Search This Blog

Sunday, 22 May 2022

TAHARUKI - 5

 







    Simulizi : Taharuki

    Sehemu Ya Tano (5)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Vijana wote wanne, walikuwa wamekaa makini na kuyafungua masikio yao kumsuikiliza kiongozi wao, Giovan, aliyekuwa anawapa maelekezo ya kazi hiyo iliyokuwa inawakabili. Ni kazi nzito ya kuhakikisha mkufu ule wa thamani unapatikana kwa gharama yoyote! Ilikuwa ni kujitoa mhanga na kuuchukua kutoka mikonononi mwa watu washenzi, ambao pia hawakupenda uchukuliwe kibwege!

    Giovann alikohoa kidogo na kusafisha koo lake, halafu akawaambia kwa sauti ndogo lakini kavu, “Jamani, tumekutana hapa tena, ili kupanga mkakati wetu wa mwisho…”

    “Ndiyo mkuu…” wote wakaitikia.

    “Habari tulizozipata ni kuwa, mkufu ule umeshaletwa hapa Paris , baada ya kuibwa kule Uingereza. Na umeletwa na vijana wa tajiri, Mokili wa Ngenge, ambaye ameuchimbia ndani ya jumba lake linalolindwa na ulinzi mkali…” akanyamaza kidogo huku akiendelea kuwaangalia.

    “Tunajua kuwa kuupata ni kazi kubwa sana , hasa ukizingatia donge nono lililotangazwa na utawala wa Malkia, limewafanya watu wengi waingie katika sakata hili la kuutafuta. Na mbaya zaidi ni kwamba hatujuani, kila mmoja anausaka kivyake, hata hivyo hiyo isitukatishe tamaa, kwani tumejipanga ipasavyo.Tajiri, bilionea wa kireno, Miguel da Silva, kutoka nchini Angola, Afrika, ameshawasili hapa Paris, leo hii, tayari kwa kukabidhiana ule mkufu, ambao alikuwa anauhitaji kwa gharama yoyote…”

    “Basi, tutakapotoka hapa, tutajipanga na kuwa karibu na jumba la Mokili wa Ngenge, tukifanya doria ya nguvu kuhakikisha kuwa mkufu ule utakapochukuliwa na bilionea yule, na sisi tuwe naye sambamba wakati anaelekea uwanja wa ndege, na kuhakikisha tunaupora kutoka mikononi mwao hata kwa kumwaga damu, mnanipata?”

    “Tunakupata mkuu!” Watu wale wanne wakajibu!

    “Ndiyo, tutajipanga kama ifuatavyo. Nyie wawili, Goppa na Chriss, mtatumia usafiri wa pikipiki yetu kubwa, yenye uwezo mkubwa wa kukabiliana na mapambano yanayotukabili…”

    “Sawa mkuu!” Wakasema.

    “Pia, mtakuwa pamoja na silaha zenu, na mtalizungukia eneo lote la mtaa wa Mtakatifu Dennis, na kuhakikisha mnalifuata gari litakalokuwa limewachukua Mokili wa Ngenge na bilionea yule, Miguel da Silva, mimi na wenzangu, Papadou na Dimitros, tutakuwa kwenye gari letu aina ya Jeep na kumwafuatilia kuhakikisha tunaupora ule mkufu kutoka mikononi mwao. Kwa ujumla nyie mtakuwa mnatulinda kwa vile mtakuwa kwenye pikipiki inayoweza kupenya sehemu yoyote, na pia tunaweza kuwapasiana mzigo huo endepo tutaandamwa na polisi, mnauonaje mpango huo?”

    “Hakika ni mpango mzuri, bila shaka tutaufanya kama ulivyopanga mkuu,”Chriss akasema kwa kuunga mkono. Halikadhalika, Goppa, Papadou na Dimitros waliunga mkono pia.

    Giovann akaendelea kuwaangalia kwa muda, huku akiridhika kuwa vijana wake walikuwa na moyo wa kazi ile. Kwa upande mwingine alikuwa na uhakika wa kuupata mkufu ule kwa jinsi walivyokuwa wamejipanga. Hata hivyo katika moyo wake, alishajenga tamaa ya kuumiliki ule mkufu yeye peke yeke endepo ungepatikana. Alipanga kuwa watakapoupata tu, basi alikuwa tayari kuwaangamiza wenzake, na yeye kuumiliki peke yake! CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Haya, kama tumeshaelewana, basi tutawanyike tukaendelee na kazi,” Giovann akawaambia.

    “Sawa mkuu,” vijana wale wakasema. Halafu wakanyanyuka na kutoka nje ya jumba lile chakavu na kwenda kuendelea kufanya uchunguzi zaidi juu ya kazi hiyo.

    Baada ya wao kutoka, wakamwacha Giovann amekaa akitafakari. Akaendelea kuyazungusha macho katika pande zote za kuta ya jengo lile chakavu, ambalo wao walikuwa wameligeuza maskani ya kupangia mipango yao . Ukweli ni kwamba alikuwa anajipongeza kwa kuweza kuuratibu mpango ule mara tu baada ya kudokezwa kuwa mkufu ule utafikia kwa Mokili wa Ngenge, mtu anayemfahamu!

    Hata hivyo, baada ya vijana wake kuondoka, naye akanyanyuka na kutoka nje kwa kupenyeza katika mlango mmoja uliokuwa umezungukwa na vichaka pamoja na miti iliyokuwa na matawi iliyofungamana. Akatokeza katika mtaa uliokuwa kimya kabisa, na kuendelea na mipango inayowakabili…

    ********

    Dereva wa teksi waliyopanda wapelelezi, Brown Lambert na Frank Mumba, alisimamisha nje ya ofisi ya magari ya kukodi ya Paris Rent A Car. Ni Kampuni mashuhuri iliyokuwa inatoa huduma kwa wateja wa aina mbalimbali, wakiwemo watalii na hata watu wa kawaida wanaohitaji huduma hiyo kwa ujumla. Baada ya kupaki teksi ile, Brown na Frank wakashuka na kuelekea ndani ya jengo la ofisi kwa hatua za taratibu, na teksi ile ikaondoka kama ilivyokuja.

    Wakafika katika eneo la Mapokezi, ambapo walimkuta mwanadada mrembo wa kizungu aliyekuwa pale. Mwanadada huyo, aliyekuwa amevalia suti nyeusi na kijisketi kifupi, aliwakaribisha kwa lugha nzuri na ya kibiashara. Kisha akawaelekeza wakae kwenye makochi yaliyokuwa sehemu ile ya Mapokezi, halafu akawaendea kwa mwendo wa madaha na kuanza kuwaulizia shida iliyowapeleke pale.

    “Karibuni niwasaidie tafadhali…” akawaambia huku akitoa tabasamu.

    “Ahsante sana , tunahitaji huduma ya gari la kukodi…” Brown akamwambia.

    “Mnahitaji gari la aina gani?Yako ya aina nyingi tu, kwa huduma za kitalii, harusi, pikiniki na nyinginezo…”

    “Tunahitaji gari aina ya Toyota Land Cruiser, kwa ajili ya shughuli za kitalii…naona hilo litatufaa...”

    “Basi, hakuna wasiwasi, ngoja nikaonane na Meneje halafu tuweze kufanya taratibu za makabidhiano…”

    “Hakuna shaka, tunakusubiri,” Brown akasema huku akiendelea kumwangalia mwanadada yule mrembo. Muda wote ule, Frank alikuwa amenyamaza kimya tu, naye pia akimwangalia mwanadada.

    Brown akalipaki gari eneo la maegesho, halafu wakashuka na kuingia ndani ya mgahawa ule, huku wakipisha na watu wa aina mbalimbali, ambao hawakuweza kuwashtukia kama walikuwa ni wapelelezi mahiri waliokuwa kazini, na pia walikuwa wamejibadili sura zao. Walipoingia ndani ya mgahawa, wakaagiza kifungua kinywa, ambacho walianza kukishambulia na huku pia wakiendelea na maongezi yao ya kikazi.

    “Frank…” Brown akamwita kwa sauti ndogo.

    “Nakusikia Brown,” Frank akasema huku akimwangalia.

    “Unajua kuwa hivi sasa tuko jirani na makazi ya Mokili wa Ngenge?”

    “ Hilo naelewa..”

    “Basi cha kufanya, tuanze upelelezi wetu hapahapa. Tupande hadi juu ya ghorofa hili, ambapo tunaweza kuona yote yanayoendelea ndani ya nyumba ya Mokili Ngenge.”

    “Ni kweli, itabidi tufanye hivyo,” Frank aliunga mkono alichopanga Brown. Hivyo basi, walipomaliza kula, wakatoka ndani ya ukumbi ule wa chakula, halafu wakazunguka hadi upande wa pili, ambapo palikuwa lifti. Wakaipanda liti ile, ambayo iliwafikisha hadi juu katika ghorofa ya kumi.

    Mwanadada yule akaondoka na kuwaacha wakiwa wamekaa pale kwenye makochi. Akaingia kwenye chumba kimoja kilichokuwa upande wa kushoto. Hata hivyo hakukaa sana mle ndani, kwani alitoka na kuwaita Brown na Frank, ambao waliingia ndani ya chumba kingine kilichokuwa upande wakulia, ambapo aliandikishiana nao mkataba kuwa wangekaa na gari lile kwa muda gani, na hatimaye kuwakabidhi gari moja aina ya Toyota Land Cruiser Short Chasis, New Model, iliyokuwa imeundwa kwa ajili ya shughuli za kitalii.

    Baada ya kukabidhiwa, wakapanda na kuondoka dereva akiwa, Brown, na Frank alikaa upande wa kushoto. Wakaondoka nalo na kuelekea katika mtaa wa Mtakatifu Dennis, uliokuwa unapita karibu na makazi ya Mokili wa Ngenge. Mtaa ule uliokuwa na pilikapilika chache, pia ulikuwa na nyumba chache za kibiashara na makazi ya watu. Pale kulikuwa na mgahawa mmoja uliokuwa ndani ya nyumba moja ya ghorofa kumi, ikiwa nayo imezungukwa na miti mingi iliyokuwa imefungamana na kujifanya ijifiche kwa sehemu ile ya chini na kubakiza sehemu ya juu kuanzia ghorofa ya tano.



    Brown akalipaki gari eneo la maegesho, halafu wakashuka na kuingia ndani ya mgahawa ule, huku wakipisha na watu wa aina mbalimbali, ambao hawakuweza kuwashtukia kama walikuwa ni wapelelezi mahiri waliokuwa kazini, na pia walikuwa wamejibadili sura zao. Walipoingia ndani ya mgahawa, wakaagiza kifungua kinywa, ambacho walianza kukishambulia na huku pia wakiendelea na maongezi yao ya kikazi.

    “Frank…” Brown akamwita kwa sauti ndogo.

    “Nakusikia Brown,” Frank akasema huku akimwangalia. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Unajua kuwa hivi sasa tuko jirani na makazi ya Mokili wa Ngenge?”

    “ Hilo naelewa..”

    “Basi cha kufanya, tuanze upelelezi wetu hapahapa. Tupande hadi juu ya ghorofa hili, ambapo tunaweza kuona yote yanayoendelea ndani ya nyumba ya Mokili Ngenge.”

    “Ni kweli, itabidi tufanye hivyo,” Frank aliunga mkono alichopanga Brown. Hivyo basi, walipomaliza kula, wakatoka ndani ya ukumbi ule wa chakula, halafu wakazunguka hadi upande wa pili, ambapo palikuwa lifti. Wakaipanda liti ile, ambayo iliwafikisha hadi juu katika ghorofa ya kumi.

    Baada ya kufika katika ghorofa ile ya kumi, wakatoka ndani ya lifti, halafu wakapandisha ngazi fupi zilizokuwa zinaishia juu, mwisho kabisa katika ghorofa ile ya kumi. Wakafikia sehemu iliyokuwa na uwazi mkubwa tu kama uwanja, ambapo pia unaweza kuona eneo lote la chini kwa umbali mrefu, na pia kuweza kuona upande wa pili wa makazi ya Mokili Ngenge. Eneo lote la kule juu lilikuwa kimya kabisa, ukizingatia hakuna mtu yeyote aliyekuwa na muda wa kupandisha kule. Ni sauti za ndege aina ya Tausi na wengineo ndiyo ziliweza kusikika na kuleta burudani ya pekee, ndani ya viunga vya mtaa ule maarufu wa Mtakatifu Dennis.

    “Huu ni muda muafaka wa kuchunguza makazi ya Mokili wa Ngenge…” Brown akasema huku akitoa darubini ndogo, lakini iliyokuwa na uwezo wa kuona mbali.

    “Ni kweli, tufanye hivyo,” Frank naye akasema.

    Brown akaiseti ile darubini na kuanza kuvuta karibu kila kitu kilichokuwa kinaendelea ndani ya makazi ya Mokili wa Ngenge baada ya bilionea, Miguel da Silva kuingia. Ukweli ni kwamba darubini ile iliweza kuvuta kila kilichokuwa kinaendelea ndani ya jumba lile kwa ukaribu zaidi. Kwa upande wa nje, kulikuwa kumezungukwa na walinzi, waliokuwa wamebeba silaha, wakiangalia pande zote, tayari kumtungua mtu yeyote asiyehitajika kulisogelea eneo lile!

    Upande wa ndani, katika jumba lile la kifahari, Mokili wa Ngenge na bilionea, Miguel, walikuwa wamejichimbia katika chumba maalum, wakiendelea na maongezi yao , na pengine wakiburudika na vinywaji baridi. Walikuwa wakiongea kibiashara kuhusu mkufu ule wa almasi aliokuwa nao Mokili. Ukweli ni kwamba ile darubini maalum, ilimwezesha Brown kuona mambo yote yaliyokuwa yanaendelea mle ndani baina ya Mokili na Miguel, kama vile ni sinema.

    “Aisee, naona wanapanga mipango ya kibiashara…” Brown akamwambia baada ya kuitoa ile darubini machoni mwake.

    “Hebu niangalie…” Frank akasema huku akichukua ile darubini na kuiweka machoni mwake. Naye akashuhudia kile kilichokuwa kinaendelea mle ndani. Ilikuwa ni kama picha ya sinema ya kusisimua…

    ********

    Walionekana Mokili Ngenge na bilionea, Miguel da Silver, wakiwa wamekaa ndani ya chumba kile maalum walichokutana. Walikaa katika makochi ya thamani kubwa, huku pande zote wamezungukwa na walinzi wa Mokili, waliokuwa makini sana kwa kile kilichokuwa kinaendelaa. Mbele yao , kwenye meza ya duara, palikuwa na briefcase ya rangi nyeusi, iliyokuwa imeihifadhi ule mkufu wa thamani kubwa.

    Kwa muda wote, Miguel naye alikuwa akiiangalia ile briefcase kwa uchu, huku akiwa na hamu ya kutaka kujua kilichokuwa ndani yake. Tuseme kwamba udenda ulikuwa ukimtoka ukizingatia alikuwa na homa kubwa ya kuupata ule mkufu ili umsaidie katika shughuli zake za madini katika mgodi wake ulioko nchini Angola . Mokili akaichukua briefcase kwa mkono mmoja, halafu akaifungua na kusema:

    “Ni vyema tuiangalie mali yenyewe…”

    “Ni jambo la maana…” akasema Miguel.

    “Ngoja niitoe…” Mokili akasema. Halafu akautoa ule mkufu wa thamani na kuuweka juu ya meza. Ulikuwa ni mkufu uliokuwa na uzito kiasi, na unaomeremeta kutokana na madini yale ya almasi yaliyoutengeneza Baada ya kuutupia macho, wote wakatabasamu!

    “Hebu utoe!” Akasema Miguel.

    “Unaiona mali hii?” Mokili akamwambia.

    “Ninauona Mokili…” Mokili akasema na kuendelea. “Ama kweli mmefanya kazi kubwa sana . Mnastahili pongezi kubwa!”

    “Ni kweli, tumefanya kazi kubwa sana . Na mpaka muda huu tunapoongea na wewe, mkufu huu unasakwa na watu wa aina mbalimbali, wakiwemo wapelelezi wa kimataifa, hasa ukizingatia lile donge nono lililotangazwa na utawala wa malkia wa Uingereza. Basi, ni jinsi gani utakavyoona mkufu huo unatafutwa!”

    “Kwa hivyo una maana kuwa itakuwa ni vigumu sana mimi kuondoka nao hapa Paris ?” Miguel akauliza kwa mshangao!

    “Hapana…usihofu. Utaondoka nao salama kabisa. Kama unavyojua mimi ni mtu mkubwa na maarufu sana hapa Paris . Hakuna ninachoshindwa, hivyo nimeshasafisha njia yote kwa kumwaga fedha. Hakuna atakayekusumbua, na isitoshe nitakusindikiza hadi uwanja wa ndege, ambapo nitahakikisha mpaka unapanda ile ndege yako mwenyewe, unanipata?” CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “ Kama ni hivyo, nimekupata Mokili,” Miguel akasema kwa sauti ndogo, halafu akaunyanyua mkono na kuiangalia saa yake. “Basi, tumalizane na mimi niondoke hapa Paris , watu hao wanaousaka mkufu huu, wanaweza kutugeuka mimi na wewe ikawa balaa!”

    “Kumalizana kutakuwa jambo la maana sana ,” Mokili naye akasema kumuunga mkono Miguel huku tama imemjaa!

    “Ngoja nikuandikie hundi kabisa,” Miguel akasema. Halafu akachukua mkoba wake na kuufunua, kisha akatoa kitabu cha Hundi, ambayo Mokili angeweza kuchukuwa pesa katika tawi lolote la Benki ya Barclays, ulimwenguni, ambapo Miguel alikuwa na akaunti zake.

    Hatua iliyofuata ilikuwa ni kuandikiana Hundi ile, juu ya malipo ya mkufu ule. Miguel akaandika huku Mokili akimwangalia kwa makini sana , na baada ya kumaliza kuandika, Miguel akamkabidhi ile hundi na Mokili akamkabidhi ule mkufu, ambao aliuweka ndani ya mkoba wake aliokuja nao kutoka Angola , nchini Afrika. Kwa vile Miguel alishakabidhiwa ule mkufu, hakuwa na muda wa kuendelea kukaa tena pale, hasa ukizingatia ulikuwa unasakwa na watu wengi, hivyo kwa yeye kuwa nao. Lilikuwa jambo la hatari sana !

    “Sina muda wa kukaa sana ,” Miguel akamwambia Mokili.

    “Hata mimi naelewa kuwa muda ni mali !” Mokili akamwambia huku wote wakinyanyuka kutoka katika makochi.

    Wakatoka nje huku wakisindikizwa na walinzi pande zote. Baada ya kufika sehemu ya maegesho, wakapanda gari lile aina ya Mercedes Benz, lenye milango sita, lililokuwa limepaki kule nje. Dereva akawafungulia milango, Miguel na Mokili, ambao waliingia ndani, wakiwa na ule mkoba uliokuwa na mkufu wa thamani, na milango ikafungwa.

    Gari likaodolewa na dereva huku nyuma likifuatiwa na gari jingine aina ya Ranger Rover, iliyokuwa na vioo vya giza, na ndani yake kukiwa na walinzi wanne wa Mokili, waliokuwa wamejizatiti kwa silaha kali, kama bunduki za rasharasha, na hata mabomu ya kutupa kwa mkono, ambavyo vyote Mokili alivipata kwa njia anayoijua mwenyewe, ukizingatia kuwa pia ni mmoja wa watu wanaowasaidia baadhi ya wapiganaji wa mistuni, waasi, katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

    Kwa ujumla wote waliokuwa ndani ya magari yale, hawakuwa na wasiwasi wowote, hadi walipotoka nje ya geti la himaya ya Mokili wa Ngenge, mtaa wa Mtakatifu Dennis. Benz likaingizwa katika barabara kuu kuelekea uwanja wa ndege. Hata hivyo, Mokili wa Ngenge hakujua kwamba hatua chache tu, kutoka pale lilipokuwa jumba lake, juu ya paa la jumba la ghorofa, wapelelezi, Brown na Frank, walikuwa wakifuatilia nyendo zao…



    ********

    Bado hali ya mtafutano ilikuwepo. Baada ya saa moja kupita, Giovan na maharamia wenzake, walikutana tena katika maskani yao , ndani ya jumba chakavu, tayari kwa kuitekeleza ile kazi yao ya kuupora mkufu ule kutoka mikononi mwa Mokili wa Ngenge, aliyekuwa na bilionea, Miguel, wakielekea uwanja wa ndege. Hakika walikuwa wamekaa tayari kukabiliana na msafara ule uliokuwa na ulinzi mkali, na muda huo walikuwa wakifuatilia muda wa kuondoka kwa msafara ule kutoka nyumbani kwa Mokili wa Ngenge, kwani kulikuwa na mtu anayewapa mawasiliano.

    Kama kawaida, Giovan alikuwa amewasimamia vijana wake, Papadou, Dimitros, Goppa na Chriss, ili kuwapangia majukumu yanayowakabili. Upande wa pili, katika uwanja mdogo uliokuwa ndani ya jumba lile, palikuwa na gari moja aina ya Jeep, lililokuwa limefunikwa turubai, na milango ikiwa wazi. Pembeni yake palikuwa na pikipiki kubwa aina ya Yamaha, ilikuwa imepaki, ikisubiri tu kutumika katika mpango ule kabambe, ambao kwa vyovyote walijua kuwa ni lazima wangefanikiwa. Muda ule, Giovan alikuwa akivuta sigara kubwa aina ya ‘Ciggar,’ na kupuliza moshi hewani kama treni ya mkaa wa mawe!

    “Nimepata taarifa kuwa msafara ndiyo umeondoka…” Giovan akawaambia vijana wake na kuongeza. “Hivyo basi, Goppa na Chriss mtaondoka na pikipiki hiyo, ambayo mtaiendesha sambamba na msafara wao unaopita katika barabara ile ya Mtakatifu Dennis, upande wa pili wa duka la vyakula, mpo?”

    “Tunakupata mkuu!” Wote wakasema kwa pamoja.

    “Pale mtakuwa macho kuangalia msafara huo wa magari, lililombeba Mokili na Miguel, hadi yatakapofika kwenye taa za trafiki. Baada ya kuika pale, msifanye chochote, mtasubiri amri yetu juu ya cha kufanya, sijui mnanipata?”

    “Tunakupata bosi, endelea…”

    “Halafu, mimi na wenzangu, Papadou na Dimitros, tutakuwa na gari hilo, Jeep, ambalo tutatumia kulifuatilia gari hilo kwa ukaribu zaidi, ambapo watakapofika kwenye taa za trafiki, tutawashambulia na kuwapora mkoba uliokuwa na mkufu huo. Baada ya kuwapora, tutawarushia nyie, ambao mtakimbia nao na kukutana ndani ya maskani yetu!”

    “Sawa mkuu!”

    “Haya, tuondoke!” CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wote wakatoka huku wakiwa na silaha zao walizokuwa wamezichimbia kibindoni, kiasi kwamba ilikuwa siyo rahisi kushtukuwa na mtu yeyote. Kundi la Giovan likaingia ndani ya lile gari na kuondoka kwa mwendo wa kasi kuelekea mtaa wa Mtakatifu Dennis, kuuwahi ule msafara wea Mokili wa Ngenge na bilionea Miguel da Silva. Lakini Goppa na Chriss walibaki nyuma huku wakivalia kofia zao za kuendeshea pikipiki, tayari kwa kuondoka. Walipohakikisha wenzao wameondoka, ndipo walipoanza kuteta jambo fulani:

    “Chriss,” Goppa akaita.

    “Sema mshirika…” Chriss akaitikia.

    “Unajua mimi nina wazo moja muhimu sana .”

    “Wazo gani?”

    “Kuhusu mkufu tunaouwania.|

    “Kwani imekuwaje?”

    “Hata tukiupata hatutafaidi kitu!”

    “Unamaanisha nini?”

    “Unafikiri bosi, Giovan alivyokuwa na tamaa, anaweza kutuacha hai? Ni lazima atatumaliza na hatimaye kuuchukua mkufu huo na kwenda kuwania hilo donge nono!”

    “Kweli nimekupata,” Chriss akasema na kuendelea. “Na mimi nilikuwa na wazo kama hilo . Tokea mwanzo machale yalikuwa yananicheza, na ninaona kama sisi tunatumika kama chambo tu!”

    “Sasa tufanyeje?”

    “Ngoja nikupe mpango. Baada ya kufanikwa kuupora kutoka mikononi mwa Mokili, najua watatupasia sisi ili tuweze kuondoka nao kwa pikipiki hii. Sasa tusingoje mpaka watupasie, bali tuwamiminie risasi hapohapo na kuwamaliza, kisha tunakimbilia kule maskani na kujua cha kufanya, mambo ni mbele kwa mbele!” Goppa akaendelea kumwambia Chriss.

    “Hakuna shaka, basi, tutafanya hivyo, na umesema jambo la maana! Tuondoke zetu!”

    Baada ya kukubaliana, ndipo walipopanda pikipiki yao na kuiondoa kwa mwendo wa kasi, kuelekea mtaa wa Mtakatifu Dennis, wakiwa na nia moja tu, kuwamaliza wenzao, na kuuchukua mkufu!

    Kazi nzito!

    ********

    Mara baada ya msafara wa magari ya Mokili wa Ngenge, kuelekea kwenye uwanja wa ndege kuanza, wapelelezi, Brown Lambert na Frank Mumba, walishuka haraka kutoka kule juu ghorofani. Baada ya kufika chini, wakaliendea gari lao aina ya Toyota Land Cruiser, lililokuwa sehemu ya maegesho, ambalo walipanda na kuondoka kuwafuatilia nyuma bila wao kufahamu. Wakati huo ilikuwa imetimu majira ya saa saba na nusu za mchana, na kwa ujumla hali ilikuwa ni shwari kabisa kwa siku ile.

    Wakiwa ni wapelelezi waliofuzu katika taaluma ile ya upelelezi, walikuwa wakichunguza pande zote, kushoto, kulia, nyuma, na mbele wanapoelekea. Na ile ilikuwa ni kuweza kujua kama kulikuwa na watu wengine waliokuwa wanawafuatilia akina Mokili wa Ngenge na bilionea, Miguel da Silva, waliokuwa ndani ya lile gari aina ya Mercedes Benz, lililokuwa linakwenda kwa mwendo wa wastani katika barabara ile kuu. Na pia, nyuma yake likifuatiliwa na gari la walinzi, aina ya Ranger Rover, lenye vioo vya giza .

    Frank na Brown hawakuamini kama kwa wakati ule walikuwa peke yao , wakiwafuatilia watu wale. Machale yalikuwa yamewacheza na kujiweka tayari kukabiliana na chochote! Ndiyo, walihisi kuwepo kwa watu hatari sana , ambao nao walikuwa wakiuhitaji ule mkufu wa thamani, baada ya kutangaziwa kwa lile donge nono kutoka kwa Malkia wa Uingereza. Na ile waligundua baada ya kuchunguza yale magari yaliyokuwa yakiongozana katika barabara ile, kwani waliliona gari lile aina ya Jeep, likiwa kama linavizia baada ya kuwaona wahusika waliokuwa ndani ya hilo gari, wakiwa wanaongea kwa kuliangalia gari la Mokili kwa muda mrefu, na ile ilikuwa ni baada ya wao kutumia ile darubini waliyokuwa nayo.

    Hatimaye magari yakafika yakafika kwenye taa za kuongozea magari, kwenye makutano ya barabara, ambapo yote yalisimama baada ya taa nyekundu kuwaka. Hivyo yakasubiri pale kusubiri taa ya kijani iwake, ambapo lile Benz lilisimama jirani kabisa jirani zaidi na taa zile na kutanguliwa na magari mawili. Wote, Mokili, Miguel na wale walinzi, waliokuwa ndani ya magari yale, walikuwa wakiangalia taa ile, wakiwa na mawazo ya kuwahi uwanja wa ndege ili angalau Mokili autue ule mzigo! Lakini upande wao wa pili ubavuni mwao, Giovan na wenzake walikuwa wanawaangalia wao ili waweze kuwapora ule mkufu!

    Taa ya kijani ikawaka! Magari yakaanza kuondoka. Lakini sekunde ileile, Watu watatu waliokuwa ndani ya gari lile aina ya jeep, lililokuwa ubavuni mwao, walichomoka wakiwa na bunduki fupifupi na kuanza kufyetua risasi mfululizo kuelekea katika magari yote mawili, lile Benz, na lile la walinzi wa Mokili Ngenge! Walikuwa ni Giovan, Papadou na Dimitros, waliokuwa wanawafuatilia kwa muda tokea walipotoka katika makazi yake kuelekea uwanja wa ndege. Walikuwa wakiwarushia risasi kwa utaalam na mpangilio wa hali ya juu. Ilikuwa kama walikuwa wanacheza sinema!

    Risasi zile ziliwajeruhi vibaya sana watu wote waliokuwa ndani ya magari yale, wakiwemo, Mokili na Miguel, na wale walinzi, ambao walishindwa kutoka kwa mara moja, hasa ukizingatia lilikuwa ni tukio la kushtukiza sana, na pia hawakutegemea kama lingetokea sehemu ya wazi namna ile. Hivyo basi majeruhi wale wakabaki wakigugumia kwa maumivu na kushindwa la kufanya! CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kufumba na kufumbua, Papadou na Dimitros wakazama ndani ya Benz na kuuchukua ule mkoba wenye mkufu wa thamani, na kuingia nao ndani ya lile gari lao aina ya Jeep. Gari likaondolewa kwa mwendo wa kasi kwa kupitia upande wa pili ambapo palikuwa na nafasi ya kupenyea. Wakati huo watu wote, wapita njia na hata madereva, walikuwa wamechanganyikiwa baada ya tukio lile kutokea, na hawakuwa na la kufanya, kwani hakuna asiyejua madhara ya risasi! Haina macho!

    Wapelelezi, Brown na Frank walilishuhudia tukio lile lilivyotokea, hivyo hawakutaka kufanya pupa. Wakapenyeza gari lao na kuanza kuwafuatilia nyuma watu wale, ambao walikuwa wakikatiza katika mitaa mbalimbali ya jiji ili kuwapoteza askari, kama waliokuwa wanawafuatilia. Walipofika katika mtaa wa nne hivi, ikatokea ile pikipiki kubwa aina ya Yamaha, ambapo juu yake walikuwepo, Goppa na Chriss, waliokuwa wamevalia mavazi maalum na kofia za kuendeshea pikipiki. Halafu wakaizuia gari ile kwa mbele, upande wa kulia, kisha wote wakaruka chini wakiwa na bunduki zao fupi!





    Tukio lile liliwashangaza Giovan na wenzake hasa ukizingatia walikuwa wamepanga kuwa wapasiane ule mkoba na siyo wao wawazuilie kwa mbele! Pale wakajua kuwa kulikuwa na hali ya usaliti na si vinginevyo! Hata hivyo walikuwa wamechelewa! Risasi zikaanza kufyetuliwa kuelekea kwenye lile Jeep, ambapo nao, Giovan na wenzake wakaanza kujibu mapigo! Mirindimo ya risasi ikarindima kwa muda wa dakika tano, na watu wote watatu, Giovan, Papadou na Dimitros wakauawa, na mkoba ukachukuliwa na wale watu wawili, Goppa na Chriss! Halafu wakapanda pikipiki yao na kutimua mbio!



    Tukio lile lilishuhudiwa na wapelelezi wale, Brown na Frank, ambapo hawakupenda kuingilia katika mapigano yale ukizingatia yalikuwa hayawahusu. Hao walichohitaji ni ule mkufu uliokuwa unagombaniwa na watu wale, ili nao waupate. Basi, nao wakaamua kuwafuatilia nyuma, Goppa na Chriss ili wajue hatima yake. Ukweli ni kwamba walishangaa sana baada ya kuona jinsi mkufu ule ulivyokuwa unatakiwa na watu wengi kuliko walivyotegemea!



    Mbio zikaanza tena!



    Ni mtafutano!



    ********



    Ving’ora vya magari ya polisi na vikosi vya uokoaji vilisikika. Magari yale yalikuwa yanaelekea katika eneo lile la tukio kwa mwendo wa kasi, ili kutoa msaada kwa majeruhi wale waliothiriwa na mapambano ya risasi! Katika eneo la tukio, palikuwa na magari yale mawili, Mercedes Benz na Ranger Rover, yaliyokuwa na matundu ya risasi na damu imetapakaa ndani na miili ya watu kulaliana.



    Baada ya kufika, walizungushia uzio na kuanza kuwatoa wale majeruhi waliokuwa katika magari yale, wakiwemo, Mokili wa Ngenge na bilionea, Miguel da Silva, ambaye naye alikuwa akigugumia kwa maumivu makali aliyokuwa nayo. Alikuwa amejeruhiwa kwa risasi begani, na damu zikimtoka kwa wingi. Hakuamini alichokuwa anakiona, kwani alishuhuia mwenyewe jinsi mkoba wake ulivyochukuliwa na mtu punde tu baada ya kushambuliwa kwa risasi ghafla na watu asiowafahamu!



    Kwa upande wa Mokili wa Ngenge, alikuwa naye amejeruhiwa kwa risasi katika sehemu mbalimbali za mwili wake. Wakati ule alikuwa na fahamu zake, akiwa haamini kile kilichokuwa kimetokea! Yaani kuporwa ule mkoba uliokuwa na ule mkufu wa almasi aliokuwa ameusotea kwa gharama kubwa sana ! Hakika hakuamini, alijiona kama mtu aliyekuwa katika ndoto ya kusisimua!



    Lakini kitu kilichowashangaza maafisa wa polisi, ni baada ya kufanya upekuzi, juu ya watu wale na kukutwa na silaha za hatari, walizokuwa nazo ndani ya gari. Hata hivyo, walichukuliwa na kupelekwa katika Hospitali ya Taifa, kwa matibabu na hatua za kisheria zichukuliwe baadaye…



    ********



    Watu wale wawili, Chriss na Goppa, wakiwa wameudhibiti mkoba ule wenye mkufu ndani yake, waliifuata barabara moja inayotoka nje ya jiji, wakiwa katika mwendo uleule wa kasi. Dereva wa pikipiki ile alikuwa ni Gopa, na Chriss alikuwa ameukamata ule mkoba huku akiangalia nyuma kama kulikuwa kuna watu waliokuwa wanawafuatilia. Brown na Frank waliokuwa wanawafuatilia wakawaacha watangulie kwanza, na mwishowe wakaiacha barabara kuu, na kuifuata barabara ya vumbi ilinayoelekea katika msitu uliokuwa na miti mingi, sehemu iliyokuwa na majengo ya zamani yasiyotumika.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kuwapotea tu, Brown aliongeza mwendo wa gari hadi walipoliona jumba moja lililokuwa upande wa kushoto mbele yao . Ni jumba la zamani sana, ambalo halikuonyesha dalili zozote za kuishi binadamu, ambalo lililozungukwa na miti iliyokuwa imefungamana na kufanya kuwe na kiza, sehemu ambayo watu wale waliokuwa na pikipiki walipoelekea na kuingia ndani yake kwa mwendo uleule wa kasi. Hakika eneo lile lilikuwa linatisha sana kwa jinsi mazingira yake yalivyokuwa.



    “Mh, umeona wameingia ndani ya jumba lile?” Frank akamwambia Brown.



    “Ndiyo, nimeona…” Brown akasema huku akisimamisha gari.



    “Sasa tufanyeje?” Akauliza Frank.



    “Hakuna jinsi, itabidi tuwaingilie…”



    “Ok, tufanye hivyo…”



    Brown na Frank wakashuka kutoka ndani ya gari huku wakiwa na silaha zao mikononi. Wakaanza kuliendea jumba lile kwa mwendo wa tahadhari bila kuonekana na mtu yeyote, kwa sababu eneo lote lilikuwa kimya kabisa, ni sauti za ndege tu ndiyo zilikuwa zinasikika. Baada ya kufika katika jumba hilo , wakabanisha pembezoni na kuchungulia kilichokuwa kinaendelea mle ndani. Kulikuwa na sauti za watu zilizokuwa zinasikika wakiongea kama walikuwa wanabishana.



    Mara milipuko ya risasi ikasikika! Walipochungulia katika upenyo, waliweza kumwona mtu mmoja, pande la baba, akiwa amekamata bastola iliyokuwa inafuka moshi. Alikuwa amewalipua, Goppa na Chriss, ambao walikuwa wamefika pale muda siyo mrefu. Mkononi mwake alikuwa amekamata ule mkoba uliokuwa na mkufu. Baada ya kuhakikisha amewamaliza, akatoka nje ya jumba lile na kuiendea ile pikipiki aliyofika nayo, ambapo aliipanda tayari kwa kuondoka. Kazi alikuwa ameshaimaliza!



    Mtu yule alijulikana kwa jina la Mario Tuzo, mtu hatari na jambazi la kutupwa, ambaye naye alikuwa anauhitaji mkufu ule tokea habari zile za mkufu huo kutapakaa katika vyombo vya habari. Ni kuhusu lile donge nono lililokuwa limetolewa, na akiwa ni mtu aliyejiamini sana , hakupenda alikose. Hivyo basi, aliamua kulifuatilia hatua kwa hatua mpaka mwisho alipopata habari kuwa maharamia walikuwa wameupata, na uko safarini kwenda nchini Angola , Afrika.



    Basi, Mario Tuzo alipowana akina Chriss wakiwaua wenzao, na yeye akawafuatilia nyuma kwa pikipiki kwa kupitia katika njia nyingine ili asiweze kushtukiwa. Akawawahi ndani ya jumba lile ili awapore ule mkufu, ambapo kweli alifanikiwa kuwakuta na kuwamaliza baada ya kutokea mabishano mafupi!



    Ndivyo ilivyokuwa!



    “Simama hapo hapo!” Frank akamwambia kwa sauti kavu!



    “Usijiguse!” Brown naye akamwambia. Wote walimnyooshea bastola zao tayari kwa kufanya chochote endepo angekataa kutii!



    “Nini?” Mario akageuka nyuma kuwaangalia watu wale waliokuwa wamempa amri! Akakutana na mitutu ya bastola imemuelekea!



    “Tupa huo mkoba chini!” Frank akamwambia.



    “Unasemaje?” Akaendelea kuuliza Mario.



    “Tupa huo mkoba chini!” Akasema Brown.



    “Kirahisi namna hiyo?” Mario akasema huku akiirekebisha miwani yake. Halafu akaiwasha pikipiki na kutaka kuondoka. Lakini pale alikuwa amefanya kosa!



    Risasi nne zilizokuwa zimetoka katika bastola mbili za Frank na Brown zilizomrusha Mario kutoka juu ya pikipiki aliyokuwa ameikalia na kumtupa pembeni! Mkoba ule ukamtoka mkononi na kuruka pembeni, na risasi zile zilikuwa zimemfumua mogongoni na kutokea upande wa kifuani! Akafa palepale!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Shenzi sana !” Frank akasema huku akiirudisha bastola yake!



    “Hatutaki mchezo!” Akaongeza kusema Brown huku akiuendea ule mkoba, ambao aliuokota na kuudhibiti.



    “Tuondoke eneo hili…” akasema Frank.



    “Ni jambo la maana!”



    Wote wawili wakapanda ile pikipiki na kuondoka katika eneo lile, kuelekea kule walipoliacha lile gari lao. Dereva akiwa ni Brown, aliiwasha ile pikipiki na kuiondoa kudi kule walipotokea kwa mwendo wa kasi huku pia wakiwa na tahadhari kubwa isije ikawa kuna watu wengine waliokuwa wanawafuatilia.



    Wakiwa njiani, Browna alipiga simu na kuomba msaada kwenye kampuni ya ndege za kukodi, aina ya helikopta, ili ifike na kuwaondoa katika eneo lile haraka, kwani hali ya hatari ilikuwa inanukia kadri muda ulivyokuwa unakwenda. Mkoba ule uliokuwa na mkufu wa thamani, ulikuwa unahitajiwa na watu wengi!



    Baada ya robo saa, mlio wa helikopta uliweza kusikika angani, ambapo baada ya rubani kuwaona pale walipokuwa, aliishusha huku ikitimua vumbi jingi. Baada ya kutua tu, akafungua mlango na kuwaruhusu, Brown na Frank kuingia ndani wakiwa na ule mkoba wao. Lile gari aina ya Toyota Land Cruiser la kukodi, waliliacha sehemu ile walipolipaki, lakini kwa kuwajulisha watu wa kampuni ile kwenda kulichukuwa.



    Rubani alipoinyanyua ile helikopta tu, waliweza kuiona gari moja aina ya Ford ikifika pale kwa kasi ya ajabu huku ikitimua vumbi. Baada ya gari lile kusimama, wakashuka watu wawili, waliokuwa na bunduki mikononi mwao. Nao walikuwa wakiufuatilia ule mkufu wenye thamani, lakini wakachelewa na kukuta, wapelelezi wale, Brown na Frank wameshautia mikononi.



    Watu wale wakabaki wamechanganyikiwa na kuiangalia ile helikopta ilivyokuwa inapaa angani, na kadri ilivyokuwa inapaa, ndiyo watu wale walivyoonekana wadogo mpaka ilipopotea, na wenyewe wakafunikwa na ule msitu mzito uliokuwa katika eneo lile.



    “Umeona?” Brown akamuuliza mpelelezi mwenzake, Frank Mumba aliyekuwa bado akiangalia chini, ne ya kioo cha dirisha.

    “Nimeona,” akajibu Frank huku akita basamu na kuacha kuangalia, kure jesha macho yake kwa Brown.



    “Nao walikuwa wanauhitaji kwa udi na uvumba...”



    “Wamechelewa...” Frank Mumba akamaliza kusema.



    “Hakika tumefanya kazi ya ziada!”



    “Ni kweli, nafikiri pia, Waingereza watafurahi kwa kure jeshwa tena kwa mkufu wao wa thamani kubwa, ulioibwa na wakora wale!”



    “Ni furaha ilioje...lakini hatujui hekaheka tutakayokutana nayo pindi tutakapofika London . Kwani kuna watu wengine ambao wanaouhitaji kwa hali na mali , ili nao waufikishe na kulipwa donge nono!”



    “ Hilo neno, lakini tutakabiliana nao!”



    Wanaume wale wawili, Frank Mumba na Brown Lambert, walikuwa wakiongea baada ya kufanikiwa kuwaepuka maadui wale waliokuwa wanawafuatilia katika kuutaka mkufu ule wa thamani, lakini wakachelewa!



    Mkoba uliohifadhi mkufu, ulikuwa umelala kan do ya kiti cha kati, uk ilindwa barabara, na hata rubani hakujua kilichokuwa ndani ya mkoba ule!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Helikopta ikazidi kukata mawimbi angani...





    *****MWISHO*****



    TOA MAONI YAKO

0 comments:

Post a Comment

Blog