Simulizi : Kosa
Sehemu Ya Tano (5)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilihisi kuangukiwa na mwili wa mwanamke baada ya kusikia mlio wa gunia likitobolewa , mawazo yangu yaliniambia nimeegemewa au nataka kukumbatiwa na Huwaida baada ya Huwaida kujaribu kuniua. Nilimpokea Huwaida nikamuweka kifuani mwangu kisha nikafungua macho kumtazama Nurulayt ambaye alikuwa nyuma ya Huwaida kwa muda huo, nilipomuona Nurulayt ameshika kile kisu kirefu ambacho mwanzo kilikuwa kisafi lakini sasa hivi kina damu nilishtuka sana na nikamtoa Huwaida kifuani kwangu halafu nikamtazama, nilipoona jeraha kubwa likiwa katika mwili wa Huwaida nilijihisi nipo ndotoni hivyo nikafikicha macho ili nione jambo lile sio la kweli lakini nilipoweka mikono usoni nikawa nahisi nimegusa kimiminika kibichi ambacho sikua nakitambua kutokana na kutojiona usoni mwangu. Nilipoitoa mikono usoni mwangu niliiangalia na hapo ndipo nikabaini kimiminika kilichonirukia usoni ilikuwa ni damu ya Huwaida, nilipomtazama Huwaida bado alikuwa mzima na anapumua kwa tabu, macho yake yalikuwa yakinitazama kwa masikitiko hadi machozi yakaanza kunitoka kwa kushindwa kuvumilia kumuona mwanamke ninayempenda akiwa akiwa katika hali hiyo. Kilio cha kimya kimya ndicho kilifuata huku machozi yakizidi kunitoka nikimuangalia Huwaida anayeonekana kuvuta hewa kwa shida kutokana na jeraha alilonalo kuwa kubwa sana, Huwaida alinyanyua mkono wake wa kulia akashika ukosi wa nguo yangu ya juu niliyovaa kisha akauvuta taratibu huku akinitazama kwa macho yanayolengwa na machozi kutokana na maumivu anayoyasikia muda huo.
"Abdul aaaargh! Abdul nini umefanya? Kama kunipenda mwanamke wa mwenzako hukutakiwa kwani sikuumbwa mzuri peke yangu ndani ya dunia hii ungepata mwanamke mwingine atakayekuwa mzuri zaidi yangu" Huwaida aliongea huku akinitazama usoni kwa sura yenye masikitiko makubwa ambayo ilinizidisha kulia kama mtoto mdogo vile.
"nisamehe Huwaida sikuwa na namna nyingine ya kufanya na sikuwa naona mwanamke zaidi yako ndani ya dunia hii, urembo wako uliniweka upofu na kukuona wewe ni zaidi wengine wote, hivyo sikuwa na jinsi zaidi ya kuamua kumteka rafiki yangu" Nilimuambia Huwaida huku machozi yakinitiririka machoni kama chemchem ya maji, kila nilipozidi kumtazama Huwaida ndivyo nilivyozidi kulia hasa alipoanza kutoa kikohozi hafifu huku akionesha kuwa anaumia sana.
"umesababisha mpenzi wangu kauawa na umesababisha na mimi nichomwe kisu na binamu yangu, sina chuki na wewe nimekusamehe kwa moyo mkunjufu lakini napenda utambue kuwa mapenzi ni sawa na mkondo wa maji hayazuiliki kwa namna yoyote kama ulivyotaka kuyazuia mapenzi yangu na Faiz. Hata kama ulimuua kimya kimya ukitarajia itakuwa ni siri jua siri ni ya mtu mmoja ikiwa ya wawili basi hiyo ni ya jamii nzima ndiyo maana mlipomfanyia Faiz hivyo nimegundua na nisingeweza kuwa nawe hata kama umefanya hivyo kwa mapenzi makubwa juu yangu." Huwaida aliongea huku akinitazama usoni machozi yakiwa yanamtoka, alisitisha kuongea kwa muda kisha akahema kwa nguvu halafu akaendelea "najua sitopona na nitamfuata Faiz wangu alipo nikiwa sina kinyongo na wewe mwanaume uliyenipenda, kiufupi nimekusameh..". Huwaida alishindwa kumalizia kauli hiyo baada ya ladha inayoonjwa na kila mtu kuwa imemfikua yeye mwenyewe, ni umauti ndiyo uliomgubika na roho yake ikawa imeachana na mwili kwa muda huo. Nilipoona katulia sikutaka kuamini ka tayari Huwaida ni marehemu na nilimtikisa huku nikiita jina lake kwa sauti kubwa iliyojaa huzuni lakini jambo hilo halikuweza kubadilika iwe Huwaida yupo hai. Kilio kilinizidi nikawa nalia huku nimeukumbatia mwili wa Huwaida, Nurulayt alipoona imekuwa hivyo alikuja kuninyanyua huku naye akiwa na machozi machoni mwake ambaye kwangu sikuyaona kama ni ya uchungu kwani yeye ndiye aliyemuua Huwaida.
"Nuru kwanini? Kwanini umefanya hivi wakati unajua kama nampenda kuliko hata nafsi yangu na ndiyo maana nilimuacha aniadhibu hata kuniua kama hanipendi ili nisiishi katika dunia hii nikiwa na maumivu" Nilimwambia Nurulayt kwa hasira baada ya kuuachia mwili wa Huwaida pale chini.
"Abdul sikuwa na jinsi zaidi ya kufanya hivi ingawa hata mimi inaniumiza kumuua binamu yangu, yote haya nilikuwa nahofia kuja kulea mtoto asiye na baba. Mimi ni mjamzito Abdul hivyo sikupenda kuja kulea mimba peke yangu au mtoto asimuone baba yake" Nurulayt aliongea huku akilia lakini sikutaka kumuelewa na niliishia kumfukuza humo ndani nikitishia kumuua ikiwa nitaiona sura yake tena, kuhusu mimba ambayo ilikuwa ni yangu sikuijali hata mara moja.
Tangu siku hiyo sikuwahi kumuona Nurulayt tena na wala sikuwahi kumpenda mwanamke yoyote hadi hii nilipokuja kumuona Sarina mwanamke mrembo aliyemzidi Huwaida kwa kila kitu tena amekuwa msaada kwangu kwa kila kitu hadi kunipa hifadhi katika nyumba yake. Nilipomfananisha na Huwaida ndipo nilipokiri kuwa kuna wazuri zaidi yake katika dunia hii, sikuhitajika nimfanyie vile rafiki yangu kwa ajili ya mwanamke.
' sikuumbwa mzuri peke yangu ndani ya dunia hii ungepata mwanamke mwingine atakayekuwa mzuri zaidi yangu' Maneno ya Huwaida aliyoniambia miaka kadhaa iliyopita kabla hajakata roho yalinijia kichwani mwangu na kunifanya nitokwe na machozi nikiwa nimekaa sebuleni nyumbani kwa Sarina bila hata kujijua kama Sarina ananitazama.
"Abdul moenie bekommerd wees nie alles wat sal eindig (Abdul usijali yote yatakwisha) Sauti ya Sarina ndiyo ilinifanya nikumbuke kama Sarina yupo karibu yangu baada ya kunipa faraja akijua yanayonifanya nidondoshe machozi muda huo ni matatizo yaliyonikumba tangu nafika ndani ya nchi hiyo. Sarina alikuja kukaa karibu yangu huku akinibembeleza kutokana na uso wangu kuwa na huzuni kubwa sana, kuukumbuka mkasa wangu na Huwaida ndiyo jambo lililonifanya nidondoshe chozi muda huo hasa nilipoyakumbuka maneno yake ya mwisho. Kumbukumbu juu ya Nurulayt nayo ikanirudia kichwani mwangu na kuhusu ule ujauzito alioniambia nikawa nina shauku ya kujua kama alijifungua salama, sikujua ni wapi nitapata majibu ya maswali yangu kwani Nurulayt sikujua alipo hadi muda huo tangu kilipotokea kifo cha Huwaida miaka kadhaa iliyopita nikiwa chuo mwaka wa kwanza.
" Abdul verduur as 'n man wat ek is bereid om te
help as ek kan(vumilia kama mwanaume Abdul nipo tayari kukusaidia kama nitaweza) Sarina aliniambia wakati ananibembeleza kuhusu suala hili.
"dankie Sarina (asante Sarina)" Nilimshukuru kwa kuonesha nia ya kunisaidia katika kipindi hichi cha matatizo bila hata kunifahamu kiundani, siku hiyo niliamua kupitisha nikiwa nipo nyumbani kwa Sarina hadi usiku nikiwa naangalia televiaheni tu bila ya kuwa na chochote cha kufanya. Usiku wa manane ulipofika ilinibidi nilale sebuleni kutokana na nyumba hiyo kuwa na chumba kimoja cha kulala, sebule, choo na bafu pamoja na jiko, Sarina alilala chumbani kwake kama kawaida na sikuwa tayari kulala naye chumba kimoja. Asubuhi ya siku iliyofuata niliwahi kuamka nikajisafisha mwili wangu kisha nikawasha televisheni ili niangalie kama kawaida kwani sikuwa na jambo lolote la kufanya, baada ya nusu saa Sarina naye aliamka akanikuta nikiwa naangalia televisheni.
" Oggend nuus(habari ya asubuhi) Sarina alinisalimia kwa uchangamfu mkubwa akiwa kavaa vazi la kulalia lenye muundo wa suruali na shati laini, nywele zake alikuwa amezibana vizuri na kunipa wasaa mwingine wa kuijua sura yake akiwa ameweka nywele kwa mtindo huo.
" veilige Ek weet nie wat jy (salama sijui wewe)" Niliikia salamu yake na nikamjulia hali yake.
"veilige(salama)" Alinijibu kisha akaingia jikoni kuandaa kifungua kinywa akiniacha nikiangalia televisheni yake iliyounganishwa na king'amuzi cha DSTV, niliangalia chaneli mbalimbali za kimataifa na mwishowe nikaikuta chaneli ya nyumbani Tanzania ikionesha kipindi cha mambo ya biashara na sasa mtangazaji wa chaneli hii iitwayo Star tv alikuwa akimhoji mkurugenzi wa kampuni zangu juu ya maendeleo ya kampuni zangu. Mahojiano hayp yalikuwa yakifanyika katika ofisi yangu iliyopo katika makao makuu ya kampuni zangu, tena meneja huyu anayeitwa anayeitwa Khalid Zaid ambaye ni mwenyeji wa Pemba alikuwa akielezea kuhusu ufanisi wa kazi wa kampuni zangu. Nilipoyaona mahojiano hayo nilikuta nikimuita Sarina jikoni
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ambaye alikuja kwa kasi kuja kuyashuhudia, katika ofisi yangu bado picha kubwa ya kwangu ilikuwa ipo pale pale ikinionesha nikiwa nimevaa suti ya gharama na tabasamu mwanana likiwa limepamba uso wangu. Khalid alipoulizwa juu ya suala la kutoonekana mwenyekiti mtendaji wa makampuni hayo ambaye ni mimi alijibu kuwa nilikuwa nipo nie ya nchi kimasomo na hata taarifa hiyo ilikuwa inajulikana na wafanyakazi wote wa kampuni zangu na yeye nimemkabidhi ofisi mpaka nitakaporudi. Nilipoyasikia maneno ya Khalid nilibaki ninashangaa sana kwani sikuwahi kumpa taarifa hiyo hata siku moja lakini yeye ametoa taarifa isiyo ya kweli katika chombo cha habari, Sarina yeye alikuwa anaangalia tu kwani hakuwa akielewa chochote kulichokuwa kinaongelewa katika televisheni kutokana na kutojua lugha ya kiswahili. Kipindi hicho alikiangalia nusu kisha akaenda kuendelea kutayarisha kifungua kinywa, alipomaliza ndipo alipokuja kuniuliza yote kuhusiana na kipindi kile kilichokwa kikirushwa. Nilianza kumfafanulia kitu kimoja baada ya kingine na niliposhindwa msamiati wowote wa kiafrikaans niliamua kutia kingereza hadi akanielewa nilichokuwa namweleza.
" baie jammer Abdul(pole sana Abdul)" Sarina aliniambia kusikiliza maelezo yangu kwa umakini.
"dankie(asante)" Nilitikia huku nikiwa nimeshika tama nikionesha kuhuzunika kwa kila kinachoonekana.
" daar is iets ernstig gaan oor dat jy nie weet( kuna jambo zito hapo linaendelea wewe hulijui)" Sarina alikisia baada ya kujifikiria kwa muda mrefu, maelezo yake kiupande mwingine yalionekana kuniingia sana nikakubaliana ingawa upande mwingine bado nilikuwa njia panda sana. Nikiwa bado najifikiria kengele ya mlango mkubwa wa kuingia ililia kuadhiria kuna mgeni yupo mlangoni, chini ya mlango bahasha ya kaki ilionekana ikipitishwa na mtu aliyepo nie. Hata Sarina alipoenda kufungua mlango alikuta tayari huyo mtu aliyeweka bahasha alikuwa ameshaondoka, Sarina aliichukua bahasha hiyo kisha akanikabidhi bila kusema lolote baada ya kuiona picha yangu ikiwa ipo juu ya bahasha. Niliipokea bahasha hiyo kisha nikaifungua kwa pupa nikitaka kujua ni nini kilichomo ndani yake, niliikuta karatasi iliyoandikwa ujumbe mzito ambao ulitakiwa kufika kwangu. Ujumbe huo uliandikwa hivi:-
'Abdul hongera sana kwa kuwapiga vijana wangu kwa uwezo wa kupigana, sasa basi nataka umalize kazi ya mwisho ya kuokoa mali zako ili uweze kujua chanzo cha kupewa kazi hizi, najua unazo dola milioni moja taslimu katika mkoba wako huo sasa unahitajika uzipeleke katika sanduku la posta la Walvis kwa namna yoyote pia nadhani utakuwa umejua kidogo hizo pesa unazoringia zinavyotafutwa na si kupewa kama unavyopewa wewe baada ya mzazi wako kufariki.
Kazi inayofuata unatakiwa ukaibe kilo 500 ya almasi iliyopo mikononi mwa Gorilla boys wanaoishi msitu wa Chirinda Zimbabwe, vijana hao wana ngome nzito sana sasa basi wewe na mwenzako mwingine mtahusika operesheni hii.
Kila heri
F.A.Z'.
Karatasi hiyo iliishia hapo kimaelezo ikawa imeacha imeniacha njia panda zaidi kwani hiyo mwenzangu sikumjua na hata hao watu wenye almasi hiyo sikujua wanaishi wapi. Nilipomtafsiria Sarina hiyo barua iliyoandikwa kiswahili alibaki akinihurumia hadi machozi yakawa yanamlenga.
" Abdul asseblief nie gaan na die gorilla seuns is
gevaarlike mense(Abdul tafadhali usiende hao Gorilla boys ni watu hatari)" Sarina aliniambia kwa huruma baada ya kumfasiria ile barua niliyotumiwa.
" Sarina ek nodig het om te gaan, my eiendom te
verlos (Sarina nahitajika niende ili kukomboa mali zangu)" Nilimwambia Sarina huku nikimfuta machozi yaliyoanza kumtoka mashavuni mwake, Sarina alianza kutokwa na machozi papo hapo nilipomueleza hivyo.
" Abdul weet die opbrengs is baie moeilik(Abdul najua kurudi huko ni vigumu sana) Sarina aliniambia kutokan na kuhofia maisha yangu katika kazi inayonikabili.
"Sarina daar is niks om te vrees nie, die basis bid
net vir my om veilig terug( Sarina hakuna cha kuhofia cha msingi niombee tu nirudi salama)" Nilimuambia Sarina muda huu alikuwa analia sana.
" Elkeen het gevoelens oor 'n ander persoon van
die teenoorgestelde geslag seks, ek pokuona vir
die eerste keer sal sekerlik 'n hartaanval.
Nilipoongea met jou vir die eerste keer beslis
myself Ek wou met jou elke uur, Abdul lief jy hoef
nie te mislei( Kila mtu ana hisia juu ya mtu mwenzake wa
jinsia tofauti, nilipokuona kwa mara ya
kwanza hakika moyo ulipata mshtuko.
Nilipoongea na wewe kwa mara ya kwanza hakika
nafsi yangu ilitamani kuwa na wewe kila saa,
Abdul nakupenda sihitaji kukupoteza)" Sarina aliongea huku akiwa amenipa mgongo kutokana na uzito wa maneno yenyewe, kwa mara ya kwanza maishani maishani nilijikuta nikitamkiwa na msichana ninayemhusudu maneno kama hayo ambayo yalinikumbusha maneno ambayo yalinitoa machozi.
"hamna kama hicho Abdul we upo juu hata usipotupia kivile tena utakuja kupata kisu kikali zaidi ya hicho ninachoenda kukuonesha leo" Maneno ya Faiza wakati anaenda kunionesha Huwaida ndiyo yalinijia kichwani mwangu na ukweli wa kauli yake ndiyo nikawa naiona imetokea baada ya kumfanyia kitu kibaya.
Nilimsogelea Sarina kisha nikamkumbatia kwa nyuma na nikambusu shingoni, Sarina aliendelea kulia tu akinisihi nisiende huko ninapotaka kwenda.
" As ons mekaar liefhet, sal ek terugkeer (kama tunapendana nitarudi) " Nilimwambia Sarina huku nikimshika na nikamgeuza nikawa natazamana naye uso kwa uso, Sarina alishindwa kuniangalia usoni na alinikumbatia kwa hisia kali. Tukiwa tumekumbatiana vilevile mlango wa mkubwa wa kuingilia ndani ukagongwa kwa nguvu pamoja na kengele kubonyezwa kwa wakati mmoja, wote tulishtuka sana kwa ugongwaji wa mlango wa namna hiyo.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" verberg(jifiche)" Sarina alinimbia haraka nami nilitoka sebuleni hadi jikoni na nikabana pembeni ya mlango wa jikoni kwa ndani, nikiwa nimebana hapo nilimsikia Sarina akimlaumu mtu aliyegonga kwa ukosefu wa ustarabu ambao aliomuonesha katika ugongaji wake wa mlango. Yule mtu naye aliomba radhi kisha akamuambia Sarina ametumwa alete mzigo hapo akijitambulisha kama mfsnyakazi wa kampuni ya usafirishaji, yule mtu alipoaga na kuondoka nilitoka hadi sebuleni nikamkuta Sarina akimalizia kufunga mlango akiwa amesimama jirani na boksi kubwa.
"Griiiiiiiiiiiiiiiiii! Griiiiiiiiiiiiiiii!" Nilipotaka kumsemesha Sarina simu yangu iliita na ikanilazimu niipokee baada ya kuona mtu anayenipigia ni yuleyule wa siku zote.
"nadhani umeuona mzigo niliouleta hapo sasa hivi ambao umepokelewa na Sarina, sasa basi ufungue na utakachokikuta humo ndani usikidharau ukitunze maana ukikidharau utakuja kujuta mwenyewe" Sauti ya yule mtu iliniambia, nilikuwa nikimsikiliza kwa umakini huku nikiuendea ule mzigo hadi nikaufikia bila hata kumuangalia Sarina aliyekuwa ananitazama kwa umakini.
Milio ya risasi iliendelea kurindima mithili ya ngoma kwenye sherehe ya kikabila, vioo vya gari letu vilitobolewa na matundu ya risasi ambazo zilikuwa zinatokea upande wa pili wa barabara. Muda huo mimi nilikuwa nimesharuka nje ya gari baada ya kuona kuwa ni hatari ndiyo ipo mbele yetu, Nurulayt naye alikuwa amesharuka nje ya gari kisha akajilaza chini kwenye miti mita kadhaa kutoka barabarani. Hali ilikuwa ngumu kwa yule askari wa uhamiaji aliyekodiwa na Nurulayt atuvushe mpakani kwani alipojaribu kutoka kupitia mlango wa kushoto ambao alikuwepo Nurulayt kutokana na mlango wa kwake kutokuwa salama kuutumia risasi ilitua mgongoni mwake na kumfanya ageuke nyuma ili aweze kumshambulia aliyemtupia risasi, yule askari alipogeuka aliinua kichwa ili aone vizuri kwani alikuwa amelala kifudifudi kutokana na risasi iliyompata mgongoni. Nikiwa nimejibanza kwenye mti mnene uliopo mita kadhaa kutoka barabarani, nilimshuhudia yule askari akitobolewa kichwa chake na risasi baada ya kuinua kichwa ili atazame upande anaotokea adui yake. Askari yule hakutoa hata neno la mwisho baada ya risasi hiyo ya masafa marefu kutoboa kichwa kisha kuendelea na safari hadi kwenye shina mti nililosimama ikapita juu kidogo ya kichwa changu kisha ikaendeleana safari.
"Abdul lala chini haraka utakufa huoni risasi imekukosa hiyo" Nurulayt aliniambia kwa sauti huku akiweka sawa bunduki aina ya short gun aliyopewa na yule askari, nililala chini kwa haraka sana na macho nikawa nayaelekeza kwenye gari letu ambalo bado lilikuwa linanguruma hadi muda huo kutokana na kutozimwa na taa bado zilikuwa zinawaka kuanzia ya ndani hadi za nje. Mlango mbele wa gari letu upande wa kiti cha kushoto cha dereva ulikuwa wazi baada ya yule askari kuufungua akijaribu kutoka nje hivyo ikawa njia rahisi sana kwa mlengaji kumuua kwani gari hii mlango mmoja ukiwa wazi basi taa ya ndani inawaka hivyo mtu wa nje anakuona kirahisi. Tukio hili ni tukio jingine linalonifanya nimshukuru Mungu katika maisha yangu kwani nafsi yangu ilinisihi nifungue kioo cha dirisha nililokaa baada tu ya kuvuka mpakani, Nurulayt naye alifanya hivyohivyo na dereva wa gari ambaye ndiye yule askari wa uhamiaji nchini Botswana wala hakufanya hivyo yeye aliendelea kuacha kioo kimepandishwa. Ndiyo maana hata kioo kilipovunjwa ni risasi iliyolengwa na ikampata begani kisha nyingine zikafuata
Tukiwa bado tumelala chini huku bunduki zetu tukiziweka tayari kwa lolote tuliwaona watu wasiopungua kumi wakiwa na bunduki aina ya AK47 karibia wote kasoro mmoa alikuwa ana bunduki aina ya sniper rifle, walikuwa wakitokea katika pori lililopo upande wa pili wa barabara.
"huyu mwenye bunduki ya wadunguaji ndiye aliyempiga dereva wetu risasi ya mgongo na ya kichwa, hivyo tunahitajika kuwamaliza wote ili tuendelee na safari la si hivyo tutakwamia hapa" Nurulayt aliongea kwa sauti ya chini huku akiweka bunduki yake sawa.
"Hatuhitaji shambulizi la risasi wapo wengi wale tunahitajika tufanye kitu cha ziada" Nilimwambia Nurulayt huku nikiishusha bunduki yake chini kwani alionekana anataka kuitumia.
"come on Abdul kitu kipi hicho zaidi ya risasi kuwamaliza" Nurulayt aliniambia akionekana hajanielewa.
"una visu hapo?" Nilimuuliza
"ndiyo ninavyo hivi hapa" Nurulayt alijibu huku akifungua sare ya askari wa uhamiaji aliyoivaa akatoa visu vinne akanipatia.
"kuwa mtazamaji mama wa mtoto wangu" Nilimuambia huku nikichukua visu, Nurulayt aliishia kutabasamu tu kisha akanikonyeza halafu akasema, " good luck ingawa sitaweza kukuona ili niwe mtazamaji". Nilitabasamu kisha nikaviweka visu mafichoni halafu nikaanza kujiburuta kama nilivyofundishwa na jeshi la jeshi la kujenga taifa kipindi namaliza kidato cha sita kwa mafunzo miezi mitatu, nilitambaa kwa umbali mrefu kidogo bila hata kujulikana na wale watu waliopo barabarani. Nilipokaribia eneo lenye nyasi ndefu niliokota kipande cha jiwe nikakirusha mbele yangu kiasi cha mita kadhaa huku nikiwatazama wale watu waliopo barabarani. Risasi zilimiminika kuelekwa upande niliorusha jiwe bila hata kuangalia kama kuna adui wanayemlenga, walipoacha kupiga risasi nilimuona yule mwenye bunduki aina ya Sniper rifle akiwalaumu waliokuwa wanapiga risasi kisha akawaamrisha waende kuangalia kuna nini. Amri hiyo waliyopewa ilinifanya nitabasamu tu kisha nikachukua majani mengi nikavijivisha mwilini mwangu kuanzia kwenye viatu hadi kwenye kofia ya sare niliyoivaa, wale watu walikuja sita upande niliokuwepo kwa kasi bila umakini na walikuwa wanapita sehemu niliyopo mimi kwani ni sehemu yenye njia ya kuelekea upande niliorusha jiwe. Walikuwa wakitembea wawili wawili kwa haraka kuwahi eneo lenye majani mengi bila hata kuonekana kama wanafuata tahadhari yoyote, walipofika usawa wangu ndipo walipojuta kuja mbio bila uangalifu kwani wawili wa nyuma niliwazoa mtama na walipoanguka nilikuwa tayari nimesharukia nikawapiga magoti ya kwenye koo kila mmojs wakatulia kama maji mtungini. Wawili wa kati niliwarushia visu vya kwenye shingo kwa haraka walipotaka kugeuka nyuma kuangalia kilichowapata wenzao, nilipomaliza hayo nilijitupa pembeni kwenye vichaka haraka sana na hata wale wawili waliokuwa mbele walipogeuka waliona miili ya wenzao isiyo na uhai ikiwa ipo njiani.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" Oooh! Shit!" Aliongea mmoja kwa sauti huku akihangaika kuchomoa simu ya upepo iliyopo kiunoni mwake bila hata kuangalia usalama wa eneo hilo kutokana na kuchanganyika na vifo vya wenzao vilivyotokea ndani ya muda usiozidi dakika moja, hakutambua kama kufanya hivyo ni uzembe mkubwa katika eneo lisilo na usalama kama hilo. Vichwa vyao tayari vilikuwa vimevurugwa na tukio la kufa wenzao na hapo ndipo nilipopata nafasi ya kufanya shambulizi jingine la kimya kimya na la ghafla, niliachia visu viwili vilivyobakia ambavyo vilitua katika shingo zao nikilenga sehemu ya shingo ambayo ni mwanzo wa koromeo. Walidondoka kama mizigo kutokana shambulizi hilo kisha wakatulia bila hata kuonekana kufurukuta wakati roho zao zikiachana na mwili, hapo ndipo nilipojiuliza kwanini hawa watu wanakufa hivi bila hata kuonesha purukushani zozote kipindi wanaiaga dunia. Maswali yangu niliona hayana mtu wa kunipa majibu hivyo sikutaka kupoteza muda eneo hilo hata kidogo, nilichukua bunduki nne zenye mikanda nikafunga usalama wa bunduki zote kisha nikazivaa mgongoni na nilichukua vibebea visasi vilivyojaa kisha nikaanza kusogea upande wa barabarani kwa kujivuta taratibu mithili ya chatu aliyemmeza mnyama ambaye hajamshibisha kisawasawa. Nilipokaribia nililitazama eneo kwa umakini kisha nikachukua bunduki moja aina ya AK47 niliyoichukua kutoka kwa wale watu niliowaua, niliiangalia nikatoa uaalama wake nikaiweka tayari kuanza shambulizi huku nikiwatazama wale watu ambao sasa hivi wamebaki wanne tu. Sikutaka kusubiri tena nilianza kuwalenga kwa mfululizo wawili wakasalimiana na ardhi wakiwa wameshaacha roho za mikononi mwa malaika mtoa roho, waliobaki ni yule mwenye bunduki ya Sniper rifle na wengine wawili wenye AK47 kila mmoja.Walikuwa wamegusana migongo yao huku bunduki zao wakiwa wamezielekeza mithili ya pembe mshabaha, kila mmoja alikuwa akilinda usalama wa wenzake kwa nyuma yake. Walikuwa wakizunguka kula upande ili wajihami kwani bunduki ile iliyowaua wenzao hawakujua imetokea wapi, walikuwa wakizunguka kuangalia pande tofauti wakionekana wamechanganywa na vifo vya wenzao. Yule mwenye sniper rifle alipoelekea upande aliopo Nurulayt wakati mwenzake akiwa nyuma yake akimlinda nilisikia mlio uliokaribiana na mzinga na wote wawili wakatupwa umbali wa mita moja toka pale waliposimama na damu ilikuwa imeanza kutoka katika vichwa vyao. Mlio huo ulipotoka na wale walipoanguka sikuona dalili za mtu yoyote kuja barabarani ingawa sauti hiyo ilikuwa ni ya bunduki aina ya shortgun, niliamua kutamba hadi nilipomuacha Nurulayt ili kuhakikisha kama ni yeye aliyepiga kwani bunduki kama iliyowapiga wale watu anayo mikononi mwake. Nilimshukuru Mungu nilipomkuta wa mama mtoto wangu salama akiwa amelala kifudifudi akiwa ameelekeza bunduki barabarani, nilimsogelea Nurulayt karibu na nilipomfikia alishtuka akanielekezea bunduki usoni kwa haraka sana akiwa amejigeuza akalala chali kwa haraka sana.
"hey ni mimi" Nilimwambia huku nikishtuka kutokana na uso wangu kutazamana na midomo miwili ya bunduki.
"muda mwingine uwe makini unapokuja kwani hiyo mijani uliyoivaa ningekutambua vipi, utakufa wewe mwanaume" Nurulayt aliniambia
"ok nimekuelewa, ile kazi ni ya mkono wako?" Nilimuuliza kuhusu wale watu wawili waliouawa na risasi moja niliyoisikia ikitokea upande aliopo.
"ndiyo, na wale watatu ni kazi ya mkono wako?" Alikiri ndiye aliyepiga ile risasi kisha akaniuliza swali.
"ndiyo, tena nina nyongeza mama" Nilimjibu huku nikiushuaha ule mzigo wa risasi mgongoni.
"vizuri nadhani wale wengine umewazima" Nurulayt aliongea
"kabisa nimetumia vile visu hata sauti hawajatoa" Nilimpa uhakika wa kumalizika kwa kazi.
"kwa sumu iliyokuwa kwenye vile visu hata maji hawaombi kama vimetua shingoni mwao, twende zetu" Nurulayt huku akijiinua kutoka pale chini alipokuwepo kisha akaanza kutembea huku akiwa ameinama na amakunja magoti kidogo. Nilimfuata kwa mwendo huo huo aliokuwa anatembea yeye hadi kwenye gari letu, Nurulayt aliuvuta mwili wa yule askari wa uhamiaji aliyekusaidia kutuvusha hadi nje ya gari kisha akaokota silaha zote za wale watu waliotuvamia akazitia ndani ya gari. Tulilikagua gari letu.kwenye matairi tukakuta ni zima halina tatizo lolote, baada ya kuona tuna uwezo wa kuendelea na safari hatukuwa na muda wa kusubiri zaidi ya kuingia ndani ya gari na safari ikaendelea kama kawaida ili tulivuke pori hilo. Hadi tunalipita pori hilo tayari ilikuwa ni saa nane usiku na sasa tulikuwa tumeingia katika mji mdogo ambao sikuujua jina lake unaitwaje, mji ulitawaliwa na ukimya kutokana na wakazi wake kuwa wamepumzika muda huo wa usiku. Nurulayt naye alizidi kubadili gia za gari akilipita eneo hilo ambalo hakunitajia linaitwaje hadi leo hii, alizidi kuwa makini na barabara huku akiwa kimya kabisa na alionekana hakutaka kuongea kabisa. Nilimuacha aendelee kuchezea usukani na mimi nikanyoosha kiti nikajilaza taratibu na usingizi ukachukua nafasi yake, nilikuja kushtuka usingizini baada ya kusikia napigwa kibao . Nilipofumbua macho nilimuona Nutulayt akiniashiria niinuke na mimi nikainuka, nilipotazama pembeni nje niliona giza bado lipo.
"vipi mbona umesimamisha gari hapa?" Nilimuuliza huku nikiangalia njia na nikagundua tupo sehemu yenye miti mingi.
"hebu vua hayo magwanda ya askariwa uhamiaji wa Botswana ni hatari kwetu" Nurulayt aliniambia huku akivua magwanda yake pamoja na viatu, nami nilivua magwanda yangu nikavaa nguo za kawaida nilizokuwa nimezivaa hapo awali. Nurulayt naye alivaa nguo zake za mwanzo na safari ikaendelea huku nikiuchapa usingizi kama kawaida. Niliamshwa kwa mara ya pili na Nurulayt tukiwa tupo katika eneo lenye mji mdogo uliochangamka ambao sikuutambua unaitwaje, kwa makadirio ilikuwa ni saa nne asubuhi kutokana na kuangalia upande ambao jua lipo tangu lilipoanza kuchomoza.
"hapa ni wapi?"Nilimuuliza huku nikipiga miayo kutokana na uchovu niliokuwa nao.
"hebu kwanza funga mdomo huo usije ukanimeza bure, hapa ni Runde hebu shuka tukapate stafustahi" Nurulayt aliniongea huku akinifunga mdomo nilipokuwa napiga miayo, nilishuka kwenye gari na Nurulayt naye alishuka kisha tukaingia kwenye mgahawa uliopo pembezoni mwa barabara. Tulipata stafustahi tukarudi kwenye gari tukaendelea na safari kama kawaida, muda huo mimi ndiye niliyekuwa dereva wa gari na ikawa zamu yake Nurulayt kulala. Hadi inatimu saa tisa alasiri tayari nilikuwa nimeshafika katika kijiji ambacho sikukijua kinaitwaje kilichopakana na msitu mkubwa sana, nilipofika hapo nilimuamsha Nurulayt ambaye alishtuka kisha akaanza kutazama mazingira ya eneo tulilopo kisha akanitazama kwa mshangao sana.
"vipi mbona hivyo?" Nilimuliza baada ya kumuona ananishangaa sana.
"Abdul naona sasa tunataka kuuana" Nurulayt aliongea kwa kulalamika.
"kivipi?"Nilimuuliza.
"mwendo gani umeutumia hadi sasa hivi uwe umefika hapa kwenye hichi kijiji jirani na msitu huu wa Chirinda" Nurulayt aliongea akionekana ameshangazwa na mwendo nilioutumua hadi nimefika hapo.
" wa kifo" Nilimjibu
"sikupi uendeshe tena utaniua we mwanaume unafikiri hii formula one" Nurulayt aliongea.
"wewe ulivyokuwa unaendesha kule Kalahari ulikuwa huoni kama utaua mtu, tema unabahati ulilala yaani ungekuwa hujalala ungekufa kwa uoga" Nilimwambia huku nikishuka ndani ya gari, Nurulayt naye alishuka kwenye kisha akaniambia, " funga milango ya gari na unifuate". Nilifunga milango nikamfuata kuelekea katikati ya kijiji ambacho pia sikukitambua kinaitwaje hadi leo hii, Nurulayt aliniongoza hadi katika mlango wa nyumba ambayo inaonekana ni ya siku nyingi ingawa ina kila dalili za kufanyiwa marekebisho. Aligonga mlango mara moja kisha akatulia kumya, mlango wa nyumba hiyo ulifunguliwa na mwanamke aliyejitanda vitenge vya kizaire ambaye hakuongea chochote zaidi ya kutuashiria tuingie ndani tu ndiye aliyefungua mlango. Sote wawili tuliingia ndani na mwanamke huyo akafunga mlango kwa makomeo kisha akatuuliza, " za safari?".CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Salama lakini sio salama sana" Nurulayt alijibu huku akimfuata yule mwanamke ambaye alikuwa anaingia katika chumba kimojawapo katika nyumba hiyo, nami niliwafuata bila hata kuambiwa niwafuate hadi ndani ya chumba hicho. Mandhari pana ya chumba chenye mitambo mbalimbali ya tarakilishi ndiyo ilionekana ipo ndani ya chumba hicho, upande mmoja kulikuwa kuna kitanda kipana cha kulala.
"jamani karibuni tena" Alituambia tena yule mwanamke.
"tushakaribia nadhani ni muda muafaka wa kujua tusichokijua Madam Rhoda" Nurulayt alimwambia yule mwanamke kisha akanigeukia mimi akaniambia "Abdul huyu anaitwa Madam Rhoda kama ulivyosikia nikimuita, alikuwa ni msaidizi wa kaka yangu Sabir ambaye aliuliwa na Faiz kama nilivyokueleza hapo awali na ndiyo yeye aliyenipa mwongozo wa kazi hii ya kumtafuta mwanangu kwa kunipatia vifaa vya kazi vya kusnzia".
Nilitabasamu baada ya kupokea utambupisho huo wa mwanamke aliyetupokea, yule mwanamke naye alitabasamu baada ya mimi kutabasamu.
"Madam huyu ni Abdul baba yake Ilham na nipo naye kwenye kazi hii" Nurulayt alimpa utambulisho wangu yule mwanamke.
"ok, sasa tuanze kueleweshana" Yule mwanamke aliongea huku akibonyeza vitufe vya tarakilishi ya mapakato iliyopo humo ndani. Kwenye tarakilishi zilikuja picha mbalimbali za kambi ambayo ilionekana ilikuwa ipo katikati ya msitu, kambi hii ilikuwa imezungukwa na minara mbalimbali yenye vibanda kwa juu ambavyo hutumiwa na walinzi wa kambi hiyo.
"jamani hii ndiyo kambi ya kundi la Gorilla katika msitu wa chirinda, ipo kilomita mbili kusini mashariki mwa barabara ipitayo katikati ya msitu huo, kambi hii ipo ni mali ya Scorpio nadhani Nuru unamfahamu" Yule meanamke alitoa maelezo halafu akamuuliza Nurulayt.
"Scorpio?! Hapana simfahamu" Nurulayt aliongea huku akivuta kumbukumbu katika halmshauri kuu ya mwili wake kama anaweza kumkumbuka lakini halmashauri kuu ambayo ni ubongo ilionesha kutolikumbuka jina hilo, hivyo yeye pia alikataa kutolikumbuka jina hilo.
"ngoja nikuoneshe picha yake labda unaweza kumkumbuka maana sikuwahi kulijua jina lake halisi zaidi ya hilo la Scorpio" Madam Rhoda aliongea kisha akafungua faili moja lililopo kwenye tarakilishi yake lililokuwa na picha ambayo sote tuliitambua kwa jina jingine kabisa.
"Faiz!" Nilisema kwa mshangao sana.
"sasa huyu ndiye mmliki wa hilo kundi ingawa kwa sasa hayupo nchi hii na hajulikani wapi alipo, Nurulayt nadhani unamfahamu." Madam Rhoda aliongea.
"muuaji aliyeutoa uhai wa kaka yangu nitamsahsu vipi? Kumbe bado yupo hai wale waasi wa Kongo tumewalipa hela nyingi wamuue wamemuacha" Nurulayt aliongea kwa uchungu sana.
"haya jamani tuendeleeni na kilichowaleta" Madam Rhoda alisema huku akifungua picha za msitu wa Chirinda sehemu ya kambi ya Gorilla boys halafu akasema, "kambi hii ina tower zisizopungua ishirini ambazo zina masniper zote sasa ukiingia bila tahadhari umeisha. Kushoto kwake ndani kuna majengo makubwa mawili ya ghorofa yenye makao makuu ya kambi hiyo, upande wa kusini mwa makao makuu hiyo ndipo kwenye ghala lenye vito vya thamani na madini mbalimbali waliyowahi kuyateka hawa watu".
ramani hii hapa itawasaidia kupata mwongozo mzuri tena inabidi muwe na bunduki aina sniper rifle kila mmoja kama mnataka muingie bila kugunduliwa kwani wale walinzi wa juu kwenye zile tower mnatakiwa muwaue mkiwa mbali ili wasiwaone wakawatungua, kumbuka wao ni sniper na ndiyo wenye kibarua kikuu cha kuilinda hiyo kambi. Je mna sniper rifle katika silaha zenu?" Madam Rhoda alieleza mwisho akatuuliza juu ya bunduki hiyo kama tunayo.
"ndiyo tunayo moja tuliyoipata kama ngawira" Nurulayt alijibu
"mnatakiwa muwe na ya pili kwani kutungua masniper ishirini sio mchezo hivyo kila mmoja anatakiwa awe na yake" Madam Rhoda alitusisitiza, kusikia suala hilo wote tuliinama chini kutokana na kutokuwa na namna ya kuipata hiyo silaha.
"hilo msijali nitawasaidia mtimize wajibu wenu, Nuru hebu lete briefscafe mbili zipo chumba ninacholala" Madam Rhoda alimuamuru Nurulayt ambaye alitoka haraka aliposikia amri hiyo kisha akarejea akiwa mikoba miwili ya kufunga kwa namba akampatia Madam Rhoda.
Nurulayt alimkabidhi mikoba hiyo Madam Rhoda ambaye aliipokea kisha akaufungua mmojawapo akatuonesha kilichopo ndani yake, bunduki aina ya sniper rifle ya kisasa ndiyo tuliyoiona ikiwa imefunguliwa na imegawamywa vipisi.
"bunduki ni hizi hapa moja mmeiona nyingine ipo kwenye hii briefscafe ambayo haijafunguliwa" Madam Rhoda aliongea kisha akaanza kuifunga taratibu hadi ilipokamilika, alipoikamilisha bunduki hiyo alitutazama kama tupo pamoja nae nasi tulitikisa vichwa kuashiria tupo pamoja nae. Aliporidhika kuwa tumeelewa namna ya ufungaji bunduki ile aliinama chini ya meza akatoa makasha mwili madogo akayaweka mezani, alipoyafungua macho yangu yalikutana na risasi ndefu ambazo mara nyingi hutumiwa katika bunduki za masafa marefu kama sniper rifle.
"risasi hizi hapa nadhani mnaelewa jinsi ya kuziweka na kuzitumia" Madam Rhoda aliongea
"hilo lisikupe tabu tunaelewa namna ya kutumia" Nurulayt alimwambia Madam Rhoda.
"ok mkishawamaliza hawa masniper wa kambi hii, mvuke uzio kwa umakini na mtumie bunduki isiyo na sauti humo ndani au iliyowekwa kiwambo cha kuzuia sauri ili vijana wa kundi hili la Gorrila wasishtuke mapema itakuwa ni hatari kwenu ikiwa watawagundua mapema. Mkifanikiwa kuwapunguza bila kugundulika mtakuwa mmepunguza idadi kubwa ya maadui kwenu, sidhani kama itakuwa ngumu kwenu" Madam Rhoda alitueleza huku akituelekeza kupitia ramani iliyopo kwenye tarakilishi yake ya mapakato, alipofikia hapo aliifunga tarakilishi yake kisha akasema, " nawatakieni kazi njema". Sote tulitabssamu baada ya kusikia hivyo kisha tukapeana naye mikono huku tukiwa tayari tumepokea makasha yenye risasi kwa ajili ya bunduki tulizopewa, tuliyaweka yale makasha kwenye mikoba tuliyokabidhiwa kisha tukatoka humo ndani tukiwa tumeongozana na madam Rhoda hadi sebuleni.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"napenda niwaage hapahapa mimi si mtokaji nje kwani natafutwa na wabaya wangu, namba ya hizo briefscafe ni 1789. Kila la heri" Madam Rhoda aliongea huku akinipatia mkono halaf akakumbatiana na Nurulayt kwa uchangamfu hafifu kisha akatufungulia mlango, tulitoka tukampungia mkono kisha tukaanza kuondoka kwa mwendo wa haraka tukiwa makini sana. Tulipita njia ileile tuliyopita awali hadi tulipoliacha gari letu ambalo lilikuwa salama, nilifungua milango nikaweka mkoba ndani na Nurulayt naye akaweka mkoba wake halafu akaniambia, "nisubiri hapahapa narudi sasa hivi". Alishuka kwenye akaingia mitaani na alirejea baada ya dakika kumi akiwa na mfuko mweusi ambao aliujaza vitu, aliingia ndani ya gari akautupa mfuko huo kiti cha nyuma halafu akasema "tuondoke fuata barabara inayoingia msituni". Nilipopata maelekezo yake niliwasha gari nikaliingiza barabarani nikaliondoa kwa mwendo wa wastani hadi nilipokiacha kijiji kisha nikaendesha mwendo niliokuwa nauendesha wakati Nurulayr akiwa amelala, niliweka gia namba tano kisha nikakanyaga mafuta hadi Nurulayt akawa ananishangaa na aliwahi kufunga mkanda wa gari kwa tahadhari ya usalama wake.
"Abdul tunakomoana siyo" Aliniambia kwa mshangao kutokana na mwenfo kasi ninaoutumia.
"kulichokutuma ukaniachia gari ni nini wakati ulisema huniachii tena, sasa leo mpaka utapike kwa mwendo huu" Nilimwambia huku macho yangu yakiwa mbele ili nisipoteze umakini kwani tulikuwa tumeingia katika eneo la msitu wa Chirinda tayari.
"haya baba Ilham we tumia mwendo huo wakati njia huijui subiri upitilize utajijua mwenyewe" Nurulayt aliniambia hivyo ili nipunguze mwenfo lakini sikupunguza na nilizidi kukanyaga mafuta huku niliwasha taa kutokana na mazingira ya msitu kuonekana kuwa giza tulipofika katikati ya msitu huo. Baada ya mwendo mrefu niliiona njia iliyoonekana kama ni njia za miguu mbili ambayo kabisa nilijua ilitokana na upitishwaji wa gari sehemu yenye majani mengi na kupelekea majani yaliyokanyagwa yakauke kabisa yakatengeza njia mbili zenye ukubwa sana na njia ya watembea kwa miguu porini. Hapo ndipo nilipopunguza mwendo kidogo kisha nikaingia katika njia hiyo nikikata kona kali hadi Nurulayt akayumba ila mkanda aliouvaa ulimsaidia, Nurulayt alinitazama kwa mshangao ambao sikuujali kabisa zaidi ya kuzidi kukanyaga mafuta ya gari nilipoingia kwenye njia hiyo. Niliendesha gari kwa umbali wa wastani kisha nikakata kona kwa kasi nikaitumbukiza gari kwenye kichaka ambacho kilikuwa kimefungamana miti, upande niloupitia kulikuwa kumevunjwa baadhi ya miti na gari hili ingawa sikuiharibu gari. Niliizima gari pamoja na taa zote kisha nikashuka nikaenda kuchukua majani nikaziba njia niliyoingilia pamoja na kulifunika gari kwa matawi ya miti, Nurulayt hadi muda huo alikuwa akihema kutokana na kona ya ghafla niliyoikata na alikuwa bado yupo ndani ya gari. Nilipohakikisha usalama wa kutosha wa gari nilirudi ndani ya gari nikaingia sehemu ya dereva nikalaza kiti nikatulia.
"Abdul hivi hii njia mpaka tunafika huku umeijuaje wakati wewe siyo mwenyeji?" Nurulayt aliniuliza.
"ramani ya madam Rhoda ndiyo imeniongoza hadi nikafika hapa, wakati tunaelekezwa mimi nilishaikariri" Nilimjibu huku nikimtazama usoni, Nurulayt naye alikinyoosha kiti chake kama nilivyonyoosha mimi akawa amegeuza shingo akawa ananitazama.
"wewe mwanaume sikuwezi hata kidogo yaani umeniweka roho juu sana" Nurulayt aliniambia huku akiniangalia kwa macho malegevu.
"mmmh! Wewe je?" Nilimuuliza.
"Abdul kuna kitu nataka nikuambie" Nurulayr aliongea jambo jingine kabisa akiacha mada tuliyokuwa tunaongea hapo awali.
"sema nakusikiliza" Nilimwambia huku nikiwa tayari kusikiliza ingawa nilihisi kitu katika macho yake, baada ya kumuambia Nurulayt hivyo aliamua kujisogeza karibu yangu akitaka kuleta mdomo karibu na kinywa changu huku macho yake akiwa kayalegeza yanaelekea kama anataka kusinzia. Alipokaribia kugusa kinywa changu nilimzuia kwani sikutaka jambo hilo litokee kwa muda huo, Nurulayt alionekana kushangaa kwa kitendo hicho kisha akawa na sura yenye masononeko ghafla.
"sio muda wake huu Nuru" Nilimwambia Nurulayt.
"Abdul please kidogo tu" Nurulayt aliniambia huku akijaribu kuleta kinywa chake kwangu na ikanibidi nimzuie tena kwani sikutaka jambo hilo litokee kwa muda huu.
"Nuru tupo kwenye kazi sasa habari hizi weka kando kabisa" Nilimwambia Nurulayt huku nikiweka sura ambayo ilimaanisha ninachokiongea.
"basi busu refu tu Abdul nipatie" Nurulayt aliendelea kunisihi nifanye anachokitaka lakini sikutaka kumuelewa.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"natambua kinachoamsha hisia zako ni busu sasa nikikupa busu yatakuwa mengine hayo Nuru, elewa tupo kazini hapa" Nilimwambia Nurulayt naye akarudi sehemu yake akatulia, ilinibidi nifanye hivyo kwani sikuwa tayari kumsaliti Sarina hata kidogo kutokana na ahadi tulizowekeana naye. Kutembea na Nurulayt kwa muda huo kwangu niliona hatia ndiyo maana nikaamua nitafute kisingizio cha uwepo wa kazi yetu, tulipumzika hapo kwa muda mfupi kisha baadae tukaanza kuaandaa silaha na tulimaliza kabla hata giza halijaingia. Giza lilipoingia kabisa tulikula chakula ambacho kilikuwa katika mfuko mweusi aliokuja nao Nurulayt halafu tukaamua kulala ili kupumzika zaidi kwa ajili ya kazi nzito ambayo tunaenda kuikabili masaa kadhaa yajayo, baada ya masaa kadhaa niliamka na nikamuamsha na Nurulayt ili tujiandae kwa ajili ya safari yetu. Tulikuwa tupo ndani ya giza nene lililozidi kutisha kutokana na miti mingi iliyopo katika msitu huo, tulibeba silaha zetu ambazo zilikuwa ni mzigo kwetu tukaelekea upande wa kusini mashariki tukiwa tunatembea kwa umakini pia kwa mwendo wa taratibu kutokana na silaha tulizozibeba kuwa nzito. Baada ya kutembea mwendo mrefu tulianza kuona waya ukiwa umekatiza katika eneo ambalo lilikuwa linaonekana kutokana na mwanga wa mwezi kupita katika eneo hilo ambalo lilionekana kukatwa baadhi ya miti, nilimuonesha Nurulayt huo waya ambao ni mwembamba wenye rangi ya fedha ambao niliuona kutokana na mng'ao wake baada ta kupigwa na mwanga wa Mwezi.
"kuwa makini nao huo ni mtego yaani ukiusukuma au ukiukanyaga hslafu ukauachia basi jua unalipuwa vipande vipande na bomu lililounganishwa na huu waya" Nurulayt aliniambia na ikanibidi niuruke lakini nilipouruka niliweka mguu pabaya nikajikuta nimezolewa kama mzigo na nipo kichwa chini miguu juu nikining'inia huku mguu wangu mmoja ukiwa umefungwa kamba juu ya mti, nilikuwa nimenaswa na mtego ambao hutumia kamba inayowekwa kitanzi chini na matawi ya miti. Ikiwa utakanyaga kwenye kitanzi kilichotegeshwa jua kuna tawi la mti ambayo liliinamishwa kwa nguvu litaifyatua ile kamba na kitanzi kitabana mguu wako. Haya ndiyo yaliyonikuta mimi na nilipomtazama Nurulayt alionekana kushtuka na alitaka kunipa kisu ili niikate lakini nilimzuia kisha nikaishika ile kamba na nikaipanda hadi juu ingawa ilikuwa ikiniumiza mikono, nilipofika mwisho wa ile kamba nilikaa kwenye tawi la mti nikatazama mbele upande tuliokuwa tunaelekea na nikavutika nizidi kuangalia kutokana na nilichokiona huko mbele. Kambi ya Gorrila boys ndiyo ilikuwa mbele ya macho yangu ikiwa ipo kwenye eneo lililokaa kama bonde lenye umbo la duara, juu ya bonde hilo kulikuwa na minara yenye vibanda ambayo tuliiona kwenye tarakilishi ya Madam Rhoda ikiwa na taa kubwa ambayo ilikuwa ikizungushwa na mtu aliyekuwa kwenye kila mnara ili kumulika maeneo ya kando ya kambi kwa ajili ya usalama wa kambi. Nilipooona mszingura yote niliifungua ile kamba mguuni na nikashuka kwenye mti huo upesi hadi chini nilipomuacha Nurulayt akiwa ananitazama pamoja na kutazama mazingira ya eneo hilo.
"kambi ipo karibu pita kushoto na mimu nipite kulia kisha tuanze kutungua masniper wote mpaka waishe, tutakutana kwenye mlango wa ghala lao wanapotunza vito na madini" Nilimwambia Nurulayt ambaye alitii na akapita kushoto na mimi nikapita kulia nikafuata mlima ambao upo jirani na kambi hiyo, hapo nikawa nipo peke yangu na niliomba Mungu nikutane na Nurulayt kwenye mlango wa lile ghala.
Nilitembea hadi kwenye ncha ya jabali lililopo kwenye kilima ambacho upande wa pili kuna kambi ya Gorilla boys, hapo nilitua silaha zangu kisha nikaichukua bunduki aina ya sniper rifle ambayo tulipatiwa na Madam Rhoda nikaiweka visimamio vyake na na nikaikagua darubini yake nikaona inafaa kisha nikaanza kupitia vibanda mbalimbali vya vinara yenye wadunguaji ishirini. Kibanda cha kwanza niliona kitupu na nilipokagua niliona mtu kalala chini, nilipokagua kibanda cha pili niliona mdunguaji wa pili akishtuka na kuanguka, hapo ndipo nikatambua kama Nurulayt ameanza kuwatungua wale wadunguaji wa kambi hii kama anatungua maembe kwenye shamba lisilo lake kwa wizi. Nami nilianza kwa kupitia kibanda ambacho taa inazungushwa nikamtungua mdunguaji wa pale na nilifanya hivyo hadi vibanda vyote vilipokuwa vitupu kutokana na Nurulayt naye kupitisha mkono katika udunguaji, nilipoona wameisha nilianza kuwalenga walinzi waliokuwawapo peke yao hadi wakaisha. Nilipoona wameisha nilibeba silaha zangu nikaanza kuteremka bondeni kuifuata kambi hiyo kwa mwendo wa kasi na wa kimya kimya hadi jirani na uzio wa kambi, niliweka baadhi ya silaha zangu chini na nikazificha kwenye kichaka kilicho jirani na eneo nililosimsma. Nilichukua bunduki aina ya UZI mbili zenye viwambo vya kuzuia sauti, Shotgun moja ya bomba mbili na MP5 moja pamoja vibebea risasi kadhaa, Shotgun pamoja na MP5 nilizivaa mgongoni huku UZI mbili zenye viwambo vya kuzuia sauti nikizishika mikononi mwangu. Bunduki hizi nilizozichagua niliwahi kusikia sifa zake kwenye mitandao na uwezo wake na hii Shotgun ya bomba mbili usiku wa siku iliyopita nilishuhudia mwenyewe ikiua watu wawili kwa risasi moja tu, hivyo niliona zinafaa kwa kazi yangu sikuwa na shaka nazo.
Niliamua kwenda mbele ya kambi hiyo kwa kupitia vichakani hadi nilipofikia lango kuu la kuingilia ndani, kwenye geti hilo kulikuwa kuna walinzi sita ambao walikuwa wapo makini kuangalia pande zote. Walinzi hapo walikuwa wamejipanga mbalimbali hivyo ikanibidi nipige hesabu za jinsi ya kuwavaa hadi nikapata mbinu, nilimpiga risasi aliyekuwa wa mwisho upande wa kushoto akaanguka chini na kupelekea walinzi wote waelekeze bunduki zao kule wakijua nipo upande ule. Walifanya kosa kubwa sana na likawagharimu maisha yao kwani niliwamiminia risasi wote wakafa papo hapo, nilitembea hadi getini haraka haraka nikaangalia sikukuta mtu na nikaamua kuingia ndani nikitembea kwa umakini na nilijibanza kwenye kingo za mahema ambapo nilisikia minong'ono ya watu ikitokea ndani kuashiria kuna kundi la watu walikuwa wanazungumza. Nilipobaini uwepo wa watu mule ndani niliamua kuzunguka nyuma nikiona ni jambo sahihi kumbe nilikuwa nimefanya kosa kubwa, nilipofika huko nyuma ya hema hilo nilisikia mlio wa kengele ndogo ikilia kwa nguvu kisha kengele ya hatari ikafuata na kupelekea eneo nililokaa libadilike liwake taa nyekundu na nilipoangalia juu ya eneo nililosimama niliona kamera ya ulinzi ikiwa inawaka taa nyekundu huku kengele ya hatari ya kambi nzima ikisikika. Nilianza kusikia vishindo vya watu wakikimbia hata hili hema nililokuwa nipo nyuma yake nilianza kusikia watu wakitoka na ikanibidi nitoe kisu nichane hema na nikaingia ndani ili nipate usalama. Nilitokea katika eneo lenye vitanda mbalimbali vya kubebana na ina meza kubwa iliyo na mabomu kadhaa ya kurusha, hema hili lilionekana kuwa na vyumba viwili hivyo ilinibidi nikague vyote na nilipoona hamna mtu nilibeba mabomu kumi ya kurusha kisha nikanyata kufuata mlango wa kutokea nikiwa na mabomu matatu mkononi na saba mfukoni. Nilipofika karibu na mlango nilijibana pembeni nikachungulia nje ambapo nilioona kundi kubwa la watu wakiwa wamechuchumaa wakimzunguka mtu mmoja ambaye alionekana kuwapa maelekezo.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"wakasalimie babu zao kuzimu hawa" Nilijisemea kisha nikachomoa pini za mabomu matatu kwa mpigo nikayarusha kwa nguvu hadi katikati yao, kishindo kikubwa kilitokea huku yakusikika mayowe ya maumivu ambayo niliyapuuzia. Nilipohakikisha hajapona hata mmoja nilitoka nikawa nakimbia kuelekea lilipo ghala lao, namshukuru Mungu nilifanikiwa kufika salama na nikamkuta Nurulayt akiwa yupo mlangoni akiningoja na aliponiona aliingia ndani nami nikaingia halafu mlango akaufunga. "Abdul unataka kuharibu kazi?" Nurulayt aliniuliza baada ya kumaliza kufunga mlango.
"ni bahati.mbaya sikujua kama kuna kamera za ulinzi hapa" Nilimwambia huku nikihema sana kutokana na matukio niliyoyafanya nilihisi yanataka kunichanganya kichwa changu kwani suala la kuua sio jambo dogo.
"humu kuna kamera za ulinzi automatic ambazo si lazima ziwe na msimamizi kwenye chumba chake, zina taa juu yake hiyo kamera ikimuona mlinzi au mtu yoyote wa humu ndani inawaka kijani na ikimuona asiyehusika inawaka nyekundu na inatoa alarm ndogo itakayosababisha alarm kuu ya humu ndani iwake na ndiyo maana alarm imelia, twende tukamalizie kazi" Nurulayt alinipa maelezo kuhusu kamera yenye uwezo ambao sikuwahi kuusikia.
Tulitembea ndani ya ghala hadi tulipona ngazi zinaingia kuelekea chini ambazo tulizifuata na tukakuta kote kupo kimya, tuliingia chini ya ardhi kabisa hadi katika eneo lenye madini tofauti yaliyopangwa vizuri katika viberenge mbalimbali vilivyopo kwenye reli maalum zinazopita kwenye mashimo maalum yaliyochongwa vizuri. Kila madini yaliandikwa uzito wake na ikatufanya tuone viberenge viwili vyenye kuunganishwa vilivyosheheni almasi vikiwa vimeandikwa kilo 600 katika kasha la madini lililopo juu ya viberenge hivyo, tulipokiona viberenge hicho tulikisukuma hadi kwenye reli zilizopo humo na tukapnda baada ya viberenge kukolea mwendo. Viberenge hivyo vilipita sehemu yenye mteremko mkali na kupelekea mwendo uongezeke, baada ya muda mfupi tulifika mwisho wa reli hizo kukiwa na uwanja mdogo wenye helikopta kubwa, pembeni kuna mashine ndogo ya kubebea mizigo yenye gia nyingi za mkono kwa ajili ya kuiongoza. Eneo hilo nalo lilikuwa tupu kabisa na halikuwa na mtu hivyo kazi yetu ikafanyika kwa urahisi kabisa, Nurulayt aliunyanyua ule mzigo wote kwa kutumia ile mashine ya kubebea mizigo akauingiza ndani ya helikopta kisha akaingia ndani akakaa sehrmu ya rubani akaniambia, "panda twende".
" unaweza kuendesha helikopta?" Nilimuuliza.
"hebu wacha maswali yako panda bwana wanakuja hao" Nurulayt aliniambia na muda huo huo tukasnza mtikisiko ambo unatokea ikipita treni, nilipanda kwenye helikopta haraka sana nikiwa nimekaa mlangoni kwa tahadhari. Nurulayt aliwasha helikopta na aliipandisha juu baada ya kuanza kuchanganya huku akiiongoza kuelekea mashariki ili aiache kambi hiyo. Helikopta ilipokuwa juu kabisa wale watu walikuwa wameshafika pale kwenye uwanja ilipokuwa imeegeshwa, walianza kutupa risasi lakini Nurulayt aliongeza mwendo akawaacha.
Baada ya kukivuka kikwazo hicho kwa mara nyingine nilijikuta nikimshukuru Mungu kwa kunifanya niwe mzima hadi muda huo tangu nilipojiweka katika mdomo wa mamba katika kambi ile, siiutarajia kama nitaweza kutoka na kuiba katika kambi ile yenye ulinzi na wapiganaji hodari sana wanaotumia silaha. Nilipomtazama Nurulayt kule mbele nilimuona yupo makini sana kuiongoza helikopta kwa mwendo wa kasi, tulikuwa tumeshaiacha kambi kwa umbali mkubwa hata ukitumia darubini utaiona kwa mbali sana na hatukuwa na wasiwasi na wale vijana wa Gorilla zaidi ya kusonga mbele.
"GRIIIIIIIII! GRIIIIIIIIIIIII! GRIIIIIIIIII! " Mlio wa simu ulisikika katika mfuko wa suruali yangu ambao ulinishtua sana kwani nilishasahau kama nilikuwa nimebeba simu kabisa katika tangu mara ya mwisho kuitumia siku ile niliyokutana na Nurulayt tangu tupoteane miaka mitano iliyopita, mlio huo pia ulimshtua Nurulayt na kumfanya atazame nyuma kwa mshangao.
"Abdul umekuja na simu tena ipo loud, huoni kama ingekuwa ni hatari kwako" Nurulayt aliniambia huku akitazama mbele kwa umakini.
"sikujua kama nina simu kwani nilishasahau kabisa" Nilimwambia huku niitoa ile simu nikaiangalia kwenye kioo na nikakuta mpigaji ni yule yule anayenipa kazi za ajabu tangu nijikute nipo Namibia.
"ipokee basi au kama hutaki izime" Nurulayt aliniambia akionekana kukerwa sana na simu niliyonayo jinsi inavyoita kwa fujo, sikuwa na jinsi kwani nisingeipokea ingekuwa ni hasara yangu na kama ningeipokea ingekuwa ni afadhali kwani sikujua huyu mtu anayejiita F.A.Z anataka kuniambia nini. Niliipokea nikaiweka sikioni bila ya kusema chochote ili nimsikilize yeye.
"Napenda niwapongeze kwa kufanikiwa kuiba almasi niliyowatuma pia naomba nikupongeze kwa kufanikiwa kutolewa hardware zangu mgongoni mwako na huyo malaya wako mkijua sitajua upo wapi ilihali unayo simu niliyokupatia mimi mwenyewe yenye Global positioning system yaani GPS, sasa basi hujaweza kunifanya nisijue uliopo Abdul hiyo GPS ya kwenye hiyo simu imeunganidhwa huku nilipo katika kompyuta zangu sasa nitajua ulipo hata uhame bara hili. Kwanza tuachane na hayo kwenye hii simu kuna ramani inayokuelekeza sehemu ya kupeleka mzigo huo sasa mpe huyo malaya alete mzigo unapohitajika, pia kumbukeni helikopta hiyo ina mafuta pungufu sasa mkijifanya mnazunguka sana jua imekula kwenu na ninahitaji mzigo huo haraka sana" Yule mtu alinipa maelekezo kisha simu ikakatwa, sikuwa na jinsi ikabidi nimuoneshe ramani hiyo Nurulayt na nimuelekeze kila kitu Nurulayt nilichoambiwa. Nurulayt alitii maelezo na safari ya kurudi sehemu iliyooneshwa ndiyo ikaanza kwa mwendo wa kasi ili tuwahi kufika eneo hilo, baada ya saa moja nilihisi helikopta ikianza kushuka taratibu na nilipoangalia chini nikaona alama ya H ya rangi nyeupe ikiwa ipo juu ya ghorofa mojawapo katika mji nadhifu sana ambao sikuujua unaitwaje hadi muda huo.
"Nuru hapa ni wapi?" Nilijikuta nikimuuliza Nurulayt.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"ni Widhoek hapo au umepasahau kabisa" Nurulayt alinitajia sehemu hiyo ambayo ndiyo mji mkuu wa Namibia tuliouacha hapo awali, sikuweza kuutambua kutokana na muonekano wake kwa juu kwani ulikuwa ni tofauti sana. Nurulayt aliishusha helikopta hadi ikatua katika alama ile ya H iliyokuwa juu ya ghorofa mojawapo ambalo niliwaona watu wengi walioshika silaha zao wakiwa wapo hapo, Nurulayt alipozima Helikopta tulishuka na kisha tukasimama mbele ya mmoja wa watu tulipwakuta hapo ambaye alitusogelea akaanza kutupekua nguo zetu achukua silaha zetu zote.
"why( kwanini)?" Nilimuuliza yule mtu aliyetupekua
"you are going to meet our Boss, weapon are not allowed. Follow me (mnaenda kukutana na bosi wetu, silaha haziruhusiwi. Nifuateni)" Yule alituambia kisha akaelekea pembeni ya eneo hilo ambalo kulikuwa na tundu kubwa kama mlango lenye ngazi zinazoingia ndani ya ghorofa hilo, tulimfuata tukiwa tumefuatwa nyuma na vijana wawili wenye silaha nzito sana. Tulishuka ngazi hizo hadi chini kisha tukaufuata ukumbi mwembamba uliotupeleka hadi kwenye mlango wenye kamera kwa juu yenye taa juu yake kama ile ya kule kambini kwa vijana wa gorilla, yule mtu aliyetukagua aliisogelea ile kamera kisha akasema "they are here Boss( wapo hapa Bosi)". Aliposema hivyo alinivuta mkono na kunisogeza karibu na ile kamera huku akiniambia "your face ( sura yako), niliinua uso wangu nikaitazama ile kamera huku kengele maalum ikilia na mlango ukafunguka. Tuliingia ndani tukiwa tumeongozana na wale watu na tukatokea katika ofisi pana yenye mandhari ya kuvutia pamoja na milango minne tofauti, mbele yetu kama mita sita kulikuwa kuna meza yenye mafaili kadhaa pamoja na kiti cha kuzunguka kilichotupa mgongo.
"kaeni kwenye makochi hapo" Sauti ile iiliyokuwa ikinipa kazi nisizozipenda ilitoa amri ikitokea katika kiti kile cha kuzunguka kilichotupa mgongo, tulikaa katika makochi yaliyopo jirani nasi yakiwa mita sita kutoka pale alipo.
"Abdul, Nurulayt hatimaye tunakutana leo hii" Aliongea yule mtu huku akuzungusha kiti kuangalia tulipo na hapo ndipo nilipoibaini sura yake halisi na nikajikuta nikishtuka sana, Nurulayt naye alishtuka sana kwani alibaini yupo ndani ya himaya ya hatari.
"FAIZ ni wewe kweli" Niliongea huku nikinyanyuka nikataka kumfuata lakini nulishtushwa na milio ya kukokiwa bunduki na nilipoangalia pembeni nilitazama na bunduki mbili aina ya SPAS-12 kutoka kwa wale watu tuliyoingia nao, sikuwa na jinsi niliishia kukaa tu palepale huku tayari nikiwa najua kilichonifanya niwe pale.
"kinachowashangaza ni kipi nyinyi? Faiz kuwa hai sio? Mlidhani atakufa kwa hila zenu mlizozifanya nyie wasomali. Abdul yaani uko radhi kujaribu kumuua rafiki yako kipenzi kisa mwanamke ambaye hakupendi mwenye mapenzi na rafiki yako kisa una pesa tu, kakwambia nani pesa inaleta mapenzi mpaka ufanye haya. Ilivyopita miaka kumi ulidhani limeisha sio?" Nilikaripiwa na nikajikuta nikiinama chini baada ya kushindwa kumtazama kutokana na maneno makali aliyokuwa anayatoa hadi machozi yakawa yanamtoka.
"Faiz nisamehe rafiki yangu" Nilijikuta nikiomba msamaha.
"wa kuniomba msamaha ni mimi kwani, muombe Faiz mwenye huruma ya kusamehe ila mimi huwa sisamehi" Yule mtu ambaye nilijua ni Faiz alitoa kauli inayoonesha kukana kama yeye siyo Faiz.
"wewe kama si Faiz ni nani?" Nilimuuliza.
"mimi ni Fauz Ally Zaid kifupi F.A.Z au Scorpio pacha wa Faiz Ally Zaid niliyeikimbia nchi yangu nikiwa na mdogo wangu Khalid na nikazamia Afrika ya kusini kutafuta maisha na nikayapata kama haya niliyokuwa nayo kwa tabu na dhiki nikiwa nina uhakika wa kuja kuipa maisha bora familia yangu lakini wewe ukaivuruga familia hiyo kwa jeuri ya pesa zako ambazo hujui zinatafutwa vipi. Pesa hizo za ulizorithi umeona ni bora uwalipe wale waasi wa Kongo wamteke Fauz halafu wawambie familia yetu walete nusu tani ya almasi kutoka katika himaya yangu mwenyewe iliyo chini vijana wangu Gorrila boys, unajua matokeo yake ni nini?...........Baba yangu Mzee Ally Zaid aliyekuwa ni mwanajeshi mstaafu akaamua kwenda kujaribu kuiba hiyo almasi akajikuta anauawa kikatili huku nikiwa sijui kama vijana wangu wamemuua bsba yangu mzazi alipokuwa ana harakati za kumkomboa mwanae, Abdul............Abdul nilijiapiza lazima ulipie kwa kukuonesha hiyo pesa inatafutwaje kama ulivyotembea na wale wanawake ili kupata dola milioni moja za kimarekani na kuiba hizo almasi ili mfe kama mlivyosababisha baba yangu afe lakini mmepona kwasababu Mungu bado anawahitaji nyinyi mashetani" Aliongea huku machozi yakimtoka na mwili ikimtetemeka kwa hasira, alipoacha kuongea mlango mmojawapo ukafunguliwa na akaingia mtu aliyetokea kuwa rafiki yangu mkubwa na pia meneja wa makampuni. Khalid Zaid ambaye yule niliyemshuhudia akiwaeleza waandishi wa habari kuwa nipo masomoni ndiye aliyeingia huku akitoa tabasamu pana sana, nilibaki nikishangaa sana kwani sikutarajia kabisa kama nitakutana naye huku kutokana na kumuamini sana.
"Khalid na wewe pia?" Nilijikuta nikiongea kwa mshangao.
"huyo anaitwa Khalid Ally Zaid na unamfahamu kama kama Khalid Zaid kwani huwa hatumii jina la kati na Faiz hatumii jina lake la mwisho, nilimtuma kwa ajili ya kukamilisha kazi hii na ukamuamini bila ya kutambua unamuamini Nyoka" Fauz aliongea huku Khalid akitabasamu.
"huyu ndiye aliyekuwa anakupeleleza na hata siku ile uliyochukua binti ambaye ni mfuasi wangu uliyeamini ni changudoa yeye ndiye aliyeusuka mpango ule mpaka ukanyonya matiti ya yule binti anayeitwa Angel aliyoyapakaa madawa ya kulevya ukalala. Pia huyuhuyu ndiye aliyekupasua mgongoni akakufunga hardware ukiwa hujitambui baada ya kunusishwa Klorofomu ukatupwa kwenye kisiwa katika bahari ya Antlantiki siku nne baadaye na ya tano ukajikuta umelala ufukweni" Fauz aliongea tena kunifahamisha juu ya Khalid, muda huohuo mlango mwingine ulifunguliwa na akaingia mtu aliyekuwa anaendeshwa kwenye kiti cha matairi na msichana ambaye sikuweza kumtambua kabisa. Walifika hadi eneo aliposimama Khalid wakiwa wamevaa kofia zilizoziba nyuso zao kwa sehemu kubwa.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Abdul umefanya kosa lililozaa maafa mengine bila ya kujijua kwa kutumia jeuri ya pesa zako na wewe ndiyo cha huyu mtu aliyekaa kwenye kiti cha matairi ashindwe kutembea tangu nampata, nadhani huyu hujamtambua ni nani ngoja umuone" Fauz alisema kisha akamfunua kofia yule aliyekaa kwenye kiti cha matairi.
"Faiz!" Niliropoka baada ya kuiona sura ya Faiz kwa mara nyingine baada ya miaka kumi kupita, Faiz alikuwa ananitazama kwa uso uliojaa na hasira sana huku akiachia tabasamu lisiloashiria furaha katika uso wake.
"unashangaa kuniona nipo hai sio fedhuli mkubwa we?" Faiz aliongea akiwa na hasira sana kisha akamgeukia kaka yake akamuambia, "Kaka ulipokimbia nyumbani ukiwa na mdogo wetu nilikuona huna maana ndiyo maana hata chuo na shuleni nilisema nimezaliwa peke yangu kumbe nina pacha wangu, nimeingia chuo nikapata rafiki nikamuona ana maana kumbe hana maana kwani ametumia watu waniteke na wamenichoma sindano ya sumu ambayo inanifanya niwe katika kiti cha matairi hadi leo hii. Ama kweli umdhaniaye ndiye kumbe siye, huyu baradhuri nilimuona anafaa kumbe hafai na nikakuona wewe hufai kumbe ndiye unafaa, Fauz huyu mtu namchukia sana" Faiz aliongea huku akitokwa na machozi, mimi mwenyewe machozi yalianza kunitoka kutokana na kujuta sana kutokana na mambo niliyomtendea rafiki yangu tukiwa chuo ingawa machozi hayakuweza kubadilisha ukweli wa jambo hilo liwe halijatokea.
"Faiz nisamehe rafiki yangu nimekosa" Nilimuomba msamaha Faiz huku nikinyanyuka ili walau nikapige magoti mbele yake anielewe lakini nilishindwa kwenda kutokana na kuwekewa bunduki kwa mara nyingine nilipotaka kwenda. Nilirudi nikakaa chini nikamtazama Nurulayt ambaye alionekana pia kujuta kwa kile alichomfanyia Faiz.
"Abdul tafadhali sana naomba usiniite rafiki yako na ukitaka nikusamehe mlete Huwaida hapa kwani nilimtumia email nilipokombolewa na anajua juu ya uovu wako na kama huwezi sitakusamehe, namtaka mpenzi wangu tu kwani sijui umemficha wapi hadi sasa" Faiz aliongea huku uso wake ukiwa umetawaliwa na hasira, nilipisikia hilo suala ikabidi nimtazame Nurulayt kisha nikasema, " Faiz haiwezekani jambo hilo kwani Huwaida niliyempenda na aliyekupenda wewe tayari ni marehemu kwa sasa".
"What! Hapanaaaa" Faiz aliongea kwa uchungu kisha akaanza kulia kwa uchungu huku mishipa ya damu ya kichwa ikiwa imemtoka, nilimuonea huruma saba ingawa chanzo cha yote nilikuwa ni mimi.
"Abdul kama Huwaida kafa basi mwnao lazima afe kwa namna yoyote" Faiz aliongea kwa uchungu.
"Kifo cha Huwaida ni mimi ndiye mhusika na si Abdul wala mtoto wetu Ilham na kama unataka kuniadhibu niadhibu ila kaka yako Fauz lazima pia naye alipe kwa kumuua Sabir kaka yangu aliyekuwa rafiki yake na mshirika na kuhusika kwangu katika kutekwa kwako nilikuwa nalenga Fauz na sio wewe" Nurulayt kwa mara ya kwanza aliingilia kutokana na kusikia suala la kutaka kuuliwa Ilham, maneno hayo yalimfanya Fauz atabasamu.
"Alaa kwahiyo umemfanya kaka yangu awe mtu wa kutembea kwa baiskeli kisa mimi kumuua Sabir na ukadhani yeye ni Fauz, sikulaumu sana najua umekosea kufananisha kwa jinsi tunavyofanana......Sabir alikuwa ni rafiki yangu sana ila amenigeuka kwa kuuwa watu wangu pia kutaka kumuua mdogo wangu kwa bomu, hivi ungekuwa wewe mtu kama huyu utamfanyaje?" Fauz aliongea na mwisho akamuuliza swali Nurulayt lililomfanya ashindwe kujibu na pia akajiona ana hatia sana kwa kufanya kile anachokifanya, Faiz alipoona Nurulayt ameshindwa kujibu swali lake alitoa ishara moja ambayo sikuielewa. Mlinzi mmoja mwenye bunduki alisogea mbele baada ya kutolewa ishara ile kisha akampatia bunduki Faiz, Faiz naye aliishika ile bunduki akaelekeza tulipo kisha akaifyatua ikatoa mlio niliousikia. Kuusikia mlio wa bunduki nilitambua haijanipiga mimi kwani bunduki ikikupiga husikii mlio wowote, nilipomuangalia Nurulayt niliona sindano yenye manyoya kama mshale wa mchezo wa dart ikiwa imemchoma begani mwake. Nurulayt aliutia ule mshale kisha akautupa chini na akabaki akiugulia maumivu, nilipomtazama Faiz nilimuona akitabasamu kisha akanielekezea bunduki mimi akiwa makini sana. Hapo mapigo yalianza kwenda mbio na ikanibidi nifumbe macho tu nikusubiria nitandikwe , mlio wa bunduki niliusikia kwa mara ya pili nikafumbua macho nikamuona Faiz akitabasamu.
"Abdul sioni kosa lako lolote lililobakia kwani umejifunza vya kutosha ila huyo mwanamke ana kosa ndiyo maana nimemuadhibu, kosa lako kubwa ilikuwa ni kutoa pesa katika mpango wa huyu mwanamke hivyo umepata funzo hiyo pesa ya urithi uliyoitoa katika mpango huo inatafutwaje" Faiz aliongea huku akinitazama halafu akamegukia Nurulayt akamuambia "Nuru hiyo ndiyo ulistahiki kwa kuhukumu watu bila kujua kama upo sahihi au haupo, sindano zilizo ndani ya bunduki hii zina sumu ambayo ikiingia kwenye damu huponi na itakuua taratibu kuanzia kiungo kimoja baada ya kingine hadi unakata roho". Faiz alipomaliza kuongea hivyo nilijikuta nikilia baada ya kusikia Nurulayt kachomwa sindano ya sumu na nikamkumbatia ingawa yeye hakuonesha kuhuzunika hata kidogo. Baada ya kusema maneno hayo Faiz alimgeukia Fauz akamwambia, " hii inawatosha wape vitu vyao", Fauz naye alitii na akamuita kijana wake mmoja akampa mkoba ambao alikuja kunipatia. Niliupokea mkoba huo nikaufungua nikakuta hati za mali zangu zote pamoja na kadi zangu za benki, niliufunga mkoba huo kisha nikatulia nikawa nawatazama ndugu wale watatu.
"Niliwaambia waandishi kuwa upo masomoni nadhani sasa muda wa masomo umeisha na umepata funzo sasa upo huru, tupatie kila tulichokupatia" Khalid aliongea huku akitabasamu, nilipoambiwa hivyo nilitoa simu nikamrushia naye akaidaka.
"Abdul natambua kama wewe ni binadamu unakosea kwani hakuna aliyemkamilifu, hivyo nimekusamehe wewe na mwenzako.....Nurulayt naomba unisamehe sana sikuwa na jibsi zaidi ya kufanya hivyo nilivyokufanyia na napenda mtambue mtoto wenu yupo nyumbani kwa Sarina mama yake wa kambo, guards take them to the room" Faiz aliongea CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walinzi walituchukua wakatutoa nje ya chumba hicho wakatupeleka chumba kingine kilicho na nguo tofauti za kike na za kiume, huko tulioga na tukabadilisha nguo kisha tukashuka hadi chini na tukachukua teksi iliyotupeleka hadi nyumbani kwa Nurulayt ambapo tulipanda gari yangu nilipewa tukaanza safari ya kuelekea nyumbani kwa Sarina. Tulifanikiwa kufika na tukashuka tukaingia ndani ya uzio kisha tukagonga mlango wa mbele tukasubiri kufunguliwa, baada ya dakika kadhaa Sarina alifungua mlango na alinikumbatia kwa furaha baada ya kuniona nimerejea nikiwa mzima. Nurulayt alikaribishwa ndani na hapo tukamsimulia kila kitu hasa juu ya Ilham kuwa ni mwanangu. "Waar is Ilham?( Yuko wapi amelala)" Nurulayt aliuliza akiwa na shauku ya kumuona Ilham
" lê(amelala)" Sarina alimjibu lakini Nurulayt alitaka amuone Ilham tu kwani hakuwa amemuona kwa miaka mitano, ilimbidi Sarina amuelekeze chumba kilipo na Nurulayt akaenda akituacha tukiongea . Aliporejea alikuwa amembeba Ilham ambaye tayari alikuwa ameamka, huku akionekana kuwa ana furaha kwa kumuona mtoto wake kwa mara nyingine.
"Anko umerudi?" Ilham aliongea aliponiona nikiwa nimejea.
"wewe sio anko yule ni baba, umesikia? Haya nenda kamsalimie baba " Nurulayt alimuambia Ilham
"ok mummy" Ilham alijibu halafu akaja kunikumbatia akiwa na furaha na mimu nikiwa na furaha kwa kumjua mwanangu.
"Sarina...dankie(Sarina......asante) Nurulayt alimshukuru Sarina kwa kumtunzia Ilham, Sarina alitabasamu kuonesha amekubali shukrani ya Nurulayt.
Nilikaa kwa Sarina kwa siku kadhaa kisha nikaenda hadi Walvis kwa rafiki yangu Jonas nikamchukua hadi nyumbani kwa Sarina, baada ya wiki mbili nilikuwa nipo Tanzania nikiwa na Sarina, Ilham, Nurulayt pamoja na Jonas ambaye nilimpatia nyumba na mtaji kama shukrani kwa msaada wake kwangu nilipokuwa nina shida aliponiokota ufukweni. Miezi miwili iliyofuata nilifunga ndoa na Sarina hapahapa Dar es salaam iliyohudhuriwa na watu mbalimbali na sherehe kubwa ikafanyika katika moja ya hoteli ninazozimiliki, furaha yangu ya kuwa na mwanamke ninayempenda katika ndoa ilitimia kuanzia siku hiyo.
Baada ya miezi mitatu tangu nifunge ndoa na Sarina hali ya kuafya ya Nurylayt ilianza kubadilika kwa baadhi ya viungo kushindwa kufanya kazi na akipolekwa hospitali ilibainika tumechelewa kwani sumu ilishasambaa mwilini kote na hakukuwa na tiba ya kumuokoa, Nurulayt aliugua kitandani kwa muda mrefu sana hadi Sarina anapata ujauzito yeye alikuwa bado ni wa kitandani. Sarina alipojifungua watoto mapacha wa kiume ambao niliwaita Haasan na Hussein yeye bado alikuwa kitandani, baada ya miaka mitatu tangu aanze kuugua Nurulayt aliaga dunia katika muda wa alasiri na akatuachia huzuni na majonzi yaliyobaki moyoni mwangu na kunipelekea nitokwe na machozi kipindi naandika mkasa huu ulionikumba. Mungu amlaze pema mama wa mtoto wangu wa kwanza na binti yangu mkubwa kati ya watoto sita niliojaliwa na Muumba, nakumbuka mazishi ya Nurulayt niliteuliwa niingie kaburini kuipokea maiti lakini nilishindwa kutokana na kulia sana hasa nikimkumbuka katika kipindi chote nilichokuwa naye.
****
Walipomaliza ukurasa wa mwisho wa shajara hiyo Hassan na Hussein wote walijikuta wakitokwa na mschozi baada ya kujua mkasa uliomkumba baba yao pamoja na mama yao wa kambo ambaye kamzaa dada yao mkubwa.
"aisee mi Mariam simtaki tena hapa nimepata funzo tosha" Hassan aliongea huku akijifuta machozi.
"kweli pesa haileti mapenzi na pesa ibilisi" Hussein aliongea huku naye akijifuta machozi.
"wanawake wapo wengi nitatafuta mwingine ngoja nimuache jamaa awe naye ili niepuke kufanya kosa kwani alichokifanya baba kimenipa funzo tosha" Hassan aliongea huku akimtazams Hussein.
"kaka hapo umeamua na umefanya busara kubwa sana, tafuta mwingine wazuri wapo wengi sana ndani ya dunia hii. Huwezi jua Mungu amekupangia nani baada ya Mariam kuchukuliwa na jamaa cha msingi badili direction ya moyo wako tu" Hussein alimshauri Hassan.
"kweli kabisa hii diary imenifunza mengi kabisa, cheki time maana nasikia tumbo linanisokota kwa njaa" Hassan alimwambia Hussein. Hussein alichukua simu yake ya mkononi akaangalia saa na alijikuta akipigwa na mshangao baada ya kuangalia saaa.
"Ebwanaeh! Time imeenda sana saa kumi hii, hebu twende tukale kwanza" Hussein aliongea kisha akasimama akaelekea mlangoni ili aelekee sebuleni, Hassan naye alimfuata kwa nyuma.
Walipofika sebuleni walikutana na wazazi wao wakawasalimia kisha wakataka kwenda kwenye meza ya chakula lakini baba yao aliwaita na akawaambia wakae kwenye kochi.
"Hussein, Hasaan" Mzee Abdul aliita majina yao.
"naam Baba" wote waliitikia kwa pamoja.
"najua mmemaliza kusoma diary yangu wanangu, je Hassan bado unataka kufanya ulichodhamiria?" Mzee Abdul aliuliza
"hapana sitafanya nimejifunza pesa si lolote katika mapenzi" Hassan alijibu.
"vizuri, niliamua kuwaacha mjue maisha yangu nyuma ili mjifunze na nyinyi wanangu. Nafurahi mmejifunza na naomba mfuate hayo mliyojifunza, ukiona umekataliwa jua kuna kizuri unaandaliwa mwanangu sasa utafute anayekupenda ili uje kuwa kama mimi Abdul na mama yenu hapa Sarina" Mzee Abdul aliongea huku Bi Sarina akitabasamu.
"sawa baba tumekuelewa" walijibu kwa pamoja.
"nendeni mkale" Mzee Abdul aliwaruhusu watoto wake, Hassan na Hussein walielekea kwenye meza ya chakula wakiwaacha wazazi wao wakiongea.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"ujue mwanzo sikuliafiki suala la wewe kuwapa watoto ile diary wasome ila sasa naona upo sahihi kabisa Mume wangu" Bi Sarina aliongea kwa sauti ya chini kumuambia mume wake.
"unajua katika suala la kuwafunza watoto inabidi muda mwingine tuwe wawazi kwao ili wajue hasara za jambo hilo mke wangu" Mzee Abdul alimwambia mke wake.
"hakika mume wangu wewe ni baba bora kwa watoto wako" Bi Sarina alimwambia mume wake.
"hata wewe ni mama bora kwa watoto, nakupenda sana" Mzee Abdul aliongea.
"nakupenda pia mume wangu" Bi Sarina aliongea huku akitabasamu.
Tangu siku hiyo Hassan aliachana na habari za kutaka kumdhuru rafiki yake na akawa na urafiki naye.
MWISHO!!
0 comments:
Post a Comment