangu, naipa siku tatu iwe imekamilika,” akajisemea.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘….Hakikisha unatimiza hilo kama ulivyosema…!’



    Alihisi sauti kama ya baba yake ikimwambia. ‘Nitatimiza,’ aliijibu.

    Siku hiyo usiku Joru hakulala vizuri, alisumbuliwa na ndoto za kutisha, ndoto za kuogofya na kumkatisha tama, mara kwa mara alishtuka na kuketi kitandani. Kemi naye alimka mara zote hizo na kumtuliza Joru, kumfariji katika mahangaiko yake. Ilipofika saa tisa usiku Joru akachuku begi lake la kawaida tu sio la kijeshi, akapanga baadhi ya vitu vyake muhimu. Aliitazama sana bastola ile aliyoichimba porini, sasa iking’aa kana kwamba ni mpya lakini utaijua kwa umbo lake kuwa ni ya kizamanai sana, Smith and Wesson, hakuwa na uhakika kwa hilo.

    “Kemi nakwenda Uganda kufanya kazi aliyonituma mzee Rutashobya, usimwambie mtu, lakini nitarudi baada ya siku tatu,” Joru akamwambia Kemi aliyekua amejivuta jirani naye kabisa.

    “Joru mpenzi, naamini kabisa utarudi na utafanikisha kazi yako, sina kinyongo na safari yako, lakini utuletee zawadi wenzako,”Kemi alimwambia Joru.



    “Usijali, baba akitoka safari ni vizuri kuleta zawadi, name nitawaletea zawadi, zawadi ya ushindi,” Joru akamwambia Kemi.

    “Baba usiende hivi hivi, japo tupeane Baraka maana nitakukosa kwa muda wa siku kadhaa,” Kemi alisema huku akisimama na kukiacha kitenge chake kikiuacha mwili nay eye kubaki kama alivyo, akamfuata Joru pale aliposimama alipokuwa akiweka vizuri mambo yake, akamfungua taulo naye akabaki vilevile, wawili hao wakaingia upya mapenzini, kitanda kikubwa kikawapokea na blanketi pana likawasitiri.



    §§§§§



    Kulipokucha, Joru akamuacha Kemi na mtoto akabeba kibegi chake na kutokomea kwenye giza la nje. Alipofika eneo la sokoni, alikuta Landrover 109 inayoelekea mpakani katika daraja kubwa la mto Kagera, hakusita bali alilipanda na kuanza safari yake. Mida kama ya saa mbili asubuhi hivi, alifika mpakani, Joru hakuwa na hati ya kusafuria lakini kwake hilo halikuwa tatizo, aliingia kenye mgahawa na kutafuta madereva wa malori, akampata mmoja, Kibinda.

    “Mambo vipi?” Joru alimsalimia jamaa huyo mfupi, mnene anayeonekana kuwa na ukorofi mwingi machoni mwake.

    “Poa, vipi brotherman, mbona kifurushi?” alimuuliza huku akiendela kunywa bia yake.

    “Wewe ndio Kibinda?” Joru akauliza.

    “Mi sipendi mtu anyeuliza majibu ujue, ee haya sema ndio mimi,” Kibinda akajiubu kwa nyodo. Mara mhudumu wa hapo akaja na chupa nyingine kwenye chano akamletea Joru. Joru akaitazama na kumtazama Yule binti, kisha macho yake akayarudisha kwa Kibinda.

    “Situmii kilevi,” akamwambia.

    “We mwanaume gani wewe, kilevi hutumii na huyo binti je humtumii? Chagua kimoja, hapa kuna sheria, ukikutana na Kibinda lazima ufanye kile anachokifanya yeye kwa wakati huo, ndiyo mtaenda sawa, kama la, potea nisikuone,” Kibinda aliongea kwa sauti yake ya kilevi.



    Joru alimtazama kijana huyo aliyekuwa akijimiminia bia kama baba yake ndiye aliyetengeneza kampuni hiyo, safari.

    “Kazi yangu hairuhusu mimi kutumia chochote kati ya ulivyovitaja,” Joru akamwambia Kibinda.

    “Kazi yako kazi gani? We una kazi wewe? Lonyalonya hivi utakuwa na kazi wewe! Basi we hunifai katika ufalme wangu, potea hapa,” Kibinda akaongea kwa sauti ya juu na kuitisha bia nyiongine.

    “Mimi kazi yangu ni kuua! Na leo ni zamu yako,” Joru akamwambia Kibinda.

    “The the the the, wewe unaweza kuua wewe? Nikikuletea mende hapa unaweza kuua wewe?” Kibinda akacheka sana, hali hii ikamletea hasira Joru, akasimama na kusogea pale alipoketi Kibinda. Kofi moja, kofi la pili, pombe zikamtoka Kibinda, akamkwida na kumuinua pamoja na unene wake, Kibinda aliinuliwa juu, miguu ikamning’inia chini.



    “Sikiliza we mpumbavu!” Joru akaanza kwa kusema, “Sasa ukitaka nisikuuwe utafanya lile ninalotaka, maana nilitaka nitumie lugha laini sasa wewe umenitaka nitumie lugha ya ukali,” Joru akamaliza.

    “Sawa kaka, hamna shida! Hamna Shida,” Kibinda alijibu, watu walianza kujaa kwenye kile kimgahawa kushuhudia kinachotokea. Joru alimuachia ghafla na Kibinda akajibwaga chini kama gunia la chumvi.

    “Twende kwenye gari yako,” Joru alimuamuru na Kibinda akafuata kama alivyoahidi.

    International, lilikuwa ni lori kubwa lenye tela la urefu wa futi arobaini limeegesha nje ya mgahawa huo, Kibinda akapanda na Joru akafuatia.

    “Unaijua Uganda vizuri?” Joru akamuuliza Kibinda.

    “Ndiyo naijua sana tu kuliko unavyofikiria,” Kibinda akajibu.

    “Nataka unifikishe hapa,” Joru akamuonesha eneo analotaka kwenda, akiwa mkononi kakamata kipande cha karatasi chenye ramani ya Uganda.

    Kibinda badala ya kujibu akatoa macho kama mjusi aliyebanwa na mlango.



    Akachukua ile karatasi ambayo Joru alimuonesha, hakuielewa hata ni nini kinachoonekana zaidi ya kuona vijimistari vilivyopita huku na kule, alichokielewa tu ni kuwa alikuwa ameshika ramani.

    “Umepaona hapa?” Joru akamuonesha kwa eneo Fulani katika ramani hiyo kwa kutumia kidole chake.

    “Nimepaona,” akajibu.

    “Unapajua?”

    “Ndiyo napajua,”

    “Nataka nifike hapa,” Joru akasisitiza.

    “Sasa kaka hapa ni mbali, na mimi siendi huku, mi naenda Mbalala, we unataka nikupeleke Jinja wapi na wapi?” Kibinda akalalamika.

    “Nitakulipa pesa nyingi,” Joru akamwambia.

    “Pesa sio tatizo kaka, hata mi nanazo, fikiria hii gari ninayoendesha ina mtambo wa GPS popote ninapoenda wananiona, unataka kibarua kiote nyasi?” Kibinda akazidi kulalamika.

    “Sawa nimekuelewa, we unataka kuniacha wapi?” Joru akahoji.

    “Mi ntakupeleka mpaka hapa njiapanda, umepaona, pale we utakwenda Jinja na mi nitakwenda Mbalala,” Kibinda akajibu huku akiwasha gari yake tayari kuvuka daraja la mto Kagera.

    ‘…Uganda, Joseph Rutashobya anakuja, hata kama sikuweza kuja kupigana nawe, lakini nakuja kumalizia kile kilichobaki…’

    Joru aliongea moyoni akiiambia maneno nchi hiyo ya Uganda wakati gari ile ilipokuwa ikilianza daraja la mto Kagera ambalo ndio mpaka mkubwa wan chi hizi mbili zilizowahi kuingia katika vita miaka ya nyuma lakini bado zote zipo katika shirikisho la jumuia ya Afrika Mashariki.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘…Maiti nyingi za wasio na hatia zilipita katika mto huu zikipelekwa na maji pasipojulikana, watoto wakabaki yatima, wamama wakabaki wajane…”

    Joru aliangusha machozi, akayatazama maji yaliyokuwa yakitirirka kuelekea Ziwa Victoria, mto Kagera ukaachwa nyuma, Joru akaendelea na safari ndani ya nchi ya Uganda akiwa na mawazo lukuki. Kibinda aliendelea kuliendesha lori lake lililokuwa likivuta mzigo mzito. Joru alikuwa akiwaza mengi sana akifikiria wapi ataanzia katika kazi yake hiyo, atajuaje mahali alipo huyo anayemtaka, alijipa moyo, ‘nitampata tu, kama kafa nitahani msiba,’ akajiwazia zaidi na zaidi.

    “Vipi kaka mbona huongei?” Kibinda aliuliza.

    “Aaa nna mambo mengi sana kichwani,” Joru akajibu.

    “Sema bwana unaweza ukakuta mi ndo nakusaidia kutatua shida yako, ushawahi kufika Uganda wewe au mara ya kwanza sasa?” Kibinda akaongea.



    “Hapana sijafika kabla, ni mara ya kwanza,” Joru akajibu.

    “Sasa Jinja unaenda kufanya nini au kwa nani?” Kibinda akauliza.

    “Naenda kumtafuta kaka yangu, nasikia ni mwnajeshi huku Uganda ila sijui yupo wapi,” Joru akadanganya.

    “Aaaa ok, pole sana, sasa huku kambi ni nyingi lakini utampata tu, mi nina rafiki yangu mwanajeshi hapo Kampala, nitakuunganisha naye kisha yeye atakusaidia kwa mapana na marefu, kama hutojali lakini,” Kibinda aliongea kwa sauti na kumalizia na cheko kubwa sana kama ilivyo kawaida yake.

    “Asante ntashukuru sana nikikutana na rafiki yako,” Joru akajibu.

    “Tena pale utafurahia maisha maana kuna totoz za ukweli kaka, kama unatumia ulevi huo mwenyewe utanitafuta kunipa mrejesho, wasichana wa Kiganda wako poa, si wachoyo, hawawezi kukunyima tena wewe mgeni, utawafaidi kikwelikweli,” Kibinda alikuwa akiendelea kuongea huku akiwa kang’ang’ani usukani wa lori kama mtu aendeshavyo baiskeli.



    §§§§§



    9

    Kanali Malyamungu. Nani asiyemjua kanali Malyamungu katika Uganda? Mwanajeshi aliyekuwa na cheo cha chini lakini mara tu, ghafla akapandishwa mpaka kuwa kanali wa jeshi, cheo alichopewa Rais wa kipindi hicho, dikteta Idd Amin na kumfanya kuwa mtu wake wa karibu sana. Mauaji mengi ya Waganda wenye vyeo mbalimbali wakiwemo maofisa wa jeshi, mawaziri, mabalozi ni yeye aliyeyatekeleza kwa amri yake, wakati mwingine kwa kutumia ajali za kutengeneza.

    Kabla ya kuwa mwanajeshi, Malyamungu alikuwa mlinzi katika lango la kiwanda Fulani na baadae alipojiunga na jeshi alipandishwa cheo haraka mpaka kufikia ngazi ya Kanali. Alikuwa ni afisa wa jeshi ambaye kila mtu alimwogopa, kila aliyemwona alitetemeka kwa hofu, alipendwa na Idd Amin na aliaminiwa katika mipango mingi hasa mipango ya siri kama ule wa kumuua askofu mkuu uliotokea miaka mingia nyuma kwa kisingizio kuwa askofu huyo alikuwa akihifadhi silaha nzito za kivita kwa lengo la kuipindua serikali iliyopo madarakani, lakini haikuwa kweli. Askofu huyo na mawaziri wengine waliuawa kwa siku moja kwa ajali ya kutengeneza lakini miili yao ilipofanyiwa uchunguzi waligundulika kuwa na matundu ya risasi. Kanali Malyamungu, aliyekuwa kiongozi wa kikosi kinachotekeleza mauaji ya aina hiyo aliutangazia umma asubuhi ya saa tano kuwa imethibitika kuwa askofu huyo alikuwa na silaha akishirikiana na Rais aliyepita, Milton Obote kutekeleza uasi dhidi ya serikali iliyopo madarakani, akaonesha na ushahidi wa silaha mbalimbali walizozikamata, lakini ilikuwa ni mchezo mchafu dhidi ya watu hao.

    Baada ya kulitumikia jeshi hilo kwa miaka mingi, akiwa amekoswakoswa na mapigano ya vita vya Kagera, Malyamungu alistahafu jeshi na kuamua kurudi kwake alikozaliwa katika eneo la Mutibwa, Jinja na kuanza maisha ya kilimo na ufugaji akiwa na mkewe na watoto wao wawili.



    Hakuwa hi kufikiri hata mara moja kuwa kuna mtu au watu watakaokuja kuulipa uovu wake, aliamini eti uovu haulipwi. Umri ulikwenda, alipostahafu, serikali ikampa na ulinzi wa kumlinda. Eneo la nyumba yake lilikuwa haliingiliki kirahisi, kamera za usalama zilitapakaa kila kona ukiachana na mbwa na walinzi waliopo katika eneo hilo.

    LORI alilopanda Joru lilifika Masaka, hapo walikutana na barabara inayotoka Kampala kuelekea Mbalala mpaka Rwanda. Kibinda akaegesha lori pembenikaribu kabisa na kituo cha mafuta cha Shell, akateremka kuliacha gari likiunguruma.

    “Oe!” akamwita Joru na kumpa ishara ya kuwa amfuate, naye akafanya hivyo. Wakafuatana na kuingia kwenye klabu moja ya usiku, klabu maarufu sana eneo la Masaka. Ndani ya klabu hiyo kulikuwa na muziki mkubwa, watu wa kila aina, wahuni na wasio wastaarabu, Malaya na makahaba waliovalia nguo na wengine kutembea na chupi tu huku wakitomaswa makalio na vijana waliokuwa humo. Joru akamfuata Kibinda mpaka katika meza moja iliyokaliwa na watu wane, Kibinda akaketi na Joru akafanya vivyo hivyo.



    “Jackson Mutebezi, kutana na jamaa yangu Joru,” Kibinda aliwatambulisha wawili hao. Wakapeana mikono, “Sasa mi si mkaaji nipo kwenye ruti zangu za kawaida, Jackson, huyu jamaa ana shida atakueleza mwenyewe kisha umsaidie mi nitapita wiki ijayo, tafadhali,” Kibinda alimaliza na tayari akawa amekwishanyanyuka.

    “Hamna tabu pal, mimi na wewe tumetoka mbali, nitampa msaada anaoutaka,” Jackson Mutebezi alimjibu Kibinda na kuagana.

    Jackson Mutebezi alimtazama Joru juu mpaka chini.

    “Unatoka wapi?” akamwuliza.

    “Tanzania, Mutukula,” Joru akajimjubu.

    “Oh good, (vizuri) napafahamu sana hapo,” Jackson akajibu.

    “Umepafamuje?” Joru akauliza.

    “Joru, ni stori ndefu sana yaani ndefu sana, sitaki kuikumbuka,” Jackson akajibu.

    “Napenda kuifahamu siku moja hiyo stori,” Joru akasisitiza.

    Jackson akamtazama Joru na kumkazia macho.



    Joru naye akabaki kumtazama kijana huyu aliyeonekana tayari yuko na pombe nyingi kichwani.

    “Sikia,” Joru akamwambia, “Mimi natoka wapi na wewe unatoka wapi havina nafasi kwa sasa cha maana ni kile kilichonileta mpaka leo niko na wewe, najua utanisaidia,” Joru alimaliza. Jackson Mutebezi akaingiza mkono mfukoni na kutoa sigara yake, akaipachika kinywani na kuibana kwa midomo yake.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ngoja nivute nipate akili, maana nikikutazama naona wewe waweza kunisaidia katika mkakati wangu Fulani,” Jackson aliyasema hayo huku akijipapasa mifukoni kutafuta kiberiti. Joru akalielewa hilo, akachomoa kiberiti chake cha gesi na kukiwasha mbele ya kijana huyo, mlio wa kiberiti uliyarejesha macho ya Jackson kwa Joru.

    “Hutakiwi kusumbuka wakati mimi nipo, vivyo hivyo sitakiwi kusumbuka wakati wewe upo,” Joru alimwambia Jackson, Jackson alimtazama Joru na kuiwasha sigara yake.

    “Asante rafiki, lete stori,” Jackson alimwambia Joru.

    “Umenambia unaijua Mtukula, niambie unaijuaje?” Joru alimwuliza Jackson. Jackson akainama kwa muda kisha akainua kichwa chake na uso wake akamuelekezea Joru.

    “Niliokota maiti ya baba yangu katika mto Kagera na tulishindwa kuirudisha Uganda tukaamua kumzika Mtukula,” Jackson aliongea kwa uchungu.

    “Pole sana Jack, hastahili kuishi yeyote aliyeyafanya haya,” Joru akamsindikiza kwa maneno.

    “Any way, tuyaache hayo, una shida gani nikusaidie kabla jua halijawia?” Jackson akamuuliza Joru.



    “Sina haja ya kujificha, nataka habari ya mtu mmoja tu, Kanali Malyamungu, anaishi wapi au kazikwa wapi bas! Nahitaji kumsalimu,” Joru aliongea huku akipumua kwa nguvu. Jacskon akamkazia macho Joru.

    “Unamjua mtu huyo?” akamwuliza Joru.

    “Simjui,” joru akajibu.

    “Ndio maana unamtafuta, kwa sababu humjui, yupo, yupo hai, wala hajafa, lakini si rahisi kumuona kwa sasa, amestahafu jeshi miaka kama saba iliyopita,” Jackson akajibu. Joru akasikiliza kwa makini sana habari hiyo iliyotolewa kwa ufupi na kijana huyo anayeonekana tangu machoni kuwa yupoyupo tu, kijana asiyejali, aliyechoka maisha.

    “Joru, we hunijui wala mi sikujui, lakini wewe ni kijana mwenzangu wote sisi tunasaka maisha, achana na huyo mtu, kabla hujafika anapoishi utakuwa marehemu tayari,” Jackson alimuonya Joru. Joru alifikiria kwa kina shauri hilo lakini hakuona umaana wake.

    “Wacha aniue, lazima niende, nipe ramani hata kama ni usiku huu, nina siku mbili tu ya kukutana na mtu huyu ili nimpe kile alichokisahau Mtukula,” Joru aliongea kwa jazba akimtazama Jackson usoni. Jackson naye macho yake aliyakaza kwa Joru, wote walitazamana kama majogoo yanayotaka kupigana, kisha Jackson akanyanyuka na kuelekea mahali Fulani akipenya penya kwenye kundi la vijana wa kike kwa wa kiume waliokuwa wakicheza muziki. Joru nae akasimama na kumfuata kwa njia hiyohiyo mpaka wote wakajikuta nje ya club hiyo, Jorru akaongeza mwendo na kumfikia Jack, akamsimamisha na Jack akatii.



    “Sikiliza kaka, mi yatima sina baba sina mama na huyo ninaye mtafuta ndiye aliyenifanya niwe hivi, nikpo tayari kwa lolote, akiniwa au nikimuwahi yote sawa,” Joru alisisitiza.

    Jackson akamtazama Joru na kutikisa kichwa, kisha akainama na kuivuta suruali yake, akaacha mguu mmoja wazi.

    “Tazama huu mguu,” akamwonesha Joru.

    “Una nini? Au umekuwaje?” Joru akauliza.

    “Huuoni? Sio mguu halisi ni wa bandia huu,” Jack akamjibu huku akimuonesha ule mguu. Joru akainama na kuupapasa na kuugongagonga, kweli ulikuwa ni mguu wa bandia, mguu uliotengenezwa kwa plastiki ngumu.

    “Haya yalinipata kwa sababu ya huyo mtu, huyo mtu alimuua baba yangu, baba yangu alikuwa ni mtu wa juu sana serikalini wakati wa Idd Amin lakini alimchinja kama kuku, nilipokuwa mtu mzima nikaamua kulipiza kisasi kama usemevyo wewe lakini sikufika popote, nilikamata na kuvunjwa mguu huu na kuambiwa nisirudie tena, sasa wewe Joru unajiamini nini kupambana na shetani Yule?” Jack akaongea kwa uchungu. Kisha akamuwacha Joru na kuondoka akaingia kwenye gari yake na uiwasha akaondoka taratibu. Mwendo kama wa mita mia moja hivi akasimamisha gari, akafungua mlango na kutoka nje, akasimama na kumtazama Joru. Baada ya dakika tano za kutazamana, Jack akaiacha ile gari na kumuelekea Joru, akasimama na kumtazama tena kana kwamba ndiyo mara ya kwanza akimuona.



    “Twende zetu, nikauoneshe unalolitaka,” Jack akamwambia Joru, kisha wote wawili wakaingia garini na kutokomea.

    “Sasa sikiliza, huyu jamaa siku hizi ana mtandao mkubwa sana wa ujambazi, na ndiyo maisha anayoishi baada ya kustahafu jeshi, lazima ujue kluwa ana masikio mengi sana, sasa we ulitakiwa tukaongee pembeni pale uliporopoka ndio maana nikaondoka, wameshasikia sasa tuko matatani,” Jack alimwambia Joru huku akikunja kona kuingia mtaa Fulani hivi. Baada ya mwendo mfupio hivi, Jack aliona gari nyingine ikiingia mtaa ule.

    “Joru geuka nyuma!,” Jack akamwambia, Joru akageuka na kuiona ile gari inayokuja.

    “Vipi?” akauliza.

    “Wanatufuata, wameshasikia tunamzungumzia boss wao, sijui hata tufanye nini maana hapa mni mawili lazima watuue, au watupeleke kwa bosi wao, Malyamungu, tumekwisha,” Jack akamwambia Joru.

    “Simama unishuhe, halafu wewe kanisubiri mbele kule,” Joru alimwambia Jack.

    “Kaka hiyo troop sio ya kuichezea au kucheka nayo, hapa cha kufanya mimi ni kufukuzana nao mpaka niwapoteze,” Jack akamwambia Joru.



    “Hapana Jack, simama mi nitawatuliza hata kama wako hamsini,” Joru alisisitiza. Jacka hakuwa na linguine alisimamisha gari na Joru akasuka garini akasimama nje kwenye kagiza hafifu kalilkokuwa kakififishwa kwa mbalamwezi pevu. Ile gari ikaja na kusimama mita chache kutoka aliposimama Joru, milango ikafunguliwa na wale jamaa wakashuka, walikuwa watatu tu, wawili wakamsogelea Joru, na mmoja akabaki nyuma akiwa na gongo la kuchezea mcjezo wa baseball, akilipigapiga mkononi kana kwamba anasubiri amri tu alitumie gongo hilo. Wale wawili waliomsogelea Joru mmoja alikuwa na bastola na mwingine alionekana kiongozi wao alikuwa mikono mitupu.

    “We ni nani, na umekuja kufanya nini?” Yule kiongozi aliyevalia suti nyeusi na kofia nyeusi pia alimuuliza Joru huku akipuliza moshi wa mtemba wake.

    “Huna hadhi ya kuniuliza swali la namna hiyo, unataka kunijua mimi?” joru aklamjibu na kumuuliza.

    “Inaonekana we tafu sana ee? Unadiriki kunijibu hivyo mimi?” Yule mtu akauliza huku akimsogelea pale alipo.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nimezaliwa ili niwe tafu, niweze kuwajibu hivi watu kama ninyi, vibaraka,” Joru alimjibu kwa dharau akisindikiza na sonyo refu lisha akageuka kama anaondoka kuelekea kwenye gari kumbe ilikuwa ni mbinu ya kuwaweka sawa.



    “Wewe! Simama kabla sijakutawanya ubongo wako,” Yule mwenye bastola alisema kwa sauti huku akivuta hatua kumfuata Joru na bastola mkononi. Ilikuwa ni nafasi hiyo anayoisubiri, Joru aligeuka kwa kasi na kuipiga teke nile bastola, ikatoka mikononi mwa Yule mtu, kisha mguu wa pili ukatua shavuni mwa Yule jamaa aliyekuwa na bastola akayumba na kwenda chini moja kwa moja. Kwa harakaharaka Joru alimuona Yule mwenye gongo akaija kasi na gongo lake juu, akampiga teke moja la mbavu Yule kiongozi wao mpaka akatema mtemba wake na kugeuka kwa Joru ndipo Joru alipomkamata suti yake na kumgeuza haraka upande wa pili na kumfaya ngao dhidi ya lile gongo lililokuwa linashuka kichwani mwake. Paaaaa! Gongo likatua kwenye paji la uso la Yule kiongozi na kumpasua vibaya fuvu la kichwa chake. Joru akamsukuma Yule kiongozi ambaye sasa alikuwa ni marahemu akambwaga chini kwa mbele, akaruka sarakasi na kuokota bastola, alipokaa sawa tu tayari alishafyatu na kufumua kifua cha Yule aliyekuwa na gongo, akapaishwa juu na gongo likichomoka mikononi mwake, akajibwaga kwenye boneti ya gari, hana uhai. Joru alimtazama Yule mmoja aliyebaki pale chini.

    “Nenda kamwambie bosi wako, nipo, nimekuja, akikuuliza nani, mwambie Israel mtoa roho katumwa na roho zote alizozitoa kwamba sasa zamu yake imefika,” Joru akafyatua risasi moja na kumvunja mkono Yule aliyebaki kisha akaisweka ile bastola kiunoni mwake na kuingia kwenye gari ya Jack.

    “Dah, kaka Joru, uko poa yaani upo kama Van Damme, vipi wamekwisha?” Jack akauliza.

    “Wamekwisha wawili ila mmoja nimemuacha apelike ujumbe kwa bosi wake,” Joru akajibu huku akijiweka vizuri kitini na Jack akiondoa lile gari kutoka eneo lile.



    §§§§§



    Haikuchukua muda taarifa zilifika kwa mhusika, mtu wa mawasiliano ambaye ni yeye tu mwenye uwezo wa kuonana na Malyamungu, akastaajabu sana kwa ushupavu wa huyo mtu aliyeweza kukisambaratisha kikosi hicho, kikosi tata. Akajishauri jinsi ya kumwambia bosi wake habarti hiyo mbaya, lakini aliposhauriana na vijana wake wengine juu ya hilo, walimshauri asimweleze, ila wafanye juu chini kumpata huyo kiumbe haraka iwezekanavyo. Uamuazi ukapitishwa na vijana wakaanza msako wa kumsaka Joru kwa hali na mali, wakihakikisha Joru haingii katika mji wa Jinja, wakati huo wengine wakipangwa kuhakikisha anakamatika hukohuko Masaka alikofanya unyama huo. Ilikuwa kazi kazi ngumu.

    Mtoto wa kwanza wa Malyamungu ndiye aliyeipata habari hiyo kuwa kikosi chake, kikosi tata kimesambaratishwa na kijana huyo huko Masaka kikiwa katika moja ya majukumu yake ya kila mara.

    Kalosi Malyamungu alihisi kuchanganyikiwa, hakuwahi kusikia vijana wa baba yake wakishindwa kirahisi namna hiyo, kila alipokaa alikuwa akiwaza jinsi ya kuongeza nguvu katika kumdhibiti mtu huyo ambaye bado alikuwa hajamjua uwezo na nini hasa anachokitaka.



    Wakati Kalosi akisumbuka akichwa kwa hilo akiwapanga vijana wake kule Masaka, Joru na Jack walikuwa njiani kuelekea Kampala, wakisogea kabisa na mji wa Jinja ambako Malyamungu ndipo alikuwa ameweka makao yake, serikali ikimpa ulinzi lakini haikujua nini kinafanyika chini ya zuria, Malyamungu alikuwa na kikosi cha vijana wa kulinda karibu sehemu mbalimbali za Uganda na hii ni kwa sababu alijua wazi kuwa ana maadui wengi aliowajenga wakati wa utawala wa nduli Idd Amin, hivyo kuona mtu anataka kulipa kisasi kwa jinsi yoyote kwake halikuwa jambo la kushangaza. Silaha alizokuwa akiziiba wakati akiwa mwanajeshi huko nyuma zilimtosha kujiwekea ulinzi wake mwenyewe dhidi ya ule wa serikali wa askari mmoja getini. Aliishi maisha ya kuwa ndani tu, ni mara chache sana alitoka nje, kila kitu alikipata akiwa ndani, alihakikisha dunia yote anayo katika sebule yake na kujua kila kinachojiri nje kuliko wewe uliye nje.



    §§§§§



    KAMPALA



    SAA kumi na moja alfajiri, Joru na Jack waliingia Kampala, mji mkuu wa Uganda, si mbali sana na Jinja. Joru na jack walifikia katika nyumba ya akina Jack kwa mapumziko mafupi kabla ya kutimiza azma yao kwa Yule wanayemhitaji, wao waliona kuwa hapo ni mahali salama na panapowafaa sana kwa shughuli yao hiyo....



    Joru na Jack walijipumzisha vya kutosha, mchana wa saa saba wote wawili pamoja walikuwa mezani kwa chakula, wakibadilishana hili na lile.

    “Sasa Joru, we umejipangaje katika kautimiza hili ulilonambia?” Jack aliuliza wakiwa chakulani.

    “Nimejipanga vya kutosha, nimechukua miaka ishirini kujiandaa kwa ajili ya hili na lazima nilitimize leo hii usiku,” Joru akajibu.

    “Sikia Joru,” Jack akamwambia.

    “Unasemaje?” Joru akamuuliza na kuacha kula akimsikiliza kijana huyo.



    “Malyamungu, ni mtu anayeogopwa sana tangu enzi zile mpaka sasa ijpaokuwa umri umemuacha, na kwa sababu anajua hilo, amejipanga sana, kuivamia ngome yake inahitaji askari au watu wenye ujuzi mkubwa sana na mb inu za kutosha za uvamizi,” Jack alimwambia Joru.

    “Niko tayari nina uwezo wa kuingia katika hiyo ngome kwa jinsi ambayo wewe mwenyewe hautodhani, na ni lazima nimmalize Malyamungu kwa mkono wangu, nitahakikisha na nina uwezo wa kuwadhibiti wale wote watakaokuwa wamemzunguka,” Joru alijigamba.

    Jack aliinama chini kwa muda, kisha akainua uso wake na kumtazama Joru kwa macho makali.

    “Napenda unavyojiamini, kubali kuniahidi kitu kimoja tu,” Jack akasema.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Niambie na nitakuahidi,” Joru alimwambia Jack.

    “Mimi ni mwanajeshi katika jeshi la Uganda, nilijaribu kulipiza kisasi kwa mtu huyu dhidi ya mauaji ya baba yangu ambaye alikuwa na cheo cha juu sana serikalini, lakini nilikamatwa, mtoto wake mkubwa, Kalosi, alinipiga risasi ya goti ambayo ilipelekea mimi kukatwa mguu, kwa huruma na hisani ya Rais Museveni, nikaachwa jeshini nikitumia mguu wa bandia kitu ambacho si rahisi popote pale duniani, lakini najua kwa kuwa mimi nimesomea zaidi maswali ya ICT,” akasita kidogo, akakohoa na kuendelea, “naomba unilipizie kisasi kwa Kalosi pia, lakini nina wasiwasi, umejiandaaje, nikimaanisha silaha?” Jack akamuuliza Joru.

    Joru akasogeza kibegi chake kidogo na kupekua ndani yake kisha akatoa bastola ya kizamani, ambayo ilikuwa iking’azwa sana na mwanga wa jua lililokuwa likipenya kupitia dirisha lililokuwa katika chumba hicho cha kulia chakula.



    “Ha! Joru, hiki nini?” Jack aliuliza kwa mshangao.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog