Simulizi : Msitu Wa Solondo
Sehemu Ya Tatu (3)
“Hapana amata, hizo ni hadithi za kale, si za kuamini, wazee wetu walitusimulia ili tuogope kabisa kuingia ndani ya msitu huu lakini ukweli ni kuwa ndani ya msitu huu wajerumani wamehifadhi vitu vingi sana na babu wa baba yangu alikuwa askari wao amekuja sana huku kuleta vitu walivyokuwa wakivichimba huku na huko katika nchi yetu! Watu wengi waliuawa na wajerumani ndio na hawakurudi tena vijijini mwao ndio maana hizo hadithi zenu zikawepo”
saringo aliongea kwa jazbaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“...hadithi zenu !!! hadithi zenu!!!”
Amata alijiwazia moyoni akijaribu kulinganisha asemayo Saringo. Amata akashusha pumzi akibaki na maswali mengi kichwani akatoa pera akaanza kutafuna huku akichezesha kichwa chake kama mtu anayefuatisha muziki fulani. Wakiwa katika hali ya ukimya sana kila mtu alizama katika mawazo yake ambayo hakuna mwingine aliyeyajua
“Dunia imekuharibu umesahau mila na desturi za nyumbani”
aliropoka Amata kumwambia Saringo, Saringo alihamaki kwa kauli ya Amata na kumtazama usoni sasa sio kwa sura ile legevu bali yenye jazba na uchungu
“Unasemaje Amata?!.. wewe unaendekeza ujinga na upumbavu wa kijijini! Hujui hata dunia upande wa pili inaendeleaje, lazima maisha yabadilike, mimi naishi mjini naelewa lakini wewe umezaliwa na kukulia huku porini utajua nini, fuata nnayokwambia”
saringo alifoka.
“ Huwezi kuniamrisha kufuata unayonambia wewe ni mwanamke tu, kama mimi nimekulia huku mshamba wa kizamani kwa nini mlinitafuta katika safari yenu hii isiyo na miguu wala kichwa, na usomi wenu na maendeleo mliyonayo mngefika wapi? Stephan yuko wapi , hellen yuko wapi? Mbona wamepotea bila kujua, na we bado zamu yako. Lazima udumishe mila na desturi, asili itabaki kuwa asili tu!”
Amata alifoka pia.
“Asili itabaki kuwa asili tu”
Maneno haya yalimchoma sana Saringo na yalimrudia mara kwa mara. Saringo akanyanyuka na kusogea pembeni, akaketi na kuikunja miguu yake kuelekea kidevuni huku akiwa kaizungushia mikono yake aliinama na kulia kwa vikwifukwifu.
Giza liliufunika msitu taratibu, sauti za ndege na mbweha zilisikika huku na huko, macho ya Amata yalikuwa yanapambana na usingizi uliokuwa unayasumbua huku wadudu nao wakifurahia kuona kiumbe hiko katika makazi yao, hakuona njia nyingine zaidi ya kutafuna matunda yake aliyoyahifadhi vyema katika mkoba suruali yake ile ya kimagereza, huku akitumia nguvu nyingi kujaribu kuangaza angaza kuona kama kuna hatari yoyote inayowakabili, alimwangalia Saringo na kugundua kuwa tayari alikuwa amelala
‘wanawake bwana!’CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
alijisemea moyoni huku akitikisa kichwa chake kuonesha kukata tamaa.
“We mbona unalala kibwege hivyo? Unafikiri uko kwenu hapa!”
alimuamsha Saringo kwa kumtikisa na kumwambia maneno hayo, saringo alinyanyua kichwa na kumtazama Amata kwa sura yenye mikunjo ya usingizi na uchovu. Amata alitabasamu na kukumbuka maneno aliyoambiwa na baba yake
‘ukitaka kuchagua mchumba mtazame anapoamka’
hapo alihakikisha baada ya kuona sura ya Saringo alipotoka katika kipande hicho cha usingizi, akarudi alipokaa na kusimama kwa muda kisha alimfuata Saringo, kibaridi kilichukua nafasi yake msituni hapo na wakiwa wamejikunyata kila mmoja kamshika mwenzie ili kupata kajoto wakapitiwa na usingizi uliowachukua kwenda ulimwengu wa mbali.
Saringo alibebwa juujuu na watu wa ajabu wenye mguu mmoja huku wakiimba nyimbo zisizoeleweka, wakizunguka naye katika mduara mkubwa ambao katikati yake kulikuwa na moto mkubwa sana, ngoma zilirindima, wengine walioketi pembeni walionekana kunywa kitu kama pombe kwenye kata kubwakubwa huku wakifurahia na kucheka kwa sauti za ajabu, Amata aliketi palepale akiangalia huku akitetemeka kwa woga wa ajabu, kijasho kilimtoka kila alipotaka kupiga kelele za kuomba msaada alijikuta sauti haimtoki na wale viumbe walimcheka sana, akajaribu kujitikisa hakutikisika kabisa kumbe alikuwa amefungwa katika mti mkubwa uliopo katika uwanja ule ambao ngoma hiyo ya ajabu ilipigwa na kuchezwa na hawa viumbe wa ajabu. Bado wale wengine waliendelea kucheza huku wamembeba Saringo juu kwa juu wakipokezana kwa furaha, mara wakamshusha na kumlaza katika jiwe kubwa lilichongwa kama ngalawa lakini halikuwa na shimo katikati, akiwa kama alivyozaliwa juu ya lile jiwe hakuweza hata kutikisika, Amata aliangalia kwa makini akitaka kujua wanataka kumfanya nini lakini kila alipojitikisa hakutikisika na kila alipofanya hivyo alisikia sauti za ajabu zikimcheka sana aliogopa na kutulia tuli kama maji ya mtungini.
Ilikuwa ni sherehe ya ajabu ambayo Amata hakupata kuiona tangu azaliwe katika dunia hii, akiwa katika hali ya kutaharuki hakupenda kuona kinachoendelea, alifumba macho yake kwa nguvu zote lakini bado akili na moyo wake vilitaka kuangalia kinachoendelea, aliyafumbua macho yake na alichokiona kilimchanganya kwa kuwa hakuelewa ni nini na kwa nini,wanawake saba waliokuwa uchi wa mnyama wakiwa wanatokea ndani ya kitu kama pango ambalo liko chini ya mti mkubwa kichwani walijitwika vitu kama vyungu wakiwa wanatembea kwa mwendo wa kurukaruka kwa kuwa walikuwa na mguu mmoja kila mmoja, waliimba nyimbo zisizoeleweka na wale wanaume waliombeba Saringo juu juu na kumlaza pale katika jiwe waliendelea kucheza ngoma ile isiyoeleweka, Amata alikuwa na woga mkuu akitetemeka mwili wote. Wanawake wale walilizunguka lile jiwe na kutua vyungu vilivyokuwa kichwani mwao, mmoja wao aliyeonekana kama ndiye kiongozi wao alitwaa chungu kimoja na kukinyanyua juu kama anayefanya sala fulani, kisha akakishusha akakiweka pembeni ya miguu ya Saringo akaingiza mikono yake na kuchota kitu kama mafuta ya kupikia na kuanza kumpaka Saringo akianzia miguuni kisha na wenzake nao wakafanya hivyo, sasa walimpaka mwili mzima huku wakiongea lugha ya ajabu ambayo Amata alijaribu kuisikiliza lakini hakuilewa
‘hawa viumbe gani?!’
Amata alijiuliza bila majibu, aliendelea kutazama kwa woga. Wanawake wale walipomaliza kazi hiyo walinyanyuka na kurudi kule walikotoka na kumuacha Saringo akiwa kalala pale aking’aa kwa mafuta yale pindi akiangazwa na mwanga wa moto ule akiwa kimya kabisa, Amata hakujua kama saringo alikuwa mzima au la maana misukosuko yote yeye alikuwa kalala kama mfu hakujitikisa wala hakufanya lolote.
Mara wale wanaume wakaanza tena ngoma yao sasa kwa uchangamfu zaidi huku wakipiga makelele ya ajabu na kurukaruka, ndipo Amata akagundua kuwa ule mguu mmoja walionao kila mmoja wao huku chini ulikuwa na kanyagio kama la kuku, mara upepo mkali ukaanza kuvuma na wao wakiwa bado wanacheza ngoma yao sasa wakionesha munkari zaidi, mara kutoka katika mti ule ambao waliingia wale wanawake joka kubwa lilibuka kwa kasi ya ajabu,
“Ssss......”
Amata alijaribu kumuita Saringo lakini sauti haikuweza kutoka hata kidogo, joka lile lilijikunjua kwa kuzunguka likiwa hewani sasa likiwa linaelekea pale alipolazwa Saringo, na liliposikia sauti hafifu ya Amata likageuka huku aliko na kutema mate kwa kasi kumtemea Amata,
******************************
..mara Amata akazinduka kutoka usingizini, alikuwa akihema kama mtu aliyekuwa akikimbizwa,
“Saringo, Saringo!”
Aliita huku akiweweseka. Alipotulia alijikuta kaloa mwili mzima na pembeni yake kuna kitu kama kata kubwa liliotelekezwa na ndani yake kulikuwa na maji kidogo, ndipo alipogundua kuwa kamwagiwa maji nandiyo ylaiyomfanya akurupuke kutoka katika usingizi wake, lakini nani alimwagia maji hakumjua wala hakumuona, wala Saringo hakumuona eneo lile, nalipoangalia vizuri aligundua kuwa hakuwa pale ambapo alipitiwa na usingizi, hapa ni mahali pengine kabisa ambapo hakupajua kabisa, aliangaza macho huku na kule lakini hakuona dalili ya mtu wala mnyama, palikuwa patupu miti ikiwa imezunguka kwa mbali na katikati palikuwa wazi ni nyasi fupifupi tu zilijaa katika eneo lile. Alijinyanyua kutoka pale alipokaa na kusimama wima, alivuta ukimya kidogo kuona kama kuna kitachotokea awe mtu au mnyama lakini hali libaki kuwa ileile ‘hapa ni wapi?’ Amata alijiuliza lakini hali ilikuwa ni ile ile, mara nyuma yake akasikia sauti ikimwita kwa kunong’ona ikirudiarudia jina lake, amata alitulia na kimya huku akiwa hajui cha kufanya, moyo ulimdunda kwa kasi akageuka taratibu kuona ni nani aliyemuita, Amata alitahamaki, hakuamini macho yake alichokiona.
Bibi kizee aliyechoka, ngozi yake imekauka kwa kukosa vitamini, macho mekundu ya kutisha, nywele zote nyeupe na unaweza kuzihesabu, miguu yenye vidole visivyo na kucha, Amata alimwangalia kwa umakini ajuza yule lakini moyoni akijawa na hofu,
‘hakika ajuza huyu angekuwa kwenye mikoa ya upande fulani wa nchi asingekuwepo hii leo hasa kwa macho yake’
mawazo haya yalipita haraka kichwani mwa Amata. Ajuza yule hakuwa hata anatikisika alisimama vilevile huku akisaidiwa kwa mkongojo ule alioushika, alimkazia macho Amata, kwa wakati huo Amata hakujua la kufanya, akimbie? Hapana, Amsalimie? Hakuna jibu, sasa afanyeje hakika ulikuwa mtihani mkubwa sana kwake,
“Amata...”
bibi yule aliita tena kwa sauti ya kukwaruza na mbaya huku akimwangalia Amata, Amata alimwangalia kwa umakini na kuanza kurudi nyuma taratibu
“Usiogope Amata, sogea hapa!”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
yule bibi alimsihi Amata huku akimuonesha ishara ya kumuita kwa mkono, Amata kwa woga alimsogelea bibi yule na alipomkaribia kabisa mwili wake ulisisimka sana na damu yake kwenda mbio, yule bibi akanyanyua mkono wake na kumpiga Amata kofi utosini, Amata aliona giza nene kisha hakuelewa chochote kinachoendelea.
Saringo aliendelea kutaabika na kuhangaika hakujua ni wapi alipo ila tu aligundua kuwa yuko ndani ya kitu kikubwa cha mviringo, giza kila upande, joto na hewa nzito alikuwa akipambana navyo wakati huo, akijaribu kunyanyuka alishindwa kabisa maana alijigonga kwa juu alijaribu kupiga kelele lakini ilikuwa kazi bure hakuna aliyemsikia huko nje kama alikuwepo. Mara kwa mbali alisikia sauti za watu wakiongea alitega sikio kwa utulivu mkubwa ili angalau asikie wanachokiongea lakini haikuwa hivyo kwani lugha waliyoitumia hakuweza kuielewa hata kidogo
‘Gwelino’
alijiwazia na mara hofu kuu ilimjaa kijasho chembamba kikaanza kumwagika kwani alijua habari za viumbe hawa ambao wanaishi katikati ya msitu huu wa Solondo na hupendelea kula moyo, utumbo, maini na mapafu ya binadamu. Saringo aliona kuwa sasa aliyokuwa akisikia juu ya Msitu wa Solondo yametimia, alijilaumu sana kwa nini na kwa vipi alijikuta akijihusisha na safari hii ngumu na mbaya, alifumba macho yake na kukumbuka maneno ya babu yake aliyokuwa akimsimulia alipokuwa mtoto juu ya safari ya Solondo, alijilaumu sana nafsi yake na roho yake yenye uroho wa utajiri
‘nani aliniambia huku kuna utajiri?alinidanganya! hapana, ni babu alinihakikishia kuwa wamezika mali nyingi huku,ah no! Alinidanganya?’
Saringo alijiuliza na kujijibu, alijilaumu na kujipa moyo, mawazo yake yakamrudisha nyuma sana na kumkumbuka babu yake Mzee Mapendo siku walipokaa wakiota moto naye akamsimulia mengi ya wakati wa ukoloni na utawala wao ambapo hapo ndipo alimsimulia juu hazina iliyofichwa na wajerumani huko Solondo..
Miaka 20 iliyopita...
kijijini kwa akina Saringo
Mzee Mapendo aliketi karibu kabisa na moto kwa kuwa yeye aliona baridi wakati wenzake walikuwa wakiona joto kali, pembeni alikuwa na kiko yake na kikombe cha maziwa, wajukuu walikuwa wamemzunguka kama unavyojua babu akaapo. Mzee huyu aliyekula chumvi nyingi alikuwa na maneno mengi ingawaje sasa hakuwa na jino hata moja kinywani mwake, alikuwa ahishiwi simulizi kwa wajukuu zake. Alipenda kujivuna kuwa yeye ni askari imara wa mkoloni aliyeogopwa na kila mtu.
“Babu!”
saringo aliita kwa sauti kijukuu, wakati huo akiwa na miaka nane darasa la kwanza.
“Enhe niambie babu yangu!!!!!”
Mzee mapendo alimuitikia kwa bashasha
“Babu vidole vyako vya miguumbona sio vitano? Viko vitatu tu!”
saringo alirusha swali la uchokozi kwa babuye
“A aaa sasa mchumba umeanza udadisi wako! Nikwambie mara ngapi? Hivi vidole vilikatika hukoooo porini huko tukiwa kazini zamani za mkoloni”
alijibu kwa kirefu.
“Mmmm babu, kazini ndio ukatike vidole!”
“Eeeee mama, tulikuwa tunapambana na maadui, mimi nimekwenda vita ya kwanza ya dunia na ya pili ya dunia, mimi askari mtiifu”
aliongeza jibu na kuedelea
“tulikuwa tunatembea mwendo mrefu kutoka kule kilima cha Saroge kwa mguu wakati huo hakuna mutuka hiz, tumetembea safari ndefu sana tunapanda milima na kushuka mabonde mpaka kuleeee mlima wa Vegani, unaujua mlima Vegani wewe?”
alimtupia swali Saringo
“Mlima Vegani? Mi siujui babu”
saringo alijibu
“Aaaaaah kweli huwezi kuujua wewe bado mdogo! Sasa kaa chini hapa nikusimulie!”
Mzee Mapendo alimwambia Saringo. Saringo akakaa chini akimtazama babu yake kwa makini huku akifuta makamasi mara kwa mara kwa mikono yake na kufanya sehemu ya kati ya mdomo na pua yake kung’aa kwa makamasi yaliyokauka.
Mzee Mapendo akaanza simulizi yake
“Tulipokuwa vijana sisi tulikuwa askari wa mkoloni, tulikuwa tunakaa hukoooo Saroge ndiyo ilikuwa kambi ya Mjerumani miaka hiyoooo, sisi tukiwa askari wakakamavu kabisa, tumefuga masharubu yetu tukisimama pale kwenye gwaride aaaaaa mjukuu yaani upepo ukipuliza utasikia kama mtu anapiga mbinja, hiyo ilikuwa ni moja ya sare yetu. Siku moja tukiwa kambini pale king’ola kililia tukatoka ndani wote tukapanga mstari, tukatangaziwa kuwa kuna mgeni amekuja kutoka ujeremani huyu Bwana alikuwa anaitwa aaa nimemsahau kidogo oooh Karl Peter, huyu Bwana alikuwa mrefu na mwenye tambo la kikakamavu haswa alikagua kikosi chetu na aliporidhika tulichaguliwa askari hodari kama kumi hivi na mimi babu yako nilikuwepo. Dhumuni ilikuwa ni kusafiri kwenda huko mlima Vegani alisema kuna mizigo ya kuchukua kupeleka sehemu nyingine. Tulianza safari asubuhi sana kupitia katikati ya pori kubwa, njiani wote tulikuwa kimya sana kila mtu akitafakari juu ya safari ile. Tulifika Vegani baada ya siku mbili, pale mlimani tulikuta watu wengi sana nilishangaa kuona mashimo makubwa makubwa na watu wakiingia na kutoka wamebeba maudongo mengi, sikuelewa ni nini kinaendelea. Pale tukapokelewa na wajeremani wengine wakatupeleka sehemu kupumzika kidogo, tukala halafu ndio tukaambiwa tunatakiwa kusindikiza msafara wa mizigo kwenda Solondo. Asubuhi yake tukaenda katika lichumba limoja kulikuwa na masanduku ya chuma mengi tu ndani yamejaa mavitu mazurimazuri, sisi hata hatukujua ni vitu gani basi tulikuwa na wapagazi wakabeba pale yale masanduku tukaanza safari ya kwenda huko Solondo” Mzee mapendo akakohoa kidogo, kisha akaendelea
“safari ile ilikuwa ndefu na ya hatari sana mjukuu wangu, tulipanda milima mikali na kuvuka mito mikubwa yenye mamba wakubwa, tulikutana na nyoka wakubwa wengine wana vichwa viwili tulipambana nao hivo hivo ndio kisa cha vidole vingine kupotea uko huko.”
“Sa mlikuwa mnaenda api?”
saringo aliulizaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Aah mjukuu wangu, mbali huko kwenye msitu kulikuwa na jiwe kubwa sana chini lina pango kubwa na shimo la ajabu humo ndio tukatengeneza eneo zuri tukachonga ngazi za kupandia na kushuka, tukatengeneza vyumba vingi sana tukahifadhi hayo mamizigo yao, kule wakaweka mamilango makubwa ya chuma na makufuli makubwa funguo wakabeba, mimi mjukuu nikaona hii itakuwa ni mali sana kwa nini wafunge hivi!!!? Tukaongozwa kutoka nje ya hilo pango... mjukuu wangu we hapo walianza kutugawanya makundi makundi kurudi lakini walipanga kutuua sote ili tusije kurudi kule pangoni, muda fulani niliona wanachukua karatasi fulani na kulisoma wakiongea kikwao na kuweka alama fulanifulani kwenye ile karatasi na miti iliyo eneo hilo na mawe walituelekeza kuchonga alama fulani fulani, kisha tukapanda mlima mmoja mkubwa na kusimika chuma kikubwa kimoja kimesimama na kingine kimekatisha katikati yake, ule ndiyo uchawi wao mjukuu, wakatuambia atakayekuja huku atakufa hatorudi tena duniani, tuliogopa sana lakini mimi nikajua huu ni ujanja tu. Mjukuu! wale watu ni makatili bwana!! sisi tulikuwa wanne na wao wawili, tukafika mtoni wakamwambia mmoja wetu avuke kwanza kumbe wanajua kuna mamba alipoingia tu mtoni wale mamba wakamkamata wakamla, halafu wenyewe wanacheka huku wanavuta kiko zao mdomoni, mimi! Mjukuu! nilikasirika sana sikujua nifanye nini, wakatuambia tupite njia nyingine, tukaendelea na safari ile huku kila mmoja wetu akiwa na mawazo mengi”
Mzee Mapendo akaendelea kuchochea kuni zake katika ule moto huku akiendelea kumsimulia habari ile mjukuu wake, Saringo, kisha akaendelea... “Safari ile mjukuu ilikuwa mbaya sana tulipita kwenye nyika kubwa, tukikutana na wanyama wakubwa sana, sasa tulifika sehemu moja kulikuwa na kama kijiji hivi, hapo palikuwa na watu wanaishi lakini watu hawa walikuwa wa ajabu sana, walipotuona walianza kufurahia na kutuzunguka wakitaka kutukamata, walikuwa wanatisha kwa sura, nywele ndefu, wamevaa ngozi, mbaya zaidi walikuwa wanakula watu. Mara tukajikuta katikati ya watu hawa, yule askari mmoja wa kijerumani alianza kuwashambulia kwa risasi kwa kutumia lile bunduki lake kubwa, walipoanza kuona wenzao wanaanguka ndipo walipopata hasira na kutushambulia kwa nguvu, walimkamata mmoja wetu na kumkata kichwa kisha niliona wengine wakinywa damu ile mbichi. Mimi nilifanikiwa kutoroka na mjerumani mmoja tukawaacha wenzetu kule, kwa kweli sijui hata nini kiliwapata. Tulipofika porini yule mjerumani akawa na hali mbaya maana alijeruhiwa sana hakuweza kutembea na kuongea kwake kukawa kwa shida sana alikuwa akitokjwa na damu nyingi mdomoni na sehemu za kisogo chake, hakuchukua muda alikufa, nikabaki peke yangu msituni niliogopa sana, nilipoangalia tulipotoka niliona tu moshi umetanda huko, mjukuu! Hivi vidole vimekatika katika kujaribu kujiokoa na hao wagwelino, hakuna nilichofanya niliamua tu kujaribu bahati yangu, nikachukua yale makaratasi yule mjerumani alikuwa nayo katika mkoba wake na lile libunduki lake, nikatembea msituni usiku na mchana, mwisho nilifika kijijini baada ya siku kadhaa, ule mkoba mpaka leo ninao nimeuning’iniza pale ukutani chumbani kwa bibi yako, ukiwa mkubwa uuchukue ule utakuwa na mambo mengi sana sawa mjukuu ah! ah! ah!, mi ndiyo babu yako shujaa...” alimaliza kwa kucheka huku akimpigapiga Saringo mgongoni.
Alipomaliza kusema hayo alikuta kumbe tayari mjukuu wake Saringo ameshapitiwa na usingizi zamani sana na kwake hadithi hiyo ya kishujaa ilikuwa inajirudia kama ndoto mbaya na ya kutisha.
*********************************
Amata alijikuta hana lakufanya baada ya kujikuta kafungwa kamba miguu yake na kuning’inizwa kwenye kitu kama goli la mpira naye yupo kichwa chini miguu juu, kichwa kilimuuma sana hata alikiona kizito, mara kwa mara alijikuta akiona giza na vitu vyeupe vyeupe viking’aa sana vikimzunguka huku na huko. Alipogeuka kwa tabu huku na huko hakuona mtu yeyote isipokuwa mandege makubwa tu yakizunguka na kutua mahali fulani, Amata aliyatambua haraka haya mandege ambayo uyaonapo ujue kuwa kuna mzoga eneo hilo, fahamu zilimrudi polepole Amata na kukikumbuka kile kizee
‘kigagula’
hakuna jirani wa kumuomba msaada, hakuna kiumbe cha kuelewa lugha yake, aliona sasa hapa hana ujanja tena alipenda afe kabla hawa jamaa hawajamfikia akiogopa kupambana na mateso makali bila yeye kujitetea. Inzi na wadudu warukao kwa jinsi zake walikuwa wakimsumbua usoni kutokana na makamasi yaliyokuwa yanamvuja na hakuweza kuyapangusa kwa kuwa mikono yake ilikuwa imefungwa kwa nyuma, alijaribu kuitikisatikisa kuona labda kamba ile inaweza kuwa imelegea lakini haikuwa hivyo. Mara ghafla aliona mti mkubwa uliopo hapo jirani ukitikisika matawi yake na alipoangalia aligundua kuwa ni nyani mmoja mkubwa yuko hapo juu, alijaribu kutoa ishara kwa kichwa labda nyani yule angeelewa kitu lakini haikuwa hivyo hata kidogo.
Kwa mbali sauti za viumbe hai zilisikika na kuongezeka zikiwa zinakaribia eneo lile, mara akamuona yule nyani akikimbia tena juu zaidi ya mti na kupiga mruzi mmoja mkali, kumbe alikuwa na wenzake eneo lile wote wakapanda miti haraka na kukaa kimya juu kana kwamba hakuna kiumbe hapo juu. Msafara mkubwa wa watu uliingia pale, watu wakutisha wanaoonekena ni makatili kwelikweli wakiwa wamejichora marangi meupe wamejichanja chale nyingi, kiunoni wamevaa tu kangozi ka kuwahifadhi maeneo yao. Mbele yao wakiongozwa na mmoja wao mwenye tambo kubwa kwelikweli akiwa amebeba lijiti lenye ncha kali linaloonekana kabisa kuwa limelowa damu, nyuma yake walifuata watu kama kumi hivi wanne wakiwa wamebeba kitu kama nyama kinachoning’inia kati ya miti miwili, wakafika pale kwenye kale kauwanja, wakasimama na kushusha ule mzigo, yule kiongozi wao aliongea lugha fulani ya ajabu ambayo Amata hakuielewa, mara wenzake waliitikia kwa kelele huku wakionyoosha juu majiti waliyoyabeba ambayo yalkikuwa na ncha kali na yamelowa kwa damu. Wawili kati yao walitoa ule mzigo, la haula !!! Amata hakuamini alichokiona mwili wa binadamu ambao umetota kwa damu kiasi kwamba hauwezi kuuelewa ni umekumbwa na masaibu gani, Amata alihisi mwili kusisimka na kuchoka kwa wakati mmoja, alitulia palepale akiangalia nini kinaendelea, wakafunga kamba ule mwili kama alivyofungwa Amata na kuja kuning’iniza kwa jinsi ile ile, Amata alijituliza na kufumba macho yake huku akipumua kwa mbali ili wasijue kama ni mzima, walipomaliza kazi hiyo, yule kiongozi wao akasogea kwa Amata na kumwangalia kwa makini sana akachukua kisu kikubwa na kikali akakamkamata Amata upande wa kushoto wa bega lake kisha akacheka kwa sauti ya ajabu na wenzake wakacheka kwa sauti hizo. Amata aliingiwa na hofu
‘mama moyo wangu’CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
alihuzunika moyoni lakini alijua basi hakuna kitachosalimika. Yule jamaa akainua bisu lake juu akashusha kwa kasi kuelekea kifua cha Amata, bila kutegemea Amata alimuona lile jitu likiganda na kuanguka kama mzigo, wenzake wakashangaa na kuangalia huku na huku na wasione mtu yeyote, walibaki kujiuliza imekuwaje kwa mwenzao, kiongozi wao, walianza kupiga makelele wakikimbia huku na huku, Amata akajua sasa amekwisha hata yeye hakuelewa kilichotokea alijigeuza kwa tabu kuangalia pale alipoanguka yule mtu, kwa macho hafifu aligundua kuwa mgongoni kwa lile jitu kunakitu kama mwiba wa mchongoma umemchoma, kwa haraka Amata aligundua kuwa hiyo ni silaha hata ri ya
‘Amazonia’
alipata faraja kuwa huwenda kuna binadamu pale aliyefanya kazi ile, kwa hiyo tumaini la maisha lilimjia tena, lakini hakuona dalili yamtu isipokuwa viumbe vile vyenye hasira vikiruka huku na huko wengine wakiwa porini kutafuta chochote, mara wakarudi na aina fulani ya majani wakayapondaponda huku wakiongea lugha ile isiyoeleweka kicha wakamkamulia maji ya majani yale mdomoni yule kiongozi wao baada ya muda kidogo akapiga chafya kama tani mfulululizo akaamka. Amata lijua hapa kazi hii labda huyualiyefungwa hapo kaifanya lakini alipomwangalia aliona ni kama mwili usio na uhai, matone ya damu yakiwa yanadondoka taratibu kutoka mwili wa mtu yule. Amata alijaribu kuangalia kwa machale mwili ule lkini hakuweza kugundua ni wa nani japo alihisi ni wa mmoja wao.
Lile jitu likaamka tena sasa likiwa na hasira na kukunja sura yake mbaya sasa halikuwa na huruma hata kidogo, lilichukua lile jiti lake kubwa kuendelea na alichodhamiria. Akiwa kainua tena jisu lake na huku kwa nyuma Amata kabanwa na mti wenye kipago na mtu mwingine ili kuhakikisha lengo lao linatimia. Kabla hajashusha jisu lile mwili wa Amata ulianguka chini, kamba iliyofungwa miguuni mwake ilikatwa kwa ustadi mkubwa sana, Amata alisikia mvumo wa kasi ya kitu kichokata kamba ile, mara moja aligundua kuwa ulikuwa mshale uliorushwa kwa uta wenye nguvu, na aina hii ya mishale ni mishale iliyotengenezwa sana na marehemu baba yake, Amata aliduwaa pale chini hakuelewa nini kinatokea kabla hajapata akili sawasawa alishuhudia mshale mvumo wa mshale mwingine ukielekea upande wake alijigeuza kifudifudi na mshale ule ulipita katikati ya fundo lililofunga mikono yake na kuchoma chini ardhini, sasa kamba ile ilikuwa imefunguka, Amata alisikia mbinja ya ajabu akajiinua haraka aliposimama akapata kizunguzungu cha ghafla kilichomrudisha chini lakini hiyo ilikuwa ni bahati kwake kwani lile jitu lilifurusha jisu lake lililolenga shingo ya Amata lakini shabaha ikakosa malengo, jitu lile lilimfuata Amata pale chini Amata kwa haraka akauchomoa ule mshale pale ardhini na kuurusha kwa mrusho hafifu lakini mshale ule ulitua jichoni kwa lile jitu, damu zikachuruzika kwa kasi, Amata alijiviringa upande wapili na kulifikia lile jisu alilinyakua na kupiga goti moja na kushindilia lile bisu mgongoni kwa lile jitu, lile jitu likatoa mkoromo wa kutisha na kukata roho. Hali haikuwa shwari eneo lile, wale wengine wakaanza kupiga kelele za ajabu na kuanza kumshambulia Amata kwa mapigo ya kifo, kutokana na uchovu aliyonao Amata aliona hapa hata kukimbia hawezi alijitahidi kufanya hiki na kile, mmoja wao alichumpa mbele ya Amata na kumkaba koo kwa mikono yake yenye nguvu na mikavu inayokwaruza, lakini mara Amata alishuhudia mshale mwingine ukizama shingoni kwa huyu mtu na kuanguka chini kama mzigo, waliobaki walipoona hayo wakaanza kutawanyika wakipiga kelele za sasa zilikuwa tofauti na za mwanzo mara kutoka mbali aliona kundi lingine likija upande ule, Amata alishindwa afanye nini, akauendea ule mwili ulioning’inia pale kuutazama vizuri. Wale viumbe waliosalia waliendelea kutandikwa na mishale isiyojulikana wapi inatokea na nani anaerusha. Amata alipigwa na butwaa alipougeuza mwili ule kwa nyuma...
*************************************
‘Kingusu’
“Ah!”
alishangaa na kufikicha macho yake kama mtu ambaye haamini ni nini alichokiona. Aligundua tu ni mwili wa binadamu wa kizungu kwa kuwa aliona baadhi ya nywele ndefu ambazo zilisalia kichwani mwa mwili ule, sura yake haikujulikana vizuri kwa jinsi ilivyogandamana na damu nyingi, Amata alijaribu kwa haraka labda angeona angalau jinsia ya mwili huu iliajue kuwa ni Hellen au Stephan, lakini kilichomshangaza mwili ule haukuwa na alama yoyote ya jinsia. Watu wale walizidi kusogea wakiwa na hari ya kufanya mashambulizi kwa adui zao, wale wenzao wote waliokuja na yule kiongozi wao walikuwa wamelala kimya juu ya ardhi bila uhai baada ya kupigwa kwa mishale isiyojulikana wapi inatoka, Amata alisikia mlio wa mbinja uliopigwa kutokea kichakani, alijua maana ya mbinja ile kwani ni baba yake alikuwa akiipiga kumuashiria kuwa hapo kuna hatari utoke haraka, Amata alishangaa maana hakujua ni nani aliyeyafanya haya yote. Alihisi kitu kikimshika bega alipogeuka alikutana uso kwa uso na nyani mkubwa mwenye kichwa cheupe, walitazamana kama sekunde kumi hivi, nyani yule alimshika mkono Amata na kumvutia msituni, Amata alimwangalia nyani yule kwa makini kule msituni ‘Kingusu’ Amata alijisemea moyoni, lakini alishangaa nyani huyu amepata wapi ujasiri au amejuaje kuwa yeye yuko huku msituni! Kwa maana nyani huyu alimuona, Amata alikaa chini ndani ya kichaka kile nyani yule alimletea baadhi ya matunda, Amata alikula na kisha nyani yule akampa ishara ya kuwa amfuate, Amata alinyanyuka na kumfuata nyani yule huku kichwani mwake akijaribu kukumbuka juu yakiumbe hiki cha ajabu..
Miaka 25 iliyopita
Kijijini kwa akina Amata.
Mzee Nkhunulaindo, baba wa Amata alikuwa ni mzee anayeogopwa sana kijijini hapo, alipenda sana utani na watu lakini hakupenda mchezo kabisa katika kazi zake, alikuwa na shamba kubwa sana lililolimwa mahindi, mpunga na mboga za ina nyingi, familia yake ya watu watatu yaani yeye mkewe na mtoto wao Amata hawakuwahi kupatwa na janga la njaa hata mara moja.
Mzee huyu mashuhuri na hodari hakuna asiyemjua kwa umahiri wake wa kupiga mishale, hii ilipelekea kila mtu kuogopa hata kuingia shambani kwake kwa kuwa alihofia kudunguliwa kwa mshale wa mzee Nkhunulaindo.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya kifo cha mkewe Bi. Vituko, mzee Nkhunulaindo alibaki akiishi na mtoto wake huyo mmoja katika nyumba yao iliyopo shambani mwao, kila siku asubuhi alimfundisha kujiandalia chai na kabla hajaenda shuleni, na aliporudi nyumbani mchana alichukua muda mwingi sana kumfundisha mambo mbalimbali ya maisha, hata Amata alipofukuzwa shule kwa kosa la kumpiga mawe mwalimu wake, Mzee Nkhunulaindo hakuona haja ya kwenda kuomba msamaha kwa mwalimu huyo kwani hakupenda hata siku moja aonekane yuko chini ya mwingine kwa kuwa tu yeye anatokea ukoo wa kichifu.
Siku moja Amata alipotoka shule alikuja na kumwambia baba yake kuwa anahitajika shuleni, bila kusita kesho yake wote waliongozana na kukutana na mwalimu wa shule hiyo
“Mzee nimekuita kukupa taarifa kuwa mtoto wako amempiga mawe mwalimu wake na kumuumiza, hivyo tumemfukuza shule kuanzia leo hii”
mwalimu alimueleza baba wa Amata. Baba wa Amata limwangalia tu mwalimu hakuna alichomwambia, baada ya muda kidogo akajibu
“Nimekusikia mwalimu, asante”
akamshika mkono mtoto wake na kuanza kuondoka.
“Jamani, sasa ndio husemi lolote, Mzee! Si tuyazungumze”
mwalimu alimueleza baba wa Amata.
“Tuzungumze nini, we umeniambia mmemfukuza shule, sasa! Ungenambia unataka umfukuze shule sawa, lakini ushamfukuza. Mbona mimi baba yake sijasoma na nakulisheni nyote hapa kijijini? Twende mwanangu.”
Aliondoka na mwanae na kurudi nyumbani. Mwalimu alibaki akishangaa na hakujua la kufanya.
Siku hiyo mzee Nkhunulando, alirudi nyumbani kwa kuchelewa sana akiwa amekunywa pombe nyingi
“Mwanangu Amata, usijali, kama wamekufukuza shule wewe utajifunza elimu dunia, elimu isiyo na gharama ila juhudi zako tu katika kutafuta maisha...”
alisema hayo kwa sauti ya kilevi huku akijitupa kwenye kiti chake cha ‘mkao wa nyani’
“Watu hatujasoma na tunaishi bwana, na wewe mwanangu utaishi, mimi baba yako nina shamba kubwa na lina kila kitu hakuna mwingine hapa kijijini ananizidi kwa ardhi. Mi chifu bwana nikuombe msamaha... we nani, wajerumani wenyewe sikuwaomba msamaha itakuwa wewe mwalimu! Ha ha ha ha... sisi tunalindwa na mizimu ya kwetu, hapa mtu achezei hapa, na wewe Amata nitakukabidhi kwa mizimu ya kwetu ikulinde na ikuongoze siku zote za maisha yako mpaka utakapoenda kuungana nao...”
aliendelea kuongea na mwisho kupitiwa na usingizi pale pale kitini.
Siku iliyofuata walikuwa pamoja shambani, Mzee Nkhunulaindo alikuwa akimfundisha mwanawe maana ya mbija mbalimbali, jinsi ya kukabili hatari za porini na kuweza kusikiliza sauti mbalimbali za msituni ilikujua huyu mnyama gani au mdudu gani, alimfundisha jinsi ya kukwepa hatari na kufikiri kabla ya kuamua.
“Amata!”
Nkhunulando aliita
“twende msituni, chukua uta na podo twende”
alimuambia Amata, Amata alifanya hivyo na wakaenda msituni, pamoja nao walichukua mbuzi mmoja mweupe na kwenda naye. Njiani waliongea mambo mengi sana, Amata alipata maelekezo mengi sana juu ya kutambua hatari za misitu, na hapo ndipo alipoanza kumsimulia habari za msitu wa Solondo na maajabu yake, Amata alisikiliza kwa makini na kuuliza maswali mengi sana juu ya msitu huo.
Amata aliendelea kumfuata baba yake ndani ya msitu ule ulio karibu na shamba lao, baba yake Amata alikuwa daima anapenda kuongozana na mtoto wake huyu, mtoto pekee aliyempata katika maisha yake, alimfundisha mambo mengi sana ya maisha ya kijijini na porini, kila asubuhi alikuwa akimfundisha kupiga mishale kulenga vitu mbalimbali, mzee huyu alifurahi sana kumuona mwanawe akijitahidi kuuvuta uta wake kwa kutumia nguvu nyingi kwa kuwa bado alikuwa na umri mdogo.
“Amata mwanangu, wewe unatakiwa kuwa jasiri kama mimi baba yako!”
Baba yake alimueleza Amata huku akimpa tunda aina ya bungo alilomchumia msituni humo.
Safari ikaishia kwenye jiwe moja jeusi lililofichwa na mimea iliyotambaa karibu jiwe zima, katikati ya jiwe lile kulikuwa na kitu kama tundu hivi, Mzee Nkhunulando akasimama kimya kama dakika tano hivi, kisha akaanza kuongea kwa sauti.
“Wazee, nimekuja, leo nimewaletea mjukuu wenu mumtambue mumuone mumjue, maana yeye ndiye atakayebaki katika himaya yetu... mumlinde na mumuongoze katika maisha yake yote..” aliongea mengi sana na kuimba baadhi ya nyimbo huku akilizungunguka jiwe lile. Mara upepo mkali ukaanza kuvuma miti yote ikiyumba kwa upepo kana kwamba inataka kukatika lakini haikuwa hivyo, ndege waliokuwa juu ya miti hiyo waliruka na kupiga kelele kwa lugha zao. Amata aliogopa sana akamshika baba yake kwa nguvu
“Usiogope mwanangu, mizimu yetu inaafikiana na lile nililowaomba, usiogope hapa ni mahali salama tu”
Nkhunulaindo alimueleza mwanawe Amata. Mara juu ya mti mmoja akashuka nyani mkubwa mweusi mwenye kichwa cheupe akasimama mbele yao,
“Inamisha kichwa Amata”
Nkhunulaindo alimwambia mwanae, wote wakainamisha vichwa kwa muda walipoinua vichwa hawakumuona nyani nyule.
“Haya chinja mbuzi huyo”
Amata alipata amri kutoka kwa baba yake, akamkamata mbuzi yule vizuri na kumchinja, damu yake wakaimwagia kwenye jiwe lile mara tatu. Upepo mkali ukavuma tena, sasa na radi ikasikika.
Baada ya hapo walirudi nyumbani, ilikuwa tayari imetimu jioni.
“Baba, yule nyani alitoka wapi?”
Amata alimuuliza baba yake
“Ule ni mzimu mwanangu, lakini huwa unatokea kwa mfano wa nyani, anaitwa ‘Kingusu’daima ukimuona usimkimbie, ujue hapo ana jambo la kukuepusha au kukulinda”
*****************************
Stephan hakuelewa kinachoendelea pale alipojikuta katikati ya kundi la viumbe wa ajabu, alishikwa na woga na kutaka kukimbia lakini hakaona hiyo si mbinu nzuri kwa wakati huo, alipogeuka huku na huku aliona kuwa viumbe wale wa kutisha walikuwa wengi sana wakubwa kwa wadogo wakiwa wamemzunguka wanamwangalia kwa macho yao yakutisha. Stephan alivumilia lakini hakika roho yake ilikuwa tayari kutoka naye alijitahidi kuitoa ili awe mfu lakini hakuweza.
‘Majini?’
alijiwazia,
‘hapana Mashetani!’CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
alijikosoa tena mwenyewe, akikumbuka hadithi za zamani alizosoma huko kwao juu ya majini, mazimwi na Mashetani ila hapo hakujua haya yapo kundi gani, kila mara mwili wake ulimsisimka kwani yalikuwa yakikoroma tu na ndiyo hiyo ilikuwa lugha yao, alipogeuka huku na huku hakumuona Hellen, woga ulimjaa sana
‘watakuwa washamla hawa!’
alijiwazia moyoni, mara nyingi alijikuta akijiwazia moyoni mawazo ambayo hayakuwa na msaada wowote, katika mawazo hayo aliiona ile nyumba yake nzuri aliyoijenga kando ya mto lakini sasa aliona kuwa hatokuja kuingia tena, aliwakumbuka wazazi wake wale wazee ambao sasa wanaishi kwenye kituo cha kulelea wazee akaona kuwa nao watakufa bila kumuona kijana wao, aliwakumbuka wadogo zake ambao baadhi yao walimshauri asiende huko bara la giza lakini hakuwasikiliza sasa aliwaona kuwa walikuwa ni watu wa pekee sana, machozi yalimtiririka hasa alipomkumbuka Hellen, binti aliyempenda sana maishani mwake ijapokuwa alikuwa ni binamu yake. Stephen hakujua nini cha kufanya isipokuwa ni kusubiri hatima yake tu kwa viumbe hawa. Akiwa kajiinamia pale chini alipokuwa amekaa, mara akasikia vishindo vikubwa sana kutokea upande wa pili wa pale alipokaa aliponyanyua kichwa kuangalia ni nini kinatokea alishangaa kuona viumbe wale wakimgombania mwenzao kana kwamba walikuwa wakigombea nyama, Amata alishuhudia jinsi walivyomtafuna mwenzao bila huruma kabisa, Stephen akafumba macho ili asishuhudie unyama huo kabisa, alijiuliza kwa nini walimfanyia vile mwenzao hakupata jibu kamili kwa kuwa hakuelewa ile lugha yao ya mikoromo waliyoitoa vinywani mwao, alibaki kuwaangalia, alijikuta akijipapasa huku na huku lakini hakuona anachokitafuta. Mara akajikuta akili ikimrudia na kujiona pale alipo yuko peke yake, alipoyaangalia tena ya madudu akaona yako bize na kula nyama ya mwenzao huku yakikoroma sana na kutimua vumbi, vishindo vyao viliifanya ardhi yote pale kutetemeka kwa nguvu, Amata akapata wazo la kutoroka wakati huo wale viumbe wakiwa na shughuli ile lakini moyo mwingine ulimkataza kabisa kufanya jambo hilo. Aliangalia tena vizuri eneo lile alilopo, akajiuliza hata akitoroka atatorokea upande gani hakupata jibu, mara alijiwazia kuwa labda Hellen hayupo mbali na pale hivyo atamuacha. Mawazo yalimsumbua kichwa chake hata hakujua lipi akubaliane nalo na lipi aachane nalo. Mara ujasiri wa ajabu ukamjia
‘potelea mbali kwanza nafsi yangu mengine baadae...’
alijiwazia na kuanza kujiburuza taratibu kwa kutumia matako akirudi nyuma nyuma huku akiwaangalia viumbe wale wasije kumgundua, moyo ukiwa unamuenda mbio akijiwazia itakuwaje watakapomuona lakini aliendelea kujikokota kinyumenyume,
“Aaaaaaaaaaaaaa help!!!!!!! ”
Stephen alipiga ukelele uliofanya viumbe wale kushtuka na kuanza kumfuata huku wakikoroma kama kawaida yao. Baada ya kujisogeza kama mita kumi na tano hivi na kujikuta mikono yake ikitumbukia kwenye kitu kama shimo kwa kuwa alikuwa akisota kinyumenyume huku amekaa katika kichaka kile hakuona hatari yoyote nyuma yake, mikono yake ilitangulia na kufuatiwa na kichwa, mwili na miguu vikimalizikia. Lilikuwa ni korongo refu sana ambalo chini yake kulikuwa na mto mkubwa, Stephen alijiona akianguka kwa kasi na lakini kabla hajafika chini alijikuta akidakwa na mkono mkubwa wenye nguvu na kurudishwa juu kwa kasi ileile, alijikuta uso kwa uso na kiumbe hiki cha ajabu kilichoonesha hasira kwa kitendo chake kile cha kutaka kutoroka, Stephene alijawa na woga akajua kuwa sasa lazima atafunwe mzima mzima, kiumbe kile kilifungua domo lake baya lenye meno marefu na kutoa mkoromo mkali uliomfanya Stephene atetemeke kwa hofu na kutokwa na mkojo bila kujijua, akiwa bado kashikwa na kiumbe kile Stephen alitulia kimya kabisa akisali kwa ukimya sala yake ya mwisho pembeni aliviona vile viumbe vingine vyote vikiwa na sura ya hasira. Yule kiumbe alimtupa chini Stephen, wakati akianguka chini kitu fulani kilimtoka kutoka katika begi lake na kuruka kwa nje mmoja wa wale viumbe akakidaka kabla akijafika chini, ilikuwa ni camera ndogo ya dijitali ambayo muda wote ilikuwa mkobani mwake lakini kutokana na misukosuko yote hii alishasahau hata kama alikuwa na kitu kile mkobani, aliwaangalia wale viumbe wakiigeuzageuza ile camera. Stephen alisikia kishindo nyuma yake na alipogeuka alikuta kiumbe kingine kimeanguka chini, aligeuka haraka kuangalia upande ule wa mwanzo, akaona wale wengine walikuwa bado wanashikashika ile camera, mara akasikia kishindo kingine tena upande mwingine alipoangalia kiumbe kingine kimeanguka, Stephen alipigwa na bumbuwazi hakujua ni nini kinachoendelea mahali pale, moyoni akaanza kujipa moyo labda Hellen yuko eneo lile ndiye anayefanya kazi hiyo, lakini pia aligeuza tena mawazo yake akaona labda Amata kwa kuwa yeye ndio mpiga mishale hodari, akiwa katika kujiuliza yote hayo mara akaona mwanga wa flash ya camera ile ukifyatuka na yule kiumbe aliyeshika ile camera akaanguka kwa kishindo na camera ile ikimtoka mikononi na kuangukia miguuni mwa Stephen ambaye wakati huo alikuwa amekaa akiugulia maumivu ya mgongo. Aliiokota camera ile na kuishika mikononi mwake akiwa na woga mkubwa akaiweka jichoni kama anataka kufotoa picha, wale viumbe walio mbele yake wakatawanyika kwa woga, Stephen akatikisa kichwa kwa ishara kwamba amegundua kuwa mwanga wa flash unawaathiri ndio maana walikuwa wakianguka kila anayemulikwa moja kwa moja na mwanga huo. Stephen akajua sasa hii ndiyo njia ya kutorokea, lakini alijiuliza mwanga huu unawaathiri kiasi gani hakupata jibu!! Alijinyanyua kutoka pale alipo na kuanza kukimbia taratibu, viumbe wale wakaanza kumfuata akasimama na kugeuka akapiga flash moja kiumbe wa mbele akaaunguka na kuangukia mti, kutokana na kishindo kile mti ule ulikatika vipande vipande, Stephen aliendelea kukimbia na mara akaona upepo mkali ukimzunguka na kumnyanyua juu, Stephen hakujielewa kwani alizungushwa kwa kasi ya ajabu akiwa kachanganyika na majani na takataka nyingi, upepo ule ulimchukua kwa muda, akiwa juu aliweza kuona viumbe wale kwa uzuri kabisa, lakini mara aliona viumbe wale wakianza kurefuka kumfuata alipo, kiumbe mmoja alinyosha mkono na kumdaka kumshusha chini, Stephen alifikishwa chini kwa nguvu kiasi kwamba alitoa ukelele wa nguvu, viumbe wale wakaanza kumgombania, Stephan alijaribu kujitikisa kwa nguvu zake zote huku akipiga makelele ya woga, mara akaanguka chini na wale viumbe wote wakarudi nyuma, Stephene alibaki kaduwaa pale chini akiwaangalia viumbe wale wenye uchu wa nyama ya binadamu lakini hakuelewa kwanini viumbe hawa wamemuachia ghafla namna ile na wala hakuwaona kama wana dalili ya kumfuata tena isipokuwa ni mikoromo yao tu iliyozidi kuwa ya kutisha. Viumbe wale walirudi nyuma na kuanza kutawanyika kutoka eneo lile, Stephen akiwa pale chini hakuelewa sababu ya wale viumbe kukimbia ovyo alihisi kabisa kuna hatari eneo lile, lakini alijiuliza je kama hiyo hatari viumbe hawa wanaiogopa kwake itakuwaje! Alikosa jibu aliendelea kuwa pale chini na mara akaona nuru ya jua ikianza kufifia na kiza kikianza kufunika eneo lote lile, jua lilipatwa na mwezi mchana ule, Stephen alipogeuka huku na huku akajikuta yuko peke yake kabisa
“God is great!” alijisemea kimoyomoyo kuonesha shukrani yake kwa aliyemuumba, alijinyanyua taratibu kutoka pale huku akichechemea alikimbia kidogokidogo kueleke machakani na kutokomea asikokujua. Safari ilimuia ngumu Stephen, hakujua wapi anaelekea, kiu, njaa, uchovu vyote vilikuwa pamoja naye, alikimbia kwa nguvu zake zote lakini nguvu zilimuishia na kuanguka chini, alijaribu kutambaa haikusaidia, koo lilimkauka kiasi kwamba hata sauti haikuweza kutoka kwa wakati huo, alilala chini katika vichaka kwa utulivu bila kujitikisa akijua kuwa sasa hakuuawa na wale viumbe lakini kiu na njaa ndiyo vitavyomuangamiza, alijigeuza na kulala chali macho yake yakiangalia anga ambalo sasa halikuwa la buluu bali lililofifia kutokana na tukio lile la kupatwa kwa jua. Usingizi mzito ulimpitia kiasi hata hakujitambua, aliamka katika dunia nyingine kabisa ambayo ilimkutanisha na wenzake wote waliopoteana katika msitu ule
‘Msitu wa Solondo’CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
katika ndoto yake akaona rafiki zake wengi aliyowaacha huko Heidenburg University, aliwaona wanafunzi wake, mara aliyaona makaburi na majitu ya kutisha yakimsongasonga huku na huko, kiza kinene kiliyashinda macho angavu ya Stephen, maswali aliyojiuliza yalibaki bila jibu, nuru ikapotea, nguvu zikamuishia, pumzi zikamtoka kwa taabu, Stephen akalala usingizi mzito.
***************************************
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment