Search This Blog

Friday, 20 May 2022

WAKALA WA GIZA - 4

 







    Simulizi : Wakala Wa Giza

    Sehemu Ya Nne (4)



    NDANI YA IKULU

        Rais Zuber tayari alikuwa ameshachanganyikiwa kwa jinsi wanajeshi hao walivyokuwa wameizunguka Ikulu pasipo kuacha nafasi hata ya  mtu aliyemo humo ndani kutoka nje bila kukamatwa, yote aliyokuwa akiyapanga humo ndani ilivuja kwa muda mfupi tu na kumfikia L.J Ibrahim ambapo alizidi kuchanganyikiwa kuhusu suala hilo. Harufu ya usaliti tayari ilianza kumzonga kwenye pua zake hadi kichwa kikawa kinamuuma, tayari alishaanza kuhisi kuwepo kwa msaliti humo ndani ya ikulu aliyekuwa akifanya mambo yote yawe mabaya. Jambo hilo lilimtatiza  sana na ndani ya muda mfupi aliitisha kikao cha wote waliomo huko ikulu kuanzia wanausalama na hata ADC, akiwa mwenye sura ya kuchanganyikiwa  hakuweza hata kuweka kalio  kwenye kiti muda wote alikuwa amesimama akiwatazama wote wa eneo hili.

                   "mnaweza kunipa maelezo ya hichi ninachowauliza?" Rais Zuber aliongea kwa nguvu, wote walikaa kimya wakwa wanamuangalia kwa umakini.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

                    "nahitaji kumjua mtu anayevujisha habari kati yenu hapa, haiwezekani mipango yote niliyoipanga asubuhi hii igundulike upesi tu kwa Ibrahim. Nani msaliti kati yenu!?" Rais Zuber aliuliza kwa hasira sana, akiwa anawatazama wale maofisa wa usalama wa taifa pamoja na mmoja wa jeshi simu yake ya mkononi iliita muda huohuo. Alipoangalia jina la pigaji alikuwa ni L.J Ibrahim, aliipokea simu hiyo na akaiweka sautu kila mtu akawa anaisikia.

                     "Ha! Ha! Ha! Ha! Zuber naona unahangaika kumtafuta msaliti sasa hivi siyo, haitasaidia kitu!" Simu hiyo ilikatwa na hasira zilimzidi sana Rais Zuber akaingiza mfukoni akatoa simu nyingine alibonyeza namba moja tu akaiweka sikioni akaongea, "njoo haraka chumba cha mkutano na vifaa vyako vyote".

        Aliwaangalia wanausalama wote wa humo ndani kisha akauliza, "simu zote mmeziacha nje sasa nani ana kinasa sauti humu ndani?

         Swali hilo liliwafanya wanausalama wote waanze kutazamana mmoja baada ya mmoja lakini hakuna aliyetoa jibu kumjibu, hasira zaidi zilimpanda Rais Zuber hadi akawa anahema kwa nguvu sana huku akiwatazama wanausalama hao ambao walikuwa  waaaminifu kwa kipindi chote alichokuwa nao. Siku hiyo baada ya kupokea simu kutokka kwa L.J Ibrahim ikimkejeli kwa mpango wake aliuongea muda huohuo, hapo ndipo alijua kuwa kuna mtu alikuwa akisababisha L.J Ibrahim ajue yote hayo kupitia kinasa sauti ambacho hakujua mtu huyo alikuwa amekiweka mahala gani. Kila aliyekuwa akimtazama uso wake haukumpa shaka naye na hapo ndipo alizidi kupagawa hakujua nani alikuwa amehusikana huko kuvujisha taarifa zake, aliwatazama watu wote na hatimaye macho yake yakatua kwa ADC wake aliyekuwa amevaa sare za kijani za jeshi la wananchi akiwa mtulivu sana asiyeonekana kama ana hofu yoyote  katika uso wake. Alimnyooshea kidole ADC huyo aliyekuwa akitembea naye katika sehemu mbalimbali akiwa nyuma yake na alikuwa ni mmoja kati ya watu aliokuwa akiwaamini, akiwa na uso wake wenye shaka juu yake alimuashiria asimame naye akatii na kusimama kisha akatoa saluti.

                       "Sina haja ya saluti yako, niambie kwanini unavujisha mambo kumpelekea msaliti wa taifa hili? Tangu uingie wewe asubuhi hii ya leo ndiyo siri zetu humu zimekuwa zikivuja. Sasa niambie kitoe kinasa sauti au aje mhusika akinase kilipo" Rais Zuber aliongea huku akimtazama ADC wake aliyekuwa amesimama kikakamavu akiwa anamtazama.

                        "Kamuti hatuna mwanajeshi mwingine humu ndani zaidi yako sasa nataka nijue ulipita vipi wanajeshi hao waliokuwa wameizunguka Ikulu nzima hadi ufike hapa kama hawakuwa wamekutuma toa kinasa sauti chako upesi" Rais Zuber aliongea  kwa kufoka, muda huohuo mlango ulifunguliwa na mtu mwenye suti nyeusi akiwa amebeba  kitu mfano wa fimbo aliingia humo ndani a. Rais Zuber alipomuona huyo mtu alitoa tabasamu la kihasira kisha akasema, "anza na ADC".

            Mtu huyo alimsogelea ADC  akamuamuru anyooshe mikono naye akatii bila shuruti yoyote, alimpitishia hiyo fimbo ambapo ilito sauti katika kila sehemu kutokana na kuwepo kwa vyuma na madini ya fedha juu ya nguo zake. Aliipitihsa mashine hiyo hadi miguuni lakini hakukuwa na cha ziada kilimchotoa sauti, baada ya kumaliza aliitazama fimbo yake hiyo iliyokuwa na kioo maalum kama cha saa ya mkononi na hakukuwa na dalili ya uwepo wa kinasa sauti chochote mwilini mwake.

                        "Mheshimiwa hana chochote zaidi ya vifungo, vyeo, nishani na mkanda ambavyo ndiyo vimefanya mashine hii itoe sauti" Alijibu huku akikisoama kioo cha kifimbo hicho alichoingia nacho. 

                        "Haya kila mmoja anyanyukea apekuliwe" Rais Zuber alitoa amri na wote wakatii wakaweka silaha zao mezani wakapekuliwa lakini hakikupatikana kinasa sauti hicho, hapo ndipo alipozidi kuchnganyikiwa  akawa hajui nini cha kufanya.  Aliwatazama kila mmoja lakini nafsi yake ilishindwa kumjua aliykuwa anahusika na hio suala, wakati akiendelea kujifikira umbile la mtu aliyekuwa amevaa amgwanda ya kijeshi alionekana akitoka ndani ya uvungu wa meza hiyo kwa taratibu sana na kwa maringo. Wanausalama wote walichukua silaha zao na wakamuelekezea kwa haraka sana, mtu huyo ambaye alikuwa amevaa kofia ya kijeshi iliyofunika uso wake kwa asilimia nyingi alitoka taratibu tena kwa maringo.

                       "Tulia hivyohivyo" Wanausalama wote waliongea huku wakimnyooshea silaha zao.



    ****



          Baada ya kuwapiga chenga mbaya wanajeshi waliotuma na M.J Mugiso, Norbert aliamua kutoka hadi maeneo ya Posta mpya akitumia njia za mkato mbalimbali ambapo alitumia mwendo mfupi akawa ameshafika. Alizunguka nyuma ya benki ya CRDB mtaa wa Azikiwe  kwa kupitia katikati ya sheli ya mafuta ya mfuta iliyopo pembezoni mwa benki hiyo, alipoimaliza sheli hiyo alivuka barabara kisha akafuata njia inzyoelekea ilipo shule ya sekodari ya wasichana ya Kisutu. Alitembea kwa umbali mfupi tu kisha akaingia kwenye lango la eneo lililokuwa limezungushiwa mabati lilipo pembezoni mwa barabara hiyo.

         Alitokea kwenye eneo lenye magari mengi yaliyokuwa yameegeshwa kwa mpangilio maalum, hapo alitembea hadi usawa wa mwisho wa eneo hilo ambapo kulikuwa na gari lake alilokuwa amekuja nalo eneo hilo. Alipolikaribia gari lake hilo alijipekua mfukoni kwa lengo la kutoa funguo lakini alisita baada ya kukitazama kioo cha giza kilichokuwa kwenye gari, alijirusha pembeni kwa haraka baada ya kuona kile alichokuwa amekiona kwenyekioo cha  gari hilo kikiwa nyuma yake. Kitendo cha yeye kutoka eneo hilo kwenye gari lake kulitokea tundu la haraka sehemu ya chini kidogo ya kioo, Norbert alipotua chini baada ya kujirusha alijibiringisha kuelekea chini ya magari mengi yaliyokuwa yameegeshwa kwa ustadi mkuba halafu akatulia akawa akitazama eneo ambalo lipo gari lake.

        Aliwashuhudia Santos na Benson wakifika haraka eneo hilo wakiwa bastola zilizofungwa viwambo vya kuzuia  sauti kila mmoja. Walipofika hapo kila mmoja alikuwa akitazama pembezoni ya gari hilo na magari mengine lakini hawakufanikiwa kumuona Norbert, waligawana kla mtu upende wake kwenda kumtafuta Norbert kisha wakaanza kutembea kwa taratibu huku risasi zao wakiwa wamezielekeza  mbele kwa tahadhari. Norbert alikuwa akiwatazama kila mmoja upande aliokuwa ameelekea ndipo na yeye akafungua kiatu  akatoa bastola ndogo ambayo huwa anaichomeka kwenye kiatu chake, alifungua na soksi yake akatoa kiwambo cha sauti ambacho alikifunga kwenye bastola hiyo.

        Alipomaliza  alitambaa hadi  mwisho wa uzio wa mabati wa eneo hilo palipokuwa kuna gari aina ya toyota landcruiser ikiwa imeegeshwa. Alijiinua kwa haraka akajibana pembezoni mwa  gari hilo kisha akatulia tuli bastola akiwa ameshika kwa tahadhari sana, alijibana eneo kwa muda hadi aliposikia mlio wa kukanyagwa kwa chupa ya plastiki ya maji ndipo akachungulia kule ulipotokea mlio ule. Machoyake yliweza kumshuhudia Benson akiwa anaelekea usawa wa lango la kuingilia eneo hilo akiwa amempa mgongo, Norbert kwa kasi ya ajabu alimuelekezea bastola yake na akaruhusu risasi mbili ambazo zilitoka zikaenda kutua mapaja ya Benson.

                    "Aaargh!" Benson aliachia ukelele wa maumivu akaenda chini moja kwa moja huku akiwa ameshikilia sehemu za uvunguni mwa mapajani mwake baada ya risasi hiyo kutua kwenye mfupa wake, ukelele huo ulimfanya Santos ajitokeze hadi pale alipo Benson akamkuta akiwa anatokwa damu nyingi miguuni.

           Kujitokeza huko naye alikuwa amefanya kosa kwani  eneo hilo Norbert hakuwa ameondoka alilokuwa hapo awali, alikuwa akimshuhudia jinsi anavyohangisha macho yake kutazama kila pande kumtafuta lakini hakuwa amemuona baada ya Norbert kujibana palepale alipokuwa awali.  Santos akiwa anashangaa hali ya Benson alirudiwa na akili ya  kujihami ajikinge na adui yake lakini wakati anarudiwa na akili hiyo tayari alikuwa ameshachelewa kwani Norbert aliikoholesha bastola yake ikatoa risasi ambayo ilienda moja kwa moja na kupiga bstola aliyokuwa ameishika, Santos alipoangalia mahali ilipotokea risasi hiyo hakumuona mlengaji yeyote kwani Norbert tayari alikuwa ameshajibana tena katika eneo alilokuwepo awali.

          Santos alisimama hapohapo akiwa hana la kufanya baada ya bastola yake kumuanguka mitaa kadhaa kutokana na nguvu ya bastola ya Norbert kuisukuma mbali, aliganda hivyo kwa muda mfupi na alipoona kimya alipiga hatua moja kuifuata bastola hapo ndipo akaganda na hatua hiyohiyo moja hakuongeza ya pili baada ya mchanga kutifuka mbele ya mguu wake. Alijua moja kwa moja ilikuwa ni risasi ile imekita ndani ya udongo na ilikuwa ni onyo asiendelee kupiga hatua zaidi, aliganda hivyohivyo kama alikuwa amegandishwa baada ya mkanda wa video kusimamishwa na muangaliaji.

                 "Geuka nyuma" Sauti ya Norbert ilimpa amri lakini hakuitekeleza mara moja akabaki akiwa amesimam vilevile, Norbeert hapo aliikoholesha bstola yake risasi ikatua kwenye ardhi  katikati ya miguu ya Snatos.

        Hapo Santos aligeuka nyuma akawa anatazamana na Norbert kwa umbali wa mita kadhaa, usawa wa bastola wa Norbert ulikuwa umemuelekea yeye ambapo angefanya kosa lolote basi basi bastooa hiyo ingekohoa kikohozi kingine na kummaliza moja kwa moja.

                 "PIga hatua kumi na tano mbele" Norbert aliongea pasipo kumjali Benson aliyekuwa ameishiwa nguvu akiwa amejilaza na bastola ikiwa ipo pembeni, Santos alipiga hatua hizo kumi na tano alizoambiwa akawa amefika umbali ambao ulikuwa ni wa takribani mita moja kutoka aliposimama.

         Baada ya kufika umbali huo ambao ulikuwa jirani kabisa na Norbert alibaki akiwa ameganda vilevile akimtazama, hapo Norbert alishusha bastola yake akaichomeka nyuma ya suruali yake kisha akamtazama Santos huku akiwa ametabasamu usoni mwake. Santos iliposhushwa silaha hiyo aliona ndiyo nafasi pekee ya kuitumia, alijifyatua kwa haraka akaja na mateke mawili ambayo yalimpata  Norbert akaenda moja kwa moja chini.

                 "Nyanyuka pusi mweusi wee!" Santos aliongea akimtazama Norbert ambaye pamoja na kupigwa na mateke hayo alikuwa akitabasamu tu, Norbert alijifyatua kiufundi akasimama wima kisha akasimama kizembe kabisa huku akimuita Santos aje ambaye hakusogea badala yake alimtazama Norbeert mkwa umakini akawa anapiga mahesabu ya jinsi ya kumkabili. Akiwa anamtazama Norbet kwa umakini akipanga jinsi ya kumkabili alijikuta akikunja sura kwa nguvu baada ya Norbert kumuonesha kidole cha kati, Santos hapo uvumilivu ukamshinda na alipiga mateke mengine ya miguu miwili lakini safari hii yaliambulia patupu baada ya Norbert kuhama pembeni kwa kasi kubwa.

                   "Usitegemee lile pigo la kimama niilokuachia litanipata tena" Norbert alisema huku akikaa kimapigano halafu akawa anamtazama  Santos ambaye alikuwa amejiweka sawa akimtazama Norbert kwa hasira.

         Mpambano baina yao uliwekwa na wote walikuwa wakipigana kwa umakini mkubwa sana, Santos alimfuata Norbert kwa kurursha ngumi mfululizo ambazo zote zilipiga hewa kwa jinsi Norberty alivyokuwa akizikwepa. Aliendelea kurusha mateke ya nguvu ambayo yalipanguliwa na Norbert ambaye hakuwa ameshambulia hata mara moja, Santos alitumia uwezo wake wote wa kupigana katika kuleta mapigo mbalimbali lakini  hakuna hata moja lililompta Norber zaidi ya yote kuishia kwenye hewa. Alibadili mfumo wa kiupiganaji akawa anatumia judo katika kupigana lakini yote haikufua dafu dafu kwani Norbert naye alikuwa akiifahamu judo vyema na aliingia kwa judo naye katika kuizuia judo, mtindo wa judo wa kuangushana Santos alitumia lakini haukufua dafu hata kidogo katika kupambana na Norbert.

       Alipomshika Norbert na kumuangusha  nayeye alifuata chini kwani Norbert naye alimshika wakanguka wote, walikuwa wakibingirishana chini katika eneo hilo. Muda huo wakiwa wanapigana hapo Benson ambaye alikuwa ameishiwa nguvu baada ya damu nyingi kumtoka alifumbua macho kwa shida akawa anatazama  kule ambapo  mwenzake anapambana na Norbert, ukungu mzito ulikuwa umetanda kwenye macho yake lakini alipoweza kumuona Norbert kwa mbali alinyanyua bastola yake ili amlenge aweze kulipa kisasi cha ndugu yake.

        Benson alifyatua risasi muda ambao Norbert na Santos walikuwa wakibingirishana pale chini baada ya Norbert kuwa upande aliolenga, risasi yake alipokuwa anataka kuifyatua tu Norbert tayari alikuwa ameshaiona. Norbert alifanya tendo la haraka kwa mbinu ya mchezo wa judo akamgeuza Santos upande aliokuwa yeye ambapo risasi hiyo ilifumua kichwa cha Santos papo hapo, huo ndiyo ukawa mwisho wa Santos na Benson alipoteza fahamu papo hapo. Walimuacha Norbert tu ambaye alisimama wima kisha akajikung'uta vumbi hadi lilipopungua kwenye nguo zake ambazo bado zilikuwa ni chafu ndipo alipomsogelea Benson pale alipokuwa amezimia, alimtazama Benson kwa dharau kisha akamkanyaga na soli za kiatu chake kooni akammaliza kabisa. Aliondoka hadi kwenye gari lake akaingia ndani akawasha na kuondoka eneo hilo kwa kasi asiweke ushahidi zaidi, nyuma aliacha masalia ambayo  ni pigo sana kwa kina L.J Ibrahim.



    ****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



        Mwanajeshi yule aliyotoka chini ya meza alivua kofia yake taratibu pasipo kujali  amri ya wanausalama hao wanaomlinda Rais, alipoivua kofia wote kwa pamoja waliiona sura ya Moses akiwa anatabsamu tu mkono mmoja akiwa amekunja ngumi. Wanausalama walipomuona ni Moses  walishusha silaha zao kasoro mmoja tu ndiye aliyekuwa akimnyooshea silaha yao huku akimtazama kwa wasiwasi mkubwa sana, Moses alimtazama mwanausalama huyo kwa sekunde kadhaa kisha akakunjua ngumi aliyokuwa ameikunja akatoa kinasa sauti akamrushia rais Zuber ambaye alikidaka akabaki akimtazama kwa wasiwasi.

                  "Muulize huyo aliyeninyooshe silaha huku wenzake wakiwa wamezishusha kuhusu hiyo hardware, kwanini aitupe chini ulipogundua msaliti yupo humu" Moses aliongea huku akimtazama mwanausalama huyo aliyekuwa amemnyooshea silaha, Rais Zuber alipatwa na mshangao wa ghafla akabaki akimtazama Mwanausalama huyo aliyekuwa akimuamini kupitiliza.

                    "Mheshmiwa jana nilipoaga kuwa naondoka sikuondoka bali nilirudi hapa kwa siri kwa msaada wa mtu mmoja tu miongoni mwa vijana wa wangu waaminifu, msaliti wako ni huyo hapo Kamudu" Moses aliongea.

                     "What! Kamudu msaliti ni wewe!" Rais Zuber aliongea kwa mshangao alkini alijikutra akinyoosha mikono juu haraka baada ya Kamudu kumuelekezea bastola yake aina ya revolver yenye uwezo mkubwa sana, watu wote waliomo humo ndani nao walitoa silaha zao wakamuelekezea Kamudu. Kamudu aliishikilia bastola hiyo kisha akamtazama kila mmoja aliyekuwa amemuolekezea bastola, alimeza funda moja la mate kisha akakaza mikono yake barabara na kidole kkwa kimeshika kifyatulio.

                      "Fanyeni ujinga na mimi nifanye upumbavu!" Kamudu aliongea kwa hasira huku midomo yake ikimcheza.







                  "Ohoo hamjanielewa siyo, shusheni silaha zenu na mtoe magazine nje mzimwage risasi zote la si hivyo  napasua kichwa chake huyu"  Kamudu aliongea kwa nguvu hadi mishipa ya kichwa ikawa inamtoka, wanausalama wote hawakuwa na sababu ya kupinga sharti hilo.

       Wote kwa pamoja walishusha silaha chini kisha wakatoa vibeba risasi ambavyo walivifungua wakamwaga risasi zote mezani hapo na bastola wakaziacha mezani hapo.

                 "rudini nyuma hatua tano kila mmoja kutoka hapo kwenye meza" Kamudu alitoa amri nyingine, wanausalama hao wakafanya kama walivyoambiwa na lakini Moses hakunyanyua mguu wake kurudi nyuma aliendelea kusimama palepale alipokuwepo awali.

                "Professa ndiyo husikii siyo" Kamudu alimfokea Moses huku akikaza kidole chake katika sehemu ya kufyatulia risasi, hilo halikumtisha Moses hata kidogo yeye ndiyo kwanza alitabasamu kama alikuwa hajaelewa kile alichoambiwa na aliketi kwenye kiti.

       Hali hiyo ilimshangaza kila mmoja hata rais mwenyewe ambaye uhai wake uikuwa ukihitajka kwa gharama yoyote ile, wote walibaki wakimtazama kwa mshangao kwani ilikuwa ni kinyume cha kazi yake ya kuhakikisha mheshimiwa hadhuriki akiwa yupo karibu naye. Kupinga jambo hilo haikutarajiwa hata na Rais Zuber mwenyewe ambaye alichoka kabisa akaona Moses alikuwa hamtakii mema, alishajikatia tamaa ya kutoka hai ikiwa Moses alikuwa akipinga amri hyio. Alibaki akiikodolea macho bunduki aina ya revolver kubwa ambayo Kamudu alikuwa ameishika akiona siku zake za kupumua zilikuwa zikihesabika kutokana na ukaidi wa Moses, alifumba macho yake mwenyewe huku akisubiri muujiza utokee wa kupona ama apigwe risasi ya kichwa.

                     "Moses fanya kama anavyokuambia tafadhali" Rais Zuber alimuambia Moses akiwa amefumba macho, Moses alitabasamu tu na hakutii jambo alilokuwa ameambiwa na amiri jeshi mkuu wa majeshi ya uliznzi na usalama.

                      "Mheshimiwa muache apasue tu kichwa chako kama ana uwezo wa kufanya hivyo lakini humu hatoki" Moses aliongea huku akiegemea mgongo wa kiti mikono akiwa amefumbata kifuani mwake.

                      "Professa  unasema nini wewe" Kamudu aliuliza kwa mshangao sana baada ya kusikia maneno hayo ambayo hakuyatarajia kuyasikia.

                 "Mpige risasi sasa unasubiri nini ila sifanyi kama uanvyoniambia" Moses aliongea, Kamudu aliposikia maneno aliona liwalo na liwe.



         Aliamua kuminya kifaytulio cha risasi akitarajia mlipuko wa bastola ndiyo utasikika lakini aliambulia kusikia mlio wa vyuma  vya ndani ya bastola tu, alishtuka haswa baada ya kusikia hivyo na aliamua kuminya tena kifyatulio hicho cha bastola lakini mlio ulikuwa ule risasi haikuwa na kitu. Hapo Moses ndiyo alicheka zaidi huku akimtazama Kamudu kwa dharau kuu, Kamudu alijikuta akiishiwa mbinu na akaona njia nzuri ilikuwa ni kumrukia Rais Zuber na kumkaba ndiyo angeweza kusalimika na balaa hilo.



        Wakati akiifikiria mbinu hiyo tayari Rais Zuber alishatoka mbio mahali alipokuwa amesimama akazunguka meza hiyo kwa upande mwingine akakimbilia eneo alilokuwa yupo Moses,  mpango wa Kamudu ulifeli papo hapo kutekelezeka kwani wanausalama wenzake waliruka kwa haraka kutoka eneo walilokuwepo wakamdaka na kumbana mikono wakamlaza  chini kwa nguvu. Walimbana mikono kwa nguvu hadi akawa amefumba macho kwa maumivu, muda huo ndiyo Moses alinyanyuka kwenye kiti alichokuwa amekaa akatumbukiza mkono wake kwenye mfuko wa kombati lake la kijeshi.

        Alitoa risasi  kumi na mbili akazimwaga mezani kisha akatabasamu, alisogea pembeni ya meza kwenye kiti hiyo kisha kajongea hadi eneo ambalo Kamudu alikuwa ameshikiliwa barabara na vijana wake waaminifu. Moses alipomfikia alichuchumaa mita kadhaa kutoka pale alipolazwa chini kifudifudi kisha akatabasamu kama kawaida yake, alimtazama mwanausalama yule msaliti kwa jinsi alivyokuwa ameuma meno kwa maumivu baada ya kubanwa mikono kwa mbinu hatari ya judo.

                     "Kamudu kosa kubwa ulilolifanya ni kweka bastola yako mguuni, ukarudia tena kosa kwa kuweka kinasa sauti chako sambamba na mkanda wa suruali wako.

       

       Ukafanya kosa jingine kukaa hapa kwenye kwenye meza suruali yake ikapanda juu bastola nikaiona, ukafanya tena kwa kwa kukitoa kinasa sauti na kukitupa chini kijanja zaidi uliposikia mheshimiwa akiulizia mwenye kinasa sauti. Hapo nilikujua wewe ni msaliti njkaitoa risasi hiyo bastola yako bila ya wewe kujua halafu nikakizima hicho kinasa sauti" Moses alimuambia jinsi alivyofanya mpango wote ambao ulidhoovisha mbinu yake ya kutaka kutoroka, maneno hayo yalimfanya Rais Zuber atoe tabasamu usoni mwake baada ya kuona alikuwa na vijana makini sana waliokuwa wakihakikisha usalama wake unakuwa sawa kwa usiku na mchana.

                  "Nakuambia Moses mshachelewa nyinyi alhamisi leo jua kesho kutwa jumamosi  jeshi lililopo hapo nje linaingia humu ndani kumtoa huyo unayemlinda" Kamudu aliongea kwa hasira.

                   "Labda niwe mfu Kamudu, jeshi la nchi na anga lipo upande wetu tuone hao wa majini watavamia kwa nguvu ya namna gani ikiwa majeshi yote ya  anga na nchi kavu bado yapo chini ya  Amiri jeshi na Meja jenerali Belinda" Moses aliongea akimsikitikia Kamudu.

                   "Na bado tu huyo atatoka humu aingie mzee Philbert Ole siku ya jumamosi" Kamudu  aliongea kijeuri zaidi.

                   "Ohoo ndiyo mliomtorosha siyo sasa tunaanza na wewe utakuwa mfano, mpelekeni chini huyo" Moses alitoa  amri na Kamudu alinyanyuliwa kwa nguvu akatolewa humo ndani na wanausalama wakabaki ADC na Rais Zuber pekee tu. Moses alipokamilisha amri hiyo alikakamaa mbele ya Rais Zuber kiheshima.

                     "Well done my boy, nafurahi kuwa na mtu kama wewe" Raiis Zuber alimpongeza Moses ambaye alitoa tabasamu tu.



    ****



        Subira huvuta heri lakini ikizidi muda mwingine heri kusubiri hutakuwa tayari, ngoja ngoja siku zote huumiza matumbo ingawa harakahraka haina baraka. Ndivyo ilikuwa kwa kwa kundi la Mzee Ole tangu walipotoka Santos na Benson kwenda kumsaka Norbert hawakuwa wamerudi hadi muda huo, waliweka subira ii wavute na lakini heri hiyo waliyokuwa wakiisubiri  ilikuwa mbali. Wakangoja vitoke vizuri kwa kuwatuma hao lakini kungoja huko kuliwachosha kabisa, hawakufanya haraka katika kungoja huko lakini muda unavyo zidi ndipo walipozidi kuwa na harak zaidi  ya jambo walilokuwa wakilingojea litimie. Muda nao ulikuwa haugandi ulizidi kuyoyoma pasipo Benson naSantos kutokea eneo hilo, walisubiri wakachoka na hatimaye wakavunja amri ya kutowapigia simu wapigiwe wao kazi ikiwa kamli.

       Walipopiga simu zao zilikuwa zikiita sana pasipo kupokelewa jambo lililozidi kuwatia hofu wote wawili, kutopokelewa kwa simu hizo kulisababisha Thomas  na Wilson waitwe na waambiwe juu ya hali hiyo iliyojitokeaza ghafla ambayo wao walikuwa hawaielewi. Hawakujijua kwamba walikuwa wamesalia watu watu watano na wawili tayari walikuwa wameshamalizwa na Norbert, kwa haraka zaidi wao waliagizwa kwenda kuwafuatilia wenzao. Thomas na Wilson walikwenda  hukuwakitumia programu ya simu ya kusaka simu za wenzao zilipo.

       Thomas akiwa na Wilson walifuata uelekeo wa simu hizo ambao uliwapeleka moja kwa moja hadi kwenye  uzio wa mabati ambao ulikuwa ukitumiwa kuegeshea magari ya wafanyakazi mbalimbali wa kampuni zilizopo katikati ya mji wakiwa wanaelekea maofisini , hapo alikuta umati mkubwa wa watu ukiwa nje ya uzio huo huku sehemu ya lango la uzio huo kukiwa na utepe pamoja na maaskari waliokuwa wapo kwenye sare. Iliwabidi waegeshe gari mbali na hapo kisha wakaenda kukaa kwenye kibanda cha fundi viatu ambapo walikuwa wamejikusanya watu wakiwa wanjadili, walipokaa kwenye kibanda hicho walijifanya hawajuani kabisa ambapo Wilson alikaa pamoja na kundi hilo la watu na Thomas akaenda kukaa jirani na fundi viatu ambapo watu walimpisha kutokana na rangi yake. Thomas akiwa ni mzungu pekee kwenye kundi hilo alivua viatu vyake kisha akamkabisdhi fundi viatu ambaye alivichangamkia kwa haraka, Wilson alijiingiza kwenye kundi la watu kama mpita njai ambaye alikuwa akitaka kujua kilichotokea eneo.

                  "jamani mimi mpita njia kuna nini hapa mbona askari wengi?" Wilson baada ya kufika kwenye hio kundi la watu.

                  "Dah kaka nchi hii imeisha ndugu, si watu wawili wameuliwa humo ndani mmoja ni mzungu fulani ana nywele ndefu mwingine black" Kijana mmoja alimuambia Wilson.

                   "duh nchi yetu inapoelekea sipo" Wilson alijifanya kushangaa lakini moyoni alikuwa akihisi tayari washapoteza wenzao wawili.

                   "Yaani ikulu imezungukwa na wajeda leo hii na mengine yanatokea sijui mzungu wa watu alikuwa kawakosea nini hao wauaji, yaani doh nasikia wamefumua kichwa na mwenzake black kaharibiwa miguu kabla hajauliwa" Mwingine alidakia akijifanya kuijua zaidi habari hiyo kwa kutumia maneno ya kuambiwa.

                    "Ndugu zanguni sina amani ya kukaa eneo hili tayari mshanitisha" Wilson aliongea huku akijifanya kaogopa habari hiyo na aliamua kuondoka eneo hilo mara moja, alielekea moja kwa moja alipokuwa ameegesha gari kisha akaingia ndani ya agari akatoa simu yake akabonyeza baadhi ya namba akaiweka sikioni.

                      "Haloo kamishna nafikiri unayo ripoti ya watu wawili waliouawa leo hii.... sasa tulikuwa tunataka utuhakikiashie je hao ni Santos na Benson......sawa nasubiri" Wilson aliongea baada ya simu hiyo kupekelewa na Kamishna  Wilfred kisha akakata alipoambiwa asuburi, alikaa ndani ya gari kwa muda mfupi tu Thomas naye akarejea akiwa amegwaya kwa taarifa aliyokuwa ameisikia juu ya mauaji yale.



        Ingawa hawakuwa na uhakika nayo tayari mioyo yao ilishaanza kuingiwa na wasiwasi waliposikia wasifu wa watu hao waliouawa, waliamua kuwasha gari na kuondoka eneo hilo baada ya simu walizokuwa wakizifuatilia kuwa zipo katika eneo lenye polisi wengi sana. Walitumia njia ya mkato ambayo ilienda kuwapeleleka mahali ilipo barabara ya Bibi Titi Mohamed mita kadhaa kutoka Vilipo vyuo vya CBE na TPSC, hapo waliingia upande wa kulia wa barabara hiyo kulekea ilipo mahakama ya Hakimu mkazi KIsutu. Walienda kwa mwendo wa kasi sana kutokana na barabara hiyo kuwa tupu ambapo iliwachukua dakika tayari wakawa wameivuka mahakama ya Kisutu na sasa walikuwa wapo kwenye makutano ta barabara ya Bibi Titi, barabara ya Ally Hassan Mwinyi na barabara inayopita kwenye mtaa wa Ohio jirani kabisa na hoteli ya Serena. Wakiwa eneo hilo simu ya Wilson iliita kwa kutetemeka mfukoni mwake na ikambidi aipokeee kwani yeye hakuwa dereva wa gari hilo, Wilson kwa haraka aliipokea simu hiyo huku akimua cha Thomas akitenda haki kwenye usukani wa gari hilo.

                      "Ndiyo Kamishna......ndiyo nakusikiliza......unasema! Oh! Shit! Tukutane baadaye Msasani tuweze kujua jinsi ya kujipanga tena upaya yasiwe mabaya... Ok in the evening" Wilson alikata simu kisha akaweka mikono mashavuni mwake kwa taarifa aliyokuwa ameisikia kutoka kwa Kamishna, alimuangalia Thomas ambaye alikuwa akimtazama kwa jicho la kuibia ili asiweze kupoteze umakini akiwa barabarani kwani tayari mataa ya eneo hilo yalikuwa yamesharuhusu.

                      "Leta ripoti Nourther" Thomas alimuambia Wilson huku akibadilisha gia kutokan na  gari hiyo kutokuwa na mfumo wa gia wa moja kwa moja.

                       "Benson na Santos hatupo nao tayari, ndiyo hao waliouawa eneo lile" Wilson aliongea kwa sauti ya kinyonge sana kutokana na taarifa hiyo aliyoipata.

                       "Ooooh! Man! Norbert anatumaliza tu, nakwambia nikimtia mikononi mwangu namkata vipange vipande" Thomas aloongea kwa hasira huku akipiga  mikono yake kwa nguvu sehemu ya pembeni ya usukani wa gari hilo, hakutetereka kwa taarifa kiasi cha kushindwa kuliongoza gari vibaya ingawa taarifa hiyo ilikuwa ni pigo kubwa kwake kwa kuwapoteza watu muhiomu kama hao  kwenye kundi lao.



       Hatari ya N001 hakika alianza kuiona ni kubwa kuliko anavyofikiria na  wakiwa wamemuacha akiendelea kufanya anavyotaka basi ingekuwa hatari kwao zaidi, sasa aliona suala la kutumia akili zaidi kuliko nguvu katika kazi hiyo ndiyo lilikuwa likihtajka zaidi. Aliamini kama wakitumia akili basi N001 anaweza kuwa mikononi mwao kwa mara nyingine na na asiweze kuwatoroka tena, Thomas hakujua kama alikuwa ni mtu aliyekuwa anapigwa na baridi usiku na anakuja kukumbuka kuwa alikuwa ana shuka tayari mapambazuko yalikuwa yameshawadia. Jambo hilo katika kulifikiria kulitenda tayari walikuwa wameshachelewa kabisa katika kuendeleza mapambano na Norbert.



    ****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



        Baada ya kutoka kuongeza pengo jingine kwa kundi la L.J Ibrahim Norbert aliongoza gari lake hadi nyumbani kwa Norene ambapo aliliingiza ndani moja kwa moja hadi katika eneo la maegesho, alishuka akiwa hatamaniki kutazamwa na mtu msafi ingawa alikuwa bado anatamanika kupendwa na mwanamke aliyekuwa anampenda. Aliingia  moja kwa moja hadi ndani ambapo alipitiliza hadi chumbani, alitumia dakika kadhaa huko chumbani kwenye bafu la ndani kujisafisha kisha akatoka akiwa amevaa suti zingine akiwa hana tai safari hii. Alitoka hadi sebuleni halafu akapitia jikoni  ambapo alimkuta Norene akiwa anapika. Hapo Norbert alimkumbatia kwa nyuma Norene kisha akambusu shingoni mwake, aliendela kumfanyia uchokozi mwingine katika mwili wake kama ilivyo kawaida yake wakiwa pamoja.

                     "Nor shida yako niunguze tu naona, kwanza niambie mbona mapema huvyo na umebadili nguo ghafla au ushapita sehemu zako nini?" Norene aliongea huku akiendela kupika

                     "Swali la kurudi mapema inabidi nikuuulize hata wewe pia kwanini umerudi mapema, sehemu yangu ya kupitia ni hii tu ipi nyingine?" Norbert aliongea huku akiwa bado amemkumbatia Norene kwa nyuma.

                     "Mh1 Haya  mshindi wewe bwana, nimerudi mapema baada ya kupewa ujumbe wako na CE na si vinginevyo. Nimemkufuata kule ofisi yako mpya nimekukosa ndiyo maana nikaamua nipite nyumbani moja kwa moja" Norene aliongea

                      "haya niambie kibabu huyo ana jipya gani au ndiyo uzeeee umeanza kumpeleka vibaya" Norbert aliongea

                       "nafikiri hali iliyochafuka Magogoni umeiona ndiyo hiyo umeitiwa, yaani nimepiga simu yako mpaka nimechoka we umeizima" Norene aliongea

                       "Yaani acha tu huko nimetibua hali ya hewa ndiyo maana nimeizima kabisa nifanye kazi kwa ufanisi zaidi, also kuhusu hiyo ishu nipo pamoja na Belinda na Gawaza kabla hata hajaniambia naona itakamilika haraka iwezekanavyo" Norbeet aliongea

                      "Sawa mume wangu ila ujichunge tu  ukumbuke mimi na mwanao bado tunakuhitaji na hiyo kazi ni ya hatari sana" Norene alipoongea maneno hayo alikuwa na sura ya unyonge sana.

                      "worry out malikia wangu kama niliweza kuifanya kazi ya hatari ugenini nikaimaliza nitashindwaje kufanya hii nyumbani" Norbet alimtoa wasiwasi Norene huku akikaa kwenye meza nyembamba ambayo huwa inawekewa  vyombo na majiko wakati wa kupika.

                     "Ok unatoka kwanza au unasubiri msosi?" Norene aliuliza

                       "Ooooh! Kitamu kinapika vitamu nitatokaje wakati sijala vitamu vilivyoandaliwa na kitamu, sinyanyui mguu hapa mpaka nile vitamu"

                     "Mhh! We nawe kwa maneno sikuwezi kabisa"

                        "uandishi wa habari upo kwenye damu,  kuwa na maneno ni sawa na gari la taka kuwa na harufu"

                       "aha! Ha! Ha!  Ha! Ha! Ha! Mwanaume wewe sikuwezi"

                         "unaniweza sana ndiyo maana uliniweka sawa bila kuchezesha msuli wowote" Norbert alipoongea maneno hayo Norene alinyanyua mwiko kwa haraka akamtisha Norbert kumpiga nao, Norbert aliinuka kwenye meza hiyo akasogea kando upesi huku akicheka.

                         "Nyoo lione jogoo pori mkubwa  wee ndiyo unayowaza hayo tu jianaume wewe"

                       "sasa ulitaka niwaze yapi wakati hadi leo yananitia uchizi na ukiyazisha nitaanza kuokota makopo" Norbert alipoongea maneno hayo Norene alishindwa hata kugeuza uso wake kumtazam na aibu ya ghafla ilimuingia akabaki akitazama sufuria ambayo ilikuwa na maakuli yakiwa ynachemka huku mwiko ulioushika ukifanya kazi ya kugeuza maakuli hayo.



       Kimya kifupi kilitanda hapo jikoni wakati Norene akiwa ndiyo anamalizia kupika chakula hicho cha mchana, Norbert asliutumia muda huo kufungua simu yake ambayo alikuwa hajaigusa kutokana na kuwa ndani ya kazi ambayo haikumstahiki kuigusa simu hiyo. Baada ya muda mapishi yalikuwa tayari na na yalipelekwa kwenye meza ya chakula yakiiwa kwenye vyombo maalum, Norbert na Norene walipakua kila mtu sahani yake na walianza kula huku wakiwa wanatazaman tu kama ndiyo walikuwa wanaonana kwa mara ya kwanza. Kilikuwa ni chakula ambacho wote kwa pamoja walikifurahia kutokana na furaha waliyokuwa nayo katika uhusiano wao, walikula kwa taratibu sana kama walikuwa akitamani kisiishe kwa haraka kutokana na ladha iliyokuwepo ndani ya chakula hicho.

                  "Ama kweli Mungu amenipa bahati mja wake" Norbert aliongea huku akipeleka kjiko cha chakula hicho mdomoni, kauli hiyo alipoitoa iliambatana na tabasamu pana katika uso wake ambalo lilimfanya Norene amtazame kwa macho malegevu kabisa.

                   "Kanijalia mrembo mwenye kila sababu ya kuitwa mke bora kwangu na mama bora kwa mtoto wangu" Norbert aliongea maneno ambayo yalimfanya Norene atabasamu.

                   "Halafu Nor tutaendelea kuwa hivi mpaka lini unajua mama kanipigia simu anauliza kuhusu ndoa" Norene aliongea kwa kulalamika.

                    "Kila kitu mipango tu mama Jerry ngoja kibarua kiishe halafu tutaongea vizuri" Norbert aliongea muda huo tayari alikuwa ameshamaliza kula, alinyanyuka kwenye kiti chake akaenda mahali lilipo eneo maalum la kunawia mikono akanawa kisha akarudi mezani ambapo alimpiga busu Norene la shavuni.

                   "Wacha niwahi" Alisema akataka kuondoka lakini Norene alimkamata koti la suti akamzuia.

                    "Khaa!  Haraka gani hiyo we jogoo pori ndiyo  hata maji usinywe hebu rudi hapa" Norene  aliongea, Norbert hakuwa na pingamizi aliamua kururdi akachukua bilauri ya maji iliyopo hapo mezani akanywa kwa haraka kisha akaondoka kutoka nje.







    KAMBI YA NGERENGERE

    MOROGORO



        Kikao cha dharura kilikuwa kimeitishwa ndani ya chumba cha mkutano katika ya kambi hiyo ambayo ndiyo kambi kubwa ya  jeshi la anga pamoja na nchi kavu, maofisa wa juu ya kambi hiyo walikuwa wameitwa kwenye hicho na mkuu wa majeshi hayo yote mawili alikuwa ametoka jijini Dar es salaam mara moja kuja kufanya kikao na wakubwa wa kambi hiyo kutoa uamuzi wake uliohitaji ufafanuzi zaidi . M.J Belinda ndiyo alikuwa amewasili ndani ya kambi hiyo baada ya kupokea taarifa kutoka wakuu wa vikosi vya anga na ardhi waliopo chini yake katika kambi hiyo, alikuwa ameingia ndani ya kambi hiyo muda mchache tu uliopita akitumia helikopta maalum ya jeshi. Taarifa aliyoipata ndiyo ilimfanya aje kwa haraka katika kambi hiyo kuja kutoa uamuzi wake kwa wanaejshi hao waliopo chini yake, ilikuwa ni lazima aje kutoa taarifa hiyo.



        Alishuka ndani ya uwanja  wa ndege wa kambi ya Ngerengere ambao upo chini ya jeshi la wananchi wa Tanzania muda mfupi uliopita,  alipitiliza hadi ndani kwenye chumba hicho cha mkutano ambacho tayari wakuu wa kambi hiyo walikuwa wameshakaa wakimsubiri. Muda huo alikuwa tayari ameshapokea heshima zote kama mkuu wa vikosi vyote viwili kwa wanajeshi hapo, alikuwa amesimama katika kiti chake kilichokuwa kimekaa  kwenye upana wa meza yenye umbo la mstatili. Wanajeshi wote waliosalia walikuwa wamekaa kwenye viti vyao vilivyopangwa sehemu ya urefu wa meza ndefu ambayo ilikuwa ndani ya chumba hicho cha mkutano. Wote  macho yao yalikuwa yapo kwa  mkuu wao  aliyekuwa amekaa kimya baada tu ya kikao hicho kuanza humo ndani, alikaa kimya kwa sekunde kadhaa pasipo kusema chochote akitazama tu amaofisa hao wa ngazi za juu wa vikosi vya anga na ardhi.

                 "Nadhani hamjajua kwanini nimekuja kutoa uamuzi mwenyewe badala ya kuridhia tu kwa simu kuwa vikosi viende kuongeza nguvu katika kuizunguka ikulu kama mkuu alivyokuwa amewapa amri makamanda wangu wakuu wa vikosi hivi" M.J Belinda alianza kuongea

                  "ok kabla sijaendelea napenda  niwasikilize Bridagia Hugo kamanda mkuu wa jeshi la anga la Brigadia  Maswe kamanda mkuu wa jeshi la ardhini ndiyo niwape sababu ya mimi kuja kutoa maaamuzi mwenyewe. Ok Kamanda Hugo unakaribishwa" M.J Belinda aliongea kwa mara nyingine na alipomaliza aliketi kwenye kiti chake huku akiiweka vyema kofia yake nyekundu katika kichwa chake, mwanajeshi  mrefu aliyekuwa   cheo cha Brigadia jenerali ambaye alivaa sare za jeshi la anga zikiwa ni za rangi ya bluu iliyopauka alisimama akatoa saluti kwa M.J Belinda. Huyo ndiye alikuwa kamanda wa kikosi cha anga ndani ya kambi hiyo Brigadia Hugo.

                   "Mkuu nusu saa iliyopita nimepata taarifa ya kupeleka kikosi cha anga kombania tatu chenye ndege zilizo na silaha ziende kwenye basement ya dharura  iliyopo ndani ya Nyambizi amabazo wanazitumia kwa sasa jeshi la maji ili ziongeze nguvu katika kuizunguka ikulu kwani bado ilikuwa na silaha kubwa sana za kumuhami mheshimiwa ambaye niliambiwa ni msaliti, nilipopata taarifa ilinibidi nikujulishe kamanda mkuu mwenye kamandi kuu kabla sijachukua uamuzi wowote na ndiyo hapo nikakujulisha. Ni hayo tu" Brigadia Hugo aliongea kisha akaketi chini alipomaliza kuongea, mwanajeshi mwingine mwenye cheo brigadia ambaye alikuwa mtu mzima kiumri alisimama kisha akatoa saluti kwa M.J  Belinda. Huyo ndiye alikuwa Brigadia Jenerali Maswe.

                 "Mkuu muda huohuo anaouzungumza afande Hugo dakika kadhaa mbele yake yaani....dakika ishirini zilizopita nimepokea amri  kutoka kwa mkuu Ibrahim nitoe amri kwa Kamanda kikosi cha Mbagala  kipeleke kombania nne zikaongeze nguvu ya kumuondoa mheshimiwa rais Ikulu kwani bado silaha ambazo zinatumika kumuhami ndani ya ikulu zilikuwa na nguvu zaidi hivyo niliambiwa niongeze kikosi atoke mwenyewe kwa hiyari baada ya kuona amezidiwa kiuwezo na silaha zetu. Nikiwa askari niliyekuwa chini yako niliamua kutoa taarifa kwako mwenye kamandi kuu kwanza kabla sijachukua uamuzi wowote na ndiyo nikakupa taarifa hiyo, ni hayo tu" Brigadia Maswe aliongea kisha akaketi chini, baada ya wakubwa hao wa majeshi yote mawili waliopo chini ya M.J Belinda kuongea M.J Belinda alisimama kisha akatoa flash ya tarakilishi akaenda hadi kilipo kioo cha tarakilishi ndani ya chumba hicho cha mkutano akaichomeka.

                     "Kabla ya sijatoa maamuzi inabidi tuangalie nani msaliti  kati ya Mkuu Ibrahim au amiri jeshi wetu mheshimiwa rais" M.J Belinda aliwaambia na hapo kioo hicho cha tarakilishi kikaanza kuonesha picha za matukio mbalimbali ambayo wakuu hao wa jeshi walikuwa hawayatambui, ilikuwa ni ule mkanda aliourekodi Norbert  akiwa ndani ya shughuli nzima na mkanda ule aliokuwa akihojiwa mzungu yule aliyekiri kila kitu juu ya mpango haramu uliokuwa umewekwa. Kimya ndani ya chumba  hicho cha mkutano kimya ndiyo kilichukua nafasi katika muda ambao mkanda huo ulikuwa ukiendelea huku kila mmoja akisikitika kwa kile ambacho alikuwa akikishuhudia, hadi mkanda huo unamalizika tayari  kila mmoja alikuwa katika hali ya kutomamini kwa kila kilichokuwa kikiendelea nyuma ya pazia. Walikiri kwamba walikuwa sahihi sana katika kusikiliza maamuzi ya Kamanda wao kwanza kabla hawa timiza maamuzi ya mnadhimu mkuu wa jeshi nchini, walikua wameujua usaliti wote uliokuwa ukifanywa na Mnadhimu mkuu wa jeshi hadi mkanda huo ulipomalizika.

                         "Nadhani mmejionea wenyewe sasa inabidi mjiulize tunafuata amri za senior mkuu au junior wake kicheo katikaa jeshi, kama tunafuata amri za senior ambaye ni mheshimiwa Rais basi tutamlinda na kama hatufuati amri zake na tukafuata za junior wake ambaye ni mnadhimu mkuu basi tutamshambulia. Wangapi wapi upande wa rais kabla sijatoa uamuzi" M.J Belinda alingea kisha akauliza swali ambalo lilifanya wakuu wote wa kambi hiyo waliopo ndani ya chumba hicho cha mutano kunyoosha mikono yao juu, wote walikuwa wapo tayari kufuata amri ya mkubwa kuliko na mwenye haki ya kulindwa ambaye ni rais Zuber.

                          "Vizuri sana makamanda, nimetumia njia hii ili mkubali wenyewe kwa mioyo yenu kuliko kutumia cheo changu kuwapa amri najua haitokuwa sawa katika jambo kama hili. Sasa basi uamuzi ni huu, vikosi alivyoviagiza msaliti wa nchi hii vitatoka kama alivyopanga ila havitakuwa upande wake bali ni kwenda kuilinda ikulu tu. Tena silaha ziongezwe zaidi kumlinda rais wetu mpendwa, ni muda wa fagio jingine la chuma nadhani kauli mbiu yake mnaijua." M.J Belinda aliongea

                         "FAGIO LA CHUMAAAA!" Alipomaliza kutoa uamuzi wake alipaza sauti ndani ya chumba hicho cha mkutano huku akiwa amenyoosha mkono wake wa kulia juu aliokuwa amekunja ngumi

                           "FAGIAAAAAAA!" Makamanda wote waliitikia kwa pamoja wakinyoosha mikono yao  ikiwa imekunjwa ngumi pia.

                             "Kufagia kuanze kwa mara nyingine"  .M.J Belinda alipotoa kauli hiyo alitoka dani ya chumba hicho cha mkutano huku makamanda wote wakisimama na kutoa saluti kwake kukubali kwa moyo mmoja amri yake ambayo ipo upande wa kiongozi mkuu wa majeshi na kuiasi amri ya Mnadhimu mkuu aliyekuwa ni msaliti wa jeshi.



    ****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



          Muda ambao kikao kilikuwa kinaisha tayari Norbert alikuwa yupo ndani ya neo la Msasani akiwa  amefika jirani na mtaa wenye maghorofa mengi sana ndani ya peninsula hiyo, aliegesha gari  jirani na bar moja iliyokuwa imeungana na nyumba ya kulala wageni. Akiwa ndani ya eneo hilo alikuwa akiwaza jinsi ya kutafuta eneo ambalo walikuwa wapo kina Wilson ndani ya  Msasani, maneno ya yule mzungu aliyemtesa siku chache ziizopita juu ya kufikia kwao sehemu ambayo ni peninsula ndiyo yalimuongoza hadi eneo hilo. Norbert alikuwa anajua wazi kuwa hakuna peninsula yeyote ndani ya jiji la Dar es salaama isipokuwa Msasani tu, hiyo ndiyo ilikuwa ni penisula pekee ndani ya  jiji la Dar es slaaam. Ndugu msomaji peninsula ni eneo la ardhi ambalo limezungukwa na maji pande tatu na upande mmoja ukiwa haujazungukwa na maji, jijini Dars es salaam eneo hio liikuwa ni Msasani tu ambayo ndiyo pekee ilikuwa imezungukwana maji ya bahari pande tatu na hakukuwa na eneo jingine lililokuwa limezungukwa na maji namna hiyo zaidi ya hilo tu.

         Norert alitambua wazi kambi ya maadui wa taifa lake analolipighania walikuwa wapo ndani ya eneo hilo na siyo jingine, alikuwa na tatizo moja tu la kutojua maadui hao walikuwa wapo ndani ya jengo gani katika eneo hilo la Msasani ambalo ni kubwa lililokuwa limesheheni majengo mbalimbali ya kifahari. Akiwa ndani ya bar hiyo aliagiza kinywaji kisicho na kilevi cha grand malt  akawa anakunywa kwa taratibu sana huku akitafakari juu ya mahali pa kuanzia, alikuwa amekaa kwenye kiti na ikambidi anyanyuke aende kwenye eneo lenye viti virefu kwenye meza nyembamba iliyopo mapokezi hapo Bar maarufu kama kaunta. Alitembea kwa mwendo wa taraatibu na alipofika akakaa kwenye kiti kimoja kirefu akaweka chupa ya kinywaji chake kwenye eneo lenye meza nyembamba ambayo watu huweka bilauri na vinywaji vyao, alitupa macho mbele akamkuta msichana mrembo sana akiwa amevaa nguo maalum za kazi akmtazama kwa tabasamu tu alipoketi kwenye kiti hicho kirefu.

                     "Sema mrembo" Norbert alimwambia msichana huyo huku akimbania jicho  halafu akatoa tabasamu lake ambalo ni kilevi kwa wasichana..

                      "Sina usemi handsome wa mapoz na masmile" Mhudumu huyo alimuambia Norbert huku akitabsamu.

                         "Utakosaje la kusema wakati kila kitu chako kinazungumza mrembo, kukuangalia tu nimepata mengi ya kuongea"

                       "Mh!"

                        "Amini hivyo ulimi unayatoa yaliyopo ndani ya moyo"

                       "Haya bwana mshindi wewe"

                        "bado sijawa mshindi kwa watoto kama nyinyi nafikiri Nouther ndiyo mshindi kwenu kwa kila wakati"

                      "Tena huyo mtu usimzungumzie kabisa simpendi sana yule mkaka"

                       "Mh!  Kwani unamjua tajiri kama yule"

                         "Hee! Msasani hii nani asiyemjua yule mkaka aliyekuwa mdogo wa rais yule aliyefungwa gerezani"

                        "Duh! Kumbe maarufu hivi"

                           "ni zaidi ya maarufu huyo mtu yaani Masaki  anamiliki nyumba nne za ghorofa mtaa wa Mwaya karibu na Supermarket  ya Shirjee i na anaringa sana yule, hapa Msasani kwenyewe mtaa wa tatu hapo ana linyumba lipo kimya mda wote kama gofu yaani halieleweki sijui wapangaji wamemdodea"

                         "mwenye hela lazima aringe kwa alichonacho life yenyewe fupi hii"

                            "kuwa na hela siyo lazima uringe handsme, mbona wewe unaonekana una hela na huringi"

                         "nina hela wapi au suti zinakudanganya mrembo, mjini kupendeza tu"

                         "mh! Nimekuona tangu unaingia na gari lako lile pale parking"

                         "Kuwa na gari siyo kuwa na hela mrembo"

                           "Haya mshindi wewe ila yule mkaka akija hapa ana kazi ya kutuita malaya sisi wahudumu anafikiri kila mtu anafanya kazi hii ni malaya"

                           "(akitabasamu)Dah kweli anakosea mrembo kama wewe kukuita malaya ningekuwa mimi kaka yake ningemchapa fimbo"

                            "Mh! Una vituko wewe(kicheko kinamtoka baada ya kusikia kauli hiyo ya Norbert)"

                             "Kweli hiyo we mrembo kabisa hebu leta mkono wake nikuoneshe" Norbert mhudumu huyo ambaye alimpa mkono bila kusita, kwa haraka aliubusu mkono wake kisha akatoa tabasamu pana.

                             "sifa hii stahiki ya kugusa papi za midomo yangu kwenye mkono wako ni kwa ajili ya msichana mrembo tu, wewe ni mrembo zaidi ndiyo maana nimegusa papi zangu za midomo hapo usifuate maneno ya yule mwenye dharau juu ya warembo kama wewe" Norbert aliongea kihisia zaidi na mwishoni akamalizia na tabasamu.

                           "(akiangalia chini) We nawee hadi naona aibu yaani"

                              "usiogope ni kawaida tu, naitwa Norbert ukipenda niite Kaila sijui mrembo unaitwa nani?" Norbert aliongea hukua akimpatia mkono wake, mhudumu huyo naye alimpatia mkono wake kwa madaha sana.

                               "(akishikana mkono na Norbert) Martha, enhee Norbert kama nishawahi kulisikia hili jina mahali. Enhee! Norbert Kaila huyu mwandishi wa habari ni wewe nini?"

                            "Hujakosea ndiyo mie hapa nipo mbele ya macho yako"

                            "(akitoa macho kutoamini) Woow! Nafurahi kukufahamu"

                               "Mimi nina zaidi ya furaha kukufahamu Martha tatizo muda unakimbia ningependa unipatie namba yako ya simu maana nina zaidi ya jingine zito kuliko huku kukufahamu"Norbert aliongea huku akitoa simu yake ya mkonnoni kisha akampa Martha ambaye aliandika namba zake kisha akapiga na simu yake iliyopo kwenye mfuko wa sketi yake ikaanza kuita, alimrudishia Norbert simu yake ambaye aliitia mfukoni.

                               "Sasa Martha ngoja niwahi mahali" Norbert aliaga huku akinyanyuka kwenye stuli ndefu aliyokuwa amekalia.

                            "Haya Norbert (akimpungia mkono Norbert)"

        Norbert kwa haraka zaidi alitoka ndani ya bar hiyo akiwa na kile alichokuwa akikitafuta ambacho kingempa mwangaza wa mahali pa kuanzia katika kazi yake, alienda kwenye maegesho ya magari ndani ya bar hiyo na akaingia ndani ya gari ambayo aliiondoa kwa mwendo wa wastani barabarani akielekea kwenye nyumba ambayo alikuwa ameambiwa na Martha baada ya kumchimba kiundani pasipo yeye mwenyewe kujijua. Ndani ya dakika tano alikuwa mtaa wa tatu kutoka pale bar lakini nyumba ile aliyoambia hakujua ipo upande gani hadi muda huo, alizunguka katika mitaa hiyo kuitafuta nyumba hiyo lakini hakuiona kabisa.

        Norbert hapo aliamua kwenda kwenye duka la vinywaji baridi baada kuegesha gari mbali na hapo akiwa na lengo la kumchimba muuuzaji wa vinywaji hivyo awze kujua nyumba hiyo ilipo, alifika kwenye duka hilo ambalo lilikuwa limewekwa dawati ambalo alilikalia huku akihema sana akionekana ni mwenye kuchoka sana. Alikaa kimya sana katika benchi hilo ikiwa ni mbinu pekee itakayomuweszesha kupata jibu la kile anachokitaka, alitulia kwa muda mrefu sana hadi pale muuzaji wa duka hilo alipomfuata  mahali alipo.

                    "Kaka mbona upo kimya kama nyumba namba 134, nakusubiri wewe nikusikilize nikupe huduma" Muuza duka huyo alimuambia.

                    "Ofuuuu! Nimechoka sana nipe koka nitulize koo" Norbert aliongea kichovu kisha kamuuliza huyo muuzaji "ukimya wangu umenifananisha na nyumba namba 134 kwani ina nini?"

                     "Braza inaonekana wewe mgeni mahala hapa hata nyumba ya Nourther huijui ile ambayo ina ukuta mrefu  sana ipo pale kona karibia eneo moja  lenye nyumba za kupangisha" Mhudumu huyo alimuambia huku akifuata kinywaji alichoagizwa.

                    "Aaah kaka we acha tu nimekulia hapa jijini lakini hata sehemu zingine sizijui ndiyo sembuse huku ugenini nlipokuja mara moja" Norbert alimuambia

                     "Kweli aise wewe mgeni hapa" Muuzaji huyo alikiri ugeni wake akiwa tayari ameleta kinywaji hiko kwenye  dawati alilokuwa amekalia Norbert.

                      "jiji kubwa kaka hili siwezi nikajua kila mtaa" Norbert aliongea huku akipiga mafunda ya soda aliyoiagiza kwa haraka sana alikuwa ana hamu ya kinywaji hikohiko kwa muda mrefu sana kumbe ilikuwa ni moja ya hila zake za kumfanya muuzajia huyo asiwe na maswali katika ubongo wake ikiwa ataondoka eneo hilo.



         Baada ya muda alikuwa amemaliza soda yote  alimrudishia muuzajichupa yake kisha akakaa kwenye dawati hilo kwa sekundee kadhaa akisanifu mazingira ya eneo hilo ambayo hayakuwa mageni sana kwake ila kutokana na kuwa yupo ndani ya kazi ilimbidi ajifanye mgeni wa mazingira hayo. Muda huo tayari alasiri ilishatokomea na sasa muda wa jua kushuka ndiyo ulikuwa ukielekea, mwangaza wa jioni wa eneo hilo ulimfanya azidi kuwa na hari ya kujua kile alichokuwa akitaka kukifahamu kila  alipokuwa akiyatazama mazingira hayo ambayo yalikuwa ndiyo yamemfanya awepo eneo hilo kikazi zaidi akisaka maskani ya wabaya wake.

         Alikaa  kwenye dawati hilo kwa muda  mrefu baada ya kumaliza soda hiyo akawa na kazi ya kuangalia mwangaza tu wa neeo hilo ambao ulikuwa ukiondoka  taratibu sana, Norbert aliutazama mwanga huo huku akitamani sana uondoke kwa haraka ili aweze kutimiza kile kilichomleta eneo hilo ambacho aliona akikifanya muda ambao mwangaza huo basi asinge kifanya kwa ufasaha kabisa. Hatimaye muda wa kuingia kwa giza uliwadia ndipo Norbert alinyanyuka kwenye dawati hilo akamuaga mwenye duka baada ya kumlipa pesa yake kisha kaanza kuembea kwa mwendo wa taratibu sana kuelekea kwenye eneo ambalo alikuwa ameegesha gari lake  mbali kidogo na duka hio la vinywaji baridi.



        Alipofika aliingia ndani ya gari na taratibu aliondoka ndani ya eneo hilo akiwa ainaifuata nyumba namba 134 katika mtaa huo ambayo ndiyo alikuwa ameambiwa na muuazaji wa vinywaji baridi wa eneo hilo, aliendesha gari kwa umbali wa mita dhaa ndipo akaona kona kali ya barabra iliyokuwa imejenga umbo la U kutokana  na uwepo wa ukuta mrefu uliokuwa  upo pembezoni kwa barabara. Norbert alikuwa akiipita ukuta wa  huo huku akisanifu vizuri kwa jinsi ilivyokuwa na ukimya mkubwa sana kuliko kawaida, ilikuwa ni  uzio mrefu sana ambao laiti mtu angeuona kwa mara ya kwanza asingedhani hiyo ni nyumba bali angedhani ni shule au taasisi. Ukimya wa eneo hilo ambalo ndani ya uzio wa ukuta huo kulikuwa na miti mingi ya kupandwa iliyo mirefu kuliko ukuta ilikuwa ikiifanya eneo hilo lizidi kuwa na ukimya wa kutisha unaoweza hata kumuogopesha mwizi asiindani ya eneo hilo.

       Norbert akiwa ndani ya gari lake akiifuata barabra hiyo yenye kona kali aliweza kuliona lango kuu la kuingia ndani ya nyumba hiyo likiwa na mitambo maalum ya kuzuia wezi kwa juu, lango hilo la eneo hilo pia lilikuwa ni lango kubwa sana ambalo lilikuwa halina hata nafasi ya mtu kuweza kuona nje. Kulikuwa na barabara iliyokuwa ikitoka barabara ya magari kwa urefu wa mita thelathini ndipo ulifikie lango hilo lililokuwa na mataa pamoja na mlango mwingine mdogo unaotumika kwa watu wanaoingi kwa miguu. Mazingira yake na jinsi ukuta ulivyokuwa mrefu ndiyo ulimpa hamasa Norbert kuweza kuifuatilia zaidi nyumba hiyo, baada ya kuisanifu vizuri nyumba hiyo aliamua kupitiliza na gari lake akaenda hadi mtaa unaofuata hadi sehemu yenye bar. Norbert aliegesha gari mahali hapo kisha akavua koti la suti yake akatoka ndani ya gari, alifunga milango vizuri na akaingia ndani ya Bar hiyo.



    Sauti ya muziki wa dansi ndiyo ilimpokea alipovuka kizingiti cha bar hiyo, ilikuwa ni muziki maridadi mojawapo wa bendi ya muziki wa dansi nchini ambayo ilikuwa ipo namba moja kwa kuporomosha burudani na kuzikonga nyoyo za  mashabiki kila wakiusikiliza muziki wao. Muziki huo ulipenya vyema kwenye masikio ya Norbert lakini haukumshawishi kukaa katika eneo hilo lililokuwa limesheheni mabinti warembo pia, macho yake yalitua kwa mabinti ambao wengine walimtolea tabasamu alipowataza lakini hakushughulika nao. Norbert alipitiliza moja kwa moja hadi mlango wa nyuma wa bar hiyo huku akiacha macho ya baadhi ya wasichana yakiwa yapo kwake kutokana na utanashati wake, alipotoka kwenye mlango wa nyuma wa bar hiyo alifuata uchochoro mwembamba unaotenganisha uzio wa ukuta wa bar hiyo na ukuta wa jengo la Bar hiyo.

     

         Uchochoro huo ulikuwa mrefu sana ambao ulikuwa na kona mbili ambazo njiani Norbert alikutana watu wawiliwawili wakiwa wapo kibinafsi zaidi katika  mwanga hafifu uliopo kwenye uchochoro huo, hadi anamaliza kona za uchohcoro huo tayari alishashuhudia mambo yaliyotosha kuikomaza akili ya mtoto ikiwa atayatazama. Alipozimaliza tu hizo kona za uchochoro alitokea pembeni ya lango la kuingilia katika bar hiyo, alitoka huku akilitazama gari lake lilipo akaliona lilikuwa lipo mahala salama. Norbert alitembea kwa miguu kufuata njia ile aliyokuwa amepita kwa gari wakati akiitalii nyumba ya Wilson ambaye anajulikana sana kwa jina la Nourther. Alitumia muda wa dakika takribani tano tu tayari akawa ameshafika kwenye uzio wa jumba hilo kwa upande wa kushoto, Norbert alitembea kama alikuwa mpita njia wa kawaida ambapo giza ambalo tayari lilikuwa limeshaanza kuingia lilimpa uwezo mkubwa kujiamini akiwa anatembea mahali hapo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

         Norbert aliendelea kutembea pembeni ya uzio huo hadi alipolivuka lango la kuingia hapo ndani akiwa ameangaia vizuri mazingira ya kuingia hapo langoni yalivyo kwa mara ya pili, mita takribani kumi za urefu wa ukuta huo tangu alipite lango hilo aliwea kuingia eneo lenye miti mingi sana iliyopo nje ya ukuta huo. Norbert aliingia katikati ya miti hiyo iliyokuwa ipo jirani na ukuta huo kisha akaupanda mmmojawapo hadi sehemu ambayo ilikuwa ni rahisi kuona kilichopo ndani ya nyumba hiyo iliyo kimya, aliangaza kila pande za ndani ya eneo hilo akisaidiwa na mwangaza kutoka kwenye taa mbalimbali zilizopo hapo ndani. Aliweza kuona eneo ambalo lilikuwa karibu na ukuta huo lilikuwa limezungukwa kwa idadi nyingi ya miti humo ndani mithili ya kulikuwa kuna maonesho maalum ya  wanyama au kulikuwa kuna upandwaji wa miti ya mazao ya misitu iliyokuwa ikitunzwa kwa manufaa ya mmiliki, umbali wa mita zaidi ya hamsini aliweza kuiona nyumba ya kifahari sana ikiwa imezungukwa na mataa mengi yaliyowezesha mazingira yake kuonekana sawia kwake. Ilikuwa ni nyumba iliyokuwa kubwa sana ambayo ilikuwa ina bustani nzuri za maua kwa pembeni yake kwa kila upande ambazo ziliifanya ionekana kama hoteli ya kisasa.

       Nyumba hiyo ilikuwa imetawaliwa na ukimya mkubwa sana ambao ulikuwa ukiifanya ionekane ni ya kipekee sana . Norbert akiwa juu ya mti huo aliendelea kusanifu mazingira ya nyumba hiyo lakini hakuridhika na usanifu wake wa macho ya kawaida tu alitaka aisanifu kwa vizuri zaidi, aliamua kuingiza mkono mfukoni akatoa kitu mfano wa kalamu mbili nene za kuwekea alama (marker pen).  Vitu hivyo ambavyo vilikuwa vimegandana alivivuta vikaachana kwa umbali wa sentimita kadhaa, ilikuwa ni darubini maalum ya kijasusi ambayo ni vigumu sana kufahamika kwa mtu yoyote kutokana na muundo wake ulivyokuwa. Norbert aliiweka darubini hiyo jirani na macho  yake kisha akaelekeza upande wa nyumba hiyo, aliweza kuyaona mazingira ya nyumba hiyo kwa ukaribu zaidi ambapo aliona vitu mbalimbali ambavyo ingekuwa ngumu sana kuviona na macho yake ya kawaida tu. Darubini hiyo iliyokuwa na uwezo wa kugundua ilipo mitambo mbalimbali inaweza kuonesha  nyumba hiyo kwa nje kwa usalama walio ndani, kupitia uwezo huo wa darubini Norbety aliweza kugundua kuwa kulikuwa kuna kamera nyingi za ulinzi ambazo nyingine zilikuwa zimefungiwa kwenye taa mbalimbali hasa maeneo yenye miti iliyo karibu sana na nyumba hiyo.



        Norbert pia aliweza kuona kuwa nyumba hiyo ilikuwa na ulinzi mkubwa katika sehemu za getini tu na sehemu zingine kulikuwa kukilindwa na mitambo maalum ya kuwaonesha wezi  ndani ya nyumba hiyo ikiwa wataikaribia. Norbert kwa kutumia darubini hiyo iliyokuwa na uwezo wa kupiga picha alipiga picha mandhari ya humo ndani ya nyumba kisha akashuka juu ya mti huo aliokuwa ameupanda, alitazama mazingira ya pembeni ya nyumba hiyo pindi aliposhuka tu kisha akafungua suruali yake sehemu ya miguuni ambapo alikuwa amevaa soksi ndefu sana  ambazo sehemu ya ugokoni mwa mguu kulikuwa kumetuna kama mchezaji wa mpira akiwa amevaa kifaa cha kulinda mguu wake. Norbert alishusha soksi zake hizo alizokuwa amezipandisha kama machezaji mpira kisha akatoa vitu mfano wa soksi ambavyo alivivaa mikononi. Baada ya hapo aligusa ukuta nyumba hiyo akaanza kupanda mithili ya mjusi anavyopanda kwenye ukuta kwa kutumia vifaa hivyo ambavyo vilimpa wepesi sana katika kupanda ukuta huo hadi juu ambapo kulikuwa na nyaya malum za umeme  kwa ajili ya kuzuia wezi. Alizivuka nyaya hizo kwa umakini mkubwa sana kwa kutumia soksi gnumi ambazo zilikuwa na asili ya mpira kwa upande mmoja ambao haungizi umeme, alipozivuka nyaya hizo alishuka ukutani taratibu kisha akatua sehemu yenye majani kama alikuwa anakanyga ardhi kwa hatua moja na kumfanya asitoe kishindo wakati anatua. Alitazama pande zote kwa upande wa kulia na kushoto na mbele yake kisha akaziweka mfukoni soksi alizopandia ukuta halafu akaanza kutembea kwa mwendo wa tahadhari, alipita katikati ya miti iliyopandwa ndani ya nyumba hiyo kwa tahadhari kubwa akikwepa sehemu zote ambazo kulikuwa kuna kamera za ulinzi alizoziona kwa darubini yake yenye uwezo uwezo wa kuvuta mionzi ya kamera.



       Akiwa katikati ya miti hiyo alitoa darubini yake kwa mara ya pili kisha akataazama mazingira ya hapo ndani kwa mara nyingine, alitazama kwa umakini mazingira ya kule ndani ya nyumba akaona kulikuwa kama alivyopaona kwa mara ya kwanza. Alirudisha darubini yake kisha akajiweka sawa aweze kusogea mbele lakini alisita baada ya kuhisi kitu kikimtambaa katikati ya miguu yake, hapo Norbert aliganda kama sanamu huku akivuta hisia hisia kile kilichokuwa kikimparza kwenye miguu yake ni nini. Akiwa yupo katika hali hiyo alisikia vishindo vya mtu akija katika eneo alilopo huku akipiga uruzi, Norbert alitazama pande zote zinazomzunguka hapoo akaona muale wa tochi ukiwa unatembea huku ukimulika chini kuashiria mmulikaji alikuwa akimulika njia yake aliyokuwa akikanyaga ili asiweze kukanyaga kile kisichotakiwa kukikanyaga katika njia yake ndani ya majani hayo ya kupandwa. Norbert aliona hatari ya kukutwa eneo hilo lakini alipopiga hatua moja alijikuta akiharibu mambo zaidi, alikanyaga kitu ambacho hakutarajia kama ndiyo kilikuwa kikimparaza kwenye mkiguu yake.

                 "NYAAAAAAAUUU!" Sauti ya paka ilisikika kwa nguvu sana baada ya Norbert kutuliza kiatu chake kwenye mkia wake, paka huyo ndiye alikuwa akimparaza kwenye eneo miguu yake akamfanya asimame kwa ghafla huku akivuta hisia juu ya kilichopo miguuni mwake. Mlio wa paka huyo ulifanya vishindo vile vilivyokuwa vikisikika vizidi kuwa vizito kuashria mtu aliyekuwa akitoa vishindo hivyo alikuwa akikimbia.



    ****



         Wakati Norbert akiwa yupo kweye haitiyati ya kudakwa na mlinzi yule ndani ya uzio wa nyumba hiyo  ambayo alikuwa nayo umbali wa mitaa zaidi ya hamsini, hali ilikuwa si shwari kabisa kwa umbali wa mita hamsini toka pale alipo. Ndani ya nyumba hiyo ambayo alikuwa yupo mbali nayo kwa mita hizo hamsini, Thomas na wenzake wote waliobakia walikuwa wamechanganykiwa haswa kwa taarifa za vifo vya wenzao waliotumwa kwenda kumdhibiti Norbert. Walikuwa wamekaa sebuleni wote kwa pamoja jioni hiyo, kila mmoja mkono ulikuwa shavuni mwake kwa kupokea taarifa hiyo,walikuwa wakimsubiri mmoja wao aliyebaki ambaye alikuwa awasili muda huo kwa ajili ya kikao.

         Ukimya ndiyo ulikuwa umetawala ndani ya eneo hilo la sebuleni ambalo lilikuwa la kupendeza sana lakini sura zao zilichangia kuifanya sebule hiyo isipendeze hata kidogo na kuonekana ni ya kuchukiza sana. Samani za kisasa ambazo zilikuwa za kupendeza ikiwa wenye nyumba hiyo watakuwa na sura zenye  kupendeza, hazikuweza kuependeza kutokana na sura za wenye nyumba hiyo kutokuwa za kupendeza hata kidogo kutokana na sura za wenye nyumba hiyo kutokuwa za kupendeza. Si L.J Ibrahim wala Mzee Ole,Thomas, Wilson au Josephine aliyekuwa na sura yenye kupendeza kati yao kwa taarifa hiyo ambayo ilikuwa ikiwatia hasira sana juu ya Norbert. Luninga ya kioo bapa ya kisasa iliyokuwa imefungwa ukutani ikionesha haikuwa hata na hadhira aliyokuwa amevutika kuiangalia kutokana na taarifa hiyo, ilikuwa ikitoa sauti pamoja kuonesha picha kwa mandhari ya humo ndani isiyo na uhai lakini si kwa viumbe vyenye uhai maana hakuna hata mmoja aliyekuwa ameitilia maanani hiyo televisheni. Wote kwa pamoja walikuwa wakimgojea kwa hamu mwenzao mmoja ambaye alikuwa hajafika tangu alipotoa ahadi yupo njiani  waweze kuanza kile kilichowafanya wawe pamoja, baada ya muda kioo cha luninga kilitoa mistari ya rangi kama zifanyavyo chaneli za televisheni zikifungwa.



       Sauti ya kengele pamoja na kubadilika kwa picha baada ya kutokea kwa rangi hiyo ndiyo vilifuata, picha iliyofuata kwenye kioo cha luninga hiyo ilikuwa ni ya mandhari ya getini ambapo ilionesha gari aina ya toyota landcruiser nyeusi ikiwa getini mwa nyumba hiyo. Kuonekana kwa picha hiyo wote kwa pamoja walinyanyua shingo zao wakitazama kioo cha luninga hiyo huku wakiwa na sura zenye ahueni baada ya subira yao kufikia kikomwe, gari hiyo iliganda kwa muda wa dakika moja getini hapo pasipo kufunguliwa kwa geti hilo.

                     "Huyu mlinzi yupo wapi mbona hamfungulii kamishna aingie hajui kama tunamsubiri yeye future IGP wetu tu"  Wilson aliongea kwa hasira hukua akikitazama kioo hicho.

                   "Usiwe na papara mdogo wangu huenda ameenda kujisaidia ni binadamu huyo kama wwe hubanwa na haja pia" Mzee Ole alimuambia Wilson kwa upole, muda huohuo alipomaliza kumtuliza hasira mdogo wake geti lilianza kufunguka na gari hiyo iliyopo getini ikaingia ndani kwa mwendo wa wastani sana.



    ****



         Vishindo vilipokaribia zaidi Norbert alifanya kitendo cha upesi zaidi cha kujirusha juu akadaka tawi la  mti ambalo alilishikilia  vyema akajivuta juu akatulia, sekunde chache baadaye alimuona mtu aliyevaa sare maalum  za walinzi akifika hapo chini akiwa amebeba tochi kubwa. Mtu huyo alimuona kupitia mwangaza wa tochi aliokuwa akioumulika chini ya miguu yake kila akitembea, mtu huyo alipofika aliangaza  kwa kumulika kwenye eneo alilokuwa amesimama Norbert awali na alimuwezesha Norbert kuona idadi kubwa ya paka wa kizungu nwenye manyoya mengi wakiwa wamelala kwa pamoja kwenye majani huku wengine wakicheza.

                 "Khaaaa! Yaani hii mipaka kumbe inapigana yenyewe bwana" Mlinzi huyo aliongea baada ya kuona alikimbia mbio nyingi zisizo na tija na akataka kuendelea kumulika maeneo ya pembeni ya eneo hilo lakini alisita baada ya mlio wa kengele maalum kusikika mfukoni mwake, aliingiza mkono kwenye mfuko wa gwanda lake la ulinzi akatoa kitu mfano wa simu akakitazama na kisha akaghairi kumulika maeneo ya jirani na hapo akatimua mbio kurudi getini.

       Muda huo ndiyo muda ambao gari ya Kamishna Wilsfredi ilikuwa ipo getini na kifaa maalum kilichokuwa kipo mfukoni mwa mlinzi huyo ndiyo kilimjulisha kupitia mitambo maalum iliyokuwa imeunganishwa na kifaa hicho iliyopo getini, nyumba hiyo ilikuwa ikilindwa na mitambo ya kisasa sana ambayo hata kwa baadh iya taasisi muhimu haikuwa nayo kabisa ndani ya nchi hii. Mitambo hiyo inayotumika kuilinda nyumba hiyo ni mitambo iliyoletwa kwa agizo maalum la Sheikh Ahmed kiongozi mkuu wa mpango mzima, mitambo hiyo iliiingia Tnazania kwa njia za panya na hatimaye ikaja kufungwa ndani ya nyumba hiyo na mafundi maalum walioletwa baada ya Wilson kujitolea nyumba yake iwe sehemu ya mpango huo. Ilikuwa imeandaliwa kwa siku nyingi nyumba hiyo ndiyo maana ikafungwa mitambo maalum  ambayo inaipa nafasi ya pili kati ya nyumba zenye ulinzi mkali ndani ya nchi ya Tanzania baada ya Ikulu ya Rais. Ulinzi wa nyumba hii haukuwa ukijulikana kama ni mkubwa kiasi hicho zaidi ya kujulikana na watu wachache tu wenye maslahi ya aina moja tu, ilikuwa ni nyumba inayoweza kujiongoza yenyewe katika suala la kugundua uvamizi wowote uliokuwa ukikairibia usawa wa vifaa vyake vilivyokuwa vimetegeshwa katika pande mbalimbali.

       Baada ya mlinzi kutoweka maeneo ambayo Norbert yupo alienda moja kwa moja kufungua geti akihofia kupewa lawama na hata kibano kwa kuchelewa huko kuufungua geti, baada ya geti hilo kufunguliwa gari aina ya toyota landcruiser nyeusi ambayo ndiyo ilionekana kwenye luninga sebuleni walipo kina Thomas ililivuka geti hilo kwa taratibu sana kisha ikongeza mwendo kupita katika barbara ya lami iliyokuwa imejengewa ndani ya nyumba hiyo. Norbert alikuwa ameshaiona gari hiyo na alishuka kwenye mti aliokuwa ameupanda kwa taratiubu sana kisha akaanza kwenda kwa mwendo wa wastani ulio na tahadhari kubwa sana, alikuwaa kilifuatilia gari hilo lililoingia getini hapo kwa umakini mkubwa sana  ambapo muda huo lilikuwa likiuzunguka mzunguko maalum uliokuwa ukiunganisha njia tatu toafati zilizokuwa zikielekea sehemu tatu tofauti ndani ya nyumba hiyo iliyokuwa kubwa sana mithili ya hoteli.



       Aliifuatilia gari hiyo hata baada ya kuupita mzunguko ikawa inaendelea mbele kuifuata nyumba waliyopo kina Thomas, kutokana na kasi ya gari hiyo ilipelekea iwahi kufika kabla hata Norbert hajasogea karibu zaidi. Hali hiyo ilimfanya Norbert atoe darubini yake palepale alipo kisha akawasha sehemu maalum ya kupigia picha,aliiweka darubuni hiyo jirani na macho yake akiwa bado yupo katika eneo lenye mitimingi ndani ya nyumba hiyo. Aliivuta karibu zaidi hiyo gari ambayo muda huo mlango wa dereva ulikuwa umefunguliwa, aliweza kumshuhudia Kamishna Wilfred akitoka ndani ya gari hiyo akionekana ni mwenye haraka zaidi. Norbert aibonyeza kitufe cha kupiga picha akampiga picha huku akitoa tabasamu kwa kuweza kupata ushahidi zaidi wa kazi yake, hadi Kamishna Wilfrd anaingia ndani ya nyumba  tayari alikuwa ameshampiga picha nyingi sana kwa haraka. Wepesi wake wa uandishi wa habari aliutumia hapo katika kubonyeza viufe vya kamera darubini hiyo kupata picha nyingi zaidi, baada ya kumaliza kuzipiga picha hizo aliibusu darubini yake kisha akasogea pembeni zaidi ya eneo alilopo ambapo aliweza kuona dirisha la sehemu ya mbele ya nyumba hiyo lakini hakuweza kuona na wala kupata kila kitu alichokuwa akikihitaji na ikambidi atumie akili ya ziada.



    ****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MBAGALA KIZUIANI

         Maeneo ya mbagala Kizuiani mbele ya kituo cha daladala cha magari yanayotoka mjini kwa mitaa kadhaa kulikuwa kuna mwanajeshi aliyenyoosha bendera nyekundu yenye kitambaa chenye kung'aa kikimulikwa na taa. Mwanajeshi huyo alikuwa amesimama mbele ya makutano ya barabra ya kilwa na inayoenda jeshini, magari yote ya barabara hiyo ya yalisimama baada tu bendera hiyo nyekundu kunyooshwa muda huo wa jioni na kupelekea foleni iwe kubwa sana katika barabara ya Kilwa. Upande wa mita kadhaa mbele kwenye sehemu ambayo kulikuwa kuna uwazi ambao unaruhusu magari yanatoka mjini kuingia upande wa kulia karibu na ofisi za TRA Mbagala napo kulikuwa na mwanajeshi mwingine aliyekuwa ameshika bendera nyekundu akizuia magari yanayotoka Zakhem yasipite eneo hilo. Ilikuwa ni jambo la ajabu sana kwa kutokea kwa jambo hilo katika eneo hilo ambalo kulikuwa kuna njia ambayo ilikuwa ikielekea kwenye kambi ya jeshi.



       Watu walijiuliza juu ya kutokea kwa hali hiyo lakini walipata majibu baada ya kuona miale ya rangi ya machungwa ikitokea kwenye ile barabara inayoelekea jeshini. Miale hiyo ilikuwa ni ving'ora vya magari makubwa sana ya kubeba mizigo ya jeshi ambayo yalikuwa na idadi kubwa sana na yaliingia kwenye barabara hiyo ya Kilwa kuelekea upande wa Zakhem, magari hayo yalikuwa yamebeba vifaru vizito sana vya jeshi ambavyo viliyafanya yatembee kwa taratibu sana. Umati wa watu waliokuwa wapo karibu na eneo hilo walibaki wakishangaa vifaru hivyo vizito ambavyo hawakuwahi kuviona vikiwa vimebebwa na magari hayo katika mazngira kama hayo zaidi ya kuviona kwenye maonesho ya kitaifa. Ubebwaji wake kwenye magari hayo ilikuwa ni  kuhofia kuharibu  pindi vitakavyotembea kwenye barabara ya lami. Magari hayo makubwa yalipoisha tu yalifuata magari ya wazi ya jeshi aina ya hummer yaliyokuwa yamejaa wanajeshi walio na silaha za kizita, magari hayo yaliingia barabrani kwa kasi kubwa zaidi huku wanajeshi hao    waliojichora usoni mwao wakishangilia kwa nguvu. Ilikuwa ni hali iliyozua maswali sana lakini watu walipoungaanisha tukio la kuzungukwa kwa ikulu na hilo la wanajeshi waliona ni uongezwaji wa nguvu ya kuzunguka ikulu. Haikuishia hapo magari yenye mizinga mizito nayo yaliingia katika barabara hiyo yakiwa na ving'ora juu, yaliingia yakiwa yamebeba wanajeshi wa kikosi maalum cha wapiga mizinga.

       Baada ya msafara huo uliochukua muda mrefu sana kuingia barabrani kuisha magari kama kawaida yaliruhusiwa kuendelea namatumizi ya barabra kwa upanmde wa magari yaliyokuwa yakirudi mjini jioni hiyo, barabara iliyokuwa ikitoka Mbagala kuelekea mjini bado ilifungwa kwa kutangulia gari ya kijeshi iliyokuwa ikitoa amri kwa magari mengine kuwekwa pembeni. Msafara huo wa magri ya jeshi ulipita barabara ya kilwa  yote hadi ulipofika bandari ukaelekea ulipo mzunguko wa barabara unaounganisha barabara  inayoenda kariakoo na inayoelekea stesheni katika mtaa wa Gerezani. Magari hayo kwa mwendo uleule yaliyokuwa yakienda yaliingia barabara ya inayopita mtaa wa gerezani kisha yakaipita hadi stesheni yakanyoosha barabra moja kwa moja hadi posta ya zamani pembezoni mwa bahari, yaliipita posta ya zamani yakaelekea kivukoni ambapo yaliingia hadi barabara ya Obama kulipokuwa kuna wanajeshi wengine wa kikosi cha maji waliokuwa tayari wapo eneo hilo.



    Kuingia kwa kikosi hicho cha jeshi la ardhi katika barabara hiyo ya Obama iliyopo mbele ya Ikulu kwa  mita kadhaa kuliwafanya wanajeshi wote waliokuwa wameizunguka Ikulu kurudi nyuma kidogo ili kuwapisha wenzao, walikuwa washapata taarifa ujio wao katika eneo hilo hivyo waliwapisha kwa hatua kadhaa nyuma na magari hayo yaliyokuwa yamebeba vifaru yakaegeshwa hapo barabrani. Magari mengine yaliyokuwa yamekuja hapo yalishusha wanajeshi wengi wa jeshi la ardhini wakiwa wapo kamili kila idara kama walikuwa wanaenda  vitani, wanajeshi hao wote waliposhuka walikaa kuangalia mbele wakiwa wameizunguka kama amri waliyopewa  na mkuu wao.

        Vifaru vizito vilivyokuwa vipo ndani ya magari makubwa ya mizigo ya jeshi navyo vilishuka taratibu kisha vikapanga mstari mmoja  mbele ya ikulu kama walivyokuwa wameagizwa, makombora yote yalikuwa yameelekezwa ikulu ikiwa ni sehemu ya kutimiza mpango waliokuwa wamepewa. wanajeshi wote wa jeshi la maji waliokuwa wameizunguka ikulu walikaa nyuma ya  wenzao waliokuwa wametangulia mbele kwa amri ya mkuu wao M.J Mugiso ambaye aliamini wote walikuwa wapo upande mmoja wa kutaka kumuondoa rais Zuber madarakani. Hawakutambua kama kikosi hicho kilikuwa kimetumwa kwa kazi nyingine tofauti na kazi yao waliyokuwa wamepewa hapo, laiti kama wangelitambua hilo basi wasingeweza kuwapisha hapo kwa ajili ya kuwaweka wao mbele kwani ni hatari sana  kwa kazi yao hiyo. Muda huohuo  ndege za kivita zenye makelele mengi sana zilipita eneo hilo kwa kasi sana na zikiwa na kazi ya kuizunguka ikulu tu  jambo ambalo lilisababisha watu waliomo ndani ya ikulu hiyo kuwa katika hali ya woga sana kila wakizitazama ndege hizo, ndege hizo ambazo mara nyingi huonekana sana katika maonesho ya sherehe za uhuru au muungano na zilipita hapo kwa tano mfululizo  kisha zikarudi katika kambi ya jeshi la anga Dar es salaam.

       Kiongozi wa vikosi vyote vilivyoingia eneo hilo alikuwa ni meja kutoka kambi ya jeshi la ardhi mbagala, meja huyo tayari alikuwa amefika eneo hilo sambamba na vikosi alivyokuja navyo eneo hilo akiwa ndiyo mtoaji wa amri kuu kwa hao. Uwepo wake eneo  ulimfanya M.J Mugiso atoke hadi kwenye eneo la jirani na njia inayoelekea lilipo lango la kuingia katika ofisi ya waziri mkuu ya hapo ikulu, M.J Mugiso alienda hadi eneo hilo ambapo kulikuwa kuna hema maalum ambalo tayari lilikuwa limewekwa na wanajeshi wa jeshi la ardhi kwa ajili ya kamanda wao waliokuja naye hapo. M.J Mugiso alipofikia eneo la jirani na hema  hilo alipokea saluti nyingi kutoka kwa wanajeshi ambao walikuwa wapo nje ya hema hilo, alipoingia ndani napo alipokea saluti kwa kila mmoja hadi kiongozi wa kikosi hicho ambaye alikuwa yupo ndani ya hema hilo akiwa amekaa sehemu moja na wanajeshi waliokuwa wataalamu wa masuala ya tarakilishi na mawasiliano kwa ajili ya kikosi cha anga.

                   "Meja Kiboni" M.J Mugiso aliongea mbele ya meja huyo

                   "Mkuu" Meja Kiboni ambaye ndiye kiongozi wa jeshi la ardhi kwa eneo hilo aliitikia.

                    "Nafikiri ushapewa taarifa zote kuwa mpo chini yangu kwa siku hizi mbili za kumuondosha msaliti wa ikulu" M.J Mugiso aliongea kwa tabasamu.

                    "Hapana mkuu sijapewa taarifa hizo, taarifa nilizopewa hadi naleta kikosi eneo hili ni kuwa niwe nasikiliza amri kutoka kwa kamanda mkuu wa  kikosi mkuu Belinda tu na si vinginevyo" Meja Kiboni aliongea maneno ambayo yalimfanya M.J Mugiso afinye uso wake kwa kutoamini.

                     "Meja taarifa zilizopo kutoka kwa Luteni Jenerali ambaye ndiye General mtarajiwa ni kwamba mtakuwa chini yangu nyote kwani mimi ndiye mkubwa hapa na pia ndege zote za kikosi cha anga zitaenda kutua kwenye nyambizi za kikosi cha maji ambapo kuna uwanja tayari upo kwa ajili yao" M.J Mugiso aliongea

                      "Mkuu taarifa niliyoambiwa ni hiyo tu siyo nyingine, nimeonywa nisifuate amri ya yoyote pasipo  mkuu Belinda kuipitisha amri hiyo kwa makamanda wangu wakuu tu" Meja Kiboni aliongea kisha akamgeukia mwanajeshi mwenye nyota mbili mabegani mwake ambaye alikuwa yupo karibu na vioo vingi vya tarakilishi ndani ya hema hilo.

                       "Unganisha video call kwa Mkuu Belinda haraka sana" Alimpa amri mwanajeshi huyo mwenye cheo cha luteni kisha akayarudisha macho alipokuwa M.J Mugiso.

                      "Sir" Luteni huyo alitii mari kisha akafanya kazi yake mara moja na ndani  muda huo kioo cha tarakilishi kilionesh alama za vidoti vikiwa vinazunguka duara huku maandishi ya kingereza yaliyosomeka 'waiting' yakitokea juu yake. Maandishi hayo yalipotoka sura ya M.J Belinda ilionekana kwenye koo hicho akiwa ameva nguo za kijeshi kasoro kichwani hakuwa na kofia, Meja Kiboni na M.J Mugiso walitoa saluti kwa alipoiona sura ya M.J Belinda kwenye kioo hicho.

                        "Belinda" M.J Mugiso aliongea akikitazama kioo hicho.

                        "Mugiso: M.J  Belinda aliitikia

                         "Mbona unaenda kinyume na amri ya mkuu Ibrahim si umeambiwa majeshi yote yawe chini yangu katika operesheni hii" M.J Mugiso alimlalamikia M.J Belinda

                         "Majeshi yaliyopo chini ya komandi yangu hayawezi kuwa chini yako hata siku moja Mugiso, wewe ni msadizi kwenye kikosi chako na mimi ni mkuu katika kikosi changu. Unapokea amri mimi natoa amri" M.J Belinda aliongea

                         "Aaah! Belinda inamaana unapinga amri ya three star general tuwe wote kwenye operesheni hii" M.J Mugiso aliongea.

                          "Amri ya kuwa wote katika eneo hili itakuwa palepale lakini si vikosi vyangu kuwa chini yako hiyo haipo kwangu. Vikosi vyangu vipo chini ya komandi yangu tu nafikiri umenielewa Mugiso, hao hawawezi kupinga amri niliyowapa" M.J Belinda aliongea

                          "Khaaa! Nini?!" M.J Mugiso aliuliza kwa hasira  sana.

                          "sisi wote ni two star general Mugiso lakini kuwa wote cheo kwenye cheo kimoja haimaanishi kwamba   hakuna mkubwa kati yetu, umenikuta kwenye cheo hiki hivyo mimi ni mkubwa ni wako tu ndiyo maana ukasaluti pamoja na Kibona ulipoiona sura yangu muda mfupi uliopita. Hivyo huna haki ya kuingilia maamuzi yangu katika misheni hii, kikosi nimeleta  hapo lakini kipo chini ya amri zangu hata kama sipo na hadi kesho  nitakapofika kitakuwa kipo chinii ya amri yangu vilevile"   M.J Belinda aliongea maeno hayo ambayo yalimkera sana M.J Mugiso lakini yalikuwa ni kweli tupu kuwa alikuwa ni mdogo kicheo kwa M.J Belinda, kuwa wote mameja jenerali hakukumaanisha kuwa hakukuwa na mkubwa kati yao.

                         "Kiboni fuata amri zangu kama nilivyokuambia tumeelewana" M.J Belinda alimsisitiza  Meja Kiboni kisha akaendelea, "Mugiso huna haki ya kuvunja amri hii na kuuifuata unapaswa kuanzia muda huu, tumeelewana".

         Maneno hayo yalikuwa ya kukera sana kwa M.J Mugiso lakini hakuwa na ulazima zaidi ya kuyafuata tu kwani aikuwa ni mdogo kwa M.J Belinda ingawa wote walikuwa wapo cheo kimoja kimoja, hakuitikia kwa kinywa chake aliposikia amri hiyo yeye alipiga saluti tu kiukakamavu kisha akatoka ndani ya hema hilo pasipo kuongeza neno lolote. Alikuwa amekasirirka sana kwa jinsi alivyokuwa akitarajia ni tofauti na aliyoyakuta huko, aliondoka moja kwa moja kurudi katika eneo alilokuwa hapo awali kwenye hema la wana maji ili kuendelea na taratibu zingine.



    ****



        Mlango wa kuingilia sebuleni ulipofunguliwa ndipo watu wote walipopata na ahueni kidogo baada ya mtu waliyokuwa wakimsubiri kuwa tayari ameshafika katika eneo hilo, waligeuza nyuso zao zisizo na dalili yoyote ya furaha kumtazama Kamishna Wilfred ambaye alikuwa ni amechelewa katika kikao hicho kuilichokuwa kifanyike muda mfupi kabla na kuchelewa kwake ndiyo kulikifanya kikao hicho kuchelewa kuanza.

                     "Mniwie radhi jamani nilikuwa nimekumbwa na mambo kifamilia ndiyo maana nikachelewa kufika ndani ya eneo hili" Kamishan Wilfred aliongea huku akielekea kwenye kochi lililokuwa tupu akaketi.

                      "hakuna kilichoharibika kamishna nadhani tuendelee na kikao chetu sasa hivi" Mzee Ole aliongea

                       "Ok jamani nafikiri mnaona mambo yanavyozidi kuwa mabaya zaidi inabidi tutafute jinsi gani ya kuweza kuyatatua la si hivyo mpango wetu utaegemea tu kwenye vkosi vya jeshi vilivyokuwa vimeizunguka ikulu  tu, nadhani mnatambua jinsi gani Norbert ambavyo amezidi kuwa hatari kwetu na tumejaribu kumteka zaidi ya mara ya mbili akatuzidi akili" Wilson aliongea

                         "Enhee! Tena kamishana kuna jambo nilisahau kukuambia kuhusu huyu Norbert, kwa taarifa nilizozipata huyu ndiye aliyemuua ndugu yako Kitoza akishirkiana na mpelelezi mwingine hatari kutoka Rwanda Hilda Alphonce katika usiku ile ambayo Kitoza na Eagle walikuwa wawaue Zuber na wenzake kama nilivyowaagiza nikiwa bado nipo ikulu" Mzee  Ole alimpa taarifa mpya kabisa Kamishna Wilfred.

                       "Nadhani unaona ni jinsi gani huyu mtu alivyo hatari Kamishna hatunao Reginald Kitoza mpelelezi hatari na aliyekuwa mkuu wa TISS ambaye ni mwenzetu, Benson, Benjamin na Santos hata Eagle ninja aliyeaminika  na kaka pia alouawa naye. Hapa huyu mtu ni hatari sana sasa inabidi tumpunguze kasi yake ya kufanya kazi ili achelewe na mpango wetu ufanikiwe kwa haraka, uharaka wake katika ujasusi wake ni hatari kwetu" Wilson alizidi kumuambia Kamishna

                        "Ok nimewalewa sasa tufanyeje? Na huyu nataka nimuue mwenyewe kwa mkono wangu kulipa kisasi cha ndugu yangu mwenyewe" Kamishna Wilfred aliongea kwa hasira aliposikia habari hiyo.

                         "Kumuua peke yako bali tutamuua sote nataka kulipa kisasi cha Benjamin pia" Josephine naye alidakia akionekana ni mwenye hasira sana

                        "Cool down Leopard Queen.....Taratibu Kamishna huyu mtu hauliwi tu kama kuku wa kizungu anayeandaliwa kutayarishwa nyama na mpishi, huyu mtu inabdi kwanza tumpunguze kasi then Mzee Ole arudi ikulu ndipo tuongeze nguvu ya kumtafuta tumuue" Thomas aliongea

                        "Enhee! Hilo ndiyo la muhimu kabisaa, na mimi ndipo nitakapopata wasaa wa kulipa fadhila zaungu kwa marehemu Kitoza kwa kuhakikisha huyu mtu anakamatwa na umuue kwa mkono wako ukishirikiana na Leopard Queen   maana yeye pekee ndiye aliyetutia hasara tangu nikiwa madarakani halafu  akaja kumpa kisa cha jinamizi mtunzi wa riwaya Hassan Mambosasa aandike akisema ni sehemu ya utafiti wake kama mwandishi wa habari" Mzee Ole aliongea

                         "Naye huyu mwandishi wa riwaya dawa yake inachemka kwa sasa maana ndiyo aliifanya nchi hii imchukie kaka yangu" Wilson aliongea

                         "Wilson hebu achana na huyo novelist sisi tudili na huyu mtu maana akizimwa basi huyo novelist hatokuwa na jipya" Thomas  aliongea

                         "Kabisa Thomas, sasa kamishna  inabidi umuwekee zengwe ashindwe kufanya kazi yake vizuri then niingie ikulu tumpe adabu kisawasawa" Mzee Ole aliongea

                         "Worry out future president, kuhusu kesi mbaya tu hapa nyumbani kwake kesho tu mtapata matokeo sasa hivi nikitoka naenda kufikiri kesi ya kumpakazia tu" Kamishna Wilfred aliongea.

                          "Tena huyu mtu zikianza ndoa ya jinsia moja aanze yeye kuwa mke kisha huyo rais kwake anayekataa dola milioni 600 kusaini mkataba kwa kujifanya mzalendo ndiyo afuate" Mzee Ole aliongea.

                          "wacha wenye kutaka fedha kama sisi tuendeshe life tupige kazi, kamishna tunakutegemea  kwa hilo our future IGP kaka akiingia ikulu tu. Chulanga hana chake yule" Wilson aliongea

                            "General mbona upo kimya hivyo siku ya leo?" Mzee Ole aliacha kuchangia kikao hicho akamuuliza  L.J Ibrahima ambye aikuwa amekaa kimya tu hajachangia chochote tangu kuikao hicho kianze.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

                              "Hapana tupo pamoja jamani, nilikuwa natafakari juu ya mpango wetu wa kuhakikisha majeshi yote yawepo ikulu maana naona kimya" L.J Ibrahim aliongea

                               "kwani bado tu air force na wa ardhini hawajafika tu au  wameasi amri tayari" Wilson aliuliza, L.J Ibrahim alipokuwa akijiandaa kujibu swali hilo simu yake ya mkononi iliita na alipoitoa kuangalia mpigaji wake alijikuta akitabasamu.

                              "Enhee! Simu ndiyo hii nilikuwa natarajiwa kupigiwa kuanzia muda huu" Alongea na wote wakaka kimya kumuacha aipokee simu hiyo, L.J  Ibrahim aliipokea simu akaongea "sema kijana... anhaa ok ok nashukuru kwa taarifa yako"

          L.J Ibrahim alikata simu kisha akawatazama wenzake akiwa amejawa na tabsamu halafu akaongea, "tayari kikosi cha jeshi la ardhi chenye vifaru, mizinga na wanajeshi kimetoka kambi ya mbagala, huyu mtu aliyenipigia ni kijana wangu yeye ameuona msafara huo  ukimalizia kulivuka daraja la reli ya tazara linalopita Mtoni mtongani".

          Kauli hiyo ilowafanya wote watoe matabsamu ya furaha na hata ikawasahulisha juu ya vifo vya wenzao ambavyo vimetokea masaa akdhaa yaliyopita ndani ya siku hiyo, kikao hicho hadi kinafikia muda huo bado kikosi cha jeshi la ardhi kilichotoka Mbagala kilikuwa hakijafikia kabisa magogoni. Kilikuwa bado kipo njiani wakati mkutano huo ukiwa unaendelea, baada ya mpango huo waliompa kamishna Wilfred autekeleze kukamilika Kamishna Wilfred alisimama kwenye kochi kisha akaaga.

             "Jamani wacha niwahi mara moja maana nimemtoroka wife hiyo ishu ya kifamilia sijaisolve bado" Kamishna Wilfred aliongea huku akimpeana mikono na kila mmoja, wote kwa pamoja walisimama baada ya kikao hicho kufikia tamati. Walitoka nje kumsindikiza Kamishna hadi alipokuwa ameegesha gari lake pasipo kutambua kuwa ndiyo walikuwa wakimpa ushahidi zaidi Norbert ambaye alikuwa akifuatilia kila hatua yao na hata ajenda yao waliyokuwa wakiipanga tayari alikuwa ameisikia baada ya kuondoka katika eneo alilokuwepo hapo awali na kusogea jirani na nyumba hiyo baada ya kuichezea mchezo mchafu mitambo ya ulinzi ya mahala hapo.



    ****



        Baada y Norbert baada ya kuzishinda nguvu kamera za ulinzi za eneo hilo kwa kutumia mionzi mikali ya darubini yake, aliweza kuzifanya zisimuone kwa muda  ambao atakuwa katika eneo hilo. alizunguka nyuma  ya nyumba hiyo na akapanda juu ya paa kisha akatembea taratibu hadi  kwa juu kwenye kibaraza kirefu cha nyumba hiyo ambacho kiikuwa kipo karibu na sebule waliyokuwa wamekaa kina Thomas. Alipofika kwenye kibaraza hicho aliweza kutega kinasa sauti jirani na dirisha la sebule hiyo ambapo aliyanasa maongezi yote yaliyokuwa yakiendelea ndani ya nyumba hiyo hadi yanamalizika, Kamishna Wilfred aliposindikizwa na wenzake wote hadi mbele ya baraza yeye alitumia darubini yake kama kawaida na kuwapiga picha wote bila wao kujijua. Norbert  picha nyingi alimpiga mzee Ole ambaye ndiyo kwanza alikuwa anamuona tangu aliposikia amelipuliwa na bomu kule njia ya kwenda Tabata siku chahce zilizopita, baada ya kupiga picha hizo alitulia huko juu hadi Kamishna Wilfred alipoondoka na wote walipoingia ndani ndipo naye alishuka kwa ujanja mkubwa wa mafunzo ya kininja aliyokuwa nayo.

        Alikimbia kwa kukanyaga vidole ambapo hakutoa sauti hadi kwenye eneo alipokuwepo awali kwenye miti mingi, alipita katika njia ya tofauti na eneo alilokuwa amepita hapo awali kuhofia kuwakanyaga tena walepaka  hadi  kwenye mti mwingine wenye majani marefu kisha akachuchumaa chini kwa ghafa baada ya kusikia uruzi mtu. Alisikia vishindo kama ilivyokuwa awali kisha vishindi hivyo vikasimama, uruzi uliendelea kuvumana Norbert akaendelea kuchuchumaa katika eneo lenye majani mengi kama pori fulani hapo. Alikuwa amekaa kwenye eneo ambalo alijuta kwanini asingekaa kwenye enoe jingine, majuto yake na kutaka kuhama katika eneo hilo yalichelewa kwani alimshuhudi yule mlinzi akifika pale kwenye majani akitazama pande zote kisha akayarudisha macho yake kwenye majani yale ambapo alikuwa amejificha Norbert. Mlinzi yule alizima tochi kisha akafungua mkanda wa suruali ya suruali yake na ndiyo hapo Norbert alijuta kwanini alichuchumaa kwenye majani mengi kama hayo, kimiminika kilianza taratibu kunyeshea majani hayo na kumlowanisha Norbert begani kwake ambapo alitulia tu ingawa ilikuwa ni zaidi ya maudhi kufanyiwa vile. Aligeuzwa choo na yule mlinzi ambaye alikuja hapo baada ya kumfungulia geti Kamishna Wilfred  kutokana na kubanwa haja ndogo kwa ghafla akaona tabu kukimbia kuelekea chooni wakati sehemu yenye faragh ipo karibu, Norbert alivumilia maudhi hayo  hadi yalipoisha na mlinzi yule ambapo aliondoka eneo hilo kwa kasi kurudi getini ambapo palikuwa ni mbali kidogo.

        Kitendo cha mlinzi kupotea katika  eneo hilo hakuwa na muda wakusubiri tena alirudi hadi pale ukutani akapanda kwa kutumia vifaa alivyopandia kwa haraka sana akatoka nje ya uzio wa nyumba hiyo  pasipo kujulikana na mtu yeyote. Harufu ya haja ndogo mbichi ndiyo ilikuwa ikitoka kwenye bega lake la kushoto lakini hakuwa na jinsi aliendelea kuivumilia kwani hakuna jinsi, shati ake lote kuanzia begani hadi kifuani lilikuwa limelowana haja ndogo ya yule mlinzi ambayo ilikuwa inatoa harufu ya pombe. Norbert alijikaza akaivumilia harufu hiyo na alitembea hadi pale Bar alipoliacha gari lake, alipofika alitoa ufunguo wake na moja kwa moja aliingia ndani ya gari lake. Kitendo cha kwanza baada ya kuingia ndani ya gari yake hiyo ilkuwa ni kuvua shati lake hilo lililogeuzwa choo na kuvaa koti la suti pekee, aliwasha gari yake akaingia barabrani na kuondoka eneo hilo ambapo mitaa kadhaa baada ya kuingia barabarani aliegesha gari pembeni.  Alilichukua shati lake na akatoa silaha zote zilifungwa kwenye shati hilo kisha akalitupa nje na akaendelea na safari yake akiwa tayari ameshapata vitu muhimu ingawa kwa mara ya kwanza alijikuta akigeuzwa choo na mwanaume mwenzake.



    ****



        Wakati kabla hata Norbert hajatoka juu ya paa la nyumba ya Wilson na kuzunguka kisha na kupetelea kwenye miti mirefu iliyokuwa imepandwa kama pori, Kamishna Wilfred alikuwa na  ari kubwa ya kuhakikisha anampa kesi Norbert itakayomfanya aishi kama digidigi. Akiwa ndani ya gari baada ya  kuagana na wenzake aliendesha kwa kasi kwa lengo la kumuwahi mkewe na  pia kuweza kufanikisha mpango wake huo aliokuwa ameupanga vizuri. Baada ya kutoka nje ya ngome ya Wilson na kuigia barabarani aliendesha gari kwa kasi sana awahi nyumbani kwake, gia za gari lake hilo alibadilisha na kuweka nyingine awahi kufika Kawe alipokuwa akiishi. Baada ya kuimaliza Msasani Kamishna Wilfred alijikuta akiishiwa tumaini la kuishi kwani alipokea ugeni mwingine tofauti ambao ulikuwa bado haujajitambulisha kuwa umewasili tayari eneo hilo. Ugeni ulikuja kumjulisha kuwa tayari ulikuwa eneo hilo baada ya kuhisi kitu cha baridi kikimgusa nyuma ya shingo yake bila ya kutarajia. Kamishna Wilfred alikuwa hajatambua kitu hicho kilikuwa nini na alipeleka mkono kukigusa lakini kitu hicho kilimkandamiza haswa, alijikuta akiongeza mwendo na kisha kufunga breki kwa ghafla baada ya kutambua kuwa alikuwa amewekewa bastola kisogoni mwake.  Gari yake ilisimama kwwa nguvu sana lakini yule aliyekuwa amemshikilia hiyo bastola hakutetereka hata kidogo, bastola hiyo iliendelea kutulia palepale kisogoni mwake vilevile.

                     "Nimefunga mkanda kamishna unafikiri nitaaanguka kwa hiyo breki na bastola inidondoke" Alisikia sauti isiyokuwa ngeni ikimuambia



       Kauli hiyo ilimfanya Kamishna Wilfred ashindwe hata kuendelea kuendesha gari baada ya kulisimamisha kwa ghafla akitegemea mtu aliyekuwa amekaa kiti cha nyuma angeyumba na bastola aliyokuwa amemuwekea imponyoke lakini haikuwa hivyo, kufunga mkanda kwa huyo mtu aliyemuwekea bastola kulimzuia kuyumba huko kwani mkanda ulishika barabara baada ya kupata mshtuko kwa jinsi gari ilivyosimamishwa kwa kasi kubwa na Kamishna Wilfred. Moyoni alilaani kabisa hiyo teknolojia ya magari kwa kuweka mtindo wa mikanda kunasa ikipata mshtuko kumzuia mtu asiyumbe au kujigonga, teknolojia hii yenye manufaa na kuweza hata umuepusha mtumiaji wa gari asiumie sana yeye aliiona haifai hata kidogo kwani imemfanya azidi kuwa katika kuti kavu badala ya kumuweka kwenye kuti bichi ajinusuru mbele ya adui yake aliyekuwa yumo ndani ya gari yake amedhibiti vilivyo. Alitulia tu kimya hakuwa na la kufanya kwani mbinu zote zilikuwa zimemuisha kabisa kwa muda huo, hakujua alikuwa ameweka kitimoto na mtu gani ambaye alikuwa yupo ndani ya gari tangu anaingia ndani ya nyumba ya Wilson   hadi anatoka kwani hakuwa amesimamisha gari mahala mpaka aseme adui huo alikuwa amepanda gari njiani.

                         "yaani tunajivunia tuna kamishna wa umri wa wastani katika nchi yetu ambaye anaonekana mzalendo kumbe mnafiki tu" Mtu huyo aliyekuwa amemuwekea bastola alimuambia, Kamishna Wilfred aliposikia sauti hiyo ambayo siyo ngeni katika masikio yake alitamani kugeuka lakini bastola aliyokuwa ameelekezewa ilimkandamiza shingoni akabaki akiwa mpole asifanye chochote

                          "Tulia hivyohivyo kamishna utanijua tu muda ukifika na hapo utaeleza kwanini unashirikiana na wasaliti wa taifa hili, kwa sasa endesha gari uelekeo wa bank club kurasini upesi sana" Mtu huyo aliongea huku akiutoa usalama wa bunduki, Kamishna Wilfred hakuwa na ubishi alitii kama alivyoelekezwa na akaendesha gari akielekea huko alipoelekezwa na mtu huyo aliyekuwa ameshikilia hatima yake kwa muda huo na nageweza kumfanyia chochote kibaya kwake.

                       "Tena endesha kwa kasi tuwahi kufika kamishana mapema si unajua jioni hii kuna foleni" Alimuamuru, Kamishna Wilfred aliendesha kama alivyokuwa ameagizwa na mtu huyo ambaye alikuwa hajamjua ni nani hadi muda huo ili kuepuka kuyapoteza maisha yake wakati bado ana malengo mengi sana ndani ya dunia hii akiwa bado hajayatimiza.



        Ilibidi awe mpole tu kwani alikuwa akifanya usaliti kwa lengo la kupata pesa na pia kwa maslahi yake mengine binafsi, sasa angeleta ukaidi wowote malengo hayo yasingetimia kamwe na ungekuwa ni mwanzo wa kuwa na hasara kwa kushiriki mpango ambao haukumpa manufaa hadi anaaga dunia. Hilo jambo hakulitaka litokee hata kidogo kwake, tayari yupo ndani ya kuti kavu na moyoni alibaki tu akijilaani kwa kutolikagua gari lake tangu anatoka nyumbani na hadi aliposimama njiani kununua vocha dukani. Aliamini kabisa kuwa adui yake alikuwa akimfuatilia na ndiyo alipanda gari lake muda huo pasipo yeye kujua. Alijiona amefanya uzembe wa hali ya juu wa kubamiza tu milango pasipo kuiweka vibanio vyake alipokimbia mara moja kwenye duka lilopo pembezoni mwa barabara alipokuwa akihitaji vocha baada ya kuishiwa kifurushi chake cha mtandao katika muda ambao hakutarajia kama kingemuishia.

                 "Kamishna leo ndiyo utajua kama wanausalama tuna ukorofi sana" Mtu huyo alimuambia wakiwa wanazidi kumaliza mitaa kueleka kurasini.

                  "we ni nani kwani Norbert siyo?!" Kamishan alijipa ujasiri akauliza kibabe  ingawa moyoni anajua ubabe wake huo usingemsaidia chochote katika hali hiyo

                   "Shida yako kunijua tu utanijua tukifika Kamishna, nimekuwa nikifuatilia nyendo zako kwa ukaribu sana"  Mtu huyo aliongea, Kamishna alisonya  huku akipiga usukani wa gari lake akizidi kujilaumu sana.

                    "shida yako nini wewe  niambie unataka kiasi gani usiendelee kunisumbua" Kamishna alijikuta akiropoka tu.

                    "Ha! Ha! Ha! Unadhani mimi ni askari mla rushwa kama wewe, mimi ni askari safi wa jeshi la polisi ninachohitaji ni wewe tu kufika mahali unapostahiki kwa usaliti wako" Mtu huyo aliongea maneno ambayo yalimfanya Kamishna Wilfred azidi kufikiria juu yake zaidi  hasa alipotaja yupo ndani ya jeshi la polisi, alimfikiria zaidi mtu huyo na alizidi kufikiri zaidi  na hatimaye akawa amemshuku jina mmoja wa maafisa aliyepo chini yake kuwa ndiyo huyo aliyekuwa nyuma yake.

                     "We John unataka nini haswa kwa mkuu wako wa kazi" Kamishan aliuliza akibahatisha kulitaja jina la huyo aliyekuwa amedhibiti humo ndani ya gari.

                       "Ha! Ha! Ha! Ha! Vizuri kwa kulijua jina langu bila kukutambulisha, ndiyo mimi DCP John Faustin nipo nyuma yake kwa sasa" DCP John aliongea huku akicheka bastola ikiwa imemueleka mkuu wake wa kazi, huyu ni mmoja wa wapelelezi wa shirika la EASA ambalo ndiyo Norbert yupo lakini yeye alikuwa ni normal service kama alivyo Moses na si secret service kama kina Norbert, Hilda na Allison.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

         Ndani ya kazi hii ya kuwaumbua wasaliti kwa mara nyingine tena akiwa yupo upande wa wazalendo kama kawaida yake, DCP John alikuwa ameingia ndani ya kazi hiyo baada ya kuhisi jeshi hilo la polisi lilikuwa na msaliti ndani yake. Alianza uchunguzi wake  kwa askari wote waliopo chini yake na hata waliopo juu yake baada ya kuhisi uwepo wa msaliti tangu kilipomalizika kikao cha dharura na mheshimiwa rais yalipotokea mauaji Yombo, hakujua msaliti kwamba alikuwa ni miongoni mwa wakubwa zake ambao alikuwa akiwaheshimu kutokana na vyeo vyao. Alipopata habari za kutumwa kwa special forces wa jeshi la polisi kwenda nyumbani kwa Moses na M.J Belinda kwenda kuwangamiza alipatwa na wasiwasi kikosi hicho kilikuwa kimetumwa na kamishana yeyote ndani ya jeshi la polisi miongoni mwa makamishna waliopo ndani ya jiji la Dar es salaam.



        Hapo alianza kuwafuatilia makamishna mmoja baada ya mwingine. Kamishna wa tatu katika kumpeleleza alikuwa ndiyo huyo Kamishna Wifred na sasa alikuwa amemnasa akiwa ndiyo msaliti haswa aliyekuwa akimtafuta ndani ya makamishna wa jeshi la polisi, alikuwa ni kibaraka wa EASA asiyefahamika kabisa kama yumo ndani ya jeshi la polisi kwa  askari yoyote zaidi ya kufahamika na wenzake wa EASA. DCP John ni mpelelezi ambaye ameshirikiana na Norbert ndani ya jeshi la polisi kwa kazi tofauti ikiwemo ndani ya kisa cha JINAMIZI wakati akiwa na cheo cha ASP (assistant superintendent police/mrakibu msaidizi wa polisi), ndani ya kisa hicho yeye ndiye alimtorosha Norbert maeneo ya Segera Tanga baada ya kuangusha kitambulisho chake akageuziwa kesi na Briton wa usalama wa taifa kipindi cha utawala wa mzee Ole. Pia ameshirikiana naye katika kisa cha SHUJAA ambapo ni yeye aliyemsaidia Norbert kuwarudisha Moses, Beatrice, Dokta Hilary pamoja na Irene kipindi wakiwa kidato ch asia baada ya kuvamiwa na wahalifu na komredi pamoja na wale wa Annie.

        Amerudi tena ndani ya kazi yake akiwa ameshughulika na msaliti ndani ya jeshi la polisi pasipo kumuambia yeyote hadi amempata, yupo njiani akiwa naye anampeleka kurasini ambapo ndipo mahala alipoona panafaa kumpeleka msaliti kama huyo. Ndani ya muda huo tayari ilikuwa imepita nusu saa na sasa wapo katika barabara ya Kilwa maeneo ya Mivinjeni, bastola bado ilikuwa imeelekea shingoni mwa Kamishna Wilfred ambaye alikuwa ametii amri ya DCP John ya kwenda wanapolekea. Aliendesha gari hadi Mtoni kwa Azizi Ally ambapo aliamriwa akate kona kuingia njia inayoeleka Kurasini aachane na barabara ya Kilwa, walienda na barabra hiyo hadi Kurasini mta wa Bank club kwenye nyumba kubwa iliyokuwa na uzio mrefu sana. Hapo aliamriwa apige honi ambapo kijana mwenye mwili mkubwa mazoezi alitoka nje hadi ilipo gari, kijana huyo alisogea kwenye dirisha la dereva akijua mhusika wa hapo ndiyo yupo mbele.



        Kioo cha nyum ya dereva kilifunguka ndipo kijaa huyo akasogea nyuma akamuona DCP John ambaye alimpa amri ya kufungua geti gari hiyo iingie ndani, kijana huyo alikimbia na kufungua geti kwa haraka gari hiyo ikaingia ndani hadi kwenye eneo maalum ambalo Kamishan Wilfred aliamriwa aegeshe gari. Aliegesha gari bila kupinga wala kuleta usumbufu wowote kwa hao waliokuwa wameushikilia uhai wake kwa muda huo, aliamriwa azime gari naye alitii vilevile hakuleta ubishi wa aina yoyote kwa  wapinzani wake ambao hakuwajua kama upinzani wao ulikuwa ukimlenga yeye pia. Aliamriwa ashuke naye alitii akashuka ndani ya gari hiyo akakutana na yule kijana aliyekuwa amefungua get akiwa tayari ameshalifunga  aada ya gari kuingia na ameshika bastola naye baada ya kumuona DCP John akiwa ameshika bastola , bastola ya yule kijana nayo ilichukua uelekeo wa mahali alipo Kamishna Wilfred. DCP John alishuka ndani ya gari naye akamuelezea bastola Kamishna Wilfred kama alivyokuwa amefanya huyo kijana.

                 "Kamishna karibu sana ndani ya nyumba ya EASA na utegemee mawili kuingia ndani ya nyumba hii ukiwa na makosa au siyo mhusika wa humu, la kwanza ni kupona ila makazi yako yatakuwa ni gerezani milele ukitoka humu na la pili ni kufa tu ukiwa umeleta  ubishi usiofaa" DCP John aliongea huku akimuashiria kwa bastola yake mahali ulipo mlango wa kuingilia katika nyumba hiyo ya siri ya kampuni ya EASA, Kamishna Wilfred ujasiri wote ulimuisha alipooona kuwa alikuwa akitazamana na mdomo wa bastola  ya DCP John kwa mara nyingine ambaye alikuwa akitabasamu tu ingawa hakuwa na faraj wala furaha iliyomfanya atabsamu kwa muda huo.

                   "Kamishnaaa! Afrika ya mashariki haichezewi na wasaliti kama nyinyi ikiwa wanausalama wake wapo kazini" DCP John alimuambia huku akiwa nyuma yake akimuangoza Kamishna Wilfrd kulekea ndani ya nyumba hiyo, yule kijana alifanya ya kufungua mlango katika kila eneo walilokuwa wakipita hadi walipoingia katika vyumba vya chini ya ardhi.



         Kamishna Wilfred alipoyaona mazingira ya eneo hilo alikuwa ameshakata tamaa ya kuishi kwani aliona uwezekano wa kutoroka humo ndani ulikuwa ni mgumu sana, moyoni alijiwa na roho iliyokuwa ikimlaumu sana tamaa yake ya pesa ndiyo ilikuwa imemponza sana hadi akaingia katika eneo hilo lenye ugumu wa kutoka kwa mtu kama yeye. Upande mwingine wa nafsi yake  ulikuwa ukimpa moyo ni sehemu ya maisha kuwa na matatizo kama hayo apige moyo konde tu anaweza kusalimika, alijipa moyo wa kusalimika akiamini kuwa aliyemsaidia akawa hajashikwa siku zote alizokuwa akifanya uhalifu atamsaidia na hapo aweze kutoka. Kamishna huyu aliyekuwa amepewa cheo kikubwa na kuaminiwa sana katika jeshi la polisi alikuwa ameshasahau kabisa kwamba anayemtegea ataweza kumnusuru eneo hilo alikuwa amemkosea kwa kiasi kikubwa sana,habari ya kuwapa viongozi wa dini pesa ili wamuasi huyo anayemtegea  kwake hakuwa nazo ila yeye alikuwa akitegemea tu kukolewa na huyo anayemuamini atakuwa ni mwokozi wake ndani ya balaa hilo zito ambalo lipo mbele yake kwa usiku huo. Usiku ambao ni usiku mmoja kati ya usiku miwili iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu iishe ili waweze kuyachukua madaraka makuu ya nchi ya Tanzania.



        Moyoni kabisa alikuwa akimtegemea Mungu  wakati walikuwa walikuwa wana mpango wakuhalalisha kile ambacho muumba alikuwa amekikataza kisihalalishwe, yote hayo aliyasahau na alikuwa akimuomba Mugnu atoke hapo salama ili asiwe amefanya kazi bure tu kuisaliti kazi yake aliyokula kiapo akitumia kitabu kitakatifu cha dini yake. Dhambi kubwa yote aliyofanya ikiwemo kuvunja kiapo kizito alichokula kipindi anajiunga na jeshi la polisi sasa ilikuwa imeanza kumtafuna yeye mwenyewe kuanzia siku hiyo,dhambi ya pili ya kutaka kuhalalisha kile alichokuwa amekipinga Mungu sasa ilikuwa ikimtafuna pia ingawa alikuwa akimuomba Mwenyezi kwa dhati ndani ya moyo wake aweze kutoka ndani ya eneo hilo.



       Ama kweli alimuona Muumba ni asiyeona huo uongo wake aliokuwa akiidanganya ndani ya nafsi yake, alikuwa akimuomba akombolewe muda huo wakati alikuwa azimia kwenda kufanya jambo baya  akitoka hapo la kwenda kushiriki kuhakikisha ule mpango wake ulikuwa unatimia vilivyo. Kamishna Wilfed usiku huo ndiyo anajikuta akijuta tangu aanze kushiriki mpango huo kwa kulipa kisasi cha ndugu yake ambaye anaamini kabisa alikuwa ameuliwa na  EASA  hata kabla hajaambiwa na Mzee Ole juu ya muuaji halisi wa ndugu yake masaa machache yaliyopita, siku zote hizo alikuwa akishiriki katika kukomoa shirika hilo pamoja na wote waliohusika katika kumuondosha Mzee Ole madarakani na kupelekea kuuawa kwa ndugu yake Reginald Kitoza aliyekuwa mtu wa karibu sana kwa Mzee Ole kama ilivyo Moses kwa Rais Zuber.

         Akiwa ametangulizwa mbele ya DCP John na nyuma ya yule kijana wa aliyewafungulia geti kwa mita takribani tatu, Rias Ole aliongozwa hadi ulipo mlango mzito wa chuma ndani ya vyumba vya chini ya ardhi ndani ya nyumba hiyo. Kijana yule alifungua mlango ule wa chuma ambao ulimhitaji kubonyeza namba maalum ukutani, ulipofunguka chumba hicho kiliwaka taa na kijana yule akaingia ndani kisha Kmaishna Wilfred akafuatia. Kamishna Wilfred alipoingia ndani ya chumba hiko aliamini kabisa uwezo wa kutoka humo ndani ulikuwa mdogo hasa baada ya kumshuhudia mtu aliyekuwa akiaminika ni mtu hatari akiwa yupo amefungwa minyororo mikononi na miguuni, mtu yule aliyekuwa akiamnika kuwa ni komando hivi sana aliamuona akiwa amepungukiwa mwili wake ule wa kimazoezi na akiwa na vidonda kadha mwilini mwake.



        Moyo wake uliingiwa na ganzi pia alimuona kijana wa special force aliyekuwa ni mmojawapo kati ya vijana aliokuwa amewatuma kumkomboa Lion kule ofisini kwa Norbert baada ya mzee yule kutotoka tangu alipoingia ndani ya ofisi ile ambayo baadaye Norbert aliacha kuitumia, alimshuhudia kijana huyo akimtazama sana kwa huruma alipofika katikati ya chumba hicho akiwa amewekewa bastola kisogoni kwake. Kamishna Wilfred alishindwa kabisa kumtazama askari wake yule waspeciala forced kutokana na matatizo aliyokuwa amemsababishia kwa kumpa amri zisizo na baraka  la jeshi la polisi lote, pia alishindwa kumtazama yule Komandoo wa kizungu aliyetiwa mikononi na Moses nyumbani kwa M.J Belinda walipotumwa kwenda kumuua mwenye nyumba ambaye ni kikwazo kwao. Kamishna Wilfred alienda kufungwa moja kwa moja kwenye kiti cha mateso ambacho kilikuwa humo  ndani ambapo kila mateka mpya anayeingia humo  lazima apitie hapo kwenye kti hicho ndiyo aende kufungwa minyororo kama wengine aliowakuta humo ndani. Baada ya kufungiwa barabraa kwenye kiti hicho cha mateso ndiyo DCP John alirudisha bastola yake kwenye pochi maalum aliyokuwa ameiweka kwapani kisha akasogea hadi karibu kabisa na kiti alichofungiwa Kamishna Wilfred, alimtazama mkuu wake wa kazi huyo kwa sekunde kadhaa huku akitabasamu halafu akasikitika sana kwa ujinga aliokuwa  akiufanya.

                      "Kamishna unafikiri nchi hii ulinzi wake ni mdogo sana hadi muweze kufanya mlitakalo, mtizame huyo mzungu aliyekuwa ni mpiganaji mzuri mkamtuma kwenda kumuua Meja jenrali Belinda alivyo, ohooo! Kiti hicho ullichokalia wewe ndiyo kimemfanya akawa vile tena kwa taarifa yako ametapika siri zenu zote.  Alikuwa mbishi sana akabanikwa korodani zake hadi akaongea ukweli na sasa hivi huo ubishi wake ushampa utasa kabisa hataweza kuzalisha hata kama akitoka humu mzima, sasa Kamishna jindae na wewe mtesaji anakuja ikifika zamu yako" DCP John alionga huku akimtazama Kmaishna Wilfred, aliacha kumtazama bada ya kumalizakuongea maneno hayo kisha akayahamisha macho kwa yule kijana wa special force.

                      "Mtazame huyo kijana wa special force katika jeshi la polisi ambaye kaumia kawa kibogoyo yote kwa ajili tu ya kufuata amri zako wewe msaliti akiwa hana uwezo wa kupinga maana wewe ni mkubwa wake, sasa hivi yupo humu akiwa ameshakata tamaa kabisa ya kuendelea kuishi Kamishna yote kwa ajili yako tu wewe ukitumia madaraka hayo uliyopewa vibaya. Kaheshimu amri zako ndiyo maana akazitii lakini leo ndiyo zimemuweka humu" DCP John aliongea huku akimtazama yule askari wa special force ambapo maneno hayo yalimfanya atokwe na mchozi baada ya kuona ameharibikiwa na maisha tu kwa ajili ya Kamishna Wilfred.

                       "Mkuu nilikuheshimu na kufuata amri zako lakini sasa nimeharibikiwa na maisha yangu tu yote kwa ajili yako wewe tu, onaaa! Nimemuacha mke wangu mjamzito nyumbani hadi leo hajui kama nimekufa au la.



         Unafikiri ataishi kwenye hali gani Kamishna ikiwa wewe umeharibu maisha yangu. Kamishna mama yangu ni mgonjwa nimemtoa shamba nimemleta mjini ili aweze kupatiwa matibabu nikitegemea kazi hii ndiyo itakayomtibu fikiria atakuwa yupo kwenye hali gani mimi nikiwa hapa, wenzangu pia wameuawa nyumbani kwa Meja jenerali yote kufuata amri zako tu fikiria wewe unayekaaa na mkeo pamoja na familia yako kwa raha ukila chakula kitamu ambacho hata tulipokuwa kazini hatukumdu kukipata. Aaaaaaargh! Kamishna umeangamiza maisha yangu ingawa bado napumua" Askari yule wa special force alilalamika huku akilia kwa uchungu akimtazam Kamishna Wilfrwd pale kwenye alipokuwa amefungwa, maneno hayo yalikuwa yamemuingia vilivyo Kamishna Wilfred akajikuta akiinamisha uso wake chini kutokana na uzito wa maneno hayo ambayo yalikuwa yamatolewa na mtu mwenye uchungu sana.

                    "Angalia sasa unaona hata aibu kumtazama sajenti Ismu kwa uovu  wako, eti unataka kumlipia kisasi Kitoza huyu msaliti aliyeshiriki mauaji ya makomandoo wa jeshi siyo. Yaani ulivyo na moyo mwepesi hadi unaona aibu kumtazama Ismu hukufaa kufanya hayo kabisa, subiri na wewe familia yako isote baada kuonja joto ya jiwe iliyowapata hawa wenzako waliofungwa hapa" DCP John aliongea huku akimtazama Kamishna Wilfred kwa masikitiko sana, Kamishna Wilfred kwa siku hiyo alijikuta akikumbuka maneno ya mkewe ambayo ambayo alimuambia siku chache baada ya kupokea habari za kifo cha Reginald Kitoza binamu yake aiyekuwa akimpenda kama ndugu yake wa damu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

                     "mume wangu naomba umuachie Mungu tu visasi  havikufai na cheo chako hiko"

                     "hapana sikubali lazima aliyemuua alipie kwa gharama yoyote ile"

                     "kumbuka alikuwa ana hatia yule na kauawa akiwa hatiani"

                     "we mwanamke ishia hapohapo nishasema nitalipa kisasi cha ndugu yangu wazazi wetu ni damu moja hivyo namuona kama ndugu yangu wa damu yule"

                     "ohooo! Sawa siishi nyumba moja na wasaliti , naenda kwetu

          (siku  mke wa Kamishna Wilfred alipoongea maneno hayo alikuwa ni ana cheo cha SP {super intendent police}, ilikuwa ni majira ya usiku ambapo mke wake aliaga kururdi kwao akipakia nguo zake kwenye begi. Kutokana na mapenzi mazito aliyonayo kwa mke wake na kuhofia kuvuja kwa adhma yake alijikuta akilegeza msimamo kimaigizo ndipo mke wake akabaki na aliamua kufanya adhma hiyo kisiri na sasa usaliti wa kusema uongo kwa mke wake pia unamtafuna leo hii).





     Lawama zake ndani ya muda huo  hazikuweza kabisa kubadilisha kile kilichokuwa kimetokea hadi akawa hapo, alizipa lawama tamaa zake lakini tayari alikuwa ameshachelewa hadi muda huo. Akiwa yupo ndani ya majuto hayo sauti ya viatu vya mtu akitembea kwa taratibu vilisikika kwa nje ya chumba hicho ambapo ndiyo kulizidi kumfanya awe na shauku ya kutaka kumjua yule aliyekuwa akija ni nani, alipowatazama kina DCP John na yule kijana wote walikuwa wakitabasamu tu. Viatu hivyo vilivyokuwa vikisikika vilizidi kukairibia eneo hilo na hatimaye aliyekuwa akitembea akaonekana mlangoni hapo Kamishna Wilfred ndiyo alizidi kuchanganyikiwa kabisa baada ya kumuona mtu aliyekuwa amepanga adhma mbaya dhidi yake akiwa ndiyo yupo mateka katika upande aliopo, alimuona Norbert akiwa amevaa suti tu akiwa hana shati na mkononi akiwa amebeba begi dogo kama la kiofisi. Norbert aliingia ndani ya chumba hiko na akamtazama Kamishna Wilfred kisha akaachia tabsamu la dharau, alimgeukia DCP John kisha akamtazama akiwa na tabasamu kwani alishaamini kuwa kazi ile ilikuwa ni mkono wake ndiyo ulikuwa umehusika hadi Kamishna Wilfred akawa yupo chini ya mikono yao

                  "Aisee John umeniwahi bwana na pia umenirahisishia kazi kabisa" Norbert aliongea

                   "Nilikuambia nitamsaka huyo kamishna aliyewatuma special forces kuja kumvamia Moses na pia kumvamia shemeji yetu Belinda sasa ni huyu hapa" DCP John aliongea

                   "kazi imekuwa rahisi sana sasa hivi" Norbert aliongea huku akimtazama  Kamishna Wilfred.

                    "Kiupande wangu imekwisha, nimemnasa alipotoka katika nyumba ile aliyoingia ambayo wamo wasaliti wenzake wote" b DCP John aliongea akazidi kumfanya Norbert ashangae kwani hakuwa akijua kuwa kama walikuwa wapo ndani ya nyumba moja muda uliopita kabla hawajatoka nyumbani kwa Wilson.

                      "Duh! Kumbe tulikuwa wote mule ndani....sasa Kamishna utakuja kuujibu umma mwenyewe imekuwa vipi wewe,Thomas, Filbert Ole, Wilson Ole na three star jeneral muwe upande mmoja. Mnamtuhumu Rais Zuber ni msaliti mkitaka kuipindua serikali yote iliyoleta maendeleo kwa muda mfupi tu kwa sababu zenu binafsi tu, ushahidi wote wa ujinga wenu ninao jua nitauachia redioni karibuni tu ili watanzania wote wausikie eti mnataka ushoga uwe rasm hapa Tanzania kisa hela tu. Ngoja usikie mwenyewe sipigi mikwara tu" Norbert aliongea kisha akatia mkono katika begi lake dogo akatoa kifaa mfano wa redio ndogo isiyotumia kanda akakiwasha, alitulia baada ya sekunde kadhaa na kisha redio hiyo ikaanza kutoa sauti ambayo alikuwa ameirekodi sambamba na kupiga picha mbalimbali bila wahusika kujijua.



       Maneno yaliyokuwa yakiongelea siku hiyo ndani ya mkutano walioutisha kina Wilson baada ya kuuawa wenzao ndiyo yalisikika ndani ya kinasa sauti  hiko, Kamishna Wilfred alijua tayari alikuwa hana ujanja kwani Norbert alikuwa ameshikilia makali na angeleta ujanja tu basi angekatwa. Alimtazama Norbert kwa sura iliyojaa huruma sana lakini huruma ile haikusaidia katika kumbadilisha Norbert awe na sura ya huruma, Norbert ndiyo kwanza alizidi kutabasamu kila alipomtazama  Kamishna Wilfred ambaye uso wake ulikuwa umejaa huruma tu kama Ngamia aliyeona kisu kikikaribia kufika kwenye shingo yake afanywe kitoweo.

                 "Kamishnaa yaani naangaliwa na mwanamke mrembo akitaka nimuonee huruma kama Josephine lakini sikumuonea huruma ndiyo nikuonee huruma wewe kidume unaejiona mjanja kufuata mkondo wa pesa na visasi visivyo na maana. Umepotea njia hapo jua hii nitahakikisha inafika redioni sasa tuone utafanyaje na ikitoka tu nakuachia huru hapo nje ya geti mchana kweupe ili wananchi wakuuwe si unajua vijana walivyochoma nyumba ya Moses bila kujua hana hatia sasa hasira zao zitawageukia nyinyi" Norbert alimuambia Kamishna Wilfred huku akimtazama kwa dharau kuu, baada ya maneno hayo yenye kuuumiza kwa Kamishna Wilfred Norbert alitoka ndani ya chumba hicho akifuatana na wenzake na wakafunga mlango na taa zikazimwa kiza kizito ndiyo kikafuata kwa mateka wao.







    ASUBUHI ILIYOFUATA

         Siku hii ijumaa ilikuwa ni siku nyingine mpya katika siku ambazo muumba alikuwa amewajalia waja wake wengi waweze kuiona siku hiyo kati ya wachache waliokuwa wameikosa kuiona siku hiyo, eneo la Magogoni hali ilikuwa ni ileile kwa wanajeshi wakiwa wameizunguka ikulu tena ndani ya siku hiyo kuongezeka kwa wanajeshi kuliwafanya raia wa kawaida waliokuwa wakishuhudia tukio hilo waamini kabisa kuwa rais wao alikuwa yupo mbioni kuondolewa ndani ya Ikulu na kuingia rais mwingine ambao watu walikuwa hawamtambui hadi muda huo. Waandshi wa habari kutoka mashirika mbalimbali ya habari duniani walikuwa tayari wameshafika na walikuwa wakirusha matangazo hayo ambayo yalikuwa yakishuhudiwa na watu tofauti kutoka mataifa mbalimbali duniani.



        Si Aljazeera,BBC,DWTV, SKY NEWS,CCTV NEWS, wala CNN waliokuwa hawajakosa kufika eneo hilo hadi asubuhi hiyo inawadia tangu wapate habari za wanajeshi kuizunguka ikulu hiyo. Wanahabari hao wa kimataifa walikuwa wamefika hapo na wakihangaika kutafuta habari kutoka kwa wanajeshi hao wakiuliza sababu ya kuizunguka ikulu hiyo, habari hiyo waliikosa na hata walipojaribu kuingia ndani ya ikulu wakamuhoji rais Zuber ambaye alikuwa hajatoka nje ya ikulku kwa siku ya pili sasa walizuiwa na wanajeshi hao waliokuwa wapo makini katika kutimiza amri ambayo walikuwa wamepewa na mkuu wao. Kikundi cha wanahabari hao wa kimataifa na hata wa kitaifa kiliamua kujitosa ndani ya siku hiyo katika kusaka habari, walijitosa na kwenda hadi makao makuu ya jeshi nchini yaliyopo Upanga ambapo kwa siku hiyo walimkuta L.J Ibrahim akiwa yupo ofisini kwa Jenerali akiiacha ofisi yake ikiwa haina mtu. Waandishi hao wa habari waliomba kumuuliza maswali machache juu ya hali hiyo akiwa yeye kama mkuu wa jeshi aliyekuwa amebakia tu katika jeshi la wananchi wa Tanzania, L.J Ibrahim kwa jinsi anavyopenda kusikilizwa na umma wa watanzania na hata duniani aliamua kuongelea kuhusu sakata hilo na akawakaribisha waandishi hao kwenye chumba cha mkutano ili aweze kuyajibu maswali hayo ya waandishi wa habari kutoka sehemu mbalimbali duniani. Waandishi hao ambao alikuwa wamejifunza lugha mbalimbali kutokana na kazi yao kuwa ya kimataifa nao hawakuichezea nafasi hiyo ili vituo vya televisheni wanavyotokea viweze kupata habari, walishusha maswali kwa L.J Ibrahim kwa mfululizo ambayo hayakujibiwa mmoja bali alitoa maelezo ambayo yalikuwa ni majibu tosha ya mswali hayo.

                       "Mmeuliza maswali mengi ambayo yalikuwa yakihitaji majibu kutoka kwangu na sitowaacha bila ya kuwapa majibu ili mtambue kisa chote cha kutoa amri hiyo ya wanajeshi wote kuizunguka Ikulu. Baada ya kuanguka utawala  wa aliyekuwa rais mheshimiwa Filbert Ole nchi hii iliijua kuwa tulikuwa tumepata kiongozi stahiki anayefaa kuwaongoza watanzania kumbe haikuwa hivyo bali tulikuwa tumepata mbaya zaidi ambaye ni zaidi hata ya aliyetangulia. Msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania alikifuta chama cha kisiasa kikuu cha upinzani ambacho kilikuwa kikiongozwa na Mzee Ole hasa baada ya kubaini kitu walichokifanya, na sisi tunasema tunamfuta madaraka rais wa nchi hii baada ya kubaini kile alichokuwa akikifanya kuwa ni kinyume na madaraka yake. Hata juma moja halijaisha tangu tumzike Jenerali wetu na komandoo wa kuaminika kati ya makomandoo kumi na mbili ambao kwa sasa kabaki mmoja tu ambaye ndiye msaidizi wangu ajaye ambaye si mwingine bali ni Meja jenerali Belinda. Uchunguzi ulibainika ya kwamba kuwa Professa Moses Gawaza alikuwa ndiyo muuaji mkuu na ndiye aliyetengeza sumu zilizokuwa zimewaua Jenerali Kulika na wanajeshi wengine wa jeshi langu na pia ndiye alihusika na mauaji ya viongozi wa dini akiwemo Askofu Edson na Mufti mkuu wa jiji la D ar es salaam. Isitoshe msaliti huyuhuyu aliyekuwa yupo ndani ya ikulu akakutana na Professa Gawaza kwa siri ilihali  anatambua ni mtuhumiwa na hakumtia hatiani alipokutana huko na mtu huyo, nilipozipata habari kupitia mtu wangu ambaye ni mmoja wasiopenda usaliti wake niliamua kumuambia atoe maelezo kwanini ameonana naye mtu huyo anayejulikana ni mtuhumiwa na hakuchukua hatua yoyote ile. Nilimpa siku saba za kutoa maelezo hayo vinginevyo Ikulu anatoka lakini yeye hakumfanya hivyo na ndiyo maana vijana wangu waliokuwa na uchungu na jenerali wao waliungana nami katika kuhakikisha anatoka Ikulu. Nafikiri maswali yenu yote nimeyajibu je kuna la ziada?"  L.J Ibrahim alitoa maelezo hayo ambayo yalikuwa na majibu ya maswali ya waandishi wa habari na akawa anasubiri kusikiliza hayo mswali ya ziada, mwandishi moja kutoka Tanzania alinyoosha mkono ambao ulikuwa umeonekana dhahiri na L.J Ibrahim ambaye alimruhusu aulize.

                "Kwa mujibu wa sheria za kitanzania hasa jeshini ni kwamba mwanajeshi yoyote mwenye kuanzia nyota huwa hapandishwi cheo chochote na yeyote isipokuwa na Amiri jeshi mkuu ambaye ndiye mheshimiwa rais, hivyo basi hakuna kiongozi yeyote mwenye mamlaka ya kumpandisha cheo mwanajeshi mwenye kamisheni na rais. Sasa General mara ya mwisho kuonekana mbele ya umma katika mazishi ya General Augustin Kulika ulikuwa na cheo cheo cha luteni jenerali au three star general iweje leo hii tukiwa tumekuja tukuone ukiwa na cheo cha four star general yaani Jenerali, je alikupandisha nani ikiwa mwenye mamlaka hayo ni tayari mmemzuia asitoke ndani ya ikulu?" Mwandishi huyo wa habari aliuliza swali hilo.

                  "Swali zuri kijana na jibu lake ni kama ifuatavyo, Zuber Ameir kwa sasa si rais na aliyenipandisha cheo hadi sasa nimekuwa jenerali kamili ni huyo ambaye ndiye ataingia pale ikulu mnamo kesho asubuhi baada ya ikulu yote kuisafisha usiku wa leo. Swali jingine" L.J Ibrahim alijiu swali hilo kisha akahitaji swali jingine la ziada, waandishi wote walikuwa wametosheka na maelezo hayo na walikaa kimya baada ya L.J Ibrahim kuhitaji swali jingine aweze kulijibu kutoka kwao. Hapo kikao kiliisha na L.J Ibrahim alinyanyuka kwenye kiti alichokuwa amekaa akafunga kikao kisha akaondoka kwenye chumba hicho cha mkutano akiwa na imani kabisa maneno yale yatakuwa yamejenga athari mpya kabisa kwa Rais Zuber akisikia kuna rais mpya tayari ameandaliwa.



    ****



       MTAA WA BREACH CANDY INDIA

    JIJINI MUMBAI, NCHINI INDIA

        Ndani ya mtaa huuu ambao upo chini ya dola ya Maharashtra katika jiji la Mumbai taarifa hiyo ya habari ya kile kilichokuwa kikitokea Tanzania ilikuwa ikishuhudiwa vizuri, watu waliokuwa na wapo ndani ya hoteli ambayo ilikuwa ipo mita kadhaa tu kutoka yalipo makao makuu ya kampuni ya kundi la Tata ambao wamiliki wa shirika la ndege,kiwanda cha magari, pamoja viwanda vingine vingi vilivyo chini ya Tata. Watu hao walikuwa wapo katika chumba kimoja cha hoteli hiyo ya hadhi ya nyota tano wakiwa wamelaliana kwa mahaba makubwa huku kioo cha televisheni kikiwa kipo mbele yao wakikitazma. Walikuwa ni watu wa jinsia moja ambao walifaa kuwa vichwa wa familia wote lakini mmoja wao yeye ndiye alikuwa ni kama moyo wa familia kwa mwenzake, mwenzake alikuwa ni kichwa wa familia tena kwa ndoa ya uhalali kwa mataifa ya magharibi. Watu hao hawakuwa wengine ila ni Askofu Valdermar(Jack Shaw) na Sheikh Ahmed wakiwa hawana nguo hata moja, wote walikuwa wakimtazama jinsi kibaraka wao L.J Ibrahim alivyokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari hadi anaondoka kwenye chumba cha mkutano cha makao makuu ya jeshi.

                   "Haaaaa! Tayari ameshajipa cheo chake kabla muda wakupewa cheo hujafika" Sheikh Ahmed aliongeaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

                    "Na wewe humjui Ibrahim alivyo yaani anapenda sana kuwa mkuu wa majeshi, ila anapendeza akiwa hivyo maana ana mwili wenye mvuto sana yaani" Askofu Vladermar aliongea huku akizishika ndevu za Sheikh Ahmed ambazo zilikuwa zimejaa kwenye kidevu chake, maneno ya kumsifia L.J Ibrahim yalimkera sana Sheikh Ahmed na aliishia kumtazama Askofu Valdedrmar kwa jicho la chuki sana.

                      "Halafu sipendi umsifie mwanaume mwingine ukiwa na mimi Shaw mbona hunielewi"  Sheikh Ahmed alikuja juu muda huohuo mithili ya moto wa makaratasi.

                      "Basi mume wangu nimekuelewa sirudiii tena"  Askofu Valdermar aliongea pasipo kuwa na haya ya kujifanya mwanamke kwa mume mwenzie, aliamua kumbusu Sheikh Ahmed mdomoni baada ya kumuona amekasirika sana.



         Hasira za Shekh Ahmed zilipoa hapohapo na sura yake ya ukali aliyokuwa akimtazama Askofu Valdermar ikarudi kwenye hali ya kawaida, busu hilo alilopigwa lilimfanya anyanyue mkono wake ambao ulikuwa pembeni ukatua hadi kwenye kalio la Askofu Valdermar. Pasipo aibu wala kuihofia hiyo sijda iliyojengeka katika paji lake la uso kwa kusujudu sana, aliliminya kalio hilo la Askofu Valdermar na kusababisha Askofu huyo afumbe macho kwa hisia. Alipoacha kumminya kalio hilo naye alimbusu mdomoni kisha macho akayarudisha kwenye kioo cha luninga ambapo tayari mazingira ya ikulu ya Tanzania yalikuwa yakionekana dhahiri baada ya kikao cha L.J Ibrahim na waaandishi wa habari kuisha.

                    "Watu weusi wajinga sana wapo radhi kuuza nchi kwa pesa tu" Sheikh Ahmed aliongea

                    "Yaani pale kama bodi ilivyopanga mpenzi tuitumie hiyo tamaa yao tupate pesa zaidi, najua Ole akikaa madarakani ule mgodi wa almasi pamoja gesi na mafuta yatakuwa yapo chini yetu tu" Askofu Valdermar aliongea.

                     "Halafu sisi tunamwaga misaada mingi kwa mashoga ili kuwashawishi watu wawe hivyo, tunajenga asasi nyingi za mashoga" Sheikh Ahmed aliongea

                       "Kabisaa mpenzi" Askofu Valdermar aliitikia huku akimbusu Sheikh Ahmed shavuni, hawakujua kuwa mambo tayari yalikuwa yemevunda huko kutokana na uwepo wa kundi la wanausalama wa EASA pamoja na maaskari waadilifu wa JWTZ.

                        "Watajiona wana maendeleo sana kumbe ndiyo tunawatia ujinga hawa, tupo nyuma ya The new wrold order daima na mzizi wetu ni uleule" Askofu Valdermar aliongea kwa sauti legevu sana.

                          "Viongozi wajinga acha sisi tuwatie ujinga zaidi wakati mwenye akili zaidi akitoka ndani ya jengo lao lile wanaloliiita Ikulu ili tumuweke kibaraka wetu tutakayemtumia daima kwa manufaa yetu wenyewe" Sheikh Ahmed aliongea huku akiuchezea mwili wa Akofu Valdermar aliyekuwa amelala juu ya kfua chake, Askofu Valdermar naye hakuwa nyuma alikuwa na kaziya kuchzea kifua cha bwana wake huyo kilichojaa bustani ya uoto mweusi wa asili wa kutoka bara Arabu.



         Walikuwa wakifurahia sana kitu hicho walichokuwa wakifanyiana lakini raha zao zilikatwa tu muda mfupi, walipokatika raha zao wote waliojikuta wakitazama pembeni kukitazama kile kilichokuwa kimewakata raha zao ambacho kiliwapa msjhangao sana. Ilikuwa ni simu ya mkononi iliyokuwa ipo sentimita kadhaa katika sehhemu ya juu ya mtoto wa kitanda ambao huwekwa taa maaulum ya kuangza humo ndani ikiwa watumiaji wa chumb hawataki kutumia taa kubwa, Askofu Valdermar alipindisha mdomo aliposikia simu hiyo kisha akajinyanyua kifuani mwa Sheikh Ahmed akaenda kuipokea.

                      "Enhee! Sema kuna habari gani mpya huko?....... tumekuona aisee hongera ni hatua kubwa mmefikia....mkimaliza mna dau nono kila mtu.......kazi njema" Askofu Valdermar aliongea alipomaliza  akakata simu akamgeukia Sheikh Ahmed aliyekuwa akimtazama muda wote aliokuwa akiongea na simu, aliweka uso kwa kudhrau kama wafanyavyo wanawake halafu akajisogeza karibu na Sheikh Ahmed akajilaza kifuani kama alivyokuwa amejilaza hapo awali.

                        "Vipi kuna jipya lipi maana nahisi ulikuwa unaongea na Ibrahim huyo?" Sheikh Ahmed aluliza

                          "wala hana jipya anataka kusifiwa tu si kingine si unajua anavyopenda kusifiwa yule aonekane ni bora sana kwa ngozi nyeupe" Askofu Valdermar aliongea kwa sauti ya taratibu sana ,Sheikh Ahmed aliposikia maneno hayo alicheka kisha aksikitika sana.

                          "Ndiyo ujinga wa ngozi nyeusi huu yaani mtu akiwa na ngozi nyeupe halafu ana hela basi wanamuona kama ni Mungu vile, wacha tuwatumie kwa ujinga wao huo" Sheikh Ahmde aliongea huku akiiweka mkono yake kwenye makalio ya Askofu Valdermar ambaye alihema kwa nguvu mithili ya mtu aliyekuwa akijigeuza ubavu wa pili akiwa usingizni, naye hakuwa nyuma katika kufanya huo upuuzi wao ambao ulikuwa ni aibu sana kwao ikiwa watasikika na jamii au kuonwa wakiufanya upuuzi huo. Walikuwa wakiufanya upuuzi huo kwenye hoteli ambazo zenye usimamizi mkali sanma kuogopa kukutwa, nyadhifa zao za kidini katika nchi zao hapo walizitumia tofauti kabisa pasipo kuwa na lepe la hulka ya kibinadamu ya kushindwa kuyafanya hayo.



    ****



    DAR ES SALAAM

         Majira ya saa nne asubuhi kwa saa za Afrika ya mashariki gari ya kijeshi yenye nyota mbili ambayo ilikuwa imeongozana na gari mbili za kijeshi zilizosheheni wanajeshi  wenye nyota tatu kila mmoja ambao walikuwa ni wa kike watupu zilifika jirani na hema ambalo lilikuwa likitumiwa na wanajeshi wa ardhi kama makao yao makuu ya muda. Waandishi wa habari walipoziona gari hizo zikiingia katika eneo hilo walizikimbilia kwa kasi sana huku kila mmoja akiwa ameweka kamera yake aweze kunasa chochote, gari hizo ziliposimama tu kundi la wanajeshi walienda kuweka mstari moja katika eneo ambalo lilkuwa mbele ya waandishi wa habari waliokuwa wakizikimbilia gari hizo ili wasiweze kufika karibu.



        Waandishi wa habari walipofika waliishia mbele ya mstari huo uliokuwa umewekwa na wanajeshi hao na hawakuvuka, walitoa kamera zao wakawa wanapiga picha magari hayo ambayo tayari wanajeshi wanawake waliokuwa wamepanda walishashuka. Maaskari hao wanawake walijipanga mstari mmoja kwa haraka sana kisha moja wao akafungua mlango wa nyuma wa gari lililokuwa na nyote mbili mbele na nyuma, M.J Belinda alionekana akishuka hapo akiwa amesuka mtindo mzuri sana ambao ulionekana dhahiri ingawa alikuwa ameuficha kwa kofia yake ya kijeshi yenye rangi nyekundu.



         Wanajeshi wote waliokuwa wapo eneo hilo walipiga saluti kwa pamoja kusababisha kamera za waandishi wa habari ziwachukue wakiwa katika hali hiyo, M.J Belinda  naye alizipokea saluti zao hao wanajeshi waliopo chini yake. Alikuwa amevaa gwanda la kijeshila jipya kabisa na kiatu kilichokuwa kinang'aa kwa dawa maalum aliyopakwa, umbo lake la kiurembo halikuweza kufichika hata akiwa amevaa gwanda hilo. Usoni alikuwa amevaa miwani nyeusi ya jua ambayo ilimfanya azidi kupendeza, M.J Belinda aliposhuka tu alitazama upande ule waliokuwa wapo waandshi wa habari akiwa amesimama mtindo ambao uliplekea kamera zao zifanye kazi ya  kupiga picha tu. Waandishi wa habari wengine walikuwa wakiweka vipaza sauti vyao mbele wakiuliza maswali ambayo hayakujibiwa na M.J Belinda zaidi ya kuwatzama tu kisha akapiga hatua kuelekea ndani ya hema la kikosi cha ardhi.





     Kiatu alichovaa na kijeshi na jinsi miondoke yake ya kike aliyokuwa anaitumia, ilimfanya aonekane kivutio kikubwa kwa jinsi anavyotembea kulekea humo ndani ya hema walipo vijana wake. Kizingatio cha umbo matata, mwili uliojaa hasa mapajani bado alionekana ni mlimbwende ingawa alikuwa amevaa nguo hizo ambazo zikionekana na raia wa kawaida huzihofu sana. Balaa alilo nalo katika mapigano ya ana kwa ana  halikuonekana kabisa kutokana na urembo wake aliokuwa nao ingawa alikuwa akifanya mazoezi sana. Muonekano wake huo kwa nyuma wakati akikaza mwendo  akiwa amewapa mgongo waandishi ulitosha kabisa kufuta mawazo potofu juu ya mwanamke kujiunga na jeshi, wote waandishi wa habari nao walithibitisha juu ya hilo.



        Dhana ambayo ambayo ilikuwa imejengeka juu ya wanawake kukomaaa na kuharibika urembo wao wakijiunga na jeshi, M.J Belinda alikuwa ameifuta kabisa kutokana na muonekano huo ambao ulichukuliwa na kamera mbalimbali za waandishi wa habari pindi alipokuwa akielekea ndani ya hema ambalo wamo vijana wake wa kazi wakichakarika. Hadi anafikia kwenye kizngiti cha hema hilo bado waandishi wa habari waliendelea kummulika na kamera zao, kamera hizo M.J Belinda hakuzijali hata kidogo yeye alisogeza kitambaa kigumu chenye asili ya  turubai kilichomo katika kizingiti cha hema hilo na kuingia ndani.

        Alipoingia tu  dani ya hema hilo alikutana saluti ya ukakamavu kutoka kutoka kwa Meja Kibona ambaye alikuwa tayari ameshatambua ujio wake katika eneo hilo pamoja na wanajeshi wote, M.J Belinda naye aliiijibu saluti hiyo kisha akavua miwani ya jua aliyovaa akaanza kuyasanifu mazingira ya humo ndani ya hema. Alitingisha kichwa kuafikiana na hali aliyoikuta humo ndani ya hema kisha akaketi kwenye kiti kilichokuwa kipo nyuma ya wanajeshi ambao walikuwa wakichakarika na tarakilishi zilizokuwa zikchukua mazingira yote ya ikulu.

                 "Kuna jipya lolote?" Aliuliza akiwa anatazama mazingira ya humo ndani

                 "jipya lililokuwepo ni taarifa ya kujiandaa na mashambulizi kutoka kwa mkuu Mugiso ambaye amesema nijiandae kutishia amani ya wote wa ikulu ikifika majira saa sita leo" Meja Kibona aliongea.

                   "Ok sasa nyinyi  si mnatambua mpo operesheni tofauti na wao, sasa basi akitoa amri hiyo tu mimi nitatoa amri yangu kazi ianze tunaelewana?!" M.J Belinda aliongea aliongea

                   "Mkuu!" Meja Kibona aliitika huku akikakamaa kijeshi.

                   "Vizuri! Nahitaji uongoze njia nikaangalie vijana na silaha zao wamejipanga vipi, hapa muache msaidizi wake atakuwa akikupa taarifa kupitia kinasa sauti maalum juu ya kitakachotokea humu uweze kutoa uamuzi" M.J Belinda aliongea

                     "Mkuu" Meja Kibona aliitikia

    "Tena radio calls zisitumike kwenye mission hii kuanzia hivi sasa tukitoka huko kukagua vikosi hakikisha viongozi wote wa vikosi vilivyopo hapa wapewe vinasa sauti muweze kusikiana, radio call zitasababisha mipngo yetu ikanaswa. Tunaweza tukanda" M.J Belinda alimuonya juu ya utumiaji wa simu za upepo ambazo ni rahisi sana kuingiliana mawasiliano na wanajeshi wa kikosi cha majini na kupelekea mpango wao uvuje kabla haujatimia, baada ya maelezo alimuambia amuongoze hadi alipovipanga vikosi vyote vilivyoingia hapo kwa platoom. Platoom ni sehemu moja kati ya sehemu tatu ya kombania ya kijeshi, sehemu hii ya kijeshi huundwa na section tatu zenye askari ishrini na saba kila moja na kuifanya platoom moja kuwa askari themanini na moja . Section nayo huwa na ashuundwa na unit tatu , unit hizi huwa na askari tisa kila moja na kuifanya section moja kuwa na askari ishirini na saba. Kombania nzima ya kijeshi huwa na askari wapatao mia na themanini na zaidi, huu ndiyo mnpagilio wa vikosi vye jeshi ambavyo hutumiwa wakiwa wapo vitani.

      Meja Kibona alitoka nje ya hema hilo akasimama ambapo wanajeshi waliokuwa wapo hapo nje walitoa heshima  kwake kutokana na yeye kuwa ndiyo mkubwa pekee baada ya M.J Belinda,  kamera za waandishi wa habari nazo hazikuacha kufanya kazi yake baada ya kujitokeza kwake. M.j Belinda alifuatia kutoka na safari hii yale macho yake malegevu yaliyokuwa yamefichwa na miwani ya giza mbele ya kamera za waandishi wa habari yalionekana dhahiri, waandishi wa habari walimpiga picha nyingi zaidi akiwa hawatilii maanani hata kidogo zaidi ya kutilia maanani heshima anazopewa na wanajeshi wake. M.J Belinda alianza kutembea akiwa sambamba na Meja Kibona huku nyuma yao kukiwa na mwanajeshi wa kike mwenye nyota mbili mabegani kwake yaani Luteni, walitembea huku wakifuatwa na waandishi wahabari kwa nyuma ambao hawakuweza kuweza kuwasogelea kutokana na kuonywa vikali sana na wanajeshi.





    ****





        Maji ra hayahaya ambayo M.J Belinda alikuwa akienda kutazama vikosi vyake ambavyo vilikuwa vimeizunguka ikulu, Thomas alikuwa yupo ndani ya mitaa ya Msasani akiwa ametoka kwenye eneo maalum ya kufanya mazoezi(gym). Alikuwa akikimbia mwendo mdogo ndani ya siku hiyo ili aweze kujiandaa vizuri katika kuikabili siku hiyo ngumu sana ambayo ndiyo siku ya mwisho ya kazi ambayo iliyokuwa imemleta nchini Tanzania. Akiwa anaendelea kukimbia na kurudi kwenye ngome yao njiani alikutana na mtu ambaye alimziba njia kwa ghfla na kupelekea asimame, mtu huyo alikuwa ni kijana muuza magazeti ambaye alimpatia Thomas bahasha pasipo kusema chochote kile kisha akapita na kuendelea na safari yake lakini Thomas alimshika mkono kwa nguvu sana. Mtu huyo alisimama akiwa amepiga hatua mbili tu baada ya kudakwa mkono kwa nguvu na Thomas, mkono wake huo uliminywa kwa nguvu sana na kupelekea ajisikie maumivu hadi akawa anajaribu kujinasua lakini hakuweza. Mikono ya Thomas ilikuwa ni imara sana na yenye nguvu kushinda mikono ya huyo mtu.

                 "Kakupa nani hii bahasha uje kunipa?" Thomas aliuliza kwa kiswahili fasaha zaidi na kuzidi kumshangaza huyo ambaye ni muuza magazeti.

                  "Kanipa mdada mmoja yupo pale mbele" Alijibu mtu huyo hukua akifumba macho kwa maumivu baada ya kubwa kwa nguvu mkono wake, alinyooosha kidole upande aliokuwa anatoka lakini hakuwa ameonesha kitu kwani hakukuwa na mtu yoyote upande huo wa aliokuwa akiunyooshea mkono. Mtu huyo alikuwa akiunyooshea mkono upande ambao kulikuwa kuna mgahwa mkubwa sana hapo maeneo ya msasani, Thomas alizidi kumbana zaidi kijana huyo baada ya kutoona mtu mbele yake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

                  "Mbona hamna mtu pale?" Alimuuliza kwa sauti ya chini huku akimkazia macho.

                  "Brooo si usifungue kwanza hiyo bahasha uangalie kama nimetuma kitu siyo kuniumiza hivyo" Mtu alilalamika na kupelekea Thomas aifungue bahasha hiyo na kukutana na karatasi ndani ambayo aliitoa kisha akaanza kuisoma.

         Ndani ya nyumba ile kuna mitambo maalum ambayo ingeweza kutukuta ikiwa ningekubali kile ulichotaka kukifanya Thomas si kwamba nilikuwa sitaki bali tungeleta matatizo isitoshe wenzetu wamekufa jana tu. Napenda utambue hata mimi nakupenda sana Thomas na hakuna msichana asiyetaka kuwa na mwanaume mzuri kama wewe, nimetoka mapema kwenye ngome si kwamba nilikuwa naenda kununua dawa kwamba kichwa kilikuwa kinaniuma sehemu niliyopigwa na kitako cha bali nilikuwa naenda kutafuta mahala tuweze kuongea na wewe ukitoka huko gym. Hatimaye nimepapata mpenzi nakusubiri kwa hamu sana my dear nipo Enot hotel chumba namba 130. Nakusubiri kwa hamu sana laazizi naomba ufanye haraka sana, nimempa hii karatasi huyo muuza magazeti na mimi nimetangulia chumbani

             Akupendaye

              Josephine'



        Thomas alipomaliza kusoma barua hiyo aijikuta akitabasamu mwenyewe kisha akamuachia mkono yule mtu ambaye aliamini alikuwa ni muuza magazeti, alimtazama huku akitabsamu baada ya kumuachia ilia muondoe hofu yule muuza magazeti kwa kitendo ambacho alikuwa amemfanyia.

                    "samahani mtu wangu" Thomas alimuambia huku akitabasamu na akili yote ilikuwa ipo kwa Josephine hasa baada ya kumaliza kuisoma barua hiyo.

                    "usijali broo najua town hatuaminani ndiyo maana ukanikamata hivyo" Mtu huyo aliongea kwa taratibu huku akiishika sehemu aliyokuwa amekamatwa kwa nguvu na Thomas akijichua kwa taratibu.



       Thomas baada ya kujiona amefanya kosa kwa huyo mtu aliingiza mkono mfukoni akatoa noti mbili za shilingi elfu kumi ambazo alimpatia kisha akaanza kukimbia kwa taratibu akielekea kwenye eneo ambalo alikuwa ameelekezwa kwa mujibu wa ujumbe huo uliokuwa umekuja kwa njia ya maandishi. Akiwa njiani kumbukumbu za usiku uliyopita masaa machache baada ya Kamishna Wilfred kuondoka na wenzake wote kuingia ndani ya vyumba vyao ndiyo zilimjia, usiku huo alikuwa amepanda juu ya ghorofa akiwa na chupa ya pomba kupitisha saa kadhaa kabla hajaenda kupumzika kwa ajili ya siku hiyo. Baada ya kukaa juu kwa takribani saa moja alirudi chini ili aende chumbani kwake kupumzika na ndiyo hapo alipomshuhudia Josephine akiwa yupo ndani ya kibukta kilaini sana ambacho kilikuwa kimemkaa sawasawa katika mwili wake hadi nguo ya ndani ikiwa inaonekana na kulifanya umbo lake tata lizidi utata. Juu Josephine alikuwa amevaa kiblauzi kidogo sana kilichokuwa kimeacha sehemu kubwa sana ya mgongo wake apmoja na kifua chake, alikuwa ameinama kwenye jokofu refu sana lilokuwa lipo sehemu ya kulia chakula pembeni ya sebule.

        Ngazi za kushukia chini kutoka kwenye kibaraza cha juu kabisa ya nyumba hiyo chenye viti ambapo ndiyo Thomas alikuwa amekaa,ilikuwa zipo katika sehemu hiyo ya kulia chakula kwa pembeni ambapo kulikuwa kunatazamana s na friji hilo. Thomas alizidi kukumbuka jinsi maungo yao ya katikati ya miguu yake yalipoumuka na kisha dalili za kuja kwa hisia kali zilipomijia baada ya kumuona Josephine ambaye alikuwa hana habari akiwa ameinama akitafuta vinywaji sehemu ya chini ya friji hilo. Tamaa yake kila alipokuwa akimuona Josephine ndani ya nyumba hiyo zilidi kiwango zaidi hasa baada ya kumuona akiwa akiwa yupo ndani ya mavazi hayo, uzalendo ulimshinda Thomas ndani ya muda huo na akajikuta akimsogelea Josephine akitembea kwa taratibu sana ilia siweze kumsikia. Alinyata zaidi hadi alipofikia meza ya chakula ambayo ilikuwa ipo karibu sana na friji ambapo aliweka chupa ya pombe kwa utaribu sana, Josephine muda huo hukuwa na habari kabisa na uwepo wa Thomas eneo hilo. Thomas akiwa bado yupo akikimbia mchakamchaka alizidi kukumbuka jinsi alivyofanikiwa kufika nyuma ya Josephine na kusikilizia kwa sekunde kadha kisha akaipeleka mikono yake akagusa kiuno kilaini cha Josephine ambacho kilikuwa kinaonekana kipana zaidi kutokana na kuwa ameinama. Josephine aliinuka haraka  sana baada ya kushikwa hivyo na kupeleka mkono mmoja wa Thomas uhame kutoka kiunoni na kutua kwenye kifua chake kichanga kilichokuwa kipo ndani ya blauzi hiyo tu, mkono mwingine wa Thomas ulikuwa umeng'ang'qnia kiuno chake huku ukilazimisha kuingia ndani ya blauzi hiyo.



        Kila alipofikiria hicho kitu akiwa ndiyo yupo mita kadhaa kuikairibia hoteli hiyo  maungo nayo yaliinuka ila kwa msaada wa nguo ya mpira aliyokuwa amevaa iliweza kumsaidia asiweze kuadhirika kwa watu waliokuwa waliopo njiani, bado mawazo ya kile kilichokuwa kikitokea jana usiku ambapo Josephine alichukia kiliendelea kurudi kwenye kichwa chake.  Alikumbuka vizuri alivyokuwa akilazimisha kuuupapasa mwili wa Josephine kutokana na papara zilizokuwa zimeuvaa ghfla mwili wake, mkono wake aliokuwa akiulazimisha kuuingiza kwenye blauzi  ya Josephine aliuhamishia haraka na kuupeleka chini ambapo mrembo huyo alikuwa amevaa kaptula laini tu pamoja na kifuniko cha mlango wake. Thomas alikumbuka jinsi alivyofanya haraka zaidi kwa kuupitiasha mkono huo kwenye mpira kifuniko hiko, alipokuwa akiyakumbuka hayo tayari alikuwa ameshakaribia lango la kuingia hoteli hiyo aliyokuwa ameelekezewa kwa mujibu wa barua ya Josephine.



       Alizidi kuongeza mwendo wake akiwa na hamu kubwa sana ya kumfikia Josephine huku kumbukumbu za kile kilichotokea usiku uliopita zikimrudia, alikumbuka jinsi mkono wake ulivyokuwa na papara sana hasa ulipoingia kwenye kifuniko kilichoziba maungo ya Josephine na kukutana hali ya bustani ndogo sana yenye dalili zote za kufyekwa. Thomas alipokumbuka hapo hisia kali zilipanda zaidi katika mwili wake, alikumbuka tena Josephine alivyoshtuka baada ya mkono wake kufika juu ya malango wake usio na komea zaidi ya pazia la mpira tu ambapo ungeingia ndaye pua hadi akamuachia Josephine ambaye alimsonya na kuondoka hapo kwenye friji kwa kasi hata kinywaji alichokuwa akikitafuta miongoni mwa vinywaji vingi usiku huo akawa hana hamu nacho tena.

        Thomas alipokumbuka hilo tayari alikuwa ameshafika kwenye mlango wa kuingia katika hni yangekua mengine. Thomas alipofikia Josephine aliachia kichwa kichwa kikali kilichompata kwenoteli ya Enot ambayo ni maarufu sana hapo Msasani, alijikuta akitabasamu mwenyewe alipokumbuka jinsi alivyopigwa kichwa na Josphine ambacho kilimuachia maumivu pasipo kumletea athari nyingine.

                  "Wanawake bwana fujo zote zile kumbe yupo katika sight" Thomas alijisemea kwa taratibu muda huo akiwa anafungua mlango wa kuingia mapokezi, aliingia mapokezi ambapo alifika kwenye dawati la wahudumu wa hoteli hiyo na akaulizia juu ya chumba hicho alichokuwa ameelekezwa.



        Aliruhusiwa moja kwa moja na kupelekwa kwenye chumba hicho alichokuwa ameelekzwa baada ya wahudumu wa hapo kuwa na taarifa ya ujio wake. Thomas alipotoka tu hapo mapokezi alipanda ngazi moja kwa moja kuelekea juu akiona lifti ilikuwa ikimchelewesdha kufika hicho chumba namba 130, alipanda ngazi hadi ghorofa ya tatu ya hoteli hiyo akatokea kwenye ukumbi mwemba uliokuwa una vyumba vingi sana. Hapo alihesabu mlango wa nne baada eneo ambalo kuna lifti kisha akatembea hadi kwenye mlango huo ulio na namba 130, Thomas alipofika hapo akazidi kukumbuka jinsi mkono wake ulivyokuwa ukitalii kwa lazima umbile lenye ngozi laini la Josephine. Hisia za nwili wake nazo zilimzidi zaidi hadi akaona dalili za wageni kukaribia, hisia hizo zilimpelekea hata asigonge mlango huo na kuufungua kwa papara. Hakujua kama kufanya hivyo lilikuwa ni kosa kubwa sana ambalo hajawahi kulifanya katika kipindi chote alichokuwa akifanya kazi hiyo, alikuwa akiongozwa na tamaa ya mwili kuliko akili zake jambo ambalo ni hatari sana kwa kazi yake hiyo hatari ya kihalifu.



        Mllango ulipotii amri ya kufunguka alimuona Josephine akiwa ameketi kitadani tu akiwa amejifunga taulo fupi ambalo lilikuwa limeacha sehemu kubwa ya mapaja yake nje, Thomas alibaki  ameduwaa kwa sekunde kadhaa na alipozinduka kutoka kwenye mduwao wake aliingia ndani ya chumba hicho kwa kasi sana pasipo kutambua alikuwa akifanya kosa jingine tena. Akiwa ameongozwa na tamaa zake alipouvuka mlango huo kwa hatua tu alihisi kitu kizito kikitua kwenye shingo yake hadi akakosa muhimili akaanguka chini akiwa hata hajamkaribia Josephine, sauti ya kufungwa kwa mlango ndiyo ilifuata baada ya kupokea ukaribisho huo uliyoifanya hadi shingo yake aione nzito kwa ghafla iliyojaa maumivu sana. Thomas alibaki akiwa haoni vizuri kwa athari ya ukaribisho huo aliokuwa ameupokea.



        Kizunguzungu cha ghafla nacho kilimkamata akiwa bado yupo chini hadi nguvu ya kuinuka akaikosa kwa muda huo akisikilizia maumivu, akiwa kwenye hali hiyo ya maumivu alitazama mbele yake kwa sentimita kadhaa akakutana na miguu ya Josephine ambayo alikuwa ameilekeza katika upande ambao unyayo wake ulikuwa umezibwa na kochi ambapo ilikuwa ngumu sana Thomas kuiona wakati anaingia ndani humo. Miguu hiyo ya kirembo ya Josephine ilikuwa ina kitu kingine cha ziada mbacho kilikuwa ni ishara tosha ya kutokuwepo kwa uhuru kwa Josephine, ilikuwa ni pingu ndiyo ishara kutokuwepo kwa uhuru kwa mrembo huyo. Pingu hiyo ambayo ilikuwa ina kamba ngumu sana ambayo ilikuwa imeingia ndani ya uvungu wa kitanda ikiashiria ilikuwa imeenda kufungwa mahall umo uuvunguni, Thomas alijua kabisa alikuwa ameingia katika pango mamba bila kujijua akijua ni shimo la huba ndiyo alikuwa akielekea kuingia.

                   "Thomas nafurahi kukuona kwa mara ya pili" Alisikia sauti ya kiume ikitokea kule ulipo ule mlango  wa kutokea humo ndani ambapo ilimfanya ageuke kwa upesi sana, alipogeuka akiwa bado yupo hapohapo kwenye marumaru alishtuka sana hadi akajivuta nyuma kuelekea upande ambao alikuwa Josephine ili aweze kupata sehemu ya kuegemesha mgongo baada ya kuwa na maumivu sana shingoni mwake.

                      "Hatimaye tunaonana yena kwa mara ya tatu Thomas vipi utatumia kinyaji gani" Sauti hiyo iliomuuliza kwa mara nyingine ikiwa ina furaha mithili ina mkaribisha  mgeni ambaye alikuwa ametarajia kama atakuja kwa ajili ya jambo la furaha zaidi ambalo alitakiwa mgeni huyo awepo.

                       "Damn!  Norbert!" Thomas aliongea huku akimtazama Norbert ambaye ndiye huyo alikuwa akimkaribisha kwa furaha ya kinafiki baada ya kumuachia pigo ambalo limemfanya siwe na nguvu hadi muda huo.

                        "Yes my best friend (ndiyo rafiki yangu mpendwa) umenikumbuka eeeh! Ni yuleyule tuliyepandwa wote ndege moja kutoka Arusha hadi Dar na ni yuleyule niliyewakaribisha kwenye mchezo wa wenye akili kule nyumbani kwa Ibrahim. Sasa karibu tena na hapa ukiwa pamoja na Josephine msichana mtamu zaidi ya vanilla niliyeuonja utamu wake uliopelekea Benjamin atake kumuua lakini kwa huruma yangu nikamuwahi ingawa alimpiga risasi ya bega kisha nikammaliza mimi" Norbert aliongea huku akimsogelea Thomas akiwa hana silaha yoyote mikononi mwake, maneno hayo aliyoyaongea yalimfanya Thomas amtazame Josephine kwa jicho la chuki akiwa bado yupo pale chini.



       Hapo aliotambua kabisa kuwa Josephine alikuwa amewadanganya siku hile alipoeleza juu ya kuuawa kwa Benson, jicho lake la chuki nalo llilipokelewa kwa kutazamwa kwa dharau na Josephine ambaye alikuwa akimchukia sana kwa udhalilishaji wake aliokuwa akitaka kuufanya usiku uliopita kwake. Josephine kila akikumbuka jinsi Thomas alivyokuwa akimshika kama alikuwa akimpapasa kahaba wa bar alizidi kukasirika

                "Thomas ulifikiri sheria hiyo ya mashoga itafanikiwa kupita Tanzania muweze kumkomoa Rais Zuber, hilo mmefeli kabisa, mashoga mtabaki kuwa nyinyi tu na nchi zenu na siyo Tanzania." Norbert alimuambia kwa dharau Thomas huku akizidi kumkashifu kwa kumuita shoga na kupelekea Thomas akasirike sana.

                  "Son of a bitch (mtoto wa mbwa)! Nani shoga?!" Thomas aliongea kwa kwa kali na ajitutumua akasimama ingawa maumivu bado alikuwa nayo na hata nguvu kwenye mwili wake ilikuwa imepungua kabisa, hasira zilezile alizokuwa akimuonya Benson na Santos wasiziendekeze sasa  zilimjia yeye na akawa nazo muda huo kutokana na maumivu aliyokuwa nayo. Alisimama kwa kujikaza ingawa bado alikuwa anayumba kwa kukosa nguvu kutokana na teke zito la shingo alilopigwa na Norbert, akiwa kasimama hivyohivyo alikunja ngumi zake kwa nguvu sana hadi mikono ikawa inamtetemeka





    ILIVYOKUWA

        Muda mfupi kabla ya Thomas  kutoka ndani ya ngome yao, Josephine alitoka wa kwanza akiwa ameaga alikuwa anaenda kununua dawa kwa ajili ya maumivu ya kichwa chake katika eneo ambalo alikuwa amepigwa na kitako cha bunduki  katika siku chache zilizopita. Haukuwa udhuru uliokuwa na uongo ndani yake bali ulikuwa ni udhuru uliokuwa na kweli tupu ndani yake, bado Josephine alikuwa akitumia dawa maalum kwa ajili ya kupunguza maumivu katika sehemu yenye uvimbe ambao ulikuwa umeazna kupungua tangu alipopigwa na kitako cha bastola na Norbert. Alitoka kwa haraka ndani ya muda huo ili aepuke pia kukutana na mwanaume aliyetokea kumchukia ndani ya siku moja iliyopita, hakutaka hata kuonana  naye kwa siku hiyo na muda huo wa asubuhi kwa jinsi alivyokuwa akimchukia mwanaume huyo. Udhalilishaji uliokuwa ukifanywa  na Thomas katika siku iliyopita bado ulikuwa ukizunguka ndani ya kichwa chake, kila akiufikiria udhalilishaji huo alikuwa akizidi kumchukia mwanaume huyo ambaye alimuheshimu kama shemeji yake kwa Marehemu Benjamin.



        Chuki aliyokuwa nayo kwa Thomas ilikuwa ni mara mbili ya chuki aliyokuwa  nayo kwa Norbert kwa kumuulia mwanaume aliyekuwa akimpenda katika maisha yake, kitendo cha kushikwa kinguvu mithili ya kahaba kilikuwa ni tusi kubwa na hakutaka hata kumuona mwanaume huyo ndani ya asubuhi hiyo akiwa na hasira iliyochanganyika na kisirani cha kike. Hasira hizo alizokuwa nazo ndiyo ilikuwa chanzo cha yeye kuumwa kichwa kwa asubuhi hiyo kwani zilikuwa zikimtesa zaidi ya hata alivyoteseka moyoni baada ya Benjamin kufa tena ikiwa sababu kubwa ikiwa ni yeye kwa kusababisha hadi akapoteza umakini wake kwa Norbert aliyesababisha kifo chake. Sehemu ya nyuma iiyokuwa imeathiriwa kwa kupigwa na kitako cha bunduki ilianza kumuuma kwa taratibu kudunda mithili ya kuna moyo wake ndani yake, kukaa mbali na eneo hilo kwa masaa kadhaa ndiyo aliona ilikuwa ni suluhisho sahihi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

         Alifanikiwa kutoka ndani ya nyumba hiyo pasipo kuonekana na Thomas aliyemuona ni adui aliyekuwa yupo ndani yao, siku hiyo hakutumia usafiri kabisa kwani maumivu hayo ya kichwa yalimfanya hata asiwe na hamu ya kuendesha gari. Alitoka hadi  nje ya geti la nyumba ihyo akitembea kwa miguu pasipokutambua kuwa lilikuwa ni kosa kubwa sana kwa yeye kutembea kwa miguu  asubuhi hiyo. Josephine alikuwa akikaza mwendo aziwahi teksi aondoke huko kwenda kununua dawa  akiwa hatambui kabisa kuwa alikuwa tayari ameshafanya kosa kubwa kwa kutoka bila usafiri wa aina yeyote ile. Alipofika mbali na ngome hiyo alihisi  kushikwa begani na mtu kama alikuwa ana urafiki mkubwa sana naye, mtu huyo alimuwekea mkono begani kisha akauzungusha karibu na shingo na akamkaba kwa namna ambayo ni vigumu sana kuonekana na wapita njia. Ilikuwa ni kabali ya utaalamu wa juu iliyoibana shingo ya Josephine kwa kutumia eneo la nyuma ya kiwiko cha mkono.



         Kabali hiyo ilimfanya Josephine aumie kwani bado alikuwa ana maumivu kichwani mwake hasa sehemu ya nyuma ya kichwa na shingo, pamoja na maumivu bado hakuonesha kuwa alikuwa ameumia mbele ya mtu huyo alitulia vilevile ingawa ishara za mwili za kwake zilikuwa zimeshaonekana na mtu huyo kuwa alikuwa amepata maumivu kwa kabali  ile aliyokuwa amemkaba. Josephine aligeuza shingo kwa haraka ingawa haikugeuka vizuri kutokana na kukabwa na mtu huyo, alimtazama yule aliyekuwa akimkaba shingoni mwake kwa muda huo na akapokewa na tabasamu pana haswa kutoka kwa Norbert. Moyo wa Josephine ulimpuka haswa kwa kukutana na mtu huyo akiwa hata hajajiandaa kinamna yoyote kukabiliana naye, uhatari wa Norbert alikuwa akiufahamu vyema  na kuukabili alikuwa akitambua kabisa kuwa maandalizi muhimu sana.



        Alikuwa ameshachelewa kabisa katika kufanya maandalizi  hayo amkabili mtu hatari kama huyo ambaye alikuwa ana akili za zaidi ya binadamu wa kawaida, Josephine akiwa bado hata hajaongeza hatua ya pili alihisi kitu kikimgusa katika mbavu zake kwa kukandamiza. Alipotazama hakuambulia chochote zaidi ya kuona koti zito likiwa limeziba sehemu ambayo mkono wa pili wa Norbert  ambao haukuwa umemkaba shingoni mwake, ugumu wa kitu hicho kilichokuwa kikimkandamiza alitambua kabisa kilikuwa na asili ya chuma au bati gumu. Josephine alisimama ghafla huku  mapigo yake ya moyo yakimuenda mbio sana, fikra zake zilikuwa zimemuambia kuwa huo ndiyo ulikuwa ni  mwisho wake wa kuishi ndani ya dunia hiyo kama wenzake waliokuwa wametangulia. Hofu ya kifo ndiyo ilimchachafya haswa kwa muda huo hadi akashindwa kutembea, alikuwa akihema kwa nguvu sana huku akitazama wapita njia waliokuwa wapo pembeni yake.

         Wapita njia nao walikuwa wapo makini sana katika kuendelea na mambo yao kwani walikuwa wapo katika kuelekea katika mchakato wa kutafuta chakula cha siku, alipoangalia mita kadhaa kutoka pale alipo aliweza kuwaona madereva wa pikipiki wakiwa wanashuhudia kile ambacho kilikuwa kimemkumba ingawa haawakuwa wameelewa uhalisia wa kitu hicho hadi muda huo. Madereva hao waliona kama Norbert alikuwa amemshtukiza mpenzi wake kumbe alikuwa amemtia nguvuni adui yake kwa namna ya kijanja kabisa, Josephine akili yake ilifanya kazi mara mbili ya kawaida na akaona atumie njia ya kike zaidi katika kujikomboa na tukio hilo. Njia pekee ya kujikomboa na  mkono wa Norbert aliona ni kupiga kelele na hakuwa na namna nyingine, hakutambua kuwa wazo lake hilo alilokuwa akilifikiri ndani ya kichwa chake tayari lilikuwa limeshajulikana na Norbert kwenye uwezo wa hali ya ju katika kufikiri.

                   "Usifikirie hilo wazo lako kelele hazitokusaidia kabisa kutoka hapa ni bora uwe mpole tu" Norbert alimuambia Josephine kisha akampiga mabusu mawili akiwa bado ameweka mkono wake  shingoni mwa Josephine, busu moja alimpiga la shavuni na jingine alimpiga la mdomoni.

                    "Tabasamu basi" Alimuambia kisha akamuongeza busu jingine pasipo kujali waendesha pikipiki waliokuwa wapo katika kituo chao wakisubiria abiria walikuwa wakishuhudia suala hilo, Josephine alijikuta akiwa hana ujanja na alitabasamu tu na kupelekea madereva hao wa pikipiki wafurahie kitendo hicho, hawakujua kabisa kama Josephine alikuwa yumo ndani ya hatari wao waliona walikuwa ni wapenzi wa kawaida tu.

                      "Piga hatua na twende ninapoenda, usijidanganye kama unaweza kunitoroka my love. Hii iliyogusa mbavuni mwake ni bastola ileile iliyokujeruhi bega nadhani unaikumbuka. Pia ndiyo aina moja na bastola uliyojaribu kuniteka nayo kule Mwembeyanga, tasabasamu basi jamani usinune hata hupendezi" Norbert alimuamuru na Josephine hakuwa na ujanja alifanya vile alivyokuwa ameamrihwa, maneno yote hayo Norbert alikuwa akuyaongea kwa sauti ya chini sana kama alikuwa akimchombeza mpenzi wake.



          Josephine naye aliachia tabsamu kila alipoambiwa na Norbert afanye ivyo na akazidi kuwapoteza kabisa kimawazo wale madereva wa pikipiki maarufu kama 'Bodaboda' , madereva hao waliona kuwa walikuwa wakipewa faida kabisa katika kuona kile ambacho hawakupaswa kukiona kwa jamii ya kitanzania. Wao waliamini utandawazi ndiyo ulikuwa ni chanzo cha watu hao kuonesha mapenzi hadharani, waliona ni sehemu moja ya burudani katika kushuhudia watu waliokuwa na mapenzi ya dhati hadi wakwa hawaoni hofu kuonesha mapenzi yao hadharani.  Norbert pamoja na Josephine walikaza mwendo hadi wakawapita madereva wa bodaboda ambapo Norbert aliwaonesha dole gumba na wote wakashangilia, alipowapita huko nyuma aliacha wakiwa bado wanawaza kile walichokiona  kwao wakiamini ilikuwa ni mapenzi makubwa kumbe ni mtu katiwa nguvuni na adui yake ambaye ni moja ya watu waliokuwa wapo katika orodha ya watu aliokuwa akiwachukia ndani ya dunia hii.

         Baada ya kuwavuka kwa hatua kadhaa Norbert alitoa Mkufu wenye kidani ambacho kinapendeza machoni kwa mtazamaji yeyote akamvisha Josephine kwa mkono ambao alikuwa ameuweka shingoni, baada ya hapo alimuachia atembee naye akiwa yupo huru kabisa huku silaha yake akairudisha kiunoni kiusiri zaidi.

                   "Ukae utambue nilichokuvalisha shingoni mwako si kidani bali ni bomu, kidani hicho ni bomu dogo  lina hatari kubwa hivyo usijione upo huru kabisa. Tuondoke bibie nimekuhamu sana" Norbert aliongea kwa tabasamu kama alikuwa akimuambia Josephine kitu cha furaha kumbe alikuwa akimuambia kitu kisichohitajika kufurahiwa kabisa labda kifurahiwe na asiye na akili timamu, Josephine aliona sana alikuwa amekamatika kwani ule mkufu aliyokuwa amevalishwa ilikuwa imekamata shingoni mithili ya mikufu ya asili maarufu kama 'culture'.

           Josephine na Norbert walitembea hadi ilipo hoteli ya Enot ambapo walichukua chumba kisha wakaenda hadi chumbani humo kinamna ileile. Muda ambao walikuwa wakiingia ndani ya chumba hicho ndiyo muda ambao Thomas alikuwa akitoka ndani ya ngome kwenda mazoezini ajiweke sawa kwa ajili ya kumaliza kazi iliyokuwa imemleta Tanzania, hakujua kabisa hiyo kazi aliyokuwa akijiandaa wala asingefanikiwa hata kufika muda huo wa kazi hiyo ili aweze kuitimiza.

           Walipoingia ndani ya chumba hicho Norbert aliweka vifaa vingine nyuma ya mlango baina ya chini ya kitasa na chini mahali ambapo komeo la kitasa lilikuwa likiingia pindi mtu anapofunga na ufunguo, kati ya vifaa hivyo viwili aliweka waya mgumu sana ambao ungeweza kuzuia mlango usifunguliwe na yeyote. Baada ya kumaliza kuviweka vifaa hivyo aliweka kidole gumba kwenye moja ya vifaa hivyo na taa nyekundu ikaonekana ikiwaka, alipomaliza kufanya hvyo alimgeukia Josephine ambaye muda alikuwa amekaa kitandani tu akiwa hana ujanja wowote zaidi ya kusali  ndani ya nafsi yake atoke salama ndani ya eneo hilo. Norbert alimtazama sana usoni jinsi alivyokuwa na hofu kisha akambania jicho moja huku akitabsamu, alimsogolea hadi pale alipkuwa ameketi akamshika viganja vya mikono yake kisha akamvuta juu akasimama bila kuleta pingamizi lolote lile.  Alipomsimamisha alimvuta upande wake kisha akaachia viganja vyake na kukikamata kiuno chake kilaini kabisa ambacho kilikuwa kimefunikwa na gauni laini, alimvuta karibu hadi kifua kilichobeba vifuu visivyokuniwa nazi kikawa kimegusa kifua chake. Norbert pasipo kujali hofu aliyokuwa nayo Josephine yeye alimbusu mdomoni huku akimpapasa sehemu mbalimbali za mwili wake, alipomuachia alimtazama huku akitabasamu lakini yeye hakulipata tabasamu kutoka kwa Josephine.

                    "Bibie huna ujanja na ukweli ndani yako tu ndiyo utakaokuokoa na si kingine, mmebaki watano katika mpango wenu kwani Kamishana tayari yupo mikononi mwetu. Sasa chagua ufe wewe au nimpate mwenzako kwa kukutumia wewe" Norbert alimuambia huku akimtazama usoni, Josephine alionekana ni mwenye kufikiria sana  alipoulizwa jambo hilo na alitumia dakika takribani dakika mbili bado hakuwa ametoa uamuzi juu ya suala aliloambiwa.

                    "Aaaah! Bibie huwezi kutoka humu kumbuka nimekufunga bomu shingoni mwako na hata pale mlangoni kuna bomu sasa jiulize utatokaje kinamna hiyo kweli,nimekupa njia ya kutoka humu sasa chaguo ni lako" Norbert alizidi kumshawishi Josephine aweze kumoata yeyote kati ya wanne waliokuwa wapo huru kwa muda huo, alimtazama Josephine usoni huku akiwa anasubiri jibu kutokana na ushawishi wake aliokuwa ameufanya.

       Ndani ya dunia hii hakuna kitu kibaya kama kuwekewa chuki na mwanamke kwani huwa moyo uliojaa kisirani na visasi sana, mwanamke ni mgumu sana kusamehe ikiwa alikuwa amefanyiwa jambo ambalo lilimuumiza ndani ya moyo wake ikiwa hakuombwa radhi. Haa akiombwa radhi pia ni vigumu sana kusamehe ndani ya muda mfupi au hata upite muda mrefu tangu akosewe, ndugu msomaji kama ulikuwa umemfanyia jambo lenye kuchukiza mwanamke kwa maslahi yako binafsi na unatambua kabisa mwanamke huyo anayajua mambo mengi yanayokuhusu  ni bora ukamuombe radhi na ukubali kujishusha. Bila ya kufanya hivyo ni jambo hatari sana kama ulikuwa na adui ambaye anafahamika wazi na mwanamke huyo, Thomas alikuwa amefanya udhalilishaji mkubwa sana kwa mwanmke asiyependa kudhalilishwa namna hiyo na hakuwa ameomba msamaha kwa udhalilishaji huo aliokuwa ameufanya usiku uliopita. Alikuwa akitambua kabisa kuwa Josehine anafahamu kila kitu kuhusu wao na alilichukulia jambo hilo ni kawaida, Thomas aliamini kabisa Josephine asingeweza kufungua mdomo wake katika kulitamka suala hilo kwa yeyote.



       Alikuwa akiamini kabisa kuwa anayeweza kushtaki suiala hilo ni yule mwanamke ambaye hajakua  kimwili na hata mwanaume hamjui, kosa kubwa hilo alilokuwa amelifanya zaidi ya makosa yote aliyoyawahi kuyatenda katika maisha yake ambayo yalimgharimu ndani ya dunia hii. Kisirani ndani ya mwanamke ni jambo la kawaida sana kama bahari kuwa na maji chumvi, hata awe na mafunzo kiasi gani ya kijasusi kama aliyokuwa anayo Josephine bado kiirani kitakuwa kipo ndani yake na ataweza kujizuia kwa mambo ya kawaida ila si kwa kudhalilishwa ikiwa ni mwenye kujiheshimu. Josephine akiwa yupo mikononi mwa Norbert aliwafikiria watu wote waliokuwa  wapo daniya kundi lao na hatimaye akaweka fikra zake kwa Thomas, alifikiria jinsi alivyokuwa akimtomasa usiku uliopita kinguvu kama alikuwa akimtomasa mcheza utupu ndani ya ukumbi wa usiku. Hasira zilimzdi sana na akaona huo ndiyo ulikuwa wakati muafaka wa kumkomesha mwanaume huyo asiyejua thamani na heshima ya mwanamke, bila kusita jambo lolote aliamua kufunguka yote kwa Norbert juu ya Thomas  ambapo alimpa mbinu nzuri adui yake ya kumnasa mwenzake ambaye ana chuki naye.



       Ama kweli chuki ni ndugu wa damu wa usaliti kuwa na mwenye chuki juu yako anaweza kukufanyia jambo baya sana, mpango wa kumnasa Thomas ulipikwa ndani ya muda huo ukapikika na ulisukwa ukasukika. Josephine alipewa karatasi ndani ya muda akaandika ule ujumbe wa maandishi ambao ulikuwa umemfikia Thomas na kumfanya aende mtegoni mwenyewe. Ndani ya eneo hilo Norbert hakuwa peke yake bali alikuwa yupo na vijana wawili wa EASA  ambao aliwaita  kisha akatoa ule waya nyuma ya mlango na kuwapa mpango huo, mmoja wa vijana hao alikuwa ni mwanamke na mwingine alikuwa ni mwanaume. Norbert alipowakaribisha vijana hao alipokea begi la wastani kutoka kwa vijana hao, begi hilo aliliweka kando humo chumbani kisha akawa anasubiri kwa hamu mpango huo ufanyike baada ya vijana hao kuondoka. Vijana walipangiwa kila kitu na Norbert ambapo mmoja alikuwa ndiye yule muuza magazeti aliyempatia ujumbe Thomas na mwingine alikuwa ni msichana aliyejifanya anampa ujumbe kisha akatoweka kabla Thomas hajamuona.

       Baada ya vijana hao kuondoka humo ndani Norbet alirudisha mitego yake kama kawaida kisha akamrudia Josephine ambaye alikuwa yupo kitandani, alimshika vile awezavyo ambapo Josephine hakutoa upinzani wowote hadi miemko ikampanda akiwa  katika hali hiyo baada ya kushikwa maeneo mabaya ya mwili wake. Mihemko mbele ya chuki ina nguvu sana na hapo Josephine akajikuta naye akienda sambamba na Norbert katika zoezi hilo, ndani ya muda mfupi tayari  Josephine alikuwa ameondolewa mavazi yote yaliyokuwa yapo mwilini mwake na Norbert akiwa amepunguza baadhi ya mavazi. Walirudi mchezo ambao walikuwa wameufanya katika chumba cha hoteli kabla hawajaaanza kuisgi kama maadui dhahiri ambao uliwachukua saa moja wakawa wameshamaliza, Norbert baaada ya kumaliza alivaa nguo zake alizokuwa amezipunguza na akaketi kwenye kochi akiwa anasubiri majibu ya mtego aliokuwa amemuwekea Thomas.

       Mtego aliowekewa Thomas ulipozaa matunda wale vijana walimpa taarifa Norbeert ambaye alimuamuru  Josephine apige simu mapokezi na kuwaambia wamruhusu aingie moja kwa moja, Thomas alipokuwa akikaribia ndani ya jengo la hoteli hiyo yule mwanamke ambaye yupo chini ya Norbert alimpa taarifa mkuu wake.   Wakati Thomas akiwa anakaribia kufika mapokezi Norbert alipata taarifa na kwa aharaka zaidi alimfunga Josephine pingu miguuni, pingu hiyo aliifunga na kamba ambayo iliingia chini ya kitanda ikaenda kufungwa kwenye chuma maalum lilipo  usawa wa dirisha. Thomas alipokuwa akikimbia kupanda ngazi yeye aliutoa ule waya wa bomu uliokuwa upo mlangoni na aliuacha mlango ukiwa umerudishiwa tu, Thomas alipofungua ue mlango akamuona nJosephine akiwa yupo ndani ya taulo baada ya kutoka kucheza kwata na Norbert na kuingia kichwakichwa. Norbert alimpa pigo zito la shingoni kisha akaufunga ule mlango pamoja na kuuweka ule waya wa bomu. Hivyo  ndivyo Norbert alivyopanga mawindo yake kwa kutumia akili na hatimaye adui yake akawa ameingia ndani ya mtego wake.



    ****



        Kuitwa shoga na Norbert ni jambo ambalo lilizidi kumvuruga kabisa Thomas, akili yake yote ya kijasusi ilimtoka  ndani ya muda huo akawa anaendeshwa na hasira tu. Hasira zake zilizidi maradufu kutokana na maumivu makubwa aliyoyapata baada ya kupigwa teke zito na Norbert lililoenda  kutua kwenye shingo yake, hasira hizo zilimfanya atumie nguvu tofauti na nguvu alizokuwa nazo muda huo ambazo hata kusimama vizuri ilikuwa tabu. Nguvu hizo za ziada zilimuwezesha kusimama hata kumfuata Norbert akabiliane, hakuwa akijali kabisa kuwa utumiaji wa nguvu namna hiyo ni jambo la hatari sana kwani kuchoka upesi hakukuwa mbali kwa mtu mwenye hali kama hiyo. Thomas akiwa hana hata muhimili wakurusha teke zaidi ya kuwa na muhimili wa kusimama alimfuata Norbert akirusha ngumi kwa nguvu sana tena zisizo na idadi, alikuwa akirusha ngumi ambazo hazikuwa zikifikia lengo na asilimia kubwa zilikuwa zikienda nje ya lengo kutokana na kuongozwa na hasira kuliko akili aliyokuwa nayo ya kimapigano.



      Norbert naye baada ya kuona lengo lake la kumpoteza kiakili adui yake limefanikiwa, alikuwa akikwepa tu ngumi hizo ambazo zilimmaliza nguvu Thomas hadi akawa anamfuata Norbert huku akiyumba kama mlevi. Nguvu zilizidi kumuishia kuliko hata zilivyokuwa zimemuishia mwanzo lakini hakujali yeye alirusha ngumi tu hovyo huku akimfuata Norbert katika kila upande aliokuwa amehama akimkwepa, ndani ya robo saa tangu aanza kupigana alikuwa akihema kwa nguvu sana huku akipepesuka na hata macho alikuwa akitazama kwa kufumba kutokana na kutokuona vizuri baada ya uchovu kumzidi kiwango. Bado hakukubali kushinwa ingawa viungo vyake vilikuwa tayari vimeshakubali, aliamua kumfuata Norbert hivyohivyo hadi nguvu zikamuishia akaanguka alipomkosa Norbert kwa ngumi yake aliyotumia mwili mzima katika kuirusha. Aliangukia kidevu chini hadi akajing'ata ulimi na maumivu aliyoyapata ndiyo yalizidi kumtia hasira hadi akawa anaona kizunguzungu, pamoja na kuchoka bado hakuwa tayari kukubali kushindwa. Alijikakamua na akajaribu kujiinua sakafuni huku mikono yake ikiwa inamsaidia katika kuinuka huko ikiwa inatetemeka, alijitahidi aweze kufika hatua ya kusimama lakini mikono ilimsaliti na hatimaye akateleza mahali pasipokuwa na utelezi na akaangukia kidevu kwa mara nyingine.

             "Aaaaaaaaargh!" Alitoa ukelele dhaifu kwa viungo yake vya mwili kumsaliti katika kumkabili Norbert ambaye alikuwa amesimama mita kadhaa  kutoka hapo alipodondoka akimtazama kwa dharau.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Damu zilikuwa zikimtoka mdomoni kwa kujing'ata ulimi kwa mara  nyingine alipoanguka na kuzidi kuimletea  maumivu ambayo ni aliyaona yamezidi kiwango, alikaa akiwa amelala kifudifudi kwa sekunde kadhaa huku akihema. Bado hakutaka kuonekana amezidiwa kiwango na Norbert yeye aliamua anyanyuke apambane hivyohivyo, aliweka tena viganja vya mikono huku akimtazama Josephine ambbaye alimbinulia tu mdomo kwa dharau tu. Hapo Thomas alipata ujasiri wa ghafla na akajikakamua viungo vyake vyote na akasimama wima ingawa muhimuli wa kusimama sawasawa hakuwa nao kwa muda huo, alihema kwa hasira sana huku akimtazama Norbert ambaye alikuwa anamsubiri aje vilevile kikondoo alivyokuwa akija hapo awali. Thomas alikuwa akihema kwa nguvu sana kutokana na kushindwa kubana pumzi, kuhema huko kulisababisha aache mdomo wazi kwa hakustahimili kuhema kwa kutumia pua pekee kwa jinsi pumzi zilivyokuwa zimemuishia. Aligeuza tena macho akamtazama Josephine pale kitandani alipokuwa amekaa huku damu ikiwa inamtoka mdomoni kutokana na kujing'ata ulimi alipojigonga kievu sakafuni, kuyumba ndiyo ilikuwa desturi yake kwa muda huo mfupi aliokuwa amepatikana katika mtego wa Norbert.

        Alijaribu tena kumfuata Norbert kwa kupiga ngumi za kizembe mfululizo lakini aliambulia patupu tu kwani Norbeet alimkwepa akaenda kusalimianaa ukuta wa chumba hicho ambao uliigonga mwamba wa pua yake kisawasawa hadi akaenda chini kwa mara nyingine,  kila alipoanguka alikuwa akinyanyua uso wake na kumtazama Josephine  ambapo alizidi kuwa na hasira zaidi kwa dharau alizokuwa akioneshwa na Josephine kwa muda huo.  Damu nazo zilikuwa zikimtoka puani pale alipojigonga mwamba huo wa pua ukutani, maumivu yalizidi ambayo yalimpa kiwewe zaidi.

                   "We malaya jua nikitoka mzima hapa ndiyo mwisho wako hutopona kabisa" Aliongea na mawazo yake  huku akimtazama Josephine kwa jicho la chuki halafu akajikaza akasimama tena, safari hakutaka kutumia nguvu zake kabisa katika kurusha ngumi.



        Alimtazama Norbert alipokuwa amesimama kisha akatazama pembeni yake akaona stuli ngumu  ambazo huwekwa kwenye meza za vioo zinazo kaa sebuleni, stuli hiyo ilikuwa imetengenezwa kwa mbao ngumu ya mpingo. Thomas hakutaka kujifikiria mara mbili alipoitazama stuli hiyo yeye aliuma meno kwa hasira  na aliinyanyua juu akiwa ameikamata kwa mikono yake miwili huku akimtazama Norbert, alimtukania Norbert mama yake mzazi kisha akamfuata kwa nguvu akiwa ameishika hiyo stuli akiwa na lengo la kutaka na kumpiga nayo.

        Alipomfikia alimpelekea stuli hiyo usawa wa kifua lakini Norbert alimkwepa, Thomas aliyumba baada ya kumkosa Norbert na hata kabla hajakaa sawa alipokea ngumi nzito  ya kwenye taya kutoka kwa Norbert. Ngumi  hiyo ilimfanya ashindwe kusimama na akawa anaelekea chini akasalimiane na sakafu kwa mara nyingine, akiwa hata hajaifikia sakafu Norbert alimuongeza teke jingine maarufu kama dochi linalopigwa chini ya vidole vya miguu. Dochi hilo la mbavu lilimfanya Thomas aende kusambaratika ukutani, mgongo wa Thomas ndiyo ulipigiza ukutani kwa uzito wa teke hilo hadi akatema damu mdmoni mwake. Thomas alipata maumivu haswa ambayo yalimfanya hata ashindwe kupumua vizuri kwa muda huo, alihisi uti wake  wa mgongo ulikuwa umekosa mawasiliano kwa muda huo uliojipigiza kwenye ukuta

                   "Aaaargh!" Ukelele wa maumivu ulimtoka Thomas  baada ya mgongo wake kusambaratika ukutani, alipotua chini alitua kwa upande mwingine wa mbavu  ambao haukupigwa dochi na Norbert. Maumivu ndiyo aliyasikia kwa mara mbili alipotua  kwa ubavu wa pili huo ambao ulikuwa haujaathirika na pigo la Norbert, maumivu hayo yalimfanya hata asiweze hata kuulalia upande alioangukia na akalala kufudifudi huku akitanua mdomo wa shida haswa. Pumzi zilikuwa zikimjia kwa tabu sana baada ya mbavu zake zote kupata maumivu alipoanguka.

                      "Aaargh!" Aliachia ukelele kwa mara nyingine huku akimtazama Norbert na hapo aliamini kabisa alikuwa amekamatika, upande mmoja wa mbavu alihisi ahueni  baada ya pigo lile na upande mwingine alihisi ndiyo kabisa ulikuwa hauna ushirikiano kabisa.



         Alijaribu kujiinua kwa mara nyingine lakini maumivu ya sehemu  ya ubavu aiyopigwa dochi na Norbert yalimfanya ashindwe kabisa kunyanyuka, aliisalimia sakafu tena akabaki akitoa miguno iliyojaa hasira tu. Norbert naye hakutaka kumuacha hata apumzike kwa sekunde kadhaa tangu amuachie pigo hilo la kuuumiza, yeye alimfuata palepale chini akashika ukosi wa fulana aliyokuwa amevaa na akamkunja. Alimuinua juu huku akimtazama kwa macho makali tofauti na ilivyokuwa hapo awali, Thomas alipoinuliwa hivyo akiwa anatazamana uso kwa uso na Norbert alimtemea mate yaliyokuwa yamechanganyika na damu usoni kisha akajaribu kiumpiga kichwa.



       Mate hayo yaliyotua usoni yalimkera sana Norbert na aliwahi kukikwepa kichwa hiko kisimpate, alipokikwepa kichwa hiko alimsukuma Thomas ukutani kisha akampiga ngumi mfululizo kifuani na kummalizia na dochi jingine la pembeni lililopiga sehemu ubavu wake aliyokuwa ameipiga hapo awali hadi mifupa ya ubavu ikatoa sauti ya kugoka. Thomas aliende chini moja kwa moja na hata kuinuka safari hii alishindwa kabisa akabaki akihema kwa tabu, Norbert alimuacha katika eneo hillo kisha akapiga hatua kadhaa hadi ulipo mlango wa choo cha ndani cha hoteli hiyo.



       Alifika kwenye eneo lililokuwa na sinki la kunawia pamoja na kioo lililopo jirani na mlango huo wa choo, alifungua koki za sinki hilo la kunawia na kupelekea maji yaanze kutirirka. Alikunja mikono ya shati lake baada ya kuona maji yanatoka,  alinawa uso wake kuondoa mate ya damu aliyotemewa kisha akafunga koki za maji. Alipomaliza  kunawa alimfuata Thomas hadi pale alipokuwa amelala akamshika mguu mmoja akawa anataka kumvuta, Thomas bado alikuwa na jeuri na hakutaka kujilegeza kwa namna yoyote.  Aliufyatua ule mguu kurusha teke kwa lengo la kukataa kuvutwa na hapo ndipo aliojizidishia majanga mengine kabisa mbele ya mtu makini kama Norbert, alipoufyatua mguu ule kwa kurusha teke Norbert alisogea kando akiwa ameushika ule mguu vilvile. Kitendo cha haraka aliupiga mguu huo teke katika maungio ya goti hadi ukapinda papo hapo kuelekea pembeni.

                   "Aaaaaargh!" Thomas alitoa ukelele mwingine wa maumivu baada ya mguu wake huo kuvunjwa huku akifumba macho kwa maumivu aliyoyapata.

        Norbert alimpofanyia kitendo hicho wala hakumjali yeye alianza kumvuta kwa nguvu kuelekea sebuleni, alimvuta hadi sebuleni akamuweka mbele kwa mitaa kadhaa kutoka Josephine alipo.



    ****



    MAKAO MAKUU YA JESHI

        Mlango wa ofisi ya mkuu wa majeshi ulifunguliwa na aliingia mtu mzima anayekaribia kuitwa mzee akiwa amevaa suti nadhifu, mtu alipoingia  tu aliketi kwenye kiti kimoja cha wageni miongoni mwa viti viwili vilivyopo ndani ya ofisi hiyo. Haukupita muda mfupi tena aliingia mtu aliyevaa kanzu, koti la suti pamoja na kofia kichwani mwake, mtu huyo alikuwa na alama nyeusi usoni mwake kuashiria kuwa ni desturi yake katika kugusisha paji la uso katika nyumba ya ibada mara tano kwa siku kila siku. Mtu huyo naye kiumri alikuwa akikaribiana na mtu mwenye suti alienda kuketi kwenye kiti cha pili kilichokuwa kipo jirani na kiti cha mwenye suti.



        Wote wawili walitazama mbele yao kwenye meza yenye makabrasha kadhaa ambayo ilikuwa na kiti kimoja, kikiwa mkabala nao, kwenye kiti hicho alionekana L.J Ibrahim akiwa amevaa mavazi ya jeshi la wananchi wa Tanzania(JWTZ) yenye rangi ya kijani kibichi pamoja kofia ya rangi hiyohiyo ikiwa na nembo la JWTZ kwa mbele. Walipotazamana na L.J Ibrahim watu hao walitabasamu na yeye pia akatabasamu kama wao, walibaki wakitazamana kwa sekunde kadhaa hadi pale L.J Ibrahim alipovunja ukimya huo kwa kuongea kile kilichokuwa kimemfanya awaite watu hao ofisini hapo.

                 "vizuri kwa kwenda na muda Mufti na Askofu, nafikiri kazi yetu inakamilika usiku wa leo kuanzia saa sita usiku. Ikifika asubuhi jueni kwamba Mzee Ole ndiye atakayeingia pale magogoni, hivyo basi tukiwa tunaelekea kumaliza kazi hii kuna wajibu ambao kama viongozi wa dini natakiwa niwape" l.J Ibrahim aliongea kisha akaweka kituo akamtazama kila mmoja usoni.

                   "hivi sasa ni saa..." L.J Ibrahim aliongea huku akiitazama saa yake ya mkononi na alipopata uhakika wa majira alisema, "Saa nne asubuhi, zimebaki saa tatu swala ya ijumaa iswaliwe kwa siku ya leo, hivyo basi mufti natambua kuwa katika siku ya leo unatoa hotuba ya ijumaa kule msikitini na vyomba vya habari vitakuwa vikiirusha hotuba hiyo kwa muda husika. Sasa  basi ni wakati wako wa kuhakikisha wananchi wanaamini kuwa Zuber ana hatia na kutoka madarakani ni lazima, propaganda ni sifa ya hotuba na hakikisha katika hotuba hiyo watu hawatotatambua kwamba upo pamoja nami wewe toa msimamo kama kiongozi wa dini".

                  "Shaka ondoa kuhusu hilo General, hotuba ipo tayari nafikiri ni muda wake tu uwadie iweze kutoka" Mufti aliitikia huku akitabasamu

                   "Vizuri sana Mufti, na kwako askofu.." L.J Ibrahim aliridhishwa na maneno ya Mufti kisha akaongea huku akimegeukia Askofu na akaweka kituo kifupi katika maneno yake. Aliendelea kuongea, "Jumapili ndiyo kazi yako katika kuhakikisha mapinduzi yanapewa baraka na waumini wote wa Katoliki, misa ya jumapili inabidi uitumie katika kuhakikisha wale waumini wote wa dhehebu la upande wako wanaukubali uongozi wa Mzee Ole na kuwa na chuki na Zuber. Wale waliokuwa na upendo na Zuber hakikisha chuki dhidi yake zinashika mizizi katika mioyo yao siyo kuchipua tu, kazi kwako Askofu. Malipo ya kazi kwa wote yatafika siku ya jumamosi baada ya mapinduzi kwenye kila akaunti ya mmoja ila Askofu yataingia nusu kwakuwa kazi yako itakuwa haijakamilika, hotuba yako ya jumapili jua ndiyo kukamilika kwa kazi yako".

                  "General hofu ondoa kuhusu hilo kila kitu kipo  ndani ya mpango na siku hii ya leo ni muda wa kuandaliwa tu maneno hayo pamoja na vifungu vya biblia ili walainike mioyo" Askofu aliongea.

                   "Yaani hakikisheni waumini wenu wanajuta kumuachia Zuber awe rais wao, nyinyi tu ndiyo mliobaki watu wa kiluteri tayari hawana imani naye kwa kitendo chake cha kukutana na Moses kwa siri. Sina la ziada niwatakie kazi njema, wanamapinduzi wenzangu" L.J Ibrahim aliwaaga wasaliti wenzake huku akinyanyuka kwenye kiti na akapeana mikono na kila mmoja wao, Askofu na Mufti walitoka ofisini humo kwa L.J Ibrahim kwa kutofuatana ambapo kila mmoja alitoka kwa wakati wake kuhofia kuhisiwa vingine.

       Hawakujua kabisa mtandao wa fagio la chuma nao ulikuwa ni mpana sana kuliko hata huo mtandao wao, wakati gari la Askofu likitoka eneo le getini kuna mwanajeshi mwenye cheo cha Sajini mtumishi aliyekuwa karibu na getini alikuwa akilitazama kwa makini sana huku akipiga picha kwa siri sana. Lilipofuata gari la Mufti alifanya hivyohivyo akiwa yupo kwenye kontena  jirani na getini hilo kwenye upande wa kuelekea ilipo Zahanati ya kijeshi, alipomaliza aliziangalia picha zake hizo na kuhakikisha zinaonekana kiufasaha zaidi.



       Alitazama pande zote na akaona yupo peke yake na hakuna aliyemuona, hapo alizituma picha hizo pamoja na picha nyingine alizotumiwa na mwenzake kama yeye aliyekuwa yupo sehemu ya katibu Mukhtasi wa Jenerali. Alitumia mtandao wa Whatsapp katika kuzituma picha hizo na alipohakikisha zimeenda alifuta picha hizo pamoja na rekodi za mtandao huo zikimuonesha alimtuma mhusika mkuu picha hizo. Baada ya hapo alibonyeza vitufe kadhaa vya simu yake kisha akamaliza na kitufe cha kupiga simu, aliitazama simu yake kwenye kioo hadi alipohakikisha imepokelewa ndiyo aliiweka sikioni.

                 "Enhee! Madam nimetuma sasa hivi fungua Whatsapp utazipata zote.....nashukuru usijali ni sehemu ya kazi yangu kama mzalendo......fagiaaa" Aliongea kwa sauti ya chini na alipomaliza kuongea na simu hiyo aliikata kisha akafuata uelekeo ilipo zahanati ya kijeshi ndani ya makao makuuu hayo ya kijeshi.



    ****



        Baada ya kumvuta na kumuweka katika eneo hilo Norbert alimfungulia pingu Josephine na cheni aliyomvalisha, aliwatazama wote wawili  kisha akatabsamu kama ilivyo kawaida yake akiwa yupo kwenye kazi kama hizo aweze kumchanganya adui yake. Bila ya kuwaambia jambo jingine lolote Norbert alifungua ule mkoba alioletewa na vijana wake na akatoa kasha la makaratasi, alilifungua kasha hilo na akatoa bomu la kutega kwa saa maarufu kama C4. Bila ya kuongea neno lolote tena alilibandika bomu hilo ukutani kisha akaliwasha, sauti ya mishale ya saa ya bomu hilo ilianza kusikika ikitembea jambo ambalo lilizidisha hofu sana kwa maadui zake wakaona kabisa mwisho wao ulikuwa umekaribia. Baada ya kumaliza kutega hilo  bomu aliwatazama maadui zake kwa dharau kuu, kisha taratibu akachukua kila kilichokuwa muhimu kwa yeye kukichukua na akasogea hadi mlangoni akaweka dole gumba kwenye bomu lilokuwa lipo mlangoni. Waya wa bomu hilo uliingia ndani ya sehemu moja ya bomu hilo la mlangoni, baada ya kuutoa waya huo Norbert aligeuza  shingo yake akawatazama maadui zake.

                 "Mna dakika tano tu za kuweza kutoka humu ndani la si hivyo nyote mtageuka vipandevipande kwa hilo bomu hapo uikutani na hili la mlangoni pia. Nikiubamiza mlango huu waya huu unajirudisha sasa atakayefungua mlango na waya huu ukawamba jua ndiyo kifo chenu wote, buriani nyote" Aliongea maneno hayo kisha akatoka ndani ya chumba hicho na akabamiza mlango, waya uliokuwa upo pale mlangoni ulijirudi na ukatga kama mwanzo.

           Josephine na Thomas wakiwa wamebaki mule chumbani walikuwa wana hofu kubwa sana juu ya bomu hilo, Thomas aljivuta kisha akakaa kwenye kochi akawa anamtazama  Josephine akiamini hakuwa na msaada mwingine zadi ya huyo mwanamke kwenye hatari kama hiyo. Alikuwa amevunjwa mguu na pia alikuwa amevunjwa mbavu na hakuwa na hata uwezo wa kusimama kwa muda huo aweze kujaribu hata  kujiokoa, Josephine alipotazamwa na Thomas yeye alimbinulia mdomo tu na hakumtilia maanani. Aliamua kuvaa gauni lake na akachukua kila kilichokuwa chake, baada ya kumaliza kuchukua vitu vyake alilitazama dirisha la kioo la hoteli hiyo kwa mara moja kisha macho yake akayarudisha kwenye bomu lililokuwa lipo ukutani. Alijikuta akimeza funda moja la mate  baada ya kuona dakika zilikuwa zimebaki mbili tu bomu hilo liweze kulipuka, kwa haraka alifungua dirisha la chumba hicho kisha akasogeza pazia na akavua viatu vyake vyenye kisigino akavishikilia.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

                       "Josephine please nisadie usiniache humu" Thomas  aliomba msaada kutoka kwa Josephine ambaye tayari alikuwa ameshaanza kupandisha mguu mmoja adirishani  aweze kutoka nje, kauli hiyo ilimfanya Josephine amuangalie Thomas kwa dharau kisha akamsonya.

                        "Go to hell" Alimuambia huku akiendelea kutoka nje, kauli hiyo ilimfanya Thomas ajirushe kutoka pale kwenye kochi hadi kitandani ambapo pako karibu na eneo la dirisha ambalo Josephine alikuwa akipanda. Bila ya kuchezea muda alijibiringisha kitandani na akasogea hadi dirishani ambapo Josephine alikuwa akimalizia kutoka  mguu wa pili, kwa haraka alimuwahi Josephine shingoni akiwa amepiga magoti kitandani na akamkaba kwa nguvu zote.

                      "Hapa hutoki mpaka utoke na mimi au tufe wote" Thomas aliongea kwa hasira huku akiwa amemkaba akiwa hajali maumivu anayoyapata katika mbavu zake, Josephine alianza kuvutwa kurudi ndani na Thomas akaona ni hatari hiyo kwa yeye kubaki hapo.



        Kujikomboa na balaa hilo aliamua kuutoa mkono wa Thomas lakini hakuweza hata kidogo na  ikabidi ashikilie upande wa dirisha kwa nguvu asiweze kuvutwa kurudi ndani, Thomas naye alizidi kumvuta Josephine ilimradi asiweze kuondoka na bomu liweze kulipuka kwani ilikuwa imebaki dakika moja na sekunde kadhaa baada ya dakika ya pili iliyobakia kukatika hadi muda huo.

        Mlio kengele ya bomu ulianza kusikika kwa taatibu dakika moja hiyo ilipokuwa ikipungua kuelekea kenye sekunde, mlio huo ulimfanya Josephine azidi kuuona umauti ulikuwa ukikaribia kwake kwani muda wowote bomu hilo lingelipuka. Alizidi kukaza mikono yake akitumia nguvu zake za kimazoezi ya kimapigano kuweza kujizuia asiiingie ndani kwani ni hatari zaidi kwake kuingia humo ndani, Thomas alizidi kumvuta kuelekea ndani na akaona alikuwa akifanikiwa baada ya mikono ya Josephine aliyokuwa ameikaza kuanza kuelegea. Naye alilegeza mikono akijua alikuwa akifa pamoja na mbaya wake aliyeweza kumfanya aingie hatarini, aliona Josephine alikuwa akikaribia kuingia ndani na aliamua kutumia nguvu ndogo huku kicheko cha kifedhuli kikimtoka.



       Loh! Salallah! Hakujua kuwa hilo ni kosa kubwa alilokuwa amelifanya kulegeza mikono yake, hakujua kabisa kuwa Josephine naye alifanya hila kulegeza mikono kwa makusudi. Akiwa anaona Josephine alikuwa akikaribia kuingia ndani, ghafla Josephine alishika dirisha kwa nguvu kisha akaachia teke la msamba kwenda juu akiwa hajali kufunuka kwa gauni lake la mpira lenye kuvutika. Teke hilo lilimpata la kwenye paji la uso Thomas hadi akalegeza mikono mwenyewe bila ya kupenda na akamuachia Josephine huku akiyumba, Josephine bila kuchelewa alikaza mikono kwenye pembe la dirisha hilo lisilo na nondo. Alitupa miguu yote miwili kurudi nyuma na ikampata Thomas ya kifuani hadi akaangukia kitandani na akabiringita kwenda chini, baada ya kufanya hivyo alitoka dirishani upesi na akatembea hadi dirisha la chumba cha pili na akashikilia bomba kwa nguvu sana.

                    "NOOOOOOO!" Thomas alipiga kelele kwa kukata tamaa alipoangukia humo dani.

          Muda huohuo muda ulikuwa umeshaisha na mlipuko mzito  ulitokea kwenye chumba alichokuwepo hadi dirisha la vioo likapasuka  na moto ukaonekana kwa nje, mayowe ya watu yalisikika baada ya mlipuko huo  na kengele maalum ya moto ikalia kwa ghafla katika hoteli hiyo. Josephine alipoona amesalimika hakutaka kusubiri tena akutwe katika eneo hilo, alipiga kisigino kioo cha dirisha la chumba cha pili hadi likavunjika hadi kikavunjika. Alitazama ndani ya chumba hicho akaona mlango wa kutoka wazi, hapo aliamua kupenyeza mkono kwenye sehemu ya kioo iliyovunjika na kufungua dirisha hilo na akaingia ndani ya chumba hicho. Hakutaka kupoteza muda yeye alikimbia hadi akatoka nje ya chumba ambapo alikuta kundi kubwa la wau likishuka kwenye ngazi za mlango wa nyuma huku wakipiga mayowe ya uoga, naye alijichanganya kwa haraka huku akipiga mayowe ya uoga kama wengine. Alijipenyeza kwenye kundi hilo la watu akishusha ngazi kwa  kasi sana kama ilivyokuwa wengine, hatimaye katika kujipenyeza huko alifanikiwa kufika nje kwa mlango huo wa nyuma na akatoka akijichanganya na watu waliokuwa wakikimbia kutoka huko kwenye mlango wa nyuma kuzunguka kwenye uzio wa hoteli hiyo kwenda kwenye lango kuu la magari na watu na magari.



    ****



        Muda ambao mlipuko unatokea Norbert hakuwa ameondoka mbali na hoteli hiyo, bado alikuwa yupo ndani ya gari karibu na lango kuu la kuingilia ndani ya hoteli hiyo akiwa na vijana wake wawili aliowatumia katika mpango huo. Baada ya bomu kulipuka vijana wake walionekana kufurahia sana wakijua kuwa kazi ilikuwa imeisha kwa wote waliomo mule chumbani, Norbert hakuwa akifurahia kabisa bali alikuwa akitazama tu kule kwenye lengo la hoteli hiyo.

                   "Mkuu nafikiri wote ni marehemu wale" Kijana wa kiume alimuambia.

                   "Si wote ila yule binti jua hakufa na katoka mzima, nimemuachia opportunity ya kuweza kujiokoa" Norbert aliwaambia.

                   "Kivipi mkuu?" Wa kike aliuliza

                   "Wakati natoka mule ndani nilimfungulia pingu na nilimvua ile cheni" nrbert alijibu.

                   "He! Bosi huoni ni hatari hiyo si mhalifu yule" Yule wa kike alimuambia

                   "Hata kama kwa sasa yule ni sawa na nyoka asiye na sumu kwetu hivyo hatuwezi  kumuhofia, nyoka mwenye sumu tayari amekufa mule kwenye bomu" Norbert aliwaambia

                   "Aaaaah! mkuu wanawake siyo watu wa kuwadharau akiwa mzima yule jua ni hatari kwa nchi" Wa kiume alimuambia.

                   "Vijana najua nikifanyacho nyinyi acheni  kama ilivyo, si niliwaambia hakufa haya muoneni huyo anatoka nje ya geti akijifanya amechanganyikiwa kama raia wengine" Norbert aliongea kisha akakatisha akawaonesha langoni wakamuona Josephine akiwa anatoka huku viatu kashika mkononi, wote walimtazama na wakajikuta wakicheka kwa jinsi alivyokuwa akiigiza kama kapatwa na kiwewe.

                   "Kiwewe cha namna gani kile ukumbuke kuvua viatu uvishike mkononi ukimbie vizuri na si kuvitupa, maigizo ya kibongo haya. Haya tuondokeni" Norbert aliongea huku akicheka na alitoa pia amri ya kuondoka eneo hilo, yule kijana wa kiume ndiye aliyekuwa upo nyuma ya usukani na aliposikia mari hiyo aliliwasha gari na akaweka gia kisha akaliingiza barabarani na kuondoka katika eneo hilo.





       Pindi Mufti na Askofu walipotoka tu ndani ya makao makuu ya jeshi, simu ya Norbeert iliita wakati akiwa na vijana wake wakikatiza katikati ya jiji la Dar es salaam baada ya kutoka Msasani kufanya tukio la kuwapunguza nguvu maadui wa taifa hili. Simu hiyo Norbet aliipokea na kusikiliza kwa makini sana kwani aliyekuwa akipiga alikuwa ni mmoja wa watu waliokuwa wapo upande wake katika kuhakikisha nchi inakua salama na kuvamiwa na wapenda pesa kuliko maslahi ya taifa, hadi simu hiyo inakatwa Norbert alikuwa ameshapokea taarifa mpya kabisa kutoka kwa M.j Belinda ambaye ndiye aliyempigia hiyo simu akampa taarifa ya kila kitu ambacho hakuwa amekifahamu kama kilikuwa kikitendeka. Ilikuwa ni majira ya saa nne na nusu inakimbilia kwenda saa tano kasoro dakika ishirini na tano, Norbert alipomaliza kuongea na simu hiyo alishusha pumzi kisha akawatazama vijana wake. Walikuwa tayari wameshaingia barabara ya Samora jirani kabisa na kituo cha reli cha Stesheni.

                          "Paki gari haraka sana" Alitoa mari na kijana wake aliitii na kuliegesha gari kando ya barabara mita kadhaa nyuma ya makutano ya barabara ya Somora na barabara inayopita mtaa wa Algeria, walikuwa wapo mbele kidogo ya ATM ya benki ya Exim ambayo ipo mitaa kadhaa kutoka ulipo mzunguko wa barabara unaojulikana kwa jina la Clock Tower.

                         "Sikia Boy we shuka uende msikiti wa Sunni karibia na duka la dawa la Shamsudin, ukanunue kanzu na kilemba kwa mara ya nyingine leo naenda kuswali Ijumaa" Norbert aliwaambia huku akitoa pesa mfukoni mwake, wote walicheka waliposikia kauli hiyo kwani wanajua kabisa mkuu wao huyo kanisa tu ilikuwa ni kituo cha polisi kwake. Kuwaambia kuwa alikuwa akienda kuswali ilikuwa ni jambo la ajabu sana kwao, hakujua kuwa kulikuwa kuna sababu ilimfanya yeye aamue kuingia  katika msikiti kwa siku hiyo ya leo.

                          "Haaaa!  Teh! Teh! Teh! Teh! Teh! Mkuu hiyo ni kali ya mwaka ila usisahau kosho najua mule  hotelini ulipotoka, nikiwa kama muisalamu sitakuruhusu uende msikitini hivyo ni dhambi kubwa sana" Kijana yule aliongea hukua akizipokea pesa za Norbert na mlango wa dereva tayari alikuwa ameshaufungua ili ashuke.

                            "Come on! Salum mimi mkristo ila sheria za dini yenu nazijua barabara na hata kiarabu hapa ni nyumbani kwake, tukitoka hapa ni kwenda kuoga hilo kosho then naenda kumsikiliza hatibu wa siku ya leo kuna jambo muhimu la kulifanya huko we kalete hiyo kanzu na kilemba" Norbert alimuambia.

                            "Sawa mkuu" Alitii amri na akashuka garini akamuacha Norbert na mwenzake wa kike waliyekuwa wapo naye kwenye mpango wa kumnasa Thomas ambaye kwa muda huo tayari alikuwa ni marehemu.

                             "mkuu leo umesilimishwa nini teh! Teh! Teh! Teh!" Yule wa kike aliuliza kiutani huku akicheka.

                              "sasa kinachokushangaza ni kipi na wewe kwani hii ni mara ya kwanza kuingia msikitini na nikaswali wakati nikiwa kazini"

                               "Lazima nishangae yaani, kanisa kwenyewe kuingia kwa tabu sana kama teja kuingia kituo cha polisi ndiyo leo hii uingie msikitini"

                               "kwani umesikia kanisani siingii?"

                               "Ndiyo mkuu huingii we umewahi kuingia lini kama kweli unaingia kanisani?"

                               "Eva sasa unaleta utani na muumini wa dhati wa dhehebu la katoliki kama mimi, nitake radhi"

                              "Haaaaa! Muumini gani wewe usiyelijua kanisa nusu mwaka sasa unaenda"

                             "Haloooo! Unaongea nini wewe wakati kila siku naenda kumuomba bwana"

                             "Mhhh! Toka zako wewe na ukijogoo umuachie nani yaani hata CE anakutambua"

                            "Weeeee! Ntake radhi jamani sasa simba atalalaje njaa kwenye msitu wenye vitoweo, anyway tuyaache hayo mara moja"

                           "ahaa! umeona inakulenga siyo unaua mada"

                           "(Akiwa na uso wa umakini) Turudi kikazi zaidi Eva utani kwa mkuu wako una mipaka pia ukumbuke"

                           "Sawa mkuu ila mimi sijapenda kumuona yule demu ulivyompa nafasi ya kujikomboa wakati ni mtu hatari na mwenye mbinu za kijasusi huoni ni hatari"

                           "Yule ni sawa na mamba asiye na meno hana hatari yoyote kwenye mpango wetu hadi unatimia"

                           "Hata kama mkuu kumbuka mamba asiye na meno akija kuota meno hatari ni ileile tu"

                            "Sasa mpaka aje kuota meno ni lini Eva si tayari nchi hii wasaliti washaondoka ukumbuke hana hatari yoyote hata wewe unamdhibiti muache tu aishi sidhani kama atakuwa na imani na kundi lake"

                             "Kwanini unasema hivyo?"

                             "Mpenzi wake mwenyewe ambaye ni mmoja wao alitaka kumuua  sasa hao waliokuwa siyo itakuwaje, na hapo ndiyo hataweza kuweka imani nao na mwishowe ni kushindwa kuendelea nao kwa hao watakaobakia baada ya fagio la chuma kupita"

                             "Haya nimekuelewa"



        Muda mfupi baadaye mlango wa gari ulifunguliwa  Salum aliingia akiwa na mfuko wa plastiki, alimkabidhi mfuko huo Norbert ambaye aliufungua kutazama kilichopo dani yake akatikisa kichwa kukubali huku akitoa tabasamu. Aliuweka mfuko huo katikati ya miguu yake na akamuamuru Saluma aondoe gari eneo hilo wawahi, zilikuwa tayari dakika ishirini zimepotea wakiwa eneo hilo wakimsubiri Salum aliyekuwa ameenda kununua kanzu na kilemba katika eneo la jirani na msikiti sunni ambao ulikuwa na wauzaji wa vitu hivyo kwa nje ya msikiti huo. Saa nne na dakika hamsini na tano au saa tano kasoro dakika tano ndiyo muda huo ulikuwa, ili wasizidi kuweka muda na kuweza kuwahi swla ya ijumaa ambayo Norbert alipanga akaswali waliamua kuondoka eneo hilo kwa kasi ya wastani ili waziwahi taa za barabarani za mtaa wa gerezani ambazo huweka sana foleni kutokana na uwepo wa askari wa usalama wa barabarani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ****



        Majira ya  saa sita na dakika arobaini na tano au saa saba kasoro robo, ndani ya msikiti maarufu jijini Dar es salam Mufti mkuu wa Tanzania alionekana akiwa ameketi nyuma ya mimbari(eneo ambalo hujengwa kama chumba jirani na eneo ambalo husimama imamu akiswalisha swala ndani ya msikiti)  hiyo akisubiri muadhini amalize adhana ya pili aweze kusimama kutoa hotuba ya siku hiyo Ijumaa. Mufti alikuwa akitazama juu yake katika eneo ambalo kulikuwa na eneo la hatibu kuweka karatasi zake anapokuwa anatoa hotuba, katika eneo hilo alijionea vipaza sauti vya televisheni na redio kadhaa ambavyo vilimfanya atoe tabasamu la ushindi akiwa anasubiri bilal wa msikiti huo amalize kutoa adhana aweze kusimama aonekane mbele ya waumini waliojitokeza katika msikiti huo kusikiliza hotuba ya swala ya ijumaa ikiwa ni sehemu ya swala hiyo.



        Mufti huyu aliamua kwenda kinyume kabisa na maamrisho ya Mwenyezi Mungu kwa kuitumia nyumba ya ibada tofauti inavyotumika, ni aibu iliyoje ndani ya nafsi yake lakini wala hakulionea aibu suala hilo la kuitumia sehemu ya ibada muhimu iliyofaradhishwa na Muweza wa yote kama daraja la kufikisha kile alichokuwa akitaka kifike kwa jamii ya kiislamu na watanzania kwa ujumla. Kawaida hotuba ya swala ya ijumaa ipo ndani ya swala ya ijumaa ndiyo maana swala hiyo huswaliwa kwa rakaa mbili tu, raka zingine mbili ambazo huzoeleka kuswaliwa muda wa adhuhuri ni hotuba ndiyo hufidia rakaa hizo. Hivyo hotuba ya swala ya ijumaa ni sehemu ya ibada, muda huo adhana ya pili ya ijumaa ikiwa inakaribia kumalizika Mufti alikuwa akijiandaa kutoa hotuba yake hiyo aliyokuwa ameiandaaa kwa lengo la kuhakikisha  waumini wa kiislamu wanaridhia mapinduzi haramu yaliyokuwa yameandaliwa na washirika wake. Bilal alipomaliza kutoa adhana ya pili dua baada ya adhana ilifuata na kisha Mufti huyo alinyanyuka  kwa mara ya pili tangu atoe salamu kabla ya adhan ya pili haijatolewa na kuruhusu kanzu yake safi pamoja na kilemba alichokuwa amekivaa kionekane mbele ya kamera za waandishi wa habari waliokuwa wapo msikitini  humo kuirusha hotuba hiyo moja kwa moja kwa hadhira.



       Alianza kwa kumshukuru Mungu kama hotuba nyingine zote zinavyoanza, kisha akashuhudia hapana Mola apasaye  kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezimungu na Muhammad (s.aw) ni mjumbe wake. Kutokuwa na hata haya ya kuwa huyo aliyekuwa akimshuhudia ili aeneze ujahili wake alikuwa akijua kila adhm ayake, Mufti aliendelea kuwausia waisalamu hao wamche Mwenyezi Mungu huku yeye mwenyewe akiwa hamchi mwenyezi mungu zaidi ya kumuonesha unafiki ulio dhahiri. Alijiusia na yeye katika kumcha Mwenyezi Mungu kama hotuba ya swala inamvyomtaka ajihusiw, huku nafsi yake ikimsuta amche Mwenyezi Mungu kiukweli na si kiuongo kama alivyokuwa akifanya  kwa tamaa ya pesa tu. Hotuba yake hiyo aliianza kwa kuzungumzia nafasi yao katika dini na pia kumuunga mkono mtu mnafiki na aliyechukua imani zao kwake kama silaha za kuwachapia wao wenyewe na pia kufanya kile akitakacho akiamini hawawezi kuamini wakisikia, aliianza hotuba hiyo kwa namna ya kisiasa zaidi ambapo haikujulikana alikuwa akiongelea nini hadi pale alipofika katikati ya hotuba hiyo. Hapo aliweza kuzivuta fikra za waumini waliohudhuria ibada hiyo kumsikiliza zaidi na pia kuwa na imani na kile alichokuwa akikiongelea kwa muda huo.



       Bila ya haya yoyote alitoa vifungu vya kitabu kitukufu Qurani na pia kutolea ushahidi wa hadithi huo ushetani wake aliotaka uridhiwe na wanachi wa kawaida, alikuwa akiongea kwa kihisia zaidi na kutoa vigezo hivyo kama kweli alikuwa akiongea kama kiongozi mkuu wa kiislamu katika kutoa msimamo wake juu ya masuala hayo. Ilikuwa ni hotuba iliyokuwa ni ndefu tofauti na hotuba zingine za swala ya Ijumaa zilizoeleka kutolewa ndani ya msikiti huo ambapo saa saba na robo ndiyo sehemu ya kwanza ya hotuba hiyo ilimalizika na Mufti aliinama sehemu ya mimbari baada ya kumaliza kusoma dua, alikaa sehemu hiyo ya mimbari akiwa haonekani kwa muda wa dakika takribani mbili na alipoinnuka alimshukuru kama alivyokuwa akianza kuhutubia kisha akaendelea na sehemu ya pili ya hotuba hiyo iliyokuwa ni hotuba ya kishetani iliyotumia nguvu na elimu ya Mufti katika kuwaaminisha waumini wasiotambua lolote lililokuwa likiendelea nyuma ya pazia.



       Sehemu ya pili ya hotuba hiyo ilichukua robo saa na saa saba na nusu akamalizia kwa kusoma dua kisha akamuamuru Bilala akimu swala watu waweze kuswali. Bilal alinyanyuka kwa haraka na akakimu swala na kama alivyopokea mari kutoka kwa Mufti, watu ndani ya msikiti huo walisimama kwa haraka na wakapanga safu kwa ajili ya kuswali swala hiyo tukufu inayoongozwa na Shetani aliyekuwa yupo katika umbile la binadamu. Mufti alikuwa tayari ameshatoka kwenye mimbari muda huo na alikuwa ameshikilia kipaza sauti akiwa yupo mbele ya safu ya kwanza, aliwahimiza watu wanyooshe safu zao huku akiangalia pande zote za za safu ya kwanza. Aliporidhika  kuwa safu ilikuwa imenyooka aliwasogeza watu waliokuwa wapo safu ya kwanza na akapata wasaa wa kuangalia safu ya pili huku akihimiza watu wanyooshe safu zao, baada ya kuridhishwa na unyooshwaji wa safu ya pili alirudi hadi mbele kwenye eneo maalum la kuswalisha na akakaa mbele ya mtu aliyekuwa yupo katikati ya safu kwanza kwa hatua moja.

                       "Allah akbar" Alifungua swala kwa takbira ya kurimia swala swala, alitulia kwa sekunde kadhaa kisha akasoma sura ambayo ni nguzo ya swala, swla hiyo ilichukua muda wa dakika takribani kumi ikawa imeisha. Waandishi wa habari walikuwa tayari wameshazima kamera zao na kipindi kilichokuwa kikirushwa moja kwa moja katika vituo mbalimbali vya luninga pamoja na redio ziizopo ndani ya Tanzania kilikatishwa kwa muda.



    ****



         Muda ambao hotuba inatolewa hadi inaisha  Norbeet alikuwa yupo ndani ya msikiti huo akiwa amevaa kanzu nadhifu sana, kilemba kilichofungwa kwa utaalamu wa hali ya juu. Kidevuni alikuwa amebandika ndevu za bandia zilizomkaa sawasawa na usoni alikuwa na sijida ya kubandika, sijida hiyo ilikuwa ni ngumu sana kujulikana kama ilikuwa ni feki kwa muumini yoyote kwa jinsi ilivyokuwa imebandikwa kwa utaalamu wa hali ya juu. Kimtazamo alikuwa hana tofauti na muumini mzuri wa msikiti kumbe kuingia kwake ilikuwa ni aghalabu sana kwa kazi maaluma kama hizo. Baada ya kutolewa salamu aliinuka kisha akafunga swala ya sunna baada ya swala, aliswali swala hiyo kisawasawa kama alikuwa ni muumini wa dini wa kiisalamu kumbe alikuwa yupo kwa kazi maalum humo msikitni.

         Ndani ya shirika la EASA ilikuwa ni jambo la kawaida sana kwa mpelelezi kama yeye na wa daraja moja yeye kujua mambo mbalimbali ya kijamii, alikuwa na elimu ya dini zote mbili yaani ukristo na uislamu kwa daraja ambalo walikuwa nalo masheikh na viongozi wakubwa wa kanisa. Ujuzi wa elimu hii ndiyo hata ulimuwezesha kujichomeka katika kundi la viongozi wa kanisa la kiluteri katika siku ya kumpokea Askofu Valdermar uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere. Sasa ametumia elimu hiyohiyo aliyokuwa amefundishwa na akiwa katika mafunzo yake kabla hajaingia kazini katika kujichomeka katika msikiti huo aweze kuswali pamoja na waumini wa dini ya kiislamu.

        Baada ya kumaliza kuswali swala ya sunna  aliwapa mikono waliokuwa wamekaa kushoto na kulia kwake, alipowapa mkono watu hao aliweka kiganja chake cha mkono huo wa kulia kifuani mwake kisha akanyanyuka hapo alipokaa na taratibu alianza kupiga hatua akikwepa baadhi ya watu waliouwa wamekaa chini wakisikiliza maneno machache kutoka kwa Mufti baada ya swala  muhimu ya Ijumaa kuweza kuisha . Norbert alifanikiwa kutoka hadi nje ya msikiti huo na akaenda hadi kwenye eneo lenye magari mengi yakiwa yameegeshwa, aliingiza mkono mfukoni na akatoa funguo kisha akabonyeza  kitufe cha rimoti kilichokuwa kipo kwenye ufunguo huo. Gari aina ya toyota Noah muundo mpya yenye rangi nyeusi ilitoa mlio pamoja na taa za pembeni kuwaka kisha mlango ukafunguka, Norbert alienda hadi ulipo mlango wa dereva wa gari hiyo akafungua kisha akaingia akaketi kwenye kiti  na akafunga mkanda. Alitulia hivyohivyo kwenye kiti hicho kwa muda wa dakika takribani ishirini, mnamo saa saba na dakika hamsini na na tano ikiwa imepita muda wa dakika ishirini na tano toka amalize kuswali swala ya ijumaa na pia  zikiwa zimepita dakika ishirini amalize kuswali swala ya sunna. Mlango wa nyuma wa gari hiyo ulifunguliwa kwa taratibu sana, alipoangalia kwenye kioo cha pembeni upande wa kushoto alimuona mwanamke aliyevaa mavazi ya kistara zaidi akiwa na binti aliyevaa nikabu (vazi ambalo huvaliwa na baadhi ya wanawake wa kiislamu kwa kuficha uso na kuacha macho mtu).

                       "Assalaam alaykum" Mwanamke huyo alisabahi

                       "Walaykum salaam" Norbert aliitikia huku akitia lafudhi ya kiarabu ndani ya maneno yake

                       "Hee! Kijana uko makini sana mwanangu na kazi yako tofauti na yule Faraji akinileta kuswali swala ya Ijumaa kila siku. Ingekuwa yeye Wallahi tungasubiri hapa nje ya gari mpaka mawaidha yote ha watu wote msikitini ndiyo naye afuate" Mwanamke huyo aliongea huu akiingia ndani ya gari na binti huyo alifuata.

                        "Mama mimi nkajua kazi yangu hivyo siwezi kuweka usubiri, lazima nfanye haraka nno nkimaliza baadiya tu basi natoka" Norbert aliongea kwa lafudhi ya kipwani.

                      "Vizuri basi Baba tuwahishe nyumbani, wee Ilham hebu funga mkanda basi usalama kwanza" Mwanamke huyo alimuambia yule binti aliyekuja naye ambaye tayari alikuwa ameshapanda naye ndani ya gari.

                       "Mama  nawee si nipo siti ya nyuma mkanda wa nini" Binti huyo aliyekuwa akiitwa Ilham aliongea akiwa hafungi mkanda kama alivyoambiwa na mama yake.

                       "Mh! Mwana mbishi wewe haya" Mwanamke huyo alimuambia

                       "Kwanza mama mimi ninaona joto ngoja nitoe hii nikabu" Ilham aliongea.

                       "Wee tena ntolee ujinga wako umeona Majid ni harimu yako hapa, ole wako ufungue naenda mwambia baba yako. Majid baba tuwahishe nyumbani" Mwanmke huyo aliongea kumkanya mwanae kisha akamuamuru Norbert awawahishe nyumbani.



        Alikuwa ni mwanamke aliyekuwa akishikilia haswa sheria za dini hadi nyingine akazidisha ndiyo maana alimuhimiza sana binti yake kufunika uso wake ingawa haikuwa ni lazima kuufunika uso kwa binti kama huyo kwa mujibu wa sheria za kiisalmu, Norbert alipopokea amri hiyo aliwasha gari kisha akaweka gia ya  kurudi nyuma aliondoe gari hilo sehemu ya maegesho ya gari ya msikitini hapo. Utaalamu aliokuwa nao katika udereva ulimuwezesha kulitoa gari hilo hadi sehemu ya wazi miongoni mwa magari yaliyokuwa yamebanana, aliliondoa gari hilo kwa mwendo wa wastani akielekea kwenye lango la hapo msikitni.



    ****

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

            SAA MOJA BAADAYE

         Ilikuwa ni muda ambao Mufti alikuwa amemaliza kujibu maswali ya waandishi wa habari ambao walikuwa wamemzonga mbele yake pindi alipotoka msikitini tu, muda huo Mufti alikuwa yupo ofisini kwake akiendelea na kazi kama kawaida baada ya kumaliza kazi aliyokuwa amepewa kwaa sharti la kupewa donge nono na washirika wake. Alikuwa ni mwenye furaha haswa baada kutoa hotuba hiyo ambayo iliibua chuki kubwa juu ya Rais Zuber, alikuwa ametoka kutibua kabisa heshima ya Rias Zuber aliyokuwa amejijengea nchini kwa kutekeleza yale yote yaliyokuwa yakihitajika kutekelezwa na wananchi.



       Muda huo hakuwa akijua kama alikuwa amelirusha bomu la machozi kwa mtu aliyekuwa naye karibu bila ya kujiziba asiathiriwe na  bomu hilo, wala hakuwa akijua bomu hilo alilolipua basi wangetokwa na machozi wote pamoja yule mtu aliyekuwa akimlenga kumlipua na bomu hilo. Alikuja kutambua kuwa hakuwa amechukua vifaa vya kujikinga na bomu hilo baadaye, bomu hilo hadi muda huo lilikuwa halijalipuka tangu alirushe na muda huo lilikuwa likielekea kulipuka. Muda wa kulipuka bomu hilo ulipokaribia simu yake ya mkononi iliita kwa fujo hapo ofisini kwake, aliitazama simu hiyo na alipoona jina la mpigaji alitoa tabasamu kisha akaipokea kwa haraka.

                "Sema General......kama kawaida yangu nimeenda vilevile...asante sana General.....sasa kazi kwenu ndiyo imeabaki kuhakikisha huyo mtu anatoka mtawala aingie rasmi.....sawasawa mapinduzi yanawezekana hapo.....hamna shida Generala mchana mwema na wewe" Alipomaliza kuongea na simu hiyo alikata simu kisha akaiweka mezani simu hiyo na akashika faili, alianza kulipitia faili hilo  kwa taratibu na haikuchukua muda simu yake hiyo ikaita tena na muda huu namba binafsi ndiyo ilionekana ikimpigia.



        Mufti aliacha kukagua faili hilo na akaichukua simu yake ya mkononi kwa mara nyingine akaitazama kuangalia mpigaji hakuona namba yoyote zaidi ya kuona neno 'Private' likiwa limejitokeza kwenye kioo hiko, Mufti aliipuuzia simu hiyo na akiiweka iite kimyakimya huku akiendelea kupekua faili. Simu iliiita mpaka ikakatika yeye aliendelea kulipekua hilo faili alilokuwa amelishika ambalo lilikuwa na kurasa nyingi sana, simu kwa mara nyingine iliiita ambapo alichukua kisha akaitazama na alipoona ni namba ileile binafsi iliyokuwa ikimpigia aliamua kubonyeza sehemu ya kuifanya simu hiyo iite kimyakimya lakini si kuiweka simu isiweze kutoa milio kwa simu zingine zitakazoingia.. Aliendelea kupekua faili alilokuwa amelishika na akaingia ukurasa mwingine wa hilo faili, alipofika kwenye ukurasa mpya wa hilo faili aliona kitu ambacho kilimfanya anyanyue mkonga wa simu ya mezani kwa haraka sana na akabonyeza namba kwenye simu hiyo ya mezani huku mkonga akiupeleka sikioni.

                     "Assalaam alaykum Ukti..... naomba uniletee hati za viwanja vile tulivyopanga tuviuzie kwa wawekezaji.....sawa nasubiri na pia mgao wako upo tayari fanya hima uje nazo ofisini kwangu nikupatie" Alipomaliza kuingia na simu hiyo ya mezani, simu yake ya mkononi iliita tena na  safari hii akaona ni usumbufu akaipokea kwani namba ilikuwa ni ileile binafsi. Bomu alilokuwa amemrushia adui yake ili limtoe machozi muda huo ndiyo lilikuwa limelipuka, sasa machozi kutokwa  wote ni jambo la kwaida sana

                    "Walaykum salaaam, nani mwenzangu....unasema nani" Aliposikia utambulisho wa mpigaji wa simu hiyo alianza kutetemeka huku mpigo ya yakimuenda mbio na alisema, "N001 nini unataka kwangu?.....Hapana Mama Ilham wangu na Ilham wamekusoea nini jamani.....no usifanye hivyo sikiliza kijana" Alipokuwa akijaribu kumuhimiza N001 ambaye  ndiye aliyempigi simu simu ilikatwa kwa ghafla.

    "Halloo haloooo!" Aliongea kwa sauti lakini mpigaji alikuwa ameshakata mawasiliano tayari.



     Ubaya wa simu binafsi ni kutoweza kumpigia mpigaji aliyepiga simu hiyo ikiwa atakata,  simu hizi huweza kukupigia tu na si kumpigia mpigaji ikiwa atakata. Jambo hili lilimfanya Mufti ashindwe kuipiga namba ya N001 ilikuwa imempigia muda huo, kila alipojaribu kuipiga simu hiyo hakuiona namba  zaidi ya kuona neno 'Private'.  Alikuwa haamini kama namba ya mpigaji ilikuwa haionekani kwa  jinsi alivyochanganyikiwa na akajikuta akipiga tena simu hiyo, matokeo ni yaleyale kila alipopiga simu hiyo kuwa hakuna namba katika rekodi za kuingia katika simu hiyo. Mufti alianza kuhema kwa shida sana alipoona namba ambayo ilikuwa ikimpa taarifa ya kushikiliwa kwa mke wake na binti wake ilikuwa haipo, taratibu wahka aliokuwa nao ulianza kumsababishia hata kofia aliyokuwa ameivaa kichwani  mwake aone ilikuwa ikimletea joto.



        Kofia yake ya bei ghali iliyonakshiwa kwa uzi uliotengeneza pambo zuri aliivua akaiweka mezani, bado joto alikuwa akiliskia mwilini mwake na ikambidi avue na koti la suti alilokuwa amevaa juu ya kanzu. Upendo aliokuwa nao kwa mke wake taratibu ulianza kumtia hofu nzito ambayo ilifanya hata mapigo yake ya moyo yaende mbio, kiti alichokuwa amekikalia alikiona kilikuwa kikimuumiza na ikambidi asimae wima ofisini hapo mikono akiwa ameweka viganja vya mikono usoni mwake kutokana na kugwaya kwa taarifa aliyokuwa amepewa na N001  katika simu aliyokuwa amempigia. Aliweka mikono hivyo usoni huku akihema kwa kasi na alipoitoa mikono usoni jambo la kwanza alilolikumbuka ilikuwa ni kuichukua simu yake ya mkononi na  kutafuta jina la dereva wake mpya aliyemtuma kwenda kumchukua mke wake na kumpeleka msikitni kwa siku hiyo ya Ijumaa.



       Alipiga simu namba ya dereva wake huyo na kuiweka simu sikioni, alisikiliza mngurumo wa kuita kwa simu hiyo hadi pale  ulipokoma baada ya simu kutopekelewa. Bado hakuchoka aliipiga tena namba ya dereva huyo na simu iliita vilevile kisha ikakatika, Mufti alizidi kupagwa akajikuta akizunguka humo ofisini kwake akiwa hana uelekeo maalum.  Taratibu kichwa kilianza kugonga kwa maumivu ya taarifa hiyo na akajikuta akikaa chini kwenye zulia ofisni kwake kama kulikuwa hamna kiti, alijifikiria kwa muda alipokaa chini kwenye zulia hapo ofisini kwake na alichukua simu yake kwa mara nyingine kisha akapiga namba za nyumbani na akaisubiria simu ilipokuwa ikiiita hadi inapokelewa.

                 "Enheee Subira!....vipi mama yako karudi hapo nyumbani......inamaana toka atoke hapo kwenda msikitini hajarejea...ok sawa mwanangu"  Alipomaliza alikata simu kisha akajikuta akimtukania tusi zito N001  tofauti na wadhifa wake unavyomtaka kuishi, alirusha mikono huku na huko huku akijifikiria cha kufanya na hatimaye akaitafuta namba ya dereva wake kwa mara nyingine na kisha akaipiga. Safari hii simu ya dereva wake huyo mpya aliyetoka kumuajiri siku chache zilizopita, ilipokelewa, Mufti ilipopokelewa hiyo simu alianza kuongea kwa wahka mkubwa hata bila ya salamu.

                   "Eheeee! Majid......walaykum salaam....ah! Ukti si kwema sana vipi  Majid  yupo wapi?.... Unasema? Kalazwa tangu saa tano kwa kubanwa na pumu.......heeee! Mbona nimesikia kenda mchukua mke wangu kumpeleka msikitini na mpaka sasa mke wangu hajarejea nyumbani.......unasemaa! Kaja dereva dereva mwingine kamuachia gari baada ya kunipigia simu nikawaahidi kuwa nitamtuma mwingine aje kuchukua gari hapo nyumbani kwake.......ooooh! Mungu wangu" Mufti alipomalizia kauli hiyo alikuwa amekaa kitako na kiwiliwili chake kililegea kisha kikamalizia kwa kuanguka kurudi nyuma fahamu zilimpotea pao hapo.



    ****



         Moja ya kitu kilichokuwa kimewahi kuleta athari kubwa tangu kuwahi kupata uhuru kwa Tanzania, basi hotuba ya Mufti ilikuwa ni miongoni mwa vitu hivyo. Baada ya kumalizika kwa hotuba hiyo tayari waumini walikuwa wameshajikusanya na ilipotimia muda huu ambao Mufti alikuwa akipokea simu ya N001 maandamano makubwa ya kiislamu ambayo hayakuwahi kutokea nchini Tanzania yalianza kuchukua nafasi yake kwenye msikiti huo ambao ulikuwa umetolewa hotuba hiyo na Mufti katika swala ya Ijumaa. Maandamano hayo yalikuwa ni maandamano yasiyokuwa na kibali na hata polisi walishindwa kuyazuia, jeshi la polisi lilikaa kando kuhusu suala hilo na hawakuthubutu kuingilia maandano.



        Kuhofia jeshi la wananchi lililokuwa likitaka kumpindua Rais kwa sababu hizohizo hawakuingilia maandamano hayo. Maandamano hayo yalipita katikati ya jiji na kisha yakapita kwenye mitaa mbalimbali, maandamano hayo yalikuja kuweka kituo jirani kabisa na ikulu kwenye upande wa barabara ya Obama mita kadhaa kutoka ikulu ilipo kwa upande wa barabara inayopita karibu na viwanja vya gofu vya Gymkhana. Hapo waumini hao wa dini ya kiislamu wasiojua chochote kinachoendela waliweka kituo tena barabarani kwakuwa barabra iyo ilikuwa haitumiki kwa muda huo, waumini hao wakiwa hawajui chochote walikuwa wakipaza sauti juu kwa nguvu wakishinikiza Rais Zuber atolewe madarakni wakidai hakufaa kuwa rais hata kidogo. Waislam hao hawakuridhika kabisa kukaa hapo katika kushinikiza Rais Zuber atolewe madarakani, walisogea mbele zaidi hadi wakafika karibu na hospitali ya Ocean road ambapo waliweka kituo nacho wakendelea kushinikiza vilevile Rais Zuber hakufaa kuwepo madarakani alitakiwa atolewe mapema.



       Kiongozi wa maandamano hayo alikuwa ni Sheikh maarufu sana ambaye yupo chini ya taasisi ambayo Mufti alikuwa akiiongoza, mtu huyo ndiyo aliwashawishi waislamu waweze kuandamana naye hadi huko baada ya kumalizika kwa swala ya Ijumaa. Ajabu kabisa aliyetoa hotuba iliyokuwa imeleta uchochezi hakuwepo kabisa kwenye maandamano hayo, waislamu hawa waliokuwa hawajui walitendalo wala hawakujiuliza kuhusu kutokuwepo kwake Mufti katika maandamano hayo. Hawakujiuliza kabisa kuwa imekuwaje huyo aliyekuwa ametoa tamko hilo ambaye alikuwa na taarifa na maandamano hayo hakuwa amejiunga nao, walikuwa hawana tofauti na wafuasi wa vyama vya siasa ambao walikuwa wakihimizwaa waandamane na viongozi wa vyama vyao huku viongozi hao wakiwa hawakushiriki maandamano hayo yenye kupinga jambo hilo kuonesha msimamo wao kivitendo na si kimaneno. Waumini hao walipoona kamera za waandishi wa habari zikiwaosogelea ndiyo walifanya sifa kabisa kwa kuzidi kupaisha sauti zao wakishinikiza hilo suala, walikuwa wapo huru zaidi kwani hakuna chombo cha dola chochote kilichokuwa kimewaingilia katika maandamano hayo yasiyo na kibali kama ilivyozoeleka kuingiliwa kwa maandamano mengine yasiyo na kibali katia nchi hii.



       Walivimbishwa vichwa zaidi walipoona kamera za waandishi wa habari zilikuwa zikichukua tukio zima, walijua kabisa kuchukuliwa huko na kamera za waandishi wa habari Rais Zuber alikuwa akiona kila kitu moja kwa moja. Kupata uhakika wakuwa ujumbe wao ulikuwa unafika moja kwa Rais Zuber wao ndiyo walizidi kupaza sauti wakimwaga shutuma mbalimbali juu yake, walikuwa ni watu wasiojua walitendalo wakitumia misimamo ya dini kwa jambo la uzushi walilokuwa wamepewa na kiongozi wao  ambaye hakuinua mguu wake katika kufuatana nao ili athibitishe kuhusu uzushi huo. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



       Waumini bila ya kutambua walikuwa wakifanya makosa waliamua kumbadili jina Rais Zuber na kumbandika jina ambalo hakuwahi kuitwa katika maisha yake yote, walisahau kabisa  alikuwa ni muumini mzuri sana na swala za ijumaa alikuwa hakosi katika misikiti labda awe ametingwa na kazi za kiofisi. Siku hiyo bila ya kujali walikuwa naye kwenye swala  na hata katika kutoa shahada wakiwa wote kwenye 'tahiyatu' (huu ni kao amnao ni nguzo moja kati ya nguzo kumi na nne za swala zilizoorodheshwa na kitabu cha fiqhi, kwa wale wasiokuwa waislamu basi nafikiri inabidi mtambue kuhusu hilo ikitajwa neno hilo ambalo maana yake kiarabu ni   maamkizi).

       Waliamua kumuita kafiri waziwazi wakisema si pamoja nao na hakufaa kuwa muislamu kwa mambo aliyokuwa ameyafanya, walimuita pia ni kinyonga ambaye alikuwa akijibadili rangi rangi kutokana na mazingira yalivyo. Walisema mbele ya vyombo kuwa rangi yake kamili walikuwa wameshaijua hivyo hawakuwa wakihitaji wao kama waislamu kuwa na kiongozi kama huyo, yalikuwa ni  maandamano yenye fujo za midomo tu tofauti na fujo zingine zilizoeleka na kufanya vitendo. Uwepo wa wanajeshi jirani na eneo hilo pamoja na uwepo wa nyumba takatifu ya ikulu kuliwafanya wasifanye fujo ya vitendo ya aina yoyote kwa kuhofia kuzua tafrani kati yao na wanajeshi, uongo  ni sumu na muda huo walikuwa wamemezeshwa na sasa ilikuwa ikifanya kazi katika miili yao.



    ****



    NDANI YA IKULU

        Hali ilikuwa tete haswa kwa Rais Zuber kila alipotazama kila kilichokuwa kikiendela nje ya ikulu, hakuamini kabisa Mufti aliyetokea kuwa na urafiki naye mkubwa na pia kuwa nae bega kwa bega kama viongozi wengine wa dini nchini ndiyo angetoa tuhuma ya uzushi kama ile hadi waumini wakaandamana hadi meneo ya jirani na Ikulu. Alikuwa akuyatazama matukio hayo kupitia kwenye luninga akiwa yupo ndani ya ofisi yake pamoja Moses, alipoiangalia hiyo taarifa aliweka viganja vya mikono yake usoni mwake mwenyewe huku akiinamisha kichwa chake chini. Aliona kabisa mwisho wake na familia yake ulikuwa umekaribia hadi muda huo, tamaa alikuwa amejikatia kabisa katika kujikomboa na suala kama hilo, Moses alikuwa akimtazama Rais Zuber tu pasipo kusema lolote na hakutaka amuoneshe ishara yoyote ya kumkatisha tamaa alipoiona hali hiyo. Moses alipoona Rais Zuber anazidi kukta tamaa katika suala hilo, aliamua kumpa moyo kwa kumbainishia nguvu zzilizopo upande wake.

                    "Mheshimiwa hakuna baya litakalotokea ikiwa sisi tupo" Moses alimuambia

                    "Ooooh! Moses come on unafikiri uongozi wangu utaendelea hapa, wananchi hawana imani na mimi tena wanashinikiza nitolewe. Jeshi lipo upande wao unafikiri nani atakuwa mwokozi wangu" Rais Zuber alilalamika

                    "Mheshimiwa cool down, everything is undercontrol hakuna kitakchoharibika hata muda huu nafikiri tuhesabu masaa machache tu heshima yako itarudi na wabaya wako watakuwa weak" Moses alimuambia

                    "But how, Belinda aanze kupinga amri za Ibrahim wakati anajua ni kinyume na amri za kijeshi huoni ni hatari maana majeshi yake  yashanizunguka"

                    "Kuzungukwa si ishara wako upande wao wale wako upande wetu daima na ikitoka hiyo amri ya kuanza kukutoa humu ndani wao ndiyo watakuwa wanakulinda wewe amini fagio la chuma lipo  upande wa rais daima na si upande wa wasaliti. Mtoaji mkuu wa amri ni wewe katika jeshi hivyo Belinda ahwezi kukusaliti"

         Muda huohuo wakiendelea kuongea mlango wa ofisi hiyo maalum iliyopo humo ikulu ulifunguliwa kwa ghafla, wote kwa pamoja walielekeza macho yao mlangoni ulipofunguliwa mlango  huo kutoka na ughafla uliotummika katika kuufungua mlango huo. Hawakuwa wametarajia kama mlango huo ungefunguliwa kwa muda huo kwani walikuwa hawana kijana wa hapo mwenye shida au dharura kubwa ambayo Mheshimiwa anapaswa kuijua kiasi cha kumfuata bila hata kuwasiliana naye kwa mawasiliano ya simu. Macho yao yote yalikuwa yapo mlangoni kwa mshangao mkuu, walipomuona huyo aliyekuwa amefungua mlnago hakuwa ni adui yao wala  kijana wao yoyote walishusha pumzi za ahueni.

                    "Mke wangu ni ufunguaji gani wa mlango huo hadi unatutisha si unajua hali ilivyo kwanini usifungue taratibu" Rais Zuber alimwambia mke wake ambaye ndiye alikuwa amefungua mlango muda huo

                     "Samahani mume wangu kama nimekukera lakini imebidi tu nije,mume wangu kumbuka Ummy ana mitihani shuleni kwao na inapasa ahudhurie katika mitihani hiyo. Watoto wote masomo wanatakiwa wahudhurie kila siku sasa kukaa ndani na kutotoka itakuwa mpaka lini jamani, huoni watoto wanapitwa na wenzao" Mke wake huyo ambaye uvumilivu wa kukaa ndani kwa watoto wake ulikuwa umeshamchosha aliongea.

                      "Khaaah! Sasa  mama Ummy kwahiyo unataka mimi nijisalimishe tu wakati sina kosa lolote" Raiz Zuber aliongea akoneshwa amekereka na maneno ya mke wake ambayo si mara ya kwanza kumuambia

                       "Sasa mume wangu unafikiri tutafanyaje kwa ajili ya maisha ya wanetu ya baadaye ikiwa tutaendelea kugoma hivi" Mke wa rais aliendelea kumuhimiza mwanmke baada ya uvumilivu kuwa umemshinda, Moses hakuwa ametia neno lolote katika maongezi hayo alikuwa  wakiwatzama tu jinsi tu na mke wake walivyokuwa wakibishana.

                        "Khaaa! Hivi we mwanamke una akili timamu kweli yaani nijisalimishe nifungwe halafu hapa Ikulu arudi Filbert Ole  kisa tu niliongea na Moses ambaye ni mtu wangu wa karibu ambaye kasingiziwa kama mimi. Haya nikishafungwa jiulize hao watoto wapate malezi ya upande mmoja na wakae na watoto wenzao wanaoamini  Baba yao alifanya baya jiulize wataishije? Akiingia Ole madarakani na  mawaziri wake watakuwa upande wake sasa jiulize kama watasoma shule moja na watoto wa hao mawaziri watakuwa na hali gani kama si kunyooshewa vidole kisa baba yao yupo ndani" Rais Zuber aliongea kwa hasira sana huku akimtazama mke wake ambaye aliingiwa na kimya cha ghafla tu bada ya kuambiwa maneno hayo.

                           "Yaani kukaa ndani hata siku tano hazijafika tayari uvumilivu ni zero je ungekaa mwezi si ungekuwa ushanigeuka wewe kama napingana maamuzi  yako hayo yasiyo na tija, kama ulikuwa na mimi katika kipindi chote nagombea na naungwa mkono na wewe ukifurahia na hata kwenye kampeni uliongozana na mmi ukiwa na furaha. Hukutambua kuwa shida inaweza kuja siku yoyote hii ni sehemu ya maisha vikwazo lazima viwepo, hivi kama kikwazo kidogo kama hiki umekosa uvumilivu na unanishauri mabovu inaonekana vikizidi utanigeuka wewe" Ris Zuber aliendelea kulalama, lawama hizo zilipofikia hapo Moses aliamua atoke humo ofisini.

                           "Samahani" Aliongea kwa kuomba radhi kwa malalamishi hayo ya mke na mume aliyokuwa ameyasikia ambayo hayakuhitajika yaingie kwenye masikio yake kwa muda huo, alikuwa akikwepa kusikia yale yasiyomuhusu na wala yasiyompasa yeye kusikia. Baada ya Moses kutoka nje matuta kwenye paji la uso wa Rais Zuber ndiyo yaliinuka kabisa na akamtazama mke wake akionesha kachukia kabisa, mke wake huyo alikuwa amekosa la kuongea baada ya kuangushiwa maneno hayo ambayo yalikuwa ni zaidi ya mzigo.

                          "Hata haya huna unakuja kuniambia mbele ya Moses mambo kama hayo unaonesha ni kiasi gani huna uvumilivu wala ustahimilivu kwenye shida wewe mwanamke, unafikiri katika kipindi hiki kigumu nani wa kunifariji mimi niweze kuwa na moyo wa uvumilivu na pia kuhakikisha nchi haiendi mrama kama si wewe. Washauri wangu watanishauri tu lakini kama sitokuwa na faraja kutoka kwako ni zero kabisa, ona Moses huyu ameamua kumsafirisha mke wake tu  kisa matatizo aliyokuwa nayo aliyajua tangu mapema kama yangemkabili. Mke wake amekuwa akimpa moyo sana na amekuwa yupo tayari arudi awe pmoja naye  lakini kutokana na uzito wa matatizo hayo amekataa kabisa, yule ni binti tu mdogo kwako mke wangu sasa jaribu kujifunza kutoka kwake kumpita umri haimaanishi umempita kimawazo wala kumpita kuolewa haimaanishi utakuwa unajua kila kitu kuhusu ndoa!" Rias Zuber aliongea kwa hasira

                           "lakini mume wangu watoto wale"

                           "Wamefanyaje?! Ndiyo wamekutuma uje kuniambia hivyo? Wao ndiyo wamekutuma uje kuniambia wako tayari baba yao niingie jela wakose malezi yangu waende shule? Sema basi!"

                            "Hapana"

                            "Inaonekana ni kiasi gani una unajali raha zadi ukisahau shida zitakuja muda wowote, sasa ni hivi jua wanajeshi wote waliokuwa wapo mbele kuizunguka ikulu wapo upande wangu na waliokuwa wapo nyuma ndiyo wapo upande wa msaliti wa nchi. Nikirudi madarakani utaenda kupumzika kwenu ili ujifunze nini maana ya ndoa"

                           "(Maneno hayo yalimshtua sana Mke wa Rias)Basi mume wangu, yasiwe hayo"



                            "Nikiweka uamuzi nimeshaweka sifuti naomba unipishe nina mjadala na kijana wangu juu ya hili linaloendelea"

                            "(Machozi yakimlenga)Mume wangu nisamehe"

                            "Nimesema nipishe niendelee na majadiliano na kijana wangu" Rais Zuber alipoongea maneno hayo alisimama kwenye kiti alichokuwa amekaa na kwenda kumshika mke mkno na kumtoa nje ya ofisi yake kisha akarudi ndani akakaa kwenye kiti chake huku viganja vya mikono vikiwa ipo kichwani mwake.



       Mke wake tayari alikuwa ameshamchanganya hadi muda huo aliokuwa amemtoa humo ndani kutokana na kukasirishwa naye, akiwa amekaa kwenye hicho kiti Moses  alifungua mlango na akarudi ndani kwa mara ya pili. Moses alienda kuketi kwenye kiti kilichokuwa mkabala na kiti cha Rais Zuber na akawa anamtazama tu  bila ya kuongea neno lolote. Hakutaka kuanza kumuongelesha neno kwa muda huo aliokuwa amechanganywa na kukata tamaa kwa mkewe na aliamua kunyamza tu, alikuwa akimtazama Rais Zuber jinsi alivyokuwa ameweka viganja vya mikono usoni mwake akionekana na mwenye kuchanganyikiwa kwa maneno ya mke wake.

                    "Yaani hawa wanawake ni zero" Rais Zuber aliwadunisha wanawake wote kwa kosa alilolitenda mke wake kwa muda huo, wala hakuwa akifikiria kama miongoni mwa wanawake hao aliokuwa akiwadunisha mmoja wao ndiyo alikuwa amemleta ndani ya dunia hii, Moses hakuchangia kabisa maneno hayo yeye aliendelea kukaa kimya tu.



    ****



                     "Baba tumefanya nini mimi na binti yangu mpaka ukatuleta huku" Mke wa Mufti alikuwa akilalamika akiwa yupo ndani ya chumba maalum na Norbert ambaye alikuwa ameshatoa kanzu na ndevu za bandia alizokuwa amezibandika, Ilham alikuwa akilia tu baada ya kupata uhakika kuwa walikuwa wametekwa na mtu ambaye walidhani ni dereva mpya wa gari yao ya nyumbani ambayo hutumika ikiwa baba yake yupo ofisini na wana ulazima wa usafiri.



        Alikuwa akimtazama Norbert kijana aliyekuwa mtanashati ambaye hakufanana kabisa na kazi aliyokuwa akiifanya hadi akawatia nguvuni hadi muda huo. Walikuwa wamefungiwa ndani ya chumba cha kisasa chenye kila kitu ndani ya nyumba ya EASA, mazingira ya chumba hicho yaliyo mazuri bado hayakuwafanya wajione kama wapo mahali salama hasa kwa jinsi walivyoingizwa humo ndani ya nyumba hiyo.

                "Mume wako mama yangu ndiyo mwenye kosa wala si wewe hivyo mtakaa hapa hadi pale atakapokiri uzushi aliokuwa akiutoa kwenye hotuba ya leo, si Mheshmiwa Rais ndiyo kashinikiza kugawa viwanja vya waislamu kwa muwekezaji ili achimbe dhahabu baada ya maeneo hayo kubainika yana madini hayo. Akiendelea kukaa kimya kuhusu hili jua na wewe hautatoka" Norbert alimwambia.

                "Sasa Baba ninakutambua wewe ni mwandishi wa habari na hiyo ni kazi ya wanausalama  kama ilikuwa ni kweli au si kweli anasambaza uzushi, kwanini unaingilia kazi  isiyokuhusu baba yangu" Mke wa Mufti aliendela kumuambia, Norbert alipoyasikia hayo maneo hakujihangaisha kujibu badala yake alitumbukiza mkono mfukoni mwake na akatoa kitambulisho chake cha kikazi akampatia mke wa Mufti. Alikipokea kitambulisho hicho kilichokuwa kipo kama kitabu kidogo na akakifungua, alishtuka sana alipokifungua kitambulisho hiko na akakirudisha kwa Norbert ambaye alikuwa akimtazama tu umakini bila ya kuongea lolote.

                  "Samahani baba yangu kwa kuingilia kazi yako" Mke wa Mufti aliomba radhi akiwa na hofu baada ya kubaini kuwa alikuwa akiongea na mwanausalama wa shirika la kijasusi la Afrika ya mashariki ambalo alikuwa akilisikia tu na hakuwahi kumuona hata mwanausalama mmoja wa shirika hilo, uoga juu ya wanausalama ambao aliwahi kuwasikia walikuwa ni hatari sana wakiwa kazini ndiyo ulimuingia muda huohuo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

                 "Sina ubaya wowote nanyi naomba mtulie na mkae humu, ukifika muda wa kuachiwa mtaachiwa nyote" Norbert aliwaambia kisha akageuka nyuma akaufuata mlango wa chumba hicho walichopo hao, aliufungua mlango na akatoka. Norbert alitokea kwenye ukumbi mwembamba na mrefu uliopo ndani ya nyumba hiyo ya EASA , pembeni ya mlango huo alikuwepo Salum  yule kijana wake aliyefanya naye kazi kule Msasani ambaye alionekana alikuwa akimsubiri yeye tu atoke humo ndani ya chumba.

                  "Vipi Salum mbona uko hapa?" Norbert alimuuliza

                  "Mkuu taarifa mpya imeingia muda huu" Salum alimuambia

                   "Enhee! Nipe ripoti" Norbert aliongea huku akianza kutembea na Salum alikuwa akifuatana naye.

                     "Mufti amedondoka kwa mshtuko ofisini kwake na hivi sasa amelazwa Aga Khan"

                   "Nilitarajia hilo suala litatokea maana udhaifu wake ndiyo upo mikononi mwetu, sasa mwambie Eva aje nimpe ujumbe aende kule akampe huo ujumbe  ataoukuta akiamka tu"

                    "Sawa mkuu"

                     "Mwambie aje ofisini sasa hivi leo hii siku ni hakuna kulala"

                      "Sawa mkuu"

       Norbert alipotoa amri hiyo alikaza mwendo kuelekea ilipo  ofisi ndani ya nyumba hiyo ya kijasusi, Salum alienda moja kwa moja kwenda kumuita Eva kama alivyokuwa ameagizwa na mkuu wake.



      Taaluma ya  mtu ni kitu kinachomfanya mtu huyo aweze kufanya ufanisi zaidi mambo yanayohusu vitu ambavyo alijifunza kwenye taaluma hiyo, wenye taaluma zao kama vile Daktari hufanya mambo mengi yanayohusu utabibu kwa ufanisi mkubwa kwakuwa ana taaluma nayo kubwa sana. Vivyo hivyo kwa waandishi wa habari hufanya mambo kwa ufanisi na wepesi wa hali ya juu kwa kuwa wana taaluma ya hayo mambo wanayoyafanya, waandishi wa habari huwa na ujuzi wa hali ya juu katika kunyaka habari ambazo zimetoka muda mfupi pasipo kueleweka na watu wa kawaida huwa wanatumia muda gani katika kuzinasa habari hizo na kuzisambaza. Muda ambao Mufti alikuwa akipelekwa hospitalini tangu akutwe amepoteza fahamu katika ofisi yake na mwanamama wa chini yake aliyemtuma amletee nyaraka, habari za kuanguka kwake tayari zilikuwa zimeshafika mikononi mwa wanahabari hata kabla hajfikishwa katika hospitali ya Aga Khan ambako ndiyo alienda kupatiwa matibabu.



       Wanahabari wenye kurasa na tovuti katika mitandao ya kijamii walizinasa habari hizo na kuziweka kwenye kurasa na tovuti zao, hata Mufti akiwa hajaanza kupatiwa huduma katika hospitali ya Aga Khan tangu afikishwe habari hiyo ilikuwa tayari imeshasaambaa mihili ya moto wa nyikani unavyosambaa kwenye nyasi kavu. Wenye tabia ya kusambaza habari mpya kwenye mitandao ya kijamii walikuwa wakisambaziana habari hiyo na hadi muda anaopatiwa matibabu karibu wananchi wote wa Tanzania waliokuwa wakitumia mitandao ya kijamii tayari walikuwa na habari hiyo. Ilikuwa ni habari ya pili iliyochukua nafasi kubwa katika vyombo vya habari ukiachia ile habari ya hotuba yake aliyoitoa mchana wa siku hiyo, muda huo wa saa tisa alasiri vijiwe mbalimbali vya vjana wanaopenda kukaa pamoja na kupiga soga walikuwa wamekaa wakiizungumzia habari hiyo.



      Moja ya vijiwe vilivyokuwa vikiizungumza habari hiyo kilikuwa ni kijiwe kimoja cha vijana maarufu sana maeneo ya Temeke Mwembeyanga kwenye kiwanja cha mpira kilichopo mita kadhaa kutoka barabara inayoelekea kwenye kona maarufu inayoitwa Davis (Davis Corner) ya Tandika. Vijana hawa muda huo wa alasiri walikuwa wakisubiri jua litulie kidogo na lipunguze ukali wa kuchoma uliokuwa umebakia waweze kucheze mpira kwa muda wa jioni, walikuwa wamekaa kwenye matairi yaliyokuwa yamechimbiwa pembeni ya uwanja huo kila mmoja akiwa ameshika viatu vyake na soksi za kupigia kandanda kwenye mpira huo wa mchangani maarufu kama Ndondo.



         Asilimia kubwa ya vijana walikuwa wamevaa nguo zilizokuwa zikionesha wazi walikuwa wapo hapo kimchezo zaidi, kuwahi kwao katika uwanja huo kulikuwa kumetoa fursa kubwa sana ya kuweza kupiga soga wakisubiri hadi muda wa muadhini wa alasiri na pia swala ya alasiri ipite ndiyo jua liwe limetulia waweze kusakata kabumbu. Walikuwa ni vijana waliokuwa hawajui kile kilichokuwa kikiendelea huko kwenye nyadhifa za juu zaidi ya kuishia kuropoka tu ili kuuepeleka muda mbele, wengi wao walikuwa wakiongea kuhusu  sakata aliloliongea Mufti na pia kuzidiwa kwa Mufti hadi akapoteza fahamu ofisini kwake. Fikra za mawazoni mwao ambazo zilinyakwa barabara na kalamu ya mwandishi ndiyo zilikuwa zikitawala maongezi hayo, wengi wao wlikuwa wakiongea kile kilichokuwa kikiwajia mawazoni mwao ambacho hawakuwa na uhakika nacho hata kidogo.



                 "Man umesikia jipu alilolitumbua Mufti na msala uliompata saa moja tu baadaye" Mmoja aliropoka.



                 "Dah! Nimeunyaka mwana, huyu Presdaa mafia mwana kamzimisha tayari" Miwngine alidakia



                  "Dah! Mama** kumbe kujenga uwanja mpya mkubwa kama wa taifa katika michezo na kutupatia huduma poa kabisa hospital alikuwa anaficha umafia mkubwa sana, jamaa kaumbua tu washamtia janga kalazwa" Miwngine alidakia.



                   "Man we acha tu ila mi naona kama kuna uduwanzi fulani pale kwenye hiyo ishu, hatuna uhakika kama ndiyo kamflotisha Mufti hadi yupo kitandani sasa hivi hajitambui" Mwingine alichangia



                    "Na wewe acha ukolo kama siyo ukweli unafikiria nini? Au kakupatia mgao nini katika mpango huo na wewe ukaenda kumzima Mufti" Yule kwanza kuchangia alimjia juu huyu aliyekuwa akitetea kuhusu hilo, wengi wao waliokuwa wamelewa maneno ya Mufti alikuwa wakimuunga mkono huyo aliyekuwa akimjia juu mwenzake alipoonesha haungi mkono kauli zao. Ilikuwa kama mzozo baada ya kutoa kauli kila mmoja akimuambia neno lake la kumkashifu.



                     "Nyinyi ndiyo makolo sure, ishu hamuipati fresh mna kazi ya kubwata mam** zenu" Aliyeittetea kauli hiyo aliwajia juu na yeye.



                      "Aaah!  Mwana huyu wa wapi huyu au Prezdaa mjomba wako nini"  Mwingine kabisa alimjia juu.



                      "acheni us****  ma**** kila mkisikia tu ni kweli siasa hizi msiwe mazoba hivyo" Naye hakuwa tayari kushindwa



                       "We kolo unaongea nini wewe" Mmojawapo ambaye alikuwa akionesha zaidi alikuwa ni kijana mwenye shari zaidi alimsukuma huyo jamaa kifuani kumrudisha nyuma baada ya kuona alikuwa wametukanwa wote.



                        "Hazard mvungie huyo hana jipya kama wa haramu vile" Mwingine alikimbilia kumzuia huyo kijana aliyekuwa yupo kishari zaidi huku akimuita jina kutokana na uchezaji wake wa uwanjani, hii huwa ni kawaida sana kwa vijana wa mtaani kupeana  majina ya wachezaji wakubwa wa Ulaya kutokana na uchezaji wa mwenzao ulivyo.



                         "Huniambiaa kitu we boya" Yule aliyekuwa yupo katika kutoamini maneno ya wenzake na pia kutoamini hotuba ya Mufti aliongea huku akimrudishia mwenzake katika kumsukuma kama alivyomfanyia.



                         "Pepe vunga na wewe basi kama unamtetea huyo Cho** Zuber juu yako" Kijana aliyekuwa akiamua ugomvi huo wa kusukumana kwa huyo Pepe na Hazard alimjia juu huyo waliyempachika jina la pepe kutokana na uwezo wake wa uwanjani.



                         "Roja na wewe acha ufala" Pepe alimjia juu huyo aliyekuwa anawaamulia



                         "Oyaa  Pepe tutakutimba ujue tutolee us****  wako" Hazard naye alimjibisha Pepe huku akimsukuma Roja apishe ili waweze kuwekana sawa, Roja alikaza mwili wake akizuia Hazrd asimsogelee Pepe.



                         "Oyaa Pepe na Hazard vungeni basi ama nini wamoja hapa tunasongeza saa tu hapa kupiga stori ishu za kupigana siyo kabisa" Roja aliamua kuwatuliza wote.



                          "haina mbaya mtu wangu" Pepe aliongea huku akimnyooshea ngumi kwa mtindo unaojulikana kama tano Roja ambaye naye alimpa tano, alimfuata pia Hazard akafanya hivyohivyo kisha wakagongesha bega kila mmoja kama ilivyo salamu ya vijana waliopoteana kwa muda mrefu sana.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



                          "Pendo moja ama nini" Hazard naye alikuwa amerudi katika hali ya kawaida alipokuwa akiongea maneno hayo wakiwa wanaonesha ishara ya amani ipo katika  urafiki wao na hakuna chochote kilichokuwa kimeharibika kwa kuzozana kwao.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog