.
Simulizi : Mkakati Wa Kuelekea Ikulu
Sehemu Ya Nne (4)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku hii Profesa Zonga akawaita waandishi wa habari na kuwaeleza mambo kadha wa kadha kubwa likiwa utabiri wa nani atakuwa Rais wa nchi hii baada ya Rais anayemaliza awamu yake kung’atuka.
Katika utabiri wake ingawa hakutaja jina, alitaja alama zote alizonazo Dr Masurufu na kutoa onyo kuwa atakayejaribu kushindana nae atapata laana na uchizi. Kwamba nyota yake ilikuwa inang’aa sana na alikuwa chaguo la Mungu pamoja na viumbe vyote.
Kwamba kumpinga ni kwenda kinyume na adhabu ya hilo ni laana, uchizi na pengine kifo. Hivyo yeye kama Profesa Zonga wa Zonga, mnajimu na mtabiri maarufu alikuwa anawaonya wote wanaotarajia kusimama kujihadhari zaidi vinginevyo hawatapa zaidi ya hasara.
Siku iliyofuata magazeti yalibeba habari hizi kwa uzito ule ule uzito uliozidi mipaka. Profesa Zonga amtabiria Masurufu kuukwaa Uraisi! Gazeti moja lilidai na kuongeza Nambari za kinajimu zimempa alama zote za ndiyo. Tayari amechukua fomu CCM. Wapinzani wake matumbo joto!
Dokta Masurufu safari ya Ikulu yaiva Lilikuwa gazeti jingine. Utabiri wathibitisha hivyo. Atakayepambana nae kuambulia laana, Uchizi! Likahitimisha
Hayakuwa haya pekee, kila moja liliibeba habari hii na kuipa umuhimu wa pekee. Hata hivyo hazikuwa habari zilizodumu sana. Kwani wanaharakati wa mashirika yasiyo ya kiserikali walimshukia Profesa Zonga na baadhi wa wahariri na wamiliki wa vyombo vya habari huku wakisaidiwa na watu walioonyesha na kutangaza nia ya kugombea urais.
“Profesa Zonga sio Mungu!” mmoja wa viongozi wa vyama vya Siasa alisema kwa jazba. “kamwe, hatuwezi kumsikiliza! Nasi tutasimamisha mgombea ili tuone kama atapata laana kweli!” Akahitimisha huku wafuasi wake wakimshangilia.
Hii sio nchi ya kishirikiana! Profesa Zonga aache unafiki na umbea wake! Walikuwa wanaharakati wengine. Yalisemwa mengi, lakini ni machache sana yaliyopewa nafasi katika vyombo vya habari na hayakupewa uzito ule le kama aliopewa Profesa Zonga. Naam! Bahasha zake kwa waandishi wa habari zilikuwa zimefanya kazi kweli.
Kule vijijini ambako walipelekewa magazeti kwa gharama za Dr Masurufu, habari zikaendelea kushika kasi, Masurufu alikuwa chaguo la Mungu pamoja na viumbe vyake. Wanakijiji wakamsubiri kwa hamu ili wasikie atakuja na kitu gani kipya cha kuwakomboa toka katika umaskini wao unaochusha na kuudhi.
Nchini Uingereza Chritopher MacDonald aliendelea kuchekelea kadiri upepo ulivyokuwa ukimuangazia Dr Masurufu. Hili la mnajimu likiwa limemfanya afurahi zaidi, hata akainua simu kumuuliza Masurufu walikolipata wazo hili.
“Ni utaratibu wake kutabiri na kuzungumza na waandishi wa habari kila baada ya muda fulani!” Akamjibu.
“Kwa hiyo ni wewe uliyemuuzia wazo hili? Maana naona limekuwa na mwitikio mzuri kweli kwa jamii!”
“Hapana! Ni mawazo yake tu. Lakini Profesa Zonga ni mtu wangu kwa kila hali. Ni yeye aliyenifanya ning’ae ughaibuni na hata Safari yangu ya Ikulu anaisimamia yeye kwa mlango wa nyuma kwa kiasi kikubwa sana tu!”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Una maana gani Dokta?”
“Sie waafrika Chris! Mambo yetu hayaendi bila nguvu za mababu na mizimu!”
Christopher akaelewa. Alishapata habari toka Steve kuwa Masurufu ameamua kuingiza masuala ya ushirikiana katika harakati zake. Na yeye kwa kuwa hakuona athari yoyote akawa amemtaka Steve amuache tu ila ahakikishe lengo lao haliathiriki.
Labda kilichomtia wasiwasi ni ile hujuma ya wadhamini bandia ambayo Masurufu alikuwa ametoa ushauri maridhawa wa kulitatua baada ya kufanya kikao ambacho Christopher pia alihudhuria kwa kutumia njia za kielectronic za mnazi wake Steve.
Hofu yake ilikuwa kama Profesa Zonga angehitaji amali ya hisa kwa kile anachokifanya baada ya Masurufu kuwa Rais.
Alipohakikishiwa kwamba Zonga hatohitaji hisa kwa kuwa alikuwa akilipwa kwa kila hatua, Christopher MacDonald akaishia kufurahi tu akiomba waendelee na harakati kama walivyopanga.

KASHFA
“Nimemaliza kazi Mkuu!” Steve alimwambia Dr Masurufu mara tu walipoingia katika chumba chao cha siri pale nyumbani kwa Dr Masurufu. “Hii ni CD yenye picha chafu za John Tengeneza ambazo amekuwa akipiga na watoto wa shule anaowarubuni na kuwaharibia maisha, John ni fataki. Hili ni faili la watu walio na wanaomdhamini kifedha ili agombee Urais.” Akatua
Masurufu akafanya pupa kuangalia watu wanaomfadhili John Tengeneza. Wengi aliwafahamu, walikuwa katika ule mtandao alioutengeneza wakati ule akiwa Waziri wa fedha. Hili likamfanya autilie shaka uadilifu anaodaiwa kuwa nao John.
“Faili hili pia…” Steve akaendelea “Lina orodha ya akaunti zake na baadhi ya mikataba aliyoingia na matajiri wa nchi ili akiwa Rais ashirikiane nao. Kwa ujumla ni faili lenye kila kitu. Na limenigharimu kuua watu wawili kulipata. Naamini hili likifika mbele ya watanzania John atabaki mtupu kabisa. Itamlazimu kuwa na moyo wa jiwe na roho ya chuma kuendelea kung’anga’nia Urais wa Tanzania sio tu kupitia CCM, bali hata nje ya hapo!” Steve akahitimisha.
“Wow!” Masurufu akashangilia akimkumbatia na kumpongeza Steve kwa kazi kubwa, ngumu na nzuri. Machozi ya furaha yakamtoka pale alipofikiria kuwa zana za kumuua kabisa kisiasa John Tengeneza zilikuwa mbele ya meza yake, zikisubiri kauli yake tu!
Christopher alifikiria nini kuniletea mtu kama Steve! Akajiuliza akijitoa kifuani kwa Steve baada ya kumpongeza tena kwa mara nyingine na nyingine!
Akaipigia simu kamati yake ya wanaumoja na kuwataka wakutane nyumbani kwake haraka. Wakati anawasubiri wajumbe wafike, akainua simu tena kumpigia Christopher kumjuza kinachoendelea na hatua waliyofikia katika kumsambaratisha John Tengeneza.
“Good Job!” Christopher akamwambia. “Ukiweza kupata taarifa za wapinzani wako wengine pia, wengine fanya hivyo. Hiyo ndiyo siasa. Siasa sio mchezo mchafu pekee bali pia ni mchezo wa kuviziana na kanuni zake ni kama zile za michezo ya mieleka unanielewa?
“Nakuelewa vizuri sana!”
“Eeh! Katika mieleka ukizubaa kidogo tu umekwisha. Ndio maana wanasema usijaribu mchezo ule. Wakati ukitafuta taarifa za hao wengine, make sure nawe huachi mianya ya taarifa zako kuvuja maana hilo likitokea hakutakuwa na maana ya tunachokifanya sasa. Okay?”
“Haina Shida! Maadamu niko na Steve, hakuna kitakachoharibika!”
“Na katika hili, mwambie Steve asiwe na huruma hata chembe!”
“Nitamwambia. Always Steve hana mzaha. Amekwishaua wawili na na kuokoa milioni mia mbili wakati akiniletea siri hii!”
Alipomaliza kuongea na Christopher, baadhi ya wajumbe walikuwa wamefika akiwemo Frank John Mariki Kampeni Meneja wake. Wote kwa pamoja wakazizunguka picha zile na kuziangalia, kabla hawajaligeukia faili na kuliperuzi.
Waliyoyakuta na kuyaona yakawafanya wajiulize kama Tengeneza aliyetajwa kuwa muadilifu na kuifanyia nchi kazi nzuri, ndiye ambaye faili lake la siri lilikuwa na zaidi ya Uvundo, je kuna muadilifu kweli nchini?
Hata hivyo wao wakiwa chui ndani ya ngozi ya kondoo, hili halikuwa shughulisha sana, badala yake walikenua kwa kupata njia ya kumuadhibu adui yao. Wakajipangia mikakati ya kummaliza John kabisa kabisa na kugawana majukumu, tayari kwa utekelezaji.
* * *
Mikakati ilitekelezwa vizuri, gazeti la Dr. Masurufu likawa la kwanza kuibuka na habari za kashfa za John Tengeneza. Kwamba alikuwa fataki na kamwe hakufaa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, kitendo chake cha kutembea na watoto wa shule na kuwaharibia maisha viongozi wa Tanzania ya kesho, hakikufaa kuungwa mkono. Kwamba alikuwa kinyume kabisa na ajenda ya watoto.
Picha kadhaa za aibu za John Tengeneza zikatolewa ukurasa wa mbele huku gazeti likidai kumiliki CD yenye kila uozo wa John. Magazeti ya udaku yakaipa uzito habari hii na kuigeza ajenda ya kibiashara ambapo kwa kuwa na habari hizo, magazeti yao yaligombewa kama njugu sokoni.
Majina ya matajiri waliomdhamini kwa makubaliano ya kuwapa vyeo yakatolewa pamoja na idadi ya fedha, mahala zilikowekwa pamoja na nambari za akaunti. Watu wakabaki midomo wazi wasiamini kama Tengeneza alikuwa hivyo anavyodaiwa.
Haya yakawa yamechokoza nyuki
Mara moja siasa zikabili uelekeo. Familia ya John Tengeneza na watu wake wakaanza kuhaha kutafuta nani aliyevujisha siri hizi hatari, ambazo zilikuwa zimehifadhiwa mbali na watu wake wawili aliwaamini vyema Mathew na Mathias, ambapo alipofuatilia zaidi aligundua kuwa watu wake hao walikuwa marehemu. Ndipo akaelewa kuwa tuhuma zile ambazo yeye zilimbomoa sana, kwa vijana wake ziliwagharimu maisha.
Ghadhabu zikampanda pale vijana wake walipomletea taarifa kwamba Dr Masurufu ndiye aliyekuwa nyuma ya njama hizi chafu. Akaanza kuwaza na kuwazua namna atakavyoweza kulipa kisasi.
Mara akaanza kupokea waandishi wa habari waliotaka kujua anasemaje kuhusu tuhuma hizo na kama anatarajia kujiengua katika kinyang’anyiro cha kuwania kuteuliwa na chama kuwa kiongozi.
Kama ambavyo huwa kwa wanasiasa wengi, naye alikanusha kwa nguvu zake zote kuwa huo ulikuwa uzushi na uongo mtupu. Aliwataja waliotoa tuhuma hizo bila hata kumpa nafasi ya kujitetea kuwa ni wanafiki na wazandiki wakubwa na kwamba kama wanafikiria atajitoa katika inyang’anyiro hicho walie tu, kwani sasa ataongeza nguvu zaidi ili hatimaye aweze kushinda na kuteuliwa na chama. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hata hivyo aliwahakikishia waandishi kwamba anawasiliana na wakili wake ili aandae taratibu za kumfikisha mahakamani kila aliyemkashifu na kumchafua ambapo atawadai mabilioni kwa mabilioni ya shilingi.
Habari hizi zilipotoka zikazusha mjadala mitaani. Kama ilivyo ada zikawachulia watanzania muda mwingi kuzijadili baadhi wakiafiki na baadhi kutoafiki huku wingi wao wakisubiria kwa hamu John Tengeneza afungue kesi.
Kesi haikufunguliwa! Badala yake walishuhudia siku kadhaa mbele magazeti megine tofauti na yale ya mwanzo, Redio na Televisheni ambavyo vilikuwa vikimuunga mkono John Tengeneza vikaibuka na habari mbaya na chafu kwa Dr Masurufu.
Kwamba licha ya kulelewa na Baba wa Taifa Masurufu alikuwa fisadi nambari moja nchini, Papa la Rushwa, Mkwepaji mkubwa wa kodi na jambazi wa kalamu. Mifano hai ya kutosha ikatolewa kulithibitisha hili, mali zake alizozipata wakati ule zikiwekwa hadharani na kutakiwa akanushe uthibitisho wa vielelezo hivyo kama anadhani anaonewa.
Sio hivyo tu, alielezwa pia namna alivyolitumia vibaya jina la Baba wa Taifa kujinufaisha, alivyolitumia Azimio la Arusha na Kampeni za uhujumu Uchumi kujilimbikizia mali pamoja na vita vya Uganda ya mwaka sabini na nane vyote kwa pamoja viliudhihirisha umma kuwa ni kweli Dr Masurufu alikuwa fisadi nambari moja nchini.
Habari hizi ambazo wengi ziliwaacha midomo wazi, baadhi wakishika vichwa kutoamini wakisikiacho, kwa Masurufu zilikaribia kuondoka na roho yake kwa kuwa alijikuta akishikwa Shinikizo la damu baadae kizunguzungu kikali kabla hajaanguka chini na kuzirai ambapo alikimbizwa hospitali ya Ocean Road zilikoanza juhudi za kuokoa maisha yake.
Habari za ugonjwa wake zikatakiwa kuwa siri kubwa hata watumishi wake ofisini hawakujua yupo wapi

Habari za ugonjwa wake zikatakiwa kuwa siri kubwa hata watumishi wake ofisini hawakujua yupo wapi!
* * *
Malumbano haya baina ya John Tengeneza na Dr. Masurufu ambayo wengine hawakuyatilia uzito sana yakawa yamempatia uhakika Samson wa ile hofu iliyokuwa ikimkabili. Hofu kwamba uchaguzi huu ulikuwa na jambo zaidi ya uchaguzi.
Awali kabla ya malumbano haya ya Tengeneza na Masurufu, alikuwa amewatembelea kwa siri wagombea Urais wasiopungua sita kwa kuwatumia vijana wake shupavu. Michael na Raymond. Akawa amejua mambo kadha wa kadha kuwahusu. Mambo ambayo pia hakuona kama yalikuwa na athari hasi kwa taifa.
Mgombea ambaye alikuwa amemvutia alikuwa Dr. Masurufu Huyu alimvutia kwa jinsi alivyoishi kama kinyonga kwa kuudanganya umma mahala anakolala.Awali alikuwa amefikiria kwamba Masurufu anafanya haya kwa sababu za kiusalama, hii ni kwa vile alifika zaidi ya mara moja katika maeneo yake na kutoona hitilafu yoyote.
Kuibuka kwa madai ya Masurufu dhidi ya Tengeneza na baadae ya Tengeneza dhidi Masurufu kukawa kumeifanya hofu yake itimie. Kwamba staili ya kinyonga ya Dr Masurufu ilikuwa inalenga kuficha mambo ambayo baadhi yametajwa na Tengeneza
Kama mpelelezi anayotegemewa na serikali, Samson Kidude aliona kuwa anawajibika kutafuta uthibitisho wa madai hayo ya Masurufu kama ambavyo alikuwa anahitimisha kupata ushahidi wa Tengeneza, ili mwisho wa siku aweze kuwakabidhi katika vyombo vya usalama wakapate malipo ya uhalifu wao.
Haraka akainua simu na kuwaita vijana wake machachari Raymond Kalolelo na Michael Kilibhaha, ambapo walifika ndani ya dakika kumi.
“Nimewaita kwa kazi moja ya haraka!” Samson akawaambia mara waliopoingia na kuketi. “Kazi ambayo nitapenda muifanye kwa uwezo wenu wote!” Akatua na kuwaruhsia nakala za magazeti yenye habari za Dr Masurufu.
Wakiwa wameshazisoma habari hizo tayari, Ray na Michael walizipitia tena haraka haraka kabla hawajayatua magazeti kando na kumtumbulia macho Samson, macho yao yakidai maelezo zaidi!
“Nahitaji uthitibitisho wa madai hayo!” Samson akasema kama aliyeyasoma macho hayo. “Ikiwezekana na ushahidi kabisa. Wakati nyie mnafanya hayo, mie nakwenda kumbana Tengeneza anieleze alikoyatoa madai haya mazito. Natumai ipo cheni ndefu nyuma yake. Cheni ambayo itatuongoza hadi penye mzizi wa tatizo ambapo tutaufukua na kuondoa utata kabisa. Naomba mwenye swali aulize!” Akatua.
Yafuatia maswali madogo madogo tu kama Masurufu aliishi wapi, mahala anakofanyia kazi familia na kadha wa kadha maswali ambayo Samson aliyajibu vizuri tu kwa kuwa alikuwa amemtembelea mara mbili na aliyajua fika mazingira ya Dr. Masurufu.
“Raymond!” Samson akaita waliposimama tayari kwa kuondoka. Raymond akamuangalia.
“Ingawa Dr Masurufu amepata kuwa mwanajeshi, sitarajii kama mtapata upinzani wa maana hasa ukizingatia alivyoacha madaraka yamlevye na kumjaza mafuta mwilini kitambi kikiwemo, Naomba mjihadhari na muwe makini!”
Ray na Michael wakatabasamu. Moyoni wakifarijika kuona Samson anavyojali maisha yao “Usihofu kaka!” wakageuka na kuondoka. Mazungumzo mafupi waliyoyafanya yakawafanya waifuate moja ya kanuni ya kazi zao.
Kutoongozana kama maandazi.
Wakagawana
Raymond akaelekea ofisini kwa Dr Masurufu wakati Michael akaelekea nyumbani kwake. Kila mmoja alisisimkwa na mwili jambo lililowaashiria kuwa walikuwa wanaingia kazini rasmi!
* * *
Dr Masurufu alizinduka masaa machache baada ya madaktari kumaliza kumtibu na kuondoka baada ya kuitaka familia yake kutomsumbua. Glady mkewe aliyekuwa akiombea mumewe aamke, akamsimamia kumkabili mithili ya jini la kutumwa.
Habari alizozipata toka kwa wapambe wa Dr. Masurufu ambao nao walikuwa mapandikizi ya John Tengeneza; kuwa Dr. Masurufu alikuwa na nyumba ndogo tofauti na yeye na kwamba ndiyo iliyokuwa ikishirikishwa katika mipango yote zilikuwa zimemchanganya vibaya hata akose simile na busara za kawaida za mwanadamu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Niko wapi Hapa?” Masurufu akauliza. Glady akamtazama kwa jicho la chuki na kumjibu, “Uko hospitali! Umeponea chupu chupu na tabia yako ya kuficha ficha!.”
“Kuficha ficha?! Mungu wangu, kumejiri kitu gani tena!” Masuruf akaweweseka akili yake ilikuwa bado hajaweza kuunganisha mambo sawa sawa na alikuwa akijitahidi kukumbuka mambo kwa uwezo wa hali ya juu.
“Kimejiri kitu gani?! Subiri tu. Na polisi wataanza kukutafuta sasa hivi!” Akapumua kwa hasira!
“Lakini Mama Masurufu…!” Steve mlinzi wao ambaye alikuwa kimya muda wote akaingilia, “…ungemuacha kwanza aji…!”
“Shut up you Idiot!” Glady akakemea.
Likawa jibu lililomkera Steve. Akaruka kutoka alipokuwa mpaka kwa Mama Masurufu, “Je,” Akamuuliza kwa hasira baridi, “unawezaje kunijibu kijeuri hali hukuniajiri wewe?”
“I don’t care!”
“Hujali siyo? Haya toka nje!”
“Sitoki!”
“Tokaah!!”
“Sitoki nakwambia!”
“Basi utatoka tu!” Steve akamshika mikono na kuanza kumvuta atoke nje. Ikatokea purukushani kidogo mpaka Dr Masurufu alipmkataza amri Steve kwa sauti dhaifu, ndipo alipomuachia na wote wakabakia wakihema kama madume ya bata yaliyotoka kupigana.
“Ahsante sana Masurufu!” Akaanza mkewe Masurufu akihema “Unanificha hata mie? Mimi mimi?!” Akajipigapiga kifuani eneo ulipo moyo na kuangua kilio. Kilio kikuu. Masurufu akashangaa maajabu haya. Swali likamtoka! “ Nimekuficha nini mpenzi wangu?”
“Hebu toka hapa na Unafiki waka, nani mpenzio? Ningekuwa mpenzio ungeweza kufanya uliyofanya bila walau kunijulisha? Mbona mimi ni mkeo? Liwazo la moyo wako, mama wa watoto wako? Mangapi nimeweza kuyaficha na kuyatunza hadi leo tuko hapa?”
“Bado sijakuelewa mama Rose?”
“Unanielewa vizuri sana, kwani nini umemtuma Steve anifukuze? Sawa, sistahili kuwa na wewe. Kwa sababu unakwenda kuwa rais wa Tanzania. Na Rais hapaswi kuwa na mke mshamba mshamba kama mimi si ndiyo?, Nashukuru sana. Nashukuru sana Masurufu!” Glady akatua na kulia tena.
Masurufu akaendelea kushangaa kwa dhati, asielewe chochote.
“Usijitie kushangaa wakati umefanya tambiko na upuuzi wako mwingine bila kuniambia. Umeingia hata katika malumbano ya kijinga na kipuuzi mpaka kufikia hatua ya kumwaga damu pasipo kunishauri. Kwa akili zako finyu wadhani ndio wapalilia Barabara yako ya Ikulu. Vyema sana! Nenda salama. Najua sina thamani tena kwako na ndio maana umepata mwanamke mwingine ambaye kwako wadhani anastahili kuwa mkeo na First Lady pindi ukiwa Rais.
Hongera kwa hilo, Ila kwa kuwa umemwaga mboga mie namwaga ugali. Nakwenda kuwa upande wa John Tengeneza na ninajua kwa taarifa zilizotoka, polisi watataka kukutembela. usijidanganye kwamba nitawaficha, nitawaeleza ukweli mtupu ikiwa ni pamoja na kuwasaidia kukwamisha ndoto zako.
Kama hiyo haitoshi nitawaeleza juu ya mkakati wako na mkataba uliofanya na akina Chris halafu tuone kama hayo unayoyataka yatatimia shenzi Taip!!”
Mama Masurufu akahitimisha na kuondoka kwa kasi kweli!
“Mama Roseeeh…!” Masurufu akaita kwa taabu. Alikuwa ameogopa kwelikweli “Mama Dani…, mke wanguuuh!” Mkewe hakumsikia na pengine alimdharau. Ilikuwa wakati huu Glady alipoufikia mlango, akaufungua kwa nguvu kabla hajaubamiza kwa hasira nyuma yake hali sauti ya “Sitakiih!” Ikiwafikia kwa taabu.
Masurufu akasikia mapigo ya moyo yakipanda tena kwa kasi hali pumzi zikimpaa “Nii…nii…niitie daktari...!” Akafaulu kusema kwa taabu na kuongeza, “Na…na… umzuie …umzuie Glady asilete madhara……madhara!”

Kitendo bila kuchelewa Steve akaruka nje, dakika ya pili akarejea na Daktari na kukuta Dr Masurufu ameshazirai tena.
Wakati daktari ameanza kumshughulikia Dr. Masurufu, Steve alikuwa ndani ya Toyota Landcruiser VX akipangua gia na kukanyaga mafuta mpaka alipofika katika mtaa ya Ohio ambapo aliliona Toyota Nissan gari la Glady Stevenson Ombwe, mke wa Dr Masurufu likiacha barabara ya Bibi titi na kuchukua ile ya Ally Hassani Mwinyi.
Akaiandama kwa busara kwa kuacha magari kadhaa mbele yake safari yao iliishia Mbezi Beach nyumbani kwa Dr Masurufu, ambako Glady alishuka na kuingia ndani kama mtu aliyechangikiwa haswaa.
“Sitaki mtu anibughudhi kabisa!” Mama Masurufu aliwaambia wafanyakazi wa ndani wakati akipitiliza ndani alikoingia na kuanza kulia.
Steve aliipaki gari yake pembeni ya gari ya Mama Masurufu naye akashuka na kuingia.
“Mama amesema hataki kusumbuliwa na mtu yoyote!” Eliza mtumishi wa ndani alikuwa amekumbuka kumwambia Steve mara alipomuona akielekea chumbni kwa Mama Masurufu. Kauli iliyomfanya Steve asimame na kutengeneza tabasamu.
“Oh! sorry” Akasema kama aliyekumbuka kitu. “Mama hajisikii vizuri, mie nataka nikachukue cheti nikamnunulie dawa!” Akawaambia.
“Ohh! Kumbe!” Alikuwa Eliza kwa unyenyekevu “Samahani, unaweza kuendelea!”
“Msijali!”
Steve akaingia ndani alikochukua dakika chache tu zilizotosha kumfaya Glady asiwe na madhara wala tishio kwa Dr Masurufu.
* * *
Sekunde chache baadae, Michael naye alikuwa anapaki gari katika viunga vya Dr Masurufu pale Mbezi Beach pembeni ya gari ya Steve na Glady. Akashuka akaukabili mlango na kubonyeza kengele.
“Karibu!” Eliza aliitika na kwenda kufungua mlango tena. “Karibu! Karibu ndani!” Akamkaribisha zaidi.
“Ahsante!” Michael akaingia ndani “Naitwa Michael ni mwandishi wa Habari, natokea Daily News!” Michael akatua na kutoa kitambulisho, akampa kitambulisho Eliza huku macho yake ya kazi yakisawiri hapa na pale kwa kasi ya ajabu.
“Shikamoo!” Alikuwa Eliza tena baada ya Michael kuketi na kumrejesha kitambilisho.
“Marahaba!
“Utakunywa nini? Soda, Juisi, Maji au kahawa?”
“Ahsante. Baba yuko wapi? Nina shida na baba kwanza. Nilikuwa ofisini nikaambiwa yuko nyumbani! Niitie nizungumze nae!”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Baba hayupo! Na hutaweza kuzungumza nae kabisa!”
“Kwa nini?” Michael akauliza kwa pupa na kihoro
“Kuna mambo yalitokea. Sijui mambo gani vile, baba akawa ameshikwa na Presha na kukimbizwa hospitali. Wakati fulani mama alitupigia simu kwamba anaendelea vizuri. Labda atatoka baadae!”
“Oooh! Poleni sana!”
“Ahsante Tumeshapoa! Michael akavuta tafakuri akijaribu kuhusianisha presha ya Dr Masurufu na zile habari za Ufisadi. Inaweza kuwa sababu? Akajiuluza kabla hajajirudi kuwa jibu la swali hilo liko kwa Masurufu. Akamtazama tena Eliza na kumuuliza
“Je amelazwa hospitali gani?”
“Nilisikia wanasema kama Ocean Road vile?! Sina hakika lakini.”
Wakati Eliza anajibu hivi, mlango wa chumba cha kulala wa cha Dr. Masurufu ukafunguliwa na Steve akatoka akiwa ameisikia Ocean Road Vizuri kabisa.
Kwa sekunde kadhaa wakatazamana kila mmoja akimsoma mwenzake. Michael alipoona muda unapita pasipo kutambulishwa akasimama na kusema “Ahsante Eliza, Nitarudi tena baadae. Mzee atakapotoka Hospitali!”
“Haya!”
Michael akamtupia jicho Stevu na kumuaga kwa kusema “Kaka Ahsante”
Steve akanyanua kichwa kukubali. Michael akatoka. Steve akamkabili Eliza na kumkazia macho mpaka Eliza akaogopa. “Yule nani” Akamuuliza.
“Ni mwandishi wa habari wa Daily News!”
“Amekuja kufanya nini?”
“Anataka kuzungumza na baba, nikwamwambia baba anaumwa yuko hospitalini Ocean Road.”
“Kwanini umemwambia yuko Ocean Road? Nani alikutuma kusema hivyo?”
Eliza akatetemeka asijue la kusema. “Nisamehe kaka, sikujua!”
“Pumbavu!” Steve akabweka kwa ghadhabu. “Usirudie tena mchezo huu sawa? Hujui kama mzee ana maadui wengi na wanaweza kumdhuru? Ukome kabisa!”
“Ndiyo kaka!” Alikuwa Eliza tena kwa woga. Steve akamuaru awaite wafanyakazi wote sita wa kasri hilo, Wakaitwa! Walipatikana wanne, wengine walikuwa nje ya nyumba kikazi.
Steve akawaonya wasithubutu tena kutoa habari za Dr Masurufu na kwamba atakayejaribu atakiona cha moto. Akawaacha wameduwaa na kutoka sekunde chache baadae akarudi na kuwaambia tena
“Mama amepumzika. Msimsumbue hata kidogo! Muacheni mpaka atakapoamka mwenyewe Sawa?!”
“Sawa!”
Akatoka na kuingia chumba chake cha kazi alikojipanga kwa muda mfupi sana kabla hajapanda gari na kurudi Ocean Road Hospitali kwa Dr Masurufu.
* * *
Njiani Michael alimpigia simu Raymond na kumtaka aje Ocean Road Hospitali kwamba Dr Masurufu alikuwa amelazwa huko baada ya kushikwa na presha.
“Nashukuru kaka, maana ilibaki sentimita chache niingine ofisini kwake! Usijali nitakuwa nawe baada ya muda mfupi tu!”
“Uje bwana, kuna njemba imenitia shaka pale nyumbani kwa Dr Masurufu! Nataka tuijadili kwa kina maana Samson hakuwahi kusema kama pale kuna mtu wa ziada. Na yule jamaa haelekei kuwa house boy!”
“Unataka kusema umetoka msambweni?”
“Hapana. Ila angalia yake kwangu kama jasusi fulani hivi! Kama vile hakufurahia mie kwenda pale!”
“Nakuja, tutaongea mengi nikifika!
“Poa!”
Ray akakata simu. Michael akampigia Samson na kumpa taarifa hizo, Samson akampongeza na kumtaka aendelee. Ulikuwa mwanzo mzuri.
Hakupata taabu kuiona wodi aliyolazwa Dr Masurufu, vile alikuwa Maarufu pale hospitali, na vile alizijua wodi za watu mashuhuri maarufu kama VIP; Michael alipitiliza moja kwa moja mpaka katika vyumba hivyo ambapo alianza kuingia chumba kimoja baada ya kingine.
Chumba cha tatu akawa amekutana na Daktari aliyekuwa akimaliza kumtibu Dr Masurufu “Ohh Michael!” Daktari akaita na kuongeza. “Hujambo?”
“Sijambo kabisa! Haya niambie Dokta Makete, Shikamoo Kwanza!”
“Marahaba. Vipi, huyu mtu wetu nini? Maana nyie mkionekana mahala kuna jambo!” Akauliza Dr Makete, mzee mwenye miaka hamsini hivi ambaye naye alikuwa mtu wa usalama
“Ni mtu wetu Dokta! Kama uvujuavyo ni mmoja wa wagombea habari zake ndizo zinazotamba. Tumenusa kitu kumhusu na ndio maana tuko hapa!”
“Ooh! Vizuri!”
“Uhakikishe anapona!”
“Hilo halina shaka.
“Na je, Itamchukua muda gani kuamka?”
“Kama masaa sita hivi. Huu mshtuko wa mara ya pili ndio umekuwa mbaya maana alikwishapata nafuu kabisa, haiweleweki ni kitu gani kilichomshitua tena na kumtia hatarini. Wengine wanaposhtuka hivi huwa wanapoteza maisha kabisa!”
Ukimya mfupi ukapita wakati Dr. Makete akimpachika dripu ya maji, alipohakikisha yanaenda vizuri akamuuliza Michael.
“Sasa?”
“Nahitaji kufanya kazi kidogo, then nitarejea baada ya hayo masaa sita atakapokuwa amerejewa na fahamu zake!”
“Haina Shida!” Makete akakubali na kutoka.
Michael akaanza upeke upeke wake. Alikagua hapa, akapachika hiki pale kabla hajuvuta droo hii na ile. Aliporidhika na kazi yake, akajiweka sawa na kuelekea mlangoni tayari kuondoka.
Alipofungua mlango tu, hamad! Uso kwa macho na Steven Lawrance Marvin ambaye alikuwa hatua kama nne hivi toka alipokuwa kitendo bila kuchelewa Steve akawa na bastola mkononi na haraka akampa Michael ishara ya kurudi alikokuwa.
Michael akajilaani na kuilaani bahati yake. Nimekuwa mzembe? Akajiuliza hali akiangalia huku na huko kama kulikuwa na raia waliokuwa wakiwangalia. Hakuna aliyewaangalia ingawa kulikuwa na watu wachache, vitendo hivyo vilifanyika ndani ya muda mfupi sana.
Michael akapima itamchukua sekunde ngapi kuingiza mkono wake chini ya kitovu na kuchukua bastola, kuondoa usalama, kumlenga Steve na kuifyatua risasi. Na itamchukua sekunde ngapi steve kukivuta kiwambo cha kufyatulia risasi. Jibu likaufanya mwili umsisimke.
Akainua mikono na kuanza kurudi ndani taratibu.
Steven akamfuata kitemi kabisa na kuufunga mlango nyuma yake kwa kutumia mguu. Kwa maringo kabisa, akamwambiaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hatimaye nimekupata mshenzi mkubwa haya niambie ukweli wewe ni nani na unataka nini kwa Dr Masurufu, Usijidanganye kuniongopea kuwa wewe ni mwandishi wa habari na unatoka Daily News!”

Steven akamfuata kitemi kabisa na kuufunga mlango nyuma yake kwa kutumia mguu. Kwa maringo kabisa, akamwambia

“Halafu ukishajua mimi ni nani ikusaidie nini?” Michael akaanza kununua muda kutafuta makosa ya Steve ili amshughulikie wakati huo huo akimsubiria Raymond.
Kabla Steve hajajibu swali la Michael, simu ya Steve ikaanza kuita. Wakati steve anahangaika kuitoa kwa mkono mmoja, Michael akaona nafasi aliyokuwa akiingojea ndio hii. Haraka akaishusha mikono na kuupleka mkono chini ya kitovu kulikokuwa na bastola yake.
Hakuwahi!
Bastola ya Steve iliyokuwa na kiwambo cha kuzuia sauti ikakohoa mara moja. Risasi ikapiga nyuma ya kiganja cha mkono wa kulia wa Michael, ikatoboa tumbo na mgongo na kutokea upande wa pili.
Michael akajikunja kwa maumivu makali na kwenda chini hali akimtolea Steve jicho la kutoamini. Bastola ya Steve ilipokohoa mara ya pili risasi ikatua katika paji la uso na kumuua Michael moja moja.
“Shenzi type!” Steve akasonya akiipeleka simu sikioni.
SURA YA NANE
VIUNGO NA DAMU ZA ALBINO
Muda si muda polisi nao wakawa wamefika nyumbani kwa Dr Masurufu na kuanza kumhoji kwa vitisho kila waliyemuona, wakitaka kujua Masurufu yuko wapi ili wamuhoji juu ya tuhuma zilizotolewa na John Tengeneza dhidi yake.
Maonyo ya Steve yakiwa yangali mabichi vichwani mwao, wafanyakazi wale wa ndani waliendelea kung’anga’ania hawajui kilichompata Dr Masurufu, wala hawajui alipo. Polisi walipodadisi zaidi, ishara za mwili zikawasaliti watumishi wa Dokta Masurufu.
Polisi wakagundua wanadanganywa ndipo walipowazoa wote na kuwapeleka Kituo cha Polisi ambapo walieleza kitu baada kulambwa vibao viwili vitatu na kutishiwa kutupwa ndani. Wakaruhusiwa baadae baada ya kueleza ukweli na ya kuandikisha maelezo yao.
* * *
Ramond aliwasili katika wodi aliyolazwa Dr Masurufu na kuingia ghafla bila hodi dakika tano baadae. Hii ilikuwa baada ya kumpigia simu Michael, na simu hiyo ikaishia kuita tu bila kupokelewa, hali gari lake lilikuwa katika maegesho ya pale Ocean Road Hospitali.
Kabla hajaifikia wodi hii alikuwa amekutana na Dr Makete kama nasibu wakati alipokuwa amekuja kuchukua dawa zilizoletwa na Lori la MSD ambalo lilipaki hatua chache toka walipokuwa wamepaki.
Ni yeye aliyemwambia kwamba Michael yuko ndani kwa Dr Masurufu na akamuelekeza wodi hiyo ilipo ambapo alianza kupiga hatua ndefu ndefu kuifuata.
Alifika anamkuta Steven amemaliza kuongea na simu.
Maiti ya Michael ilikuwa imeondolewa na kusukumiwa mvunguni mwa kitanda cha Dr Masurufu. Ile damu iliyotapakaa pale sakafuni inamtisha na haraka anapeleka mkono nyuma ya mgongo kwa minajili ya kutoa bastola. Lakini anachelewa kwani tayari alikuwa anachungulia mdomo wa Bastola ndogo ya kisasa aina ya 36 Calibre iliyotengenezwa na Mrusi.
Tabasamu la uchungu likamtoka moyoni akistaajabu wepesi usio wa kawaida wa Steve. Kwa wepesi ule ule, Raymond nae akafyatua teke kali kwa kutumia mguu wake wa kulia akaipigia teke bastola ya Steve nayo ikarushwa kando.
Wanaume wakaanza kuzungukana
Raymond akatisha kushoto na kurusha pigo la kwanza katika mtindo wa karate. Steve akalikwepa. Pigo la pili Hola! La tatu na la nne. Yote yakakata upepo. Raymond akashangaa zaidi asijue kakutana na mtu gani. Akabadili mtindo wa mapigano na kuanza kuruka kama bondia mwenye uzito mwepesi akitupa mapigo mazito mazito kwa staili ya kung-fu. Mapigo ya kifo.
Bado steve aliendelea kuyapoteza mapigo yake kama mzaha, hali akitabasamu kwa dharau. Mara Raymond akarusha pigo la kininja, mara Taekwondo, mara KickBoxer! Ilikuwa kazi bure. Hakuingiza hata pigo moja katika mwili wa steve.
Steve alipoona amemchosha vilivyo Ramond, ndipo alipoikamata mikono yake ambayo ilikuwa imekuja kwa lengo la kumpiga karate katika chembe ya moyo, akaizungusha na kumnyanyua Ramond kwa kasi ya ajabu na kwa njia ya Judo amshusha na kumbwaga chini kwa nguvu. Maumivu makali yakampata mgongoni.
Akamfuata na kumnyanyua tena kwa njia ilele ile ya Judo akampigiza tena chini kwa nguvu “Mama nakufaaah!” Ramond akapiga unyende mkali wa maumivu.
“Unakufa kweli” Akamwambia kwa dhihaka wakati akimkusanya na kumnyanyua tena. Akamwambia “Ni wachache sana waliowahi kupambana na mimi na wakatoka salama. Wasalimie kuzimu!”
Alipomtua tena mara ya tatu, uti wa mgongo wa Raymond ukavunjika! Raymond akalia kama mtoto mdogo. Steve akamsogelea pale chini na kumnyuka makonde kadhaa ya haja, Ray alipotepeta kabisa, Steve akakiinua kichwa chake na kumvunja shingo.
Baada ya kumuua Raymond ndipo Steve alipotambua kuwa mahali pale hapakuwa salama hata kidogo, Hii ni kwa vile kama watu aliowaua walikuwa wametumwa, basi lazima aliyewatuma atataka kujua matokeo ya kazi yake.
Na vile Dr Masurufu alikuwa angali amepoteza fahamu, Steve akaona mambo yanaweza kuwa magumu zaidi kama Polisi watafika hapo na kumkuta anang’aa ng’aa macho. Akatoka nje na kuchukua kigari cha kubebea wagonjwa, akakiingiza wodini na kumpakia Dr Masurufu.
Akampeleka mpaka katika gari lake na kumuingiza.
Madaktari na walinzi walipomuulizia majibu ya kina yalikuwa yanawasubiri, kwamba wameamua kwenda kumuuguzia nyumbani chini ya uangalizi wa Daktari wa familia. Wakamruhusu. Walipoumuuliza ilipo hati ya ruhusa, discharge card. Akaingiza mkono mfukoni, ukatoka ukiwa na noti kadhaa. Akamkabidhi mmoja wao.
“Za nini?!” Mmoja akasaili kwa macho.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Tusaidiane ndugu zangu, nyumbani wanamuhitaji haraka!”
Wale walinzi wakatazamana. Halafu wakaelewa na kutabasamu. Wakamfungulia geti akatoka taratiibu kwa amani na kutokomea zake.
Ni mtu mmoja tu aliyeingiwa na mashaka baada ya kuambiwa Dr Masurufu ameondoka. Mtu huyu Dr. Keneth Makete ambaye alikuwa maliwato wakati Steve alipoondoka na Dr. Masurufu; yeye alikimbilia moja kwa moja katika chumba alichokuwa Dr Masurufu ambapo damu zililimlaki.
Alipoangalia chini ya mvungu, Maiti ya Raymond yalikuwa bado hata hayajapoa wakati ile ya Michael damu zilikuwa zimeanza kuganda. Haraka akainuka na kurudi ofisini kwake ambako alijua cha kufanya.
* * *
Frank aliingia hima katika hospitali hiyo ya Binafsi ambayo ilikuwa Sinza kijiweni ambako alimkuta Steve amejiinamia. Akamsogelea na kumsaili.
“Vipi Master?!”
“Mambo sio hata kidogo, hata naanza kupata mashaka kama harakati zetu zitafanikiwa”.
“Kwani kumezidi kitu gani tena?”
“Tengeneza ametuweza kweli! Sijui zile ziri za Masurufu alizipata wapi? Yaelekea Polisi wamezipata na kuamua kuzifuatilia, Taasisi ya kuzuia Rushwa hali kadhalika. Wachilia mbali usalama wa Taifa ambao nahisi wapo nyuma! Naona matumaini yamepungua sana!”
“Mungu wangu!” Frank John akamudu kutamka. “Sasa tutafanyeje maana naona kama vile tunanza kuwa wakimbizi ndani ya nchi yetu wenyewe!”
“Ndiyo maana nimekuita tushauriane”
“Mie nadhani tungesubiri kwanza Masurufu aamke ili tujadiliane nae kwa kina, kwa sababu namna mambo anavyoyaendesha anajua mwenyewe. We siri kama zile unaweza kuzipata wapi kama sio mtu wake wa karibu sana. Mie mwenyewe kuna Baadhi ya mambo ndio nayaona mle. Pengine akiamka anaweza kuwa na hisia nani amehusika. Pengine mkewe. Tutajuaje?”
“Inawezekana, maana jinsi Mama Masurufu alivyompandishia mumewe pale hospitali, inatia mashaka kama wangali wanazungumza lugha moja.”
“Eti? Wamegombana na mkewe? Hebu nipe habari!” Frank aliomba.
Steve akamsimulia yote. Frank akabaki ameshika kichwa kwa mshangao. Kutokea hapo walijadiliana kwa muda lakini baadae waligundua kuwa hawaendi mbele wala kurudi nyuma. Wakawa hawana budi kusubiri Masurufu aamke wamuulize. Wakaendelea kusubiri.
Masurufu alizinduka masaa manne baadae na baada ya huduma zaidi za hapa na pale, Dr Masurufu alijikuta akiwa na nafuu kabisa kiasi cha akili yake kutulia na kutafakari mambo kwa upana wake. Na katika hali hiyo waliweza kufanya majadiliano ya kina pia.
Ambapo mwisho walikubaliana Masurufu aendelee kujificha hapo hospitali kwa muda wakati Frank akisawazisha mambo kwa kuwanunua wanahabari ili wasiendelee kukuza mambo, kununua viongozi wa hospitali na ikiwezekana hata polisi ili mambo yafunikwe na Dr. Masurufu atakapojitokeza hali iwe shwari kabisa kabisa.
Masurufu pia alipendekeza John Tengeneza auawe ili kukishawishi chama kupeleka uteuzi wa wagombea mbele kwa kuwa hili litasaidia wao kupata muda wa kujipanga vizuri kuondoa makosa yote na kurejesha imani ya jamii iliyotoweka juu yake.
Kitu ambacho walikikubali.
* * *
Taarifa kwamba Raymond na Michael wameuawa na Dr Masurufu kutoweka zilikaribia kumfanya Samson Kidude awehuke kwa kihoro. Akakanyaga mafuta ya gari kwa hasira akivunja na kukiuka sheria za usalama barabarani hadi pale alipojikuta amewasili katika viunga vya Ocean Road Hospital ambako Dk Makete alikuwa Akimsubiri.
Akampokea na kumpa maelezo machache kabla hajamuongoza mpaka katika chumba alichokuwa amelazwa Dr Masurufu, ambacho wakati huu kilikuwa kimesheheni damu na harufu ya maiti. Wakainua kitanda na kukisogeza pembeni, maiti ya Raymond na Michael zikaonekana.
Roho ilimuuma kuona vijana wake walivyouawa kikatili. Akafumba macho na kutoa heshima za mwisho kwa vijana wake hawa aliowapenda na kuwaamini, moyoni akijilaani ni kwa nini hakujipa yeye jukumu la kuja kukabiliana na Masurufu, akiwaacha vijana wake wakienda kwa Tengeneza.
Akainama na kuchukua miwani ya Michael iliyokuwa hatua chache toka ilipo maiti ya Michael, akanyofoa vitendea kazi kadhaa katika shati la Raymond halafu akazifunika shuka maiti zile na kutoka, akimtaka Dk Makete awaite Polisi ambao Awali walikuwa wamezuiliwa wasifanye chochote ili wapige picha na kuchukua alama halafu azihifadhi maiti hizo mochwari.
Kutoka pale Ocean Road, safari yake iliishia katika maabara yake ambako alifika anavitumbukiza vifaa vile katika mashine yake. Picha za matukio waliyopitia Michael na Raymond zikatokea, picha ya Steve ikijionyesha vizuri zaidi. Akai-print na kuihifadhi.
Dakika chache alikuwa katika simu akitoa maagizo haya na yale kwa Mzee Chilonga ambaye naye alijua cha kufanya.
Kiza kilipoanza kubisha hodi kilimkuta akiwa katika sebule ya jumba la kifahari la Dk Masurufu, mbele yake akiwepo Eliza na watumishi wengine watano. Hofu kwamba huyu ni polisi uliwazidishia wasiwasi hata wasijue familia yao inakabiliwa na kitu gani hata polisi waizingire mara kwa mara.
“Mnaweza kuniambia huyu ni nani?”Akawauliza huku akiwapa picha ya Steve. Watumishi wale wakaitazama kwa zamu na kubakia na hofu huku wakitegeana nani aongee. Hii ni kwa kuwa maonyo ya Steve yalikuwa yangali mabichi vichwani mwao.
“Je” Akawauliza tena “Mnamfahamu?”
Baadhi wakatikisa kichwa kukubali, wengine wakikataa.
“Ni nani?”
“Ni... ni... ni mlinzi wa baba aliyerejea nae toka Ulaya!”. Joyce ambaye alipata msukosuko kuzidi wenzake pale walipochukuliwa na polisi mara ya kwanza akaamua kusema, akihofu kwamba pengine ile hadithi ya kuchukuliwa tena mpaka Polisi inaweza kujirudia tena.
“Anaitwa nani?
“Sisi tumemzoea kwa jina moja la Anko Steve!”
“Yuko wapi?”
“Humu huwa haingii mara kwa mara, huingia kwa dharura tu na mara nyingi anapoingia huwa ameitwa na baba. Nyumba yake ni ile pale!” Akajibu tena Joyce akiisota nyumba ya Steve ambapo kwa hapo walipokaa, ilikuwa mgongoni kwa Samsoni.
Samsoni akageuka na kutazama nyuma, akakiona kijumba kidogo mfano wa nyumba yenye vyumba viwili na sebule pembeni sana ya geti la kuingilia na kutokea ndani. Ilizungukwa na maua mengi kiasi cha kufanya isionekane sawa sawa nyakati za mchana, ingawa kwa jioni hii ikiwa inawaka taa ilionekana vizuri zaidi. Akashangaa kwa nini hakuwa ameiona nyumba hii katika mara zote alizofanya safari za siri hapo nyumbani kwa Dk Masurufu.

“Ndio kusema yupo nyumbani kwake?”Akaendelea kusaili.
“Sidhani!” Sasa akajibu Eliza.
“Kwa nini?” Samsoni akamgeukia.
“Mara ya mwisho ilikuwa mchana wakati mama aliporejea kutoka hospitali akiwa hajisikii vizuri na kuomba asisumbuliwe. Anko Steve akaja baadae, akazungumza nae na kwenda kumnunulia dawa huku akituonya tusimsumbue mama wala kutoa habari za mahali alikolazwa Baba.”
Samsoni akasikia moyo wake unapiga kwa nguvu.
“Je,” Akauliza “ Na toka muda huo, mama hajaamka na Steve hajarudi?”
“Hatujui kama ni hivyo au lah!”
“Kwa nini?”
“Kwa kuwa baada ya yule mwandishi wa habari kutoka, na anko Steve kutukemea, na yeye kuondoka, Polisi waliingia hapa na kuanza kutafuta habari za mzee, ambapo walitusomba wote baada ya kuwaambia hatujui alipo mzee, wenyewe wakisema tunawaongopea.
Kituoni tulilazimika kusema ukweli ambapo tuliachiwa baada ya kuandika maelezo. Nyakati za jioni polisi walikuja tena kutaka kuongea na mama lakini mlango wake ulikuwa bado umefungwa kitu kilichotufanya tuhisi kuwa kama mama hakutoka wakati sisi tulipokuwa polisi; basi atakuwa bado amelala.
“Chumba chake kiko wapi?”
“Kile pale! Lakini huwa haruhusu kabisa kuamshwa, anaweza kutufukuza kazi, mama ni mkali sana!”
“Hatawafukuza!” Samsoni akawatia moyo akiinuka na kwenda kuukabili mlango. Akaugonga mara kadhaa bila jibu. Akarudi nyuma na kuurukia kwa miguu yote miwili. Lilikuwa pigo takatifu. Mlango ukatii na kufunguka na kufanya Samsoni atue ndani.
Kile alichokihofia ndicho kilichokuwa. Mama Masurufu alikuwa amefariki kwa risasi ya kichwa. Alilala kwa utulivu juu ya kitanda chake hali dimbwi la damu likijitenga pembeni nae juu ya kitanda hicho hicho.
Kushoto kwake kulikuwa na bastola ndogo ambayo Samson alihisi pengine mama Masurufu alikuwa anataka kupambana na Steve muda mfupi kabla ya kifo chake. Samson akachoka.
Mama Masurufu alifanya nini mpaka Steve na Masurufu wake wampe adhabu kali hivi? Akajiuliza asipate jibu. Akatoka nje na kuwapigia simu Polisi. Wakati Polisi wanakuja yeye akatoka nje na kwenda kuyakabili makazi ya Steve ambako mshangao ulikuwa unamsubiri.
Nyumba ya Steve ilijengwa imara na kitu mfano wa zege kama sio chuma. Milango na madirisha yake vilikuwa imara kiasi kwamba pengine ungehitaji silaha mfano wa RPG kufungua. Samson alifanya kila alichoweza kufungua bila mafanikio.
Polisi wakafika na kuichukua maiti ya mama Masurufu baada ya taratibu nyingine kufuatwa. Familia nzima ikasombwa na kupelekwa Polisi ambako walijikuta wakihenyeshwa kwa maswali ambayo majibu yake hawakuyajua.
Samsoni aliendelea kuitafiti nyumba ya Steve mpaka pale alipopokea simu kwamba mmoja wa watu waliotangaza nia ya kugombea urais kupitia chama Tawala alikuwa ameuawa kikatili.
Samsoni akalazimika kuwaita vijana wake wengine wawili ambao aliwataka walinde tu nyumba ya Dk Masurufu na pale watakapomuona Steve amerudi wasimfanye chochote badala yake wampigie simu na atakuja mara moja
Wakakubali, Samsoni akaondoka.
* * *
Leo Profesa Zonga alikuwa tofauti na siku zote.
Uso wote ulikuwa mwekundu na alikuwa akitetemeka kwa hasira huku macho yote ameyatoa kwa namna iliyotisha na kuogofya kabisa, hali msaidizi wake Mwile wa Mwilenga akiwa na kazi ya kuwatuliza waungwana waliopanda kichwani kwa Profesa Zonga na kutishia amani.
“Umefanya makosa Masuuuuh! Makosa makubwa Masurufu. Sasa waungwana wamekasirika wanataka kuitoa roho yangu, wanataka kuangamiza familia Masurufu. Umefanya nini sasa!”Zonga aliendelea kulalamika akitikiswa kwa nguvu.
“Basi waungwana muwasamehe! Ni watoto, wangali wanajifunza bado!” Mwilenga akasihi akimgeukia Dr Masurufu aliyekuwa amejiinamia kwa hofu hali akitetemeka kwa uoga.
“Sema tawire!” Mwilenga akamfokea Masuru kwa sauti kali na kuongeza “Utakufa wewe!”
Masurufu akakurupuka na kubweka “Tawire”
Profesa Zonga akasikitika na kulia. “Sasa mimi nitafanya nini kukusaidia wewe hali umevunja masharti eeh Masurufu?!”
“Tusaidie baba, tumekosa!”
“Haya nipe jini langu!” Profesa Zonga akaomba.
“Jini?” Masurufu akashangaa akiogopa zaidi. Akauliza
“Je, Uliwahi kunipa jini Profesa?”
“Mwileeeh!” Sauti ya Profesa sasa ikawa kama mwangwi!” Mwile akakurupuka na kuanguka kifudifudi mbele ya Zonga!
“Rabaika Sayid yangu!”Akajibu akitetemeka kwa uoga.
“Huyu anaongea kitu gani?”
Mwile akainuka na kumtazama Dk Masurufu kwa jicho kali. Masurufu akazidi kuogopa. Akamwambia akingali amemtumbulia macho. “Hukumbuki kupewa kitu chochote na Sayid yangu?!”
“Kitu.... kitu...!” Dr Masurufu akavuta tafakuri. Hakukumbuka chochote.
“Sikumbuki maulana. Mungu na mtume sikumbuki kabisa!”
Mwile akatikisa kichwa kwa masikitiko kufuatia jibu hili. Akisema, “Siku ile ya kazi ulipovunja nazi sabini kwenye tendegu la mlango hukupewa kitu wewe?”
Ndiyo kwanza akakumbuka! Kwamba baada ya zoezi lile lililomchosha sana, mwisho wa siku alipewa karatasi iliyoandikwa maneno ya kiarabu na kuambiwa ahakikishe anatembea nayo kila anapokwenda ila asiingie nayo chooni wala msikitini na aliweke mbali pindi anapomkaribia mkewe.
“Ile karatasi?”Akauliza kizembe zembe.
“Ndilo jini linaloombwa na Sayid yangu hilo!”
Machozi yakamtoka Masurufu. Ni kweli alikuwa amevunja masharti, siku chache tu toka atoke kwa Profesa alijisahau na kuingia nalo chooni, alipojitahidi kujilinda na hilo, siku nyingine mkewe akambana akajikuta akifanya mapenzi naye hali karatasi hilo limo mfukoni mwake.
Ni kutokea hapo ndipo aliponunua mkebe maaalum akaliweka katika gari na kutembea nayo kila alipokwenda. Ukweli huu ukamfanya aone dunia ikimuinamia hali walimwengu wakimdhihaki na kumkebehi.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nipe jini langu haraka!” Alikuwa Profesa tena kwa makelele.
“Lipo katika gari yangu ambayo ipo nyumbani, toka niliposhikwa na presha sijalitumia tena. Labda nimtume Frank akalilete!”
“Haina haja... Haina haja Masu!! Mwanangu umemtenda na ametoroka. Shida zote hizi anazileta yeye kwa kuwa tu hukuheshimu makubaliano yetu! Umenitenda Masu, Umenitenda Masuuh!” Profesa Zonga akatetemeka na kulia zaidi, Mwile akimpoza hali Dr Masurufu akiomba msamaha.
Ilikuwa ni baadae sana jini lililomtoroka Masurufu lilipokubali kurudi kumsaidia tena Dr Masurufu lakini kwa sharti la kupatiwa lita kumi na tano ya damu ya albino, viganja vitano vya mikono, mikono minne, nyayo mbili na moyo mmoja!
Yalikuwa masharti yaliyomtisha Dr Masurufu kupita kiasi. Ilibakia sentimita chache arejewe na presha tena. Kwa dakika kadhaa aliomboleza akitaka abadilishiwe masharti au atoe fedha badala yake, hakukubaliwa.
“Hapa una mawili tu, “Profesa Zonga alimwambia baadae baada ya mashetani wake kuondoka. Akaendelea, ama utimize masharti uupate urais au uache kiti wangu aitafune familia yako na wewe mwenyewe!”
Yote yalikuwa magumu. Masurufu hakujua afanyeje.
Kikao baina yake na Steve na Frank hakikuwa na matunda ya kujivunia kabisa. “Frank!”Akaita baadae baada ya kuona hawaendi popote. “Itakubidi ushughulikie hili!
Frank akajamba. “Eti… eti nini vile?!!” Hakuamini.
“Ndiyo Frank! There is no way. Jitahidi kadiri ya uwezo wako, mahitaji ya Profesa yapatikane haraka iwezekanavyo ndani ya siku chache tu ikiwezekana tatu tu!”
“Lakini Dokta... lakini!”
“Naelewa unachotaka kusema. Naelewa pengine kuliko unavyotaka nielewe. Lakini kumbuka hakuna lisilowezekana chini ya jua. Usione watu wanakuwa wasemaji wa Ikulu au wanampangia rais cha kufanya, mamlaka hayo hutokana na majukumu kama haya.
Kama unavyojua Steve hawezi kusimamia hili kwa kuwa sio kazi yake, lakini pia baada ya kuwaua wale makachero wa polisi kule hospitali, hatuoni kama ni busara aendelee kuzagaa zagaa mitaani. Mimi pia sitaweza kwa kuwa natafutwa na vyombo vya usalama kujibu tuhuma alizotoa Tengeneza.
Ndio maana nimeomba fursa ya kujificha hapa kwa Profesa Zonga ili aweke mambo sawa ndipo nijitokeze. Nikiwa na waungwana wa Profesa Zonga baada ya kulishughulikia hili vizuri nitajitokeza kifua mbele nikiwa na majibu ya hoja zote, tena majibu timilifu kabisa!”
Akatua kwa muda kuona Frank anayapokeaje maelezo yale. Alipoona kimya akaendelea.
“Hii ni kadi yangu ya ATM, niliamua kuzigawanya kadi hizi kwa ajili ya dharura kama hizi. Humo kuna milioni ya mia moja, neno la siri ni mkakati. Chukua fedha unazoweza, kodi watu unaowataka ili mradi tu zoezi hilo litimie ndani ya siku mbili au tatu.
Kingine unachopaswa kukumbuka ni kuwa maji tumeshayavulia nguo, hatuna budi kuyaoga. Hivyo ni lazima tupambane bila kuinua mikono wala kurudi nyuma. Na ole wao tuitie Tanzania mikononi…!”
Masurufu akahitimisha. Ikawa hotuba iliyomjaza mori na kumtia hamasa Frank. Akapokea kadi ya ATM na kuondoka.
* * *
“Stupid! Stupid! Bastard! Christopher McDonald alilalama kwa sautii kali kiasi cha kuyaumiza masikio ya Steve. Uso ukambadilika na kuwa mwekundu mithili ya papai bivu.
“Nani alimtuma aingie katika siasa za kuchafuana hali anajielewa fika si msafi, ilikuaje aanze ugomvi wa mawe hali nyumba yake ni ya vioo? Sie tulimpa fedha akanunue uongozi yeye kanunua matusi! Shiit!”Aliendelea kulalamika wakati Steve akimueleza hali halisi na karata ya mwisho anayoicheza Masurufu.
“Sikiza Steve!” Alikuwa McDonald kwa hasira mwisho wa maongezi yake na Steve.
“Endelea kuangalia upepo ukoje. Hakikisha humwachi hata hatua moja. Ukiona mambo huku saa nane huku saa tisa, hakikisha unamrejesha mikononi mwetu haraka iwezekanavyo na lazima arejeshe gharama zetu zote! Okay?!”
“Haina shida!”
“Huo Mkakati wake mwingine unauonaje?”
“Wa kutafuta viungo vya Albino?”
‘Ndiyo!”
“Hata mie umenishangaza. Sioni ni vipi damu au viungo vya mtu vinaweza kurekebisha hali hii Ndio maana alipotaka kunishirikisha nikamwambia hiyo siyo kazi iliyonileta!”
“Na huyo anaeishughulikia anaweza kuiendesha vizuri maana isije kuwa mnachota maji kisimani ili kwenda kujaza bahari!”
“Nadhani anaweza. Awali alikuwa na hofu lakini baadae akatuliza akili na kuanza kuitekeleza. Nahisi atafanikiwa. Na unajua nini,huyu mtabiri sijui mnajimu huku anakubalika sana. Ana timu kubwa ya viongozi na watu wengine mashuhuri. Ngoja tuone, pengine atafanikiwa!”
“Katika hilo hakikisha huchezi pata potea Steve!”
“Usihofu bosi, ninajua ninachokifanya!”
Wakaagana.

* * *CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Milioni thelathini alizopewa Emanuel Kuho na Frank John yakiwa ni malipo ya awali zilimchanganya akili, akajifungia ndani akipanga mpango mzima wa kutekeleza matakwa ya Frank. Katika hili alijikuta akisafiri mikoa michache tu kwa kutumia ndege ya kukodi na aliporidhika na uchunguzi wake ndipo alipokuja tena kwa Frank na kuchukua theluthi nyingine ya fedha, tayari kwa utekelezaji.

ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment