Search This Blog

Friday, 20 May 2022

QUEEN MONICA - 1

 







    IMEANDIKWA NA : PATRICK CK



    *********************************************************************************



    Simulizi : Queen Monica

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kumepambazuka tena na habari kubwa iliyotawala mitandao ya kijamii na katika vyombo mbali mbali vya habari Tanzania asubuhi hii ni habari iliyochapishwa katika jarida la The Face ambalo ni maarufu kwa habari za mitindo na urembo duniani ,inayohusiana na matokeo ya utafiti uliofanyika barani afrika kuhusu masuala ya urembo. Ukurasa wa mbele wa jarida hili maarufu ulipambwa na picha kubwa ya mwanamke wa kiafrika mwenye uzuri uliotukuka akiwa ndani ya tabasamu kubwa na huku kukiwa na maandishi makubwa yaliyosomeka QUEEN OF AFRICA. Ukurasa wa nne wa jarida hili kuliandikwa habari ndefu inayohusiana na picha ile ya yule mwanamke aliyeupamba ukurasa wa mbele.Habari hiyo ilielezea kwa kina kuhusiana na matokeo ya utafiti uliofanywa na jarida hilo barani afrika matokeo yaliyoonyesha kuwa msichana Monica Benedict Mwamsole anayetokea Tanzania ambaye picha yake iliwekwa katika ukurasa wa mbele wa jarida lile ndiye mwanamke mrembo zaidi barani afrika. Habari hii ilisababisha kuwepo kwa mijadala mingi katika mitandao ya kijamii na katika vyombo mbali mbali vya habari duniani.Watu walimjadili Monica na wengi ambao hawakuwa wakimfahamu walitaka kumfahamu ni nani huyu msichana hadi atajwe kuwa ndiye mrembo zaidi kuliko wote barani Afrika. Monica Benedict Mwamsole ana umri wa miaka 25 .Ni mtoto wa pili na wa mwisho kwa mzee Benedict na bi Janet Mwamsole.Monica anatokea katika familia iliyobarikiwa utajiri mkubwa.Baba yake mzee Benedict Mwamsole ni mmoja wa mabilionea wakubwa wanaotambulika na kuheshimika ndani na nje ya nchi .Kwa uchache tu mzee Benard anamiliki kampuni kubwa ya usafirishaji ,kiwanda kikubwa cha kutengeneza mvinyo wenye soko kubwa katika nchi za ulaya,anamiliki pia biashara nyingine kubwa kubwa ndani na nje ya nchi. Monica mwenye urefu wa futi 5.9 ni msichana mwenye ngozi nyororo na weupe wa kung’aa.Ana nywele ndefu ambazo huzitengeneza katika mtindo wa kipekee ambao humfanya awe na uzuri usioelezeka.Monica amebarikiwa mwili mzuri mwembamba wastani ambao huwafanya wengi waamini ameufanyia upasuaji na kuufanya uonekane vile. Kielimu Monica ni msomi mwenye shahada katika mahusiano ya kimataifa .Ukiacha sifa na uzuri wa nje Monica ana sifa za kipekee za ndani.Ni msichana mpenda watu asiye na makuu licha ya kuogelea katika bahari ya utajiri mkubwa wa familia yao.Pamoja na uzuri wake uliopelekea apewe jina la Black Angel au malaika mweusi,Monica hakuwa na majivuno aliongea na kila mtu ,hakuchagua mtu wala tabaka Fulani la watu kuwa nao karibu.Aliwasikiliza wote waliomuendea na shida mbalimbali na kuwasaidia kadiri alivyoweza.Alikuwa na taasisi yake aliyoianzisha kwa ajili ya kusaidia watu wenye matatizo mbali mbali lakini akilenga zaidi watoto na wazee wasiojiweza.Kwa ujumla Monica alikuwa ni mwanamke mwenye sifa lukuki na kipenzi cha watu.Alipendwa na wakubwa na wadogo. Alipohitimu elimu yake ya juu,Monica alichagua kufanya kile ambacho alikuwa anakipenda kwa dhati toka akiwa mtoto mdogo yaani mitindo.Alipenda sana mambo ya mavazi na urembo hivyo alianzisha kampuni yake inayojishughulisha na masuala ya mitindo kampuni ambayo imeliteka soko la afrika mashariki kutokana na aina ya mitindo ya mavazi wanayoibuni iliyotokea kupendwa sana na watu wengi. Kwa ufupi huyu ndiye Monica Mwamsole ambaye jina lake maarufu nchini Tanzania ni malaika mweusi jina ambalo alipewa kutokana na uzuri wake na matendo yake.Taarifa za yeye kutangazwa na jarida la The Face kuwa ndiye msichana mrembo zaidi barani Afrika hazikuwashangaza wengi waliomfahamu bali walikubaliana na matokeo ya utafiti huo na kuwapongeza watafiti ,Monica alistahili heshima hiyo ya kuwa mrembo wa afrika.



    Sauti ya ndege mkubwa aliyekuwa akilia karibu na dirisha ilimstua Monica toka katika usingizi .Huku akionekana kukerwa na sauti ile iliyomstua usingizini akainuka na kukaa. “ oh no ! Huyu ndege ameniharibia ndoto yangu tamu..” akawaza Monica,akainuka kitandani na kujinyoosha halafu akatazama saa ndogo yenye nakshi za dhahabu iliyoko mezani “ Ni saa mbili na robo sasa,muda umekwenda sana natakiwa niwahi ofisini leo nina miadi ya kuonana na Daniel ambaye alisema atamleta rafiki yake anayehitaji kuchangia katika mbio tunazoziandaa.Nashukuru wadau wengi wanazidi kujitokeza na kuniunga mkono katika mpango wangu wa kujenga shule ya watoto wenye mahitaji maalum.Nina hakika jambo hili litafanikiwa kwani limepata mwitikio mzuri kwa watu wengi matajiri kwa wasio na uwezo.” Akawaza huku akivaa nguo zake za mazoezi na kujiandaa kwa ajili ya kufanya zoezi la asubuhi.Ni kawaida yake kila aamkapo asubuhi kutembea kwa miguu kilometa kadhaa kabla ya kwenda ofisini.Alipokuwa tayari akatoka na kwenda kwanza kuwasalimu watumishi wake wa ndani waliokuwa katika harakati zao za kawaida za asubuhi akaongea nao mawili matatu na kutoa maelekezo kadhaa kisha akatoka nje na kusalimiana na kijana mtunza mazingira na mwisho akawajulia hali walinzi wake wanaolinda nyumba yake halafu akaanza zoezi lake la kutembea.Haya ndiyo maisha ya kila siku ya Monica,kila asubuhi kabla hajafanya chochote lazima kwanza ahakikishe amewasalimu watu wote anaoishi nao nyumbani kwake na kujua hali zao na ndipo huendelea na ratiba nyingine za siku. “ Sikufanya makosa kuamua kuhamia huku.Ni kuzuri ,kuna hewa safi na utulivu wa kutosha.Japokuwa ni mbali na mji lakini hiyo hainipi taabu ninachohitaji mimi ni kuishi sehemu tulivu kama hii kusikokuwa na makelele wala uchafuzi wa hewa.Huku ninapata hewa safi toka baharini tofauti na mjini” akawaza Monica wakati akipanda kilima kidogo. “ Hata hivyo eneo hili bado jipya na lina changamoto nyingi,miundo mbinu bado si mizuri,hakuna maji ya uhakika,umeme barabara n.k.Natakiwa kukutana na wakaazi wa eneo hili na kwa pamoja tujadili namna ya kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabili.Wanahitaji huduma za afya,shule n.k so I must help them.I want to change this place.Kwa sasa panaonekana ni kijijini lakini ndani ya miaka michache ijayo patakimbiliwa na kila mtu .Nina ndoto ya kulifanya eneo hili kuwa mji mzuri sana na wa kupendeza” akawaza Monica akiendelea na mazoezi yake Alirejea nyumbani na moja kwa moja akaelekea chumbani kwake akaoga na kujiandaa kwa ajili ya kuanza shughuli zake za siku.Alipomaliza kujiremba akajitazama katika kioo na kutabasamu halafu akawasha simu zake.Jumbe nyingi zikaingia mfululizo akakaa kitandani na kuanza kuzipitia kwa haraka haraka na mojawapo ya jumbe hizo ulitoka kwa baba yake ambao ulikuwa na neno moja tu “Congraturations ” Monica akatabasamu “ Baba ananipongeza kwa jambo gani? Kuna chochote nimekifanya kinachostahili pongezi? Ngoja nimpigie niongee naye anieleze sababu ya kunipongeza” akawaza Monica na kumpigia simu baba yake. “ Hallow Monica” akasema mzee Benedict Mwamsole baada ya kupokea simu ya Monica “ Goodmorning dady” “ Good morning my sweetie,umeamkaje? “ Nimeamka salama dady,vipi nyie huko wote wazima? “ Sisi sote wazima wa afya,hofu kwako “ “ Mimi pia mzima dady.Nimepata ujumbe wako sasa hivi” akasema Monica huku akitabasamu “ Nimekutafuta sana jana usiku lakini simu yako haikuwa ikipatikana ndiyo maana nikakutumia ujumbe ule.Bado hujaacha tabia yako ya kuzima

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    simu usiku” akasema mzee Ben.Monica akacheka kidogo na kusema “ C’mon dady,you know me.Nina kazi nyingi mchana kutwa kwa hiyo ikifika usiku kichwa changu na mwili vyote vinakuwa vimechoka mno that’s why when I go to bed I switch off everything.By the way you congraturated me,hongera kwa jambo gani baba? Akauliza Monica “ Ina maana bado hujapata habari?!! Akauliza mzee Ben “ Habari zipi baba? Kama nilivyokwambia kwamba mimi huzima kila kitu usiku na halafu mimi si mpenzi sana wa kutazama taarifa za habari katika luninga kwani taarifa nyingi zimejaa mambo ya siasa na mimi kama unavyonijua I hate politics.Kuna taarifa gani kwani? Akauliza Monica kwa wasiwasi kidogo “ Monica unatakiwa uachane na huo utaratibu wako wa kuzima simu usiku na ujenge pia utamaduni wa kufuatilia vyombo vya habari” “ Kwani kuna nini baba? Akauliza Monica “ Too bad kama bado mpaka sasa hujapata taarifa.Ni kwamba umetangazwa na jarida la The face la Marekani katika toleo lake la mwezi huu lililotoka jana usiku kwa huku kwetu ambayo ni mchana kwao kwamba wewe ndiye msichana mrembo zaidi barani afrika.Hongera sana Monica.You deserve it” akasema mzee Ben “ What?? That cant be true..Me? Monica akashangaa “ kweli Monica.You are the most beautifull woman in Africa.Your beauty is amazing and I’m so proud of you” akasema mzee Ben Macho ya Monica yakaanza kuloa machozi “ Monica !! akaita mzee Ben “ Naam baba” akaitika Monica huku akifuta machozi “ Ouh Monica you are crying again “ “ I’m sorry dady si unajua machozi yangu yako karibu.Ninapokuwa na furaha iliyopitiliza hujizuia kushindwa kutoa machozi” akasema Monica “ Sawa Monica basi endelea na shughuli zako ila napenda tu kukutaarifu kwamba tunaandaa sherehe ya kukupongeza kama familia kwa jambo hili kubwa” akasema Ben “ Ahsanet Dady.See you later “ akasema Monica na kukata simu akavuta pumzi ndefu na kuinua mikono yake akatazama juu “ Oh my God who am I to deserve all these? Akasema Monica halafu akaiwasha kompyuta yake na kuingia mtandaoni ili kuthibitisha kile alichoambiwa na baba yake. Katika akaunti yake ya barua pepe kulikuwa na ujumbe toka kwa uongozi wa jarida la The Face ambao walimtaarifu kuwa kutokana na utafiti wao walioufanya barani afrika kwa muda wa miezi kumi na moja yeye ameonekana kuwa ndiye mwanamke mrembo kuliko wote barani afrika.Walimueleza kwa krefu kuhusiana na namna walivyofanya utafiti wao na kwa namna yeye Monica alivyoweza kuibuka kuwa mrembo zaidi Afrika.Mwisho walimtaarifu kuwa watatuma timu ya wawakilishi wao waje kuonana na Monica ikiwa ni pamoja na kumkabidhi zawadi yake ya ushindi na kuzungumza naye masuala kadhaa yanayohusiana na mitindo afrika.Walimtumia pia nakala ya tolea lililotoa matokeo hayo.Nje ya jarida lile kulikuwa na picha kubwa ya Monica akiwa katika tabasamu “ oh my Gosh its true.....its true...” akasema kwa furaha huku michirizi ya machozi ikionekana mashavuni pake. “ Dah ! siku yangu imeanza kwa furaha namna hii.Sikutegemea kabisa kama jambo hili lingetokea.Najifahamu mimi ni mzuri lakini sikuwahi kuota kuwa siku moja nitaweza kutangazwa kuwa mrembo kuliko wote afrika.Nakumbuka watu wa jarida la The Face waliwahi kuja kuniona nikaongea nao nikawaeleza shughuli zangu,wakanihoji mambo mengi kuhusiana na maisha yangu na wakanipiga picha nyingi za kutosha ila sikufahamu kama walikuwa katika utafiti.Mimi nilidhani walikuwa katika mojawapo ya kazi zao za kila siku za kukusanya taarifa za mitindo na urembo. Walitakiwa waniweke wazi nini walichokuwa wanakifanya kuliko kunistukiza namna hii lakini hata hivyo I’m happy.Wamenifanya nijulikane ghafla sana duniani.Oh my God I real don’t know how to thank you for this ...” akawaza Monica na kurekebisha poda usoni akatoka na kwenda moja kwa moja katika chumba cha chakula ambako tayari kulikwisha aandaliwa stafstahi.Alikunywa chai haraka haraka na kisha akaagana na watumishi wake akaondoka kwenda kazini



    Mzee Benedict Mwamsole baada ya kumaliza kuongea na mwanae Monica simuni akamgeukia mke wake na wote wawili wakatazamana na kutabasamu “ Mbona unanitazama hivyo Ben? Akauliza Bi Janet Mwamsole .Ben akambusu mkewe na kusema “ Monica amerithi uzuri wako .Yeye ni mrembo afrika nzima lakini wewe ni mrembo wa dunia nzima.Una uzuri wa kipekee kabisa” akasema mzee Benedict “ Thank you Ben” akasema mke wake “ Halafu kuna kitu kingine umebarikiwa nacho ambacho wengi hawana” “ Kitu gani hicho Ben? “ Huzeeki.Umri umesogea sana lakini bado unaonekana ni kama vile una miaka thelathini .Tazama mimi karibu kichwa changu chote kitakuwa cheupe kwa mvi lakini wewe bado unaonekana mbichi.Unajua sana kujitunza na jambo hili umemuambukiza hata mwanao Monica anajua kujitunza na ndiyo maana ameweza kuonekana mrembo zaidi ndani ya mamilioni ya wasichana warembo barani afrika.” Akasema mzee Ben na kumbusu mke wake “ Ben unajua sana namna ya kunifanya nitabasamu.Maneno yako huniingia taratibu na hujikuta nimehama kifikra toka katika dunia hii na kujiiona niko katika ulimwengu mwingine kabisa.Umebarikiwa kinywa chenye maneno matamu .Nadhani hata mwanao Nathani amerithi hilo toka kwako na ndiyo maana amekuwa anapapatikiwa na wanawake kila kukicha.Ana maneno matamu kuweza kumlainisha mwanamke yeyote”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mzee Ben akajikuta akiangua kicheko kwa maneno yale ya mke wake “ Unanifurahisha sana Janet.Hao wanawake wanaompapatikia Nathani si kwa sababu ya maneno yake matamu bali kwa pesa zake.Nathani bado ni kijana na anapenda sana starehe.Ukiwa na pesa huhitaji kuwa na maneno matamu ili kumpata mwanamke mrembo bali pesa huongea yenyewe bila hata ya wewe kufumbua mdomo wako utakipata kile unachokihitaji.Hata hivyo nadhani ni wakati muafaka sasa wa kukaa na kumkanya Nathani kuhusiana na tabia yake ya kuendekeza starehe kupindukia.Tukimuacha aendelee namna hii mwisho wake hautakuwa mzuri hata kidogo.Umri unakwenda na anatakiwa atafute msichana mmoja mzuri atulie naye kuliko kuruka ruka anakofanya sasa hivi.Isitoshe sisi tumekwisha kuwa wazee anatakiwa ajiandae kusimamia miradi yetu kwani yey endoye mtoto mkunwa“ akasema mzee Ben “ Hilo unalosema Ben ni la kweli.Huyu mtoto tunatakiwa tumkanye aachane kabisa na tabia yake hii mbovu ya kubadilisha wanawake kama nguo.Halafu vipi kuhusu huyu Monica? “ Monica ana nini ? akauliza Ben .Bi Janet akainuka na kukaa mzee Ben naye akafanya hivyo “ Monica ana miaka 25 hivi sasa,tayari ana kila kitu katika maisha yake na hakuna kitu anachokikosa.Kinachonipa wasi wasi ni kwamba amekuwa mgumu sana kuweka wazi masuala yake ya kimahusiano.Mpaka leo hii mimi sifahamu mwanaume wake ni yupi ,hatujui nini mipango yake kuhusu jambo hili? Nafahamu sera yetu ni kutokuingilia masuala binafsi ya watoto hususan mahusiano lakini nimeanza kuingiwa na woga kwa sasa baada ya Monica kupata umaarufu mkubwa.Wanaume watamsumbua sana na wengi watakaomfuata ni watu wenye pesa ambao hutumia nguvu yao ya pesa kuwarubini wanawake na kuwapata kimapenzi.Nina wasi wasi mwanangu anaweza kushindwa kumpata mwanaume mzuri wa ndoto zake .Ninahitaji Monica ampate mwanaume mzuri mwenye kumpenda kwa dhati na ambaye atamfanya awe na furaha siku zote katika maisha yake “ akasema Bi Janet Mzee Ben akakuna kichwa kidogo na kusema “ Hilo unalolisema ni la kweli kabisa.Monica anatakiwa awe muangalifu sana kwa sasa baada ya kupata umaarufu mkubwa.Umaarufu ni kama ua lenye harufu nzuri ambalo huwavutia nyuki kulifuata na kuchukua asali na utamu ukiisha huliacha ua likinyauka na kupukutika mtini.Wanaume hasa wenye pesa ni sawa na nyuki ambao huvutika na uzuri na umaarufu wa msichana na hutumia nguvu yao ya fedha kumpata na wakisha fanikisha haja zao humuacha na kwenda kutafuta wanawake wengine kama nyuki wanavyoliacha ua lililoisha utamu na kwenda kutafuta au lingine.Monica anatakiwa awe makini sana.Hata hivyo.....” akasema mzee Ben na kunyamaza kidogo kana kwamba kuna kitu anakikumbuka “ Nini Ben ? akauliza mkewe “ Kuna kitu nimekumbka.Monica ana ukaribu sana na Yule Daniel mtoto wa mzee Swai.Unamuonaje Yule kijana anaweza kumfaa Monica? Ni kijana msomi ana sura nzuri,ana adabu na familia yao ni watu wa karibu sana na sisi isitoshe ni watu matajiri .Nadhani Daniel ni kijana mzuri kwa Monica.Unaonaje kuhusu hilo? Bi Janet akaguna na kumtazama Ben kwa macho makali “ You don’t know anything about that guy!! “ Kwani Daniel ana tatizo gani? Mbona mimi namuona ni kijana mzuri tu ?

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “ Daniel is a snake.!! Hafai kabisa Yule kijana kuwa hata na ukaribu na Monica.Baada ya kugundua ukaribu wake na Monica nilimfanyia uchunguzi nikagundua kuwa ni kijana mshenzi sana.Ana tabia chafu mno.Ana wanawake karibu kila kona ya jiji.Anawabadilisha wanawake kama nini sijui.Daniel hafai hafai kabisa tena nina mpango wa kumuonya Monica aache kabisa kuwa karibu naye” akasema Bi Janet huku sura yake ikionyesha wazi alikwisha anza kukasirika “ Dah ! sikuwa nikifahamu tabia zake kama ni hizo.Anyway tuachane na hayo mambo tutazungumza siku nyingine nataka tujadili namna ya kuandaa sherehe ya kumpongeza Monica kwa mafanikio haya makubwa aliyoyapata.Hiki walichokifanya The Face kumtaja kuwa ndiye mwanamke mrembo zaidi afrika ni suala kubwa hii ni bahati kubwa kwa familia yetu kwa hiyo lazima tufanye sherehe kubwa ya kumpongeza” “ Sawa ben niachie mimi suala hilo nitalishughulikia” akasema Bi Janet ***************** Monica aliwasili katika jengo zilimo ofisi zake.Ni jengo la ghorofa mbili analolimiliki yeye mwenyewe.Kama ilivyo kawaida yake akasalimiana na walinzi wake baada ya kushuka garini pamoja na baadhi ya wafanyakazi waliokuwa nje kisha akaingia ndani.Mapokezi hakukuwa na mtu akapanda moja kwa moja katika ghorofa ya kwanza ambako kazi zote za ubunifu hufanyikia hapo lakini hakukuwa na mtu ila kompyuta karibu zote zilikwisha washwa .Monica akashangazwa kidogo kwa hali ile “ Where is everyone? akajiuliza na kuchukua simu akataka kupiga mara akatokea Jesica mmoja wa wafanyakazi aliyekuwa akihema kwa kasi.. “Madam ..!! akaita Jessica “ Jessica kuna nini mbona hivyo? “ Madam its Linah ..!! akasema Jessica na kumstua Monica “ Linah ?? amefanya nini? Akauliza Monica kwa wasi wasi “ Ameanguka ghafla .Twende ukamuone..” akasema Jessica na kugeuka akaanza kutembea haraka haraka Monica akiwa nyuma yake “ nini kimemtokea Linah? Akauliza Monica lakini Jessica hakumjibu kitu.Walipanda hadi katika ghorofa ya pili kulikokuwa na ofisi ya Monica pamoja na ukumbi mdogo wa mikutano.Jessica akaufungua mlango wa ukumbi ule mdogo wa mikutano kwa kasi akaingia ndani,Monica naye aliyekuwa amkimfuata nyuma akaingia kwa kasi na mara akakutana na kitu ambacho hakuwa amekitarajia.. “ Surprise !!!!... ikasikika sauti kubwa toka kwa wafanyakazi waliokuwa wamekaa katika mojawapo ya kona ya ukumbi ule wakiwa na nyuso zenye furaha .Linah msaidizi wa Monica alikuwa amesimama mbeye yao akiwa na maua huku akiwa na tabasamu zito “ Oh my Gosh !!..akasema Monica kwa mshangao ..Taratibu Linah akamsogelea Monica na kumpa maua “Congraturations queen of Africa” akasema Linah .Kwa mara nyingine Monica akajikuta akimwaga machozi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alikuwa na furaha iliyopitiliza.Wafanyakazi wake walimpongeza kwa kutangazwa kwake kuwa ndiye mrembo kuliko wote afrika.Baada ya pongezi Monica akaomba aongee machache “ Thank you..!! akasema Monica na kufuta machozi “ Thank you so much for this wonderfull surprise.Nimefurahi kupitiliza na ndiyo maana mnaona machozi yananitoka.Ahsanteni sana ndugu zangu” akanyamaza akafuta machozi na kuendelea “ Hiki kilichotokea kwa mimi kutangazwa kuwa mrembo kuliko wote Afrika ni mafanikio ya juhudi zenu.Nimeonekana mimi kwa sababu ninyi ndio mlioniinua na kunifanya nionekane kwa hiyo ushindi huu ni wa kwenu ninyi.Mnatakiwa mjipongeze papo hapo napenda kuwaasa kuwa tunatakiwa kuongeza bidii ya kazi ili tufike mbali zaidi ya hapa tulipofika.Tutakaa pamoja na kujadili namna tutakavyoweza kuitumia fursa hii iliyojitokeza lakini kwa sasa tufungue shampeni na tugonganishe glasi tutakieni heri na kupongezana kwa mafanikio haya makubwa” akasema Monica.Shampeni ikafunguliwa wote wakashangilia halafu kila mmoja akaenda kuendelea na kazi.Monica aliingia ofisini kwake akajiegemeza kitini hakuwa na hamu ya kufanya kazi yoyote. “ Why me Lord? Katika wanawake wote hawa wa afrika wenye uzuri usioelezeka why me? Akajiuliza Monica akainuka na kuanza kuzunguka zunguka mle ofisini na mara siku ya mezani ikaita akaunyanyua mkono wa simu “ Hallow “ akasema “ Madam kuna wageni wako hapa mapokezi” “ Ni akina nani? “ Ni Mr Daniel na mwenzake” “ Ok waruhusu waje moja kwa moja” akasema Monica halafu kwa haraka akaingia katika kijichumba kidogo kilichomo ndani ya ofisi yake ambacho hukitumia kujirembea akarekebisha poda usoni na kutoka tayari kuwapokea wageni wake.Baada ya dakika kama nne hivi mlango ukagongwa akaruhusu mgongaji



    aingie ndani na ndipo walipojitokeza vjana wawili watanashati.Daniel Swai na mwenzake.. “ Karibuni sana” Monica akawakaribisha wageni wake katika sofa nzuri zilizokuwamo mle katika ofisi yake.Muhudumu akafika na kuwakirimu wageni kwa vinywaji na maongezi yakaanza.Daniel ndiye aliyeanzisha maongezi “ Monica huyu ni rafiki yangu anaitwa Dr Marcelo Richard.Yeye kama atakavyojieleza mwenyewe anayo taasisi yake ya kuwahudumia wagonjwa wenye matatizo ya saratani ya damu. Baada ya kumueleza kuhusiana na jambo unalokusudia kulifanya naye akajikuta ameguswa na akaomba aje atoe mchango wake..” akasema Daniel halafu akamgeukia Dr Marcelo “ Dr Marcelo huyu ni rafiki yangu anaitwa Monica Mwamsole ambaye Jarida la The Face limemtaja kuwa ndiye mrembo kuliko wote barani Afrika.” Akafanya utambulisho Daniel halafu akainuka na kwenda kumpa mkono Monica “ Hongera sana Monica kwa mafanikio haya makubwa.Unastahiili kuvishwa taji hilo” akasema Daniel na wote wakacheka. “ Ahsante sana nashukuru.Nimeweza kuonekana kutokana na uungwaji mkono toka kwa wadau kama ninyi ambao kila mara mmekuwa mstari wa mbele kuniunga mkono kwa kila jambo” Akasema Monica halafu akainuka na kumfuata Dr Marcelo “ Dr Marcelo nafurahi sana kukufahamu.Karibu sana .Hapa ndipo ofisini kwangu.Nina kampuni yangu inayojishughulisha na masuala ya ubunifu wa mitindo ya mavazi vile vile ninayo taasisi inayojishughulisha na matatizo mbali mbali yanayowahusu watoto wadogo na wazee

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wasiojiweza.Nitakutembeza uone namna kazi zinavyofanyika hapa.Huyu mwenzio Daniel yeye ni mwenyeji hapa anakuja mara kwa mara,ni rafiki yangu wa siku nyingi toka tukiwa wadogo “ akasema Monica.Dr Marcelo akatabasamu na kusema “ Nashukuru sana Monica kwa makaribisho mazuri.Daniel alinieleza kuhusiana na jambo ulilokusuidia kulifanya nikaguswa na nikaomba anilete kwako ili niweze kufahamu kwa undani zaidi juu ya jambo lenyewe na vile vile mimi na taasisi yangu tuweze kutoa mchango wetu kwa hiyo naomba katika orodha yako ya wadau uniongeze na mimi.” Akasema Dr Marcelo “ Ahsante sana Dr Marcelo kwa kuwa mmoja wa wadau wangu.Karibu sana.Mchango wa wadau kama ninyi unahitajika sana” “ Usijali kuhusu hilo Monica tuko pamoja..” akasema Dr Marcelo halafu ukapita ukimya mfupi wa sekunde kadhaa “ Taasisi yako inashughulika na masuala gani? akauliza Monica “ Taasisi yangu inajishughulisha na kuwahudumia wagonjwa wanaosumbuliwa na saratani ya damu.Tuna hospitali tunakowatibu wagonjwa hawa ambayo ni kumbu kumbgu ya baba yangu Dr Richard aliyefariki kwa maradhi hayo ya saratani ya damu” “ Ouh I’m so sorry “ akasema Monica.Baada ya sekunde kadhaa Dr Marcelo akaendelea “ Hospitali yetu ina wagonjwa zaidi ya themanini tunaowahudumia kwa sasa.Hatuna wafadhili wa nje bali ni hospitali inayosimamiwa na familia japokuwa tunapata msaada kidogo kutoka serikalini lakini hilo si tatizo kwetu kwani kama familia tumekwisha azimia kulifanya hilo kumuenzi baba yetu aliyefariki kwa maradhi hayo ya saratani ya damu kwa hiyo tunatumia kila tunachokipata kutoka katika miradi kadhaa ya familia kuwahudumia wagonjwa katika hospitali yetu.” Akasema Dr Marcelo “ Hongera sana Dr Marcelo kwa namna wewe na familia yako mlivyojitolea kuwahudumia wagonjwa hao wenye mahitaji makubwa.Matibabu ya saratani ni ghali sana lakini ninyi mnajinyima na kuwahudumia wagonjwa.Mungu atawabariki kwa hilo mnalolifanya.Sisi sote tuna malengo yanayofanana.Mimi na taasisi yangu tunataka kujenga shule kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum ambao wana ulemavu wa kutoona na kutosikia.Tumegundua idadi ya watoto wenye ulemavu wa aina hii imeongezeka zaidi kwa hiyo tumeamua kujenga shule maalum kwa ajili yao kwani changamoto wanazozipata ni nyingi sana.Ili kulifanikisha hilo tunahitaji kiasi kikubwa cha pesa ndiyo maana tumekuwa tunapita kwa wadau mbali mbali ili kuomba misaada yao ya hali na mali.” Akasema Monica na kwenda kufungua kabati kubwa akatoa makaratasi manne makubwa yenye picha za majengo ya shule wanayotazamia kuijenga akamuonyesha Dr Marcelo . “ Kwa hiyo Dr Marcelo majengo tunayokusudia kuyajenga ndiyo haya.Pamoja na kuzunguka kwa wadau mbalimbali kuomba msaada lakini kuna mambo kadhaa amabyo tumekusudia kuyafanya ili kuweza kutunisha mfuko wetu wa ujenzi.Kwanza tumeandaa mbio za nusu marathoni ambazo zitakuwa ni maalum kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa shule hiyo.Wadau mbalimbali tayari wamekwisha jitokeza kutuunga mkono na kujiandikisha kushiriki katika mbio hizo. Baada ya mbio hizo tutaandaa pia onyesho

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    la mavazi ambalo nalo lengo lake ni hilo hilo kukusanya fedha kwa ajili ya shule hiyo na mwisho kabisa tutaandaa chakula cha usiku maalum kwa ajili ya lengo hilo pia tutawaalika watu mbali mbali,viongozi na makampuni, hata wewe na taasisi yako mtaalikwa pia.Tuna imani kabisa baada ya kukamilisha mipango hiyo tutakuwa tumekusanya kiasi cha kutosha cha fedha tayari kabisa kuanza ujenzi.Kwa hiyo wewe na taasisi yako mtachagua mnataka kushiriki katika tukio gani aidha mbio,nyesho la mavazi , chakula cha usiku au vyote” akasema Monica na wote wakacheka. “ Monica pamoja na kwamba tuna mzigo mkubwa mimi na familia yangu kuwahudumia agonjwa wa saratani kama nilivyokueleza lakini kwa jambo kubwa kama hili la kuchangia ujenzi wa shule hiyo ya watoto wenye mahitaji maalum ni jambo kubwa na la msingi sana ambalo lazima tulichangie.Mimi na taasisi yangu tutashirki katika matukio yote matatu kuanzia mbio hadi chakula cha usiku.” “ Nashukuru sana Dr Marcelo” akasema Monica. “ Katika hizi mbio mlizoziandaa kwanza kabisa tutachangia kiasi cha shilingi milioni themanini na vile vile tutatoa msaada wa kitabibu kwa washiriki wote watakapopata matatizo yoyote wakati wa mbio hizo.Matibabu yote tutayatoa bure kabisa.Katika onyesho la mavazi pia tutatoa mchango wetu na katika chakula tutachangia pia.Tutashirikiana bega kwa bega kuhakikisha jambo hili linafanikiwa.” Akasema Dr Marcelo.Monica akainuka na kumpa mkono Dr Marcelo. “ Ahsante sana Dr Marcelo .Nashukuru sana kwa msaada huo mkubwa.Wadau kama ninyi mnahitajika sana ili kuwasaidia watu wenye matatizo mbali mbali” akasema Monica.Bila kupoteza wakati Dr Marcelo akatoa kitabu cha hundi katika mkoba wake na kuandika hundi ya shilingi milioni themanini akamkabidhi Monica. Baada ya maongezi ya zaidi ya saa moja Monica akawachukua Daniel na Dr Marcelo akawatembeza sehemu mbali mbali za jengo lile na kuwaonyesha kazi wanazozifanya pamoja na hatua mbali mbali za ubunifu wa mavazi.Baada ya kuzungukia sehemu zote wakaagana Daniel na Dr Marcelo wakaingia katika gari lao na kondoka,Monica akarejea ofisini kwake. “ Ahsante Mungu kwa uungwaji mkono mkubwa ninaoupata toka kwa wadau mbali mbali.Najua jambo hili litafanikiwa kwa nguvu zako.Endelea kuwawezesha wadau mbali mbali wazidi kujitokeza wajitolee michango yao ili tuweze kukulifanikisha jambo hili la kujenga shule ya watoto wenye mahitaji maalum.” Monica akaomba na mara akamkumbuka Dr Marcelo “ Wengi wananiunga mkono lakini Dr Marcelo na taasisi yake wametoa mchango mkubwa kupita wote.Ningepata wadau kumi kama hawa ningepiga hatua kubwa sana katika jambo hili” akawaza na kutabasamu “ He’s so handsome.Ni mpole na ana moyo wa huruma .Hata hivyo yeye na familia yake wanaonekana ni watu wenye kujiweza sana kifedha na ndiyo maana wameweza kumudu kuwahudumia watu wenye matatizo ya saratani ya damu.Nimefurahi sana kukutana na mtu mwenye malengo na mtazamo kama wa kwangu.Sote tuna lengo moja la kuwahudumia watu wenye matatizo mbali mbali.” Akawaza Monica

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Dr Marcelo umemuona Monica? Akauliza Daniel wakiwa garini baada ya kuondoka ofisini kwa Monica.Dr Marcelo akatabasamu na kusema “ Nimemuona.She’s hot.She’s an angel.Anastahili kabisa kuwa mrembo kuliko wote Afrika.” Akasema Dr Marcelo na kumfanya Daniel aangue kicheko “ Kwa kweli anastahili.Ni msichana mwenye uzuri wa kipekee kabisa wa ndani na nje.Waliomtaja kuwa mrembo wa afrika hawakukosea.” Akasema Daniel na kimya kifupi kikapita.Baada ya sekunde kadhaa Daniel akasema “ To be honest I love that woman so much .Nimekutana na wanawake wengi sana lakini kati ya hao wote hakuna kama Monica.I’m a champion when it comes to women lakini kwa Monica nadhani kuna dalili za kugonga mwamba.Si mwanamke rahisi kama nilivyodhani.Nimekuwa naye karibu kwa muda mrefu nimejaribu kutumia kila aina ya ufundi nilio nao kumpata lakini sijafanikiwa ila sijakata tamaa nitafanya kila linalowezekana hadi Monica awe wangu.” Akasema Daniel.Dr Marcelo hakusema kitu akabaki kimya.Alionekana kuzama katika mawazo ya ghafla. “Daniel ana haki ya kuchanganyikiwa kwa uzuri wa Monica. Kwa muda mrefu amekuwa akimsifia sana Monica kuwa hajawahi kuona msichana mrembo kama yeye leo nimeamini maneno yake.Monica ni kifaa hasa.Nilipomuona tu mwili wangu wote ukanisisimka nikaingiwa na baridi ya ghafla.Utadhani ninatazamana na malaika kumbe ni mwanadamu mwenzangu.” Akawaza Dr Marcelo “ Baada ya kumuona Monica leo naona kama akili yangu imechanganyikiwa kabisa na ninahisi kumpenda ghafla. Nimesisimkwa mno na sijui kama nitaweza kuendelea na msimamo wangu wa kutojiingiza katika mahusiano ya kimapenzi.Nahisi kuna nguvu Fulani iliyonisukuma kutaka kuonana na Monica.Yawezekana kuonana kwetu ni kwa sababu maalum” akawaza na kumtazama Daniel aliyekuwa akiongea na simu na mmoja wa wanawake zake “ Daniel anakiri kwamba anampenda sana Monica na ameahidi kufanya kila linalowezekana hadi ahakikishe anampata.Namfahamu vizuri huyu jamaa ni kijana mchafu sana wa tabia na siku zote amekuwa akitumia utajiri wake kuwapata na kuwachezea wanawake wengi tu hapa mjini .Ni mtu mwenye tamaa ya ajabu sana na akisha timiza haja zake humuacha mwanamke na kwenda kutafuta mwingine.Sintokubali afanye hivyo kwa Monica.Hawezi kupeleka uchafu wake kwa mwanamke malaika Yule.Monica hastahili kabisa kuchezewa.Daniel tayari amekwisha watoa machozi wanawake wengi tu hapa mjini na sintakubali hata kidogo amtoe machozi Monica.Mwanamke kama Yule anastahili mtu mwenye kumpenda kwa dhati ambaye hatamtoa chozi.She deserves someone like me ambaye nitamtunza na kumlinda kama mboni ya jicho langu lakini tatizo ni hii saratani...” akanyong’onyea ghafla “ Safari hii nitauvunja mwiko na nitajiingiza katika mapenzi.Monica ameustua sana moyo wangu.Potelea mbali litakalotokea na litokee tu lakini lazima niwe na Monica kwani nahisi ndiye mwanamke wa maisha yangu.Kuhusu Monica na Daniel lazima niuvuruge uhusiano wao kwani sitaki kabisa huyu jamaa aendelee kuwa karibu na Monica.Najua kunaweza kutokea uadui mkubwa kati yetu lakini sijali hilo ,kama tukiwa maadui na iwe lakini nitafanya kila niwezalo kwanza kumlinda Monica na pili kuhakikisha ninampata na anakuwa mpenzi wangu hata kama ni kwa kipindi kifupi“ akawaza Dr Marcelo

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    iku ilikuwa ndefu sana na ilipotimu saa mbili za usiku Monica akawasili nyumbani kwa wazazi wake ambako alikaribishwa kwa furaha kubwa .Kwa pamoja walipata chakula cha usiku na Monica akafahamishwa kuhusiana na sherehe itakayoandaliwa pale pale nyumbani kwao siku inayofuata kwa ajili ya kumpongeza kwa mafanikio yake na kubwa zaidi ni kwa yeye kutajwa kuwa ndiye mwanamke mrembo zaidi barani afrika.Baada ya mazungumo yaliyowapeleka hadi saa tano za usiku Monica akaaga na kutaka kuondoka lakini wakati akielekea katika gari lake mama yake akaomba waongozane ana jambo anataka waongee. “ Jambo gani mama? Akauliza Monica wakati wakieleka katika gari. “ Monica kuna jambo moja ambalo nimekuwa nataka kuzungumza nawe kwa muda mrefu kidogo lakini kwa kuwa nafasi inakuwa finyu sana nimeona niongee nawe sasa hivi.Ni kuhusu Yule kijana rafiki yako Daniel mtoto wa mzee Swai” “ Ndiyo mama nakusikiliza” akasema Monica “ Nafahamu kuwa tumekuwa na ukaribu mkubwa na familia yao,wewe na yeye mmekuwa marafiki toka mkiwa wadogo lakini kwa siku za karibuni nimegundua ukaribu wenu umeongezeka sana.Hilo ni jambo jema lakini ilinilazimu kumfanyia uchunguzi ili kumfahamu ni kijana wa aina gani,kuzifahamu tabia zake yote hii ni ili kujua kama anaweza akakufaa kama ukiamua kuingia naye katika mahusiano .Utanisamehe kwa kufanya hivyo bila kukutaarifu lakini ni kwa ajili ya ya faida yako.” “ Usijali mama hilo ni jambo jema na zuri kwani si rahisi kumfahamu vizuri kila mtu anayenizunguka” akasema Monica “ Ahsante Monica.Nilifanya uchunguzi wangu na nikagundua kwamba kijana Yule ni mchafu sana wa tabia.Ana wanawake karibu kila kona ya jiji.Anautumia utajiri alionao kwa ajili ya kuwarubuni wanawake na kuwatumia kimapenzi kisha huwaacha .Ni tabia mbaya sana aliyonayo na ndiyo maana nikataka nikuonye mapema ili ujihadhari naye.Kaa naye mbali hafai kabisa yule kijana .Jihadhari asije akakurubuni ukaingia katika mtego wake.Ninafahamu kuna kitu anakitafuta kwako kwa hiyo kaa naye mbali kabisa” akasema Bi Janet. “ Ahsante mama kwa tahadhari hiyo lakini hata mimi ninamfahamu vizuri Daniel na nimekwisha chukua tahadhari kubwa kuhusu yeye.Ninazifahamu tabia zake ni chafu na ninakuhakikishia kwamba hapa kwangu amekutana na mwamba na hataweza kuleta uchafu wake kwangu.” Akasema Monica “ Ninashukuru kusikia hivyo Monica.Chukua tahadhari kubwa na hasa kwa sasa ambapo jina lako linavuma kila kona ya dunia,watakuja wanaume wengi watakaovutwa na umaarufu wako. Jihadhari nao sana.” “ Ahsante mama kwa tahadhari hiyo lakini unanifahamu vizuri msimamo wangu hakuna yeyote atakayekuja kwa tamaa zake atakayefanikiwa.” Akasema Monica na wote wakacheka “

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Lakini Monica kuna jambo lingine nataka nikuulize” “ Uliza mama” “ Ni muda mrefu sasa tumekuwa tunasubiri taarifa toka kwako lakini mpaka leo hii kimya” “ Taarifa gani mama? Akauliza Monica huku akicheka “ Kuhusiana na mchumba.Mbona hutuelezi chochote? Bado hujampata? Akauliza Bi Janet na wote wakacheka “ Mama suala hili linahitaji umakini mkubwa sana katika kufanya uchaguzi kwani siku hizi watu wamekuwa walaghai mno na mapenzi ya kweli ni nadra sana kupata kwa hiyo ninajitahidi kupata muda wa kutosha kufanya uchaguzi na uchunguzi wa kutosha kujiridhisha na yule nitakayekuwa nimemchagua.Sitaki niumizwe mama na ndiyo maana nimekuwa makini sana katika hilo.Endeleeni kusubiri kidogo na pindi nikiwa tayari wewe utakuwa wa kwanza kufahamu.” Akasema Monica “ Nashukuru sana kusikia hivyo Monica.Basi mimi nakutakia kila la heri na ufanikiwe kumpata mwanaume bora na si bora mwanaume.” “ Ahsante mama nakuahidi nitakuletea mwanaume ambaye wewe mwenyewe utamkubali na utampenda pia” akasema Monica akaagana na mama yake



    akaingia garini na kuondoka kuelekea nyumbani kwake “ Kumbe hadi mama tayari amegundua kuhusu tabia chafu za Daniel.Natakiwa kuanza kukaa naye mbali ili asije haribu sifa yangu.Ukaribu wetu unaweza kuzua maswali mengi kwa jamii na wakadhani labda tuna mahusiano .Natakiwa haraka sana kupunguza mazoea naye “ akawaza Monica akiwa garini kurejea nyumbani kwake. Alifika nyumbani kwake na kuwajulia hali watumishi wake wote na kisha akaingia chumbani kwake akaoga na kujitupa kitandani.Kichwa chake kilijaa mawazo “ Jambo aliloliongea mama ni jambo la msingi sana.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ni wakati sasa wa mimi kumtafuta mwanaume wa maisha yangu.Umri unakwenda kwa kasi na wakati wa kumpata mwanaume wa ndoto zangu ni sasa.Nimezungukwa na wanaume wengi wazuri wenye sifa na tabia nzuri lakini si kazi nyepesi kujua ni yupi anayeweza kunifaa.Umakini mkubwa sana unahitajika katika hili.” Akawaza Monica halafu sura ya Dr Marcelo ikamjia akatabasamu “ Dr Marcelo ni kijana mpole mtanashati na mpenda watu.Katika wanaume wote niliokutana nao na walionizunguka yeye namuona yuko tofauti sana.Nilimtazama machoni wakati tukiongea pale ofisini kwangu nikagundua kitu katika macho yake kwa namna alivyokuwa ananitazama. Jicho lile linanipa picha Fulani kwani mimi si mtoto mdogo kufahamu mtu ambaye anahitaji kitu Fulani toka kwangu.Siwezi pia kuudanganya moyo wangu lakini kwa kweli lazima nikiri kuwa hata mimi nilihisi moyo wangu umestuka sana pale nilipomuona .Kwa kweli amenigusa sana moyoni na kuna kila dalili kwamba kuna kitu kinazunguka kati yetu.Hata hivyo sipaswi kuwa na haraka sana ninachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kumchunguza Marcelo ni mtu wa aina gani ,ana tabia gani na kama anaweza kunifaa kwani kuna kila dalili kwamba ameugusa moyo wangu” akawaza Monica akainuka na kukaa “ Tena itakuwa vizuri kama nitamualika katika sherehe niliyoandaliwa nyumbani kesho.Nikiwa naye karibu nitaweza kumfahamu vizuri sana ni mtu wa aina gani “ Monica akatabasamu kidogo “

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    That’s a good I dea.Natakiwa kumualika Dr Marcelo katika sherehe ya kesho nyumbani kwetu.Lakini tatizo ni je amekwisha oa? Kama ana mke lazima ataambatana naye na mimi ninahitaji awe peke yake ili nipate nafasi nzuri ya kumfahamu.” Akawaza Monica “ Inawezekana kweli Dr Marcelo akawa ana mke? Nakumbuka sikuona pete ya ndoa katika kidole chake lakini hata hivyo kuna njia moja tu ya kufahamu kama ameoa ama vipi.Natakiwa kumtumia ujumbe wa kumualika katika sherehe ya kesho aje na mke wake.Kama hatakuwa na mke atanijulisha.” Akawaza Monica na kuchukua simu yake akamuandikia ujumbe wa mualiko Dr Marcelo na kumtumia .Baada ya kama dakika tatu hivi toka autume ujumbe ule ukaingia ujumbe katika simu yake uliotoka kwa Dr Marcelo akaufungua haraka haraka. “ Monica ahsante sana kwa mwaliko.Nitafika bila kukosa” ndivyo ulivyosomeka ujumbe toka kwa Dr Marcelo.Baada ya kuusoma Monica akatabasamu na kuandika tena ujumbe mwingine “ Usisahau kuja na wifi yangu” Baada ya dakika moja ukaingia ujumbe “ Wifi yako hayupo niko mwenyewe bado sijaingia katika daraja la ndoa” “ Wow !! Kumbe bado hajaoa.” Akawaza Monica huku akitabasamu.Akaandika tena ujumbe mwingine “ I hope utakuwa tayari na mchumba naomba uje naye.Itapendeza sana kama ukiongozana naye” Baada ya sekunde kadhaa ukaingia ujumbe toka kwa Marcelo “ Bado sina mchumba,siko katika mahusiano yoyote ya kimapenzi kwa sasa” “ Mhh !! hiki anachokisema Dr Marcelo ni cha kweli? Inawezekanaje akakosa mke au hata asiwe katika mahusiano yoyote? Ni nadra sana kukutana na kijana mzuri kama Yule halafu akawa hana mchumba wala mahusiano.Kuna haja ya kumchunguza na kumfahamu Dr Marcelo kwa undani kama ni kweli anachokisema basi lazima atakuwa na tatizo..” akawaza Monica na kuandika ujumbe mwingine wa kumjibu “ Ahsante kwa kukubali mwaliko wangu.Tafadhali ufike bila kukosa.Usiku mwema” akautuma na baada ya muda ukaingia ujumbe mwingine toka kwa Marcelo “ Ahsante nashukuru .Usiku mwema nawe” “ Dah !! kuna kitu ninahisi cha tofauti sana kila ninapowaza kuhusu Dr Marcelo.Kesho nitamfahamu vizuri zaidi” akawaza Monica na kuzima simu zake akalala



    Tayari ni saa kumi na mbili za jioni siku iliyofuata na wageni walioalikwa katika sherehe ya kifamilia ya kumpongeza Monica kwa kutajwa kuwa msichana mrembo kuliko wote Afrika,walikwisha anza kuwasili katika jumba la kifahari la bilionea mzee Benedict Mwamsole.Kulikuwa na bendi ya muziki ikipiga kuwatumbuiza wageni waliowahi kuwasili bila kusahau vyakula na vinywaji vya kila aina. Saa mbili za usiku muongoza shughuli akawataarifu wageni walikwa kuwa muda wa kuanza shughuli ulikuwa umewadia na hivyo kila mtu anatakiwa achukue nafasi yake .Huku bendi ikiendelea kutumbuiza Nathaniel Mwamsole kaka wa Monica akashuka ngazi akitokea ghorofani akiwa ameongozana na msichana mmoja mrembo sana.Wageni wakasimama wakimshangilia na akaelekezwa sehemu ya kukaa.Baada ya dakika tano Mzee Benard akiwa ameshikana mkono na mkewe nao wakashuka ngazi taratibu wakipita katika zuria jekundu ,watu wote wakasimama wakiwashangilia.Mzee Benard akaelekezwa sehemu yake ya kukaa iliyoandaliwa maalum kwa ajili ya familia “

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Waheshimiwa wageni waalikwa tunayemsubiri hivi sasa ni malkia wa Africa ambaye atashuka muda si mrefu.Naomba mara tu atakapotokea wote tusimame tumshangilie kwa nguvu huku tukiongozwa na bendi. “ akasema muongoza shughuli.Watu wote walioalikwa katika sherehe ile waliopata zaidi ya mia mbili walielekeza macho yao mlangoni kumshuhudia mwanamke mrembo kuliko wote Afrika atakapotoka.Baada ya kama dakika tano hivi mlango mkubwa ukafunguliwa akajitokeza mwanamke mwenye uzuri usioelezeka na wageni wote wakashangilia kwa nguvu.Taa zote zikawashwa na eneo lote likawa jeupe kwa mwanga.Monica akashuka ngazi taratibu na kutembea katika zuria jekundu kwa madaha huku akipunga mkono.Mzee Benard na mkewe wakampokea Monica na kwenda kumkalisha katika kiti maalum kilichoandaliwa kwa ajili yake.Sherehe ikaanza rasmi. Ilikuwa ni sherehe nzuri ya kukata na shoka.Kila aliyekuwamo mle ndani alisuuzika vilivyo.Kulikuwa na kila aina ya knywaji na chakula.Ratiba ya mwisho ilikuwa ni muziki na vinywaji.Baada tu ya kufungua muziki na watu kujimwaga kuusakata muziki,Monica akaanza kuzunguka ukumbini akisalimiana na watu mbali mbali waliohudhuria sherehe ile na hatimaye akawasili katika meza aliyokuwa amekaa Dr Marcelo na watu wengine watatu.Akawasalimu na kuketi maongezi na vinywaji vikaendelea. “ Dr Marcelo would you mind if I show you around? Akauliza Monica na kwa haraka Dr Marcelo akainuka wakaondoka pale bustanini wakaelekea katika sehemu nyingine kulikokuwa na bwawa la kuogelea. “ Nyumba yenu ni kubwa sana na nzuri” akasema Dr Marcelo “ Hapa ni kwa wazazi wangu mimi siishi hapa kwa sasa.Ni nyumba kubwa na hata kama sote tungeamua kuishi hapa bado tungetosha kabisa kwani kuna vyumba vya kutosha” akajibu Monica wakati wakiketi katika meza iliyokuwa imeandaliwa vinywaji .Dr Marcelo akamtazama Monica na kutabasamu “ Hongera sana Monica .Usiku wa leo umependeza kupita maelezo.Umebarikiwa uzuri wa ajabu sana na sintachoka kurudia tena na tena kuwa waliokutaja kuwa mwanamke mrembo afrika hawakukosea kabisa.Unastahili heshima hiyo kutokana na uzuri ulio nao” akasema Dr Marcelo “ Ahsante sana Dr Marcelo.Hata wewe umependeza sana nadhani kupita vijana wote waliohudhuria sherehe hii” akasema Monica na wote wakacheka “ Sijamuona Daniel,kwa nini hajahudhuria? Dr Marcelo akauliza.Monica akanywa funda moja la mvinyo mwepesi na kusema “ Daniel hujamuona hapa kwa sababu sikumualika.” Akasema Monica “ Hukumualika?!! Dr Marcelo akashangaa “ Ndiyo sikumualika.Hii ni sherehe yangu na ninachagua watu wa kuhudhuria.Sikutaka Daniel ahudhurie” akasema Monica “ Unajua nimeshangaa kidogo kwa sababu ninavyofahamu wewe na Daniel ni marafiki wakubwa.Kuna tatizo lolote limetokea kati yenu? Akauliza Dr Marcelo “ Hapana hakuna tatizo lolote ila niliamua tu kutokumualika Daniel” akasema Monica “ Dr Marcelo let’s forget about Daniel, ni masuala yangu mimi na yeye kwa hiyo yasichukue muda wetu.Kwanza napenda kukushukuru sana kwa kufika ingawa nilitegemea ungekuwa na ubavu wa pili pembeni yako lakini hakuna kilichoharibika” akasema Monica na wote wakaangua kicheko “ Kama nilivyokueleza jana Monica kuwa bado sijafikia daraja hilo” akajibu Dr Marcelo

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “ Usijali Dr Marcelo hakuna tatizo lolote unajua suala kama hili halitaki haraka.Ni suala la kuendea taratibu na umakini wa kutosha unahitajika kwani dunia ya sasa mambo yamebadilika mno.Lakini hata hivyo kwa kijana mwenye hadhi kama yako ukisema huna mke wala hata mchumba inakuwa vigumu kidogo kuamini “ akasema Monica na wote wakaangua kicheko tena “ Ni kweli Monica kama nilivyokueleza jana kuwa mpaka sasa sina mke,mchumba au hata rafiki wa kike kama unaamisha mpenzi japokuwa marafiki wa kawaida wa kike ninao na mmojawapo ukiwa wewe.Vipi kuhusu wewe mbona leo uko peke yako? Yuko wapi mzee?” akauliza Dr Marcelo na wote wakacheka “ Mimi pia ni kama ulivyo wewe mpaka sasa bado sina mpenzi.” Akasema Monica huku akitoa kicheko kidogo “ Usinitanie Monica.Haiwezekani kabisa msichana kama wewe mwenye uzuri wa malaika ukose mpenzi.Thats not true na siwezi kuamini kabisa” akasema Dr Marcelo “ Kwani kuna kitu gani kigumu kuamini Dr Marcelo? Ni kweli sina mpenzi hadi sasa na huo ndio ukweli” akasema Monica “ Nimeshangaa Monica kwa sababu kwa maisha yetu haya ya sasa wasichana wengi wazuri wameugeuza uzuri wao kama mtaji wa kupata unafuu wa maisha ..” akasema Dr Marcelo “ I’m different Dr Marcelo.Mimi sifanani na hao kitabia.Mimi ni mwanamke ninayejitambua na ninaitambua thamani yangu kwa hiyo siwezi kuutumia uzuri wangu kama mtaji” akasema Monica “ Hongera sana kwa hilo Monica ndiyo maana sintachoka kusema kwamba waliokutaja kuwa mrembo wa Afrika hawakukosea.Waliangalia mambo mengi” “ Ahsante sana Dr Marcelo” akajibu Monica Wakati Monica na Dr Marcelo wakiendelea na maongezi bustanini ,hawakujua kama bi Janet alikuwa akiwafuatilia toka walipotoka mahala ilipokuwa inafanyika sherehe.Wakiwa kati kati ya maongezi mara bi Janet akajitokeza. “ Mama !!.akasema Monica kwa mshangao hakuwa ametegemea kabisa kama mama yake angefika pale katika bwawa la kuogelea. “ Monica samahani kwa kuingia ghafla kuna jambo nilitaka tuongee lakini tutaongea baadae,endeleeni na maongezi yenu” akasema Bi Janet “ Ahsante mama ila naomba ukutane na Dr Marcelo Richard.Yeye ni rafiki yangu na ana hospitali ya kuwahudumia wagonjwa wenye maradhi ya saratani ya damu. Ni mmoja kati ya wadau waliojitoa kwa hali na mali kufanikisha ule mradi wangu wa shule ya watoto” akasema Monica na kumgeukia Dr Marcelo “ Dr Marcelo huyu ni mama yangu mzazi anaitwa Bi Janet Mwamsole” Dr Marcelo akainuka na kumsalimu bi Janet kwa adabu.Kisha salimiana Bi Janet akaondoka na kuwaacha Monica na Dr Marcelo wakiendelea na maongezi yao. “ Dr Marcelo Richard !! akanong’ona bi Janet wakati akiondoka pale katika



    bwawa la kuogelea walikokuwa wamekaa Monica na Dr Marcelo “Kwa nini Monica aamue kuacha maeneo yote mazuri kwa kukaa na kuzungumza akaamua kuja kukaa huku katika bwawa la kuogelea? Is something going on between them? Nahisi kuna jambo linaendelea kati yao na ndiyo maana wameamua kujitenga huku? Hata hivyo kwa muonekano wa haraka haraka Yule kijana anaonekana kuwa ni kijana mwenye adabu sana na msomi mzuri.Mimi si mtoto mdogo kwa namna walivyokuwa wamekaa inaonyesha kabisa kuna kitu kinachoendelea kati yao .Natakiwa kumfanyia uchunguzi wa kina huyu Dr Marcelo ili nimfahamu ni mtu wa aina gani na kama hana tabia nzuri basi nimkanye Monica aachane naye angali mapema.Yule mwingine Daniel sijamuona hapa ninahisi yale maneno niliyomueleza jana yamefanya kazi.” Akawaza Bi Janet na kumtafuta kijana mmoja anaitwa Bakari ambaye ni mmoja wa vijana anayemtumia katika shughuli zake nyingi “ Bakari kuna kazi ninataka unifanyie na ninahitaji majibu yake kwa haraka kesho” akasema Bi Janet “ Kazi gani mama? “ Unakumbuka niliwahi kukupa kazi ya kumchunguza Yule kijana rafiki wa Monica anaitwa Daniel? “ Ndiyo nakumbuka mama” “Sasa nataka uifanye kazi kama ile.Kuna kijana mmoja nataka kupata taarifa zake za kina.Anaitwa Dr Marcelo yuko na Monica hivi sasa bustanini wanaongea.Nataka kazi hiyo uianze usiku huu wa leo.Wafuatile kila wanachokifanya na uone kama kuna chochote kinachoendelea kati yao” “ Sawa mama nitafanya hivyo .Tegemea taarifa nzuri yenye kila unachokihitaji” akasema Bakari



    Taarifa za kuwepo kwa sherehe kubwa nyumbani kwa akina Monica zilizoandaliwa na familia yake kwa ajili ya kumpongeza zilimfikia Daniel na kumshangaza sana.Hakutegemea kabisa kama kungeweza kufanyika sherehe kama ile bila yeye kualikwa au hata kujulishwa hasa kutokana na ukaribu wake na Monica na vile vile ukaribu wa familia zao.Alijiuliza maswali mengi sana na hakuweza kupata jibu. “

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Haijawahi kutokea hata mara moja toka kwa Monica kufanya jambo kubwa namna hii bila kunijulisha.Siku zote anapokuwa na jambo huwa ananifahamisha lakini kwa hili hajanijulisha na wala hajanialika,what happened? Nini kimesababisha asinialike? Halafu kingine nasikia Dr Marcelo alikuwepo.Yaani mtu ambaye amefahamiana jana tu na Monica amealikwa lakini mimi ambaye nimekuwa na Monica kwa miaka mingi hata taarifa sina kwanini Monica ananifanyia hivi? Kuna kitu gani nimekosea? Akajiuliza na kuchukua simu akazitafuta namba za Monica akapiga lakini simu ya Monica haikuwa ikipatikana.Akapiga namba za simu za Dr Marcelo lakini hazikuwa zikipatikana.Akampigia Hidaya msichana ambaye ni rafiki yake Monica ambaye anafahamiana naye na ambaye ndiye aliyemjulisha kuhusiana na sherehe ile baada ya kutomuona . “ Hidaya “ akasema Daniel baada ya Hidaya kupokea simu “ Unasemaje Danny? “ Nini kinachoendelea hivi sasa hapo shereheni? “ Kinachoendelea hivi sasa ni muziki na vinywaji? “ Monica unaweza ukamuona hapo? “ Monica kitambo sana sijamuona sijui amekwenda wapi? “ Dr Marcelo naye unamuona hapo ? “ Daniel watu ni wengi hapa kwa hiyo si rahisi kumuona mtu kwa haraka ila nilimuona hapa kuna wakati alikuwa anaongea na Monica na hivi sasa kila mtu amejichanganya kucheza muziki” “ Basi naomba ukimuona Monica umpe simu yako niongee naye kwa sababu nimejaribu kumpigia simu yake haipatikani” “ Sawa Daniel nitafanya hivyo mara tu nitakapomuona” akasema Hidaya na kukata simu.Daniel akaitupa simu sofani “ Kwa nini Monica amenifanyia hivi? Kuna tatizo gani kati yangu naye? Nimekuwa na ukaribu sana na Monica na hajawahi kunitenga katika jambo lake lolote.Lazima kuna kitu kilichosababisha nisijulishwe au nisialikwe.Nitamtafuta Monica anieleze nini kimetokea hadi aniache mimi mtu wake wa karibu na wa siku nyingi na amualike Dr Marcelo ambaye amefahamiana naye jana tu.” Akawaza Daniel akiwa amejawa na hasira



    r Marcelo aliwasili nyumbani kwake saa saba za usiku baada ya sherehe kumalizika.Uso wake haukukaukiwa tabasamu .Alikuwa na furaha iliyopitiliza. “ For he first time in my life I’m happy.Nina furaha ya ajabu sana leo na usiku huu wa leo utaingia katika historia yangu kwani ni usiku wa kwanza ulionifanya nikawa na furaha na ni usiku wa kwanza katika maisha yangu I feel I’m in love.I think I’ve found the woman of my dreams.Ninaamini Monica ndiye mwanamke wa ndoto zangu kwani kati yetu kuna muunganiko .We feel connected to each other .Sijawahi kuhisi kuwa karibu na mwanamke yeyote kama ilivyonitokea kwa Monica.Mimi na yeye tumefahamiana jana lakini utadhani urafiki wetu ni wa miaka mingi.Nadhani ni wakati sasa wa kuufungua ukurasa mpya katika maisha yangu.Ukurasa wa mapenzi.Sihitaji kukata tamaa kuhusu maisha yangu,nahitaji kuwa na mawazo chanya kuhusu maisha yangu .I want to live long because of Monica.” Akaendelea kuwaza Dr Marcelo .Akachukua simu yake na kuzitafuta namba za Monica kwa dhumuni la kumpigia na kumshukuru kwa usiku ule mzuri lakini simu ya Monica haikuwa ikipatikana “ Nitaonana naye kesho.Lazima nianze kuchukua hatua za haraka za makusudi kuupalilia urafiki wetu.Tayari kuna kila dalili kuwa hata yeye Monica ananihitaji kuwa rafiki yake.Kitendo cha kumuacha Daniel ambaye ni rafiki yake mkubwa na wa siku nyingi akanialika mimi ni wazi kuwa ananihitaji niwe karibu yake.Nadhani tayari amekwisha zifahamu tabia za Daniel na ameanza kujitenga naye.Hii ni nafasi yangu kuitumia.Najua Daniel akigundua kwamba nimekuwa na ukaribu na Monica urafiki wetu utatetereka sana lakini sijali kuhusu hilo.Uhusiano wa Daniel na Monica natakiwa kuuzika kabisa.Monica anatakiwa awe na mwanaume mwenye heshima zake kama mimi .” akawaza Dr Marcelo

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    onica hakurejea nyumbani kwake baada ya sherehe kumalizika bali alienda kujipumzisha katika chumba chake kilichokuwapo katika nyumba ya wazazi wake. “ Mama alitaka kuongea nini na mimi hadi akanifuata kule bwawani nilikokuwa na Dr Marcelo na alijuaje kama niko kule? Akajiuliza akiwa amejilaza kitandani “ Hata hivyo hakuna ubaya wowote kwani alitukuta tukiwa katika mongezi ya kawaida.” akawaza Monica na kutabasamu “ Hakuna siku nimejawa na furaha katika maisha yangu kama leo.Nina furaha ya ajabu sana.Sherehe imefana sana kila mtu amefurahi na kwa hili napaswa kuwashukuru sana wazazi wangu kwa kunijali .Kitu kingine kilichonifanya niwe na furaha ni Dr Marcelo.Nimepata leo nafasi ya kukaa naye karibu tukaongea japo kwa muda mfupi lakini ni mtu ambaye naweza kusema kwamba amenigusa sana.Ni kijana mwenye tabia nzuri,ana moyo wa huruma na ana malengo makubwa .Natamani kama ningepata muda mrefu zaidi wa kukaa na kuongea naye...” akawaza na kuinuka akakaa. “ Oh no !! I think Im falling in love so quickly..” akasema kwa sauti ndogo “ Kwa hili siwezi kubishana na moyo wangu kuwa tayari nimeanza kumpenda Dr Marcelo .Hata yeye kuna kitu nimekigundua kutoka kwake .Kuna kila dalili kuwa kuna kitu kipo kati yetu .Naomba Mungu hisia hizi tulizonazo ziwe za kweli “ Uso wa Monica ukajaa tabasamu kubwa “ Siwezi kusema moja kwa moja kuwa Dr Marcelo is the right guy for me hadi hapo nitakapomchunguza lakini lazima nikiri kuwa amenisisimua na katika kipindi hiki cha masaa machache tulichofahamiana nimemsoma vya kutosha na moyo wangu unaniambia kwamba anaweza akanifaa.Pamoja na hisia hizi kali nilizo nazo juu yake bado sitakiwi kuwa na haraka.Natakiwa kwanza kumfanyia uchunguzi wa kina nimfahamu ni mtu wa aina gani” Mara akakumbuka kitu “ Dr Marcelo amenisaidia niweze kumuweka pembeni Daniel.Ni kweli mimi na Danny tumekuwa karibu na kwa kipindi kirefu lakini kwa sasa simuhitaji tena karibu yangu.Nimekwisha lifahamu lengo lake kwangu na sitaki kumpa nafasi ya kuwa karibu yangu.Sitaki kuzungukwa na watu wachafu wa tabia kama yeye.Nitakuwa karibu na Dr Marcelo ambaye anaonekana ni kijana mwenye tabia nzuri tofauti kabisa na Daniel.” Akawaza Monica



    Kumekucha tena siku nyingine imeanza.Saa nne za asubuhi Monica akawasili ofisini kwake.Akiwa mapokezi akataarifiwa kwamba Daniel alikuwa juu ghorofani akimsubiri .Alifika toka saa mbili za asubuhi. “ Huyu jamaa anaonakana atanisumbua sana.I must find a way to drive him away from me..” akawaza Monica huku akipanda ngazi kuelekea juu .Alisalimiana na wafanyakazi wake halafu akaelekea ofisini kwake akamkuta Daniel akiwa katika sofa nje ya ofisi yake akimsubiri.Pembeni yake kulikuwa na maua mazuri . “ Daniel “ akasema Monica huku akijilazimisha kutabasamu “ Monica” akasema Daniel akiinuka akamfuata Monica akamkumbatia. “ Goodmorning queen of Africa” akasema Daniel “ Goodmorning Daniel” akasema Monica huku akiifungua ofisi yake akamkaribisha Daniel ndani. “ Daniel karibu sana.You are so early today” akasema Monica “ Yes I’m so early today.Nimefika hapa kama mfanyakazi “ akasema Daniel na wote wakacheka “ Hii si kawaida yako Daniel.Kuna tatizo lolote? Akauliza Monica huku akipanga vitu vyake mezani halafu akaenda katika sofa alikokuwa amekaa Daniel “ Sikuweza kupata usingizi usiku ndiyo maana nimewahi sana kuja asubuhi ya leo” akasema Daniel “ Kuna tatizo gani Daniel? Kitu gani kimekukosesha usingizi? Akauliza Monica.Daniel akamtazama Monica kwa sekunde kadhaa kisha akasema “ Monica me and you we’re long time great friends,right? “ Yeah..We’re great friends” akajibu Monica “ Kwa nini ukanifanyia hivi? “ Nimekufanyia nini Daniel? “

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa nini hukuniambia kama umefanyiwa sherehe ya kupongezwa na wazazi wako? Kama hukutaka nihudhurie lakini basi ungenitaarifu tu ingetosha.Hujawahi kunifanyia kitu kama hiki toka tumefahamiana .Nimesononeshwa sana na jambo hili na ndiyo maana sikuweza kupata usingizi usiku wa leo .Nimejiuliza maswali mengi ni kitu gani nimekukosea hadi ukashindwa kunialika katika sherehe yako kubwa kama hii ili nifurahi pamoja nawe? Tafadhali naomba unieleze Monica kama kuna jambo lolote baya nimekufanyia ili nikuombe msamaha na ili siku nyingine usinifanyie jambo kama hili ulilonifanyia” akasema Daniel.Monica akamtazama kwa makni na kusema “ Daniel kwanza naomba unisamehe sana kwa hiki kilichotokea.Ni kweli jana kulikuwa na sherehe iliyofanyika nyumbani kwa wazazi wangu kwa lengo la kunipongeza kwa mafanikio yangu.Ni sherehe ndogo iliyoandaliwa na wazazi na iliandaliwa kwa haraka na hata mimi sikuwa nimetaarifiwa uwepo wa sherehe hiyo.It was a surprise na walioalikwa katika sherehe hiyo karibu wengi walialikwa na wazazi bila ya mimi kufahamu” akasema Monica “ Lakini ulimualika Dr Marcelo.” Akasema Daniel.Monica akanyamaza kidogo akavuta pumzi na kusema “ Nilikuwa na Dr Marcelo jana jioni tukijadiliana mambo kadhaa kuhusiana na shughuli ambazo mimi na taasisi yangu tunakusudia kuzifanya nilipopigiwa simu na mama akanitaka nifike nyumbani haraka sana hivyo nikaongozana na Dr Marcelo na tulipofika kule nikakuta kumeandaliwa sherehe.”Monica akadanganya “ Ahsante kwa taarifa hiyo lakini ungenitaarifu kuhusiana na uwepo wa sherehe hiyo ningekuja hata kama imefika katikati. “ “ Samahani kwa hilo Daniel.It wont happen agai......” kabla Monica hajamaliza alichotaka kukisema mlango ukafunguliwa akaingia Linah msaidizi wake akiwa amebeba kikapu cha maua mazuri sana. “ Madam kuna mzigo wako umeletwa hapa sasa hivi “ akasema Linah “ Wow ! what a beautiful flowers.Yametoka wapi haya? Akauliza Monica huku akiinuka na kuyapokea maua yale akayaweka mezani. “ Kwa mujibu wa mtu aliyeyaleta anasema ameagizwa na Dr Marcelo” “ Dr Marcelo ? Daniel akasema kwa mshangao.Linah akampa karatasi ya kusaini kwamba amepokea mzigo .Monica akasaini Linah akatoka . “ Dr Marcelo amekutumia maua haya? Akauliza Daniel.



    Monica hakujibu kitu akabaki anayatazama maua yale mazuri huku akitabasamu “ Inaonekana mmekuwa marafiki wakubwa tayari hadi mtumiane maua? Akauliza Daniel huku sura yake ikionyesha wazi kuwa hakuwa amependezwa na kitendo kile cha Dr Marcelo kumtumia Monica maua. “ Stop that Danny.Kwani kuna ubaya gani kwa Marcelo kunitumia maua? Isitoshe I love flowers” akasema Monica na mara simu yake ikaita alikuwa ni Dr Marcelo “ Hallow Dr Marcelo” Monica akapokea simu ile mbele ya Daniel “ Good morning Monica” akasema Dr Marcelo “ Good Moring Marcelo.Umeamkaje? “ Nimeamka salama Monica sijui wewe” “ Mimi niko poa kabisa.Ahsante sana kwa maua mazuri.Nimeyapokea muda mfupi uliopita” akasema Monica huku akitabasamu “ Umeyapenda? “ Kwa nini nisiyapende? I love flowers ,nimeyapenda sana maua uliyoyaleta” akasema Monica na mara Daniel akainuka na kumfanyia Monica ishara kuwa anaondoka . “ Nashukuru sana kama umeyapenda maua niliyokutumia Monica.Lengo ni kukushukuru kwa siku ya jana ilikuwa ni nzuri .Mimi si mtokaji sana wa kuhudhuria sherehe au kwenda sehemu za starehe muda mwingi niko kazini lakini kwa siku ya jana nimefurahi mno.Ahsante sana Monica” “ Nafurahi kusikia hivyo Dr Marcelo.Unajua mara nyingi tunajikuta tukitumia muda mwingi kwa ajili ya kazi zetu na kujisahau kama na sisi tunahitaji kufurahi kama watu wengine. Ni muhimu kutenga muda walau mara moja kwa wiki kupumzisha na kuburudisha mwili.” “ Usemayo ni ya kweli Monica.Basi naomba nikuache uendelee na kazi zako tutakutana kesho kutwa katika mbio.” “Sawa Dr Marcelo.Ahsante sana na uwe na siku njema” akasema Monica na kukata simu.Akayatazama tena maua yale aliyotumiwa na Dr Marcelo “ Dr Marcelo ni mtu anayenifanya nitabasamu kila siku.Hiki alichokifanya anaweza akafikiri kuwa ni kidogo lakini ni kitu kikubwa kwangu.” Akawaza Monica na kukumbuka kitu “

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Daniel tayari amekwisha anza kuwa na wasiwasi kuhusu ukaribu wangu na Dr Marcelo .Nimeiona sura yake baada ya kushuhudia maua yaliyotoka kwa Dr Marcelom hakupendezwa.Najua hili ni jambo linaloweza kuzua mtafaruku katika urafiki wao kwani ni marafiki wakubwa lakini mimi ndiye mwenye kuamua ninataka kuwa na ukaribu na nani na kwa sasa nimemchagua Dr Marcelo.Sitaki kuendelea na ukaribu na Daniel.Nataka kama ikiwezekana urafiki wangu naye ufike mwisho.Sina tabia ya kuchagua marafiki lakini kwa sasa itanilazimu kufanya hivyo nataka kuwa na marafiki wasafi wenye tabia na mienendo mizuri ili niweze kuwa mfano kwa wengine kwani kwa sasa mimi ni mtu ninayeangaliwa sana kwa kila ninachokifanya” akawaza Monica na kumuita Linah akampatia yale maua aliyokuja nayo Daniel “ Nenda kayaweke huko na tafadhali naomba siku nyingine Daniel akija hapa asiruhusiwe kuja kuingia bila ruhusa yangu” “ Sawa Madam” akajibu Linah na kutoka



    “ Bado siamini eti urafiki wa Dr Marcelo na Monica umekuwa mkubwa kiasi cha kufikia hatua ya kutumiana maua.Nimewakutanisha juzi tu na leo urafiki wao umekua kana kwamba wamekutana miaka kumi iliyopita!! That wont happen.Halafu jana Monica ameniacha mimi rafiki yake wa miaka mingi toka utotoni akamualika Marcelo mtu aliyefahamiana naye juzi kwa nini lakini? Cha kushangaza zaidi Marcelo amemtumia Monica maua.Hii ni wazi urafiki wao unaanza kuota mizizi na kuna kila dalili kuwa tayari Dr Marcelo ameanza kuvutiwa na Monica.I wont let it happen.Natakiwa kufanya kila niwezalo kuhakikisha kwamba urafiki wao haufiki kokote.Nikizubaa zubaa hapa nitakosa kila kitu.Siwezi kukubali kumkosa Monica.Nimeupalilia urafiki wetu kwa muda mrefu sana na siwezi kuja kushindwa sasa labda mimi si Daniel Swai” akawaza Daniel huku sura yake ikiwa imejikunja akionekana wazi kukasirika sana. “ Kwanza kabisa kuna mambo ambayo natakiwa kuyafanya kwa haraka sana.Kwanza natakiwa kuonana na Marcelo na kumkanya aachane kabisa na Monica.Najua anaweza akakasirika lakini hakuna namna lazima nimueleze ukweli kwamba Monica ni wangu na lazima aachane naye haraka sana.Kama ni ukaribu basi uwe ni wa kawada na asijaribu kabisa kuingiza masuala ya mapenzi kwa sababu nimekwisha mueleza toka jana kuwa ninampenda Monica na niko katika harakati za kumpata.Sintakubali hata kidogo atokee na avuruge mipango yangu.Potelea mbali kama urafiki wetu utavunjika lakini kwa ajili ya Monica niko tayari kwa hilo “ Daniel akauma meno kwa hasira wakati akielekea katika hospitali inayomilikiwa na familia ya akina Marcelo.Alifahamika sana mahala hapa kwa kuwa amekuwa akija mara kwa mara ,akapokelewa vizuri na kutaarifiwa kuwa Dr Marcelo alikuwa anazungukia wagonjwa.Hakutaka kuondoka akaamua kumsubiri hadi atakapomaliza shughuli zake. Saa sita za mchana Dr Marcelo akarejea ofisini kwake huku akionekana kuwa na kazi nyingi,akastuka alipomkuta Daniel. “ Daniel!! Akasema “ Dr Marcelo” akasema Daniel “ Karibu sana.Umekuja muda mrefu? “ Ndiyo nimekuja kitambo kidogo” “ Karibu sana Danny.Leo niko katika heka heka kuna wagonjwa wawili hali zao si nzuri na ndiyo maana nimetumia muda mrefu wodini.” “ Ouh usijali Dr Marcelo” akasema Daniel huku akiketi kitini. “ Karibu sana Daniel..” akasema Dr Marcelo baada ya kumuona Daniel akiwa kimya huku akimtazama kwa macho makali “ Dr Marcelo utanisamehe kwa kuchukua muda wako lakini nitajitahidi kuongea kwa ufupi sana kile kilichonileta hapa.” “ Karibu..” akasema Marcelo “ Nilitaarifiwa jana na Hidaya kuhusiana na sherehe aliyoandaliwa Monica na wazazi wake.nIliambiwa na wewe ulihudhuria” “ Yah nilihudhuria ilikuwa nzuri .Ilifana mno.I wish ungekuwepo” akasema Dr Marcelo “ Too bad kwamba sikualikwa achilia mbali kujulishwa kwamba kuna kitu kama hicho.” “ Lakini Monica ni rafiki yako mkubwa ,kwa nini hakukujulisha kama kuna sherehe imeandaliwa nyumbani kwao? Akauliza Dr Marcelo “ Sifahamu kwa nini lakini naona kama vile urafiki wetu umeingiliwa na mdudu na ndiyo maana hakunitaarifu kama kuna shrehe nyumbani kwao.Hajawahi kutokea Monica akafanya jambo lolote kubwa bila ya kunitaarifu.Mimi na yeye tumekuwa marafki kwa muda mrefu toka tukiwa wadogo .Familia zetu ni marafiki wakubwa kwa hiyo urafiki wetu haukuanza jana.Nimestuka sana kwa hiki alichonifanyia Monica lakini inawezekana kwa sababu ilikuwa ni sherehe ya kustukiza ndiyo maana akanisahau mimi mtu wake wa karibu.” Akasema Daniel “ Surprise party?!! Dr Marcelo akashangaa “ Ndiyo.Anasema hakunialika kwa sababu ilikuwa ni surprise party” “ Hapana haikuwa surprise party.Mbona mimi amenialika usiku wa kuamkia jana? Kama ingekuwa ni surprise asingenialika siku moja kabla

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Inawezekana kabisa labda hakutaka uhudhurie na ndiyo maana hakukutaarifu” akasema Dr Marcelo.Maneno yale yalionekana kumchoma sana Daniel ambaye aliinama akafikiri kidogo halafu akainua kichwa na kusema “ Inawezekana hayo unayoyasema ni ya kweli .Inawezekana hakutaka nihudhurie katika sherehe hiyo lakini pamoja na hayo bado Monica ndiye mwanamke peke ninayempebnda kuliko wote.Yawezekana alikuwa na sababu zake na ndiyo maana akafanya hivyo alivyofanya lakini siwezi kumchukia kwa hilo wala kumlaumu kama kuna tatizo atanieleza.” Akasema Daniel “ Yah “ akajibu Dr Marcelo “ Kabla ya kuja hapa nimetoka ofisini kwa Monica nimeonge a naye na tumeweka mambo sawa .Wakati nikiwa pale ukaingia mzigo wa maua ukitokea kwako.Nikastuka kidogo kwamba mmefahamiana juzi tu na Monica halafu leo hii tayari mmeanza kumtumia maua.Nimejiuliza maswali mengi maua yale yalikuwa kwa ajili gani? Ni ya pongezi,au ya nini? Usije ndugu yangu ukaanza kunizunguka wakati nimekwisha kueleza kwamba mimi Monica ndiye mwanamke ninayemtaka na nimeupalilia urafiki wetu kwa miaka mingi na nimekwisha weka ahadi lazima nihakikishe nimempata.” Akasema Danel huku akicheka kidogo.Dr Marcelo akastuka sana kwa kauli ile ya Daniel “ Unajua uuhh..nilimtumia maua yale..you know me..ninapenda kushukuru..” akasema Dr Marcelo. “ Ni vizuri kama itakuwa hivyo na si vinginevyo.Marcelo naomba nirudie tena kukuweka wazi kwamba ninampenda Monica sana zaidi ya ninavyoweza kukueleza na kwa hiyo niko tayari kufanya jambo lolote lile kwa ajili ya kuhakikisha ninampata kwa hiyo basi naomba ulifahamu hilo na usithubutu kufanya mchezo wowote wa kujaribu kunizunguka.Nikigundua kama unanizunguka I swear I’ll forget that you are my friend and we’ll become enemies.Umenielewa Marcelo? Akauliza Daniel .Marcelo hakumjibu kitu akabaki anamtazama. “ Umenielwa Marcelo? Akauliza Daniel safari hii kwa ukali kidogo “ Daniel kuna kitu sijakielewa hapa.Unadai kwamba Monica ni msichana wako nikimpigia simu sasa hivi atakiri hilo? Akauliza Dr Marcelo ambaye naye alionekana kukereka sana na maneno yale ya Daniel “ Unataka kumaanisha nini Marcelo? Akauliza Daniel uso ukiwa umejikunja “ Ninataka nipate uhakika wa hayo unayoyasema kama kweli Monica ni mpenzi wako” “ Sijasema kwamba Monica ni mpenzi wangu nimesema kwamba ninataka awe mpenzi wangu na sijaanza leo nimeanza kuipalilia njia miaka mingi iliyopita na kuna kila dalili za kuelekea katika kulifanikisha hilo hivi karibuni kwa hiyo nakuomba usiwe kikwazo cha mimi kushindwa kulifanikisha hilo.Toka nimekutambulisha juzi naona kumekuwa na mabadiliko makubwa kwa Monica.” Akasema Daniel “ Daniel kuhusu maelewano yako na Monica kubadilika ghafla mimi si wa kulaumiwa kwani siwezi kuingia ndani ya moyo wa mtu na kujua anawaza nini .Hayo ni masuala yenu ninyi wawili mkae na mtafute namna ya kuyatatua na ninaomba mimi nisihusishwe kabisa.Halafu hata kama nikitaka kuanzisha mahusiano ya kimapenzi hakuna wa kunizuia kwani Monica yuko huru na hafungwi na mahusiano yoyote” Akasema Dr Marcelo kwa sauti ya juu “ Marcelo naomba usijaribu kutafuta ugomvi na mimi .Mmi ni mtu mbaya sana nikikasirishwa kwa hiyo kama unataka kuziona hasira zangu basi endeleza mahusiano na Monica.Nimekwisha kwambia kwamba Monica ni wangu .” “ Daniel naomba tafadhali usijaribu kunitisha.Huna uwezo wa kunizuia nisiwe na Monica.Mwenye uwezo huo ni Monica peke yake kwa hiyo kama huna jambo lingine la kuniambia tafadhali naomba uondoke ofisini kwangu kabla sijaita walinzi wakutoe kwa nguvu.” Akasema Dr Marcelo kwa ukali huku akisimama.Daniel naye akasimamana kumkaribia “ Please Marcelo don’t try me!!! Akasema Daniel kwa hasira “ Kwenda zako Daniel huna lolote la kunitisha .Kama ungekuwa kidume kweli kwa miaka hii yote uliyokuwa na ukaribu na Monica basi ungekwisha mpata lakini pale umegonga ukuta kwani Yule si kama hao makahaba ambao umezoea kuwarubuni kwa vihela vyako.” Akasema Dr Marcelo na ghafla Daniel akamvuta koti na kutaka kumkaba lakini Dr Marcelo akamsukuma kwa nguvu akaanguka chini. “ Get out of my office right now kabla sijakuharibu sura yako ..!!! akasema Dr Marcelo kwa ukali “ Marcelo hvi ni wewe unayethubutu kunifanyia hivi kweli??? Akauliza Daniel akiwa bado amekaa chini “ Daniel naomba uinuke haraka sana uondoke kabla hasira zangu hazijapanda nikajikuta nimekufanyia kitu kibaya ambacho nitakijutia !!! akasema Marcelo kwa ukali.Taratibu Daniel akainuka “ Marcelo this isn’t over...Umeuwasha moto ambao hutaweza kuuzima.Mimi na wewe hivi sasa ni maadui wakubwa na sasa utanifahamu kama mimi ndiye mwenye jiji hili.” Akasema Daniel



    Hunitishi Daniel.Tena ninakuonya kwamba kaa mbali kabisa na Monica na usithubutu kumsogelea.Hakutaki kabisa karibu yake wewe mchafu wa tabia.If I ever see you near Monica agan it’ll be you or me..!! akasema Marcelo . “ Get prepared Marcelo!!! Akasema Daniel na kutoka akiwa amejaa hasira.Dr Marcelo akavuta pumzi ndefu na kuketi kitini “ Nilijua tu jambo kama hili lazima litatokea.Lakini ni bora nikaingia katika mgogoro na Daniel kuliko kumuacha akawa karibu na Monica.Niko tayari kwa lolote kwa ajili ya Monica.Yule ni mtu mwenye heshima kubwa sana na siko tayari kuona akiingia katika ulaghai wa mtu kama Daniel.Ni bora nikayapoteza maisha yangu katika kumpigania Monica kuliko kukubali akawa katika mapenzi na Daniel.Mimi simuogopi na hawezi kunifanya chochote” akawaza Dr Marcelo na kuchukua simu akampigia Monica “ Hallow Dr Marcelo” akasema Monica “ Monica samahani sana kwa kukusumbua tena” “ Bila samahani Dr Marcelo” akasema Monica “ Daniel was here.Kumetokea mtafaruku kati yetu” “ oh my God !! is everything ok? Are you ok? Akauliza Monica kwa wasi wasi “ Usijali Monica hakuna tatizo tulipisha tu kauli.” Akasema Marcelo “ Alikuwa anataka nini Daniel? “ Alikuja kunikanya nisiwe karibu nawe kwa sababu anakusudia uwe wake.Wewe nay eye mna mahusiano yoyote ya kimapenzi? “ Hapana mimi na Daniel hatuna mahusiano yoyote yale ya kimapenzi ni marafiki wa kawadia toka tukiwa wadogo.Tafadhali naomba asikusumbue huyo” akasema Monica kwa ukali “ Hata mimi nilimwambia kwamba hawezi kunizuia nisiwe karibu nawe bali wewe ndiye mwamuzi kama niwe karibu nawe au vipi.Ameondoka na hasira na vitisho vingi.” “ Pole sana Dr Marcelo na samahani sana kwa kilichotokea.” Akasema Monica “ Usijali Monica.Hili si tatizo kubwa kwangu ila nimeona ni vema kama nitakutaarifu kilichotokea na kinachoendelea kati yangu na Daniel ili usisikie kwa watu ukashangaa” akasema Dr Marcelo “ Ahsante Dr Marcelo .Again I’m so sorry and dont worry I’m gong to handle it” “ Thank you Monica.Have a good day” “ You too “ akajibu Monica na kukata simu “ Huyu Daniel sasa amefika pabaya.Kitendo cha mimi kuwa karibu na Dr Marcelo kimemuumiza sana.Kumbe lengo lake la kuwa karibu nami ni kuniweka katika orodha ya wanawake aliotembea nao.Hapa kwangu amekwaa kisiki.Lazima nimkanye asimfuate kabisa Dr Marcelo.Anatakiwa apambane na mimi na si Dr Marcelo..” akawaza Monica na kuchukua simu akampigia Daniel “ Hallow Monica” akasema Daniel baada ya kupokea simu “ Daniel nataka unieleze kitu kimoja tu,ulikwenda kufanya nini kwa Dr Marcelo?? Akauliza Monica kwa ukali “ Calm down Monica..” “ Calm down?!! Nataka unieleze umekwenda kufanya nini kwa Dr Marcelo? “ Monica I’m sorry.Real I am.Naomba tuzungumze suala hili wakati umetulia.Let us find sometime and we can talk” “ Nataka unieleze sasa hivi kwa nini umemfuata Dr Marcelo na kumtusi pamoja na kumtolea vitisho? “ Monica taarifa ulizopewa si za kweli,sijamtusi wala kumtisha lakini hata hivyo naomba tuzungumze jambo hili wakati tumetulia.Hivi sasa mimi nina hasira na wewe una hasira pia kwa hiyo hatuwezi kuzungumza.Nitakutafuta wakati umetulia na tutaongea ila I’m sorry for what happened “ “ Wa kumuomba samahani si mimi bali Dr Marcelo ambaye ulimfuata na kumtolea vitisho kwamba asiwe karibu na mimi.Wewe ni nani hadi unipangie watu wa kuwa karibu nao.Umeniudhi sana Daniel” “ I’m so sorry Monica.Ndiyo maana nikasema kwamba nitatafuta nafasi wakati sote tumetulia tutaongea kuhusu suala hili,ila naomba samahani sana kama nimekuudhi Monica” “ Ni kweli nimechukia lakini wa kumuomba samahani si mimi bali ni Dr Marcelo ambaye umemfuata na kumtolea vitisho.Ukitaka nikusamehe nenda kwanza kwa Dr Marcelo na umuombe msamaha ndipo na mimi nitakusamehe” akasema Monica na kukata simu “ I’ll never say sorry to that bastard...Sintaweza kumuomba msamaha Dr Marcelo wakati yeye ndiye aliyenichokoza kwa kuingia kwenye anga zangu.Narudia tena I’ll never say sorry to him na Monica lazima nitampata tu.Hana ujanja kwangu.” Akasema Daniel kwa hasira

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    KINSHASA – JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO. Msafara wa magari zaidi ya kumi na tano uliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa N’djili jijini Kinshasa.Ni msafara wa rais wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.Ulinzi ulikuwa mkali hapo uwanjani kama ilivyo kawaida ya rais huyu ambaye huwa na ulinzi mkali sana.Taratibu za kiusalama zikafuatwa na mlango wa gari la kifahari la rais ambalo ni la kipekee kwa marais wa afrika ukafunguliwa ,akashuka akiwa mwingi wa tabasamu na kisha akaanza kutembea katika zuria jekundu akisalimiana na viongozi mbali mbali waliojipanga mstari kumuaga.Kisha agana na viongozi mbalimbali rais akaingia katika dege lake kubwa la kifahari aina ya Boeing 747 tayari kwa safari ya kuelekea nchini Tanzania kwa ajili ya mkutano wa wakuu wa nchi za maziwa makuu. David Bikumbi Mukaya Zumo ni rais anayeongoza taifa kubwa la jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.Ana umri wa miaka 43 na anatajwa kuwa rais kijana zaidi barani afrika.Anatokea katika familia ya kitajiri sana.Baba yake mzee Patrice Mukaya Zumo ni mmoja kati ya matajiri wa kubwa sana na wanaoheshimika nchini Congo na afrika.Toka akiwa mdogo David aliishi na kupata elimu yake nchini Ufaransa na hadi alipohitimu sahahada yake ya uzamivu katika masuala ya uchumi ndipo aliporejea nchini Congo na kwa ushawishi wa baba yake ambaye alimtaka arudi Congo na ajihusishe katika masuala ya siasa.David hakuwa mtu anayefahamika sana nchini Congo lakini kwa ushawishi wa baba yake ambaye ni tajiri anayejulikana na kuheshmika sana nchini Congo David alijulikana na kukubalika kwa haraka na hatimaye ulipofika uchaguzi David akachaguliwa kugombea na kwa mshangao wa wengi aliibuka mshindi kwa kura nyingi. David Zumo ni rais ambaye anatajwa kufanya mambo mengi makubwa katika nchi ya Congo kwani toka aliposhika madaraka uchumi wa Congo umepaa kwa kiwango cha kushangaza.Kumejengwa viwanda vingi ambavyo vimetengeneza ajira nyingi.Huduma za elimu na afya zimeboreka kwa kiwango cha juu mno.Miundo mbinu imeboreshwa kwa kiwango kikubwa kwani wakati akiingia madarakani alikuta kukiwa na kilometa chini ya 3500 za lami na ameboresha hadi kufikia kiasi cha kilometa zaidi ya 30000 za lami kwa nchi nzima.Anatajwa kuwa rais pekee ambaye katika kipindi cha uongozi wake ameweza kuleta amani nchini Congo kitu ambacho wananchi wa Congo walikuwa wanakihitaji kwa muda mrefu.Ameweza kukaa na makundi ya waasi wakakubaliana kusitisha mapigano na kuufungua ukurasa mpya wa watu wa Congo kuijenga nchi yao.Ni rais ambaye anatajwa na tafiti mbali mbali zilizofanyaka kuwa katika maraisi wote waliowahi kuitawala nchi hii tajiri David Zumo ndiye ndiye rais anayependwa zaidi nchini Congo hasa kutokana na mambo aliyoyafanya.Amefanikiwa kulifanya taifa la Congo kuwa taifa kubwa na lenye nguvu kiuchumi na kijeshi. Pamoja na kazi kubwa ya kuibadili Congo aliyoifanya David Zumo na kuifanya iwe mojawapo ya nchi inayoongoza kwa uchumi mkubwa lakini kuna mambo mengine makubwa aliyoyafanya ambayo yaliweka doa katika utawala wake.Kikubwa alichokifanya David ambacho kilimuwekea doa kubwa na kumfanya apigiwe kelele na jumuiya za kimataifa ni kitendo cha kukutaka kuibadili Congo kuwa nchi ya kifalme nay eye kutawazwa kuwa mfalme wa kwanza wa Congo.Tayari maandalizi ya jambo hilo yamekwisha kamilika na kilichokuwa kinasubiriwa ni wananchi kupiga kura ya maoni kuamua jambo hilo. Ukiacha hilo la kutaka kuibadili Congo kuwa nchi ya kifalme David ni mmoja wa marais wachache matajiri wakubwa duniani anayetajwa kujilimbikizia kiasi kikubwa cha mali.Ni raisi ambaye anaongoza kwa utajiri barani afrika.Anatajwa kuwa tajiri wa kwanza Afrika.Ndiye rais pekee afrika mwenye ndege yake binafsi kubwa na ya kifahari aina ya Boeng 747 iliyogharimu kiasi cha dola milioni 530 za Marekani.Ni ndege ya kifahari mno.Ukiacha hiyo ndege anamiliki pia shirika lake kubwa la ndege la Dav air lenye ndege kubwa zaidi ya hamsini zinazofanya safari ndani na nje ya Congo.Anamiliki pia mahoteli na biashara nyingine kubwa kubwa nje ya Congo . Ni rais anayeishi maisha ya anasa kubwa pengine kuliko wote afrika.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog