Simulizi : Siri Ya Miaka 20
Sehemu Ya Nne (4)
***********
Kule millz hotel alionekana tom akiwa kaishika bunduki huku jicho lake moja likichungulia ndani ya lenzi iliyopo juu ya bunduki hiyo kuelekea kwenye mlango wa kutokea nje ya ukumbi huo... huku kidole chake kikiwa tayari kwenye kitufe cha kufyatulia risasi.... alikaa tayari kama edo akitokeza tu afyatue risasi..
kule nje ya millz hotel bony aliwafatilia watu wale aliona wameingia kwenye ngazi ya kutumia umeme(lift) aliona yule mmoja kabofya kitufe kimeandikwa 28C.......bony alianza kukimbia kuelekea upande wa juu kwa kutumia ngazi za kawaida kwa sababu bony alikuwa ni mtu wa mazoezi kila siku hivyo hakuweza kuchoka alikimbia kwa kasi utadhani anashuka kumbe anapanda kuelekea upande wa juu.. alipofika ghorofa ya 28...alijibanza sehemu ya ukuta kisha akachungulia aliona watu wale wameingia kwenye chumba no:555
*********CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kule mlimani city edo alitoka nje huku kaongozana na mchumba wake grace....
mtom aliweza kumuona edo aliweka shabaha katikati ya paji lauso wa edo... ile anataka kubofya kitufe cha kufyatulia risasi mara ghafla...
ile anataka kubofya kitufe cha kufyatulia risasi mara ghafla Edo alijikwa kwenye ngazi akatereza!!!!! kutokana alikuwa na ulevi kichwani mwake Edo akadondoka chini lakini hakupata jeraha...Shit" Error Target...alijisemea tom..ghafla simu ya tom iliita alipoitoa na kuitazama aligundua bony alikuwa anampigia tom hakuipokea simu ile aliamua kuikata..kisha akatazama ule upande wa mlimani city kwa kutumia lenzi iliyopo juu ya bunduki ile aina ya SNIPER CONVO-R7 alitahamaki Edo hakuepo tena eneo lile alipojaribu kuangaza huku na kule hakuweza kumuona edo.... aisee huyu mwanaharamu kanivurugia mpango wangu kwa kupiga simu ile ningejua hata nisingeshughulika na simu... alijisemea tom... kisha akatoka pale dirishani na kurudishia kioo kwa kukisukuma upande......mambo uamekwenda ndivyo sivyo"" alisikika tom akiwaambia vijana wake wa kazi walio kuwemo ndani ya chumba hicho...
*********
Ule upande wa nje bony alinyata kuelekea kwenye mlango ule namba 555....
kabla hajafika alihisi mlango ule unafunguliwa akajibanza kwenye ukuta....kisha akachungulia kwa umakini wa hali ya juu...aliona yule moja wa vijana wa tom katoka nje ya chumba'',, ni yule aliyepigana nae kikumbo kwenye mlango wa kuingia ndani ya ukumbi kule mliman city....mtu yule aliangaza angaza pande zote misha akarudi ndani....
Tom alianza kuandaa mpango mwingine mbadala... alimuamuru yule mtu atoke nje akachukue laptop kwenye gari ili atafute kenye mtandao huenda akaona mambo yanayomuhusu edo..ili amchuguze kiundani zaidi.. yule mtu alitokanje kisha akaelekea kunako lift... alivyoingia tu na bony pia akaingia ndani ya lifi huku kavalia kofia iliyoficha uso wake hivyo hakutambulika kwa haraka...
mtu yule aliyevalia suti ya bluu hakumjali bony alihisi ni moja ya wateja waliokodi vyumba katika hotel hiyo kisha kisha akabonyeza kitufe kilichoandikwa GROUND ili lift ishuke chini kabisa ya jengo hilo... naye bony akabonyeza kitufe kilichoandikwa 20C lift ilianza kushuka chini...ilipofika grorofa ya 20 lift ilisimama na mlango ukafunguka.... bony alitoka nje mara ghafla kabla hajamaliza hatua moja kutoka ndani ya lift aliachia teke kali aina ya ROUND KICK..teke lile lilikwenda moja kwa moja kwenye upande wa sikio la yule kijana wa kazi wa tom... kabla hajakaa sawa bony alirusha ngumi kali ya mkono wa kusho aina ya ambakati.. yule mtu alidondoka chini na kupoteza fahamu... kisha bony akarudi ndani ya lift
akabonyeza kitufe kilichoandikwa TOP yani lift ipande juu mwisho wa jengo.... kisha mlango ukajifunga.
***********
kule mlimani city Alionekana edo akiwa ndani ya gari lake alilopewa na mama yake... ni gari ambalo alikuwa analitumia marehemu baba yake.. eso alikuwa akionge na grace juu ya mpango wa harusi yao lakini grace alisema ni vyema...kwa kuwa mama yangu umemfahamu pia ni vyema nikakupeleka kwa baba yangu pia umfahamu lakini yeye anaisgi Dodoma alihama dar es salaam miaka mingi iliyopita au unasemaje??? aliuliza grace"" Edo hakuwa na pingamizi walikubaliana hivyo...... grace alifuragi sana baada ya kukubaliwa ombi lake la yeye na edo kwenda Dodoma kumtambulisha kwa baba yake mzazi na Grace
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
**********
kule MILLZ HOTEL tom alipo ona zimepita dakika kadhaa yule mtu hajarudi aliamuru yule kijana wake mwingine ashuke kule upande wa chini amwambie yule mtu afanye haraka alete laptop... mtu yule alifata amri ya bosi wake akatoka nje kisha akaanza kuzipiga hatua kuelekea kunako lift... wakati huo huo bony alikuwa ndani ya lift kutokea upande wa juu kule alipokwenda kumficha yule kijana wa tom ili mpango wake wa kumnasa tom usiharibike..... yule mtu aliyeagizwa na tom alibonyeza kitufe cha kuisimamisha lifti ikifika ghorofa hiyo ya 28C... lift ilifika ilipofunguka alikutana uso kwa uso na bony.... mtu yule alimtambua bony... alimkimbika vyema sikuile alimtoboa mguu kwa kupiga msumari na nyundo ukaingia kwenye mguu.... mtu yule alimjua vyema bony ni moto wa kuotea mbali aligeuka nyuma na kuanza kutimua mbio kuelekea chumba namba 555 bony alianza kumkimbiza alijua endapo mtu huyo akifanikiwa kuingia mdani ya chumba hicho namba 555 basi mpango wake wa kumnasa tom utaharibika... bany alimkimbiza alipomkaribia huwezi amini kilichotokea bony alimrukia yule mtu kama goli kipa"" wote wakadondoka chini kwenye vigae.
Mtu yule alirusha ngumi ngumi lakini bony aliipangua na kumdhibiti madhubuti.. mtu yule... ghafla alichomoa kisu na kudunga bony sehemu ya paja... bony alimuachia mtu yule alichoropoks akanyanyuka na kuanza kukimbia...bony alimkimbiza mtu yule alipomkaribia aliruka huku akiachia teke kali lililompiga mtu yule upande wa mgongo mtu yule alidondoka punde bony alimnasa mtu huyo.... alimpiga ngumi moja ya kwenye koo.... mtu yule alitulia tuli.. kisha bony akamviruta mtu yule mpaka kwenye upande wa choo kilichokuwa katika korido ya ghorofa ya 28C..
kisha akanyata lakini aligundua kuwa camera zilizokuwa zimetegesha katika korido zilikuwa zikirecord tukio zima....
aliamua kutafuta ni wapi chumba cha mawasiliano ya camera kilipo.(Control room) alifanikiwa kukipata alinyata na kufungua mlango lakini chumba hicho kilikuwa kimefungwa kwa kutumia namba za siri... bony ni moto wa kuotea mbali alitoa Grover's nyeusi na kuzivaa kwenye viganja vyake kisha aliingiza namba ambazo WANA IT wanazijua... ""namba hizo ni maalumu kwa kufungua kitu chochote kilichofungwa kwa namba za siri( computerlise) baada ya kuingiza namba hizo mlango ulifunguka kisha akaenda moja kwa moja mpaka kwenye kompyuta iliyokuwemo ndani humo... alifita matukio yote ya siku nzima ambayo yarirekodiwa na camera zile zilizoyegeshwa eneo zima la kuizunguka MILLZ HOTEL.. kisha akizima camera zote.... bony alipohakikisha kazima camera alitoka upande wa nje na kufunga mlango ile...... alianza kuzipiga hatua kuelekea kule ambapo kipo chumba namba 555.
***********
kule mlimani city Sandra alianza kuingiwa na wasiwasi kwa ninj Edo amechelewa kurudi ukumbini humo wakati ni sherehe yake... sandra hakupendezwa na mitendo hicho aliamua kuchukua simu yake na kumpigia Edo.... edo aliipokea simu ile kisha akasema ok Mom nakuja sipo mbali nipo hapa nje kwenye packing ya magari.....kisha Edo alitoka ndani ya gari lake pamoja na grace wakaanza kuzipiga hatua kuelekea kunako ukumbi.. wakati huo tom alikuwa makini kutazama ule upande amboa ulikuwepo ukumbi kwa kutumia binoculars (Darubini) alitazama kwamuda mrefu lakini hakufanikiwa kuona kile alichotarajia.... aliamua kutoka dirishani hapo....
wakati tom anaondoka kutoka sehemu lilipokuwa dirisha ndio wakati ambao Edo alikuwa akifumgua mlango wa kuingia ndani ya ukumbi hivyo tom hakuona kwa sababu alikuwa katoka dirishani tayari.. lakini tom alianza kuingiwa na wasiwasi kwa nini vijana wake wa kazi wamechelewa kurudi... alichukua simu na kupiga namba ya simu ya mmoja kati ua vijana wake wale wawili..simu iliita bila kupokelewa... tom alizingukazunguka chumbani humo huku kashikilia darubini yake.... alipo ona simu haipokelewi aliamua kurudi pale dirishani akaendelea kutazama ule upande wa mliman city kwa kutumia binoculars (darubini)
**********
ule upande mwingine bony alimpigia simu sandra.
kutokana na muziki kuwa mkubwa ndani ya ukumbi ule sandra aliamua kuto nje ili aongee na simu kwa utulivu... sandra alipotoka nje tom aliweza kumuona sandra kwa kutumia darubini.. haraka haraka tom aliisogelea ile bunduki yake hatari aina ya SNIPER CONVO-7R akachungulia kwa jicho lake moja kutazama ule upande aliokuwa amesimama sandra.... aliweka shabaha vyema katikati ya kifua cha sandra upande wa moyo... alipohakikisha kamuweka Target alipeleka kidole chake taratibu katika kitufe cha kufuaturia risasi.....
**********
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ule upande mwingine bony alikuwa anamwambia sandra kuwa tom yupo jijini dar es salaam
MILLZ HOTEL"" sandra alionekana kuisikiliza simu kwa umakini wa hali ya juu kisha akazipiga hatua za haraka haraka kuelekea kule alipolipaki gari lake ili aongee na simu ile.....kumbe sandra alipokuwa anazipiga hatua hizo za harakaharaka ziliharibu Target ya Tom.... na kwakuwa kulikuwa na magari mengi yaliyopaki hivyo magari hayo yalimziba sandra""" tom hakuweza kumuona tena sandra.
Tom alikasirika sana.. ghafla alimuona sandra akizipiga hatua kutokea ule upande yalipokuwa yamepaki magari.... TOM aliweka shabaha kisha akapeleka kidole chake kwenye kitufe cha kufyatulia risasi... alifyatua risasi ilikwenda moja kwa moja mpaka kwenye kichwa cha sandra papohapo alidondoka chini na kupoteza maisha... yes.. i got you bitch(nimekupata malaya wewe)
ghafla bony aliingia kwa kuvamia huku kashika bastola mkononi akiielekezea ule upande aliokuwepo tom...
" tulia hivyo hivyo kabla sijasambaratisha ubongo wako"alisema Bony ..........kisha Tom alinyanyuka akageuka taratibu huku akinyanyua mikono yake juu.. tom ni moto wa kuotea mbali wakati ananyanyua mikono juu ghafla alitoa bastora ni kitendo cha sekunde... kisha akafyatua risasi huku akiruka upande mwingine... risasi ilikwenda moja kwa moja mpaka kwenye mkono wa boni akaachia bastora ikadondoka chini...alipotaka kuichukua bastola ""hey tulia hivyo hivyo ulivyo kisha nyanyua mikono yako juu... bony alihisi ni utani hakuitii amri ya tom ghafla tom alifyatua risasi nyingine iliyo kwenda moja kwa moja mpaka tumboni mwa bony... "" bony aliishiwa ngu na kudondoka chini...
tom alisogea jirani kabisa na bony kisha akafyatua risasi ikaingia kichwani mwa bony... bony alitulia tuli.. na kuiaga dunia.... kisha tom akafungua mlango na kutoka upande wa nje... akaanza kuzipiga hatia za bila wasiwasi kuelekea kunako lift.. aliingia ndani ya lift na kushuka chini kabisa... na kutokomea kusikojulikana
************
ule upande mwingine kule mliman city... mziki ulisimamishwa ghafla na dj akatangaza kuwa kuna mauwaji yametokea upande wa nje... kuna mama mmoja kauwawa... Edo alitazama pande zote hakumuona mama yake... aliamoa kutoka nje ili sone huenda huyo mtu aliye uwawa ni mama yake... alipofika nje alistahajabu alistuka sana baada ya kuona mtu aliyeuwawa ni mama yake...Edo alilia kwa uchungu... sana alikumbatia maiti ya mama yake huku damu zikiendelea kutoka kwenye lile tundu alilopigwa risasi..
kisha edo alifanya mpango ili maiti ya mama yake ipelekwe mochwari.. na kisha maiti ile ilipelekwa mochwari.... kisha Edo akafuata taratibu zote na mwili ukahifadhiwa katika Hospital ya MUHIMBILI.
Grace alimuonea huruma sana mchumba wake Edo alimfariji kwa kumkumbatia na kumwambia manene yenye faraja.. baada ya muda waliondoka...Ilibidi usiku huo grace akalale nyumbani kwa kina Edo....
*********
palipokucha taratibu za mazishi zilifanyika kisha sandra alizikwa...
******BAADA YA MIEZI MIWILI KUPITA*******
mama aliniambia kuwa baba yangu aliuwawa lakini hakuniambi nani muuwaji!!!! ya wezekana huyo muuwaji aliye muuwa baba yangu ndiye kamuuwa na mama yangu pia...haiwezekani lazima nilipize kisasi MUNGU NISAMEHE KWA HILI"" alijisemea moyoni Edo....
aliichukuwa simu ya mama yake na kuiwasha kisha akaanza kukagua kagua"" aliona namba fulani ilikuwa ikiwasiliana na mama yake mara kwa mara pia alisoma SMS aligundua mambo mengi Edo alihisi kuna kitu kilikuwa kinaendelea... namba hiyo ilikuwa imeandikwa kwa jina la Bony...alipojaribu kuipigia namba ile haikupatikana.. lakini alisoma SMS moja ambayo ilikuwa inaelekeza nyumbani kwa bony...
Edo alielekea mpaka kwenye ile nyumba ambayo ilitolewa maelekezo kwenye SMS iliyokuwemo kwenye simu ya mama yake jinsi ya kufika kwenye nyumba hiyo... Edo alifanikiwa kuiona nyumba hiyo.. alipofika getini alipiga hodi lakini hapakuinesha dalili yoyote ya kuwepo mtu ndani.. aliamua kuruka uzio na kuingia ndani... kisha akapitia dirishani kuingia upande wa ndani kabisa... Edo alianza kukagua sehemu zote alipofungua droo mdogo ya kwenye kabati la nguo.. aliona karatasi nyingi... alipojaribu kutazama moja moja... aliona karatasi zimeandikwa jina la baba yake!!! Edo alistuka... aliposoma kwa umakini aligundua zilikuwa ni NYARAKA hati miliki ya mali za baba yake... Edo hakuamini.... inamaana mama ndiye alimuuwa baba yangu!!!!! ili azimiliki mali za baba yangu... bila sha huyu anaye ishi humu ni mwanaume wake!! alijisemea moyoni huku uso wake ukionekana kujawa hasira na chuki ya hali ya juu edo aliamini kuwa mama yake ndiye aliyefanya njama ya kumuuwa baba yake edo. ..
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
wakati Edo bado yumo ndani ya bony... kumbe tom naye hakuwa mbali na eneo hilo alikuwa yupo njiani kuelekea kwenye nyumba ya bony ili akazichukue nyaraka zile kwa kuwa bony kamuuwa... hivyo hakuwa na wasiwasi.. tom alifika nje ya nyumba ya bony.. kisha akafungua geti kwa funguo za bandia na kuingia ndani ya uzio mara ghafla.
Mara ghafla Tom alihisi kuna mtu upande wa ndani... alisita kuingia... wakati huo huo Edo alikuwa anatoka upande wa nje kwa kupitia dirishani huku kazishikiria nyaraka zile... kutokanakana dirisha lilikuwa upande wa nyuma hivyo wakati Edo anatoka Tom akuweza kumuona kisha Edo alipanda juu ya ukuta wa uzio na kuruka upande wa nje na kundoka alikwenda moja kwamoja paka alipokuwa amelipaki gari lake haikuwa mbali sana na maeneo hayo...
Tom alitoa bastola na kuingia huku akizipiga hatua za kunyatia alinyata huku akizunguka kwenye madirisha huku masikio yake yakiwa makini kusikiliza upande wa ndani... alipo ona ukimya alizipiga hatua mpaka kwenye mlango"" alitoa funguo zake za bandia na kufungua mlango... kisha akaingia nda huku macho yake yakitazama kwa umakini wa hali ya juu... alikuta mlango wa chumba kimoja upo wazi aliingia kwa tahadhali kubwa aliona hakuna mtu... alirudisha bastola yake kwenye koti kisha akaanza kukagua sehemu zote huenda akazipata nyaraka zile....lakini hakufanikiwa"" huyu mwanaharamu kaficha wapi nyaraka hizo!!!!?alijisemea moyoni tom.. huku akionesha kukata tamaa ya kuzipata nyaraka hizo... wakati anataka anaondoka aliona simu ilikuwa juu ya kitanda....aliichukua simu ile na baada ya kupekuwapekuwa simu hiyo aligundua kuwa ni ya Sandra...... bila shaka Edo aliingia humu ndani na huenda nyaraka hizo kazipata.. alijisemea tom
kumbe edo alisahau simu hiyo kitandani hapo baada ya kusoma nyaraka zile...alichanganyikiwa kukuta ni hati miliki ya mali za baba yake.. hivyo kipindi anatoka chumbani humo hakukumbuka kuchukua simu ile... tom alikasirika sana akatoka chumbani humo kwa jazba na kuondoka zake..
*************
Ule upande mwingine Edo alifika nyumbani kwao... lakini alionekana kuwa kuna kitu kinasumbua akili yake... grace aliligundua hilo kwa hakuzoea kumuona edo katika hali hiyo... alimshauri kuwa amtafute yule mwanadada aliyekuwa sekretari wa marehemu baba yake.... huenda akawa anafahamu baadhi ya mambo yaliyokuwa yakiendelea kwenye Kampuni ya baba yake.
kumbe wakiti huo huo Tom alikuwa anaandaa mpango wa kwenda kumuuwa sekretari yule... aliamini huenda akaja kutoa siri kwa sababu miaka ishirini iliyopita sekretari huyo aliona baada ya tom kuacha kompyuta ikiwa inawaka huku ikionesha faili la siri lililokuwa likionesha ni wapi zimehifadhiwa nyaraka hati miliki ya mali za Jimy...siku ile tom alimuona sekretari huyo akitokea ndani ya ofisi ya marehemu Jimy...ambayo kwa kipindi hicho alikuwa anaitumia tom ofisi hiyo... tom alikuwa anapafahamu alipokuwa akiishi sekretali huyo anayeitwa Amida. alivamia nyumbani kwa Amida usiku huo na kumchinja amida alipoteza maisha...
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment