Simulizi : Shujaa Wa Taifa
Sehemu Ya Nne (4)
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mara katika hali isiyotarajiwa G master kijana hatari na mratibu wa mauaji ya watu wote na matukio mabaya wa banguli akaruka na kuupiga mkono wa banguli ambapo bastola ikadondoka kutoka katika mkono wa banguli.
Bila kuchelewa akamuwahi banguli na kumkaba shingo kwa mkono wake huku akifuatiwa na kumuwekea bastola kichwani.
“Zarish njoo huku!” akaongea G master huku akimwelekeza Zarish akae nyuma yake.
Zarish akatii!
“nipisheni nyie wapumbavu la sivyo namuua mkubwa wenu” akapaza sauti G master kuwaelekezea walinzi walioshika silaha zao kumuelekea yeye.
G master akawa akiwageuka huku na huku bado akiwa kashika silaha kujaribu kujilinda, banguli bado yupo mikononi mwake.
Wakafanikiwa kutoka nje.
Akaamuru afunguliwe mlango wa gari atumiayo waziri huyo ambayo ilikuwa ni bullete proof huku ikisemekana kuwa na speed ya ajabu zaid ya gari zote jijini ntovo.
Akafunguliwa milango ya gari hilo.
“fungueni geti kabla sijatoa ubongo wa mkuu wenu na hakikisheni mnaweka silaha zenu chini” akazidi kuongea G master aliyemweka telo Banguli.
Rafiki zake watatu G master afanyao nao kazi za banguli mara zote, wakaingia ndani ya gari hilo wakifuatiwa na mwanadada Zarish.
Gari ikawashwa nah apo ndipo G master akamsukumia Banguli pembeni na yeye kuingia ndani ya gari hilo na kufunga mlango.
Risasi ndizo pekee zililindima kuifukuzia gari hiyo iliyoanza kuondoka kwa kasi kutokea getini mwa jengo hilo.
Bila kuchelewa askari nao wakachukua magari yao na kuanza kuifukuza gari hiyo.
Mtaani ikawa ni patashika nguo kuchanika, risasi tu ndizo zilizokuwa zikiungurumishwa kutoka katika gari za maaskari kuielekeza katika gari ya G master na wenzake ambapo ndani yake akiwepo mwandada Zarish aliyesababisha yote hayo.
Askari hao walijaribu kulenga magurudumu ya gari hiyo ili wapate kuidondosha kama walivyojua gari hiyo ilikuwa na bullete proof kwahiyo mahali pengine tofauti na magurudumu hakutakuwa na badiliko lolote la gari hiyo.
Bado gari aliyomo G master na wenzake ikazidi kusaga lami kuwaepuka askari hao wenye hasira kali. Na kwakuwa gari hiyo ilikuwa na speed kuliko gari lolote la katika ofisi ya waziri yule hivyo maaskari walifanikiwa kuachwa kwa umbali mrefu mno na hata baade kupotea kabisa machoni mwao gari hilo.
Na baadae walipokuja kuliona gari hilo lilikuwa ni tupu limeshatelekezwa pembezoni mwa barabara.
Hasira ndizo pekee zilimtawala banguli baada ya ripoti hiyo ya kutokamatwa kwa G master na wenzake. Hivyo akawaamuru askari wa nchi nzima wahakikishe G master na wenzake wanatiwa mikononi eidha wakiwa wazima au wamekufa.
Mikakati ya kuitekeleza oda hiyo kutoka kwa mkuu ikaanza mara moja.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
***
G master na wenzake wakiwa na mwanadada Zarish walipofanikiwa kuwaacha askari wale hawakuchelewa, hivyo wakaamua kuingia ndani ya msitu wa tini kwa ajili ya kuokoa Maisha yao.
“nimechoka kweli!” Zarish aliongea huku akimaanisha lile aliongealo kwa kuketi chini.
“jikaze twende, hapa bado haijawa sehemu salama kabisa kwa Maisha yetu twende mama!” G master akaongea huku akiushika mkono wa Zarish.
“hapana siwezi kwenda Zaidi, n ahata nikienda huko tutaishia wapi si bora tu nibaki hapa waniue”
“unasemaje wewe?” kijana mmoja wa G master akauliza huku akiukunja uso kumsogelea Zarish,”yaani si tumehatarisha Maisha yetu kwa ajili yako alafu unaleta uku**, si bora ungebaki kule kule ufe” kijana huyo akaongea kwa jazba huku akitaka kumnasa kibao Zarish, lakini G master akamzuia.
Mara,” hands up!” ikasikika sauti kuwaelekea.
Wote wakashtuka na walipogeuka wakakutana na sura zilizojikunja haswa kumaanisha lile wanalolisema, bastola kuwaelekezea.
Alikuwa ni mwanadada tiffa pamoja na makomandoo saba waliolihasi jeshi la zambe. G master na kundi lake hawakuwa na ujanja Zaidi ya kunyoosha mikono juu.
Tiffa alivyomtazama Zarish alimkumbuka kuwa ni msanii maarufu mno katika nchi ile na mpaka hatua ya mwisho mwanadada huyo kuwa kibaraka wa banguli adui wa wananchi mheshimiwa banguli alizipata, hivyo kumuona mwanadada huyo mahali hapo aliamini kabisa itakuwa ni mtego wa serikali kuja kuwakamata wao.
Si Zarish tu hata uwepo wa G master kijana mwarifu ambaye serikali ilimbeba, moja kwa moja aliikubali Imani yake kuwa ujio wa vijana hao basi yawezekana umbali si mrefu kuna maaskari, umakini wa hali ya juu ukamvaa.
“nyinyi ni wakina nani?” mmoja wa makomandoo kati ya makomandoo wale saba aliongea huku akiilekeza bastola yake kwa mateka wao.
“naomba ushushe silaha tutawaeleza, maana sisi ni kama nyinyi tu” G master aliongea huku akiwa kanyoosha mikono yake juu baada ya kuwagundua vizuri watu wale ambao hata yeye alipewa misheni ya kuwatafuta baada ya taarifa iliyokuwepo kuwa vijana hao wamehasi jeshi.
“ongea hivyo hivyo we kibwengo!” tiffa aliye na hasira kali hasa ukizingatia kumpoteza mtu aliyempenda akaongea kwa jazba.
“sisi tulikuwa ni wafanyakazi wa waziri banguli ambaye ndiye rais wa hii nchi nyuma ya pazia, huyu dada kipindi yupo pale aliweza kung’amua siri ya kuteswa kwa mwandishi nguli bwana Afordias ndani ya nyumba ya waziri yule…” CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Afordias!!??? Huyu huyu?” makomandoo wote akiwemo na tifa wakauliza kwa mshangao, iweje wanazipata taarifa za mtu aliyesemekana kufa siku nyingi eti kumbe yupo mzima tena ndani ya nyumba ya kiongozi? Huku serikali yenyewe ilitangaza kutompata mtu huyo. Hilo ndilo lililowafanya washtuke.
“ndio huyo huyo, kiukweli hajafa yupo hai na aminini banguli ndio mtu mbaya katika nchi hii na mkubwa wa majeshi kwani wanafanya kazi kwa kushirikiana kwa ukaribu mno, rais kawekwa chini ya ulinzi na watu hawa” G master akatoboa siri
“nmmh” tiffa akaugumia kuonesha lile alisikialo ni geni kwake.
“aya endelea huyo mwanadada alivyong’amua siri za pale ikawaje?” komandoo akamwamuru aendelee na story yake.
Basi G master akaendelea kusimulia harakati zote zilizotokea hadi yeye kutoroka na mwanadada Zarish akiwa na wenzake.
“ ha ha ha ha ha ha haaaa” mwanadada tiffa akashusha silaha yak echini huku akijawa na kicheko mara baada ya kusikia habari ile.
Wote wakamshangaa hawakujua nini kilikuwa kikimchekesha kiasi hiko.
Alicheka na kufanya ainame na hata kufikia hatua ya kudondoka chini kwa kunogewa na kicheko hicho. Sio kundi la G master pekee lilikuwa likimshangaa hata wenzake pia walimshangaa kwani hawakujua ni nini kimemsababishia mwenzao acheke vile.
Tiffa baada ya kuridhika na kicheko chake akasimama na kuanza kuongea huku kicheko kikionesha bado kipo kwani aliongea huku akicheka.
“mlidhani ule msemo wa akimaliza kwetu atakuja na kwenu uliwekwa tu eee? Nadhani leo mmeuelewa maana ya msemo huu, nyinyi sin do mlikuwa mnashirikiana nae kutoa roho za watu na hata wakina wananchi tulipokuwa tunasema mkaona oooh wanaongea shiiit, BANGULI is an evil wallahi mnaona sasa yaliyowakuta?” tiffa aliufikisha ujumbe huo wa maneno ambao kwa kweli uliwachoma mno G master, Zarish na wenzake wakabaki kukiri kwa mioyo yao.
Mara wakiwa wanaendelea na mazungumzo yao, wakasikia milio ya gari ambazo zilikuwa zikipita kwa kasi katika barabara ipitayo nje ya msitu huo.
Wote wakashtuka!
Wakaandaa silaha zao vizuri!
Taratibu wakajisogeza karibu na barabara hiyo kuangalia kuna nini. Walifanikiwa kuona msululu wa gari za polisi zikipita kwa kasi katika njia hiyo.
“tondokeni!” komandoo mmoja ambaye ndiye alichukua uongozi mara baada ya kupotea kwa D’oen akapaza sauti kutoa amri.
Wote wakakimbia kutokomea ndani zaid ya msitu huo!
hapo ndipo muungano wa makundi mawili hayo ukaanza.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
****
Jenerali Hambabe akiwa kwa kunyenyekea anaonekana ofisini kwa waziri banguli ambapo kuna mambo yamempelekea kutaka kuzungumza na mkuu huyo wa nchi.
Bila kuchelewa anakaribishwa katika ofisi hiyo na kuanzisha mazungumzo na waziri huyo kiburi na gaidi mwenye majivuno.
“mheshimiwa kuna jambo moja nahitaji tulijadili, nadhani hilo jambo laweza kuwa na manufaa kwetu sisi sote” Hambabe akaanzisha mazungumzo hayo.
Banguli akabaki kumsikiliza kwa umakini wa hali ya juu.
Hambabe akaendelea kuelezea swala lake.
“kuna ishu hii ya mitandao” akaongea huku akisita kidogo kusoma upepo wa waziri huyo aliyemuogopa kupita maelezo, alipoona hakuna reaction mbaya katika sura ya waziri huyo ndipo akaendelea.
“unajua sasa hivi kama jeshi tupo katika kipindi kigumu mno, kuna makomandoo wamehasi jeshi ni kitu ambacho ni kibaya kuliko ubaya wowote. Sasa hatujui hawa wanajeshi wapo wapi na wana mipango gani kupitia sisi, uoni ni hatari hii?”
“enheee nini point yako naona unazunguka kiongozi ebu twende na muda” banguli aliyejawa na kiburi akaongea.
“nachoomba ni hivi network system ya nchi ifunguliwe ili tuweze kuwasaka hawa watu kiteknolojia Zaidi ambapo hatutatumia nguvu nyingi, na naamini utaporuhusu na mitandao ya kijamii kupitia data bsae za watu mbalimbali tutawapata tu” akaongea mkuu huyo wa majeshi ambaye hakuwa na kauli mbele ya banguli.
Banguli akakaa kwa muda kidogo akifikiria kabla hajaongea
“ vipi haitoweza kuleta shida habari zetu za ndani kusambaa na hatimaye kufikia kufika kwa umoja wa mataifa?”
“ hiyo haina shida mkuu, wewe ruhusu tu tutaweka sharia kali za kimitandao zitakazofanya mtu yeyote hasitoe taarifa iusiayo nchi hii, trust me lazima tuwakamate”
“mmmh bado napata ukakasi wa hilo, nahisi kama sio jema”
“hapana mkuu hili la kuzuia mitandao ndio baya Zaidi kwani hata nchi ingine itakapokuwa imepata taarifa zetu na kuamua kupanga mikakati ya kuvamia tutapata wapi taarifa? Turuhusu tu!”
Basi baada ya ushawishi wa mkuu huyo katili wa majeshi kwenda kwa waziri katili wa mambo ya ndani ya nchi, wakakubaliana kuifungulia mitandao ya kijamii.
Na haikuchukua muda mitandao sasa ikawa wazi.
Hakika hilo likawa ni kosa.
Wananchi walifurahi mno kwani haikuwa tu kunyima uhuru wa mawasiliano bali pia kiliweza kunyima ujiingiziaji wa kipato kwa raia wan chi hiyo waliotegemea biashara za mitandaoni yaani online trading. Kwahiyo kufunguliwa kwa mitandao hiyo ikawa ni moja ya hatua kuelekea ushindi kwa wananchi wan chi ya zambe.
Hata upande wa kundi la G master walioungana na makomandoo walioamua kulihasi jeshi kwa ajili ya kuitetea nchi waliifurahia hatua hiyo iliyofikiwa na serikali hiyo.
Hivyo kupitia simu zao za mikononi waliweza kuperuzi vitu mbalimbali vitakavyoweza kuwasaidia kuweza kuikomboa nchi.
Mwanadada tiffa akiwa anapitia mtandao wa youtube alifanikiwa kunogewa na kipande kimoja cha utangulizi wa simulizi iendayo kwa jina la DUKA LA ROHO. Utangulizi ule uligusa kabisa hali ya nchi yake na mchakato wake mzima wa kutaka kupata technique kali za kivita.
Alipoamua kuifuatilia simulizi hiyo ndipo aligundua kuwa inapatikana katika channel ya simulizi mix.
Uamuzi wa kusubscribe kwa ajili ya kuendelea kuburudika na mbinu zilizotumiwa na frank man mansai kuiokoa nchi kutoka kwa majambazi ukamjia.
Mbali na kuburudika aliweza kusoma mbinu mbalimbali zilizotumiwa na kachero huyo katika harakati za ukombozi wa taifa lake. Wewe mpenzi msikilizaji unaweza ipata simulizi hii ndani ya youtube chanel ya simulizi mix kwa kusbcribe kabisa ili kuweza kujua ni mbinu zipi hizo zilizotumiwa na frank mansai.
Basi kupitia faida za mitandao ya kijamii, makundi hayo mawili lile la G master na wenzake pamoja na tiffa na makomandoo waliweza kujinoa na kuanza mikakati mipya ya kuweza kuikomboa nchi yao mara baada ya mkakati ule wa awali kufeli.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
****
MWAKA MMOJA BAADAE
Ndani ya mji mdogo wa kitibi mbali kidogo na jiji la ntovo kwa takribani kilometa 120 katika nchi ya zambe kunazuka tafrani kubwa mara baada ya kutokea mauaji ya ghafla na kibaya Zaidi wengi waliokuwa wakiuawa ni watendaji wa serikali pamoja na watumishi wa jeshi la polisi.
Nchi nzima iliingia taaruki wananchi walihama makazi yao kwa kuhofia vifo hivyo.
Magaazeti na vyombo mbalimbali na mitandao ya kijamii pia ilinogeshwa kwa habari hiyo ya kusikitisha.
Si wananchi tu ndio waliokuwa wakitaharuki kutokana na hali hiyo bali hata serikali kuu pia nayo ilikuwa ikishangaa tukio hilo lililogeni kabisa katika nchi hiyo.
Kikao cha kwanza kabisa cha siri kilichohudhuriwa na wajumbe wake wanne yaani waziri banguli, mkuu wa majeshi jenerali Hambabe, waziri mkuu na IGP wa jeshi la polisi kilijadili swala hilo hili kuhakikisha kuwa hakuna yeyote kati yao aliyepanga tukio hilo. Kwasababu waliamini wao ndio wapangaji wakuu wa matukio ya kimauaji nchini humo. Lakini cha kushangaza hakuna hata mmoja aliyekubali kuwa yeye ndiye amepanga mauaji hayo.
Hapo ndipo hofu zikazidi kutanda mioyoni mwao. Kama si wao basi ni nani? Wakati wao ndio waasisi na waanzilishi wa matukio yote ya hatari nchini humo? Wakabaki na sintofahamu kubwa.
Hivyo mikakati ya kutuma askari wao eneo hilo ili wakapambane na watu hao waliozuka ghafla ukaanza.
Hali hiyo ikawa imesambaa katika maeneo mbalimbali duniani mara baada ya swala hilo kushikiliwa ipasavyo na dada mmoja aliyejizolea umaarufu mitandaoni fetty diva mara baada ya kuwaamasisha wananchi washirikiane na hao wauaji ili waweze kuwaua maaskari ilimradi ukombozi kutoka katika vifungo kwa wananchi hao uweze kupatikana.
Serikali ilitamani iweze kupambana na binti huyo, basi kipind banguli akiwatuma askari wake katika mji wa kitibi wengine aliwatuma kwenda kumkamata mdada huyo nje kidogo ya nchi ya zambe katika visiwa vya kuzu lakini hawakufanikiwa kutokana na utata wa binti huyo. Je binti huyo alikuwa na utata gani? Na kwanini aliamua kuitendea hivyo serikali? Ebu tuendelee utapata kujua majibu ya hayo yote.
Askari kundi la kwanza lililopelekwa yalirudi majina yao tu miili yote iliachwa huko.
Katika hali nyingine ya taharuki iliyozuka ni pale wauaji hao walipoenda mbali na kuteka wananchi, tena wanamume ndio waliokuwa wakitekwa.
Kundi lingine la maaskari walitumwa kwenda kupambana na watu hao lakini nao hawakuweza kubadilisha lolote Zaidi ya kurudi majina yao tu huku wenyewe wakiwa ni maiti tupu.
Serikali ili kuondoa hofu swala hilo la mauaji hayo kwa wananchi ndipo wakazuia vyombo vya habari au mwandishi yeyote kwenda kuchukua taarifa eneo hilo na kuzisambaza.
Hakika hiyo ilikuwa ni njia pekee kweli ya kuweza kupunguza hofu kwa wananchi wasiojua nini chanzo cha mauaji yale kwani habari za mauaji hayo zilipungua!
Na kwa mbali hofu ya wananchi juu ya swala hilo ikaisha lakini ukweli wa mauji wa askari na viongozi wa serikali ukabaki pale pale.
***
Mwandishi na mtangazaji mahiri kutoka katika redio ndogo ndani ya mkoa wa njozo bwana felix mwenda anasikitishwa na habari zile za mauaji yanayoendelea kuwasakama askari wa n chi yake. Na kinachomuuma ni kile kitendo serikali kutoruhusu waandishi kuweza kuandika taarifa ile.
Ndipo kwa kujiamini anaamua kuchukua vifaa vyake na kufunga safari kutokea mkoani kwake hadi katika mji wa kitibi yanapoendelea mauaji hao.
Umahiri wake katika kuchukua matukio ya mauaji ndani ya mji huo na kuchambua habari hizo licha ya zuio la serikali la kusambaza habari za mauaji hayo, yeye anaamua kupingana na serikali na kuamua kurusha habari hizo kwenye mitandao ya kijamii na hata kwenye gaazeti mama la UPENDO alilokuwa akiliuzia habari hizo. Hali hiyo ilimpelekea umaarufu mkubwa na kujikuta kila kona likitajwa jina lake.
Hata mara kibao mwanadada fetty diva katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram alitokea kumsifia mara kibao na kuwaambia waandishi wengine waache uoga na waige mfano kutoka kwake.
Felix aliendelea na kuzichambua habari za huko lengo likiwa ni kuhakikisha taarifa hizo zinafikiwa kila mahali. Alishangaa uamuzi wa serikali wa kuzuia utangazaji wa matukio ya huko. Hakuona umuhimu wa kuweka siri ilihali wananchi na askari wao wanaendelea kupotea tu.
Basi hali hiyo ikazidi kuendelea. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hapo ndipo serikali ikaamua ilitume jeshi lake la wananchi wa n chi hiyo kwenda kushughulikia wauaji hao mara baada ya polisi na majeshi mengine ya usalama kushindwa kufanya lolote juu ya mauaji hayo.
Jeshi likaingia na kuweka kambi katika jiji hilo kwa siri.
****
Timu nzima ya mwanadada tiffa, makomandoo na ile ya G master walifurahishwa mno na taarifa za kuuwawa kwa viongozi wa serikali na askari kwani kitendo kile walikiunga mkono mno ni kama aliyekuwa akifanya mauaji hayo alikuwa katika mipango yao.
Ila kihere here cha kutaka kugundua huyo anayesimamia mpango mzima wa mauaji hayo ni nani kikawavaa.
Hivyo bila kuchelewa na wao kwa usiri mkubwa wakaianza safari yao kutoka katika msitu watini walikojificha awali na kuelekea katika mji wa kitibi yanapoendelea mauaji hayo.
Walifanya hivyo kwa lengo la kuongeza nguvu kwa wauaji hao na vile vile kwakuwa askari wengi walikuwa wakitumwa kwenda katika mji huo basi hiyo ilikuwa ni point yao ya ushindi kuweza kuwavamia kwa kuwashtukiza askari hao, ikiwa ni moja ya kuwapunguza askari hao.
Baada ya safari ya mwendo wa muda mrefu na misukosuko ya hapa na pale kuhakikisha hawaonekani, kwasababu tayari walikuwa ni watu wanaotafutwa na serikali wakafanikiwa kufika ndani ya mji huo. Wanaweka kambi msituni.
Wanachimba mahandaki na kutulia na kuanza kupanga mikakati ya wapi pa kuanzia na jinsi ya kumpata muuaji huyo.
Kupitia akiba zao za vyakula wanatoa na kuanza kula!
Siku hiyo ikapita bila kupata dalili zozote za muuaji lakini habari za kuuliwa kwa askari walizipata ndani ya mji huo huo waliofikia.
Siku iliyofuata asubuhi na mapema mwanadada tiffa anaonekana ndio wa kwanza kuamka kutoka katika handaki alilojihifadhi. Anapiga mwayo mreefu na kuichukua silaha yake, anaiweka begani na kuanza safari ya kutafuta sehemu ambayo angeweza kujisaidia.
Akiwa mbali na eneo hilo alilowaacha wenzake wakiwa bado wamelala, anafanikiwa kujiificha tayari kwa kujisaidia. Mara akahisi kuna mtu nyuma yake akimsogelea.
Umakini wa hali ya juu unamuingia na hapo ndipo kwa haraka anainyakuwa silaha yake na kugeuka nayo mazima akiwa kasimama!
Uso kwa uso na mdomo wa pistol ulioelekezewa kwake ambapo na yeye anafanikiwa kuinyoosha silaha yake kubwa.
Wanabaki wote wawili wameganda wakinyoosheana silaha zao!
Waliendelea kuganda kwa kunyooseana silaha hizo hadi pale mwanamume mrefu aliyevaa kofia ya kijeshi alipovua kofia hiyo kutoka katika kichwa chake huku akishusha silaha yak echini taratibu.
Tiffa hakuyaamini macho yake, ilibaki kidogo azimie kwa furaha.
“D’oen!” tiffa akaita huku bado akiwa kwenye mshangao
“ndio mimi mama!”
Tiffa akatupa silaha chini na kumkimbilia D’oen kisha kumkumbatia kwa furaha.
Akamkumbatia huku akili
“jaman D kumbe upo hai baba!” aliongea tiffa kwa masikitiko makubwa mno huku machozi yake yakilowanisha bega la D’oen.
“nipo hai mama!” D’oen akaongea kwa uchungu huku na yeye akilia kiume.
Hakika ilikuwa ni furaha ya ajabu kwa mwanadada tiffa. Ni vipi mpenzi msikilizaji mtu uliyepotezana nae muda mrefu na kufikia hatua hata ya kujua kuwa amefariki lakini unakutana nae? Ni ipi furaha yake? Hakika ni furaha ambayo haina mfano.
“kwanini upo hapa tiffa?” D’oen akauliza baada ya kuachiana kutoka katika kumbatio hilo.
“ni story ndefu D kwanza hapa sipo peke yangu! Nipo na wenzangu tumeweka kambi kule” tiffa akaongea huku akionesha upande wa kambi yao.
“oooh kwahiyo bado upo na makomandoo wangu?”
“ndio nipo nao, na wewe kwanini upo hapa?” tiffa akauliza
“kwani hujasikia taarifa kuhusu mauaji ya viongozi wa serikali na pamoja na askari?” D akamuuliza swali badala ya kujibu moja kwa moja swali lake lile.
“nimesikia”CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“basi mimi na timu yangu ndio wasababishaji, nilikuahidi tiffa lazima nihakikishe serikali hii inaondoka madarakani kwa hali yeyote ile na hata aliyesababisha mauaji ya baba yako atakufa na yeye soon!” D’oen akaongea kwa msisitizo wa hali ya juu.
“ilikuwaje na risasi zote zile hukufa?”
D’oen akacheka baada ya swali hilo.
“nilikuambia komandoo siku zote hafi na hata akifa kabla hajatimiza lengo lake basi lazima damu yake ilipize kisasi, twende nikaonane na timu utajua tu haya yote” D’oen akaongea huku akimshika tiffa mkono na kuelekea kwa upande waliopo timu ya tiffa.
Tiffa alifurahi mno na ile faraja yake ikarejea akajiona kama tayari ameshashinda vita hiyo na yupo na D’oen wakianza Maisha yao mapya.
Kumbe haikuwa hivyo safari bado ilikuwa ndefu mno tena mabonde na makorongo ndio njia yao katika safari hiyo.
Wakawafikia ambapo waliwakuta tayari wameshaamka!
Makomandoo wakabaki wameshangaa na kama isingikuwa komando mwenzao huyo kuwepo na mwanadada tiffa mahali hapo nadhani wangekimbia maana walibaki wameduwaa wakimtazama!
Tiffa akabaki akiwa mwenye tabasamu nene!
Zarish alimkumbuka vizuri D’oen siku ile walipokutana katika bar ya kismart. G master nae alimfahamu vizuri D’oen licha ya kukutana bar ya kismart na kukorofishana, lakini pia usiku walipofika katika eneo hilo yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kukutana na D’oen.
Ilikuwa ni kipindi alipowaacha wenzake na kuelekea eneo la mbali kidogo kwa ajili ya kuzurura. Njiani ndipo alikutana na D’oen na kwakuwa walikuwa na visa tangu kismart bar ambapo G master alimletea ubabe D’oen hivyo baada ya kukutana walianza kuzichapa kavu kavu huku kila mmoja hasijue lengo la mwenzake kuwepo eneo hilo.
Ngumi zao ziliendelea hadi pale waliposhtuliwa na risasi zilizowakosa kosa na kugonga miti kutoka kwa wanajeshi wa zambe.
Kila mmoja alikimbia kivyake.
Hivyo kitendo cha kukutana wote tena mahali hapo kama timu kiliwaacha na maswali vichwani mwao.
D’oen akatabasamu kisha akamfuata G master na kumpiga piga begani kama ishara ya Amani na upendo.
“kama umejigundua na kuamua kuwa mtu mwema huo ndio uanaume, jana nilivyokuona nilifikiri umekuja na jeshi la banguli” akaongea huku akiwa mwenye tabasamu tele.
G master akabaki mwenye matabasamu mfululizo.
“na wewe mrembo umefikaje katika timu hii ya kazi, risasi na viuno wapi na wapi?” D’oen akaongea kidhiaka huku akimshika shavuni Zarish.
Zarish akabaki ameinamia chini akiona aibu.
“master imekuaje kwani mbona mi iselewe ujue” komandoo mmoja akaongea huku akimuangalia D’oen kwa mshangao.
D’oen akamtazama komandoo huyo kwa bashasha kabla ya kujibu
“komandoo huwa hafi, mmeisahau hii kauli ya mwalimu wetu achebe aliyetufundisha kozi hii ya ukomandoo?”
D’oen akatoa kauli hiyo kutoka kwenye kinywa chake na kufanya makomandoo wenzake waikumbuke kauli hiyo. Wakatikisa vichwa vyao kukubali.
“ndio master lakini tunaomba utueleweshe ilikuwaje kuwaje hadi leo hii tunakuona hai ilihali nchi nzima ilijua ushakufa?” komandoo mmoja akaongea kwa shauku ya kutaka kujua.
D’oen akatafuta sehemu nzuri na kuketi, wote wakamsogelea.
“ni uwezo wa mung utu mimi kuwa hai, na yote haya wa kushukuriwa ni mwanadada fetty diva” aliongea kauli hiyo bado akiwaacha wenzake kwenye dimbwi la maswali lukuki.
“fetty diva huyu huyu wa mitandaoni?” tiffa akahoji kuonesha kutokubaliana na kauli ya D’oen. Ni vipi mwanadada yule ambaye hakuwa hata na nguvu ya kuongoza jeshi ashukuriwe na mwanakaka komandoo? Akabaki ameganda akisubiri jibu kutoka kwa D’oen.
“yea huyo huyo, na naweza sema bila yeye wote nyinyi msingeniona leo hii, ana ubinadamu sana yule dada, ana roho ya utu vile vile hapendi kuona mnyonge akidhurumiwa haki yake” D’oen akaongea.
“enhee tuambie kivipi kakusaidia”
D’oen akaachia tabasamu pana kisha akaanza kutoa hadithi nzima tangu anapigwa risasi hadi leo hii kuonana na wenzake akiwa mzima.
JINSI ILIVYOKUWA
D’oen baada ya kushambuliwa na risasi kadhaa kutoka katika mikono ya waziri banguli, alijitosa ndani ya bahari baada ya kuruka kutokea darajani.
Japokuwa maumivu ya risasi zile alikuwa akizisikia ila alijitahidi kuweza kupotea eneo hilo. Ilikuwa ni bora kwake aweze kuuliwa na chochote ndani ya maji hayo kuliko kujisalimisha katika mikono ya banguli kwani kwake aliona ni ishara ya udhaifu na isingekuwa na maana ya yeye kwenda miezi tisa kuenyea ukomandoo.
Kipindi alipokuwa mafunzoni katika mafunzo ya ukomando aliweza kufundishwa jinsi ya kuvumilia kwa muda mrefu ndani ya maji bila kupumua.
Hivyo kupitia mafunzo hayo aliweza kustahimili hali ile ya majini na kufanikiwa kupiga mbizi kwa muda mrefu kuweza kujikimbiza katika eneo lile.
Aliweza kutembea chini ya maji kwa umbali mrefu mno na huko ndipo akajiibua.
Lakini kadri alivyokuwa akijitahidi kuogelea kulitafuta eneo la nchi kavu ambapo kwa macho ya kawaida hakuweza kuona ndipo nguvu zilivyokuwa zikimuisha hasa hasa kutokana na maumivu ya mwili wake kutokana na risasi zile.
Akiwa katika hatua ya mwisho ya kukata tamaa ikambidi amwombe mola wake hata atakapoichukua roho yake basi ahakikishe amemleta mtu mwingine wa kuweza kuipatia ushindi na ukombozi nchi yake.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hapo ndipo taratibu macho yake yaliyopoteza nguvu yakajifumba!
Na hakuweza tena kutambua nini kiliendelea baada ya macho yake kukata mawasiliano.
Alipokuja kufumbua macho alishangaa kujiona yupo ndani yah ema.
Alijishangaa sana na alipojaribu kujinyanyua kitandani hapo ndipo akagundua amewekewa dripu mkononi mwake.
“mungu wangu nimekwisha!” akajisemea
Moja kwa moja fikra zilimpelekea kuwa yupo katika mikono ya askari wa n chi yake.
Taratibu akabaki amejilaza pale pale akisubiri hatma ya watu aliowadhania wamemteka yaani banguli na kundi lake.
Mara alisikia vishindo vya mtu kuelekea alipo yeye.
Akajaribu kuuvuta mkono wake usiotundikiwa dripu taratibu akakishika chuma kilicholala karibu na kitandani alipolazwa yeye.
Huku akiomba mungu na katika fikra zake alijua kabisa kama sio banguli basi atakuwa ni askari wake yeyote, kwahiyo akajiandaa kwa ajili ya kurusha chuma hicho yeyote atakayeingia kiweze kumpata.
Mara hatua za mtu huyo zikakoma bila kujulikana aliishia wapi.
Mara za mtu mwingine tena zikaanza kusikika kuja upande ule ule wa hema hilo.
“huyo sasa atakuwa banguli kabisa” D’oen akajisemea huku sasa akikivuta kile chuma vizuri na kukitegesha ili atakapoingia tu akiachie.
Mara hatua za huyo tena zikakoma.
Kwa mbali akasikia watu hao wakiongea kwa kunong’onezana.
Maongezi yao yalidumu takribani dakika tano kabla mmoja hajaamua kuweka maamuzi ya kuondoka na kumuacha mwenzake pale.
Mtu huyo akasogea upande mwingine wa hema hilo ambapo ndipo kulikuwa na mlango wa kuingilia, ndipo D’oen akaweza kugundua mtu huyo kashika silaha ya moto mara baada ya kukiona kivuli cha mtu huyo katika hema hilo baada ya kupigwa na mwanga wa jua.
Mtu huyo akazipiga hatua kuingia ndani.
Ndipo D’oen akakiandaa chuma kile kukirusha.!
“oooooh ssssssss” D’oen akaachia yowe mara baada ya kuumia mkono kutokana na maumivu aliyoyapata katika harakati za kukirusha chuma kile, ni wazi mkono huo ulikuwa katika madhara ya risasi zile.
Mtu aliyeingia ndani humo naye akashtuka .
Kwa haraka akamkimbilia D’oen na kumweka vizuri kabla ya kutoa pole.
“oooh pole sana” sauti nzito ya mtu huyo aliye na sura isiyoonesha mchezo huku akiwa na mavazi ya kaki ikachombeza akiwa kamfikia D’oen.
D akatulia na kumuangalia mtu huyo lakini sura yake haikuonesha kuwa ni raia wa zambe.
“nipo wapi hapa?” D’oen akahoji akaimtazama mtu yule.
“pumzika tutakuelezea kila kitu, upo sehemu salama kabisa” mtu huyo akaongea huku akichukua baadhi ya dawa ya miti shamba na kuanza kuzipaka sehemu za D’oen zenye vidonda.
Akamaliza na kuchukua bakuli lililopo mahali hapo, akamuoneshea D’oen kilichomo ndani yake.
“ni risasi?!” akahoji D kwa mshangao baada ya kukiona kilichomo ndani ya bakuli lile.
“sio risasi tu, ni kwamba zimetoka katika mwili wako zote hizi” akajibu mtu huyo
“ngapi hizo?” D’oen akauliza kwa mshangao baada kuonesha kutoamini yaani risasi zilikuwa nyingi ndani ya bakuli hilo, leo hii aambiwe zimetoka katika mwili wake nab ado yupo hai? Haikumuingia akilini.
“15, ambapo tatu tumezitoa katika bega lako la mkono wa kushoto, mbili mkono wa kulia, tatu mgongoni,tano mguu wa kulia na mbili kwenye kalio lako la kushoto” mtu huyo akaeleza kwa msisitizo mkubwa.
D’oen hakuamini kabisa maneno yale aliyoambiwa nah apo ndipo akaanza kuhisi maumivu ni kama vile ndo ametoka kupigwa risasi hizo muda huo.
Akaanza kuhisi maumivu ya kila sehemu alipoelezwa amepigwa risasi.
“na tumeweza kuzitoa risasi zote, ila cha kushukuru mungu hakuna hata risasi moja iliyovunja mfupa hata mmoja wa mwili wako, kwahiyo tarajia kurudi katika hali yako ya awali soon” mtu huyo akaongea.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mara kutokea kwenye mlango wa hema hilo akaingia mwanadada mmoja mfupi wa wastani na mnene pia wa wastani aliye na uso wa bashasha na ucheshi.
“wow mgonjwa wetu umepata nafuu” akaongea mwanadad huyo huku akiwaelekea D pamoja na mtu mwingine yule.
Akaketi karibu na D’oen.
“lakini ninyi ni wakina nani na hapa nipo wapi?” D’oen akauliza huku akijitahidi kukaa kitako lakini akashindwa na kubaki amejilaza tu.
“kwanza pole kwa yaliokukuta” mwanadada yule kwa sauti yake ya madaha akaongea huku akimshika D’oen nywele zake,”mimi naitwa fetty diva” akajitambulisha.
“na huyu mwenzangu anaitwa barnabas, na huku tupo timu ya watu watatu mmoja wetu ametoka kidogo kuna dawa ya kiasili amekufatia ambayo inakausha vidonda haraka, huyo anaitwa santos. Nadhani swala la sisi ni wakina nani tumekujibu si ndiyo? Bado la hapa ni wapi, si ndiyo ee?” mwanadada huyo aliyejitambulisha kwa jina la fetty diva akaongea huku akimuuliza na maswali D’oen, ambaye alitikisa kichwa kuafiki.
Akaendelea,” hapa upo katika kisiwa cha uzunwi ndani ya nchi ya kinte, sisi wote unaotuona hapa ni watu wa zambe lakini tunaichukia zambe kupita maelezo, na si kama tunaichukia zambe kama nchi, la hasha bali tunachukia uongozi wa zambe, kiongozi mkubwa wa zambe ndiye amenifanya mimi niishi hivi, si kama napenda laa, na nadhani si sisi tu ndiye niliyefanyiwa ubaya na kiongozi huyo ni wengi sana, sema wamenyamaza kwa sababu ya kuhofia kufa, naapa kwa mungu wangu mmoja siku ambayo nchi ya zambe itajipatia uhuru wake kutoka kwa viongozi hawa naamini hapo ndipo kila mtu ataamua kuuweka ukweli na uovu wa kiongozi huyo katili wa zambe”
Dada huyo aliongea kwa masikitiko na moja kwa moja katika kichwa cha D’oen alivuta taswira ya kiongozi huyo anayezungumziwa si mwingine bali ni banguli, waziri aliyejali tumbo lake kuliko utu kwa wananchi wake.
D’oen akajisikia faraja kujiona yupo mikononi mwa watu wenye malengo sawa na yake.
“ilikuwa ni usiku wa jana kipindi tunavua samaki kwa ajili ya kuweza kujipatia kitoweo cha usiku huo hapo ndipo tuliona kitu cha kushangaza yaani tulikuvua wewe katika nyavu zetu ukiwa haujitambui, hapo ndipo tulikuchukua, tujikoka kuni nyingi kwa kuwasha moto ili kuweza kukupatia joto ambalo lingekuondoa katika baridi kali ya baharini. Baadae ndipo tuligundua mwili wako ukiwa na matundu mengi nah apo ndipo tulihisi yaweza kuwa ni risasi” fetty diva alianza kueleza story ya wao kumpata D’oen lakini akanyamaza kidogo na kumeza mate kisha akaendelea,”hapo ndipo tukaenda kumchukua dokta wangu ambaye huwa ananitibu sana katika hospitali moja katika mji huu wa kinte, alipokuja na vifaa vyake aligundua ni kweli mwili wako una risasi tena nyingi mno na uwezo wa kupona aliuacha kwa mungu wako, basi aliangaika kuzitoa hadi hapo aliposema zimekwisha zote zilikuwa ni risasi kumi na tano, hizo hapo kwenye bakuli” fetty akaongea huku akielekeza kidole chake kwenye lile bakuli lenye risasi alizooneshwa awali D’oen.
“basi baada ya hapo akaondoka na kutushauri tutumie dawa za kiasili za kutibu kabisa, ndo hapa sasa unaendelea na matibabu” fetty akamaliza hadithi hiyo ambayo D’ akakumbuka chanzo cha risasi hizo. D’oen Akatafakari kwa muda kabla hajamgeuzia swali mwanadada fetty diva.
“ na wewe ulisema ni mzawa wa zambe? Na ulijuaje kama mimi ni mtu wa zambe?”
Fetty akatabasamu baada ya swali hilo.
Akajiweka vizuri kisha akajibu swali hilo
“kipindi wewe unashiriki mashindano ya kimataifa ya utunguaji na kushinda unafikiri dunia ilivyokuwa na umbea iliacha kukutangaza? Ilikutangaza vizuri sana nah apo ndipo nchi yetu uliipatia sifa, na picha zako nyingi zilisambaa kwenye magaazeti ya huku nje, hapo ndipo nikakujua shujaa wetu n ahata nilipokuona jana sikupata shaka kukufahamu”
D’oen akatabasamu kusikia maneno hayo kutoka katika midomo ya mwanadada huyo, tayari katika fikra zake alishafikiria ukombozi wa n chi yake upo tayari. Na alitamani angekuwa mzima ili aweze kupambana na magaidi wan chi hiyo waliojificha kwenye kivuli cha uongozi.
“na wewe kiongozi gani wa zambe alikufanyia ubaya na kwa nini?” D’oen akamtupia swali hilo fettydiva.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“utajua tu muda ukiruhusu, subiri kwanza upone” fetty diva akaongea huku akijinyanyua mahali hapo na kutoka nje.
****
Basi D’oen akaendelea na matibabu na taratibu kadri siku zilivyokuwa zikizidi kwenda ndipo nay eye akapata unafuu wa mwili wake. Na miezi sita baadae aliweza kusimama kabisa na kuwa imara.
Hii ni kutokana na ukomavu wa mwili wake kutokana na mafunzo makali ya kikomandoo aliyopitia. Mwili wake ulikomaa haswa kwani muda mwingine wakati wa mazoezi yao aliweza kupigwa na nondo kwenye miguu, basi hali hiyo ilimpelekea kukomaa kwa mwili wake.
Baada ya miezi sita hiyo mwili ukarudi kama awali na maumivu ya risasi yakapotea, akabaki na makovu tu katika mwili wake.
Hapo ndipo mwanadada fetty diva akaamua kutumia faida ya komandoo huyo kuweza kumueleza kisa cha yeye kumchukia kiongozi mmoja wa nchi hiyo ya zambe. Alijua kabisa kupitia D’oen basi angeweza kulipiza kisasi na hakujua kuwa nje ya mji huo D’oen na yeye alikuwa na mpango wa kulikomboa taifa hilo hilo la zambe.
Hivyo fettydiva akaamua kumpata D’oen historia nzima ya tangu yupo zambe hadi kufika katika mji huo na chanzo cha yeye kufika katika mji huo wan chi ya kinte.
Story iliyosimuliwa na mwandada fetydiva kumuadithia D’oen ilikuwa hivi:
mwanadada fetty diva alikuwa ni mwanadada mwenye furaha sana katika familia yao, japo alikuwa ni mtoto anayelelewa na mzazi mmoja lakini hilo halikumnyima furaha. Mama ndiye alikuwa kichwa katika familia hiyo iliyo jumla ya watoto watatu yaani fettydiva akiwa ndiyo mtoto wa kwanza huku akifuatiwa na wadogo zake wawili wa kiume ambao ni mapacha yaani santos na barnabas. Baba na mama yao walitengana baada ya miezi michache santos na barnabas kuzaliwa. Kisa kwakweli watoto hao hawakuweza kukijua.
Mama yao alikuwa ni mwakilishi wa wananchi katika bunge la nchi ya zambe kwa tiketi ya chama pinzani, ni mwanamama wa aina yake asiyeogopa mtu yeyote, mwenye uwezo wa kujenga hoja na kuitetea.
Na hayo ndiyo malezi aliyokuwa akiwalea watoto wake hao, hakutaka watoto wake hao waishi Maisha ya kumuogopa yeyote Zaidi ya mungu, hivyo aliwajenga kiroho na kimwili.
kupelekea misimamo ya mwanamama huyo bungeni ndipo akapewa jina la utani na wabunge wenzake wa upinzani n ahata wa chama chake,’kigingi’.
Na kweli alikuwa ni kigingi haswaa kwani hoja mpaka anaikubali ujue ina mashiko na faida kwa wananchi wa jimbo lake na taifa kwa ujumla.
Tabia yake hiyo iliwachukiza viongozi wengi wapenda matumbo yao, n ahata banguli ambaye kipindi hicho alikuwa mbunge ambaye alionesha uwezo kupinga hoja na kukitetea chama chake, alimchukia mno mama fetty.
Banguli nae kupitia uwezo wake wa kuongea na kukilind a chama chake ndipo rais wa n chi hiyo yule ambaye kabla ya ELIAS STANFORD (Elias kipindi hicho alikuwa waziri mkuu) akamtunuku uwaziri wa mambo ya nje ya nchi, kabla hajapewa uwaziri wa mambo ya ndani alipoingia ELIAS STANFORD madarakani, ambapo masikini STANFORD aliingia mkenge kumchagua waziri huyo kuwa wa mambo ya ndani, laiti kama angelijua mapema suala la yeye kupinduliwa na kijana huyo basi asingelimchagua kijana huyo kujihusisha na wizara nyeti kama ile.
Hoja iliyokuwa ikiwasilishwa bungeni ya kufungia mitandao ya kijamii, upinzani wengi waliipinga vikali lakini walipoongwa pesa na hata nyumba, uwezo wao wa kuichambua hoja hiyo ukapungua. Lakini upande wa mwanamama ambaye ni mama wa watoto watatu akaipinga vikali hoja hiyo na hata mara kibao mawaziri mbalimbali wenye manufaa na hoja hiyo hususani banguli walipomfata faragha bado mama huyo alionesha msimamo wake wa kuikataa sheria hiyo ambayo haikuwa na manufaa hata kidogo kwa wananchi Zaidi ya kuwaumiza wale wanaotegemea shughuli zao za kijamii kupitia mitandao hiyo.
Mama huyo alipoona bungeni anakuwa mwenyewe na hakuna mwingine anayeipinga hoja hiyo ndipo akaanza kuwaamasisha wananchi ikiwezekana waandamane hadi bungeni kushinikiza wabunge wao wasiipitishe hoja hiyo.
Hilo likawa ni kosa!CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Banguli hakuweza kumvumilia.
Siku hiyo akiwa anatoka nyumbani kwake kwa ajili ya kwenda kwenye shughuli zake za kila siku za kitaifa ndipo alijiwa na ugeni wa ghafla.
Alikuwa ni banguli na walinzi wake wawili.
“habari yako mama kigingi!” banguli akasalimia huku akionesha tabasamu
“salama vipi muheshimiwa?”
“safi unaenda wapi tena wakati mguu huu ni wako?” banguli akaongea huku akijichekesha chekesha
“mbona nina safari kidogo kuna tatizo kidogo kwenye jimbo langu”
“aaah ebu tuongee kidogo, hilo tatizo la jimboni mwako limeshaisha” banguli akaongea huku akianza yeye kuingia ndani ya nyumba hiyo ya mbunge huyo.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment