Simulizi : Queen Monica
Sehemu Ya Pili (2)
aada ya kuingia ndegeni alisalimiana na walinzi wake pamoja na wasaidizi wake akaenda pia katika chumba cha marubani akasalimiana nao na moja kwa moja akaelekea katika chumba maalum cha rais kiilichokuwa na kila kitu kuanzia ofisi,ukumbi wa mikutano chumba cha kulala n.k.Baada ya dakika chache dege likapaa kuelekea Dar es salaam. Akiwa katika chumba chake cha mikutano alijadiliana mambo kadhaa na wasaidizi wake alioambatana nao kisha akawaomba wamuache apumzike kidogo.Baada ya wasaidizi wale kundoka akamuita Jean Pierre Muyeye mmoja wa wasaidizi wake anayemtumia katika mambo yake mengi binafsi. Haraka haraka Muyeye akafika .David alikuwa ameelekeza macho katika kompyuta yake ndogo baada ya kama dakika mbili hivi akainua kichwa na kumtazama Muyeye. “ Muyeye tunakwenda Dar es salaam lakini tukiwa huko kuna jambo ambalo nataka ulifanye.” Akasema David “ Niko tayari mkuu” akajibu Jean Pierre Muyeye kwa adabu.David akamgeuzia Muyeye kompyuta ile ndogo ambayo kulikuwa na jalada la jarida la The Face lililopambwa kwa picha ya mwananke mmoja mrembo sana aliyekuwa ndani ya tabasamu pana “ Umemuona huyo mwanamke katika hilo jarida? Akauliza David “ Ndiyo mzee nimemuona.” “ Vizuri.Jina lake anaitwa Monica Benedict Mwamsole ni mtanzania.Ni mtoto wa mfanya biashara mmoja mkubwa pale jijini Dar es salaam anaitwa Benedict Mwamsole” David akanyamaza akamtazama Muyeye na kuendelea “ Tukifika Dar es salaam wakati ninaendelea na kikao wewe utakuwa na kazi moja tu nataka ukusanye taarifa za kumuhusu huyu msichana.Nataka mpaka jioni ya leo uwe umepata taarifa sahihi na za kutosha kuhusu Monica. Tafadhali Muyeye jambo hili ni muhimu sana kwangu na kazi hii unatakiwa uifanye kwa umakini na kwa usiri mkubwa.Baada ya kuzipata taarifa hizo nitakuelekeza nini cha kufanya” akasema David Zumo na baada ya maelekezo machache Muyeye akatoka na kumuacha rais peke yake mle ofisini.David akaelekeza tena macho katika kompyuta yake akaanza kuzitazama picha mbali mbali za Monica alizozikuta mtandaoni “ Monica Benedict Mwamsole..” akasema kwa sauti ndogo “ Hakika huyu msichana ana uzuri wa kipekee sana na anastahili kuwa mrembo kuliko wote Afrika.” Akawaza na kupiga funda kubwa la mvinyo mkali “Katu siwezi kukubali msichana mrembo kama huyu akanikosa.Ugonjwa wangu mimi ni wanawake wazuri kama hawa.Lazima nifanye kila linalowezekana kuhakikisha ninampata .Lazima awe mke wangu.Kama yeye ni malkia wa afrika basi mimi ndiye mfalme wa Afrika.Monica anastahili kuwa na mtu kama mimi ili aishi kweli yale maisha ya kimalkia.” Akawaza David na unywa tena funda lingine la mvinyo “ Macho yangu yameona wanawake wengi lakini si kama huyu.Monica ni mwanamke wa tofauti sana.Wanawake wenye sura kama hizi tumezoea kuwaona katika michoro ya wachoraji mahiri lakini kumbe kuna wengine wapo kweli na mmoja wao ni huyu Monica.I swear lazima nimpate huyu mwanamke.Kwa namna yoyote ile lazima nimpate ” Akaendelea kuwaza David huku dege lake likiwa angani kuelekea Dar es salaam.
Daniel hakutaka kuelekea sehemu nyingine yoyote baada ya kutoka kwa Dr Marcelo akanyoosha moja kwa moja kwa Muktar rafiki yake anayefanya biashara ya kuuza vipuri vya magari na ambaye huwa wanashirkiana mambo mengi. “ King Daniel !! akasema Muktar baada ya kumuona Daniel akiingia dukani kwake “ Leo kulikoni asubuhi namna hii? Gari lina matatizo? Akauliza Muktar.Hakuwa amezoea kuonana na Daniel mida kama ile. “ Kwani kuna ubaya nikija dukani kwako asubuhi Muktar? Akauliza Daniel “ Hakuna ubaya Danny lakini nimeuliza tu kwa sababu sijazoea kukuona maeneo haya asubuhi. Karibu sana Daniel..” akasema Muktar na kumtazama Daniel usoni akagundua kuwa kuna kitu hakiko sawa “ Daniel kuna tatizo? Akauliza Muktar “ Daniel nimekuja kwako unishauri .” akasema Daniel na Muktar akamuongoza hadi katika ofisi yake . “ Kuna tatizo gani Daniel? Akauliza.Daniel akavuta pumzi ndefu na kusema “ Muktar nadhani unamfahamu Monica” “ Monica Yule rafiki yako? “ Ndiyo” “ Ninamfahamu vizuri.Nini kimetokea? “ Muktar wewe unanifahamu vizuri mimi ugonjwa wangu ni vimwana warembo.Nimekuwa na ukaribu na Monica kwa muda mrefu sasa na sikufichi ndugu yangu Yule mtoto amenichanganya mno.Sijawahi kuchanganyikiwa kwa mwanamke kama ilivyonitokea kwa Monica.Pale akili yangu imefika mwisho ,ninampenda Monica zaidi ya ninavyoweza kueleza.Monica ana mradi wake mkubwa anataka kuuanzisha anataka kujenga shule ya watoto walemavu kwa hiyo anahitaji fedha nyingi.Ameandaa mbio za nusu marathoni ili kukusanya fedha toka kwa watu mbali mbali.Kuna Yule rafiki yangu Dr Marcelo naye baada ya kusikia kuhusu jambo hilo akataka kuchangia nikamkutanisha na Monica wakaongea na akatoa mchango wake lakini mara ghafla naona mambo yamebadilika.Monica na Dr Marcelo wamekuwa na ukaribu mkubwa sana.Jana kulikuwa na sherehe iliyoandaliwa nyumbani kwa wazazi wa Monica kumpongeza lakini cha kushangaza kwa mara ya kwanza toka nimekuwa na ukaribu na Monica hakunialika katika sherehe hiyo na badala yake akamualika Dr Marcelo.Nilipopata taarifa hizo nilishangaa sana na asubuhi ya leo nikawahi ofisini kwa Monica ili anieleze ni sababu gani iliyopelekea asinialike katika sherehe yake lakini wakati tukiongea akaingia msaidizi wake akiwa na kikapu cha maua yaliyotoka kwa Dr Marcelo.Nilikasirika nikaondoka bila hata kumuaga nikaelekea moja kwa moja kwa Dr Marcelo kumuonya akae mbali na Monica kwani Monica ni wangu .
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sikuweza kuelewa na Dr Marcelo na tukataka kugombana.Ameniudhi sana Yule paka na hapa nilipo nina hasira kama za Mbogo.Dr Marcelo ameonyesha kila dalili kuwa anamtaka Monica na hata Monica ameonyesha dalili za kuvutiwa na Marcelo.Muktar nimechanganyikiwa and I don’t know what to do.Tafadhali naomba unishauri nini cha kufanya? Akasema Daniel.Muktar akatoa sigara akawasha na kupiga mikupuo kadhaa kisha akasema “ Una hakika Monica anaweza akawa amevutiwa na Marcelo au ni urafiki wa kawaida tu? “ Muktar laiti ungemuona namna Monica alivyotabasamu baada ya kupokea maua yaliyotoka kwa Daniel ungekubaliana nami kuwa tayari ameanza kuvutiwa na Yule mjinga.I swear I’m going to destroy that bastard !!!..akasema Daniel na kugonga meza “ Daniel punguza hasira kidogo ili tujadili namna ya kulimaliza suala hili.” “ Muktar nina hasira sana na ninaweza kufanya chochote kile kwa aili ya Monica.!! Akasema Daniel “ Kibaya zaidi Marcelo amempigia simu Monica na kumueleza kwamba nimemfuata na kumtishia maisha yake jambo ambalo limemkasirisha sana Monica.Muktar sikutaka kabisa kumuudhi Monica.I don’t know what to do” akasema Daniel na kuinama chini
Daniel siku zote ninakuelezaga kwamba wewe ni mtu mwenye hasira nyingi kwa hiyo jitahidi siku zote kudhibiti hasira zako.Kitendo ulichokifanya cha kumfuata Marcelo ni wazi hakikuwa kizuri.Kwa hapa jambo hili lilipofika inahitajika busara zaidi kuweka mambo sawa”” akasema Muktar ,Daniel akamtazama kwa macho makali “ Unataka kumaanisha nini Muktar? Akauliza “ Namaanisha kwamba tayari ulikwisha jenga mahusiano mazuri na Monica na njia ilikuwa nyeupe kumpata lakini kwa hiki ulichokifanya cha kumfuata Marcelo tayari kimetia doa ile taswira nzuri uliyoijenga kwa Monica.Ili kuijenga tena taswira nzuri kwa Monica unatakiwa kufanya jambo ambalo naamini kwako litakuwa gumu lakini lazima lifanyike.Unatakiwa ukamuombe msamaha Monica “ akasema Muktar “ Tayari nimekwisha fanya hivyo lakini imeshindikana,amenipa sharti ambalo ni gumu kwangu” Akasema Daniel “ Amekupa sharti gani Monica? “ Amesema eti nikamuombe msamaha Marcelo jambo ambalo katu siwezi kulifanya” akasema Daniel na kuukunja uso.Muktar akamtazama na kusema “ Kama Monica ndivyo anavyotaka please do it..” “ No !! No !! no.!!.siwezi katu kufanya kitu kama hicho .Siwezi katu kumuomba msamaha Marcelo wakati ni yeye ndiye aliyeingia katika anga zangu .Kama Monica hatanisamehe kwa sababu tu sijamuomba msamaha Marcelo let it be ila siko tayari kabisa kabisa kwenda kumpigia magoti Yule mbuzi na kumuomba msamaha.But I swear I’ll destroy him....!! Atanitambua mimi ni nani!! Siwezi kumkosa Monica kwa sababu yake!!! Akasema Daniel huku akigonga meza kwa hasira na kuinuka “ Daniel tafadhali punguza hasira na usifanye hicho unachodhamiria kukifanya.Usijingize tena katika matatizo mengine yasiyokuwa na msingi.Tafuta njia nyingin......” akasema Muktar lakini kabla hajamaliza Daniel akasema kwa sauti kali “ Huna chochote cha kunishauri Muktar.Wewe nawe ni kama wao tu.I wont come to you again for advice.....!! akasema kwa ukali na kuondoka “ Kama ni kumkosa Monica acha nimkose lakini si kumpigia magoti Yule mshenzi Marcelo.Yeye ndiye sababu ya mimi kumkosa mwanamke ninayempenda kuliko wote and I’m going to show him who I real am.Nitamuonyesha kwamba hili jiji ni langu..!! akawaza huku akiuma meno kwa hasira baada ya kuondoka dukani kwa Muktar
Saa saba na dakika kumi na tisa Monica aliwasili Jasmina Restaurant walikopanga wakutane na Dr Marcelo kwa ajili ya chakula cha mchana.Kitendo alichokifanya Daniel kumfuata Marcelo na kumtolea vitisho kilimuudhi sana Monica na hivyo akampigia simu Dr Marcelo akamuomba wakutane mchana ili waweze kuongea kilichotokea. Monica alishuka katika gari akaangaza angaza na mara akamuona Dr Marcelo akimpungia mkono akamfuata.Walikaa sehemu tulivu huku wakifurahia mandhari nzuri ya bahari.Muhudumu akafika na kuwasikiliza wakaagiza chakula na wakati wakisubiri chakula wakaendelea na maongezi mengine “ Dr Marcelo japokuwa sote tuna shughuli nyingi za kufanya lakini nimeona ni vyema kama tukakutana mchana huu ili tuongelee kilichotokea asubuhi.” Akasema Monica “ I’m so sorry Monic..” akasema Dr Marcelo lakini kabla hajamaliza Monica akamzuia “ Dr Marcelo mimi ndiye ninayepaswa kukuomba samahani kwa kilichotokea.Mimi ndiye chanzo cha haya yote.I’m so sorry Dr Marcelo nimekusababishia matatizo na rafiki yako mkubwa” akasema Monica “ Usijali Monica.Mimi na Daniel ni marafiki wa siku nyingi .Hii ni mara yetu ya kwanza kukorofishana lakini nina uhakika tutaelewana tu.” Akasema Daniel “ Baada ya kutoka kwako Daniel alinipigia simu na kuniomba msamaha lakini nikamwambia kwamba aje kwanza akuombe msamaha ndipo arudi kwangu kuniomba msamaha,alikuja tena kwako ? akauliza Monica “ Hapana hakurudi.Ninamfahamu Daniel ni kijana mwenye kiburi sana hasa kutokana na utajiri alionao na katu hangeweza kurudi kuniomba samahani.Yeye anadai kwamba mimi ndiye niliyemuingilia katika mahusiano yake,anadai wewe ni mpenzi wake.Ni kweli? Akauliza Dr Marcelo na kumfanya Monica atoe kicheko. “ Hata kama wanaume wangeisha kabisa katika dunia hii na angebaki Daniel peke yake katu hawezi kuwa mpenzi wangu.Ninamfahamu vizuri na ninazifahamu tabia zake chafu.Ukaribu wetu ni wa kawaida tu na hakuna zaidi ya hapo.Kama nilivyokueleza kuwa mimi nay eye tumekua pamoja toka tukiwa wadogo na hata familia zetu ni marafiki” Akasema Monica Chakula kikaletwa wakaendelea kula kimya kimya “ Dr Marcelo ..” akaita Monica. “ Naomba tafadhali mpuuze Yule mjinga na maneno aliyoyasema.Yule bado ni kijana na hana malengo yoyote zaidi ya kuutumia kwa fujo utajiri wa baba yake kwa anasa.Ninafurahi sana kukutana na kijana kama wewe ambaye una malengo makubwa na pamoja kwamba familia yako ina uwezo lakini hujatopea katika anasa na starehe na badala yake umeelekeza kila shilingi unayoipata katika kuwahudumia watu wenye matatizo.Endelea na moyo huo Dr Marcelo na Mungu atakubariki na atakuzidishia wewe na familia yako.” “ Ahsante sana Monica kwa maneno hayo yenye busara” akasema Dr Marcelo “ Kuna jambo lingine ambalo nataka nikushauri” akasema Monica “ Nakushauri uvunje kabisa urafiki na Daniel.Nimegundua si kijana mzuri na hafai kabisa kuwa rafiki yako.Wewe na yeye tabia zenu ni tofauti kabisa. Kifupi ni kwamba hamuendani.Nakushauri tafuta rafiki wa karibu mwenye tabia njema na mwenye malengo makubwa ya maisha tofauti na Daniel ambaye kila kukicha yeye anawaza starehe tu” akasema Monica “ Monica mawazo yako ni kama niliyonayo kichwani.Nimewaza sana kuhusu jambo hilo na nimekwisha dhamiria kwamba mimi na Daniel urafki wetu uishie hapa .Kwa kitendo alichonifanyia leo sintaweza kabisa kuendelea na urafiki naye” akasema Dr Marcelo “ Good.Thats a wise decision.” “ Vipi kuhusu wewe ,? Nina wasi wasi anaweza akaja kukuletea matatizo pia.” Akasema Dr Marcelo “ Hata mimi tayari nimekwisha anza kuchukua hatua za kumuweka Daniel mbali kabisa nami.Sitaki kabisa ukaribu naye.Hata mama yangu amenishauri nifanye hivyo na ndiyo maana ukaona hata katika sherehe ile niliyofanyiwa ya kupongezwa na familia sikumualika,yote hii ni kwa sababu sitaki tena ukaribu naye.Usijali hana uwezo wa kunifanya chochote.Mimi ndiye muamuzi ni mtu gani ninayetaka awe karibu yangu.” Akasema Monica “ Monica ninakuahidi hapa kwamba Daniel akithubutu kukufanyia jambo lolote lisilo la kistaarabu I swear I’ll destroy him.Mimi ni mtu mzuri sana lakini sintaweza kuvumilia hata kidogo kumuona Daniel au mwingine yeyote akikufanyia vurugu. Malaika kama wewe unapaswa kuheshimika na kila mtu” akasema Dr Marcelo na kutazamana na Monica wote wakatabasamu. “ Wow ! what a gentleman.Macho yake yanaonyesha wazi anamaanisha anachokiongea.Ni mapema sana kusema lakini ninaziona kila dalili za mwanaume Yule wa ndoto zangu kwa Dr Marcelo.Ana kila sifa ya mwanaume bora.Kinachonishangaza ni kwa nini kijana kama huyu mwenye kila kitu,ana sura nzuri,ana moyo wa huruma na anajali,ukiacha yote ni kijana tajiri,mpaka leo hana mpenzi? Ana tatizo lolote? Nahisi kuna mambo ya ndani yanayomuhusu Marcelo ambayo napaswa kuyafahamu.” Akawaza Monica. Walimaliza kula kisha wakaendelea na maongezi kuhusiana na mbio za nusu marathoni zinazotarajia kufanyika siku inayofuata.Baada ya kutoka hapo wakaondoka wote na kuongozana kwenda kuangalia maandalizi ya mbio hizo yaliyokofikia.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Saa kumi na mbili kasoro za jioni Bakari mmoja wa wafanyakazi wa Bi Janet ambaye humtumia katika shughuli zake mbali mbali,alirejea katika makazi ya Benedict Mwamsole na kumkuta Bi Jane tayari amekwisha rejea nyumbani . Moja kwa moja akamfuata na kumpa majibu ya kazi aliyokuwa amemtuma jana yake. “ Madam kazi uliyonituma nimeimaliza na haya hapa ni majibu yake.” Akasema Bakari akiwa amesimama mbele ya Bi Janet kwa adabu “ Ahsante sana Bakari kwa kuikamilisha kazi hii kwa haraka.” Akasema Bi Janet na Bakari akamkabidhi bahasha . “ Humu kuna kila kitu kuhusiana na Dr Marcelo” akasema Bakari “ Una hakika taarifa zote zilizomo humu ni sahihi? Akauliza Bi Janet “ Ndiyo Madam .Taarifa zote zilizomo humo ni za uhakika “ akasema Bakari. “ Good.” Akasema Bi Janet,akachana hundi na kumpatia Bakari,akatoa karatasi zilizokuwamo katika bahasha ile akaanza kuzipitia moja baada ya nyingine.Kulikuwa na nyaraka kadhaa zikionyesha mambo mbali mbali kuhusiana na Dr Marcelo kuanzia taarifa zake za kifedha,mali anazomiliki n.k.Ilimchukua zaidi ya saa moja na nusu kuipitia ripoti ile kuhusiana na Dr Marcelo akavuta pumzi ndefu na kumuita mtumishi wake amletee maji ya kunywa kisha akazama katika dimbwi la mawazo “ Dr Marcelo is a good guy .A very good guy na anaweza kusema kwamba huyu kijana anaweza kumfaa sana Monica.Hana sifa yoyote mbaya kama Yule mshenzi Daniel .Anatoka katika familia tajiri ,ni msomi mzuri,hajawahi kuoa na ana kila sifa nzuri lakini ana tatizo moja kubwa ambalo siwezi kukubali akawa na Monica japokuwa kuna kila dalili kwamba Monica ameanza kuvutiwa naye.” Akavuta pumzi ndefu na kutazama tena karatasi zile kwa makini “ Dr Marcelo ana saratani ya damu !!.Oh my God why it have to be him?? Hii ina maana hana maisha marefu kwa sababu ya ugonjwa wake huu kwa hiyo siwezi kukubali akawa na Monica.Siko tayari kumuona mwanangu akiwa mjane katika umri mdogo.Inaniuma kumkosa kijana kama huyu lakini sina namna nyingine ya kufanya zaidi ya kuwatenganisha haraka sana kabla ya mahusiano yao hayajafika mbali na kuota mizizi.Mungu atamjalia Monica na siku moja atampata mwanaume wa ndoto zake ambaye hatakuwa na tatizo lolote” akawaza Bi Janet na kuinuka akaelekea chumbani kwake.
baada ya kuwasili jijini Dar es salaam, David Bikumbi Mukaya Zumo rais wa jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo alipokelewa na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Tanzania katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius nyerere halafu akapelekwa moja kwa moja katika hoteli atakayofikia ambako alipata mapumziko mafupi kabla ya kuelelekea ikulu kuonana na rais wa Tanzania Ernest Mkasa ambaye alikuwa na mazungumo naye ya faragha kabla ya kuanza kikao cha maraisi wa nchi za maziwa makuu. Alipokewa ikulu na mwenyeji wake wakawa na mazungumzo ya faragha na baada ya hapo akaelekea katika hoteli ya White Panda ambako kuliandaliwa mkutano kati yake na raia wa kongo wanaoishi nchini Tanzania.Aliongea nao mambo mengi na kisha akarejea hotelini kwake kujipumzisha na kujiandaa kwa ajili ya mkutano wao unaotarajiwa kuanza kesho. Saa moja za jioni Jean Pierre Muyeye msaidizi wa David Zumo akarejea.Toka walipowasili Dar es salaam Muyeye alikuwa anafanya kazi moja tu aliyotumwa na mkuu wake ya kufuatilia na kukusanya taarifa kuhusiana na binti afrika Monika Mwamsole. “ Nipe taarifa nzuri Muyeye” akasema David Zumo akiwa sebuleni amepumzika akipata mvinyo “ Mkuu nimeifanya kazi uliyonituma na nimeikamilisha.” Akasema Muyeye “ Kazi nzuri sana Muyeye.Nipe taarifa hizo” akasema David Zumo. Jean Pierre Muyeye akamueleza David kila kitu alichokipata kuhusiana na Monica.Uso wa rais huyu tajiri barani Afrika ukajenga tabasamu kubwa sana baada ya Muyeye kumaliza kumpa taarifa ile. Akainuka na kumimina mvinyo katika glasi akampatia Muyeye “ Muyeye unastahili kunywa pamoja nami mvinyo huu ghali zaidi ambao hunywewa na watu maarufu.Mambo uliyoyafanya ni makubwa na unastahili kunywa pamoja nami” akasema David na kugonganisha glasi “ Umenifurahisha sana Muyeye kwa kazi hii uliyoifanya hadi ukapata taarifa hizi.Naomba nikiri kwamba kwa upande wako unaweza ukaona ni kazi ndogo umeifanya lakini kwangu mimi ni kitu kikubwa sana umekifanya.” Akasema David na kunywa funda moja “ Kazi hii ya leo ni hatua ya kwanza.Kesho nataka tuingie katika hatua ya pili.Nataka kesho ushiriki katika mbio hizo fupi kama mwakilishi wangu na baada ya mbio hizo nataka uonane na Monica umfikishie ujumbe wangu.Mweleze kwamba ninahitaji kuonana naye kesho jioni kwa chakula cha usiku hapa hotelini kwa lengo la kujadili kuhusiana na mradi wake wa ujenzi wa shule ya watoto wenye ulemavu.Nimeguswa sana na ninahitaji na mimi kuchangia katika mradi huo.Ninataka kujadili pamoja naye anieleze kwa kina ni sehemu ipi hasa ninayoweza kuchangia ” akasema David Zumo “ Mkuu nitafanya kama ulivyoagiza na kesho utakutana na Monica.” Akasema Muyeye na kuzidi kumfurahisha David Zumo “ Monica mwamsole ..!! akasema David kwa kunong’ona baada ya Jean Pierre Muyeye kutoka.Akaifungua kompyuta yake na kuzitazama tena picha za Monica zilizopo mtandaoni akanywa funda kubwa la mvinyo akatabasamu “ Huyu ndiye hasa mwanamke anayepaswa kuwa na mtu kama mimi.Ana kila sifa ya mwanamke ninayemtaka. Naapa katu sintamuacha lazima nimpate ,Monica lazima awe wangu .Nitatumia kila nguvu niliyonayo mpaka nihakikishe ninampata kimwana huyu anayeikimbiza Afrika.Uzuri wake umenisisimua mno na siwezi kukubali mwanamke mrembo kama huyu asiwe wangu”
Ni saa tano za usiku sasa Mzee benedict Mwamsole na mke wake Janet wako chumbani kwao wakijipumzisha baada ya shughuli za kutwa nzima. “ Ben kuna jambo lilitokea jana na sikutaka kukwambia mapema nilitaka kwanza nifanye uchunguzi wangu” akasema Janet “ Ni jambo gani hilo kwa sababu nawe huishiwagi mambo” akasema mzee Ben huku akitoa kicheko kidogo “ Katika sherehe ya Monica jana Daniel Yule kijana wa mzee Swai hakuwepo inaonekana hakualikwa.Nadhani Monica aliyafanyia kazi maneno yangu” “ Uliongea na Monica kuhusu suala hilo? Akauliza mzee Ben “ Ndiyo niliongea naye na kumtahadharisha kuhusu ukaribu na Daniel “ akasema bi Janet “ Hukupaswa kufanya hivyo.Monica ataona kama vile tunaingilia masuala yake binafsi” akasema Ben “ Hapana siwezi kukaa kimya wakati ninamuona kabisa mwanangu yuko karibu na chui mwenye ngozi ya kondoo.Nilimtahadharisha awe muangalifu asije akaingia katika mitego ya Yule kijana.Kutomuona Daniel jana katika sherehe ni dalili za wazi kwamba tayari amekwisha anza kumkwepa kijana yule mchafu wa tabia.” Akasema bi Janet na baada ya sekunde kadhaa akaendelea “ Jana wakati sherehe ikiendelea Monica alikuwa anazunguka zunguka kusalimia watu mbali mbali walioalikwa na baadae akapotea ghafla .Nilikuwa nikimfuatilia na nikamuona akiondoka na kijana mmoja hivi mtanashati sana ambaye ni mara ya kwanza kumuona naye wakaeleka kule kwenye bwawa la kuogelea ambako kuliandaliwa meza .Nadhani Monica alipanga kukutana na kijana Yule kule ili waongee mambo yao.Niliwafuatilia na kuwakuta wakiwa wamezama katika maongezi na kwa namna nilivyowakuta kuna kila dalili kwamba kuna kitu kinaendelea kati yao.” Akanyamaza tena na baada ya muda akaendelea. “ Kijana huyo anaitwa Dr Marcelo Richard.Kwa mujibu wa Monica ni kwamba kijana huyo ni mmoja wa wafadhili wa mradi wake wa kujenga shule ya watoto walemavu.Lakini kwa mtazamo wangu kuna kitu zaidi ya ufadhili nilichokiona kati yao.Kama kawaida yangu nilifanya utafiti wangu nilitaka kumfahamu Dr Marcelo ni kijana wa namna gani” “ Umepata majibu gani ? akauliza mzee Ben “ Dr Marcelo ni kijana msafi wa tabia,ni msomi mzuri,anatoka katika familia tajiri ,hajawahi kuwa na mke na hana tabia chafu za kubadilisha wanawake kama alizonazo Daniel.Anaongoza hospitali inayofadhiliwa na familia yake inayohudumia wagonjwa wa saratani ya damu.Kwa ujumla ni kijana mwenye sifa nzuri na ni kijana anayeweza kumfaa sana Monica ila kuna tatizo moja.” Akasema Bi Janet na kunyamaza “ Tatizo gani hilo? Akauliza Ben.Bi Janet akavuta pumzi ndefu na kusema “ Dr Marcelo ana tatizo la saratani ya damu”.. Zilipita kama dakika mbili za ukimya mzee Ben akasema “ Kwa namna ulivyowaona kuna dalili zozote za Monica na huyo Dr Marcelo
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kuwa katika mahusiano? Akauliza mzee Benedict ” Mimi ni mtu mzima na nimeyapitia mambo haya ,ni wazi kuna dalili za kupendana kati yao” akajibu Bi Janet “ Kama tayari kuna dalili hizo na wakati huo huo unadai kwamba kijana huyo ana saratani ya damu ambayo kiuhalisia hatakuwa na maisha marefu ,unashauri nini kifanyike? “ Ben hapa hakuna mjadala kuna kitu kimoja tu cha kufanya ni kuwatenganisha Monica na huyo kijana.” Akasema Bi Janet.Mzee Ben akafikiri kidogo na ksuema “ Sikatai wazo lako lakini huoni kuwa hatutakuwa tunamtendea haki Monica tukisema aachane na kijana anayempenda? Mimi kwa matazamo wangu kama Monica anampenda huyo kijana basi awe naye ila aelezwe ukweli kwamba kijana huyo ampendaye ana maradhi ya saratani ya damu ili afanye uamuzi yeye mwenyewe kuliko kungilia masuala yake ya kimahusiano.” Akashauri Ben “ Hapana Ben.Sitaki mwanangu awe mjane katika umri mdogo.Nataka Monica ampate mwanaume ambaye hana kasoro hata moja.Huyu Dr Marcelo ni kijana mwenye sifa zote lakini tatizo lake ni hilo moja tu la ugonjwa huo unaomsumbua.” Akasema bi Janet “ Kumpata mtu asiye na kasoro yoyote katika ulimwengu huu wa sasa ni ngumu sana.Nashauri tukae na Monica tuongee naye na tumueleze ukweli kwamba kama anampenda Dr Marcelo basi afahamu kwamba anasumbuliwa na maradhi ya saratani ili yeye mwenyewe afanye uamuzi kuliko sisi kumuingilia katika maisha yake.Monica ni msichana mkubwa sasa na ana uwezo wa kufanya maamuzi kuhusu maisha yake kwa hiyo usimnyime nafasi hiyo mhimu ya kupanga maisha yake .Kama anampenda Dr Marcelo kwa dhati ya moyo wake basi lazima atakubaliana na mapungufu yake yote ikiwemo na ugonjwa huo unaomsumbua “ akashauri mzee Ben “ Haopana siwezi kukubaliana na hilo Ben.Monica bado ni msichana mwenye ndoto nyingi za maisha kwa hiyo anatakiwa ampate mwanaume ambaye atamsaidia kuzitimiza ndoto hizo na si ampate mwanume ambaye baada ya kipindi kifupi atakuwa kitandani na Monica kuutumia muda wake mwingi kumuhudumia na kusahau kuhusu ndoto zake. Siwezi kukubali mwananagu abebe mzigo wa kuhudumia mtu mgonjwa .Na vipi iwapo watapata watoto ambao nao watarithi maradhi hayo ya saratani ya damu? Maisha ya Monica yatakuwa ni kuuguza wagonjwa .Sikubaliani na hilo.Monica ana fursa nyingi sana za kumfikisha mbali na siko tayari kumuona akizizima ndoto zake kwa sababu eti ya mapenzi.Wanaume hawajaisha .Dunia hii bado ina mamilioni ya wanaume vijana wazuri na nina hakika Monica atampata mmoja wa maisha yake.” Akasema Bi Janet “ Lakini Janet tukifanya hivyo hatutakuwa tumemtendea haki mtoto.Tumuache Monica mwenyewe afanye maamuzi kuhusu maisha yake “ akasema mzee Ben “ Ben tutakuwa wajinga na tutachekwa na dunia kama ndoto za Monica zitazimika huku tukiona kwa
kigezo eti cha kumuacha awe huru kuchagua kuhusu maisha yake.Sisi kama wazazi lazima tutumie vyema nafasi yetu kuhakikisha mtoto anakuwa na maisha mazuri yenye furaha.Kama wewe hauko tayari kwa hilo niachie mimi.Nitahusika kwa chochote kitakachotokea .Wewe kaa pembeni niache mimi nibebe mzigo wote wa lawama kama zitakuwepo lakini siwezi kukubali kumuona Monica akijiingiza katika mahusiano yasiyo na manufaa kwake” akasema Bi janet.Mzee Ben hakutaka tena kuendelea na mjadala ule akageuka upande wa pili “ Tutafanya kosa kubwa kuingilia mahusiano ya Monica.Kama anampenda huyo daktari mimi sina kipingamizi chochote kama ndiye chaguo lake .Suala la kumpangia awe na nani ni mambo ya miaka ya zamani sana.Zama hizi watoto wako huru kufanya uchaguzi wa watu wanaowataka wawe nao katika mahusiano.Hata hivyo siwezi kukaa kimya na kumuacha Janet afanye atakavyo.Nitamuita Monica nitaongea naye na kumuweka wazi kama anampenda huyo daktari kwa moyo wake wote basi afumbe macho na aweke pamba masikioni ili asisikie ya watu bali aendelee naye .” akawaza mzee Benedict. “ Benedict bado ana mawazo ya kizamani sana.Zama hizi tunaangalia mambo mengi kabla ya kuamua kuwa na mtu Fulani kimahusiano.Siwezi na sema siwezi kukubali kumuacha Monica aingie katika mahusiano na Dr Marcelo wakati nikifahamu kabisa kuwa Yule kijana hana kitu chochte atakachomletea Monica zaidi ya furaha ya muda mfupi na kitakachofuata hapo ni kilio na majonzi.Sitaki Monica aachwe mjane katika umri mdogo.Ni bora hata Daniel anaweza akabadilika kuliko huyu ambaye hana maisha marefu .Nitawatenganisha” akawaza Bi Janet.
Kumepambazuka tena ni siku ya jumamosi na jiji la Dar es salaam likiwa limeamshwa na tukio moja kubwa ambalo ni mbio za nusu marathoni zilizoandaliwa na Monica kwa lengo la kuchangisha fedha za ujenzi wa shule ya watoto wenye ulemavu wa kutoona na kusikia. Kuanzia saa kumi na mbili za asubuhi maelfu ya wakaazi wa jiji la Dar es salaam tayari walikuwa wamewasili katika viwanja ambako mbio hizo zingeanzia.Watu walihamasika vya kutosha na ndiyo maana wakajitokeza kwa wingi mno. Saa mbili za asubuhi mgeni rasmi akawasili ambaye ni waziri wa habari sanaa na michezo ambaye naye alikuwa mshiriki katika mbio hizo.Utepe ukakatwa na mbio zikaanza rasmi. Monica alikuwa akikimbia sambamba na mgeni rasmi pamoja nao walikuwepo pia baba na mama yake ambao walikuja pia kumuunga mkono.Alikuwepo pia Dr Marcelo ambaye timu yake ya madaktari ilikuwapo katika mbio hizo kwa ajili ya kutoa huduma ya kitabibu kwa wale wote watakaopatwa na tatizo lolote .Vile vile wafanyakazi wengine wa taasisi yake walishiriki pia katika mbio hizo.Miongoni mwa washiriki wa mbio hizo alikuwa ni Daniel akiwa na kundi la marafiki zake.Alitamani sana kama angeweza kupata nafasi ya kuzungumza na Monica lakini hakuipata nafasi hiyo ya kuonana na Monica.Aliumia sana kumuona Monica akiwa karibu na Dr Marcelo. “Mimi ndiye niliyetakiwa niwe pale karibu na Monica kwani nmemsaidia sana kuandaa mbio hizi lakini ametokea Yule mshenzi Marcelo ameniharibia kila kitu.Naapa lazima nimfundishe adabu.Nimeujenga urafiki na Monica kwa miaka mingi na kwa gharama kubwa lakini amekuja na kuuvuruga kwa siku moja tu.Hapana sikubaliani kabisa na hilo lazima nimfunze adabu” Akawaza Daniel huku akiendelea na mbio taratibu. Hatimaye mbio zikamalizika na ukafika wasaa wa mgeni rasmi kuwatunuku zawadi washindi toka makundi mbali mbali waliofanya vizuri katika mbio hizo lakini kabla ya kutoa zawadi mgeni rasmi alikuwa na machache ya kuongea.Wakati mgeni rasmi akitoa maneno machache kwa washiriki kabla ya kukabidhi zawadi,Linah msaidizi wa Monica akamfuata na kumvuta pembeni. “ Madam Monny,kuna mtu anahitaji kukuona anasema ana ujumbe wako toka kwa rais David Zumo wa jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo” akasema Linah “ Kutoka kwa rais wa Kongo? Akauliza Monica “ Ndiyo” akajibu Linah “ Unamuamini huyo mtu ni mkweli? Akauliza Monica “ Anaonekana ni mkweli” akajibu Linah.Monica akafikiri kidogo na kusema “ Kwa sasa mgeni rasmi anatarajia kukabidhi zawadi kwa washiriki waliofanya vizuri,mwambie nitaonana naye baada ya shughuli zote kumalizika” akasema Monica na kurejea jukwaani. “ Rais wa Kongo !! akawaza “ Ana ujumbe gani kwangu? Akajiuliza “ Ngoja nitafahamu baada ya shughuli kumalizka.Halafu nilimuona Daniel na alionekana kutaka sana kuongea nami lakini sitaki kumpa nafasi hiyo . Ni kijana asiye mstaarabu hata kidogo.Kitendo cha jana kumfuata Dr Marcelo na kumtolea maneno ya kejeli na vitisho na kujitangazia kwamba mimi ni mpenzi wake sijayapenda kabisa.” Akawaza Monica. Mgeni rasmi akatunuku zawadi kwa washiriki waliofanya vizuri na kilichofuata
baada ya hapo ni burudani ya muziki toka kwa wasanii mbali mbali walioshiriki pia katika mbio hizo .Monica akaagana na mgeni rasmi pamoja na baadhi ya watu wengine walioshiriki mbio hizo na mara akakutanisha macho na Daniel “ Monica..Monica..tafadhali naomba unipe dakika mbili tu” akasema Daniel.Monica akatabasamu na kumpa mkono “ Hallow Daniel.” Akasema na kumfanya Daniel atoe tabasamu pana “ Hallow Monica” akasema Daniel “ Daniel nashukuru sana umehudhuria .Nilikuwa na wasiwasi pengine hutaweza kuhudhuria leo” akasema Monica “ Kwa nini nisihudhurie jambo kubwa kama hili Monica? Siwezi katu kufanya hivyo.Hata hivyo ninaomba samahani sana kwa yale yaliyotokea..” akasema Daniel lakini Monica akamkatisha “ Daniel hapa si mahali pa kuongelea masuala yale.Hapa tuko katika masuala mengine kabisa.Tutatafuta nafasi ya kuongelea suala hilo siku nyingine na mahala pengine” Akasema Monica “ Sawa Monica ila napenda kukuhakikishia kwamba hakuna mtu au kitu chochote kinachoweza kuuvunja urafiki wetu.Mimi na wewe ni marafiki hadi mwisho wa nyakati” akasema Daniel “ Sawa Daniel.Nimefurahia uwepo wako ila kwa sasa utanisamehe nina watu wengi ninaotakiwa kuonana nao na kuwashukuru pia kwa kufika kwao.Tutawasiliana zaidi” akasema Monica na kuondoka. “ Daniel amefurahi sana kwa namna nilivyomuonyesha tabasamu kana kwamba hakuna kilichotokea lakini hajui kama moyoni nimetokea kumchukia sana kwa kitendio alichokifanya” akawaza Monica na kumfuata Linah “ Linah yuko wapi huyo mjumbe wa rais wa Kongo? Akauliza Monica. “ Yuko pale katika gari anakusubiri” akasema Linah na kumuongoza Monica moja kwa moja hadi alipokuwa Jean Pierre Muyeye.Alikuwa nje ya gari moja la ubalozi wa Kongo akiwa na taulo begani na chupa ya maji .Naye alikuwa ni mmoja wa washiriki wa mbio hizo.Linah akawakutanisha na kuwaacha waongee “ Monica naitwa Jean Pierre Muyeye ni msaidizi wa David Bikumbi Mukaya Zumo rais wa jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.” Akajitambulisha Muyeye “ Nafurahi sana kukufahamu Pierre Muyeye na nimefurahi sana kwa kushiriki mbio hizi.” Akasema Monica “ Ahsante sana Monica.Jambo hili ni zuri na ndiyo maana nimeshiriki nikimuwakilisha rais wa Kongo ambaye ndiye aliyenituma nishiriki” “
Kweli !! akauliza Monica kwa furaha “ Ndiyo.Yeye ndiye aliyenituma nije nimuwakilishe katika mbio hizi.Yuko hapa nchini kwa ajili ya mkutano wa marais wa nchi za maziwa makuu mkutano unaoanza hii leo na kama angekuwa na nafasi angeweza kushiriki yeye mwenyewe ila kwa kuwa hana nafasi amenituma mimi nimuwakilishe” akasema Muyeye “ Dah ! nimefurahi kupita maelezo kwa rais wa Kongo kuamua kushiriki katika shughuli hii muhimu.Mfikishie
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
shukrani zangu za dhati kwa jambo hili.” Akasema Monica “ Mheshimiwa rais hakunituma nije kushiriki tu kukimbia bali amenipa pia na ujumbe mwingine mkubwa na wa muhimu sana” akasema Muyeye na kutulia kidogo akamtazama Monica na kusema “ Mheshimiwa rais ni mtu wa kusaidia sana taasisi mbali mbali zinazofanya mambo makubwa kwa jamii na hata kule Kongo amekuwa akisaidia sana taasisi mbalimbali .Jana alipofika hapa Tanzania akapata taarifa za kuwepo kwa mbio hizi ulizoziandaa zenye lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya kujenga shule ya watoto wenye ulemavu.Ameguswa sana kwa jambo hilo na kwa hiyo anataka kutoa mchango wake .Hakutaka kunipa mimi mchango wake niulete bali anataka akukabidhi ana kwa ana .Kwa hiyo amenituma nikwambie kwamba anahitaji kuonana nawe usiku wa leo kwa ajili ya chakula maalum na akukabidhi mchango wake.Anaomba ukutane naye katika hoteli aliyofikia ya Kobe Village ” Monica akastuka na kuiweka mikono yake kifuani mahala uliko moyo.Akamtazama Muyeye kwa sekunde kadhaa na kusema “ Pierre Muyeye ninashindwa nikupe jibu gani kwa ufupi nimestushwa kidogo na mwaliko huu wa rais David.Sikuwa nimetarajia kabisa kama mtu wa kutoka mbali angeweza kuguswa na juhudi zangu wakati watu wa hapa hapa nchini wanashindwa .Hii ni heshima kubwa sana na niko tayari kuonana na mheshmiwa rais.” Akasema Monica “ Ahsante sana Monica.Mheshimiwa rais atafurahi sana kwa kukubali kuonana nawe.Nakuahidi hutajutia uamuzi wako wa kukubali kwenda kuonana naye.Ni mtu mwenye moyo wa kusaidia na tayari amekwisha wasaidia watu wengi sana kwa hiyo hii ni fursa kwako ya kuweza kufanikisha mipango yako.Ukifika mueleze mipango yako yote unayokusudia kuifanya na ninakuhakikishia Monica lazima David atakusaidia “ akasema Muyeye. “ Ahsante sana Muyeye nitafanya hivyo” “ Sawa Monica basi kwa kuwa umekubali mimi nitamjulisha habari hizi na saa moja na nusu za jioni utakuja kuchukuliwa na gari la ubalozi kupelekwa hotelini kuonana na mheshmiwa rais” akasema Muyeye akaagana na Monica akaondoka zake. “ Dah ! ama kweli huu ni mwaka wangu.Mbona mambo mazuri yanaongozana namna hii? Naamini Mungu ananitumia ili kuwasaidia watu wake wenye matatizo na ndiyo maana anaelekeza mambo mazuri namna hii kuja kwangu.Rais wa Kongo kuguswa na jambo ninalolifanya ni mafanikio makubwa sana kwangu.” Akasimama kidogo akelekeza macho jukwaani kulikotoka shangwe kubwa kutokana na mambo makubwa aliyokuwa anayafanya mmoja wa wasanii wakubwa aliyekuwa anatumbuiza lakini akili yake haikuwa jukwaani alikuwa mbali sana kimawazo “ Nimewahi kuzisikia taarifa za rais huyu wa Kongo kuwa ni rais tajiri kuliko wote afrika.Kama kweli ana nia ya dhati ya kutaka kunisaidia basi nina hakika mipango yangu itakwenda kama
nilivyokusudia.Napaswa kumshukuru sana Mungu kwa jambo hili” akawaza Monica na kuelekea moja kwa moja mahala walikokuwa wamekaa wazazi wake akaomba wasogee pembeni waongee. “ Monica hongera sana zimekuwa ni mbio nzuri sana na zenye mafanikio.Muitikio umekuwa mkubwa na watu wamehamasika sana.Hongera kwa hilo juhudi zako zinaonekana na nina hakika Mungu ataendelea kukubariki ili mambo yako yaendelee vizuri uzidi kuwasaidia watu wengi wenye uwezo” akasema mzee Benedict “ Ahsante sana baba.Usemayo ni sahihi kabisa nina haki ya kumshukuru Mungu kwani ni kweli jambo hili limefana kwa kiwango ambacho sikuwa nimekitarajia.Japokuwa tumefanya umasishaji mkubwa lakini sikuwa nimetegemea kama watu wangehamasika na kujitokeza kwa maelfu.Ninamshukuru sana Mungu kwa kunisaidia jambo hili limekwenda vizuri” akasema Monica “ Nimemuona Daniel hapa “ akasema bi Janet.Monica akacheka kidogo na kusema “ Mama hapa si mahali pa kuliongelea hilo.Tutapata wasaa tutaongea ila kuna jambo moja ambalo nimeona ni vyema endapo nitawashirikisha ninyi wazazi wangu” “ Ni jambo gani hilo? Akauliza mzee Benedict “ Nimetoka kuongea na mtu moja anaitwa Jean Pierre Muyeye msaidizi wa rais wa Kongo” akasema Monica na kunyamaza kidogo “ Ameshiriki katika mbio akimuwakilisha rais wa Kongo lakini alikuwa na ujumbe pia kutoka kwa rais ambaye yuko hapa nchini kwa ajili ya mkutano wa marais wa nchi za maziwa makuu unaofanyikia hapa Dar es salaam.David Zumo rais wa Kongo ameguswa na kile ninachotaka kukifanya na ameamua atoe mchango wake kwa hiyo amenikaribisha hotelini kwake nikaonanaye naye jioni ya leo ili aweze kunikabidhi mchango wake.Kwa mujibu wa Pierre Muyeye,David amekuwa akisaidia sana watu wengi na hasa wanaofanya mambo makubwa kwa jamii.Nimeona niwashirikishe jambo hili ili mnishauri japokuwa tayari nimekwisha mkubalia Muyeye kuwa nitaonana na rais wa Kongo jioni ya leo.Mnasemaje kuhusu hilo ? akauliza Monika. Mzee Benedict na mke wake wakatazamana kisha mzee Benard akasema “ Monica milango ya mafanikio inazidi kufunguka na sasa imekwenda mbali zaidi .Naweza sema kwamba hii ni fursa kwako kufanikisha malengo yako yote kwani kila unachokifanya kinakwende vizuri na hata watu wakubwa tayari wameanza kuziona juhudi zako na wamejitokeza kukuunga mkono.Nenda kaonane na David Zumo kama alivyokuomba.Ni tajiri namba moja afrika na anaweza akakusaidia sana.Nadhani hakuna haja ya kuongea mambo mengi sisi tunakubaliana na ulichokifanya na tunakutakia kila la heri.Utakaporejea utakuja kutujuza kitakachokuwa kimejiri huko” akasema mzee Benedict.Monica akawakumbatia wazazi wake kwa furaha Shughuli zilizopangwa kufanyika siku hii ya jumamosi zilikamilika na watu wakatawanyika.Monica akawaacha wasaidizi wake wakiendelea na kumalizia shughuli ndogo zilizobaki akaondoka kwa ajili ya kwenda kujiandaa kuonana na rais wa Kongo David Zumo
Tayari inakaribia saa moja za jioni na muda wa Monica kwenda kuonana na David Zumo ukikaribia lakini bado Monica alikuwa anatafuta nguo nzuri atakayovaa usiku huo.Kitandani kulikuwa na magauni manne ameyaweka .Kila moja ni zuri lakini hakujua avae lipi.Akasimama akayaangalia magauni yale na mwisho akaamua kuchukua gauni jekundu akavaa pamoja na koti refu jepesi la rangi nyeusi.Ama kweli ungebahatika kuonana naye usiku huu ungewapa hongera waliosema kwamba Monica ni mrembo kuliko wote Afrika.Alipendeza kuliko kawaida.Akajitazama katika kioo akatabasamu “ Mtu ninayekwenda kuonana naye ni mtu mzito kwa hiyo lazima nipendeze .Ingekuwa ni mtu wa kawaida tu nisingejiremba hivi ningeenda kawaida tu.Huyu ni rais wa nchi kwa hiyo ninalazimika kupendeza “ akawaza Monica na mlango wa chumba chake ukagongwa,akaenda kuufungua akakutana na mtumishi wake Maria “ Madam nimepigiwa simu na walinzi kuna wageni wako wanasema wanatoka katika ubalozi wa Kongo hapa nchini” akasema Maria “ Ahsante Maria wakaribishe sebuleni ninakuja sasa hivi” akasema Monica na kuendelea kujipamba na baada ya muda akachukua pochi yake na kutoka chumbani kwake akaelekea sebuleni ambako kulikuwa na watu watatu wamekaa na wote wakashindwa kuzuia mshangao wao baada ya kumuona Monica . “ Jean Pierre Muyeye” akasema Monica huku akitabasamu.Muyeye akainuka na kumpa mkono Monica “Madam Monica” akasema Muyeye na wale watu wengine alioongozana nao wakasimama wakamsalimu Monica “ Nadhani uko tayari tunaweza kuondoka? Akauliza Muyeye “ Ndiyo tunaweza kuondoka “ akasema Monica kisha wakaongozana hadi nje wakaingia katika gari la ubalozi wa Kongo wakaondoka . “ Ama kweli msichana huyu ana uzuri wa kipekee kabisa.Ninavyomfahamu David Zumo anapenda sana watoto wazuri kama huyu na nina hakika kabisa lengo lake si kuchangia miradi ya Monica kama anavyotaka bali anamtaka Monica kimapenzi.” Akawaza Muyeye wakati safari ikiendelea. Hatimaye wakawasili hoteli ya kifahari yenye hadhi ya nyota tano ya Kobe Village hoteli ambayo maraisi wengi wanapotembelea Tanzania hufikia.Ni hoteli inayotajwa kuwa na huduma za hali ya juu na bei ya juu zaidi kuliko zote afrika mashariki.Gari likasimama na haraka haraka Muyeye akashuka na kuufungua mlango wa upande aliokaa Monica ,akashuka kisha akamuomba amfuate wakapanda lifti kuelekea ghorofani kilipo chumba cha rais David Zumo.Walinzi wa rais David walikuwa tayari na taarifa za ujio wa Monica hata hivyo hawakumruhusu apite hivi hivi bila kukaguliwa wakaukagua mkoba aliobeba na kuhakikisha hakukuwa na silaha au kitu chochote hatarishi alichobeba.David Zumo ni mmoja wa maraisi wanaotajwa kuwa na ulinzi mkali sana miongoni mwa marais wa afrika. Jean Pierre Muyeye akamuongoza Monica kuingia katika sebule kubwa ya
chumba cha rais David Zumo ambaye wakati wakiingia alikuwa akiongea na simu lakini mara tu alipomuona Muyeye akiwa ameongozana na Monica akasitisha maongezi na mtu aliyekuwa akiongea naye simuni “ Mungu wangu..!! huyu Monica ni binasamu wa kawaida kweli?? Uzuri wake unanipa shaka sana yawezekana akawa ni kiumbe mwingine huyu” akawaza David Zumo.Pierre Muyeye akasimama kwa adabu na kusema “ Mheshimiwa rais mgeni wako huyu hapa amefika salama” akasema Muyeye na kumgeukia Monica “ Madam Monica huyu ndiye mwenyeji wako ,rais wa jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo,David Zumo.Karibu sana Madam” akasema Muyeye na kuinama kwa adabu kuonyesha heshima kisha akatoka nje na kumuacha David Zumo akiwa na Monica peke yao mle ndani “ Monica karibu sana.” Akasema David huku akimpa mkono Monica “ Ahsante sana mheshimiwa rais” akajibu Monica kwa adabu na David Zumo akamkaribisha sofani. “ Monica ni furaha yangu kukutana nawe usiku wa leo na kabla ya yote ninapenda kwanza kusema ahsante sana kwa kukubali mwaliko wangu wa kutaka kuonana nawe usiku huu.” Akasema David Zumo rais mwenye haiba ya aina yake “ Hata mimi nimefurahi sana kukutana nawe mheshimiwa rais kwani nimekuwa nikikusoma na kukutazama kupitia vyombo vya habari lakini leo hii nimekutana nawe ana kwa ana.Ni heshima kubwa sana kukutana nawe mheshimiwa rais” akasema Monica huku akitabasamu “ Nafurahi kusikia hivyo Monica.Jambo la pili nataka nikupongeze sana kwa mafanikio makubwa uliyoyapata na hasa kwa kutangazwa na jarida kubwa la the Face kuwa mwanamke mrembo zaidi barani Afrika.Hongera sana unastahili heshima hiyo kubwa.Heshima hii uliyopewa na jarida la The Face imekupaisha hadi nje ya mipaka ya Tanzania na kutufanya hata sisi wengine ambao hatukuwa tumekufahamu hapo kabla kukufahamu.Hongera vile vile kwa mambo ambayo umekuwa ukiyafanya kwa jamii.Tanzania inapaswa kujivunia sana kuwa na mtu kama wewe” akasema David “ Ahsante sana David.Napenda na mimi nitumie nafasi hii kukupongeza sana kwa kazi kubwa uliyoifanya katika nchi yako ya Kongo.Ni kazi kubwa na ya kutiliwa mfano.Kongo ya sasa si ile ya miaka ile.Hongera sana mheshimiwa rais” akasema Monica na kuufanya uso wa David Zumo ukachanua kwa tabasamu kubwa kisha akainuka na kufungua chupa ya mvinyo akammiminia Monica katika glasi na kumpatia “ Samahani Monica nilipaswa kukukaribisha kinywaji toka ulipoingia lakini tumejikita moja kwa moja katika maongezi.” Akasema David “ Ahsante sana mheshimiwa rais” akajibu Monica na kunywa funda dogo la mvinyo... “ Monica usiku wa leo nina maongezi kadhaa kuhusiana na miradi ya kimaendeleo unayoifanya lakini kabla ya yote ningependa kwanza kukukaribisha kwa chakula cha jioni nilichokiandaa kwa
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
heshima yako.Karibu kwa chakula Monica” akasema Monica kisha David akamuongoza kuelekea katika chumba cha chakula ambamo chakula maalum kilikwisha andaliwa .David Zumo akamkaribisha Monica mezani kwa ajili ya chakula.Baada ya kula wakarejea tena sebuleni kuendelea na maongezi yao. “ Monica sitaki nichukue muda mrefu sana wa kuongea nawe usiku huu sitaki mwenzi wako awe na wasi wasi.Unajua sisi wanaume hata kama akiwa na uhakika kwamba umekuja sehemu salama kuonana na rais lakini bado hawezi kukosa kuwa na wasiwasi.Kwa hiyo naomba nijielekeze moja kwa moja katika ile ambacho nimekuitia hapa usiku huu” akasema David Zumo na kumfanya Monica atoe kicheko kidogo. “ Mbona unacheka Monica? Akauliza David Zumo ambaye anatajwa kuwa ni rais ambaye huongea kwa hisia kubwa “ Hakuna wasi wasi wowote mheshimiwa rais kwani sina mume bado kwa hiyo tunayo nafasi ya kuongea mambo mbalimbali kama utapenda” akasema Monica na uso wa David ukajenga tabasamu “ Nilimuuliza swali la mtego ili nijue kama ana mpenzi au hana lakini kumbe hana mpenzi.” Akawaza David Zumo na kusema “ Monica nimefuatilia baadhi ya shughuli unazozifanya na nimejikuta nikiguswa sana.Hongera sana kwanza kwa kujitoa kusaidia jamii yako.Ni wengi wanajitahidi kufanya kama unavyofanya lakini wengi hawafanyi kwa kujitolea kama unavyofanya.Nimeguswa zaidi sana na huu mradi wa kujenga shule ya watoto wenye ulemavu wa kutoona na kutosikia ambao unautafutia fedha.Naona tuanzie hapo nataka kupata taarifa za kina kuhusiana na mradi huo na wapi umefikia hadi sasa na nini kinahitajika na kama kuna miradi mingine pia ningependa kuifahamu ni ipi na nini kinahitajika.Watu kama ninyi mnatakiwa kuungwa sana mkono kwa kila hali” akasema David na kunywa funda la mvinyo. “ Ahsante sana mheshimiwa rais kwa kunikaribisha usiku huu .Ni heshima kubwa umenipa ya kunikaribisha mahala hapa .Ahsante kwa chakula kizuri.Vile vile napenda nikushukuru sana kwa kuonyesha kuguswa na baadhi ya kazi ninazozifanya hususani mradi huu wa ujenzi wa shule ya watoto wenye ulemavu wa kutoona na kutokusikia.Msaidizi wako Jean Pierre Muyeye aliniambia kwamba kama usingekuwa na mkutano leo hii nawe ungehudhuria mbio hizo” akasema Monica na kuachia tabasamu “ Ni kweli Monica laiti kama nisingekuwa na kikao leo hii ningeungana nawe katika mbio hizo lakini kwa vile sikuwa na nafasi nikalazimika kumtuma Muyeye aje aniwakilishe” akasema David “ Ahsnate sana mheshimiwa David kwa ushiriki wako.Kwa ufupi tu ni kwamba mimi nina taasisi ambayo hushughulika kutatua matatizo mbalimbali ambayo imejielekeza zaidi katika matatizo ya watoto na wazee wasiojiweza ambao ni kundi linaloonekana kusahaulika sana.Tumekuwa tukitoa misaada mbali mbali mahospitalini kusaidia watoto wadogo na hata wazee kwa kuwajengea makazi bora,kuwasaidia huduma za afya
chakula na mambo mengine .” akanyamaza akameza mate na kuendelea “ Katika utafiti tulioufanya tumegundua kuna kundi moja limesahaulika sana ni la watoto wenye ulemavu wa kutoona na kutosikia kwa pamoja.Kundi hili linazidi kuongezeka na kwa takwimu tulizonazo ni zaidi ya watoto mia nne na hamsini wenye ulemavu wa aina hii.Tumegundua watoto wenye ulemavu wa aina hii wanakumbana na changamoto nyingi sana katika maisha yao kwa hiyo kwa vile jukumu la taasisi yangu ni kuwahudumia watoto tumeamua kulibeba jukumu hili la kuwasaidia watoto wenye aina hii ya ulemavu kwa kuwajengea shule yenye miundo mbinu rafiki na ambamo wataishi na kutapata elimu na malezi.Ujenzi wa shule unakadiria kugharimu zaidi ya shilingi bilioni mia tatu za kitanzania.Itakuwa ni shule ya aina yake na tunategemea kuifanya iwe ya kimataifa kwani kwa miaka ya mbele tutakuwa tukipokea watoto kutoka hata katika nchi nyingine jirani ” Monica akanyamaza akanywa funda dogo la mvinyo akaendelea “ Tumejaribu kutafuta wafadhili kutoka nje ya nchi lakini tumejikuta tukikumbana na vikwazo mbalimbali hivyo nikaona ni bora kama tukijitajidi kufanya jambo hili wenyewe kwa kuanzia na nguvu zetu kidogo tulizonazo.Kwa hiyo tumeazimia kufanya mambo kadhaa ili kukusanya fedha za kuanza ujenzi wa shule hiyo .Tumeazimia kufanya mambo matatu.Kwanza ni kuandaa mbio za nusu marathoni ambazo zimefanyika leo na kushirikisha watu toka nchi mbalimbali maalum kabisa kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa shule hii na ninashukuru muitikio umekuwa mkubwa na tumevuka lengo tulilokusudia kukusanya.Huu umekuwa ni mwanzo mzuri sana .Baada ya mbio tutaandaa onyesho la mavazi ambalo nalo litakuwa maalum kwa ajili ya kukusanya fedha .Litakuwa ni onyesho kubwa kuwahi kufanyika afrika mashariki kwani tumewaalika wabunifu na wanamitindo wakubwa duniani na lengo likiwa kutunisha mfuko wa ujenzi wa shule hii.Baada ya onyesho hilo la mavazi tutaandaa pia chakula maalum tutakachowakaribisha watu mbali mbali viongozi wa serikali,mashirika na watu binafsi ambao watachangia fedha.Baada ya matukio hayo matatu ninaamini tutakuwa na kiasi cha kutosha kutuwezesha kuanza ujenzi wa shule hiyo.Kwa hiyo mheshimiwa rais hiyo ndiyo mipango ambayo mimi na taasisi yangu tumepanga kuifanya ili kuweza kupata fedha za ujenzi wa shule hiyo ya watoto wenye ulemavu wa kutoona na kusikia” akasema Monica na kuinua glasi ya mvinyo akanywa funda dogo kama kawaida yake .David Zumo naye akanywa funda kubwa la mvinyo na kusema “ Hongera sana Monica .U mwanamke jasiri sana ambaye juhudi zako zinastahili kuungwa mkono.Umeonyesha ujasiri mkubwa na kwa hilo lazima nikupongeze.Kama nilivyokueleza awali kwamba mimi nimeguswa sana na jambo hili na niko tayari kukusaidia.Fedha zinazohitajika kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo ni nyingi na pengine baada kukusanya fedha katika matukio hayo yote matatu fedha zinaweza zisitoshe .Kabla sijasema kiasi ambacho mimi nitachangia katika ujenzi huo unategemea kupata kama shilingi ngapi katika matukio hayo yote matatu? “ Tunatarajia kukusanya kiasi cha shilingi bilioni ishirini hadi hamsini.” “ Ni kiasi kidogo sana ambacho itachukua muda mrefu kuikamilisha shule hiyo.Ninaiona kiu ya kutaka kuimamilisha shule hiyo kwa wakati lakini kikwazo kitakuwa ni fedha.Mimi kwa upande wangu nitachangia kiasi cha shilingi bilioni mia mbili na sabini .Nina hakika kwa kiasi hicho hatua kubwa itakuwa imepigwa “ akasema David.Monica akapatwa na mstuko hakuwa ametegemea kama David Zumo angeweza kuchangia kiasi kikubwa kama kile cha fedha.Kwa sekunde kadhaa akabaki ameduwaa akimtazama David aliyekuwa akitabasamu halafu akainuka na kwenda kumpa mkono
“ Mheshimiwa rais ahsante sana kwa msaada huu mkubwa ambao sikuwa nimeutarajia kabisa.Kiasi hiki kikubwa ulichokitoa kinakwenda kuimaliza kabisa shule hiyo.Ahsante sana mheshimiwa rais na sijui hata nikushukuruje kwa msaada huu mkubwa.Watu wa Kongo wana bahati sana kukupata rais mwenye moyo wa huruma kama wewe” akasema Monica na kwa furaha aliyokuwa nayo akashindwa kujizuia kutoa machozi.Akatoa kitambaa na kufuta machozi. “ Samahani mheshimiwa rais ni kawaida yangu kila ninapokuwa na furaha iliyopitiliza hushindwa kujizuia machozi kunitoka “ akasema Monica “ Usijali Monica.Toka moyoni nimeguswa sana na jambo hili unalolifanya na ndiyo maana niko tayari kutoa kiasi chochote cha mchango kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye matatizo mbalimbali.Mungu ametujaalia wachache kuwa na utajiri ili tuutumie utajiri huo kwa wale masikini wasiokuwa na uwezo .Kwa hiyo ninatamini sana katika kusaidia watu masikini na ninawapenda sana wale wanaojitolea kuwasaidia watu masikini. Kwa hiyo naomba ufahamu kuwa mchango huu mdogo nilioutoa nimeutoa kwa moyo mmoja na si kwa sababu ya utajiri nilio nao.” Akasema David Zumo “ David huu si mchango mdogo kama unavyosema .Ni mchango mkubwa sana na ninaiona namna ndoto yangu ya kuwasaidia watoto hawa wenye mahitaji makubwa.Ahsante sana mheshimiwa rais kwa kuifanya ndoto yangu iwe kweli.Nimeupokea mchango huu kwa moyo mmoja na ninakuahidi kiasi hiki cha fedha ulichokichangia kitatumika kama kilivyokusudiwa” akasema Monica “ Monica mimi niko pamoja nawe na nitakuunga mkono katika kila jambo ambalo umekusudia kulifanya kwa jamii yako.Ukiacha shule hii unayotarajia kujenga ,ni jambo lipi ambalo umekusudia kulifanya iwapo ungepata fedha za kutosha? Akauliza David Zumo “ Kwa sasa akili yangu nimeielekeza katika shule hii ya watoto hawa wenye mahitaji maalum lakini kuna mambo mengi ambayo kama ningekuwa na fedha za kutosha ningeweza kuyafanya .Kuna jambo ambalo nimekuwa nalifikiria pia nalo ni kuhusu kujenga kambi za wazee.Hii ni sehemu kubwa ya jamii ambayo imeonekana kusahaulika kabisa.Wazee wanapata wakati mgumu sana na imefikia hatua uzee unaonekana ni kama adhabu.Nataka kuwe na kambi kwa ajili ya kuwatunza wazee katika kila mkoa ambako watapatiwa huduma mbali mbali na watakuwa na uzee mzuri.Hiyo ni ndoto yangu nyingine baada ya kumaliza kwanza suala hili la shule ya watoto wenye uhitaji” akasema Monica “ Monica naomba ufahamu kuwa siku zote mimi nitakuwa pamoja nawe katika mipango yako yote na nihesabu kama mdau namba moja wa miradi yako ya kusaidia jamii na nitawaleta pia wadau wengine rafiki zangu ambao kwa pamoja tutakupa ushirikiano mkubwa.Kitu cha msingi unachotakiwa kufanya ni kuwa na mawasiliano ya karibu na kila pale unapohitaji msaada Fulani usisite kuniambia.” Akasema David “ Ahsante sana mheshimiwa rais sintasita kukutaarifu jambo lolote au kila pale nitakapokuwa nimekwama katika kitu chochote.Ahsante sana kwa kuwa msaada mkubwa kwangu.Ni Mungu pekee ndiye atakayekulipa kwa namna ulivyojitoa kusaidia watu wake wenye matatizo mbali mbali” akasemaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ Dah !! siamini macho yangu.Nilikuwa nazungumza na binadamu au malaika? Akajiuliza David kisha akajimiminia tena mvinyo na kuunywa wote “ Monica si binadamu wa kawaida .Kwa muda huu mfupi niliokaa naye nimegundua kwamba ni binadamu wa kipekee kabisa.Nimekutana na wanawake wengi lakini sijawahi kukutana na mwanamke yeyote mwenye walau kuukaribia uzuri wa Monica.Huyu ni mwanamke ambaye sintakubali nimkose katika maisha yangu.Nitafanya kila niwezalo hadi nihakikishe nimempata Monica.” Akasema David na kunywa tena mvinyo.Alionekana ni kama mtu aliyechanganyikiwa alikuwa anazunguka zunguka mle sebuleni. “ Nimeanzisha vita lazima nihakikishe ninaimaliza na ninashinda.Ninasema ni vita kwa sababu naamini Monica anawachanganya wanaume wengi kwa uzuri wake na wengi lazima wameweka ahadi kama yangu ya kuhakikisha wanampata kwa hiyo lazima kuna ushindani mkubwa hapa na ndiyo maana nikasema kwamba hii ni sawa na vita ya kumgombania mwanamke.Najua lazima atakuwa na mpenzi wake na ni wazi huyo mpenzi wake lazima atakuwa ni mtu mwenye fedha nyingi lakini lazima atapambana na mimi tajiri namba moja afrika kwa hiyo hakuna tajiri anayeweza kuniumiza kichwa mimi na hakuna mwanamke anayeweza kukataa kuogelea katika bahari ya utajiri labda awe malaika.Hata Monica nina hakika hana ubavu wa kunikataa.Lakini hata hivyo ninatakiwa kujenga mazoea ya karibu sana na wazazi wake.Nikifanikiwa kuwaweka karibu wazazi wake basi nitakuwa nimeshinda vita hii bila kutumia nguvu kubwa.” Akawaza David na kunywa tena funda kubwa la mvinyo “ Monica lazima awe wangu...Nitakuwa mwanaume mwenye furaha sana duniani kama nitakuwa na Monica mwanamke ambaye hata mke wangu ambaye niliamini ni mzuri kuliko wote niliowahi kuwaona hamfikii hata robo.Utajiri nilionao utakuwa na maana kama nitampata Monica.” Akaendelea kuwaza David Zumo.
aada ya kutoka kuonana na rais David Zumo,Monica alimuelekeza Jean Pierre Muyeye ampeleke moja kwa moja nyumban kwa wazazi wake.Usiku huu hakutaka kwenda nyumbani kwake. “ Huu ni kama muujiza kwangu,sikuwa nimetegemea kabisa kupata kiasi hiki kikubwa cha fedha kwa haraka namna hii ili kukamilisha mradi ule mkubwa.Nilikuwa na uhakika wa kuzipata lakini sikujua ningezipataje.Ahsante Mungu kwa kuendelea kusimama nami na kunifanikishia mambo yangu.” Akawaza Monica wakati safari ya kurejea nyumbani ikiendelea “ David Zumo ..” akawaza na kutabasamu baada ya picha ya David kumjia kichwani “ Nimepata bahati ya kipekee ya kukutana uso wa uso na rais huyu mwenye sifa lukuki na kikubwa zaidi ana roho nzuri pengine kupita marais wote . Ni rais ambaye amelifanya taifa la Kongo kuwa taifa kubwa afrika.Uchumi wake umepaa kwa kasi kubwa.Naweza kusema kwamba raia wa Kongo wana bahati sana ya kumpata rais mpenda watu kama huyu.Ni rais anayeguswa na matatizo ya watu.” Akawaza Monica na kukumbuka maongezi yake na David. “Toka moyoni nimeguswa sana na jambo hili unalolifanya na ndiyo maana niko tayari kutoa kiasi chochote cha mchango kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye matatizo mbalimbali.Mungu ametujaalia wachache kuwa na utajiri ili tuutumie utajiri huo kwa wale masikini wasiokuwa na uwezo .Kwa hiyo ninatamini sana katika kusaidia watu masikini na ninawapenda sana wale wanaojitolea kuwasaidia watu masikini. Kwa hiyo naomba ufahamu kuwa mchango huu mdogo nilioutoa nimeutoa kwa moyo mmoja na si kwa sababu ya utajiri nilio nao.”. Maneno haya ya David Zumo yakaendelea kuzunguka katika kichwa cha Monica. “ Ni wazi alitoa mchango wake huu kwa moyo na wala si kwa utajiri alionao.Sijui nitamshukuruje mtu huyu.Sioni namna bora ya kumshukuru zaidi ya kumuombea ili awe na moyo huo huo wa kusaidia watu wenye matatizo mbali mbali “ akaendelea kuwaza Monica. Alifika nyumbani kwa wazazi wake akaagana na akina Muyeye akaelekea ndani.Benedict na mkewe tayari walikuwa wamelala Monica akawaamsha.Walishangazwa sana na ujio ule wa Monica usiku ule. “Monica is everything ok my dear? Akauliza Bi Janet mama yake Monica kwa wasi wasi “ Msihofu jamani hakuna tatizo” akajibu Monica kuwatuliza wazazi wake walioanza kuwa na wasi wasi “ Samahani kwanza kwa kuwaamsha ila nisingeweza kulala bila kuja uonana nanyi usiku huu” akasema Monica “ Kwani kuna nini Monica? Akauliza Bi Janet “ Nimetoka kuonana na rais wa jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo David Zumo” akasema na kunyamaza
Nini kimetokea huko? Akauliza bi Janet aliyeonekana kuwa na shauku kubwa ya kutaka kufahamu kilichojiri “ Mambo yamekwenda vizuri sana.Nimeonana na David tumeongea na kikubwa alichohitaji kuonana nami ni kwa ajili ya kuchangia katika mradi wangu wa shule .Alitaka kufahamu nimefikia wapi kuhusu mradi huo nikamueleza hatua ninazochukua kukusanya kwanza fedha kabla ya kuanza ujenzi.Baada ya kumpa mchanganuo wote wa mradi ndipo akatoa mchango wake.Gharama nzima ya mradi ni kiasi cha shilingi bilioni mia tatu na yeye ametoa mchango wa shilingi bilioni mia mbili na sabini “ akasema Monica na kumkumbatia mama yake “ Wow !! this is wonderfull !! akasema bi Janet akiwa na mshangao “ Bilioni mia mbili na sabini!!!..akasema mzee benedict naye akiwa katika mshangao “ Mwanangu una bahati kubwa sana.Katika dunia ya leo hakuna binadamu anayeweza akakupatia kiasi kikubwa kama hicho cha pesa.Huyu rais ni mtu mwenye moyo wa ajabu sana.” Akasema mzee Benedict “ Ni kweli baba.Hata mimi mpaka sasa bado naona jambo hili ni kama ndoto lakini ni kitu cha kweli kabisa” akasema Monica na machozi yakaanza kumtoka baba yake akamkumbatia na kumfuta machozi “ Ouh my queen you are crying again” akasema mzee benedict “ I cant help it dady.Nina furaha iliyopitiliza.Ndoto yangu ya muda mrefu inakwenda kutimia.Nilikuwa naumiza kichwa sana namna nitakavyoweza kupata fedha za kuniwezesha kuijenga shule hiyo,nilikuwa namlilia Mungu sana na amesikia kilio change na hatimaye fedha zimepatikana” akasema Monica “ Monica unapaswa kumshukuru sana Mungu kwani amekupa upendeleo wa ajabu.Kila uchao anazidi kukufungulia milango ya mafanikio.Anazina juhudi zako na moyo wako wa kusaidia watu wenye matatizo mbali mbali na ndiyo maana amekuwa anakubariki kila siku” “ Usemayo ni ya kweli kabisa baba.Ninapaswa kumshukuru sana Mungu kwa Baraka zake hizi.Hiki kilichotokea leo naona ni kama muujiza tu.Sikuwa nimetegemea kama David Zumo angeweza kutoa kiasi hiki kikubwa cha fedha.Nimezoea kupewa msaada wa milioni kadhaa lakini si mabilioni mengi kama haya.” “ Monica Yule ni rais na vile vile ni tajiri namba moja kwa hiyo ulikuwa unazungumza na mtu mkubwa sana na si wale uliowazoea wa kutoa ahadi za milioni moja moja.Huyu ni mtu mzito na ndiyo maana ametoa mchango mkubwa kulingana na uwezo wake” “ Ukiacha mchango alioutoa kwa ajili ya shule ,ameahidi pia kunipa ushirikiano nitakapoanza ule mradi wangu wa kujenga makambi ya wazee katika kila mkoa.David ni mtu anayeonekana kuguswa sana na matatizo ya watu wanyonge na ndiyo maana hata watu wa nchi yake wanampenda na wamekubali kubadili vifungu vya katiba ili David atawale kwa miaka mingi.Tukiachana na hayo kuna jambo lingine” akasema Monica na kunyamaza
Jambo gani hilo Monica? Akauliza Bi Janet “ David anahitaji kuonana nanyi kesho jioni” Mzee Ben na mkewe wakatazamana “ Anataka kuonana nasi? Kuna nini kwani? Akauliza mzee Ben kwa furaha iliyochanganyika na wasi wasi “ Hakuna chochote kibaya ila anahitaji tu kuwafahamu.Aliniuliza kama wazazi wangu bado wako hai nikamjibu ndiyo akasema kwamba anahitaji kuwafahamu” akasema Monica “ Wow ! tutakwenda kuonana naye.Huu ni mwaliko mkubwa sana.Ni heshima kubwa kualikwa na mtu mkubwa kama huyu.Tutakwenda kuonana naye hiyo kesho” akasema mzee Ben. Baada ya maongezi yaliyochukua takribani saa nzima Monica akaenda kulala katika chumba chake kilichopo hapo katika nyumba ya wazazi wake Alijitupa kitandani lakini macho hayakuonyesha dalili zozote za kupata usingizi.Kuna kitu kimoja tu ambacho kilikuwa kimejaa kichwani kwake ni David Zumo. “ Sijawahi kukutana na mtu mwenye roho nzuri kama David.Ni tajiri namba moja afrika lakini hana majivuno ni mcheshi na kinachonivutia zaidi kwake ni moyo wa huruma alio nao kuweza kusaidia watu wenye matatizo mbali mbali.” Akawaza Monica akiendelea kujigeuza kitandani. “ Kukutana na kujenga urafiki na mtu kama David ni mwanzo wa kuelekea katika mafanikio makubwa na kutimiza ndoto zangu nyingi nilizonazo.Hii naweza kusema kwamba ni bahati ya kipekee sana kuwa na ukaribu na mtu kama huyu ambaye anaweza kunifanikishia mipango yangu mingi ya kusaidia jamii masikini.Naamini nikipata nafasi ya kutosha ya kuongea naye kuna mambo mengi ambayo anaweza akanisaidia kama vile kujenga zahanati kwa ajili ya akina mama vijijini mahala ambako kuna changamoto kubwa ya huduma za afya nk.” Kichwa cha Monica kilikuwa na mawazo mengi sana kuhusiana na David Zumo na ilimchukua muda mrefu kupata usingizi.
Japokuwa hakuweza kupata usingizi wa kutosha usiku kutokana na kichwa chake kujawa na mawazo mengi lakini Monica aliwahi kudamka asubuhi akajiandaa kwa ajili ya kuianza siku.Alipata kifungua kinywa kabla hata ya wazazi wake hawajaamka kisha akatumia gari la mama yake akaelekea nyumbani kwake .Alisalimiana na wafanyakazi wake kama ilivyo ada halafu akaelekea chumbani kwake ambako alioga na kubadili mavazi akajiweka tayari kwa ajili ya kwenda kazini.Wakati akiendelea kujiandaa simu yake ikaita.Akaichukua na kutazama mpigaji zilikuwa ni namba ngeni kabisa katika simu yake. “ Hallow “ akasema baada ya kubonyeza kitufe cha kupokelea “ Hallow Monica” ikasema sauti ya upande wa pili ambayo Monica aliweza kuitambua mara moja ilikuwa ni sauti ya David Zumo “ Mheshimiwa rais ..!! akasema Monica “ Umeamkaje Monica? ‘ Nmeamka salama Mheshmiwa rais ,sijui wewe” “ Mimi niko salama.Nimeona nikupigie asubuhi hii kujua maendeleo yako” “ Nashukuru sana mheshimiwa rais kwa kunijulia hali.Ninaendelea vizuri “ akasema Monica huku sura yake ikiwa na tabasamu kubwa “ Nafurahi kusikia hivyo Monica.Nataka nikushukuru vile vile kwa kukubali mwaliko wa kuja kuonana nami jana” “ Mheshimiwa rais mimi ndiye ninayepaswa kukushukuru kwa kunialika jana na kwa mchango mkubwa ulionichangia.” “ Usijali Monica huu ni mwanzo tu wa kukuunga mkono katika juhudi zako za kusaidia watu wenye uhitaji.Nitashirikiana nawe katika mambo mengi.” Akasema David Zumo “ Ahsante sana mheshimiwa rais” “ Monica leo tunamaliza mkutano wetu wa wakuu wa nchi za maziwa makuu lakini sintaondoka kwani nilikuahidi kwamba ninahitaji kuonana na wazazi wako jioni ya leo.Nitafurahi zaidi iwapo utaongozana nao” “ Usijali mheshimiwa rais nitakuja nao .Tunashukuru sana kwa heshima hii kubwa unayotupa familia yetu” akasema Monica “ Haya nashukuru sana Monica .Tutaonana hiyo jioni” akasema David Zumo na kukata simu. “ oh my gosh !! He called me ....” Akasema Monica kwa furaha akiwa ameiweka mikono yake kifuani “ Sikutegemea kama David Zmo anaweza akanipigia simu.Huyu ni mtu mkubwa sana kunipigia simu mtu kama mimi ni heshima kubwa.Ninajiona mwenye bahati kubwa kuwa na ukaribu na mtu kama huyu.” Akawaza Monica na kuchukua mkoba wake akatoka kuelekea ofisini kwake. Akiwa garini bado kichwa cha Monica kiliendelea kujawa na mawazo mengi kuhusiana na David Zumo na hasa msaada mkubwa aliomsaidia. “ Its like I’m going crazy.David zumo amenikaa kichwani kwangu ghafla na kila dakika namuwaza yeye tu. Nadhani ni kutokana na ukarimu wake wa ajabu.” Akawaza Monica akiendelea na safari ya kuelekea ofisini kwake. Aliwasili ofisini kwake na kusalimiana na wafanyakzi wake kama kawaida yake na kisha akaelekea ofisni
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
.Mara tu alipoingia ofisini kwake akakuta kuna bahasha nyeupe juu ya meza ,akaitazama ilikuwa imeandikwa jina lake.Akamuita Linah msaidizi wake akamuuliza kuhusiana na bahasha ile “ Madam bahasha hii imeletwa na mtu jana usiku na kwa vile hakukuwa na mtu yeyote akaiacha getini kwa walinzi.Nilipofika asubuhi nikakabidhiwa ili nikupe” “ Ni nani huyo mtu ? hakutaja jina lake? Akauliza Monica “ Kwa mujibu wa walinzi mtu aliyeleta bahasha hiyo hakutaja jina lake” akasema Linah.Monica akaishika bahasha ile akaifungua taratibu akakutana na faili ambalo llikuwa na jina na picha ya Marcelo Richard. “ Dr Marcelo !! Hili mbona linaonekana ni faili la hospitali ? akajiuliza Monica na kulifungua akaanza kulisoma.Faili lile lilikuwa na taarifa za Dr Marcelo ambazo zilionyesha kwamba alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya saratani ya damu. “ oh my God !! is this true?? Akajiuliza Monica na kuanza kulipitia tena “ Nani kaleta hili faili hapa na kwa makusudi gani? akajiuliza Monica na kuanza tena kulipitia lile faili.Alihisi kijasho kinamtoka. “ Yeyote aliyelileta faili hili hapa lazima lengo lake lilikuwa ni ili nifahamu kuhusu ugonjwa huu wa Dr Marcelo.Nani basi anayeweza kufanya kitu kama hiki? Kama lengo lake ni mimi kufahamu kuhusu ugonjwa wa Dr Marcelo anataka nini kitokee? Akaendelea kujiuliza. “ Kwa nini Dr Marcelo hajanieleza kuhusu maradhi yanayomsumbua? Aliogopa nini kunieleza? Au inawezekana kwa sababu tumefahamiana hivi karibuni ndiyo maana hakuwa tayari kunieleza .Ngoja nimpigie simu nimuulize kuhusiana na faili hili na namna lilivyofika hapa” akawaza Monica na kuchukua simu zake akatafuta namba za Dr Marcelo akapigia.Simu ikaita mara ya kwanza na kukatika bila kupokelewa,akapiga tena mara ya pili lakini haikupokelewa.Akaingiwa na wasi wasi “ Kwa nini hapokei simu? Inawezekana labda anatazama wagonjwa? Akajiuliza Monica na kujaribu kupiga tena.Safari hii ikapokelewa lakini Dr Marcelo aliongea kwa sauti ya chini kidogo na Monica akagundua utofauti katika sauti yake “ Hallow Monica” akasema Dr Marcelo. “ Dr Marcelo uko wapi? “ Monica nilipatwa na matatizo kidogo niko hapa kituo cha polisi” “ Nini kimetokea Dr Marcelo? Akauliza Monica “ Jana usiku nikiwa katika zamu ya kuwatazama wagonjwa kuna watu walivamia nyumbani kwangu na kuchukua baadhi ya vitu vyangu vya kwa hiyo nimekuja hapa polisi” akasema Dr Marcelo na Monica akabaki kimya. ‘ Monica “ akaita Dr Marcelo “ Dr Marcelo I need to see you now” akasema Monica “ Monica kuna nini ? “ Dr Marcelo naomba tuonane sasa hivi kuna suala la muhimu sana nataka tuongee” akasema Monica.Dr Marcelo akafikiri kidogo na kusema “ Sawa Monica uko wapi sasa hivi? “ Niko hapa ofisini kwangu”
Nisubiri ninakuja hapo sasa hivi” akasema Dr Marcelo “ Hapana usije hapa naomba tukutane Savana Garden” akasema Monica na kukata simu akavuta pumzi ndefu “ Faili hili ninahisi linaweza kuwa ni moja ya vitu vilivyoibwa toka nyumbani kwa Dr Marcelo jana usiku na likaletwa hapa.Laiti kama tungeweza kumpata mtu aliyelileta hapa ingekuwa rahisi sana kumfahamu aliyevunja nyumbani kwa Dr Marcelo.Lakini nini hasa lengo la huyu mtu kunionyesha faili hili? Akaendelea kujiuliza bila kupata majibu akalichukua faili lile na kuondoka kuelekea mahala alikopanga akutane na Dr Marcelo.Njiani alijaribu sana kuwaza kuhusiana na mtu aliyelileta faili lile ofisini kwake na kusudio lake lakini hakuweza kupata jibu. “ Najaribu sana kuwaza bila kupata jibu nini hasa lengo la huyu mtu kuniletea faili hili? Lakini kuna mtu mmoja tu ambaye akili yangu inanituma kwamba ndiye anaweza kuwa amefanya jambo hili .Ni Daniel.Hakupenda kabisa ukaribu wangu na Dr Marcelo na alidiriki hata kumfuata na kumtolea vitisho akimtaka aachane kabisa na mimi akidai kwamba mimi ni mpenzi wake.Ni yeye tu anayeweza akafanya jambo kama hili na lengo lake kubwa ni kunitenganisha mimi na Dr Marcelo.Alitaka nifahamu kuhusiana na ugonjwa wa Dr Marcelo “ akawaza Monica. “ NI wazi lengo lake ni hilo kwamba nifahamu Dr Marcelo ni mgonjwa wa saratani ya damu na kwamba hana maisha marefu sana .Ouh poor Daniel kwa nini amefanya hivi? Nina hakika ni yeye tu hakuna mwingine anayeweza akafanya jambo la kijinga kama hili” akawaza Monica akachukua simu na kuzitafuta namba za simu za Daniela akampigia “ Monica” akasema Daniel kwa mshangao kidogo baada ya kupokea simu “ Daniel uko wapi? Akauliza Monica “ Bado niko nyumbani najiandaa kuelekea katika shughuli zangu.Wewe uko wapi? “ Naomba usitoke ninakuja hapo hapo nyumbani kwako sasa hivi” “ Kuna nini Mon....” akasema Daniel lakini kabla hajamaliza Monica akakata simu “ Kwa hiki Daniel alichokifanya ananifanya nimchukie zaidi na zaidi.Hakuna analoweza kulifanya kunitenganisha na Dr Marce....” Akawaza Monica na kustuka “ Masikini Marcelo.Kwa nini hakutaka kunieleza mapema kuhusiaana na kile kinachomsumbua? Aliogopa nini kunieleza kama ana maradhi ya saratani ? Japo ameniudhi kwa kunificha kuhusu hali yake ya kiafya lakini nimeumia sana kwa kuufahamu ugonjwa alionao.Nina wasi wasi sana pengine hatakuwa na maisha marefu.It hurt so much.Nimefahamiana naye hivi karibuni na tayari moyo wangu ulikwisha anza kumpenda kwa sababu ana sifa zote za mwanaume wa ndoto zangu lakini baada ya kuyafahamu maradhi yake yanayomsumbua kumeniweka njia panda.Nashindwa kufanya maamuzi.” Akawaza Monica na kwa mbali macho yake yakaonekana kuwa na michirizi ya machozi “ Nina mafanikio makubwa katika kila ninachokifanya lakini sijawahi kupata mafanikio katika masuala ya mapenzi.Mpaka leo bado sijabahatika
kumpata mwanaume ambaye ataufanya moyo wangu usimame.Kidogo Dr Marcelo alikuwa anakaribia kufikia vigezo vyangu na niliamini ni mwanaume pekee anayeweza kunifaa lakini suala hili la ugonjwa tayari limeweka doa mipango yangu.It’s obvious siwezi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Dr Marcelo tena badala yake ataendelea kuwa rafiki yangu wa karibu sana.Inaniuma lakini sina namna nyingine ya kufanya.Yawezekana labda Marcelo hakuwa fungu langu ,sintokata tamaa nitaendelea kumlilia Mungu ili siku moja aniletee mwanaume ambaye amemuandaa kwa ajili yangu.” Akaendelea kuwaza Monica Aliwasili katika makazi ya Daniel,akafunguliwa geti akaingia ndani ,akashuka garini na moja kwa moja akaelekea sebuleni.Daniel akataarifiwa kuwa Monica tayari amekwisha wasili akashuka haraka kwenda kuonana naye. “ Monica ..’ akasema Daniel kwa furaha huku uso wake ukiwa katika tabasamu ,akamsogelea Monica na kutaka kumkumbatia ,akamzuia “ Monica kuna tatizo gani? Mbona unaonekana hauko sawa? Akauliza Daniel.Monica akamtazama kwa macho makali na kulitupa lile faili mezani “ Daniel mimi na wewe tumekuwa watu wa karibu sana na sikutegemea kabisa kama ungeweza ukafanya kitu cha kijinga kama hiki ulichokifanya.” Akasema Monica kwa ukali Daniel akabaki na mshangao “ Monica kuna nini? Akauliza Daniel “Unajifanya hujui ulichokifanya? Ninashukuru ulichotaka nikifahamu nimekifahamu lakini nakuhakikishia kwamba hautakipata kamwe ulichokikusudia.” Akasema Monica.Daniel akalichukua lile faili na kulifungua,sura yake ikaonyesha mstuko mkubwa “ Monica what is this? Akauliza Daniel “ Unajifanya hujui kilichomo humo? Akauliza Monica “ Monica hili ni faili linalomuhusu Dr Marcelo !! “ Ulitaka nifahamu kuhusu ugonjwa wa Dr Marcelo ? Nashukuru umenisaidia nimeufahamu lakini nakuhakikishia kwamba jambo unaloliota katu halitakuwa.Ulitaka niufahamu ugonjwa wake ili nisiwe karibu naye kwani lengo lako ni kuwa na mimi lakini nakuhakikishia kwamba kwa hilo umekosea sana.Mimi nitaendelea kuwa na Dr Marcelo kwani ni mtu ambaye nimemchagua kuwa rafiki yangu wa karibu na hata kama nikiamua kuingia katika mahusiano naye ya kimapenzi hakuna wa kunizuia kwa hilo na sintojali ugonjwa wake kwani ndiye mwanaume anayenifaa . “ akasema Monica kwa hasira “ Monica naomba unisikilize kwa makini.Mimi sijafanya jambo kama hili na katu siwezi kufanya kitu kama hiki za zaidi ya yote nimekuwa karibu na Dr Marcelo na sikuwahi kulifahamu jambo hili.Hajawahi kunieleza kama anasumbuliwa na maradhi ya saratani ya damu.Kingine ni kwamba ni kweli mimi na Dr Marcelo tulipishana kauli lakini sina sababu yoyote ya kufanya hivi hata kama ningekuwa nafahamu kuhusu ugonjwa wake.Nimekuwa nawe karibu kwa muda mrefu unanifahamu vizuri sina tabia kama hivi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwanza jana usiku nilikuwa nyumbani toka saa moja za jioni tulikuwa na kikao cha familia sasa ningewezaje kufanya kitu kama hicho? Believe me Monica..” akasema Daniel Monica akamtazama kwa makini na kuichukua bahasha ile “ Daniel tafadhali naomba ukae mbali kabisa nami.I don’t want you near me anymore.Tabia zako ni chafu na siwezi kuwa na ukaribu na mtu mwenye tabia chafu kama zako.” Akasema Monica kwa hasira akaanza kupiga hatua kutoka mle ndani “ Monica please..!! akasema Daniel na kumkimbilia Monica akamshika mkono “ Daniel please don’t ever touch me !!! akasema kwa ukali na mara toka ndani akatoka mwanamke mmoja akiwa amevaa nguo za ndani pekee.. “ Daniel whats going here?? And who is she??Akauliza Yule mwanadada mweupe mwenye nywele ndefu “ Margreth please go inside..!! akasema Daniel kwa ukali lakini yule mwanadada akazidi kumsogelea Daniel na Monica ambaye alisimama kwa hasira “ Daniel kuna tatizo lolote na huyu kahaba? Akauliza Margreth .Kwa hasira Monica akamnasa kibao kikali na kuondoka akaelekea katika gari lake,Daniel akamfuata na kumtaka waongee lakini Monica hakuwa tayari akawasha gari na kuondoka kwa hasira. “ Kwa mara ya kwanza leo katika maisha yangu nimeitwa kahaba.Sijawahi kukosewa heshima kiasi hiki.Lakini kwa kofi lile nililomnasa Yule kahaba nadhani nimemtendea haki.Tabia ya Daniel ni chafu sana na sitaki kabisa kuwa karibu naye.Nina hakika baada ya maneno yale niliyomweleza hatathubutu kunikaribia tena.Lakini..” Akawaza Monica na kusita kidogo “ Nimemtazama Daniel machoni he’s not the one who did this.Ukilichukulia kwa haraka haraka suala hili unaweza ukadhani labda Daniel ndiye muhusika mkuu na usipokuwa makini unaweza hata kumchukulia hatua lakini Daniel hahusiki kabisa na hiki kilichotokea.Ni nani basi aliyefanya hivi? Akaendelea kujiuliza Monica “ Nina hakika kabisa aliyefanya jambo hili lengo lake kubwa ni kutuvuruga mimi na Dr Marcelo tusiwe na mahusiano lakini ni nani huyu na kwa nini anataka mimi na Dr Marcelo tusiwe karibu?? Swali hili likamuumiza sana kichwa. Aliwasilli Savana Garden moja kati ya sehemu nzuri na tulivu,watu wengi hupenda kuja kupumzika hapa,kuna bustani nzuri ya majani na miti.Aliegesha gari na kufungua mlango na kabla hajashuka akatokea Dr Marcelo “ Monica” akasema Dr Marcelo “ Dr Marcelo umeshafika” “ Nimefika kitambo sana.Habari yako? “ Habari yangu nzuri.Habari yako nawe? Akauliza Monica huku akiufunga mlango wa gari wakaongozana kutafuta sehemu ya kukaa. “ Pole sana Dr Marcelo kwa mkasa uliokukuta.” Akaanzisha maongezi Monica “ Ahsante Monica.Kama nilivyokueleza simuni, jana nilikuwa katika zamu ya usiku nikiwatazama wagonjwa na nilipofika nyumbani nikakuta kasiki langu ambalo huhifadi vitu vyangu vya muhimu liko wazi na baadhi ya vitu vyangu havipo.
Hakuna mlango au sehemu yoyote iliyovunjwa ila kasiki langu nimelikuta wazi na vitu vyangu vy amuhimu havipo.Mtu aliyefanya uhalifu huo lazima atakuwa ni mtu anayenifahamu vyema hadi akazifahamu namba za siri za kufungulia kasiki langu” “ Pole sana .Ni vitu gani walivyovichukua ? akauliza Monica na Dr Marcelo akasita kidogo “ Uhhm wamechukua vitu vyangu vya muhimu .Kuna faili langu lenye nyaraka muhimu sana pamoja na baadhi ya vitu vingine.” “ Unaishi na nani? Nyumbani kwako hakuna ulinzi? Akauliza Monica “ Hapana sijaweka mlinzi.Ni sehemu salama sana na ndiyo maana sina haja ya kuweka mlinzi.Hakuna ninayeishi naye ila kuna mtmishi wa ndani huja kial siku asubuhi akafanya kazi na kuondoka saa kumi lakini huyu hawezikufanya hivi na isitoshe hata funguo za chumba change hana” akasema Dr Marcelo “ Hujafunga kamera za ulinzi? Akauliza Monica “ Hapana sijafunga” “ Unatakiwa uimarishe ulinzi nyumbani kwako ikiwa ni pamoja na kufunga kamera za ulinzi.Vipi polisi wana taarifa zozote za mtu aliyefanya uhalifu huu? “ hapana bado hawana taarifa zozote na wanaendelea kuchunguza “ akasema Dr Marcelo.Ukimya mfupi ukapita Monica akauliza “ Dr Marcelo samahani kwa maswali yangu kama polisi lakini ni kutokana na kuguswa na jambo hili “ “Usijali Monica uliza chochote unachotaka” “ Kuna mtu yeyote unayemuhisi kufanya uhalifu huu? Kuna yeyote unayedhani anapafahamu vizuri nyumbani kwako hadi akaweza kulifungua kasiki unalohifadhi nyaraka zako muhimu? Lakini kabla hujanijibu swali langu kuna kitu nataka nikukabidhi” akasema Monica na kulitoa faili lile la Dr Marcelo na kumpatia.Mikono ikamtetemeka.
“ Umelitoa wapi faili hili? Akauliza Dr Marcelo “ Nimelikuta ofisini kwangu asubuhi.Kuna mtu amelipeleka jana usiku akawaachia walinzi ili wanipatie leo asubuhi.” Akasema Monica na kuliona jasho usoni kwa Dr Marcelo “ Walinzi wanaweza kumfahamu mtu huyo? “ Hapana nimewadadisi hawamkumbuki” “ Umesoma kilichomo ndani ? akauliza Dr Marcelo “ Ndiyo Dr Marcelo nimelisoma na ninafahamu kila kitu kilichomo humo ndani” Ukimya wa sekunde kadhaa ukapita Dr Marcelo akiendelea kulikodolea macho faili lile. “ Daniel..!! akasema Dr Marcelo kwa sauti ndogo “ Unasema nini Dr Marcelo? Akauliza Monica “ Daniel.!!Nimetafakari sana toka jana usiku kuhusu ni nani anayeweza kunifanyia hivi lakini baada ya kunieleza kuhusu faili hili tayari nimepata picha ni mtu mmoja tu ambaye amelifanya jambo hili.Ni Daniel. Aliapa kufanya chochote ili kuuvuruga urafiki wetu na ndiyo maana akasuka mipango ya kulipata faili hili ili uweze kuliona.Damn you Daniel..I’m going to teach you a lesson !!! akasema Dr Marcelo kwa hasira “ It’s not him” akasema Monica “ What ??? akauliza Dr Marcelo ambaye alikuwa amepandwa na hasira kali “ Its not him.It’s not Daniel “ akasema Monica Dr Marcelo akamtazama Monica kwa hasira na kusema “ It’s him.Hakuna mwingine ambaye anaweza akafanya jambo hili zaidi yake” akasema Dr Marcelo “ Hapana Dr Marcelo Daniel hahusiki kabisa na suala hili.” “ Are you sure Monica? Akauliza Dr Marcelo “ Yes I’m sure” akajibu Monica. “ Kabla sijafika hapa nimetoka kuonana na Daniel na amekana kuhusika katika jambo hili.” “ Do you believe him?? Akauliza Dr Marcelo “ Yes I do believe him” akajibu Monica na ukapita ukimya “ Dr Marcelo kuna mtu aliyefanya jambo hili na si Daniel.You have to find the right person who did this but not Daniel.By the way kwa nini hukunieleza ukweli kuhusiana na wewe kusumbuliwa na maradhi ya saratani ya damu? Akauliza Monica.Dr Marcelo akashindwa ajibu nini midomo ikabaki inamcheza. “ Uliogopa nini Dr Marcvelo kunieleza ukweli? Akauliza tena Monica “ Monica listen to me please.” Akasema Dr Marcelo “ Kwanza samahani sana kuhusu suala hili lakini kama unavyofahamu hatuna hata wiki moja toka tulipofahamiana kwa hiyo nisingeweza kukimbilia haraka haraka kuanza kukueleza mambo makubwa kama haya.Hili si jambo dogo lakini hata hivyo nisingeweza kukuficha lazima ningekueleza.” “ Dr Marcelo muda mfupi wa kufahamiana si kigezo.Ni kweli tumefahamiana katika muda usiozidi wiki moja lakini where are we now?.Ni marafiki
.Ni marafiki wakubwa kuliko hata wale ambao nimekuwa nao toka utotoni.Urafiki wetu una nguvu kubwa na ndiyo maana nikashangaa sana kwa nini usinieleze kuhusiana na suala hili toka siku tulipokutana.? I’m so dissaponed with that” akasema Monica “ Monica I’m sorry.Im real very sorry lakini kama nilivyokueleza awali kwamba nisingeweza kukurupuka tu na kuanza kukueleza kuhusu suala hili.Ni jam.....” Akataka kuendelea Monica akamkatisha “ Uliogopa nini kunieleza Marcelo? You don’t trust me? Akauliza Monica “ I was scared..” akajibu “ Scared?? Scared for what?? Akauliza Monica .Dr Marcelo hakujibu akabaki kimya. “ Answer me Dr Marcelo” akasema Monica “ I was scared to loose you..” “ Loose me!! Monica akashangaa “ Ndiyo Monica” akajibu Dr Marcelo “ ungenieleza ukweli kuhusu hali yako ya kiafya ungenipoteza vipi? Akauliza Monica “ Monica let me be honest .Nilipokuona kwa mara ya kwanza nilishindwa kujizuia kukupenda na ndiyo maana nikaogopa endapo ungefahamu kuhusu hali yangu hii usingeweza kukubali kuwa na mtu kama mimi.I love you Monica more than I can explain lakini ugonjwa wangu huu kwa sasa umefikia katika hatua mbaya na sintakuwa na muda mrefi wa kuishi ndiyo maana ninafanya siri.Sijawahi kujihusisha katika mahusiano yoyote toka nilipofahamu kuwa nina maradhi haya .Kwa ufupi I’ve never been happy.Nilipokuona nilikupenda ghafla na nilitaka walau katiak siku zangu chache zilizobaki niwe na furaha na ndiyo maana sikukueleza jambo ” akasema Dr Marcelo na kukawa kimya.Baada ya kama dakika mbili Monica akainua kichwa macho yake yalikuwa na machozi akasema “ Sikiliza Dr Marcelo.Ikitokea kama umempenda mtu kwa moyo wako wote kama unavyosema unanipenda basi unapaswa kumueleza ukweli mtu huyo toka siku mnapoonana.Kama kuna jambo ambalo unadhani anapaswa kulifahamu basi mueleze kutokea siku hiyo na usisubiri hadi atakapolifahamu mwenyewe .Ulipaswa kunieleza kuhusu suala hili mapema kabisa bila kusubiri .Kwa sasa unadhani nitakuamini tena? Akauliza Monica “ Tafadhali naomba uniamini Monica” akasema Dr Marcelo “ How can I trust you Marcelo wakati umenificha jambo hili kubwa? Nilikuweka karibu yangu sana kwa sababu nilikuona ni mtu ninayeweza kumuamini .Naomba nikueleze kuwa hata mimi tayari nilianza kuhisi kitu kwako lakini ni vipi kama ningeingia katika mahusiano nawe wakati sijui kama una maradhi haya japokuwa haayaambukizi lakini tukafurahi kwa siku chache tu halafu ukaondoka na kuniachia majonzi ? Marcelo umeniumiza sana and I cant trust you anymore” akasema Monica “ Monica please trust me.I love you.I real do..” akasema Dr Marcelo “ Dr Marcelo naomba tafadhali tuachane na masuala hayo na tuongelee kuhusu suala la kumtafuta nani aliyefanya jambo hili.Aliyefanya hivi ni wazi alikuwa na makusudi yake na ninaamini lengo lake
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Dr Marcelo naomba tafadhali tuachane na masuala hayo na tuongelee kuhusu suala la kumtafuta nani aliyefanya jambo hili.Aliyefanya hivi ni wazi alikuwa na makusudi yake na ninaamini lengo lake ni mimi kuliona faili hili na kufahamu kuhusu hali yako ya kiafya.Nini anakusudia nikifahamu kuhusu hali ya afya yako?? Hapo ndipo mahala pa kujiuliza” “ Aliyefanya hivi alikuwa na lengo moja tu la kuharibu mahusiano kati yangu nawe.Lazima aliyefanya hivi atakuwa akifahamu kuwa toka tumefahamiana mahusiano yetu yamekuwa mazuri sana na hilo halimpendezi ndiyo maana nikasema kuwa lazima atakuwa ni Daniel kwani ni yeye ambaye anafahamu kuhusu ukaribu wangu mimi na wewe” akasema Dr Marcelo “ Trust me Marcelo,Daniel is not the one who did this.Kuna mtu mwingine aliyefanya hivi.Unatakiwa kushirikiana sana na vyombo vya dola ilikuweza kumbaini mtu huyu ni nani..” akasema Monica.Daniel akainam akafikiri kwa dakika kama tatu halafu akainua kichwa na kusema “ Kwa upande Fulani naweza kukubaliana nawe Monica .Mtu aliyefanya hivi lazima ni mtu anayenifahamu na ndiyo maana akweza kujua muda ninaorudi nyumbani na hivyo akaweza kuingia ndani mwangu bila hata ya kuvunja mlango na kufungua kasiki.Lazima ni mtu ambaye ananifahamu vyema kiasi kwamba akaweza kuzifahamu namba za siri za kufungulia kasiki.Monica ninaanza kupata picha hili si suala dogo kama ninavyodhani.” Akasema Dr Marcelo na kuzama katika mawazo halafu akasema “ Naweza kukubaliana nawe kwamba Danel hahusiki katika jambo hili.Hajawahi kuingia chumbani kwangu na wala hajui namba za kufungulia kasiki langu.” Akasema Dr Marcelo “ Do you believe me now? Akauliza Monica “ Yes I do.Nimejaribu kutafakari kwa haraka haraka na nimeona Daniel hawezi kuhusika katika suala hili.” “ Kama si Daniel,nani basi aliyefanya jambo hili? Akauliza Monica .Dr Marcelo akabaki kimya akitafakari.Baada ya tafakari ya muda Dr Marcelo akainuka ghafla kana kwamba amekumbuka kitu akasema “ Monica I need to go,nitawasiliana nawe baadae.” Akasema na kuinuka akaanza kupiga hatua za haraka kuelekea mahala lilipo gari lake,Monica akabaki anashangaa. “ What happened? Mbona Marcelo ameondoka kwa haraka namna hii ? Kuna kitu amekikumbuka? Akajiuliza Monica huku naye akiinuka na kuelekea katika gari lake. “ Lazima mtu aliyefanya jambo hili anamfahamu vyema Dr Marcelo.Ni nani huyo na lengo lake ni nini? Akajiuliza Monica akiwa garini “ Ngoja niachane na suala hili la Dr Marcelo nielekeze akili katika masuala yangu ya msingi.Kwa sasa ngoja nikaonane na wataalamu wangu juu ya suala la kuanza ujenzi wa shule .Sitaki kupoteza muda , wakati tayari pesa imepatikana.Ujenzi lazima uanze mara moja.Sijui nitatumia neno gani kumshukuru David Zumo kwa msaada wake huu mkubwa alionisaidia.” Akawaza Monica.
Kichwa cha Dr Marcelo Richard kilikuwa kizito kwa mawazo mengi aliyokuwa nayo baada ya kuachana na Monica. “ Nahisi kama vile kichwa changu kimebeba mzigo mzito .Suala hili linaanza kunichanganya kichwa changu sana na sielewi nifanye nini kumpata mtu aliyeingia chumbani kwangu na kufungua kasiki langu.Kinachonishangaza zaidi kwa nini mtu huyu atake Monica afahamu kama ninasumbuliwa na saratani ya damu? Jibu la haraka haraka ninalopata ni kwamba lengo lake ni mimi na Monica tusiwe karibu na kwa hilo nadhani amefanikiwa kwani I’ve already lost Monica.Mipango yangu yote niliyokuwa nayo kuhusu Monica imeyeyuka.Tayari kila kitu kilianza kwenda vizuri na Monica alionyesha kila dalili ya kunikubali lakini baada ya kufahamu kwamba mimi nina maradhi ya saratani ya damu na kwamba sina maisha marefu hayuko tayari kuwa na mimi tena.Nani huyu lakini aliyenifanyia ukatili huu mkubwa? I’ve never been happy in my life.Nilitegemea japo kwa mara ya kwanza katika maisha yangu niwe na furaha baada ya kukutana na Monica lakini binadamu wakatili wameivuruga mipango yangu yote .I swear I must find the person who did this to me.” Akawaza Dr Marcelo na kuuma meno kwa hasira. Alielekea moja kwa moja nyumbani kwake.Ndani alikuwepo mtumishi wake wa kazi za ndani ambaye huja asubuhi na kuondoka saa kumi za jioni akiendelea na kazi.Dr Marcelo akashuka garini na moja kwa moja akaelekea katika mlango mkubwa wa kuingilia sebuleni akajaribu kuuchunguza kwa makini lakini haukuwa umevunjwa sehemu yoyote. “ Mvamizi huyo lazima alitumia funguo bandia kufungua mlango kwani hakuna sehemu mlango huu ulikovunjwa .Siwezi kabisa kumuhusisha mama Salama katika jambo hili kwani yeye ana funguo za milango mitatu tu.Huu wa sebuleni ,wa nyuma ya nyumba na wa geti.Hajawahi kungia chumbani kwangu kwani hata kama ni usafi huwa ninafanya mimi mwenyewe.Aliyeingia chumbani kwangu ni mtu mtaalamu sana” akawaza na kuelekea chumbani kwake.Akalifungua kasiki akalichunguza halafu akaenda kukaa kitandani “ Niwataarifu polisi kuhusu kupatikana kwa faili hili la taarifa zangu za ugonjwa? Akajiuliza “ Nikiwataarifu lazima watakwenda kuanza kumuhoji Monica,jambo ambalo sitaki litokee kwani hahuski chchote na jambo hili.Ngoja niachane na wazo hili .Monica ana mambo mengi kwa sasa kwa hiyo sitaki kumbughudhi kwa mambo mengine “ akajilaza kitandani na kuzama mawazoni lakini ghafla akakurupuka baada ya kukumbuka kitu. “ A book..!! akasema “ NImekumbuka kile kitabu..!! akaenda haraka katika kasiki akachungulia lakini kitabu hakikuwemo.Akafungua kabati lake kubwa la kuhifadhia vitabu akapangua kitabu kimoja kimoja lakini kitabu anachokitafuta hakikuwemo “Nakumbuka kitabu nilikihifadhi humu katika kasiki .Wamekichukua.oh my God” akasema Dr Marcelo na kushika kiuno. “ Kulikuwa na tsh milioni thelathini na nane katika kasiki lakini hizo hazikuguswa hata senti moja badala yake
wakachukua baadhi ya vitu kama faili hili na hicho kitabu.Ninachojiuliza kwa nini wachukue kitabu waache fedha? Kitabu kile kina thamani gani? akajiuliza na kuanza kurudisha kumbu kumbu nyuma. DAR ES SALAAM 2005 Hali ya jiji la Dar es salaam ni ya mvua kubwa na mitaa miingi imefurika maji,katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, Dr Marcelo Richard anawasili na ndege ya shirika la ndege la Tanzania akitokea masomoni nchini China.Uwanjani hapo alipokewa na dada yake Julieth “ Vipi hali ya mzee anaendeleaje? Akauliza Dr Marcelo wakiwa garini “ Mzee hali yake si nzuri na madaktari wametueleza ukweli kwamba he wont make it.Imekuwa vizuri umekuja kwani mzee hana muda mrefu sana wa kuishi” akasema Julieth. Waliwasili nyumbani kwao ambako kila aliyekuwapo alikuwa na sura ya majonzi makubwa kutokana na hali ya Dr Richard Wendelic Richard bingwa wa magonjwa ya moyo kuzidi kudhoofika .Dr Richard aliyekuwa akifahamika kwa umahiri wake katika upasuaji wa moyo alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya saratani ya damu .Pamoja na jitihada zote za familia yake kujaribu kumtibu lakini hakukuwa na unafuu wowote na madaktari waliihakikishia familia yake kuwa Dr Richard hataweza kupona maradhi yanayomsumbua. Baada ya Dr Marcelo kuwasili akitokea nchini China alikokuwa akisomea masuala ya neva za fahamu Dr Richard akawataka watu wote mle chumbani watoke wamuache yeye na Dr Marcelo . “ Marcelo nashukuru sana umekuja kwa wakati kama nilivyoagiza.” Akasema Dr Richard akavuta pumzi ndefu na kuendelea “ Nadhani tayari umekwisha pewa taarifa na ndugu zako kwamba matibabu yameshindikana na hakuna namna tena so I have to die.Ninafurahi kwamba ninakufa lakini mmoja wa wanangu ni daktari lakini ningekushauri baada ya kumaliza masomo yako kuhusu neva za fahamu ,usomee pia kuhusu maradhi yanayokuja kwa kasi na kuua watu wengi hivi sasa ,maradhi ya saratani ya damu.Nimekushauri kwa muda mrefu sana usomee kuhusu maradhi haya lakini haukuwa tayari.Nataka leo niweke wazi kwa nini nilikuwa nakusisitiza sana kuhusu kusomea maradhi ya saratani ya damu.” Dr Richard akavuta pumzi ndefu akamtazama mwanae kwa makini.Mvua kubwa ilikuwa inanyesha huko nje na radi zikimulika “ Marcelo wewe pia una saratani ya damu” “ What ?? Dr Marcelo akastuka sana “ Una saratani ya damu pia” akasema Dr Richard.Dr Marcelo akastuka kama vile ameona dudu la kutisha akamtazama baba yake kwa macho makali “ Tell me its not true dady !! akasema Dr Marcelo “ Its true Marcelo” akasema Dr Richard.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
dr Marcelo akamtazama baba yake kwa karibu dakika mbili huku machozi yakimtoka akasema “ No that’s not true .Kama ningekuwa na tatizo hilo kwa nini miaka hii yote nisijue kama nina saratani hiyo ya damu? I’m fine na sina tatizo lolote.Please dady don’t lie to me kwa sababu tu unataka nkasomee kitu unachokitaka wewe” “ I’m not lying to you my son.Its true.Una chronic mylegonous leukemia.Hii ni saratani ya damu ambayo husambaa taratibu sana na mtu mwenye aina hii ya saratani anaweza akapata dalili chache au asiwe kabisa na dalili kwa miaka mingi kabla ya ugonjwa kufumuka na kuanza kumshambulia.Kwa hiyo Marcelo naomba unsikilize ninachokushauri mwanangu,hakikisha umesomea maradhi haya ya sarataniya damu ili uweze kujisaidia wewe mwenyewe na vile vile kuwasaidia wengine wanaosumbuliwa nayo” akasema Dr Richard “ Dady no ! that’s not true..!! “ Its true my son.Samahani sana kwa kutokufahamisha kuhusu jambo hili mapema sikutaka nikuchanganye katika masomo yako.Tafadhali zingatia hayo ninayokwambia na utaishi miaka mingi.Jambo lingine ambalo ninataka ulifanye baada ya mimi kufariki,ukisha hitimu masomo ya saratani ya damu nataka kama familia mjenge hospitali kubwa ya kuwahudumia wagonjwa wa saratani ambayo itakuwa ni kwa kumbu kumbu yangu. “ akanyamaza kidogo halafu akaendelea “ Jambo la mwisho ambalo nataka ulifanye,..” akasema Dr Richard akamuomba Marcel;o amsaidie kunyanyuka pale kitandani akatembea taratibu hadi katika kasiki lililokuwa ukutani akalifungua na kutoa kitabu “ Kitabu hiki ni muongozo wako kila pale utakapokuwa umepatwa na tatizo lolote katika kazi zako za kitabibu.Mimi kimekuwa ni msaada mkubwa sana kwangu katika maisha yangu ya kitabibu na kwa kuwa sasa maisha yangu ya kitabibu yanakwenda kufikia mwisho ninakukabidhi wewe.Kitabu hiki kitakupa muongozo wa mambo mengi hususan mambo ya kitabibu .Mimi nimekuwa daktari mkubwa na kuheshimika afrika ni kwa sababu ya kitabu hiki.Kitabu hiki si kitabu rahisi kukielewa na kabla hujaanza kukisoma kuna mtu ambaye unapaswa kuonana naye ambaye atakupa maelekezo ya jinsi ya kukisoma kitabu hicho. Naomba uchukue kalamu na uziandike namba hizi ntakazokutajia.Halafu jambo lingine kitabu hiki ukitunze sana asiruhusiwe kukishika mtu mwingine yeyote zaidi yako” Akasema Dr Richard na kumtajia Dr Marcelo namba za simu akaziandika katika kijitabu. Dr Marcelo akafuta jasho baada ya kumbukumbu ile kumjia “ Sikuwahi kukifungua kitabu kile kukisoma kwani toka nilipokabidhiwa na baba siku ile nilizunguka nacho nchi mbai mbali nilizosoma na niliporejea hapa nyumbani nilikihifadhi katika kasiki na kukisahau kabisa hadi leo hii nilipokikumbuka.Nini kiliandikwa katika kitabu kile? Aliyekichukua anafahamu umuhimu wake? Anafahamu kilichoandikwamo? Akajiuliza Dr Marcelo “ Ninakumbuka siku ile baba wakinikabidhi kitabu hicho alinitajia namba Fulani nikaiandika katika kitabu
changu cha kumbu kumbu na sikuwahi kupiga namba hiyo.Aliniambia kwamba kabla ya kukisoma kitabu hicho ningehitaji maelekezo toka kwa huyo mtu aliyenipa namba zake .Nakumbuka kitabu kile cha kumbu kumbu nilichoandika namba zile kilijaa na nikakihifadhi katika kabati langu la kutunzia vitabu. “ akawaza Dr Marcelo na kutoka mbio hadi katika chumba chake cha kusomea akafungua kabati kubwa la kuhifadhia vitabu na kuanza kukitafuta kitabu alichoandika namba zile alizopewa na baba yake.Haikuwa kazi rahisi kutokana na vitabu vingi alivyokuwa navyo.Ilimchukua zaidi ya saa mbili kuweza kukipata.Alikuwa ameloa jasho mwili mzima.Haraka haraka akaanza kuzitafuta namba zile na akazipata. “ Nimezipata namba za mtu huyu ambaye angenipa maelekezo kuhusu kitabu kile ,nifanye nini sasa? Akajiuliza na mara akapata wazo,akachukua simu na kumpigia Monica “ Dr Marcelo” akasema Mnica baada ya kupokea simu “ Monica samahani kwa kukusumbua.” “ Bila samahani Dr Marcelo” “ Monica nina tatizo nahitaji kuonana nawe sasa hivi” akasema Dr Marceo na zikapita sekunde kadhaa “ Uko wapi sasa hivi? Akauliza Monica “ Niko nyumbani kwangu” akasema “ Naomba tukutane Savana garden” akasema Monica Bila kupoteza wakati akatoka haraka kwenda kukutana na Monica
“ Dr Macelo kuna tatizo gani? akauliza Monica baada ya kukutana na Dr Marcelo mahala walikopanga wakutane.Uso wa Dr Marcelo ulionyesha wazi kwamba kuna jambo lililokuwa linamsumbua akavuta pumzi ndefu na kusema “ Monica naomba kwanza nikushukuru kwa kusimamisha shughuli zako na kuja kunisikiliza.Ahsante sana kwa kunithamini” akasema Dr Marcelo “ Usijali Dr Marcelo,nieleze kuna tatizo gani? akauliza Monica.Dr Marcelo akainamisha kichwa kwa sekunde kadhaa halafu akasema “ Monica,tulipoachana nilielekea moja kwa moja nyumbani kutuliza akili na kujaribu kulitafakari suala lililotokea kwa makini zaidi. Wakati nikijaribu kulitafakari suala hilo na kuitafakari dhamira ya mtu aliyefanya jambo lile nikakumbuka kitu Fulani” akanyamaza “ Jambo gani hilo Dr Marcelo? Akauliza Monica “ Wakati baba yangu akiwa katika siku za mwisho za uhai wake ,nilikuwa masomoni nchini China ikanilazimu kurejea nyumbani na siku niliyorejea nilikuwa na maongezi naye.Alinieleza kwamba kutokana na ugonjwa wake wa saratani ya damu uliokuwa unamsumbua hataweza kupona.Alinieleza mambo mengi ikiwa ni pamoja na kunisisitiza kwamba nihakikishe nimesomea kuhusu saratani ya damu.” Akanyamaza kidogo halafu akaendelea “ Katika maongezi hayo ndipo aliponipa wazo la kujenga hospitali ya kuwahudumia wagonjwa wa saratani ya damu kwa kumbu kumbu yake.Pamoja na yote aliyonieleza kuna mambo mawili makubwa.Kwanza alinieleza kwamba nilikuwa na saratani ya damu pia.Sikuwa nikilifahamu hili kwani sikuwahi kuwa na dalili zozote za saratani lakini akanieleza kwamba aina ya saratani niliyokuwa nayo ni chronic myelogenous leukemia ambayo ni aina ya saratani inayosambaa taratibu na huchukua miaka hadi kugundua.” Marcelo akanyamaza tena akainamisha kichwa na baada ya sekunde kadhaa akasema “ Tukiachana na hilo kuna jambo lingine ambalo sikuwa nimelitilia maanani lakini leo nikiwa natafakari juu ya hiki kilichotokea ndipo nilipolikumbuka.Siku ile nilipoongea na baba alinipa kitabu Fulani chenye jalada gumu la kijani akanieleza kwamba ni kitabu muhimu sana ambacho natakiwa nikitunze na nihakikishe hakuna atakayekisoma zaidi yangu.Alinieleza kwamba kitabu kile ni muongozo wangu katika kazi zangu za kitabibu na mambo mengine mengi.Kwa maelekezo aliyonipa ni kwamba kila pale nitakapokuwa na tatizo katika masuala yangu ya kitabibu au masuala binafsi basi nikitumie kitabu hicho chenye kila kitu ndani yake lakini akanieleza kwamba kabla sijakisoma kitabu hicho kuna mtu ambaye natakiwa kuwasiliana naye ambaye atanipa maelekezo ya namna ya kukitumia .Alinipa namba za simu za mtu huyo nikaziandika katika kijitabu Fulani.Toka aliponipa kitabu hicho sikuwahi kukisoma au hata kukifungua kujua kilichomo ndani yake.Baada ya kumaliza masomo yangu nilikihifadhi kitabu hicho katika kasiki langu na sikuwahi kukigusa tena.Leo hii ndipo nilipokikumbuka na nilipokiangalia lakini hakikuwemo katika kasiki.Mtu aliyefungua kasiki alikichukua .Nikazikumbuka namba za Yule mtu ambaye baba alisema kwamba nimpigie ili anipe maelekezo ya namna ya kukitumia kitabu hicho.Nilikitafuta kitabu nilichoandika namba hizo nikakipata na
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment