Search This Blog

Sunday 22 May 2022

NYUMA YA PAZIA - 1

 





    IMEANDIKWA NA : ASNARY HUSEIN



    *********************************************************************************



    Simulizi : Nyuma Ya Pazia

    Sehemu Ya Kwanza (1)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kazi kubwa ya kufanya kwake ilikuwa ni kuliongoza jopo la mawakili na wanasheria wote chini ya kampuni yake ya mawakili ijulikanayo kama NEW VISION ADVOCATES.Haikuwa kazi kubwa kuwapata wateja mbalimbali waliohitaji msaada katika kesi zao tena kesi nzito kwani kampuni yake ilikuwa ikisifika kwa kutoa wanasheria waliotambua sheria.Hakuwa mwingine bali ni Mh.Harold Maebo aleyefahamika sana kwa jina la Mr.Maebo.Alikuwa na makamo ya miaka 45 hivi,kichwa chake kikiwa tayari kinanyemelewa na nywele nyeupe yaani mvi.Alikuwa mcheshi na mchapakazi aliyetambua kazi yake vizuri hukua akiiendesha kampuni hiyo.Hakuna mfanyakazi wake hata mmoja aliyemchukia wala kutofurahishwa nae bali walifarijika sana kuwa chini ya uongozi wake Mr.Maebo.

    * * * * * * * * *

    "Za asubuhi Mariam?" alitoa salamu Mr.Maebo wakati akiingia ofisini kwake kwa mwendo wa haraka.

    "Nzuri Boss,shikamoo!" Aliitikia Mariam mmoja kati ya wafanyakazi wake.

    "Marahaba,naomba Mafaili ya jana ambayo hukuyaleta" aliagiza.

    "Sawa boss"Aliitikia Mariam hukuakipekua mafaili hayo.

    Haukupita muda aliingia ofisini kwa Mr.Maebo na kuyaweka mezani.

    "Asante mama eh!"Alitania Mr.Maebo.

    "Haya"

    "Lakini boss......."Aliongea Mariam.

    "Naaam!"

    "Jana ulipoondoka alikuja mtu fulani hivi alikuwa akikuulizia."

    "Alikuwa na shida gani?"Aliuliza Mr.Maebo kwa shauku.

    "Hakunambia chochote nilipomuuliza shida yake ila alinambia atakuja."

    "Mh!yukoje yukoje...."Alianza kudadisi.

    "Ni mrefu mwenye mwili mkubwa uliojengeka vizuri kabisa kama vile anafanya zoezi la kubeba vyitu vizito na ana nywele fupi yani kwa ujumla ni mtanashati sana."Alielezea Mariam.

    "Ok!"

    "Hakuacha namba ya simu?"Aliuliza tena Mr.Maebo.

    "Hapana...."Alieleza huku akitikisa kichwa.

    "Sawa mama kaendelee na kazi mama"

    "Sawa Boss!"Aliitikia huku akiufuata mlango na kufungua kitasa.

    Alibaki akifikiria ni nani aliyemtembelea siku hiyo na alikuwa na shida gani hadi asimueleze sekretari wake?

    "Ah!Potelea mbali atakuja tu!"Aliamua kupotezea huku akianza kuangalia kazi katika mafaili yale.

    * * * * * * * * * * *

    Alikuwa ni mrefu tena mtanashati aliyejua kupangilia mavazi huku akinogeshwa na uzuri wa sura yake.Ni Joachim Bartazar mmoja kati ya wafanyakazi wa kampuni ya HAMSHOT ENTERPRENEURS LTD. Alikuwa ni meneja wa kampuni hiyo.

    "Ah!sijui ntamkuta na leo huyu mzee?"Alikuwa akijiuliza wakati akisubiri foleni katika mitaa ya Buguruni.

    "Halafu sikuchukua namba yake!!"

    Alikanyaga mafuta mara tu walipo ruhusiwa kuendelea na safari zao aliufuata upande wa kushoto kama vile anaelekea barabara ya Karume.Alikanyaga mafuta hadi mtaa wa Samora na kupaki karibu na jengo moja kubwa lenye bango la NEW VISION ADVOCATES LTD.Alishuka kwenye gari lake aina ya Toyota Landcruiser VX.Alilifuata lango kuu la kuingilia jengo lile.Moja kwa moja hadi ghorofa ya pili hakutaka kuongea na mtu hivyo alinyooka moja kwa moja hadi kwa Sekretari aliyeonana nae siku iliyopita.

    "Halloow dada"Alitoa salamu yake Joachim Bartazar.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hi kaka"Aliitikia Mariam.

    "Safi nahisi leo nimemkuta au........"

    "Yah hata usijari naomba usubiri kidogo"

    "Worry out (usiwe na shaka)"Aliongea huku akitoa tabasamu.

    Alikamata simu ya mezani na kubonyeza namba fulani kisha akaweka sikioni kusikiliza.

    "Halloow Boss...."Aliongea Mariam.

    "Boss yule mgeni wako kafika.............."

    "Nimruhusu aingie........"

    "Sawa Boss"Alimaliza huku akimuangalia yule mgeni.

    "Kaka kata kushoto mlango wa mwisho wenye jina la Mr.Harold Maebo hapo hapo"Alimueleke

    za.

    "Asante bibieh!"

    Aliachana na Mariam na kuufuata uelekeo alioelekezwa.Alianza kuuona huo mlango na alipo ufikia aliusukuma na kuingia ndani.

    "Haaaaaa!it's you? (Ni wewe?)"Aliinuka katika kiti huku akishangaa ujio wa Joachim Bartazar.

    "Ni mimi mzee......"Aliitikia Joachim.

    "Nahisi kazi imeisha Joachim....."Aliongea huku akiupokea mkono wa Joachim.



    "Haaaaaa!it's you? (Ni wewe?)"Aliinuka katika kiti huku

    akishangaa ujio wa Joachim Bartazar.

    "Ni mimi mzee......"Aliitikia Joachim.

    "Nahisi kazi imeisha Joachim....."Aliongea huku akiupokea

    mkono wa Joachim.

    "Usijali mzee"

    "Nakuamini sana kijana wangu......."

    "Asante mzee....." alidakia Joachim.

    "Kwa hiyo vipi......." Aliuliza Mr. Maebo.

    "Usjali mzee hapa si mahala pake, tukutane Safari Inn kama kawaida mzee" Aliongea huku akiinuka na kuondoka.

    Alitoka nje na kulutia moto gari lake.



    * * *



    Alikuwa tofauti na umzaniavyo kwani mara baada ya kutoka 9uba hakutaka kujulikana wapi alikoelekea huku akitafutwa bila mafanikio yoyote. Kama alivyojulikana na wengi au marafiki zake kuwa huyu ni Joachim Bartazar na ni Meneja katika Kampuni inayohusika na Usimamizi wa Kibiashara pamoja na Masoko iliyojulikana kama the HAMSHOT ENTERPRENEURS Co LTD basi. Hakuna aliyejua kuwa kijana huyo mtanashati na mcheshi kiasi kile alikuwa akicheza michezo hatari kiasi ambacho kinaweza kugharimu maisha yake aliyonayo. Hilo hakulijali ila aliendelea kucheza michezo hiyo na kumfanya akomae katika kufuatilia mambo mengi ya siri za Vigogo kibao Jijini hapo. Hakupenda kuwa na mahusiano bali alitamani sana kufanya hivyo ila sheria zake mwenyewe hazikumruhusu kufanya hivyo. Alikua mzuri katika Mapambano ya ana kwa ana huku yakimfanya kujinyakulia tuzo nyingi kutokana na hilo wakati alipokuwa chuoni pake nchini Cuba.

    Alikuwa na furaha sana siku hiyo kwani alikuwa amemkumbuka sana rafikiye Mr. Harold Maebo jambo lililomfanya atabasamu. Aliamua kuelekea kwake ili ajiandae kwa kukutana tena jioni na mzee yule mkarimu. Alikuwa makini sana na kila hatua aliyotembea huku akilazimika kuangalia nyuma na pembeni ili kugundua chochote au yeyote anae mfuatilia. Kama aliyelijua hilo aligundua uwepo wa gari moja nzuri sana aina ya Range Rover Sport aliyowahi kuiona katika maeneo fulani hatarishi.

    "Mh....wamejuaje nko huku hawa washenzi au waliniona wakati naenda pale ofisini nini?"Alijiuliza kichwani pake.

    "Ngoja niwaonyeshe hawa washenzi kuwa mimi ni mshenzi......."Alijinadi kimoyo moyo.

    Haraka aliiacha barabara kubwa na kuifuata barabara iliyompeleka mitaa mingine kabisa hakuwa na malengo nako, lakini aliwaona wakipitiliza kama vile wakimtangiza. Yeye aligeuza gari na kurudi alipotokea.

    "Wajinga kweli wanadhani mie rahisi kiasi hichio....."Alijigamba huku akilizidishia moto gari lake. Alipotelea mitaani akiwa hana pa kwenda.



    * * * *



    Siku hiyo furaha yake iliongezeka maradufu kutokana na ujio wa Joachim ofisini pake. Kila mfanyakazi aliliona hilo na kila aliyemuuliza ndio alimzidishia furaha.

    "Boss vipi leo mbona hivi......"Aliuliza Mariam.

    "Vipi kwani...."CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Furaha uliyonayo inashangaza yani"

    "Ha ha aha aha ha!!! Mama unanifurahisha sana sana hapa nilipo na miaka yangu yote hii unataka ninune nife eeh....."Aliongea kwa utani Mr. Maebo. Lilikuwa jibu kwa kila aliyemuuliza mzee yule. Alipo maliza muda wake wa majukumu katika ofisi yake haraka hakutaka kupoteza muda aliinuka na haraka alilifuata gari lake aina ya Toyota Prado TX na kulitia moto kuelekea Mikocheni kuliko kuwa na maskani yake.

    Hakuchelewa kufika kutokana na kutokuwepo kwa foleni barabarani muda ule. Alipofika kwake alilipaki gari lake nje na kuingia ndani ya geti kwani ilikuwa desturi yake pale anapokuwa na safari mara baada ya kurudi kutoka ofisini kwake.

    "Halooow my wife I'm back home (halooow mke wangu nimerudi nyumbani)"Alitania Mr. Maebo kama ilivyokuwa ada yake.

    "Yani we mzee haujaacha tu mambo yako"Alikazia mke wake.

    "Yaani ninavyokupenda mke wangu alafu nisifurahi kukuona"Alikazia masihala yake.

    "Haya bwana pole na kazi mme wangu"

    "Asanteee.......ila nina njaa my wife"

    Alielekea chumbani kwake na kuoga kisha akabadili nguo na kurudi sebureni kisha kula chakula alichoandaliwa na mkewe. Alipomaliza aliinuka.

    "Vipi mbona vizuri wapi tena baba....."Aliuliza Mkewe.

    "Leo naenda kuonana na mtu wa muhimu sana ila sichelewi kurudi eti eeehh..."Alimwambia.

    "Haya mi nipo"

    "Sichelewi kwa heri"aliaga na kuondoka.

    Alidandia gari na kulitia moto kuelekea Safari Inn walipokubaliana na Joachim. Alikuwa na furaha kwa hilo.

    Alikuwa hajamaliza mita 500 ghafla gari lake lilipata ajali ambayo ilisababisha Mr. Maebo kupoteza maisha palepale. Taarifa za kifo chake zilisambaa ndani ya nusu saa baada ya ajali kutokea. Kila aliyemfahamu alisikitishwa na kifo hicho lakini Joachim hakuwa na taarifa hizo.



    * * * *



    Alikuwa spidi huku akiangalia saa yake kwani alidhani amechelewa miadi yake na Mr. Harold Maebo na ndipo simu yake iliita;

    " Nani tena....."Alikiuliza.

    Alisimamisha gari na kuangalia nani aliyempigia, ilikuwa namba ngeni kabisa wala hakuitambua aliamua kuipokea;

    "Yes!! Halooow"

    "Ha ha ha eti Joachim Bartazar "Aliongea kwa kejeli mtu yule aliyepiga.

    "Yap!! Lakini sijakujua wewe ni nani?!"Alishangaa.

    "Huna shida ya kunijua ila kwa taarifa yako huyo unamuita boss wako Mr. Harold Maebo kaisha kwenda na maji umebaki wewe na hiyo timu yenu sasa chagua unanipa faili au hunipi"Aliongea kwa jeuri na kutishia mtu yule.

    "Utanisamehe faili sina na sitishiki kihivyo"

    "Sheeenz sasa chagua kufa alafu na faili nilipate au ulete hilo faili tumalizane"

    "Pole sana nasikitika ya kuwa faili huwezi kulipata kaka mkubwa bye...."Aliongea kwa ujasiri mkubwa na kukata simu.

    Hakutaka kuamini alichosikia kwenye masikio yake kuwa Mr. Harold Maebo hivi sasa ni marehemu.

    Aliahirisha safari na kuelekea Hospitali ya Muhimbili ili akalithibitishe hilo kwa macho yake. Alipofika katika Hospitali ile hakutaka kuuliza chochote ila aliufuata uelekeo wa Mochwari ili akamuone.

    "Kaka!!!samahani hairuhusiwi muda huu kuelekea huko..."Aliongea mmoja kati ya Manesi waliokuwa na zamu siku hiyo.

    "Unajua mie ni nani?"Alimuangalia huku akikunja uso na kuupoteza ule uso wake wa huruma na upole.

    "Haisaidiii"

    "Mie ni Afisa wa Jeshi la Wananchi na nna kazi nafanya humu....."Aliongea huku akimuonyesha kitambulisho chake cha bandia.

    "Samahani sana afande.... Sikujua ndio maana"

    "Usijali nani muhusika wa kule"Aliongea huku akinyoosha kidole katika mlango wa Mochwari.

    "Yumo ndani afande"aliitikia kwa woga kama mwanzo.

    "Sawa jisikie huru"

    "Sawa"

    Haraka aliufuata ule mlango huku akiangalia huku na huku ili kuakikisha usalama wake. Mara baada ya kufanikiwa kuingia mle ndani allipokelewa na harufu kali ya madawa ya kutunzia maiti. Alimuona yule muhusika akiendelea na kazi yake huku akiwa hana taarifa na ugeni mle ndani. Joachim alimfuata na kumshika bega, hakushituka bali aligeuka na kumuangalia tu. Joachim alishangaa sana kwa kile alichokiona kwani mhudumu yule alikuwa akiuweka sawa mwili wa Mr. Maebo ili autunze katika friza ya kutunzia maiti. Alishutuliwa na sauti ya mfanyakazi yule.

    "Kijana shida yako"

    "Sogea"Aliongea Joachim.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "We vipi?" Alishangaa yule mfanyakazi kwani mtu aliyekuwa nae hakuwa mhusika ila tu alijifanya kama ndio kiongozi wa pale.

    "Nimesema sogea...lAliongea kwa ukali na kumsogeza.

    "We vi......."Alikatishwa kauli na mkono uliokuwa na bastola mkononi uliokuwa ukimuangalia huku mlengaji akiwa bize kuangalia ile maiti iliyolala pale kitandani.

    "Dah....yani wamemuua?"Alijiuliza kwa sauti Joachim.

    "Kwani vipi huyu ni nduguyo?"Aliuliza kwa mshangao yule mhudumu wa chumba kile.

    "Kafa kwa nini?"Aliuliza Joachim.

    "Ngoja niangalie faili lake!"Alijibu yule mhudumu.

    "Lilete hapa"Alimpokonya lile faili.

    "AJALI shit......hubu lete glavu haraka"Alishangaa na kuaguza haraka.

    "Sawa"

    Alizivaa na kuanza kuiangalia ile maiti kwa ufasaha huku akiigeuza geuza.

    "Hili ni tundu la risasi"Aliongea Joachim na yule mhudumu kuitikia kwa kichwa.

    "Nipe mkasi"Aliagiza tena .

    Alipopatiwa aliuingiza na kuchokonoa kisha akatoka na risasi.

    "Haaaaaaaa!!! Kweli" alionge yule mhudumu kwa mshangao.

    Alitoa simu yake na kumpiga picha za ushahidi marehemu na kutoka. Hakutaka kupoteza muda aliingia ndani ya gari lake na kuto simu yake kisha akaiangalia ile namba mpya iliyompa taarifa zile. Alijaribu kuitafuta lakini hakufanikiwa kwani aliambiwa namba haipatikani kwa wakati ule.

    "Shit....!!!!" Aliirudisha simu yake kwenye kopo maalum lilikuwa na kazi hiyo katika gari lake.

    "Kanikosea sana na atanipenda mchezo wangu"aliongea na kuliondoa gari lake maeneo ya maegesho yale



    "Shit.........."alirudisha simu yake kenye kopo malum lililokuwa na kazi katika gari lake.

    "Kanikosea sana na atanipenda mchezo wangu" aliongea na kuliondoa gari lake maeneo ya maegesho yale.

    Aliamua kuliekezea nyumbani kwake. Njiani alikuwa na mawazo mengi huku picha za matukio ya kifo cha Mr. Harold Maebo kama vile sinema ya kuigiza. Alikumbuka mambo mengi sana kuhusiana na mzee yule kwani yeye ndie aliyempokea na kumuingiza ndani ya kikosi kile cha Usalama cha siri cha NDA (National Defence Agency) kilichokuwa kikifanya kazi ya kufuatilia Ujangiri, Ujambazi, Ufisadi na mambo yote yaliyohusu nchi huku kikiwa hakifahamiki. Yeye ndie aliyempokea wakati akitokea nchini Cuba mara baada ya kuwasili na hakuna aliyeju chochote.

    "Fight for your Country Joachim (Pambana kwa ajili ya nchi yako Joachim)" alikuwa akikumbuka moja ya maneno ya maneno yake.

    "Wewe ni komando na hakuna anaeweza kukuchezea kirahisi na ndio maana nilivutiwa kukuleta hapa najua unaweza".



    Aliingia kwake na kupaki gari kisha akaeleka ndani. Hakutaka hata kukaa sebuleni moja kwa moja aliingia chumbani kwake kisha akalifunua Zuria lililokuwa limetandazwa mle chumbani. Alifunua na kukutana na kijimlango cha chuma, hakutaka kuchelewa aliingia ndani yake kwa msaada wa ngazi iliyokuwa ndani yake. Alielekea moja kwa moja katika sanduku kubwa na kulifunua na kisha akatoa simu tatu kisha iweka ile aliyokuwa nayo. Alitoa moja na kupiga simu makao makuu ya NDA;

    "Haloow.......Ajenti namba 79 hapa naongea."aliongea Joachim.

    "Nakusikia Ajenti nikusaidie nini?"aliuliza Opareta.

    "Nahitaji ruhusa kwani makamu mkurugenzi ameuawa Mr. Harold Maebo na nimepigiwa simu natikiwa kuuawa kwa hiyo kabla ya kazi yao nataka wao watufahamu sie ni akina nani"aliongea Joachim kwa hasira.

    "Kweli Ajenti tumepokea taarifa za kifo hicho na Sauda ndie aliyetoa taarifa mapema."

    "Swala la kazi je????......" aliuliza tena.

    "Tunihitaji kukutumia taarifa maalum kuhusu kazi hiyo Ajenti"

    "Naomba angalia hizi namba na IMEI za simu iliyotumika katika kunipigia kisha ufuatilie GPS na taarifa zake".aliongea huku akiandika namba zile katika kompyuta iliyokuwa katika chumba kile.

    Baada ya muda aliambiwa maelezo kuhusu hiyo namba;

    "Mwenye namba anaitwa MALIK

    TAU RAZAQ anafanya kazi Mlimani City Centre na simu aliyotumia ni Samsung S3 na IMEI zake............."

    "Achana nazo angalia kwa sasa yuko wapi....."alimkatisha yule Opareta.

    "Namba haipatikani kwa sasa ila kwa sasa inaonekana yuko karibu na Le Grand Casino, mtaa wa Azikiwe Posta."aliongea.

    "Asante sasa naomba ukae online ili unipatie taarifa zake naelekea huko sasa hivi."aliongea haraka haraka huku akiweka kifaa cha sauti sikioni.

    "Nahisi unanisikia.....Opareta"Aliongea tena Joachim.

    Alitoka na kufunga haraka na kulifuta gari lake. Alikanyaga moto na kulifanya gari lile kufanya kazi kwa uwezo mkubwa. Alikimbiza gari na kumfanya mara kwa mara avunje sheria za barabara.

    "Kaelekea wapi hivi sasa!?"alikuwa akimuuliza Opareta wake.

    "Yuko eneo hilo hilo fanya haraka Ajenti"Alimjibu na kumfanya Joachim kuzidisha spidi za gari hiyo.

    "Sawa"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hakutaka kupoteza muda mara baada ya kukutana na foleni ndefu barabarani. Alilipaki gari lake na kuchukua bodaboda ili awahi.

    "Posta shilingi ngapi?"aliuliza huku akipanda kabla hajajibiwa.

    "Elfu kumi kaka."

    "Poa,lete niendeshe" alikubali huku akiikamata mwenyewe pikipki aina ya Boxer 150-C. Aliitoa na spidi ya hali ya juu huku akimrusha roho aliyembuba.



    * * * *



    National Defence Agency kama ilivyofahamika na majasusi wake. Kilikuwa kikosi cha siri kilichoanzishwa na Jeshi la Nchi ila kwa siri kubwa huku Serikali ikiwa haina taarifa wala habari yoyote ya uwepo wake. Hakuna ambaye alikifahamu katika uongozi ule kwani waanzilishi wote waliuawa ili kukificha kikosi kile cha siri. Kama alivyofahamika Mr. Harold Maebo hakuwa tu mmiliki wa kampuni ya sheria bali alikuwa kiongozi mkubwa sana tena wa siri kjatika kikosi kile cha NDA. Mara tu baada ya kuhusika katika kupambana na jeshi kubwa la Uganda mwaka 1977 na kuweza kurudi akiwa salama aliweza kujizolea sifa nyingi na kuwa mmoja kati ya vigogo wakubwa kijeshi. Lakini hakuishia pale alikutana na upinzani mkubwa mara baada ya kujikuta akiwa mmoja kati ya wapelelezi wakubwa walioitwa na CIA kutoka Afrika. Aliheshimik kutokana na utendaji kazi wake hadi akatunukiwa cheo kile wakati alipoingizwa katika kikosi kile hatari cha siri. Alikiongoza vizuri huku akiangalia nani anafanya kazi nzuri ili aingie katika kikosi kile na ndipo alipomuona kijana James Jacob aliyetegemewa kuwa hatari katika kikosi cha JWTZ ( Jeshi la Wananchi Tanzania ) mara baada ya kuchukua mafunzo ya kikomandoo na kufuzu vizuri sana nchini Cuba. Hakutaka utani ila alimuwahi akiwa Airport kabla hata Jeshi halijamuijia.

    "Karibu tena Tanzania...." aliwambia mara baada ya kumpokea yeye.



    "Karibu tena Tanzania...." aliwambia mara baada ya kumpokea yeye.



    * * * *



    Alipofika eneo lile alimuuliza Opareta;

    "Nakusikiliza wapi yupo sasa hivo?"

    "Hapo ulipokata kulia na upo nae karibu" Alijibu Opareta.

    "Sawa hebu muangalie kavaaje?" aliuliza Joachim.

    "Sina huo ewezo kwenye hii kompyuta yetu labda nitumie Satellite na hiyo inaonyesha mambo mengi kuhusu sie ko angalia tu." Alijibu Opareta.

    "Okey" Alijibu Joachim.

    Lakini wakati anafikilia alistuliwa na yule dereva wa pikipiki.

    "Vipi kwani kuna mtu unamtafuta?."

    Joachim hakujibu bali alibaki akijiuliza nini afanye ili ampate hiyo mtu.

    "Kwani unamuona kwa kutumia kitu gani?" aliuliza Joachim.

    "GPS ya IMEI yake." Alijibu Opareta.

    "Hack namba anayotumia"

    "Sawa ngoja nijaribu "

    "Yap.......tayari...........ni hii hapa..........+255710783876" Aliongea na kumfanya Joachim azikamata kwa haraka zaidi.

    "Sawa" Aliitikia Joachim.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Muda ile aliipiga ile namba na kuisika ikiita.

    "Halloow" Iliitikia sauti upande wa pili mara baada ya simu kupokelewa.

    "Naam...upo wapi?" Aliuliza Joachim mara baada ya simu kupelewa.

    "Nko Casino sasa hivi nitafute kesho" Ndivo alivojibu.

    "Le Grand Casino au wapi?"

    "Yah kwani uko nje au vipi?" Aliuliza bila kufahamu nani aliyepiga.

    "Ndio niko nje njoo mara moja"

    "Sawa namuagiza mtu akuijie"

    "Sawa"

    Aliitikia Joachim huku akikaa tayari.



    * * * *



    Papaa Paul kama alivyofahamika akiwa na mabosi wenzake ambao kazi yao ni kufuja Mali za nchi. Alikuwa ni moja kati ya mabosi wazito katika Jiji lile la Dar huku kikosi chake cha Rising Mafias kikiwa kinaogopeka kwa kufanya mauaji ya kutisha. Haikutaka kufahamika nani mmiliki wa kikosi kile hatari. Lakini hilo Mr. Harold Maebo aliliona na kumpatia jukumu la kufuatilia suala hilo Joachim. Ilikuwa rahisi kusikia mauaji tametokea na wauaji kuwa ni kikosi cha Rising Mafias huku wakihusika na wizi na upotevu wa pesa ndefu ya Nchi. Polisi waliliacha na kuliona ni tatizo la kawaida kabisa kama la magonjwa kama vile VVU , au Kipindupindu kama kawaida kabisa. Joachim alilifuatilia na kugundua uwepo wa Wakubwa walioweka mikono yao katika kikosi kile uhatari au kama walivyo fahamika kwa watu Jeshi Jeusi. Alipata msululu wa majina yaliyohusika na kikosi kile na ndipo ilipofahamika kua wa kuna mfanyakazi wa kampuni ya mauzo alikuwa mpelelezi na alikuwa na kazi ya kulipeleza Jeshi Jeusi. Nao hawakutaka kumpotezea waliamua kumuagiza Jack Loyce moja kati ya mamasenari ( Mamuruki) wa kikosi kile hatari. Hakuwa mwepesi wa kazi hivyo ndio maana wakamua kumtumia yeye aifanye kazi hiyo. Kilicho mshangaza Jack Loyce ni uwezo wa mtu ambaye alikuwa akimpeleleza kwani alikuwa mwepesi wa kuruka mitego yake mingi tena kwa akili sana. Alikaa akakumbuka siku aliyomuona akitoka ofisini kwake na kuamua kumfata mwanzo hadi mwisho wa safari yake ambapo ulikuwa katika ofisi za wakili za NEW VISION ADVOCATES. Mara alikaa muda kidogo kisha alitoka na kuondoka spidi eneo lile yeye hakutaka kumuacha ila alikuwa nae sahani moja. Lakini baada ya muda alimuona mtu wake akikata kushoto na kumpotea. Aliamua kurudi hadi ofisi zile ili atambue alienda kuonana na nani. Mara baada ya Mr. Harold Maebo kutoka ndio alitambua uwepo wa Joachim pale kwani alimtambua mzee yule katika mambo fulani yaliyohusu kundi lao la Rising Mafias.

    Aliamua aanze na mzee yule hivyo haraka aliamua kumpigia Papaa Paul na kuomba ruhusa ya kazi ile na kuruhusiwa kwa lolote. Alikuwa na mzee yule wakati akiingia kwake na kumpotezea huku akilipaki gari la ke aina ya Range Rover Sport kwa mbali. Alifungua mlanvo wa nyuma na kutoa sanduku dogo aina ya Briefcase na kuifungua. Alitoa vifaa fulani kisha akaanza kuviunganisha na kutoa bunduki ndefu iliyounganishwa na kiwambo cha sauti. Aliiwekea risasi na kiukoki huku ikonyesha uko tayari kwa kazi iliyo kuwa mbele yake. Hakutaka masihara na alichokuwa akikifanya siku zote. Haikumchukua muda aliliona gariaina ya Toyota Prado TX ikija. Aliitambua gari ile ya Mr. Harold Maebo hivyo aliiweka vizuri bundiki yake aliyoiunganisha na huachilia risasi iliyopenya katika kioo na kuingia katika kifuani cha Mr. Harold na kufumua moyo wake hali iliyo sababisha apoteze uelekeo na kuanguka na gari alilpomaliza alijiakikishia halakuwa na ushahidi wowote ulioonekana zaidi ya gari kwani ilionekana amepata ajali tena mbaya sana. Alipanda gari lake na kupotelea mbali. Hakupoteza alimpigia Joachim mara baada ya kupata namba yake aliyoipata katika ofisi yake. Alishangaa yule alikuwa mtu gani asiye ogopa vitisho vyake mara baada ya kumpigia. Aliliona kazi ni ngumu aliamua kuagiza moja kati ya madereva taxi wamfuatilia Joachim anakaa wapi il iwe rahisi kumpata.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ila nitatumia namba nyingine kukupatia jibu...." Ndio alivo jibu yule dereva taxi.

    "Sawa ila pigs siri mi nitakupa kiasi chocote Sawa...." Alijibu Jack Loyce na kuondoka zake.

    Aliondoka na kuelekea Le Grand Casino mara baada ya kuongea na dereva taxi yule. Ilipopita muda wa masaa matatu aliona namba mpya hivyo aliuona urahisi wa kazi na kuelewa yule alikuwa dereva taxi aliyemuagiza hivyo Aliamua kumuita ndani.

    "Bill nenda kamlete mgeni wangu pale nje" Aliagiza Jack Loyce.

    "Sawa"



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog