Simulizi : Sahihi Ya Kifo
Sehemu Ya Nne (4)
Siku kama hiyo ya jumamosi chuoni hapo kuna kuwa na disko ndani ya ukumbi wa chuo na baadhi ya wanafunzi huwa wanachaguliwa kucheza nyimbo za aina mbalimbali ilikuonesha uwezo wao na vipaji vyao,
Rafiki zake na victoria waliweza kugundua kuwa victoria ameanza kumpenda david hivyo walianda mpango na kuongea na wanachumba wenzie na david kuwa itakapofika muda wa kucheza basi david acheze na victoria na wengine waliobaki watacheza na wao,
Swala hilo lilionekana jema sana kwa washikaji zake na david maana waliona sheshe kaingia kwenye kichaka cha simba hivyo hakuna jinsi zaidi ya kumlarua tu na kumla nyama, mpango huo ulikubalika,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mida ya saa mojamoja hivi usiku wanafunzi walionekana kujiandaa vyema, wenye kuazima nguo waliazima, na wenye kugongea marashi waligongea ilimradi kila mtu aonekane maridadi siku hiyo mbele ya wavulana na mbele ya wasichana ndani ya ukumbi huo,
Mipango yote hiyo wakati ikiendelea david hakuwa na taarifa yoyote ile, yeye alijiandaa kawaida maana hakuwa mpenzi sana wa mziki na mipango yake ilikuwa ni kwenda kuangalia kwa muda tu na kumuona mtoto victoria kisha arudi zake bwenini,
sauti ile ya mziki uliokuwa unasikika ukumbini ulianza kuwa kusanya watu eneo lile.wengi walipendeza na nguo zao za anasa,wengine walionesha mizuka yao kwa kucheza nje hata kabla ya kuingia ndani acha wale waliokuwa wamekumbatiana kwenye giza wakiendelea na mambo yao ya ajabu ambayo haya stahiri kuonwa na watoto,
yote hayo david aliyaona na kubaki kusikitika tu na kuendelea kuzunguka kumtafuta victoria, wakati akiwa anashangaa ghafla alikuja msichana mmoja kwa nyuma ,hakika alikuwa mrembo sana, akamshika kiuno david hali iliyomfanya ageuke kwa haraka sana, kitendo kile cha kugeuka haraka na yule dada alikuwa anataka kumkumbatia basi wakajikuta wanadondoka chini na yule dada akiwa juu ya david,,
watu waliwazunguka na kuanza kuwa pigia makofi hata wale waliokuwa mbali walitamani kutaka kujua kuna nini eneo lile hivyo nao hawakusita kusogelea,
umati huo uliokuwa unasogea alikuwepo na victoria pia, ndani ya dakika chache kila mtu aliweza kushuhudia kitendo kile na yule dada alifurahi sana kwa tukio lile maana alikuwa kajipatia umaarufu mkubwa kumkumbatia mwanaume asiye kuwa na mpango na wanawake halafu anapendwa na wengi,
david alijitahidi kumsukuma yule dada pale chini na akafanikiwa, alinyanyuka kwa hasira na kuanza kuwasukuma watu wampishe ili apite andoke zake, alipo wamaliza ghafla mbele yake akamuona victoria aliyekuwa anataka kuanza kulia,
kwakuwa kila mmoja alikuwa anampenda mwenzie hivyo nyuso zao ziliteseka kwa aibu na victoria kuanza kukimbia eneo lile na david kumfuata kwa nyuma, watu hawakuelewa kinachoendelea zaidi walizidi kushangilia tu kwa kujionea filamua ya mapenzi ya bure,
Victoria alikimbia mpaka akapotezana na david, hivyo david akawa anazidi kumtafuta maeneo yote yale ya chuo lakini hakumuona kwa muda huo
Hasira za victoria zilimpeleka mpaka kwenye stoo ya chuo ambayo ilikuwa na kiza na kuanza kulia, alijilaumua sana kwa kuchelewa kumwambia hisia zake mwanaume aliye mpenda kwa muda mfupi na akiwa ndani ya maumivu alilia sana huku akiendelea kufikiria na maneno ya upweke yakamtoka,,,,
“”nani ambaye atauokoa moyo wangu kwenye mafuriko haya ya machozi eeh jaman nimechoka kuwa mtumwa wa kumtumikia bwana maumivu, nani aje kuwa mkombozi wangu na kunifariji kwa kipindi hiki kigumu eeh?
Victoria alijuta kuwa na moyo wa upendo kwa kuwa ulikosa mtu wa kuutunza, machozi hayo alimkumbuka mtu aliye kuwa na ahadi naye ya kukutana, na aliya kumbuka maneno matamu aliyokuwa anatumiwa hivyo alihisi moyo wake unaweza kupata faraja kupitia mtu huyo bila ya kujua mtu mwenyewe ni david aliyempenda bila kumwambia pia ndiye aliye mfanya yeye kuwa mahali hapo ambapo si salama kwa usiku huo,
Victoria hakuwa na budi kuanza kulitafuta jina la mtu huyo kwa jinsi alivyo liweka yeye ili ampigie waonane, wakati anaendelea kulitafuta kumbe david alikuwa amekaribia maeneo hayo ya stoo na alishtushwa na mwanga wa simu uliokuwa unaonekana kule stoo na hisia zikaja huenda atakuwa victoria hivyo ikabidi aufuate ili awe na uhakika kama kweli ni victoria,
David hakuchukua muda mpaka kufika kwenye mlango wa stoo na alianza kuchungulia mle ndani na kugundua kuwa yule ni victoria kwa kusaidiwa na ule mwanga wa simu uliokuwa unammulika mrembo huyo ambaye david mwanzo alimuita Qeen tz,
kabla victoria hajalipata jina la mtu anayetaka kuonana nae ghafla rafiki yake akamtumia ujumbe ulikuwa unamuuliza,
“uko wapi”?
victoria alisonya na kuendelea kutafuta jina la mtu wake bila kujibu ujumbe huo ndipo rafiki yake huyo akaamua kumpigia na wimbo uliokuwa unaita ni huu,,,,,,,
“I’m so lonely broken angel”
“I’m so lonely,listen to my heart”
“one and only broken angel”
“come and save me, before I fall apart”
Victoria pia hakuweza kupokea hata hiyo simu mpaka nyimbo hiyo iliyoendana na upweke alionao ma iliyomuongezea machozi ilipo kata yenyewe,
David aliusikia wimbo huo pale nje na kilio cha mtoto mzuri victoria ndipo alipojitokeza na maneno matamu ya mahaba yalitoka kwa sauti inayo sisitiza upendo,,,,,
“niko hapa kukutoa upweke ulionao”
Sauti hiyo iliushtua sana moyo wa Victoria alitamani kumjua huyo mtu aliye ingia humo ndani japo alihiisi kama sauti anaifahamu vile, ndipo alipommulika usoni kwa kutumia mwanga wa simu na kugundua kuwa ni david,
Mdomo wenye ulimi mzuri ndani yake na uliojaaliwa kutamka maneno mazuri ya upendo ulitaka kusema kitu lakini ulipingwa na sauti iliyo shiba ya shababi david kwa kauli yenye kusisitiza mahaba,,,,,,
“Victoria moyo wako unaweza kutoka kwenye mafuriko ya machozi kama utaruhusu kuliachia tabasamu ulilolificha kwa muda mrefu kwa mtu unaye mpenda na kuhisi kuwa anaweza kuwa baharia wako atakaye kufikisha nchi ya furaha yenye upepo na kijua cha mapendo ya dhati na kuepukana na visamaki pamoja na vichura vidogovidogo vilivyokuja na tamaa ya maji ambavyo kiangazi ikifika havionekani”
“Wengi watakuhitaji kwa muda mfupi lakini ni kwasababu ya kutaka kutimiza kiu yao ya uzinzi tu ila mimi david niko hapa kwa ajili ya kutaka kulinda uzuri wako usipotee na kuharibiwa na watu wasio jua thaman yako fikiria leo nafuta chozi lako kwa maneno ya dhati toka moyoni mwangu ambayo sijawahi kumueleza mwanamke yoyote yule katika ulimwengu huu lakini kwako yameweza kutoka tena bila hata ya kujali ile namba ya siri ambayo kwa mwanaume mwenye kujielewa ni lazima ndio aifanye kuwa funguo ya moyo si nyingine ni tabia pekee,, hilo kwangu sikujali tafadhali naomba upokee maombi haya ambayo tayari yamesha pitigwa saini ya upendo”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Victoria alizidi kuweweseka manaa hakuamini kama angeweza kukutana na mwanaume aliye mpenda kwa dhati katika mazingira hayo, kicheko cha furaha kilicho changanyika na aibu kiliendelea kumtesa moyoni mwake, miguu yake ikawa na kazi ya kuchimbachimba chini huku vidole vyake vya mkono wa kulia akivinyonya kama mtoto mdogo aliye kuwa na hamu ya ziwa la mama yake, aliinua uso wake uliokuwa unang’a hata kama kulikuwa na kiza na kumrembulia jicho david, jecho lenye kope za asili na majimaji ndani yake ambayo yalizidi kumfanya david kujipa asilimia 99% za kumpata Victoria,
Miguu yao ilionekana kupiga hatua ndogo ndogo wakisogeleana kwa hisia mpaka ku kawa na umbali wenye mita sifuri(zero distance) na kilichoendelea hakisimuliki,
Ndani ya muda wa kama saa moja na nusu hivi walionekana wakitoka kwenye chumba hicho kilichokuwa na kiza huku nyuso zao zikiwa na furaha,
Victoria kila walipo kuwa wana tembea umbali wa hatua tano lazima aegemee kifua cha david huku akiachia kicheko ambacho kilimfanya david atabasamu na kumuachia busu la msisimko shavuni mwake,
Kutembea kwao pamoja walivutia wengi ambao walikodoa mi macho kuwa tizama na kutaka kuhakikisha kama yule ni david au siye, wakawa na kazi ya kutaniana tu na kukimbizana kwenye viunga vya maua chuoni hapo hata habari ya disko wakawa wamesahau kabisa,
Moyo wa david ukawa umeingiwa na furaha ya ajabu ambayo hakuwahi kuipata kwenye maisha yake lakini Victoria mwanamke wa kwanza ameweza kuibadilisha akili ya david na kumuingiza sehemu ambayo wengi wana lia,
Rafiki zake na Victoria waliokuwa wana mtafuta walibaki midomo wazi walipo wakuta pamoja wamekumbatiana huku wakiwa wameegemea mti, kila mmoja wao alionekana kufurahia mahusiano yao kwa kuwa waliendana sana.
Siku nyingi zilikatika na habari zili sambaa chuoni hapo juu ya watu hao wawili kuwa katika mahusiano ya kimapenzi, waliokuwa wanampenda Victoria waliumia kwa kumkosa hata yule Emmanuely regan aliye mtenda alianza kuona wivu jinsi watu walivyo kuwa wana wasifia kwa kuendana kwako,
Wasichana wengi nao walijitahidi kutaka kutoa kasoro za Victoria kwa kuwa walikuwa wanampenda david lakini jitihada zao ziligonga mwamba kwa wawili hao kushikamana kupita kiasi,
****************************************
Miaka minne ya david kukaa chuoni ikawa imewadia ni baada ya kumaliza mtihani wao wa mwisho na kila mmoja kuwa ndani ya mavazi yalio fanana kama sale ya siku hiyo maalumu ya kuhitimu ambayo yaliandaliwa mahafali makubwa chuoni hapo watu wengi walihuzulia wakiwemo wazazi wa wanafunzi lakini wengi wao walikuwaa ni wakutoka pale pale Rwanda,,
Victoria na david walikuwa miongoni mwa wanafunzi ambao hawakuwa na watu wa kuwasindikiza katika mahafali hayo, japo huzuni ilimtawala sana kwa kuona wazazi wa wenzie lakini Victoria alijua wajibu wake kwa david hivyo alimliwaza kwa maneno matamu na kumwambia kuwa yeye ndio mama yake, hivyo awe na mana ndani ya moyo wake,
David alizidi kuonesha upendo kwa Victoria maana alipata faraja aliyoikosa kwa muda mrefu na kwa wakati muafaka ambao alikuwa kwenye mawazo mazito,
Watu walikusanyika eneo maalumu ambapo viti vya wahitimu vilitengwa karibu na wazazi na vile vya wanafunzi wengine viliwekwa kando kidogo
Meza kubwa iliyokuwa mbele aliweza kuwepo mgeni rasmi ambaye ni rais wa nchi hiyo muheshimiwa paul kagame akiwa ameambatana na familia yake ambao walikuwa wame kaa pembeni kidogo,
Muongozaji shuhuri aliweza kusoma ratiba itakayo waongoza ili kukamilisha mahafalli hayo, taratibu zote zilifuatwa na kabla ya mgeni rasmi muheshimiwa paul kagame kusimamishwa alitakiwa kusimama mwanafunzi mmoja kwa ajili ya kuwa kilisha wengine kwa kusema kitu ambacho kitaweza kuwasaidia huko mtaani wanako kwenda na wale watakao baki chuoni hapoa ili mgeni rasmi naye aweze kutoa mchango wake katika chuo hiko kwa kuendeleza na kukuza maendeleo ya elimu nchini Rwanda,,
Mkuu wa chuo alipelekewa majina matano ya wanafunzi ili achague atakaye wakilisha wanafunzi wote chuoni hapo,kula ya mkuu wa chuo ilidondokea kwa mtoto wa alfredi kazinge ambaye ni david na jina hilo kutangazwa mbele ya wanafunzi wote na muhusika alitakiwa kwenda mbele ya hadhara ile ya watu wengi kwenda kuzungumza mambo ya msingi,,,,,,
Waliokuwa wanasikia tu habari za david bila kumjua muhusika walifurahi sana maana ndio ilikuwa nafasi pekee ya wao kumuona, sauti za makofi zilisikika kwa wingi kumkaribisha kijana huyo mtanashati aliye pata bahati ya kuzungumza ili kumkaribisha rais wa nchi hiyo mheshimiwa paul kagame,
Jambo hilo lilimfanya david kupata uwoga maana hakujiamani kama ni yeye ndiye anaye hitajika kwenda pale mbele ya hadhara ile kubwa japo alikiri jina lililo tajwa ni la kwake, Victoria aliye kuwa karibu alimshika began a kumuomba ajikaze na kujiamani kama mwanaume aende,
Wengi walitamani wangeitwa wao lakini aliye chaguliwa ni kijana aliyeonekana mnyonge sana chuoni, vidole vingi vilikwenda kwa david na minon’gono mingi kusikika,
makofi yalizidi david alipo nyanyuka na kuanza kuelekea kule ilipo maiki ya kuongelea
Jambo hilo lilimfanya david kupata uwoga maana hakujiamani kama ni yeye ndiye anaye hitajika kwenda pale mbele ya hadhara ile kubwa japo alikiri jina lililo tajwa ni la kwake, Victoria aliye kuwa karibu alimshika began a kumuomba ajikaze na kujiamani kama mwanaume aende,
Wengi walitamani wangeitwa wao lakini aliye chaguliwa ni kijana aliyeonekana mnyonge sana chuoni, vidole vingi vilikwenda kwa david na minon’gono mingi kusikika,
makofi yalizidi david alipo nyanyuka na kuanza kuelekea kule ilipo maiki ya kuongelea ,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wingi wa makofi uliwafanya watoto wale wa kike wa paul kagame kuwa na shauku ya kumuona huyo david aliyekuwa umbali kidogo kabla haja isogelea maiki, mwendo wa david na tabasamu alilo kuwa analiachia lili wachanganya wasichana wengi hata walio kuja kwa niaba ya ndugu zao nao mioyo yao ilikiri kuwa david ni mtu mwenye kila sifa ya kuitwa mwanaume na kugombaniwa,,
Ndani ya hatua chache alifanikiwa kuifikia ile maiki iliyosimamishwa na kuanza kukohoa kidogo ili kuwa weka watu katika umakini wa kusikiliza kitakacho ongelewa, alipo maliza alipepesa macho yake huku na huko kutafuta pozi la kuanzia ndipo alipo gongana macho kwa macho na mtoto wa rahisi paul kagame,
David akiachia tabasamu na kuonesha hana mpango naye japo yule dada alianza kuleta mikao ya ajabu baada ya kuangaliwa na david,
Akili ya david ilipokaa sawa na kuona kimya kimetawala ndipo alipo anza kusema mambo ya msingi na kwa faida ya wote kutoka moyoni mwake baada ya kutoa salamu kwa wote,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
“maisha ni kama kivuli cha mti ambacho kadri muda unvyo sogea ndivyo kivuli huama na kubadilika hivyo mimi na wewe wote kama vinajana tusikubali kukatishwa tamaa na mtu wa aina yoyote ile maana cheko la usoni wakati mwingine linakuwa ni mlinzi wa roho mbaya iliyokuwa moyoni, hiki tulicho kipata chuno hapa basi kiwe ni chenye kuleta upendo kwenye familia zetu, tusije kumzalau baba au mama kwa elimu tulio ipata, akili zetu zinabidi zifanye kazi ipasavyo na kuamini kuwa hata kama baadhi ya wazazi wetu hawajafanikiwa kupita hata katika chumba kimoja cha darasa lakini wao ni wajuzi kuliko sisi tulio pita madarasa mengi ambayo yanaweza kuleta viburi mbele za watu kwa kujiona kuwa sisi ni wathamani zaidi kuliko yule mtoto unaye muona kaweka mikono nyuma barabarani na kukuonesha jicho la haruma pale unapokuwa unakula vitu vitamu, hakupenda kuwa katika hali ya udhuni lakini alitamani naye siku moja ashike peni na karatasi abadilishe maisha kama wewe,
Tusimnyanyase yule msichana wa kazi mdogo ambaye ni kama mama yako wa pili pale nyumbani hata kama ni mdogo maana ndiye anaye anayekuandalia chakula na kukufanyia kazi zote japo umri wake hauruhusu kufanya kazi zile ila in sababu ya shida tu,
Kwanini umuone in kama mtu wa kupita hali ya kuwa anatabia nzuri inayo mpendeza kila mtu, tafadhali elimu isifanye kuwabagua watu maana hatujui kesho utakuwa nani kutokana na maisha kuwa kama kivuli cha mti”
Maneno hayo david aliyazungumza kwa sauti ya upole na palipo stahili kukemea baya alikemea lakini alikuwa ameanza kusindikizwa na chozi la huruma kutokana alichokuwa anakisema alikuwa ana maanisha,,,,,,,
“huenda huyo msichana wa kazi utakaye mnyanyasa au kumfanya ndio mke wenu wa pili wewe na baba yako kutokana na pesa zenu na kumpatia ugonjwa ambao utamfanya ajute kwenye maisha yake anaweza kuwa ni Nisha,,,,,,,,,
“Nishaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!” sauti za hadhira iliyokuwa pale walirudia jina hilo la nisha kwa mshangao na kuonekana kujiuliza ni nani huku david naye akiwa kajishtukia maana haikuwa dhamira yake kumtaja mdogo wake kipenzi hivyo alipatwa na mshtuko wa ghafla papo hapo na kuachia maiki ile kishindo kizito kilisikika in baada ya mwili wa david kufika katika ardhi---
Mama!!!!!!!!!!!! Yesu kristu!!!!!!!!!!!!!!!, mtumeeeeeeeeeee!!!!!!!!! Maskini ni nini hiki tena???????? Mayowe ya watu yalisikika kwa mshangao, wapo walioshika mioyo yao na wengine kushika vichwa vyao, Victoria alichanganyikiwa mkono wake ulishika ile nguo aliyo vaa yenye urefu uliokuwa unataka kubuluzika, machozi yalianza kumlenga mlenga huku akiomba njia ili awahi pale alipo dondoka kipenzi chake ambaye aliapa kutomuacha haka kama ardhi yote itageuka na kuwa bahari,
Umati wa watu ulimfanya Victoria kuchelewa kumuona david yupo katika hali gani pale alipo dondoka ni baada ya kuwa waliokuwa karibu kumbeba na kumuwahisha katika zahanati ya chuo, alibaki kusimama tu kuangalia jinsi david alivyokuwa anakimbizwa ili kwenda kuokoa maisha yake,
Mkuu wa chuo alisimama na kuomba radhi kwa kilicho tokea na kusisitiza utulivu uendelee ili wamalize shughuli salama, rafiki zake na Victoria walikwenda kumchukua victoria pale alipokuwa amesimama na kumrudisha kwenye kiti,
Ndali ya dakika kadhaa hali ikawa shwari kiasi Fulani lakini kulikuwa na minong’ono midogo midogo, wengi walikshindwa kuelewewa kilichokuwa kinaendelea na walitamani kumjua nisha ni nani? Hata Victoria naye alishindwa kujielewa vile na kutulia pale alipokuwa amekaa alitaman kunyanyuka aelekee kule alipo pelekwa david,
Moyo wa wivu ndio uliokuwa unamsumbua Victoria kwa wakati huo maana naye hakumjua nisha ni nani kutokana na david kutomuleza siri ya maisha yake na mengi yalio mkuta, utaratibu wa mahafari uliendelea kama kawaida na rais paul kagame kutoa pongezi kwa david ambaye hakuwepo hapo kwa ujumbe mzuri alio utoa kwa wenzie na kusisitiza ufuatwe na kutekelezwa,
,
Makofi mengi yalipigwa kuashiria wapo pamoja na rais na kuwa watafanya kama alivyosisitiza,
Rais paul kagame alivyomaliza hotuba yake, utaratibu ulifuatwa kama kupewa vyeti vyao, kupata chakula na kunywa, wanafunzi walipiga picha nyingi kwa ajili ya ukumbusho na wengine kubadilishana namba za simu pamoja na barua pepe kwa ajili ya mawasiliano maana waliokuwa wanasoma hapo wengi walikuwa wanatoka mataifa tofauti tofauti,
Familia ya muheshimiwa paul kagame ilipata fursa ya kwenda kumuona david ambaye alikuwa anaendelea vizuri baada ya kupewa huduma hapo kituoni na kwakuwa tatizo lake lili kuwa in la muda mfupi tu basi aliruhusiwa na kujumuika na wenzake, watoto wa kike wa rais waliomba kupiga picha na david za mapozi tofauti ambayo mengine yalizidi kumkera Victoria maana hawakuruhusiwa kwa wakati huo kufanya chochote kutokana na uwepo wa rais pale,
Baada ya rais kuondoka david akawa huru kuungana na wenzie rasmi na kupiga nao picha, wengi walichukua namba zake hata wale waliokuwa wana mchukia walinyoosha mikono kuwa wameshindwa vita nay eye hivyo wakaendeleza amani tu, kila mtu alitoa kinyongo chake na kukumbatiana,
Mkuu wa chuo alimletea david vyeti vyake ba kumpiga kofi la pongezi begani kwa ujumbe mzuri alio utoa na kumtakia kila rakheri katika maisha yake huko anako kwenda azidi kuwa hamasisha watu kufanya mambo ya msingi,
Na wamwisho alikuwa mama mwenye nyumba mtarajiwa Victoria , walipiga picha nyingi sana zilizo ashiria upendo wa dhati hata kama atakaye ziona alikuwa hawezi kuuliza kama walikuwa wapenzi maana zilijitambulisha zenyewe, watu wengi walitoa machozi kwa kuachana na ukiangalia walisha zoeana hasa rafiki zake na Victoria ambao wengine walitokea, Ghana, Kenya na Burundi.
Hivyo ndivyo safari na maisha ya chuo kwa david yalivyo malizika na siku aliyofuata safari ikawa imewadia kurudi nchini Tanzania kuendelea na shughuli yake pevu ya kumtafuta helman.
********************************
Magari ya aina tofauti yaliegeshwa upande wa kushoto na wa kulia kwa kutenganishwa na barabara ndogo iliyopita kati, watu wa mataifa mbali mbali wenye rangi nyeupe na nyeusi walikuwa wakipishana wengine wakiingia na wengine wakitoka, wafanya kazi wenye sale za suruali nyeusi na mashati myeupe huku wakiwa na vitambulisho vya ajira yao vilivyokuwa viki ning’inia shingoni waliendelea kusukuma mikokoteni midogo ya kisasa iliyipakia mabegi walizidi kupendezesha eneo hilo ambalo lilikuwa na miti myembamba na mirefu ambalo lilitambulishwa kwa jina moja la mtu anaye kumbukwa na kutamani arudi kila siku inayo itwa,aliyepigania uhuru wan chi hii yenye sifa ya kuitwa kisiwa cha amani ambayo sasa inaelekea kupotea kutokana na wapuuzi wachache waliokuwa na nia ya kutaka kujifaidisha wao na familia zao, ni “JULIUS NYERERE INTERNATIONAL AIRPORT” (uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius nyerere)CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kofia ya zambarau na tisheti ya zambarau vilivyo changiwa na suruali ya jinsi nyeusi pamoja na viatu aina ya jodani yenye uwekundu maeneo yalio karibia soli ya kiatu hicho ndivyo vilimfanya david kung’aa zaidi pale uwanja wa ndege wa juliasi akiwa kamshika mkono qeen tz wake Victoria ambaye aling’arishwa na nywele za kizungu zilizo iva kwa weusi na kuzibana kwa kibanio cha rangi ya pinki iliyoendana sawa na rangi ya kiatu alicho vaa huku vikitoautisha na suruali nyeupe iliyombana kiasi na kuonesha maungo yake, ile brauzi yenye rangi ya goldi na iliyokuwa inameremeta kwa nakshi zake hakika Victoria zilimpendezesha sana,,
David alisimama na kutoa simu yake ambayo kulikuwa na picha ya Victoria kwenye kioo na kutafuta namba ya afande criss kisha kupiga na punde ikawa imepokelewa, david alipokuwa anataka kuuliza kuwa afande criss amesiamama wapi kwa bahati nzuri macho yao yakagongana na afande criss akawa anampungia mkono huku akionesha uso wa furaha kwa kumuona david kwa maranyingine tena akiwa katika muonekano tofauti kabisa,
Baada ya kuzunguka kutoka mle ndani wakakumbatiana kwa furaha kila mmoja alikiri kumkumbuka mwenzie, Victoria alibaki akiwanshangaa tu na tabasamu lake la uchokozi, wawili hao afande criss na david walipo maliza kulakiana mdomo wa afande criss ilitaka kuuliza kitu juu ya Victoria lakini alipomtazama david walibaki kucheka tu maana afande criss alikuwa mtu mzima aliweza kuelewa kilichoendelea kati yao,
Wote walitembea kwa furaha na kuelekea kwenye gari la afande criss lakini Victoria alitaka kuweka kipingamizi kwenda kwa kina david japo alipompigia mama yake akawa hampati kwenye simu hivyo david alimuomba na kusaidiwa na afande criss waeleekee kwanza kwako halafu watampeleka Victoria nyumbani kwako, mtoto wa kike akawa hana kipingamizi mbele ya kipenzi chake alikubali na safari ikaanza kuelekea mabibo external nyumbani kwa afande criss,
Baada ya purukushani za foleni huko barabarani walipokuwa hatimaye waliweza kufika external mabibo ambapo david alieza jinsi masomo yalivyokuwa huko na kila kitu ambacho alichokuwa anakijua alimtambulisha Victoria kwa afande criss na kumdanganya Victoria kuwa yule ni baba yake akiwa na maana hakutaka maswali mengi hapo baada na Victoria kuujua undani wake mapema hivyo na baada ya kula na kunywa david ilibidi aage na kumsindikiza Victoria mpaka kwako lakini aligoma kuingia ndani na kuahidi kuwa atakwenda siku nyingine,
Japo Victoria alichukia lakini hakukuwa na jinsi david alirudi mpaka kwako ambapo afande criss alikwenda tena kazini:
***************************
Chini ya usiku wa nyota na mwezi david akiwa juu ya kitanda chake baada alitafakari na kupanga mipango yake ya kuanza kumtafuta mdogo wake nisha na kuingia vitani rasmi maana tayari ngao ya elimu anayo anauwezo wa kuingia mahali popote anapo pataka,
Aliwaza na kuwazua wapi aanzie akawa amepata jibu nini cha kufanya alijisema moyoni,
“kesho inabidi nifanye kila linalowezekana niende morogoro alipokuwa amefungwa mzee wangu na kupoteza maisha na kuzikwa kama mbwa wa mitaani aliyegongwa na gari, lakini inabidi niifanye kuwa siri asijue Victoria wala afande maana wanaweza leta kipingamizi na naweza kupokea maswali mengi kutoka kwa Victoria ukiangalia kwa sasa sijapnaga kumuambia chochote kile,”
Chini ya usiku wa nyota na mwezi david akiwa juu ya kitanda chake baada alitafakari na kupanga mipango yake ya kuanza kumtafuta mdogo wake nisha na kuingia vitani rasmi maana tayari ngao ya elimu anayo anauwezo wa kuingia mahali popote anapo pataka,
Aliwaza na kuwazua wapi aanzie akawa amepata jibu nini cha kufanya alijisema moyoni,
“kesho inabidi nifanye kila linalowezekana niende morogoro alipokuwa amefungwa mzee wangu na kupoteza maisha na kuzikwa kama mbwa wa mitaani aliyegongwa na gari, lakini inabidi niifanye kuwa siri asijue Victoria wala afande maana wanaweza leta kipingamizi na naweza kupokea maswali mengi kutoka kwa Victoria ukiangalia kwa sasa sijapnaga kumuambia chochote kile,”
Hayo ndiyo yalikuwa mawazo ya david na mpango aliokuwa mauandaa, asubuhi na mapema david aliamka na kujiandaa vyema, alipokuwa anatoka nje alikutana na afande criss ambaye naye alikuwa anaelekea kazini, afande alimuulizaa swali david baada ya kumuona amejiandaa asubuhi subuhi,,,,,,,
“vipi david unasafari?
“ aah jana nilisahau kukwambia victoria leo wanasherehe kwako mtoto wa baba yake mdogo anaolewa hivyo amenialika na inawezekana nisirudi mpaka kesho” david alimdanganya afande criss
“Ooh hakuna shida kikubwa kuwa makini tu na tueane taarifa kama kunatatizo na ngoja nikupatie pesa kidogo” afande criss alizungumza
“Hapana baba pesa ninayo ya kutosha hakuna shida labda kama itapunguwa basi nitakujulisha”
Afande criss alimuelewa david na akampa ruhusa japo taarifa ameipata asubuhi hakujali maana david Alisha kuwa mtu mzima sasa hivyo kila mmoja alikwenda kivyake na david kuelekea kwenye kituo kikubwa cha mabasi ubungo na kuchukua gari ya kampuni ya abood iliyokuwa inaelekea morogoro,
Huzuni ilimjia baada ya kukumbuka jinsi alivyopotezana na mdogo wake kipenzi nisha nay eye kunusurika kufa kwa shtuma za wizi, mpaka gari inaanza kuondoka david mchozi mwembamba ulikuwa unamshuka taratibu, alichukua kitambaa na kujifuta.
**********************************
Ndani ya msaa matatu akawa amefika stendi kuu ya mabasi ya mjini morogoro msamvu kisha kuchukua gari ndogo kuelekea kinguluila gerezani alikokuwa amefungwa marehemu baba yake,
Umbali wa kutoka hapo mjini mpaka kufika huko gerezani haukuwa mkubwa sane hivyo aliweza kufika mapema na alipoliona geti la gereza alimkumbuka marehemu baba yake sana, alipiga hatua mpaka kwa mlinzi na kujiandikisha kuwa anaelekea kwa mtunza kumbukumbu wa gereza,
Mlinzi huyo alimuelekeza ofisi ya mtunza kumbukumbu na david hakuchelewa alielekea huko na alipo fanikiwa kuonana naye walisalimiana na david kueleza shida yake ambayo afisa huyo alitaka kuipinga lakini david alimpitia kiasi cha fedha na akaridhika,
Ndipi alipo simama afisa huyo na kwenda kwenye droo kisha kurudi na daftari moja ambalo lilichoka choka na kumkabidhi david na david alimuuliza,,,,,,,,,
“Unauhakika kuwa hili ndilo daftari lililokuwa linatumika kuandikisha watu wanaokuja kutembelea wagonjwa kipindi hicho marehebu baba yangu alipo fungwa hapa?
“Ndio ninauhakika” alijibu yule afisa
Ndipo david alipoanza kulikagua taratibu na kwa umakini wa hali ya juu klitafuta jina la mtu wa mwisho aliye kwenda kumtembelea marehemu baba yake kabla ya kifo chake,
Uso wa david ulibadilika ghafla na kuiva kwa hasira baada ya kulikuta jina na sahihi iliyopigwa ya mtu huyo wa mwisho kwenda kumuona marehemu baba yake kabla ya kifo chake lakini jina lililo andikwa pale ni HELSON ambalo kila akitafakari aliona linaendana kabisa na HELMAN alijiuliza na kuingalia ile sahihi iliyopigwa pale ili aweze kuikariri hata hivyo aliona bado itakuwa kazi kuiweka kichwani ndipo alipomzugisha yule afisa na kumwambia,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
“nahisi umekosea hili daftari tafadhali niangalizie lingine wakati nikimalizia kulikagua hili”\
Yule afisa aliponyanyuka na kwenda kutazama daftari lingine david alichana ile sehemu iliyopigwa sahihi na kukichukua kile kipande cha karatasi.
Kisha kukiweka kwenye mfuko wa suruali yake haraka na kujikausha kwa utulivu wa hali juu kabisa.
“bwana mkubwa hakuna lingine zaidi ya hilo maana yote ni ya miaka ya nyuma zaidi jaribu kuangalia vizuri na kwa umakini zaidi” alizungumza yule afisa wakati ametoka kutafuta daftari lingine,CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Dah mbona kazi inataka kuwa ngumu kwa upande wangu maana nimeangalia kila karatasi kwa uwangalifu lakini sijafanikiwa kuoma chochote kile” alizungumza david iliamradi tu afanye ukweli kuwa uwongo na ndipo yule afande alipo sema,,,,,
“ngoja nami nikusaidie kutazama labda naweza kuliona huenda wewe umechoka kwa uchovu wa safari na kuwa na papala”
“Aah usijali muheshimiwa achana tu na hiyo kazi nitakuja siku nyingine kwa ajili ya hii kazi tu, hivyo usisumbuke ndugu” David alimpinga kisha kumuongezea kiasi cha fedha na yeye kunyanyuka na kuanza safari ya kuondoka huku yule afisa akibaki anashangaa shangaa tu pale mezani kwake.
Siku hiyo David alilala kwenye nyumba ya wageni mjini Morogoro na asubuhi ilipofika akaanza safari ya kurudi jijini Dar es salaam akiwa na wazo jipya kichwani mwake la kuanza harakati za kumtafuta Nisha dada yake kipenzi walioachana miaka mingi huku helman akiendelea kuzunguka mawazoni kwake kwa hasira,
Muda aliotoka Morogoro mjini David aliweza kufika Dar es salaam mapema sana, alishuka kwenye gari kisha kutafakari kwa muda na kuchukua hatua ya kumpigia simu mpenzi wake Victoria, wazo hilo lilimjia baada ya kutaka kuleta uhalisia kwa afande Criss amini kwamba kweli David alilala kwenye sherehe nyumbani kwa kina Victoria,
Baada ya muda Victoria alikuja maeneo ya ubungo mataa na kukutana na David, kila mmoja alimlaki mwenzie kwa furaha bila kujali umati wa watu waliokuwa wanapishana, furaha ilitawala kwenye mioyo yao maana kila mmoja alikuwa anampenda mwenzake toka ndani ya moyo,
“Unatoka wapi mpenzi wangu saa hizi na mbona nilikuwa sikupati kwenye simu?”Victoria alimuuliza David ambaye aliyekuwa anafikiria jibu la kumpa,,,,
“ni kweli Victoria hapa ninavyo kueleza nilikuwa kituo cha polisi baada ya kukosana na mtu lugha na ndio sababu ya kukupigia wewe maana nimemdanganya baba kuwa nili lala kwenu kulikuwa na sherehe hivyo naomba msaada wako ili aamini tulikuwa wote maana akijua kama nilikuwa kituoni atanigombeza kwa nini sikumpigia simu aje kunitoa na mimi jambo hilo sikutaka kulifanya maana mimi ndiye niliye kuwa na makosa”
David alizidi kuwa cheza shere afande Criss na Victoria na wote wakiaamini alayokuwa akiyasema, Victoria alimpatia pole nyingi david ambaye alimdanganya bila yeye kujua kuwa anachezewa akili,
Hawakuchuka muda kufika kutokana na umbali mfupi uliokuwepo kutoka ubungo mpaka mabibo external nyumbani kwa kina david hivyo nyayo zao zilikanyaga kikanyagio cha kufutia vumbi na uchafu mwingine kilichopo pale mlangoni ambapo walikuta viatu na David alihisi afande Criss yupo ndani, hodi moja ilitosha kwa afande criss kusikia na kuwa karibisha waingie,
“ooh wanangu karibuni sana na mna bahati maana ndio nilikuwa nataka kuelekea kazini baada ya kurudi mara moja” afande Criss alizungumza kabla hata wakina David hawaja kaa chini,
“Asante sana baba tunekaribia za tangu jana?” David alimshukuru baba yake anaye mlea afande criss na kumuuliza swali
“namshukuru mungu salama japo nilikuwa mpweke maana nilishazoea kuwa wawili na nyie poleni na uchovu wa sherehe” alizungumza afande Criss
“Mmh tumesha poa baba lakini samahani kwa kutokualika” Victoria naye aliingilia maongezi na kumjibu afande criss wakati david akiendelea kutabasamu kwa kificho baada ya kuona dili lake linaenda sawa hakuna aliyemshtukia kama alikuwa Morogoro kwenye shughuli pevu.
“Uwepo wa David tu unatosha kuniwakilisha mimi wala usiwe na hofu kabisa mwanangu” alizungumza afande Criss,
Baada ya maongezi hayo ya kutakiana hali, afande Criss alimtazama David kisha kumuambia,,,,,,
“David, ni rahisi sana mtu kufa kwa maji aliyo ridhia mwenyewe kuyanywa kuliko yule anaye tapatapa mtoni au baharini”
Usemi huo aliozungumza afande criss uliwafanya Victoria na David kutazamana kwa mshangao kisha David kumuuliza afande criss,,,
“unamaana gani baba kwa usemi huo?”
“maana yangu ni kwamba aliyekuwa kwenye mahusiano na mpenzi mmoja ni rahisi sana kupata magonjwa ya zinaa kama hutokuwa mwaminifu kwa mwenza wako hivyo basi ni jambo la kushukuru kupata mchumba mzuri kama Victoria mimi nawatakia kila la kheri katika mapenzi yenu maana kuna jambo zuri ambalo nataka kukueleza mbele ya mwenzio”
afande Criss alizungumza.na David alijikusanya na kukaa vizuri kisha kuuliza kwa shauku,,,
“lipi hilo tena baba?”
“David kwa bahati nzuri jana nilipokuwa hapa natazama runinga kuna rafiki yangu mmoja alinipigia tukawa tunazungumza maongezi ya hapa na pale ndipo aliponieleza kuwa katika shirika lake linaloshungulika na masuala ya kusaidia vijana kujikwamua kutoka katika hali tete kama uvutaji wa madawa ya kulevya pamoja na kusaidia watoto yatima, sasa aliyekuwa muhasibu wake ametoroka na kiasi cha fedha ambacho kilitumwa kutoka landon na wafadhili waliojitolea kusaidia shirika hilo hivyo anashida ya muhasibu mwingine atakaye kuwa mwaminifu, nami nikaona sio mbaya kumueleza sifa zako juu ya masuala ya kibiashara uliyosomea na ufaulu wako naye ameridhika bila hata kuona vyeti vyako kwa kuwa ananiamini lakini keshokutwa utakapo kwenda kuanza kazi hiyo ubebe na vyeti vyako kwa heshima zaidi na awe na uhakika kwa macho yake mwenyewe” afande Criss alizungumza
Habari ya kazi ni jambo jema kabisa, kila atakaye pata taarifa ni lazima afurahi kutokana na tatizo la ukosefu wa ajira nchini japo kuwa vijana wanaweza kujiajili wenyewe,
David alionekana kuwa na sura ya huzuni japo ilikuwa sio rahisi kuigundua, lakini afande criss aliweza kuijua kutokana na utuuzima alio kuwa nao, Victoria naye tabasamu la kirafiki lilimtoka huku akimwangalia david aliyekuwa anajilazimisha kufurahi,
Jambo lililomfanya david kuwa na huzuni ni baada ya kusikia shirika analoenda kufanya kazi ni la watoto yatima, ndipo mawazo mengi yaka mjia kumkumbuka Nisha ambaye mpaka kwa muda huo hakujua yupo katika hali gani mzima au amekufa? Pia ni miaka mingi imepita tangu wapotezane ni matarajio yake kumuona akiwa msichana mkubwa na mwenye akili timamu kama atakuwa bado yuko hai.
“David vipi mbona umebadilika ghafla hukufurihia kupata kazi?” aliuliza afande criss
“Mmh hapana baba nilikuwa najaribu kufikiria ugumu nitakao upata maana si unajua sikuwahi kufanya hata mazoezi ya kazi nilipokuwa chuo?’alimjibu
“Hahahahah david usitufurahishe sisi ila usiwe na wasiwasi ulichokisoma ndicho utakacho kitumia na mengine utaelekezwa hapo hapo kazini sawa mwanangu?”
******************************
Furaha yenye huzuni ndani yake ikawa imemaliza siku david alimrejesha Victoria kwao lakini kwa bahati mbaya mama Victoria hakuwepo muda ambao david yupo pale, hivyo hakukaa sane nae ilimbidi arudi nyumbani kwao akapata chakula cha usiku kisha kumuaga afande criss na kuelekea chumbani,,CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Aliwasha taa na kwenda kufungua begi lake ambayo aliweka suruali aliyoivaa siku alivyo kwenda gerezani alikokuwa amefungwa marehemu baba yake miaka ya nyuma kisha kuingiza mkono na kukitoa kile kipande cha karatasi chenye sahihi ambayo alihisi ni ya helman japo jina alilo likuta ni halson, aliitazama vizuri sana kisha kukihifadhi ndani ya pochi yake ndogo ya mfukoni na kuamua kujipumzikia kutokana na uchovu.
Siku iliyofuata david aliamka asubuhi na mapema na kufanya baadhi ya kazi ndogo ndogo kama kumyooshea afande criss sale zake za kazi na baada ya afande kuelekea kazini naye akatoka.
Alikwenda mpaka maeneo ya ubungo stendi na kuingia kwenye steshenari moja iliyokuwa karibu na chuo cha the amazon kisha kuitoa chapa nyingie ile sahihi ili ziwe nyingi hata kama moja inaweza kupotea basi awe na akiba,
Alikotoka kulikuwa na sehemu nyingi za kutolea chapa lakini alikwenda maeneo hayo kwa jukumu kubwa kabisa la kuanza kumtafuta dada yake kipenzi,
David alijitahidi kuulizia kila watu ambao aliwaona wakiombaomba na vikundi vya watoto wa mitaani, walio wakubwa na hata watoto kama wangeweza kumfahamu nisha, lakini bila mafanikio mpaka jua likawa linaelekea kutua upande wa magharibi,,
Ndipo David alipo amua kwenda kukaa kwenye mgahawa mmoja na kupata chakula maana kazi ilikuwa nzito kwake hata hamu ya kula hakuwa nayo, wakati akiendelea kujipatia chakula chake pale ghafla macho yake yaliweza kumuona msichana mmoja aliyevaa nguo fupi yenye rangi nyekundu na kichwani chake kikiwa kimepambwa na nywele za kizungu huku moshi mwingi wa sigara ukimtoka mdomoni david alimtazama sana lakini hakuweza kufanikiwa kumuoni usoni kwa umbali mchache aliokuwa amekaa nae na hakutaka kumkazia sana macho lakini kilicho mshangaza ni kuona yule msichana kazungukwa na mipombe mikali juu ya meza yake,
Ndipo David alipo amua kwenda kukaa kwenye mgahawa mmoja na kupata chakula maana kazi ilikuwa nzito kwake hata hamu ya kula hakuwa nayo, wakati akiendelea kujipatia chakula chake pale ghafla macho yake yaliweza kumuona msichana mmoja aliyevaa nguo fupi yenye rangi nyekundu na kichwani chake kikiwa kimepambwa na nywele za kizungu huku moshi mwingi wa sigara ukimtoka mdomoni david alimtazama sana lakini hakuweza kufanikiwa kumuoni usoni kwa umbali mchache aliokuwa amekaa nae na hakutaka kumkazia sana macho lakini kilicho mshangaza ni kuona yule msichana kazungukwa na mipombe mikali juu ya meza yake,
Kitendo hicho david hakukubali akili yake ilikuwa imesha changanyikiwa kila msichana anaye muona yupo katika mazingira yasio eleweka basi akili yake inarudi kwa nisha na kujiuliza vipi huko alipo anaishi vipi? Na ndipo alipo nyanyuka kwenye meza yake na kwenda na kuanza kumsogelea yule dada ambaye umri wake unaonesha si mkubwa, sauti za hatua za david zilimshtua yule dada ghafla yule dada alipoiona sura ya david alionekana kutetemeka huku mikono yake ikichukua pochi yake iliyoendana na nguo yake nyekundu na punde tu david alivyomkaribia yule dada alikurupuka na kuisukuma ile meza na zile chupa za pombe zilianguka na kuvunjika, watu waliokuwa pale walishtuka na kugeuza shingo zao kutaka kujua kuna nini,
Lakini david bila kumuona vizuri usoni yule dada alitoka mbio na miguu ya david haikusita kuanzisha mashindano ya riadha kumkimbilia yule dada ili apate kumjua na kwa nini alikimbia
Hatua zake yule dada hazikumfikisha mbali David akawa amemfikia, lakini yule dada alizidi kuonesha uwoga kwa David baada ya kupiga magoti na kuanza kulalamika,,
“tafadhali kaka yangu usinikamate ni shida tu lakini sikupenda kuuza mwili wangu nipate kipato,ndugu zangu wananitegemea na hapa ninavyokwambia nina watoto wawili wako kwa jirani yangu mpaka nitakaporudi ndio naenda kuwa chukua, hawana baba, mimi ndio baba na mimi ndio mama hivyo kama utanikamata watazidi kuwa katika maisha magumu kuliko haya ya sasa”
Yule dada alimwaga mchozi wa maumivu, kilio chake kiliweza kusimamisha watu waliokuwa wanapita kando, ila david alishindwa kumuelewa anazungumza nini mpaka dakika hiyo, ilimbidi amuuinue pale chini alipokuwa amepiga magoti na kumjibu jibu ambalo wangeenda sawa kwanza iliajue tatizo lilikuwa ni nini,,,,,,,
“usijali dada yangu sitokukamata, ondoa shaka kabisa moyoni mwako twende ukaendelee na starehe zako halafu uniambie kwa upana zaidi naweza kukusaidia”
Yule dada hakuamini alichokisikia toka kwa david kuwa anaweza msaidia, basi waliongozana wote mpaka kwenye zile meza na wakaamua kukaa meza moja ili yule dada aweze kueleza tatizo lake,
“Unaitwa nani dada?” david aliuliza
“Mwajuma” alijibu yule dada huku akifuta mchozi na kuingiza makamasi ndani
“Ooh jina zuri lakini kwanini ulinikimbia wakati na kusogelea?” alizungumza David
“Akili yangu haipo sawa sasa maana ni jana tu wenzangu wamekamatwa na askari kule buguruni kwa ajili ya kufanya miili yao mtaji, na mimi nilifanikiwa kuwa kimbia na wame weka baadhi ya picha zangu kwenye mitandao kwamba natafutwa kwa kwenda kinyume na maadili ya kitanzania kkuuza mwili hivyo kila anaye nisogelea na jua ni askari tu kwani wewe sio askari maana umesema utanisaidia? Alizungumza mwajuma na kumuuliza swali David.
“Hapana mimi sio askari na ujio wangu pale kwako nilihisi unatatizo maana mtu wa kawaida hawezi kunywa pombe nyingi vile zenye ukali” aliungumza David
“ni kweli kaka yangu nimefanyiwa kitu sio kizuri kabisa kwenye maisha yangu nimezalishwa watoto kabla ya umri wangu lakini bora ya hivyo ila mwanaume mwenyewe akaaamua kunifukuza na kunitishia kuniua endapo kama nitatoa taarifa polisi ndio maana nikaamua kujihusisha na biashara hii ya kuuza mwili na kwasasa ninaiishi na virusi vya ukimwi ambavyo sijaelewa nilipo vitoa kutokana na idadi kubwa ya wanaume niliokuwa na tembea nao tena wengine bila kinga kwa kuwa waliniahidi kunipa pesa nyingi”
David huruma ilizidi kumuuingia moyoni mwake maana anashindwa kujua kuwa Nisha atakuwaje maana akiangalia sababu za huyo dada in matatizo yalio mfanya kujiuza na nisha mdogo wake ambaye siku ya kwanza tu kufika jijini akapotezana nae, hajui yu hali gani mpaka sasa.
Mkono wake haukusita kuingia mfukoni na kutoa kitambaa kufuta mchozi wa kiume uliokuwa unachuruzika shavuni kisha kumuambia,,,
“Pole sana dada yangu kwa mataizo hayo lakini usijali huwa kuwa binaadamu kama hujakumbana na changamoto kama hizo na sisi wanaume wengi ndio tulivyo huwa tunapenda kupanda lakini mavuno hatuyataki, na huyo mwanaume wako yuko wapi?” david alimuuliza,
“Yuko haphapa dar es salaam na anapesa nyingi sana pia ni mtu mzima wa makamu anamke na mtoto mmoja wa kiume ambae hana utofauti na wewe kwa muonekano, mimi nilikuwa kimada tu kwake na akaamua kunizalisha ila baada ya mke wake kuanza kugundua kuwa anamahusiano na mimi ndipo alipo nitelekeza kwa kumuhofia mkewe aliposema kuwa atamhuharibia siri zake”
Akili ya david ilikaa sawa kidogo baada ya kusikia mwajuma kataja neon siri, hivyo hakusita kumuuliza,
“Kwani anasiri gani kubwa ambayo mpaka kufikia hatua ya yeye kuhofia?” david alimuuliza.
“Inavyosemekana ni jambazi na swala la kuua kwake ni kama kunywa maji kila mtu amalizapo kula ndio maana nikaamua kukaa kimya tu ili nami nisije kupoteza maisha yangu na kuwaacha watoto wangu” mwajuma alizidi kumpasulia david undani wa maisha yake japo david alishindwa kuamini maana ndio mara ya kwanza wameonana na yule dada kawa muwazi kwake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mmh dah sasa huyo mzee anaitwa nani na anaishi wapi?” david aliuliza,
“Anaishi mbezi beach yeye na familia yake yote na kwa jina ambalo hakuna Malaya asiye lijua anaitwa Helman mapesa, ni hii imetoakana na jinsi alivyokuwa anamwaga pesa nyingi kila anapokuta wasichana wrembo hasa wadogo wadogo ili kuwapa tama ya kukubali kuwa na yeye”
Moyo wa david ulishtuka baada ya kulisikia jina la mbaya wake anaye mtafuta kila kona ya jiji la dar lakini bila mafanikio likitajwa tena kwa sifa mbaya ambazo hata yeye anamtafuta kutokana na ukatili alio ufanyia familia yake, alivuta kiti mbele na kumuuliza kwa umakini mkubwa sana,,,
“Umesema anaitwa nani huyo mzee?”
“Helman mapesa” mwajuma alimjibu
“ Unaweza kuwa na picha zake ambazo mmewahi kupiga pamoja” david akachacha maa kumtaka kumjua huyo helman mapesa mwenye sifa za ukatili
“Ndio ninazo lakini zipo nyumbani kwangu” mwajuma alimjibu
“Samahani naomba tuelekee huko nyumbani kwako ukanioneshe hizo picha nakuomba sana” david alizidi kumbembeleza yule dada mpaka mwajuma akaingiwa na wasiwasi,na kumuuliza,,
Mbona unaonekana unataka kumjua sana wewe ni askari nini? Mwenzio na hofia maisha yangu,watoto wangu wasije kuishi kwa mashaka kwa hilo sitoweza kukusaidia kaka kwaheri”
Mwajuma alivyoona maswali yanazidi kuwa mengi akaamua kumuacha David pale alipo na kuondoka zake huku akimuachia kitisho,,
“ukinifuata na kuitia mwizi na kuheshimu, kama msaada wenyewe ndio huo wa kutaka kuniingiza kwenye matatizo basi, kama unataka kumjua tafuta madangulo nimekwambia hakuna Malaya asiye mjua”
David hakuwa na jinsi maana maeneo yale anayakumbuka vizuri sane aliponusurika kuuwawa kwa shtuma za wizi siku ya kwanza kabisa alipokuwa anaingia jijini, alimuuangalia yule dada ambaye aliamua kupanda boda boda na kuishia zake.
Alinyakuwa mkono wake na kuangalia saa ambayo ilimuonesha kuwa ni saa mbili kasoro, ikabidi achukue simu yake na kumpigia afande criss kisha kumueleza kuwa atachelewa kurudi nyumbani siku hiyo, na alipomaliza mazungumzo naye alinyanyuka baada ya kuwa ameshalipia chakula na kupanda daladala iliyokuwa inaelekea Buguruni,
Dereva wa dalala alijitahidi kuikwepa foleni iliyokuwa barabarani mpaka kufika buguruni ambapo david alishuka na kuulizia sehemu ambayo kuna wanawake wanao jiuza,
Watu hawakuwa na roho mbaya walimuonesha, japo walimuuliza maswali machache na kumpa ushauri juu ya afya yake kwa kwenda kuchukua wanawake wanao uuza miili yao,
Wanawake walionekana ni wengi na wenye umri mdogo waliopendezeshwa na nguo zao fupi za anasa, david alizidi kushangaa kuona mpaka watu wazima wenye umri ambao ungeweza kufanana na marehemu mama yake pia wakifanya biashara ya kuuza miili yao lakini hakutaka kuhoji sana hilo, aliwasogelea na kuanza kuthaminisha kama anachagua nguo dukani mwishowe aliweza kumpata mwanamke mmoja ambaye ni mzuri kimuonekano lakini uzuri wake ulijitia doa kwa biashara aliyokuwa anaifanya, walikubariana bei na david akaahidi kumpatia marambili yake kama atakubali kumsaidia katika mambo yake,
Yule dada hakuwa na shida kwakuwa yupo kipesa zaidi alikubali na kuongozana na david mpaka kwenye nyumba moja ya wageni iliyochoka choka japo ilikuwa inatumiwa sana na wenyeji ipo uswahilini ambayo haikuwa mbali na kile kituo chao cha biashara ya kuuza miili.
Dada yule ambaye alijitambulisha kwa jina la salome akataka kuanza kaziyake ya kumfurahisha david kwa kutaka kumpatia penzi lakini haikuwa hivyo david alimuomba asubiri kwanza wazungumze,ndipo alipomuuliza swali,,,
“unamjua Helman mapesa?”
Swali hilo lilimshtua yule dada na kuanza kuwa na hofu kidogo na kujibu,,,
“ndio na mfahamu kwanini umeniiuliza” salome naye aliuliza swali
“Mmh ni rafiki yangu hivyo aliniambia kuwa hakuna mtu asiye mjua hivyo nilitaka kuhakikisha tu” alijibu david
“Helman mapesa kiukweli hakuna mtu asiye mjua mbali na pesa zake lakini ni mnyanyasaji sana mimba nyingi amekataa na ukimlazimisha anakutishia kukuua hivyo wanasichana wengi huamua kukaa kimya tu” salome alizungumza
“Aisee lakini mimi nilikuwa sijui hilo maana sikuwa nae muda mrefu nimekuja hivi karibuni tu kutoka arusha, na vipi kuhusu mwajuma unamfahamu?”david alizungumza
“Mmh mwajuma na mfahamu si yule anaye kaa jangwani? naye ni mmoja wa wanawake ambao wametelekezwa na Helman mapesa lakini kaka samahani sana Helman mapesa huwa hapendi mambo yake yatangazwe ovyo mimi naogopa.
Salome alikuwa nazungumza kwa wasiwasi sana na ghafla hali ya hewa ikaanza kubadilika mapanzia ya ile nyumba ya wageni yakaanza kupepea kwa upepo mkali uliokuwa unavuma, david alinyanyuka na kuanza kuyafunga punde si punde mlango wa chumba hicho alichokuwa david na salome hodi ikawa inagongwa, david aligeuka na kuutazama mlango kwa muda na kumwambia salome aende kuufungua,
Salome alikwenda na kufanya hivyo alipo maliza kufungua tu ule mlango ukasukumwa kwa nguvu na watu walio shiba wakaingia mle ndani huku wakiwa wameshika mitutu ya bunduki
David alipokuwa anataka kuwa hoji alipigwa na kitako cha bunduki na kudondoka chini, mikono yake ikiendelea kusugua yale maumivu ya pale kifuani alipokuwa amepigwa,, salome aliingiza kichwa chake chini ya uvungu wa kitanda kwa uwoga,,
“Ole wake mtu yoyote apige kelele humu ndani tunammaliza hapahapa” alizungumza mmoja kati ya wale majambazi huku wengine wawili wikichungulia nje ambapo magari ya polisi yakiwa yanapita kwa kasi na baada ya muda kimya cha magari na vuguvugu la polisi kule nje wale majambazi walitoka mbio mbio bila kuwafanya chochote kina david.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hawa bila shaka watakuwa wametoka kufanya tukio mahali sasa wanakimbizwa na polisi”alijisemea david moyoni.
Salome baada ya kuona hali imekuwa tulivu alinyanyuka na kukusanya vitu vyake huku akijisema mwenyewe ovyo,,
“kuanzia leo mimi umalaya basi” akawa anaondoka kwa kuchanganyikiwa,,
“ Salome chukua basi pesa yako ya usumbufu” david alizungumza,
“Sitaki kaa nayo tu” alijibu salome wakati anaishia kwa kasi,
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment