Search This Blog

Sunday, 22 May 2022

HEKA HEKA - 4

 







    Simulizi : Heka Heka

    Sehemu Ya Nne (4)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku nyingine wakiwa katika mijadala yao kama hii Eve alileta mambo mapya.

    “Banzi hivi una umri gani rafiki yangu?

    “Duuuh, leo naona una mada nyingine mpya. Mwezi wa kenda natimiza miaka 39!

    “Hongera sana kwa umri na unaonekana unatunza mwili wako vizuri!

    “Asante, japo nadhani nastahili pole au kupewa tahadhari”

    “Kwa nini Banzi?

    “Umri wangu na mambo yangu haviendani?

    “Sijakuelewa”

    “Jana nilikuwa naongea na mama yangu ambaye yuko taabani hospitali, alikuwa analalamikia kitendo cha mimi kutokuwa na mke wala watoto. Anasema naishi kama ndege”

    “Lakini hilo si suala la kukulaumu sana, kwani inawezekana unakamilisha mipango yako ili ufanye hivyo! Eve alijibu kwa kusisitiza

    “Ingekuwa hivyo nadhani mama asingekuwa ananisema, lakini naweza sema miye ni kama mtu ambaye naishi tu na kutimiza malengo ya watu wengine kama John Kificho” Hapo ndipo mjadala mkali ukazuka wa jinsi watu wengine wanyotumiwa na taaluma za kufikisha malengo ya watu wengine ili hali wao wakiachwa kuwa wahanga wa gharama za mafanikio ya hao watu. Ni mjadala huu ndo uliowafikisha kugundua kuwa Eve na Banzi walikuwa na shida mbili tofauti. Wakati Banzi akiwa na shida ya fedha za kujenga maisha yake, Eve yeye hakuwa na shida ya fedha bali mpenzi. Walivyojiangalia, hakuna ambaye angeweza kuwa jibu la mwenzie, ila jambo moja walikubaliana baada ya mjadala mrefu, nalo ni kuwa kila mtu ana ufunguo wa kuelekea kutatua shida ya mwenzie.

    Eve alikuwa na jukumu la kumpa Banzi wazo la kumsaidia kupiga bingo, ili hali Banzi alikuwa na kazi ya kutumia ukomandoo wake kufanikiwa kutekeleza wazo la Eve na kumsaidia Eve.



    Eve alikuwa na shida ya kumpata na kummiliki Jacob Matata ili hali comandoo Banzi alitaka kutumia hali iliyopo kujinufaisha kwa kupata fedha nyingi.

    “Sikiliza Banzi, mzee Harken Kalm anamtaka Jacob na Regina kwa udi na uvumba, John Kificho anakutegemea katika ulinzi na kutekeleza mipango yake ya siri. John Kificho anakulipa fedha kidogo sana tofauti na kazi unayomfanyia. Fanya kitu! Ila hakikisha nampata Jacob Matata akiwa hai”

    “Huo ni mpango mgumu sana ila naona unamanufaa, ngoja nijaribu kubuni vitendo vyake nione utafanyaje kazi” Banzi alisema huku akikuna kichwa kwa tafakari.



    *** Kaazi kwel-kwel!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Banzi ni Komandoo kama alivyomwambi Eve, si Komandoo wa kujiita ni baliwa kutunukiwa baada ya kufuzu mafunzo ya juu kabisa yanayomfanya mtu kuitwa jina hilo. Amewahi kufanya kazi nyingi za hatari, japo nyingi zikiwa ni nje ya nchi kama vile Holland, Ugiriki na Cambodia. Kwa sasa hakuna kitu anahitaji zaidi ya pesa, ndo maana serikali ilipomtaka baada ya kuhitimu mafunzo alikataa na kusema atakuwa anafanya kazi binafsi.



    Ili kutekeleza mawazo aliyokuwa amepewa na Eve, simu ya kwanza kupiga ilielekea ofisini kwa mzee Harken Kalm, ikimtaka pesa ilia pate taarifa za walipo Jacob Matata na Regina. Ni simu hiyo ndo ilimfanya mzee Harken Kalm atume vijana wake watafute wapi alipo mtu aliyepiga hiyo simu bila mafanikio.



    Simu ya pili kupiga iliingia moja kwa moja ofisini kwa mkurugenzi wa ofisi fukuzi, Bi. Anita.

    “Ennhe niambie habari uliyonayo? Bi Anita alimuuliza Banzi

    “Ni kuhusu rafiki yangu Jacob Matata, najua alipo. Kama hutajari napenda kuwa kwenye oparesheni itakayokwenda kumchukua”

    “Banzi! Umesahau kanuni namba nne?

    “Samahani mama si unajua uzee. Kwa hiyo?

    “Cover 9” Alijibu Bi. Anita

    “Assurance? Banzi alisema

    “asilimia mia!

    Jibu la mwisho ndo lilimfanya Komandoo Banzi aende posta saa nane na dakika saba usiku ili kuangalia sanduku lake la barua kwa maelekezo toka ofisi fukuzi. Na kweli alikuta karatasi yenye mistari minne tu. “BANZI FANYA MNADA KWA AJILI YA KUFILISI MALI YA MDAIWA JACOB, BANKI ITALIPA SHS 716”. Comandoo Banzi alikunja hiyo karatasi na kuiweka mfukoni. Akaaangaza angaza kama anyetafuta sanduku jingine la barua, alipoona namba 716 alifungua kwa kutumia funguo zake malaya na kuweka karatasi nyingine tofauti na ile aliyokuwa amechukua toka sanduku lake.



    Aliondoka haraka eneo hilo la kuchukulia barua na kurudi alipokuwa amaeegesha gari lake. Aliingia ndani ya gari na kutia moto, lakini gari haikuwaka. Wakati anataka kutafuta nini kimetokea alipigwa na kitu kama nyundo ya kilo tano kichwani akaapoteza fahamu papo hapo.



    ********



    Mfumo wa usalama aliokuwa ameujenga John Kificho, haukuwa wa kumwamini mtu yeyote katika wafanyakazi wake. Kwa hivyo haikumchukua muda mrefu kugundua kuwa urafiki wa Eve na Banzi haukuwa na lengo zuri kwake. Hivyo akaweka utaratibu wa kufuatilia kila walilokuwa wakifanya hawa watu wawili. Baadaye akawa amepata taarifa kamili juu ya mpango wa Banzi kujitafutia pesa kupitia mateka wake wawili – Jacob Matata na Regina.



    Mara moja John Kificho akaagiza kukamatwa kwa Banzi na Eve.

    Banzi alipozinduka alijikuta akiwa kwenye chumba amefungwa pamoja na Eve na Jacob Matata. Kazi! Eve alimwangalia Banzi kwa jicho la kukata tamaa.



    Hali ya Jacob Matata ilikuwa imeshaanza kutengemaa japo bado alikuwa amefungwa kama siku zote. Kwa masaa kadhaa yaliyopita amekuwa akipewa chakula. Hii ilikuwa ni jitihada za John Kificho kumteka Regina kwa kumpendezesha.

    Jacob hakuelewa kilichotokea kwa Banzi na Eve, ila alijua fika kuwa kuna kosa hawa watu watakuwa wamelifanya. Nini? Alijiuliza.



    *******



    Kama ilivyokuwa awali, Regina hakuwa anaruhusiwa kuingia peke yake ndani ya chumba walichokuwa mateka. Aliruhusiwa kuwa sehemu baadhi tu za jumba hilo. Kwa nyakati mbali mbali alifanikiwa kukutana na wafanya kazi wa jumba hilo na kuongea nao, japokuwa hakuwa anafurahia maongezi nao maana walikuwa wanamwogopa sana maana John alimtambulisha kama malkia wao na mar azote aliwaonya kuwa hatasita kuua mtu yeyote atakaeonekana kukosea mbele ya Regina.



    “Sara “ Regina alimwita nesi mmoja aliyekuwa amesimama kama anayesubiri kitu

    “unangoja nini hapo” Regina aliuliza

    “Hapana dada, nilitaka kutupa hii” alisema huku akimwonesha kikaratasi kisha akakitupa kwenye chombo cha kuwekea taka hapo mlangoni. Kwa sababu asizozijua, Regina alipata shauku ya kujua ilikuwa kitu gani. Basi alipoondoka yule nesi, alitembea hadi kilipo kile chombo cha taka na kuchukua kilichotupwa. Ilikuwa ni kijikarastasi kidogo, alikifungua kujua ni nini, ndipo akakutana nay ale maandishi “BANZI FANYA MNADA KWA AJILI YA KUFILISI MALI YA MDAIWA JACOB, BANKI ITALIPA SHS 716”. Moyo ulimripuka kuona jina la Banzi na Jacob yako katika karatasi moja, na ilionyesha kama ni ujumbe ambao hata hivyo hakujua maana yake. Shahuku ya kutaka kujua maana ya ujumbe huo ilimjaa. Akakificha kile kikarata.



    Siku hiyo alitafuta sana ilia pate nafasi ya kwenda kuwaona mateka, na kweli alifanikiwa kuingia akiwa na mlinzi mmoja. Shahuku yake ilikuwa kujua maana ya ile karatasi, hivyo alitafuta namna hadi akaionyesha mbele ya macho ya Jacob Matata kwa kuiweka mgongoni wakati yeye anaongea na Banzi.



    Jacob Matata alipoisoma hiyo kararatasi mara moja akaelewa ilimaanisha nini. Akajua pia kuwa Banzi alikuwa na mawasiliano na ofisi fukuzi. Regina aligeuka kumwangalia Jacob akijua fika kuwa atakuwa tayari ameshasoma ile karatasi. Ndiyo! Jacob alionyesha kila dalili kuwa alikuwa amesoma ila pia alikuwa naonyesha ishara kwa macho. Regina aliangalia kwenye mikono ya Jacob ambako ndiyo mamcho yalikuwa yakielekea kama kumtaka Regina aangalie. Akaona Jacob anamwonyesha ishara ya kutaka kalamu na karatasi. Kumbuka wakati huu Jacob hakuwa anaweza kusikia wa kuona kutokana na kufungwa mdomo na kuwekewa vifaa vya kumzuia kusikia masikioni. Regina alielewa, kwa usiri mkubwa alichukua kalamu na kile kijikaratasi akakiweka kwanye kiganja cha Jacob Matata. Kisha akaondoka chumbani humo.



    Siku iliyofuata, Regina alikuwa na hamu kama nini ya kwenda chumba cha mateka, alijua fika kuwa kutakuwa na ujumbe toka kwa Jacob – kwenye karatasi. Hivyo alitafuna sana sababu na wakati wa kuingia ambapo hakukuwa na watu wengi. Aliingia, na kama alivyo tarajia Jacob alimpa karatasi ile ndogo ambayo upande wa pili iliandikwa “REGINA PELEKA POSTA 716. HILI SHIMO LINA MADINI WEKA MCHIMBAJI. JACOB” Regina alielewa kuwa alitakiwa kwenda posta kupeleka ile karatasi. Hakujua atafanikiwaje maana popote alipokwenda kulikuwa na ulinzi mkali sana.



    Alitafuta safari ya kwenda mjini kufanya manunuzi, alikwenda duka moja akanunua nguo, chini ya ulinzi mkali tena akiwa na John Kificho, lakini alifanikiwa kumwomba mhudumu mmoja ampelekee bahasha yake posta. Wakaondoka.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku nyingine alivyoenda kuwaona mateka, Jacob alionyesha ishara ya kutaka kalamu na karatasi. Akafanya kama alivyofanya wakati uliopita. Mara hii tena akaenda kwenye lile duka languo kwa kisingizio kuwa anarudisha baadhi ya nguo ambazo hazikuwa zimemkaa vizuri. Akamwomba yule mtu ampeleeke tena, posta haikuwa mbali toka lilipokuwa duka, hivyo huyo kijana akaenda. Alinunua stempu na kutumbukiza barua.Ila wakati anatumbukiza barua kuna mtu alimuhoji kuwa nani alimtuma barua, hakujali alijibu haraka. Akaondoka kurudi dukani haraka, kwa jinsi ilivyo karibu alifanikiwa kuwakuta Regina na timu yake bado wapo. Kijana hakuwa peke yake wakati anarudi, tayari timu ya ofisi fukuzi ilikuwa pamoja naye.



    ******



    Karatasi ye ujumbe “REGINA PELEKA POSTA 716. HILI SHIMO LINA MADINI WEKA MCHIMBAJI. JACOB” ilifika ofisi fukuzi.

    Mara moja Bi. Anita aliweka wachimbaji kwenye mgodi. Alituma vijana wake posta ambayo barua hiyo iliwekwa. Kijana mmoja aliwekwa duka la kununulia stempu, mwingine aliwekwa kwenye masanduku ya kuchukulia barua na mwingine kaunta ya posta na mwingine sehemu ya kupumzikia. Ni yule kijana aliyekuwa kwenye duka la kunulia stempu ndo alifanikiwa kuona barua iliyokuwa imekusudiwa kutumwa kwao wakati muuza duka la nguo alipokuwa ananunua stempu.



    Mawasiliano yalifanyika na kwa vile muuza duka hakuwa makini alipoulizwa kuhusu hiyo barua litoa jibu ambalo liliwasaidia mashushu hao kujua mambo yameiva.

    Baada ya masaa kadhaa, nyumba ya John Kificho ilikuwa chini ya uchunguzi na ulinzi mkali wa vijana wa ofisi fukuzi, uchunguzi huo na ulinzi ulifanyika kwa siri kubwa kiasi kuwa hakuna aliyehisi shida.



    “mpaka sasa tuna taarifa na kila kitu tulichokuwa tunakihitaji ili kuendesha operesheni kwenye nyumba ambayo tunaamini Jacob ameshikwa mateka”



    *******



    Ni duka kubwa la kuuza Paka walio hai kati kati ya kariakoo. Duka hili linatazamana na kituo cha mafuta kiitwacho Big Bon. Muuzaji wa paka hao bwana Mushi alikuwa ameshauza idadi ya kutosha hadi jioni hiyo ilipokuwa inaingia. Wakati akiwa amechukua funguo kwa ajili ya kuanza kufunga duka la ili asimamie zoezi la kuwalisha Paka ambao wanangoja kuuzwa, mara akaingia mteja. Mteja huyo alipoingia hakuongea kitu kwa sekunde kadhaa bali alibaki akiwa amemwangalia tu mwenyeji wake, muuzaji. Ghafula bwana Mushi akajikuta nafsi yake inakinaika na uwepo wa mteja huyu. Akataka kumfukuza lakini maadili ya biashara hayakumruhusu kufanya hivyo. Ikabidi aendelee kusubiri mteja wake aongee

    Mambo mawili yalimfanya Mushi kutopenda ujio wa mteja huyo saa hizo. Kwanza ni jinsi mgeni huyo alivyokuwa akitazama, macho yake yalikuwa kama ya Paka mwenye kichaa aliyekosa chakula kwa wiki nzima. Pili hakuingia kirafiki kama wateja wengine bali alikuwa na harufu ya shari. Mteja akatabasamu na kujisogeza jirani na meza ya mbele ya kuuzia dukani hapo. Mushi alichefuka na tabasamu hilo. Mteja alinyanyua mikono yake na kuimwaga kaunta, mushi alipoiangalia salio la uvumilivu wake kuhusiana na mteja huyu lilikwisha. Maana mikono hiyo ilikuwa kama mikono ambayo haijaoshwa ya mtu aliyeshinda kwenye kazi ya mtu aliyeshinda kwenye kuchanganya zege.

    "Nikusaidie nini? Mushi alimudu kutamka

    'Nataka Paka' sauti ilitoka. Mushi alikereka na kutiwa hofu na hiyo sauti.

    'aina gani, wangapi?

    'wale wenye asili ya Amazoni, dume, mkubwa' Sauti ilikoroma tena.

    'Hao ni dola Sabini na tano, na una bahati amebaki huyo mmoja tu' Mushi alisema huku akijilazimisha kutabasamu.

    'Bahati yako kuwa yupo huyo, maana ungeniambia ni kwa nini unakuwa na duka la kuuza paka wakati huna paka' sauti hiyo ilionya taratiibu lakini kwa jinsi ilivyo, tabasamu la kulazimisha liliondoka usoni kwa Mushi.

    'Hii hapa' Mteja alisema huku akiwa ameshika noti ya dola mia moja. Mushi aliipokea huku akiwa macho yake yakiwa yanatathini mkono ya mteja. Mteja alibaini mshangao wa Mushi juu ya mikono yake.

    'Chukua hela acha kushangaa shangaa usije zikwa ukiwa hai wewe'. Mushi aligutuka, akachukua hela.



    Mteja alipokuwa anaondoka, Mushi alibaki na mshangao. Wateja wengine huja na vyombo maalumu vya kubebea paka, lakini mteja huyu alimkaba paka wake kwa mkono mmoja kwa namna ya ajabu. Na kutoka naye taratiibu bila hata ya kuaga.

    'Dunia ina mambo' Mushi alijikuta akijisemea kwa sauti ya kunong'ona huku akiwa anafunga duka lake. Hakuwa na hamu ya mteja mwingine tena jioni hiyo.



    Mteja mwenyewe akiwa na Paka wake mkononi alitembea taratibu, kichovu. mkono wa kushoto ulishikilia Paka, mkono wa kulia aliupumzisha kwenye mfuko wa koti refu la rangi ya kaki alilokuwa amevaa. Miguu yake mirefu miembamba ilirushwa taratiibu kuikanyaga lami ya kariakoo ili kuruhusu mwili wake kujibeba kwenda akili ilikotaka aende.



    Kwa kawaida mwezi Februari katika jiji la Dar es salaam huwa ni kipindi cha mvua. kuna watu huifurahia mvua hiyo lakini kuna wengine huwa ni kama adhabu kwao. kwa mfanyabiashara yeyote wa kariakoo au yeyote ambaye angelazimika kutumia Kariakoo kila siku kwenda kwenye shughuli zake basi wakati kama huu wa mvua hali huwa si nzuri. tope, maji kujaa barabarani, watu kutabisha vyoo vyao na kero zinazofanana na hizo huwa adhabu kwa wahusika wa Kariakoo.



    Jioni hii kulikuwa na kila dalili ya mvua kunyesha, upepo mkali ulioandamana na radi ulikuwa umefanikiwa kuwafanya watu kukimbia ovyo, kufunga maduka yao na kugombania daladala na kuwaacha wa mama wenye watoto migongoni kuwa wahanga zaidi wa hali hii kwani hawakuwa wepesi sana kukimbia na kupanda dala dala kwa kupitia madirishani kama wengine wengi walivyo fanya.



    Hivyo wengine walikimbia, wengine walifunga maduka, wengine walidandia dala dala nakupiatia madirishani, wengine walionekana kuparamia Boda boda, ill mradi kila mtu hali ilimfanya aharakishe ili kuwahi mvua iliyokuwa na kila dalili za kuanza kunyesha. Lakini mteja huyu alitembea taratiibu kama awali huku kicha chake kainamisha chini, akiwa kabeba paka wake na mkono mwingine mfukoni.



    Alitembea hivyo hadi upande wa kulia lilipo soko kuu la kariakoo na kuingia bara bara kuu kuelekea eneo ilipo shule ya Uhuru, mahali zinapopaki daladala za Mbagala. Hapo alipanda dala dala ya kuelekea Mbagala. Paka alikuwa ameshajitahidi kujikwamua mikononi mwa mmiliki wake huyu mpya, lakini jitihada zake zote zilikwamisha na mkono ule wa kulia ambao ulimbana sawa sawa.



    Mteja huyo wa Mushi alitulia tuli kwenye kiti chake akiwaacha baadhi ya watu kumshangaa namna alivyokuwa amebeba paka mkubwa namna ile bila wasi wasi. walipofika Saba saba aliomba kuteremka. Hakukuwa na kituo eneo aliloomba kuteremka ila sauti yake ilmfanya konda kumwamuru dereva kusimamisha gari.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Jamaa aliteremka na kuanza kutembea taratiibu kama ada yake, huku akiacha macho ya abiria kadhaa waliokuwa ndani ya ile dala dala yakimsanifu na baadhi wakimuhusudi wa kwa jinsi alivyokuwa amekaa kibabe kibabe.



    Alitembea hivyo hadi alipoifikia gari moja ya kifahari iliyokuwa imeegeshwa jirani na baa moja maeneo ya shirika la Salvation Army. Alipofika, kijana mmoja alishuka toka ndani ya gari na kumfungulia jamaa huyo mlango wa abiria. Bila kusalimiana jamaa aliingia na gari ikaondolewa kwa fujo. Huyo ndiye Ben au Kiroboto, hayo ndiyo yalikuwa maandalizi yakke ya mwisho kabla ya kwenda kwenye himaya ya John Kificho. Kabla ya kwenda dukani kwa Mushi kununua paka hao Kiroboto alikuwa amemtembela Mr. Gebo, safari hiyo nayo ilikuwa katika maandalizi ya kutembelea jumba la John Kificho usiku ule.



    Mr Gebo alikuwa sebuleni kwake, majira ya saa kumi na mbili, alisikia kama karatasi inapulizwa na upepo halafu ghafula akahisi kama gunia zito linapita usoni. Hakusikia maumivu yoyote, ila baada ya litu hicho kupita usoni fahamu zilimtoka. Aliporejewa na fahamu ilkuwa saa moja na nusu usiku. Hakuwa amejeruhiwa popote, alikagua nyumba yake kila kitu kilikuwa mahali pake, hata zile dola zake za kimarekani kama elfu kumi hivi zilizokuwa kitandani alizikuta palepale. Alipoingia maktaba ndipo alipogundua tofauti. Ilikuwa imekaguliwa vema. Lakini haikuwa rahisi kwake kujua nini kilikuwa kimechukuliwa. Ndiyo Kiroboto alivyokuwa ameinghia na kutoka kwenye nyumba ya Mr. Gebo mchoraji ramani maarufu jijini Dar es salaam, amabye matajiri wengi akiwemo John Kificho walipenda kumtumia na masikini walishindwa kwa sababu ya gharama zake. Kiroboto aliondoka na ramani yake mkononi. Alijua pigo alilokuwa amempa Mr Gebo lingemchukua masaa kadhaa kuzinduka ila angekuwa salama. Koroto alijua wapi pa kupiga na kwa malengo gani.



    ********

    Wakati Kiroboto akiwasili nyumbani kwa John Kificho majira ya saa mbili na dakika tano usiku. Hali ilikuwa tulivu eneo hilo. Alisimama kama mti kwa muda wa saa nzima akiwa na mashine yake ndogo kama darubini akiangalia jinsi walinzi walivyokuwa wakizunguka na kamera za usalama zilivyokuwa zimewekwa.



    Saa ya ukutani iliyoko chumbani kwaJohn Kificho ilipoonyesha kuwa ni saa tano na unusu. Kificho na Regina tayari walikuwa kitandani.

    “Regina mpenzi, unaonaje makao mapya? John Kificho aliuliza wakiwa ndo wameingia kitandani kulala.

    “Mmmmmh si mbaya, sema sikuzoea kuwa sehemu nzuri kama hivi, asante sana John. Nimeanza kukuzoea na nimeanza kuwazoea watu humu. Kingine lazima nikuambie sikutegemea ungekubali kumfungulia Jacob ili awe huru mule chumbani, naamini ipo siku utamwachia baada ya kupona” Regina alisema huku akiangalia darini. Tangu amefika hapo amekuwa akilala chumba kimoja na John lakini hawajawahi kufanya mapenzi, John aliafiki hilo kwa vile aliamini Regina anahitaji muda wa kutulia kiakili na kimwili ili awe tayari kwa hilo.

    “Unajua pamoja na utajiri nilio nao, bado nina moyo wa utu, nina huruma sana na nadhani baada ya Jacob kupota nitamfanya aawe mmoja wa wakuu katika biashara zangu” John Kificho alisema

    “Hilo nalo ni wazo….” Kabla Regina ahajamaliza walisikia kishindo, wote wakashituka. Wakati John ananyanyuka ili achkue bastola yake, mara nyumba yote ikawa giza.



    Jacob aliliona hilo akajiweka sawa, Vijana wa ofisi fukuzi walikuwepo nao waliona wakajua mambo yameiva, Banzi aliona lakini alikuwa hoi baaa ya kupata kipigo kikali toka kwenye lile jitu ambalo lilishaachilia kipigo kwa Jacob siku chache zilizopita. Ben maarufu kama Kiroboto alikuwa kazini, alishafikia sehemu ya kuu inayosambaza umeme kwenye nyumba ya John Kificho. Alijua kukiwa na giza wajanja ndiyo huwa wepesi na huru zaidi kuliko kukiwa na mwanga. Alikuwa amevalia kininja siku hiyo, hiyo ilimkumbusha alivyokuwa kwenye misitu ya Amazon kule marekani kama sehemu ya mafunzo yao. Akili yake ilimwambia kuwa awe makini kwa vile anapambana na mtu ambaye alikuwa akimshinda mara zote walizotakiwa kupigana wakiwa mafunzoni chini Cuba. Hivyo alitaka kumshinda Jacob kwa mara ya kwanza wakiwa kwenye kazi.



    Ilivyo ni kuwa, nyumba ya John kificho ilikuwa imejitenga na nyumba nyingine, si kwamba ilikuwa porini, ila John alikuwa amenunua eneo kubwa sana na kwenda kuweka makazi yake katikati ya eneo hilo. Wengi waliona kama halitendea halali eneo hilo kwa vile ilikuwa ni moja ya maeneo ya thamani katika jiji la Dar. Serikali mara kadhaa ilijaribu kulikomboa eneo hilo ili kuligawa kwa watu wengine lakini nguvu ya pesa ilizima majaribio yote. Ilikuwa ni nyumba ya ghorofa mbili, na pia ilikuwa na ghorofa moja kwenda chini. Ilikuwa imezungukwa na miti na migomba mingi, aliyekuambia kwa migomba haiwezi kustawi Dar kwa sababu ya udogo wake amekudanganya, inategemea tu una nguvu kiasi gani. Pesa ina weza kuhamisha mlima. Migomba ilikuwa imestawi na kunawili. Kulikuwa na video kamera karibia kila eneo kuzunguka jumba hilo ambalo mipaka ya eneo lake ilikuwa imezungukwa na ukuta mrefu ambo kwa juu uliwekewa nyaya za umeme. Kila kona kuzunguka nyumba hiyo kulikuwa na walinzi ambao walikuwa na silaha za kisasa. Walinzi ambao walikuwa wafundishwa na kuiva. Kwa kifupi eneo hilo lilikuwa salama kabisa.



    *********



    Pamoja na ulinzi ule, haikuwa taabu sana kwa mtu kama Kiroboto aliyekuwa amekamilika kila idara. Hakuwa na papara, alipofika nje ya ukuta wa kuzunguka nyumba ya John Kificho, Ben ama Kiroboto alizunguka kwa nje hadi pale alipopata mti mmoja mkuwa uliokuwa kwa jirani na ukuta huo. Aliupana kwa stahili ya aina yake huku mkono mmoja akiwa kamshika paka wake aliyemnunua Kariakoo, mgongoni akiwa na kibegi chake chenye vifaa vichache vya lazima kwa usiku huo. Alipopata tawi ambalo aliridhika nalo alitulia tuli. Mbu waliokuwa wakimshambulia wala hakuwa kama anawasikia, uvumilivu ni zoezi la kwanza ambalo mtu yeyote wa aina yake hufundishwa. Alitulia juu yam ti huo kama Bundi, shingo na macho tu ndiyo vilipepeswa. Muda wake ulipofika akatingishika. Aliikunja ramani yake aliyokuwa ameiiba kwa Mr. Gebo, kaichomeka mgongoni.

    “Its time for game” Alijiambia kwa kunong’ona. Alimchukua yule paka wake aliyekuwa amemnunua kwa bwana Mushi kule kariakoo. Akamfunga vidude vitatu viliyofanana na mpira mdogo. Alikifunga kimoja shingoni, kingine akakifunga mgongoni na kingine mkiani. Alipojiridhisha na hilo akamrusha huyo paka ndani ya ukuta. Alianza kukimbia kuelekea lilipokuwa jingo la nyumba hiyo. Mlipuko mdogo wa kwanza uliposikika, Kiroboto alitabasamu. Walinzi walikimbilia ulipotokea mlio huo mdogo amba ukubwa wake ni kama puto lililopasuliwa. Yule paka aliendelea kukimbia kuelekea upande mwingine. Mlio wa pili uliposikia, Kiroboto aliruka toka juu yam ti aliokuwa akatua ndani pasipo kufanya ukulele wowote.



    Alitembea kama kivuli, hata alipomfikia mlinzi aliyekuwa jirani naye, milinzi huyo alihisi kama upepo unapita wakati shingo yake ilipovunjwa kwa pigo moja tu. Alitembea ule mwendo wake wa kasi pasipo kufanya ukulele, alikuwa akienda kama kivuli kinapita, hata alipomfikia mlinzi mwingine, mlinzi huyo alihisi kitu lakini wakati akiipa akili yake nafasi ya kupambanua kinachoendelea, alishapitiwa tayari na Kiroboto. Tayari alikuwa ameshaufikia ukuta wa nyumba. Miti na migomba kuzunguka njyumba hiyo ilikuwa msaada tosha kwake maana kasi yake na shabaha yake isingeweza kuzuiwa na yeyeto pale.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mlio mdogo wa tatu ulitokea ndani, Kirobot alitabasamu “Amazon Cat” alinong’ona kwa jeuri. Hiyo ilimkumbusha jinsi paka hao walivyo wa ajabu ajabu, aliwajua wakati wakiwa kwenye mafunzo kwenye misitu ya Amazon kule marekani ya kaskazini. Sasa patashika zilisikika kila kona ya nyumba. Akili ya Kiroboto haikuwa ikimwofia mtu mwingine Zaidi ya Jacob Matata.

    Alijua fika kuwa ili kukamilisha zoezi lake hilo ilikuwa ni lazima kabiliane naye na kukabiliana naye ilimaanisha yeye kufa au Jacob kufa. Alitambaa na ukuta kama buibui, kwa vile walinzi walikuwa wakikimbia huku na huko ilikuw rahisi kwake kuingia ndani kwa kutumia lango kuu. Hapo kwa msaada wa ile ramani aliyoiba kwa Mr. Gebo alishaelewa sehemu kuu ya kuwasha na kuzimia umeme katika nyumba hiyo ‘main switch’ ilikuwa wapi. Haikumchukua sekunde nyingu kusababisha giza la ghafula katika jumba hilo lote. Alitulia kidogo ili macho yazoee giza, kwa mtu kama yeye alijua giza ndiyo sehemu nzuri Zaidi ya kupambania. Kwenye giza kasi yake na shabaha huongezeka.



    Jacob naye alifurahia kuona kumekuwa na giza nyumba yote, alitembea hadi kwenye mlango wa chumba alichokuwa amefungiwa. Wakati huu hakuwa amefungwa kama siku zote, hii ilifuatia ombi la Regina kwa John Kificho.

    “si mbaya sana” Jacob alijisema baada ya teke lake kufungua mlango aliokuwemo. Mlinzi aliyekuwa jirani na mlango huo alisikia kishindo cha lile teke kwenye mlango. Alipofika mlangoni alishangaa kukuta uko wazi, alipotaka kuingia alishitukia kitu kama mbao kikiufunika uso wake. Wala hakupata hata nafasi ya kuguna, taya lile kofi la Jacob lilishauchukua uhai wake.



    Jacob alinyata taratiibu kuelekea upande mwningine wa jingo hilo ambako kulikuwa na vyumba vingi, mpaka wakati huu hakuwa anajua nini kinaendelea, ila alijua ni wakati muafaka kwake kufanya mambo ya muhimu kwanza. Aliambaa ambaa na kibalaza kimoja hadi alipofikia mlango uliokuwa na maandihi yaliyosomeka ‘JIKONI’. Hadi kufika hapo alikuwa ameshapishana na walinzi kadhaa ambao walikuwa wakihaha pasipo kujua nini kinaendelea. Jacob aliujaribu mlango wa hicho chumba, ulikuwa wazi, akaingia. Humo alichukua kama dakika tatu hadi tano hivi, alipomaliza alijifuta mdomo kwa kiganja chake ksiha akanywa maji mafundo machache. Alitulia akiwa amesimama kama mtu anayesali, alikuwa akiikusanya akili iunganike na mwili wake. Aliporidhika kuwa sasa mwili uko tayari kuchuku amri zote ambazo zingetolewa na akili, alisikia damu inamkimbia mwilini, hali ya kupambana ilimvaa na alikuwa tayari kwa lolote.



    Alitoka chumbani humo akiwa ameshikilia kisu, alitemmbea taratiibu kulelekea upande ambao kulikuwa na purukushani nyingi. Kabla hata hajafika mbali, alimwona yule Paka wa Kiroboto akija upande huo, Jacob alimwangali halafu akajinong’oneza “Amazon Cat, Kiroboto yuko hapa, itakuwa mchezo mzuri” alimwacha yule paka apite, alichaelewa kuwa alikuwa anafuata harufu. Hivyo nay eye akageuka kurudi jikoni, aliingia jikoni, macho yalikuwa yameshazoea giza, wakati akiingia yule paka alikuwa akihangaika na masufira. Alikuwa akitafuta chakula. Jacob alisimama mlangoni yule paka alihisi mlangoni kuna mtu, akageuka, macho yake ya bluy yakang’aa. Jacob alimsogelea, yule Paka aliruka ili kumshambulia Jacob, lakini kasi na shabaha yake ilizidiwa na ile ya mkono wa Jacob, alitoa mlio mkali wakati shingo yake ilipokuwa akiminywa kama mtu aminyavyo mkate. Alikata roho, Jacob alimtupa yule paka mlangoni halafu akaendelea na safari yake.



    Alitembea mpaka sehemu ambayo alihisi kuwa ni sehemu ya kuingilia upande mwingine wa jumba hilo, ambako kwa hisia zake aliona ndiyo yangekuwa makazi ya John Kificho. Wakati akitaka kuujaribu mlango alihisi kuna kitu nyuma yake. Aligeuka kama umeme, macho yake yakakutana ana kwa nan a like jitu lilokuwa likimpa vipigo vya mauti. Alishusha pumzi, akajipanga tayari kwa shughuli. Lile jitu lilimtazama tu kwa macho ya hasira huku likipumua kwa fujo. Jacob aliweza kuusikia mwili wake ukiwa katka hali bora kabisa, ile safari yake ya jikoni ilishaanza kulipa.



    Lile jitu lilimvamia Jacob na kuachilia vipigo vitatu mfululizo, Jacob aliviona vyote na kuvikwepa ka kasi ya ajabu. Wakati bado linajizungusha Jacob aliachilia mateke matatu yote yalitua kwenye mwili wa hilo dude, likayumba. Kabla halijakaa sawa Jacob aliruka juu kama tai, kwa kutumia kiganja chake akalitandika lile dude shingoni na kutua chini kwa mapigo makali mawili ya Kung fu, lile jitu likaguna. Likainama, Jacob akaona hiyo ndiyo ingekuwa nafasi nzuri ya kulimalizia, alilivamia ili alivunje shingo, alishangaa alipokutana na shingo ngumu kaka mbao. Wakati huo huo likamdaka Jacob na kumbamiza ukutani. Kwa kasi likamfuata Jacob pale chini ili liikanyage shingo yake, Jacob aliona hilo kwa kasi ya ajabu na shabaha ya Tai, kisu kilichorushwa na Jacob kilizama shingoni mwa lile jitu. Likatoa mlio wa maumivu, likalegea. Jacob kaachia karate nyingine mbili amabazo zililipeleka chini lile jitu. Sasa likawa linahema na kuguna kwa fujo na hasira. Jacob alilisogelea jitu hilo ka lengo la kumaliza kazi, wakati ameshalifikia akasikia mvumo kama wa karatasi inayosukumwa na upepo. K wa kasi aliruka toka aplea lipokuwa na kutua upande mwingine, wakati huo huo pigo la mauti lilokuwa limeachiwa na Kiroboto likiwa linapita kapa. Kwa kasi ile ile, Kiroboto alijipindua na sasa akawa anatazamana ana kwa ana na Jacob Matata.

    Kiroboto alifanya ishara ya kininja, Jacob akajibu, wakajipanga.

    “Its my pleasure Jacob” Kiroboto alinong’ona

    “All the best Ben” Jacob alijibu, kasha akasikia kitu kama karatasi inasukumwa na upepo. Alishajua maana yake, aliponyea wakati pigo la Ben au Kiroboto likipita juu ya kichwa chake. Jacob aliachia teke la mbele lilipokwepwa akalirudisha kwa nyuma, mguu wake ukadakwa na Kiroboto. Kiroboto akausukuma ule mguu kwa nguvu Jacob akarushwa hewani lakini akatua chini akiwa amepiga magoti. Kuona hivyo Kiroboto akaja mzima mzima ili amchukue Jacob kwa pigo la kifo, lakini alipofika alikuta patupu, Jacob alikuwa akimsubiri Kiroboto atue, akampa ngumi mzibu, Kiroboto akazibuka, akafunikwa kwa teke ndama, Kiroboto akateteleka. Jacob damu ilikuwa inamchemka wakati huo. Alikwenda kama ananyata kwa kasi ya kimbunga ili amzoe Kiroboto, lakini Kiroboto alishamsoma, akakwepa na kumpa kichwa Jacob, Jacob akaona nyota. Kasi iliyokuwa inatumika, shabaha, na ukali wa mapigo ungedhani uko unaangali zile sinema za mapigano, kumbe niwatanzania wawili waliokuwa wakipigana.



    Kiroboto alitoa mapigo manne mfululizo, mawili yakamwingia Jacob. Jaco akayumba. Kiroboto alikuja na wimbi jingine ambalo lilikuwa na lengo la kuvunja taya za Jacob akamwona na kujipinda kidogo, kasha akaachia vipigo viwili ambavyovilimpeleka Kiroboto chini. Kiroboto akaguna, kasha mlio wa mguu kuvunjika ulisikia mara baada ya teke kali kama radi lilipotua mguuni kwa Kiroboto. Jacob akanesa na akawa anamkabiri Kirobot, mara akasikia sauti kali ya kike

    “Jacooooooob” Halafu ile sauti ikazimwa ghafula. Jacob akaegeuka kuangalia sauti inakotoka, hilo lilikuwa kosa kubwa kutosha kuadhibiwa. Alijikuta yuko chini baada ya pigo la Kiroboto, alijipinda ili kukwepa la pili kasha akajifyatua na kumkumba Kiroboto ambaye alikuwa amesha vunjika mguu. Kirobot alishaona maji marefu, alirka juu kuelekea upande mwingine, Jacob alipogeuka Kiroboto alikuwa ameshatoweka. Alielewa maana yake, akakimbia kuelekea upande ambao sauti ya kike ya kuomba msaada ilitokea. Alipofika alipoliacha lle jitu akakuta halipo. Akafungua mlango kuingi upande mwingine wa jingo ambako alihisi ndipo makazi ya John kificho yalikuwepo. Alipofikwa sehemu ya uwazi alitokea mlinzi mmoja, Jacob alijirusha chini akawa anajiviringisha kama tairi huku risasi zilizokuwa zikimiminwa na mlinzi huyo zikimkosa kosa. Alisimama alipofika nyuma ya ukuta uliokuwa nyuma ya ngazi za kupandia ghorofani. Yule mlinzi alikuja kwa kasi akidhani Jacob alikuwa amekwenda upande mwingine, alipofika usawa na alipokuwa amejibanza Jacob, kiganja cha Jacob kilitua kwenye shingo yake na kuua baadhi ya mishipa yake ya fahamu. Akaanguka chini akiwa maiti tayari. Jacob alichukua bunduki aliyokuwa amebeba huyo jamaa, kasha akaanza kunyata. Kulikuwa na ngazi za kushuka chini kwenda kwenye jumba lililokuwa chini ya ardhi na kulikuwa na ngazi zilizoelekea juu ghorofani. Wakati bado anajiuliza kuwa aelekee wabi mara sauti ikasikika tena.

    “Jacob, nakufa!!! Sauti hiyo ilitokea ubande wa chini, hivyo Jacob akaanza kukimbia kuzifuata ngazi zilizokuwa zikielekea chini ya ardhi kabla hajasiki.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Stop, Don’t! Ilikuwa ni sauti aliyokuwa anaifahamu. Akageuka na kukutana na macho makali ya Bi. Anita. Kabla hajasema lolote kikasikika kishindo kizito kilichotikisa jingo lote na eneo zima, Jacob aliruka akamkumba Bi. Anita huku na kujibingirisha naye huku moto mkubwa uliokuwa umetokea ardhini ukiruka na kupita juu yao. Walipokuja kutulia ili wasimame, Jacob akajikuta anataza kwenye viatu vya mtu aliyekuwa amesimama jirani na pale alipoangukia. Hakutaka kujishauri Zaidi alijisukuma kwa mikono na kujirushia upande mwingine mbali na hiyo miguu. Aliposimama akaliona lile jitu amabalo lilikuwa katika hali ya kutisha.





    “Run….Boss, kimbia” alisema huku akielekea kulikabili lile jitu. Alipolifikia, lilianguka chini na kuacha kishindo kikubwa. Jacob akajua limeshakwisha hivyo akageuka na kuanza kutoka nje. Alipokuwa amepiga kama hatua nne hivi akasikia

    “Jacob, angaliaaaa” Sauti ya kike ilipiga kelele wakati huo huo akasikia mlio wa bastola ikikohoa. Ilijirusha, alipotua chini aligeuka kwa kasi, akamwona Eve akiwa chini huku damu zikiwa zinambumbujika kifuani. Risasi ambazo zilikuwa zimekusudiwa kumwingia yeye zote zilikuwa zimemwingia Eve, baada ya Eeve kuruka ili kumwokoa Jacob. Bastola bado ilikuwa mkononi mwa lile jityu ambalo wakati huo lilikuwa limechia tabasamu la kifedhuri usoni. Lilikuwa linapigania pumzi zake za mwisho, lakini hata hivyo lilikuwa limekusudia kuondoka na Jacob kama si Eve kuliona na kuruka kumkinga Jaco.



    Jacob alikimbilia lilipokuwa lile jitu, alichukua ile bastola, kasha akalimiminia risasi kibao kichwani. Lilitoa mlio wa kutisha kasha likakata roho. Jacob alikimbia alipokuwa Eve, alipiga magoti, akamnyanyua na kumkumbati huku Eve akiendelea kutokwa na damu. Eve aliweza kumwona Jacob, japo alikuwa kwenye maumivu makali lakini alitabasamu na kujitahidi kumkumbatia Jacob.

    “Ja….j…a..a..ja…ja… jacob, nan… a…nana kupenda, ni..ni.ni.n.n.i.b.u.su! Eve alisema kwa shida huku tabasamu likiwa usoni. Jacob aliinama akambusu Eve. Japo alijikaza asilie lakini Jacob ilimuuma kuona Eve anamfia mikononi. Akiwa katika hali hiyo, alihisi mkono unamgusa begani, alipogeuka akakutana na uso wa Bi. Anita, mkurugenzi wa ofisi fukuzi.



    *****



    Wiki moja baada ya Jacob kufanikiwa kutoka Mikononi mwa John Kificho, ilikuwa yenye visa na vituko vya ajabu ajabu. Si kwa Jacob Matata, bali idara ya jeshi la Polisi na viongozi mbali mbali.Matukio ya kushangaza yalikuwa yanatoke na hakuna aliyekuwa anajua chanzo chake wala mwisho wake.

    Huyu mheshimiwa alikuwa ni mmoja wa wahanga wa matukio hayo. Masaa kadhaa yalikuwa yamepita tangu ajilaze kwenye mchanga wa fukwe ya bahari ya hindi maeneo ya mbezi. Eneo hili lilikuwa giza na kulikuwa na mbu wataabishaji ambao hata hivyo kutokana na jambo lilikuwa likimtatiza kichwani na moyoni hakuweza kuhisi usumbufu wowote toka kwa mbu hao. Alijisikia kukereka kuona wenzie hawafiki lakini alipoangalia saa yake ya dhahabu aliyokuwa amevaa mshale ulimwonyesha kuwa ndo kwanza ilikuwa saa nne kasoro dakika tatu. Walikubaliana wakutane saa tano kamili, hivyo ilimaanisha kuwa ilikuwa bado takribani saa moja na dakika tatu ili waanze mazungumzo yao. Alisimama, akaangali mawimbi kama anayesikiliza muziki wake, baada ya dakika chache akakaa tena. Aliendelea kukaa, kusimama na kijisonya mwenyewe hadi pale wazo la kwenda sehemu ya kuuzia vinywaji lilipomjia. Alinunua chupa kubwa ya mvinyo na kuanza kuunywa kwa fujo. Mvinyo huo uliitibua zaidi akili yake.

    Ilipofika saa tano kamili watu wanne waliku wamekaa pale ufukweni kimya kabisa, kila mmoja akifikiri lake. Waliokuwa wamefika ni Mheshimiwa Mboka , Said na Mondina. Walikuwa wanawasubiri waheshimiwa Nungwana na Luzwilo.

    'ndugu zangu, nimewaiteni hapa kufuatia hali ya utata ambayo imejitokeza hivi karibuni. Kama mjuavyo tangu kutoweka kwa John Kificho na Harken Kalm , wenzetu wawili wameshatoweka na haijulikani waliko. Huku jitihada za kuwatafuta zikiendelea ni wazi kuwa kuna jambo ambalo ama limejulikana au linakwenda kujulikana kuhusu sisi! Ni wa wazi kuwa waheshimiwa wote waliotoweka ni wanachama katika kundi letu la siri. Nimeshawasiliana na Frank kumuelezea juu ya wasi wasi wetu anasema leo watakuwa na kikao huko Hispania kujadili hali hii....naomba tuwe katika hali ya hadhari kubwa, na nawashauri msisafiri ovyo ovyo' aliongea Mheshimiwa Mboka na kutulia, bila shaka kuwaachia wenzie waongee lolote. Kimya cha muda kilipita ambacho kilizaa hofu Fulani, katika kimya hicho ndipo sauti ya Mheshimiwa Mondina ilipotoka. "tulipanga tukutane hapa na wote tulikuwa na taarifa hizo lakini nashangaa wenzetu wawili hawapo. Labda kama mheshimiwa Mboka una taarifa zao?

    "hapana mheshimiwa Idrisa, sina taarifa zozote, nimejaribu kupiga simu zao lakini hazipatikani' Mheshimiwa Mboka alisema kwa sauti yenye hofu kiasi. Kikao kilikwisha na wote walitawanyika.

    ****

    “miye nachoweza kusema, huyu jamaa ni hatari, maana ni mwepesi kama upepo na mapigo yake na mguso wake ni imara kama chuma. Ni mtu ambaye japo miye ni mwanajeshi, tena mwanajeshi hasa lakini sikuweza kufanya lolote mbele ya kasi yake na uimara wake. Japo ameniteka ila ninamhusudu sana ujuzi wake”

    “Miye kabla sijapambana na mtekaji alipita paka mmoja mkubwa, ndipo akatoke mtu ambaye ni mwepesi kama upepo, mapigo yake huwa nayaona kwenye filamu tu” huyu naye alisimulia

    “Nami pia alipita paka lakini nilishangaa kuona “Amazon Cat” maeneo yetu kama yale. Maana hao ni paka adimu sana” aliongea mheshimiwa Nungwana kama mtu anayeota. Wote wawili waliingizwa katika chumba hiki kwa nyakati tofauti. Sababu ya kutekwa kwao hawakuijua, ila hawakuhitaji maelezo kuambiwa kuwa wametekwa. Wote wawili walitekwa sehemu tofauti na mazingira tofauti tofauti wakati wakijiandaa kwenda kwenye kile kikao ufukweni mwa bahari. Kutokana na jinsi kila mmoja alivyomuelezea mtekaji, walikuja kukubaliana kuwa hakuna shaka kuwa mtekaji wao alikuwa ni mmoja. Kitendo cha wao kuwekwa sehemu moja kilithibitisha hilo. 'anataka nini na katumwa na nani? Ndilo swali walilokuwa wakijiuliza bila majibu.

    ****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mwanzo ilikuwa siri kati ya vyombo vya usalama na wakubwa. Ikawa ni taarifa za ki interejensia lakini baadaye haikuwa siri tena. Watu wote walijua. Wasio muhimu na watu muhimu, wa masaki na wa manzese, waheshimiwa na wakata nyasi, wote walijua kuwa kuna shida katika taifa. Magazeti yaliandika, Radio zilitangaza, Televisheni zilionyesha, mitandao ya kijamii iliandika na ikajadiliwa kuwa waheshimiwa watano wametoweka na hawajulikani waliko. Kila mtu alijaribu kubuni kuhusu kutoweka kwao. Wapo waliosema wamekimbia nchi baada ya kujiridhisha na utajiri wao. Wengine walipinga hilo wazo na kusema waheshimiwa hao wasingeacha familia zao nyuma katika hali tata kama hiyo. Wengine walisema wameawa, laikini wakatilia shaka kwa kusema kuwa maiti za waheshimiwa hao zingepatikana. Vyombo vya usalama vya hadharani na sirini vilikuwa kazini kutafuta ukweli juu ya suala hilo. Kila mbinu ikitumika kuhakikisha waheshimiwa hao wanapatikana.

    ****

    Kitendo cha kutowekakwa waheshimiwa wanne ndani ya siku mbili kilimchanganya sana mkuu huyu wa usalama. Hakuwahi kusikia hapo kabla kuwa hali kama hiyo imewahi tokea.



    Hiki kilikuwa na kikao cha tatu ndani ya siku hii. Kilianza majira ya saa moja jioni.

    'nataka unapotoa ripoti yako utoe na mapendekezo ya nini kifanyike baada ya hapo' aliunguruma mkuu huyo wa usalama. 'kamati hii inategea kupata ripoti Ya kwanza itatoka kwa afande Lucas amabye ataeleza mazingira na juu ya taarifa za utekwaji wa Mheshimiwa Luzwilo, afande Mwita atatueleza juu ya mheshimiwa Nungwana, afande Numbi atatueleza juu ya Mheshimiwa Motie, afande Ngesi juu ya mheshimiwa Nitwa. Bila kupoteza muda tuanze na afande Lucas'.

    'Afande, uchunguzi wetu ulianzia nyumbani kwa Mheshimiwa Luzwilo. Tulifanikiwa kuongea na wana familia na walinzi. Mke wa Mheshimiwa anasema ilipofika majira ya saa kumi na mbili jioni, wakiwa chumbani hapo nyumbani, mumewe alipokea simu, simu hiyo ni kama ilikuwa akimkumbusha juu ya miadi fulani. Neno pekee ambali mheshimiwa aliongea kwenye simu hiyo ni 'nakuja comrade' kisha akakata simu. Baada ya simu hiyo mheshimiwa alivalia lakini si kama mtu anayekwenda sehemu rasmi, maana alikuwa kama mtu anayekwenda bustanini tu Alipotoka alimwambia mke wake 'nitarudi baada ya masaa mawili kuna rafiki zangu nakwenda kuwaona'. Mke wa mheshimiwa anasema hiyo ndiyo ilikuwa mara ya mwisho kumsikia na kumwona mume wake. Baadae tumewahoji walinzi wa hapo nyumbani kujua kama walimwona mheshimiwa akitoka muda huo aliosema mkewe. Askari wawili walio zamu wamekana kabisa kuwahi kumwona mheshimiwa akitoka. Baadae tukawahoji watumishi wa nyumbani hapo kama kuna yeyota alibahatika kumwona Mheshimiwa akitoka. Watatu walikana kumwona ila wawili wanakiri kumwona akitoka. Mmoja anasema alimwona akifungua mlango wa sebuleni kwenda nje. Mwingine anasema alimwona akielekea upande wa kuegeshea magari. Baadae tukawauliza hawa wawili waliokubali kama wanakumbuka jinsi mkeshimiwa alivyokuwa amevaa. Wote walitueleza sawa na ambavyo mkewe mheshimiwa alituambia jinsi mumewe alivyokuwa amevaa. Baadae tukamtafuta dereva wa mheshimiwa. Dereva anasema mheshimiwa alimuruhusu kutoka jioni ile kwa vile hakuwa anatarajia kutoka hivyo alitarajia kurudi nyumbani kwa mheshimiwa asubuhi ya kesho yake. Hivyo haamini kama mheshimiwa alitoka jioni hiyo, kama alitoka basi anadhani alitoka kwa miguu ambayo hiyo sasa inatofautiana na yule mfanyakazi wa bustanini anayedai alimwona akielekea sehemu ya kuegeshea magari. Dereva anasema hakuwahi kumwona mheshimiwa akiwa anatoka nyumbani kwa miguu. Mke wa mheshimiwa pia anaondoa uwezekano wa mumewe kuondoka nyumbani kwa miguu. Kijana wa bustanini aliulizwa kama aliwahi kusikia gari ikiwashwa na kuondoka pindi mheshimiwa alipoelekea sehemu ya kuegeshea magari. Kijana huyo anasema hakumbuki kama gari iliwashwa. Baada ya hapo tulitoka na kuanza kuangalia mazingira ya nje ya nyumba ya mheshimiwa Luzwilo Lupimo. Huko hatukuona lolote jipya. Ila askari wanasema kama siku tatu nyuma kulikuwa na kichaa ambaye alipendelea kupita eneo hilo mara kwa mara na mara nyingene alikaa hapo kwa muda na kuondoka. Wanasema tangu mheshimiwa atoweke hawajamwona tena kichaa huyo. Tumejaribu kila namna kumtafuta kichaa huyo lakini hatujafanikiwa kumpata. Ila tumearifiwa kuwa kichaa huyo aliwahi kuonekana kwa nyakati tofauti tofauti kwenye maenea ya mbele ya nyumba wanazoishi waheshimiwa waliotoweka. Kote huko hajaonekana mara baada ya matukio. Mkuu, mapendekezo yetu ni kuangalia uwezekano wa kumpata kichaa huyo na pia kuendelea na uchunguzi wa kujua chanzo cha kutoweka kwao na kujua walipo waheshimiwa hao' alimaliza Afande Lucas na kukabidhi ripoti yake. Huku akiamini ameeleze yote aliyotakiwa kutaelezea. Lucas aliulizwa maswali na makamanda wengine waliokuwepo kikaoni hapo ka ufafanuzi zaidi. Aliyajibu na kisha makamanda wengine wakatoa taarifa zao. Taarifa zilitofautiana maelezo na mazingira ya kutoweka na maeneo waliyokuwepo waheshimiwa hao. Kitu kimoja kilitokea kwenye taarifa ilionyesha kuwa yule mtu kicha alioneka akiwa maeneo jirani waliyokuwepo waheshimiwa kabla ya kutoweka.

    'naona kuna mambo matatu hapa ambayo yanaweza kutupa mwanga; kwanza ni huyu kichaa, pili ni ile simu ya wisho aliyopigiwa mheshimiwa Luzwilo Lupimo na tatu tujue kama kwenye maeneo yoote ambayo hawa waheshimiwa walitoweka kuna namna yoyote tunaweza pata ushahidi wa kutufikisha ama kwa huyo kichaa au mtekaji. Makamanda wengine mtaendelea kufuatilia kama nilivyowagawia, ila kuanzia sasa afande Tiko wewe utafuatilia kote ili kuweza kuunganisha matukio na mwenendo wa upelelezi wa jambo hili. Naomba kazi yetu tufanye kwa kasi na umakini mkubwa. Wakati huo huo, ulinzi kwa waheshimiwa wengine uimalishwe sana......alimaliza mkuu wa usalama na kuwaruhusu maafande watawanyike kwa ajili ya utekelezaji wa waliyokubaliana.



    ****



    Jacob alicheka, aliangalia tena computer iliyokuwa mbele yake, kisha akakuna kichwa. Hatimaye alikuwa na jibu la mchezo mzima, alishaelewa Regina atakuwa wapi na namna ya kuwapata John Kificho na Harken Kalm, zile dakika ishirini alizoomba kuingia kwenye jumba lililokuwa linateketea la John kificho zilikuwa zimempa ufunguo. Alihitaji muda na akili iliyotulia kuumliza mchezo mzima. Alizima computer yake, akanyanyuka.



    ******

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Saa moja na dakika arobaini na tano Mpelelezi Jacob alikuwa maeneo ya Upanga, alipaki gari lake nyumba ya tatu toka ile aliyokuwa amekusudia kwenda jioni hiyo. Alitembea taratibu huku macho yake yakiwa yanaangali nyumba aliyokuwa anaiendea. Ilikuwa ni moja ya zile nyumba za shirika la nyumba ambazo zilikuwa na ghorofa moja. Alipoifikia nyumba aliyokuwa anaitaka badala ya kwenda kwenye lango kuu la mbele la uzio wa nyumba hiyo, alijipenyeza kwenye uchochoro mmoja uliokuwa unaitenga nyumba hiyo na ile ya jirani. Ilikuwa imezungushiwa ukuta mbao hata hivyo ulikuwa umeshachoka sana. Ukuta huo ulikuwa mfupi, kiasi kuwa hata kuku aliyekurupushwa angeweza kuuruka bila shida. Jacob alitembea taratiibu huku akisanifu jinsi nyumba hiyo ilivyokuwa. Sehemu ya mbele kulikuwa na majani yaliyokuwa yameota na iliashiria kuwa hakukuwa na mtu alikuwa anaishi katika nyumba hiyo. Alipofika sehemu ambayo ukuta wa ua wa nyumba hiyo ulipokuwa unaishia, aliruka kama mchezo vile akawa ameingia ndani. Ilikuwa imetimu saa mbili na dakika sita, kwa vile hakukuwa na taa yoyote eneo la nje la nyumba hivyo, giza lilikuwa linashindana na mwanga wa taa toka nyumba za jirani. Jacob alinyata taratibu kusuogelea mlango wa upande wa nje. Aliufikia mlango na akasimama kama kivuli kwa dakika kadhaa kusikiliza kama kulikuwa na mchakato wowote tokea ndani. Palikuwa kimya kabisa. Ilikuwa nyumba ya shirika la nyumba yenye ghorofa moja, lakini hakukuwa na dalili ya kuishi kiumbe yeyote ndani ya nyumba hiyo. Aliujaribu mlango wa nyumba hiyo, ulikuwa umefungwa na alipounyonga mlio wake uliashiria kuwa haukuwa umetumika kwa muda mrefu.

    Wakati akiwa amekata tamaa na kutaka kuanza kuondoka alisikia mlio wa kama kiti kusogezwa. Akili yake ikashituka na matumaini yakapata uhai. Alichukua funguo malaya akaingiza kwenye kitasa cha mlango, mlango ukakubali. Aliusogeza taratibu, kasha akaanza kunyata kuelekea upande wa mbele ambako kulikuwa na sebule na mlango wa mbele wa kuingilia nyumba hiyo. Alitembea hivyo na kukagua vyumba vyote vilivyokuwa sehemu hiyo ya chini lakini hakuambulia lolote. Hayo aliyafanya kimya kimya mno kiasi hata kama kungekuwa na panya ndani ya nyumba hivyo wasingekeza kuhisi tofauti yoyote. Aliporidhika kuwa alikuwa amekagua vema sehemu ya chini, aliamua kupanda ngazi kwenda upande wa juu. Alizipanda ngazi taratibu kwa mwendo wa kunyata. Alipofika kwenye korido iliyokuwa inavigawa vyumba vya upande wa juu, alitembeza macho yake na mara moja yakakwama kwenye mwanga uliokuwa unatoka kwa chini ya mlango wa chumba cha kati kati upande wa kushoto.



    Teke moja la mguu wa kulia liliufungua mlango na Jaco akajikuta anatazamana na chumba kilichokuwa kimejaa vifaaa vya mawasiliano. Kulikuwa na meza moja na kiti ambacho kilikuwa kimekaliwa na mzee mmoja aliyekuwa na miwani mikubwa machoni kwake. Hakujitete wala hakujitingisha bali alikuwa ametazama tu kama aliyekuwa anatarajia jambo kama hilo kutokea.





    “Bila shaka unaitwa Jacob Matata” Sauti iliyochoka na iliyokwama kwama ya kizee yam zee huyo ilisema huku akigeuka kuangalia mlangoni ambapo Jacob Matata alikuwa amesimama imara bastola mknoni ikiwa imemwelekea mzee huyo.

    “Hujakosea, bila shaka ni mzee Vicent? Jacob alijibu kasha akauliza

    “Hujakosea, sitaki kushindana na wewe. Nilikuwa nikingoja kwa hamu siku ambayo nitaonana na wewe” Alisema yule mzee huku akimwangalia Jacob kwa macho yake yaliyokuwa yameingia ndani.

    “Hapa nilipokaa sina uwezo w kutoka kasha nikaendelea kuwa hai, nimekuwa hivi kwa muda wa miezi sita sasa tangu walipoanza kutekeleza mpango wao huu” Alisema mzee Vicent

    “Mpango gani? Jacob alihoji

    “Najua ndicho kilichokuleta hapa. Lakini kabla sijakuambia, nitoe hapa nilipo kasha twende sehemu nyingine tukaongee maana leo wana ratiba ya kuja kuniletea chakula na kuchuku taarifa wanazozitaka” Alisema mzee Vicent huku midomo yake ikiwa inatetemeka.

    “Chini ya hiki kiti nilichokaa kuna bomu, ambalo nikinyanyuka tu zito wangu ukaondoka lialipuka” aliongeza mzee Vicent.

    “Okay nimeshaelea” Jacob alisema huku akiiinama, akanyanyua suruali yake kile kiatu chake cha ngozi kilichokuwa kilefu hadi jirani na magoti kilioneka. Kwa pembeni ya kiatu hico kulikuwa na mifuko midogo midogo iliyokuwa imewekwa vitu mbalimbali. Mfuko mmoja ulikuwa umebeba kisu, alikichomoa kasha akapiga magoti. Kwa kutumia kisu chake akaanza kuchokonoa chini ya mbao ya iliyokuwa chini ya kiti hicho. Ilivyo ni kuwa, kile kiti alichokuwa amekalia mzee Vicent kilikuwa juu ya mbao kubwa pana kiasi kuwa miguu yote ya kiti ilisimama juu yake. Mbao ile ilikuwa inafunika kitu kama shimo ambalo ndani yake ndimo kulikuwa na bomu. Hivyo Jacob alijua ni lazima alitegue lile bomu ili yeye na mzee huyo waweze kutoka salama ndani ya nyuma ile.Ilimchukua Jacob Matata dakika kumi kuweza kutegua lile bomu.

    “Sasa nimeanza kuamini yaliyokuwa yanasimuliwa kukuhusu wewe! alisema mzee Vicent kwa mshangao.

    “Bomu ulilotegua ni la kisasa mno, ingehitaji mtu mtaalam sana kuweza kulitegua” Jacob alitabasamu hakusema kitu. Alichkua simu yake akabonyeza namba kadhaa kasha akasubiri.

    “Enoce, hebu njoo hapa upanga nyumba namba 41A kuna mzigo nataka uuchukue ukauweke sehemu salama” Jacob alisema kasha akakata simu bila kungoja jibu.

    “Kaa hapa ngoja niwasubiri wageni wako huko chini, lakini kabla sijaenda hebu nipe taarifa nazozitaka” Jacob alisema huku akiwa anaiwekea bastola yake kiwambo cha kuzuia sauti, akili yake tayari ilikuwa imekaa kimapambano.

    “Jacob, mpango huu ni mkbwa ni zaidi ya Regina na Eve, ni zaidi ya biashara haramu ambazo Herkan Kalm na John Kificho wanafanya. Hiyo yote ilikuwa ni geresha tu na kukupotezea muda. Muda wote walikuwa wanakuogopa wewe. Jambo moja unatakiwa kujua ni kwamba, Kificho na Harken Kalm hawajui kuwa wako katika mpango mmoja, maana wamehusishwa kwa njia tofauti sana. Kama umeweza kufika hapa basi sasa nina hakika unaweza kutinua mpango wao kama ambavyo wakekuwa wakikuhofia. Miye nimukuwa nikitumika kama mtambo wa kuunganisha na kuwezesha mawasiliano tu, ila sijui mambo mengi ndani ya mpango huu. Nilikuwa natafuta uhuru wangu ili nirudi katika maisha yangu ya kawaida ndiyo maana nikatuma ule ujumbe ulioukuta kwenye komputa iliyokuwa chumbani kwa John kificho baada yay eye kutoroka. Akitaka kupata njia ya kufikia kiini cha mpango huu, inabidi umwone mheshimiwa...” Kabla hajamalizia kusema, mlango wa chumba kile ulipigwa teke, kama umeme Jacob aliruka pembeni na kupisha risasi zilizokuwa zimeelekezwa kwake ziingie kwenye kifua cha mzee Vicent. Jacob hakuchelewa, alichia risasi tatu, ambazo zote zilimpata yule kijana pale mlangoni akadondoka. Jacob alisimama haraka na kuelekea mlangoni huku bastola tyake yenye kiwambo cha kuzuia sauti ikiwa imara mkononi. Alipofika mlangoni, bastola yake ilipigwa teke, ikaangukia pembeni. Kasha teke ambalo lilikuja kama mtego wa panya uliofyatuka likatua kifuani kwake na kumfanya Jacob arudi nyuma. Mateke mawili yaliyofuata aliyaona, kasha akrusha ngumi yake ya kulia ikatua kwenye shingo ya huyo jamaa. Jamaa karusha ngumi tatu zilizotoka kama umeme, moja ikampata Jacob ambaye naye akajibu kwa shoto lake ambalo lilimpeleka huyo jamaa chini, kabla jamaa hajainuka, Jacob alimpa mateke matatu ya mbavuni, mbavu kadhaa zilivunjika. Jamaa kalegea. Jacob alimsogelea kwa nia ya kumhoji huyo, jamaa. Lakini hata kabla hajamfikia huyo jamaa Jacob alimwona akiwa amekaza macho kwenye dirisha ambalo Jacob alikuwa amelipa mgongo wakati huo, Jacob akahisi kitu, akajirusha pembeni, huku nukta chache tu risasi zikimkosa na kumuua yule jamaa. Kisha aksikia kishindo akajua muuaji alikuwa amesharuka toka pale dirishani upande wa nje. Haraka akamrudia mzee Vicent, ambaye alikuwa akipigania roho yake. Alimtingisha kuona kama anaweza kushituka. Mzee vicent alifungua macho, alitabasamu. Akajitahidi kuinua mkono wake, akaingiza kifuani kwake, alipoutoa alikuwa ameshikilia chuma kidogo kilichokuwa na umbo la pembe nne kilichokuwa kikining’inia kwenye mkufu wake. Akakiweka mkononi kwa Jacob kasha akafungua kinywa chake ili kusema kitu, alijitahidi sana hadi mwishowe akanong’ona “fu fu ..”. Alivyosema hivyo akapumua kwa nguvu kasha akatulia. Jacob alimwachia kasha akakurupuka kutoka nje. Wakati anafika nje akapigwa na mshangao mwingine pale alipokutana na maiti ya Enoce yule kijana aliyekuwa amemwita toka ofisi fukuzi ilia je amchukue mzee Vicent. Aliangaza macho huku na huko lakini hakuona kitu. Alikiangalia kile chma alichokuwa amepewa na mzee vicent, hakuelewa kwa nini mzee vicent alimpa kile chuma. wakati anataka kupiga hatu hatua kuelea kwenye lango la kutokea nje, alisikia mlio wa gari likiondolewa kwa kasi. Akakurupuka kuelekea njea lakini mara kile chuma kikaanguka, akarudi ili akiokote, ndipo alipokuta kimefunguka kama mkebe vile. Kikaratasi kidogo kikaonekana. Jacob alikichukua haraka. Kilikuwa na maandishi madogo sana lakini Jacob aliweza kuyasoma, kilikuwa kimeandika; Makongo juu # 091. Jacob aliangalia saa yake, ilikuwa imeshatimu saa nne kasoro usiku.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    *******

    Ilipofika saa tano na robo usiku, Jacob tayari alikuwa ameshapata ilipokuwa nyumba namba 091, makongo juu. Alishangaa alipogundua kuwa nyumba hiyo ilikuwa ya mheshimiwa Mondina.

    “kwenye Dunia ya sasa kila kitu kinawezekana” Jacob alijisemea baada ya kuwa ameshaparamia ukuta wa nyumba hiyo na kutua sehemu ya ndani ya ua wa nyumba hiyo. Ukiingalia nyumba hiyo ilikuwa sawa na nyumba nyingine ambazo waheshimiwa wanazimiliki. Ilikuwa vyumba ya mheshimiwa ambayo ilikuwa imetanda kwenye viwanja kama viliwi hivi ambavyo nyumba za kawaida zingeweza kujengwa. Bustani yake, mapambo yake pale nje, gari zilizokuwa zimepaki, taa zilizokuwa zikiwaka ilikuwa ni sababu tosha ya kujibu swali la kwa nini watu wanagombania na kung’ang’ania uongozi hata kama hawauwezi. Kila kitu kilipendeza. Jacob alinyata hadi alipofikia dirisha la nyumba hiyo. Ndani kulikuwa giza tupu, alizungukia vyumba kama vitatu vyote vilikuwa giza, alipokaribia chumba ambacho kilikuwa na mwanga akasikia vishindo vya mtu ambavyo viliashiria alikuwa akija upande ambao yeye alikuwepo. Alijibanza kweye nguzo moja ya chuma na kuonekana kama sehemu ya chuma hicho. Askari alitembea taratibu kasha akampita Jacob. Jacob alimwangali yule askari hadi alipopotelea. Akarudi pale diridhshani akatega sikio.

    “Alaaaah huyu Jacob ni hatari sana kawezaje kujua tulipokuwa tumemficha Vicent? Sauti iliongea kwa jazba. Jacob alajitahidi kutafuta namna ya kuona ndani lakini kulikuwa na pazia zito sana hakuweza kumwona mwongeaji.

    “Sikiliza Kificho, inabidi utafute namna ya kumdhibiti Jacob, wakati huo huo nitajaribu kutumia vijana wangu walioko wizarani ili waweze kunipa taarifa za kutusaidia kumpata huyumkichaa. Pamoja na kumzuzu na wale wasichana lakini bado anazidi kuja karibu na sisi, shenzi sana huyu. Wewe fanya kazi yako ila atajua miye Mondia ni nani” Sauti hiyo ililoloma kwa hasira.

    “Pumbavu sana huyu Jacob, kazi inaelekea mwisho nay eye ndiyo anajitia kimbelembele ila atadhibitiwa tu” Alisikika ila safari hii alionekana kuwa akijisemea mwenyewe. Kimya kilipita huku Jacob akiwa pale dirishani anatafakari. Akakata shauri aingie ndani kumuhoji yule muheshimiwa. Hakutaka kumsumbua yule askari, lakini aliona hakuwa na namna. Aliangaza macho yake huko na huko kasha kaliona kopo likiwa jirani na mti wa mpapai. Aliliendea na kulipiga teke kasha akaenda kujibanza kwenye nguzo aliyokuwa amejibanza awali wakati yule askari alipokuwa anapita. Muda si mrefu alisikia vishindo vya mtu akiwa anakuja, safari hii yule askari alipofika usawa wa pale alipokuwa amesimama Jacob, Jacob alimtanika yule askari kiganja cha shingoni, akaanguka chini bila ya kutoa kelele yoyote. Jacob alitembea hadi upande wa mbele wa nyumba, kwa kutumia funguo zake Malaya au wazungu husema master keys aliweza kufungua na kuingia ndani. Japo alijua chumba cha mhesimiwa kilikuwa upande gani lakini ilimchukua dakika kadhaa kuweza kukifikia kile chumba kutokana na jinsi ile nyumba ilivyokuwa imejengwa. Vyomba vingine vyote vilionekana kutokuwa na watu. Hilo lilimshangaza Jacob kwani achilia mbali kuwa ilijulikana kuwa mheshimiwa Mondina alikuwa na familia, lakini kwa kawaida ya familia za kiafrika ndugu akisha kuwa na uwezo sehemu kubwa ya jamaa yake huamia kwake na kuishi hapo hatan kama hawana mpango wowote. Kitendo cha jumba hilo kuonekana kutokuwa na mtu mwingine kilimuachia maswali mengi. Alipofika chumba ambacho alihisi ndicho hasa cha Mondia, Jacob alishikira vizuri bastola yake, akaugusa mlango akakuta uko wazi. Aliusukuma taratibu kwa kidole cha kati kasha akatanguliza mguu wa kulia kwa mtindo wa kuusukuma taratibu. Hakuwa anataka kumdhuru Mondia ila alitaka kumhoji ili amweleze kuhusu huo mpango ambao mzee Vicent aliusema. Ilionyesha wazi kuwa mzee Vicent alishajua kuwa Mondia anahusika ndiyo maana akamwachia Jacob ule ujumbe. Jacob alichungulia ndani, hakutaka kumpa nafasi Mondia ya kuwa na kutumia bastola yake kitendo ambacho kingesababisha makelele na majirani kuita polisi. Hivyo alitaka amuwahi na kumketisha kitako ili kwa ustaarabu au kwa nguvu aseme anachojua. Jacob alichungulia ndani, macho yake kwanza yalitua kitandani ambako hakukuwa na mtu, lakini pia yakavutwa na kitu sakafuni. Alipoangalia vema kaona kitu kama maji ila yenye rangi nyekundu yanatambaa sakafuni. Damu, Jacob alitahamaki, akaingia ndani kwa haraka, hakuchelewa kuuonamwili wa mheshimiwa modnia tayari ukiwa maiti. Alitoka nje haraka na kuanza kutafuta yeyote ambaye angekuwa amefanya kitendo kile. Alizunguka kila mahali lakini hakuona chochote. Alirudi ndani na kuanza kupekua kama angeweza kupata taarifa yoyote, lakini pamoja na utaalamu wake wa kupekua hakufanikiwa kupata chochote. Akiwa maekata tamaa, alitembea taratibu kuondoka mule chumbani. Alipokuwa amefika upande mwingine wa nyumba hiyo ambako kulikuwa na vyumba vingi pia, mara akasikia kitu kinaunguruma, aliposikiliza visuri akagundua muungurumo ulikuwa unatokea uapnde aliokuwa ametoka.akarudi aharaka upande ule, mlio ulikuwa unatoke chumbani kwa Mondia amabye sasa alikuwa marehemu. Aliingia chumbani, aksikiliz tena, mara moja akainama uvunguni, akaiona simu iliyokuwa inauguruma bado. Alipoishika ndipo ikaacha kuunguruma. Aliichukua ile simu. Akaangalia namba ya mpigani akakutana na neno “private number”. Akifutika mfukoni, kasha akatoka zake. Alipofika je alienda, upande ambao aliruka ukuta kuingilia. Wakati anajiandaa kuruka mambo mawili yalitokea. Alisiki yule askari akipiga kelel hovyo hku akikimbia kuelekea ndani. Wakati huo huo akaona “amazon cat” akipita kwa kasi kukimbilia upande mwingine wa jumba hilo.

    “Shiiiiit Kiroboto” Jacob alisema kisha akaparamia ukuta kama paka akaruka na kutua upande wan je wa ukuta akatokomea zake. Alijua ameshachelewa, Kiroboto alikuwa ameshamaliza kazi asingekuwa maeneo hayo muda huo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ****



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog