Search This Blog
Monday, 23 May 2022
Sunday, 22 May 2022
MKANDA WA SIRI - 5
Simulizi : Mkanda Wa Siri
Sehemu Ya Tano (5)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ilikuwa usiku wa manane akiwa amelala mbele ya duka moja pale Tandika. Alihisi kupapaswa na mtu mapajani, mwanzoni alidhani ni ndoto, lakini baada ya kuhisi akizidi kupapaswa ghafla alifumbua macho, ndipo alipokutana na vitu viwili kwa mpigo. Alikutana na Kisu kirefu pamoja na sura ya kutisha ya Dula Mbabe. Mbabe wa Tandika. Jamaa alikuwa anataka kumbaka Binunu, Binunu sio kwamba hakuwa tayari kubakwa tu, pia hakuwa amewahi hata kufanya mapenzi kwa hiyari yake. Sasa ataingiaje katika ulimwengu wa mapenzi kwa mtindo wa kubakwa? Kilichofuatia baada ya pale kilitikisa jiji zima la Dar es salaam. Kichwa cha Dula Mbabe kiliokotwa Temeke Sudani, kiwiliwili kisicho na miguu cha mtu asiyejulikana kiliokotwa mbele ya Temeke hospitali huku miguu ikiokotwa katika dampo la Yombo. Polisi hawakupata shida kujua kwamba viungo vile ilikuwa ya mtu mmoja, Dula Mbabe. Jambazi waliyekuwa wanamsaka kwa muda mrefu bila mafanikio. Hawakujishughulisha kumsaka muuaji, walijua itakuwa ni kisasi toka kwa majambazi wenzie baada ya kudhulumiana mali za wizi.
Huo ndo ulikuwa mwanzo wa Binunu kuuwa...
Sababu kuu ya kuwa mkatili kiasi kile ni kwamba, Binunu alianza kuwa mtoto wa mtaani akiwa na umri mdogo sana, na kwa kiasi kikubwa mtaa ndio uliobadiri akili na vitendo vya Binunu. Hata mpango wa kwenda kuvamia kasri ya Abdullah ili kuupora mkanda ni yeye ndiye alikuwa ameupanga. Mpango wa kutumia spray za ocer na foner, huku yeye akiziita kwa ujumla spray zile kama OcaFona. Richard alishangaa sana uwezo wa akili wa Binunu katika kupanga. Alikuwa ameshafanya operesheni kadhaa na watu tofautitofauti, watu mahiri katika medani, lakini hii waliifanya kwa ufanisi mkubwa zaidi, walipata walichokitaka bila kutumia nguvu, na mipango ya Binunu ikienda sawa kwa asilimia mia. Alimkubali sana mwanamke yule na kufikia hatua ya kumwamini na kumpa mkanda wa siri kwenda nao Dar akamkabidhi Martin. Lakini kwa bahati mbaya kabisa meli ya MV Donors ikiwa na Binunu pamoja na mkanda ilizamishwa kwa hila za Malolo katikati ya bahari Hindi. Ajari ilikuwa mbaya sana, kuliko ajari yoyote ya meli iliyowahi kutokea katika kisiwa cha Zanzibar. Ajari ilikuwa na madhara kwa Binunu pia, alijigonga vibaya katika kisogo na kupoteza kumbukumbu pamoja na kuchanganyikiwa. Pamoja na ujasusi wake wote lakini Binunu akili ilimpaa. Kama alikuwa na akili angalau za kuweza kujuta basi labda angejuta kiuwendawazimu kwa kitendo chake cha kujiingiza katika operesheni ile. Ni kudra za Mwenyezi Mungu tu ndizo zilizomuokoa Binunu. Alisukumwa na maji ya bahari yaliyompeleka hadi ufukweni. Na nusu saa baadae aliokotwa na wavuvi wawili, na baada ya muda mrefu wa kushauriana wavuvi wale waliamua kumpeleka katika uwanja wa Maisala. Huku wakilichukuwa wao begi dogo likiloning'inia mgongoni mwa Binunu. Begi lenye mkanda wa siri lilichukuliwa na wavuvi huku Binunu akicheka kiuwendawazimu. Na kutokea yote yaliyotokea...
SASA leo Binunu aliyebadilishwa na mtaa alikuwa ana kwa ana na Chifu, mtu aliyeamini kuwa ndiye aliyewaua wazazi wake wapendwa miaka kumi na saba iliyopita. Na taswira mbaya ya wazazi wake ilimjia tena kichwani mwake. Aliwaona wakiwa hawana uhai wamelaliana chini. Huku damu za baba yake mzazi zikuwa zimemtampakaa mama yake mzazi, ilikuwa ni taswira mbaya sana ya kusikitisha ambayo Binunu aliishuhudia akiwa na umri mdogo. Kumbuka mama yake alikuwa ametoka kubakwa kabla hajauwawa. Taswira ambayo haikuthubutu kutoka katika ubongo wake kwa muda wa miaka kumi na sababu. Na taswira ile mbaya ya wazazi wake ilimpandisha hasira maradufu. Kwa haraka alinyoosha mikono yake yote miwili na kumkaba shingoni kwa nguvu. Huku kidole gumba cha mkono wa kulia akikikandamiza katika koromeo la Chifu. Chifu macho yalimtoka pima!
Mkono wa kulia wa Chifu ukaushika mkono wa kushoto wa Binunu, na mkono wa kushoto wa Chifu ukaushika mkono wa kulia wa Binunu. Akijaribu kuitoa mikono ya Binunu shingoni mwake, lakini hakuweza!
Mikono ya Binunu ilikuwa imara, haikusogea hata chembe. Na kilitokea kitendo cha ghafla. Binunu alimpiga Chifu kichwa takatifu katikati ya utosi wake!
Chifu hakukitegemea kabisa kitendo kile, Binunu alimstukiza sana, wakati yeye akihangaika kuitoa ile roba pale shingoni, Binunu alifanya kitu kingine.
Chifu alichanganyikiwa.
Na muda uleule, Utosi wa Chifu ulivimba kitu kinachoitwa nundu. Chifu naye hakukubali. Hakuwa tayari kudhalilishwa kiasi kile, tena na mwanamke. Aliacha kuushika ule mkono wa kushoto wa Binunu na kuutumia kurusha ngumi ya nguvu kuelekea katika shavu la kushoto la Binunu. Yule mwanamke aliyekulia mtaani aliikwepa ngumi ile kwa ustadi mkubwa sana, huku akiutoa mkono wa kulia katika shingo ya Chifu na kuutumia kurusha ngumi yake ya nguvu, ngumi iliyompata Chifu bara'bara katika mbavu upande wa kushoto. Jamaa alitoa mguno mdogo wa maumivu. Binunu alitanua mikono yake yote miwili mithili ya mtu anayetaka kupaa angani na kuibamiza kwa nguvu zake zote katika kichwa cha Chifu. Mkono wa kulia ulitua katika sikio la kushoto la Chifu na mkono wa kushoto ulitua katika sikio la kulia la Chifu. Masikio yote mawili ya Chifu yalipatwa na pigo lile. Alisikia mivumo mibaya masikioni mwake kutokana na pigo lile liitwalo Malaika.
"Ni sababu gani iliyokufanya uwaue wazazi wangu?" Binunu aliuliza kwa sauti kubwa yenye ghadhabu.
Chifu alikaa kimya.
Alikuwa anamtazama tu yule mwanamke. Siyo kama alikaa kimya kwa jeuri ama kiburi, la hasha alikuwa hajasikia chochote alichoulizwa. Bado masikioni mwake kulikuwa na mivumo kutokana na pigo baya la Malaika alilopigwa. Binunu alihisi jamaa hataki kujibu swali lake. Hasira zilizidi kumpanda. Alirudia tena kupiga pigo lilelile la Malaika. Ni mivumo ya vuuuu vuuuu iliendelea maradufu katika masikio yote ya Chifu. Chifu alibaki mdomo wazi, chozi la uchungu la kiume lilimdondoka sakafuni.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Saa 9: 04 A.M
Katika kisiwa cha Pemba bado wakina Malkia walikuwa wanamsubiri Ayoub. Hawakutaka kutoka pale mpaka waonane nae na kuongea nae. Bado walikuwa na imani kwamba pale ndipo kwenye jibu la mkanda wa siri.
Baada ya masaa mawili, Ayoub alikuwa anarejea katika kibanda chake. Akiwa amebeba mfuko wa rambo uliosheheni samaki wabichi. Akiwa umbali kama wa mita miamoja aliwaona watu wanne wakiwa wamekaa mbele ya kibanda chake. Kati ya watu wale alimfahamu mtu mmoja tu.
"Wale wengine ni kina nani?" Ayoub alijiuliza kimoyomoyo.
Hakuwa na miadi na wageni kwa siku ile. Ayoub aliendelea kwenda katika kibanda chake bila kujua kwamba alikuwa anaisogelea hatari. Kwa mwendo wa taratibu Ayoub aliendelea kuelekea katika kibanda chake dhaifu. Kibanda alichokitengeneza kwa dharura tu baada ya kuhama kwa lazima katika nyumba aliyokuwa amepanga awali. Alitembea huku akiwa na mashaka mengi sana ndani ya moyo wake. Moyo ulikuwa unamdunda pasi na kawaida. Ni mara ya tatu sasa katika maisha yake moyo kumdunda namna ile....Hakuwahi kudundwa na moyo kiasi kile tangu siku ile alivyouwawa baba yake na siku aliyovamiwa chumbani kwake na watu wasiojulikana. Matukio mawili ambayo yamebaki kuwa kitendawili kwake hadi leo. Hakujua vyanzo vyake, hakujua sababu zake. Matukio ya kutisha ambayo yalimtoa Ayoub katika hali aliyokuwa nayo akiwa mtoto, hali ya ucheshi, na matukio hayo yalimtengeneza Ayoub katika hali aliyonayo sasa, hali ya ukimya na upole.
Na hapo ndipo wakina Malkia nao walimuona....
Wakina Malkia walivyoona mtu anaelekea pale wote walisimama wima. Wakijua mtu wa kulifumbua fumbo lao lililodumu mwezi mzima alikuwa amewasili. Mtu muhimu kwa mustakabali wa mkanda uliowapotea kimaajabu. Na sasa walikutana.
"Wageni wako hawa Mwenyekiti" Yule mvuvi aliyewapeleka pale alisema baada ya salamu.
"Ahaaa, nashukuru sana kaka" Ayoub alisema huku akiziangalia kwa zamu sura za wageni zilizopo mbele yake. Alijaribu kuziuliza kumbukumbu zake lakini zilimjibu kwamba hakuwahi kukutana na sura kama zile tangu azaliwe.
"Karibuni sana wageni wangu" Ayoub alisema kwa sauti ya upole yenye kuonesha ukarimu ndani yake.
"Naitwa Angel Michael, huyu anaitwa Maziku Donge na huyu anaitwa Jackson Fued..." Malkia aliwatambulisha wenzake na yeye mwenyewe kwa majina ya uwongo huku akiwaonesha kwa vidole wenziwe wakati wa utambulisho.
Huku wote wakimwangalia yule jamaa kwa pamoja.
"Nashukuru sana kuwafahamu... Mimi kwa majina ninaitwa Ayoub...Ayoub Mbembati, ni mwenyekiti wa BMU ya hapa...karibuni sana" Ayoub alisema kwa sauti yake ya upole.
"Ayoub Mbembatiii!" Wote walisema kwa pamoja kwa taharuki, kasoro yule mvuvi aliyewasindikiza. Mstuko dhahiri ulionekana kwa wageni wale watatu. Walianza kuangaliana kwa muda.
Hawakuyaamini masikio yao.
Mstuko na taharuki ile ilipokewa kwa namna tofauti na yule mvuvi msindikizaji pamoja na Ayoub mwenyewe. Kwanini wageni washangae namna ile kwa kusikia tu jina la Ayoub. Kuna tatizo...tatizo gani sasa?
Mdundo wa hofu wa moyo wake ulioanza pindi tu alipowaona kwa mbali wageni wale ulimthibitishia Ayoub kwamba ulikuwa sahihi, na wale wageni hawakuwa watu wema. Hawakuwa wema kwa vipi, hakujua, alichojua ni kutafuta namna ya kujiokoa. Ilimfunukia kwamba pale hapakuwa mahali salama.
"Ayoub Mbembati..." Malkia alitamka kwa sauti ndogo ya kuchoka. Lilikuwa jina ambalo hakutaka kulisikia kabisa kwa wakati ule. Jina lile lilikuwa na thamani, tena thamani kubwa sana miezi miwili iliyopita, lakini siyo sasa. Sasa halikuwa na thamani kabisa.
*****
Kule Kisarawe hali ilikuwa ngumu sana kwa Chifu Abdullah. Binunu alikuwa amechachamaa kwa jazba na hasira. Ulikuwa ni wakati mgumu sana kwa Chifu. Pengine ingekuwa enzi zake asingeweza kunyanyaswa kiasi kile na yule mwanamke, lakini sasa umri ulikuwa umemtupa mkono. Binunu alitumia vizuri udhaifu huo wa Chifu. Alikuwa ameshampiga mabao ya masikio mara tano sasa. Chifu alikuwa hawezi kabisa kujitetea. Kichwa chote kilikuwa kinamuuma vibaya sana. Na Binunu hakuwa na dalili kabisa ya kuacha kumpiga kwa namna ileile, sehemu ileile, kwa nguvu ileile. Na Chifu aliona asipojitahidi kujibu anachoulizwa atakufa kifo kibaya. Atakufa akiwa kiziwi. Pamoja na maumivu makali na mivumo isiyoisha masikioni mwake lakini sasa alijitahidi kumsikiliza ili amjibu.
"Kwanini uliwauwa wazazi wangu?" Binunu aliuliza kwa ukali huku akitambua kuwa Chifu alikuwa hasikii. Na kweli Chifu hakusikia, lakini alijibu. Chifu aliona mdomo wa Binunu jinsi ulivyokuwa unacheza.
Alimuelewa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"M..ka...nda!" Chifu alisema kwa sauti ya kukatakata. Binunu alisikia vizuri sana jibu la Chifu. Na muda uleule alikumbuka sauti ya kukwamakwama ya baba yake siku ile wakati anakata roho. Jinsi ikivyokwamakwama na kumwambia kuwa mkanda anao Ayoub.
"Inamaana mkanda tulioenda kuuiba kwenye kasri juzi ndio mkanda alioniambia baba miaka kumi na saba iliyopita kuwa upo kwa Ayoub?" Binunu alijiuliza kimoyomoyo...huku akikumbuka tukio lile na kudhani limetokea juzi tu, kumbe ulikuwa mwezi sasa umepita.
Na kumbukumbu hiyo ilimzidisha hasira maradufu.
Binunu alipandwa na hasira maradufu huku akiwa hailewi kabisa mambo yale yalivyokuwa yanatokea. Sasa alipata kitendawili kipya kabisa kichwani mwake...Hakuelewa kwanini sasa kina Martin walikuwa wanauhitaji ule mkanda. Mkanda wa siri uliosababisha kifo cha wazazi wake wapendwa. Mikono ya Chifu ilikuwa imeziba masikio yake yote mawili, ikizuia mapigo yale ya hatari sana kutoka kwa Binunu. Binunu sasa aligairi, hakufanya kama alivyofanya awali. Alibadili kitendo...
Alimshika Chifu shingoni kama alivyomshika awali, kwa kasi Chifu nae aliacha kuziba masikio na kuipeleka mikono yake juu ya mikono ya Binunu.
"Na hii ni kwa niaba ya baba!" Binunu alitamka maneno hayo huku akimpiga Chifu kichwa takatifu, kichwa cha nguvu mara mbili ya kile alichompiga awali.
Chifu alijaribu kukwepesha kichwa chake, lakini kasi ya Binunu kupeleka kichwa kile ilikuwa ni zaidi ya kasi ya Chifu aliyoitumia kukwepa.
Kilimpata!
"Na hiyo kwa niaba ya mama..khabithi wewe!" Binunu alisema huku akipiga ngumi ya nguvu kwa mkono wake wa kulia, ngumi iliyotua katikati ya uso wa Chifu. Chifu aliinama chini huku akiwa ameshika uso wake kwa viganja vyake vyote viwili. Binunu alikuwa amempiga palepale kilipotua kichwa.
"Na hiyo kwa niaba ya mzee Mbembati...baradhuli mkubwa wewe!" Teke kali toka kwa Binunu lilimpata bara'bara katikati ya miguu yake. Kumbuka Chifu alikuwa uchi wa mnyama. Teke lile lilimrusha juu Chifu na kumpelekea kwenda kujigonga vibaya sana ukutani. Chifu alilala chali akiwa hoi bin taaban. Pumzi zake zilikuwa zinatoka kwa mbali sana. Alikuwa anapigania hewa ili aweze kuishi. Bila wasiwasi wowote Binunu alimsogelea taratibu Chifu, mguu wake wa kulia alimuwekea Chifu kifuani na kuanza kumkandamiza kwa nguvu. Madonge makubwa ya damu yalitoka mdomoni mwa Chifu. Alikuwa anatapika huku sura yake ikiwa imechakaa vibaya sana. Sura ikiwa haina matumaini ya kuishi. Binunu alinyanyua juu ule mguu wake wa kulia na kuurejesha chini kwa kasi sana na nguvu kubwa, mguu ulitua palepale ulipotua awali, katika kifua cha Chifu. Chifu alitapika madonge ya damu huku akiunguruma mithili ya Simba mzee. Binunu hakuwa na huruma hata kidogo, hakumhurumia Chifu, sasa alinyanyua juu mguu wake wa kushoto na kupiga katika sehemu za siri za Chifu, kumbuka Chifu alikuwa uchi wa mnyama.
Na pigo lile lilitua vizuri sana.
Chifu alitoa ukelele mkali, na kuanza kulia mithili ya mtoto mdogo. Binunu aliinama pale chini na kumshika Chifu shingoni. Alilishika koromeo la Chifu kwa vidole vyake viwili, kidole gumba na kidole cha shahada. Na kuanza kulivuta. Macho yalimtoka pima Chifu mithili ya kijusi aliyebanwa na mlango. Maumivu akiyoyapata Chifu yalikuwa hayana mfano, na kwa bahati mbaya kwake alishindwa kabisa kujitetea, msaada pekee kwake ulikuwa ni kupiga makelele, alikuwa anapiga tu makelele yasiyo na maana yoyote kwa Binunu. Binunu alilibinya lile koromeo la Chifu, kitendo kilichofanya amlize Chifu apendavyo. Yule mwanamke akalivuta bwana koromeo. Alilivuta kwa nguvu nia yake ni kulitoa nje!. Roho ya Chifu haikutaka kukaa tena katika mwili ule uliokuwa unapitia katika mateso makali sana. Roho haikuweza kuvumilia maumivu yale. Roho ya Chifu iliruka juu na kwenda kuzimu. Chifu alikata roho akiwa anapitia maumivu makali sana, maumivu ambayo hakuwahi kuyafikiria hata siku moja, maumivu makali ilikuwa kama anachunwa ngozi akiwa hai.
Binunu aliingia ndani, alilivua lile gauni. Alijifuta damu za Chifu zilizomtapakaa mwilini kwa kutumia lilelile gauni, sasa alivaa suruali ya jeans nyeusi na tshirt ya bluu, chini alivaa raba nyeusi zilizomkaa vema bila hata kujua nguo zile za nani. Alitoka nje ya nyumba ile na kutokomea kusikojulikana.
*****
"Wewe kumbe ndo Ayoub Mbembati..?" Malkia aliuliza kwa sauti yake ya uchovu. Sauti isiyokuwa na matumaini yoyote. Walikuwa wamecheza mchezo uitwao pata...potea.
"Ndio mimi Angel, mimi ndiye Ayoub...kwani kuna tatizo gani?" Ayoub alijibu kwa sauti yenye mashaka na kumalizia kwa kuuliza swali. Hakuna aliyenyanyua mdomo wake kumjibu Ayoub. Wote walitazamana tena, kisha wakatikisa vichwa vyao kwa masikitiko. Hali iliyozidi kumchanganya Ayoub pamoja na yule mvuvi msindikizaji. Wakina Malkia hawakuwa na la ziada pale, haikuwa na maana yoyote kujibu swali la Ayoub. Kumbukumbu mbaya zilipita vichwani mwao.
Wewe kumbe ndo Ayoub Mbembati..?" Malkia aliuliza kwa sauti yake ya uchovu. Sauti isiyokuwa na matumaini yoyote. Walikuwa wamecheza mchezo uitwao pata...potea.
"Ndio mimi Angel, mimi ndiye Ayoub...kwani kuna tatizo gani?" Ayoub alijibu kwa sauti yenye mashaka na kumalizia kwa kuuliza swali. Hakuna aliyenyanyua mdomo wake kumjibu Ayoub. Wote walitazamana tena, kisha wakatikisa vichwa vyao kwa masikitiko. Hali iliyozidi kumchanganya Ayoub pamoja na yule mvuvi msindikizaji. Wakina Malkia hawakuwa na la ziada pale, haikuwa na maana yoyote kujibu swali la Ayoub. Kumbukumbu mbaya zilipita vichwani mwao.
***
Yaliyotokea miaka kumi na saba iliyopita..
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
SIKU ile Mzee Issa alivyopigwa risasi na akiwa katika harakati za kukata roho, kwa sauti ya kukatakata aliyoitoa akiwa anapitia katika maumivu makali, alimwambia mwanae mpendwa Binunu kuwa mkanda upo kwa Ayoub. Baba Binunu kwa kauli ile alikuwa anamlenga Binunu pekee lakini kwa bahati mbaya sana kauli ilisikiwa na watu wote pale sebuleni. Kauli yenye thamani sana ilisikiwa na masikio mabaya pia, masikio yasiyopaswa kabisa kuisikia kauli ile kulingana na unyeti wake. Ndipo msako wa kina Chifu ulipobadili mwelekeo. Badala ya kuusaka mkanda wa siri kama walivyokuwa wanafanya awali, sasa walianza kumsaka Ayoub kwa udi na uvumba....wakiamini kuwa Ayoub ndiye mwenye mkanda kama alivyosema baba yake Binunu kumwambia mwanae wakati anakata roho. Wakina Chifu hawakuhangaika kabisa na yule mtoto, hawakumfanya chochote, walimuacha akilia huku akizilalia maiti za wazazi wake. Na ndio kosa kubwa waliolifanya kina Chifu, walisahau kwamba umuuwapo nyoka lazima utenganishe kichwa na kiwiliwili. Wao waliondoka na jina tu la mtu muhimu kwao, huku wakimuacha hai mtoto Binunu. Na kama walidhani ni kazi rahisi kumpata Ayoub kisha kuupata mkanda, basi walikuwa wamejidanganya sana.
Hiyo haikuwa kazi rahisi hata kidogo.
Walitumia miaka kumi na saba kumtafuta bila kujua huyo Ayoub anakaa wapi, ingawa kwasasa walikuwa na maelezo mengi sana kuhusu maisha ya Ayoub huko nyuma lakini hawakujua kabisa kwasasa Ayoub anaishi wapi. Na hata hao waliowaleza wakina Chifu maisha ya Ayoub ya awali hawakujua kwa sasa Ayoub yuko wapi. Baada ya kupita miaka hiyo ndipo upelelezi wa kina Chifu ulipowafikisha mahali alipo Ayoub na mkanda wa siri. Naaam, kina Chifu walifika katika kisiwa cha Unguja. Ni kweli kuwa Ayoub alikuwa na mkanda mahali fulani katika chumba alichopanga huko Unguja. Siku zote tangu aupate mkanda ule aliutunza mahali pa siri, mahali alipokuwa anapajua yeye pekee, lakini ulikuwa humohumo katika chumba kidogo alichopanga. Na katika miaka yote hiyo alikuwa bado hajaungalia mkanda una nini ndani yake, hakujua ni vitu gani vilivyopo katika mkanda ule vilivyosababisha madhila makuu kwa baba yake na yule mzungu. Ingawa hakuwa na video lakini hiyo haikuwa sababu ya kutouangalia mkanda ule. Yeye hakutamani hata kidogo kuuangalia. Alikuwa hapendi hata kuliangalia kava tu la mkanda ule kwakuwa ulikuwa unamrejeshea kumbukumbu mbaya sana za nyuma. Picha mbaya na ya kutisha aliyoiona wakati baba yake anakata roho ilimjia pindi tu aukumbukapo mkanda ule. Na alikuwa anapata HOFU kuu moyoni. Kabla hajahamia katika kibanda akaacho sasa ambacho ndipo walipomkuta wakina Malkia, Ayoub alikuwa amepanga mjini Unguja. Sababu iliyomfanya ahame kwenye nyumba hiyo ya Unguja ilitokea mwezi mmoja uliopita.
Siku hiyo, Ayoub alikuwa anarejea nyumbani kwake toka matembezini saa nne usiku. Alikuwa anarudi nyumbani kwake akiwa hana wasiwasi wowote ule. Historia mbaya ya mambo yote yaliyotokea miaka kadhaa iliyopita ilikuwa imeanza kufutika kichwani mwake. Alifungua mlango wa chumba chake na kuingia ndani, alipiga hatua za taratibu kuifata swichi ili awashe taa iliyopo mle chumbani kwa lengo la kupata mwanga. Lakini hakuifikia swichi......Kitu ambacho hakuwa anakifahamu kabla..yeye alidhani yuko peke yake mle chumbani, kumbe haikuwa hivyo, hakuwa peke yake, kulikuwa na wageni walioingia kwa siri sana ndani ya chumba chake saa mbili kabla ya yeye hajarejea toka matembezini. Ayoub alikuwa chumba kimoja, tena gizani na wageni wabaya na wenye lengo baya sana. Ndani ya kiza kinene katika chumba cha Ayoub kulikuwa na wageni wawili walioingia bila hata kukaribishwa na mwenyeji wa chumba kile. Namna waliyoitumia kuingia mle ndani walikuwa wanaijua wao wenyewe. Wageni hao wasio rasmi, mmoja alikuwa anaitwa Peter Kissali na mwengine alikuwa anaitwa Malolo Abdallah.
Peter alikuwa amekaa juu ya kitanda kilichochakaa kilichokuwa kinamilikiwa na mmiliki wa chumba kile. Wakati mgeni mwengine, Malolo alikuwa amekaa katika kiti pekee cha mbao ambacho kilikuwepo katika kona moja ya chumba kile. Kutokana na giza la kutisha Ayoub aliingia bila kuhisi kabisa kama kuna watu chumbani mwake mpaka pale alivyosemeshwa na sauti asiyoijua wakati akielekea kuwasha swichi ya umeme.
"We are in OMS, and now we need M..." Peter alisema kwa lugha ya mafumbo tena kwa lugha ya kiingereza.
Ayoub sio tu hakuelewa maana ya maneno yale pia hakuelewa kabisa ile sauti iliingia vipi mle ndani. Mstuko alioupata kutokana na kusikia sauti ile hauna mfano. Alistuka sana...hakutegemea kabisa. Alibaki amesimama wima huku akitetemeka kwa woga katikati ya chumba chake.
"Tuko katika operesheni mkanda wa siri, na sasa tunahitaji mkanda" Malolo aliyatafsiri kwa kiswahili maneno ya kiingereza yaliyoongelewa na Peter.
Na sasa mstuko wa Ayoub ulizidi maradufu. Ayoub alihisi mambo aliyoyakimbia Kilwa sasa yalikuwa yamemfata Unguja, tena yamesubiri miaka kumi na saba ili yarejee tena.
"Mkanda wa ....." Ayoub hakumaliza alichotaka kusema.
"Mkanda aliokupa baba yako mzazi, mzee Mbembati miaka kumi na saba iliyopita huko kwenu Kilwa, ndio huo mkanda ambao tunautaka sisi..." Peter alimalizia maneno ya Ayoub kwa maringo na kujiamini sana.
Ayoub alibabaika sana!
"Tumeingia kirafiki, tumekuwa werevu maana tumekusubiri kirafiki pia, na sasa tunaongea kirafiki, tupe mkanda kirafiki, ili tuondoke kirafiki na ubaki kuwa rafiki yetu" Malolo alisema huku akinyanyuka toka kule konani mwa chumba, katika kiti alichokikalia.
Ayoub alikuwa hana ujanja wowote ule wa kimapambano. Alikuwa sio mtu wa kuzoea misukosuko na mikikimikiki kabisa na hata angekuwa mtu wa hivyo mle ndani alikuwa peke yake, na hakujua maadui zake wako wangapi. Ingawa hadi sasa alikuwa ameshasikia sauti za watu wawili tofauti. Aliongea.
"Mzee hakuwahi kunambia nikukabidhini ninyi mkanda .." Ayoub alijibu kizembe sana.
"Hahaha, alikwambia umkabidhi nani sasa?" Peter alicheka kwa dharau huku akimtupia swali Ayoub.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Utatupa hutupi!" Malolo nae alidakia kwa kauli aliyoitoa kimamlaka.
Ayoub alikaa kimya.
"Hatujaja kwa shari, usitulazimishe tuondoke kwa shari, tupe mkanda kijana!" Peter aliacha kucheka na kutahadharisha akiwa bado amekaa pale kitandani bila wasiwasi wowote.
"Niwape ama nisiwape?" Hayo ni mawazo yaliyopita katika kichwa cha Ayoub. Mawazo yaliyopita kwa mtindo wa swali. Ayoub alikuwa anajiuliza mwenyewe, awape mkanda ama asiwape?.
"Siwapi" Alijijibu pia mwenyewe, kimoyomoyo, akimaanisha kuwa kwa njia yoyote ile hatoutoa mkanda.
"Utatupa!" Peter alisema kuijibu kauli ya Ayoub ambayo aliisema kimoyomoyo. Ayoub alistuka sana. Kwani lile lilikuwa jibu la jibu lake alilojijibu mawazoni tu. Jamaa alijibu swali lililokuwa linapita kichwani kwake. Ayoub aliona ni jinsi gani kwamba alikuwa na watu hatari sana chumbani mwake. Jinsi gani alivyo karibu na hatari. Watu wenye kuweza kujibu hata vitu vinavyopita kichwani mwake.
'Na kwa mara ya kwanza Ayoub alijuta kwa kitendo chake cha kutouangalia mkanda ule'
Lakini pamoja na umahiri mkubwa waliouonesha watu wale ambao hakuzijua hata sura zao kutokana na giza nene lililokuwa mle chumbani, hakukata tamaa. Aliamua kufanya kitu.
'Hapa nitafute nafasi ya kuufikia mlango ili nikimbie, mbio ndio usalama wangu pekee wa kujiokoa..mbio kali sana za kujiokoa na kifo'
Ayoub alipiga hatua ndogo sana kwa mguu wake wa kushoto, lengo ni kutaka kurudi nyuma na kutafuta namna ya kujiokoa. Hatua ambayo ilielekea upande ulipokuwa mlango. Ilikuwa hatua ndogo sana ya kimyakimya tena katika giza nene. Lakini cha ajabu mguu ule wa kushoto uliopiga hatua ile haukufika chini. Ulisimamishwa na sauti ya Peter!
"Unaenda wapi Ayoub, usilete hila yoyote hapa, hila toka kwako inamaanisha unahamu ya KIFO! na bila shaka tutaikamilisha hamu yako dogo" Peter alisema kwa umakini mkubwa huko neno kifo akilitaja kwa sauti kubwa tofauti na yale maneno mengine.
Mguu wa kushoto wa Ayoub ulikuwa umeganda hewani ukining'inia. Akiwa hajui aurudishe alikoutoa ama akanyage alipotaka kuupeleka. Alikuwa anawaza harakaharaka kichwani mwake lakini hakupata jibu. Atapata vipi jibu wakati alikuwa na mawazo mvuragano. Mawazo ambayo yalienda sambamba na mshangao.
"Jamaa wana macho aina gani hawa? wamewezaje kuuona mguu wangu katika giza kama hili?" Kwa mwendo wa taratibu Malolo alimfata pale aliposimama Ayoub. Ayoub sasa alimuona japo kwa shida maana macho yake sasa yalianza kuzoea giza. Na hapo ndipo alipoanza kuelewa sababu ya wale jamaa kumuona, walikuwa wamekaa muda mrefu mle chumbani na walikuwa wamelizoea giza. Ayoub sasa alijitahidi kuiangalia sura ya jamaa aliyekuwa anamfata, angalau ajue kama aliwahi kukutana nae sehemu nyingine tofauti na leo, au aihifadhi kichwani ili aitambue siku nyingine kama atapata nafasi ya kufika siku hiyo. Pamoja na jitihada zake zote lakini hakufanikiwa kabisa kuiona sura ya mtu yule. Malolo alizikatisha jitihada za kuona za Ayoub.
Ghafla, Malolo aliufyatua ule mguu wa kulia uliobaki chini. Ilikuwa kazi rahisi sana kwakuwa Ayoub alikuwa amesimamia mguu mmoja. Ayoub alienda chini mithili ya gunia la mpunga ! Hakujiandaa kabisa na tukio lile na hata angejiandaa angeenda tu chini, aligaragara chini huku akilia kwa uchungu uliochanganyika na majuto.
"Usijaribu kuleta ujanja wowote hapa kama bado unapenda kuwa mvuvi katika sayari hii...tofauti na hivyo utaenda kuwa mvuvi kuzimu, kama huko kuzimu kuna bahari!" Peter alitahadharisha akiwa bado amekaa palepale kitandani. Kijana Ayoub alikuwa hajazoea kabisa shuruba...yeye alizoea kusumbuana na samaki lakini sio kusumbuana na binadamu wenzake. Akiwa pale chini alikuwa analia huku damu zikimchuruzika mdomoni, na hapo ndipo alifikia uamuzi mgumu sana katika maisha yake, aliamua kuwapa mkanda wale jamaa ili kuokoa maisha yake.
"Na..wa..pa M..ka..nda..." Ayoub alisema kwa sauti ya kukatakata iliyoonesha kuwa alikuwa anapitia katika maumivu. Alinyanyuka taratibu toka pale sakafuni na kusogelea swichi ya umeme ili awashe taa.
"Usiwashe taa!" Malolo alisema kwa ukali.
Lilikuwa katazo zuri la Malolo kwa wakati ule lakini katazo lile liliharibu kabisa ushindi upande wao. Ayoub alichukua kiti alichokuwa amekalia Malolo awali na kupanda darini. Aliutoa mkanda na kuwakabidhi. Alikabidhi mkanda katika mikono mibaya huku mikono yake ikitetemeka na macho yake yakitoa machozi mfululizo.
'Na kwa mara nyingine tena Ayoub alijuta kwa kitendo chake cha kutouangalia kitu kilichomo katika mkanda ule' Majuto ni mjukuu.
Jamaa waliuchukua mkanda wa siri mikononi mwa Ayoub na kutokomea nao. Bila kuiona sura ya Ayoub. Bila Ayoub kuziona sura zao. Waliingia na giza, na walitoka na giza.
Asubuhi ya siku iliyofuata Ayoub alihama ile nyumba bila kupenda, alihama kwa kudhani wale jamaa wangerejea tena na kumdhuru. Hakuonana tena na wale majamaa mpaka baada ya mwezi mmoja. Watu walewale walikuwa wamemfata Ayoub tena kudai mkanda ambao waliuchukua wao wenyewe chumbani kwa Ayoub usiku wa giza kali. Lilikuwa ajabu la nane la Dunia!
Ulikuwa ni mwezi wa mashaka mazito na upelelezi mkali toka katika jeshi la Polisi kwenda kwa watu wawili. Vikosi vya jeshi la Polisi vikiongozwa na Koplo Baruani viliendelea na msako wao ambao kwa sasa ulielekea kufeli, tunaweza kuuita msako uliofeli wa kumsaka kijana Martin Nguzu, jamaa anayetuhumiwa kumuua mtu ndani ya gari bandarini. Msako huo ulienda sambamba na msako wa kumsaka Mr Na na na, mzungu aliyeacha taharuki kubwa sana katika hoteli ya Grand villa. Koplo Baruani alitumia mbinu zake zote alizofunzwa katika chuo cha upolisi, CCP Moshi, koplo Baruani alitumia pia mbinu za ziada alizotunukiwa na Mwenyezi Mungu. Pamoja na kutumia mbinu hizo mbili alizozipata katika sehemu kuu mbili alizoziamini sana lakini jina la Martin Nguzu lilibaki kuwa kama msamiati mgumu ambao haukuwahi kutokea katika lugha yake adhimu ya Kiswahili. Na kuhusu Mr Na na na, ilikuwa ni sentensi tata yenye utata mwingi sana, ambao kwa mwanafunzi wa kiwango chake cha elimu hakuweza kuutatua utata huo.
Pengine alichokuwa anakosea Koplo yule kijana pamoja na Jeshi la Polisi kwa ujumla ni kufanya upelelezi ndani ya upande mmoja tu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hawakutilia maanani kabisa kuhusu upande wa pili wa Muungano, kisiwa cha Zanzibar. Upande ambao ndipo yalipokuwa majibu ya maswali yao yote.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ilikuwa umepita mwezi mmoja na wiki kadhaa toka kifo cha Shanta wa bandarini, kijana mbabe kuliko wote bandarini, Mansour. Leo hii ilimkuta Koplo Baruani akiwa nje ya nyumba anayoishi Martin pindi akiwa jijini Dar es salaam. Nusu saa ilimuweka koplo Baruani katikati ya mlango wa nyumba ile, kasimama mithili ya sanamu la pale Posta. Alikuwa anabisha hodi bila ya kujibiwa. Pamoja na jitihada zake za kuisaka nyumba ile hadi kuipata lakini kitu ambacho alikuwa hajakifahamu bado.....Martin alikuwa anaishi nyumba ile mara chache sana akiwa jijini Dar es salaam. Mara nyingi hata akiwa Dar es salaam alikuwa analala katika hoteli mbalimbali. Sababu kuu za kuhamahama zikiwa ni hisia zake, alikuwa anazisikiliza sana hisia zake juu ya mahali pa kulala. Hisia zikimkataza anaacha, hisia zikimwambia anafanya. Koplo Baruani alivyoona kimya baada ya kubisha hodi kwa muda mrefu, aliamua kumtafuta Mwenyekiti wa mtaa wa Magomeni Mapipa ili apate ruhusa ya kuingia katika nyumba ile na kuipekua. Ilimchukua nusu saa nyingine kumpata Mwenyekiti wa mtaa. Na sasa walikuwa watu watano mbele ya mlango wa nyumba ya Martin. Walikuwa Mwenyekiti wa mtaa wa Magomeni, wajumbe wawili, shahidi mmoja na Koplo mwenyewe. Walivunja mlango wa nyumba na kuingia ndani. Ilikuwa ni nyumba ndogo yenye vyumba vitatu, bafu na sebule safi ya kisasa. Walipita chumba kimoja baada ya kingine, kwa umakini na tahadhari kubwa sana walijaribu kupekua kila sehemu waliyoihisi inaweza kuwa na lolote, lakini hawakulikuta hilo lolote. Baada ya saa moja walikaa sebuleni na kujadiliana.
"Kwani Martin amehamia lini mtaa huu?" Koplo Baruani alimuuliza mzee Nondo ambaye ndiye alikuwa Mwenyekiti wa mtaa wakiwa wamesimama sebuleni.
"Ana kama miaka mitano sasa kama sikosei.." mzee Nondo alijibu baada ya kufikiria kidogo.
"Kwani nani alikuwa rafiki yake mkubwa hapa mtaani?" Koplo Baruani aliuliza tena baada ya kuandika maelezo kidogo katika kijitabu chake. "Kwa kweli huyu kijana hajawahi kuwa na rafiki hapa mtaani, alikuwa ni mtu wa kuingia na kutoka, ukimuona leo tarajia kumuona tena baada ya miezi mitatu" Kijana mmoja aliyeitwa kama shahidi katika upekuzi ule alijibu.
"Mtu anaweza kuishi miaka mitano mtaani bila kuwa na urafiki na mtu yeyote, inawezekana kweli hiyo Mwenyekiti?"
"Ni ngumu sana Afande, lakini kwa huyo kijana anayekaa nyumba hii ni nyepesi sana, na amelithibitisha hilo, akwambialo Uledi ni ukweli mtupu" Mwenyekiti alijibu.
Baada ya kuongea hili na lile Koplo Baruani aliagana na watu wale, aliagana nao huku akiahidi kuwa atarejea tena kama atakuwa na sababu ya kurejea, pia aliwaachia namba yake ya simu ya mkononi ili wampigie pindi tu Martin watakapomuona pale mtaani. Naye alichukua namba zao. Koplo Baruani aliondoka huku akiwa bado ana maswali mengi sana juu ya mtu aitwaye Martin Nguzu lakini kwa bahati mbaya sana kwake hakuwa na wa kumuuliza.
*****
"Kumbe wewe nd'o Ayoub, Ayoub Mbembati? daaah tumefanya a big mistake, we can call it " the mistake of the year..!" Malolo alisema kwa sauti kubwa, huku moyoni mwake akiwa anatamani Ayoub aseme yeye sio Ayoub Mbembati. Lakini itatokea vipi hiko anachokitamani? Mbele yao alikuwa amesimama mtu, na alikuwa Ayoub halisi, Ayoub Bin Mbembati.
Ayoub alistuka sana kuisikia sauti ile ikiwa katika mshangao namna ile. Kumbukumbu zake zilirudi kwa kasi sana hadi mwezi mmoja uliopita, wakati alipopata wageni asiowatarajia gizani, na kuporwa mkanda wa siri bila kupenda.
"Usiwashe taa!" Ayoub badala ya kujibu swali la Malolo, ama kukili maelezo ya Malolo, yeye alikumbuka karipio la kutowasha taa alilopewa chumbani kwake gizani. Na ndipo alipoikumbuka kwamba sauti ambayo ilimpa karipio lile, sauti ambayo ilimkataza kwa nguvu asiwashe taa ya chumbani kwake mwezi mmoja uliopita ilikuwa mbele yake, sauti ileile, sauti yenye kupenda kukaripia wanyonge. Hakuwahi kulisahau karipio la sauti ile ubongoni mwake. Alilikumbuka siku zote zilizofuata baada ya karipio lile. Sauti ile ilikuwa imeshajirudia mara kadhaa katika ndoto alizoota baada ya siku ile, ilikuwa ni miongoni mwa sauti mbaya zaidi kuzisikia katika maisha yake, ilikuwa ni sauti mbaya iliyokuwa inamilikiwa na mtu aliyeondoka na mkanda wa siri katika usiku wa giza. Kamwe hakuthubutu kuisahau ile sauti hasa ikiwa katika mtindo wa kukaripia.
"Mkanda si mliuchukua nyinyi lakini..." Ayoub aliropoka akiwa katika hali ya kutetemeka. Kauli ile ilisikiwa na wote, kauli ambayo haikueleweka kabisa na yule mvuvi msindikizaji, lakini kauli ilieleweka, tena ilieleweka vizuri sana na wakina Malolo. Wote walitazamana. Waliielewa maana ya kauli ya Ayoub. Ilikuwa inamaanisha kwamba walikuwa wameenda sehemu siyo sahihi. Walishauchukua mkanda toka mikononi mwa Ayoub mwezi mmoja sasa. Na leo wameenda tena.
"Usiwashe taa!" Peter nae alikumbuka kauli ya Malolo siku ile. Sauti Iliyokuwa inamkataza Ayoub asiwashe taa.
"Labda angewasha taa siku ile, leo hii tusingesumbuka namna hii..ona sasa tumepotea maboya kizembe sana" Mawazo hayo yalipita kichwani mwa Peter. Na ilikuwa kweli, wasingewasha taa wangekuwa na taswira ya Ayoub vichwani mwao, na wangemtambua Ayoub kabla hawajahangaika na kwenda Pemba, wangemtambua pale tu walipomuona kwenye runinga tangu wakiwa Kisarawe.
Upande wa Ayoub alikuwa anatetemeka vibaya sana. Aliamini kwamba wale ndio watu aliokuwa nao katika chumba chenye giza, watu hatari sana wenye kusoma hadi mawazo ya mtu yapitayo kichwani.
"Mkanda walishauchukua sasa wamefata nini tena kwangu, bila shaka leo wamekuja kunimaliza, siku ile walifata mkanda na leo bila shaka wamefata roho yangu! Nina mkosi gani mimi?..." Inawezekana kweli kwamba Ayoub alikuwa na mkosi. Maana alikuwa amepitia na kushuhudia mambo makubwa na mazito sana katika maisha yake. Na bado mambo hayo yalikuwa yanamuandama.
"Mwendawazimu katuuza aisee..." Peter alisema kwa nguvu. Akiwa na maana kuwa Binunu kawauza kwa kuwaonesha mtu sie, lakini kauli ile ilimstua vibaya sana yule mvuvi msindikizaji.
"Hapana jamani, huyu ndiye aliyepo katika picha yenu, ni mwenyekiti wetu wa BMU, wala sijawauza, hebu iangalieni vizuri picha yenu halafu mumuangalie na huyu, au labda mniambie mapacha." Mvuvi msindikizaji alilalama.
"Shut up! Tena funga kabisa mdomo wako mchafu, hatuko katika maigizo hapa, nitakupasua tumbo lako sasahivi na kuutawanya utumbo wako hewani!" Malkia alifoka kwa nguvu huku akirusha mikono yake hewani. Akionesha jinsi atakavyousambaza utumbo wa mvuvi msindikizaji.
Jamaa aliogopa sana. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hakutegemea kabisa kama watu wale walikuwa wakali namna ile, Mvuvi hakuweza kujizuia majimaji mepesi yasiiloweshe suruali yake, mkojo mwembamba ulimtoka bila kupenda, mkojo mwembamba ulimtoka bila kujua. Kila mmoja aliuona mkojo ule lakini hakuna aliyeujadili. Na tangu hapo wala hakuthubutu kufungua tena mdomo wake ulioitwa mchafu kuchangia chochote. Ingawa kichwani mwake kulikuwa na swali likilojirudia mara kwa mara.
"Hawa jamaa ni wakina nani?, na kuna nini kati yao na Mwenyekiti?" Alitamani sana kuuliza lakini wala hakuthubutu kabisa kulitoa swali lile nje ya mdomo wake mchafu, aliliacha likijiuliza ndani ya ubongo wake. Nani anayewaza kutamani kuuona utumbo wake ukitapakaa hewani.
Sasa Binunu aliingia katika mitaa ya Kisarawe akiwa na akili timamu kabisa. Kila kitu kilichotokea huko nyuma katika maisha yake kabla ya ile ajari mbaya ya meli kilirejea kwa kasi kubwa sana katika akili yake. Kumbukumbu zake adhimu zilizokuwa zimepotea takribani mwezi mmoja sasa zilikuwa zimerejea, kasoro vitu vichache ambavyo vilikuwa vimetokea mara ya mwisho baada ya meli ya Mv Donors kuzama. Hivyo ndivyo vitu pekee ambavyo hakuvikumbuka kabisa. Hakukumbuka baada ya ajari ile mkanda ulielekea wapi?. Alijaribu kukumbuka lakini kumbukumbu zilimgomea kabisa.
"Nakumbuka nilikaa kwenye kiti, baada ya kama ya saa moja meli ilianza kwenda mrama, kishaaaa.....yes.. lilitolewa tangazo la tahadhari, nakumbuka niliutoa mkanda baada ya tangazo lile na kuuvirigiza katika mfuko wa nailoni. Baada ya muda mfupi maji yalianza kuingia kwenye meli, nilisukumwa vibaya sana na yale maji......halafu, halafu kikatokea nini vileeeee, ah mbona nimesahau, aaah yes nimekumbuka.....nilimuona Ayoub Mbembati akiongea katika runinga....nooo sasa kwenye ile meli nilitokaje? Na mkanda utakuwa uko wapi?"
Kwa mara ya tano sasa alijaribu kukumbuka matukio yaliyotokea baada ya yeye kuingia katika meli, lakini aliishia kukumbuka hayo tu. Saa mbili sasa zilikuwa zimepita tangu Binunu akae katika msingi wa nyumba isiyoisha karibu na soko la Kisarawe. Alikuwa amekilaza kichwa chake juu ya magoti yake. Alikuwa akijaribu kuwaza upya juu ya mustakabari wa operesheni ya mkanda wa siri.
"Hii ni operesheni ya ajabu sana kuwahi kuifanya katika maisha yangu. Nilikodiwa na wakina Martin Hisia kufanya OMS bila kujua kuwa OMS ni Operesheni inayonihusu kwa asilimia mia moja. Niliingizwa katika operesheni ya kusaka kitu kinachonihusu kabisa lakini bila kujua. Kumbe ilikuwa ni operesheni ya kusaka kitu kilichopoteza maisha ya baba yangu mzazi. Operesheni ya kusaka kitu kilichoondoka na maisha ya mama yangu mzazi. Wazazi wangu walikufa kikatili sana kwa sababu ya mkanda tukiousaka katika OMS...Mkanda ule sijui utakuwa na nini ndani yake? Yaani Baba alikubali kufa kinyama namna ile lakini si kuuachia mkanda kwa watu wale wabaya, wenye nia mbaya bila shaka. Hivi mkanda huo utakuwa na nini lakini ndani yake?" Binunu sasa aliinua kichwa chake toka magotini na kuangalia mbele. Alikuwa anaangalia mbele lakini alikuwa haoni chochote kile. Alikuwa mbali sana kimawazo.
"....kwa sasa nina majukumu makuu mawili tu hapa duniani. Na majukumu hayo labda nd'o sababu ya mimi kuendelea kupumua mpaka sasa. Baada ya kuyamaliza majukumu hayo bila shaka nitakuwa nimekamilisha sababu ya mimi kuletwa Duniani. Nitakuwa tayari kufa! Najua ni majukumu mazito sana lakini lazima niyatimize, na hiyo ni kwa ajili ya wazazi wangu waliotokea kuwa wema kwangu kuliko mtu yeyote yule duniani..." Katika macho ya Binunu kulikuwa na majimaji mepesi yanatiririka alipokumbuka juu ya wazazi wake, maji yalishuka kwa kutengeneza michirizi myembamba katika mashavu yake laini.
Binunu alikuwa analia, na alikuwa analia baada ya miaka mingi sana kupita bila kulia. Hakukumbuka lini mara yake ya mwisho kulia, ingawa alikumbuka kwamba yeye alikuwa ameshawaliza watu wengi sana katika maisha yake. Na mtu wa mwisho alitoka kumliza saa mbili zilizopita.
"....nina jukumu zito sana la kulipa kisasi kwa wote waliosababisha vifo vya wazazi wangu wapendwa, pamoja na jukumu hilo zito lakini pia nina jukumu lengine zito, jukumu la kuusaka mkanda wa siri popote pale ulipo, kwa njia yoyote ile lazima niupate ule mkanda. Yaani ni LAZIMA!..." Binunu aliwaza huku neno la mwisho akijikuta amelitamka kwa sauti kubwa. Kitu kibaya sana kwake, hakuwa na kumbukumbu kabisa kama kwa mara ya mwisho mkanda alikuwa nao yeye. Alikumbuka mambo ya zamani sana na kusahau ya hivi karibuni.
Kule visiwani kina Malolo iliwafunukia kwamba walikuwa wamekosea. Walikuwa wameenda kwa mtu asiye sahihi. Lilikuwa ni kosa la kiufundi. Malolo alimpa ishara kwa siri Peter, ishara ile ya siri toka kwa Malolo ilisafiri kwa njia ya siri pia na kufika hadi kwa Malkia. Na wote watatu walielewana. Malkia alimuaga Ayoub akiwa na tabasamu tele usoni mwake. Alikuwa siye Malkia yule aliyemkoromea na kumtisha Mvuvi msindikizaji muda mfupi uliopita. Huyu sasa alikuwa mwanamke mrembo mwenye tabasamu la kirembo sana. Tabasamu lenye kuweza kumpumbaza mwanaume yeyote yule rijali, na kutoa hata asichoambiwa kutoa. Ayoub hakuwa hata na nguvu ya kuagana na watu wale. Ingawa aliliona tabasamu la Malkia lakini hakuwa hata na hisia za kupumbazwa na tabasamu lile ghali. Alibaki mdomo wazi huku akiwatazama tu wageni wake. Wale jamaa hawakujari. Walianza kuondoka huku Ayoub na Mvuvi msindikizaji wakiingalia migongo ya wababe wale watatu hadi ilipopotea katika upeo wa macho yao.
Ilikuwa ni safari kuelekea Kisarawe.
Laiti wangejua walichokuwa wanaenda kukutana nacho?
Ayoub na yule mvuvi msindikizaji sasa walibaki wanatazamana wenyewe, wakiwa hawaamini kabisa kama wamebaki salama, hawakuwa wanaelewa lengo la watu wale kuwaacha. Ulikuwa ni kama mchezo wa kuigiza wakina Steven Marashi na Ruby. Lakini ukweli ni kwamba huu haukuwa mchezo wa kuigiza. Ulikuwa ni mchezo wa kweli, wale majamaa waliondoka huku wakiwa hawajawagusa hata kucha zao wavuvi wale wawili!
Kisarawe..saa 05:08 P.M
Wakina Malkia waliwasili katika mji wa Kisarawe mida ya saa kumi na moja jioni. Walikuwa wamerudi tena katika maficho yao ya muda mfupi baada ya kukikosa walichokifata huko Pemba. Malolo alikuwa ndiye katangulia mbele wakati wanaingia ndani, mle sebuleni. Nyuma yake alikuwa anafatiwa na Peter na wa mwisho wa msafara ule wa watu watatu alikuwa Malkia, mwanamke wa kipemba hatari sana!
Alipofika tu ndani ya sebule Malolo alihisi harufu ya kifo! Harufu ya kifo cha binadamu. Haikuwa shida hata kidogo kwa Malolo kujua kwamba mle ndani kulikuwa na mwili wa binadamu, na ulikuwa unatoa harufu ya kifo. Malolo alikuwa amecheza michezo hatari mingi sana, na kukutana na harufu za vifo mara nyingi sana.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Bloody bastard.." Malolo alisema kwa sauti ndogo sana huku kwa haraka akiitoa bastola yake kiunoni ...mwanaume alikuwa tayari kwa lolote.
Tayari kuuwa!
Tayari kufa!
Ingekuwa mimi au wewe tungerudi nyuma tena kwa hofu kubwa sana, lakini Malolo hakuwa mimi au wewe, yeye alisonga mbele akiwa makini zaidi huku mdomo wa bastola yake ukiwa umetangulia mbele, tayari kwa kuitungua hatari yoyote ile mbele yake.
Peter na Malkia walisikia sauti ya Malolo ingawa ilisemwa kwa sauti ya chini sana, pia walikiona kitendo kilichofanywa na Malolo. Moja kwa moja wakajua mambo si salama ndani ya nyumba ile, mambo si shwari maskani mwao. Nao wakatoa bastola zao viunoni. Wakati Malkia alitoa bastola moja, aliyoishika imara kwa mkono wa kulia. Peter alitoa bastola mbili toka kila upande wa kiuno chake, mikono yake yote miwili sasa ilishika bastola. Peter alikuwa anangalia kushoto na kulia kila baada ya sekunde moja, sekunde hii akiangalia kushoto, sekunde inayofuata basi aliangalia kulia. Alikuwa anapiga hatua kila baada ya kuridhika kuwa kuna usalama pande zote mbili, hatua ambayo iliruhusu na Malkia nae apige hatua lakini kwa aina tofauti. Yaani Ilipendeza sana kuwangalia. Malkia yeye alikuwa amegeuka nyuma, akiiangalia hatari yoyote itokayo nyuma yao, alikuwa anarudi kinyumenyume lakini kwa tahadhari na umakini mkubwa sana. Huku kupiga kwake hatua kulifuata baada ya hatua ya Peter, ambaye nae aliruhusiwa na Malolo. Kila mmoja alikuwa anamlinda mwenzake huku akiwa anamsaka adui. Kwa mwendo wa kunyata na kwa 'style' ile ya aina yake walifika hadi sebuleni kabisa.
Malolo ndiye alikuwa wa kwanza kumuona, alikutana uso kwa uso na uso wa Chifu huku mwili wake ukiwa umelala hovyo sakafuni karibu na meza ya runinga. Malkia alikuwa wa mwisho katika msafara ule na kumbuka kuwa alikuwa amegeuka nyuma, lakini cha kushangaza na kustaajabisha alikuwa ndiye wa kwanza kufika katika mwili usio wa uhai wa Chifu pale sakafuni.
"Chifuuuuuu" Malkia aliita kwa nguvu huku akiutikisa mwili ule lakini Chifu hakuitika. Ataitika vipi wakati hakuwa katika ulimwengu huu? Wale wanaume wawili hawakuzubaa. Walikuwa wanatanguliza bastola zao kabla ya kugeuka kila upande wakiohisi adui anaweza kutokea, vidole vyao vya shahada vikiwa katika triga tayari kwa kuifyatua hatari. Ndani ya mioyo wao walikuwa na uchungu mkubwa sana, walikuwa na hasira kali sana, walikuwa na huzuni kuu. Lakini hawakutaka kuendeshwa na hisia kama Malkia. Ilibidi wazidhibiti hisia zao ili nao wasiingie katika mikono ya adui. Ukweli ni kwamba ilikuwa inawauma sana maana kumkuta Chifu katika hali ile ilikuwa ni habari mbaya sana kwao.
"Chifu ameuwawa! Chifu, Chifuuu, nakuomba please usife Chifu, usife mpaka nitakapokuletea mkanda niliokuahidiiiiiiii....." Malkia alithubutu kusema kwa sauti yenye majonzi makuu, huku aliutikisa kwa nguvu mwili wa baridi tena uliokuwa mtupu wa Chifu. Ukimya ulikuwepo pale sebuleni uliharibiwa vibaya sana na kelele za majonzi za sauti ya Malkia.
"Shiiiiiiiiii!" Malolo alimnyamazisha Malkia huku akiwa ameweka kidole chake cha shahada cha mkono wa kushoto katikati ya mdomo wake.
"Ni hatari sana hiyo" Peter alisema kwa sauti ndogo sana. Malkia alinyamaza kulia kwa sauti, lakini hakunyamaza kulia kwa kutiririsha machozi, machozi yalimmiminika kama mtoto mdogo. Kwa mara nyingine tena Binunu alikuwa analiza mtu siku ile. Jamaa walimwangalia mwanamke yule aliyekuwa anapitia katika machungu makubwa sana lakini hakuna aliyeenda kumbembeleza, wao wenyewe walikuwa hawaijua hatma ya usalama wao mle ndani.
"Siku nitakayokufa hakika mtazikuta maiti mbili, yangu na ya huyo atakayeniuwa, nachukia sana kifo lazima nipambane sana ili kukiepuka...Chifu hawezi kufa kizembe hata siku moja!" Chifu alishawahi kuwaambia maneno hayo wakina Malolo, na Peter aliyakumbuka pale sebuleni. Na ndipo alipopata cha kufanya, alimpa ishara Malolo, na aliielewa.
Waliitekeleza.
Vijana wale wawili walianza kuingia ndani ya nyumba huku wakimuacha Malkia pale sebuleni akiwa ameulalia mwili wa Chifu. Hakika lile lilikuwa PIGO MUJA'RABU kwa Malkia. Walienda kukagua sehemu moja baada ya nyingine ili kuona kama kuna maadui ndani au labda maiti ya pili kama alivyowaahidi Chifu juu ya siku atakayokufa.
Baada ya nusu saa jamaa walikutana tena sebuleni. Wakiwa idadi ileile, watatu na mwili wa Chifu ukiwa umelala bado sakafuni ukiwa hauna uhai...huku Malkia akiwa pembeni ya mwili ule. Akiwa amekaa kitako, amenyoosha miguu yake, kaupakata ule mdoli uliokuwa unamilikiwa na Binunu, Malkia alikiwa ametoa macho akiwa anashangaa kitu kisichoonekana. Alikuwa anaongea maneno yasiyoeleweka. Amini, usiamini.....Akili ya Malkia haikuweza kustahamili uzito wa kifo cha mtu wa karibu yake sana, mtu aliyekuwa analala nae kitanda kimoja, shuka moja. Wakishirikiana kila wanachopaswa kushirikiana wanandoa. Ama kweli mapenzi ni kitu cha ajabu sana. Malkia alikuwa amestahamili maumivu mengi sana katika maisha yake, maumivu ya kuumiza sana lakini leo hii alishindwa kabisa kuvumilia maumivu ya mapenzi. Mume anauma wewe! CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ugonjwa kama aliokuwa nao Binunu leo hii ulimrudia yeye, na mdoli aupendao Binunu leo hii alikuwa anaupenda yeye. 'What goes around, comes around'
Daah! Malkia alikuwa amechanganyikiwa katika siku ileile ambayo Binunu alikuwa amerejewa na akili pamoja na kumbukumbu zake za maisha yake ya nyuma.
MWISHO WA MKANDA WA SIRI SEASON 1
MKANDA WA SIRI - 4
Simulizi : Mkanda Wa Siri
Sehemu Ya Nne (4)
Upande wa Malolo, 'Laptop' ilifunguka, aliingiza namba ya siri, akabofya 'icon' iliyoandikwa 'my documents', yakafunguka mafaili mengi, akawa anatafuta faili analolitaka, akalipata. Lilikuwa limeandikwa 'Dangerous People in Mission' akalibonyaza hilo faili, nalo likadai namba ya siri, aliweka namba ya siri tofauti na ile ya awali, likafunguka. Akaanza kutafuta jina la yule mzungu katika orodha ya watu kumi. Mtu wa tatu katika orodha ile alikuwa Brown Van Dyke, akabofya hilo jina, kompyuta ikadai tena namba ya siri, akaiweka namba ya siri lakini tofauti na zile namba za siri za awali. Likafunguka! Akamsogezea Malkia ile laptop ili amuoneshe Brown Van Dyke ni nani? " Malkia alifumbua macho, aliipokea laptop na kuanza kusoma. Alitumia masaa mawili kusoma habari ile ndefu kuhusu Brown. Malkia alikuwa anajikuna kichwa kila baada ya sekunde kumi. Maelezo kuhusu Brown yalimuingia hasa. Baada ya kumaliza kusoma alimwangalia Malolo akiwa amekata tamaa. Jasho linammwagika, kiyoyozi cha kwenye gari hakikumsaidia kabisa. Malolo aliongea.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Lazima Peter aje Zanzibar, yeye pekee ndo ataweza kupambana na Brown. Brown ni moto! .....tena ni moto wa kuotea mbali!"
"Peter anakuja leo....." Malkia alijibu kwa sauti ya chini sana.... Malkia maji yalikuwa yamemfika hapa! Na ilikuwa kama Malkia alivyosema....
Sasa wote waja Zanzibar, shughuli imekuwa ngumu sanaaa..
Lazima Peter aje Zanzibar, yeye pekee ndo ataweza kupambana na Brown. Brown ni moto! .....tena ni moto wa kuotea mbali!"
"Peter anakuja leo....." Malkia alijibu kwa sauti ya chini sana.... Malkia maji yalikuwa yamemfika hapa! Na ilikuwa kama Malkia alivyosema....
Saa tatu kamili asubuhi Peter aliwasili katika visiwa vya Zanzibar. Akiwa amevaa suti yake kali nyeusi, viatu vyeusi na miwani nyeusi, alifika Zanzibar akiwa ndiye tumaini pekee katika mapambano ya kuusaka mkanda wa siri. Malolo Abdallah ndiye mtu aliyeenda kumpokea Peter bandarini. Walitoka katika viunga vya bandari na kutoka nje, mahali alipopaki Malolo gari. Wakaingia ndani ya gari. Malolo katika usukani, Peter katika kiti cha abiria.
"Peter mwendawazimu tumeshikwa pabaya sana safari hii..." Malolo alianza kuongea punde tu walipoingia ndani ya gari.
"Kivipi Malolo, mbona unaweweseka kwa mambo madogo sana Malolo" Peter alisema huku akijiweka sawa kitini.
"Hebu fikiria mwenyewe Peter, wale jamaa wana Martin Hisia pamoja na Brown Mrusi, wale jamaa ni watu hatari sana bro"
"Malolo una woga sambamba na kitete, woga ni kitu kibaya sana katika misheni kama hizi, hutakiwi kuogopa hata siku moja Malolo, hutakiwi kumuogopa adui, ukimuogopa adui jua umeshampa nafasi ya kushinda...ngoja nikwambie kitu, Martin Hisia ni mtu kama wewe, Brown ni binadamu kama wewe, kwanini uogope? Acha tukapambane, tukapambane huku tukiweka uwoga pembeni."
Baada ya maneno hayo Malolo alikumbuka maneno aliyoambiwa na Malkia juu ya woga. Aliamua kukaa kimya. Na hawakuongea tena mpaka walipofika kasrini mbele ya Malkia. Malkia alimueleza kila kitu Peter, na Peter alielezea hatua alizozichukua huko Dar pindi tu aliposikia kuwa Mkanda umepotea. Wote walishangaa kusikia kuwa Peter ndiye aliyemuuwa yule jamaa bandarini.
"Huyo msichana uliyemuelezea hapa yuko wapi sasa, au ndo amepotea kabisa..." Peter aliuliza baada ya maelezo marefu ya kujulishana walipofikia.
"Msichana tunaye Peter, anaishi sebuleni, analala kile chumba cha mwisho ..." Malkia alisema huku akionesha kwa kidole mahali kilipo chumba akicholala Binunu.
"Malkia bwana....Kumbe mkanda wa siri tunao halafu tunahangaika na kupata uwoga usio na maana". Peter alisema akiwa na uhakika kabisa.
" Unasema!!! ...Mkanda tunao? Uko wapi? Eti Peter?”
"Malkia punguza jazba....huyo msichana ndiye mkanda wa siri. Huwezi kumtenganisha msichana na mkanda wa siri. Ni yeye ndiye aliyetumwa kuupeleka mkanda Dar kwa Martin bila shaka....kwa vyovyote vile msichana ndo binadamu pekee hapa duniani ambaye anajua mahali sahihi ulipo mkanda wa siri"
"Inawezekana uko sahihi Peter, lakini huyo msichana ni Mwendawazimu Peter, hana hili wala lile, how atajua mahali ulipo mkanda?"
"Nakwambia Malkia hata kama huyo dada ni Mwendawazimu lakini yeye ndiye anapajua mahali mkanda wa siri ulipo, siku ambayo akili zake zitarudi ndio siku hiyohiyo ambayo mkanda wa siri utarudi mikononi mwetu, la msingi ni kumlea vizuri, kumlea kama mtoto mdogo Ili kuiweka saikolojia yake sawa. Ipo siku atapona tu, na akipona atasema mahali mkanda wa siri ulipo, na sisi kuibuka washindi"
"Sasa Peter .....vipi kuhusu wakina Brown na Martin Hisia?"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ngoja nikuulize kitu Malkia..we unafikiri kina Martin sasahivi wanahaha kuutafuta mkanda au wanamtafuta huyo msichana?"
"I think wanamtafuta huyu msichana"
"Sio you think Malkia, huo ni ukweli, wanamsaka huyu msichana...walimkabidhi yeye mkanda, bila shaka wao wanajua kwamba mahali ulipo mkanda anapajua yeye, sasa we unadhani kwanini walitaka kukuvamieni hapa usiku, wakati wanajua mkanda walishauchukua hapa?....jibu mbona rahisi sana halihitaji hata kutumia four figure?" Malkia alikaa kimya.
Maneno ya Peter yalikuwa kweli tupu. Alitafuta neno la kusema...lakini hakulipata.
"......amini wanajua wakimpata huyo msichana ndio wameupata mkanda, sasa sisi tunae huyu msichana, ambaye kwa sasa thamani yake ni sawa na mkanda sasa kwanini tuhangaike? Achana na madetector, achana na kina Martin Hisia, watatumalizia energy zetu tu bure, tudeal na huyo msichana, Msichana ni muhimu zaidi kwa sasa, siri zetu zote za kule Amboni ziko mikononi mwake"
"Aisee fact, nimekuelewa sana chizi" Malkia alitingisha kichwa juu-chini na kusema maneno hayo.
Sasa mchezo pande zote mbili ulikuwa unaongozwa na watu wenye akili sana. Peter Kisali P.A.K Mwendawazimu kwa upande wa kina Chifu na Brown Kolarov P.A.K Brown Mrusi kwa upande wa kina Martin Hisia.
Kitu cha kwanza kushauri Peter ili kufanikisha misheni hii ni kuacha kabisa kuwafatilia wakina Martin Hisia, kwake yeye kina Martin Hisia ndio walipaswa kuwafatilia wao, sio wao kuwafatilia. Kina Martin ndio waliopaswa kumtafuta Binunu kwa nguvu zote maana nd'o mwenye kujua mahali ulipo mkanda wa siri, ushauri ambao ulikubaliwa kwa mikono miwili na Malkia pamoja na watu wote katika kambi ile, na kitu cha pili, Peter alichoshauri ni kuhama katika kasri ama kuhama kabisa katika mji wa Zanzibar. Kwakuwa maadui zao walishayajua makazi yale na muda wowote wangeweza kuvamia na kumteka Binunu. Alishauri watafute sehemu nyingine yoyote wakaishi wakati wanasubiria Binunu arejee katika hali yake ya kawaida.
Kwa mara nyingine tena wote walikubaliana na ushauri huo wa busara sana. Waliona kama alivyoshauri Peter....... Kasri si sehemu salama tena, lazima wakae napo mbali. Wazo hili nalo lilipitishwa.
Siku ileile usiku, kwa kutumia ndege ndogo ya kukodi....Chifu, Malolo, Malkia, Peter na daktari wa familia walihama Tanzania Visiwani na kuhamia Tanzania bara, katika mji uitwao Kisarawe, katika mkoa wa Pwani, mji uliopo nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam.
Upande wa kina Martin Hisia wao walihama katika mji wa Unguja. Walijua nyumba ile ilishagunduliwa na detector ya maadui zao. Muda wowote wanaweza kuvamiwa. Ulikuwa ushauri toka kwa Brown Mrusi. Na ukakubaliwa na wote. Kina Martin nao walihama katika kisiwa cha Unguja, na kuhamia katika kisiwa cha Pemba, katika mji uitwao Chakechake. Lakini kina Martin walikuwa wanaenda Unguja mara kwa mara kwa minajili ya kumsaka Binunu Issa.
MWEZI Mmoja Baadae. Hali ya Binunu bado ilikuwa vilevile. Alikuwa Mwendawazimu anayeishi ndani katika nyumba moja ya kisasa huko Kisarawe, Mwendawazimu anayepatiwa kila kitu kwa ajili ya malezi ya bora ya akili yake, kile kidonda kikubwa kilichokuwa nyuma ya kisogo chake kilikuwa kimepona sasa ingawa kilikuwa kimeacha kovu baya sana. Muda mwingi Binunu alikuwa anaongea maneno yasiyoeleweka huku mara chache akiongea maneno mawili yanayoeleweka...mkanda wa siri. Kila akitaja maneno hayo watu wote walikuwa makini kumsikiliza ili kujua atasema neno gani lengine kuhusu mkanda. Binunu hakuwahi kusema hilo neno walilolisubiria. Pamoja na kutosema neno hili lakini walijiona wamefanya uamuzi sahihi, walikuwa wanasubiri kwa hamu siku ambayo Binunu atasema neno walilolitarajia siku zote... Kuwatajia mahali Mkanda ulipo.
Pamoja na daktari wa familia kuwa karibu sana na Binunu kuhakikisha afya ya akili ya Binunu inakaa sawa lakini pia walijaribu kumpeleka Hospitali kadhaa kujaribu kumtibu, walipewa majibu ya kutia moyo mengi sana lakini majibu ya kutia moyo toka kwa madaktari bingwa yalikuwa hayajaleta hiyo hali iliyoitwa ya matumaini wakiyoizungumzia madaktari. Maana hali ya Binunu ilikuwa vilevile kama siku ile walivyompora katika viwanja vya Maisala.
Chifu Abdullah hali yake sasa ilikuwa nzuri. Alikuwa amerudi katika hali yake ya kawaida kabisa. Peter alifanya kazi kubwa sana ya kumjenga kisaikolojia Chifu. Muda mwingi aliutumia kumpa imani kwamba mkanda ulikuwa umepatikana. Peter alimwaminisha Chifu Abdullah na kuwaaminisha watu wote kwamba Binunu ndiye alikuwa mkanda. Pamoja na kuamini hivyo na kuwa na matumaini makubwa kwamba mkanda ambaye kwao ulikuwa ni Binunu ulikuwa mikononi mwao, Lakini hali ilikuwa siyo ya kuleta matumaini hata kidogo, ni mwezi sasa ulikuwa umepita tangu Binunu awe mwendawazimu kamili.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Huko Chakechake Pemba, hali ilikuwa ya kukatisha tamaa. Hawakumuona Binunu wala hawakujua lolote kuhusu mkanda. Ni mwezi sasa ulikuwa umepita lakini hawakuwa wamemuona Binunu wala Mkanda. Licha ya kwenda Unguja mara kadhaa kule katika kasri ya Chifu, lakini hawakumkuta mtu yeyote wa maana zaidi ya Walinzi walio na dalili zote za kutokujua lolote. Walishawateka walinzi watatu, licha ya kuwatesa sana lakini walisema hawajui mahali waliko mabosi wao...na sura zao zilimaanisha..walikuwa hawajui mahali walikoenda wakina Chifu. Wakina Martin walikuwa wanaelekea kushindwa sasa, hawakuweza kabisa kujua Chifu na familia yake wamehamia wapi.
Upande wa jeshi la Polisi hawakuacha kumsaka Martin Nguzu hata siku moja. Koplo Baruani alikuwa anafatilia kesi mbili ambazo hakujua kabisa kama zina uhusiano. Kesi inayomuhusu Martin Nguzu kwa kumuua mtu ndani ya gari na kesi ya inayomuhusu mzungu aliyemvamia muuza madini katika hoteli ya Grand Villa, mzungu aliyetambulika kama Mr Nanana. Koplo Baruani alikuwa kazini kila siku kuwasaka watuhumiwa hao wawili, lakini hakupiga hatua yoyote. Yeye aliwasaka kwa nguvu sana katika jiji la Dar es salaam, wakati Martin Hisia na Brown Mrusi walikuwa katika nyumba moja waliyopanga huko Chakechake, Pemba. Angewapata vipi?
Kisarawe Saa 8:00 P.M
Ni mwezi na wiki moja ilikuwa imepita, tangu mambo yale ya ajabu yatokee kule Zanzibar. Ilikuwa siku ya jumatatu na ulikuwa ni muda wa kuangalia taarifa ya habari. Wote walikuwa sebuleni katika nyumba ya kisasa waliyokodi kwa muda wa mwaka mmoja ili kuisubiri hali ya Binunu itengemae. Chifu na Malkia walikuwa wamekaa katika sofa zuri la watu wawili, wakiwa wamekumbatiana. Huku Malolo na Peter wakiwa wamekaa katika sofa la mtu mmojammoja. Peter akiwa upande wa kulia wa sebule, na Malolo upande wa kushoto, wakati Malkia na Chifu wakiwa wamekaa katika sofa lililokuwa katikati ya sebule. Binunu, yeye alikuwa amekaa chini, pembeni ya sofa la Peter. Akiwa kajiinamia chini anautazama mdoli wake huku akicheka mara kwa mara, kama ilivyo ada yake.
Taarifa ya habari toka katika televisheni ya Taifa..TBC, ilikuwa inaendelea, huku mtangazaji mahili wa kituo hiko anayejulikana kwa jina la Gabriel Zacharia akisoma habari kwa uweledi mkubwa sana, zilikuwa habari za kitaifa.
Ghafla! Binunu aliacha kuuangalia mdoli wake na kwa umakini mkubwa sana aliiangalia runinga. Kilikuwa ni kitendo cha ghafla sana lakini kilionwa na Peter. Wakati wengine wote wakiwa makini na taarifa ile ya habari, Peter aliacha kuitazama taarifa ya habari na kumwangalia Binunu. Umakini wa ghafla uliooneshwa na yule msichana uliivuta akili ya Peter. Binunu alikuwa ametulia tuli. Mdoli akioutazama muda mfupi uliopita alikuwa ameutupa pembeni, kicheko ambacho huwa kinamtawala siku zote leo kilikuwa kimekata ghafla. Binunu alikuwa makini mithili ya mtu mwenye akili timamu, tena zaidi hata ya mtu mwenye hizo akili ziitwazo timamu. Alikandamiza mikono yake chini ya sakafu huku akiunyanyua mwili wake kwa juu. Kilikuwa kitendo kilichochukua sekunde zipatazo kumi na tano. Sasa Binunu alikuwa amesimama wima. Peter alikuwa makini kuwaangalia vitendo vya kushangaza viliavyoanza kuoneshwa kwa ghafla na yule msichana wasiyemjua jina, ambao wao waliamua kumpachika jina la Mkanda. Kwa maana hiyo Peter alikuwa anamtazama jinsi Mkanda alivyosimama.
"Kaona nini huyu? Leo kausahau hata mdoli ambao alikuwa analia hata ukimtishia tu kumnyang'anya?" Hayo ndio maswali makuu yaliyopita mawazoni mwa Peter.
"Kuwa na subira, leo huyu msichana atakufumbulieni fumbo mkilolisubiri siku nyingi" Sauti nyingine toka ndani ya nafsi yake ilimjibu. Yalikuwa majibizano kati ya mawazo na nafsi ya Peter, na Peter aliisikiliza nafsi yake.
Aliamua kusubiri.
Binunu P.A.K Mkanda alikuwa imara, amesimama wima, huku macho yake yote mawili yakiwa makini yakitazama kilichokuwa kinaoneshwa katika runinga, macho yaliyojaa mshangao, sawa na macho ya mtu yeyote yule mwenye akili timamu lakini ambaye alikuwa ameona kitu kilichomstaajabisha sana.
"Kaona nini huyu?" Mawazo ya Peter yaliuliza tena, nahisi yalikuwa yamechoka kusubiri. Mawazo yaliamini kuwa...ngoja ngoja yaumiza matumbo!
"Nimekwambia subiri, kuwa na subira huyu mwanamke atakuonesheni kitu leo" Nafsi ya Peter iliendelea kusisitiza subira. Nafsi iliiamini kwamba subira yavuta heri.
Binunu sasa alipiga hatua ndogo kwa mguu wake wa kulia kuelekea mbele, kisha ikafuatiwa na hatua nyingine ndogo kwa mguu wake wa kushoto. Alipiga hatua zipatazo tatu toka kwa kila mguu, alifika mbele ya runinga. Sasa akavuta umakini wa kila mtu pale ukumbini.
Wote walimuona sasa.
Binunu sasa alipiga hatua ndogo kwa mguu wake wa kulia kuelekea mbele, kisha ikafuatiwa na hatua nyingine ndogo kwa mguu wake wa kushoto. Alipiga hatua zipatazo tatu toka kwa kila mguu, alifika mbele ya runinga. Sasa akavuta umakini wa kila mtu pale ukumbini.
Wote walimuona sasa.
Ukumbi mzima ulikuwa unamwangalia yeye, kila mmoja akionesha mshangao wa hali ya juu. Chifu na Malkia ambao walikuwa wamekumbatiana pale sofani, waliachiana taratibu bila wenyewe kujua, Malolo nae alikuwa mdomo wazi akiangalia kitendo kile cha ajabu kilichokuwa kinaoneshwa na Binunu. Binunu hakuwapa muda wa kutafakari sana, alinyoosha mkono wake kulia, huku kidole chake cha pili toka kidole gumba kikiwa mbele, kidole maarufu kama kidole cha shahada. Binunu alikuwa anaonesha kitu kwenye runinga, ama alikuwa anamuonesha kidole mtu. Watu wote walipigwa na butwaa!
"Ana nini huyu?" Chifu aliuliza kwa sauti ndogo sana, lakini ilisikiwa na watu wote pale ukumbini, ingawa walimsikia, hakuna hata mtu mmoja aliyejihangaisha kumjibu. Kila mmoja akili yake ilikuwa makini na yule msichana, na sio kujibu maswali ya Chifu, kwanza wangemjibu nini? Wao wenyewe walikuwa katika mshangao. Binunu alinyoosha mkono wake huku bado kile kidole cha shahada kikiwa mbele takribani kwa sekunde sita. Kisha aligeuza shingo yake kuangalia kulia, upande aliokaa Peter, kisha aligeuza shingo yake taratibu kuelekea upande wa kushoto, upande aliokaa Malolo. Kisha aligeuka nyuma, akiwaangalia wakina Chifu. Alirudisha tena uso wake mbele, kwenye runinga....kwa sauti ndogo sana yenye uhakika na kumaanisha alisema.
"Huyu ndiye anao mkanda wa siri"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati Chifu, Malkia na Malolo wakiwa makini na Binunu, na kushangazwa na kauli iliyotolewa na Binunu. Peter alifikiri kwa haraka, aliona wakizubaa watakosa kitu muhimu sana. Watamkosa mtu mwenye mkanda wa siri kwa mujibu wa maneno ya Binunu. Alivyofikiria tu hayo na kauli ya Binunu ilijirudia tena kichwani kwake.
"Huyu ndiye mwenye Mkanda wa siri"
"Lazima nifanye kitu..." Peter alijisemea kimoyomoyo. Peter aliacha kumwangalia Binunu. Macho yake aliyapeleka katika runinga, kukiona hicho kilichomnyanyua Binunu toka pale chini, kukiona hicho kitu au mtu aliyemfanya Binunu kutamka maneno yale yenye thamani kubwa sana kwao, maneno ambayo ni mwezi na wiki moja sasa walikuwa wanayasubiri. Kama alivyohisi Peter tangu ile siku ya kwanza aliposimuliwa mkasa huu na Malkia, na kusema kwamba ipo siku isiyo na jina Binunu atasema mahali mkanda ulipo, ni yeye aliyeshauri wamlee vizuri tu Binunu ili ajione yupo katika mikono salama, ili asiwe na shaka yoyote siku hiyo ikifika. Siku hiyo ya kufikirika ilikuwa imesadikika sasa. Binunu amewaonesha mtu mwenye mkanda wa siri. Ilikuwa ni jukumu lao wao kupiga hatua mbele, hatua muhimu, hatua zenye kuleta mafaniko. Na mafanikio pekee yalikuwa ni kuupata mkanda! Peter aliona uzembe waliokuwa wanaendelea kuufanya pale sebuleni, yeye hakutaka hata kidogo kuwa sehemu ya uzembe huo. Aliacha kumwangalia Binunu, alingalia runinga. Ili kukiona hicho kilichomnyanyua Binunu pale sakafuni na kuuacha mdoli aupendao. Alijua kwa vyovyote vile kilichomstua Binunu kilikuwa runingani. Sasa kwanini yeye azubae kwa kumwangalia Binunu ambaye wanae siku zote.
Habari ilikuwa inahusu mambo ya uwekezaji wa maliasili za bahari. Mtu mmoja alikuwa anaonekana katika runinga akiongea kwa kujiamini sana. Peter alijua cha kufanya, harakaharaka aliitoa simu yake mfukoni na kumpiga picha mvuvi yule. Kisha alimgeukia Binunu, ambaye alikuwa katika hali yake ileile, huku akimuonesha kidole yule mtu kwenye runinga. Nae alimpiga picha akiwa katika ile hali ya kumuonesha kidole yule mtu. Na ile habari iliisha.
Binunu alipigwa na butwaa kubwa sana kwa kutomuona tena yule mtu pale mbele. Alitulia tuli. Mkono wa kulia kaushusha sasa, alibaki kasimama wima. Ilikuwa kama kuna kitu kilikuwa kinapita kichwani mwake.
"Vipi jamani mbona kimya?" Ilikuwa sauti ya Dokta wa familia aliyeingia pale sebuleni akitokea chumbani. Wote waliweka vidole vyao vya shahada mdomoni wakimwashiria anyamaze. Na Dokta alinyamaza.
Ghafla, Binunu alitoa kicheko kikubwa, alirukaruka juu mara tatu, kisha alicheka tena....alisema, Mkanda, mkanda..kauli aitoayo siku zote tangu alipopata madhila haya, sio ya kauli ya kumaanisha kama aliyotoa pindi alipomuona yule mtu katika runinga. Watu wote walikuwa kimya, huku Dokta akiwa kasimama mlangoni na mshangao wake, kwake hakukuwa na jipya pale, ile ilikuwa hali ya siku zote ya mgonjwa wake, yale yalikuwa maneno ya siku zote ya Binunu. Kilichomshangaza Dokta ni Binunu kuwa mbali na mdoli wake. Hilo pekee ndio lilikuwa ajabu.
"Au ndo kinachowashangaza wenzangu?" Alijiuliza mwenyewe, hakuthubutu kuuliza kwa nguvu.
Binunu alipandwa na kichaa, alijizungusha mwenyewe mara tatu, huku akipiga kelele. Kisha alikimbia mbio fupi na kwenda kuunyanyua haraka mdoli wake pale chini. Aliutazama kwa umakini sana. Akarukaruka tena, kisha akasimama. Akacheka tena kiuwendawazimu. Kisha akajipweteka chini palepale alipokaa awali. Na kuendelea kuchezea mdoli wake, ilikuwa kama hakijatokea kitu. Binunu alikuwa amepona muda mfupi uliopita lakini sasa alikuwa mwendawazimu tena!
Kitendo kile kiliacha maswali mengi sana kwa kina Malkia. Huku wa kuwajibu alikuwa Binunu peke yake, Binunu ambaye hakukuwa na matumaini yoyote kwamba atawajibu kitu, ataelewa kitu, atakumbuka kitu, Binunu sasa alikuwa Mwendawazimu!
"Nini hii jamani, ina maana gani hii, eeeeh...?" Malkia aliuliza kwa nguvu, kwa sauti iliyojaa hamaniko.
"Kuna kitu!" Malolo na Chifu walijibu kwa pamoja ingawa kila mtu kwa maneno yake.
"Hata mimi naamini hivyo, na iko hivyo......Bila shaka kuna kitu, ni kitu gani sasa?" Malkia aliuliza tena.
"Mkanda alimkabidhi yule jamaa mkanda" Malolo alisema akiwa na uhakika mkubwa. Akimaanisha Binunu alimkabidhi yule jamaa mkanda.
".....na kwa bahati mbaya ile habari imeisha, hatukuwa makini kumwangalia vizuri yule jamaa" Chifu alidakia ile kauli toka kwa Malolo.
"Tumefanya kosa la kiufundi, yatupasa tusubiri marudio ya taarifa ya habari, kama sio saa nne usiku basi saa tano, au asubuhi katika kipindi cha Jambo Tanzania!" Malkia aliwaambia wenzake. Wote walitikisa vichwa kusikitika, kasoro Peter na yule Dokta aliyekuwa bado kasimama pale mlangoni.
"Sijaelewa mnazungumzia nini?" Dokta aliuliza huku akipiga hatua kuingia sebuleni.
"Mkanda wa siri..." Chifu alijibu kwa sauti iliyochoka.
Na ukumbi mzima ulikuwa kimya!
Peter alinyanyuka taratibu pale sofani, huku akiwa ameishika simu yake mkononi. Macho nane yalikuwa yanamwangalia yeye. Macho ya Chifu, Malkia, Malolo na Dokta. Peter hakujari wingi wa macho yalikuwa yanamwangalia, alimsogelea Binunu pale chini na kupiga magoti mbele yake. Alimkaribia kabisa, lakini Binunu hakujishughulisha kumwangalia Peter hata kidogo, yeye alikuwa makini akiutazama mdoli wake. Watu wote mle ndani walikuwa wanamshangaa Peter.
"Unataka kufanya nini Peter?" Daktari aliropoka.
Lakini hakupata bahati ya kujibiwa. Peter alinyoosha mkono wake wa kulia ambao ulikuwa umeshika simu yake hadi karibu na uso wa Binunu. Binunu alitazama kidogo kile kilichoshikwa na yule jamaa.
E bwana wee, Alimuona!
"Mkandaaaaaa..!" Binunu aliropoka kwa nguvu. Huku mdoli wake aupendao akiurusha hewani. Binunu alirudia tena kusema yale maneno kwa sauti kubwa. Maneno yaliyoleta matumaini makubwa sana katika moyo wa kila mtu pale ukumbini.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Huyu ndiye anao mkanda wa siri" Binunu alisema huku akiiangalia ile picha katika simu ya Peter kwa umakini mkubwa sana, ilikuwa mithili ya mwanafunzi yupo katika chumba cha mtihani, akijitahidi kulikumbuka jawabu ambalo alikariri asubuhi ya siku ya mtihani na kumpotea ghafla baada ya kuliona swali ndani ya mtihani.
Saa 6: 01 A:M
Usiku uleule kwa kutumia mashine waliyokuwa nayo 'waliiprint' ile picha toka katika simu ya Peter. Sasa kila mmoja alikuwa na picha ya mvuvi mwenye mkanda wa siri mkononi mwake.
Wakiisubiri kesho kwa shauku kubwa sana.
*****
Asubuhi na mapema..... Malolo, Malkia na Peter walikuwa safarini kuelekea katika kisiwa cha Pemba...kumsaka yule jamaa ambaye walikuwa na picha yake mkononi tayari. Walijiridhisha kwa kuangalia tena taarifa ya habari alfajiri na kupata jina la mahali alipokuwa anaishi yule mvuvi, kwa bahati mbaya kabisa taarifa ya habari haikutaja jina la mvuvi, zaidi ya kutaja cheo chake, kwa mujibu wa taarifa ya habari toka katika Televisheni ya Taifa, Jamaa alikuwa ni mwenyekiti wa B.M.U ( Beach Management Unit) katika kisiwa cha Pemba.
Waliondoka huku pale Kisarawe alibaki Chifu, Binunu na Dokta wa familia.
Hawakujua....hawakujua!
Yaani laiti wangejua? Bora hata wasingeenda..
Ukiondoa kina Malkia ambao walikuwa wameenda Pemba kwa waliobaki, Binunu ndiye alikuwa wa kwanza kuamka. Aliamka dakika thelathini baada ya wakina Malkia kuelekea Pemba. Alitoka chumbani kwake na moja kwa moja alienda sebuleni, na kukaa mahali palepale alipokaa jana, sehemu anayokaa siku zote tangu wahamie Kisarawe. Alikuwa anapepesa macho huku akiangalia hapa na pale. Alikuwa anaongea peke yake maneno ambayo bila shaka hata yeye mwenyewe alikuwa hayaelewi maana yake, lakini cha ajabu yeye mwenyewe ndiye alikuwa anacheka kutokana na maneno yake. Kwa hakika Binunu alikuwa kichaa dhahiri.
Dakika thelathini baadae Chifu nae aliamka. Moja kwa moja alielekea sebuleni. Akiwa amejifunga taulo tu kiunoni huku juu akiwa amevaa 'vest' nyeupe aina ya spider. Chifu alikuwa anapiga mluzi akiufatiza wimbo wa kihindi wa All is Well, wimbo mzuri uliopamba tamthilia ya kihindi ya 3 Idiots.
Chifu sasa alikuwa na amani, amani iliyotokana na uhakika, alikuwa na uhakika kwa kikosi kilichoelekea Pemba iwe isiwe lazima kitarejea na Mkanda. Wale ni watu makini aliowatumia miaka kadhaa sasa, na walikuwa wameshafanya operesheni ngumu na za hatari tena zaidi ya hii. Ikiwemo Operesheni Pambana na Simba, Operesheni iliyoanza kama biashara lakini baadae ikageuka na kuwa vita! Chifu alimkumbuka kiongozi wa operesheni hii ya sasa, Malkia. Mwanamke wa kipemba aliyetoka kuwa mfanyakazi wake wa ndani lakini kwasasa aligeuka kuwa mpenzi wake. Mwanamke aliyemfundisha mwenyewe ukatili, ambaye kwa sasa amekuwa katili zaidi yake. Mwanamke mwenye kutumia akili za kuzaliwa kuwahi kutokea hapa duniani.
Chifu alimkumbuka Malolo, mwanaume wa shoka, mwanaume mahiri katika mapambano ya ana kwa ana. Alitingisha kichwa kukili uwezo wa Malolo. Malolo alikuwa ni mtu sahihi kabisa kuwemo katika operesheni hii.
Mwisho alimkumbuka Peter, alivyomkumbuka Peter aliguna tu mwenyewe kwa sauti kubwa, na kuacha kupiga mluzi, hakuwa na maneno mazuri zaidi ya kumuelezea Peter.....
Chifu alipiga hatua mpaka sofani, alienda kukaa katika sofa lilelile alilokaa jana yake, tofauti ni kwamba jana alikaa na mkewe lakini leo alikaa peke yake. Alitulia tuli huku akiangalia runinga.
Runinga ilikuwa inaonesha kipindi cha magazetini.
"Wataalamu wamesahau kuzima hata runinga? Kweli wanapenda kazi"
Chifu alisema huku akichukua kikopo kidogo kilichokuwepo pale mezani. Alikifungua na kumimina unga mweupe katika kiganja chake cha mkono wa kulia. Alivyouona tu ule unga madenda yalimtoka. Ni miaka arobaini na tatu sasa tangu aanze kuutumia unga ule, unga ulioitwa haramu na Serikali lakini kwake ulikuwa halali, tena halali tamu lakini hadi leo alikuwa hajauzoea bado, akiuona tu lazima madenda yamtoke. Unga wa ajabu sana ambao humpa hisia za ajabu siku zote. Kiganja chake cha mkono wa kulia chenye ule unga laini mweupe alikipeleka usawa wa pua yake.
Alianza kuunusa taratibu.
Mara Dokta wa familia alienda sebuleni, walisalimiana na Chifu, baada ya maongezi ya kama dakika mbili Dokta alimuaga Chifu kuwa anaenda kufuata dawa za Binunu.
Akaondoka.
Sasa Chifu alikuwa yeye na Binunu. Chifu akiwa makini juu ya ule unga mweupe kiganjani mwake huku mara chache akiangalia runinga ili kufahamu habari kuu za siku ile kama zilivyoandikwa na magazeti.
Dakika zipatazo tano aliangalia katika runinga, dakika ya sita ilipotimu alihamishia macho yake kwa Binunu. Alimwangalia kwa sekunde zipatazo thelathini, kisha akarudisha macho yake katika runinga, macho ya Chifu hayakudumu sana katika runinga, yalirudi katika kiganja chake, alitabasamu na kuuvuta kwa pupa ule unga wote uliobaki pale kiganjani, alitoa mguno wa raha.
Baada ya kuuvuta ule unga, kwa kasi macho yake yalirudi tena kwa Binunu.
Binunu alikuwa hana hili wala lile, alikuwa hajui yuko mahali gani, hajui yuko na watu aina gani, yeye alikuwa anaongea tu kila neno lililomjia katika akili yake dumavu iliyochanganyikiwa.
Safari hii macho ya Chifu yalidumu kwa Binunu kwa takribani dakika moja, kisha yalirudi tena katika runinga. Alimkuta msomaji wa magazeti akisoma habari za michezo, yeye na habari za michezo wapi na wapi, aliachana na runinga. Sekunde tatu tu macho yake yalirudi kule yalikokuwa dakika moja iliyopita, kwa Binunu. Safari hii macho ya Chifu yalikutana na kitu cha ajabu, akili ya Chifu ilipumbazwa kwa nusu dakika. Alimwangalia kwa jicho tofauti mwanamke yule aliyechanganyikiwa. Sehemu za kati za mapaja yake zilivimba kidogo. Hisia zake zilimwambia kitu kingine kabisa.
Bila kutumia akili wala kuwaza mara mbili Chifu, alikuwa tayari amelevywa na ule unga haramu aliouvuta hivi punde, alinyanyuka taratibu kwenye sofa na kuanza kumfata Binunu pale chini.....
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Chifu Abdullah alimfikia Binunu pale chini. Kwa mara ya kwanza tangu aanze kuishi na Binunu ndio aliuona uzuri halisi wa Binunu. Na uzuri ule ulibariki moja kwa moja nia haramu ya Chifu ambayo kwa kiasi kikubwa ilichochewa na ule unga haramu aliouvuta. Unga ambao siku zote akiuvuta kitendo kinachofuata ni kufanya ngono, kama alivyofunzwa na mwalimu wake wa mapenzi na unga miaka arobaini na tatu iliyopita.
Chifu alifika hadi mahali pale alipokuwa amekaa Binunu, alisimama huku akimwangalia Binunu kwa chini, tena akimwangalia kwa jicho lenye kuonesha maana halisi ya matamanio, denda la matamanio lilimdondoka tena, na kuishia kusambaa kifuani kwake, ingawa safari hii denda lile lilimdondoka kwa dhamira tofauti na ile ya awali.
Mwanzoni madenda yalimdondoka kwa hamu ya unga haramu, unga alioanza kuuvuta akiwa na miaka kumi na saba tu na sasa akiwa na miaka sitini lakini bado aliganda katika matumizi ya unga ule. Ukimuuliza Chifu kiumbe gani ambaye hawezi kumsahau hapa duniani, asingetumia hata sekunde tatu kufikiria, harakaharaka angekujibu ni mwanamke aitwaye Wema Shayo. Mwanamke mzuri wa kichaga aliyemuingiza Chifu katika matumizi mabaya ya madawa ya kulevya.
*****
Alikuwa na umri wa miaka kumi na saba tu Chifu alipotokea kumpenda sana Wema Shayo, alimpenda kwa maana sahihi ya kuitwa upendo wa dhati. Lakini yule mwanamke hakuwa tayari kabisa kumkubalia Chifu ombi lake, sio kwamba hakumpenda Chifu la hasha alimpenda sana ila kulikuwa kuna kizuizi ambacho kilimfanya amkatae. Upande wa Chifu hakukata tamaa. Siku zote alimuelezea Wema kiasi gani alikuwa anampenda sana, na alishaandika barua mara kadhaa za mapenzi kuuelezea upendo wake wa dhati kwa Wema, lakini yule mwanamke alishikilia msimamo wake, alikataa katakata.
Siku moja usiku Chifu na Wema walikutana kama bahati mbaya katika uwanja wa Mbagala Zakheim kulikuwa na maonesho ya sinema. Chifu aliitumia vizuri siku ile kumuelezea Wema jinsi anavyompenda.
"Mimi siyo kwamba sikupendi Abdullah, ila kuna KIZUIZI, sipendi kabisa uingie katika mtego huo, hutotoka, wewe ni mwema sana kwangu, kwanini nikutese... !" Wema alisema baada ya kuyatafakari kwa kina maneno ya ushawishi toka kwa Chifu.
"Kizuizi gani hiko kinachoweza kutokutuunganisha mimi na wewe Wema, amini nakupenda kwa dhati na niko tayari kufanya chochote kile ili kukiondoa hiko kizuizi, naapa Wema " Chifu aliongea kwa kumaanisha.
"Una hakika Abdullah?" Wema aliuza kwa sauti yake ya upole. Sauti iliyopenya moja kwa moja hadi katika moyo wa Chifu.
"Sijawahi kukudanganya Wema na sitothubutu hata siku moja kukudanganya, kwanza kukudanganya wewe ni sawa na kuudanganya moyo wangu"
Wema alimwangalia Chifu kwa sura yake ya upole na kuanza kulia, Chifu alimsogeza Wema na kumuweka katikati ya kifua chake, alianza kumpangusa machozi kwa mkono wake wa kulia mwanamke yule wa ndoto zake.
"Unanipenda kweli Abdullah?" Wema aliuliza kwa sauti ya kwikwi.
"Nakupenda zaidi ya neno lenyewe nakupenda linavyomaanisha, nakupenda zaidi ya unavyofikiria, kumbuka ni miezi saba sasa imepita tangu nilivyokutamkia kwamba nakupenda, pamoja na majibu yako ya kukatisha tamaa lakini bado nimeonesha kama nakupenda, amini nakupenda kwa dhati Wema na sio kwamba nakutamani kama wafanyavyo wanaume wengine, nakupenda toka katika uvungu wa moyo wangu, wewe ni kila kitu kwangu....." Chifu aliongea kwa kumaanisha.
"Abdullah na mimi nakupenda sana, ila......" Wema hakumalizia kusema, Chifu alimkatisha.
"Wema, Wema, Wema.. ila nini sasa, nitamkie na wewe kama unanipenda kama nikupendavyo, nami nipate faraja ndani ya moyo wangu..."
"Mi..mi ..ni te..ja..." Wema alitamka maneno hayo kwa sauti ya kitetemezi.
"Eti!" Chifu alishangaa huku macho kayatoa pima.
"Na siwezi kushiriki tendo la ndoa mpaka nivute unga..." Wema aliendelea kuongea kana kwamba hakuona mshangao wa Chifu.
"......na na huyo ninayeshiriki nae vilevile awe ametumia pia..hapo ndipo hujisikia raha!" Wema alipigilia msumari wa mwisho katika jeneza la Chifu.
Kwa haraka Chifu alimuacha Wema na kusogea nyuma hatua kama mbili, alikuwa anahema juujuu. Huku akimwangalia mwanamke yule toka utosini mpaka miguuni.
Hakuamini.
Hakuamini.
Hakuamini.
Maneno yale alitamani yawe ameyasikia ndotoni.
"Au naota?" Alijiuliza mwenyewe kimoyomoyo.
Chifu aliuma kwa nguvu mdomo wake wa chini kwa meno kama ni ndoto basi aamke. Ingawa aliumia lakini hakuamka, hakuamka kwa kuwa ile haikuwa ndoto. Ilikuwa ni kweli... Wema mwanamke ampendae alikuwa mbele yake. Na kama kweli neno ampendae bado lilikuwa na maana kwake mpaka sasa, ilimpasa atumie madawa ya kulevya.
Mtihani mkubwa!
"Nimekuelewa Wema, kwa kuwa kesho sinema itakuwepo tena tukutane hapahapa uwanjani tuone tumefikia wapi, yanipasa nikafikirie kwanza"
"Sawa lakini nakuomba usimwambie mtu Abdullah, hakuna anayeijua siri hii zaidi yako, na yule aliyefanikiwa kunivutisha madawa kwa mara ya kwanza..ambaye nitakwambia siku nyingine kuhusu yeye" Wema aliongea sauti yenye kuonesha kujuta.
Abdullah aliitikia kwa kichwa.
Usiku wa siku ile Abdullah hakulala, alikuwa anawaza na kuwazua. Ukweli ni kwamba alikuwa anampenda sana Wema, sana tena sana, lakini alikuwa anachukia sana matumizi madawa ya kulevya. Je ni halali kufanya haramu ili upate ukipendacho?
Hadi asubuhi aliamka na swali hilo.
Aliamka na hakuwa na jibu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mchana wa siku ile aliona saa zinaenda kwa kasi sana, na hatimaye saa mbili usiku ilifika, muda wa sinema.
Usiku wa kufanya maamuzi magumu!
Siku hiyo Wema alienda mapema sana katika viwanja vya Mbagala Zakheim, huku akimsubiri Abdullah kwa hamu kubwa sana, ukweli ni kwamba nae alikuwa anampenda sana.
Abdullah alikuwa amejiinamia chumbani kwake akiwaza aende ama asiende. Kwenda kwenye sinema ilimaanisha kwenda kumuona mwanamke wa ndoto yake, kwenda kwenye sinema kulimaanisha kwenda kufungua ukurasa mzuri wa mapenzi na mwanamke ampendae, kwenda sinema pia ilimaanisha kuanza rasmi kutumia madawa ya kulevya. Alikuwa anampenda sana Wema, lakini alikuwa hayapendi hata kidogo madawa ya kulevya.
"Nitatumia mara moja tu, kisha nitamshawishi Wema tuache. Nampenda sana Wema, kwanini nisiuoneshe upendo wangu kwake kwa hili? Nisipoenda ataamini kuwa nilikuwa simpendi. Baadae ya kuwa mpenzi wangu nitamshawishi kwa kumwambia madhara ya madawa ya kulevya naamini atanielewa na tutaacha tu..." Baada ya kuwaza maneno hayo alinyanyuka taratibu kitandani na kuelekea katika uwanja wa sinema.
Ilikuwa ni saa tano usiku, Wema alikuwa ameshakata tamaa, akiamini ametoswa na Abdullah. Alikuwa amesimama huku akiangalia sinema lakini alikuwa haelewi kitu, ndipo alipostuka baada ya kuhisi akishikwa bega na mtu, aligeuka nyuma akiwa na ghadhabu, ghadhabu ya kutoswa.
Alipigwa na butwaa!
Alikuwa anatazamana na Chifu. Walikumbatiana kwa nguvu, kila mmoja akilia.
Wiki moja baadae Chifu alianza rasmi kutumia madawa ya kulevya.
*****
Pale ukumbini Chifu aliinama na kumshika mikono yote miwili Binunu aliinuka taratibu, huku akiendelea kuongea maneno yake yasiyoeleweka, na bila kujua sababu ya kunyanyuliwa. Sasa wote walikuwa wamesimama wima, wanatazamana!
Chifu alimsukuma Binunu katika lile sofa ambalo alikaa Peter jana yake. Binunu alidondoka mzimamzima.
Na Chifu alimsogelea.
Katika kichwa chenye akili iliyochanganyikiwa ya Binunu kuna mambo yalikuwa yanapita mithili ya sinema. Ule msukumo mbaya toka kwa Chifu ulimfanya Binunu akumbuke miaka kumi na saba iliyopita. Alikumbuka jinsi mtu mmoja alivyomsukuma mama yake mzazi kwa namna ileile na kuangukia sofani vile vile kama alivyoanguka yeye leo. Alikuwa na miaka tisa tu kipindi hiko, lakini mambo yaliyotokea siku hiyo yalijirudia kichwani mwake mithili ya sinema leo, tena akiwa amechanganyikiwa.
Chifu alimsogelea Binunu na kulinyanyua kwa juu gauni la pinki alilolivaa Binunu.
Jinsi gauni lile lilivyonyanyuliwa Binunu alikumbuka jinsi gauni la mama yake mzazi lilivyonyanyuliwa kwa namna ileile miaka kumi na saba iliyopita huko Kilwa Masoko. Sinema iliyopo kichwani mwake ilimuonesha kuwa gauni la mama yake lilivyofunuliwa vile aliona jinsi baba yake mzazi alivyotoa ukelele mkali wa ghadhabu kuashiria kukerwa na kitendo kile alichokuwa anafanyiwa mkewe kipenzi. Laiti Chifu angejua vitu alivyokuwa anaviona Binunu akilini mwake, ni bora angemwachia tu.....
Sasa Chifu aliishika nguo ya ndani ya Binunu na kuanza kuivua kwa mtindo wa kuivuta kwa nguvu....
Kina Malolo walifika katika kisiwa cha Pemba. Kila mmoja akiwa na ile picha ya mvuvi mkononi mwake.
Wale walikuwa ni watu makini, na walijua sehemu sahihi ya kwenda kumsaka yule mvuvi, walienda katika fukwe ya bahari. Na kutokana na umaarufu wa mtu waliyekuwa wanamtafuta hawakupata shida kabisa kumpata mvuvi aliyekuwepo katika picha ile. Mtu wa watatu tu kumuuliza aliwaambia kila kitu kuhusu mvuvi huyo, tena na kuwasindikiza hadi katika kibanda cha yule mvuvi. Ndani ya mioyo ya kina Malkia ilikuwa ni furaha isiyo na kifani, kazi yao ilitokea kuwa rahisi sana...walikuwa wanaamini ndani ya robo saa mkanda utakuwa tena mikononi mwao, iwe kistaharabu ama kwa nguvu. Wakichoamini wao huyo jamaa alipewa mkanda na yule msichana baada ya kutokea ile ajari mbaya ya meli ya MV Donors, kumbe wala haikuwa hivyo...
Ayoub Mbembati alikuwa ni mvuvi aliyejipatia umaarufu muda mfupi sana katika kisiwa cha Pemba. Hii ilitokana na hekima, busara, upole, uwajibikaji na uchapakazi. Uvuvi ilikuwa ni kazi yake kuu tangu alivyohamia katika kisiwa cha Pemba miaka kadhaa iliyopita...uvuvi ilikuwa ni kazi aliyoirithi toka kwa baba yake mzazi, mzee Mbembati. Na kutokana na makuu aliyoyapitia Ayoub ndomana alitokea kuwa na sifa hizo.
Ayoub alikuwa mvuvi, lakini mvuvi duni akiyetumia zana duni. Na bado maisha yake yaliendelea kuwa duni. Baba yake mzazi alifariki akiwa duni pia, tena alifariki kifo kibaya sana mbele ya Ayoub, ni Ayoub pekee ndiye aliyeijua sababu ya kifo cha baba yake. Kifo kilichoacha vitendawili kadhaa mpaka leo. Na sababu ya kifo hiko ambayo ilikuwa ndani ya kifua chake ndiyo iliyomfanya ahame kimyakimya katika mji wa Kilwa Masoko na kuibukia katika kisiwa cha Pemba, mzee Mbembati alifariki kifo kibaya sana akimfata mkewe mwezi mmoja tu baada ya kufariki kwa ugonjwa wa malaria.
Ayoub Mbembati, kitu pekee alichorithi toka kwa baba yake mzazi ni mkanda, mkanda ambao ulisababisha kifo cha kikatili cha baba yake, mkanda ambao ndio uliomfanya ahame bila kupenda katika mji aupendao na kwenda kuishi ugenini, lakini cha kusikitisha mkanda haukudumu sana mikononi mwake.....yaliyotokea hadi leo bado yalikuwa bado katika kichwa chake.
Shirika la W.W.F lilipeleka mradi wa kutunza mazingira ya bahari na maliasili za bahari Pemba, na mikoa mingi yenye bahari na maziwa katika nchi ya Tanzania. Mradi ulioleta matumaini kwa wakazi wa jamii za kivuvi, ikiwemo wakazi wa kisiwa cha Pemba. Wananchi walitakiwa kutunza na kulinda mali za bahari, hapo ndipo vilipoanzishwa vikundi vilivyojulikana kama Beach Management Unit ( BMU) kwa ajili ya kufanya doria baharini na nchikavu kwa lengo la kupiga vita uvuvi haramu, kulinda bahari na mali zake, na Ayoub Mbembati ndipo alipochaguliwa kuwa mwenyekiti wa BMU...Na cheo hiko ndicho kilichomfanya aonekane kwenye taarifa ya habari ya TBC akielezea umuhimu wa kuhifadhi bahari, na kuonwa na Binunu Issa.
*****CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kule Kisarawe hali ilikuwa mbaya sana kwa Binunu. Chifu shetani alikuwa kamkalia kohoni. Alikuwa anataka kumbaka Binunu. Sasa nguo ya ndani ya Binunu ilikuwa katikati ya mapaja yake.
Kichwani sinema ya ajabu ya Binunu iliendelea, alikumbuka jinsi siku ambayo mama yake alikuwa anafanyiwa kitendo kama kile. Sinema ilimuonesha kwamba nguo ya ndani ya mama yake mzazi ilipofika maeneo yale baba yake alikurupuka kwa hasira. Lakini hakufika akikotaka kwenda. Alipigwa kwa nguvu na kiwiko cha bunduki katika paji la uso wake.
Baba yake damu zilimbubujika!
Damu za kwenye sinema zilimkumbusha kitu kipya kabisa leo...
Naam...Binunu sasa alikumbuka !
Sasa haikuwa sinema, ilikuwa dhahiri shahri, Binunu alikumbuka mtu aliyekuwa anamfanyia vile mama yake alivuta vitu fulani kabla hajamfanyia kile kitendo kibaya mama yake mzazi, alivuta kama alivyovuta huyu wa leo. Tena aina ya vikopo walivyotoa hivyo vitu alivyokuwa anavuta huyu aliye mbele yake leo, na aliyembaka mama yake miaka kadhaa iliyopita vilikuwa vinafanana. Vikopo vyeusi vyenye rangi nyeupe, vikopo vilivyotengeneza taswira ya mnyama Pundamilia.
Na taulo la Chifu lilianza kufunguka...
Chifu alikuwa anaendeshwa na hisia zilizotokana na madawa ya kulevya zaidi badala ya akili zake za asili. Madawa ambayo siku zote humshauri kama yanamvyomshauri leo, baada ya kuvuta ni ngono. Kama ukipata nafasi ya kumuuliza Chifu faida ya unga ule angekwambia moja tu, unga ulimfanya ampate Wema Shayo, mwanamke aliyempenda zaidi hapa Duniani, baada ya hapo unga ulimsukumia Chifu katika engo mbaya sana, ulimtoa kwa kasi sana toka kuwa binadamu wa kawaida hadi kuwa mnyama. Na yote hayo yalisababishwa na pesa, ilimpasa apate pesa ili aweze kununua unga, ambao sasa ulikuwa umeweka kambi ya kudumu katika mishipa ya damu yake. Hapo ndipo alipoanza kuwa mwizi, tabia mbaya ambayo hakuwa nayo kabisa hapo kabla, alianza kuiba vitu vidogovidogo vya nyumbani kwao, aliporidhika alihamia vitu vikubwa, aliiba runinga, deki na friji, na kwenda kuuza kwa bei rahisi ili apate pesa ya kwenda kununulia unga. Maneno ya wazazi wake hayakusaidia kitu, ilikuwa ni kama wanampigia mbuzi gitaa. Alivyomaliza vitu nyumbani kwao alihamia katika nyumba za jirani, na hatimaye aliiba popote pale alipoona cha kuiba. Nguvu za madawa ya kulevya zilimpeleka vibaya, na hapo ndipo alipopanda ngazi rasmi, toka mwizi wa kawaida mpaka jambazi, kumbuka alikuwa na miaka kumi na nane tu hapo. Baada ya kupanda ngazi ndipo alipopata wazo jipya, wazo ambalo lilibarikiwa na mpenzi wake, Wema Shayo. Alizamia meli na kwenda Afrika ya kusini...eti kutafuta maisha. Huko ndiko Chifu alikobadilika hasa.
Kwa mara ya kwanza huko ndiko aliua mtu, Mzulu aliyemfanyisha kazi kwa ujira wa kupewa madawa ya kulevya. Baada ya Chifu kumaliza ile kazi, Mzulu alijifanya mjuaji kwa kudhani anaweza kumdhulumu mtoto yule...kumbe Chifu alikuwa mdogo kwa umri lakini mkubwa kwa matendo, hasa matendo ya kikatili. Kilichofuatia hapo Mungu pekee ndio anajua, lakini kwa alichomfanyia yule Mzulu kilimpeleka kaburini na yeye kuhukumiwa kifungo cha maisha jela akiwa mtoto mdogo sana. Jela ikamfundisha shurba Chifu, ukatili, umajinuni na ubabe, pamoja na umri wake mdogo lakini yeye nd'o alikuwa mwamba katika gereza lililokuwepo katika mji wa Soweto.
Na huko ndipo lilipoibuka jina la Chifu, Chifu sasa akawa Chifu wa Gereza la Soweto, na jina lake la awali la Abdullah kufutika kabisa masikioni mwake.
Na baada ya miaka miwili ya jela ndipo mfumo wa kubadilishana wafungwa kati ya Tanzania na Afrika Kusini ulianzishwa, na Chifu alikuwa mmoja wa wafungwa wa mwanzoni waliofaidika na mfumo huo hasa kutokana na umri wake kuwa mdogo, alirudishwa jijini Dar es salaam, alifikia katika gereza la Ukonga.
Hapo Chifu alikuwa na miaka ishirini....
Na sasa Chifu alikuwa yu tayari kumuingilia Binunu. Alimtanua miguu yake kwa nguvu pale chini na kuingia kwa kati.....
Sinema ya kutisha iliyopo kichwani mwa Binunu ilimkumbusha kitu, siku mama yake alivyofanyiwa kitendo kama kile. Siku mama yake alivyoingiliwa kwa kati namna ile alifanya kitu. Naye alifanya kitu hichohicho ambacho alichofanya mama yake miaka kumi na saba iliyopita. Naye aliamua kufanya kitendo hikohiko. Kitendo kama kilichofanywa na mama yake mzazi miaka kumi na saba iliyopita. Binunu alikumbuka vizuri sana kuwa mama yake alimng'ata shingoni upande wa kulia yule jamaa aliyekuwa amemuingilia kati kwa lengo la kumbaka. Naye alidhamiria kufanya hivyohivyo, kama alivyokuwa anaoneshwa katika sinema yake kichwani. Alimwangalia yule jamaa upande wa kulia shingoni kwa lengo la kumng'ata. Upande uleule wa shingo aliong'ata mama yake miaka kumi na saba iliyopita, jamaa alikuwa na kovu!
E bwana wee!
Binunu akili zake zote zilirudi.
"Wewe ndiye uliyembaka mama yangu" Binunu alisema kwa sauti nzito yenye kukwaruza. Chifu aliduwaa...ilikuwa kama ameona mdudu wa kutisha sana, na yeye hakuwa na uwezo wa kujitetea wala kujiokoa....ilikuwa kama mgonjwa ambaye amepigwa sindano ya ganzi lakini akishuhudia jinsi kidonda chake kibichi kikivyoshonwa huku yeye akiwa hasikii maumivu..Chifu hakuamini kabisa kama maneno yale yalikuwa yametoka kinywani mwa Binunu.
"Kwanini mlimuua baba yangu mzazi?" Binunu alibadilisha aina ya sentensi na maana ya sentensi, mwanzo ilikuwa kauli taarifa, sasa ilikuwa katika muundo wa swali. Mwanzoni alimuulizia mama yake, na sasa alimuulizia baba yake. Sasa Chifu alisimama wima, akiwa uchi wa mnyama. Akimwangalia Binunu kwa woga na mashaka. Raha iliyokuwa ikiletwa na madawa ya kulevya ilikata ghafla. Raha ambayo aliyoanza kuipata mara tu pale alipoanzisha uhusiano na Wema Shayo na hadi leo alikuwa anaipata kila avutapo unga. Raha ambayo alihakikisha inamfikia hadi katika gereza la Ukonga kwa njia yoyote ile. Na baada ya kuaminika na mtu aliyekuwa anaingiza kwa siri raha ile gerezani yeye ndiye aliyepata bahati ya kuwa msambazaji, kazi aliyoifanya kwa ufanisi mkubwa sana. Hadi wauzaji wa madawa wakubwa walipotamani kumtoa gerezani ili atoe huduma ya usambazaji nje ya gereza. Haikuwa kazi ngumu kutoka gerezani kama unavyoweza kufikiria. MONEY TALKS! na Chifu alirejea tena uraiani baada ya kukaa gerezani kwa muda wa miaka mitano.
Na hapo alikuwa na miaka ishirini na mitano tu.
Alivyotoka nje ya gereza alikuta kila kitu kimebadilika, wazazi wake wapendwa walikuwa wamehama walipokuwa wanakaa na nyumba ilikuwa imeuzwa. Wema Shayo, mwanamke aliyekuwa anampenda sana, alikuwa ameshafariki miaka mitatu iliyopita baada kupigwa na raia wenye hasira kali baada ya kukamatwa alipoenda kuiba katika duka la Mhindi mmoja Kariakoo. Hapo ndipo Chifu alipopata wazazi wapya, wazazi wake wapya walikuwa madawa ya kulevya, na Chifu alipata mpenzi mpya, mpenzi wake mpya alikuwa madawa ya kulevya. Hakujishughulisha kuwatafuta wazazi wake kama asivyojishughulisha kutafuta mpenzi mpya. Aliendelea na kazi yake mpya aipendayo ya kusambaza madawa ya kulevya katika mikoa yote ya Tanzania. Huku Chifu akiwa hamjui hata 'Boss' wa biashara hiyo. Lakini aliifanya kwa moyo wake wote na ufanisi mkubwa kama ilivyo ada yake. Na hapo ndipo Chifu alianza kuwa Chifu kweli.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ulimbaka mama yangu mbele yangu, mbele ya baba yangu, Mlimuuwa baba yangu mbele ya macho yangu, mbele ya macho ya mama....mlimpiga risasi kikatili sana, mama nimpendae mlimbaka kisha mlimuuwa kwa kumkaba shingoni, tena ni wewe ndiye ulimkaba..na kumuuwa mama yangu mpendwa bila huruma yoyote, niambie ni kosa gani kubwa walilowafanyia wazazi wangu? Hadi mkawafanyia vitendo vya kikatili namna ile? Baba alikuwa mwalimu mwema kwa wanafunzi wake na wananchi wote, alikuwa mshauri mwema kwa kila mtu, alikuwa tumaini jema, mtu asiye na ugomvi na mtu yeyote yule, mama alikuwa mama mwema asiyejua kabisa kugombana na watu, alikuwa mithili ya baba, labda ndomana walipendana na kuoana, walikuwa wanafanana tabia, na wahenga waliwahi sema " ndege wanaofanana huruka pamoja', kwanini sasa mliwafanyia vile ndege wale wazuri wafananao kwa tabia njema???" Binunu alikuwa anauliza maswali huku akinyanyuka sofani kumfuata Chifu.
"Hiyo tabia uiitayo njema ndiyo ilimponza marehemu baba yako..." Chifu aliongea kizembe bila kujitambua.
"Amma!" Unasemaje bwege wewe?" Binunu alimaka kwa hasira huku akiendelea kumsogelea Chifu akiwa kafura kwa hasira. Ama kwa lugha nyepesi tunaweza sema hatari ilikuwa inamsogelea Chifu. Tena hatari kubwa sana!
Binunu alikuwa anacheka kwa dharau huku akimsogelea Chifu. Chifu aliendelea kurudi nyuma taratibu. Huku moyo ukimdunda kwa kasi kubwa sana!
"Yaani mlimuuwa baba yangu kikatili namna ile, yaani ulimbaka mama yangu kisha ukamuua kinyama sana, eti leo unaniambia kizembe tu....ni tabia njema yake ndio sababu ya kumuua baba, nd'o sababu ya kumuua na kumbaka mama, ulisikia wapi tabia njema ikaleta matokeo mabaya tena ya kusikitisha namna ile, ngoja nikwambie kitu mzee.....tabia njema siku zote huleta matokeo mema, na tabia mbaya ndio huleta matokeo mabaya, iko hivyo.... matokeo mabaya kama yatakayokukuta wewe leo hii na hii yote ni kutokana na tabia yako mbaya ya kuuwa watu wenye tabia njema.." Binunu alisema kwa jazba sasa, wakiwa wamekaribiana kabisa na Chifu.
Sebuleni sasa palikuwa hapatoshi, Binunu alikuwa amerudiwa na akili zake zote zilizokuwa zimeenda kusikojulikana, tena na akili za ziada zilikuwa zimerudi. Amerejewa na kumbukumbu zake zilizopotea tangu siku ile ilipotokea ajari ya kupangwa ya MV donors. Kitu ambacho Chifu labda alikuwa hajui. Binunu sasa hakuwa Binunu yule aliyekuwa anamfahamu kabla...
Kipindi kile akiwa mtoto dhaifu aliyekuwa haelewi chochote wakati wazazi wake wanauliwa. Kwa sasa Binunu alikuwa amepitia mengi sana tangu siku ile ya mauaji ya wazazi wake, miaka kumi na saba iliyopita. Vitu vilivyomjenga na kuwa mwanamke hatari sana. Kuuwa kwake ilikuwa ni mchezo rahisi sana kuliko mchezo wowote rahisi unaofahamu wewe. Binunu alikulia mtaani akiwa na miaka kumi na moja tu. Baada ya miaka miwili ya mateso toka kwa ndugu wa wazazi wake. Alipoingia mtaani, mtaa ulimpokea na kumfunza mambo mengi sana. Mtaa ukamfundisha njia moja tu kama bado anataka kuendelea kuishi, kutumia nguvu ili kupata kila kitu. Naye alilielewa vizuri sana somo hilo, alitumia nguvu ili ale, alitumia nguvu ili avae, alitumia nguvu ili alale, alitumia nguvu ili kujitetea kwa lolote lile baya kwake, kubakwa na kadhalika...
Mtaa ukamtoa kwa kasi toka kuwa kiumbe dhaifu wa kike na kumpeleka kuwa kiumbe mkorofi sana. Asiyeogopa mtu yeyote yule duniani. Kumbuka alikuwa na umri wa miaka kumi na moja tu, na hapo ndipo alipobatizwa jina baya la Chokoraa. Kutokana na ubabe wake uliokubuhu Binunu aliogopwa na kila mtu kuanzia Tandika sokoni na hatimaye akawa homa ya jiji Dar es salaam nzima, dunia ya wababe ilitambua kwamba kuna mbabe mmoja wa kike aitwaye Binunu. Wabeba mzigo, wahuni, mateja walitambua Binunu ni nani, mwanamke mwenye umbo dogo lakini mwenye nguvu ya mapambano, huku mwalimu wake wa medani hiyo ukiwa ni mtaa.
Baada ya miaka saba kupita....Binunu alihama katika ubabe wa mtaani na wizi mdogomdogo na kuingia kwenye ujambazi. Akawa jambazi, Binunu alikuwa jambazi kweli. Akaanza kutumika katika matukio mbalimbali makubwa ya kijambazi, kuvamia benki na kupora pesa, kuvamia vituo vya mafuta na supermarket mote kutafuta pesa. Na mara zote alifanikiwa, alifanikiwa kuiba na kuua! Fani yake mpya ya ujambazi ikamfundisha kitu kipya katika medani, kutumia akili, sasa Binunu akawa anatumia nguvu alizozipata mtaani na akili alizozipata katika ujambazi. Kwa kifupi Binunu alikuwa ni muuaji wa kukodiwa aliyekamilika, anauwa kwa nguvu, anaiba kwa akili na kisha baadae kulipwa pesa. Aliishi hivyo toka alipo timu miaka kumi na nane mpaka miezi mitatu iliyopita alipofatwa na Martin kwa ajili ya operesheni aliyoahidiwa pesa nyingi sana, Operesheni Mkanda wa Siri. Bila kujua operesheni hii sio ilikuwa ya kukodiwa tu na kuvuna pesa kama zilivyo operesheni zingine. Bila kujua ‘OMS’ Ilikuwa inamhusu yeye kwa asilimia miamoja. Mkanda wa siri ukiotafutwa ndio ulikuwa sababu ya kuondoa maisha ya wazazi wake hapa duniani..... Bila kujua Martin Hisia alimuingiza Binunu katika Operesheni iliyompelekea Binunu maamuzi kuwa ni yake kulipa kisasi cha vifo vya wazazi wake ama kujua sababu za vifo vya wazazi wake pamoja na wauaji, na kwasasa chaguo lilikuwa ni lake, maana mbele yake alikuwa na mmoja wa watu waliowauwa wazazi wake. Na ushahidi ulionesha hivyo, na kwa bahati nzuri mwenyewe kakili kwa mdomo wake. Binunu aliingia kwenye operesheni inayomhusu lakini bila kujua, aliingia kwa miguu yake yote miwili.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alitoka Dar es salaam mwezi mmija na wiki moja iliyopita na kwenda katika visiwa vya Zanzibar, ili kuungana na Richard katika ‘OMS;. Binunu hakuwa amesomea ujasusi darasani kama ilivyo kwa Brown, lakini maisha magumu aliyopitia mtaani yalimfanya kuwa zaidi ya jasusi. Na kufikia kiwango cha kukodiwa katika ‘OMS’. Maisha yote magumu ya mtaani unayoyajua wewe Binunu alikuwa ameshayapitia, na kufuzu kwa kiwango cha juu, mitihani yote wanayopitia watoto wa kike wa mitaani Binunu aliyapitia na yote alifuzu kwa kiwango cha juu. Mtaa ndio uliomfundisha kuuwa ili kutetea haki yake, mtaa ulimfundisha kuuwa ili kutetea heshima yake. Katika maisha yake ya mtaani aliua mtu kwa mara ya kwanza akiwa na miaka kumi na sita tu. Alimuua jamaa akiyeitwa Dula Mbabe.
ITAENDELEA
Subscribe to:
Posts (Atom)