.
Simulizi : Mkakati Wa Kuelekea Ikulu
Sehemu Ya Tano (5)
* * *CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku mbili za kusubiria zikaanza kumchosha Samson. Hata hivyo hakuchoka. Aliendelea kusubiri tu. Kitu fulani kiliendelea kumwambia kuwa lazima tu Steve au Masurufu watarudi katika nyumba hiyo kukamilisha masuala yao fulani fulani.
Hakutaka kuamini mara moja kuwa baada ya mauaji yale yaliyopelekea kupotea kwa Steve na Masurufu hata wakasakwa katika viunga vyote bila kupatikana kwamba watakuwa wameyeyuka moja kwa moja. Na hili alilipa nguvu kufuatia lile angalizo.
Naam! Angalizo alilotoa kwa mzee Anderson Chilonga, ambalo kwa hakika lilikuwa limefanya kazi ipasavyo. Mipaka yote ilikuwa imefungwa kwa ajili ya Masurufu na Steve, askari wenye picha zao waliwekwa kila palipohisiwa kuwa panaweza kumtoa mtu nje ya Dar es salaam.
Tishio kwamba uchaguzi huu utakuwa na tatizo liliwasumbua vichwa takribani maafisa wote wa usalama pamoja na maafisa wa jeshi la polisi kiasi cha kila mmoja kuhaha kutaka kuweka hali sawa.
Akiwa anapata taarifa zote toka kwa rafiki zake waliomo ndani ya jeshi la polisi na vyombo vingine vya usalama, Samson alijiona kama aliye hatua moja mbele katika mapambano hayo kwa kule kumfahamu kwake Steve na ofisi yake yake Siri.
Ofisi ambayo alikuwa amejaribu kuifungua kwa mbinu zake na kutofanikiwa.
“Maadamu taarifa zinasema hajatoroka nje, na kwamba inawezekana kuwa wameamua kujificha kwa dharura, basi watarudi tu na hapo ndipo kiama chao kitakapotukia!” Samsoni aliamua na kuendelea kusubiri.
* * *
Kipindi kilichofuatia kilikuwa kigumu zaidi kwa jeshi la polisi, vyombo vya usalama na serikali kwa ujumla. Maisha ya raia wenye ulemavu wa ngozi maarufu kama Albino yalianza kuwa hatarini na kuwafanya waishi kwa mashaka mazito.
Ilianzia Kigoma, mmoja akauawa na kunyofolewa baadhi ya viungo vyake, kabla hili halijaisha ikafuatia Tabora kabla Mwanza nako mambo hayajaharibika.
Nchi ikatikisika na kuzomewa na mataifa ya nje.
Wanaharakati wakaandama na kulaani, hali Albino wenyewe wakianza kuishi kwa hofu pasipo kujua nani atafuata kesho. Wakahaha kuomba Serikali iwasaidie na kuwalinda. Ulinzi miongoni mwao ukaongezwa. Polisi wakaapa kuwakamata wote walioendesha unyama huo..
Alipouawa Albino mwingine kule Shinyanga na maiti yake kuonekana siku ya pili ikiwa imeharibika vibaya, ndipo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliposimama na kutoa hotuba kali na kutaka watuhumiwa wa vitendo hivi wawe wamekamatwa na kufikishwa mbele ya sheria haraka iwezekanavyo. Akamtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi aiongoze oparesheni hiyo na kumpelekea moja kwa moja taarifa.
Hatua hii ilifuatiwa na ile ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kububujikwa na machozi wakati alipokuwa akisikiliza kisa cha mmoja wa Albino walionusurika katika kadhia hiyo ambaye hata hivyo alikatwa viganja vya mikono yake miwili. Akamuagiza Mkuu wa Polisi kuhakikisha maharamia hao wanakamatwa.
Mkuu wa Polisi akamuahidi kulifanyia kazi. Ahadi ambayo aliitimiza.
* * *
Wakati hali ikiwa tete hivi Emanuel Kuho, wakala wa Frank aliyekuwa amepanga Mwanza Hotel; alikuwa amepungukiwa na lita tatu tu za damu, pamoja na kiganja kimoja kutimiza yale mahitaji ya Bosi wake Frank.
Kwa mujibu wa wa Robinson mtu aliyempa jukumu la kumtekelezea kazi hiyo kwa shilingi milioni tatu kwa kila kiungo, laki tisa kwa kila lita moja ya damu alikuwa amehakikishiwa kwamba upungufu huu wa leo ungeweza kumalizwa kabisa.
Kiasi alijisikia mwenye furaha isiyo kifani. Hii ni kwa vile ndege ya kukodi ilikuwa ikimsubiri uwanjani. Hivyo alijua muda si muda Robinson atamletea amana yake naye ataondoka usiku huo huo na kurejea Dare s salaam ambako atamkabidhi Frank mali yake naye atamaliziwa fedha zilizosalia na kuwa miongoni mwa mamilionea.
Hakuona ni kwa nini asipambe na kusherehekea.
Naam, akainua simu na kumwita mmoja wa wahudumu wa Hotel ile ambapo alimuagiza chakula, vinywaji na kitu kingine kimoja zaidi. Mhudumu akaondoka amekenua baada ya kupewa ahsante ya shilingi elfu ishrini.
Dakika chache baadae Emanuel alikuwa katikati ya maguberi mawili ya kike wakiogelea katika msitu wa vinywaji na makulaji. Alikula, kunywa na kufanya mapenzi na malaya wale mpaka pale alipopigiwa simu kwamba mzigo wake ulikuwa tayari. Ni hapo alipowatimua wale vyangudoa .
“Nawashukuruni sana, sasa mnaweza kwenda!”
“Jamani mara hii”, Mmoja akalalamika kwa geresha hali moyo ukimpaa kwa furaha baada ya kukabidhiwa kibunda cha shilingi laki moja kwa kazi ya kipuuzi kabisa.
“Msijali, mie naingia katika majukumu mengine na nikiwahitaji tena, nitamjulisha Peter nae atawaleta!”
“Kweli?”
“Kabisa!”
“Usijali, tukikutana tena utafurahi mara mbili ya hapa!”
“Nitashukuru!”
Wanawake wakavaa na kuondoka. Naye akaingia bafuni, kuoga na kuvalia nadhifu. Malipo ya Robinson akayaandaa na kuyaweka kwenye bahasha kabisa.
Hakika, Robinson alifika baadae. Na hakuwa pekee. Alikuwa na Polisi ambao walimkamata Emanuel Kuho kama kuku, na kumpeleka kituoni ambako aliminywa vizuri na kurupoka kila kitu ikiwemo ndege ya kukodi aliyokuja nayo kutoka Dar es salaam ambayo ilikuwa ikimsubiri Uwanja wa ndege.
Polisi wakabaki wanashangaa, mtu kukodi ndege kutoka Dar es salaam hadi Mwanza kwenda kufanya mauaji tu.
Dakika chache baadae, Robinson, Kuho, maafisa wa Polisi pamoja na watuhumiwa wengine zaidi wa matukio ya mauaji ya Albino, walikua hewani kurejea Dar es salaam wakitumia ndege ile ile ya kukodi iliyokuwa ikimsubiri Emanuel Kuho.
Moyoni, maafisa wale wa polisi walikuwa wamkimshukuru Mungu kuona kwamba zoezi lililokuwa kubwa kiasi cha kupigiwa kelele mpaka na Rais mwenyewe, licha ya kuwa gumu, lakini limekuwa fupi na lenye manufaa kwao.
Ilikuwa ni baada ya jitihada za kuwapeleleza waliofanya mauaji na vitendo vya ukatili dhidi ya Albino kutozaa matunda ndipo lilipokuja wazo la kuimarisha Ulinzi dhidi ya Raia wenye ulemavu huo kwa polisi wenye silaha kujichanganya katika familia zenye raia hao.
Wazo ambalo limekuwa na manufaa kwa kuwa watu waliokuja kufanya uhalifu walikamatwa kirahisi na walipobanwa wakawa wamewaleta mpaka kwa Robinson ambaye aliwapeleka mpaka kwa Kuho ambaye naye alikuwa mbioni kuwafikisha miguuni kwa Frank.
Kama ilivyokuwa kwa Kuho, Frank nae alikamatwa siku hiyo hiyo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
SURA YA TISA
HATI YA KUMKAMATA MASURUFU
Ilikuwa ni lazima arejee katika makazi yao ili kukamilisha jukumu moja zito aliloagizwa na Christopher McDonald. Hivyo akiwa anajua fika kuwa nyumba ya Dr Masurufu imeshakuwa eneo la makachero, Steve alichukua kila aina ya tahadhari ikiwemo hii ya kuingia usiku akitumia moja ya milango ambayo hutumika kwa nadra sana.
Bahati haikuwa yake, kwani eneo aliloamua kulitumia kwa kuingilia lilikuwa jirani sana na eneo alilojificha Samson kidude ambaye wakati huu alikuwa ameanza kusinzia. Zile kukuru kakara ambazo zilifanyika kwa utaratibu uliolenga kuzifanya zisitoe ukelele zikawa zimemuamsha.
Akasimama imara sambamba na ukuta, mavazi yake meusi yakimfanya awe sehemu ya kiza hicho. Alitulia kwa utulivu mpaka Steve alipomaliza kukuru kakara zake na kuanza kupiga hatua fupi fupi zenye umakini wa aina yake kuelekea jengo kuu ndipo Samson alipomwambia.
“Karibu nyumbani shujaa!”
Steve akashtuka na kugeuka haraka kwa kasi mkono wake ukisafiri kwa kasi kuelekea kule iliko bastola yake. Akajikuta amechelewa kwani tayari alikuwa anatazamana na mdomo wa bastola ya kisasa aina ya Colt 50 iliyotengenezwa na Mjapani. Kwa kila hali Samson alikuwa amemuwahi.
“Unanishangaza! Uliwezaje kuwaua vijana wangu kijasiri kule hospitali, halafu ushindwe kuja mchana katika makazi yako tena utumie milango isiyotumika!”
“Wewe ni nani?” Steve akauliza akiwa na lengo la kumvizia Samson aweze kumpotezea silaha yake. Lengo ambalo Samson pia alilijua! Samson akatabasamu. Akimwamuru Steve asogee mbele kulikokuwa na uwanja na mwanga wa kutosha. Steve akatii.
“Unataka kunijua siyo, utanijua tu. Lakini kwanza niambie kwa nini ulimuua mama Masurufu?”
“Siyo mimi niliyemuua!”
“Ni wewe! Watumishi wote wa Dr Masurufu walikuona. Wewe ndiye uliyekuwa mtu wa mwisho kuingia chumbani kwake, na toka ulivyotoka hakuna yeyote aliyeingia mpaka maiti yake ilipoonekana juzi!”
“Nakwambia sio mimi niliyemuua, hutaki shauri yako!”
“Unajifanya jeuri siyo? Utafika wakati utatapika kila kitu. Na Dr Masurufu umemficha wapi?”
“Sijui unaongea nini! Mimi ni mlinzi tu!”
“Unakuaje mlinzi mpumbavu kiasi hicho usiyejua wapi alipo bosi wako?
Kimya.
“Mikono juu!” Akaamrisha. Steve akatii.
Samson akamsogelea. Ilikuwa fursa adhimu ambayo Steve alikuwa akiisubiri kwa hamu. Kwa uangalifu wa hali ya juu Samson akaanza kumkagua Steve akichukua silaha hii na ile na kifaa hiki na kile toka katika mwili wa Steve na kukitupa kushoto.
Ulikuwa ni wakati huu Steve aliposhusha mikono yake kwa nguvu, ikatua katika kichwa cha Samson na hapo hapo akaachia teke kali lililopiga bastola ya Samson ikapotelea kizani. Wakati huo huo akapeleka mapigo mawili ya karate ambayo licha ya Samson kuyakinga, bado yalimpeleka chini.
Steve akamuacha Samson ainuke. Tukio hili likamshangaza Samson, Steve alikuwa na nafasi nzuri ya kuendelea kumshambulia lakini akamuacha. Steve akamuhimiza ainuke.
“Inuka ujiandae. Bila shaka ni Samson Kidude. Nimekuwa nikisikia sifa zako tu, pamoja na kwamba nimetumwa na bosi, nataka nihakiki, je ni kweli sifa hizi unazo au wamekuwa wakikuvisha kilemba cha ukoka. Inuka Samson, inuka!”.
Samson akainuka. “Bosi wako ni nani?” Akauliza.
“Haikuhusu!” Steve akajibu kijeuri huku akimzunguka “Mind your business!” Akaongeza akitupa pigo la kungfu. Samson akaliona na kulipoteza. Akarusha lingine na lingine. Samson akayapoteza.

Alipoona amepoteza mapigo ya kutosha ya Steve na Steve anaelekea kuchoka , ndipo naye alipoanza kutupa pigo moja moja. La kwanza Steve akalikwepa, Samson aliporusha teke, Steve akalidaka na wakati anajiandaa kuunyonga mguu, Samson alijipindua na kumpiga teke jingine zito katika shavu la kushoto kwa kutumia mguu uliobaki chini na Steve akaenda chini pamoja na Samson.
Wakati huu Samson alikuwa ameshaweza kumsoma vizuri Steve na kugundua mitindo yote anayotumia, hivyo yeye aliyapoteza mapigo ya Steve katika mitindo ya Steve na kutoa ya kwake mitindo tofauti kabisa.
Mitindo ambayo ni aghalabu kwa wanafunzi wa kawaida kuijua kutoka kwa walimu wao. Yeye Samson aliijua mitindo hii kwa kuwa mwalimu wake wa Tai-chi kule Hong Kong alimpenda kupita kiasi, akawa amemfundisha kila alilolijua huku akimpa siri za ndani za kushinda mapambano magumu.
Na kila Samson alipozitumia mbinu hizo, hakuwahi kushindwa. Na hapa wakati anaziutumia mbinu hizi, alifaulu kumnyuka Steve kama mtoto. Hili lilimshangaza na kumuumiza sana Steve pengine kuliko kipigo alichopokea maana kila alivyojitahidi ajikurupushe na kuonyesha uwezo, ndiyo alivyozidi kuchezea kichapo.
Kutahamaki akawa hoi pale sakafuni, uso ukiwa hautamaniki.
“Haya inuka na uniongoze ndani, nione mlichokifungia mle. Natumai sasa unaweza kujibu maswali yangu vizuri!” Samson alitamba baada ya kuhakikisha amempokonya Steve silaha zote vikiwemo vidonge vya sumu ambavyo labda pengine Steve angevitumia kujiua akizidiwa kabisa na Samson.
Steve akajizoazoa pale na kuinuka. Roho ikimuuma kuona namna alivyonyanyaswa na kudhalilishwa na mtu mweusi kutoka Afrika. Akaapa kumuua Samson kidogo kidogo kwa mateso makali mara tu atakapomtia Samson mikononi.
Akanza kuongoza kuelekea lilipo jumba la Dokta Masurufu!
“Siyo huko!” Akafoka Samson. “Nipeleke katika kile kijumba chako!
Yes! Steve akafurahi kimoyomoyo akimuongoza Samson. Nakuonea huruma kaka, akaendelea kusema kimoyomoyo. Kunirudisha katika chumba kile ni sawa na kumrejesha mamba mtoni baada ya kumshinda katika nchi kavu!CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hatua chache toka kilipo kijumba kile, Steve aliinama na kuutoa mfuniko fulani uliokuwa sawa sawa na ardhi. Samson akamtazama vizuri zaidi bastola mkononi huku akiwa tayari kuzuia hila zozote ambazo Steve angeweza kuzifanya.
Steve hakufanya hila, badala yake alibonyeza bonyeza pale chini kulikokuwa na mfuko ule, kutahamaki mlango wa kile kijumba ukaanza kufunguka kidogo kidogo kwa kuzama ardhini. Lango la kijumba kile lilipobaki wazi, Steve akawa wa kwanza kuingia ndani. Samson akamfuata kidogo kidogo kwa hadhari zote, naye alipoingia ndani tu mlango ukaanza kujifunga.
“Nani kakuruhusu ufunge mlango?” Akafoka Samson “Fungua mlango haraka!” Akaamuru macho yake yakizunguka huku na huko. Yakalakiwa na mandhari ya kupendeza na kuvutia. Kijumba kile kilikuwa kimejengwa kwa mtindo wa namna yake, hali ndani kukiwa na nafasi kubwa ya kutosha kuingia hata Fuso mbili na zikaenea bila tabu.
Samson akashangaa kwa nini muda wote aliokuwa anakuja hapa kumpeleleza Masurufu hakujiwa na wazo la kukitembea kijumba hiki. Kijumba ambacho kilielekea kubeba kila kitu. Samson akafoka zaidi “Fungua mlango nakwambia!”
Steve akatabasamu, nguvu zikiwa zimeanza kumrejesha akauliza kwa maringo.
“Unaogopa nini na hali umeshanishinda katika mapambano ya mikono? Na hali ukingali umeshika bastola?!”
“Nimesema fungua mlango!”
“Na nikikataa je?”
“Nakupa nafasi moja ya mwisho!” Samson akatua na kumeza mate. Safari hii mlango ukiwa umejifunga kabisa. “Ukileta ujeuri zaidi nitajua la kufanya na hutapata zaidi ya hasara. Haya fungua mlango!”
“Okay nitafanya upendandavyo!” Alikuwa Steve kwa maringo akivuta hatua kuelekea ukutani kulikokuwa na swichi mfano wa zile za kuwashia umeme. “Mlango unafunguka sasa hivi Sir!” Steve akasema akibonyeza mojawapo ya zile swichi.
Kilichotokea Samson hakukitegemea.
Alijishtukia akigongwa na kitu kizito kisogoni mfano wa kitako cha Bunduki ambacho kilimfanya ashindwe kujihimili akajikuta akianguka kifudifudi hali bastola ikimtoka mkononi na kuangukia mbele.
Akajitahidi kuamka kadiri alivyoweza ili apambane na Steve, akashindwa, akaona nguvu zikipungua kwa kiasi mwilini mwake hali macho yakiona giza. “Shit!” Akaguta kwa nguvu akiilani bahati yake. Sauti pia haikutoka.
Akapoteza fahamu!
“Shenzi taip!” Steve akasonya wakati akiokota bastola ya Samson aliyelala kama mzoga hatua chache mbele yake. Akamtazama Samson na kutikisa kichwa kwa masikitiko “Umekwisha Samson! Akasema kwa mnong’ono mzito akiondoa kiwambo cha kuzuia usalama katika bastola yake.
* * *
Baada ya kupokea simu hii, Inspekta Kimaro alilazimika kuondoka katika hafla ya kumpongeza Askari mwenzao wa ngazi za juu aliyerejea toka Masomoni ambapo alikuwa amepata alama nzuri kiasi cha kuipa sifa Tanzania. Na jeshi liliamua kumuandalia hafla kumpongeza. Miongoni mwa watu walioalikwa na kuhudhuria alikuwa Inspekta Kimaro ambaye wakati huu aliwaomba radhi wenzie kwa maelezo kuwa kuna dharura, akapanda gari yake na kuelekea ofisini kwake ambako alikuta wageni wawili wakimsubiri, Kachero Inspekta Mathias na Sub Inspekta Mina.
Hawa walisimama mara tu Kimaro alipoingia, wakakakamaa huku wakiinua mikono na kupiga saluti miguu yao ikiwa sawa kabisa. Sauti zikawaponyoka kwa pamoja,
“Jambo Afande!”
“Jambo!” Inspekta Kimaro akajibu akizunguka nyuma ya meza yake na kuketi. “Enhe?” akasema hali akiitoa kofia kichwani na kuitua mezani. “Leteni taarifa. Nimelazimika kuacha sherehe kuja kuwasikiliza kwa ajili ya unyeti wa kazi niliyowatuma. Nawasikiliza!” Akatua.
“Tunaomba utayarishe hati ya kumkamata Dr Masurufu!” Akasema Mina na kuongeza “Na zoezi hili lifanyike haraka iwezekanavyo, ikiwezekana usiku huu huu atiwe mbaroni!”
“Kitu gani? Msiniambie kama Masurufu anahusika!”
“Tunakwambia Mkuu. Masurufu anahusika kwa kila hali na yupo kila mahali. Kwanza mali zake nyingi ni za wizi na magendo. Uchunguzi tulioufanya kwa kutembelea miradi iliyoanishwa katika kashfa zilizotolewa dhidi yake na Marehemu John Tengeneza unathibitisha hivyo.
Ameshiriki pia kuiba fedha zilizo katika akaunti ya madeni ya ndani na nje, ana hisa katika kampuni zote zilizoshiriki katika kulihujumu Shirika hata likapata hasara ya mamilioni ya Shilingi. Baadhi ya hasara hizo, taifa lingali linaendelea kuzipata hadi leo hii tena kwa kulipa mamilioni ya shilingi. Hapana Inspekta, masurufu anatakiwa kusimama kizimbani akapate malipo ya uhalifu wake!” Mathias akatua.
“Kama hiyo haitoshi”, Mina akaongezea “Ameshiriki pia kusababisha vifo vya Michael na Raymond wa Usalama wa Taifa, amemuua mkewe pia kwani alama za vidole zilikutwa katika wodi aliyokuwa amelazwa Masuruf pale Ocean Road, ndizo ambazo pia zimekutwa katika kitasa cha mlango wa ndani wa chumba cha Dr Masurufu ambapo mkewe alikutwa amekufa.
Alama hizo hizo zipo pia katika usukani wa baadhi y magari. Tunaamini alama hizi ni za Steve kama tulivyoambiwa na Samson na kuthibitishiwa na Frank ambaye amesema ni Steve aliyemuua pia John Tengeneza. Kwa hiyo utaona kama Steve ni mlinzi wa Masurufu na ndiye anayetokea kila penye mauaji, yanayoambatana harakati zake za kutaka kwenda Ikulu, Masurufu hawezi kukwepa tuhuma na ukweli huu!”
Alama hizo hizo zipo pia katika usukani wa baadhi y magari. Tunaamini alama hizi ni za Steve kama tulivyoambiwa na Samson na kuthibitishiwa na Frank ambaye amesema ni Steve aliyemuua pia John Tengeneza. Kwa hiyo utaona kama Steve ni mlinzi wa Masurufu na ndiye anayetokea kila penye mauaji, yanayoambatana harakati zake za kutaka kwenda Ikulu, Masurufu hawezi kukwepa tuhuma na ukweli huu!”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mina anaye akatua. Inspekta Kimato akauliza.
“Na kuhusu yule mtuhumiwa wa jana?”
“Frank siyo?” Mathias akajibu kwa Swali
Kimaro akatikisa kichwa akakubali
“Ni huyo aliyetufanya tuje tuombe hati ya kumkamata Masurufu. Jana tumemminya kiasi cha kutosha na ametapika kila kitu. Kwamba hata vifo vya Albino vilivyokuwa vimeshamiri, vinatokana na mahitaji ya Dr Masurufu ambaye anatimiliza matakwa ya Profesa Zonga ili hatimaye Dr Masurufu aweze kwenda Ikulu.
“Mungu wangu!” Inspekta akamudu kutamka “Profesa Zonga pia yumo?!”
“Kwa mujibu wa Frank ambaye ilifikia mahali akashindwa kabisa kuyavumilia mateso tuliyokuwa tukimpa, amesema Albino hawa wasingeuwawa kama Dr Masurufu asingevunja masharti ambapo ilitakiwa dawa na viungo vya Albino kumsafisha, na ndipo yeye alipopewa jukumu hili pamoja na kitita cha milioni mia moja, ambapo naye alilikabidhi jukumu la kutafuta viungo vya Albino kwa Emmanuel Kuho!” Akatua Mathias.
“Isitoshe,” Mina akaendelea “Frank amethibitisha pia kuwa ni Masurufu aliyetoa amri ya Tengeneza kuuawa, na kwamba sasa hivi Dr Masurufu na Steve wamejificha nyumbani kwa Profesa Zonga wakingojea damu ya Albino ili wasafishe mambo na kujitokeza hadharani wakiwa na nguvu mpya!” Mina akamalizia.
Ilitosha! Inspekta akachoka. Mikono akaitua mezani na kujiinamia.
Ilimuumiza kuona Masurufu Hussein Masurufu, mtoto wa mpigania Uhuru maskini, aliyesoma na kukua chini ya ulezi wa baba wa taifa ndiye aliyeangukiwa na tuhuma zote hizi. Hakuweza kuunganisha mambo mara moja na kuweza kuupata mzizi kuwa ilikuwaje hata mtu kama Masurufu aliyetegemewa kuwa hazina na rasilimali ya taifa ageuke kuwa mwiba kwa taifa.
Alishindwa kutambua mara moja pia nini huwa kinatokea kwa watu mpaka wengine wanakuwa waadilifu sana kama alivyo yeye ambapo starehe yake ni kuona watu wote wanaishi kwa haki na usawa chini ya amani, utulivu na upendo wakifanya kazi zao kwa uhuru na furaha; Na inakuwaje wengine wanakuwa wahalifu sana kiasi cha kutaka kukwapua hata kile kidogo ambacho wananchi wa kawaida wamekipata kwa ngama baada ya kukitolea jasho jingi.
Watu kama hawa hakujua walipaswa kupewa adhabu gani kati ya kunyongwa, kufungwa maisha na kuachiwa huru kama alivyofayika Mengistu Haile Maryamu
Kama ningekuwa mimi… Akawaza …ningemfunga kifungo cha maisha mahala pa wazi ili kila mmoja aweze kumuona na kumsusuika. Pengine ingesaidia kuifanya mioyo ya vijana wetu ambayo kwa sasa ni kama imeandaliwa kujengwa na kumea ndani ya ufisadi, kuweza kuhofia na kuuacha mfumo huo.
Naam! Inspekta Kimaro aliendelea kuona athari ya maisha wanayoishi watanzania kama hatua madhubuti hazitachukuliwa kuizuia hali hii. Kwamba ukabila unarejea kwa kasi ya ajabu, vyama vya makabila baadhi vikiachwa vichipue kama uyoga na kumea kila nafasi ilipopatikana.
Watu wakijisikia kama wana wajibu wa kutoa rushwa hata baada ya kupewa huduma inayostahili ambayo ni haki yao kimsingi. Hali ambayo imewafikisha watanzania mahala ambapo wameamini kama hujulikani kwa maana ya kuwa mtoto au mtu mwenye nasaba na kigogo au mfanyabiashara fulani na huna chochote kitu mfukoni, huwezi kupata msaada au huduma yoyote ile.
Hili pamoja na lile ma mgawanyo usio sawa wa rasilimali za taifa, pengo kati ya masikini na matajiri ambao licha ya kuishi katika sayari moja, bado matajiri wamekuwa na maisha yao wakimiliki dunia yao yenye kila kitu chao kama makazi, shule, hospitali, magari na hata starehe zao.
Maskini pia nao wamekuwa na makazi kwenye dunia yao, wakichangia huduma duni kutoka katika shule zao almaarufu kama shule za akina Kayumba. Si hilo tu wamekuwa pia na Hospitali zao, usafiri wao wa daladala na starehe zao ambazo ni aghalabu sana kutofutiana na ile starehe anayoipata mbwa kwa kukalia mkia wake.
Inspekta Kimaro aliendelea kuiona hatari kubwa inayoinyemelea Tanzania zaidi ya hii ya Dr Masurufu. Hatari ya nchi kugeuka kuwa ya kifisadi na kila mwenye kinafasi chake anataka ale na kula na kula hadi asaze! Na pengine amalize chote na kingine akaweke akiba nje ya nchi ili atakapostaafu na kuzeeka aishi kama yuko peponi.
Kwa ujumla hatari ilikuwa kubwa sana. Kubwa mno! Na kama mkereketwa wa uhuru wa kweli, amani ya kweli na upendo wa kweli, Inspekta Kimaro alikuwa anaamini kwa dhati kwamba ilitakiwa kuchukuliwa hatua. Hatua madhubuti ambayo ingeizuia Tanzania kutumbukia katika shimo la kupoteza dira na mwelekeo inakoelekea sasa, yenyewe ikidhani inaelekea katika maziwa na asali.
Lakini nani na kuchukua hatua hiyo? Akajiuliza na kuendelea …wakati kila mmoja anaona kwamba hili ni jukumu la mwenzake? Lilikuwa swali gumu kwa kila hali. Akaachana mawazo hayo na kuusogelea mkonga wa simu. Akampigia mkuu wa Jeshi la Poisi kwa ajili ya kupata kibali cha kumkamata Dr Masurufu.
Kama ilivyokuwa kwake, IGP anae alishtuka kusikia habari za Dr Masuruf na Profesa Zonga, hata hivyo baada ya kujadiliana na watu anaofanya nao kazi hatimaye aliidhinisha na muda mwingi baadae, hati ya kukamatwa kwa Dr Masurufu, ikawa imetolewa rasmi.
* * *
Wakati Steve anainua bastola ili ampige Samson risasi ya mguu kwa lengo la kumpunguza makali ili aweze kumtesa vizuri, simu yake ikaita. Christopher MacDonald alikuwa upande wa pili akitaka kujua mambo yanakwendaje na kama jukumu alilompa Steve lilikuwa limemalizika au lah.
“Nalikamilisha sasa hivi mkuu, baada ya dakika ishirini hivi utapata majibu!”
Akamjibu akificha kueleza hali halisi ikiwemo kipigo alichokipata toka kwa Samson. Akiwa mtu asiyependa kukata tamaa haraka alimuhakikishia kuwa mambo bado sio mazuri sana ingawa hatarajii kuwa yanaweza kuwa mabaya zaidi ya hapo.
“Nakutegema Steve, muangalie sana Masurufu, binafsi naanza kukosa imani nae!”
“Namuangalia vizuri bosi, na angalizo lako lingali hai akilini mwangu. Ninachokuahidi ni kitu kimoja tu Cris, sitakuangusha bosi wangu. Sijawahi kumuangusha mteja wangu na sitakaa niangushe mtu!” Akatua. Ilikuwa sawa na kiapo.
“Vizuri Steve, kuna la ziada?”
“Hakuna!”
WakaaganaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Steve akainamana na kumuangalia Samson vizuri akiukubali na kustaajabia uwezo wake wa kupigana. Ile dhana kwamba afrika hakuna wapiganaji wazuri, akaifuta. Wazo la kumpiga risasi ya mguu kumpunguza makali likiondoka.
Akajikuta akitaka kumjua vizuri na kujua anajua mangapi kuwahusu! Habari za yeye kuhusika na vifo vya mama Masurufu na akina Michael huyu alizipata vipi na kwa nini aliitilia mashaka nyumba hii ambayo ni kweli imehifadhi kila kitu. Je amewahi kuitembelea kabla, na kwanini amsumbirie yeye tu hadi usiku?
Ni haya yaliyomfanya atamani kumuhoji Samson. Akamgeuza kuangalia pale alipopigwa na kile chuma kilichopachikwa ukutani kiufundi. Jeraha lilikuwa kubwa kiasi, damu ikiwa imetoka kwa uchache. Kwa kadiri alivyojua, mtu aliyepigwa na chumba ile huchukua kati ya dakika arobaini na tano na saa moja kurejewa na fahamu tena.
Hivyo kabla ya muda huo, alihitaji kufanya maandalizi kadhaa ikiwa ni pamoja na kumchoma Samson sindano ya kumpunguza nguvu ili asiweze kuleta ushindani wa maana na kumfanya ashindwe kutimiza lengo. Na baada ya hapo ndipo angeitimiza ile ahadi yake ya kumuua kikatili kwa mateso makuu ili Samson ajutie kitendo cha kujiingiza katika mambo yasiyomuhusu, ikiwa ni pamoja na kumuadhibu yeye steve.
Ni hapa alipoanza kumpekua Samson na kumsachi hapana na pale na kutoa kila alichokuwa nacho Samson zikiwemo zile silaha ambazo zilikuwa mbali kabisa ambazo macho au mikono ambayo haijafuzu isingweza kuziona kamwe.
“Yu nani mtu huyu!” Steve akajikuta akijiuliza. Maana silaha na vifaa nilivyokuwa vimefichwa katika mwili wa Samson vikamfanya ajue kuwa hachezi na mtoto kama alivyokuwa amefikiria awali, bali anacheza na wazoefu wanaojua kitu gani wanafanya. Majasusi kama yeye.
Kabla hajaendelea zaidi, simu yake ikaita tena
Masurufu alikuwa upande akikabiliwa na hatari ya kukamatwa. Steve akaikumbuka ahadi yake kwa Christopher MacDonald ambayo ilikuwa sawa na kiapo. Akamtamzama samson na kufikiria kama anaweza kupata fahamu karibuni. Uwezekano ulikuwa mdogo.Hata hivyo akajikumbusha uimara wa jingo hili. Akajiuliza kama atamfungia Samson kwa nje, kamwe samson asingweza kufungua mlango na kutoroka kwa kuwa mlango ule ulihitaji tarakimu za siri ambazo alizijua yeye tu.
Akazificha silaha na zana za Samson, akamvuta na kumuhifadhi mahala pazuri akimfunga kamba kwa tahadhari akatoka, akaiparamia gari na kukimbilia kwa Profesa Zonga kumuokoa Dr Masurufu katika hatari ya kukamatwa na polisi.
SURA YA KUMI
MAMBO HADHARANI
Aliwahi dakika kadhaa kabla polisi hawajafika. Akamkuta Dr Masurufu akitetema hovyo huku akiwa anashindwa hata kufikiria vizuri. Nusura Steve aangue kicheko pale alipoona Suruali ya Dr Masurufu ikiwa imelowana. Hata hivyo akajizuia na kuuliza.
“Kumezidi kitu gani tena?”
“Frank amekamatwa!”
“Mungu wangu!” Moyo wa Steve ukapiga kite na kuanza kudunda vibaya.
“Amekamatwa lini na kwa nini?” Akauliza kwa kihoro hali akijitahidi kuirudisha akili yake katika hali ya kawaida ili aweze kufikiria na kuamua vizuri. Alikuwa na hakika kuwa akiiruhusu hofu na woga vimtawale itafika mahala atashindwa kujihimili na matokeo yake ni kujikojolea kama alivyofanya Masurufu na kuishia mikononi mwa Polisi ambapo mchezo utakuwa umekwisha.
“Amekamtwa jana. Ni kuhusu ile issue ya Albino!”
“Mie nilijua tu…” Steve akalaumu. Hata hivyo akajirudi. Huu haukuwa wakati wa lawama. Alichotakiwa kufanya ni kuiepusha hatari inayowakabili, huku akifiria umuhimu wa kurudi nyumbani kwa Dr Masurufu kumuua Samson na kuchukua vifaa vyake muhimu tayari kwa kutoweka nchini.
“Sasa ninyi mmejuaje kama mnakuja kukamatwa”
“Kuna kiongozi mmoja wa vyombo vya usalama, ngazi ya juu amempigia Simu Profesa Zonga. Akamwambia ajihadhari polisi wanajua kama amemficha Dokta Masurufu na wanakuja kumkata usiku huu!.
“Ni huyo pia aliyewapa habari za Frank kukamatwa?”
“Ndiyo. Alimueleza Profesa Zonga kuwa Frank amekamatwa baada ya kutajwa na watuhumiwa wa mauaji ya Albino na baada ya kuteswa Frank ametamka kila kitu. Ilikuwa ni baada ya hati ya kukamatwa kwangu kutolewa ndipo kigogo huyo alipompigia simu Profesa ili kumtahadharisha! Na hili nahisi lilijiri kwa kuwa Profesa ana timu kubwa viongozi wa ngazi za juu anaowahudumia.
“Kwa nini wakukamate kwa hati?”
“Nina historia na nchi hii Steve, mimi ni mtoto wa mpigania Uhuru kwa Baba. Pamoja na baba nimelelewa pia na muasisi wa Taifa hili anayeheshimika sana. Isitoshe nimekuwa Mbunge, Waziri na baadae Balozi na ningali Balozi hadi leo hii. Ndio maana nahisi wameona siwezi kukamatwa kienyeji! Kwa upande wa pili ni bahati mbaya sana kuona kwamba mkakati wangu hauelekei kuzaa matunda. Nasikitika sana. Nauonea aibu mwisho wangu!”
“Hutakamatwa Dokta!” Akamjibu kumpa moyo. Akaendelea “Believe me or not! Uko na Steve Lawrance Marvin. Ukiwa mimi daima uko salama!”
“Kiasi naamini Steve. Nakuamini! Ila… Ila….!” Dr Masurufu akakwama, Steve akamuelewa “Usijali” Akamwambia na kumuuliza tena. “Kwa hiyo Profesa Zonga yuko wapi?”

“Ameenda Ikulu!” Ameenda kumuomba Rais amlinde na kadhia hii! Mwenyewe akidai anasingiziwa na maadui zake!”
Ilikuwa kauli iliyofamfanya Steve acheke kwa uchungu
“ Na Rais naye anaweza kumsaidia?!”
“Sasa mimi nitajuaje Steve”
“Okay! Tuna muda mchache sana. Jiandae tuondoke”
“Tunakwenda wapi?”
“Vita vyetu tumezidiwa hatuna budi kukimbia ili tukaongeze nguvu!”
“Na Polisi Je?” Masurufu aliendelea kuwa na wasiwasi.
“Hilo niachie mimi!”
“Lakini bado hujaniambia tunakwenda wapi?”
“Nje ya nchi! Ila tunapitia nyumbani mara moja kuna kazi ya kufanya kabla hatujaondoka!” Steve akahitimisha.
“Mie sina neno!” Masurufu akakubali. Kumbe angefanya nini? Wakaondoka. Dakika tano baadae, gari ya polisi ikaingia. Maelezo waliyoyapata yakawafanya waelekee Mbezi Beach, nyumbani kwa Dr Masurufu.
* * *
Samson Kidude alizinduka dakika kumi baada ya Steve kuondoka. Chumba kilikuwa na giza na kichwa kilikuwa kikimuuma vibaya. Aliposema ajigeuze ndipo alipogundua pia alikuwa amefungwa imara kabisa. Akatulia na kutuliza akili hali akijitahidi kutafakari kwa nguvu.
Kwa mbali macho yake yalianza kuzoea giza, akaweza kuziona kamba alizofungwa. Akili yake ilipotulia na kuanza kufanya kazi vizuri, ikawa imemchukua dakika tano tu kujifungua kamba na kuipata swichi ya taa.
Akiwa katika nuru ile, sasa aliweza kukikagaua chumba kile vizuri. Alikwishagundua kwamba vitu vingi katika chumba kile vilikuwa vikiendeshwa kwa kutumia mitambo maalumu inayotumia umeme. Kwa maana hii ilihitajika akili zaidi, kuliko nguvu.
Akitembea hapa na pale , Samson alianza kuona mitambo mbalimbali ambayo hakujua kazi yake mara moja, akajikuta akiwa na kazi mbili ya kusoma na kujaribu katika kujaribu akagundua kwamba nyingi zilikuwa silaha, baadhi zilitupa hata risasi. Ndipo akagundua ni kwanini alipigwa na kitu kilichomfanya azirai.
Akijua kwamba ugunduzi na pengine kutoka kwake ndani ya jela hii kunaongozwa na kujaribu, Samson hakukoma. Aliendelea kugusa hapa na pale na katika kugusa gusa hivi mara ukuta uliokuwa unamkinga mbele asione kitu, ukaachana na mbele yake inatokea ofisi nzuri sana. Ofisi ya kifahari hasa.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Udadisi unamshika, anasahau maumivu na kupiga hatua za taratibu kuisogelea. Mbele yake juu ya meza ile aghali, mbali ya kompyuta, simu ya mezani, kitufe cha ramani, mafaili na vifaa vingine vya kiofisi; pia kulikuwa na maandishi yaliyochongwa kisanifu kabisa kwa kutumia dhahabu yaliyosomeka Hon. E. Dr Masurufu. H. Masurufu, President of United Republic of Tanzania.
Samson akatabasamu kwa uchungu. Ile dhahabu iliyotumika kuchonga jina lile ingeweza kujenga Hospitali kama sio shule kadhaa za Sekondari. Nyuma ya meza ile aghali kabisa kulikuwa na kiti maridhawa kilichozidia vile vinavyoitwa Executive chair kwa uzuri. Ukiacha hivi kulikuwa na makabati kadhaa, mashubaka ya vitabu, droo za chuma za mafaili na vingine kadha wa kadha.
Vyote viliashiriia kitu kimoja dhahiri, ukwasi uliokithiri.
Samson akajikuta juu ya kiti kile cha kifahari na meza ile aghali, akaanza kupekua mafaili kadhaa yaliyojazana pale juu ya meza. Mihutasari ya mikutano, hati za ukodashaji helkopta, Orodha ya timu ya kampeni na mipango mbalimbali ya ushindi vilikuwa baadhi ya vitu alivyoviona na kuvipitia kwa haraka, baadhi vikiusisimua moyo wake.
Hatosheki na nyaraka za juu ya meza, anavuta droo moja baada ya nyingine na kupitia kila nyaraka kwa umakini na wepesi wa hali ya juu. Nyaraka mbalimbali zinatokea na hizi zinakuwa msaada mwingine kama sio ushahidi wa kuyathititisha madai ya Tengeneza dhidi ya Masurufu.
Anapohitimisha zoezi hili, anarudi mezani na kuwasha kompyuta inamdai neno la siri anapoingiza jina la Masurufu kompyuta inafunguka. Anaanza kuita faili moja baada ya jingine. Anasoma na kusoma na kusoma. Akiwa katika zoezi hili anagundua kuwa kompyuta imeunganishwa na mtandao wa Internet. Hili linamfanya ajitumie kila anachikiona kinafaa katika barua pepe yake.
Kutahamaki likaja faili la Mkakati wa Kuelekea Ikulu, Samson akafanya kulifungua kwa pupa. Haikuwa rahisi. Lilimdai neno la siri. Akajaribu majina yote ya Dr Masurufu na vitu alivyohisi vina uhusiano naye bado haukufunguka “Shit!” Samson akaguta na kusonya.
Akakata tamaa na kuachana na mkakati huo, akaendelea kuita na kusoma mafaili mengine. Kulikuwa na mafaili mengi tu na kila moja lilikuwa na umuhimu wake. Ni katika moja ya mafaili hayo alipokuta nambari za siri za kufungulia sefu.
Akahamisha macho kutoka katika kompyuta na kuyazungusha tena humo ndani. Hakukuwa na sefu. Wakati anajiaanda kupuuza akakumbuka. Kwamba masefu ya siku hizi ili kubana matumizi ya nafasi na pengine kuyaficha, huwa yanayejengwa sambamba na kuta, wakati mwingine hupigwa rangi moja na ukuta kabisa. Jambo ambalo hukuwia vigumu kujua kama kuna sefu humo ndani.
Ni wazo hili lililomfanya anyanyuke pale kitini akaanza kuusanifu ukuta akifunua hiki na kile. Na pale kulipokuwa na picha ya Mlima Kilimanjaro ambayo ilikuwa imekaa kama pambo, akakuta vinamba kama vile viliyovyopo juu ya Briefscase.
Akazibonyeza nambari za siri, alipomaliza tu sefu lile maridhawa likafunguka.
Masalalee! Hayo mamilioni ya shilingi na dola za kimarekani yaliyojipanga na kulala kwa utulivu yalikaribia kumpofusha macho hata akajikuta akimeza mafunda kwa mafunda ya mate.
Zilikuwa fedha nyingi mno na kiasi Samson hakujisumbua hata kufikiria kukisia thamani yake. Chini kabisa ya fedha zile kulikuwa na droo ambapo ndani yake kulikuwa na Suitcase ndogo iliyoandikwa siri. Moyo ukamdunda Samson Alipoifungua Suitcase hiyo, ndipo alipoikuta nakala ngumu ya Mkakati wa kuelekea Ikulu pamoja na mkataba baina yake na G-8 Original.
Samson akivitwaa na kuvisoma.
Akakutana na mambo mazito mazito ambayo hakuyafikiria kama mtanzania wa kawaida wachilia mzalendo kama anaweza kufikiria kuvitenda kwa nchi yake. Ukatili ulioje. Alipomaliza kuusoma mkakati na mkataba wake, alikuwa akitetembeka kwa hasira na uoga. Hakutaka kufikiria kama yale aliyoyaona yakitekelezwa Tanzania itakuwaje.
Naam! Kwa mawazo yake huu haukuwa mkakati wa kuelekea Ikulu tu bali mkakati wa kuiuza Tanzania ukiwa umeambatana na mkataba wake! Hujuma iliyoje kwa Taifa hili maskini!
“Hapana!” Samson akaamua kwa dhati “Nitakuwa radhi kufa kuliko kuiacha Tanzania ichukuliwe na manyang’au!” Kama hiyo haitoshi akaapa kuwapeleka kuzimu wote walio nyuma ya mkakati huu.
Muda si mrefu Samson, kupitia dirishani akaona gari, Toyota Land Cruiser VX likiingia na kusimama hatua chache mbele kidogo ya kijumba alichokuwemo. Kupitia dirisha lile ambalo lilimuwezesha wa ndani kumuona wa nje na wa nje kutomuona wa ndani, Samson akashuhudua Dr Masurufu na mlinzi wake Steve wakishuka. “Naam…!” Akajiambia “Kazi imeanza!”
Ingawa hakuwa na silaha. Alijijasirisha na kujitayarisha kuwapokea akidhamiria kupambana nao kufa na kupona mpaka atakapowashinda nguvu na kuwatia mbaroni. Alipokuwa akihifadhi vitu vile vizuri ndipo jicho lake lilipotua juu ya meza kwa mara nyingine tena akawa ameiona simu.
Akajilaumu kwa nini hakupiga simu ofisini kwake, polisi au kwa Anderson Chilonga kumuomba msaada. Wazo likamjia kwamba akimbilie simu na kupiga kuomba msaada. Wazo hili lilizidi kupata nguvu kutokana na ukweli kwamba atakuwa akipambana na watu wawili wakiwa katika chumba chenye mitambo yenye silaha nyingi ambayo wapinzani wake wanazijua vizuri kuliko yeye.
Hata hivyo akapima uharaka wa kila jambo. Kwamba itamchukua dakika ngapi kuiendea meza, kupiga simu na kupokelewa na yeye kueleza shida yake, na itawachukua sekunde ngapi Steve na Dr Masurufu kumfikia yeye pale alipo.
Akaachana na wazo hili na kujikusuru kupambana nao.
Wakati Steve na Masurufu wanaanza kuifuata ile nyumba, gari nyingine Landlover Difender ikaingia kwa fujo. Askari wenye silala zaidi ya kumi na mbili ambao walikuwa wamejificha katika bodi ya gari, sasa wakajitokeza wakizipunga silaha zao hewani huku mmoja wao akibweka “Mko chini ya ulinzi!”
Steve akaduwaa kwa sekunde mbili hivi.
Ulikuwa ni wakati huu pia baadhi ya askari walipoanza kuruka na kuchukua nafasi. Samson akiendelea kuchungulia katika dirisha akamshukuru mungu kuona amemuelewa na kumletea msaada. Kwa askari wale wenye silaha zile, Samson akajua ingewawia vigumu Steve na Masurufu kuwashinda. Maskini kumbe hakumjua Steve vizuri.
Sekunde iliyofuata, Steve alimkamata mkono Masurufu na kwa kasi ya ajabu akafungua mlango wa VX na kumsukumia ndani, wakati huo huo akaruka mpaka upande wa pili wa dereva, akafungua mlango na kuingia garini kwa kasi ile ile vitendo vyote hivyo vilitokea ndani ya nukta tatu au nne hivi.
Akawasha Land Cruiser na kuirudisha nyuma kwa nguvu na kwa spidi kali kabisa ambapo aliwagonga askari wanne kati ya sita waliokuwa pale mbele. Wawili waliosalia akawamaliza kwa Bastola na haraka haraka akawageukia wengine waliokuwa wakishangaa na kuwadonoa mmoja baada ya mwingine kwa kutumia bastola yake yenye kiwambo cha kuzuia sauti.
Ni pale polisi walipokuja kutahamaki wamebaki wawili ndipo walipokurupuka na kuanza kummiminia risasi Steve. Walimimina risasi za kutosha hasa muda si muda wakasikia Steve akipiga yowe baada ya kupigwa risasi mkononi.
Pamoja na maumivu, Steve akaing’oa tena Landcruiser VX na kuitoa kwa kasi kubwa kuelekea ilipo nyumba ya kuishi ya Dr Masurufu ambako aliugonga ukuta, ukabomoka na kuingia ndani.
Askari wale waliendelea kumimina risasi hadi zilipowaishia kulipokuwa kimya, ndipo walipiga simu kituoni na kuomba waongezewe nguvu. Muda si muda gari nyingine iliyokuwa na askari wa kutosha wenye silaha ikafika.
Polisi waliokuwepo wakawapa wenzao taarifa kwa ufupi, ambapo kundi la askari wenye silaha wakaizunguka nyumba ya Dr Masurufu ili kuimarisha ulinzi. Wengine wakaingia ndani kwenda kumkamata Steve na Masurufu, .
Kule ndani Samson alijitahidi alivyoweza kupiga kelele za kuomba msaada na kufungua mlango haikuwezekana. Alipochoka kabisa akampigia simu Mkuu wake wa kazi Anderson Chilonga pamoja na msaidizi wake Assia na kuwaeleza kinachojiri katika nyumba ya Dr. Masurufu na kule alikofungwa yeye.
Hawa wakamtoa hofu na kumwambia wanakwenda huko mara moja. Samson akashukuru na kuendelea kuangalia sinema ile kupitia dirishani.
Ndani askari wale walilikuta gari likiwa tupu. Wakiongozwa na michinzi ya damu ambayo bila shaka ilitoka katika jeraha la Steve, Polisi wale waliingia mpaka katika chumba fulani ambacho kulikuwa kama stoo hivi.

Ndani ya kile chumba kulikuwa na vikorokoro vingi na mfuniko wa kitu kama chemba ya choo hivi. Pembeni ya chemba hiyo kulikuwa na kidimbwi kidogo cha damu ambacho askari wale walihisi kama Steve aliitumia sehemu ile kujiganga. Askari walipojiridhisha kuwa hakukuwa na mahala pengine ambapo mtu angeweza kujificha, wakaifunua chemba ile ambayo haikuwa imefunikwa vizuri
Ngazi zinazoelekea chini zikawalaki.
Handaki! Wakapigwa na butwaa la mshangao wakati wakiingia chini Haraka. Ndani kulikuwa na vyumba vinne, vyenye shehena mbalimbali za mizigo ambayo hawakuitambua mara moja. Hakukuwa na muda wa ukaguzi, silaha zao zikiwa tayari tayari wakaongoza kukifuata kijinjia chembamba chenye kiza kilichokuja kuwatoa ufukweni mwa bahari ya Lindi.
Mahala walioibukia kulikuwa na boti mbili speed boat! Katikati ya Boti hizo kulikuwa na uwazi mkubwa ulioashiria kuwa Speed boat moja ilikuwa imeondoka. Walipotupa macho Baharini hawakuweza kuona chochote zaidi ya giza lililotamalaki na kufunika bahari nzima.
Mawasiliano yakafanyika haraka kuwataka askari walio mjini waagize boti za Doria zilizomo katika Bahari ya Hindi waitafute, kuifukuza na kuikamata haraka boti hiyo ambayo ilikuwa ikiwatorosha watuhumiwa wao Dr Masurufu Hussein Masurufu na mlinzi wake Steve.
Wao wakarudi kuwapa taarifa wenzao.
Wakakuta tayari Inspekta Kimaro ameshafika, alikuwa anawaangalia askari wake waliouawa na Steve kwa uchungu na masikitiko makuu, hali majeruhi wakimueleza ilivyokuwa. Inspekta Kimaro hakuwa pekee, alikuwa pamoja na Mkurugenzi msaidizi wa Usalama wa Taifa Chilonga Anderson Chilonga, Msaidizi wa Samson Assia Khalifa pamoja na maafisa wengine wa polisi.
Vitu aina kwa aina vya Dr Masurufu vikiwa vimekusanya pamoja baada ya kumfungulia Samson kwa kutumia Mtaalamu wa mitambo ya kijasusi kutoka jeshi la Polisi la Tanzania.
Kutoka hapo safari ya kuelekea Makao makuu na baadae Usalama wa Taifa ilianza ambako Samson kidude alikuwa na mengi ya kueleza mbele ya Inspetka Kimaro, Anderson Chilonga, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Katibu Mkuu wa chama, Mwenyekiti wa Chama Tawala pamoja na Rais anayemaliza muda wake.
Mwisho wa maelezo yake, Samson aliwakabidhi Mkakati wa Dr Masurufu wa kuelekea Ikulu, ule mkataba wa kishetani baina ya Dr Masurufu na G-8 Original, pamoja na taarifa za uwepo wa mabilioni kwa mabilioni ya shilingi katika Ofisi na handaki la Dr Masurufu kule Mbezi Beach.
Viongozi wa usalama pamoja na Rais walibubujikwa na machozi ya furaha wasiamini kile wakisikiacho. Kwa mara nyingine tena Samson kidude kwa kushirikiana na jeshi la Polisi na Vyombo vya Usalama alikuwa wameliepusha taifa toka katika hujuma hizo nzito.
Kwao hizi zilikuwa taarifa za ushindi kwa kila hali.
Taarifa za matumaini. Taarifa ambazo zingetoa onyo kwa G-8 Original na kuwajulisha kuwa huu ulikuwa mwanzo wa Tanzania kujinasua toka katika ukoloni mamboleo. Ukoloni wa kifikra, ukoloni wa kuandaliwa sera na mifumo isiyokuwa na tija kwa wananchi wa kawaida.
Naam! Taarifa hizi zilikuwa sawa na pigo lililonyooka.
Rais aliwataka wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha Dr Masurufu anakamatwa na kurejeshwa kizimbani ili sheria ichukue mkondo wake pamoja na wote walioshiriki katika kadhia la Dokta Masurufu. Akawaamrisha viongozi wa chama kumchukulia hatua za kinidhamu ndani ya chama kwa jinsi alivyoshiriki kukichafua na kukipaka matope na akataka hatua hizo zichukuliwe haraka.
Akawataka wakurugenzi wa Usalama waiboreshe ofisi ya Samson na kuhakikisha anapata kila anachohitaji. Kwa upande wa rasilimali fedha zilizokamatwa nyumbani kwa Masurufu, Rais aliamua kuwa zitaelekezwa katika shughuli za maendeleo ya jamii ili kuchangia katika harakati za kupunguza umasikini wa kipato na kuboresha maisha.
Ilikuwa ni baada ya kila mmoja kuahidi kuyafanyia kazi maagizo ya Rais ndipo, Samson Kidude alipoanza kupokea pongezi za dhati kutoka kwa kila mmoja. “Sidhani kama nastahili pongezi hizi peke yangu!” Akasema kwa upole na kuendelea “Kila mmoja amefanya kazi, hivyo yafaa tujipongeze wote hasa jeshi la Polisi!”
Wakampigia makofi.
* * *
SURA YA KUMI NA MOJA
MALIPO YA UHALIFU
Tarehe mbili, mwezi Mei, Kamati kuu ya Chama ilikutana katika kikao chake cha dharura, na pamoja na mambo mengine. Ililiondoa jina la Dr Masurufu Hussein Masurufu kutoka miongoni mwa watu wanaotarajiwa kuwa wagombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi.
Kamati pia ilichuja baadhi ya majina na kumfuta John Tengeneza ambaye alikuwa amepoteza maisha hata hivyo haya hayakuvuruga ratiba ya uchaguzi.
Akiongea na vyombo vya habari katika ukumbi wa mikutano wa Dodoma Hotel, Katibu Mkuu wa Chama alisema walikuwa na wajibu wa kuondoa jina la Dokta Masurufu toka miongoni mwa wagombea kwa kuwa alikiuka, miiko maadili na kanuni za chama cha Mapinduzi wakati akishiriki katika kinyang’anyiro hicho.
Katibu alisema Dr Masurufu amekiuka kanuni hizo kwa kuingia mkataba wa kihuni na mabepari wanaotaka kufaidi rasilimali za Tanzania bila jasho, kushiriki kwa vitendo vya ufisadi na kupora rasilimali za taifa na kujilimbikizia mali toka wakati wa vita vya Kagera, Azimio la Arusha, Uhujumu Uchumi hadi katika misamaha ya kodi zaidi akiwa mshirikiana.
Hata hivyo aliwataka wananchi kutoihukumu CCM kwa vitendo vya Dokta Masurufu kwamba hivyo vilikuwa vitendo binafsi vya mtu na kwamba licha ya kila dini kuhubiri mema na kukataza mabaya, bado baadhi ya waumini wa dini hizo wamezama katika mambo yote waliyokatazwa kama ulevi, uzinzi, uongo, ulaghai, wizi, usenganyaji na kadhalika. Kwa hiyo huwezi kuihukumu dini kwa kuwa na watu kama hawa.
Alisema watu kama Dr Masurufu waliingia katika chama kwa bahati mbaya kama vile jiwe lipatavyo fursa ya kuingia katika sahani ya ubwabwa na katu huu sio mpango wa chama kuwa na watu kama hawa na ndio maana kila wanapobainika hutemwa mara moja kam jiwe liliko katika ubwabwa linavyotemwa pindi likiingia kinywani na kutafunwa.
Akifafanua zaidi alisema safari ya jiwe kuelekea katika sahani ya ubwabwa ilianzia mbali toka shambani. Ambapo mpunga ulivunwa na kukusanywa. Ni pale tu ulipoanikwa ndipo jiwe lilipojiingiza kinyemela! Hata ulipoanuliwa juani na kupigwa au kutwangwa na pengine kukobolewa jiwe liliendelea tu kung’ang’ania.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Safari ya kuupeleka mchele sokoni, mama akaja kuununua na kuuchagua, kuupepeta na kuuchuja, Bado tu jiwe liliendelea kuwemo. Hatimaye mchele unapikwa na kugeuka wali, unapakuliwa katika sahani, jiwe bado limo tu. Na lilivyo na tabia mbaya, jiwe hili hukimbia katika sahani ya baba au ya mgeni na kutoa tafsiri kwamba mama hajui kupika.
Akawataka wananchi wajue kuwa hata katika CCM bado kuna mawe mengi na wataendelea kuyatoa kadri yatakapobainika kwani sio matarajio ya chama kuwa na mawe! Akawataka wananchi wajitokeze kwa wingi siku ya uchaguzi na kuichagua CCM kura nyingi.
Hotuba yake iliwasisimua na kuwavutia wengi. Habari hizo zilipotoka zikawafanya watu washike vichwa kwa uchungu na mshangao. Wasiamini kama Masurufu huyu, aliyezaliwa na mpigania Uhuru, akasomeshwa na kulelewa na baba wa Taifa ndiye anayefanya haya.
“Laiti Mwalimu angelikuwepo na kujionea kizazi alichokilea na kukisimamia kinavyopotoka?” Baadhi waliwaza kwa hitimisho, wakisikitika na kuondoka.
Naam! Siku chache baadae Profesa Zonga, Frank, Kuho, Robison na wauaji wenzao wa raia wenye ulemavu wa ngozi nao walifikishwa mahakamani. Ushahidi wao ukiwa dhahiri na mwingine wakiwa nao, upelelezi ulifanyika haraka na muda mfupi baadae wakawa wamehukumiwa kifungo cha maisha na kazi ngumu jela.
* * *
Baada ya chenga za hapa na pale zilizowachukulia muda na fedha za kutosha, hatimae Steve na Masurufu walifika Afrika Kusini wakiwa wamemaliza akiba yao yote. Steve akampigia simu Christopher McDonald ambaye aliwatumia ndege ya kukodi iliyowafikisha Uingereza.
Christopher aliwapokea vizuri akaenda nao mpaka ofisini kwake na wakampa habari za kina kwa mara nyingine, habari ambazo zilikuwa zaidi ya zile alizozipata kupitia vyombo vya habari vya BBC na CNN.
“Hongera Steve!”Akamwambia baadae. “Umefanya kazi nzuri kumleta Masurufu. Hii ni theluthi nyingine ya malipo yako. Kesho utamaliziwa theluthi iliyobakia na tutakuruhusu urudi zako Miami! Tayari tumekuandalia hoteli nzuri ya kufikia”.
Akatua na kujiwashia sigara, akatoa moshi mwingi na kupuliza hewani. Halafu akamgeukia Masurufu, “Wewe nenda kapumzike bila shaka G-8 watapenda kuyasikia haya unayonieleza.
“Chris naomba tena, niko chini ya miguu yenu. I’m very very sorry Chris!” Machozi yakamtoka.
“Najua! Lakini kesho tutaongea mengi zaidi!”
Alipomaliza kusema hayo walikuja watu wawili, mmoja akamchukua Masurufu na mwingine akamchukua Steve wakaondoka nao hadi katika Hotel ya nyota tano pale Uingereza. Kila mmoja akakabidhiwa chumba chake.
Steve alipobaki peke yake akainua ile briefcase yake yenye fedha na kuifungua. Badala ya fedha, ukatoka moshi fulani mweupe. Ulikuwa na harufu nzuri hujaona na ulimuingia Steve moja kwa moja puani.
Steve alipokuja kutahamaki kwamba anavuta sumu, tayari alikuwa amekwisha chelewa, nguvu zilikuwa zikipungua mwilini mwake kwa kasi ya ajabu. Akajitahidi kuinuka akimbilie bafuni akapate maji ambayo yalikuwa dawa ya sumu hii, hakuweza, akaanguka vibaya, mwili ukikosa nguvu hata ya kujikokota.
“Shiit!” Akajitahidi kujuta akijilaani na kuilani bahati yake. Sauti pia haikutoka. Akili ikapoteza uwezo wa kufikiri akaanza kudidimia katika shimo lefu la kiza ambalo halikuwa na mwisho. Ukawa mwisho wake.
* * *
Dr Masurufu alikuja kuchukuliwa siku ya pili asubuhi na kupelekwa katika chumba fulani ambako alikuta timu yote ya G-8 Original ikimsubiri.
Hapo tena akatakiwa kueleza kilitokea nini, hata mpango wao ukafeli licha ya wao kuwekeza mamilioni kwa mamilioni ya shilingi. Akijua hii ndiyo nafasi yake ya mwisho, Masurufu alieleza hatua kwa hatua mpaka hali ilipofikia.
“Umenisikitisha sana Masurufu!” Akasema Christopher mwisho wa simulizi. “Ulishindwa nini kuomba ushauri kabla? Kwa hasara uliyotuingiza tuambie ni kwa nini hustahili kufa!”
“Kufa?” Masurufu akashtuka. “Oh! Hapana jamani… No… Nooooh! Nina mipango mbadala ambayo itarejesha fedha mliyotoa na faida. Nina familia na wazazi wanaonitegemea! Nina… Nina…!”Alisema mengi ambayo hayakuwaelea G-8 Original, zaidi akiomba msamaha na kwamba katika mpango mwingine atakuwa makini zaidi. Ataomba ushauri na kadhalika.
“Okay!Unaweza kwenda!” Akaambiwa alipomaliza kusema.
Masurufu hakuyaamini masikio yake, kirahisi hivi. Akawaza na kuuliza kutaka uhakika “Eti umesema?”
“Unaweza kwenda!”
“Je” Akatua akiwatazama mmoja baada ya mwingine “Mmenisamehe?”
Wajumbe wakatikisa kichwa juu na chini kukubali. Dr Masurufu akaomba dua, kumshukuru Mungu na kuwashukuru Christopher McDonald na wenzake. Kabla hajainuka akaanza kuvuta hatua na kuondoka.
Alipoukaribia mlango tu, Christopher McDonald akatoa bastola na kumpiga Dr Masurufu risasi ya kisogo ambayo ilimpaisha na kumsomba mzima mzima, ikampigiza ukutani kwa nguvu. Alipotua chini alikuwa maiti.
“Number one!” Masurufu akasema baada ya kubonyeza mahala ukutani. Dakika hiyo hiyo akaingia mwanaume mmoja mwenye asili ya kichina aliyechanganya damu na mjapani. Huyu alikuwa Ben Tapeli.
“Niko hapa Sir!”
“Vipi kazi ya hotelini?” Akamsaili.
“Imekwenda vizuri sana. Steve ameingia kuzimu jana jioni kwa kutumia ileile sumu hatari tuliyoipata South Korea. Hakukuwa na upinzani kabisa. Alikufa mara moja. Bila shaka anamkaribisha mwenzie sasa hivi!” Akihitimisha kwa utani.
Akina Christopher wakacheka.
“Ilikuwa ni lazima afe. Uzembe wake wa kutomsimamia Masurufu vyema umemgharimu!”
“Kabisa bosi!”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Tafadhari tuondolee huu mzoga ndani. Unastahili kuwa chakula cha samaki baharini!” Akaamrisha. Jamaa akaanza kutekeleza kazi aliyotumwa, akiacha Christopher akiwaomba radhi wenzie kwa kufeli kwa mpango wao.
Walipomsamehe ndipo walipoanza kuumiza vichwa kutafuta namna ya kulipiza kisasi kwa watanzania na serikali yao kufidia hasara waliyoingia. Walidhamiria kutoka na mkakati ambao utakuwa sawa na pigo takatifu sana. Pigo lenye nguvu kupita kiasi. Pigo litakalofanya sio tu Tanzania na Afrika ilie pekee bali na kusaga meno!
Waliendelea kutafuta.
* * *
Maiti ya Dr Masurufu yaliokotwa kando kando mwa ufukwe wa Bahari katika jimbo moja nchini Ufaransa. Iliwachukua muda mfupi tu Polisi kugundua kuwa walikuwa wameuokota mwili wa aliyekuwa anataka kugombea urais wa Tanzania kutokana na nyaraka zilizokutwa mfukoni mwake.
Habari hizi zilipofika Tanzania, hakuna aliyelia!
MWISHO.

0 comments:
Post a Comment