Simulizi : Queen Monica
Sehemu Ya Tano (5)
wewe tunapaswa tuongee.Ahsante kwa taarifa hizi njema na kuyang’arisha tena maisha yangu.I love you so much” Akasema Ernest na kumbusu Janet kisha
akatoka mle chumbani. “ Sikutegemea kabisa kama siku moja jambo hili litakuja kufika hapa.Sikutaka kumueleza Ernest lakini kwa hali ilivyo sikuwa na ujanja
ilikuwa lazima nimueleze ukweli kabla mambo hayajawa magumu kwani sina hakika kama suala hili litakuwa na mwisho mzuri.I’m so scared” akawaza Janet
baada ya Ernest kutoka mle chumbani. “ Ngoja niondoke hapa niwahi nyumbani leo jioni kuna kikao kati yetu na
Monica cha kumueleza kuhusiana na ombi la David Zumo la kutaka kumuoa.Naomba Monica akubali kwani inaweza ikaleta amani kidogo kwa Ben na kuupoza
upepo huu mbaya unaoanza kuvuma.Endapo akikataa basi mambo yanaweza kuwa magumu sana kwa upande wangu.” Akawaza Janet huku akivaa nguo zake na
yeye akaondoka “ Dah ! bado siamini maneno aliyonieleza Janet kuwa Monica ni mwanangu.Lakini Janet hawezi kusema uongo kwa jambo kubwa kama
hili.Lazima kweli Monica atakuwa ni mwanangu.Nilikwisha kata tamaa kabisa ya kumpata mrithi wangu lakini hatimaye nimempata.Nina furaha iliyopitiliza.”
Akawaza Ernest akiwa katika gari lake akirejea ikulu “ Hata hivyo kuna mambo ambayo natakiwa kuyafanya.Kwanza kabisa nataka nipate uhakika kuwa kweli
Monica ni mwanangu kwa kufanya kwa siri kipimo cha vinasaba.Jambo hili ni la muhimu na linatakiwa kufanywa kwa siri kubwa sana.Baada ya kupata uhakika
kama kweli Monica ni mwanangu kuna suala la pili kubwa ambalo limekuwa linaniumiza kichwa toka nilipolisikia ni hili la kwamba David Zumo anataka
kumuoa Monica.Hili ni jambo ambalo silikubali kabisa kwani japokuwa wote ni marais lakini sina maelewano mazuri na David Zumo kwa hiyo sitaki kabisa
mtu huyu amuoe mwanangu Monica.Nitafanya kila linalowezekana hadi jambo hili lishindikane.Kuhusu Ben huyu hawezi kuniumiza kichwa nitatafuta namna
ya kumdhibiti ” Akaendelea kuwaza Ernest Alifika ikulu akaoga na kubadili nguo kisha akamuita Mukasha mmoja wa wasaidizi wake anayemuamini sana . “
Mukasha kuna jambo ninataka unisaidie” “ Ndiyo mzee” akajibu Mukasha kwa adabu “ Nahitaji kumpata kijana moja mahiri sana katika mambo ya uchunguzi
ambaye ninaweza kumuamini na kumtumia katika kazi zangu binafsi za kiuchunguzi na ambaye ni mkweli na hatatoa siri za mambo nitakayomtuma.Unaweza
kunitafutia kijana huyo miongoni mwa vijana tulionao? Akauliza mheshimiwa rais Ernest Mkasa.Mzee Mukasha akainama akakuna kichwa kidogo akafikiri
halafu akasema “ Mheshimiwa rais sina hakika kama unaweza ukakubaliana nami kwa hili nitakalokwambia” akasema Mukasha “ Mukasa nieleze chochote
nitakusikiliza .” Akasema Ernest “ Mheshmiwa rais kuna jambo ambalo sina hakika kama unalifahamu na kama unalifahamu basi hauna taarifa za kutosha
kuhusiana nalo” “ Ni jambo gani hilo Mukasha? Nieleze usihofu tafadhali.Najua kuna mambo mengi ambayo siyafahamu na ninafichwa ila wewe kama mtu
wangu wa karibu kama kuna jambo unalifahamu naomba usinifiche tafadhali.Nieleze ukweli wote” “ Sawa mheshimiwa rais” akasema Mukasha na kukohoa
kidogo halafu akasema “ Mwaka mmoja kabla haujaingia madarakani raia saba wa Tanzania madereva wa malori yaliyobeba chakula kupeleka nchni Somalia
walitekwa nyara
na wanamgambo wa kikundi cha Alshabaab.Wanamgambo hao waliitaka serikali ya Tanzania itoe kiasi kikubwa cha fedha ili wawaachie watu hao lakini serikali
ya Tanzania haikuwa tayari.Walitoa muda ambao kama Tanzania ingeshindwa kulipa kiasi hicho cha fedha basi wangewaua madereva hao .Rais aliyekuwa
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
madarakani wakati huo hakuwa tayari kukubaliana na matakwa ya wanamgambo hao hivyo akaunda kikosi kidogo cha watu ambao aliwatuma kwenda
Mogadishu kuwakomboa madereva hao.” Akasema Mukasha “ Ninalifahamu jambo hilo” akasema rais “ Nakubali mheshimiwa rais hili ni jambo linalofahamika
na watu wengi lakini kuna jambo ambalo wengi hawalifahamu kuhusiana na kikos hicho cha wanajeshi ishirini na sita kutoka katika kikosi cha kupambana na
ugaidi kilichotumwa kwenda kuwarudisha nyumbani watanzania waliotekwa na Alshabaab.” “ Kulikuwa na jambo gani Mukasha? Akauliza Ernest “ Kulikuwa
na mtu mmoja kutoka idara ya ujasusi ambaye ndiye aliyewaongoza wanajeshi hao kufika mahala walipokuwa wamefichwa madereva hao waliotekwa.Kijana
huyo anaitwa Austin January lakini jina lake halijatajwa katika orodha ya watu waliokuwemo katika kikosi hicho.” “ Austin January? Akauliza Ernest “ Ndiyo
mzee.” Akajibu Mukasha na baada ya muda akaendelea “ Kikosi kile kilichotumwa kilifanikiwa kupambana na wanamgambo wa Alshabaab na kufanikiwa
kuwakomboa mateka na kuwarudisha nyumbani lakini Austin January hakurejea tena nyumbani.” “ Nini kilitokea? Alikufa? Akauliza Ernest “ Ilitolewa taarifa
fupi tu kwamba Austin alipotea katika mapambano na hawakujua aliko . Walihitimisha kwamba kuna uwezekano mkubwa atakuwa aliuawa.Lakini ukweli wa
jambo hili uko hivi,Austin hakufa kama ilivyodaiwa bali wakati wakiendelea na mapambano dhidi ya wanamgambo alipigwa risasi na mmoja wa wanajeshi wa
Tanzania makusudi kabisa kwa lengo la kumuua na akatelekezwa hapo akiwa hana fahamu.Alipopata fahamu alijikuta akiwa katika kambi ya wanamgambo wa
Alshabaab ambao walimtibu na alipopona walihitaji kulipwa fedha nyingi sana ili wamuachie.Austin alifahamu kabisa kwamba alipigwa risasi makusudi hivyo
hakutaka tena msaada wowote kutoka serikali ya Tanzania .Aliyemsaidia kumkomboa kutoka kwa mikono ya Alshabaab kwa kulipa fedha nyingi sana ni baba wa
mchumba wake mfanya biashara tajiri ambaye alilipa kiasi cha fedha kilichokuwa kinahitajika na Austin akawa huru.Hakurejea tena Tanzania na kwa sasa anaishi
nchini Afrika kusini ambako ameachana kabisa na mambo mengine yote na anafanya kazi ya kusimamia miradi ya baba mkwe wake.Ana maisha mazuri hivi sasa
na anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni na mpenzi wake Marie.” “ Oh my God !! Umezipata wapi taarifa hizi? Akauliza Ernest “ Nina ukaribu na huyo tajiri
ambaye alimsaidia Austin kutoka mikononi mwa
Alshabaab.Sababu ya kutaka kuuawa mpaka leo hakuna anayeifahamu imebaki ni siri yake Austin lakini kuna hisia kwamba kuna watu ndani ya serikali ambao
walitaka kumuua kwani inaonekana kuna suala ambalo aliligundua linalowahusisha watu wakubwa serikalini na ndiyo maana akatakiwa kuuawa .Ni kijana
mtiifu sana ,anayejituma na asiyependa kupindisha ukweli.Kama kweli unahitaji kijana mwaminifu ambaye unaweza kumtuma kufanya kazi zako binafsi basi
ninakushauri kumtafuta Austin.Tunao vijana wengi wazuri hapa katika idara yetu ya usalama wa taifa ambao wanaweza wakafanya kazi vizuri lakini hakuna
kama Austin.” Akasema Mukasha .Ukimya ukatanda mle chumbani baada ya muda Ernest akasimama akaenda kuegemea kabati la vitabu akazama mawazoni na
baada ya muda akasema “ Kwa maelezo haya mafupi uliyonipa nimepata picha ya haraka haraka kwamba Austin ni mtu sahihi ninayemtaka lakini ugumu unakuja
namna ya kumpata.” “ Mheshimiwa rais ili uweze kumpata Austin itakubidi kwanza uzungumze na baba mkwe wake.Ni mtu wangu wa karibu nitamtafuta ili
uweze kuzungumza naye” “ Jitahidi ili niweze kuzungumza naye jioni ya leo nijaribu kumshawishi kama anaweza kukubali kumruhusu Austin aje kunifanyia
kazi hata kama ni kwa muda mfupi na niko tayari kumlipa kiasi chochote cha fedha atakachohitaji” akasema Ernest “ Mheshimiwa rais naomba nikuweke wazi tu
kuwa suala hili haliwezi kuwa rahisi kwani kwa sasa Austin ameachana kabisa na mambo haya ya ujasusi na anajishughulisha na biashara.Sina hakika kama
atakubali ombi lako” akasema Mukasha “ Nitaongea vizuri na baba mkwe wake na nina hakika yeye akimwambia jambo hawezi akapinga.Nitatumia kila aina ya
ushawishi hadi Austin akubali kuna kufanya kazi yangu.” Akasema Ernest.
Ilikuwa ni siku ndefu sana kwa Monica.Alizunguka sehemu mbali mbali na Daniel akiwa na lengo la kutuliza kichwa chake kutokana na mambo mengi
yaliyokuwa yanamsumbua na kubwa likiwa ni suala la Dr Marcelo. Saa kumi na mbili za jioni baada ya kutoka hospitali kumuona Dr Marcelo alirejea nyumbani
kwao ambako alikuwa na maongezi na wazazi wake usiku huo.Aliekea moja kwa moja chumbani kwake akaoga na kujiweka tayari kwa ajili ya kukutana na
wazazi wake. “ Siku imekuwa ndefu sana,namshukuru Daniel kwa kujitolea kuungana nami siku ya leo na siku yangu imekwenda vizuri.Nashukuru vile vile Dr
Marcelo naye anaendelea vizuri japokuwa mpaka sasa hajaweza kuzungumza lakini hali yake inatia matumaini .Namuombea Mungu aweze kupona na wale wote
waliofanya kitendo kile cha kinyama wakamatwe na kufikishwa mbele ya sheria lakini hata hivyo bado kuna maswali mengi ambayo ningependa kumuuliza Dr
Marcelo pindi atakapoanza kuongea.Kuna mambo ambayo nahitaji kuyafahamu kutoka kwake” akawaza Monica akainuka na kutoka chumbani kwake akaelekea
sebuleni kwa wazazi wake. “ Monica,karibu sana..” akasema mzee Benedict aliyekuwa amekaa sebuleni akisoma gazeti “ Ahsante baba,umeshindaje leo?
Akauliza “ Nimeshinda salama Monica.Vipi rafiki yako anaendeleaje? Akauliza mzee Benedict “ Anaendelea vizuri.Hali yake ni tofauti na jana japokuwa bado
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
hajaanza kuzungumza lakini madakatari wametuhakikisia kwamba atapona na atarejea katika hali yake ya kawaida” akasema Monica “ Mungu atamsaidia
atapona” akasema mzee Benedict “ Where is mother? “ Bado hajarudi si unajua mama yako huwa ana shughuli nyingi “ akasema mzee Ben na mara simu yake
ikaita .Akatazama mpigaji halafu akainuka akasogea pembeni akaipokea “ hallow Gordon” akasema mzee Benedict “ Mzee nimekupigia kukupa majibu ya ile
kazi uliyonituma” akasema mtu wa upande wa pili ambaye mzee benedict alimuita kwa jina la Gordon. “ Good..Tel me the good news.....” akasema mzee
Benedict na kulazimika kugeuka baada ya kusikia sauti ya mke wake akisalimiana na Monica baada ya kurejea. “ Mzee nimemfuatilia mama kama
ulivyonielekeza .Kwanza alikwenda ofisini kwake halafu akatoka akaelekea saluni akatumia kama dakika arobaini na tano kisha akaondoka na kuelekea katika
duka la vipodozi .Alipotoka hapo akaelekea katika kiwanda cha nguo ,ambako alitumia kama nusu saa hivi halafu akatoka na kuelekea White Rhino hotel.Pale
aliingia katika ofisi ya meneja wa hoteli akatumia kama dakika kumi halafu akatoka na kuelekea katika presidential suit namba tano akaingia mle na baadae rais
aliwasili na akaelekea pia katika chumba kile kile alichokuwamo mama Janet.Walikaa mle kwa muda wa zaidi ya nusu saa na kisha rais akatoka.Baada ya dakika
kumi toka rais atoke mama Janet naye akatoka akaelekea ofisini kwake ambako amekaa hadi jioni hii na akatoka hakupita tena sehemu nyingine yoyote akarejea
moja kwa moja nyumbani .Nimemuona akiingia ndani ndipo nilipoamua kukupigia na kukujlisha kuhusu mizunguko yote ya mama Janet
kwa siku ya leo” akasema Gordon.Mzee Benedict akavuta pumzi ndefu na kusema “ Gordon ahsante sana .Umefanya kazi nzuri .Naomba uendelee kumfuatilia
kwa wiki mbili zaidi na kila siku nataka unipe majibu “ akasema mzee Benedict na kukata simu akageuka akamtazama mke wake aliyekuwa ameketi sofani
akiongea na Monica “ I knew it.Nilijua tu kwamba lazima watakuwa wanakutana.Na leo nina hakika walikutana kujadiliana kuhusiana na suala hili la
Monica.Sasa nimeanza kupata picha kumbe siku hizi zote Janet amekuwa akinizunguka.Amekuwa na mahusiano ya siri na Ernest mkasa.I swear I’m going to
destroy them both lakini kabla ya kufanya chochote natakiwa kwanza kukusanya ushahidi wa kutosha .Ngoja niendelee kumchunguza Jane kwa wiki mbili zaidi
ninaamini kuna mambo mengine mengi ambayo ninaweza kuyafahamu .” akawaza Benedict na kurejea sebuleni .Baada ya kuoga Janet akaungana na mumewe na
Monica wakapata chakula kisha wakaenda kuketi barazani kwa ajili ya maongezi. “ Monica najua umechoka sana kwa mizunguko ya siku kwa hiyo naomba
nisichukue muda wako mwingi nataka niende moja kwa moja katika lile ambalo tumekuitia jioni ya leo.” Akaanzisha mazungumzo mzee Benedict “ Kwanza
kabisa napenda kukushukuru kwa kutukutanisha na mtu mkubwa sana afrika na duniani rais David Zumo.Ni mtu mzuri na ana moyo wa kusaidia.Jana
nimeongea naye mambo mengi sana na ameniahidi mambo mengi makubwa na mojawapo ikiwa kuniinua hadi kufikia kiwango cha kuweza kuingia katika kikao
cha mabilionea mia moja wa dunia .Hili si jambo dogo lakini kwa David Zumo linawezekana na ameahidi kuhakikisha linafanikiwa.” Akasema Benedict “ That’s
good news.David ni mtu mwenye moyo wa ajabu sana.Anaonekana kuvutiwa mno na familia yetu.Tuna bahati sana ya kuwa na ukaribu wa ghafla wa mtu kama
huyu.Baba hii ni fursa ambayo hutakiwi kuiacha.Itumie vyema” akasema Monica “ Usemalo ni la kweli Monica familia yetu imekuwa na bahati sana kwa kuwa
na ukaribu na David Zumo. Ni fursa ambao tunatakiwa kuitumia kwani kuwa na ukaribu na mtu mkubwa kama huyu si suala dogo” akasema mzee Benedict
halafu ukapita ukimya mfupi “ Monica kama nilivyokueleza kuwa jana nimeongea mambo mengi na David Zumo lakini miongoni mwa mengi tuliyoongea kuna
jambo kubwa “ akasema Ben na kunyamaza kidogo kisha akaendelea “ David Zumo amevutiwa sana nawe.Amekiri kwamba hajawahi kuona mwanamke
aliyemgusa mtima wake kama wewe hivyo ameamua kuweka wazi hisia zake kuwa anakupenda sana na anataka kukuoa” “ Baba !! akasema Monica kwa
mshangao na kusimama.Ni wazi alistushwa sana na kauli ile toka kwa baba yake “ Monica najua umestushwa sana na kauli hii lakini .....” “ Hakuna lakini..how
could you do this to me father? Akauliza Monica
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ Monica tafadhali naomba unisikilize “ akasema bi Janet akainuka na kumshika mkono Monica akamketisha chini. “ Monica najua kauli hii
aliyoisema baba yako imekustua sana kwani si taratibu zetu sisi watanzania jambo kama hili kutamkwa namna hii.Masuala kama haya ya mtu kumpenda Fulani
na kufikiria hata kumuoa hayajazoeleka kupitia kwa wazazi bali muhusika mwenyewe kama amemuona binti akampenda humfuata akaongea naye wakakubaliana
wakaanzisha urafiki na baadae taratibu za uchumba huanza na mwisho huwa ni ndoa na hizo ndizo taratibu zetu tulizozizoea” “ Exactly..Hata mimi ninafahamu
hivyo.Hata kama David Zumo anadai kwamba ananipenda alipaswa kuongea nami moja kwa moja na si kwa kuwatumia ninyi kwani mwenye maamuzi ya
mwisho kama nikubali au nikatae ni mimi.!! Akasema Monica kwa sauti ya juu kidogo.Ben na mkewe wakabaki kimya wakimtazama.Baada ya sekunde kadhaa
za ukimya Monica akasema “ I’m sorry,sikupaswa kupandisha sauti namna ile ni kutokana na mstuko nilioupata.” Akasema Monica “ Monica utatusamehe sana
kwa jambo hili lakini anachokisema baba yako ni kukufikishia tu maneno aliyoyatamka David zumo ambayo sisi baada ya kuyatafakari tumeona ni jambo zuri
tu.Kwa kifupi ni kwamba David Zumo hajaamua kutumia zile njia zetu za kawaida labda kwa ugeni na kutokufahamu taratibu zetu lakini bado hakijaharibika
kitu kwa kuamua kutueleza sisi kile kilichopo moyoni mwake.Ametuweka wazi kwamba anakupenda,na lengo lake kubwa ni kutaka kukuoa.Kwa muda mrefu
sasa tumekuwa tunasubiri siku utakayotuambia kwamba tayari umepata mchumba kwani umri unazidi kwenda na hatujapewa taarifa zozote lakini baada ya
David Zumo kujitokeza tumeona ni mpango wa Mungu kwani mwanaume mwenye vigezo ambayo wote tunavihitaji.Monica mwanangu David Zumo ni
mwanaume ambaye kila mwanamke anaota kuwa naye.Japokuwa hatumfahamu undani wake lakini ni mtu ambaye ukikaa naye dakika chache unamfahamu ni
mtu wa namna gani.Ni mpole,mnyenyekevu,si mtu mwenye kujikweza licha ya utajiri alionao,ni mpenda watu ana moyo wa kusaidia na sifa nyingine kede kede.
Sisi kwa upande wetu tumeona huyu ni mtu ambaye anakufaa sana Monica.Vil......” Monica hakumpa nafasi mama yake aendelee akaingilia kati “ Mama tafadhali
naomba usiendelee zaidi nimekwisha kusikia na kukuelewa.Nimelisikia ombi la David Zumo .Ninamfahamu David na japokuwa nimefahamiana naye kwa siku
mbili tu naweza kusema he’s a good man .Pamoja na hayo siwezi kutamka chochote kwa usiku huu kwamba ombi lake nimelipokea ama vipi .Mimi pia nina
mipango ya maisha yangu kwa hiyo nipeni nafasi ya kutosha kuweza kulitafakari jambo hili kwa kina kabla sijatamka chochote. “ akasema Monica “ Lakini
Monica hakuna ubaya kama tukilijadili suala hili kwa pamoja kwa sababu ni suala lenye manufaa kwetu
sote.Sisi kama wazazi siku zote ni jukumu letu kuona mwanetu unampata mwanaume bora ambaye unaweza ukaishi naye bila matatizo na si bora mwanaume na
ndiyo maana baada ya David Zumo kutoa yake ya moyoni tumeona ni mtu ambaye anakufaa na anaifaa familia yetu.” Akasema mzee Ben “ Kwa kuongezea hilo
alilolisema baba yako,endapo utachagua kuolewa na David Zumo utaingia katika ulimwengu mwingine kabisa ulimwengu wa mabilionea.Utajiri wote wa David
Zumo utaumiliki wewe pale utakapomzalia mtoto ambaye atakuwa mrithi wa mali zake .Monica hii ni fursa kubwa imejitokeza katika maisha yako ambayo
hutakiwi kuiacha.Mungu amekufungulia milango ya Baraka zake kwa hiyo unatakiwa uzitumie vyema fursa zote unazoletewa.” Akasema bi Janet “ Monica
usisahau vile vile” akasema Ben “ wewe ni mtu ambaye umejitolea kuihudumia jamii na una mipango mingi kama huu wa kujenga shule ya watoto
walemavu,nafahamu una mpango pia wa kujenga vituo vya kulelea wazee wasiojiweza katika kila mkoa na mambo mengine mengi lakini yote haya yanahitaji
fedha nyingi ambazo upatikanaji wake unaweza kuchukua miaka mingi na pengine malengo yako yasifanikiwe.Lakini utakapochagua kuolewa na David Zumo
kila kitu ambacho umekuwa unakiota kukifanya kitafanikiwa kwa sababu kile ni kisima cha fedha.Utajenga mashule,vituo vya wazee na kila
unachokihitaji.Utajulikana dunia nzima na utasaidia si Tanzania tu bali hata jamii nyingine zenye uhitaji duniani.Monica hii ni fursa ambayo unatakiwa uitumie”
akasema mzee Ben .Monica akawatazama na kusema “ Wazee wangu nimewasikia na kuwaelewa yale yote mliyoniamba lakini naona wote mmeegemea katika
suala moja tu la utajiri wa David Zumo.Kila mnapoongea hamuachi kutaja utajiri na fedha za David.Kama nikiamua kuolewa na David si kwa sababu ya fedha
bali moyo wangu umenituma hivyo kwa hiyo hakuna haja ya kujaribu kunishawishi kwa kutumia kigezo cha fedha.Ni watu wangapi ambao wamekimbilia
kuolewa na watu matajiri kwa kufuata pesa na mali lakini wameishia kulia kila uchao? Hata ulalie godoro la fedha lakini kama hampendani kwa dhati ya mioyo
yenu itakuwa kazi bure kwani katu hamtakuwa na furaha katika maisha yenu.Kwa hiyo wazee wangu mimi nimewasikia na kama nilivyosema naombeni mnipe
muda wa kulitafakari hili suala na nitawapa jibu kwamba nimekubali ama vipi” akasema Monica “ Usijali Monica jipe muda ulitafakari jambo hili kwa undani
na uchambue faida zake na hasara kama zipo halafu utatupa jibu lakini sisi kama wazazi hatuna tatizo lolote na jambo hili tumelipa Baraka zetu kwani lina faida
kwetu na kwako pia kwa hiyo kila kitu tunakuachia wewe.” Akasema mzee Benedict kisha akainuka akaelekea chumbani kwake na kuwaacha Monica na mama
yake “ Mama what you are trying to do is unfair..Kwa nini lakini mnataka kufanya kitu kama hiki? Kwa nini mmekubaliana na mtu bila kwanza kukaa na mmi
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
mkanisikia na mimi nina mawazo na
mipango ipi? Kwa mara ya kwanza napenda kuwaambia kwamba hamjanitendea haki.Haya ni maisha yangu na mimi ndiye ninayechagua nani niwe naye nani
atanifaa na siangalii kama ni tajiri au masikini bali ninachoangalia mimi ni mapenzi ya kweli.Ninyi mmeangalia upande mmoja tu wa utajiri na ndiyo maana
mmekubali kirahisi ombi la David na japokuwa hamjanieleza nina hakika lazima mtakuwa mmemuhakikishia David kwamba jambo hili linawezekana na
mumempa matumaini makubwa kwamba ombi lake lazima litakubaliwa.Kwa nini mmenifunga mikono namna hii? Kweli mama hamjanitendea haki” akasema
Monica na kuinama chini “ Monica naomba usikwazike mwanangu kwa jambo hili.Sisi hatujaamua kitu chochote bali tumekufikishia ujumbe tu na mwamuzi
wa yote ni wewe.Sisi hatuna maamuzi yoyote juu ya maisha yako lakini pale tunapoona tunahitaji kutoa ushauri wetu basi kama wazazi lazima tufanye
hivyo.Kwa hiyo Monica usihuzunike na kudhani labda sisi tunakupangia maisha yako lakini wewe ndiye mwenye uamuzi wa mwisho kuhusu hatima ya maisha
yako” akasema Janet “ Lakini mama kwa namna jambo hili mlivyoliweka ni wazi kwamba tayari mmekwisha amua kwamba niolewe na David Zumo.Mmeweka
msisitizo mkubwa sana kwa jambo hili kwa sababu amewaahidi kuwasaidia kiuchumi na kuwa matajiri wakubwa duniani.Thats not fair at all” akasema Monica “
Monica sisi kama wazazi siku zote huwa tunahitaji wanetu waishi maisha mazuri na ndiyo maana hatulali ili kuhakikisha tunawajengea watoto maisha yaliyo
bora na yenye furaha.Sisi hatujakulazimisha kuolewa na David Zumo lakini kwa mtazamo wetu tumeona David Zumo ni mtu ambaye anaweza akakufaa sana
kutokana na sifa alizonazo.Miaka inazidi kwenda Monica na hadi sasa bado hujatuletea mchumba unataka kuolewa lini mwanangu? Unataka ufunge ndoa wakati
sisi tumekwisha fariki? Huu ni wakati wako mzuri sana wa kuingia katika maisha ya ndoa na kwa kuwa amejitokeza mwanaume ambaye sisi tunaona anakufaa
basi usiiache nafasi hii.Kila mwanamke katika hii dunia anaota kuolewa na mwanaume bora mwenye uwezo anayeweza kumtunza na kwako ametokea
mwanaume wa aina hiyo ambaye ni tajiri mkubwa wa afrika kwa nini basi umuache? Mimi kama mama yako nakushauri Monica kama bado huna mchumba hadi
sasa basi David anakufaa sana.Hata kama unahisi humpendi kwa sasa lakini ukiwa naye utajifunza kumpenda na utafurahia kuwa naye.Achana na hayo mambo ya
moyo ambayo yamekuwa yakitamkwa kila siku kwamba sijui moyo umependa ni uongo mtupu zama zimebadilika na siku hizi wengi wanaangalia sana kutimiza
ndoto zao na mengine yote yatakuja huko huko mbele ya safari.” Akasema Janet.Monica akainama akaonekana kujawa na mawazo mengi .Akainua kichwa na
kusema “ Mama sijawahi hata mara moja katika maisha yangu kuhisi kwamba hamnitendei haki lakini kwa hili mlilonifanyia ni wazi hamjanitendea haki
kabisa.Mnataka niolewe na mtu ambaye licha ya kwamba ana pesa lakini tayari ana
ndoa yake !! “ akasema Monica na kuinamisha kichwa “ Monica hili lisikuogopeshe ,David ana mke ndiyo lakini mpaka leo hii mke wake hajaweza kumzalia
mtoto.Hawezi kushika mimba.Hii ni nafasi yako sasa ya kuumiliki utajiri wa David kwa kumzalia mtoto ambaye atakuwa mrithi wa mali zake.Monica mimi ni
mwanamke na kama nafasi hii ningeipata enzi za usichana wangu katu nisingekubali iniponyoke.Ninakwambia hivyo kama mama yako kwa sababu ninapenda
maisha yako yawe mazuri.Lakini hata hivyo wewe ndiye muamuzi wa maisha yako.Utaamua mwenyewe unataka kuishi maisha ya namna gani.Ila nakushauri
Monica fikiria na fanya maamuzi yenye kufaa” akasema bi Janet akaagana na Monica na kila mmoja akaelekea chumbani kwake. “ Umejaribu kumshawishi?
Akauliza Benedict “ Uphhh..nimejitahidi sana kumshawishi na kumueleza kuhusu faida zitakazopatikana endapo atakubali kuolewa na David Zumo.Anaonekana
ana msimamo lakini kwa sasa bado amestushwa na suala hili hakuwa amelitegemea ninaamini atakapokaa akatulia akatafakari anaweza akafanya maamuzi
mazuri.Nimejitahidi sana kumpa somo na kama akipuuzia shauri zake.Nafasi kama hizi huwa hazitoke mara mbili.Wanawake wengi wanaota kupata bahati kama
hii na hawaipati yeye kaipata na anaweka misimamo yake kama mwanasiasa.” Akasema Janet “ Amechukua tabia yako ya kuwa na msimamo usioyumba
.Nakumbuka misuko suko iliyokupata wakati ule ulipopata mimba ukiwa bado shuleni na kila mtu akakutaka ukaitoe.Familia yako wakakutaka uchague shule
au mapenzi na ukachagua mapenzi.Hukuyumba na wala hukupepesa macho kuchagua kuwa na mimi na tabia hii ndiyo anayo Monica.” Akasema Benedict “ Oh
Ben bado unazikumbuka nyakati zile.Katu siwezi kusahau namna familia yangu ilivyosimama na kunitaka nikaitoe mimba ya Nathan.Kwa wakati ule sikuwa na
kitu chochote nilichokuwa ninakifikiria katika akili yangu zaidi yako.Ulikuwa umenikaa katika kila mshipa wa mwili wangu.I was madly in love with you,my
first love” akasema Janet na wote wakacheka. “ Kwa kweli ule ulikuwa ni mfano wa penzi la kweli.Hukusita kunichagua kijana masikini kama mimi ambaye
kwa ule sikuwa na mbele wala nyuma .Nililazimika kukatisha masomo ili niweze kutafuta kibarua cha kuweza kukutunza wewe na mtoto.Lazima nikiri kwamba
sijawahi kuwa na wakati mgumu kama ule lakini kila niliporejea nyumbani ulikuwa na tabasamu usoni na ulikuwa ndiye mfariji wangu mkubwa.Pamoja
kwamba hatukuwa na fedha ,tulikuwa na maisha ya taabu but we were happy.Tuliishi maisha ya furaha hadi pale tulipokutana na Ernest.” Akanyamaza na
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kutazama chini.Wote wakabaki kimya “ He changed our happy life.He changed us.He took our love away.He turned us to monsters” akasema Benedict kwa sauti
ya unyonge “ Please Ben don’t say that.You are hurting me “ akasema Janet “ It’s not me hurting you it’s the truth” akasema Ben “ Baada ya kuanza kupata fedha
maisha yetu yalibadilika.Kila kitu kikabadilika.” Akasema Ernest “ Si kweli Ben,mambo yalibadilika kiuchumi lakini mapenzi yetu hayakubadilika.Ni kweli
tulipitia vikwazo kadhaa katika kuelekea maisha mazuri na kuna nyakati tulitetereka lakini bado tumesimama pamoja hadi leo.I loved you Ben and I will always
love you” akasema Janet “ Are you sure that you still love me? Akauliza benedict “ yes I do” akajibu Janet “ Ben tusihukumiane kwa mambo yaliyopita ndiyo
maana nikasema kwamba kuna nyakati tulitetereka .Sote tulifanya makosa,tusameheane na tuangalie yaliyoko mbele yetu.NInakupenda sana” akasema Janet na
kumbusu Ben “ What a liar.Unadhani sifahamu mambo unayoyafanya ? Laiti ningegundua mapema namna ulivyo katu nisingekubali kujiingiza katika mapenzi na
wewe nyoka mkubwa we” akawaza Ben
onica aliingia chumbani kwake na kuketi sofani .Alihisi kichwa kizito kutokana na kujawa na mawazo mengi.Jambo aliloelezwa na wazazi wake usiku ule
lilimchanganya mno akili yake “ Sikutegemea kabisa kusikia hiki nilichokisikia usiku wa leo toka kwa wazazi eti Davi Zumo anataka kunioa” akawaza halafu
akavua viatu na kujilaza sofani “ David Zumo ni mtu mkubwa,ni rais mwenye nguvu na tajiri namba moja Afrika.Kusema kwamba amenipenda na anataka
kunioa si kitu kidogo.Hili ni jambo kubwa kwake,kwangu na kwa nchi zetu pia.Ninatakiwa kutafakari kwa makini sana kuhusu suala hili na kuchukua maamuzi
yenye kufaa.Oh m y gosh ! kichwa changu nahisi kimejaa na kinashindwa kufikiri sawa sawa” akainuka akabadili mavazi akatoka na kuelekea katika bwawa la
kuogelea akajitumbukiza majini akaanza kuogelea.Mara nyingi awapo na jambo kubwa linalomsumbua kichwa chake hupenda sana kuogelea.Wakati akiogelea
bado kichwa chake kiliendelea kujaa mawazo kuhusiana na David Zumo. “ Nilijiuliza sana sababu ya David Zumo kutoa msaada ule mkubwa kumbe alikuwa na
lengo lake na msaada ule alionipa ni moja kati ya njia za kutaka kufanikisha lengo lake la kuanzisha mahusiano na mimi.Amenifahamu kwa muda gani hadi
afikie hatua ya kufanya maamuzi ya kutaka kunioa? Nia yake ya kutaka kunioa inatoka moyoni au amevutiwa tu na uzuri wangu? Ninahisi yawezekana akawa
amevutiwa na uzuri wangu na hasa baada ya kutangazwa mrembo zaidi Afrika na anataka kutumia jina na utajiri wake kunipata.Endapo angekuwa na nia ya dhati
kwangu angeweza kuieleza mimi mwenyewe wazi wazi lakini hakufanya hivyo na badala yake akawaeleza wazazi ili wao wanishawishi mimi nikubali kuolewa
naye.Thats an old style.Wazazi nao kwa tamaa ya utajiri walioahidiwa wanajitahidi kufanya kila wawezalo kunishawishi nikubali kuolewa na David.Sijawahi
kubishana nao hata mara moja na wanaitumia fursa hiyo kunishawishi.I’m confused and I don’t know what to do” akawaza na kuzama chini halafu akaibuka “
Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nitatofautiana na wazazi.Sintakubaliana nao kwa hiki wanachotaka nikifanye” akawaza na kuzama tena chini ,akaibuka
“ Simfahamu David Zumo kiundani,sizifahamu tabia zake,sifahamu ananipenda kiasi gani.Ninafahamu kitu kimoja tu kuhusu David kwamba ni tajiri namba
moja Afrika.Zaidi ya hilo sifahamu chochote kuhusu yeye na siwezi kukubali au kufurahia kuolewa na bilionea huyu ambaye bado simfahamu vyema.”
Akaendelea kupiga mbizi kuzunguka bwawa. “ Suala la ndoa si suala rahisi kama wao wanavyolichukulia.Ni jambo linalohusu moyo zaidi kuliko mali .Kama
isingekuwa matatizo yaliyomtokea Dr Marcelo ,ni mwanaume ambaye tayari nilikwisha aanza kuvutiwa naye .Ana sifa nyingi kati ya zile ninazozihitaji kwa
mwanaume wa maisha yangu,lakini naye kama ilivyo kwa David Zumo bado simfahamu vyema na kuna mambo mengi ambayo nahitaji kuyafahamu kuhusu yeye
lakini kwa sasa its already late.kwa mambo yaliyotokea mimi na yeye tutaendelea kuwa marafiki wa kawaida tu.Namuomhea aweze kupona na aendelee
na maisha yake” Monica akatoka ndani ya maji akaelekea chumbani kwake “ Ni lini basi nitampata mwanaume wa ndoto zangu ambaye hatakuwa na kasoro?
Kila mwanaume ninayempata na kudhani labda anaweza kunifaa nagundua ana kasoro Fulani.Lakini sichoki kusubiri ,ninaamini siku moja nitampata tu
mwanaume aliyeumbwa kwa ajili yangu .Nitaendelea kumuomba Mungu ili iwe mapema zaidi kwani jambo hili linaniumiza sana moyo wangu.Nadhani ni muda
muafaka sasa wa kuwa na mume ,kuwa na familia .Sitaki kupata watoto wakati nikiwa na umri mkubwa.” Akawaza akiwa amejilaza kitandani na mara sura ya
David ikamjia akatabasamu “ David Zumo “ akasema kwa sauti ndogo halafu akainuka na kwenda kuketi sofani “ Kwa muda mfupi niliokutana naye kuna vitu
kadhaa nimevigundua kwake.Ana sura nzuri,anaonekana anajali na mwenye moyo wa kusaidia japokuwa naamini msaada ule mkubwa alionisaidia ulikuwa kwa
ajili ya kujenga ukaribu kati yangu na yeye lakini anaonekana ana roho nzuri.” Akainuka na kurejea kitandani “ Kama ningekuwa tayari ninamfahamu
vizuri,naona David angeweza kunifaa sana lakini tatizo bado simfahamu vyema halafu moyo wangu unakuwa mzito kumkubali japokuwa naamini kuna faida
nyingi ambazo naweza kuzipata kama nikikubal kuolewa naye.Faida kubwa hasa ni kiuchumi.Nikiwa na David nitaweza kutekeleza miradi yangu mingi
ninayokusudia kuianzisha hapa nchini hususan ule mradi wa kujenga kambi za wazee kila mkoa kila wilaya.David ni mtu mwenye pesa na anaweza akanisaidia
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
hilo likawezekana na taasisi yangu inaweza kujulikana duniani kote na kupata wafadhili wengi.Jina langu litakuwa kubwa na kujulikana duniani kote” Ghafla
Monica akastuka kama aliyekuwa usingizini.” “ Oh my gosh !! sijui kwa nini ninawaza mambo kama haya ambayo ni wazi hayawezekani.Siwezi kuolewa na
David Zumo hata kama ni rais na tajiri namba moja Afrika.Nitaolewa na mtu ambaye moyo wangu utamridhia na si mtu kwa sababu ya utajiri wake.Bado ninayo
imani kwa mungu kwamba ataniletea mwanaume Yule ambaye amemuandaa kwa ajili yangu.” Akawaza Monica na mara akajiwa na wazo “ Lakini mbona
inaonekana kama suala hili nimelifanyia maamuzi ya haraka sana? Akajiuliza “ Ni kweli jambo hili nimelitolea maamuzi ya haraka sana .Kuna ubaya gani endapo
nitalipa walau muda kidogo? Mimi nadhani hili ni wazo zuri,nilipe nafasi jambo hili nilitafakari kwanza kabla ya kutoa maamuzi ya haraka haraka.Hakuna ubaya
wowote endapo nitaamua kujipa muda katika suala hili na papo hapo nitakuwa nikimsoma David Zumo ni mtu wa namna gani na pengine ninaweza nikajikuta
nikibadili mawazo” akawaza “ Kama nikiamua kulipa nafasi suala hili basi itanilazimu kujenga ukaribu na David .Oh my gosh ! I’m so scared”...akatazama juu
kwa sekunde kadhaa na kuendelea kutafakari “ Kuna sauti inaniambia kwamba nisiogope,niwe jasiri.Ngoja niisikie sauti
hiyo na nilikabili suala hili .Yawezekana ikawa ni bahati yangu na ninaipiga teke.” Akawaza Monica na kuanza kuutafuta usingizi *******************
Imekwisha timu saa tano za usiku ,bado rais wa Tanzania Ernest Mkasa alikuwa ofisini kwake akiwa na mkurugenzi wa habari wa ikulu wakijadiliana masuala
kadhaa,mara mlango ukafunguliwa akaingia mzee Mukasha.Rais alipomuona Mukasha akamuomba mkurugenzi wa habari waonane asubuhi wamalizie
maongezi yao akamkaribisha Mukasha. “ karibu Mukasha “ akasema Rais .Mukasha akaeti sofani “ Mheshimiwa rais nimefanikiwa kumpata Mr Boaz” akasema
Mukasha “ That’s good news.Umezungumza naye chochote? “ Hapana mheshimiwa rais,sijaongea naye chochote ila nimemueleza kwamba wewe ndiye
unayetaka kuzungumza naye.Kwa sasa yuko katika biashara zake Comoro na ameniomba nimpigie baada ya dakika kumi na toka tulipoongea simuni hadi sasa
tayari muda huo umekwisha pita.Ngoja nimpigie” akasema Mzee Mukasha na kuzitafuta namba za bilionea Boaz akampigia.Simu ikaita na baada ya muda
ikapokelewa “ hallow Mr Boaz,Mukasha ninaongea ,niko na rais hapa.Tayari una muda mzuri wa kuzungumza naye? “ Ndiyo Mr Mukasha.Nipe nizungumze
naye” akasema Boaz na Mukasha “ Habari yako Mr Boaz” akasema Ernest “ Habari yako mheshimiwa rais?Pole sana na majukumu mazito ya kuongoza nchi”
akasema Boaz “ Ahsante sana Mr Boaz.Natumai hii ni mara yetu ya kwanza kuzungumza.” “ Ndiyo mheshimiwa rais.” “ Nafurahi kukufahamu Mr Boaz,naamini
huu utakuwa ni mwanzo mzuri wa kujenga mahusiano mazuri baina yetu.Wafanya biashara wakubwa kama ninyi mnapaswa kuwa karibu na watu kama sisi ili
tuweze kuwasaidia.Mimi mwenyewe nimekuwa mfanya biashara ninazifahamu changamoto wanazokumbana nazo wafanya biashara kwa hiyo ukiwa karibu na
mtu kama rais ni jambo lenye manufaa makubwa.Kuna nyakati unaweza kukwama lakini neno langu moja tu likakukwamua” akasema Ernest huku akicheka
kidogo “ Usemayo ni ya kweli mheshimiwa rais.Umuhimu upo mkubwa lakini tatizo ni namna ya kuwafikia ninyi wakubwa.” Akasema Boaz. “ Usijali Mr Boaz,
nitakupatia namba yangu ya simu na muda wowote ukihitaji msaada wa aina yoyote ile utanitaarifu nitakusaidia” “ Nashukuru sana mheshimiwa rais” “ Mr Boaz
nimeambiwa na Mr Mukasha kwamba kwa sasa uko safarini Canada kwa hiyo sitaki kuchukua muda wako mwingi naomba nielekee moja kwa moja katika suala
la msingi lililonifanya nikutafute” akasema Ernest na kunyamaza kidogo kisha akasema “ Mr Boaz ninataka kuzunguza nawe kuhusiana na mtu mmoja anaitwa
Austin January”
“ Austin?!! Boaz akastuka “ Ndiyo Mr Boaz.Nimeelekezwa hivi sasa ulo naye na anafaya kazi katika moja ya kampuni zako” “ Ndiyo mheshimiwa rais,Austin
anafanya kazi katika mojawapo ya kampuni zangu nchini Afrika ya kusini” “ Mr Boaz ninahitaji kuonana na Austin” akasema Rais na kumfanya Boaz atoe
kicheko k idogo “ Mheshimiwa rais hilo ni jambo ambalo halitawezekana kwasasa.Austin hawezi kurejea tena Tanzania kutokana na mambo yaliyowahi
kumtokea .Nadhani utakuwa unafahamu mambo yaliyomkuta “ “ Ndiyo Boaz ninafahamu japokuwa tukio hilo lilitokea wakati bado sijaingia madarakani na
nilipoinga madarakani nilipewa taarifa ya tukio hilo japokuwa sikuelezwa ukweli wote.Nimeufahamu ukweli hivi karibuni na ndiyo maana nimekupigia
kukuomba unisaidie kuonana na Austin.Ningeweza kuzungumza naye moja kwa moja lakini nimeona ni vyema kama nikiongea nawe kwanza kwani yuko chini
ya himaya yako.Please help me” “ Hujakosea mheshimiwa rais na ninakushukuru kwa busara hiyo lakini sina hakika kama Austin anaweza akakubali kuonana
nawe.Hivi sasa amekwisha sahau yote yaliyotokea na anaishi maisha mazuri na si mimi wala mtu yeyote anayeweza kumshawishi Austin akakubali ombi lako.He
hate Tanzania” akasema Boaz “ Mr Boaz tafadhasli naomba ujaribu kwa kila namna unavyoweza kumshawishi akubali kuonana nami,ni muhimu sana.” Akasema
Ernest “ Mheshimiwa rais natamani sana kukusaidia,au labda unieleze unamuhitaji Austin kwa jambo gani hasa? “ Kuna kazi binafsi nahitaji anifanyie” “ Kazi ?!
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
akasema Boaz na kutoa kicheko kidogo “ Austin amekwisha achana na hizo kazi mheshimiwa rais.Nakushauri mheshimiwa rais jaribu kutafuta kijana mwingine
miongoni mwa vijana wako akufanyie kazi yako na usipoteze muda kuhusu Austin” “ Mr Boaz nakubaliana nawe kwamba kutokana na mambo yaliyomkuta
Austin inaweza kuwa vigumu kwake kukubali kuonana nami lakini kwa kupitia kwako inaweza kuwa rahisi na akalegeza msimamo wake.Mimi na wewe
tunaweza kuingia makubaliano kwani jambo kama hili haliwezi kwenda hivi hivi.Niko tayari kwa makubaliano yoyote ili mradi nifanikiwe kuonana na
Austin.Niambie unahitaji nini nikupatie nawe unisaidie nionane na Austin” akasema Rais na Boaz akasikika akivuta pumzi ndefu kisha akasema “ Mheshimiwa
rais wewe ni rais wangu ,ninakuheshimu sana ,ninaiona nia yako ya kutaka kuonana na Austin na siwezi kufanya makubaliano yoyote nawe katika suala hili
kwani itakuwa ni kukukosea heshima kiongozi wangu.Nitakusaidia uweze kuonana na Austin.Nitajitahidi kumshawishi japo haitakuwa rahisi lakini naamini
atakubali.Ila ninachokuomba mheshimwa rais pale nitakapokuja kwako kuomba
msaada wako naomba usinitupe mkuu wangu” “ Mr Boaz nakushukuru sana na ninakuahidi kuwa dakika yoyote ukihitaji msaada wangu wa aina yoyote ile
usisite kunitaarifu nitakusaidia” akasema rais “ Ahsante mheshimiwa rais kwa ahadi hiyo.Sasa naomba nikuache upumzike nitawasiliaa nawe tena baada ya
kuzungumza na Austin” akasema Boaz akaagana na rais na kukata simu “ Oh thank you Lord.Sasa nina uhakika wa kumpata Austin.Boaz ameonyesha uungwana
mkubwa.By the way huyu Boaz ni nani hasa? Anashughulika na biashara gani? Akauliza Ernest “ Boaz ni bilionea mtanzania anayemiliki biashara kubwa kubwa
nchini Afrika kusini.Amewekeza sana huko lakini hata hapa nyumbani amewekeza pia ana miradi kadhaa mikubwa.Nitajitahidi kukusanya taarifa zake na
kukuletea” akasema Mukasha “ Nitashukuru sana Mukasha.Ahsante kwa msaada huu mkubwa wa kunikutanisha na Boaz na hatimaye nitampata Austin .Naomba
sasa twende tukapumzike imekuwa ni siku ndefu lakini yenye mafanikio makubwa” akasema Ernest ****************** Monica alidamka saa kumi na mbili za
asubuhi na bila kuaga mtu yeyote akaondoka kuelekea hospitali kumtazama Dr Marcelo.Bado kichwa chake kiliendelea kusongwa na mawazo mengi kuhusiana
na suala aliloelezwa na wazazi juu ya ombi la rais David Zumo.Alifika hospitali lakini hakuna aliyeruhusiwa kuingia ndani ya chumba hicho kutokana na hali ya
Dr Marcelo kubadilika ghafla kwa hiyo madaktari walikuwa katika heka heka za kujaribu kuidhibiti hali hiyo.Ndugu na jamaa wote waliofika kumjulia hali Dr
Marcelo walikuwa nje wakiwa na wasiwasi mkubwa.Monica akiwa miongoni mwa watu waliokuwa nje wakisubiri taarifa ya daktari juu ya hali ya Dr Marcelo
akastuka baada ya kuguswa bega.Akageuka kumtazama aliyemgusa akakutana na Julieth dada yake Marcelo “ Habari za asubuhi Monica.Naitwa Julieth ni dada
wa Marcelo” “ Ninakufahamu Julieth.Tayari Daniel alikwisha nitambulisha kwako” “Good.Can I have a word with you Monica? Akasema Julieth wakasogea
pembeni kidogo “ Unasemaje Julieth? Akauliza Monica “ Monica kuna jambo nataka kukuuliza ila utanisamehe kwa kuwa ni la kibinafsi zaidi” “ Usihofu
Julieth uliza” “ Dr Marcelo ni kaka yangu ,mimi na yeye baba yetu mmoja lakini mama zetu ni tofauti.Marcelo ni mtoto wa pekee kwa mama yake na mimi kwa
mama yangu niko peke yangu pia.Maisha ya Marcelo naweza kusema kwamba yametawaliwa na usiri mkuwa.Kuna mamo mengi tusiyoyajua kuhusu yeye.Kwa
sasa hali yake inazidi kuwa tete na kuna wasi wasi yawezekana akapoteza maisha kwa mujibu wa daktari alienieleza leo kwamba hali yake si nzuri .Toka
alipopata matatizo haya umekuwa ukifika hapa hospitali mara kwa mara kumjulia hali na
unaonekana kuguswa sana .Naomba kuuliza wewe na Marcelo mna mahusiano yoyote? Au kwa lugha nyepesi ninyi ni wapenzi? Akauliza Julieth na kumfanya
Monica atoe kicheko kidogo “ Usinielewe vibaya Monica nimeuliza hivyo kwa makusudi ili hata likitokea la kutokea basi tujue marehemu ameacha mchumba
au hata kama kuna mtoto” “ Hilo ni suala zuri na la muhimu sana julieth lakini mimi na Dr Marcelo hatuna mahusiano yoyote ya kimapenzi.Sisi ni marafiki wa
kawaida .Nimefahamiana naye hivi karibuni na aliyetukutanisha ni Daniel ambaye amekuwa rafiki yangu wa muda mrefu toka tukiwa wadogo.Kwa muda huu
mfupi tuliofahamiana tumekuwa marafiki wakubwa na mtu yeyote angeweza kudhani labda sisi ni marafiki wakubwa wa muda mrefu au hata wapenzi.”
Akasema Monica. “ Ahsante kwa majibu hayo Monica.Hata mimi nilihisi labda yawezekana mkawa ni wapenzi.kaka yangu ana bahati sana ya kupata marafiki
wazuri lakini mpaka leo hii hatujawahi kumfahamu mpenzi wake” akasema Julieth “ kwa hiyo Marcelo hajawahi kuwa na mpenzi? Akauliza Monica “ Sisi kama
ndugu zake hatulifahamu hilo kwani amekuwa msiri sana kuhusiana na kuweka wazi mahusiano yake” akasema Julieth “ Poor Marcelo.Mungu amsaidie apone
na aendelee na maisha yake.He’s a good person.Watu waliofanya kitendo hiki tayari wamekwisha fahamika na kukamatwa? Akauliza Monica “ Hapana bado
hawajafahamika ila jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi kuwabaini na kuwatia nguvuni.” Akajibu Juliet “ Ninasali sana kumuomba Mungu ili watu hawa
waliofanya ukatili huu wapatikane na kufikishwa mbele ya sheria.Kinachoniumiza zaidi mchana wa siku ile ya tukio nilikutana naye kuna jambo alikuja
kunieleza.Niliingiwa na hofu kuhusiana na usalama wake nikamuomba aje akae nyumbani kwangu kwa muda hadi hapo masuala yake yatakapopatiwa ufumbuzi
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
lakini akakataa na jioni ya siku hiyo akapigwa risasi.Inaniuma sana na ndiyo maana siachi kuja kila siku kumjulia hali” akasema Monica na machozi yakamtoka “
Pole Monica .Hili ni tukio linalotuumiza sote na tuzidi kumuomea Marcelo apone” akasema Julieth .Baada ya dakika tano daktari akatoka na kuwataarifu kuwa
hali ya Marcelo inaendelea vizuri akawatoa hofu na kuwataka warejee nyumbani Baada ya kutoka hospitali Monica akaelekea moja kwa moja nyumbani
kwake.Alisalimiana na wafanyakazi wake pale nyumbani halafu akaenda chumbani kwake “Kichwa changu ni kama vile kinabebeshwa mzigo mzito zaidi ya
uwezo wake.Ninawaza hadi nahisi kufika mwisho wa uwezo wangu wa kufikiri.Huku kuna suala la David Zumo na huku kuna suala la Marcelo.Yote haya
yananich......” akastuliwa toka mawazoni na mlio wa simu akaitoa katika pochi akatazama mpigaji.Zilikuwa ni namba ngeni.Akazitazama vizuri na kugundua
hazikuwa ni namba za Tanzania.Akasita kidogo halafu akaipokea “ Hallow’ akasema kwa wasi wasi kidogo “ Hallow Monica.David Zumo ninaongea
hapa.Habari za asubuhi.? Vipi maendeleo yako? Monica akastuka sana baada ya kuisikia sauti ile ya David “ Hallow mheshimiwa rais” akasema kwa sauti yenye
kukwama kwama “ Monica nimefurahi sana kuisikia tena sauti yako nzuri.Vipi maendeleo yako? “ Ninaendelea vizuri mheshimiwa rais” “ Nafurahi kusikia
hivyo,ila nakuomba unite David inatosha sana” “Sawa mhe....oh samahani David..” akasema Monica na wote wakacheka “Monica utanisamehe kwa kukupigia
asubuhi hii naamini hukuwa umerajia simu toka kwangu.Lengo kubwa ni kutaka kujua maendeleo yako na pili kukufahamisa kwamba mimi ni mlezi wa umoja
wa vijana wa Congo.Umoja huu lengo lake kubwa ni kuwajenga vijana kifikra watambue wajibu wao kwa taifa na kwa jamii.Kila mwaka wanachama wa umoja
huu hufanya kongamano kubwa na kujadili mambo mbali mbali na changamoto zinazowazunguka kama vijana.Mwaka huu kongamano hilo linafanyika hapa
Kinshasa na mimi kama mlezi wao nimealikwa kulizindua.Monica kuna jambo ambalo sikuwa nimelipanga hapo kabla lakini baada ya kukutana nawe nimeona
kuna ulazima wa wewe kuwa mmoja wa watoa mada katika kongamano hilo.Mchango wako utawasaidia vijana wengi wa kike na wa kiume kujitambua wao ni
akina nani na wafanye nini ili watimize malengo yao ya maisha.Kwa hiyo Monica napenda nitumie nafasi hii kukukaribisha rasmi katika kongamano la tisa la
umoja wa vijana wa Congo.Uwepo wako utawapa hamasa vijana wengi.” Akasema David “ David nimefurahi kwa mwaliko huo lakini nashindwa nikujibu nini
kwani imekuwa ni ghafla mno na sijajiandaa kabisa kwa jambo hil..” Monica hakumaliza sentensi David akasema “Monica tafadhali naomba usiseme
hapana.Nafahamu nilipaswa kukutaarifu toka mapema kuhusiana na suala hili lakini sikuwa na mawazo hayo.Baada ya kuondoka Tanzania nimetafakari na
kuona kuna umuhimu mkubwa sana wewe kuhudhuria katika kongamano hilo.Tayari nimekwisha wataarifu viongozi wa umoja huo kwamba na wewe
utakuwepo na vijana wametangaziwa na kwa taaarifa nilizozipata ni kwamba vijana wamehamasika mno kuihudhuria katika kongamano baada ya kusikia uwepo
wako.Kwa hiyo Monica nakuomba tafadhali usiniangushe.Naomba ukubali mwaliko huu rasmi toka kwangu” akasema David.Ukimya mfupi ukapita .Monica
akatafakari kasha akasema “ Mheshimiwa rais kwa hili ulilolifanya hujanitendea haki hata kidogo.Ulipaswa kunitaarifu kwanza ili nithibitishe ushiriki wangu
kabla ya kuutangazia umma.” Akasema Monica akanyamaza na kuendelea “ Hata hivyo,tayari umenifunga mikono na siwezi tena kusema hapana.Nitahudhuria
kongamano hilo” “ Ahsante sana Monica.Nashukuru mno.Hii ni heshima kubwa umenipa” “ Lini linafanyika kongamano hilo? Akauliza Monica “ Linaanza
kesho.Kwa hiyo jioni ya leo nitatuma ndege yangu binafsi kuja kukuchukua hapo Dar es salaam” akasema David Zumo.Ukimya ukatanda tena baada ya muda
Monica akasema “Sawa David” “Ahsante Monica.Nitawasiliana nawe baadae mchana wa leo” akasema David na kukata simu “Dah ! Kweli David amedhamiria
kufanya kila awezalo kutafuta ukaribu na mimi.Amenibana katika kona na nisingeweza kusema hapana.Hili ni jaribu kubwa na taratibu najiona kama vile
ninaelekea kuanguka.Ninapoisikia sauti ya David nahisi kutetemeka kwa ndani.Nahisi amefanya hili makusudi kabisa ili apate nafasi ya kuwa na mimi.Lakini
hata hivyo hii ni nafasi yangu pia ya kumsoma na kumfahamu vizuri ni mtu wa aina gani hasa.Ngoja niende Congo kwa sababu naona kuna nguvu kubwa
inanitaka niende kuonana na David “ akawaza na kuoga akajiandaa akatoka kuelekea ofisini kwake.Njiani bado kichwa chake kilikuwa na mawazo mengi na hata
alipofika ofisini kwake alishindwa kufanya kazi yoyote.Kikubwa alichokuwa anakiwaza ni safari ya kwenda Congo.
NINI KITATOKEA MONICA AKIWA CONGO? ATAKUBALI KUOLEWA NA DAVID ZUMO? AUSTIN JANUARY ATAKUBALI KUREJEA TANZANIA?
NANI KAMPIGA RISASI DR MARCELO NA KWA NINI ? #USIKOSE KUENDELEA NA SIMULIZI HII KATIKA SEASON 2#
MWISHO WA SEASON 1
MWISHO
0 comments:
Post a Comment