Simulizi : Mzigo
Sehemu Ya Tano (5)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ilikuwa ni siku miongoni mwa siku ambazo sitazisahau katika maisha yangu.Ni kumbukumbu nyingine mbaya kabisa kuwahi kutokea.Haiwezi kufutika kwenye kumbukumbu zangu abadani.
Ilikuwa ni Jumanne tulivu. Jerry alinifuata,ilikuwa ni siku
ambayo Jerry aliniambia natakiwa kukutana na tume
maalum iliyoundwa na kamati maalum iliyoundwa na Mheshimiwa Rais kutafuta chanzo na tiba ya mauaji ya
albino.Nakumbuka siku hiyo Jerry hakuwa na furaha kabisa.Alikuwa mtu mwenye huzuni na mawazo mengi.
Kuna nini? Nilijiuliza!
Nilimuona akiwa mwenye hasira kali na kukunja ngumi kwa hasira,vitu vingi alikuwa akiniashiria kwa mkono tu. Jinsi alivyokuwa niliogopa hata kumuuliza.Macho yake
yalikuwa yameiva na kufanya wekundu.
Huyu alikuwa na jambo tu,tena jambo zito!Nilishindwa
kabisa kumuuliza.
“Twende!” Alisema kwa kauli fupi huku maelekezo mengine
yote yakifuata kwa ishara. Nilipotoka nje ndipo nilipobaini kuwa jengo lile lilikuwa ni la ghorofa nne. Lilikuwa karibu na shule ya sekondari ya Wasichana ya Kunduchi.
Halikuwa mbali na kitengo maalum cha Sayansi ya bahari cha chuo kikuu cha Dar es salaam.
“Vipi kuna nini leo Jerry!” Nikauliza baada ya uvumilivu
kunishinda.
“Mambo si mazuri Kajuna tutaongea vizuri tukifika ofisini.
Tukaingia ndani ya gari Toyota land cruiser.
Haikutuchukua muda mrefu kufika mnazi mmoja.
Tukapanda ngazi za jengo lile taratibu huku nikiwa na hofu
kubwa ya kwenda kusikia nini kilichotokea.Kidogo hali ya
Jerry ilikuwa imerudi kawaida ingawa hakuweza kuongea
chochote .
Ghafla,nikamuona akibadilika kutoka kwenye furaha na
sura yake kurudi kama mwanzo.
“Bwana kajuna umekutana na mengi sana umeishi katika
kipindi cha mpito,kipindi kigumu ajabu!lakini kubwa
ninaloweza kusema ni kuwa Mungu amekuchagua
kulikomboa taifa kutoka kwenye aibu kubwa inayolikabili.
Mara nyingi yamekuwa yakitokea mauaji ya albino lakini vyombo vya usalama havijapata ufumbuzi wa kadhia hiyo,hivyo ninachokiona hapa ni kuwa Mungu amekuchagua,kwa kuwa Mungu amekuchagua basi unatakiwa uwe mfanoCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
wa manabii…..” Akatulia kidogo na kunikazia macho huku akiniacha kwenye mshangao mkubwa zaidi.
” Umepoteza mpenzi,nasikitika kukufahamisha kuwa umepoteza rafiki pia lakini naomba haya yote
yasikurudishe nyuma Taifa linakutegemea kwani mambo
uliyofanya ni mazito na yanastaajabisha” Akatulia kidogo na kuonesha huzuni na wasiwasi wa kile anachotaka kukizungumza.
“Naomba ieleweke kuwa wote hawa wanaingia kwenye
historia kama wapigania haki za binadamu tuwaombee
Mungu huko waliko” Akatulia huku akiwa ameshika tama.
Niliogopa sikutaka aniambie kuwa Ommy naye kauwawa,sikutaka kabisa kusikia habari hiyo moyo ulienda mbio.
Ingawa alishatanguliza pole kwa kueleza juu ya mpenzi
wangu lakini pia aligusia rafiki jambo lililonitia hofu.
Nilikuwa natetemeka.Nafikiri umeona vitu vya kutisha
vingi,kidogo utakuwa mzoefu. Bado sikumuelewa.
“Nifuate!” Aliniamrisha nami nikamfuata kuelekea kile
chumba kidogo.Kulikuwa na jokofu moja kubwa,niliogopa
kutokana na fikra nilizoanza kuwa nazo kuhusu Ommy.
Akafungua lile jokofu nikamtazama kwa hofu kubwa zaidi.
Nilikuwa natamani kumzuia lakini nilikuwa nimeyavulia
nguo maji.Nilikuwa nimeushika mkono wake kwa nguvu ili asifungue lakini nilishachelewa Akafungua!
*********
Tulifika maeneo ya Posta saa 12.30 jioni.Nilikuwa sina
raha.Kitendo cha Ommy kuuwawa na kuachwa bila
kiwiliwili kilinifanya nitamani sana kukutana na Samsoni
kipusa ‘Bonge’.Nilikuwa nimemchukia kuliko mtu yeyote duniani.Sikuwa na uhakika kama risasi niliyompiga siku ile kule Mbagala ilimuua au ilimjeruhi.Mtu wa pili
niliyemchukia zaidi ni Martin kisha nilihisi chuki kwa wote
wanaohusika na mauaji ya albino.Angalau sasa nikiwa na Jerry nilikuwa najihisi kuwa na amani.Picha ya kichwa cha Ommy ambacho nilikiona kwenye jokofu ilinitia simanzi kila iliponijia kichwani.Wakati tukipanda ghorofa la jengo lile la wizara ya mambo ya ndani nikakumbuka kitu,nilikuwa sijamuuliza jerry Ommy kauwawa vipi?
“Hivi ilikuwaje Ommy akauwawa?”
“Ni hadithi fupi sana,tulipoondoka hapa na kukuacha Ommy aliniomba afike nyumbani kwake mara moja maana ni siku nyingi hajafika huko.Sikumzuia kwa sababu nilijua wewe ndio unayetafutwa zaidi kuliko Ommy.Sikuweza kufikiria kuwa anaweza kuandamwa kiasi kile.Nikashangaa
kuona siku ile hakurudi tena. Jambo hilo likanitia mashaka
tukajaribu kuwasiliana na vituo vyote vya polisi,ndipo
siku ya pili tukapata taarifa kuwa Polisi wameokota kichwa cha mtu huko Kigamboni.Nikafuatilia ndipo nikabaini kuwa Ommy ameuwawa.
Uchungu niliousikia siku hiyo ulinikumbusha kifo cha
Betty.Huzuni yangu ikakusanya majonzi ya misiba miwili.
Kwanini mimi,Rafiki sina,mchumba nae…..
********
Saa 12.45 Tuliingia katika moja miongoni mwa ofisi nyeti katika jengo lile.Moyo wangu ulianza kwenda kasi tena.
KATIBU MKUU,maandishi hayo makubwa yalikuwa kwenye kibao chembama ambacho kilikuwa mbele ya meza moja ndefu kikimtambulisha mtu mnene ambaye alikaa mbele ya
meza ile.Licha ya yule mnene kulikuwa na watu wengine
mle ndani,niliogopa sana. Wengi wao sura zao hazikuwa ngeni machoni mwangu.Niliweza kumwona Kamanda wa polisi wa Tanzani IGP akiwa miongoni mwa watu waliohudhuria mkutano huo ambao sikuutarajia.Kulikuwa na watu wapatao watano.
“Karibu Jerry vipi umetuletea mgeni?” Sauti nene ya yule
mzee ilisikika.Jerry akanionesha kiti nikaketi. Wageni au watu waliokuwepo mle ndani walionekana kushangazwa na ujio wangu. Ni wazi kuwa hawakupewa taarifa hapo kabla.
“Tulikuwa tunakusubiri bwana Jerry,umechelewa sana!”
Sauti nyingine ya mtu ambaye nilikuja kutambua baadae kuwa ni naibu waziri wa mambo ya ndani ilisikika.
Jerry hakusema kitu akaenda moja kwa moja mpaka kule
mbele ambako kulikuwa na kiti karibu kabisa na kile cha
katibu mkuu.Nilishindwa kuelewa Jerry ana cheo gani
mpaka aonekane kuwa muhimu kiasi hiki.Akakaa.
“Kwanza niwaombe radhi kutokana na kuchelewa kwangu!”
Alianza Jerry huku akipangusa uso wake kwa kitambaa.
Kisha akaendelea
“Kuchelewa kwangu kumekuwa na faida kwetu na kwa kikao chetu cha leo,lakini kabla sijafika huko naomba
niwatambulshe kwenu huyu kijana ambaye anaitwa Kajuna!”Baada ya kutaja jina hilo wote wakanigeukia na
kunikazia macho.
“Nafikiri jina lake sio geni kwenu huyu ndio yule kijana
tuliyekuwa tunamtafuta sana tukimuhusisha na mauaji
hapo kabla.Pia napenda kukupa haki yako Bwana kajuna kwa kukutambulisha hawa waliopo hapa mbele ni tume maalum iliyoundwa na muheshimiwa Rais kuchunguza mauaji ya albino yanayoendelea hapa nchini,kutokana na uzito na ugumu wa jambo lenyewe tume hii imekuwa ikifanya kazi yake kwa usiri mno.Kutoka kulia ni naibu Waziri wa Ulinzi na usalama wa raia Muheshimiwa Hashim
Bakari,anayefuata ni mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Bi
Anna Ngonyani wa tatu ni Katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani Enerst Shadi,huyo mwingine ni mkurugenzi wa usalama wa Taifa Bwana Zakaria Mkude na mwisho ni kamishina maalum wa jeshi la polisi bwana Stefano Nyimbo!” Akatulia na kunikodolea macho
“Pia yupo Jaji Sebastian Pinda ambaye nafikiri hayuko
mbali na eneo hili kwani niliambiwa nae atakuwepo hapa!”
Kabla hajamaliza kuongea mlango ukafunguliwa akaingia mtu ambaye nilihisi kuwa ndiye Jaji aliyetajwa.
Sikukukosea kwani Jerry alinitambulisha kwa huyo Jaji.
Baada ya hapo Jerry akaanza kutoa habari zangu kuanzia
mwanzo hadi nilivyokutana nae.”
Ukafika muda ambao nilitakiwa kuthibitisha kama yale yaliyosemwa na Jerry ni ya kweli.Nikathibitisha huku
nikikumbusha baadhi ya vipengele ambavyo vilisahaulika.
Ilikuwa ni mshangao wa wazi katika macho yao.Bila shaka ni kutokana na vile nilivyotafsirika mwanzo kuwa ni muuaji na miongoni mwa wahusika wa biashara hiyo
ambayo haikubaliki kabisa.
Ikafika zamu ya maswali,nikaulizwa maswali mengi lakini nikayajibu kwa ufasaha.Katika maisha yangu sikutegemea kama itatokea siku ambayo nitapeana mkono na waziri,Kwa mara ya kwanza nilijikuta nikipewa mikono na watu hawa nyeti serikalini tena kwa heshima kubwa.Kwa mara ya kwanza toka nianze kukabiliana na tukio hili nilianza kuhisi furaha kwenye nafsi yangu. Angalau wazee hawa ambao walikuwa kwenye kikao maalum cha kutafutaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ufumbuzi walinipa moyo.
Nikamkumbuka sana afande Edwin ambaye alikuwa anataka kuning’oa meno bila ganzi,nilitamani sana angekuwepo akaona jinsi wakubwa wake walivyoniheshimu na
kunithamini.Kama si kifo cha Ommy basi hii ilikuwa ni
siku ambayo ningefanya sherehe,kupeana mkono na Jaji,waziri,katibu mkuu na mkurugenzi wa nini sijui huko juu,lilikuwa jambo la faraja kwangu.
Ukafika muda ambao maazimio yalitakiwa kupitishwa,jambo la kwanza lilikuwa ni kusaidiwa mzigo,ikaamuliwa kuwa kuanzia muda huo kamati ile nyeti ndiyo itakayokuwa na jukumu la kuwatunza Stela na Johari pia liliwekwa azimio la kufanyika upelelezi wa siri ili kuwabaini wote waliokuwa wanashirikiana na muheshimiwa Waziri kufanya
vitendo vile vya kishetani. Sambamba na hilo nilipewa
heshima kwa kupewa nakala ya upelelezi wao wa mwanzo
pale walipoishia.Katika nakala hiyo iliwagusa zaidi wavuvi wa samaki ambao walikuwa wakitumia viungo hivyo vya binadamu wenzao kwa dhana kuwa vinasaidia kupata samaki wengi. Haikuwa nakala ambayo ilionesha uozo wa viongozi,labda kwa sababu mbele ya jamii kiongozi alionekana mtu safi asiye na tatizo lolote.Kwaya,nyimbo,mashairi na ngonjera vilimfanya aonekane mtu safi mbele ya jamii.
********
Saa 3.11 tulifika maeneo ya Yombo Abiola,tukaenda moja
kwa moja nyumbani kwa Ommy ambako Stela na Johari niliwaacha huko.Huku nikiwa na furaha niligonga mlango kwa nguvu kidogo. Nililakiwa na ukimya. Nikagonga mara ya pili lakini bado kulikuwa kimya. Tukatazamana na Jerry.
Nikaanza kushikwa na hofu. Nikashika kitasa na kufungua.
Ndani kulikuwa na giza. Moyo ulikuwa unapiga kwa nguvu sana.Ujasiri na furaha niliyokuwa nayo vikatoweka.
Nikapapasa ukutani nikaipata swichi.Nilipowasha taa ndipo nilipozidi kuingiwa na woga. Damu ilikuwa imetapakaa pale sakafuni.Hakukuwa na yeyote mle ndani.
Jerry akatembea kwa kutumia vidole vya mbele vya miguu yake huku akiwa na bastola mkononi.Aina hii ya bastola nilikuwa sijawahi kuiona hata katika filamu. Baadae alinifahamisha kuwa ilikuwa inaitwa Luger au P00
Parabellum ilianza kutumiwa na majeshi ya kiswisi mwaka
1900 hadi 1949.Akaufikia mlango wa chumba ambacho
walikuwa wanalala Stela na Johari,mlango ulikuwa
umefungwa.
“Johari ni mimi Kajuna,fungua tafadhali!” Nikasikia nyayo za mtu ambaye alikuwa anakuja kufungua mlango.
Nilijiuliza maswali mengi ndani ya muda mfupi sana. Ina maana stella amekufa? Au ni Johari ……Swali lolote
nililotaka kujiuliza lilikatishwa na mtu aliyefungua mlango
ule.Jerry alikuwa mwepesi ajabu.Kitendo cha kitasa cha
ule mlango kuguswa tu Jerry alikuwa ameruka na kujibanza upande wa kushoto wa ukuta ulioshikilia mlango
ule.Nilishusha pumzi baada ya kumuona aliyefungua
mlango ni Johari .
“Stella yuko wapi?” Lilikuwa ni swali lililokuja ghafla kabla
hata ya salamu.
“Yupo huku chumbani.
“Na hizi damu…”
“mbona hutulii kwanza tukusimulie?” Nikamuona stella akitoka mle chumbani. “Tulivamiwa aliongea stella huku akionesha wazi kuwa na hofu.
“Watasimulia kwenye gari kwa sasa hili eneo lishaonekana halina usalama!” aliongea Jerry baada ya kugundua kuwa
wote wako salama.
Tukiwa kwenye gari stella akaanza kusimulia jinsi
walivyovamiwa na mtu mwenye kisu.Walijitahidi
kupambana naye.Stela aliweza kumpiga huyo jamaa kwa stuli usoni.Inasemekana jamaa alivuja damu vibaya lakini aliwahi kukimbia. Kutokana na maelezo yao nikabaini huyo mvamizi hakuwa na uhusiano na kundi la Bonge,alikuwa ni mwizi wa kawaida ambaye alibeba kisu ili aweze kujihami ikitokea dharura.
Jerry aliendesha kwa kasi kutokana na bara bara kutokuwa na msongamano muda huo.Ni Jerry pekee ndiye aliyekuwa anajua wapi tunaelekea.Tukaiacha barabara ya Pugu tukafuata ile ya Mandela.Saa 4.02 tulikuwa maeneo ya Mbezi Luis.Tukafika mbele ya jumba moja kubwa.
Tulipofika karibu na lango akapiga honi mara tatu. Mlango ukafunguliwa na mtu ambaye nilihisi kuwa ni mlinzi.
Tukashuka kwenye gari tukasalimiana na yule mlinzi,kisha tuka tambulishwa kwa mlinzi ambaye alikuwa anaitwa Ibrahim Kondo.Tukaachwa ndani ya Jumba lile ambalo halikuwa na watu wengine mle ndani,lakini ajabu!Lilikuwa na kila kitu.
*********
Tulikaa ndani ya jumba lile kwa siku tatu huku tukiwa chini ya uangalizi maalum wa Jerry.Jambo ambalo lilinifurahisha ni kutembelewa na tume ile iliyoundwa na Rais.Pamoja na furaha niliyokuwa nayo bado nilitamani sana kukutana na
Bonge.Ommy na Betty walinifanya nitamani sana kukutana naye.Kama ile bastola niliyompiga siku ile ilimpata basi ni heri kubwa na kama ilimjeruhi LAZIMA NIMUUE.
“Hivi humu ndani tutakaa hadi lini?” Aliuliza Stella na
kunikatisha mawazo yangu. “Nafikiri saa ya ushindi ikifika!” Nilimjibu huku nikimiminia maji kwenye glasi.
“Unafikiri tutashinda?” Aliuliza tena
“Tutashinda lakini vita itakuwa ndefu!”
“Kivipi?” Safari hii Johari naye alinirushia swali.
“Hata wakikamatwa hawa wanaotusumbua bado kuna
mlolongo wa watu wenye roho za kishetani ambao wana mawazo kama yao!”
“Hao utapambana nao vipi?”
“Haliwezi kuwa jukumu langu peke yangu ni jamii mzima
hususani viongozi wa dini ndio hasa wanatakiwa
kubadilisha nyoyo za watu.”
Huku nikiwa kwenye lindi la mawazo nikasikia lango
linafunguliwa,nikachungulia dirishani.Alikuwa ni Jerry.
Nikamuona akiliingiza gari lake sehemu ya kuegeshea.
Baada ya kushuka akatembea taratibu kuja kule tuliko.
Muda huo Stella na Johari wao walikuwa chumbani kwao wakitazama luninga. Urafiki wao ulinifariji sana kwani angalau Johari alianza kurudi kwenye hali ya kawaida.
Mara mlango ukafunguliwa,Jerry akiwa mwenye furaha
alikuja pale nilipokaa akanisalimia huku akinishika mkono kwa nguvu na kuutikisa kwa furaha.
“Leo Rais katoa kibali cha kukamatwa muheshimiwaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
mwingine!” Aliongea Jerry huku akionesha furaha ya wazi kabisa
“Ni nani huyo muheshimiwa?”
“Naibu waziri wa Bunge!”
“Naye pia anahusika?”
“Yeye na mkuu wake wote wanahusika!”
“Saa ngapi atakamatwa?”
“Hivi ninavyozungumza vijana kutoka makao makuu ya polisi wameelekea nyumbani kwake wengine ofisini kwake ili kokote ambako atakuwepo muda huu aweze kukamatwa!”
“Na wale wengine?”
“Tunaandaa kikosi maalum unatakiwa kujiandaa kwani leo usiku utatupeleka huko iliko nyumba ya Samson Kipusa”
“Ina maana tajiri mkubwa kama yule mulikuwa hamfahamu wapi anaishi?” “Hapana,yule ana nyumba yake Mbezi inaonesha hiyo nyumba ambayo wewe umeitaja ni maalum kwa shughuli zao!”
Habari ile ilikuwa ya kufurahisha kwangu.Niliona masaa yakienda taratibu mno.
********
.Hali ilikuwa tulivu mno,usingeweza kuamini kuwa hii ndio ile barabara ya Mbagala ambayo inakuwa na msongamano mkubwa wa magari.
Magari yalikuwa machache mno hivyo kuifanya safari yetu mimi na Jerry kuwa rahisi.
“Umechukua bastola yako?” Aliuliza Jerry.
“Ndiyo” “Naomba niione!” Nikampa.
“Hii sio mzuri,chukua hii ya kwangu!” Akanipa bastola
nyingine ambayo haikuwa nzito kama ile ya kwangu.
“We,utatumia nini?”
“Kisu na mikono!” Nilimwangalia kwa mshangao.
Tukafika maeneo ya Kongowe.Tukaicha gari kwa mlinzi wa shule ya sekondari ya St.Matthews.Tukatembea taratibu kana kwamba tunaenda harusini.
“Tangulia!” Jerry alinihimiza. Nikawa mbele akaniacha
takribani hatua kumi.Ule upande ambao tulitoroka nikiwa na Johari ndio tulioutumia kuingilia ndani.
Ndani kulikuwa na nyasi na maua ambayo hayakutuzwa
vizuri.Tukasikia nyayo za mtu ambaye alikuwa anakuja
kule nyuma. Jerry akakimbia kwa kasi bila kufanya vishindo akaenda kuegemea ukuta wa jengo lile. Nikataka
kumfuata .Akaniashiria kwa mkono kuwa nisimame pale
pale.
Huyu jamaa ananiuza nini? Niliwaza baada ya kuona
sehemu ambayo aliniambia nisimame ni ya wazi mno.
Nikasimama palepale.Dakika chache baadae akatokea
mlinzi.
“We nani?” aliuliza mlinzi huku akijiweka tayari kwa kwa shambulizi.Hakuwahi kufanya lolote,nilishuhudia aina ya mateke ambayo nayaona kwenye filamu za kichina likitua katikati ya koo la yule mlinzi.
“Kumbe Jerry ni mtu hatari namna hii?” Niliwaza baada ya kumuona yule mlinzi akianguka kama gunia. Akaniashiria kwa mkono niende kule aliko.Nikamfuata bila kusita.
Akaniamrisha nilale chini. Tukaanza kutambaa kama nyoka,nilikuwa nasikia maumivu ya tumbo lakini nilivumilia na kufuatisha vile alivyokuwa anafanya.
“We Pembe uko wapi?” Ilisikika sauti nyingine.
“Njoo huku!”Alisema Jerry jambo lililinifanya niingiwe na
hofu kwani lazima yule mtu angeshangazwa na sauti
ile.Huyu alikuja na tochi. Alishaanza kuingiwa na mashaka.
Sijui ni staili gani ilitumiwa na Jerry kuinuka pale chini
kwani hata kwenye sinema nilikuwa sijawahi kuiona.
Nilimshuhudia akimrukia yule jamaa na kumpiga kabali ya
nguvu.Baada ya dakika moja yule jamaa alikuwa hajitambui.Akamlaza pale chini tukaondoka.
“Inaonesha kulikuwa na walinzi wawili tu huku nje!”
Sikumjibu nikaendelea kumfuata .Tukaingia.Ndani
kulikuwa kimya bila shaka hakukuwa na watu mle ndani.
Tulitembea kwa kujiamini ndani ya nyumba ile kubwa.
Wakati tunasonga mbele tukasikia sauti ya watu waliokuwa wanaongea.Jerry akachungulia kwenye tundu la ufunguo la chumba kilichokuwa kinasikika sauti za watu”
“Tuondoke hatari!” Alininong’oneza.
Kama tulivyoingia ndivyo tulivyoondoka.
“Tuna bahati sana Kajuna, kazi itaisha mapema kuliko
nilivyofikiria!” Aliongea tukiwa mbali kidogo na eneo lile.
“Kwa nini?” Nilimuuliza.
“Karibu wahusika wote muhimu wako humu ndani bila
shaka wana kikao muhimu!” Tulikuwa tumefika pale
tulipoliacha gari. Tukangia kwenye gari .Gari iliendeshwa
kwa kasi kubwa mpaka nikahisi kuwa ajali iko karibu.
Sikujua kwanini Jerry aliamua kuondoka badala ya kuwa
shambulia wale jamaa.
Tulitumia dakika kumi na mbili tu kutoka Mbagala hadi
makao makuu ya jeshi la Polisi.
“Nisubiri hapo kwenye gari!” alisema huku akikimbia
kuelekea ndani ya jengo lile la makao makuu ya Polisi.
Baadhi ya polisi waliokuwa pale nje walimsimamisha kwani
aliwatia hofu kwa kitendo kile cha kukimbia. Alipotoa
kitambulisho chake kila mmoja alisimama pembeni baada
ya kumpa heshima yake ya kiaskari.
Dakika chache baadae alikuwa anashuka kutoka kwenye
jengo lile la makao makuu ya jeshi la polisi nchini. Nyuma
yake alikuwa anafuatwa na askari polisi mwenye nyota
moja begani.
“Samahani Kajuna, wewe utakuja na askari ambao
watahitaji msaada wako kwa kuwaelekeza eneo la tukio.”
Akaniacha kwa Polisi yule mwenye nyota moja. Akaondoka
kwa kasi kurudi Mbagala.
***
Hali ilikuwa shwari hivyo kuruhusu msafara wetu wa
magari matatu kuwa huru barabarani. Bastola ambayo
nilikuwa naitumia ilishachukuliwa na Jerry. Mimi nilikuwa
sina silaha ya aina yoyote kitendo ambacho kilinikosesha
raha sana.
Tulikuwa tunakaribia kufika eneo la tukio jukumu langu
lilikuwa ni kuwaelekeza tu ndio maana sikupewa silaha.
Dakika chache baadae tukawasili eneo la tukio.
Nikaambiwa nibaki pale kwenye gari. Kwa unyonge
nikakaa pale nikiwaangalia askari jinsi walivyokuwa
wanagawana pande za nyumba ile. Nilishangaa sikumuona
Jerry kwenye kundi lile. Wakati nikimfikiria JerryCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
nikashtushwa na Mlipuko wa silaha. Askari walikuwa
wamepindukia ndani. Nikawa nasikia mfululizo wa milipuko
hiyo. Ingawa nilikuwa na hamu ya kwenda moja kwa moja
eneo la tukio nilijikuta nikitetemeka pale nilipokaa. Upande
wa kushoto wa nyumba ile nilimuona mtu akiruka ukuta na
kuanza kukimbia, Mungu wangu! Alikuwa Martin.
Nilijilaumu kwanini sikung’ang’ania kupewa silaha kwani
ningeuburudisha moyo wangu kwa kumlipua muuaji huyu.
Nikaanza kusikia vilio vya watu ambao bila shaka
walikuwa wamepigwa risasi huko ndani. Nilimuona wazi
Martin akiingia kwenye jengo moja bovu. Kabla sijaamua
lolote kuhusu Martin nikaona lango la nyumba ile
likifunguliwa. Nikawaona askari wawili wakiwa wamebeba
kitu kama machela. Waliposogea karibu ndipo nilipogundua
kuwa walikuwa wamembeba Samson Kipusa. Alikuwa
hajiwezi. Bila shaka alikuwa anatibiwa mle ndani kutokana
na risasi niliyompiga siku niliyotoroka. Nilijisikia furaha
sana kumkomesha mshenzi huyu. Akaletwa mle kwenye
gari.
“Kijana muangalie huyu” aliongea askari mmoja huku
wakirudi tena ndani. Hakuwekwa kwenye gari alilazwa pale
nje, leo utajiri wake haukuwa na thamani tena. Duh! Kweli
mshahara wa dhambi ni mauti. Askari walifanya kazi yao
inavyotakiwa. Nilimwangalia Bonge alikuwa anapumua kwa
shida sana. Nikamfuata pale chini alipolazwa
Nikamkandamiza kwa nguvu kisha nkamziba pua na
mdomo. Jamaa alitapatapa hatimaye akakata roho. Nikarudi
pale niliposimama huku nikijihisi utulivu moyoni.Nilifanya
hivyo kwa kuchelea maamuzi ya mahakama kwani kama
angesimama mahakamani akatumia pesa zake vibaya
ungesikia kaachiwa huru au kafutiwa makosa ya mauaji na
sasa anashtakiwa kwa kosa la kutumia utajiri wake vibaya
au kosa la kutotoa taarifa mapema. Kosa hilo lingemfanya
aumikie kifungo cha miezi sita au mwaka mmoja.
*********
Saa 8. 54 kazi ilikuwa imekwisha kwani Martin aliuwawa
baada ya kuwaelekeza Polisi kule alikojificha. Huku tukiwa
na furaha tulikuwa tunarudi uwanja wa vita. Katika msafara
wa kurudi tuliongezewa magari manne kwani tulikuwa na
maiti nne za majambazi na mateka saba. Upande wetu
alijeruhiwa askari mmoja tu! Wananchi wengi wa maeneo
ya Kongowe na Mbagala rangi tatu walishangazwa na
milipuko ya risasi. Wengi walikuwa nje ya majumba yao
baada ya kusikia ving’ora vya polisi. Walisimama kando ya
majumba, nahisi walikuwa wanajiuliza maswali yasiyo na
majibu kwani hawajawahi kuona msururu wa magari ya
polisi kama ambao niliongozana nao siku hiyo. Wengine
walikuwa wamevaa misuli, wengine mabukta tu, kwa
upande wa kina mama wengi wao walitoka na kanga moja
huku wengine wakiwa na magauni ya kulalia tu. Ama kwa
hakika lilikuwa tukio la aina yake.
Nilikuwa na furaha mno kurudi tena kwenye ulimwengu wa
kawaida. Angalau sasa nilijua kuwa jina langu litakuwa safi
mbele ya jamii.
Saa 9.36 nilifika mafichoni kwetu kule Mbezi. Stella na
Johari walikuwa sebuleni eti walisema kuwa hawakulala
walikuwa wananisubiri kwa hamu ili wajue nini kimetokea.
Niliwasimulia kila kitu kilichotokea.
***
Ilikuwa ni asubuhi ya siku ya tatu baada ya tukio lile la
kuvamia Mbagala. Afrika mashariki ilitikiswa kwa habari
nzito za kukamatwa kwa waziri na naibu wake, Mbunge na
wafanyabiashara kadhaa kwa tuhuma za biashara ya ngozi
za binadamu na ushirikina wa kutumia viungo vya Albino.
Watu wengi walionekana kwenye vituo vya kuuzia
magazeti. Ni siku ambayo magazeti yaliisha mapema sana.
Habari hizo zilinisafisha na kunitaja kuwa shujaa. Nilijihisi
kama mtu niliyezaliwa upya.
Wakati nikiwa kwenye furaha ile mara akaingia Jerry.
“Kajuna nina habari za kufurahisha sana kwako, serikali
imekuzawadia nyumba kubwa ya kifahari, gari pia una
nafasi ya kwenda kusoma huko Cuba kwani kuanzia sasa
wewe ni muajiriwa katika idara yetu!” Nilikuwa kama naota
sikuamini.
“Hivi ninavyokuambia nimeitwa ofisi ya Rais kufuatilia
barua yako pia Rais anataka kuonana na wewe!”
Hilo la Rais kuonana na mimi lilinitisha sikuona kama
ninauwezo wa kukabiliana na Rais katika maongezi. Jerry
akaondoka akatuacha mimi Stella na Johari .
“Leo nataka nikawasalimie wazazi wangu!” Niliwaambia
Johari na Stella. “Kajuna!” Stella aliniita kwa sauti ndogo
wakati naelekea chumbani kwangu. Nilipogeuka
akanitazama kwa aibu kisha akatamka neno ambalo hata
Johari alilisikia.
“Nakupenda!” Neno hilo lilikuwa kama kisu kwenye moyo
wangu. Pale niliposimama nilikuwa nawaona vizuri wote
wawili, Johari akatembea kwa haraka kunifuata kule niliko.
Akanishika mkono na kunivutia kwake kisha
akaninong’oneza sikioni.
“Kajuna umeniokoa, sasa unataka kuniua?” Kabla sijamjibu
nikashikwa mkono mwingine na Stella. Johari akaja mbele
yangu akakilaza kichwa chake kifuani pangu. Kila mmoja
alikuwa anaonesha mapenzi kwangu. Nikawa navutwa huku
na huku hali iliyoniweka njia panda. Ghafla, Stela
akaniacha na kumfuata Johari, kidogo niliingiwa na
wasiwasi.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Johari!” Alisikika Stela kwa sauti iliyotulia.
“Nakutakia maisha mema na kajuna. Nampenda hilo liko
wazi lakini nahisi wewe una haki zaidi kwake…………”
Hakumaliza machozi yalikuwa yanadondoka na kufanya
michirizi kama ya chemchem inayokaribia kukauka.
Nikamtazama tena Johari kwa macho yaliyojaa mapenzi,
nikamvuta upande wangu. Nikamkumbatia kwa nguvu.
“Nataka kufunga ndoa na wewe Johari uko tayari?”
Akacheka na kuruhusu mwanya wake wa kuvutia
kujidhihirisha katika macho yangu.
“Uamuzi wa busara!” Alisikika Stela ambaye alikuwa nyuma
yangu. Nilipogeuka nikamuona anatabasamu. Machozi
yalikuwa yamekauka.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment