Search This Blog

Sunday, 22 May 2022

KOSA - 4

 







    Simulizi : Kosa

    Sehemu Ya Nne (4)



    "fungua mzigo sasa usiutazame tu" niliambiwa na mimi nikatii nikaufungua mzigo huo ambao uliniacha nikiwa nimepigwa na bumbuwazi kwa kile nilichokiona, hata Sarina naye alipigwa na bumbuwazi kwa alichokiona ndani ya boksi hilo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "vizuri kwa kuufungua mzigo huo, sasa kama unataka ujute maishani mwako kidharau hicho ulichokikuta humo ndani na kama hupendi kujuta basi ukitunze nilichokukabidhi kwani si mali yangu ila kipo chini ya uangalizi wangu" Sauti ya kwenye simu ilinisisitiza kisha simu ikakatwa.



    Macho yangu yote niliyaelekeza ndani ya boksi hilo kwa kutazama kile nilichokiona ndani yake, sikutegemea kabisa kama nitaletewa mzigo mwingine wakati tayari nina gunia zito la mchanga katika kichwa changu ambalo linaonekana kunizidia uzito. Mtu huyu anayenipa tabu zote hizi nilimuona kama amepanga kuniongezea uzito akijua tayari nimeelemewa ili nianguke, ndani ya boksi hilo kulikuwa kuna mtoto wa kike wa kisomali apataye miaka kumi au tisa kama ungekadiria umri wake. Alionekana ni binti mrembo na mwenye kuvutia ikiwa utamtazama machoni, alikuwa na nywele ndefu sana zenye rangi nyeusi sana. Sura ya mtoto huyu niliifananisha kama niliwahi kuiona mahali lakini sikuwa nakumbuka ni wapi niliiona, nilibaki nikimshangaa huku moyoni nikichoka kabisa kutokana na kuhisi nimeelemewa na mzigo mwingine wa kumtunza huyu binti mdogo na mrembo ambaye nilihisi hakuwa na hatia yoyote mpaka aletwe mbele yangu mimi aje kuteseka akikosa matunzo ya wazazi wake. Binti mdogo mwenye kila sifa ya kuitwa mzuri hata akiwa mkubwa basi angekuwa ni tishio kwa urembo wake ambao unaonekana mapema tu akiwa na umri huo, akiwa ndani ya boksi alikuwa yupo ndani ya usingizi mzito sana kwani nilimtingisha hakuonekana kuamka kabisa. Alivyolala ndani ya boksi hilo ni wazi alikuwa anaumia na hata angeamka angejihisi maumivu kwa jinsi alivyojikunja, nilimtoa kwenye boksi na nikamlaza kwenye kochi ili aweze kulala vizuri kutokana na kujikuta nikiingiwa na huruma ya ghafla kila nikimuangalia jinsi alivyolala hapo kwenye boksi. Sarina alibaki kapigwa na butwaa baada ya kumuona mtoto huyo na hata nilipokuwa ninayafanya yote hayo yeye alibaki akishangaa kama mtu aliyepumbazika, alikuja kutoka kwenye kupumbazika huko baada ya kusikia kilio changu cha chinichini kilichoanza kunipata baada ya kupewa mzigo mwingine. Sarina alipoona kilio changu kinazidi alinisogelea halafu akaniambia, " Abdul huil nie jy is 'n man, 'n bepaling van die

    hart(Abdul usilie wewe ni mwanaume, kuwa mkakamavu)".

    " Sarina seer het ons net gelaat word, wat nie die

    man wat ek mkisea weet wat?(Sarina inauma we acha tu, sijui huyu mtu nimemkosea nini?) Niliongea huku nikibubujikwa na machozi na macho yangu yote nikiwa nimeyaelekeza alipo msichana mdogo niliyemtoa kwenye boksi, hakustahili kuletwa kwa mtu mwenye matatizo kama mimi tena asiye na mbele wala nyuma huku ugenini kwenye nchi yawatu.

    " nou was sy sy skuld Wat my bring ng, nie sal jy

    ly sonder enige skuld( sasa huyu binti kosa lake ni lipi mpaka niletewe mimi, huoni kama atateseka bila ya kuwa na hatia" Niliendelea kulalamika huku machozi yakiwa yananitoka bila hata kuonesha dalili yoyote ya kuonesha kikomo chake kinakaribia, Sarina alizidi kunitazama na huzuni hasa nilipozidi kulia mtoto wa kiume kwa kumuhurumia msichana niliyetewa.

    " Sarina het niks om te dra, sy deel van die slaap

    en doen sy deel te kos. U is my hulp, nou sy

    was om te sien of dit is 'n las en sal ly( Sarina sina cha kuvaa, sina sehemu ya kulala na wala sina sehemu ya kupata chakula, Wewe ndiyo msaada kwangu, sasa huyu binti huoni kama ni mzigo na atateseka)" Niliendelea kuongea huku machozi yakinitoka kila nikimtazama msichana niliyeletewa, Sarina alipoona ninazidi kulia alinikumbatia bila kusema chochote na alipoacha kunikumbatia alinibusu kwenye paji la uso halafu akaenda hadi pale alipolazwa yule binti halafu akaketi jirani naye. Alimnyanyua yule binti kichwa chake akakiweka kwenye mapaja yake kisha akaanza kuzichezea nywele za binti huyo, nilibaki nikimtazama huku kilio changu nikiwa nimekisitisha nikimtazama yeye tu.

    " Abdul as ek is nuttig vir jou, dan is dit nuttig om

    te sy dogter sal wees, ek toevallig baie lief en ek

    kan nie laat dit om te ly wanneer ek kan steun teCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    gee(Abdul ikiwa mimi ni msaada kwako basi huyu binti nitakuwa msaada kwake, nimetokea kumpenda sana na siwezi nikamuacha ateseke wakati uwezo wa kumsaidia ninao)" Sarina aliongea huku akimtazama yule binti kwa huruma sana, maneno hayo yalinifanya nimuone Sarina ni mwanamke wa kipekee sana kwani si jambo rahisi kwa mwanamke mwingine wa kawaida na wenye mioyo ya aina hiyo duniani laiti tungewahesabu na kuwaweka katika asilimia basi wangekuwa ni asilimia mbili kati ya asilimia mia moja. Sarina ni mwanamke wa kipekee sana kwa uamuzi huo aliouchukua, nilijikuta nikienda kukaa karibu naye katika lile kochi halafu nikachukua miguu ya yule binti nikaipakata kwenye mapaja yangu kama Sarina alivyokipakata kichwa chake. Sarina aliniangalia nilipofanya hivyo halafu akatabasamu bila hata kuniambia jambo lolote, na mimi nilitabasamu kisha nikamvuta Sarina nikambusu mdomoni halafu nikamuambia " Sarina is lief vir jou en ek ophou om jou lief te

    hê, is jy beslis unieke vrou (Sarina nakupenda sana na sitoacha kukupenda, hakika wewe ni mwanamke wa kipekee)". Maneno hayo yalimfanya Sarina atabasamu kisha akaniegemea begani huku mkoni wake ukiwa umeshika shingo yangu, tukiwa tupo namna hiyo msichana tuliyetewa alianza kupiga chafya mara mbili huku akifikicha macho yake. Wote wawili tulishtuka na tukawa tunamtazama huyu binti kwa mshangao wa kutaka kutaka kumuona akifungua macho yake, binti alipopiga chafya mara ya tatu alifumbua macho taratibu na akashtuka baada ya kutuona sisi ambao ni wageni kwake.

    "nyinyi wakina nani? Hapa ni wapi?" Binti huyu aliongea kiswahili fasaha huku akirudi nyuma kwa wasiwasi kabisa na hapo ndipo nikatambua kuwa anaongea kiswahil, Sarina alishangaa sana kwani lugha hiyo hakuwa anaitambua kabisa.

    "hapa ni sehemu salama" Nilimwambia kwa kiswahili ili kumtuliza nikimuacha Sarina akiwa haelewi chochote.

    "mmenihamisha kwingine sio, sitaki namtaka mama yangu" Binti huyu alianza kulia huku akigaragara lakini niliwahi kumtuliza kisha nikampa maneno mazuri yaliyomfanya awe na sisi, alipotulia kabisa tulimketisha katikati yetu mimi na Sarina.

    "mtoto unaitwa nani?" Nilimuuliza kwa upole.

    "Ilham" Alijibu

    "sikiliza mtoto mzuri nipo tayari kukusaidia, umuone mama yako. Lakini kwanza tuambie ulikuwa wapi kama unakumbuka na ikiwezekana utueleze yaliyokukuta kwa ufupi" Nilimwambia huku nikimshika kichwani nikimtazama kwa macho ya huruma sana. Nilipomuuliza hivyo alijibu, "nilikuwa nikitoka shule tu nikajikuta nimekamatwa nikawekewa kitambaa mdomoni, nililala nilipokuja kuamka nikajikuta nipo nisipopajua".

    "polee Ilham, unakumbuka ilikuwa lini?" Nilimuuliza huku nikimshika bega tena safari hii nilipiga magoti mbele yake. Ilham nilipomuuliza hivyo alinitajia tarehe, mwezi na hadi siku aliyokamatwa pamoja na mwaka, nilibaki nikiwa nimepigwa na butwaa baada ya kubaini kwamba siku aliyokamatwa Ilham ni miaka mitano iliyopita hivyo amefungiwa kwa miaka mitano hadi inafika siku hiyo tunamkuta ndani ya boksi. Nilimfasiria Sarina yote aliyokuwa akiyaongea Ilham ambayo pia yalimshangaza hata yeye, Ilham mwenyewe alionekana kutoelewa muda aliokaa ndani.

    "kwenu ni wapi na unaishi na nani?" Nilimuuliza

    "Kwetu ni Mwanza naishi na mama" Ilham alijibu

    "Pole sana mtoto mzuri baba yako yupo wapi?" Nilimuuliza, swali hilo llionekana lilikuwa ni gumu kwa Ilham na akashindwa kulijibu akabaki akiwa ameinamisha uso wake chini.

    "Mtoto mzuri utakaa na sisi hadi tutakapokupeleka kwa mama umesikiaeh! Mimi naitwa anko Abdul na huyo hapo ni anti Sarina" Nilimwambia maneno yaliyoambatana na utambulisho mimi na Sarina, Ilham alionesha kuyakubali hayo maneno halafu akamtazama Sarina akiwa anatabasamu pana usoni mwake. Ilham alimkumbatia Sarina huku akitabasamu na Sarina naye akampokea.

    " Algehele as 'n ma en kind(Mnapendeza kama mama na mtoto)" Nilimwambia Sarina huku nikitabasamu na yeye akatabasamu alipisikia maneno hayo ambayo hayakueleweka kwa Ilham.

    "Anko umesemaje mbona sijakuelewa?" Ilham aliniuliza baada ya kusikia naongea kiafrikaas nikiwa hapo

    "katoto hapa sio Tanzania, hivyo hatuongei kiswahili hiki ni kiafrikaas" Nilimwambia Ilham maneno yaliyomshangaza sana kwani mwanzo hatukumuambia alipo ni nchi gani. Ilham alizidi kushangaa sana na ikabidi nimueleze ukweli juu ya eneo ambalo tupo na nchi yake, pia nikamueleza juu ya Sarina kutojua kiswahili.

    "Anko basi mimi hata kifaransa naongea au anti Sarina naye hawezi" Ilham alianza kuchangamka hapohapo hadi akanifanya na mimi nifurahi.

    "unaweza kweli kifaransa? Ngoja nikujaribu" Nilimwambia kimasihara huku nikionesha tabasamu ambalo lilimfanya na yeye atabasamu, Sarina alikuwa akituangalia huku akitabasamu baada ya kumuona Ilham ana furaha.

    "ndiyo naweza tumefundishwa shuleni toka Nursery" Ilham aliendelea kuweka uchangamfu wake wa kitoto.

    " Ce est là?(hapa ni wapi?)" Nilimuuliza kwa lugha ya kifaransa ili nimpime kama anajua kifaransa au hajui kwani na mimi nilikisoma kifaransa nilipokuwa shule ya sekondari pia katika biashara nilikuwa nakitumia kuzungumza na wafanyabiashara wa kifaransa.

    " Maintenant que vous me avez dit vous-même ici,

    ce est la Namibie, pourquoi me demandez-vous

    à nouveau?(umeniambia mwenyewe hapa ni Namibia, kwanini unaniuliza tena?)" Ilham aliniambia kwa kifaransa fasaha kabisa hadi nikawa namshangaa na kicheko ndicho kilichofuata kwangu na kwa Sarina.

    " Je me demande pourquoi je demande même

    quand il se dit

    (hata mimi nashangaa kwanini anakuuliza wakati amekuambia mwenyewe)" Sarina naye aliongea kifaransa kwa mara ya kwanza tangu nifahamiane nae, sikuwa na natambua kama Sarina anajua kifaransa na hapo ndipo nilipobaki nikimshangaa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " vous vous demandez pourquoi Abdul, je parle

    français? Les gens parlent plusieurs langues

    Namibie de six(unashangaa nini Abdul, Mimi kuongea kifaransa? Namibia watu wanaongea lugha zaidi ya sita)" Maneno hayo ya Sarina kwa lugha ya kifaransa ndiyo yalinishangaza sana kwani sikutambua kama raia wa nchi hii wanajua lugha zaidi ya moja.

    Maongezi baina yetu yaliendelea ndani ya muda mrefu na furaha ikiwa imetawala maongezi yetu hasa baada ya kuongezeka kwa Ilham katika nyumba hii, Ilhama alikuwa ni binti mchangamfu sana kutokana na kutawaliwa na akili za kitoto. Muda wa mchana ulipowadia ilinibidi nimwambie Sarina kuhusu suala kupeleka pesa kule kwenye sanduku la posta nililopewa namba zake, Sarina alinishauri nizitume zote kwa njia ya posta katika ofisi ya posta ya mjini Widhoek kwenda kwenye sanduku la posta la ghuba ya Walvis. Wazo lake hilo nililiafiki na muda huo huo wote tukaingia kwenye gari kuelekea zilipo ofisi za posta pembezoni mwa barabara ya uhuru (Independence avenue) katika jiji hilo, niliamua kuwa makini sana kwani nilikuwa nina wasiwasi wa kutafutwa kutokana na tukio nililolifanya katika hoteli ya Widhoek siku iliyopita. Njiani Sarina alininunulia kofia ambayo ilinisaidia kuficha sehemu kubwa ya uso wangu, yeye alivaa kawaida sana kutokana na shungi alilolivaa siku iliyopita isingekuwa rahisi kumtambua. Ilham hatukuwa na wasiwasi naye wala hakuwa ana wasiwasi wa chochote, yeye alivaa kawaida tu, baada ya dakika kadhaa tulifanikiwa kufika zilipo ofisi hizo na taratibu zote za kutuma pesa kwenda sanduku la posta la ghuba ya Walvis ikafanywa. Tulifanikiwa kutuma pesa hizo kisha tukaondoka mahala hapo salama kabisa bila hata kusumbuliwa na hofu ya nafsi ya kuwaona askari waliopo katika ofisi hizo za posta, usukani nilimuachia Sarina safari mimi nikapumzika. Sarina aliendesha gari siku hiyo akipita sehemu mbalimbali ambazo zina maduka ambazo alinifahamisha kama ni maduka aliyoachiwa na baba yake na ndiyo yanayomfanya awepo mjini, tulimaliza kutembelea maduka hayo yote na tukarudi nyumbani muda wa mchana tukiwa tumefurahia kuzunguka sehemu mbalimbali tukiwa pamoja. Siku hiyo tulishinda nyumbani baada ya kurudi safari hiyo hadi jioni inaingia tukiongea mambo mbalimbali, kuna muda Ilham alilala na ukawa uhuru kwetu katika kuongea zaidi. Muda Sarina alinisimulia historia ya Maisha yake kwa ufupi na mimi nikamsimulia yangu pia huku nikiruka kisa changu na Faiz. Kukikwepa kwangu kicho hakukudumu kwani Sarina alitaka nimsimulie historia yangu katika mapenzi baada ya yeye kuanza kunisimulia yake, kwakweli ilinikuwa ni jambo gumu sana kumuelezea juu ya jambo nililolofanya huko nyuma ambalo sitaki linirudie kichwani mwangu. Ilikuwa ni jambo gumu sana kumueleza kisa hicho nikihofia kuvurugika kwa upendo wake kwangu ulioanza kuchipua siku hiyo hiyo, machozi yalianza kunitoka nilipofikiria kisa hicho ambacho ndiyo chanzo cha mimi kujiingiza katika unywaji wa pombe pamoja na ununuaji wa machangudoa hadi najikuta nchini hapa kwa mara ya mwisho. Hofu ya kumpoteza niliona inanijia waziwazi na jambo hilo sikuhitaji litokee, ningeamua kukaa kimya ningeonekana simkweli hivyo jambo pekee nililoliona wakati huo ni kueleza ukweli kwani dunia haina siri hata siku moja na ukitaka siri fanya jambo la peke yako vinginevyo ukifanya na mtu mwingine jua hiyo siri itajulikana hata kama huyo mtu awe bubu. " est dans l'histoire, ni l'histoire m'a rappelé que je

    aimerais que quelqu'un, je si je aimais je

    ai trouvé que je ai fait une grosse erreur(ni katika historia nisiyopenda kuikumbusha wala kuihadithia, nilipendwa nisipopendwa nikajikuta nimefanya kosa kubwa" Nilijikakamua nikamueleza kwa ufupi nikitumia lugha ya kifaransa ninayoielewa zaidi kuliko kiafrikaas, Sarina alinitazama kwa umakini sana aliposikia maneno hayo na alikuwa akiniangalia kwa macho yanayohitaji niendelee kumsimulia. Nilishusha pumzi kisha nikaanza kuongea ukweli mtupu kuhusu mambo yaliyotokea nyuma hadi pale Huwaida alipouawa, nilimuelezea kila kitu sikutaka kumficha na machozi muda huo yalikuwa yameshika hatamu katika macho yangu. Nilimaliza kwa kumsimulia kuhusu Nurulayt kuwa na ujauzito kisha nikamtazama yeye nimuone alipokeaje historia yangu, Sarina alionekana kuwa na sura masikitiko sana nilipomaliza kumsimulia haya.

    " . Abdul.......Abdul a fait une très grosse erreur

    que vous devez être pardonné et offensé, devrait

    être libre de trouver le pardon dans votre cœur

    pour votre ami(Abdul.....Abdul umefanya kosa kubwa sana ambalo unahitaji usamehewe na uliyemkosea, inabidi uwe huru moyoni mwako kwa kupata msamaha wa rafiki yako)" Sarina aliongea kwa masikitiko huku akinitazama usoni kwa huruma. Sarina aliongea suala la ukweli kabisa kwamba nilikuwa nahitaji msamaha wa Faiz ili niwe na amani ya moyo, lakini ningeanzia wapi wakati sindano ya sumu aliyochomwa Faiz ilikuwa inamuua siku moja inafuata ya tangu Huwaida afariki. Nilimueleza juu ya kutowezekana kwa suala hilo huku nikimsihi asinichukie kutokana na kosa hilo nililotenda kipindi cha nyuma, nilimueleza kwa jinsi ninavyompenda sikuwa tayari kutengana naye.

    " Abdul avait fait il ya dix ans ne existait pas, ici

    parler à mon copain que je aime Abdul(Abdul aliyefanya jambo hilo miaka kumi iliyopita hayupo, hapa naongea na Abdul mpenzi wangu ninayempenda sana) Sarina aliongea huku akinitazama usoni akiwa na tabasamu pana halafu akanisogeza mdomo wangu karibu na wake tukabadilishana kimininika kisichotoa kiu wala kujaza tumbo. Zoezi hilo lilitupendeza sana na tukajikuta tukiendelea nalo, tulipokuja kuacha kila mmoja alikuwa snatabasamu. Tuliendelea na zoezi letu kwa mara ya pili huku nikivua shati langu na Sarina akivua nguo yake ya juu, tulijikuta tukibaki na nguo za ndani pekee na joto lilikuwa kali sana. Kupunguza joto ilinidi niende nikawashe feni la hapo ukumbini, upande ulipo feni ilibidi nimpe mgongo wakati naenda kuliwasha kwani swichi ya kuliwasha feni ilikuwa upande huo, nilipopiga hatua mbili kwenda kwenye swichi Sarina aliona kitu kilichomfanya anifuate akiniambia nisimame kwanza. Aliponifikia alinishika katika ya mgongo huku akiniuliza, " Avez-vous déjà tricoter?(umewahi kushonwa?)", nilikataa akaniuliza juu ya alama ndogo ya mshono iliyopo mgongoni mwangu ambayo nilikuwa siijui.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ukweli ni kwamba sikuwahi kushonwa mgongoni hata siku moja kwani sikuwahi kuumia hadi nikashonwa na wala sikuwahi kufanyiwa upasuaji wowote hadi nishonwe mgongoni, Sarina alikuwa akinishika sehemu ambayo alisema kuna mshono na hapo nikahisi kuna alama ipo mgongoni mwangu. Sikuijua hiyo alama niliwahi kupatwa na nini hadi nikawa hivyo, Sarina aliendelea kuishika ile alama kwa namna ya kupapasa huku akinibusu shingoni kwangu hadi nikaanza kujihisi nina hali tofauti kabisa katika mwili wangu kutokana na msisimko uliokuwa ninaupata. Nilipowasha feni la hapo sebuleni ilikuwa ni mwanzo wa jambo lililowaka katika miili yetu lililohitajiwa kuzimwa na kwa kupata kile ambacho hatukuwa nacho katika miili yetu, ilikuwa ni mambo ambayo hayawezi kuelezeka kwa maandishi kwa kila hatua kwa mtu mwenye maadili timamu ya rika zote za umri ni safari ya ajabu isiyotakiwa kusimuliwa kwa mwingine ili kuepuka vichochezi na ushawishi kwa wengine kutaka kusafiri kama hii. Niliweza kusafiri kwa saa na dakika kadhaa katika safari hii isiyokuwa na karaha kwa wahitaji wake hadi nilipofikia kituo kikuu cha mwisho cha safari hii, Sarina alikuwa naye yupo pamoja nami katika kwa kila hatua na hata nilipotua mzigo mwisho wa safari hii naye alitua mzigo vilevile. Tulipomaliza wote tulienda bafuni tukajisafisha kisha Sarina aliingia jikoni kuandaa chakula cha jioni na mimi nikakaa sebuleni nikawa naangalia runinga kama kawaida yangu, niliwasha nikaangalia chaneli za Tanzania kujua kinachojiri nikawa nimeshasahau kabisa suala la Sarina kuuona mshono mgongoni kwangu. Nikiwa naangalia televisheni simu yangu iliita kwa mara nyingine huku jina la mpigaji likionekana ni lile la mtu anayenipa kazi nisizozipenda kila kukicha, niliipokea simu kisha nikaiweka sikioni nikatulia kimya bila kuongea chochote.

    "sasa muda wa kazi umewadia inabidi ujiandae mwenzako anakusubiri katika kibanda cha simu kilichopo jirani na hoteli ya Hilton, inabidi umchukue uende nae atakapokuelekeza. Pia hongera kwa kumtafuna Sarina" Aliniambia kisha akakata simu, nilibaki nikiwa nina hasira hasa kutokana na mambo anayonifanyia huyu mtu akionesha kuniona kila ninachofanya. Kwa mara nyingine nilianza kuyafikiria mambo ambayo ninafanyiwa na huyu ambaye anaonekana ananiona kwa kila hatua yangu, nilifikiria matukio yote hadi pale Sarina aliponiambia kuhusu alama ya mshono iliyopo mgongoni kwangu. Nilijaribu kukumbuka filamu mbalimbali za kipelelezi nilizowahi kuziangalia na nyingine za mapigano ambapo zilinikumbusha juu ya uwepo wa kifaa kidogo mithili ya punje ya ngano ambacho mtu akiwekewa mwilini mwake hujulikana alipo na kipi akifanyacho. Awali nilipokuwa nikiziangalia filamu hizo tangu nikiwa mdogo nilikuwa nahisi ni uongo wa wazungu lakini hapo nikaanza kuziamini moja kwa moja na nikabaki nikiwa nina shauku ya kukitoa hicho kitu nahisi ndicho kilichopo mwilini mwangu.

    Sarina alipomaliza kupika nilimueleza juu ya kila kitu nilichoambiwa na mtu aliyenipigia simu na nikachukua wasaa huo kumueleza kuwa inabidi nimuage ili niweze kwenda kuifanya kazi hiyo. Ilikuwa ni jambo gumu kulikubali kwa Sarina kwani alihofia usalama wangu katika sehemu ninayoelekea, nilimbembeleza akatulia na kukubaliana na uamuzi wangu na nilimpa ahadi kwamba ningerejea tu nitakapomaliza kazi hiyo kutokana na uwepo wa Ilham kwake ambaye kutunzwa kwake ni dhamana yangu. Pia uwepo wa mapenzi yangu kwake nj jambo jingine lililonifanya nimpe ahadi , nilitakiwa niuvae ujasiri ambao niliuvaa wa kutengana na huyu mwanamke niliyempenda kuliko kitu chochote kwa wakati huo. Ilham alipoamka naye nilimuaga ingawa sikumuambia naenda kufanya nini kwa muda huo, baada ya kumaliza kula chakula cha usiku niliondoka rasmi nikiwa nina vitu vyangu vya muhimu. Nilitumia gari yangu ambayo nilipewa na Jasmin baada ya kumburudisha kwa usiku mzima, gari ambayo ni gari yenye kasi zaidi duniani pia ni gari ghali sana niliamua kuitumia usiku huo na hata kwa safari zangu zinazofuatia. Nilipotoka nyumbani kwa Sarina nilikuwa nina kitita cha pesa ambacho nilipatiwa na Sarina kwa ajili ya matumizi ya dharura njiani, niliendesha gari kwa mwendo mkali ambao ulinifikisha katika hoteli ya Hilton kwa muda wa dakika takribani tano tu. Nilisogea hadi kwenye kibanda cha simu kilichopo jirani na hoteli hiyo ambapo nilimkuta mwanamke mrefu na mwembamba aliyevaa sweta lenye kofia pamoja na suruali akiwa amesimama, kofia ya sweta alilolivaa ilikuwa imefunika sehemu kubwa ya uso wake kiasi cha kutoweza kumtambua. Nilisogeza gari karibu na kibanda hicho cha simu kisha nikapiga honi mara moja na kupelekea yule mwanamke aje kwenye mlango wa mbele ulio pembeni ya dereva kwa upande wa kushoto. Niliruhusu mlango ufunguliwe naye akafungua kisha akakaingia ndani ya gari akaketi.

    "lets go (twende)" Aliniambia kwa kingereza tena kwa sauti ninayoijua kabisa ingawa uso wake sikuwa nauona kabisa, ili niuone uso wake vizuri ilinibidi nimvue kofia aliyoivaa kichwani na hapo ndipo moyo wangu ulipiga kwa nguvu hadi nikahisi ulikuwa unataka kupasuka kwani sikutegemea kumuona mwanamke huyu niliyemuona muda huo.

    "Nurulayt!" Nilijikuta nikutamka kwa mshangao baada ya kuiona sura ya Nurulayt kwa mara ya kwanza tangu miaka kumi ipite katika siku ambayo Huwaida alipoteza maisha, Nurulayt aliposikia natamka jina lake alinitazama vizuri usoni mwangu kwani mara ya kwanza hakuwa ameniangalia usoni.

    "Abdul! Ni wewe kweli?!" Nurulayt alijikuta akiniuliza kwa huku akinishika mashavuni mwake kwa viganja vya mikono yake, niliitikia kwa kichwa nikikubali kama ndiyo mimi huku mapigo yangu ya moyo yakinienda mbio. Nurulayt alikuwa kashaanza kutiririkwa na machozi ya furaha kwa kuniona mimi kwa mara nyingine kwani nilipomtazama nilimuona akinitazama huku akiwa na tabasamu lenye kuashiria kurudi kwa matumaini yaliyopotea kwa muda mrefu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "vipi unaishi huku siku hizi" Nurulayt aliniuliza akiwa anahema kwa nguvu kwa mshtuko uliotokana na kuiona sura yangu mahala hapo.

    "hapana Nuru ni matatizo ndiyo yamesababisha niwe huku, vipi wewe unaishi huku?" Nilimueleza kisha nikamuuliza swali, Nurulayt aliposikia swali langu alijiinamia kwa muda wa sekunde kadhaa kisha akainua kichwa akanitazama macho yakiwa yana na machozi.

    "Abdul sijui hata nianze kukueleza vipi?" Nurulayt aliongea kisha akaanzs kulia kwa sauti ya chini iliyoambatana na kwikwi.

    "usilie Nuru we nieleze" Nilimuambia huku nikimuinua kichwa, aliponyanyua kichwa chaks nilimfuta machozi yaliyoanza kumtiririka mashavuni mwake.

    "kwanza tuondoke hapa haraka sana" Nurulayt aliniambia huku akijifuta michirizi ya machozi iliyoanza kumtoka mashavuni mwake, nilimkubalia Nurulayt kisha nikaweka gia ili nirudishe gari nyuma niondoke lakini nilishtuliwa na kioo cha gari langu ambacho ni cha guza kikigongwa. Nilipoangalia nje niliwaona walinzi wanne wa hoteli ya Hilton wakiwa wameongozana na wanaume watatu ambao wawili kati yao walikuwa na sare za jeshi la polisi la nchini Namibia na mmoja alikuwa amevaa kiraia. Kengele ya hatari ililia katika kichwa changu nikajua moja kwa moja tukio nililolifanya hapo hotelini limekuwa kesi na watakuwa wamelikariri gari langu, nilipomuangalia Nurulayt naye alinisihi nisifungue na uoga ulionekana dhahiri kwenye macho yake. Wale walinzi wa hoteli waligonga kioo cha gari kwa fujo kisha mmoja wao akataka kuufungua mlango lakini nilikuwa nimeshaibana, nilipotazama nyuma niliona kuna magari mawaili ya polisi yamekaa yamekaa sambamba yakiacha uwazi ambao ungeweza kupita gari dogo linaloendeshwa na dereva mzoefu. Nilipowaangalia wale walinzi wa hoteli niliwaona walikuwa wanajadiliana jambo na wala maaskari kisha mmoja wa walinzi akawa anaishika bunduki yske vizuri akija kwenye kioo kwa mwendo wa kukazana. Nilipoona hivyo nilijua nini kinafuata hivyo nilimtazama Nurulayt nikamuambia, "funga mkanda". Nurulayt alifunga mkanda kwa haraka kisha akatulia, yule mlinzi alipokaribia kioo akalenga kioo kwa kitako cha bunduki aliyoishika ili avunje kioo awezs vifunga mlango afunguo mlango, mimi nilipoona hivyo nilikanyaga mwendo wa gari kwa nguvu na gari ikaanza kurudi nyuma kwa kasi ya ajabu hadi pale magari yalipoacha upenyo nikimuacha yule mlinzi akiwa ameanguka chini. Nililipitisha gari kwenye upenyo ule kisha nikalizungusha mithili ya pia kugeukia upande niliotoka, nilipohakikisha gari lipo sawa barabarani nilibadilisha gia nikitoa gia ya kurudi nyuma na nikanyaga mwendo kwa nguvu kuelekea upande wa kusini nikiwaacha wale maaskari wapo mdomo wazi jinsi nilipita kwenye uwazi ulioachwa na magari yao bila hata kuchubua gari. Nikiwa barabarani nilikuwa nikibadilisha gia kila muda na kuifanya gari ikimbie kwa kasi hadi nikawa naingiwa na hofu kwani sikuwahi kuendesha gari yenye mwendo mkali kama hii bugatti niliyopewa na Jasmin, nilipoaangalia nyuma nilikuwa siwaoni hata hao maaskari Niliona taa ndogo ya rangi bluu ikiwa inawaka yenye kama antena ya redio ndogo.

    "Shit! wamenibandikia GPS hawa" Nilisema huku nikikanyaga breki kwa nguvu halafu nikashuka nikaenda hadi nyuma, niliiong'oa ile antena nikaitupa halafu nikarudi ndani ya gari nikaendelea kuendelea kuendesha gari tena safari hii Nurulayt akawa ananielekeza pa kwenda. Baada ya kuhakikisha tumewapotea polisi kabisa tulielekea nje kidogo ya jiji la Widhoek katika kitongoji ambacho sikukijua jina na hata leo hii pia silijui, Nurulayt aliniongoza hadi kwenye nyumba yenye uzio mrefu pamoja na geti lililochakaa , alishuka hapo akafungua geti nikaingiza gari ndani kisha akafunga. Nilishuka kwenye gari nikaingia ndani nikimfuata yeye aliyetangulia kuingia katika nyumba iliyopo ndani ya uzio huo, nilikaribishwa katika nyumba isiyo na samani za kutosha zaidi ya viti vichache, makochi na meza.

    "Abdul karibu sana hapa ndipo ninapoishi" Nurulayt alinikaribisha kwa mara ya pili akiwa amekaa kwenye kochi la watu watatu sebuleni hapo.

    "asante Nuru, kumbe umejijenga hivi ukiwa huku ugenini hongera" Nilimwambia huku nikikaa jirani naye kisha nikamwambia, "enhee nipe mkasa mzima uliokufanya uwe huku".

    "Ni miaka mitano sasa imepita tangu nilipompoteza mwanangu na nikapopigiwa simu nije nchi hii nikitakiwa nifanye mambo ya kihalifu kwa miaka sita ndiyo nimpate mwanangu, sasa hata ulivyoniona pale nilikuwa nikikusubiri ingawa sikujua kama ni wewe ili twende Zimbabwe tukaibe kilo 500 ya almasi" Nurulayt alieleza sababu ya yeye kuwa katika nchi hii.

    "inamaana upo huku kwa ajili ya kumkomboa mwanao?" Nilimuuliza

    "si mwanangu peke yangu bali ni mwanetu, Abdul kumbuka mara ya mwisho nilikuambia nimebeba ujauzito wako. Sasa huyu aliyetekwa ndiye mtoto wetu" Nurulayt aliongea

    Maneno yake hayo yalinifanya nijifukirie kwa umakini kisha nikamuuliza, "unamjua aliyemteka?"

    Nurulayt alitikisa kichwa kukataa kama hamjui kisha akawa ananitazama usoni akiashiria anatala kunisikiliza nitakavyosema juu ya hilo.

    "inaonekana tunasumbuliwa na mtu mmoja ambaye sijui lengo lake ni nini?" Niliongea huku nikimtazama usoni.

    "tena anaonekana anajua kila hatua yetu na nyendo zetu" Nurulayt naye akadakia.

    "ni kweli usemayo kwani nimejigundua nina hardware baada ya kuona mshono ambao siujui" Nilmwambia Nurulayt kisha nikamsimulia kilichonikuta nikificha habari za Sarina na Ilham na nikamalizia hadi pale tulipoonana. Baada ya kumsimulia kisa hicho nilimuomba anisaidie kukitoa kifaa nilichohisi kipo mwilini mwangu naye akakubali bila ya kuweka walakini wowote. Nurulayt aliniamuru nimfuate nilipomuambia hivyo nami nikatii, tulienda kwenye chumba kimojawapo katika nyumba hiyo chenye mandhari ya wodi ya hospitali ambayo yalinishangaza sana katika nyumba hiyo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "usishamgae sana Abdul kwa mtu kama ninayefanya kazi haramu kama uhalifu lazima niwe na sehemu ya kujitibia majeraha madogo madogo ninayoweza kujitibu, lala hapo unioneshe hiyo alama ya mshono" Aliongea huku akinionesha sehemu ya kulala nami nikatii nikatii nikavua shati nikalala kifudifudi pale aliponioneaha. Nurulayt alichukua kifaa kilicho na umbo la mkasi uliochongoka kwa mbele akanitoboa pembeni ya mshono kisha akaingiza mkasi huo ndani ya ngozi yangu, nilikuwa nasikia maumivu kwa kitendo alichonifanyia lakini sikuwa na jinsi ilnibidi nivumilie tu. Nurulayt alitoa vitu mfano wa mbegu ya ngano vikiwa viwili mwilini mwangu, aliviweka kwenye mkebe wa hospitali wa chuma kisha akanionesha.

    "hizi ni hardware mbili tofauti ambazo uliwekewa katika mwili wako, moja hutumika kuonesha mahali ulipo na nyingine imenasa mfumo wako wote wa neva za fahamu na kila chochote unachokifanya waliokufunga hivi vitu wanajua" Nurulayt aliongea huku akinifunga jeraha lililotokea baada ya yeye kupitisha mkasi mgongoni.

    "asante sana, nafikiri ni muda wa kazi sasa tuliyopangiwa" Niliongea huku nikivaa shati baada ya Nurulayt kumaliza kunitoa vifaa vilivyokuwa vipo mwilini mwangu.

    "inabidi tuondoke hapa kuelekea huko tunapoelekea kwa ajili ya kumkomboa Ilham namuhitaji mwanangu tu" Nurulayt kwa kutaja jina la Ilham ambaye ana jina sawa na binti tuliyepewa mimi na Sarina, niliishia kushtuka tu lakini sikutaka kujiwekea uhakika asilimia mia kuwa yule ndiyo mwanangu na hata ningemuambia Nurulayt kuwa ninaye yupo kwa mpenzi wangu asingeweza kuniamini kwani mwanzo nilimficha nilipomsimulia juu ya masaibu yaliyonikuta. Hivyo niliamua kukaa kimya tu bila kumuambia jambo lolote juu ya Sarina na Ilham, Nurulayt aliniongoza hadi chumba kingine ambacho ukutani mwake kulikuwa kuna mageti ya kutokea nje. Ndani ya chumba hicho kulikuwa kuna gari aina ya diffender yenye rangi nyeusi isiyo na sehemu ya kuwekea mizigo, pia kulikuwa kuna silaha za kila aina za kupambana humo ndani ambazo nyingine nilikuwa sizijui.

    "Abdul kutumia bunduki si unajua?" Nurulayt aliniuliza huku akiniangalia usoni.

    "najua sana" Nilimjibu huku nikikumbuka kuwa nilipomaliza kidato cha sita nilipitia jeshi kama sheria ya Tanzania ilivyo kwa wahitimu, mafunzo ya kulenga shabaha bado yalikuwa yapo kichwani hivyo niliona ndiyo wakati muafaka wa kuyatumia katika kuokoa kila kilicho changu hadi mwanangu ambaye bado hakuwa huru kwa wazazi wake. Napenda nilishukuru jeshi la kujenga taifa kwa kunipa mafunzo haya ya kivita na hata ya kutumia silaha kwani mwanzo sikuyaona umuhimu wake niliyaona ni mateso niliyokuwa nayapitia tu ingawa nilizingatia mafunzo yote, faida ya mafunzo haya ndiyo niliiona katika siku hiyo ambayp ilihitajika nikomboe kila kilicho changu.

    "kurutuu! Shonaa tuliaa nyungu juu" Maneno ya maafande wakati nipo katika mafunzo ya kijeshi yalinirudia kichwani yalikuwa yanahusu kusimamia ngumi chini ukiwa umeambatanisha mikono yote, mazoezi haya ndiyo cha mimi kuweza kuhimili silaha ya aina yoyote na hata Nurulayt aliponiambia suala la silaha wala sikuwa na wasiwasi nalo.

    "mmh! Umejifunzia wapi?" Nurulayt aliniuliza baada ya kumkubalia kuwa najua kutumia bunduki.

    "depo miezi mitatu silaha nimeweza kushika, na bastola nimejifunza mwenyewe kwani nilikuwa nimenunua kwa ajili ya ulinzi nilipokuwa Dar" Nilimjibu Nurulayt huku nikitabasamu naye akatabasamu.

    "poa chukua silaha kiasi chako uingize kwenye gari hiyo katikati ya viti vya nyuma vuta kapeti ya gari kuna sehemu ipo na mlango, funguo uziweke humo" Nurulayt aliniambia huku akienda sehemu yenye silaha.

    Nilienda sehemu yenye silaha nikachagua bastola za aina mbili pamoja na maboksi kadhaa ya risasi, kwa bunduki kubwa nilichukua bunduki aina ya UZI ya nchini Israel ambayo imeundwa na mwanajeshi wa kiyahudi anayeitwa Uziel Gal mwaka 1948. Bunduki hii ni moja kati ya bunduki hatari duniani yenye uwezo kupiga risasi mfululizo kama ilivyo AK47, MP5 na nyinginezo, nilibeba risasi za kutosha na viwambo vya kuzuia sauti nikaenda kuviweka pale nilipoelekezwa.

    "vipi visu hubebi?" Nurulayt aliniulixa huku anipatia visu sita vikubwa, nilivipokea visu hivyo bila ya kusema chochote nikaviweka kwenye gari kisha nikamtazama kama anaweza kuniambia la ziada.

    "panda tuondoke" Nurulayt aliniambia nami nikazunguka mbele kwenye mlango wa pembeni ya dereva nikapanda.





    Usukani wa gari hili ulikamatwa na Nurulayt na safari ya kuelekea pori la Chirinda ikaanza mara moja baada ya geti lililokuwa lipo humo ndani kufunguliwa na kifaa maalum, baada ya gari kutoka geti lile lilijifunga tena kama ilivyokuwa awali na tukawa tupo nie ya nyumba hiyo kwa upande mwingine kabisa. Ilikuwa ni majira ya saa tano kasoro za usiku barabara ilikuwa tulivu sana kuliko kawaida, tulikuwa tukipishana na magari machache tu njiani yaliyokuwa yanaitumia barabara kwa muda huo. Tulirudi hadi katikati ya jiji la Widhoek kuifuata barabara ambayp sikuijua inaitwaje hadi muda huo, Nurulayt aliifuata barabara hiyo kuelekea mashariki ya jiji la Widhoek kwa mwendo wa kasi sana. Alikuwa akiweka gia na kutoa gia nyingine huku akicheza na usukani kwa umakini sana na kusababisha gari hii iende mwendo mkali hadi ikawa inatoa mlio kama wa kulalamika kwa kuendeshwa mwendo huo, gia tano za gari hii zilitumiwa ipasavyo na Nurulayt kama anaendesha gari ya mashindano hali iliyonisababisha nifunge mkanda mwenyewe kwani mwanzo sikuwa nimefunga mkanda. Baada ya muda mfupi tulikuwa tumeingia kwenye eneo la jangwa lisilo na majani wala nyumba za watu, tulipongia katila jagwa hilo ambalo nalijua kwa jina la Kalahari ndiyo mwendo wa gari ulizidi . Nurulayt hakuonekana kujali sana kwa mwendo aliokuwa anautumia yeye ndiyo alizidi kukanyaga mafuta hadi mshale wa mngurumo wa gari ukafika sehemu yenye alama nyekundu huku kengele ya hatari ikigonga kwa fujo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "we mwanamke sikuwezi hata kidogo" Nilimuambia huku nikisikitika kwa mwendo aliokuwa anautumia Nurulayt

    "kwanini unasema hivyo?" Nurulayt aliniuliza huku macho yake yakiwa makini kuangalia mbele.

    "huu mwendo sijui upo mashindano ya formula 1" Nilimwambia kuhusu mwendo anaoutumia tena niliufananisha mashindano maarufu ya magari ya formula 1 yenye magari yanayooenda kwa kasi sana, maneno yangu yalimfanya Nurulayt atabasamu kisha akasema "we unataka tutembee mwendo wa harusini unafikiri tutafika leo Abdul yaani hapa hatujafika Botswana halafu tunaelekea Zimbabwe".

    "Mh! Haya suka twende kazi" Nilimwambia kukatisha mazungumzo yetu kisha nikakaa kimya na sikuongea hadi Nurulayt alipopunguza mwendo akaingia kwenye sheli iliyopo pembezoni mwa barabara.

    "vipi mafuta yamepungua?" Nilimuuliza.

    "hayajapungua ila yanahitajika yaongezwe" Nurulayt alijibu huku akishuka kwenye gari baada ya gari kuliegesha gari jirani na mashine ya kujazia mafuta, Nurulayt alilipa pesa na gari ikajazwa mafuta hadi tenki lote likajaa kisha akarudi kwenye gari lakini hakukaa kwenye kiti cha dereva bali alikaa kwenye viti vya nyuma na kiti cha dereva kikabaki kitupu kama kilivyo.

    "Nuru mbona unakaa huko mbona sikuelewi ?" Nilimuuliza huku nikigeuka nyuma nikamtazama.

    "Abdul huelewi nini au mimi kuachia usukani kuja kukaa huku?" Nurulayt aliniuliza.

    "ndiyo maana yake hicho ndicho nisichokielewa" Nilimwambia.

    "Abdul hapa tupo karibu na West gate na West gate camp katika jangwa hili la Kalahari, mbele kidogo kiasi cha mita 500 kuna mpaka wa Trans Kalahari ambao unatenganisha nchi hii na Botswana na una ulinzi mkali. Sasa basi hatuwezi kuuvuka mpaka huo bila ya kuwa na mtu ambaye ni askari wa pale, nimetoka kwenye kiti cha dereva ili kumpisha askari niliyemkodi kwa ajili ya kutuvusha atuvushe" Nurulayt aliongea kunielewesha juu ya mpango wake ambao nilikuwa siujui kabisa.

    "hapo sawa nimekuelewa" Nilimwambia kukubali kuuelewa mpango wake mzima alioupanga, maelezo yake yaliniridhisha na nikatazama mbele.

    " sasa sikiliza" Nurulayt aliniambia huku akinivuta bega, niligeuka kumtazama ili kumsikiliza nini anachotaka kuniambia.

    "katika kazi kama hizi usipende kuwa muongeaji na muulizaji wa maswali sana, unatakiwa uwe kimya Abdul ingekuwa mwingine tayari ameshakupiga risasi" Nurulayt aliniambia huku akinitazama kwa umakini usoni, nilimsikiliza maneno yake kisha nikashusha pumzi halafu nikasema "poa" nikageuka mbele. Baada ya muda takribani dakika kumi kupita mlango wa dereva ulifunguliwa na mtu mwenye mavazi ya kiaskari aliingia ndani ya gari kisha akatutazama akasema, "samahani kwa kuchelewa".

    Askari huyu aliwasha akaliingiza barabarani na safari ikaendelea wote tukiwa kimya bila ya kuongea chochote, baada ya dakika tano tulikuwa tumefika sehemu hiyo ya mpaka ambayo ilkuwa na ukaguzi wa magari yanayotoka na kuingia nchini Namibia. Mpaka huo ulikuwa na njia mbili ambayo moja yanapita magari yanayokwenda nje ya nchi na nyingine yanapita magari yanayoingia ndani ya nchi, tulipokaribia eneo hilo yule askari aliwela gari kando akatuomba tumsubiri anarejea sasa hivi. Alishuka ndani ya gari akaenda kwenye ofisi zilizopo hapo mpakani, tulibaki tukiwa tunamsubiri na alirejea baada ya dakika takribani tatu kisha akaingia ndani ya gari safari ikaendelea tukawa tunaelekea kwenye mpaka kuvuka. Alipofika eneo la ukaguzi alitoa kadi na makaratasi akawaonesha askari ambao walimruhusu kupita bila hata kumuuliza lolote, tuliendelea na safari tukivuka bango kubwa linalo tukaribisha nchini Botswana. Yule askari aliendesha gari kwa mwendo wa mita takribani 400 kisha akashuka akatuaga akikutakia safari njema, baada ya askari kuondoka Nurulayt alirudi kwenye usukani kama kawaida na safari ikaendelea kwa mwendo ule ule wa kilevi. Baada ya saa moja tangu tuvuke pale mpakani tulitokea kwenye mji mdogo uliokuwa umechangamka sana, ilikuwa yapata saa saba za usiku na ilitubidi tuegeshe gari kando ya barabara ili tupumzike humo humo ndani ya gari kwa ajili ya usalama wa

    vitu vyetu, tulilala usingizi wa mang'amng'am hadi kunakucha tukaendelea na safari yetu. Usukani wa gari kama kawaida ulikamatwa na Nurulayt na mwendo wa gari aliupunguza kwa sababu tulikuwa tumeingia katika makazi ya watu. Tulitembea kwa umbali wa kilomita kadhaa tukawa tumefika sehemu yemmnye barabara mbili ambayo moja inaelekea kushoto na nyingine inaelekea kulia, Nurulayt alipokaribia njia hizo aliweka gari pembeni na jirani na mgahawa aliweka breki ya mkononi huku akiliacha gari likiwa linawaka.

    "twende tukanywe chai saa tatu hii" Aliniambia huku akiteremka garini nami nikamfuata bilab kuongea jambo lolote, tuliingia ndani ya mgahawa. Tulipata kifungua kinywa kwa pamoja na tulipomaliza tulirudi garini na safari ikaendelea huku macho yangu yakiwa dirishani kuangalia mandhari ya nchi hii kwa upande wa sehemu wanazoishi watu wenye hali ya chini. Baina ya zile njia zilizokuwa zimegawanyika sisi tulifuata njia ya upande wa kushoto, tulienda kwa mwendo wa masaa kadhaa tukawa tumefika sehemu yenye mji mdogo uliochangamka sana.

    "hapa panaitwa Maun ni sehemu iliyo karibu na hifadhi ya wanyama kwa upande wa kushoto na delta ya mto Okavango kwa upande huo huo" Nurulayt alinielezea juu ya sehemu iliyokuwa ipo mbele yetu.

    "ok" nilimuitikia kwa ufupi tu kisha nikakaa kimya nikimuacha Nurulayt acheze na usukani wa gari, Nurulayt naye hakuwa muongeaji sana baada ya kunielezea hivyo alikaa kimya akaelekeza umakini wake barabarani. Haikupita hata nusu saa tangu alivyonieleza hivyo usingizi mzito ulinichukua kutokana na uchovu nilionao uliotokana na kutolala usinfizi wa kutosha, nilikuja kuamka baada ya kusikia napigwa kibao huku jina langu likiitwa.

    "Amka wewe tukale jioni hii"Nurulayt aliniambia nilipofumbua macho kumtazama, hapo nilibaini giza llishaanza kuingia na tulikuwa tunaonana kupitia taa ndogo iliyopo ndani ya gari.

    Nilipiga muayo mrefu kisha nikamtazama Nurulayt ambaye alionekana kuchoka sana.

    "shuka bwana twende au wewe huhisi njaa?" Nurulayt aliniuliza baada ya kuona namtazama bila ya kushuka kwenye gari.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "hapa ni wapi?" Nilimuuliza bila hata kujali maneno aliyoniambia.

    "bwana hebu shuka huko mwanaume una maswali kama mwanao, nahisi kachukua tabia yako" Nurulayt aliongea huku akinisukuma nishuke. Muda huo yeye alikuwa tayari ameshafungua mlango wa upande wake alikuwa anasubiri mimi tu nishuke, nilifungua mlango nikashuka chini kisha nikaenda hadi upande aliopo Nurulayt ili aniongoze kuelekea hiyo sehemu ya kwenda kula kwakuwa nilikuwa mgeni ndani ya eneo hilo.

    "yaani wewe na mwanao mkikaa na mimi nahisi mtaniua maana mna maswali mengi kama polisi" Nurulayt aliendelea kuongea huku akinishika mkono kuelekea ndani ya nyumba moja yenye milango mikubwa ambayo ilikuwa ipo mbele yetu.

    "huyo mtoto kachukua tabia zako mimi unanipakazia tu" Nilijitetea kimasihara na kusababisha Nurulayt anisukume begani kimasihara.

    "Loh! Lione yaani mwanao nimekaa naye kwa miaka mitano tu lakini alipoanza kuongea kazi nilikuwa nayo ya kujibu maswali tu, na sasa nakutana na baba mtu habari ni hiyohiyo tu yaani kama mnanihoji vile" Nurulayr aliongea akiingia ndani nami nikamfuata, tulikuwa tumeingia kwenye mgahawa mdogo wenye watu wachache jioni hiyo. Nurulayt aliagiza chakula kama ilivyo kawaida yake halafu akaja kuketi meza moja nami, chakula kililetwa na kila mtu akawa anashughulika katika kulijaza tumbo lake. Hatukuongea hadi tulipotoka tularudi ndani ya gari, Nurulayt alienda kukaa kwenye kiti cha changu na mimi nikakaa kwenye usukani.

    "tunaelekea wapi sasa, nahitaji nijue sio unaniachia usukani tu bila kusema cjochote" Nilimwambia Nurulayt.

    "hapa tupo Nata kwenye njia tatu zinapokutana, fuata barabara inayoenda kusini mashariki hadi katika mji unaoitwa Francistown" Nurulayt aliniambia huku akikinyoosha kiti cha gari miayo ikimtoka mdomoni mwake, niliwasha gari nikaingiza barabarani na safari ikaendelea kuutafuta mji wa Francis town nikiwa nimewasha taa za gari kwani nuru ya anga ilishaanza kupotea. Baada ya dakika thelathini tangu niingize gari barabarani Nurulayt alikuwa tayari yupo kwenye usingizi mzito sana na kama isingekuwa mkanda wa gari angekuwa kajigeuza ovyo hadi kufikia kuiparamia gia ya gari, siku hii niliendesha gari kwa mwendo wa kasi nikiomba tufike salama kwani sikuwa mwenyeji wa barabara ninayoitumia na alama za barabarani ndiyo kitu pekee kilichonisaidia kuniongoza katika barabara hiyo. Hadi inatimu saa nne ya usiku tayari nilikuwa nimeshafika katika mji wa Francistown uliopo kilomita 185 kutoka Nata nilipotoka, nilipofika hapo ndipo nikamshtua Nurulayt usingizini na nilimtaarifu tumefika tayari.

    "ingia hiyo barabara inayoelekea kushoto na uende hadi utapokuta sheli yenye supermarket" Nurulayt aliniambia maneno hayo alipomaliza alirudi tena kulala.

    Niliingiza gari barabarani kwa mara nyingine nikawa naelekea barabara inayoenda kushoto kati ya barabara tatu zilizopo mbele yangu, barabara hizi kwa Tanzania ningezifananisha na makutano ya barabara ya Segera yanayokutanisha barabara tatu zinazoelekea Tanga mjini, Kilimanjaro na Mkoa wa pwani. Eneo la Nata na hili la Francistown lilifanana kila kitu muundo wa makutano ya barabara zilivyo, niliamua kuwa makini na alama za barabarani kwani hizo ndizo zilikuwa msaada kwangu katika kuniongoza na barabara ya huku ili niweze kufika salama bila hata kupata ajali yoyote. Nilitumia kiasi cha dakika 45 nikawa nimefika katika sheli aliyonielekeza Nurulayt, hapo nilimuamsha tena na nikamtaatifu kuwa nimeshafika. Nurulayt aliamka kisha akatazama mazingira ya hapo kwenye sheli halafu akashuka akaniambia," sogeza gari sehemu ya kuwekea mafuta". Nilisogeza kama alivyoniambia kisha akaongea na na mhudumu wa hapo sheli, alipomaliza alichukua mpira wa kujazia mafuta akatia mafuta hadi mshale wa mafuta katika kioo cha plastiki kilichopo chini ya usukani kikaonesha tenki la gari limejaa. Alifanya malipo kisha akarejea ndani ya gari alipokuwa awali, alipokaa kwenye kiti nilimuangalia usoni nilitarajia aseme lipi juu ya hii safari.

    "Mbona unaniangalia hivyo?" Nurulayt aliniuliza.

    "nahitaji kujua nini kinachofuata Nuru" Nilimwambia huku nikiwa sijatoa jicho langu usoni mwake.

    "ok ok ni hivi, nusu kilomita kutoka hapa kuna mpaka wa Ramekgwebana unaotenganisha Botswana na Zimbabwe. Hivyo inabidi uruke kiti cha nyuma kuna askari wa uhamiaji atakuja kutuvusha hapa kama tulivyovuka kule Trans kalahari border" Nurulayt alinipa maelezo ya mpango unaofuatia. Baada ya dakika kadhaa tangu anipe maelezo hayo nilimuona askari wa mmoja aliyebeba mkoba mkubwa mgongoni akija hadi kwenye gari letu usawa wa mlango wa dereva, alipofika niliamua kuruka kiti nyuma kwani nilijua fika ndiye mtu tunayemsubiri. Yule askari alifungua mlango wa gari akaingia huku akiwa anahema sana akiwa na mkoba wake ambao aliupakata mapajani alipokaa kwenye kiti cha gari.

    "mambo si mazuri huko" Askari aliongea huku akitutazama kila mmoja.

    "vipi huko kuna nini?" Nurulayt aliuliza

    "muda mfupi uliopita hapo mpakani walipita watu wakiwa na gari yenye mizigo mingi ambayo haikujulikana ni vitu gani, walipekuliwa wakakutwa na na unga na walipotaka kukamatwa wakaanzisha vita ndogo. Wamefanikiwa kukimbia na gari lao la mizigo kuingia mpaka Zimbabwe kinguvu lakini waliishia msituni wa jirani na mpaka, na hivi ninavyokuambia wanafanya majibizano ya risasi na askari na mpaka mzima umemwagwa askari" Yule askari alieleza sababu ya mambo kutokuwa mazuri huko mpakani.

    "sasa itakuwaje?" Nurulayt aliuliza akionekana kuchanganyikiwa sana na maelezo hayo.

    "njia pekee ya kuvuka pale mpakani ni kuvaa sare za kama hizi zangu na viatu" Aliongea yule askari huku akifungua mkoba mkubwa alioingia nao akatupatia sare za askari wa uhamiaji pamoja na viatu vya kijeshi.

    "mkivaa nguo za askari wa uhamiaji mtajulikana ni askari waliongezwa na makao makuu kwenda kupambana na hawa wasafirishaji madawa ya kulevya na mtaruhusiwa kupita. Badilisheni hapahapa" Yule askari alituambia.

    "ok hamna shida ila wewe inabidi ushuke tubadilishe nguo kwani mimi ni mwanamke na huyu ni mzazi mwenzangu, hupaswi kuniona nikibadili nguo labda yeye kwakuwa hakuna asichokijua katika mwili wangu" Nurulayt alimuambia yule askari

    "mh! OK hamna shida" Yule askari alinitazama kwa jicho la pembeni halafu akatabasamu akaonesha kukubaliana na maneno ya Nurulayt, alishuka ndani ya gari kwa haraka na sisi tukabadilisha kwa haraka halafu tukamuita tulipomaliza kuvaa. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hapo safi kabisa yaani mpo kama askari wa uhamiaji, chukueni na hizi bunduki mzishikilie ili wakituona wajue mnaingia kazini" Yule aliongea baada ya kutuona tukiwa tumevaa magwanda ya askari wa uhamiaji, alifungua ule mkoba tena akatoa bunduki mbili aina ya short gun akatupatia pamoja na mikanda ya risasi. Safari ya kuelekea kwenye mpaka wa Ramekgwebana iluanza na askari yule ndiye aliyekuwa dereva, gari letu lilipoingia barabarani alitoa king'ora cha kubandika akampatia Nurulayt ambaye alikiweka juu ya paa la gari. Mpakani tulifanikiwa kupita bila matatizo na kweli kulikuwa kuna maaskari wengi wakiwa na wana silaha kama hizi tulizokabidhiwa, safari yetu iliendelea na tukawa tumeingia kwenye pori lililopo mwanzaoni mwa nchi ya Zimbabwe. Furaha ilidhihirika machoni mwetu kwa kufanikiwa kukivuka kikwazo kile lakini furaha hii haikudumu kwani dosari kubwa iliingilia furaha hii, tukiwa tupo katikati ya pori usiku majira ya saa sita milio ya risasi ilianza kusikika na vioo vya gari letu vikaanza kupasuka.Yule askari ambaye ndiye aliyekuwa dereva wetu alitoa ukelele wa maumivu akiachia usukani wa gari

    na gari likaingia pembeni ya barabara nusura ligonge mti baada ya yeye kuwahi kukanyaga breki ya gari.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog