Search This Blog

Friday, 20 May 2022

MSITU WA SOLONDO - 5

 







    Simulizi : Msitu Wa Solondo

    Sehemu Ya Tano (5)



    Amata alipiga ukelele baada ya kumuona swahiba wake Golam katika dimbwi la mahaba na wasichana wale akataka kwenda katika chumba kile lakini alizuiwa na bibi yule

    “huwezi fika walipo”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    bibi kizee alimwueleza Amata.

    “Nyie binadamu mnatusumbua sana, kuna mambo mengi tunataka kwenu hasa hisia na akili”

    bibi kizee alimueleza Amata huku akimuongoza kusikojulikana na nyuma yao kulifuatiwa na mabinti wale warembo wenye nywele zinazoning’inia mpaka chini ya viuno vyao. Walifika eneo tulivu sana lililojaa kila aina ya ufahari, Amata alikaribishwa kuketi katika jiwe moja kati ya mengi yaliyokuwa hapo. Na mabinti wale waliowafuata waliwazunguka na kuketi chini, Amata aliwatolea macho mabinti wale muda wote

    “Amata!”

    bibi kizee aliita

    “jambo mnalolifanya ni jambo la hatari sana, sisi wenyewe na maarifa yetu yote ya nguvu ya chini hatuwezi jaribu, tumeshashindwa muda mrefu”

    bibi kizee aliendelea kumueleza Amata naye alisikiliza kwa makini

    “Gorino ni viumbe hatari, si binadamu wale hata sisi wametuzidi uwezo”

    bibi kizee aliendelea kumuasa Amata, Amata alimsikiliza huku akipepesa macho yake huku na kule. “Tamaa yenu binadamu ndiyo inawafikisha pabaya, kwa nini hamridhiki?”

    bibi aliendelea kuongea na Amata ambaye kwa wakati huo akili yake haikuwa hapo hata kidogo. “Bibi, naomba unisaidie, bila shaka wewe unajua wenzangu wote walipo”

    Amata alimkatisha bibi kizee. Cheko la ajabu lilimtoka bibi yule

    “Kijana nitakusaidia lakini kwa sharti moja, na wewe unisaidie”

    bibi alijibu na kutoa la moyoni

    “sema bibi, nipo tayari kukusaidia”

    Amata alidakia na kujibu,

    “mimi nataka roho hai ya Kelume”

    bibi alitoa ombi lake

    “Kelume! Ni nani huyo?”

    Amata kwa mshangao aliuliza

    “ha ha ha ha ha! Kelume ni kiongozi wa Gorino, nataka roho yake hai”

    Bibi kizee alimjibu Amata, Amata alifikiri sana juu ya ombi lile na alipoinua kichwa chake kumtazama bibi yule alikutana uso kwa uso na Bundi mkubwa aliyesimama juu ya kipande cha mti kilichopo mbele hapo, Amata alimtazama bundi yule mara bundi yule aliruka na kutokomea mbali. Amata alinyanyuka pale alipoketi alipoangalia huku na huko aligundua kuwa yuko mahali tofauti na alipokuwa mwanzo, alitulia kidogo na kuvuta akili.

    Alivuta hatua chache mbele yake na kupanda juu ya jiwe kubwa lililopo hapo, na alipofika juu alijilaza kifudifudi na kuangalia kwa makini pande zote, kwa mbali aliona kitu kama mlima na chini yake aliona kama kusanyiko kubwa la watu, Amata hakuelewa vizuri kama ni watu au ni nini, aliteremka kutoka katika jiwe lile na kusonga mbele kupitia katika vichaka vyenye miiba na mawe ilimradi tu afike mahali ambapo angeona kwa uzuri zaidi. Aliteremka bonde kubwa kwa taabu sana na alipofika chini aliendelea kwenda kwa umakini zaidi kuelekea upande ule alipowaona wale watu, jua lilianza kuchwea na kagiza mororo kalianza kuufukuza mwanga hafifu ulioujaza msitu huo, Amata alijibanza katika jiwe mojawapo na kutulia akisubiri giza litawale ili ajue nini cha kufanya.







    **************************************





    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Hellen alitulia kimya akifuatilia nyendo za mtu huyo ambaye alikuwa akiingia pangoni mle kwa kunyata, akiwa bado na kamba miokononi na miguuni alijiegemeza katika ukuta wa pango lile. Yule mtu aliendelea kusogea alipo Hellen, akanyoosha mkono wake na kumshika mguu Hellen, Hellen hakuleta tabu yoyote alitulia tu kuona nini kinaendelea, yule mtu alimburuza Hellen hadi nje ya pango, ‘Gorino’ Hellen alishangaa na kuingiwa na woga, sasa alijaribu kujinasua lakini hakuweza kwa kuwa alikuwa amefungwa kamba mikono na miguu, mtu yule alitoa tabasamu baya ambalo Hellen alitema mate, kwa kitendo hiko alistukia kofi moja kali lililomrusha upande wa pili, Hellen alilia kwa uchungu. Huku akijigalagaza kama mtoto. Lile pande la mtu likamjia tena Hellen lilimwangalia kwa sura yake ya kutisha iliyopakwa vitu vya ajabu na kuchanjwa chale nyingi, harufu yake ilimfanya Hellen kuhisi kichefuchefu, Hellen aliliangalia lile jitu ambalo lilionekana lina uchu wa kitu fulani toka kwa hellen, likaanza kuongea lugha isiyojulikana, Hellen hakuelewa chochote kinachosemwa aliendelea kulitazama lilipokuwa linamfuata pale alipo, Hellen alijaribu kujisogeza lakini hakuweza. Lile jitu likamkamata Hellen kwa mkono wake wenye nguvu na kumuinua kutoka pale alipokuwa amekaa, likamwangalia na kuanza kumshikashika makalio na mapaja huku mkono mmoja likiwa limemshika bega Hellen, Hellen alihisi maumivu makali sana begani mwake na hakupenda hata kidogo jitu lile lilivyokuwa linamshikashika namna ile lakini hakuweza kujinasua, lile jitu likaanza kumshika kiunoni taratibu likapitiisha mkono wake kifuani na kuanza kuyaminya matiti, Hellen hakuvumilia hata kidogo alijivuta nyuma kidogo na kuachia kichwa kilichompata kwenye mwamba wa pua, damu nyingi zikaanza kuvuja kwenye pua ya jitu lile, hasira zikatawala, lile jitu likachukua mti uliochongwa mbele ambao walitumia sana katika kutoa mioyo ya binadamu, liliunyanyua na kumshambualia Hellen, Hellen alinyayua mikono yake kujikinga uso, mti ule ulipita karibu na uso wa Hellen, Hellen aligeuka upande wa pili na kushudia mikono yake ikiwa huru kumbe mti ule ulikata zile kamba, kazi! Hellen akiwa chini alijifungua kamba za miguu kwa haraka na kusimama kulikabili jitu lile ambalo lilikuwa bado linajaribu kufuta damu zile. Lile jitu lilipotahamaki lilimuona Hellen akianza kukimbia, lilitoa kamba kiunoni na kuirusha miguuni kwa Hellen, Hellen aliruka samasoti moja na lipotua aligeuka nyuma kuliangalia jitu lile lililokuwa likimfuata kwa kasi, Hellen aliruka teke maridadi lililotua shavuni kwa jitu lile lakini halikuonekana kutetereka hata kidogo, Hellen alipotua chini alipiga goti moja na kujizungusha kwa kasi na kumpa ngwara maridadi lakini jitu lile halikuanguka. Hellen alijinyanyua na kurudi nyuma hatua chache kupanga mashambulizi upya kabla hajajiweka sa alijikuta akipata gumi moja la shavu lililompeleka chini, alijibiringisha na kunyanyuka haraka hakujali maumivu wala damu zilizomtoka mdomoni, alipata gumi linigine nalo likampeleka chini sasa hakuweza kunyanyuka mara moja alitambaa kama mtoto kuelekea kule kulikoangukia ule mti wa yule gorino, jitu lile lilipoona mbinu ya Hellen likamfuata Hellen kwa kasi lakini alichelewa Hellen alichukua ule mti na kujigeuza haraka na kuwa chali, jitu lile lilijirusha kuchukua ule mti lakini badala ya kuuchukua lilijikuta likitua kwenye ncha ya jiti lile ambalo lilididimia katikati ya kifua chake, lilitoa macho mpaka likakata roho, Hellen alilisukuma kwa miguu yake na kulitupa pembeni. Hellen alinyanyuka na kuliangalia lile jitu likiwa najiti lake kifuani

    ‘kumbe na mi naweza’

    alijisemea moyoni, ndipo alipogundua kuwa jino moja lilitoka mdomoni mwake na mawili yamelegea, alitema mate yaliyochanganyika na damu, aliendelea kutema lakini aliona damu ile haiishi aliondoka taratibu eneo lile na kuingia ndani zaidi ya msitu ule, hakuwa hata na hamu ya kutaka kujua nini kimejiri katika msafara ule. Alikimbia taratibu huku akipambana na nyasi ndefu miti yenye miba na mawe yaliyomfanya mara nyingi kupunguza mwendo wake huo. Hellen alijikuta amechoka lakini hakukata tamaa huku akiwa anasali kimoyomoyo aliendelea kukimbia na kuomba akutane na mmoja wao lakini haikuwa hivyo aliendelea kukimbia na kuomba asikutane na wanyama au viumbe wabaya.

    Giza lilianza kuitawala nuru, Hellen akawa amechoka sana akaanza kutembea taratibu na kwa kuwa alikuwa anaogopa giza aliona njia pekee ni kujificha sehemu au kupanda juu ya mti. Akiwa katika usingizi alisikia mlio wa ngoma kwa mbali kidogo, moyo ulimlipuka na kwenda mbiyo maana aliitambua ngoma hiyo ‘Gorino’alijiwazia akijua kuwa kumbe hawakwenda mbali na walipomuacha, ndiyo maana hata yule mmoja alifanikiwa kurudi kirahisi. Hellen alijitahidi kupanda kwa shida kwenye mti mmojawapo angalau ajiepushe na wanyama wapitao huko chini, na alipokuwa juu ndipo alipogundua kuwa mti ule ulikuwa umebeba mtango uliotambaa vizuri na matango makubwamakubwa yakining’inia

    “Thanks God!”

    Hellen alijikuta akiongea kwa sauti na kuanza kuyashambulia matango yale kwa fujo, aliporidhika akapitiwa na usingizi akiwa amekumbatia tawi la mti huo.







    **********************************************************







    Alipozinduka ulikuwa usiku mzito sana aliona kwa mbali moto ukiwaka na ngoma zikirindima, Hellen aliangalia na kupata shauku ya kwenda japo alijua ni Gorino waliopo huko kwa kuwa alishauzoea mdundo wa ngoma ile, alipiga moyo konde akashuka kwa uangalifu wa hali ya juu, aliweka miguu chini taratibu na kutazama huku na kule alipoona usalama upo alianza kutembea taratibu kulikabili bonde kubwa ambalo chini huko ndiko alikoona moto ule

    ‘itakuwaje wakinikamata’

    alijiuliza bila kupata jibu, lakini hakusita alisonga mbele kwa kujiamini lakini kila muda aligeuka nyuma kutazama kama kuna yeyote anayemfuata, mara moja akiwa katika kugeuka nyuma alijikuta akitereza na kuporomoka katika bonde refu, alijipiga katika miti na mawe kadhaa yaliyopo katika poromoko hilo.





    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/





    ******************************







    Saringo alinyata kwa ustadi sana akihakikisha hakuna anayeona hata unyasi ukitikisika, punde si punde alitokea kwenye jiwe kubwa sana jeusi ambalo juu yake limebeba mawe mengine yaliyokaa katika mitindo tofauti. Saringo hakuwa na woga hata kidogo akiamini kabisa kuwa kama kufa ni kufa tu, aliendelea kunyata kulizunguka jiwe lile ambalo lilichukua eneo kubwa sana, huku akisikia midundo ya ngoma na nyimbo asizozielewa alijaribu kutafuta sehemu ambayo angeweza kuona ni nini kinaendelea, akiwa katika kuzunguka alichuchumaa nyuma ya jiwe moja ambalo lilikuwa na tundu katikati na kupitia hapo aliweza kuona ngoma ile japo kwa taabu kidogo. Ghafla alihisi mkono wa mtu ukimshika bega, taratibu Saringo aligeuka kwa woga kwa kuwa alikuwa hajui ni nani aliyemshika bega, moyo ulimlipuka na kwenda mbio baada ya kuona gorino wawili wamesimama nyuma yake, alijinyanyuka pale alipokuwa amechuchumaa na kuegemea jiwe akitazamana na wale gorino walioonekana kuwa na hasira kali.



    Giza liliivamia nchi, sherehe ya kafara ya Gorino ilianza kwa kuwasha moto katia mienge mingi waliokuwa nayo, ngoma na nyimbo zilirindima katika msitu ule, huku na huku katika mawe yale walionekana kuzunguka na kumwaga vitu fulani fulani. Saringo alitulia kimya kabisa katika moja ya jiwe alilohifadhiwa lakini aliweza kuona kila kinachoendelea mahali pale. Mbele ya jiwe hilo aliweza kuona kitu kama shimo kubwa linaloelekea chini na giza nene lilitawala ndani humo, Saringo alijiuliza kama hapo ndiyo mahali pale alipoelezwa na babu yake au bado alikuwa hajafika, lakini hakuwa na la kufanya kwa kuwa mpaka muda huo hakujua ni nani kafa au yuko hai katika kundi lao zaidi ya Golam aliyepotea msituni.



    Mbala mwezi ilianza kung’aa na sherehe ya kafara ilizidi kunoga, Saringo hakuwahi kuona ngoma kama hiyo ya ajabu katika maisha yake, lakini jinsi ilivyochezwa ilimvutia sana na hata wakati mwingine alicheka japo hakutoa sauti. Mara watu wawili wakaja hadi pale alipo na kumfungua kisha kutoka nae moja kwa moja katikati ya ngoma ile, Saringo alijaribu kujinasua lakini mikono ya gorino ilikuwa na nguvu za ajabu Saringo hakuweza hata kutikisika alipiga kelele lakini hazikusaidia, alijikuta katikati ya gorino waliomzunguka huku na huku, Saringo hakuwa na ujanja, hakuwa na lakufanya alibaki kutazamana na Kerume aliyevimba kwa hasira maana katika utaratibu wa mwanamke hakuruhusiwa kuwepo eneo la kafara. “Beliiiigo!!!”

    Kerume alitoa ukelele na ngoma ile ilinyamaza kimya kikuu kikatawala

    “ Losa, losa, losa ilo seleke”

    akimaanisha “hii hii hii ni laana” kwa hasira alizokuwa nazo Kerume hakuweza kujizuia alimsogelea saringo na kumpiga makofi kadhaa ya nguvu yaliyompeleka chini, wafuasi wa Kerume walimnyanyua na kumsimamisha wima, Saringo alikuwa akitweta kwa uchungu na hasira lakini hakuwa na cha kufanya. Kerume aliangalia huku na huku na kumyang’anya mfuasi wake mmoja mti aliokuwa akiutumia katika ngoma ile na bila kuchelewa aliunyanyua na kuuteremsha kwa pigo lisilo huruma kifuani mwa Saringo, Saringo alipiga ukelele wa uchungu pale jiti lile lilipotua mwilini mwake, akapiga magoti na kudondoka chini kifudifudi damu zikimmwagika.

    Kerume alinyoosha mikono yake juu na kutoa ishara fulani. Mwili wa Saringo uliondolewa katika eneo lile na ngoma ile ilianza upya. Ngoma ilipokolea mmoja wa mateka alitolewa pangoni akiwa na kamba shingoni akivutwa kama mbuzi na kupandishwa juu ya jiwe mojawapo lililo katikati ya kiwanja kile na kulazwa chali, Kerume alishuka kutoka alipokaa na mti wake maalumu kwa kazi hiyo, aliunyanyua na kushusha pigo moja kifuani mwa mtu yule alipouchomoa mti ule ulitoka na moyo, yowe la uchungu lilisikika na mtu yule uhai ukamtoka, wengine walitega midomo yao kunywa damu iliyokuwa inaruka kwa kasi kutoka katika mwili ule. Ngoma ilizidi kuchanganya, gorino wengine walionekana wakitoka katika pango lile na mtu mwingine ambaye alikuwa ni mbishi sana na hakutaka kabisa kwenda, kipigo alichopewa hakikuwa cha kawaida mpaka alipopoteza nguvu walimbeba na kumrusha katika pango lingine kubwa zaidi. Joka kubwa lilimdaka kabla hajafika chini na kumviringa kisha kupotea nae pangoni. Kelele za Gorino zilisikika kwa nguvu zaidi wakishangilia kwa kuwa kafara yao ilipokelewa.



    Damu nyingi ziliendelea kumtoka Saringo pale alipotupwa na Gorino ambao walikuwa wakijiandaa kumchuna ngozi ili wapate nyama kama walivyoagizwa, kwa kuwa wao hawakujuwa kama mtu yule amekufa au la, waliendelea kuchuna kamba na kunoa vitu kama visu walivyotaka kutumia kwa kazi hiyo. Walimchukuwa Saringo na kuanza kumfunga kamba mikononi ili wamning’inize tayari kuchuna ngozi ile, walipotaka kumnyanyua ndipo mmoja alisukumwa na mkono wa Saringo kwa nguvu hafifu sana akajua kumbe hajafa

    “soliti igola!”

    alimwambia mwenzake akimaanisa mbona hajafa. Alichukua jiti lake na kutaka kumdidimiza Saringo moyoni lakini kabla hajatimiza azma yake alianguka chini na kurusharusha miguu na mikono huku na huku uhai ukimtoka. Mwenzake aliangalia huku na huku hakuona mtu

    Mwenzake aliangalia huku na huku hakuona mtu alipomwangalia mwenzake alikuta mshale umemdidimia katika koromeo na macho yamemtoka pima, alitazama huku na huku hakuona mtu tena aliweka mikono yake mdomoni akitaka kupiga mbinja akachelewa kichwa chake kilitawanywa na ubongo wote ukamwagika hakuweza hata kufurukuta alirushwa na kuangukia upande wa pili, mwingine alikuwa mbali kidogo akiandaa hiki na kile akashtushwa na kishindo kile akarudi na njiani akakuta kiwiliwili cha mwenzake, alitazama vizuri na kujigeuzageuza, akanyanyuka na kuelekea kule walikokuwa wakitaka kumchuna Saringo, alipofika alikuta mwili usio na uhai wa mwenzake nao umelala pale lakini hakuona ile nyama yao, alionekana wazi kuchanganyikiwa hakujua afanye nini, katika kuzubaa huko kamba ilimnasa shingoni na kumnyanyua juu alirusharusha miguu lakini taratibu sana roho iliacha mwili, mwili wa marehemu yule ulianguka chini na kutulia kimya.



    Hellen aliipachika bastola yake kiunoni, akisaidiana na Amata waliubeba mwili wa Saringo aliyeonekana bado anapumua kwa mbali, Hellen alijitahidi kumpa tiba angalau kuokoa damu iliyobaki na kufunga jeraha lile kwa kutumia blauzi yake, Hellen aliamua kubaki na kanguo kepesi ka ndani tu baada ya kuichana blauzi yake ili kumsitiri Saringo, Amata alileta maji na kumnywesha Saringo ambaye alionekana kupoteza nguvu nyingi sana hasa kwa kutokwa na damu, kimvua chembamba kilinyesha usiku ule na hii ilikuwa ni ahuweni kubwa kwa Saringo, Hellen aligundua kuwa pigo lile la Kerume kwa saringo halikutua sawasawa moyoni kwake sipokuwa lilipiga chini kidogo na kuvunja mbavu karibu mbili tatu za juu za upande wa kushoto. Amata aliingia porini nakuja na aina fulani ya majani ambayo aliitafuna na kuweka katika jeraha lile na kufunga vizuri. Walipohakikisha Saringo yupo salama wakaanza kupanga mikakati jinsi ya kuvamia eneo lile, kundi lile la Gorino liliwatisha sana kila walipojiangalia silaha walizo nazo zisingeweza kufanya chochote. Hellen aliifungua ile karatasi aliyopewa na Amata akaangalia vizuri mchoro ule na maandishi yote yaliyoandikwa mle akagundua kuwa pale katika lile jiwe ndiyo kuna pango la hazina.

    “Tupite nyuma ya jiwe, ili tuwatokee kwa nyuma”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hellen alimuambia Amata kwa kiswahili cha kubabaisha, Amata aliangalia vizuri eneo lile ambalo kwa wakati huo halikuwa umbali wa kutisha waliweza kuona kila kitu kinachoendelea, walimuacha Saringo pale baada ya kumuhifadhi vizuri na wao kuteremka bondeni kisha kwa mwendo wa kunyata walilizunguka eneo lile na kutokea kwa nyuma kama walivyopanga. Walitafuta eneo zuri ambalo wangejificha lakini pia wangeweza kuona vizuri ili kujua nini wafanye, Amata na Hellen walijificha vizuri katika kichaka kidogo lakini si mbali na eneo lile huku wakiwa makini kuona kama kuna chochote cha kuwasumbua, alilivua podo lake na kuhesabu mishale ilobaki, si haba ilikuwa kama ishirini na tano na alipotazama kundi lile alikuta kuna Gorino zaidi ya mia moja Amata alichanganyikiwa akamtazama Hellen ambaye wakati huo naye alikuwa akihesabu risasi alizonazo baada ya kupewa kikasha kile na Amata si haba zilikuwa kama mia na ishirini akamnyoshea alama ya dole gumba Amata naye akajibu kwa mtindo uo huo.

    “Subiri hapa mi nasogea mbele nione wanafanya nini!”

    Amata alimueleza Hellen

    “Wapo kwenye kafara hata mimi nilikuwa kwenye msafara huo, wanaua watu, kuna watu kama kumi na tano hivi”

    Hellen alimueleza Amata. Amata alijivuta taratibu mpaka karibu na jiwe kubwa lakini hamad! Alijikuta amekutana na Gorino aliyeko katika ulinzi wa eneo hilo, Amata alimtazama na kabla Gorino yule hajakaa vizuri alijikuta akipaa hewani kwa ngwala safi aliyopigwa na Amata, alitua kama mzigo na alipofika chini bisu kubwa la Amata lilidimia kifuani mwa Gorino yule na kupoteza uhai. Amata alitazama huku na huku kuhakikisha usalama kisha akaendelea kusogea upande wa pili kulizunguka jiwe lile, kabla hajakata kona alimuona Gorino mwingine aliyekuwa kasimama akitazama upande mwingine Amata alifikiri atumie mbinu gani kumuondoa lakini alikosa kwa kuwa hakuwa tayari kutumia uta wake kwani alibakiwa na mishale michache, alifikiri kama atumie mikono kumkabili lakini akaona inaweza kuwa mbinu mbaya endapo atazidiwa nguvu, aliokota jiwe la kutosha na kulirusha kwa nguvu zote na kumpiga kisogoni, Gorino yule aliyumba na alipokaa sawa aligeuka nyuma uso uso kwa uso na Amata, Gorino alirusha jiti lake kwa Amata lakini Amata aliepa kwa ustadi na shabaha kukosa uelekeo, Amata alidakwa koo hata akajikuta anakosa nguvu alijikusanya na kupiga kifuti kimoja kati maeneo nyeti ya Gorino yule, kutokana na maumivu yale alimuachia Amata ambaye alichukua nafasi hiyo kumtandika mateke mawili ya usoni yaliyomfanya anyanyuke kisha Amata akajirusha mzimamzima na kutua kwa miguu miwili kifuani mwa Gorino yule ambaye aliyumba tena na kujipigiza kwenye jiwe, damu zilimtoka kwa wingi kisogoni akajibwaga chini na uhai ukaambaa zake, maiti! Amata alipanda polepole juu ya jiwe lile lakini kwa kuwa alikuwa haoni anakoelekea kumbe mmoja wa Gorino alikuwa kule juu, Hellen alimuona vizuri sana Gorino yule lakini alifikiria afanyeje kama angetumia bastola yake basi ile kelele ingewashtua wengine, moyoni aliteseka lakini hakujua afanye nini alibaki kutazama tu kitachotokea. Amata alishika vizuri jiwe la juu ili ajivute lakini mara akahisi kitu kimemkanyaga, hakusita aliendelea kujivuta na hapo alijikuta ameshikwa mikono yake na yote miwili na Gorino yule na kuvutiwa juu ya jiwe lile, Amata alijinyanyua na lipo simama wima alimpiga kichwa Gorino yule na kumsindikiza kwa makonde mfululizo, Gorino alipepesuka lakini Amata alimdaka na kumgeuzia upande wa pili ambapo alimponyoka na kuanguka kutoka juu ya jiwe lile kabla hajafika chini joka kubwa lilichomoza kutoka pangoni na kudaka juu kwa juu na kuteremka nae chini mpaka pangoni Amata alibaki na bumbuwazi.







    ***************************************









    Kule chini ngoma ya Gorino iliendelea na kafara ziliendelea kutolewa, tayari watu karibu watano walikwishauawa kinyama na eneo lote lilikuwa likinuka damu lakini kwa Gorino hiyo ilikuwa ni sherehe kubwa sana waliimba na kucheza wala hawakujua kama kuna wenzao waliokwishapoteza maisha kati usiku huo. Kerume akiwa juu ya jiwe lililochongwa kama kiti na wafuasi wake aliendelea kusherehekea karamu ile ya damu zalondigo, huku akitafuna nyama mbichi. Alitolewa mtu mwingine tayari kwa kafara akapandishwa juu ya jiwe lile la kutolea kafara ambapo wakishamkata kichwa lazima kidondokee pangoni na damu yake kutiririka kuelekea uko huko ambako wao waliamini kuwa Kolilo ndimo anamoishi. Alikuwa ni kijana wa makamu aliyekuwa akileta upinzani wa hali ya juu ili asipelekwe katika jiwe lile, Gorino walimshika vizuri na kumburuza kumpeleka jiweni walimpandisha na kumfunga panapotakiwa tayari kwa kutoa kafara ya damu.

    Hellen kutoka mbali aliweza kuona kila kinachoendelea na alipoona huyo kijana akamkumbuka kwa kuwa alifungwa jirani yake wakiwa kama mateka kule msituni, alilia kwa uchungu, akachukua bastola yake akaiweka sawa ‘liwalo na liwe’

    akajisemea moyoni akaanza kuitafuta shabaha lakini hakujua nani hasa anayemlenga Kerume au wafuasi wake

    ‘atakayenyanyua mkono wake tu ninaye’

    alijisemea huku akiuma meno aliweka bastola yake na domo la revolver lilikuwa tayari tayari kutekeleza litakachoamriwa na mkono wa Hellen. Gorino walipiga kelele kama ishara ya kutekeleza agizo la Kerume, Gorino mmuaji ambaye mwili wake wote ulichafuka damu ya binadamu alinyayua juu lile jiti lake tayari kwa kazi, kabla hajashusha alipaishwa juu na kujibwaga kama mzigo jeraha kubwa lililokuwa kifuani mwake lilimfanya ashindwe kuyashinda mauti, bastola ya Hellen ilifuata maagizo sawasawa. Amata akiwa juu ya lile jiwe alishtushwa na mlio ule na moja kwa moja alijuwa kuwa Hellen keshafyatua risasi na kuwachokoza Gorino. Hali ya eneo lile ilivurugika gorino walitawanyika eneo lote kutafuta adui wao wakiwa na munkari wa kuua yeyote watakeyemuona. Amata alitegemea kwa hali ile wote wangeweza kumuacha Kerume ili amtoe uhai kama alivyokubaliana na Bibi kizee lakini haikuwa hivyo gorino karibu ishirini walimzunguka Kerume wakirukaruka huku na huko ingekuwa wamasai tungesema wamepandisha mori. Gorino walizunguka wakiwa hawajui ni nani wananemtafuta sherehe imevurugika, Amata alijikuta akinaswa kwa kamba mguuni ambayo ilimuangusha kutoka juu ya jiwe lile mpaka chini na uta wake ukimtoka mkononi Gorino ailiyemvuta kwa kamba ile alinyanyua jiti lake ili kumchoma lakini haikuwa hivyo wakati kageuka kuangalia juu alijikuta kichwa chake kikifumuliwa kwa risasi kutoka kwa Hellen, Hellen alihama haraka kutoka katika kichaka kile na kukimbilia nyuma ya mbuyu mkubwa uliopo mahali hapo, sasa kwake ilikuwa ni kama kulipa kisasi kwa yote ambayo walimfanyia akiwa mateka, hakutaka hata kidogo kumpoteza Amata katika macho yake, alibaki bado anamwangalia pale alipoangukia, akiwa anajizoa zoa Gorino mmoja alikuwa akimjia kwa kasi akifuatiwa na wengine nyuma yake huku wakipiga kelele yule wa mbele hakufika kwani nae alipaishwa juu na kifua chake kilifumuliwa vibaya na risasi nyingine ya Hellen, Amata kwa haraka alinyanyuka na kuokota uta wake lakini kabla hajajiweka sawa alipata pigo moja la mgongoni alihisi kupigwa na kitu ka jiwe aligeuka kwa kasi na kuchomoa jisu lake pigo moja la shingo liliruhusu jisu lile kupenya Amata akalichomoa wakati huo akimsindikiza na teke kali la nyuma gorino wa pili ambaye alipepesuka bila uelekeo na kuangukia kando. Kerume alipagawa na kuchuka uta wake wenye nguvu ya ajabu aliweka mchale wake na kuuvuta shabaha kuelekea kwa Amata aliuachia na kasi uliotoka nayo haikuwa rahisi binadamu wa kawaida kuuepa...



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ********************************************



    KIUMBE cha ajabu kilimtokea Saringo katika maficho yake, Saringo ambaye wakati huo hali yake ilizidi kuwa mbaya kwa kupoteza damu nyingi alikuwa ametulia kimya hana la kufanya na alikuwa akiangalia tu nini kitatokea. Alitamani sana kwenda kuwasaidia wenzake kwa kuwa aliona jinsi walivyobanwa na Gorino katika mapambano yale lakini alishindwa kabisa. Alijikaza lakini alikuwa anaogopa mno jinsi kiumbe kile kilivyoonekana, kilisimama mbele ya Saringo na kumwangalia kisha kikamsogelea na kunyoosha mkono wake kuelekea jeraha la Saringo. Kiumbe kile kilikuwa na vidole virefu na kadiri ya umbali vilikuwa vikirefuka kuelekea kwa saringo na alimpogusa jeraha Saringo alihisi ganzi mwili mzima na kuzirai.

    Bibi kizee alikuwa akipita eneo la mapambanao kwa umbo la Bundi lakini alishindwa kabisa kutoa msaada wowote ka Amata na Hellen, hakuwa mbali kwa kuwa kile alichokubaliana na Amata kilikuwa bado hakijatimia. Katika eneo lile ilikuwa vigumu kwake kujigeuza na kuwa katika umbo lingine kutokana na uchawi wa hali ya juu ambao Gorino waliuweka eneo lote la tambiko, hivyo ilikuwa ni vigumu kwa viumbe vingine kutawala eneo lile au hata kupita ilikuwa ni vigumu kwao. Na katika pambano la Gorino kumuondoa bibi kizee na wasichana wake eneo lile ilikuwa kazi ngumu kwa kuwa kila mmoja alikuwa na zindiko lake mahali pale, lakini Kerume kwa kutumia uta wake wa kichawi aliweza kuwashinda bi kizee na wasichana wake ambao hata wao miaka mingi nyuma walikuwa wakifanya matambiko yao hao, na humo ndani ya pango walihifadhi vitu vyao vingi ambavyo Kerume alipowashinda alifunga kwa kuzindika na nguvu zake za kichawi hivyo bi kizee na wasicana wake wakawa kama watumwa wa Gorino. Bibi kizee alimuomba Amata Roho ya Kerume akimuahidi kumpatia kila atakachopata.

    Saringo alikimbia taratibu kuelekea eneo la mapambano alimuona Hellen alipokuwa akipambana na Gorino wale kwa kutumia bastola yake ambayo ilikuwa karibu na kwisha risasi. Amata akiwa na uta wake mkononi sasa lengo lake lilikuwa ni kumtafuta Kerume lakini katika pango aliloingia kulikuwa na walinzi watano baada ya mmoja kuuawa, akiwa katika mwendo wa kuchechemea alijaribu kukwepa vishale vya Gorino ambavyo vingi vilimwandama yeye.

    Hellen hakuamini kumuona Saringo eneo lile, Saringo aliingia katikati na mkononi akiwa na kitu kama mfupa ambao aliutumia kama silaha kwa kuwapigia Gorino wale lakini alichoshangaa ni kuwa kila aliyempiga nao hakuweza kupona, aliendelea kupambana na Gorino waliosalia eneo lile kwani wengine wlitawanyika hawakuonekena ila walijificha kwa kuwa hawakujua la kufanya. Kingusu aliwaandama walinzi wa Kerume kwa kupiga mishale kwa ustadi mpaka walipoukiambia mlango wa pango aliloingia Kerume, Amata alipotaka kuingia alihisi kitu kumpiga kichwani akarudi nyuma na kuangalia juu mmoja wa Gorino alimpiga Amata kwa kutumia kitu kama nazi, Amata alipanda juu ya jiwe na kumrushia kisu kilichompata sawia kifuani. “Amataaaaaaaaa!!!!!” sauti kali ya Saringo ilimfanya Amata ageuke nyuma kitendo hicho ndicho kikamfanya apone kutoka katika msahale uliopigwa kutoka pangoni, mshale wa Kerume mshale wa kichawi usiokwepeka na binadamu, Amata alipepesuka na kuanguka chini, alimuona Kerume akitoka Pangoni na kuja nje, Amata alijiinua haraka na kusimama kidete uso kwa uso na Kerume. Kerume alimvamia Amata kwa nguvu Amata akaepa upande na kumpiga ngwala lakini Kerume aliruka na kusimama sawia, akageuka na kumpiga Amata na kikoto cha mfupa Amata aliyumba na kuanguka karibu na mlango wa pango, Kerume alimfuata akiwa na hasira lakini kabla hajamfikia Amata, Kingusu alifyatua mshale uliopita mbele ya uso wake pale alipoukwepa, Kerume aligeuka na kutazama juu ya mti akamuona nyani mkubwa “Beselo sito!” akimaanisha ‘huu ni mwisho’ akachukua mchanga na kuupulizia kule alipo nyani yule punde si punde nyuki walijaa eneo hilo na kuanza kuuma kila aliyekuwepo. Hellen na Saringo walilala chini lakini haikusaidia, nyuki walimzingira Hellen aliyekuw akijaribu kukimbia kutafuta pa kujificha, Hellen aliumwa na nyuki wnegi waliompelekea kukosa nguvu na kuanguka chini, Saringo hakuwa na la kufanya juu ya nyuki wale wakali.

    Amata alipata muda wa kunyanyuka na kuegemea jiwe, Kerume alinyanyua jiti lake na kumchoma Amata kifuani lakini Amata alibonyea chini na jiti lile likapiga kenye jiwe, Amata alipita katikati ya miguu ya Kerume na kutokea nyuma yake aliruka teke la kusukuma na kutua mgongoni mwa Kerume ambaye aliyumba kwenda mbele na kabla hajageuka mshale wa Amata ulikuwa njiani alipogeuka tu uso kwa uso na mshale ule lakini Kerume aliudaka kwa mdomo wake akaugeuza na kuurusha kwa mdomo na mshale ule ulichomoka kwa kasi ya ajabu, Amata alishindwa afanyeje lakini kabla hajaamua jambo mshale ule ulikosa nguvu na Amata akaudaka kwa mikono yake. Kerume kwa kutumia kikoto chake cha mfupa alimpiga Amata mapigo ya kifo lakini Amata alikwepa yote kwa ustadi huku akirudi nyuma mwisho Kerume alirusha kikoto kile Amata alikwepa, Hellen alikuwa anajaribu kunyanyua uso wake ndipo alipohisi maumivu makali katika paji la uso, kikoto cha mfupa kilichorushwa na Kerume kilitua usoni kwa Hellen, Hellen aliona giza kuu likiyavamia macho yake, kutoka pale alipodondoka wakati akishambuliwa na nyuki alijilaza tena.

    Amata alipigwa kichwa na Kerume, alijitoa kwenye mikono ya Kerume na kurusha ngumi mfululizo ambazo zilimpata Kerume lakini hakutetereka hata kidogo. Amata alijifanya kukimbia kuelekea kwa Saringo na Kerume alimfuata, Saringo alimrushia Amata ule mfupa na Amata alipoudaka tu aligeuka na kumtandika Kerume kichwani, Kerume aliyumba na kabla hajatulia Amata alimpiga tena kichwani pigo ambalo lilimpeleka chini Kerume hakiwa hajiwezi, akiwa anatambaa kujisogeza na Amata alikuwa akitembea kumwangalia, akamkanyaga kichwani na kukishindilia kichwa kile katika mawe. Upepo mkali ukaanza kuvuma miti yote ikawa ikiyumba kwa kasi ya ajabu, vumbi lilitimka eneo lote. Amata aliona mwanga wa ajabu uliong’aza eneo lote, mwanga wa rangirangi za kumetameta, Amata akanyanyua uso wake kuangalia mbele na juu ya jiwe lile alimuona Saringo kasimama akiwa na upanga mkononi, upanga uliokuwa ukitoa mianga ya ajabu na mkono wake wa pili ameshika kichwa cha chui.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Saringo!” Amata aliita huku akiondoa mguu wake pale alipomkandamiza Kerume.

    “Mimi sio Saringo” alisema mwanamke yule huku akishuka mpaka pale chini alipolala Kerume, sasa akiwa uso kwa uso na Amata. Akampa Amata kile kichwa cha chui kisha akanyanyua upanga wake juu kwa mikono miwili. Kelele zilisikika msituni za watu wakilia na kuomboleza, upepo nao aulizidi kuvuma eneo lote, Saringo bandia akashusha upanga na kukata Shingo ya Kerume, kichwa chake kiliachana na kiwiliwili lakini cha kushangaza kiwiliwili kile hakikutoa hata tone la damu. Saringo bandia akakitupa kichwa cha Kerume katika moto uliokuwa ukiwaka eneo lile kisha akachukua kichwa cha chui kutoka kwa Amata na kukisemea maneno fulani ambayo Amata hakuyaelewa na kukipachika kile kichwa cha chui katika kiwiliwili cha Kerume na muda huo huo Kerume akageuka Chui mkubwa wa kutisha, Saringo bandia aliongea maneno fulani na Chui yule akakimbilia msituni.

    Amata alibaki mdomo wazi huku akionekana na sura ya woga, akageuka nyuma na kumuona Hellen akiwa kalala chini akamfuata na kumtazama alionekana kama hana uhai, aliyageuza macho yake na kuona tayari ni mfu. Amata alidondosha chozi, mara akasikia kama kundi la watu likija mahali pale alipogeuka aliona kundi la Gorino likiwa limesimama nyuma yake.

    “Usiogope Amata” yule Saringo bandia alisema

    “Hao wote ni mateka wangu, hawana nguvu tena kwa kuwa Kerume zindiko la kichwa cha chui amerudi alikotoka” aliendelea

    “Hapo unapowaona hawajaja wenyewe wamekamatwa na kuletwa. Tumerudi kwenye himaya yetu ya Msitu wa Solondo, katika pango la Mtukufu Baghoza hakuna aliye juu yetu ila wote wako chini yetu, na sasa ni zamu yetu kutoa kafara kwa Baghoza” Saringo bandia aliongea na Amata wakati Amata akiwa bado kamshika Hellen ambaye tayari mwili wake ulikuwa wa baridi kabisa.

    “Amata, umefanya kazi tuliyokuwa tumeishindwa kwa karne na karne, unastahili zawadi kubwa kuliko unavyofikiria.” Saringo bandia alimwambia Amata

    “U nani wewe? Mbona unafanana na Saringo?” Amata aliuliza

    “Mimi ni Baghoza, kinara wa roho zisizoonekana. Unisamehe Amata, nilimkuta Saringo anakata roho nikauchukua mwili wake lakini hapa tunavyoongea ameshakufa” Saringo bandia aliinamisha kichwa kuonesha masikitiko

    “Baghoza!” Amata alitamka na kupiga magoti mbele ya Saringo bandia, akaendelea

    “Kuliko kunipa zawadi yoyote, naomba nirudishie uhai wa watu wangu”

    “Ha ha ha ha ha haaaaaa, Baghoza hata kama ndiye mleta mauti na mtoa uhai, siwezi kukutimizia hilo kwa sababu moja” akatulia kidogo kisha akaendelea “Solondo si eneo la kuishi ninyi binadamu, kama sisi hatuji kwenu na sisi hatupendi mje kwetu. Mnafata nini huku?” Saringo bandia aliendelea kumwambia Amata

    “Wewe hukutaka kuja huku, hata hujui huku kuna nini, ila hawa wenzako wana tamaa ya mali na utajiri hata ijapokuwa wanajifanya wanafanya utafiti, sisi tuna uwezo wa kuona fikra zenu. Amata kumbuka tamaa mbele mauti nyuma, kwa tamaa yao wote wamekufa na hawataamka tena. Ila wewe kwanza umetusaidia kurejesha himaya yetu hatuna budi kukupa zawadi, na ukishaondoka hapa sisi tutaendelea na ibada yetu ya kafara” Saringo bandia alisema hayo huku akiwa na upanga wake mkononi. Aliunyoosha upanga wake na ukaanza tena kutoa ile miale ya mwanga iliyoangaza eneo lote pale katika jiwe, mara upepo ukaanza tena kama mwanzo sasa ulikuwa wa kuzunguka na ukakusanya vumbi kubwa kisha katikati ya upepo ule Amata aliona kama mtu kasimama na ulipotulia alimuona bibi kizee kasimama pale na hakumuona tena yule Saringo bandia. Yule bibi kizee akamsogelea Amata, akainua mkono wake na kutoa pete iliyokuwa iking’aa sana iliyowekwa jiwe la yaspi safi na kwa ndani ilikuwa na madini kutoka sayari ya Uranus. Amata akaipokea na kuigeuzageuza ilikuwa ikitoa rangi nyinginyingi.

    “Vaa katika kidole cha kati mkono wa kushoto” bibi kizee alitoa maelekezo. Amata akavaa na alipomaliza aliona mji mkubwa sana mbele yake majengo marefu marefu na wanawake wazuri warembo wa kuvutia wenye nywele ndefu, hakika mji ule ulikuwa ni wa kipekee, cha ajabu aliona wanawake tu na ailipogeuka nyuma yeke alijikuta kazungukwa na wadada wengi sana, Amata alistaajabu aliyoyaona hapo, akanyanyua mkono wake na kuitoa pete ile kidoleni, akajikuta yupo palepale msituni na mbele yake bibi kizee akimwangalia, aligeuka nyuma na kuona hakuna wale wasichana isipokuwa Gorino walioletwa pale.





    “Vaa katika kidole cha shahada mkono wa kushoto” bibi kizee alimwambia Amata. Amata akavaa pete ile katika kidole cha shahada, mbele yake aliona moto mkubwa ukiwaka katika shimo, cheche kubwa za moto zilikuwa zikiruka na kurudi shimoni, alisikia vilio vya watu wakilia kwa maumivu makali na kusaga meno, Amata aliangalia vizuri na kuona watu wengi wasio na idadi. Amata akatoa machozi akalia kwa vikwifukwifu kwa kuwa aliwaona Hellen, saringo, Stephan na Golam wote wakiwa katika mateso hayo. Aliivua pete ile na kuishika mkononi. Alijikuta tena na bibi kizee.

    “Bibi kwanini rafiki zangu wapo huku?” Amata aliuliza

    “Watu wote wenye tamaa ya mali huishia huko, huwezi kuingia Solondo ukafika kwenye jiwe hili kama una tamaa ya mali. Hizi mali ni zetu, kila penye madini na sisi tupo na tunayalinda sana. Hawa Gorino walitufukuza hapa na kuchukua wao, wakamuweka huyo nyoka wao wa ajabu, huyo hakuwa nyoka wa kawaida, mshale wa Kingusu ndiyo umemmaliza huyo Nyoka.” Bibi kizee alimueleza Amata na kisha akanyanyua kichwa chake kuangalia angani akaendelea kusema

    “ Mwezi umekuwa mpevu, huu ni muda wetu. Amata naomba tuagane, pete hiyo utaivaa kila utapoitaji kuonana na sisi, utaivaa kidole cha kati kisha utaigonga kwa kwenzi mara tatu utafunguliwa mlango, ukigonga mara nne utaomba chochote tutakupa. Tahadhali, usiigonge mara moja wala usiigonge mara mbili.” Bibi kizee alimuasa AmataCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sasa pita katikati ya hilo pango kubwa, huko chini utakuta mambo mengi sana usiogope utakutana na viumbe wa ajabu usiogope, teremka chini mpaka ngazi ya kwanza kutoka ya saba utakuta milango imejipanga nenda mlango wa kwanza kutoka wa tano fungua uingie pale utakuta vitu vingi sana chagua kadiri ya uwezo wako uende zako” bibi alimaliza kuongea

    “Bibi, nitajuaje njia ya kwenda kwetu? Hata nilivyokuja sijui” Amata aliuliza tena

    “Amata muda umeisha tunataka tuanze kazi yetu, nenda sasa ingia haraka kimbia, imetosha, tena usigeuke nyuma kabisa” sauti ya bibi ilianza kuwa ya kutisha yenye mwangwi wa ajabu. Amata aliiuacha mwili wa Hellen na kuingia pangoni kwa kasi, nyuma yake alisikia radi kali na ngurumo za ajabu.

    ???

    GIZA nene lilitanda kila kona ya pango lile, Amata hakuweza hata kuona wapi anaelekea, alivuta hatua fupifupi kwa kuwa alihisi kama akiteremka ngazi, nyuma yake alisikia tu kama vitu vikianguka na watu wakipumua kwa nguvu alitamani kugeuka lakini alikumbuka maneno ya Baghoza, alijikaza na kusonga mbele, alizidi kuteremka chini zaidi huku akipapasa kwa kuwa hakuweza kuona hata umbali wa urefu wa mkono wake. Woga ulimtawala, nguvu zilimpungua alihisi akikosa hewa ya kutosha, akiwa bado anaendelea kuteremka alihisi amekanyaga kitu, akarudisha mguu kisha akakanyaga tena akuhisi kile kitu, akaendelea kuteremka ndipo alipohisi mguu wake ukishikwa na kitu kama mikono akaanza kusikia sauti kama ya siafu wengi waliokuwa wakitembea, Amata alifikiri kurudi nyuma lakini alikumbuka maneno ya Baghoza, moyo wake ulikosa la kuamua akanyanyua mguu kwa nguvu lakini bado hakuweza ndipo alipoinama kushika kilichopo mguuni alijikuta akipigwa kofi la utosini lililompelekea kudondoka katika ngazi zile na kuviringika kuelekea chini zaidi. Alisikia sauti za vicheko zikimsindikiza na alipofika chini kabisa utulivu ulirejea kama mwamnzo, sasa hakuweza kusikia vya nje wala vya ndani. Amata alinyanyuka na kuketi, kila mara mwili ulimsisimka lakini hakuweza kuona chochote katika pango lile. Alipokumbuka maelekezo aliyopewa na bibi kizee Amata alihisi kupata ganzi kani hakukumbuka kuhesabu ngazi alizoshuka hivyo hakuweza kujua yuko ngazi ya ngapi, alijishika kichwa na kujilaumu nafsi yake kisha akasimama na kuendelea kushuka lakini hakukuta ngazi za kushuka bali ukuta ulimkinga hakuweza kusonga mbele, aliposhika kushoto na kulia kote aliona vivyo hivyo, hakuwa na budi zaidi ya kurudi nyuma ili aweze kuhesabu ngazi zile. Lakini akiwa katika kutafakari afanyeje maana aliambiwa asithubutu kugeuka nyuma, aliikumbua pete yake aliyopewa na bibi kizee aliunyanyua mkono wake na kuigonga kwa kutumia kwenzi mara nne pete ile ikabadilika na kuwa ya buluu,

    “ninaomba msaada nimepote pangoni na kuna giza sana” Amata alimaliza kusema kisha kutulia kama sanamu. Upepo mwanana ukaanza kuvuma katika pango lile mara Amata aliiona mienge iliyotundikwa pembeni ya ukuta ule ikiwaka mmoja baada ya mwingine, baada ya muda mfupi pango lile lilikuwa linang’aa, Amata alichomoa moja ya mienge ile na kuanza kupanda ngazi zile kwa kurudi nyuma bila kugeuka. Aliendelea taratibu mpaka alipofika mahali alipoelekezwa, pale akakuta kuna lango kubwa bila kuchelewa na mwenge wake mkononi akaingia na kuvuta hatua chache alihisi kuna viumbe vikipita mbele na nyuma yake vikiwa katika shughuli mbalimbali lakini hakuweza kuviona kwa macho. Pango lilijawa na nyzi nene za buibui kila kona zikiashiria kuwa humo ndani ni muda mrefu hakujaingiwa na mtu. Katika kutazama uku na huku akaona milango kadha wa kadha imejipanga na kuwekwa makufuli makubwa. Alihesabu milango ile lakini ilikuwa ngumu sana kwa kuwa aliona kama inamzunguka, alikata tamaa mara akakumbuka maelekezo ya bi kizee akaaza kuhesabu tena sasa akaupata mlango aliyouhitaji, mlango mkubwa wenye kufuli nene akajaribu kutoa yale mabuibui na kuufikia. Mlango ule ulikuwa na picha ya kichwa cha nyoka mkubwa sana, Amata aliusogelea na akaona kichwa kile kinapata uhai na kufungua mdomo wake tayari kutema mate, Amata aliogopa na kurudi nyuma, alipojaribu kusogea tena ikawa vilevile. Amata akanyanyua mkono wake akaigonga pete yake mara nne “fungua” akatamka neno hilo. Mara aliona kufuli lile likifunguka kana kwamba kuna mtu aliyefungua na mlango ukajisogeza kwa ndani, Amata akajitoma ndani, chumba kilikuwa ni kitupu pembeni kabisa kulikuwa na jeneza lililochongwa michongo ya ajabu ajabu. Amata alisimama na kuliangalia jeneza lile lililojaa vumbi akalishika kufungua, alipoondoa mfuniko wake alipigwa na bumbuwazi, kulikuwa na ngazi zikishuka kuingia shimoni, Amata aliingia na kufuata ngazi zile kuteremka chini kabisa ya shimo lile, ndani ya shimo lile mlikuwa na giza nene, Amata alishuka taratibu akisaidiwe na ule mwenge alioushika mkononi mwake alipokaribia chini alianza kuona vitu viking’aa kutokana na ule mwanga wa mwenge alioushika. Amata alitabasamu alipoona vitu vile vilivyojawa vumbi na buibui kufanya makao yake, sahani, vikombe, vitu mbalimbali vya thamani vilivyotengenezwa kwa madini ya dhahabu, almasi, vito vya madini mbalimbali kama yaspi, quartz, marmar. Amata alibakia kaduwaa hajui wapi shike wap aache, alipouona mkufu alimkumbuka rafiki yake Chausiku ‘huu utamfaa’ alijiwazia. Alizunguka huku na huku na hakujua afanye nini. Alibaki kufikiria hatima ya maisha yake na mawazo yake yalisafiri dunia nyingine akimkumbuka Chausiku binti Saidi ambaye ni muda mrefu hakumuona.





    HATIMA

    Amata akiwa juu ya jiwe kubwa alikuwa na furaha sana alipomuona mtoto wake akicheza na mama yake Chausiku binti Saidi, alitabasamu alipowaona wakikimbizana pale katika nyasi za kijani sana zilizojawa kila aina ya rutuba.

    Moyo wake uliridhika na ulijawa na furaha alipotazama nyumba yake nzuri kijijini pale, mashamba makubwa aliyokuwa akimiliki, sasa hakuwa mkulima wa jembe la mkono bali alikuwa akimiliki trekta kubwa, mifugo iliyokuwa hapo ilizidi kupendezesha eneo kubwa lililomilikiwa na kijana Amata.

    Amata alikuwa akiangalia picha alizotengeneza kutoka katika kamera ile ndogo aliyoichukua kwa Stephan, picha za kutisha, picha za Solondo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliteremka kutoka katika jiwe lile na kuungana na familia yake katika mchezo ule mzuri, walicheza na kufurahi pamoja Amata, Chausiku na mtoto wao. Hakika Chau alikuwa ana haki ya kuwa na furaha kwani alikataa wanaume wengi sana ili kumsubiri Amata atoke gerezani hakujua hata kidogo masaibu yote yaliyomkuta katika safari yake ya hatari. Alijawa na furaha tu alipomuona kijana huyu yupo pale kijijini lakini sasa akiwa mtu tofauti sana, alimkumbatia kwa furaha zote na baada ya muda mfupi wawili hawa walifunga ndoa na kuishi pamoja na kujenga familia yenye furaha.

    Na hapa msemo wa wazee ulitimia...

    ‘Ridhiki ya Mbwa iko miguuni mwake’



    MWISHO



0 comments:

Post a Comment

Blog