Simulizi : Msitu Wa Solondo
Sehemu Ya Nne (4)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Saringo akashtushwa na kitu kilichomgusa mgongoni kitu kama tone la maji baridi sana, akafumbua macho taratibu kuangalia nini kilichomgusa,mwanga mkali ukamfikia machoni alipotazama juu akagundua kuwa kumbe alikuwa ndani ya kitu kama chungu kikubwa ambacho kifunikwapo giza lake huwezi kuona hata umbali wa sentimeta mbili, alijishauri kutoka mle ndani lakini aliogopa kwa kuwa hakujua nini atakachokikuta huko nje,alitega sikio lake kwa umakini asikie chochote kitakachosemwa na waliopo huko nje lakini hakuna alichosikia isipokuwa mvumo tu wa upepo mkali ambao hata hakujua unatoka wapi na unaelekea wapi, hofu ilimtoka kidogo na kuchukua uamuzi ‘natoka liwalo na liwe’
alijisemea moyoni
‘ah! Lakini vipi nikikutana na haya majitu huko nje si yatanifanyia mbaya!?’
nafsi nyingine ilimuuliza moyoni ‘ah! Kama kufa ndo nshakufa ngoja nitoke mengine ntajua ukohuko’ alijipa moyo tena kisha kwa nguvu zote alijinyanyua na kujitokeza juu ya ule mdomo wa kile chungu, alichokikuta huko nje hakutegemea kwanza vumbi kali lilimfikia machoni na kumfanya apate shida kwa macho yake kupambana na vumbi lile alijitahidi kufungua jicho mojamoja lakini ilikuwa ngumu, upepo mkali wenye vumbi na matakataka ulifunikiza eneo lote alilopo hata asiweze ona vizuri, bila kusita alipanda kwenye kile chungu na kujirushia nje, akiwa amelala kifudifudi alijinyanyua shingo yake na kuangalia kilichopo japo kwa taabu alisikia kelele na vitu kama nyimbo zilizokuwa zikisikika upande wa pili wa msitu huo, Saringo taratibu alianza kutambaa kwa staili ya nyoka kuelekea kule alikosikia nyimbo zile alihisi kuwa akisimama atembee wangemuona kwa urahisi. Akiwa kachafuka na vumbi lile aliendelea kujisongeza kwa taabu lakini hakuona dalili zozote za kiumbe eneo lile, alipofika ndani ya vichaka alijinyanyua na kukaa kitako akiegemea mti mmojawapo, kelele zile zilisikika kwa nyuma katika umbali mfupi tu, zingine zikishangilia na zingine zikilia, Saringo alijawa na hofu pale tu alipoona mbele yake kiumbe kifupi kikimtazama kwa umakini, alishikwa na hofu kuu alianza kutetemeka na mapigo ya moyo kumuenda mbio, kiumbe kile kilitoa mngurumo wa ajabu huku kikinyanyua sura yake kuangalia juu kama kikiita wengine, domo lake kubwa liliachama na ulimi wake mweusi kujitokeza nje, Saringo alinyanyuka na kuanza kutimua mbio lakini kabla hajafika mbali alijikuta akitumbukia kwenye korongo refu na kufikia kwenye tope zito ambalo hata kujigeuza ilikuwa tabu, tope lenye kunata, alijigeuza huku na huku lakini alihisi uzito sana, alipoangalia alikotoka aliona viumbe kama vile alipovihesabu vilikuwa yapata vitano hivi, pembeni aliona mzizi mkubwa na mrefu ulioning’inia kutoka mti mkubwa uliopo juu ya korongo lile, Saringo alikumbuka mafunzo aliyoyapata alipokuwa katika mafunzo ya jeshi la kujenga taifa, aliushika mzizi ule na kwa taabu sana alianza kupanda kutoka mle ndani ya tope lile zito, alijivuta kuelekea juu taratibu aliweza kufanikiwa huku viumbe wale wakiwa wamesimama palepale Saringo hakuogopa aliendelea kukwea kwa ujasiri mkubwa mpaka kufika juu katika shina la mti ule alijaribu kutazama huku na huku hakuona tena viumbe wale, alijinyanyua na kuanza kufuata kule alikosikia kelele zile, baada ya kutembea mwendo kama wa dakika kumi na tano hivi alijikuta katokea kwenye eneo lile alikokuwa akisikia kelele zile, Saringo alishika midomo yake kwa kutoamini alichokiona pale.
alijinyanyua na kuanza kufuata kule alikosikia kelele zile, baada ya kutembea mwendo kama wa dakika kumi na tano hivi alijikuta katokea kwenye eneo lile alikokuwa akisikia kelele zile, Saringo alishika midomo yake kwa kutoamini alichokiona pale, watu wengi sana waliujaza uwanja ule wake kwa waume wakicheza ngoma za ajabu kabisa katika mduara mkubwa, pembeni yao kwa juu kulikuwa na kitu kama jukwaa hivi hapo aliketi mtu mmoja aliyeonekana kama ndio kiongozi wao, mkononi alishika fimbo kubwa na juu ya fimbo hiyo kulikuwa na fuvu la binadamu lilionekana kama la mtoto mdogo hivi, pembeni yake alizungukwa na wanawake wengi waliokuwa nusu uchi kwa kuacha vifua na sehemu kubwa ya miguu yao ikiwa wazi, ilionekana ni sherehe kubwa sana watu hawa wa kutisha walikula na kunywa wakicheza ngoma yao hiyo kwa kila aina ya mtindo wakiwa wamejipamba kwa michoro ya ajabu ajabu katika miili yao, katikati ya mduara huo kulikuwa na watu walioonekana wamefungwa kamba kwa hesabu ya haraka haraka Saringo alipata kuwa wapo kama kumi natano ‘ha! Ina maana huku kuna viumbe kama sisi!’ Saringo alijiuliza lakini jibu hakupata kwa kuwa aliona wengine wakiwa wamefungwa kamba na kuwekwa pale katikati. Saringo alitulia pembeni ya mti ule ili ajue ni nini kitaendelea eneo lile maana sherehe hii haikuleta maana kwake hata kidogo. Aliendelea kujibanza palepale mwili wake ukiendelea kushambuliwa na mbung’o wenye njaa ambao sasa walipata kitoweo bila jasho, uchovu ulimkabili hata kusababisha mwili wake kudhoofu kwa hilo, hakujua hatima yake, hakujua wenzake wako wapi au wamepatwa na nini, hali hii ilimfanya msichana huyu mrembo mwenye maringo na mikogo ya aina aina awe kama kichaa asiye na msaada ukiongeza na matope ambayo sasa hata yeye alishasahau kama yamemganda mwilini mwake alibaki tu kujiinamia kwenye kichaka kile kidogo, machozi yalimlengalenga na macho yake kulowa alimlilia nani hakujua, Saringo alituli palepale kama mtu aliyegongewa kwa misumari hakuthubutu kujitikisa kwa kuwa alihofu kuwa kwa kufanya hivyo angewafanya watu wale wajue kuwa yupo pale.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Saringo aligutushwa pale ngoma ilipoongeza kasi na watu kuongeza nguvu za kucheza, mara yule mtu aliye kama kiongozi alinyanyuka na kupiga kelele akinyanyua juu fimbo yake, watu wawili walitokea nyuma ya kiti chake kile wakiwa wamemshika mtu mwingine wakitumia nguvu kumleta pale mbele ya kile kiti, mtu yule alionekena kuwa mkaidi na kutumia nguvu kujinasua lakini watu wale wenye nguvu na tambo kubwa walimdhibiti na kumfikisha pale mbele ya yule kiongozi, kiongozi yule alipiga tena kelele na wale waliokuwa wakicheza ngoma walishangilia kwa kwa kelele za ajabu kisha wakasimama na kugeukia upande ule ambao yupo yule kiongozi wao. Wale watu walifunga yule mateka wao kwenye kisiki cha mti kilichowekwa mahali pale na mmoja wao akachukua mti wenye kipago kama cha manati na kuipachika shingo ya yule mateka kiasi kwamba hawezi kupata pumzi, yule kiongozi alipiga tena ukelele na wale watu wote wakashangilia kwa kelele zile zile, yule kiongozi akachukua jiti kubwa lenye ncha kali na kulididimiza kifuani mwa yule mateka alipolichomoa lilitoka na moyo wa binadamu, damu ziliruka kwa kasi na watu wote wakaanza kushangilia kwa nguvu, ngoma ikaanza upya na kucheza kukaanza tena, yule kiongozi akarudi kwenye kiti chake cha enzi akiwa na ule moyo mkononi huku akionesha kufurahia kile alichofanya. Saringo alisisimka mwili wote na kupata ganzi akaanza kulia kwa vikwifukwifu akiwaomboleza wenzi wake wote na kujijutia nafsi yake maana alijua sasa maiti yake haitaonekena hata na rafiki zake bali italiwa na wanyama na ndege wa Msitu wa Solondo. Giza lilipoanza ingia moto mkubwa uliwashwa mahali pale na sherehe ile iliendelea kwa muda kisha ikasimama, yule kiongozi akaongea maneno machache ambayo Saringo hakuyaelewa maana yake ni nini kwa kuwa walitumia lugha isiyoeleweka. Baada ya maneno yale machache wale watu walishangilia tena kwa sauti kubwa na mara wakawanyanyua wale waliokuwa wamefungwa pale chini na kuwaongoza kuelekea mahali fulani, Saringo aliendelea kuangalia msafara ule ukiingia msituni
‘lazima nione mwisho wake’
alijisemea nakuanza kuufuata msafara ule kwa kupitia pembeni ili tu wasije kumuona. Msafara ule ulipita katikati ya misitu minene Saringo hakujua hata ni wapi wanakoelekea yeye aliendelea kufuata tu kwa kuwa aliamini kuwa labda kati ya wale ambao wamefungwa inawezekana kuna wenzake alijipa moyo nakuendelea kuufuata kwa pembeni huku akimuomba Mungu wake amlinde japokuwa hata kanisa au msikiti hakuujua. Saringo aliona mara nyingi mtu mmoja ambaye alichoka sana katika mateka wale, mara mara kwa mara alikuwa akishindwa kuendelea na safari ile lakini wao hawakujali bali walimburuza na kumyanyua kwa nguvu ili aendelee na safari ile, saringo alishikwa na huruma ya kike lakini hakuthubutu hata kuthubutu kufanya lolote maana alijua hapa akionekana tu itakuwa zamu yake kutolewa moyo kama waliotangulia, alizidi kuufuata msafara ule bila kuchoka huku akichuma kila akionacho porini humo na kula ilimradi tu hakikuwa kichungu wala hakikuwa sumu. . Kiu na njaa vilisumbua koo na tumbo lake akiwa anahemea juju kwa uchovu na kibaridi cha usiku ule kikiendelea kumpa nguvu kidogo Saringo hakuchoka, mwili wote ukiwa umegandamana na matope hata alisahau hili nia na lengo yake ilikuwa tu ni kuona mwisho wa msafara ule uliokuwa umekusanya mateka wale. Mwanga wa mienge iliyowashwa na watu wale ilangaza vema ndani ya msitu ule
‘kama akina Amata hawako kati ya mateka wale sasa wako wapi? Watawezaje kufika katika pango lile tunalolikusudia hali mchoro wa njia yote anao Stephan!’
wazo hilo lilimjia daima na ha po akagundua kuwa si ajabu yuko peke yake ndani ya msitu huu, alijaribu kufikiria uwezekano wa hawa wenzake kuwa pamoja lakini hakuna muunganiko wa matukio ambayo yangewafanya wakutane ‘Stephen na Hellen walipotea pangoni nikabaki mimi na Amata, ah! Amata yupo wapi?’ alijiuliza mwenyewe huku akiendelea na safari asiyoijua ni wapi inaelekea. Akiwa katikati ya msitu ule saringo alichoka sana akainama na mikono yake kushika magotini, alihisi kama mkono wa mtu ukimuinua kichwa chake alipoinuka hakuona mtu yeyote mahali pale, hofu ilimjaa akarudi nyuma kidogo na kugeuka uku na huko lakini hakuona mtu zaidi ya miti ya msitu ule iliyozunguka mahali pale, mara akasikia sauti ya kuning’ona ikimwita
“Saringo, Saringo!!!”
Saringo aliangaza uku na huko hakuona mtu mbele yake kulikuwa na mbuyu mkubwa sana aliangalia juu ya mti ule hakuna kitu, mauzauza! Alianza kuondoka polepole mara akajikwaa kwenye kitu kama kamba na kuanguka kifudifudi akasikia vicheko vya kike vikimcheka kwa kujirudiarudia, Saringo aliogopa sana moyo ukaanza kwenda mbio akajishika kifuani japo kuhakikisha kuwa moyo huo hautatoka nje! Vicheko vile vilitulia na hali ilikuwa ya utulivu kama mwanzo ni miti tu iliyokuwa ikitikiswa na upepo ndiyo iliyotawala giza hilo, mbala mwezi ilianza kung’aza eneo hilo, Saringo alisimama kimya akijua sasa msafara ule utakuwa umempotea hata asijue wapi ulipo.
Akiwa katika kutafakari hayo yote alisikia sauti za watu wakiongea mara mtoto akilia mara vicheko sauti hizi zilikuwa zikitoke pande mbalimbali mara aligeuka nyuma hakuona mtoto alitazama kushoto na kulia hakuona watu, Saringo alizidi kuingiwa na hofu akaanza kutimua mbio kama kichaa, akipita vichakani, alihisi kama mtu anakimbiza nyuma yake lakini hakumuona, alizidi kukimbia huku akitweta kwa nguvu bado alisikia vishindo vya mtu vikimfukuza nyuma yake, akasimama na kugeuka nyuma ‘liwalo na liwe’ alijiambia, lakini hakuona mtu na vishindo vile havikusikika tena, alihisi kuchanganyikiwa zaidi, alipoanza kutembea alihisi kama mtu yuko pembeni yake naye akitembea, saringo akasonya mara akasikia misonyo zaidi ya kumi kutoka pande tofauti, akaanza kukimbia tena sasa kwa kasi zaidi, nyuma yake alisikia vishindo sasa sio vya mtu mmoja bali ni wengi wakimfukuza, saringo alikimbia kwa kasi yake yote huku moyoni akiomba Mungu amsaiidie katika hili, akiwa katika mbio hizo alijikwaa na kuanguka vibaya pale alipoangukia kulikua na mzoga wa mnyama wa skunyingi sana ambao kwa wakati huo ulibaki mifupa tu, alihisi kama mtu akimshika shingoni kumyanyua, Saringo akaokota moja ya ile mifupa na kugeuka kwa kasi tayari kwa shambulizi, vumbi kubwa lilitimka mbele yake kama upepo wa kisulisuli miti na manyasi ya eneo hilo iliyumbayumba bila muelekeo, mara kukawa kimya kumetulia kabisa, Saringo akainua mkono wake kuangalia ule mfupa ‘waoh!!!!’ alishangaa, aligundua kuwa inawezekana viumbe hivi visivyoonekana vinaoghopa aina hii ya mifupa, akachukua na kuupachika kwenye pindo la suruali yake na mwingine akaushika mkononi, akaanza kujaribu kuutafuta ule msafara kama angeuona tena!
**********************************
Miaka saba ilopita
Heidelberg University-Ujerumani
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Chuo kikuu cha Heidelbeg, (Heidelberg University, Ruperto Carola) ni chuo kikuu cha tafiti kilichopo katika jiji la Heidelbeg, Baden-Württemberg, Ujerumani. Kilianzishwa mnamo mwaka 1386, ni chuo kikongwe sana huko Ujerumani na ni chuo cha tatu kujengwa katika Utawala wa Warumi. Heidelberg kimekuwa chuo kinachotoa elimu mchanganyiko tangu mwaka 1899. Leo hii katika chuo hiki kuna vitivo kumi na mbili na kinatoa shahada, shahada ya uzamili na shahada ya juu.
Katika chuo hiki ndipo Bw Stephen Van Leuwen alipokuta na Bi Hellen Schurman wakiwa wakufunzi katika kitivo hii ya mambo ya kale, hawakuzoeana kirahisi kama unavyofikiria wewe sasa hivi bali walifanya kazi chuoni hapo takribani miaka mitano. Siku moja Stephen alipata safari ya kikazi kwenda Chuo kikuu cha Humboltd nacho cha uko huko Ujerumani kuona mabaki ya mjusi mkubwa (dinosauria) yaliyokuwa yamepelekwa huko Ujerumani yakitokea katika moja ya makoloni yao lililojulikana kama Deutche Ost Africa (Tanzania bara ya sasa), katika ziara hiyo ya kikazi ndipo alipopata nafasi ya kuongea na Bi Hellen kwa mara ya kwanza, wakiwa katika kubadilishana mawazo ndipo walipogundua kuwa huko katika bara la giza kuna mambo mengi ambayo wao kama watafiti wa mambo ya kale iliwapasa kuyafahamu.
“Ningependa siku moja kufanya safari ya uchunguzi huko Africa”
Hellen alimueleza Stephen
“Inawezekana kwa kuwa pia kuna historia kubwa sana ya Mjerumani, kwa nini usiitafiti? Twaweza kufanya hilo na kuandika kitabu ambacho kitasaidia kufundishia na pia kuongeza elimu yetu!” Stephen alikazia
“Lakini tutafanya tafiti juu ya nini?”
Hellen aliuliza
“Inabidi tukae tuangalie pamoja, kwa kuwa kuna mambo mengi sana ya kufanyia utafiti”
Stephan alijibu huku akiwa katika harakati za kuwasha sigara yake ili avute.
“Samahani sipendelei sigara!”
Hellen alimwambia Stephan
“Oh! Sorry Miss!!!”
Stephan aliomba radhi na kuzima sigara ile
Mazungumzo yao yalikuwa marefu sana, waliongea mengi sana juu ya mambo kale na historia mbalimbali, lililotokana na mazungumzo hayo lilikuwa ni kufunga safari ya kitafiti huko Africa, lakini wasiwasi wao ulikuwa ni nini cha kufanyia utafiti na wapi pa kwenda.
Walirudi tena Heidelberg kuendelea na kazi, mara kwa mara kila mmoja alikuwa ana hamu ya kuonana na mwenzake ili tu kubadilishana mawazo katika hili, Hellen alidhamiria toka ndani ya moyo wake kufanya tafiti mojawapo katika Africa lakini aliogopeshwa na habari nyingi za huko Africa, mara alikata tamaa na mara alijipa matumaini hasa alipokumbuka safari yake aliyoifanya miaka kadhaa nyuma akiwa mwanafunzi katika misitu ya Amazonia aliamini duniani hakuna msitu unaoweza kuufikia huo kwa kila hali. Kwa upande wa Stephan alitokea kumpenda sana Hellen hasa kwa umbo lake zuri la kike waswahili wangeliita namba nane, mwanadada huyu mfupi, mcheshi anayeonekana ni mjuzi wa mambo aligonga mhuri wa penzi katika moyo wa Stephan, kijana jasiri kutoka Poland aliyelelewa na baba yake ambaye alikuwa mwanajeshi aliyepigana vita ya I ya dunia, hakuwa muongeaji sana lakini pia hakuwa mtu wa kukubali kila kitu alichoambiwa, alipenda kusoma na kuchunguza mambo mbalimbali hasa ya kutatanisha, kwa muda huu alivutiwa na wazo la Hellen la kufanya utafiti huko Africa lakini bado hakujua ni nini wangeenda kufanya huko, tangu siku hiyo alianza kusoma vitabu mbalimbali vinavyohusu Africa ili labda angeona chochote cha kufanyia utafiti, haikuwa rahisi sana kwani katika maktaba ya chuo hicho kulikuwa na vitabu zaidi ya elu kumi vyote vikizungumzia mambo kale hasa ya Africa, vitabu hivyo vilimpatia habari za kutisha sana juu ya Africa lakini alijipa moyo hasa alipokumbuka safari yake akiwa mwanafunzi huko Misri katika mapyramid aliamini hakuna sehemu yoyote duniani ambayo ni ngumu kuishi zaidi ya huko ambako ni jangwa na vumbu muda wote.
Stephan, kijana jasiri kutoka Poland aliyelelewa na baba yake ambaye alikuwa mwanajeshi aliyepigana vita ya I ya dunia, hakuwa muongeaji sana lakini pia hakuwa mtu wa kukubali kila kitu alichoambiwa, alipenda kusoma na kuchunguza mambo mbalimbali hasa ya kutatanisha, kwa muda huu alivutiwa na wazo la Hellen la kufanya utafiti huko Africa lakini bado hakujua ni nini wangeenda kufanya huko, tangu siku hiyo alianza kusoma vitabu mbalimbali vinavyohusu Africa ili labda angeona chochote cha kufanyia utafiti, haikuwa rahisi sana kwani katika maktaba ya chuo hicho kulikuwa na vitabu zaidi ya elu kumi vyote vikizungumzia mambo kale hasa ya Africa, vitabu hivyo vilimpatia habari za kutisha sana juu ya Africa lakini alijipa moyo hasa alipokumbuka safari yake akiwa mwanafunzi huko Misri katika mapyramid aliamini hakuna sehemu yoyote duniani ambayo ni ngumu kuishi zaidi ya huko ambako ni jangwa na vumbu muda wote.
Siku moja akiwa ndani ya maktaba akipitia vitabu mbalimbali, Stephen alimuona msichana mrembo, mrefu wa wastani mwenye mwendo wa madaha, Stephen alijikuta akishindwa kuendelea kusoma kitabu kile na badala yake macho na mawazo yote yalimuelekea msichana yule mweusi mwenye nywele fupi aliyekuwa akiingia maktaba mle kwa ajili ya kujisomea kama ilivyo ada, alimtazama mpaka alipokaa, maadam alikuwa ndani ya maktaba ile basi alijua kwa vyovyote ni mwanafunzi wa chuo hicho alivutiwa hasa na rangi yake iliyotunzwa vizuri.
‘A girl from dark continent!’
alijiwazia moyoni, ilikuwa ni mara yake ya kwanza kumuona mtu mweusi hakuamini anachokiona bali alijiuliza tu jinsi alivyosikia habari za bara hilo la giza na kumbe kuna viumbe vizuri kama hivi vinaishi, haikumuingia akilini hata kidogo. Alinyanyuka alipoketi na kutoka maktabani kwa kuwa alipoangalia saa yake alijikuta kuwa anatakiwa katika kipindi, alichukua baiskeli yake na kuelekea alikotakiwa.
Hamu ya Stephan ya kufanya utafiti katika bara lile la giza ilizidi kuchukua nafasi katika moyo wake na hasa alipomuona msichana huyu mweusi, mrembo mwenye kila aina ya mvuto. Alimtafuta tena Hellen na kumueleza juu ya azma hiyo na juu ya yule msichana mweusi,
“Labda anaweza kufahamu mambo mengi kuhusu Africa!”
Hellen alimueleza Stephan kwa shauku. Walikubaliana kumtafuta ili wajue mengi juu ya alikotoka na hapo ndipo waanze kuandika kile kitabu chao cha utafiti.
Siku tatu baadae...
Ruperto Carola Cafe
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hellen na Stephan walionekana wenye furaha sana hasa kwa wazo lao lile walilolipata maana walijua wazi kuwa pindi tu watapokamilisha zoezi hili watakuwa juu sana kitaaluma, kiu yao ya kitafiti hasa juu ya mambo ya kale ilikuwa kubwa sana, lakini bado hawakujua hasa ni nini wanachotaka kukifanya sasa, ni kitu cha hatari kiasi gani wanachokifikiria, Hellen alijiuliza tu kama itakuwa safari kama ile ya Amazonia iliyomchuku wiki tatu kuikamilisha akiishi na wa-Indios na wa-Amazonia ambako alikutana na hatari ndogondogo tu, Stephan aliichukulia labda itakuwa safari kama ile ambayo aliifanya huko Hamunatra katika jangwa la Misri ndani ya mapyramid yaliyosadikiwa kuzikwa watawala wa nchi hiyo nyakati za kale kabisa, wote wawili walijiona ni mashujaa sana kwa safari zao za utafiti walizozifanya katika maisha yao.
Stephan alishusha taratibu kikombe chake cha kahawa na kukiweka katika kijimeza kidogo ndani ya mgahawa huo huku akiendelea na maongezi ya hapa na pale na Bi Hellen. Binti mweusi alikuwa amekaa katika kimoja cha viti vitatu vilivyozunguka meza hiyo akiwa na makaratasi machache mkononi mwake.
“Naitwa Saringo!”
alijitambulisha kwa Hellen na Stephen, hili lilitukia mara baada ya hawa wawili kujitambulisha kwake. Mazungumzo machache yalipita kati yao hasa ya kufahamiana na kujuana zaidi, Stephen na Hellen walivutiwa na uchangamfu wa Saringo, Saringo aliwaambia mambo mengi sana juu ya Africa hasa eneo ambalo yeye anatoka,Deutche Ost Africa, Stephen na Hellen walivutiwa sana na habari za huko na walipenda kujua kama ni kweli au ni za kutunga tu za mababu wa kale. Saringo aliwasimulia mengi sana hasa aliyosimuliwa na babu yake mzee Koloto, baada ya mazungumzo hayo saringo aliwagusia juu ya stori ya babu yake alipokuwa askari wa wajerumani na alivyokuwa akiongoza misafara ya wapagazi kuingia misituni na kuficha vitu visivyojulikana huko kisha kuuawa, “No! Kwa nini waliwaua? Lazima kuna kitu” Hellen aliuliza kwa mshtuko
“Labda hawakutaka warudi tena huko, kuhofia kuchukua mali zao”
Stephen alijibu
“ndiyo, ndiyo, hakika kabisa babu alinambia waliwaua ili wasiweze kurudi, lakini yeye alinusurika na kufanikiwa kubaki hai”
Saringo aliwaeleza na kutoa zile karatasi chache zenye michoro ya ajabu na maandishi ya kijerumani. Kwa Stephan haikuwa kitu kigeni michoro ile kwani aliitumia sana alipokwenda huko Hamunatra, kwa haraka haraka aliweza kuisoma na kutambua kilichofichwa katika michoro ile.
Stephen alitikisa kichwa kuashiria amegundua kitu, akanyanyua kikombe chake cha kahawa na kunywa kidogo.
“Vipi? Stephen!”
Hellen aliuliza kwa shauku ya kutaka kujua. Stephen alitikisa tena kichwa na kugeuza geuza mdomo wake, mara alionekana kukunja uso, mara kutabasamu, akaiweka ile karatasi chakavumezani, na kunyanyua kichwa kumwangalia Saringo.
“Bingo!”
Stephen alitamka neno hilo na kuamka alipokaa akazungukazunguka huku akiwa amefungamanisha mikono yake kwa nyuma kisha akarudi akaketi tena,
“Saringo! Unajua Msitu wa Solondo?”
Stephen alimrushia swali Saringo, Saringo akaitikia kwa kutikisa kichwa, Stephen akaendelea “unajua Gereza Saroge?”
Saringo akaitikia tena kwa kutikisa kichwa,
“good! We have to face a big adventure!”.
Stephen akachukua zile karatasi na kuzikunja vizuri kisha akampatia Saringo
“tunza, urithi ulioachiwa na babu yako”
Saringo alizipokea na kuziweka mkobani.
“Kama tunaamua kufanya utafiti huu, basi na tujiandae vema sisi watatu ila lazima tupate nguvu ya watu wa ziada kuukabili msitu wa Solondo.”
Stephen aliwaeleza akijua kwamba washaelewa kila kitu,
“Stephen!”
Hellen aliita
“ tueleze kwanza kuna nini ulichokiona kisha ndiyo tuone pamoja cha kufanya”
Hellen alimueleza Stephan.
“Ok! Kadiri ya mchoro huu wakoloni wa kijerumani walipokuwa wanaitawala Deutch Ost Africa walipata vitu vingi sana ikiwemo mali za aina mbalimbali, kwa hiyo walichokifanya ni kuzificha ili vizazi na vizazi vyao vija kuchukua na kuupata utajiri huu mnono, Babu yake Saringo aliifadhi kitu kikubwa asichokijua, huu ni urithi usiopimika kwa mjukuu wake.”
Stephen alimaliza maneno yake na kuwafumbua macho wadada hawa wawili ambao walibaki kutazamana bila kujua wanachotazamania ni nini! Walizungumza masuala machache na kukubaliana kuanza shughuli hii ya utafiti wa wapi zilipo mali hizo, na jalada la utafiti huu wakaliita ‘Msitu wa Solondo’.
Saringo alizama kwenye mawazo mazito sana na daima alijaribu kuunganisha habari hii aliyoisikia kwa Stephan na ile aliyoelezwa na babu yake mzee Koloto miaka mingi nyuma, alijaribu kufikiria kama kuingia ndani ya msitu ule ni wazo linalowezekana au la, kwa maana alishasikia mengi juu ya msitu ule, hakuwahi kufikiri kwenda huko hata siku moja lakini sasa mawazo makubwa mawili yanagongana kichwani kwake moja likimtaka aende na lingine likimzuia na kumuonesha hatari zote zinazomkabili, alifikiria juu ya mali hiyo aliyoisema Stephen ambayo mpaka hapo hakuna alojua ni mali gani iliyofichwa, Saringo alibaki hajui la kufanya.
Hellen kwa upande wake aliona wazo la kwenda huko ni zuri lakini alifikiria adha za porini akilinganisha na zile alizopata akiwa huko Amazon, hakujua aamue nini, alifikiri kuwa endapo watafanikiwa kufika mwisho wa safari yao salama atakuwa ni milionea wa kutupwa mara alijiuliza itakuwaje endapo asirudi huko akaona kuwa maiti yake haitaonekana hata kwa ndugu zake, alikata tamaa na kuona kuwa hilo ni wazo hasi kabisa kwa wakati huo.
Stephen alikuwa na mambo mengi kichwani, alijua kama akifanikisha safari hiyo si tu atakuwa kitaaluma lakini pia ataukwaa utajiri usokifani kutokana na mali hizo zilizowekwa porini, alifurahi sana kwa ugunduzi huo hata siku hiyo maisha yake yalibadilika na kuanza kuishi kama kibopa mmoja hivi, wanafunzi wake walimshangaa sana alipoingia katika kipindi akiwa na furaha ya ajabu sana, alifundisha kiasi kwamba muda wa kipindi chake ulikuwa hautoshi, kila saa aliangalia saa yake ile aliyoipenda sana.
Saringo aliona sasa ndoto zake zimetimia baada ya kujua kuwa amepata watu ambao wameweza kugundua siri ile ambayo yeye hakuijua kirahisi, aliamua kwenda kusoma katika chuo hicho ili naye apate kujua na kwa bahati mbaya au nzuri anakutana na watu ambao wanafahamu na wameshafanya tafiti kama hizo. Saringo aliiona hiyo ni bahati kubwa sana kwake na aliona kile alichokisubiri kwa miaka mingi kitendawili ambacho hakukijua tatuzo lake sasa kimefika mwisho. Alishusha pumzi kwa nguvu na kujinyoosha pale juu ya kitanda chake huku akitafakari hili na lile ‘nani wa kutupeleka msituni?’CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
alijiuliza lakini hakupata jibu, alikumbuka tu mahitaji aliyoambiwa na Stephen
‘mtu anayejua misitu, mwenye nguvu na mkakamavu, nani! Cjui’
alijiuliza na kujijibu kwa namna isiyosawa, Saringo alikuwa kama aliyechanganyikiwa katika kichwa chake, hakujua anachofikiri wala anachokiwaza. Kila alipoamua kuingia ndani ya msitu ule akili yake ilimtoa na kumuuliza maswali yasiyo na ukomo, alimkumbuka mjomba wake Golam ambaye mara tatu alijaribu kuingia katika msitu huo wenye maajabu na kukutana na vitu ambavyo havielezeki na hata mara ya mwisho aalikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa, bangi, gongo vurugu nyingi za mtaani ilikuwa ndiyo kawaida yake. Lakini hakuna kitu kilichomsumbua sana saringo kama jinsi gani ya kupata sehemu ya pili ya ramani ile maana ile ilkuwa ni nusu na nusu nyingine je ilikuwa wapi, hilo lilikuwa swali ambalo halikupata jibu hata kidogo
‘hata kama tukienda msituni tutafikaje kwenye maficho haya, hatuna sehemu ya pili ya mchoro huu, babu alinambia kipande kingine kilibaki kwa yule askari wa kundi la pili, mh! Yuko wapi? Alikufa, mzima au alikitupia wapi au kukificha wapi kipande kile, utata!!!’
Saringo alikosa jibu hata usingizi ulimchukua.
********************************
Kutoka juu ya kilima kile Hellen alianguka baada ya kuteleza vibaya alipokuwa katikati ya msafara ule wa wale watu katili wasio na chembe ya huruma, alining’inia kwa kamba ile iliyofungwa kiunoni mwake, akiwa amechoka na uso wake umesawajika vibaya kwa matope, damu zilizoganda zilimfumba macho, njaa ya siku kadhaa haikupata tiba yake, Hellen alibaki akining’inia kwenye korongo lile huku watesi wale wakimvuta kurudi juu, msafara ulisimama kwa muda. Hellen alifikishwa juu na kujumuishwa na wengine na msafara ule uliendelea, ‘Gwerino’ watu wanaokula nyama za watu daima walikuwa wakifanya matambiko katika mawe na mapango makubwa yaliyopo katikati ya msitu wa Solondo. Siku ya matambiko ilikuwa imefika na katika siku hii hutoa damu za watu na kumwaga kwenye mawe yale ambayo wao waliamini Miungu yao ndimo inamoishi, siku hiyo hawakula kabisa nyama za watu kwa kuwa zote walizipeleka Mzimuni. Msafara ulizidi kuingia ndani kabisa ya msitu ule watu wapatao kama kumi na tano walifungwa kamba viunoni na shingoni wakikokotwa huku wakipigwa sana. Hellen kati ya msafara ule alikuwa amechoka sana hata alitamani afe na asifike anakopelekwa, wenzake aliowakuta wamefungwa hakuwajua hata mmoja wao hakujuwa hata wametokea wapi, hakuelewa lugha inayoongelewa na hawa Gwerino, kibaya zaidi alichokishuhudia ni jinsi wanavyoua watu na kula nyama zao wengine wakinywa damu mbichi, Hellen aliona kuwa hii sio dunia aliyoijua kweli hili ni bara la giza, mara kadhaa amepoteza fahamu na alipozinduka alijiuliza kwa nini alikuja kwenye safari mbaya kama hii. Msafara uliendelea, watu walikuwa ni wengi sana wenye mienge mikononi, magongo makubwa, mavazi yao yakutisha yaliyotengenezwa kama ngozi wengine walivaa vidani ambavyo vilikuwa ni mifupa ya vidole vya watu. Kila Hellen alipoona haya alihisi akili yake kuchanganyika na ubongo, Hellen alichoka kabisa hakuweza kuendelea na safari ile alianguka tena na sasa hali ilikuwa mbaya zaidi hakuweza kusogea hata kidogo. Msafara ulisimama na yule kiongozi alishuka kutoka kwenye kiti kile cha enzi kilichobebwa na wanaume wapatao nane hivi walioshiba kwelikweli.
“Kusisi libiko?”
yule kiongozi aliwauliza waongoza msafara kwa sauti ya kutisha yenye kukwaruza akimaanisha
‘kumetokea nini’
huku akiwa anajongea taratibu na fimbo yake ambayo juu imepambwa na fuvu la binadamu.
“Libiko sinzota, kucholo londigo!”
alijibiwa na kiongozi wa msafara akimaanisha ‘hapa kuna kafara moja imechoka haiwezi kufika’ yule kiongozi akatikisa kichwa kuashiria ameelewa alichoambiwa
“Kucholo? Losa fo, libeso kolilo, a la to”
aliongea kwa kufoka huku akizungukazunguka akimaanisha‘imechoka, basi na tuitoe sasa ili miungu ifurahi’ alimaliza na kuigonga chini fimbo yake kwa nguvu na kupaaza sauti huku mkono wake mmoja ukiwa juu
“I lee se?”
na msafara wote ukajibu
“seeee!!!!”
akimaanisha ‘ni sawa?’ msafara ukajibu ‘sawa’ . wale waliokuwa wakilinda mateka wale wakamfungua kamba Hellen na kumnyanyua wakasonga nae mbele kidogo, maana katika utaratibu wao kama kafara haiwezi kufika mzimuni basi mnaweza kutolea popote na damu yake ndiyo mtayoipeleka mzimuni pamoja na moyo. Walifanya mduara na wote walianza kugonga fimbo zao chini wakirudiarudia neno lile
“Se, se, se, se”.
Hellen alifungwa mikono kwa nyuma na kupigishwa magoti kisha mtu mmoja lisimama nyuma yake na kumuwekea mti wenye mfano wa kipago cha manati mgongoni na kamba moja iliyomzunguka shingoni ikavutwa nyuma mgongo wa Hellen ukapinda na kifua chake kutangulizwa mbele tayari kwa kazi hiyo. Yule kiongozi alizunguka kwa mbele na kukabidhiwa ule mti uliochongwa maalumu kwa kazi hiyo akaunyanyua juu na yule kiongozi alizunguka kwa mbele na kukabidhiwa ule mti uliochongwa maalumu kwa kazi hiyo akaunyanyua juu na alipotaka kuushusha kukipasua kifua cha Hellen alisita ghafla, akashusha mti ule taratibu, watu wote walinyamaza kimya kabisa wakiwa hawajui nini kinachoendelea
“Ifime, letose seleke, ke la londigo?, bease keloya londigo”
kiongozi yule aling’aka kwa hasira akimaanisha ‘laana, hii sio kafara ni mwanamke huyu?, ivueni nguo hii kafara’ watumishi wa kiongozi yule mara moja walimfungua kamba Hellen na kumvua blauzi yake iliyochakaa kwa uchafu wa aina tofauti, kiongozi yule akamwangalia Hellen na kumeza funda kubwa la mate alipoona chuchu zile nyekundu zilivyosimama kama mishale ya saa sita
“seleke!”
alitamka neno hilo huku akijipiga mkono wake wa kulia kifuani mara kadhaa akimaanisha ‘laana’, katika utaratibu wao ilikuwa kafara lazima awe binadamu wa kiume na si wa kike, muda wote walipomkamata Hellen hawakujua kama ni mwanamke kwa jinsi alivyovaa suruali ile ya jeans, kilichomshtua kiongozi yule ni jinsi alivyoona vitu vilivyotuna kifuani mwa Hellen ndipo alipofikiri kuwa huyu ni mwanamke na walipomvua blauzi ile waligundua kuwa ni kweli. Wote walijipiga kifuani kwa mkono wa kuume wakirudia neno lile ‘seleke’. Hellen aliondolewa kwenye kundi lile la mateka wengine, akiwa bado amechoka sana alitembea kwa tabu, yule kiongozi alimwita mmoja wa majemadari wake na kumnong’oneza kitu kisha alitoa ishara msafara ule uendelee. Hellen aliingizwa kwenye kitu kama pango na kuwekwa pale huku akiwa amefungwa kamba za miti ili asitoroke. Msafara uliendelea usiku ule na mateka wale sasa walikuwa wamebaki kumi na nne.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akiwa mle pangoni, Hellen hakuwa na lolote la kufanya alitulia tu akisubiri mwisho wake ufike, hakujua ni kwa nini alifungwa pale, macho yake yaliendelea kupambana na giza nene lililotawala msitu ule, mbu na mbung’o walifurajhia kupata damu wasiyoitarajia, hakika ilikuwa ni sherehe kwao usiku ule. Hellen alishuhudia mwanga ule wa mienge ya watesi wake ukitokomea msituni, alitafakari sana lakini hakupata njia ya kumtoa mahali pale, alibaki tu amejikalia huku machozi yakimtoka. Katika msitu ule ni mivumo ya miti na upepo tu iliyosikika na milio ya ndege wasiyopendwa na binadamu, bundi. Akiwa katika kutokujielewa Hellen alihisi vichaka vikitikisika aliogopa sana akaanza macho kuangalia ni kitu gani kilichokuwa hapo, hakuweza kufanya lolote kwa kuwa alikuwa amefungwa kwa kamba mikono na miguu yake, alibaki kuangalia tu kitachotokea, mara aliona kama mtu akitokea vichakani mle akinyata kuelekea pango lile, Hellen alitulia akiangalia nyendo zote za kiumbe kile, mtu yule alizidi kunyata kana kwamba kuna watu ambao hakupenda wamuone alisogea mpaka karibu kabisa na mlango wa pango lile, akiwa anamulikwa kwa mbalamwezi hafifu iliyotoke nyuma yake Hellen hakuweza kuona hata sura ya mtu huyu, alijua tu kwa vyovyote atakuwa ni mmoja wa atesi wake ambaye labda amerudi kuja kujifaidia teka lile baada ya kujua kuwa alikuwa ni mwanamke. Hellen alijibanza kwenye kiambaza cha pango lile akiwa kimya kabisa bila hata kujitikisa alisubiri tu kuona mtu huyo atafanya nini kwake.
************************************************
Amata alipumzika vya kutosha katika kichaka kile ambacho alihifadhiwa na yule nyani, alinyanyuka na kujinyoosha viungo na kujikuta yuko fiti kwani yule nyani alimletea chakula pamoja na mizizi mbalimbali ili kumrudishia nguvu ambazo zilipotea kwa mateso yale, Amata aligeuka huku na kule lakini hakumuona Kingusu eneo lile, Amata alitoka ndani ya kichaka kile na kuangaza huku na huko akanyanyua mkono wake na kubana vizuri midomo yake kisha akapiga mbinja kali ya kumuita Kingusu, alisubiri kidogo lakini hakuona dalili ya Kingusu kuwa mahali pale, alipogeuka kurudi alipokaa alikuta uta wake na podo viko pale akavichukua na kuvibeba tayari kwa safari lakini aende wapi? Hata yeye hakujua. Alipiga hatua mbili tatu akasimama tena hakujua bado ni nini anachotakiwa kufanya, baridi kali ilikuwa ikimpa taabu lakini alijitahidi kuivumilia japo mara kwa mara alikuwa akitetemeka. Akiwa katika kutafakari hili na lile kwa mbali aliona kitu kama moshi kikitokea katikati ya msitu ule, Amata aliangalia kwa makini sana moshi ule na akagundua kuwa kule lazima kuna watu, lakini alibaki kujiuliza maswali mengi ni watu wa namna gani hao, au ni vie viumbe vya ajabu ndivyo viishivyo huko lakini hakupata jibu. Aliendelea kuuangalia moshi ule na akaamua kuelekea uko huko ili akaone kulikoni ‘liwalo na liwe’ alipiga moyo konde na kuanza safari huku moyoni akiwakumbuka wenzake wote ambao mpaka muda huo hakujua wapi walipo japo mmoja wao tu, alijiona sasa kabaki peke yake na kilichobaki ni kufanya juu chini kutoka ndani ya msitu ule na kurudi kijijini kwa kuwa hakujua hata aelekee wapi na upande gani, akili yote ilikuwa ni kurudi alikotoka lakini sasa hakujua hata ni wapi alipo. Alitembea kwa hadhari kubwa sana ndani ya msitu huo kuelekea kule alikoona moshi ule alidhamilia kukabiliana na hatari iwayo yote atakayokutana nayo, mara kwa mara alitembea na kuangalia nyuma maana alihisi kama kuna watu wanaomfuata lakini alipuuzia tu kwa kuwa yeye alifahamu mambo mengi sana juu ya misitu. Amata alipita vichakani na alipopata nafasi mara alikimbia na mara alitembea, alipoendelea mbele mara ghafla alijikuta akitokea kwenye ukingo kama wa shimo kubwa alisimama na kuangaza macho huku na huku hakuona mwisho wa bonde lile, bonge kubwa lililofunikwa na miti mikubwa iliyoshonana kwa namna ya ajabu, Amata alipigwa na bumbuwazi hakujua afanyeje kuendelea na safari yake alipoangalia kule kulikokuwa kukitokea moshi ule aliona bado unaendelea kufuka lakini mahali bado pakali mbali, alipoangalia bonde lile lilikuwa ni kubwa na la ajabu hakuwahi kuona kitu kama hicho, Amata aliamua kushuka bondeni kule kwa kutumia mizizi ya miti mikubwa iliyokuwa ikining’inia aliweka uta na podo lake vizuri na kuanza kuteremka taratibu, kila mara aliangalia aendako na atokako lakini aliona hafiki chini, mara ghafla mzizi ule ukakosa nguvu na kukatika Amata alipiga ukelele na kuanguka kwa kasi kuelekea bondeni alijipiga kwenya baadhi ya miti na kupata michubuko kadhaa mwilini aliendelea kupiga ukelele lakini hakukuwa na mtu eneo hilo isipokuwa ndege wa mwituni, kasi ya kuporomoka chini iliongezeka kila nukta Amata alijua sasa hata akifika chini asingepona, alijikuta anadondokea kwenye kitu kama nyavu kubwa, hakuamini alichokiona uoto uliyojishonashona kama wavu ulimdaka Amata naye alikuwa salama, aligeuka kuangali chini akaona sasa si mbali sana kumbe angeweza hata kuteremka tu kwa kujirusha tu. Alijirusha mpaka chini na kutua kwenye lundo la majani makavu akatulia dakika kadhaa lakini hakuona chochote, aliendelea kutembea kwa hadhari kubwa sana na taratibu kuelekea kule alikoona moshi ule, katika kutembea kule alisikia sauti ya mandege makubwa yakilialia Amata alijua popote penye ndege wale lazima kuna mzoga, alisimama na kusikiliza kwa muda huku akijaribu na kuvuta harufu kuona kama kuna harufu ya kitu chochote kilichooza, haikuwa hivyo. Amata alichomoa moja ya mshale wake katika podo na kuupachika vizuri utani kauvuta kwa mvuto wa wastani kisha taratibu alinyata kuelekea walikojaa ndege wale alipokaribia eneo lile alitulia kimya kuangalia vizuri hakuelewa anachokiona kama ni mzoga wa mtu au mnayama, Amata aliingiwa na woga kidogo aliushusha uta wake uliokuwa tayari kwa kujeruhi na kuushika kwa mkono mmoja alipoangalia kwa makini eneo lile hakukuwa na mzoga wowote Amata alisogea na kushuhudia tu madonge ya damu nzito nzito yametapakaa eneo lile alipigwa na bumbuazi hakuelewa aliyepata masaibu haya ni binadamu au mnyama aliiangalia damu ile kwa makini sana ilionekena tukio hilo halikutokea muda mrefu, Amata alitazama huku na huku na kuona michirizi mingine ya damu imeelekea porini aliifuata kwa hadhari kubwa huku uta wake ukiwa umeshikwa tayari kwa kutoa pigo, akiangalia nyuma na mbele kwa haraka haraka aliendelea kufuata damu zile, mbele kidogo alikuta damu zile zimepotea, alisimama na kuangalia huku akijigeuza taratibu pande zote nne za dunia, akiwa pale chini alihisi kama tone la maji limemdondokea, Amata akanyanyua kichwa chake kuona kulikoni, hakuamini macho yake, mwili wa mwanadamu uliyoraluliwa vibaya ulikuwa kwenye moja ya matawi ya mti ule ukining’inia, Amata aliuangalia mwili ule ukiwa pale juu, machozi ya uchungu yalimdondoka nguvu zikamuisha na hasira ikaanza kuchukua nafasi yake, alitamani amuone aliyefanya unyama ule kama ni mnyama au ni kiumbe wa aina gani, Amata alikwea mti ule na kuuteremsha mwili ule mpaka chini akaulaza na kuangalia vizuri
‘Stephan!’CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
alijisemea moyoni huku akilia aliugeuzageuza, akaweka mkono wake shingoni mwa mwili ule labda angehisi joto lakini mwili ulishatawaliwa na baridi, alijaribu kugusa kifuani kuona kama kuna dalili ya uhai ah wapi! Amata alijishika kichwa na kukosa la kufanya
‘mwanaume chini!’
alijisemea mwenyewe huku akibubujikwa na machozi mwili wa Stephan ukiwa umelala bila uhai, aikuwa na majeraha ambayo yalionesha kwa vyovyote kuwa ameuawa na mnyama mkali. Amata alibaki amekaa kimya karibu kabisa na mwili ule, akiwa na maswali mengi kichwani mwake akijiuliza na kujijibu
‘vipi wale wanawake wawili, bado wako hai au nao wamekufa?’
Amata akauchukua mwili ule na kufanya shimo la kumtosha Stephan ambaye kwa sasa alishakuwa marehemu, akamsitili kwa heshima iliyomfaa, akafanya tuta mahali pale na kuweka kitu kama msalaba, akasimama mbele ya kaburi lile na kutoa saluti ya heshima
“kwa heri kamanda, Hellen na ndugu zako hawatakuona tena”
Amata akachukua uta wake na kuanza kuondoka, mara akasita na kugeuka nyuma alikumbuka karatasi zile ambazo Stephen daima alikuwa anazisoma ili kupata uelekeo sahihi alitazama eneo lile hakuweza kuziona, taratibu aliamua kurudi kule michirizi ya damu ilipotokea, Mungu si Athumani alizikuta japo zilipeperuka kwa upepo ila hazikwenda mbali sana pamoja nazo aliokota na ile camera ndogo vyote akavitia kwenye mfuko wake wa suruali ile ya jela na kuendelea na safari yake, poli kwa poli Amata alitokea kwenye uwanda mkubwa ulioonekana kama umetandikwa zuria la kijani aliangalia kwa makini akaokota kipande cha mti na kukirushia lol! Kumbe kuna maji, akaendelea kuambaaambaa na ukingo wa bwawa hilo lakini lengo lake yeye ilikuwa ni kuvuka na kuelekea upande wa pili lakini atavukaje ndiyo lilikuwa tatizo, aliendelea kufuata ukingo ule mpaka alipokuta sehemu nyembamba ambayo aliona hapa angeweza kuvuka kwa urahisi, alipokuwa akijiandaa mara akaona maji yale yakitikisika, akaangalia kwa makini hakuona kitu, Amata akarudi nyuma kidogo mbali na mto ule ili kuona nini kilichopo ndani yake, alikaza macho kutazama magugumaji yale yaliyotuama vizuri juu ya maji ambapo kama huna subira basi unaweza kutumbukia ukijua ni ardhi kavu. Wazo likamjia Amata akaingia porini na aliporudi alikuwa na digidigi mkononi akamrusha majini, La haula! Mamba wakubwa walijinyanyua kugombania nyama ile ambayo hata kwa vipi isingewatosha wote, Amata akapigwa na butwaa baada ya kuona jinsi alivyogundua siri hiyo, akakaa chini akiwa hajui la kufanya lakini kichwani mwake akiwa anafikiri jinsi gani angeweza vuka kwenda upande wa pili ambako lengo lake ni kufika kule kunakofuka moshi akiamini kabisa lazima kuna binadamu wanaoishi huko ila mara kwa mara alijiuliza itakuwaje kama watakuwa ni Gorino alijua kuwa huo utakuwa ndiyo mwisho wake jinsi watakavyomtafuna
Wazo likamjia, akaingia tena msituni na kufanya mawindo kidogo, akapata mnyama mkubwa kidogo, akamkatakata vipande vya kutosa kisha akasogea pale kwenye yale maji, Amata akamwaga nyama zile kwa ustadi mkubwa na mamba wale walipokuwa wakigombania yeye alitumia mwanya huo kupita juu ya migongo yao kwa kasi na kufanikiwa kufika upande wa pili, alianguka kwenye majani kisha akaangalia kazi aliyoifanya ilivyokuwa na mafanikio, mamba waliendelea kugombania nyama wakati Amata alishafanikiwa lengo lake, aliamka na kujikung’uta majani yaliyoshikana na nguo yake na kuendelea na safari kuelekea kule alikouona moshi ule, sasa Amata alijikuta kwenye msitu wa upande wa pili, msitu wa kutisha wenye mawe mengi na makubwa, yeye hakujali japo huku uoto mwingi ulikuwa wa miba, alihisi kupambana na hatari nyingi kuliko alikotoka lakini alijipa moyo na kuendelea kutembea msituni mle japo kwa taabu sana.
***********************************************************
Msafara wa wagorino ulitokomea katikati ya msitu, na kulipopambazuka ulikuwa umefika mahali hasa palipokusudiwa, katika utaratibu wao walitakiwa kutoa kafara usiku wa saba baada ya jua kupatwa na mwezi. Tukio hilo liliwafanya wao waamini kuwa Mungu wao amekasirika hivyo inampasa kuombwa msamaha kwa kumwaga damu na kula nyama, daima walimtoa yoyote kati yao ikiwa hawajapata binadamu wa kumtoa kafala kutoka jamii nyingine. Safari hii waliamini kuwa Mungu wao ‘Kolilo’ atafurahi kwa kupata damu nyingi hivyo kuwaondolea laana ‘seleke’ kwa kuwa walikamata msafara wa waarabu waliokuwa wakipita huko Solondo katika pilikapilika za kutafuna hazina ile ya kale, tamaa mbaya. Gorino waliwateka wote na kuwatesa sana, waliwaua na kugawana nyama kwa ajili ya kitoweo, baada ya kuona kitendo kile cha jua kupatwa na mwezi walijua Kolilo amechukia hivyo inabidi atolewe sadaka ya msamaha, ndipo walipoazimia waliobaki wote wapelekwe mzimuni na watolewe kafara safi.
Katika pilikapilika za kulinda himaya yao ndipo walipomkuta Hellen kando ya mto akiwa amekaa na hajui la kufanya. Hellen alipowaona akajua sasa amepata msaada kumbe kaingia mikononi mwa Gorino ‘wala watu’. Binadamu hawa wa ajabu walifurahia kupata windo bila jasho, Hellen aliongea lugha zote lakini wenzake wakabaki kucheka maana hawakuelewa, walianza kumtomasatomasa wakitaka kugawana minofu ya kiumbe huyu aliyenona sana na wengi wao walivutiwa na nyama ya makalio na mapaja kwa kuwa yalijaa hasa, lakini kabla hawajafikia azma yao ya kumcharangacharanga alitokea mwenzao ambaye aliwaamuru windo lile lipelekwe kwa kiongozi wao kwanza halafu yeye aamue ni nini cha kufanya.
Walimfunga kamba Hellen na kuenda nae katika ngome yao, moja kwa moja walimfikisha kwa kiongozi wao aliyejulikana kama ‘Kelume’ kwa cheo chake, yeye akaamua kua Hellen achanganywe na wale waarabu wengine ili asubiri zamu yake ya kuliwa nyama, mpaka hapo hakuna aliyegundua kuwa huyu ni mwanamke. Hellen hakujua la kufanya zaidi ya kupata mshtuko alipoona matukio yanayoendelea pale, mauaji ya kinyama huku ngoma ya ajabu ikichezwa na wanawake kwa wanaume ambao kwa ujumla ni kama walikuwa uchi kwani walijifunika tu sehemu za siri. Ngoma hii ilimkera sana Hellen kwa jinsi ilivyochezwa, kwake aliona watu hawa hawana hata chembe ya adabu lakini wenzake kwao ilikuwa ni burudani na maisha ya kawaida, kwani mara kadhaa alishuhudia wakifanya ngono bila kujali na wenzao wakishangilia, mara waliletewa nyama kwenye vyungu vikubwa tu na kula wakifurahi, nyama ya watu. Hellen alizimia alipoona jinsi Kelume anavyoua mmoja wa mateka na kumtoa moyo kisha kushangilia sana na kuilamba damu iliyouzunguka moyo huo, wengine wakinya damu katika bakuli. Hellen alihisi kufika dunia ya ajabu, alizidiwa na harufu mbaya ya damu, ubongo wake ulichafuka kwa kuona matukio yote yale, alizimia mara kwa mara.
Hata alipofungiwa katika lile pango kwake ilikuwa ni shida tu maana alijua wazi kuwa wakimaliza kazi yao huko watarudi kwake, alitamani afe lakini haikuwezekana, akimbie lakini alifungwa kamba, hakuna msaada.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Lito, seki londigo Kolilo isom”
amri ilitoka kwa kelume akimaanisha ‘simama, kafara ya kolilo imefika’ msafara ulisimama alfajiri ile katika jiwe kubwa jeusi lililochongoka juu kama kichuguu cha mchwa, hapa ndipo walipotolea kafara yao, nje yake kulikuwa na mawe mengine mengi mengi yaliyojipanga katika mtindo tofauti. Msafara uliweka kambi kusubiri giza liingie ili kalamu ya kafara itolewe, kwa kuwa kafara yao hutolewa tu wakati wa mbalamwezi na si vinginevyo. Mateka wale walichukuliwa na kuwekwa kwenye pango maalumu ndani ya jiwe lile ili kusubiri wakati, huku nje gorino wakiendelea na ibada zao kwa Kolilo.
Ndani ya jiwe lile kubwa lililoko juu ya mlima mmojawapo kati ya mingi katika msitu wa Solondo mlikuwano na shimo kubwa na ndani ya shimo hilo kulikuwa na mashimo mengimengi yenye giza la kutisha, mara nyingi nyakati za usiku huonekana vitu vya ajabu katika eneo hili vinavyosadikiwa ni mashetani. Gorino wao wanaamini kuwa hapo ndipo Kolilo anapoishi kwa hiyo huja kutoa sadaka ya damu na nyama ya moyo katika jiwe hilo.
*******************************************************
Amata alijikuta mbele ya gofu, alitazama gofu lile kuona kama kuna dalili zozote za kiumbe kuishi lakini hakuona, polepole alisogelea banda lile liliojengwa kwa mawe na miti, lilikuwa kimya kabisa, kabla hajalifikia kabisa alilizunguka kuona labda kuna chochote au yeyote, lakini jambo la ajabu lilitokea kila alipozunguka alijikuta bado yupo upande uleule, akastaajabu na kushindwa la kufanya akabaki amesimama akiiangalia nyumba ile hali mshale wake tayari upo utani kwa shambulizi. Kutoka nyuma yake akasikia kitu kama ndege kikipipiga mbawa na ghafla juu ya banda lile akatua Bundi mkubwa ambaye Amata hakuwahi kuona maishani. Akavuta uta wake na alipouachia mshale ule uliondoka kwa kasi kumuelekea Bundi yule lakini alishokishuhudia ni mshale kudakwa na Bundi yule vizuri na kwa ustadi mkubwa kwa kutumia mdomo, Amata akabaki mdomo wazi na kushusha uta wake chini taratibu. Bundi yule akatuwa chini na mara upepo wakisulisuli ukavuma vumbi likatimka na majani kupepea kila mahali, alipofumbua macho alikuta ajuza kasimama mbele yake, bibi wa umri mkubwa, Amata alimkumbuka bibi yule
“usiogope Amata”
ajuza akamsihi Amata kisha akaendelea
“umeingia kwenye Himaya yangu, na nilijua utafika tu”.
Amata alimkazia macho bibi yule kisha akamuuliza
“wewe ni nani?”
bibi yule alitoa cheko la kutisha lililomfanya Amata kurudi nyuma hatua chache, cheko lile likatulia na bibi yule sasa alikuwa na macho mekundu sana “mimi si binadamu kama wewe” bibi akamwambia Amata
“huku binadamu kama wewe hawawezi kuishi wala kufika wengi hufa na sisi huwala nyama”
kisha akaendelea
“nimekuona muda mrefu sana na nilikuwa nakufuatilia, sisi tunawaogopa sana ninyi binadamu, lakini tumewazidi maarifa”
aliendelea kuongea bibi yule kwa sauti yake ya kutisha.
“Unatafuta nini huku Solondo?”
bibi akamuuliza Amata
“nimewasindikiza rafiki zangu, wamekuja kufanya utafiti wa hazina ya kale, inasemekana ipo huku” Amata alijibu kwa kitetemeshi. Cheko baya lilimtoka bibi yule Amata akaingiwa na woga mkuu
“wapo wapi rafiki zako?”
bibi akauliza
“sijui tumepoteana wote msituni ila mmoja amekufa nimemzika porini”
Amata alijibu kwa sauti ya shida, kofi zito lilitua kwenye shavu la Amata na kumpeleka chini. “Umeniuzi sana mimi na wenzangu, kwa nini umeondoa nyama yetu ambayo sisi tulikuwa tukiikausha? Halafu ukaifunga tusiweze kuichukua?”
bibi yule sasa aliongea kwa hasira na kumsogelea Amata, Amata alirudi nyuma kwa woga. Hapo ndipo Amata alipogundua kuwa kifo cha Stephen kilitokana na huyu bibi, hasira ilitawala roho ya Amata alitamani kulipiza kisasi lakini alijua hapo hatofua dafu alibaki katulia tu na kumeza mate ya hasira.
Bibi yule alinyoosha mikono yake juu na alipoishusha Amata alihisi kama kuna watu wametua kutoka juu lakini hakuwaona kwa macho
“fumba macho!”
bibi yule alimwambia Amata na Amata akafanya hivyo. Amata alihisi kaupepo mwanana kisha kwa mbali akasikia sauti ikimwambia
“fumbua macho”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
na alipofumbua aliona wasichana wazuri ajabu mbele yake, uzuri wao hajawahi ona maishani mwake Amata alistaajabu na kujiuliza kama wale walikuwa ni binadamu kweli au la, alifikicha macho yake na kutazama tena, bibi yule akamshika mkono Amata na kumpeleka ndani ya banda lile, Amata alisikia sauti za watu waliozama katika mahaba zikizidi kuongezeka, sauti za watu walio katika raha ya ajabu, sauti zile zikaanza kumletea kumbukumbu fulani Amata, akavuta hisia kali “Golaaaaaaammmmm!”
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment