Simulizi : Sahihi Ya Kifo
Sehemu Ya Pili (2)
Kitendo kile kilinifanya nianze kukimbia kuwahi familia yangu ili nijue kama ipo salama nilifika nyumbani na kukuta geti lipo wazi nikaelekea sebleni nikakuta makochi yamesogezwa na vitu vipo katika mpango usio eleweka nili nibidi niite kwa hofu,,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
”Magrety Magrety?
”Abee mume wangu”aliitika kisha kuja pale sebuleni kutokea chumbani kwa David akiwa ameshika kifaa cha kudekia kisha kuniuliza,,,
“Mbona mapema Alfred kuna usalama kweli huko?
”Usalama upo kiasi ila habari za kifo cha Sagu ndio limekuwa gumzo la jiji huko nje”
”kuna mtu aliye kuja hapa” nilimuuliza
”hapana hajaja mtu”alijibu
”Kwanini umeuliza hivyo”?aliniuliza
”Maana geti lipo wazi”
”Ooh walikuja wazoa taka watakuwa walisahau kufunga lakini huja nijibu kwanini umewahi kurudi?alijibu na kuniuliza nami nikamueleza sababu iliyo nifanya niwahi kurudi.
****************
Miaka kama mitatu ilipita mke wangu akapata ujauzito ambao mtoto ndio huyu dason na uchunguzi ulifanyika juu ya kifo cha sagu ila wakafanikiwa kumkamata cholo yule mnyaruanda ilisemekana kuwa helman alihonga pesa nyingi sana mpaka yeye hakuhusishwa katika ile kesi.
Mpaka siku moja nikiwa nimetulia na magrety nikapokea ujumbe kutoka kwenye namba ambayo alijitambulisha moja kwa moja kuwa yeye ni helman na kunipa vitisho,,,,
”NAJUA KUWA WEWE NDIYE ULIE TOA TAARIFA KITUONI MPAKA CHOLO AMEKAMATWA NA KAMA ISINGE KUWA PESA ZANGU LEO NA MIMI NINGEKUWA GEREZANI SASA UTAKIONA KILICHOMFANYA NYOKA KUKOSA MIGUU KAMA SIO KUFA WEWE BASI FAMILIA YAKO ITAKUWA KWENYE MATATIZO NA HIVYO VIKISHINDIKANA UTAMFUATA CHOLO GEREZANI KWA GHARAMA YOYOTE ILE”
Huo ndio uliokuwa ujumbe wa mwisho kutumiwa na Helmani kabla ya kuundaa mpango wake ulionifanya mpaka nikaenda gerezani
Vitisho kutoka kwa Helman ndio ikawa sehemu ya maisha yangu kwa kipindi chote hicho japo tangu tukio la mauaji ya marehemu Sagu sikuwahi kumtia machoni zaidi ya kupata ujumbe huo nami sikutaka kujua yuko wapi maana kwa kiasi fulani hali iliaanza kuwa shwari kutokana na jeshi la polisi nchini kuwa makini na matukio kama hayo.
Nami umakini ukazidi kwa familia yangu na kuzidisha upendo kwa wanangu na kumngojea kwa hamu kiumbe kilicho kuwa tumboni kwa Magrety na ufanisi wangu wa kazi ukawa umerejea kama kawaida hivyo amani kwa ujumla ikawa imerejea nje hata ndani ya moyo wangu ikawa nikitoka tu kazini sina sehemu ya kwenda zaidi ya kuelekea nyumbani,
Jumatano moja iliyo pambazuka na hali ya mvuamvua kulikuwa na watu wengi nje walio kuwa wana subiri kuingia ofisini kwangu kwa ajili ya kusaini fomu za mikopo ili wakaendeleze biashara zao na wale walio kuwa ndio wanaanza kuchukua mikopo walikuja na kopi za hati za nyumba zao pamoja na picha baada ya taratibu zote kufuatwa kama wasaidizi wangu kwenda kuhakiki nyumba hizo na sahihi kuwekwa na mdhamini kama mtu alizaminiwa nyumba.
Kazi ilikwenda vizuri wengi niliwakamilishia huduma walizo kuwa wanahitaji lakini hofu ilirudi tena baada ya kupata mteja aliyetambulika kwa jina la Khaji Kipeneko baada ya kunionesha fomu yake iliyokuwa na sahihi yake na ya mdhamini ila ile ya mdhamini nilikuwa na ifananisha na ya Helman alipo nionesha na picha ya nyumba nikahakiki kuwa ni kweli ni ya Helman macho yalipepesuka marambili mbili kisha ni kamtazama yule jamaa kwa makini na kumuuliza kwa dhihaka,,,,,
“aliyekudhamini nyumba hii ya thamani ni nani yako maana anaonekana ana moyo sana”
“ni bosi wangu” alinijibu
Mdomo wangu ukapata kigugumizi kidogo na wala sikuta kuendelea tena maana anaye kuwa mfanya kazi wa Helman lazima watakuwa wanashirikiana katika maswala yao ya ujambazi tu nikamsainia haraka haraka na kumueleza siku ya kuja kuchukua mkopo wake na kumruhusu aondoke maana alisha niharibia siku. Na bahati yeye ndiye aliyekuwa wa mwisho hivyo nami sikuchelewa ilinibidi niondoke kwa kuomba ruhusa ya uongo.
Nikiwa njiani ndani ya gari langu BMW230 huku mvua ya rasharasha ikiwa inaendelea na kifaa maalumu cha kusafishia kioo kikiwa kinabadilisha upande kwenda kulia na kushoto iliniweze kuona vizuri hakika macho yangu yalimuona yule jamaa mwenye jina la Khaji Kipeneko akiwa na Helman kwenye mgahawa mmoja ambao haukuwa mbali sana kutoka pale benki na kama kuna jambo walikuwa wana lijadili hivi, ilinibidi nisimame na kuwaangalia vizuri walipo liona gari langu walinyanyuka na kuondoka.
Nilifikiri kwa muda pale huku kichwa changu nikiwa nime kiinamisha kwenye usukani,
“ kwamba maisha haya nitaishi mpaka lini na kwa nini niwe mtumwa wa elimu yangu mwenyewe?
“Helman yeye ni nani kwangu mungu ? Hapana, sasa kwanini nimuhofie? nilijiuliza maswali mengi na kujijibu mwenyewe, ilinibidi nichukue maamuzi ya kumfuata anieleze kama kuna sababu nyingine inayo mfanya aendelee kunifatafata maana ni miaka mitatu imepita lakini bado anataka kuendelea kuwa kikwazo kwangu.
Nilifungua mlango wa gari kwa hasira bila kujali mvua iliyo kuwa inaanza kuchanganya na kumfuta Helman kule waliko kuwa wanaelekea na yule kibalaka wake Khaji Kipeneko nilifika mpaka maeneo yale lakini njia ilikuwa nyeupe sikujua waliingilia upande gani, ilinibidi nirudi kwenye ule mgahawa na kutulia kidogo kushusha pumzi kidogo mpaka muhudumu alipo kuja na kumuagiza aniletee bia ya Kilimanjaro ya moto.
Nilikunywa bia ile taratibu mpaka nikamaliza japo nilihisi inaweza ikanipunguzia mawazo lakini haikuwa hivyo, nikatoa waleti yangu mfukoni na kumuita muhudumu ili nimpatie fedha yake cha ajabu alicho nijibu alinifanya nimpatie maneno yasio stahili kuambiwa binaamu,,,
“ mbona umeshalipiwa hicho kinywaji’? aliniambia
“Na nani”?
“Amesema ni kwambie mgomvi wako” alinijibu yule muhudumu
“Wewe dada unakichaa? Utawezaje kupokea pesa toka kwa mtu mwingine wakati kinywaji nimekunywa mimi na isitoshe umeniona nimekuja peke yangu hapa embu nitokee usoni mwangu”
nilimjibu na kumtupia pesa usoni naye akainama akaziokota na kuniomba radhi ambayo sikumjibu kisha akaondoka, jibu lile alilo nijibu kuwa mgomvi wako ndiye aliye kulipia nilijua yawezekana kuwa Helman bado yupo maeneo yale nilinyanyuka na kutaka kuweka waleti mfukoni baada ya kuitoa nilipokuwa nataka kumpatia fedha yule muhudumu, lakini kumbe kutokana na zile papala niliangusha pale chini badala ya kuweka mfukoni kama ilivyokuwa nia yangu.japo kwa muda huo sikujua.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilimfuata yule muhudumu na kumuuliza aliye nilipia yuko wapi alinionesha sehemu ambayo aliyo kuwepo mwanzoni lakini baada ya kwenda mimi sikumuona yule dada allisema
“ alikuwa hapa mida sio mirefu wakati mimi nakuja kwako” nilikasirika sana ilinibidi niondoke zangu nyumbani.
Nilipofika nilimkuta Magrety pamoja na Nisha wamejipumzisha kwenye makochi kutokana na mzigo aliokuwa nao tumboni mwake. Nilielekea mezani na kujiandalia chakula mwenyewe, nilipo kuwa naanza kula tu David naye alikuwa anarudi kutoka shuleni basi nikaungana naye pamoja tukala wote, kisha nikaelekea chumbani kutafakari mpaka Magrety naye alipo amka nakunikuta nipo chumbani
“eeh mme wangu umerudi saa ngapi tena”? aliniuliza
“Muda mrefu mpaka nimekula we ulikuwa bado ume lala na Nisha wako pembeni sikutaka kuwa sumbua”
Basi baada ya maongezi hayo mafupi ilinibidi nimueleze kilicho nikuta siku hiyo naye alinipa wazo,
“Baba David mme wangu swala hili sasa naona linazidi kuelekea pabaya zaidi maana huyu Helman inaonekana ni sugu na anaweza akakusababishia matatizo makubwa maana haiwezekani kipindi chote hiki awe bado anakufuatilia halafu bila kosa lolote lile cha msingi hapa kesho twende tukatoe taarifa kituoni hata kama kuna jambo lita tokea basi polisi lisiwe geni kwao”
“Nimekuelewa mke wangu mpendwa nitafanya hivyo kweli hali hii inazidi kuniogopesha sana hasa nikifikiria usalama wa familia yangu”
Tuliweza kukubaliana maamuzi yetu mimi na mke wangu kilicho baki tulikuwa tunaomba uzima kwa mwenyezi mungu tufike salama siku inyofuata ili tuelekee kituoni;
Waswahili wana sema mwenye nacho huongezewa kwangu usemi huo ulichukua nafasi baada ya kuongezewa matatizo niliyo kuwa nayo,
Asubuhi na mapema wakati nikiendelea kujiaanda ili nieleke kituoni na baada yapo ndio niende kazini, sikujua kilicho nisukuma kuwasha luninga yangu ya chumbani ambayo ilikuwa inatangaza habari mpya,,
“ndugu watazamaji wa kipindi chetu cha ” matukio yetu” siku ya leo tunaamka na habari ambayo imeshika katika habari zote tulizo nazo,
“Gari lililo kuwa linasafirisha fedha jana jioni kutoka Dar es salaam kwenda Tanga lilivamiwa na majambazi wasio julikana na kuwajeruhi baadhi ya maaskari waliokuwa wana linda gari hilo ila kwa bahati nzuri kuna baaadhi ya vielelezo ambavyo vimeweza kuonekana eneo la tukio ni pamoja na waleti iliyokuwa na vitambulisho ambavyo vinasemekana ni vya mmoja wa wafanyakazi wa benki ya NMB akitambuliwa kwa jina la Alfred kazinge pamoja na bastola moja ambayo ilionekana kutumiwa katika tukio hilo na kwa taarifa tulizo nazo ni kwamba polisi wanaelekea kumkamata mtuhumiwa baada ya kuthibitisha kuwa vifaa hivyo ni vya muhusika wa tukio hilo kwa uthitisho ulio tolewa na meneja wake wa tawi la magomeni”
Nilizima luninga ile haraka na kusimama kwa muda bila kujua cha kufanya na kutoamini nilichokiona na kukisikia kwa masikio yangu mawili,mpaka nilipo kumbuka mazingira ambayo nitakuwa nimeangusha ile waleti ndipo nilipo gundua kuwa ni pale mgahawani niligeuka nyuma kumtazama Magrety aliye kuwa kitandani nika mkuta kashika kichwa na mdomo ukimtetemeka kwa hofu, nilitupa macho yangu chini kisha kuyainua na kupiga hatua kumsogelea na kumwambia,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
“ Magrety mke wangu hapa sina njia nyingine ya kukwepa kesi hii maana ile waleti ni kweli yangu na vile ni vitambulisho vyangu pia kama unakumbuka ile bastola nilisha wahi kuishika tena bila gropsi na wale mapacha walikuwa na grops walivyo ichukua kwangu yawezekana huu mpango ulikuwa endelevu ulioandaliwa
“ pia kwa kipindi chote hicho yawezekana ikawa haikutumiwa na kama ilitumiwa basi watumiaji walivaa gropsi ili zile alama za mikono zikipimwa zionekane ni za kwangu Helman namjua anaakili sana ya kijambazi japo mimi sio muhusika inanibidi nikimbie tu ilibaadae nije kulea familia yangu nakuomba usiwaambie chochote hawa watoto maana wanaweza kuishi kwa hofu sana katika maisha yao nami napenda wawe na amani”
Nilibusu tumbo la mke wangu na kukiomba radhi kiumbe kilichopo ndani..,,,,,,,,,
“ewe malaika usiye jua chochote kinacho endelea naomba unisamehe sana kwa uwamuzi ninao uchukua wa kuondoka bila ya wewe kuzaliwa maana utakosa upendo wangu kwa muda na sina ninachoweza kukuachia kwa sasa zaidi ya kumbukumbu za maumivu utakazo kuja kuzikuta utakapo zaliwa na kujitambua.
Maneno hayo niliyo kiambia kiumbe kilichopo tumboni yali mchoma sana Magrety alisikia uchungu usio na mipaka, machozi yalianzisha ujirani na mashavu yalitililika vyakutosha acha makamasi yalio kuwa yana toka kwa kupiga hodi hata kile kilio cha kwikwi kikachukua nafasi kinywani mwake. Nami sikutaka kupoteza muda zaidi ya kuingia kwenye droo na kuchukua kiasi kidogo cha fedha ambacho nilikiweka kama akiba na kingine kumuachia Magrety kwa ajili ya familia yangu na kuhusu hati za mali alikuwa anajua wapi zilipo.
nikampiga busu la mwisho na yeye ambalo lilimfanya azidi kutoa machozi na kutaka kunizuia nisiondoke lakini sikutaka kumuendekeza nikatoka kwa nguvu mpaka nje kisha nikafungua geti na kurudi kwenye BMW230 na kuiwasha na kutoka mpaka nje ya geti
wakati najaribu kunyoosha matairi vizuri ilinianze kuondoka ghafla nikaona vikofia vya polisi vikibembea kwa nyuma ya gari lao walikuwa ni wengi waliobebwa nyuma ya gari hilo huku mitutu ya bunduki ikiwa mbele ya vifua vyao ilinibidi nijisalimishe mwenyewe tu.,
walishuka hata kabla gari lao halija simama vizuri na kunivamia moja kwa moja walinijua baada ya kuoneshwa na meneja wangu ambaye ndiye alie waleta nyumbani kwangu.
Walikamata mikono yangu na kunifunga pingu kwa nyuma baada ya kuigeuza mikono yangu kisha kunirudisha mpaka ndani kwangu askari wengine walijigawa kwenye vyumba vingine wakikagua kama kuna siraha au zana zingine amabazo zina husiana na ujangili kiukweli nilijisikia vibaya sana nilipo waona watoto wangu pamoja na mke wangu walivyo kuwa wananililia lakini askari hao hawakujali lolote walishindwa hata kumuhurumia mke wangu kwa hali aliyo nayo, walikuwa wakimsukuma kila alipo kuwa ananisogelea na kunililia,
Sikuweza kujikaza katika hali hiyo nami machozi yakawa yananitoka kila nikiwatazama familia yangu ikitapatapa kwa kukosa msaada hata wa kubembelezwa, maaskari hao walipo maliza ukaguzi wao walinitoa nje huku nikiwa bado nina pingu mikononi jambo ambalo lilinifanya nione aibu kutokana na wingi wa watu hasa majirani zangu walivyo kusanyika kushuhudia tukio hilo, nilipandishwa kwenye gari lao kama ng’ombe wanao pelekwa mnadani kisha kuondoka kuelekea kituoni.
Walikamata mikono yangu na kunifunga pingu kwa nyuma baada ya kuigeuza mikono yangu kisha kunirudisha mpaka ndani kwangu askari wengine walijigawa kwenye vyumba vingine wakikagua kama kuna siraha au zana zingine amabazo zina husiana na ujangili kiukweli nilijisikia vibaya sana nilipo waona watoto wangu pamoja na mke wangu walivyo kuwa wananililia lakini askari hao hawakujali lolote walishindwa hata kumuhurumia mke wangu kwa hali aliyo nayo, walikuwa wakimsukuma kila alipo kuwa ananisogelea na kunililia,
Sikuweza kujikaza katika hali hiyo nami machozi yakawa yananitoka kila nikiwatazama familia yangu ikitapatapa kwa kukosa msaada hata wa kubembelezwa, maaskari hao walipo maliza ukaguzi wao walinitoa nje huku nikiwa bado nina pingu mikononi jambo ambalo lilinifanya nione aibu kutokana na wingi wa watu hasa majirani zangu walivyo kusanyika kushuhudia tukio hilo, nilipandishwa kwenye gari lao kama ng’ombe wanao pelekwa mnadani kisha kuondoka kuelekea kituoni,
Mama David japo na hali yake ile alijaribu kulikimbiza gari lile kama mwanamke mwenye kichaa lakini hata hivyo hatua zake hazikumchukua mbali na kudondoka chini hiyo ndio ilikuwa mara ya mwisho kuiona famila yangu na kuwaona kina David wakimlilia mama yao pale alipo dondoka chini hata mahakamani hawakuja si kujua walipatwa na nini huko nyuma.
Mahakama ikatoa hukumu ya mimi kuhukumiwa kifungo na mali zangu zote kutaifishwa na kupigwa mnada ndipo familia yangu ikawa imekuja huku katika nyumbaa hii niliyo ijenga kwa siri na Dason alizaliwa huku na hakuweza kunijua baba yake mpaka nilipo toka gerezani kwa msamaha wa Rais.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hata hivyo wakati natoka gerezani nilikutana na mwanamke mmoja aliyekuwa rafiki wa mke wangu ambaye alikuwa anaijua familia yangu vizuri aliniambia kuwa ana ushahidi kuhusu tukio lililo kuwa limetokea ambao unaweza ukanisaidia pia kulipwa fidia au kurudishiwa mali zangu lakini kikubwa alicho kisema ni kwamba.
“ushahidi huo Helman amesikia kuwa ninao mimi baada ya kutonywa na mafanyakazi mwenzangu hivyo ananitafuta kwa hudi na uvumba na mimi pale hotelini kwetu nilipo kuwa nafanya kazi nimeacha kwa kuona maisha yangu yata kuwa hatalini”
lakini kabla hajamaliza maongeza nilimuona katanua mdomo kwa kupigwa na butwaa na macho yake yakiangalia eneo ambalo mimi nili lilipa mgongo nilipo geuza shingo nilimuona Helman ambaye alikuwa ananifananisha hivi na yawezekana hakuamini kama ningeweza kutoka jela kwa wakati ule na alionekana kuchanganyikiwa baada ya kuniona mimi na yule mama rafiki wa mke wangu mwenye ushahidi hivyo hatukuwa na jinsi zaidi ya kukimbia na huko mbele tukapotezana kila mmoja akapita njia ya peke yake ndipo nami nilipo fanya haraka kwenda ubungo na kupanda abood ya kuja huku Morogoro.
Hofu yangu iliyo kuwa inanifanya ni mkataze David asiende mjini ni kwamba Helman yaweze kana anajua kuwa mimi huo ushahidi nilichukua kwa yule mama ambaye anaitwa Magdalena hivyo japo si rahisi kumkumbuka David kwa kuwa miaka mingi imepita na David amekuwa sana lakini dunia haina siri yawezekana tu akajulikana na akapata matatizo makubwa sana zaidi ya haya niliyo yapata mimi. Hayo ndiyo matukio yaliobadilisha maisha yangu.
***************************************
Baada ya mzee kazinge kumaliza yalio mtokea mpaka kufikia katika hali ile aliyokuwa nayo sasa kila mtu alichoka kwa kweli wengi walidondosha machozi na kumuhurumia hata David akawa amejua ukatili alio fanyiwa baba yake japo kumbukumbu ya machache alikuwa nayo akili mwake lakini kiini cha matatizo alikuwa hakijui sasa ndio amejua mtoto wa kiume hata Nisha naye aliye kuwa mdogo kwa wakati ule ameweza kujua alicho fanyiwa baba yake na Dasoni yeye ndio amekuwa kama Nisha wazamani asiye jua chochote zaidi ya kuona kama watu wanasimulia hadithi za bibi na babu tu,
Ndugu mwenyekiti alivyo taka kuongea neno alikatishwa na sauti ya mama Coolin ambaye alikuwa amebeba chakula alicho enda kukiandaa kwa ajili ya mgonjwa,,,
“jamani tumechelewa kupeleka chakula cha mgonjwa na sasa yaelekea saa tisa kasoro na kule ilikuwa ni saa saba ndio tulitakiwa twende tatizo kufuata mahitaji sokoni mpaka kuandaa na mikaa yenyewe ya siku hizi hii ndio imenichelewesha Davidi mwanangu twende haraka tukaombe tuingie hata kama tumechelewa wanaweza waka tuelewa”
David alinyanuka akawa anaelekea kule alipo mama Coolin ili ampokee kikapu cha chakula na mzee Kazinge naye akaona si vibaya kwenda kumuona mkewe japo uso wake ulikuwa bado una aibu kwa alicho mfanyia mkewe,
Waliongozana wale watatu mpaka barabarani na kuchukua bajaji kuelekea Hospitali huku wakijadili ni jinsi gani wanaweza wakalipa ile bili ya mgonjwa kule Hospitali maana walifanyiwa msaada kutokana na hali yake kuwa mbaya, maongezi hayo walienda nayo mpaka yalipo wafikisha hospitali,
Walifika getini na kumuomba mlinzi awarusu waingie kutokana na hali walio muacha nayo mgonjwa halafu alibaki mwenyewe, kwa kuwa mlinzi naye binaadamu aliwaruhusu na walipo ruhusiwa tu mama Coolin akawaomba watangulie maana alisahau hata kununua maji ya kunywa mgonjwa hivyo akaelekea kwenye duka lililopo karibu na Hospitali hiyo ya gairo,
David akawa yupo na baba yake mzee Kazinge akimuelekeza njia za kupita ili waweze kufika kwenye chumba ambacho mama yake alikuwa amelazwa, na ndani ya dakika kadhaa wakiwa wanakaribia chumba kile na David alimwambia baba yake,
“ Baba inabidi nionane na daktari kwanza maana chumba hicho hawaruhusiwa kuingia kama hodi zingine za wagonjwa wa kawaida”.
Akamuacha baba yake pale akiwa amesimama na yeye kuelekea kwa Daktari lakini alipo fika hakumkuta ofisini mwake ilimbidi arudi kule alipo baba yake sasa wakati ana mkaribia tu baba yake, aliona mlango wa chumba alicho lazwa mama yake kitanda kilicho kuwa na mtu aliye funikwa kuanzia kwenye miguu mpaka kichwani kinatolewa na yule daktari akawa anatoka kwenye kile chumba
Daktari alipo muona David na yule mzee macho ya Daktari yalionekana kumkazia sana mzee Kazinge kwa muda kisha kumuangalia David aliye duwaa kukiangalia kile kitanda kilicho kua kinasukumwa kupelekwa asiko kujua, Daktari alipo maliza kuwangalia alisikitika
Kusikitika kule kwa daktari kulimpa wasiwasi mzee kazinge hakuelewa kwanini Daktari alifanya vile hivyo alibaki akishangaa tu,
Miguu ya David ilianza kupiga hatua ndogo ndogo kuelekea kwenye kile kitanda, kadri alivyo kuwa anazidi kusogea ndivyo mwendo ukawa unaongezeka na baadae mbio zikachukua nafasi.
Alifika kwenye kile kitanda na kuwasukuma baadhi ya manesi walio kuwa upande wake na kuufunua ule mwili uliokuwa umefunikwa, maskini wa mungu macho ya David yalianza kuwa na chemchem za machozi alipo hakiki kuwa mama yake ndio ameaga dunia,
Dokta alimpa pole sana David na baadhi ya manesi wakawa wanambembeleza na kumshika alivyokuwa anajitupa tupa chini kwa kumlilia mama yake kipenzi, uchungu alio kuwa anausikia David alihisi yupo kwenye mpaka wa uhai na umauti,
Mzee Kazinge naye akawa kajisogeza eneo lile kwa aibu kubwa iliyo mjaa usoni mwake japo ni kweli alikosea kwa kitendo kile cha kumpiga mkewe wakati anaumwa ila chozi la upendo mpevu lilimtoka wakati kitanda kile alicho bebwa marehemu Magrety kikipelekwa kwenye nyumba ya kuhifadhia maiti.
Mama Coolin alipo fika naye alikuta hali si shwari pale, hata maji yenyewe alio kuwa amefata aliya dondosha chini na kujumuika katika kilio hicho, baadhi ya watu walio kuwa wema waliwabembeleza na Daktari aliwaomba waelekee ofisini kwake akawape utaratibu na sababu za kifo cha mama David
Wakati wakielekea kwenye chumba cha Daktari, David alilia sana kumlaumu baba yake kwa kitendo alicho kifanya mpaka mama yake kupoteza uhai wake.ila hakuwa na jinsi ndio imesha tokea ilimbidi aendelee kulia kimyakimya tu kama mwanaume.
Walipofika tu ofisini kwa dakatari walikaribishwa na Dokta akaanza kuwa eleza,,
“Kwanza poleni sana kwa msiba ulio wapata ila hii ni sehemu ya maisha ya binaadamu hivyo hatuna budi kulikubali hili ambalo lipo mbele yetu lakini pia tumejitahidi kwa kila tunavyoweza kuajribu kuokoa maisha ya mgonjwa wetu lakini tumeshindwa maana mungu ndio mwenye uwezo zaidi”
“Lakini kikubwa kilicho sababisha kifo chake mbali na maradhi ya moyo aliyo kuwa nayo inaonekana alipigwa huyu marehemu maana damu imevia kwenye ubongo na hii ni hatari sana kwa uhai wa binaadamu”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Na swala hili hatuwezi kulifumbia macho hata kidogo kwa sababu kila siku vyombo vya habari vinatangaza juu ya matatizo kama haya na serikali ina mikakati migumu sana juu ya kesi kama hizi”
Daktari alipo maliza kuongea David alimwangalia baba yake kwa jicho la hasira sana na uso uliojaa udhia wa fadhaa mpaka Daktari alipo tia neno
“Bila shaka wewe ndie mume wa marehemu”aliuliza Dokta
“ndio mimi Daktari” mzee Kazinge alijibu lakini swali hilo lilimfanya ateseke kwa aibu
“Najua wewe ndie muhusika wa kipigo cha marehemu mkeo kwa maelezo niliyo nayo hivyo hatuna budi kukuchukulia hatua maana kama nitakuacha na maelezo ya kifo cha mkeo niliyo andika na weza nikafungwa mimi”Daktari alizungumza na alipo maliza alichuku simu yake ya mezani na kupiga,
“hallo afande nakuomba uje hapa ofisini kwangu”? alimpigia simu askari ambaye huwa alikuwa getini na bila kuchelewa alifika ofisini kwa Daktari na kupewa maelezo kisha akamfunga pingu mzee Kazinge na kuanza kumpeleka kituoni kwa kosa alilo fanya la kukiuka haki za binaadamu kwa kumsababishia mkewe kifo,
Huzuni ilizidi kutawala moyoni mwa Davidi kilio kiliongezeka moyoni mwake akawa anajilaumu kwa kumueleza Daktari ukweli ile asubuhi alipo muhoji maana alijua shida na mateso yataanza kuomba makazi katika familia yake,
Dakatari aliwapa utaratibu jinsi watakavyo weza kuchukua maiti yao kwa ajili ya mazishi,
Basi hapo hawakuwa na jinsi zaidi ya kuelekea nyumbani na kuwapa taarifa wengine juu ya msiba huo ulio wafika,
D avid alikuwa anajiuliza ni jinsi gani wadogo zake wata upokea msiba huo maana ndio wanabaki yatima mama ameaga dunia na baba gerezani kwa mara ya pili.
Ujio wao tu pale mtaani watu wazima walishaanza kuhisi kuwa kuna tatizo, David jicho lilikuwa jekundu na kilio cha kugugumia kiliendelea, mama Coolin naye ndala zake mkononi kanga iliyojikaza ikawa mkanda kwenye kiuno chake acha kile kilemba alicho jifunga kichwani kilicho timka timka, mwendo wa haraka uliwafikisha kwenye nyumba ya kina David,. Mayowe yakaanza kwa masikitiko ya majonzi kwa kuondokewa na mama yake, majirani wakaribu wakawa wanavutika na kilio kile amabacho kiliashiria kuwa ni msiba.
Ndani ya muda mchache tu taarifa za kufariki Magrety mama yake na David zikawa zimesambaa kijijini hapo Gairo, mama muksini naye aliposikia hakutaka kuwaambia kina Nisha pamoja na Dasoni alichokifanya ni kuwa shika mikono na kuelekea kule msibani,
walipo kuwa wana karibia walishtushwa na sauti za vilio ambavyo vilikuwa vinatokea nyumbani kwako, nisha alipo taka kuuliza kuna nini ghafla akamuona kaka yake david aki wakimbilia na huku akitoa machozi nao wakapokonyoka mikononi mwa mama muksini na kumkimbilia kaka yao.
walipokutana kati david akapiga magoti ili alingane nao urefu kisha kuwa kumbatia, aliwaangalia huku akivuta makasi ndani, hali ile ya huzuni aliyo onesha kwa wadogo zake ilizidi kuongeza simanzi kwao hasa alipo ongea maneno ambayo hata kama dasoni alikuwa mdogo aliweza kuelewa kuwa sasa ni yatima wa mzazi mmoja,,,,,,
“nisha mdogo wangu mama ameatucha wenyewe hatuna kimbilio sisi wadogo zangu, baba nae ndio hivyo…….” Aliongea maneno hayo kwa sauti ambayo lazima utadondosha chozi kama ukimsikia mpakashindwa kumalizia baba yake amefanya nini.
Mama muksini alimnyakuwa david pale alipo kuwa amepiga magoti na baadhi ya wazee wengine wakaja kumsaidia kisha waka mchukua david na kwenda kumbembeleza mama muksini nae hakuwaacha nisha na dasoni hivyo nae alienda kuwa bembeleza, kiukweli mama muksini alitokea kuwa penda sane watoto hao.
Maturubai yaliweza kufungwa watu wakawa wamejigawa wanawake upande wao na wanaume upande wao, stuli iliwekwa njia panda ya kwenda sehemu ya wanawake na wanaume hao kisha kiungo kidogo maarufu kama kitunga kiliwekwa juu yake kikiwa na picha nyingi za marehemu mama david ambazo zilipigwa alama x kumaanisha kuwa huyu ndie marehemu aliye fariki,
Mama muksini alimnyakuwa david pale alipo kuwa amepiga magoti na baadhi ya wazee wengine wakaja kumsaidia kisha waka mchukua david na kwenda kumbembeleza mama muksini nae hakuwaacha nisha na dasoni hivyo nae alienda kuwa bembeleza, kiukweli mama muksini alitokea kuwa penda sane watoto hao.
Maturubai yaliweza kufungwa watu wakawa wamejigawa wanawake upande wao na wanaume upande wao, stuli iliwekwa njia panda ya kwenda sehemu ya wanawake na wanaume hao kisha kiungo kidogo maarufu kama kitunga kiliwekwa juu yake kikiwa na picha nyingi za marehemu mama david ambazo zilipigwa alama x kumaanisha kuwa huyu ndie marehemu aliye fariki,
wengi wasio mjua marehemu walipita kwenye stuli hiyo na kutazama picha hizo wengi walisikitika na maneno mengi kuwatoka mdomoni mwao hasa walipo oona picha aliyo piga na familia yake ambayo aliyo wakumbatia watoto wake vipenzi,,,
“maskini watoto wake hawa wawili wadogo kweli sijui watakuwa kwenye mazingira gani? Alikuwa anajisemea mmama moja ambaye alikuwa akitazama picha hizo.
Muda ulivyozidi kwenda mkusanyiko ulizidi kuwa mkubwa hasa kwa habari zilizo zidi kusambaa kuwa amefariki kwa kipigo japo wengine walizungumza mengi ambayo yasio na ukweli kama vile, alifumaniwa ndio sababu ya kupigwa, lakini hayo yalikuwa ni maneno ambayo hutokea kwenye mkusanyiko wa watu au jambo ambalo lina utata. Ila walio jua walitulia tu wakitafakari msibao huo na nini cha kufanya.
Wazee wakaribu na marafiki wa mzee kazinge waliitana na kuweka kikao kutaka kujadili taratibu za mazishi bila kumsahau david pia alijumuishwa katika kikao hicho maana alishakuwa mtu mzima na alikuwa na uwezo wa kutoa maamuzi au kupinga jambo ambalo ataona si bora kufanyika,,,,
“Ndugu zangu tumekusanyika hapa ili tuweze kujua tunafanya nini juu ya msiba huu ambao umemfika mwenzetu wa kufiwa na mkewe na matatizo ambayo yeye yamemkuta wengi tumesikia sikia juu juu tu kama amekamatwa na polisi na yupo kule kwenye kituo kidogo kwa kosa la kumsababishia mkewe kifo jambo hilo ni kweli kwa maelezo ambayo tumeletewa na mwanamke huyu,,alimuonesha mama coolin.
“ ambayo yeye aliyapata toka kwa daktari walivyo kwenda jioni hii kwa ajili ya kupeleka chakula na hata waliweza kushuhudia maiti ya mama davidi ikipelekwa sehemu maaulumu ili kuuhifadhi mwili huo, mpaka taratibu zitakapo kamilika na kwenda kuchukuliwa kwa ajili ya mazishi” alizungumza mzee nyomolage ambaye alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kikao hicho kutokana na ukaribu alio kuwa nao kwa mzee kazinge.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“na kama mnavyo jua ndugu yetu mzee kazinge tumeishi nae hapa kwa miaka mingi sana na hana ndugu hapa na hakuna anayejua mawasiliano yao jambo tunalo lijua sisi in kuwa wazazi wake walikuwa wanaishi mkoani tanga na walisha faliki muda mrefu hivyo sisi ndio tumekuwa ndugu zake hatuna budi kubeba majukumu haya ili tumpumzishe mkewe mahali salama hata uko atakapo kwenda basi ahisi kweli alikuwa anaishi na binaadamu na sio watu na sasa nafikiri kikao kimeanza rasmi tuweze kusikia mawazo yenu tuyapatie ufumbuzi kwa haraka” hayo yalikuwa maneno ya mzee nyomolage ambaye alizidi kuonesha utu kwa familia ya mzee kazinge.
Kidole cha kwanza kilikuwa ni cha mama coolin ambaye alianza kwa kuchangi yanayo hitajika hospitali, alijifikicha macho yake kwanza na sauti iliyo karibia kukauka kutokana na kulia sana ilianza kuzungumza,,,,,
“jamani wakati tunampeleka mgonjwa hospitali hatukuweza kulipa chochote kile in msaada tu tulifanyiwa na yule daktari kutokana na hali ya marehemu ilivyo kuwa mbaya hivyo kuna kiasi cha fedha tunadaiwa ndipo pia tunaweza kuchukua mwili wa marehemu”wazo hilo la mama coolin lilisikilizwa na ufumbuzi ukatolewa na mtu akateuliwa kwenda kukusanya michango kwa waliohudhulia msibani.
“pia me nafikiri tungeweza kwenda kuomba ili hata mzee kazinge aje kumzika mkewe na kuona nana na familia yake huku akisindikizwa na akari nahisi tuna weza kukubaliwa kwa hili maana si mnajua kule alipo anaweza asitoke mpaka siku ya kwenda mahakamani na nchi yetu mnaijua hii sio chini ya miaka mitatu utasikia bado wapo kwenye uchunguzi” hilo lilikuwa wazo la mzee kombo.
Mawazo hayo yalijadiliwa na kupatiwa ufumbuzi na baadhi ya watu walichaguliwa ambao kesho ikifika salama basi watajigawa wengine watakwenda kulipia gharama za matibabu na kuuchukua mwili wa marehemu ambapo hata bajeti ya jeneza ilisha pigwa kutokana na kiasi cha michango kilicho patikana jioni hiyo iliyokuwa inaelekea magharibi na wengine watakwenda kuonana na mkuu wa kituo cha polisi ili mzee kazinge aweze kwenda kuhudhulia mazishi ya mkewe na kwenda kuwaaga familia yake na watakao baki watabaki kuchimba kaburi ambalo david alipendekeza lichimmbwe nyuma ya nyumba yao, na muda wa mazishi ulipendekezwa utakuwa na saa kumi na nusu jioni na watu wakatangaziwa yote yaliojili kwenye kikao hicho.
Mpaka kikao kinaisha watu waliweza kula kisha kila mmoja kujichukulia nafasi kwenye turubai na kuweka ubavu wake na wengine wakiendelea kuombeleza.
***************************
Sauti zile za mapambio zilizo kuwa zinaimbwa na wana mama ziliweza kuwaamsha walio lala pale nje kwenye maturubai na kuwa fanya waanze pilika pilika za kujiandaa ili kila mmoja ashike njia ya kwenda sehemu husika kukamilisha mambo aliyokuwa amepangiwa ndani ya saa kuminambili hiyo asubuhi,
Baada ya wote kukusanyika safari ikaanza kuelekea kituo cha polisi na hospitali, kwa bahati nzuri wote wakawa wamefanikiwa wale wa hospitali kuupata mwili wa marehemu na kuuhifadhi kwenye jeneza ambalo wali linunua nje ya hospitali karibu na jengo la kuhifadhia maiti kisha kurudi nao nyumbani na wale wa kituo cha polisi waliambiwa abaki mmoja ambaye watarudi wote ma gari la polisi mpaka kwenye mazishi.
Ilipofika mishale ya saa tisa maandalizi ya kuuwaga mwili wa marehemu yaka andaliwa na mapambio yakaanza kuimbwa na wanakwaya ambao walialikwa na padri nae akawa anafungua biblia yake kutafuta maandiko matakatifu ambayo ataweza kuyasoma kwenye hadhara hiyo iliyo kusanyika msibani hapo na baada ya muda aliweza kuyapata na kwaya ikasimama na maandiko matakatifu ya kaanza kusomwa,,,,,,,
“kwa jina la baba na la mwana, alitoa ishara ya msalaba kisha kuendelea,hakika kila mpandaji mazao atavuna kile alicho kipanda na bwana mungu wetu leo amevuna kwenye familia hii ya mzee alfredy kazinge ili kukamilisha kazi yake kutokana na tukio hili na maana ya sisi kukusanyika hapa ili tujifunze kuwa na sisi siku moja tutalala hapa mbele na kusomewa kama huyu marehemu ndugu yetu magrety john tumuombe bwana mungu wetu atuepushe na madhambi ambayo tuna yafanya amina”
padri alimaliza kutoa neno na funzo kwa walio hai ili waweze kujifunza kupitia mwili wa magrety ambao uliwekwa mbele pamoja na picha yake kubwa aliyo kuwa ameipiga enzi za uhai wake, wakina david pamoja na wadogo zake walinyolewa vipala kama wafiwa na kuvaa nguo zao nyeusi kisha kuketi kwenye viti vya mbele ambavyo viliandaliwa na kutazama jeneza lala mama yao.
Padri aliweza kutoa ruhusa ya kuungalia mwili wa marehemu magrety kwa mara ya mwisho ili kuelekea kwenye njia ambayo inaweza kumpeleka motoni au peponi kutokana na matendo aliyo kuwa anayafanya enzi za uhai wake.
Watoto wa marehemu waliweza kushikiliwa katika kipindi hicho kigumu cha kuuaga mwili wa mama yao kipenzi, hasa david ambaye alikuwa anafikilia mambo mengi kama mzigo ambao alio achiwa wa kulea familia akiangalia ndio kwanza ametoka kumaliza kidato cha sita na matokeo hayajatoka na kazi hana jambo hilo lilimuongezea sana sononeko moyoni mwake,
Waliomshikilia waliianza kushindana nae nguvu alipo nga’ang’ania kwenye mwili wa mama yake huku akiushika kwenye paji la uso na kuutikisa huku akiuuambia,,,
“mama amka mama mi najua umelala tu mama yangu amka basi utuone wanao tunavyo hangaika na machozi kututoka kwa huzuni unayo tuachia” maneno hayo yaliwafanya hata walio mbali kusogea eneo ambalo walilo kuwa wanaagia mwili huo baada ya kusikia sauti ya david ikiongea na maiti tena kwa masikitiko.
ghafla vumbi na upepo mkali ukaanza kutanda eneo hilo na hali ya hewa ikaanza kubadilika, mbigu juu ikaanza kuwa nyeusi kutokana na mawingu yalio kuwa yameanza kutawala ikabidi zoezi la kuaga lisitishwe na watu wakabeba jeneza kuelekea nyuma ya nyumba ambapo ndipo kaburi lilipo chimbwa na hapo watu wakatumbukia ndani ya kaburi kulipokea jeneza hilo na wengine wakibaki juu kulishusha kwa kamba ambayo ilipitishwa pembezoni mwa jeneza hilo.
“baada ya zoezi hilo kukamilika watu walio kuwa ndani ya kaburi walitoka kisha padri akasoma harakaharaka kisha kuchukua udongoulio kuwa kwenye chepeo na kuanza kuumimina juu ya jeneza hilo ambalo lilishwa tumbukizwa kwenye kaburi na kumalizia na maneno haya,,,,
“wewe in vumbi na utarudi kuwa vumbi jina la bwana lihimiliwe” sauti za watu zilisikika zikijibu amin.
Kisha chepeo lenye udongo kugeuzwa kwa david naye akachota udongo kabla hajaweka udongo tu kwenye kabuli alishtushwa na sauti ya gari lililokuwa linakuja kwa kasi eneo la kaburi hilo lakini kabla halija simama alimuona baba yake akiwa na pingu mkononi akiruka kwenye gari kabla hata ya askari kushuka kwenye gari hilo la polisi na kuanza kukimbia huku akilalamika kwa sauti akimuomba magrety amsubiri, lakini kila mmoja hakuamini kwa alicho kisikia maskioni mwake in baada ya kusikia mlio wa risasi aliyo pigwa mzee kazinge na askari aliye dhani kuwa anataka kutoroka kupitia umati ule wa watu david hakukubali
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Aliuchukua ule msalaba alio kuwa ameushika mtu aliye mpokea wakati yeye akiweka udongo kwenye kaburi na ndio ikawa silaha yake, alimtazama yule askari aliye mpiga risasi ya mguu mzee kazinge na kuaanza kumfuata kwa kumkimbilia alipomsogelea alinyakuwa ule msalaba kwa kunguvu zake zote iliampige nao kichwani lakini jambo hilo halikufanikiwa baada ya askari wenzie kuudaka msalaba huo na kumshika david kwa kumbana mikono yake kwa nyuma,,
Uso wa david uliiva kwa hasira kila alipofikiria jinsi mama yake alivyo patwa na umauti na matatizo yalio mpata baba yake, kiukweli mambo hayo yote yaliweza kumpunguzia david moyo wa ubinaadamu na maneno yalioufanya mioyo ya maskari wale kupanda kooni lakini wakuwa na lakufanya,,,
“mtu malize wote sasa si ndio kazi yenu inavyo watuma kupiga risasi ovyo kwa wananchi wenu?
“elimu yenu inawasaidia nini sasa hakuna mncho kumbuka juu ya wananchi zaidi ya kuwapa kesi hata kama hawana hatia nimalizeni kama mnajua sana kupiga risasi ni uweni nasema piga hiyo risasi yako mbona unachelewa, fikirieni in mzigo gani nilio kuwa nao hii yote imesababishwa na nyinyi kuto kuwa makini na kufuatilia mambo kwa undani zaidi.”
Malumbano yaliendelea na baadhi ya watu hawa kujua lakufanya kutokana na mshtuko wa risasi na zile vulugu zilizo kuwa zinaendelea pale kaburini, wengine walikimbia kwa kuhofia maisha yao,mtawanyiko huo wa watu walishindwa kuelewa mzee kazinge yuko wapi na hali yake ikoje,
Kumbe baada ya kupigwa risasi ile ya mguu pale alipokuwa ameangukia aliweza kujivuta taratibu mpaka kwenye kaburi la mkewe na kujitupa mle ili wazikwe wote maana alihisi anastahili kufa kwa mateso anayo yapata kwa miaka yote tena bila sababu ya msingi.
Watu walirudishwa tena mahali pale lilipo kaburi la mama davidi baada ya manyunyu ya mvua kuanza hata davidi aliachiwa na wale askari, hapo ndipo walipo gundua kuwa mzee kazinge yupo mle ndani ya kaburi,,,,,
“jamani hii familia kama mungu haioni vile in misuko suko kila kukicha eeh mungu wasaidie hawa,,
“Mmh inatia huruma kwa kweli watazame watoto wake walivyo kuwa na huzuni “
Hayo maneno yaliwatoka watu tofauti katika eneo hilo na wakati huo wakina mzee nyomolage walitumbukia ndani ya kaburi na kumtoa mzee kazinge, taarifa ziliweza kuwafikia mapaparazi ambao walitoka kwenye kwenye vituo tofauti tofauti kama vile redio,magazeti na hata wale wa televisheni ili kukusanya habari hiyo amabayo walijua kuwa lazima itawapatia pesa ya kutosha kutokana na uzito watukio hilo picha nyingi zilipigwa ili kupendezesha magazeti..
Padri aliamrisha wazike maana mvua ilianza kuwa kubwa watu walimfukia mama david kwa haraka ili mvua ile iliyo kuwa inanyesha isije ikaleta balaa lingine wakashindwa kuufukia mwili wa marehemu magrety.
David alilia sana maana hakuamini kama mama yake ndio safari yake imefika mwisho,
Wale askari walimshikilia mzee kazinge ambaye alikuwa anavuja damu kwenye mguu ule ulio kuwa umepigwa risasi, mama muksini nae hakuwaacha watoto wake nisha na dasoni.
Hayo maneno yaliwatoka watu tofauti katika eneo hilo na wakati huo wakina mzee nyomolage walitumbukia ndani ya kaburi na kumtoa mzee kazinge, taarifa ziliweza kuwafikia mapaparazi ambao walitoka kwenye kwenye vituo tofauti tofauti kama vile redio,magazeti na hata wale wa televisheni ili kukusanya habari hiyo amabayo walijua kuwa lazima itawapatia pesa ya kutosha kutokana na uzito watukio hilo picha nyingi zilipigwa ili kupendezesha magazeti..
Padri aliamrisha wazike maana mvua ilianza kuwa kubwa watu walimfukia mama david kwa haraka ili mvua ile iliyo kuwa inanyesha isije ikaleta balaa lingine wakashindwa kuufukia mwili wa marehemu magrety.
David alilia sana maana hakuamini kama mama yake ndio safari yake imefika mwisho,
Wale askari walimshikilia mzee kazinge ambaye alikuwa anavuja damu kwenye mguu ule ulio kuwa umepigwa risasi, mama muksini nae hakuwaacha watoto wake nisha na dasoni.
Upepo ulizidi na mvua ikawa kubwa na weusi ulio sababishwa na mawingu ukawa umetawala kijijini hapo na bahati nzuri zoezi la mazishi likawa limeisha japo kwa shida watu walitawanyika kuikimbia mvua ile, askari nao wakataka kuondoka na mzee kazinge lakini mzee kazinge aliomba azungumze na wanae hasa david ndipo alipoitwa david baada ya mama muksini kuondoka na kina nisha kwa kuwa wale ni watoto na hali ile ya hewa ingeweza kuwaletea homa,
”David mwanangu hakika umeelewa binaadamu walivyo naomba ujifunze kupitia matatizo haya penda kuwa mtu wa kusikiliza na kuongea kidogo tu ili uweze kuwajua wabaya wako, usiwe na papala kutaka kupata mali zako fuatilia taratibu iliuweze kukamilisha ushahidi utakao weza kuwarudisha tena nyinyi katika maisha mazuri ambayo mwanzo mimi nilikuwa naishi, sasa nakuruhusu nenda mjini karudishe mali zako wewe na wadogo zako nakukabidhi famulia hii uilee kadri utakavyo weza ili wasije kupata machungu zaidi pale watakapo tukumbuka sisi na ukifika huko mtafute yule mama anayeitwa magdalena ambaye aliniambua kuwa anaushaidi utakao weza kurudisha mali zenu nakutakia kazi njema na maisha mema uwezekano wangu wa kutoka gerezani ni mdogo sana kwaheri mwanangu wasalimie wanangu waambie nawapenda sana”
Alipo maliza tu kusema askari nao wakamkokota mpaka kwenye gari lao kisha kuondoka nae david hakuwa na cha kufanya zaid ya kuangalia tu lile gari huku moyo wake ukiwa umesha badilika kuwa wa simba kwa yeyote atakaye leta mchezo na familia yake. Mvua ile kubwa iliyo kuwa inamnyeshea ilikuwa in kama vipande vya barafu ambavyo vina peperushwa na upepo hakujali jambo ilo mpaka watu wazima walipo kwenda kumtoa pale kwenye ile mvua kwa nguvu,
Akili ya david ilikuwa imesha changanyikiwa kwa matukio ambayo yamemtokea mfululizo tena yalikuwa chini ya umri wake lakini hakuwa na budi kukubaliana nayo ili ajue wapi anaanzia, mpaka pilika pilika zote zinaishia ilikuwa tayari imeshatimia mishale ya saa kumi na mbili jioni, hivyo kutpokana na ile mvua wengi walikwenda majumbani kwao ila wale walio kuwa karibu na familia ile ndio walio baki kwa kina david kuwa fairiji kama vile mama coolin, mama muksini kina mzee nyomolage na wengine,
Baada ya siku tatu swala la msiba likawa limeisha kilicho baki ilikuwa in kujua kuwa wata wasaidia vipi wale watoto hasa nisha na dasoni amabo walikuwa wadogo maana david anakabiliwa na majukumu mazito ya kutaka kurudisha haki ya familia yake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mama muksini hakuchoka alijitolea kuwa chukua na kuwalea lakini akasema kwa sasa mume wake hayupo yupo safari kwa muda wa miezi sita sasa maana anafanya kazi katika mbuga za wanyama hivyo huchukua muda mrefu mpaka kurudi lakini kwa sasa hana muda atakuwa amerudi baada ya siku kama nne hivi mbele hivyo atazungumza nae ili ajue na yeye atalipokea vipi na kama atalikubali jambo hilo basi atakaa nao na kujitahidi kuwa somesha mpaka pale mungu atakapo wasaidia kupata kazi yao.
Wote walikubaliana juu jambo hilo david alikuwa hana chakusema zaid ya kuwasikiliza tu japo kichwani mwake alikuwa anaonekana kufikiria jambo fulani ambalo hakutaka kuliweka wazi kwa wakati huo mbele ya hadhara ile ya watu wake wakaribu,
Sikuzilikatika na bwana wa mama muksini akawa karejea kutoka ile safari yake aliyo kuwa amekwenda alipo fika tu nyumbani kwake aliwakuta kina nisha na dasoni wana jilia chakula cha mchana jinsi alivyo kuwa na roho mbaya baba ya huyu japo alizipata taarifa za msiba na matatizo waliyo yapata watoto hao alidiliki kumuita mke wake na kumuuliza swali mbeye ya watoto hao mke wangu kituo hiki cha kulelea watoto yatima kimesajiliwa lini maskini wa mungu nisha alipaliwa na chai kusikia maneno yale ya kejeli
“mume wangu maneno gani hayo unazungumza mbele ya hawa watoto ndio kwanza umetoka safari si ungepumzika kwanza kisha tuyazangumze vizuri’?mama muksini alimwambia mumewe
Ghafla mama muksini kalamba kibao cha uso aja kaa sawa kasukumwa aelekee chumbani, nisha kuona vile akanyanyuka na kumshika mkono dasoni wakakimbia mama muksini alipo taka kuwa fuata mumewe akamzuia na kumpa maneno ya vitisho,,,
“kama utathubutu kutoa mguu wako hapa ndani na kuwafuata wale watoto jua kwamba ndio umevunja pingu tulio funga mimi na wewe, nimekaa mimi na wewe miaka kibao hapa hata kusema mume wangu leo nimejisikia kichefuchefu hakuna halafu unataka kuniletea vipaka vyako hapa ndani baradhuli mkubwa wewe”
Mama muksini matumaini yake ya kutaka kuwalea kina nisha yaligeuka na kuwa fadhaa, kilio kikamsindikiza mpaka chumbani na huko kukawa hakuna neno walilo kuwa wanazungumza zaidi ya mumewe kumsema tu kwa kujichukulia maamuzi kama yeye ndie mtafutaji.
Nisha akawa anamkimbiza dasoni waelekee nyumbani kwao lakini hakika mwenyezi mungu in mkubwa na alipangalo yeye hakuna anayeweza kulipangua na watu wanaweza kushilikisha maamuzi yake na uchawi kama tatizo likielemea kwenye famila moja wakati,
Walipo kuwa kwenye mwendo huo ambao ulisababishwa na kitendo kilichofanywa na mume wake mama muksini cha kuongea kauli za kuwanyanyapa watoto wale na kumpiga mkewe kwa sababu yao kiliwafanya kutokuwa makini wakati wakikimbia maana machozi pia yalikuwa yanawatoka kwa hasira punde si punde sauti iliyokuwa inaomba msaada ilisikika,,,,
“mama nakufaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!”
Hapohapo na sauti za vioo vya gari lile kubwa lililo kuwa limepakia viazi vilisikika vikivunjikavunjika, watu wengi walionekana kukimbilia eneo lile kutaka kujua nini kilichotekea huko.
“”ajali jamani ajali mungu wangu ni wakina nani hawa” watu walikuwa wanazungumza
Baada ya watu kuwa wengi na kulizunguka gari lile lililo ingia mtaloni na kuona maiti ya mtoto mmoja wakiume baadhi ya watu walio kuwa wamemjua mtoto huyo waliangua kilio papo hapo na kila mmoja yalimtoka mengi mdomoni,,,,
“Kijiji hiki kina wachawi sana wamewakosea nini familia hii ni juzi tu tumetoka kumzika mama yao leo mtoto huyu naye ameaga dunia”
“Maskini dason ameaga dunia bila hatia”
“Nani ameaga dunia? Mtu mmoja aliuliza alihisi kama amesikia vibaya vile,
“ ni dasoni mtoto wa mzee kazinge”
jamaa yule alivyosikia vile alitimua mbio kumfuata david nyumbani kwao na alifika haraka sana maana hapakuwa mbali sana na ajali ilipo kuwa imetokea, alinzaa kugonga huku akihema,
“david david david!!!!
Kila alipo kuwa anaita akawa hajibiwi akaamua kuchungulia dirishani hakuamini alicho kiona kitu alicho kuwa anataka kukifanya david,,,,,
We david nakuomba usijiue rafiki yangu, nakuomba sana sio kitu kizuri unachotaka kuki fanya kwa wakati huu fikiria wadogo zako, kwanza mguu huu nimekuja kwako kunatatizo limewapata wadogo fanya haraka twende acha hicho unacho taka kukifanya hakina faida nakuomba…
David aliachia kikombe kile kilichokuwa na maji machache na kuzimwaga dawa zile zilizo kuwa mchanganyiko kwa mshangao baada ya kusikia wadogo zake wamepatwa na tatizo, alizubaa kwa muda na kukurupuka kufungua mlango kisha kutoka nje yule jamaa akampokea mlangoni na kuanza kukimbia nae mpaka kwenye tukio lile
Alifika pale na kuukuta mwili wa mtoto mdogo umefunikwa na kanga alipo ufunua alimkuta dason,,
Maskini wa mungu david alilia kama mtoto mdogo vile, makamasi yalishuka mpaka mdomoni mwake ghafla akamkumbuka nisha,,
“Nisha wangu yuko wapi jamani”
“ nisha dada uko wapi njoo dada umejificha wapi”??
david akawa anaita huku anazunguka kila upande watu hawana la kufanya maana wengine wakujua kama watoto hao wapo wawili ila baadhi ya watu walio kuwa wana mjua wakawa wazunguka kwenye majani kumsaidia kutafuta na wengine wakajumuika pia,,,
“jamani kuna mtoto wa kike huku ila bado anahema” mzee mmoja alifanikiwa kumuona nisha.
David ilimbidi aelekee kule alipofika alimkuta nisha kaumia vibaya baada ya vioo vile kumchana mgongoni na vingine kung’a ng’ania mwilini mwake watu hawakua na muda wa kupoteza wakamkimbiza nisha hospitali na kumuacha david pale na maiti ya dasoni.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tarifa ziliwafikia kina mama muksini na mumewe hofu ikatanda kwao, mzee nyomolage naye aliyekuwa shambani kwake aliweza kupata taarifa hizo naye aliwahi kufika kwenye tukio ambapo alikuta polisi wameshafika pale wakifanya taratibu zao ambapo iligundulika kuwa na dereva wa gari hilo naye amefariki dunia.
Hivyo polisi walitoa agizo kuwa wanandugu waka zike maiti ya mtoto huyo dason maana ilikuwa imeharibika vibaya na isingeweza kukaa mudamrefu ingeaza kutoa harufu,
Hawakua na budi kufanya hivyo taratibu zote zilifuatwa kaburi lilichimbwa pembeni ya mama david na david kwa mara ya pili alibeba msalaba wa mdogo wake.
Dasoni alifukiwa akawa amemfuata mama yake mbele za haki yani ikawa pigo ndani ya pigo.
David alizidi kuisha kiafya kutokana na mambo yalio kuwa yanamkabili na hakuwa na msaada wa maana japo alishukuru kwa moyo waliouonesha kina mzee nyomolage juu yake,
Usiku na mchana ulipokezana na siku zikasogea nisha naye akawa ametolewa hospitali na kupewa taarifa juu ya kifo cha dasoni kiukweli alilia kama msiba ulikuwa unaanza upya vile.
Wazee walikaa kikao nakulijadili swala la msiba ulivyo mfika dason hali ya kuwa alikabidhiwa mama muksini. nisha ilimbidi kueleza kilichotokea, na ndipo wanakijiji wakafikia muafaka kuwa watamtenga mume wake na mama muksini.
Wakati kikao kilipo kuwa kinakaribia mwisho alikuja afisa mmoja ambaye alijitambulisha na kusema kuwa ametoka mahakama ya wilaya akawapa barua kuwa mzee kazinge atafikishwa mahakamani kesho hivyo wanaombwa familia yake kufika huko
Wazee hao waliipokea barua na kuisoma na muda uliwaonesha kuwa saa saa tatu asubuhi wanahitajika kwenda kusikiliza hukumu ya alfredi kazinge katika mahakama hiyo ya wilaya
****************
Adhana ya saa kumi na moja alfajiri iliyokuwa inawakumbusha waislamu kwenda kufanya ibada iliweza kumuamsha david toka usingizini na kuegemea mto ulio kuwa kitandani na kuonekana akitafakari jambo fulani hivi ambalo liliweza kumyanyua pale kitandani na kuelekea chumbani kwa wazazi wake.
Aliwasha mshumaa ili aweze kupata mwanga kisha kufungua sanduku dogo ambalo lilikuwa limewekwa chini ya uvungu wa kitanda na kutoa baadhi ya makaratasi ambayo yalikuwa na picha ndogo ya mzee kazinge kwa juu upande wa kulia.
Aliyangaalia kwa makini maelezo yale ambayo yalikuwa yanaonesha uhitimu wa chuo kikuu cha biashara ambacho alisoma mzee kazinge, kisha akatoa albamu ya picha na kuanza kuzitazama moja baada ya nyingine alitoa tabasamu kidogo baada ya kuona picha ya baba yake kwa mavazi ya kizamani aliyokuwa amevaa lakini hali hiyo ilibadilika ghafla baada ya kuona picha aliyo piga baba yake na marehemu mama yake siku ya ndoa yao,
David hakusita kupeleka kiganja chake cha mkono kwenye sura ya marehemu mama yake nakuanza kukizungusha juu ya picha hiyo, alikumbuka upendo wa marehemu mama yake tangu alivyo kuwa hai mpaka umauti unamfika hivyo aliinyakuwa picha hiyo mpaka kwenye mdomo wake na kumpa busu la heshima mama yake na baada yapo akatoa ishara ya msalaba iliyomaanisha pumzika kwa amani.
Alizibeba baadhi ya picha kama kumbukumbu na kuelekea chumbani kwa nisha, aliufungua mlango taratibu bila kuingia ndani akawa anamwangalia mdogo wake kipenzi aliye bakia, alihuzunika baada ya kutupa macho kwenye kitanda cha pembeni ambacho alikuwa analalia marehemu dason, david alishindwa kuvumilia aliufunga ule mlango kisha kuelekea chumbani kwake.na kuziweka zile picha kwenye mkoba wake na kutoka nje kuandaa kifungua kinywa cha asubuhi ili waweze kuelekea mahakamani muda utakapo wadia.
Alizibeba baadhi ya picha kama kumbukumbu na kuelekea chumbani kwa nisha, aliufungua mlango taratibu bila kuingia ndani akawa anamwangalia mdogo wake kipenzi aliye bakia, alihuzunika baada ya kutupa macho kwenye kitanda cha pembeni ambacho alikuwa analalia marehemu dason, david alishindwa kuvumilia aliufunga ule mlango kisha kuelekea chumbani kwake.na kuziweka zile picha kwenye mkoba wake na kutoka nje kuandaa kifungua kinywa cha asubuhi ili waweze kuelekea mahakamani muda utakapo wadia.
Kabla ya masaa machache mbele kuelekea mahakamani walikuwa wamesha maliza kupata kifungua kinywa yeye na mdogo wake na mzee nyomolage akawa amewapitia kuelekea mahakamani ambapo kulikuwa na umbali kiasi kutoka nyumbani kwako hivyo walipanda bajaji ili kukimbizana na muda kama ulivyooneshwa kwenye barua ile.
*******************
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kooooooooooooooooooooooooooooti”’ sauti iliyo kuwa inawaandaa walio kuwa mahakamani ilisikika na watu walinyanyuka mlango wa hakimu ulifunguliwa na hakimu akatoka na kugonga nyundo moja mezani na kesi ikawa inaanza baada ya upande wa mshtakiwa mzee kazinge kupandishwa kizimbani.
Mzee kazinge alivyo kuwa kizimbani alipepesa macho huku na kule ndipo alipo muona mzee nyomolage ambaye nae alitoa ishala kuwa tupo pamoja lakini alionekana kujiuliza dason yuko wapi maana kwenye benchi lile aliweza kumuona nisha na david tu, wakati akiendelea kutafakari alishtuliwa kwa kuulizwa swali
“wewe ni dini gani”
“Mkristu wa romani katoliki”alijibu mzee kazinge na kukabidhiwa biblia kisha kuambiwa ainyakue juu kwa mkono wakulia na afatishe manen haya,,
“mimi alfred kazinge naapa kuwa nitakacho kisema in cha kweli ukweli mtupu mungu nisaidie”
Hivyo ndivyo mzee kazinge alivyo apishwa na kesi ikaunguluma takribani masaa sita mpaka mzee kazinge kukutwa na hatia ya kusababisha kifo cha marehemu mkewe magrety, japo ingeweza kuwa kesi ya kuua bila kukusudia lakini kutokana na kukosa wakili wa kumtetea nyundo za kifungo cha maisha zikagongwa na askari kwenda kumtoa pale kizimbani kisha kumfunga pingu mikononi mwake na kuelekea nje kwenye gari la polisi ili kupelekwa gerezani morogoro mjini ambako ndipo yatakuwa makazi yake mapya yenye shida na kila taabu amabayo umewahi kuisikia.
Maaskari walipo kuwa wanashusha nae ngazi za mahakamani hapo mbele walimkuta david akiwa kamshika nisha mkono huku akilengwalengwa na machozi lakini nisha alishindwa kuyazuia hivyo yakawa yanatoka kama maji kufuata mkondo wake.
Askari hao waliweza kumpa muda mchache wa kuzungumza na familia yake,,
“david,, dason yuko wapi?
Aliuliza mzee kazinge na david hakuwa na cha kumjibu kutokana na uchungu alionao ambao ulimfanya mpaka kushindwa kuongea hivyo alibaki kumwangalia nisha tu ambaye alizidi kulia tu.
Ndipo mzee nyomolage alipo msogelea mzee kazinge na kumshika begani na kumueleza kwa utaratibu,,
“pole sana mzee mwenzangu kwa matatizo haya, dason naye tumpe mpoteza kwa ajali ya gari”
Mzee kazinge alinyakuwa miguu yake bila kupenda na kuelekea kwenye gari la polisi huku akicheka kicheko ambacho kilichanganyika na kilio ndani yake, kwa mtazamo tu wa wale maaskari walijua hii tayari ni dalili ya kuchanganyikiwa hivyo waliwasha gari lao na kuwaachia kina david wingu la mavumbi usoni mwao.hapo mzee nyomolage akawachukua na kuanza safari ya kurudi nyumbani kwao.
Walifika mishale ya saa kumi na moja jioni hivi hivyo mzee nyomolage akajipigapiga mfukoni mwake na kwenda kuwanunulia chakula mgahawani ili wapate nguvu na kweli waliweza kula kwa maneno ya faraja aliyo kuwa anawapatia mzee huyo kuwaahidi kwamba ataishi nao hapo nyumbani kwao kama baba yao.
Kiza kilipokuwa kinaanza kuchukua nafasi mishale ile ya kuelekea saa kumi na mbili david alizunguka nyuma ya nyumba yao ambapo kulikuwa na makabuli ya mama yake na mdogo wake dason. Alifika na kukaa katikati ya makabuli yale mawili na kutoa mchozi wa hasira huku akiongea maneno ya kisasi,,,,
“ mama na dason najua kuwa miili yenu isingeweza kufukiwa hapa kama mwanaharamu helman asinge msababishia baba matatizo kwa tamaa zake za pesa, mimi kesho naondoka hakika haki hii iliyopotea mikononi mwenu itarudi mikononi mwetu na heshima ya baba itarudi kwamba hakuhusika na ujambazi wa fedha za benki naombeni mlale salama kwa amani nitazidi kuwa ombea amin.”
David aliweza kuzungumza na makabuli yale akiamini kuwa mama yake na mdogo wake wanamsikia alichukua udongo wa kaburi la mama yake na wa kaburi la dasoni kisha kuuchanganya pamoja kama ishara ya upendo kwake hata huko walipo waweze kuonana kwa imani aliyo kuwa anaamin.
Wakati ananyanyuka na kujikung’uta vumbi la pale chini alipo kuwa amepiga magoti alimuona mzee nyomolage nyuma yake kumbe alimsikia yote aliyo kuwa anayazungumza ndipo mzee huyo alipoanza kumpa nasaha,,,,,,
“david mwanangu ni mapema mno wewe kuondoka hapa maana bado akili yako haija tulia sawa sawa na pia jambo hili linahitaji mipango ya hali ya juu sana kutokana na uzito wake hivyo tafadhali subiri kwanza tafadhali”
Wakawa wanazungumza huku kuelekea ndani lakini david yakawa yanaingilia huku yana tokea kule aliona kama mzee huyu anamchanganya zaidi maana hakuna kilicho baki zaidi ya kwenda kumtafuta helman tu.
“mzee kwa unachozungumza mimi siwezi kubaki hapa tena kitakachotokea kitajulikana mbele ya safari nita jua tutakula nini na tutaishi vipi mimi na mdogo wangu nisha”
“nisha? Mzee nyomolage alishtuka kusikia kuwa david anataka kuondoka na nisha
“David tafadhali nakuomba ni bora kama umeamua kweli unataka kuondoka nenda mwenyewe nisha muache mimi nitakaa nae huyu utaenda kupata nae shida kumbuka kuna maradhi na ujangili wa kila haina huko unakoenda fikiria huna hata pakufikia mtaishi vipi?
Mzee huyo alimueleza david lakini david hakuelewa akamwambia,,,
“ kama muda wakulala ukifika utalala kule chumbani kwangu na pia kesho nikiondoka nakuomba utulindie nyumba yetu” david aliingia chumbani kwa wazazi wake na kufunga mlango kwa hasira.
Mzee nyomolage kutokana na ukaribu aliokuwa nao na mzee kazinge hivyo alijitolea kuchukua majukumu ya ubaba na kuanza kumkemea david pale mlangoni,,,
“david hilo swala la kuondoka na nisha halitowezekana hata kidogo tambua hata baba yako alikukataza wakati ule kuhofia uhai wako mpaka akaamua kukupa siri ambayo hukuistairi kuijua kwa wakati ule nasema nisha atabaki na mimi hapa”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
David mle chumbani aliko kuwa amekaa alijiziba maskio asiweze kusikia kile alicho kuwa anazingumza mzee nyomolage lakini kutokana na sauti ile ya ukali maneno yaliweza kupenya kwenye ngoma zake za skio na alipoona mzee yule kamaliza kuongea aliinama chini na kuvuta kile kisanduku na alipo kifungua alitoa kiasi cha pesa kisicho pungua laki moja na nusu ambacho zilikuwa zinahifadhiwa na marehemu mama yake kisha kusema kwa furaha kiasi,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
“pesa hizi hakika zitatosha kutufikisha da es saalam inabidi kesho niamke asubuhi na mapema kisha kutoroka na mdogo wangu
Alipomaliza kujifariji juu ya mpango wake wa kutoroka kutokana na kiasi hicho kidogo cha fedha alichonacho lakini kwake kilikuwa ni kikubwa alipanda kitandani na kuanza kulifikiria jiji lenye kila sifa, na kila mtoto anayezaliwa basi hutamani kufika mahali huko, japo swala la kuwa atafikia wapi lilikuwa linamchanganya hilo hakujali kwa wakati huo, pia alijitahidi sana kutafakari kwa uzito kuhusu nisha akawa anawaza kwa kina,,,
“ndani ya ardhi ya kijiji hiki nimesha zika watu wawili muhimu huku nikishuhudia kwa macho yangu, vipi nikiondoka nikimuacha nisha hapa si ndio hata kaburi lake sito liona kabisa?
“hapana mzee nyomolage, kwa hili naomba unisamehe sana kwa kweli najua unalengo zuri na sisi lakini siwezi kumuamini yoyote yule kwa sasa lazima niondoke na mdogo wangu maana huyu ndie mama niliyebaki naye”
Baada ya mawazo hayo aliyokuwa anawaza na kujiuliza maswali kisha kujijibu mwenyewe alivuta pumzi ndefu na kuiachia, alitega maskio yake nje kwa muda akagundua kuwa pako tulivu sana, akajikusanya kisha kupiga hatua mpaka mlangoni nakuufungua kwa taratibu iliusipige kelele ambazo zinaweza kumuamsha mzee nyomolage,
Alitoa kichwa kwanza akachungulia pale sebuleni na kwambali akasikia sauti ya mzee nyomolage ikikoroma kule alipo lala, ndipo alipotoa mwili mzima na kunyata kwa uwangalifu kuelekea chumbani kwa nisha, alipo fika alianza kumtikisa nisha ili aamke,,,,,
“nisha nisha nisha??,
“abee” nisha aliitika kwa mshtuko
“shiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii” david nae alimfanyia ishara ili atulie na kuanza kumpa maelekezo.
“sikia nikwambie mdogo wangu kesho alfajiri sane jogoo la kwanza tu inabidi uwe umesha amka na uweke nguo zako mbili tatu kwenye mkoba wako mdogo ilituanze safari”
“tunaenda wapi kaka? Nisha aliuliza
“ we fanya kama nilivyo kuagiza na usije kujiandaa kwa kelele maana sitaki huyui mzee ajue kama tunaondoka hivyo kuwa mwangalifu kwa hilo sawa mdogo eeh”
“Sawa kaka”
“haya pumzika na mimi ngoja nika lale usiku mwema” maelekezo hayo yalionekana kueleweka kwa nisha hivyo david nae akaelekea kulala.
**********************************
Sauti za mbwa walio kuwa wanabweka pamoja na zile za ndege wa usiku ziliweza kuusindikiza usiku huo ambao ulikuwa unasubiriwa kwa hamu na david uweze kuisha,
hivyo ulikuwa ni muda mzuri wa david kujiandaa na kuhakikisha kama pesa zipo salama na zimetimia, alipo hakiki hilo hakuwa nahaja na kitu kingine maana nguo zake zilikuwa chumbani kwake ambapo mzee nyomolage amelala.
Alipofungua mlango wa chumbani kwake ili atoke nje akamuamshe nisha alijikuta akiachia tabasamu baada ya kumuona nisha pale mlangoni kuwa amesha jiandaa na ndio alikuwa anataka kumgongea kaka yake ili waanze safari ambayo yeye hakujua wanaelekea wapi lakini aliamua kumtii kaka yake maana akijua ndio kimbilio lake kwa wakati huo,
Walifanikiwa kufungua mlango mkubwa wa kutokea nje bila ya mzee nyomolage kusikia chochote na safari ikawa imeiva chini ya mbaramwezi na nyota zile za alfajiri ambazo zilikuwa zinaishia ili kulipisha jua.
Walitembea kwa mguu umbali mrefu kidogo mpaka kufika kituo kidogo cha mabasi madogo yaendayo morogoro mjini na bila kuonwa na mtu yoyote yule ambaye alikuwa anawafahamu,walipowasili tu kwa bahati nzuri waliweza kupata kiahisi kimoja ambacho kilibakiza siti tatu tu ili kianze safari hivyo yeye na nisha pamoja na abiria mwingie waliweza kumalizia nafasi hizo na gari kuondoka.
Ndani ya saa moja na nusu tu walianza kuona magari mengi barabarani yakiwa kwenye foleni,,umati mkubwa wa watu wakigombania daladala ilikuwahi makazini acha wale wasichana waliokuwa wanajirejesha majumbani kwako baada ya kutoka katika biashara ya ngono na nguo zao za anasa pale jirani na kituo kikubwa cha mabasi msavu panapoitwa itigi macho yao yaliweza kujionea vingi ambavyo vingine david aliviona muda mrefu sane,
Wale madada waliokuwa wamevaa nusu uchi wakizani kuwa ndio uzuri au wanaweza kumvutia mwanaume walimfanya david amwangalie dada yake kipenzi nisha na kutafakari vipi kama dada yake atakuja kuishi katika mazingira yale? Lakini aliishia kusikitika tu kuona kuwa wamekosa maadili mema.
Kuwaza kule kulikatika baada ya gari walilokuwa wamepanda kuingia kwenye stendi ndogo iliyokaribu na stendi kubwa ya magari yaendayo mikoani maarufu kama stendi ya dodoma.waliweza kushuka hapo na kuanza kuvutwavutwa na na wale wapiga debe na kuulizwa mnakwenda wapi dar,mwanza, kigoma au wapi?
“Dar es salaam” david alijibu
Ndipo mpiga debe huyo alipo ongozana nao na kuelekea kwenye stendi kubwa ya mabasi yaendayo mikoani na kuwafikisha mpaka kwenye basi la abood liliokuwa mbioni kuondoka na alipo pewa chake akaondoka zake, david alikata tiketi za watu wawili yeye na mdogo wake kisha wakaingia kwenye gari na kutafuta siti zao kwa kuuliza uliza, watu wengi walionekana kuwashangaa kutokana na muonekeno wao maana tumeshazoea kuwa kila tunaposafiri basi lazima tupendezze lakini kina david walikuwa kama vile wanakwenda shambani kwa kwa ajili ya kilimo kutokana na kukurupuka kwao.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Honi ya kujiandaa ilipigwa na baada ya dakika chacbe tu gari ikaanza kuchanja mbuga kuiacha morogoro mjini na kuelekea dar es salaam, nisha alionekana kufurahia safari hiyo maana hakuwahi kupanda gari tangu alipoanza kujitambua kwa kiasi fulani.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment