Simulizi : Queen Monica
Sehemu Ya Tatu (3)
kuzipata hizo namba ambazo ni hizi hapa” akasema Dr Marcelo na kumpatia Monica zile namba . “ Umejaribu kupiga namba hizi? Akauliza Monica “ Hapana sijajaribu kupiga.I’m scared” akasema Dr Marcelo “ Kwa hiyo hujui kitabu hicho kina nini ndani yake? Akauliza Monica “ Ndiyo Monica.Kama nilivyokueleza kwamba sikuwahi kukifungua toka baba alivyonikabidhi.Sikutaka kabisa kujua ndani yake kuna nini” akasema Dr Marcelo. “ Unadhani aliyekichukua anaweza kuwa na ufahamu wa kilichomo ndani ya kitabu hicho? Akauliza Monica “ Sifahamu Monica ila ninahisi kitu kama hicho kwa sababu mtu huyo hakuwa na nia na fedha bali baadhi tu ya vitu kwani ndani ya kasiki kulikuwa na fedha kiasi cha shilingi milioni milioni thelathini na nane lakini hazikuguswa hata senti moja badala yake akachukua faili langu la matibabu pamoja na hicho kitabu.Ninahisi yawezekana labda alilenga katika vitu hivyo pekee” akasema Dr Marcelo “ Hili suala mbona linanikanganya sana.” Akasema Monica “ Kweli Monica suala hili limenikanganya hata mimi na sielewi malengo ya huyo mtu.Lengo la kwanza ni kuufichua ugonjwa wangu kwako lakini sijui lengo la kukichukua hicho kitabu ni nini.Laiti nigekuwa nafahamu kilichomo ndani ya kitabu hicho ningeweza kupata walau mwanga lakini sikuwahi kukifungua kitabu hicho na sielewi kuliandikwa nini.” akasema Dr Marcelo “ Piga hizo namba za huyo mtu ambaye ulielekezwa kwake ili akupe maelekezo ya kukisoma kitabu hicho uongee naye ” akasema Monica “ Monica I’m scared.Ni miaka mingi imekwisha pita ” akasema Dr Marcelo “ Hutakiwi kuogopa Dr Marcelo.Nina hakika huyo mtu anaweza akakupa mwanga ili tufahamu kilichomo ndani ya kitabu hicho na tukijua kilichomo basi inaweza kuturahishia kufahamu lengo la mtu aliyekichukua kitabu hicho.” Akasema Monica.Dr Marcelo akaziandika namba zile katika simu yake halafu akataka kupiga akasita. “ Piga Dr Marcelo usiogope” akasema Monica lakini Dr Marcelo bado alionyesha uoga.Monica akaichukua ile simu ya Dr Marcelo na kupiga zile namba simu ikaanza kuita “ Simu inaita” akasema Monica na kumpatia Dr Marcelo simu “ Hallow” ikasema sauti nzito ya kiume upande wa pili baada ya kupokea simu “ Hallow..” akasema Marcelo “ Naongea na nani tafadhali” akauliza Yule mtu upande wa pili “ Naitwa Dr Marcelo,nilipewa namba hiz......” Kabla hajamaliza kujieleza simu ikakatwa “ Amekata simu” akasema Dr Marcelo kwa wasi wasi “ Kwa nini hakutaka kukusikia ulichotaka kumueleza na kukata simu haraka haraka? Au ulikosea namba?Akauliza Monica “ Monica namba hizi sikuzikosea niliziandika kwa makini sana na baba alinitaka nizirudie mara mbili ili ahakikishe kama nimeandika kwa usahihi.” Akasema Dr MarceloCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mimi nadhani kuna umuhimu wa kuwashirikisha polisi suala hili ili wafahamu kinachoendelea na ikwezekana wazifanyie uchunguzi hizo namba.Nimeanza kuwa na wasi wasi sana Dr Marcelo” “ NI wazo zuri lakini nataka kwanza nifanye uchunguzi wangu mwenyewe kuhusiana na kitabu hicho na baada ya hapo ndipo nitavishirikisha vyombo vya uchunguzi” akasema Dr Marcelo “ Kwa hiyo umepanga kufanya nini Dr Marcelo? “ Sijapata jibu bado nifanye nini lakini nitapata tu jibu wapi pa kuanzia uchunguzi wangu” akasema Dr Marcelo.Ukimya mfupi ukapita halafu Monica akasema “ Is your mother still alive? Akauliza Monica “ Sikuwahi kumfahamu mama yangu.Niliambiwa kwamba mama yangu alifariki baada ya kufanyiwa upasuaji wakati akijifungua mimi.Kwa hiyo sikupata bahati hata ya kukaa naye kwa dakika moja.Baada ya mama kufariki baba alioa mwanamke mwingine ambaye ndiye aliyenilea na ambaye hadi sasa bado yuko hai.” “ Dah pole sana kwa kuwapoteza wazazi wako wote wawili” akasema Monica “ Ahsante Monica.Ni kazi ya Mungu” “ Umefikiria kumuuliza mama yako kuhusiana na kitabu hicho? Hudhani kama anaweza kufahamu chochote juu ya kitabu hicho? Akauliza Monica “ Uhhm sikuwa nimelifikiria hilo kwani kitabu kile baba alikuwa anakificha sana na sina hakika kama mama alikuwa anakifahamu” akasema Dr Marcelo “ Dr Marcelo you have to ask her.Wanandoa wana tabia ya kuelezana mambo hata yale ya ndani kabisa kwa hiyo usiogope kumuuliza pengine anaweza kuwa anafahamu jambo Fulani kuhusiana na kitabu hicho ambalo linaweza kukusaidia.” Akasema Monica “ Monica wazo lako ni zuri sana.Nadhani hiyo ni sehemu nzuri kwa kuanzia.Nitakwenda kuongea na mama na kama ana lolote analolifahamu najua lazima atanieleza” akasema Dr Marcelo “ Dr Marcelo kuna kitu kingine ambacho nataka nikushauri.” “ Kitu gani hicho Monica? “ Tukio hili lililotokea limenipa wasi wasi sana na kwa kuwa hatuelewi lengo la huyu mtu aliyediriki kuingia chumbani kwako na kuchukua baadhi ya vitu vyako vya muhimu.Kwa kuwa bado uchunguzi unaendelea nashauri uchukue tahadhari kubwa kuhusu usalama wa maisha yako.Ulinieleza kwamba unaishi mwenyewe na nyumbani kwako hakuna mlinzi .Nakushauri kwa hali ilivyo sasa hivi undoke pale nyumbani kwako kwa muda.Njoo uishi kwangu kuna ulinzi na usalama wa kutosha.Nina nyumba kubwa ya kutosha hata watu mia moja.I don’t care what people will say but what I care is your safety.Come live with me for a while.Mambo yakitulia utarejea nyumbani kwako “ akasema Monica ” Monica ahsante sana kwa wazo hilo na kwa kujali usalama wangu lakini Usijali nitaendelea kukaa pale pale kwangu,nitaweka walinzi wa kulinda.I’ll be safe” “ Are you sure? Akauliza Monica “ yes I’m sure.I’ll be fine Monica” “ Sawa Dr Marcelo kama umenihakishia kwamba utakuwa salama mimi sina tatizo.” “ Monica naomba niende nikaonane na mama sasa hivi.Nitakujulisha atakachonieleza nitakapoongea naye” akasema Dr Marcelo “ Sawa Dr Marcelo mimi naelekea nyumbani nakwenda kujiandaa kuonana na David Zumo rais wa Kongo usiku wa leo” “ Rais wa Kongo? Akauliza Marcelo kwa mshangao kidogo “ Ndiyo” “ Do you know each other? Akauliza Dr Marcelo “ Yes we do” akasema Monica na kwa sekudne kadhaa Dr Marcelo akabaki anamtazama Monica halafu wakaanza kutembea kueleka katika maegesho yaliko magari yao. “ Dr Marcelo if you change your mind,my place is the best place for you” akasema Monica “ Ntakujulisha Monica usijali” akasema Dr Marcelo wakati anaingia garini akaondoka
Saa mbili na dakika kumi za usiku iliwakuta Mzee Benedict mwamsole,mkewe Janet na mtoto wao Monica katika hoteli ya kifahari ya Kobe village alikofikia David Zumo.Usoni kwa mzee Benedict hakukukauka tabasamu pana alikuwa na hamu sana ya kuonana na David Zumo kiongozi mwenye sifa kubwa afrika na dunia. Monica na wazazi wake walipokewa na wasaidizi wa David wakapelekwa bustanini ambako ndiko David alipanga akutane nao .Ilikuwa ni sehemu iliyoandaliwa vizuri na kulikuwa na ulinzi mkali kama kawaida ya kila mahala anapokuwapo David Zumo.Walikaribishwa na wahudumu waliovalia nadhifu wakaendelea na vinywaji wakati wakimsubiri David “ This place is amazing.Pamoja na utajiri wangu wote sijawahi kufika mahali hapa.Tumezoea kuona sehemu kama hizi zenye uzuri wa kushangaza katika mahoteli makubwa ya huko ulaya .Nimefurahi sana kuona hata hapa nyumbani tuna sehemu nzuri kama hizi” akasema mzee Ben. Wakati wakiendelea na maongezi ,David Zumo akiwa na walinzi wake akashuka ghorofani na kueleka moja kwa moja bustanini kukutana na wageni wake.Wote wakasimama baada ya David kuwasili pale bustanini wakasalimiana .David alikuwa na furaha kubwa kuonana na wazazi wa Monica.Walinzi wa David wakajitenga mbali kidogo na mahala walipokuwa wamekaa akina David ili kuwapa nafasi ya kuzungumza mambo yanayowahusu kwa uhuru zaidi “Nimefurahi sana kuwafahamu Bwana na Bi Benedict na Janet Mwamsole.” Akaanzisha maongezi David Zumo. “ Hata sisi tumefurahi sana kukutana nawe mheshimiwa rais .Ni heshima kubwa umetupa ya kukutana nawe.” Akasema mzee Benedict “ Nisingeweza kuondoka bila kuonana nanyi.Leo tumemaliza mkutano wetu wa marais wa nchi za maziwa makuu lakini nimelazimika kubaki ili kukutana nanyi.” Akasema na kunywa funda la mvinyo kisha akaendelea “ Jana nimekutana na Monica,nilimualika hapa kwa chakula na maongezi baada ya kuguswa sana na mambo anayoyafanya kwa jamii.Nilipofika hapa Tanzania nilisikia kuhusiana na mradi wake wa kujenga shule ya watoto wenye ulemavu wa kutokuona na kusikia.Niliguswa sana na jambo hilo na nikaona siwezi kuondoka bila kuunga mkono juhudi kama hizi za Monica na ndiyo maana nikamualika hapa nionane naye ili niweze kutoa mchango wangu mdogo na nikajikuta nikitaka kuonana na wazazi wake.Kwa hiyo karibuni sana wazee wangu tule tunywe tufurahie mafanikio ya Monica” akasema David “ Tunashukuru sana mheshimiwa rais .Kama nilivyokueleza mwanzo kuwa hii ni heshima kubwa umetupa .Binafsi sikuwahi kuhisi kama siku moja ningeweza kukutana nawe ana kwa ana kwa hiyo leo ni siku yangu ya furaha sana kukutana na rais ambaye nimekuwa nikitamani sana kukutana naye katika maisha yangu “ akasema mzee Benedict na sura ya David Zumo ikajenga tabasamu kubwa . Walipata chakula na kisha wakaendelea na maongezi .Wakati maongezi yakiendelea simu ya Monica
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ikaita.Akaitoa na kutazama mpigaji ,alikuwa ni Daniel. “ Excuse me” akasema na kusogea pembeni kuipokea simu ile “ Hallow Daniel” akasema Monica kwa sauti ndogo “ Monica where are you? Akauliza Daniel.Monica akagundua kitu katika sauti ya Daniel “ Niko hapa Kobe village hotel “Akajibu Monica..Ukapita ukimya wa sekunde kadhaa “ Daniel kuna nini You sound strange” akasema Monica “ Sikiliza Monica kuna taarifa ambazo si nzuri hata kidogo nimezipokea muda si mrefu” “ Taarifa gani hizo Daniel? Akauliza Monica kwa wasiwasi “ Monica I know you are strong woman and please I want you to be strong for what I’m going to tell you” akasema Daniel “ Daniel please tell me.What happened? Akauliza Monica “ Dr Macelo amepigwa risasi muda mfupi uliopita na watu wasiojulikana” “ What ?!! akauliza Monica kwa mshangao “ Dr Marcelo amepigwa risasi” akarudia Daniel “ Oh my God !! akasema Monica na kukaa kimya.Alistuka mno. “ Monica..” akaita Daniel “ Daniel tell me he’s not dead” “ Nimepigiwa simu na dada yake Julieth na amesema kwamba Marcelo amekimbizwa hospitali kuu ya St Lucia .Mimi ninaelekea huko .Tafadhali kama utapata nafasi uje huko hospitali” akasema Daniel “ Oh my God! ninakuja huko sasa hivi? Akasema Monica na kukata simu akarejea mezani akamuita mama yake “ Mama nimepokea simu sasa hivi kuwa Dr Marcelo amepigwa risasi” “ What ??Lini? bi Janet akashangaa “ Jioni hii.” Akajibu Monica “ Oh my God !!!... is he dead? “ Sifahamu hali yake ikoje ila amekimbizwa hospitali kuu ya St Lucia.Mama nahitaji kwenda huko sasa hivi ” “ Monica huwezi kuondoka katikati ya maongezi.Mheshimiwa rais ametupa heshima kubwa sana.Subiri hadi tutakapomaliza maongezi ndipo utakwenda lakini kwa sasa hapana.Wewe ndiye uliyetuunganisha sisi na David kwa hiyo huwezi kuondoka hapa na kutuacha peke yetu” akasema bi Janet “ Dr Marcelo is my friend mother so I need to get there at once !! akasema Monica “Hata kama ukiwahi kufika pale what will you do?.Utamponya? Hebu tuliza kichwa Monica .Kitu cha muhimu kwa sasa ni kumuombea ili aweze kupona kwa sababu kama amekimbizwa hospitali ni jukumu la madaktari kuokoa maisha yake.Lets us get back to the table now and keep your smile on!! akasema bi Janet wakarejea mezani Monica alijitahidi kutabasamu lakini bado sura yake ilionyesha kuna kitu kinamsumbua.Sura yake ilionyesha mstuko. “ Monica kuna tatizo lolote? Mbona unaonekana kubadilika ? akauliza David Zumo baada ya kuona mabadiliko katika sura ya Monica
samahani sana mheshimiswa rais nimepokea simu ambayo si nzuri,kuna rafiki yangu amepigwa risasi jioni hii yuko hospitali.” “Pole sana Monica,unahitaji kwenda hospitali sasa hivi? “ Kama sintakuwa nimeivuruga ratiba ya leo ,ndiyo” “ Hakuna kitakachoharibika Monica.Nenda hospitali .Kama kuna chochote ninachoweza kusaidia tafadhali usisite kunieleza” akasema David Zumo na kumuita moja wa walinzi wake akamnong’oneza kitu kisha mlinzi Yule akamuomba Monica amfuate.Monica akainuka akamuaga David na wazazi wake lakini ghafla mama yake naye akainuka. “ Nadhani itakuwa vyema nikiongozane naye “ akasema bi Janet “ Hilo ni wazo zuri pia “ akasema David.Monica na mama yake wakaondoka kuelekea hospitali. “ Mr Benedict,sasa baada ya wanawake kuondoka mezani tuongee kama wanaume.” Akasema David Zumo na kumimina mvinyo katika glasi akapiga funda kubwa na kusema “ Benedict nimekufuatilia nimegundua wewe ni mmoja wa mabilionea wakubwa wa hapa Tanzania.Biashara zako zinakwendaje? Akaulzia David Zumo “ Ni kweli mheshimiwa rais mimi ni mmoja wa wafanya biashara wakubwa.Ninamiliki biashara kadhaa kubwa hapa nchini na hata nje ya nchi.Kibiashara ninaendela vizuri japokuwa changamoto hazikosekani na hasa ushindani katika masoko umekuwa mkubwa sana bain aya viwanda vyetu vya afrika na bidhaa toka viwanda vya ulaya.” Akasema mzee Benedict “ Benedict ninafurahi kwa kuwa kuanzia sasa utakuwa mmoja wa watu wangu wa karibu kibiashara.Ninawapenda wafanya biashara kwani hata mimi pia ni mfanya biashara kwa hiyo usijali kuhusu changamoto zilizopo” akasema David Zumo na kunywa tena funda la mvinyo kisha akaendelea “ David tuweke mambo mengine yote pembeni ,kuna jambo moja la muhimu sana ambalo nataka kulijadili nawe” akasema David halafu akatoa sigara toka katika mkebe akaiwasha na kuvuta mikupuo kadhaa akapuliza moshi kisha akasema “Benedict wewe ni mtu mkubwa na ajiri lakini bado haujafikia kile kiwango cha kimataifa.Nina mawazo ya kukufanya mtu mmoja mkubwa na mwenye nguvu yaani tajiri mkubwa.Nataka kulipaisha jina lako liwe miongoni mwa matajiri wakubwa wanaojulikana dunia kwani kwa sasa unajulikana zaidi hapa Tanzania na afrika mashariki na baadhi ya nchi chache za ulaya unakouza bidhaa zako za mvinyo.Nataka ujulikane dunia nzima,na siku moja ushiriki katika vikao vya matajiri mia moja wa dunia hii.” “ Matajiri mia moja? Sijawahi kusikia kitu hicho” akasema Benedict “ Huwezi kufahamu kwa kuwa wewe bado ni mfanya biashara mdogo licha ya kuwa bilionea.Kuna kikao kinafanyika mara mbili kila mwaka kinachowakutanisha matajiri mia moja wa dunia kutoka katika kila kona ya dunia.Katika kikao hiki mambo mbali mbali huzungunzwa na nikuibie siri kwamba kikao hiki kina nguvu kubwa ya
kufanya maamuzi kuhusiana na uchumi wa dunia.Ni kikao kizito na hata wakuu wa nchi nyingi hasa zile tajiri huwa wanakuwa makini sana na maamuzi ya kikao hiki kwa hiyo nataka siku moja na wewe ushiriki kwani katika ukanda huu wa afrika mashariki kati na kusini hakuna mtu mwingine anayeingia katika kikao hicho zaidi yangu.Kwa afrika tuko watatu tu mimi na raia wengine wawili wa kutoka Nigeria.” Akasema David Zumo “ Dah ! Mwili umenisisimka sana kwa maelezo hayo.Sikuwa nikilifahamu jambo hilo na nItashukuru sana kama ukiniwezesha niweze kuwa na sifa za kuingia katika kikao hicho cha matajiri wakubwa duniani.” Akasema Benedict.David Zumo akavuta mkupuo mmoja mkubwa akatabasamu halafu akatazama juu na kupuliza moshi mwingi kisha akasema “ Kuingia katika kikao hii cha matajiri wakubwa mia moja wa dunia si kitu rahisi.Unatakiwa uwe tajiri kwelikweli na kuna kamati ya kukutathmini kama una vigezo .Ni jambo kubwa lakini endapo ukifanikiwa linakuwa na faida hata kwa nchi pia. Usiogope Benedict mimi nitakuwezesha utaingia katika kikao hicho kwani mimi ni namba nne kwa watu matajiri duniani kwa hiyo niko katika kikao kingine cha watu kumi ambacho kina nguvu kupita kikao hiki cha watu mia moja.Watu hao kumi ndio tunaoamua tuzungumze mambo gani au tufanye nini na wapi.Nitakuwezesha Benedict utashuhudia mwenyewe namna mambo yanavyoendeshwa katika hii dunia na ukiingia katika kikao hicho utaona kule ulikotoka ulikuwa kama wale vijana wanaozunguka na bidhaa zao mitaani wakizitembeza hapa Tanzania kuna jina mnawaita” “ wanaitwa Machinga” “ Sawa kabisa utajiona kama vile nawe ulikuwa Machinga” akasema David na wote wakaangua kicheko.David akawasha sigara nyingine na kupiga mkupuo mrefu akapuliza moshi mwingi na kumtazama mzee Benedict ambaye alikosa kitu cha kuongea kwa furaha kubwa aliyokuwa nayo. “Benedict,kama nilivyokueleza kwamba uwezo wa kukuingiza katika orodha ya watu mia moja matajiri duniani ninao lakini kuna jambo ambalo nitalihitaji toka kwako na ambalo nina imani liko ndani ya uwezo wako kwa hiyo kama ukikubaliana nami basi jihesabu kuwa ndani ya muda mfupi utapaa na kuingia katika orodha ya matajiri wa dunia” akasema David huku akitabasamu “ Ni jambo gani hilo mhesimiwa rais? Niambie na ninakuhakikishia kwamba nitalitekeleza kwa nguvu sana” akasema Benedict “ Vizuri sana.” Akajibu David Zumo na kuvuta mikupuo kadhaa ya sigara halafu akanywa funda moja la kinywaji kisha akasema “ Benedict ni jambo rahisi tu kwako na sina hakika kama litakuwa na ugumu wowote.Ninahitaji kumuoa mwanao Monica” Sura ya mzee Benedict Mwamsole haikuweza kuzuia kuuficha mstuko alioupata.David Zumo akamtazama na kutabasamu kisha akasema “ Monica ni mwanao na nina imani una uwezo wa kumshawishi akakubali ombi langu la kutaka kumuoa.Kutoka moyoni mwangu napenda kukuhakikishia kwamba ninampenda sana Monica kuliko mwanamke yeyote niliyewahi kumpenda chini ya jua. Ninataka awe mke wangu na nitamfanyia mambo makubwa sana ambayo hakutegemea kufanyiwa hapa duniani.Nitamfanya kuwa malkia wa kweli wa afrika .Naomba sana mzee wangu unikubalie jambo hili na umshawishi mwanao akubaliane na ombi langu.Endapo jambo hili likifanikiwa nakuahidi kwamba nitakuwezesha kwa kiasi ambacho hukukitegemea na nitakufanya mmoja wa watu wakubwa afrika na dunia.Utavuma kila kona ya dunia kwa utajiri.” Akasema David na kuvuta sigara yake.Bado Benedict alikuwa kimya
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Benedict hilo nililoliomba ni jambo kubwa kwako? Liko nje ya uwezo wako? Akauliza David baada ya kuona mzee Benedict amekuwa kimya “ Hapana mheshimiwa rais,hili si jambo kubwa kwangu na liko ndani ya uweo wangu.Ninaweza kumshawishi Monica akubaliane na ombi lako na ninataka kukuhakikishia kwamba hawezi kukataa lakini .....” “ Lakini nini? Akauliza David Zumo “ Lakini wewe tayari una mke mheshimiwa rais” akasema Benedict.David akanywa funda moja la mvinyo na kusema “ Ni kweli nina mke lakini kwa ajili ya Monica niko tayari kwa lolote.Mke niliyenaye mpaka sasa hatujabahatika kupata mtoto kwani hawezi kushika mimba.Nina mali nyingi sana na mpaka sasa sina mrithi.Ninataka nimuoe Monica ili anizalie mtoto,tutengeneze familia .Nimekwishaongea na mke wangu juu ya jambo hilo na tumekubaliana kwamba nikimpata mwanamke ambaye nitapendezwa naye basi nizae naye na kumpata mrithi wangu tatizo lilikuwa kumpata huyo mwanamke .Huu ni mwaka wa nne ninajaribu kutafuta mwanamke ambaye atanigusa moyo wangu lakini sijafanikiwa hadi nilipompata Monica ambaye ameigusa sakafu ya moyo wangu.Tafadhali Benedict naomba sana ufanikishe hilo jambo.Nataka niwe mwanaume mwenye furaha nikiwa na Monica.” Akasema David Zumo “ Mheshmiwa rais nakuomba ondoa wasi wasi kabisa jambo hili litawezekana na Monica atakubali kuolewa nawe.Nadhani hii ni mipango ya Mungu kwani kwa muda mrefu sasa tumekuwa tukijiuliza ni lini Monica atatutambulisha mchumba wake. Amekuwa akitafuta mchumba ambaye atamfaa na sasa Mungu amemjibu na amemletea mtu ambaye alikuwa anamsubiri kwa miaka mingi.Mheshimiwa rais ,naamini Monica aliumbwa kwa ajili yako.Wewe ndiye hasa mwanaume wa ndoto zake ,Yule ambaye amekuwa anakusubiri .Nina hakika hata yeye mwenyewe atafurahi sana atakaposikia taarifa hizi.” Akasema mzee benedict na kumfanya David Zumo atoe tabasamu kubwa.Wakagoganisha glasi kwa furaha. ************** Monica na mama yake waliwasili St Lucia hospital na moja kwa moja wakaelekea katika chumba cha upasuaji ambako Dr Marcelo alikuwa amekimbizwa.Nje ya chumba cha upasuaji walikuwepo watu kadhaa miongoni mwao alikuwepo Daniel. “ Daniel anaendeleaje Dr Marcelo? Akauliza Monicca “ Hali yake bado si nzuri ameingizwa katika chumba cha upasuaji kwa hiyo tusubiri taarifa za madaktari.” Monica akashindwa kujizuia machozi kumtoka “ Monica please don’t cry.We need to be strong for him” akasema Daniel “ Inaniuma sana Daniel.Jioni ya leo nimekutana naye tukaongea mambo Fulani na nikamueleza kwamba nina wasi wasi na usalama wake nikamkaribisha akaishi nyumbani kwangu lakini akakataa.Ni kama vile nilihisi jambo baya lingeweza kumtokea” Akasema Monica na machozi yakaendelea kumtoka “ Nani aliyefanya kitendo hiki? Akauliza Monica “ Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote iliyotolewa na polisi wanaendelea na uchunguzi wao juu ya tukio hili.” Akasema Daniel halafu akamshika mkono Monica
akaenda kumtambulisha kwa ndugu za Dr Marcelo waliokuwa wamekaa kwa huzuni nje ya chumba cha upasuaji.Monica na mama yake wakawafariji na kuungana nao kusubiri upasuaji umalizike.Kila aliyekuwapo pale alionekana kuwa na sura ya wasi wasi mkubwa.Kadiri muda ulivyozidi kusonga ndivyo idadi ya watu ilivyozidi kuongezeka kwani Dr Marcelo ni mmoja wa watu waliokuwa wanafahamika na kupendwa sana na watu wengi. “ Dr Marcelo ni mmoja wa marafiki zangu wakubwa na wa muda mrefu.Toka tulipokutana tumekuwa marafiki wakubwa,tumeheshimiana na hata siku moja haijawahi kutokea tukapishana kauli.Kila mmoja alimfahamu vizuri mwenzake akayafahamu madhaifu yake na hiyo ndiyo iliyotuwezesha tukawa marafiki wakubwa.Ni mara ya kwanza imetokea tukapishana kauli na ninakijutia sana kitendo kile.Kinachoniuma sana,right now Marcelo is fighting for his life and I don’t have time to say I’m sorry.Inaniuma sana.Sikutaka urafiki wetu uishe namna hii” akasema Daniel na akashindwa kujizuia machozi kumtoka “ All its because of me.Mimi ndiye niliyekuja kuuvuruga urafiki wenu na kuwapelekea mkakorofishana hadi kufikia hatua ya kutoleana maneno machafu.I’m so sorry Daniel.” Akasema Monica “ Usijilaumu Monica.Sisi sote tumefanya makosa.Tunachotakiwa kufanya hivi sasa ni kumuombea Marcelo ili aweze kupona” akasema Daniel Saa saba na dakika ishirini Dr Marcelo akatolewa katika chumba cha upasuaji na kupelekwa katika chumba cha wagonjwa walioko katika hali ya hatari.Daktari akawaita baadhi ya ndugu wa Marcelo ofisini kwake akawafahamisha kwamba upasuaji umefanyika vizuri na kwa mafanikio lakini bado mgonjwa alikuwa hajatolewa katika hali ya hatari “ Can we see him? Akauliza Julieth dada yake “ Hata mkimuona kwa sasa hawezi kuongea bado yuko katika usingizi” akasema daktari “ Daktari tunaomba turuhusiwe kuingia kumuona ndugu yetu ili tuwe na uhakika kama bado yuko hai ama vipi.” Akaomba Daniel ambaye naye alikuwemo miongoni mwa watu walioingia ofisini kwa daktari kupewa maelezo ya kuhusu hali ya Dr Marcelo.Familia ya Dr Marcelo inamfahamu sana Daniel na wanamchukulia ni kama ndugu yao kutokana na ukaribu mkubwa alionao na Dr Marcelo. Baada ya kuomba sana daktari akawaruhusu waingie watu watano katika chumba alichokuwa amelazwa Dr Marcelo lakini wakiwa wamevaa mavazi maalumu.Haraka haraka wakajichagua watu watano na miongoni mwao walikuwemo Daniel na Monica.Wakavalishwa mavazi maalum wakaingia ndani ya chumba alimolazwa Dr Marcelo.Kulikuwa na mashine mbali mbali zilizokuwa zimeunganishwa katika mwili wa Dr Marcelo aliyekuwa amelala kitandani hana fahamu. “ I’m so sorry Dr Marcelo.Sikutegemea kabisa kama siku moja ungeweza kulala hapo kitandani namna hii huna fahamu ukipigania maisha yako.Please Marcelo fight for your life because we still need and love you.You
need to come back because I want to say how sorry I am for those awfull things I said to you.I love you brother..” akawaza Daniel huku machozi yakimtoka .Kila aliyekuwamo mle chumbani alikuwa anawaza lake lakini ghafla kikatokea kitu kilichowastua wote,mashine yenye kuonyesha mwenendo wa mapigo ya moyo ikaanza kutoa mlio.Haraka hakara madakatri wakaitwa na kutoka kila kona wakaanza kukimbia kuelekea katika chumba alimolazwa Dr Marcelo na kuwataka ndugu wote watoke.Mashine ile ilionyesha kwamba moyo wa Dr Marcelo ulisimama kufanya kazi yake .Juhudi za kuustua moyo ili uendelee na kazi zikaanza lakini juhudi zote zikaonekana kushindwa kufanikiwa. “ I’m so sorry.He’s gone” Dr Mchemo akawaambia madaktari wenzake baada ya kumpima na kuhakikisha kweli amefariki.Kwa huzuni Madaktari wakaanza kutoka mle chumbani na kuwaachia wauguzi kazi ya kuundoa mwili ule wa Dr Marcelo kuupeleka katika chumba cha kuhifadhia maiti Wakiwa nje ndugu na jamaa wa Dr Marcelo walishuhudia wadaktari wakitoka ndani ya chumba kile wakiwa vichwa chini.Dr Mchemo akawataka ndugu tu wa karibu waende ofisini kwake.Kwa namna madaktari walivyotoka ndani ya kile chumba haikuhitaji tena maelezo mengi juu ya kilichotokea.Watu wengine tayari wakaanza kuangua vilio.Daniel aliyekuwa amesimama na Monica alistushwa mno na jambo lile akamshika mkono Monica na kwa haraka wakaelekea katika chumba ulimo mwili wa Dr Marcelo .Wauguzi walikuwa bado wanajiandaa ili waanze kuzifungua baadhi ya mashine zilizokuwa zimeunganishwa mwilini mwa Dr Marcelo.Monica akashindwa kujizuia kuangua kilio kikubwa ,Daniel akamkumbatia na kumsihi anyamaze.Ghafla kikatokea kitu ambacho hakuna aliyekuwa amekitarajia. Mashine yenye kuonyesha mwenendo wa mapigo ya moyo wa Dr Marcelo ambayo bado haikuwa imeondolewa ikaanza kufanya kazi kuashiria kwamba moyo wa Dr Marcelo ulianza kufanya kazi tena “ What ???!! Daniel akastuka na kuwastua wale wauguzi ambao waliacha kufanya kazi zao na kubakiwa na mshangao wasiamini macho yao.Ni kweli mashine ile ilionyesha moyo wa Dr Marcelo ulikuwa unafanya kazi tena.Haraka haraka mmoja wao akatoka mbio huku akipiga ukelele kuwaita madaktari ambao walijaa mle chumbani .Lilikuwa ni tukio la ajabu ambalo hakuna aliyewahi kulishuhudia.Kila mmoja mle chumbani ilikuwa ni mara yake ya kwanza kushuhudia kitu kama kile.Watu wote waliokuwa wakilia wakanyamaza baada ya kupata taarifa za kilichotokea. Ulikuwa ni mshangao kwa kila mtu.Ni jambo ambalo halikuzoeleka mtu ambaye tayari alikwisha thibitishwa na madaktari bingwa kuwa amefariki kuzinduka.Madaktari hawakutaka kutoka mle chumbani wakiendelea kufuatilia hali ya Dr Marcelo ili waone kama kuna chochote kitakachotokea lakini vipimo vyote vilionyesha kila kitu kilikuwa kinaendelea vizuri.
Saa tisa za usiku Monica na mama yake wakiwa wameongozana na walinzi wa David Zumo wakarejea nyumbani.Mzee Benedict tayari alikwisha rejea nyumbani kitambo na hakuwa amelala alikuwa amekaa sebuleni akiwasubiri warejee. “ Vipi hali ya huko ikoje? Mgonjwa anaendeleaje? Akauliza mzee “ Mhh !! kilichotokea huko si kitu kidogo.” Akasema bi Janet. “ Nini kimetokea He’s dead? Akauliza mzee Benedict “ Hapana hajafariki” akasema bi Janet na kuvuta pumzi ndefu.Monica alikuwa ameinama hakuweza kuongea chochote “ Hebu niambieni nini kimetokea huko? Akauliza.Monica akasimama “ Dady I’m so tired .I have to go sleep now,mother will tell you everything” akasema Monica “ Sawa Monica nenda kapumzike tutaonana asubuhi.Usiondoke bila ya kuona nami kwanza nina mambo ya muhimu sana ya kuzungumza nawe” akasema mzee Benedict naye akainuka akamshika mkono mke wake wakaongozana kuelekea chumbani kwao. “ Jane nini kimetokea huko hospitali? Akauliza Ben “ Ni mambo makubwa Ben.Kwanza mmemaliza salama na mheshimiwa rais? “ Ndiyo tumekuwa na mazungumzo mazuri sana yenye mafanikio makubwa.Nitakueleza kila kitu naomba kwanza unieleze kilichotokea hospitali” akasema Ben “ Kilichotokea hospitali leo imebaki ni gumzo.Kila mtu ameshikwa na mshangao.Nilikuwa nasoma mambo haya katika vitabu lakini leo hii nimeshuhudia kwa macho yangu.” “ Nini kimetokea Jane? “ Dr Marcelo Yule rafiki wa Monica aliyepigwa risasi alifanyiwa upasuaji na baada ya upasuaji akapelekwa katika chumba cha uangalizi maalum.Akiwa mle ,wakaruhusiwa baadhi ya watu wake wa karibu akiwamo Monica kuingia na kumuangalia japokuwa hakuwa na fahamu.Wakati wakiwa mle ndani mashine ya kuonyesha mwenendo wa mapigo ya moyo ikaonyesha kwamba moyo haukuwa ukifanya kazi,madaktari wakafanya kila jitihada kuustua moyo ili uendelee na kazi lakini zikashindikana na Marcelo akafariki dunia.Wakati madaktari wametoka na kuwaacha wauguzi washughulikie kuiondoa maiti ndipo kilipotokea kitu cha ajabu sana.Moyo wa Marcelo ghafla ukaanza kufanya kazi tena.He came back to life again.Jambo hili limemshangaza kila mtu na hakuna aliyetaka kuamini.Hadi sasa bado madaktari wanaendelea kuulizana nini kimetokea kwa sababu ni wazi Dr Marcelo alikuwa amefariki dunia kabisa.Ben haya ni maajabu makubwa sana na katika maisha yangu sijawahi kuyashuhudia ni mara ya kwanza leo kushuhudia mtu aliyefariki akirejewa na uhai.” Akasema Bi Janet “ Dah ! kweli huu ni muujiza mkubwa.Mambo haya huwa yanatokea mara chache sana duniani.” Akasema mzee Ben “ Kweli ni muujiza.Hakuna aliyekuwa ametegemea.Wote tulijua Marcelo tayari amekufa and its over lakini baada ya muda moyo wake ukaanza kufanya kazi tena kweli ni muujiza.Madaktari hawatalala leo wakijaribu kuchunguza nini kimetokea” akasema Bi Janet
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa hiyo hali yake ikoje kwa ujumla? Akauliza Ben “ Mpaka sisi tunaondoka hali yake ilikuwa inaendelea vizuri.Mashine zote zilionyesha maendeleo yake ni mazuri” “ Monica ameumizwa sana na jambo hili.” Akasema Ben “ Ni kweli Ben.Jambo hili la kupigwa risasi kwa rafiki yake Marcelo limemuumiza sana.Kuna kitu nimekigundua leo.Inaoneana wazi kabisa Monica anampenda sana huyo Marcelo na kama hisia zangu zilivyokuwa sahihi siku ile nilipowakuta kule bwawani usiku wakiongea nilijua kabisa lazima kulikuwa na kitu kinachoendelea.Tatizo ni kwamba jambo hilo halitawezekana kwani Marcelo ni mgonjwa na sina hakika kama Monica analifahamu hilo.Kuna ulazima wa kumueleza mapema kuhusu jambo hili kabla hawajaenda mbali zaidi.” Akasema bi Janet “ Tuachane na hayo ya hospitali.Nini kiliendelea tulipoondoka? Akauliza Janet “ Mlipoondoka kumekuwa na mazungumzo mazito lakini yenye manufaa makubwa kwetu.” “ Haya nishirikishe na mimi kilichojiri” akasema Janet “ Kuna mambo kama mawili makubwa tuliyoongea.Kwanza David Zumo alinieleza kwamba amenifuatilia na kugundua kuwa mimi ni mfanyabiashara bilionea hapa nchini lakini akasema kwamba anataka kunifanya niwe mfanyabiashara mkubwa zaidi nijulikane afrika na duniani kwa ujumla.Kuna kikao ambacho hukutanisha mabilionea mia moja wa dunia anataka siku moja na mimi niwepo katika kikao hicho” akasema Ben “ Wow ! hizo ni habari njema.Mtu huyu ni mwema sana.Ana moyo wa kusaidia na ndiyo maana hata Mungu anambariki” akasema bi Janet kwa furaha “ Ni kweli Jane.Huyu mtu ana moyo wa kusaidia na toka moyoni ameahidi kunipaisha kimataifa.Lakini kuna jambo moja analihitaji toka kwangu,toka kwetu” Ben akanyamaza kidogo na kusema “ David Zumo anampenda Monica.Anataka kumuoa” akanyamaza baada ya mke wake aliyekuwa amekaa kitandani kuinuka na kumtazama kwa macho makali sana. “ Tell me it’s a joke Benedict” akasema bi Janet “ Hapana si utani Janet.Ametamka David Zumo kwa mdomo wake kuwa anampenda na anataka kumuoa Monica.” Akasema Ben .Mke wake akasimama akamtazama benedict “ oh my God why it have to be her?? Akauliza Janet.Ben akatabasamu na kusema “ Mwanetu ana bahati ya kipeke sana.Kila siku milango yake ya mafanikio inazidi kufunguliwa.Yote hii ni kwa sababu ya upendo wake mkubwa kwa watu.Juzi tu ametangazwa kuwa mrembo kuliko wote afrika na leo hii tajiri namba moja afrika anajitokeza na kutaka kumuoa.Huoni hizo ni Baraka ? Hii ni bahati ya kipekee sana .” Akasema mzee Ben.Mkewe akaendelea kumtazama kwa hasira “ Umemjibu nini? Akauliza Janet “ Ningemjibu nini zaidi ya jibu moja tu la ndiyo” akasema Ben “ Benedict are you crazy? Akauliza bi Janet
Kwani vipi Janet.Jambo hili lina ubaya gani? Mtu kama David ndiye ambaye Monica amekuwa akimuhitaji.Tumesubiri kwa muda mrefu Monica ampate mwanaume mzuri wa kumfaa na Mungu amejibu maombi yake amemletea mwanaume wa maisha yake,ambaye anampenda kwa moyo wake wote.Wanasema mvumilivu hula mbivu,Monica amevumilia kwa muda mrefu na sasa ni wakati wake wa kuzila mbivu kwani anakwenda kuwa malkia halisi wa afrika .Anakuwa mke wa tajiri namba moja wa af..” “ Oh my God !! Benedict are you crazy??!!!! Akauliza bi Janet kwa hasira “ Janet kuna tatizo gani katika hilo? That what we’ve been dreaming for her,right?.Monica kumpata mwanaume atakayempenda ilikuwa ni ndoto yako kubwa na sasa kuna tatizo gani wakati ndoto hiyo imetimia tayari? Amejitokeza mwanaume mwenye sifa unazozitaka.David bado kijana ,ni raisi wa nchi,ni tajiri namba moja afrika kwa ujumla ni mtu mwenye sifa zote za kumuoa Monica.Zaidi ya yote anakwenda kutusaidia sana kiuchumi.Anakwenda kutupaisha imataifa zaidi na sisi tutaingia katika orodha ya matajiri wa dunia kwani uwezo huo anao.” Akasema Benedict Mke wake akamtazama kwa hasira huku akihema mfululizo na kusema “ Toka moyoni mwako unakubali kweli Monica aolewe na David Zumo? Akauliza.Bila kupepesa macho mzee Ben akajibu “ Kwa moyo mweupe kabisa ndiyo,nataka Monica aolewe na David Zumo.Sina kipingamizi chochote katika jambo hilo kwani naamini Yule ndiye hasa mwanaume anayemfaa...” Bi Janet akamtazama mumewe na kutikisa kichwa “ Sikutegemea kama siku moja unaweza ukawa na akili za kijinga namna hiyo.How could you be so stupid Benedict? Kauli ile ikampandisha hasira mzee Benedict akainuka kwa hasira “ Am I stupid?? Akauliza kwa hasira “ yes you are stupid.Unamuangamiza mwanao huku ukiona.Huoni kuwa huo ni ujinga uliopitiliza?” “ Mjinga ni wewe hapa ambaye hutaki kuona mwanao akiwa na furaha.Kila mwanaume ambaye mwanao anampata wewe unamkataa.Unataka aolewe na nani na shetani? Sasa mimi natoa kauli yangu ya mwisho kuwa Monica ataolewa na Daviz Zumo.Hiyo ni kauli yangu ya mwisho na hakuna wa kuipinga.Kesho asubuhi nitaongea na Monica na kumfahamisha kuhusu jambo hili na ninaamini hata yeye mwenyewe atakubali” “ Why are you doing this Benedict? “ Hii ni kwa faida ya Monica.Nataka Monica aishi maisha mazuri na yenye furaha.Hii si nafasi ya kuiacha..” akasema Benedict “ Unafanya kwa ajili ya Monica au kwa ajili yako mwenyewe? “ Both..Kwa ajili ya Monica na kwetu pia” “ Please let me out of this.Katu siwezi kushiriki katika mambo ya kipumbavu kama hayo.” Akasema bi Janet kwa hasira “ Tafadhali Jane naomba usinidharau .Mimi nimekwisha amua na hakuna wa kupingana na mimi.Mimi ndiye mwenye
kauli ya mwisho humu ndani.” Akasema mzee Benedict kwa hasira akionekana kukasirishwa sana na kauli ile ya mke wake.Bi Janet naye akapandwa na hasira akasema “ Benedict umenilazimisha nifanye kile ambacho sikuwa nimekikusudia kukifanya kwa hiyo naomba unisikilize kwa makini sana” Akasema bi Janet na kuvuta pumzi ndefu “ Kwanza kabisa napenda nikukanushe kuwa wewe si mwenye kauli ya mwisho humu ndani bali mimi ndiye mwamuzi wa mwisho wa jambo lolote humu ndani.Kwa muda mrefu nimekuachia ufanye maamuzi kwa sababu ya kukuheshimu lakini humu ndani mwenye madaraka ya kusema kitu kiwe ni mimi.I’m the head of this house and not you.You are just a man but you are nothing. “ akanyamaza na kumtazama mzee Benedict aliyekunja sura yake kwa hasira “ Nani aliyekwambia kwamba wewe ndiye mkubwa wa nyumba hii? Akauliza Benedict kwa hasira “ Benedict ninapoongea nataka utulie nani kakupa ruhusa ya kuzungumza wakati sijamaliza? Ngoja nimalize kuzungumza na wewe ndipo utazungumza.Umenilazimisha mwenyewe nifanye hivi kwa hiyo usinione mbaya.” Akasema Janet na kumtazama Benedict kwa hasira “ Kwa kuwa nilikwisha kueleza awali kuwa mimi ndiye mwenye kauli ya mwisho humu na ndiye kiongozi basi kauli yangu ya mwisho ni kwamba Monica haolewi na David Zumo.Thats final.Ni afadhali akaolewa na Yule mtu aliyekufa akarudi kuliko kuolewa na David..” akasema Janet “ Janet you must be insane..!!! Yaani Monica aolewe na Yule mfu? That will never happen.Ninasema hivi Monica ataolewa na David Zumo na hakuna wa kulipinga hilo si wewe wala nani.Najua unasema kwamba wewe ndiye mwenye kauli ya mwsho kutokana na sehemu kubwa ya mali tulizonazo kuwa zimetokana nawe lakini hiyo hainifanyi nishindwe kusimama kama mwanaume katika masuala makubwa ya watoto wangu.Sina shida na mali zako kwani muda si mrefu nitakuwa na mali nyingi kushinda hizi dunia yote watanifahamu lakini linapokuja suala la watoto huna kauli yoyote na ninaomba usijaribu kufanya chochote kulifaya suala hili lishindikane.I swear Janet nitafanya kitu ambacho hukuwa umekitazamia..!!! akasema mzee Benedict kwa hasira “ Benedict utanifanya nini? Utanua? Chunga maneno unayoyangea Ben wakati unafahamu kabisa unaongea na nani.Nakushangaa umetowa wapi kiburi cha kuongea nami namna hiyo wakati unanifahamu fika kwamba mimi ni mtu wa namna gani.Nakuonya Ben achana kabisa na suala hili.Sitaki kabisa uingilie masuala ya watoto wangu ” “ They are my children !! Huwezi kunipangia chochote juu ya watoto wangu .Nimesema Monica ataolewa na David Zumo and that’s final.Ninakuomba usiongee chochote tena nisije nikakufanya kitu kibaya usiku huu nikabaki najuta” Bi Janet akamtazama kwa hasira na huku midomo ikimtetemeka akasema “ Nilikwambia kwamba unanilazimisha nifanye kila ambacho sikuwa nimekusudia kukifanya.Unanivuta mikono kufanya jambo gumu sana kwangu lakini sina namna nyingine ya kufanya zaidi ya kukueleza ukweli ili tulimalize suala hili ambalo ni wewe mwenyewe umelianzisha.I’m not ready to see you send my daughter to the hell so I’m going to fight with all my strength I have.Kwa kuanzia nataka nikuweke wazi kuhusu jambo moja.Monica is not your daughter”
Mzee Benedict akamtazama mkewe kwa hasira halafu akajikuta akitabasamu na kuachia kicheko “ Sijawahi kuona mwanamke mjinga kama wewe katika hii dunia.Huyu mtoto ulimzaa vipi bila mimi? Akauliza na kuachia kicheko kidogo “ Narudia tena Monica si mwanao.Lifahamu hilo na utambue kuwa huna mamlaka ya kuamua chochote juu yake.” Akasema Janet. “ Unasema nini Jane? Monica si mwanangu ? akauliza mzee Benedict “ Nadhani umenisikia vizuri nimerudia mara mbili kukueleza kuwa Monica si mwanao.” Akasema Jane. “ Kama si mwanangu ni nani? Mjomba wangu? Akauliza mzee Benedict “ Nisikilize vizuri na unielewe,Monica si mwanao.Si damu yako.Monica ana baba yake.Wewe ni mlezi wake tu.” “ That’s not true.!! That,s a lie..!!! akasema mzee Benedict kwa hasira. “ Its not a lie my dear Benedict.Its the truth.Monica is not your daughter.I’m sorry I lied to you about this” akasema Janet “ Hapana si kweli.Hii ni janja yako ya kutaka jambo hili lisifanikiwe.” Akasema Benedict “ Benedict uko tayari kufanya kipimo cha DNA kuthibitisha hiki ninachokisema? Akauliza Janet.Mzee Benedict akabaki kimya amesimama akimtazama mke wake “ Nijibu Banedict uko tayari tukapime ili uthibitishe Monica si mwanao? Akauliza bi Janet .Uso wa mzee Benedict ukaloa jasho akakaa kitandani akaweka mikono kichwani. “ Anachokisema huyu mwanamke kinaweza kuwa kweli au ni sehemu ya ulaghai wake ili kuufanya mpango wangu na David Zumo ushindwe kufanikiwa?Why she’s doing this? Akawaza mzee Benedict huku jasho likimtiririka. “ Siwezi kukubali huyu mwanamke akanishinda na kuyakosa yale yote niliyokubaliana na David Zumo” akawaza Benedict na kuvuta droo yake iliyoko kitandani akatoa bastora na kumfuata mkewe aliyekuwa amekaa upande wa pili wa kitanda machozi yakimtoka.mzee Benedict akamuwekea bastora kichwani “ tell me the truth Janet,or I’ll kill you !!.. akasema mzee Benedict “ Ben that’s the truth” akasema Janet.Mzee Ben akamtazama kwa hasira na huku mkono wake uliokuwa na bastora ukimtetemeka kwa hasira “ Kama unadai mimi si baba yake nani basi ni baba yake? Akauliza mzee Benedict. “ Put the gun down Benedict you are not going to shoot me.” Akasema Janet na kuushika mkono wa mzee Benedict uliokuwa na bastora taratibu akaushusha chini. “Sit !! akasema Janet kwa sauti kali na mzee Benedict akaketi kitandani pembeni yake. “ I’m sorry Ben..Real sorry.This is the sercret I’ve kept for years but I cant keep it any longer.Ni wakati sasa wa kuufahamu ukweli wote.” Akasema Janet “ Just tell me who is the father of Monica ” akasema mzee Benedict Janet akafikiri kidogo na kusema “ Ernest Mkasa” akasema Janet na kumfanya mzee Benedict amrukie kama Simba na kumkaba koo. “ How could you do something like that Janet??!! Akauliza Benedict kwa hasira .Janet akajitutumua kwa nguvu na kumsukuma Ben akaanguka chini. “ Huyu mjinga alitaka kuniua.”akawaza Janet huku akikohoa mfululizo. Mzee Benedict akaegemea kitanda akilia machozi.Janet akageuka akamtazama na kumsogelea akamshika bega.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ Benedict I’m very sorry” akasema bi Janet “ Janet tumekuwa pamoja kwa miaka mingi hadi sasa tumekuwa wazee.Tumepitia mambo mengi sana makubwa,mazuri na mabaya,mimi na wewe tuna historia kubwa lakini katika safari yetu hii ya maisha hadi hapa tulipofika hakuna siku ambayo nimewahi kuumia na kujuta kukutana nawe kama siku hii ya leo.Naomba nikuweke wazi kuwa umeuchana chana moyo wangu .Ni kweli wewe ndiye chanzo cha hizi maIi zote ingawa tunaolifahamu hilo ni mimi na wewe tu lakini kwa hili ulilolifanya naapa sintakusamehe kamwe.I’ll never forgive you Janet.Ulidai kwamba Ernest ni rafiki yako na anatusaidia kuondokana na umasikini lakini kumbe unatembea naye !!” Akasema mzee Benedict huku mwili ukimtetemeka kwa hasira. “ Hata usiponisamehe Ben I don’t care.Nilifanya nililopaswa kulifanya kwa ajili ya kutusaidia kuondoka katika maisha yake magumu tuliyokuwa nayo.Bila kufanya vile katu tusingekuwa na maisha haya.” Akasema bi Janet kwa sauti kali. “ Sasa nimegundua kwamba kwa miaka hii yote ambayo tumeishi wote tumeishi katika ulaghai mkubwa.Hukuwahi kunipenda hata kidogo.” Akasema Benedict “ Kama nisingekuwa nakupenda Ben nisingekuwa nawe hadi muda huu” akasema Janet “ Lier !!Huna hata chembe ya upendo ndani mwako .Mwanamke una roho ya kishetani.Sikujua kama una roho mbaya namna hii.Kwa nini usingenieleza jambo hili toka mapema nijue? “ Samahani kwa hilo Ben.Nakiri nilifanya kosa kutokukueleza.Niliogopa kukueleza kwa sababu niliogopa ungeumia sana kwani nafahamu namna unavyonipenda.Nimeishi na siri hii moyoni kwa muda mrefu na nimekuwa nikijaribu kutafuta ujasiri wa kukueleza lakini nimeshindwa. Hili ni jambo la aibu na ndiyo maana sikutaka lijulikane.Nisamehe Ben .Nisamehe sana.Najua nimekuumiza mno.Hata mimi ninaumia vile vile kwani sijui uso wangu nitauweka wapi pindi Monica akilifahamu jambo hili.Tafadhali naomba tusilifanye jambo hili kuwa gumu Ben.Tushauriane nini cha kufanya.” Akasema Janet kwa sauti ya chini. Mzee Benedict aliendelea kuinamisha kichwa alikuwa na mawazo mengi.Akainua kichwa na kuuliza “ Ernest anafahamu kuwa Monica ni mwanae? Akauliza mzee Ben “ Hapana hafahamu kama Monica ni mwanae” akasema Janet “ Kwa nini hukumueleza ukweli? Akauliza Ben na Janet akashindwa kujibu kitu akabaki kimya “ Answer me Jane kwa nini hukumueleza ukweli Ernest kuhusiana na Monica? “ Because I don’t love him.Ninamfahamu Ernest si mtu mzuri na ndiyo maana sikutaka afahamu Monica ni mwanae kwani kama angefahamu basi angeweza kumchukua kitu ambacho sikuwa tayari.Sikutaka Monica akaishi na Ernest” akasema Janet na kuinamisha kichwa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ How could you ..!.” akasema Ben lakini akajikuta akishindwa kumalizia alichotaka kukisema akainamisha kichwa .Baada ya muda akauliza “Niambie nani ni
baba wa Nathan? Akauliza mzee Ben “ Ni wewe” akajibu Jane “ Are you sure? “ Yes..!! “ Niambie Jane nani ni baba wa Nathan kwa sababu sikuamini tena kwa
lolote lile.” “ Nathani ni mtoto wako,uamini usiamini lakini huo ndio ukweli.Nathani ni mwanao na hilo halina ubishi.” “ Vyovyote utakavyosema Jane kaa ujue
kuwa sintokuamini tena ,una roho ya kishetani” “ Usianze kunitusi Ben..” akasema Janet “ Sikutusi Jane huo ni ukweli.You are a devil !! “ Don’t call me a devil
Ben ..Kama mimi ni shetani na wewe utakuwa nani? Usijifanye malaika hapa Ben.We’re both devils.Tumefanya mambo mengi mabaya kwa hiyo huu si muda wa
kuanza kushutumiana nani shetani nani malaika.Jambo limetokea na tunachopaswa kukifanya kwa sasa ni kujadili tunatokaje katika dimbwi hili la matope kwani
sote tumepakaa matope na tunatakiwa tuyafute matope haya kabla watu hawajauona uchafu huu tulioufanya ” Akasema Jane “ Usiseme tumepakaa matope wewe
ndiye uliyepakaa matope na si mimi.Kama ni aibu basi itakuwa juu yako na si mimi.” Akasema Ben “ Ben usidhani sifahamu uchafu wako.Watoto wangapi
umezaa na wanawake wako huko nje unadhani siwajui? Ninakufahamu vizuri sana Ben na ninafahamu kila unachokifanya .Ninafahamu makahaba wako wote
unaotembea nao na ndiyo maana nikasema kwamba tunatakiwa tujisafishe matope haya tuliyopakaa kabla siri zetu hazijaanza kutoka nje ya nyumba hii.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akasema Janet.UKapita ukimya wa dakika tano mzee Ben akasema “ Ukitaka kujisafisha matope hayo unayoyasema anza kwa kumueleza ukweli
Monica.”akasema mzee Ben na Janet akabaki kimya. “ Ni jambo gumu sana lakini lazima ulifanye.Lazima Monica ajue ukweli wote” “ Ben I cant do that.She’s
going to hate me forever” “ Kwa hiki ulichokifanya unastahili kuchukiwa.Ni jambo baya mno umelifanya Jane.Anastahili akuchukie sana kwa sababu
utamsababishia maumivu makubwa.Utazivuruga ndoto zake nyingi alizonazo” akasema Mzee Ben. “ Ben I don’t want to hurt my daughter.Please let’s keep this
secret between us. Hakuna yeyote anayefahamu kuwa Monica si mwanao zaidi yangu.Lets us take this secret to our graves.Monica ataendelea kuwa mwanao na
familia yetu itaendelea kuwa moja na yenye amani.Tukimueleza ukweli atatuchukia mno na ataumia sana jambo ambalo sitaki litokee kwani ninampenda sana
Monica.Wewe utabaki kuwa baba yake kwani umemlea kwa upendo mkubwa toka akiwa mdogo hadi leo hii.Nakuomba Ben tusikubali jambo hili likaivuruga
familia yetu.Tumetoka mbali sana na huu
ni wakati wa kufurahia matunda ya kazi ngumu tuliyokwisha ifanya huko nyuma na si kuibua mifarakano.Sote tumefanya makosa mengi .Wewe pia Ben una
watoto wa nje ambao ninawafahamu lakini sijawahi kukuuliza chochote kuhusu jambo hilo kwa hiyo hakuna msafi kati yetu.” Akasema Janet.Mzee Ben
akainamisha kichwa akafikiri kwa muda kisha akasema “ Kama unataka iwe hivyo lazima tukubaliane jambo moja” akasema Ben “ Jambo gani Ben? “ Monica
aolewe na David Zumo” “ What ???.. Janet akastuka “ Umenisikia vizuri Jane,kama unataka jambo hili liendele kuwa siri na mwanao asilifahamu basi ridhia
Monica aolewe na David Zumo na kila kitu kitakuwa kimekwisha.” “ Hilo haliwezekani Ben.Ninasema hilo sikubaliani nalo” “ kama hukubaliani nalo basi
lazima Monica aufahamu ukweli wote and she’ll hate you forever.Do you want her to hate you??Si yeye peke yake atakayekuchukia bali Nathan pia .Wote
watakuacha peke yako.Unataka hilo litokee? Akauliza mzee Ben.Janet akabaki kimya “ Ukimya huo unaonyesha kwamba hauko tayari kwa hiyo basi
tunakubaliana kuwa Monica aolewe na David Zumo” akasema mzee Ben.Janet akafikiri kwa muda kisha akasema “ Ben please don’t do that.We are sending our
daughter to hell !!..Utajiri wa David Zumo hauna uhalali.Ameuchuma utajiri wake kutoka kwa raia masikini wa Kongo,amekuwa akifuja rasilimali za nchi yake
kwa hiyo utajiri wake una laana.Kukubali Monica aolewe na David ni kumuingiza mwananetu katika laana hiyo.Tafadhali Ben tusifanye hivyo.” Akasema Janet
huku akitoa machozi “ Janet huo ndio msimamo wangu ambao siwezi kuubadili.Monica lazima aolewe na David Zumo.Kuna faida nyingi sana kwa jambo hilo
kwa hiyo kama ukitaka tuendelee kuishi kwa amani na furaha Monica lazima akubali kuolewa na David Zumo.” Akasema Ben na kuinuka akatoka mle chumbani
akaelekea sebuleni katika ukuta kulikuwa na picha kubwa waliyopiga wote kama familia.Akaitazama na kulengwa na machozi
“ Sikujua kama siku moja Jane angekuja kuniumiza kiasi hiki. Ninafahamu ni mwanamke mwenye roho ya ukatili lakini sikutegemea kama angefikia kufanya
jambo hili.Nilimpenda sana Jane toka tukiwa bado vijana wadogo na nilikuwa tayari kufanya jambo lolote kwa ajili ya kuwa naye.Nilikubali kufanya mambo
mengi tu ya hatari kwa lengo moja tu la kuishi naye maisha mazuri lakini leo ameniumiza sana na sijui Monica ataumia vipi akilifahamu jambo hili.” Akawaza
na kwenda kuketi sofani “ Ernest Mkasa.!! Akasema kwa sauti ndogo na kukunja sura “ Kumbe Jane alikuwa na mahusiano ya siri na Ernest.Dah !! ama kweli
hakuna rafiki wa kweli katika hii dunia.Ernest ni rafiki yetu mkubwa na ambaye alijitolea sana kutusaidia kwa hali na mali hadi tukafika hapa tulipofika lakini
kumbe alikuwa na lengo lake nyuma ya pazia.Simuamini tena Jane na nina hakika hadi sasa bado yeye na Ernest wanaendeleza mahusiano yao.What am I going to
do ?? akajiuliza mzee Ben .Alihisi kichwa kimekuwa kizito sana akajilaza sofani “ Ernest Mkasa wa sasa si Yule wa kipindi kile tuliyekuwa tukimfahamu.Kwa
sasa ni mtu mkubwa ,and he’s very powerfull.Ni rais wa Tanzania.Ni mtu ambaye nilimuamini sana na sikutegemea kama angeweza kunifanyia usaliti mkubwa
kama huu.Japokuwa kwa sasa ana nguvu kubwa lakini siwezi kumuacha hivi hivi lazima nitafute namna ya kupambana naye.I must fight him.” Akawaza mzee
Benedict “ Nimepitia mambo mengi sana magmu na ya kusikitisha lakini sijawahi kuumia kama nilivyoumizwa na jambo hili la kuambiwa Monica si
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
mwanangu.Ninawapenda Monica na Nathan kuliko kitu chochote katika hii dunia na kwa sababu hiyo nitapambana kwa ajili yao.Monica ataendelea kuwa
mwanangu hadi siku ninaondoka katika dunia hii na hakuna wa kulibadili hilo.Hata hivyo I must do something ..” akawaza na kuinuka akaenda tena kuitazama
ile picha waliyopiga wote kama familia wakiwa na nyuso zenye tabasamu “ I must destroy Ernest Mkasa.” Akawaza na kufungua mlango akatoka na kukaa
kibarazani akitazama angani “ Ernest is my best friend,amenisaidia sana hadi kufika hapa nilipofika lakini kwa hili alilolifanya katu siwezi kuvumilia,I must
destroy him.” Akawaza huku sura yake ikionyesha wazi kuwa alikuwa amedhamiria kukifanya kile alichokuwa anakiwaza “ Yes I must destroy him...Siwezi
kuvumilia kufanyiwa kitendo kama hiki.Ernest Mkasa must be destroyed.” Akawaza na kupiga ngumi ukutani kwa hasira halafu akaelekea sebuleni na kukaa
sofani kichwa chake kikiwa kizito kwa mawazo. Janet Mwamsole alikaa kitandani na alishindwa kuyazuia machozi yasimtoke. “ My family is falling apart..!!
akasema kwa sauti ndogo na kuchukua kitambaa akafuta machozi. “ I took years to build this family lakini kwa kosa moja nililolifanya miaka zaidi ya ishirini
iliyopita kazi yote kubwa niliyoifanya kwa miaka mingi imekuwa bure.Familia yangu inakwenda kugawanyika.Monica akigundua kwamba Ben si baba yake
mzazi hakutakuwa na familia tena.Atanichukia sana na hatataka kuniona tena.Si yeye peke yake bali familia nzima watanichukia.Nitabaki peke yangu.Hapana
sitaki hilo litokee.Familia hii niliyonayo ni kila kitu kwangu kuliko hata hizi mali nilizonazo kwa hiyo nitafanya kila niwezalo kuhakikisha familia hii
haigawanyiki.Ngoja nikubaliane
na hiki anachokitaka Ben yaani Monica aolewe na David Zumo.Japokuwa moyo wangu hautaki jambo hili lakini hakuna namna lazima nikubali ili mimi na Ben
tuweze kwenda sawa.” Akawaza na kufuta tena machozi “ Sikutaka mtu yeyote aifahamu siri hii lakini sijui kitu gani leo kimenifanya niitoe.Ni siri ambayo
niliapa kwenda nayo kaburini lakini kwa kuamua kuiweka wazi kwa Ben nimevuruga kila kitu.Ben will never trust me again.Ninampenda Ben sana na hata yeye
ananipenda sana na sikufanya jambo hili kwa makusudi bali ilinilazimu kufanya mapenzi na Ernest Mkasa.Sikuwa na namna nyingine ya kufanya zaidi ya kufanya
vile .” akawaza Jane na kuanza kukumbuka historia ya nyuma alikotoka na Benedict DAR ES SALAAM “ Janet tafadhali naomba ufanye kila linalowezekana
uweze kunitoa humu ndani.Wewe ndiye pekee ninayekutegemea ukishindwa wewe basi maisha yangu yote yatamalizikia gerezani.” Akasema kijana mmoja
aliyekuwa amesawajika.Mwanamke aliyekuwa akionge anaye mwenye uzuri wa kipekee akafuta machozi na kusema “ Ben nimejitahidi sana kufanya kila
linalowezekana lakini mpaka sasa sijafanikiwa .Kesi hii mawakili wengi wanaiogopa kwani kijana uliyemgonga na kufa ni mjukuu wa mmoja wa waziri mstaafu
ambaye ana heshima kubwa hapa nchini.Kila mwanasheria ambaye ninamtafuta atusimamie katika kesi hii anakuwa na mashaka kama anaweza akashinda.” “
Janet you have to do something.Mimi sikuwa na makosa bali wao ndio walionigonga na gari lao na inaonekana walikuwa wamelewa.Kwa nini hawataki
kulizingatia hili na wanataka waniangamize wakati sina hatia? Tafadhali Jane ninakutegemea sana.Wewe ndiye unayeweza kuniokoa katika hili.Tafadhali naomba
unisaidie Jane.Nikiendelea kukaa humu ndani mipango yetu yote itashindwa kufanikiwa.Dont you believe me Jane?” Akauliza Ben.Janet akafuta machozi na
kusema “ I believe you Ben.Nitakwenda kutafuta namna nyingine ya kufanya.Usivunjike moyo mpenzi wangu.Mungu atatusaidia na tutashinda hii kesi.”
Akasema Janet na kuagana na mpenzi wake akatoka mle gerezani huku machozi yakimtoka.Hakutaka kupoteza muda akaingia katika teksi iliyompeleka pale
gerezani akamuamuru dereva aondoke. “ Huu ni mkosi gani unanikuta mimi? Kwa nini maisha yangu yamebadilika na kuwa magumu namna hii? Sikuwahi hata
mara moja kuhisi kuwa maisha yangu siku moja yatakuwa namna hii .Wazazi wangu ni matajiri lakini hawako tayari kunisaidia kwa namna nilivyowakorofisha.
Akawaza Janet na kufuta machozi “ Laiti kama nisingejiigiza katika mahusiano na Ben na kupata mimba yote haya yasingetokea.Hivi sasa ningekuwa mbali sana
na ningekuwa na maisha mazuri lakini nilishawishika na kuingi akatika mahusiano na Ben na sasa haya ndiyo yanayonikuta.Hakuna wa
kumlaumu kwa maisha haya kwani nimeyataka mwenyewe ninachopaswa ni kusimama na kupambana kumtoa Ben gerezani kwani nikishindwa kufanya hivyo
atafungwa.Kesi hii inamuendea vibaya sana.Si yeye aliyesababisha ajali ile lakini kwa kuwa mtu aliyefariki katika ajali hiyo ni mjukuu wa mwanasiasa basi kesi
yote inamuangukia yeye.I must save him” akawaza Janet kisha akamuelekeza dereva ampeleke Papaya supermarket. “ Baba anaweza kabisa kunisaidia katika
jambo hili.Natamani nikampigie magoti nimuombe msamaha ili anisaidie lakini hatakuwa tayari.Msaada anaonisaidia wa kumlea mwanangu Nathani unatosha
.Lazima nipambane mwenyewe.Namshukuru mama ambaye amekuwa akinipa msaada mkubwa sana kama si yeye sijui ningeishi vipi hapa mjini.” Akawaza Janet
. Dereva taksi akamfikisha Janet, Papaya supermarket akashuka na kuanza kupiga hatua kuelekea ndani kununua mahitaji aliyoyataka lakini mara akastuka baada
ya kumuona mtu Fulani akiwa amekaa nje ya gari la kifahari akiongea na mwenzake “ Ernest !! akasema kwa mshangao na kisha akaanza kupiga hatua
kumuendea.Yule kijana naye alipomuona Janet akastuka sana “ Janet !! akasema na kisha wote wakakumbatiana. “ Jane is that you?? Akauliza Ernest “ Ni mimi
Ernest.” Akajibu Jane.Ernest akamuomba samahani Yule mtu aliyekuwa anaongea naye wakakubaliana kukutana siku nyingine “ Jane sikutegema kabisa kuuoana
nawe.I’ve been searching for you everywhere lakini sijafanikiwa kukuona” akasema Ernest “ Mbona nipo Ernest nimejaa tele hapa mjini.Ninapambana tu na
maisha.Vipi wewe maisha yako yanakwendaje? Akauliza Jane “ Mambo yangu siwezi kusema ni mabaya.Ni kama unavyoniona” akasema Ernest huku
akitabasamu “ Vipi wewe mambo yako yanakwendaje? Akauliza Ernest lakini Janet akasita kidogo “ Jane una haraka sana? Kama huna haraka sana tunaweza
kupata nafasi tukakaa mahali tukaongea? “ Bila tatizo” akasema Jane na kwenda kumlipa dereva taksi pesa yake kisha akaongozana na Ernest hadi katika gari
lake la kifahari wakaondoka “ Jane nilihitaji sana kukuona lakini kila ninayemuuliza hana habari zako na hakuna anayejua unapoishi” akasema Ernest wakiwa
garini.Jane akatabasamu na kusema “ Maisha yangu sitaki yajulikane ndiyo maana sitaki kumuelekeza rafiki yangu yeyote mahali ninakoishi.” Akasema Jane
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hawakuwa na maongezi mengi garini kwani muda mwingi Ernest alikuwa akiongea na simu.Waliwasili La 403 Casino wakashuka garini na kuingia ndani ya
kasino lile ambalo Ernest alionekana kujulikana sana kwani alisalimiana na watu mbalimbali aliowakuta mle ndani .Ernest akamuongoza Jane hadi katika
chumba kimoja kizuri kikubwa “ Jane karibu sana La 403 Casino.Hii ni moja ya biashara ninazozimiliki kwa sasa” akasema Ernest na kumfanya Jane astuke . “
That’s not true” akasema Jane “ Its true Jane.Kitu gani kinachokufanya usiamini? Akauliza Ernest huku akicheka “ Ernest nimestuka tu sikutegemea kabisa kama
ungeweza kumiliki kitu kikubwa kama hiki” akasema Janet “ Si hii moja tu bali ninazo biashara nyingine nyingi tu sehemu mbalimbali .You are talking to a
man.” Akasema Ernest kwa majigambo “ Hongera sana Ernest.Umejitahidi sana .Nakumbuka hata tukiwa shule ndoto yako siku zote ilikuwa ni kuwa mtu
mkubwa.Sasa nimeyaamini maneno yako” akasema Janet.Ernest akafungua friji akatoa kinywaji na kumkaribisha Janet.Halafu akasema “ Haya Janet nieleze
maisha yako yakoje? Akasema Ernest na uso wa Janet ukachanua kwa tabasamu pana. “ Ouh Jane uzuri wao bado ule ule na sasa umezidi maradufu.Lile
tabasamu lako ambalo lilikuwa linanipa uchizi bado lipo.You are so beautifull Jane” akasema Ernest “ Ernest bado hujaacha yale maneno yako tu” akasema Anna
na kunywa funda dogo la kinywaji “ Niambie Jane.Maisha yako yanakwendaje? Tell me everything about your life” akasema Ernest.Janet akavuta pumzi ndefu na
kusema “ Ernest sijui nianzie wapi kukueleza kuhusu maisha yangu.Lakini kwa ujumla naweza kusema kwamba maisha yangu si mazuri sana.Si maisha yale
ambayo nilikuwa ninaota kuyaishi.Naweza kusema kwamba ndoto zangu sijaweza kuzitimiza.” Akasema Jane.Ernest akamtazama halafu akanywa kinywaji
kidogo akapokea simu iliyokuwa ikiita kisha akamgeukia Jane
“ Jane kwa nini lakini uliyaharibu maisha yako namna hii? Haukupaswa kuishi maisha ya namna hii.Baba yako ni mtu tajiri alikusomesha katika shule nzuri sana
ambayo wanasoma watoto wa watu wazito lakini sijui nini kikatokea ukaingia katika mapenzi na Yule kijana ambaye hakuwa wa kiwango chako ukapata mimba
na kuacha shule.Kwa nini ulifanya hivyo Jane? “ Ernest naweza kukubali kwamba nilifanya makosa sana kupata mimba ile wakati nikiwa shule lakini siwezi
kumlaumu mtu yeyote kwani nilifanya maamuzi mimi mwenyewe.” “ Unadhani ulifanya maamuzi ya busara? Akauliza Ernest “ Kwa macho ya wengi hapana
lakini kwangu mimi ndiyo.Nilifanya maamuzi sahihi.” Akasema Janet na ukimya ukatanda.Janet hakuonyesha kupendezwa na swali lile la Ernest “ Baada ya
kupata mimba ile baba alinitaka nikaitoe ili niendelee na masomo lakini sikuwa tayari ,akaniambia nichague mawili kati ya mapenzi na shule nikachagua
mapenzi.Nlifanya hivyo kwa kuwa ninampenda sana Ben na ndiyo maana nikawa tayari kuacha kila kitu kwa ajili yake kwa hiyo maisha haya ninayoishi sasa
niliyachagua mwenyewe.This is love,true love.” akasema Janet.Ernest akanywa kinywaji na kusema “ I see.Lakini nimekuwa najiuliza swali hili kila siku bila
kupata jibu” “ Swali gani Ernest? Akauliza jane “ Jane ulikuwa ni msichana mzuri kuliko wote shuleni na kila mwanaume alikuwa anataka kukupata .Shule yetu
ilijaa vijana watoto wa mabilionea lakini katika hao wote hukumuona hata mmoja hadi ukaenda kuzama mapenzini na Yule kijana asiye na mbele wala nyuma
.Alikupa nini Yule kijana? Ana kitu gani ambacho wengine hawana? Janet akatabsamu na kusema “ Alichonacho Ben hakuna mwanaume mwingine chini ya jua
ambaye anaweza kuwa nacho that’s why I gave up everythuig for him” akasema Jane.Ernest akainua glasi akanywa funda lingine na kusema “ Anyway tuachane
na hayo Jane nafahamu msimamo wako kwani nimekuhangaikia kwa miaka mingi lakini sikufanikiwa kupata hata busu” akasema Ernest na wote wakacheka “
Niambie hivi sasa unaishi wapi? Unafanya kazi gani? Maisha yako yakoje? “ Ernest kama nilivyokueleza ni kwamba maisha yangu ninayajua mwenyewe.Si
mazuri sana kama yale niliyokuwa natazamia kuishi.Mimi na mume wangu tunaishi maisha ya kawaida sana kama watu wengine.Sina kazi yoyote mpaka sasa ila
Ben ydeye amekuwa anajishughulisha na biashara ya boda boda.” “ Boda boda?!! Akauliza Ernest kwa mshangao “ Ndiyo mbona umeshangaa? Akauliza Jane “
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment