IMEANDIKWA NA : KEVIN MPONDA
*********************************************************************************
Simulizi : Ufukwe Wa Madagascar
Sehemu Ya Kwanza (1)
JINAMIZI la ndoto mbaya isiyoeleweka likanipelekea nitupe miguu na mikono yangu huku na kule huku nikikisukasuka ovyo kichwa change katika hali ya kukataa kabisa kukubaliana na kile kilichokuwa kikiendelea kunitokea ndotoni. Hali ile ikapelekea jasho jepesi lianze kunitoka sehemu mbalimbali mwilini huku mapigo ya moyo wangu yakienda mbio isivyokawaida.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati nikiwa katika hali ile mara hisia zangu zikanitanabaisha kuwa simu ya mezani iliyokuwa sehemu fulani mle ndani ilikuwa imeanza kuita. Tukio lile likapelekea koo langu likauke kwa ghafla huku nywele zikinicheza kichwani kwa hofu. Hata hivyo mara hii milango yangu ya fahamu ilikuwa makini zaidi huku nikiishirikisha akili yangu kikamilifu katika kuniletea taarifa za kuaminika kama tukio lile lingekuwa katika mlolongo mrefu wa yale matukio ya ndotoni au lah!.
Ile simu bado iliendelea kuita na mwito wake ukageuka kero masikioni mwangu. Hatimaye nikayafumbua macho yangu taratibu nikiyatembeza mle ndani kutazama huku na kule na hapo nikakutana na ukungu wa giza nene machoni mwangu. Hali ile ikanipelekea niyatulize vizuri mawazo yangu huku nikijaribu kufikiria vizuri kuwa pale ningekuwa wapi. Jibu la haraka sikulipata hivyo nikapeleka mikono yangu huku na kule nikipapasa. Kwa kufanya vile taratibu fahamu zangu zikaanza kurejewa na uhai.
Nilikuwa nimelala kitandani chumbani kwangu na ile simu iliyokuwa ikiita halikuwa tukio la ndotoni kama nilivyokuwa nimedhani hapo awali. Ilikuwa ni simu ya mezani iliyokuwa mle ndani chumbani kwangu tena juu ya meza fupi ya fomeka yenye droo mbili chini yake iliyokuwa upande wa kushoto wa kitanda changu.
Nikiwa pale kitandani sikuweza kukumbuka haraka kuwa ni wakati gani usingizi ulifanikiwa kunichukua muda mfupi mara baada ya kumaliza kutazama filamu ya kutisha ya Drag Me To Hell usiku ule. Hata hivyo nilikuwa na hakika kuwa muda ule ungekuwa ni usiku wa manane kutokana na uwepo wa hali ya utulivu wa kutisha ndani na nje chumba kile.
Ile simu juu ya mezani pembeni ya kitanda changu ikaendelea kuita na mara hii nikashawishika kutaka kuipokea huku nikijiuliza kuwa mpigaji wa simu ile ya mezani niitumiayo mara chache angekuwa nani. Jibu sikulipata hivyo hatimaye nikalitupa shuka pembeni kisha kwa msaada wa swichi iliyokuwa kando ya kitanda nikawasha taa ya mle chumbani huku akili yangu ikiwa imeanza kupoteza utulivu.
Usingizi ukiwa bado haujanitoka vizuri nikayafikicha macho yangu na kupiga mwayo hafifu wa uchovu huku nikivinyoosha viungo vyangu mwilini. Nilipoyatuliza macho yangu kutazama saa ya ukutani mle ndani haraka nikagundua kuwa ilikuwa tayari imetimia saa nane na robo usiku.
Kitendo cha kukumbuka kuwa nilikuwa nimeizima simu yangu ya mkononi kabla ya kulala kikaupelekea moyo wangu upige kite kwa nguvu na hapo kijasho chembamba kikaanza kunitoka. Haraka nilikuwa nimekumbuka kuwa ile simu ya mezani mle ndani ilikuwa ikitumika kwa shughuli za kiofisi tu na hivyo hakuna mtu yeyote wa kawaida aliyekuwa akiifahamu zaidi ya ofisi yangu ya idara kuu ya taifa ya ujasusi jijini Dar es Salaam.
Hofu ikiwa imeanza kuniingia moyoni nikaitazama tena ile simu ya mezani kwa wasiwasi huku nikianza kuhisi jambo la hatari. Hata hivyo sikutaka kuendelea kusubiri ile simu iendelee kuita zaidi kwani ilikuwa mbioni kukata baada ya kuita kwa muda mrefu.
Hivyo nikajisogeza pembeni ya kile kitanda kivivuvivu na kisha kuupeleka mkono wangu juu ya ile meza ili kuipokea ile simu. Hata hivyo kabla sijaifikia ile simu ikawahi kukata na tukio lilelikautowesha kabisa usingizi wangu kichwani badala yake nikabaki nikiikodolea macho ile simu kama guruneti la kutupa kwa mkono huku akili yangu taratibu ikizama kwenye tafakuri ya kuanza kuwaza kuwa mpiganaji wa simu ile angekuwa nani na angekuwa na shida gani usiku wa manane kama ule.
Kitambo cha kirefu cha ukimya kikapita na wakati nikiwa mbioni kukata tamaa mara ile simu ya mezani ikaanza kuita tena mle ndani. Sikutaka ile simu iendelee kuita zaidi hivyo haraka nikakinyakuwa kiwambo chake na kukiweka sikioni huku nikiipa akili yangu utulivu wa hali ya juu.
Mara tu nilipoipokea ile simu sauti ya upande wa pili ikanitanabaisha kuwa mzungumzaji upande wa pili alikuwa ni mkuu wa idara ya taifa ya ujasusi Brigedia jenerali Ibrahim Gambari. Kitendo cha kuisikia sauti adimu ya kamanda yule machachari kikanipelekea nimeze funda kubwa la mate kuutuliza mtima wangu huku nikianza kuhisi jambo lisilo la kawaida.
“Vipi kijana wangu umelala?” sauti nzito na tulivu ya Brigedia jenerali Ibrahim Gambari ikaongea kwa utulivu huku ikionekana dhahiri kuwa mbali na usingizi.
“Ndiyo mzee bado nipo usingizini” nikajibu kwa jazba huku nikihisi karaha ya kukatishwa usingizi wangu kwa swali lisilokuwa na maana na hapo nikamsikia Brigedia jenerali Ibrahim Gambari akiangua kicheko cha ghafla na kicheko kile kilipokoma akaongea
“Tangu lini mtu aliyeko usingizini akapokea simu na kujinadi kuwa yupo usingizini?”
“Sasa mzee una maana gani ya kuniuliza kuwa nimelala wakati unaona kuwa nimeipokea simu yako na sasa tunaongea vizuri kwenye simu?” nikamuuliza Brigedia jenerali Ibrahim Gambari huku donge la hasira za kupokonywa lepe langu la usingizi likigoma kushuka kooni.
Mtu yeyote ambaye ingelikuwa ni mara yake ya kwanza kunisikia nikizungumza na Brigedia jenerali Ibrahim Gambari katika mazungumzo yetu ya kawaida asingesita kuhitimisha kuwa tulikuwa ni watu wenye uhasama mkubwa.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hata hivyo hali hiyo haikuwa kweli kwani pamoja na utofauti mkubwa wa cheo na umri kati yangu na Brigedia jenerali Ibrahim Gambari lakini tulikuwani marafiki wakubwa sana. Siku zote tukitaniana kwa furaha kama baba na kijana wake hata katika masuala ya msingi ingawa utani wetu ulikuwa na mipaka katika mazingira fulani hususanpale linapotokea jambo makini la kikazi. Hivyo sikuwa nimeona ugumu wowote katika kumjibu vile yule jemadari wangu mwenye lukuki ya nishani za kijeshi kifuani na mabegani mwake.
“Washa runinga yako na weka chaneli 232, nitakupigia muda mfupi baadaye”. Sauti ya Brigedia jenerali Ibrahim Gambari ikaongea kwa msisitizo pasipo chembe yoyote ya mzaha.
“Kuna nini afande?” nikamuuliza kwa shauku hata hivyo nilikuwa nimechelewa kwani ile simu tayari ilikuwa imekatwa upande wa pili. Akili yangu ikiwa imeanza kupoteza utulivu sikutaka kupoteza muda hivyo haraka nikakirudisha kile kiwambo cha simu mahala pake kisha nikachukuwa rimoti ya runinga kubwa ya mle chumbani iliyokuwa juu ya meza pembeni ya ile simu ya mezani na kuwasha runinga iliyokuwa sehemu ya mbele ya kitanda.
Ile runinga ilipowaka nikapeleka kwenye chaneli 232 na macho yangu yalipotulia nikaweza kunasa vizuri picha ya kile kilichokuwa kikiendelea katika stesheni ile ya runinga. Breaking news ama taarifa za dharura zilikuwa zikirushwa moja kwa moja na kituo kile cha runinga kutoka mji mkuu wa nchi ya Burundi uitwao Bujumbura.
Mwandishi wa habari wa shirika la habari duniani liitwalo The Reuters akifahamika kwa jina la Boubakar Konte, raia wa Bukinafaso alikuwa akiripoti taarifa za jaribio la mapinduzi ya kijeshi lililofanyika muda mfupi nchiniBurundi. Picha ya nyuma ya mwandishi yule wa habari iliwaonesha raia wa nchi ya Burundi ambao wengi wao walikuwa vijana wakikatisha katika mitaa mbalimbali ya jiji la Bujumbura huku wakiwa na matawi ya miti mikononi katika namna ya kushangilia kwa furaha na kuunga mkono jaribio lile la mapinduzi ya kijeshi.
Ilikuwa ni habari mbaya na ya kushtukiza kwangu kwa vile nilikuwa sipendi kabisa suala la mapinduzi ya kijeshi kama mtindo wa kubadili uongozi wa serikali katika nchi za Afrika. Lakini kitendo cha kuwaona wananchi wa Burundi wakiendelea kushangilia jaribio lile la mapinduzi ya kijeshi katika mitaa mbalimbali ya jiji la Bujumbura kilikuwa kimeniacha njia panda.
Niliendelea kuitazama habari ile huku mawazo mengi yakipita kichwani mwangu hasa pale nilipokumbuka kuwa rais wa nchi hiyo ndugu Pierre Nkurunziza alikuwa jijini Dar es SalaamTanzania kukutana na viongozi wengine wa nchi kwenye mkutano wa 13 wa viongozi wa nchi za Afrika mashariki ambapo suala la kutetereka kwa amani ya nchi ya Burundi ilikuwa ni ajenda mojawapo katika mkutano huo.
Ilikuwa ni habari ya kusikitisha sana hata hivyo akili yangu bado ilikuwa ikisumbuka katika namna ya kutaka kufahamu tukio lile lilikuwa likitaka kuhusishwa vipi na mimi au Brigedia jenerali Ibrahim Gambari au nchi ya Tanzania kwa ujumla.
Nikiwa nimeanza kuzama kwenye tafakuri mawazo yangu yakahamia kwa Brigedia jenerali Ibrahim Gambari na nilipokuwa katika harakati za kuupisha utulivu kichwani mwangu katika namna ya kutafuta hoja ya msingi kutoka kwenye habari ile mara ile simu ya mezani mle ndani ikaanza kuita tena. Sikuwa na shaka kuwa Brigedia jenerali Ibrahim Gambari alikuwa akirejea tena hewani hivyo nikasogea karibu na kukikwapua tena kile kiwambo cha simu na kukiweka sikioni
“Umewasha runinga yako na kuweka chaneli 232?” sauti ya Brigedia jenerali Ibrahim Gambari ikaongea tena kwa utulivu upande wa pili wa simu ile.
“Ndiyo afande”
“Umeona nini?”
“Jaribio la mapinduzi ya kijeshi nchini Burundi” nikaongea kwa utulivu huku nikishindwa kuelewa uelekeo wa maongezi yale.
“Vizuri sana!, kuna jambo la haraka tunalopaswa kufanya” Brigedia jenerali Ibrahim Gambari akaendelea kuongea kwa msisitizo.
“Jambo gani?” nikauliza kwa shauku.
“Hatuwezi kuzungumza kwenye simu. Jiandae kwa kazi, nitamtuma dereva wangu aje akuchukue baada ya nusu saa. Huwenda ikawa ni safari ya siku mbili hadi tatu hivyo ni vizuri kabla ya kuondoka ukaweka kabisa mambo yako sawa”
“Safari ya kuelekea wapi?” nikauliza kwa hasira kwani akili yangu haikuwa tayari kujiingiza kwenye mambo ya hatari ukichukulia kuwa ile ilikuwa ndiyo kwanza siku ya nne tangu nilipoanza kuitumikia likizo yangu ya mwaka. Hata hivyo ni kama niliyekuwa nikijiongelesha mwenyewe kwani ile sauti ya Brigedia jenerali Ibrahim Gambari ilikuwa imekwishatoweka upande wa pili wa ile simu na ile simu kukatwa.
Akili yangu ikiwa imeanza kupoteza utulivu huku mitupo ya mapigo ya moyo wangu ikiongezeka dabali, taratibu nikakirudisha kile kiwambo cha simu mahala pake huku hofu ikiwa imeanza kuniingia. Hisia zangu zikanitanabaisha kuwa hoja ya Brigedia jenerali Ibrahim Gambari haikuwa na uzito mwepesi kama yalivyokuwa maelezo yake.
Safari ya siku mbili tatu ingeweza kuwa ya muda wa wiki moja, mwezi, au miezi, mwaka hadi miaka kutegemeana na yatakayojiri mbele ya safari yenyewe. Safari haikuwa na shida yoyote tatizo lilikuwa kwenye namna ya safari yenyewe hususan pale roho yangu inapotumika kama nishati ya safari hiyo. Hata hivyo sikuwa na namna ya kufanya zaidi ya kutii amri kama sheria zetu za kijeshi zinavyotutaka.
Nilifahamu nini maana ya kuzingatia muda hivyo haraka nikaamka kitandani na kutandika vizuri kitanda ambapo pia niliweka sawa vitu vyangu mle ndani. Nilipomaliza nikavua pajama yangu na kuelekea bafuni kujimwagia maji. Nilipotoka kuoga ilikuwa tayari imetimia saa nane na nusu usiku hivyo dakika chache zilikuwa zimesalia kabla ya kutimia muda wa nusu saa ambao dereva wa Brigedia jenerali Ibrahim Gambari tayari angekuwa amefika pale nyumbani kunichukua.
Vifaa vyangu muhimu vya kazi nikavitia ndani ya begi langu dogo la mgongoni lenye mifuko mingi yenye vipenyo tofauti ambapo mle ndani pia niliweka nguo zangu chache muhimu za kubadilisha.
Baada ya muda mfupi nikawa nimemaliza kujiandaa huku nikiwa katika mwonekano mpya wa suruali nyeusi ya jeans, buti ngumu za ngozi miguuni, fulana nyekundu yenye mstari mweupe kifuani, shati zito la jeans la rangi ya samawati, saa ya kijasusi mkononi na kofia nyeusi ya kapelo.
Wakati nikitoka nje na kufunga mlango wa mbele wa nyumba yangu nikaliona gari la jeshi aina ya Nissan Patrol likiegesha mbele ya nyumba yangu kando ya mti mkubwa uliyokuwa eneo lile.
Dereva wa gari lile akawasha taa za mbele na kuzima mara mbili katika namna ya kunifahamisha kuwa tayari alikuwa amefika kunichukua nami bila kupoteza muda mara tu nilipomaliza kufunga mlango haraka nikashuka ngazi za baraza yangu nikielekea kwenye lile gari.
Dereva wa lile gari la jeshi Nissan Patrol nilimfahamu kwa jina moja tu la Mayunga mwenye cheo cha Koplo na vilevile askari komando wa daraja la pili. Kijana tuliyeelekeana kwa umri, mrefu na mweusi mwenye macho makali na mikono imara, mtu asiye na maneno mengi lakini mcheshi.
Nilipolifikia lile gari nikafungua mlango wa mbele na kuingia ndani. Dereva wa lile gari Koplo Mayunga akanipigia saluti kwa heshima zote na kunisalimia kwa utulivu kwani alikuwa akikifahamu vizuri kwa cheo changu cha kijeshi cha Luteni nami nikaitikia salamu yake kwa bashasha zote.
“Pole na majukumu” nikamwambia huku nikitabasamu wakati alipokuwa akinipokea begi langu dogo na kuliweka siti ya nyuma.
“Nishapoa afande wangu, nikupe pole wewe uliyemwacha shemeji yangu usiku wa manane kama huu kajikunyata mwenyewe kitandani”
Maelezo ya Koplo Mayunga yakapelekea wote tuangue kicheko hafifu mle ndani huku kila mmoja akionekana kufurahishwa na utani ule na hapo safari yetu ikaanza. Tulipofika njiani nikamuuliza Koplo Mayunga kama alikuwa akifahamu lolote juu ya wito wangu usiku ule. Hata hivyo alinijibu kuwa alikuwa hafahamu chochote ingawa alinidokeza kuwa hata yeye alikuwa ameamshwa usiku ule na kutakiwa kumpeleka Brigedia jenerali Ibrahim Gambari ofisini kwake. Kusikia vile haraka hisia za hatari zikaanza kujengeka kichwani mwangu huku nikizama kwenye tafakuri.
Muda huu wa usiku manane jiji la Dar es Salaam lilikuwa limemezwa na utulivu wa aina yake. Magari machache yalionekana kukatisha barabarani wakati safari yetu ilipokuwa ikiendelea. Katika baadhi ya mitaa maarufu wasichana waliokuwa wakifanya biashara ya ngono maarufu kama dada poa walionekana kujaribu bahati zao kwa wanaume wapita njia na hali ile ilinisikitisha sana.
_____
Saa tisa na nusu usiku Koplo Mayunga aliegesha gari lile Nissan Patrol kwenye viunga vya maegesho ya magari vya ofisi ya taifa ya idara kuu ya ujasusi eneo la Upanga jijini Dar es Salaam. Nami bila kupoteza muda nikamshukuru kwa huduma yake ya usafiri kisha nikachukua begi langu na kufungua mlango nikishuka.
Wakati nikitembea kuelekea kwenye ofisi zile za makao makuu ya idara ya ujasusi nikayatembeza macho yangu kutazama huku na kule nikilipeleleza jengo la ghorofa la ofisi zile zenye ulinzi wa kuaminika masaa ishirini na nne wiki nzima. Nikaiona taa ikiwa inawaka kwenye chumba kimoja kilichokuwa kwenye ghorofa ya pili ya jengo lile na hapo nikawa na hakika kuwa mkuu wa idara ya taifa ya ujasusi Brigedia jenerali Ibrahim Gambari alikuwa akinisubiri ofisini kwake.
Walinzi makini wa jengo lile hawakujisumbua kunizuia kwani walikuwa wakinifahamu vizuri kuwa mimi ni nani. Hivyo wakanisalimia kwa heshima zote za kiaskari wakati nilipokuwa nikiharakisha kupanda ngazi za jengo lile kuelekea ghorofa ya pili ilipokuwa ofisi ya jemadari yule chakaramu.
Ofisi ya Brigedia jenerali Ibrahim Gambari ilikuwa mkono wa kushoto mara baada ya kumaliza kupanda ngazi za kuingia ghorofa ya pili kwenye korido pana, hatua chache baada ya kuipita ofisi ya usalama wa taifa ya sera na mipango ambayo kwa wakati huu ilikuwa imefungwa.
Hatua chache zilizofuata nikawa nimeifikia ofisi ya mkuu wa idara ya ujasusi Brigedia jenerali Ibrahim Gambari. Nilipofika mlangoni nikasimama na kuupimia utulivu wa mle ndani. Ofisi ilikuwa tulivu na hapakuwa na sauti yoyote ya maongezi iliyosikika mle ndani hivyo nikahisi kuwa Brigedia jenerali Ibrahim Gambari huwenda alikuwa peke yake mle ndani. Bila kupoteza muda nikaanza kugonga hodi pale mlangoni. Ukimya kidogo ukapita kisha kutoka mle ndani ya ofisi nikasikia sauti nzito ya kiume yenye mamlaka ikiniambia.
“Ingia ndani Tibba”
Ruhusa ile ikanipelekea nikikamate vizuri kitasa cha ule mlango kisha nikakizungusha haraka na kuusukuma ule mlango kwa ndani huku nikipiga hatua zangu za kijeshi kuingia mle ndani. Hii haikuwa mara yangu ya kwanza kuingia kwenye ofisi ya Brigedia jenerali Ibrahim Gambari hivyo wakati nikiingia mle ndani tayari nilikuwa na picha kamili ya mandhari ya ofisi ile.
Ilikuwa ni ofisi pana yenye zulia jekundu sakafuni na meza ndefu ya ofisini yenye viti ishirini na viwili. Viti kumi na mbili upande wa kushoto na viti vingine kumi na mbili upande wa kulia. Haraka nikayatembeza macho yangu mle ndani na namna ya mpangilio wa viti kwenye ile meza kubwa ya ofisini nikahisi kuwa kikao kizito kilikuwa kimefanyika mle ndani muda mfupi uliyopita.
Brigedia jenerali Ibrahim Gambari alikuwa ameketi nyuma ya meza yake kubwa ya ofisini mwisho wa ofisi ile upande wa kushoto akiwa katika uso wa kusawajika huku akiwa ameegemea kiti chake cha ofisi. Ukimya ndani ya ofisi ile ukanifanya nisikie sauti hafifu ya hatua zangu wakati nilipokuwa nikikatisha kuelekea kwenye ile meza ya ofisini ya Brigedia jenerali Ibrahim Gambari. Mara moja nilipoitazama sura ya jemadari yule haraka nikatambua kuwa tayari mambo yalikuwa segemnege.
Brigedia jenerali Ibrahim Gambari alikuwa ameketi kwenye kiti chake cha ofisini huku mche wa sigara ukiteketea taratibu kwenye pembe ya mdomo wake na macho yake yakitazama karatasi ndogo aliyokuwa ameishika mkononi. Nilipomchunguza vizuri haraka nikatambua kuwa hapakuwa na mazingira ya kuleta mzaha kama vile ilivyokuwa kawaida yetu. Juu ya meza ile ya ofisini kulikuwa na vitabu na mafaili machache yaliyopangwa kwa ustadi pembeni ya kibao kidogo kilichochongwa vizuri kwa maandishi ya kutanabaisha cheo cha kamanda yule pamoja na kidau cha wino na mhuri wa ofisi.
Upande wa kushoto wa ofisi ile kulikuwa na picha kubwa ya baba wa taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na picha nyingine za viongozi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania zikiwa zimetundikwa ukutani. Upande wa kulia kulikuwa na rafu kubwa ya mbao iliyosanifiwa kwa ustadi wa hali ya juu. Ndani ya rafu ile kulipangwa vitabu na mafaili chungu nzima yaliyoshika vumbi na kupoteza nuru kutokana na kuhifadhiwa kwa muda mrefu ingawaje mazingira ya mle ndani yalikuwa nadhifu na yanayovutia kwa mpangilio wa samani za kisasa. Mbele ya ofisi ile ukutani kulikuwa na ramani tatu kubwa. Ramani moja ya nchi ya Tanzania, ramani ya pili ya bara la Afrika na ramani ya tatu ya Dunia
Hatimaye nikaifikia ile meza ya ofisini ya Brigedia jenerali Ibrahim Gambari na macho yetu yalipokutana nikafunga mguu na kupiga saluti moja ya nguvu mbele ya jemadari yule. Brigedia jenerali Ibrahim Gambari akaitikia salamu yangu ya kijeshi kwa utulivu kisha akanikaribisha niketi kwenye kochi moja la sofa lililokuwa likitazamana na ile meza yake mle ndani.
Naam! sasa nilikuwa ana kwa ana nikitazamana na mwanausalama na kamanda yule wa jeshi Brigedia jenerali Ibrahim Gambari. Umri wa miaka hamsini na miwili bado ulikuwa haujatosha kabisa kuzipokonya nguvu zake mwilini. Macho yake makali yakanitazama kwa makini pasipo kusema neno lolote huku akionekana kuipa utulivu akili yake. Alipoiegemea mikono yake pale juu ya meza na kuketi vizuri akavunja ukimya.
“Karibu sana Tibba!” Brigedia jenerali Ibrahim Gambari akaongea huku akinipa mkono wa karibisho.
“Nashukuru sana afande” nikamwitikia jemadari yule kwa utulivu huku akili yangu ikiwa bado kwenye tafakuri ya kutaka kufahamu dhumuni la wito ule. Mara tu nilipoketi kwenye lile kochi Brigedia jenerali Ibrahim Gambari akanitazama kwa uyakinifu kabla ya kuvunja ukimya.
“Huwenda ukawa umeshangazwa sana na wito wangu usiku wa manane kama huu” kisha akaweka kituo kidodo na kukohoa kabla ya kuendelea.
“Lakini huu ni wajibu wetu sote tuliyoukubali kwa ridhaa yetu wenyewe tangu tulipojiunga na jeshi la wananchi wa Tanzania na kuweka kiapo cha kufa na kupona cha kulitumikia jeshi hili” Brigedia jenerali Ibrahim Gambari akaweka kituo tena kasha akanitazama kwa utulivu na hatimaye kunipa ile karatasi aliyokuwa ameishika mkononi. Haraka nikanyoosha mkono wangu kuipokea ile karatasi kisha nikajiegemeza vizuri kwenye lile kochi nikayapitia maelezo yaliyokuwa kwenye karatasi ile.
Mara tu nilipoanza kusoma yale maelezo kwenye ile karatasi mapema nikatambua kuwa ile karatasi ilikuwa ni faksi na faksi ile ilikuwa imetumwa masaa machache yaliyopita kutoka kwenye ofisi kuu ya ubalozi wa Tanzania jijini Bujumbura nchini Burundi.
Nilipomaliza kusoma maelezo yaliyokuwa kwenye faksi ile haraka nikatambua nini dhumuni la wito ule wa usiku. Ile faksi ilikuwa imetumwa na kitengo cha usalama cha ubalozi wa Tanzania nchini Burundi ikieleza kuwa balozi wa Tanzania nchini Burundi, Meja jenerali mstaafu ndugu Adam Mwambapa alikuwa ametekwa na watu wasiofahamika muda mfupi baada ya jaribio la mapinduzi ya kijeshi kufanyika nchini humo. Mara tu nilipomaliza kusoma taarifa ile moyo wangu ukapoteza utulivu kabisa huku kijasho chepesi kikianza kunitoka sehemu mbalimbali za kwa mwili wangu.
“Nini kimetokea?” hatimaye nikauliza kwa udadisi huku nikiyapeleka macho yangu kumtazama kamanda yule mbele yangu.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Bado ni kizungumkuti kwani hadi wakati huu hakuna yeyote anayefahamu kinachoendelea. Mimi pia nimeshtuka kama wewe na kwa kweli hizi ni taarifa za kustaajabisha na kusikitisha sana” Brigedia jenerali Ibrahim Gambari akaongea katika hali ya simanzi huku taratibu akiviminyaminya vidole vyake vya mikononi katika hali ya kuupisha utulivu kichwani mwamke.
“Mna uthibitisho gani juu ya taarifa hizi?” nikamuuliza Brigedia jenerali Ibrahim Gambari kwa utulivu huku nikirudia kusoma kwa makini maelezo ya kwenye ile faksi.
“Hakuna namna ya kupingana na taarifa hizo kuwa siyo za kweli au lah!. Kama unavyoona mwenyewe faksi hiyo imetumwa na idara ya usalama ya ubalozi wetu wa nchini Burundi”
“Mmejaribu kupata maelezo ya kina juu ya hili tukio?” nakauliza kwa udadisi.
“Tumekosa ushirikiano wa kutosha kutoka kwa maafisa usalama wa nchini Burundi kutokana na hali ya tete ya usalama wa nchi hiyo ilivyo kwa sasa” Brigedia jenerali Ibrahim Gambari akaongea kwa utulivu huku akiupeleka mche wake wa sigara mdomoni na nilipomtazama nikatambua bado alikuwa akitafakari juu ya lile tukio la kutekwa kwa balozi Adam Mwambapa.
“Hili ni tukio la kushangaza sana” nikaongea kwa utulivu huku nikiendelea kutafakari yale maelezo kwenye ile faksi.
“Pia ni pigo kubwa kwa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na idara yetu ya ujasusi”
“Wewe una mtazamo gani juu ya suala hili?” nikamuuliza kamanda yule.
“Bado ni mapema sana kutoa mwelekeo sahihi wa hili tukio la utekaji wa balozi wetu Adam Mwambapa ingawa naweza kulihusisha na hali ya machafuko ya kisiasa yaneyoendelea nchini Burundi” Brigedia jenerali Ibrahim Gambari akaongea kwa utulivu baada ya kuitoa sigara yake mdomoni na kupuliza wingu zito la moshi wake pembeni na hapo kikafuatia kitambo kifupi cha ukimya baina yetu huku kila mmoja akionekana kuzama kwenye tafakuri nzito kichwani mwake. Niseme kuwa balozi Adam Mwambapa hakuwa mgeni kabisa katika fikra zangu kwani kabla ya kustaafu jeshi na kuteuliwa na rais kushika wadhifa wa balozi wa Tanzania nchini Burundi aliwahi pia kushika nyadhifa nyingi za kijeshi ikiwemo cheo cha mnadhimu mkuu wa jeshi la wananchi Tanzania. Hivyo alikuwa ni mtu mzoefu sana kwenye masuala ya kijeshi ya ulinzi na usalama na alivimudu vyema vyeo vyake vyote kwa weledi wa hali ya juu. Ndiyo kisa hata baada ya kustaafu jeshi serikali haikutaka mchango wake upotee hivihivi hivyo rais akamteua Meja jenerali mstaafu ndugu Adam Mwambapa kuwa balozi wa Tanzania nchini Burundi miaka minne iliyopita.
Kiongozi yeyote wa jeshi hasa mtu aliyewahi kushika madaraka ya juu jeshini kama Meja jenerali mstaafu ndugu Adam Mwambapa inapotokea kuwa ametekwa au kutoweka katika mazingira ya kutatanisha huwa ni tishio kubwa kwa serikali iliyopo madarakani na hata kwa usalama wa nchi kwa ujumla. Kwani kiongozi wa jeshi wa namna ile aliyelitumikia jeshi kwa miaka mingi huwa anafahamu siri nyingi za nchi yake hususani katika masuala ya usalama. Hivyo yeyote aliyemteka jemadari yule mstaafu wa jeshi la wananchi Tanzania ndugu Adam Mwambapa kwanza alipaswa kuwa ni mwanajeshi au kikundi cha kijeshi chenye maarifa ya juu sana katika medani za mapambano ya kijeshi. Vilevile utekwaji wake ulipaswa kuwa na sababu za msingi za kuhalalisha kitendo hicho kwa watekaji.
Niliendelea kutafakari kwa sababu hizo zingekuwa zipi na wakati nikiwa katika hali ile mara hisia mbaya zikanijia na hapo moyo wangu ukapoteza utulivu kabisa pale nilipowaza kuwa huwenda watekaji hao walitaka kupata taarifa fulani kutoka kwake. Taarifa ambazo bila shaka zilikuwa na mahusiano ya moja kwa moja na serikali ya Tanzania kama siyo vyombo vyake vya ulinzi. Nani anayeweza kufanya tukio la namna ile na kwa sababu gani?. Nikajiuliza pasipo kupata majibu.
Nikiwa nimezama kwenye tafakuri ile akili yangu ikaenda mbele zaidi katika kuunda hoja kichwani. Nikaanza kuziorodhesha nchi zote za Afrika ya Mashariki nikianzia kwa Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, na hatimaye Burundi. Nilipomaliza nikaanza kutathmini vizuri hali ya mahusiano ya kisiasa yaliyopo baina ya nchi hizi za Afrika Mashariki. Tathmini yangu ikanieleza kuwa mahusiano ya nyanja zote baina ya nchi zile bado yalikuwa mazuri ingawa kulikuwa na misuguano ya kawaida ya hapa na pale. Nilipotafakari kwa kina juu ya misuguano hiyo bado haikuweza kuniridhisha kuwa ingeweza kuwa sababu toshelevu ya kutekwa kwa balozi wetu tena na moja ya nchi hii jirani iliyopo kwenye ushirika wa jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki. Hivyo nikaishilia kumeza funda kubwa la mate huku akili yangu ikiendelea kusumbuka.
“Kikao cha wanausalama kilichomalizika muda mfupi uliyopita kabla ya wewe kufika hapa kimeazimia kuwa itakuwa ni vyema sana tukikubadhi jukumu hili wewe” maelezo ya Brigedia jenerali Ibrahim Gambari yakawa yamezirudisha fikra zangu mle ndani na hapo nikayapeleka macho yangu kumtazama kwa makini kana kwamba sikuwa nimemsikia kwa makini kamanda yule.
“Una maana gani?” nikamuuliza kamanda yule kwa utulivu huku nikifahamu fika uelekeo wa maongezi yake.
“Hatuwezi kulifumbia macho suala hili kama unavyojua kuwa ndugu Adam Mwambapa ni kiongozi mkubwa serikalini na jeshini. Yeyote aliyemteka bila shaka anataka kupata taarifa nyeti kutoka kwake kuhusiana na serikali yetu na vyombo vyetu vya usalama. Hiki ndiyo tunachodhani wote kwa pamoja ndiyo kisa tukaona kuwa tukutume nchini Burundi ukatafute ukweli juu ya mashaka tuliyonayo” Brigedia jenerali Ibrahim Gambari akaweka kituo huku akiyakung`uta majivu ya sigara yake kwenye kibeseni kidogo cha majivu kilichokuwa pale juu ya meza halafu akayapeleka macho yake kunitazama kwa utulivu.
“Lakini hii ni kazi ngumu sana na ya hatari kufanywa na mtu mmoja” nikatumbukiza hoja yangu huku nikimtazama Brigedia jenerali Ibrahim Gambari katika sura ya kukata tamaa.
“Hakuna mtu aliyesema kuwa hii ni kazi rahisi hasa kwa kuzingatia hali ya usalama ya nchi ya Burundi ilivyo kwa wakati huu. Hata hivyo tunaamini kuwa ni wewe tu utakayeweza kuifanya kwa ufanisi na kutuletea majibu mazuri ya hakika ndani ya muda mfupi huku sisi tukiwa nyuma yako kukupa msaada wowote utakaouhitaji” Brigedia jenerali Ibrahim Gambari akaweka kituo kidogo akikohoa kusafisha koo lake kabla kuendelea.
“Tanzania ni nchi yenye bahati sana kwa kutokumezwa na majanga ya chuki ya ukabila ukifananisha na hizi nchi nyingine zilizosalia za Afrika Mashariki. Hii inatokana na Mungu mwenyewe kumjalia hekima ya juu sana baba wa taifa hili Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ya kuzitumia vizuri tofauti zetu za rangi ya ngozi, imani na makabila katika kutengeneza mshikamano thabiti wa kutufanya tuwe wamoja.
Wapo wapumbavu wachache wanaojaribu kupenyeza nadharia ya udini na ukabila katika mfumo wa maisha ya watanzania wakijitafutia manufaa yao. Ndiyo maana hata sasa katika baadhi ya taasisi za serikali au binafsi aina ya wafanyakazi wake itakutanabaisha kuwa nadharia ya udini na ukabila bado inaabudiwa na kuzidi kuota mizizi. Hali hii ni mbaya sana kwa sababu hujenga.....
...chuki ya muda mrefu na pale chuki hiyo inapokomaa huzaa machafuko ambayo mtanzania wa kwaida itamgharimu kupambana kufa na kupona kuipigania pumzi yake”
“Lakini nionavyo mimi hali hii hutegemeana sana na utashi wa kiongozi aliyeko madarakani, kwani kama kiongozi ana utashi mdogo na mbinafsi na washauri wake ni watu anaofanana nao kimtazamo ni rahisi kumuona anatoa fursa nyingi kwa watu wa dini yake au kabila lake pasipo kuangalia mustakabali mzima wa taifa. Kwa kufanya hivyo jamiii ya mlengwa wa kushoto hujihisi kutengwa na hivyo ubani wa chuki ya udini na ukabila kuzidi kufukiza” nilimaliza kuongea huku nikipiga mwayo hafifu wa uchovu.
“Tunataka kiongozi ambaye ataweza kutufanya wamoja pamoja na uwepo wa tofauti katika imani na makabila yetu. Kwa mfano, Rwanda na Burundi ni nchi ambazo watu wake wanabaguana kwa ukabila kwa kiwango cha juu sana. Hali hiyo imepelekea kunawiri kwa chuki mbaya ya ukabila miongoni mwao. Chuki ambayo imeondoa kabisa hali ya kuaminiana wenyewe kwa wenyewe katika kila maeneo. Ndiyo maana migogoro na machafuko ya kisiasa ni vigumu kumalizika kabisa katika nchi hizi. Kama Tanzania haitalivalia njuga hili suala la udini hapa nchini basi na sisi pia hatutakuwa salama kwa siku za usoni” Brigedia jenerali Ibrahim Gambari akaweka kituo akivuta sigara yake taratibu na alipoitoa sigara ile mdomoni na kuupuliza moshi wake pembeni akaendelea.
“Napenda uelekee nchini Burundi kufanya hii kazi huku tayari ukiwa na picha kamili kichwani kuwa unaenda kuonana na watu wa namna gani. Jaribio la mapinduzi ya kijeshi lililotangazwa usiku wa leo nchini Burundi siyo jambo geni sana katika nchi hiyo. Nchi ya Burundi inaundwa na mjumuiko wa makabila matatu lakini yasiyo na uwiano sawa kwa ujumla wa hesabu yake. Raia wa Burundi wa kabila la Hutu ndiyo wengi zaidi kwa asilimia 85, asilimia 14 katika sehemu iliyosalia inaundwa na kabila la Tutsi ambao wengi wao ndiyo walioshikilia nyadhifa za juu serikalini na jeshini. Asilimia moja iliyosalia inaundwa na watu wa kabila la Twa ambalo ni kabila la wawindaji. Hivyo ukitazama utagundua kuwa watu wa kabila la Hutu ni wengi zaidi katika jumla ya idadi ya raia wanchi hiyo.
Mapinduzi ya kijeshi nchini Burundi yalianza kutokea mwaka 1976 wakati serikali ya rais Michael Micombero wa kabila la Tutsi ilipopinduliwa kijeshi na mtutsi mwingine Kanali Jean-Baptiste Bagaza kwa sababu alizozijua yeye mwenyewe. Baada ya Kanali Jean-Baptiste Bagaza kuingia madarakani chini ya chama chake cha UPRONA-Unité pour le progrès National, aliendelea kuongoza nchi hiyo hadi mwaka 1984 ambapo joto la demokrasia lilikuwa limekolea vizuri.
Uchaguzi mkuu wa rais ulipofanyika Burundi haukuleta mabadiliko yoyote kwani Kanali Jean-Baptiste Bagaza na chama chake cha UPRONA walijinadi kuibuka na ushindi wa kishindo wa silimia 99.6 dhidi ya wapinzani wao na hivyo kuendelea kubaki madarakani. Ingawa utafiti unaeleza kuwa uchaguzi huo haukuwa wa haki kama zilivyo chaguzi nyingi za nchi za bara la Afrika” Brigedia jenerali Ibrahim Gambari akaweka kituo akikohoa kidogo na kuyakung`uta majivu ya sigara yake kwenye kile kibeseni kidogo cha majivu ya sigara kilichokuwa pale mezani kabla ya kuendelea.
“Hata hivyo utawala wa Kanali Jean-Baptiste Bagaza ulishutumiwa vikali kwa kuliwekea vikwazo kanisa la Roman Catholic ambalo lina waumini asilimia 65 ya raia wote wa nchi ya Burundi kwa kile kilichodaiwa kuwa kanisa hilo lilikuwa likiingilia mambo kadhaa ya serikali. Kufuatia hali hiyo serikali ya Kanali Jean-Baptiste Bagaza haikuendelea kutabaruku zaidi madarakani kwani ilipofika mwezi Septemba 1987 wakati Kanali Jean-Baptiste Bagaza alipokuwa amesafiri kwenda jijini Quebec nchini Canada kuhudhuria mkutano wa viongozi wa nchi zinazongumza lugha ya kifaransa. Serikali yake ikapinduliwa na binamu yake Meja Pierre Buyoya na hivyo utawala mwingine wa jeshi kushika hatamu. Baada ya kusikia juu ya mapinduzi hayo Kanali Jean-Baptiste Bagaza haraka alirudi nchini mwake lakini uwanja wa ndege wa Bujumbura ulikuwa tayari umefungwa. Hivyo Kanali Jean-Baptiste Bagaza akakimbilia jijini Nairobi lakini Kenya ilikataa kumpokea hivyo akaelekea nchini Uganda na baadaye kutorokea nchini Libya ambapo huko alipewa hifadhi ya ukimbizi wa kisasa.
Mara baada ya Meja Pierre Buyoya kujiingiza madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi na kutangazwa kuwa rais wa nchi ya Burundi tarehe 2 Oktoba mwaka 1987. Alitangaza haraka kubadili katiba ya nchi hiyo na kuondoa vikwazo vyote vilivyokuwa vimewekwa na serikali ya Kanali Jean-Baptiste Bagaza dhidi ya kanisa la Romanic Catholic hasa kwa kuwa yeye alikuwa muumini wa kanisa hilo.
Meja Pierre Buyoya akaendelea kushikilia madaraka ya nchi ya Burundi hadi pale ulipofanyika unaosemekana uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia tarehe 27 mwezi Juni mwaka 1993. Katika uchaguzi huo uliosemekana wa kweli na wa haki, Melchior Ndadaye mhutu aliibuka mshindi na kutangazwa kuwa rais wa nne wa nchi hiyo. Hata hivyo Melchior Ndadaye hakufanikiwa kutimiza ahadi zake za kukuza uchumi wa nchi ya Burundi na kupunguza chuki ya ukabila baina ya waburundi kwani alishika madaraka kwa kipindi cha miezi mitatu tu kabla kupinduliwa kijeshi na hatimaye kuuwawa tarehe 21 Oktoba 1993.
Mapinduzi ya kijeshi dhidi ya serikali ya rais mhutu Melchior Ndadaye na kuuwawa kwake na mawaziri wake sita kuliamsha hisia kali za chuki kwa watutsi dhidi ya wahutu nchini Burundi na hivyo kupelekea kulipuka kwa vita kali ya ukabila kati ya watutsi na wahutu nchini humo, hivyo ukafanyika umwagaji damu wa kutisha. Katika mazingira hayo waliompindua rais Melchior Ndadaye na hatimaye kumuua hawakupata nafasi ya kushikilia dola hivyo ndugu Francois Ngeze, mwanasiasa wa kawaida akawekwa kuwa rais na kushikilia utawala wa nchi hiyo kwa muda.
Hata hivyo Ngeze alikataa kuwapa ushirikiano wa kutosha viongozi wote wa mapinduzi ya kijeshi na badala yake akamuita aliyekuwa waziri mkuu wa kipindi hicho kabla ya mapinduzi hayo ya kijeshi, mama Sylvie Kinigi, mtutsi ambaye alikuwa ameyakimbia mapinduzi hayo na kuomba hifadhi kwa ubalozi wa Ufaransa.
Makamanda wa jeshi hawakuwa na namna ya kukataa hivyo wakakubali kuwa mama Sylvie Kinigi ashikilie uongozi wa nchi kama rais wa mpito wakati katiba ya nchi hiyo ikifanyiwa marekebisho baada ya ile katiba ya awali kupelekea machafuko makubwa ya kisiasa na umwagaji mkubwa wa damu uliotokana na vita ya ukabila.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ilipofika mwezi Januari mwaka 1994, bunge la nchi ya Burundi likamchagua ndugu Cyprien Ntaryamira ambaye hapo awali alikuwa waziri wa kilimo enzi za utawala wa rais Melchior Ndadaye kuwa rais wa nchi hiyo. Rais Cyprien Ntaryamira alikuwa mhutu hivyo kitendo cha mhutu kuchaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo kiliamsha hisia tofauti kwa watutsi raia wa nchi hiyo. Waziri mkuu mtutsi mama Sylvie Kinigi akamtambua Cyprien Ntaryamira kama rais hata hivyo muda mfupi baadae akajiuzulu wakati rais Cyprien Ntaryamira akiapishwa na hivyo nafasi yake kuchukuliwa na ndugu Anatole Kanyenkiko. Kwani mama Sylvie Kinigi alikuwa akionekana kuwa ni mkosoaji na mtu wa kuogopwa kwa namna ya uongozi wake. Muda mfupi baada ya kujiuzulu mama Sylvie Kinigi akaondoka nchini Burundi” Brigedia jenerali Ibrahim Gambari akaweka kituo huku akinitazama kwa utulivu na kisha kuniuliza.
“Nadhani unayafuatilia vizuri maelezo yangu”
“Ondoa shaka” nikamwambia na hapo akaendelea.
“Rais wa Burundi ndugu Cyprien Ntaryamira na rais wa Rwanda kipindi hicho ndugu Juvénal Habyarimana, wote wahutu, waliuwawa jioni ya tarehe 6, Aprili, 1994 kwa shambulio la kulipuliwa kwa ndege yao wakati ndege hiyo ilipokuwa ikijiandaa kutua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kigali nchini Rwanda. Tukio hilo lilipelekea mauaji ya kimbari nchini Rwanda.
Baada ya kifo cha rais Cyprien Ntaryamira uongozi wa nchi ya Burundi ukachukuliwa na ndugu Sylvestre Ntibantunganya ambaye hapo awali alikuwa ni spika wa bunge la Burundi ambaye pia kwa kabila ni mhutu. Hata hivyo ndugu Sylvestre Ntibantunganya hakufaidi sana madaraka yake kwani ilipofika tarehe 21 mwezi Julai mwaka 1996, waasi wa kihutu walivamia kambi moja ya wakimbizi nchini Burundi na kuua watu zaidi ya 300. Tukio hilo likapelekea rais Sylvestre Ntibantunganya siku mbili zilizofuata aikimbie ikulu na kwenda kujificha kwenye ubalozi wa Marekani nchini Burundi.
Jeshi likachukua madaraka ya nchi ya Burundi tarehe 25 mwezi Julai mwaka 1996 na aliyekuwa waziri wa ulinzi ndugu Firmin Sinzoyiheba akatangaza kupitia redio ya taifa kuwa Meja Pierre Buyoya mtutsi ndiye rais wa serikali ya mpito. Mapinduzi hayo yalipingwa vikali na taasisi za kimataifa akiwemo rais wa Marekani wa kipindi hicho Bill Clinton, katibu mkuu wa umoja wa mataifa wa kipindi hicho ndugu Boutros Boutros-Ghali na katibu mkuu wa umoja wa Afrika wa kipindi hicho, mtanzania mwenzetu ndugu Salim Ahmed Salim. Hivyo hayo yalikuwa ni mapinduzi ya kijeshi mara ya nne kuwahi kufanyika nchini Burundi na pia ya mara ya pili kwa Meja Pierre Buyoya kutwaa madaraka ya nchi hiyo.
Kufuatia hapo vikwazo mbalimbali vikawekwa na tasisi za kimataifa ili kuibana serikali ya Meja Pierre Buyoya juu ya namna yake kutwaa madaraka kwa mapinduzi ya kijeshi. Hata hivyo kufuatia vyombo mbalimbali vya asuluhishi hatimaye Major Pierre Buyoya akakubali kukabidhi madaraka mwaka 2003 ambapo aliyekuwa makamo wake wa rais ndugu Domitien Ndayizeye ambaye ni mhutu akaapishwa kuwa rais wa nchi hiyo wa serikali ya mpito. Madaraka ambayo aliyoyashikilia hadi tarehe 26 mwezi Agasti mwaka 2005 alipomkabidhi kiti cha uongozi wa nchi hiyo ndugu Pierre Nkurunziza baada ya kuibuka mshindi kwenye uchaguzi mkuu wa rais wa nchi hiyo” Brigedia jenerali Ibrahim Gambari akaweka kituo kisha nikamuona akimalizia kuvuta sigara yake na kipisi kidogo kilichosalia akakitupia kwenye kile kibeseni cha majivu pale mezani kisha akasogeza nyuma kiti chake cha ofisini na kusimama.
Upande wa kulia wa sehemu ile kulikuwa na kabati kubwa la mbao, Brigedia jenerali Ibrahim Gambari alipolifikia lile kabati akafungua na kuchukua chupa ya chai na vikombe viwili vya dongo, mkebe mdogo wa kuhifadhia sukari na pakiti moja ya kahawa. Aliporudi pale mezani akafungua ile chupa ya chai na kumimina maji ya moto kwenye vile vikombe kisha akaichana ile pakiti ya kahawa na kumimina kahawa mle ndani. Vijiko vichache vya sukari ya Kilombero vikatosha kutengeneza mchanganyiko makini wa kahawa yenye harufu nzuri na ladha ya kuvutia.
“Karibu tupashe tumbo joto” Brigedia jenerali Ibrahim Gambari akanikaribisha baada ya kumaliza kukoroga mchanganyiko ule kwenye vile vikombe kisha akanyanyua kikombe kimoja na kukishika hewani. Kwa ishara ile nikafahamu kuwa alikuwa akinisubiri tugongeshe vikombe vyetu kama ishara ya umoja na urafiki wetu ama Cheers. Mara tu tulipogongesha vikombe vyetu hewani kila mmoja akavuta funda moja la kahawa na kukiweka kikombe chake mezani.
“Nashukuru sana kwa kahawa maana tumbo langu lilikuwa limepoa mno” nikaongea kwa utulivu huku nikitabasamu.
“Kahawa ni kinywaji kizuri sana hasa wakati wa baridi” Brigedia jenerali Ibrahim Gambari akaongea kwa utulivu kisha akaweka kituo. Nilipomtazama haraka nikajua kuwa alikuwa akifikiria jambo fulani lakini hatimaye akavunja tena ukimya.
“Ukirejea kwenye maelezo yangu ya hapo awali sasa utagundua kuwa nchi ya Burundi tangu ilipopata uhuru wake kutoka kwa mkoloni mwaka 1962, tayari imeshatawaliwa na viongozi kumi na moja hadi kufikia wakati huu. Mapinduzi ya kijeshi yamefanyika mara nne na ndiyo maana hapo awali nikakueleza kuwa mapinduzi ya kijeshi katika nchi ya Burundi siyo jambo geni. Hivyo ni vizuri kuwa utakapokuwa unaingia kwenye nchi hii uwe unafahamu vizuri hali ya usalama wa nchi hiyo jinsi ilivyo” Brigedia jenerali Ibrahim Gambari akaweka kituo akinyanyua kikombe na kuvuta funda jingine la kahawa huku akinitazama.
“Balozi Adamu Mwambapa alikuwa akiishi na familia yake huko nchini Burundi?” nikamuuliza jemadari yule huku na mimi nikikizoa kikombe changu pale mezani na kuvuta funda moja la kahawa.
“Hapana!, familia yake ipo Tukuyu mkoani Mbeya, kwenye nyumba yake aliyoijenga baada ya kustaafu. Ingawa mara kwa mara familia yake husafiri na kwenda kumsalimia huko jijini Bujumbura nchini Burundi, hususani pale anapokuwa ametingwa kwa muda mrefu na shughuli za kiofisi zinazo mnyima muda wa kurudi nchini Tanzania na kuisalimia familia yake”
“Familia ya balozi Adam Mwambapa imeshafahamishwa juu ya kutekwa kwake?”
“Bado haijafahamishwa kwani hata sisi wenyewe hatuna muda mrefu sana tangu tulipopata taarifa hizi. Kutakapopambazuka tutafanya utaratibu za kuipasha habari familia yake hasa baada ya kuandaa mazingira stahiki”
“Vyombo vya habari je vinafahamu?”
“Tumekubaliana kutovujisha taarifa hizi kwa vyombo vya habari. Hatutaki idara yetu ya usalama ionekane dhaifu na serikali ilaumiwe kwa kutokuwajibika ipasavyo kuwalinda viongozi wake. Hili ni agizo kutoka kwa rais lakini vilevile kuvujisha kwa taarifa hizi kwa waandishi wa habari kunaweza kumfanya mtu yeyote aliyehusika na tukio hili kuipima vizuri nguvu yetu ya usalama na hivyo kutukwepa kiulaini. Hivyo tumeonelea kuwa mambo yote yawe kimyakimya hadi hapo tutakapokuwa tumefanikiwa kwenye mipango yetu”
“Mmefanya vyema” nikaongea kwa msisitizo huku nikionesha kufurahishwa na hoja ile. Brigedia jenerali Ibrahim Gambari akavuta tena funda jingine la kahawa na kuweka kikombe chake juu ya meza kisha akakohoa kidogo na kuendelea.
“Tunataka uende jijini Bujumbura nchini Burundi ukapeleleze kwa kina juu ya hili tukio la kutekwa kwa balozi wetu na ni matumaini yetu kuwa kwa moyo wako wa uzalendo utarudi salama hapa Dar es Salaam huku ukiwa umeongozananaye. Sitarajii kuwa itakuwa ni kazi rahisi lakini naamini kuwa utaifanya kwa weledi wako wote na kuiletea heshima kubwa idara yetu ya ujasusi na serekali yetu kwa ujumla” Brigedia jenerali Ibrahim Gambari akaongea huku akinitazama kwa macho yake chakaramu. Ukimya wa mle ndani ukanipelekea nisikie kelele za mapanga boi ya feni namna yalivyokuwa yakikata upepo kwa utulivu kwenye ya dari ya ofisi ile.
“Rais wa Burundi kwa sasa yuko wapi?”
“Yupo hapa jijini Dar es Salaam kuhudhuria mkutano wa 13 wa viongozi wa nchi za Afrika Mashariki huku suala la machafuko ya kisiasa nchini Burundi likiwa ni ajenda kuu ya mkutano huo”
“Anafahamu juu ya kile kinachoendelea sasa hivi nchini kwake?”
“Nina hakika kuwa huwenda anafahamu lakini kwa wakati huu hawezi kuwa na msaada wowote kwetu. Tunachokifanya sisi ni sehemu ya wajibu wetu wa kikatiba katika kuhakikisha usalama wa raia wetu ndani na nje ya nchi. Hivyo hatuna sababu yoyote ya kuendelea kusubiri”....
“Ni kweli” nikaongea kwa utulivu na hapo nikamuona Brigedia jenerali Ibrahim Gambari akivuta mtoto mmoja wa meza yake ya ofisini kisha akachukua nyaraka fulani na kunikabidhi. Nilipozipokea na kuzichunguza kwa makini nikagundua kuwa zilikuwa ni pasipoti tatu za kimataifa za kusafiria.
Pasipoti ya kwanza ilinitambulisha kama raia wa Tanzania na kazi yangu ni mfanyabiashara mwenye jina la Paul Masha. Pasipoti ya pili ilinitambulisha kama mnyarwanda, kazi yangu dereva na jina langu ni Jean Baptiste Gatete na nilipochunguza vizuri katika zile nyaraka nikaona leseni ya udereva yenye utambulisho wa jina la Jean Baptiste Gatete, raia wa Rwanda. Pasipoti ya tatu na ya mwisho, ilinitambulisha kama raia wa Burundi mwenye jina la Céléstine Desire Bizimana, kazi yangu mfanyabiashara.
Nilipozikagua vizuri zile pasipoti nikagundua kuwa zote zilikuwa zimegogwa mihuri mara kadhaa katika vituo fulani vya uhamaji mipakani katika nchi zile katika namna ya kuonesha kuwa tayari nilikuwa nimefanya safari kadhaa maeneo hayo. Pia katika nyaraka zile kulikuwa na kadi tatu za ATM za benki tofauti zilizokuwa nchini Rwanda na Burundi. Mbali na kadi zile pia kulikuwa na vitambulisho vinne vyenye majina yangu.
Kitambulisho cha kwanza kilinitambulisha kama kada wa chama kilichokuwa madarakani nchini Burundi cha CNDD–FDD-Conseil National pour la Défense de la Démocratie-Forces de Défense de la Democratie. Kitambulisho cha pili kilinitambulisha kama kada wa chama pinzani cha siasa nchini Burundi kiitwacho MSD-Mouvement pour la Solidarité et la Démocratie na kitambulisho cha tatu kilinitambulisha kama kada wa chama kingine pinzani cha siasa nchini Burundi kiitwacho ADC-l´Alliance des Democrates pour le Changement au Burundi (ADC-Ikibiri). Kitambulisho cha mwisho kilinitambulisha kama kada wa chama kingine pinzani cha siasa nchini Burundi kiitwacho FNL-Forces Nationales de Libération hapo mwanzo chama hicho kikifahamika kama PALIPEHUTU-FNL, kikundi hatari cha waasi kilichokuwa kikipigania maslahi ya watu wa kabila la wahutu nchini Burundi.
Kwa kweli nyaraka zile muhimu zilikuwa zimenishangaza sana. Sikujua ni wakati gani nyaraka zile zilikuwa zimeandaliwa hata hivyo nilikuwa nikiifahamu vizuri idara yetu ya ujasusi chini ya Brigedia jenerali Ibrahim Gambari namna ilivyokuwa makini katika kuratibu harakati za kijasusi. Hususani pale linapojitokeza suala la dharura kama la kutekwa kwa balozi wetu nchini Burundi, Meja jenerali mstaafu ndugu Adam Mwambapa. Kwa kweli nilikuwa nimeridhishwa vizuri na maandalizi yale ya safari ya kijasusi ya kushtukiza.
Brigedia jenerali Ibrahim Gambari akavuta funda jingine la kahawa na alipokiweka kile kikombe pale mezani akanyanyua mkono na kuitazama saa yake ya mkononi kabla ya kuvunja tena ukimya.
“Taarifa za kiintelijensia zinaeleza kuwa tayari wimbi kubwa la wakimbizi kutoka nchini Burundi limeanza kumiminika kwenye kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu, Kasulu mkoani Kigoma hapa kwetu Tanzania. Hivyo tumeona kuwa lisingekuwa jambo la busara kuwa wakati wakimbizi hao wakiendelea kuingia hapa nchini wewe upishanenao katika njia hiyohiyo ukienda nchini Burundi. Sidhani kama hiyo ni njia salama isitoshe yeyote aliyefanya tukio hili huwenda akawa ametega mitego yake katika njia hiyo kumnasa mtu wetu yeyote tunayekusudia kumtuma.
Kwa hiyo tumeonelea kuwa itakuwa vyema ukiingia nchini Burundi kwa kutokea jijini Kigali nchini Rwanda na nyaraka nilizokupa bila shaka zinatosha kukamilisha mpango huo. Wakati utakapokuwa kwenye harakati nadhani unajua ni namna gani ya kuwasiliana na mimi au idara yetu ya ujasusi. Hivyo ni matumaini yangu kuwa utakuwa ukinijulisha kwa ukaribu kila hatua utakayofikia” Brigedia jenerali Ibrahim Gambari akahitimisha maelezo yake kisha akaitazama tena saa yake ya mkononi na aliporidhika na mwenendo wa majira yake akakinyakua kile kikombe chake cha kahawa pale mezani na kugida funda la mwisho la kahawa. Alipokitua kile kikombe pale juu mezani tayari kilikuwa tupu.
Nilifahamu kuwa tukio lile lilikuwa limeashiria kuwa maongezi yetu mle ndani na Brigedia jenerali Ibrahim Gambari yalikuwa yamefika tamati. Hivyo na mimi nikachukua kikombe changu cha kahawa pale mezani na kugida mafunda mfululizo hadi pale kahawa ile ilipoisha na wakati nikifanya vile Brigedia jenerali Ibrahim Gambari alikuwa akinitazama kwa utulivu.
Nilikuwa wa kwanza kusimama muda mfupi kabla Brigedia jenerali Ibrahim Gambari kufanya hivyo na hapo nikafunga mguu wangu na kupiga saluti ya heshima mbele ya jemadari yule ambapo aliitikia vyema na kunipa mkono wa kuagana.
“Nakutakia safari njema yenye mafanikio Tibba. Tambua kuwa nimekupa jukumu hili kwa sababu nakuamini sana kijana wangu” Brigedia jenerali Ibrahim Gambari akaongea kwa sauti tulivu ya kusihi na katika sauti yake nikaiona hali ya huruma na unyenyekevu huku simanzi na masikitiko yakiwa yamejificha nafsini mwake.
“Mungu atanitangulia” nikaongea kwa utulivu huku nikilazimisha tabasamu usoni mwangu ingawa tabasamu hilo lilikataa kabisa kuumbika pale nilipoanza kutafakari juu safari zangu za kijasusi namna zilivyokuwa zikitawaliwa na mazingira ya hatari katika kuupigania uhai wangu. Wakati nikilichukuwa begi langu na kulitundika begani Brigedia jenerali Ibrahim Gambari akanikabidhi tiketi ya ndege ya shirika la ndege la RwandaAir yenye jina langu ambayo ingenisaidia kusafiri hadi jijini Kigali nchini Rwanda kabla ya kuendelea mbele na safari yangu.
“Mayunga atakupeleka hadi uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere” Brigedia jenerali Ibrahim Gambari akaongea kwa utulivu huku akinitazama. Nikaipokea ile tiketi na kuichunguza kwa makini na kwa kufanya vile nikaliona jina langu la bandia la Paul Masha na hapo tabasamu hafifu likaniponyoka usoni. Tiketi ile ya ndege ilikuwa ikinionesha kuwa ningesafiri saa kumi usiku na ndege ya shirika la ndege la RwandaAir iliyokuwa ikitokea jijini Nairobi kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta nchini Kenya.
“It is our responsibility to defend the respect of our government and the territories of our country as well!” Brigedia jenerali Ibrahim Gambari akaongea kwa utulivu huku akinipigapiga begani kwa mkono wake na kutabasamu katika namna ya kunitia moyo.
“I love my country sir! and not my government” nikamwambia Brigedia jenerali Ibrahim Gambari huku na mimi nikimpigapiga begani kwa ucheshi kisha nikaanza kuzitupa hatua zangu taratibu nikiondoka kwenye ofisi ile.
Muda mfupi baadaye nikaufikia mlango wa ile ofisi na kuufungua huku nikiwa na hakika kuwa macho ya Brigedia jenerali Ibrahim Gambari yalikuwa nyuma yangu yakinisindikiza. Mara nilipoufungua ule mlango nikageuka na kumtazama tena Brigedia jenerali Ibrahim Gambari na nilichokiona usoni mwake lilikuwa ni tabasamu la mwisho la kuagana huku jemadari yule akiwa ameitia mikono yake mifukoni. Bila kupoteza muda nikamtupia tabasamu jepesi la buriani kisha nikatoka nje ya ofisi ile na kufunga mlango.
_____
Nilimkuta Koplo Mayunga akiwa tayari amepitiwa na usingizi huku ameuegemea usukani wa gari lile la jeshi Nissan Patrol, katika eneo la maegesho ya magari la ofisi zile za makao makuu ya idara ya ujasusi jijini Dar es Salaam. Askari yule makini akawahi kushtuka kutoka usingizini wakati nikiukaribia mlango wa mbele wa gari lile na hapo akawahi kushusha kidogo kioo cha mlangoni na kunitazama. Kisha akajisogeza upande wa pili akifanya jitihada kidogo za kufyatua kabari ya mlango ule. Bila kusubiri zaidi nikaufungua ule mlango wa sehemu ya abiria kando ya dereva na kuingia ndani. Koplo Mayunga akanikaribisha kwa bashasha zote huku uso wake ukitengeneza tabasamu hafifu la kichovu kwani macho yake legevu yaliashiria kuwa alikuwa katikati ya lepe zito la usingizi.
“Nipeleke uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere bila kupoteza muda kwani nina safari nzito ya kikazi” nikamwambia Koplo Mayunga huku nikilitupia begi langu kwenye siti ya nyuma na kisha kufunga vizuri mkanda wa siti yangu tayari kuanza safari.
“Vipi afande kuna usalama?” Koplo Mayunga akaniuliza kwa udadisi wakati akiwasha gari na kulitoa kwenye yale maegesho.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mambo siyo shwari ndugu yangu, nimekabidhiwa jukumu zito na sina budi kuwajibika” nikaongea kwa utulivu wakati tulipokuwa tukiyaacha maegesho yale.
“Pole sana afande wangu!” Koplo Mayunga akanifariji huku akiliondoa gari kwenye maegesho yale na kuingia mitaani.
“Nishapoa!” nikaongea kwa utulivu huku akili yangu ikianza kuzama kwenye tafakuri ya kina juu ya safari ile ya kijasusi isiyoeleweka vizuri. Koplo Mayunga hakuwa mtu wa maneno mengi hivyo baada ya pale kikafuatia kitambo kirefu cha ukimya wakati tulipokuwa tukiiacha barabara ya mtaa mmoja na kuingia barabara ya mtaa mwingine kuelekea uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam.
Tulikuwa tumefika mbali katika safari yetu wakati Koplo Mayunga alipoyarudisha tena mawazo yangu mle ndani na kuniuliza.
“Unasafiri na ndege ya saa ngapi afande?”
“Saa kumi usiku huu”
“Ondoa shaka kwani tutawahi kufika kiwanja cha ndege mapema zaidi” Koplo Mayunga akaongea kwa utulivu akinitia moyo hata hivyo sikutia neno badala yake nikayapeleka macho yangu dirishani nikitazama mandhari ya barabara za jiji la Dar es Salaam usiku ule.
Hali ya hewa ilikuwa tulivu na giza zito lilikuwa limetanda angani. Wakati tukiendelea na safari njiani tulipishana na magari machache na kwa kuwa wakati ule wa usiku hapakuwa na foleni za magari hivyo mwendo wetu ulikuwa wa kasi sana na hivyo kuyapeleka magurudumu ya gari letu kuteleza kwenye barabara ile ya lami kama kambare kwenye tope. Wakati ule wa usiku maduka yaliyopakana na barabara za jiji la Dar es Salaam yalionekana kufungwa na baadhi ya magari yalionekana kuegeshwa kwenye sehemu za wazi au kwenye gereji bubu.
Niliitazama mitaa ile ya jiji la Dar es Salaam huku kichwani nikijiuliza kama ningepata nafasi nyingine ya kuizuru mitaa ile nikiwa hai. Hisia zangu ziliniambia kuwa nilikuwa nikielekea kukabiliana na jambo kubwa la hatari sana ingawa picha kamili ya hatari hiyo ilikataa kuumbika kichwani. Nikaendelea kuzikumbuka ndoto zangu za ujanani za kuwa na mafanikio mazuri kama kuwa na mke mwema na watoto wenye siha njema lakini sasa ndoto zile nilianza kuzitilia mashaka kama kweli zingetimia wakati nilipoziweka kwenye tathmini ya mzani wa kifo.
Kama isingekuwa kiapo cha kazi ya jeshi leo hii ningeweza kabisa kukataa ombi la Brigedia jenerali Ibrahim Gambari kisha na ningeandika barua ya kuomba kustaafu na baada ya kulipwa mafao yangu ningeamua kufanya biashara au shughuli nyingine halali za kujiingizia kipato kama walivyo watanzania wengi. Lakini jambo hilo kwa sasa lisingewezekana kwani woga ulikuwa ni kinyume kabisa na taratibu za jeshi letu. Hata hivyo japokuwa kazi ya ujasusi ilikuwa ni kazi ya roho mkononi lakini niseme kuwa nilikuwa nikiipenda sana kuliko kazi yoyote nyingine duniani hali iliyonipelekea niifanye kwa weledi wa hali ya juu na jitihada za aina zote na hivyo kunipelekea kila nitumwapo nirudi na majibu mazuri ya kushangaza huku ugumu wa kazi yenyewe ukiendelea kuwa siri yangu moyoni. Nikiwa bado nimezama kwenye tafakuri ile nikajikuta nikiyakumbuka makovu matatu ya risasi yaliyokuwa kwenye paja langu la mguu wa kushoto na makovu mengine ya misumari yaliyokuwa viganjani ambayo nilikuwa nimeyapata kwenye harakati zangu mbalimbali za kajasusi. Kwa kweli nikajikuta nikimeza funda kubwa la mate kuzitowesha kumbukumbu zile mbaya.
Mawazo yangu yaliporudi tena mle ndani ya gari nikashtuka kuwa tayari tulikuwa tumefika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Mara baada ya kuvuka geti la kuingilia kiwanjani pale Koplo Mayunga akaendesha gari taratibu huku akiyatembeza macho yake huku na kule akitafuta sehemu nzuri ya maegesho na baada ya muda mfupi hatimaye akawa amepata sehemu nzuri ya maegesho na kusimama.
Sikuwa na muda wa kupoteza kwani kwa mujibu wa ratiba iliyokuwa kwenye tiketi ile ya ndege niliyopewa na Brigedia jenerali Ibrahim Gambari ni kuwa zilikuwa zimesalia dakika ishirini tu kabla ya ndege ya shirika la ndege la RwandaAir kuanza safari yake ya kuelekea jijini Kigali nchini Rwanda. Hivyo bila kupoteza muda nikafyatua kabari ya mkanda wa siti yangu kisha nikachukua begi langu kutoka ile siti ya nyuma na kushuka. Koplo Mayunga alitaka kushuka garini na kunisindikiza hata hivyo nilimshukuru na kumtaka asipoteze muda wake kwani nilikuwa na muda mfupi sana kabla kuanza safari yangu kuelekea jijini Kigali nchini Rwanda hivyo tukaagana bila yeye kushuka.
Koplo Mayunga akaniaga kwa kunipungia mkono dirishani huku akinitakia safari njema yenye mafanikio katika harakati zangu. Nikamshukuru huku nikiliacha tabasamu langu likijivinjari usoni mwangu ingawaje moyoni nilihisi kuwa ni kama aliyekuwa akiniambia pumzika kwa amani mpiganaji.
_____
Mtikisiko uliotokea baada ya magurudumu ya ndege ya shirika la ndege la RwandaAir, Boeing 737-800 kuanza kutua kwenye kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Kigali International Airport ukanishtua kutoka usingizini. Nilipoyafumbua macho yangu nikayatembeza taratibu mle ndani ya ndege nikitazama huku na kule na kwa kufanya vile nikagundua kuwa abiria wenzangu wote mle ndani walikuwa macho tayari wamejiandaa kwa tukio lile la kutua kwa ndege. Hivyo haraka nikajua kuwa ni mimi tu ndiye ambaye nilikuwa sijaisikia sauti ya msichana mrembo mhudumu wa ndege ile wakati alipokuwa akiwatangazia abiria wa ndege ile kufunga mikanda wakati ndege ile ilipokuwa ikijiandaa kutua.
Kushoto kwangu alikuwa amekaa mama mmoja wa kinyarwanda ambapo nilikuwa nimemtambua haraka kutokana na mwonekano wake huku akiwa na watoto wake wawili, mmoja wa kike na mwingine wa kiume. Hata hivyo watoto wale walikuwa wamepitiwa na usingizi huku wamezuiliwa vyema na mikanda ya siti za ndege ile. Nilipoyapeleka macho yangu kutazama dirishani mara moja nikauona mwanga hafifu wa pambazuko la alfajiri na hapo nikakumbuka kuitupia macho saa yangu ya mkononi. Majira yalionesha kuwa tayari ilikuwa imetimia saa kumi na mbili na robo alfajiri na hapo nikajua kuwa tulikuwa tumetumia muda wa masaa mawili na dakika ishirini tangu tulipoanza safari kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam hadi uwanja ule wa ndege wa kimataifa wa Kigali nchini Rwanda...
Muda mfupi baada ya ndege yetu kusimama mbele ya jengo la uwanja ule wa ndege mlango wa ndege ulifunguliwa na hapo abiria wakaanza kushuka. Usingizi wa masaa mawili safarini ulikuwa umenipunguzia uchovu kwa kiasi kikubwa hivyo nikafyatua mkanda wa siti na kusimama. Nililichukua begi langu dogo la mgongoni kutoka sehemu maalum ya kuwekea mizigo kwenye sehemu ya juu ya ndege ile kisha nikaunga kwenye foleni ya abiria waliokuwa wakishuka. Abiria tuliyokuwa tukishuka kwenye ndege ile tulikuwa wachache na hapo nikakumbuka kuwa ndege ile ilikuwa ikielekea Entebbe International Airport, kiwanja cha ndege cha kimataifa cha nchi ya Uganda.
Mara tuliposhuka kwenye ile ndege tukaingia kwenye jengo kubwa la kiwanja kile cha ndege cha Kigali lenye migahawa ya kisasa na ofisi mbalimbali za utawala zikiwemo ofisi za uhamiaji za nchi ya Rwanda. Kwa kuwa sikuwa na mzigo wowote mkubwa nikawatangulia abiria wenzangu wenye mizigo nikipenya haraka na kulifikia dirisha moja la ofisi za uhamiaji ziliyokuwa pale kiwanjani.
Nilipofika kwenye dirisha lile nikapenyeza vibali vyangu vyote vya kusafiria kwenye dirisha dogo la kioo la chumba kidogo kilichomhifadhi msichana mmoja mlimbwende aliyeonekana kuyazingatia vema maadili ya kazi yake kwa uchangamfu wa sura yake. Msichana yule afisa uhamiaji akavipokea vibali vyangu vya kusafiria huku akinipa pole ya uchovu wa safari na kuliachia tabasamu lake maridhawa likizitongoza fikra zangu.
Mambo yote yalikuwa chapuchapu kwani yule afisa uhamiaji alimaliza haraka kuingiza taarifa zangu kwenye kompyuta yake kisha akagonga mhuri kwenye hati yangu ya kusafiria na kuniruhusu kuingia rasmi nchini Rwanda. Bila kupoteza muda nikaipokea hati yangu ya kusafiria na kuitia mfukoni huku tabasamu langu la kichokozi likizigalagaza vibaya hisia za afisa yule mlibwende. Kisha nikamkonyeza kidogo kumchombeza huku nikianza kuzitupa hatua zangu kwa utulivu kuliacha eneo lile. Afisa yule uhamiaji akabaki ameduwaa kwa furaha huku macho yake yakinisindikiza nyuma yangu hadi pale nilipopotea mbele yake.
Hali ya hewa ya baridi ya wastani yenye kiasi kikubwa cha unyevunyevu ikanikumbusha kuwa sikuwa nchini Tanzani, jijini Dar es Salaam kama nilivyozoea na badala yake hali ile ilikuwa ni ishara tosha kuwa tayari nilikuwa nimeikanyaga ardhi ya nchi ya Rwanda, jijini Kigali.
Nilikuwa na kiasi kidogo cha faranga za kinyarwanda ambacho nilikuwa nimekipata baada ya kubadilisha kwa shilingi za kitanzania kabla ya kuanza safari yangu jijini Dar es Salaam katika duka moja la kubadilisha fedha za kigeni lililokuwa kule kwenye kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Da es Salaam.
Hii haikuwa mara yangu ya kwanza kufika nchini Rwanda hususani jijini Kigali hivyo kwa kiasi fulani sikuwa mgeni kabisa wa mazingira yale ingawa sikuwa nimewahi kufika jijini Bujumbura nchini Burundi. Hivyo mara baada ya kutoka nje ya uwanja ule wa ndege wa kimataifa wa Kigali dereva mmoja wa teksi mjanja akaniwahi haraka kabla ya wenzake baada ya kuhisi hitaji langu. Mzee yule wa makamo mrefu na mwembamba mwenye sura ya ucheshi akiwa amevaa kofia nyeusi ya pama, shati jeupe na sweta jeusi, suruali ya kijivu na makubasi ya ngozi miguuni akawahi kunifungulia mlango wa teksi yake hata kabla sijaafikiana naye na kumueleza hitaji langu. Kwa ushawishi ule sikuwa na pingamizi hivyo nikaingia ndani.
Mara tu nilipoingia ndani ya ile teksi yule dereva wa teksi akanisemesha kwa lugha ya kinyarwanda na alipoona kuwa sielekei kumuelewa akabadili lugha na kunisemesha kwa kifaransa. Sikuwa mgeni wa lugha ile kwani miongoni mwa lugha nilizokuwa nikizifahamu na kuzizungumza vizuri ilikuwa ni lugha ya kifaransa. Idara yangu ya kijasusi ilikuwa imenipeleka jijini Paris nchini Ufaransa kujifunza vizuri lugha ya kifaransa kwa muda wa miaka mitatu. Kisha miaka miwili mingine nikiitumia jijini Lisbon nchini Ureno kujifunza vizuri lugha ya kireno na hatimaye mwaka mmoja nikiutumia katika chuo kikuu cha Cape town nchini Afrika ya kusini kukipiga vizuri msasa kiingereza changu.
“Toi c'est un Rwandais?” Wewe ni mnyarwanda? dereva yule akaniuliza
“Non, je ne suis pas un Rwandais, je suis un Burundais” Mimi siyo mnyararwanda, mimi ni raia wa Burundi, nikaongea kwa utulivu
“Oh! donc toi c'est un Burundais, bienvenu à Kigali. Moi je suis un Tutsi, et toi?” Oh! kumbe wewe ni raia wa Burundi, karibu sana Kigali. Mimi ni mtutsi wewe je?
Nikaupisha utulivu nikimtazama mzee yule huku nikiwa nimeshtushwa na namna hisia za ukabila zilivyokuwa zikimtafuna nafsini mwake kwa kitendo cha kujitambulisha kwangu kuwa yeye ni mtutsi. Hata hivyo sikutaka kutofautiana na hisia zake.
“Moi aussi je suis un Tutsi, bien que je ne peus pas parler cette langue” Mimi pia ni mtutsi ingawa siwezi kuzungumza lugha hiyo. Maelezo yangu yakampelekea yule mzee aangue kicheko hafifu kabla kuniambia
“Ça ne m'etone pas, car la plus part de jeunes de ce jours ne connaîssent pas leur langue maternelle” Sishangai kwanini vijana wengi wa zama hizi hawajui kuzungumza lugha zao za asili, wengi wanadhani ni ushamba.
Maelezo yale yakapelekea wote kwa pamoja tuangue kicheko hafifu cha katikati ya maongezi na kabla kicheko kile hakijafika ukomo yule mzee dereva wa teksi akaniuliza.
“Tu ne m'a pas encore dis là où tu vas?” Bado hujaniambia unaelekea wapi?
“Amaine moi à Nyabugogo, où il ya la guarre des bus qui maine vers Bujumbura” Nipeleke Bugogo ilipo stendi ya mabasi ya kuelekea Bujumbura.
Kitambo kifupi cha ukimya kikafuatia wakati mzee yule dereva wa teksi akiitoa teksi yake kwenye maegesho yale ya teksi ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kigali. Sehemu ya maegesho teksi maarufu kama Kanombe Airport Park na kuingia barabara ya KK 18 Avenue na wakati tukiingia kwenye barabara ile nikakumbuka kumuuliza yule dereva.
“Ça coute combine d'ici jusqu' à Nyabugogo?” Ni pesa kiasi gani kutoka hapa hadi Nyabugogo?
“30 franc seulement mon jeune garçon” Faranga 30 tu kijana wangu, yule dereva wa teksi akaniambiaCHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Amaine moi, s'il vous plait!” Nipeleke tafadhali!
Safari yetu ikaendelea na tulipofika mbele kidogo sehemu kulipokuwa na barabara pacha tukaiacha barabara ya KK 18 Avenue na kuingia upande wa kushoto tukiifuata barabara ya mtaa wa KK 218. Safari yetu ikaendelea mbele na baada ya kitambo kifupi cha safari ile tukawa tumeifikia barabara nyingine pacha. Tulipofika pale mara nikamuona yule mzee dereva wa ile teksi akiingia upande wa kulia akiiacha barabara ya mtaa wa KK 271 kushoto kwake na kuingia barabara ya upande wa kulia ya Airport View. Wakati tukiendelea na safari mara nikakumbuka kumuuliza yule dereva.
“Est ce que, je peus trouver le bus qui va à Bujumbura ce matin?” Nitaweza kupata basi la kuelekea Bujumbura asubuhi hii?
“Ne t'inquiéte pas!” Ondoa shaka!, yule mzee akaniambia kabla ya kuendelea.
“Ce matin il y a beaucoup de bus, qui vont à Bujumbura, Nairobi, Kampala, jusqu' à Kigoma Tanzanie” Muda huu wa asubuhi mabasi huwa ni mengi sana pale, kuelekea Bujumbura, Nairobi, Kampala hadi Kigoma Tanzania.
Wakati tukiendelea na safari nikayatembeza macho yangu taratibu kutazama kwenye vioo vya ubavuni vya lile gari ili kuchunguza kama kungekuwa na gari lolote likitufuatilia. Niliporidhika kuwa hakuna gari lolote lililokuwa limetufungia mkia nyuma yetu nikageuka na kumtazama yule dereva wa teksi kabla ya kuanza kuyatathmini vizuri mandhari ya eneo lile tulilokuwa tukilipita. Kitu cha kwanza kilichokuwa kimenivutia ni juu hali nzuri ya usafi iliyokuwa katika jiji la Kigali pamoja na mpangilio mzuri wa makazi ya watu ingawaje kwa wakati ule watu wengi walikuwa majumbani mwao.
Baada ya kitambo kifupi cha safari yetu hatimaye tukawa tumetokezea kwenye barabara kuu ya magari iliyokuwa ikifahamika kama barabara ya KN 5. Mara tu tulipoingia kwenye barabara ile tukashika uelekeo wa upande wa kushoto huku upande wa kulia kwetu tukiiacha sehemu ya maegesho ya teksi ya eneo la Remera inayofahamika kama Remera Taxi Park. Baada ya kuingia kwenye barabara ile mwendo wetu ukaongezeka huku dereva yule wa teksi akionekana kuwa makini na sheria zote za barabarani wakati tulipokuwa tukipishana na magari machache na watembea kwa miguu kando ya barabara ile.
Safari yetu ikiwa inaendelea mimi nikatumia wasaa ule kufanya utalii usio rasmi. Kwanza nikaiona Ndoli Joint Supermarket upande wa kushoto kwenye mzunguko wa barabara kuelekea tawi la benki ya Equity eneo la Kisimenti na sehemu ulipo uwanja wa mpira wa miguu wa Amahoro. Tulipoupita mzunguko ule wa barabara tukaendelea mbele na safari huku nikiyashuhudia majengo marefu ya ghorofa yaliyokuwa yamepakana na barabara ile upande kwa upande wa kushoto na kulia.
Safari yetu ikiwa inaendelea upande wa kushoto nikauona mgahawa wa kisasa wa kiitaliano uitwao Sole Luna Italian ukifuatiwa na hoteli ya Beauséjour. Bado tuliendelea na safari tukiifuata barabara ile kuu ya magari. Baada ya kitambo kirefu cha safari ile hatimaye tukawa tumeufikia mzunguko mkubwa wa barabara uitwao KG 2 Round About baada ya kulipita jengo la bunge la Rwanda upande wa kulia. Mara tu tulipomaliza kuuzunguka mzunguko ule wa barabara mbele yetu nikaliona jengo la Casino Kigali. Dereva wa ile teksi akaiacha barabara KN 5 upande wa kushoto ielekeayo eneo la Kigali Centenary Park akiifuata barabara ya RN 3.
Safari ikaendelea na wakati tukiendelea kuifuata barabara ile mbele kidogo upande wa kulia nikaliona jengo la Discover Rwanda Youth Hostel, kisha jengo la British High Commission upande wa kushoto. Tulipozidi kusonga mbele upande wa kulia nikaiona hoteli yenye hadhi ya nyota nne iitwayo Hotel Umubano, kisha tukalipita jengo la Carnegie Mellon University la nchini Rwanda. Barabara ile ilikuwa ikikatisha kwenye eneo lenye majengo mengi yaliyokuwa yakitumika kama ofisi za serikali ya Rwanda na taasisi nyingi za kimataifa. Yule dereva wa teksi akionekana kuanza kuchoshwa na ukimya uliokuwa ukiendelea kushika hatamu mle ndani akanichokoza kwa swali.
“Tu viens d'où?” Unatoka wapi?
“Je vien du Congo Kinshasa” Natokea Congo Kinshasa, nikamjibu kwa utulivu dereva yule wa teksi na hapo akaendelea kuniuliza.
“Pour quoi tu n'a pas dessandu à l´aéroport de Bujumbura?” Kwanini hukushukia uwanja wa ndege wa Bujumbura?
“L'avion que je me suis envolé avec, passé ici à Kigali, et j'ai vu que c'est ne pas mauvais si j'atterrisse ici, et aller à Bujumbura par bus” Ndege niliyopanda ilikuwa inapitia hapa Kigali hivyo nikaona siyo vibaya kushukia hapa ili niende Bujumbura kwa usafiri wa basi. Maelezo yangu yakampelekea yule mzee dereva wa teksi ageuke kidogo na kunitazama kisha kitambo cha ukimya kikafuatia huku nikiwaza kuwa huwenda alikuwa akiyatafakari kwa kina yale maelezo yangu. Safari ikaendelea na baada ya kitambo kifupi cha safari ile mara nikamuona tena yule dereva wa teksi akigeuka na kutazama upande wa kulia wa ile barabara kabla ya kuvunja tena ukimya akiniuliza.
“Tu as vis votre ambassade du côté droit?” Umeziona ofisi za ubalozi wenu upande wa kulia?. Swali la yule dereva wa teksi likanipelekea haraka nigeuke na kutazama upande wa kulia wa ile barabara na hapo nikaliona jengo la ofisi za ubalozi wa Burundi. Kuliona lile jengo kukanifanya nikumbuke kuwa nilikuwa nimemdanganya yule dereva wa teksi kuwa mimi ni raia wa Burundi hivyo haraka nikajua kwendana na maongezi yale.
“Oui, j'ai déjà été là plusière fois, quand j'ai travaillé ici au Rwanda” Ndiyo, nimewahi kufika pale mara kadhaa wakati nilipokuwa kikazi hapa Rwanda. Nikamwambia yule dereva wa teksi huku nikiyapa utulivu macho yangu kulitazama lile jengo lenye ofisi za ubalozi wa Burundi nchini Rwanda.
Tulipofika mbele kidogo upande wa kulia nikaliona jengo kubwa la ghorofa la ofisi kuu ya idara ya uhamiaji ya nchi ya Rwanda ama Rwanda Immigration and Emigration. Safari ikaendelea na tulipolipita lile jengo mbele kidogo tukakutana na mzunguko mwingine wa barabara ambapo tuliuzunguka taratibu na kushika uelekeo wa upande wa kulia tukilipita jengo la ghorofa la hoteli ya Grill Marks kwa upande wa kulia. Safari yetu bado ikaendelea na baada ya kitambo kifupi cha safari ile mbele tukaja kukutana na barabara pacha. Tulipofika pale tukaiacha barabara ya KN 8 Avenue upande wa kulia na kunyoosha mbele tukiifuata barabara ya mtaa wa KG 704 iliyokuwa ikikatisha katikati ya makazi ya watu wenye afya kiuchumi. Wakati tukiingia kwenye barabara ile yule dereva wa teksi akavunja tena ukimya akiniambia.
“J'ai eu linformation qu'll y a eu un type d´attentat contre le gouvernement de president Nkurunziza à Bujumbura au Burundi” Nimesikia vyombo vya habari vikitangaza kuwa kumefanyika jaribio la mapinduzi ya kijeshi dhidi ya serikali ya rais Nkurunziza, Bujumbura nchini Burundi.
“Oui, même moi aussi je l'ai compris, et je pense que c´est pour ce la même les vols iternationaux à l'aéroport, de Bujumbura ont été areter, à cause de l'insécurite” Ndiyo, hata mimi nimesikia, nadhani ndiyo maana hata safari za ndege za kimataifa zimesitishwa kwenye uwanja wa ndege wa Bunjura kuhofia usalama.
Bado tuliendelea na safari yetu na tulipofika mbele tukaingia upande wa kulia tukiifuata barabara ya mtaa wa KG 702 halafu mbele kidogo tukakutana na barabara ya RN 3. Tulipoifikia barabara ile tukaingia upande wa kushoto tukiifuata barabara ya KN 8 Avenue. Mara tu tulipoingia kwenye barabara ile mwendo wetu ukaongezeka na nilipochunguza nikagundua kuwa tulikuwa tukizunguka kurefusha safari. Tukio lile likanifanya nigutuke kuwa yule dereva wa teksi alikuwa akifanya ujanja wa kunizungusha ili hatimaye anitoze pesa nyingi kwa safari ile. Hata hivyo nilimezea kwani kwa upande mwingine nilikuwa nimefurahi kwa kulitalii jiji lile la Kigali nchini Rwanda japo kwa sehemu tu.
Kufikia wakati ule sehemu nyingi za jiji la Kigali zilikuwa zimeanza kuchangamka huku watu wakijitokeza na shughuli nyingine za kibinadamu zikianza kufanyika katika baadhi ya maeneo. Maduka yalikuwa yameanza kufunguliwa na baadhi ya ofisi za kutoa huduma muhimu kama benki na posta...
Baada ya kitambo kifupi cha safari ile mara tukalipita jengo la BK ATM upande kulia na kisha kukatisha katikati ya kituo cha kujazia mafuta cha Hashi Energy upande wa kushoto na kituo kingine cha kujazia mafuta cha Kobil upande wa kulia. Baada ya safari fupi mbele kidogo tukaja kukutana na barabara nyingine kubwa ya magari iitwayo KN 7. Tulipofika pale tukaingia upande wa kulia tukiifuata barabara KN 7 kwa upande wa kulia.
Sasa tulikuwa tukielekea eneo la Nyabugogo sehemu ilipokuwa stendi kuu ya mabasi ya kuelekea jijini Bujumbura nchini Burundi. Baada ya safari ndefu hatimaye tukawasili stendi kuu ya Nyabugogo ya mabasi ya kuelekea maeneo ya mbali na jiji la Kigali na nje ya nchi ya Rwanda. Maeneo kama Bujumbura nchini Burundi na Kigoma nchini Tanzania. Yule dereva wa teksi akataka kunishushia kando ya kituo cha maegesho ya teksi cha stendi kuu ya Nyabugogo hata hivyo kwa kuwa sikutaka kusumbuliwa na madereva wa teksi waliokuwa eneo lile hivyo nikamwambia anishushie nje ya jengo la Banque Commerciale du Rwanda. Umbali mfupi kutoka yalipokuwa makutano ya barabara ya Kigali kwenda Gatuma. Barabara ya KN 1 na ile barabara ya KN 20 Avenue.
Bila kupoteza muda nikachukua wallet yangu kutoka mfukoni na kuhesabu faranga 20 za pesa ya kinyarwanda na kumpa na wakati akizipokea na kuzihesabu nikamwambia.
“Merci pour votre meyen de transport” Nashukuru kwa usafiri. Yule dereva wa teksi haraka akamaliza kuhesabu zile pesa na kuzitia mfukoni huku uso wake ukitengeneza tabasamu la kirafiki.
“Ne te derange pas, d'autre fois quand tu arrives à l'aéroport, et tu as besoin de transport, chercher moi au nom de Gael Mugenzi” Ondoa shaka wakati mwingine ukifika pale kiwanja cha ndege, ukihitaji usafiri niulizie kwa jina la Gael Mugenzi. Nikatikisa kichwa huku nikitabasamu katika namna ya kumuonesha yule dereva wa teksi kuwa nilikuwa nimeafikiana vizuri na hoja yake huku nikifahamu fika kuwa uwezekano wa mimi kuonana naye ulikuwa mdogo na pengine mahusiano yetu yalikuwa yakiishia pale.
“Ne te derange pas!” Ondoa shaka!, nikaongea huku nikifungua mlango wa ile teksi na kushuka.
“Bon voyage Monsieur” safari njema ndugu, yule mzee dereva wa teksi akaniambia na kuniaga kwa kunipungia mkono dirishani huku tabasamu lake la kibiashara likigoma kwenda likizo kisha akageuza teksi na kushika uelekeo wa kule tulipotoka.
Niliendelea kusimama eneo lile nikiitazama ile teksi namna ilivyokuwa ikitokomea mitaani kisha nikashika uelekeo wa kwenye lile jengo la Banque Commerciale du Rwanda, eneo lile la Nyabugogo.
Kulikuwa na magari machache yaliyokuwa yameegeshwa nje ya jengo lile la benki wakati nilipokuwa nikikatisha kuelekea ndani ya lile jengo. Mara tu nilipoingia mle ndani nikashtukia kuwa benki ile ndiyo kwanza ilikuwa inafunguliwa muda ule kwani mle ndani kulikuwa na wateja wachache sana. Niliuacha upande wa kushoto kwenye ofisi za benki ile zinazoshughulika na masuala ya mikopo na huduma kwa wateja nikashika uelekeo wa kulia kwenye madirisha matano ya kuta za vioo yaliyokuwa na wahudumu wa benki ile. Nilichagua dirisha moja lenye msichana mrembo mfanyakazi wa benki ile kisha nikapenyeza kadi yangu ya visa nikitaka kuchukua pesa ya kutosha ambayo kwa namna moja au nyingine nisingeweza kuitoa kupitia mashine za ATM za benki ile zilikokuwa nje ya lile jengo.
Msichana yule akanisalimia kwa bashasha zote huku akionekana kubabaika kidogo na uzuri wangu na kwa kweli niseme kioo cha kabati langu kule nyumbani kwangu Dar es Salaam siku zote hakikuacha kuniridhisha kuwa nilikuwa miongoni mwa wanaume wachache wenye mvuto wa hali ya juu kwa wasichana warembo wa sampuli ile. Nilihudumiwa haraka baada ya kumaliza kujaza fomu ya kutolea pesa kupitia kadi yangu ya visa na baada ya muda mfupi kupita nikakabidhiwa kiasi kile cha pesa katika dola za kimarekani. Kisha nikatenga kiasi kingine cha pesa kutoka katika zile dola za kimarekani na kukibadili kwenda kwenye pesa ya faranga za Burundi. Nilipomaliza nikamshukuru yule msichana mrembo mfanyakazi wa ile benki kwa kunifanyia kazi ile kwa haraka isiyo ya kawaida na kwa kweli roho yangu haikutaka nimuache hivihivi. Hivyo nikampa yule dada ahsante ya pesa yenye thamani ya mlo mmoja kamili wa mchana kwenye hoteli ya daraja la tatu huku nikiitia pesa yangu mfukoni na kushika uelekeo wa nje ya lile jengo la benki ya biashara ya Rwanda.
Saa yangu ya mkononi ilionekana kuwa ilikuwa ikielekea kutimia saa mbili kasoro asubuhi wakati nilipokuwa nikitoka nje ya benki ile kuelekea eneo ilipokuwa stendi ya mabasi ya kuelekea jijini Bujumbura nchini Burundi. Jua lilikuwa limeanza kuchomoza ingawaje hali ya hewa ilikuwa ya baridi ya kiasi na siyo kama lile joto la jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania. Pilika za watu zilikuwa zimeanza kushamiri na hivyo kuupelekea mji ule kuanza kuchangamka. Tofauti na vile hapakuwa na ziada nyingine kwani miji mingi ya bara la Afrika kwa namna moja au nyingine ilikuwa ikifanana kwa mandhari na maendeleo.
Maelekezo kupitia kwenye mabango ya kando ya barabara hatimaye yakanifikisha kwenye ofisi za mabasi ya kuelekea jijini Bujumbura nchini Burundi katika stendi ile ya Nyabugogo. Kama yalivyokuwa maeneo mengi ya stendi za mabasi hususani katika nchi za Afrika basi stendi ile ya mabasi ya Nyabugogo kuelekea jijini Bujumbura nchini Burundi ilikuwa imetawaliwa na pilikapilika nyingi za kibinadamu. Pilika za wachuuzi wa biashara ndogondogo, wauza magazeti, wauza matunda kwenye masinia, migahawa midogo kwa ajili ya kuuza vyakula kwa wasafiri na maduka ya bidhaa mbalimbali kuzunguka eneo la stendi ile.
Wafanyakazi wa ofisi zile za mabasi walinipokea kwa bashasha zote hata hivyo hali niliyoikuta katika ofisi zile ilinitia wasiwasi siyo kidogo. Kulikuwa na abiria wengi katika ofisi za mabasi ya stendi ile na mizigo ya abiria ilikuwa imetelekezwa katika namna ya kuashiria kuwa huduma za usafiri zilikuwa zimesitishwa kwa muda ingawaje wafanyakazi wa ofisi zile bado walikuwa wakiendelea kukatisha tiketi kwa abiria waliokuwa wakiendelea kufika eneo lile.
Hatimaye nikaamua kuwauliza abiria niliyowakuta eneo lile na baada ya kudadisi nikagundua kuwa safari za mabasi yote ya kuelekea jijini Bujumbura nchini Burundi zilikuwa zikisuasua kutokana na hali ya machafuko ya kisiasa iliyokuwa ikiendelea nchini humo. Kwa kweli hali ile ilinikatisha tamaa kwani taratibu nilianza kuona dalili za kutofika jijini Bujumbura kwa siku ile. Niliendelea kujishauri na hatimaye nikaamua kuachana na wazo la kukata tiketi baada ya kuhisi kuwa huwenda kungetokea usumbufu mkubwa wakati wa kudai nauli zetu pale ambapo ingetokea kuwa safari za kwenda jijini Bujumbura zingesitishwa rasmi.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nikiwa bado nipo lile eneo la stendi ya mabasi ya Nyabugogo nikasimama na kuanza kuyatembeza macho yangu eneo lile katika namna ya kuzichunguza sura za abiria waliokuwa eneo lile wakisubiri usafiri wa kuelekea jijini Bujumbura nchini Burundi. Kwa kufanya vile nikagundua kuwa akina mama na watoto walikuwa wachache sana eneo lile ukilinganisha na vijana na wazee.
Nikiwa bado ninaendelea na uchunguzi wangu dhidi ya watu waliokuwa eneo lile mara nikajikuta nikivutiwa na msichana mmoja aliyekuwa amesimama peke yake mbali kidogo na eneo lile. Alikuwa msichana mrefu na mweusi mwenye haiba nzuri ya kuvutia. Nywele zake nyeusi ndefu na laini alikuwa amezifunika kwa kofia kama yangu. Sura yake ndefu kiasi yenye macho makubwa ya kike na legevu. Pua yake ndefu na mdomo laini wenye kingo pana kiasi zilizopakwa lipstick ya rangi nzuri ya chocolate pamoja na vishimo vodogo mashavuni mwake vilinifanya nibabaike kidogo kwa uzuri wake wakati nilipomtazama. Msichana yule alikuwa amevaa fulana nyepesi nyeupe iliyoyaficha vyema matiti yake imara yenye ukubwa wa wastani na juu yake alikuwa amevaa shati zito jeusi la kitambaa cha jeans.
Nikiwa na hakika kuwa msichana yule alikuwa hafahamu chochote kuwa nilikuwa nikimtazama kwa kificho nikaendelea na udadisi wangu. Kiuno chake chembamba kiasi chenye misuli imara kiliizuia suruali yake ya rangi nyeusi ya jeans iliyolichora vyema umbo lake matata lenye kuitaabisha vibaya nafsi ya mwanaume yoyote asiyekuwa na msimamo. Miguuni alikuwa amevaa buti ngumu za ngozi na kwa kweli msichana yule alikuwa akipendeza sana. Hisia za upweke zikiwa zimeanza kunitawala nikaanza kuvuta picha juu ya namna gani nitakavyokuwa baada ya kufanikiwa kutengeneza urafiki na msichana yule mlimbwende. Mgongoni alikuwa amebeba begi.
Hatimaye miguu yangu ikawa myepesi ghafla na hivyo kujikuta nikipiga hatua zangu za kivivuvivu kumsogelea huku uso wangu ukianza kutengeneza tabasamu la kirafiki. Msichana yule akawahi kugeuka na kunitazama wakati nilipokuwa nikimkaribia na hapo nikamsalimia.
“Bonjour Mademoiselle” Habari za asubuhi Dada. Msichana yule akageuka kunitazama kwa mshangao kidogo kabla ya kulegeza uso wake na kutabasamu
“Bonjour Monsieur” Hatimaye akaitikia salamu yangu huku akinitazama kwa utulivu na kweli ukaribu ule ukanipelekea niutathmini vizuri uzuri wa msichana yule. Mfinyanzi alikuwa ametulia kwa makini wakati wa kumuumba kisura yule!
“Tu vas aussi au Burundi?” Unaelekea Burundi, nikamuuliza yule mlimbwende
“Oui!” Ndiyo! yule msichana akaitikia huku akitikisa kichwa chake taratibu na kunitazama usoni katika namna ya kukubali kisha akaniuliza.
“Et toi aussi tu te dirige vers le Burundi?” Na wewe pia unaelekea Burundi?
“Oui, Mais, c'est ma première fois d'aller au Burundi” Ndiyo, lakini ni mara yangu ya kwanza kwenda Burundi. Yule msichana akanitazama kidogo kwa utulivu huku uso wake ukishindwa kuonesha tashwishwi yoyote na hatimaye akaniuliza tena.
“C'est ne pas un bon mement d'aller visiter Bujumbura, que-ce-que tu vas faire au Burundi” Huu siyo wakati mzuri wa kwenda kutembea Bujumbura. Unaenda kufanya nini Burundi?. Swali la yule msichana likaipelekea haraka akili yangu kuchangamka huku nikitunga uongo mzuri kichwani na hatimaye nikapata wazo.
“Je vais chercher mon grand frère, il est là depui longtemps, il est partis chercher la vie, et pour le moment je n'ai pas des communication avec lui” Naenda kumtafuta kaka yangu, kwa muda mrefu amekimbilia huko kutafuta maisha na sasa sina mawasiliano naye. Nikaongea kwa kujiamini huku uso wangu ukiendelea kutengeneza tabasamu la kirafiki na kwa hakika tabasamu langu lilifanikiwa kuziteka hisia za mlimbwende yule kwani nilimuona akipumbazika na uzuri wangu.
“Bujumbura c'une grande ville, comment-est-que tu vas chercher quelqu'un sans avoir ses informations?” Bujumbura ni mji mkubwa, utawezaje kumtafuta mtu bila ya kuwa na taarifa zake? yule msichana akaniuliza huku akinitazama na hapo nikatabasamu kidogo na kuangua kicheko hafifu kisichokuwa na maana yeyote kisha nikamwambia.
“Je sais que c'est une chause difficile, mais je n'ai pas le moyen. Ça fait cinq ans que je n'ai rien compris de lui. La darnière fois qu'on a communiqué, il a dit qu'il hapité à l'avenue de la jeunesse au bord de la route de la chaussé du peuple Murundi” Nafahamu kuwa ni jambo gumu lakini sina namna. Miaka mitano imepita bila ya kusikia chochote kutoka kwake. Mara ya mwisho tulipowasiliana alisema kuwa anaishi mtaa wa Avenue de la Jeunesse kando ya barabara ya Chaussee du peuple Murundi.
“Oh! je connais cet avenue, c'est ne pas loin du centre ville. Quand on va arrive à Bujumbura je vais te diriger” Oh! naufahamu vizuri huo mtaa, haupo mbali sana kutoka katikati ya mji. Tukifika Bujumbura nitakuelekeza. Nikayafurahia sana maelezo ya msichana yule huku nikihisi kuwa nilikuwa nimepata rafiki mzuri mwenyeji wa jiji la Bujumbura.
“Ja vais te remercier beaucoup” Nashukuru sana. Nikamwambia yule mlimbwende
“Moi j'arrive à l'avenue Bulevard du ler Novembre dans la ville de Bujumbura” Mimi nitafikia mtaa wa Boulevard de ler Novembre jijini Bujumbura. Yule msichana akaniambia.
Nikamtazama msichana yule kwa utulivu huku nikitabasamu katika namna ya kuzidi kutengeneza urafiki naye. Mitaa mingi ya jiji la Bujumbura nilikuwa nikiifahamu kupitia ramani ndogo ya nchi ya Burundi niliyopewa na Brigedia jenerali Ibrahim Gambari kabla ya kuanza safari yangu jijini Dar es Salaam. Kitambo kifupi cha ukimya kikapita huku kila mmoja akiupisha utulivu kichwani mwake na nikiwa katika hali ile swali fulani likanijia kichwani.
“Tu es de Bujumbura?” Wewe ni mwenyeji wa Bujumbura?. Nikamuuliza.
“Qui, mais c'est ne pas du tuot” Ndiyo, japo siyo sana. Yule mrembo akaniambia huku akinitazama katika namna ya kuonesha kufurahishwa na maongezi yangu.
“C'est le voyage de combien d'heures d'ici?” Ni safari ya masaa mangapi kutoka hapa?. Nikamuuliza yule mrembo na baada ya kufikiri kidogo akanijibu.
“Dans sept heures ou huit heures si l'atmosphere et calme” Masaa saba hadi nane kama hali ya hewa ni tulivu.
“Comment est la securité?” Vipi kuhusu hali ya usalama?. Swali langu likampelekea yule mlimbwende atabasamu kidogo huku akinitazama na hapo nikapata nafasi nzuri ya kuyaona meno yake meupe yaliyopangika vizuri na vishimo vyake mashavuni. Alikuwa msichana mrembo sana ambaye katika kumbukumbu zangu sidhani kama niliwahi kuonana na msichana kisura wa namna ile. Tabasamu lake lilipokoma akavunja ukimya.
“Le gouvernement seforce a securisé cette route, mais il y a des mauvais actes pendant la nuit” Serikali inajitahidi kudumisha usalama katika barabara hii ingawa kumekuwa na vitendo vya kiharamia nyakati za usiku.
“Tu as déjà voyage pendant la nuit?” Umewahi kusafiri nyakati za usiku? Nikamuuliza yule dada na swali langu likampelekea anikate jicho la kiaina na namna ya utazamaji wake ukanitia mashaka kidogo.
“C'est comme ça que les qents disent” Watu ndiyo wanavyosema. Jibu lile likanipelekea nigeuke vizuri na kumtazama usoni msichana yule na kwa kufanya vile nikawa nimegundua kuwa maelezo ya mrembo yule yalikuwa hayaendani kabisa na mwonekano wa sura yake. Hali ile ikapelekea maswali chungu mzima yaanze kuibuka kichwani mwangu. Sikujua kwanini nilishikwa na hali ile ya wasiwasi lakini moyo wangu ulikosa utulivu kidogo ingawa nilimezea na kuendelea kutabasamu kabla ya kuzidi kumchombeza zaidi kisura yule.
“Tu ne m'a pas encore dis votre nom la belle?” Hujaniambia unaitwa nani mrembo?. Nikamuuliza huku nikitabasamu.
“Moi?” Mimi?. Yule mrembo akaniuliza kwa kujibalaguza huku akifahamu fika kuwa swali langu lilikuwa likimlenga yeye. Angalau nikaliona tena tabasamu lake maridhawa likichomoza usoni mwake na kuusuuza vizuri mtima wangu...
“Oui!, je vois que c'est ne pas mauvais qu'on seconnaissent, si ça ne te derange pas” Ndiyo! nimeona siyo vibaya tukafahamiana, kama hutojali. Nikaongea kwa utulivu huku nikimtazama yule kisura.
“Je m'appelle Amanda Egide, et vous?” Naitwa Amanda Egide, wewe je?
“Je m'appelle Jean Baptiste Gatete” Naitwa Jean Baptiste Gatete. Nikamwambia yule mlimbwende kwa kujiamini kana kwamba lile lilikuwa jina langu halisi.
“Toi c'est un Rwandais?” Wewe ni mnyarwanda?. Amanda akaniuliza na swali lake likaibua hisia mpya kichwani mwangu huku nikishindwa kuelewa nini maana ya swali lile.
“Oui, mais pour le moment je vis à Lubumbashi en D R Congo” Ndiyo, ila kwa sasa naishi Lubumbashi, jamhuri ya kidemokrasia ya nchi ya Kongo. Jibu langu likampelekea Amanda ageuke vizuri na kunikata jicho tena na nilipomtazama usoni sikuona tashwishwi yoyote usoni mwake na badala yake alikaa kimya akiupisha utulivu kama afikiriaye jambo fulani. Hali ile ikaniacha njia panda na kwa kuwa sikupenda hali ile ya ukimya iendelee kutawala hivyo nikavunja ukimya na kumuuliza tena Amanda.
“Tu penses qu'on va trouver le transport aujourd'hui?” Unadhani leo tutapata usafiri?
“Je n'ai pas la précision, mais ça dependra de l'état de la sécurité au Burundi” Sina hakika ingawa itategemea na hali ya usalama itakavyokuwa nchini Burundi. Amanda akaniambia huku akiitazama saa yake ya mkononi.
Tuliendelea kuongea hili na lile huku nikimuuliza maswali Amanda juu ya mambo mbalimbali ambayo kwa namna moja au nyingine nilikuwa na hakika kuwa yangeweza kunisaidia katika harakati zangu mbele ya safari. Kwa kweli nilikuwa nimefurahi sana kumpata rafiki na mwenyeji wa jiji la Bujumbura na vitongoji vyake. Kwani kwa namna nyingine nilikuwa nimeanza kupata matumaini kuwa safari yangu isingekuwa na vikwazo sana katika kuzifikia sehemu muhimu nilizokuwa nikizihitaji mara baada ya kufika jijini Bujumbura. Wakati tukiendelea na maongezi nikagundua kuwa idadi ya wasafiri wa kuelekea jijini Bujumbura ilikuwa ikiendelea kuongezeka taratibu kwenye zile ofisi za yale mabasi huku dalili za kuanza safari zikizidi kufifia.
Ilipotimia saa tano asubuhi matumaini ya kupata usafiri wa kuelekea jijini Bujumbura nchini Burundi yakawa yametoweka kabisa baada ya wafanyakazi wa ofisi zile za mabasi kutoa tamko kwa abiria waliokuwa pale kuwa serikali ya nchi Rwanda ilikuwa imetoa tamko la tahadhari ya usalama kupitia waziri wake wa ulinzi. Kuwa safari zote za kuelekea jijini Bujumbura nchini Burundi zilikuwa zimetolewa tamko la kusitishwa kutokana na hali ya machafuko ya kisiasa ilivyokuwa ikiendelea kuota mizizi katika nchi hiyo. Taarifa zile zikaibua zogo la aina yake baada ya abiria waliokata tiketi eneo lile kuanza kudai nauli zao.
Kwa kweli nilikata tamaa sana hasa kwa kuchukulia kuwa nilikuwa tayari nimepoteza muda wangu mwingi eneo lile na hasa nilipoanza kuwaza kuwa kutokana na hali ile nisingeweza tena kupata nafasi ya kusafiri na mlimbwende yule Amanda. Njaa nayo ilikuwa imeanza kuniuma hivyo nilichowaza ilikuwa kwanza ni kutafuta mgahawa wowote wa jirani na eneo lile ambapo ningepata mlo wa nguvu huku nikipanga hatua inayofuata. Nilipomtazama Amanda naye nikamuona kuwa ni kama aliyekuwa amekatishwa tamaa sana na tamko lile la kusitishwa kwa usafiri wa kuelekea nchini Burundi. Hata hivyo sikuweza kufahamu kuwa alikuwa akiwaza nini kichwani mwake.
“Est-ce qu'il y a un bon restaurant dans ce milien, là où on peut prendre le petit dejeuner?” Kuna mgahawa wowote mzuri eneo hili ambapo tunaweza kupata kifungua kinywa?. Nikamuuliza Amanda.
“Le restaurant du coin des amis, il est derière le bâtiment de Kigali Nightmare, c'est ne pas loin d'ici” Mgahawa wa kona ya marafiki upo nyuma ya jengo la Kigali Nightmare, siyo mbali sana kutoka hapa. Amanda akaniambia kwa bashasha zote huku akionekana kufurahishwa na wazo langu.
Muda mfupi baadaye tulikuwa ndani ya mgahawa wa kisasa wa Le Restaurant du coin des amis uliyokuwa nyuma ya jengo refu la biashara la Kigali Nightmare, barabara ya mtaa wa KN 8. Ulikuwa ni mgahawa mzuri wa kisasa wenye huduma zote muhimu kama aina ya vyakula mbalimbali vya watu wa mataifa tofauti na utulivu wa kutosha. Tulipoingia mle ndani nikagundua kuwa kulikuwa na raia wengi wa kutoka nje ya nchi ya Rwanda husani wazungu ambao wengi walikuwa ni wafaransa ambao niliwatambua haraka baada ya kuwasikia vizuri wakizungumza lugha ya kifaransa.
Hatimaye tukatafuta meza moja iliyojitenga kwenye kona moja ya mgahawa ule na kuketi. Sehemu ile tuliyoketi ilituwezesha sote kuona nje ya mgahawa ule kupitia kuta safi za vioo zilizokuwa zikitazamana na barabara pana ya lami. Mhudumu mmoja wa mgahawa ule alipokuja kutusikiliza nikamuagiza Hot chocolat chaud na supu nzito ya ng’ombe yenye saladi na chapati tatu za unga wa ngano wa ata. Amanda yeye akaagiza wali wa kuku na saladi ya mboga za majani.
Vyakula vile vilipoletwa na mhudumu tukaanza kuvishambulia huku kila mmoja akionekana kuwa na njaa na wakati tukianza kupata mlo ule ndiyo nikapata wasaa mzuri wa kumchunguza Amanda kwa jicho la wiziwizi. Hisia zangu zikanipelekea nijisikie furaha kwa kuketi pamoja na msichana yule mrembo hasa pale nilipogundua kuwa watu wengi waliokuwa mle ndani ya ule mgahawa walikuwa wakitutazama kwa jicho la wivu. Hakika tulipendeza sana na kuonekana kama wapenzi tulioshibana na kuendana vizuri sana.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati nikiendelea kupata mlo nikagundua kuwa hata Amanda naye alikuwa akinitazama kwa jicho la wizi. Hata hivyo sikutaka kumnyima nafasi ile hivyo mara kwa mara nikawa nikizuga kutazama nje ya mgahawa ule kupitia kuta safi za vioo vya ule mgahawa. Pamoja na yote macho ya Amanda hayakuhama kwangu badala yake yalikuwa makini kufuatilia kwa karibu kila tukio nililokuwa nikilifanya.
Mara kwa mara nilipoacha kutazama nje ya mgahawa ule niliyatembeza macho yangu kuzitazama sura za watu waliokuwa mle ndani na kwa kufanya vile nikagundua kuwa mle ndani kulikuwa na huduma ya Wi-Fi (Wireless Fidelity). Huduma ya mtandao wa intaneti kwa mtu yeyote mwenye kifaa kinachoweza kunasa taarifa za kimtandao wa intaneti kama simu za kisasa za mkononi au kompyuta.
Hali ile ikanipelekea nipate wazo la kuwasiliana na mratibu wangu wa safari za kijasusi na vilevile mkuu wa idara ya taifa ya ujasusi Brigedia jenerali Ibrahim Gambari jijini Dar es Salaam Tanzania. Lengo langu likiwa ni kutaka kumueleza kuwa tayari nilikuwa nimefika nchini Rwanda na sasa nilikuwa katika harakati za kuelekea jijini Bujumbura nchini Burundi. Hivyo nikaichukua simu yangu ya mkononi na kuiunganisha na huduma ile ya mtandao wa intaneti ndani ya ule mgahawa. Tukio ambalo pia lingempelekea Brigedia jenerali Ibrahim Gambari kupitia GPRS aweze moja kwa moja kuitambua sehemu ile niliyokuwa.
Mtandao wa intaneti uliponasa vizuri kwenye simu yangu ya mkononi nikaandika taarifa fupi ya ujumbe wa elektroniki nikimueleza Brigedia jenerali Ibrahim Gambari hatua niyofikia kwenye harakati zangu. Wakati nikifanya vile Amanda akawa akinitazama kwa kuibaiba hata hivyo sikumtilia maanani. Ule ujumbe wa taarifa fupi ulipoenda nikaizima simu yangu na kuitia mfukoni huku nikiliachia tabasamu langu maridhawa likielea usoni. Mara tu ule ujumbe ulipoenda na kisha kuizima simu yangu kabla ya kuitia mfukoni nikashangaa kumuona Amanda naye akiitoa simu yake ya mkononi haraka kutoka mfukoni na kuitazama kisha akayahamishia macho yake kunitazama kidogo kabla ya kuyahamisha pembeni. Nikamuuliza kama kulikuwa na shida yoyote.
“Est-ce qu'l y a un problème?” Kuna shida yoyote?
“Non, je regardè le temps” Hapana, nilikuwa natazama muda. Amanda akaniambia huku akiendelea kupata mlo na wakati tukiendelea kula akili yangu ikawa ikiendelea kusumbuka katika namna ya kuwaza kuwa ni kwa namna gani ningepata usafiri wa kuelekea jijini Bujumbura nchini Burundi kwa siku ileile.
“La nouriture d'ici goûte bien” Chakula cha hapa kina ladha nzuri. Huku akitabasamu Amanda akaniambia.
“C'est juste, laisse moi parler que je n'ai jamais mangé la nouriture qui goûte bien ici au Rwanda, comme à ce restaurant” Ni kweli, niseme kuwa sijawahi kula mlo wenye ladha nzuri hapa nchini Rwanda kama kwenye mgahawa huu. Nikamwambia Amanda huku nikitabasamu.
Maongezi baina yetu yakaendelea ndani ya ule mgahawa huku tukiendelea kupata mlo taratibu na sote tulionekana kufurahishwa na urafiki ule ulioanzia njiani. Amanda alinieleza mambo mbalimbali kuhusu nchi ya Burundi ambayo hapo mwanzo nilikuwa siyafahamu na mimi sikuacha maongezi yale yaelemee upande mmoja hivyo nikawa nikitia vionjo vya hapa na pale vilivyompelekea Amanda ajikute akicheka mara kwa mara.
Tulipomaliza kupata mlo tukaagiza juisi ya parachichi tukishushia taratibu kusindikiza maongezi yetu huku kichwani nikiendelea kufikiria juu ya safari yangu ya jijini Bujumbura nchini Burundi.
Ilipofika saa nane mchana nikaanza kuhisi kuwa tulikuwa tumetumia muda mwingi kukaa ndani ya mgahawa ule kwani hata wale watu waliotukuta mle ndani nao walikuwa wamehudumiwa na hatimaye kuondoka. Hivyo nikamuita mhudumu mmoja wa ule mgahawa na kulipa bili ya ule mlo wote tuliokula mimi na Amanda. Niliporudishiwa chenchi nikamuomba Amanda kuwa tuondoke eneo lile na bila upinzani wowote Amanda akakubaliana na ombi langu hivyo tukachukua mabegi yetu na kutoka nje ya ule mgahawa tukirudi tena kule kwenye ile stendi ya mabasi ya Nyabugogo.
Tulipokuwa tukitembea njiani nikanunua gazeti moja la nchini Rwanda liitwalo La Nouvelle Relève lililokuwa likiandikwa kwa lugha ya kifaransa baada ya kuona taarifa fulani kwenye gazeti lile iliyokuwa ikielezea kwa kina juu ya hali ya machafuko ya kisiasa iliyokuwa ikiendelea nchini Burundi.
Mara tu tulipofika kwenye ile stendi ya mabasi ya Nyabugogo haraka nikagundua kuwa wale abiria wengi waliokuwa eneo lile wakisubiri usafiri wa kuelekea jijini Bujumbura nchini Burundi hawakuwepo. Nilipoendelea kuchunguza nikagundua kuwa zile ofisi za yale mabasi kwenye ile stendi bado zilikuwa wazi hali iliyonipelekea niingiwe na wasiwasi kuwa huwenda usafiri wa dharura ulikuwa umepatikana wakati mimi na Amanda tulipokuwa tukipata mlo kwenye ule mgahawa.
Amanda akawahi kuuliza kwa wale wafanyakazi wa ofisi za yale mabasi kama kulikuwa na usafiri wowote ulioondoka kuelekea jijini Bujumbura kwa kipindi kile ambacho hatukuwepo pale stendi. Wale wafanyakazi wakatuambia kuwa hapakuwa na basi lolote lililosafirisha abiria kuelekea nchini Burundi huku wakitufafanulia kwa kina juu ya tamko lililotolewa na waziri wa ulinzi wa serikali ya Rwanda juu ya kusitishwa kwa safari zote za kuelekea nchini Burundi kufuatia hali ya machafuko ya kisiasa iliyokuwa ikiendelea nchini humo tangu jaribio la mapinduzi ya kijeshi lilipofanyika.
Maelezo ya wale wafanyakazi wa ofisi za yale mabasi yakanipelekea niondoe kabisa matumaini ya kupata usafiri wa kuelekea jijini Bujumbura nchini Burundi kwa mabasi yale badala yake akili yangu ikaanza kuchangamka nikianza kufikiria njia mbadala. Nikiwa katika hali ile mara nikamuona Amanda akiniacha pale niliposimama na kwenda kuzungumza na kijana mmoja aliyekuwa amesimama kando ya eneo lile kama mtu aliyekuwa akitusikilizia. Nilimuona Amanda akizungumza na kijana yule na baada muda mfupi wa maongezi yale Amanda akageuka na kunionesha ishara ya kuniita kwa mkono akinitaka nimfuate pale aliposimama na yule kijana. Nikafanya vile na nilipowafikia pale waliposimama kupitia maongezi yao nikaelewa kuwa kulikuwa kumepatikana usafiri wa mtu binafsi wa kuelekea jijini Bujumbura nchini Burundi. Hivyo yule kijana alikuwa ni mhusika mmojawapo wa gari hilo ambalo kwa mujibu wa maelezo yake ni kuwa gari hilo lilikuwa limeegeshwa nyuma ya kituo kimoja cha kujazia mafuta kilichokuwa jirani ne eneo lile. Akihofia kukamatwa na askari endapo angeliegesha gari lile pale stendi na kutafuta abiria. Kwani tayari serikali ya Rwanda ilikuwa imetoa tamko la usitishwaji wa safari za kuelekea nchini Burundi.
Nikamuuliza yule kijana kuwa nauli ingekuwa faranga ngapi za pesa ya kinyarwanda na hapo akatueleza kuwa alikuwa akitoza dola za kimarekani 50 kwa kila abiria mmoja. Nikageuka kumtazama Amanda nikitaka kufahamu kama alikuwa akilichukuliaje suala lile. Amanda akanifanyia ishara kuwa nisiwe na wasiwasi wote kwani usafiri wa magendo wa namna ile ulikuwa ni jambo la kawaida kufanyika katika stendi ile hususani pale inapotokea shida ya usafiri. Maelezo ya Amanda yakanipelekea nisione sababu ya kuwa na wasiwasi hivyo nikakubaliana na wazo lile na hapo kwa pamoja tukaanza safari ya kuelekea kwenye hilo gari huku yule kijana akituongoza mbele yetu.
Wakati tukitembea mara kwa mara Amanda alikuwa akigeuka na kunitazama katika namna ambayo kwa kweli sikuweza kuielewa. Hata hivyo niliipa akili yangu utulivu huku nikiendelea kutafakari juu ya kazi iliyokuwa ikinikabili mbele yangu.
Baada ya mwendo mfupi wa safari yetu hatimaye tukawa tumekifikia kituo kimoja cha kujazia mafuta kiitwacho Hass Petroleum kilichokuwa nyuma ya ile stendi kuu ya mabasi ya Nyabugogo. Kituo hicho kikipakana na duka kubwa la vipuli vya magari.
Tulipolikaribia vizuri eneo lile mara nikaliona gari moja aina ya Land Rover 110 lenye muundo wa kizamani la rangi ya kijivu likiwa limeegeshwa kando ya kituo kile cha kujazia mafuta. Tulipolifikia lile gari nikagundua kuwa mle ndani kulikuwa tayari kuna watu watatu. Mbele kulikuwa na dereva wa lile gari. Mwanaume mwenye umri wa kukadirika wa kati ya miaka thelathini na tano hadi arobaini, mrefu na mweusi mwenye macho makali akiwa amevaa kofia nyeupe ya pama na koti zito jeusi la kujikinga na baridi. Alikuwa ameketi kwenye ile siti ya dereva akiendelea kusubiri abiria. Ile sehemu ya abiria nyuma yake kulikuwa na watu wawili, vijana wa makamo yangu. Mmoja mrefu na mwembamba na mwingine mfupi na mnene.
Tulipolifikia lile gari tukawasalimia wale watu waliokuwa mle ndani ya gari kiungwana na wote wakaitikia kwa pamoja. Hata hivyo mimi sikukaa kwenye zile siti zilizokuwa mbele kama wale watu tuliyowakuta walivyokuwa wamekaa ila badala yake nikafungua mlango wa nyuma kabisa wa lile gari na kuketi kwenye siti za kutazamana.
Amanda akaonekana kutaka kupingana na uamuzi wangu wa kukaa kule nyuma lakini mara akaghairi msimamo wake pale alipoona nikimfanyia ishara kwa kichwa kuwa aingie kule nyuma ya lile gari ili tukae wote. Hivyo nayeye akafanya vilevile na alipoingia kule nyuma ya gari akaenda na kuketi mbele yangu upande wa pili na kutokana na muundo wa siti za lile gari mtindo ule wa ukaaji ukatupelekea tujikute tukitazamana huku tabasamu lake maridhawa likiendelea kuziadhibu vibaya hisia zangu...
...Yule kijana aliyetuleta kwenye lile gari alipoona kuwa tayari tumeingia akageuza na kurudi kule tulipotoka na hapo nikajua kuwa alikuwa akienda kutafuta abiria wengine wa kujaza nafasi zilizosalia. Dereva wa lile gari akageuka nyuma haraka na kudai nauli na hapo nikapata nafasi ya kuiona vizuri sura yake. Macho yake makali yakatutazama kwa utulivu huku akitengeneza tabasamu jepesi usoni mwake lililoyapelekea meno yake yaliyopoteza mng’ao kwa ukungu wa moshi wa sigara wa miaka mingi kuonekana vizuri huku akiwa ameibana njiti moja ya kiberiti kwenye pembe ya mdomo wake. Hata hivyo macho ya dereva yule nikayaona yakajikita zaidi kwenye kumtazama Amanda na hapo nikajua kuwa jamaa alikuwa amebabaishwa sana na uzuri wa Amanda.
Bila kupoteza muda nikachukua wallet yangu kutoka mfukoni na nilipoifungua nikahesabu noti zenye thamani ya dola mia moja na kumpa yule dereva kama malipo ya nauli yangu na Amanda. Amanda kuona vile akajibalaguza kwa kujidai kuwa anataka kujilipia hata hivyo nikamfanyia ishara kuwa aachane na mpango wake.
Yule dereva akazipokea zile pesa na kuanza kuzihesabu na wakati akifanya vile na mimi nikapata wasaa mzuri wa kuweza kulipeleleza lile gari pamoja na wale abiria tuliowakuta mle ndani. Wale abiria wawili walionekana kuwa ni vijana waliokuwa na hamsini zao na sikuwatilia maanani. Hatimaye nikayahamishia macho yangu nikimtazama yule dereva huku nikitafakari namna alivyokuwa amemtazama Amanda na kisha kunikata jicho la kiaina kabla ya kuipokea ile pesa yangu. Lile gari Land Rover 110 lilikuwa ni la mtindo wa zamani ingawa bado lilionekana kuwa bado ni imara na lenye uwezo mzuri wa kumudu safari yetu. Ingawa sikuwa na uzoefu na safari za namna ile lakini niliamini kuwa maeneo mengi ya bara la Afrika yalikuwa yakifanana hivyo nikaupisha utulivu huku nikijaribu kuvuta picha ya kule tulipokuwa tukielekea.
Wakati nikiendelea na tathmini yangu mara yule kijana aliyetuleta pale awali nikamuona akija huku akiwa ameongozana na abiria wengine wanne. Walipofika kwenye lile gari, abiria wawili wakaingia kule mbele na wale abiria wawili waliosalia wakaingia kule nyuma tulipokuwa mimi na Amanda. Walikuwa ni vijana watatu na mzee mmoja na hivyo kupelekea Amanda awe ndiye msichana pekee mle ndani. Wale vijana walipoingia mle ndani tukawapisha wakae mbele yetu huku mimi na Amanda tukiendelea kukaa sehemu ya nyuma kabisa ya lile gari. Tulisalimiana vizuri na wale vijana na baada ya pale kila mmoja akaendelea na hamsini zake hata hivyo kule nyuma ya gari tukawa tayari tumeenea na hivyo kupelekea abiria mmoja tu kusalia kabla ya kuanza safari yetu.
Kwa muda mrefu tukaendelea kukaa ndani ya lile gari eneo lile huku ukimya ukiendelea kutawala mle ndani. Mara kwa mara nikamuona Amanda akinitazama na kila macho yetu yalipokutana kila mmoja alitabasamu pasipo kuongea neno lolote ingawa nilipomchunguza vizuri Amanda nikagundua kuwa macho yake yalikuwa na uchovu mwingi. Yeyote ambaye angetutazama angeweza kudhani kuwa mimi na Amanda tulikuwa ni wapenzi tulioshibana au pengine tulikuwa ni mke na mume lakini ukweli ni kwamba siri tulikuwa tukiifahamu sisi wenyewe. Tukiwa katika hali ile hatimaye Amanda akapitiwa na usingizi na kukiegemeza kichwa chake juu ya begi lake la mgongoni alilokuwa amelipakata mapajani mwake. Nikamuhurumia sana Amanda kwa hali ile lakini sikuwa na namna ya kumsaidia.
Hali ya ukimya ilipoonekana kuzidi kutawala mle ndani nikaanzisha mada za hapa na pale kwa wale abiria wenzangu katika namna ya kuchangamsha watu lakini hata hivyo mwitikio ulikuwa hafifu sana na hapo nikagundua kuwa ile ilikuwa ni nchi nyingine yenye tamaduni tofauti kabisa na nchi yangu ya Tanzania ambapo utu, undugu na urafiki lilikuwa ni suala la kawaida kabisa. Kiasi kwamba katika mazingira kama yale maongezi ya kirafiki lingekuwa ni jambo la kushabikiwa na kufurahiwa sana.
Kupitia vioo vya madirisha ya lile gari niliweza kuliona wingu zito la mvua lililokuwa likijitengeneza taratibu angani na hivyo kuashiria kuwa mvua kubwa ilikuwa mbioni kunyesha.
Ilipotimia saa kumi na moja jioni safari ikaanza baada ya abiria mmoja aliyekuwa akisubiriwa kupatikana. Yule kijana aliyekuwa akitafuta abiria akaingia mbele kwenye lile gari na kukaa kwenye siti ya abiria upande wa kushoto wa dereva na yule abiria mwingine aliyepatikana akaingia na kukaa kwenye ile siti ya abiria iliyokuwa ikifuatia baada ya ile siti ya nyuma kabisa tuliyoketi na hapo safari ikaanza.
Tulipokuwa tukiondoka eneo lile Amanda akashtuka kutoka usingizini kisha akanitazama kidogo kabla ya kuyahamisha macho yake kuwatazama kwa makini wale abiria wote waliokuwa mle ndani. Alipoyarudisha tena macho yake kwangu akatabasamu kidogo kama kawaida yake huku myumbo wa gari lile barabarani ukimpotezea umakini. Tukabaki tukitazamana tu ingawa kila mmoja alikuwa amezama kwenye fikra zake.
Dereva wa lile gari Land Rover 110 alionekana kuwa mzoefu sana na mwenye kuvijua vizuri vichochoro vingi vya jiji la Kigali. Hivyo akawa akiendesha kwa mbwembwe huku akiwa makini kuchagua barabara za kupita kwa kuhofia kusimamishwa na askari wa usalama barabarani.
Muda mfupi baadaye taratibu tukaanza kuliacha jiji la Kigali nyuma yetu katika mwendo wa masafa marefu huku sauti pekee iliyokuwa ikisikika mle ndani ya gari ikiwa ni ile sauti ya muungurumo wa injini ya lile gari na mnuko wa harufu nyepesi ya mafuta ya petroli. Muda mfupi baadaye tukawa tumeifikia barabara kuu ya kuelekea nchini Burundi.
Mara tu tulipoingia kwenye ile barabara nikageuka kutazama nyuma kupitia kwenye kioo cha mlango wa nyuma wa lile gari na hapo nikagundua kuwa mwendo wetu ulikuwa wa kasi mno. Hali iliyopelekea ile taswira ya yale majengo marefu ya ghorofa ya katikati ya jiji la Kigali na nyumba za makazi ya watu kutoweka taratibu katika upeo wa macho yangu kadiri lile gari Land Rover 110 lilivyokuwa likichanja mbuga kwenye barabara ile. Muda mfupi baadaye hatimaye tukawa tumetokomea kabisa mbali na jiji la Kigali na kuanza kuingia kwenye barabara iliyokuwa ikikatisha katikati ya vichaka na miti mirefu ya msituni tukishuka mabonde na kupanda milima mwendo wa kasi.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Safari ikiwa inaendelea nikaanza kuzichunguza tena nyendo za watu waliokuwa mle ndani kisha nikayapeleka macho yangu kwa yule dereva wa lile gari. Niliporidhika na mwenendo mzima wa ile safari nikaingiza mkono kwenye begi langu nikilichukua lile gazeti la La Nouvelle Relève nililolinunua wakati tulipokuwa tukitoka kwenye ule mgahawa wa Le Restaurant du coin des amis wakati ule na Amanda. Kisha nikalifunua hadi nilipoufikia ukurasa wa tatu sehemu kulipokuwa ni zile taarifa za machafuko ya kisiasa yaliyokuwa yakiendelea nchini Burundi. Kulikuwa na maelezo mengi katika habari ile lakini nilijaribu kwa kila hali kuisoma kwa haraka taarifa ile huku nikiruka maelezo mengine yasiyokuwa na umuhimu kwangu na hivyo kusoma dondoo muhimu tu.
Maelezo aliyonipa Brigedia jenerali Ibrahim Gambari kabla ya kuanza safari yangu ya kijasusi jijini Dar es Salaam nikagundua kuwa hayakuwa yametofautiana sana na kile kilichokuwa kimeandikwa katika taarifa ile. Hata hivyo kulikuwa na ziada nyingine niliyokuwa nimeipata katika ile taarifa. Kwanza niligundua kuwa kiongozi wa jaribio la mapinduzi yale ya kijeshi ya kuiondoa madarakani serikali ya Burundi ya rais Pierre Nkurunziza mwenye cheo cha Meja Jenerali akifahamika kwa jina la Godefroid Niyombare. Taarifa zile zikaendelea kueleza kuwa Meja jenerali Godefroid Niyombare hapo kabla aliwahi kushikilia madaraka ya cheo cha Military chief of staff na vilevile aliwahi kuwa balozi wa Burundi nchini Kenya na pia aliwahi kuwa mkuu wa idara ya ujasusi ya nchi ya Burundi.
Taarifa zikaendelea kueleza kuwa wakati wa vita ya kikabila nchini Burundi, Meja jenerali Godefroid Niyombare alikuwa kamanda wa kijeshi wa kihutu katika kikundi cha kijeshi cha waasi cha wakati huo kikifahamika kwa jina la CNDD-FDD-Conseil National pour la Défense de la Démocratie-Force pour la Défense de la Démocratie na vilevile aliwahi kushiriki katika mazungumzo ya amani na kikundi kingine cha waasi cha FNL-Forces Nationales de Libération. Baada ya vita hiyo ya kikabila Meja jenerali Godefroid Niyombare alipewa cheo cha mkuu wa majeshi ya Burundi chini ya utawala wa rais Pierre Nkurunziza.
Ilipofika Februari 2015 Meja jenerali Godefroid Niyombare akaenguliwa kwenye cheo cha mkuu wa idara ya ujasusi nchini Burundi na rais Pierre Nkurunziza baada ya walaka wake wenye kurasa 10 kuvuja. Walaka ambao aliuandika katika kumkosoa rais Pierre Nkurunziza juu ya kuandaa mazingira ya kutawala nchi zaidi kwa muhula wa tatu. Kitu ambacho kilikuwa ni kinyume kabisa na katiba ya nchi hiyo.
Tarehe 13, mwezi Mei, mwaka 2015 kupitia kituo binafsi cha redio nchini Burundi, Meja jenerali Godefroid Niyombare akatangaza rasmi kuing'oa madarakani serikali ya rais Pierre Nkurunziza kupitia tukio la mapinduzi ya kijeshi wakati rais Pierre Nkurunziza alipokuwa jijini Dar es Salaam nchini Tanzania kuhudhuria mkutano wa 13 wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki. Chini ya habari ile pia kulikuwa na taarifa nyingine iliyoeleza kuwa Meja jenerali Godefroid Niyombare pia aliwahi kushiriki katika mpango wa amani barani Afrika nchini Somalia-African Union Mission to Somalia.
Nikasoma maelezo mengine kuwa Meja jenerali Godefroid Niyombare pia aliwahi kuwa kwenye kamati ya mipango ya kikundi kilichokuwa kikifahamika kwa jina la IMBONERAKURE ingawa sikuweza kufahamu IMBONERAKURE maana yake nini kwa vile pale hapakuwa na maelezo ya kujitosheleza. Hatimaye nikamalizia kusoma taarifa ile kwenye lile gazeti kisha nikalikunja na kulichomeka kwenye mfuko wa pembeni wa begi langu. Nilipomtazama Amanda nikagundua kuwa alikuwa tayari amepitiwa tena na usingizi.
Lile gari lilikuwa likienda mwendo kasi ingawa hata hivyo yule dereva alionekana kuwa makini sana huku akionekana pia kuizoea vizuri ile barabara. Nikayatembeza tena macho yangu kuwatazama abiria wengine waliokuwa mle ndani na hapo nikagundua kuwa hata wao walikuwa wamepitiwa na usingizi. Nikaendelea kuwatazama kwa utulivu watu wale huku wakionekana kuelemewa sana na uchovu. Hata hivyo pamoja na mimi kuwa na uchovu mwingi lakini kamwe sikuuruhusu usingizi unichukue kwa kuzingatia vigezo viwili vikubwa. Kwanza nilikuwa mgeni kabisa wa barabara ile na mazingira yake. Pili binafsi niliona kuwa lilikuwa ni jambo gumu sana na la hatari kwa mtu aliyeko usingizini kuweza kujitetea kikamilifu pale inapotokea hatari ya namna yoyote.
Miale hafifu ya jua la machweo ilikuwa mbioni kutoweka katika safu za milima mirefu yenye misitu mizito ambapo barabara ile ilikuwa ikikatisha kando yake na hivyo kulifanya wingu jepesi la giza kutanda angani. Hata hivyo mwanga mkali wa taa za mbele za lile gari Land Rover 110 ulijitahidi kwa kila hali kulifukuza giza lile lililotanda mbele ya ile barabara wakati gari lile lilivyokuwa likijitahidi kukata upepo na kutokomea mbele zaidi. Kupitia kwenye vioo vya madirisha ya lile gari niliweza pia kuona manyunyu hafifu ya mvua iliyotokana na wingu zito lililokuwa limetanda angani. Hakuna aliyekuwa akiongea na hivyo mle ndani ya gari kulitawaliwa na kiasi kikubwa cha ukimya wa namna yake. Safari bado ilikuwa ikiendelea.
_____
Nilikuwa nimezama katikati ya tafakuri nzito nikiwaza namna ya kuanza harakati zangu mara baada ya kufika jijini Bujumbura nchini Burundi pale niliposhtushwa na kupungua ghafla kwa mwendo wa lile gari letu. Haraka nikainua kichwa na kuyatembeza macho yangu nikitazama huku na kule na hapo haraka nikaona kizuizi cha barabarani kilichokuwa umbali mfupi mbele yetu kabla ya kuanza kupanda mlima. Mvua kubwa ilikuwa ikinyesha na usiku tayari ulikuwa umeingia.
Wakati tukikikaribia kile kizuizi haraka nikagundua kuwa kulikuwa na askari watatu wa barabarani katika kizuizi kile. Askari mmoja alikuwa amesimama katikati ya barabara mbele ya kizuizi kile akimuonesha dereva wetu ishara ya mkono kuwa apunguze mwendo na kusimama. Askari wawili waliosalia mmoja alikuwa amesimama upande wa kushoto na mwingine alikuwa amesimama upande wa kulia wa barabara ile. Askari wale wote walikuwa wamevaa makoti marefu ya mvua huku wamezishika vyema bunduki zao mkononi.
Kitendo cha mwendo wa lile gari letu kupungua ghafla kikawapelekea wale abiria wengine washtuke kutoka usingizini haraka na kutazama kule mbele huku Amanda akiwa miongoni mwao.
Nikiwa bado nimeketi mle ndani nikayahamishia macho yangu tena kwa yule dereva wetu huku nikijaribu kumchunguza kama alikuwa na wasiwasi wowote juu ya lile tukio la kusimamishwa kwetu na wale watu walioonekana kuwa ni askari wa usalama barabarani. Sikuona tashwishwi yoyote usoni mwake badala yake nikamuona akikazana kupangua gia za lile gari Land Rover 110 huku taratibu akipunguza mwendo. Nikayahamisha tena macho yangu kumtazama Amanda pale alipoketi na hapo nikagundua kuwa hata yeye alikuwa amezama katika kuwatazama wale askari waliokuwa wakitusimamisha.
Hatimaye gari letu likasimama hatua chache mbele ya yule askari kando ya ile barabara sehemu kulipokuwa na kile kizuizi kisha yule dereva akageuka nyuma haraka na kutuambia.
“Si un policien vous interoge, disez que nous allons à Huye aux enterrement” Askari akiwauliza mwambieni kuwa tunaelekea Huye kwenye msiba. Sote tukatikisa vichwa taratibu kuonesha kukubaliana na hoja yake kisha yule dereva akafungua mlango wa gari na kushuka taratibu akipiga hatua zake za woga kumfuata yule askari wa usalama barabarani. Tukio lile likanipelekea nizidi kuwa makini zaidi kumtazama yule dereva kule alipokuwa akielekea huku mara kwa mara macho yangu yakiwatazama wale askari wengine kule waliposimama.
Kikapita kitambo kifupi cha maongezi kati ya yule dereva na yule askari wa usalama barabarani na wakati huo wote mimi nilikuwa makini kuwatazama. Mwishowe nikamuona yule dereva wetu akichukua wallet yake ndogo kutoka mfukoni na kuifungua kisha akatoa noti moja na kumpa yule askari. Yule askari akaipokea ile noti haraka na kuitia mfukoni kisha taratibu akaanza kupiga hatua zake akilisogelea gari letu. Yule askari alipolikaribia lile gari akageuka na kumuuliza yule dereva wetu kwa sauti ya ukali.
“Où est-ce que vous alez?” Mnaelekea wapi?
“Nous allons à Huye Monsieur” Tunaelekea Huye bwana mkubwa. Nikamsikia yule dereva akimwambia yule askari na hapo nikamuona yule askari akizunguka na kuja nyuma ya lile gari na wakati yule askari akija kule nyuma ya gari akawa akitukata jicho la hadhari watu wote tuliokuwa mle ndani. Yule askari alipofika kule nyuma ya gari akafungua ule mlango na hapo wote tukageuka na kumtazama kwa shauku, na yeye akatutazama kidogo mmoja baada ya mwingine kwa udadisi kabla ya kumuuliza yule dereva.
“Tu transportes les passagés?” Unabeba abiria eh?
“Non!” Hapana!
“Et les gents qui sont ici dereiere?” Na hawa watu huku nyuma ni akina nani?. Yule askari akamuuliza yule dereva kwa hasira huku akitukodolea macho...
...“Non! commandant, nous sommês des frères, nous allons au deil” Hapana! afande, sisi ni ndugu tunaenda msibani. Yule dereva akajitetea huku akilazimisha tabasamu la kirafiki usoni mwake. Yule askari akamtazama yule dereva kwa makini kabla ya kumwambia.
“Donne moi votre permis de conduire” Nipe leseni yako ya udereva. Yule askari akamwambia yule dereva huku akiyahamisha macho yake kututazama tena.
“Comment vous allez?” Habari zenu?. Yule askari akatuuliza na hapo wote tukamwitikia kwa pamoja.
“Nous allons bien!” Nzuri!. Sote tukaitikia na hapo yule askari akachunguza kule nyuma ya gari tulipoketi na hatimaye kufunga mlango huku akiipokea leseni ya udereva ya yule dereva wetu na kuanza kuikagua. Kitambo kifupi cha ukimya kikapita wakati yule askari wa usalama barabarani akiendelea kuikagua leseni ya yule dereva wetu na wakati akifanya vile wale askari wenzake wakawa tayari wamekwisha karibia lile gari letu. Hata hivyo sikupenda yafanyike mahojiano zaidi kwa kukwepa kupoteza muda mwingi eneo lile na kuzuia kuibuliwa kwa mambo mengine yaliyokuwa yamefunikwa.
Hata hivyo hatimaye bahati ikaangukia upande wetu kwani haukupita muda mrefu mara nikamuona yule askari akimrudishia leseni yake yule dereva wetu na hivyo kuturuhusu kuendelea na safari. Dereva wetu akaipokea ile leseni na kushukuru huku akiingia kwenye gari. Wale askari wengine wakawahi kuondoa kile kizuizi cha barabarani kilichokuwa kimeandikwa kwa lugha ya kifaransa POLICE CONTROLE au kwa lugha ya kiingereza POLICE CHECK POINT. Muda ule ule bila ya kupoteza muda dereva wetu akawasha gari na kuingia barabarani huku akijitahidi kwa kila hali kutabasamu mbele ya wale askari wakati akiondoka eneo lile kwa kasi. Angalau moyo wangu ukapata utulivu baada ya kuona tukiondoka eneo lile la kizuizi pasipo rabsha yoyote.
Mwendo wetu ulikuwa siyo wa kubabaisha. Baada ya mwendo mfupi wa safari yetu mbele kidogo tukavuka daraja na tulipoingia upande wa kulia tukaanza kupanda mlima mkubwa. Wakati tukianza kupanda ule mlima nikageuka nyuma na kuwatazama wale askari wa barabarani na hapo nikawaona kuwa wote walikuwa wamesimama katikati ya ile barabara nyuma yetu wakitutazama namna tulivyokuwa tukitokomea mbele yao. Nikaendelea kuwatazama wale askari na kadiri gari letu lilivyokuwa likitokomea ndivyo taswira ya askari wale ilivyokuwa ikitoweka machoni mwangu. Hatimaye tukatokomea kabisa mbele yao katika barabara ile tukikatisha katikati ya msitu mnene wenye giza zito huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha. Hali iliyopelekea barabara ile izidi kutisha wakati ule wa usiku.
Safari ikiwa bado inaendelea kikafuatia kitambo kirefu ukimya mle ndani na hapo nikayatembeza tena macho yangu taratibu kuwatazama wale abiria wenzangu waliokuwa mle ndani. Sikuona tashwishwi yoyote katika nyuso zao na kila mmoja alionekana kushika hamsini zake. Nikageuka kumtazama Amanda na hapo nikamuona kuwa bado alikuwa akitazama kule nyuma tulipotoka. Nilichokiona usoni mwake ilikuwa ni hali ya kupoteza utulivu na kwa namna nyingine nilimuona ni kama aliyekuwa amezama kwenye fikra fulani. Kuanzia pale sikumuona tena Amanda akilala na badala yake mara kwa mara tukawa tukitazamana na hatimaye nyuso zetu kuishia kwenye tabasamu zito la kupimana hisia huku mawazo mengi yakiendelea kupita kichwani mwangu.
Safari ilikuwa ndefu lakini yule dereva wetu alijitahidi kuwa makini huku akiendesha kwa mwendo kasi lakini wenye tahadhari za aina zote. Baada ya kitambo kirefu cha safari yetu wale abiria wengine waliokuwa mle ndani wakawa wamepitiwa na usingizi tena na hivyo kupelekea watu watatu tu mle ndani tuwe macho. Yaani mimi, yule dereva wa lile gari na Amanda hata hivyo hakuna aliyemsemesha mwenzake.
Safari ikaendelea huku tukivuka mabonde na milima, misitu minene na vichaka, madaraja na kona mbalimbali za ile barabara. Njiani tukapishana na wanyama wadogo kama Fisi, Digidigi, Fungo, Nguruwe mwitu, Paka shume,Kicheche,Dondoro na Swala waliokuwa wakivuka barabara kwa mwendo kasi baada ya kushtushwa na makelele ya injini na mwanga wa gari letu. Safari bado ikaendelea huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha. Njiani katika baadhi ya maeneo tukakatisha katikati ya makazi ya watu lakini kwa wakati ule wa usiku nyumba zile zilionekana kama vichuguu yatima kwani wakazi wake wengi walikuwa usingizini kwenye nyumba za Tembe.
_____CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tulikuwa tumemaliza kushuka mteremko mrefu kabla ya dereva yule kukata kona kali kuingia upande wa kushoto na kulikaribia daraja ambalo mara baada ya kulivuka tungeanza kupanda mlima mwingine wakati nilipohisi tena kuwa mwendo wa gari letu ulikuwa ukipungua kwa ghafla. Hisia mbaya zikanijia akilini na hapo haraka nikainua kichwa na kuyapeleka macho yangu kule mbele ya lile gari kutazama. Miale mirefu ya mwanga mkali wa taa za lile gari Land Rover 110 ukafichua vizuri kile kilichokuwa mbele yetu kwenye ile barabara. Kitu ambacho bila shaka kilikuwa kimempelekea yule dereva wetu kupunguza mwendo wa gari kwa ghafla.
Kiasi cha umbali usiopungua mita sitini mbele yetu kulikuwa na mawe makubwa yaliyokuwa yamepangwa barabarani katika namna ya kuzuia gari lolote kupita na kuendelea na safari yake. Nikageuka haraka nikiyatembeza macho yangu kuwatazama abiria wenzangu waliokuwa mle ndani na hapo nikajua kuwa wote walikuwa usingizini isipokuwa mimi, dereva wa lile gari na Amanda ambaye kwa wakati ule na yeye alikuwa makini sana akitazama kule mbele ya gari. Amanda akanikata jicho la haraka la kunitahadharisha huku akirudia kutazama tena kule mbele. Nikiwa nimeupisha utulivu akilini mwangu, mitupo ya mapigo ya moyo wangu yakaongezeka mara dufu huku nywele zikinicheza kwa hadhari.
Nilipomtazama dereva wa lile gari haraka nikagundua kuwa alikuwa ameanza kuchachawa huku damu ikianza kumchemka mwilini kwa hofu. Tukio lile likampelekea yule dereva aanze kupangua gia huku akipunguza mwendo taratibu.
Haraka nikayapeleleza mazingira yale na kugundua kuwa hapakuwa na uwezekano wa kuyakwepa yale mawe kwa kupita kando ya ile barabara. Kwani ile barabara ilikuwa nyembamba na kando yake kulikuwa na miteremko mikali iliyokuwa imemezwa na misitu minene ya mvua. Hivyo kwa mahesabu ya haraka hapakuwa na namna ya kuendelea na safari yetu pasipo kusimama na kuyaondoa yale mawe ya kizuizi cha barabarani. Hisia zangu zikaniambia kuwa mambo hayakuwa shwari tena hivyo nilipaswa kufanya maamuzi ya haraka kabla macho yangu hayajaniletea tafsiri ya taswira mbaya iliyokuwa mbioni kuumbika kichwani mwangu. Mara moja nikayapeleka macho yangu kumtazama Amanda na macho yetu yalipokutana niliweza kuiona hofu iliyokuwa imejengeka usoni mwake na hapo nikamshika mkono wake taratibu huku macho yangu yakimueleza nini tulichopaswa kufanya muda ule. Tukiwa katika hali ile akili yangu ikarudishwa mle ndani baada ya mlio mkali wa risasi kusikika eneo lile.
Sasa nilikuwa na hakika kuwa tulikuwa tukielekea kukabiliana na utekaji na wakati nikitafakari nikawaona watu wawili wakijitokeza mbele yetu kwenye vichaka vilivyokuwa kando ya eneo lile huku mikononi wakiwa wameshika bunduki. Sikuona namna ya kuchomoka na ushindi wa haraka katika mkasa ule hivyo haraka nikafyatua komeo la ule mlango wa nyuma wa lile gari huku tayari nikiwa nimemuonesha ishara fulani Amanda kuwa asishtuke na kupiga kelele kisha nikamshika mkono haraka na kumsukuma nje na mimi nikafuatia. Hata hivyo mimi niliwahi kufika chini mapema zaidi nikitua kwa mgongo wangu ingawa sikuumia kutokana na begi langu nililokuwa nimelivaa vyema mgongoni.
Amanda aliwahi kuniangukia kwa juu na begi lake mgongoni na kweli nilijisikia faraja sana kwa tukio lile la kuangukiwa na mrembo kisha kwa mtindo wa sarakasi wa judo nikaikamata vyema mikono yake na kuibana miguu yake. Halafu nikamvuta na hapo tukawa tukijiviringisha haraka kama gurudumu la gari tukiiacha barabara ile na kupotelea kwenye kichaka kilichokuwa jirani na eneo lile. Kitu kilichonishangaza zaidi ni kuwa Amanda alikuwa mwepesi sana kuufahamu mtindo ule sarakasi wa judo huku akiendana vyema na mijongeo yangu na baada ya muda mfupi tukawa tumepotelea kwenye kichaka kizito kilichokuwa jirani na eneo lile.
Amanda alikuwa ameshtuka sana na kushikwa na hofu kutokana na tukio lile hata hivyo alikuwa makini sana kufuata maelekezo yangu. Muda mfupi uliyofuata tukajibanza kwenye kichaka kile kando ya barabara na hapo nikapata nafasi nzuri ya kutazama kile kilichokuwa kikiendelea kule mbele kwenye lile gari. Dereva wa lile gari letu Land Rover 110 alikuwa amepagawa haraka baada ya kuhisi jambo baya lilikuwa mbioni kutokea kule mbele. Hivyo akaingiza gia na kukanyaga mafuta akiongeza mwendo na kwa kweli sikuweza kutambua haraka dhamira ya tukio lile. Hata hivyo yule dereva hakufika mbali kwani muda ule ule nikasikia mlio mkali wa risasi huku lile gari Land Rover 110 ikiendelea kutimua mbio. Muda mfupi baada ya pale kukafuatiwa na milio miwili mingine ya risasi ambayo haraka nilishtushwa na matokeo ya kazi yake.
Risasi moja ilikuwa imepasua kioo cha mbele cha lile gari Land Rover 110 na kuacha tundu dogo lililozungukwa na nyufa nyingi usawa wa siti ya yule dereva na nilipochunguza kwa haraka nikashikwa na hamaki. Risasi ile ilikuwa imekifumua vibaya kichwa cha yule dereva na kutoboa bodi la lile gari ikiendelea mbele na safari. Ile risasi ya pili ilikuwa imepasua gurudumu la upande wa kushoto wa lile gari na hivyo kulifanya lile gari liende likiyumbayumba barabara nzima kabla ya hatimaye kugota kwenye yale mawe huku injini yake ikiendelea kuunguruma. Amanda akataka kupiga yowe la hofu hata hivyo nikawahi kumzuia kwa kumziba mdomo kwa kiganja changu.
Tukiwa kwenye kile kichaka tumejibanza tukaendelea kutazama kule mbele. Kikapita kitambo kifupi cha ukimya eneo lile na hapo nikaanza kuona watu fulani wakianza kujitokeza kwenye vichaka vilivyokuwa kando ya eneo lile. Nilipowachunguza haraka watu wale nikagundua kuwa idadi yao walikuwa saba na wote walikuwa vijana wa makamo yangu huku wakiwa na bunduki zao mikononi. Niwatazama haraka vijana wale na hapo nikashikwa na hasira kwa namna walivyokuwa wakijitapa na kuangua vicheko vya ushindi.
Wakati wale watekaji wakiendelea kusherehekea ushindi wao ghafla nikamuona mtu mmoja akitoka ndani ya lile gari Land Rover 110 na kuanza kutimua mbio akirudi kule tulipotoka. Hata hivyo yule mtu hakufika mbali kwani kufumba na kufumbua nikasikia mlio wa risasi kisha nikamuona yule mtu akitupwa hewani na kupiga yowe kali ya uchungu. Nilipomchunguza haraka mtu yule nikamkumbuka vizuri kuwa alikuwa miongoni mwa wale vijana wawili tuliokuwa tumekaa nao kule nyuma ya lile gari. Yule kijana alipoanguka chini akatulia kimya huku uhai ukiwa mbali na nafsi yake kwani ile risasi iliyofyatuliwa ilikuwa imepenya upande wa kushoto wa mgongo wake na kuacha tundu kubwa la moyo linalovuja damu.
Baada ya muda mfupi lile gari likawa tayari limezingirwa na wale vijana wenye bunduki mikononi huku wakilipigapiga bodi la lile gari ubavuni kwa mikono yao. Nilipowatazama wale vijana nyusoni mwao nikagundua kuwa hakuna aliyekuwa na hofu ya kumwaga damu ya mtu hata kidogo.
“Mumanuke mwese vubavuba!”. Nikamsikia kijana mmoja miongoni mwao akifoka kwa hasira na kwa kweli sikuweza kufahamu maana ya maneno yale ingawa haraka niliifahamu lugha ile kuwa ilikuwa ni kinyarwanda. Nikakumbuka kuwa nilikuwa nimemdanganya Amanda kuwa mimi ni mnyarwanda niliyekuwa nikiishi jijini Lubumbashi nchini D.R.Congo. Hata hivyo sikutaka maneno yale yanipite hivihivi bila ya kujua maana yake hivyo nikageuka na kumuuliza Amanda.
“Qu'est-ce que it dit?” Anasemaje?. Swali langu likampelekea Amanda ageuke na kunitazama kwa mshangao kisha akaniambia kwa sauti ya kunong’ona iliyojaa hofu.
“Il dit que dessandez vous tous”. Anawaambia kwa lugha ya kinyarwanda wale watu waliomo ndani ya lile gari kuwa.
“Kuwa wote shukeni chini haraka”. Nikamtazama Amanda kwa utulivu huku nikitafakari kisha nikayapeleka tena macho yangu kutazama kwenye lile gari na hapo nikamsikia kijana mmoja miongoni mwa wale vijana akifoka kwa sauti.
“Kandi ntihagire uwibeshya ngo yiruke”. Qu'il n'ause pas personne de dessandre. Amanda akanitafsiria kwa kifaransa akimaanisha.
“Asithubutu mtu yoyote kukimbia”. Mwingine akasikika akiongea kwa ghadhabu baada ya wale watu kwenye lile gari kuanza kushuka chini kwa haraka ya hofu.
“Zana ibyo ufite byose ntugire icyo uhisha”. Enleves toutes chause que vous avez et mattez-les par terre, ne cachez pas. Amanda akaniambia kwa kifaransa akimaanisha.
“Toa kila kitu ulichonacho na uweke chini na usijaribu kuficha kitu”. Yule kijana akaendelea kufoka kwa hasira huku wale abiria wenzetu wakiendelea kushuka kwenye gari kwa hofu.
Kwa kweli nilifadhaishwa na kushikwa sana na hasira juu ya tukio lile huku akili yangu ikiendelea kusumbuka katika namna ya kutaka kupambana na wale watu hatari na kuzima kabisa jaribio lile la kishenzi na la kinyama kuwahi kufanyiwa binadamu. Hata hivyo nafsi yangu ikanionya juu ya mpango wangu wa kuingilia kwani wale watu walikuwa makini sana huku wakijipanga katika mtindo wa kulizunguka lile gari. Wakilipa mgongo na kuelekeza bunduki zao katika pande zote tayari kukabiliana na rabsha yoyote ambayo ingejitokeza. Mwenzao mmoja tu ndiye aliyekuwa akishughulika na wale abiria wenzetu. Na wakati wale abiria wenzetu wakiendelea kushuka yule kijana mtekaji akaendelea kufoka kwa kinyarwanda.
“N'Imana iravuga ngo udakora ntakarye” Amanda akaendelea kunitafsiria kwa kifaransa baada ya kufahamu kuwa nilikuwa sikijui kinyarwanda.
“Même Dieu le déclare, ce lui qui ne travaille pas qu'il ne mange pas”. Hata Mungu anasema asiyefanya kazi na asile. Nilimsikiliza Amanda kwa utulivu na kuyaelewa vizuri maelezo yake kwa lugha ya kifaransa na hapo nikajikuta nikisikitika kwani wale watu hatari walikuwa wakiyatumia maneno ya Mtume Paulo katika kitabu cha Biblia kubariki kitendo chao kile cha kishetani.
Wale abiria wenzetu wakaendelea kushuka huku kila mmoja akijipekua na kutoa vitu vyake vyote mifukoni na kuviweka pale chini barabarani pamoja na mizigo yao iliyokuwa kwenye lile gari. Yule kijana mtekaji hatari akawa akimpekua mtu mmoja baada ya mwingine katika namna kuhakikisha kuwa hakuna aliyeficha kitu huku akiwavua wale abiria viatu na kila aliyemaliza kupekuliwa akawa akisogea mbele na kusimama.
Baada ya muda mfupi hatimaye wale abiria wenzetu wakamaliza kushuka kwenye lile gari na ule upekuzi ukafika kikomo. Yule mzee, abiria mwenzetu bahati mbaya baada ya kupekuliwa akawa amekutwa na pesa nyingi alizokuwa amezificha kwenye nguo yake ya ndani. Mara nikamuona yule kijana hatari akimtazama yule mzee kwa hasira kisha akamzaba makofi mawili ya nguvu...
....yaliyompelekea yule mzee apepesuke lakini hata hivyo hakuanguka na aliposimama vizuri akaambiwa asogee mbele hatua sita. Haraka nilifahamu nini maana ya agizo lile na hapo hasira zikanipanda. Nikataka nitoke pale kichakani na kwenda kuingilia kitendo kile cha kinyama lakini Amanda aliwahi kunizuia akinivuta mguu wangu kwa nguvu zake zote hali iliyopelekea mtikisiko hafifu katika kile kichaka tulichojificha. Tukio lile likampelekea mmoja wa wale watekaji aliyekuwa akitazama ule upande wetu ahisi kitu na kuanza taratibu kusogea eneo lile. Sote tukajibanza na kutulia kimya huku kila mmoja akiusikiliza vyema mwenendo wa mapigo yake ya moyo namna yalivyokuwa yamepoteza utulivu kwenye kichaka kile. Yule mtu hatari akiwa ameielekeza bunduki yake kwenye kile kichaka akaendelea kusogea taratibu pale tulipojibanza lakini hatimaye nikamuona akisita na kusimama huku akitazama pale tulipojibanza kwa makini. Wale wenzake wakawa wamegeuka na kumtazama yule mwenzao kwa shauku lakini kitendo cha yule mtekaji hatari kusita na kugeuza akirudi kule alipotoka kikawapelekea na wale wenzake nao waache kumtazama na kuendelea na hamsini zao.
Nikameza funda kubwa la mate na kumshukuru Mungu kwa kutuepusha na ule mtutu wa bunduki ya yule mtekaji aina ya AK-47 iliyotuama vyema katika mikono yake chakaramu. Nikageuka kumtazama Amanda pembeni yangu na hapo nikamuona ameganda kama sanamu akionekana kutoamini vizuri kile kilichotokea mbele yetu. Muda uleule sote tukashtushwa na milio kadhaa ya risasi na hapo tukageuka na kutazama kule kwenye lile gari.
Risasi nne za yule mtekaji hatari zilikuwa zimeacha matundu yakivuja damu katika sehemu ya tumbo na kifua cha yule mzee aliyetuhumiwa kuficha pesa kwenye nguo yake ya ndani huku pesa zake zikichukuliwa. Yule mzee akapiga yowe dogo la hofu kisha akaanguka pale barabarani na kutulia kimya kifo tayari kikiwa kimemchukua.
Kwa kweli nilisikitika sana na kushikwa na ghadhabu juu ya tukio lile hata hivyo sikuwa na namna ingawa roho iliniuma sana. Wakati hali ile ikiendelea mara nikamuona kijana mmoja miongoni mwa wale watekaji akichepuka na kwenda kuipekua ile maiti ya yule kijana wa kwanza kabisa ambaye aliuwawa wakati alipokuwa akijitahidi kutoroka. Mchezo mzima uliokuwa ukiendelea eneo lile ulikuwa kama mkanda wa video ya kubuni. Hata hivyo lilikuwa ni tukio halisi huku mimi nikiwa miongoni mwa watazamaji.
Wakati lile sakata likiendelea eneo lile mara nilimuona mmoja wa wale watekaji akiingia ndani ya lile gari na kupitisha msako na alipotoka nje akawauliza wale abiria wenzetu waliosalia.
“Mwari muri bangahe hano imbere?”. Vous etaitent à combien ici?. Amanda akanifafanulia kwa kifaransa akimaanisha.
“Mlikuwa wangapi humu ndani?”
“Twari icumi”. Abiria mmoja akajibu kwa woga huku akitetemeka kwa hofu na nilipogeuka kumtazama Amanda akanitafsiria kwa kifaransa juu ya yule abiria alivyojibu.
“On était à dix”. Tulikuwa kumi. Jibu la yule abiria mwenzetu likawapelekea wale watekaji watazamane kwa mshangao kabla ya mmoja wao kuuliza.
“Ko mbona muri amunani babiri barihehe?”. Vous êtes à huit, où sont les deux?. Nilipomtazama Amanda akaniambia akimaanisha kuwa yule kijana mtekaji alikuwa akiwauliza wale abiria kuwa
“Mbona mko nane, waili wako wapi?”. Lile swali likawapelekea wale abiria wenzetu watazamane na kushangaashangaa huku dhahiri wakionekana hawajui kile kilichokuwa kimetokea na hapo nikawa na hakika kuwa hakuna mtu aliyetuona wakati tulipokuwa tukiruka kwenye lile gari mimi na Amanda. Wale watekaji wakatazamana kidogo na sikuona kama walikuwa na muda wa kuendelea kusubiri zaidi kabla ya mmoja wao kufoka kwa hasira.
“Mwese mujye ku murongo”. Vous tous à l ligne. Amanda akaniambia akimaanisha kuwa yule mtekaji alikuwa akiwaambia wale abiria.
“Haya wote pangeni mstari”. Wale abiria walipopanga mstari yule mtekaji akatoa amri nyingine akisema kwa kinyarwanda.
“Nimuririmbe, igishoro cy’umukene ni imbarage ze!”. Chanter, le capitale d’un povre c’est ses forces!. Akimaanisha.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Imbeni, mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe!”
Ilikuwa ni amri ya udhalilishaji na ya fedheha hata hivyo niliwaona wale abiria wenzetu wakianza kuimba kwa hofu na wakati wakifanya vile wale watekaji wakawa wakiangua kicheko cha dhihaka huku baadhi yao wakikusanya vile vitu walivyowapora wale abiria pale chini barabarani na ile mizigo yao. Niliendelea kutazama kilichokuwa kikiendelea eneo lile hata hivyo nafsi yangu haikuniruhusu kuingilia tukio lile kwani sikuwa na silaha yoyote na wale watekaji walionekana kujizatiti kila eneo na bunduki zao mkononi. Wale abiria walipomaliza kuimba yule mtekaji akafoka kwa sauti akiwaambia wale abiria.
“Ntimuzibeshye guca muri uyu muhanda mwijoro ikindi gihe”. N'oser plus de passé cette route pendant la nuit. Amanda akaniambia kwa kifaransa akimaanisha kuwa yule mtekaji alikuwa akiwaambia wale abiria wenzetu kuwa.
“Msithubutu tena kupita barabara hii nyakati za usiku”. Hofu ikanishika wakati nilipoyasikia vizuri maelezo yale kutoka kwa Amanda na wakati nikiendelea kutafakari nafsi yangu ikashtushwa na ule unyama uliokuwa ukifanyika eneo lile.
Wale watekaji wote walikuwa wamewasogelea wale mateka pale walipokuwa wamesimama kisha mwenzao mmoja akawapa ishara ya kichwa ambayo muda mfupi uliofuata nilielewa maana yake. Wale watekaji wakaielekeza mitutu ya bunduki zao kwa wale mateka na hapo nikasikia milio kadhaa ya risasi. Zile risasi zilipokoma wale mateka wote wakawa wameanguka chini wakiugulia majeraha ya zile risasi na baada ya muda mfupi lile eneo lote likamezwa na ukimya wa kifo.
Kwa kweli nilihuzunishwa sana na tukio lile hasa pale nilipowakumbuka wale abiria wenzetu wakati tulipokuwa tukianza safari yetu jioni ile kule stendi ya Nyabugogo jijini Kigali Rwanda siku ile. Amanda akataka kupiga yowe la hofu hata hivyo niliwahi kumziba mdomo baada ya kuhisi hatari ambayo ingetukabili pindi wale watekaji ambapo wangelisikia yowe lile pale kichakani.
Wale watekaji walipomaliza kuutekeleza ule unyama wao haraka wakachukua vile vitu walivyopora na kuanza kukimbia wakilitoroka eneo lile. Sikuwa na namna yoyote ya kufanya badala yake nikajitahidi kumbembeleza Amanda aliyekuwa ameanza kuangua kilio cha kwikwi huku akitetemeka kwa hofu.
Tuliendelea kujibanza kwenye kile kichaka kwa muda usiopungua robo saa tukiendelea kutathmini hali ya usalama wa eneo lile. Nilipojiridhisha kuwa wale watekaji hatari wangekuwa tayari wametokomea msituni sikuona sababu ya kuendelea kujibanza kwenye kile kichaka. Hivyo nikasimama taratibu na kutoka kwenye kile kichaka nikijitokeza kwenye ile barabara. Hata hivyo nilimuonya Amanda na kumtahadharisha kuwa aendelee kujibanza kwenye kile kichaka na kuendelea kuchunguza hali ya usalama wa eneo lile huku nikimtaka anishtue pale ambapo angehisi jambo lolote la hatari.
Nilijitokeza kwenye barabara ile kwa tahadhari na kuanza kutembea taratibu nikielekea kwenye lile gari huku nikiyatembeza macho yangu kutazama huku na kule. Mvua kubwa bado ilikuwa ikiendelea kunyesha na kupitia mvua ile niliweza kusikia kelele za mjongeo wa maji mengi yaliyokuwa yakiendelea kukatisha kwenye lile daraja lililokuwa umbali mfupi nyuma yetu. Muda mfupi uliofuata nikawa nimefika kwenye ile sehemu iliyokuwa na ile miili ya wale abiria wenzetu waliouwawa. Kwa kweli roho iliniuma sana wakati nilipokuwa nikiitazama miili ile. Damu nyingi ilikuwa imesambaa eneo lile. Niliendelea kuwatazama wale watu waliolala pale chini na kwa kweli sikuona dalili ya uhai kwa mtu hata mmoja.
Nikiwa na hakika kuwa macho ya Amanda kule kichakani yalikuwa makini kuzitazama nyendo zangu nikaendelea kutembea hadi nilipolifikia lile gari pale lilipokuwa limegotea kwenye yale mawe. Nilipofika nikaanza kulizunguka lile gari nikilichunguza kwa makini na hapo nikagundua kuwa halikuwa limepata uharibifu mkubwa zaidi ya kioo chake cha mbele kilichokuwa na tundu dogo la risasi na gurudumu moja la mbele la upande wa kushoto lililokuwa limepasuliwa kwa shambulio la risasi za wale watekaji.
Bila kupoteza muda nikaufungua ule mlango wa dereva na kuushusha chini ule mwili wa yule dereva ambao ulikuwa umeharibiwa vibaya kwa shambulio la risasi kichwani. Wakati nikiushusha chini mwili ule nikajikuta nikimkumbuka dereva yule namna alivyokuwa makini kuimudu safari yetu barabarani. Nilipomaliza kuushusha ule mwili nikauburuta na kwenda kuulaza kando ya ile barabara kisha haraka nikarudi kwenye lile gari na kuanza kufanya upekuzi mle ndani.
Ndani ya muda mfupi nikawa nimefanikiwa kupata sanduku dogo jeusi la chuma lenye vifaa vya matengenezo ya dharura ya lile gari juu ya sanduku lile kukiwa na maandishi meupe yanayosomeka vizuri Tools box. Nilipolifungua sanduku lile baada ya pekuapekua ya hapa na pale nikafanikiwa kupata jeki ya gari na spana kadhaa muhimu. Muda mfupi uliofuata nilikuwa mbele nje ya lile gari upande wa kushoto nikitia jeki na kulifungua lile gurudumu lililopasuliwa kwa shambulio la risasi la wale watekaji.
Kazi ya kulifungua lile gurudumu niliifanya kwa wepesi wa hali ya juu na ndani ya muda mfupi tu nikawa nimefanikiwa kulifungua lile gurudumu na kulikokota haraka hadi kule nyuma ya gari ambapo nililipandisha na kulihifadhi mle ndani. Kisha nikalifungua gurudumu la akiba lililokuwa limefungwa nje ya ule mlango wa nyuma wa lile gari. Nilipomaliza nikalikokota haraka lile gurudumu na kwenda kulifunga kule mbele. Hata hivyo nilikuwa makini katika kutathmini mazingira ya eneo lile na kujihami na kitu chochote kibaya ambacho kingekuwa mafichoni kuninyemelea.
Upepo mkali ulikuwa ukivuma sambamba na mvua kubwa iliyokuwa ikiendelea kunyesha eneo lile lenye mabonde na miinuko yenye misitu na giza nene. Ndani ya muda mfupi nikawa nimemaliza kufunga lile gurudumu na nilipochungulia ndani ya lile gari nikauona ufunguo wa lile gari ukiwa mahala pake. Haraka nikaenda mbele ya lile gari na kuanza kuyasogeza yale mawe kando ya barabara. Nilipomaliza na kuridhishwa na kazi yangu nikapiga mruzi mwepesi kumshtua Amanda kule kule kichakani.
Kitambo kifupi cha ukimya kikapita kisha taratibu na kwa tahadhari nikamuona Amanda akijitokeza kwenye kile kichaka yalipokuwa maficho yetu huku mgongoni akiwa na yale mabegi yetu. Nilipomtazama vizuri nikagundua kuwa bado alikuwa amishikwa na woga na wasiwasi mwingi. Nikawahi kumpokea yale mabegi kisha nikafungua mlango wa nyuma wa lile gari Land Rover 110 na kuyatupia ndani. Wakati nikiufunga ule mlango wa nyuma wa lile gari Amanda tayari alikuwa ameshaingia ndani ya gari na kuketi kwenye siti ya abiria iliyokuwa kando ya dereva. Hivyo haraka nikarudi kule mbele ya lile gari ambapo niliufungua mlango wa dereva na kuketi nyuma ya usukani. Kisha nikatumia muda mfupi kufuta mabaki ya damu yaliyotokana na majeraha mabaya yule dereva aliyeuwawa kwa shambulio la risasi nikitumia kitambaa kidogo kilichokuwa nyuma ya ile siti ya dereva.
Ndani ya muda mfupi tu nikawa nimemaliza zoezi lile na kukitupa nje kile kitambaa. Nilipoyapeleka macho yangu kumtazama Amanda nikagundua kuwa alikuwa ameacha kulia ingawa bado alionekana kuwa ni mtu mwenye woga na wasiwasi mwingi kama ambaye bado haamini kile kilichokuwa kimetokea eneo lile muda mfupi uliopita. Macho yetu yalipokutana Amanda akajitahidi kuumba tabasamu hafifu usoni mwake hata hivyo hakufanikiwa kwani badala yake alionekana ni kama mtu anayetaka kulia na kucheka kwa wakati mmoja. Hata hivyo nikaumba tabasamu hafifu la matumaini usoni mwangu huku nikimuuliza.
“Comment, tu es bien”. Vipi upo sawa?.
“N'aye pas doute”. Ondoa shaka. Amanda akaongea kwa utulivu akiniambia. Sikupenda tuendelee kukaa eneo lile hivyo haraka nikafunga ule mlango wa dereva na kuvaa mkanda wa siti. Muda mfupi uliofuata nikawasha gari na kuondoka kwa kasi eneo lile huku mawazo mengi yakipita kichwani mwangu wakati nilipoanza kuwakumbuka wale abiria wenzetu waliouwawa ambao tulikuwa nao pamoja kwenye lile gari muda mfupi uliopita. Kwa kweli nilishikwa na huzuni isiyoelezeka kuwa nikishindwa kujilaumu au kujipongeza kwa kutokuingilia kati udhalimu ule na kuyaokoa maisha yao. Wakati nikiendelea kufikiri zaidi sikuona kama nilipaswa kulaumiwa pale nilipokumbuka kuwa sikuwa na silaha yoyote ya kujitetea wakati tukio lile la mauaji ya wale abiria wenzetu lilipokuwa likitokea. Vilevile wale watu hatari watekaji walionekana kuwa makini sana kwa kutoruhusu tukio lolote ambalo lingepelekea kuvurugika kwa mipango yao. Kisha nikamkumbuka Amanda na kuwaza kuwa hata yeye alikuwa kikwazo wakati nilipotaka kuingilia unyama ule huku nikiwaza kuwa huwenda hata yeye aliiona hatari ambayo ingetukabili sote endapo ningejitia kuingilia kati.
Mshale wa mafuta katika dashibodi ya lile gari Land Rover 110 ulionesha kuwa bado kulikuwa na mafuta ya kutosha kwenye lile gari ingawa sikuwa na hakika kama mafuta yale yangeweza kutufikisha hadi mwisho wa safari yetu. Kwani sikuwa nikiufahamu vizuri umbali uliokuwa umesalia mbele yetu. Wakati nikiingiza gia na kukanyaga mafuta nikageuka na kumuuliza Amanda kwa utulivu.
“Est-ce qu'il y a un tragé d'ici jusqu' au frontiere de Rwanda et Burundi?. Kuna umbali mrefu kutoka hapa hadi ulipo mpaka wa nchi ya Rwanda na Burundi?. Swali langu likapelekea kitambo kifupi cha ukimya mle ndani huku Amanda akionekana kufikiria jambo fulani kisha akaongea kwa utulivu.
“Pas moin de trois heures de voyage”. Siyo chini ya safari ya masaa matatu kutoka hapa tulipo. Jibu la Amanda likanipelekea nigeuke na kumkata jicho kidogo kabla ya kugeuka na kutazama mbele huku nikimwambia.
“Ne t'en fait mon amour, maintenant nous sommês bien”. Ondoa shaka mpenzi sasa tupo salama. Amanda akageuka na kunitazama, safari hii uso wake ukionekana kujawa na furaha ya tumaini kama mtu aliyepewa ahadi ya uhai wa milele.
Mwendo wangu wa kuendesha gari ulikuwa wa uhakika huku nikishuka mabonde na kupanda milima katika baadhi ya maeneo na kukatisha kwenye sehemu zenye misitu mizito iliyojitenga mbali na makazi ya watu. Kuna wakati barabara ile ilikatisha katika miji midogo ya nchi ya Rwanda yenye nyumba duni za udongo hata hivyo hatukusimama. Wakati wote tukiendelea na safari Amanda alikuwa kimya ingawa usingizi ulionekana dhahiri kuwa mbali naye huku...
...akionekana kusumbuliwa na kumbukumbu ya yale matukio ya nyuma. Kila nilipokuwa nikiona kuwa ukimya ulikuwa ukizidi kushika hatamu mle ndani ya gari nilimchangamsha Amanda kwa maswali machache na utani wa hapa na pale nikijitahidi kumsahaulisha kwa muda yale yote yaliyotokea nyuma yetu. Hata hivyo sina hakika sana kama nilifanikiwa kwa kiwango nilichokitaka.
“Je te remerci Jean de m'avoir sauve´”. Nashukuru sana kwa kuyaokoa maisha yangu Jean. Amanda akaniambia kwa utulivu huku akitabasamu na hapo nikageuka tena na kumtazama huku nikiangua tabasamu hafifu.
“Si c'est ne pas Dieu, à ce coment on serait de morts”. Kama siyo Mungu huwenda muda huu tungekuwa wafu. Nikaongea kwa utulivu na hapo Amanda hakutia neno badala yake akatikisa kichwa chake kidogo akionesha kukubaliana na hoja yangu na kisha kikafuata kitambo kidogo cha ukimya huku Amanda akionekana kama anaewaza jambo fulani. Hatimaye akavunja tena ukimya na kuniuliza.
“J'ai pensé que tu parles le kinyarwanda?”. Nilidhani kuwa unafahamu kuzungumza kinyarwanda?.
“Non!, mois c'est une Rwandaise mais, me parents sont partis à Lubumbashi au Congo et j'etais encore très joune. C'est pour ce la que je n'ai pas eu la chance d'apprendre le kinyarwanda”. Hapana!, mimi ni mnyarwanda lakini wazazi wangu walihamia Lubumbushi nchini Congo mimi nikiwa bado mdogo sana. Hivyo sikupata nafasi ya kujifunza kinyarwanda. Nilijitahidi kudanganya hata hivyo Amanda hakuzungumza neno lolote badala yake alikaa kimya akiupisha utulivu huku akitazama nje kupitia dirishani na nilipomtazama nikajua kuwa alikuwa amezama tena kwenye tafakuri.
Swali la Amanda kwa namna moja au nyingine lilikuwa limeamsha hisia zangu na kuyaruhusu mawazo mengi kuanza kupitia kichwani. Kwani kwa namna moja au nyingine nilianza kuhisi kuwa Amanda alikuwa ameanza kushikwa na wasiwasi juu ya nyendo zangu. Hata hivyo nilifahamu kuwa sikupaswa kumlaumu juu ya mashaka yake dhidi yangu.
Mvua kubwa ilikuwa ikiendelea kunyesha katika barabara ile iliyokuwa ikikatisha katika eneo kubwa lenye misitu minene. Mvua ile sasa ilikuwa ikikokota takataka nyingi za msituni kutoka milimani. Takataka hizo zikikatisha barabarani na kuporomokea mabondeni hali iliyopelekea nipunguze mwendo na kuongeza katika nyakati tofauti ili kujihami na ajali. Hata hivyo mwendo wangu bado ulikuwa wa kasi mno lakini makini kwelikweli.
_____CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Saa yangu ya mkononi ilionesha kuwa nilikuwa nimeendesha gari kwa muda wa saa moja na robo tangu tulipoanza safari ile na Amanda baada ya lile tukio la utekaji na mauaji ya kule msituni kufanyika.
Wakati nilipoyapeleka macho yangu kutazama kwenye dashibodi ya gari nikashtuka kuona taa ndogo ya njano ikiwaka na mshale wa mafuta ukienda kombo na hapo nikajua kuwa mafuta kwenye lile gari yalikuwa yakielekea kuisha. Hali ile ikanitia hofu kwani kwa mujibu wa maelezo ya Amanda ni kuwa tulikuwa tumebakiwa na umbali mrefu kabla ya kuufikia mpaka wa nchi ya Rwanda na Burundi.
Bila shaka Amanda alikuwa ameshtushwa na hali ya mashaka iliyokuwa usoni mwangu baada ya kutazama mwenendo wa mafuta kwenye dashibodi ya lile gari. Hivyo haraka akageuka kunitazama kabla ya kuniuliza kwa shahuku.
“Est-ce qu'il y a un problèm?”. Kuna shida yoyote?.
“Le carburant va ceterminer d'ici là, est-ce qu'il y a une station aux environs?”. Mafuta yanaelekea kuisha, kuna kituo chochote cha kujazia mafuta karibu na hapa?. Nikamuuliza Amanda huku nikilipuuza lile swali lake na hapo Amanda akatulia kidogo kama anayejaribu kukumbuka. Kisha akayapeleka macho yake kutazama nje kupitia dirishani na hapo nikajua kuwa alikuwa akijaribu kuyakumbuka mazingira yale. Alipogeuka kunitazama akaniambia.
“Il ya l'une devant nous, mais c'est plus de deux kilometre d'ici où sommes. Est-ce que le carburant est terminé?”. Kipo kituo kimoja mbele yetu lakini ni zaidi ya mwendo wa kilometa mbili kutoka hapa tulipo. Vipi mafuta yameisha?. Amanda akaniuliza kwa wasiwasi.
“Ça cedirige vers la fin, et on risque de ne pas continuer avec le voyage”. Yanaelekea kuisha na huwenda tukashindwa kuendelea na safari. Nikaongea kwa utulivu huku nikijitahidi kuudhibiti vizuri usukani wa lile gari kwenye kipande kile korofi cha barabara.
“Dieu aide nous”. Mungu tusaidie. Nikamsikia Amanda akiongea katika namna ya kukata tama hata hivyo mimi sikutia neno lolote.
Mara baada ya kukivuka kipande kile kifupi korofi cha barabara mbele kidogo tukaanza kupanda mlima na wakati tukipanda ule mlima nikatembeza macho yangu kutazama huku na kule. Tulikuwa tukiyakaribia makazi ya watu na kitendo cha kuanza kuona makazi yale ya watu kikafufua matumaini nafsini mwangu huku nikiwaza kuwa huwenda tulikuwa tukikikaribia pia kituo cha kujazia mafuta. Nikajikuta nikifarijika baada ya kuwaza kuwa hata kama ingetokea kuwa tumekosa mafuta eneo lile lakini kitendo tu cha kuyafikia makazi ya watu ilikuwa ni usalama tosha kwetu.
Mara tu tulipomaliza kuupanda ule mlima tukaanza kushuka mteremko mrefu mbele yetu na wakati tukishuka nikaanza kuuona mji mdogo wenye nyumba nyingi. Nyumba hizo baadhi zikiwa ni za kisasa na nyingine kuukuu za vijijini. Nikamuuliza Amanda kama alikuwa akilifahamu jina la mji ule na hapo akaniambia kuwa jina ule mji lilikuwa limemtoka kidogo. Tuliendelea kushuka kwa kasi na uchunguzi wangu ukaniletea majibu kuwa ule mji haukuwa na umeme. Baadhi ya wakazi wake walikuwa wakitumia majenereta na wengine paneli za sistimu za umeme wa jua. Ulikuwa ni mji mkubwa kiasi lakini kwa wakati ule wa usiku wa manane sikumuona hata mtu mmoja akirandaranda barabarani.
Tulipomaliza kushuka ule mteremko tukaanza kukatisha katikati ya makazi ya watu barabara ile ilipokuwa ikipita na kando ya barabara ile nikaona maduka, baa, mashine za kusaga na zahanati. Lakini kwa wakati ule vyote vilikuwa vimefungwa.
Tuliendelea kukatisha katikati ya yale makazi ya watu wa mji ule mdogo kisha tukaingia upande wa kulia tukiifuata ile barabara na kwa kufanya vile tukajikuta taratibu tukianza kuuacha ule mji mdogo nyuma yetu. Sasa macho yangu yakawa makini kutazama huku na kule nikitarajia kuona kituo cha kujazia mafuta kando ya barabara ile. Sikuona kituo chochote cha kujazia mafuta na tulikuwa tukizidi kuuacha ule mji mdogo nyuma yetu na hali ile ikanipa mashaka hata hivyo sikusimama.
Nilipokuwa mbioni kutaka kumuuliza Amanda juu ya kituo kile cha kujazia mafuta ambacho hapo awali alinihakikishia kukifahamu mara ghafla nikakiona kituo kimoja cha kujazia mafuta upande wa kulia mara baada ya kuvuka daraja lenye mto uliyopakana na mianzi mingi kando yake.
Sasa sikuwa na mashaka kuwa kituo kile cha kujazia mafuta ndiyo kile kilichokuwa kimezungumziwa na Amanda hapo awali wakati nilipomuuliza. Muda mfupi uliyofuata nikachepuka upande wa kulia na kwenda kuegesha gari kwenye upande wenye pampu ya kujazia mafuta ya petroli chini ya paa kubwa la kituo kile cha kujazia mafuta.
Kulikuwa na maroli mawili ya mafuta yaliyokuwa yameegeshwa kando ya kituo kile na zaidi ya pale hapakuwa na gari lolote jingine eneo lile. Mara tu tuliposimama kutoka kwenye ofisi ya kituo kile cha kujazia mafuta kilichokuwa kando ya eneo lile ambacho kilikuwa kikiwaka taa. Mlango wa ofisi ile ukafunguliwa kisha akatoka mwanaume mmoja mrefu ambaye sikuwa na mashaka kuwa alikuwa mfanyakazi wa kituo kile huku akiwa amejifunika kwa mwamvuli na mkononi ameshika kurunzi. Wakati yule mtu akija pale tuliposimama nikamuona mtu mwingine akisogea taratibu eneo lile na nilipomchunguza haraka nikagundua alikuwa ni mlinzi wa pale kutokana na mavazi yake na bunduki aliyoishika mkononi.
Bila kupoteza muda nikalichukuwa begi langu na nilipolifungua nikachukua kiasi cha fedha kisha nikafungua mlango na kushuka nikielekea nyuma kwenye tenki ya mafuta ya lile gari. Nilipofika nikauondoa mfuniko wa lile tenki haraka na wakati huo tayari yule mfanyakazi wa kile kituo cha mafuta alikuwa tayari amekwishafika eneo lile. Hivyo tuliposalimiana nikamwambia ajaze mafuta kwenye lile tenki huku wote tukiwa tumejikinga mvua na ule mwamvuli. Zoezi lile likafanyika kwa muda mfupi tu na mafuta yalipojaa nikamlipa yule mfanyakazi wa kile kituo cha kujazia mafuta kiasi cha pesa nilichopaswa kulipa kisha nikachepuka kidogo kwenda kwenye choo cha kile kituo kushusha haja ndogo. Muda mfupi baadaye nikarudi na kuingia kwenye gari na hapo safari yetu ikaanza tena tukiondoka eneo lile na kuingia barabarani.
Wakati tukianza safari ile nikakumbuka kuliweka vizuri lile begi langu na nilipokuwa nikifanya vile nikashtukia kuwa hali ya lile begi ilikuwa tofauti na vile nilivyokuwa nimeliacha baada ya kutoa zile fedha za kujazia mafuta. Kwa uchunguzi wa haraka nikajua kuwa lile begi lilikuwa limefanyiwa upekuzi wa hila na usio na umakini kiasi cha kunifanya nigutuke haraka. Kwa kweli moyo wangu ulipoteza kabisa utulivu ingawa kamwe sikuruhusu hali ile ionekane usoni mwangu.
Hapakuwa na mtu mwingine niliyekuwa nimemuacha mle ndani isipokuwa Amanda. Kwa kweli nilihisi hali ya baridi nyepesi ikiutafuna mtima wangu hasa pale nilipokumbuka swali la Amanda kuwa kwanini mimi nilikuwa sifahamu kuzungumza kinyarwanda wakati hapo awali nilikuwa nimejinadi kwake kuwa mimi ni mnyarwanda. Amanda alikuwa amelipekuwa begi langu kwa siri kutafuta nini?. Nikajiuliza kichwani hata hivyo nikapiga moyo konde na kujipa uvumilivu ingawaje kwa namna fulani nikaanza kujionya juu ya kuwa makini na mtu niliyekuwa nikiongozana naye kwenye ile safari. Nikiwa katika hali ile mara Amanda akaniuliza kwa utulivu huku akitazama mbele.
“Tu restes à Bujumbura jusqu' à quand?”. Utakaa kwa muda gani Bujumbura?.
“Après avoir vu mon grand frère je n'aller pas tarder, je veux rentrer à Lubumbashi au Congo”. Mara baada ya kuonana na kaka yangu sitakaa sana nitarudi nyumbani Lubumbashi nchini Congo. Nikamwambia Amanda wakati nilipokuwa nikiingiza gia na kukanyaga mafuta na kuzidi kutokomea mbali na ule mji mdogo.
“Et comment si tu ne parviens pas à seracontrer avec votre grand frère?”. Na vipi usipofanikiwa kuonana na huyo kaka yako?. Amanda akaniuliza kwa udadisi.
“Il faudra que je rentre à la maison très tôt”. Itabidi nirudi nyumbani mapema. Nikamwambia Amanda huku nikijitahidi kuumba tabasamu hafifu usoni mwangu kasha baada ya hapo kikafuatia kitambo kifupi cha ukimya na nilipomtazama Amanda nikajua kuwa bado alikuwa kwenye mawazo.
Nilipoitazama saa yangu ya mkononi nikagundua kuwa ilikuwa ikielekea kutimia saa saba usiku. Mvua bado ilikuwa ikiendelea kunyesha katika barabara ile iliyokuwa ikikatisha msituni kwenye mabonde na milima. Ukimya wa usiku ule ukatupelekea tusikie vizuri ile sauti ya makelele ya ile injini ya gari wakati nilipokuwa nikiingiza gia na kukanyaga mafuta katika nyakati tofauti.
Sasa tulikuwa mbali kabisa na ule mji mdogo nyuma yetu huku angalau tukiwa na hakika na safari ile. Amanda alikuwa msichana mrembo sana ambaye mwanaume yeyote angejisikia fahari sana walau kubadilishana naye mawazo. Hivyo kitendo kile cha kusafiri peke yetu kwenye lile gari kilikuwa kimeamsha hisia za furaha kubwa moyoni mwangu kwa kuambatana na mrembo yule kando yangu. Nikiwa katika mawazo yale mara Amanda akazirudisha fikra zangu mle ndani kwa kuniuliza.
“Tu as la femme et des enfants?”. Una mke na watoto?. Swali lile likanipelekea nitabasamu kidogo huku nikigeuka kumtazama Amanda.
“Je ne suis pas encore marié, et je n'ai pas une fiancée”. Bado sijaoa na wala sina mchumba. Nikaongea kwa utulivu huku nikishindwa kuelewa uelekeo wa maongezi yale ingawa kwa namna moja au nyingine yalielekea kunifurahisha. Kitambo kifupi cha ukimya kikapita kisha nikageuka na kumuuliza Amanda.
“Et toi, tu es mariée?”. Na wewe vipi umeolewa?. Swali langu likampelekea Amanda atabasamu kidogo huku akiviminyaminya vidole vya mikono yake kama mtoto anayedeka kisha akaniambia huku akigeuka na kunitazama. Lile tabasamu lake maridhawa likikataa kwenda likizo usoni mwake.
“Je ne suis pas encore mariée mais j'ai un fiancé”. Sijaolewa ila nina mchumba. Amanda akaniambia kwa utulivu huku akijitahidi kusahau yaliyopita.
“Où est votre fiancé?”. Mchumba wako yuko wapi?. Nikamuuliza.
“Il est en Amerique pour les études”. Yupo masomoni nchini Marekani. Amanda akaniambia kwa kujisifu akijitahidi kunionesha ni kwa namna gani alikuwa na bahati ya uhakika wa maisha mazuri kwa kuolewa na mwanaume msomi ingawa nilimtazama kidogo na kumhurumia wakati nilipowaza kuwa atakuwa katika hali gani pale ambapo huyo mwanaume anayemtarajia aolewe naye abadili mawazo ghafla na kumuoa msichana mwingine.
“Très bien, s'ans doute vous aller vous mariés très tôt quand il rentrel!”. Vizuri sana, bila shaka mtafunga ndoa yenu mapema sana jamaa atakaporudi. Nikamwambia Amanda huku moyoni nikijihisi wivu kwa kutokuwa na nafasi yoyote katika moyo wa mlimbwende yule wa ajabu.
“Oui, si Dieu le veut”. Ndiyo, Mungu akipenda. Huku akionesha furaha usoni na kujiona kuwa ni msichana mwenye bahati Amanda akaniambia kwa ujivuni.
“Il s'appelle comment?”. Anaitwa nani?. Nikamuuliza Amanda huku wivu ukinisimanga moyoni.
“Jean-marie”. Amanda akaniambia kwa kujiamini na kwa kweli jibu lake likapandisha wivu mkubwa moyoni mwangu hali iliyonipelekea nimeze funda kubwa la mate kuupoza mtima wangu. Nikabaki nikimuonea wivu Jean-marie kwa kuopoa malkia wa nguvu kiasi kile.
Kwa kweli niliumudu vyema usukani wa gari na mwendo wangu ulikuwa siyo wa kubabaisha nikipanda milima na kushuka mabonde kama upepo huku akili yangu ikijikita katika kuwaza hali ya mambo itakavyokuwa baada ya kufika jijini Bujumbura nchini Burundi. Nikiwa katika mawazo yale mara Amanda akaniuliza tena...
Kwa kweli niliumudu vyema usukani wa gari na mwendo wangu ulikuwa siyo wa kubabaisha nikipanda milima na kushuka mabonde kama upepo huku akili yangu ikijikita katika kuwaza hali ya mambo itakavyokuwa baada ya kufika jijini Bujumbura nchini Burundi. Nikiwa katika mawazo yale mara Amanda akaniuliza tena.
“Il ya une chose que je doute avec”. Kuna kitu bado nina wasiwasi nacho. Amanda akaongea kwa utulivu na hapo nikageuka na kumtazama kwa shauku huku nikishtushwa na maongezi yale.
“La quelle?. Kitu gani?. Nikamuuliza Amanda huku nikimkata jicho hata hivyo Amanda aliendelea kutabasamu kisha akaniuliza.
“Un beau homme comme toi, tu n'as pas une femme ni une fiancée?”. Mwanaume mzuri kama wewe kusema kuwa hujaoa na huna mchumba?. Swali la Amanda likanipelekea nitabasamu kidogo na kuongea.
“Crois moi, mais aussi c'est le temps de chercher mon partenaire”. Niamini, lakini hata hivyo nadhani muda wa kutafuta mwenza wangu pia umefika. Niliangua kicheko hafifu huku nikiendelea kukanyaga mafuta na kutokomea kwenye barabara ile na kwa kweli akili yangu haikuwepo kabisa katika masuala ya mapenzi kama Amanda alivyokuwa akidhani. Badala yake akili yangu ilikuwa imejikita katika kuwaza namna ya kuanza harakati zangu mara baada ya kufika jijini Bujumbura.
_____
Tulikuwa tumetembea umbali usiopungua kilometa hamsini na ushei katika barabara ile iliyopakana na misitu mizito, tukivuka madaraja, kupanda milima na kushuka mabonde katikati ya giza nene na mvua kubwa ya masika isiyokuwa na kikomo pale Amanda alipoamua kuvunja ukimya ulioanza kuota mizizi mle ndani ya gari.
“Diminuer la vitesse!”. Punguza mwendo!. Ghafla Amanda akaniambia huku akionesha hakika kuwa nilikuwa sijakiona kile alichokuwa amekiona katika barabara ile mbele yetu.
“Qu' est-ce qu'il ya?. Kuna nini?. Nikamuuliza Amanda huku nikipangua gia za gari lile kwa fujo kama niliyeshikwa na wazimu. Kitendo ambacho hata mimi mwenyewe sikupenda.
“Au côté gaushe là devant, il y a une voiture en panne”. Pale mbele kuna gari limeharibika. Amanda akaniambia kwa taharuki huku akinionesha kwa kidole chake mbele ya ile barabara upande wa kushoto. Nikaendelea kupangua gia na kupunguza mwendo kwa pupa huku macho yangu yakijitahidi kufuata uelekeo wa kile kidole cha Amanda. Nilipoyatuliza vizuri macho yangu nikaliona gari jeupe aina ya Landcruiser hardtop likiwa limeegeshwa barabarani huku nyuma yake kukiwa na matawi kadhaa ya miti yaliyokatwa na kulazwa barabarani kama alama ya kutambulisha kuwa gari lile lilikuwa limeharibika.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Niliendelea kupangua gia na kupunguza mwendo huku macho yangu yakilitazama lile gari kwa udadisi. Gurudumu moja la nyuma la lile gari lilikuwa limefunguliwa na kulazwa chini huku sehemu yake ikiwa imenyanyuliwa na kuwekwa juu ya kipande cha gogo. Chini kwenye uvungu wa lile gari niliiona miguu ya mtu fulani aliyelala ikiwa nusu imetokeza nje na kunipelekea niamini kuwa gari lile lilikuwa likifanyiwa matengenezo. Nikaendelea kupunguza mwendo huku nikiendelea kulitazama lile gari na nilipotazama juu yake kwenye carrier nikagundua kuwa lile gari lilikuwa limebeba shehena kubwa ya mzigo uliokuwa umefunikwa vizuri kwa turubai.
Nilipoendelea kupunguza mwendo na kuzidi kulikaribia lile gari nikagundua kuwa ndani ya lile gari kulikuwa na watu ingawa jinsia na idadi yao ilikuwa ni vigumu kuifahamu haraka kutokana na giza lililokuwa mle ndani. Haraka nikayapeleka macho yangu pembeni kumtazama Amanda na hapo nikagundua kuwa alikuwa amesogea karibu zaidi na kioo cha mbele cha ile gari kutazama kule mbele. Amanda hakusema neno lolote ingawa nilikuwa na kila hakika kuwa alikuwa akifahamu kuwa nilikuwa nikimtazama. Haraka nikawaona wanaume wawili wakija nyuma ya ile gari na kutupungia mikono katika namna ya kututaka tusimame ili watuombe msaada.
“Arrête toi, je pense qu'il ont besoin d'aide”. Simama, nahisi wanahitaji msaada. Amanda akaniambia kwa msisitizo katika namna ya kunihimiza nisimame. Wale watu wakaendelea kutupungia mkono kwa bidii huku mmoja akitumia shati lake alilolivua haraka baada ya kuhisi huwenda hatukuwaona.
“Arrête toi!”. Simama!. Amanda akaendelea kunisihi. Kwa kweli nilijikuta katika wakati mgumu wa kuamua nisimame au niendelee na safari kwani kumbukumbu ya lile tukio la utekaji lililokuwa limetokea masaa machache yaliyopita kule nyuma yetu tulipotoka ilikuwa bado haijatoweka katika fikra zangu.
Hatimaye nafsi yangu ikaingiwa na hali ya utu hivyo nikazidi kuminya breki na kupunguza mwendo zaidi nikitafuta sehemu ya maegesho hatua chache baada ya kulipita lile gari bovu. Lakini wakati nikiwa katika harakati zile mara ghafla nikawaona wanaume wengine wawili mbali na wale wa awali waliokuwa wakitusimamisha wakichomoza gizani kutoka upande wa kushoto wa lile gari na kuanza kukimbia taratibu wakija pale tuliposimama. Tukio lile likaupelekea moyo wangu ushtuke na kupoteza utulivu kabisa huku nafsi yangu ikianza kunisimanga katika namna ya kunilaumu kuwa huwenda nilikuwa nikifanya maamuzi yasiyokuwa sahihi kwa kusimama eneo lile.
Wale watu waliokuwa wakikimbia kutufuata walikuwa wamesaliwa na hatua chache kutufikia pale tulipoegesha gari wakati nafsi yangu iliposukumwa kufanya maamuzi magumu. Sikuruhusu aina yoyote ya mjadala mwingine kuzitongoza fikra zangu hivyo haraka nikaingiza gia na kukanyaga mafuta nikiliingiza lile gari barabarani. Mshangao uliomvaa Amanda haukutofautiana sana na ule uliowapata wale watu nyuma yetu wakati nilipowatazama kupitia kioo cha ubavuni cha lile gari Land Rover 110. Wale watu kuona vile wakasimama ghafla na kuweka mikono yao vichwani katika namna ya kukata tamaa kama wachezaji wa mpira wa miguu waliokosa penati ya mwisho katika mchezo fainali. Amanda akageuka na kunikata jicho la mshangao lenye hasira iliyotokana na kupuuzwa kwa hoja yake.
“On ne peut pas s'arrêter, ce milien ne pas bon”. Hatuwezi kusimama kwani hii sehemu siyo salama. Nikaongea kwa msisitizo huku nikionekana kupuuza waziwazi ombi lile kwani hisia zangu zilikuwa zimenitanabaisha waziwazi kuwa kusimama pale ilikuwa ni sawa na kuhatarisha usalama wetu.
Amanda akaendelea kunitazama kwa hasira kana kwamba nilikuwa nimefanya dhambi kubwa iliyomshangaza hata shetani mwenyewe. Hata hivyo sikutaka kabisa kukubaliana na hisia zake na vilevile sikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakiamini mawazo ya mtu mwingine hususani katika mazingira hatarishi kama yale.
Kupitia vioo vya ubavuni vya lile gari Land Rover 110 niliendelea kuwatazama wale watu nyuma yetu huku wakiwa wamesimama katikati ya barabara na kuendelea kulitazama gari letu namna lilivyokuwa likitokomea mbele yao bila matumaini ya kusimama. Hatimaye Amanda alipoona kuwa simsemeshi akaamua kuegemea vizuri siti yake huku akigeuka na kutazama dirishani dhahiri akionekana kununa na hali ile ikawa afadhali kubwa kwangu.
Mvua ilikuwa ikiendelea kunyesha na sauti pekee iliyokuwa ikisikika katika misitu ile ilikuwa ni ile sauti ya muungurumo wa injini ya lile gari letu wakati tukipanda milima na kushuka mabonde.
_____
“Il y a la voiture qui vient derière nous”. Kuna gari linakuja nyuma yetu. Sauti hafifu ya Amanda ikazirudisha fikra zangu mle ndani ya gari baada ya kitambo kirefu cha ukimya na hapo nikageuka haraka na kumtazama Amanda kama ambaye sikuwa nimemsikia vizuri maelezo yake.
“Qu'est qu'il y a?”. Kuna nini?. Nikamuuliza Amanda kwa shauku huku nikigeuka kidogo na kumtazama kabla ya kuyarudisha macho yangu kutazama tena mbele ya gari.
“Régarder les paraprises de côtés”. Tazama kwenye vioo vya gari ubavuni. Amanda akaniambia kwa hamaki na hapo haraka nikayapeleka macho yangu kutazama kwenye vioo vya ubavuni vya lile gari. Macho yangu yalipotulia vizuri mara nikauona mwanga mkali wa taa za mbele za gari lililokuwa likija kwa kasi nyuma yetu.
“La voiture…?”. Gari…?. Nikajiuliza kwa mshangao wakati jibu ninalo.
“C'est la voiture qu'on a passé qui été en panne”. Ni lile gari lililoharibika tulilolipita kule njiani. Amanda akaniambia huku akiendelea kutazama kwenye kioo cha ubavuni cha gari kilichokuwa upande wake.
“Cette fois-ci cette voiture est dépannée?”. Mara hii tu lile gari litakuwa limepona?. Nikamuuliza Amanda kwa wasiwasi huku nikiendelea kutazama kwenye kioo cha ubavuni cha lile gari letu.
“Même moi aussi je suis étoné, et elle vient très rapide”. Hata mimi nashangaa na linakuja kwa kasi sana. Amanda akaniambia huku dhahiri akionekana kuanza kuingiwa na hofu.
Niliendelea kulitazama lile gari namna lilivyokuwa likija kwa kasi na kutukaribia nyuma yetu huku akili yangu ikianza kutafakari juu ya tukio lile lisiloeleweka akilini mwangu. Baada ya muda mfupi lile gari hatimaye likawa limetufikia na nilipolichunguza vizuri nikapata hakika kuwa lilikuwa ni lile gari tulilolipita kule nyuma njiani. Ingawa sikuwa nimefahamu tatizo la lile gari lakini hata hivyo haikuniingia akilini kuwa ndani ya muda mfupi tu kiasi kile lile gari lingekuwa tayari limepona na kuendelea na safari yake. Hivyo tukio lile lilinipa wasiwasi mwingi.
Nikiwa naendelea kutafakari mara lile gari likaanza kutupita kwa kasi ya ajabu. Tukio lile likanipelekea nipunguze mwendo wa gari letu nikilipisha lile gari litupite kwa uhuru na kuendelea na safari yake. Hata hivyo hilo halikutokea kwani mara baada ya lile gari kutupita ghafla nikaliona likipunguza mwendo na kwenda kutuzuia kwa mbele. Kwa kweli nilishikwa na hofu na taharuki isiyoelezeka nikijitahidi kwa kila namna kulikwepa lile gari lakini ufundi wangu katika udereva iligonga mwamba. Kwani bila ya kupenda nilijikuta nikiligonga lile gari kwa nyuma na hapo sauti ya kishindo kikubwa ikasikika huku vioo na taa za nyuma za lile gari mbele yetu vikipasuliwa vibaya na ngao ngumu ya lile gari letu Land Rover 110 .Ilikuwa ajali mbaya lakini ya makusudi.
Amanda akapiga yowe la hofu hata hivyo ule haukuwa muda wa kushauriana baada ya kuhisi nini ambacho kingefuatia baada ya pale. Hivyo haraka nikajisogeza karibu na ule mlango wa kando ya Amanda kisha nikavuta kabali ya ule mlango kwa juu na kuufungua kwa teke moja la nguvu. Ule mlango ulipofunguka nikamfanyia Amanda ishara ya kichwa kuwa ashuke haraka na akimbie akajifiche kwenye msitu mkubwa uliokuwa kando ya ile barabara. Amanda akashikwa na hofu na nilipomuona hanielewi nikamwambia.
“Va te casher à la foret et toute chase qui va arriver n'oser pas de sometrer”. Nenda kajifiche msituni na chochote kitakachotokea usithubutu kujitokeza. Nilimwambia Amanda huku nikimsisitiza hata hivyo sikumuona akionesha dalili zozote za kukubaliana na hoja yangu.
“Je n'y vais pas moi même sans toi”. Siendi peke yangu bila wewe. Hatimaye Amanda aliniambia huku akitikisa kichwa chake kuonesha kukataa.
“N'aye pas peure mon amour, je serai bien”. Wala usihofu mpenzi nitakuwa salama. Nikamsisitiza Amanda huku nikihisi kuwa sikuwa na muda mrefu wa kuendelea na majadiliano yale. Haraka nikayapeleka macho yangu kutazama kule mbele kwenye lile gari na hapo nikauona mlango wa dereva ukifunguliwa taratibu kisha akashuka mwanaume mmoja aliyevaa suruali ya jeans na fulana mchinjo ya rangi nyeupe huku kichwani akiwa amevaa kofia ya pama na mkononi alikuwa ameshika bunduki aina ya Smg.
Sasa nilikuwa na hakika kuwa mambo hayakuwa shwari tena. Nilitamani sana nishuke kwenye lile gari pamoja na Amanda kisha tuanze kukimbia tukipotelea kwenye ule msitu mkubwa uliokuwa kando ya ile barabara. Hata hivyo haraka nikajikuta nikipingana na wazo lile pale nilipohisi kuwa kulikuwa na uwezekano mkubwa wa kukamatwa endapo ningeamua kukimbia huku nikiwa nimeongozana na Amanda. Kwani nilikuwa nimemchukulia Amanda kama walivyokuwa wasichana wengine wa kawaida wasiokuwa na mazoezi yoyote ya mwili. Vilevile kutokana na mazingira yale sikuwa na silaha yoyote ya kujihami. Kwa kifupi nilipoteza kabisa matumaini ya kutoroka salama eneo lile. Hatimaye nikageuka haraka na kumshawishi Amanda kwa mara ya mwisho nikimnong’oneza na kumsihi.
“S'il vous plaît allez ma cherie”. Tafadhali nenda mpenzi. Sauti yangu ilikuwa ni yenye kusihi na kushawishi sana hali iliyompelekea Amanda anitazame kwa makini kama mtu aliyesikia habari mpya kabisa masikioni mwake. Kisha pasipo upinzani wowote nikamuona akiyachukua yale mabegi yetu mawili halafu haraka akausukuma ule mlango wa gari na kushuka chini akianza kukimbia kuelekea kwenye ule msitu uliokuwa kando ya ile barabara. Niliendelea kumtazama Amanda namna alivyokuwa akipotelea kwenye ule msitu hadi alipotoweka kabisa machoni mwangu. Nilipoyarudisha macho yangu kutazama nje ya gari nikagundua kuwa lile gari letu Land Rover 110 tayari lilikuwa limezingirwa na wanaume sita walioshika bunduki zao vyema mikononi.
Kuona vile ghafla moyo wangu ukapiga kite kwa nguvu, koo likanikauka huku jasho jepesi la hofu likianza kunitoka sehemu mbalimbali za mwili wangu. Kwa sekunde kadhaa nikajikuta nimeganda nyuma ya usukani wa gari kama sanamu huku akili yangu ikikataa kabisa kufanya kazi. Hatimaye nikayainua macho yangu na kuanza kuyatembeza taratibu nikitazama nje kupitia vioo vya madirishani.
Miongoni mwa wale watu sita, wanne haraka niliwakumbuka. Wawili kati yao walikuwa ni wale waliokuwa wamesimama nyuma ya lile gari wakitusimamisha wakati tulipokuwa tukiwapita kule msituni. Wale watu wengine wawili nikawakumbuka vizuri kuwa walikuwa ni wale waliotukimbilia baada ya kulisimamisha gari letu kule msituni. Wawili waliosalia sura zao zilikuwa ngeni kabisa kwangu ingawa sasa nilikuwa na hakika kuwa huwenda walikuwa wamejificha wakati wenzao walipokuwa wakijitahidi kutusimamisha kule msituni.
“Descendez vous tous!”. Wote shukeni chini!. Mara nikamsikia mmoja wao akifoka kwa sauti huku akilipigapiga lile bodi la gari kwa kitako cha bunduki yake mkononi. Sikuwa na namna ya kukaidi amri ile hivyo taratibu nikafungua mlango wa gari kwa unyonge na kushuka chini. Hata hivyo sikupiga hatua yoyote ya mjongeo mbali na eneo lile. Kitendo kile kikawapelekea wale watu wanne wanaume wanisogelee na kunizunguka. Kisha mmoja wao akawasha kurunzi yenye mwanga mkali na kunimulika usoni. Tukio lile likanitia hasira hata hivyo nilijionya kutofanya purukushani za aina yoyote eneo lile badala yake nikaipa akili yangu utulivu huku nikihisi hatari ilikuwa ikininyemelea kwa kasi ya risasi.
“Est-ce qu'il y a un problème?”. Kuna tatizo gani?. Nikawauliza wale watu huku kwa hila nikianza kuzikagua vizuri nyendo zao. Hata hivyo nilijikuta nikikabiliana na maumivu makali ya ngumi mbili kavu za mgongoni kutoka kwa mtu aliyekuwa nyuma yangu na kunifanya niheme juu juu kama niliyeamshwa na njozi mbaya kutoka usingizini. Wakati nikiugulia maumivu yale nikajikuta tena nikichapwa makofi mawili ya nguvu usoni yalionipelekea nione maluweluwe mbele yangu...
*********
***************
**************************CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ta femme est très belle”. Mke wako ni mrembo sana. Yule mtu akaongea kwa utulivu huku akitabasamu kisha akageuka na kumtazama Amanda usoni huku akipiga hatua taratibu kumsogelea pale aliposimama halafu nikamsikia akimuuliza Amanda.
“Où est de I'argent?”. Pesa ziko wapi?. Lile swali likampelekea Amanda ageuke kidogo na kunitazama hata hivyo sikuona tashwishwi yoyote usoni mwake. Kisha akamtazama tena yule mtu hatari kiongozi wa wale watekaji na kumwambia.
“Je les est caché à la brousse”. Nimezificha kule msituni. Amanda akaongea kwa utulivu huku akionekana kujawa na hofu.
“Tu es sure?”. Una uhakika?. Yule mtu akafoka huku akimtazama Amanda kwa makini usoni.
“Oui”. Ndiyo. Amanda akaitikia kwa woga kisha nikamuona yule mtu mtu akageuka na kuwatazama wale wapambe wake wawili.
“Toi et toi, allez avec lui pour prendre cet argent, et qu'il n'ose pas faire la rusé”. Wewe na wewe, nendeni naye mkachukue hizo pesa na asithubutu kufanya hila. Mara baada ya yule mtu kutoa amri wale wapambe wake wawili wakaanza kuongozana na Amanda wakielekea kule msituni na wakati wakiondoka Amanda akageuka tena na kunitazama na namna ya utazamaji wake nikahisi kuwa kulikuwa jambo fulani ambalo mimi sikulifahamu. Hata hivyo nikajipa subira huku sote tukiwatazama Amanda na wale watu namna walivyokuwa wakitokomea kwenye ule msitu wa jirani na ile barabara.
Wakati lile tukio likiendelea na kuonekana kuwachukua sana wale watekaji waliosalia pamoja na kiongozi wao. Mimi akili yangu ilikwishaanza kuchangamka huku nikiiona kuwa ile ndiyo ingekuwa nafasi pekee ya kujiokoa. Haraka nikayatembeza macho yangu kuwapeleleza vizuri wale watekaji. Mmoja alikuwa kiasi umbali wa hatua zisizopungua nne kutoka pale chini nilipokuwa nimekaa na mwenzake alikuwa mbali zaidi akiwa amesimama nyuma ya lile gari huku akivuta bangi. Yule kiongozi wao alikuwa hatua moja zaidi mbele yangu huku akiwa amejikita katika kutazama kule msituni walikopotelea Amanda na wale wapambe wake.
Sikuona kama kungekuwa na nafasi nyingine nzuri ya kucheza na akili za wale binadamu kama ile. Mikono yangu ikiwa imefungwa na kukazwa kikamilifu kwa nyuma kama mbawa za kuku, nikafanya tukio moja la kushangaza lakini hatari na makini. Nilikusanya nguvu za kutosha kisha kufumba na kufumbua nikajibetua na kuuzungusha chini mguu wangu wa kulia nikimchota mtama maridadi wenye ufundi wa hali ya juu yule kiongozi wa wale watekaji mbele yangu. Ambapo alishikwa na taharuki ya aina yake wakati alipokuwa akitupwa hewani na kuweweseka kama aliyepagawa na jinamizi baya ndotoni. Yule mtu alipotua chini akajikuta tayari ameenea vizuri kwenye kabari matata ya miguu yangu iliyomnyima nafasi ya kuhema vizuri huku macho yakiwa yamemtoka kwa mshangao. Tukio lile lilikuwa limepelekea ile bastola yake mkononi imponyoke na kuangukia kando yangu.
Mahesabu yangu yalikuwa yameenda vizuri kwani haraka nikaiokota ile bastola huku yule bwege akiendelea kufurukuta bila ya mafanikio. Wale wenzake kuona vile wakataharuki wakizielekezea bunduki zao kwangu. Risasi moja iliyofyatuliwa na mmoja wa wale watekaji nikawahi kufanya hila haraka nikijipindua na yule mateka wangu na kupelekea ile risasi ipekenye na kuvunja mfupa wa paja la yule kiongozi wao na hapo nikamsikia yule mtu akipiga yowe kali la maumivu na kulaani kitendo kile kwa matusi mzito mazito ya kila sampuli.
Nikafurahi na kuangua kicheko cha dhihaka nikimpongeza yule mtu kwa tabasamu. Tukio lile likampelekea yule aliyefyatua ile risasi ashikwe na kihoro kwa kumtindua risasi kiongozi wake kwa kutokuwa makini. Yule kiongozi wao ambaye sasa nilikuwa nimemtuliza vizuri kwa kabari yangu matata akaendelea kutukana matusi ya aina zote duniani huku akilalamika kwa maumivu makali ya jeraha la risasi na kulaumu kwa kitendo kile. Ilikuwa kama mchezo wa kuigiza jukwaani lakini chochote kilichokuwa kikifanyika pale lilikuwa ni tukio la kweli.
“Déposez vos armes, si non je vais mourir avec votre mari”. Tupeni silaha chini vinginevyo nitakufa na huyu mume wenu. Nikafoka kwa hasira nikiwaambia wale watekaji wawili na bunduki zao mkononi. Hata hivyo nikawaona ni kama wanaotaka kunipuuza hivyo kwa kuwahakikishia kuwa nilikuwa sifanyi mzaha nikajipinda mgongo ili kuiruhusu mikono yangu iliyoshika ile bastola ya yule bwege iweze kupata mhimili mzuri wa shabaha. kisha nikavuta kilimi cha ile bastola.
Lilikuwa shambulio makini kwani ile risasi ilipenya kwenye goti la yule kiongozi wao niliyemtuliza vizuri kwa kabari yangu na hapo akapiga yowe kali la maumivu huku akijitahidi kufurukuta bila mafanikio. Kwani bado nilikuwa nimemdhibiti vizuri kwa ile kabari yangu miguuni. Yule mateka wangu kuona vile akaanza kulalamika kwa kulia huku akifoka kuwaambia wale wapambe wake.
“Ecoutez vous les idiots, déposer vos armes au bien vous voulez que je meure?”. Msikilizeni nyinyi wapumbavu, tupeni silaha zenu chini au mnataka mimi nife?. Yule kiongozi wao akafoka kwa hasira akiwaambia wale wapambe wake huku akiwa bado nimemtuliza vizuri kwenye kabari yangu matata ya miguuni. Wale watekaji wengine kuona vile hawakuwa na pingamizi tena badala yake wakaweka bunduki zao chini huku wameshikwa na mshangao wasijue la kufanya. Kwa kweli nilifurahishwa sana na kitendo chao kile cha nidhamu na utii kwa kiongozi wao. Nilipohakikisha kuwa tayari walikuwa wameweka silaha zao chini nikawaambia.
“Bien!, alors rentez cing pas en arrière”. Vizuri!, haya rudini nyuma hatua tano. Wale watekaji kusikia vile wakasita kidogo wakitazamana lakini waliponiona nikijipinda tena na kuielekezea ile bastola mikononi mwangu kwa yule kiongozi wao wakaingiwa na hofu na kuanza kurudi nyuma kama nilivyowaamuru.
Wale watekaji waliporudi nyuma katika umbali wa kuridhisha nikageuka na kumwambia bosi wao kuwa anifungue zile kamba zilizokuwa zimefungwa na kukazwa mikononi mwangu kwa nyuma huku bado nikiwa nimemtundika kabari kwa miguu yangu. Yule mtu akasita kidogo lakini alipoona nikizidi kuibana miguu yangu na kuzidi kumpa wakati mgumu wa kuhema ikabidi aipitishe mikono yake nyuma yangu na kuanza kuifungua ile kamba taratibu huku macho yangu yakiwa makini kuwatazama wale wapambe wake pale waliposimama.
Zoezi la kuzifungua zile kamba likafanyika kwa muda mfupi sana huku nikihofia kukutwa na wale watu walioongozana na Amanda kwenda kule msituni ule muda mfupi uliopita Yule mtu alipomaliza kunifungua, mikono yangu ikarudiwa tena na uhai huku mishipa yake ikianza kuruhusu mjongeo mzuri wa damu kupita na kuitowesha ganzi mikononi mwangu. Hatimaye nikaifungua ile kabari na kusimama huku nikiinyooshanyoosha mikono yangu. Kitendo cha kuifungua ile kabari yangu ya miguuni kikampelekea yule kiongozi wao aanze kukohoa na kuhema ovyo huku akilishika koo lake kwa viganja vyake na macho yametoka pima.
Wale wapambe wake wakiwa bado wamesimama wasijue la kufanya nikaamua kuwashangaza. Kufumba na kufumbua nikageuka na kuwachapa risasi za kutosha. Wale watu wakapiga mayowe ya maumivu wakianguka chini na kutapatapa ovyo kabla ya kutulia huku kifo kikiwa tayari kimewachukua. Sasa nikageuka na kumtazama yule mtu aliyeonekana kuwa ndiye kiongozi wao ambaye sasa alikuwa akijitahidi kuinuka pale chini bila mafanikio kwani miguu yake yote miwili ilikuwa na majeraha ya zile risasi zangu.
Yule kiongozi wao kuona vile akaanza kusota taratibu akiondoka eneo lile huku akinitazama kwa woga. Hata hivyo tukio lile lilikuwa ni sawa na kutapatapa tu kwani yule mtu hakufika popote badala yake mimi nilikuwa nyuma yake nikimfuata taratibu pasipo kutia neno lolote. Jamaa akaendelea kusota na alipoona kuwa jitihada zile zisingemfikisha popote hatimaye ilifika sehemu akaamua kukaa huku damu nyingi ikiendelea kumtoka kwenye yale majeraha yake ya risasi. Kisha akaanza kuniomba msamaha akinisihi kuwa tusameheane na nisimdhuru. Sikusema neno lolote kwani hoja ile haikuwa katika mipango yangu.
Nilianza kwa kumchapa risasi moja ya goti lake la mguu wa kushoto kisha nikaendelea na goti la mguu wake wa kulia huku yule mtu akiendelea kupiga mayowe ya maumivu makali. Yule mtu akaendelea kulalamika sana akiniomba msamaha na kunisihi nimuache lakini ilikuwa kazi bure kwani niliunyoosha tena mkono wangu na kuielekeza tena ile bastola kwenye bega lake la kushoto kisha nikavuta kilimi cha ile bastola na kuuchangua vibaya mfupa wa bega lake. Yule mtu akapiga yowe na kubweka kama mbwa wakati maumivu yale makali ya risasi yalipokuwa yakisambaa haraka mwilini mwake.
Nilimkumbuka vizuri yule mtu namna alivyonitemea mate usoni kwa dharau na kunichapa makofi kadha wa kadha wakati nilipokuwa nimefungwa kamba mikononi ule muda mfupi uliopita. Kwa kweli sikuona sababu ya kumuacha mtu yule aendelee kuishi. Nilitaka afe kifo cha aibu na chenye maumivu makali ya risasi nilizokuwa nimepanga kumuadhibu nazo taratibu katika maeneo tofauti ya mwili wake ambayo yangekichelewesha kifo chake ili iwe kama fundisho kwa vitendo vile vya kiharamia vya utekaji wa magari vilivyokuwa vukiwanyima raha wasafiri wa barabara ile nyakati za usiku na mchana.
Nilikuwa katika harakati za kujiandaa kumchapa risasi nyingine ya bega la kulia yule kiongozi wa watekaji wakati niliposhtushwa na mlio wa risasi kutoka kwenye ule msitu wa jirani na barabara alipokuwa Amanda na wale watekaji wawili. Tukio lile la mfyatuko wa risasi likanishtua sana na kuniletea hisia mbaya zisizoelezeka. Hivyo nikajikuta nikiganda kama nyamafu huku shughuli za mwili wangu zikisimama kwa sekunde kadhaa. Masikio yangu yakasumbuliwa na ugeni wa kelele za mbawa za ndege ambao walikuwa wakijitahidi kuyakimbia matawi ya miti mirefu ya msitu ule baada ya ndege wale kushtushwa vibaya na ile sauti mbaya ya ule mlio wa risasi.
Nikiwa bado nimeyatega masikio yangu mara nikashtushwa tena na mlio mwingine wa risasi kutoka kwenye msitu ule na hapo hofu juu ya usalama wa Amanda ikazidi kuzimeza hisia zangu taratibu kama sindano ya sumu kali isambaavyo mwilini. Moyo wangu ukashikwa na mfadhaiko huku ukianza kwenda mbio isivyo kawaida. Miguu yangu nayo ikawa mizito kupiga hatua huku jasho jepesi likianza kunitoka sehemu mbalimbali za mwili wangu. Hata hivyo hali ile haikuendelea zaidi kwani muda uleule mara nikahisi nikipigwa pigo moja la nguvu na kitu kizito nyuma ya kichwa change. Nikajitahidi kujitetea bila mafanikio badala yake nikajikuta nikikabiliana na maumivu makali yaliyoanza kusambaa taratibu mwilini yakitokea sehemu ya nyuma ya kichwa changu.
Nikaanza kuhisi kuwa hali yangu ilikuwa ikizidi kuwa mbaya kadiri sekunde zilivyokuwa zikiyoyoma. Kichwa changu nacho kikawa kizito mno kama niliyebebeshwa mzigo mzito kichwani nisioweza kuumudu. Nilitamani kufungua mdomo ili nipige yowe la kuomba msaada lakini nikajikuta nikiishilia kufumbua mdomo tu huku ile sauti ikigoma kabisa kutoka na hivyo kuishilia akilini mwangu tu. Macho yangu nayo yakaanza taratibu kupoteza nguvu ya kuona. Hatimaye shughuli mbalimbali za mwili wangu nazo nikazihisi kuwa zilikuwa mbioni kusitisha utendaji wake. Nikajiuliza ni kitu gani kilichokuwa kikinitokea lakini kabla sijapata jibu nikaanza kuhisi taratibu nilikuwa nikiishiwa nguvu mwilini na hatimaye kuanguka chini. Nilitamani sana kufumbua macho na kuona nini kilichokuwa kikinitokea eneo lile lakini hilo halikuwezekana kwani macho yangu yalikuwa yakizidi kuwa mazito sana na hatimaye nikaanguka chini kabisa kama bondia aliyetupiwa konde zito la kichwani na mpinzani wake.
Nikiwa pale chini sijielewi vizuri mara kwa mbali nikasikia mlio mwingine wa risasi hata hivyo safari hii nilihisi kuwa risasi ile ilikuwa imefyatuliwa umbali mfupi kutoka pale chini nilipokuwa nimeanguka. Nilijitahidi kusimama lakini sikuweza kwani taratibu fahamu zangu zilikuwa zikinitoka na kunifanya nijihisi mzembe sana kwa kusumbuliwa na maradhi nisiyoyafahamu. Hatimaye nikalala chini kabisa nikiwa sina uwezo wa kufanya chochote. Nikiwa nimelala pale chini huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha mara nikaanza teja kuhisi kuwa nilikuwa nikinyanyuliwa taratibu na kitu nisichokijua na ingawa nilijitahidi kuleta pingamizi la kila namna hata hivyo sikufanikiwa. Muda mfupi baada ya pale sikuweza tena kufahamu kilichoendelea.
_____
Niliyatega masikio yangu kwa makini huku nikijaribu kutafakari kuwa pale nilikuwa wapi. Sikusikia sauti ya kitu chochote na utulivu wa eneo lile ulikuwa ni wa hali ya juu kiasi kwamba nafsi yangu ilianza tena kuingiwa na hofu.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilikuwa nimerudiwa na fahamu, hisia zangu zilinitanabaisha hivyo huku nikikumbuka vizuri masaibu yote yaliyonitokea kule barabarani msituni wakati nilipopambana kikamilifu na wale watekaji. Sikuweza kufahamu nini kilichokuwa kimenitokea wakati macho yangu yalipokuwa yamejikita kutazama upande ule wa msitu alipokuwa Amanda na wale watekaji wawili baada ya milio ya risasi kusikika na kisha fahamu zangu kuchukuliwa na pigo zito la nyuma ya kichwa changu na baada ya pale sikufahamu kilichofuata. Hata hivyo nikapiga moyo konde na kumshukuru Mungu kwa kuniweka hai hadi wakati ule kwani niliamini kuwa mambo mengine ningekuja kuyafahamu baadaye.
Nilikuwa kitandani nimelala kwenye foronya laini na mto wa kuegemeza kichwa. Sikusikia upepo mkali, baridi wala yale manyunyu makubwa ya mvua zile za masika za kule msituni. Hivyo nilikuwa na kila hakika kuwa nilikuwa ndani ya nyumba. Nyumba ile ilikuwa ya nani na nilifikaje fikaje pale?. Nikajiuliza bila kupata majibu hali iliyonipelekea niyafumbue macho yangu taratibu na kuanza kuyatembeza huku na kule katika kutathmini vizuri mandhari yale.
Nilikuwa kwenye chumba kikubwa chenye kitanda kikubwa cha samadari, cha futi sita kwa sita, cha mbao ngumu ya mnin’ga, chenye droo mbili upande wa kushoto. Mbele ya kitanda kile kulikuwa na runinga pana ya inchi arobaini na mbili. Sistimu ya kisasa ya muziki aina ya Jvc, deki ndogo ya runinga yenye kutumia cd na flash disc, vyote vikiwa katika meza nzuri nyeusi ya kioo.
Upande wa kushoto wa kile chumba kulikuwa na kabati kubwa la kisasa la nguo hata hivyo kabati lile lilikuwa limefungwa. Pembeni ya kabati lile kulikuwa na kochi moja la sofa huku kando yake kukiwa na meza fupi ya mbao yenye simu ya mezani na kitabu kidogo chenye orodha ya majina ya watu na kampuni zilizokuwa zikitumia huduma ile ya simu ya mezani ama landline. Kwenye kona ya chumba kile upande wa kushoto kulikuwa na mlango. Nilipouchunguza mlango ule nikagundua kuwa ulikuwa ni wa kuelekea kwenye chumba kidogo cha maliwato na bafu.
Niliendelea kuyatembeza macho yangu taratibu nikitazama ukutani na hapo nikaona picha mbili kubwa nzuri za kuchorwa zikiwa zimetundikwa sehemu mbili tofauti. Moja ilikuwa ni ya mama wa kiafrika akiwa amembeba mtoto wake kwa mbeleko mgongoni na picha nyingine ilikuwa ya ua zuri la rangi nyekundu lililochorwa kwa ustadi wa hali ya juu. Picha zote mbili zilikuwa ndani ya fremu nzuri za kioo na kuzifanya zionekane vizuri katika zile kuta nyeupe na...
... na Burundi. Mbali na kadi zile pia kulikuwa na ramani ndogo ya kukunja ya kijasusi niliyokuwa nimepewa na mratibu wangu wa safari za kijasusi Brigedia Jenerali Ibrahim Gambari. Muda mfupi kabla ya kuanza safari yangu jijini Dar es Salaam, Tanzania. Kwa kweli nilijikuta nikiishiwa nguvu pale nilipohisi kuwa kulikuwa na uwezekano mkubwa wa nyaraka zile muhimu za kijasusi kuwa tayari zingekuwa zimeonwa pale ambapo Amanda angeamua kufanya upekuzi kwenye begi langu wakati fahamu zikiwa zimenitoka.
Hata hivyo sikuwa na namna ya kufanya kwani chochote ambacho kingetokea nilipaswa kujipanga kukabiliana nacho ingawa uzima wa afya yangu kilikuwa ni kipaumbele cha kwanza. Hatimaye nikameza funda kubwa la mate nikijitahidi kuyatowesha mawazo yale kichwani mwangu huku zile dawa za kutuliza maumivu zikiendelea kufanya kazi mwilini.
_____
Sikuweza kufahamu ni wakati gani lepe hafifu la usingizi lilikuwa limefanikiwa kuziteka fikra zangu pale kitandani wakati nilipokuwa nikiendelea kuwaza hili na lile juu ya safari yangu ile ya kijasusi, pale niliposhtuka kutoka usingizini baada ya kitasa cha mlango wa kile chumba kusikika kikizungushwa taratibu na ule mlango kufunguliwa ukisukumwa kwa ndani.
Hisia zangu zikanitanabaisha kuwa yule alikuwa Amanda na alikuwa akija mle ndani kuniletea chakula. Hivyo nikageuka taratibu nikitabasamu na kuyapeleka macho yangu kuutazama ule mlango wa kile chumba huku nikitarajia kumuona Amanda akiwa na sinia kubwa lenye maakuli. Hata hivyo hilo halikutokea na badala yake mbele yangu nikajikuta nikikabiliana na mshtuko usioelezeka.
Ule mlango ulipofunguliwa Amanda akaingia mle ndani huku akiwa ameongozana na wanaume watatu, warefu na weusi wenye miili iliyojengeka imara. Huku wote wakiwa wamevaa sare za jeshi la wananchi wa Burundi na kofia za bereti vichwani mwao. Jamaa walikuwa wamepanda hewani kisawasawa na namna ya mikono ya gwanda zao ilivyokuwa imekunjwa niliweza kuiona misuli yao imara ya mikononi namna ilivyotuna kikamilifu kwa mazoezi ya nguvu yasiyokuwa na kikomo. Haraka nilipowachunguza nikagundua kuwa walikuwa ni makomandoo waliofuzu vizuri katika medani za masuala ya kijeshi na hapo koo langu likanikauka ghafla kwa hofu. Mapigo ya moyo wangu yakaanza kunienda mbio huku baridi nyepesi ikisafiri katika maungo yangu. Hali ile ikanipelekea nijihisi kuwa nimepona kabisa yale maradhi yangu na kuanza kujilaumu kuwa nilikuwa nikipoteza muda wangu pale kitandani.
Sasa nilikuwa na hakika kuwa Amanda alikuwa ameniuza tena kwa bei ya rejareja isiyokuwa na majuto yoyote katika nafsi yake na kwa kweli sikutaka haraka kuamini vile. Wale wanajeshi huku wakiwa wameongozana na Amanda wakazitupa hatua zao kwa tahadhari huku wakitembea kikakamavu katika namna iliyonipelekea niweze kuzisikia vizuri buti zao ngumu miguuni namna zilivyofanikiwa kwa kiasi kikubwa kuitetemesha sakafu ya kile chumba. Nilitamani nilitupe kando lile blanketi nililojifunika kisha nikurupuke na kuanza kutimua mbio. Lakini hilo halikuwezekana kwa kuwa muda haukuniruhusu kufanya vile na wale watu walikuwa ni kama tayari wameshanifikia pale kitandani nilipolala. Mbali na vile pale kitandani sikuwa na nguo hata moja ya kunisitiri, hali iliyonipelekea sasa niamini kuwa Amanda alikuwa amenifanyia hila kwa kunivua nguo ili hata zikitokea purukushani zozote nisiweze kukimbia loh!.
Wale wanajeshi walipofika pale kitandani nilipolala wakajigawa katika mtindo wa kukizunguka kile kitanda. Mmoja akaja na kusimama nyuma yangu, mwingine upande wa kushoto na mwingine upande wa kulia. Amanda yeye akasimama mbele ya kile kitanda huku akinitazama kwa tabasamu la kinafiki lenye tafsiri ya ushindi. Nikiwa nimeshikwa na mshtuko wa hali ya juu, nikayatembeza macho yangu taratibu nikizikagua vizuri sura za wale watu kisha nikaweka kituo nikimtazama Amanda huku nikijitahidi kuumeza mshtuko niliokuwa nao moyoni. Amanda akanitazama na baada ya kitambo kifupi akavunja ukimya akiniambia.
“Jean ne t'enfait pas c'est sont mes amis, ils vont t´aider”. Jean, hawa ni marafiki zangu, watakusaidia. Maelezo ya Amanda yenye kila namna ya chuki na usaliti yakanipelekea nitabasamu kidogo kujifariji na kuitowesha hasira iliyokuwa imeanza kuchemka moyoni mwangu na hapo nikamuona yule mwanajeshi wa upande wa kulia akisogea kidogo pale kitandani huku tabasamu la kifidhuli likijitokeza taratibu usoni mwake na mikono yake ameishikamanisha mbele yake. Kwa heshima akajitambulisha.
“Je m'appelle Major Pascal Karibwami, je suis contant de te voir ici”. Naitwa Meja Pascal Karibwami, nafurahi sana kukuona hapa. Yule mwanajeshi akaongea kwa kujiamini huku akinipa heshima zote utasema mimi nilikuwa mkuu wake wa kazi. Alikuwa mwanaume mrefu na mweusi kama mjaruo. Hali iliyonipelekea niyaone vizuri macho na meno yake meupe wakati alipokuwa akitabasamu. Alipomaliza kujitambulisha mwenzake naye akasogea na kujitambulisha kwa nidhamu zote hali iliyonipelekea nishikwe na mduwao.
“Staff Surgent Anatole Nkunda”
Wakati yule mwanajeshi mwingine akijitambulisha nikageuka na kumtazama na sura yake ikanitia mashaka. Macho yake yalikuwa makubwa yenye uchovu lakini yanayoonya. Uso wake mrefu ulikuwa umetulia kama maji ya kisima na ijapokuwa alikuwa amevaa kofia ya bereti lakini kofia ile ya kiafande ilikuwa imetuama vizuri kwenye upara wake unaowaka na usiokuwa na unywele hata mmoja. Isipokuwa mishipa ya damu iliyotuna na kusambaa kichwani kama mizizi ya mmea wa mhindi. Yule afande akakaza sura akinitazama utasema alikuwa akivishwa medani ya heshima na amiri jeshi mkuu. Alipomaliza kijitambulisha yule askari mwenzake aliyekuwa nyuma yangu nikamsikia naye akijitambulisha. Hata hivyo sikuweza kumuona kutokana na namna nilivyokuwa nimelala pale kitandani isipokuwa sauti yake ilikuwa nzito mno.
“Corporal Adolphe Sahinguvu”
“Je ne, veux pas l'aide de qui que ça sole”. Sihitaji msaada wa mtu yeyote. Nikaongea kwa jazba hata hivyo wale maafande wakaishia kuangua kicheko cha dharau ambacho kilinishangaza sana na kunitia hasira. Kicheko kile kilipokoma nikamsikia yule mwanajeshi mkubwa kwa cheo aliyejitambulisha kwangu kama Major Pascal Karibwami akiniuliza kwa utulivu.
“Comment ça va camarade?”. Vipi komredi unajisikiaje?.
“Je ne me sens pas bien, et je suis trés enfamé”. Sijisikii vizuri na nasikia njaa sana. Nikaongea kwa utulivu huku nikianza kuhisi usalama wangu ulikuwa ukielekea kudorora mbele ya uwepo wa watu wale. Ingawa taratibu za kijasusi zilikuwa zikinionya kutomuamini mtu yeyote katika mazingira yoyote lakini kwa kweli sikuwa nimetarajia kabisa kuwa Amanda angekuja kunisaliti tena katika mazingira kama yale. Hata hivyo nilijionya kuwa ukorofi wowote ambao ningeamua kuuleta katika mazingira yale usingenisaidia kitu kwani afya yangu bado ilikuwa dhaifu. Hivyo nikaishia kumeza funda kubwa la mate kuipoza hasira yangu kifuani.
“On ne t'a pas encore donner à manger?”. Hujapewa chakula?. Major Pascal Karibwami akaniuliza kwa utulivu huku akitabasamu. Ingawa nilikuwa na hakika kuwa alikuwa akinidhihaki hata hivyo ilinibidi nimjibu.
“Oui”. Ndiyo.
“Ne t'enfaite pas, nous allons te donner à manger”. Usijali sisi tutakupa chakula kingi na utashiba vizuri. Meja Pascal Karibwami akaniambia huku akiendelea kutabasamu na nilipomtazama usoni nikashtushwa na tabasamu lake la kinyama. Hali iliyonipelekea nizidi kushikwa na mashaka juu ya hatima yangu.
“Qui etes des qui?”. Nyinyi ni akina nani?. Nikawauliza wale watu huku nikifoka kwa kitendo kile cha kuchezewa akili yangu kama mtoto mdogo.
“Ne te derange pas, dans peu de temps tu vas nous connaître”. Ondoa shaka, muda siyo mrefu utatufahamu vizuri sisi ni akina nani. Meja Pascal Karibwami akaniambia huku akikenua meno yake na kunitazama kwa furaha. Alipoyatoa macho yake kwangu akayatembeza taratibu akimtazama Amanda pamoja na wale askari wenzake kisha akayarudisha tena pale kitandani nilipolala na kuniambia kwa sauti tulivu lakini yenye kumaanisha.
“Nous venons te prendre camarade”. Tumekuja kukuchukua komredi. Maelezo ya Meja Pascal Karibwami yakanipelekea nishikwe na mshangao huku nikishindwa kuelewa kuwa alikuwa amenuia nini. Hatimaye nikamuuliza huku nikiwa nimeanza kushikwa na wasiwasi juu ya kauli ile.
“Vous m'amainer où?”. Mnanipeleka wapi?. Swali langu likawapelekea wale maafande wote mle ndani waangue kicheko kana kwamba nilikuwa nimeongea kitu cha kipuuzi na cha kuchekesha sana. Wakati wale watu wakiendelea kucheka nikiwa pale kitandani nikamtazama Amanda na kitendo cha kumuona akiungana na wale watu kunicheka kikanitia gadhabu. Kile kicheko chao kilipofika kikomo Meja Pascal Karibwami akaniambia kwa hadhari huku akinitazama.
“Nous t'amainons à l'hospitale parceque votre santé ne pas bonne”. Tunakupeleka hospitali kwani afya yako siyo nzuri.
“Qui vous a dit que je veux l'aide d'aller à l'hospitale?”. Nani aliyewaambia kuwa nahitaji msaada wa kupelekwa hospitali?. Nikamuuliza kwa jazba yule mtu huku nimeshikwa na hasira kwa kudhihakiwa.
“Si tu es bien, pourquoi maintenant tu dors ice de dans comme une femme aceinte?”. Sasa kama wewe ni mzima kwanini unalala lala humu ndani kama mama mjamzito?. Meja Pascal Karibwami akaniuliza na kuwapelekea wale watu wote mle ndani waangue kicheko.
Kwa kweli nilishikwa na hasira hasa nilipokumbuka namna nilivyomuokoa Amanda kutoka katika ile mikono ya wale watekaji kule njiani msituni.
“Je ne veux pas l'aide de qui que ça sole”. Sihitaji msaada wa mtu yoyote. Nikaongea kwa msisitizo na hapo nikamsikia yule mwanajeshi aliyekuwa nyuma yangu akiniambia kwa kufoka.
“Arreter de s'opposer toi singe!”. Acha ubishi wewe tumbili!. Hali ile ikanipelekea nimuulize Amanda kwa hasira.
“Amanda, qu'est-ce qu'evolue ici de dans, je n'arrive pas à te comprendre?”. Amanda, nini kinachoendelea humu ndani, mbona sikuelewi?.
“Sans doute tu es troublé Jean, qui est Amanda?”. Bila shaka umechanganyikiwa Jean, Amanda ndiyo nani?. Amanda akanimbia huku akiangua kicheko cha dhihaka.
“C'est toi!”. Si ni wewe!. Nikamwambia Amanda kwa mshangao huku nikijihisi kuchanganyikiwa kwa kutumbukia katika mkasa ule wa hatari. Meja Pascal Karibwami akaangua kicheko hafifu kabla ya kuniambia.
“C'est pour quoi je te dis que nous venons t'amainer à l'hopital, votre inteligence n'est pas bonne, tu vois tu es entré de baptiser les gents le noms qui ne sont pas les leur!”. Ndiyo maana nikamwambia kuwa tumekuja kukuchukua tukupeleke hospitali. Akili yako siyo nzuri, huoni unavyowabatiza watu majina yasiyo yao?.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Je ne vous comprend pas?”. Mbona siwaelewi?. Nikawauliza wale watu kwa hasira hata hivyo swali langu likawapelekea wale watu waangue tena kicheko wakinidhihaki. Kisha Meja Pascal Karibwami akaniambia kwa utulivu huku akitabasamu.
“Ne t'enfait pas camarade, nous allons te faire comprendre”. Usihofu komredi, tutakuelewesha. Kisha nikamuona Meja Pascal Karibwami akiwafanyia ishara fulani ya kichwa wale askari wake hali iliyonipelekea nihisi jambo baya lilikuwa likielekeza kutekelezwa juu yangu.
Muda uleule lile blanketi nililokuwa nimefunikwa pale kitandani likaondoshwa kwa kasi na yule mwanajeshi aliyekuwa amesimama kushoto kwangu. Nilijitahidi kulizuia lakini kutokana na udhaifu wa mwili wangu sikufanikiwa. Hivyo nikajikuta nimebaki uchi kama nilivyozaliwa pale kitandani. Muda siyo mrefu mara nikamuona yule mwanajeshi mwenye cheo cha Koplo ambaye hapo awali alikuwa amejitambulisha kwangu kama Koplo Adolphe Sahinguvu, akizunguka kwenye kile kitanda na kunishika miguu. Kisha akanivuta chini kwa nguvu zake zote hali iliyonipelekea nitue pale chini sakafuni kwa matako na hivyo kupelekea maumivu makali yanisambae mwili mzima. Nilijitahidi kujitetea lakini ilikuwa kazi bure kwani mapigo ya mateke mgongoni na mabegani mwangu yakazidi kunipelekea niishiwe na nguvu kizunguzungu kikanishika na kunipelekea nijihisi kutaka kutapika.
Wale watu waliporidhika kuwa kile kipigo kilikuwa kimenilegeza kiasi cha kutosha, wakaamua kuniacha huku nikihema ovyo. Damu sasa ilikuwa ikinitoka puani, sehemu ya juu ya jicho langu la kulia ilikuwa imevimba na kuchanika huku ikivuja damu taratibu. Mdomo wangu nao ulikuwa umechanika sehemu yake ya chini na hivyo kunipelekea nihisi ladha nyepesi ya chumvi ya damu iliyokuwa ikivuja kwenye jeraha lile. Ikafikia hatua nikawa siwezi kuona vizuri mbele yangu. Nikiwa pale chini sijielewi vizuri baada ya kuleweshwa na ule mkong’oto wa nguvu kutoka kwa wale watu mara kwa shida nikamuona yule askari mwenye cheo cha chini kabisa kuliko wenzake akanisogelea pale nilipokuwa na kuanza kunifunga kamba mikononi na miguuni. Sikuweza kuleta upinzani wowote kutokana na hali yangu ya kiafya kuzidi kuzorota. Yule askari alipomaliza kunifunga zile kamba akaambiwa neno fulani la kirundi na yule Meja Pascal Karibwami ambalo muda mfupi baadaye nilifahamu vizuri maana ya neno lile kupitia vitendo. Kwani muda uleule yule mwanajeshi aliyenifunga zile kamba akanizoa pale chini sakafuni mzegamzega na kujitwisha begani huku nikiwa uchi wa mnyama bila nguo yoyote ya kujisitiri mwilini.
Huku nikiwa ninaning’inia begani kwa yule askari muda uleule safari ya kutoka mle ndani ikaanza huku yule askari aliyenibeba akitangulia mbele. Nyuma akafuatia Amanda na wale wanajeshi wengine. Hali yangu kiafya ilikuwa mbaya sana hata hivyo nilijitahidi kuituliza akili yangu na kuyachunguza vizuri mazingira yale.
Mara tu tulipotoka kwenye kile chumba tukajikuta kwenye korido pana kiasi iliyokuwa ikitazamana na milango mitatu upande wa kushoto ambayo kwa wakati ule yote ilikuwa imefungwa. Upande wa kulia wa ile korido kulikuwa na dirisha kubwa la kioo lililofunikwa kwa pazia refu na mwisho wa dirisha lile kulikuwa na mlango uliofungwa...
...Tulipoipita ile korido tukaingia upande wa kushoto ambapo tuliifuata korido nyingine fupi na mwisho wa korido ile nikauona mlango mwingine ukiwa umefungwa. Hata hivyo hatukuufikia mlango ule na badala yake mbele kidogo tukachepuka na kuingia upande wa kulia sehemu kulipokuwa na mlango mwingine. Mara tulipoufikia ule mlango yule mwanajeshi aliyenibeba akaufungua na hapo tukajikuta tukitazamana na ngazi za mbao za kushukia sehemu ya chini zilizotengenezwa kwa ustadi. Wale watu wakiwa nyuma yetu mara tukaanza kuzishuka zile ngazi kwa makini tukielekea sehemu ya chini ya lile jengo na wakati tukishuka zile ngazi nikayatega masikio yangu vizuri na kushangazwa na ukimya wa eneo lile. Kwani kwa namna nyingine ni kama ni sisi tu peke yetu ndiyo tuliokuwa mle ndani ya lile jengo kutokana na utulivu wa kushangaza uliokuwa mle ndani.
Tukaendelea kushuka zile ngazi na ndani ya muda mfupi tukawa tumefika sehemu ya chini mwisho wa zile ngazi katika ukumbi mpana ulioonekana kutumika kama sebule kubwa ya kisasa yenye samani za kila aina. Kama seti mbili za makochi makubwa ya sofa, meza moja kubwa ya kulia chakula, rafu kubwa ya vitabu, kabati la vyombo ukutani na sistimu kubwa ya muziki. Nilipenda kuendelea kuipeleleza vizuri sebule ile kwa macho yangu hata hivyo sikupata nafasi kwani yule mwanajeshi aliyenibeba hakuonekana kujali kitu chochote na mwendo wake ulikuwa wa kijeshi huku nikining’inia begani mwake kama gunia la viazi.
Hatimaye tukakatisha katikati ya sebule ile na wakati tukifanya vile nikabahatika kuiona picha moja kubwa iliyokuwa imetundikwa ukutani katika kuta moja ya ile sebule. Ilikuwa ni picha ya kiongozi mmoja mkubwa wa jeshi la wananchi wa Burundi hata hivyo sikuweza kuliona jina la kiongozi yule kutokana na mwendo kasi wa yule bwege aliyenibeba. Ingawa nilifanikiwa kuinakili vizuri sura ya yule kiongozi wa kijeshi kwenye ile picha ukutani.
Mara tulipofika kwenye kona ya ile sebule nikagundua kuwa kulikuwa na mlango lakini haraka nikafahamu kuwa ule mlango ulikuwa haujafungwa kwani yule bwege aliyenibeba akakishika kitasa chake na kuufungua ule mlango pasipo pingamizi lolote. Ule mlango ulipofunguka tukawa tumetokeza kwenye korido nyingine lakini fupi na mwisho wa korido ile kulikuwa na dirisha refu na jembamba la kioo na upande wa kushoto kulikuwa na ngazi nyingine za kushuka chini zaidi ya lile jingo. Hali ile ikanipelekea nigundue kuwa ile nyumba ilikuwa ni jengo la ghorofa kutokana na zile ngazi ingawa sikuweza kufahamu lilikuwa ni jengo la ghorofa ngapi.
Tulipozifikia zile ngazi tukaanza kushuka chini tena na nilipochunguza eneo lile nikagundua kuwa zile zilikuwa ni ngazi za mwisho kabla ya kufika sehemu ya chini kabisa ya lile jengo.
Amanda na wale viongozi wawili wa kijeshi walikuwa hatua chache nyuma yetu na wote walikuwa makini kunichunguza. Baada ya muda mfupi hatimaye tukawa tumefika kwenye sehemu ya chini kabisa ya lile jengo tukitokezea kwenye korido pana kiasi lakini yenye kona nyingi za kuweza kufanikiwa kumchanganya mtu yoyote ambaye ingekuwa ni mara yake ya kwanza kufika eneo lile. Hata hivyo nilikuwa makini kuzihesabu kona za korido ile wakati tulipokuwa tukizipita moja baada ya nyingine. Zilikuwa kona nane zilizokuwa zikitazamana na milango ya vyumba vingi vilivyofungwa. Hatimaye korido ile ikatufikisha mbele ya mlango mkubwa wa mbao.
Tulipofika pale yule bwege aliyenibeba akaufungua ule mlango na baada ya ule mlango kufunguka nikaanza kuhisi nini kilichokuwa kikielekea kutokea. Wale watu walikuwa bila shaka wamepanga kunisafirisha mbali na eneo lile kwa sababu nisizozifahamu kwani hatua chache mbele ya mlango ule gari la kijeshi aina ya Tdi-Discover lilikuwa limeegeshwa huku milango yake ya nyuma ikiwa wazi.
Tulipofika nyuma ya lile gari yule mwanajeshi aliyenibeba akanibwaga nyuma ya lile gari kama gunia hali iliyonipelekea nitue vibaya na kulalamika kwa maumivu makali. Hata hivyo hakuna aliyeonekana kujali badala yake kule nyuma akapanda yule mwanajeshi aliyenibeba na yule mwenzake mwenye cheo cha Sajenti kisha wakafunga ile milango ya nyuma. Amanda na yule Meja Pascal Karibwami wao wakaingia sehemu ya mbele ya lile gari na muda mfupi uliofuata safari ikaanza.
Hisia zangu zikanitanabaisha kuwa nilikuwa nikipelekwa katika mazingira hatari zaidi yenye usiri wa hali ya juu na yasiyokuwa na haya na matendo yoyote ya kinyama. Hata hivyo sikuwa na namna yoyote ya kuweza kujitetea na vioo vya lile gari vilikuwa vimewekwa tinted nyeusi hivyo ilikuwa vigumu kwa mtu aliyekuwa ndani ya lile gari kuweza kuona nje vizuri. Lakini sikukata tamaa badala yake niligeuka taratibu wakati lile gari lilipokuwa likiondoka eneo lile na kwa kufanya vile nikafanikiwa kuiona kwa sehemu tu ile nyumba tuliyotoka.
Ilikuwa ni nyumba ya ghorofa nne iliyozungukwa kwa bustani nzuri ya maua na miti ya vivuli iliyopandwa katika utaratibu maalum lakini unaopendeza. Mbele ya lile jengo la ghorofa chini yake kulikuwa na gari moja bovu la kijeshi aina ya Tata pamoja na lile gari Land Rover 110 tulilosafiri nalo kutoka jijini Kigali nchini Rwanda. Nikaendelea kuyachunguza mandhari yale hata hivyo sikuweza kuona ziada nyingine na badala yake kadiri tulivyokuwa tukitokomea mbali na eneo lile ndivyo taswira ya lile jengo la ghorofa na mandhari yake ilivyokuwa ikitoweka machoni mwangu. Kutokana na miti mingi mikubwa na mirefu iliyokuwa imepakana na ile barabara hafifu ya magari iliyotawaliwa na mawe mengi madogomadogo na vichaka vya nyasi ndefu kando yake. Hatimaye ile taswira ya lile jengo la ghorofa na mandhari yake ikatoweka kabisa machoni mwangu.
Nikiwa bado nipo uchi huku nimefungwa mikono na miguu yangu mara baada ya taswira ya lile jengo la ghorofa na mandhari yake kutoweka machoni mwangu nikageuka kuwatazama wale wanajeshi niliokuwa nimekaa nao kule nyuma ya gari. Kwa kufanya vile nikakutana na macho yao makali yaliyonionya huku wakionekana kucheza vizuri na nyendo zangu. Sikuwasemesha neno lolote badala yake nikamtazama kila mmoja na kutabasamu kama mwendawazimu. Hata hivyo sikufanikiwa kuzilainisha nyuso zao kwani wale wanajeshi walionekana wapo kikazi zaidi huku sura zao wamezikaza kama ambao wapo kwenye gwaride la heshima. Sikuipenda hali ile ya ukimya kwa vile sikujua nini walichokuwa wakiniwazia vichwani mwao. Hivyo kwa kutaka kuilainisha mioyo yao nikawauliza.
“Où allons-nous?”. Tunaelekea wapi?. Nikawauliza wale wanajeshi huku nikiendelea kutabasamu hata hivyo hawakunijibu badala yake wakanitazama kama jiwe la barabarani. Sikuwasemesha tena badala yake nikageuka tena na kutazama nje kupitia dirishani.
Tulikuwa tukisafiri kwenye kipande cha barabara ya msituni yenye vichaka hafifu na miti mikubwa kando yake huku nikijaribu kuchunguza kama kungekuwa na nyumba yoyote ya jirani na eneo lile. Sikuona nyumba nyingine na lile eneo ni kama lilikuwa limejitenga. Hatimaye nikageuka na kutazama kule mbele ya gari na hapo nikamuona Amanda ndiye aliyekuwa akiendesha lile gari huku Meja Pascal Karibwami akiwa ameketi kwenye siti ya abiria kando yake. Hata hivyo hakuna aliyemsemesha mwenzake hali iliyopelekea mle ndani kutawaliwe na ukimya wa kushangaza utasema tulikuwa tukielekea kwenye msiba mkubwa uliotushtua sana.
Nikamchunguza Amanda na kugundua kuwa alikuwa dereva mzuri na makini sana kuliko vile nilivyokuwa nikimchukulia wakati ule tulipokuwa tukisafiri kutoka stendi ya mabasi ya Nyabugogo jijini Kigali nchini Rwanda.
Amanda alikuwa amenisaliti na kuniuza kwa bei nafuu kwa watu wale hatari bila kulifahamu kosa langu ingawa hadi kufikia pale nilianza kuamini kuwa Amanda naye alikuwa mwanajeshi wa jeshi la wananchi wa Burundi kwani vinginevyo sikuona mahusiano mengine kati ya wale watu hatari na Amanda. Mazingira ya mle ndani yakanieleza kuwa sikuwa sehemu salama tena na kwa vyovyote vile hisia za wale watu bila shaka zilikuwa zimejikita katika kuamini kuwa mimi ni jasusi kutokana na zile nyaraka muhimu zilizokuwa kwenye begi langu kwani niliamini kuwa Amanda angekuwa tayari amewaonesha wale watu. Hivyo kwa tafsiri ya haraka ni kuwa nilikuwa nikipelekwa sehemu fulani kufanyiwa mahojiano ya kulazimishwa nizungumze kuwa mimi ni nani na nilikuwa nimefika pale nchini Burundi kufanya nini. Kwa kweli niliingiwa na hofu, wasiwasi na mashaka pale nilipowaza kuwa nilikuwa nikielekea kukabiliana na kifo cha mateso makali. Hatimaye nikameza funda kubwa la mate kuikabili hofu ile.
Baada ya safari ndefu kidogo ile barabara ikachepuka upande kulia na kuanza kushuka mteremko mkali wenye barabara mbovu yenye mashimomashimo. Hata hivyo Amanda alijitahidi kwa kila hali kuumudu usukani wa lile gari na baada ya muda mfupi tukawa tumetokezea kwenye barabara ya lami. Tayari kulikuwa kumepambazuka na jua la asubuhi lilikuwa limeanza kuchomoza hali iliyonipelekea niweze kuona kwa unafuu zaidi nje ya lile gari.
Mara tu tulipoingia kwenye ile barabara ya lami tukashika uelekeo wa upande wa kushoto wa ile barabara tukisafiri katika mwendo wa kasi na wakati wote nilikuwa makini kuchunguza mandhari ya barabara ile. Kitu pekee kilichonishangaza ni kuwa wakati tukisafiri katika barabara ile njiani hatukupishana na gari hata moja. Baada ya mwendo mfupi wa safari yetu hatimaye tukaja kukutana na barabara nyingine ya lami ambayo ilikuwa kubwa zaidi ukifananisha na ile tuliyotoka. Mara tu tulipoingia kwenye barabara ile tukaanza kupishana na magari mengi kiasi lakini yakiwa katika mwendo kasi kana kwamba hapakuwa na kituo ama makazi ya watu karibu na eneo lile.
Upande wa kushoto wa barabara ile niliona mabango matatu makubwa ya matangazo. Bango la MTN, bango la benki ya wananchi wa Burundi na bango lingine la kampuni ya mawasiliano ya Airtel. Nikakumbuka kuwa kabla ya kufika pale Bujumbura nchini Burundi, Amanda alikuwa ameniambia kuwa angefikia mtaa wa Boulevard de 1er Novembre jijini Bujumbura. Hivyo nilijitahidi kwa kila namna kuchunguza kama kungekuwa na kiashiria chochote kuwa pale ni wapi. Hata hivyo lilikuwa jambo gumu kwani Amanda alikuwa akiendesha lile gari kwa kasi sana kiasi kwamba sikupata nafasi nzuri ya kufanya uchunguzi wangu kwa wepesi.
Njiani tulikutana na vijana wengi waliokuwa wakiimba nyimbo nyingi za kizalendo za nchi ya Burundi huku wakilisifu jeshi la wananchi wa Burundi kwa kufanya jaribio la mapinduzi ya kijeshi. Huku mikononi wakiwa wameshika matawi ya miti na kuyapunga hewani kwa furaha. Wale vijana walipokuwa wakiliona lile gari letu la kijeshi wakawa wakilishangilia kwa furaha huku wakilipisha bila upinzani wowote. Kupitia tukio lile nikajifunza kitu kuwa wananchi wa Burundi hususan vijana wengi walikuwa wameshachoshwa na utawala uliokuwa madarakani wa serikali ya nchi ile.
Baada ya muda mfupi wa safari yetu mara nikaanza kuhisi kuwa tulikuwa tukishika uelekeo wa katikati ya jiji la Bujumbura kwani kadiri tulivyokuwa tukiendelea na ile safari nikawa nikiyaona majengo marefu ya ghorofa na makazi ya watu yaliyopangwa vizuri kando ya barabara ile. Nilipochunguza vizuri kupitia dirishani nikawaona polisi wa Burundi wakiwa wametanda kila kona katika namna ya kukabiliana na maandamano yale huku wakitumia mabomu ya machozi, mbwa wakali wa polisi na magari yenye maji ya kuwasha. Hata hivyo wale polisi hawakutuwekea kizuizi cha namna yoyote badala yake wakawasalimia wale wanajeshi walioniteka na kuturuhusu tuendelee na safari yetu.
Zile dawa za kutuliza maumivu alizokuwa amenipa Amanda mapema alfajiri ile zilikuwa zimenisaidia kwa kiasi kikubwa. Kwani yale maumivu ya kichwa yalikuwa yamepungua sana na sasa nilianza kuhisi kuwa kichwa changu kilikuwa kimeanza kuwa chepesi ingawa njaa tumboni bado ilikuwa ikiniuma sana. Safari yetu bado iliendelea na kwa tathmini yangu dhidi ya mandhari ya barabara ile ni kuwa bado tulikuwa mbali na jiji la Bujumbura, kwani tulifika sehemu tukawa mbali kabisa na yale makazi ya watu. Ingawa bado niliweza kuyaona yale majengo marefu ya ghorofa yakiwa mbali kidogo na barabara ile.
Ile barabara kando yake ilikuwa imepakana na miti mizuri ya kivuli iliyopandwa katika utaratibu unaopendeza ingawa bado sikuweza kumuona mtu yeyote akitembea kwa miguu kando ya barabara ile. Ile barabara ilikuwa ngeni kabisa machoni mwangu. Labda ningeweza kuufahamu uelekeo ule endapo ningekuwa na ile ramani yangu ndogo ya kijasusi. Hivyo ilifika sehemu nikashindwa kabisa kuelewa kama tulikuwa tukielekea katikati ya jiji la Bujumbura au tulikuwa tukitokomea mbali na jiji lile.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya mwendo wa safari usiopungua muda wa nusu saa hatimaye tukaja kukutana na kizuizi cha mawe makubwa matano yaliyokuwa yamepangwa barabarani, katikati ya daraja kubwa la barabara ile ambapo mto mkubwa ulikuwa ukikatisha eneo lile. Haraka nikayapeleka macho yangu kutazama mawe yale makubwa mfano wa majabali huku nikikikumbuka kile kizuizi cha mawe cha kule msituni barabarani yalipotokea yale mauaji ya abiria wenzetu wakati tulipokuwa tukitoka jijini Kigali nchini Rwanda. Hata hivyo sikutarajia tukio kama lile kutokea katika mazingira kama yale.
Yale mawe yalikuwa yamepangwa katikati ya lile daraja hivyo tulipofika pale tukasimama na nilipochunguza upande wa kushoto wa ile barabara nikashtuka kuiona maiti moja ya mwanaume ikiwa imetelekezwa kando ya ile barabara. Huku maiti ile ikionekana kuwa na majeraha makubwa ya risasi kichwani. Hapakuwa na mtu yoyote eneo lile na kwa namna fulani uwepo wa ile maiti ya mtu eneo lile ulinitia mashaka. Niliendelea kulichunguza eneo lile kwa tahadhari na hapo nikaona magurudumu mengi ya magari yalikuwa yamewashwa moto na kutelekezwa ovyo eneo lile huku yakiendelea kuteketea taratibu na hivyo kufukiza wingu kubwa la moshi mweusi angani. Kulikuwa pia na vipande vya magogo makubwa ya miti pamoja na chupa nyingi zilizokuwa zimevunjwa eneo lile. Kwa tathmini ya haraka ni kuwa muda mfupi uliopita sehemu ile ilikuwa imeshuhudia rabsha za aina yake. Bila shaka mvua kubwa ilikuwa imenyesha usiku wa kuamkia siku ile kwani ule mto ulikuwa umejaa na maji yake yalikuwa yamevurugika kwa tope zito lililokokotwa kutoka sehemu mbalimbali za mto ule na hivyo kuyafanya maji yale yawe makendu na yanayosafari kwa kasi mno.
Amanda akawahi kusimamisha gari haraka umbali wa hatua chache kabla ya kile kizuizi cha yale mawe mbele yetu. Kisha yule mwanajeshi mwenye cheo cha Koplo ambaye hapo awali alikuwa amejitambulisha kwangu kwa jina la Koplo Adolphe Sahinguvu. Ambaye pia alikuwa miongoni mwa wale wanajeshi wawili waliokuwa nyuma ya lile gari wakinilinda. Haraka akafungua ule mlango wa nyuma wa lile gari na kushuka kisha akaanza kuelekea kule mbele kulipokuwa kumewekwa kizuizi cha yale mawe.
Hatua zake zilikuwa za hakika na nilipoendelea kumchunguza nikamuona akiingiza mkono nyuma ya kiuno chake na kuchomoa bastola ambapo aliikamata vyema mkononi. Koplo Adolphe Sahinguvu alipoyafikia yale mawe yaliyopangwa kule mbele kuzuia ile barabara akatazama tazama huku na kule kisha akaanza kuyaondoa yale mawe moja baada ya jingine akiyasogeza kando ya ile baabara na sote tuliokuwa ndani ya lile gari tukajikuta tukimtazama...
...Hata hivyo nikagundua kuwa yale mawe kutokana na ukubwa wake yalikuwa mazito mno. Hivyo kasi ya Koplo Adolphe Sahinguvu ya kuyatoa yale mawe pale barabarani ilikuwa ndogo mno huku akitumia nguvu nyingi. Ukimya ukaendelea kutawala mle ndani huku sote tukiendelea kumtazama Koplo Adolphe Sahinguvu namna alivyokuwa akikukurika na zoezi lile. Hata hivyo yule Koplo Adolphe Sahinguvu alipofanikiwa kuliondosha jiwe la pili nikamuona akihema ovyo huku akionekana kuanza kukata tama na zoezi lile. Muda mfupi baadaye nikamuona akisimama kwa uchovu huku amejishika kiunoni akihema ovyo. Baadaye taratibu nikamuona akigeuka na kutazama pale tulipoegesha lile gari na hapo nikamuona akinyoosha mkono na kuanza kuita kwa kiganja chake katika namna ya kuonesha kuwa alikuwa akiomba msaada kwa mwenzake.
Tukiwa mle ndani ya lile gari kila mtu akaoneka kuelewa vizuri maana ya wito ule. Tukio lile likampelekea yule mwanajeshi mwenye cheo cha Staff Surgent ambaye hapo awali alikuwa amejitambulisha kwangu kwa jina la Anatole Nkunda. Ambaye pia wakati ule ndiyo alikuwa amebakia peke yake kule nyuma akinilinda, ageuke haraka na kunitazama na hapo macho yake makubwa na mekundu yaliyohifadhi kumbukumbu ya kila unyama yakanionya. Muda uleule nikamuona Staff Surgent Anatole Nkunda akiichomoa bastola yake kutoka mafichoni katika gwanda lake la kijeshi kisha taratibu akauelekeza mdomo wa ile bastola yake katikati ya paji langu usoni huku ameikaza sura yake kama aliyepigwa ngumi ya mgongo. Halafu kwa sauti ya kunong’ona yenye chuki akaniambia.
“Ne pas déplacer, chaque étape a une seule balle”. Usithubutu kusogea, kila hatua yako moja ina risasi yake. Lilikuwa onyo la dhahiri lisilohitaji ufafanuzi. Staff Surgent Anatole Nkunda kweli alikuwa akimaanisha na kwa kutaka kunihakikishia juu ya onyo lake akanichapa kofi moja la usoni kisha ni nikamuona akiingiza tena mkono wake mfukoni na kuchukua mfuko mweusi wa nguo na kunivalisha kichwani. Nilijitahidi kwa kila namna kupingana na kitendo kile nikikiyumbisha yumbisha kichwa changu huku na kule katika namna ya kumpotezea malengo yule mtu. Lakini hata hivyo sikufanikiwa badala yake nikajikuta nikikabiliana na maumivu makali ya makofi mawili ya nguvu niliyozabwa shingoni na kunipelekea nihisi kutaka kutapika huku ule mfuko tayari ukiwa umevalishwa vizuri kichwani mwangu.
Mara baada ya yule askari kumaliza kunivisha ule mfuko muda uleule nikamsikia akishuka chini kule nyuma gari tulipokuwa na hapo nikajua kuwa alikuwa akienda kule mbele ya gari kumsaidia yule mwenzake kuyaondoa yale mawe yaliyowekwa barabarani. Tukio lile likaamsha hisia mpya kichwani mwangu na hapo wazo fulani likatumbukia katika fikra zangu na kunipa mzuka wa matumaini. Uzoefu katika harakati nyingi za kijasusi nilizowahi kushiriki au kuzishuhudia ni kuwa hukumu ya mtu yeyote anapokamatwa akifanya ujasusi katika nchi nyingine huwa ni kifo, tena kifo chenyewe huwa ni cha mateso makali na ya kinyama yenye kutaabisha mwili, nafsi na roho. Hivyo mara tu jasusi anapokamatwa tumaini lake pekee huwa ni katika kutoroka na hivyo kupelekea kila nafasi ya kutoroka inayojitokeza kuwa ni hatua ya muhimu kwake katika kuepukana na kifo cheye uchungu wa mateso makali.
Hivyo nilifahamu fika kuwa mwisho wa safari ile nilikuwa nikienda kukabiliana na kifo chenye uchungu na mateso makali baada ya mahojiano ya kina na kwa kweli sikupenda kwenda kufa kifo cha kondoo mpole huku nimeinamisha kichwa chini. Kwanza sikutaka kufa mapema huku kazi niliyotumwa nikiwa hata kuianza sijaianza kwani huo ndiyo ungekuwa upumbavu nambari moja. Suala la kifo kwangu haikuwa hoja ya kunishtua kwani ni dhahiri kuwa kila mtu atakufa hapa duniani apende au asipende. Lakini kufa huku nikiwa sijafanikiwa kutekeleza hata sehemu tu ya kile nilichokuwa nimetumwa kukitekeleza ilikuwa ni zaidi ya hoja kubwa katika maisha yangu. Kamwe sikuogopa kufa lakini kufa kifo cha mbinde au kufa kijerumani na tai shingoni kwangu ilikuwa ni heshima kubwa zaidi ya ile ya buti zangu za kijeshi na ile bendera kubwa ya taifa kulifunika jeneza langu wakati wa safari yangu ya mwisho kuelekea kaburini itakapofanyika hapa duniani.
Kwangu jambo muhimu lilikuwa ni kucheza na muda vizuri bila kuipuuza akili ya adui yangu. Hivyo wakati yule Staff Surgent Anatole Nkunda akishuka kwenye gari na kuniacha kule nyuma peke yangu sikutaka kupoteza muda. Kwa maana nyingine ni kuwa sikuona kama kungekuwa na nafasi nyingine nzuri kama ile katika kutimiza mpango wangu. Japokuwa nilikuwa nimefunikwa ule mfuko mweusi wa nguo lakini tayari taswira ya mandhari yale ilikuwa imenasa vizuri katika fikra zangu. Bila kupoteza muda nikaanza kuzifungua haraka zile kamba za mikononi mwangu kwa msaada wa meno. Lakini wakati nikiwa katikati ya harakati zile mara nikahisi kuwa miongoni mwa wale wanajeshi wawili walioenda kuyaondoa yale mawe barabarani kule mbele kwenye lile daraja mmoja wapo alikuwa akirudi ghafla kule nyuma ya gari nilipokuwa.
Huku hofu ikiwa imeanza kuniingia sikuona kama lingekuwa ni jambo la busara kuendelea kusubiri badala yake haraka nikajilaza chini pale nilipokuwa kwenye lile gari kisha taratibu nikaanza kujiviringisha nikiangukia nje chini ya lile gari. Bado nilikuwa na kumbukumbu nzuri juu ya mandhari yale niliyoipata kabla ya kuvalishwa ule mfuko mweusi. Hivyo nikatua chini ya lile gari pasipo kusababisha mshtuko wowote kisha kwa kasi ya gurudumu la gari haraka nikajiviringisha nikipotelea chini ya lile gari huku nikiwa uchi wa mnyama na mikono na miguu yangu bado ikiwa imefungwa kwa kamba na ule mfuko mweusi umevalisha kichwani mwangu. Nikiwa chini ya lile gari niliweza kuzikia vizuri hatua za yule mtu aliyekuwa akirudi kule nyuma ya lile gari.
Huku nikifahamu fika kuwa muda siyo mrefu siri yangu ya kutaka kutoroka ingefichuka baada ya yule mtu kufika kule nyuma ya gari na kunikosa sikutaka kupoteza muda. Kwa mujibu wa kumbukumbu kichwani mwangu ni kuwa ule mto uliokuwa ukikatisha chini ya lile daraja ulikuwa ukitokea upande wa mashariki ukisafiri kuelekea upande wa magharibi na kutoka pale nilipokuwa sikuwa mbali na kingo ya lile daraja la ule mto kwa upande ule wa magharibi. Hivyo sikuwa na muda wa kusibiri zaidi badala yake nikaanza tena kujiviringisha nikitokea chini ya lile gari kuelekea kwenye kingo moja ya lile daraja huku shughuli za mwili wangu bado zikiendeshwa kwa hisia kwani kichwani bado nilikuwa nimefunikwa na ule mfuko mweusi wa nguo.
Muda uleule mara nikasikia sauti mbaya ya risasi umbali mfupi kutoka pale nilipokuwa hata hivyo sikusita katika dhamira yangu badala yake nikaongeza kasi zaidi katika kujiviringisha na kuelekea kwenye kingo ya lile daraja. Risasi ya pili iliyofyatuliwa ikauparaza kidogo ule mfuko mweusi niliovalishwa kichwani kisha ikagonga chuma kimoja cha lile daraja na kusababisha ukulele mbaya masikioni mwangu. Risasi ya tatu huwenda ilikuwa na shabaha makini zaidi lakini mlengaji yule hakuwa makini kwani niliisikia ikichana anga bila matokeao yoyote nyuma yangu huku mimi nikiwa tayari nimeshaifikia kingo ya lile daraja na kujiachia kwenye yale maji mengi ya ule mto yaliyokuwa yakisafiri kwa papara za aina yake.
Kufumba na kufumbua nikawa nimemezwa na yale maji na kupotelea ndani ya ule mto. Nilikuwa nimefanya uamuzi wa ujasiri na wa hatari sana kwa kujitosa ndani ya ule mto hata hivyo sikuwa na namna kwani niliiona kuwa ile ndiyo ingekuwa namna pekee ya kujiokoa kutoka katika mikono hatari ya wale watu. Yale maji yakanisomba na kunizamisha chini kabisa ya ule mto sehemu ambayo japokuwa sikuwa na kipimo maalum lakini niliweza kuhisi kuwa nilikuwa kwenye kina cha zaidi ya futi kumi na tano kwenda chini. Yale maji yalikuwa na nguvu mno na kule chini ya ule mto kulikuwa na mawe hali ambayo ilikuwa hatari sana kwangu kwa vilevile mikono na miguu yangu bado ilikuwa imefungwa huku kichwa changu kimefunikwa kwa ule mfuko mweusi.
Nilijigonga begani kwenye jiwe moja huku yale maji yakinisomba na kunipigiza magongoni kwenye jiwe la pili na kufanikiwa kunichana upande wa kushoto wa mgongo wangu. Jiwe la tatu lenye ncha kali likanichana nyuma ya paja langu la mguu wa kushoto na kunisababishia jeraha lenye maumivu makali sana. Hata hivyo sikuwa na namna kwani yale maji yalikuwa yakinikokota ovyo katika namna yalivyotaka.
Huku nikiwa nimeanza kuingiwa na hofu ya kujeruhiwa vibaya na yale mawe hatari chini ya ule mto nilijitahidi kujitetea kwa kila namna lakini kitendo cha miguu na mikono yangu kuwa imefungwa kilininyima ushindi wa haraka. Hivyo nikawa nikiendelea kusombwa na yale maji huku mikono yangu nikiwa nimeitanguliza mbele katika namna ya kukipa ulinzi kichwa changu. Hata hivyo kadiri muda ulivyokuwa ukizidi kusonga nikawa naanza kuhisi kuishiwa na pumzi ya kuzidi kutabaruku ndani ya yale maji mengi ya ule mto yenye kuzizima.
Woga wa kifo ukiwa umeanza kuniingia nikawa nikijitahidi kupapasa huku na kule kutafuta jiwe ambalo ningelishikilia kikamilifu ili yale maji ya ule mto yasiendelee kunisomba zaidi na kunipeleka kule mbele ya ule mto. Hata hivyo mahesabu yangu ni kama yalikuwa yamegonga mwamba kwani kule mbele kadiri ule mto ulivyokuwa ukizidi kutokomea ndiyo yale mawe yalivyokuwa yakizidi kuwa madogo zaidi kiasi kwamba hayakuwa na msaada wowote. Badala yake yale mawe yalikuwa yakizidi kumezwa na mchanga laini wa chini ya ule mto na hali ile ikanifanya nizidi kukata tamaa ya kutoka salama kwenye ule mto wenye maji mengi.
Nilikuwa nimesafirishwa umbali mrefu na yale maji ya ule mto huku pumzi ikiwa mbioni kuniishia pale nilipojikuta nimenasa kwenye kitu fulani nisichokijua. Nilipojaribu kupapasa vizuri nikagundua kuwa nilikuwa nimenasa kwenye gogo kubwa la mti lililokuwa likiteleza sana kutokana na kukaa kwa muda mrefu kwenye yale maji. Kwa kweli ilikuwa ni bahati ya kipekee ambayo kamwe haikuwa katika fikra zangu. Matawi yaliyopishana ya lile gogo yalikuwa yamekinasa kiwiliwili changu na hivyo kunizuia nisiendelee mbele. Hivyo nikaileta ile mikono yangu mdomoni na kuanza kuzifungua zile kamba mikononi mwangu na kwa kuwa zoezi lile nilikuwa nimelianza muda mfupi kabla ya kujitumbukiza katika ule mto zile kamba hazikunipa upinzani mkubwa.
Ndani ya muda mfupi nikawa nimemaliza kuzifungua zile kamba na kuiacha mikono yangu huru kisha haraka nikajivua ule mfuko mweusi wa nguo kichwani mwangu. Kitendo cha kujivua ule mfuko kikanifanya niweze kuhisi vizuri wingi wa yale maji ya ule mto. Yalikuwa maji mengi sana labda ningeweza kuufananisha ule mto na mito kama mto Kilombero wa mkoani Morogoro au mto Rufiji mkoani Pwani nchini Tanzania. Kwani kulikuwa na mito mingine midogomidogo iliyokuwa ikitiririsha maji yake katika mto ule.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nikiwa bado nimenasa kwenye tawi la ule mti nikajipinda na kuanza kujifungua haraka zile kamba za miguuni na kwa kweli mapafu yangu yalikuwa yakihangaika ovyo kutafuta hewa. Nilikuwa nimetumia muda mwingi ndani ya yale maji na endapo ningeendelea kukaa zaidi mle ndani ya mto basi muda siyo mrefu ningeishiwa nguvu na hatimaye kupoteza maisha. Baada ya hangaika hangaika ya hapa na pale hatimaye nikafanikiwa kuzifungua zile kamba za miguuni na hivyo kujinasua kutoka kwenye lile tawi la mti. Yale maji ya mto yalikuwa na nguvu sana na kule mbele ule mto ulikuwa umezidi kutanuka na bila shaka kina chake cha maji pia kuongezeka.
Sikuwa na nguvu za kutosha za kuendelea kupambana zaidi na yale maji istoshe pumzi nayo ilikuwa mbioni kuniishia hivyo niliamua kulitumia lile gogo kama nyenzo muhimu ya kujiokoa. Nikayakamata vizuri matawi ya lile gogo nikiyatumia vizuri kujitafutia sehemu nzuri ya kulikumbatia lile gogo la ule mti. Muda mfupi uliofuata nikawa nimefanikiwa kupanda juu ya lile gogo na hapo nikalikumbatia vizuri na kuanza kusota nalo taratibu nikiitumia miguu na mikono yangu kujivuta. Ilikuwa ni kazi ngumu na ya hatari kwani lile gogo katika baadhi ya maeneo yake lilikuwa limekwishaanza kuoza na lilikuwa likiteleza sana. Lile gogo lilikuwa ni la mti mkubwa wa mvule uliokuwa kando ya ule mto. Mmomonyoko mkubwa wa udongo kando ya ule mto uliosababishwa na maji mengi ulikuwa umetia udhaifu mkubwa katika mizizi na shina la ule mti na hivyo kuupelekea ule mti kuangukia ndani ya ule mto huko siku za nyuma.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment