Simulizi : Angamizo
Sehemu Ya Pili (2)
Walitoka nje ili kumwangalia Raiya ameenda wapi? Hawakumuona.
Hawakujua ameelekea wapi? Aliyeyuka mithili ya upepo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baadae Mayasa aliaga na kuondoka kwao huku Abdul akibaki na wingi wa mawazo. Abdul alisinzia akiwa na mawazo mengi. Lakini kutokana na uchovu wa kutoka Same na ukijumlisha mawazo aliyomletea Raiya ndio yalimchosha kabisa, alilala fofofo.
Saa kumi usiku simu yake ilitoa mlio wa sauti alioutega Kwa ajili ya mwitikio wa ujumbe mfupi. Ikimaanisha kuna meseji mpya iliingia.
'Umeuchokoza moto. Niliacha zamani ukatili. Wewe unajitahidi kunirudisha huko. Nilikuwa katili sana zamani. Kama hupendi nirudie tabia zangu za zamani nakuomba achana na kikaragosi. Nitakuuwa, nitamuuwa pia. Nakupa siku tatu za kufikiria juu ya suala hili. Mimi bado nipo Arusha.
Namaanisha!" Abdul alikaa kitandani na kuurudia kuusoma ujumbe ule mara tano. Jasho lilikuwa linamtiririka kama maji. Akamtumia ule ujumbe na Mayasa.
Hakuujibu.
Na hajaujibu mpaka leo!
Asubuhi na mapema watu wanne walienda katika chumba cha Abdul. Walikuwa wamefuatana na kiongozi wa hosteli. Mshauri wa wanafunzi na Raisi wa Chuo. Walimuita pembeni na kumwambia.
"Sisi ni askari wa kituo kikuu cha Polisi Arusha. Unahitajika kituo cha Polisi kwa mahojiano kidogo"
"Nimefanya nini jamani ?"
"Utajua hukohuko kituoni" Askari mmoja alimnyanyua kwa nyuma suruali yake na kupelekwa kituoni. Alikuwa anatembelea vidole sasa. Wanafunzi wenzie walimuonea huruma pale chuoni.
Hakujua amefanya nini? Hawakujua amefanya nini?
Baada ya kufika kituoni ndipo alipoambiwa kosa lake. Eti alituhumiwa kwa kumuua Mayasa! Na ujumbe wake wa vitisho kutoka kwanye simu yake yake ulikutwa katika simu yake. Na ulitumika kama ushahidi. Alihemewa sana.
Alilia sana.
Aliuona mwisho wa ndoto zake umetimia. Akajua ataozea jela. Aliwekwa selo akisubiri ushahidi ukamilike. Akiwa ndani ya selo Abdul aliwaza mambo mengi sana. Moja kwa moja alijua kama kweli Mayasa ameuwawa basi Raiya ndiye mhusika mkuu wa kifo cha Mayasa. Lakini ujumbe ule aliomtumia Mayasa ulikuwa unamweka mashakani. Alikuwa analia mithili ya kichanga. Afande aliyekuwa anaitwa John ndiye alipewa jukumu la kupeleleza kesi ya kifo cha mtoto wa Makamu wa Raisi wa Zanzibar. Afande John alianza kumhoji Abdul kwanza. Mtuhumiwa wa kwanza wa mauaji yale.
" Unaitwa nani? "
"Abdul "
"Majina matatu !!"
"Abdul Ramadhani Washiro"
"Kabila? " CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Msukuma "
"Nambie uhusiano wako na Mayasa ?"
"Alikuwa mwanafunzi mwenzangu"
"Hamkuwa na uhusiano wa kimapenzi ?"
"Hapana, alikuwa ni rafiki yangu wa kawaida "
"Sasa kwanini uliamua kumuua rafiki yako?"
"Sijamuua mimi afande "
"Soma huu ujumbe "Askari ule ujumbe aliyomtumia Mayasa baada ya kutumiwa na Raiya. Ujumbe wa vitisho!
Ulisomeka' Umeuchokoza moto. Niliacha zamani ukatili. Wewe unajitahidi kunirudisha huko. Nilikuwa katili sana zamani. Kama hupendi nirudie tabia zangu za zamani nakuomba achana na kikaragosi. Nitakuuwa, nitamuuwa pia. Nakupa siku tatu za kufikiria juu ya suala hili. Mimi bado nipo Arusha.
Namaanisha'
"Alinitumia Raiya ujumbe huu, mimi nilimfowadia tu Mayasa."
"Raiya ndio nani ?"
Alimsimulia afande John kila kitu kuhusu ugomvi wao na Raiya. Alirudishwa selo na afande John alikwenda kwa kina Raiya kumhoji. Hakuwa anapajua , na wala Abdul alikuwa hapajui. Ila alisema atapajua tu. Afande john alifanikiwa kufika nyumbani kwa dada yake Raiya. Baada ya kumuonesha kitambulisho cha Polisi, Raiya alishangaa sana.
"Jamani, wewe ni askari wa tatu kuja kunihoji leo"
"Walikuja maaskari wengine hapa ?"
" Ndio na mmoja katoka nusu saa iliyopita"
"Walikuwa na vitambulisho ?"
"Ndio walinionesha"
"Unayakumbuka majina yao?"
"Nayakumbuka sana kwa kuwa majina yao wote yanafanana"
"Wanaitwaje?"
"Wote wanaitwa John"
Afande John alisikia kizunguzungu na mivumo isiyoeleweka masikioni mwake Ilikuwa taarifa ya kushangaza sana.
"Itabidi nikakuhoji kituoni " Afande John aliona pale siyo mahali salama pa kufanyia mahojiano. Walifuatana na Raiya kuelekea kituoni. Hapakuwa na umbali mkubwa sana toka nyumba aliyokuwa anakaa Raiya hadi kituo kikuu cha Polisi Arusha. Raiya alikuwa anakaa katika nyumba ya dada yake aliyokuja kukaa kwa muda mahsusi ili kutekeleza aliyoyakusudia, kutenganisha penzi la Abdul na Mayasa kama akivyoamini yeye kuwa walikuwa wapenzi.
"Raiya hebu nambie vizuri kuhusu hao askari waliokuja kukuhoji kwako."
" Ndiyo kama nilivyokwambia Afande. Walikuja askari wawili kunihoji. Mmoja alikuja asubuhi na mwingine alikuja muda mfupi kabla hujaja wewe. Na wote walitaka maelezo yangu kuhusu kifo cha Mayasa na uhusiano wangu na Mayasa na Abdul"
"Wewe uliwajibu nini?"
"Yule wa kwanza sikumjibu kitu. Maana aliniacha kwenye mstuko mkubwa sana baada ya kunambia Mayasa amefariki. Sikuamini kama Mayasa amefariki..nilikuwa nalia tu kila alichokuwa ananiuliza . Askari yule alifanya kazi ya kunibembeleza tu, akaondoka"
"Askari wa pili je ?"
"Yeye alinikuta nimetulia sasa. Nilimueleza kila kitu kuhusu ugomvi wetu mimi, Mayasa na Abdul."
"Alisemaje baada ya maelezo yako?"
"Aliandika kwenye kitabu chake na kuondoka" Afande John alishusha pumzi ndefu. Akajua ngoma sasa imekuwa nzito. Akamfungia Raiya selo na kutoka nje kwenda kutafakari. Alikaa chini ya mwembe mrefu uliokuwepo pale nje ya kituo. Akiwaza na kuwazua. Simu yake ikawa inaita. Namba ilikuwa ngeni. Zilitokea namba tu. Akaipokea na kuiweka sikioni.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Hallo"
"Hallo nani mwenzangu ?"
"Huna haja ya kulijua jina langu. Cha muhimu acha kuifatilia hiyo kesi utauwawa bure. Au unahamu ya kumuweka eda mkeo?"
Aliandika kwenye kitabu chake na kuondoka" Afande John alishusha pumzi ndefu. Akajua ngoma sasa imekuwa nzito. Akamfungia Raiya selo na kutoka nje kwenda kutafakari. Alikaa chini ya mwembe mrefu uliokuwepo pale nje ya kituo. Akiwaza na kuwazua. Simu yake ikawa inaita. Namba ilikuwa ngeni. Zilitokea namba tu. Akaipokea na kuiweka sikioni.
"Hallo"
"Hallo nani mwenzangu ?"
"Huna haja ya kulijua jina langu. Cha muhimu acha kuifatilia hiyo kesi utauwawa bure. Au unahamu ya kumuweka eda mkeo?"
"Usinitishe kijana"
"Nitakuuwa!"
"Huna jeuri hiyo"
"Unajifanya kiburi"
"Nitawakamata wote wauaji waoga!' " Utaenda kutukamata kuzimu.."
Afande John alihisi amerukiwa na kitu kama maji maji utosini. Aligusa kwa mkono wake wa kulia. Aligusa yale maji. Sauti ya kwenye simu ilianza kucheka. Ghafla ngozi ya afande John ilianza kuvuka. Afande John alitupa simu chini, alisikia maumivu makali sana. Alikufa taratibu kwa maumivu makali sana! Alikufa aina ya kifo sawa na alichokufa Mayasa!
Sasa ilikuwa mshikemshike. Mauaji ya Polisi kuuwawa nje ya kituo. Ilizua mambo mengi. Mauaji haya ya pili yaliwafanya Polisi wafikirie nje ya boksi. Watuhumiwa wawili wapo ndani, lakini Afande John kauwawa akiwa nje. Bila shaka na wauaji walewale waliomuuwa Mayasa.
Mauaji hayo yalilitikisa Jiji la Arusha. Arusha iligeuzwa nje ndani kumtafuta muuaji au wauaji. Hawakupata fununu zozote. Polisi walibaki gizani.
Mayasa alikuwa Mtoto wa mkubwa Serikalini. Serikali ilituma wapelelezi mahiri watatu. Kwenda Arusha kumsaka muuaji. Walienda wapelelezi watatu. Lakini kila mmoja alivuliwa ngozi kwa siku yake. Waliuwawa kwa maji yaleyale yaliyomuua Mayasa. Maji yaleyale yaliyomuuwa afande John. Mmoja alikutwa amekufa hotelini kwake, akiwa amelala. Ngozi ikiwa imejitenga na mwili wake. Wapili alikutwa amekufa akiwa kwenye gari lake. Aina ileile ya kifo alichouwawa mwenzake. Wa mwisho aliuwawa mgahawani. Akiwa anakula chakula cha usiku.
Hali sasa ilitisha sana !
Ndani ya selo hali Abdul Ilikuwa mbaya sana. Polisi hawakuwa wamempiga hata kidogo . Lakini alikuwa amechoka taabani. Alichoka kimwili. Alichoka kimawazo. Kifo cha Mayasa kilimuumiza sana kichwa. Akilini mwake alijua Raiya anahusika kwa asilimia zote. Aliukumbuka sana wema wa Mayasa. Mayasa alikuwa kama malaika kwa Abdul. Mayasa alikuwa mwanamke mwenye roho ya kipekee sana. Alimsaidia bila ya sharti lolote. Alimkumbuka kila dakika mle selo. Sasa alimchukia sana Raiya. Chuki kwa Raiya ilianza taratibu. Lakini sasa ilikuwa imeota mizizi. Alimwona ni adui yake namba moja duniani. Adui kwa kumuua Mayasa. Rafiki mwenye upendo wa kweli kwake. Wazazi wake hawakuwa wanajua kama yuko jela. Na wala hakutaka kuwaambia, maana hata angewaambia isingesaidia lolote, maana hakuna atakayeenda Arusha. Wasingekuwa na nauli ya kwenda Arusha. Alikuwa anaijua hali ya uchumi ya nyumbani kwao. Aliacha kuwaambia akihofia kuwapa presha za bure. Wakati akiwa anawaza hayo, mlango wa selo ulifunguliwa. Aliingia askari mmoja wa kike. Alikuwa na sura ya huzuni. Alikuja kumpa taarifa mbaya ya kifo. Taarifa ya kifo cha Afande John !
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Inamaana Raiya kamuua na Afande John ?"
" Sidhani kama Raiya anahusika. Afande John amefariki wakati Raiya yuko selo"
"Unasema!"
"Ndio hivyo Abdul, hebu tuambie mtu mwengine unayehisi anaweza kuwa nyuma ya mauaji haya Abdul ?"
"Hakuna nilijualo Afande kweli sijui kitu afande" Alisema huku machozi yanamtoka . Alirudishwa selo baada ya mahojiano mafupi na askari yule wa kike. Sasa akaona uzito na ugumu wa kesi hii iliyokuwa inamkabili. Akaamua kuwaeleza wazazi wake Bagamoyo kwa simu. Hakuwa na jinsi sasa. Alikuwa anahitaji hekima za wakubwa. Alikuwa anahitaji sana majaliwa ya Mungu. Kutoka katika mkasa huu mzito. Aliwaomba askari wampe simu ili awapigie wazazi wake. Awataarifu juu ya kukamatwa kwake.
Walimruhusu.
Alimueleza baba yake mzazi, Mzee Washiro juu ya kukamatwa kwake na Polisi na tuhuma za mauaji zinazomkabili. Alisikitika sana baba yake. Kwa mara ya kwanza alimsikia baba yake akilia kwenye simu. Alipatwa na uchungu sana. Abdul alikuwa mtoto wake wa kwanza kati ya watoto saba. Alikuwa ndiye tumaini hai la familia yake. Mtoto aliyesoma zaidi ya wote katika familia yake. Habari ya kutuhumiwa kwake kwa kesi ya mauaji, kwa baba yake ilikuwa mithili ya kuzimika ghafla kwa mshumaa pekee akioutegemea gizani. Pamoja na yote alimuahidi kitu. Alimuahidi lazima aende Arusha punde atakapopata pesa. Abdul alijua baba yake hatokukwenda Arusha karibuni. Na pengine hatokwenda kabisa. Na anaweza kuozea jela Arusha bila kumuona ndugu yake yeyote. Walikuwa mafukara sana nyumbani kwao. Lakini kidogo alipata imani. Kwakuwa nyumbani kwao walikuwa wanafahamu sasa kuwa mtoto wao yupo katika matatizo makubwa ugenini.
***
Kwa upande wa Polisi wa Arusha Ilikuwa hekaheka ndani ya Jiji. Walitafuta wachuna ngozi wale wasio na huruma bila mafanikio. Walimkamata kila waliyemuhisi, lakini hawakufanikiwa kumkamata muuaji halisi. Ilikuwa kama ametoweka ghafla Arusha. Jiji lilibaki likisubiri Muuaji yule katili ataibukia wapi?
Baada ya wiki mbili yalitokea mauaji mengine. Safari hii katika Jiji la Mwanza . Mauaji ya aina ileile kama yaliyotokea Arusha. Katika Chuo kikuu cha St Augustine cha huko jijini Mwanza kuna mwanafunzi aliuwawa kikatili. Alikuwa anatoka kujisomea usiku akielelekea Hosteli. Alinyang'anywa njiani roho yake. Maiti yake iliokotwa asubuhi katika uwanja wa mpira wa chuo ikiwa haitamaniki. Ngozi iliokotwa upande wa goli la kaskazini. Kiwiliwili kisicho na ngozi kiliokotwa karibu na goli la kusini. Yalikuwa mauaji ya kinyama sana. Yaliowaacha na uwoga mkubwa sana wanafunzi wa Chuo hiko kikubwa jijini Mwanza.
Mwanafunzi huyo alikuwa ni mtoto wa waziri wa ujenzi, Mheshimiwa Karimu Nduguga. Polisi wa Mwanza nao wakalipata hekaheka kama ilivyokuwa kwa wenzao wa Arusha, wa kumsaka muuaji huyo asiye na huruma. Lakini hawakumpata na wala hawakukaribia kumpata.
Ndipo hali ya hatari ikatangazwa nchi nzima, na Waziri wa wa mambo ya Ndani ya nchi, Mheshimiwa Frank Chali. Ilitolewa tahadhari hasa kwa watoto wa viongozi wakuu wa chama na Serikali. Watoto wa vigogo wakawa wanalindwa hasa. Huku doria za Polisi zikishamiri Tanzania mzima.
Abdul na Raiya waliendelea kusota selo. Sasa walihamishiwa Gereza kuu Arusha.Ilikuwa kwa usalama wao kama Polisi walivyosema.
Wiki mbili zilipita maisha yao yakiwa selo. Ilikuwa siku ya jumatatu asubuhi. Ya wiki ya tatu tangu wahamishiwe Magereza. Abdul alitolewa selo na kupelekwa katika chumba cha mahojiano cha Gereza lile. Siku hii alihojiwa na mtu mpya. Hakuwa wa gereza la Arusha. Maana wengi ailikuwa anawafahamu sasa.
"Unaitwa nani ?"
"Naitwa Abdul Ramadhani " "Niambie kwa kifupi unavyolielewa sakata hili ?" Alimsimulia kila kitu tangu safari yangu ya kutoka Bagamoyo hadi nilivyofika Arusha.
"Unajua Kwa nini umewekwa ndani? "
"Ndio"
"Kwanini ?"
"Kwa ajili ya usalama wangu."
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Sasa mimi nataka nikutoe nje Abdul "
"Ati !"
"Ndio nataka uisaidie Polisi ukiwa nje"
"Nahofia usalama wangu, wataniua vibaya "
"Usiwe na shaka. Utakuwa na mimi kila hatua utakayopiga. Naitwa Daniel Mwaseba"
"Usiwe na shaka. Utakuwa na mimi kila hatua utakayopiga. Naitwa Daniel Mwaseba" Abdul alistuka sana kusikia jina hilo. Hakuna Mtanzania ambaye alikuwa halijui jina la Daniel Mwaseba . Alikuwa mpelelezi namba moja Tanzania. Alikuwa mtu hatari kuliko hatari yenyewe. Alishawahi kuliokoa Taifa hili katika matatizo makubwa sana. Aliliokoa kutoka katika hila mbaya za maadui zetu. Alikuwa kijana makini, mpiganaji, mzalendo wa kweli kwa nchi yake. Kuja kwa Daniel Mwaseba kwenye kesi hii Abdul akajua mambo yamefikia pagumu. Mbele ya Daniel alikuwa radhi atolewe. Aliamini atakuwa salama.
Alikubali.
Walitoka Gerezani wakiwa wamefuatana na Daniel Mwaseba. Alijisikia fahari kufuatana na Daniel. Njiani alikuwa anamuuliza hili na lile. Yeye alikuwa anajibu kwa mkato tu. Daniel alikuwa anampekeka Kijenge juu kwenye nyumba aliyopangiwa na jeshi la Polisi kuishi kwa muda. Hosteli haikuwa sehemu salama kwake tena. Walishuka kwenye gari ya Daniel wakiwa sambamba. Walikuwa wanakatisha barabara ili waingie katika nyumba aliyopangiwa. Wakati wakiwa katikati ya barabara gari dogo aina ya Noah nyeusi ilikuja kwa kasi kwa lengo la kutaka kuwagonga. Abdul aliliona lakini hakuwa na jinsi ya kufanya. Liliwakaribia sana. Kwa kasi ile Abdul alijua lazima wagongwe. Lazima wafe yeye na Daniel Mwaseba. Kilikuwa kifo dhahiri usoni mwao.
Ghafla Abdul alijikuta amerudi nyuma kwa haraka sana. Gari lilipita sentimita chache sana na pale waliposimama na Daniel. Kilikuwa ni kitendo cha haraka sana. Abdul hakuelewa amerudi vipi nyuma kwa kasi ile. Akamwangalia Daniel Mwaseba alikuwa anatabasamu, hana wasiwasi wowote. Huwezi jua kama kiliwakosa kifo sikunde chache zilizopita.
"Mwanzo nzuri" Abdul alimsikia Daniel akinong'ona mwenyewe.
"Hivi limetukosaje lile Gari ? Halafu alidhamiria kutugonga kwa makusudi"
"Nilikuvuta mkono" Daniel alijibu jibu fupi na kumshika mkono Abdul, wakarejea kwenye gari yake.
Kwenye gari hakuongea neno. Alikuwa kimya, makini na usukani huku akipiga mluzi. Akiimba wimbo usioeleweka. Lakini akiangalia kwenye vioo vya pembeni vya gari kila mara.
"Hivi kitu gani cha siri alichowahi kukwambia Mayasa?" Ghafla Daniel alimuuliza swali Abdul huku akiwa anaangalia mbele.
"Hakuna kitu cha siri alichowahi nambia Mayasa"
"Una uhakika Abdul? Nakuuliza hili kwa ajili ya maisha yako. Kuficha hakukusaidii kitu"
"Kweli kaka Daniel. Hakuna siri yoyote aliyowahi nambia Mayasa."
Safari yao ilishia kituo kikuu cha Polisi Arusha. Walikaa kaunta pamoja na Daniel na askari mwengine. Mara simu ya mezani ya pale kaunta ikaita.
"Hallo"
"Napiga toka Magereza Arusha"
"Ehh nambie Afande"
"Kuna tatizo hapa Magereza"
"Tatizo gani Afande ?"
"Yule mwanamke aliyewekwa mahabusu kwa ajili ya usalama wake amefariki!!!"
"Nani ?"
"Raiya" CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Unasemaa !"
"Ameuwawa Afande"
"Natuma askari sasa hivi"
"Sawa" Yule askari aliwaambia taarifa ya kifo aliyoipokea. Ilikuwa ni taarifa ya kifo cha Raiya, iliwastua sana. Lilikuwa pigo la ghafla na la kushangaza sana. Mtu kufariki akiwa mikononi mwa askari siyo tatizo sana. Lakini mtu kuuwawa mikononi wa askari ilikuwa ni tatizo kubwa sana. Tena ndani ya Gereza lenye ulinzi mkali kama la Arusha. Yalikuwa maajabu.
Walifuatana Abdul na Daniel kuelekea Magereza. Daniel hakutaka kumuacha Abdul hata sekunde moja. Alijua lazima wauaji watataka kumuua. Kwa vyovyote walikuwa wanataka kupoteza ushahidi kwa kuuwa. Daniel aliamini kwa kumtumia Abdul ndipo atakapowatia mkononi kwa urahisi wauaji. Alimtumia kama chambo. Alijua kwa vyovyote atakuwa anawindwa auwawe!
Waliwasili Magereza majira ya saa nne asubuhi. Walikuta hali ya gereza ikiwa shwari na vikundi vidogovidogo vya askari wakijadiliana. Walienda moja kwa moja kwa mkuu wa Gereza. Baada ya salamu walianza kuongea.
"Ilikuwaje mkuu"
"Mnamo mida ya saa tatu asubuhi alikuja mtu. Alidai yeye ni ndugu na Raiya. Baada ya kumkagua askari walimruhusu aingie. Hakuwa na kitu chochote cha hatari. Baada ya kama dakika nne aliaga anaondoka, na marehemu alirudi selo. Lakini baadae askari walipoenda kwenye selo yake walimkuta ameuwawa kikatili sana"
"Marehemu alipomuona huyo mtu alionesha dalili yoyote ya kumtambua?"
"Siwezi kujibia hilo ngoja tumwite askari aliyekuwa zamu" Mkuu wa Gereza alimpigia Simu huyo askari. Baada ya kumaliza wakaendelea na maongezi yao
"Kwanini mnahisi huyo mgeni ndiye anahusika Katika mauaji ?"
"Marehemu hakuongea na mtu mwengine yeyote baada ya yule mgeni kuondoka"
Baada ya maelezo hayo yule askari aliyepigiwa simu na mkuu wa Gereza alikuwa ameshafika. Yeye alisema hakuwa makini kuchunguza kama mgeni na marehemu walikuwa wanajuana ama lah. Yeye aliwakutanisha tu na kuondoka. Bila kutafiti chochote. Waliongozana na mkuu wa magereza pamoja na Daniel kwenda kuuangalia mwili wa marehemu Raiya. Ilikuwa ni picha mbaya sana ambayo haitafutika kichwani kwa Abdul hadi leo. Picha mbaya ilioje kumkuta binadamu unayemfahamu kachunwa ngozi mithili ya Ng'ombe. Abdul alikuwa anamchukia sana Raiya lakini siku ile alitoa machozi kwa ajili ya yake. Alimuonea huruma sana. Alijua kapitia maumivu makali sana akiwa anaipigania roho yake. Mwili usio na ngozi uliwekwa hapa. Na ngozi iliyokusanywa iliwekwa pale...! Hali ilikuwa ya kutisha sana. Hakuna aliyeongea kwa zile dakika tano walizokaa katika chumba. Abdul alimwangalia Daniel usoni. Alikuwa anatabasamu bila wasiwasi wowote. Walirudi ofisini kwa mkuu wa Gereza. Sasa Abdul aligundua tabia moja ya Daniel. Huwa anatabasamu kila mambo yanapokuwa magumu. Alimwona Daniel anatabasamu mbele ya maiti ya Raiya iliyouwawa kinyama.
Daniel Mwaseba na Abdul waliondoka pale Magereza wakiacha mwili wa marehemu Raiya ukipakiwa kwenye gari kupelekwa hospitali. Abdul alikuwa mwenye majonzi sana. Watu wawili waliojitolea kumsaidia kwa hali na mali walikuwa wamefariki kwa tofauti ya masaa machache sana. Ni mkosi gani huu.
Njiani alimuona Daniel Mwaseba akitabasamu. Akajua kuna kitu cha kakiona. Tena bila shaka cha hatari.
"Tunafuatwa" Alimsikia akisema kwa sauti ndogo.
"Ama zetu, ama zao "
Waliifuata njia iliyokuwa inaelekea Moshi mjini kutokea Arusha. Abdul roho inamdunda sana. Daniel alikuwa hana wasiwasi hata kidogo. Akiendelea na mluzi wake usioeleweka. Abdul aliangalia kwenye kioo cha pembeni naye aliona. Gari tatu nyeusi aina ya Noah zilikuwa zinawafuata kwa kasi kubwa sana. Daniel alikuwa makini na usukani. Alipofika Tengeru alikata kulia. Wakawa wanaelekea barabara ya vumbi iliyokuwa inaelekea katika Chuo cha Maendeleo ya jamii, Tengeru. Zilikuwa mbio kali sana kwenye barabara ya vumbi. Jamaa walianza kurusha risasi. Daniel alikuwa dereva makini. Alihakikisha hawadhuriki na risasi zile.
Na hawakudhurika.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Daniel aliingiza gari ndani ya Chuo cha Tengeru. Hakutegemea kama ataiingiiza gari Chuoni kwa kasi ile. Abdul alidhani atakata kulia njia inayoelekwa chuo cha Sayansi cha Nelson Mandela. Haikuwa hivyo lakini. Sasa Ilikuwa patashika ndani ya Chuo cha Tengeru. Walikuta wanachuo wengi wapo nje. Baada ya kufunga breki walishuka haraka haraka na kujichanganya na kundi la wanachuo waliokuwa wanaelekea kunywa chai mgahawani. Waliziona zile Noah tatu nazo zikifunga breki kali . Vumbi lilitimka.
Baadhi ya wanafunzi wa kike wakipiga kelele za uwoga, wa kiume walikuwa wanashangilia. Bila kujua nini kinatokea . Walishuka jumla ya watu kumi na tano toka katika Noah zile tatu. Wote na bunduki mkononi.
Abdul na Daniel walikuwa washaingia Mgahawani. Lakini waliona kila kilichokuwa kinafanyika kule nje karibu na geti ya kuingilia Chuoni. Wanafunzi walianza kukimbia hovyo. Jamaa moja alipiga risasi tatu hewani. Sasa lilikuwa vurumai. Wanafunzi walikimbia hovyo huku wakipiga kelele za taharuki. Wakajigawa wale majamaa. Watano walielekea madarasani. Wawili walienda maktaba. Watatu walienda uelekeo wa ofisi za walimu, na watatu wengine walielekea vimbwetani na wawili walikuwa wanaenda Mgahawani walipokuwa kina Daniel. Daniel aliinuka pale kwenye meza akaenda kujificha nyuma ya mlango wa Mgahawa ule. Abdul alibaki palepale mezani pamoja na wale wanafunzi.
Hali ya hofu ilitawala ndani ya Mgahawa.
Wote waliwashuhudia watu wale wawili wakija Mgahawani na silaha zao mkononi. Wanafunzi walikuwa na hofu kubwa, walikuwa wanalia kimyakimya. Wale watu waliingia Mgahawani kwa umakini mkubwa sana. Abdul alikuwa anasubiri hatua atakayoichukua Daniel kule nyuma ya mlango. Alikuwa na imani nae sana. Akaingia wa kwanza. Akaingia wa pili.
Ghafla yule jamaa mmoja alidondoka chini. Watu wote walistuka mule Mgahawani. Abdul akamwangalia Daniel kule nyuma ya mlango alikojificha. Aliiona mdomo wa bastola yake ukiwa unafuka moshi. Akajua bastola ya Daniel imetumika. Na ilikuwa imefungwa kiwambo cha kuzuia sauti. Na bila shaka risasi ilitua mgongoni kwa yule jamaa. Yule jamaa mwengine alibabaika sana. Hakujua nini kimempata mwenzie. Mgahawa sasa ulikuwa kimya. Kila mtu alitulia kusubiri hatma ya roho yake.Yule jambazi mwengine aligeuka nyuma kuangalia kule mlangoni. Alikutana nayo!!
Alipigwa risasi ya utosini. Damu chache ziliwarukia baadhi ya wanafunzi waliokuwa karibu naye. Nae alielekea kuzimu bila ya kuaga. Sasa Daniel alitoka kule mlangoni. Akazivuta zile maiti mbili na kwenda kuzificha nyuma ya mlango. Hakuwa na wasiwasi kabisa. Alikuwa kama anavuta magunia ya mkaa tu.
"Wanafunzi wote laleni chini haraka. Atakayejifanya mjuaji tu shauri yake !!" Daniel alisema huku na yeye akilala chini.
Baada ya kama dakika kumi sauti za mlango zilisikika tena. Aliingia jambazi aliyevaa sawa na wale wenzake. Suti nzuri nyeusi na shati jeupe ndani. Na bunduki iliyotayari kuuwa wakati wowote itakapoamrishwa. Huyu aliingia bila umakini wowote. Bila shaka alitegemea Uwepo wa wenzake mle ndani. Hivyo yeye hakuwa makini sana.
" Chugaaa" alianza kuita.
"Naam" Aliitikiwa. Daniel aliitikia ule wito huku akinyanyuka alipokuwa amelala. Jamaa aliashangaa sana. Akiwa Kwenye mshangao Daniel aliachia risasi iliyozama katika tumbo la yule jamaa. Alikufa na mshangao wake usoni.
Daniel aliivuta ile maiti tena na kwenda kuiweka nyuma ya mlango nayo. Ulikuwa ni mchezo hatari sana lakini Daniel aliucheza bila uwoga wowote. Kosa moja tu lingesababisha kifo. Wanafunzi wengi walikuwa wameshajikojolea pale sakafuni kwa uwoga.
Abdul sasa kidogo alianza kuwa mzoefu. Mzoefu wa kuona maiti. Mzoefu wa kuona watu wakiuwawa. Watu wote walikuwa wameikumbatia sakafu kasoro Daniel pekee. Alikuwa amesimama akiangalia kule nje. Simu moja ya wale marehemu ilikuwa inaita kule nyuma ya mlango.
Daniel alienda kuipokea.
"Chuga hapa"
Alisema simuni.
"Yah, waje wawili " Daniel alijitambulisha kuwa yeye ni Chuga. Na kuomba watu wawili waje mgahawani. Hawakuchelewa.
Walikuja haraka sana. Wakati Daniel akiwa bado yupo kulekule nyuma ya mlango. Alikoenda kupokea simu. Wauaji waliingia ndani huku wakimwacha Daniel kule nyuma ya mlango. Hawakufikiria kabisa kama kuna hatari. Abdul jicho lake lilikuwa linaangalia nyuma ya mlango, kwa Daniel kuona atafanya nini ?. Alimuona akijishika kiuno. Alitoka na visu viwili. Kimoja amekishika kwa mkono wa kulia na kingine mkono wa kushoto. Alivirusha vyote kwa mpigo na kwa nguvu visu vile kuelekea kwa wale majamaa. Vyote vilitua shingoni. Kila mmoja na chake. Walienda chini kama mizoga. Nilimuona Daniel akitabasamu. Majambazi watano sasa alikuwa kawamaliza kimya kimya mule Mgahawani.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Mara kundi la majambazi wote kumi waliobaki kule nje lilikuwa linakuja Mgahawani wakiwa wanakimbia....
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment