Search This Blog

Friday, 20 May 2022

SAHIHI YA KIFO - 1

 







    IMEANDIKWA NA : ISSA MMBAGA



    *********************************************************************************



    Simulizi : Sahihi Ya Kifo

    Sehemu Ya Kwanza (1)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Jua lilikuwa likiaga upande wa mashariki na kwenda kuungana na magharibi ili kukamilisha siku, huku likisindikizwa na hali ya hewa yenye ubaridi kwa mbali, ndege pia walipeperusha mbawa zao kutafuta makazi ambayo yatawafanya walione jua la kesho hata baadhi ya nyumba za jirani zilionekana kufuka moshi kama ishara ya maandalizi ya chakula cha usiku. Sauti za wakina mama pia zilisikika zikiwaita watoto wao kurudi nyumbani ili kuepukana na dhoruba za giza litakapo kuwa kubwa, wengine wakiwatuma wakubwa kwenda kununua mafuta ya taa na mishumaa ili waweze kupata mwanga.

    Lakini nyumba ya kina David ambayo ndio ilikuwa ikionekana yenye thamani katika kijiji hicho cha Gairo mkoani Morogoro ilikuwa tofaauti baada ya kuzongwa na huzuni pamoja na mabishano ya hapa na pale juu ya swala la David kutaka kwenda mjini baada ya kumaliza elimu yake ya kidato cha sita katika shule ya sekondari Gairo.

    Familia ilikuwa imekusanyika katika kitanda cha mama yao mzazi ambaye alikuwa hoi kutokana na maradhi ya moyo yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu. ambayo yalisababishwa na mshtuko alioupata baada ya kupata taarifa juu ya mumewe kuhukumiwa kifungo kutokana na ubadhirifu wa fedha uliotokea katika benk ya NMB

    Tawi la magomeni aliyokuwa akifanya kazi miaka ya nyuma huko kwenye jiji la maraha na uchafu wote Dar es saalam.

    Mzee Kazinge alisema “…………swala hili halito wezekana hata kidogo, bora ya hawa wadogo zako ndio wange lilia kwenda, lakini sio wewe maana unakumbuka nini kilichotokea huko unakotaka kwa kauli ya mwisho nasema baki hapa kijijini ”.



    Baada ya kumaliza kuongea kwa jazba na hasira mzee Kazinge alinyanyuka na kutoka nje.

    “Baba!! Baba!!...”.David alimuita baba yake kwa sauti ya unyenyekevu lakini mzee huyo hakugeuka nyuma.

    David alimwangalia mama yake kwa huzuni sana kisha kumueleza,,,,

    “Mama safari hii ni kwa sababu yako huenda nikafanikiwa kupata pesa huko zitakazo saidia kufanikisha kufanyiwa upasuaji”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “najua mwanangu unanipenda mama yakoniendele kuishi lakini fikiria pia kama utaondoka hapa hakuna wa kunihudumia, wewe ndio tegemeo langu, baba yako mwenyewe hali yake ndio hiyo unayoiyona tangu ametoka jela amechanganyikiwa, pombe ndio imekuwa furaha yake, nakuomba ubaki baba yangu kama Mungu amepanga niiishi nitaishi lakini kama hakupanga basi kazi yake haina makosa”

    Mama yake aliendelea kumsisitizia;

    “…kingine wadogo zako ata wahimiza nani kusoma hata kuwatunza pia”? Alimuuliza David.

    Lakini David hakujibu swali hilo alibaki anamuangalia tu mama yake aliyekuwa anazungumza kwa shida pale kitandani.

    Maneno hayo yalimuumiza sana David. machozi yakamtoka, lakini alijikaza kiume baada ya kuona wadogo zake wamenyong’onyea na kukosa amani ndani ya mioyo yao kutokana na maneno aliyoyasema mama yao na malumbano yalio kuwa yakiendelea hapo ndani ndipo alipo wavuta na kuwapakata na kuongea nao kwa utaratibu..........

    ”msijali wadogo zangu mimi sitoondoka na wala mama hatokufa alikuwa anatania tu sawa Dason?

    “ndiyo”Dason aliyekuwa mdogo wake wa mwisho alijibu

    Nisha? Aliimuita

    “Abee” aliitika

    “Haya nendeni jikoni mkaandae mimi nakuja kupika sawa”?

    “Sawa kaka”.alijibu Nisha mdogo wake wa pili



    Mzee Kazinge alivyotoka alielekea kilabuni ambako wanauza pombe za kienyeji ili kukamilisha furaha yake kama mkewe alivyoeleza, alirudi nyumbani akiwa amelewa sana hata alipokuwa njiani aliropoka maneno ambayo yalionekana kuendana na ukweli wa maisha yake……..,

    ”Elimu yangu mwenyewe imenipeleka gerezani!!!

    ”Nimekosa nini katika nchi hii”?

    ”kipi bora kuwa mjinga au kuwa na elimu?

    ”Ama kweli Serikali ina siri kali!!!.

    Aliongea maneno hayo njia nzima mpaka alipofika nyumbani kwake, Familia yake ilikuwa imesha lala baada ya kupata chakula cha usiku ambacho kiliandaliwa na David, wakati huo ilikuwa ya pata kama mishale ya saa nane usiku, kijiji kizima kilikuwa kimya hivyo sauti yake iliweza kuamsha baadhi ya majirani. Aligonga mlango wa nyumbani kwake zaidi ya mara nne lakini hakuna alieamka ndipo alipo zunguka nyuma na kumgongea David dirishani,,,,,

    ”David, David....,

    ”Naamu” sauti yenye usingizi iliitika

    ”Mimi nagonga we husikii eeh? Aliuliza kwa ukali

    “nakuja baba” alimjibu

    Ndipo alipo nyanyuka kitandani na kwenda kufungua mlango,ghafla David alijikuta akipokea kipigo kutoka kwa baba yake,,,,

    ” mimi na wewe nani baba humu ndani eeh? Alimuliza David huku akiendelea kumpiga.

    ”haiwezekani mimi nigonge mara zote hizo wewe upo ndani kama ndiye mwenye nyumba hii”

    Hasira hizo pia ziliendana na swala la David kutaka kwenda mjini maana alilihusisha pia wakati kipigo kikiendelea,,,,,,

    “unataka nikuzike mapema huko unakotaka kwenda?”

    ”unajifanya hujui kilicho mfanya mama yako aje huku kijijini wakati niko gerezani?” alimuuliza

    Bila kujibiwa aliendeleza kipigo ambacho kilimfanya David aanze kuhisi maumivu mpaka kufikia hatua ya kulia kwa sauti kubwa kama mtoto mdogo wakati ni dume linalo kimbilia miaka ishirini na ushehe.

    Kilio cha David kiliwatoa majirani majumbani kwao hata mama yake alipokisikia kilio cha mwanae alijitahidi kwenda kumuamulia japo alikuwa hoi,kama ilivyo misemo ya Waswahili samaki mmoja akioza wote wameoza mama yake naye akajumuishwa katika kipigo hicho bila kujali afya yake,

    Hali ilizidi kuwa mbaya kwa mama David mpaka majirani walipo wasili eneo la tukio na kumshika mzee Kazinge.

    ”jamani muwaisheni hospitali haraka huyu mama” sauti za watu zilisikika huku wengine wakimbembeleza David.

    ”Mwenye namba ya gari la hospitali apige upesi bila hivyo tutachelewa” wazo lilitolewa na kufanyiwa kazi haraka iwezekanavyo na baada ya muda gari likawa imewasili.

    Nisha na Dasoni pia waliamka baada ya zogo kuwa kubwa hivyo walijikuta wakilia bila kujua kinacho endele kutokana na umri wao, japo Nisha alikuwa kigoli na Dason ni mdogo asiye pungua miaka tisa.

    Mama Muksini ambaye alikuwa wa makamo alipowaona aliwafuata na kuwachukua, kisha kumuongezea kanga nyingine Nisha maana maumbile yake yalikuwa yameanza kuonekana. hasa nyonga na chuchu zilizo chongoka kwa kuwa alitoka na kanga aliyo lalia tu.

    ”Sasa jamani huyu mzee kazinge tumpeleke kwa mwenyekiti wakati mkewe akiwaishwa hospitali”,alizungumza mzee Nyomolage.

    Safari ikaanza baada ya kujigawa makundi mawili ambapo mzee Nyomolage, mama Muksini akiwa na kina Dason na mzee Mtepa pamoja na mzee Kazinge mwenyewe wao walielekea njia ya kwa mwenyekiti lakini kwa kumshikiria mzee kazinge asije akawakimbia na pombe zake alizo kuwa nazo kichwani.

    David,Stallone,Junior na mama coolin wao walielekea hospitali kumpeleka mama David.

    Safari ya kwa mwenyekiti haikuchukua muda maana hapakuwa mbali sana na kwa kina David ndani ya dakika kadhaa wakawa wamewasili na mzee Nyomolage ndie aliyegonga mlango......



    ”mwenyekiti,,mwenyekiti” sauti mbili tu zilitosha kumuamsha mzee maige ambaye ndie alikuwa mwenyekiti.



    Mwenyekiti aliamka na kutoka nje akiwa amebeba taa ya chemli iliimsaidie kuona kutoka na kuto kuwa na umeme nyumbani kwake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ”Vipi jamani mbona usiku na mkusanyiko mkubwa kuna nini!!? Aliuliza mwenyekiti kwa mshangao,

    Mzee Nyomolage alionekana kuwa kiongozi wa msafara kwasababu alikuwa jirani sana na mzee kazinge hivyo swali hilo alijibu yeye,,,,,



    ”tumemleta mzee Kazinge alikuwa anawafanyia vulugu familia yake na hivi tuna vyoongea mkewe amewaishwa hospitali hali yake si nzuri ndugu mwenyekiti”.



    ”Mzee Kazinge tatizo nini mpaka unaleta vulugu kwa familia yako eeh? Mwenyekiti aliuliza



    ”umesha sema familia yangu nyinyi inawahusu nini mbona mnakuwa wambea kuingilia mambo yasio wahusu? We mwenyekiti si umelala na familia yako nani aliyekuja kuku uliza kwa nini umelala eeh ni jibu sasa”?



    Majibu ya mzee kazinge yalionekana dhahiri kutoeleweka kutokana na pombe aliyokuwa amekunywa iliyo mlewesha kufikia hatua ya kutojua anazungumza nini na mbele ya nani.



    ” Mzee Nyomolage na wenzio embu mfungeni kamba kisha muingizeni ndani mpaka kesho panapo majaaliwa pombe ikiwa imemusha kichwani tutaendelea na mshauri haya”alizungumza mwenyekiti.



    Zoezi hilo likafanyika kwa haraka.



    ”Ndugu mwenyekiti basi na mimi naomba watoto hawa wa mzee kazinge nikalale nao maana kwao hakuna mtu kaka yao pia ameelekea hospitali”.mama Muksini alionesha huruma kwa watoto hao Nisha na Dason



    ”Hakuna shida mama ila kesho mjitahidi kuwahi ilitujue tunafanya nini juu ya tatizo hili.



    ”Sawa na shukuru tutajitahidi” alijibu mama Muksini kwa heshima.



    Muda huo huo mzee Nyomolage na wenzie walielekea majumbani kwao na ilikuwa yapata kama saa kumi kasoro hivi,njia nzima mazungumzo yalikuwa juu ya swala hili.

    *************



    Daktari alimtoa mikono David kisha kumshika begani na kumueleza........



    ”hali ya mama yako inaridhisha kiasi ila kuna mambo inabidi tukazungumzie ofisini kwangu”



    Walifuatana mpaka ofisini na dokta alianza kumu uliza baadhi ya maswali,,,

    ”kijana tatizo lilikuwa ni nini mpaka mgonjwa anafikia hali ile mnaendelea kukaa naye nyumbani?



    Swali hilo lilionekana ni kama kusifiwa na kipofu umependeza, hivyo David alikaa kimya kutafakari huku mawazo yalio kuwa yanaelea kichwani mwake ni kwamba,,,



    ”kama nikimueleza kilichotokea baba anaweza kuwa katika wakati mgumu”



    wakati akiendelea kutafakari daktari alimuuliza kwa mara ya pili na David akajibu,,



    ”matatizo ya kifamilia tu daktari” ila macho yake yalionekana kuogopa hivyo yalimfanya daktari kuhisi kuwa anamdanganya ndipo alipo mchimba mkwara kutaka kujua ukweli,,



    ” Kijana haya ni maisha ya mama yako ukifanya mchezo unaweza ukayapoteza huku unajiona, mimi natakiwa kuandika taarifa juu ya mgonjwa huyu unafikiri nitaandika nini? Mama yako ameonekana ana majeraha sehemu za usoni, hali ambayo hata wewe unayo hivyo basi mama yako hatopata huduma nyingine mpaka taarifa zake zitakapo kamilika pia kumbuka kwamba kwa sasa ametibiwa kutokana na hali yake kuwa mbaya lakini bila hivyo tusinge weza kumpokea bila maelezo kutoka kituo cha polisi na baada ya wiki mbili anatakiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo wake ukichelewa inabidi asafilishwe kwenda india gharama zitakuwa juu yenu serikali haito changia chochote kwa kuwa huu ni uzembe uliofanyika” Daktari aliongea kwa hasira na kuhamaki.



    Maneno hayo yalizidi kumpa wakati mgumu David maana akifikiria baba anaumuhimu kwake na mama ana umuhimu kwake nini afanye? Akajikuta yupo njia panda na chozi jembamba likaanza kumtoka mtoto wa kiume.



    Baada ya mpigano wa mawazo kichwani mwake akaona bora amueleze tu juu ya tatizo ambalo limemkuta mama yake ili kuokoa maisha yake.



    Daktari akawa anaendelea kuandika maelezo hayo kwenye faili lake na alipo maliza akamruhusu David aende nyumbani warudi mchana na chakula huenda mgonjwa akawa anauwezo wa kupeleka japo kitu mdomoni.

    Daktari alipogeuza macho aliona tangazo lililo bandikwa ukutani likisema ,,,,,,,



    ”PINGA UNYANYASAJI KWA WANAWAKE NA TETEA HAKI ZA BINAADAMU” TANGAZO HILI LIMELETWA KWENU NA WIZARA YA AFYA IKISHIRIKIANA NA H ISANI YA WATU WA MAREKANI” Daktari alipo maliza kulisoma alimwangalia David

    ambaye pia macho yake yalilenga kwenye tangazo lile, Tangazo hilo lilimfanya Daktari kupata wazo nini afanye juu ya mzee kazinge.



    David aliondoka ofisini kwa daktari akiwa na huzuni huku akifikiria hatima ya wazazi wake,alifika kwa wenzie ambao walikuwa wa mesha amka , na macho yao yakigeuka huku na kule ni dhahiri yalikuwa yana mtafuta David hatimaye walimuona ameegemea ukutani akiwa amewapa mgongo,wote walijikuta wakimuita kwa pamoja David..........!!!!!!



    Ndipo mama Coolin alipo nyanyuka kutoka kwenye benchi na kwenda kusimama karibu naye.,,,

    ”ulikuwa wapi maana tulikuwa na wasiwasi kuto kuwepo kwako” aliuliza mama Coolin



    David alijikaza na kujitahidi kumjibu japo alikuwa na kazi ya kuubembeleza moyo wake ambao una majonzi,alivuta pumzi ya ndani na kumwambia,,,,



    ”nimetoka kwa Daktari”

    ”kasemaje ”? Mama coolin aliuliza kwa hofu,

    “hali ya mama inaridhisha kiasi tofauti na alivyo kuja pia anatakiwa kufanyiwa upasuaji ambao unagharimu kiasi ki kubwa cha pesa kama kita chelewa ugonjwa ukizidi atatakiwa asafirishwe kwenda india kwa matibabu zaidi”



    Kisha akakaa kimya kwa muda na mboni za macho yake yakielekea kwenye chumba alicho mama yake ukimya huo ulimfanya azidi kuduaa mpaka alipo shtuliwa na kina Stallone ambao nao walimsogelea,CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Vipi jamani mbona kimya kimezidi kuna usalama”? aliuliza Junior,

    “Kiasi chake upo” mama Cool alijibu,



    Baada ya maongezi hayo David aliwaambiwa waelekee nyumbani huku yeye akianza kujongea. Na wenzie wakimfuata na safari hiyo iliyoanzishwa ya kuelekea nyumbani wakiwa kwa miguu ikawa inasindikizwa na maongezi ya hapa na pale kama mama Coolin kuwa eleza wenzie kilichojiri kwa Daktari kama yeye alivyo elezwa na David .

    Walichukua muda wa masaa mawili mpaka kufika njia panda ya mtaani kwao ambayo ndio iliyo onekana kutaka kuwatenganisha kabla ya kuagana ili kila mmoja akaendelee na shughuli zake ikiwemo kupumzika kutokana na uchovu wa usiku kucha, Davidi alipo taka kuelekea kwao taswira zilianza kuelea kichwani mwake kwamba kitendo anachotaka kuki fanya si cha kiuungwana cha kutaka kuondoka bila kutoa shukrani zake kwa wema alio fanyiwa na majirani zake alipo kumbuka usemi mmoja kutoka kwa mwalimu wake uliosema,,,,,,,



    “mwenye busara hujifunza kwa mateso yake” ndipo alipo thubutu kunyakuwa kinywa chake na kutoa tabasamu la kirafiki lililosindikizwa na maneno ya upole yalio mfanya mama Coolin kutoa chozi lenye mchanganyiko wa furaha na huzuni huku wakina stallone na junior midomo yao kuonekana kutaka kusema neno,,,,



    “Akili yangu iliyokuwa na upeo mdogo wa kufikiria leo imeweza kuongezeka baada ya kufikishwa katika ulimwengu wa faraja ndani ya masaa saba ya shida, ambayo yalio nifanya niweze kumjua mwalimu wa maisha na kujua nini maana ya tatizo, huenda maneno yangu yasisadiki moyoni kwenu ila naomba mzipokee shukrani zangu za dhati mimi na familia yangu akiwemo mama yangu kipenzi,ninyi ni binaadamu mnao stahili kuishi katika hii dunia”

    David alizungumza maneno hayo kwa unyenyekevu sana ili walio msaidia mpaka mama yake kufika hospitali wajue kuwa msaada wao unamuhimu na ameujali kuliko ambavyo wao wangeweza kufikiria maana wema ni akiba.



    Junior nae alizidi kumpa moyo wa ujasiri kukabiliana na tatizo ambalo lipo mbele yake,,,

    “David, thamani ya mtu inakuja pale yeye mwenyewe anapo jithamini hivyo hatukuwa na budi kuonesha ushirikiano wetu kwako juu ya tatizo lako isitoshe sisi ni vijana ambao tuna tarajia kuja kuwa wazazi wa baade tusipo pendana na kujaliana matatizo yetu hata watoto zetu hawato pendana hizi ni changamoto katika maisha tupo pamoja mpaka mwisho wa tatizo hili.



    Upendo huo ulio oneshwa hapo ulimfanya kila mmoja kujiona ni miongoni mwa watu wema sana katika dunia maana kila mmoja alitambua thamani ya mwenzie.

    mama Coolin pia aliweza kuahidi kuandaa chakula cha mgonjwa hivyo aliomba aruhusiwe awahi kukipika, basi wote wakakumbatiana na kila mmoja kuelekea kwake.



    *****************



    Ukimya ulio tanda kwenye nyumba ya kina David ulimuogopesha sana na akiangalia milango yote imefungwa jukumu la kuanza kuita lika chukua nafasi mdomoni mwake,,,

    Baba!!!!!!? Baba!!!!..,? nisha !!!!!? Lakini bila mafanikio zaidi ya sauti zilizo kuwa zinajirudia rudia kumkera tu maskioni mwake ghafla alishtuka alipo vutwa shati kwa nyuma na shingo yake ilipo geuka kumbe alikuwa ni Dasoni hakuwa na budi kuitoa ile sura yenye mikunyanzi usoni mwake na kumbeba mdogo wake kipenzi,

    Alipo taka kumuuliza nisha yuko wapi macho yake yaliweza kumuona kwa mbele Nisha akija huku akiambatana na mama Muksini, walipo wasili karibu yake mama Coolini alimueleza,,,,,



    “milango niliifunga jana baada ya nyie kwenda hospitali baba yako tulimpeleka kwa mwenyekiti hivyo alilala huko kutokana na pombe alizo kunywa na huu mguu tulikuwa tunaelekea huko ila Dasoni ndiye alie wahi kukuona wakati ukija hapa ndio maana akakukimbilia”

    Alipo maliza aliuliza hali ya mgonjwa na jibu likawa lilelile alilo wapa wakina mama Coolin.



    “Basi tuongozane twende wote huko”David alimueleza mama Muksini,



    “David jihurumie na wewe ungeoga kwanza kisha uendee nyumbani kwangu Yule masichana wangu wa kazi akupatie chai ndio uje maana hiyo kesi haiwezi kuendeshwa bila wewe kuwepo”mama Muksini alimueleza David baada ya kumuhurumia lakini kwa David haikuwa hivyo,,



    “nashukuru sana kwa ukarimu wako lakini kiukweli sina hata hamu ya kula kitu chochote kile kwa sasa ni vyema tuwahi huko kwa mwenyekitini ili tujue kinachoendelea huenda hata yeye Baba akawa na wasi wasi juu ya hali ya Mama”



    Mama Muksini kutokana na maelezo ya David akawa hana kipingamizi ikabidi waongozane kuelekea kwa mwenyekiti na walipo anza kuiona ile bendera ya chama cha mapinduzi (ccm) iliyo chakaa ikipepea juu ya mlingoti David alifanikiwa kumuona Baba yake akiwa na mwenye kiti wakitoka ndani kwenda kwenye mabenchi ambayo wakina mzee Nyomolage walisha wasili kitambo huku akiwa amesha funguliwa zile kamba alizo fungwa usiku na pombe zilisha kwisha kichwani. Moyo wa hasira ulimshika David alipo kumbuka hali ya Mama yake kule hospitalini lakini alijikaza,,,



    Miguu yao ilipo kanyaga eneo lile macho makavu ya David yalionza kubadilika rangi kutaka kuwa mekundu kutokana na hasira yalipo gongana na mzee Kazinge ana kwa ana na moyo wa mzee kazinge ukionekana kuteseka na aibu kwa kitendo alicho kifanya maana Alisha elezwa yote yalio tokea na mwenyekiti wakati walipo kuwa wanajibizana akiwa anafunguliwa zile kamba alizo fungwa.



    Bila kuchelewa ndugu mwenyekiti akaanzisha kikao na swali kwa David juu ya hali ya mgonjwa kwanza.. Jibu alilo toa David lilizidi kuchokonoa aibu iliyo jificha kwa mzee kazinge kufikia hatua ya kuinama chini lakini mwenyekiti aliendelea kuuliza maswali mengi mengi ambayo yalichukua muda mwingi mzee Kazinge kuya jibu mpaka ilipo timia saa saba kasoro hakuna jibu wala sababu ya msingi ambayo iliyomfanya mzee kazinge kumpiga David na mkewe.



    Mwenye kiti ndipo alipo amua kutaka kukata shauri kwa kuruhusu mzee Mazinge apelekwe kituo kidogo cha polisi kwa matatizo aliyo msababishia mkewe mpaka kulazwa.



    Kutokana na hatua aliyofikia mwenyekiti ilimtisha mzee Kazinge alipofikiri kuiacha familia yake kwa mara ya pili tena kwa ujinga , na yeye kwenda gerezani, kilimuumiza sana na kuleta mlipuko mkubwa wa mamumivu mwilini mwake na chozi la kujilaumu likaanza kumtoka hali ambayo ilileta huzuni kubwa kwa kina Dason na Nisha,.

    Ali watazama na kufikiria kama mkewe atakufa hospitali ni zahiri safari hii ataukumiwa kifungo cha maisha.ndipo macho yake yalipomtazama David kisha kugeukia upande wa kina Nisha na Dason ambao walipakatwa na mama Muksini kisha kuanza kusema,,,,,



    “Mwenyekiti kwanza naomba radhi kwa niliyo yafanya naamini kwangu ni hasira na pombe ambazo ndizo zilizo nifanya nitende hivi, pia familia yangu ambayo naipenda sana najua ni vigumu kuomba radhi kwenu lakini naomba mnisamehe pia mkaniombee msamaha kwa mama yenu maana nikienda kituoni huenda nisionane na nyie tena wala mama yenu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “ Kikubwa ni kwamba familia hii sio maskini ila kuna mambo ambayo yamejificha leo ninge penda kuwa eleza zile kumbukumbu ambazo niliapa hazito saulika katika maisha yangu yote David najua unajua ulicho kiona kwa macho yako ila chanzo hukijui. Tega sikio ili ujue kwanini nilikukataza usiendee mjini kwa wakati huu. Wote walijikuta kukaa kimya huku macho na maskio ya David yakikaa kiudadisi kutaka kujua chanzo

    Mzee kazinge anaanza kuwa simulia,, ilikuwa mwaka 2002

    Ilikuwa mwaka 2002 ndani ya jiji la dar es saalam nikiwa mfanyakazi katika NMB banki iliyopo tawi la magomeni katika kitengo cha mikopo, kitengo hicho kilinifanya nifahamiane na watu wengi sana na wenye tabia tofauti kutokana na ukalimu nilio nao.



    Japo niliiamini kuwa hata uwe mwema kiasi gani lazima utakuwa na maadui wanao kuzungua, hao pia nili jitahidi kuishi nao.kila ofisi utakayo kwenda kama ikiwa na wafanyakazi thelathini basi kumi na watano lazima walikuwa wanalifahamu jina la Alfred Kazinge



    Miaka ilivyozidi kwenda huku nikiwa tayari nina watoto wa wili David na Nisha, jina langu lilijulikana zaidi ndani na nje ya jiji la dar es saalam hasa na wafanya biashara waliokuwa wanaingia na kutoka. nilikuwa na pokea simu nyingi sana kiasi ambacho zingine zikawa zinaleta ugomvi kwa mke wangu magrety .(mama david)



    Umaarufu huo ulianza kuniletea dosari katika kazi yangu baada ya kumpata rafiki Helman ambaye ndio nikamfanya ndugu yangu wakaribu baada ya kuhamia hapo jijini dar es salaamu kutokea mkoani Tanga ambapo ndipo walipo baadhi ya ndugu zangu. Na makaburi ya wazazi wangu yalipo.



    Bwana Helman alianza kunifanya nichelewe kurudi nyumbani kwangu kwa kunipitisha sehemu nyingi za anasa na kunikutanisha na marafiki zake ambao wengi walionekana ni wenyeji wa Arusha,.kila walipo kaa walikuwa wanazungukwa na wasichana ambao nilikuwa nashindwa kuwaangalia kwa mara ya kwanza kutokana na nguo zao za anasa walizo kuwa wanavaa.



    Hivyo sehemu hizo za starehe zilinifanya kumgeuza mke wangu magrety kuwa mlinzi wa nyumba na mtunza muda kwa kuangalia saa ya ukutani ni saa ngapi narudi na alipo sikia honi ya gari majukumu ya kufungua mlango pia aliyabeba na alinivumilia sana hata nilipo amia dunia nyingine yenye utembeaji wa kupepesuka( ya ulevi)



    Bwana Helman alianza kunifanya nichelewe kurudi nyumbani kwangu kwa kunipitisha sehemu nyingi za anasa na kunikutanisha na marafiki zake ambao wengi walionekana ni wenyeji wa Arusha,.kila walipo kaa walikuwa wanazungukwa na wasichana ambao nilikuwa nashindwa kuwaangalia kwa mara ya kwanza kutokana na nguo zao za anasa walizo kuwa wanavaa.



    Hivyo sehemu hizo za starehe zilinifanya kumgeuza mke wangu magrety kuwa mlinzi wa nyumba na mtunza muda kwa kuangalia saa ya ukutani ni saa ngapi narudi na alipo sikia honi ya gari majukumu ya kufungua mlango pia aliyabeba na alinivumilia sana hata nilipo amia dunia nyingine yenye utembeaji wa kupepesuka( ya ulevi)



    Nakiri kuwa sikuwahi kumpiaga mke wangu hata nilivyo kuwa katika hali hiyo. Ilifika kipindi nikawa na kosa hata muda wa kuzungumza na watoto wangu vipenzi japo kwa wakati huo David ndiye aliye kuwa na akili ya kunijibu na kunielewa nini na zungumza pia kwa utoto wa Nisha wa kuzunguka zunguka na kupiga kelele pale subuleni wakati wa mazungumzo ya hapa na pale ili kuendelea kujenga amani na upendo niliukumbuka pia;



    Namshukuru sana mke wangu siku ya jumamosi majira ya saa tatu usiku nikiwa tayari nimejiandaa kutoka ndipo alipo niweka chini na kunikumbusha mateso niliyo yapitia wakati na soma shida ngapi nili pata na leo na tumia fedha bila kujali kuwa kuna watu wenye shida duniani pia hata upande wa penzi lake, baba yake alikuwa na fedha kiasi ambacho yeye aliweza kuniibia na kunipatia ili niweze kuendeleza masomo yangu na kujikimu kwa mahitaji madogo madogo.



    Hakika jambo hilo lili niingia kichwani na kuona kuwa Helman sio rafiki mzuri kwangu sikuchelewa niliingiza mkono mfukoni na kutoa nokia yangu kisha kubonyeza vitufe 0654000092 na kupiga sekunde kadhaa simu ikaanza kuita na muda huo huo ikapokelea nilicho anza kukisikia ni kelele nyingi za mziki na sauti za wanawake tofauti ,hivyo nilijua tayari wamesha wasili baa na wenzie wanakunywa pombe tu, akanzaa kuongea,,,



    “hallo uko wapi wewe mbona tunakusubiri hutokei”? Aliuliza Helman kwa sauti ya juu ili aweze kusikika kutoka na eneo alilopo

    “Helman naomba usogee sehemu yenye utulivu kidogo ili tuzungumze”nilimwambia

    “Eeh uko wapi sasa? maana huku warembo wanakusubiri kwa hamu uje kuwa mwagia pesa”



    sauti hiyo aliyo ongea Helman, Magrety aliweza kuisikia alizidi kujua vitendo alivyo kuwa na vifanya mme wake,Alfredy, aibu ikamshika Alfred ndipo alipo zungumza kwa ukali,,,,,



    ”Sikia Helman kuanzia sasa urafiki wetu mimi na wewe umeisha siwezi kutelekeza familia yangu sababu yako na hata ukija ofisini nita kuhudumia kama wateja wengine na sio kama rafiki yangu pia nyumbani kwangu sikuhitaji”



    kisha akakata simu. upande wa Helman akawa anaendelea kulalamika,,,,,

    “hallo?,hallo? Lakini bila mafanikio alipo itazama simu yake akagundua kuwa ilisha katwa muda mrefu , oooh shit!!! Ndio neno li lilo mtoka.Helman



    Akaondoka kwa mwendo wa haraka kuelekea walipo wenzie walio kuwa wanajiburudisha na warembo alifika huku akihema na kuzungumza kwa jazba…

    “Jamani mpango wetu unaanza kuharibika yani kama huyu jamaa ameotea dili vile au kuna mtu kamvujishia huyu eeh?



    Wote walihamaki! Na mmoja wao kuuliza kwanza kafanyaje kwasababu leo si ndio tumepanga akija tumalize kila kitu na tujue mchongo tuna useti vipi?



    “Alfred amekataa kuja na kasema kuwa hataki urafiki na mimi maana mimi sio rafiki mzuri kwa maneno haya huoni kama kanishtukia? Helmani alizungumza na kuendelea kusema kwa hasira huku akipigapiga mikono yake kwenye meza.

    wakataka kuharibiana wenyewe ndipo walipo kubaliana wafanye jambo.

    ****************

    Nilipo kuwa naomba radhi kwa mama David ghafla muito mfupi kwenye simu yangu uliita nilipo angalia nikakuta ni namba ngeni imenitumia ujumbe nilishikwa na woga nilipo ona ujumbe ulio andikwa,,,



    “KAZI YETU KWAKO HAIJAISHA MPAKA LENGO LETU LITA KAPO TIMIA”



    kisha mbele akaandika maneno yalio ashiria kucheka,,,

    ”hahahaha!!!!!!!”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilipigwa na butwaa hali iliyo mfanya mke wangu mama David kuwa na wasiwasi naye akaichukua ile simu na kusoma ujumbe ule, kabla hajamaliza ghafla hodi ikawa inagongwa kwa nguvu sana wote tulizidi kushikwa na woga kila mmoja aliwaza huenda ni Yule aliye tuma ujumbe ule wa vitisho? lakini hatukuwa na uhakika tukajikuta tumesogeleana na bahati nzuri Nisha na David kila mmoja alikuwa chumbani kwake hivyo hawakuweza kujua kile kilichoendelea pale sebleni.



    Ikabidi nijikaze na kumwambia mama David alekee chumbani maana hatujui nani anaye gonga majira yale ya usiku na hatukuwa na mazoea ya ugeni wa usiku bila taarifa na getini amepita vipi mtu huyo anaye gonga mlango nilitazama huku na kule nikakuta mchi wa kinu kidogo nika uchukua nakuelekea mlangoni hakika sikuamini nilicho kiona mbele ya macho yangu



    Nguvu ziliniishia na ule mchi mdogo nilio ushika ulianguka chini kisha nikashusha pumzi ndefu, kumbe alikuwa ni Sagu kijana ambaye alikuwa anasimamia ujenzi wa nyumba yangu hii ninayo ishi sasa hapa gairo ambayo niliamua kuijenga kwa siri na huku mbali kwa sababu kama kampuni ingejua najenga wangeanza kunifuatilia na kuhisi huenda nikawa naihujumu.



    Basi nilimkaribisha japo aliuliza maswali ya hapa na pale mbona na hema kiasi kile na nimeshika mchi kama navizia kitu fulani cha hatari lakini nilimpa majibu yalio mlizisha na hakujua kilicho kuwa kina endelea kwa muda huo, hivyo tuliketi na kuanza mazungumzo,,,,,



    “Sagu mbona usiku na bila taarifa? Nilimuuliza

    ”aisee bosi samahani kwani nilijaribu kupiga simu yako ila mtandao ulikuwa unasumbua” alinijibu



    Nikamtazama kwa makini lakini kila nilipo taka kumuliza swali getini aliingiaje mdomo wangu ulikuwa mzito niliwaza mambo mengi kichwani mwangu kwa muda mchache nilio kuwa na mtazama mpaka sauti ya mke wangu Magrety iliposikika kutokea chumbani ,,,,,



    ”Eeh shemeji umekuja saa ngapi? Alimuuliza Sagu kwa kuzuga

    “Muda mrefu shemeji yangu wazima hapa? sagu Alijibu na kuuliza hali

    “Sisi wazima mnatunyima nini huko?Magrety aliuliza huku akiweka kisura cha kujichekesha asishtukiwe kama alitoka kwenye hofu

    “huko tuta wanyima nini zaidi ya mvua zinazoendelea kunyesha na viazi kuzidi kunawaili”?



    Baada ya mazungumzo hayo mafupi Magrety alinyanyuka na kwenda kumuandalia chakula Sagu nasi tukawa tunaendelea na mazungumzo,,,,



    “Mmh Sagu niambie ujio wako kama unautofauti na siku nyingine?nilimuuliza

    “hapana bosi ni ulele tu vifaa vya ujenzi vimepungua hivyo nime ona bora nije ili nimalizane na wewe ukabidhiwe nyumba yako baada ya muda mfupi”alinijibu

    “basi hakuna shida kesho nitakupatia fedha ili ukaendelee na ujenzi” nilipo mjibu nikanyanyuka na kumuaga na kumtakia usiku mwema wakati yeye akielekea kula na kwenda kwenye chumba cha kumpumzika maana alikuwa sio mgeni.



    Usiku nilipata usingizi wa mang’amu ng’amu sana niliwaza kila neno ambalo mke wangu aliniambia na kuufikiria zaidi ule ujumbe nilio tumiwa, mke wangu alizidi kunionea huruma kwa hali ilivyo badilika ghafla kutoka kwenye furaha mpaka kufikia huzuni ambao hata yeye hakutegemea kwa muda ule kama ungeweka makazi ndani ya mioyo yetu, ila kinywa chake hakikusita kutamka maneno haya ambayo yalimpendeza mungu,,

    “mme wangu kesho tukiamka salama tuelekee kanisani tuka fanye maombi maana hali ina anza kuwa tete”

    Hakika nilijikuta nikimporomoshea mvua nyingi ya mabusu usoni mwake kisha nikamueleza,,

    “mke wangu wewe ni mwanamke ambaye umetumwa kuja kunibadilisha mimi katika dunia hii na kunipa faraja ambayo wengine wanaikosa nakushukuru sana mama David” nilizungumza maneno hayo huku uso wangu ukionesha masikitiko makubwa kwa yote niliyo yafanya nyuma.



    Mke wangu akanisogelea taratibu na kuniangalia kwa sekunde kadhaa usoni kisha akaachia tabasamu la kimahaba na kulaza kichwa chake juu ya kifua changu ,

    kutoka kwenye tabasamu lile niliweza kuhisi alichofikiria huenda hakuamini kama nimeamua kubadilika kwa muda mfupi kiasi kile.

    kule kumisi kulala mapema na mimi kulimfanya apitiwe na usingizi mapema lakini kwangu ilikuwa tofauti mpaka kulipo kucha baada ya kumshwa na jogoo la kwanza.



    Tuliamka wote tukajiandaa na kuibeba familia yangu kwenye gari yangu aina ya BMW230 safari ikawa kuelekea kanisani kama mke wangu alivyo nishauli lakini kabla hatuja fika nilimshua Sagu njiani ambaye pia tuliongozana nae kutoka nyumbani na kumpatia kiasi cha fedha kwa ajili ya vifaa vya ujenzi na nauli ya kurudi Morogoro.na baada ya muda tukawa tumefika kanisani ibada iliendelea vizuri ila tulikaa mabenchi tofauti mimi na mke wangu, na watoto wetu walienda kukaa na watoto wenzao kwa kuwa tulikuwa tumechelewa hivyo mabenchi mengi yalikuwa na nafasi chache.



    Wakati ibada ikiendelea nilihisi kutekenywa na kitu mfukoni nilipo toa ilikuwa ni simu yangu ambayo niliweka muito wa kimyakimya ili isipige kelele tukiwa ibadani, macho yangu yalipigwa na bumbuwazi kuona tena namba ngeni ikiwa imetuma ujumbe ambao nilianza kuwa na mashaka nao, ujumbe wenyewe ulisomeka hivi,,



    “TUKO NJE TUNA KUSUBIRI UKITOKA UJE KUCHUKUA MZIGO WAKO”



    Maneno hayo kwa kweli yalizidi kuniogopesha maana nikagundua kuwa kuna watu wameanza kunifuatilia kama ni swala la kwenda kanisani mawazo tulipata usiku mimi na mke wangu ndipo tukaamua kuwaanda na watoto wetu tukaja kanisani sasa wamejuaje kama tupo kanisani moyo ukaanza kuingiwa na wasiwasi juu ya Sagu.



    Nilishindwa kuvumilia kukaa ndani ya kanisa hivyo nikatoka kwa mwendo wa haraka hali iliyo wafanya walio karibu nami kunishangaa maana nilionekana kama mtu aliyechanganyikiwa huku nikiwa na bonyeza vitufe kutafuta namba ya Sagu nilivyo fika tu nje ikawa tayari inaonekana mbele ya mboni zangu hapo mkono wangu ukaanza kubonyeza kile kitufe cha kijani kumpigia sagu na kuweka simu sikioni nilizidi kushikwa na hasira baada ya kujibiwa,,,,



    ”Ndugu mteja namba unayopiga kwa sasa haipatikani jaribu tena baadae”



    Nilipiga zaidi ya mara nne na jibu likawa lile lile na mawazo ya ule ujumbe wa kwanza ukawa kama umenitoka kwa muda kichwani baada ya kuchanganywa na muhudumu aliye nijibu wakati nikiwa na mpigia Sagu, sikuwa na jinsi ilinibidi nichukue maamuzi ya kutaka kurudi tena ndani ya kanisa,nilivyo piga hatua tatu kabla sijaukalibia mlango wa kanisa ujumbe mwinigine ukaingia hapo ulinifanya nigeuke nyuma na kupepesa macho yangu pande zote kama nitamuona yoyote ambaye anafahamiana na mimi huenda nikamjua huyu anaye nitumia ujumbe usio eleweka kama huu uliongia na kunieleza kuwa……..CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “VIPI IBADA IMEISHA MBONA UMEWAHI KUTOKA?”



    Hapo sikuchelewa tena nikapiga haraka namba hiyo iliyo nitumia ujumbe bahati nzuri ikawa imepokelewa mdomo ukawa na kihere here cha kuongea,,,

    ”Hallo? Hallo?

    Hallo?hallo?



    nikajikuta naongea peke yangu, nilipo toa sikioni kuingalia ilikuwa bado ipo hewani nilizidi kuchanganyikiwa mpaka nikaanza kujuta kwanini nilienda kanisani na familia yangu maana imeshaonekana ni hatari inayo taka kunikumba lakini ghafla nikasikia sauti kwa mbali ikiongea ndipo nilipo weka tena simu sikioni,



    Hallo? Nilizungumza na bahati nzuri muhusikia naye alianza kuzungumza ila nilishtuka baada ya kusikia ananza kutaja jina langu tena ilikuwa ni sauti ya kike,,,

    “Hallo mr.Alfred kazinge”? alizungumza nami sikutaka kupoteza muda nikamjibu kwa sauti ya ukali bila kujali eneo nililopo

    “Wewe ni nani na unataka nini toka kwangu”? Nilihamaki

    ”hahahahaha” alicheka kwa dharau kisha akaendelea kujitambulisha

    ”haina haja ya kunijua jina maana haito saidia cha msingi toka hapo ulipo na sogea mbele utakuta kuna gari aina ya range nyekundu imepaki uje kuchukua mzigo wako.



    Nami nilifanya kama walivyo niagiza ilinibidi nielekee mahali nilipo elekezwa, mwendo wa hatua kadhaa tu ulinifanya niwe nimewasili eneo lile na nilipokuwa nashanga shanga mara kioo cha gari lile aina ya range kikashushwa na mkono ukaonesha ishara ya kuniita nikasogea mpaka kwenye dirisha lile lakini aliyetoa kichwa chake nje huku uso wake ukiwa umefichwa na miwani meusi hakua mwanamke kama sauti niliyo isikia kwenye simu, alikuwa mwanaume tena aliye kuwa amekomaa sana kwa mtazamo.





    Nilipotaka kujua kama kuna mwanamke mle ndani iliniweze kumuuliza anashida gani na mimi, nafasi hiyo nilinyimwa baada ya kukabidhiwa bahasha kubwa ya kaki iliyo kuwa imetuna kiasi kisha gari hilo kuondoka kwa mwendo kasi sana lakini nilipo taka kuifungua bahasha hiyo ilinijue kuna nini nilishtushwa na breki iliyo kuwa imebanwa ghafla kama vile dereva anayetaka kukwepa ajali ya kugonga, hivyo uso wangu ulibidi utazame kwenye gari lile ila nilicho kiona ni yule jamaa aliye nikabidhi ule mzigo akitazama nyuma yangu huku akitingisha kichwa chake kama amegundua kitu fulani hivi.



    Nilipotaka kujua kama kuna mwanamke mle ndani iliniweze kumuuliza anashida gani na mimi, nafasi hiyo nilinyimwa baada ya kukabidhiwa bahasha kubwa ya kaki iliyo kuwa imetuna kiasi kisha gari hilo kuondoka kwa mwendo kasi sana lakini nilipo taka kuifungua bahasha hiyo ilinijue kuna nini nilishtushwa na breki iliyo kuwa imebanwa ghafla kama vile dereva anayetaka kukwepa ajali ya kugonga, hivyo uso wangu ulibidi utazame kwenye gari lile ila nilicho kiona ni yule jamaa aliye nikabidhi ule mzigo akitazama nyuma yangu huku akitingisha kichwa chake kama amegundua kitu fulani hivi. Nilipogeuka alikuwa

    Ni mama David na David hapo akili yangu ikabidi ichekeche kwa haraka na jibu nililo pata ni kwamba yule jamaa atakuwa amejua kuwa hii ni familia yangu na nilipo mgeuzia shingo kwa mara ya pili nilizidi kuogopa baada ya kumuona ametengeneza umbo la bastola kwa kutumia kiganja chake cha kulia na kuonesha ishara kuwa atawashuti, kisha gari hilo likaacha vumbi na kuishia zake,hata hamu ya kutaka kujua kilichopo kwenye ile bahasha sikuwa nayo nilicho kifanya ni kwenda kumshika mkono David na kumwambia Magrety akamchukue Nisha tuondoke nyumbani ila kwa hasira nilitaka kumchapa vibao Magrety kwa maneno aliyo niambia,,,,,,,,



    ”mume wangu tatizo nini mbona ibada haija isha”?

    “fanya kama nilivyo kuambia kamchukue nisha haraka macho huna hata sauti husikii? Niilizungumza kwa sauti ya ukali bila kujali kuwa baadhi ya watu walikuwa wana tutazama



    Magrety hakukaidi agizo hilo, walipo wasili tu niliwasha gari safari ikawa kuelekea nyumbani hakika mwendo nilio kuwa naenda nao kama askari wa barabarani wangeniona wasingee sita kunikamata niliwakosakosa kuwagonga watoto wenye tabia za kucheza barabarani lakini nilimshukuru mungu baada ya kufika salama.



    Mimi na mke wangu tukaelekea chumbani huku nikiwa nimeshika ile bahasha mkononi na kina David kuwaacha sebuleni baada ya kuwa nimemuonya David asithubutu hata kunyakua mguu wake kuutoa nje pia amuangalie Nisha asicheze mbali naye nilifikia kukaa juu ya kitanda huku mama David akiwa ana lalamika mwenyewe

    “maisha gani haya tunayoanza kuishi?

    ”Hatuna amani nayo kabisa au kuna mtu umemkosea mme wangu? Aliniuliza .



    ”Hakuna mtu niliye mkosea wala kumdhulumu haki yake mimi mwenyewe na shangaa haya yanayo tokea ghafla hivi!!! ila yote ni mitihani tu katika maisha mke wangu inabidi tupambane nayo sio wote watakao kupenda wengine ni wanafiki”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilibidi niwe mpole na kusimama kama mwanaume kwenye nyumba maana mke wangu asije kupoteza dira kabisa hata ya kutoa mawazo kama na mimi ningeamua kunyong’onyea.

    Baada ya kumuona kidogo anaanza kutulia nikaichukua ile bahasha na kuanza kutaka kuifungua ila mke wangu akauliza,,

    ” kuna nini humo”?

    ”Ngoja tufungue kwanza ili tujue kuna nini” nilimjibu

    Nikatoa gundi iliyo kuwa imebandikwa kama kufuli ya bahasha na kilichokuwa ndani kila mmoja alishika mdomo, tulitazamana kwa mshangao kisha nikaingiza mkono ndani ya ile bahasha nilicho anza kutoa yalikuwa ni maburungutu ma tano ya fedha mpya na kila burungutu lilikuwa na kiasi cha milioni tano hivyo jumla yalikuwa yana thamani ya milioni ishirini na tano

    ”Nilijiuliza fedha hizi ni za nini? Wakati huo mke wangu alizidi kupagawa na macho yalimtoka na kuendelea kutazama ile bahasha.

    Nilipo ingiza mkono mara ya pili nikatoa karatasi iliyo kuwa imeviringisha kitu fulani kigumu na nilipoikunjua mapigo ya moyo yaliongeza kasi na mke wangu alinyanyuka pale kitandani tulipo kuwa tumeketi kwa mshtuko na kusema kwa sauti ya mshangao,,,,



    ”aaah bastola”? Yesu kristu balaa gani hili mume wangu? Aliuliza maswali yasiyo kuwa na majibu.

    Niliishika bastola ile kisha kuigeuza geuza zaidi ya mara mbili baadae nikagundua kuwa karatasi ile iliyoviringisha bastola ilikuwa na maandishi yalio nipa maelekezo juu ya ile bahasha,,,,,,,,



    ”HIZO FEDHA NI KIASI CHA AWALI KABLA YA KAZI TUNAYO TAKA KUKUPA, NA KAZI ITAKAPO KAMILIKA UTAMALIZIWA KIASI KAMA HICHO PIA HIYO BASTOLA SIO KIFAA KITAKACHO TUMIKA KATIKA KAZI YAKO ILA UTAKITUMIA KUIMALIZA FAMILIA YAKO KWA MKONO WAKO MWENYEWE KAMA UTAKAIDI AGIZO LETU.

    ITAKAPO FIKA SAA 4:30 USIKU NJOO TUKUTANE PALE LANDMARK HOTELI YA RIVERSIDE UBUNGO.KWA MAZUNGUMZO ZAIDI BILA KUSAHAU HIYO BASTOLA ”0768606510 NDIO NAMBA UTAKAZO TUMIA KUTUTAFUTA UKIFIKA.



    Ujumbe huo nilio kuwa na usoma kwa sauti ili mke wangu pia asikie ukazua taflani kwa muda huo baada ya mke wangu kupandwa na hasira na kuanza kunipigapiga na mikono yake kifuani huku akilia na yote hayo ni kwasababu ya upendo alionao kwa watoto wake,,,,



    ”sitaki mimi Alfred hayo mambo yako kama ulikuwa unafanya na wenzio mmalizane wenyewe sio kutuingiza na sisi watoto wangu nawapenda sana”



    Alilalamika kwa muda kisha kuondoka chumbani kwa hasira na kwenda kwa watoto wake nami nilibaki chumbani nikiendelea kufikiria ni kwanini yanatokea haya kuna nini nilicho kifanya kwa mtu? Japo mawazo yakawa yananijia na kuanza kumshtumu pia Helman lakini kila nikijiuliza mara mbilimbili ni kipi nilichomkosea sikupata jibu na kama kukataa mimi na yeye tusiwe marafiki ndio anifanyie hivi mbona mambo yanayo nitokea ni makubwa kuliko hilo la urafiki? Hayo ndio mawazo yalio kuwa yana zungukazunguka ndani ya kichwa changu.



    Magrety alishinda na watoto wake siku nzima bila kurudi chumbani wala kuniita kwenye chakula japo hata kama angeniita nisinge weza kula maana yalio nikuta kwa muda mfupi nilihisi kushiba, nami nilishinda ndani mpaka kiza kika ingia nilipo tazama saa yangu ikawa inaniambia ni saa 3:30 usiku hivyo nikaona muda huo unanifaa sana kujiandaa ili kwenda kuonana na wapuuzi nisio wajua. Maana kutoka magomeni mpaka maeneo ya ubungo ningeweza kumudu foleni kwa muda huo.wa usiku.



    Nilipo maliza tu kujiandaa nikachukua biblia yangu kisha kupiga magoti chini ya kitanda na kuanza kumuomba mwenyezi mungu..

    .

    ”eeh Mungu baba mimi kijana wako nina nyoosha mikono yangu kwako kwa kuwa wewe ndio unaye jua vinavyo onekana na visivyo onekana naomba unilinde mimi na familia yangu,umlinde mke wangu kipenzi na huko niendako naomba nirudi salama maana sijui ninacho endea ila ni katika hali ya kuilinda familia amin,



    Baada ya sala hiyo fupi nilirudiaha biblia yangu kabatini kisha kuchukua ile bastola na kuiseti vizuri.



    wakati naendelea na kitendo hicho Magrety akaingia, alishtushwa na kitendo nilicho kuwa nakifanya maana usoni mwangu nilisha tengeneza v na kama alijua nilichokipanga vile kwamba kama kuna mtu atanilitea ujinga na muua hapo hapo. Magrety alinisogelea na kunieleza



    ”Nakuomba mume wangu usiende huko tafadhali tupige simu kituo cha polisi kwanza kama kwenda basi uende na maaskari”



    kipindi hicho wakati anazungumza hasira zake zilikuwa zimemuisha na kwa bahati mbaya kukasirika kwake kwa mara ya kwanza ndiko kuliko nifanya nijitolee maisha yangu kwenda huko kama kufa ni kafe maana najua nitakufa kishujaa kwa kuilinda familia yangu kama baba anaye jali na kuipenda familia.



    Nilipo kuwa nataka kutoka Magrety akawa ananikataza nisiondoke nilicho, kifanya nika msukumia kitandani huko na kumpa onyo asipige simu kituoni maana hatuwezi jua kuwa hao jamaa wana nia gani na wameweka mitego gani hivyo tuna weza kuongeza tatizo badala ya kulipunguza.



    kisha nikatoka mle chumbani na kumuacha Magrety akilia kilio cha kwikwi nami nikaanza safari ya kuelekea huko,

    wakati nimeshika komea la mlango wa kutokea nje nikakumbuka kitu kichwani ilinibidi nielekee chumbani kwa Nisha nikambusu shavuni wakati akiwa amelala kisha kwenda na chumbani kwa Davidi pia alikuwa amesha lala nilimshika kichwani na kumuambia maneno ya kiume,,,,



    ”David wewe ndio kidume changu cha baadae na kiongozi wa famila hii mungu aendelee kuku kuza na ukuwe salama ili baadae uje kulinda familia yako kama mimi leo ninavyo jitolea maisha yangu juu yenu”



    Nilirudi vyumbani kwao kuwaaga maana sikujua huko ninako kwenda kama nitaweza kurudi hai

    au maiti, baada ya hapo safari yangu ikawa imeiva sasa nilitoka na kuwasha BMW230 yangu

    kuelekea huko na ndani ya dakika kadhaa nikawa nimefika eneo husika nikatoa simu yangu na kuanza kubonyeza vile vitufe husika kama namba ilivyo kuwa inajieleza 0768606510 nika piga na simu ikaanza kuita na baada ya sekunde tu nikasikia sauti niliyo ifahamu kabisa

    Ikisema hallo??!!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilipo mjibu kuonesha kwamba ninamskia alinipatia maelezo,,,

    ”Alfred subiri hapo hapo nimeshakuona”



    Nilitamani kumuita jina lake ili nijue kama ni yeye au nimefananisha sauti, tatizo simu ikakatika ghafla,nilipo itazama ilikuwa imekatwa kusudi,

    Niliendelea kusubiri kama alivyonielekeza huku kichwani na mimi nikipanga maarifa yangu nifanyeje kama litatokea tatizo juu ya uhai wangu.



    Baada ya dakika kupita sauti za viatu zikawa zinasikika zikinisogelea nilipotazama mbele nikaona warembo wa wili walio panda kiasi,wenye shingo ndefu na nyembamba zilizo pambwa na mikufu ambayo ni ghari kununua pia hata miili yao ilikuwa ni myembamba japo kuanzia kiunoni walitenga kiasi kwa vijana wa sasa wanawaita umbo namba nane.

    walivaa nguo zilizo fanana, makoti mafupi yenye rangi nyeusi pamoja na vimini, .mikono yao ilivalishwa gropsi zilizo fanana na rangi ya makoti yao sura, zao zenye weusi uliong’a uliwatambulisha kuwa wao ni waafrika halisi, sura hizo ni kazi kuzitofautisha kama huja zizoea.



    Nilishangaa walivyo jigawa, mmoja akakaa upande wangu wa kulia na mwingine kushoto hapo uvumilivu ulinishinda ikabidi niwaulize kwa ukali ili kujihami,,,,,

    ”nyie ni wakina nani”?

    Twin killers(mapacha wauaji) walinijibu huku wakiwa wameweka sura ya ukatili

    ”Kwa hiyo mnataka nini sasa”? niliwauliza nami kwa ukatili maana nilijua wanawake ni waoga hivyo wanaweza kutishika lakini kumbe ndio nikawa nime wachochea, wakanishika mikono yangu yote wakiwa wamegawana kila mmoja na upande wake.



    Nilipojitikisa kwa nguvu zangu zote ili waniachie kumbe bastola yangu niliyokuwa nimeiweka kwa nyuma walisha itoa bila mimi kujua na kuniwekea kichwani,,, moja alizungumza,,

    ”Songa mbele haraka we kijana”



    Kutokana na jinsi alivyo zungumza kile kiswahili chake nikaanza kuhisi kuwa hawa si watanzania, wakanikukusa hivyo hivyo huku nikiwa na weka hali ya ubishi mpaka tulipo fika nyuma ya ile hoteli ambapo kulikuwa na meza moja iliyo jitenga kwenye maua mengi marefu na mwanga hafifu wa taa zenye rangi tofauti,na kulikuwa na bwawa la kizungu pembeni(swimming pool)



    Meza hiyo ilikuwa imezungukwa na watu wapatao saba walio shiba vilivyo wote wakiwa wame simama kumzunguka mtu moja ambaye yeye aliketi kwenye kiti nikahisi huenda huyu ni bosi wao nikaanza kuogopa,



    Sauti ya kofi ilisikika kutoka kwa yule jamaa aliye keti na kuwaambia wale madada kwa lugha nilio weza kuitambua kuwa ni kinyaruanda, ila siku bahatika kujua maana ya yale maneno.

    baada ya ishara hiyo ya kofi wakaniachia kisha nika sogezewa kiti nami nika keti pamoja nae.

    Alinitazama kwa dharau halafu akachukua simu yake iliyo kuwa juu ya ile meza na kupiga, sikujua ni nani aliye kuwa ana mpigia ila alisema,

    ”hallo? eeh tumesha muandaa” kisha aka kata simu

    Ndani ya muda mchache nilishtuka baada ya kuguswa bega kwa nyuma nilipo geuka alikuwa ni Helman, nilinyanyuka kwa kuhamaki nikarudia kumuita tena,

    ”Helman ni wewe unae nifanya kukosa furaha mimi na familia yangu?

    Alicheka kisha akasema,

    ”Alfred raha unajinyima mwenyewe wewe na familia yako mbona tulivyo kuwa marafiki haukukosa amani”?aliniuliza lakini sikumjibu.





    Alinitazama kwa dharau halafu akachukua simu yake iliyo kuwa juu ya ile meza na kupiga, sikujua ni nani aliye kuwa ana mpigia ila alisema,

    ”hallo? eeh tumesha muandaa” kisha aka kata simu

    Ndani ya muda mchache nilishtuka baada ya kuguswa bega kwa nyuma nilipo geuka alikuwa ni Helman, nilinyanyuka kwa kuhamaki nikarudia kumuita tena,

    ”Helman ni wewe unae nifanya kukosa furaha mimi na familia yangu?

    Alicheka kisha akasema,

    ”Alfred raha unajinyima mwenyewe wewe na familia yako mbona tulivyo kuwa marafiki haukukosa amani”?aliniuliza lakini sikumjibu.



    Naye akaja aka kaa kwenye kiti, yule jamaa niliye mkuta amekaa pale mezani mara ya kwanza wakati naingia akawaruhusu wale mabaunsa pamoja na wale madada mapacha waondoke hivyo tukawa tumebaki watatu pale mezani na Helman akanzaa kuniambia lengo la mimi kuwepo pale,,



    ”Alfred kwanza unatakiwa ujue duniani kuna watu na viatu, sasa leo nakuweka wazi kuwa mimi si katika watu ila ni kiatu, kuunda urafiki na wewe sio bure ila ni kwa maana ili nitengeneze pesa kupitia mgongo wako hivyo kazi ninazo taka kukupa ni mbili ya kwanza,

    ” nataka uwe unanipa taarifa kila gari la fedha linapo kuwa linasafirisha fedha kutoka benki moja kwenda nyingine ili tuweze kuchukua chetu mapema”.

    Na kazi ya pili,

    ”Unatakiwa uni pambe kwa meneja wako kuwa mimi ni mteja mzuri sana katika swala la mikopo ili niweze kuwa naye karibu na aniamini hata siku mambo yakibuma achukue muda kujua kama ni mimi ndiye na husika atakapo sikia tetesi juu yangu”



    Jicho lili nitoka na kutetemeka baada ya kugundua maelezo yake yana maanisha kuwa yeye ni jambazi na ndio kazi iliyo kuwa inamuweka dar es salaam hata hivyo hakuishia hapo aliniangalia kisha akamuangalia yule jamaa mwingine na kunitambulisha,



    ”huyu jamaa anaitwa Cholo yeye ni mtu wa Rwanda ninafanyanae kazi hii kwa muda wa miaka mingi sana na yeye ndiye anaye nichoresha dili nyingi sana za kwao na wale mapacha amekuja nao huku tanzania kwa kuwa kule nchini kwao wameshashtukiwa na wana tafutwa na polisi”



    Maneno yake yalinifanya nizidi kumchukia Helman maana alikuwa anataka kunishirikisha katika kazi ambazo hata cheti chake sina nilinyanyuka kwa gadhabu na kumwambia,

    ”hiyo kazi yako fanya na hao hao wakimbizi wenzio lakini sio mimi, siwezi kuwa kama kunguru wako hawa mapacha walio kimbia nchi yao wakati ni raia halali wa Rwanda naenda kutoa taarifa kituoni”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Nilipo maliza kuzungumza niligeuza mwili wangu na kuanza kupiga hatua kuondoka, zilipofika hatua tano mbele Helmani akaniita nilisimama kwa sekunde bila kumgeukia kisha ndio nikageuza shingo yangu,



    miguu ilitaka kuishiwa nguvu nilipo muona baunsa mmoja akimleta Sagu huku nguo zake zikiwa zimeloa damu na kisha kumtupa chini pale pembezoni mwa bwawa la kizungu(swimming pool) nilirudi haraka haraka na kumsogelea Sagu.



    nikagundua kuwa walimchoma kisu dakika kadhaa nyuma baada yakuona tundu lililo kuwa lina toa damu nyingi na yule baunsa akiwa ameshika kisu kilicho lowa damu ila alikuwa bado anapumua nikaanza kumuuliza kwa sauti iliyo kuwa inakaribisha mchozi,,

    ”Sagu imekuaje mdogo wangu umefanya nini na hawa wamekujuaje wewe eeh? Wakati huo nilikuwa nimepiga magoti na kujaribu kumuinua nikimshika mabega yake,

    ndipo alipo anza kunieleza.,,,,,



    ”hawa jamaa waliwahi kutuona mimi na wewe nilipo kuja mara ya kwanza kununua vifaa vya ujenzi siku za nyuma kule karia koo na inavyoonesha walianza kukufuatilia muda sana kabla hata ya Helman aja kufuata moja kwa moja na kuanzisha urafiki na wewe na tulipo achana walinifuata na kuniuliza kuwa nina uhusiano gani na wewe, nili waambia nakusaidia tu kubeba vifaa vyako maana sikujua wanalengo gani na nilikuwa siwajui hivyo ilinipa ugumu kujitambulisha moja kwa moja, ndipo walipo nipatia pesa na namba zao za simu niwe na wapa taarifa zako, kiufupi mimi ndiye niliye rahisisha Helman kuanzisha urafiki na wewe”



    Maneno ya Sagu yalinipandisha hasira lakini huruma ilinijia kila nilipomtazama na hali aliyo nayo kwa wakati ule, lakini sikujua bado sababu ilio wafanya waamue kmchoma kisu mpaka nilipo muuliza swali hilo Sagu na kunijibu,,



    ”walipo nipatia zile namba na pesa hawakujua kama mimi sikai hapa dar es saalam na walipo kuwa wana hitaji taarifa zako nilikuwa nakupigia na kuzua jambo lolote lile kuhusu ujenzi halafu nikawa na kuuliza swali ambalo walilo kuwa wanataka kujua huku nikijichekesha chekesha ili ujue kama ni utani”



    ” sasa kumbe mdogo wake na Helman alikuwa anasoma chuo kikuu cha mzumbe aliniona siku moja Morogoro mjini ndipo alipo mpigia simu kaka yake na kumueleza kuwa ameniona,

    baada ya muda Helman alinipigia na kuniuliza niko wapi na mimi nikamdanganya kuwa nipo dar es saalam, na neno alilo niambia ni kuwa anataka kuonana na mimi.jumapili”



    ” hapo sikuwa na jinsi zaidi ya kuelekea stendi ya mabasi msamvu na kuchukua gari kuja huku ili asijue kama nilikuwa Morogoro ndio sababu ilio nifanya nije usiku ule wa jumamosi bila taarifa nyumbani kwako na jumapili ile nilivyo wapa taarifa kuwa nipo na wewe wenzie waliamini kuwa nipo hapa dar na ulivyo nishusha pale ndipo nilipo kuja kuonana na Helman,”



    ”kwakuwa Helman anamuamini sana mdogo wake ilibidi anipeleleze kwa kunipa kipigo mpaka nilipo kubali kuwa nilikuwa Morogoro na kisu hiki wamenichoma nilipo kataa kuwaeleza ni kitu gani na fanya kule Morogoro hivyo hawajui kama unajenga, siri yako mimi ndio nakufa nayo”



    Mpaka Sagu anamaliza kunieleza njama nzima waliokuwa wanaifanya ya kunizunguka mimi mchozi ulikuwa umesha lowesha shavu langu lote,





    kimya kweli kilitawala kwenye kinywa cha Sagu kumbe alisha kata roho, hasira zilinipanda ,nilipo geuka kwenye meza walio kuwa wameketi kina Helman ilikuwa nyeupe kumbe wakati walivyo mtupa Sagu pale chini wakakimbia maana walijua hato weza kupona na ile ni kesi ya mauaji na ghafla maskio yangu yakaanza kusikia ving’ola vya polisi

    Ndipo nami nilipo pata akili ya kukimbia, niliongoza moja kwa moja mpaka kwenye

    BMW230 na kuiwasha na mwendo wa kasi ukachukua nafasi barabarani, nilipishana na magari yasiyo pungua matatu ya polisi yakielekea land mark hotel kwenye tukio japo sikujua ni nani aliye wapa taarifa, hilo si kujali kwa wakati huo kilicho kuwa akilini mwangu ni kutoka eneo lile maana kama ningeonekana wange hisi kuwa ni mimi nahusika na mauaji kwa ushahidi wa nguo zangu kulowa damu nilizozipata wakati nime mpakata marehemu Sagu,



    kila nilipo kuwa na simama kwenye foleni hofu ilizidi kunielemea moyoni mwangu mpaka nafika getini kwangu sikuamini kama nimeweza kujitoa kwenye eneo lile la hatari, nilichukua simu yangu na kumpigia Magrety(mama David) aje kunifungulia geti lakini simu yake ikawa haipatikani na usiku ndio ulikuwa unazidi kuwa mnene japo siku angalia saa ila nili hisi yaweza kuwa ni kama saa nane hivi.



    Nilishuka kwenye gari na kwenda kuluka ukuta kisha nikaenda kumgongea dirishani aniletee funguo za geti, alipo kuwa analeta funguo akataka kupiga kelele baada ya kuziona damu kwenye shati langu akijua labda mimi ndiye nilie jeruhiwa nikamtuliza na kumwambia tuta yazungumza chumbani, nikafungua geti na kuingiza gari ndani.



    Magrety alikuwa amesimama kwenye kizingiti cha mlango akinisubiri nilimsogelea na kumshika kiunoni ili asiwe na hofu na kwenda naye chumbani. Huko ndipo kimbembe kilipo anza baada ya Magrety kushindwa kuniamini juu ya damu nilizo nazo aliongea kwa wasiwasi huku akinipapasa maeneo ya tumboni kama angeweza kuliona jeraha lakini haikua hivyo, baada ya kulikosa ndipo sauti ya ukali na yenye kuogopa ikamtoka,,,,,



    ”Alfred umeua mume wangu?

    ”sijaua mke wangu? Nilimjibu

    “Mbona umelowa damu zimetoka wapi kumbuka uliondoka na ile bastola huku ukiwa na hasira balaa gani hili lina ikumba nyumba yangu!!!!!!!!!!!” alizungumza Magrety



    Nikachua akili kichwani, kwamba kama nita mwambia Sagu amefariki litazuka jambo lingine usiku ule ili nibidi ni mbembeleze tuzungumze kesho ili hofu na jazba alizo nazo zipungue, nilimshika kwenye paji lake la uso na kumtazama kwa jicho la huruma kwenye mboni za macho yake kwa dakika kadhaa bila kumwambia chochote kisha nikamuacha chumbani nami nikaelekea bafuni kuoga ili kutoa taka mwili pamoja na zile damu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati natoka bafuni huku nikijifunga funga taulo vizuri nikashangaa kumuona mama David amekasirika vibaya yani na akiwa ameshika simu yangu mkononi nilipo muuliza nini tatizo alinijibu kwa kuniuliza swali,,,



    “Kati yako na Helman nani ameusika na mauaji ya Sagu”?



    Moyo ulinipasua ghafla, amejuaje huyu? Ndio swali nililojiuliza kichwani mwangu nilipo itazama ile simu nikaona mwanga kwenye kioo hauja zimika nika hisi huenda kuna mtu amepiga au ametuma ujumbe,nikampokonya ile simu kwa nguvu na nilipo itazama nikaona ujumbe ulio kuwa umefunguliwa muda si mlefu aliye tuma alitumia namba ngeni hivyo sikumjua muhusika ni nani na alisema,,,,,,,



    ”ukijifanya mjanja naenda kutoa taarifa kituoni juu ya mauaji ya Sagu”



    Sikuwa na jinsi ilinibidi nimueleza ukweli tu mke wangu kwa kilicho tokea kule nilipo toka, hapo kidogo akawa kanielewa, akanyanyuka na kwenda kuchukua biblia kabatini na tukamuomba mwenyezi azidi kutuepusha na mabalaa. Tulipo maliza nikamuomba ni lale maana asubuhi natakiwa kuwahi kazini kama mambo mengine tutazungumza kesho na kujua nini kitaendelea.



    Asubuhi na mapema nikaamka nikajiandaa huku moyo wangu ukiwa na hofu maana sikujua nini hatima ya tukio lile baada ya polisi kwenda pale hotelini,nika toka nje kuelekea kwenye gari langu ili ni wahi kazini lakini sikuweza kufanya hivyo kutokana na kuona damu kwenye siti niliyokuwa nimekalia jana usiku hivyo ilinilazimu ni pande bodaboda mpaka kazini.



    Wakati naendelea na kazi pale ofisini kwangu akaja mfanya kazi mwenzangu akiwa na gazeti lililo andikwa ,,,,



    ”mtu mmoja auwawa na watu wasio julikana usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya landmark iliyopo maeneo ya river side ubungo na jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi kuwa baini wauaji hao”

    huku gazeti hilo likiwa limewekwa picha kubwa kwa mbele ya marehemu Sagu iliyo pigwa kwenye tukio hilo.



    Hali ilizidi kuwa tete kwa upande wangu siku hiyo nilijikuta kukosa amani kabisa tangu nilipo ona picha ile kwenye lile gazeti, ufanisi wangu wa kazi ulipungua ilipofika mishale ya saa saba mchana ilinibidi niombe ruhusa kwa meneja kuwa naumwa ili nikapate muda wa kupumzika kutokana na hekaheka za jana na kujadili swala lile na mke wangu.



    Mchana huo nilipanda daladala kurudi nyumbani huko pia walizidi kunichanganya maana kulikuwa hakuna jambo walilo kuwa wanazungumza zaidi ya tukio lile la mauaji ya Sagu

    ”jamani duniani kuna watu wa katili sana unawezaje kutoa uhai wa mwenzako kama kuku”

    Utazani wao hawajaumbwa au hawato kufa” hizo zilikuwa sauti za abilia walio kuwa nyuma yangu wakionesha kusikitika juu ya tukio lile.



    Daladala ilipofika kwenye kituo changu nilishuka nakuongoza njia ya nyumbani kwangu, baada ya kupita nyumba kadhaa kabla sijafika kwenye nyumba yangu nilistaajabu kumuona Cholo yule jamaa wa kinyaruanda niliyetambulishwa na Helman akitokea maeneo ya nyumbani kwangu nilisimama kuhakikisha kama ni yeye au kupagawa kwangu tu, lakini alivyo sogea alikuwa ni yeye kweli, naye alipo niona alishtuka pia aliningalia kwa jicho la shari kisha akaongeza mwendo wa kutembea.



    Kitendo kile kilinifanya nianze kukimbia kuwahi familia yangu ili nijue kama ipo salama nilifika nyumbani na kukuta geti lipo wazi nikaelekea sebleni nikakuta makochi yamesogezwa na vitu vipo katika mpango usio eleweka nili nibidi niite kwa hofu,,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ”Magrety Magrety?

    ”Abee mume wangu”aliitika kisha kuja pale sebuleni kutokea chumbani kwa David akiwa ameshika kifaa cha kudekia kisha kuniuliza,,,

    “Mbona mapema Alfred kuna usalama kweli huko?

    ”Usalama upo kiasi ila habari za kifo cha Sagu ndio limekuwa gumzo la jiji huko nje”

    ”kuna mtu aliye kuja hapa” nilimuuliza

    ”hapana hajaja mtu”alijibu

    ”Kwanini umeuliza hivyo”?aliniuliza

    ”Maana geti lipo wazi”

    ”Ooh walikuja wazoa taka watakuwa walisahau kufunga lakini huja nijibu kwanini umewahi kurudi?alijibu na kuniuliza nami nikamueleza sababu iliyo nifanya niwahi kurudi.

    ****************

    ITAENDELEA  

0 comments:

Post a Comment

Blog