Search This Blog

Sunday, 22 May 2022

TAALUMA ILIYOPOTEA - 4

 





    Simulizi : Taaluma Iliyopotea

    Sehemu Ya Nne (4)



    Nilitoka pale na kupanda gari yangu kuelekea nyumbani, nilifika na kuingia ndani kisha nikampigia simu Haleed.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nimefika” nilimuambia huku nikionekana kutetemeka.

    “mumeo yupo?” aliniuliza kwa makini sana.

    “Hayupo hapa alisema anaenda morogoro mida hii” nilimjibu na yeye alikaa kimya kwa muda kidogo kisha nilimsikia kama akifanya kitu kwenye laptop yake.

    “hapo chumbani kwenu, ukienda upande wa chooni kwa juu ya dari unaona kama kimfuniko hapo na kama inaning’inia, nenda mpaka hapo ukiwa na stuli kisha uniambie” , hofu ilizidi kunijia na sikuelewa kabisa ni nini kilikuwa kinaendelea, ila kwakuwa nilitaka kujua kila kitu nilichokuwa sikifahamu basi ilinibidi nifanye yale niyawezayo, nilienda kama alivyoniagiza mpaka pale na kusikiliza tena maelekezo yake;

    “panda juu ya stuli kisha shikilia iyo kamba taratibu na uanze kuivuta taratibu sana kisha uitoe hiyo stuli uendelee kuivuta, sikiliza kwa makini namaanisha taratibu kwakuwa ukivuta kwa pupa alaem italia na hutakuwa na cha kujibu zaidi ya kupoteza kila kitu, zima simu yako ya kazini acha simu ambayo kazini hawaifahamu ili ufanye mambo kwa ustadi, namaanisha taratibu sana itafunguka na nitakupa maelezo ya ziada” sikuitika tena, nilikuwa nimelowa kama nilinyeshewa na mvua, nilikuwa na muonekano ambao usingemshawishi mtu kuwa nilikuwa waziri, sikufanania kwasasa kwaile hofu niliyokuwa nayo.

    Nilivuta ile kamba taratibu kama alivyonielekeza na hapohapo niliona ngazi ikishuka taratibu, nilipigwa na butwaa kwakuwa sikujua ilikuwaje muda wote nimeishi kwenye ile nyumba na kuoga lile bafu ila sijawahi kuona vitu vya namna ile.

    “Tayari” niliongea kwasauti ya kunong’ona.

    “panda taratibu sana na hapo juu kushoto kuna ‘switch’ bonyeza kisha taa zitawaka, usiwe na haraka tayari nimeshahakikisha kuwa mumeo hayuko dar kwasasa, ukiwasha taa, usihangaike na utakayoyaona huko, kuwa makini tu na kile ambacho nakuelekeza, angalia kwenye hayo majokofu hapo mbele yako utaona kitasa ukutani nenda kivute kwa kwenda chini na utaona kama umeme umepungua kiasi flani, hapo inamaana umezima kamera zote za ulinzi hapo kwako ikiwa ni pamoja na zilizopo huko ndani, mbele kidogo kuna maboksi makubwa yapite kisha kushoto kuna kompyuta iwashe kisha ingiza neno la siri 45RQ54, itawaka kisha nitakupa maelekezo mengine”, mpaka hapo nilikuwa na maswali mengi sana kichwani kwangu lakini hakukuwa na muda wa kuyatafutia majibu. Sikujua yale majokofu yalikuwa na kazi gani au yale maboksi yalikuwa na nini ndani yake.

    Niliwasha ile kompyuta, na nilikuta picha ya mtoto mdogo wa kike lakini sikuijali sana zaidi ya kuendelea kusikiliza maelezo aliyokuwa akinipa Haleed;

    “sasa hapo nenda kwenye ‘local disk C’ kisha nenda ‘program files’ utakuta kuna file limeandikwa ‘hardwares’ lifungue utakuta ‘folder’ limeandikwa ‘apparent’ lifungue ndani yake utakuta linguine limeandikwa ‘zip folder’ lifungue utakuta kitu kimeandikwa ‘bit locker encrypted code’ nakili hizo namba kisha rudisha kila kitu kwa makini, rudisha kila kitu kama ulivyokikutwa na ujiweke safi kisha nitakupigia simu kwa maelekezo zaidi” alimaliza kuongea hayo na kisha alikata simu. Nilirudisha kila kitu kama kilivyotakiwa na kabla sijatoka nilifungua moja ya jokofu lililokuwa karibu yangu, ndani yake lilikuwa na maboksi ambayo sikuweza kuyatambua lakini niliona jiana juu yake yakiwa yameandikwa ‘President’s Cargo, CC +255’, sikuwa na hata chembe ya uelewa wa kile nilichokiona pale, nilifunga lile jokofu na kuwasha tena zile kamera kisha niliondoka, nilirudisha kila kitu na kushuka kisha niliingia bafuni nikaoga na kubadili tena nguo, niliwasha simu ya kazini na kumuuliza katibu muktasi wangu kama kuna mtu yoyote alikuwa ananiulizia na aliseme alikuwepo lakini naibu waziri alishalishughulikia hilo.

    *****

    Nilipiga simu ya Haleed lakini haikuwa inapatikana na baada ya muda niliona namba ngeni ya simu ikiingia kwenye simu yangu, niliipokea na hapo nilishukuru kwakuwa alikuwa Haleed;

    “Madam washa gari lako njoo ofisini kwako utanikuta hapa, kumbuka kila kitu kiko sawa uwapo mbele za watu, usionyeshe any sign of fear(dalili yoyote ya woga) ili mambo yaende sawa, kuwa mvumilivu na maswali yako yote nitakujibu” alinieleza hayo na kabla hatasijaongea chochote alikuwa ameshakata simu. Haikuwa kawaida mimi kuendesha gari mwenyewe au kuwa mbali na ofisi yangu bila mtu yoyote kujua, lakini leo niliwakwepa watu na nilitamani kupata likizo japo ya wiki mbili ili nitafute majibu ya maswali mengi niliyokuwa nayo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Niliingia kwenye gari na kuliwasha kisha nilikamata njia ya kuelekea posta na baada ya muda kiasi nilifika eneo la ofisini, pale ambapo huwa napaki gari langu kulikuwa na gari limepaki pale hivyo nilienda kupaki pembeni yake na nilishuka nikawa nafunga mlango wa gari, nilisikia tena simu yangu ikiita na nilivyopokea nilisikia maneno machache sana, na simu ilikatwa.

    “ingia kwenye hii gari pembeni yako” nilifunga mlango wa gari yangu na kuingia kwenye ile gari kisha tuliondoka na kuelekea kurasini, ila mbele kidogo kabla hatujafika simu yangu iliita na alikuwa Nicholas, nilimueleza Haleed kuwa mume wangu alikuwa anapiga, kisha aliniambia nikae kimya na nimpe ile simu yangu.

    “Mkuu habari aisee” alimsalimu Nicholas na kisha alianza kucheka kama vile walikuwa wanajuana.

    “Vipi za siku nyingi” nilisikia akimsemesha Haleed swali linguine.

    “salama, sasa mama leo namuendesha mimi, mana hali ya usalama sasa hivi sio njema sana, yeye yuko kwenye kikao hapa Peacock Hotel simu aliacha kwenye dash body hapa” alimdanganya na ilionekana kuwa Nicholas aliridhika, kisha Haleed alinirudishia ile simu.

    “Haleed,,,” sikumaliza hata kuongea alinikatisha.

    “ndio najua una maswali mengi sana ungependa kuyafahamu lakini nakuahidi hakuna kitu ambacho hutafahamu ila kwasasa twende huku”, aliingiza gari mpaka nyumba moja iliyokuwa imejificha na tulipofika tuliingia ndani kabisa kulikuwa na chumba chenye kompyuta na vifaa vingi, vya umeme, nilikuta pia kijana mmoja aliyekuwa busy na zile kompyuta.

    “Shikamoo muheshiwa” alinisalimia lakini sikupenda sana alivyoniita muheshimiwa, na kabla sijaitika Haleed aliniambia niketi kisha nilimpatia zile namba.

    “unaweza kuhuck sasa hivi” alimuuliza yule kijana ambaye hata hivyo alionekana kuwa amepagawa au alikuwa na tatizo la kiakili.

    “yeah naweza, siumekuja na BLC,” aliuliza hivyo lakini sikujua ni nini, alimpatia zile namba na muda huohuo, ilikusikika sauti za watu wakiongea, yule kijana alichukua simu yangu akaibonyezabonyeza kisha alinipa ‘earphone’ na mimi nilianza kusikia sauti za wale watu wakipanda juu ya kuyapitisha makontena bandarini na ilionekana kama waliongea na mtu kwa upande wa pili, sauti ambayo niliigundua kuwa ilikuwa ya baba yangu. Sikufahamu walichokipanga vizuri kwakuwa nilikuta ile habari katikati.

    “Leo hii majokofu mengine yataingizwa nchini usiku kupitia bandari ya Dar na kupelekwa morogoro, baba yako ndiye mmiliki wa mzigo huo akishirikiana na mumeo” aliniambia Haleed na sikujua kulikuwa na ubaya gani kama ilikuwa ni majokofu tu.

    “sioni tatizo la hilo” nilimweleza Haleed na kuonyesha kuwa sikuwa na haja na taarifa yake.

    “si majokofu tu ni madawa ya kulevya yanayokwenda kuuzwa nchi za jirani, biashara hii baba yako asingeweza kuifanya bila kuhakikisha wewe unaolewa na Nicholas” alinieleza na hicho kilizidi kunishtua.

    “Kwanini” niliuliza huku nikimgeukia Haleed.

    “toka kipindi ukiwa mdogo baba yako akiwa ndo kwanza anaanza maisha alikuwa na rafiki yake aliyekuwa anaitwa Mark ambaye walikuwa nae kwakipindi chote mpaka pale ambapo baba yako alipomtoa uhai wake wakiwa njiani kutoka Ngorongoro na kusingizia kuwa walipata ajali, yule mzee ni baba yake na mdogo na Nicholas, hvyo baba yake Nicholas alilazimika kuanza ushirikiano na baba yako baada ya mdogo wake kufa na wakati huo baba yako alijiingiza kwenye siasa lakini bado walifanya biashara ya pembe za ndovu, Nicholas alijiingiza kwenye biashara na kumuua baba yake ili arithi utajiri, hata hivyo mda mfupi baadae mama yake alifariki na hivyo sasa kila kitu kilikuwa mikononi mwako, alijua siri nyingi sana za baba yako na alikuwa akikupenda toka siku nyingi. Aliongea na baba yako juu ya kukuoa lakini baba yako alikataa kipindi akiwa balozi, kipindi cha kampeni kilipokaribia walikubaliana kuwa akuoe ili kutoruhusu mtu mwingine kuingilia mambo ya biashara zao, hivyo ili kutofanya watu wahoji ukaribu wao na mahusiano yao kibiashara, kwaiyo ilikufanikisha hayo ilikuwa ni lazima pia Frank aondoke, hivyo kuteswa na kudhulumiwa kwa Frank kulikuwa na sababu nyingi sana” alimaliza na kuvuta pumzi kidogo, kila alipomtaja Frank nilijikuta nikilia lakini alininyamaza kwakuniambia safari bado ni ndefu lazima niwe mvumilivu.

    “kwanini unaniambia hayo saa hizi” nilimuuliza huku machozi yakinitoka.

    “Kwakuwa mimi ni mmoja wa watu walioumizwa na dhuluma za mzee wako, ndio maana niliamua kukusanya ushahidi wote huu” alinishtua kwa ile kauli lakini sikuelewa nimuulize swali gani.

    “H,,,haa….” Sikujua cha kuongea ila alinikatisha.

    “baba yangu ni mzee Awadhi Jiratu, nadhani ulishawahi kumsikia, alikuwa mmiliki wa eneo ambalo mmejenga nyumba yenu kabla ya kwenda ikulu, lile eneo zamani sana lilikuwa la kwetu na kulikuwa na nyumba yetu, baadae baba alikuja kulichukua kibabe na hawakumlipa fidia, alipokwenda mahakamani alizungushwa na mwisho wa siku alikufa kwenye mazingira ya kutatanisha, na mama yangu pia na huyu unayemwona ni mdogo wangu, amesoma mambo ya uhandisi wa kompyuta, ila aliporudi na kuanza kufufua tena ile kesi alitengenezewa ajali iliyomfanya akili zake hazipo, haijulikani vyeti vyake viko wapi tumeshafanya juhudi za kuomba atumiwe tena vyeti vyako toka india ila pale wizara ya elimu wamezuia barua yake na wala polisi hawataki kutoa taarifa yake ya kupoteza kwa vyeti vyake hadi leo, hapo hajielewi kitu, mimi nilibahatika kuingia kwenye majeshi haya na baadaye niliingizwa usalama, kuna mambo mengi yanafanyika siyapendi lakini nimeamua kukusanya ushahidi huu siku nyingi kwakuwa niliumia zaidi kwa kilichomtokea Frank kuliko kilichowatokea wazazi wangu, kwaiyo kama unataka kujua ukweli na kuepukana na hiyo zambi tulia nikueleze kila kitu na kama utahitaji kunishitaki hata mimi kwa kufumbia macho haya basi nitakuwa tayari kuwa wakwanza kushitakiwa” alinitazama machoni na niligundua kuwa machozi yalikuwa yakimtoka ila alikuwa akijitahidi kuyazuia kitu ambacho mimi sikuwa tayari kukizuia, tuliendelea pale na ile kazi ya kuweka vile vitu vyote kwa pamoja na baada ya pale tulipanda gari tena na kurudi ofisini kwangu. Nilikuwa na kila kitu kwenye mkoba wangu na Haleed aliniambia nisiruhusu dereva wangu aniendeshe kuanzia siku hiyo.

    ****

    Kesho yake asubuhi nilikuwa na kazi za kufanya na nilihakikisha nazifanya kwa ustadi mkubwa sana na kwa haraka na baada ya pale, niliondoka na kwenda kutembelea vikundi vya kina mama wa wilaya ya kisarawe, mda wote nilikuwa nikijichekesha usoni lakini moyoni nilikuwa na mawazo mengi sana, kazi za ofisini sasa niliziona kama mzigo mkubwa nisiouhitaji, mwanangu alikuwa akikaa na dada wa kazi na kunywa maziwa ya ng’ombe mda wote kwakuwa tu sikuwa na muda wa kukaa nae, kilichoniuma zaidi ni kuwa nilijiingiza kwa muuaji na kufanikiwa kuzaa nae, mwanangu alizaliwa na mtu hatari mwenye utajiri wa kutisha usio halali, ama kweli usione mtu anapesa na anatabasamu ukadhani kuwa alipata kihalali pesa zake. Kilichoniumiza kichwa zaidi ni wapi nitaanzia lakini kwakuwa Haleed alikuwa mtu makini niliamini atanisaidia.

    ****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Jioni ya siku hiyo nikiwa nimetulia kabisa na mwanangu nyumbani, nilipokea simu kutoka kwa Nicholas aliyekuwa kazini na kuniambia kuwa nijiandae tunaelekea kwenye tafrija ya wadau wa mfuko wa mashirika binafsi iliyoandaliwa na benk ya exim na tafrija hiyo ingefanyika Kilimanjaro Kempisky, sikutaka kumkatalia kwakuwa alikuwa ni lazima aende, hivyo nilijiandaa na muda kidogo alikuja nyumbani na yeye akajiandaa.

    Tuliingia katika ukumbi uliopo Kilimanjaro kempisky na sherehe ilianza, kulikuwa na watu mbalimbali na mara nyingi Nicholas alikuwa akiniacha na kwenda nje kupokea simu na muda mwingine alionekana akiwa anaongea na wazee Fulani kama wakipanga kitu pale. Nilikaribishwa pale jukwaani niweze kusema lolote na mimi nilipanda na kutoa neno kidogo lakini wakati naongea niliona mtu akinikonyeza na sikumtambua vizuri nilipotoka pale juu nilienda mpaka pale alipokuwa na ndipo nilipogundua kuwa alikuwa ni Haleed;

    “umekuja kufanya nini hapa” nilimuuliza

    “kuna wageni leo hotelini hapa ndio mana nipo kuhakikisha usalama wa wenzetu” alinijibu huku akitabasamu.

    “ni kina nani hao wageni” niliuliza huku tukitembea kuelekea upande kulikokuwa na viti.

    “Mtoto wa mfalme wa Saudia yupo kwenye hii hoteli, ni siri kwakuwa hakuja kwa mambo ya kiserikali, anashughuli zake na anakutana usiku huu na baba yako” nilishtuka kidogo lakini sikujua kwanini alikuwa anataka kukutana na baba yangu na kwanini hakuja kiserikali bali kisirisiri.

    “usifikirie sana kwakuwa hata mumeo nae anahusika, amekuja anataka kupewa eneo la kusini kwaajili ya kuchimba mafuta lakini watatangaza kama uwekezaji wa hoteli, usiku huu kuna kikao kinafanyika hapa lakini usijihusishe na lolote, weka akili yako mbele, na mimi ndiye nitakupeleka nyumbani usiku huu nimepewa taarifa na mumeo” aliniambia na kupokea ujumbe kwenye simu kisha akinipigapiga begani kama ishara ya kuniambia nisubiri kisha aliondoka, nilitoka pale na kwenda chooni, ila nilipokuwa nikijitazama kwenye kioo niliona mtu kasimama nyuma yangu.

    “We still need to talk, don’t make things”(bado tunahitaji kuongea) aliniambia yule mtu aliyekuwa amesimama nyuma yangu niliogopa lakini nilipogeuka alikuwa yule msichana aliyekuja kuongea na mimi pale ofisini.

    “Beatrice what are you doing here”(unafanya nini hapa) nilimuuliza huku nikimtazama.

    “you are denying Frank his right by staying quite”(unamnyima Frank haki yake kwa kukaa kimya) aliniambia huku machozi yakimtoka.

    “yeah I know but….” Alinikatisha.

    “Not here, not now, let’s tomorrow Lunch time hotel at 10:30AM” (sio hapa na sio sasa, tukutane kesho saa 4:30 asubuhi Lunch time hotel) alinikabidhi kikaratasi kilichokuwa na namba yake ya simu na kisha aliondoka. Nilitoka pale na kuifuata pochi yangu pale nilipoiacha, nilikuwa natembea na ushahidi wote nilioupata toka kwa Beatrice na ule wa Haleed kila nilipokuwa naenda, nilificha ile CD na ile ‘memory card’ kwenye mkoba wangu ndani kabisa. Baada ya hapo Haleed alikuja na kunichukua kisha tuliingia kwenye gari na kuondoka.

    “Haleed kuna kitu bado nahitaji kujua” nilimuuliza wakati tukiwa njiani.

    “Yeah najua ni kuhusu yule mtoto uliyemuona” kama vile aliissoma akili yangu.

    “ndio” nilimjibu.

    “yule ni mtoto wa Nicholas, alizaa na mwanamke mmoja ambaye hatujui alienda wapi, huyo mtoto amefariki akiwa na miaka mitatu, walikufa kwenye ajali ya meli” alinijibu kwakifupi kabla ya kushtuka akiwa anahangaika kuikwepesha gari kwani mbele yetu kulikuwa na gari kubwa la mafuta likija kwa kasi. Hofu ilianza kunijaa na Haleed alijitahidi kukwepa na kwenda pembeni ila ile gari ilizidi kuja upande wetu na hapo nilisikia mlio mkubwa.

    Sikujua nini kimetokea bali nilikuja kujikuta nikiwa hospitali ya Regency, niliposhtuka nilimuona Nicholas akiwa pale pamoja na baba yangu na msaidizi wangu wa kazi ofisini.

    “uko wapi mkoba wangu” lilikuwa swali la kwanza kuuliza.

    “hatujafanikiwa kuokoa chochote kwenye gari, liliwaka moto palepale,” alinijibu Nicholas na hapo nilihisi kama vile nazimia.

    “na Haleed yuko wapi”, hakuna aliyenijibu kila mtu aliangalia pembeni, nilichomoa ile mirija na kunyanyuka lakini walinishika,

    “nauliza Haleed yuko wapi” niliuliza kwa nguvu na kwa hasira.

    “HALEED AMEFARIKI” alinijibu baba yangu.



    “Shida kaumbiwa binadamu, kila kikutokeacho katika maisha yako, kinatokea kwasababu, yawezekana iyo sababu ukawa unaipenda au huipendi lakini hiyo haifuti ukweli kuwa mambo hutokea kama yalivyopangwa. Kuna muda mambo hutokea kwa vile sisi tumetaka au kuyaruhusu yatokee kutokana na mgando wa hisia zetu na mpauko wa namna ya ufikiri wetu. Ukipatwa na jambo la kukukatisha tamaa rudi nyuma uanze upya baada ya kujitafakari, fikiria zaidi juu ya utu wako kabla hujajiingiza kwenye mambo yatakayoharibu maudhui ya ubinadamu wako na kuripotosha njia zako na ubinadamu wako. KILA KITU HUANZA NA WEWE,” HII NI SEHEMU YA KUMI,,,ANDIKA HIVI..



    **FRANK ANAHADITHIA**



    “…….nianze kwa kukupa pole kwa kazi nzito ya kulitumikia taifa ambalo ulininyima nafasi ya kuwa mmoja wa kuliletea maendeleo, Mh. Rais, utakumbuka kuwa ni zaidi ya miaka mitano sasa umenifanya niishi kwa shida tabu na masumbuko yote kwasababu ndogo tu ya kisiasa, ni zaidi ya miaka mitano sasa naishi maisha ambayo sikuwahi kuyaota toka nizaliwe, sina cha kujivunia na nimekuwa kama kifaranga kisicho na mzazi wake, miaka zaidi ya mitano ya uchungu, matesho na taabu kwangu ni zaidi ya miaka mitano ya raha, umaarufu wa kisiasa na faraja kwako.

    Mh. Rais katika dunia ya sasa, uvumilivu una mwisho kwakuwa hata miaka ya binadamu kuishi imepungua. Labda nirudi nyuma na kukumbusha yaliyonitokea wakati wa miaka hii mitano uliyoamua kujifanya mungu na kuniadhibu kwa makosa nisiyoyajua.



    1. Ulifanikisha kunitenga na jamii yangu, jamii ambayo ingenufaika na uwepo wangu kama binadamu lakini zaidi kama mtu ambaye ningeweza kutoa msaada mkubwa kwa jamii yangu, leo hii hata jamii yangu ikiniona hainiamini na wala kunihitaji kabisa, nimekuwa kama ndezi au nguruwe pori kila niendako nawindwa na kuonekana kama adui au msaliti, kitu ambacho ni wewe mheshimiwa mwenye vyeo na pesa ndio umesababisha, pesa zako zisizo halali ndizo ulizozitumia kama fimbo ya kunichapia, na hakika kwa miaka mitano na miezi kadhaa umenifanya nione dunia kama si sehemu nzuri ya mimi kukaa. Jamii hainitambua na wengine wanadai nimekufa, haya yote ni matakwa yako mkuu na wewe pekee na fedha na vibaraka wako ndio mnaojua nini maana ya yote haya.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    2. Umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kunitenga na Natasha, msichana kipenzi wa maisha yangu. Nikukumbishe tu kuwa Natasha hakuwa anahitaji wadhifa ama pesa ama chochote ili aweze kuwa msichana bora, Natasha alihitaji mapenzi ya kweli, kujaliwa na kulindwa, hayo ndiyo mambo aliyoyahitaji. Lakini kwa kushiba pesa ulibadili tafsiri ya mahusiano na mapenzi na kuiweka kama maagano ya kupendana na kushirikiana ya watu wenye kipato sawa tu, lakini sio kweli mkuu kwakuwa hata wewe ulikuwa na kipato cha chini kwa mujibu wa historia yako lakini ulimuoa mama Natasha akiwa ni mtoto wa Chifu. Wewe kunitenganisha na Natasha lilikuwa jambo moja lakini mbinu ulizozitumia kunitenganisha nae, zimeniletea maumivu makubwa katika maisha yangu yote, nilikuwa tayari kuwa na Natasha hata kama angekuwa ni mtoto wa masikini wa mwisho duniani. Mapenzi yangu kwa Natasha hayakuegemea wala kuangalia kipato chako au uzuri na weledi wa wake wa mambo ya maisha ila nafsi yangu ilikuwa tayari kuwa nae kwakuwa Natasha alikuwa na mapenzi ya kweli na si mbabaishaji. Kunisaidia kwa Natasha ilikuwa ni msaada wa kibinadamu ambao alijisikia yeye kuguswa toka ndani ya moyo wake kunisaidia pale nilipohitaji kusaidiwa, Natasha alikuwa ndiye kitu pekee na mtu pekee aliyekuwa amebaki kwenye maisha yangu. Nilimpenda na ninampenda Natasha licha ya mali na vyeo alivyokuwa navyo kipindi hicho na kwasasa. Naamini kabisa kwa sumu uliyomnywesha ya uongo, hila na dhuluma, Natasha amebadilika na kuwa ni mtu mwingine kabisa, iliniuma sana siku niliyomuona Natasha akilia kwa jambo ambalo sio la kweli, siku ambayo hila na ufedhuli wako uliyabadili mapenzi ya Natasha kwangu na kuwa chuki, siku uliyoacha ukweli upotee ili uongo na dhuluma yako itawale, lakini amini nakuambia, mungu si wako peke yako. Nimeishi kwa maumivu makubwa ya mapenzi kwa kipindi chote cha miaka mitano, nimehangaika kwakuwa tu nilimpenda mtu ambaye baba yake aliijua kuitumia dola na wadhifa wake kuniangamiza kabisa. KAMA ILIPANGWA MIMI

    KUWA NA NATASHA BASI JUA NI MUDA TU HAUJAFIKA.



    3. Umefanikiwa kwa asilimia zote kabisa kuipoteza elimu niliyoihangaika kwa maisha yangu yote niliyoishi kabla, umezima ndoto zangu zote na kila nilichokipanga kimeyeyuka mithili ya barafu liyeyukavyo ndani ya maji ya moto. Malengo na mipango yote imegeuka kuwa mfu na sasa ni historia ya uchovu wa fikra iliyotawala ubongo wangu. Mh. Rais nilikuwa mtoto wa kiume katika familia masikini sana ambayo hata pesa ya kula kuna muda ilitushinda, kipindi baba yangu anaumwa nililazimika kwenda kuchimba mashimo ya kuweka minara ya simu ili wachina wanilipe ujira wa shilingi elfu tano kwa siku nije nihudumie wazazi wangu, wakati wote huu nilikuwa nasoma. Nilihangaika kuwatunza wazazi wangu lakini sikufanikiwa kwakuwa muda wao wa kuishi hapa duniani ulitimia. Hata hivyo kazi iliendelea kuwa ngumu kwakuwa nikiwa chuoni nililazimika kuhakikisha marehemu dada yangu anakula na kwenda shule na hata kodi ya nyumba pia ilikuwa juu yangu. Juhudi zote hizi nilizofanya zilikuwa ni kwaajili ya kutimiza ndoto zangu, masika yalikuja na kiangazi kilitawala, changamoto za kimaisha na mchoko wa wa akili haukunifanya niache kupafikiria pale nitakapo kufika. Nilikuwa na ndoto kubwa kama wewe ulivyowahi kuwa na ndoto ya kuitawala Tanzania na bila kuingiliwa na mtu yoyote yule umeweza kutimiza ndoto zako. Nikukumbushe kuwa kwasasa elimu ambayo nina ushahidi nayo ni elimu yangu ya kidato cha sita tu, vyeti na kumbukumbu zote za elimu yangu ya sheria umeipoteza kama moshi wa sigara upoteavyo angani, umenifanya niishi maisha ya kuhisi naota siku zote, maisha ya ukimbizi ndani ya nchi niliyohangaika kuuiimba na kuisifia siku zote za maisha yangu ya kabla. Sijutii kabisa na sitegemei kabisa katika maisha yangu kuwa nitajuta kujuana au kukutana na Natasha. S I J U T I I. Ila najuta na nitajuta daima kuishi dunia yenye watu kama wewe. Umefuta kila kitu nilichokiandika kwa wino wa ufikiri wangu, umechoma kila kitu nilichokisumbukia usiku na mchana kukiweka sawa, umeharibu imani na uelewa wangu juu ya mambo ya msingi, umeruhusu ujinga wa fikra mgando zitawale maamuzi yako na kutenda kwa jinsi nguvu ya pesa na udhalimu wa vyeo ulivyokuelekeza badala ya utashi na busara ya kibinadamu inavyokuambia. Umeifanya hasira na mafikirio yako mabovu kuwa ndo msingi wa maamuzi yako ukasahau haki za wengine na kuharibu ya wale wasiokuwa watoto wako au ndugu zako. Umeua wengi katika kutafuta umaarufu wa kisiasa na nguvu ya kifedha, mikono yako imejaa damu nyingi za watu wasio na hatia. Leo hii ungekuta pengine ndoto zangu za kuwa na msingi bora wa maisha na Natasha imetimia, pengine ndoto yangu ya kufuta dhana ya kijana masikini kubaki kuwa masikini ingekuwa imetimia. Ningekuwa moja ya watu ambao wangetetea maslahi na haki ya wananchi lakini kwakuwa wewe ni tajiri na mtu mwenye cheo ukajigeuza Herode na kuifanya Tanzania ni nyumba yako. Nimeteseka sana kwa kuishi mbali na yale niliyokaribia kuyatimiza.



    4. Ukumbuke kuwa, umenidhalilisha na kunifanya nionekane kama muhalifu na mtu nisiye na maadili, ulinifungulia kesi ya kubambikiwa ya madawa ya kulevya, kitu ambacho hakikuwa cha kweli, lakini kwa ustadi mkubwa ulifanikiwa kupenyeza fikra hizo kwa jamii nzima na kwa Natasha, ulifanikiwa kunitumia kama mtaji wa kisiasa pale ulipoamua kutangaza kuwa natumiwa na wapinzani wako wa kisiasa. Unafahamu fika kuwa si kweli uliyoyaongea yote, unafahamu fika kuwa mimi nilikuwa kijana mwema na mtiifu kwa wakubwa zangu na wadogo zangu, sikuwa na kashfa yoyote ile wala kuwahi kufikishwa polisi hata kwa kutoa ushahidi wa jambo lolote, niliishi bila makuu wala bila kugombana na mtu katika maisha yangu yote, hii ilikuwa ni katika kuepuka mambo yasiyo ya msingi kuniharibia mfumo na utaratibu wa maisha yangu. Lakini kwakuwa ulikuwa na nguvu zaidi ya Goliath na ulikuwa na pesa zilizokuwezesha kuwa kila mahali wakati wowote utakao, ukazitumia katika kufifisha ndoto za kijana ambaye hakuwa na madhara hata kwa mfanyakazi wako wa ndani. Mimi ni sehemu ndogo sana ya jamii ya watanzania, ni sehemu ndogo sana inayotengeneza ukamilifu wa utanzania na Amani ya kitanzania, kuondolewa kwangu katika jamii hii hakuleti athari yoyote ila ya wazi lakini athari ya kificho, itakumbukwa daima na nafsi zijuazo ukweli na kuuishi ukweli kuwa umeingia madarakani kwa dhuluma na damu ya kila aliyeonekana kuwa kikwazo mbele yako, ulitengeneza uongozi kwa damu za watu na dhuluma ya haki, ulikiuka misingi ya utawala bora na maadili ya uongozi na kujitwika mzigo wa ubepari na udikteta uliotukuka. Nikukumbushe kauli ya mwanafalsafa wa kimarekani aliyeitwa Joe Batten yeye alisema “THE FIRST TASK OF A LEADER IS TO KEEP HOPE ALIVE”(Kazi ya kwanza ya kiongozi ni kuyafanya matumaini yaishi), hii ni kazi ambayo wewe kama kiongozi ulikuwa nayo, lakini ulishindwa kuyafanya matumaini ya watu wengi yaishi na badala yake ulituvunja moyo wachache kwa faida yako binafsi. Ulinizushia kesi nyingi lakini moja wapo ni ya kutaka kumua msichana kipenzi nimpenda, na ulifanikiwa kwa asilimia zote kutumia vyanzo vyako na vijana waliofundishwa kuutengeneza uongo ufanane na ukweli kunibebesha mzigo wa dhambi isiyonihusu, sikuogopa kwenda jela au kunyongwa ila niliogopa na kutetemeka pale nilipogundua kuwa ninaweza kufa huku Natasha akibaki kujua kuwa kweli nilitaka kumuua. John C. Maxwell aliwahi kusema “A LEADER IS THE ONE WHO KNOWS THE WAY, GOES THE WAY AND SHOWS THE WAY”(Kiongozi ni yule aijuaye njia, aiendaye njia na aonyeshae njia), Je wewe kama Rais leo utaonyesha njia gani ya kupinga ukatili wa watu wasio na uwezo wakati wewe waijua njia ya dhuluma? Ingekuwaje ingekuwa ni mtoto wako anafanyiwa hayo uliyonifanyia mimi?CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    5. Mwili wangu umejaa majeraha mengi na hata siwezi kukaa bila shati mbele za watu na wakaamini kuwa mimi si jambazi. Nimepigwa sana na kuonewa kwaajili ya wewe, umenitupa kwenye nchi ya watu na sikuwa na Amani kwani kila aliyeniona alijua sikuwa mtu mwema, umenifanya nisiaminike na watu walionipa msaada mkubwa nchini mwao kwakuwa tu sikueleweka historia yangu wala mambo yangu, kama haikuwa wewe kuninyanyang’anya kila kitu katika maisha yangu, kama haikuwa nguvu ya pesa uliyolewa na kujisahau kisha kwa makusudi ya ulemavu wa akili yako ukaamua kunifanya kondoo wa kafara basi leo hii nisingekuwa na majeraha haya, kwasasa nasubiri siku ya kufa kwakuwa ugonjwa wa tetenasi ulioshambulia mwili wangu hauwezi kutibika tena kwa gharama ambayo naweza kuilipia, mwili wangu umefadhaika na kudhoofika kwakuwa tu wewe uliamua kunifanya mimi kama mnyama wa kuchinja ili ufanikiwe, mlinipiga na kunichoma na vitu vyenye ncha kali bila kunitibu, mliniumiza na kunitumatupa kama jani la muembe lidondokavyo toka mtini. Hukujali afya yangu wala thamani yangu kama binadamu mwenzio ila maslahi yako na uchu wa madaraka viliusonga ubongo wako mchanga usiweze kuwaza na kufikiri. Mh. Rais mwanafalsafa wa kimarekani Elbert Hubbard aliyeishi kati ya mwaka 1856-1915 aliwahi kusema “ONE MACHINE CAN DO THE WORK OF FIFTY ORDINARY MEN. NO MACHINE CAN DO THE WORK OF ONE EXTRAORDINARY MAN” (Mashine moja inaweza kufanya kazi ya ya watu hamsini wa kawaida. Hakuna mashine inayoweza kufanya kazi ya mtu mmoja asiyewakawaida), mimi si mtu wa kawaida, mlifanikiwa kwanamna mlizoweza kuniangamiza kabisa, lakini hamjaweza kuangamiza kile ninachokiamini na kile nikijuacho, uanasheria na ujuzi wangu wa sheria haukuwa kwenye vyeti mlivyonidhulumu ila sheria ipi kichwani mwangu na kwenye damu yangu. HAMTAWEZA KUNIMALIZA BILA YA NYIE KUUMBUKA.



    6. Mh. Rais, nikukumbushe maneno ya mwenyekiti wa Vincent Astor Foundation ya nchini marekani, bibi Brooke Astor aliyewahi kusema “POWER IS THE ABILITY TO DO GOOD THINGS FOR OTHERS”(Nguvu ni uwezo wa kufanya mambo mema kwa ajili ya wengine), wewe katika uongozi wako hukuamua kufanya mambo mema kwa wengine bali uliamua kuruhusu tu wale waliokubaliana na wewe na wale wasiokujua waendelee kuishi ila wale walioleta changamoto katika maisha yako uliamua kuwatanguliza kuzimu. Nikiwa nchini Madagascar nilikuwa mvuvi na sio mwanasheria, nilikuwa mwanachi wa Madagascar na sio mtanzania, nilikuwa mkimbizi na sio mtu huru, niliishi kwa kuijua leo yang utu na sio kesho yangu, maisha kwangu yalikuwa ni tanuru la moto lililoichoma ngozi yangu kila dakika niliyokuwa ndani yake, tabu machungu na kudhalilika ilikuwa sehemu ya maisha yangu wakati

    wewe ukiwa unastarehe ikulu kwa kodi ya watanzania masikini.



    7. Napenda kukukumbusha maneno ya muandishi mashuhuri James A. Baldwin, aliyesema “LOVE DOES NOT BEGIN AND ENDS THE WAY WE SEEMS TO THINK IT DOES, LOVE IS A BATTLE, LOVE IS WAR, LOVE IS GROWING UP” ( mapenzi hayaanzi na kuish kama tunavyofikiri, mapenzi ni mapigano, mapenzi ni vita, mapenzi ni kukua), nilipoanza mapenzi na mwanao niliyategemea changamoto na vita inayohusu mahusiano yangu mimi na yeye, ila sikutegemea vita na mapambano ya dhuluma na chuki kama uliyoyafanya wewe.

    Nimekuandikia waraka huu kukukumbusha juu ya machache kati ya mengi uliyonifanyia, nimerudi kutoka Madagascar na nina uhakika unayotaarifa hiyo, kama huna taarifa basi nakutaarifu kuwa nimesharudi na niko Afrika kwa sasa, nilishaanza maisha yangu na kujaribu kusahau yaliyowahi kunitokea lakini sikufanikiwa kwakuwa baada ya kuonana na Natasha katika foleni ya ubungo, nilirudia machungu baada ya kupigwa na wananchi wakidhani ni mwizi kisa tu nilikuwa nikimkimbia mtu aliyedhani mimi ni adui yake. Umeniumiza sana katika maisha yangu na sasa nategemea kufa siku yoyote kama sitapata matibabu ya haraka..ila sitakufa kabla wewe hujafa... mh, mtunzi wa mashairi wa kispanyola Miguel Cervantes aliwahi kusema “TO BE PREPARED IS HALF VICTORY”(Kujiandaa ni nusu ya ushindi), najiandaa kufa ila najiandaa pia KUKUUA, ni vizuri na wewe ukajiandaa kufa kama mimi ninavyojiandaa kufa, uwezo wangu wa kuvumilia umefika mwisho na hakuna chochote cha kunipa moyo tena, ila sitakubali kuondoka duniani kabla ya kuhakikisha wewe haupo. Ulianzisha mapambano ambayo yamemaanisha mwisho wa matumaini yangu, ulifanya matumaini yafe na sasa kilichobaki ni uchovu. Mcheza mpira maarufu nakocha wa zamani wa Marekani anayeitwa Vincent Lombardi aliwahi kusema “LEADERSHIP IS BASED ON SPIRITUAL QUALITY;THE POWER TO INSPIRE OTHERS TO FOLLOW” (Uongozi ni ubora wa kiroho, yani nguvu ya kuwavutia wengine wakufate), uongozi wako wa kibabe na kiuaji umenivutia na mimi niwe muuaji.



    MWISHO: James A. Baldwin aliwahi kusema “THE MOST DANGEROUS CREATION IN ANY SOCIETY IS A MAN WITH NOTHING TO LOSE” (Kiumbe hatari katika jamii yoyote ni mtu asiye na chakupoteza)..Natasha alikuwa ndio kitu pekee nilichobakiwa nacho na kwakuwa sasa sina cha kupoteza YOU WILL NEVER TOUCH ME MR. PRESIDENT (Hutaweza kunishika Mh. Rais),,,IMARISHA ULINZI WAKO KWAKUWA MUDA WOWOTE NA SAA YOYOTE NITAUFATA UHAI WAKO NA HAKUNA ATAKAYENIZUIA. Ukipenda sambaza waraka huu kwa vyombo vya habari ili nchi ijue kuwa umebakiza mda mchache kufa.

    NI MIMI FRANK.”

    Niliufunga vizu ule waraka na kuutumbukiza kwenye ile bahasha kisha niliiandika jina la Rais na sio cheo chake, niliupeleka ofisi za EMS nikalipia na safari ya kuletwa ule waraka kwa njia ya ndege ilianza kisha nilimtumia nakala nyingine kwa nyia ya anwani yake ya barua pepe niliyoipata kwenye tovuti ya ikulu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “ Kama duniani tukisema jicho kwa jicho, yani atakayekukosea na wewe ulipize kisasi basi dunia nzima itakuwa na vipofu. Kuna muda katika maisha yetu inapotokea mtu anakushinda kwa kuongea basi busara ni wewe kujitahidi kwa kadiri uwezavyo umshinde kwa kunyamaza. Kisasi cha kweli ni kile cha kujitahidi usiwe kama huyo aliyekutendea baya. Kama alikuulia ndugu yako na sasa yeye ni muuaji basi jitahidi na wewe usiwe muuaji. Kusamehe ni jambo la msingi kwakuwa kila mtu anahitaji kusamehewa kwa kutokuwa mkamilifu. Kushindwa kusamehe ni sawa na kunywa sumu ya panya alafu unakaa ukisubiri panya afe…” SOMA, TAFAKARI, JIFUNZE TENDA”,,HII NI SEHEMU YA KUMI NA MOJA,,,ANDIKA HIVI..

    **NATASHA ANASIMULIA**

    Wengi wanadhani kuwa na pesa na vyeo lukuki ndio furaha tosha katika maisha, lakini si kweli, pesa ni sehemu ndogo sana ya furaha ya kweli, upendo na Amani ni kitu pekee kinachoweza kumfanya mtu ajisikie wa thamani katika hii dunia. Nilikuwa waziri na mke wa kijana tajiri, nilikuwa nimetoka kwenye familia yenye pesa na kikubwa nilikuwa mtoto wa rais wa nchi, nilikuwa namiliki nyumba nyingi jijini na mali kedekede nilikuwa na miradi na mshahara mzuri, mapato yangu kwa mwezi pamoja na mshahara wangu ilikuwa ni zaidi ya milioni 90, sikuwa na matumizi makubwa kwakuwa nilikuwa nikihudumiwa karibu kila kitu na serikali, mume wangu alikuwa ni mtu mwenye pesa nyingi na ambaye hakuhangaika hata siku moja kujua kuhusu mshahara wangu. Lakini mali zote hizi na utajiri na vyeo pamoja na elimu niliyokuwa navyo vilishindwa kuniletea furaha ya kweli na Amani ya moyo.

    “nataka kuondoka hapa hospitali” nilimuambia Nicholas aliyekuwa amekaa pale pembeni yakama vile malaika asubiriaye wito wa mungu.

    “hapana huwezi kuondoka mke wangu kwakuwa bado daktari bado hajakuruhusu” aliniambia hukua akinibembeleza pale lakini nilianza kulia bila kujua kwanini nililia kiasi kile, sikutaka kumuambia Nicholas chochote kwakuwa nilijua angeweza kufanya chochote ili ukweli usijulikane.

    “hapana sio lazima daktari aondoke, nataka kuondoka najisikia niko sawa, tafadhali naombeni mnitoe hapa hospitali nikaendelee na kazi zangu” niliongea hayo huku machozi yakizidi kunitoka, nililia sana kusikia Haleed amefariki,siku iyo jioni saa 10 nilitoroka pale hospitali na kuchukua tax mpaka kwangu, Nicholas hakuwepo, nilivaa vizuri na kuamua kuondoka mpaka kwa Haleed ambapo nilikuta watu wakiwa wanaelekea makaburini. Sikuamini macho yangu kuwa msaada pekee nilioutegemea ulikuwa umeondoka duniani, sikujua pa kuanzia wala pa kuishia. Matumaini yote yalipotea na mshumaa wa matumaini uliokuwa ukiwaka sasa ulikuwa umezimika na mbele lilikuwa giza nene lisilonipa matumaini ya kuuweka ukweli wazi. Watu walikuwa wanalia sana na hiyo ilinifanya nijione kama vile nina hatia.

    “habari yako mheshimiwa” ilikuwa sauti ya mtu aliyekuwa nyuma yangu, niligeuka na hapo nilimuona kijana mrefu akiwa amevaa suti nyeusi na miwani nyeusi.

    “nikusaidie nini” lilikuwa swali la kwanza kumuuliza kabla ya salamu au chochote.

    “nimekuja kukufata” aliniambia huku akiangalia upande wa pili wa barabara kana kwamba alikuwa akinielekeza kuwa nielekee huko.

    “wewe ni nani” nilimuuliza na yeye aliingiza mkono mfukoni kisha alitoa kitambulisho kilichomuonyesha kuwa ni kijana wa usalama wa taifa.

    “siondoki hapa” nilimjibu na kuendelea na kuangalia kule watu walipokuwa wakielekea.

    “madam kuna vitu nahisi unahitaji kuvichukua” aliniambia tena na hapo niliamua kumgeukia kisha nilimuona akielekea kule kwenye lile gari na mimi nilimfuata, nilipofika pale alinifungulia mlango namimi niliingia ndani.

    “madam nisikilize kwa makini, uko hatarini haijalishi wewe ni nani na baba yako ni nani, unatakiwa kuwa makini kuliko kawaida. Najua Frank alipo, lakini siwezi kufika wala kuelewa njia, naelewa nchi tu na atakuja siku yoyote kumaliza alichoanzisha baba yako. Haleed ameuliwa kwa maelekezo ya baba yako na kwa ushauri wa mume wako baada ya wao kugundua kuwa alikuwa akikuelekeza juu ya mambo yaliyokuwa yanahatarisha maisha yao na biashara zao, sina mengi ya kuongea ila kuwa makini, hii begi hapa chukua utaifungua ukifika kwako au popote, nitakupigia simu nikihitajika kufanya hivyo ila vinginevyo sitarajii kuonana tena na wewe” alinikabidhi mkoba wa kike kisha alinipa mkono akini kabla sijashuka kwenye gari nilimuuliza tena swali.

    “Frank yuko wapi?” nilimuuliza huku nikiyazuia machozi yangu.

    “madam mimi sijui alipo ila alionekana Kenya mara ya mwisho alipoonekana pia aliandika barua kwenda kwa rais na sasa itaanza kujadiliwa mda wowote, zaidi ya hapo hakuna nilijualo” alinijibu kwa sauti ya kumaanisha kuwa hakujua chochote.

    “Unamjua Haleed?” nilimuuliza huku nikilia, nilisikia uchungu kila nilipomkumbuka Haleed, alikuwa kijana mtiifu na wakati wote nilipojuana nae alikuwa makini kufanya kazi zake na mwepesi katika kutafuta taarifa na ulinzi.

    “Niliajiriwa ndani ya hii taasisi miaka miwili baada ya Haleed kuajiriwa, ye ndo aliyenipokea na kunifundisha mambo mengi sana juu ya hii kazi, alikuwa mwalimu wangu kipindi naanza kazi na hata siku moja kabla hajafa niliongea nae, siku ambayo anauwawa niliona kila kitu, wakati naenda kumuangalia pale hospitali, nilipofika na kukuta kile chumba kimefungwa na mapazia yote yamefungwa nilipata wasiwasi na kutafuta namna ya kujua kwanini kumefungwa, nilifanikiwa kuona ndani baada ya kuhangaika kidogo, niliona akiuwawa lakini sikuwa na la kufanya” aliongea huku nikishuhudia kabisa machozi yakimtoka lakini alikuwa akiyazuia.

    “na Frank umemjuaje” nilimuuliza maswali yale lakini sikutaka majibu yake kwakuwa yangeniumiza.

    “Frank nilisoma nae, namfahamu vizuri sana, hakuwa rafiki yangu lakini nafahamu juhudi zake na namjua ni mtu mtaratibu” nililia sana kwa kila alichoniambia lakini hatukuwa na muda wa kuongea sana, nilishuka kwenye gari na kwenda mpaka nilipokuwa nimeegesha gari yangu, nilifungua mlango na kuingia ndani ya gari ghafla nilishtuka baada ya kusikia sauti ya mtu ndani ya gari;

    “Mke wangu usifanye hivyo, unahitaji matibabu na sio kuja msibani” alikuwa Nicholas na sijui aliingiaje kwenye gari yangu.

    “Nicholas umeingiaje kwenye gari yangu?” nilimuuliza kwa sauti yenye mshituko.

    “nimetumia funguo ya akiba” alinijibu huku akitabasamu.

    “Nicholas hii ni gari yangu, huna ruhusa ya kufungua na kuingia ndani kama mimi sipo labda iwe nimeiegesha nyumbani lakini sio ukute gari yangu nje ya nyumbani uifungue ndani na kuingia, niheshimu kama mkeo. Ungepiga simu ili nije hapa kama ulitaka kuniona lakini si kuingia kwenye gari yangu bila mimi kujua, usirudie tena sijapenda” niliongea kwa hasira na huku machozi yakinitoka, kila nilipomuona Nicholas kwasasa nilimuona kama shetani, sikuwahi kumgombeza au kumropokea toka anioe lakini leo hii yeye mwenye hakuamini.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “nisamehe mke wangu kipenzi, sikumaanisha kukuudhi, ila nataka urudi hospitali ukapate matibabu zaidi, daktari ameshauri urudi hospitali na pia wewe ni waziri si vyema kuwa unatembea peke yako au kuja maeneo ya hatari peke yako, kama hawakuwekei walinzi mimi binafsi nitakuwekea walinzi, unaumwa na kuendesha gari mwenyewe sio vizuri, unaweza kusababisha ajali, sitaki kabisa” aliongea kwa sauti ndogo ya upole iliyojaa na kutawala ndani ya gari lakini iliyokuwa kelele ndani ya masikio yangu, yeye alikuwa kiti cha nyuma cha gari ile na mimi nilikuwa kwenye kiti cha dereva, nilimsikiliza huku nikiwa natazama bado ile nyumba ya Haleed kwa mbali na kukumbuka siku aliyonileta pale na kunionyesha ile video ya hawa mbwa..

    “Natasha tumeelewana?” alirudia kuuliza baada ya kuona nilikuwa kimya huku machozi yakinitoka.

    “Nicholas, nilipopata ajali juzi nilikuwa naendeshwa na dereva mzoefu, Haleed alikuwa dereva mzoefu kabisa hiyo haipingiki, alikuwa akiendesha kwa mwendo wa kawaida lakini haikujulikana ilikuwaje tukapata ajali, kwaiyo mimi kudhurika sitadhurika au kupata ajali kwakuwa eti naendesha gari peke yangu, hapana nitadhurika au kupata ajali pale watakapoamua iwe hivyo, sihitaji walinzi, mungu ndiye mlinzi pekee muaminifu, ndiye dereva pekee atakayenikinga na ajali za kutengeneza, kwahiyo usijali mume wangu, usijali kabisa, huu ni mwanzo wa maisha yangu pia” niliongea huku nikitokwa namachozi, nilikuwa nimejawa na hasira hasa kwakuwa Nicholas alijifanya kama vile hajui kilichotokea.

    “Sijakuelewa” aliniuliza na mimi niligeuka nikavuta kiti kikarudi nyuma na kumshika kisha nilimbusu na kumtazama usoni.

    “Nakupenda sana mume wangu”, nilimtazama kwa muda wa dakika mbili alikuwa kama amepigwa na butwaa.

    “Nicholas nahitaji kuondoka, naomba unipishe kwenye gari langu au kama tunaondoka wote tuondoke”. Nilimsemesha huku nikiwasha gari gari tayari kwa kuondoka, nilikuwa na maumivu makali sana sehemu ya mbavu lakini sikutaka kuonyesha kama nina hayo maumivu, Nicholas alishuka kwenye gari na mimi niliondoka pale na kwenda hadi ofisini, nilipofika niliingia ofisini kwangu, nikafunga mlango, nilikaa nikalia sana na ghafla nilipitiwa na usingizi nikiwa pale kwenye kiti, nilishtuka baada ya simu ya ofisini kuanza kuita.

    “Hallo” niliipokea kwa sauti ya uchovu,

    “Mheshimiwa kuna mtu amepiga simu anataka kuongea na wewe” ilikuwa sauti ya katibu muktasi wangu.

    “sihitaji kuongea na mtu yeyote,,” nilimuambia kwa ile sauti yenye mchoko.

    “amesema ni muhimu” aliniambia vile na hapo nilikaa sawa na kumruhusu aniunganishe na ile simu.

    “madam ni mimi” niliishikia ile sauti na lile jina aliloniita nikawa nimeshaelewa kuwa yule alikuwa ni yule kijana.

    “madam gari yako imeweka ‘car tracking device’ ya kuwafanya wajue kila unakoenda, imefungwa vinasa sauti huko ndani kwaiyo kuwa makini sana” kabla sijamuuliza chochote simu ilikuwa imeshakatika, nilijaribu kumwambia yule katibu muktasi atafute ile namba lakini hakuweza kuipata. Nilirudi tena ofisini na kuufunga mlango kisha nilifungua ule mkoba na kutazama ndani, nilikuta boksi dogo la nokia ya tochi nikalifungua na kukuta ‘memory card’ haraka haraka niliwasha ngamizi yangu pale na kuichomeka ile memory card.

    “jamani nimewaita hapa kwakuwa kuna dosari ambayo itatugharimu wote. Haleed ameamua kutusaliti na kuamua kuleta mambo yatakayoweza kuhatarisha Amani ya nchi yetu. Haleed anamkanda aliourekodi ukituonyesha tukipanga kwenda kummaliza yule kijana Frank na amepanga kumpa Natasha huo mkanda, ili atambue ukweli wa kila kitu, nyie wote ni mashahidi wa namna ambavyo tulitumia gharama kubwa na ufundi kufanikisha lile jambo hivyo kuendelea kuona usaliti huu unatugharimu ni kulea ujinga.” Sauti hiyo ndiyo nilianza kuisikia pale nilipochomeka ile ‘memory card’, ilikuwa sauti ya baba yangu, haikuonyeshwa video lakini niliweza kuitambua iyo sauti, niliendelea kusikiliza;

    “sasa tunafanyaje” iliuliza sauti ya mtu ambaye sikumtambua.

    “ni rahisi sana, wote tuna uzoefu na mambo haya, tunachofanya hapa ni ‘perfect murder’(kijasusi ni kumuondoa mtu bila kuacha ushahidi au wasiwasi wa mtu kuhoji), tunafahamu wote kanuni za ‘perfect murder’ na niwakumbushe tu kuwa 1. Hutakiwi kuua mbele ya hadhara au sehemu yenye watu, na unatakiwa uwe umevaa ‘gloves’,,2. Silaha lazima iwe ile isiyoacha maswali..3. Muuaji mwenyewe yani wewe unayeua jitahidi sana kufanya mauaji yaonekane kama ni mtu alijiua mwenyewe au ni uzembe wake,,4. Ondoa ushahidi, usiache ushahidi wa chochote hata kipande cha nywele yako, ukifanya kinyume itakuwa ni ‘Imperfect murder’..5. Ondoa maiti, unaweza kuanzisha moto kwa mkubwa utakaounguza kila kitu, au kumtosa baharini,,6. Chochea lawama kwa mtu au kitu kingine ili jamii imtazame yeye kama muuaji. Hizi ndizo mbinu, lakini kwenye hili tutatumia ajali, ili Haleed apelekwe hospitali kisha kule tutachomoa mipira ya oksijeni atakayokuwa amewekewa pale ambapo tutakwenda kumuona,gari ya kusababisha ajali itakuwa ni gari kubwa na moto utawaka ili kuunguza kila kitu, tunakijana wetu anakuja kufanya cleanup (kusafisha) ili ahakikishe hakuna ushahidi kesho yasubuhi” iliongea sauti ile na kutoa maelezo marefu, niliirudia tena kipande kile na kugundua kuwa yule aliyeongea alikuwa Nicholas, nilikuwa nimelowa kwa machozi na jasho lakini niliendelea kusikiliza.

    “Kwaiyo utaratibu ukoje” aliuliza mtu mwingine.

    “Kesho nitakwenda kwenye sherehe na mke wangu, na kwakuwa tayari wana urafiki na ushahidi mwingine mke wangu anatembea nao kwenye begi yake basi huo ndo utakuwa wasaa, Haleed atapangiwa kwenye hotel ya Kempisky kesho ili kuwapa muda wakutane, kisha baadaye nitamuomba amrudishe, huku nje mmoja wenu ataweka ile ‘tracker’ na mtakuwa na GPS ili kujua wanakopita, hakikisha mnagonga upande wa dereva, narudia tena,,kwenye gari kutakuwa na mke wangu kipenzi, na ni waziri na ni mtoto wa rais hivyo asiumie zaidi ya kupata mshtuko, huo ndio utaratibu, no names, we go dark (hakuna majina, hii ni siri).” Sikusikia tena kitu kingine zaidi ya vitu kuvutwa ikimaanisha kikao kile kiliisha, huku nikitokwa na machozi kama mtoto nilifungua tena lile boksi na kukuta ‘memory card’ nyingine kisha niliiweka na hii ilikuwa ikionyesha siku Haleed alivyouawa pake hospitali mbele ya Nicholas, niliona kijana mmoja akichomoa ile mipira ya oksijeni aliyowekewa na taratibu Haleed alianza kuhangaika na baadaye alikata roho kisha yule kijana alirudishia ile mirija, kisha Nicholas alimuamuru yule kijana amuite dokta na ikaonekana kama dokta alikuja na kumuambia kuwa Haleed ameshakata roho, na video hiyo iliishia hapo.

    Tayari nilikuwa nimeshachoka na machozi yalizidi kunitoka ila sikujua wapi pa kuanzia, sikuwa tayari kuonyesha tena kuwa nilifahamu kilichokuwa kikiendelea kwa kuwa nilijua itakuwa ni hatari, ila sasa nilijielekeza katika kutafuta suluhisho la namna ya kumpata Frank na kumuokoa.

    “ngrii,,,ngrii” ilikuwa simu ya mezani ikiita, niliipokea na kusikia sauti ya baba yangu.

    “habari Natasha” alinisalimu kwa sauti ya unyonge.

    “Salama shikamoo muheshimiwa” aliitika na baada ya kuniuliza maswali mengi kuhusu afya yangu alinieleza sasa kilichomfanya anipigie simu;CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “nina kikao hapa ikulu naomba uwepo ni dakika kumi kuanzia sasa” aliongea hivyo na mimi sikumuonyesha kukataa au kuwa sikuwa kawaida, sikuwa na jinsi zaidi ya kuwa kawaida nikiwa mbali na watu kwakuwa bado nilihitaji kupata ushahidi zaidi ingawaje sikujua kabisa ule ushahidi nitaupeleka wapi. Nilitoka ofisini na kumpigia simu dereva wangu kisha alikuja na sasa niliamua kutumia gari la ofisi, nilifanikiwa kufika ikulu japo nilikuta nimechelewa kidogo lakini watu walikuwa wakinisubiri, nilipotazama haraka nilimuona mkuu wa polisi, mkuu wa jeshi la wananchi, mkurugenzi wa usalama wa taifa, waziri wa ulizi, waziri wa mambo ya ndani, mkurugenzi wa makosa ya jinai na mkuu wa kitengo cha upelelezi wa jeshi la polisi, kisha kulikuwa na vijana nane ambao nilitambulishwa kwamba ni makomandoo kutoka jeshi la wananchi. Hofu ilinijaa lakini sikuwa nelewa kwanini niliitwa pale, nilikabidhiwa karatasi iliyokuwa inakurasa tatu noisome, nilishtuka baada ya kuisoma kwakuwa ilikuwa ni waraka ulioandikwa na Frank kwenda kwa rais, lakini ule waraka ulinishangaza kwakuwa Frank alikuwa anakiri kuwa alijaribu kuniua akashindwa lakini sasa hivi alikuwa ajipanga kufanya shambulio kubwa nchini Tanzania, hakueleza sababu ya yeye kufanya hivyo lakini alisema tu kuwa atafanya hivyo siku yoyote, nilikuwa kama nimechanganyikiwa lakini niliomba ruhusu kidogo nikatoka na hapohapo nilikimbia hadi ofisini kwa baba yangu, nilipoingia nilifunga mlango kisha nilianza kupekea kwenye makaratasi yake, baada ya kupekua sana sikuona chochote ila baada ya kutazama chini ya meza niliona bahasha iliyokuwa imeandikwa anuani yake, niliifungua ndani na nikakuta waraka wa Frank wenye kurasa saba, niliufungua na kuutoa nakala palepale kwakuwa kulikuwa na mashine ya kunukulisha. Kisha niliingiza ndani ya nguo yangu na kutoka nje taratibu, nilikwenda mpaka kwenye kikao na nilikuta wameshaanza, na mimi nilikuwa nikimsikiliza yule komandoo mmoja kijana akielezea;

    “,,,kwaiyo hapa ili tuweze kupambana lazima tujue yeye ni ‘Mass Murder’ yani anaweza kuwa ni muuaji ambaye anaweza kuwa anaua watu zaidi ya wanne kwa wakati mmoja kwa eneo moja au ni ‘Spree Killer’ yani muuaji anayeua watu wawili au zaidi katika maeneo miwili tofauti lakini kunakuwa hakuna cooling off (hakuna kupumzika), au ni ‘Serial Killer’ kwamba anaua watu watatu au zaidi katika matukio tofauti lakini huwa yeye ana ‘cooling off’ (anapumzika kati ya tukio moja na lingine), na hawa wauaji wa kundi hili huwa wanachagua watu wa kuua na anakuwa na orodha na huwa ni watu makini wasioweza kujulikana, na lazima tujue kama ni ‘Serial Killer’ je ni ‘visionary’ yani anaua kwakuwa anasikia sauti ndani yake zikimuamuru au watu Fulani, hawa wengi ni wenye matatizo ya ukichaa au mapepo na matatizo mengine ya kisaikolojia, au tujue ni ‘mission oriented’ yani anayeua kwa kuwalenga watu Fulani ambao anaamini hawana faida kwa dunia au nchi au eneo Fulani na anaamini wao wakifa maisha yatakuwa sawa, au yeye ni ‘Hedonistic Killer’ yani anaua kwakuwa anasikia raha kuua na hawa mara nyingi haui mpaka ambake huyo anayemuua au afanye naye mapenzi, au ni ‘power oriented’ kwamba anaua ili aonyeshe nguvu yake juu ya wale asiowapenda.” Alimaliza kuelezea na sasa alikwenda kukaa kisha wote kwa pamoja walikubaliana kuwa Frank ni muuaji ambaye anataka kuua kwakuwa hawapendi watu waliokuwa ndani ya serikali, walikubaliana kuwa watatuma wapelelezi na makomandoo kumi na tano kwenda Kenya eneo la Nyahururu na Garisa nchini Kenya ambapo ndipo inasemekana waraka huo ulitokea, na waliwasiliana na uongozi wa Kenya na kupata kibali cha kuingia nchini Kenya, kikao kilipoisha nilitoka haraka na kwenda ofisini kwangu kisha nilirudi tena mpaka ikulu na kukabidhi barua ya kujiuzulu rasmi cheo changu cha uwaziri, baba yangu alionekana kama hanielewi lakini sikumpa muda nilitoka na kurudi nyumbani kisha nilipanda kwenye ile ngazi ya bafuni na kwenda kule juu ila nilishangaa baada ya kukuta ni kweupe na hakukuwa na kitu, nilibadilisha nguo na hapo simu yangu iliita nilipopokea alikuwa yule kijana.

    “nini mpango wako” lilikuwa swali la kwanza kabla ya kusalimiana.

    “Sijui hata, nimejuzulu uwaziri” nilimuambia huku nikihema kwa kasi.

    “umefanya vibaya kwakuwa hatutakuwa na taarifa kamili juu ya kinachoendelea ila kikubwa ni kuwahi Kenya kabla wao hawajamuwahi Frank” aliniambia na kuniomba tukutane Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere muda mfupi ujao kwa safari ya kuelekea Kenya, kisha alikata simu.

    Nilivaa hijabu nyeusi na miwani iliyoficha kabisa mwonekano wangu, nilibeba kiasi cha pesa milioni nane, kisha nilishika njia kuelekea Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere, nilifika pale na yule kijana alinipigia simu na kunielekeza sehemu ya kuchukua tiketi yangu, nilipokuwa nikitoka kuchukua tiketi niliona watu wengine kule wakiingia kwenye ndege na ndege ilianza kupandisha ile ngazi ikiashiria kutaka kuondoka, nilipotazama kwa makini mtu wa mwisho nilionekana kumfahama, nilikimbia mpaka pale lakini ndege ilishaanza kuondoka, nilipiga kelele yuele jamaa aliyekuwa akiongoza ndege pale aligoma kuacha kuiruhusu na ndipo nilipoamua kuvua ile miwani na kutoa kitambaa kile kichwani, aligundua kuwa nilikuwa waziri na hapo alimuonyesha yule rubani ishara ya kusubiri, polisi walishafika pale na nilieleza kuwa kuna mtu ndani ya ndege nilikuwa nikimuhitaji kwakuwa ofisi yangu ilikuwa na shida naye, walifatilia mtu wa mwisho kuingia na walipomleta alikuwa ni Beatrice.

    “Unaenda wapi?” nilimuuliza kwa lugha ya kingereza.

    “Narudi kwetu, nimekata tama ya kumpata Frank” alinieleza huku akilia.

    “Frank yuko kwenye matatizo na anahitaji msaada, siwezi mimi mwenyewe, naomba unisaidie na sina muda wa kukueleza, tutaongea tukiwa ndani ya ndege, ila kwasasa achana na begi lako, mimi nitakulipa mara nne ya utavyopoteza” nilimvuta mkono tukielekea kule kwenye, eneo la kutolea tiketi kisha tulikata tiketi na kuingia kwenye ndege, kwenye viti vyetu kulikuwa na mtu wa tatu na nilipomtazama alikuwa yule kijana.

    Ndege iliondoka saa 8 mchana kuelekea Kenya.



    “Usichana ni wa thamani kuliko jinsia nyingine yeyote, msichana bila msimamo huwa ni sawa na choo cha kulipia, yeyote mwenye pesa ya kukidhi hitaji la kodi ya kutoa haja yake, huingia na kutoa kisha huondoka na kuacha harufu na uchafu wake. Usichana ni sawa na chakula kilichohifadhiwa kwenye bakuli zuri na safi kikiwa kimefunikwa, ikitokea chakula hiki huingizwa vijiko na kila apitae na kufunua bali ni wazi kuwa mlaji wa mwisho hukuta kikiwa kimechacha, nani awezaye au apendaye kula kilichochacha?? Thamani halisi ya utu wa binadamu haifananishwi na kitu chochote, mwanaume awapo na wanawake wengi huambiwa ni mjanja, mkali, kiwembe, anabahati, ila msichana amilikie japo wanaume wawili huambiwa ni ‘malaya’,,nani anayetaka kuwa na Malaya? Wasichana ni muhimu na wathamani kuliko wavulana na hii ni kwakuwa wao si dhaifu kwetu kama sisi tulivyo dhaifu kwao. HESHIMU UTU WAKO,,HESHIMU MWILI WAKO. Ulishawahi kujiuliza ungejisikiaje kusikia kuwa mama yako alikuwa tapeli wa mapenzi na Malaya wa kupindukia??? Basi kama huwezi kujiheshimu, heshimu wanao wajao au waliopo” HII NI SEHEMU YA KUMI NA MBILI



    …nilipofika kwenye ndege baada ya kukaa tu nilianza kuusoma ule waraka alioutuma Frank, niliusoma kwa makini mstari kwa mstari, mpaka nikamaliza kurasa zote saba, kisha nilichukua ule niliopewa kwenye kikao nao nikaupitia kwa makini mstari kwa mstari mpaka nikamaliza, nilichokuja kugundua ni kuwa sahihi ya huu wa pili niliopewa kwenye kikao ilikuwa imeghushiwa na pia maneno ya huu wa pili ambao ndio uliosambazwa kwenye kikao kile haukusema ni kwanini Frank alikuwa akija kufanya shambulio na ulificha mambo mengi sana, ambayo kama yangejulika kwenye kile kikao basi kusingekuwa na haja ya wao kuhangaika. Nilimpatia Beatrice ule waraka akasoma, nilimshuhudia akilia na hii ilinionyesha dhahiri kuwa Beatrice huenda alikuwa na mahusiano na Frank lakini sikuwa na uhakika na wala sikutaka kuamini hivyo kwakuwa kitendo cha yeye kuhangaika kumtafuta Frank tu kilitosha kunipa wivu wa kimapenzi.

    “Kwaiyo yote haya yalitokea mbele yako” aliniuliza Beatrice huku akinitazama kwa hasira. Sikuwa na la kujibu zaidi ya kulia, nilijiona mwenye hatia kwakuwa sikuweza kuishughulisha akili yangu na kuwaza hata kidogo juu ya yale niliyoambiwa na kuyasikia juu ya Frank, sikujua Frank angenifanya nini kama angeniona lakini sikujali sana kwani nilichojua hata yeye anafahamu kuwa hatia yangu ni mimi kushindwa kumsikiliza na kumpa nafasi ya kumuamini. Beatrice alinieleza kila kitu kuhusu Frank toka alipokuwa akifanya kazi kwao na mpaka pale alipopigwa na kutaka kuuwawa, nililia kwa uchungu sana kwakuwa mimi ndiye nilikuwa chanzo cha yote hayo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “nadhani muda wa kulia umekwisha, sasa ni muda wa kufanya mambo kwa vitendo, ni ama tunamuokoa Frank au wao wanamuua, habari ya kulia sahauni kwa muda, habari ya woga sahauni kwa muda, sasa hivi ni kazi tu, mda mfupi ujao tutatua Nairob, sitaki woga, ikibidi kufanya kitu ambacho hujawahi kufanya usisite, wao ni wauaji waliosomea, wakikuwahi hubaki, hivyo na nyinyi mkiwawahi iwe ndo mwisho” aliongea yule kijana kwa sauti ya polepole lakini wote tulimuelewa, alikuwa makini kupita maelezo na hakuwa na mchezo na mtu yeyote, sura yake tu alionekana kuwa aliposema hakuna kulia alimaanisha.

    ****



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog