Search This Blog

Sunday, 22 May 2022

BONDE LA MAUTI - 3

 







    Simulizi : Bonde La Mauti

    Sehemu Ya Tatu (3)



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Na kwa sasa hana wazo jipya la kutengeneza mashine iliyo bora kushinda zote.Hakika niliwaza sana bila kupata mwanga wa mawazo yangu maana tayari nilikwisha kuona dalili zote za kushidwa kutengeneza kitu walicho hitaji na kwa kuwa nawajua watu hawa hawana mzaha kwenye kazi zao basi nilikiona tayari kifo ni zawadi yangu sitahiki.Maanda lizi yalianza baada ya wiki mbili hivi baada ya kuchagua eneo la kufanyia kazi nilianza kufanyia utafiti vifaa nitakavyovitumia kutengeneza mtambo.Projekti yangu ilinichukua miezi sita nikifanyia utafiti madini niliyo yapata kutoko Kongo.Niliweza kugundua madini yale yana uwezo wa kuzalisha umeme wa kudumu tena wenye nguvu nyingi mno.Kwa kuwa nilikuwa ni mtu wa kwanza kuyafanyia kazi madini yale ilinibidi nichukue muda wa kutosha katika utafiti ili ili niweze kutokeza kiumbe bora zaidi ama mashine yenye uwezo kushinda zote.Katika eneo hili kulikuwa na maroboti mengi yakitengenezwa ambayo sikuweza kujua kazi yake nini hasa kwa maana watu hawa wanaonekana wana nguvu kuliko majeshi makubwa ya nchi zenye nguvu.Projekti yangu iliweza kukamilika kwa asilimia 100%.Nilihifadhi katika talakilishi yangu ya mpakato mfumo mzima wa mashine zangu nitakazo zifanyia kazi. Mashine ya kwanza ambayo niliiteuwa kuitengeneza ilikuwa ni ndege ya kivita ambayo niliipatia jina la projekit Eno1.Ndege hii ilikuwa ni kubwa kidogo yenye uwezowa kubeba tani moja tu.Mmonekano wake ulikuwa ni wa duara.Ilikuwa na uwezio wa kushambulia pande zote na pia ingeweza kuendeshwa kwa kutumia computer bila kuwa na rubani.Nikiwa katika hatua za mwishoni kuikamilisha ndege hiyo chombo chetu kilipata hitilafu kubwa katika mfumo wake wa ingine hivyo ilitubidi miradi isimamishe upesi turudi tena arithini.Hivyo injini za dharula zikawashwa na chombo kikageuza safari yake na kurudi katika eneo waliko kielekeza.Baada ya wiki chombo kiliweza kutua katika msitu wa Amazonia. Tangu wakati huo hadi hii leo miaka mitano imepita tukihishi hapa na shughuli zetu za kutengeneza mashine zilisitishwa kwa muda.Kwa hiyo we kaa ukijua upo katika chombo hiki ambacho si rahisi kuweza kujua maana mahali kilipo ni kama arthi na anaye weza kukiendesha chombo hiki ameshikiliwa na serikali ya Marekani na hakiwezi kufanya kazi pasipo kupata alama yake ya mkono na ndiyo maana shuguhuli ilibadilishwa ikawa ni kuuza siraha za maangamizi na mradi wao mkubwa ume simamishwa kwa muda hadi apatikane mtu mwenye kuendana na mzee yule aliye kitengeneza. Hakika simulizi la dokta Eriki lilinigusa sana maana sikutegemea kama watu hawa wana mtandao mkubwa hivyo na nguvu walinayo ilinipa mashaka makubwa hasa kulinganisha na nchi yangu niliona ni sawa na hakuna hata ukileta jeshi lote litapukutishwa na kubaki majivu. Asante sana Dokta kwa kuniweka wazi katika masuala haya. Ujue nina sababu ya kukwambia ukweli huu maana mbele yako kuna kibarua matata ukifanya uzembe unapoteza uhai wako. Baada ya miezi miwili niliweza kuwa tayari nimezoea maisha ya kambi hii ikiwa ni pamoja na kujua kuendesha vyombo mbalimbali vya kivita ikiwamo ndege na matenki.Nilifun dishwa mitindo ya mapigano mbali mbali na dokta Erick. "Kesho jiandae kuingia katika chumba cha maabara kwa ajiri ya kufutwa kumbukumbu zako." Hakika nilishutuka mno maana nilizani wameshagahili kumbe ni kutusaulisha hapo ndipo nilipo kumbuka kwa hawa ni adui tu na si watu. "Usiwe na wasiwasi mwingi nitakusaidia japo kwa uwezo wangu nilio nao.Unaweza kuchukua kidonge hiki ukimeze na hakika hata wakifanya scani utaonekana umepoteza kumbukumbu ila we utakuwa nazo bado.Ila kumbuka unapaswa kufanya jambo jingine ukitoka katika chumba hicho.Maelekezo utayapata ukitoka katika chumba hicho. ***************************** Nikiwa katika chumba changu tayari kuelekea katika chumba cha kufutwa kumbukumbu nilikimeza kidonge hicho baada ya muda niliweza kuona kizungungu zungu kisha nikapoteza nuru katika macho yangu.Kikajikuta ninaanguka chini na kuzimia.....

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Nilipo pata fahamu zangu baada ya kuwa nimemeza kidonge nilicho pewa na docta Erick nilijikuta katika mashine kubwa aina ya Scaning system.Hapo ndipo niliutambua ukweli wa Doct Erick maana kama si yeye ningelikuwa mtu mwingine kabisa maana uhatari wa watu hawa nauona kwa macho yangu mawili.

    Nilitolewa kwenye mashine hiyo nikiwa nimefugwa mikanda kwenye kitanda kigumu cha chuma chenye magurudumu.Kwa muda huo sikujua napelekwa wapi maana niliingizwa katika chumba kingine cha mitambo ambacho niliweza kuzishuhudia mashine za kisasa zikiwafanyia upusuaji binadamu.Na wengi nilio waona katika chumba hiki walionekana hawana viungo vyao vya mwili hasa miguu na mikono.mashine hizi zilifanya kazi ya ajabu kweli kwani watu hawa ziliwapachika vyuma kwenye sehemu zao zenye kasoro.Kila mashine ilifanya kazi yake kwa ufasaha mno maana niliona jinsi utendaji wake unavyo zidi kwenda.

    Hakika bado siku jua lengo lao la kuniweka pale kwenye mashine hizo. Walikisukuma kitanda changu hadi kenye computer kubwa iliyo kuwa inaziongoza mashine zilizo kwenye chumba hicho.Docta wa kike alinisogelea na kunitizama kwa makini kisha akaandika ripoti yake kwenye computer yake.Nilifanyiwa vipimo mbalimbali na kila kitu kilinakiliwa kwenye Computer. "jina lako nani umri wako unatokea nchi gani?" Aliniuliza binti huyo maswali yake yote sikujibu chochote kile maana nishajua nipo nafanyiwa uchunguzi kama kweli nimepoteza kumbukumbu. Baada kujilidhisha na uchunguzi wake nilifunguliwa mikanda iliyo kuwa imenifunga kisha yule doct wa kike akaniamru nimfwate. Safari yetu ilikomea kwenye ukumbi mnene wenye watu wengi walio onekana ni vibopa maana walionekana kama watu wazito kwa mtazamo wa haraka. Niliingizwa katika chumba ambacho niliwakuta watu wengine wenye mavazi kama yangu na woote walikuwa kimya.Hakuna aliye msemesha mwenzake.*****SIKU TATU NYUMA****

    Baada ya doct Erick kumpatia kidonge Nel alikimeza na kisha akazimia asijue kipi kina endelea.

    Doct Eric alingia kwenye chumba cha Nel akiongozana na Doct mwingine wa kike wakiwa na kitanda cha magurudum kwa ajiri ya kummbea mgojwa wao.Walimpakia kwenye kitanda hicho na safari ya kumchukua maabara ikaanza.

    Ndani ya maabara hîi ya kisasa mno yenye mashine za kila mtindo alilazwa nel kwenye kitanda maarum chenye mionzi mikali mno ya kijani.

    "Samahani doct unaweza ukanipisha katika chumba maana kuna jambo nahitaji kulifanyia kazi nikiwa peke yangu ila kabla kwenda niletee na sindano ya huyu jamaa nim dunge mapema maana akipata nafuu ni balaa mno."

    Ni maneno ya kusihi aliyo yaonge doct erick akimsihi doct mwenzake ampe nafasi ya kufanya uchunguzi akiwa mwenye juu ya kijana wake.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Hakika sitaweza kukusaliti ndugu yangu na nitafanya hivi kwa ajiri ya nchi yangu maana sina cha kuilipa kwa yote ambayo nchi yangu imenifanyia zaidi ya hili." Yalikuwa ni mawozo ya Dr.ERIC baada ya kuwa amepewa ruksa ya kumfanyia upasuaji kijana wake maana hakutaka ajulikane yeye ni na kwanini yuko pale kwa muda wote. ¤¤NDANI YA KAMBI HII ¤¤ Katika ofisi ya mkuu wa kambi ya BONDE LA MAUTI. Halikuwa akitafakali juu ya kuifanya kazi ya kuutawala ulimwengu unakaribia maana kwa asilimia kubwa alisha vuruga amani ya nchi nyingi na sasa alikuwa mpango wake ulikuwa ni kutafuta nchi vibaraka watakao kuwa chini yake. "Si rahisi kuukwepa mtego huu maana mpenda pesa nitampa pesa na mwenye kuitaji nguvu nitampa.Lakini atakaye shidwa kunifuatisha bonde litamhusu.Mpango huu wapatie wote wa hasisi na wawakilishi wangu.Na kingine hakikisha mnatengeneza siraha bora za maangamizi kwa ajiri ya nchi zitakazo kaidi mpango wetu mahususi hasa za kibailojia. Kidogo nisahau kitu Dr Erick ametengeneza nilicho mwambia akifanye maana namjua jinsi alivyo na kiburi cha kimya kimya na hawamu hii asipo fuata maelekezo yangu naiteketeza familia yake" Mkuu wa kambi hii ya BONDE LA MAUTI alikuwa akionge na mshiriki wake wa karibu mno ambaye ni mzee wa makamo.Kama unamkumbuka huyu ndiye alimleta Dr.Erick kutoka Kongo. "Ndiyo mkuu nimekuelewa nitafanya kama utakavyo na mpango wa kuwapata vibaraka kesho kutwa nita ongea na waasisi wote walio pande zote za dunia ili tuweze kutekeleza mpango wetu mapema.Taarifa nzuri iliyo toka maabara ni kwamba Dr.Erick katengeneza tayari mfumo wa kuwaunda maaskari shujaa ulio katika muundo wa virusi N002 ambavyo kwa mjibu wake ni bora kuriko roboti za chuma yaani askari akidugwa virusi hivi anakuwa na uwezo mkuba kuliko binadamu wa kawaida. Ila uwezo wake unaweza ukamnyanganya kama akishidwa kufuata amri uliyo mpa kwa kutumia virusi vya N003. Ripoti ndiyo hiyo mkuu toka maabara." "Huyu Dr.ana uwezo wa ajabu kabisa na kila kukicha ananishangaza kwa kipawa chake alicho nacho.Ila kuna kitu kwenye ugunduzi wake hajakupatia kabisa wala ujakigundua.FOMLA ya virusi hivi alivyo viunda na madhara yake ajakwambia hapo kuweni makini." "Ni kweli mkuu ila kanambia fomla hipo katika mfumo wa virusi na mchoro wake ninao kwenye computer yangu na nakala nishakutumia kwenye kifaa chako mkuu." "Hapo unaweza kwenda maana kidogo nimekuwa na matumaini maana hawa watu weusi si waaminifu kabisa na siwapendi sana zaidi ya kupenda walicho nacho." Baada ya kumaliza majadiliano yao mzee huyu mwenye machachari alitoka katika ofisi ya mkuu wake na kuelekea katika chumba mawasiliano ili akatoe taarifa ya kikao cha dharula kwa wanachama wote. ¤¤¤NDANI YA MAHABARA ¤¤¤ DR.Erick aliendelea na upasuaji kwa kijana wake ambapo ilionekana anafanya kitu cha tofauti kwa mwenzake maada ilibidi amfanyie kitu hicho akiwa peke yake kwa ajiri ya kumlinda dhidi ya maadui wasimjue yeye ni nani. Huyu ndiye alikuwa ni ufunguo wa fomla yote maana alimpandikiza vitu zaidi ya wenzake watakao fanyizwa baadae. "Najua utapata shida kuilinda fomla hii ila kumbuka itakuwa ni zawadi kwako na nchi yangu itunze kuliko vyote maana wewe ndiye utaikomboa dunia kwa madhara yajayo ya viumbe hawa wasio na utu." Alikuwa akiongea Dr.Erick kwa sauti ya chini akiendelea na shughuli ya kumpandikiza mashine kijana wake.Ni kana kwamba maneno aliyo kuwa anayaongea Dr.Erick yalipenya kama ndoto kichwani mwa Nel.Lakni hakuweza kujibu maana alikuwa kazimishwa na dawa alizo lishwa. Akiwa katika hatua za mwisho Dr.Erick alipata ugeni wa gafla ndani ya chumba cha upasuaji. "Ongera kwa kazi Dr. Nimeona kazi yako ilivyo bora na nzuri ila kuna vitu naona bado unavifichaficha.....



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Kwa nini umejifanya mjanja siku hizi au umesahau kilicho kufanya uwe mtumishi wa sehemu hii tukufu ukiwa ni wewe mweusi tu mwenye wadhifa wa juu.Ongera kwa hatua yako maana naona unataka kunipanda kichwani ili uwe mkubwa wangu.Kabla sijaondoka nipatie fomla hiyo haraka maana umeanza wewe acha nifuate ili tuone nani zaidi kati yako mwanzilishi na mimi mtaalamu." "Fomla sina Dr mkuu kaichukua yote.Nimebaki na kopi yake tu.Na kingine naomba utoke nje nimalizie kazi yangu maana sipendi kuichafua kabisa." "Wewe nyani mweusi ndiye wa kunijibu hivyo au umenisaha mimi ni nani? Natoka ila utalipa kwa hili na fomla lazima unipe halisi na si kopi maana naona jinsi ulivyo mbinafsi." Baada ya mtu huyu kutoka Dr Erick aliutoa mchoro halisi wa fomla nzima ya kutengeneza virusi hatari vya maangamizi pamoja virusi vya N001,2,3 . Akitabasam kidogo anaifungua lap top yake na kuanza kuandika kila kitu kilicho kwenye fomla hii.Baada ya kukamilisha zoezi hilo ana hiunganisha lap top yake kwenye mfumo wa computer nyingine iliyo kwa kijana wake.Data zote alizo ziandika zinaanza kuingia katika mfumo wa fahamu wa neli. "Ngoja nije nione kama utapata kitu maana umezidi na kupenda vitu laini . Na huu ndiyo utakuwa wakati wako wa mwisho katika utawala wako labda urudi Israel tena ukasomee teknologia nyingine maana hata naona si mahali pako." Dr Erick alijiwazia moyoni mwake na kutabasam baada ya kuwa amemfanyia ujuma rafiki yake mwisirael Obadi.Huyu ndiye ameshirikiana naye katika utafiti wao wa virus ila Dr.Erick ndiye alipewa kazi ya kuchora Fomla.Baada ya kuona virusi hivyo kamili vikioneka vilivyo hapo ndipo alihamua kubadilisha fomla nzima na akatengeneza mbadala yake lakini yenye nguvu karibu na ya kwanza. Na tayari mfumo wa kwanza kisha aka uhamishia kwa kijana wake. **TURUDI KATIKA UKUMBI BAADA YA SIKU MBILI KUPITA*** "Karibu Dr.Erick uweze kutupatia maelekezo ya program yako ili wajumbe wapate kuwa makini kwa mazungumuzo yafuatayo" Dr.Erick alikaribishwa kwenye ukumbi huo ulio sheheni vibopa ambao kwa mtazamo tu wa macho utawajua wao ni akina nani maana walinukia pesa kwa harufu isiyo weza kuisha kamwe.Lakini moyoni walikuwa wachafu zaidi ya choo cha wagojwa wa kuhara.Hawa ndiyo walikuwa wakiratibu mauaji katika nchi mbali kama vile Rwanda,Kongo,Somalia na kwingineko.Hakika utu si mavazi bali mtu alivyo kwa ndani yaani mwenendo na matendo yake.Kama dunia ingelikuwa na watu hawa pekee isingelikaruka kabisa kwa wanyonge. "Karibuni wajumbe nyote kwa kututembelea katika falme yetu tukufu iliyo na ngome nzito isiyo na udhaaifu milele.Mbele yenu ni mimi Dr:Erick nikiwa ni kwa ajiri ya kuonyesha Program mpya kabisa kwa ajiri ya kuibadili dunia na kuifanya kuwa kitu cha kutamanika hakika. Tazameni kwa umakini video hii na mimi nitawapa maelekezo muhimu". Dr. Erick anasogea pembeni na project{sinema} inawasha. Hapo ndipo unaonyesha michoro mingi iliyo kama ramani.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ..Ilianza kujitokeza kwenye ukuta ulio mbele ya ukumbi huo.Hakika kwa uwezo wa teknolojia iliyo kuwa inaonyesha mbele ya macho yao ulikuwa mkubwa mno kiasi kwamba ingelikuwa ngumu kwa mtu wa kawaida kuamini kama kwenye ulimwengu huu kuna mambo makubwa kiasi hicho tena yaliyo buniwa na binadam aliye dhaifu na duni lakini kwenye ukweli hakuna la kupingika. Video hiyo ya michoro ya kisayansi ilichukua saa moja na nusu ikionyeshwa kwenye ukumbi huo wa kisasa wenye hadhi ya hali ya juu lakini walio ndani yake wakiwa ni wauaji wa halaiki kwa kupenda wenyewe maana wao ndio walikuwa wawakilishi wa shirika hili la BONDE LA MAUTI katika mataifa mbalimbali.Video hiyo iliweza kuisha kwa kuonyesha wasifu wa kemikali zilizo tumika kuunda program za virusi hatari vya N00.2,3 Hakika ukumbi mzima ulilipuka kwa furaha kubwa mno maana kitu walichokitegemea kwa miaka mingi mno kipo kamili tayari kwa matumizi na wamekipata bila garama kama walivyo kuwa wanafikilia hapo mwanzo. "Asanteni sana wajumbe kwa usikivu wenu na hiyo ndiyo program yetu kamili ambayo sikuifanya mwenyewe maana nisipo wataja watu hawa basi itakuwa ni dhambi nzito kwangu maana watu hawa wamefanya mengi zaidi na akili yao nyingi imetumika katika kufanikisha hii program.Labda nianze na master wa computer na si mwingine ni mrembo wetu matata hapa ndani ya falme hii tukufu naye ni DR.Anitha kutoka Urusi akiwa ndiye mtu pekee duniani kuweza kudurufu komputa zote bila kushutukiwa na mtu yeyote. DR.Anitha naomba uje mbele uwape salamu kidogo wajumbe maana wanaweza kujua natania nikisema wewe ni mrembo kuliko na una hatari kwa ulimwengu wa digital .'' Dr.Anitha alipanda jukwaani na kuanza kuwapungia mkono wajumbe wote walio kuwa kwenye ukumbi huuakionyesha tabasam lake matata ambalo kama utamuona anatabasam kama wewe ni mwanaume lijari unaweza kusema anakuita.Maana alikuwa ana sifa zote za kuitwa mrembo.Hakika Mungu alimpatia vitu vizuri mno maana alipendelewa kwa kila kitu.Lakini roho yake ilivyo ni bora ungekutana Osama maana hakuwa huruma akiwa kazini na ndiyo maana akaonekana katika watu hawa wenye roho mbaya kama shetani maana wote wanatamani dunia isipate amani kwa tamaa zao za kijinga. "Asanteni nyote kwa kufika kwenu hapa maana muda umepita sasa kablahatujaonana hivi.Karibuni tena katika ulimwengu wa digitali maana siku si nyingi nitampata mrithi wangu wa uhakika aliye zaidi yangu katika masuala haya ya teknolojia ambaye atakuwa amechukua kila kitu ninacho kijua na huyo ndiye mtu wa kwanza kufanyiwa majaribio yetu ya virusi hivi vya N00.2,3.Hakika nimshukru sana DR Erick na mwenzake kwa ugunduzi huu wa teknologia mpya ambayo hivi karibuni itaugeuza ulimwengu na kuuchukua eneo jingine kabisa maana wamefanya mambo ambayo sikupata kuyafikilia kama yapo ulimwengu huu wa tatu.Mara ya kwanza nilifiklia hawa si binadam maana teknologia yao haiwezi kuingiliwa na mtu mwingine yeyote zaidi ya wao wenyewe ndio wanaweza kuivunja. Asanteni sana kwa kunisikiliza na karibuni katika ofisi yangu kwa maelezo zaidi ya haya maana kazi ndo imeanza sasa. Alimaliza hivyo Dr.Anitha ambaye alitoa maelekezo kinaganaga na ukumbi mzima ukampigia makofi ya kumpongeza maana kwa maelezo aliyo yatoa walijiona tayari ni washindi wa kazi iliyo mbele yao. DR.Erick alikisogelea tena kipaza sauti na kuendelea kuongea na wajumbe hao juu ya program yao ilivyo. '' Mtu aliye fanikisha kwa kiasi kikubwa kuitengeneza progra hii si mwingine huyu ni ginias wa Israel yoote na ni mbuni wa maroboti ya TTS20000 akiwa ndiye mtu pekee aliye tumika kuiongoza program nzima katika mfumo wa komputer na katika michoro tulimtegemea yeye pekee kuwaeza kufanikisha mpango wetu wote.DR KATRA karibu sana mbele ili uwape maelezo wajumbe " "Asante DR ERICK kwa uaminifu wako maana nilijua utakuwa umechukua program nzima maana mwanzo sikukupenda kabisa hasa nilipo hona unapenda kukaa peke yako kumbe hapo ndipo unapo toa ujuzi asante kwa yote najua utakuwa una kitu umekificha hasa kuhusu mimi maana hapa wengi hawakujui kama mimi ninavyo kujua maana wewe tumesoma pamoja na mimi nilikuwa katika timu yako.Kwanini usijulikane mbele ya wajumbe ili upate msaada maana najua lazima una tatizo kubwa na mimi nalijua kiundani na mbinu za kulitatua tatizo lako maana siku ikijulikana upo hai bila shaka hautakuwa salama .Wewe ni........

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Ni mtu muhimu katika falme hii na wewe pekee ndiye unaye jua fomla yote kwa usahii.Miaka kumi iliyo pita tukikuwa katika chuo kimoja cha teknologia wewe ndiye ulikuwa mtu mweusi pekee na wewe ndiye uliweza kufanikiwa katika mtihani ule wa kutengeneza robot ndege ya kisasa lakini jambo la kushangaza umekuwa mpole kama unikumbuki." Hakika Dr. Erick alishaanza kushutuka maana alihisi huenda Katra anakwenda kumhanika mbele ya hathara kumbe yalikuwa ni maneno yake ya kujionyesha anamjua vizuri kuliko wote pale. Lakini maneno ya DR.Katra hayakupuziwa na wajumbe hawa maana wao walitaka ndio waipate teknolojia ambayo aliwahi kuifanyia mtihani chuoni kabla ya kuwa hapo.Kwa hiyo walianza kujadili kimya kimya uwezo wa Dr Erick. "Kwa siku ya leo maelezo ya program hii naishia hapo ,lakini kila mtu atapata nakala ya fomla hii kwa kiasi lakini oligino itabaki mahali fulani palipo salama na vipande vyake muhimu vimefichwa mahali pengine kwa hapo nawakilisha maana maamuzi mengine namhachia kiongozi wa hapa." Dr Erick alimaliza maelezo yake na kisha akatoka kwenye ukumbi huo na kuelekea kwenye chumba cha komputa ambcho DR.Anitha alikwisha kutangulia maana alikuwa amemaliza mazungungumzo yake na alitakiwa kuwapa maelezo ya fomla kupitia njia ya intanet na alitakiowa awaandae vijana ambao tayari wamedugwa virusi vya N002,3 ili wajumbe waone jinsi wanavyo fanya kazi zao. "Karibu DR.Erick na ongera kwa kazi yako nzuri maana sikuamni kama utanipa nafasi kwenye hii projekit yako ya hali ya juuhakika nashukru sana kwa wema wako maana umenifanya niweza kufahamika kwa njia kubwa na hapa kazi yangu itakuwa yenye thaman zaidi.Lakini kuna kitu hakija kaa sawa hasa kuhusiana wewe na Dr.Katra kuna kitu gani kati yenu maana kila mara anakuandama na si kwa wema maana hata juzi niliweza kumsikia akihitaji umpatie program yeye na alikutusi sana ila kuna kitu hapo kinaendelea maana si bure tu mtu akuchukie.Naomba unambie huenda nikapata pa kukusaidia" "Usijari Dr.Anitha haya mambo ni makubwa mno na kisasi chake bado hajakitimiza maana nimemzidi mengi tangu nikiwa chuo kwa hiyo lengo lake ni kutaka kuniangusha kabisa ili yeye aweze kuwa juu zaidi yangu na teknolojia yake iwe kubwa mno lakini hatoweza maana nimemjua mapema na atabaki na kisirani chake hadi kifo kimkute maana hii teknologia ni kubwa mno kuliko elimu yake aliyo nayo. waandae vijana ambao tayari umewadunga virusi na wamekamilika niwapitie kama wame kwisha kuwatayari " "Vijana wako wako vizuri sana labda mtu wako amekataa kusema nasisi nimemtazama katika mwili naona yupo sawa ila yeye yuko tofauti na wengine kwa kila kitu maana inaonyesha ana nguvu zaidi ya hawa wote na yeye ndiye anaweza kujiongoza mwenyewe je hili aliwezi kuwa tatizo.? "hilo si tatizo mimi ndiye nimemfanya awe wa pekee ili aweze kutekeleza kitu kimoja kama kutatokea hatari katika kambi hii hasa kama virusi vitasababisha hatari maana kama tulivyo kwisha kuona kama program itakuwa imefeli watu hawa wanaweza kuleta madhara kwa ulimwengu mzima maana wao tu ni zaidi ya bomu kama waki ongozwa na kichaa." " unataka kusema anaye weza kuizuia program hii ni kijana wako tu.?maana nimeona mfumo tofauti kwake na yeye pekee anaweza kujitambua na mbona ujaliweka wazi jambo hilo mapema .maana kama mkuu akijua itakuwa ni hatari kubwa mno. "kwa hiyo unataka kumwambia mkuu ili iwe hatari?ama unafurahia kuona dunia ijayo inaisha kwa tamaa za watu hawa sema ili nijue "? "Hapana simaanishi hivyo nina hofu kubwa juu yako hasa jinsi unavyo fanya kitu hatari na kisha unafanya kitu cha kuzuia hatari hiyo mara moja uoni kwamba ni kama unawatania watu hawa na ujue na mimi nimeambiwa nitengeneze virusi vya kuangamiza vitakavyo sambaza kwenye intanet na bado sijajua njia ya kuvizuia kama vitaleta madhara makubwa kwa watu." " Hebu achana na hayo mambo huu si wakati wake tukawaone makomandoo wa kibailogia tuwape na maelekezo ya kufuata." Madaktari hawa waliingia kwenye chumba walicho kuwamo makomandoo hawa wa kibailogia wakiwa na tabasam zito machoni mwao maana waliweza kuwaona watu wao jinsiwalivyo makini kusikiliza kikao cha wajumbe kwa umakini mno . "Habari zenu vijana natumaini mmeweza kusikia kikao hicho kwa umakini na tayari mmeweza kujua nyinyi ni akina nani hasa sasa ni hivi kila mmoja atafanya kazi kutoka kwa watu maalum na mtafuata amri toka kwa mkuu ambaye mt amjua baada ya kujua kuitumia program iliyo katika miili yenu.Nyote hapo mna kitu cha pekee katika miili yenu na kitu hicho ni zawadi ya kwenu.Kwa hiyo majaribio yafuatayo msiniangushe kabisa maana yoote mnaweza kuamru mwili ufanye kitu cha pekee.Nel wewe hapo ndiye utaanza katika majaribio haya na jina lako la mwanzo life kwa sasa maana wewe ndiye N001 kwa hiyo utaweza kuongoza program upendavyo na unaweza kuongoza mashine zote kwa kuzihamru utakavyo kwa hiyo kawaonyeshe kwamba wewe ndiye wa kwanza katika malengo yangu na wewe pekee ndiye mkombozi wa wanyonge."



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog