IMEANDIKWA NA : HALFANI SUDY
*********************************************************************************
Simulizi : Angamizo
Sehemu Ya Kwanza (1)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kumekucha Arusha. Jiji lilipo kaskazini mwa nchi ya Tanzania. Siku ilianza kwa manyunyu ya mvua na radi kidogo katika jiji la Arusha. Kutokana na manyunyu hayo ya mvua, hali ya ubaridi iliongezeka katika jiji la Arusha. Baridi iliyowafanya watu wengi kuyakumbuka makoti yao na kuyatia mwilini.
Siku hiyo ilikuwa ya furaha sana kwa Abdul Washiro. Ilikuwa siku ambayo alikuwa anatimiza ndoto kubwa sana katika maisha yake. Alichaguliwa kujiunga na chuo cha uhasibu Arusha. Jumatatu hiyo ndio Ilikuwa siku yake ya kuripoti pale chuoni.
Abdul alikuwa na furaha sana. Hata ile hali ya baridi haikumchukiza kabisa. Hakuwa anaihisi baridi kabisa. Mawazo yake yote yalikuwa juu ya kutimiza ndoto hiyo kubwa sana katika maisha yake. Wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza walikusanyika katika ukumbi wa chuo kwa ajili ya usajili. Walikuwa wanafunzi wengi sana kutoka mikoa mbali mbali Tanzania, waliokwenda jijini Arusha kuisaka elimu.
Baada ya maelezo ya awali ya utambulisho toka uongozi wa chuo pale ukumbini sasa ulifika muda wa kupanga foleni ili usajili uanze.
Kila mtu alikuwa anagombea nafasi ya kukaa mbele ili angalau asisote sana kwenye foleni. Ilikuwa ni fujo sana . Abdul alikaa kwenye kiti cha plastiki akiangalia vurugu zile.
Hakuwa na wasiwasi wowote, alijua maadamu amechaguliwa kujiunga na chuo kile, basi atasajiriwa tu.
Baada ya fujo kutulia, Abdul naye alienda kujiunga kwenye foleni. Alikuwa mtu wa mwisho katika foleni ile ya usajili. Alikaa kwenye foleni huku akiwaza safari yake ya elimu ilipotokea.
***
Abdul aliwaza jinsi alivyosoma kwa shida shule ya Sekondari Bagamoyo. Wazazi wake hawakuwa na uwezo wa kumsomesha. Hivyo alipata shida sana kupata mtu mwenye moyo wa kumsomesha. Ilibidi mchana asome sana, ili jioni afanye biashara ndogondogo ya kuuza karanga ili aweze kupata hela ya mahitaji madogomadogo ya shule. Baba yake Abdul alikuwa mvuvi . Lakini pesa akizopata kutokana na kazi yake ya uvuvi zilitosha kuilisha familia yake tu. Hii ilitokana na Mzee Washiro kuwa na familia kubwa ya watoto saba. Mama yake hakuwa na kazi zaidi ya kuchuuza samaki mtaani, samaki wa mumewe. Inamaana ilikuwa sawa na kusema, baba na mama yake Abdul walikuwa wanafanya biashara moja. Baba anavua samaki, tena kwa zana dhaifu za uvuvi na mama anawauza kwa kuwachuuza mtaani.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Katika watoto wote saba wa baba na mama Abdul. Abdul pekee ndio alikuwa anasoma shule. Wengine wote hawakutaka hata kusikia neno shule. Hawakuona umuhimu wa shule. Waliona kaka yao akivyoteseka kwa ajili ya kusoma. Kupata sare, madaftari na michango midogomidogo ilikuwa shida. Nduguze Abdul wote walikuwa wanashinda pwani wakijitafutia ridhiki. Hata hivyo hawakuwa wanapata ridhiki ya kutosha. Pamoja na shida zote hizo, Abdul alijitahidi sana katika masomo ili afanikiwe, na kuisaidia familia yake iliyotopea katika dimbwi la umaskini. Ukweli ni kwamba alikuwa anafanya vizuri sana darasani. Siku zote alikuwa anaamini elimu ndio mkombozi wake. Elimu ndio silaha pekee ya kuishika kwa maskini kama yeye. Na aliishika kweli elimu. Mungu hamtupi mja wake, alifanikiwa kumaliza kidato cha nne pale shule ya Sekondari Bagamoyo, na kufaulu vizuri sana. Abdul alichaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano katika shule ya Sekondari Ndanda. Pamoja na kuijua thamani ya elimu, lakini alipofaulu kwenda Ndanda, Abdul pia aliitambua thamani ya pesa. Alijua kwamba kumbe pesa na elimu vilikuwa vinaenda sambamba. Abdul hakuwa na pesa kabisa ya kuweza kumpeleka shule. Kwanza nauli kutoka Bagamoyo hadi Mtwara, mkoa iliyopo shule hiyo Ilikuwa mtihani. Hapo hujajumlisha pesa ya ada pamoja na vitu vingine vya shule. Ndoto yake ya kusoma Abdul ilikomea hapo. Alihisi hawezi tena kuendelea na kusoma. Hata wazazi wake walimwambia hivyo. Baba yake alikuwa na jukumu zito la kuhakikisha familia inakula, familia inatibiwa, familia inavaa pia . Hakuwa na kipato cha kutosha kumuwezesha Abdul kwenda Mtwara kusoma. Abdul alikuwa na akiba ya shilingi elfu kumi iliyotokana na biashara zake za kuuza karanga jioni. Kumbuka Abdul ndiye alikuwa mkubwa katika familia hii. Alikuwa na ndugu sita nyuma yake, wote wakimwangalia yeye. Aliamua kuzifuta kabisa fikra za kukata tamaa. Aliamini kukata tamaa ni dhambi kubwa sana katika maisha. Aliyakumbuka vizuri maneno ya Mwalimu wake wa Kiswahili wakati anasoma pale Bagamoyo sekondari.
"Usipende kukata tamaa ukiwa bado unaishi. Pambana hadi pumzi yako ya mwisho. Hakuna linaloshindakana chini ya jua". Maneno hayo ya mwalimu wake yalijirudia katika kichwa chake. Aliapa lazima asome kwa njia yoyote ile. Alikuwa anajiona mwenye wajibu wa baadae kuwasaidia wazazi wake. Kusaidia ndugu zake pia.
"Lazima nisome" Alihisi maneno hayo anayesema polepole maneno hayo. Haikuwa hivyo, yalisikiwa na mtu aliyekuwa mbele yake katika foleni ile ndefu ya usajili.
"Unaonekana una mawazo sana kaka" Sauti nyororo ya dada aliyekuwa mbele ya Abdul ilipenya kwenye masikio yake.
"Hapana, sina mawazo dada"
"Mbona unaongea peke yako sasa ?" Abdul hakujibu.
"Naitwa Mayasa"
"Naitwa Abdul"
"Tunaweza kuonana baadae sehemu tofauti na hapa?"
"Bila shaka"
Walibadilishana namba zao za simu palepale kwenye foleni. Zoezi la usajili lilichukuwa saa zipatazo tano. Hatimaye Abdul akasajiriwa kama mwanafunzi wa chuo cha uhasibu.
Baada ya kusajiriwa, Abdul alienda katika hosteli za chuo kupumzika. Alijilaza kitandani huku akikumbuka misukosuko ya safari yake ya kusaka elimu. Alikumbuka alivyoteseka kipindi kile anatafuta hela ya ada pamoja na ya matumizi ili aende kusoma shule ya Sekondari Ndanda. Alienda kuomba serikalini lakini hawakumuelewa. Alienda kuomba kwa Mbunge wake naye hakumuelewa . Hakupata hela ya ada, hakupata hela ya nauli. Bado alikuwa na elfu kumi ndani, chini ya mto wake wa kulalia.
Ilikuwa bado wiki moja ili shule ifunguliwe. Na Abdul akaanze kidato cha tano. Sasa ndoto yake ilikuwa inaanza kuyeyuka. Hakuwa na njia ya mkato ya kumpeleka shule.
" Si ruhusa kukata tamaa katika maisha ukiwa bado unaishi.." Kauli ya mwalimu wake ilijirudia tena katika kichwa chake.
"Sasa kwanini mimi naruhusu kukata tamaa nikiwa bado ninaishi. Tena na afya tele. Haiwezekani!
"Lazima niende Mtwara nikasome"
Usiku wa siku ile alipata wazo. Wazo ambalo lilipewa baraka na kichwa chake. Aliamua kwenda Mtwara kwa miguu. Alikuwa ameamua hivyo.
Usiku ule ule aliweka vitu vyake vyote sawa. Tayari kwa safari. Asubuhi aliwaambia wazazi wake.
"Baba na Mama mimi leo naenda shule "
"Umepata ada mwanangu ?" Mama yake alimuuliza kwa sauti yake ya upole.
" Hapana"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Sasa utaenda vipi shule ?" Baba yake alimuuliiza nae.
" Kwa miguu"
"Miguu ?"
"Ndio wazazi wangu. Lazima niende Mtwara kusoma. Na nimeamua kwenda Mtwara kwa miguu !" Alisema akiwa anajiamini sana.
"Hivi Abdul unaujua umbali wa Mtwara kutoka hapa ?"
"Siujui, lakini nitafika "
"Ni mbali sana Mtwara, huwezi kwenda kwa miguu Abdul " Mama yake alimwambia kwa sauti yake ya upole.
"Nimeshafunga kila kitu changu. Ilibaki kuwaaga nyinyi na ndugu zangu. Nakubali Mtwara ni mbali. Lakini bila elimu safari yetu ya kuelekea kwenye mafanikio inazidi kuwa mbali. Bora niumie kwa kutembea kwa miguu kuisaka elimu. Kuliko kuumia kwa umaskini huu uliotukuka. Umaskini umeweka kambi nyumbani kwetu. Hautaki kutuacha hata kidogo. Na kitu pekee kinachoweza kuufukuza umaskini huu kipo Mtwara. Lazima niende Mtwara "
"Tufanye utaenda Mtwara kwa miguu. Je hela ya ada utaitoa wapi ?" Baba alimtupia swali zito. Alifikiria kidogo akajibu.
"Nitajua huko huko Mtwara. Lakini lazima nifike Mtwara kwanza. Mambo mengine yatajijibu huko huko."
Wazazi wake hawakuwa na jinsi. Walimruhusu aende Mtwara . Mama yake alikuwa analia machozi kwa kumuonea huruma Abdul. Baba yake alikuwa anamhurumia pia. Abdul alikuwa jasiri na imara katika msimamo wake. Alidhamiria kwenda kusoma Mtwara kwa njia yoyote ile . Baba aliwaita ndugu zake wote. Akawaambia juu ya safari ya Abdul ya kwenda shuleni Mtwara, tena kwa miguu. Ndugu zake wote walisikitika sana. Kila mmoja aliingia ndani na kutoa akiba aliyojiwekea na kumpa. Abdul alianza safari yake ya kutoka Bagamoyo kwenda Mtwara akiwa na elfu ishirini tu. Familia nzima aliiacha kwenye majonzi makuu. Hakujari. Hakusikitika. Alidhamiria kwenda kusoma. Alidhamiria kweli kwenda Mtwara kwa miguu.
Abdul alikuwa jasiri na imara katika msimamo wake. Alidhamiria kwenda kusoma Mtwara kwa njia yoyote ile . Baba aliwaita ndugu zake wote. Akawaambia juu ya safari ya Abdul ya kwenda shuleni Mtwara, tena kwa miguu. Ndugu zake wote walisikitika sana. Kila mmoja aliingia ndani na kutoa akiba aliyojiwekea na kumpa. Abdul alianza safari yake ya kutoka Bagamoyo kwenda Mtwara akiwa na elfu ishirini tu. Familia nzima aliiacha kwenye majonzi makuu. Hakujari. Hakusikitika. Alidhamiria kwenda kusoma. Alidhamiria kweli kwenda Mtwara kwa miguu.
***
Abdul alikuwa katikati ya mawazo, simu yake iliita. Aliangalia kwenye kioo cha simu yake, alikuwa Mayasa.
Aliipokea na kuanza kumsikiliza.
"Hallo"
"Mambo Abdul ?"
"Safi Mayasa, nambie"
"Nipo tu, nilikuwa na ombi moja Abdul"
"Nakusikiliza"
"Naomba nikualike chakula cha usiku leo"
"Haina shida, wapi ?"
"Tukutane Tengeru hoteli saa mbili usiku"
"Sawa Mayasa "
"Sawa baadae"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Simu ikakatwa.
Abdul alipoambiwa habari ya chakula cha usiku. Alikumbuka kitu. Alimkumbuka Raiya. Mwanamke aliyesoma nae shule ya Msingi kule Bagamoyo na kuja kukutana nae kama bahati jijini Dar es salaam. Alikutana nae kama bahati siku ile anatembea kutoka Bagamoyo kuelekea Mtwara kwa miguu. Siku ile alitembea kweli kwa miguu kutoka Bagamoyo hadi Dar es salaam. Alipofika Mwenge ndipo alipokutana na Raiya akiwa anauza duka la simu pale Mwenge. Ni Raiya ndiye aliyemuona na kumwita Abdul.
"Mambo Abdul ?"
"Safi Raiya, za siku ?"
"Nzuri, vipi mbona na begi mkononi, unaenda wapi ?"
"Mtwara"
"Mtwara utapata gari sahivi. Saa saba hii Abdul ?"
"Naenda kwa miguu"
"Miguu ?"
"Ndiyo Raiya"
Abdul alimsimulia kila kitu Raiya kuhusu maisha yake. Alivyofika mwisho aliukuta uso wa Raiya hautamaniki. Umelowa kwa machozi. Alimuonea huruma, na kuahidi kumsaidia.
"Ngoja nikupe hela hii ukapumzike Hotelini. Halafu kesho nitakusafirisha Mtwara. Na pesa ya ada nitakupa"
"Ahsante sana Raiya yaani sijui nikushukuru vipi dada yangu."
"Jioni nikifunga hapa nitakupigia simu tukapate chakula cha usiku sehemu"
"Sina simu Raiya" Raiya alitoa simu moja iliyokuwa kwenye droo pale dukani na kumkabidhi. Kwa siku ile alimuona Raiya Mungu mtu.
Alienda kutafuta chumba cha kupumzika Kebby hoteli lilikuwa jibu lake. Akaingia ndani na kukaa kitandani. Aliitoa ile simu aliyopewa na Raiya na kuichaji Kebby hotel ilikuwa hoteli nzuri ya kisasa yenye gharama nafuu iliyokuwa Kijitonyama. Ilikuwa na kila kitu ndani. Kwa Abdul Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kulala kwenye hoteli kubwa kama ile. Siku ile ilikuwa ni moja ya siku aliyokuwa na furaha sana. Ndoto yake ya kusoma ilikuwa inaenda kutimia. Tena inatimizwa na mtu ambaye hakutegemea kabisa. Kweli usimdharau mtu yeyote duniani. Ingawa yeye na Raiya hawakuwa marafiki kipindi wanasoma, lakini walikuwa wanaheshimiana sana. Heshima ile bila shaka ilimpa moyo Raiya wa kumsaidia leo hii.
Saa moja kamili walikutana na Raiya pale Kebby hoteli. Kulikuwa na mgahawa mzuri wa kisasa mbele ya hoteli ile. Walikaa na kupata chakula cha usiku. Wakati wanakula waliongea mambo mengi sana na Raiya. Raiya alimsimulia mambo mengi sana Abdul kuhusu maisha yake. Kumbe kwa sasa Raiya alikuwa mke wa mtu. Alimsimulia mateso aliyokuwa anayapata toka kwa mumewe. Mumewe hakuwa anampa vizuri haki yake ya ndoa .
" Sasa Abdul mimi nitakupa hela" "Nitashukuru sana yaani dada yangu"
"Lakini kwa sharti moja tu"
"Nipo tayari kufuata sharti lolote Raiya"
"Kweli ?"
"Kweli nakwambia"
"Nitakupa shilingi laki tano leo. Na nitakuwa nakutumia matumizi kila utakapohitaji. Lakini naomba twende chumbani ukaniridhishe Abdul. Ukaupe nafuu moyo wangu. Ukanipe vile nilivyovikosa tangu niolewe na mume wangu na tutakuwa tunafanya hivyo kila nitakapokuwa nahitaji" Abdul alipigwa na butwaa.
Kwanza hakutegemea kupata msaada mkubwa kama ule kutoka kwa Raiya. Ulikuwa msaada mkubwa uliokuja wakati akiouhitaji sana. Kwa Abdul, laki tano Ilikuwa ni zaidi ya msaada. Tatizo lilikuja katika sharti lake. Raiya alikuwa anataka kufanya mapenzi na Abdul. Lilikuwa sharti gumu sana kwa Abdul. Pesa alikuwa anazitaka sana lakini kufanya mapenzi Na Raiya tena mke wa mtu alikuwa hataki kabisa.
"Umenielewa Abdul ? " Nimekuelewa Raiya, lakini wewe mke wa mtu"
"Kwahiyo ? "
"Utakuwa humtendei haki mumeo"
"Hizi laki tano ninazotaka kukupa wewe nimemuibia yeye. Je kumuibia hela zake ni kumtendea haki?" Raiya aliongea huku akimuonesha burungutu kubwa la pesa.
"Kama hutaki pesa nenda kwa miguu Mtwara" Abdul alikuwa katika wakati mgumu sana wa kufanya maamuzi katika maisha yake. Alijikuta anakubali kufanya mapenzi na Raiya, siyo kwa kumpenda ila kwa kupenda kusoma. Aliamua kuutumia mwili wake kwa manufaa ya maisha yake ya baadae. Walivunja amri ya sita ndani ya Kebby hoteli.
***
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Abdul alistuka na kuangalia saa yake ya mkononi. Akakumbuka alikuwa na ahadi na Mayasa saa mbili usiku Tengeru. Na sasa Ilikuwa saa moja kamili. Alijiandaa kwa ajili ya kwenda kutekeleza ahadi hiyo. Alioga. Akavaa suruali yake nzuri ya jeans pamoja na T-shirt nyeupe iliyoandikwa maneno kwa rangi nyeupe
'Napenda Riwaya'.
Chini alivaa raba nyeupe, zenye nembo ya Ocafona. Alijupulizia pafyumu. alikuwa ananukia vizuri sana. Akaenda Tengeru hoteli. Alifika hotelini saa mbili na dakika mbili usiku. Alimkuta Mayasa ameshawasiri. Mayasa alimlaki kwa furaha kubwa sana. Walikaa na Mayasa na kuongea mambo mbalimbali hadi saa nne usiku. Ndipo Mayasa alipotaka kujua sababu ya Abdul kuwa na mawazo na kuongea peke yake.
"Abdul"
"Naam"
"Kwanini unaonekana mtu mwenye mawazo sana ?"
"Niko sawa Mayasa"
"Hauko sawa Abdul, unafikia hatua ya kuongea peke yako Abdul, Nini tatizo?"
"Kweli nina matatizo Mayasa, ila tutafute sehemu iliyotulia zaidi ya hapa nitakueleza. Wewe ushakuwa rafiki yangu sasa sina budi kukwambia kila kitu kinachonisibu "
"Nitafurahi sana, sehemu gani unadhani itakuwa nzuri kwako? "
"Popote patakapokuwa pametulia zaidi ya hapa"
"Sawa kesho jioni nitakupigia. Tutaenda Moshi. Kule kuna bustani moja nzuri sana kwa maongezi"
"Sawa Mayasa"
Baada ya maongezi yaliyodumu kama dakika arobaini na tano Mayasa na Abdul walirejea Arusha kwa kukodi teksi pale Tengeru. Mayasa alimuacha Abdul hosteli za chuo, na yeye kuelekea nyumbani kwao.
Kesho yake jioni, Abdul na Mayasa walienda Moshi. Walienda sehemu nzuri zaidi. Palikuwa sehemu tulivu. Penye maua mazuri na majani machache yaliyopandwa kwa ustadi mkubwa. Kulikuwa na meza zilizokaa mbali mbali. Walichagua meza moja.
Walikaa na Mayasa. Abdul alianza kumsimulia historia ya maisha yake. Alimsimulia Mayasa historia yake kuanzia Bagamoyo. Magumu yote aliyopitia katika kusoma. Alimsimulia jinsi alivyokutana na Raiya. Na mkataba wa ngono alioingia na Raiya. Sasa alikuwa mtumwa wa ngono wa Raiya. kumpa penzi Raiya kila atakapojisikia, naye kumhudumia katika matatizo yake yote.
"Ukweli sikuwa nampenda Raiya. Sikuwa napenda mkataba ule wa ngono. Niliuchukia sana. Lakini sikuwa na jinsi Mayasa. Nilikuwa napenda kusoma. Ilibidi nifanye akivyotaka Raiya. Naamini Raiya nae hakuwa ananipenda. Alinipenda mimi kwa ajili ya ngono. Nilimaliza kidato cha sita kwa kusomeshwa na Raiya chini ya mkataba ule wa ngono. Matokeo ya kidato cha sita yalipotoka nilifaulu. Nilichaguliwa kusomea udaktari. Katika Chuo cha uhasibu hapa Arusha. Ambapo ndipo jana nilikutana na wewe."
"Daah pole sana Abdul. Hakika umepitia makuu. Umekuwa mtumwa wa mapenzi. Sasa una mpango gani Abdul ?"
"Natamani kujitoa katika utumwa huo. Lakini sina jinsi Mayasa. Elimu yangu inamtegemea Raiya. Maisha yangu yanamtegemea Raiya. Nitakapomaliza Chuo na kupata kazi hapo ndipo nitakuwa nimejivua utumwa. Utumwa wa mapenzi kama ulivyouita ".
" Nataka nikusaidie Abdul bila sharti lolote. Dhamira yangu ya ndani nimeamua kukusaidia. Nimependa harakati zako za kuitafuta elimu. Unaonesha unapenda kusoma, na una akili sana."
Nataka nikusaidie Abdul bila sharti lolote. Dhamira ya ndani ya moyo wangu nimeamua kukusaidia. Nimependa harakati zako za kuitafuta elimu. Unaonesha unapenda kusoma, na una akili sana."
"Nashukuru sana Mayasa. Wewe ni mwanamke mwenye moyo wa ajabu sana."
Walimaliza kuongea na Mayasa saa nne usiku. Walikodi gari iliyowarejesha Arusha mjini. Sasa Abdul alihamia himaya mpya. Himaya ya Mayasa, alimkabidhi kila kitu Mayasa kuhusu maisha yake, kasoro moyo tu. Alipunguza mawasiliano na Raiya na kuongeza mawasiliano na Mayasa.
***CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ilikuwa siku ya jumatano jioni ya wiki ya pili tangu waanze chuo. Abdul alikuwa na Mayasa wanajisomea darasani muda wa jioni.
Simu ya Abdul iliita.
Alikuwa Raiya anapiga.
" Wewe unajifanya kiburi sikuhizi eeh. Mimi nimekusomesha umefika Chuo unajifanya mjanja. Sasa kesho nakuja huko huko Arusha nione kinachokuzuzua. Ole wako nisikie una mwanamke" Bila salamu Raiya aliwaka kwenye simu. Abdul hakumjibu. Alikata simu na kuizima kabisa. Hamu ya kusoma ilimuisha. Mayasa alisikia kila kitu alichosema Raiya. Raiya alikuwa alimkaripia kama mtoto Abdul na kwa nguvu. Alimuonea sana huruma. Hamu ya kusoma ilimuisha. Alimuaga Mayasa na kurudi hosteli. Alifika kitandani na kulala chali. Alifikiria mustahabari wa maisha yake. Alijiona ni mtu mwenye mikosi. Aliulaumu umaskini wake. Aliulaumu umaskini wa wazazi wake. Machozi yalitoka yenyewe taratibu. Akauhisi mkono laini ukimfuta machozi. Alifumbua macho yake na kuangalia. Alikuwa Mayasa.
"Acha kulia Abdul. Nimejitoa kukusaidia kwa lolote kaka yangu. Naamini tutaushinda mtihani huu.Tutamshinda Raiya. Sitokubali ulie tena." Mayasa alimbembeleza sana Abdul. Mwishowe akamwelewa. Akanyamaza.
Ilipita wiki moja tangu Raiya ampe vitisho vyake Abdul. Hakutokea Arusha wala hakumpigia simu. Akajua labda amekata tamaa. Akawa anaishi maisha yake kama kawaida. Furaha ikarejea tena. Huku akimtegemea Mayasa kwa kila kitu. Naye hakuchoka. Alimsaidia Abdul.
Upande wa darasani alikuwa anafanya vizuri sana katika masomo. Alikuwa na uwelewa mkubwa sana. Mayasa hakuwa mzuri sana darasani. Alijitahidi kumsaidia kila alipopata nafasi. Alielewana sana na Mayasa. Walifatana muda wote. Walijisomea pamoja. Walikuwa mithili ya chanda na pete. Kila mwishoni mwa wiki walikuwa wanatoka nje ya jiji la Arusha kutembea na Mayasa.
Siku moja jumamosi Abdul na Mayasa iliwakuta Same. Sasa walikuwa marafiki walioshibana. Abdul alikuwa anafahamu sasa baadhi ya vitu vya Mayasa. Kumbe baba yake Mayasa alikuwa, Ally Hamisi. Makamu wa raisi wa Zanzibar. Baba yake alikuwa mtu mkubwa sana Serikalini lakini hakuna hata siku moja aliyemtamkia mdomoni Abdul. Alisikia tu kutoka kwa watu wa pembeni. Siku waliyoenda Same, walirudi chuoni saa kumi na mbili jioni kutoka. Same Ilikuwa mbali kidogo na Jiji la Arusha. Mayasa alimrudisha kwanza Abdul hosteli ili na yeye arudi kwao. Walienda Same na gari Mayasa. Walipofika karibu na chumba cha Abdul, nje walikutana na Justus. Kijana aliyekuwa wanakaa chumba kimoja pale hosteli.
"Daah afadhali umerudi Abdul, kuna mgeni wako ndani"
"Nani ?"
"Simfahamu, ila amefika zamani sana"
"Sawa kaka"
Waliingia ndani na Mayasa. Wakiwa hawana wasiwasi hata kidogo. Walipofungua mlango na kuingia ndani walimwona msichana amelala kitandani kwa Abdul. Wote walistuka sana! Walipomwangalia kwa makini, Abdul alimgundua msichana yule.
Alikuwa Raiya .
"Naitwa Raiya Mohamedi" Aliongea huku akimwangalia Mayasa usoni.
"Naitwa Mayasa Ally" Mayasa nae alijibu kwa kujiamini.
"Wewe ndiye unajifanya unajua kutembea na wanaume wa watu ?"
"Sema kilichokuleta "
"Kilichonileta ndio hiki ninachoongea "
"Usione vyaelea dada......"
"Sina muda wa kuongea na wewe"
"Abdul ?" Raiya aliita.
Hakuitika.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Umenisaliti kwa sababu ya hiki kikaragosi ?" Abdul alikaa kimya anamwangalia tu.
"Kumbuka nilipokutoa Abdul, Kumbuka Siku ile pale Mwenge, ningekuacha ungekutana na hiki kikaragosi leo? " Raiya aliongea maneno yaliyomuingia kidogo Abdul.
Pamoja na madhaifu yake kadhaa lakini Raiya alikuwa na mchango mkubwa sana katika maisha ya Abdul hadi alipofikia sasa.
"Sasa chagua moja Abdul. Utakuwa na mimi au huyu?" Raiya aliongea kwa jazba.
Abdul alibaki njia panda.
Raiya na Mayasa wote walikuwa na mchango mkubwa katika maisha yake. Na wote walimwangalia yeye kusubiri jibu langu.
"Mayasa siyo mpenzi wangu" Alijua ametamka kwa sauti kumbe sauti haikutoka nje. Mdomo ulikuwa unatetemeka tu.
"Chagua Abdul"
"Achague nini, mimi Abdul siyo mpenzi wangu"
"Ni nani yako sasa ?"
"Rafiki yangu tu"
"Hahaha siku zote mapenzi yanaanzia kwenye urafiki, Ok marafiki. Basi mimi ni mke wa Abdul. Nasema naomba muvuunje kabisa huo urafiki wenu. Siutaki, siutaki, siutaki hata kuusikia. Mkewe nimesema!"
"Raiya wewe ni mke wa Abdul ?"
"Hilo jibu uliza swali "
"Una hakika Raiya ?"
"Ndio"
"Na Salehe je, unamwitaje Raiya ?" Swali hilo allouliza Mayasa lili mstua sana Raiya. Hali sasa ilibadilika mle ndani.
"Mimi ni Mayasa Ally Hamisi, unanikumbuka ?" Mumeo Salehe ni kaka yangu. Mtoto wa mama mdogo Fatma. Au nimpigie Salehe nimuulize kama kakuacha ?" Mayasa aliongea huku akitafuta namba za Salehe katika simu yake. Raiya sasa alikuwa amechoka hoi. Hajui lipi aseme, lipi aache. Alikosa kauli kabisa.
Ghafla alitoka nje ya hostel kwa ghadhabu mithili ya roketi, bila ya kuaga. Abdul aligundua kitu kimoja kuhusu Mayasa. Mayasa alikuwa msichana msiri sana. Alimficha cheo cha baba yake hadi sasa. Pia kumbe alikuwa anamficha kama Raiya ni wifi yake, hakumwambia kabla. Alianza kumwangalia Mayasa kwa jicho la kumuogopa sasa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" Usijari Abdul. Raiya ni wifi yangu lakini yeye hakuwa ananijua. Tulionana na Raiya siku moja tu. Tena siku ya harusi yake na kaka Salehe. Hata wewe ulivyonisimulia historia ya maisha yako. Ulipotaja jina la Raiya sikujua kama Raiya wifi yangu, sikufikiria kabisa. Leo nilivyomwona hapa ndio nimemkumbuka ". Mayasa alinijibu kitu ambacho nilikuwa nakifikiria.
"Sawa Mayasa nimekuelewa"
Walitoka nje ili kumwangalia Raiya ameenda wapi? Hawakumuona.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment