.
Simulizi : Mkakati Wa Kuelekea Ikulu
Sehemu Ya Tatu (3)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Faili lako hili hapa bosi!” Sekretari alimwambia Christopher mara tu alipoingia katika ofisi yake na kulitua faili juu ya meza. MacDonald aliinua macho kutoka katika Laptop aliyokuwa ameiinamia muda wote na kumwambia.
“Ahsante Suzane, unaweza kuendelea na shughuli zako!”.
Suzane alisimama kwa heshima, akageuka na kuondoka. Alipogusa kitasa cha mlango tu, MacDonald alimwita tena.
“Beeh!”Akarejea na kusimama tena kwa heshima mbele ya bosi wake. “Suzane?” MacDonald aliita akingali ammeiinamia kompyuta.
“Mie hapa bwana wangu!”
“Ule mpango ulimaliza kuuchapa?”
“Ndio bwana, tena niliutuma kwa barua pepe kwa wana G-8 kama ulivyoamuru. Baadhi wameleta maoni na baadhi wameusifu. Nilikuwa sijafanya hitimisho pale utakapouona na kutoa maoni yako ya mwisho!” “Vizuri!” MacDonald akaendelea kuchapa. “Vizuri sana. Ndio maana nakupenda sana sekretari wangu. Naomba uziprint hizo coments zao na niletee haraka!”
“Nitafanya hivyo!”
“Tena wapigie simu G-8 wote, waambie tuonane mahala palepale pa siku zote haraka iwezekanavyo. Sawa?”
“Sawa bosi!”
Suzane alipoondoka, MacDonald aliinua faili alilolileta Suzane na kuanza kulipekua. Alilipekua kwa haraka huku akinakili baadhi ya vitu kadhaa pembeni kwa kalamu.
Alifanya hivi mpaka alipofika kwenye ukurasa fulani ambao aliutazama kwa makini kabla hajaachia tabasamu la haja lililofanya sura yake iwe na mng’ao wa aina yake. Tabasamu hili liliendelea kwa muda kadiri alivyozama katika kuusoma ukurasa wa faili lile. Mara kadhaa, tabasamu lilikomaa sana hata akakaribia kucheka kabisa, lakini hakucheka. Kutoka hapo aligeukia Laptop akataipu kidogo kabla ya kile alichokitaka kufunguka. Ilikuwa ni tovuti mpya. Tovuti ya Steven Lawrence Marvin.
Ni wakati anasoma taarifa za Steven katika tovuti hii ndipo alipogundua mtu huyu alikuwa muhimu kwao kwa kiasi gani. Alikuwa na habari nzuri hasa, nzuri alizozihitaji MacDonald.
Suzane aliingia tena kuleta alichotumwa na bosi wake pamwe na kutoa taarifa kwamba akina G-8 walikuwa njiani. MacDonald akamshukuru, Suzie akaondoka.
Alipomaliza, akageukia maoni ya wenzake ambayo yalikuwa na uzuri usiochusha, wenzake walipofika walimkuta amekwishamaliza kuyapanga maoni yake vizuri. Na sasa alimwita Suzie kwa ajili ya kufanya hitimisho.
Kwa takribani saa moja na nusu, MacDonald na wenzake walikuwa wakiwajadili vijana watatu wenye sura, rangi na mionekano tofauti kutoka mabara kama sio mataifa mbalimbali ya Ulaya.
Kila mmoja alikuwa amechukuliwa kwa namna yake, maelezo yake yakachujwa na kuhifadhiwa katika faili la siri la Christopher. Huu ukiwa mwanzo, MacDonald alihakikisha anakutana na kila mmoja, akazungumza nae na kupima uelewa wake, halafu akampa jaribio na matokeo ya majaribio haya, ikawa ni makubaliano ya kuingia mikataba na watu hawa kwa matarajio ya kuwatumia baadae.

Katika vijana hao wanne alikuwemo Wallace George. Huyu alikuwa raia wa New Zealand. Mrefu kiasi, mnene wa kadiri mwenye mwanya mzuri ambao daima uliwaumiza wanawake kila alipotabasamu.
Huyu mbali ya ujuzi wake wa karate na kungfu, pia alikuwa hodari wa kujipenyeza mahala, kutega bomu na kuondoka pasipo kujulikana. Ingawa alikuwa mweupe pee, uwezo wake wa kiakili na kule kule kuweza kwake kujibadili kwa kwa kuvaa nguo zinazofanana na aendako, kulimfanya apoteze jina lake la Wallace na Kinyonga kuchukua nafasi yake.
Ukiacha huyu kulikuwa na William Peter. Miaka yake arobaini na moja ilikuwa amemtoa kabisa katika ujana ingawa sura na mwili wake pamoja na ule mtindo wake wa unyoaji ndevu vilimfanya aonekane kijana wa miaka kati ya ishirini na sita na thelathini na nne. Mama yake alikuwa na asili ya Japani wakati baba alikuwa mzungu wa Uingereza.
Huyu alikuwa mkali wa judo na kumchezea shere adui yake hata akachoka kabla hajatimiza lengo. Mara nyingi alikuwa akiwafanyia hili maadui zake, akawachosha kwa hila, na walipochoka na kumpuuza ndipo nae alipofanya vitu vyake! Ilikuwa aghalabu sana kwa willy kushindwa kutekeleza mipango aliyotumwa kufanya. Ni rekodi hii iliyomfanya atumwe na Mataifa mbalimbali katika kutekeleza mipango ya siri.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Halafu alikuwepo Steven Lawrance! Huyu alikuwa mbantu haswaa kwa kuwa wazazi wake wote wawili walikuwa wamerekani wenye asili ya kiafrika. Kutokuwa na uhakika wa chakula, ubaguzi wa rangi na umasikini uliochusha na kuudhi vilikuwa vimemsukuma katika mkondo hasi wa maisha. Mkondo uliomfanya akulie katika maisha duni hujaona, maisha ambayo yaligeuka na kuwa ya uchokoraa pale wazazi wake walipofariki mmoja baada ya mwingine wakiwa wameachiana hatua ya miaka miwili miwili.
Akajikuta akijilea mwenyewe kwa ushauri toka kwa watoto machokoraa wenzake waliokuwa wakiishi katika vitongoji mbalimbali katika jiji la New York walijipatia chochote toka kwa yeyote. Katika malezi haya alijikuta akithamini vitu viwili tu, chakula na starehe. Starehe ya wanawake na pombe.
Haikumchukua muda kugundua kuwa chakula na starehe ambavyo daima huwa havikopwi visingeliweza kupatikana bila fedha. Na fedha hawakuwa nazo wakajingiza katika wizi na udokozi.
Mara nyingi walifanikiwa. Zile siku kadhaa walizoangukia katika mikono ya raia wenye hasira walijikuta wakichezea kipigo cha haja kilichowafanya waone umuhimu wa kujifunza sanaa ya mapigano, wakajifunza.
Ni katika wakati huu kipawa cha Steven kilipoonekana. Alikuwa na upeo wa hali ya juu. Aliyafuata maelekezo ya walimu wake barabara, mazoezi ya nadharia yakafanyika katika kule Gym wakati ya vitendo alifanya katika mitaa mbalimbali ama katika mikusanyiko ya mapigano.
Matokeo ya mazoezi haya yakawa ni jina lake kujulikana huku polisi wakimtafuta kwa udi na uvumba. Staili yake ya kupiga mapigo mazito ya kushtukia ilimfanya awe anaua kama mchezo.
Halafu akakamatwa na kufungwa katika lile gereza la Guantanamo.
Gerezani alikutana na mateso ya kila namna. Mateso ambayo badala ya kumfunza awe raia mwema, yalimfanya awe katili zaidi huku mikasa ya aina kwa aina waliyokuwa nayo wafungwa wenzake ikichangia kumfanya awe zaidi ya nduli.
Adhabu zikamkomaza, mateso yakamjenga. Chuki yake dhidi ya binadamu na ulimwengu ikashamiri, haja yake ya kupata fedha ili afanye starehe nayo ikashika hatamu, huku akipanga kutoroka katika gereza hilo mara tu upenyo utakapopatikana.
Hakufaulu kutoroka, alitoroshwa!
Genge la MAFIA lililokuwa limesikia sifa zake lilifanya kila njia hadi kumtorosha. Kazi kadhaa alizopewa badae ambazo alizifanya bila ufanisi wa maana ndizo zilizopelekea kiongozi wa Mafia wakati ule ambaye alifahamika kwa jina moja tu la Biggie aamue kumuendeleza.
Alimpeleka katika shule za hali ya juu za karate, kung fu, kick boxing na judo. Alipofuzu akampelekea katika majeshi yao ya siri ambako alijifunza ukomandoo ambako pia alifuzu vizuri sana. Akawa na shabaha hujaona.
Hitimisho ikawa ni kupelekwa mashirika mbalimbali ya kijasusi ambao kulikuwa na marafiki zake, huko alijifunza ujasusi wa kiwango kilichowafanya hata walimu wake wamuhusudu na kumng’ang’ania. Kutoka hapo akarejea katika kundi lake la Mafia na kuanza kuihangaisha Serikali ya Marekani na washirika wake. Wakawa wakifanya vitu watakavyo kana kwamba walikuwa wamejitangazia uhuru wa Taifa lao dogo ndani Marekani.
Uhalifu wao haukuishia ndani ya Marekani pekee, Walivuka mipaka mpaka Asia, Ulaya na Afrika ambako MAFIA ilikuwa na maslahi. Chini ya uratibu wa Steven Lawrence, hakuna mpango walioupanga ukashindwa.
Hili likamfanya Steve pia kutimiza azma yake ya kupata fedha na starehe. Alistarehe haswaa huku utanashati wake wa mavazi ya heshima, suti za kaunda, suruali za vitambaa na vingine vikimtofautisha na wenzake wengi.
Ilikuwa ni baada ya Biggie kufariki na Bill Clintoni kuingia madarakani hali akiwa na ukwasi wa maana ndipo Steven alipotundika bastola na kuamua kustaafu! Mara chache alitumiwa na watu wenye mahitaji kama ya MacDonald kwa malipo manono kwa kazi maalumu na alipozimaliza kazi zao alirejea kuwa raia mwema.
Mwisho wa kikao, MacDonald na wenzake walikubaliana kumtumia Steven Lawrence Marvin kama mlinzi wa Daktari Masurufu. Hii ilikuwa baada ya kuzichambua na kuridhika na sifa zake. Ule ubantu wa Steve ukiwa sababu nyingine.
Siku chache baadae MacDonald alikutana na steve na kuingia nae mkataba. Kazi za Steve zilikuwa chache tu kuhakikisha anaumwaga ubongo wa yeyote anayetishia kutofanikiwa kwa harakati za Dokta Masurufu. Kumvunja shingo ikibidi na mgongo yeyote anayejitia kumjua jua sana Masurufu kwa lengo la kumkwamisha. Jukumu kubwa zaidi ilikuwa Steve kuwapa taarifa hasa za hali halisi inavyoendelea.
Akina MacDonald hawakuwa wajinga, walijua Dokta Masurufu ni Mtanzania, anakwenda kuonana na watanzania wenzake kwa ajili ya Tanzania yao. Hujui wataongea nini na ndani hasa ya mioyo yao kuna nini. Uzalendo unaweza kuwashinda nguvu nao wakajikuta wakikusaliti ukawa umepoteza nguvu, fedha na muda!
Hivyo mbali ya kupokea taarifa za maendeleo na utekelezaji wa mkakati wao toka kwa Masurufu mwenyewe, pia walitaka wapokee taarifa nyingine kutoka kwa Steven ili kuona kama Masurufu hafanyi hila. Na katika hili waliazimia kumuamuru Steve amuue Dokta Masurufu kama kungelikuwa na hila yeyote.
Halafu wakampa theluthi ya malipo ya Awali. Yalikuwa malipo ya kutakakata yaliomfanya Steve aahidi kufanya kazi hiyo kwa moyo wake wote. Theluthi mbili akiahidiwa kupewa pengine na zaidi kama atalisimamia zoezi vizuri.
Kilichofuata baadae ni kumkadidhi Steve kwa Dokta Masurufu.
“Huyu atakuwa mlinzi wako!” Alimwambia siku chache kabla ya Masurufu kuondoka.
“Wow!” Masurufu alifurahia akimshika mkono MacDonald “Nashukuru sana. Umefikiria kitu muhimu sana. Rais mtarajiwa ana maadui wengi ati?!” Wakacheka
“Lakini vipi uwezo wake?”
MacDonld akatabasamu. “Hauna shaka. Katika watu tulionao huyu ni the best, na zaidi ni mbantu mwenzio tunaamini hatapata shida kujichanganya na wabantu wenzie. Ukiwa na shida yeyote mueleze nae atatatua katika namna itakayokufurahisha. Shida yeyote isipokuwa ya kifedha sawa?
“Sawa!”
Ikawa hivyo. MacDonald akaondoka. Steve akaanza kazi hapo hapo. Akamfunga Dokta Masurufu vifungo vizuri, akakagua na kusafisha ofisi, akakagua gari yake na vingine vingi. Baadae akakaa nae na kumuhoji maswali machache kuhusu mpangilio wa ratiba yake kwa siku, nyumbani kwake huko Tanzania na mengine mengi.
Masurufu alimueleza yote kwa moyo mkunjufu.
“Vizuri!” Steve alisema baadae kwa kiswahili akiifunga laptop yake. “Nimeingiza utaratibu huu katika programu zangu ambazo wakati mwingine hufanya kazi bila ya mimi kuwepo! Tafadhali usibadili utaratibu huu bila kunijulisha!”
Masurufu akashangaa “Unajua kiswahili? Tena kizuri hivi umejifunzia wapi?”
“Niliwahi kufanya kazi Congo enzi zile ikitwa Zaire chini ya Mobutu Seseseko kuku Ngbedu wa Zabanga. Kule ndiko nilikopata hamu ya kujua lugha hii. Hata hivyo nilijifunza China sio siri lugha yetu ni nzuri sana!”Akahitimisha kwa kusifu.
“Ahsante! Na je, Congo ulikwenda kufanya nini?”
Steve akatabasamu. Akajibu “Kazi ndogo tu ya kumtoa Mobutu madarakani na kumweka Kabila!”
“Kumbe?” Masurufu akashangaa kiasi akiogopa.
“Ndiyo !” Steve akajibu. Ukapita ukimya wa muda. Steve akauvunja kwa kumuuliza. “Kwa hiyo tumeelewana?”
“Kuhusu utaratibu?”
“Ndiyo!”
“Nimekuelewa, ila sidhani kama nikiwa nyumbani Tanzania nitaweza kuufuata utaratibu kama nilivyojiwekea. Siunajua wagombea urais taratibu na ratiba zao hupangwa na wapambe?”
“Najua! Tukifika huko tutapanga zaidi na kujipanga upya. Muhimu ni taarifa tu baina yangu na wewe!’
“Haina shida!” Masurufu alikubali.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Steve akaondoka.
Akiwa ameyaacha maelezo yale palepale ofisini, Masurufu alishangaa alipojikuta anapigiwa simu usiku na Steve na kuambiwa.
“Kuna kitu hakipo sawa bosi!”
“Kitu gani?” Masurufu akauliza kwa mshangao akijikagua.
“Hujaenda kuudurusu mpango wako na wakati huu umelala kwenye kochi badala ya kitandani!”
“Ni kweli!” Masurufu akakubali akishangaa Steve amejuaje hali hawakuwa wanaishi pamoja. Akaongeza “Nilichoka mno baada ya mizunguko mingi ya kutwa nzima ya leo!”
“Nilikwambia taarifa ni muhimu bosi!”
“Kumradhi Steve!”
“Usijali. Usiku Mwema!”
“Kwako pia!”
Wakaagana. Masurufu akaingia ndani. Kabla ya kulala Masurufu alipekuwa kila mahali kuona kama kulikuwa na kamera mahali au kitu kingine chochote kinachosafirisha muenendo wake kwa Steve, hakukiona.
Hii ilijiri kwa kuwa hakuwahi kumleta Steven hapo nyumbani kwake. Alipochoka alipanda kitandani, akamkuta mkewe Glady akimsubiri, wakafanya mapenzi ya kutosha. Walipotosheka, walianza kumjadili MacDonald, Steve na baadae safari yao ya Tanzania kabla hawajalala.
Alipofika ofisini kesho yake, alimkuta Steve ameshafika tayari. Wakasalimiana kwa bashasha kabla ya Steve hajamuliza Masurufu swali jingine! “Jana usiku ulikuwa ukitafuta nini?”
Masurufu akatoa macho “What? Unasemaje Steve?”
“Unaelewa vizuri sana ninachokisema!”
Masurufu akatabasamu na kuangalia chini kwa aibu. Atakuwa ameona pia nilivyokuwa nikifanya mapenzi na Glady! Akawaza kwa uoga na hasira. Sasa ulinzi gani huu unaoninyima hata faragha? Hata hivyo alijirudi pale alipogundua kuwa yeye ni mtaka cha uvunguni. Hana budi kuinama. Bila kujibu chochote akamuacha Steve akitabasamu kwa ushindi, akaingia ofisini kwake na kuchapa kazi.
SURA YA TANO
DAR ES SALAAM – FEBRUARY 2005
Ilikuwa asubuhi njema kwa kila hali. Asubuhi yenye afya kama kawaida ya jiji la Dar es salaamu. Tayari miale ya jua ambayo awali alikuwa ya dhahabu, ilikuwa imeanza kuikumbatia ardhi baada ya hekaheka za kuibusu zilizoanza toka alfajiri kumalizika.
Haliwi kumbatio la faraja hata kidogo. Lile joto lake ambalo awali lilikuwa na vuguvugu lililoufariji mwili hata kuufanya ulitamani milele, sasa lilikuwa kali lililouchoma sio mwili pekee bali hata ardhi na vyote na vyote ilivyobeba na kuifanya ardhi ianze kuzalisha miale ya kujitetea na adha ya makali ya jua.
Kama ilivyo ada jiji lilikuwa limeanza kuchangamka. Watu walikuwa katika pilika pilika za maisha yao ya kila siku pengine kwa ajili yakujitafutia mkate wao wa kila siku. Harakati hizi zingeweza kulinganishwa na harakati za siafu wafanyao kazi kwa bidii kila mmoja kwa namna yake bila usimamizi maalumu.
Katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zamani DIA, hali ilikuwa hivi. Watu walikuwa wengi sana. Sare zao za chama zilizobeba picha ya Dokta Masurufu Hussein Masurufu, vibendera vidogo vya mikono na bendera kubwa kwa pamoja viliufanya uwanja wote kuakisi rangi mbili maridhawa, kijani na njano.
Vile vikundi vya sanaa ambavyo wakati huu vilikuwa vikitumbuiza kwa ngoma za asili, vikundi vya matarumbeta, ngoma za asili, ngongoti na Brass Band kwa pamoja viliendelea kupafanya uwanjani hapo kuwa na uhai zaidi kuliko eneo lolote hapo kipawa.
Ukiacha hawa walikuwepo waandishi wa habari kutoka karibu vyombo vyote vya habari vikichukua tukio hili la kihistoria. Redio moja na Televisheni mbili zikirusha matukio haya moja kwa moja kutoka hapo uwanjani, Live! Hawa mbali ya kuwa walikuwa wamewekewa eneo lao maalum ili waweze kupata kila kitu kwa ubora unaotakiwa, bado kila wakati waliliacha eneo lao na kujichanganya na watu, kwa lengo la kupata hili na lile.
Upande mwingine wa uwanja walikuwepo vigogo wa chama ambao hawakuwa maarufu na pengine mashuhuri katika vyombo vya habari. Hawa walikaa na watu wengine wa nyota tano ambao walishindwa kulivumilia baridi lililomo katika vyumba vyao vya VIP pale Air port na kuja kuangalia shamra shamra hizi za kurejea kwa Dokta Masurufu.
Kona nyingine walikuwemo mabalozi wa nchi anuai ambao walikuwa wameombwa kushiriki na kukubali. Hawa waliketi sambamba na mawaziri kadhaa ambao kwa makusudi walikuwa wameondoa nia zao za kushiriki katika kinyang`anyiro hicho ili wampe nguvu Dokta kwa matarajio ya kupata vyeo nyeti zaidi wakati Masurufu atakapokuwa rais wa nchi hii.

Kona ya mwisho walikuwepo wazee wa chama waliopigania uhuru. Hawa walikuwa wamemuona Masurufu kama chaguo pekee kwa kule kuwa miongoni mwa vijana waliolelewa na Mwalimu. Miongoni mwa hawa alikuwepo baba yake Kapteni Husein Masurufu!
Muda si muda mvumo wa ndege ulianza kusikika hewani na kuwafanya watu wainue nyuso zao na kuangalia juu. Picha ya ndege ndogo ikawalaki. Jinsi ilivyokuwa haikuwa rahisi kugundua ni ndege ya aina gani.
Kadiri muda ulivyokuwa ukienda ndivyo ndege ile ilivyozidi kuikaribia ardhi, taaswira yake ikiongezeka na kuwa kubwa hali iliyowafanya watu waanze kuitambua. Maandishi madogo Gulf Air ways SHT-511 yakaonekana ubavuni na kuwavutia wengi kwa namna yalivyotengenezwa kwa namna ya kuvutia kabisa.
Dakika chache baadae ndege hiyo ndogo ya kukodi yenye uwezo wa kuchukua watu thelathini ilikuwa ikisota na kutafuta parking kandokando ya uwanja, sio mbali sana na pale walipokuwa wakitumbuiza Brass Band.
Ndege iliposimama tu, haraka wale waheshimiwa walisogea na kuweka mstari mmoja mnyofu ambao vigogo kama sio vingunge aina kwa aina walijipanga kati yake. Vikundi vya burudani, ngongoti na vinginevyo vilikaribia kujivunja viuno kwa kucheza.
Mlango wa ndege ukafunguliwa, watu wakaanza kutoka mmoja baada ya mwingine. Dokta Masurufu alikuwa watano kushuka akifuatiwa na mkewe na Steven.
Mara tu alipochomoza uwanja mzima ukalipuka kwa vigelegele. Rais…Rais…Rais! Akasimama mlangoni tabasamu paana likiupamba usowe, akainua mkono na kuwapungia waliokuja kumpokea. Shangwe zikazidi, hali wapiga picha wakipigana vikumbo kutaka kupata picha bora zaidi.
Sekunde kadhaa zikayoyoma akiwa amesimama katika lango la ndege, halafu akaanza kushuka ngazi. Aliposhuka chini vijana wa skauti wakamfuata na kumvisha skafu na shada la maua, halafu akaenda katika mstari wa vigogo na kuanza kuwasalimu mmoja baada ya mwingine.
Wapo waliomkumbatia, waliomuombea dua, waliompongeza kwa uamuzi wake na kumwambia tuko nyuma yako. Basi kila mmoja alimwambia lake. Kutoka hapo aliangalia sanaa kidogo, akajibu maswali ya wanahabari kwa ufupi sana, kabla hajajifungia katika chumba cha VIP pale uwanjani na kuteta na wazee wa chama. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alipotoka safari iliishia New Afrika hotel ambako wazee wa mkoa wa Dar es salaam na vitongoji vyake walikusanyika. Ni hapo alipotangaza nia yake ya kugombea wadhifa huo mkubwa kabisa katika nchi na sababu zake, kwamba alikuwa ameamua kugombea awapeleke watanzania katika nchi ya maziwa na asali.
Kwamba ilikuwa ni aibu kwa watanzania kuwa masikini na kutegemea misaada wakati ni miongoni mwa nchi tajiri kabisa duniani. Yeye alitaka kutumia utajiri kuongeza pato la wananchi ili iwe walau dola tano kwa siku tofauti na chini ya dola moja kwa sasa, pamoja na kukuza uchumi wanchi na thamani ya shilingi ya Tanzania.
Alisema chini ya utawala wake, wabadhirifu wa mali wa mali za umma na mafisadi wataadhibiwa na kufilisiwa, ataboresha huduma ya afya kwa mama na mtoto ili kupunguza vifo vya uzazi, ataongeza shule na kuboresha kiwango cha taaluma ili wahitimu waweze kuingia vizuri katika soko la ushindani wa ajira.
Vitu kama ajira kwa vijana, miundo mbinu, mazingira, mifumuko ya bei, kilimo cha kutegemea mvua, ukosefu wa soko la uhakika wa mazao na bidhaa za kitanzania, aliwahakikishia kuwa vinaweza kupatiwa ufumbuzi baada tu ya kuleta mjadala wa kitaifa, amabao utawashirikisha watanzania wote na kuwapa fursa ya kushiriki kwa vitendo katika kugawanya rasilimali za taifa kwa usawa na kuamua zielekezwe sekta gani kukabili changamoto za kimaisha.
Alidai muundo wa Bajeti ya serikali yake utaanzia chini na kupanda juu na angehakikisha kila mtanzania anashiriki na daima angeheshimu mawazo hayo kwa kurudisha Bajeti hiyo kama ilivyo na kamwe asingepokea vipaumbele kutoka Benki ya Dunia, Shirika la fedha duniani, Shirika la biashara ulimwenguni pamoja na Umoja wa nchi nane tajiri zaidi duniani.
Kwa ujumla hotuba yake ya kutangaza nia ilikuwa nzuri iliyomvuta kila mmoja. MacDonald alikuwa ameiandaa vizuri sana baada ya kutafiti mahitaji halisi ya watanzania.
Mwisho wa kikao, kila mzee alipewa posho ya nauli ya shilingi tano, hali waandishi wa habari wakipewa shilingi milioni moja kila mmoja.
Wakati huu Masurufu hakusahau kuwaomba wamuunge mkono na kupigania kwa kila hali nae atawawezesha kila patakapokuwa na tukio. Wazee na waandishi kwa pamoja walimuahidi Masurufu sio tu kumpa zaidi ya ushirikiano pekee, bali na kumuunga mkono pia.
Kwa kutumia ndege ileile ya kukodi Dokta Masurufu na timu yake, vingunge adhaa wa chama pamoja na waandishi wa wahabari walisafiri pamoja mpaka Dodoma ambako Dokta Masurufu alichukua fomu ya chama ya kuomba kuteuliwa kugombea urais kwa Katibu mkuu wa chama na kulipa shilingi milioni mbili!
* * *
Siku ya pili magazeti yote yalibeba habari za Dokta Masurufu kwa uzito wa pekee. Baada ya Redio, Televisheni na mitandao kuzionyesha katika namna ivutiayo. Ni Masurufu tu nabii anayekubalika kwao! Lilinadi gazeti moja.
Hatimaye nuru ya mafanikio imeng’aa Tanzania, Masurufu kuipeleka nchi katika maziwa na asali! Lilidai gazeti jingine. Mkombozi aja! Hili liliripuka kwa maandishi mazito meusi na kufuatiwa na vichwa vingine vidogovidogo. Ni Dokta Masurufu Hussein aliyezaliwa na mpigania uhuru na kulelewa na mwalimu. Amewahi kuwa mbunge na waziri. Ripoti yake ya uadilifu inatisha. Hotuba yake yawaliza wazee wa Dar es salaam. Hili lilikuwa gazeti jingine.
Dokta Christopher MacDonald aliendelea kuzitazama habari hizi kwa furaha na matumaini makuu.“Umekuwa mwanzo mzuri, mwanzo wa kuitwaa Tanzania na kuiweka mikononi mwangu! Hatimaye...” Aliwaza kwa furaha akiipitia tena ripoti ya awali kutoka kwa Steve. Kila kitu kilikuwa shwari, mambo yanakwenda kama yalivyopangwa na kwamba sasa ilikuwa imeanza ile safari muhimu ya kuwafuata wanachama mia mbili kila mkoa.
Jukumu ambalo walijua watalimaliza kama mzaha. Ni hili lililomfanya ainue simu na kumpigia Dokta Masurufu na kumpongeza kwa kazi nzuri kabla hajamuuliza kama ana tatizo lolote. Masurufu alipojibu hana, Christopher alimtakia kazi njema na kumuagizia mtu mmoja zaidi kwa ajili ya ushauri wakati wa kujaza fomu hiyo ya chama ya kuombea kuteuliwa kuwa mgombea.
Masurufu alikubali tu, Christopher akazidi kufurahi.
* * *
Wakiwa mbioni kumaliza zoezi la kupata wadhamini mia mbili kila mkoa katika mikoa kumi ya Tanzania Bara na miwili ya Tanzania visiwani, na zoezi likiwa linaenda vizuri, ndipo Frank Meneja wake alipomfuata na kumjuza kuwa mambo si shwari kama yanavyoonekana.
Kwamba ulikuwa umepangwa mkakati kabambe wa kumwangusha wakati huu wa kura za maoni kwa kumfanyia rafu. Akiwa amefundishwa na Christopher McDonald kutopuuza lolote, Dk Masurufu alijikuta akimkaribisha shushushu huyo Frank John ambaye pia alikuwa Msaidizi wake mkuu.
“Unasema mambo si shwari?” Alimuuliza.
“Ndiyo mkuu, na muda si muda yataharibika kabisa kama hazitachukuliwa hatua madhubuti za kulinusuru hili. John Tengeneza sio mtu mzuri hata kidogo!”
“Huyu Tengeneza ni nani?”
“Ni mmoja wa watu waliotangaza nia ya kugombea urais kwa mwaka huu kupitia chama tawala na kama ulivyo wewe, naye ana nafasi kubwa ya kufanya vizuri?”
“Mie mbona simfahamu vizuri?”
“Mara hii umesahau kuwa umeishi nje ya Tanzania kwa takribani mwongo mmoja na ushei? Tengeneza ni jamaa aliyeibuka siku za karibuni akiwa ndani ya serikali ya awamu ya tatu ambapo amefanya vingi na mengi!”
“Na kuhusu fedha je? anaweza kuwa na fedha kama nilizonazo mie?”
“Hilo siwezi kulisemea. Lakini mpaka mtu ameamua kugombea urais ambacho ni cheo cha juu kabisa nchini, bila shaka atakuwa amejiandaa vya kutosha!” Frank akatua.
Msurufu akainua kichwa na kufikiria.
Moyowe ukianza kupiga kwa hofu. Alikuwa ameelekeza nguvu zake kwa wagombea watatu tu ambao kwao alikuwa na hofu nao. Wagombea hao ni Jakaya Mrisho Kikwete, Salim Ahmed Salim na Frederick Tluway Sumaye walikuwa wamemtisha kutokana na rekodi zao za uongozi na namna walivyotumikia chama, serikali na wananchi.
Hawa alikuwa amewasoma na kuwatambua vya kutosha na tayari alikuwa ameshapata namna ya kuwashinda. Namna ambayo alikuwa na uhakika na mafanikio yake kwa asilimia tisini na tisa kwa moja.
Kuibuka kwa John Tengeneza, kukamfanya akune kichwa mara mbili kufikiria namna ya kumpiku. Kilichomuumiza ni ule ukweli kuwa sasa atakuwa na maadui wanne badala ya watatu wa awali ambao alitakiwa kuwafanyia faulo ili hatimaye mwisho wa siku Halmashauri kuu na kamati kuu ya chama viweze kumpitisha kwa kura zote kuwa mgombea uraisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM.
“Sawa!” Masurufu akapumua baada ya kukosa fikra za maana. Akaendelea. “Turudi kwenye pointi yetu. Tengeneza amefanya nini?”
“Ameandaa mpango wa kukuangusha kwa kupandikiza wadhamini wasio na sifa katika fomu zako za kuomba kudhamin!”
“Kitu gani?” Masurufu akashtuka.
“Ndiyo hivyo. Na tayari amefanikiwa. Robo tatu ya watu waliojitokeza kukudhamini ni feki na yeye anasubiri kikao cha uteuzi tu aweze kukuwekea pingamizi!”
“Mungu wangu!” Masurufu akamudu kutamka. Ukimya ukapita. Ukimya huo uliodumu kwa muda ulivunjwa na Masurufu mwenyewe kwa kuomba aelezwe kwa kina hili limetokeaje!
Frank akamueleza kinagaubaga toka alivyopewa jukumu la kuwa Meneja wa Masurufu, na alivyowajibika kutafuta habari za wapinzani wake ili kupambana nao vizuri, mikakati aliyoweka na namna alivyoweza kujipenyeza katika ngome mbalimbali za waliotarajiwa kuwa wapinzani wa Dk Masurufu ndani ya chama kwa kuwatumia vijana wake ambao alikuwa amewapandikiza huku na huko.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ni mmoja wa vijana wake hao aliyemletea kanda ndogo ya Cassette Tape recorder ambayo alikuwa amepewa na kuingia nayo katika moja ya vikao vya John Tengeneza. Ni baada ya kusikiliza ndipo alipogundua kuwa John alikuwa amefaulu kumtegea watu wasio na sifa wakati akitafuta kudhaminiwa na walikuwa wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kuwa robo tatu ya watu waliomdhamini Dk Masurufu walikuwa watu wao. Ni hapo alipokimbia kwa Dokta Masurufu na kumueleza kila kitu.
“Hiyo tape recorder iko wapi?” Akauliza mwisho wa maelezo ya Frank.
“Hii hapa!” Frank akajibu akiitoa na kumpa.
Masurufu akaipokea, Frank akaaga na kuondoka. Alipofika mlangoni tu Masurufu akamwita tena. “Kuna haja ya kuandaa mkutano mwingine wa wanaumoja haraka iwezekanavyo. Tafadhali waandae wajumbe, ndani ya muda mfupi tu, tuwe tumekutana. Sawa?”
“Hakuna tatizo Mkuu! Nitaandaa na kukujulisha!” Akajibu.
“Vizuri Frank, unaweza kwenda. Ahsante kwa taarifa. Umefanya kazi nzuri sana. Ndio maana nakupenda Frank. Endelea kupambana. Tutakapoiweka nchi mikononi mwetu tutafidia usumbufu wote huu!”
“Usijali Mkuu!Naielewa hali ilivyo!” Akajibu tena na kuondoka
Alipobaki pekee, akaikabili redio yake na kuitumbukiza ile Tape recorder. Alichokisikia kilikaribia kuufanya moyo wake usimame kwa hofu. Alipomaliza, akabonyeza mahala katika meza yake na muda si muda Steve akawa mbele yake, akamwambia bila kumwangalia,

“Niko hapa mkuu!”
“Hali si shwari Steve!”
“Kumezidi kitu gani tena bosi?”
Masurufu akaitwaa ile tape recorder pale mezani na kumpa. Akamwambia, “Kaisikilize kwanza halafu uje tuzungumze!”
Bila kuongeza neno, Steve akaipokea na kupotelea nje kulikokuwa na makazi yenye ofisi yake. Muda mfupi baadae akarejea na akiwa amechoka kama alivyochoka Dk Masurufu awali.
“Nimesikia Mkuu na nimeiona hatari inayotunyemelea! Nasubiri amri yako tu nifanye nini kuzuia hili!”
“Vizuri Steve. Hili ndilo nililokuitia. Yako mengi ya kufanya lakini ningependa tujadiliane kwanza.
“Niko tayari! Nadhani pia kuna umuhimu wa kumjulisha Christopher! Maana hii ni vita, na tayari imeanza. Tunatakiwa kujibu mapigo!” Steve akatua.
“Bado sijamuarifu Chris! Mambo mengine naona kama vile yako ndani ya uwezo wetu. Huyu John Tengeneza tunammudu kabisa! Ni bahati nzuri njama hizi tumezigundua mapema!”
“Nikingali nakusikiliza bado Mkuu!” Alikuwa Steve.
“Nakuja huko. Kwanza nataka utumie uwezo wako kujua yote yaliyo nyuma ya John Tengeneza. Sitapenda auawe kwa kuwa kifo chake kinaweza kufanya uchaguzi usogezwe mbele na hivyo kutuchelewesha zaidi!”
“Una maana gani bosi?
“Nataka kujua udhaifu wake ukoje, ana madhambi kiasi gani, ana shilingi ngapi benki, watu gani anaowategemea kumuwezesha kiuchumi, na kadhalika. Sawa?!”
“Sawa!”
“Jukumu hili lifanyike haraka iwezekanavyo. Yupo Frank, Yule kampeni meneja wangu aliyewezesha Tape record hii kurekodiwa. Yeye atakusaidia kupita pale usipoweza kupita nimaana kukupa taarifa. Yeye pia ana vijana wanaojua mengi ambao wanaweza kukusaidia kwa namna moja au nyingine! Je,” Masurufu Akauliza alipofika mwisho, “Kuna la ziada?
“Hakuna” Steve akajibu. Mwili ukimsisimka. Sasa alikuwa anaingia msambweni rasmi. Masurufu alipoona hana la ziada, akamwambia
“Unaweza kwenda Steve! Nakutegemea sana!”
Steve akaondoka.
* * *
Kikao kilichofuata kilikuwa nyeti na kikubwa kuliko vingi vilivyotangulia. Hiki kilikuwa kimefanyika Dodoma Hotel kwa siri baada ya kufanya uhakiki wa majina ya wadhamini na kugundua kuwa ni kweli kulikuwa na mamluki wasio na sifa waliopandikizwa kwa Dk Masurufu, ili baadae Masurufu awekewe pingamizi na kuondolewa.
Kingine kilichopelekea kikao hiki kuwa nyeti na kikubwa ni ule ukweli waliokuja kuugundua wakati wa uhakiki kuwa Dk Masurufu hakuwa anakubalika sana kwa wanachama wa CCM kama walivyokuwa wamefikiria awali.
Licha ya kwamba tayari walikuwa wamenunua gazeti moja makini pamoja na watendaji wake, kukodi Televisheni mbili na redio mbili pamoja na kupata ahadi ya sapoti kubwa toka magazeti ya udaku na kampuni kubwa za matangazo; Bado Masurufu hakuwa anakubalika sana.
Hili pamoja na lile la wadhamini, yakawa sababu ya kuwepo kama sio umuhimu wa mkutano wa huu kufanyika, ambao kwao ulitarajiwa kuja na mwarobaini wa matatizo yote hayo. Kichwa kiliwauma wajumbe wa kikao hiki, bongo zikachemka, wakaumba na kuumbua vitu mbalimbali ili mwisho wa siku viweze kuwavusha salama katika kikombe hiki cha Uchaguzi Mkuu.
Taarifa ya awali iliyotolewa na Steve haikuwa tofauti sana na ile aliyopewa Frank. Kwamba John Tengeneza alianza mikakati ya kwenda Ikulu mapema zaidi na alikuwa amewekeza mtaji mkubwa kwa wananchi.
Vile alikuwa Mkuu wa polisi na alifanya kazi nzuri sana iliyomvutia kila mmoja kwa kukomesha ujambazi na kudumisha amani na usalama, vile alikuwa kwenye taasisi ya kuzuia rushwa na alikuwa vilevile amefanya kazi nzuri ya kuzuia ufisadi, ubadhirifu wa mali za umma na vile alikuwa na rekodi nzuri za kiutendaji, muadilifu kwa maana halisi, ingemuwia vigumu sana Dr Masurufu kutoa ushindani wa maana kwa Tengeneza pasipo kuingiza hila.
Pamoja na kwamba Steven alikuwa anaendelea kuhakiki uwezo wa Tengeneza kifedha, Masurufu hakutaka kujiongopea kwamba Tengeneza hatokuwa na uwezo huo kwa sababu kama ameweza kumpachikia mamluki na kuwasambaza katika baadhi ya mikoa ya Tanzania, na kama amedhamiria kweli kuutwaa ukuu wa nchi, itakuwa maajabu kama hana fedha za kutosha.
Ni hili lililomtisha na kumuogopesha Dr Masurufu, kwamba anaweza kupoteza muda na fedha na asipate hicho anachokitaka. Alipowafikiria G-8 Original na tishio lao kwake akajikuta akikosa raha kabisa. Ni hapo alipoamua kuitisha kikao hiki cha wanaumoja. Kikao hiki kilikuwa na kazi moja tu, kuzipitia changamoto zilizokuwa mbele yao na kupanga mikakati ya ushindi wa kishindo ndani ya chama.
Wakijadili changamoto hiyo, wajumbe waliona ugumu wa kumkabili Tengeneza. Kila walichofikiria waliona kama hakiwasaidii kwenda mbele badala yake kilikuwa kikiwarudisha nyuma. Wakiwa wamekata tamaa kabisa, ndipo mjumbe mmoja alipokuja na wazo la kumchafua Tengeneza kwa kumpachikia kashfa na kuiandalia ushahidi wa kubuni ambao ungekuwa radhi kuung’ang’ania ukweli huo hata mbele ya vyombo vya habari na mahakama.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kashfa gani, hilo likaachwa mikononi mwa timu ya propaganda.
Kumalizika kwa hili kukafanya waijadili mikakati ya ushindi baada ya chama kumpitisha Dr Masurufu kuwa mgombea wake. Suala la kujiuza lilipewa umuhimu wa kwanza.
Baada ya majadiliano ya kina walikubaliana kuendelea kutafuta vyombo vya habari vinavyoukubalika na kuwanunua watendaji wake, kutengeneza tovuti zitakazokuwa zikiendeleza utafiti wa nani anakubalika zaidi na matokeo yalenge kumpendelea Dr Masurufu.
Mkakati wa kutengeneza fulana za kutosha, kanga, vilemba, vitenge, miamvuli, vishikio vya funguo, mifuniko ya matairi ya magari na vingineyo nayo haikusahaulika. Uandaaji wa vitu kama mchele, chumvi, sukari na mafuta bila kusahau pombe kwa ajili ya kuwarubuni wapiga kura wa vijijini na mjini nao ukapangwa.
Takwimu ya wanaotarajiwa kupiga kura ikafanywa kwa kutumia takwimu za Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufuatia orodha ya watu waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura. Kila mwananchi alitengewa Shilingi elfu ishirini ambazo angepewa kwa awamu tatu.
Awamu mbili za mwanzo, wangepata shilingi elfu tano tano pamoja na kilo za mchele sukari, unga na nusu lita ya pombe za kienyeji. Awamu moja ya mwisho kila mmoja angepata shilingi elfu kumi pamoja na kitenge, mwamvuli au kilemba kwa akina mama. Kofia, vizibao, mabazee ya chama na vuvuzela kwa wanaume.
Wakifanya tathmini ya mwisho wa kikao, Masurufu na wenzie waliona kuwa mkakati huu, na ule wa kuwanunua wajumbe watakaoshiriki kikao cha uteuzi kwa kuwatengea milioni kumi kila mjumbe mmoja ikiwa ni pamoja na kucheza rafu kidogo hapa na pale bila kusahau ule mpango mama wa kuwanunua wagombea wenzake wenye uchumi uliokonda, kwa pamoja utawasaidia kwenda Ikulu kiulaini kabisa.
Walihitimisha kwa kugawana majukumu na fedha na kutakiwa kuwasilisha taarifa za maendeleo ya majukumu yao mara kwa mara kwa Frank John ambaye alikuwa mkuu wao wa kazi na Kampeni Meneja wa Dk Masurufu Hussein Masurufu.
SURA YA SITA
SAMSON KIDUDE
Kutoka kuongea na Inspekta Kimaro, Kamishna wa jeshi la polisi kukawa kama kumeiamsha akili ya Samson Kidude mithili ya betri iliyotolewa chaji. Akiendesha gari yake taratibu aina ya Toyota RAV 4 kutokea hapo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi; Samsoni alijikuta akiwa na mawazo mengi kupita kiasi.
Mawazo yaliyomfanya naye aanze kuutazama uchaguzi huu kwa macho mawili, ule ushabiki wa kawaida akauweka pembeni. Huu ukiwa ni uchaguzi wa tatu wa mfumo wa vyama vingi vya siasa baada ya ule wa kwanza wa mwaka 1995 ambao haukuwa shwari hata kidogo.
Ukafuatiwa na ule wa mwaka 2000 ambapo Benjamin Mkapa alikuwa anamaliza awamu ya pili ya ngwe yake, ambapo akiwa ni rais bado na Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi aliweza kusimamia vyema hata ukamalizika salama salimini.
Huu wa mwaka 2005 ulikuwa mgumu kwa kila hali. Mgumu kwa maana kwamba chama kilikuwa kinaingia katika kura za maoni na baadae uchaguzi mkuu bila yule kinara wake maridhawa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere!
Huu ukiwa na ziada ya kitu kimoja zaidi. Watu wakiwa wameelevuka kupita kiasi. Hawana uoga hata chembe wakikisoa chama, Rais na serikali yake bila hofu. Mafisadi wakiwa wametamalaki kila kona hali kila mwananchi akigeuka na kutaka kuwa mjasiriamali wa kutaka kupata faida tu bila kujali wananchi wenzake, bila kujali kama amepewa dhamana na umma au hajepewa, bila kujali kama ni kiongozi au lah.
Hili pamoja na lile la minong’ono ya fulani kafanya hiki au huyu anatarajia kufanya kile, kwa pamoja vikamfanya Samson Kidude aone kwamba hastahili kukaa na kuamini kuwa hali ni shwari pasipo kuchukua hatua.
Mpaka anafika ofisini kwake Upanga bado alikuwa hajaamua aanze na lipi kati ya mengi ambayo alifikiria kuyafanya. Akaingia na kujitupa nyuma ya meza yake juu ya kiti cha kuzunguka. Muda si mrefu mlango ukagongwa akaingia katibu muhtasi wake na nakala za magazeti. Akayatua juu ya meza ya Samson na kumwambia,
“Magazeti yako hayo hapo. Bila shaka yametimia!”
“Ahsante,” Samson akajibu na kuyaangalia tu kama hayaoni.
“Je?” Assia, Katibu Muhtasi wake akauliza “Ungependa kunywa nini?”
“Mara hii umesahau kinywaji changu? Nikuambie mara ngapi kuwa…!”
“Kumradhi bosi!” Assia akawahi. “Nakuletea!” Akatoka.
Kutoka kwa Assia kukamfanya arejee kuyaangalia magazeti. Kama Rais anashindwa kufanya maamuzi magumu ajiuzulu! Kilinadi kichwa cha habari cha gazeti moja mashuhuri. Kichwa hiki kikamkumbusha Samsoni sakata la kongamano la Mwalimu Nyerere Forum. Wanaosema Rais hawezi kufanya maamuzi magumu ni wehu! liliandika gazeti jingine.
Ukafuatia mlolongo wa majibizano uliochusha na kuudhi. Akaanza kufikiria chanzo cha wazee hawa kutoheshimiana na kutoleana majibu ya hovyo. Alikuwa amemuomba Katibu wake amkusanyie magazeti yote yenye taarifa hizo kwa imani kwamba kulikuwa na chokochoko zilikuwa zikiandaliwa na huu ulikuwa mwanzo tu .
Na alikuwa amefuatilia kwa kiasi na kutogundua lolote la maana zaidi ya hisia tu kuwa baadhi ya maswahiba wa Rais walikuwa wameamua kumzunguka baada ya yeye kutoonyesha msaada wa aina yoyote kwao wakati wa matatizo yao. Zaidi ya hii sababu nyingine iliyotajwa ilikuwa ni ya watu hao kutoingizwa katika madaraka.
Samson hakuona kama hili linaweza kuwa sababu ya amani kutoweka katika kipindi hiki tete cha kuelekea uchaguzi mkuu. Hata hivyo aliamua kuyaitisha tena magazeti haya baada ya yale mazungumzo yake na Inpekta Kimaro ambaye alikuwa na wasiwasi na uchaguzi mkuu.
Muda si muda katibu muhtasi wake Assia akaingia na kumtengea kahawa. Alipoondoka Samsoni akaendelea kuyaperuzi magazeti kwa umakini wa hali ya juu kwa matumaini ya kukutana na kitu kipya. Hakukutana nacho.
Akaanza kuona kama anajipa mzigo wa bure usiokuwa na tija wala mafao!

Ilikuwa ni saa kumi na mbili na dakika ishirini na mbili jioni wakati Dk Masurufu alipopaki gari lake nje ya nyumba ya Profesa Zonga wa Zonga kule Kimara Baruti. Akashuka na kupokelewa kwa bashasha zote baada ya kupiga honi iliyomtambulisha.
“Nimekuja tena Maalim!” Akamwambia mara alipoingia katika ofisi ya Profesa Zonga iliyokuwa juu ya Bangaluu hilo alilomjengea miaka ile ya kisogoni!”
“Karibu Mkuu! Kumezidi kitu gani tena?”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nafasi Mkuu. Toka nitangaze nia maadui wameniandaa na kuitishia kabisa nafasi yangu. Naomba unisaidie, wewe ni tegemeo na kimbilio langu pekee. Nakuomba Profesa!”
Profesa Zonga akachukua karatasi kadhaa, kidau cha wino mwekundu wa zafarani na kipande cha mti. Wakati huo huo akamwita msaidizi wake na kumtaka aandae chetezo na ubani. Msaidizi yule Mwilenga wa Mwile akaandaa vitu upesi upesi.
“Fatiha!” Alikuwa Masurufu baadae akinyunyiza ubani katika chetezo. Moshi ulipoanza kufuka naye akaanza kuandika, huku akitamka maneno aliyoyajua mwenyewe kwa kushirikiana na Mwile. Zoezi hilo lilidumu kwa takribani dakika kumi na tano hivi. Alipomaliza akamwambia.
“Masurufu!”
“Tawire Profesa!”
“Hakuna tatizo!”
“Eti?”
“Umesikia sahihi. Sioni tatizo lolote. Nyota yako ingali inang’aa sana. Bado una nguvu za kutosha kuingia Ikulu bila wasiwasi wowote. Hakuna cha nani wala nani wote nawaona hapa wanakufukuzia kwa mbali kabisa. Na nakuhakikishia hawatakushika.
Uso wa Masurufu ukakunjuka, tabasamu la wastani likatokeza usoni mwake. Akasema.
“Yaweza kuwa kweli. Ila kuna huyu John Tengeneza yaelekea ameshanitengeneza, maana kila ninapokanyaga nakuta ameishapita na kuacha madhara mbele yangu, ndiyo maana nimekimbilia kwako.
Profesa akamtumbulia macho asimuelewe. “Una maana gani Dokta?”
Hapo tena Dokta Masurufu akaeleza yote yaliyofikia baina yake na Tengeneza na namna alivyotaka kumuingiza mkenge wa wadhamini.
“Na wewe umechukua hatua gani?” Profesa Zonga akauliza na kujibiwa. Halafu akafanya tafakari ya kina, kabla hajaliandika tena jina la Tengeneza katika mitambo yake na kuanza kulitengeneza upya!”
“Hana lolote!”Akasema baadae na kuongeza “Waungwana wamethibitisha hivyo!”
“Kweli?”
“Kabisa kabisa. Ila …” Profesa akatua na kupiga funda la kahawa chungu. Masurufu akasimamisha masikio. Profesa akaendelea.“Inatubidi tufanye vitu kadhaa. Kwanza ni tambiko. Hili inabidi likafanyike kwenye milima ya uluguru na Pwani usiku wa kesho na inabidi liambatane na sadaka ya kondoo kumi na tano na mbuzi watano. Lengo la hili itakuwa kupata baraka ya mizimu ya uluguru na pwani na kama unavyojua Ikulu iko Dar es salaam mahala ilipo mizimu hiyo.
Pili inabidi tuififize nyota ya Jonh Tengeneza na wenzake. Hapa tunahitaji ng’ombe fahali mweusi, nazi sabini na moja, vyungu saba , nyembe saba, sindano saba, ndimu saba, chumvi ya mawe na madawa ya kufifiza nyota ambayo yanapatikana Mombasa na bonde la mto Rufiji. Baada ya hapo utakuwa huru kufanya lolote na chochote mpaka utakapokikalia kile kiti cha enzi. Kiti cha nchi!”
“Kuhusu gharama?” Maana sifikirii kama vitu hivyo naweza kuvipata kwa kuwa nina mambo mengi ya kufanya na muda hautoshi kabisa.
“Gharama ya kazi na vifaa haitazidi milioni kumi!”
“Haina shida!” Masurufu akaifungua briefcase yake na kutoa vitabu viwili vya hundi, akaandika hundi mbili kila moja ya milioni tano na kumkabidhi Profesa Zonga.
“Hili tumelimaliza! Je” Akauliza Masurufu, “Kuna jingine?”
“Lipo! Tena hili ni muhimu kupindukia!”
“Lipi tena?”
“Yaelekea mipango yako mingi inaratibiwa na mkeo Glady, siyo?”
“Uko sawa kabisa!”
“Hilo ni kosa. Waungwana hawataki kabisa mambo ya wanawake!” Moyo wa Masurufu ukafanya pah! Hakujua ni vipi anaweza kumweka mbali mkewe katika kipindi hiki ambacho wamekuwa bega kwa bega kuhakikisha kwamba wanaingia Ikulu. Asili ya safari hiyo hata uwezo wa kipesa alionao ukiwa ni juhudi za mkewe kipenzi anayempenda sana!
“Kwanini Profesa?”
“Swali zuri Dokta! Umeuliza vizuri sana. Waungwana wasichopenda kutoka kwa wanawake ni zile damu zao za kila mwezi ambazo sio siri huwa zinawasumbua sana katika kutekeleza mambo yao. Mfano hapa tunatengeneza tambiko kuweka sawa mambo yetu, mkeo akipata hedhi tu kazi yote tuliyofanya inakuwa ni bure. Vivyo hivyo katika kumfunga nyota John Tengeneza!
Masurufu akachoka. Alimjua vizuri sana mkewe, uchakalikaji wake na jinsi alivyo mjenga hoja mzuri na asiyejubali kushindwa kirahisi. Kumwambia tu akae pembeni eti kwa kuwa Profesa Zonga amesema, ingekuwa sawa na kuchokoza mzinga wa nyuki.
“ Kwa… kwa… kwani hakuna njia nyingine Profesa?”
“Haya sio matakwa yangu, Dokta. Mie ni tarishi tu. Wenyewe wapo na wanatoa amri ya kila kinachofanyika!”
“Lakini… lakini…?”
“Unautaka urais au huutaki?”
“Nautaka!”
“Basi kafanye yanayotakiwa kufanywa. Kwa heri!”
Dr. Masurufu akaondoka kinyonge.
* * *
“Kuna simu yako toka Ikulu!”Assia alimwambia Samsoni mara tu alipopokea simu yake. Usingizi ulikuwa umeanza kumnyemelea baada ya mawazo kupigana vikumbo katika kichwa kutafuta jambo ambalo hata yeye hakulijua sawa sawa. Akamuuliza Assia!
“Atakuwa mzee Chilo bila shaka!”
“Ndiyo!”
“Okay, niunganishe!”
“Vipi Samson?” Sauti ya Mzee Chilo ikasikika.
“Salama mkuu, Shikamoo!”
“Marahaba. Ni hivi punde tu nimetoka kuongea na rais na bado ningali katika viunga vya Ikulu. Naomba tuonane katika ofisi ya yangu ya siri iliyopo pale Ubungo Plaza. Yaelekea kukawa na dharura!”
“Sawa mkuu!” Samsoni akajibu.
“Okay!” Kwaheri!” Mzee Chilo akaaga na kukata simu.
Naam! Kumekucha sasa! Samson akawaza akitabasamu baada ya kuutua mkonga wa simu chini. Dharura kwake ilimaanisha kazi. Na kazi mpaka unapoona ameingilia mzee Chilo baada ya kufanya kikao baina yake na Rais, haiwezi kuwa kazi ndogo hata kidogo.
Mzee Chilo alikuwa Mkurugenzi Msaidizi wa usalama wa taifa, ambaye alikuwa akiongoza Idara ya ulinzi na usalama wa taifa. Samson kidude ambaye awali alikuwa mwajiriwa wa jeshi la polisi idara ya upelelezi wa makosa ya jinai akiwa na cheo cha Sub Inspekta; hakuwa akimjua kabisa mzee Chilonga Anderson Chilonga almaarufu kama Chilo.
Kumjua kwake kulikuja kama nasibu tu, wakati alipojikuta ameingia katika mkasa mmoja uliohusisha ubadhirifu mkubwa wa mali za umma kupitia kampeni ya kitapeli ya kufua umeme bandia, mkasa ambao uliratibiwa na vigogo wakubwa wakiwemo wa jeshi la polisi ambao kimsingi walikuwa mabosi wake.
Samsoni angali anakumbuka vizuri sana kuwa ufuatiliaji wa mkasa ule ambao mwanafasihi Hussein ameuandikia kitabu na kukiita Nipe Roho Yako ulimfanya aponee chupuchupu baada ya kugundua uozo mkubwa uliokuwa ukilipeleka taifa katika hujuma nzito ambayo ingeiingiza taifa katika machafuko.
Hujuma hizo ambazo zilipelekea Rais kuwatimua kazi wakuu wa usalama, maafisa wa jeshi la polisi na wasaidizi wao, pia zilipelekea Rais kuvunja Baraza la wasaidizi wake baada ya kumfuta kazi waziri wa umeme na madini. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ni baada ya matokeo hayo ndipo alipoanza kuwindwa auwawe, na suluhisho likawa ni yeye kuacha kazi ya upolisi na kuanza kuishi kwa kujificha. Mambo yalipotulia akajitokeza akiwa mfanyabiashara. Biashara ambazo ziliwafanya viongozi waliosalia katika kadhia hiyo kuacha kumuwinda baada ya kumpa onyo zito wakiamini hatokuwa tishio tena kwao.
Akiwa katika hali hii, Samsoni Kidude alijikuta akiachama pale alipokuja kuchukuliwa na kupelekwa ikulu, ambapo Rais na Mkurugenzi wa usalama wa taifa walikuwa wakimsubiri. Huko alitakiwa kueleza sababu ya kuacha kazi hali taifa likihitaji mchango wake.
Ikiwa nafasi aliyoililia muda mrefu, Samson alimueleza Rais kinagaubaga wa yale aliyogundua na ulafi uliomo miongoni mwa watu wanaolisimamia jeshi la polisi. Akamuhakikishia kwamba hatoweza kurudi kazini asilani labda kwa mtindo mwingine.
Baada ya majadiliano ya kina ndipo ilipokubaliwa Samson arejee kazini kwa siri machoni pia wengine akiwa Mfanyabiashara na raia wa kawaida. Afanye kazi zake kwa uhuru na mtindo atakaoona unafaa na akiwa na tatizo amuone mzee Chilonga ambaye atakuwa mshauri na kiongozi wake, Nao wanaweza kuripoti moja kwa ima kwa Mkuu wa usalama wa Taifa au Rais mwenyewe. Hatua hii ilifuatiwa na vigogo wachache waliosalia katika kadhia ile ambao walikuwa wamempa onyo Samson, nao kukamatwa na kufunguliwa mashtaka.
Katika hili Samson aliruhusiwa pia kuwatumia watu alioona wanafaa ili kufanikisha mipango yake, kitengo chake ambacho kiliitwa maalum kikitengewa bajeti ya kutosha toka Usalama wa Taifa.
Ridhaa ya haya toka Ikulu ndiyo iliyomfanya afungue ofisi yake pale Upanga na akamuajiri mrembo Assia Khalifa mwenye ziada ya akili na maarifa kuwa sio tu katibu Mhutasi wake, bali pia mlinzi na msiri wake. Kabla ya Ofisi kuanza kazi, alipelekwa nje ya nchi alikojifunza zaidi ya ujasusi na ukomandoo.
Naam! Alikuwa na haki ya kusema kumekucha. Chilonga huwa hamwiti bure. Hii itakuwa mara ya pili baada ya ile ya mwanzo ambapo mwito wake ulimuingiza katika sakata jingine zito lililoitwa EPA, Eleza Pesa Alipozificha! Sakata ambalo mbali ya kumfanya ayaweke rehani maisha yake mara kadhaa na kunusurika katika dakika za lala salama; pia sakata hilo lilikuwa limemuachia mke mzuri sana, Shuwena Mhasibu Jamaldin!
Mazungumzo yake na Chilo yalikuwa mafupi tu.
Kwamba nchi ilikuwa inaingia katika jaribio lingine la kihistoria.
Jaribio la Uchaguzi pasipo baba wa Taifa. Wenye hila na chokocho tayari wamekaa macho juu wakisubiria kuona litakalotokea. Wengine wakitamani kuona amani na utulivu tuliodumu nao kwa takribani miaka arobaini na tano sasa inatoweka na kuwa kinyume chake.
Manyang’au, mafisadi na waroho wa mali za umma wameanza kutupa karata zao kuhakikisha wanavuna. Haya pamoja na ile hofu ya Inspekta Kimaro ambayo aliifikisha kwa Mnadhimu Mkuu, nae akaitupa kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi aliyeitua kwa Rais na Rais kuirudisha kwa Chilonga, kwa pamoja viliwajulisha kuwa hawapaswi kulala tena.
“Rais ameruhusu kutumia kila rasilimali tunayoitaka!” Chilo akahitimisha.
“Hakuna shida, mwambie asiwe na wasiwasi, Tutajitahidi kadiri ya uwezo wetu na mambo yatakuwa shwari tu, midhali haya yamefika mapema sioni kama kuna shida tena!” Samson akajibu.
Likaondokea kuwa jibu lililompa faraja Mzee Chilonga Anderson.

Masurufu aliingia kwake akiwa na unyonge ule ule. Juhudi za kuuondosha na kujivika uchangamfu bandia zilikuwa zimekwama mithili ya jitihada za mlevi chakari anayejitahidi asipepesuke mbele za watu anaowaheshimu.
Mkewe alimgundua mapema tu na kuanza kuhoji sababu!
“Hakuna kitu!” Masurufu alikuwa amemjibu hivi mara kadhaa huku akijivika uchangamfu ambao nao haukukawia kumtoroka. Mara kadhaa alijikuta amemsahau mkewe na kuzama katika dimbwi la mawazo akivuta fikara.
“Masurufu!” Mkewe alimwita tena.
“Naam!”
“Unajua unanishangaza unapoendelea kung’ang’ania hakuna kitu hali mwili, akili na roho yako vikikusaliti!” Akamtazama vizuri “Una nini wewe? Enhe? Hebu niambie Sweetie wangu!”
Hatia zikamuelemea Masurufu. Akashindwa kumuangalia Glady usoni.
“Unajua kama mficha maradhi kifo humuumbua?” Lilikuwa swali linguine la mkewe.
“ Najua!” Akajibu kwa moyo mzito.
“Na unajua kama mchuma janga hula na wa kwao?”
“Sikiliza mama Rose!” Masurufu akashindwa kuvumilia. “Huna haja ya kunihimiza kwa misemo na methali kama mtoto wa shule ya msingi. Mie ni mtu mzima. Najua hicho unachokihofia zaidi ya unavyotaka kufikiria. Nimekwambia mara zote hakuna kitu mpenzi wangu. Sijawahi kukudanganya na sitakaa nije nikudanganye!”
“Lakinii!” Mkewe akapoa. “Body Language inakusaliti mume wangu. Kama kuna tatizo niambie, kumbuka mimi ni kila kitu kwako!”
“Sio nikumbuke tu. Bali najua fika. Kwamba wewe ni kila kitu kwangu. Hebu niamini basi kuwa mabadiliko yangu haya ni hali ya kawaida tu!”
“Mh! Sawa dia!” Mkewe akakubali
“Aksante kwa kunielewa.”
Ukapita ukimya mfupi.
“Baba Rose!” Mkewe akaita tena na kuuvunja ukimya
“Rebeka Laaziz!”
“Leo uliniaga kwamba unakwenda kwa Profesa Zonga!”
Moyo wa Masurufu ukapiga kite kwa nguvu. Kite kilichoambatana na mshituko mdogo ambao Glady aliuona sawia. Akajifanya kama hajaona kitu na kuendelea. “Ila hujaniambia kilichojiri, tafadhali naomba uniambie basi!”
“Profesa kasema hakuna tatizo kabisa, Tengeneza sio tishio na ametutaka tuendelee na mipango yetu kama tulivyoipanga!”
Kitu fulani kikamfanya Glady au mama Rose ahisi kuwepo kwa walakini katika sentensi hii. Hata hivyo kwa kuwa alishamuona mumewe na kugundua kuwa kuna kitu anachokificha, Glady hakuendelea na maswali zaidi.
Hata changamoto alizokutana nazo katika jukumu la kuanzisha asasi ya kuwasaida wanawake kama wake wengine wa marasi waliotangulia, yakiwa ni maandalizi ya kuwa First Lady, akawa amesahau kumueleza mumewe huyu Dokta Masurufu.
Badala yake alijikuta akishika majukumu halisi kama mama nyumbani na mwisho wa yote akajikuta ameanguka kitandani chini ya mumewe. Hata baada ya kufanya mapenzi ya kina, bado Dr Masurufu hakuwa tayari kumueleza mkewe chanzo cha kupotea kwa furaha yake na kuingiwa na unyonge.
Siku ya pili usiku kwa kutumia kwa kutumia ndege ya kukodi walikuwa katika Chinole katika milima ya Uluguru wakifanya tambiko. Mizimu iliwahakikishia tena baada ya kunywa damu ya kutosha kuwa hakuna kitachomzuia Dr Masurufu kuingia Ikulu.
Maelezo ya mizimu, mazingira ya maeneo yenyewe pamoja na mtikisiko aliokuwa nao Profesa Zonga kwa pamoja vilimhakikisha kuwa nchi ilikuwa yake kwa kila hali.
Masikini laiti angelijua kuwa kuna mtu alitangulizwa kule msituni kisha mti mkubwa ukapasuliwa na yeye kuingizwa ndani yake ili aongee kama mzimu…!CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kumalizika kwa zoezi hilo kulifuatiwa na zoezi jingine zito la kufifiza nyota ya John Tengeneza na wenzake siku ya pili yake. Hili lilifanyikia Kerege Bagamoyo. lilikuwa zoezi fupi lililochukua wastani wa masaa matatu hivi ambapo Dr Masurufu aliogeshwa, kisomo kikasomwa, ngo’mbe mweusi akachinjwa Masurufu akaruka damu yake na kichwa kikazikwa chini, ndani ya kinywa cha kichwa hicho kukiwa na majina ya wabaya wote wa Dokta Masurufu.
Zoezi hili lilifuatiwa na uvunjaji wa nazi sabini na moja uliofanywa na Masurufu mwenyewe! Ukaangaji wa nyembe, sindano, na chumvi ya mawe na vingine vingi. Mpaka shughuli inakwisha, moyo wa Masurufu ulikuwa kwaatu kabisa, aliamini kuwa safari ya Ikulu sasa imeiva barabara!.
Ambacho hakukijua ni kwamba miongoni mwa wapambe wake aliowaamini na kuambatana nao kila mahali, mmoja alikuwa akimpelekea habari zote mkewe Glady Stevenson Ombwe!
* * *
ITAENDELEA

0 comments:
Post a Comment