Search This Blog

Friday, 20 May 2022

QUEEN MONICA - 4

 







    Simulizi : Queen Monica

    Sehemu Ya Nne (4)



    Lazimka nishangae Jane.Baba yako analalia fedha lakini wewe unaishi kwa kutegemea kipato cha boda boda? “Ndiyo Ernest.Fedha alizonazo baba ni zake na

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wala hazinihusu mimi.Nimejifunza kuishi kutokana na kipato chetu kidogo and we’re happy with our life.Kuna nyakati mama amekuwa ananisaidia hapa na pale



    namshukuru sana kwa kuendelea kunilea” akasema Jane “ Jane utanisamehe kwa hili lakini si kwamba ninadharau kipato hicho cha mumeo lakini kwa



    mwanamke kama wewe unapaswa uwe na maisha mazuri sana katika jumba kubwa la kifahari uwe na magari yako ya kifahari kwa ufupi



    unatakiwa uishi kama malkia.” Akasema Ernest na ukimya ukapita “ Jane tuachane na hayo mambo yamekwisha pita tuangalie ya sasa na mbele.Baada ya



    kupotezana kwa miaka mingi tumekutana tena na japokuwa kila mmoja kwa sasa tayari ana maisha yake lakini hii haituzuii kuendeleza urafiki wetu.Kwa ufupi



    ni kwamba mimi kwa sasa nina mchumba anaitwa Miriam na kama ikimpendeza Mungu ndiye ambaye nitafunga naye ndoa kwa hiyo sote tuko katika



    mahusiano.” Akasema Ernest na kunywa funda la mvinyo akaendelea “ Jane nimeguswa sana na maisha yako japokuwa hujanieleza kwa undani ila nafahamu



    kuwa hukupaswa kuishi katika aina hii ya maisha kwa hiyo mimi kama rafiki yako ambaye kwa sasa nina uwezo mkubwa nataka nikusaidie nikutoe katika



    maisha haya na ufikie yale maisha uliyokuwa unayahitaji and please don’t say no.This is just a help for a friend and nothing else.” Akasema Ernest na Janet



    akatabasamu “ You know how to tie my hands Ernest lakini hata hivyo umekuja kwa wakati muafaka kabisa.I real need your help right now” akasema Janet “



    Thank you Jane for accepting my help.Tell me what do you want me to help? Janet akavuta pumzi ndefu na kusema “ Ben alikuwa anaendesha gari ambalo



    aliazima kwa mmoja wa rafiki zake akiwa barabarani alipata ajali na katika ajali hiyo mtu mmoja alifariki dunia.Inasemekana mtu huyo aliyefariki dunia ni



    mjukuu wa mmoja wapo wa wanasiasa wakubwa hapa nchini kwa hiyo kuna shinikizo kubwa la kutaka Ben afungwe ingawa hakuwa na hatia kwani yeye ndiye



    aliyegongwa lakini kibao kimegeuka na anatajwa kuwa ndiye aliyegonga.Nimejitahidi sana kutafuta msaada wa kisheria sehemu mbali mbali lakini wengi wa



    mawakili wanaigopa kesi hii kwani wanafahamu kuwa hawatashinda na kuharibu sifa yao.Ernest nahitaji wakili wa kuweza kumsimamia Ben katika kesi hii



    kwani bila kumpata wakili mzuri atafungwa.Sitaki Ben afungwe kwani yeye ndiye kila kitu kwangu.Tafadhali Ernest kama una uwezo wa kunisaidia katika hilo



    naomba unisaidie ” akasema janet machozi yakamtoka.Ernest akainuka akamsogelea akamfuta machozi na kusema “ Usilie Janet.Niachie mimi suala hilo na



    ninakuhakikishia litakwisha na hutaamini macho yako.” “ Real ??! “ Niamini Jane.Kwanza hesabu kama suala hilo tayari limekwisha kwani liko ndani ya uwezo



    wangu.” “ Ahsante sana Ernest” akasema Janet kwa furaha na kumkumbatia Ernest kwa nguvu “ Hilo ni moja,lakini baada ya kesi kumalizika nataka nimfundishe



    Ben kazi.Nataka aanze kufanya biashara kubwa kubwa na kupata fedha nyingi kuliko biashara hiyo anayoifanya ya boda boda.Nakuhakikishia Jane nitafanya kila



    lililo ndani ya uwezo wangu hadi mtakuwa watu matajiri.” “ Ahsante sana Ernest .Naamini ni mpango wa Mungu kutukutanisha kwani nilikwisha kata tamaa na



    sikujua ningefanya nini” akasema Janet.



    Kumbu kumbu hii ikamtoa machozi Janet. “ Ernest alifanikiwa kumtoa Ben gerezani na kesi ikamalizika.Mpaka leo sifahamu alifanya nini kulimaliza suala lile



    lakini nilichokuwa nakitaka mimi ni Benedict atoke gerezani. Baada ya Ben kutoka gerezani ndipo maisha yetu yalipobadilika.Ernest changed our life.Sidhani



    kama ninapaswa kumshukuru au kumlaani kwa hapa alipotufikisha lakini moyoni ninajuta kumfahamu ” akawaza Janet. Mzee Benedict bado alikuwa amekaa



    sofani akiwa na mawazo mengi.Alikumbuka mambo mengi kuhusiana na safari ya maisha yake toka alipokutana na Janet lakini kubwa ni siku aliyokutana na



    Ernest kwa mara ya kwanza na maisha yake yakabadilika DAR ES SALAAM - LA 403 CASINO Kiza tayari kimetanda angani gari la kifahari lilipofunga breki



    katika maegesho maalum kwa ajili ya watu muhimu tu wanaokuja katika kasino hili.Mlinzi mwenye sare maalum za ulinzi aliyekuwa akilinda eneo lile la



    maegesho akasogea na kuufungua mlango na toka ndani ya gari lile akashuka Benedict Mwamsole na mke wake Janet. “ Wow ! Sijawahi kufika hapa katika



    kipindi chote cha maisha yangu.” Akasema Benedict kwa mshangao mkubwa kutokana na uzuri wa mahali pale.Dereva akashuka garini na kuwataka wamfuate.



    Hii ilikuwa ni jioni ya siku ambayo mahakama ilimuachia huru Ben kwa kutokuwa na ushahidi wa kutosha kuhusiana na shitaka lililokuwa linamkabili.Ilikuwa



    ni siku ya furaha kubwa kwa Ben na kipenzi chake Janet.Usiku huu walifika hapa La 403 Casino kuja kuonana na mtu aliyefanikisha kuachiwa huru kwa Ben



    ambaye ni Ernest Mkasa aliyewataka wafike hapa kuonana naye na kuzungumza mambo ya muhimu sana kwa ajili yao Dereva aliwaongoza hadi katika ghorofa



    ya juu kabisa ya kasino hili kubwa ambako walimkuta Ernest akiwasubiri.Aliwakaribisha kwa furaha kubwa.Kuliandaliwa chakula kizuri na vinywaji na bila



    kupoteza muda wakala kwanza chakula halafu maongezi yakaanza “ Sasa tunaweza kuanza maongezi yetu” akasema Ernest “ Ernest awali ya yote mimi na mume



    wangu tunapenda sana kutoa shukrani zetu za dhati kwako kwa kuweza kulianikisha suala hili la kuimaliza kesi ile iliyokuwa inamkabili.Sitaki kufahamu



    umefanyaje lakini shida yetu sisi ni kesi ile imalizike.Ahsante sana Ernest.Tuna deni kubwa kwako” akasema Janet na kwa mbali machozi yakamlenga “ Janet



    ninyi ni marafiki zangu na niko tayari kufanya jambo lolote lile kwa ajili ya kuwasaidia marafiki zangu kwa hiyo nilifanya nililoweza kufanya ili kuimaliza ile



    kesi.Kwangu mimi haya ni mambo madogo sana” akasema Ernest na kutabasamu akaelekeza macho kwa Ben “ Benedict pole sana kwa matatizo lakini kwa



    mwanaume matatizo ni sehemu ya maisha yetu .Kukaa jela si dhambi kwani tukiwa kule tunaamini kuwa tunaimarika zaidi na kuitazama dunia kwa



    jicho la tatu.Ninaamini kwa muda uliokaa uko tayari umekwisha imarika vya kutosha.You are now a man” akasema Ernest “ Usemayo ni ya kweli Ernest.Nikiwa



    kule nimekutana na mambo mengi ambayo sikuwa nimeyafahamu hapo kabla,japokuwa sikuwa nimefungwa bado lakini nikiwa mahabusu nimekutana na watu



    wengi wenye makosa na tabia mbali mbali.Kama unavyosema nimeimarika.Nimejifunza mengi.Nashukuru sana kwa jitihada zako za kunitoa gerezani” akasema



    Ben “ Usijali Ben.Nilikutana na Jane siku moja akiwa anakwenda supermarket na akanieleza tatizo lako.Mimi na Monica ni marafiki wa muda mrefu,tumesoma

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wote sule moja hadi alipopata yale matatizo na kuacha shule tukapotezana mimi nikaendelea na masomo na harakati nyingine za maisha .Tulipokutana tena



    amekutana na mtu mwingne tofauti na Yule aliyemfahamu tukiwa shule.Now I’m a man. “ akasema na kuwasha sigara akavuta halafu akaendelea “ Sijifu lakini



    ninaweza kusema kwa sasa niko katika orodha ya watu matajiri hapa nchini.Ninamiliki biashara kadhaa kubwa kubwa na hata hili kasino ni la kwangu pia



    ninalimiliki kwa asilimia mia moja.Watu wengi wanashangaa nimewezaje kuwa na utajiri huu mkubwa ndani ya kipindi hiki kifupi na katika mri huu



    mdogo.Wengine wanasema yawezekana mali hizi nilizonazo ni mali za baba kwani wanamfahamu baba yangu ni mtu tajiri lakini baba ana mchango mdogo sana



    sehemu kubwa ya mali nimeitafuta mwenyewe mwenyewe kwa jasho langu.Kila kitu kinawezekana .Ukiwa na nia na kuweka bidii utafanikiwa katika kila jambo



    unalolifanya.Kwa hiyo hata ninyi pia mnaweza mkayabadili maisha yenu na mkafika hapa nilipo mimi na kuishangaza dunia.” Akanyamaza akainua glasi yake



    yenye pombe kali akanywa na kuvuta mikupuko kadhaa ya sigara kisha akasema “ Usiku wa leo nimewaiteni hapa ili kuongea mambo ya msingi sana kuhusiana



    na mustakabali mzima wa maisha yenu.” Akanyamaza tena akavuta sigara akapuliza moshi mwingi na kuendelea “ Janet alinieleza japosi kwa undani sana



    kuhusiana na maisha yenu kwamba hayakuwa mazuri na mimi kama rafiki nimejitolea kwa hali na mali kuwasaidia na kuwaondoa katika hali mliyonayo



    sasa.Nitawaelekeza njia lakini mnatakiwa mfanye kazi kwa bidii sana na kwa kujituma ili kujikwamua kwa hiyo kabla sijasema lolote nataka nipate uhakika toka



    kwenu kama kweli mnaumizwa na aina ya maisha mnayoishi na mnataka kuachana nayo na kuwa matajiri kama mimi” akasema Ernest na kuvuta tena sigara



    yake.Benedict na Janet wakatazamana na kisha Jane akasema ` “ Ernest hakuna mtu anayeufurahia umasikini kwa hiyo kama kuna njia ambayo una jua inaweza



    kutusaidia kutukwamua kutoka katika hali hii ngumu tafadhali tuonyeshe njia hiyo na sisi tupite tuweze kujikwamua” akasema Jane “ Nafurahi kusikia



    hivyo.Nitawasaidia” akasema na kuinua tena glasi yenye pombe akanywa na kuwatazama akina Jane kwa makini usoni



    “ Kwa kuwa mmekiri kuwa mko tayari kufanya kazi ili kuachana na umasikini mlionao basi nitawaonyesha njia lakini nataka niwahakikishie kwamba si kazi



    rahisi na inahitaji moyo mgumu na kikubwa ni kwamba pindi nitakapowaeleza nini mnatakiwa mfanye there is no turning back.Tunaelewana ndugu zangu?



    Akauliza “Tunakuelewa Ernest.” Wakajibu Janet na Ben “ Vizuri.Usiku huu nitawatambulisha kwa washirika wangu ambao ninafanya nao kazi .Tuna biashara



    mbali mbali tunazifanya gizani.Ninaposema gizani sina maana ya usiku bali ni biashara zile ambazo serikali imekuwa inazipiga vita.Siwafichi ndugu zangu ni



    vigumu sana kuendelea na kuwa tajiri kwa biashara za kufanya mchana.Utaendelea na kuwa tajiri kama mimi kutokana na biashara za gizani.Kuna biashara mbali



    mbali ambazo tunazifanya mimi na washirika wangu lakini kubwa ambayo kwa sasa ina pesa nyingi mno ni biashara ya pembe za ndovu .” akanyamaza na kuvuta



    sigara yake.Janet na Ben wakatazamana.Ernest akaendelea “ Biashara ya pembe za ndovu ni biashara ambayo inaweza ikawatoa katika umaskini kwa haraka sana



    kwani soko lake ni kubwa mno duniani kwa sasa. Kutokana na kupanuka kwa soko hilo la pembe za ndovu duniani na kasi ya kutoweka kwa tembo katika



    hifadhi zetu serikali imeongeza ulinzi katika hifadhi na hivyo kufanya upatikanaji wa meno ya tembo uwe mgumu .Kwa sasa ni kama vita kati ya wawindaji na



    askari wa wanyamapori.Lakini naomba nisiwatishe kwa sababu katika mtandao wetu kuna watu wazito wakiwemo pia watu wakubwa serikalini kwa hiyo kwetu



    sisi ni kazi rahisi tu na hakuna ugumu mkubwa tunaokutana nao.” Akanyamaza akanywa pombe yake kali na kusema “ Mimi sikuwa na ufahamu wowote kuhusu



    mambo haya ni baba yangu ndiye aliyeniingiza katika mtandao huu na mimi nitawaingiza ninyi kwa kuwa kwa sasa mimi ndiye kiongozi wao.I swear to you



    endapo mtazingatia masharti na kujituma umasikini utabaki historia kwenu” akasema Ernest. Mzee Benard akajifuta jasho lililokuwa linamtiririka kwa wingi



    baada ya kumbu kumbu ile kumjia.



    Usiku ule ndipo maisha yetu yalibadilika.Ernest alitokea kuwa mtu wetu wa karibu na alitusaidia sana japokuwa haikuwa kazi rahisi lakini mimi na Janet



    tulishirikiana bega kwa bega na kama alivyosema Ernest maisha yetu yalibadilika.Ilikuwa ni biashara ya hatari kubwa na mara kadhaa tulinusurika kifo lakini



    hatukukata tamaa na mwishowe tukafanikisha malengo yetu tukawa matajiri wakubwa.Mara kadhaa niliwahi kukamatwa na kuweka gerezani lakini kwa msaada



    wa Ernest na mtandao wetu nilitoka gerezani.Ernest ni mmoja wa watu ambao ninawaheshimu sana na kila leo ninajiona kama nina deni kubwa kwake kwani



    hata baada ya kuwa rais bado ameendelea kutusaidia katika masuala mbali mbali ya kibiashara lakini sikuwahi kujua kama alikuwa na mahusiano na mke wangu



    na hadi wakafikia hatua ya kuzaa mtoto.Kwa hili alilolifanya la kukosa uaminifu linanifanya niyafute yale yote mazuri aliyoyafanya kwetu.I must destroy



    Ernest.” Akawaza Ben.Akiwa bado amesongwa na mawazo mengi mke wake Bi Janet akatoka chumbani na kwenda kuketi karibu na mumewe. “ Ben..” akasema



    Bi janet kwa sauti ya upole.Ben akainua kichwa akamtazama “ Ben I’m real sorry for the awfull things I said to you tonight.Sikupaswa kutamka maneno kama



    yale kwa mtu muhimu kama wewe.Ni hasira tu zilizonifanya nikatamka maneno yale.Nisamehe sana Ben.Nimetakafakarinimeliona kosa langu.Sikupaswa kabisa



    kukutamkia maneno yale.” Akasema Bi Janet.Ben akavuta pumzi ndefu na kusema “ Jane mimi na wewe tumetoka mbali mno na tuna historia kubwa lakini kwa



    mara ya kwanza katika maisha yangu nathubutu kutamka kwamba umeniumiza sana.Sijawahi kukutamkia neno hili hata siku moja lakini leo nataka ufahamu hilo



    kuwa umeniumiza sana si kwa maneno uliyoyatamka bali kwa usaliti ulionifanyia.Sikutegemea kabisa na wala sikuwahi kuota kama siku moja ungeweza



    kunisaliti hadi kufikia hatua ya kuzaa mtoto halafu ukanificha jambo hili kwa miaka hii yote hadi leo .I’m hurt ,deeply hurt” akasema Ben.Mkewe bi Janet



    akafuta machozi na kusema “ Ben nadhani unafahamu namna ninavyokupenda.Nilikupenda toka angali ukiwa kijana usiye na kitu chochote usiye na mbele wala



    nyuma.Niliwakataa vijana wengi waliotoka katika familia tajiri kwa ajili ya kuwa nawe.Hata nilipopata ujauzito wa Nathan na ukanisistiza kwamba nikatoe

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kwani hukuwa na uwezo wa kunihudumia wakati huo ukiwa mwanafunzi nilikataa na hata familia yangu iliponitaka nikatoe ili niendelee na masomo nikakataa



    pia na baba akaniambia nichague kati ya wewe au shule nikakuchagua wewe.I gave up everything for you Ben.Baba alikwisha niandalia maisha makubwa mazuri



    lakini niliviacha hivyo vyote kwa sababu ya upendo mkubwa nilio kuwa nao kwako.Nimeishi nawe maisha ya umasikini mkubwa na hata siku moja sikuwahi



    kujilaumu wala kujutia maamuzi yangu niliyoyafanya.Sikuwahi kumlaumu mtu yeyote kwa maisha niliyokuwa naishi kwani ni maisha niliyochagua kuishi na



    nilikuwa na furaha sana.Kama kukusaliti ningeweza kukusaliti wakati ule tukiwa katika maisha ya dhiki kubwa laini nilikuwa mvumilivu na sikuthubutu



    kufanya hivyo” akasema Janet



    Yote uliyoyasema nakubaliana nayo aslimia mia moja na ninamshukuru sana Mungu kwa kumpata mwanamke kama wewe ambae ni kwa jitihada zako kubwa



    leo hii tuko hapa tulipo lakini hayo yote uliyoyafanya pamoja na upendo mkubwa ulio nao kwangu yanatiwa doa na kitu kimoja tu kwamba umezaa nje ya ndoa



    tena na mtu ambaye ni rafiki yetu mkubwa.Nakubali hata mimi nimefanya usaliti na nina watoto kadhaa nje ya ndoa yetu na sikuwahi kukueleza na utanisamehe



    kwa hilo lakini ni kwa watu ambao si wa karibu yetu au unaowafahamu.Wewe umetembea na kuzaa na mtu wetu wa karibu sana.Ni aibu kubwa hii.Tutaziweka



    wapi sura zetu Jane jambo hili siku moja likivuja kwa watu? Akauliza Ben.Janet ambaye machozi hayakukauka machoni pake akasema “ Ernest ni mtu ambaye



    alikuwa ananitaka sana kimapenzi toka tukiwa shule lakini hakufanikiwa.Na hata tulipokutana tena baada ya miaka mingi na akajitolea kutusaidia bado alikuwa



    anaendelea na zile jitihada zake za kunitaka kimapenzi lakini nilijitahidi sana kumkwepa na kumueleza ukweli kwamba jambo hilo haliwezekani kwani penzi



    langu mimi nimelitoa kwa mtu mmoja tu ambaye ni wewe.” Akanyamaza akafuta machozi na kusema “ Kuna ule wakati ulikamatwa nchini China nikamfuata



    kwa ajili ya msaada.Akaahidi kukusaidia lakini kwa sharti moja tu kwamba lazima nifanye naye mapenzi.Kwa wakati ule sikuwa na mtu mwingine ambaye



    ningeweza kumkimbilia na kumuomba msaada zaidi ya Ernest hivyo nikalazimika kufanya naye mapenzi lakini kwa lengo la kutaka msaada wake.Baada ya



    kufanya naye mapenzi akakusaidia ukaachiwa na baadae ndipo nilipogundua kwamba nina ujauzito wa Ernest.Niliogopa sana kukueleza jambo kama lile la aibu



    na wala sikumueleza Ernest na mpaka leo hii hajui kama Monica ni mtoto wake.Hii ilikuwa ni siri yangu ambayo nilipanga kwenda nayo kaburini lakini ni jambo



    lililokuwa linaniumiza sana .” akasema Janet.Ben akawaza na kuuliza “ Ilitokea mara moja tu au bado mnaendelea na mahusiano kwa siri? “ It happened just



    once..” Akasema Janet “ Nitafanya uchunguzi wangu na endapo nitagundua kwamba wewe na Ernest bado mna mahusiano na kwamba mnakutana kwa siri I



    swear I will destroy you both.God will forgive me for that but I swear I will destroy you.Uwezo wa kufanya hivyo ninao!!! Akasema Benedict na kuinuka



    akaelekea chumbani na kumuacha mke wake pale sebuleni ***************** Sauti ya mlango kugongwa ilimstua mzee Ben toka usingizini,akamtazama



    mkewe aliyekuwa pembeni yake ambaye bado alikuwa katika usingizi ,taratibu mzee Ben akainuka na kwenda kuufungua mlango akakutana na Monica “ Monica



    “ akasema Mzee Ben “ Shikamoo baba” “Marahaba you are so early today” “ Ndiyo baba nimeamka mapema nataka nikamtazame rafiki yangu Dr Marcelo



    aliyepigwa risasi jana lakini kabla sijaelekea hospitali nimeona nije nikuone



    kama ulivyokuwa umeniagiza jana kwamba nisiondoke bila kuja kukuona” akasema Monica “ Sawa Monica.Nisubiri ninawe uso nikupeleke hospitali” akasema



    mzee Ben na kuingia bafuni akajimwagia maji haraka haraka .Wakati anatoka bafuni akamkuta mke wake tayari ameamka. Hawakusalimiana akavaa haraka



    haraka. “Unaenda wapi Ben? Akauliza Jane “ Nakwenda hospitali na Monica” akajibu Ben na kutoka akaongoza na Monica hadi katika gari wakaondoka



    kuelekea hospitali.Mara tu Benedict na Monica walipoondoka Janet akachukua simu na kuzitafuta namba Fulani akapiga baada ya muda ikapokelewa “ Hallow



    Madam Jane” ikasema sauti ya upande wa pili ya mtu aliyepokea simu “ Mukasha samahani kwa kukusumbua asubuhi hii lakini nina jambo la muhimu nataka



    unisaidie” “ Bila samahani Madam Jane.Nikusaidie nini? “ Nataka kuonana na Ernest leo” “ Leo ?? “ Ndiyo Mukasha.Nataka kuonana naye leo.Tafadhali fanya



    kila linalowezekana hadi nionane na Ernest leo” akasema Janet “ Sawa madam Jane ngoja nijitahidi nione nitakavyofanya ,nitakujulisha baadae” “ Ahsante sana



    Mukasha.Nakutegemea sana tafadhali usiniangushe” akasema Jane na kukata simu “ Lazima nionane na Ernest leo nimueleze kwamba tunatakiwa tuwe makini



    sana kwa sasa kwani Ben anatuchunguza.Ninamfahamu Ben huwa anamaanisha anachokisema na amedhamiria kweli kufanya uchunguzi kuhusu mimi na



    Ernest.Kwa miaka mingi nimekuwa katika mahusiano ya siri na Ernest bila ya Ben kujua.Najuta kwa nini niliamua kumueleza ukweli Ben kwani nimetibua na



    mambo mengine ambayo sikutaka yajulikane.Nina mambo mengi ambayo Ben hayajui kuhusu mimi na akifanya uchunguzi anaweza akayagundua.Natakiwa



    kuwa makini sana kuanzia sasa.Kosa dogo tu linaweza kusababisha matatizo makubwa.Ninampenda sana Ben lakini hata Ernest ninampenda pia ni mtu ambaye

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    nimuhimu pia kwangu,sitaki litokee jambo ambalo litanifanya nimkose mmoja wapo wa watu hawa ” Akawaza Jane



    “ Baba ulisema jana nisiondoke bila kuja kukuona.Kuna jambo lolote ulitaka kunieleza? Akauliza Monica wakiwa garini wakielekea hospitali “ Ndiyo Monica



    .Kuna jambo ambalo tunataka kuzungumza nawe lakini itakuwa ni baadae tukiwa pamoja na mama yako.” “ Ni jamb......” akasema Monica lakini mara simu yake



    ikaita,akazitambua namba zile “ David Zumo” akasema na kumfanya mzee Ben atabsamu “ Pokea” akasema “ Hallow mheshimiwa rais” “ Hallow Monica habari



    za asubuhi? Umeamka salama? “ Nimeamka salama mheshimiwa rais sijui wewe” “ Nimeamka salama Monica.Vipi hali ya rafiki yako? “ Hivi sasa ninaelekea



    hospitali kujua hali yake lakini hadi jana usiku hali yake ilikuwa inaendelea vizuri.” “ Sawa Monica nimekupigia kukujulia hali na vile vile kukufahamisha kuwa



    asubuhi ya leo nitaondoka kurejea Kongo .Nimefurahi sana kukutana nawe ana kwa ana na ningependa sana kama ningeweza kuonana nawe kabla ya kuondoka



    lakini kutokana na majukumu uliyonayo haitawezekana ila tutazidi kuwasiliana” akasema David “ Ahsante sana mheshimiwa rais.Ninashukuru sana kwa msaada



    mkubwa ulionisaidia.Nakuombea usafiri salama natumai tutazidi kuwasiliana” “ Ahsante Monica.Karibu sana Kongo.Nitakutumia mwaliko rasmi wa kuja



    kutembea Kongo” “ Sawa nitashukuru sana mheshimiwa rais” akasema Monica “ Kwa heri Monica” akasema David na kukata simu “ He’s a good person”



    akasema mzee Ben baada ya Monica kumaliza kuzungumza na David “ Ndyo baba,David zumo ni mtu mzuri ana roho nzuri.Anapenda sana kusaidia” akajibu



    Monica na safari ikaendelea hadi walipofika hospitali. Tayari Daniel na watu wengine walikwisha fika pale hospitali kumtazama Dr Marcelo ambaye alikuwa



    anaendelea vizuri.Tayari alikwisha fumbua macho lakini hakuweza kuongea .Bado tukio lililotokea la Dr Marcelo kurejea na uhai baada ya kuwa amekwisha



    thibitishwa kufariki liliendelea kuwa vinywani mwa watu na wengi walitaka kuthibitisha kama tukio lile ni kweli limetokea. Monica na baba yake waliondoka



    pale hospitali baada ya kuridhika kuwa hali ya Dr Marcelo ilikuwa inaendelea vizuri.Moja kwa moja walirejea nyumbani Monica akaenda chumbani kwake



    kujiandaa kwa ajili ya kuelekea kazini kwake,mzee Ben naye akaelekea chumbani kwake ambako alimkuta mkewe Jane “ Anaendeleaje Dr Marcelo? Akauliza



    Jane “ Anaendelea vizuri ,amekwisha fumbua macho lakini bado hajaweza kuzungumza chochote.” “ Poor Marcelo.Mungu atamsaidia atapona” akasema Jane. “



    Tayari umemueleza Monica ulichotaka kumueleza? Akauliza Jane “ Hapana sijamueleza.Tutamueleza wote wawili jioni ya leo” akasema mzee Ben “ Sawa Ben”



    akasema Janet



    onica aliwasili ofisini kwake lakini hakuweza kufanya chochote kwani kichwa chake kilikuwa na mawazo mengi sana na kubwa lililomuumiza kichwa ni



    kuhusiana na tukio la kupigwa risasi Dr Marcelo. “ Ni nani aliyempiga Dr Mareclo risasi na kwa nini? Akajiuliza “ Inawezekana tukio la kupigwa risasi



    linahusiana na lile la kupotea kwa vitu vyake na hasa kitabu alichopewa na baba yake? Akaendelea kujiuliza Monica bila kupata jibu ,na moja kati ya simu zake



    tatu za mezani ikaita akaipokea. “ Dada Monica,Daniel yuko hapa mapokezi anahitaji kuonana nawe,” akasema msichana wa mapokezi.Monica akafikiri kidogo



    na kusema “ Sawa mruhusu aingie ndani” akasema Monica .Baada ya kama dakika tatu hivi mlango wa ofisi ya Monica ukafunguliwa na Daniel akaingia. “



    Daniel karibu sana.Umepata taarifa zozote za kuhusiana na Dr Marcelo? Akauliza Monica “ Nimeongea na dada yake Julieth muda mfupi uliopita



    amenihakikishia kwamba Marcelo anaendelea vizuri .” akasema Daniel huku akiketi kitini. “ Oh thank God “ akasema Monica “ Monica samahani sana kwa



    kufika hapa kwani najua ulinieleza awali kwamba nisifike tena ofisini kwako lakini imenilazimu kuja.” Akasema Daniel “ Oh Daniel forget about what



    happened.Sote tulikuwa na hasira na tuliongea mambo ambayo hayakutoka moyoni.Unakaribishwa hapa muda wowote Daniel” “ Thank you” akasema Daniel



    halafu ukapita ukimya mfupi “ Monica sina amani toka jana, hili suala zima la Macelo limenichanganya sana na nimekuwa najiuliza maswali mengi bila



    majibu.Kwanza mtu kaingia chumbani kwake akavunja kasiki na kuchukua baadhi ya vitu muhimu na moja ya vitu alivyovichukua ni faili lenye kuonyesha Dr



    Marcelo ni mgonjwa wa saratani ya damu uliloletewa hapa.Baada ya tukio hilo Marcelo anapigwa risasi na watu wasio julikana na halafu cha kushangaza zaidi



    Marcelo akafariki na kurejea tena.Hili ni suala ambalo binafsi limenifanya nikose usingizi.Nimeona nije kwako kwa pamoja tulijadili suala hili pengine



    tunaweza kupata mwanga Fulani” akasema Daniel “ Hata mimi jambo hili limenichanganya sana.Kwanza sifahamu lengo la mtu aliyelileta lile faili kwangu na



    vile vile sifahamu kwa nini amepigwa risasi.Simfahamu Dr Marcelo kwa undani sana kwani tumefahamiana si muda mrefu lakini wewe ni rafiki yako wa siku



    nyingi na unamfahamu kiundani unadhani anaweza kuwa na ugomvi na mtu yeyote? “ Dr Marcelo ni mtu ambaye hana ugomvi na mtu yeyote.Ni mtu mpole sana



    na hapendi magomvi.Kila mtu anashangaa kwa nini amepigwa risasi” akasema Danie “ Jana mchana alinipigia simu akanitaka nionane naye na tulipokutana



    akaniambia kitu Fulani .Alisema kwamba wakati akitafakari aligundua kwamba katika vitu vilivyochukuliwa na mtu aliyefungua kasiki lake ni kitabu ambacho



    aliwahi kupewa na baba yake kabla hajafariki.” “ Kitabu? Akauliza Daniel



    Kitabu? Akauliza Daniel “ Ndiyo alisema kwamba kuna kitabu alipewa na baba yake ambacho ni mwongozo katika kazi zake za kitabibu na kabla hajakisoma



    kitabu hicho alipewa namba ambazo alitakiwa apige ili apewe maelekezo ya namna ya kukitumia kitabu hicho.Kwa mujibu wa Dr Marcelo ni kwamba hajawahi



    kukifungua kitabu hicho kujua kiliandikwa nini lakini jana baada ya kukumbuka kwamba nacho kimepotea ikamlazimu azitafute zile namba alizopewa apige



    kwa ajili ya kupewa maelekezo akapiga lakini simu ikapokelewa na kukatwa na jioni ya siku hiyo akapigwa risasi.Cha kushangaza zaidi mtu huyo alichukua



    kitabu hicho pamoja na lile faili akaacha mamilioni ya fedha yaliyokuwamo katika kasiki” Akasema Monica.Daniel akatafakari na kusema “ Monica jambo hili



    ulilonieleza limezidi kunichanganya zaidi na kulifanya suala hili kuzidi kuwa gumu.Kitabu hicho kina nini hadi huyu mvamizi akichukue na kuacha mamilioni

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ya fedha yaliyokuwamo katika kasiki? Akauliza Daniel na wote wakabaki kimya baada ya sekunde kadhaa Daniel akakumbuka kitu. “ Monica kuna kitu



    nimekumbuka.Siku moja nilikuwa na Marcelo sehemu Fulani usiku tukipata kinywaji .Hii ilikuwa ni baada ya kumaliza masomo yake nchini China.Alinieleza



    kwamba anatakiwa akafanye upasuaji wake wa kwanza kwa binti mmoja ambaye anasumbuliwa na tatizo la mishipa ya fahamu ya kichwa.Usiku huo alikuwa na



    wasiwasi mwingi na hakusita kunieleza kuhusu wasi wasi alionao kwani kwa hali ya mgonjwa huyo ilivyo ni wazi kama angefanyiwa upasuaji lazima



    angepoteza maisha.Uliponieleza kuhusu hicho kitabu nimekumbuka kitu,usiku huo alinieleza kwamba ili kuifanya operesheni hiyo analazimika kwenda kupitia



    mwongozo wake.Hakunieleza ni mwongozo upi anakwenda kuusoma lakini baada ya kunieleza kuwa alipewa kitabu cha mwongozo na baba yake sasa nimepata



    picha kwamba Marcelo alikuwa anamaanisha kwenda kuusoma mwongozo ambao ni hicho kitabu alichopewa na baba yake.” Akasema Daniel “ Nini kilitokea



    kwa mgonjwa? Akauliza Monica “ Alifanikiwa kumfanyia upasuaji.He saved her.” “ Wow !..akasema Monica “Kama ni hivyo ni wazi Marcelo alikisoma kitabu



    hicho na akafanikiwa kuokoa maisha ya mgonjwa, kwa nini basi Marcelo anidanganye kuwa hajawahi kukisoma hicho kitabu? “ Hata mimi nashangaa” Akajibu



    Daniel na ukimya ukapita “ Nakumbuka msichana ambaye alimfanyia upasuaji ule alipona akawa rafiki yake sana na walikuwa wakionekana pamoja sehemu



    mbali mbali na sote tukajua labda wamekuwa wapenzi .” “ Unamfahamu? Akauliza Monica “ Ndiyo ninamfahamu anaitwa Lilian.” “ Marcelo hakuwahi



    kunieleza kuhusu jambo hilo “ akasema Monica “ Marcelo ni msiri sana wa mambo yake mengi.Hata hili suala la saratani ya damu ya damu sikuwa nikilifahamu



    pamoja na ukaribu wetu wa muda mrefu.” Sasa unashauri nini Daniel ,tuwasiliane na familia yake tuwape taarifa hizi? Akauliza Monica “ Hapana let us stay out



    of this.Suala hili si jepesi kama tunavyodhani.Kuna vyombo vya usalama ambavyo vinafanya uchunguzi na hakuna ulazima wa sisi kuingilia uchunguzi wao.”



    Akasema “ Lakini Daniel,hatuwezi kuwa na taarifa kama hizi ambazo zinaweza kusaidia uchunguzi halafu tukakaa kimya.Lazima na sisi tutoe mchango wetu”



    akasema Monica “ Monica,Marcelo ni rafiki yetu lakini kwa suala hili nakuomba tusijihusishe kabisa labda hadi hapo tutakapoombwa .Tuviachie vyombo vya



    usalama vifanye kazi yake .Tunachotakiwa kufanya ni kumuombea Marcelo apone haraka” akasema Daniel.Monica akainamisha kichwa akazama katika mawazo



    kisah akasema “ Daniel nadhani nahitaji kupumzisha kichwa.Haya mambo yamenifanya nishindwe hata kufanya kazi yoyote leo japokuwa nina kazi nyingi za



    kufanya.Take me somewhere Daniel where I can clear my mind.” Akasema Monica.Huku akitabasamu Daniel akamshika mkono wakatoka mle ofisini



    wakaondoka.



    Ernest Mkasa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania akitokea kukagua maendeleo ya upanuzi wa bandari ya Dar es salaam alielekeza msafara wake uingie



    White Rhino hotel.Hii ni moja ya hoteli inayomilikiwa na rais huyu .White Rhino hotel imesambaa katika nchi mbali mbali za afrika na katika baadhi ya nchi za



    Ulaya.Mara nyingi Ernest hupenda kuja hapa kupata chakula,kupumzika katika bustani nzuri zenye wanyama mbali mbali na wakati mwingine hukutana na



    wageni wake kwa ajili ya maongezi ya faragha. Alipokewa na watumishi wa hoteli akasalimiana nao halafu akaongozana na meneja wa hoteli hadi katika lifti



    wakapanda ghorofani “ Tayari Jane amekwisha fika? Akauliza Ernest kwa sauti ndogo “ Amekwisha fika mheshimiwa rais,yupo chumbani anakusubiri” akajibu



    meneja wa hoteli Walipanda hadi ghorofa ya ishirini na mbili wakashuka na kuelekea katika mlango ulioandikwa Presidential suit 5.Ernest akawafanyia ishara



    walinzi wake wabaki nje ,meneja wa hoteli akamfungulia mlango rais akaingia ndani.Katika sofa zuri jeupe alikuwa amekaa mwanamama mmoja ambaye licha



    ya umri wake kuonekana kuwa mkubwa lakini sura yake bado ilionyesha uzuri wa aina yake.Uso wa Ernest ukachanua kwa tabasamu pana sana baada ya kuiona



    sura ile nzuri ya Yule manamama ambaye alisimama na kumfuata Ernest wakakumbatiana kwa furaha “ I missed you Janet.I missed you so much” akasema



    Erbnest na kumbusu Janet “ I missed you too Ernest” akasema Janet na kumkumbatia Ernest kwa nguvu zaidi wakanyonyana ndimi na huku wote wakihema kwa



    kasi na kutoa miguno wakavua nguo na kuingia katika mtanange .Dakika kumi na tano zilitosha sana kumaliza mtanange ule ambao uliwaacha wote wawili



    wakihema kama wakimbiaji wa mbio ndefu. “ Jane sijui nikwambie nini “ akasema Ernest huku akimtazama Janet “ Kwa nini Ernest? “ Pamoja na kwamba umri



    wetu umesonga sana lakini kila ninapokutana nawe ninazikumbuka zile enzi zetu za ujana.Unanifanya nijione bado ni kijana sana” akasema Ernest na wote



    wakacheka “ Ernest you don’t have an idea how much I missed you.Wewe ni tofauti sana na wanaume wengine wote ambao nimewahi kukutana nao.Ninapofanya



    nawe mapenzi hata kwa muda mfupi ninaipata raha ambayo siwezi kuipata toka kwa wanaume wengine.Wewe utabaki kuwa shujaa wangu daima” akasema Janet



    na kumbusu Ernest.Ukapita ukimya mfupi Ernest akasema “ Jane ulimssitiza Mukasha kwamba unahitaji kuonana nami leo na kwa msisitizo uliompa nikajua



    kuna jambo la msingi sana na ndiyo maana nikasitisha ratiba zangu za mchana wa leo ili nipate nafasi ya kukutana nawe.So tell me sweetheart Kuna jambo



    unataka kunieleza? Jane akavuta pumzi ndefu na kusema “ Ndiyo Ernest kuna jambo la muhimu nataka kukueleza “ Nieleze Jane” akasema Ernest “ Nimekuja



    kukueleza kwamba Ben tayari amehisi kuna kitu kinaendelea kati yetu .” “ What ? How? Akauliza Ernest akiwa katika mstuko mkubwa “ Sifahamu amejuaje



    lakini amenihakikishia kwamba atafanya



    uchunguzi wake na endapo atagundua kwamba ni kweli sisi tuna mahusiano basi ama zetu ama zake.Kwa hiyo Ernest we have to put an end to what we’re



    doing” akasema Janet .Ernest akamtazama kwa macho ya uoga na kusema “ Jambo hili limenishangaza sana.Tumekuwa tunakutana kwa siri kwa zaidi ya miaka



    ishirini sasa lakini ninachojiuliza why now? Kwa nini ahisi sasa? Akauliza Ernest ,Janet hakujibu kitu akabaki kimya “ Jane tafadhali naomba unieleze nini



    kimetokea hadi Ben akahisi mimi na wewe tuna mahusiano kwa sababu hainiingii akilini kabisa kwa miaka hii yote Ben aje ahisi leo mimi na wewe tuna

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    mahusiano.” “ Hakuna tatizo lolote Ernest,nadhani kuna tetesi atakuwa amepewa” akajibu Jane “ Kapewa na nani? Jane naomba tafadhali unieleze



    ukweli.Ninakufaamu vizuri kuliko mtu mwingine yeyote kuliko hata mumeo.I know that you are hiding something from me.Tafadhali Jane mmi na wewe



    tumekuwa tunaelezana siri zetu hata zile kubwa.Nieleze kuna tatizo gani ? Ben amehisi vipi kuwa mimi na wewe tuna mahusiano? Ninakusisitiza unieleze



    ukweli kwa sababu ninamfahamu vizuri Ben .Kama amesema atafanya uchunguzi basi lazima atafanya na endapo atagundua kwamba mimi na wewe ni kweli



    tuna mahusiano basi suala hilo litachukua sura mpya.Ben anakupenda sana na kwa ajili yako anaweza akafanya jambo lolote baya kwetu na hasa hasa



    kwangu.Najua hawezi kuniua kwa silaha lakini kama unavyojua Ben ananifahamu kiundani,anaifahamu historia yangu chafu ya nyuma kwa hiyo ni rahisi sana



    kwa mtu kama huyu kuniharibia taswira yangu kwa jamii.Ni kweli nimepitia mambo mengi machafu katika kutafuta utajiri na hadi nimefika hapa katika nafasi



    hii kubwa ya uongozi wa nchi.Endapo wananchi watafahamu historia ya rais wao wanayempenda nina hakika nitakuwa rais wa kwanza duniani kupigwa mawe na



    wananchi hadharani.Kabla hatujafika huko natakiwa kujua nini kimetokea ,nini kinaendelea ili niweze kuchukua hatua za haraka kama zitahitajika ili kuzuia



    madhara yanayoweza kutokea endapo jambo hili litagundulika,lakini endapo utaendelea kunificha na mambo yakaharibika basi nitakua na kitu kimoja tu cha



    kufanya “ akasema Ernest na kunyamaza akamtazama Janet “ Whats that Ernest? Akauliza jane “ To kill Ben” akasema Ernest kwa sauti ndogo.Jane akastuka



    akamtazama Ernest kwa macho makali “ Mbona umestuka Jane? Akauliza Ernest “ Ernest tafadhali naomba usithubutu kuwaza kitu kama hicho.Ukimuua Ben



    it’ll be the end of us all.Ben is all I have na kwa ajili yake niko tayari kufanya lolote hata kama ni baya kwa hiyo nakuomba mawazo machafu kama hayo uyaweke



    pembeni kwani endapo utafanya kitu kama hicho utaingia katika vita na mimi na unajua mimi ni mbaya kuliko hata Ben.” Akasema Janet “ Janet najua



    unampenda sana Ben na uko tayari kwa lolote kwa ajili yake na ninafahamu pia kwamba wewe ni mbaya zaidi lakini usisahau kuwa mimi ndiye niliyewabadili



    mkawa hivi mlivyo leo,mambo yote niliwafundisha mimi kwa



    hiyo msisahau kuwa mimi ndiye mwalimu wenu na nina roho mbaya kama ya shetani kwa mtu anayenikorofisha na kutaka kuchezea maslahi yangu.So my dear



    Jane don’t wait for the situation to get ugly,tell me everything now!! Akasema Ernest “ Hakuna ujanja I have to tell him the truth.Bila hivyo mambo yanaweza



    kuwa mabaya sana.Ben na Ernest wote ni watu wenye hasira na wasiokubali kushindwa kirahisi kwa hiyo endapo hawa wawili wataingia katika uadui basi



    haitakuwa vita ndogo.Itatuhusisha wengi.Sitakiwi kuacha jambo hili likafika huk....” Janet akastuliwa na sauti ya Ernest “ Janet muda unakwenda na nina mambo



    mengi ya kufanya.Kama kuna jambo unataka kunieleza basi wakati wake ni sasa” akasema Ernest akainuka na kuanza kuvaa “ Naomba ukae chini Ernest”



    akasema Janet .Ernest akakaa kitandani “ Ernest kuna tatizo kubwa” “ Nieleze Jane ni tatizo gani hilo? Akauliza Ernest.Janet akavuta pumzi ndefu na kusema “



    Ni jambo ambalo limetokea miaka mingi iliyopita wakati ule Ben alipokamatwa nchini China na nikakufuata kukuomba umsaidie ,ukatoa sharti kwamba ili



    umsaidie ni lazima nikubali kufanya mapenzi nawe.Sikuwa na namna nyingine ninakubali kuanzisha mahusiano nawe lakini tulipofanya mara moja tukanogewa



    na kuchonga mzinga tukaendelea kulamba asali hadi hii leo.Kuna jambo lilitokea ambalo sikukueleza na sikutaka kukueleza wewe au mtu yeyote Yule lakini



    kutokana na hali ya mambo inavyokwenda nimejikuta sina ujanja zaidi ya kumueleza Ben na ndiyo chanzo cha haya yote ambayo yanataka kutokea” akasema



    Janet “Nini kimetokea Jane? Akauliza Ernest kwa wasi wasi.Jane akakohoa kidogo kurekebisha koo halafu akasema “ Ernest wakati wa mahusano yetu ya



    mwanzo kipindi Ben akiwa nchini China kuna jambo lilitokea.” “ Nieleze Jane mbona hutaki kuniambia ni jambo gani hilo lilitokea? “ We had a daughter”



    akasema Jane.Uso wa Ernest akaonyesha mstuko mkubwa sana.Akasimama na kumtazama Jane kwa uoga. “ Hebu rudia tena kile ambacho umekitamka Janet”



    akasema Ernest “ Nimekwambia kwamba we had a daughter” “ Oh my God !! akasema Ernest na kwenda dirishani akachungulia nje na kurudi kwa kasi akapiga

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    magoti pembeni ya Janet “ Janet please tell me it’s not a lie” akasema Ernest ambaye alionekana kama mtu aliyechanganyikiwa “ Its true Ernest “ akajibu Jane.



    Ernest machozi yalianza kumlenga “ Oh my God !! akasema na kusimama akachukua kitambaa na kujifuta machozi “ Kwa nini hukuwahi kunieleza jambo hili



    mapema? Kwa nini unanieleza leo ? akauliza Ernest huku bado machozi ya furaha yakiendelea kumtoka “ Ernest hii ilikuwa ni siri yangu ambayo niliapa kufa



    nayo na sikutaka mtu yeyote alifahamu jambo hili.Nisingeweza kukueleza kuhusu suala hili kwani nakufahamu you are a monster.Watoto



    wako watatu umewatoa kafara katika kufanikisha mambo yako ya utajiri.Sikutaka mwanangu naye afanywe kama ulivyowafanya wanao wengine.Endapo



    ningekueleza mapema kuhusu suala hili ni wazi lazima ungemchukua mtoto jambo ambalo sikutaka litokee.” Akanyamaza na kumeza mate.Ernest alikuwa ni



    kama mtu aliyechanganyikiwa “ Oh my God..Oh my God !!! akasema Ernest na halafu akaenda tena kupiga magoti mbele ya Janet “ Tell me Janet where is my



    daughter..ouh sorry where is our daughter? Akauliza “ Mwananetu yupo .Ni Monica” akasema Janet na kuzidi kumchanganya Ernest “ Monica? Akauliza kwa



    mshangao “ Ndiyo ni Monica” “ Monica malkia wa Afrika? “ Ndiye huyo.” Akajibu Janet.Ernest akainua mikono juu ishara ya kumshukuru Mungu halafu



    akamtazama tena Janet “ Janet tafadhali naomba unihakikishie kwamba hiki unachonieleza ni kitu cha kweli na si masihara” akasema Ernest “ kwa nini nifanye



    masihara katika jambo kubwa kama hili? Siwezi kukutania Ernest ni kweli mimi na wewe tuna mtoto ambaye ni Monica.” “ Ben analifahamu jambo hili?



    Umemueleza? “ Ndiyo anafahamu nimelazimika kumueleza ukweli” “ Amesemaje? Akauliza Ernest “ Kama ilivyo kwa mwanaume yeyote haikuwa habari nzuri



    kwake ambayo hakuwa ametegemea kuisikia.Alistuka sana .Ben anampenda sana Monica na haikuwa rahisi kuamini kuwa si mwanae lakini amekubaliana nami



    na hatuna mgogoro mkubwa ila hatuwezi kuwa sawa tena kama zamani tayari kuna doa kubwa limeingia katika ndoa yetu .Ben ameumia sana na



    kilichomuumiza zaidi si mimi kuzaa nje ya ndoa kwani hata yeye anao watoto aliowazaa nje ya ndoa ingawa amenificha lakini ninawafahamu na sina ugomvi



    naye katika hilo ,ila kilichomuumiza zaidi ni mtu niliyezaa naye yaani wewe.Hakutegemea kabisa mtu kama wewe ungeweza kumfanyia kitendo kama hiki hasa



    kwa namna mnavyoheshimiana.Amekasirishwa sana na hilo na ndiyo maana ameahidi kufanya uchunguzi kubaini kama mimi na wewe bado tunaendelea na



    mahusiano yetu na ameahidi kufanya kitu kibaya sana kama akigundua kuhusu hilo ndiyo maana nimekuja kukuomba kwamba kwa sasa tusimame kwanza



    kukutana hadi hapo baadae mambo yatakapotulia ndipo tuendelee” akasema Janet.Ernest akaketi pembeni yake akamshika mikono



    Janet nimekosa neno la kusema kwa surprise hii kubwa uliyonifanyia.Ninauona ni kama muujiza umenitokea.Watoto wangu wote tayari nimewapoteza na



    niliamini kuwa nitakufa bila ya kuwa na mrithi wa mali zangu .Kuniambia kwamba una mtoto wangu kumenipa furaha ambayo siwezi kuielezea na ndiyo maana



    unaniona niko kama mtu aliyechanganyikiwa .Hizi ni taarifa nzito sana kuwahi kuzisikia .Ouh Janet Janet ...” akasema Ernest na kumkumbatia Janet akamwagia



    mabusu “ Kuna swali moja ambao nataka unijibu.Ilikuaje hadi ukamueleza Ben suala hili? Najua lazima iko sababu so tell me” “ Ernest naomba nikueleze



    ukweli kwamba Monica nimemlea katika maadili makubwa sana ni mwanamke anayejitambua na anayejithamini sana.Mpaka leo pamoja na umaarufu wake bado



    hatujamfahamu mpenzi wake.Ni binti anayejitunza sana. Amekuwa karibu na wanaume kadhaa ambao baada ya kuwafanyia uchunguzi nimekuwa nikibaini



    kasoro kadhaa kwao lakini Monica ana imani kwamba si muda mrefu atampata mwanaume Yule ambaye amekuwa akimuhitaji kwa maisha yake yote”



    akanyamaza akameza mate na kuendelea “ Juzi alikuja rais wa jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo David Zumo ambaye baada ya kusikia kuhusiana na shule



    ambayo Monica anataka kuijenga kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wa kutokuona na kusikia ,akaguswa na akataka kuchangia mchango wake.Alimualika



    Monica katika hoteli alikofikia na kweli akampatia mchango mkubwa wa mabilioni ya fedha.Siku iliyofuata akatualika mimi na Ben kukutana naye tukaenda na



    wakati tukiendelea na chakula tukapata habari kuwa mmoja wa marafiki wa Monica amepigwa risasi ikanilazimu mimi na Monica kuondoka na kwenda hospitali



    nikamuacha Ben na David wakiongea.Katika maongezi yao David Zumo aliweka wazi nia yake ya kutaka kumuoa Monica.” “ What ?? !! Ernest akastuka sana “



    David Zumo ameweka wazi nia yake ya kutaka kumuoa Monica.Amedai kwamba anampenda sana na kwamba atatupa msaada mkubwa kiuchumi na kutupaisha



    kimataifa.Ben alikubali lakini mimi sikukubaliana hata kidogo na suala hilo na ndiyo hapo ugomvi wetu ulipoanzia ikanilazimu kumueleza Ben ukweli kuwa



    hana kauli yoyote juu ya Monica kwani si mwanae wa damu.Ben alitaka kwenda kumueleza Monica kuhusu jambo hili ,nikamzuia asifanye hivyo lakini kwa



    makubaliano maalum.” “ Makubaliano gani hayo? Akauliza Ernest “ Tumekubaliana kwamba suala hili litabaki siri yetu lakini Monica aolewe tu na



    David.Sikuweza kulikataa hilo kwani siko tayari kuyaharibu maisha ya Monica au kuivuruga familia yangu Monica atakapofahamu kuwa Ben si baba yake

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    mzazi.” “ No that’s not going to happen.Mwanangu aolewe na David Zumo? Hapana hiyo haiwezekani kabisa.I swear I wont let that happen !! akasema Ernest “



    Ernest nisikilize kwa makini .Hakuna chochote unachoweza kufanya kuhusu suala hili kwa sasa na hautafanya chochote kuzuia jambo hili lisifanyike.Tayari



    tumekwisha fanya maamuzi na lazima uyaheshimu.Monica ataolewa na David Zumo that’s final !! akasema Janet kwa sauti ya ukali “ Janet kama Monica ni



    mwanangu kweli kama unavyodai siko tayari aolewe



    na David Zumo.Japokuwa ni tajiri namba moja afrika lakini siko tayari amuoe mwanangu. !! akasema Ernest “ Ernest nimekwisha kwambia kwamba huwezi na



    usijaribu kulivuruga hilo.” Ernest akamtazama Janet kwa macho makali na kusema “ Kwa maana hiyo hutamtambulisha Monica kwangu kuwa mimi ni baba



    yake mzazi? “ Hapana.Hiyo itabaki ni siri yetu sisi watu watatu na Ben ataendelea kuwa baba yake.I want to save my family from falling apart.Pindi Monica



    akitambua kuwa Ben si baba yake mzazi familia yangu itameguka na nitabaki mwenywe.Familia yangu ni kitu kikubwa sana kwangu kuliko hata mali nilizonazo



    kwa hiyo nitailinda kwa gharama zozote zile.” Akasema Janet “ Monica nakubaliana nawe kwamba suala hili kama Monica akilifahamu litamuumiza na kweli



    familia yako itavurugika sana lakini na mimi nina haki kama baba na yeye Monica ana haki ya kumfahamu baba yake mzazi.Kama hukunipa haki ya kumlea



    mwanangu huwezi kumnyima Monica haki ya kumfahamu baba yake mzazi.” “ Ernest ninafahamu unazo haki kama baba mzazi lakini ninakuomba sana kwa sasa



    tuliache suala hili kama lilivyo.Hii ni hatua kubwa imefanyika umefahamu kuwa una mtoto na hata kama ukifa leo basi mrithi unaye.Muache aolewe na David



    Zumo na aendelee na maisha yake na suala hilo niachie mimi nitajua kitu cha kufanya.Nakuahidi ntamleta kwako Monica akufahamu.Haitakuwa rahisi lakini



    nakuahidi kwamba lazima nitamleta Monica akufahamu ila kwa sasa naomba tuyaache mambo yatulie kwanza .Suala hili twende nalo taratibu hatua kwa hatua



    lakini tukienda nalo kwa kasi tutaharibu kila kitu” akasema Janet.Ernest akainama akafikiri kwa muda na kusema “ Sawa Janet nimekuelewa japo kidogo lakini



    nataka nikushukuru kwa kuamua kunieleza ukweli wa jambo hili.Nashukuru kwa kuniletea habari njema sana ambazo zimeirudisha furaha ya maisha yangu



    ambayo nilikwisha ipoteza.Nipe muda na mimi nikatafakari kwa siku ya leo suala hili halafu nitakwambia nimefikiria tufanye nini kuhusu namna bora ya



    kulimaliza hili suala .” “ Ernest kwa sasa hatutaweza kuonana kama utanihitaji basi utanipigia simu na kama kuna suala la kujadili basi tutajadili lakini



    hatutaweza kuonana tena kwa hivi karibuni.” “ Sawa nimekuelewa Jane.Nitatafuta kila namna hadi nionane nawe tena kwani bado kuna mengi ambayo mimi na





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog