Simulizi : Sahihi Ya Kifo
Sehemu Ya Tatu (3)
Ndipo mpiga debe huyo alipo ongozana nao na kuelekea kwenye stendi kubwa ya mabasi yaendayo mikoani na kuwafikisha mpaka kwenye basi la abood liliokuwa mbioni kuondoka na alipo pewa chake akaondoka zake, david alikata tiketi za watu wawili yeye na mdogo wake kisha wakaingia kwenye gari na kutafuta siti zao kwa kuuliza uliza, watu wengi walionekana kuwashangaa kutokana na muonekeno wao maana tumeshazoea kuwa kila tunaposafiri basi lazima tupendezze lakini kina david walikuwa kama vile wanakwenda shambani kwa kwa ajili ya kilimo kutokana na kukurupuka kwao.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Honi ya kujiandaa ilipigwa na baada ya dakika chacbe tu gari ikaanza kuchanja mbuga kuiacha morogoro mjini na kuelekea dar es salaam, nisha alionekana kufurahia safari hiyo maana hakuwahi kupanda gari tangu alipoanza kujitambua kwa kiasi fulani.
David nae aliegemea kwenye siti akiutafuta usingizi huku mawazo hayakuacha urafiki na kichwa chake, hakika mwendo wa gari hilo ulikuwa in mkubwa sane hata abiria waliokuwa na roho nyepesi walianza kupiga kelele kumuomba dereva apunguze mwendo lakini hata ivyo ikawa kazi bure kwao na mwendo huo ulio anzia saa mbili asubuhi mjini morogoro uliweza kuwafikisha jijini dar es saalam saa tano asubuhi hivyo waliweza kutumia muda wa masaa matatu tu mpaka kufika hapo..
Abairia wakaanza kushuka kwenye basi hilo na kulakiwa na ndugu zao waliokuja kuwa pokea,,kina david nao walishuka na kuanza kushikana mikono kwa hofu maana sifa za jiji hilo waliweza kuzisikia kupitia vyombo mbalimbali vya habari hivyo david ilimbidi awe makini kidogo, alisimama pembezoni mwagari hilo akitafakari pakwenda alipopata wazo la kutaka kutoka kwanza mle nisha alimwambia david,,
“kaka nimesahau mkoba wangu kwenye gari mle ndani”
“Aah nisha nawewe mbona mzembe hivyo?
Aliongea kwa kuchukia david maana aliona kama anamchanganya hivi ndipo alipo muacha nisha pale nje nayeye kuelekea ndani ya gari kuufuata ule mkoba, alipofika kweli alifanikiwa kuukuta sasa wakati anatoka alihisi kama amepatwa na upofu hivi kutokana na kutomuona nisha pale nje alipo muacha na kila alipo jaribu kuwauliza wale walikuwa nae karibu walimjibu hawaju pia wapo waliomtukana na kumpa maneno ya kejeli,,,
“we vipi umesikia sisi tumekuja kulinda watu hapa embu chukua time bwana unatuzingua tu hapa”
David aliweza kuwashtua watu kwa kelele alizo kuwa anapiga kumuita nisha huku akikimbia kimbia ndani ya stendi hiyo kama mtu aliye pandwa na maleria kichwani vile machozi yalimtoka lakini hakuna hata binaadamu mmoja aliye thubutu kushiriki huzuni na matatizo yalio mpata hapo la kupotelewa na dada yake.
Kule kuchanganyikiwa alitoka mpaka ndani ya ile stendi ya ubungo na kuanza kuparamia watu ovyo kumuulizia mdogo wake lakini mbuzi wa masikini hazai na kama akizaa huzaa dume basi ndicho kilicho mkuta david baada ya kumparamia mama mmoja hivi kwa ghafla na kuweza kumshtua yule ama kinywa chake kilitoa sauti,,,
“mwiziiiiiiiiiiiii huyooooooooo jaman anataka kunibia mwizi!!!!!!!!!!! Mwizi!!!!!!!!!!!!!!!”
Yale mayowe yaliokuwa yanapigwa na yule mama yaliweza kukusanya kundi kubwa la watu wenye silaha ya kila aina walio beba matofali, wengine walikuja na matairi maskini david wa watu kila alipotaka kutafuta njia ya kulikimbia kundi lile kubwa la watu nafasi alikosa kilio cha hofu kilimtokaaa
“Jamani sio mwizi mimi mnisamehe jamani tafadhalini naombeni mnielewe”
kutokana na kulalamika kwa david baadhi ya watu waliokuwa wana utu waliweza kuhisi yawezekana kweli sio mwizi hivyo wakawa wanaanza kumtetea,,
“mwacheni jamani embu tumsikilize mliona wapi mwizi aliyekuwa amekubuu analia kama mtoto msije mkauwa mtu asiye na hatia”
Wenye roho mbaya wakawa wanataka kuwajumuisha wale waliokuwa wanamtetea david,,,
“ Haiwezekani wamezoea hawa nyie huyu mwenzenu mnashilikiana nae”
Wakawa wanawavuta vuta na wale jamaa, zogo lile kubwa lilimfanya askari wa barabarani aliye karibu kusogea eneo lile na kujitahidi kuwazuia kitendo cha kutaka kujichukulia sheria mkononi
“embu subirini kwanza jamani huyu kashafika kwenye mikono ya sheria hakuna tatizo”
askari yule akawa anawatuliza raia wale wenye asila kali kisha kuuliza wakati akiwa amemshika david aliyekuwa anajitazama tazama michubuko michache aliyeipata na machozi kumtoka,,,,
“yuko wapi aliye ibiwa? Afande aliuliza
“mimi ndiye aliyekuwa anataka kuniibia” yule mama alijitokeza
“kwahiyo ajakuibia ila alikuwa anataka kukuibia? Afande alimuuliza yule mama
“ndiyo”alimjibu
Askari yule alimwangalia david na kumkuta na mkoba wa kike ameushika mkononi kisha kuuliza tena,,,,
“Na huu mkoba wa nani?
Kabla david hajajibu sauti za watu waliokuwa wanalazimisha kumtoa david kwa yule afande wakawa wanasema maneno mengi sane tofauti,,,,
“huo atakuwa kashamliza mtu huyu mwangalie macho yake yenyewe yamekaa kiwizi wizi”
“Oya mbona tunamchelewesha huyo tumuue”
Zogo likataka kuanza tena ndipo yule afande akamwambia yule mama amfuate kuelekea ndani ya stendi ambapo kuna kituo kidogo cha polisi na huko kila mmoja alitoa maelezo yake lakini ya david yalionekana kuto kusikilizwa hivyo alipelekwa mahabusu na alikaa huko kwa muda wa miezi mitatu mpaka alipotoka baada ya kuonekana upande wa mashtaka hakuna ushirikiano hivyo jarada lake likafungwa..
************************************
Mawazo mazito yaliyo kuwa yanachanganya akili na ubongo wa david yalimfanya kudhohofika sana,kiasi kwamba hata ukimtazama hutamani kurudia,mara nyingi alikuwa mtu wa kurandaranda mitaani kana kwamba kuna kitu cha thamani anakitafuta kwenye maisha yake,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
hakuna aliye jua david anasumbuliwa na nini kutokana na kukaa kimya muda wote.kipindi hicho jua lilikuwa kali sana watu wengi wa jijini dare s salaam walionekana kutembea na miamvuli na nguo zao zilikuwa nyepesi kutokana na joto,wengine waliketi kwenye migahawa wakipata vinywaji baridi kupoza koo zao, hata wasichana warembo na kina mama walipumzika ndani ya saluni waki jipamba na wengine kufanya umbea kama ilivyo kawaida ya wanawake.
Ndani ya saluni moja iliyopo manzese iliyo tambulika kwa jina la “mwanamke urembo”mwana mama mmoja aliyekuwa amevaa dela jeupe lenye nakshi zinazo ng’a akitengenezwa nywele zake huku akipiga domo ghafla alisikika
“ yesu wangu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!”
Nini tena? Madada wa mle ndani waliuliza
lakini bila kutoa jibu alinyanyuka aliko keti na kukimbilia nje huku akionekana kushangaa kila upande wa eneo lile,wale madada pia walimfuata na kumuuliza tena,
“vipi shoga mbona unatutisha? Halafu cheki unavyo hema haraka kuna nini?
“mmh acheni tu nilivyo kuwa pale kwenye kioo kuna kijana nimemuona akipita kwa nje lakini sina uhakika kama ni yeye maana david ninaye mjua pamoja na familia yake hawezi kuwa katika hali ile niliyo muona,yupo mchafu mchafu pia amekonda sana sijui amepatwa na nini?
“ Chaajabu nafika nje simuoni yani kama kumwaga maji ardhini kipindi cha kiangazi ndivyo david alivyotoweka
”
“.pole mama Victoria huenda ukabahatisha kumuona tena siku nyingine”
,wanawake wenzie walikuwa wakimpatia moyo wa kutokata tama.
Safari ile ya david ya kurandaranda mitaani alijikuta akitokea magomeni ambao walikuwa wakiishi zamani,kabla ya kuhamia gairo mjini morogoro,
bila kutegemea david katikati ya barabaraa alijikuta akisimama huku macho yake yakitazama nyumba moja ya kifahari iliyoko mbele yake
,ile hamadi gari aina ya” opa” lipo miguuni kwa david liki mpigia honi,pipipiiiiiiiiiiiiiiiiiii iliapishe barabarani lakini david hakusikia kutokana na kupigwa na butwaa kwa alicho kiona mbele yake,,,
kelele za watu zilisikika,,,,,,
“mtumeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!,mamamaaaaaaaaaa!!!!!!!mungu wanguuuu!!!!!!,”
zote hizo zilikuwa juu ya david kunusurika kugongwa na gari.hapo ndipo dereva wa gari hilo alipoteremka na kuanza kumtoa david barabarani huku akimsukuma na kumpa maneno yaliyo karaisha moyo wa david,,
“we kijana unaleta pombe mpaka barabarani au bangi zenu mnazo vuta na jua hili zina wazingua kama wazazi wako wameshindwa kukulea sisi tutakunyoosha bwege we huku akiendelea kumsukuma”
hatimaye david akadondoka chini,akawa anamtazama dereva huyo kwa hasira, alitamani kumrarua rarua kama simba mwenye njaa akimkamata swala,lakini david aliamua kunyanyuka kwa upole na dereva kuishia zake.
David aliendelea kuingalia nyumba hiyo kwa huzuni huku akiwa anasonga taratibu kuelekea pembezoni mwa nyumba hiyo ambako kulikuwa na mti mkubwa wenye kivuli na hewa safi kisha kuketi mahali hapo.
mawazo ya david yalimrudisha sikiu chache zilizopita na kuhisi kwamba mbele ya macho yake kwenye ile nyumba ya kifahari kuna watoto wawili dason na nisha ambao walikuwa wadogo zake vipenzi wakicheza juu ya nyasi zilizo ng’a kutokana na rangi yake ya kijani,
jicho lililojaa huruma na majonzi likaanza kutoa mchozi taratibu huku sauti ya chini ikisikika kugugumia
”mhmhmhmhmh”
kama unavyojua damu ni nzito kuliko maji david alishindwa kuisaliti nafsi, sauti ya david ilisikika mtaa mzima ikiita nishaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!,
hata ndege waliokuwa juu ya ule mti mkubwa waliruka na pia watu waliokuwa wakipita kandokando ya barabara shingo zao zilionekana kugeuka huku na kule kwa shauku ya kutaka kujua sauti ile ya huzuni na majonzi ilikuwa inatokea wapi
David aliendelea kulia kwa uchungu bila majina ya wadogo zake vipenzi dason na nisha kukauka mdomoni mwake.aliketi mahali hapo mpaka kiza kikaingia,alipigwa na baridi la usiku na kung’atwa na mbu,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
hatimaye david kwenye mikono ya askari waliokuwa doria usiku ule wa manane,hakuna msaada alioambulia zaidi ya kipigo kutoka kwa askari hao wakizani kuwa ni kibaka,shati lake lenye rangi ya kijivu lililowa damu hata mguu wake wakushoto uliteguka kutokana na kupigwa virungu vya ugoko,alipelekwa mpaka kituo cha polisi kilichopo hapo magomeni bila kupewa huduma yoyote ya kwanza, siku hiyo david hakulala kabisa kutokana na maumivu makali aliyo ya pata.
Asubuhi ilipofika askari waliokuwa zamu usiku ule walipeleka ripoti kwa mkuu wa kituo ikiambatanishwa pamoja na majina ya watuhumiwa hao.,Afande cris ambaye alikuwa mkuu wa kituo alipopitia taarifa hizo anakuta jina la “david kazinge” alihisi kama analifahamu jina hilo hasa la kazinge, ndipo alipo muita afande juma na kumwambia…..
”nenda kawatoe watuhumiwa wote walio kamatwa usiku na wapange foleni mara moja sawa?
“Sawa afande”,
afande juma alifuata agizo hilo bila kipingamizi alielekea mahabusu na kuwaamrisha watoke nje
“haya haya toka haraka na panga foleni mara moja huku akiwapiga na virungu migongoni”
.baada ya zoezi hilo kukamilika afande cris aliitwa nakuanza kuwatazama watuhumiwa usoni kwa makini huenda akabahatisha kumjua david kazinge,akawa anakwenda anarudi anakwenda anarudi mwishowe aliweka kirungu begani kwa kijana mmoja na kumuuliza kwa ukali,,,,,
” wewe ndiye david kazinge?
Sauti yenye kutetemeka ikiambatana na woga ilijibu,,,,,
” ndi ndio mimi afande” david alijibu
.”haya nifuate ofisi kwangu”alimueleza david
.afande cris alikuwa ametangulia na david nyuma akimfuata huku akichechemea,walipo fika ofisini afande cris aliketi, david akawa amesimama moyo wake ulikuwa na hofu kwakuwa hakujua kwanini yupo pale.
ndipo afande cris alipo muamuru kukaa,,,
” hey! david alishtuka,
“unaweza kukaa”,alipo keti akawa anamtazama afande cris atazungumza nini,,
.
“ Wewe ni mtoto wa mr.kazinge ambaye alikuwa anafanya kazi benk ya nmb? afande alimuuliza swali david
David alikubali,
Jesus Christ!!,afande alishangaa na kuuliza,,,,
“Ina maana baba yako hajatoka gerezani mpaka leo?
Bila kujibiwa aliendelea,,,,
“Kwa hali uliyonayo ni dhahiri umekosa mahitaji muhimu kwa muda mrefu”
“,kwa hiyo kwasasa mnaishi wapi wewe na family yako na imekuaje mpaka wewe kuwepo hapa kituoni?
Afande criss alimuuliza david huku akionekana kuguswa sana na hali ya david
. Macho ya david yalionekana kumwangalia afande criss kwa huruma na mdomo wake ukionekana unataka kujibu lakini aliishia kutaja,,,,
” fa, fa fa!!!!”
ghafla akadondoka chini na kupoteza fahamu papo hapo.
Afande chriss alishtushwa sana na kitendo kile ndipo alipo waita maafande wenzie kisha kumbeba kwenye gari ya polisi na kumu waisha hospitali iliyopo hapo magomeni.
*************************
Upande wa mama victoria ambaye alimuona david kule saluni, alionekana kukosa amani tangu alipo muona david,
alijikuta akifikiria mambo mengi sana hasa ukweli na siri nzito alio nayo ndani ya moyo wake, alitamani kuonana na familia ya kina david ili awaelezee juu ya ukweli huo lakini hakupata nafasi hiyo maana hakujua wapi wanapatikana,CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
baada ya kufikiri kwa muda mrefu alipata wazo la kuwatafuta bila kujua wapi anaanzia...
Upande wa mama victoria ambaye alimuona david kule saluni, alionekana kukosa amani tangu alipo muona david,
alijikuta akifikiria mambo mengi sana hasa ukweli na siri nzito alio nayo ndani ya moyo wake, alitamani kuonana na familia ya kina david ili awaelezee juu ya ukweli huo lakini hakupata nafasi hiyo maana hakujua wapi wanapatikana,
baada ya kufikiri kwa muda mrefu alipata wazo la kuwatafuta bila kujua wapi anaanzia...
Muda ulikwenda masaa yalikatika, kule hospitalini david alionekana kupata fahamu baada ya kupewa huduma nzuri katika hospitali hiyo,wakati huo afande criss alikuwa katika dirisha la muhasibu akilipia bili ya matibabu,
,saa ambayo anajirejesha hodini alimkuta david akijitahidi kujiinua pale kitandani,tabasamu lilionekana kwenye uso wa afande criss baada ya kuona hali ya david inaendelea vizuri,
ndipo alipo msogelea na kumshika kichwani huku akimwangalia usoni na kumwambia maneno ya faraja,,,
”David mwanangu pole sana ninachokuomba kuwa na amani kwenye moyo wako,
Hutorudi tena kituoni tutaenda kuishi wote sawa”? David alitingisha kichwa kukubali.
Afande criss alipomaliza tu kuongea sauti ya dokta ilisikika,
”Unaendeleaje david”?
”Nzuri tu dokta namshukuru mungu,”
Baada ya mazungumzo na david dokta akawa ana ongea na afande criss,
”Afande,,.mgonjwa wako hana tatizo kubwa ila kilichokuwa kina msumbua ni msongo wa mawazo yaliyo ambatana na njaa ambayo yalipelekea mzunguko wa damu kuwa mdogo ndio maana alipoteza fahamu hivyo chukua cheti hiki ukanunue hizi dawa zita msaidia na sasa mnaweza kwenda.dokta alitoa ruhusa.
Bila kupoteza muda safarari ya kuondoka ikaanza wakiwa na gari ile ya polisi,afande cris alimpeleka david hotelini kisha kumpitisha dukani na kumnunulia nguo kadhaa za kuanzia,
Walifika mabibo external ambapo afande cris alikuwa akiishi,
David alkaribishwa vizuri nyumbani kwa afande cris lakini ukimya wa nyumba hiyo ulimfanya david kuuliza,,,
”mkeo na watoto zako wako wapi?
Afande cris alitabasamu kidogo kutokana na swali ambalo david amemuuliza kisha kumjibu,,
”tume tengana muda mrefu sasa na hapa naishi mwenyewe tu kwakuwa na wewe upo basi angalau nyumba itakuwa imechangamka”
David alionekana kutoamini ukarimu alio kuwa ameoneshwa na afande cris kwa muda mfupi,
Alitaka kumuuliza maswali mengi zaidi lakini alikumbuka usemi wa baba yake kuwa
”usimuamini yoyote yule pia penda kuwa mtu wa kusikiliza na kusema kidogo tu ili upate kujua mengi zaid.”
Hivyo david akafunga kinywa chake na kuendelea kusikiliza afande criss akizungumza tu;
********************************
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mwaka huo ulikatika na david akawa amesha mueleza afande criss yote yalio mkuta na juhudi za kumtafuta nisha zikawa zinaendelea ila hakumwambia swala la ushahidi kuhusu mwanamke ambaye baba yake alimwambia akifika mjini amtafate na afande criss kumuahidi kuwa atakuwa nae bega kwa bega mpaka atakapo fanikiwa kupata mali zake,,
Siku moja ya mapumziko mishale ya saa mbili usiku wakati taarifa ya habari inatangazwa waziri wa elimu alitangaza kuwa matokeo ya kidato cha sita sasa yapo hewani na kiwango cha ufaulu kimeongezeka kwa asilimia 65 toka yale ya awali yalio kuwa na asilimia43,
Taarifa hizo zilimshtuwa sana david maana na yeye alikuwa anahusika katika mtanange huo
Hivyo afande cris naye hakuchelewa akaenda kuchukua laptop yake na kuanza kutafuta namba ya mtihani ya david ambayo alimueleza tayari,
Nyuso za furaha zilionekana usoni kwa kila mmoja baada ya kuona matokeo ya david kuwa amefaulu kwa kupata daraja la pili hasa yale masomo yake ya sayansi,
Lakini ghafla tu furaha ya david ilikatika na afande cris alimuuliza,,,,
”vipi david hukuridhika na daraja ulilo pata? Swali hilo david hakujibu na mchozi mwembamba ukaanza kumtoka,
Afande criss ilibidi amuulize tena,,,
”David mwanangu tatizo nini embu niweke wazi basi?
Ndipo alipo nyakuwa kinwywa chake na kusema,,,,,
”nafanikio haya madogo nilitamani wangekuewepo familia yangu hapa lakini sina jinsi”’
Afande cris alizidi kumpa maneno ya kiume david na kumueleza jumatatu wataenda morogoro mpaka gerezani alipo mzee kazinge na atapata kuzungumza naye david jicho lilimtoka------------
Ile siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu ya kwenda kijijini kwa kina david ikawa imewadia, david alionekana kubadilika kutokana na siha nzuri ya uso aliokuwa nao kutakata na maji yale ya chumvi ndani ya jijini lenye kila aina ya ufuska na wingi wa watu jiji la dar es saalam,
Afande cris kazi yake ilikuwa kuachia tabasamu tu kwa david maana alikuwa kanyonga tai ya kiuutuuzima shati lake la mikono mirefu renye rangi ya zambarau lilijitosheleza vizuri ndani ya suruali ile nyeusi achia mbali kile kizibao kilichoendana na rangi ya suruali,
Nywele zake alizofuga kiasi na kuzitana vizuri zilizidi kung’aa hasa kutokana na mafuta maalumu kwaajili ya nywele, hakika shida ndizo zilizo kuwa zinauficha ushababi wa david lakini kwa hali ya sasa hakuna mwanamke ambaye akaambiwa lugha ya ushawishi wa kimapenzi akakataa kwanza ni lazima huyo mwanamke atapata uwoga kwa kutojiamini kusimama na david,
Afande cris na david waligonisha matabasamu yao kisha kupanda kwenye ile mazda yenned namba za usajiri Tz6210, kisha mafuta kukolezwa safari kuelekea morogoro, foleni ile ya pale maeneo ya kimara mpaka mbezi kwa msuguli iliwapotezea kama dakika 45 hivi walipo imaliza mazda ikawa imepamba moto,,
Injini ya gari ile iliweza kuwatunzia heshima yao kwa kutowasumbua njiani mpaka walipo kuwa wanaingia kwenye ardhi ile yenye sifa ya kuwa na udongo mwekundu na kunyimwa bahari, hiyo ni ndani ya milima ya uluguru Morogoro
Hapo morogoro mjini waliweza kupumzika kwenye bar moja inayoitwa makuti
Kupata vinywaji na chakula kupoza njaa kidogo baada ya kuwa wametembea njiani kwa muda usio pungua masaa matau hivyo walikuwa wanatoa uchovu wa safari hiyo,
Wahudumu waliokuwa wana wahudumia walitamani kwenda kwenye meza hiyo mara kwa mara kutokana na mvuto wa david japo mwenyewe aliweza kujua kuwa wasichana hao walikuwa wanajigonga gonga kwake lakini kwa upande wake hakujali yani kama moyo wake wa upendo ulipigwa kufuli na matatizo yalio kuwa yana muandama kwa muda mrefu,
Hapo ilikuwa sio mwisho wa safari walikuwa na saa moja na nusu hivi mpaka kufika gairo kijijini kwa kina david hivyo walivyo maliza kula na kunywa mazda ikawashwa upya na kuchukua barabara inayoelekea dodoma ili waweze kufika gairo eneo maarufu kwa ulimaji wa viazi vitamu,
Ndani ya saa saba na mchana wakawa wapo ndani ya kijiji cha gairo, watu wengi walianza kulishanga lile gari lilikuwa linaelekea nyumbani kwa kina david maana palionekana kuwa kimya kwa muda mrefu sana, majani mengi yaliota kuzunguka ile nyumba ambapo ilikuwa in dalili tosha kwamba kulikuwa hakuna mtu,
Jambo hilo pia lilimshangaza david sana yani, hakujua kwa nini pale nyumbani pako vile,iliwabidi washuke haraka na david akaanza kugonga lile geti,,,,,
“mzee nyomolage, mzee nyomo lage!!!!!!!!!!!!!!!!!!!, lakini kimya kilizidi na mwangi ndio uliokuwa unamjibu kama yeye alivyokuwa anaita,
Lakini punde tu kuna mmama mmoja hakuwa mbali na pale akawa anawapigia kofi kama ishara na kuwaoneshea mkono kama ishara ya kuwaita, afande cris alimtazama na david kisha wakaelekea kule alipo yule mama,
Walivyofika yule mama aliwaomba waelekee nyumbani kwake ambako kulikuwa si mbali sane na pale na huko aliwakalibisha na kuanza kuzungumza,,,,
“david baba yani mmekuwa maarufu kijiji kizima hakuna asiyejua habari zenu ,hakuna asiyetoa chozi kwa ajili yenu kila mtu anawa hurumia nyie!!!!!!!
Maneno hayo bado yakawa yanamuweka katika wakati mgumu sane david na afande criss walishindwa kumuelewa yule mama alikuwa ana maana gani ilibidi david ambembeleze azungumze kitu ambacho wanaweza wakamuelewa,,
“mama tafadhali in yale yale au kuna mengine yametokea maana hali ya nyumbani kwetu sijaielewa!!!, wakati naondoka tulimuacha mzee yomolage pale nyumbani lakini tunafika kuna onesha hakuna dalili zozote zile za kuwepo na mtu wala vitu ndani kwa kuwa ule mwangi nilikuwa nausikia kama vile nyumba ipo tupu nakuomba mama tueleze ukweli mzee nyomo lage yuko wapi?????
David sasa hali ikaanza kubadilika kwake na machozi kuonekana kulenga lenga kwake hapo afande cris kama mtu mzima naye alichukua nafasi ya kuzungumza na yule mama iliawaeleze hali halisi iliyo tokea ndipo yule mama ikabidi awaeleze kilichotokea,,,,,
“ilikuwa ni siku moja ililyokuwa na mvua kiasi ambapo watu wengi walikuwa wakipishana kuikimbia mvua ile kuelekea ma kwao nami nikiwa mmoja wao niliyekuwa naikimbia ile mvua kuja nyumbani kwangu, sasa wakati na pita nilisikia kelele mle ndani kwenu zikijibizana na sauti niliyoweza kuitambua ni ya mzee nyomolage ikilalamika kujibu maswali ila ile iliyokuwa inauliza sikuweza kuitambua,,,,,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“watoto wa alfred wako wapi wewe mzee eeh? Kunamtu alikuwa anauliza kwa ukali sane
“Sijui mimi jamani walipoenda, nimewatafuta sana kila kijiji lakini sikuwapata na ukweli sijui watakuwa kijiji gani kwa sasa” mzee nyomolage nilimsikia akijibu swali hilo kwa sauti ya machozi tena nikasikia sauti za watu wengine zikimuuliza swali hilohilo la kuwaulizia nyinyi,,
Ghafla niliwaona watu ambao walikuwa wamejazia wasio pungua watatu na mmoja aliyekuwa amvaa suti na miwani ya kitanashati wakitoka mle ndani na kupanda kwenye gari kisha kuishia punde tu alitoka mzee nyomolage na kutimua mbio kuelekea kusiko julikana mpaka leo hii hatuji kama mzima au amekufa,
Wanakijiji ambao nao walipata kuliona tukio hilo kwa mbali kama mimi niliye jibanza kwenye mti kushuudia tukio hilo tuliaandamana mpaka kwenye serikali ya kijiji na kutaka swala hili lifatile kisheria kuna tatizo gani mpaka familia hii inyanyasike kiasi hiki na yote hayo yalibebwa na tukio zito ambalo tulipata kusikia kwamba na baba yako mzee kazinge amefariki huko akiwa gerezani na kuzikwa na serikali baada ya kukosa ndugu,,
hicho ndicho kilichotokea yani mungu ashukuliwe kuwaepusha wewe na nisha katika tatizo hili yawezekana kizazi chenu kingeishia siku ile kama nanyi mngekuwepo,,
***********************
Maneno hayo yalimfanya afande criss alijisikia aibu sana kwakuwa na yeye in mmoja katika vyombo vya dola na baada ya david kushikwa na hasira na kulalamaika kwa kilio ambacho alikuwa anailaumu serikali nzima.,,
Afande cris alizungumza na yule mama na kushukuru kwa ujumbe ambao walimpatia kisha kumbembeleza david anyamaze iliwajue wanaanzia wapi kulifatilia tatizo hilo,,
Baada ya kuwaza na kuwazua afande alitoa wazo waende kwanza shuleni kwako alikosoma david wakachukue vyeti vyake vya form six lakini kabla hawajaelekea huko afande alimuuliza swali yule mama,,
“sasa mbona na ule mlango umefungwa in nani aliyeufunga na wakati mzee nyomolage alikimbia?
“ni mimi ndie niliyempa kufuli mwenyekiti alipokuja kuhakikisha na serikali ya kijiji baada ya kusikia mzee nyomolage amekimbia hivyo funguo zingine ni nazo mimi kama mnazihitaji naweza kuwapatia” afande cris alizihitaji ili wakaangalie usalama wa mle ndani,
Zoezi hilo lilifanyika wakawa wamekwenda mle ndani na kwa bahati nzuri vitu muhimu walivikuta kama vile picha na vyeti vya kidato cha nne vya david na walikwenda shule wakapatiwa vyeti vya kidato cha sita na siku hiyo wali lala kwa huyo mama na asubuhi yake safari ya kwenda gerezani kutaka kujua kilichomuua mzee kazinge ni nini na swala hilo afande cris kuahidi kuwa atalifatilia-
Ndami ya david alikuwa anaona kama wanachelwa vile kufika kule gerezani, mawazo ya hasira yalikuwa yanakuja kichwani mwake juu ya afande criss kuona ndio wale wale tu kama maaskari wengine, uso uliiva kwa hasira kila akifikiria matukio yaliokuwa yanaongozana,afande crss nae alisha gundua gadhabu anayo ipata david kwa wakati ule hivyo alijitahidi kuendesha gari hilo kwa mwendo kasi mpaka lilipo wafikisha salama kwenye kwenye gereza alilokuwa amefungwa afande mzee kazinge,
Walifika getini na kufuata utaratibu wa kujiandikisha jina lako, mahali unapoishi na mtu unayekwenda kumtazama,. Swala hilo halikuwa gumu kwako, walijiandikisha lakini ujanja alioutumia afande criss ulikuwa wahali ya juu sana alimnong’oneza david sikioni kisha matokeo ya yale aliyo mwambia kwa siri yalikuwa ni haya,,
Kwakuwa afande criss alikuwa in mtu mzima pia hakuvaa kipolisi alikwenda kama raia wa kawaida hivyo yeye aliandika anakwenda kwa mkuu wa gererza na divid aliangalia jina moja la juu baada kama ya majina matano hivi akaliandika kuwa anakwenda kumuona mtu yule kumbe hata kumjua hamjui ila lengo lilikuwa in kutaka kuonana na wafungwa angalau anaweza akapata chochote kitu juu ya kifo cha baba yake..
Kwakuwa afande criss alikuwa in mtu mzima pia hakuvaa kipolisi alikwenda kama raia wa kawaida hivyo yeye aliandika anakwenda kwa mkuu wa gererza na divid aliangalia jina moja la juu baada kama ya majina matano hivi akaliandika kuwa anakwenda kumuona mtu yule kumbe hata kumjua hamjui ila lengo lilikuwa in kutaka kuonana na wafungwa angalau anaweza akapata chochote kitu juu ya kifo cha baba yake..
Walivyo maliza wote walitoka kwa pamoja na kila mmoja alikwenda kwenye upande wake lakini afande alizi kumsisitiza david awemakini katika uulizaji wake, na yeye alikwenda kuonana na mkuu wa gereza na maongezi yao yakaanza baada ya kuwa amefika ndani ya ofisi,,,
“habari ya kazi mheshimiwa? Afande criss alimsalimia yule mkuu wa kituo
“salama tu habari yako na wewe?
“Namshukuru mungu niko salama:” afande criss alijibu
“Mmmh nikusaidie nini? Ule mkuu wa kituo alimuuliza afande criss
“mheshimiwa mimi ni ndugu yake na marehemu alfred kazinge ila sikuwepo hapa nchini kwa muda kidogo na nimekwenda nyumbani kwake kule gairo sikufanikiwa kuikuta hata familia yake zaidi ya kukuta makaburi mawili la mwanane na mkewe na taarifa za majonzi ambazo zimenifanya nije hapa hivyo nilikuwa napenda kujua ndugu yangu alikufa kwa ugonjwa gani na wapi alipo zikwa”
Jicho lilimtoka yule mkuu wa kituo na kuanza kukuna kichwa akitafuta jibu la kumpatia afande criss na baada ya kujishauli kwa muda kidogo aliweza kumwambia ,,,
“kwanza pole sana kwa msiba ulio kupata na hata hivyo kifo chake kimetuhudhunisha sana hapa gerezani alfred alikuwa na ucheshi sana kila mmfungwa alikuwa nanamtania lakini kumbe ucheshi huo tulishindwa kuutambua mapema kuwa alikuwa ameanza kuchanganyikiwa mpaka siku moja walipo kuwa wanafanya usafi mdogo wa gereza hili kulimalima na kufyeka majani alijaribu kuchukua kifaa kimoja na kutaka kujiua lakini wenzie walimuwahi na kumpeleka gerezani na baada ya siku tatu hivi alikutwa amekufa pembeni ya pembeni ya kuuta wa gereza ambapo wenzio walikuwa wanalima na uchunguzi wa polisi ulipofanyika tuligundua kuwa amekufa kwa sumu na wala hatujua aliitoa wapi naa kuuamua kuinywa hivyo ndivyo tulivyo mpoteza alfred kazinge”
Pumnzi ndefu ilishuka kwa afande criss na kumwangalia yuke mkuu wa gereza aliyekuwa anajiangaisha pale kwenye kiti huku akionekana akili yake haipo sawa na kisha kumuuliza tena,,,,,
“Na alizikwa na nani?CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Serikali ndio ilimzika baada ya kuwa hakuna ndugu hata mmoja aliyekuja”
Kwa maelezo aliyo sema yule mkuu wa gereza na kutokana na uzoefu wa kazi yake ya kipolisi afande criss aliweza kugundua kuwa kuna kitu kinafichwa pale basi hakutaka kupoteza muda alimshukuru yule mkuu wa gereza na kumuaga kuwa anaondoka basi walipeana mikono kisha afande criss kutoka nje,.
Na upande wa david yeye alilitumia jina lilelile ambalo aliiandika kwenye kile kitabu na kuitiwa yule mfungwa mwenye jina la frank mgaya ambaye au kwa jina lake la utani walikuwa wanamuita sir/side in kutokana na ucheshi aliokuwa nao. Na kuanza kuonge nae,,
“samahani sana kaka najua hunijui na wala mimi sikujui lakini niliweza kupata jina lako pale kwenye kitabu cha wanao wasili na ombi langu kubwa ambalo kama utanisaidia basi mimi kuanzia leo nitakuw anakuja kukusalimia na kukuletea chochote ambacho utakuwa uanataka kutoka nje” david alizungumza,
Yule jamaa frank mgaya aliposikia maswala ya kuleteana vitu hakutaka kulemba akijiweka vizuri kutaka kusikiliza hilo jambo amabalo anataka kuambiwa na david ndipo alipomuuliza,,,
“ namjua alfred kazinge ambaye sasa in marehemu?
Frank kabla hajajibu alikuwa kama amelisahau jina hilo hivyo akawa kama nanjaribu kulikumbuka hivi ndipo na yeye akamuuliza swali david iliapate uhakika,,,,
“umesema kuwa sasa in marehemu?
“ndiyo” david alimjibu na ndipo yule mfungwa frank alipokuwa amekumbuka na kumwambia,,
“aaah nimekumbuka ungesema Bob “k” ndio jina mbalo kila mmoja alikuwa analijua hapa kutokana na kule kudata kwake na mambo aliyokuwa anayafanya kwani wewe nani yako? Frank alimuuliza david
“ni baba yangu mzazi”
“Sasa rafiki yangu ulikuwa wapi mpaka baba yako anakufa kinyama na kuzikwa na wafungwa kama vile mbwa yani dah kiukweli bob k alichofanyiwa lilikuwa sio jambo la kiuungwana kabisa wengi walishuhudia tu mazishi yake lakini wachache ndio ulishuudia kifo chake na mimi in kiwepo yani kama unamungu sana kukutana na mimi yani” frank alimwambia david na david sasa akaa mkao wa kula kusikiliza kilicho tokea baada ya kumuiliza ilikuwaje,,,,,,,,,,,,
“siku moja tulikuwa tumetoka kumaliza usafi tukawa tuna kula na ukweli mzee wako alikuwa ameanza kuchanganyikwa bila watu wengi kujua kwakua alikuwa anaucheshi sana lakini hata hivyo kuna baadhi ya mambo alikuwa anayafanya lazima mtu ushtuke kidogo kuwa huyu mtu hayupo sawa
sasa tulipokuwa tunaendelea kula tukaona kuna watu kama wanne hivi wamekuja mmoja akiwa mevaa suti nyeusi na wengine walikuwa wamejazia jazia hivi na bob k yeye alikuwa amejitenga na sisi ambao tulikuwa karibu na eneo lile lakini ili kuwa si rahisi kutuona, basi wale jamaa walionekana kuelekezwa na askari alipo kuwa bob k na wakafika mpaka pale na kumzunguka wakijifanya wanacheka nae kumpa mikono ilikutengeneza uhalisia wa udugu,
lakini bob k alipigwa na butwaa kumuangalia yule jamaa aliye kuwa amevaa suti nyeusi kisha kujipiga piga kichwani kulazimisha kukumbuka kitu, wakati tukio hilo la bob k kupigwa na butwaa mmoja kati ya wale akatoa kitu kwenye koti lake na kuweka kwenye chakula cha bob na mwingine akampiga na gazeti kichwani na kuliacha pale kisha kuondoka zao na baada ya muda tu ndipo tuliposikia bob k amefariki dunia na ukweli hakuna hata mmoja aliyejitokeza kufuatilia swala hili ila nimeshangaa sana unasema wewe mwanae na ulikuwa wapi siku zote?
“Nilikuwa shuleni”: david alimjibu kwa mkato na kuonekana kutafakari jambo hivi kisha kumuuliza tena yule mfungwa,,
“hilo gazeti liliandikwa nini”
Kiukweli mimi sikufanukiwa kuliona ila waliokuwa zamu kufanya usafi kule kwenye ofisi ya mkuu wa gereza waliliona na kuja kusema kuwa bob k alikuwa na matatizo sane ya kumpoteza mkewe sijui nini mambo mengi sana si alikuwa nakaa gairo?
“ndiyo”
“Basi mle pia waliandika baada ya washkaji wengine waliokuwa wanatokea huko kulala mika kuwa wamempoteza ndugu yao wa kutoka kijijini kwako”
Wakati maongezi yakiendelea muda wao ukawa umeisha hivyo yule mfungwa alirudishwa gerezani na david alimpatia dole kuwa usijali tuko pamoja kisha david kuondoka na alipofika nje alikutana na afande criss wakawa wanaelekea kwenye geti kubwa la kutokea nje lakini wakati wanaenda afande criss aligundua kuwa amesahau funguo npale kwenye meza ya mkuu wagereza ilimbidi arudi moaka kule na alipo fika mlangoni alimsikia yule mkuu wakituo akiongea na simu iliyomshtua afande criss-Baada ya kusikia manane haya,,,,,,
“ee bwana ule mpango umeharibika kuna,,,,,,,!!!!!!!” wakati hajamalizia kusema kuwa kuna nini kuna askari alikuwa anapita pale nje alihisi kama afande cris ametega sikio ndipo alimpomhtua kwa kumwambia,,,,
””nikusaidie nini mzee wangu?afande criss alijiumauma na kusema,,,,
“asanate sana kjiana naingia humu sema nilisahau in mlango gani hivyo nikawa anafananisha hii sauti lakini sasa nimegundua kuwa ni humu ninakotakiwa kuingia”
Yule askari alistupa macho yake juu ya mlango wa mkuu wa gereza na kukuta kibao kimeandikwa “ofisi ya mkuu wa gereza” kisha akarudisha macho yake kwa afande criss ambaye naye hakutaka kupoteza muda akausukuma ule mlango bila kubisha hodi na kuingia mle ndani,
Mkuu wa gereza aliposikia mlango wake unafunguliwa alikata ile simu haraharaka na kujifanaya anatafuta baadhi ya nyaraka pale juu ya meza yake na afande criss naye akajifanya kama hakusikua hata neno moja ambalo lita mfanya ajaue pakuanzia. Alimuomba ladhi yule mkuu wa gereza kwa kuingia bila kubisha hodi na kuchukua funguo zake na kutoka zake huku akiwa na jambo kichwani na kumuachia maswali yule yule mkuu wa gereza aliyokuwa anajiuliza na kujipa majibu yasio kuwa na uhakika,,,,
Alitoka njee kabisa na kuungana na david kisha kuanza safari ya kuelekea ndani ya jiji la dar es salaam. Ndani ya gari walitumia umbali huo mpaka kufika dar es salaam kwa kuambizana kila mmoja alichokipata walivyo jigawa iliwajue wapi pa kuanzia,
Maelezo ya david yalimpa afande criss uwanja mkubwa sane wa kufikiria nini afanye ili wa weze kukamilisha ushahidi bila ya kujua kuwa kuna mtu ambeye david alimsikia kuwa anaushahidi ambao ungeweza kuwasaidia lakini naye pia hakusema jambo hilo kwa afande criss akihisi asije akamfanyia kama yale ya aliyofanyiwa marehemu baba yake na helman,
Safari ilizidi kunoga kwa kila mmoja kutoa wazo lake juu ya swala hilo mpaka walipofika jijini na moja kwa moja gari ilianza kukataa mitaa na kuelekea nyumbani kwa afande criss, kila mmoja alikuwa amechoka kutokana na uzito wa jambo hilo akifikiria ni wapi pakuanzia maana kama utakurupuka unaweza kufungwa wewe ndivyo afande criss alivyokuwa anawaza,,,
Afande criss alimuangalia david ambaye aliyeonekana kuchoka zaidi hasa kwa mawazo ya jinsi babaye alivyo uwawa kikatili na kuzikwa kama mbwa lakini hakuna mtu aliye jali wala kufatilia swala hilo ndipo afande criss alipo mwambia david ampatie vile vyeti vyake vya form four na form six kisha akaanza kuviangalia kwa makini na kugundua kuwa katika somo la hesabu pia david alifanya vizuri amabalo linaweza kumpa fursa ya yeye kusomea kitu ambacho yeye alikuwa anakifikiria ilikiweze kuleta urahisi katika uchunguzi wake,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Afande cris alimuita david ambaye alikuwa mbali kimawazo na kumwambia,,,,
“david kuna wazo nimelipata!”
“Lipi hilo? David aliuliza na kukaa mkao wa kula
“embu somea shahada ya mambo ya kibiahara”afabde criss alimwambia, lakini david alionekana kupinga
“kwa nini afande mimi nina ndoto zangu za kutaka kuja kuwa daktari bingwa wa moyo iliniuma sane mama yangu alipokufa kwa ugonjwa huo hivyo inanibidi nisomee udaktari ilinije kushuhudia mgonjwa anakufa kwa ugonjwa wa moyo mbele yangu, mimi siwezi kusome hayo maswala ya kibiashara afande” david alikataa katakata lakini afande criss ndipo alipoamua kumuelewesha na kumfafanulia vizuri zaidi,,,,,,,,,
“david sikia in kwambie kumbuka kuwa baba yako alikuwa anafanya kazi benk maana yake alisomea maswala ya kibiashara hivyo na marafiki wake wengi in lazima watakuwa in wafanya biashara hata matatizo yake yametokana na fedha za benki ambazo in za biashara kwa hiyo sasa wewe ukisomea maswala hayo in rahisi kuwajua watu wengi waliokuwa wanafanya biashara na baba yako, matajiri wengi utawajua na huenda huko ukapata wapi helmani anapatika na nina uhakika yeye kukukumbuka sio rahisi kwa kuwa umekuwa sana na mpaka utakapo maliza masoma yako utazidi kuwa mbaba na mimi nitakuwa nimepata baadhi ya vitu katika uchunguzi wangu umenielewa?’
David alionekana kufikiria swala hilo na kuona limemuingia akilini na kuona kweli linaweza kuwapa nafasi ya pakuanzia na urahisi wa kumjua helman anapopatikana, hivyo david alikubaliana na ushauri wa afande criss, na afande criss alinyanyuka alipoketi na kumpiga kofi la pongezi begani kwake kisha kuelekea chumbani kwake,,
Baada ya siku kadhaa kukatika afande criss kumbe alifanya mawasiliano nchi moja ya jirani hapo rwanda na nakupata chuo cha kibiashara ambacho ndicho alichoprndrkrza david akasome na david alikubali hilo na mipango ya safari ikawa imeandaliwa na david akaelekea huko na atakaa kwamuda wa miaka minne bila kurudi nchini tanzania,,
Chuoni huko david alipokelewa vizuri na baadhi ya wanafunzi wa kirwanda ambao kiswahili kwao ilikuwa ni tatizo kidogo na gata kama wakizungumza kuna utoauti na watanzania hivyo wengi wao walipenda kuzungumza kingereza na lugha ya kwako,
Maisha ya david yalianza kubadilika chuoni hapo baada ya kumpata rafiki mmoja wa kiume alieitwa gozbety lakini yeye alikuwa anapenda kujiita gozbety CT 234 ambaye ni mwenyeji wa hapo hapo rwanda, siku moja walipokuwa wanapata chakula cha mchana katika mgahawa wa hapo chuoni kwako na kupeleka kufikia katika mazungumzo yaliomfanya david kushikilia kijijo cha chakula kwa muda kidogo bila kukipeleka mdomoni Baada ya kumuuliza,,,,,
“kwanini unajiita gozbety CT 234? Gozbety alimwangalia david kwa makini sana kisha kumueleza,
Maisha ya david yalianza kubadilika chuoni hapo baada ya kumpata rafiki mmoja wa kiume alieitwa gozbety lakini yeye alikuwa anapenda kujiita gozbety CT 234 ambaye ni mwenyeji wa hapo hapo rwanda, siku moja walipokuwa wanapata chakula cha mchana katika mgahawa wa hapo chuoni kwako na kupeleka kufikia katika mazungumzo yaliomfanya david kushikilia kijijo cha chakula kwa muda kidogo bila kukipeleka mdomoni Baada ya kumuuliza,,,,,
“kwanini unajiita gozbety CT 234? Gozbety alimwangalia david kwa makini sana kisha kumueleza,
“david rafiki yangu jina hili lina silinzinto sana ambayo inazidi kuniumiza na kunifanya kuwa mkiwa kwa muda sasa na hapa nikimaliza masomo yangu nitaelekea tanzania huko kuna baba yangu mdogo ni tajiri sana na ana makampuni yake ya kibiashara pia nitasikitika kukuacha hapa chuoni rafiki yangu nilitamanikama wote tungekuwa tunamaliza mwakani lakini wewe bado unamika miwili mbele lakini usijali ukifika tanzania tutatafutana tu”
Maneno hayo yalikuwa yanaongelewa kwa lugha ya kingereza na kuchanganya na kiswahili kidogo yaliendelea kuwapotezea muda hapo mgahawani lakini david alikuwa na shauku ya kutaka kujua kwanini anajiita CT 234 ndipo alipo muuliza tena,,,,
“gozbety hujaniambia kwa nini unanjiita jino hilo bado na lina siri gani?
Gozbety alicheka na kumwambia mbona unaonekana unashauku ya kutaka kujua sane david?, usijali nitakwambia tu rafiki yangu japo sijawahi kumwambia mtu yoyote yule kwenye maisha yangu hata mpenzi wangu mwenyewe hajui ila“Ninachokuomba iwe siri yako maana kama huyo baba yangu mdogo akijua kuwa nimemueleza mtu juu ya siri la jina hili anaweza kunifanya kitu kibaya kwa kuwa si baba yangu mdogo wa kuzaliwa na baba yangu hapana, ila nimetokea kumuheshimu kutokana na baba yangu mzazi kufanya kazi kwake kwa muda mrefu japo mwanzoni sikujua kuwa wanafanya kazi gani kutokana na umri wangu kuwa mdogo lakini baada ya kukua na kujitambua nilielezwa na watu kuwa baba yangu alikuwa anafanya kazi ya ujambazi na akakamatwa huko tanzania,
“Lakini siwezi kuamini maneno ya watu sana na kuacha kumuamini yule aliyekuwa karibu na baba yangu na kufanyanae kazi kwa muda mrefu maana yeye alinimbia kuwa walikuwa wanafanya biashara yakuuza magari yaliokuwa yamesha tumika kwa muda mchache na kuyauza kwa watu hivyo baba yangu kazi yake ilikuwa ni kuyasambaza sehemu mbalimbali,
“Siku moja baba yangu alipokuwa anajiandaa kutaka kuyasafirisha magari bandalini ndipo polisi wakazingira nyumba yake na kuingia ndani kuanza kukagua na hatimaye walikuta bunduki kama tano hivi na risasi kazaa hicho ndicho kilicho msababisha akamatwe, na nilipomuuliza baba yangu huyo mdogo zile bunduki zilitoka wapi aliniambia kuwa kuna rafiki yao mmoja ambaye alikuwa nafanya kazi benki ndiye aliyetuma watu kuzipeleka pale baada ya kushindwana bei katika gari moja zuri aina ya masidinzi benzi na kutoleana maneno ya kashfa mbele za watu hivyo rafiki yao yule hakupenda kuzalilishwa mbele za watu akaamua kumuabisha kwa aina hiyo ili baba yangu aonekane jambazi
“na kuhusu jina hili la CT 234 nimeliweka kama kumbukumbu ili hata watoto wangu watakapo zaliwa waweze kukumbuka kwa urahisi maana litakuwa linatamkwa na wengi bila ya watu hao kujua lina maana gani, hii herufi C ni jina la baba yangu mzazi lina maana ya Cholo na T ni Tanzania na hiyo namba 234 ni namba ya usajiri ya ufungwa wa baba yangu huko tanzania, hivyo ndivyo nilivyo amua kuweka kwamfumo huo hata watoto wangu wakiulizwa huko baadae watasema” babu yetu alikuwa anaitwa cholo alifungwa tanzania kwa namba yake 234 hivyo ndivyo nilivyo amua kuweka”
“baba yangu aliweza kufungwa tanzania japo ni raia wa rwanda ni kutokana na huyo baba yangu mdogo kufanya mipango ya kumsajili kama raia wa tanzania kwa kuhonga pesa haraka haraka ili kesi isiwe kubwa na isiweze kumuingiza na yeye kama jambazi kwa kumuajili raia wa rwanda bila kibali chochote kile.
“Kiukweli rafiki yangu david inaniuma sana kila nikikumbuka alichofanyiwa baba yangu na huyo jamaa wao wa benki nilitamani kumjua japo jina tu lakini baba yangu mdogo hakuniambia kwa wakati huo alinificha kutokana na jazba niliyokuwa nayo ambayo ingenipelekea kushindwa kusoma na kudili kumfanyia kitu kibaya jamaa huyo yeye na familia yake maana imenifanya nimeishi maisha ya bila baba kwa muda mrefu,,
Gozybety alipomaliza kueleza siri ya jina lake kwa david alishangaa kumuona david jicho limemuiva na kuwa jekundu mchozi mwembemba ukimtililika huku misuli ya kwenye mikono yake ikiwa imekaza kama mtu anayejiandaa kupigana lakini alijitahidi kujizui kuonesha fadhaa yake pale baada ya kukumbuka maneno ya marehemu baba yake yaliokuwa yanasema….
“utulivu wako ndio utakao kufanya ujue mengi na kuzipata mali zako”
Japo alijitahidi kujizuia lakini jina la cholo ndilo lilikuwa linaelea ndani ya kichwa chake maana analijua vizuri ni mmoja wa watu walio panga mpango wa baba yake kufungwa kwa mara ya kwanza na ndio matatizo mengine yakaanza kuongozana lakini alicho ambiwa na gozbety kuhusu kufungwa kwa baba yake mzazi cholo, anaona kinataka kumuangamiza yeye na wakati waliofanya ubaya ni wao,CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
akafikiri kwa muda na kutaka kujua huyo baba yake mdogo wa tanzania ni nani ili apate uhakika juu ya cholo anayezungumziwa yule ambaye alikuwa anashirikiana na adui yake mkubwa helman ambaye amemfanya mpaka kupoteza ndoto zake za kuwa daktari na kusomea maswala ya kibiashara ili ampate kwa urahisi au mwingine?
Alipokuwa anataka kumuuliza Gozbety jina la baba yake mdogo huyo wa tanzania walikatishwa na mayowe yaliokuwa yanapigwa na wanafunzi hapo chuoni wakilalamika kuwa bweni la wasichana linawaka moto,
wote walikurupuka na kwenda kusaidia huko, watu walionekana kuchanganyikiwa,wengi walikimbia mahali pasipo julikana wengine walikuwa wanataja majina ya watu waliokuwa wapo ndani ndipo gozbety aliposikia jina la mpenzi wake ambaye alikuwa anaitwa Segito kuwa yupo ndani na moto unazidi kuongezeka,
Nguvu ya mapenzi ikamsukuma gozbety kukimbia na kuingia mle ndani ya bweni ili ikiwezekana amuokoe mpenzi wake lakini kwa bahati mbaya alizidiwa na moshi mle ndani alipoteza maisha na hiyo baada ya kuwa uchunguzi umefanyika na kugundua kuwa katika watu sita walioaga dunia na ajali hiyo ya moto mmoja alikuwa ni mwanaume aliye kwenda kuwasaidia ambaye alitambulika kwa jina la gozbety,
Kifo cha gozbety kilichukua sura mpya kwenye moyo wa david maana alikuwa bado anahitaji kujua mambo mengi sana kupitia yeye hasa kutaka kuhakikisha kuwa helman ndiye baba mdogo wa gozbety?
Taratibu za mazishi zilifanyika kwa wanafunzi waliopoteza maisha na ajali hiyo ya moto, wageni wengi walihuzulia msiba huo akiwemo rais wa nchi hiyo paul kagame akiambatana na wanae, msiba huo ulihuzunisha wengi sana maana ulikuwa ni waghafla,
kwa kuwa ajali haina kinga basi ilibidi wakubaliane na tukio hilo la moto ambao chanzo chake kilikuwa ni shoti ya umeme,
siku zilikatika baada ya wanafunzi kupata mapumziko mafupi ili ikiwezekana waweze kupunguza mawazo ya tukio hilo lakini david hakurudi tanzania alipata hifadhi kwa rafiki mwingine ambae hawakuwa karibu sana ila walifahamiana kutokana na kusoma kozi moja,
muda ukawa umewadia wa kurudi chuoni na walikuta mambo yamebadilika kiasi fulani baada ya yale majengo yalio kuwa yameungua kurekebishwa na kupakwa rangi upya,wengi walifurahi kukutana kwa mara nyingine na kusimuliana mambo mengi ya mtaani kwao, hasa yalikuwa maswala ya kimapenzi ndio yaliochukua nafasi kubwa katika maongezi yao,
Lakini david muda mwingi alikuwa kimya sana na nakujitenga na wenzie, hali hiyo kuna watu walikuwa wanahisi analinga na kujisikia sana hata wengine walidriki kusema ile sababu ambayo kila mtu wa kutoka nchi nyingine anapokuwa kwenye nchi ya wenyeji huonekana wa thamani sana hivyo utanzania wa david pia ulimuongezea umaharufu chuoni hapo.
Madada wengi walimpenda kwa ukimya wake huo na walitamani kuwa naye kwakuwa hawakuwahi kusikia kuwa anamahusiano ya kimapenzi na msichana yoyote yule chuoni hapo japo kwa uzuri alionao na weusi wake ulio kuwa una waka waka na kumeremeta, wapo waliojipeleka wenyewe lakini david aliwajibu kwa ustaarabu wa hali ya juu hata kama walikataliwa lakini walijisikia fahari kukaa nae,
Siku moja usiku david alikaa kwenye kitanda chake huku wengine wakiendelea na maongezi ya hapa na pale, wenye kuongea na simu na wapenzi wao waliongea na wenye kurudia kusimulia lile tukio la moto lilivyotokea waliendelea kusikitika,
Utulivu wa david pale juu ya kitanda ulimfanya kuanza kufikiria vitu vingi sana alimkumbuka sana mdogo wake nisha hakujua kama yuko hai au amekufa,alitamani kuwahi kurudi tanzania iliakafanye harakati za kujaribu tena kumtafuta maana alimtafuta mara ya kwanza bila mafanikio,
Lakini maneno aliyokuwa ameyazungumza marehemu gozbety yalichukua utawala kwenye kichwa chake aliyatafakari kwa kina sana na kujiuliza maswali mengi ambayo alipata majibu baada ya kuchekecha akili na kulinganisha matukio akajua kabisa kuwa huyu baba yake mdogo wa marehemu gozbety ni helma tu hakuna mwingine,
Alijaribu kufikiria tena kwanini maelezo yake gozbety yaonekane ni yakutaka kulipa kisasi kwa familia yake akahisi kuwa ni dhahili helman amenywesha sumu ya maneno ili apate usaidizi wa kutaka kuendelea kuingamiza familia yake na hapo aliapa kwa sasa yuko tayari kufa au kufungwa, popote atakapo kutana na helman na kumjua basi kitakachotokea hapo itakuwa habari ya kusikitisha tanzania nzima na haitosahaulika kamwe,
Mawazo hayo yalimsindikiza mpaka akapitiwa na usingizi, alipoamka mida ile ya saa mbili asubuhi akaangalia ratiba yake na kuona kuwa anakipindi majira ya saa nne ndipo alipo jiandaa na kuchukua vifaa vyake na kuelekea kwenye darasa moja ambalo lilikuwa halina mtu yoyote yule ili akajisomee wakati anasubiria kipindi, ukimya wa darasa lile ulimridhisha david na kwenda kukaa kwenye kona kabisa ya darasa maana alikuwa hapendi kelele wala kujichanganya na wenzie kutokana na matatizo aliyo nayo hivyo aliogopa siku moja asije akayasema mbele za watu na kila mtu kujua kilichompata na kuwa mada chuoni hapo,
Alipo kuwa akiendelea kujisomea ghafla alishtuka alipohisi kama kuna mtu amepita kwa kasi nje, alipepesa macho yake kutazama ni nani huyo aliyepita lakini hakufanikiwa kumuona,ndipo alpoendelea kujisomea,
Ndani ya muda huo mchache masikio ya david yaliweza kusikia sauti nyembamba ya mtoto wa kike ikitokea nje ya dirisha ambalo lilikuwa karibu na yeye, sauti hiyo kwa mara ya kwanza iliweza kumvutia david japo bado hajafanikiwa kumuona kwa sura na kikubwa na kilichomshngaza ni kusikia akilia kuyalalamikia mapenzi tena kwa lugha ya kiswahili fasaha kabisa ambapo hajawahi kumsikia mtu yoyote yule akizungumza kiswahili fasaha hata kama baadhi ya wa nyaruanda wengine chuoni hapo walikuwa wanajaribu jaribu ila kiswahili hicho kilikuwa ni tofauti kabisa hivyo masikio yake akayatega kusikiliza maneno haya,,,,,,,,
“hii ni sayari gani jaman kila siku watu wanalia nimekosa nini mimi? Au sikustahili kuishi kwenye sayari hii ya mapenzi mbona niliingia kwa furaha na ninatoka kwa machozi,kumpenda kwangu naonekana malaya leo,sioni faida ya kuishi ni bora kupoteza maisha kuliko kuishi kwenye sayari isiyokuwa na upendo na mimi”
Maneno hayo dada huyo alikuwa akiyazungumza huku machozi yakimtoka alijutia kupenda sana mpaka kufikia kuchukua maamuzi ya kutaka kujiua na hilo ndilo swala david lililomfanya kunyanyuka pale alipokuwa amekaa na kutoka nje kuifuta sauti ile nzuri iliyokuwa ina yalalamikia mapenzi kwa lugha ya kiswahili,CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alipofika alimkuta msichana huyo amejiinamia chini akizidi kulia kwa uchungu alisimama kwa sekunde hivi akitafakari ataanza vipi kumuongelesha yule mdada na yeye mazoea na wasichana hana lakini alipo kuwa anajifikiria yule dada pale chini alihiisi kuwa kunamtu kasimama mbele yake, alipo nyakuwa kichwa chake na kugundua kuwa yule mtu aliyesimama ni mwanaume alimrukia na kuanza kumpigapiga na mikono yake laini huku akimwambia,,,,
“ I hate boys just leave me alone please, I hate you go,”( tafadhali naomba uniache mwenyewe nawachukia wavulana, nakuchukia nenda)
dada huyo alizidi kumpigampiga david huku akirudia maneno hayo kwa lugha ya kingereza bila kujua anaye mwambia lugha hiyo naye anajua kiswahili kama yeye alivyo kuwa ana lia kwa lugha ya kiswahili,
“ I hate boys just leave me alone please, I hate you go,”( tafadhali naomba uniache mwenyewe nawachukia wavulana, nakuchukia nenda)
dada huyo alizidi kumpigampiga david huku akirudia maneno hayo kwa lugha ya kingereza bila kujua anaye mwambia lugha hiyo naye anajua kiswahili kama yeye alivyo kuwa ana lia kwa lugha ya kiswahili,
David alikuwa akimtazama tu jinsi alivyokuwa anampiga piga na kufikiri huenda yule dada naye anamawazo kama yake kuwa hapo chuoni hakuna mtu anayejua kiswahili kwa kutokana na wengi wao walikuwa ni wanyaruanda na kutoka mataifa mengine ambayo yanazungumza kiingereza, lakini akajikaza na kumuuliza swali kwa kiswahili,,,,,
“Dada unamatatizo gani yanayokusumbua mpaka unataka kujiua?
Ghafla tu yule dada alijikuta kaacha kumpiga na kumsukuma david na kuanza kuduwaa kwa alichokisika maskioni mwake kwa lugha ya kiswahili ndipo na yeye alipomuuliza swali david huku akitetemeka maana alihisi kama anaota vile,,,,,,,
“we, we ni mtanzania??
David alitingisha kichwa kukubali kuwa ndio yeye ni mtanzania, lakini kukubali kule kulimfanya david kuchanganyikiwa kwa muda ndipo alipo chukua maamuzi ya kugeuka nyuma na kuondoka kwa mwendo wa haraka kuelekea bwenini kwao, alifika na kujitupa kwenye kitanda hata dhana zake alizobeba kwa ajili ya kujisomea aliziacha kule kule darasani,
Yule dada alibaki akijiuliza maswali na kuonesha hali ya kutoamini kwa alicho kisikia na kukiona mbele yake hivyo mawazo yale ya mapenzi aliyokuwa nayo mwanzo na tukio hilo lilimuongezea msongo wa mawazo kwa muda huo mchache, alidondoka palepale chini na kupoteza fahamu, watu waliokuwa karibu na maeneo yale walishtushwa na kile kishindo na kuanza kuelekea kule sauti ya kishindo ilipotokea na kumuona yule dada kadondoka chini na damu zikimtoka puani,
Walimbeba juujuu na kumuwaisha kwenye zahanati ya chuo hiko, wauguzi walimpokea kwa haraka na kumlaza kwenye kitanda kisha kumuongezea maji ambayo yaliweza kusaidia kurudisha fahamu yake kwa haraka zaidi,
marafiki zake hawakuwa mbali kutaka kujua hali ya rafiki yao inaendeleaje baada ya kupata taarifa kwa wanafunzi walio mbeba hivyo wakawa wanamfariji na kujaribu kumchekesha kwa vituko vya hapa na pale ilimradi aweze kupoteza mawazo aliyo kuwa nayo maana walishajua kuwa huyu atakuwa kapoteza fahamu baada ya kutendwa na mpenzi wake aliyekuwa anaitwa Emmanuel Regan,
Kichwa cha david kikawa kimeongeza wazo lingine la kuwaza, aliifikiria sana ile sauti ya yule dada japo ilikuwa na majonzi lakini bado ilizidi kuvutia, aliutafakari ule ufupi wake kiasi aliokuwa nao ambao ulimfanya david kuachia tabasamu la upendo hapo kitandani alipokuwa,
Alivuta picha na kujiuliza swali,vipi kama ataweza kumkumbatia msichana huyo mwenye muanya kwa juu na aliye kata nywele zake kiasi ambazo zilikuwa zina ng’aa kutokana na weusi wake ambao ulizidi kufanya ile rangi yake ya usoni inayotaka kufanana na maji ya kunde kuonekana zaidi ni nini kitatokea?
jibu la kimahaba na bashasha likaja akilini mwake na kujijibu
“ Ni dhahili ataweza kusikia mapigo ya moyo wangu yanavyodunda kwa haraka zaidi kwa ajili yake”
Mawazo hayo yalimfanya david kuchelewa kipindi darasani, na siku hiyo ikawa imepote bule,
Siku iliyofuata yule dada akawa ameruhusiwa kule zahanati kwa kuwa tatizo lake halikuwa kubwa sana na kikubwa alichoshauriwa ni kupunguza mawazo,
David alionekana kwenye viunga vya maua chuoni hapo akizunguka zunguka kujaribu kumtafuta yule dada ambaye hakujua atampata vipi maana hakuwa na chochote ambacho kingeweza kumrahisishia kumpata kama vile jina hata mchepuo aliokuwa anasoma,
Wahenga walisema mola hamtupi mja wake usemi huo uliweza kumsaidia david,baada ya kumtafuta dada huyo kwa muda mrefu bila mafanikio akaamua kutaka kujirejesha bwenini kupumzika alipokuwa anataka kuchukua njia ambayo itamtoa mazingira yale ya chuoni na kumfikisha bwenini alimuona yule dada akiwa wanabadirishana namba simu na msichana mwenzie ili amuelezee jinsi mpenzi wake Emmanuely regan alivyo mtenda, david hakuremba alijibanza kwenye mti uliokuwa karibu na kumvizia yule dada amtajie mwenzie namba zake,
Yule dada alipokuwa anazitaja namba zake ambazo ni +250768000092, masikio ya david yakayapa ushirikiano mzuri vinganja vyake na kuanza kuziandika kwenye simu yake, basi wale madada walipomaliza kubadirishana namba kila mmoja akachukua njia yake bila kujua kama kuna mtu ambaye alikuwa amejificha jirani yao,
Tukio hilo lilizidi kumuongezea david furaha na kutaka kusahau kama anamatatizo makubwa, ali zihifadhi namba kwenye simu yake na kuipa jina la Qeen tz, maana alikuwa hamjui jina lake,
Shughuli za masomo ziliendelea kwa furaha siku hiyo kwa david na alitamani usiku ufike haraka ili aweze kujaribu bahati yake kwakuwa huyo dada alikuwa katoka kwenye maumivu siku mbili nyuma hivyo alihisi lazima kutakuwa na ugumu wa hali ya juu,
Ombi lake lilifanikiwa jua lilielekea magharibi na sauti za mbu zikawa zinamsumbua david wakati akiweka chandalua chake vizuri, kisha kuchukua mto na kuegesha kichwa chake kwa juu na kuanza kubonyeza vitufe kulitafuta jina la Qeen tz, alipolipata akabonyeza kitufe cha kijani ambacho kina ruhusu simu kutoka au kupokea wakati ikiingia na baada ya kuweka skioni kuzikiliza kama inaita alijibiwa,,
“simu unayopiga kwa sasa inatumika jaribu tena baadae”
ujumbe huo ulibadilisha sura ya david na furaha yake kutaka kupotea, alijaribu zaidi ya mara nne lakini jibu likawa ni lilelile mpaka alipokata tamaa na kunza kusinzia ghafla alishtushwa na wimbo mfupi ulikowa unaashiria kuwa kuna ujumbe umeingia ambao na kuaza kujibizana lakini lugha iliyokuwa inatumia hapo ni kiingereza,
“mambo? Ndio ujumbe ulio ingia kwenye simu ya david na akanza kuuijibu,
“poa”
“Sijui mwenzangu nani maana hii namba in ngeni kwangu” yule dada aliuliza
“mimi ni mtu mwenye pendo wa kweli ninaye toka kwenye sayari ya kufuta mchozi na kuwa patia furaha wenye majonzi kama wewe” alionge david
“Mmh wewe mbona unanichanganya na majibu yako namba yangu amekupa nani kwanza? Aliuliza yule dada
“Kuna ubaya nikiwa nayo” david naye alimuuliza swali
“Hapana ila lazima tujuane kwanza na najue namba yangu umepata wapi kama hivyo siwezi kukaa na namba mpya kwenye simu bila kuijua sawa eeh” yule dada alivyojibu tu ule ujumbe ilionekana wazi amekasirika ndipo david alimpo mjibu,,,CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“sikuzote hakuna upendo wa zamani kwa mwanamke unaye mpenda jinsi namba yangu ilivyokuwa mpya kwako ndivyo mimi nitakavyo kuwa mpya ndani ya moyo wako kama utaruhusu kupokea pendo langu kama unavyo pokea ujumbe wangu”
david aliona bora afunguke kwa staili ya kumuweka kwenye mabano yule dada wa katanzania,
na kweli yule dada alizidi kuchanganyikiwa maana majibu aliyokuwa anayapokea kwa david hakuwahi kuyasikia kwa mwanauume yoyote yule ndipo alipomuomba kesho asubuhi waonane kwenye kiunga kimoja cha maua kilicho karibu na jengo kuu la ofisi za chuo hiko david alikubali lakini akamuuliza tena swali yule dada,,
“unaitwa nani lakini maana jina lako limejificha ndani ya moyo wangu na alitaki kutoka kwa kuwa onaonekana umechukia na macho yangu yanausumbu moyo kutaka kuona jina lako kwa mara nyingie huenda nilikuwa na kosea hata katika kuliandika katika kitabu changu cha matukio ambapo jina lako ndilo lililofungua ukurasa wa kwanza wakitabu hicho ila hata kama nilikuwa nakosea lakini jina lako ni zuri sana tafadhali naomba unitumie jina lako iliniliandike vizuri kwenye kitabu changu”
David aliona yule dada kasha chukia na maaongezi yalikuwa yanakaribia kuisha kwa muda ule na jina alikuwa bado halijui ndipo alipoamua kutumia ujanja huo kana kwamba alikuwa analifahamu tangu zamani ila alikuwa analikosea katika kuliandika,
Ndege mjanja huna kwenye tundu bovu yule dada akaingilia kwenye mtego huo na akatuma jina lake akihisi tayari lina fahamika kwa mtu anaye jibizana nae akasema,,
“Jina langu linaandikwa hivi Victoria”
David baada ya ujumbe huo aliokuwa anausubiria kwa hamu kuingia na kuusoma alifurahi sana mpaka wenzie mle ndani wakawa wanashangaa huyu jamaa siku zote huwa kimya vipi leo mbona amekuwa na furaha ya ajabu sane lakini david aliendelea kugeuka geuka na kuliangalia lile jina mara kwa mara kisha kujifunika shuka ili apate usingizi mapema kesho iwahi kufika------- Miale ya jua iliyo kuwa inapenya dirishani iliweza kumfanya david afunue shuka na kuchungulia nje na kuona wanafunzi wenzie wakiendelea na usafi wa nguo zao siku hiyo ya jumamosi ambayo wengi walikuwa hawana vipindi japo wachache walikuwa navyo,
Alifumba macho yake na kuanza kusali kumshukuru mungu wake kwa kumuamsha salama kisha kunyanyuka kitandani na kutandika vizuri na safari ya kuelekea bafuni ikafuata,
Ndani ya muda mchache akawa kasha maliza kujianda na kuelekea kwenye mgahawa wa chuo kujipatia kifungua kinywa,
marashi aliyo yapaka david yalikuwa na harufu nzuri sana yalionekana kama yanaendana na nguo zake alizovaa asubuhi hiyo,ilikuwa ni pensi nyeupe na singrendi nyeupe yenye picha kubwa yakuvutia na zile sendro zake nyeupe,
Wengi alio pishana nao waligeuka kumtazama kwa muonekano mzuri aliokuwa nao david, acha baadhi ya wavulana wenzie waliokuwa wanamsimamisha kuulizia jina la marashi aliyo yapaka maana yalionekana kuwavutia sana,
Alifika mgahawani hapo na kuagiza vitafunwa pamoja na chai ya maziwa akajipatia na kushiba vizuri kisha kuondoka, kurudi bwenini, kila alipo pita au kukaa mahali popote pale basi akiondoka ni lazima aache mada kwa watu,
walimzungumzia kwa mengi mazuri na mabaya, japo sifa nyingi nzuri alikuwa anazipata kutoka kwa wasichana, wavulana wengi walikuwa wanamchukia kutokana na baadhi ya wasichana waliokuwa wanatongozwa wengi wao walikuwa wana sema kuwa wanawachumba tayari naukiwauliza walikuwa wana mtaja david hivyo kitendo hicho kilikuwa kina wakera sana,
david alifika kitandani kwake na kuchukua simu yake ambayo alisahau kutoka nayo, alipoiangalia akakuta ujumbe mpya kutoka kwa victoria uliomuomba ifikapo saa saba mchana wakutane kwenye mgahawa wa chuo kupata chakula cha mchana na waweze kufahamiana kwa sura maana victoria alikuwa hajui kama anayetaka kuonana naye walisha wahi kukutana na akazimia kwa kutoamini kumsikia mtu akizungumza kiswahili chuoni hapo,
******************************
Kila mmoja wao alionekana kuwa na shauku ya kutaka kuonana na mwenzie japo victoria alikuwa katoka kuumizwa lakini alivutika na maneno aliyokuwa anatumiwa na david kwenye simu,
Muda uliobaki kabla ya kukutana waliweza kuutumia kufanya shughuli zao za hapa na pale mpaka kijua kilipokuwa kikali na kukili kuwa sasa ni muda muafaka wa kwenda kukutana,
David alijipigilia jinsi nyeusi na tisheti jeupe ambalo halikuwa na doa hata ya andishi moja na chini kuvaa kiatu ambacho kiliendana na rangi ya tisheti lake,
weusi wake mzuri wenye kuwaka waka ulizidi kuonekana kutokana na nguo ile nyeupe aliyokuwa amevaa, alipojihakikishia kuwa yuko sawa na hana tatizo lolote lile basi hakuwa na budi kuanza safari yake ya kuelekea kuonana na mtoto mzuri victori,
Moyo ulikuwa una mdunda david maana hajawahi kuongea na mwanamke ana kwa ana kuhusiana na mapenzi hivyo alihisi atakuwa na wakati mgumu sana siku hiyo,
Alipokuwa anaukaribia mlango wa kuingia ndani ya mgahawa huo alisikia sauti ambayo ndiyo ilimfanya mapaka kuchukua maamuzi ya kutoa hisia zake za moyoni, ikizungumza na simu
Alipogeuka nyuma waligongana macho kwa macho, victoria alidosha pochi yake chini kwa mshtuko na david ilibidi azuge kama ndio alikuwa anatoka mle ndani ya mgahawa hivyo alimpita na kurudi alipo tokea,
victoria aligeuza shingo yake kumtazama david ambaye alikuwa anaishia basi akabaki kuvuta pumzi ndefu ambayo ile harufu ya marashi aliyopaka david kuingia kwa wingi puani mwake,
Akili ile ya mahaba ilipomtoka victoria alishtuka kuona baadhi ya watu wakimtazama na wengine kucheka kwa kitendo alichokuwa anakifanya, aliinama na kuokota pochi yake kisha kuingia mle mgahawani huku akiwa anahema kwa haraka, aliketi kwa muda kumsubiri mtu aliyekuwa na ahadi naye bila kujua mtu mwenye ndiyo david aliye pishana nae,aliendelea kusubiri lakini bila mafanikio,maana david hakurudi tena muda huo,
Hivyo victoria naye ikabidi aondoke kwa hasira kwa kufanywa kama mtoto mdogo mgahawi pale,lakini furaha ilikuwa inakuja kila alipokuwa anakumbuka jinsi david alivyompita na kuacha harufu nzuri ya marashi,
********************
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku kama hiyo ya jumamosi chuoni hapo kuna kuwa na disko ndani ya ukumbi wa chuo na baadhi ya wanafunzi huwa wanachaguliwa kucheza nyimbo za aina mbalimbali ilikuonesha uwezo wao na vipaji vyao,
Rafiki zake na victoria waliweza kugundua kuwa victoria ameanza kumpenda david hivyo walianda mpango na kuongea na wanachumba wenzie na david kuwa itakapofika muda wa kucheza basi david acheze na victoria na wengine waliobaki watacheza na wao,
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment