Search This Blog

Friday, 20 May 2022

SAHIHI YA KIFO - 5

 







    Simulizi : Sahihi Ya Kifo

    Sehemu Ya Tano (5)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ole wake mtu yoyote apige kelele humu ndani tunammaliza hapahapa” alizungumza mmoja kati ya wale majambazi huku wengine wawili wikichungulia nje ambapo magari ya polisi yakiwa yanapita kwa kasi na baada ya muda kimya cha magari na vuguvugu la polisi kule nje wale majambazi walitoka mbio mbio bila kuwafanya chochote kina david.



    “Hawa bila shaka watakuwa wametoka kufanya tukio mahali sasa wanakimbizwa na polisi”alijisemea david moyoni.



    Salome baada ya kuona hali imekuwa tulivu alinyanyuka na kukusanya vitu vyake huku akijisema mwenyewe ovyo,,

    “kuanzia leo mimi umalaya basi” akawa anaondoka kwa kuchanganyikiwa,,

    “ Salome chukua basi pesa yako ya usumbufu” david alizungumza,

    “Sitaki kaa nayo tu” alijibu salome wakati anaishia kwa kasi,,



    David naye hakuwa na jinsi ilibidi aondoke huku akiwa amesha pajua nyumbani kwa kina mwajuma baada ya salome kulitaja eneo ambalo analokaa mwajuma,

    Alifika nyumbani kwao usiku sana na kumkuta afande criss akiwa kachukua pale sebuleni baada ya kumpa onyo,,,



    “David najua umekuwa sasa lakini tabia hii ya kuchelewa kurudi tena usiku siipendi kumbuka bado unakazi nzito mbele yako na hujui mbaya wako nani mpaka sasa hivyo kuwa makini”



    David alitingisha kichwa kukubali na kuomba radhi kisha akawa anataka kuelekea chumbani kwake kulala lakini alipogeuza mgongo tu afande criss alimuita na kumwambia,,



    “david, kumbuka kesho inabidi twende kwenye ile ofisi ukaanze kazi hivyo jiandae vizuri na uwahi kuamka usiku mwema”

    “Sawa baba” david alijibu kwa unyonge kisha kuelekea chumbani huku akiwa kashika ile bahasha yake aliyotoka nayo kutoa chapa ya sahihi aliyotoka nayo kule gerezani.



    mwili wa david ulikuwa umechoka kwa pilika pilika za mchana kutwa hivyo aliweza kulala fofofo. Mpaka alfajiri alipo amshwa na hodi ambayo ilikuwa inagongwa na afande criss kwa ajili ya kijiandaa ili waelekee maeneo ya posta ambao ofisi ya shirika linaloshughulika na kukomboa vijana kutoka hali tete na watoto yatima. Linaloitwa “upendo toka moyoni”



    David alijinyakuwa pale kwenye kitanda na kwenda kujiandaa na baada ya muda akawa yuko tayari hivyo wakaongozana na afande criss mpaka posta kwenye shirika la” upendo toka moyoni” kisha kuonana na bosi wa shirika ilo ambaye alifurahi sana kuona uwepo wa david,



    Bossi huyo ambaye aliweza kumtambulisha david kwa wafanya kazi wengine ambao walikuwa wakifanya kazi hapo kwa muda mrefu, david alioneshwa ofisi yake ambayo ilikuwa na hadhi ya kuitwa ofisi na baada ya hapo akaanza kuelekezwa jinsi ya ufanyaji wa kazi na kupewa maelezo mengi kuhusu shirika hilo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Jioni ilipofika baada ya muda wa kazi kuisha, wakati david akirudi kuelekea kwao akiwa amepita barabara ya morogoro aliweza kumuona mtu kwa mbali kama mwajuma akihangaika ndipo alipoomba ashushwe pale maeneo ya jagwani, japo hali ilikuwa si shwari maana maji yalikuwa yanataka kujaa kutokana na mvua zilizokuwa zikiendelela kunyesha kwa msimu huo,



    Alimfuatilia kimyakimya na kumkuta akihamisha baadhi ya vyombo vyake kupeleka kwa jirani baada ya nyumba aliykuwa anakaa maji kuingia ndani na baadhi ya vitu kuharibika,mwajuma alishtuka kuona uwepo wa david pale maana hakuwahi kumuelekeza anapoishi, alimtazama kisha mwajuma akajifanya kama hajamuona vile na kuamua kutaka kuondoka, david alimuita kwa upole na kumsogelea kisha kumuomba,,

    “samahani mwajuma, jaribu kunielewa mimi sio askari na wala sina nia mbaya ya kutaka kukuingiza matatizoni ila ninalengo la kutaka kukusaidia kama utanipa picha ya huyo jamaa anayeitwa Helman mapesa”



    Kabla mwajuma hajajibu chochote kile, sauti ya mtoto wa kike ikawa inasogea huku akiwa kambeba mtoto mdogo mgongoni ambaye alikuwa analia na kutetemeka na baridi kisha kusema,,,

    “mama njaa inauma”



    David alimwangalia mwajuma na kumuuliza,,,

    “hawa ndio watoto wako?”

    Swali hilo lilimfanya mwajuma kujisikia aibu kujibu maana hali waliokuwa nayo watoto wake ilikuwa haiendani na uzuri wake wala kama david alivyomuona siku ya kwanza kule kwenye mgahawa maeneno ya ubungo, david akawa anahuakika kuwa hawa ni watoto wa mwajuma maana wasingeweza kuja na kumuita mama kisha kumlalamikia njaa, hivyo david akainama na kumuuliza yule mkubwa amabye kidogo alikuwa anajua kuongea,,,



    “unaitwa nani mtoto mzuri?”

    “Nisha” kile kitoto kilijibu jibu ambalo lilimfanya david ashtuke kidogo na kumuuliza tena,

    “Nani amekupa jina hili zuri”

    “mama” kilijibu kile kitoto,



    David aliingiza mkno mfukoni na kutoa elfutano kisha kumpatia yule mtoto, na kujinyakuwa pale alipokuwa amesimama na kuanza kuzungumza na mwajuma,,,

    “mwajuma tazama hali ya watoto wako ilivyo na hili baridi, pia fikiria eneo hili si salama kuishi cheki mvua kidogo tu imeweza kuingia mpaka ndani ya nyumba yako vipi kuhusu mafuriko yakija huoni kama unaweza kuipoteza familia yako? Tafadhali nioneshe hizo picha mimi nikusaidie.



    Maneno hayo yaliweza kugusa moyo wa mwajuma lakini jibu alilompatia david lilikuwa halina faida kwa upande wa david,,,



    “kaka nashukuru kwa kuonesha moyo wa kuguswa na tatizo langu, nami ningeweza kukusaidia lakini kwa bahati mbaya maji haya yalioingia ndani yameharibu vitu vingi na albamu ya kuwekea picha imeharibika yani picha niliyobaki nayo ni ya rafiki yangu kipenzi niliyo ibandika juu ya ukuta. ambaye sikuweza kuishi naye kwa muda mrefu akanipotea na sijui wapi alipokwenda ni muda mrefu sana tangu nikiwa bado msichana mdogo sana ndio maana ilikumuenzi nikaamua jina lake kumpatia huyu mwanangu Nisha”



    David hakuamini alichokisikia ikabidi aulize tena umesema rafiki yako alikuwa anaitwa nani?

    “Nisha” mwajuma alijibu,

    “Tafadhali naomba unioneshe picha ya huyo rafiki yako nakuomba sana, nitakupa kiasi chochote cha fedha ambacho unataka pia nitakuhamisha hapa ambapo unakaa tafadhali naomba unisaidie yani hiyo ni muhimu kuliko hata hiyo iliyopotea ya Helman mapesa” david alionesha huzuni



    Mwajuma akawa anashindwa kuelewa kwanini david kila anachotajiwa yeye anakitaka kukiona lakini hakuwa na jinsi ikabidi waongozane na david mpaka chumbani ambako kulikuwa na maji ambayo yalikuwa yanakaribia magoti huku baadhi ya vitu ambavyo vilikuwa havija tolewa vikiwa vinaelea juu juu,



    David bila hata kujali yale maji akaingia na viatu moja kwa moja na ndipo mwajuma aliponyoosha kidole juu kumuonesha ile picha ndogo iliyokuwa pale juu ya ukuta, na kwakuwa david alikuwa mrefu hivyo aliweza kunyoosha mkono tu na kuitoa ile picha.



    Picha ilishikwa vizuri kwenye mikono ya david na kuanza kuitazama kwa makini kwa kuisogeza karibu na macho yake, jicho lilibadirika na rangi na kuanza kudodosha mchozi wa hasira uliochanganyika na huzuni, kiganja chake kikawa kinapapasa juu ya uso kwenye ile picha kisha kuinua sura yake na kumtazama mwajuma na kumwambia,,,,,,

    “mwajuma huyu ni nisha wangu kabisa”



    huku mdomo ukitetemeka kwa uchungu mwajuma hakumuelewa na akaamua kumuuliza swali,,,,

    “unamaana gani kusema nisha wako na unalia kwa nini?”

    “naamaanisha ni mdogo wangu kabisa wa kuzaliwa naye tumbo moja na nina mtafuta leo kesho lakini bila mafanikio mpaka sasa nimepotezana naye muda mrefu sasa na kwasasa anaweza kuwa na umri kama wako na huenda akaitwa mama pia kwani wewe ulikutana naye wapi?”david alijibu na kuuliza swali,



    “nisha japotulikuwa wadogo lakini aliweza kunisaidia nilipotaka kubakwa na wahuni majira ya saa 4 usiku maeneo ya manzese darajani mahali ambapo ndipo yalipokuwa makazi yangu kabla sijaaingia kwenye ulimwengu wa kujiuza, alinisaidia kupiga mayowe na watu wakaja kutusaidia na kuna mama mmoja akaamua kutupa hifadhi kwake lakini kumbe alikuwa anafanya biashara ya kuuza mwili hivyo nasi tukajiunga naye, kiukweli mimi na nisha tumeingia kwenye biashara hii tukiwa na umri mdogo sana na sidhani kama nisha alikuwa amesha kuwa vizuri kwa wakati ule lakini hatukuwa na jinsi kwa kuwa tulikuwa hatuna pakwenda ilibidi tukubaliane na hali, lakini nisha kitendo kile cha kuuza mwili hakuridhika nacho japo alikuwa mdogo ila alikuwa na upeo mkubwa wa kufikiria ndio maana akaamua kutoroka na sikujua alipo elekea, nilitamani kujua kilichomkuta lakini alikataa kunieleza kabisa”



    Mwajuma aliweza kumpa maelezo david japo yalikuwa mafupi lakini yalieleweka, mpaka mwajuma anamaliza kusema hayo naye mchozi ukawa unamtoka.david alijilazimisha kumbembeleza mwajuma kisha kutoa kiasi cha fedha kumpatia na kumwambia akachukue chumba kwenye nyumba ya wageni halafu kesho waonane ili ajue atamsaidiaje kisha david kuelekea kwao.



    Siku hiyo ilikatika na david siku inayofuata alionana na mwajuma na akaamua kumsaidia kumpangia vyumba viwili maeneo ya kimara, kitendo hicho mpenzi wake Victoria aliweza kukusikia na akahisi huenda atakuwa in kimada cha david hivyo ugomvi baridi ukachukua nafasi katika penzi lao na Victoria kumtaka akajitambulishe kwao na ikiwezekana waoane,swala hilo david alilikubali lakini akamuambia asubiri kidogo mpaka atakapoweka mambo sawa ndio atakwenda huko kujitambulisha,

    **************************************

    Miaka miwili ilikatika bila ya david kuvuna chochote kile maana hakufanikiwa kumpata nisha wala helman japo alikuwa anamuwinda kule maeneo ya mbezi beach alipoelekezwa kuwa ndipo anapoishi yeye na familia yake na mungu aliweza kujaalia david kwakuwa alianza kujitegemea mwenyewe kwenye nyumba nzuri ya kupanga na kuwa na usafiri wake binafsi.



    Siku moja jumatatu asubuhi bosi wa shirika hilo aliitisha kikao cha ghafla baada ya kupokea wageni wawili asio wajua wakisema kuwa wanataka kuwekeza kwenye shirika hilo hivyo wafanya kazi waliombwa wachangie mawazo yao na david akapewa fursa ya kwanza kabisa,,,,



    “bosi mimi mtazamo wangu kama muhasibu wa shirika nafikiri kwa sasa tusiwapokee mpaka mwaka unao fuata ili tuweze kumaliza mikataba na wawekezaji wengine”



    David alitoa mtazamo wake lakini wafanya kazi wengine walionekana kuupinga vikali hivyo wazo lake likaonekana halina maana, na hapo sekretali ikabidi aagizwe akawaite wale wageni wawili waliokuwa wanaonekana wa heshima ila baadhi ya wafanyakazi wa kike wakawa wananyoosha nyoosha vidole kwa mgeni mmoja,

    Baada ya muda ikabidi mikataba iletwe iliwaandikishahe na sehemu za kujaza zilikuwa sehemu ya mwanaseheria upende wa mwekezaji na upande wa mwenye shirika, sehemu ya mwekezaji mwenyewe na bosi wa shirika na sehemu ya mwisho ni ya muhasibu na wote waliweza kujaza vyema na nafasi ya mwisho ilikuwa ni ya muhasibu ambaye ni david, baada ya karatasi kuzunguka kwa watu wengine pale mezani na ikawa imemfikia yeye,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati akiendelea kukagua walipo weka sahihi wengine kabla ya yeye kuweka hakuamini alicho kiona kwenye zile karatasi hasa pale kwenye nafasi ya mwekezaji mkuu, mkono wake ulitetemeka mpaka ile peni aliyokuwa ameishika ikaanguka chini, watu wakaanza kumshangaa usoni baada ya kuona sura inabadrika na kuwa ya kigaidi na moyo wa kinaadamu ukamtoka david ghafla ni baada ya kuionaa sahihi inayofanana na ile aliyotoka nayo kule gerezani ambayo in ya mtu wa mwisho kwenda kumuona marehemu baba yake na yawezekana ndio alikuwa anahusikia na mauaji ya baba yake,



    David aliinua macho yake yalionza kuloa mchozi na kuwatazama wale wageni kwa makini usoni kisha kuita kwa nguvu Helmannnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnn!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!-------------“

    Sauti ile ya david ilimshtua kila mtu mle ndani, wote waliduwaa, helman kwa mshtuko akajikuta kaitika naam, masikio ya david yalivyosikia tu helman kaitika na macho yake kukiri kumuona mbaya wake, viungo vya mwili wa david havikusita kujipa ushirikiano kwa pamoja, baada ya matukio yaliomtokea kujirudia kichwani mwake ghafla david akamrukia helman na kuanza kumpatia kipigo cha hasira cha harakaharaka bila kujali bosi wake aliyekuwepo pale huku maneno ya fadhaa yakimtoka mdomoni mwake,,,,,,,



    “huyu ni muuaji kabisa hastaili kuishi katika dunia hii ya waugwana hata kidogo, baradhuli mkubwa huyu”

    watu walijitahidi kumshikiria david wakati helman akiwa kaumizwa kiasi na damu chache kumtoka usoni, yule mwenzie aliye kuja na helman pale ofisi akaona mambo yamesha haribika hivyo akatafuta upenyo akakimbia, kitendo kile kilmshtua bosi wake na david akahisi ya wezekana kweli kuna tatizo hapo, ikabidi apige simu kituoni kilichokuwa karibu na posta ya zamani, huku helman akiwa ameshikiliwa na wafanya kazi wa pale.



    david alikuwa bado na hasira moyoni mwake alikasirika sana wenzie walivyomshika kama yeye ni mtuhumiwa vile, walipokuwa wanajisahau tu, david alikuwa anataka kumrukia tena helman,

    Helman alishindwa kumjua david mpaka dakika hiyo japo alishajua atakuwa ni mmoja kati ya watu ambao Alisha wahi kuwafanyia ubaya maana ndio ilikuwa tabia yake.



    Muda si mrefu askari wakawa wamefika eneo la tukio walivyouliza tatizo na kupewa kwa ufupi basi hawakuwa na jinsi wakaamua kuwafunga wote pingu maana kulikuwa hakuna ushahidi wa kutosha kwa muda huo na kosa alilolifanya david in kujichukulia sheria mkononi ndio maana naye akalazimika kufungwa pingu,





    Helman alishindwa kumjua david mpaka dakika hiyo japo alishajua atakuwa ni mmoja kati ya watu ambao Alisha wahi kuwafanyia ubaya maana ndio ilikuwa tabia yake.



    Muda si mrefu askari wakawa wamefika eneo la tukio walivyouliza tatizo na kupewa kwa ufupi basi hawakuwa na jinsi wakaamua kuwafunga wote pingu maana kulikuwa hakuna ushahidi wa kutosha kwa muda huo na kosa alilolifanya david in kujichukulia sheria mkononi ndio maana naye akalazimika kufungwa pingu,



    Wakati wanatoka ndani ya ofisi kuelekea kwenye gari ya polisi kwa ajili ya safari ya kuelekea kituoni, david alimkuta mpenzi wake Victoria ambaye alishakuwa mjamzito wa miezi tisa na aliishi na mimba hiyo kwa mashaka na mama yake maana david alikataa kwenda kujitambulisha mapema lakini mama yake na Victoria hakutaka kumfukuza mwanae tangu alivyogundua ni mja mzito wa miezi miwili, na sasa baada ya kuilea mimba mpaka kufikia miezi tisa hakutaka Victoria ajifungue bila mwenye ujauzito kumjua, hivyo akamlazimisha amtafute aliye mpa ujauzito na aende naye kumtambulisha hiyo ndio sababu iliyomfanya Victoria kwenda ofisi kwa david muda huo,



    Lakini hali aliyoikuta ilikuwa si shwari kabisa alikosa muda wa kuzungumza na david maana alikuwa chini ya ulinzi wa polisi, na Victoria alishindwa kuelewa kinachoendelea maana david hakuwahi kumueleza chochote juu ya masiha yake aliyopitia huko nyuma,

    Macho yao yenye huzuni na upendo ndani yake yalitazamana wakati david alivyokuwa anapandishwa kwenye gari na Victoria akiendelea kuwa vuta mashati wale askari kutaka kujua mpenzi wake kafanya nini ila jibu alilopewa ni kwamba aende kituoni huko atajua yote yaliojiri.



    Victoria hakuwa na jinsi ilimbidi achukue simu yake huku akiwa na hofu moyoni na kuanza kumpigia mama yake kumpatia taarifa,,,,,



    “Hallo mama ,baba wa ujauzito huu amepata matatizo na hapa naelekea kituo cha polisi kilichopo karibu na posta ya zamani”

    Mama yake naye alipata mshtuko juu ya taarifa hizo akamjibu,,

    “nakuja mwanangu sasa hivi”

    Gari ya polisi ilivyoondoka na Victoria hakuchelewa, akapanda pikipiki na kuwa fuata kule walipokuwa wanaelekea.

    ***************************

    Walifika kituoni na askari wakaanza kumuhoji david,,,

    “Kwanini umechukua sheria mkononi kumpiga mtu bila kosa” alihoji askari mmoja

    “Huyu anamakosa mengi sana ambayo serikali wanayafumbia macho,haki yake ya kuishi imeshakwisha hapa duniani lazima awafuate aliowatanguliza kwa hila zake na mkono wake mwenyewe kuliko kuendelea kuishi tena kwa jeshi hili la nchi yetu lenye sera ya mwenye pesa hana kosa,,,,,”

    David alikuwa na jazba akawa anazidi kutoa uwozo wa serikali bila kujali eneo alilopo, kitendo hicho askari walichukia na kuanza kumpa kipondo kwanini anaidharau serikali lakini david hakukubali alizidi kutoa maneno ya kashfa huku akicheka kicheko kilichoambatana na dharau,,,,,

    “hahahahah hakuna maumivu makali kama yale yanayohifadhiwa moyoni tena bila kujua yanaishalini,hivyo nipigeni tu maana ndio manafikiri suluhisho bila kuchunguza na kutaka kujua ukweli uko wapi,

    “ nini faida ya wewe kusoma? Au kuwa askari maana yake huna utu moyoni mwako ambao unashindwa kujua maumivu anayoyapata kiumbe kisicho na hatia na kumtumikia yule ambaye kesho atakuja kukugeuka utakaposhindwa kumtimizia jambo lake, jaribuni kutumia akili kabla hamja fanya maamuzi”



    David alizidi kuwapa maneno makali huku akiendelea kupigwa na marumbano hayo yaliweza kusikika na mkuu wa kituo ambayo yalionekana kumkera sana ndipo alipotoka nje na kufanya jambo ambalo david alizidi kushangaa,,,,,,

    “Helman,,!!!!!

    “Freizo!!!!!!

    Mkuu wa kituo hicho alishangaa kumuona rafiki yake kipenzi helman yupo ndani ya pingu na helman alishangaa kumuona rafiki yake yupo pale kituoni tena akiwa na cheo maana ni muda mrefu sana hawa kuonana.



    “vipi mbona wamekufunga pingu tatizo nini?” aliuliza mkuu wa kituo na wakati huo Victoria anawasili mle ndani na helman alipomuona Victoria akamkumbuka wakati wanapandishwa kwenye gari kupelekwa kituoni hivyo alijua huyu ni mpenzi wake na david tu japo kwa wakati huo bado hajamjua kama ni mtoto wa marehemu alfred kazinge ndipo alipoamua kusema,,,



    “hawa vijana wa sasa hivi si unajua tena wanataka kwenda sawa na wakubwa, niliwahi kumuona sehemu moja ya starehe huko akiwa kazungukwa na wanawake sasa kuna msichana mmoja na mjua kati ya wale waliokuwa wamemzunguka ikabidi ni muuite na alipokuja nikamueleza nilicho muitia na nilipotaka kuondoka akaniomba in mpatie lifti maana hakuona faida ya kukaa na huyu mtoto sasa nafikiri huyu kijana alihisi kuwa nina mahusiano na yule changudoa ndio leo tumeonana katika maswala ya kujenga taifa akanikumbuka akaanza kunirukia na kunishambulia vikali”



    Victoria alichukia kusikia maneno yale yaliokuwa yanazungumzwa na helman, aliamini moja kwa moja kuwa ni kweli maana helman alikuwa mtu mzima na muonekano wake kama humjui lazima uwamini anachokisema, Victoria aliangua kilio pale kituoni, akawa anamsogelea huku mkono wa kushoto akiwa kajishika kiuno na wakulia kashikilia mimba yake kubwa na kuanza kutoa maneno ya hasira,,,,



    “David kumbe ulikuwa unakataa kuja kujitambulisha kwa sababu ya huo ujinga unao ufanya huko sehemu za starehe? In bora ungeniambia mapema kama huniitaji, tazama nimegombana na mama yangu juu ya ujauzito huu kwa kukaa kimya bila kukutaja, kumbe wewe ni mshenzi eeh kwanini lakini umenifanyia hivi?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Victoria alilalamika kwa uchungu, david akashindwa aseme lipi maana hasira zilimpanda mpaka akawa anashindwa kuongea alibaki akiita tu jina la helman huku jicho limemuiva alipotaka kusema kitu ghafla waliingia watu wawili kwa haraka, mwanaume mmoja na mwanamke mmoja ambaye naye alikuwa mja mzito ambao ulionekana unalingana kabisa na ule wa Victoria,,

    “Baba vipi uko salama kweli maana nilipigiwa simu na mtu nisiyemjua kuwa umekamatwa na polisi na kwa bahati nzuri sikuwa mbali mimi na mke wangu hivyo ndio maana nimekuja haraka tatizo nini lakini?”

    yule mwanaume kulikuwa na dalili zote kuwa in mtoto wa helman maana alivyoingia tu alianza kumuita baba lakini david hakuwa na uhakika mpaka aliposibitisha kwa kauli ya helman,,,,,

    “usijali john mwanangu jambo la kawaida tu na nafikiri litaisha tu maana huyu kijana ndiye aliyekuwa ananiletea fujo(alimnyooshea kidole david).

    ndipo john mtoto wa helman pamoja na mkewe ambaye ni mmjamzito wakamuangalia kwa pamoja david ambaye mchozi ulikuwa unamtoka maana alinyimwa kabisa nafasi ya kusema,

    macho ya david yalishikwa na kigugumizi kila alipokuwa anamtazama yule mke wa john mtoto wa helman, alimsahili kutoka juu mpaka chini zaidi ya mara mbili mpaka john akamuuliza kwa ukali,,



    “wewe vipi mbona mnamtazama sana mke wangu kiasi hicho” na helman naye akapata nafasi ya kukazia neon ambalo lilizidi kuweka uwaminifu kwa Victoria ni kweli david alikuwa msharati,

    “Kazoea huyo maana hata mimi kanidhuru kwa sababu ya wanawake”aliungumza helman

    Kwakuwa mkuu wa kituo hicho bwana freizo alikuwa anamfahamu helman basi askari wa hapo walishindwa kuingilia maongezi hayo maana hayakuwa chini yao tena ndio maana yakawa yanaendelea kama mchezo wa kuigiza,,



    “uso wako haupotei, kichwani mwangu nakiri hata kama ungekuwa umezeeka lakini kamwe usingeweza kutoka kichwani mwangu, tazama ulivyokuwa sasa unafanana kabisa na mama” david alijitahidi kunyakuwa mkono na kumuonesha ishara yule mke wa john kuwa amsogelee jambo ambalo kila mtu alishangaa na kushindwa kumuelewa kwa nini anazungumza vile na kutoa ishara kama zile mpaka mdomo wake na ulimi wake kushirikiana kutoa maneno ya unyenyekevu yalioonesha upendo wa dhati kabisa,,,



    “Nisha! Nisha!”

    David alimuita mke wa john lakini hakuitika yule madada, hakuchoka akamueleza,,

    “Nisha mdogo wangu siamani kama bado unaishi na leo nimekuona tena! Mimi ni kaka yako david nisha mbona hunijibu dada? Kumbuka shida ngapi tumepata mimi na wewe leo hii unashindwa kuniita kaka kama zamani tafadhali nijibu mdogo wangu, ndoto zangu nikuwa na wewe kwenye dunia hii maana ndiye ndugu yangu uliyebaki,sikuzote ulizokuwa mbali lakini bado ulikuwa unaishi nami kichwani mwangu”

    Macho ya david yalikuwa na uhakika kabisa kuwa yule mke wa john mtoto wa helman ni nisha mdogo wake lakini alichokuwa anashindwa kuelewa mbona hajibiwi kila akimuita ndipo alipotaka kutoka kwa nguvu pale chini ya ulinzi wa polisi ili amsogelee karibu, huenda nisha akamkumbuka david,lakini alizuiwa na askari, hapo sasa ndipo wakawa wamehamsha zaidi hasira za david na mdomo wake haukusita kuongea kwa nguvu,,,,



    “umepewa nini nisha mdogo wangu hii sio familia ya kuolewa nayo huyu helman ndio anahusika na kifo cha baba yetu kule gerezani na ndio chanzo cha matatizo yote haya lakini serikali imemmfumbia macho na bado kaona haoitoshi kaamua kukuteka kupitia mwanae,,,,,”

    David kabla hajamaliza kusema yule mke wa john alikana jina hilo tena kwa sauti ya ukali,,,

    “tafadhali wewe kaka, sikujui na wala hunijui mimi siitwi nisha na wala sina ndugu, utakuwa umenifananisha, jina langu naitwa “Nashrifa” kama umenifananisha na hao machangudoa wako wanaokufanya mpaka uvamie wakwe za watu hapa umekosea upo hapo?”



    Jibu la nashrifa ambaye ni mke wa john mtoto wa helman lilizidi kumkera david na askari wote wakacheka kwa daharau, walijasahau kuwa lile ni jengo la serikali na haki ilikuwa inatakiwa kufuatwa lakini wakawa wanatazama tu yule marumbano, david mchozi ukazidi kumtoka mpaka Victoria mpenzi wake aliyekuwa pembeni akaanza kumuonea huruma na alilikumbuka jina la nisha wakati wako chuo nchini Rwandalilimfanya david kupoteza fahamu mbele ya umati wa watu chini ya ugeni wa rais paul kagame, lakini hakuwa na chakusema hapo naye akaangua kilio cha kwikwi baada ya kuona mpenzi wake anadhalilishwa,



    Na kilicho washangaza zaidi Victoria na david pamoja na askari wengine ambao waliokuwa wanajielewa na kujua haki ni baada ya mkuu wa kituo ndugu freizo kutoa amri kuwa helman afunguliwe pingu na david awekwe mahabusu kwa kosa la kumdhalilisha helman, david hakujali hilo kikubwa kwa wakati huo alikuwa anamataka nisha wake tu ndipo aliposema,,,,

    “wewe ni nisha mdogo wangu mimi sijui hilo jina la nashrifa umelipata vipi? Na mgongoni kwako una alama ya kovu ambalo nilitegemea lingekuwa pigo kwako maana ulilipata kwenye ajali iliyosababisha mdogo wetu dason kupoteza maisha siku chache baada ya kumzika mama yetu mzazi.



    Mchozi ulimtoka david wakati anazungumza na kuona bado mdogo wake nisha kama anaonekana kutoelewa kinachoendelea, lakini maneno hayo kwa upande wa john yalionekana kumuingia baada ya kuwaza,,,,

    “inawezekana kuna ukweli ya haya anayoyasema huyu jamaa maana huyu ni mke wangu mimi na ni kweli anahilo kovu mgongoni na hakuna mtu ambaye angeweza kujua zaidi yangu kwakuwa mimi ndio nina uhuru na mwili wake na hajawahi kuvaa nguo ambayo inamuonesha mgongo kwa kuhofia hilo kovu lisionekane,,,,,”



    John mtoto wa helman alipokuwa anaendela kuwaza jambo hilo ghafla mama Victoria na afande criss walionekana wanaingia kwa pamoja na hakuna aliyekuwa anajua kama wapo safari mmoja kwakuwa kila mmoja alikuja kivyake na walikutana tu hapo mlangoni,,

    Victoria baada ya kumuona mama yake alimkimbilia na kumkumbatia huku akilia kwa uchungu, afande criss alivyo ingia wale askari wadogowadogo walimpa heshima yake kikamanda kwa kuwazidi cheo,

    Macho ya mama Victoria yalifanikiwa kumuona david na nisha aliweza kumkumbuka sana kwakuwa alikuwa mkubwa mkubwa wakati enzi za uhai wa mama yake alipokuwa anakwenda kuwasabahi na aliweza kumkumbuka nisha maana sura yake ilikuwa inafanana kabisa na rafiki yake kipenzi marehemu magrety,



    Alihisi kama maajabu na kutoamini alichokiona baada ya kumuona na helman pale, mama victoria hakusita kusema neno na kwenda kumkunja helman,,,

    “wewe muuaji cheki ulivyofanya familia hii kuwa kama watoto wa ndege, umedhurumu mali za wazazi wao na kuwasababishia matatizo,

    “David, nisha( aliwaita) huyu ndio mwenye malizenu na ushahidi upo wa kutosha,,,”

    askari ikabidi wamtoe mama Victoria kwa nguvu baada ya kumkunja helman na helman akaanza kumkumbuka yule mama uwoga ukaanza akumtawala moyoni mwake maana aliona mwisho wake umefika, zogo lile wakati likiendelea ghafla kishindo kizito kikasikika na kutazama alikuwa nisha kadondoka na povu likawa linamtoka mdomoni,

    Mama Victoria alimwachia helman na kumkimbilia nisha pale chini alipokuwa amedondoka, david alijiona ni mwenye kuandamwa na kivuli cha matatizo baada ya kuona mdogo wake kipenzi anataka kupoteza maisha mbele yake,

    Kauli za majonzi zikamtoka david,,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Askari ikabidi wamtoe mama Victoria kwa nguvu baada ya kumkunja helman na helman akaanza kumkumbuka yule mama uwoga ukaanza akumtawala moyoni mwake maana aliona mwisho wake umefika, zogo lile wakati likiendelea ghafla kishindo kizito kikasikika na kutazama alikuwa nisha kadondoka na povu likawa linamtoka mdomoni,

    Mama Victoria alimwachia helman na kumkimbilia nisha pale chini alipokuwa amedondoka, david alijiona ni mwenye kuandamwa na kivuli cha matatizo baada ya kuona mdogo wake kipenzi anataka kupoteza maisha mbele yake,

    Kauli za majonzi zikamtoka david,,

    “ nisha siku zote ulikuwa mbali nami leo unataka kunitoka mbele ya macho yangu!!!, tafadhali nisubiri twende huko pamoja na familia hii iwe imefika mwisho hakuna baba, mama wala watoto”



    Tukio hilo lilizidi kukichanganya kituo cha polisi, raia wengine waliokuwa nje walibaki wakijiuliza kulikoni?

    David alijitahidi kumuamsha nisha kwa kumtikisa lakini hakufanikiwa, povu ndio kwanza lilizidi kumtoka mdomoni mwake, mama Victoria pamoja na afande criss walipokuwa wanajitahidi kumtoa pale chini alipokuwa amemkumbatia mdogo wake ,hawa kufanikiwa kwa kuwazidi nguvu.



    David alipoona hali ya nisha inazidi kuwa mbaya, alinyanyuka kwa hasira na kutupa jicho la kumtafuta helman kasimama upande gani, alipomuona tu, alipiga hatua mbili na kurusha ngumi yenye ujazo ili kumdhuru helman, lakini wahenga husema hasira hasara, ngumi hiyo ilimkosa helman na kwenda kumpata kipenzi cha roho yake Victoria ambaye nae alikuwa mjamzito. Papo hapo mwili wa Victoria pia ukawa chini ya sakafu na damu kuanza kumtoka sehemu za siri.



    Ghafla mwanga wa kamera ukaonekana kumulika eneo hilo, kumbe waandishi wa habari walikuwa wamesha wasiri eneo la tukio, afande criss alitoa agizo kwa mkuu wa kituo hicho cha polisi kuwa helman na david wawekwe mahabusu ila ziwe tofauti kisha wagonjwa wa wahishwe hospitalini haraka.



    Kichwa cha kila mtu kilionekana kuchanganyikiwa kwa kuhofia kesi kuwa kubwa na kulaumiwa kwa uzembe hivyo afande freizo nae aliwaamuru askari wake kwa kuwa fokea wafanye kama agizo lilivyotoka kwa afande criss.

    John mtoto wa helman alimbeba mkewe nisha na kumtoa nje ya kituo ili waelekee hospitali huku nisha akiwa kabebwa na askari,

    vinasa sauti vilikuwa karibu kunasa habari na picha kupigwa kwa wingi, baadhi ya askari wakazungushia uzio wa kamba za njano kwa haraka ili umati uliokuwa umekusanyika wakae kando, hata waandishi wa habari wakawa wanakatazwa kuchukua habari.

    Mama Victoria mchozi ukawa unamtoka kama maji kwenye macho yake, viatu na vitu vingine alivyokuwa amekwenda navyo aliviona vizito, hata nguo alizokuwa amezivaa alihisi zinataka kumvuka, tumbo la ghafla likamshika hivyo alijikaza na mtandio wake kiunoni kama dawa ya haraka kwake na safari ikawa kuelea agakani hospital ambayo haikuwa na umbali wa kutosha kutokea hapo.



    Pale kituoni zogo likawa lanaendelea kati ya afande criss na afande freizo ambaye ni mkuu wa kituo hicho, kutokana na uzembe ambao afande freizo ameufanya wa kuweka kikao kisicho cha maana na watuhumiwa bila kuchukua maelezo ya kutosha na kufungua jarada la kesi.

    Walibishana hatimaye walifikia muafaka, jarada la kesi likafunguliwa na kuandaliwa kwa kupelekwa mahakamani.

    Afande criss baada ya kuweka kila kitu sawa akamuachia mwenye kituo chake na kuwafuata walio tangulia hospitali huku david akibaki na butwaa kwa kutojua nini kitakachoendelea kwa dada yake wa dhati pamoja na kipenzi chake cha roho Victoria, alizidi kuhisi yawezekana pia asitoke gerezani kama mkewe atapoteza maisha, kumbukumbu za kifungo cha marehemu baba yake” Alfred kazinge” zilimjia na kuona kinataka kuendana na kifungo chake kwa kuwa naye amemsababishia matatizo mkewe Victoria.

    Afande criss alifika agakani hospital na kukuta Victoria pamoja na wifi yake nisha wamesha pelekwa kwenye vyumba vya wa mama wajawazito” leba” tayari kwa kupewa huduma ya kwanza, huku mama Victoria akionekana kuzunguka zunguka kwa kuchanganyikiwa na jicho la hasira kumtupia john mtoto wa helman japo hisia zao zilikuwa kwenye mlango wa wagonjwa wao wakimsubiri dokta ili kujua usalama wa wagonjwa wao.

    “vipi jamani hali za wagonjwa wetu zinaendeleaje hapa?” aliuliza afande criss.

    “Bado si buheri, ndio wameingizwa kwenye vyumba vya matibabu muda mchache uliopita” alijibu john kwa unyonge

    Afande criss alipokuwa anataka kuzungumza na mama Victoria alikatishwa na sauti ya mlango uliokuwa unafunguliwa na dokta,

    Dokta alivyotoka hakuwa na muda wa kupoteza, alitoa macho na kurusha mikono kuongea kwa msisitizo,,,

    “ mgonjwa wenu victoria hali yake si nzuri kwa sasa kutokana na damu nyingi kumtoka na kupoteza kiwango kikubwa cha damu na yupo mbioni kujifungua kutokana na mtikisiko alioupata, hivyo damu ya haraka yenye grupu A+ inahitajika ili tuweze kujitahidi kuokoa maisha yake yeye na mwanae la sivyo tunaweza kumpoteza mama au mtoto”



    Vichwa vilizidi kuwa uma, walijishauri kwa haraka na mama Victoria kujitolea kutoa damu kuokoa maisha ya mwanae, wote walielekea kwa dokta kufanikisha zoezi hilo, kama ilivyo ada kifo cha nyani miti yote huteleza, baada ya kuchukua vipimo vya mama victoria ikaonekana damu yake haiko kundi sawa na la mwanae, hivyo afande criss akajitolea pia, nae majibu ya kawa yale yale.



    Aliyebaki kuchukuliwa vipimo alikuwa ni john mtoto wa helman, alipoombwa kutoa damu yake alikataa na kusema kuwa,,,

    “mwacheni afe kwani mimi ananihusu nini?, yani kwa shutma zote ulizo mpa baba yangu pale kituoni na kumdhalilisha sasa hivi nijipendekeze kutoa damu yangu hali ya kuwa mzee wangu anaweza kuozea jela na msababishaji ni wewe siwezi kufanya kitu kama hicho”, alikata kauli.



    Maneno hayo yalimuumiza sana mama Victoria na kuwezakupandisha presha yake hatimaye kudondoka chini na kupoteza fahamu, john alipoona vile akataka kuondoka lakini aibu ikamshika akarudi na kukubali kuchukua vipimo, yawezekana maisha ya Victoria yalikuwa mikononi mwa john, baada ya vipimo, damu zao zilionekana kuendana bila shida ya aina yoyote ile, papo hapo dokta alitoka na kwenda kwenye kile chumba walichokuwepo wagonjwa wake na kutoa agizo la uandilizi wa vifaa kwa ajili ya upasuaji ili waweze kumzalisha, kutokana na hali yake ya kutojitambua asingeweza kujifungua kwa njia salama.



    Wakati wakiendelea kumuhudumia Victoria ambaye hali yake ilikuwa mbaya zaidi kutokana na kupoteza damu nyingi, nisha nae aliyekuwa amewekewa chupa ya maji ili kurudisha fahamu yake baada ya kupotea kwa muda, alianza kupiga kelele za uchungu, madaktari na manesi wengine walijikusanya na kuumuandaa nae pia kwa ajili ya kujifungua, kwake ilikuwa al-hamdulilah maana hakuhitaji upasuaji, njia salama ilitumika.



    Siku hiyo ilikuwa kama ya miujiza kwa familia hiyo kutokana na matatizo waliyo pitia na mpaka walipofikia, sauti nyembamba ilisikika ya mtoto mchanga ikilia kwa sauti kali, nyuso za furaha zikatawala kwa manesi na madaktari waliokuwa wanamuhudumia Victoria, japo hali ya Victoria ilikuwa si nzuri lakini manesi walisema

    “ hongera Victoria kwa kupata mtoto mzuri wa kike na mwenye afya”

    Hazikupita hata dakika kumi na tano upande wa nisha alipokuwa anazalishwa sauti yenye uzito kiasi iliyoashiria kuwa ni mtoto wa kiume amezaliwa ilisikika, unaweza kusema kuwa ni zaidi ya miujiza lakini amini kuwa sauti hiyo ya mtoto wa kiume aliyezaliwa na nisha ndio ilionekana kurudisha fahamu ya mama Victoria na alijikuta akiropoka,,,

    “nime pata bwana ewe mungu ashukuriwe”

    afande criss pamoja na john ambao walikuwa karibu kumpepelea walishangazwa na kauli yake, lakini mshangao uliwatoka pale sauti ya viatu vya madokta iliposikika ikiwasogelea na kuachia tabasamu kwa kujipongeza kwa kazi nzuri walioifanya kisha kuwaambia,,,

    “ hongereni mungu ameweza kusikia maombi yenu, kwa taarifa nzuri ni kwamba Victoria hali yake si mbaya sana na amefanikiwa kupata mtoto wa kike mwenye afya nzuri, kisha dokta wa pili akamalizia kwa kusema huku akimwangalia mama victoria,,,

    “ mama hongera sana kwa bwana mzuri uliyempata kutoka kwa nisha.

    Furaha isiyo na kifani iliwatawala kwa muda mfupi, japo john alikuwa anaona haya kwa alichokifanya na kilichokuwa kinamsaidia ni kwamba mama Victoria baada ya kurudiwa na fahamu hakujua kilichotokea muda mchache ulio pita hivyo wote walijumuika kwa pamoja.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mungu ametenda maajabu kwa familia hiyo kwa kuwapa mapacha wa nje waliopishana dakika chache tu katika kuzaliwa kwao, ghafla nesi mmoja alitoka na kuwa salimu kisha kuzungumza,,,

    “mnaweza kuja kuwaona watoto mara moja halafu mkawaandalie wagonjwa wenu chakula pia hamtaweza kuzungumza nao kwa kuwa bado, wapo katika hali ya mapumziko, wote walizidi kufurahi na kwenda kufanya hivyo, waliwashika na kuwa chambua kiungo kimoja baada ya kingine na kutoa mfanano juu ya wazazi wao na siku ilikatika kwa namna hiyo.

    ********************



    Siku inayofuata asubuhi na mapema afande criss alikwenda kituoni alikokuwa amefungwa david, nakufuatilia utaratibu unakwendaje, taarifa alizopewa ni kwamba jarada la kesi limeshapelekwa mahakamani, na walikuwa wanasubiriwa wao tu, pamoja na mashahidi ambao kila mtuhumiwa amemtaja,

    Kwa upande wa david kazinge, amesema kuwa mshahidi wake ni mama Victoria na helman mshahidi wake ni mwanae john, ghafla na john mwenyewe akawa anatokea nae akapatiwa maelezo hayo.

    Afande criss hakuwa na budi kumpigia mama Victoria na kumueleza juu ya taarifa hizo, na mama Victoria alikubali kwenda kutoa ushahidi huo baada ya kutoka hospitali ambapo mkwe wake pamoja na mwanae walipokuwa wamelazwa.



    Watuhumiwa walitolewa mahabusu na kupelekwa mahakamani, huku wakisindikizwa na jopo kubwa la waandishi wa habari, mheshimiwa hakimu alipowasiri watu walisimama kwa heshima kisha kukaa na watuhumiwa kupandishwa kizimbani,



    Kwa kuwa wote walikuwa ni wakristu basi waliapishwa kwa bibilia takatifu na kuahidi kusema ukweli mtu,

    Mahojiano yaliendelea na maelezo yalisikilizwa kwa pande zote mbili kwa usawa na umakini mkubwa kabisa kisha kesi kuahirishwa mpaka saa saba mchana kuanzia muda wa saa mbili walipokuwa wameanza,

    Saa saba ilipofika kesi ikaanza upya na mama Victoria alikuwa amesha wasiri mahakamani hapo tayari kwa kutoa ushahidi,

    Hakimu alianza kumuita john kama mshahidi wa upande wa mshtakiwa , nae akapamda kizimbani kutoa ushahidi wake baada ya kuapishwa ,aliulizwa maswali mengi na wakili wa davdi ambayo alishindwa kuyajibu mpaka aliporuhusiwa kwenda kuketi, na mama Victoria kupandishwa kizimbani kama mshahidi wa mwisho aliyekuwa anasubiriwa,



    Baada ya kupewa uwanja wa kutoa ushahidi alimtazama helman kwa hasira na jazba ya hali ya juu kisha kusema haya,,,,

    “ mheshimiwa hakimu mimi sina mengi ya kuzungumza ila ni kutoa ufafanuzi tu kwa ufupi kwa kile nilichokiona.

    Wakati nikiwa kama muhudumu wa landmark hoteli iliyopo maeneo ya riverside ubungo, nilipata kumuona yule mheshimiwa( alimyooshea kidole helman) akiwa na wenzie walioshiba kiasi pamoja na wasichana wa wili ambao walikuwa na sifa za kuwa mapacha kwa mfanano wao, wakiwasiri pale majira ya saa moja moja usiku na gari moja nyeusi kisha kuchukua chumba ambacho kilitustaajabisha baadhi ya wahudumu ambao tulikuwa na upeo wa kufikiri baada ya watu hao wasiopungua wanne kuingia kwa pamoja katika chumba hicho, kwa kuwa vyumba hivyo vinakamera ambazo si rahisi kuziona na mara nyingi huzimwa mpaka pale mteja anapokuwa na shida ya kutaka kitu flani humohumo chumbani basi huwashwa na kuelekezwa baada ya kuwa tayari ameshapiga simu mapokezi,



    Hivyo kwakuwa mimi nilikuwa na mashaka nao kutokana na muonekano wao, nilikwenda kuwa kwa siri kwenye zile swichi ambazo zipo ukutani pale mapokezi kisha kuzima ile television inayoonesha maeneo yote ya hoteli ili wengine wasiweze kujua kilichokuwa kinaendelea na kuanza kupiga kelele kwa hofu au kuwatonya nami nikapoteza maisha yangu.



    Baada ya kukaa ndani humo kwa muda mrefu niliwakuta wanatoka kisha kuzunguka nyuma ya hoteli na kuchukua meza moja na kuketi lakini huyu mheshimiwa sikumuona, kiukweli nilipunguza ufanisi wangu wa kazi kwa muda na sikujua kwa nini nilikuwa ninamashaka juu yao ila nafikiri ni uwezo na miujiza ya mungu tu kutaka kunionesha uharifu waliokuwa wanaupanga, ilipofika majira kama ya saa nne hivi nilimkuta mheshimiwa huyu akitoka huku akizungumza na simu ambayo ilionesha kuwa ni ya siri kutokana na umakini aliouweka usoni mwake, hivyo alivyo maliza kushusha zile ngazi na kuelekea kule walipokuwa wenzie mimi nikawasha ile televisheni baada ya kuhakikisha kuwa nipo mwenyewe, na nilichokiona na kukisikia niliogopa, ghafla nilishtuliwa na mfanya kazi mwenzangu wa kiume aliyekuwa nyuma yangu na nafikiri aliweza kuona lakini hakuelewa, kutokana na uwoga niliitoa ile kanda ya kisasa “COMPACT DISC” ( CD) na kutoka nayo haraka bila kujali kitakachotokea kwa bosi, toka moyo wangu ulipokili kuwa yaliokuwa yanazungumzwa ni mipango ya uharifu,



    Baada ya kukaa ndani humo kwa muda mrefu niliwakuta wanatoka kisha kuzunguka nyuma ya hoteli na kuchukua meza moja na kuketi lakini huyu mheshimiwa sikumuona, kiukweli nilipunguza ufanisi wangu wa kazi kwa muda na sikujua kwa nini nilikuwa ninamashaka juu yao ila nafikiri ni uwezo na miujiza ya mungu tu kutaka kunionesha uharifu waliokuwa wanaupanga, ilipofika majira kama ya saa nne hivi nilimkuta mheshimiwa huyu akitoka huku akizungumza na simu ambayo ilionesha kuwa ni ya siri kutokana na umakini aliouweka usoni mwake, hivyo alivyo maliza kushusha zile ngazi na kuelekea kule walipokuwa wenzie mimi nikawasha ile televisheni baada ya kuhakikisha kuwa nipo mwenyewe, na nilichokiona na kukisikia niliogopa, ghafla nilishtuliwa na mfanya kazi mwenzangu wa kiume aliyekuwa nyuma yangu na nafikiri aliweza kuona lakini hakuelewa, kutokana na uwoga niliitoa ile kanda ya kisasa “COMPACT DISC” ( CD) na kutoka nayo haraka bila kujali kitakachotokea kwa bosi, toka moyo wangu ulipokili kuwa yaliokuwa yanazungumzwa ni mipango ya uharifu,

    haukupita muda hoteli ikawa imechafuka baada ya kutokea mauaji ya kijana mmoja ambaye hakufahamika jina lake ila aliuwawa na mmoja watu aliokuwa nao huyu mheshimiwa na hapo ndipo nilipomuona marehemu alfedi kazinge akiikumbatia kwa uchungu na kuililia maiti ile na kilichoendelea hapo sikujua japo nilijengewa na hofu huenda alfredi naye alikuwa anahusika ila ilikuwa si kweli baada ya kwenda na kuisikiliza cd ile kwa umakini na kugundua kuwa nae walipanga kumuua kama atakaidi agizo lao la kushirikiana nao katika kuweka mipango ya uvamizi wa gari la pesa, niliamua kuacha kazi katika hoteli hiyo kwa kutetea maisha yangu kutokana na taarifa nilizo zipata kuwa mheshimiwa huyu amejua ukweli kuwa cd yenye ushahidi wa mambo waliokuwa wanayapanga nilikuwa nayo mimi hivyo walikuwa wananitafuta kwa udi na uvumba na kila kitu mtajionea wenyewe katika cd hiyo ambayo nimewapatia kama kielelezo cha kukamilisha ushahidi, pia kinachoshangaza zaidi ni kwamba nyumba na baadhi ya mali za marehemu alfred kazinge zinamilikiwa na huyu mheshimiwa hali ya kuwa familia ya marehemu imekuwa na kuishi katika mazingila magumu sana. Hivyo muheshimiwa hakimu naomba jambo hili lifatilie kwa makini na adhabu kali itolewe kwa mtuhumiwa, mpaka hapo sina cha ziada.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Pumzi nzito ilionekana kushuka kwa helman baada ya mama victoria kuonekana kuweka kila kitu bayana, kutokana na aibu iliyokuwa inamtesa, helman hakusita kuinamisha uso wake uliokosa haya kipindi cha nyuma,

    Mheshimiwa hakimu akaludi upande wa helman na kumuuliza,

    “ mheshimiwa unachochote cha kujitetea au kupinga ushahidi ambao umetolewa na mshahidi upende wa mashtaka?”

    “Sina mheshimiwa, ila kuna kitu naomba kuzungumza kabla hukumu kali haijaja juu yangu kisha maneno yangu yaje kuwa funzo kwa wengine wote ambao ni waumini wa tabia kama yangu” .

    helman alizungumza kwa huruma huku mikono yake ikionekana kutokauka machoni kama mtu anayefuta machozi yaanzayo kutoka. Maneno yake yalimstua sana mwanae john na baadhi ya watu wengine waliokuwa wamekuja kusikiliza kesi hiyo ambayo ilionekana kupotea kwa muda na kuwa tena na uzito kutokana na waandishi waliowahi kuisikia na kuifatilia kipindi cha nyuma kuipata tena na kutaka kuhakikisha haki inafanyika kwa wakati huo.



    “unaweza kuzungumza tu mheshimiwa helman” hakimu aliruhusu na watu wakakaa mkao wakusikiliza hicho ambacho mtenda dhambi na mfitini mkubwa anachotaka kukizungumza,



    Sauti nzito iliyotoka kwenye koo la helman kwa ishara ya maandilizi ya kuongea ikaongeza ukimya kwa wasikilizaji na hapo maneno yake ya mwisho yakaanza kumtoka,,,,,,

    “ mheshimiwa hakimu, mwanangu john na wengine mnaosikiliza, mimi ni binaadamu kama nyinyi lakini tofauti yetu ni kwa yale niliyo yatenda, tamaa na ukosefu wa utu moyoni ndio yalionipelekea kuwa na kiroho ya kinyama,

    leo na kili mbele ya mahakama hii tukufu na kwa mwenyezi mungu na wote naomba mnisamehe,

    mahakama hii tukufu ni haki yake kunifunga kwa niliyoyatenda na mwenyezi mungu ni haki yake kunichoma kwa dhambi zote zinazonihusu, labda kwa huruma yake mungu anaweza kunihurumia kwa kuwa ni mwingi wa kusamehe.

    Niliyo mtendea marehemu alfed kazinge ambaye nilimuua kwa sumu kali niliyomuekea kwenye chakula chake kule gerezani kinguruila mkoani morogoro, nikishirikiana na mkuu wa gereza hilo ambaye nilimpatia rushwa ya kutosha ya kuniruhusu kuingia ndani ya gereza na kufanya yale niliyo yataka, pia nilimuua mfanya kazi wa marehemu Alfred kazinge ambaye pia alikaidi kushirikiana nami vilivyo. Hao ni baadhi tu ambao nyie mnaweza kuwa fahamu ila wapo wengi nilioweza kuwapoteza katika dunia hii pale tu walipokaidi kutii amri yangu”

    Helman alizidi kumimina yale yaliokuwa kifuani mwake,

    John mwanangu,( alimuuita kwa kumtazama) najua umekuwa katika maisha ya kifahari na kila raha ndani yake, lakini hukujua ni wapi mali hizo nimezipata na hukujua baba yako nafanya kazi gani ya kuniingizia kipato kikubwa kiasi cha kukufanya wewe uwe na furaha na kujivunia kuwa na baba kama mimi, leo inabidi utambue na ujifunze na wala usijaribu kupita katika njia hii ambayo mimi nimepita maana hutokuwa na furaha maisha yako yote”

    Helman alipomaliza kumpa usia mwanae wa pekee akaendelea kusema,,

    “mheshimiwa hakimu, baada ya kumfanyia vitimbi na kumtengenezea kesi ya uporaji wa fedha, marehemu Alfred kazinge mpaka kuhukumiwa kufungwa kutokana na wizi huo, shirika la benki aliyokuwa anafanyia kazi ikaamua kufanya mnada wa kuuza mali zake ili kuweza kufidia kwa uchache deni hilo, lakini kutokana na roho ya kinyama niliyokuwa nayo nikafanya mpango wa kuongea na meneja wa benk hiyo kisha mali zake zote zikafanywa mnada kwangu kwa kiasi kidogo cha fedha hivyo basi nakili kuwa mimi si mmiliki halali wa mali hizo, naomba mahakama hii tukufu iweshahidi na kuzirudisha mali hizo katika mikono ya david na familia yake nami niko tayari kwa hukumu itakayotolewa na Mahakam hii, kwa yote niliyoyafanya” helman akawa amemaliza kutoa uozo wake ambao ulipeleka hata ya kutokuwa na haja ya kwenda kuitazama cd iliyotolewa na mama Victoria kama ushahidi,

    Kila mtu alistaajabu kwa alichokizungumza helman, hakuna aliye amini kutokana na roho yake mbaya ya kidharimu kama angeweza kukiri na kusema yote aliyowahi kuyafanya,

    John mchozi ukawa unamtoka kama mvua ianzayo kunyesha kwa kasi,baada ya nyundo kugongwa mezani wote walikaa kimya na hakimu akaanza kuzungumza,,,,

    “kutokana na vifungu vya kesi ya mauaji na udhurumaji wa mali, mahakama hii tukufu inamhukumu ndugu helman kifungo cha maisha yeye pamoja na mkuu wa gereza ambaye walishirikiana katika kuandaa mpango wa kumuua Alfred kazinge, hivyo baada ya hapa askari watakwenda mkoani morogoro na kumtia mbaroni kisha kwenda jela moja kwa moja, na pia mali zote zitakabidhiwa kwa david kazinge ambaye ni mtoto wa kwanza wa marehemu”

    Hakimu aligonga nyundo mezani ya kuashiria kuwa kesi imekwisha, na askari walikwenda kumfunga pingu tayari kumpeleka gerezani kwenda kutumikia kifungo,

    Jino la furaha lilionekana kwa david ambaye alikuwa anakumbatiana na afande criss pamoja na mama Victoria huku akitoa shukrani zake za dhati kwa ushirikiano waliomuonesha,

    Kilio nacho ndio kikawa rafiki wa john wakati akimtazama baba yake akipelekwa nje kwaajili ya safari ya gerezani,

    Mawakili walipeana mikono kwa kumaliza kesi hiyo na waandishi wa habari wakijaribu kusogeza kamera zao kutaka kumuhoji david maswali mbalimbali juu ya kilichotokea, lakini ghafla umati wote uliokuwa ndani ulishtushwa na sauti ya risasi pamoja na sauti ya maumivu iliyosikika,

    Walipokimbilia nje kutazama kilichotokea, walikuta mwili wa helman ukimalizikia kukataa roho baada ya kujipiga risasi ya kichwa mwenyewe kwa bastola aliyo pola kwa mmoja wa askari waliokuwa wanampeleka kumpandisha kwenye gari kuelekea gerezani, hilo liliendelea kuwa faida kwa waandishi wa habari kuendelea kupiga picha, john alizidi kuchanganyikiwa maana alimpoteza baba yake pamoja na mali zote hakujua wapi aanzie,

    David pamoja na mama Victoria waliaamua kuondoka kwa kuwa tukio hilo lilikuwa aliwahusu ni kazi ya serikali, na kumuacha afande criss akijumuika na askari wenzie kulikabili tatizo hilo na hatimaye mwili wa helman ulipelekwa hospitali kwa maandilizi kisha kwenda kuhifadhiwa mochwari kwa ajili ya mazishi baada ya makabidhiano ya mali kukamilika.

    ************

    Siku iliyofuata wanasheria wakiambatana na john ambaye alikuwa na majonzi, walikwenda kukabidhi mali kwa david akiwa chini ya usimamizi wa afande criss, na baada ya makabidhiano David alipigiwa simu na mama Victoria ambaye alidamkia hospitali, kuwa wapo njiani wakirudi nyumbani wamepata ruhusa toka kwa daktari,

    David aliwapa maelezo huku akiwa na furaha kuwa waende moja kwa moja kwenye nyumba yao tayari wamesha kabidhiwa, na baada ya muda mchache furaha ilizidi kuongezeka kwenye familia hiyo pale alipo ziona sura za watu wake wa muhimu nisha pamoja na kipenzi chake Victoria wakishuka kwenye gari huku watoto wakiwa wameshikwa na mama Victoria pamoja na dereva ambaye aliwaleta pale.

    David aliwasogelea watoto na kuwa busu kama ishara ya upendo kisha kumtazama nisha ambaye alianza kutoa mchozi baada ya kumkumbuka kaka yake david, hisia zao za kindugu zilipozungumza moyoni mwao walijikuta wakikumbatiana kwa furaha huku mikono ya david ikifuta machozi ya dada yake,CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kitendo hicho kilipokuwa kinaendelea john alikuwa bado hajaondoka baada ya kuwa tayari amesha kabidhi dokomenti zote za mali hivyo alioona hana chake alikwenda kwa mama Victoria ambaye alimbeba motto wa kiume wa nisha na kusema,,,,

    “ nipeni mwanangu nikaishi naye mwenyewe nanyi muendelee na maisha yenu”

    john alizungumza hivyo huku akinyoosha mikono tayari kwa kupokea mtoto, ghafla mambo yakawa si mambo baada ya nisha kutoa kauli ambayo iliwafanya kutoamini hata kama familia ya kina john iliwatendea ubaya lakini alikuwa amekamilisha kauli isemayo siri ya mwana aijuaye mama,,,,

    “we, we, ishia hapo hapo tena usijaribu hata kukigusa hicho kiumbe na mikono yako haramu uliyolisi kutoka kwa baba yako dharimu aliyenifanya kuishi maisha ya tabu na shida, tambua huyo mtoto hakuhusu hata kidogo, tena john ukae mbali nami sioni hasara kukudhuru name kupoteza maisha kwa hasira na uchungu kila nikikumbuka mlichotufanyia”

    Nisha alizungumza kwa hasira na kujikuta ananguvu japo ndio alikuwa anatoka hospitali, maneno hayo david alikuwa bado hajaelewa vizuri kuhusu huyo mtoto alipokuwa anataka kuhoji alikatishwa na john aliposema,,

    “nashrifa tambua hiyo ni damu yangu nina haki ya kuchukua kile nilichokipanda hivyo angalia kauli zako isitoshe najua kabisa mimi na wewe hatuwezi kuendelea tena ndio maana namtaka mwanangu nikaishi mbali nanyi”

    “ sikia nikwambie we mwanaume, kwanza siitwi nashrifa, uliniteka kiakili na kunipa jina hilo kwa kuwa sikuwa na kumbukumbu zozote juu ya familia yangu na wala wewe hukujua chochote kuhusu familia yangu, jua kuwa naitwa nisha alfredi kazinge mtoto wa pili kwenye familia yetu, na huyu( alimuonesha david) ni kaka yangu kipenzi na ninampenda sana, leo naomba utambue john, siku uliyonikuta pale buguruni majira yale ya usiku nilikuwa nimetoka kufukuzwa na mama mwenye nyumba ambaye nilikuwa na mfanyia kazi zake za ndani baada ya kugundua kuwa ni mjamzito na aliyenipatia alikuwa ni mwanae na hata nilipotaja kuwa ujauzito ni wa mwanae wote walinishambulia kwa matusi na kipigo kisha kunifukuza, nilishindwa kukwambia ukweli na kukudanganya kuwa ujauzito ni wa kwako kwakuwa nilikuwa sina pakwenda na msaada wako nilikuwa nauhitaji kwa hilo nakushukuru kwakuwa ulinisaidia kwa usiku ule, nafikiri umeshajua ukweli unaweza kwenda aliyotufanyia baba yako yanatosha usitake kuanzisha balaa lingine”

    Nisha aliweka kila kitu bayana na kila aliyeyasikia maneno yale aliamini na hakukuwa na haja ya kuhoji chochote kwakuwa mzazi mwenyewe ameweza kuweka siri yote kwenye masikio ya hadhira hata david akawa ameshajua maisha aliyopitia dada yake kwa muunganiko wa matukio aliyo yapata kutoka kwa rafiki wa nisha na kuunganisha hayo ambayo mwenyewe ameyasema kwa muda huo,

    Kiukweli john alichoka kwa kuvuta na kutoa pumzi kubwa, alijiona ni aliyekosa thamani mbele ya kila mtu aliyekuwapo pale, uso wa aibu ulimshika kwa yote aliyoyafanya marehemu baba yake helman, haukupita muda askari wa wili walikuja na kumkamata john huku wa kiwa na kijana mmoja ambaye alikutwa na madawa ya kulevya akitaka kuyasafirisha nje ya nchi, na alipoulizwa na kupewa kibano ndipo alipomtaja john helman ndio mmiliki wa mzigo huo hivyo john alikamatwa na kupelekwa kituoni na kuwaacha familia iliyopoteana kwa muda mrefu ikiingia kwenye nyumba ambayo walizaliwa na kucheza humo miaka mingi iliyopita, david alikumbuka mengi sana ambayo yaliokuwa yakifanyika ndami humo, sura ya marehemu baba yake na mama yake zilimjia huku zikitabasamu kwa furaha, alihisi ni ishara kuwa sasa wanaweza pumzika kwa amani huko walipokwenda na ndipo alipo mgeukia nisha ambaye alikuwa ameketi kwe kochi kisha kwenda kumnyanyua mtoto wa kiume aliyezaliwa na nisha na kumchukua mwanae wa kike aliyezaa na kipenzi chake Victoria na kuwaweka pamoja na kusema,,,,,

    “tunakushukuru mungu baba kwa kuweza kurudisha furaha yetu kupitia mapacha hawa wa nje ambao kila mmoja anaonekana kufanana na mzee aliyefanana nae jinsia”

    Baada ya sara hiyo fupi alianza kumyakuwa mtoto wa kiume wa nisha nakusogea naye mpaka kwenye kizingiti cha mlango na kumyooshea juu na kusema,,,,

    “nakushukuru mungu baba kwa kuweza kumpatia dada yangu mtoto wa kiume ambaye leo hii atakwenda kuwa mlisi wa jina la marehemu babu yake, kuanzia leo mtoto huyu ataitwa “ALFRED”

    Alipomaliza kumbatiza jina mtoto huyo alikwenda kumkabidhi kwa mama yake nisha, kisha kumchukua mwanae wa kike na kusogea naye kwenye kizingiti cha mlango na kumyooshea juu na kusema,,,

    “upole na huruma aliyokuwa nayo mama yetu, zote ziende kwa mtoto ambaye atalisi jina la bibi yake, kuanzia sasa mtoto huyu ataitwa “MAGRETH”

    Magreth mpya alipopewa jina lala bibi yake alikabidhiwa kwa mama yake na wote walicheka na kufurahi kwa furaha.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *********

    Baada ya miezi kadhaa kupita Victoria na nisha walifunga ndoa na baadaye david alifikiria na kuona raha ya mtoto alelewe na wazazi wote wawili hivyo alijitahidi kadri ya uwezo wake akamtafuta mwanaume aliyempatia ujauzito dada yake na kumshawishi wawe pamoja na kumwambia kuwa wememsamehe bila kinyongo cha aina ya yoyote ile, Jackson ambaye ni baba magreth wa sasa alikubali kuwa pamoja na nisha na wao pia wakafunga ndoa na kusamehana yote yalio pita,

    Taarifa za ndoa ya nisha zilifanikiwa kumfikia john mtoto wa helman huko gerezani ambapo naye alihukumiwa kwa kosa la uuzaji wa madawa ya kulevya ndani na nje ya nchi, hivyo kutokana na nguvu ya mapenzi na upendo aliokuwa nao kwa nisha ukiachilia mbali udhalilishaji alioupata wa kulea mimba ambayo si yak wake akaamua kujimaliza kwa kisu walipokuwa wakifanya kazi za gereza na kumfuata marehemu baba yake helman kuzimu aliko elekea.

    Ama kweli mwisho wa ubaya ni ubaya, na jasho la mtu hali liliwi

    Ridhiki anagawa mungu tafuta ya kwako nawe utafanikiwa;



    ---- --------------MWISHO-----------------



0 comments:

Post a Comment

Blog