Search This Blog

Sunday, 22 May 2022

ANGAMIZO - 3

 







    Simulizi : Angamizo

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Majambazi watano sasa alikuwa kawamaliza kimya kimya mule Mgahawani.



    Mara kundi la majambazi wote kumi waliobaki kule nje lilikuwa linakuja Mgahawani wakiwa wanakimbia. Bila shaka walihisi kuna kitu cha hatari. Sasa ilikuwa hatari zaidi. Abdul nae alianza kutetemeka mwili mzima kwa hofu. Alimwangalia Daniel kule nyuma ya mlango, alimshangaa hakuwa na hofu kabisa mwanaume yule. Kwa hakika Daniel hakuwa binadamu wa kawaida. Kila hatari inavyomkaribia yeye anazidi kuwa mtulivu na tabasamu lisiloisha usoni mwake. Wale jamaa waliingia ndani ya Mgahawa. Pale nyuma ya mlango sasa Daniel Alikuwa ameshika bastola mbili mkononi. Ndani ya nusu dakika watu wote kumi walikuwa chini. Wote walikuwa wameuwawa na Daniel. Wanafunzi wote walisimama na kumpa mkono wa pongezi Daniel. Alikuwa shujaa kwao. Alikuwa shujaa zaidi kwa Abdul. Walimhusudu sana Daniel. Abdul alimhusudu zaidi Daniel. Walitoka eneo la Chuo huku Daniel akiwapigia simu Polisi waje kutoa maiti zile. Wao walielekea moja Kwa moja kituo cha Polisi Arusha.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    SURA YA PILI



    Katika nyumba moja iliyopo mtaa wa Mikocheni, Dar es salaam. Kulikuwa na kikao. Kikao kilihusisha watu watano. Kati ya watu hao watano. Kulikuwa na wanajeshi wanne wenye vyeo vikubwa jeshini na raia mmoja wa kawaida. Walikuwa wanajadili mpango wao walioupa jina la Angamizo.

    Katika kikao kile mtu mmoja tu ndiye ambaye hakuwa mwanajeshi, Salehe.



    Kikao hiki kiliitishwa baada ya kuingia doa katika mpango wao. Ilikuwa hivi, siku ya ijumaa Salehe alichelewa kurudi nyumbani. Mkewe Raiya alijisikia mchomvu sana. Alichukua laptop ya mumewe ili apoteze mawazo. Kipindi hicho Raiya alikuwa na wakati ngumu sana katika maisha ya ndoa yake. Mumewe alikuwa bize sana. Vikao visivyoisha hadi saa tisa ya usiku. Kutokana na ubize huo Raiya akahisi anasalitiwa kwa kutopewa haki yake ya ndoa. Kumbe hakuwa anasalitiwa. Mumewe alikuwa bize na Mpango haramu ulioitwa Angamizo.

    Hakuwa anampa haki yake ya ndoa mkewe. Alibadilika kabisa. Muda mwingi alikaa peke yake kuipanga sawa mipango yake. Siku hiyo akiwa anachezea laptop ya mumewe. Ndani ya laptop ya mumewe Raiya aliliona faili liliandikwa Siri. Akalifungua bila wasiwasi wowote. Ndani ya faili hilo ndimo alikuta mambo yaliyomtisha sana. Mpango wa Angamizo ulipangwa utekelezwe baada ya miaka miwili. Ulikuwa Mpango hatari ulioratibiwa na watu hatari sana. Siku alipoliona faili lile lenye siri toka Kwenye laptop ya mumewe kesho yake ndipo alipokutana na Abdul. Akiwa anatoka Bagamoyo, na kuanzisha uhusiano haramu. Ulikuwa uhusiano haramu lakini ulioleta faida kubwa kwa Taifa baadae.



    Siku zilivyosonga mbele Salehe alihisi mabadiliko toka kwa mkewe. Akahisi huenda anatoka nje ya ndoa yao.

    Anamsaliti!

    Siku zote alikuwa anamlalamikia kuhusu suala la unyumba. Lakini Sasa alikuwa halalamiki tena. Akaanza kumchunguza. Baada ya uchunguzi wake Salehe akagundua kila walichokuwa wanafanya na Abdul. Mbaya zaidi Salehe aligundua pia kuwa Raiya amegundua mpango wao wa Angamizo. Na akajua kwa vyovyote Raiya lazima atamsimulia mtu wake wa karibu. Ambaye ni Abdul.

    Sasa Salehe alianza kumfatilia Raiya kwa kila hatua aliyopiga. Siku Aliyomuaga kuwa anakwenda Arusha alimkubalia lakini hakumwacha peke yake. Alimfatilia!

    Ndipo alipogundua kwa kina kila kitu kuhusu uhusiano wao na kuamua kuwaangamiza wote kwa sumu kali na hatari iitwayo Proxine!



    Ndani ya kikao kile ilikuwa ni kutupiana lawama. Wanajeshi wote wanne walikuwa wanamtupia lawama Salehe. Kwa kuweka rehani Mpango wao hatari. Salehe alijitetea sana. Lakini hakueleweka kabisa. Wakati wanaendelea na mazungumzo yao, simu ya Salehe iliita.



    "Halo"



    "Bon, Arusha"



    "Nambie Bon"



    'Mambo mabaya sana"



    "Kuna nini tena ?"



    "Tumepoteza wapiganaji kumi na tano leo"



    "Unasema !!!"



    "Ndio hivyo Salehe, kumi na tano wameuwawa "



    "Sisi tumefanikiwa lakini?"



    "Hatujafanikiwa "



    "Kwanini Bon..hadi sasa anapumua?"



    "Ni msumbufu sana kaka"



    "Inamaana ni Abdul ndiye aliyewauwa wapiganaji wetu kumi na tano"



    "Ndio Abdul, ila yuko na mwenzie. Ni watu hatari sana"



    "Nakuja na Avira na Avast kwa ndege ya jioni, kummaliza mwenyewe"



    "Itakuwa poa kaka".

    Simu ikakatwa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Jioni ya siku ile baada ya kikao. Salehe akiongozana na Avast na Avira walikuwa wanaelekea jijini Arusha. Kwa kazi moja tu. Kuhakikisha Abdul anauwawa. Avast na Avira walikuwa wauaji hatari. Wauaji wanaojua aina zote za mauaji. Walikuwa makomandoo toka Nigeria walioletwa kwa ajili ya kuleta Angamizo nchini Tanzania. Ni hawa wauaji wanaotumia sumu hatari ya Proxine kuwaua watu kinyama. Asubuhi ya leo walikuwa Arusha kutekeleza kifo cha Raiya akiwa gerezani.Na sasa wanarudi tena Arusha kukatisha maisha ya Abdul. Hawakuwahi kushindwa wanapoamua kuuwa mtu. Walikuwa makini sana na kazi yao.



    Asubuhi ya leo walikuwa Arusha kutekeleza kifo cha Raiya akiwa gerezani.Na sasa wanarudi tena Arusha kukatisha maisha ya Abdul. Hawakuwahi kushindwa wanapoamua kuuwa mtu. Walikuwa makini sana na kazi yao.



    Walitua jijini Arusha saa moja kamili usiku. Walipanga asubuhi ndio waanze kazi yao ya kumsaka Abdul. Hawakuwa na wasiwasi hata kidogo. Walikuwa na uhakika hata kama askari wote Arusha watakaa nje ya kituo cha Polisi alikokuwemo Abdul, waliamini lazima watamuuwa. Walikuwa na mbinu na hila zote za kijasusi. Waliamini watamuua tu. Walijiamini.

    Daniel Mwaseba alimwacha Abdul amemfungia katika chumba cha siri pale Polisi. Chumba kikichojulikana na baadhi tu ya Polisi. Kilikuwa chumba kinachotumiwa kwa nadra sana. Tena kwa sababu maalumu. Daniel alienda kufanya kazi. Aliyanasa maongezi ya Kwenye simu kati ya Bon na Salehe kutoka Kwa rafiki yake aliyekuwa anafanya kazi katika kampuni ya simu waliyotumia Bon na Salehe kuwasiliana. Alihisi kuna kitu kutoka kwa mumewe Raiya. Hivyo aliongea na rafiki yake anase na kurekodi simu zote za Salehe. Hivyo alisikia simu zote zilizoingia na kutoka katika simu ya Salehe. Ikiwemo simu aliyopiga Bon kwenda kwa Salehe. Na Daniel sasa alikuwa uwanja wa ndege wa Arusha akiwasubiri wageni wake.



    Daniel aliiona ndege waliyopanda Salehe, Avast na Avira ikitua pale uwanja wa ndege wa Arusha. Aliwaona watu wale watatu wakishuka kwa kujiamini sana. Macho ya Daniel yalikuwa makini sana na wale majamaa mawili, Avast na Avira. Macho yake yalimwambia hawakuwa watu wa kawaida. Aliwaona walivyoshuka kwenye ndege na kupanda kwenye gari aina ya Noah nyeusi. Sawa na zile alizofukuzana nazo asubuhi. Aliifuata nyuma Noah ile akiwa na pikipiki yake. Avast na Avira hawakuwa watu wa kawaida. Huwa wanaweka tahadhari kabla ya jambo halijatokea. Leo walivyoshuka tu kwenye gari walihisi watafuatwa. Walikuwa makini sana. Wakati Daniel akiwafata akina Avast na Avira kutoka uwanja wa ndege, kina Avast walikuwa makini sana na magari yaliyokuwa nyuma yao. Baadae kidogo waliitilia shaka pikipiki iliyokuwa inawafata nyuma. Wakawa wanasubiri muda muafaka wamtie mikononi mfuatiliaji. Wakawa wanaendesha gari taratibu wakiipigia hesabu ile pikipiki. Walikuwa na sumu yao hatari ya Proxine.Tayari kwa kuitumia muda wowote itakapobidi.



    Msafara uliwafikisha kwenye mzunguko wa Azimio la Arusha wakielekea stendi kuu Arusha. Walipofika mbele kidogo Daniel alibadili njia. Hakuwafata tena. Wakati wao wakinyoosha yeye alikata kulia njia iliyokuwa inaelekea uwanja wa mpira wa Shekhe Amri Abeid. Alipofika usawa wa geti la uwanja akasimama. Mle ndani ya gari walishangaa ile pikipiki wakiyoitilia shaka imepotea ghafla. Wakawa wanaangaza huku na huko hawakuiona ile pikipiki. Walipofika mbele kidogo walisimamisha gari yao. Daniel sasa alikuwa anatembea kwa miguu. Aliwaona jinsi maadui zake walivyobabaika. Akagundua walishajua kuwa wanafuatwa. Akajipongeza kwa uamuzi wake wa kuchepuka. Kina Avast walijifanya kutengeneza gari yao. Salehe aliingia uvunguni wakati Avast Na Avira walikuwa wanaangazaangaza huku na kule kumtafuta mwendesha pikipiki. Dereva alikuwa ametulia tuli kwenye usukani, alikuwa ni Bon. Mbinu wakizozitumia kina Avast, Daniel alikuwa ndio Mwalimu wa mbinu hizo. Alijificha kwenye mti mmoja akisubiri wafanye kosa lolote. Awaadhibu.

    Alikaa robo saa. Kosa halikutokea. Avast na Avira hawakuwa watu wa kufanya makosa kizembe. Walikuwa watu wanaoijua kazi yao.

    Baada ya robo saa walipanda kwenye Gari yao na kuondoka. Daniel aliachana nao. Akijua ipo siku watakutana tu. Alirudi nyumbani kwake mtaa wa maji ya chai kwa kutumia pikipiki yake. Usiku nzima hakulala. Alikuwa anafikiria ni kitu gani wanachotaka kufanya watu wale.

    Hakupata jibu.



    Asubuhi na mapema alienda kituoni. Alimkuta askari mmoja yupo kaunta.Alikaa na kuongea nae pale kaunta. Saa moja na nusu asubuhi alikuja mgeni alijitambulisha kama ndugu wa Abdul. Daniel kumuona tu mtu yule alimtambua. Alikuwa mmoja ya watu watatu aliowafatilia usiku wa jana yake usiku.



    Daniel alitabasamu.



    "Habari Afande"



    "Nzuri vipi hali yako?"



    "Kwema, kuna ndugu yangu nimekuja kumwangalia"



    "Anaitwa nani ?"



    "Abdul"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Unatokea wapi ?"



    "Bagamoyo"



    "Sawa"



    Jamaa alionesha tabasamu la matumaini kwa mbali. Aliyekuwa anaongea na na yule polisi ni Avira. Komandoo toka Nigeria. Daniel akiwa pembeni alikuwa anamwangalia huku anatabasamu. Alimkumbuka vizuri sana. Daniel aliomba kuongozana na yule mtu kumpeleka kwa Abdul. Sasa Daniel aliongozana na Avira kwenda kumwangalia Abdul. Abdul alikuwa amefungiwa kwenye chumba cha siri. Kilikuwa chumba chenye kila kitu ndani yake. Alipewa na msichana mmoja aliyekuwa anamsaidia kazi ndogo ndogo mle ndani. Aliona mlango ukifunguliwa. Walikuwa wanakuja kama marafiki wa kawaida. Yule mtu alinyoosha mkono ili wasalimiane na Abdul. Mkono wenye Proxine!!



    Daniel alipiga ukelele mkali, akimkataza Abdul kushikana mkono na yule mtu. Abdul alirudisha mkono wake kwa haraka wakati yule mtu akizidi kuupeleka kwake. Daniel Mwaseba alirusha teke lililoupiga mkono wa yule jamaa. Ukaanza mpambano sasa.



    Yule jamaa alirusha ngumi mbili zilizopanguliwa na Daniel kwa ustadi mkubwa. Akarusha teke moja maridadi lililompata Daniel kwenye mbavu. Alikuwa anataka kutoa kitu mfukoni Daniel alimzuia kwa kungfu kali ya mkononi. Jamaa kwa ghadhabu alirusha kichwa kilichokwepwa na Daniel. Hadi hapo Daniel hakufanya shambulio lolote zaidi ya lile la kuzuia mkono wa yule jamaa usigusane na wa Abdul. Na lakuzuia asitoe kitu mfukoni yule jamaa. Jamaa alirusha ngumi mbili Daniel alizikwepa kwa ufundi mkubwa. Jamaa alitaka kutoa kitu mfukoni Daniel alimzuia kwa teke kali lililompata barabara mkononi. Jamaa Sasa alikuwa na hofu. Alisimama na kurusha kofi la nguvu Daniel , Daniel alikwepa tena. Jamaa alirusha kofi lengine Daniel akakwepa. Sasa Ulikuwa mwendo wa makofi kutoka kwa yule Jamaa na Daniel alifanikiwa kuyakwepa yote.

    Sasa jamaa akaanza kulia. Alijaribu kuingiza mkono mfukoni Daniel alimzuia kwa kumpiga ngumi kali ya uso. Jamaa alisimama.

    Ghafla akaanza kuumuka. Abdul macho yalimtoka pima!. Ngozi ya yule jamaa ilikuwa inavuka !. Lilikuwa tukio la kusikitisha sana. Tukio la kuogofya sana. Jamaa ngozi yake ilikuwa inashuka chini taratibu. Alikufa kifo kinachofanana na cha Mayasa. Alikufa kifo kinachofanana na cha Raiya. Alikufa kifo kinachofanaa na cha afande John. Yule jamaa nae alivuka ngozi.



    Kumbe yule jamaa alishika ile dawa inayoitwa Proxine pale alipotaka kumsalimia Abdul kwa mkono. Na alivyokuwa anataka kutoa kitu mfukoni alikuwa anataka kutoa dawa nyingine ili ajipake dawa kuzuia madhara ya ile dawa. Lakini alichelewa. Daniel alikuwa anamzuia kwa pigo kila alipotaka kuitoa ile dawa hiyo. Alijua atakufa, ndiomana alianza kulia kabla. Siku zote mshahara wa dhambi ni mauti...



    Daniel alimsogelea taratibu na kuanza kumuuliza Abdul kwa upole.



    "Kuna kitu wanahisi unacho. Wanataka kukuua ili kisitoke nje. Unahisi wanataka kitu gani Abdul?"



    "Mimi sina kitu kaka Daniel. Sijui hata wananitakia nini ?"



    "Kipo kitu Abdul"



    "Kitu gani sasa kaka Daniel ?"



    "Mayasa alishawahi kukupa kitu chochote enzi za uhai wake ?"



    "Amewahi kunipa vitu vingi lakini siyo vya kudumu"



    "Raiya alikupa nini cha kudumu ?"



    "Hamna zaidi ya hii simu "



    "Hebu ilete "

    Akampa.

    Daniel aliiangalia ile simu kwa makini. Aliigeuza nyuma. Aliifungua ile simu kule nyuma. Kule inakokaa betri ilidondoka chini karatasi ndogo. Abdul alishangaa sana. Hakuwa ameweka karatasi yoyote kwa kuwa hakuwahi kuifungua simu ile tangu alivyopewa na Raiya. Daniel akaisoma kwa sauti ndogo ile karatasi.



    Daniel aliiangalia ile simu kwa makini. Aliigeuza nyuma. Aliifungua ile simu kule nyuma. Kule inakokaa betri ilidondoka chini karatasi ndogo. Abdul alishangaa sana. Hakuwa ameweka karatasi yoyote kwa kuwa hakuwahi kuifungua simu ile tangu alivyopewa na Raiya. Daniel akaisoma kwa sauti ndogo ile karatasi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Kwenye laptop ya mme wangu kuna faili la limeandikwa Siri. Linahusu mpango wa kuangamiza watoto wa viongozi wa nchi hii na mambo mengine mengi ya siri sana. Abdul jaribu kulifikisha suala hili kunapohusika ili kuliokoa Taifa hili " Abdul alishangaa sana. Sasa alimhusudu sana Raiya. Alimuona ni mtu mwenye akili kuliko mtu yeyote duniani. Raiya kumbe alikufa na siri kubwa sana. Abdul alimhusudu zaidi Daniel. Aligundua kitu alichokaa nacho miaka miwili bila kutambua . Alikiri Daniel hakuwa mtu wa karne hii. Alikuwa na akili na uwezo wa ziada. Daniel alitoka nje na kile kikaratasi. Baada ya dakika kumi na tano waliingia askari wawili kuutoa mwili wa yule jamaa. Daniel alitoka nje kwa nia moja tu. Kumtafuta mume wa Raiya popote alipo. Ilikuwa lazima ampate popote atakapokuwa !



    ***



    Upande wa kina Avast ilikuwa ni patashika na taharuki kubwa. Ilikuwa yapata saa saba ya mchana sasa, Avira hajarudi. Ilikuwa ajabu. Avira hakuwahi kufanya kazi muda mrefu namna hii. Avira hufanya mambo kwa haraka na kwa uhakika. Hiyo ndio sifa kuu ya Avira. Alitekeleza kazi ya kumuua Raiya robo saa tu alivyoenda magereza. Leo saa zaidi ya tano alikuwa hajarudi. Walimsubiri.

    Walimsubiri sana.

    Hakurudi.

    Na hajarudi mpaka leo!



    Daniel alivyotoka palepale moja kwa moja alienda kwa dada yake Raiya. Alienda na kumuulizia mtaa na namba ya nyumba akiyokaa Raiya huko Dar es salaam ilipo.

    Baada ya kuelekezwa Daniel aliweka 'booking' ya ndege ya kwenda Dar es salaam kesho yake asubuhi.

    Aliipata.



    Usiku ule ulikuwa mgumu sana kwa Avast na Salehe. Wakaanza kuhisi huenda Avira amekamatwa. Wakawa wanahofia endapo Avira atakuwa kakamatwa anaweza kutoa siri. Siri pekee ambayo hawakutaka itoke ilikuwa kwenye laptop, nyumbani kwa Salehe, Dar es salaam. Wakapanga kesho Avast aende Dar es salaam kuichukua ile laptop. Ili siri isifike mikononi mwa adui.



    ***



    Daniel Mwaseba ndiye alikuwa wa kwanza kufika nyumbani Kwa Salehe Mikocheni. Hakupata shida sana kuingia ndani ya nyumba ya Salehe. Hakukuwa na ulinzi wowote kwenye nyumba ile. Aliruka ukuta na kuingia ndani. Aliitafuta laptop ndani ya chumba cha Daniel. Chumba hakikuwa na vitu vingi sana. Kulikuwa na kitanda kikubwa, meza ya kujirembea na kabati kubwa la nguo. Robo saa ilitosha kukipata alichokuwa anakitafuta ndani ya nyumba ile kubwa. Aliikuta laptop ndani ya kabati la nguo chumbani katika chumba cha kulala cha Salehe. Aliiweka laptop yenye siri nzito kwenye begi na kuanza kutoka. Hakutaka kuifungua mle ndani. Aliona ile siyo sehemu salama. Alipita sebuleni akafungua mlango wa sebule wa kutokea nje. Sasa akawa anatembea katika uwanja mpana kulielekea geti la nyumba ile. Alilikaribia kabisa geti. Zilibaki hatua kama tano ili Daniel atoke nje ya nyumba ile.

    Ghafla! Geti lilianza kufunguka lenyewe. Aliingia mtu Avast ! Pacha wa Avira aliyemuuwa kwa mateso makubwa jana, kule Arusha. Sasa Daniel Alikuwa anatazamana macho kwa macho na Avast.

    Wote wakiwa Na bastola mkononi!



    Avast alikuwa anauangalia sana mfuko alioubeba Daniel. Akajua ndani ya mfuko ule kipo alichokifuata. Laptop yenye siri nzito !



    "Wanaume wanaojiamini hawapambani kwa silaha. Tuweke silaha chini na tuoneshane ubabe" Avast aliongea kwa sauti yake mzito na ya kujiamini yenye lafudhi ya kinigeria. Aliongea kwa majigambo sana. Daniel alitii, kwa sababu nae alijiamini. Alitaka kumuonesha Avast jinsi Wanaume wa kweli wanavyopigana. Wote waliweka bastola chini. Sasa ulikuwa mpambano wa nguvu. Mshindi alitakiwa kuondoka na laptop ile yenye siri nzito. Ndani ya sekunde thelathini walikuwa wanaangaliana tu . Kila mmoja akifikiria jinsi ya kumuingilia mwenzie. Avast ndiye alitangulia kushambulia. Avast aliruka juu na kumuelekezea Daniel mateke mawili ya nguvu kuelekea kifuani mwa Daniel. Mateke yale yalitua sawia kwenye kifua chake. Nguvu ya mateke yale yalimfanya Daniel adondoke chini. Huku mfuko wenye laptop nao ukidondoka chini!

    Daniel alinyanyuka kivivu. Avast alirusha teke la kulia lililokuwa linaenda mbavuni kwa Daniel. Alijaribu kulipangua lakini alizidiwa nguvu na uzito wa teke lile. Lilimpata kidogo Kwenye mbavu.

    Aligumia kwa maumivu. Avast alirusha ngumi na wakati uleule Daniel alirusha ngumi. Ngumi zile zilikutana katikati. Ila Daniel ndiye aliyepata madhara. Ngumi ya Avast ilikuwa na nguvu zaidi. Daniel aliumia mkono. Sasa Daniel akajua akitumia nguvu atapigwa. Yule jamaa alikuwa hatari sana. Sasa aliona ulikuwa wakati wa kutumia zaidi akili . Avast alirusha mateke mawili kwa mpigo. Kwa miguu miwili tofauti. Moja lilimpata Daniel kwenye mbavu ya kushoto na lengine mbavu za kulia. Daniel alidondoka chini kwa nguvu. Alikuwa ameumia mbavu vibaya sana. Avast alitoa kichupa kidogo cha dawa ya Proxine , akapaka kwenye kiganja chake na kumsogelea ili ampake Daniel pale chini alipokuwa amelala. Ile anataka kumgusa Daniel alijisogeza kwa nguvu na kwa haraka. Avast aligusa sakafu... Daniel alinyanyuka sasa. Akawa makini zaidi. Akijua kosa moja tu linaondoka na maisha yake. Alisimama imara sasa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Avast nae alikuwa anataka kufanya haraka ili ile sumu ya Proxine isimdhuru mwenyewe. Ilikuwa na uwezo wa kukaa kiganjani kwa dakika kumi tu. Baada ya hapo ingemdhuru yeye mwenyewe. Daniel akajua hiyo ni nafasi pekee ya kumshinda Avast. Avast alirusha teke lililompata Daniel kwenye shingo. Teke lile lilimpeleka Daniel chini bila kutaka. Avast akawa anamsogelea tena ampake Proxine. Hakumgusa, alikutana na ngumi takatifu ya pua, damu zikaanza kumtoka. Avast hakujigusa pua. Kujigusa pua Ilikuwa inamaanisha kujivua ngozi. Kujiua mwenyewe kwa sumu kali ya Proxine.

    Wote walikuwa wamesimama, wanaangaliana kama majogoo. Avast alirusha kofi kwa kutumia ule mkono wake wa kulia wenye sumu ya Proxine . Daniel aliliona kofi lile. Alinesa kidogo likapita jumla. Daniel alipata nafasi. Kwa kutumia mkono wake wa kushoto alipiga ngumi ya nguvu kwenye mbavu za Avast. Avast aligumia kwa maumivu makali. Alitamani kujishika mbavu lakini hakuruhusiwa na Proxine. Proxine sasa ikawa zuio kwake mwenyewe. Avast mbavu zilikuwa zinamuuma huku damu zinachuruzika puani. Alikosa umakini, hakuweka kinga usoni. Daniel aliitumia vizuri hiyo nafasi. Alipiga ngumi mbili za haraka usoni kwa Avast. Avast Akawa anaona nyotanyota. Avast aliyumba kutokana na uzito wa zile ngumi, lakini hakuanguka. Daniel alirusha teke kali lililompata Avast kwenye goti lake. Alienda chini taratibu. Kama Avira, Avast alikuwa analia naye. Alikiona kifo kwa mbali kikimsogelea. Proxine ilianza kuleta mrejesho. Alijaribu kutoa dawa ya kuiondoa ile sumu ya Proxine, akaishika mkononi. Akitaka kufungua kile kichupa ili aondoe ile sumu hatari. Alichelewa, teke kali la Daniel liliupiga ule mkono ulioishika ile dawa. Chupa ilidondoka sakafuni na kuvunjika!

    Avast sasa alilia kwa sauti kama mtoto mdogo. Alilia Kwa sauti kali! Daniel alikuwa anacheka kimoyomoyo. Auwae kwa upanga siku zote huuwawa kwa upanga. Daniel aliruka "double kick". Miguu yake yote miwili ilitua kwenye kifua cha Avast. Avast alitapika damu. Huku akitapika damu ngozi yake ilianza kuvuka taratibu. Daniel hakusubiri. Alichukua lile begi lenye laptop na kutoka nalo nje akiwa anakimbia. Akitafuta hotel salama na kujifungia ndani peke yake.Tayari kuifungua ile laptop yenye siri nzito. Moyo wake ulikuwa unamwenda kasi alipoliona faili lililiandikwa Siri. Akabofyabofya kidogo. Sasa akatulia na kuanza kulisoma. Ghafla mlango ulifunguka kwa kasi! Ulikuwa umevunjwa kwa teke zito. Waliingia wazee wawili wakiwa wamevaa suti nzuri nyeupe.



    "Hatujaja kuua. Tumefata laptop tu !" Mzee mmoja alisema.



    "Hamuwezi kuipata laptop mpaka mniuwe kwanza" Daniel nae alijibu. Wale wazee walicheka kwa sauti kwa pamoja.

    Walijiamini sana.



    Daniel atafanya nini mbele ya wazee hawa? Je watafanikiwa kuipata Laptop yenye siri?



    "Hatujaja kuua. Tumefata laptop tu !" Mzee mmoja alisema.



    "Hamuwezi kuipata laptop mpaka mniuwe kwanza" Daniel nae alijibu. Wale wazee walicheka kwa sauti kwa pamoja.

    Walijiamini sana.

    Wazee wale walitoa bastola. Midomo miwili ya bastola ilikuwa inamuangalia Daniel.

    Hakuihofia.

    Yeye alitabasamu tu. Wale wazee wawili Walikuwa wamenuna hasa.Tabasamu lile la Daniel waliliona kama dhihaka toka kwa Daniel. Wakawa wanamsogelea taratibu pale kitandani alipokaa. Daniel aliacha kuwaangaalia. Akawa anaitazama ile laptop. Ikifanya alichoiagiza.

    Ilikubali.

    Kichwani alifikiria cha kufanya. Jamaa walimkaribia sasa. Zilibaki hatua kama tano wamfikie kabisa. walikuwa makini. Walikuwa wanamtambua Daniel. Walijua kosa moja tu lingewagharimu maisha yao yote .



    "Simama juu" Mmoja aliamrisha. Daniel alisimama taratibu.



    "Mikono juu!" Yule yule wa mwanzo alitoa amri nyingine Daniel alinyoosha mikono yake juu. Yule aliyetoa amri alimsogelea huku yule mwengine akiwa amebaki palepale. Akimnyooshea bastola yake. Jamaa alimpekua Daniel harakaharaka. Alipata visu viwili na bastola moja. Hivyo viliwekwa sehemu ya kawaida. Silaha alizoweka sirini hakuzipata. Zilihitaji mtu anayejua kupekua hasa. Akaishika ile laptop. Bila kuitazama akaifunga. Wakawa wanarudi kinyumenyume sasa.



    "Naitwa kaspersky " yule aliyempekua Daniel alisema.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Naitwa Zwangendaba" Na yule aliyekuwa kimya muda wote alisema.

    Wakatokomea na laptop mbio.



    "Tutakutana tu " Daniel alisema kimoyomoyo, huku akitabasamu. Akatoka nje taratibu. Kwa utulivu mkubwa. Kama hajatizamwa na midomo miwili ya bastola dakika chache zilizopita. Alitembea kwa madaha. Kwa mwendo wa kujiamini. Huku akijiuliza kwanini wale jamaa walimwacha akipumua. Akawacheka ujinga. Hawakujua kuwa walifanya kosa la karne. Daniel Mwaseba alikuwa zaidi ya wanavyomfahamu. Akarandaranda mitaa ya Mikocheni bila uelekeo maalumu. Aliranda makusudi. Alikuwa anachunguza kama kuna mtu anamfatilia. Hakumwona mtu. Akaingia kwenye "internet cafe" moja. Akalipia masaa mawili. Akaifungua email yake. Aliikuta akichokitaka. Daniel aliikuta email iliyotumwa muda mfupi uliopita. Aliwapongeza wamiliki wa hoteli ile aliyokuwa mwanzo kwa kuweka "wireless internet'. Aliikuta email aliyojitumia yeye mwenyewe muda mfupi uliopita alivyokuwa kule hotelini. Kabla ya wale jamaa hawajamvamia. Kichwa cha email kilisomeka "SIRI ". Daniel akatabasamu tena. Sasa alianza kuisoma. Alianza kuisoma ile email yenye siri nzito!



    ***



    "Hili ni Angamizo. Macho yasiyohusika hayapaswi kabisa kuona maandishi haya.... " Ghafla Daniel alihisi anapapaswa bega. Daniel aligeuka. Alikuwa anatazamana uso kwa uso na Zwangendaba.



    " Sasa nimekuja kuichukua roho yako rafiki yangu " Alimnong'oneza Kwa sauti ndogo iliyopenya vizuri katika sikio la kushoto la Daniel. Kwa mara ya kwanza mapigo ya moyo yalimpiga Daniel. Hakutegemea kabisa watu wale kuwa mahali pale muda ule. Hakutegemea kabisa kukamatwa kirahisi namna ile. Alihisi Kutekenywa na kitu kigumu mbavuni. Akaelewa. Alikuwa ameguswa na bastola kwenye mbavu zake.



    "Simama juu" Zwangendaba alinong'ona tena. Daniel alisimama. Watu wote ndani ya 'internet cafe' hawakuelewa nini kinaendelea. Kila mtu alikuwa anatazamana na kompyuta yake. Daniel alikuwa anatekwa kimya kimya. Kaspersky naye aliingia ndani ya internet cafe. Akaisogelea ile kompyuta akiyoitumia Daniel. Akaifuta ile email ya siri. Akarudi nje wakapanda kwenye Noah yao nyeusi. Safari ya kwenda kusikojulikana iliaanza.



    Ndani ya gari ilikuwa kimya. Hakuna aliyeongea. Wale majamaa wawili walikuwa wanavuta bangi kwa fujo ndani ya gari. Gari yote ilitapakaa moshi wa bangi. Yalikuwa mateso kwa Daniel. Hakuwa mvutaji hata wa sigara. Lakini hakuruhusu hata kukohoa. Alijua kukohoa tu ataonekana dhaifu mbele ya watu wale. Safari isiyojulikana ilifika mwisho. Ilikuwa nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam. Kulikuwa na kibanda kidogo porini. Kibanda kilichojitenga na nyumba za watu. Walimuweka kwenye kibanda hicho. Daniel alishuhudia migongo ya Kerspersky na Zwangendaba ikitokomea. Daniel walimfungia kwenye kibanda hicho.



    Kilikuwa kibanda kidogo chenye mlango mmoja tu. Hakukuwa na madirisha wala sehemu yoyote ya kutolea au kuingiza hewa. Walimfungia kinjenje. Alisikia muungurumo wa gari, jamaa walitoweka kwa kasi kwa gari yao. Kwenda kutekeleza mpango wao hatari wa Angamizo. Hawakutaka kumuua Daniel. Nia yao Daniel ashuhudie Angamizo litakaloikumba Serikali yake. Walimuacha hai ili ateseke kwa kuona Angamizo hilo.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Abdul aliendelea kukaa kule kwenye chumba cha siri cha Polisi Arusha. Alikuwa ameshachoka sasa. Alikuwa anautamani sana uhuru wake. Hakumuona Daniel ndani ya siku tatu. Alikuwa anatamani kumuona Daniel. Maana yeye ndio alikuwa tumaini lake pekee la kuurudisha uhuru wake tena. Alianza kukonda kwa mawazo.



    Upande wa Polisi nao ulichanganyikiwa sana. Kutoonekana kwa Daniel kwa siku tatu bila mawasiliano lilikuwa jambo la kushangaza sana. Wakahisi huenda Daniel yuko katika matatizo makubwa. Walimtafuta kila sehemu waliyoifikiria bila mafanikio yoyote.



    Kule Ndani ya kibanda kile Daniel aliteseka sana. Kulikuwa na joto kupita kiasi. Ukijumlisha na njaa pamoja na kiu kikali alichokuwa nacho, yalikuwa mateso makubwa sana. Alivyoachwa tu Daniel siku ileile alitafuta njia ya kujiokoa bila mafanikio. Mlango ulikuwa ni geti gumu la chuma. Ukuta wa tofali ulikuwa mrefu wa kunyooka mgumu kuupanda. Kwa juu ziliezekwa bati za udongo. Ndani kulikuwa na giza kiasi cha kutotambua usiku au mchana. Hakukuwa na madirisha kabisa katika kibanda kile. Dakika ya kwanza tu aliyowekwa Daniel alianza kutafuta namna ya kujiokoa. Hadi leo siku ya tatu hakuipata. Na wala hakuwa na dalili ya kuipata.Alidhohofika sana kwa mawazo. Alidhohofika sana kwa njaa. Sasa alilala chini akiwa amekata tamaa. Alikuwa anakisubiri kifo. Huku akisikitika siyo tu kwa kutozitimiza harakati alizozianzisha duniani. Hapana, alisikitika kwa kutofanikiwa angalau kujua watu wale walikuwa na siri gani wakiyoilinda namna ile. Alikuwa amelala chini huku akikoroma sasa. Hakuwa na nguvu sasa. Ndipo likamjia tumaini. Akakumbuka kitu pekee kinachoweza kumuokoa mahali pale. Mungu. Daniel alipiga magoti kwa shida na kuanza kumuomba Mungu. Hakuwa mhudhuriaji kabisa wa nyumba za ibada. Lakini leo alikwama kweli. Alimuomba Mungu kitu kimoja tu. Amuokoe katika mdomo wa mauti ili akaitetee nchi yake. Aliomba ndani ya nusu saa. Hakikutokea kitu. Sasa aliamua kulala akiwa amekosa matumaini kabisa. Daniel alimuona malaika mtoa roho akimsogelea. Alikata mawasiliano na dunia. Alilala usingizi mbaya huku akikoroma.



    ***



    Ni siku ya tatu leo mke wazee Washiro hakwenda kuchuuza samaki mtaani. Alikuwa anamhudumia mtu aliyemuokota mumewe, Mzee Washiro. Katika mizunguko yake ya kutafuta matunda ya mabungo porini ili akayauze sokoni Bagamoyo apate pesa ya nauli ili aende Arusha kumwangalia mwanae aliyekuwa mikononi mwa Polisi. Mzee Washiro alikutana na kitu cha ajabu.



    Ni mwezi sasa tangu mwanae Abdul alipompigia simu na kumueleza kuwa amepatwa na matatizo Arusha. Mwanawe alikamatwa Kwa kosa la kumuua mtoto wa makamu wa Raisi wa Zanzibar. Siku ya tatu baada ya kuacha kazi yake ya uvuvi ambayo aliona inamuingizia pesa polepole aliamua kuingia msituni kutafuta matunda hayo ya porini na kwenda kuyauza sokoni. Sasa alikuwa na akiba ya elfu kumi na tano ndani. Siku ya nne aliyoenda msituni kutafuta mabungo, hakurudi na mabungo. Alirudi na mwili wa mtu aliyepoteza fahamu. Siku hiyo alikiona kibanda kidogo kilichokuwepo katikati ya msitu. Mzee Washiro alikisogelea kwa tahadhari. Alisikia mtu akikoroma ndani ya kibanda hiko. Bila shaka alikuwa katika matatizo makubwa. Alivunja kufuli ya kibanda kile kwa kutumia jiwe kubwa , alimkuta mtu aliyekuwa akiyekoroma ndani yake. Alimchukua na kumpeleka nyumbani kwake. Tangu siku hiyo Daniel alikuwa anahudumiwa na mama Washiro. Mama yake mzazi na Abdul. Hawakuwa na uwezo wa kumpeleka hospital. Daniel alihudumiwa kwa dawa za kienyeji. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku ya pili leo fahamu za Daniel hazikuwa zimerejea.

    Siku ya tatu alfajiri walisikia makelele katika chumba cha mgonjwa wao. Daniel alikuwa analia usingizini. Mzee Washiro alienda chumbani na kumkuta Daniel akigaragara kitandani. Alikuwa anataja neno moja tu. Angamizo!

    Mzee Washiro hakuelewa Maana ya maneno hayo. Lakini alijawa na furaha moyoni kuona mgonjwa wao amepata nafuu. Siku hiyo ndio ilikuwa mwanzo wa Daniel kurejea duniani. Ilihitajika lishe bora tu ili Daniel arudi katika hali yake ya kwaida. Maana hakuwa na jeraha lolote mwilini.



    "Nashukuru sana mzee kwa msaada wako" Daniel alisema siku moja.



    "Usijari kijana"



    "Umenisaidia sana. Umenitoa kwenye ufu na kunirudisha duniani. Mungu akubariki sana! "



    Amina"



    "Sasa mzee naomba uniazime simu yako niwajulishe ndugu zangu hali yangu" Mzee Washiro alimpa simu Daniel Mwaseba. Simu aliyopiga Daniel ilizua chereko upande wa pili. Daniel alipiga simu kwa Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP John Rondo alifurahi sana. Kwani alihisi Daniel ameuwawa.



    Nusu saa baadae helkopta ya kijeshi ilitua ndani ya mji wa Bagamoyo na kumbeba Daniel na kumpeleka Dar es salam kwa uangalizi maalumu. Daniel alimuahidi Mzee Washiro ipo siku atarudi tena kulipa fadhila kwa aliyomfanyia. Daniel alienda Dar es salaam kwa lengo Moja tu, kupata lishe bora ili kurejesha siha yake. Arudi katika mapambano haya mazito.



    Kutokana na matunzo na vyakula akivyokula Dar es salaam, baada ya wiki moja hali ya Daniel ilirudi kama zamani. Baada ya kupona Daniel kabisa alisimuliwa na IGP Rondo madhara waliyoyafanya wauaji kipindi chote alichokuwa kuzimu. Walishaua watoto wa vigogo wengine watano. Toka katika mikoa tofauti .Walishaua wapelelezi kumi na moja na raia wema ishirini. Wote waliwauwa kwa mtindo uleule. Wa kutumia sumu kali ya Proxine.



    "Nchi sasa ipo katika hali ya hatari sana. Tegemeo pekee ni wewe Daniel. Najua ulishapiga hatua flani katika upelelezi wako. Nchi inakutegemea sana. Raisi anakutegemea sana. Watanzania wanakutegemea sana. Hebu nenda kaumalizie upelelezi wako." IGP John Rondo alikuwa anaongea kwa sauti ndogo na yenye hisia.



    "Usijari mkuu. Nakuahidi ndani ya siku tatu nitakuwa nishawaonesha hawa mahayawani mimi ni nani?

    Hii ni ahadi mkuu"



    Usijari mkuu. Nakuahidi ndani ya siku tatu nitakuwa nishawaonesha hawa mahayawani mimi ni nani ? Hii ni ahadi mkuu"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Unajua nakukutegemea sana Daniel" Daniel sasa aliingia kazini kwa kasi mpya. Alibeba dhima ya Taifa. Nyuma yake kulikuwa na Watanzania zaidi ya milioni arobaini wakimtegemea yeye.

    Wakimtumaini yeye pekee.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog