Search This Blog

Sunday, 22 May 2022

UFUKWE WA MADAGASCAR - 3

 







    Simulizi : Ufukwe Wa Madagascar

    Sehemu Ya Tatu (3)





     Mvua bado ilikuwa ikiendelea kunyesha na hali ile ilikuwa nafuu kwangu kwani wakati nikiendelea na safari matone makubwa ya mvua ile yakawa yakiosha uvundo mwilini mwangu uliotokana na masalia ya takataka zilizokuwa ndani ya lile pipa.

     Muda mfupi uliofuata nikawa nimetoka kwenye kile kichochoro na kuingia barabarani huku kwa tahadhari nikiendelea kupita kandokando ya kuta ndefu zilizoyazunguka majumba ya kifahari ya eneo lile. Mwisho wa ile barabara kulikuwa na barabara nyingine iliyokatisha hivyo nilipoifikia ile barabara nikaingia upande wa kushoto huku nikiendelea kutembea kwa tahadhari na mara kwa mara nikawa nikigeuka na kutazama nyuma kama kungekuwa na mtu yeyote aliyekuwa akinifuatilia. Sikumuona mtu yeyote nyuma yangu hivyo hali bado ilikuwa...

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    shwari. Ile barabara ilikuwa ikikatisha moja kwa moja mbele ya ile suparmaket niliyoegesha gari langu hivyo nilinyoosha moja kwa moja.

     Wakati nikilifikia lile gari langu nikachepuka kidogo na kujibanza kwenye kona moja ya ukuta katika namna ya kuchunguza hali ya usalama wa eneo lile na niliporidhika kuwa hali bado ilikuwa shwari nikavuka barabara na kuelekea kwenye gari langu kwa tahadhari huku mkono wangu wa kushoto ukiwa umekikamata vyema kilimi cha bastola yangu kwenye mfuko wa koti langu tayari kukabiliana na rabsha yoyote ambayo ingejitokeza eneo lile. Hatimaye nikalifikia gari langu na baada ya kulizunguka kidogo kukagua usalama wake na kuridhishwa nikafungua mlango wa dereva na kuingia mle ndani. Koti langu la mvua nikalivua na kulitupia siti ya nyuma kasha bila kupoteza muda nikawasha gari na kuondoka eneo lile huku mawazo mengi yakipita kichwani mwangu.

     Kwa namna moja au nyingine nilianza kuamini kuwa tukio la kutekwa kwa balozi Adam Mwambapa lilikuwa limetekelezwa na kikundi cha wanajeshi wachache wa jeshi la wananchi wa Burundi ingawa bado sikuweza kufahamu dhamira ya watekaji hao. Nilikuwa nimeanza kushawishika kwenda kuripoti juu ya tukio lile kwa maafisa usalama waandamizi wa nchini Burundi hata hivyo hali ile ya machafuko ya kisiasa iliyokuwa ikiendelea nchini Burundi ilinionya kuwa kwa kufanya vile huwenda ningejitumbukiza kwenye hatari ya kugharimu uhai wangu badala ya kutatua tatizo kama ilivyokuwa lengo langu.

     Mvua kubwa bado ilikuwa ikiendelea kunyesha na wakati nikiendelea na safari yangu mbali na kile kitongoji cha Chaussée P.L. Rwagasore nikagundua kuwa mifereji mingi ya maji iliyokuwa ikipakana na barabara za kitongoji kile ilikuwa mbioni kufurika kwa maji ya mvua kubwa iliyokuwa ikiendelea kunyesha. Nikaendelea kuendesha gari kwa kasi nikikitoroka kitongoji kile huku mara kwa mara nikiyapeleka macho yangu kutazama vioo vya ubavuni vya lile gari kuona kama kungekuwa na gari lolote lililokuwa likinifungia mkia kwa nyuma. Sikuona gari lolote hivyo hali bado ilikuwa shwari.

     Baada ya mwendo mrefu wa safari yangu nikivizunguka vichuguu kushuka mabonde na kupanda milima hatimaye nikapita mbele ya jengo refu la ghorofa la Vaya residence apartments services. Nilipolipita lile jengo upande wa kushoto baada ya safari fupi nikakunja kona upande wa kulia nikipanda mlima mfupi katika barabara ya Chaussée P.L. Rwagasore. Mwendo wangu ulikuwa wa kasi mno hivyo baada ya muda mfupi nikawa nimeyafikia makutano ya barabara ya Chaussée P.L. Rwagasore na barabara ya Avenue Belvedere. Nilipoyafikia yale makutano nikapunguza mwendo na kuingia barabara ya Avenue Belvedere nikianza kushuka mteremko mkali wa barabara ile kuelekea mjini.



     _____

     Saa tano na dakika kumi usiku niliegesha gari langu katika viunga vya maegesho ya magari vya jengo la New Parador Residence kando ya barabara ya Boulevard du 28 Novembre. Mvua bado ilikuwa ikiendelea kunyesha na nje ya jengo ile kulikuwa na magari machache yaliyoegeshwa.

     Nilikuwa nimeyakumbuka vyema maelezo ya Hidaya kuwa siku ile ambayo hakuhudhuria kazini Balozi Adam Mwambapa alikuwa amealikwa na maafisa waandamizi wa serikali ya Burundi kuhudhuria kikao juu ya hali tete ya machafuko ya kisiasa iliyokuwa imeanza kutokea nchini Burundi. Kwa mujibu wa maelezo ya Hidaya aliyoyapata kutoka kwa Balozi Adam Mwambapa ni kuwa mkutano ule ungefanyikia katika ukumbi wa lile jengo la New Parador Residence ndiyo kisa nikawa nimefika pale.

     Kabla ya kushuka kwenye gari nikatulia kwa dakika chache nikitathmini vizuri mandhari yale. Eneo la mbele la maegesho ya magari ya lile jengo kulipandwa miti mirefu ya kivuli aina ya Quercus virginiana katikati ya bustani nzuri ya maua baina ya sehemu moja ya maegesho ya gari na sehemu nyingine. Kulikuwa na taa hafifu za ardhini zilizokuwa zikimulika eneo lile na hivyo kulifanya lile eneo lipendeze.

     Nilipozidi kuchunguza nikagundua kuwa kulikuwa na magari machache madogo yaliyokuwa yameegeshwa eneo lile. Mbali na magari yale madogo pia kulikuwa na basi moja la wanafunzi wa shule ya sekondari ya Eldoret ya nchini Kenya, lori moja kubwa la kubebea watalii wa masafa marefu na gari moja jeusi aina ya Nissan Caravan lililokuwa limeegeshwa upande wa kushoto mwisho wa lile jengo.

     Upande wa kulia wa eneo lile kulikuwa na kibanda kidogo chenye mashine mbili za ATM za benki. Mashine moja ya ATM ya Banque de Crédit de Bujumbura na mashine nyingine ya ATM ya Banque de la République du Burundi. Kulikuwa na watu wachache katika foleni za wahitaji huduma kuelekea kwenye zile mashine za ATM na wengi wao walikuwa ya wazungu wa kutoka nje ya bara la Afrika. Pembeni ya mashine zile za ATM kulikuwa na bustani ya nyasi laini zilizokatiwa vizuri na kupendeza na katika bustani ile kulikuwa na sehemu za kupumzika zenye viti na meza chini ya miamvuli mikubwa yenye rangi za kupendeza. Nilipoyatembeza macho yangu kwa utulivu nikagundua kuwa hapakuwa na mtu yeyote eneo lile labda kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikiendelea kunyesha.

     Jengo la New Parador Residence lilijengwa kwa ufanisi wa hali ya juu kiasi kwamba taa nzuri zilizokuwa zikiwaka kwenye ghorofa zake zililipelekea jengo lile lionekane kama meli kubwa ya kupendeza iliyotia nanga kwenye bandari ya nchi kavu. Chini ya lile jengo kulikuwa na supermarket moja kubwa, maduka ya nguo za kisasa, ofisi za mashirika ya simu, ofisi za Dstv, Dhl na maduka mawili ya kubadilishia fedha za kigeni.

     Hatimaye nikalichukua lile koti langu jeusi la mvua na kulivaa kisha nikafungua mlango wa gari na kushuka. Taratibu nikaanza kukatisha kwenye viunga vile vya maegesho taratibu nikielekea mbele wa lile jengo sehemu kulipokuwa na mlango mkubwa wa kioo na varanda pana yenye ngazi iliyofunikwa kwa kofia nzuri ya zege.

     Wakati nikiendelea kutembea nikawa nikiyatembeza macho yangu kwa utulivu kutazama huku na kule kuchunguza kama kungekuwa na mtu yeyote ambaye angekuwa akizifuatilia nyendo zangu. Sikumuona mtu yeyote wa kumtilia mashaka hivyo hatimaye nikazifikia zile ngazi na kuanza kuzipanda tatatibu kisha nilipoufikia ule mlango wa kioo nikausukuma na kupotelea ndani.

     Kulikuwa na vijana wawili wahudumu wa ile hoteli waliokuwa wamesimama kando ya ule mlango wa kuingilia kwa ndani. Vijana wale waliovaa sare za kazi, suruali nyeusi, makoti ya suti ya rangi nyekundu na kofia nyeupe kichwani wakanipokea kwa bashasha zote huku wakinionesha tabasamu la kirafiki kwenye nyuso zao. Nikawashukuru vijana wale kwa ukaribisho wao na kuendelea na safari yangu nikitembea juu ya kipande mstatili cha zulia jekundu kuelekea sehemu ya mapokezi ya hoteli ile huku nikiendelea kuyatembeza macho yangu kupeleleza mandhari ya mle ndani.

     Upande wa kushoto mara baada ya kushuka ngazi chache chini kulikuwa na ukumbi mkubwa wenye meza nyingi za kulia chakula zenye umbo duara zilizozungukwa kwa viti nadhifu vyenye foronya laini. Meza zile zilikuwa zikimefunikwa kwa vitambaa visafi vya rangi nyeupe na juu yake kuliwekwa kadi ngumu za kupendeza zenye orodha ya vyakula na vinywaji vinavyopatika katika hoteli ile. Karatasi laini nyeupe za tishu za kufutia mikono na vifaa vyote muhimu vya kujipatia maakuli kama uma, visu na vijiko. Vikasha wiwili vidogo kimoja cha kuwekea chumvi ya mezani na kingine cha vijiti vya kuchokolea meno. Pembeni ya meza zile kulikuwa na makochi mazuri ya sofa yaliyopangwa kuzizunguka meza fupi za vioo katika mpangilio mmoja unaovutia. Nilipozidi kuchunguza mwisho wa ukumbi ule nikaiona kaunta kubwa ya vinywaji.

     Madirisha makubwa ya vioo ya ukumbi ule yalikuwa yamefunikwa kwa mapazia marefu yenye rangi nzuri za kupendeza. Ukutani kulikuwa na runinga pana za flat screen zilizokuwa zikiendelea kurusha taarifa kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Bujumbura zikielezea juu ya hali ya machafuko ya kisiasa iliyokuwa ikiendelea kufuka moshi nchini Burundi.

     Nilipotazama vizuri ndani ya ule ukumbi nikaona kuwa kulikuwa na watu wachache waliokuwa wameketi mle ndani wakijipatia mlo na vinywaji huku kwa makini wakiendelea kufuatilia taarifa zilizokuwa zikirushwa kupitia zile runinga. Ukumbi ule mkubwa ulikuwa umetenganishwa na ile sehemu ya mapokezi kwa ukuta mkubwa wa kioo unaomruhusu mtu yeyote kuweza kuona mle ndani bila usumbufu wowote.

     Nilipogeuka kutazama upande wa kulia nikauona ukumbi mwingine mdogo wenye nguzo mbili kubwa katikati yake. Kulikuwa na watu wachache kwenye ukumbi ule, wazungu kwa waafrika wakiendelea na maongezi yao ya hapa na pale katika makochi mazuri ya sofa yenye meza fupi za mbao. Watu wale wakijipatia vinywaji, wengine wakivuta sigara na kutazama mechi za mpira wa miguu za ligi za ulaya zilizokuwa zikioneshwa kwenye runinga tofauti zilizotundikwa ukutani. Wahudumu wa hoteli ile walikuwa wakiendelea na taratibu zao za kutoa huduma kwa wateja kama ilivyo ada.

     Wakati nilipokuwa nikiifikia kaunta ya mapokezi ya ile hoteli mle ndani nikawaona vijana wawili waliovaa sare za kazi zinazofanana na za wale vijana wengine walionikaribisha kule mlangoni na wote walikuwa warefu na weusi wenye maumbo imara na miili iliyojengeka vizuri. Mhudumu mmoja alikuwa akizifuta bilauri ndefu za vinywaji kwa kitaulo kidogo kilichokuwa begani mwake na kuzipanga vizuri katika rafu ya mbao iliyokuwa ukutani eneo lile. Mwenzake alikuwa akiandika taarifa fulani kwenye kitabu kidogo kilichokuwa juu ya meza ya ile kaunta na aliponiona haraka akaacha kile alichokuwa akikifanya na kunikaribisha kwa tabasamu zuri la kibiashara na mimi bila ajizi nikawahi kumsalimia.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Comment va le travail?’’. Habari za kazi?.

    “Bien frère, je peus t?aider?”. Salama kaka sijui nikusaidie nini?. Yule kijana akanijibu kwa bashasha zote za kirafiki huku akinitazama kwa makini huku akikunja vizuri mikono ya shati lake.

    “Je suis I?officien de I?ambassade de Tanzanie ici à Bujumbura. Je veus savoir s?il y a eu une reunion de dirigents qui a eu lieu dans votre”. Mimi ni afisa wa ubalozi wa Tanzania hapa Bujumbura. Nataka kufahamu kama kulikuwa na mkutano wowote wa viongozi wa serikali uliofanyikia hapa siku ya juzi. Nikaongea kwa utulivu huku nikiwatazama wale vijana kwa makini. Swali langu bila shaka lilimshtua kidogo yule kijana na hapo nikamuona akinikata jicho la udadisi kabla ya kugeuka na kumtazama mwenzake pale kaunta. Nikahisi jambo fulani nisilolielewa hata hivyo sikutia neno lolote. Yule kijana akageuka na kunitazama tena.

    “Pardon!, nous ne sommes pas permis de donner auqu?une information, peut être allez voir notre directeur’’. Samahani!, haturuhusiwi kutoa taarifa zozote za kiofisi labda ukamuone meneja wetu.

     Yule kijana akaniambia kwa utulivu huku akinitazama na kwa kweli sikuona tashwishwi yoyote usoni mwake. Kitambo kifupi cha ukimya kikapita huku nikigeuka nyuma na kuyatembeza macho yangu taratibu katika namna ya kupeleleza sura za watu zinazostahili kutiliwa mashaka mle ndani. Sikumuona mtu yoyote akinitazama hivyo nikayarudisha macho yangu kwa yule kijana na kuweka kituo.

    “Où est le bureau de votre directeur?”. Ofisi ya meneja wenu iko wapi?. Nikamuuliza yule kijana mhudumu na mara ile tena nikamuona akigeuka na kumtazama mwenzake pasipo kusema neno lolote kisha akayarudisha macho yake tena kunitazama.

    “Au cinquieme niveau dans la chambre numero 302”. Ghorofa ya tano chumba namba 302. Yule kijana akaniambia kwa utulivu huku akinitazama na hapo nikakumbuka kutumbukiza ombi langu.

    “Fais un coup de téléphone et dis lui qu?il ya qulqu?un qui veut le voir”. Piga simu mueleze kuwa kuna mtu anahitaji kumuona. Nikamwambia yule kijana na baada ya kusita kidogo nikamuona akinyanyua kiwambo cha simu ya mezani iliyokuwa pale juu kwenye meza ya kaunta na kukiweka sikioni kisha nikamuona akibonyeza tarakimu kadhaa. Muda mfupi uliofuata ile simu ilikuwa hewani na hapo nikajua kuwa yule kijana alikuwa akiwasiliana na meneja wa ile hoteli ingawa mazungumzo ya simu yalipoanza sikuambulia kitu chochote kwani lugha ya mawasiliano iliyokuwa ikitumika baina ya yule kijana mhudumu na meneja wa ile hoteli ilikuwa ni kirundi ambayo mimi sikuifahamu. Yale mazungumzo ya simu yaliposimama nikamuona yule kijana akigeuka na kuniuliza.

    “II demande qui etes vous?’’. Anauliza kuwa wewe ni nani?.

    “Dis lui que c?est I?officié de I?embassade de Tanzanie ici au Burundi”. Mwambie kuwa mimi ni afisa kutoka ubalozi wa Tanzania hapa nchini Burundi. Nikamwambia yule kijana huku taratibu nikivigongesha vidole vyangu juu ya sakafu ya ubao wa ile kaunta. Yule kijana akayahamishia maongezi yake tena kwenye ile simu kisha baada ya maongezi mafupi akaikata ile simu na kukirudishia kile kiwambo mahala pake. Muda uleule akageuka tena na kunitazama akivunja ukimya.

    “Allez maintenant, il est dans la chambre numero 302, il vous ettend”. Nenda sasa hivi yupo chumba namba 302 anakusubiri. Yule kijana akaniambia.

    “A la fin de ce comptoire du côté droit tu vas voir I?assacaire. Ça sera bien si vous partez vite, parcequ?il reste avec un peu de temps avant qu?il ferme son bureau cette nuit’’. Mwisho wa hii kaunta upande wa kulia utaona lifti. Itakuwa vizuri ukiwahi maana amebakiwa na muda mfupi kabla ya kufunga ofisi yake usiku huu. Yule mwenzake akasisitiza.

    “Je vous remercis beaucoup”. Ahsanteni sana.

     Nikawashukuru wale vijana na kuanza kuondoka eneo lile. Niliiacha ile kaunta ya mapokezi na kushika uelekeo wa upande kulia nikitembea kwa utulivu na baada ya kuipita nguzo moja kubwa ya ule ukumbi upande wa kushoto nikaiona lifti ya lile jengo. Nilipochunguza vizuri nikagundua kuwa ile lifti ilikuwa ikishuka hivyo nikasimama na kusubiri mtu aliyekuwa...





    ...akishuka kwenye ile lifti atoke kisha nikaingia mle ndani na kubonyeza kitufe ukutani nikiiamuru ile lifti inifikishe ghorofa ya tano ya lile jengo. Mlango ulipojifunga ile lifti ikaanza kupanda juu na wakati ule mawazo mengi yakawa yakipita kichwani mwangu.

     Nilianza kwa kukumbuka mambo yote yaliyojili tangu siku ile ya kwanza nilipoondoka jijini Dar es Salaam nchini Tanzania kuja pale Bujumbura nchini Burundi. Kisha nikamkumbuka yule msichana mrembo wa ajabu aitwaye Amanda niliyesafiri naye kutoka jijini Kigali nchini Rwanda namna alivyonisaliti kwa wale wanajeshi na kugeuka mwiba mchungu katika safari yangu. Nikiwa katikati ya mawazo yale nikamkumbuka Hidaya kabla ya mawazo yangu kuhamia tena kwa yule mtu aliyejitambulisha kwangu kwa jina la Jean-Baptiste Nibizi muda mfupi kabla ya kuuwawa kwa risasi kwenye ukingo wa ule mto mkubwa kando ya daraja la barabara ielekeayo mbali na jiji la Bujumbura.

     Hatimaye mawazo yangu yakahamia nyumbani kwa Balozi Adam Mwambapa muda mfupi uliopita nikikumbuka namna nilivyopambana na lile jitu hatari na hatimaye kuchomoka na ushindi mwembamba katika pambano la kukata na shoka. Mwishowe mawazo yangu yakahamia kwa yule kijana mfanyakazi wa nyumbani kwa Balozi Adam Mwambapa aliyejitambulisha kwangu kwa jina la Sundi. Kitendo cha kumkumbuka Sundi kikayapelekea mawazo yangu yaweke nanga kwenye mjadala mzito juu ya Padri Aloysius Kanyameza.

     Kitendo cha ile lifti kugota haraka kikayarudisha mawazo yangu mle ndani na hapo nikashtukia kuwa tayari nilikuwa nimefika kwenye ghorofa ya tano ya lile jengo la New Parador Residence. Mlango wa kile chumba cha lifti ulipofunguka nikalitengeneza vizuri koti langu na kutoka nje.

     Sasa nilikuwa nimetokezea kwenye korido pana iliyomezwa na utulivu wa aina yake. Korido ile ilikuwa ikipakana na milango mingi ya vyumba kwa upande wa kushoto na kulia. Nikasimama kidogo nikiichunguza korido ile kwa utulivu. Katikati ya ile korido kulikuwa na kitufe kikubwa chekundu cha kengele ya hatari pembeni ya mtungi mkubwa wa gesi ya kuzimia moto wa dharura. Kwenye dari ya korido ile kulikuwa na taa ndefu za tubelight za mtindo wa kupendeza zilizokuwa zikiangaza mwanga wa wastani katikati ya korido ile na hivyo kuyafanya mandhari yale tulivu yapendeze. Lile jengo lilikuwa kubwa hivyo na ile korido nayo ilikuwa ndefu kiasi kwamba sikuweza kuona mwisho wake vizuri.

     Hatimaye nikaanza kutembea taratibu nikiichunguza kwa makini milango yote iliyokuwa ikitazamana na ile korido. Juu ya ile milango kulikuwa na vibao vidogo vya rangi ya kijivu vilivyokuwa na utambulisho wa namba ya chumba husika. Nikaendelea kutembea taratibu kwa utulivu huku nikiyatembeza macho yangu huku na kule kutazama zile namba milangoni. Haikuwa hadi pale nilipofika katikati ya korido ile upande wa kulia ndiyo nikauona mlango wenye kibao kilichochongwa vizuri namba 302.

     Kwa sekunde kadhaa nikasimama nikiutazama mlango ule kwa makini. Jambo moja lilinishangaza kidogo huku nikijiuliza kama kweli ule mlango ulikuwa ni wa kuelekea ofisini kwa meneja wa ile hoteli kwa nini hapakuwa na utambulisho wowote pale mlangoni unaoelezea kuwa ile ni ofisi ya meneja wa ile hoteli?. Huku nikiendelea kujiuliza kwa nini ofisi ya meneja wa hoteli kubwa kama ile iwekwe ghorofa ya tano ya lile jengo badala ya kuwekwa ghorofa ya chini ambapo ndiyo ingelikuwa rahisi zaidi kufikiwa na wateja wanaohitaji huduma. Nikaendelea kujiuliza pasipo kupata majibu hata hivyo muda haukuwa rafiki kwangu hivyo hatimaye nikausogelea ule mlango na kubofya kitufe kidogo cha kingele kilichokuwa kando yake.

     Ulipita muda mrefu pasipo mwitikio wowote wa kutoka ndani ya kile chumba na hali ile ikanisukuma nisogee tena pale mlangoni na kubofya kile kitufe cha kengele. Mara moja tu kengele ile ilipoanza kuita tena mara nikauona ule mlango ukifunguliwa taratibu na mbele yangu akasimama mwanaume mmoja mfupi mwenye sura ya umbo duara, macho makubwa, pua ya kibantu na mdomo wenye kingo pana uliozungukwa na ndevu zilizokatiwa vizuri. Mwanaume mfupi na mnene mwenye kitambi cha ukwasi huku amevaa suti ya kodrai ya rangi ya udongo, shati la rangi ya kijivu na tai nyeusi shingoni. Nilipomchunguza vizuri mtu yule nikaridhika kuwa alifaa kuitwa meneja wa hoteli ile kwa namna ya haiba yake. Tabasamu hafifu la kirafiki likaanza kuumbika usoni na hapo yule mtu akavunja ukimya akinikaribisha na nilipomtazama nikagundua kuwa umri wake haukwenda mbali zaidi ya miaka arobaini.

    “Bien venu Monsieur et tu as de la chance, parceque je me préparer a quitté le bureau”. Karibu sana ndugu, tena una bahati sana maana ndiyo nilikuwa najiandaa kufunga ofisi. Yule mtu akanikaribisha kiungwana na wakati nikiingia mle ndani akanipa mkono na tabia yake ile ya ukarimu ikawa imenivutia sana. Ule mlango nyuma yangu ukafungwa.

    “Merci beaucoup”. Ahsante sana. Nikaitikia kwa furaha huku nikipiga hatua zinazopwaya ndani ya ofisi ile ngeni kabisa machoni mwangu huku taratibu nikiyatembeza macho yangu kutazama mandhari ya ile ofisi.

     Ilikuwa ofisi kubwa yenye mandhari tulivu ya kuvutia. Upande wa kulia kulikuwa na kiti kikubwa cha sofa nyuma ya meza kubwa ya ofisini yenye majalada mengi yaliyopangwa moja juu ya lingine, bendera ndogo ya mezani ya taifa la Burundi, kidau cha wino, mhuri, kompyuta moja ya mezani na simu ya mezani pembeni yake. Kando ya ile meza kulikuwa na kabati kubwa la mbao lenye nyaraka za kiofisi kando ya sefu moja ya chuma.

     Nikaendelea kuyatembeza macho yangu taratibu mle ndani na kwa kufanya vile upande wa pili wa ile ofisi nikaliona dirisha kubwa ukutani likiwa limefunikwa kwa mapazia mawili marefu. Upande wa kushoto wa ile ofisi kulikuwa na seti moja ya makochi mazuri ya sofa nyuma ya meza fupi ya kioo yenye ua zuri juu yake na pembeni ya makochi yale ukutani kulitundikwa runinga pana flat screen iliyofungwa sistimu ya nzuri mziki. Nilipotazama kwenye kona moja iliyokuwa upande wa kushoto wa ile ofisi nikauona mlango na hapo nikahisi kuwa ule ulikuwa ni mlango wa kuelekea sehemu ya maliwato ya ile ofisi ingawa sikuwa na hakika ya moja kwa moja hata hivyo ule mlango ulikuwa umefungwa. Ofisi ilikuwa nzuri na yenye mandhari ya kisasa yaliyonogeshwa na hewa nzuri ya kiyoyozi kilichokuwa mle ndani. Sakafuni kulikuwa na zulia zuri la rangi ya chanikiwiti lenye manyoya laini ya kupendeza. Nilipochunguza vizuri kando ya dirisha kubwa la mle ndani nikakiona kipoza maji.

    “S?il vous plais, assaiez-vous”. Tafadhali karibu uketi. Yule meneja wa hoteli akanikaribisha niketi kwenye kochi moja la mle ndani baada ya kuniona nikisitasita huku yeye akizunguka na kwenda kuketi kwenye kile kiti cha ofisini kilichokuwa nyuma ya ile meza yake ya utukufu.

    “Merci”. Ahsante. Nikashukuru na kwenda kuketi kwenye kochi moja la sofa la mle ndani lililokuwa karibu na ile meza ya ofisini. Kitambo kifupi cha ukimya kikapita huku nikiutumia muda wangu kuyazoea vizuri mandhari yale na hali ile ya ukimya ilipokuwa mbioni kushika hatamu nikavunja ukimya baada ya kukohoa kidogo kusafisha koo langu.

    “J?ai besoin de voir le directeur de cet hôtel, sans doute c?est toi”. Nahitaji kuonana na meneja wa hii hoteli, bila shaka ndiyo wewe. Nikaongea kwa utulivu huku nikimtazama yule mtu mfupi mbele ya kile kiti cha ofisi.

    “C?est moi”. Ndiyo mimi. Yule mtu akaitikia kwa utulivu pasina mashaka yoyote kisha akakohoa kidogo kusafisha koo lake kabla ya kuendelea.

    “Je m?appelle Monsieur Vital Desire Habonimana, le directeur de cet hôtel. Quel est votre nom?. Naitwa ndugu Vital Desire Habonimana, meneja wa hoteli hii. Jina lako nani?. Yule mtu mfupi akamaliza kujitambulisha huku akinikodolea macho nami nikakohoa kidogo kabla ya kuvunja ukimya.

    “Je m?appelle James Lusungu I?officié de I?embassade de Tanzanie ici à Bujumbura. Je vous savoir si le jour avant hier notre ambassadeur a arrivé ici à I?hôtel partucipé à la reunion”. Naitwa James Lusungu, afisa wa ubalozi wa Tanzania hapa Bujumbura. Nataka kufahamu kama juzi balozi wetu alifika hapa hotelini kwako kuhudhuria mkutano”. Nikadanganya kwa kujiamini huku nikimtazama yule mtu kwa makini. Kitambo kifupi cha ukimya kikapita huku yule mtu mfupi akinitazama kwa utulivu kama anayefikiria jambo fulani pasipo kuonesha tashwishwi yoyote usoni mwake halafu baada ya kuitazama saa yake ya mkononi akavunja tena ukimya.

    “Pourquoi ne pas rentre au bureau et demande cette question aupès de votre ambassadeur?”. Kwa nini usirudi ofisini na kumuuliza Balozi wako swali hilo?. Maelezo ya yule mtu yakanishangaza na haraka nikagundua kuwa kulikuwa na namna fulani ya jeuri katika maelezo yake tofauti kabisa na wakati ule alipokuwa akinikaribisha mle ndani muda mfupi uliopita. Hata hivyo kwa kuwa tayari nilikuwa ndani ya ofisi yake tena nikiwa na haja yangu binafsi nikaamua kujipa uvumilivu huku nikilazimisha tabasamu la kirafiki usoni mwangu.

    “Notre ambassadeur maintenant il est en voyage vers Dar es Salaam Tanzania”. Balozi wetu sasa hivi yuko safarini anaelekea Dar es Salaam Tanzania. Nikaongea kwa kujiamini huku nikidanganya na hapo yule mtu mfupi akaangua kicheko cha ghafla kilichonishangaza na kuniacha kwenye mduwao wa aina yake. Kicheko kile kilipofika ukomo yule mtu akaongea kwa utulivu kama mtu aliyefyatukwa na akili kichwani.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Un homme adulte comme toi, tu n?as pas honte de tromper?”. Mtu mzima kama wewe hivi huoni aibu kudanganya?.

     Maelezo ya yule mtu mfupi meneja wa hoteli ile yakanipelekea nihisi kuwa huwenda nilikuwa nikifahamika vizuri na mtu yule kuliko vile nilivyokuwa nikidhani. Hata hivyo nikapiga moyo konde na kumeza funda kubwa la mate kuitowesha hofu moyoni mwangu huku dalili zikiashiria kuwa mambo hayakuwa shwari tena mle ndani.

    “Donc toi, tu connais là où est I?embassadeur Adam Mwambapa?’’. Kwa hiyo wewe unafahamu mahali alipo Balozi Adam Mwambapa?. Nikamuuliza yule mtu kwa jazba kidogo. Yule mtu akacheka tena huku akijishika kidevu chake kifahari kabla ya kuniuliza.

    “Tu veus savoir là où est votre embassadeur ou tu veus savoir si le jour avant hier il a partucipé à la reunion ici à I?hôtel?”. Unataka kufahamu mahali alipo balozi wako au unataka kufahamu kama juzi alihudhuria mkutano hapa hotelini?.

    “Les tout” Vyote. Nikamjibu kwa jazba.

    “Ne te trompes pas camarade en pensant qu? on est te connait pas qui tu es”. Usijidanganye komredi ukidhani kuwa hatukufahamu vizuri kuwa wewe ni nani”. Yule mtu mfupi akaniambia huku akiangua kicheko hafifu cha dhihaka.

    “Je ne comprends pas, tu parles quoi?”. Mbona sikuelewi unaongea nini?. Nikamuuliza yule mtu kwa hasira za kudhihakiwa.

    “Bien venu camarade j?ai pensé que tu sera encore malin et echaper à cet obstacle”. Karibu sana komredi nilidhani kuwa mara hii ungekuwa mwerevu kuruka kiunzi hiki. Sauti kavu ya kiume kutoka nyuma yangu ikazungumza kwa utulivu hali iliyonishtua na kunipelekea nigeuke haraka kutazama nyuma yangu na kwa kufanya vile nikajikuta nikitazamana na mdomo wa bastola yenye uchu aina ya Type 64 Silenced iliyofungwa kiwambo maalum cha kuzuia sauti. Moyo wangu ukapiga kite kwa nguvu kisha kijasho chepesi kikaanza kunitoka sehemu mbalimbali mwili wangu.

     Sasa nilikuwa na hakika kuwa nilikuwa nimejiingiza kwenye himaya ya adui pasipo kujua na pale ndiyo nikafahamu kwanini yule mtu mfupi mbele yangu aliyejinadi kuwa ni meneja wa ile hoteli alikuwa akiongea kwa kujiamini sana ule muda mfupi uliopita. Jambo la kushangaza zaidi ni kuwa ile bastola nyuma yangu ilikuwa imeshikwa na yule kijana wa mapokezi ya ile hoteli aliyekuwa akifuta glasi kwa kile kitaulo kidogo wakati ule nilipokuwa nikiingia kwenye ile hoteli kati ya wale vijana wawili wahudumu wa ile hoteli waliokuwa ile sehemu ya mapokezi kule chini. Yule kijana aliyenishikia bastola nyuma yangu bado alikuwa katika sare zake za kazi huku usoni akitengeneza tabasamu jepesi la ushindi wenye dhihaka na kejeli.

     Kwa kweli sikuwa nimetarajia kabisa kuwa vijana wale niliowakuta kule sehemu ya mapokezi ya ile hoteli kuwa walikuwa ni mamluki waliopandikizwa eneo lile kwa ajili ya kufanikisha mpango wa kuninasa. Mara moja nikakumbuka namna vijana wale walivyokuwa wakitazamana wakati nilipokuwa nikizungumza nao kule chini sehemu ya mapokezi ya ile hoteli na hapo nikagundua kuwa kumbe kulikuwa na jambo lililokuwa likiendelea baina yao dhidi yangu.

     Hata hivyo sikuweza kuelewa ni kwa namna gani yule kijana aliyenishikia bastola nyuma yangu alikuwa amefanikiwa kuingia mle ndani pasipo kufanya kelele yoyote ya kunishtua. Hisia zangu zikanitanabaisha kuwa nilikuwa nimekutana na watu hatari na professional katika harakati za kijasusi. Nikapiga moyo konde na kumeza funda kubwa la mate kuupoteza mshtuko mkubwa usoni mwangu kisha nikageuka na kumtazama yule mtu mfupi mbele yangu aliyejinadi kwangu kuwa ndiye meneja wa ile hoteli kisha nikavunja ukimya.

    “Quelle obstacle?”. Kiunzi gani?. Nikauliza kwa kujiamini ingawa haraka niligundua kuwa sauti yangu ilikuwa imeanza kupwaya. Swali langu likaibua kicheko kingine cha ghafla kwa wale watu ingawa sikuweza kufahamu hasa ni kitu gani kikubwa katika swali lile kilichowapelekea wale watu waangue kicheko cha ghafla vile kama makahaba waliohongwa bia kaunta. Kicheko kile kilipokoma yule mtu mfupi mbele yangu akavunja ukimya na kuanza kuongea huku akinitazama kwa makini na nilipoyachunguza macho yake nikagundua kuwa hayakuwa na huruma hata kidogo.

    “Premier j?aimerais t?appelle Tibba Ganza, et non tes noms de massonge les quels tu utilises pour depasser les frontierres de nos pays”. Kwanza ningependa kukutambua kama Tibba Ganza na siyo hayo majina yako ya uongo unayoyatumia kwa ujanja kuvuka mipaka ya nchi zetu. Yule mtu mbele yangu akaongea kwa hakika huku akionekana kuwa na taarifa nyingi juu ya nyendo zangu hali iliyonipelekea nihisi kuwa wale watu walikuwa na ushirika mmoja na Amanda. Hivyo sikuwa tena na shaka kuwa hata taarifa zangu walikuwa wamezipata kutoka kwake...



    “Si tu n?as pas des reponses, alors laisser moi partir”. Kama huna majibu basi wacha mimi niondoke. Nikamwambia yule mtu mfupi mbele yangu huku nikifahamu fika kuwa tayari usalama wangu ulikuwa mashakani na hivyo nilipaswa kuwa makini sana na watu wale. Nikaanza kusimama nikitaka kuondoka hata hivyo sikufanikiwa kwani yule kijana nyuma yangu akanizaba makofi mawili ya nguvu kichwani kisha akamalizia kwa kunitandika ngumi moja ya mbavuni iliyonirudisha chini niendelee keti pale kwenye lile kochi kwa mkono wake mmoja uliokomaa kama mbao ya mninga.

    “Resté comme ça toi singe et n?ose pas de bouger”. Tulia hivyo hivyo wewe tumbili na usidhubutu kujitikisa. Yule kijana mwenye sare za mhudumu wa hoteli ile nyuma yangu akanionya na kwa kweli maumivu ya kile kipigo chake yalikuwa makali mno mwilini. Masikio yangu yakawa yakisikia sauti kali ya mvumo huku maumivu ya mbavu zangu yakinifanya niheme juu juu. Tukio lile likampelekea yule mtu mbele yangu aangue tena kicheko cha dhihaka kilichosindikizwa na mluzi mwepesi. Hatimaye nikamuona yule mtu mfupi akiingiza mkono wake mfukoni na kuchukua sigara kutoka katika pakiti. Alipoitia ile sigara mdomoni akajiwashia kwa kibiriti chake cha gesi na kuvuta mapafu kadhaa na kisha kuupuliza moshi wake angani tukio lililoonekana kumfurahisha sana. Hatimaye akuvunja ukimya.

    “Ne te trompe pas camarade tu vas nullpart. Nous etions etrer d?attendre cette chance pour lontemps et on ne peut pas le laisser faire encore’’. Usijidanganye komredi kwani huwendi popote. Tumekuwa tukiisubiri hii bahati kwa muda mrefu na hatuwezi kuichezea tena.

    “Qui etes-vous et vous avez quel problème avec moi?”. Ninyi ni akina nani na mna shida gani na mimi?. Nikawauliza wale watu kwa jazba na hapo nikamsikia yule mtu mfupi mbele yangu akinijibu kwa msisitizo.

    “C?est mieu de ne pas nous connaître”. Ni afadhali usitufahamu.

    “Je pense que vous avez la confision”. Nahisi mmechanganyikiwa. Nikawaambia wale watu kwa hasira na kabla sijamaliza kuongea yule kijana nyuma yangu akanitandika ngumi mbili za mgongo zilizonipelekea nihisi maradhi ya kichomi cha mbavu. Kwa kweli nilisikia maumivu makali mno yaliyonipelekea niheme ovyo huku yule kijana nyuma yangu akanivua lile koti langu na kuanza kunipekua. Alipomaliza akawa amefanikiwa kuipata ile bastola yangu iliyokuwa mafichoni tukio lile likampelekea atabasamu kabla ya kunizaba kofi moja la nguvu usoni kiasi cha kunifanya nione maruweruwe mbele yangu.

    “Tu as parvenu à nous echapé deux fois, mais c?est ne pas ce tour”. Ulifanikiwa kututoroka mara mbili lakini siyo sasa hivi. Yule kijana nyuma yangu akanionya huku akinisukasuka ovyo kwa mkono wake shingoni na kwa kweli kitendo kile kiliniudhi sana hata hivyo nilijipa uvumilivu.

    “Dis nous camarade, où arrive votre travail?”. Tuambie komredi kazi yako imefikia wapi?. Yule mtu mfupi mbele yangu akaniuliza huku akikung?uta majivu ya sigara yake kwenye kibakuli kidogo cha majivu ya sigara kilichokuwa juu ya ile meza ya ofisini.

    “Vous m?avez donné quelle travail ou bien vous avez la confision?” Kazi gani mliyonipa au mmechanganyikiwa?. Nikamuuliza yule mtu mfupi mbele yangu huku hasira zimenipanda na kwa kweli utulivu wa nafsi ulishapotea kabisa moyoni mwangu. Muda uleule mara nikamuona yule mtu mfupi aliyeketi kwenye kile kiti cha ofisini mbele yangu akisogeza kile kiti nyuma na kusimama kisha akapiga hatua zake hafifu kunikaribia pale kwenye kochi nilipoketi. Alipofika akanipulizia moshi wake wa sigara usoni kisha ghafla akanitandika ngumi mbili za tumbo huku akitabasamu kama hayawani. Maumivu makali yakasambaa mwilini mwangu na nilipomtazama usoni yule mtu nikaliona tabasamu lake la kinyama namna lilivyochanua.

    “Dis nous qu?est ce que tu es venu faire ici au Burundi?”. Tuambie umefuata nini hapa nchini Burundi?.

     Tukio lile likanipelekea nimkate jicho kali la hasira yule mtu huku nikitamani kusimama na kumtia adabu. Hata hivyo nafsi yangu ilinionya pale nilipoukumbuka ule mdomo wa bastola nyuma yangu namna ulivyokuwa ukitazamana na kisogo changu kwa uchu. Hivyo nikaamua kujipa utulivu.

    “Soyez vigilant je pense que vous avez la confision et la personne que vous cherchez c?est ne pas moi’’. Hebu kuweni makini nahisi mmejichanganya na mtu mnayemtafuta siyo mimi. Nikawaambia wale watu huku lengo langu likiwa ni kuzidi kuununua muda, kujitoa hatiani lakini vilevile kuipa akili yangu utulivu katika kufikiria nini cha kufanya ili kujinasua katika mtego ule.

    “D?accord, parceque tu ne veu pas nous dire de ta volonté, alors nous allons t?a mainer là où on va t?obliger de parler”. Okay, kwa kuwa hutaki kutuambia kwa hiari yako basi tunakupeleka sehemu utakayolazimishwa kutuambia. Yule mtu mfupi mbele yangu akaniambia kwa dhihaka.

    “Où est-ce que vous m?amainer?”. Mnanipeleka wapi?. Nikamuuliza yule mtu mfupi kwa shauku.

    “Attends, dans peu de temps tu vas voir”. Subiri muda siyo mrefu utaona. Yule mtu mfupi mbele yangu akiniambia huku akiirekebisha vizuri tai yake shingoni na kupitia maelezo yake nikafahamu kuwa alikuwa akimaanisha alichokuwa akikiongea. Sikutaka kuendelea kusubiri kwani nilifahamu fika nini ambacho kingefuatia baada ya pale. Hivyo kufumba na kufumbua nikageuka kwa pigo moja makini la kareti lililoipokonya vizuri bastola ya yule kijana nyuma yangu huku nikitupa teke farasi maridadi nyuma yangu lililomtupa vibaya yule kijana nyuma yangu kwenye ile meza ya ofisini na kumbwaga kama gunia. Yule kijana akanitukana tusi zito huku akinilaani kwa shambulizi lile makini la kushtukiza.

     Nikawahi kujitupa kando ya lile kochi hata hivyo yule kijana nyuma yangu hakunipa nafasi ya kujipanga badala yake akawahi kunichapa teke zito la kifuani lililonitupa ukutani na kunisababishia maumivu makali mno. Hata hivyo nilipoanguka tu chini nikawahi kusimama haraka na kujipanga. Pigo la pili la teke la yule kijana lilipokuja nikawahi kuliona hivyo nikalipangua kama mchezo kwa mikono yangu miwili kisha kwa nguvu zangu zote nikamsukumia yule kijana kwenye lile kabati la mle ofisini. Yule kijana hakuwa na namna ya kujitetea hivyo akajikuta akiparamia lile kabati kama kipofu na hatimaye kuanguka nalo sakafuni na hivyo kusababisha droo za lile kabati kufunguka na nyaraka zote za mle ndani kutawanyika ovyo.

     Yule mtu mfupi kuona vile akawahi kutumbukiza mkono wake kwenye koti lale la suti kuchukua bastola ili anilenge. Kuona vile nikawahi kujitupa kwenye lile kochi la sofa la mle ndani kisha nikabinuka nalo na kulifanya kama ngao ya kujikinga na risasi za yule mtu mfupi huku nikitafuta namna ya kujiweka mbali na hatari ile.

     Zile risasi za yule mtu mfupi zikawa zikinikosakosa na nilipoona hatari inazidi kunikaribia nikanyanyuka na lile kochi mzegamzega nikimfuata yule mtu mfupi aliyejinadi kwangu kuwa ndiye meneja wa ile hoteli. Hata hivyo haraka niligundua kuwa yule mtu mfupi hakuelekea kuwa meneja wa ile hoteli kwani alionekana kuwa makini zaidi kwenye mapigano baada ya kulikwepa lile kochi kama mchezo kwa kuruka hewani huku amechanua msamba wa nguvu jambo ambalo kamwe sikuwa nimelitarajia kutokana na ufupi wake. Hata hivyo sikumsubiri yule mtu mfupi amalizie mbwembwe zake hivyo alipotua chini tu nikawa tayari nimemfikia na kumsindikiza kwa pigo matata la teke lililomtupa chini huku akipiga yowe la hofu.

     Hata hivyo furaha yangu haikukamilika kwani wakati nilipokuwa nikigeuka nikajikuta nikitandikwa teke moja la shingo na yule kijana mwenye sare za mhudumu wa ile hoteli. Maumivu makali yakasambaa mwilini huku nikipepesuka ovyo kurudi nyuma kama bondia aliyepigwa konde zito la kichwani na mpinzani wake. Nilipokuwa mbioni kutafuta mhimili wa kusimama yule kijana akaniwahi kwa kunitandika pigo lingine la teke la kifuani liitwalo Hook kick lililonilevya vibaya baada ya kujipigiza ukutani huku maumivu makali yakisambaa mwilini kama niliyetupiwa tofali gumu za zege.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Pigo lile likawa limempelekea yule kijana mwenye sare za mhudumu wa ile hoteli anogewe na mafanikio yale hivyo haraka akinifikia na kutupa mapigo matatu ya Kung-fu ambayo niliyaona vizuri na kuyakwepa kwa ulaini kama upepo. Pigo lake la tatu shingoni kwangu nikalipangua na hapo nikapata nafasi nzuri ya kutupa ngumi mbili kwenye koo lake kisha nikamchapa mapigo matatu makini yaliyotia udhaifu mkubwa tumboni mwake na kumsababishia kichefuchefu cha ghafla. Kisha nikamalizia kwa kumchapa teke moja matata la korodani lililompelekea abweke kama mbwa koko huku akupepesuka kama mlevi na kuanguka chini.

     Yule mtu mfupi aliyejinadi kwangu kuwa ndiye meneja wa ile hoteli kuona vile akawahi kuiokota bastola yake sakafuni kule ilipoangukia hata hivyo hakufanikiwa kwani niliwahi kulishika pindo la lile zulia dogo alilokanyaga ambalo lilikuwa katikati ya ile ofisi. Kisha nikalivuta lile zulia kwa nguvu na hivyo kumchota yule mtu mfupi mtama mzuri wa aina yake uliyompaisha hewani kama bwege na alipotua chini akafikia juu ya ile meza fupi ya kioo na kuvunjika mkono. Ile meza ikavunjika vipande vipande huku yule mtu mfupi akipiga yowe kali la maumivu.

     Yule kijana mwenye sare za mhudumu wa ile hoteli alikuwa tayari ameshakusanya nguvu za kutosha hivyo kuona vile akaokota lile koti langu na kunirushia kichwani pale nilipokuwa huku akinifuata kwa kasi ya ajabu. Haraka nikajua kuwa lengo lake lilikuwa ni kunifunika kwa hila na lile koti ili hatimaye apate nafasi nzuri ya kunishambulia. Hata hivyo niliwahi kuishtukia mapema hila ile hivyo nikawahi kulinasa lile koti hewani kwa mguu wangu wa kushoto kisha nikalizungusha kwa kasi na kumtupia yule kijana ambapo lilimfikia vizuri na kumziba usoni. Yule kijana alipokuwa akihangaika kulitoa lile koti usoni nikawa tayari nimemfikia hata hivyo alikuwa mpambanaji mwenye ujuzi wa hali ya juu kwani japokuwa alikuwa haoni mbele yake lakini alijitahidi kwa kila namna kuyazuia vyema mapigo yangu akianzia kichwani, kifuani na tumboni. Hatimaye akafanikiwa kuliondoa lile koti usoni mwake na kulitupa kando.

     Sasa tukawa tukipambana kwa mapigano ya ana kwa ana huku kila mmoja akijitahidi kumsoma vizuri mwenzake. Pigo moja la yule kijana sikuliona mapema hivyo lilitua vibaya tumboni mwangu na kwa kuwa sikuwa nimejiandaa maumivu yake yakanifanya nihisi kutaka kutapika. Pigo lake la pili la kareti likatua shingoni mwangu na hapo sekunde kadhaa nikahisi kukatika kwa mawasiliano kati ya shingo yangu na sehemu nyingine za mwili wangu.

     Haraka nikarudi nyuma na kuishika shingo yangu nikiigeuza geuza huku na kule hadi pale niliporidhika kuwa ilikuwa imerudi mahala pake ndiyo nikajipanga. Pigo la tatu la teke liliponijia nikawahi kuinama kidogo na kuliacha likikata upepo angani bila mafanikio na hapo nikageuka kwa hasira na kumchapa yule kijana ngumi tatu makini za mgongoni. Alipogeuka nikamuwahi kwa kichwa makini kilichoupasua vibaya mwamba wa pua yake na kumtupa nyuma huku damu nyingi ikianza kumtoka puani. Yule kijana akiishika pua yake kwa maumivu makali mno huku akitukana kila aina ya matusi na alipoona hali inazidi kuwa mbaya haraka akachomoa kisu chake cha mkunjo kutoka mafichoni. Hivyo wakati nilipokuwa nikimkaribia bila kujua pigo lake moja likanichana begani na kupelekea damu nyingi ianze kunitoka kwenye lile jeraha.

     Mchezo wa visu japokuwa nilikuwa nikiumudu vizuri lakini kamwe sikuupenda kwani kosa moja la kutokwepa vizuri shambulio lilikuwa likileta matokeo yenye athari mbaya kwa mhanga. Pigo lingine lilipokuja nikajitahidi kulikwepa hata hivyo nilichelewa kidogo kwani kile kisu kilinichana vibaya mkononi na kunisababishia jeraha lingine linalovuja damu. Yule mwenzake mfupi alikuwa tayari amepata nguvu mpya hivyo akasimama na kunifuata kwa kasi huku akipega makelele kama mwehu. Hata hivyo hakunifikia kwani alipokuwa akinikaribia nikamrudisha kule alipotoka kwa teke moja makini la kinyume nyume lililomtupa kwenye ile meza kubwa ya ofisini na kubinuka vibaya.

     Pigo lingine la yule kijana liliponijia nikawahi kulipangua kwa nguvu zote na hapo kile kisu mkononi kikamponyoka na kurukia hewani. Ilikuwa nafasi nzuri kwani nilijirusha hewani na kukiwahi kile kisu kabla hakijatua kisha nilipoanguka chini nikajiviringisha haraka mbali na eneo lile kwa mtindo wa kininja halafu kwa wepesi wa ajabu nikakizungusha kile kisu na kukitupa kwa yule kijana mwenye sare za mhudumu wa ile hoteli. Yule kijana akajitahidi kukikwepa kile kisu bila mafanikio.

     Shabaha yangu ilikuwa makini sana kwani kile kisu kilisafiri angani na hatimaye kupenya kwenye tumbo la yule kijana huku sehemu tu ya mpini wake ikibaki nje. Yule kijana akapiga yowe kali la hofu hata hivyo alikuwa na roho ngumu kama paka kwani badala yake akasimama kwa ghadhabu huku akikichomoa kile kisu tumboni mwake na kuanza kunifuata kwa hasira kama zombi. Kweli nilishangazwa sana na tukio lile kwani yule kijana hakuelekea kujionea huruma hata kidogo kutokana na damu nyingi iliyokuwa ikimtoka kwenye lile jeraha tumboni mwake.

     Haraka nilipogeuka kumtazama yule mtu mfupi aliyejinadi kwangu kuwa ndiyo meneja wa ile hoteli nikamuona kuwa alishaikamata vyema bastola yake na kuanza kuielekezea kwangu. Sikuwa na mashaka yoyote kuwa endapo mtu yule angevuta kilimi cha ile bastola asingenikosa hata kama angekuwa mzembe wa shabaha kwa kiasi gani.

     Nikiwa tayari nimeiona hatari ile sikutaka kutoa nafasi hivyo nikasubiri kidogo yule kijana anifikie kisha nikamkwepa kidogo na kumsindikiza kwa teke maridadi kuelekea kwa yule mtu mfupi. Bila shaka yoyote mahesabu yangu yalikuwa makini kwani wakati yule kijana akitupwa kwa pigo langu upande ule na yule mtu mfupi aliyejinadi kwangu kuwa ndiye meneja wa ile hoteli naye akawa tayari amefyatua risasi pasipo kuwa makini.

     Kufumba na kufumbua nikamuona yule kijana akitupwa hewani kwani risasi za yule mtu mfupi zilikuwa tayari zimefanikiwa kulifumania vizuri pafu lake la upande wa kushoto. Nikamsikia yule kijana akipiga yowe hafifu la maumivu na alipotua chini akatikisa kidogo na kutulia sakafuni huku roho yake ikiwa mbali na mwili...



    Wakati yule mtu mfupi aliyejinadi kwangu kuwa ni meneja wa ile hoteli akiwa ameshikwa butwaa kwa kitendo cha kumuua mwenziwe mimi nikawahi kujitupa kando ya eneo lile karibu na lile kochi la mle ofisini lilipokuwa limeangukia lile koti langu jeusi la mvua. Kisha nikaupenyeza mkono wangu kwenye mfuko wa koti lile na kuchomoa bastola na mara hii sikutaka kupoteza muda. Hivyo risasi moja niliyoiruhusu kufanya safari ikasafiri kwa shabaha makini na kukisambaratisha vibaya kiganja cha mkono cha yule mtu mfupi na hapo ile bastola ikamponyoka mkononi huku akiwa ameingiwa na hofu kuu. Ndani ya sekunde chache tayari nikawa nimemfikia yule mtu pale alipokuwa amesimama huku akiwa anaweweseka ovyo kwa hofu ya maumivu kama mwehu.

     Yule mtu mfupi kuona vile akawahi kujihami kwa kurusha teke hata hivyo lilikuwa pigo dhaifu kwani niliwahi kulidaka kisha nikamchota mtama maridadi kupitia mguu wake mmoja uliosalia chini. Pigo lile likampelekea yule mtu atue chini kwa matako na kupiga yowe kali la maumivu huku akiponyokwa na tusi zito mdomoni. Alipotaka kuinuka akajikuta akitazamana na mdomo wa bastola yangu mkononi. Hofu iliyomuingia ikamrudisha chini taratibu huku akiona aibu kunitazama usoni.

    “Qui etes-vous?”. Wewe ni nani?. Nikamuuliza yule mtu kwa hasira.

    “Leonidas Ndikumagenge”. Yule mtu akajitambulisha kwa hofu.

    “Vouz aves quel problème avec moi?”. Mna shida gani na mimi?. Nikamuuliza yule mtu hata hivyo hakunijibu badala yake akainamisha kichwa chake chini. Sikumkawiza badala yake nikamzaba makofi mawili ya nguvu kumuweka sawa kabla ya kumuuliza tena.

    “Vous etes envoyer par qui?”. Mmetumwa na nani?. Nikamkwida tai yake shingoni yule mtu na kumuuliza huku akiugulia maumivu ya ule mkono wake uliovunjika na kile kiganja chake nilichokisambaratisha kwa risasi.

    “Je ne sais pas”. Sifahamu. Yule mtu mfupi akinijibu kwa mkato na hapo nikamzaba tena kofi la usoni lililompelekea azidi kuona maruweruwe huku akiendelea kuugulia maumivu. Nikazidi kumkwida shingo yake kwa ile tai huku nikiendelea kumuuliza.

    “Vous etes à combien dans ce battument?”. Mpo wangapi kwenye hili jengo?.

    “Nous sommes trois”. Tuko watatu. Yule mtu mfupi akanijibu kwa hofu na hapo nikamtazama kidogo huku nikitafakari juu ya lile jibu lake. Hatimaye nafsi yangu ikajiridhisha kuwa huwenda mtu yule alikuwa akizungumza ukweli pale nilipowakumbuka wale vijana wawili walionikaribisha kule mapokezi ambao mmoja wapo ndiye yule niliyetoka kupambana naye muda mfupi uliopita mle ndani. Hatimaye nikayapeleka tena macho yangu kumtazama Yule mtu mfupi pale chini.

    “Tu sais quoi consernant le Pretre Aloysius Kanyameza?”. Unafahamu nini kuhusu Padri Aloysius Kanyameza?. Nikamuuliza tena yule mtu mfupi huku nikiusukasuka ovyo ule mkono wake uliovunjika.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Je ne sais rien, et je ne lui conais même pas”. Sifahamu chochote na wala simjui. Yule mtu mfupi akaongea kwa tabu huku akilalama kwa maumivu makali ya majeraha yake mikononi. Nilifahamu fika kuwa alikuwa akinidanganya kupitia jibu lake hata hivyo katika mazingira yale sikuona kama alikuwa tayari kuzungumza ukweli wowote. Kitambo kifupi cha ukimya kikapita mle ndani huku nikifikiria nini cha kufanya na nilipokuwa katika hali ile yule mtu akavunja tena ukimya akiongea kwa shida.

    “N?esaye pas de fuire tu ne vas pas arrivé loin, parceque nos gents sont partout”. Usijaribu kutoroka hutofika mbali kwani watu wetu wapo kila mahali. Nikamsikiliza vizuri yule mtu na hapo nikagundua kuwa alikuwa akijitahidi kuniogopesha kuwa bado sikupaswa kuitwa mshindi katika vita ile. Hata hivyo nikalipuuza onyo lake kumtupia swali lingine.

    “Où est I?autres?”. Yule mwenzako yuko wapi?.

    “II est dans votre vehicule là dehors il vous attend”. Yupo kwenye gari lako kule chini nje ya hoteli anakusubiri. Maelekezo ya yule mtu mfupi yakanipelekea nishikwe na mshangao. Kumbe wale vijana wawili niliyowakuta pale mapokezi kule chini kwenye ile hoteli walikuwa mamluki waliopandikizwa katika namna ya kuhakikisha kuwa ninakamatwa mapema kabla sijafika mbali katika harakati zangu. Hivyo yule kijana mwingine wa pale mapokezi alikuwa ameenda kunivizia kwenye gari langu ili ikitokea kuwa nimewatoroka mwenzake aweze kunimaliza kiulaini. Mawazo yale yakapelekea tabasamu jepesi kuumbika usoni mwangu.

    “Comment s?appelle l?autre”. Anaitwa nani?.

    “Il s?appelle Blaise”. Anaitwa Blaise Tugiramahoro. Yule mtu mfupi akanijibu kwa uoga na nilipomkata jicho la hadhari akanyoosha maelezo.

    “II s?appelle Blaise Tungiramahoro’’. Anaitwa Blaise Tugiramahoro.

     Nikamsikiliza yule mtu kwa utulivu na wakati nilipokuwa nikijiandaa kumuuliza swali lingine mara ghafla nikasikia ile kengele ya nje ya mlango wa kile chumba ikilia. Nilipoyatega vizuri masikio yangu ile kengele ikanitanabaisha kwa nje ya kile chumba mlangoni kulikuwa na mtu aliyekuwa akihitaji kuingia mle ndani. Haraka nikayarudisha tena macho yangu kumtazama yule mtu mfupi mateka wangu na sikuona kama angekuwa na taarifa zozote nyingine muhimu za kunisaidia. Hivyo nikainyanyua bastola yangu mkononi na kabla yule mtu hajazungumza alichotaka kuniambia risasi zangu mbili tayari zilikuwa mwilini mwake. Risasi moja kwenye moyo kifuani mwake na risasi nyingine shingoni pasipo kelele yoyote mle ndani kwani bastola yangu ilikuwa imefungwa kiwambo maalum cha kuzuia sauti.

     Muda mfupi uliofuata nikawa tayari nimeufikia ule mlango wa kile chumba na kabla ya kuufungua nikainama na kuchungulia kwenye tundu la funguo kwenye kitasa cha ule mlango. Nilichokiona kule nje ya ule mlango kikanitahadharisha kuwa mambo hayakuwa shwari. Mwanaume fulani aliyevaa sare za mhudumu wa ile hoteli alikuwa amesimama nje ya ule mlango wa kile chumba. Sura yake, kiwiliwili wala sehemu yake ya chini sikuweza kuiona kutokana na udogo wa lile tundu la funguo pale mlangoni. Hata hivyo mtu yule mkononi alikuwa ameshika sinia lenye chupa moja ya mvinyo mwekundu wa kifaransa Château Lascombes na glasi moja ndefu yenye karatasi nyeupe ya tishu ndani yake. Nilipozidi kuchungulia vizuri nikashtukia kuwa chini ya lile sinia yule mtu alikuwa ameshika bastola.

     Sasa sikuwa na shaka tena kuwa hatari ilikuwa mlangoni. Hata hivyo niliwaza kuwa kuendelea kusubiri zaidi pasipo kufungua ule mlango kungeweza kumpelekea yule mtu aliyesimama pale mlangoni kuingiwa na wasiwasi na hivyo kutafuta namna nyingine ya kunikabili. Hivyo haraka nikaichomeka bastola yangu nyuma kiunoni na kuufungua taratibu ule mlango huku tabasamu la kirafiki likiwa usoni mwangu. Yule mtu aliyekuwa akibisha hodi nje ya ule mlango haraka nilipomchunguza nikamkumbuka kuwa alikuwa ni yule kijana mwingine kati ya wale vijana wawili walionikaribisha vizuri muda mfupi uliopita kule chini ya ile hoteli sehemu ya mapokezi. Ambaye yule mtu mfupi aliyejinadi kwangu kuwa ndiye meneja wa ile hoteli ambaye sasa alikuwa marehemu mle ndani alikuwa amemnasibu kwa jina la Blaise Tigiramahoro. Alikuwa ni yule kijana aliyesemekana kunisubiri kwa kunivizia kwenye gari langu kule nje chini ya ile hoteli.

    “Oh! bien venue monsieur”. Oh! karibu sana ndugu. Nikamkaribisha yule kijana kwa utulivu huku usoni nikiwa nimeumba tabasamu la kirafiki. Hata hivyo haraka niliweza kuuona mshtuko mkubwa usoni kwa yule kijana kiasi cha kumpelekea asite kuingia mle ndani. Lakini tabasamu na macho yangu vikamshawishi aingie na huku nikizidi kuufungua zaidi ule mlango wakati huo nikijitahidi kuuegemea ule mlango. Yule kijana ikabidi anitazame kidogo huku usoni mwake akilazimisha tabasamu ingawa nilipomchunguza vizuri nikafahamu kuwa macho yake hayakwendana kabisa na lile tabasamu lake badala yake alionekana kujawa na wasiwasi mwingi. Hata hivyo akajikaza na kuniitikia kwa utulivu ingawa sauti yake ilipwaya kidogo.

    “Merci beaucoup!”. Ahsante sana!. Yule kijana akaitikia huku akiingia mle ndani kwa tahadhari na sinia lake mkononi. Sikuwa na muda wa kupoteza hivyo mara baada ya yule kijana kuingia mle ndani haraka nikaufunga ule mlango nyuma yake. Hata hivyo yule kijana alikuwa amejiandaa kwani mara tu alipoingia mle ndani haraka akalitua lile sinia chini na kugeuka huku akiwa na bastola yake mkononi.

     Nikiwa nimejiandaa kwa tukio lile sikutaka kumpa nafasi ya kuonesha umahili wake yule kijana hivyo kabla hajamalizia vizuri kuielekeza bastola yake kwangu tayari nilikuwa nimegeuka na kuvuta kilimi cha bastola yangu mkononi. Risasi yangu moja ikatoboa pafu lake la kulia huku risasi nyingine ikiacha tundu dogo linalovuja damu nyingi kwenye moyo wake. Yule kijana akapiga mweleka wa nguvu na alipoanguka chini akatikisika kidogo na kutulia.

     Muda haukuwa rafiki tena kwangu kwani nilifahamu fika kuwa muda siyo mrefu washirika wa watu wale wangeweza kuhisi kilichowasibu wenzao kwenye kile chumba na hivyo kufika mle ndani haraka jambo ambalo kamwe sikupenda litokee kabla sijatoka kwenye kile chumba cha ile ofisi na hatimaye kutokomea mbali kabisa na lile eneo.

     Hivyo nilianza kwa kupitisha upekuzi wa haraka mle ndani. Kupitia zile nyaraka za kiofisi zilizokuwa kwenye kabati la mle ndani na droo za ile meza kubwa ya ofisini niliweza kugundua kuwa meneja wa ile hoteli alikuwa haitwi jina la Vital Desire Habonimana kama yule mtu mfupi alivyojinadi pale awali. Meneja wa ile hoteli alikuwa akifahamika kwa jina la ndugu Alain Basuzuguye.

     Hatimaye nilimaliza kufanya upekuzi katika zile nyaraka za kiofisi kwenye lile kabati na zile droo za ile meza ya ofisini pasipo kupata kitu kingine chochote cha maana. Hivyo nikahamishia upekuzi wangu kwenye ile miili ya wale watu niliyopambana nao na kuwaangamiza mle ndani. Kitu kilichonishangaza kama siyo kunishtua ni kuwa katika mavazi ya wale watu niligundua vitu vidogo vyeusi mfano wa vifungo vilivyonasishwa vizuri kwenye kosi za mashati yao. Nilipoendelea kuchunguza haraka nikagundua kuwa vile vidude vilikuwa ni vifaa pandikizi vya mawasiliano ya kijasusi viitwavyo UHF-Voice Transmitters vinavyoweza kunasa mazungumzo ya watu waliopo ndani ya umbali wa futi thelathini na tano na kuyasafirisha mawimbi ya maongezi hayo katika umbali usiopungua mita mia tatu au sawa na urefu wa viwanja vitatu vya mpira wa miguu.

     Nikavitazama vifaa vile vya mawasiliano kwa utulivu huku mawazo mengi yakipita kichwani mwangu. Kwa namna moja au nyingine nilikuwa na kila sababu ya kuamini kuwa maongezi kati yangu na wale watu mle ndani yalikuwa yamesikika na mtu au watu fulani waliokuwa ndani ya lile jengo la hoteli au mbali na ile hoteli sehemu fulani ambayo sikuifahamu. Nilipozidi kuwaza nikaja na hitimisho kuwa kulikuwa na uwezekano mkubwa kuwa mtu au watu hao waliokuwa wakifuatilia maongezi yale baada ya kupoteza mawasiliano na wenzao wa mle ndani sasa wangekuwa katika jitihada kubwa za kukifikia kile chumba cha ile ofisi ya meneja wa ile hoteli kama siyo kulifikia lile jengo la hoteli ikiwa ni sehemu ya mkakati wao katika kuhakikisha kuwa sitoroki na kuwaacha solemba.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Nilifahamu hatari ambayo ingenifikia endapo ningeendelea kupoteza muda wangu ndani ya kile chumba. Hivyo haraka nikavitupa sakafuni vile vifaa vidogo vya mawasiliano ya kijasusi kutoka katika miili ya wale watu na kuvikanyaga kwa buti zangu ngumu miguuni nikivisaga kuviharibu. Kisha haraka nikasogea kwenye dirisha la ile ofisi na kusogeza pazia kando nikitazama kule chini nje ya lile jengo. Kwa kufanya vile nikashikwa na mstuko kidogo. Chini ya lile jengo usawa wa dirisha la ile ofisi nikawaona wanaume watatu waliovaa sare za kijeshi wakioneshana kwa vidole vyao katika kile chumba cha ofisi nilichokuwa ndani yake. Tukio lile kwangu ilikuwa ni ishara mbaya hivyo haraka nikalirudishia vizuri lile pazia pale dirishani huku moyo wangu ukiwa umeanza kupoteza utulivu. Haraka nikaelekea kwenye ule mlango wa mle ndani kuelekea kile chumba cha maliwato. Nilipofika nikaufungua ule mlango kwa tahadhari bastola yangu ikiwa mkononi katika namna ya kuchunguza usalama wa mle ndani. Sikuona kitu chochote cha maana hivyo nikaufunga ule mlango huku akili yangu ikianza kufanya kazi ya ziada katika kufikiria ni kwa namna gani ningeweza kulitoroka lile jengo pasipo kukabiliana na upinzani mwingine mbele yangu.

     Nikiwa katika ile hali kuendelea kufikiria mara nikawa nimepata wazo. Haraka nikaisogelea maiti ya yule kijana wa mwisho kupambana naye mle ndani kisha nikaanza kumvua zile sare za mhudumu wa ile hoteli upesi. Nilipomaliza nikazivaa nguo zile haraka juu ya nguo zangu ingawa zilikuwa na mabaka ya damu hata hivyo nilijitahidi kuzitengeneza kwa kila namna katika namna ya kuondoa viashiria vya haraka vya kutiliwa mashaka na mtu yeyote ambaye angenitazama juu juu. Nilipomaliza nikalichukua lile koti langu la mvua na kulikunja vizuri kisha nikalichukua lile sinia lenye ile chupa ya kinywaji na glasi nikilibeba kwa uangalifu. Baada ya kujihisi nimeuvaa vyema muonekano wa mhudumu wa ile hoteli nikaivua kofia yangu kichwani na kuikunjia ndani ya lile koti nililolishikilia vizuri chini ya lile sinia. Bila kupoteza muda nikavaa kofia ya mhudumu wa ile hoteli na kuitengeneza vizuri kichwani mwangu. Niliporidhika vizuri na muonekano wangu nikafungua mlango wa kile chumba na kutoka huku nikiiweka vizuri ile chupa ya ule mvinyo juu ya lile sinia ili kuficha yale madoa ya damu yaliyokuwa kifuani kwenye lile vazi la mhudumu wa ile hoteli nililolivaa.

     Nilipotoka nje ya kile chumba nikashika uelekeo wa upande wa kulia nikielekea mwisho wa ile korido sehemu kulipokuwa na ngazi za kushukia chini ya lile jengo. Sikutaka kutumia lifti kushuka chini ya lile jengo kwa kuanzia ghorofa ile kwani kufanya vile ningetengeneza ushahidi wa wazi kwa mtu yeyote aliyekuwa akinifuatilia. Hivyo nilipofika mwisho wa ile korido nikaanza kushuka zile ngazi kwa haraka nikielekea chini kwenye ghorofa ya nne ya lile jengo. Wakati nilipokuwa nikishuka zile ngazi nikakutana na wanaume wawili waliovaa suti nadhifu nyeusi wakipanda zile ngazi kwa pupa na nilipowatazama haraka nikawatambua kuwa hawakuwa watu wa kawaida kutokana na muonekano wao. Wakati nikipishana na watu wale hawakusalimiana na mimi badala yake nikawaona haraka wakiipeleka mikono yao kwenye mifuko ya makoti yao ya suti huku wakinitazama kwa macho ya mashaka. Hata hivyo haraka nilibadili dhamira yao kwa kuwasalimia vizuri huku nikitabasamu. Wale wanaume hawakuitikia salamu yangu badala yake wakanipita na kuendelea na safari yao huku...



    ...wakigeuka na kunitazama kwa mashaka wakiendelea kuzipanda zile ngazi kwa bidii. Sikugeuka tena nyuma kuwatazama badala yake nikakazana kuzitupa hatua zangu kuendelea mbele na safari.

     Nilipomaliza kushuka zile ngazi nikawa nimetokezea kwenye korido ya ghorofa ya nne ambapo nilishika uelekeo wa upande wa kushoto nikielekea mwisho wa ile korido sehemu kulipokuwa na lifti ya lile jengo ili nishuke chini. Hata hivyo wakati nilipokuwa nikiikaribia ile sehemu ya lifti ya lile jengo mara ghafla nikakiona kile chumba cha lifti kikitia nanga kwenye korido ya ile ghorofa ya nne kisha mlango wake ulipofunguka akatoka mwanaume mmoja mweusi, mrefu na mwenye misuli imara ya nguvu mwilini huku akiwa amenyoa upara. Macho ya mtu yule yalikuwa yamefichwa vizuri nyuma ya miwani nyeusi. Yule mtu alikuwa amevaa suti nyeusi ambayo kutokana na ukubwa wa mwili wake wenye misuli imara suti ile ilionekana kama ambayo haimtoshi vizuri kwa namna ilivyombana katika baadhi ya maeneo ya mwili wake huku weusi wa ile suti na rangi yake vikimpelekea aonekane kama mpingo.

     Kitendo cha kumuona yule mtu akija ule upande wangu kikaupelekea moyo wangu ulipuke kwa hofu huku kwa tahadhari nikiipapasa bastola yangu chini ya lile sinia nililolibeba mkononi baada ya kuanza kuhisi hali ya hatari. Yule mtu kuona vile akawahi kuupeleka mkono wake kwenye mfuko wa koti lake la suti huku akinikazia macho kunitazama kwa makini. Nikameza fundo kubwa la mate huku nikijitahidi kutabasamu hata hivyo ni kama tabasamu langu liliishia njiani kwa hofu na kunipelekea nionekane kama ninayetaka kucheka pasipo kitu cha kuchekesha. Yule mtu aliponikaribia akazidi kukaza uso wake kunitazama huku taratibu akipunguza urefu wa hatua zake huku mkono wake mmoja ukiwa bado upo kwenye mfuko wa ndani wa koti lake la suti. Haraka nikagundua kuwa alikuwa akiipapasa bastola yake mfukoni tayari kukabiliana na chochote.

     Hofu ikiwa imeanza kuniingia nikapiga moyo konde na kumeza funda kubwa la mate kuitowesha hofu iliyoanza kujengeka nafsini mwangu na katika harakati za kurudisha hali ya kujiamini wakati nikipishana na yule mtu nikamuuliza huku nikilazimisha tabasamu la kirafiki usoni mwangu.

    “Y at-il quelque chose de mal patron?”. Kuna tatizo lolote bosi?.

    “Occupe toi de tes affaires”. Fuata mambo yako. Yule mtu akanijibu kwa jeuri huku taratibu akiutoa mkono wake mfukoni na kunipiga kumbo hafifu huku akiendelea na safari yake. Kwa sekunde kadhaa moyo wangu ukawa ni kama ulioshika ganzi huku baridi nyepesi ikisambaa mwilini mwangu. Hata hivyo nilijitahidi kwa kila namna kuimeza hofu yangu huku nikiendelea mbele na safari yangu pasipo kugeuka nyuma.

     Wakati nikikifikia kile chumba cha lifti nikagundua kuwa kilikuwa kimepanda ghorofa ya juu kumpeleka mtu mwingine hivyo nikabonyeza kitufe cha kushuka chini kuiita ile lifti. Ile lifti iliposhuka na mlango wake kufunguka haraka nikaingia mle ndani na kubonyeza kitufe cha kushuka ghorofa ya chini kabisa ya lile jengo.

     Wakati nikishuka chini ya lile jengo la ile hoteli mawazo mengi yakawa yakipita kichwani mwangu. Kupitia wale wanaume wawili niliopishana nao wakati nikishuka zile ngazi kuelekea ghorofa ya nne ya lile jengo na yule mtu matata niliyepishana naye muda mfupi uliopita kwenye ile korido. Sasa nilikuwa na hakika kuwa uwepo wangu kwenye lile jengo la hoteli ulikuwa ukifahamika na adui zangu lakini vilevile nilipokumbuka juu ya vile vifaa vya kijasusi nilivyovigundua kwenye miili ya wale watu niliopambana nao kule ofisini. Ilikuwa ni ishara tosha kuwa nilikuwa nimejitumbukiza kwenye mkasa hatari wa mapambano dhidi ya watu wenye ujuzi wa hali ya juu katika masuala ya kijasusi. Hivyo nafsi yangu ikazidi kunionya kuwa niwe makini sana na nyendo zangu.

     Ndani ya muda mfupi kile chumba cha lifti kikawa kimefika ghorofa ya chini kabisa ya lile jengo la ile hoteli New Parador Residence. Mlango wa kile chumba cha lifti ulipofunguka nikatoka nje na kupishana na wanaume wengine wawili ambao haraka waligeuka na kunitazama kabla hawajaingia kwenye ile lifti. Mara tu nilipotoka kwenye kile chumba cha lifti sikutaka kutoka nje ya lile jengo kwa kupitia ule mlango mkubwa uliokuwa sehemu ya mbele ya ile hoteli. Hivyo haraka nikashika uelekeo wa upande wa kushoto nikipotelea gizani nyuma ya ile sehemu ya mapokezi ya ile hoteli huku nikijitahidi kutoyavuta macho ya mtu yeyote ambaye angekuwa akinitazama.

     Sikuwa mwenyeji wa mazingira yale hivyo kwa kila namna nilijitahidi kuwa mwangalifu. Nyuma ya ile sehemu ya mapokezi nikatokezea kwenye korido pana yenye mwanga hafifu. Nikaanza kuufuata uelekeo wa korido ile pasipo kutambua ilikuwa ikielekea wapi huku mara kwa mara nikigeuka nyuma kutazama kama kulikuwa na mtu yoyote ambaye angekuwa akinifuatilia. Sikumuona mtu yoyote hivyo hali bado ilikuwa shwari. Nilipofika kule mbele nikagundua kuwa ile korido ilikuwa imebadili uelekeo na kufuata upande wa kulia na niliposoma kibao elekezi kwenye ile korido nikagundua kuwa ule uelekeo ulikuwa ni wa kwenda kwenye sehemu za maliwato ya wahudumu wa ile hoteli. Hivyo nikauacha ule uelekeo na kuanza kushuka ngazi zilizokuwa mbele ya kona ya ile korido sehemu yenye giza. Niliporidhika kuwa nimetokomea kabisa gizani sehemu ile nikalitelekeza chini lile sinia kisha nikazivua zile sare za mhudumu wa ile hoteli na kulivaa vyema lile koti langu jeusi la mvua. Ile chupa ya mvinyo mwekundu wa gharama wa kifaransa Château Lascombes nikaitia kwenye mfuko wa koti langu na kuzidi kushuka zile ngazi gizani.

     Nilipofika chini kabisa ya zile ngazi nikashika uelekeo wa upande wa kushoto nikitembea katika uchochoro mwembamba wenye giza nene. Nilitamani kuwasha kurunzi yangu mkononi hata hivyo nilijikuta nikisita kufanya vile baada ya kuhisi kuwa mwanga wake ungeweza kumvuta mtu yeyote ambaye angekuwa eneo lile.

     Baada ya safari fupi hatimaye nikaanza kuuona mwanga hafifu wa taa kabla ya kusikia maongezi ya watu eneo lile. Nilipochunguza nikagundua kuwa nilikuwa nimetokezea kwenye sehemu ya jiko la ile hoteli na wakati nikiendelea kutembea nikahisi kuwa nilikuwa nikilikaribia zaidi lile eneo la jiko la ile hoteli. Kwa mbali niliweza kuwaona wapishi katika sare zao za kazi wakiendelea na shughuli zao kwenye jiko lile. Hewa ya mle ndani ilikuwa nzito kidogo kutokana na moshi mwingi na joto kali ambalo lilikuwa likitoka kwenye ile sehemu ya lile jiko.

     Niliendelea kutembea kwa utulivu na nilipokaribia lile jiko upande wa kulia nikaiona korido nyingine ambayo chini yake ilikuwa imetandazwa mabomba mengi ya maji, gesi na nyaya za umeme huku eneo lile likitawaliwa na harufu ya mnuko wa mafuta ya vyakula.

     Hatimaye nikauacha ule uelekeo wa lile jiko la ile hoteli na kuanza kuifuata ile korido ya upande wa kulia kwa tahadhari huku mara kwa mara nikigeuka na kutazama nyuma kama kungekuwa na mtu yeyote akinifuatilia. Baada ya umbali mfupi wa safari yangu mara nikauona mlango mmoja wa chumba cha stoo. Nilipochunguza vizuri nikagundua ule mlango ulikuwa wazi na ndani yake kulikuwa na watu kutokana na minong?ono hafifu iliyokuwa ikisikika. Kwa tahadhari nikaupita mlango wa kile chumba na kuendelea mbele na safari yangu na baada ya hatua chache nikakutana na korido nyingine inayokatisha mbele yangu. Nilipofika kwenye ile korido nikasimama na kuanza kulichunguza eneo lile kwa makini.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Kulikuwa na giza zito eneo lile ingawa kupitia mwanga hafifu uliopenya kutoka lile eneo la jiko niliweza kuona kwa shida mandhari yale. Ile korido kwa upande wa kulia ilikuwa ikielekea kwenye tenki kubwa la maji ya akiba ya ile hoteli na nilipochunguza vizuri nikagundua kuwa hakukuwa na uelekeo mwingine baada ya ile sehemu yenye lile tenki la maji. Hivyo nikaamua kushika uelekeo wa upande wa kushoto nikitembea katikati ya korido nyembamba inayotazamana na vyumba vyenye mitambo ya umeme huku bastola yangu ikiwa imetuama vyema mkononi.

     Baada ya muda mfupi nikawa nimetokezea kwenye sehemu kubwa ya wazi yenye mitambo mingine mikubwa ya umeme wa lile jengo likiwemo jenereta kubwa umeme wa dharura. Nilipofika pale nikasimama tena nikiyapeleleza vizuri mazingira yale na kwa kufanya vile upande wa kulia nikauona mlango mkubwa wa wavu na nondo za chuma kuelekea sehemu ya nyuma ya ile hoteli. Hisia zangu zikanieleza kuwa angalau nilikuwa kwenye eneo salama lenye unafuu wa kutoroka kwangu ingawa kwa namna moja au nyingine nilikuwa nikiamini kuwa mpaka kufikia wakati ule lile jengo la ile hoteli New Parador Residence lingekuwa chini ya uangalizi mkali wa watu waliokuwa wakifanya mawasiliano na wale watu niliopambana nao kule juu kwenye ile ofisi ya meneja wa ile hoteli ghorofani.

     Nilipoitazama saa yangu ya mkononi nikagundua kuwa muda ulikuwa umeenda sana hata hivyo nilihisi mafanikio kidogo katika kazi yangu. Hatimaye nikaikamata vyema bastola yangu mkononi na kuanza kulitoroka taratibu eneo lile lakini mara moja nikiwa katika harakati zile mara nikajikuta nikimezwa na mshtuko wa aina yake. Moyo wangu ukapiga kite kwa nguvu na kupoteza utulivu huku nywele kichwani zikinicheza.

     Hatua chache kutoka pale lilipokuwa lile jenereta la umeme wa dharura wa lile jengo la hoteli kulikuwa na mtu aliyesimama na sikuweza kuelewa ni kwa namna gani mtu yule hakuweza kushtukia uwepo wangu eneo lile. Ingawa kulikuwa na giza zito lakini miali hafifu ya mwanga wa taa uliopenya kutoka nje ya lile jengo uliniwezesha kumuona kwa shida kidogo yule mtu. Alikuwa mrefu zaidi yangu mwenye umbo lenye afya njema na alikuwa amevaa suti nadhifu ambayo sikuitambua haraka rangi yake kutokana na giza la ile sehemu na nilipomchunguza vizuri yule mtu nikagundua kuwa mkononi alikuwa ameshika bastola.

     Yule mtu alikuwa akitazama upande mwingine wa lile eneo huku akiyatembeza macho yake huku na kule kama atafutaye kitu na hapo nikawaza kuwa huwenda yule mtu alikuwa mbali na lile eneo muda mfupi uliopita kabla ya kufika pale. Niliwahi haraka kurudi nyuma na kujibanza kwenye kona moja ya ukuta wa eneo lile huku kwa makini macho yangu yakimtazama yule mtu.

     Kitambo kifupi cha ukimya kikaumeza mshtuko wangu huku nikiendelea kumtazama yule mtu kwa makini na bastola yangu mkononi. Baada ya kitambo kifupi mara nikamuona yule mtu akianza kuzitupa hatua zake kwa tahadhari kuja pale nilipojibanza huku akionekana kama aliyehisi jambo fulani. Macho yangu yakiwa makini kumtazama yule mtu nikaanza kujiandaa kumkabili. Hata hivyo kabla hajanifikia mara nikaona taa ndogo ya kijani ikiwaka kwenye sehemu ya ukosi wa koti lake la suti shingoni. Tukio lile likampelekea yule mtu asite kuendelea mbele na safari yake badala yake haraka akaupeleka mkono wake shingoni kurekebisha kifaa chake cha mawasiliano. Uzoefu wangu ukanitanabaisha kuwa kulikuwa na mtu mwingine mbali na eneo lile aliyekuwa akitaka kuwasiliana na yule mtu bahati mbaya sana maneno machache ya lugha waliotumia kuwasiliana watu wale sikuielewa ingawa nilikuwa na kila hakika kuwa ilikuwa ni lugha ya kirundi.

     Muda mfupi baada ya mawasiliano kwenye kile kifaa cha mawasiliano cha yule mtu kukatika hewani mara nikamuona yule mtu akisitisha kuja pale nilipokuwa nimejibanza na badala yake haraka akabadili uelekeo akikatisha kwenye ile korido niliyotoka na kutokomea gizani. Kwa sekunde kadhaa nikaendelea kujibanza eneo lile huku nikiupisha utulivu nafsini mwangu. Ile sauti ya hatua hafifu za yule mtu taratibu ikaendelea kutokomea mbali na eneo lile na hatimaye kukoma kabisa. Sasa nilikuwa na kila hakika kuwa yule mtu alikuwa shirika moja pamoja na wale watu hatari waliokuwa wakiisaka roho yangu kwa udi na uvumba.

     Kitambo kifupi cha ukimya kikapita wakati nikiendelea kufanya tathmini ya hali ya usalama wa eneo lile. Nilipojiridhisha kuwa hapakuwa na mtu mwingine eneo lile taratibu nikayaacha maficho yale kwa tahadhari na kuelekea kwenye ule mlango mkubwa wa nondo na wavu. Nilipofika na kuuchunguza vizuri ule mlango nikagundua kuwa lile geti lilikuwa limefungwa kwa mnyororo mkubwa na kufuli moja imara hata hivyo sikupata upinzani wowote kwani mfukoni nilikuwa na funguo zangu maalum kwa ajili ya kushughulika na maeneo korofi kama yale. Hivyo kwa tahadhari nikaifungua ile kufuli na kisha kuufungua na ule mnyororo. Nilipotoka nje nikaurudishia vizuri ule mlango na kulifunga lile geti kama nilivyolikuta.

     Sasa nilikuwa nimetokezea sehemu ya nyuma ya lile jengo la New Parador Residence na mbele yangu niliweza kuona mabwawa matatu makubwa ya kupigia mbizi katika uwanja mkubwa wenye nyasi nzuri za kijani kibichi. Mabwawa yale yalikuwa yamezungukwa na viti maalum vya kupumzika chini ya miavuli mikubwa yenye rangi za kupendeza. Umbali mfupi baada ya ile sehemu yenye yale mabwawa ya kupigia mbizi kulikuwa na viwanja vitatu vikubwa vya michezo. Kiwanja kimoja cha mpira wa kikapu, kingine cha mpira wa mikono na kiwanja cha mwisho kilikuwa cha mazoezi ya viungo ya kawaida.

     Eneo kubwa lililosalia lilikuwa ni la kiwanja cha mpira wa golf hata hivyo kiwanja kile kilizungukwa na sehemu nzuri zenye viti visivyohamishika vya kupumzika vilivyokuwa chini ya miti mirefu ya vivuli. Mandhari ile ilikuwa ni ya kupendeza sana hata hivyo nilipoendelea kulichunguza lile eneo sikuweza kumuona mtu yeyote ingawa hali ile haikuwa kigezo tosha cha kunihakikishia kuwa eneo lile halikuwa chini ya ulinzi.

     Nikiwa bado nayatathmini vizuri mazingira yale kando ya ule mlango mkubwa wa wavu na nondo mara ghafla nikauona mwanga mkali wa kurunzi ikimulika mulika mle ndani kwenye lile eneo la chini la lile jengo nilipotoka muda mfupi iliopita. Haraka nikawahi kusogea kando na kujibanza huku nikichungulia na kutazama mle ndani. Kwa kufanya vile nikawaona wanaume wawili wakiwa na bastola zao mikononi huku mmoja akiwa ameshika kurunzi mkononi mwake.

     Kulikuwa na mabishano hafifu baina yao ingawaje sikuweza kuambulia kitu kupitia ile lugha waliyokuwa wakiizungumza ambayo niliihisi kuwa ilikuwa ni lugha ya kirundi. Hata hivyo kupitia vitendo niliweza kuhisi kiini cha mabishano yale baina ya wale watu wawili.

     Yule mtu aliyeshika ile kurunzi mkono wake mwingine ulikuwa umezishika zile sare za mhudumu wa ile hoteli ambazo muda mfupi uliopita nilikuwa nimetoka kuzivua na kuzitelekeza mle ndani gizani. Yule mtu alikuwa akimuonesha mwenzake zile nguo huku akimfokea kwa jazba dhahiri akionekana kushikwa na hasira. Kupitia tukio lile nikafahamu kuwa mpango wangu wa kutoroka kwenye lile jengo haukuwa siri tena kwani wale watu hatari tayari walikuwa wameing?amua vyema hila yangu...



    Tayari wasiwasi ukiwa umeanza kuniingia mara nikawaona wale watu wakisogea kwenye ule mlango mkubwa nondo na wavu na kuanza kumulikamulika kwenye ule mnyororo na lile kufuli huku wakionekana kushikwa na mshangao baada ya kuona ile sehemu ikiwa imefungwa vizuri. Muda mfupi uliofuata mara nikamsikia yule mtu aliyeshika ile kurunzi mkononi akimwambia jambo fulani yule mwenzake kisha akazima ule mwanga wa kurunzi mkononi mwake na hapo wale watu wakaanza kuondoka haraka eneo lile.

     Nilikuwa na kila sababu ya kuamini kuwa watu wale walikuwa bado hawajakata tamaa juu yangu na sasa walikuwa katika harakati za kubuni mkakati mwingine makini zaidi wa kunikamata kabla sijafika mbali hivyo sikutaka kuendelea kupoteza muda wangu zaidi eneo lile. Haraka nikayaacha yale maficho yangu kando ya ule mlango mkubwa na kuanza kuambaa mbaa kwa tahadhari nyuma ya lile jengo huku mara kwa mara nikiyatembeza macho yangu huku na kule kutazama kama kungekuwa na mtu yeyote eneo lile. Mvua kubwa ilikuwa ikiendelea kunyesha na huwenda hali ile ndiyo iliyokuwa imepelekea mazingira yale kukimbiwa na watu. Hata hivyo kidole cha mkono wangu wa kushoto kilikuwa kimetulia vyema juu ya kilimi cha bastola yangu ndani ya mfuko wa koti langu tayari kukabiliana na rabsha yoyote ambayo ingejitokeza mbeleni.

     Wakati nikitembea ikafika sehemu mwanga wa taa za nyuma za lile jengo ukawa ukinimulika hali iliyonipelekea nichepuke haraka kando ya lile jengo na kupita chini ya miti na baada ya muda mfupi nikawa nimetokezea nyuma ya kile kibanda chenye mashine za ATM kilichokuwa kando ya lile jengo la ile hoteli hata hivyo sikumuona mtu yeyote eneo lile. Ile sehemu yenye viti na miamvuli ya kujipumzishia nyakati za jua nayo haikuwa na mtu hata mmoja bila shaka kutokana na ile mvua kubwa iliyokuwa ikiendelea kunyesha.

     Kwa kukwepa kutiliwa mashaka na mtu yoyote nikaamua kukatisha nyuma ya kibanda cha mlinzi wa ile hoteli nikielekea kwenye lile eneo la maegesho ya magari mbele ya ile hoteli huku nikiwa makini kuchunguza kama kungekuwa na mtu yeyote eneo lile. Muda mfupi uliofuata nikawa nimelifikia lile eneo la maegesho ya magari la ile hoteli na mara moja nilipochunguza nikagundua kuwa kulikuwa na magari mawili yaliyoondoka na gari moja liliongezeka baada ya mimi kuingia kwenye ile hoteli. Nilipochunguza lile gari lililoongezeka nikagundua kuwa lilikuwa ni gari aina ya Landcruiser Vx jeupe.

     Sikutaka kuendelea kupoteza muda zaidi eneo lile kwani tayari nilikuwa nimeanza kuhisi mambo hayakuwa shwari tena hivyo mara tu nilipolifikia gari langu nikalikagua haraka kisha nikafungua mlango na kuingia ndani. Bila kusubiri muda uleule nikawasha gari na kuyaacha yale maegesho huku bado nikiendelea kuyatembeza macho yangu huku na kule kuchunguza kama kungekuwa na mtu yeyote aliyekuwa akizifuatilia nyendo zangu. Sikumuona mtu yoyote na baada ya muda mfupi nikawa nimetoka kabisa nje ya geti la mbele la ile hoteli.

     Wakati nikiwa katika harakati za kutokomea mbali na ile hoteli mara kwa mbali nikawaona watu wawili wakitoka kwa kasi kwenye mlango wa mbele wa ile hoteli na kuelekea kwenye lile eneo la maegesho ya magari la ile hoteli. Kitendo cha kuwakumbuka wale watu wawili wenye kurunzi walioondoka ile sehemu ya chini ya ile hoteli nikahisi nini ambacho kingefuatia baada ya pale. Hivyo nikaongeza mwendo na kuzidi kutokomea mbali zaidi na eneo lile.

     _____

     Bado nilikuwa katika barabara ya Boulevard du 28 Novembre na mwendo wangu wa gari haukuwa wa kubabaisha. Mvua kubwa ya masika ilikuwa ikiendelea kunyesha na giza zito lilikuwa limetanda angani hali iliyopelekea magari machache kwa wakati ule kuonekana barabarani. Wakati nikiendelea na safari yangu moyoni nikawa nikiomba kuwa nisikutane na kizuizi kingine chochote cha barabarani ambacho kingenitia hatarini.

     Niliendelea na safari yangu huku mara kwa mara nikitazama nyuma yangu kupitia vioo vya ubavuni vya gari ili kuona kama kuna gari lolote lililonifungia mkia au lah!. Mambo bado yalikuwa shwari kwani sikuliona gari lolote nyuma yangu hata hivyo sikupunguza mwendo. Muda mfupi baadaye nikayapita makutano ya barabara ya Boulevard du 28 Novembre na barabara ya Chaussée P.L. Rwagasore nikiiacha hoteli ya City Hill upande wa kulia. Hatimaye nikaipita barabara ya Avenue De L?UNESCO upande wa kushoto mbele kidogo baada ya kulipita jengo la kiwanda cha sabuni.

     Nilipoyafikia makutano ya barabara ya Boulevard du 28 Novembre na ile barabara ya Avenue de la Dynastie upande wangu wa kulia nikaliona gari jeupe aina ya Landcruiser kama lile nililoliona kwenye lile eneo la maegesho ya magari la New Parador Residence likiingia kwenye barabara ile na kuanza kunifuata kwa nyuma. Wasiwasi ukaniingia huku nikitafuta hakika kama gari lile lilikuwa likinifungia mkia au lilikuwa kwenye hamsini zake. Nikaendelea kulichunguza lile gari kupitia vioo vya ubavuni vya gari langu huku nikiendelea na safari kwa umbali mrefu katika barabara ile hata hivyo lile gari nyuma yangu halikuniacha.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Wasiwasi ukiwa umeanza kuniingia akili yangu ikaanza kufikiria namna ya kukabiliana na hatari ya namna yoyote ambayo ingenikabili endapo watu waliokuwa ndani ya lile gari wangekuwa na dhamira mbaya na mimi. Lakini wakati nikiwa katika harakati za kupanga mikakati ya kujihami mara nikashangaa kuliona lile gari nyuma yangu likipunguza mwendo na kuingia upande kushoto kuifuata barabara ya Aveneu du I?universite iliyokuwa ikieleke chuo kikuu cha Burundi. Mara moja nilipolichunguza vizuri lile gari ubavuni nikaiona nembo kubwa ya Université du Burundi inayolitambulisha gari lile kuwa ni mali ya chuo kikuu cha Burundi. Kuona vile nikaachia msonyo mrefu mdomoni huku taratibu utulivu ukianza kutafuta hifadhi moyoni mwangu na hapo nikaingiza tena gia na kukanyaga mafuta nikiendelea kuchanja mbuga.

     Wakati nikiendelea na safari mawazo mengi yakawa yakipita kichwani mwangu yaliyokusanya mlolongo mrefu wa matukio yote yaliyotokea tangu siku ile nilipoondoka jijini Dar es Salaam kuja pale Jijini Bujumbura nchini Burundi. Hatimaye mawazo yangu yakaweka kituo na kukumbuka mambo yote yaliyotokea kwenye lile chumba 302 cha ghorofa ya tano ya lile jengo la ile hoteli New Parador Residence nililotoka muda mfupi uliopita. Nikawakumbuka vizuri wale watu niliopambananao na kufanikiwa kuwaangamiza huku wote wakijifanya kuwa ni wafanyakazi wa ile hoteli. Kwa kweli sikuweza kufahamu walikuwa wakifanya vile kwa maslahi ya nani, waliwezaje kunifahamu na kujua kuwa ningefika pale kwenye ile hoteli.

     Hata hivyo nilipoyakumbuka vizuri maelezo ya yule mtu mfupi aliyejinadi kwangu kuwa ndiye meneja wa ile hoteli angalau nikapata faraja kidogo. Bila shaka ule ulikuwa ni mpango ulioandaliwa kikamilifu na watu waliomteka balozi Adam Mwambapa na huwenda walikuwa wakifahamu vizuri kuwa nilikuwa pale jijini Bujumbura kwa kazi moja tu ya kumtafuta balozi Adam Mwambapa. Nikaendelea kukumbuka vizuri maelezo ya yule mtu mfupi aliyejinadi kwangu kwa jina la Vital Desire Habonimana huku akionekana kunifahamu vizuri kiasi cha kulitaja jina langu halisi pasipo kigugumizi cha namna yoyote. Maswali mengi yakaanza kuibuka kichwani mwangu.

     Mtu yule alilifahamu vipi jina langu wakati mimi na yeye hatukuwahi kufahamiana hapo kabla?. Uongozi wa ile hoteli uliwezaje kuwaruhusu watu wa namna ile kutekeleza mpango wao mchafu wa kutaka kuniangamiza?. Jambo gani lilikuwa likiendelea kiasi cha kupelekea Balozi Adam Mwambapa kutekwa?. Nikaendelea kujiuliza maswali mengi pasipo kupata majibu ingawa kwa namna moja au nyingine niliamini kuwa tukio la kutekwa kwa Balozi Adam Mwambapa lilikuwa limeratibiwa na kutekelezwa kwa utaalam wa hali ya juu maana Balozi Adam Mwambapa hakuwa mtu wa kuingilika kirahisi pamoja na umri kumtupa mkono. Mwishowe mawazo yangu yakahamia kwa Padri Aloysius Kanyameza ambaye yule kijana aitwaye Sundi alikuwa amenigusia na kunitaka nikamtafute.

     Nikaendelea kuwaza huku nikijiuliza ni kwa namna gani mtumishi huyo wa kiroho alikuwa ameingia kwenye mkasa huu hatari. Sundi alikuwa akifahamu nini kuhusu Padri Aloysius Kanyameza na kwanini aliangua kicheko hafifu katikati ya maumivu makali ya jeraha lake kubwa la kisu tumboni wakati nilipokuwa nikimuuliza maswali machache juu ya tukio la kutekwa kwa Balozi Adam Mwambapa?. Majibu sikuyapata na kwa kweli hali ile ilikuwa imenipelekea nijihisi ni kama niliyekuwa nimetupwa kwenye shimo refu la msongo wa mawazo pasipo dalili ya mtu yeyote kunitupia kamba ya kuniokoa kutoka katika kadhia ile.

     Mawazo yangu yaliporudi mle ndani ya gari nikashtukia kuwa tayari nilikuwa nimeyafikia makutano ya barabara ya Boulevard du 28 Novembre na barabara ya Avenue de I?imprimerie upande wa kushoto kando ya kiwanda kidogo cha kusindika samaki wa kutoka Ziwa Tanganyika. Kitendo cha kuyaona makutano yale ya barabara kikanipelekea nipunguze mwendo na kuingia upande wa kushoto nikiifuata barabara ndefu ya Avenue de I?imprimerie eneo la Ntahangwa iliyokuwa ikikatisha katikati ya makazi ya watu.

     Muda mfupi baada ya kuingia kwenye barabara ile mbele yangu nikakutana na kizuizi cha barabarani cha askari jeshi wakiwa katika makoti yao marefu ya mvua na bunduki zao mkononi. Askari mmoja akaingia barabarani na kunipiga mkono wa kunitaka nisimame. Kwa kweli nianza tena kuingiwa na wasiwasi huku taratibu nikipunguza mwendo wa gari kukikaribia kile kizuizi. Wakati nilipokuwa nikiendelea kupunguza mwendo mara nikawaona askari wengine wawili wakijitokeza kando ya barabara ile na kuingia barabarani huku wakiwa na bunduki zao mikononi katika namna ya kuonesha msisitizo kuwa nilipaswa kusimama.

     Sikuwa na namna ya kufanya hivyo taratibu nikaanza kupunguza mwendo huku nikivificha vifaa vyangu muhimu vya kazi na nilipoyapeleka macho yangu kutazama kwenye vioo vya ubavuni vya gari langu ghafla nikajikuta nikishikwa na mshtuko. Lile gari Landcruiser jeupe nililokuwa nimeliacha kwenye vile viunga vya maegesho ya magari vya New Parador Residence sasa lilikuwa umbali wa mita chache nyuma yangu. Niliweza kulikumbuka vizuri lile gari kupitia sahani ya namba zake na gurudumu moja la akiba lililokuwa limefungwa juu ya boneti ya lile gari. Kwa kweli nilitamani nishuke kwenye gari na kuanza kutimua mbio nikipotelea kwenye vichaka vya jirani na eneo lile hata hivyo nafsi yangu ilinionya kuwa huwenda lile lisingekuwa jambo rahisi kama nilivyodhani kwani kile kilikuwa kizuizi kikubwa zaidi cha barabarani na chenye askari jeshi wengi zaidi kuliko vizuizi vyote nilivyowahi kukabiliana navyo pale jijini Bujumbura hadi kufikia wakati ule.

     Wakati nikisimama eneo lile mara nikaona kuwa kulikuwa na magari mengine mawili yaliyokuwa yamesimamishwa kando ya ile barabara eneo lile yakifanyiwa upekuzi na askari jeshi wengine walioshika bunduki zao mkononi. Nikiwa nimesimama katikati ya ile barabara mara nikamuona yule askari aliyewahi kunisimamisha pale barabarani akizitupa hatua zake taratibu kusogea pale nilipokuwa nimesimamisha gari langu huku akiwa ameikamata vyema bunduki yake mkononi. Kuona vile ikabidi nishushe kioo cha mlangoni taratibu huku nikimtazama yule askari katika uso wa mashaka. Hata hivyo sikuweza kumuona vizuri usoni kutokana na kofia ya koti lake la mvua iliyokuwa imeukinga vyema uso wake.

    “Bonsoir mon commandant?’’. Habari za usiku afande?. Nikawahi kumsalimia yule mwanajeshi hata hivyo hakuitikia na wala sikuona tashwishwi yoyote usoni mwake badala yake akanikata jicho kali la hadhari. Aliponifikia akajipangusa maji ya mvua usoni kwa kiganja chake na kisha kuniambia kwa sauti ya ukali.

    “Mettez votre vehicule.`a côté de la route”. Egesha gari lako pale kando ya barabara. Sikutaka kuleta ubishi wowote hivyo taratibu nikaendesha gari langu na kwenda kuegesha mbele kidogo kando ya ile barabara hata hivyo sikushuka kwenye gari.

     Kitambo kifupi kilipopita mara nikamuona yule mwanajeshi akisogea taratibu pale nilipoegesha gari langu kando ya ile barabara. Alipofika akainama kidogo dirishani akichunguza chunguza mle ndani ya gari kabla ya kuniuliza kwa utulivu.

    “D?où venez vous cette nuit?’’. Unatoka wapi usiku huu?.

    “Commandant, je viens de I?université de Burundi”. Natoka chuo kikuu cha Burundi afande. Nikadanganya huku nikiongea kwa kujiamini kana kwamba sikuwa na wasiwasi wowote nafsini mwangu. Kitambo kifupi cha ukimya kikapita huku yule askari akanitazama kwa makini kabla ya kuniambia.

    “Montre moi votre carte”. Nioneshe kitambulisho chako. Yule askari akaniambia huku akiendelea kunitazama kwa makini. Akili yangu ikasumbuka kidogo kisha nikakumbuka kuwa katika droo iliyokuwa kwenye dashibodi ya lile gari Hidaya alikuwa ameniwekea kitambulisho feki kinachonitambulisha kama afisa wa ubalozi wa Tanzania pale nchini Burundi. Hivyo haraka nikaifungua ile droo na kuchukua kile kitambulisho na kumkabidhi yule askari. Yule askari akakipokea kile kitambulisho na kukipitishia macho haraka kisha akanirudishia huku akinitazama kwa makini kabla ya kuniuliza.

    “Où allez vous?”. Unaelekea wapi?.

    “Je vais à I?avenue de I?OUA chez moi”. Naelekea mtaa wa OAU nyumbani kwangu. Nikamjibu yule afande huku nikijitia kutazama saa yangu ya mkononi katika namna ya kuashiria kuwa alikuwa akinichelewesha.

    “Ouvrez le capot du vehicule, je veus controler”. Fungua buti ya gari nahitaji kukagua. Yule askari hatimaye akaniambia huku akijitia kutabasamu hata hivyo sikupingana na ombi lake badala yake nikavuta kabari ya buti ya lile gari chini ya usukani na hapo ile buti ya gari ikafunguka. Yule askari kuona vile taratibu akielekea nyuma ya gari langu kuchunguza kwenye buti. Nikiwa ndani ya gari nikaendelea kuomba kimoyomoyo kuwa Mungu aniepushe mbali na hatari yoyote ambayo ingejitokeza eneo lile.

     Nikaupisha utulivu kichwani mwangu huku nikitazama nyuma ya gari kupitia vile vioo vya ubavuni na kwa kufanya vile mara nikashikwa na mshtuko. Niliwaona wanajeshi nane haraka wakisogelea karibu na kulizingira lile gari jeupe Landcruiser lililokuwa limenifungia mkia nyuma yangu huku wanajeshi wale wakiwa na bunduki zao mkononi. Haraka nikahisi kuwa kulikuwa na jambo la hatari lililokuwa likielekea kutokea eneo lile.

     Kwa sauti ya ukali na mara nikamsikia mmoja wa wale wanajeshi mwenye cheo cha Meja akiwaamrisha watu wote waliokuwa ndani ya lile gari jeupe Landcruiser washuke chini. Hata hivyo pamoja na amri ile ya ukali bado sikuona dalili za mtu yeyote kutaka kushuka kwenye...

    ...Lile gari badala yake ukimya usio na majibu ukaendelea kutawala eneo lile. Wakati yale yakiendelea yule askari nyuma ya gari langu akawa amemaliza kufanya upekuzi kwenye buti ya gari akimulika kwa kurunzi yake mkononi. Hivyo akafunga haraka ile buti ya gari kule nyuma na kupitia kioo cha ubavuni nikamuona akija tena kule mbele kwa haraka na alipofika pale dirishani akainama kidogo na kuniambia.

    “D?accord, vous pouvez continuer avec votre voyage”. Okay, unaweza kuendelea na safari. Yule afande akaniambia hata hivyo nilisita kidogo kwa vile nilikuwa sijamsikia vizuri na macho yetu yalipokutana akanifanyia ishara kwa kichwa akinitaka niondoke eneo lile.

    “Merci, bon travail”. Ahsante, kazi njema. Haraka nikamwambia yule afande huku nikiingiza gia na kuanza kuondoka sehemu ile.

    “Et vous aussi”. Na wewe pia. Yule afande akaitikia huku akianza kurudi kule nyuma kando ya barabara lilipoegeshwa lile gari jeupe Landcruiser. Haraka nikalitoa gari kwenye kile kizuizi na kuingia barabarani na wakati nikifanya vile nikaanza kusikia majibizano ya risasi nyuma yangu yakifanyika kati ya wale wanajeshi wa kile kizuizi na watu waliokuwa ndani ya lile gari Landcruiser.

     Lile gari lilikuwa limeanza kuondoka kwa kasi kunifuata nyuma yangu pasipo kufanyiwa ukaguzi hivyo wale wanajeshi walikuwa wakilizuia lisiondoke. Hata hivyo dereva wa lile gari alikuwa amedharau ile amri ya wale askari na hivyo kuamua kuondoka pasipo ruhusa. Lile gari halikufika mbali kwani risasi za wale askari zikawa zimefanikiwa kupasua magurudumu yake na hivyo kulifanya lile gari liende kwa mwendo wa kuyumba yumba barabara nzima kabla ya kusimama. Nikapunguza mwendo kidogo baada ya kukipita kile kizuizi nikitaka kushuhudia nini ambacho kingefuatia baada ya pale. Lile gari jeupe Landcruiser liliposimama milango yake ikafunguliwa kwa ghafla kisha wakashuka wanaume wanne na kuanza kutimua mbio wakielekea kwenye pori lililokuwa jirani na eneo lile. Muda uleule mara nikamuona mmoja wao akisombwa vibaya na kutupwa hewani kwa shambulio la risasi za mmoja wa wale wanajeshi kabla hajalifikia lile pori huku majibizano ya risasi yakiendelea. Sikutaka tena kuendelea kupoteza muda wangu eneo lile hivyo nikaongeza mwendo na kuzidi kutokomea.

     _____

     Baada ya muda mrefu wa safari yangu hatimaye nikawa nimeifikia barabara ya Chausseé du Peuple Murundi. Ilikuwa ni barabara pana ya kisasa kama zilivyokuwa barabara nyingi za mijini hata hivyo ile barabara ilikuwa imejitenga sana na makazi ya watu ikikatisha katikati ya vichaka vizito vya miti, mawe na nyasi ndefu. Hivyo haraka nilifahamu kuwa usalama katika barabara ile ulikuwa hafifu sana kwani baada ya mwendo mfupi tu wa safari yangu nikaanza kuziona maiti za watu zikiwa zimezagaa ovyo barabarani na kutelekezwa. Nilipoendelea kuchunguza vizuri kwenye barabara ile nikayaona magurudumu chakavu ya magari yakiendelea kuteketea kwa moto pamoja na vizuizi vya mawe makubwa katika baadhi ya maeneo ya barabara ile. Kuona vile ikabidi nipunguze mwendo na kuanza kuchagua sehemu za kupita. Sikumuona mtu yoyote katika ile barabara na hali ile ilinitia wasiwasi kidogo.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Athari za jaribio la mapinduzi ya kijeshi nchini Burundi zilikuwa zimeanza kujitokeza. Barabara za mitaa mingi ya jiji la Bujumbura zilikuwa zimeachwa upweke baada ya kukimbiwa na watu waliokuwa wakitafuta usalama wa roho zao. Kila eneo sasa lilikuwa likinuka harufu ya moshi wa risasi na magruneti ya kutupa kwa mkono. Maiti za watu nazo zilikuwa zimezagaa ovyo kila mahali. Hali ya amani katika nchi ya Burundi ilikuwa ikizidi kuwa tete kwa vile haikufahamika hadharani kuwa uongozi wa serikali ya nchi ya Burundi ulikuwa chini ya nani kwa wakati ule. Nilipolikumbuka lile gari jeupe Landcruiser lililokuwa limenifungia mkia kule nyuma nikaanza kuhisi kuwa wale watu waliokuwa ndani ya lile gari na wale wengine niliyopambana nao kwenye kile chumba cha ofisi ya meneja wa ile hoteli ya New Parador Residence walikuwa shirika moja katika kumteka balozi Adam Mwambapa. Nilihisi kuwa kulikuwa na jambo kubwa la hatari lililofichika katika mkasa mzima wa kutekwa kwa balozi Adam Mwambapa hata hivyo hadi kufikia wakati ule bado nilikuwa sijapata vizuri penyenye yoyote ya kile nilichokuwa nikipeleleza.

     Mawazo yangu yaliporudi mle ndani nikashtuka kuwa tayari nilikwishaufikia mzunguko mkubwa wa barabara uliozikutanisha barabara kubwa tano. Katikati ya makutano yale kulikuwa na bustani nzuri ya miti ya maua iliyokatiwa vizuri ikizungukwa kwa nguzo ndefu zenye taa nzuri za barabarani. Nilipoufikia ule mzunguko wa barabara nikapunguza mwendo na kuingia upande wa kushoto na wakati nikifanya vile nikapishana na magari machache eneo lile. Muda mfupi uliofuata nikaiacha barabara ya Avenue de l?OAU upande wa kushoto na kuingia barabara ya Boulevard Mwambutsa upande wa kaskazini nikikipita kituo cha kujazia mafuta cha EBS Petroleum upande wa kulia. Barabara ya Boulevard Mwambutsa ilikuwa barabara pana ya kisasa iliyopakana na mifereji ya maji taka iliyojengewa vizuri kando yake huku ikipakana na miti mirefu ya kivuli na hivyo kuifanya igubikwe na utulivu wa aina yake.

     Nilipoitazama ramani yangu ndogo ya kijasusi nikagundua kuwa kutoka pale nilipokuwa sikuwa mbali sana na Le Tulip Hôtel Africaine ambayo kwa mujibu wa uchunguzi wangu kupitia zile nyaraka muhimu zenye orodha ya mienendo ya mawasiliano ambayo Hidaya alikuwa ameipata kwa opareta ni kuwa simu ya mezani ya ofisini kwa Balozi Adam Mwambapa ilikuwa imetumika kufanya mawasiliano mengi kuelekea kwenye hoteli ile muda mfupi kabla ya mapinduzi yale ya kijeshi.

     Baada ya mwendo wa robo saa katika barabara pana ya lami iliyokuwa ikikatisha katikati ya mashamba na iliyopakana na miti mirefu na vichaka vya hapa na pale hatimaye nikaja kuiona Le Tulip Hôtel Africaine upande wa kushoto kiasi cha umbali usiopungua mita mia mbili kando ya barabara ile.

     Ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuiona hoteli ile hata hivyo sifa zake zilikuwa zimeyafikia masikio yangu kwa muda wa miaka kadhaa iliyopita kutoka kwa marafiki na wakuu wangu wa kazi ambao walikuwa wamebahatika kuitembelea hoteli ile huko siku za nyuma mara kwa mara wakati walipokuwa wakifika pale nchini Burundi kwa safari za kikazi. Mojawapo ya taarifa nilizokuwanazo ni kuwa Le Tulip Hôtel Africaine ilikuwa ni hoteli yenye hadhi ya nyota tano na ilikuwa ikimilikiwa na mwekezaji mmoja wa jijini Bujumbura ambaye alikuwa ni raia wa Ufaransa.

     Bango kubwa lenye tangazo la hoteli ile barabarani likanipelekea nipunguze mwendo na kuingia upande wa kushoto nikiifuata barabara nyembamba kiasi iliyofunikwa kwa changarawe na kupakana na miti mirefu ya kivuli iliyozungukwa na bustani ya maua ya kupendeza yenye hewa safi ya upepo wa asili. Le Tulip Hôtel Africaine sasa ilikuwa mbele yangu na ilikuwa ni hoteli kubwa yenye mandhari tulivu ya kupendeza.

     Katika bustani nzuri iliyoizunguka hoteli ile kulikuwa na mabwawa makubwa ya kuogelea, sehemu zenye viti maalum vya kupumzikia chini ya miti mizuri ya kivuli aina ya Hopea odorata pamoja na vibanda vidogo vya faragha. Ile barabara niliyoingia ilikuwa ikimulikwa kwa mwanga hafifu wa taa zilizokuwa kando ya ile barabara juu ya vinguzo vifupi vya chuma. Katika lile jengo la ghorofa la ile hoteli wakati ule wa usiku niliviona baadhi ya vyumba vikiwa vinawaka taa ghorofani. Wakati nikiwasili nje ya ile hoteli nikaiona milingoti mitano yenye bendera zinazopepea taratibu. Zilikuwa ni bendera za nchi za Afrika mashariki na bendera ya taifa la Ufaransa na Marekani na sehemu ya mbele chini ya hoteli ile kulikuwa na magari mengi yaliyoegeshwa.

     Hatimaye nikawa nimefika mbele ya ile hoteli ambapo baada ya hangaika ya hapa na pale nikawa nimepata sehemu nzuri ya maegesho ya gari langu. Kabla ya kushuka kwenye gari nikatulia kidogo nikifanya tathmini nzuri ya mandhari ya hoteli ile na baada ya muda macho yangu yakaridhika kuwa ilikuwa ni hoteli nzuri mno ingawaje majengo yake yalikuwa ni ya mtindo wa kizamani kidogo. Nilipoendelea kuchunguza nikagundua kuwa nyuma ya ile hoteli kiasi cha umbali usiopungua mita mia tano kulikuwa na msitu mkubwa wa miti ya kupandwa kama ule wa Sao Hill uliopo mkoani Iringa ingawa ukubwa wa msitu ule sikuweza kuufahamu.

     Mvua bado ilikuwa ikiendelea kunyesha na giza nalo lilikuwa zito ingawa mara kwa mara giza lile lilitoweshwa na mwanga mkali wa radi kutoka angani. Sikuweza kumuona mtu yeyote nje ya hoteli ile mbali na walinzi wawili waliokuwa ndani ya kibanda kidogo kando ya eneo lile. Hivyo nikalichukua koti langu la mvua na kulivaa huku bastola yangu nikiitia ndani ya mfuko wa lile koti. Baada ya kujitazama kidogo kupitia kioo cha mbele chini ya paa ya lile gari na kuridhika na mwonekano wangu nikafungua mlango wa gari na kutoka nikikatisha katikati ya lile eneo la maegesho ya magari kuelekea mbele ya ile hoteli. Wakati nikitembea nikihakikisha kuwa hapakuwa na mtu yeyote aliyekuwa akinifuatilia nyendo zangu eneo lile.

     Nilipofika mbele ya ile hoteli nikapanda ngazi kumi na mbili za varanda yenye sakafu nzuri ya tarazo iliyoandikwa kwa ufundi mkubwa jina la hoteli ile kisha nikausukuma mlango mkubwa wa kioo na kutokomea ndani. Kama zilivyokuwa hoteli nyingi za kimataifa duniani Le Tulip Hôtel Africaine haikuwa tofauti. Sehemu yake ya mapokezi ilikuwa na umbo la nusu duara iliyozungukwa na meza nzuri ya kaunta ya mbao ya mti wa Jacaranda iliyokuwa ikitazamana na makochi meupe ya ngozi laini ya sofa.

     Niliwakuta wazungu watatu eneo lile, wawili wanaume na mmoja mwanamke wakiwa wameketi kwenye yale makochi ya sofa huku upande wa pili kukiwa na wanaume wengine wawili waafrika kama mimi na kila mtu alionekana kuzama kwenye hamsini zake. Pale sehemu mapokezi nikawakuta wahudumu wawili, kaka na dada wakiwa katika sare zao nadhifu za kazi za mashati meupe yenye kola za rangi ya kijivu na suruali za rangi ya kijivu huku shingoni wakiwa wamevaa tai ndogo nyeusi zilizowapendeza. Yule mhudumu wa kiume alikuwa amejitenga kando akizungumza na mwanaume mmoja niliyemhisi kuwa alikuwa ni raia wa Nigeria kutokana na lafudhi ya kiingereza chake na aina ya mavazi aliyovaa. Yule mhudumu wa kike alikuwa akihitimisha kuongea na simu ya mezani wakati nilipokuwa nikiifikia ile kaunta ya mapokezi hivyo haraka akairudishia ile simu mahala pake kisha uso wake ukiwa umefanikiwa kutengeneza tabasamu zuri la kirafiki akageuka na kunitazama.

    “Soeur, comment va le travail?”. Dada, habari za kazi?. Nikawahi kumsalimia huku usoni nikitengeneza tabasamu la kikazi na hapo nikamsikia yule dada akinikaribisha kwa sauti nyororo ya kike.

    “Bien frère bienvenu, je peux t?aider?”. Nzuri tu kaka karibu nikusaidie.

    “Merci beaucoup soeur, je suis venu voir mon visiteur”. Ahsante sana dada, nimekuja kumuona mgeni wangu. Nikamwambia yule dada huku nikimtazama usoni kwa bashasha zote za kimapenzi hali iliyompelekea akwepeshe macho yake pembeni huku akiangua tabasamu lenye kimelea cha aibu na kisha kujiziba mdomo kwa kiganja cha mkono wake. Alikuwa msichana mrembo sana kiasi kwamba lile tabasamu likavipelekea vishimo vidogo mashavuni mwake kuchomoza vizuri na kuuteka vibaya mtima wangu.

    “Il est dans la chambre numero combien?”. Yupo chumba namba ngapi?. Yule dada mhudumu akaniuliza kwa utulivu huku akinitazama. Tukio lile likanipelekea nikohoe kidogo na kuvunja ukimya.

    “Deux jours passé j?ai appellé de l?ambassade de Tanzanie ici à Bujumbura en parlant avec quelqu?un de la réception qu?il puisse reserver une chambre pour mon visiteur. Je ne sais pas vous I?avais donne la chambre numero combien”. Siku mbili zilizopita nilipiga simu hapa kutoka ofisi ya ubalozi wa Tanzania hapa Bujumbura, nikaongea na mtu wa hapa mapokezi kuwa aniwekee chumba kwa ajili ya mgeni wangu. Sijui mtakuwa mlimpatia chumba namba ngapi. Nikamuuliza yule dada mhudumu wa hoteli na hapo yule dada akanitazama kwa uyakinifu kama mtu anayejaribu kuvuta kumbukumbu zake kisha nikamuona akikichukua kitabu kikubwa chenye taarifa za wageni wa ile hoteli kilichokuwa kando yake pale juu mezani. Muda uleule nikamuona akianza kufunua kurasa za kile kitabu kwa utulivu hadi pale alipoufikia ukurasa fulani ndiyo akaweka kituo akiyapitia maelezo fulani yaliyokuwa kwenye ule ukurasa. Hatimaye nikamuona akiinua tena macho yake kunitazama.

    “Oh! c?est vrai que je vois ces coordonés dans le registre de visiteurs son nom c?est Pierre Okongo, n?est ce pas?”. Oh! ni kweli naona maelezo ya mgeni wako yapo hapa kwenye kitabu cha wageni, jina lake anaitwa Peter Okongo, au sivyo?. Yule dada mhudumu akaniambia huku akiyapeleka macho yake kunitazama tena.

    “C?est bien lui, il est dans la chambre numero combien?”. Huyo ndiyo mwenyewe, yupo chumba namba ngapi?. Nikadakia haraka na kuuliza huku jina la Pierre Okongo likianza kuzitekenya upya fikra zangu.

    “II est dans la chambre numero 403 au sixième niveau”. Yupo chumba namba 403 ghorofa ya sita. Yule dada akaniambia kwa utulivu huku akinitazama kwa makini. Kwa kitambo kifupi nikaupisha utulivu kichwani mwangu huku nikifikiria jambo fulani kabla ya kuvunja ukimya.

    “Tu peux appeller pour me confirmer s?il est de dans à cet heure?”. Unaweza kupiga simu kunihakikishia kama yupo ndani kwa muda huu?. Yule dada akatikisa kichwa chake haraka akionesha kukubaliana na ombi langu kisha akaisogeza ile simu ya mezani pale mapokezi na kukiweka kiwambo cha simu sikioni kwake. Alipobofya tarakimu kadhaa ile simu ikaanza kuita upande wa pili na hapo yule dada mhudumu akayahamishia macho yake kunitazama tena. Ile simu iliendelea kuita hadi pale ilipokata na hapo nikamuona yule dada akiipiga tena kwa mara nyingine. Akalirudia lile zoezi mara kadhaa pasipo ile simu kupokelewa na hatimaye yule dada akaikata ile simu na kurudishia kiwambo chake mahala pake.

    “Je pense qu?il n?est pas là, parceque le téléphone de sa chambre appelle mais personne ne décroche”. Nadhani atakuwa ametoka maana simu ya chumbani kwake inaita muda mrefu bila ya kupokelewa. Yule dada mhudumu akaniambia huku akinitazama katika namna ya kunionea huruma kwa kitendo cha kupishana na mgeni wangu.

    “D?accord, je peux trouver la chambre à côte de celle de mon visiteur?”. Okay, ninaweza kupata chumba jirani na hicho cha mgeni wangu?”. Swali langu likampelekea tena yule dada anitazame kwa mshangao kidogo lakini hatimaye akayahamishia macho yake kuitazama tena ile kurasa katika kile kitabu cha taarifa za wageni. Kitambo kifupi cha ukimya kikapita kisha nikamuona tena yule dada akiinua macho yake na kunitazama kabla ya kuniambia..



    “Toutes les chambres à côté de celle de ton visiteur sont occupés peut être celle qui est en face de sa chambre”. Vyumba vyote vya jirani na yeye naona vimejaa labda uchukue chumba kinachotazamana na chake upande wa pili wa korido.

    “J?apprécierai”. Nitashukuru. Nikamwambia yule dada kisha nikanyanyua mkono kuitazama saa yangu ya mkononi na nilipojiridhisha na mwenendo wa majira yake nikageuka nyuma na kuyatembeza macho yangu taratibu kuchunguza kama kungekuwa na ongezeko la mtu mwingine eneo lile. Sikumuona mtu yeyote mwingine hivyo hali bado ilikuwa shwari. Baada ya kumaliza kufanya malipo ya chumba yule dada muhudumu akanikabidhi funguo ya chumba na kunielekeza sehemu kulipokuwa na lifti ya lile jengo la hoteli kuelekea juu.

     Muda mfupi uliofuata nikaliacha lile eneo la mapokezi na kushika uelekeo wa upande wa kulia. Mbele kidogo nikaingia upande wa kushoto na baada ya kuupita mlango mkubwa wa kuelekea sehemu ya maliwato uliokuwa upande wa kushoto hatua chache mbele yangu nikakiona chumba cha lifti cha kuelekea ghorofa za juu za lile jengo la hoteli Le Tulip Hôtel Africaine. Kwa sekunde kadhaa nikasubiri kile chumba cha lifti kishuke chini kwa vile kulikuwa na watu wakishuka chini ya lile jengo. Kile chumba kilipofika chini na mlango wake kufungua wazungu wawili mwanamke na mwanaume wakatoka na kunisalimia huku wakishika hamsini zao. Nikawahi kuingia ndani ya kile chumba cha lifti kisha nikabonyeza kitufe kuiamuru ile lifti inipeleke ghorofa ya sita ya lile jengo. Muda mfupi uliofuata kile chumba cha lifti kikaanza kukwea juu ya lile jengo huku mawazo mengi yakipita kichwani mwangu.

     _____

     Mandhari ya ghorofa ya sita ya lile jengo la Le Tulip Hôtel Africaine jijini Bujumbura yakanitanabaisha vizuri kuwa ni kwa sababu gani hoteli ile ilikuwa imepewa hadhi ya nyota tano. Kile chumba cha lifti kilipotia nanga na kugota ghorofa ya sita na mlango wake kufunguka nikatoka nje na kujikuta katikati ya korido pana yenye utulivu wa hali ya juu. Kwa sekunde kadhaa nikasimama na kuyatathmini vizuri mandhari yale. Kulikuwa na hewa safi iliyokuwa ikisambazwa taratibu na viyoyozi viwili kimoja kikiwa mwanzo wa ile korido na kingine mwisho. Sakafu ya korido ile ilifunikwa kwa zulia jekundu lenye umbo mstatili na hapakuwa na kitu kingine cha ziada zaidi ya utulivu mkubwa wa kistaarabu. Dari ya ile korido ilitengenezwa kwa gypsum nzuri ya rangi nyeupe na katika sehemu za dari ile kulining?inizwa taa nzuri zilizozungukwa na vitenga maridadi vya wavu mwepesi unaopitisha mwanga.

     Taratibu nikaanza kutembea katikati ya ile korido huku nikiyatembeza macho yangu upande huu na ule kutazama namba zilizokuwa juu ya milango ya vyumba vilivyokuwa vikitazamana na ile korido huku kidole changu kimoja kikiwa tayari kimetuama vyema kwenye kilimi cha bastola yangu ndani ya mfuko wa koti. Nikaendelea kutembea taratibu hadi nilipofika katikati ya ile korido na hapo nikasimama.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Nikiwa katikati ya ile korido nikagundua kuwa kulikuwa na korido nyingine ya ile ghorofa iliyoingia upande wa kushoto na hivyo kunipelekea niweze kuielewa vizuri ramani ya lile jengo kuwa ilikuwa ni katika mtindo wa herufi T. Nikaendelea kuyatembeza macho yangu eneo lile na kwa kufanya vile nikagundua kuwa kutoka pale nilipokuwa nimesimama namba za milango ya vyumba vile mbele yangu bado ilikuwa chini ya namba ya kile chumba nilichokuwa nikielekea. Hivyo hisia zangu zikanieleza kuwa chumba namba 403 kingekuwa kwenye ile korido ya upande wa kushoto wa lile jengo. Hivyo haraka nikabadili uelekeo wangu nikiacha kuifuata ile korido mbele yangu badala yake nikashika uelekeo wa upande wa kushoto nikiifuata ile korido.

     Ilikuwa korido ndefu sana inayoniwezesha kuona vizuri hadi mwisho wake na korido ile ilikuwa ikitazamana na milango mingi ya vyumba kwa upande wa kushoto na kulia. Niliendelea kutembea katikati ya korido ile huku taratibu nikiyatembeza macho yangu milangoni. Nilipofika katikati ya ile korido nikapishana na mwanaume mmoja aliyetoka katika chumba jirani na eneo lile ambapo alinisalimia kwa heshima zote na kushika hamsini zake akiniacha niendelee na safari yangu.

     Nilikuwa mbioni kukata tamaa wakati nilipokiona chumba namba 403 upande wangu wa kulia hatua chache kabla ya kufika mwisho wa ile korido. Moyo wangu ukapiga kite kwa nguvu kama niliyeona jambo la kushangaza na la hatari mno. Sikujua ni kwa namna gani hali ile ilinitokea hata hivyo niliziheshimu sana hisia zangu. Taratibu nikausogelea ule mlango na kuuchunguza kwa utulivu. Ulikuwa ni mlango mkubwa na imara wa mbao ngumu. Juu ya mlango ule kulikuwa na nafasi ndogo iliyozibwa kwa kioo chenye mawimbi kisichomuwezesha mtu yeyote aliyeko nje kuweza kuona vizuri ndani ya kile chumba. Hata hivyo kupitia kioo kile nikaweza kugundua kuwa taa ya ndani ya kile chumba ilikuwa imewashwa na hivyo kushikilia kuwa kama mwenyeji wa kile chumba hakuwa mle ndani basi huwenda alikuwa ametoka kidogo kwa safari ya fupi au hakuwa mbali na eneo lile.

     Nilitaka kupata hakika kama mwenyeji wa kile chumba alikuwepo mle ndani au lah!. Hivyo baada ya kuyatembeza macho yangu kwenye ile korido na kuridhika kuwa hakukuwa na mtu mwingine eneo lile nikausogelea ule mlango na kubofya kengele ya mlangoni. Ile kengele ikaanza kuita na tukio lile ikapelekea hamasa ya kipekee nafsini mwangu na hivyo kuifanya taswira ya kufikirika ya mtu aitwaye Pierre Okongo kuanza kujengeka machoni mwangu. Maswali kadhaa yakaanza kuibuka kichwani mwangu nikijiuliza kuwa Pierre Okongo ni nani na alikuwa ametumbukiaje katika mkasa ule. Hata hivyo nilijionya na kujipa tahadhari kuwa nilipaswa kuwa makini zaidi katika nyendo zangu kwani bado sikuwa na hakika vizuri juu ya adui yangu.

     Ile kengele ya mlangoni ikaendelea kuita mle ndani ya kile chumba pasipo dalili zozote za ule mlango kufunguliwa na hatimaye ikafika ukomo bila majibu. Nikarudia tena kubofya ile kengele ya mlangoni mara kadhaa hata hivyo sikujibiwa wala ule mlango kufunguliwa. Hali ile ikanipelekea niyaamini maelezo ya yule dada mhudumu wa kule mapokezi nilipotoka kuwa mwenyeji wa kile chumba huwenda alikuwa ametoka kidogo kutokana na lile tukio la simu ya kile chumba kuita kwa muda mrefu bila kupokelewa.

     Nafsi yangu ikanitanabaisha kuwa nilipaswa kujipa subira kwanza katika kutafuta hakika ya hisia zangu. Hivyo nikauacha mlango wa kile chumba na kuhamia upande wa pili wa ile korido kwenye mlango wa chumba kingine nilichokuwa nimekabidhiwa ufunguo wake na yule dada mhudumu wa mapokezi wa ile hoteli kule chini. Nilipofika nikauchukua ule ufunguo kutoka mfukoni na kuupachika kwenye tundu la kitasa cha ule mlango ambapo nilipoutekenya kidogo ule ufunguo mlango wa kile chumba ukafunguka na hapo nikausukuma taratibu kuingia mle ndani.

     Nilipoingia mle ndani ya kile chumba nikaufungua ule mlango nyuma yangu na kusimama nikitathmini vizuri mandhari ya mle ndani. Kilikuwa chumba kikubwa sana na chenye nafasi ya kutosha. Mle ndani upande wa kulia kulikuwa na kitanda kikubwa cha mbao chenye godoro la foronya laini lililofunikwa kwa shuka safi za rangi nyeupe. Sakafu ya kile chumba ilifunikwa kwa zulia zuri la rangi ya kijivu lenye maua mekundu. Upande wa kushoto wa kile kitanda kulikuwa na kabati zuri la nguo la ukutani pembeni ya dirisha kubwa la kile chumba lililofunikwa kwa mapazia marefu na mepesi yanayoruhusu hewa safi kupenya mle ndani. Upande wa kulia wa kile chumba kando ya kile kitanda nikauona mlango mmoja na hapo nikajua kuwa ule ulikuwa ni mlango wa kueleke kwenye chumba cha maliwato. Kiyoyozi makini kilichokuwa sehemu fulani kwenye kona ya kile chumba kilikuwa kikiendelea kusambaza hewa safi mle ndani pasipo kuzingatia uwepo wa mtumiaji. Kulikuwa na makochi mawili ya sofa upande wa kushoto wa kile chumba nyuma ya meza ndogo fupi ya mbao yenye kibakuli kidogo cha majivu ya sigara juu yake. Makochi yale yalikuwa yakitazamana na seti moja kubwa ya runinga aina ya Sonny Blavia ya inchi 44 iliyofungwa vizuri ukutani na kuunganishwa na king’amuzi cha chaneli nyingi za kimataifa. Niliposogea karibu na yale makochi nikaiona simu moja ya mezani iliyokuwa juu ya stuli moja ya mbao yenye miguu mitatu iliyokuwa kwenye kona ya kile chumba. Pembeni ya simu ile kulikuwa na kitabu kikubwa cha rangi ya samawati chenye orodha ya majina na namba za simu za watu na makampuni mbalimbali ya nchini Burundi.

     Niliwaza kuwa mle ndani ingekuwa ni sehemu tulivu ya kumsubiri Pierre Okongo mwenyeji wa kile chumba cha upande wa pili wa ile korido kilichokuwa mkabala na mlango wa kile chumba changu. Hata hivyo kabla ya kuketi kwenye kochi nikazunguka mle ndani kwa utulivu kukipeleleza vizuri kile chumba. Niliporidhika na hali ya usalama ya mle ndani nikarudi na kuketi kwenye kochi moja mle ndani.

     Kwa mara ya kwanza tangu nifike pale jijini Bujumbura nikajihisi kuwa angalau nilikuwa sehemu salama yenye upweke japokuwa hali ya usalama wa mle ndani haikuwa ya hakika. Nikatulia mle ndani nikifikiria juu ya hili na lile na hatimaye mawazo yangu yakawa yamehamia kwa yule mtu mwenye jina la Pierre Okongo huku nikijaribu kuvuta picha kuwa mtu huyo angekuwa ni mtu wa namna gani. Kwa namna moja au nyingine nilikuwa na kila sababu ya kuamini kuwa Pierre Okongo angekuwa ni msaada mkubwa katika kujibu maswali mengi yaliyokuwa yakikisumbua kichwa changu. Nilikuwa nimekumbuka kuwa kulikuwa na mawasiliano mengi yaliyokuwa yamefanywa kati ya simu ya mezani ya ofisini kwa Balozi Adam Mwambapa na sehemu ya mapokezi ya hoteli ile na sasa nilianza kuamini kuwa Pierre Okongo ndiye aliyeonekana kuwa mlengwa mkubwa wa mawasiliano yale.

     Nikiwa nimeketi kwenye kochi mle chumbani mawazo mengi yakawa yakipita kichwani mwangu. Nilihisi uchovu mwingi mwilini hata hivyo sikuruhusu usingizi unichukue badala yake nikaendelea kuyatega vizuri masikio yangu kwa utulivu nikisikilizia hatua za mtu yeyote ambaye angejitokeza na kuukaribia mlango wa kile chumba 403 cha jirani kilichokuwa mkabala na kile chumba changu.

     Muda uliendelea kusonga pasipo dalili za mtu yeyote kusikika akiusogelea ule mlango wa kile chumba cha jirani kwenye ile korido. Hata hivyo sikukata tamaa kamwe kwani nilikuwa nimejiapiza kusubiri hadi hapo utafiti wangu utakapozaa matunda. Muda bado uliendelea kusonga huku nikiendelea kusubiri na nikiwa katika hali ile wazo jipya likanijia kichwani baada ya kukumbuka kuwa mle ndani kulikuwa na simu ya mezani. Wazo fulani lilikuwa limenijia kichwani na kunifanya nione kuwa kulikuwa na umuhimu wa kumueleza Hidaya juu ya mambo yote yaliyojiri tangu mara ya mwisho tulipoachana.

     Nikaitazama saa yangu ya mkononi na kugundua kuwa muda ulikuwa umesonga sana hali iliyonipelekea niamini kuwa kwa muda ule huwenda Hidaya angekuwa tayari ameshalala nyumbani kwake. Hata hivyo nilifahamu kuwa Hidaya alikuwa msichana makini asiyependa kuendekeza usingizi hususani katika hali tete kama ile. Hivyo nikaichukua ile kadi ndogo yenye namba za simu zilizoandikwa kijasusi kwa mtindo wa herufi na mchoro wa ramani ndogo mfano wa ua zuri la kuchora ambalo mtu yeyote wa kawaida asingeweza kuitambua ramani ile kuwa ingeweza kunifikisha nyumbani kwa Hidaya.

     Ilikuwa ni ile kadi niliyopewa na Hidaya asubuhi ile wakati tulipoonana kule kwenye ofisi za ubalozi wa Tanzania nchini Burundi. Nikamata kadi ile mkononi kisha nikanyakua kiwambo cha ile simu ya mezani mle chumbani na kubonyeza tarakimu za siri zilizokuwa kwenye ile kadi. Nilipomaliza tu ile simu ikaanza kuita upande wa pili hivyo nikakiweka vizuri kile kiwambo cha simu sikioni mwangu na kuanza kusikiliza. Ilikuwa ni kama bahati kwani ule mwito wa simu ulipokuwa mbioni kufika ukomo ile simu ikapokelewa upande wa pili. Hata hivyo mpokeaji wa ile simu hakuzungumza neno lolote huku dhahiri akionekana kunitegea kwa kutokuwa na hakika kuwa mpigaji wa simu ile angekuwa nani kama zilivyokuwa tabia za ujasusi.

    “Hidaya…”. Hatimaye nikavunja ukimya na kuita kwa sauti tulivu ya chini lakini pia inayosikika vizuri hata hivyo Hidaya hakuitikia mapema badala yake nikasikia kelele kidogo kama mtu anayejiweka sawa baada ya kuzinduka kutoka usingizini.

    “Hidaya ni mimi hapa Tibba”

     “Tibba…?”

     “Ndiyo ni mimi Tibba Ganza shemeji yako mwandamizi”. Nikaongea kwa msisitizo huku tukio lile la kupokelewa kwa simu yangu likinifurahisha.

    “Vipi Tibba, kwema?”. Hidaya akaniuliza kwa mashaka huku akitamani kucheka.

    “Ondoa hofu mimi niko salama kabisa labda wewe”

     “Mimi naendelea vizuri, vipi upo kwa wifi yangu Veronica?”. Hidaya akaongea huku akiangua kicheko hafifu cha kimbea chenye kimelea cha wivu wa starehe zangu.

    “Mh! si afadhali ningekuwa kwa huyo Veronica”

     “Sasa upo wapi muda huu?”

     “Nipo Le Tulip Hôtel Africaine ndani ya chumba kimoja kizuri cha daraja la kwanza namsubiri mwenyeji wangu”

     “Mbona hukuniambia kuwa una mwenyeji mwingine hapa jijini Bujumbura?”. Hidaya akaniuliza na hapo haraka nikatambua kuwa lile lilikuwa swali la hila kwa vile alitaka kusikia mengi zaidi kutoka kwangu kama ulivyokuwa ujanja wake. Hivyo nikaikwepa haraka hoja yake kwa kumtumbukizia swali langu.

    “Umewasiliana na Chifu usiku huu?’’

     “Ndiyo”

     “Anasemaje?”

     “Nimemueleza kuwa tayari tumeonana na sasa upo kazini ukiendelea na majukumu yako”

     “Umefanya vizuri sana”. Nikaongea kwa utulivu huku nikiyatafakari maelezo yale na wakati nikiwa katika hali ile Hidaya akavunja ukimya.

    “Vipi Tibba ulifika nyumbani kwa Balozi Adam Mwambapa?’’. Hidaya akaniuliza kwa shauku...

    “Nimetoka huko muda siyo mrefu lakini mambo siyo shwari”

     “Una maana gani?”

     “Kutokana na mazingira niliyoyaona nimejiridhisha kuwa Balozi Adam Mwambapa ametekwa na bahati mbaya sana tukio la kutekwa kwake limegharimu maisha ya watu wengi wasio na hatia”

     “Una maanisha kuwa kuna watu waliouawa?” Hidaya akaniuliza kwa hofu.

    “Walinzi wake wote”

     “Oh! my God”. Hidaya akaongea kwa masikitiko na nilipotega vizuri sikio langu kwa mbali nikamsikia akishusha pumzi katika namna ya kukata tamaa juu ya taarifa ile kisha kukafuatia kitambo kifupi cha ukimya wa tafakari.

    “Balozi Adam Mwambapa alikuwa akiishi na nani nyumbani kwake?’’. Nikawahi kumuuliza Hidaya baada ya kukumbuka kiini cha mawasiliano yale.

    “Zaidi ya yeye mwenyewe, walinzi wake na kijana wake mmoja wa kazi simfahamu mtu mwingine”. Hidaya akanijibu kwa hakika.

    “Kijana wake wa kazi!...”. Nikajisemea moyoni huku nikimkumbuka Sundi. Yule kijana aliyekuwa na jeraha kubwa la kisu tumboni niliyemkuta chumbani kwa Balozi Adam Mwambapa muda mfupi kabla hajakata roho.

    “Kijana wa kazi wa nyumbani kwa Balozi Adam Mwambapa anaitwa Sundi?”

     “Sundi Masele”. Hidaya akaniweka bayana kisha akakohoa kidogo na kuniuliza kwa mashaka.

    “Mungu wangu Sundi amefanya nini tena?”

     “Ameuawa hata hivyo nilipata nafasi ya kuzungumza naye kwa kifupi kabla ya kifo chake. Alitaka nimtafute Padri mmoja wa kanisa la katoliki la hapa jijini Bujumbura aitwaye Aloysius Kanyameza. Umewahi kumsikia popote Padri huyo?”

     “Sundi amekufa…!. Mungu wangu ni unyama gani huu?’’. Nikamsikia Hidaya akisononeka na kushusha pumzi taratibu katika namna ya kukata tamaa hata hivyo sikuona kama ule ungekuwa ni wakati wa majadiliano hivyo haraka nikaelekea kwenye hoja yangu.

    “Niambie Hidaya, unaweza ukawa unafahamu chochote kuhusu Padri Aloysius Kanyameza?”. Hoja yangu ikapelekea kitambo kifupi cha ukimya kupita kisha kwa sauti dhaifu nikamsikia Hidaya akinijibu.

    “Hapana sifahamu chochote kwani hilo jina ni geni kabisa masikioni mwangu. Kwani imekuwaje Tibba?”

     “Bado nipo kwenye uchunguzi Hidaya hivyo taarifa yoyote inaweza kuwa na umuhumu kwangu. Bado sijapata uelekeo sahihi wa kile ninachokipeleleza hivyo pia sina lolote la kukwambia kwa sasa”

     “Sasa kuhusu huyo Padri Aloysius Kanyameza je unadhani kuna lolote ninaloweza kukusaidia?”

     “Hapana Hidaya hili lipo nje ya uwezo wako. Acha tu nitajua namna ya kufanya”

     “Kama ni hivyo sawa”

     “Jambo moja tu…”

     “Ondoa shaka Tibba niambie tu”. Hidaya akaniuliza kwa shauku.

    “Naomba kutakapo pambazuka uwatume vijana wakaiondoe ile miili nyumba ya Balozi Adam Mwambapa. Hakikisha jambo hilo linafanyika kwa usiri mkubwa nadhani unaelewa vizuri ninachomaanisha”

     “Ondoa shaka Tibba nitafanya hivyo. Unadhani ni vyema kumueleza Chifu juu ya hatua uliyofikia?”

     “Siyo jambo la lazima sana lakini pia siyo vibaya kumueleza kwani ni yeye ndiye atakaye shughulikia utaratibu wa kusafirisha hiyo miili hadi Dar es Salaam”

     “Sawa, kuna kingine?”. Hidaya akaniuliza huku usingizi ukionekana kuwa mbali na nafsi yake.

    “Ni hayo tu kwa sasa chochote kingine kitakachojiri tutafahamishana baadaye kadiri muda utakavyoruhusu”. Nikaongea kwa utulivu huku nikiitazama saa yangu ya mkononi.

    “Tibba…”

     “Naam nakusikia Hidaya”

     “Bado hujaniambia kuwa mwenyeji wako hapo hotelini ni nani?”. Swali la Hidaya likanipelekea nitabasamu kidogo baada ya kufurahishwa na tabia yake ya kutokupitwa na jambo.

    “Mtu anayefahamika kwa jina la Pierre Okongo. Kwa mujibu wa uchunguzi wangu ni kuwa huyu ndiye mtu aliyewasiliana na Balozi Adam Mmwambapa muda mfupi kabla ya tukio la kutekwa kwake”

     “Kuwa mwangalifu Tibba”

     “Kifo kitakapokuja hakuna wa kukizuia Hidaya ingawa nimekuwa nikipishana nacho mara kwa mara”

     “Mh! kumbuka Veronica bado anakuhitaji”. Hidaya akachombeza utani huku akiangua kicheko hafifu cha umbea.

    “Ushaanza mambo yako mimi nitakuwezea wapi wewe”. Sote tukaangua kicheko na kwa kuwa sikuwa na jambo lingine la maana la kuzungumza kicheko kile kilipofika ukomo nikaona nimuage kabisa Hidaya.

    “Usiku mwema”CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     “Ahsante Tibba na wewe pia. Nakutakia kila la heri katika kazi yako”

     “Nashukuru sana hata hivyo unisamehe sana kwa kukuharibia usingizi wako”

     “Ondoa shaka wala usijali”

    Hatimaye nikaagana na Hidaya na kisha kurudishia kile kiwambo cha simu ya mezani mahala pake. Kwa sekunde kadhaa nikatulia pale kwenye kochi huku nikiupisha utulivu kichwani mwangu. Kwa kweli sikuweza kufahamu kama nilikuwa nikipiga hatua yoyote kwenye uchunguzi wangu. Hata hivyo nilikuwa na kila sababu ya kuamini kuwa yeyote niliyekutana naye au niliyekuwa nikielekea kukutana naye alikuwa akihusika na mkasa huu. Masaa yalikuwa yakizidi kuyoyoma na mvua nayo ilikuwa ikiendelea kunyesha wakati mawazo mwengi yakipita kichwani mwangu.

     _____

     Sikuweza kufahamu ni kwa namna gani usingizi ulikuwa umefanikiwa kuniteka nyara nikiwa bado nimeketi kwenye lile kochi mle chumbani. Hata hivyo kitendo cha kushtuka kutoka usingizini na kujikuta bado nikiwa kwenye mazingira salama kikanitia faraja. Nikausogeza mkono wangu karibu na kuitazama saa yangu ya mkononi na hapo majira yake yakanitanabaisha kuwa nilikuwa nimeponda usingizi kwa muda wa saa moja kasoro dakika chache nikiwa bado nimeketi kwenye lile kochi. Nikajikuta nikijilaumu kwa kuwa mzembe kiasi kile kwa kuuruhusu usingizi unichukue mzima mzima. Adui mjanja angeweza kuitumia nafasi ile adimu kutimiza dhamira yake mbaya. Nikawaza huku nikipiga mwayo hafifu na kuvinyoosha viungo vyangu mwilini.

     Nilipotuliza fikra zangu nikawaza kuwa muda ule nilioutumia kuuponda usingizi ningeweza kumruhusu Pierre Okongo au mtu mwingine yeyote kuweza kuufikia ule mlango wa chumba cha jirani na hatimaye kuingia mle ndani pasipo kumsikia. Hali ile ikanipelekea nishindwe kufahamu kama bado nilikuwa ndani ya muda au nje ya muda katika kumsubiri mwenyeji wangu. Mwishowe nafsi yangu ikanionya kuwa huwenda nilikuwa nikimsubiri mtu nisiyekuwa na hakika naye hivyo nikasimama na kuelekea kwenye dirisha la kile chumba. Nilipofika nikasogeza pazia kando na kutazama nje chini ya lile jengo.

     Nyuma ya lile jengo kulikuwa na bustani nzuri ya maua na viwanja vya mazoezi na mbele ya viwanja vile kulikuwa na msitu mkubwa wa miti ya kupandwa. Sikuweza haraka kutambua msitu ule ulikuwa umeishia wapi kwa kule mbele hata hivyo ulikuwa umeshona sana na hivyo kuupelekea uonekane unatisha sana kwa nyakati zile za usiku wa manane. Mara moja au mbili mwanga mkali wa radi ulimulika kwenye msitu ule na kutengeneza nuru kubwa ya ghafla iliyoniwezesha walau kuona sehemu tu ya msitu ule wa kutisha. Mvua bado ilikuwa ikiendelea kunyesha hata hivyo nilihisi kuwa ilikuwa imepungua kidogo. Zaidi ya pale sikuweza kuona kiumbe chochote eneo lile na hali ile ikanitanabaisha kuwa masaa yalikuwa yameenda sana.

     Mwishowe nikaliacha lile dirisha na kufunika pazia vizuri kabla ya kuelekea mlangoni. Sikuona kama kuendelea kusubiri zaidi mle ndani kungeweza kufanikisha majibu ya maswali yangu kichwani hivyo nilipoufikia ule mlango nikaufungua taratibu na kutoka. Mlango ulipofunguka nikatoka na kuchungulia kwenye ile korido. Sikumuona mtu yeyote eneo lile na ukimya ule ulikuwa kama wa kifo. Hatimaye nikatoka kabisa nje ya kile chumba na kuufunga ule mlango nyuma yangu. Kwa sekunde kadhaa baada ya kutoka kwenye kile chumba nikasimama katikati ya ile korido nikitaka kutafuta salama ya eneo lile. Sikumuona mtu yeyote hivyo hali bado ilikuwa shwari.

     Nilipoyapeleka macho yangu kutazama juu ya mlango wa kile chumba namba 403 nikashangaa kuona kuwa ile taa ya mle ndani ya kile chumba ilikuwa bado ikiwaka. Tukio lile likaibua maswali mengi kichwani mwangu huku nikishikwa na wasiwasi kuwa huwenda mwenyeji wa chumba kile alikuwa bado hajarudi. Nikajiuliza kama kweli mwenyeji wa chumba kile angekuwa bado hajarudi ingenichukuwa muda gani kumsubiri mtu nisiyekuwa na miadi naye. Jibu la haraka sikulipata hivyo pia sikuona sababu ya kuendelea kusubiri badala yake taratibu nikausogelea mlango wa kile chumba na kubofya kitufe cha kengele ya mlangoni. Miito kadhaa ya ile kengele ya mlangoni ikasikika kwa mbali ndani ya kile chumba pasipo dalili za kufunguliwa kwa ule mlango. Nikarudia tena na tena kubofya kitufe cha ile kengele hata hivyo ule mlango haukufunguliwa wala mtu yeyote kujitokeza na hali ile ikazidi kunitia mashaka.

     Hatimaye nikaanza kuhisi kuwa nilikuwa nikipoteza muda wangu bure kwa kufanya utafiti usiokuwa na tija. Hivyo nikaachana na lile zoezi la kubofya kile kitufe cha kengele pale mlangoni badala yake nikausogelea karibu ule mlango na kushika kitasa chake huku tayari nikiwa nimevaa glovu nyepesi mikononi ili kukwepa kuacha alama za vidole vyangu eneo lile. Nikiwa nimeridhishwa na hali ya usalama wa eneo lile taratibu nikakizungusha kile kitasa na kuusukuma ndani ule mlango. Hata hivyo jitihada zangu hazikufua dafu kwani ule mlango ulikuwa umefungwa.

     Bila kupoteza muda nikaingiza mkono wangu mfukoni na kuchukua mkungu wa funguo malaya ambapo nilianza taratibu kujaribu funguo moja baada ya nyingine kwenye kile kitasa cha ule mlango. Baada ya hangaika hangaika ya hapa na pale hatimaye ule mlango ukafunguka hivyo nikachomoa funguo na kuitia mfukoni.

     Nilianza kwa kuusukuma taratibu ule mlango kwa mkono wa kulia huku mkono wangu wa kushoto ukiwa umeikamata vyema bastola yangu tayari kukabiliana na rabsha za aina yoyote ambazo zingejitokeza mbele yangu. Hata hivyo sikukutana na upinzani wowote badala yake ule mlango ukatii amri kama nilivyotaka hivyo haraka nikaingia mle ndani ya kile chumba na kuurudishia ule mlango nyuma yangu.

     Kwa sekunde kadhaa nikiwa nimesimama mlangoni ndani ya kile chumba nikajikuta nimeshikwa na taharuki isiyoelezeka. Moyo wangu ukapoteza utulivu kabisa huku kijasho chembamba kikianza kufanya ziara sehemu mbalimbali za mwili wangu.

     Katikati ya kitanda kikubwa cha mle ndani chini ya dari ya kile chumba mwili wa mwanaume mmoja mzee wa kizungu mwenye umri wa kukadirika kati ya miaka hamsini hadi sitini ulikuwa ukining’inia kwenye waya mwembamba uliofungwa shingoni na kutundikwa darini. Kwa kweli nilistaajabu sana kwa tukio lile. Yule mzee wa kizungu alikuwa amevaa mavazi ya kitakatifu, joho refu jeupe na kofia nyeupe ya kasisi yenye alama ya msalaba mwekundu mbele yake. Sikuwa na shaka yoyote kuwa mtu yule alikuwa amenyongwa siku moja au mbili zilizopita kwani mwili wake ulikuwa imeanza kutoa harufu mbaya inayoweza kumtapisha mtu.

     Chini ya lile joho yule mtu alikuwa amevaa suruali nyeusi na viatu vyeusi vya ngozi. Mkononi alikuwa ameshika kitabu kitakatifu cha Biblia kilichozungushiwa rozari na kifuani pake alikuwa amening’iniza kidani cha msalaba mkubwa uliotiwa nakshi ya madini ya shaba katika baadhi ya maeneo yake. Ulimi na macho vilikuwa vimemtoa kiongozi yule wa kiroho kutokana na ule waya mwembamba ulioikaba vibaya shingo yake kiasi cha kuuzuia mzunguko wa damu kichwani mwake.

     Haikuwa maiti ya kurudia kuitazama mara mbili mbili. Yule mtu alikuwa amenyongwa tena katika mazingira ya kibabe sana. Uchunguzi wangu ukahitimisha hivyo. Hata hivyo nilihisi kuwa halikuwa jambo rahisi kwani mandhari ya mle ndani yaliashiria kuwa kulikuwa kumetokea patashika ya aina yake. Shuka za pale kitandani zilikuwa zimevurugwa ovyo na mito yake kutupwa sakafuni. Kabati la nguo la ukutani la mle ndani lilikuwa limeachwa wazi ingawa ndani yake hapakuwa na kitu chochote. Simu ya mezani mle chumbani ilikuwa imeangushwa chini ingawa haikuwa imeharibika. Droo za kitanda zilikuwa zimefunguliwa na kuachwa wazi na katika meza ndogo ya mle ndani iliyokuwa pembeni ya kitanda juu yake...





    Kulikuwa na chupa kubwa ya mvinyo mwekundu aina ya Merlot ulikuwa nusu huku glasi mbili zikiwa kando yake. Kupitia zile glasi mbili pale mezani na ule mzinga wa pombe nikajiridhisha kuwa mle kulikuwa na watu wawili waliokuwa wakiyasindikiza maongezi yao kwa kile kinywaji na bila shaka mtu huyo mwingine ndiye angekuwa amehusika kumnyonga kinyama yule Padri wa kizungu mle ndani. Niliposogea karibu na kuchunguza pale juu ya ile meza nikaona kalamu na karatasi ingawa karatasi ile nilipoichunguza vizuri nikagundua kuwa ilikuwa haijaandikwa kitu chochote juu yake.

     Kwa sekunde kadhaa nikasimama huku taratibu nikiyatembeza macho yangu mle ndani kupeleleza kama kungekuwa na kitu kingine cha kuziteka hisia zangu. Sikuona kitu chochote cha ziada kwani mandhari ya kile chumba hayakutofautiana kabisa na kile chumba nilichotoka. Jambo moja la kushangaza ni kuwa runinga iliyokuwa mle ndani ilikuwa ikiendelea kurusha matangazo yake kama kawaida. Kwa kweli sikuweza kupata picha kamili juu ya kilichokuwa kikiendelea mle ndani hadi kupelekea tukio la kunyongwa kwa yule padri wa kizungu. Hata hivyo kupitia ile kalamu na karatasi juu ya ile meza fupi mle ndani nilihisi kuwa huwenda yule Padri alikuwa amelazimishwa kutoa taarifa fulani na alipokataa kutoa ushirikiano mnyongaji akawa amepata sababu ya kutimiza adhma yake. Bado sikuweza kufahamu kilichokuwa kikiendelea mle ndani ingawa jina la Pierre Okongo sasa lilianza kupata nafasi kubwa ya kujadiliwa kichwani mwangu. Nikaendelea kujiuliza kuwa Pierre Okongo ni nani na yule Padri wa kizungu aliyenyongwa mle ndani alikuwa ameingiaje kwenye mkasa huu hatari usioeleweka. Bado sikupata majibu hivyo mawazo mengi bado yalikuwa yakipita kichwani mwangu.

     Hatimaye nikaisogelea karibu maiti ya yule Padri wa kizungu huku nikiwa nimeziba pua yangu kwa kiganja ili kujikinga na ile harufu mbaya ya uvundo kisha nikaanza kiufanyia uchunguzi kwa kuipekua mifukoni. Nilipomaliza kufanya upekuzi wangu nikawa nimefanikiwa kupata kitabu kidogo cha sala ambapo nilipokipekua vizuri ndani yake nikaona kuwa kilikuwa kimegongwa mhuri wa kutambulisha kuwa kitabu kile cha sala kilikuwa ni mali ya kanisa la Katoriki dayosisi ya jimbo moja lililokuwa katikati ya jiji la Bujumbura. Zaidi ya pale sikuona kitu kingine cha ziada hivyo nikachukua kile kitabu kidogo cha sala na kukitia mfukoni.

     Ghafla wakati nilipokuwa nikiendelea na uchunguzi wangu dhidi ya ule mwili wa yule Padri wa kizungu mle ndani mara nikasikia sauti za vishindo vya hatua za watu wakikimbia nje ya ile korido kuukaribia mlango wa kile chumba. Haraka nikahisi kuwa jambo la hatari lilikuwa mbioni kunikaribia hivyo sikutaka kusubiri badala yake haraka nikakatisha kwenye kile chumba kuelekea dirishani huku nikijipa tahadhari. Nilipofika pale dirishani nikasogeza pazia pembeni na kufyatua komeo la dirisha pana la kioo na kulifungua lile dirisha. Vile vishindo vya watu vikaongezeka kwenye ile korido na hatimaye kuja kukomea nje ya ule mlango wa kile chumba kisha ukimya mfupi ukafuata kabla ya kusikia kelele za kitasa cha ule mlango kikichokolewa kwa funguo.

     Niliwahi kufungua lile dirisha haraka nikachungulia kule nje nikitazama kama kungekuwa na uwezekano wowote wa kutoroka eneo lile. Hata hivyo muundo wa jengo lile haukunipa nafasi nzuri ya kutimiza haraka azma yangu kwa kuwa hapakuwa na sehemu nzuri ya kuning’inia mbali na vijukwaa vifupi vilivyokuwa chini ya madirisha ya lile jengo. Hata hivyo nilipoendelea kuchunguza nikaliona bomba moja lililokuwa likisafirisha maji ya mvua kutoka sehemu ya juu ya paa la ile hoteli kwenda chini ya lile jengo. Lile bomba lilikuwa kiasi cha umbali wa mita kadhaa upande wa kushoto likipita kando ya dirisha la chumba kingine kilichokuwa jirani. Haraka nikawahi kujilaza pale dirishani kisha nikawihi kutanguliza miguu yangu nje ya lile dirisha. Kiwiliwili changu kilipopita nikamalizia kwa kuning’inia nje ya lile dirisha kwa mikono yangu huku nikiwahi kurudishia lile pazia na kulifunga lile dirisha kwa nje. Sasa nilikuwa nimening’inia kwenye ukingo mdogo wa lile dirisha na uzito wote mwilini ulielekea kuilemea mikono yangu.

     Nikiwa bado nimening’inia pale dirishani nikageuka na kutazama kule chini na ule umbali ukanionya kuwa namna yoyote ya kukosa umakini katika kuning’inia pale dirishani kifo kilikuwa tayari kunipokea. Hata hivyo sikutaka kuondoka haraka pale dirishani kabla sijatafuta hakika ya wale watu waliokuwa kule nje mlangoni koridoni wakifanya jitihada za kuingia mle ndani.

     Muda mfupi uliofuata ule mlango wa kile chumba ukasikika ukifunguliwa kwa kishindo cha nguvu kazi ya hali ya juu. Ule mlango ukafunguka kwa pupa na kujipigiza ukutani. Nikawahi kujivuta juu na kuchungulia mle ndani ya kile chumba kupitia uwazi mdogo ulioachwa na pazia la kile chumba pale dirishani. Nilipochungulia nikawaona wanaume wawili wakiingia mle ndani huku kila mmoja akiwa na bastola yake mkononi. Walikuwa wanaume warefu na weusi wenye miili iliyojengeka imara. Japokuwa watu wale hawakuwa wamevaa sare za jeshi lakini wajihi wao ulitosha kunitanabaisha kuwa walikuwa ni askari jeshi waliohitimu vizuri mafunzo ya juu ya kijeshi.

     Kitu kilichonistaajabisha ni kuwa watu wale hawakuonekana kushtushwa kabisa na lile tukio la kunyongwa kwa yule Padri wa kizungu mle ndani badala yake walijikita katika kumtafuta mtu mwingine ambaye bila shaka mtu huyo alikuwa mimi. Nikamuona mwanaume mmoja kati ya wale wanaume wawili walioingia mle ndani akichepuka haraka na kuelekea kwenye chumba kidogo cha maliwato kilichokuwa kwenye kona ya kile chumba cha kulala ambapo alipofika akafungua mlango wa kile chumba kwa tahadhari na kutazama tazama mle ndani. Alipoona mle ndani hakuna mtu akarudi tena pale chumbani. Yule mwenzake akaendelea kusimama pale mlangoni huku akionekana kuchukua tahadhari za kiusalama za kila namna kujihami.

     Nikiwa bado nimening’inia pale dirishani nikaendelea kuwachunguza wale watu hata hivyo haraka niligundua kuwa sura zao zilikuwa ngeni kabisa machoni mwangu. Hali ikanipelekea nijiulize maswali kadhaa kichwani mwangu kuwa watu wale walikuwa akina nani na walikuwa na shida gani. Wote walikuwa wamevaa suti nyeusi, mashati ya kijivu na tai nyeusi shingoni mwao huku kichwani wakiwa wamevaa kofia nyeusi nadhifu za pama. Yule mwanaume mmoja akaendelea kufanya upekuzi mle ndani na aliporidhika kuwa hapakuwa na mtu mle ndani nikamuona akimwonesha ishara fulani yule mwenzake pale mlangoni na hapo nikamuona yule mwenzake pale mlangoni akiwasha kifaa cha mawasiliano kilichokuwa shingoni mwake na kupelekea habari kwa mtu wa tatu ambaye sikumuona mle ndani.

     Wakati yule mtu wa mlangoni akiendelea kumpasha taarifa huyo mtu wa tatu ambaye hakuwa mle ndani mara nikamuona yule mwenzake akigeuka na kutazama pale dirishani kama aliyehisi jambo fulani na kwa kutaka kuzitafutia hakika hisia zake nikamuona taratibu akipiga hatua zake hafifu za tahadhari kusogea pale dirishani nilipokuwa nimening’inia kwa nje. Kuona vile nikaamua kujidhatiti ili kukabiliana na rabsha zozote ambazo zingejitokeza. Hata hivyo mikono yangu ilikuwa imeanza kuchoka kuning’nia pale dirishani na hali ile ilizidi kunipa wasiwasi. Hata hivyo kabla yule mtu hajafika pale dirishani nikawa tayari nimekusanya nguvu za kujisogeza kando ya lile dirisha nikiendelea kuning’inia. Mikono yangu ilikuwa imeanza kutetemeka kutokana na nguvu nyingi niliyokuwa nikiitumia kuubeba uzito wa kiwiliwili changu na ingawa kulikuwa na hali ya hewa ya baridi kufuatia mvua za masika zilizokuwa zikiendelea kunyesha lakini mwilini nilianza kuhisi hali ya joto kali.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Yule mtu alipofika pale dirishani akasogeza pazia na kufungua lile dirisha akitazama tazama kule chini ya lile jengo. Hata hivyo niligundua haraka kuwa hakuwa ameniona kutokana na giza lililokuwa eneo lile na baada ya kuridhika na uchunguzi wake usio makini nikamsikia akimwambia neno fulani la kirundi yule mwenzake kule mlangoni kisha akatoa sigara kutoka mfukoni na kuiwasha akianza kuivuta taratibu pale dirishani. Kwa kweli nilikuwa nimeanza kuchoka kuning’inia pale dirishani hivyo nilianza kuona hatari ya kujiachia mzimamzima bila kupenda na hatimaye kuanguka chini ya lile jengo. Hata hivyo ule umbali wa chini ya lile jengo ulikuwa umenionya kuwa kujiachia pale ilikuwa ni sawa na kujiua kwa kifo cha aibu na woga wa kujisalimisha kwa wale watu.

     Nikiwa mbioni kuishiwa nguvu pale dirishani niliponing’inia nikageuka tena na kulichunguza vizuri lile bomba la kusafirishia maji ya mvua kutoka sehemu ya juu ya lile jengo. Mara moja uchunguzi wangu makini ukabadilisha mawazo yangu kuwa sikuwa sahihi na sikupaswa kuyategemeza maisha yangu kwenye lile bomba kwani niligundua haraka kuwa lile bomba lilikuwa na udhaifu mkubwa katika baadhi ya maungio yake kutokana na kutofanyiwa ukarabati madhubuti wa mara kwa mara hivyo hofu ikajipenyeza upya moyoni mwangu.

     Kadiri hali yangu ilivyokuwa ikizidi kuwa mbaya mawazo ya kutaka kupiga kelele na kumshtua yule mtu pale dirishani ili aniokoe yakawa taratibu yakianza kuniingia akilini mwangu kwani niliamini kuwa kwa muda usiozidi dakika tano baada ya pale hata nguvu za kusogea tena eneo lile nisingekuwa nazo tena. Nikiwa katika hali ile mara nikamsikia yule mtu aliyesimama pale mlangoni akimuita yule mwenzake wa pale dirishani. Muda uleule yule mtu aliyesimama pale dirishani akasitisha starehe yake ya kuvuta sigara kisha kile kipisi cha sigara akakitupa nje lakini bila kutarajia kile kipisi cha sigara kikaangukia kwenye vidole vyangu pale nilipong’inia na kuniunguza hata hivyo sikushughulika nacho kwani nguvu zilikuwa mbioni kuniishia. Haukupita muda mrefu mara nikamsikia yule mtu pale dirishani akifunga lile dirisha na kurudishia lile pazia. Muda mfupi uliofuata nikausikia mlango wa kile chumba ukifunguliwa na kisha kufungwa baada ya pale ukimya ukafuatia.

     Sikuwa na sababu nyingine ya kuendelea kusubiri kwani nguvu za mikono yangu zilikuwa mbioni kuniishia na hali yangu ilikuwa ikizidi kuwa mbaya hivyo taabu nikakusanya nguvu na kufanikiwa kuupandisha mguu wangu mmoja pale dirishani. Nilipofanikiwa kuupandisha mguu mwingine nikawahi kushika pembe moja ya lile dirisha ambapo nilijivuta kwa nguvu zangu zote hadi pale nilipofanikiwa kukaa pale juu dirishani huku nikihema ovyo. Sikutaka tena kugeuka na kutazama chini ya lile jengo kwani kizunguzungu kilikuwa kimenishika vilivyo kutokana na msukumo mkubwa wa damu kichwani mwangu. Nilipojaribu kulifungua lile dirisha nikagundua kuwa yule mtu aliyekuwa amesimama pale dirishani muda mfupi uliopita alikuwa amelifunga lile dirisha kwa ndani kwa komeo hivyo hapakuwa na namna mbadala ya kurudi mle ndani bila ya kupasua kile kioo cha pale dirishani.

     Bila kupoteza muda nikaikamata vizuri pembe moja ya lile dirisha kisha nikapiga kiwiko kimoja cha nguvu pale dirishani. Kioo cha lile dirisha kilipopasuka nikapenyeza mkono na kufyatua komeo na muda mfupi uliofuata nikawa nimerudi mle ndani ya kile chumba. Sikutaka kupoteza muda tena mle ndani hivyo haraka nikaelekea kwenye mlango wa kile chumba huku kidole changu kikiwa tayari mbele ya kilimi cha bastola yangu iliyokuwa ndani ya mfuko wa koti langu. Nilipofika pale mlangoni taratibu nikaufungua ule mlango kisha kwa tahadhari nikachungulia kwenye ile korido. Sikumuona mtu yeyote kwenye ile korido hivyo hali bado ilikuwa shwari. Hatimaye nikatoka kwenye kile chumba na kuingia kwenye ile korido. Niliwakumbuka wale watu wawili waliotoka mle ndani ya kile chumba muda mfupi uliopita kuwa wangekuwa wamekwisha toweka na kushika hamsini zao hata hivyo niliamini kuwa hadi kufikia wakati ule wale watu wasingekuwa wamefika mbali sana na eneo lile. Hivyo kwa kukwepa kukutana nao mara tu nilipotoka nje ya kile chumba nikashika uelekeo wa upande kulia wa ile korido nikitembea kwa tahadhari huku mara kwa mara nikigeuka na kutazama nyuma.

     Mwisho wa ile korido upande wa kushoto kulikuwa na lifti na wakati nikifika eneo lile nikagundua kuwa kile chumba cha lifti kilikuwa kipo ghorofa ya 12 ya lile jengo. Hivyo nikabonyeza kitufe kando ya ule mlango kuiita ile lifti pale nilipokuwa. Kulikuwa na muda kidogo wa kusubiri kwani kile chumba cha lifti kiliendelea na safari yake hadi ghorofa ya 14 na hapo nikajua kuwa kulikuwa na mtu kwenye ile ghorofa ya 14 aliyekuwa ameiita ile lifti akitaka kushuka chini ya lile jengo. Hivyo baada ya muda mfupi kupita kile chumba cha lifti kikaanza kushuka chini.

     Wakati nikiendelea kusubiri kile chumba cha lifti kinifikie mara nikajikuta nikishtushwa na sauti ya kishindo cha hatua za mtu aliyekuwa akikimbia kuja kwenye ile korido. Wasiwasi ukiwa tayari umeanza kiniingia nikageuka na kutazama kule mwanzo wa ile korido ambapo kulikuwa na korido na nyingine iliyokatisha mbele yake. Haukupita muda mrefu mara nikawaona wale wanaume wawili hatari wakitimua mbio na kuingia kwenye ile korido kunifuata huku bastola zao wamezishika mkononi. Niliwakumbuka vizuri wale watu kuwa ndiyo wale waliokuwa wametoka kwenye kile chumba chenye yule Padri wa kizungu aliyenyongwa muda mfupi uliopita na sikuwa na mashaka kuwa mlengwa wa mbio zile nilikuwa mimi.

     Wasiwasi ukiwa umenishika taratibu nikageuka na kuchunguza lile eneo kama kungekuwa na mwanya wowote wa kutoroka. Kwa mara ya kwanza nikajikuta kwenye wakati mgumu baada kuhisi kuwa hapakuwa na sehemu yoyote ya kukimbilia na wale watu sasa walikuwa wakinikaribia kwa kasi ya ajabu. Sikuwa na namna ya kufanya hivyo haraka nikaingiza mkono kwenye mfuko wa koti langu na kuikamata vyema bastola yangu tayari kuanzisha mapamana. Wale watu ni kama tayari walikuwa wameishtukia janja yangu kwani mmoja aliwahi kufyatua bastola kunilenga ila kutokana na kule kukimbia kwake akawa amekosa shabaha hivyo ile risasi ikaniparaza begani na kwenda kupasua kioo cha dirisha lililokuwa mwisho wa ile korido tukio lile likasababisha sauti kali ya mpasuko wa kile kioo. Kuona vile nikaamua kujibu mashambulizi. Risasi mbili nilizofyatua zikawakosa wale watu hata hivyo zilifanikiwa kuipunguza kasi yao ya kunifikia ingawa wale watu bado hawakukata tamaa. Tukaendelea kutupiana risasi huku kila mmoja akichepuka na kujibanza kwenye kona za milango ya vyumba vilivyokuwa vikipakana na ile korido. Wale watu hawakutaka kunipa nafasi ya kuwatoroka hivyo wakawa wakinitupia risasi nyingi lakini zisizokuwa na shabaha nami sikuacha kuwaandama wale watu kwa risasi zangu na kwa kufanya vile nikafanikiwa kumpata mmoja begani.

     Nikiwa mbioni kukata tamaa mara kile chumba cha lifti kikawa tayari kimefika kwenye ile korido na mlango wake ulipofunguka nikajitupa ndani kinyume nyume huku nikiendelea kujibu mashambulizi dhidi ya wale watu. Wale watu walitamani sana nisifanikiwe kuwatoroka hata hivyo risasi zangu ziliwazuia kunifikia kwa wepesi. Hatimaye ule mlango wa kile chumba...

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ...cha lifti ukafunga na ile lifti ikaanza kushuka chini ya lile jengo. Mle ndani ya kile chumba cha lifti hakukuwa na mtu mwingine yeyote na hali ile niliipenda. Sasa akili yangu ikaanza kujiandaa namna ya kukabiliana na hatari yeyote ambayo ingejitokeza baada ya kufika chini ya lile jengo.

     Sikufanikiwa kwani wakati kile chumba cha lifti kinafika ghorofa ya tatu ya lile jengo la Le Tulip Hôtel Africaine ghafla taa ya mle ndani ikazima na kisha kile chumba cha lifti kusimama. Kwa sekunde kadhaa nikaganda kama nyamafu nikishikwa na taharuki isiyoelezeka sambamba hofu kuanza kupenya taratibu moyoni mwangu. Hisia zangu zikanitanabaisha kuwa nilikuwa nimejitumbukiza kwenye hatari nyingine na tukio lile huwenda lingekuwa ni mtego wa kuninasa mzimamzima kama siyo hitilafu ya umeme ya kawaida.

     Kutokana na mfumo wa kile chumba cha lifti hapakuwa na hewa iliyokuwa ikiingia au kutoka mle ndani hivyo nilianza kuishiwa pumzi taratibu huku nikitokwa na jasho jingi mwilini. Hata hivyo nilijipa uvumilivu huku nikijipa matumaini kuwa kama lile lingekuwa ni tatizo la umeme wa kawaida basi jenereta la umeme wa dharura wa lile jengo lisingechukua zaidi ya dakika tatu kabla kuwaka na hivyo safari yangu ingeendelea kama kawaida.

     Hata hivyo kile nilichokuwa nikikiwaza hakikutokea kwani ule umeme haukurudi wala kile chumba cha lifti kuendelea na safari. Kwa zaidi ya dakika mbili nikakaa mle ndani na baada ya kuona hakuna uelekeo sikutaka kusubiri zaidi kwani hewa ya mle ndani ya kile chumba ilikuwa tayari imeanza kuwa nzito kiasi cha kunipelekea nianze kuhema kwa tabu. Haraka nikaingiza mkono mfukoni kuchukua kurunzi yangu ndogo ya kijasusi yenye mwanga mkali na kuanza kumulikamulika mle ndani. Kwa kufanya vile nikakiona kifuniko kidogo kilichokuwa sehemu ya juu katikati ya kile chumba cha lifti kikiwa kimefungwa kwa skrubu.

     Bila ya kupoteza muda nikadandia kuta za kile chumba kwa miguu yangu na kuanza kufungua ule mfuniko kwa kisu changu kidogo chenye mkusanyiko wa vifaa vingi muhimu kama kiberiti cha gesi, bisbisi, uma mdogo, kijiko, opena na vifaa vingine vidogo vidogo muhimu. Baada ya muda mfupi nikawa nimefanikiwa kuufungua ule mfuniko na kuuweka kando huku moyoni nikiomba kuwa ule umeme wa lile jengo usirudi haraka kabla ya kukamilika kwa operesheni yangu.

     Nilipouondoa ule mfuniko nikapenyeza kichwa changu kwenye lile tundu kule juu na kuanza kumulika. Kule juu kulikuwa na nyaya nyingi zinazopishana na machuma mengi yaliyoshikilia kile chumba cha lifti. Mle ndani hewa ilikuwa imeanza kuwa nzito na joto nalo lilikuwa likiongezeka taratibu. Nilianza kuzifuatilia zile nyaya na nilipohisi kuwa zisingenifaa chochote nikaamua kuachana nazo. Nilipoendelea kuchunguza vizuri nikauona mpira mwembamba uliopenya kwenye tundu ndogo kama la pipa la maji. Nilipoufuatilia ule mpira nikagundua kuwa ulikuwa ni mpira wa kiyoyozi cha kile chumba hivyo nikachukua kisu na kuukata kisha nikaanza kuuvuta. Muda mfupi uliofuata nikawa nimefanikiwa kuunyofoa ule mpira na hapo hewa safi na nyepesi ikaanza kupenya mle ndani na hapo akili yangu ikaanza kupata afya njema huku mwili wangu ukirudi katika hali yake ya kawaida. Sasa suala la hewa safi mle ndani likawa limerudi katika hali yake ya kawaida.

     Nikaendelea kukwea juu zaidi ya kile chumba cha lifti nikipenya kwenye vile vyuma vya juu vilivyoshikilia kile chumba. Kulikuwa na mitambo mingine ya kuendeshea mjongeo wa kile chumba cha lifti ambayo hata nilipojitahidi kuichunguza mitambo ile bado sikuweza kufahamu namna ya ufanyakazi wake wa kazi. Baada ya kuvipita vile vyuma juu yake nikakutana na mfuniko mwingine wa chuma chepesi ambapo kulikuwa na nyaya nyingi za umeme zilizofungwa pamoja zilizokuwa zimepenya kwenye tundu dogo lililokuwa kwenye pembe ya ule mfuniko. Niliposogea karibu na kuchungulia kwenye lile tundu dogo kule juu nikaona uwazi mkubwa. Kwa msaada wa ile bisibis nikafungua kile kifuniko na kupenya zaidi kule juu. Muda mfupi baadaye nikawa nimetokezea sehemu salama zaidi iliyokuwa juu ya kile chumba katika eneo la wazi lililoniwezesha kuona vizuri kule juu ya kile chumba cha lifti na sehemu ya nje ya lile jengo kupitia kuta safi za kioo.

     Upande wa kushoto eneo lile nikaliona bomba kubwa la chuma ingawa sikuweza kufahamu kuwa lile bomba lilikuwa likielekea wapi. Hata hivyo nilishawishika kulifuata lile bomba nikihisi kuwa huwenda lingekuwa msaada mkubwa katika kulitoroka eneo lile. Hivyo haraka nikalisogelea lile bomba na kujilaza juu yake kisha nikaanza kusota kwa tumbo nikielekea kule mbele lile bomba lilipokuwa likielekea. Lile bomba lilikuwa refu sana likipenya kwenye vipenyo kadhaa vya lile jengo.

     Hatimaye nikafika sehemu ambapo lile bomba lilikuwa limebadili uelekeo na kuingia upande wa kulia. Nilipofika eneo lile sehemu ya chini nikaona vyumba vingi vinavyopakana na eneo kubwa la wazi. Hisia zangu zikanitanabaisha kuwa nilikuwa nimetokezea kwenye eneo la maliwato. Nilifurahi sana hivyo nikajiachia kwenye lile bomba na kutua kwenye vyoo vya wanaume vya ghorofa ile.

     Kulikuwa na vyumba vitano vya vyoo eneo lile vilivyokuwa vikitazamana na eneo la wazi lenye masinki ya kunawia na vyoo vidogo vya marumaru vya haja ndogo ukutani. Mle ndani hapakuwa na mtu na mlango wa eneo lile ulikuwa umefungwa. Nikaachana na ule mlango wa eneo lile na kaingia kwenye choo kimoja. Nyuma ya kile choo kulikuwa na dirisha dogo la kioo linaloniwezesha kupenya vizuri hivyo nikafyatua komeo lake na kufungua lile dirisha. Halafu pasipo kupoteza muda nikapanda juu ya choo cha kukaa cha marumaru cha mle ndani kisha nikakanyaga tenki dogo la maji ya kusukumia uchafu na kuanza kupenya nikitoka nje ya kile chumba. Bado lile jengo lilikuwa limegubigwa na giza kila mahali na hali ile niliipenda sana kwani yeyote aliyekuwa akinifuatilia asingeweza kuniona kwa urahisi.

     Mara baada ya kutoka kwenye lile dirisha nikaning’inia kwenye jukwaa dogo la zege lililokuwa chini ya lile dirisha huku nikitafuta namna ya kushuka kule chini ingawa sasa nilikuwa na matumaini ya usalama wangu kwani ule umbali wa kule chini ulikuwa umepungua. Nilipoendelea kuchunguza upande ule nikauona mti mmoja mkubwa wa kivuli hata hivyo matawi ya mti ule yalikuwa yameishia ghorofa ya pili hivyo ingenilazimu kushuka chini kwa ghorofa moja zaidi kabla ya kuyafikia matawi ya ule mti.

     Sikuwa na namna nyingine ya kufanya hivyo nikaanza kuning’inia kwa tahadhari nikitoka dirisha la chumba kimoja kwenda dirisha la chumba kingine na ndani ya muda mfupi nikawa nimelifikia lile bomba dhaifu lililokuwa likitiririsha maji ya mvua kutoka kwenye paa la juu la lile jengo la ile hoteli. Nilipolifikia lile bomba nikaning’inia kwa tahadhari nikisota taratibu kushuka chini huku nikiwa mwangalifu lisije likakwanyuka na kuniangusha chini. Hivyo baada ya muda mfupi nikawa nimefanikiwa kulifikia paa dogo la dirisha la chumba kimoja cha ghorofa ya pili hivyo nikaliacha lile bomba na kurukia juu ya lile paa dogo la lile dirisha.

     Nikiwa pale juu ya lile paa nikatulia kwa muda nikayatembeza macho yangu kulipeleleza vizuri eneo lile. Sikumuona mtu yeyote hivyo hali bado ilikuwa shwari na bila kupoteza muda nikajilaza tena juu ya lile paa nikianza kusota taratibu nikilifuata tawi moja la mti mkubwa wa kivuli uliokuwa kando kidogo na lile dirisha. Hatimaye nikawa nimelipata tawi moja imara lenye uwezo wa kuubeba uzito wangu bila mashaka yoyote. Taratibu na kwa tahadhari ya hali ya juu nikaanza kukwea lile tawi nikishuka chini ya ule mti. Macho yangu bado yalikuwa makini kulichunguza eneo lile. Muda mfupi uliofuata nikawa nimefanikiwa kushuka chini ya ule mti. Hata hivyo kabla ya kuondoka eneo lile nikatulia kidogo nikipeleleza kama kungekuwa na mtu yeyote eneo lile na niliporidhika kuwa bado nilikuwa salama nikachepuka na kuanza kutembea kwa tahadhari kando ya ukuta wa Le Tulip Hôtel Africaine nikipita kwenye vichaka vya maua ya kupandwa kuelekea mbele ya ile hoteli.

     Wakati nikitembea nikawa nikiwakumbuka wale watu waliokuwa wakinifuatilia kule nyuma na lile gari jeupe Landcruiser na hatimaye kuzuiliwa na kile kizuizi cha askari jeshi kule barabarani na hapo nikajikuta nikiwahusisha wale watu na hawa niliofanikiwa kuwatoroka kwenye ile korido ya ghorofa ya tano ya lile jengo la hoteli muda mfupi uliopita. Sasa nilianza kuamini kuwa mpango wa kutekwa kwa Balozi Adam Mwambapa usiku ule kule nyumbani kwake ulikuwa umepangwa na kutekelezwa na kikundi cha askari jeshi wachache wa jeshi la wananchi wa Burundi huku nikishindwa kuelewa lengo lao.

     Mvua bado ilikuwa ikiendelea kunyesha na giza zito lilikuwa limetanda kila mahali. Nilichokuwa nikiwaza kichwani ni kuondoka haraka eneo lile kabla masaibu mengine hayajanikuta eneo lile. Nikaendelea kutembea kwa tahadhari nikilizunguka lile jengo la hoteli kuelekea kule mbele nilipokuwa nimeegesha gari langu. Nilikuwa na kila hakika kuwa wale watu waliokuwa wakinifuatilia kule ghorofani wakati watakapofanikiwa kukifungua kile chumba cha lifti na kushikwa na mshangao mimi ningekuwa tayari niko mbali na eneo lile nikitokomea na jambo hilo lingenipa faraja sana.

     Hata hivyo mambo hayakwenda kama nilivyokuwa nimetarajia kwani wakati nikifikia mbele ya lile jengo la hoteli mara nikaliona gari moja la jeshi aina ya Nissan Patrol likiingia kwa kasi na kuegesha katika maegesho ya mbele ya ile hoteli. Kisha kabla ya mlango wa lile gari kufunguliwa haraka nikamuona mtu mmoja akichepuka kutoka sehemu ya mbele ya ile hoteli na kulifuata lile gari. Nilipozidi kuchunguza nikagundua kuwa yule mtu alikuwa miongoni mwa wale watu wawili niliotoka kupambana nao na hatimaye kufanikiwa kuwatoroka kule juu ghorofani kwenye ile korido ingawa sikuweza kufahamu yule mwenzake alikuwa wapi kwa wakati ule. Yule mtu alipofika kwenye lile gari kioo cha dirishani kikashushwa na hapo nikamuona yule mtu akiongea na mtu mwingine pale dirishani huku akimuelekeza kwa kidole juu ya lile jengo la ghorofa la ile hoteli.

     Nilihisi jambo fulani lisilo la kawaida kuelekea kutokea eneo lile hata hivyo sikuweza tena kulifikia lile gari langu pale kwenye yale maegesho kwani lile gari Nissan Patrol lilikuwa limechukua nafasi kando ya gari langu baada ya gari jingine lililokuwa pale kuondoka. Haukupita muda mrefu mara nikaona milango ya lile gari Nissan Patrol ikifunguliwa kisha wakashuka wanaume kumi na moja pamoja na mbwa wawili wakubwa aina ya German Shephered wenye urefu sawa na ule wa ndama wa kisasa. Lile gari Nissan Patrol lilikuwa dogo kuweza kuwabeba wale watu wote hata hivyo kwa kuwa ililazimishwa basi iliwezekana. Sasa nilitambua kuwa kikosi cha kunisaka kilikuwa kimeongezwa kama moja ya mkakati makini wa kuhakikisha kuwa sipati mwanya wowote wa kutoroka.

     Wale watu walioshuka kutoka kwenye lile gari walikuwa wamevaa makoti marefu ya kijeshi ya mvua na mikononi walikuwa wameshika bunduki. Muda mfupi uliofuata nikawaona watu wawili wakielekea pale kwenye gari langu baada ya kuelekezwa na yule mtu wa awali. Wale watu walipofika wakalizunguka gari langu na kuanza kulikagua kwa tahadhari kisha nikamuona mmoja akitia utundu na kufungua mlango wa lile gari langu akiingia mle ndani. Sikuweza kufahamu kwa haraka kuwa lipi lilikuwa lengo la yule mtu hata hivyo nilihisi kuwa chochote ambacho kingefanyika ndani ya lile gari bila shaka kingekuwa katika moja ya mikakati yao mingi ya kutaka kunikamata kama siyo kuniangamiza kabisa.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Wakati wale watu wakiendelea kushughulika na gari langu mara nikamuona yule mtu wa awali aliyevaa suti akiongozana na watu watatu miongoni mwa wale watu walioshuka kutoka kwenye lile gari la jeshi wakielekea kwenye ile hoteli. Wale watu sita waliosalia nikawaona wakijigawa katika makundi mawili yenye watu watatu na kila kundi moja likawa likiongozwa na mbwa mmoja. Kundi moja likashika uelekeo wa upande wa kushoto wa lile jengo la hoteli na kundi jingine likashika uelekeo wa upande wa kulia wakija kwenye ile kona ya lile jengo nilipokuwa nimejibanza.

     Nikiwa nimeanza kuhisi hatari ambayo ingenikabili sikutaka kuendelea kusubiri zaidi eneo lile kwani kwa namna moja au nyingine sikuona tena kama kungekuwa na uwezekano wa kuondoka pale kwa kutumia lile gari langu. Hivyo taratibu nikayaacha yale maficho yangu na kuanza kuondoka eneo lile nikirudi kule nyuma ya lile jengo nilipotoka huku nikiwaza namna ya kulitoroka eneo lile kabla wale watu hatari hawajanifikia.

     Mvua kubwa ilikuwa ikiendelea kunyesha na nilitambua kuwa hali ile ingeweza kuathiri uwezo wa wale mbwa kunusa ardhini. Hata hivyo niliamini kuwa pale ambapo wale mbwa wangeniona isingewachukua muda mfupi kabla ya kunifikia na hiyo ingekuwa hatari zaidi kwangu.

     Nilikumbuka kuwa nyuma ya lile jengo la hoteli kulikuwa na msitu mkubwa wa miti ya kupandwa hata hivyo kulikuwa na kipande kirefu cha uwanda kabla ya kuufikia ule msitu ambao hata hivyo nilikuwa mgeni kabisa wa mazingira yale. Nafsi yangu ikanitanabaisha kuwa ndani ya ule ndiyo ingekuwa sehemu salama ya kukimbilia katika kuisalimisha roho yangu. Hivyo mara tu baada ya kufika nyuma ya ile hoteli nikachepuka nikiliacha lile jengo kwa tahadhari na kuanza kukimbia kuelekea kwenye ule msitu. Hata hivyo kabla sijafika mbali na eneo lile mara ghafla umeme wa lile jengo la hoteli ukarudi na hivyo kupelekea taa za nyuma ya lile jengo kuwaka na kuangaza kila mahali. Kwa kweli nililaani vibaya kitendo kile cha umeme kurudi mapema kabla sijatimiza azima yangu. Nilipogeuka kutazama upande wa kushoto wa ile hoteli nikawaona watu wawili miongoni mwa wale watu watatu waliopita upande wa kushoto wa ile hoteli. Yule mwenzao mmoja aliyekuwa na yule mbwa sikumuona na wala sikuweza kutambua kuwa alikua ameshika uelekeo upi.

     Wale watu wakawa kama waliosita ghafla baada ya kuniona eneo lile na mimi kuona vile hofu ikaniingia moyoni haraka na hivyo kushawishika kuwa nianze kutimua mbio. Hata hivyo nilijionya juu ya kuanza kutimua mbio za ghafla kwani kwa namna moja au nyingine nilihisi kuwa kwa kufanya vile ningeweza kutengeneza hakika juu ya hisia za wale watu dhidi yangu. Hivyo nikaamua kukazana nikiongeza urefu wa hatua zangu kuelekea kule msituni huku nikiwatazama wale watu kwa jicho la pembe. Hata hivyo baada ya kutafakari nikagundua kuwa ile ilikuwa hila dhaifu sana ya kuweza kuwahadaa watu wale kwani kitendo cha wale watu kuniona nikiharakisha kutembea kikawapelekea na wao waanze taratibu kutimua mbio wakinifuata. Kuona vile nikazidi kuchanganya miguu nikikimbia kistaarabu hata hivyo wale watu hawakuniacha kwani haraka nikawaona wakiaongeza mbio na kukatisha chini ya miti ya kivuli ya eneo lile kunifuata.

     Hatimaye sikuona tena sababu ya kuendelea kupoteza muda kwa kujifanya kuwa watu wale hawakuwa na hamsini na mimi hivyo nikakusanya nguvu na kuanza kutimua mbio za uhakika nikikatisha kwenye ule uwanda kuelekea kule msituni huku nikiwa nimechukua tahadhari za kila namna. Nilipogeuka nyuma kutazama nikawaona wale watu nao wakitimua mbio...

    ...Kunifukuza huku mmoja akipuliza filimbi kuwashtua wenzake. Mwendo wangu haukuwa wa kubabaisha huku moyoni nikiamini kuwa ile ndiyo ingekuwa nafasi yangu nzuri ya kuwatoroka wale watu. Hata hivyo kabla ya kufika mbali mara nikaanza kusikia risasi zikifyatuliwa nyuma yangu. Hofu ikaanza kuniingia hata hivyo sikupunguza mwendo kwani niliamini kuwa kwa kadiri nilivyokuwa nikitimua mbio kupotelea kule mbele gizani ndivyo ambavyo nilivyokuwa nikiwapotezea malengo ya shabaha ya wale watu nyuma yangu. Hata hivyo wale watu hawakuniacha badala yake wakaendelea kunifukuza huku wakiendelea kunifyatulia risasi. Nilipoona ile mvua ya risasi inazidi kuninyea nikachomoa bastola yangu kutoka kwenye mfuko wa koti langu na kugeuka nyuma nikijibu mashambulizi lakini wakati ule sote tulikuwa gizani hivyo utupaji wangu wa risasi ulikuwa ni kama wa kubahatisha.

     Hata hivyo kwa kufanya vile nikafanikiwa kumtungua mmoja miongoni mwa wale watu wawili kwani ghafla nilikuwa nimesikia sauti ya mtu akipiga yowe gizani nyuma yangu huku kukifuatiwa na kukoma kwa yale mashambulizi ya risasi nyuma yangu. Hata hivyo sikupunguza mwendo badala yake nikazidi kukata upepo kwa kasi ya mwanariadha mahiri nikielekea kwenye ule msitu mbele yangu. Wakati nikiendelea kutimua mbio nikawa nikijitahidi kutazama mbele yangu katika namna ya kutathmini vizuri mandhari ya ule msitu kwa usalama wa roho yangu.

     Kwa kufanya vile kiasi cha umbali wa mita zisizopungua hamsini mbele yangu nikagundua kuwa kulikuwa na uzio mrefu wa seng’enge uliotenganisha eneo la ile hoteli na ule msitu mkubwa wa kupandwa. Nikaanza kupatwa na mashaka juu ya kufanikiwa kuuvuka ule uzio wa seng’enge salama kabla ya wale watu waliokuwa wakinifukuza nyuma yangu hawajanifikia. Nikiwa katikati ya fikra zile mara nikashangaa nikipigwa kumbo la nguvu lililonitupa kando bila jitihada zozote za kujihami na nilipotua chini nikajikuta tayari nipo chini ya kifua shupavu cha mbwa mkubwa mwenye uchu na windo lake. Nikajitahidi kufurukuta pasipo mafanikio kwani ile bastola yangu ilikuwa imeangukia mbali kidogo na eneo lile na ukubwa wa mbwa yule na nguvu zake hazikunipa ruhusa ya kufurukuta. Yule mbwa akawa akipenyeza kichwa chake ili aniume shingoni. Kwa kushtukia hila ya yule mbwa nikawahi kumzuia kwa mkono wangu wa mmoja na lile likawa kosa kubwa kwani yule mbwa haraka akaudaka mkono wangu kama adakavyo mfupa. Meno yake makali yakapenya na kuikamata vyema mifupa ya mkono wangu na tukio lile likasababisha maumivu makali yasambae mwilini mwangu.

     Niliendelea kufurukuta pale chini pasipo mafanikio na hali ile ikazidi kunitia hofu kwani niliamini kadiri nilivyokuwa nikiendelea kukaa chini ya himaya ya yule mbwa ndivyo wale watu kule nyuma yangu walivyokuwa wakikaribia kunifikia.

     Baada ya kufurukuta kwa kitambo hatimaye nikafanikiwa kuunasua mkono wangu kutoka kinywani kwa yule mbwa. Hata hivyo ni kama niliyekuwa nimefanya kazi bure kwani safari hii yule mbwa haraka aliuachia mkono wangu na kuniuma begani huku akiunguruma kwa hasira na kujaribu kunikwaruza kwa kucha zake kifuani mwangu.

     Hofu ikiwa imeanza kuniingia sikutaka kuendelea kudhibitiwa tena na mnyama yule aliyezidiwa akili nyingi na binadamu. Hivyo haraka nikaingiza mkono mfukoni na kuchukua kisu mkunjo kisha nikamchapa yule mbwa kwa pigo moja madhubuti lililolichana vibaya tumbo lake na kupelekea utumbo wake kuchungulia nje. Hata hivyo yule mbwa hakuniachia na badala yake ni kama niliyekuwa nimempandisha hasira yule mbwa kwani kwa nguvu zake zote akajitahidi kuninyofoa begani na hapo maumivu makali yakasambaa mwilini. Nilipoona kuwa yule mbwa haelekei kuniachia nikamchapa mapigo mengine matatu ya kisu kwenye koo lake nikiazimia kumtia adabu. Safari hii yule mbwa hakufurukuta tena badala yake akasimama kimya akinitazama kama anayejiandaa kuimba wimbo wa taifa lake na hapo nikajua kuwa mapigo yangu yalikuwa yamemuingia vizuri. Yule mbwa hakuwa na ujanja tena hivyo bila kupoteza muda nikamsukuma kwa miguu yangu akiangukia kando kama mzigo na kuanza kulia kwa sauti ya huruma.

     Haraka nikajiviringisha kando na kuikota bastola yangu kisha nikasimama na kuendelea kutimua mbio nikielekea kwenye zile seng’enge. Nilipozifikia zile seng’enge nikaanza kuziparamia kwa fujo. Zile seng’enge zikanichana vibaya mikononi kiasi cha kunisababishia majeraha mabaya yanayovuja damu hata hivyo sikuzembea kwani niliamini kuwa ile ndiyo ingekuwa salama yangu.

     Nilipokuwa nikikaribia kufika juu ya ule uzio wa seng’enge mbwa mwingine akawa tayari amenifika na kunirukia akiuma kiatu changu mguuni. Nikajitahidi kujinasua bila mafanikio na nilipoona muda unaenda nikageuka na kumchapa yule mbwa risasi moja ya kichwa iliyomtupa chini na kutulia kimya na hapo nikapandisha mguu wangu na kuangukia upande wa pili wa ule uzio. Pasipo kusubiri nikasimama tena na kuanza kutimua mbio nikipotelea kwenye ule msitu mzito wa kupandwa wenye giza la kuzimu. Sikufika mbali mara nikaanza kusikia mvua ya risasi ikinisindikiza nyuma yangu hata hivyo sikugeuka nyuma badala yake nikaendelea kutimua mbio na baada ya muda mfupi nikawa nimetokomea kabisa ndani ya ule msitu.

     Sasa nilikuwa nimetomea ndani ya ule msitu na hisia zangu zikanitanabaisha kuwa nilikuwa nimeingia kwenye ulimwengu mwingine. Japokuwa nilikuwa nimetoka kukiepuka kifo cha mateso makali nyuma yangu lakini mazingira ya msitu ule yalikuwa yamenisababishia aina nyingine ya hofu nisiyokuwa na hakika nayo. Ingawa miti ya ule msitu ilikuwa imepandwa kitaalam na katika mistari minyoofu lakini giza la mle msituni lililohanikizwa na kelele za bundi liliniletea hisia mbaya. Hata hivyo sikupunguza mwendo wala kurudi nyuma badala yake nikaikamata vyema bastola yangu mkononi na kuendelea kutimua mbio nikizidi kutokomea ndani zaidi ya ule msitu.

     Mvua ilikuwa ikiendelea kunyesha na manyunyu yale yalirudisha nguvu mpya mwilini mwangu. Yale majeraha ya begani na mkononi yalikuwa yakiendelea kuvuja damu huku maumivu makali yakiendelea kusambaa mwilini. Hata hivyo sikuwa na namna kwani kwa namna nyingine ilikuwa ni afadhali kukabiliana na maumivu yale kuliko kifo kilichokuwa kikinifukuza nyuma yangu.

     Baada ya mwendo mrefu wa kutimua mbio hatimaye nikawa nimefika kwenye eneo la ndani zaidi la msitu ule lililonipelekea nianze kuingiwa na hisia mbaya. Nywele zikanicheza, damu ikanichemka mwilini huku mapigo ya moyo wangu yakienda mbio isivyo kawaida. Utulivu ukiwa mbioni kutoweka kabisa moyoni mwangu hatimaye nikaingiza mkono kwenye mfuko wa koti langu na kuchukua kurunzi yangu ndogo ya kijasusi kisha haraka nikaiwasha na kuanza kumulika eneo lile. Nilichokiona kikanishtua sana kama siyo kuniogopesha.

     Kulikuwa na kundi kubwa la fisi waliokuwa wakigombea minofu ya maiti za watu wafu. Fisi wale wakashtuka baada ya kuuona mwanga wa kurunzi yangu mkononi. Baadhi ya wale fisi wakaingiwa na mashaka hata hivyo wengine walionekana kunipuuza na kuendelea kujipatia kitoweo kile cha aibu na fedheha kwa binadamu. Kuona vile nikaanza kuokota mawe na kuanza kuwarushia wale fisi kwa hasira hata hivyo walionitii walikuwa wachache huku wengi wao wakiacha ile mizoga ya wafu na kuanza kujikusanya taratibu wakinisogelea na kunizunguka. Kuona vile nikaamua kuitumia bastola yangu mkononi kujihami na kwa kuwa bastola yangu ilikuwa na kiwambo maalum cha kuzuia sauti kazi ikawa rahisi tu. Risasi zangu zikawaangusha fisi watatu eneo lile huku wakibweka ovyo na kuwapelekea wale fisi wengine waanze kuniogopa wakigeuka nyuma na kuanza kutimua mbio wakitokomea mbali na eneo lile. Kitendo cha wale fisi kukimbia mbali na eneo lile kikanipelekea nipate nafasi nzuri ya kuanza kulipeleleza kwa makini eneo lile.

     Baada ya kumulika eneo lile kwa muda mrefu nikitumia kurunzi yangu mkononi hatimaye nikagundua kuwa kulikuwa na miili ya watu sita iliyoharibika vibaya huku ikiwa imevuliwa nguo na kufungwa kwenye miti mikubwa iliyokuwa eneo lile. Niliposogea karibu na kuichunguza ile miili nikagundua kuwa wale watu walikuwa wameuawa kwa kufyatuliwa risasi kifuani na tumboni mwao. Nilipoendelea kuchunguza nikagundua kuwa kati ya wale watu wanawake walikuwa wawili na wanaume walikuwa sita kwa idadi yao na kwa makadirio ya umri wao watu wale walionekana ni wenye umri wa kati ya miaka thelathini na tano hadi sitini.

     Uchunguzi wangu ukanitanabaisha kuwa wale watu walikuwa wamepitia mateso makali kutokana na hali mbaya ya miili yao kabla ya kuuawa kinyama. Watu wale walikuwa wamefungwa sehemu tatu kwenye miili yao kwa kamba ngumu zilizokazwa huku kila moja akiwa amefungwa kwenye mti wake. Walikuwa wamefungwa miguuni, kiunoni na shingoni huku macho na ndimi zao zimewatoka kiasi cha kuogopesha kurudia kuwatazama mara mbili. Miili ya watu wale ilikuwa imevimba sana na kuanza kuharibika ikitoa harufu mbaya na sikuona dalili zozote za uhai kwa watu wale. Kwa kweli nilijikuta nikishikwa na hasira dhidi ya unyama ule usiyomithirika. Ingawa sikuweza kufahamu kuwa watu wale walikuwa wametenda kosa gani hata hivyo sikuona kama ule ungekuwa ni ujira waliostahili kupewa. Machozi yakanitoka na hapo nikafumba macho kuyazuia yasidondoke ardhini.

     Niliendelea kusimama eneo lile kwa tahadhari huku nikijiuliza ni kosa gani walilolifanya wale watu hadi wastahili kufanyiwa unyama ule wa kishenzi. Wakati nikiendelea kuwachunguza wale watu nikajikuta nikivutiwa zaidi na maiti ya mwanaume mmoja mwenye umri kati ya miaka arobaini na tano hadi hamsini. Mwanaume yule alikuwa amefungwa kwenye mti wa mwisho uliokuwa upande wa kushoto huku macho yamemtoka akitazama katika uelekeo tofauti kabisa na wenzake. Kupitia macho ya yule mtu nikawa nimehisi jambo fulani lisilo la kawaida na hapo nikajikuta nikishawishika kuanza kufuata uelekeo wa macho ya yule mtu kule yalipokuwa yakitazama.

     Baada ya kutembea umbali wa takribani mita zisizopungua ishirini nikaliona shimo moja jembamba lililokuwa kando ya kichuguu kidogo. Nilipomulika kwa kurunzi yangu kutazama ndani ya lile shimo nikaona kuwa lilikuwa limejaa maji kufuatia mvua kubwa ya masika iliyokuwa ikiendelea kunyesha. Nilipoendelea kuchunguza kwenye maji ya lile shimo nikaziona nguo zikielea. Nilipoendelea kuzichunguza zile nguo nikagundua kuwa zilikuwa ni mchanganyiko wa nguo za kike na za kiume tukio lililonipelekea moja kwa moja niamini kuwa zile nguo zingekuwa ni za wale watu waliouawa kinyama na kufungwa kwenye ile miti ya ule msitu. Hisia zangu zikanipelekea nihisi kuwa kulikuwa na jambo nililokuwa nikipaswa kulifahamu zaidi juu tukio lile lisiloeleweka. Hivyo nikasogea karibu na lile shimo na kuziopoa zile nguo kwa kijiti kidogo nilichokiokota kando ya dimbwi lile. Mvua bado ilikuwa ikiendelea kunyesha na giza zito lilikuwa limetanda kwenye ule msitu na hivyo kuupelekea ule msitu uzidi kutisha.

     Nafsi yangu ikanisukuma nianze kujihisi kuwa ni kama niliyekuwa nikipoteza muda wangu bure kwa kujishughulisha na mambo yasiyonihusu. Hata hivyo kwa kuwa sikuwa na jambo lingine zito lililokuwa likinisubiri mbele yangu kwa usiku ule sikuona kama nilikuwa nikipoteza muda wangu bure. Hivyo baada ya kuziopoa zile nguo na kuziweka kando ya lile shimo nikaanza kuzipekua taratibu. Idadi ya zile nguo na jinsia ilikuwa imeendana na ile idadi ya wale watu waliokuwa wameuawa na kufungwa kwenye ile miti pale msituni hivyo sikuwa na shaka yoyote kuwa zile nguo zilikuwa ni za wale watu.

     Nikiwa nimeanza kuhisi jambo fulani lisilo la kawaida haraka nikaanza kuzipekua zile nguo huku mara kwa mara nikigeuka na kuyatembeza macho yangu eneo lile katika namna ya kujihakikishia usalama wangu. Hatimaye nikawa nimemaliza kuzifanyia upekuzi zile nguo ambapo nilipata funguo tatu za magari tofauti na funguo moja ambayo sikuweza kuifahamu haraka kuwa ilikuwa ni funguo ya kufungulia kitu gani pamoja na kitambulisho kimoja cha mfanyakazi chenye utambulisho wa jina la Jean Aristide Wamba. Kitambulisho kile chenye jina la Jean Aristide Wamba kilikuwa kimemtambulisha mhusika yule kama meneja mkuu wa Banque de la République du Burundi iliyopo Avenue Des Non Aligens jijini Bujumbura. Chini ya kitambulisho kile nikaziona taarifa nyingine muhimu kama sanduku la posta, barua pepe, nukushi na namba za simu ya ofisini. Nikaendelea kukichunguza vizuri kile kitambulisho huku nikishindwa kuelewa nini kilichokuwa kikiendelea eneo lile. Zile kelele za wale fisi zikaanza kusikika tena wakiikaribia ile mizoga ya wale watu waliofungwa kwenye ile miti baada ya kuona hakuna mwendelezo wa upinzani. Kwa kweli nilijikuta nikishikwa na hasira hata hivyo sikuwa na namna ya kufanya kwani nilifahamu fika kuwa ingekuwa ni kazi ngumu kupambana na wale fisi wasiendelee kuitafuna ile mizoga ya wale wafu.

     Huzini ikaniingia na kunipelekea nifumbe macho yangu na kumeza funda kubwa la mate kuitowesha hasira iliyokuwa ikifurukuta vibaya moyoni mwangu dhidi ya unyama ule wa aibu kufanyiwa binadamu. Hatimaye nikaichukua ile funguo moja isiyoeleweka na kile kitambulisho cha kazi na kuvitia ndani ya mfuko wa koti langu. Lakini wakati nikiwa katikati ya harakati zile kwa mbali mara nikaanza kusikia kelele za vishindo hafifu vya watu fulani wakija upande ule. Nilipogeuka nyuma na kutazama nikaona miale ya kurunzi nne ikimulika kuja eneo lile. Sikuwa na mashaka yoyote kuwa watu wale wangekuwa ni wale niliyokuwa nimewatoroka kule Le Tulip Hôtel Africaine muda mfupi uliopita. Hivyo sikutaka tena wale watu wanikute pale badala yake kwa tahadhari ya hali ya juu nikaanza kuondoka eneo lile na kushika uelekeo wa upande wa mashariki wa ule msitu. Nilipofika mbele nikachanganya miguu na kuanza kutimua mbio nikiwakimbia wale watu nyuma yangu.

     Mvua kubwa ilikuwa ikiendelea kunyesha na kufuatia giza nene lililotanda angani ule msitu ulikuwa ukitisha mno. Hata hivyo hatari ya wanyama wakali ambao wangekuwa kwenye msitu ule kwangu ilikuwa ni afadhali zaidi kuliko kukabiliana na wale watu hatari waliokuwa nyuma yangu.

     Sikukumbuka kutazama saa yangu ya mkononi hata hivyo nilihisi kuwa nilikuwa nimetumia muda usiopungua nusu saa kabla ya kukutana na mteremko mkali ndani ya ule msitu wenye majabali makubwa katika mikingamo yake. Nilipofika eneo lile nikapunguza mwendo na kuanza kushuka taratibu na kwa tahadhari huku bastola yangu ikiwa mkononi tayari kukabiliana na hatari yoyote ambayo ingejitokeza mbele yangu.

     Hata hivyo wakati nikiendelea kushuka ule mteremko nikahisi kuwa kutoka pale sikuwa mbali sana na barabara kwani mara moja au mbili niliweza kusikia kelele za muungurumo wa injini ya gari zikivuma eneo lile ingawa sikuweza kufahamu barabara ile ya magari ingekuwa upande gani kutoka pale nilipokuwa. Niliendelea kushuka ule mteremko na baada ya mwendo mfupi nikaanza kuona sehemu ya wazi iliyojitenga na ule msitu mbele yangu iliyosongwa na vichaka...

    ...vya miti hafifu na nyasi ndefu. Nilipofika kwenye lile eneo nikaanza kukatisha katikati ya vichaka vile na kadiri nilivyokuwa nikiendelea mbele na safari yangu ndivyo zile kelele za muungurumo wa injini ya gari ulivyokuwa ukizidi kusikika. Hatimaye nikawa nimetokezea sehemu ya wazi kabisa na mbele yangu nikaiona barabara ya lami. Huwenda magari machache yalikuwa yametangulia kukatisha eneo lile kwani kwa mbali nilisikia makelele ya injini ya gari yakiyoyoma kabla ya kukoma na hivyo eneo lile kugubikwa na ukimya.

     Sikutaka kuendelea kupoteza muda eneo lile kwani nilikumbuka kuwa nyuma yangu kulikuwa na wale watu waliokuwa wakinifuatilia. Hivyo nikaanza kutembea kwa tahadhari kandokando ya barabara ile nikishika uelekeo wa upande wa kushoto baada ya kuhisi kuwa ule ndiyo ungekuwa uelekeo sahihi wa kuelekea mjini.

     Wakati nikiendelea kutembea nikaanza kuhisi kuwa angalau nilikuwa kwenye mazingira salama kidogo ukifananisha na kule nilipotoka ingawa bado sikuacha kuchukua tahadhari huku mara kwa mara nikigeuka na kutazama nyuma. Wakati nikiendelea kutembea mawazo mengi yakawa yakipita kichwani mwangu. Matukio yote yaliyojiri tangu nifike jijini Bujumbura yalikuwa yameniacha hoi sana kifikra na sasa mawazo yangu yalikuwa yamejikita katika kile chumba namba 403 cha ghorofa ya sita ya Le Tulip Hôtel Africaine aliponyongwa yule Padri wa kizungu. Hadi sasa sikuweza kufahamu ni sababu gani iliyokuwa imempelekea kiongozi yule wa kiroho kunyongwa kinyama namna ile.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Nilikumbuka maneno ya mwisho ya Sundi Masele mfanyakazi wa nyumbani kwa Bolozi Adam Mwambapa wakati aliponieleza kuwa nimtafute Padri Aloysius Kanyameza kuwa ni yeye ndiye angeweza kunipa taarifa nilizozihitaji. Kwa kweli sikuweza kufahamu ni wapi ambapo ningempata huyo Padri Aloysius Kanyameza kwa pale jijini Bujumbura lakini kitendo cha kumuona Padri yule kiongozi wa kiroho akiwa amenyongwa vibaya katika kile chumba kilichosemekana kukodiwa na mtu aliyesemekana kuitwa Pierre Okongo kilikuwa kimeniacha njia panda. Nikaendelea kutafakari huku nikihisi kuwa huwenda yule mtu aliyenyongwa kwenye kile chumba ndiye angekuwa huyo Padri Aloysius Kanyameza. Hata hivyo nilikuwa nimesita katika kuamini hivyo kwani jina la Kanyameza lilikuwa limenitatiza kidogo kwa kuwa lilikuwa ni jina la asili la watu wa Burundi ambao ni waafrika weusi kama mimi na yule alikuwa ni Padri wa kizungu kwa muonekano wake. Kwa kweli fikra zangu bado zilikuwa njia panda ingawa kwa namna moja au nyingine nilijiridhisha katika kuamini kuwa kama Pierre Okongo ndiye aliyekuwa amehusika na kifo cha yule Padri kwenye kile chumba namba 403 cha Le Tulip Hôteli Africaine basi kwa namna moja au nyingine alikuwa na mahusiano ya moja kwa moja na wale watu walikuwa wakiniwinda. Pierre Okongo ni nani na anahusika vipi kwenye huu mkasa?. Nikaendelea kujiuliza pasipo kupata majibu hata hivyo niliamini kuwa ukweli ungekuja kufahamika muda mfupi mbele ya safari.

     Nikiwa naendelea kutembea kandokando ya ile barabara mawazo yangu yakajikuta yakihamia kwenye ule msitu niliotoka muda mfupi uliopita. Mara hii nikajikuta nikiwakumbuka wale watu waliouawa kinyama kwa kupigwa risasi huku wakiwa wamefungwa kwa kamba kwenye ile miti ya ule msitu. Kwa kweli niliuona ni kama ulikuwa mkasa uliokuwa ukujitegemea huku nikishindwa kabisa kufahamu kilichokuwa kikiendelea. Nilipoendelea kiwaza hisia fulani zikaanza kujengeka kichwani mwangu juu ya mauaji yale. Kupitia kile kitambulisho cha kazi nilichokikuta mfukoni kwenye zile nguo za wale watu waliouawa kule msituni ambazo nilikuwa nimeziopoa kwenye lile dimbwi la maji nilikuwa nimeamini kuwa miongoni mwa wale watu wafu alikuwepo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Jean Aristide Wamba ambaye kama kitambulisho kile kilivyoeleza mtu yule alikuwa ni meneja mkuu wa Banque de la République du Burundi.

     Kama zile taarifa kwenye kile kitambulisho zilivyokuwa zikieleza binafsi niliamini kuwa meneja mkuu wa benki ya taifa kama ile alikuwa ni mtu muhimu sana katika suala zima la uchumi wa nchi. Hivyo kwa namna moja au nyingine wadhifa mkubwa wa mtu yule nisiyemfahamu nikaanza kuuhusisha na sababu ya kifo chake au vifo vya wale watu na suala la kimaslahi ingawa bado sikuweza kufahamu kuwa maslahi hayo yangekuwa katika mtazamo upi. Hatimaye mawazo yangu yakahamia kwa msichana mrembo mfanyakazi wa Havana Club aitwaye Veronica. Nilikuwa nimemuahidi Veronica kuwa ningemtembelea nyumbani kwake usiku ule mara baada ya kutoka kazini saa mbili usiku lakini sasa ilikuwa ikielekea kutimia saa nane usiku kwa mujibu wa majira ya saa yangu ya mkononi. Nikaendelea kuwaza kuwa huwenda ungekuwa usumbufu mkubwa kwenda kumgongea Veronica nyumbani kwake usiku ule hata hivyo nikapiga moyo konde na kujipa matumaini kuwa baada ya kufunguliwa mlango kwa kila hali ningejitahidi kumuelewesha kwa kila hali huku nikimpa sababu za uongo zilizonipelekea kuchelewa kufika kwenye miadi kwani vinginevyo sikuwa na sehemu nyingine ya kulaza mbavu zangu kwa usiku ule.

     Wakati nikiendelea na safari yangu mara nikasikia muungurumo wa gari likija na nilipogeuka nyuma yangu kutazama nikauona mwanga hafifu wa taa za mbele za gari ukichomoza. Haraka nikawahi kuchepuka na kujibanza kichakani kando ya ile barabara. Muda mfupi uliofuata mara nikaliona gari ndogo aina ya Land Rover likikatisha eneo lile na nilipochunguza kwa makini nikawaona wanaume watatu ndani ya lile gari. Nikashawishika kutaka kujitokeza na kuomba lifti hata hivyo nafsi yangu ikawahi kunionya haraka juu ya kufanya vile pale nilipofikiria juu ya hatari ambayo ingenifika endapo wale watu kwenye lile gari wangekuwa ni miongoni mwa wale wanajeshi waliokuwa wakinisaka. Hivyo nikaendelea kujibanza kwenye kile kichaka nikiliacha lile gari linipite na kutokomea mbele ya safari.

     Muda mfupi baada ya lile gari kutokomea nikatoka kwenye kile kichaka na kurudi barabarani nikiendelea mbele na safari yangu.

     Mvua bado ilikuwa ikiendelea kunyesha na ingawa nilikuwa sifahamu jiografia ya makazi ya jiji la Bujumbura lakini nilianza kuona athari ya mafuriko makubwa kuelekea kutokea endapo mvua ile ingeendelea kunyesha zaidi. Mara kwa mara nikaendelea kutembea kandokando ya ile barabara huku nikigeuka nyuma kutazama kama ningewaona wale watu waliokuwa wakinifuatilia kule msituni. Bado sikuwaona wale watu na sikuweza kufahamu kuwa walikuwa wamekwamia wapi hata hivyo niliendelea kujipa tahadhari.

     Baada ya safari ndefu ya kutembea kwa miguu mara nikakutana mteremko mkali na chini ya ule mteremko kulikuwa na daraja kubwa. Nilipovuka lile daraja nikaanza kupanda mlima. Ilikuwa ni kabla sijamaliza kuupanda ule mlima mara nikasikia tena muungurumo wa gari nyuma yangu na nilipogeuka kutazama nikauona mwanga wa taa kali za mbele za gari lililokuwa likija nyuma yangu. Uzoefu wangu wa magari ukanitanabaisha kuwa lile lilikuwa ni gari kubwa. Tumaini jipya likafufuka moyoni mwangu hivyo haraka nikachepuka tena na kujificha kwenye kichaka kilichokuwa kando ya ile barabara. Haukupita muda mrefu mara nikaliona lile gari likishuka ule mteremko kwa kasi na lilipopita tu pale darajani likaanza taratibu kupanda mlima hali iliyonipelekea nihisi kuwa lilikuwa limebeba mzigo mzito. Kadri lile gari lilivyokuwa likikaribia usawa wa kile kichaka nilichokuwa nimejibanza kando ya ile barabara ndiyo nilivyofanikiwa kuliona vizuri lile gari. Lilikuwa ni lori kubwa la mizigo aina ya Fuso.

     Nafsi yangu ikaniambia kuwa ule ungekuwa wakati muafaka katika kupiga hatua nyingine zaidi katika harakati zangu. Hivyo wakati lile lori likikatisha eneo lile na kuanza kupanda ule mlima haraka nikatoka kwenye kile kichaka kando ya barabara na kuanza kulikimbilia lile lori la mizigo kwa nyuma. Kwa kuwa lile lori lilikuwa likipanda mlima taratibu hivyo ndani ya muda mfupi tu nikawa tayari nimelifikia na nilipochunguza ile sehemu ya nyuma ya lile lori haraka nikagundua kuwa ilikuwa imefunikwa kwa turubai kubwa ili kuukinga mzigo uliokuwa mle ndani usilowane na ile mvua iliyokuwa ikiendelea kunyesha.

     Nikaendelea kulikimbilia lile lori huku mara kwa mara nikigeuka nyuma na kutazama kama kungekuwa na mtu yeyote nyuma yangu. Sikumuona mtu yeyote hivyo hali bado ilikuwa shwari. Nilipolifikia lile lori kwa nyuma nikadandia na kuanza kupanda juu ambapo nililifungua lile turubai na kulisogeza kando kiasi cha kuniwezesha kuufungua ule mlango wa nyuma wa lile lori. Muda mfupi uliofuata nikawa nimefanikiwa kuingia mle ndani huku nikiwa tayari nimechukua tahadhari za kila namna za kujihami endepo mle ndani ningewakuta watu. Hata hivyo kwa kuwa kule nyuma kulikuwa kumefungwa na kufunikwa na lile turubai hivyo matumaini ya kuwakuta watu mle ndani yalikuwa hafifu sana. Mara tu nilipoingia mle ndani haraka nikachukua kurunzi yangu kutoka mfukoni na kuiwasha nikiangaza angaza mle ndani.

     Lile lori lilikuwa limebeba magunia ya vitunguu na bila shaka lilikuwa likielekea jijini Bujumbura kwenye maeneo ya masoko na hali ile ikanipa matumaini ya kufika mjini pasipo usumbufu wowote. Lile lori likaendelea kupanda ule mlima kwa mwendo wa taratibu huku injini yake ikilalamika vibaya kila gia moja ilipokuwa ikipanguliwa na gia nyingine kuingizwa kutokana na ule mzigo mzito lililoubeba. Hata hivyo baada ya safari ndefu hatimaye lile lori likamaliza kupanda ule mlima na hapo mwendo kasi ukaongezeka tena.

     Mvua bado ilikuwa ikiendelea kunyesha huku mara kwa mara nikisogeza lile turubai na chungulia kule nyuma barabarani kutazama kama kungekuwa na gari lolote likilifungia mkia lile lori. Bado hali ilikuwa shwari kwani magari machache yaliyojitokeza na kulifuata lile lori kwa nyuma yalilikaribia na hatimaye kulipita yakiendelea mbele na safari zao. Bado lile lori liliendelea kuchanja mbuga likiendelea na safari na kwa vile kule mbele miinuko ilikuwa imepungua hivyo mwendo wa lile lori nao ulikuwa umeongezeka.

     Moyoni niliendelea kuomba kuwa tusikutane na kizuizi cha barabarani mbele ya safari. Wakati safari ikiendelea mawazo mengi yakawa yakipita kichwani mwangu huku nikijaribu kuunganisha mlolongo wa matukio yote yaliyojiri tangu nilipoanza safari yangu ya kijasusi jijini Dar es Salaam nchini Tanzania. Mawazo yangu hatimaye yakahamia kwa Veronica huku nikijiuliza kama muda ule angekuwa tayari kunifungulia mlango wa nyumba yake na kunipokea kwa furaha kama wakati tulivyoachana kwenye ule mgahawa Havana Club asubuhi ile. Uzoefu wangu ulinieleza kuwa wanawake ni viumbe wanaoweza kubadilika ghafla kutegemea na nyakati na hisia zao hivyo upo uwezekano kuwa mara ya kwanza unapo onana na mwanamke akakuchangamkia na kukufurahia lakini muda mfupi baadaye mkipoteana na kuonana tena akakupuuza haraka na kukuchukia vibaya bila sababu za msingi. Moyoni niliomba sana kuwa Veronica asiwe miongoni mwa wanawake wenye hulka hiyo.

     Safari ikiwa inaendelea nikaanza kuvuta picha namna nitakavyopokelewa na Veronica kwa bashasha zote kisha kuvuliwa nguo zangu na kutayarishiwa maji ya moto ya kuoga na baadaye kuandaliwa chakula kitamu cha kirundi kilichopikwa kwa ufundi wa hali ya juu na kutiwa vikorombwezo vyote vya mapishi. Kufika pale nikajikuta nikiomba tena kimoyomoyo kuwa sebuleni kwa Veronica kusiwe na makochi ili baaada ya kuoga na kupata mlo mzuri moja kwa moja anifungulie chumba chake na kunikaribisha kitandani kwake. Picha ya kufikirika iliyofuata baada ya pale ikaniacha nikitabasamu peke yangu katikati ya giza nene lililokuwa kule nyuma ndani ya lile lori la mizigo.

     Ghafla nikiwa katikati ya mawazo yale mara nikahisi dereva wa lile lori alikuwa akijitahidi kupangua gia na kupunguza mwendo wa lile lori. Mawazo yangu yakahama, moyo wangu ukapoteza utulivu huku baridi nyepesi ikipenya kifuani mwangu. Haraka nikasogea na kusogeza lile turubai pembeni nikichungulia kwa tahadhari kule nyuma barabarani. Loh! koo langu likakauka ghafla baada ya kuliona lile gari la jeshi Nissan Patrol nililoliona likiingia na kuegesha kule mbele ya Le Tulip Hôtel Africaine likiwa umbali wa hatua chache nyuma ya lile lori. Dereva wa lile gari Nissan Patrol alikuwa amewasha taa za hadhari katika namna ya kumuashiria yule dereva wa lile lori asimame haraka.

     Nikiwa na hakika kuwa wale watu kwenye lile gari Nissan patrol hawakuwa wameniona nikaendelea kuchungulia kupitia uwazi mdogo uliokuwa kwenye pembe ya lile turubai la lori. Kwa kufanya vile mbele ya lile gari nikawaona wanaume wawili ambao wote niliwakumbuka haraka kuwa walikuwa miongoni mwa wale watu kumi na moja walioshuka kwenye lile gari wakati lilipowasili na kuegesha kule nje ya Le Tulip Hôtel Africaine. Sasa nilikuwa na kila hakika kuwa mlengwa wa tukio lile la kusimamishwa kwa lile lori nilikuwa mimi. Bila kusubiri zaidi akili yangu ikaanza kufanya kazi ya ziada nikifikiria namna ya kujinasua kwenye hatari ile. Kwa kweli nilikuwa nimechoshwa sana na ile tabia ya kufuatwafuatwa kila niendapo hivyo uvumilivu wangu nao ulikuwa ukingoni.

     Dereva wa lile lori akaendelea kupangua gia taratibu huku akionekana kutafuta sehemu nzuri ya maegesho kwani lile eneo la barabara lilikuwa limekaa vibaya sana kutokana na uwepo wa kona nyingi na kupakana na bonde kubwa upande wa kulia. Kitendo cha dereva wa ile Nissan Patrol kuliona lile lori likikawia kusimama kikampelekea aongeze mwendo zaidi na kulipita lile lori kwa kasi huku akiwa na lengo la kwenda kuliwekea lile lori kizuizi kwa mbele. Nafsi yangu ikaniambia kuwa ile ndiyo ingekuwa nafasi nzuri ya kuitorosha roho yangu mbali na wale watu hatari waliokuwa kwenye lile gari. Hivyo wakati lile lori likipunguza mwendo na kusimama baada ya kuwekewa kizuizi cha ghafla na ile Nissan Patrol kule mbele mimi nikaitumia nafasi ile kutoka haraka nyuma ya lile lori kisha nikajirusha chini kwa mtindo wa kininja nikijiviringisha kama gurudumu la gari na hatimaye kupotelea kwenye kichaka kilichokuwa kando ya ile barabara.

     Kabla ya kutoweka eneo lile nilitaka kwanza kupata tathmini ya hakika kuwa wale watu waliokuwa wakinifuatilia kwenye lile gari Nissan Patrol walikuwa akina nani. Hatua chache mbele kutoka pale niliporuka lile lori likapungua mwendo na kusimama umbali mfupi nyuma ya ile Nissan Patrol. Muda uleule nikawaona wanaume wanne wakishuka kutoka kwenye ile Nissan Patrol huku wakiwa na bunduki zao mikononi. Nilipowachunguza wale watu nikagundua kuwa hawakuwa watu wa kufanya mzaha hata kidogo. Mmoja wao akaielekeza bunduki yake juu na kufyatua risasi kadhaa katika namna ya kutengeneza hofu kwa wale watu waliokuwa ndani ya lile lori kule mbele. Haukupita muda mrefu mara nikawaona tena wanaume wawili kati ya wale wanaume wanne walioshuka kutoka kwenye ile Nissan Patrol wakichepuka na kulizunguka lile lori kwa nyuma na bunduki zao mikononi.

     Mara nikamsikia mwanaume mmoja kati ya wale wanaume wawili waliobakia kule mbele ya lile lori akitoa amri ya kuwataka wale watu waliokuwa kwenye lile lori washuke chini mara moja. Muda uleule nikamuona yule dereva wa lile lori akifungua mlango na kushuka chini taratibu huku akiwa ameongozana na vijana wawili wa kiume na mwanamke mmoja. Yule mtu...

    ...aliyetoa amri ya kuwataka watu wote waliokuwa kwenye lile lori washuke chini akamsogelea yule dereva na kuanza kumshushia kipigo cha nguvu huku yule mwenzake akiingia mbele ya lile lori na kufanya upekuzi. Kule nyuma ya lile lori wale wanaume wawili wenye bunduki mkononi wakausogelea ule mlango wa nyuma wa lile lori kwa tahadhari kisha mmoja akashika kamba fupi iliyokuwa ikining’inia na kukwea kule nyuma akiingia mle ndani ya lori na kuanza kufanya upekuzi. Hata hivyo kitendo cha kuukuta ule mlango wa nyuma wa lile lori ukiwa wazi kikawa kimewapa mashaka na hapo nikawaona wale watu wakijipa tahadhari na kugeuka eneo lile wakiyatembeza macho yao taratibu kulipeleleza lile eneo la vichaka vilivyokuwa kando ya ile barabara.

     Nikahisi kuwa hatari ilikuwa mbioni kunifikia kwenye kile kichaka nilichojibanza kando ya barabara hivyo taratibu nikakiacha kile kichaka na kuanza kushuka kwenye lile bonde msituni kando ya ile barabara. Nikaendelea kushuka kwenye lile bonde hadi nilipofika chini na hapo nikakutana na mto mkubwa wenye mawe mengi ambao kwa wakati ule ulikuwa mbioni kufurika kufuatia mvua za masika zilizokuwa zikiendelea kunyesha. Hisia zangu zikanitanabaisha kuwa kutoka pale nilikuwa karibu sana na kitovu cha jiji la Bujumbura hivyo nikaanza kutembea taratibu kando ya ule mto nikiufuata kule mbele unapoelekea.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Baada ya safari ya kitambo kirefu hatimaye nikafika sehemu ambapo mto ule ulikuwa ukikatisha chini ya daraja kubwa lenye barabara ya lami juu yake. Nikiwa chini ya lile daraja nikayaona magari machache madogo yakikatisha juu ya lile daraja. Sikuwa na shaka yoyote kuwa sasa nilikuwa karibu sana na eneo la mjini lenye makazi ya watu hivyo nikauacha ule mto na kupanda juu ya lile daraja nikishika uelekeo wa magharibi baada ya kuliona bango kubwa la barabarani linaloelekeza majina ya vitongoji vya jiji la Bujumbura na umbali wake kutoka pale. Kulikuwa na umbali mfupi kabla ya kufika katikati ya jiji la Bujumbura hivyo nikaendelea kutembea kwa utulivu kando ya barabara ile huku mara kwa mara nikigeuka na kutazama nyuma yangu kama kungekuwa na gari au mtu yeyote akinifuatilia. Sikumuona mtu yeyote wala gari hivyo hali bado ilikuwa shwari.

     _____

     Teksi niliyoikodi kutoka kwenye kituo cha kujazia mafuta cha Hash Petroleum nje kidogo ya jiji la Bujumbura kando ya ghala kubwa ya kuhifadhia mafuta ghafi ikanishushia hatua chache kabla ya ilipokuwa nyumba namba 37 ya shirika la nyumba la taifa la Burundi kwenye barabara ya Boulevard de I?independence nyuma ya uwanja mkubwa wa mpira wa miguu wa Prince Rwagasore Stadium. Akili yangu ilikuwa imechoka sana kutokana na pilika za kutwa nzima hivyo sikutaka kuanzisha maongezi ya aina yoyote na dereva yule badala yake nikamlipa pesa yake na kushuka.

     Ile teksi iliposhika hamsini zake na kutokomea mbali na eneo lile nikavuka barabara huku nikitazama majira kwenye saa yangu ya mkononi. Mara moja nikagundua kuwa ilikuwa ikielekea kutimia saa nane na nusu usiku. Nikaendelea kutembea taratibu huku utulivu katika mtaa ule ukinipa hadhari ya namna yake. Nilipofika mbele nikasimama kidogo kando ya ile barabara nikiyatembeza macho yangu kwa makini kuyapeleleza mandhari yale na niliporidhika na tathmini yangu nikaanza tena kutembea taratibu huku mikono wangu mmoja ukiwa ndani ya mifuko ya koti langu umeikamata bastola.

     Lile eneo lilikuwa la hifadhi ya nyumba za taifa la Burundi hivyo hata makazi yake yalikuwa yamepangwa vizuri yakitenganishwa kwa barabara nzuri za lami. Nyumba aliyokuwa akiishi Veronica ilikuwa kwenye ghorofa ya pili upande wa kushoto baada ya kuipita bustani ndogo ya maua. Uchunguzi wangu ulihitimisha vile. Muda ulikuwa umesonga sana hivyo matumaini ya kumkuta Veronica akiwa macho kwa tafsiri nyingine yalikuwa madogo sana. Hata hivyo niliona kuwa kuchelewa kwenye miadi ilikuwa ni afadhali kuliko kutokufika kabisa.

     Wakati nikiendelea kutembea kandokando ya ile barabara kumbukumbu juu ya Veronica wakati nilipoonana naye asubuhi ile ndani ya Havana Club ikaanza kujengeka taratibu kichwani mwangu. Veronica alikuwa msichana mrembo sana ambaye mwanaume yeyote angejisikia fahari kuwa naye. Umbo lake matata na sauti yake nyororo vilikuwa vimeuteka vibaya moyo wangu na kunipelekea nijihisi kuwa nimekuwa mateka wa nafsi mbele yake.

     Baada ya kitambo kifupi cha safari yangu nikachepuka upande wa kulia na kuanza kuifuata barabara ndogo ya watembea kwa miguu iliyotengenezwa kwa vitofali vidogo vilivyounganishwa kwa ustadi wa hali ya juu. Barabara ile ikikatisha katikati ya majengo marefu ya ghorofa ya shirika la nyumba la taifa huku kando yake ikipakana na bustani nzuri za maua. Nilipoingia kwenye barabara ile haraka nikajihisi mpweke kwani giza lilikuwa zito mno na mvua nayo ilikuwa ikiendelea kunyesha. Ingawa baadhi ya nyumba zilikuwa zikiwaka taa kwenye baadhi ya majengo ya ghorofa ya eneo lile lakini mwanga wa taa zile haukuwa na msaada wowote katikati ya lile giza nene.

     Nilipoupita mstari wa kwanza wa nyumba za ghorofa macho yangu yakawa makini zaidi wakati nikiukaribia mstari wa pili. Kidole changu kikiwa kimetuama vyema kwenye kilimi cha bastola ndani ya mfuko wa koti langu wala sikuwa na wasiwasi wowote. Nilipoufikia ule mstari wa pili wa nyumba za ghorofa nikachepuka na kuingia upande wa kushoto. Mara moja nikageuka nyuma kuangalia kama kungekuwa na mtu yeyote akinifuatilia. Sikumuona mtu yeyote hivyo hali bado ilikuwa shwari.

     Kulikuwa na gari moja dogo jeupe aina ya Toyota double cabin iliyokuwa imeegeshwa chini mbele ya jengo la ghorofa la kwanza. Nilipolichunguza vizuri jengo lile nikagundua kuwa taa zake zote zilikuwa zimezimwa na hivyo kuashiria kuwa wakazi wa jengo lile walikuwa tayari wamekwisha lala usiku ule.

     Nilipolifikia lile jengo la pili la ghorofa nikasimama na kulichunguza kwa utulivu na umakini wa hali ya juu. Tathmini yangu ikanitanabaisha kuwa lile jengo lilikuwa na ghorofa saba na kama lilivyokuwa lile jengo la kwanza jengo lile nalo lilikuwa limemezwa na giza zito kila mahali. Taa zote za lile jengo zilikuwa zimezimwa na hivyo kuashiria kuwa wakazi wake walikuwa wamelala. Upande wa kulia chini ya lile jengo nikaziona ngazi za kuelekea sehemu ya juu ya lile jengo.

     Kabla ya kupanda zile ngazi nikasimama nikizitazama kwa utulivu na nilipohisi kuridhishwa na hali ya usalama wa eneo lile nikaanza kupanda zile ngazi taratibu kuelekea ghorofa ya pili. Hali ilikuwa tulivu hivyo wakati nikipanda zile ngazi nikawa nikisikia sauti dhaifu ya hatua zangu kwa kadiri nilivyokuwa nikijongea. Nikaendelea kuzipanda zile ngazi kwa utulivu huku mara kwa mara nikisimama na kuyapa masikio yangu utulivu wa hali ya juu.

     Hatimaye nikamaliza kupanda zile ngazi na kujikuta nimetokezea kwenye korido ya ghorofa ya pili. Ilikuwa korido pana na ndefu sana kiasi kwamba sikuweza kuona mwisho wake. Mara tu nilipofika kwenye ile korido nikasimama tena nikiupima utulivu wa eneo lile. Bado hali ilikuwa shwari na hapakuwa na kiashiria chochote cha uwepo wa kiumbe hai eneo lile.

     Kutokana na giza zito lililokuwa limetanda kwenye ile korido sikuweza kunasa picha halisi ya mandhari yale. Hivyo taratibu nikautumbukiza mkono wangu kwenye mfuko wa koti na kuchukua kurunzi ambapo niliiwasha na kuanza kumulika kwenye ile korido. Mara moja nilipochunguza nikagundua kuwa ile korido ilikuwa ikitazamana na milango mingi iliyochorwa namba juu yake. Uchakavu wa ile milango katika baadhi ya maeneo ikawa ni ishara tosha kuwa lile jengo lilikuwa likekula chumvi nyingi pasipo kufanyiwa ukarabati wa kuridhisha. Niliyakumbuka vizuri maelezo ya Veronica asubuhi ile aliponiambia kuwa alikuwa akiishi nyumba namba 37 katika ghorofa ya pili ya jengo lile hivyo nikajipa moyo kuwa bado nilikuwa sijapotea.

     Taratibu nikaanza kutembea kwenye ile korido huku nikimulika na kuchunguza zile namba za milangoni. Baada ya kitambo kirefu kupita nikilifanya zoezi lile hatimaye nikauona mlango mmoja wenye namba 37 ukiwa katikati ya ile korido. Haraka nikazima kurunzi yangu na kuitia mfukoni kisha nikausogelea ule mlango na kuupima utulivu wa mle ndani kwa kutega sikio langu kwa karibu. Niliporidhika kuwa mambo yalikuwa shwari nikaanza kugonga taratibu pale mlangoni.

     Niligonga mara kadhaa bila ule mlango kufunguliwa na hali ile ikaanza kunitia wasiwasi kuwa huwenda nilikuwa nimekosea mlango. Hata hivyo nilipoyatupia macho yangu pale mlangoni na kuiona namba 37 juu ya ule mlango nikapata matumaini kuwa bado nilikuwa sehemu sahihi. Hivyo nikaendelea kugonga tena kwa kishindo zaidi. Hata hivyo ule mlango haukufunguliwa wala kuwepo kwa dalili zozote za uwepo wa mtu mle ndani. Taratibu hisia mbaya zikaanza kupenya nafsini mwangu na kunipelekea nianze kuhisi kuwa huwenda Veronica alikuwa amenidanganya. Kwa nini Veronica anidanganye na alikuwa na sababu gani ya kunidanganya?. Nikajiuliza pasipo kupata majibu na hali ile ikaniacha njia panda. Nilipokumbuka begi langu dogo la shanta la mgongoni nililomuachia Veronica nikaanza kujilaumu kwa kuwa mwepesi wa kumuamini mlimbwende yule kutokana na kubabaishwa vibaya na uzuri wake.

     Sasa nilikuwa njia panda katika kuamua uelekeo. Upande mmoja wa nafsi yangu ukawa unanisukuma kuwa niondoke eneo lile na kwenda kutafuta malazi katika hoteli yoyote ambayo ingekuwa jirani na eneo lile hadi hapo kutakapopambazuka huku upande mwingine wa nafsi yangu ukinisukuma kuwa niufungue ule mlango kwa hila na kuingia mle ndani huku nikiwa tayari kukabiliana na kitu chochote cha hatari ambacho kingetokea. Hata hivyo wakati nikiwa katikati ya hali ile mara ghafla nikasikia kitasa cha ule mlango kikichokolewa kwa funguo na kisha ule mlango kufunguliwa taratibu. Mwanga hafifu kutoka ndani ya kile chumba ukasababisha mshangao wa kipekee nafsini mwangu.

     Msichana mzuri Veronica alikuwa amesimamia pale mlangoni. Kwa sekunde kadhaa nikasimama pale mlangoni nikimtazama Veronica huku macho yangu yakishindwa kuamini kama kweli msichana yule mzuri alikuwa ni yeye. Alikuwa Veronica hatimaye nafsi yangu ikanitanabaisha vile. Hata hivyo hakuwa Veronica yule niliyeonana naye kule Havana Club asubuhi ile akiwa katika sare zake za kazi kwani usiku huu uzuri wake ulikuwa umeongezeka maradufu na kuzichakaza vibaya hisia zangu. Nimewahi kukutana na wasichana wengi wazuri na warembo katika pilikapilika zangu lakini niseme kuwa Veronica alikuwa zaidi yao wote. Alikuwa amevaa nguo nyepesi ya kulalia, nightdress nyeupe iliyolichora vyema umbo lake maridhawa kuwahi kutunukiwa mwanamke wa duniani na hivyo kupelekea nguo yake nyekundu ya ndani kuonekana bila kificho chochote.

     Macho yake legevu yaliyotoka kupambana na usingizi wa mang’amu ng’amu yakasimama yakinitazama kwa tuo kama mtu ambaye haamini anachokiona mbele yake. Hatimaye tabasamu jepesi likaanza kuchomoza usoni mwake na kunipelekea nijihisi kuwa sikuwa nimekosea mlango.

     Hisia zangu zikiwa taabani macho yangu chakaramu yakaanza kufanya ziara ya kushtukiza kifuani pake na hapo kupitia kivazi chake chepesi nikasiona chuchu zake laini zilivyosimama kwa utulivu juu ya milima miwili isiyofahamu adha yoyote ya volkano. Kitovu chake laini chenye kishimo kidogo kikitengeneza ziada nyingine ya uzuri wake. Macho yangu yalipofika kiunoni pake nikaiona nyonga yake laini yenye mifupa miteke iliyopakana na mzigo imara wa makalio yaliyotuama vyema kiasi cha kumpelekea aonekane kama aliyeficha vipande vya mikate mapajani. Wakati nikiwa katika hali ile ya mduwao mara Veronica akavunja ukimya baada ya kuitazama saa yake ya mkononi.

    “Gilbert…”

     “Veronica…”

     “Kwa nini umechelewa?” Veronica akaniuliza huku akijitahidi kudhibiti donge la hasira ya wivu kooni mwake. Ingawa tulikuwa tukielekea kufungua ukurasa mpya wa mapenzi na mlimbwende yule lakini hisia zangu zilinitanabaisha mapema kuwa Veronica alikuwa msichana mwenye wivu mkubwa juu yangu.

    “Naomba kwanza unikaribishe ndani mpenzi”. Nikamsihi kwa utulivu huku usoni nikiumba tabasamu jepesi la kirafiki.

    “Karibu ndani”. Veronica akanikaribisha kwa sauti dhaifu ya kinyonge huku akinipisha pale mlangoni. Bila kutia neno nikavua koti langu na kulitundika begani kisha nikaingia mle ndani na hapo Veronica akaufunga ule mlango nyuma yangu.

     Wakati Veronica akimalizia kufunga ule mlango na kugeuka mimi tayari nilikuwa nimelitupa koti langu sakafuni kisha nikamkaribia pale mlangoni na kumshika kiunoni bila ruhusa yake hata hivyo nikashukuru kuwa sikukutana na upinzani wowote. Veronica akanitazama machoni kisha tabasamu maridhawa likachomoza usoni mwake.

    “Kwanini umechelewa hivi mpenzi?”. Veronica akaniuliza kwa utulivu huku akiipitisha mikono yake nyuma ya shingo yangu na kupelekea chuchu za matiti yake kukitekenya kifua changu na kupelekea joto kali la mwili wake linifanye nijisikie faraja ya aina yake. Nilipomtazama Veronica machoni nikayaona machozi ya furaha yakianza kumtoka.

     Veronica alikuwa na kiu sana ya penzi langu na sikutaka kuamini kuwa nilikuwa mwanaume wake wa kwanza lakini niseme kuwa hisia zetu ziliendana kwa kiwango cha juu kabisa kwa wapenzi. Kwa kiganja changu taratibu nikamfuta machozi lakini huwenda tendo lile halikuwa na umuhimu wowote kwake kwani haraka aliuondoa mkono wangu machoni mwake kisha akanivuta karibu na hapo ndimi zetu zikakutana. Nilichoweza kusikia baada ya pale ilikuwa ni sauti nyepesi ya pumzi yake namna ilivyokuwa ikipenya kwa fujo kwenye matundu ya pua yake sambamba na miguno isiyoeleweka ya mahaba. Nilitaka kuleta pingamizi kwa vile nilikuwa mchafu nikinuka jasho la kutwa nzima lakini sikufanikiwa.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Kama mtu aliyepandwa na wazimu wa mapenzi Veronica akanivua kofia yangu na kuitupilia mbali kisha akapenyeza mikono yake kifuani mwangu na kuanza kunivua nguo kwa pupa. Nilipotaka kumzuia akaning’ata mkono.

    “Gilbert…”

     “Naam Veronica…”

     “Ulikuwa wapi mpenzi mbona umechelewa?”. Veronica akaniuliza kama mwehu huku akiufungua mkanda wa suruali yangu kwa pupa.

    “Naomba unisamehe mpenzi kwa kuchelewa”. Nikanong’ona.

    “Ulikuwa wapi?”. Veronica akaniuliza na wakati nilipokuwa nikijiandaa kutunga uongo ndimi zetu zikaingia tena kazini zikitekenyana taratibu mdomoni. Ingawa nilikuwa jasusi hatari wa...

    Japokuwa nilikuwa jasusi hatari wa kuogopwa lakini mbele ya mlimbwende yule nilikuwa kama mbwa muoga mbele ya chatu mwenye njaa kali. Veronica akavuta kamba nyembamba ya kivazi chake kiunoni na hapo kivazi kile kikaanguka chini na kumuacha na nguo yake nyekundu nzuri ya ndani huku harufu nzuri ya manukato yake ikinishawishi kuendelea na hatua inayofuata.

     Sikuwa na ujasiri wa kupingana zaidi na hizia zangu hivyo taratibu nikaupeleka mkono wangu ndani ya nguo ya ndani ya Veronica na kuanza kuyatomasa makalio yake laini yaliyoshiba minofu. Veronica akashtuka kidogo na kuachia mguno hafifu wakati mkono wangu mwingine ulipokuwa ukiyatomasa matiti yake taratibu. Ndimi zetu zilipoachana ulimi wangu chakaramu nikautembeza taratibu shingoni na hatimaye sikioni mwake na hapo nikasikia sauti yake hafifu mguno wa mahaba. Veronica hakuweza kuvumilia tena hivyo haraka akaishusha chini nguo yangu ya ndani na kuupeleka mkono wake akizichezea malighafi zangu na kunipelekea nianze kuhema ovyo.

     Muda mfupi uliofuata tulikuwa kwenye kochi kubwa la sofa lililokuwa pale sebuleni huku kila mmoja akiwa amepandwa na wazimu wa mapenzi. Veronica alikuwa msichana mtundu sana aliyeyamudu vyema mapenzi kiasi cha kunipelekea nijihisi kama mvulana wa sekondari. Pamoja na ufundi wangu wote wa mapenzi lakini kwake bado sikuweza kufua dafu kwani alinidhibiti vyema pale kwenye kochi mimi chini yeye juu huku nikiitazama mijongeo hafifu ya kiuno chake wakati alipokuwa akipanda juu na kushuka chini taratibu.

     Tulikuwa kwenye ulimwengu mzito wa mapenzi na dunia ilikuwa kama kisiwa cha raha kwa ajili yetu. Veronica alikuwa amezitendea vyema hisia zangu na raha niliyoipata macho yangu hayakuweza tena kumtazama usoni.

     _____

     Kwa mara kwa kwanza tangu nitoke jijini Dar es Salaam nilikuwa nimelala usingizi mtamu wa kueleweka. Ilikuwa tayari imetimia saa kumi na moja na robo alfajiri wakati niliposhtuka kutoka usingizi. Veronica alikuwa bado yupo usingizini huku kichwa chake amekilaza kifuani kwangu pale kwenye kochi. Mguu wake mmoja ulikuwa katikati ya mapaja yangu huku mkono wake mmoja ameuzungusha shingoni mwangu na kwa mbali niliweza kusikia sauti hafifu ya mkoromo wake wa uchovu. Penzi zito la Veronica lilikuwa limeamsha ari mpya nafsini mwangu na kupitia ukaribu ule kitu fulani kilikuwa kimeanza kujengeka moyoni mwangu. Kwa namna moja au nyingine Veronica alikuwa ameuteka moyo wangu na sasa nilianza kuona ugumu wa kuwa mbali naye katika harakati zangu.

     Taratibu nikayatembeza macho yangu kuipeleleza vizuri sebule ile. Ilikuwa sebule ndogo yenye samani za kawaida kama seti moja ya makochi ya sofa na meza ndogo ya chakula iliyozungukwa na viti vinne iliyokuwa upande wa kushoto kwenye sebule ile. Katikati ya sebule ile kulikuwa na meza nyingine fupi na nzuri ya mbao ya mti wa msonobari iliyofunikwa kwa kitambaa cheupe kizuri chenye maua mekundu ya kufuma kwa mkono. Juu ya meza ile kulikuwa na ua zuri ndani chungu cha udongo mfano wa kibuyu cha asili kilichofinyangwa kwa mkono. Sakafu ya mle ndani ilifunikwa kwa zulia maridadi la rangi za kupendeza na katika kuta safi nyeupe za sebule ile niliziona picha mbili kubwa za kuchora za wanyama wa mwituni na kalenda nzuri zikiwa zimetundikwa. Kupitia zile samani za pale sebuleni haraka nikatambua kuwa kipato cha Veronica kilikuwa cha chini sana ingawa alionekana kuishi maisha ya daraja la kati kwa kadiri alivyoweza.

     Upande wa kulia wa ile sebule nikauona mlango uliofunikwa kwa pazia jepesi. Hisia zangu zikanitanabaisha kuwa ule huwenda ulikuwa mlango wa kuelekea chumbani.

     Nilipokumbuka kazi ngumu iliyokuwa mbele yangu sikuona sababu ya kuendelea kulala pale sebuleni hivyo taratibu nikamsogeza Veronica pembeni yangu na kisha kuketi na wakati nikifanya vile maumivu makali ya majeraha yangu yakapenya mwilini

     Mara moja nilipoyatazama yale majeraha ya mbwa mikononi mwangu nikaanza kuingiwa na wasiwasi wa kuugua maradhi mabaya ya kichaa cha mbwa kwa vile sikuwa na hakika yoyote juu ya afya ya wale mbwa walionishambulia usiku wa jana kule Le Tulip Hôtel Africaine. Tumbo langu lilikuwa dhaifu sana kwa vile usiku wa jana sikuwa nimetia kitu chochote tumboni. Penzi zito la msichana Veronica usiku uliopita lilikuwa limenipelekea nisahau njaa kali iliyokuwa ikinitafuna tumboni. Haraka nikasimama pale kwenye kochi na kuanza kuichunguza ile nyumba kwa utulivu. Nilipomaliza nikagundua kuwa ile nyumba ilikuwa na chumba kimoja cha kulala, sebule, jiko, choo na bafu.

     Nililikuta begi langu la mgongoni nililomuachia Veronica asubuhi ya jana kule Havana Club likiwa juu ya meza ndogo iliyokuwa kando ya kitanda chumbani kwake. Haraka nikaingia bafuni kuoga nilipotoka mwili ulikuwa tayari umepata nguvu mpya ambapo nilijiandaa vizuri na kubadili nguo. Kulikuwa na vifaa muhimu vya huduma ya kwanza kwenye begi langu hivyo nilijifanyia tiba muhimu dhidi ya yale majeraha kwa kujichoma sindano ya kuzuia maradhi ya kichaa cha mbwa. Nilipomaliza nikaelekea sebuleni ambapo nilimkuta Veronica akiendelea kuuponda usingizi pale kwenye kochi. Sikumuamsha badala nikaliokota koti langu na kofia na kisha kuelekea bafuni ambapo nilivisafisha vizuri na kuvitia mwilini. Sasa nilikuwa katika muonekano mpya wa suruali nyeusi ya jeans, fulana ya rangi ya kijivu, kofia nyeusi ya kapero, koti jeusi la mvua na buti ngumu za ngozi miguuni.

     Nilipotoka bafuni nikaelekea jikoni na baada ya pekuapekua ya hapa na pale nikakuta hotpot yenye chakula kizuri cha ndizi za matoke zilizopikwa kwa ufundi wa hali ya juu huku zikiwa zimechanganywa vizuri na samaki wa ziwa Tanganyika waitwao Mukake. Sikuwa na shaka yoyote kuwa chakula kile kilikuwa kimeandaliwa na Veronica kwa ajili yangu usiku wa jana. Pembeni ya hotpot ile kulikuwa na chupa ya chai ambapo nilipoifungua ndani yake nikaona maziwa fresh. Kile chakula kilikuwa kingi hivyo tungeweza kula mimi na Veronica na kushiba vizuri kabla kila mmoja hajaelekea kwenye harakati zake. Hivyo haraka nikapasha moto kile chakula kwa jiko la gesi na kuchemsha yale maziwa.

     Ni wakati nilipokuwa mbioni kumaliza zoezi lile la kuandaa chakula pale niliposhtushwa na mkono laini ukinishika begani. Mara moja nikashtuka na kugeuka nyuma huku moyo wangu ukianza kupoteza utulivu lakini kitendo cha kumuona Veronica kikauyeyusha haraka mshtuko wangu na kusababisha tabasamu jepesi lichomoze usoni mwangu. Veronica alikuwa amenyata taratibu kutoka sebuleni kwenye kochi na hatimaye kusimama nyuma yangu. Ingawa macho yake yalikuwa na kila dalili za uchovu lakini tabasamu lake maridhawa lilirudisha uhai mpya usoni mwake na kumpelekea aonekane mwanamke mzuri na mrembo sana kupita wote niliowahi kuwaona duniani.

     Mwanga hafifu wa pambazuko la alfajiri uliokuwa ukipenya taratibu mle ndani ukaniwezesha kuiona hazina matata iliyojificha katika umbo la mlimbwende yule. Veronica alikuwa amesimama nyuma yangu kama alivyozaliwa bila nguo yoyote ya kujisitiri mwilini mwake. Loh! nywele zangu zikasimama wima, moyo wangu ukacheza kidogo kisha mdomo wangu ukaachama huku nikimkodolea macho ya uchu kama fisi aliyeona mfupa.

    “Mbona umeamka mapema mpenzi?”. Sauti nyororo ya Veronica ikaziachia huru fikra zangu na kuzirudisha kwenye ufikirivu wa kawaida na hapo nikaunyanyua mkono na kuitazama saa yangu ya mkononi.

    “Sasa hivi ni saa kumi na mbili kasoro mpenzi”. Nikaongea kwa sauti hafifu ya kirafiki na hapo nikamuona Veronica akishikwa na mshangao.

    “Khe! kumbe kumeshapambazuka!”

     “Kazini unaingia saa ngapi?”. Nikamuuliza.

    “Saa moja na nusu asubuhi”. Veronica akanijibu kwa sauti hafifu huku akionesha kukerwa na ratiba ile.

    “Hata leo Jumapili?”

     “Kila siku mpenzi”. Mara moja nikamtazama Veronica na kumhurumia hata hivyo sikuwa na namna na hatimaye nikavunja ukimya.

    “Nenda kaanze kujiandaa utakapomaliza chakula kitakuwa tayari mezani”. Maneno yangu yakampelekea Veronica atabasamu kidogo kisha akanitupia macho usoni na macho yetu yalipokutana hisia za mapenzi zikafufuka upya nafsini mwetu.

    “Gilbert…”

     “Naam Veronica”

     “Je t?aime a la fol?ie”. Nakupenda hadi najihisi kuchanganyikiwa.

    “Moi aussi”. Mimi pia.

    “S?il vous plaît, ne me quitte pas mon amour”. Tafadhali usiniache mpenzi wangu.

    “Jusqu? à ce que la mort nous sèpare”. Hadi kifo kitakapotutenganisha. Nikaongea kwa utulivu huku nikiruhusu tabasamu langu kuchanua usoni. Veronica akanisogelea na kunibusu mdomoni kisha taratibu akageuka na kuondoka na hapo nikapata kuona vizuri mtikisiko maridhawa wa umbo lake chakaramu. Kwa mara ya kwanza nikahisi nafsi yangu ilikuwa imepata utajiri mkubwa wa furaha isiyoelezeka.



     Ilipofika saa kumi na mbili na nusu Veronica alikuwa tayari amekwishamaliza kujiandaa. Alipotoka chumbani akanikuta nikiwa nimeketi tayari kwenye ile meza ya chakula sebuleni huku taratibu nikipekua kurasa moja baada ya nyingine ya kile kitabu kidogo cha sala nilichokipata kwa yule padri wa kizungu aliyenyongwa kule kwenye kile chumba 403 cha Le Tulip Hôtel Africaine nikijaribu kuchunguza kama ningeweza kuvumbua kitu chochote cha kunisaidia katika harakati zangu. Kurasa ya mwisho ya kitabu kile haikuongeza ziada yoyote katika kile nilichokuwa nikikifahamu hapo awali hivyo nikafunika kile kitabu na kukitia mfukoni huku macho yangu yakiwa kwa Veronica nikijidai kuwa nilikuwa katika harakati za kuombea chakula.

     Asubuhi hii Veronica alikuwa amependeza zaidi katika muonekano wa vazi la kitenge cha wax na kilemba kilichofungwa kwa ufundi wa hali ya juu kichwani mwake. Kama ningekuwa promota wa mitindo ya mavazi ya kiafrika sikuwa na shaka yoyote kuwa Veronica angeweza kuniletea ushindi wa kuaminika. Nilipomuuliza juu ya sare zake za kazi akaniambia kuwa angebadili mavazi baada ya kufika kazini kwake.

     Wakati tukipata mlo pale mezani kila mmoja akawa amejikita katika kumdadisi mwenzake na hapo nikapata nafasi ya kujua mambo machache kuhusu Veronica ingawa kwa upande wangu aliambulia uongo katika kila swali aliloniuliza.

     Saa moja asubuhi kasoro dakika tano tulimaliza kupata kifungua kinywa na kisha kushushia na mvinyo mtamu wa Chateau Lascombes nilioupata kwenye kile chumba cha ofisi ya meneja wa New Paradol Residence usiku wa jana kutoka kwa yule mtu wa mwisho niliyepambana naye. Mvinyo ule ulikuwa umeamsha ari mpya katika miili yetu na kutuchangamsha vizuri kasi cha kupunguza nishai machoni. Veronica akaondoa vyombo na kwenda kuvisuuza jikoni, aliporudi akachukuwa pochi yake ya begani na hapo tukatoka nje ya nyumba ile na kufunga mlango.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Asubuhi ile hali ya hewa ya jiji la Bujumbura ilikuwa imepoa zaidi, manyunyu hafifu ya mvua yalikuwa yakianguka kutoka angani kulikotanda wingu zito la mvua kiasi cha kuweza kuizuia miale ya jua la asubuhi kutua vizuri ardhini. Kufuatia lile jaribio la mapinduzi ya kijeshi jiji la Bujumbura ni kama lilikuwa limelala kwani wakazi wake hawakuwa huru sana kurandaranda mitaani kama ilivyokuwa desturi yao badala yake hofu ilikuwa imetanda kila kona.

     Mara baada ya kuyaacha maskani ya Veronica tulishuka kwenye jengo lile la ghorofa la shirika la nyumba la taifa na kushika uelekeo wa ilipo barabara ya Boulevard de Independence. Wakati tukitembea macho yangu yalikuwa makini kutazama kila mahali katika namna ya kuchunguza kuwa hapakuwa na mtu yeyote aliyekuwa akitufuatilia nyendo zetu.

     Tulipoyafikia makutano ya barabara ya Boulevard de Independence na barabara ya Avenue de Litalie, Veronica akanishawishi kuwa tuvuke makutano yale na kuendelea kutembea kidogo kwa kuifuata barabara Boulevard de I?independence kwani mbele kidogo tungekuja kukutana na kituo cha maegesho ya teksi nje ya kiwanda cha kuchapisha magazeti. Lilikuwa wazo zuri hivyo nilikubaliana na Veronica bila ubishi wowote kwa vile niliona kuwa kutembea kwa...



    ...miguu umbali mrefu ingekuwa ni hatari zaidi kwetu sote kwa vile nilivyokuwa nikisakwa na wale watu hatari. Veronica alitaka kujua kuwa nilikuwa nikielekea wapi, nikamdanganya kuwa nilikuwa nikielekea katikati ya jiji kukutana na mfanyabiasha mmoja mkubwa wa pale jijini Bujumbura na bila shaka jibu langu lilikuwa na ushawishi mkubwa kwani hakudiriki kuniuliza tena. Aliponiuliza juu ya yale majeraha ya usiku wa jana mwilini mwangu jibu tayari nilikuwa nalo mdomoni kuwa nilikuwa nimepata ajali ya bodaboda baada ya dereva kukosa umakini barabarani na kwa kumthibitishia nikaapa mbele yake kuwa kamwe sitatumia tena usafiri wa bodaboda hata kama nina haraka ya namna gani.

     Nje ya kiwanda cha kuchapa magazeti kando ya barabara ya Boulevard de I?independence tukakuta maegesho ya teksi. Kitu cha ajabu ni kwamba madereva wa teksi wa eneo lile hawakujisumbua kutugombea badala yake nilimuona dereva mmoja wa teksi kijana wa makamo akiangua tabasamu la kibiashara pindi alipomuona Veronica na hapo nikajua kuwa Veronica alikuwa ni mteja wake wa kuaminika. Hatukupoteza muda hivyo tukafungua milango ya nyuma ya teksi ile na kuzama ndani. Muda uleule ile teksi ikaacha maegesho na kuingia barabara huku yule kijana dereva wa teksi akijitia uchangamfu wa kila namna katika kuhakikisha kuwa ananizoea, nafasi ambayo kamwe hakuipata. Kwa kukwepa mizunguko isiyo na ulazima dereva wa teksi akaifuata barabara ya Boulevard de I?independence akiendesha kwa mwendo wa haraka.

     Safari ilipoanza tu nikaanza kuchunguza kama tungefungiwa mkia na gari nyingine nyuma yetu lakini hilo halikujitokeza. Baada ya mwendo mrefu wa safari yetu hatimaye tukayafikia makutano ya barabara ya Boulevard de I?independence na barabara ya Boulevard de I?uprona. Tulipoyafikia makutano yale dereva akaingia upande wa kushoto akiifuata barabara ya Boulevard de I?uprona na hapo kumbukumbu nzuri ya mandhari yale ikanijia akilini mara tu baada ya kuzipata ofisi za ubalozi wa Ufaransa mbele kidogo upande wa kushoto. Haraka nikagundua kuwa tulikuwa tumeingia kwenye ile barabara iliyokuwa ikipakana na Havana Club.

     Kulikuwa na magari machache katika barabara ile hivyo mwendo wetu uliongezeka na baada ya muda mfupi wa safari ile teksi ikasimama nje ya Havana Club. Veronica akashuka haraka na kuniaga kwa vile muda wa kuingia kazini kwake ulikuwa tayari umefika. Alipotaka kumlipa dereva wa teksi nikamsihi aache na kumuahidi kuwa ni mimi ndiyo ningemlipa. Hivyo tukaagana na Veronica kwa makubaliano kuwa tungeonana usiku kule nyumbani kama ilivyo ada na hapo dereva wa ile teksi akatia moto gari tukielekea katikati ya jiji la Bujumbura. Hakukuwa na gari lililokuwa likitufungia mkia nyuma yetu hivyo bado mambo yalikuwa shwari.

     _____

    “Un lideur de Coup d'état militaire du pay de Burundi géneral Godfroid Niyombare et ses compagno is sont arrêtés”. Kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi nchini Burundi generali Godfroid Niyombare na washirika wake wakamatwa.

     Zilikuwa habari za kushtua zilizoamsha hisia mpya moyoni mwangu. Mtangazaji wa kituo kimoja maarufu cha redio cha jijini Bujumbura alikuwa akimalizia kutangaza taarifa ile wakati dereva wa teksi alipovunja ukimya ulioshamiri mle ndani ya teksi tangu kuanza kwa safari yetu kwa kuwasha redio ya gari. Mara moja nilipomtazama dereva yule nikagundua kuwa alikuwa hajafurahishwa kabisa na taarifa ile kwa namna uso wake ulivyobadilika na hapo nikajifunza kuwa raia wengi wa nchini Burundi huwenda walikuwa wamefurahishwa na mapinduzi yale ya kijeshi hivyo kukamatwa kwa wahaini wale wa jaribio la mapinduzi ya kijeshi kulikuwa kumewavunja moyo sana wa kusimikwa kwa utawara mpya kama dereva yule alivyoonesha hisia zake za waziwazi.

     Kwa kukwepa kutengeneza vielelezo rahisi kwa mtu yeyote aliyekuwa akinipeleleza nyendo zangu nilikuwa nimeamua kukodi teksi nyingine mara baada ya yule dereva wa teksi wa Veronica kumtaka anishushie katikati ya jiji la Bujumbura nje ya ofisi kuu za shirika la posta. Dereva wa ile teksi alipotokomea nikavuka barabara na kutembea hadi mtaa wa tatu ambapo nilikodi teksi nyingine na kumtaka dereva wa teksi ile mwanaume mrefu wa asili ya kitutsi mwenye umri kati ya miaka thelathini na tano hadi arobaini anipeleke eneo linaloitwa Bubanza.

     Wakati nilipoinua mkono na kuitazama saa yangu ya mkononi nikagundua kuwa muda wa saa moja tayari ulikwishapita tangu kuanza kwa safari yetu ya kuelekea eneo la kaskazini ya jiji la Bujumbura. Sehemu kubwa ya nchi ya Burundi ilikuwa imemezwa na ukimya wa hofu. Wanajeshi watiifu wa serikali ya Rais Pierre Nkurunziza sasa walikuwa wametanda kila kona kuanzia mitaa ya jiji la Bujumbura hadi kwenye barabara zinazokwenda mbali na miji. Vizuizi vya askari wa barabarani vilikuwa vimeongezwa na upekuzi wa magari na watu waliokuwa wakitoka na kuingia mijini ulikuwa ukifanyika.

     Mazingira hayakuwa rafiki kwa mtu yeyote mgeni wa nchi ya Burundi hivyo kwa kukwepa kusababisha migogoro hatari yenye upotevu wa muda wenye kugharimu uhai wangu kwenye vizuizi vya barabarani nikaamua kutumia kitambulisho changu bandia kinachonitambulisha kwa jina Céléstine Desire Bizimana kama kada mwandamizi wa chama kilichopo madarakani nchini Burundi cha CNDD-FDD-Conseil National pour la Défense de la Démocratié-Forces de Defense de la Démocratié. Hivyo katika kila kizuizi tulichosimamishwa askari walipoona kitambulisho changu hawakunitilia mashaka yoyote badala yake walituruhusu tuendelee na safari katika nyuso za kiungwana.

     Barabara ya kuelekea eneo la Bubanza lililopo maili nyingi kaskazini mwa jiji la Bujumbura ilikuwa mbaya mno isiyokuwa na lami yenye mashimo na makorongo karibu kila mahali. Kufuatia mvua za masika zilizokuwa zikiendelea kunyesha baadhi ya madaraja madogo madogo yalikuwa yamesombwa na mafuriko. Hivyo dereva yule wa teksi alijikuta akitumia akili na nguvu za ziada katika kufanikisha safari ile kwenye barabara mbovu ya kidongo chekundu iliyokuwa ikikatisha katikati ya misitu mizito. Njiani katika baadhi ya maeneo tulikutana na makundi ya raia wa Burundi wengi wao wakiwa wanawake na watoto wakiwa na mizigo yao vichwani huku wakitembea kwa hofu kandokando ya barabara ile kukimbia mapigano katika miji yao na kwenda kutafuta hifadhi ya kikimbizi katika maeneo yenye usalama nafuu mashariki mwa D.R. Congo.

     Niliwatazama watu wale na kujikuta nikiwaonea huruma sana kwa namna walivyokuwa wakitaabika kwa kuisaka amani kwa udi na uvumba. Ilikuwa taswira ya kusononesha mno kiasi cha kushawishika kutaka kumwambia dereva wa ile teksi asimamishe gari ili tumchukue mama mmoja mwenye watoto sita wadogo waliodhoofika afya baada ya safari ndefu ya kutembea kwa miguu bila chakula wala maji. Hata hivyo niliachana na mpango ule baada ya kuhisi kuwa mara baada ya kumuona mama yule na watoto wake tukiwasaidia wakimbizi wengine wangetaka nao wasaidiwe jambo ambalo lisingewezekana na huwenda lingeamsha chuki na hasira dhidi yetu.

     _____



     Baada ya kitambo kirefu cha safari hatimaye tukafika sehemu yenye njia panda. Mara moja tulipoanza kukaribia eneo lilie dereva wa ile teksi akaanza kupunguza mwendo na hapo nikayahamisha macho yangu kutoka dirishani na kutazama kule mbele ya gari. Nilichokiona kwenye ile njia panda kikapelekea baridi nyepesi isambae moyoni mwangu. Maiti nyingi za watu waliouwawa muda mfupi uliopita zilikuwa zimezagaa eneo lile huku wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto. Taratibu nikashusha kioo cha dirishani na kuchungulia nje na hapo simanzi na hasira vikanishika.

     Ulikuwa ni ukatili wa aina yake kuwahi kufanyiwa binadamu. Watu wale walikuwa wameuwawa kwa kupigwa mapanga kichwani. Maiti za wanawake zilikuwa uchi wa mnyama katika namna ya kuaminika kuwa walikuwa wamebakwa na wavamizi kabla ya kuuwawa. Baadhi ya zile maiti zilikuwa zimezagaa barabarani. Dereva wa ile teksi akawa kama anayepunguza mwendo ili asimame kisha tushuke tukasaidiane kuziondoa zile maiti na kuziweka kando ili tuweze kupita.

     Lilikuwa wazo zuri kwa vile hatukuwa na sehemu nyingine ya kupita lakini moyo wangu ukasita kidogo baada ya kulichunguza vizuri lile eneo. Nafsi yangu ikanitanabaisha kuwa hatukuwa sehemu salama. Mbele yetu kulikuwa na barabara nyingine iliyokuwa ikikatisha na eneo lile lilikuwa limepakana na msitu mzito wenye miti mirefu iliyozingirwa na vichaka vinavyotisha. Nilipotazama vizuri kule mbele kwenye makutano ya zile barabara nikaona bango dogo jeupe lenye mshale mweusi unaoelekeza upande wa kulia juu yake kumeandikwa Bubanza 20KM Est.

     Dereva wa ile teksi akionekana dhahiri kuingiwa na hofu akageuka na kunitazama kama anayetaka nimruhusu asimame hata hivyo nikakataa kwa kutingisha kichwa hali iliyosababisha mshangao usioelezeka usoni mwake. Nilifahamu kuwa lile lilikuwa jambo gumu kwake kwani kwa vyovyote vile ili kupita eneo lile yule dereva angelazimika kuzikanyaga zile maiti kwa magurudumu ya gari katika baadhi ya sehemu. Hata hivyo hapakuwa na namna nyingine kwani wale watu tayari walikuwa wafu hivyo usalama wetu ulikuwa muhimu zaidi kwa kuzingatia kuwa wafu hawakuwa na cha kupoteza.

     Huku jasho likianza kumtoka dereva wa ile teksi akatia gari moto na kuanza kuzikanyaga zile maiti za wafu mbele yetu na wakati akifanya vile mimi nikawa makini kulichunguza lile eneo. Lilikuwa eneo linalotisha na hapakuwa na dalili zozote za makazi ya watu.

     Tulikuwa mbioni kabisa kuifikia ile njia panda wakati nilipogeuka nyuma na kuona kikundi cha wanaume kikichomoza kutoka msituni kando ya ile barabara na kuanza kutufuata huku mikononi wakiwa na silaha za jadi na bunduki. Muda uleule mara tukaanza kushambuliwa kwa risasi. Kuona vile nikamuhimiza yule dereva wa teksi aongeze mwendo na hapo nikachomoa bastola yangu kutoka kwenye mfuko wa koti na kuanza kujibu mashambulizi baada ya kufungua mlango wa nyuma na kujilaza chini.

     Ingawa watu wale walijitahidi kwa kila namna kutuzuia huku wakilishambulia gari letu lakini hawakufanikiwa kwani niliwadondosha mmoja baada ya mwingine kwa risasi zangu zenye shabaha makini huku yule dereva wa teksi akizidi kutia moto gari. Muda mfupi tukawa tumeyafikia yale makutano ya barabarana hapo yule dereva wa teksi akaingia upande wa kulia akitimua mbio zisizo za kawaida. Nikaendelea kuwatazama wale watu waliosalia nyuma yetu wakiendelea kutufukuza hata hivyo tuliendelea kuwaacha kwa umbali mrefu na hatimaye tukawapotea kabisa tukiendelea kuchanja mbuga kwenye barabara nyembamba ya vumbi iliyokuwa ikikatisha katikati ya misitu minene.

     Kulikuwa na matundu machache ya risasi nyuma ya gari na kwenye kioo cha nyuma dirishani zaidi ya pale hapakuwa na athari nyingine katika uvamizi ule. Wakati tukiendelea na safari mara kwa mara nilimtazama yule dereva wa teksi na kumuona ni kama aliyekuwa akijuta kuambatana na mimi. Sasa alikuwa akinitazama kwa woga wa hali ya juu kupitia kioo cha mbele cha ndani ya gari na macho yetu yalipokutana niliona namna hofu ilivyolipuka usoni mwake. Bila shaka alikuwa ameshtushwa na kitendo cha mimi kumiliki silaha na kuitumia kwa ufundi wa hali ya juu.

     _____CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



     Mara baada ya kuvuka daraja la mto mkubwa uliokatisha katikati ya msitu mkubwa tukaingia upande wa kushoto. Hatukufika mbali sana mara nikamuona dereva wa ile teksi akipunguza mwendo na kabla sijamuuliza kuwa alikuwa akifanya vile kwa sababu gani akawahi kugeuka nyuma na kuniambia.

    “Puis je aller pour un court appel s?il vous plait”. Naomba niende nikajisaidie kidogo tafadhali.

    “D'accord”. Sawa. Nikamruhusu huku nikimtazama yule dereva kwa mashaka kidogo. Yule Dereva wa teksi akaegesha gari kando ya ile barabara na kushuka. Mara tu aliposhuka akageuka na kunikata jicho na namna ya utazamaji wake ukanitia mashaka kidogo. Waswahili husema moyo wa binadamu ni kama kichaka kizito kwani nilipenda kufahamu kuwa mtu yule alikuwa akiniwazia nini kichwani mwake na kama alikuwa amabanwa kweli na haja au alikuwa akifanya hila. Majibu sikuyapata kwa vile Mungu alikuwa ameninyima binadamu uwezo huo hivyo nafsi yangu ikabaki imetawaliwa na hisia tu na hapo nikabaki nimeketi nyuma ya ile teksi huku nikimtazama yule dereva wa teksi namna alivyokuwa akizitupa hatua zake kwa utulivu kuelekea kichakani kando ya ile barabara huku mara kwa mara akigeuka nyuma na kunitazama. Hatiamye yule dereva wa teksi akapotelea kwenye kichaka kikubwa kilichokuwa kando ya ile barabara na hapo nikahisi kuwa huwenda alikuwa ameshikwa na tumbo la kuhara kwa namna alivyokuwa akizidi kuharakisha na kuzipangua nyasi ndefu akizidi kutokomea ndani ya kile kichaka. Ingawa sikupenda tusimame barabarani sehemu ya wazi kama ile lakini niliheshimu vizuri matatizo ya binadamu hivyo nikabaki garini nimeegemea siti huku nikiendelea kutazama nyuma ya ile barabara kupitia kioo cha ndani cha mbele kwa dereva huku mawazo mengi yakipita kichwani mwangu.

     _____



     Kama siyo tabia mbaya ya kupenda kula ovyo vyakula vya barabarani pasipo kuzingatia usafi wa upishi basi maradhi ya tumbo la kuhara huweza pia kusababishwa na hofu ambayo binadamu hukutana nayo. Dereva wa teksi huwenda alikuwa ameshikwa na hofu baada ya yale mapambano dhidi ya wale wavamizi wa kule barabarani tulipotoka. Nikajikuta nikiwaza hivyo baada ya kuyatuliza tena mawazo yangu mle ndani ya gari.

     Lakini sasa wasiwasi tayari ulikuwa umeanza kuniingia baada ya kuitazama saa yangu ya mkononi na kugundua kuwa dakika chache zilikuwa zimesalia kabla ya muda wa nusu saa kutimia tangu yule dereva wa teksi alipoingia kule kichakani. Muda wa nusu saa kwa mtu aliyechafukwa na tumbo la kuhara kichakani nikaanza kuuona kuwa ulikuwa ni mwingi sana hivyo nikaanza kuingiwa na hofu kiasi cha kuanza kushawishika kuwa nishuke kwenye ile teksi na kuelekekea kwenye kile kichaka ili nikamsihi yule dereva wa teksi aharakishe haja yake ili tuendelee na safari kwa vile nilianza kuhisi kuwa nilikuwa nikielekea kuchelewa kule niendako. Hata hivyo baada ya kujishauri sana hatimaye nikaamua kutoa msamaha wa dakika tano za nyongeza huku nikiamini kuwa muda wowote kuanzia pale yule dereva wa teksi angejitokeza kichakani huku uso wake ukiwa na faraja baada ya kuutua mzigo mzito.

     Hata hivyo wakati nikiendelea kusubiri mle ndani ya teksi nikaona kuwa siyo vibaya kulichunguza lile gari kwa kuyatembeza macho yangu hapa na pale. Kwa kufanya vile mara moja nikagundua kuwa funguo za gari hazikuwepo kwenye swichi yake chini ya usukani. Hivyo kwa tafsiri nyingine ni kuwa dereva wa ile teksi alikuwa amendoka na funguo za gari wakati ule aliposhuka na kwenda kujisaidia kichakani. Dereva wa ile teksi alikuwa na maana gani kuondoka na funguo za gari wakati alikusudia kutumia muda mfupi tu kamaliza haja yake kichakani?. Au huwenda alikuwa amehofia kuwa kuacha funguo za gari mle ndani kungeweza kunipa fursa nzuri ya kutokomea na gari lake wakati yeye akiwa kichakani anapambana na haja yake?. Majibu sikuyapata hivyo wasiwasi sasa ulikuwa dhihiri nafsini mwangu.

     Hatimaye sikuona sababu ya kuendelea kusubiri zaidi mle ndani ya ile teksi hivyo nikafungua mlango na kushuka huku mkono wangu wa kushoto ukiwa umeikamata vyema bastola ndani ya mfuko wa koti langu. Kwa sekunde kadhaa nikasimama pembezoni ya ile barabara nikifanya tathmini dhidi ya mazingira yale na kwa kufanya vile hisia zangu zikanitanabaisha kuwa tulikuwa kwenye eneo la msitu mzito wenye miti mirefu na mikubwa iliyokula chumvi nyingi katika sehemu isiyokuwa na makazi ya watu. Nilipoyatega kwa makini masikio yangu kwa mbali niliweza kuzisikia sauti za tetere zikihanikiza juu ya miti iliyokuwa eneo lile.

     Hatimaye nikaanza kutembea taratibu kukifuata kile kichaka kilichokuwa kando ya ile barabara alichokuwa amepotelea yule dereva wa teksi. Mara tu nilipoingia kwenye kile kichaka mashaka yakazidi kuniingia baada ya kutomuona yule dereva na badala yake nikauona uchochoro mwembamba wa nyasi zilizolala chini muda mfupi uliopita baada ya mtu kupita eneo lile. Sikuwa na shaka yoyote kuwa yule dereva wa teksi ndiye ambaye angekuwa amepita eneo lile na kuendelea kule mbele. Kwanini yule dereva wa teksi aliamua kwenda mbali zaidi na eneo lile kama kweli alikuwa ameshikwa na haja ya ghafla?. Nikajiuliza tena bila kupata majibu.

     Hata hivyo nikaamua kuanza kuufuata ule uchochoro wa nyasi zilizokanyagwa chini ya miti mikubwa na mirefu ya mivule huku nikilichunguza lile eneo kwa makini na tayari kukabiliana na hatari yoyote ambayo ingejitokeza mbeleni. Bado sikuona dalili za uwepo wa mtu yeyote eneo lile.

     Umbali niliotembea kwa miguu nikiufuata ule uchochoro wa nyasi zilizolala kwa kukanyagwa ulikuwa zaidi ya mita mia mbili na ule uchochoro ulionekana kuzidi kusonga mbele zaidi hali iliyonitia mashaka. Nilipozidi kuwaza sikuona sababu yoyote ya mtu aliyebanwa na haja ya ghafla iwe ndogo au kubwa kutembea umbali wa zaidi ya mita mia mbili msituni eti kutafuta sehemu nzuri ya kujisaidia. Hivyo haraka nikaanza kuhisi hatari ingawa niliendelea kujipa moyo kwa kumuita yule dereva wa teksi pasipo mafanikio yoyote. Mwishowe nikakata tamaa lakini kabla sijaamua kurudi kule barabarani ilipoegeshwa ile teksi nikataka kujipa hakika zaidi na uchunguzi wangu. Hivyo nikachagua mti mmoja mrefu wenye ukubwa wa wastani na kuanza kuukwea.

     Muda mfupi baadaye nikawa nimemaliza kukwea na kufika juu ya ule mti na hapo nikapata nafasi nzuri ya kuona mandhari ya eneo lile. Kwa mbali niliweza kuona milima na mabonde, vichuguu, misitu na nyasi ndefu zinazoweza kuwaficha wanyama hatari wa porini kama simba, mbwa mwitu, chui au fisi. Lakini bado hapakuwa na dalili zozote za uwepo wa binadamu eneo lile na jambo lile lilinishangaza sana. Nikiwa bado pale juu ya mti nikaendelea kulichunguza lile eneo la msitu kwa utulivu huku nikitarajia kumuona yule dereva wa teksi katikati ya kichaka au nyasi ndefu akimalizia haja yake lakini hilo halikutokea badala yake nikaishia kumuita yule dereva kwa kila namna hali iliyowapelekea ndege wa porini wanisikilize kwa makini na hatimaye kunicheka. Mwishowe nikaona kuwa nilikuwa nikipoteza muda wangu bure hivyo taratibu na kwa tahadhari ya hali juu nikashuka chini ya ule mti na kurudi kule barabarani ilipoegeshwa ile teksi.

     Majira ya saa yangu ya mkononi yakanitahadharisha kuwa muda haukuwa rafiki sana kwangu hivyo nilipoifikia ile teksi nikafungua mlango wa dereva na kuingia ndani. Funguo za gari hazikuwepo mahala pake lakini kwa kuwa nilikuwa na weledi mzuri katika ufundi wa magari nikabomoa swichi ya gari na kutafuta nyaya fulani mbili ambapo nilipozigusanisha kidogo mchuma ukatoa majibu chanya. Kwa dakika chache nikaiacha injini ya ile gari ikiunguruma kwa hasira huku nikipiga honi mfululizo ambazo zingeweza kumshtua yule dereva wa teksi kokote alikokuwa karibu na eneo lile kichakani. Yule dereva wa teksi hakujitokeza na jambo lile likazidi kunichanganya akilini. Mwishowe sikuona sababu ya kuendelea kusubiri zaidi hivyo nikatia moto gari na kuingia barabarani nikitoweka mbali na eneo lile katikati ya barabara iliyopakana na misitu mizito yenye milima na mabonde huku mawazo mengi yakipita kichwani mwangu...

    Kanisa la Katoliki la Diocèse de Bubanza lilikuwa kando kidogo ya mji mdogo wa Bubanza kaskazini mwa jiji la Bujumbura, kilometa chache upande wa kulia baada ya kuachana na barabara ya vumbi inayoelekea mto Ruzizi ulipo mpaka wa nchi ya Burundi na D.R.Congo upande wa magharibi. Tofauti na jiji la Bujumbura mji mdogo wa Bubanza haukuwa na pilika nyingi za watu magari na shughuli nyingi za binadamu. Barabara zake zilikuwa duni sana, huduma za kijamii kama maji safi, hospitali za kisasa, shule zilikuwa zinahesabika. Sikuwa na shaka yoyote kuwa taarifa za jaribio la mapinduzi ya kijeshi nchini Burundi zilikuwa tayari zimewafikia wakazi wa mji ule na kupelekea mashaka dhidi ya usalama wao.

     Baada ya ulizauliza ya hapa na pale kwa wenyeji wa mji ule hatimaye nikalifikia kanisa la katoliki jibo la Bubanza kando kidogo ya mji ule. Nikafurahi kukuta misa ilikuwa ikiendelea. Nje ya kanisa lile kulikuwa na magari machache ambayo nilipoyachunguza vizuri nikagundua kuwa yalikuwa ni mali ya kanisa lile kutokana na maelezo yaliyokuwa yameandikwa ubavuni. Miongoni mwa magari yale nikaliona gari la Askofu mkuu wa jimbo, gari la padri na lori moja la hospitali ya Catholic Mission de Bubanza. Magari yale yakiwa yameegeshwa katika sehemu maalumu ya kuegesha magari mbele ya minara mikubwa ya masanamu.

     Taratibu nikaegesha ile teksi na kushuka huku nikiyatembeza macho yangu kulichunguza vizuri eneo lile. Ukubwa wa kanisa ungeweza kumeza watu elfu moja bila usumbufu wowote. Upande wa kushoto nilipochunguza nikaona kuwa lile kanisa lilikuwa limepakana na hospitali ndogo ya mission ya kikatoliki ambayo bila shaka ndiyo ilikuwa tegemeo kubwa la wakazi wa kitongoji kile. Upande wa kulia kanisa lile lilipakana na ofisi za makasisi na watawa wa kikatoliki pamoja na jengo la kituo kidogo cha kanisa cha kulelea watoto yatima. Upande wa nyuma ya kanisa nisingeweza kuona chochote ingawa mandhari yake yalipambwa kwa miti ya kupandwa. Kwa kuwa misa ilikuwa ikiendelea sikumuona mtu yeyote nje ya kanisa lile hivyo taratibu nikaanza kuzitupa hatua zangu kuelekea ndani ya kanisa lile huku macho yangu yakijitahidi kusoma maelezo yalikuwa sehemu ya juu ya mlango wa kuingilia kanisani yanayosomeka Cathédrale Christ Roi Diocèse de Bubanza, yaani Kanisa la Kristo Mfalme Dayosisi ya Bubanza.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Nilipofika karibu na mlango wa kuingilia mle kanisani taratibu nikaanza kupanda ngazi kuelekea kwenye baraza kubwa ya lile kanisa. Muda mfupi uliofuata nikawa nimemaliza kupanda zile ngazi huku nikizipita nguzo mbili za sanamu za mitume wa Kristo na bikira Maria huku nikiutathmini muonekano wangu kama ungeshabihiana na baadhi ya waumini waliokuwa mle ndani ya kanisa. Anga lilikuwa limeshaanza kufunikwa tena na wingu zito kuashiria kuwa mvua ingenyesha.

     Hatua zangu madhubuti wakati nikiingia mle kanisani zikatengeneza kishindo hafifu na hapo nyuso za waumini waoga zikageuka na kunitazama kwa woga kama shetani aliyeingia kanisani kuungama dhambi zake. Sikupenda kuvuta macho ya watu wala kuonekana kivutio hivyo mara moja nikapunguza mwendo nikitembea taratibu huku nikiyatembeza macho yangu huku na kule kuzitazama nyuso za watu wa mle ndani na vilevile nikitafuta sehemu nzuri ya kukaa mle ndani ambapo macho yangu yangeweza kufanya tathmini vizuri.

     Hatimaye nikaenda kuketi mwisho wa benchi la tatu kutoka nyuma ya kanisa sehemu walipokuwa wameketi wanaume wawili wazee na kijana mdogo wa shule ya msingi. Wakati nikiketi baadhi ya watu wakageuka nyuma na kunitazama kidogo kisha wakayarudisha macho yao kutazama mbele kwa muhubiri ingawa wapo baadhi ya watu waliendelea kunitazama bila haya yoyote. Sikumbuki mara ya mwisho kuingia kanisani ilikuwa ni lini ingawa tathmini yangu ilinitanabaisha kuwa huwenda misa ile ilikuwa na waumini wengi zaidi kushinda misa nyingine zilizotangulia asubuhi.

     Lilikuwa kanisa kubwa lenye paa refu na imara. Ukutani kulikuwa na madirisha makubwa marefu ya vioo vyenye mchanganyiko wa rangi ya njano, nyeupe na kijani na katikati ya madirisha yale kulichorwa picha ya bikira Maria akiwa amempakata mtoto Yesu. Labda niseme zilikuwa ni picha za kufikirika kwani teknolojia ya upigaji na utengenezaji wa picha ni dhahiri haikuwepo nyakati za Yesu alipokuwa hapa duniani. Kila baada ya madirisha mawili ya kanisa lile kulikuwa na nguzo ndefu zilizotoka chini hadi juu kushikilia paa la kanisa lile na nguzo zile zilikuwa zimechongwa kwa ustadi sanamu za mfano wa wanafunzi kumi na wawili wa Yesu huku wakiwa wamemwinamia Yesu miguuni kama ishara ya utukufu. Juu ya sanamu zile kulikuwa na msalaba mkubwa wa kuchongwa uliotiwa nakshi za kupendeza. Mbele ya kanisa lile ilipo altale upande wa kushoto na kulia kulikuwa na vyumba vya kuungama dhambi na juu ya vyumba vile kulikuwa na ngazi ndefu za kuelekea sehemu ya juu ya kanisa lile zilikofungwa kengele kubwa mbili za kanisa.

     Macho yangu yakatulia kutazama mishumaa mikubwa iliyowekwa kwenye vikombe maalum vya shaba vilivyokuwa ukutani ikiendelea kuangaza mle kanisani. Nilipochunguza vizuri mle ndani nikagundua kuwa idadi ya watoto ilikuwa ndogo sana ukilinganisha na idadi ya wanaume na wanawake, wazee kwa vijana.

     Askofu wa jimbo alikuwa mbele ya kanisa na wasaidizi wake wakishirikiana kikamilifu kuendesha misa ile na wote walikuwa katika mavazi ya kanzu nyeupe zenye misalaba myekundu katikati huku baadhi ya wale wasaidizi wakiwa wameshika chetezo kufukiza ubani. Lugha kuu iliyokuwa ikitumika kuendesha ibada ile ilikuwa ni lugha ya kirundi kilichochanganyika na kifaransa na hapo nikafanikiwa kuokota neno moja moja la kifaransa ambapo nilipoyaunganisha nikapata maana iliyozifungua kidogo fikra zangu. Mahubiri yale yalikuwa yamelenga katika kutilia mkazo suala la amani nchini Burundi huku mhubiri akionekana kukemea vitendo vya uvunjifu wa amani na machafuko ya kisiasa yaliyokuwa yakiendelea nchini mle huku akitumia mifano mingi kutoka kwenye kitabu chake cha kuongozea misa. Waumini walionekana kumkodolea macho mhubiri yule huku wakimsikiliza kwa makini na kutafakari.

     Mimi sikuwa miongoni mwa watu waliofika pale kanisani kushiriki misa ingawa suala la kumuabudu na kumcha Mungu ni jukumu la kila mwanadamu. Hivyo wakati misa ile ikiendelea fikra nyingi zikawa zikipita kichwani mwangu nikiwaza juu ya Padri Aloysius Kanyameza ambaye kupitia kile kitabu kidogo cha sala nilichokikuta mfukoni mwake nilikuwa na kila sababu ya kuamini kuwa alikuwa miongoni mwa makasisi wa kanisa lile. Niliamini kuwa kuonana na Padri Aloysius Kunyameza kungeweza kunifungulia njia katika upelelezi wangu na hatimaye kumfikia mtu aliyefahamika kama Pierre Okongo ambaye ni yeye ndiye angeweza kutegua kitendawili cha nani aliyehusika na kifo cha yule Padri wa kizungu aliyenyongwa ndani ya kile chumba 403 cha Le Tulip Hôtel Africaine.

     Kulikuwa na watu wachache waliokuwa wakiendelea kunitazama mle kanisani na kwa kuwa sikupendezwa na tukio lile nikayapeleka macho yangu kuwatazama watu wale na macho yetu yalipokutana wakaona aibu na kutazama kwingine huku dhahiri wakionekana kusubiri kwa hamu misa ile ifike ukingoni ili wakaendelee na shughuli zao. Kwa kufanya vile nikafanikiwa kuyafukuza macho ya watu wengi na wale wachache waliokomaa kunikodolea macho nikawapuuza kwa kutoa kile kitabu kidogo cha sala na kuanza kukipitia ingawa fikra zangu kamwe hazikuwa pale kitabuni. Mawazo juu ya yule dereva wa teksi aliyetoweka katika mazingira ya kutatanisha kule msituni njiani bado yalikuwa yakiitafuna nafsi yangu.



     _____



     Sikuwa na shaka yoyote kuwa misa ile ilikuwa ikielekea ukingoni na wakati yule askofu akiendelea kuhubiri mimi macho yangu yalikuwa kitabuni kuununua muda huku nikijiuliza kama kweli nasaha zile zilikuwa zikiwaingia vizuri wale waumini akilini mwao au lah!. Hatimaye mawazo yangu yakahamia kwa Hidaya huku nikijaribu kufikiria namna atakavyosumbuliwa na maafisa usalama wa nchini Burundi mara baada ya lile gari nililokuwa nikilitumia la ubalozi wa Tanzania kuonekana katika maegesho ya viunga vya Le Tulip Hôtel Africaine.

     Sauti ya muungurumo wa gari lililokuja ghafla na kuegesha nje ya lile kanisa ikazirudisha fikra zangu mle ndani ya kanisa na hapo taratibu nikafunika kile kitabu kidogo cha sala mikononi mwangu na kugeuka nyuma nikitazama pale mlangoni. Kitambo kifupi cha ukimya kikapita na wakati huo nikashtukia kuwa watu wengi mle kanisani nao walikuwa wamegeuka nyuma kama mimi na kutazama kwenye ule mlango wa kuingilia mle kanisani huku wakionesha hamasa ya kutaka kufahamu ni nani ambaye angeingia mle kanisani baada ya muungurumo wa lile gari nje kufika ukomo.

     Muda mfupi uliofuata mara watu watatu wakaingia mle kanisani na muonekana wao ukanipelekea nishikwe kidogo na mduwao. Wanaume wale watatu walikuwa wamevaa suti nadhifu nyeusi na miwani myeusi machoni mwao. Miili yao ilikuwa imejengekea vyema kwa mazoezi ya nguvu na lishe ya uhakika. Urefu wao ulishabihiana na walikuwa weusi mno labda ningeweza kuwaita wajaluo kama siyo wenye asili ya Sudani ya kusini. Askofu wa kanisa lile akasita kidogo kuendelea na mahubiri baada ya kuwaona wale watu wakiingia mle ndani tukio lile likapelekea kanisa zima ligeuke na kutazama nyuma pale mlangoni kabla ya askofu yule kuendelea.

     Umahiri wangu wa kuzisoma vizuri sura za watu na tabia zao ukanitanabaisha kuwa wale watu hawakuwa waumini wa kawaida kwani kwa sekunde kadhaa wakasimama pale mlangoni wakiyatembeza macho mle ndani kisha nikamuona mmoja wao akitembea kwa utulivu katikati ya kanisa kuelekea mbele ambapo alitafuta sehemu na kuketi upande wa kulia. Mtu wa pili akatembea kwa utulivu huku akitafuta sehemu ya kuketi upande wa kushoto katikati ya lile kanisa. Yule mtu mmoja aliyesalia akayatembeza macho yake kutazama pale nyuma nilipoketi kabla ya kuanza kupiga hatua zake taratibu na hatimaye kuja kuketi nyuma yangu hali iliyonishawishi nitake kugeuka nyuma na kumtazama ingawa sikuthubutu kufanya hivyo. Sasa macho yangu yalikuwa makini kuwatazama wale wanaume wawili walioketi kule mbele ya kanisa na mara moja nikatambua kuwa kila mmoja alikuwa akijishughulisha katika kuzikagua kwa siri nyuso za watu waliokuwa mle ndani.

     Nilipoendelea kuwachunguza vizuri wale watu taratibu kumbukumbu zikanijia akilini na kupelekea kijasho chepesi kuanza kunitoka maungoni. Haraka nikawa nimemkumbuka mtu mmoja miongoni mwao kuwa alikuwa miongoni mwa wale watu wawili niliopishana nao wakati nikitoka kule Le Tulip Hôtel Africaine. Loh! harufu ya matata ikaanza kunijia akilini kuwa huwenda mlengwa wa ziara ile ya kushtukiza nilikuwa mimi na hapo nikaanza kujiuliza kuwa kama mimi ndiyo ningekuwa mlengwa wa ziara ile wale watu walijuaje kuwa mimi niko pale tena nikiwa ndiyo kwanza nimefika pale kanisani muda mfupi tu uliyopita?. Jibu sikulipata ingawa sasa nilikuwa makini zaidi na nyendo zangu. Hata hivyo bado nikahisi kuwa wale watu hawakuwa wameniona.

     Wakati nikiwa katika harakati za kuamua nini cha kufanya mara misa ile ikafikia ukomo na hapo tukaingia kwenye kipindi cha matoleo baada ya sala fupi kufanyika. Utaratibu wa matoleo ya sadaka ukatulazimu sote mle ndani tusimame na kuanza kupanga mistari miwili minyoofu katikati ya kanisa kuelekea mbele vilipokuwa vyombo vya matoleo. Nikasubiri watu wote wanyanyuke kwenye lile benchi nililoketi kisha nikaunga mstari huku yule mtu nyuma yangu akionesha kunitegea kwa hila ili nitangulie.

     Baada ya mgogoro mfupi wa nafsi yangu hatimaye nikaona kuwa nisingefanikiwa kufanya hila kwa kuwa foleni ile ilifuata utaratibu maalum kuwa watu wa benchi la mbele wangesimama na kuelekea mbele kutoa sadaka zao na kufuatiwa na watu benchi la nyuma. Hivyo kabla ya yule mtu nyuma yangu mimi ndiyo ningestahili kutangulia vinginevyo ningeonekana mtu wa ajabu. Bila kusita nikasimama na kuunga mstari huku macho yangu yakiwa makini kuwatazama wale watu kule mbele. Wale watu hawakuunga mstari kwenda kule mbele kutoa sadaka kama waumini wengine walivyofanya badala yake wakasimama wakitazamana kama wanaopeana ishara fulani kisha nikaona wakigeuka na kutazama pale nilipokuwa na tukio lile likanipelekea nishtukie kuwa wale watu walikuwa wameniona kwani haraka macho yetu yalipogongana wakayakwepesha macho yao pembeni na kutazamana huku wakijitia kuzirekebisha vizuri tai zao shingoni.

     Wakati nikifika katikati ya kanisa na kuunga ule mstari wa matoleo taratibu nikauingiza mkono kuipapasa bastola yangu kwenye mfuko wa koti langu na kitendo cha kuikuta bastola yangu ikiwa imetulia vyema mahala pake kikanifurahisha. Nilipogeuka kutazama nyuma macho yangu yakakutana na macho ya yule mtu aliyekuwa ameketi nyuma yangu muda mfupi uliopita yakiwa yamejificha nyuma ya vioo vyeusi vya miwani yake. Yule mtu akatabasamu kinafiki huku mkono wake mmoja tayari ukiwa umezama kwenye mfuko wa koti lake la suti na hapo nikajua nini maana ya tukio lile. Sikuwa na shaka kuwa yule mtu nyuma yangu alikuwa akinionya kuwa hila yoyote ambayo ningeileta alikuwa tayari kunichapa risasi. Hata hivyo yule mtu alionekana kucheza vizuri na akili yangu kwani hakutoa bastola kutoka kwenye mfuko wa koti lake la suti badala yake akatoa noti moja ya faranga ya kirundi huku akitabasamu na kuyapelekea meno yake meupe yaonekane bila kificho.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Pasipo kuonesha tashwishwi yoyote nikageuka na kutazama mbele huku nikitembea taratibu katika ule mstari kwenda kutoa sadaka. Wakati nikiendelea kutembea kwenye ule mstari mara nikawaona wale watu wengine wawili wakisogea taratibu kutoka sehemu zao walizokuwa na kunikaribia pale kwenye mstari huku kila mmoja akiwa ameutia mkono wake ndani ya mfuko wa koti lake la suti. Hisia zangu zikanitanabaisha kuwa nilikuwa nikiandaliwa mtego wa kukamatwa mzimamzima. Nikiwa tayari nimeishtukia hila ile nikajikuta nikitabasamu moyoni huku akili yangu ikifanya kazi ya ziada. Wale watu waliponifikia mmoja akatangulia na kujichomeka kwenye ule mstari mbele yangu huku yule mwenzake akitembea kando sambamba na mimi ingawa hakuingia kwenye ule mstari kupanga foleni.

     Taratibu nikageuka na kuyatembeza macho yangu mle ndani ya kanisani na umati ule wa watu ukanitanabaisha kuwa wale watu wasingeweza kuzitumia bastola zao katika mazingira yale hivyo nafsi yangu ikaniambia kuwa nilipaswa kurelax. Wakati tukilifikia kapu moja la sadaka mara nikamuona yule askofu aliyekuwa akiongoza misa akifunga vitabu vyake vya kuongozea misa kisha wasaidizi wake wawili wakasogea kwa unyenyekevu na kuvichukua vile vitabu na msalaba mkubwa kisha wakaanza kuondoka taratibu pale madhabahuni wakielekea kwenye mlango uliokuwa upande wa kushoto mbele ya lile kanisa. Walipoufikia ule mlango wakaufungua na kuingia mle ndani kisha ule mlango ukafungwa nyuma yao. Pale madhabahuni akabakia mtawa mmoja na watumishi wengine wa kanisa ambao bila shaka walikuwa wameachiwa jukumu la kufunga misa.

     Wale watu sasa walikuwa wamenikaribia zaidi mmoja mbele, mwingine nyuma na yule mwingine akiwa kando yangu. Sikupenda kuzongwa namna ile hivyo kwa kuwa pale mbele kulikuwa na vyombo vingi vya kutoa sadaka mara nilipofika pale mbele nikachepuka kando kukifuata chombo cha mbali zaidi cha kutolea sadaka. Wale watu kuona vile wakashtuka na kuanza kunifuata hata hivyo wakati wakinifikia tayari nilikuwa nimeshatia sadaka yangu kwenye kapu na kurudi haraka kwenye ule mstari hivyo wale watu wakapishana na mimi wakati nikirudi. Bila kupoteza muda nikaharakisha na kuunga mstari wa matolea kwa mbele huku nikiuchunguza ule mlango wa ofisi ya askofu. Kwa kufanya vile nikaona kuwa upande wa kushoto pale mbele madhabahuni kulikuwa na nguzo na kando ya nguzo ile kulikuwa na ngazi. Nilipozichunguza zile ngazi nikagundua kuwa zilikuwa zikielekea kwenye ule mlango wa ile ofisi ya askofu.

     Haraka nikageuka kuwatazama wale watu kule nyuma na hapo nikagundua kuwa walikuwa wakishangaa shangaa kwa kutoniona baada ya kutoka kutoa sadaka. Nafasi nzuri ambayo kamwe nisingeiacha iende hivihivi hivyo nilipoifikia ile nguzo ya kanisa nikachepuka kidogo na kuanza kupanda zile ngazi za kuelekea ofisi ya askofu. Watu wachache wakageuka na kunitazama kwa mshangao hata hivyo sikuwatilia maanani. Mara tu nilipoingia kwenye ile korido nikawaona wale wasaidizi wa askofu wakitoka kwenye kile chumba cha ofisi ya askofu kisha wakaelekea mbele hadi sehemu kulipokuwa na mlango mwingine ambapo waliufungua na kuingia mle ndani. Nikaendelea kutembea kwa tahadhari kwenye ile korido huku mara kwa mara nikigeuka nyuma kutazama. Sikuwaona wale watu hatari niliyowatoroka hivyo nikajua kuwa bado walikuwa wakinitafuta.

     Nilipoufikia ule mlango wa ofisi ya askofu sikubisha hodi badala yake nikaufungua ule mlango na kuingia ndani. Macho ya mwanaume mwenye umri wa miaka hamsini na ushei yakanipokea kwa chuki isiyoelezeka kana kwamba tulikuwa tukifahamiana hapo kabla. Mwanaume yule akiwa katika mavazi yake ya kitumishi nyuma ya meza kubwa yenye lukuki ya vitabu vya kiroho, majarida na maandalio ya masomo ya kanisa. Askofu yule akanitazama kwa hadhari huku akionekana kuwa na wasiwasi mwingi.

     Ile ofisi ilikuwa kubwa na ya kisasa. Upande wa kulia kulikuwa na kabati moja la mbao na makabati mawili mengine ya chuma na pembeni ya makabati yale kulikuwa na sanamu kubwa ya bikira Maria chini ya kalenda kubwa ya kirumi. Sakafuni kulikuwa zulia zuri la rangi nyekundu. Upande wa kushoto ukutani kulikuwa na rafu ya mbao iliyopangwa vitabu vya dini na juu ya rafu ile kulikuwa na mishumaa. Pembeni ya rafu ile ukutani kulikuwa na runinga kubwa iliyounganishwa na chaneli nyingi za dini. Mara moja tu nilipoingia mle ndani hali ya hewa nyepesi ikanifanya niyatembeze macho yangu mle ndani na hapo nikakiona kiyoyozi kimoja ukutani...

    "Bonjour”. Habari. Nikamsalimia yule askofu huku nikiupuuza mshangao wake.

    “Qu?est-ce que a besoin d?ici?”. Unataka nini hapa?. Yule askofu akaniuliza kwa jazba.

    “Une brève conversation, s?il vous plaît, puis-je rester?”. Maongezi mafupi tu na wewe, tafadhali ninaweza kuketi?. Taratibu nikaongea huku nikikisogelea kiti kimoja kilichokuwa mkabala na ile meza ya yule askofu. Chuki sasa ilikuwa dhahiri machoni kwa yule askofu hata hivyo nilikuwa tayari kukabiliana naye ingawa kwa namna nyingine nilishindwa kuelewa chuki kwa mtumishi wa Mungu kama yule ingetokana na nini. Hatimaye nikavuta kiti na kuketi baada ya kuchoka kusubiri ukaribisho rasmi kwani nilimuona yule askofu akiinama na kuendelea na hamsini zake kana kwamba uwepo wangu haukuwa na maana yoyote mle ndani. Nikachukizwa sana na aina ile ya dharau vinginevyo ningeweza kumtia adabu yule askofu hata hivyo lile halikuwa suala lililonifikisha pale hivyo nikaishia kujipa utulivu wa nafsi. Yule askofu akaondoa miwani yake usoni na kuiweka pale mezani kisha akayafikicha macho yake kivivu na kupiga mwayo hafifu kisha akaiegemeza mikono yake mezani katika uso wa chuki na ghadhabu kabla ya kuongea.

    “J?ai beaucoup de travail à faire, ce n?est pas temps pour rencontrer de gens. Qui vous a permis d?entrer dans mon bureau”. Nina kazi nyingi za kufanya, huu siyo muda wa kuonana na watu. Nani aliyekuruhusu uingie ofisini kwangu?.

    “J?ai besoin de parler avec toi”. Nahitaji kuongea na wewe. Uso wangu ukiwa mbali na mzaha nikaongea kwa utulivu huku nikimtazama yule askofu. Yule askofu akanitazama kwa mshangao kisha nikamuona akitabasamu kwa dharau kabla ya kuniambia.

    “D?accord, vous pouves parler”. Okay, zungumza.

     Hata hivyo wakati nilipokuwa nikijiandaa kutoa hoja yangu yule askofu akaniuliza.

    “Qui est-tu?” Wewe ni nani?.

     Swali la yule askofu likanipelekea niketi vizuri na kuiegemeza mikono yangu pale mezani na nilipomtazama machoni nikavunja ukimya.

    “Désolé pour le travail de Dieu. Je m?apelle Géorge Ntahimana”. Kwanza pole sana na kazi ya Mungu. Mimi naitwa Géorges Ntahimana. Wakati nikimaliza kujitambulisha mara nikashangaa kumuona yule askofu akitabasamu na muda mfupi uliofuata tabasamu lake likageuka kicheko kikubwa kilichoniacha na mduwao wa aina yake ingawa sikutia neno lolote. Yule askofu akaendelea kucheka kama mwehu na kicheko chake kilipokuwa ukingoni akavunja ukimya.

    “Utilise to nom de Tibba Ganza, tu sera bien éntendu”. Tumia jina lako la Tibba Ganza utaeleweka vizuri. Maneno ya yule askofu yakanifanya nishtuke huku nikishangazwa na kulijua jina langu. Kwa kweli nilistaajabu sana, sasa nilifahamu kuwa taarifa zangu nchini Burundi zilikuwa zimezagaa kila kona. Nimefahamika vipi na nani anayesambaza taarifa zangu?. Nikajiuliza bila kupata majibu hata hivyo sikuonesha tashwishi yoyote usoni.

    “Appelle-moi de toute façon”. Unaweza kuniita upendavyo.

    “Et pourquoi tu me menteque tu est Géorges Ntahimana alors que tu t?apelle Tibba Ganza?”. Sasa kwa nini unidanganye kuwa wewe ni Gèorges Ntahimana wakati unaitwa Tibba Ganza?” Yule askofu akaongea huku akiendelea kucheka.

    “Je ne t?ai pas menti, c?est toi quia voul de m?apelle ça”. Sijakudanganya ila ni wewe ndiye umeniita hivyo. Nikaongea kwa hasira kidogo huku nikianza kuchoshwa na tabia ile ya dharau.

    “D?accord, tu as quel probléme?”. Okay, una shida gani?. Yule askofu akaniuliza huku akinikazia macho.

    “J?ai bésoin de voir du prêtre Aloysius Kanyameza”. Nahitaji kuonana na padri Aloysius Kanyameza. Nikaongea kwa utulivu na hapo yule askofu akanikata jicho kama mtu anayetafuta hakika ya maneno yangu kisha akavunja ukimya.

    “Pourquoi?”. Unamuhitaji wa nini?.

    “Son amie proche”. Mimi ni rafiki yake wa karibu. Nikadanganya na hapo yule Askofu akaangua tena kicheko cha dhihaka.

    “Mais le prêtre Aloysius Kanyameza nest jamais dit nous àpropos de toi?”. Mbona padri Aloysius Kanyameza hakuwahi kutuambia juu ya habari zako?.

    “Peut être n?a fait cela pour ses propres raisons”. Huwenda alifanya hivyo kwa sababu zake binafsi. Maelezo yangu yakampelekea tena yule askofu aangue kicheko cha dhihaka kisha akavunja ukimya akinipuuza.

    “Ne mentes-moi parce-que je conais chaque chose à propos de toi. Est-ce-que tu pense que je ne conais pas que c?est toi qui lui a tue’?. S’il vous plais leve-toi et partir. Dieu te jugera à son”. Usinidanganye kwani nafahamu kila kitu kuhusu wewe. Unadhani sifahamu kuwa wewe ndiye uliyemuua?. Tafadhali simama uende zako. Mungu atakuhukumu kwa muda wake.

    “Vous ne saves pas de quoi vous parlez”. Hujui unachozungumza. Nikaongea kwa msisitizo na hapo yule askofu akanitazama kwa dhihaka kisha akavuta mtoto wa meza yake ya ofisini na kutoa picha nne ambazo alizitupia pale mezani mbele yangu bila kutia neno. Haraka nikasogea pale mezani na kuzitazama vizuri zile picha na mara moja nilipoziona nikashtuka sana. Zilikuwa ni picha nilizopigwa na kamera za usalama wakati nilipokuwa ndani ya kile chumba 403 cha Le Tulip Hôtel Africaine wakati nikiupekuwa ule mwili wa yule padri wa kizungu aliyenyongwa.

     Mara moja nikagundua kuwa huwenda picha zile zingekuwa zimenaswa na kamera maalum ya siri iliyokuwa imepandwa mle ndani. Nikaanza kujilaumu kwa kutokuwa makini kiasi cha kupigwa picha zile bila kushtukia. Lakini jambo moja lilikuwa limenishangaza sana. Picha zile ziliwezaje kumfikia yule askofu tena mapema kiasi kile?. Nani alifahamu kuwa ningefika pale hadi akatanguliza picha zile kuniwekea ukuta katika kupata taarifa muhimu za upelelezi wangu?. Maswali meni yakaanza kupita kichwani mwangu na nilipomtazama yule askofu nikaanza kuhisi kuwa alikuwa miongoni mwa watu wale hatari waliokuwa wakinisaka usiku na mchana.

    “Ce n?est pas moi qui là tué prêtre Aloysius Kanyameza”. Mimi siyo niliyemuua padri Aloysius Kanyameza. Nikaongea kwa utulivu huku nikiendelea kuzitazama zile picha kwa makini.

    “Je te conceille jeûne hôme di être loi de cette casse parce-que ton âme sera en danger”. Nakushauri kijana kaa mbali na hili suala vinginevyo uhai wako utauweka matatani. Yule askofu akaongea kwa hadhari huku akiviminyaminya vidole vyake pale mezani.

    “Je suis ici pour aider atraper celui qui là tue”. Nipo hapa kusaidia kumnasa yeyote aliyehusika na kifo chake.

    “Qui est mort?”. Kifo cha nani?. Yule askofu akaniuliza huku akiyafikicha macho yake na kisha kuitia miwani yake machoni na hapo akanitazama kwa utulivu.

    “Prêtre Aloysius Kanyameza”. Padri Aloysius Kanyameza. Nikaongea kwa msisitizo huku mawazo mengi yakipita kichwani mwangu kisha baada ya kukohoa kidogo nikaendelea.

    “Que-ce que tu pense come la cause de sa mort?”. Unadhani ni sababu ipi iliyopelekea kifo chake?. Swali langu likampelekea yule askofu taratibu aangue tabasamu la dharau huku akinitazama kisha akaegemea kiti chake cha ofini baada ya kuyabetua mabega yake.

    “Coment puis je connaitre?”. Mimi nitajuaje?. Lilikuwa jibu lililonikatisha tamaa sana na kunipelekea kwa sekunde kadhaa nimtazame yule askofu pasipo kutia neno ingawa akili yangu ilikuwa imezama katika kufikiri juu ya nini kilichokuwa kikiendelea. Taratibu nikayahamisha macho yangu na kuanza kuyatembeza mle ndani nikiichunguza tena ile ofisi kana kwamba ndiyo nilikuwa nimeingia mle ndani muda mfupi uliopita. Hisia za kushindwa katika harakati zangu zilikuwa zimeanza kunisimanga kiasi cha kunipelekea nishindwe kufahamu kama nilikuwa nikipiga hatua au nilikuwa nimejitumbukiza kwenye mkasa usiyonihusu. Taswira mbaya ya yule padri wa kizungu aliyenyongwa vibaya kwa waya na kutundikwa katikati ya chumba 403 cha Le Tulip Hôtel Africaine haraka ikaumbika tena akilini mwangu na kuibua hoja ambazo majibu yake yangehitaji mazingira rafiki.

    “Prêtre Aloysius Kanyameza a un amie qui sapelle Pierre Opango?”. Padri Aloysius Kanyameza amewahi kuwa na rafiki yeyote anayeitwa Pierre Opango?. Hatimaye nikavunja ukimya na kumuuliza yule askofu huku nikirejesha macho yangu kwake. Yule askofu akanitazama na mara ile hakutaka kutumia kifaransa tena katika maongezi yetu.

    “Nadhani swali hilo ni yeye mwenyewe ndiye anayeweza kukujibu”.

    “Ningekuwa na uwezo wa kuongea na marehemu huwenda wewe ungekuwa mtu wa mwisho kukufikia”. Maelezo yangu yakampelekea yule askofu anikate jicho lenye kila kaishiria cha kuchoshwa na maongezi yale kabla ya kuongea kwa utulivu huku akinitazama.

    “Muda siyo mrefu utapata nafasi nzuri ya kufanya mahojiano naye huko kuzimu”. Yule askofu akaongea kwa kujiamini kisha akasogeza nyuma kiti chake cha ofisini na kusimama huku akiendelea kunitazama. Maneno ya yule askofu yakawa yameniacha njia panda na hapo nikaanza kuhisi jambo la hatari. Hatimaye akavunja tena ukimya na kuendelea.

    “Najua kwanini upo hapa nchini Burundi, najua nini kilichokuleta hapa hivyo hakuna namna unayoweza kunificha Tibba”. Yule askofu akaweka kituo akikohoa kidogo kisha akaendelea tena.

    “Kwa miaka mingi nchi yako Tanzania imekuwa ikijizolea sifa nyingi kutoka kwa mabwana wakubwa wa nchi za magharibi eti kuwa ni kisiwa cha amani. Sifa hizo zimekuwa zikiwavimbisha kichwa na kuwapelekea mjione kuwa kweli mna amani kiasi cha kuingilia taratibu za nchi nyingine na kujipa nafasi za usuruhishi wa migogoro kana kwamba kweli mna amani wakati chaguzi zenu zinatawaliwa na mizengwe ya uibaji wa kura na ubadilishwaji wa matokeo. Tanzania haina amani labda niseme kuwa ina idadi kubwa ya wanaume wengi waoga kama wanawake”. Yule askofu akaweka kituo akinitazama ingawa nilipomchunguza nikagundua kuwa alikuwa akijipa utulivu katika kufikiri jambo fulani. Kisha akaendelea tena

    “Tanzania ndiyo nchi pekee ambayo waziri wake anaweza kutumia shilingi milioni kumi, pesa za wananchi walipa kodi kununulia mboga ya kula na familia yake, na bado wananchi wakamchagua tena ili aendelee kuwatumikia. Tanzania ndiyo nchi pekee ambayo waziri wake anatafuna pesa za walipokodi shilingi bilioni moja na kujinadi mbele ya waandishi wa habari kuwa eti pesa hiyo ni vijisenti tu, na bado raia wake wakakaa kimya bila kufanya chochote. Tanzania ndiyo nchi pekee ambayo kiongozi wa nchi anafanya safari zaidi ya 360 nje ya nchi kwa pesa za walipakodi huku raia wake wamekaa kimya bila kuchukua hatua yoyote.

     Tanzania ndiyo nchi pekee duniani ambayo wanyapori wake wanatoroshwa kwa ndege ya jeshi ya nchi nyingine kwenda ughaibuni huku viongozi wa nchi wakijitia kutofahamu chochote huku raia wake wakiishilia kulalamika majumbani mwao bila kuchukua hatua yoyote. Wapinzani wa vyama vyenu vya siasa wanakamatwa, wanapigwa, wanadhalilishwa na kusekwa rumande wakifunguliwa mashtaka ya kipuuzi huku raia wenu wamekaa kimya tu wasione tatizo lolote. Sisi siyo waoga kama nyinyi na tumeikataa hali hiyo. Tunataka kuona nchi ya Burundi yenye umoja na usawa na hatutaki katu kuingiliwa mambo yetu”. Yule askofu akaweka kituo na hivyo kunipa nafasi nzuri ya kuyatafakari vizuri maneno yake.

     Katika baadhi ya hoja zake niliona kuwa huwenda alikuwa sahihi kabisa lakini sikuona kama pale palikuwa mahala pake. Ni dhahiri kuwa askofu yule alikuwa ameshikwa na jazba na mara moja nilipomchunguza nikagundua kuwa alikuwa akifahamu mengi yaliyojificha nyuma ya kifo cha padri Aloysius Kanyameza kuliko nilivyodhani. Nikameza funda kubwa la mate kujipa utulivu nafsini mwangu huku macho yangu yakiendelea kumtazama yule askofu kwa makini na sasa alikuwa ametia mikono yake katika mifuko ya joho lake.

    “Nani aliyekupa habari zangu?”. Hatimaye nikavunja ukimya kwa kumuuliza yule askofu na hapo nikajikuta nikishtushwa na kicheko chake. Kicheko chenye kila mikogo ya dhihaka na kejeli.

    “Ningekueleza lakini nadhani hilo siyo suala lililokuleta hapa”. Hatimaye yule askofu akaongea huku akitabasamu na kwa mara ya kwanza nikajikuta nikikabiliana na msongo mkubwa wa mawazo. Nikahisi kuwa taarifa zangu zote sasa zilikuwa kiganjani kwa adui. Nani aliyewapasha watu wale habari zangu?. Nikajiuliza pasipo kupata majibu hata hivyo nilipomtazama yule askofu nikamuona kuwa ndiye angekuwa chanzo cha kwanza cha taarifa muhimu nilizokuwa nikizihitaji. Hivyo kichwani nikaanza kupanga mahesabu namna nitavyoitupa vyema karata yangu.

    “Nahitaji msaada wako tafadhali”. Nikaongea kwa sauti ya utulivu.

    “Chochote kuhusu masuala ya kiimani na kanisa…?”

     “Hapana, ni kuhusu padri Aloysius Kanyameza, chochote unachofahamu kuhusu kifo chake”

     “Unahitaji vipi taarifa za kifo chake wakati mshukiwa wa kwanza wa kifo chake ni wewe?. Unapoteza muda wangu bure hapa. Simama utoke ofisini kwangu”. Yule askofu akafoka kwa jazba na hapo nikasogeza kiti nyuma na kusimama.

    “Kama utapata nafasi ya kurudi nchini kwako salama nenda ukamueleze bosi wako kuwa kazi aliyokutuma imekushinda”. Yalikuwa maneno ya karaha na yenye kufedhehesha na mimi sikuwa tayari kamwe kukubaliana nayo. Hivyo nikapanga namna ya kumkabili yule askofu kibabe huku nikiamini kuwa angekuwa na majibu ya kuridhisha. Hata hivyo sikufanikiwa kwani wakati nikijiandaa kumkabili yule askofu nikajikuta nikitazamana na mdomo wa bastola yenye uchu mikononi mwa yule askofu. Koo likanikauka ghafla, baridi nyepesi ikaanza kusambaa mwilini mwangu huku mapigo ya moyo yakipoteza kabisa utulivu.

    “Huwendi kokote tulia hapohapo, huu ndiyo mwisho wako”. Yule askofu akanionya huku akiwa makini na nyendo zangu. Kwa kweli nilistaajabu sana kwa vile sikuwahi kufikiria kuwa kiongozi wa kiroho kama yule angeweza kuwa muumini namba moja wa mtutu wa bunduki na hapo nikashusha pumzi na kumtazama kwa utulivu.

    “Ni watu wangapi umefanikiwa kuwauwa kwa mkono wako hadi sasa?”. Nikamuuliza yule askofu kwa utulivu huku nikimtazama, lengo langu likiwa ni kuununua muda zaidi.

    “Wengi sana sikumbuki hata hivyo nafurahi sana kuua mtu kwa manufaa ya taifa langu”

     “Ni manufaa yapi unayoyazungumzia?”. Nikamuuliza kwa udadisi.

    “Wewe siyo raia wa nchi hii hivyo siyo rahisi ukanielewa”

     “Kwa hiyo kwa kuniua mimi unadhani kuwa utatimiza hiyo nadharia ya uzalendo dhidi ya nchi yako?”

     “Hilo halikuhusu, toa bastola yako na uiweke mezani. Nakusihi usithubutu kufanya hila kwani risasi yangu moja tu inaweza kubadili jina lako” Yule askofu akanionya na maneno yake yalikuwa dhahiri na hali ile ikanitia mashaka.

    “Nadhani hujui unachokifanya”. Nikaongea kwa utulivu huku akili yangu ikipiga mahesabu namna ya kujinasua kwenye hatari ile.

     Mdomo wa ile bastola ya yule askofu sasa ulikuwa umbali mfupi mbele yangu. Utayari wa kidole chake kwenye kile kilimi cha bastola ukanitahadharisha kuwa mtikisiko hafifu ungeweza kuruhusu risasi kupenya kichwani mwangu na kuacha tundu dogo linalovuja damu na huo ndiyo ungekuwa mwisho wangu. Hivyo sikutaka kupuuza hata hivyo wakati nikiendelea kufikiria namna ya kukabiliana na tukio lile ghafla mlango wa ile ofisi nyuma yangu ukafunguliwa kwa kasi ya ajabu na kabla sijageuka vizuri kutazama nyuma yangu nikazabwa kofi zito la shingoni. Haraka nikaupeleka mkono wangu mafichoni kuifikia bastola yangu. Bahati mbaya mko wangu ukaishia njiani kwani kwa mtindo hatari wa judo ule mkono ukadakwa njiani na kuzungushwa kwa kasi ya ajabu na kufungashwa mgongoni kwangu kisha nikachezea kichapo cha ngumi mbili makini za mbavuni. Mwili ukatengeneza mitetemo dhaifu, maumivu makali yakasambaa mwilini, mbavu zikabana na hapo kichomi dhaifu kikanipelekea niachame mdomo wazi na kuhema taratibu kama bata aliyemeza gololi ya moto.

    “Tulia hivyo hivyo kenge weh!”. Sauti kavu ya kiume kutoka nyuma yangu ikanionya. Muda uleule nikapigwa kabari matata shingoni iliyoniruhusu kuhema kwa shida na nguvu iliyotumika ilikuwa kubwa mno kana kwamba nilikuwa nimekaidi agizo. Sikuweza kufurukuta kwani kabari ile ilikuwa kama pingu kiasi kwamba kadili nilivyokuwa nikijitahidi kujinasua ndivyo kipenyo cha koo langu kilivyozidi kupungua. Wakati nikiwa katika harakati za kujipanga mara nikaanza kufanyiwa upekuzi wa haraka na mikono miwili makini iliyokuwa ikifanya kazi ile ikanitanabaisha kuwa nyuma yangu kulikuwa na wanaume wawili makini.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Zoezi la upekuzi hatimaye likafika ukomo huku bastola yangu na vitambulisho vyangu vikichuliwa na adui. Yule mtu alipomaliza kunipekua akageuka na kunizaba makofi mawili ya nguvu usoni na hivyo kunipelekea nione taswira tofauti za nyota kubwa na ndogo kabla ya kamasi nyepesi za damu kuanza kuchuruzika puani na maumivu niliyasikia ni kama niliyepigwa na kipande cha ubao wa mninga. Kiganja cha mkono wa yule mtu kilikuwa kimekomaa kama simenti.

    “Safi sana mwanaharakati wetu, tulikuwa na wasiwasi kuwa pengine ungeshindwa kumdhibiti huyu kunguni”. Yule mtu aliyenipiga kabari nyuma yangu nikamsikia akizungumza kwa sauti kavu ya kibabe. Nikashindwa kuelewa nani alikuwa akiambiwa maneno yale. Lakini kitendo cha kumuona yule askofu akitabasamu nikajua maneno yale yalimhusu yeye.

    “Kazi imekuwa rahisi sana kama mnavyoona. Hivi mlijuaje kuwa angekuja hapa?”. Yule askofu akawauliza wale watu huku bastola yake bado amielekezea kwangu.

    “Imekuwa kama bahati kwani tulipewa habari na François”. Yule mtu nyuma yangu akafafanua.

    “François ndiyo nani?”

     “Mwanaharakati mwenzetu dereva wa teksi tuliyempandikiza katikati ya jiji la Bujumbura”. Maneno ya yule mtu alitenipiga kabari nyuma yangu yakanipelekea nishtuke. Haraka nikawa nimemkumbuka yule dereva wa teksi aliyenitoroka kule barabarani msituni na kupitia maelezo yake sikuwa na shaka yoyote kuwa ndiye aliyesemekana kuwapasha habari zangu wale watu hatari. Loh! kwa kweli sikuwa nimemfikiria kabisa yule dereva wa teksi hata chembe kuwa angekuwa miongoni mwao.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog