Search This Blog

Sunday, 22 May 2022

TAALUMA ILIYOPOTEA - 5

 





    Simulizi : Taaluma Iliyopotea

    Sehemu Ya Tano (5)



    Tulishuka uwanja wa ndege wa Jomo Kenyata, na kuondoka haraka kuelekea Thika, tulipofika pale ilikuwa tayari inaelekea mida ya usiku, tulishuka na pale tukapelekwa kwenye nyumba Fulani ambayo hatukuifahamu, nilikuwa nina uwoga lakini nilipomtazama Beatrice alionekana kuwa haogopi kitu.

    “Karibuni sana, msiogope kila kitu kitaanzia hapa” aliongea yule kijana na kufungua mlango ilia atoke nje.

    “Hujatuambia jina lako” nilimuambia huku nikimtazama alikokuwa akielekea.

    “naitwa Hussein, hilo ni swali la mwisho kuniuliza kwasasa, mnavyokuwa hamnifahamu vizuri inakuwa salama zaidi kwenu” alijibu na kuondoka.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “mpango wenu ni nini?” aliuliza Beatrice.

    “tunakwenda kumuokoa Frank kama nilivyokuambia” nilimjibu huku nikiendelea kuvuta pumzi.

    “naelewa ila ninachotaka kujua ni je, mna fahamu alipo kabisa?” aliuliza Beatrice aliyeonekana sasa kuona kama kukaa pale ni kupoteza muda.

    “sijui ila kwenye kikao pale walisema ni wapi barua hiyo ilipotokea kwakuwa ilikuwa na muhuri wa ofisi za EMS za sehemu hiyo” nilimjibu huku nikinyanyuka na kwenda dirishani kuangalia wapi Hussein alielekea.

    “na huyu kijana umemjuaje” aliuliza tena.

    “simjui vizuri lakini yeye ni rafiki wa kijana aliyenisaidia kabla”, nilimjibu na hapo akili yangu ilirudi nyuma na kuanza kumkumbuka Haleed, nikajikuta nimeduwaa pale dirishani ila nilishtuliwa na sauti ya mlango uliokuwa ukifunguliwa. Aliingia Hussein akiwa na kijana mwingine mmoja aliyeonekana kuwa na asili ya kisomali.

    “huyu anaitwa Twalib, ni rafiki yangu na hivyo kwasasa ni rafiki yenu pia, yeye ni mtaalamu wa mambo ya ramani na alikuwa rubani wa ndege za kivita nchini Somalia kabla ya kuacha kazi, atawafundisha namna ya kutumia GPS na ramani, mimi nitatoka na muda si mrefu nitarejea, tutaanza safari masaa miwili kuanzia sasa, hivyo mna masaa miwili ya kujifunza vitu vingi na kuelewa, tunachokifanya ni hatari, hivyo uelewa wako wa unachoelekezwa ndio utakao kuweka mbali na hatari, weka masikio yako na akili yako kwenye maelekezo, uliza kama huelewi, usipoelewa unasogeza maisha ya Frank karibu na mdomo wa bunduki” alimaliza na kuondoka kisha nilisikia wakiongea na Twalib alirudi pale tulipokuwa.

    “nifateni huku” aliongea kingereza chenye lafudhi ya kisomali na kutoka pale kisha tulimfata, ile nyumba ilikuwa porini kiasi na kulikuwa na giza mule ndani, alituchukua kisha akafungua mlango mmoja wa chuma tukaingia ndani na yeye aliwasha taa, kilikuwa ni chumba kikubwa kama darasa, kulikuwa na kompyuta na vifaa vingine ambavyo sikuvifahamu.

    “hii ni sehemu ya kufunzia watu juu ya mafunzo ya jiografia, satellite, ramani na maswala ya anga, nilitengeneza hii sehemu na nilikuwa nikifundisha vijana wengi waliotaka kusomea urubani kwa siri” alianza kueleza huku akiwasha kifaa kilichokuwa mbele yake.

    “kwanini iwe ni kwasiri” Beatrice aliuliza.

    “Kwakuwa ni hatari” alijibu na kuanza kutufundisha.

    “GPS, inakusaidia kujua ulipo au sehemu unayotaka kwenda, sasa kwenye hili mnaloenda kufanya mtatumia simu na si kifaa chenye ili iwe rahisi kwenu, (huku akitugawia simu), hizo ni sumsung android zenye GPS tayari, sasa ukiifungua hapo kwakuwa hatuna muda sana utaanza kutafuta sehemu uliyopo au ile unayotaka kwenda kupitia kiboksi cha chini hapo kwenye kioo cha simu, wakati huo intanet itakuwa inafanya kazi ya kutafuta kupitia ‘google map’ na baadaye itakupatia sehemu uliyoitafuta, ukiikuza itazidi kukupa maeneo yaliyopo kwenye eneo hilo ulilokuza….” Somo liliendelea pale kwa muda wa nusu saa na tulikuwa tumeshamaliza, tulielewa vizuri sana na muda mfupi aliingia Hussein pale ndani.

    “kila mmoja ameelewa?” aliuliza Hussein huku akinywa maji aliyokuja nayo pale, na sisi tulitingisha kichwa kuashiria kuwa tulielewa.

    “tumebakiwa na lisaa limoja na dakika 20 tu, hatuna muda wa kupoteza, naomba nifateni” aliongea Hussein na kuelekea sebuleni pale kisha tulimfata, alisukuma lile kochi pale sebuleni na kuvuta lile kapeti kubwa zito mpaka alipoona kitu kama mfuniko mkubwa wa chuma, tuliona akiingiza funguo na kuungua kisha ulianza kufunguka taratibu kisha alianza kuingia yeye kwa ngazi iliyokuwa ikionekana pale, Twalib alikuja na kutupa tochi ndogo kisha na sisi tulishuka kwa zamu, sikuwa na uelewa wa hata kilichokuwa kikiendelea pale ila nilifanya kwakuwa kila kitu kilifanika katika jina la ‘okoa Frank’, tulipofika kule chini kulikuwa na giza nene na kulikuwa kunatisha, hewa ilikuwa nzito sana na kulikuwa na joto la hatari na harufu ya ubani ilisikika kwa mbali. Hussein alikwenda mpaka mbele kidogo na kuwasha taa, mwanga ulitawala pale ndani na tulisikia pia hewa nzuri ikianza kupajaza pale ndani, ilikuwa ni kiyoyozi kikitupa faraja ya muda.

    “zoezi hili litachukua nusu saa tu, kanuni ni ileile, ukishindwa kuelewa kwa wakati ujue unamsogeza Frank kwenye mdomo wa bunduki” alituambia huku akitutazama kwa makini, kisha alitusogeza karibu na meza iliyokuwa nyuma yetu.

    “tuna muda wa nusu saa wa kujifunza kuhusu bastola na kuitumia, kwanza lazima ujue kanuni za matumizi ya bastola,,1. Unatakiwa mar azote uielekeze kwenye sehemu salama kama umeishika, usiielekeze katika upande ambao ikitokea ikafyatuka italeta madhara au kuwafanya watu washtuke. 2. Usiweke kidole chako kwenye ‘trigger’ (kitufe cha kuruhusu risasi itoke) mpaka uwe tayari kwa kulenga na 3. Usiiziruhusu risasi zikae kwenye njia yake mpaka uwe tayari kwa kuitumia.. hizo ndizo kanuni tatu za msingi, lakini kwa hili la kwetu, mda wote kidole kiwe karibu na ‘trigger’ pale tutakapofika sehemu ya hatari,” nilikuwa naogopa sana lakini niliuficha woga wangu, Beatrice alionekana kuwa makini na siye hata na chembe ya woga, tulianza kufundishwa namna ya kushika bastola na namna ya kutembea tukiwa tumeishika, namna ya kunyata, jinsi ya kujaza risasi na mwisho tuliingia kwenye kulenga ambapo tuliingizwa kwenye chumba maalumu kilichokuwa na sehemu za kulengea shabaha, ilipotimia nusu saa tuliachana na zoezi hilo na tayari tulikuwa na uelewa kiasi japo bado kuna vitu nilikuwa sielewi lakini nilijua nitaelewa mbeleni.

    Tuliondoka pale chini na kurudi mpaka juu sebuleni kisha tulionyeshwa sehemu ya kuoga na tulipomaliza Hussein alituatia hijab mpya mbili na kutuambia kuwa hayo ndiyo mavazi tukatayovaa, lakini kwa ndani alituambia tuvae suruali za jeans alizokuwa nazo ameleta na flana nyingine, kabla ya kuvaa hijabu hizo alituvalisha kama kikoti kingine alichotuambia kuwa ni ‘bullet broof’ kwaajili ya kuzuia risasi ukipigwa isiingie ndani ya mwili, mambo yote haya yalikuwa mageni kwangu kwakuwa sikuwa nina uhakika kama nitaweza, nilifahamu kabisa kuwa ile ilikuwa ni safari yangu ya kifo lakini bado ilinilazimu kuijaribu.

    “Beatrice utachukua hii bastola, inaitwa Colt M1911, ni nzito ila nyepesi wakati unapiga, tayari ina risasi na kuikoki ni kama tulivyoelekezana, Natasha wewe utachukua hii hapa inaitwa Jericho 941, ni nyepesi, tayari inarisasi, zote mtazichomeka kiunoni nyuma, pia simu zenu ziwe kwenye mifuko yenu, na zisizimwe” aliongea na kuanza kutuweka vitu flani masikioni ambavyo sikuvijua ni nini.

    “haloo, mnanisikia?” aliongea Hussein na tulimsikia kupitia vile vidude alivyotuwekea masikioni. Tuliitikia na yeye alihakikisha kuwa tulimsikia. Alinyanyua simu na kupiga akiwa anaongea na mtu mwingine ambaye mda mfupi alikuja pale akiwa na mifuko mikubwa miwili.

    “huyu anaitwa Sandra, atakuwa na sisi kwenye safari yetu, yeye ni dereva, na hiyo kwnye mifuko ni chakula, fanyeni haraka mle hapo kwa dakika kumi tuanze safari” aliongea Hussein na kuondoka pale, kwa mbali pembeni nilisikia wakiongea kuwa walipungukiwa na pesa kiasi Fulani.

    “Hussein” nilimuita na yeye alikuja.

    “nilikuja na pesa kiasi cha kutosha” nilimueleza huku nikifungua begi langu dogo.

    “sasa kwani umeshazibadilisha?” aliniuliza.

    “ndio nilibadilishi mda mfupi nilipofika pale uwanja wa ndege” nilimuambia na kutoa kiasi cha pesa, kisha nilimpatia yeye na kingine nilimpa Beatrice na mimi kubakiwa na kiasi kingine, waliondoka pale na yule dada kisha muda mfupi Hussein alirudi pale akatuambia tufunge macho kisha aliomba dua na sasa tuliondoka na kuingia kwenye gari, saa zetu zilionyesha ilikuwa ni saa tano kasoro usiku na maeneo ya pale hayakuwa na taa wala mwanga zaidi ya ule wa gari.

    “Sandra yuko wapi” aliuliza Beatrice.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “ametangulia tutamkuta mbele huko” aliongea Hussein na kuwasha gari na kwa mwendo wa kasi sana safari ilianza, ilikuwa ni Range Rover ya zamani lakini ilikuwa na kasi ya ajabu, baada ya mwendo kama wa dakika tano hivi tulisimama sehemu na Hussein alishuka, kisha tuliona Sandra akipanda na safari ilianza.

    “Hussein kaenda wapi”, niliuliza kwa namna ya mshangao.

    “ametangulia tuendako” alijibu Sandra na hapo hakuongea tena, alikimbiza gari na baada ya mwendo wa takribani masaa sita tulikuwa katika msitu mkubwa sana. Sandra alituambia tushuke na kila mmoja awe tayari na bastola yake mkononi, hofu ilinijaa sana na sikujua inakuwaje pale, nilianza kutetemeka lakini suti ya Hussein ilijirudia ndani yangu ‘mnapokosea ndo mnamuweka Frank karibu na mdomo wa bunduki’, nilijikaza na hapo alituambia tuvue zile hijab na kubaki na suruali na sisi tulifanya hivyo, kisha alianza kutuongoza njia taratibu.

    “sikilizeni, woga hakuna hapa, leo nyie ni wanajeshi haijalishi ni kina nani mlikuwa, Beatrice utaenda njia hii (huku akionyesha njia iliyoonekana pembeni yake), mimi nitaenda mbele na Natasha utakaa hapa uangalie kama kuna mtu anakuja, msizitumie bastola zenu mpaka ikibidi, taarifa zote ni kwa sauti ya chini, mkiongea kila mmoja atamsikia mwenzake hivyo hakuna haja ya kupayuka, ukimuona mtu kama hana mwelekeo wa kukudhuru na hajakuona, muache apite” aliongea Sandra na wao waliondoka, nilikaa pale kimya nikijiegemeza kwenye mti na kuanza kulia taratibu, ilikuwa ni hatari ambayo sikuwahi kuiwaza, baada ya muda wa kama dakika kumi nilisikia kupitia vile vidude vya masikioni sauti ya Sandra akiniambia niwashe gari na kuelekea upande walioelekea wao, nilirudi kwenye gari na kuwasha gari, wakati naondoka nilisikia mngurumo mkubwa na nilipotaka kuondoka kitu kikubwa kiliruka na kuangukia mbele ya kioo cha gari kisha mngurumo uliendelea, nilipotazama kwa makini niliona vitu kama meno marefu na hapo niligundua kuwa ulikuwa ni mdomo wa samba, niliendelea kukanyaga mafupa huku mapigo ya moyo yakienda mbio lakini sikufika popote nilisikia gari likigonga mti kwakuwa aliniziba nisione mbele, mkojo ulikuwa ushanitoka na sasa nilianza kulia, niliangalia bastola yangu sikuiona pale kiunoni nikakumbuka wakati napanda kwenye gari niliirushia kiti cha nyuma, nilijaribu kurudisha gari nyuma lakini ilikwama kwenye tope, nilijaribu kuongea ili wanisikie lakini kile kidude cha masikioni kilikuwa kimedongoka, yule simba alizidi kupiga kelele na wengine walianza kuja na kulizunguka gari, kioo cha kiti cha nyuma kilikuwa wazi kwa nusu na simba mmoja alikuwa akijaribu kupenyeza kichwa chake, sikujua nini cha kufanya zaidi ya kupiga makelele ambayo hata hivyo yalizidiwa na kelele zile za wale simba, nilitazama pale pembeni kulikuwa na kisu, ujasiri ulinijia nikabeba kile kisu na kumchoma jichoni yule simba aliyekuwa akipenyeza kichwa chake na hapo nilikuwa kama nimewachokoza, katika maisha yangu sikuwahi kuota kilichokuwa kikienda kunitokea pale, simba wale waliendelea kukwaruza vile vioo na kufanikiwa kutoa mipira iliyokuwa ikishikilia vile vioo, nilibinua kiti taratibu na kuinama kuiokota ile bastola kwenye kitu cha nyuma;

    “ngriiiii” nilisikia sauti nyuma yangu na nilipogeuka nilikuta nguo yangu imeshikiliwa na ukucha wa mguu wa simba aliyepenyeza miguu yake, sikuwa na namna zaidi ya kuanza kuomba mungu kwakuwa kama ningegeuka ilikuwa akamate nywele zangu na kunichomoa kupitia ule uwazi wa mlango wa kiti cha nyuma, nilishaifikia na kuishika bastola yangu ila sikuwa na jinsi ya kuitumia, nilijivuta kwenda mbele wakati bado nimeinama lakini bado nilikuwa navutwa kwenye kioo, na sasa niliishiwa nguvu na kile kioo pale kikavunjika kisha alinikamata na kuingiza kichwa ndani, niligeuka haraka na sikujua ilikuwaje ila nilijikuta nimefyatua risasi na yule simba aliniachia, nilikaa nikajibanza huku nimekaa nikiwaangalia wale wengine lakini nilisikia mlio wa bunduki na hapo niliona wakikimbia huku wengine wakidondoka pale, wakati nashangaa ni nini kimetokea, malango wa gari nilisikia ukifunguliwa hapo nilifyatua risasi bila kujua kisha nilisikia kitu kikidondoka, nilifungua mlango taratibu na kumkuta Hussein akiwa chini, ndipo nilipojua kuwa nilimpiga yeye risasi, nilichukua simu yangu na kubonyeza namba moja kisha nilimpata Beatrice kwenye simu;

    “Mbona huji tunakusubiri huku” aliongea Beatrice na huku nikiwa kwenye sauti ya kutetemeka niliwaeleza kilichotokea, kama muda wa dakika kumi walifika pale.

    “shika hii” Sandra alinikabidhi bastola yake na kuanza kumuangalia Hussein, alichomoa kitu kama kipakiti kidogo na kumuwekea puani kisha Hussein alishtuka. Wote tulivuta pumzi na kukaa chini, Hussein alishtuka na kuamka kisha alifungua shati lake;

    “kuweni makini tutauana wenyewe aisee” aliongea Hussein na kuvua ile ‘bullet proof’, tuliisukuma ila gari na kufanikiwa kuichomoa pale. Kisha safari ilianza, nilikuwa bado nikilia kichinichini huku nimemlalia Beatrice, Hussein alikuwa kiti cha mbele akiendelea kusoma ile ramani na Sandra alikuwa akiendesha huku akimtania Hussein kuwa kama sio ile Bullet Proof angekuwa marehemu, nilichogundua kwa muda ule ni kuwa Hussein na Sandra walikuwa ni wapenzi, kwakuwa muda mwingi Sandra aliokuwa akimwangalia Hussein alikuwa alimuangalia katika namna iliyoashiria hivyo, kilichonisumbua kichwa ni maswali mengi kuhusu wao na kwanini walihatarisha maisha yao ili wamtafute Frank.

    “kutoka hapa mpaka hapo sehemu sio mbali na si salama kama tutaenda na gari” nilimsikia Sandra akimueleza Hussein wakati huo walikuwa wamezima taa za gari na gari pia walizima.

    “bai kaeni hapa nisubirini, mimi naenda” aliongea Hussein.

    “hapana nisubirini nyie, nitaenda mimi” aliongea Sandra na kabla hata ya Hussein kujibu Sandra alikuwa ameshashuka na kuanza kukimbia kuelekea huko alikosema, kwa mbali tulisikia sauti ya mbwa wengi wakibweka.

    “Hussein tumfate, hao mbwa watamdhuru” Beatrice aliongea.

    “hapana atakuwa salama usijali ana uzoefu” aliongea Hussein kwa sauti iliyojaa ujasiri, kisha alikuwa makini kuangalia kule alikokuwa akielekea Sandra, baada ya dakika kama kumi Sandra alirudi pale akiwa na mzee mmoja aliyekuwa akionekana kama mmasai, walipopanda kwenye gari walisalimiana na Hussein na hapo alianza kuulizwa maswali.

    “Frank unamjuaje?” lilikuwa swali la kwanza toka kwa Hussein.

    “simfahamu Frank, namfahamu Shadrack, alipokuja huku alibadilishwa jina na kuitwa Shadrack” aliongea yule mzee.

    “alikuja kufanya nini” nilimuuliza.

    “hapana usijibu hilo swali” Hussein alimwambia yule mzee na yeye hakunijibu kitu.

    “Hussein nina haki ya kujua mambo yanayomuhusu Frank” nilimuambia huku nikilia.

    “hatujaja kujua habari za alichokuwa anafanya Frank, tumekuja kumtafuta Frank, maswali ya kuuliza yatahusu alipo na kama mtu anamjua, tukifanikiwa kumpata yeye atakueleza alichokuwa akifanya huku” aliongea Hussein na wakati huo mimi nilikuwa bado nikitokwa na machozi.

    “Natasha njoo chini” aliongea Hussein na mimi nilishuka.

    “utajua kila kitu tukimpata Frank, hawa watu hawatashirikiana na sisi kama tutaanza kuhoji shughuli zao” aliniambia Hussein na mimi nilimuelewa na kunyamaza kisha tulirudi kwenye gari.

    “kwaiyo tunampataje Frank” aliuliza Sandra.

    “mtatoka kwenye hili pori na kukamata Garissa road kisha mtakwenda mpaka Dadaab, pale kuna kambi ya siri, ni hatari sana lakini mkifika pale semeni mmetumwa na Gharib Osien, na mnakwenda kuonana na Meja Tom, mkifika pale mtaongea nae na yeye ndiye atakayewaruhusu muonane na Frank” aliongea yule mzee na kushuka. Saa ya mkononi ilionyesha kuwa ilikuwa ni saa 9 kasoro ya usiku, gari liligeuzwa na kuanza kuitafuta barabara ya Garissa, mwendo wa kilomita tano mbele tulianza kusikia sauti za helkopta zikielekea upande ule tulikokuwa tunaelekea sisi, simu ya Hussein ilianza kuita na yeye aliipokea;

    “hallo” aliongea na baada ya mazungumzo ya sekunde chache nilimsikia akiuliza.

    “kwaiyo wao wanauhakika kuwa yupo kwenye iyo kambi?” aliuliza na inaonekana kama vile upande wa pili ulimjibu kuwa ndio.

    “sawa nitahakikisha yuko salama” alikata simu na kuvuta pumzi.

    “kuna nini Hussein” aliuliza Beatrice.

    “wanajeshi wa Kenya pamoja na wale makomandoo wanaelekea huko tuendako” aliongea kwa sauti iliyokuwa inatafuta suluhisho.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mara ghafla gari Sandra alikata kona na kuingia njia nyingine huku akizidi kulikimbiza lile gari.

    “unafanya nini Sandra?” aliuliza Hussein.

    “njia hii kutakuwa kuna ulinzi mbele, naijua njia ya kutokea nyuma ya ile kambi” aliongea na Hussein alikaa kimya, umbali wa zaidi ya kilomita 12 tulisikia mizinga mikubwa ikilia na moto mkubwa uliwaka kwa mbali, tulisimamisha gari pale na kushuhudia ule moto mkubwa, nililia sana baada ya Hussein kuniambia kuwa walikuwa wanelipua ile kambi ambayo ndipo alipokuwa Frank, wakati hayo yakiendelea simu ya Sandra iliita tena. Na baada ya kuongea nao kama dakika kumi hivi bila kusema chochote aliwasha gari na kuondoka kwa kasi ya ajabu.

    “ Frank hayupo kambini, atakuwepo Sild ropper saa 12 asubuhi kukutana na mtu” aliongea Sandra huku akiendesha gari kwa kasi. Alilikimbiza gari sana majira ya saa 11 na nusu tulikuwa tumeshakaribia Sild ropper, tulienda kwa mwendo wa taratibu na tulipofika pale, tuliegesha gari yetu ng’ambo kidogo ya barabara, na majira ya saa 12 na dakika kumi ilikuja defender TDI ya kijivu na kupaki upende wa pili kisha nilimshuhudia Frank akitoka na kuingia ndani ya lile jingo, tulikaa pale nje kwa zaidi ya lisaa lizima ila hakutoka mtu yoyote, Sandra alishuka na kuamua kwenda hadi pale, aliingia ndani ya lile jingo na muda sio mrefu tuliona akitoka huyu amefungwa mikono yote kwa nyuma akisindikizwa na vijana watatu wenye bunduki.

    “tokeni wote kwenye gari shuka chini” aliamuru mmoja wa wale vijana, kisha wote tulishuka chini.

    “hey, sisi sio watu wabaya, tumekuja kumfata Shadrack ni rafiki yetu,” aliongea Hussein

    “Shadrack hana rafiki na hayupo hapa” aliongea mmoja wa wale vijana.

    “ameingia huko ndani na tumemuona” aliendelea kuongea Hussein huku akimsogelea yule kijana, alipomkaribia alimpiga mtama na kumnyang’anya ile silaha kisha alimuweka chini na wale vijana wawili pia.

    “jamani sisi hatutaki tufike mbali, Shadrack yupo kwenye hatari na sisi tumekuja kumtafuta hapa kwakuwa tumemuona” aliongea Hussein.

    “kweli vile Shadrack ameshaondoka hapa na anasafari leo japo hajasema anakwenda wapi” aliongea yule kijana mmoja na Sandra aliondoka na Beatrice kuelekea kule ndani, kisha walitoka nje wakiwa hawana matumaini.

    “itakuwa ni kweli, kuna gari inaonekana imeondoka kupitia uwani mda sio mrefu” aliongea Sandra na wote tuliondoka pale na kwenda kwenye ile gari Frank aliyokuja nayo, baada ya kuikagua Hussein hakukuta chochote, tuliondoka pale na wale vijana walirudi ndani, tuliingia kwenye gari lakini kabla hatujaondoka tuliona vumbi likitimka kwa mbali, Sandra aliwasha gari na kuingia njia nyingine ya vumbi kisha tulienda tulipaki gari kwenye kichaka na kukaa kimya tukiangalia kwa mbali kilichokuwa kikiendelea, zilikuja gar inane pale na wote walikuwa na silaha, wakaizingira ile nyumba na baada ya muda sio tulisikia milio ya risasi na kimya kilitanda kidogo, kisha walitoka wale watu na kuondoka, tuliwasha gari na kuelekea tena kwenye lile eneo. Tulipofika pale Hussein alishuka na kukimbilia kule ndani tena, aliokota yale makasha ya risasi na kurudi nayo, walivyoyatazama alieleza kuwa wale walikuwa ni wale makomandoo waliotumwa, wakati akiyatazama yale makasha pale tulishangaa kuona Sandra akitoa mlio wa maumivu, kioo cha mbele kilikuwa kimetoboka na usoni alitoa damu;

    “Beatrice ruka kiti ya mbele washa gari geuza kuna mtu kule mbele anafyatua risasi kuelekea huku” Beatrice aliruka kiti cha mbele na wakati anageuza gari risasi nyingine ilivunja kioo nikaishuhudia ikipenya kichwani kwa Hussein, nilianza kulia lakini haikusaidia, Beatrice alianza kuliendesha gari kwa kasi na kwa mbali niliangalia nyuma yule mtu alishuka toka juu ya mti na kusimama pale barabarani akiangalia tulikokuwa tukielekea, nilimgusa Sandra na kugundua alikuwa ameshafariki na Hussein pia alikuwa amefariki, sikujua nini kinaanza zaidi ya kulia tu pale. Mbele kidogo tulisimamisha gari na Beatrice alilalia usukani wa gari huku wote tukilia kwa uchungu, ni kama giza lilitanda mbele yetu na hapohapo nilipofuta machozi nilishangaa kuona gari mbele yetu.

    “Beatrice” nilimuita Beatrice na yeye akashtuka alipotazama mbele aliona yule mtu akishuka kwenye gari huku akiwa na bunduki mkononi, aliwasha gari na kukaa bila kufanya chochote huku akimuangalia yule mtu aliyekuwa sasa akikaribia gari tulilokuwepo.

    “Beatrice, geuza gari tunakufa” nilimuambia huku nikilia lakini Beatrice hakusema chochote zaidi ya kutokwa na machozi na jasho, alipiga ishara ya msalaba na kukanyaga mafuta kuelekea kwa yule mtu aliyekuwa mbele ya gari letu na kumgonga kisha gari liliruka na kwenda kupindukia pembeni.

    “Beatrice, Beatrice,,,ooo mungu,,Beatrice please,,usiniache mwenyewe, Beatrice,,,,,” nilimuita Beatrice lakini sikusikia mapigo yake ya moyo tena yakidunda, gari ilikuwa imepinduka na usukani ulimbana kifuani.



    “Kuwa mwanamke/mwanaume ambaye ungependa binti/kijana wako awe nae, kuwa na tabia ya msichana/mvulana ambaye ungependa mwanao amuoe. Kuna muda sisi hufanya vitu ambavyo tusingependa watoto wetu wafanyiwe, hivi umeshajiuliza je ungependa mtoto wako wa kike awe na mtu mwenye tabia kama zako??au mtoto wako awe na msichana kama wako??, unapenda sana kutembea na wamama za watu je ulishajiuliza ungejisikiaje kugundua mama yako anatembea na kijana mwenzio? Unapenda sana kutembea na wababa za watu je itakuwaje mwanao kutembea na wazee unaofanya nao kazi ofisini? Mtawa wa kanisa katoliki aliyejulika kwa jina la mama THEREZA aliwa kusema ‘kama ikitokea kila mtu akafagia eneo lake kila asubuhi basi kila siku dunia nzima itakuwa sadi’…Acha tabia ambazo zinahatarisha uhai wa hadhi yako kwa wanao. KUWA SEHEMU YA MABADILIKO UYATAKAYO…MABADILIKO HUANZA NA WEWE”…HII NI SEHEMU YA KUMI NA TATU,,,ANDIKA HIVI..



    ***FRANK ANAHADITHIA***

    KNT-308 sniper riffle, yenye uwezo wa kulenga umbali wa mita 800, imetengenezwa Turkey na inayouzwa dola za kimarekani elfu 2 sawa na shilingi milioni sita za kitanzania ndiyo silaha niliyokuwa nayo kwenye begi langu. Alichokianzanisha muheshimiwa raisi nilikuwa nakwenda kukimaliza, aliharibu maisha yangu lakini asubuhi ya leo nilipoamka nilipanga kufa na nilipanga kufa nae. Hakuna wa kunikamata, hakuna wa kunizuia, hasira yangu ilikuwa ni kubwa kupita mlango wa pepo, akili mawazo yangu na nafsi yangu vilijaa unyama mtupu na hakuna nilichofikiria zaidi ya kuua.



    **MIEZI KADHAA NYUMA**

    Nilikuwa nchini Kenya ikiwa ni mwezi mzima toka niingie Kenya na kukutana na rafiki yangu wa siku nyingi niliyesoma naye chuo kimoja bwana Charles, nilimueleza kila kitu kilichotokea kwenye maisha yangu na yeye aliniahidi kunipa hifadhi nyumbani kwake, niliishi kwa Charles na kumsaidia biashara zake za kila siku za uuzaji wa vifaa vya magari, yalikuwa maisha ya utumwa sana lakini niliyavumilia mda wote, kwakuwa Charles alikuwa akifanya kazi shirika la umoja wa kimataifa basi kazi nyingi aliniachia mimi nimsaidie lakini aliyekuwa mkurugenzi wa Kampuni yake alikuwa ni Elieth au mama Debra kama alivyojulikana, niliiishi nyumbani kwa Charles kwa muda mfupi lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida nilianza kuchoshwa na vituko vya mama Debra, nakumbuka kuna siku baada ya kufungwa mahesabu yote ya ofisi kwa jioni hiyo hakukuwa na mfanyakazi mwingine kazini na Elieth alinipigia simu kutaka kujua nilipokuwa, nilipomueleza nilikuwa bado kazini alikata simu na muda sio mrefu alifika na kuanza kuuliza kama kulikuwa na wafanyakazi wengine pale ofisini na mimi nilimjibu hapana;

    “Frank kuna jambo nataka unisaidie” alisema Elieth huku akinitazama kama vile alikuwa akisoma fikra zangu, Elieth alikuwa moja kati ya wanawake warembo sana katika jiji la Nairob, alikuwa mweupe na mwenye umbo la kueleweka lakini alikuwa ni kiburi na mwenye misimamo ya kiume.

    “jambo gani shemeji” nilimuuliza huku nikiendelea kukusanya vitu vyangu pale mezani.

    “Frank nakupenda” nilishtuka na kuacha yale makabrasha pale, nilipoinua macho na kumtazama alikuwa ameshafungua vifungo vya ile blauzi aliyokuwa ameivaa, moyoni nilijua nia yake ilikuwa ni kupiga kelele iwapo ningemkatalia, nilimtazama huku nikitabasamu na kumvuta kuelekea kwangu kama vile nilikuwa nikimkumbatia kisha nilishika blauzi yake taratibu na kuanza kuvifunga vifungo vyake huku bado macho yangu alikuwa yakimtazama yeye usoni.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Elieth haya mambo ni kupanga, kwaiyo usijali, tutapanga lakini si vyema kuja hapa ofisini na kuyaleta hayo, zipo sehemu nyingi tunaweza kwenda na kufanya hivyo, vuta subira” nilimuambia hayo huku nikiwa nimeshamaliza kumfunga vifungo kisha nilinyanyua vitu vyangu na kumshika mkono taratibu nikimshauri tuondoke nyumbani naye alikubali tukarudi nyumbani, nilichojifunza pale ni kwamba Charles alikuwa ‘busy’ sana na kazi kiasi cha kumsahau mkewe, na si kwamba Elieth alikuwa amenipenda ila hapna Elieth aliniona mimi mwepesi kupatikana mda wowote mwili wake ukihitaji, alizidi kunisumbua na kila mara nilijitahidi kumpa maneno ya kumpa moyo ajue muda si mrefu nitakubaliana na ombi lake lakini sasa vituko vilizidi na kuna muda alinifata chumbani kwangu akiwa na nguo fupi ya kulalia tu,,sikuwa na hisia na yeye sio tu kwakuwa alikuwa ni mke wa ndoa wa rafiki yangu hapana ila ni kwakuwa nilikuwa na mawazo ambayo hayakuniruhusu kuwaza juu ya mapenzi au kitu chochote. Elieth hakujua kwanini mtu mzima kama mimi niliyepaswa kuwa na familia yangu nije kukaa nyumbani kwao. Yeye alidhani kuwa nilikuwa mfanya kazi tu na alinichukulia hivyo, nilipokuja kwao nilimuomba Charles asimwambie chochote kuhusu maisha yangu kwakuwa sikutaka yeyote afahamu.

    Baada ya vibweka na mitego ya Elieth kunichosha niliamua kuondoka nyumbani kwa Charles na kuacha kazi kwenye Kampuni yake na hapo nilikwenda kupanga sehemu nyingine kabisa mbali na wao, lakini siku moja Elieth alikuja kunifata na hapo sikuwa na namna zaidi ya kumweleza kwanini sina hisia, nakumbuka alilia sana siku hiyo na aliniahidi kuwa asingenisumbua tena, kesho yake alikuja na kunipatia kiasi cha pesa ili nianzishe biashara, hivyo nilianza biashara ya kusafirisha vitu kupeleka Somalia na wiki moja tu nilikutana na Feisal kijana msomi wa kisomali na aliyeamua kuniingiza kwenye kundi la THE PATRIOTS lililokuwa na sera sawa na kundi la Alshabaab, makundi haya miwili yote yaliendesha mafunzo sawa, niliingia kwenye kundi lile nia yangu ikiwa moja tu, kujifunza namna ya kuwa na roho kama ya baba yake Natasha, roho isiyojua utu na thamani ya binadam, roho ya unyama na tama ya madaraka, nilitaka kuwa na roho itakayoondoa ubinadamu wangu na kunipachika nafsi ya chui. Nilipoingia kwenye kundi la the Patriots kitu cha kwanza kujifunza ilikuwa ni uvumilivu wa maumivu, yani kutokutoa siri hata utishiwe maisha yako, kuamini kuwa unaweza kujitoa muhanga kwa jambo ambalo unadhani kuwa linaenda kinyume na maagizo ya mungu, tulifundishwa mafunzo ya ukomandoo na kulenga shabaha, nilikuwa moja ya watu bora kwa kulenga shabaha katika wiki mbili tu niliozoishi pale kambini, nilikuwa silali, kila mara ilikuwa ni muda wa mazoezi kwangu, lakini hakuna hata mmoja aliyejua lengo langu pale zaidi ya Feisal, nilikuwa na hasira na kila nilichokuwa nakifanya, nakumbua kuna kipindi nilipiga ngumi gunia la mchanga likatoboka na hapo ndipo nilipowekewa watu wanichunguze na ya mimi kuja kwenye lile kundi, lakini hakuna aliyeweza kufahamu, nilijifunza mbinu zote za kijasusi kwa muda wa miezi mitatu, na baada ya hapo nilirudi nchini Kenya na kuishi Dadaab nikifanya kazi na watu wa pori hilo kupitisha vitu vya magendo na shughuli nyingine, kila siku nilikuwa nikikimbia kilomita 30 ili kujipanga kwa pumzi, lakini nilikuja kukata tama siku niliyoumwa na kwenda hospitali nikaambiwa kuwa nina ugonjwa uliotokana na maambukizi ya tetenasi na kwasasa nilitakiwa kuwekwa sehemu ya uangalizi wa karibu, ilikuwa ni gharama kubwa lakini pia ndani ya mwili wangu kulikuwa na uvimbe uliofanya damu isipite vizuri kwenye mwili wangu na hii ni kutokana na mlolongo wa kipigo nilichokipata kwenye maisha yangu, afya yangu ilikuwa inadhoofika lakini nilijilazimisha kwa kumeza Dextro energy ambayo ni dawa ya kuongeza nguvu za mwili, baada ya kukaa pale ndipo niliandika waraka kwa rais nikimkumbusha makosa yake na siku ya kifo chake, nilifanikiwa kuwa na rafiki ndani ya majeshi ya Kenya naye alinitaarifu kila kitu juu ya makomandoo wa Tanzania waliotumwa kuja kunitafuta na hivyo niliamua kuondoka nchini Kenya siku hiyo na kuelekea tena Somalia, kitu kilichokuwa kikinicheleweza ilikuwa ni silaha niliyoagiza kutokea Turkey iliyokuwa iingizwe Pwani ya Somalia siku mbili baada ya wale makombandoo kuingia Kenya, nilipoipata niliweka vitu vyangu sawa na kurudi Tanzania, sikuwa nina shida tena na Natasha kwakuwa nilijua kama hakunielewa kipindi nikiwa mwema, asingenielewa muda huu nikiwa mtu mnyama kuliko unyama wenyewe, asingenielewa kwakuwa alishalishwa sumu isiyoweza kutoka ndani ya kichwa chake. Sikutaka kuonana nae kwakuwa ningeweza kubadili akili yangu kitu ambacho sikuwa tayari kitokee, mpaka nilikuwa nina orodha ya watu wawili wa kuwaondoa duniani, wakwanza alikuwa Nicholas, mume wa Natasha ambaye inasemekana ndiye aliyefadhili shughuli ya kuteswa kwangu ili awe na Natasha na mwingine ni baba yake na Natasha amabaye kila niklimfikiria nilikuwa nikiishiwa pumzi, nilitamani nimchemshe supu ili kila nafsi iliyofia mikononi mwake ifurahi, nilikuwa namchukia kuliko kitu chochote, alikuwa ni mzuri wa uso ila ni katili kuliko ukatili wenyewe, kila nilipowaza na kumfikia nilihisi hasira zangu zikigonga mwili wangu mithili ya nyundo ya fundi mwashi.

    Niliondoka nchini Kenya baada ya wale makomandoo kuingia na siku hiyo nilifanikiwa kujipenyeza katika kundi la watalii lililokuwa likipanda Mlima Kilimanjaro kupitia Kenya, baada ya safari ndefu ya mzunguko nilitokea Rombo na hapo nilipanda basi la Meridian Coach tayari kwasafari ya kwenda Dar es Salaam. Mda wote akili yangu ilipanga mazingira ya kuonana na rais kwakuwa lilikuwa ni jambo gumu kuliko kawaida, ulinzi uliimarishwa kila mahali lakini niliamini kwakuwa sikuwa na cha kupoteza basi hakuna pia cha kuogopa, nilijipanga kwa ustadi mkubwa sana kulitikisa jiji na nchi kwa ujumla na mwisho nilipanga kujiua mwenyewe au kujisalimisha polisi ili nikahukumiwe kunyongwa.

    “Abiria wote inueni vichwa vyenu na kama we ni mwanaume umevaa kofia vua” ilikuwa sauti ya askari aliyepita akikagua watu waliokuwa kwenye gari, alikuwa ameshikilia picha kubwa mkononi kwake kwa kwambali niliiona ikiwa na sura yangu lakini nilikuwa sina madevu kama niliyokuwa nayo sasa hivi, nilijiamini na kuvuta pumzi kisha yule askari alinisogelea na kunitazama kwa makini.

    “we mbona kama mnafanana na huyu jambazi” alinisemesha yule askari huku akizidi kunitazama, lakini sikumuongelesha nikajifanya kama vile sikuwa nimemuelewa asemacho. Baada ya ukaguzi huo waliondoka lakini yule askari alionekana kunitilia shaka sana kwani hadi anaondoka alikuwa akinitazama.



    *****

    Safari iliendelea na nilifanikiwa kufika Kibaha maili moja nikashuka na kutafuta nyumba ya kulala wageni, sikutaka kufika kabisa jijini kwakuwa sikuwa nafahamu usalama wa jiji ukoje. Kesho yake niliamka saa 11 asubuhi na kwenda mpaka Dar, nilifika maeneo ya posta saa 12 asubuhi na kununua suti moja nyeusi kisha niliondoka na kwenda mpaka kariakoo ambapo nilionana na kijana mmoja wa kihindi niliyeagizwa kwake na Feisal ili kumpatia kikaratasi ambacho sikujua kilikuwa cha nini, baada ya kumpatia alinipatia kiboksi kidogo;

    “hiki cha nini mimi, huu ujumbe nilipewa siku nyingi sana kabla sijatoka Somalia kwenda Kenya na aliniambia siku nikipanga kuja Tanzania nikuletee hiki kikaratasi, na sina mpango kabisa wa kurudi tena Somalia kwahiyo nakushauri mtumie kwa njia yoyote uwezayo” nilimuambia hayo na kuondoka lakini nilimsikia akiniita, nikasimama na kumsikiliza.

    “Feisal anafahamu kuwa umerudi Tanzania na jana alinipigia simu, akaniambia kuwa utakuja hapa, hichi kikaratasi hakijaandikwa kitu, ni kama utambulisho tu kuwa ni wewe unayetakiwa kuja hapa” aliongea polepolekwa lafudhi ile ya kihindi huku akinitazama usoni kwa macho makali.

    “kwahiyo” nilimuuliza.

    “take this box, open it when you are alone, we do not know each other, I wish you the best of lucky”(chukua hiki kibox ukifungue ukiwa peke yako, mimi na wewe hatujuani na ninakutakia mafanikio mema) alinikabidhi na kuondoka.

    Nilitoka moja kwa moja na kwenda kukodi chumba pale Valley View hotel maeneo ya kariakoo, nilipofika chumbani nilifungua lile boksi na kukuta kitambulisho chenye picha yangu lakini jina lilikuwa tofauti, kilikuwa ni kitambulisho cha kunitambulisha kama afisa wa usalama wa taifa, nilifurahi sana japo sikujua namna ya kufanya. Haraka haraka nilifunga kile chumba na kuondoka kwenda kuelekea Kibaha kufata vitu vyangu vingine nilivyoviacha ili nirudi kuanza kazi.



    *****

    Asubuhi kabisa majira ya saa moja kamili nilikuwa nimeshang’oa kamera zote za nyumba ile nakufanikiwa kuingia sebuleni.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Habari yako ewe mkuu” nilimsalimia wakati akijiandaa kutoka, suti niliyokuwa nimevaa ilimfanya ajue mimi nilikuwa mmoja wa walinzi wake hivyo hakugeuka kunitazama baada ya yeye kuitika. Nilisogea mpaka kwenye jokofu lililokuwa pale sebuleni na kulifungua kisha nilimimina mvinyo kwenye ‘glass’ na kuanza kunywa, wakati huo yeye alikuwa bado akihangaika kufungwa tai yake.

    “nenda hakikisha gari iko sawa nataka kuondoka kwenda kuonana na rais” aliniambia huku akiwa bado amekigeukia kioo, nilisogea mpaka nyuma yake na kusimama kisha nilivua ile kioo na yeye alipoangalia kwenye kioo aliniona na kushtuka, aligeuka haraka na kuiwahi ile bastola yake iliyokuwa juu ya kiti, sikuwa na wasiwasi niligeuka taratibu huku nikinywa ule mvinyo.

    “hahaa, ulikosea sana kuniacha niishi, huwezi tena kuniua kwasasa kwakuwa mimi tayari nimekufa, mimi ni mfu” aliikoki bastola yake na kuninyooshea akiniamuru nilale chini lakini mimi nilisogea tena mpaka kwenye kabati nikachukua glasi nyingine na kuweka mvinyo na kwenye ile ya kwangu niliongeza kisha nikamsogelea na kutaka kumpa ila alirudi nyuma na kubonyeza kile kitufe cha kuruhusu risasi itoke lakini haikutoka, alizidi kukoki lakini wapi haikutoka.

    “ni bora ukaungana na mimi tu kupata mvinyo ndugu Nicholas Mtemvu” nilimsogelea tena na yeye alizidi kutetemeka na kurudi nyuma ili afungue mlango lakini mlango ulikuwa umefungwa.

    “karibu mvinyo Nicholas, huwezi kwenda popote wala kufanya chochote, kwaiyo karibu tuongee” nilimueleza huku nikimtazama usoni, nilikuwa nikimuonyesha tabasamu lililomueleza wazi kuwa nilikuwa nikimaanisha.

    Nyumba ya Nicholas ni ngumu sana kwa mtu kuingia lakini wakati niko Somalia nilifanikiwa kuipata ramani ya nyumba hiyo kupitia kwa Feisal, niliifahamu ile nyumba na mfumo wake wa usalama ulivyo, asubuhi na mapema nilipoamka nilifika pale na kukutana na mlinzi niliyempa karatasi ya kusaini nikijifanya kuwa mtu wa usalama wa taifa niliyetumwa kuleta mzigo wa Nicholas na hivyo alitakiwa asaini yeye kuwa aliupokea ule mzigo, kalamu aliyotumia kusainia ilikuwa ni ya kwangu iliyokuwa imepakwa unga wa madawa ya kulevya yaliyokuwa na sumu kali ambayo kama ikitokea ukainusa mda huohuo unadondoka, alipomaliza kusaini alijishika pua na hapohapo alidondoka na mimi nilimsogeza pembeni taratibu na kumfunga mikono na kumjaza makaratasi mdomoni ili akishtuka asipige kelele akasikika, nilifanya hivyo kwa walinzi wote na kufanikiwa kuingia ndani.



    ***

    Nicholas bado alikuwa akihaha pale sebuleni asijue cha kufanya, mtoto wao hakuwepo siku hiyo aliondoka na msichana wao wa kazi kwenda nyumbani kwa kina Natasha na hiyo ilikuwa ni nafasi nzuri sana kwangu kufanya nitakacho.

    “Nicholas, pesa ina nguvu sana, pesa inaweza kukufanya uwe popote saa yoyote ile, inaweza kukufanya umuoe msichana yoyote yule, uwe na gari lolote lile, inaweza kukupa furaha ya muda mfupi na mrefu, lakini pesa haiwezi kukwamisha hasira za masikini mdhulumiwa” nilimwambia maneno hayo huku nikizunguka, huku na kule pale chumbani, nilikwenda mpaka kwenye kimeza kidogo walipokuwa wameweka picha zao nikachukua ile picha waliyopiga na Natasha siku ya harusi yao, nilihisi kama machozi yakinitoka nilipomtazama Natasha kwenye ile picha na kunikumbuka enzi za uhai wa mapenzi yetu;

    “Nicholas, nilikukosea nini mpaka kustahili yote uliyoyafanya wewe na baba mkwe wako? Ni siasa, biashara, au ni nguvu ya pesa?, kwanini uliamua kushiriki kuifukia taaluma yangu? Lipi liliwafanya mniharibie utu wangu na ubinadamu wangu? Kwanini, mmefanikiwa kuzima kila kitu ambacho nilikianzisha kwa nguvu zangu, mlikuwa na pesa na uwezo wa kunitenganisha na Natasha kwa njia ya Amani lakini si kwa kuninyang’anya hata kile kidogo ambacho nilikuwa nacho” nilisikia uchungu sana kwakuwa kila nilipojiuliza ni lipi kosa langu mpaka wao kunifanyia hivyo sikuona.

    “kaa kwenye kochi Nicholas” nilimgeukia na kumwambia akae kisha alikuja kukaa pale huku akizidi kutetemeka.

    “Nataka unijibu maswali yangu machache kisha nitaondoka” nilimwambia huku nimekaa kwenye kiti mbele yake na yeye alitikisa kichwa akimaanisha kuwa yuko tayari kunijibu.

    “Natasha yuko wapi” lilikuwa swali la kwanza ambalo hata hivyo alionekana kutofahamu.

    “sijui ila nilisikia alikwenda Kenya kukutafuta” alijibu huku akizidi kutetemeka.

    “kwanini unamfanya Natasha ahangaike kiasi hicho, huoni kuwa ananipenda ndio mana anaenda kunitafuta? Kwanini unataka kununua mapenzi kwa fedha na mali zako?.. je una mango gani wa kumtafuta na kumrudisha nyumbani? Nilimuuliza kisha nilinyanyuka na kuanza kuwaza ni nini kitakuwa kimempata huko Kenya kwakuwa sikujua kabisa angewezaje kunipata.

    “nimetuma vijana wangu wakamtafute” alinijibu.

    “ni nani anamsaidia kazi ya kunitafuta” nilimuuliza huku akili yangu ikiwa bado haifanyi kazi, nilikuwa dhaifu sana kila niliposikia kuwa Natasha alikuwa kwenye matatizo, nilijua kabisa hataweza maisha ya kunitafuta huko alikoambiwa niko.

    “aliondoka na msichana flani anaitwa Beatrice ni mgeni toka Madagascar nilisikia, na kijana mwingine ambaye hatukuweza kupata jina lake pale uwanja wa ndege kwakuwa hakuandika jina lake” nilishtuka na kumgeukia.

    “umesema Beatrice!!!?” nilimgeukia tena na kumsogelea karibu.

    “ndiyo, ni raia wa Madagascar” alijibu na hapo ndiyo aliongeza ugumu wa mambo kabisa, nilichukua simu yangu na kuanza kutafuta namba za simu za mtu ambaye angenisaidia kuwatafuta.

    “ndio habari yako” nilongea na mtu wa upande wa pili aliitikia kisha sikuwa na mengi ya kusema.

    “kuna watu wangu wawili, wanawake, mmoja anaongea Kiswahili na mwingine hawezi Kiswahili, wako nchini Kenya wananitafuta lakini watakufa kabla ya kunipata, naomba msaada wako mzee, naomba waje kwangu wakiwa wazima” nilimuomba mtu aliyekuwa upande wa pili wa simu.

    “kesho” alijibu hivyo na kukata simu, sikujua nini maana ya kesho lakini sikutaka kujua zaidi.

    “Nicholas, nilikuja hapa kukuambia tu ujiandae, mimi nimeshajiandaa pia baba mkwe wako anajiandaa na yeye kesho wote nyinyi mtaondoka, kila mmoja atakufa ni muda tu haujafika” nilinyanyuka pale na kuondoka zangu, nilifika nje ya geti na kuchukua bajaji nilipofika mbele kidogo nilishuka na kuanza kutembea kwa mguu kupita baadhi ya maene, kisha nikatokeza njia kuu na kupanda gari kurudi kariakoo, nilichukua vitu vyangu katika ile hoteli na kuondoka kuelekea hoteli nyingine.



    KESHO YAKE

    Ilikuwa siku ya jumamosi asubuhi niliweka vifaa vyangu tayari kabisa kwa kumaliza kazi, niliamka na kusali ili mungu anisamehe kile nilichokuwa naenda kukifanya siku hiyo, nilipanga kumkatakata vipandevipande rais wa nchi yangu aliyesababisha nipoteze kila kitu, niliweka bunduki yangu matata ya KNT-308 sniper riffle, kwenye begi na kuondoka mpaka eneo ambalo nilikuwa nimepanga ningekaa siku hiyo kwakuwa nilikuwa nikiifahamu ratiba ya rais ya siku hiyo yote.



    *****

    Muheshimiwa rais alitoka ikulu na kwenda kutembea katika ufukwe wa bahari akiwa na walinzi wake kama kumi na sita waliomzunguka kila sehemu, nilikuwa umbali wa mita mia saba nikiwa na juu kabisa ya meli ya Mv. Mipango iliyokuwa imetia nanga baharini.

    “tiiiii,,,,,,,tiiiii” simu yake ilikuwa ikiita na hapo nilimuona kupitia darubini iliyokuwa kweny ila mashine, mlinzi wake alimsogelea na kumpa ile simu.

    “Yes Nicholas” aliitikia kwa furaha.

    “Honorable President, am sorry that it’s not as you expected, am here to take what I owe you”(muheshimiwa rais, samahani kwakuwa si kama ulivyotaraji, niko hapa kuchukua kile ninachokudai)

    “Who are you?” (wewe ni nani) aliuliza kwa sauti ya chini.

    “unataka kujua mimi ni nani?” nilikata simu na haraka niliweka jicho kwenye ile bunduki kisha kwa haraka kabisa nilikuwa nilianza kuchezesha kidole katika kitufe cha kuruhusu risasi(trigger) mara kumi na tano tu na walinzi wake walikuwa wamebaki watano pale waliokuwa yeye alikuwa amekimbia na kujificha kwenye mti akiwa amebakiwa na mlinzi mmoja, niliipiga tena ile simu yake na alipopokea alikuwa akiongea kwa kutetemeka.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “sema chochote unachotaka nitakupa” aliongea huku akitetemeka.

    “natumaini sasa umejua mimi ni nani, nitafata ninachokitaka, huyo mlinzi mmoja atakusaidia” nilikata simu na kukunja mashine yangu kisha nilishuka taratibu mpaka chini kimya kimya kisha nikavaa nguo za mabaharia na mtungi wa oksijeni nikazama ndani ya maji na kuondoka.

    Majira ya saa 7 mchana taarifa ya habari ilitangaza lile tukio lakini hawakusema ni nani alifanya hivyo ila ulinzi uliimarishwa ndani ya jiji la Dar es Salaam na maeneo yote ya ikulu, usiku huo rais alikuwa na uzinduzi wa mfuko mpya wa hifadhi za jamii uliokuwa ufanyike Ubungo Plaza lakini walitangaza kuwa uliahirishwa.

    “ngriiiii,,,,,ngriii” ulikuwa mlio wa simu yangu na ile simu ya Nicholas nilikuwa nimeizima kabisa kwa wakati huo.

    “halloo” niliitikia ile simu.

    “katika saa ya ubungo, kwenye stendi ya daladala, saa 10 kamili” aliongea yule mtu wa upande wa pili wa simu lakini hata hivyo sikujua ni nani na alikuwa na maana gani, kabla sijaongea kitu alikata simu, hapo ilikuwa imebaki dakika 15 tu kufika saa 10 kamili na mimi nilikuwa Rombo green view hotel, nilikodi pikipiki na haraka nilifika pale lakini nilikaa mbali ng’ambo ya barabara ili niweze kuona ni nani anafika pale mda ukifika, lakini ilipofika saa kumi kamili hakukuwa na mtu wala dalili ya mtu pale, nilitaka kuondoka lakini niliponyanyua mguu nilihisi kitu kimeegemea mguu wangu, kutazama chini ilikuwa ni kabegi kadogo nikakabeba na kuondoka, nilizunguka na pikipiki mpaka chuo kikuu cha Dar es Salaam na kuingia darasa moja lililokuwa karibu na barabara nikafungua ile begi ndogo na kukuta kitambulisho na ndevu za bandia, nilijua yule alikuwa ni yule muhindi wa Feisal, kulikuwa pia na ratiba ya shughuli iliyoahirishwa ambayo sasa ilikua ianze saa 12 jioni katika hoteli nyingine katikati ya jiji, niliondoka na kujiandaa vizuri kisha nilivaa kile kitambulisho cha mfuko wa hifadhi ya jamii na nilifanikiwa kuingia mpaka ukumbini, mda wote macho yangu yalikuwa kwa rais na walinzi wake siku hiyo walikuwa wengi sana. Alielezea pia kuhusu jaribio la kutaka kumuua lakini alijisifu kuwa kwa vile yeye ni kamanda huyo aliyetaka kumuua alishindwa baada ya kuzidiwa nguvu na kukimbia. Akiwa anatoka pale juu kwenye hotuba yake niliona akipelekewa simu na mlinzi wake mmoja, kisha alipokea na kuondoka pale kisha alikuwa akisindikizwa na walinzi wake akaelekea kama anakwenda kwenye chumba kimoja pale ndani kisha aliwaambia walinzi wake wasubiri pale nje, haraka bila ya kuweka wasiwasi kwa mtu yeyote nilizunguka mpaka upane wa pili wa ukumbi na kufanikiwa kuona sehemu ya kupanda kwenye dari la ile gorofa nilifanya taratibu kabisa na kufunika ule mfuniko vizuri kila mnikaingia juu na kuchomoa waya zilizokuwa zinahusika na mfumo wa ufunguaji mlango kwa kadi maalumu na hapo malango wa chumba alichoingia ulijifunga bila yeyote kujua, nilitambaa na ukuta taratibu mpaka sehemu nyingine iliyokuwa na mlango wa dharura na kwakutumia kichuma maalumu cha kufungulia milango nilibahatika kuufungua ule mlango na kuingia bila yeye kusikia kwakuwa alikuwa makini kuongea na simu.

    “Kwahiyo umemuua Natasha?” aliuliza na inaonekana simu ya upande wa pili ilijibu ndio, alikaa chini na kuhika kichwa bado akimsikiliza yule jamaa.

    “Robeen tumemuua mwanangu, na tumemuua waziri, sikuwa tayari kwa hilo ila kwa upuuzi wako ulizima simu yako” alikata simu na kuonekana akifuta machozi.

    “Mr. President” nilimuita na alipogeuka alikutana na ngumi nzito ya pua



    “Usiinue hisia za mwenzake kama hauko tayari kumpenda, usifanye hisia za mwenzake chumba cha kufanyia mazoezi, hisia na mihemko ni vitu vyenye kuweza kumfanya binadamu afanye chochote, kila mtu hufanya jambo kwasababu amesukumwa na hisia, zaweza kuwa za chuki au za upendo, katika mapenzi hisia hutufanya tusikie raha lakini hisia hutufanya tulie na kujuta, kuna wakati kwa tama za mwili tunajikuta tukiwafanya wengine watupende kwa kuzifanya hisia zao ziamini kuwa tunawapenda pia. HAKUNA KITU KIBAYA KAMA KUJIAMINISHA KUWA MTU ANAKUPENDA NA KUMBE YEYE ANAJUA KINYUME,,,USIAMSHE HISIA ZA MTU USIYEKUWA TAYARI KUMPENDA”,,,HII NI SEHEMU YA 14



    Nilinyanyua uso nikamuona akinifata bado huku akichechemea, nilijinyanyua pale nilipokuwa nimeinama lakini alikuwa ameshanifikia, nikajitahidi sana kujivuta ilininyanyuke lakini sikuweza kwakuwa nilikuwa nimebanwa.

    “Tafadhali usiniue, tafadhali” nililia lakini alinisogelea mpaka pale na kuvua ile kofia, kisha aliweka kidole kwenye kile kitufe cha bastola na kuanza kukivuta taratibu.

    “paaaa” sauti kubwa ilisikika na hapohapo nilimuona akidondoka, sikujua nini kimetokea pale, nilianza kurudi nyuma huku nikiangalia ni nini kimetokea, niliimsogelea pale alipokuwa ameanguka yule jamaa,nikapiga magoti chini kwa uchovu na kunyanyua ile bastola yake lakini wakati napeleka mkono nilishtuka kukanyagwa mguu na hapohapo nilanza kutetemeka tena, nikanyanyua uso wangu taratibu na kuanza kumtazama yule aliyenikanyaga.

    “hauhitaji bastola” alinipa mkono na sikuweza kumtambua lakini hakuwa anaongea Kiswahili.

    “wewe ni nani” niliuliza huku nikitetemeka.

    “haijalishi, usiponijua itakuwa ndio uzima wako” alizidi kunisogezea ule mkono na kwa hali ya uoga nilimpa mkono wangu.

    “tuondoke, hakuna muda wa kusubiri” aliniambia lakini sikuwa tayari kuondoka kwakuwa sikumfahamu na sikujua yeye atakuwa nani.

    “siendi popote” nilimtazama, alikuwa amefunga kitambaa usoni na kuacha macho tu.

    “ni lazima sio ombi” aliniambia kwa sauti ya kumaanisha.

    “rafiki yangu, amebanwa na usukani wa gari, amefariki, siko tayari kumuacha hapa” nilimuambia huku nikielekea kwenye gari.

    “acha wafu wazike wafu wao, tuondoke” nilishtushwa na kauli yake ile na kusimama kisha niligeuka na kumtazama.

    “kama hatutamtoa hapa basi sitaenda popote, sikujui na sijui kwanini unataka kuniondoa hapa na sijui unakotaka kunipeleka” niliaenda pale kwenye gari na yeye alinifata na taratibu tulianza kunyanyua yale mabati yaliyokuwa yamesonga kisha tukanyanyua na kile kiti taratibu na kufanikiwa kumtoa.

    “koh koh” nilirukaruka na kuinama, alikuwa yuko hai.

    “ee mungu wangu, Beatrice, Beatrice, niangalie Beatrice,” nilimuita Beatrice huku nikimgusagusa, na taratibu niliona akifungua macho, machozi ya furaha yalinitawala sana.

    Kwa muda mfupi sana na mgumu niliokuwa na Beatrice niliweza kujua kuwa Beatrice ni msichana jasiri sana na hakuwa na woga mar azote alipokuwa na hasira, hakuwa muongeaji sana lakini alifanya kila jambo kuhakikisha kuwa Frank anaepukana na matatizo, kilichoniacha njia panda ni uhusiano wa Beatrice na Frank, nilishindwa kujua kuwa wanamahusiano ya kimapenzi au la, nilijua kwasasa kama Frank angejitolea kunisamehe basi ndio ungekuwa mwanzo wa mapenzi yetu mimi na yeye, lakini sikujua mapenzi ya Frank kwa Beatrice, swala hili kwa upande mwingine wa kichwa changu liliniumiza sana na sikuwa tayari kabisa kumkosa Frank muda huu hata kama ningeambiwa alikuwa shetani. Sikutaka kuwa na chochote duniani zaidi ya Frank na mwanangu, nilipanga kumuua Nicholas iwapo nitamkuta mbele yangu, chuki aliyopandikiza ili nimchukie Frank ilizidi mara dufu na kumgeukia yeye, na sasa nilikipenda kifo kuliko kumpenda yeye, sikujua ningemfanya nini baba yangu niliyempenda kwa kila hali lakini muda ambao ningebahatika kuonana naye ndio ningejua itakuwaje.



    **MIAKA 19 KABLA**



    “Natasha Rweikaza” nilisikia jina langu likiitwa wakati niko maktaba usiku nikijisomea, ilikuwa sauti ya sista Fransisca aliyekuwa mlezi wetu pale shuleni.

    “abee sista” niliitika kwa taratibu.

    “nenda ofisi ya sista mkuu unaitwa” niliondoka mpaka ofisini na kumkuta sista mkuu ambaye kwa pale ndiye aliyekuwa mkuu wa shule.

    “Natasha kesho asubuhi unatakiwa uende nyumbani, baba yako anakuhitaji na amepiga simu kasema kuwa anahitaji ufike mapema hivyo asubuhi sista Mage atakupeleka Uwanja wa ndege ili upande ndege ya asubuhi kwaajili ya safari ya kuelekea Dar” alinieleza hayo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “kuna nini Sista?” nilimuuliza lakini hakunieleza chochote zaidi ya kuniambia niondoke kwenda kujiandaa.

    Asubuhi ya siku hiyo niliamka mapema na kuondoka na ndege ndogo ya saa kumi na mbili mpaka uwanja wa ndege ambapo nilichukuliwa na gari hadi nyumbani, nilipofika nilikuta na mzee anataka kutoka hivyo aliniambia nikabadilishe nguo twende hospitali mama anaumwa. Nilifanya harakaharaka na tuliondoka, kipindi hiki baba yangu alikuwa ni waziri, baada ya kufika hospitali nilikuta mama yangu akiwa hoi kitandani”

    “mama utapona usijali” nililia huku nikizidi kumkumbatia.

    “hapana,,siwezi kupona tena,,sitaweza, kuwa makini na baba yako, uwe binti mwema” aliongea maneno hayo tu na kukata roho akiwa mikononi mwangu, sikuwa na uelewa wa ukimya wake mpaka madaktari walivyokuja na kumfunika kisha walituambia kuwa amekufariki, maneno ya mwisho ya mama yangu sikuyaelewa, nilikuwa kama nimechanganyikiwa kwakuwa sikujua nini kilikuwa kinatokea, baada ya kukaa muda mrefu na kumaliza masomo yangu ya sekondari ndipo nilisikiaga kuwa baba yangu hakuwa mwaminifu kwa mama yangu na walikuwa na ugomvi mkubwa toka zamani sana nikiwa mdogo, hivyo kifo cha mama yangu kilikuwa na mkono wa baba yangu, baada ya mimi kumaliza elimu ya sekondari baba yangu aliteuliwa kuwa balozi baadaya kuachana na uwaziri, hapo alikuja jioni ya siku moja na kunieleza kuwa alitaka kuoa kwakuwa sasa akiwa kama balozi alihitajika kuwa na mke, kwakuwa nilimpenda sana baba yangu na nilikuwa nikihitaji awe na furaha muda wote basi sikuwa na pingamizi kabisa na swala hilo, lakini nilimpa sharti moja tu kuwa nisingependa amlete huyo mwanamke nyumbani pale ili kuzidi kulinda heshima ya mama yangu kwakuwa ile nyumba ilikuwa ni jasho lake, baba alikubali na alifanikiwa kumuoa Lucrecia Mganyizi na walianza kuishi kama mke na mume, nilimpenda Lucrecia kwakuwa nilimpenda baba yangu na sikutaka aumie kwa kuona namchukia mke wake lakini ndani ya moyo wangu, sikumpenda kabisa kutokana na tabia zake za Kiswahili, lucrecia alikuwa ni mtumishi wa ubalozi japo alikuwa ni msomi sana lakini hiyo ilishindwa kuifukia tabia yake ya uvivu na kupenda starehe.

    **SASA**

    Beatrice alifungua macho na na hapo yule mtu aliita gari na muda si mrefu iliingia gari ndogo kisha wote tulipanda kwenye gari na ndani ya gari kulikuwa na daktari aliyeanza kumtibu Beatrice, alimchoma sindano na kumvua ile blauzi kisha alimfunga kitambaa maeneo ya kuzunguka mbavu, tulikuwa bado tunasafiri na baada ya masaa miwili tulikuwa tumeshafika Nairob.

    “Tunaelekea wapi” niliuliza.

    “Tunaenda Tanzania” aliongea yule jamaa .

    “Lakini Frank hajapatikana” nilimwambia hivyo lakini badala ya kunijibu alinyanyua simu yake ya mkononi na kupiga, kisha nilisikia akiongea;

    “naelekea Tanzania kusaidia kumalizia, akipiga simu kuuliza au kusema chochote mwambie kesho” alisema hayo na alikata simu.

    “Kesho kuna nini?” nilimuuliza.

    “ni vizuri usipojua” alinijibu na hapo waliegesha gari kisha wakashuka na kwenda kununua vyakula, walikuwa vijana watu watatu, dereva, yule daktari na yule jamaa mwingine lakini waliporudi walikuwa wawili tu, dereva na yule jamaa, yule daktari hakuwepo, walitupa vyakula vile na kwakuwa tulikuwa na njaa kweli tulianza kula kwa kuvifakamia, baada ya kumaliza kula tuliendelea na safari na Beatrice sasa alikuwa amepata nguvu ya kuongea japo aliongea kwa shida lakini ilikuwa hivyo. Tulipitiwa na usingizi mkubwa kwa muda mrefu sana na nilipokuja kushtuka tayari ilikuwa usiku na saa ilionyesha kuwa ilikuwa ni saa 9 ya usiku, nilishtuka na kuanza kusikia harufu ya sigara, nilipotazama tulikuwa ndani ya gari bado na yule jamaa alikuwa nje akiongea na simu.

    “umempatia kila alichokuwa anahitajika kuwa nacho?” aliuliza na inaonekana alijibiwa ndiyo kisha alikaa kimya kidogo kisha alianza kuongea tena.

    “niko nao, yeye hajui, andaa sehemu kwenye maficho kule, kisha mtafute kwa namba nitakayokutumia na umpe eneo hilo, hakuna namba za gari hakuna alama za mikono, mpe ujumbe huo” alimaliza na kukata simu.

    Nilitamani kukimbia lakini sikujua pale tulipo ni wapi na nisingeweza kukimbia nikamuacha Beatrice, baada ya yeye kumaliza kuvuta ile sigara alirudi kwenye gari na safari ilianza, muda wote huo Beatrice alikuwa amelala. Tuliendelea na safari mpaka kesho yake tena saa 10 jioni ndiyo niliona tukichomoza jijini Dar es Salaam, nilianza kuhisi kuwa yule jamaa alitumwa na Nicholas kuja kunifata, kitu ambacho sikuwa tayari kukiona kikitokea mimi kupelekwa kwa Nicholas au baba yangu.

    “siko tayari kurudi kwa Nicholas wala kwa baba yangu” nilimueleza yule jamaa.

    “nakupeleka unapopataka” alisema hayo na hapo alirudi nyuma na kunifunga mikono, midomo yangu aliiweka plasta kisha walinifunga kitambaa cheusi usoni, Beatrice alikuwa amelala bado kwahiyo hawakuhangaika nae, sikujua tunakoenda lakini baadaye tulishushwa kwenye jumba moja lililoonekana kuwa halikai mtu na lilikuwa porini.



    **FRANK ANAHADITHIA**

    Ile ngumi ilimfanya aende chini na kuzimia palepale, simu yangu ya mkononi iliita na nilipoangalia alikuwa yule kijana wa Feisal.

    “ndio” niliipokea.

    “niko nje” nilikata simu na kuvua lile koti nililokuwa nimevaa, kisha nikavuta mfuko niliokuwa nimeuficha kwenye lilikoti, nilifungua dirisha na kutazama nje nikatazama chini na kuhakikisha kuwa yule kijana alikuwa pale, niliwaha ile tochi ndogo na kumpa ishara na alikuwa tayari amenielewa, harakaharaka nilichukua kamba ndefu ya manila niliyokuwa nimeiweka kwenye ule mfuko, nilimfunga kiunoni na kufungua lile dirisha kisha nilimpitisha na taratibu nikaanza kumshusha huku nikishikilia ile kamba ili asidondoke, nilifanya zoezi hilo kwa dakika mbili na tayari yule kijana alikuwa ameshampokea na kumuingiza kwenye gari kisha yeye aliondoka nae. Niliweka kila kitu sawa na kutoka tena kupitia ule mlango na kuufunga vizuri kwa kutumia kile kichuma maalumu nilichokuwa nacho, nilipita njia ile ile niliyopita nakurudishia zile nyaya zinazomwezesha kufungua milango na nilishuka kisha nikaingia kwenye ‘lift’ nakuondoka, nilifika pale chini nikakaguliwa vyema na kuondoka na njia yangu kuelekea sehemu nyingine.

    ***

    “how are you my friend”(habari yako rafiki yangu), nilimuita akiwa amenipa mgongo na alipogeuka alikutana na kibao cha macho kilichomfanya ashindwe kuona vizuri kisha nilimkamata na kumnyanyua.

    “huu ndio muda Nicholas” alipokea ngumi ya pua kama ishara ya kuanza kwa mwisho wa mwanzo waliouanzisha. Alikuwa nje ya nyumba yake akiongea na simu ya magendo hivyo sikuwa na shida sana nilimpandisha kwenye ukuta na kumuangushia upande wa pili na mimi nilipanda na kumfata hukohuko, pale nilimbeba na kusimamisha tax ambayo nilimwambia dereva wake kuwa yule ni jamaa yangu na amelewa hajiwezi hivyo anipeleke mpaka maeneo ya mbali kidogo na pale, na baada ya umbali wa kilomita moja nilishuka na yule kijana wa Feisal alikuwa ameshafika, tukambeba na kuondoka naye.

    Akili yangu ilikuwa haifanyi kazi vizuri, nilikunya pombe sana wakati nikiwa njiani kuelekea kwenye eneo maalumu tulioliandaa, Feisal alinipigia simu ya na kuniambia kuwa nishirikiane na kijana wake na yeye alikuwa njiani kuja lakini niliarifiwa kuwa tayari alikuwa ameshafika na muda wowote angefika eneo la tukio.

    Tuliondoka bila kutiliwashaka mpaka kitunda na kumuingiza Nicholas ndani ya lile jumba tukamuweka pamoja na baba mkwe wake kisha tuliwamwagia majina hapo walizinduka.

    “mko chini ya himaya yangu” niliwaambiwa wakati wakinitazama, sikujua nianze kwa zoezi gani ili kuwazindua akili zao. Nilimtoa mmoja mmoja na kuwakalisha kwenye kiti kisha niliwafua mashati na kuwafunga mikono na miguu na kuwaacha vifua vyao vikiwa wazi.

    “Frank, niko tayari kukuachia Natasha ili uniache niishi” aliniambia Nicholas huku akilia.

    “Natasha hajawahi kuwa ni wako, hajawahi kuwa wako hata siku moja acha upumbavu, usingetumia hila Natasha asingekuwa mke wako leo” nilimsemesha kwa hasira huku nikimtazama usoni, alikniudhi sana kwa ile kauli kwakuwa alidhani kuwa mimi kuwa na Natasha ilikuwa hisani, nilichukua ile plaizi iliyokuwa karibu na kumfinya mbavu mpaka nilipohakikisha nimetoka na kipande cha Nyama, alilia sana kama mtoto lakini sikujali hata kwa asilimia 1.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mzee, hapa unavyoniona, tetenasi imenila sana, nikihitaji kupona ipo haja ya mimi kukaa hospitali zaidi ya miezi mitatu tena hospitali ya bei kubwaa ili nitibiwe sawia, haya yote yalitokea kwakuwa wewe na huyu jamaa na wale wengine waliokuwa wanakusikiliza waliamua kunifanya siku moja niishi maisha haya, niwe mtu wa kusubiri kufa” nilimuambia mzee Rweikaza huku nikitokwa na machozi.

    “Niko tayari kukupeleka hospitali yoyote unayotaka, niko tayari kukupa nuru mpya ya maisha Frank, niko tayari kijana wangu” alikuwa akiongea huku akitetemeka, nilimsogelea na kupeleka ile plaizi kwenye mbavu nikambana mpaka nilipoona jasho, machozi na makamasi vimeujaza uso wake, niliendelea na lile zoezi kwa lisaa limoja mfululizo mpaka nilipohakikisha mwili wao umejaa vidonda, walikuwa wanalia kama watoto.

    “naomba niletee mifuko na nailoni minne na kibiriti” nilimuagiza yule kijana na kwa haraka aliniletea ile mifuko nikaiwasha na kusubiri ishike moto vizuri ili matone yake niwadondoshee kwenye vile vidonda, kulia kwao kulianza kufuta machungu yangu ya miaka yote, nilipokuwa Somalia nilifundishwa kuwa kisasi kizuri ni kile ambacho kabla ya kumuua adui wako unamfanya ayahisi maumivu uliyoyasikia kipindi yeye akiwa mtesaji. Niliwadondoshea yale matone mwili mzima na walilia kuliko kawaida kisha baaya ya kuhakikisha wamelowa matone na nailoni nilivaa ‘gloves’ na kuanza kubandua yale matone yaliyoganda na kuwaachia vidonda vikubwa vya moto, zoezi la kubandua yale matone yaliyokuwa yameganda lilikuwa la kuumiza kuliko lile zoezi la kuwadondoshea yale matone.

    “Frank kuwa na utu” aliongea yule mzee aliyeonekana kuelekea kufa, tulimchoma sindano ya kumuongeza nguvu na kumfanya awe tena na nguvu, nia ikiwa ni kumuonyesha kuwa kulikuwa na watu wanaoweza kufanya yale yasiyofikiriwa kufanywa kwa binadamu, wakati wote huo yule kijana nilimwambia awe anachukua video ili kesho na kesho kutwa vizazi na vizazi vijifunze ubaya wa kumdhulumu mtu haki yake.

    “leta yale maji” nilimuagiza yule kijana na haraka alileta maji ya pilipili yaliyochanganywa na chumvi na kisha nilianza kuwamwagia taratibu sana.

    “ayaayayaaa,,,Frank unanidhalilisha mimi ni rais, nitakupa chochote,,ayayayaaaa” mzee Rweikaza alilia kama mtoto lakini hiyo haikujalisha.

    Baada ya kuwafanyia hayo niliwamwagia spirit mwili mzima na kuwasugua na brashi ngumu ya chuma mpaka walipopoteza fahamu, baada ya kuwashtua muda mrefu bila wao kushtuka niliambua kuchukua ile plaizi na kuanza kukata vidole, nilipokata kidole cha mzee Rweikaza alishtuka hapo hapo na kuanza kulia, nilifanya hivyo huku nikimmwagia spirit na kumuweka chumvi ili kukata damu asife haraka, nilimaliza vidole vyake vyote na alizimia kwa mara nyingine kisha nilianza kwa Nicholas ambaye baada ya kumaliza vidole vya mkono mmoja alikuwa ameshazimia.

    “Feisal yuko hapa” aliniambia yule kijana.

    “mruhusu” aliingia Feisal

    “kila kitu kiko sawa?” aliuliza Feisal alipofika pale, alifunga macho baada ya kuwaona jinsi walivyokuwa, alitoka pale na kurudi tena na watu.

    Nilishtuka sana kumuona Natasha mbele yangu akiwa na Beatrice, nilikaa kama vile nilipigwa na butwaa lakini kabla sijamtazama vizuri Beatrice alikuwa ameshaujaza mwili wangu kwa kumbatio la uchungu, nilimkumbatia Beatrice na kukumbuka sana kipindi nikiwa kwao.

    “Frank am glady you are alive”(Frank ninafuarahi uko salama) aliniambia Beatrice na kunibusu, nilimshika nakumtazama usoni kisha nikamkumbatia tena. Natasha bado alikuwa akilia pale na kuona aibu hata kunifata, nilimtazama na kuiona siku ya kwanza niliyompenda Natasha. Nilimfata na kumkumbatia huku machozi ya majonzi yakinitoka.

    “nisamehe Frank” alilia akiongea hayo lakini kabla sijajibu chochote nilisikia sauti ya Feisal na kugeuka.

    “Honorable Mr. President do you remember me” (Muheshimiwa rais unanikumbuka?), mzee Rweikaza alikuwa ameshaamka na Feisal alikuwa akimsemesha, sikujua kuwa Feisal alikuwa na yake pia katika hili. Nilimuona mzee Rweikaza akiangalia kama vile alikuwa anasinzia.

    “My name is Feisal Kareem Ahmed, the son of the former Captain Ahmed Kareem of the People’s Militia, who was also your business partener in 1996, but you betrayed him by raping my mother and later on you killed her, then killed my father when he was about to know who killed his wife, later on you killed Zarack who to me is my young brother just because he saw you when you killed my father”(Jina langu naitwa Feisal Kareem Ahmed, ni mtoto wa Kapteni wa zamani wa jeshi la wanamgamb, aliyekuwa pia mfanyabiashara mwenzako mwaka 1996, lakini ulimsaliti kwa kumbaka mama yangu na baadaye ulimuua, na baadaye ukamuua baba yangu alipokuwa karibu kujua nani alimuua mkewe, baadaye ulikuja kumuua Zarack ambaye ni kaka yangu kwakuwa tu alikuona ukimuua baba yangu), aliongea Feisal na kuvua miwani kisha rais alionekana kumtazama vizuri huku akizidi kutetemeka, Natasha aliendelea kulia na alizunguka kisha kumuangalia baba yake.

    “Natasha, niokoe” alilia mzee Rweikaza. Natasha alimsogelea tena Nicholas na kuanza kumlaumu kwa kumuingiza katika matatizo na kabla hatujatulia tulisikia Nicholas akilia kwa uchungu, kugeuka tulikuta Natasha amezamisha kisu kwenye utosi wa Nicholas mara mbili na hapohapo alikata roho. Wakati bado nashangaa kilichotokea Natasha aliondoka na kwenda kumchoma tena baba yake kile kisu lakini nilimrukia na kile kisu nilizama begani badala ya kichwani.

    Feisal alikichomoa kile kisu na kukipitisha shingoni kwa mzee Rweikaza kama vile alikuwa akichinja kuku, na Beatrice alipata mshtuko na kuzimia, baada ya dakika kumi aliinuka na tulimwaga mafuta ya petrol kwenye lile jingo na kulichoma moto.

    **KESHO YAKE**

    “Mimi naondoka kurudi Somalia, hali ya msako ni kubwa hivyo nitaondoka leo usiku, na nashauri hata nyie pia kila mtu aondoke, mpaka sasa inajulikana kuwa ni Frank aliyemteka rais kwakuwa aliandika ule waraka, na mimi nimetuma jana usiku ile video mliyochukua ya Hukumu ya rais na maelezo marefu juu ya maovu yake yote na ule waraka wake. Kama mtataka tunaweza kuondoka wote na huko Beatrice. Natasha unaweza kubaki kwakuwa ushahidi hakuna sehemu ambayo wewe unahusishwa, kwenye makaratasi niliyowatumia nimeandika kuwa tulikuteka hivyo, unaweza kubaki” aliongea Feisal tukiwa kwenye nyumba nyingine huko kibiti.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nataka kurudiana na wewe Frank, nataka kuanza maisha mapya na wewe na mtoto wangu tafadhali” kabla sijaongea chochote nilishtuliwa na kauli ya Feisal.

    “HAMUWEZI KUOANA, NYINYI NI NDUGU, MZEE RWEIKAZA NI BABA YAKO FRANK, yule aliyefariki kipindi kile sio baba yako, mama yako alikuwa na mahusiano na mzee Rweikaza kipindi hicho kabla hajafanikiwa kimaisha, lakini alimtelekeza mama yako wewe ukiwa na miezi nane na ulilelewa na mwanaume aliyekuja kwenye mahusiano mapya na mama yako, mzee Rweikaza hakuwahi kulijua hilo lakini nililijua hilo kwakuwa nilimfahamu mzee Rweikaza, na majibu ya damu zenu hayo hapo” aliongea kauli iliyonifanya nikae chini na kuchoka kabisa.



    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog