Simulizi : Shujaa Wa Taifa
Sehemu Ya Tano (5)
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hakuwa na namna mama huyo hivyo ikabidi na yeye arudi ndani kumsikiliza waziri huyo ana nini la kuongea naye.
Akaongozana nao hadi sebuleni na kuketi.
“sasa mheshimiwa hakuna lingine lililonileta hapa Zaidi ya kuongea na wewe kwa mara ya mwisho tujue unaungana na sisi kwenye hoja yetu au laa” banguli akaanza kuongea huku uso wake ukionesha hauna masihara.
“mkuu kumbe mimi bado hujanielewa ee, nimeshasema kule bungeni siitaki ile mada naipinga haina manufaa kwa wananchi wetu kwanini lakini tuitumikie? Wakati ni Dhahiri itakuwa na hasara nyingi kuliko faida” mwanamama huyo akaendelea kuonesha msimamo wake.
“sikia unajua sisi tunaweza tukaipitisha hoja ile kivyovyote, so usione kuja kwetu hapa basi tumejishusha sana, sasa ngoja tuone utaenda kuongelea wapi. Watu tunakufata kistaharabu hutaki kuelewa, wewe ni wa kifo tu, mkataa pema pabaya panamuita” akaongea banguli huku akisimama.
Mara muda huo huo fetty diva aliyepo chumbani ambapo alikuwa akisikia maongezi hayo akajisogeza taratibu na kujibanza kwenye pembe ya ukuta kujaribu kutazama ni kipi kinachoendelea.
Akaanza kuangalia kwa kuchungulia!
Akamshuhudia waziri huyo akiomba gloves na kuzivaa kwenye viganja vyake vya mikono.
Kwa uchungu na masikitiko makubwa fetty diva akashuhudia mama yake akizibwa mdomo na kukabwa koo.
Kukabwa huko kulifuatia na kutapa tapa kwa mama huyo.
Aliendelea kutapatapa kwa kurusha miguu yake huku na kule hadi pale roho yake ilipoachia mwili wake.
Fetty alilia kwa uchungu huku sauti ikiwa haitoki ni baada ya kushuhudia mauaji hayo ya kikatili yaliyokuwa yakiendelea mbele ya macho yake. Alitamani aende kupambana nao lakini alijua lazima watamuua tu na yeye hivyo akabaki ametulia hapo hadi watu wale walipomaliza na kuondoka.
Ndipo akamsogelea mama yake na kuanza kulia kwa uchungu.
Hata wadogo zake pia walivyorudi kutoka shule ambapo walikuwa ni wanafunzi wa kidato cha tatu waliushuhudia msiba huo mzito.
Hakika walilia hadi tone la mwisho.
Taarifa za kifo cha mama huyo kikasambaa nchi nzima ya zambe na vyombo mbalimbali vya habri vikawa na habari hiyo iliyosomeka kwa kichwa kikuu,’MBUNGE AUAWA KIKATILI’.
Viongozi mbalimbali wa kisiasa pamoja na wananchi walisikitisghwa mno na msiba ule, na hata wengine walielezea hali hiyo wazi wazi kwenye mitandao ya kijamii.
Kila mahali habari ndio ikawa hiyo na taifa kwa ujumla likasikitika.
Maiti hiyo ilipelekwa hospitali kwa ajili ya uchunbguzi n ahata baadae taarifa ikatoka kuwa mama huyo kafa kwa kukosa hewa baada ya kukbwa kwenye koo. Hapo ndipo maiti hiyo ikakabidhiwa kwa familia na mazishi yaliohudhuriwa na wanasiasa na viongozi mbalimbali akiwemo banguli yakafanyika.
Fetty alitamani mno amrukie banguli kila alipokuwa akimuona kwenye msiba huo. Na hata kuna muda alimjia juu kwakuitoboa siri yake ya mauaji kipindi mheshimiwa huyo akiwa katika orodha ya waagaji.
“umefurahi ee kuiondoa roho ya mama yangu, si ndio?” aliongea kwa jazba kumuelekea banguli asiye na chembe hata ya aibu.
“jaman huyu ndiye aliyemuua mama yangu huyu, kwa macho yangu nimemshuhudia, kwanini hayupo gerezani badala yake yupo hapa, tena anashiriki mazishi ya aliyemuu?” fetty akaendelea kulalama kwa jazba.
Askari wakamzuia binti huyo kwa kumshika na kumtoa eneo hilo. Bado japokuwa alitolewa lakini aliendelea kupaza sauti kuachia maneno hayo.
Watu wakabaki vinywa wazi na kuna walioyaamini maneno ya mwanadada huyo lakini kuna pia waliyoyapuuza na kuona tu ni kuchanganyikiwa kwa kumkosa mama yake aliyempenda sana. Swali lililobaki katika vichwa vya wengi ni vipi fetty awaache watu wote waliopo msibani hapo na amfuate kiongozi huyo? Ikabaki kuwa lisemwalo lipo.
Mazishi yakapita salama lakini banguli akaingiwa wasiwasi baada ya kugundua kuwa binti yule amefahamu mchezo mzima wa mauaji yale. Hivyo harakati za kumpoteza binti huyo zikaanza.
Fetty diva akatonywa mchezo mzima kuwa si salama kwa yeye kuendelea kuishi katika nyumba ile kwani yaweza kuwa ni hatari kwake, eidha ahame mji au nchi kabisa.
Hapo ndipo uamuzi wa kuiama nchi hiyo ukamjia.
Huku akisaidiwa na kiongozi wa chama cha upinzani akafanikiwa kukatiwa tiketi kwenda kuishi nchi ya kinte yeye na wadogo zake.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Bila kuchelewa mpango huo wa siri ukafanywa na hapo ndipo mwanadada huyo na wadogo zake wakahamia nchi ya kinte.
Ndipo wakatafuta makazi yao pembezoni mwa bahari inayotenganisha nchi hiyo ya kisiwa pamoja na nchi ya zambe. Kwa msaada wa kiongozi huyo wa upinzani kwa kusaidiana katika shida mbalimbali aliweza kuishi Maisha yasiyo na bughuza katika mji huo.
***
“basi hivyo ndivyo ilivyokuwa” mwanadada fettydiva aliongea huku tayari machozi yakiwa yashalowanisha uso wake baada ya kuimazliza hadithi hiyo yenye kugusa mno.
Historia ile ilimgusa sana D’oen akaanza kumbembeleza mwanadada huyo.
“na hivyo huku tunaishi kimatumaini ipo siku tutalipiza kisasi, mimi na ndugu zangu hawa, hatujajiweka kilele mama hivyo tumeamua kujifunza mbinu mbalimbali za kivita, na tuna Imani tutamuondoa gaidi yule aliyepoteza furaha yetu” akaongea fetty akionesha bado chuki kwa banguli.
“mbegu walioipanda wenyewe hakika itawarudia” aliongea D kwa masikitiko,”na mimi zile risasi mlizozitowa katika mwili wangu si mwingine aliyesababisha bali ni huyo huyo banguli”
Fetty akashtuka mara baada ya kauli hiyo ya D’oen!
‘unamaanisha amekupiga hadi wewe mwanajeshi wa taifa lao? Mimi nilidhani umevamiwa na majambazi”
“hapana ni yeye, nchi imeenda katika hali mbaya sana” D’oen akaongea nah apo ndipo akampa story nzima za hadi yeye anapigwa risasi zile. Fetty diva alishtuka mno na alilia sana kuisikitikia nchi yake.
Basi wakaungana kuwa wamoja na kuhakikisha lazima waikomboe nchi hiyo.
Mafunzo makali ya kivita wakayaanza yakiongozwa na D’oen kuhakikisha santos na barnabas wanaiva kwa ajili ya kwenda kufanya ukombozi wa nchi yao.
Baada ya kuhakikisha wameiva ndipo wakaanza sasa mikakati ya kuivamia nchi hiyo.
Wakatoa ramani ya nchi hiyo na sehemu nzuri ya kuingilia waliona ni mashariki mwa nchi hiyo kwani ndio wapo karibu napo.
Waliuchagua mji wa kitibi na mbinu yao ya kwanza ilikuwa ni kuua viongozi wa serikali tu pamoja na askari kimya kimya kwani kuuliwa kwa hao wangepelekea kupatikana kwa banguli n ahata Hambabe.
Mbinu ya pili ilikuwa ni kuteka wanamume wote kuanzia miaka 18 na kuendelea, lengo ni kuwahamasisha kuhusu movement ya kuikomboa nchi yao na hata watakapoamua kujitokeza basi wawe na jeshi kubwa la wananchi.
Mbinu ya tatu ni mwanadada fetty diva yeye abaki katika mji wa nchi ya kinte acheze na akili za wananchi kwenye mitandao. Yaani awaamasishe kupambania haki, ikapangwa na tarehe ambayo fetty atahamasisha maandamano ya nchi nzima ndio siku ambayo D’oen na jeshi lake watajitokeza live na kundi la wananchi.
Basi mbinu hizo zilipokamilika ndipo D’oen akiwa na santo pamoja na barnabas wakaamua kuingia katika mji huo mashariki ya nchi ya zambe.
Mauaji ya kimya kimya baada ya kuweka kambi katika mji huo ndio yaliyokuwa yakifuata. Askari wengi waliotumwa walifanikiwa kuuwawa na vijana hao kimya kimya na silaha zao kuchukuliwa. Mbinu ya pili nayo ya kukusanya wananchi ikafuatia ya kuteka wananchi wenye jinsia ya kiume na kuanza kuwahamasisha kuhusu ukombozi wa nchi na pia wakafundishwa jinsi ya kupambana kwa kutumia silaha.
D’oen akafanikiwa kumaliza hadithi nzima ya yeye kuwa hai, ni baada ya kuwaelezea timu yake walio na shauku ya kutaka kufahamu nini kilimpata mpaka kuonekana hai licha ya watu wote kujua amekufa.
Wote wakafurahi na ushindi ule walioupanga kwa takribani miaka mingi huko nyuma sasa wazi wazi uliweza kuonekana.
“kahiyo hao wananchi na vijana hao wawili wapo wapi?” tiffa akauliza
“ninao, kambi yetu si mbali na hapa yaani mkikohoa hapa kule tunasikia”
Kipindi wakiendelea na mazungumzo hayo mara miungurumo ya risasi ikaanza kusikika.
Wote wakashtuka!CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kila mmoja akaielekea silaha yake na kuingia vichakani kwa ajili ya kujihami.
D’oen akiwa anatembea mwendo wa tahadhari kujaribu kuangalia ni nini kinaendelea ghafla akapigwa teke la mgongoni lililomdondosha chini.
Teke ambalo linamtenganisha mbali na silaha yake.
Akasimama kikomandoo na kuangalia ni nani aliyempiga teke hilo.
Uso kwa uso na komandoo aliyekuwa akimtafuta kwa udi na uvumba kwa muda mrefu sana, ambaye alipelekea kifo cha Rafiki yake hance si mwingine ni komandoo msaliti Izzy.
Izzy akamnyooshea bastola D’oen.
Izzy akashtuka kidogo baada ya kumuona D’oen akiwa hai.
“kijana msaliti wa taifa lako na jeshi kwa ujumla leo ndio mwisho wako” izzy akaongea baada ya kumgundua aliyepo mbele yake ni D’oen.
D’oen akabaki akimwangalia izzy kwa hasira pima.
“siku zote anayeuwa huwa habagein kama ananunua nyanya vile ni kushoot tu, nakuruhusu piga risasi kama unaweza” D’oen akaongea huku akionesha kujiamini kwa hali ya juu.
Taratibu izzy akaweka silaha chini kisha akakunja mikono yake ishara ya kuhitaji wapigane ngumi.
“ona oen umeharibu cv yako wakati ilibidi uwe mtu muhimu sana katika jeshi, sasa hivi mimi sio mwenzio ni major sasa, sio mtu wa mchezo kabisa na niahidiwa ukuu wa majeshi, hiyo yote ni kwa sababu ya uzalendo wan chi yangu” aliongea izzy kwa majigambo
“uzalendo upi huo ambao unasababisha mwanajeshi mwenzako auwawe kwa manufaa yako binafsi? Leo ngoja nikuoneshe sasa faida ya usaliti” D’oen akaongea huku akikunja ngumi barabara.
Wakasogeleana!
Hapo ndipo izzy akarusha ngumi moja nzito iliyotua katika kidevu cha D’oen na kufanya acheue damu.
Kabla hajatulia D’oen akaongezwa na teke lengine lililotua kifuani kwake ambalo lilimfanya adondoke chini.
D’oen akajinyanyua chini kwa upesi kukwepa teke la izzy lililo na lengo la kumsaga pale chini. Akajipanga upya kwa ajili ya mashambulizi.
Izzy kwa speed ya light akarusha ngumi moja nzito lakini D’oen akaikwepa na kumuacha yeye na ngumi ya mbavuni.
“aaaaaah” izzy akatoa yowe kuonesha uchungu wa ngumi ile.
Akainama chini akiugulia ngumi ile ambayo ilikuwa ni mithili amepigwa na jiwe.
“njoo meja! Come on boy!” D’oen aliongea kiutani akimwita izzy huku akiwa ananesa nesa.
Izzy akaamka kwa nguvu na kumfuata D’oen kwa teke la hewani, lakini kabla halijatua tayari D’oen akalidhibiti teke lile kwa kulizuia kwa teke msimamo.
Izzy akaanguka chini kama gunia.
“oooh jaman meja pole sana” D’oen akaongea kumdhiaki izzy aliyedondoka chini na kuachia yowe la usingizi.
Izzy akaamka chini hapo kwa hasira, kwa upesi wa hali ya juu akachomoa kisu chake kutoka kwenye kiuno chake na kutaka kumshindilia D’oen katika shingo ni kama vile D’oen aliliwaza hilo akaudaka mkono huo na kuanza kumshindilia ngumi nyingi nyingi za mbavuni.
Ni kelele tu ndizo zilizokuwa zikitolewa na izzy.
Mara
“fyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu” risasi iliyopita mithili ya umeme na kugonga kwenye mti jirani nayo ikasikika.
D’oen akashtuka alipoangalia risasi ile ilipotokea ndipo aliona kundi la wanajeshi waliovaa mavazi ya jeshi la zambe wakizim imina risasai kuelekea upande wake.
Akamwacha izzy na kubinuka sarakasi kadhaa na kuifikia silaha yake akainyakua na kutokomea katika hali ya kimaajabu.
Wakafika eneo hilo na kumkuta mkuu wao akiwa hoi kwa kipigo.
Wakagawana majukumu, wengine wakambeba kiongozi huyo kumpeleka katika kambi yao na wengine wakazidi kuzama ndani kuendelea kumtafuta D’oen. Risasi tu ndizo zilikuwa zawadi zao za kushtukiza bila hata ya kujua mpigaji alikuwa eneo lipi.
Kimya kimya wanajeshi hao wakapoteza Maisha nah apo ndipo D’oen aliye na silaha akatokea.
Akaanza kupiga hatua kuelekea kwenye kambi yake kwenda kungalia wenzake wapo wapi.
Alipofika kwenye kambi hiyo alikuta miili ya wananchi ikiwa imetapakaa tayari roho zao zilishaomba pumziko kwa muumba wao. Hakuumia sana pale alipoziona na maiti za askari wa jeshi la taifa jeshi la banguli.
Akaweka ishara ya msalaba kifuani mwake kuwaombea wananchi wale waliokufa kwenye mapambano.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Upande wa mwanadada tiffa nae aliendelea kurushiana risasi na wanajeshi kadhaa aliokuwa akikutana nao, alikadhalika kwa makomandoo vilevile.
G master upande wake nae alishachanganyikiwa baada ya kuona maiti ya vijana wake aliokuwa akifanya nao kazi zikiwa zimepigwa risasi. Aliumia sana lakini hakukata tamaa aliendelea na mapambano, ambapo hali hiyo ndio ilizidi kumpa mshawasho wa kupambana na askari wale.
Akiwa anaendelea na safari taratibu kuwafuata maadui zake ndipo alihisi nyuma yake kuna mtu lakini kabla hajageuka tayari bastola ilishawekwa juu ya kichwa chake.
“usijaribu kutikisa hata ukope wa macho, tulia hivyo hivyo” sauti kutoka nyuma yake ikaongea.
Akajaribu kuitafakari sauti ya mtu huyo aliyesimama nyuma yake akiwa kamweka telo ilikuwa ikimjia kabisa kana kwamba alishawahi isikia sehemu flani lakini kumbukumbu ya huyo ni nani bado haikumjia kwa haraka.
“tembea mwendo huo huo usigeuke nyuma wala nini aya ongoza mbele” sauti ile ikaamrisha.
Akatii.
“haya simama hapo hapo” sauti ikaamrisha.
Akasimama!
“aya geuka!”
Akageuka!
Macho yake yalikutana na sura ngeni
“wewe ni nani?” G master akauliza
“haupaswi kujua Zaidi ya kutii amri ntakayo kuhamrisha” mtu huyo akaongea huku akiikoki silaha yake kwa uzuri.
“nyinyi ni wapumbavu sana mnaifanya hii nchi kama yenu sasa leo ntakuonesha cha moto nadhani utaenda kusimulia vizuri wauaji wenzako huko kuzimu mbwa wewe” mtu huyo akazidi kumpa wakati mgumu G master.
G master akabaki ameduwaa asijue la kufanya.
Mara
“hey usifanye hivyo acha!” ikasikika sauti ikipaza kumuelekeza mtu yule aliyemwelekezea bastola G master.
Ilikuwa ni sauti ya D’oen akimkataza santos ambaye ndiye amemweka telo G master.
“huyo ni mwenzetu, nilikuambia ukimwona mtu yeyote mwenye mavazi ya jeshi ndio sio mwenzetu lakini mwenye mavazi ya kiraia kama huyu ni mwenzetu” D’oen akaongea
Santos akashusha silaha yake chini.
Wakaungana na kuanza safari ya kuwatafuta wenzao, kwani siku hiyo ndio siku waliopanga na mwandada fetty diva kwamba kutakuwa na maandamano ya wananchi. Kwahiyo walitakiwa wajioneshe ili waweze kuungana na wananchi hao.
Hatimaye wote wakafanikiwa kukutana! Mwanadada tiffa, Zarish, barnabas, santos, D’oen,G master, makomandoo na wananchi waliobaki wakakutana kwa ajili ya kupanga kuungana na wananchi waliopo uraiani kupigania nchi yao.
“leo ndio siku ambayo nchii inaenda kuwa huru, kwahiyo tutatoka hapa wote kwa umoja wetu na kuingia mtaani kuungana na wananchi wengine ambao leo wapo kwenye maandamano, kulingana na strategy yetu kila mji lazima ushiriki maandamano hayo yenye lengo la kumuondoa banguli na HAmbabe. Tumeelewana?” D’oen akaongea akiwa amekusanya jeshi lake la ukombozi.
Wote wakaitikia huku wakiwa wenye furaha sana.
Wakati huo huo D’oen akiwa anaendeleza mazungumzo yale katika kikao kile mara mwanga mwekundu kuonesha kuwa alikuwa kwenye target ya silaha ukatembea tembea kulenga kifua chake.
Mwanadada Zarish ndiye pekee aliyeuona mwanga ule.
Akashtushwa na hali ile. Ndipo akajinyanyua kwenda kumsukuma D’oen ili hasiweze kudhuriwa na silaha ile lakini kabla hajamfikia tayari risasi kutokea kwenye silaha ile zikaachiwa…..
Taharuki kubwa ikazuka katika eneo lile mara baada ya mwanadada Zarish kudondoka chini kutokana na risasi zile zote kutua mgongoni mwake.
D’oen alipotupa macho zilipotokea risasi zile ndipo akamuona izzi akitokomea eneo hilo baada ya kuona shabaha yake haijafanikiwa.
D’oen akachukua bastola na kusogea eneo ya uwazi kisha kuanza kumrenga, na kama unakumbuka D’oen ni mtunguaji mzuri sana hivyo akafanikiwa kuachia risasi zilizotua kichwani mwa kijana huyo. Bila kuomba maji naye izzy akawa ameshakata roho.
Hilo likawa pigo kwa jeshi hilo liongozwalo na D’oen lakini haikuwazuia kuweza kuendelea na taratibu zao za kuikomboa nchi yao.
Wakaufunika mwili huo na kuuacha.
Wakaanza safari kuingia uraiani.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walipokuwa wakikutana na mtu yeyote mwenye mavazi ya kiaskari walikuwa wakishoot tu na kuendelea mbele kwa mbele kuelekea ofisi ya mkuu wa mkoa huo.
D’oen, tiffa na makomandoo pamoja na G master na santo pamoja na barnabas ndio walioongoza maandamano hayo huku wakiwa na silaha za moto, nyuma yao kundi kubwa la wananchi waliokuwa wakiimba nyimbo za ukombozi ndio waliokuwa wakija.
Wananchi walihamasishika kupitia mitandao ya kijamii nao waliungana na kundi hilo kadri lilivyokuwa linakatiza katika nyumba za watu.
Ule uoga wa siku zote wa wananchi hao ukawekwa pembeni wakaamua kuungana na lao kuwa moja. Na hata felix nae akiongoza kundi la waandishi wa habari wakaungana na kundi hilo kuelekea ofisi ya mkuu wa mkoa.
Hadi wanafika ofisi hiyo ya mkoa tayari wananchi kama wote wakawa wameshakusanyika eneo hilo.
Askari walijaribu kupiga mabomu ya machozi lakini wapi wananchi hawakuweza kutawanyika hivyo wakabaki wakiwaangalia maana kutokana na wingi wao basi wasingeongefanya lolote kuwazuia, wananchi walikuwa ni wengi mno.
Upande wa jiji la ntovo na majiji mengine nayo yalifanya hivyo hivyo kwa kupitia ushawishi wa mwanadada fetty diva kutokea mitandaoni.
Maandamano hayo katika jiji la ntovo ndiyo yalikuwa funika mno maana wananchi wote waliungana na kwenda kujirundika nje ya ofisi ya waziri wa mambo ya ndani yaani ALBERTO BANGULI. Askari walijaribu kuwazuia wananchi hao wenye hasira kali lakini baada ya wananchi hao kuwahamasisha askari hao nao wakajikuta wakiungana na wananchi kushinikiza mkubwa wao jenerali hambabe na banguli waachie nchi haraka iwezekanavyo.
Hakika banguli hakuwa na ujanja hata chembe.
Aliamua kujifungia ndani ya ofisi yake kujaribu kutafuta njia ya kuwakimbia wananchi hao.
Na kila alipochungulia dirishani kuangalia nje alikutana na kundi lukuki la wananchi hao wenye hasira kali.
Alitamani ardhi ichimbuke adumbukie.
Na alijilaumu sana kuendelea kubaki ndani ya nchi hiyo kipindi maandamano yakiendelea. Kupuuza kwa wananchi wake aliowazoea kila siku kuwa hawana lolote ndilo lililomponza na kusababisha kuendelea kuwepo mpaka muda huo ndani ya ofisi hiyo.
Upande mwingine nae jenerali hambabe ilikuwa ni patashika kwani wanajeshi wake walimgeuka na kumwimbia nyimbo za kujiudhuru kwa kiongozi huyo.
Naye akabaki tumbo joto.
***
Mwanadada tiffa baada ya kuhakikisha wananchi wa kitibi wameshafanya lile analolihitaji hakuona tena umuhimu wa kuendelea kuwepo hapo, hivyo akamshawishi D’oen waende ntovo sehemu ambayo mbaya wake alikuwa akipatikana.
Lile wazo la kulipiza kisasi cha mauaji ya hayati baba yake yalimuingia moyoni mwake. D’oen hakupinga hivyo wakaanza safari ya kuelekea jiji hilo.
Wakachukua gari ya mkuu wa mkoa aliye ofisini mwake na kuondoka wawili hao wakiwaacha makomandoo na wenzao wengine pamoja na wananchi wenye hasira kali.
Mwanadada fetty diva naye hakuona umuhimu wa kumuacha mtu aliyesababisha mauaji ya mama yake aendelee kuishi ama kupewa adhabu na mtu mwingine hivyo alifunga safari kutokea mji wan chi ya kinte kuelekea ntovo kwa dhamira ya kisasi hicho.
***
D’oen na tiffa wanafanikiwa kufika ndani ya jiji la ntovo na breki yao ya kwanza ni katika ofisi ya mkuu wa majeshi wan chi hiyo.
Wanafanikiwa kupokewa na wanajeshi kama wote nje ya ofisi hiyo wakishinikiza kiongozi huyo ajihudhuru.
Wanajeshi wote wakawashangilia D na tiffa baada ya kuwaona
“komandooo! komandoo! komandoo!” sauti za wanajeshi hao zikapazwa kumshangilia D.
D nae akafurahi.
Wanajeshi hao wakamkimbilia na kumbeba D’oen juu juu huku wakiendeleza sifa kwa kijana huyo
“shujaaa! Shujaa! Shujaaa!”
Tiffa akabaki akifuta machozi ya furaha kwenye mashavu yake hakuamini kama ipo siku itafikia watalikamilisha lile lilokuwa likimkereketa.
D’oen akashushwa!
“sikilizeni sasa!” akaongea D’oen na wote wakatulia kumsikiliza.
“kwanza hicho kijeneral uchwara kipo?” akahoji
“kipo” wakajibu kwa sauti
“yupo wapi?”
“ofisini kwake!”CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“aaah kwanini mnamuacha ofisini aendelee kula kiyoyozi cha kodi zenu, kamleteni hapa”
Baada ya amri hiyo wanajeshi wakaivamia ofisi hiyo baada ya kuuvunja mlango uliokuwa umefungwa kwa ndani. Baadae wakarejea na HAMBABE waliyembeba juu juu.
Wakamshusha chini ya miguu ya tiffa na D’oen.
“we tulia” waliongea kumuamrisha baada ya kuonesha utundu.
Tiffa alipokuwa akimwangalia ndipo mawazo ya baba yake yakamjia. Na ndo hapo akajisemea kimoyoni,’kumuacha huyu ni sawa na kumsaliti baba yangu’
Baada ya kauli hiyo akachomoa bastola kiunoni mwake na bila kubagein akazipachika risasi kadhaa katika kichwa cha hambabe.
Hambabe akadondoka chini kama gunia na hapo ndio ukawa mwisho wake.
HAMBABE akafariki.
Wanajeshi kwa furaha wakambeba D’oen na tiffa juu juu kuelekea ofisi ya waziri wa mambo ya ndani yaani banguli.
Wakafanikiwa kufika katika eneo hilo.
Walifarijika mno baada ya kuona wananchi kama wote wakiwa nje ya ofisi hiyo ya kiongozi huyo. Wakamshusha D’oen na ndipo wananchi wakawapokea kwa shangwe yaani
“mashujaa! Mashujaa! Mashujaa!” huo ndio wimbo uliowapokea.
Wakaomba njia kuelekea kwenye ofisi hiyo, wakapishwa.
Wakiwa mlangoni wakashangaa mlango ukivunjwa na banguli kufuatia nyuma ya mlango huo ambao kwa pamoja wakadondoka chini!
“aaaaaaaahaaaaaaaaaaaaaaa” banguli akaachia yowe la uchungu.
Wakiwa wapo kwenye bumbuwazi ni nini kimempata hadi kurushwa nje kiasi hicho. Mara mwanadada fetty diva mwenye upanga mkononi akatokea mlangoni pale.
Hapo ndipo wananchi wakalipuka
“fetty diva! Fetty diva! Fetty diva!” wakamshangilia kwa kelel za hali ya juu. Ni nani asiyemjua na ushawishi wake na mitandao?
Fetty diva akapunga mkono kuwasalimia.
“jamani wananchi nadhani wengi mimi mnanijua na mnaelewa ni jinsi gani nilivyokuwa na uchungu na serikali hii” fetty diva akaongea huku akiwa mwenye hasira mno na kigugumizi chake cha muda mrefu kikaanza kusikika kwa mbali.
“sana dada, ongea ongea” wananchi wakaongea
“basi aliyesababisha mimi niichukie serikali ni huyu, huyu ndiye aliyemuua mama yangu mzazi na watu wengi wanaopotea katika hii nchi huyu ndio muuaji mkubwa, huyu ni jambazi” fetty aliongea kwa uchungu.
Banguli alibaki akilia na huku akionesha kuomba msamaha.
“sasa leo namuua hapa mbele yenu kama nadhiri niliyoiweka lazima nilipize kisasi cha mama yangu” fetty akaongea maneno hayo huku akiunyanyua upanga wake juu na kuushusha katika utosi wa banguli, damu ziliruka na kumrukia fetty diva usoni na katika mavazi yake.
Wananchi wenye roho nyepesi wakafumba macho yao.
Hapo ndipo roho ya mwanadada fetty diva ikatulia baada ya kisasi kile. Akatupa panga chini na kunyoosha mikono km mtu anayetaka kukumbatiwa. D’oen na tiffa ndio walikuwa wa kwanza kumkumbatia baadae wanajeshi wakaja nyuma yao na wananchi wakaja kwa nyuma ya wanajeshi na wote kukumbatiana kwa pamoja.
Ilikuwa ni kilio tu cha ushindi ndicho kilichozuka ndani ya jiji hilo la ntovo.
Picha mbalimbali zikapigwa n ahata video pia kupitia waandishi wa habari wa nchi waliokosa uhuru muda mrefu.
Dunia nzima ikalipokea tukio hilo.
****
Ndipo ukaguzi ukafanywa ndani ya nyumba ya waziri banguli na hapo ndipo ilipatikana miili mbalimbali ya watu ambayo ilikuwa imeshaoza n ahata Afordias nae akakutwa akiwa tayari amekufa.
Huo ndio ukawa msiba wa taifa.
Nchi ikakabidhiwa ndani ya mikono ya ELIAS STANFORD ambaye baada ya kukabidhiwa akawasomba ndani wale viongozi wote waliokuwa wakishirikiana na banguli.
Jeshi la wananchi lote likapanguliwa na hata jeshi la polisi nalo na kuwekwa mfumo mpya wenye kutetea haki za wananchi na si kukandamiza. D’oen akafanikiwa kupewa cheo cha kuliongoza jeshi la nchi hiyo huku tiffa akiwa ni second in command wake yaani msaidizi wake. Wale makomandoo wenzake walipangiwa nafasi nzuri tu jeshini, na G master nae baada ya mafunzo machache akapewa nafasi ya kujiunga na jeshi hilo naye akapewa nafasi kubwa.
Santos na barnabas wao wakaendelezwa kimasomo na kupatiwa ajira serikalini kiulaini.
Mwanadada fetty nae pia akatafutiwa ajira na Maisha yao yaliendeshwa vizuri yeye pamoja na ndugu zake kupitia serikali.
Felix nae kutokana na mchango wake katika kurusha habari bila woga akafanikiwa kupewa kazi ya uandishi wa habari wa ikulu.
Maisha ndio yakaenda kwa staili hiyo.
Nchi ikarejea katika Amani yake ya awali na serikali ikabaki ikitendea wema raia wake kwa kuwafanya haki.
***
SIKU TATU BAADAE
D’oen na tiffa baada ya ushindi ule waliamua wakajipongeze, hivyo wakaitafuta hoteli moja kubwa sana katika jiji la ntovo na kuamua kuitumia kwa ajili ya kupata vinywaji.
Kiukweli tiffa na D’oen walikuwa si wanywaji wa pombe lakini siku hiyo kutokana na furaha yao ya kunusurika na vifo wakaamua wanywe.
Wakanywa sana na kujikuta wote wamelewa chakali.
Hapo ndipo uamuzi wa kipumbavu wa wawili hao wa kuamua kukodi chumba ndani ya hoteli hiyo ukawajia.
Bila kuchelewa wakakodi chumba na kujikuta wamelala wote.
Ibirisi hakuwaacha usiku huo kucheza na hisia za miili yao na kujikuta wakivunja ile amri kuu ya sita kwamba USIDHINI. Wawli hao wakajikuta wakitumbukia katika dimbwi zito la mahaba.
Asubuhi ilivyofika wawili hao walishtuka mno baada ya pombe kuwatoka kichwani na kujikuta wakiwa katika kitanda kimoja tena wakiwa kama walivyozaliwa yaani watupu.
Tiffa aliona aibu mno lakini moyoni alifurahia lile kutokea kama hapo awali alipokuwa akitaka kuwa na kijana huyo aliyeuteka moyo wake.
Hawakuwa na jinsi kwakuwa wote walikuwa tayari washakufa washaoza kwa kila mmoja hivyo wakajikuta wakiingia kwenye uhusiano na hapo ndipo wakapoamua kuanza kulifanya tendo hilo upya wakiwa kichwani bila pombe. Wote wakaoneshwa kufurahishwa baada ya dakika tisini ya mchezo huo.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“D” tiffa akaita baada ya mchezo huo
“naam!” sauti nzito ya D’oen ikaitikia
“unakumbuka nilikuahidi zawadi tutakapokuwa tumefanikisha kifo cha hambabe?”
“yes honey nakumbuka!”
“basi ndio hii nlokupa leo”
“oooh wow asante sana” D’oen akaongea huku akimwachia busu tiffa. Busu hilo likawazamisha katika romance zito.
Ahadi kemkem za kuoana zikawasakama!
Baada ya kutambulishana kwa ndugu na jamaa wa pande zote mbili ndipo ndoa yao iliyohudhuriwa na watu mbali mbali akiwemo rais STANFORD ikafungwa.
Huo ndio ukawa mwanzo wa Maisha ya furaha ya wawili hao.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment