Search This Blog

Friday, 20 May 2022

MZIGO - 4

 







    Simulizi : Mzigo

    Sehemu Ya Nne (4)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bado alikuwa na msimamo wa kutaka kufa,alinishangaza na kuniacha kinywa wazi. Ghafla!Nikasikia honi ya gari kutoka nje. “Twende!” akakataa.Sikuwa na muda wa kupoteza nikampiga kofi kali la shavu,akayumba nakuangukia kitandani. “Pumbavu twende!” Nilifoka huku nikimuongezea ngumi ambayo ilimuangushia tena kitandani pale alipojaribu kuinuka.Nikamwonesha kile kisu ambacho dakika chache zilizopita nilikitumia kwa mauaji,akashtuka hakutegemea kama nitachukua hatua kali namna ile.Nilikuwa nimebadilika nilikuwa Kajuna Mwingine kabisa. “Nimesema twende!” Alikuwa hana hiyari zaidi ya kunifuata.Nilimshika mkono nikaanza kukimbia kuelekea mlangoni. Nasema hakuwa na hiyari,naye alikuwa anakimbia kunifuata kwani nilimshika kwa nguvu ili asije akaleta tena upuuzi wake.Nikamuona mlinzi anahangaika kufungua komeo ambalo lilikuwa limeshikia lango,bado honi zilikuwa zinapigwa.Sikutaka kupoteza muda niliuacha mkono wa Johari nikakimbia kwa kasi.Laiti ungebahatika kuniona jinsi nilivyokuwa nakimbia usingeweza kunitofautisha na mtu anayeshiriki mashindano ya mbio za mita mia moja.Kwa kuwa nilikuwa sijavaa viatu na ule mngurumo wa gari vikamfanya mlinzi ashindwe kugundua kuwa kuna mtu alikuwa anamfuata.Nilipomkaribia alikuwa anataka kufungua komeo la mwisho.Hakuwahi! Nikamrukia,tukapiga mwereka mzito akataka kupiga yowe,alichelewa! Nilididimiza kisu kile kikubwa katikati ya mdomo wake kikatokea nyuma ya shingo yake.Nilikuwa nimekata mawasiliano yake ya sauti.Nikamwacha akigaagaa kupigania roho yake.Nikakiingiza kisu mfuko wa nyuma wa suruali yangu.Nikarudi kwa Johari nikamshika mkono tukawa tunakimbia kuelekea nyuma ya nyumba ile.Hakukuwa na mlango. Ukuta haukuwa mrefu lakini nilijua wazi kuwa Johari hawezi kupanda ule ukuta.Kwa ujasiri wa ajabu nikamweka Johari mgongoni. “Nishike vizuri!” nilimwamrisha.Kwa jinsi nilivyokuwa mkali na alivyo nishuhudia nikiuwa watu alijua sitaki mchezo hivyo hakuleta ubishi.Alijishikia vizuri mgongoni kwangu nikaruka na kudaka juu kwenye matofali.Kwa kutumia nguvu zangu zote nikajivuta hadi juu ya ukuta.Kisha nikaangukia upande wa pili.Nyuma ya ule ukuta kulikuwa na nyumba nyingi ambazo ujenzi wake ulikuwa haujakamilika.Eneo hili lilikuwa na nyumba chache ambazo zilikuwa zinaishi watu.Kwa kuwa giza lilikuwa limeingia sikupata hofu ya kukamatwa. Johari hakuwa na nguvu ya kukimbia nikambeba kwa mikono miwili.Alikuwa kimya akisubiri hatma yake. Huku ni kiwa na kile kisu chenye damu nikaingia kwenye jengo moja ambalo lilikuwa halijamalizika ujenzi wake. “Mwanamke! Tulia hapa.”Niliongea kwa ukali. Nikamwacha Johari mle ndani.Nikarudi kule nilikotoka.Nikaenda mbele ambako kulikuwa na lile lango lakuingilia.Nikajificha kwenye kichaka.Bado lile gari lilikuwa linapiga honi kwa fujo.Angefungua nani? mlinzi alikuwa amekufa.Nikasikia sauti ya hatua za miguu ya mtu aliyekuwa anakimbia kuelekea getini. “Mungu wangu,nani kafanya huu ushenzi?” Nilimsikia huyo mtu akiropoka kwa kihoro bila shaka baada ya kuiona maiti ya yule mlinzi.Bado yule mtu hakutosheka na mshtuko huo akaendelea kumimina matusi mazito ya kulaani kitendo kile. Nikashuhudia lango likifunguliwa.Gari likataka kuingia halafu nikaona dereva anasita na kurudi nyuma.Wanaume wanne wakashuka kutoka kwenye ile Rav4,wote walionekana watu ambao wamenawiri kwa fedha. Sikumtambua hata mmoja zaidi ya Bonge.Walikuwa wamebaki vinywa wazi. “Nini kinaendelea hapa!” aliuliza Bonge kwa mshtuko. “Yule mshenzi amemuua Dula na Suma huko ndani halafu amemalizia na huyu Peter!” “yuko wapi alifoka Bonge akiwa ameanza kuingia ndani!” “Ametoroka!Tena ametoroka na ile mali yetu mpya!” Jinsi jamaa walivyoshtuka huwezi kuamini.Kama wangenikamata muda ule nafikiri kulikuwa hakuna mjadala





     “Dawa ya muheshimiwa waziri ishatengenezwa?” alihoji mmoja. “Hapana mkuu ilikuwa yule binti achinjwe leo usiku lakini keshatoroshwa sijui itakuwaje!” “hii damu ni mbichi sana inaonesha tukio si la muda mrefu msake mpaka umpate!” Ilikuwa ni amri kali. Wakaingia ndani huku wakiongea maneno ambayo sikuweza kuyasikia vizuri. Mungu mkubwa, jinsi jamaa walivyo kuwa wamechanganyikiwa inafurahisha. Waliingia ndani wakasahau kufunga milango ya lile gari. Nikazunguka nyuma haraka. Nikambeba tena Johari , sikuwa na uhakika kama ninaweza kuwahi kabla hawajafika. Nikiwa nimembeba Johari mikononi nikamwingiza ndani ya lile gari. Sikuwa na leseni ya udereva lakini nilikuwa naweza kuendesha kwani mara mojamoja rafiki yangu Salumu Kapirimba rafiki yangu niliyesoma naye sekondari alinifundisha. Nikawa nahangaika kutaka kuwasha. Huku nikitetemeka nikawasikia jamaa wakitembea kwa kasi kuja liliko gari. Hofu ilianza kunitawala upya. Upande fulani nilianza kujilaumu kwanini nilikuja huku kwenye gari wakati sina taaluma ya udereva. “Mtafuteni haraka!” Nilisikia sauti ya Bonge akiendelea kufoka. Gari lilikuwa linakataa kuwaka. Mungu wangu! Johari ambaye alikuwa upande wa kulia aliinuka na kunipa ishara ya kutaka nimpishe. Sikufanya ubishi nikampisha. Nikaishika vizuri bastola yangu. Nilikuwa sijawahi kutumia bastola, lakini kwa uzoefu wa kuangalia filamu mbalimbali sikuwa na wasiwasi wa nini cha kufanya. Nikafyatua kitunza usalama cha bastola ile. Johari alikuwa ameiwasha gari. Kwa kuwa lango lilikuwa halijafungwa nikawaona wale jamaa wakija kwa kasi kulifuata lile gari. Sikutaka kuchelewa nikaishika vizuri bastola. Kutokana na giza hawakuweza kuniona vizuri. Nikalenga shabaha katika kifua cha bonge nikaifyatua. Mlipuko mkubwa ukawashtua majirani. Wale watu wakapatwa na kihoro baada ya kumuona Bonge akirushwa juu na kuanguka chini baada ya kumpata risasi ile. Alikuwa ameanguka kama mzigo. Sikuwa na uhakika kama alikufa au alikuwa mzima. Nikatabasamu baada ya kumuona Johari akiirudisha ‘rivasi’ gari ile. Kisha akaiondoa kwa kasi. Ilikuwa ni patashika nguo kuchanika kwani tulishambuliwa kwa risasi mfululizo. Hata hivyo Mungu alikuwa upande wetu. Tukatoka salama na kuingia barabarani. Gari lilikuwa linaendeshwa kwa kasi ambayo sikuitarajia. “Kumbe unaweza gari!” Nilimsemesha Johari ambaye muda wote alikuwa kimya.Akatabasamu, kisha akacheka na kuruhusu mwanya wake kuonekana. Alipokuwa anacheka mashavu yaliweka vishimo vidogo vilivyovutia sana. Hapo nikagundua kuwa Johari alikuwa mwanamke mrembo. Sura yake kidogo ilinifanya nisahau kama nipo kwenye wakati mgumu. Nilisahau kabisa kuwa nina kisu chenye damu huku nikiwa nimeshika bastola mkononi. “Please hide your pistol!” Johari alinishtua. Nikaweka bastola mfukoni. Kitendo cha Johari kutabasamu na kuanza kuongea kilinipa nguvu na faraja kubwa sana. Angalau nusu ya upweke niliokuwa nao ilianza kupotea. Nilikuwa na shauku kubwa ya kujua aliyomsibu Johari lakini haukuwa muda muafaka. Niliendelea kumkazia macho huku nikistaajabia uzuri wake. *** Tukaitelekeza gari kituo cha magari cha Temeke mwisho, kwani inavyoonesha hawa jamaa walikuwa na mtandao mpana hivyo nilihofu kama tutaendelea kuitumia tungekutana na askari wa usalama barabarani ambao wangetukamata na kuturudisha katika mikono yao. Sikupenda hilo litokee! Kama niliyeota dakika chache baadaye nilianza kusikia ving’ora vya gari la polisi vikija maeneo yale. “Giza lishaingia gari nishaitelekeza kwa leo hawanipati abadani!” Niliwaza baada ya kuhisi kuwa huenda hao polisi wamepewa taarifa zangu hivyo wananitafuta. Tulitembea kwa miguu huku nikiwa sina shati wala viatu miguuni. Watu walikuwa wanatushangaa sana. Tulijitahidi kupita vichochoro ambavyo havikuwa na watu wengi hadi tulipotokea maeneo ya Abiola. Ili kuogopa usumbufu nikaamua kupita nyuma ya kituo cha Polisi. Hatimaye nikatokea nyumbani kwa Ommy. Nilikuwa natamani sana kuonana na Ommy ili anijulishe kile kilichojiri siku ya mwisho ambayo nilijikuta hospitali. Licha ya kutaka kujua Ommy ndiye pekee niliyemuona kuwa mshirika wangu wa karibu kwenye matatizo yale. Angekuwa mtu mwingine siku niliyomueleza kuhusu mzigo wa almasi pengine angeweza hata kuniua kwa tamaa ya utajiri wa haraka. Ommy alikuwa mtu na pia utu alikuwa nao. *** Hali ya nyumbani kwa Ommy kidogo ilinitia mashaka. Nyumba ilionekana kupooza. Ilikuwa kama gofu, hakukuwa na dalili zozote za uhai kwenye nyumba ile. Hali ile ilinishangaza sana, haikuwa dalili nzuri kwangu kwani ilimaanisha kuwa Ommy ana siku nyingi hajalala pale ndani. Kwa kuwa pale tulipokuwa tunauficha ufunguo nilipafahamu vizuri sikupata shida. Niliinua lile tofali, nilishangaa kuuona ufunguo ukiwa na kutu. Hii ilimaanisha kuwa Ommy alikuwa na siku nyingi zaidi ya vile nilivyofikiri hajakanyaga pale nyumbani. Nikafungua mlango na kuingia ndani. Ndani hakukuwa na mabadiliko yoyote zaidi ya vumbi na buibui ambao walishageuza kuta za nyumba ile kuwa makazi yao ya kudumu. “kimetokea nini?!?” nilijiuliza kwa mshangao. Nilianza kurudiwa na huzuni ambayo ilishapotea. Yuko hai kweli? Nikaingia kwenye chumba changu. Nikafungua mfuko mdogo wa begi langu, “uhuuuu!” Nikashusha pumzi baada ya kuziona zile fedha nilizokuwa nimezihifadhi zikiwa salama. Sikuwa na haja ya kuzihesabu kwani hata kama zingepungua ningemuuliza nani? Niliacha laki sita na elfu hamsini. Niliporudi sebuleni nikamkuta Johari akiwa amekaa kwenye sofa. Alikuwa amechoka sana. “Utahitaji kuoga?” aliitikia kwa kichwa. Nikaangalia kwenye ndoo zote zilikuwa na maji kama tulivyoacha mara ya mwisho. “Mh! Hii hatari sana ina maana Ommy akurudi tena nyumbani.” Nikakagua vitu vingi mle ndani vilikuwa kama tulivyoacha mara ya mwisho. Katika vitu ambavyo sikutamani kusikia muda ule ni kifo cha Ommy. Moyo ulikuwa unaenda kasi ajabu! Nikamwekea Johari maji bafuni akaenda kuoga. Wakati yuko bafuni ndipo nikakumbuka kuwa mfukoni kuna kisu chenye damu. Nikakitoa mfukoni na kukiweka pale mezani. Nikaiangalia vizuri ile bastola. Sikuwa mtaalamu wa mambo ya silaha hivyo sikuweza kujua ni bastola ya aina gani na inatoka nchi gani, labda angekuwepo Ommy. Nikakumbuka kitu, nikaenda kwenye chumba cha Ommy. Kama nilivyotegemea, nikalikuta begi ambalo lilikuwa na viungo vya albino likiwa juu ya Meza ndogo. Juu ya lile begi kulikuwa na barua. Bila shaka ulikuwa ni ujumbe kutoka kwa Ommy. Nikatabasamu, angalau nilianza kufarijika kidogo baada ya kuuona ujumbe ule. Nilikuwa na matumaini angalau ya kupata taarifa kuwa Ommy katoroka au vinginevyo na si kifo chake. ***** Nilikagua tena lile begi, nikashangaa kuona vile viungo vya albino havijaharibika. Nilipoangalia vizuri nikagundua kuwa kuna dawa maalum ilikuwa imewekwa. Kumbe ndio maana nilisafiri na mzigo huu bila kusikia harufu. Nikachukua ile barua iliyoachwa na Ommy nikaiweka mfukoni. Sikutaka Johari alione lile begi nilihofu angeweza kujisikia vibaya kisha akarudia ule msimamo wake wa awali. Nikalifunga vizuri nikaliweka uvunguni mwa kitanda. Nikarudi sebuleni nikamkuta Johari akiwa amekaa pale kwenye sofa. Alikuwa amevaa nguo zake zilezile. Alikuwa amevaa blauzi ya rangi ya kijani na sketi ndefu ya kijivu. Nywele zake zilikuwa zimetunzwa vizuri kiasi cha kunishangaza kwani mazingira tuliyokutana nilitegemea nywele zake zingekuwa hovyo hovyo. Kabla sijaanza kumuhoji lolote nikaamua kuanza kusoma barua ya Ommy. Rafiki yangu mpendwa; Naandika barua hii nikiwa sina uhakika kama tutakuja kuonana tena, kama tutaonana basi itakuwa ni heri kubwa na iwapo hatutaonana basi naomba Mungu atukutanishe katika kivuli cha wapenda haki huko mbinguni. Siku zote nimekuwa nikikuthamini kwa kuwa nimekuona ni rafiki mwema na mpenda haki, Mungu akubariki kwa hilo. Ninaandika nikiwa sina uhakika kama utaisoma barua hii! Sina uhakika kama bado uko hai au umekufa. Kama umekufa naamini Mungu ataufikisha ujumbe huu huko uliko kwenye mapumziko ya milele. Kajuna ulikuja kwangu kama mzaha nami nikakupokea lakini kupitia kwako yamekuja bainika mambo mazito sana. Lengo la ujumbe wangu huu ni kukusimulia kwanza jinsi tulivyoachana siku ile. Nilikuwa nawasiwasi huenda ukafikiri kuwa nilikusaliti, haikuwa hivyo kajuna. Wakati wewe unaingia ndani nikawaona watu wenye bastola wakikufuatilia. Nikaamua kutoka kwenye yale maficho yangu kisha nikawafuata taratibu hadi ulipotekwa ukaingizwa kwenye lile gari. Gari ilipokuwa inaelekea Tandika ndipo nikaigonga na kusababisha ile ajali iliyotokea. Kumbe wale washenzi walisoma namba za gari langu wakawa wananifuatilia nyendo zangu. Nami nikawa nafuatilia nyendo zao. Nimegundua mambo mengi sana mojawapo ni kuhusika kwa baadhi ya vigogo kwenye ushirikina mkubwa wa viungo vya albino. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Tafadhali naomba uwe makini na sehemu hii: Wanaohusika ni baadhi ya wabunge kwa sababu za kisiasa, wavuvi na wafanyabiashara wakubwa. Kiongozi wao ni mheshimiwa Stefano Kenge waziri wa bunge na usimamizi wa vikao vya serikali, pia naomba ufahamu kuwa yule Bonge ndiye Samson Kipusa mfanyabiashara mkubwa wa madini ambaye pia ana tuhuma mbalimbali za ujambazi. Uwezo wangu wa kuchunguza umeishia hapo lakini sina uhakika na uhai wangu na wako lakini napenda kukuahidi kuwa sitarudi nyuma. Kama watakuuwa nitalipa kisasi, na kama wataniua naomba upambane hadi tone la mwisho. Najua unaweza kufikiri kuwa ni kazi kubwa lakini nakuhakikishia kuwa Mungu yuko pamoja nasi. Kama mungu atatukutanisha tutaongea mengi sana.Mwisho naomba uchukue namba hii 0756 465 265, hii ni namba ya mtu ambaye nahisi atakusaidia sana anaitwa Jerrome Mtuvu. ALUTA KONTINUA. Hayo ndiyo maneno ya mwisho kwenye barua hiyo. Maneno hayo yalinitia simanzi . Nikainamisha kichwa chini huku nikifikiria upya kuhusu Ommy, mtu ambaye ameamua kuutoa moyo wake kupigania maslahi ya wengine. Nilimfananisha na wanamapinduzi mbalimbali wa Afrika kama Kwame Nkurumah wa Ghana na Samora Machel wa msumbiji. Tuna watu wachache sana wa aina hii katika kizazi chetu cha sasa. Hakuna wazalendo wa kweli na hawatatokea tena. Nani atakuwa tayari kuipigania nchi iliyojaa dhuluma na ufisadi? Nani yuko tayari kwenda kutoa taarifa ya uhalifu wakati baadhi ya polisi wana urafiki mkubwa na majambazi. Nani yuko tayari kutoa hata taarifa ya mtu aliyechomwa kisu mtaani, lazima ataogopa kwani bila shaka atakuwa mtuhumiwa namba moja huku akisota gerezani kusubiri upelelezi wa muda mrefu wa Polisi ukamilike. Moyo huo alikuwa nao Ommy na wachache ambao ni vigumu kuwafahamu. Nilitamani zirudi zama za wazalendo wa ukweli kama kina Nelson Mandela na wengineo kama yeye. Niliinua Macho nikatazama saa iliyokuwa ukutani, Ilikuwa ni saa 6.01 usiku nikagundua kuwa Johari alikuwa na njaa ingawa hakutaka kuongea. Nikaenda kuoga haraka haraka, nikabadili nguo kisha nikaenda kutafuta chochote kwenye baa ambazo zilikuwa hazijafungwa ili tuweze kula mimi na Johari. *** Aluta kontinua! maneno ya Ommy yalijirudia kichwani kwangu huku nikimtazama Johari ambaye alikuwa anamalizia zile ndizi za kuchomwa. Kitu kimoja kilikuwa kinaichanganya akili yangu, Ommy alikuwa amenipa namba ya Jerrome Mtuvu eti nikaombe msaada kwake wakati nafahamu fika kuwa ndiye yule mnafiki aliyekuwa ananihoji polisi kisha akanirudisha katika mikono ya Bonge ambaye sasa nilimfahamu kwa jina la Samson Kipusa. “Au na yeye alilaghaiwa na Jerrome kuwa ni mtu mzuri akamuamini?” Niliwaza. Johari alikuwa amemaliza kula, muda wote alikuwa kimya akinitazama ili ajue nini kitafuata. “Johari!” nilimwita, kabla hajaitika nikaendelea “Tuna mengi ya kuongea, tena mengi sana lakini kwa leo inabidi tupumzike!” nikainuka pale nilipokaa nikatumia ishara ya mkono kumtaka anifuate. “Utalala hapa!” Nilimwonesha kile kitanda nilichokuwa nalalia wakati Ommy akiwepo. “Peke yangu!?” “sasa ulitaka ulale na nani?” Nilimuuliza kwa mshangao kidogo.











     “Siwezi kulala peke yangu kajuna, watanikuta……” “Kina nani?” nilimkatisha. “tafadhali usiniache Kajuna naogopa kulala peke yangu!” alikuwa na hofu ya kweli, sikuwa na jinsi. Tukalala kitanda kimoja. Tukalala mzungu wa nne. Kwa jinsi nilivyochoka sikuchelewa kushikwa na usingizi, nikalala. Ilitakiwa mtu mwenye moyo wa jiwe. Ndiyo lakini mzungu wa nne yataka moyo. Usiku haukuwa mzuri kwa Johari , alikuwa anashtuka na kuweweseka sana. Akashindwa kulala upande wake akageukia upande wangu. Akawa amelala huku amenikumbatia. Ilikuwa hatari. Wee thubutuu! Nani kakwambia bila kupima siwezi. Nikaomba Mungu usiku uishe salama. Niliweza, inawezekana mambo mengine tunayaendekeza tu. *** Niliamka mapema zaidi. Nikakaa sebuleni, sikuweza tena kuendelea kukumbatiwa na Johari pale kitandani. Sina roho ya chuma. Ingawa alikuwa anafanya hivyo kutokana na woga wake kwangu ilikuwa adhabu tosha, kuna wakati niliweza kujisahau nikahisi kuwa nimekumbatiwa na Betty, pia niliweza hata kumpapasa pale nilipojisahau. Ah…. Yamepita. Jambo kubwa lililokuwa linaumiza kichwa ni jinsi nitakavyotoka mle ndani kwenda kupata mahitaji bila kujulikana. Nilihisi pengine sura yangu ilishakuwa maarufu kwenye magazeti. Sina uhakika kama magazeti yalishaautaarifu umma juu ya kitendo changu cha kutoroka na kufanya mauaji makubwa. Nikavaa mawani ya jua ambayo alikuwa anatumia Ommy siku za jua kali. Hakuwa akiitumia mara kwa mara hivyo bado ilikuwa kama mpya ingawa ilikuwa ni ya muda mrefu. Sehemu ya kwanza ilikuwa ni kituo cha magazeti. Nikakusanya magazeti mengi, sikujali ni ya lini kwani muda mrefu nilikuwa kwenye dunia ya nusu wafu. Nikaenda dukani, nikanunua vitu mbalimbali bila kusahau chupa ya chai. Kama kawaida ya mitaa kama hii, kulikuwa na vibanda vingi vya kina mama wauza chakula. Vibanda hivi vilikuwa vimepambwa kwa sanaa ambayo ilitafsiri hali halisi ya maisha ya Mtanzania, Karibu vibanda vyote vilikuwa vimezungushiwa kanga au vitenge vilivyochoka. Watu wengi hususani makapera walikuwa wakipata huduma zao humo. “Niwekee vikombe sita tafadhali” “Sita haviingii humu, vitano na nusu tu!” “haya weka vitano, unifungie na chapati tano” yule mama mnene akanifungia chapati zangu nikaondoka kurudi nyumbani. Wakati narudi ndipo nilipopatwa na mshtuko baada ya kuwaona watu wawili wakinifuata kwa hatua za haraka. Nilipowatazama vizuri nikamkumbuka yule mmoja. Alikuwa yule dereva wa gari lilonichukua na kisha kupata ajali kabla sijajikuta niko hospitali. Ina maana hakufa? Nilijiuliza. Kitu ambacho kilinifanya nimtambue kuwa ni yeye ni unene wake na ile nundu iliyoota kwenye paji la uso. Tofauti na siku ya kwana kuna kitu cha ziada kilikuwa kimeongezeka kwenye sura yake. Jicho, alikuwa hana jicho moja nahisi lilipotea siku ya ajali. Kwa kuwa nilishafika karibu na nyumbani sikutaka wafahamu pale nilipo. Hata hivyo nahisi walikuwa hawajagundua kuwa nimewaona maana ingawa walikuwa wanakuja kasi bado walikuwa kama ni watu wanaonivizia. Nikaamua kutumia vizuri fursa hiyo kwa kufuata barabara inayoelekea makaburini. Nikaongeza kasi nami nikiendelea kujifanya sijawaona, mara kwa mara niliinua mkono wangu nikijifanya kuangalia saa. Nilikosea, nilikosea sana kwani mbele yangu niliwaona watu wengine wakinifuata. Sasa ni wazi nyuma kulikuwa na watu mbele pia. Hapo nikaamua kukona na kufuata kichochoro ambacho kinaelekea kituo cha polisi Makangarawe. Nilipofika mbele nikaingia kwenye nyumba mbovu ambayo ilikuwa inatumika kama dampo la kutupia takataka. “Amepotea?” Nilisikia watu wakiulizana. “Inavyoonesha anaishi kule bondeni tatizo ni ninyi mliokuwa mbele yake inaonesha kuna mmoja amemtambua, sisi tulikuwa tunamfuatilia vizuri na hakujua kama anafuatwa!’ “Sasa?” “Ni vizuri tukiweka doria maeneo haya kuanzia leo.” “Hilo ni wazo la kipuuzi, bosi amesema yule jamaa ana akili sana. Sidhani kwa mtu mwenye akili kuweza kuendelea kukaa hapa baada ya kugundua kuwa anatafutwa.” “Dah, sure mwana hapa tumempoteza tuondoke zetu si unaona hata nyumbani kwake haonekani kabisa?” Nikasikia sauti za nyayo za watu, bila shaka walikuwa wanaondoka. Nikaondoka pale mafichoni na kuelekea nyumbani. Johari alikuwa ameamka. Alionekana kuwa na mawazo mengi na hasira. Nikamsogelea nikambusu shavu la kulia, akaniangalia kwa kustaajabu. “Wewe! huogopi?” “niogope nini?” Nilimuuliza “Si wanasema ni nuksi kumbusu albino?” “Kwani kila linalosemwa lina ukweli?” “Mh, we hujui kama lisemwalo lipo?” “Wapo waliosema dunia imefika mwisho na hatukuuona!” Nikacheka kisha nikampiga mabusu mfululizo ili kumuondoa hofu. Kabla ya kunywa chai nikaanza kusoma magazeti. Vichwa vya habari vilinitisha, vilikuwa na habari ambazo kwa wasomaji wa kawaida ni za kusisimua. Zilinitisha. Gazeti moja liliripoti kuwa MTUHUMIWA ATOROKA NA KUFANYA MAUAJI MENGINE. Habari hii ilikuwa inaeleza juu ya mauaji ya walinzi wa Samson Kipusa huku ikielezea pia kupigwa risasi kwa Samson mwenyewe. Taarifa iliendelea kueleza kuwa kwa sasa Samson amelazwa katika wodi ya wagonjwa mahututri pale Muhimbili baada ya kujeruhiwa vibaya kwa risasi. Habari ikamalizia kuhusu uporaji wa gari ambalo lilitelekezwa Temeke. Nikamimina chai kwenye kikombe nikampa Johari . “kunywa rafiki yangu!” Johari akatabasamu huku akinitazama kwa macho yaliyojaa aibu. Akaanza kunywa chai huku akinitazama jinsi nilivyokuwa nasoma magazeti. Baada ya kumaliza kusoma magazeti hayo ambayo yalinitisha nikamimina chai kwenye kikombe. Sikutaka kuumiza kichwa kwa habari hizo ambazo zilikuwa zinaonesha kuwa mimi ni jambazi sugu. “Johari.” “Abee.” Akaitika. “Nadhani muda umefika sasa wa kuweza kuelezana kile kilichosababisha tukutane mimi na wewe.” “Nitaanza kukusimulia mimi kilichotokea hadi tukakutana kisha nitasikia kutoka kwako” kisha nikamsimulia kila kitu. Alikuwa ananisikiliza kwa makini na kutokwa na machozi hasa pale nilipomsimulia kuhusu mpenzi wangu Betty na habari za ule mzigo wa Mwanza. *** “Naitwa Johari Iyina Mayala, ni mzaliwa wa Shinyanga katika wilaya ya Mwadui. Mimi ni mtoto wa pili katika familia ya mzee Mayala ambaye aliwahi kuwa diwani katika kata tofauti za Shinyanga mjini. Mama yangu mzazi alifariki dunia nikiwa kidato cha nne shule ya sekondari ya Biashara ya Shinyanga . Wakati wa uhai wa mama yangu niliishi kwa furaha sana kwani alinijali na kunithamini. Matatizo yalianza kujitokeza baada ya kifo cha mama yangu. Kuna wakati baba yangu alikuwa ananiambia maneno ambayo yalikuwa yananitia uchungu sana. Alikuwa ananiambia wazi wazi kuwa mimi ndiye ninatia nuksi katika familia. Maduka yake hayaendi vizuri, magari yanaharibika mara kwa mara eti chanzo ni mimi. Ikafikia wakati akaamua kuoa mwanamke mwingine. Akatulia kidogo na kunywa maji, kisha akaendelea. Huyo mama alipokuja ikawa mwanzo wa mashaka na mateso, nilikuwa nimefundishwa kuendesha gari wakati wa uhai wa mama yangu. Mara moja moja nilikuwa nachukua gari na kwenda nalo mjini. Wengi walinisifia kuwa nilikuwa dereva nzuri, lakini baada ya kuja mama mwingine nikawa nimezuiwa kabisa kutumia magari hayo kwa madai kuwa eti nitayatia mkosi. Nilianza kuumwa kichwa mara kwa mara kutokana na mawazo!” akatulia na kuanza kutokwa na machozi. “Enhee, endelea!” nikamuhimiza baada ya kumuona amesita kusimulia. “Ikatokea siku ambayo siwezi kuisahau katika maisha yangu. Siku hiyo alikuja mtu ambaye nilihisi kuwa ni mganga wa kienyeji. Akawa anaongea na baba. Toka nianze kunyanyaswa nilikuwa nimejenga tabia ya kujificha na kuwasikiliza baba na mama walikuwa wanaongea nini kuhusu mimi. Nikiwa karibu na dirisha niliweza kusikiliza vizuri sana maongezi yao. Nikamsikia yule mganga akiongea. “Kama ni ubunge utaupata lakini masharti yake kidogo ni magumu!” “Masharti gani?” aliuliza baba “Mizimu inataka kafara ya mkono wa kulia na mguu wa kushoto wa albino” nilimuona baba akishtushwa na kauli hiyo. “hivi imewahi kweli kutokea kafara ya aina hiyo!?” Aliuliza tena baba. “Toka siku za nyuma kafara za aina hii tumekuwa tukizifanya, ili kukwepa mikono ya sheria tuliamua kupandikiza imani kuwa albino huwa hafi bali hupotea, lakini siku hizi mambo yameanza kuwa wazi kutokana na uwingi wa vyombo vya habari!” Baba alikuwa ametulia huku akimsikiliza kwa makini yule mzee hali iliyonitia hofu. “Unataka kuniambia nikifanya hiyo kafara nitafanikiwa?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “siwezi kukudanganya mzee katika orodha yangu nina wavuvi wa samaki na wafanyabiashara wa madini, hakuna hata mmoja ambaye amewahi kuja kulalamika kuwa hajafanikiwa. Tena nilitaka kusahau katika orodha ya wateja wangu yupo waziri mmoja anaitwa……” sijui alitaja jina gani sina kumbukumbu kama alisema ni muheshimiwa Kenge au kingi.” Akatulia tena na kunifanya niwe na hamu kubwa ya kuendelea kumsikiliza. “Baada ya kuongea vile baba akamweleza yule mganga kuwa ana mtoto wa kike ambaye ni albino, yule mganga akacheka sana, kisha nikamsikia akisema “Kama una mtoto wako mwenyewe hata ukiutaka uraisi utaupata.” “Ah! Hapana kwa sasa nahitaji ubunge kwanza labda uchaguzi unaokuja.” Nikashtuka baada ya kauli hiyo. “Ina maana baba yuko tayari kuniangamiza?” nilijiuliza huku nikisikia uchungu sana. “Ili umtumie vizuri inabidi achukuliwe mzima kwani itanisaidia kufanya kafara ya watu wengi kwa pamoja. “niko tayari kumtoa mwanangu ili mradi niupate huo ubunge!” aliongea baba kitu ambacho kilinifanya nipatwe na msthuko mkubwa. Sikutaka kupoteza muda nikaamua kutoroka, nikaenda kujificha kwenye jengo moja ambalo bado lilikuwa halijakamilika liko mtaa wa kaunda. Nikakaa humo hadi usiku. Maisha yangu yakawa ya kutangatanga kwani mara kadhaa nilipita majalalani kutafuta chakula na ilipofika usiku nilitafuta gofu nikalala hapo. Maisha yangu yalikuwa hivyo kwa siku kadhaa, nilikonda nikadhoofika. Matangazo yakatolewa kuwa natafutwa nimepotea! Ni kipindi kigumu ambacho siwezi kukisahau kwani niliishi kama kichaa. Ulifika muda ikawa hatima ya maficho yangu kwani nilipatwa na homa, nikaenda kwenye zahanati ya daktari ambaye ni rafiki mkubwa wa baba kwani naye ni kada mwenzake wa chama. Nahisi yeye ndiye aliyetoa taarifa kwa baba kuwa niko pale. Baada ya dakika arobaini wakati nasubiri huduma ghafla nikamuona baba anaingia pale zahanati akiwa ameongozana na watu wanne wote wakiwa wanaume. Nilipatwa na mshtuko nikapoteza fahamu. Nilipozinduka nikajikuta nimefungiwa kwenye chumba cha wageni. Baada ya siku saba ndio nikasafirishwa kuja Dar, nikawekwa kwenye chumba kile kama ulivyonikuta! ” akamaliza kusimulia na kunifanya nitafakari zaidi. Inakuwaje mtu anaamua kuitoa damu yake sadaka, huku ni kupoteza mwelekeo. “Ulisafirishwa vipi kutoka Shinyanga?” Nilimuuliza. “Nakumbuka siku hiyo ilikuwa Ijumaa asubuhi. Kule chumbani nilikofungiwa walikuja watu wanne. Yule mganga, baba na wengine wawili ambao sikuwafahamu, ingawa yule mmoja nilisikia akiitwa Martin mwingine sikubahatika kusikia jina lake. Yule mganga akachukua kitu kama mkia wa ng’ombe akawa ananipiga nao kichwani huku akiongea maneno ambayo sikuyaelewa” “Wakati anafanya hivyo haukupiga kelele!” “Hapana nilishakata tamaa tena ajabu nilitamani zaidi kifo kuliko kitu kingine thamani yangu ilikuwa mbele ya Mungu duniani sikuiona tena, ndio maana ulipotaka kuniokoa nilikukatalia Nashukuru kwani umeonesha ubinadamu mkubwa kwangu!” “Usijali, enhe ikawaje?” “Kisha yule mtu mbaya ambaye wanamwita Martin akanichoma sindano, baada ya dakika chache nikalala. Nilipoamka ndo nikajikuta nipo kule ulikonitoa.”





     ******** Katika habari za magazeti yale ilinivutia makala ya gazeti moja ambalo nililihifadhi ili nilisome baadae.Nililitunza kwa sababu makala yake ilinivutia kidogo nilipanga kuisoma baada ya kumaliza mahojiano na Johari .Ilikuwa na kichwa cha habari kilichosomeka UKWELI KUHUSU MAUAJI YANAYOENDELEA habari yenyewe iliandikwa kwa mtindo wa makala hivyo nililazimika kuisoma kwa vipande vipande.Kipande kimoja kiikuwa na maandishi ambayo mwandishi alililalamika kuwa vyombo vya usalama havikuwa makini kwani haiwezekani matukio yote yale ya kutisha niyafanye mimi tena bila sababu za msingi,mwisho akamaliza kwa ahadi ya kueleza kiini cha yote yale toleo lijalo.Kwa kuwa lile gazeti lilikuwa linatoka kila siku nikaamua kusubiri siku itakayofuata nione mwandishi ataeleza nini anachokijua.Yule mwandishi alikuwa anafahamika kwa jina la Stela Mangungu. “Hivi huyu Stella mada nyingine anazoanzisha haogopi?” niliwaza. Nilianza kuhisi hatari inayomwandama mwandishi huyu kwa makala aliyoandika.Najua wazi nia yake ya kuandika kiini cha yote katika toleo linalokuja inatokana na mawazo yake binafsi. “Lazima nimsaidie la sivyo atakufa huyu!” Niliwaza. Namshukuru Mungu kuwa mpaka kufikia muda huo akili yangu ilikuwa inafanya kazi kwa wepesi wa ajabu sana.Nikaikumbuka simu iliyoachwa na marehemu Merina. Nilikuwa nimeshamkabidhi Ommy,nikaenda kuitafuta kwenye mabegi yake,nikaiona.Alikuwa ameihifadhi kwenye mfuko wa pembeni wa begi.Haikuwa na chaji. Nikaenda katika kibanda kinachotoa huduma za simu.Nilitaka niichaji simu ile lakini yule jamaa alikuwa na chaja za aina mbalimbali hivyo nikaamua kununua kununua chaja ambayo nitaimiliki mwenyewe. Nikarudi nyumbani kwenda kuchaji ile simu. Saa 7.15 simu ilikuwa imejaa chaji.Nikampigia Stella yule mwandishi wa gazeti la UKOMBOZI.Nashukuru huu utaratibu wao wa kuandika namba za simu baada ya makala ndio ulionisaidia sana.Stella alikuwa hewani. “Unaongea na na Sebastian Mumba hapa!” niliongopa. “Nikusaidie nini?” sauti ya kike iliuliza. “Nahitaji kuonana na wewe nitakupata vipi?” “Unajua unaongea na nani?” “Bila shaka ni Stella Mangungu!” “Ok!Njoo nyumbani saa kumi na mbili,naishi kinondoni nyuma ya shule ya sekondari ya Ridhwaa seminary shuka kituo cha mkwajuni.Ukifika maeneo hayo uliza kwa mzee Mwakasungura! ” Nikakata simu kisha nikaanza kuitafuta namba ya Ommy. Nilipoipata nikapiga,hakupatikana!.Kidogo nikaingiwa na hofu,yuko wapi Ommy?Wakati nikiwaza hilo mara simu ikaanza kuita. Alikuwa ni Stella. “Enhe,sema!” “Samahani nilikuwa nataka kujua wewe ni nani na una shida gani?” “Nafikiri nimeshakueleza kuwa naitwa Sebastian Mumba,nimevutiwa na ile makala yako juu ya mauaji ya kutatanisha yanayoendelea hapa nchini kidogo nimeona unaelekea kwenye ukweli hivyo nataka kukusaidia ili uandike kitu sahihi na siyo makala kama Insha za sekondari!”Nikasikia akishusha pumzi kwenye simu. “Sawa!” alijibu baada ya kuwa hewani kwa sekunde kadhaa bila kuongea. ******** Niliwaza sana jinsi gani nitafika mitaa ya Kinondoni nikiwa mtu ninayetafutwa kila kona.Nikacheka baada ya kupata wazo.Johari akawa ananitazama kwa mshangao bila kuuliza wala kuongea chochote.Alikuwa na mawazo mengi sana.Bila shaka alikuwa anataka kujua hatima ya yote haya itakuwa nini.Nikatoka kwenda kununua mahitaji muhimu ikiwa ni pamoja na vifaa vya kazi ambayo nilitarajia kuifanya usiku huo. Nikanunua redio ndogo aina ya Rising,redio hii ilikuwa inarekodi.Nikanunua mikanda mitatu ya ‘tape’ ambayo ilikuwa haijarekodiwa chochote. Pia nikanunua vazi aina ya kanzu na baraghashia. ********* Daladala nililopanda liliwasili Kinondoni mkwajuni saa 11.00,ilikuwa ni saa moja kabla ya muda tuliokubaliana kukutana.Nilitembea taratibu kuelekea upande nilioelekezwa na Stella.Simu nilikuwa nimeiacha hivyo sikuweza kumfahamisha Stella kuwa nimefika na sikutaka afahamu ujio wangu.Sikuwa na shida ya kuonana na stela muda huo nilikuwa na mawazo yangu binafsi.Nilijua wazi kuwa Stella atakufa kama sitatoa msaada kwake. Tatizo kubwa ambalo lingemgharimu Stela ni kitendo changu cha kuwatoroka wale Mashetani. Pengine Stella angeweza kuhisiwa kupata habari kutoka kwangu.Jukumu lao kubwa lilikuwa ni kumfunga mdomo.Lazima wangemtafuta Stella. Kwa kuwa nilishaingia kwenye mapambano haya ya aina yake nilikuwa na jukumu la kuhakikisha Stela anakuwa salama. Nikiwa ndani ya vazi la kanzu na baraghashia nikaanza kutembea taratibu kuelekea mbele kidogo kutoka pale kituoni. “haloo kijana,unaweza kunielekeza nyumbani kwa Mwakasungura” nilimuuliza kijana mdogo ambaye alikuwa anacheza mpira na wenzake “nyumba ileee!” alinionesha kwa kidole nyumba ambayo haikuwa mbali kutoka pale niliposimama,huku akionesha wazi kukerwa na kitendo changu cha kukatisha burudani yake.Nikatembea taratibu kuifuata nyumba ile.Sikuwa na wasiwasi kwa sababu vazi la kanzu na kibaraghashia vilinifanya nipewe Salam aleikum nyingi sana.Hii ina maana kuwa sikutambulika licha ya baadhi ya magazeti kuchapisha picha yangu. Ingawa jua lilikuwa linaelekea kuliaga jiji la Dar es salaam sikuthubutu kabisa kuvua miwani ile ya jua,niliogopa kutambulika kwa urahisi zaidi.Nilipofika usawa wa ile nyumba sikusimama hadi kwenye banda la chips ambalo lilikuwa jirani. “Naomba chips mayai!” “poa ustadhi wangu!” Alinijibu muuzaji baada ya kuagiza mlo huo ambao unapendwa sana jijini Dar. “Zikauke sana ustadhi wangu?” Aliuliza tena. “Eee kausha!” Nilimjibu huku nikimeza mate kwa hamu ya mlo huo. Chips zilikuwa tayari kwenye sahani. Nilianza kula taratibu huku nikitembeza macho yangu hapa na pale kwa namna ambayo mtu yeyote asingeweza kugundua kuwa nilikuwa kwenye kazi fulani. “Inaelekea biashara ni ngumu mbona sioni wateja?” nilimuuliza muuzaji “wateja wa hapa wengi ni wa usiku” alinijibu.Nikawa nimeanzisha maongezi ya kuongelea hili na lile kuhusu biashara ili mradi nicheleweshe muda. Baada ya kuona chips ambazo nilikuwa nakula taratibu mno zinaisha nikaagiza soda,yote ikiwa ni moja ya mbinu za kupoteza muda. Nilikuwa nakaribia kukata tamaa ndipo nilipoliona gari la kampuni ya magazeti ya Ukombozi likiingia. Likasimama mbele ya nyumba ya Mwakasungura. Nililijua kwa sababu nyuma lilikuwa na nembo kubwa ya kampuni ile.Kama nilivyotarajia aliyeteremka alikuwa ni Stella.Ukweli sikuwa na shida ya Stella,nilikuwa nawahitaji wale wauaji.Kwa jinsi nilivyowafahamu nilijua wazi ni lazima watamfuatilia Stella kutokana na makala aliyoandika.Nikatulia pale kwenye banda la chips kwa muda mrefu kidogo hatimaye nikaamua kuondoka na kutafuta eneo lingine ambalo lisingekuwa mbali na pale kwa Stella. Bado hali ilikuwa shwari kitu ambacho kilinipa moyo kuwa huenda wauaji walikuwa hawana mpango na huyu dada. Nikaamua kuondoka na kurudi kituo cha daladala. Nikasimama hapo nikisubiri gari za buguruni.Nuru ya jua ilikuwa imetoweka kabisa. Taa zilizokuwa zinawaka kwenye majengo mbalimbali zikaanza kuchukua utawala wake. “Lakini kwanini nisionane naye? Watamuua huyu!” Nilijiuliza.Nilikata shauri kurudi kwa Stella. Nilipofika nikabisha hodi,mzee wa makamo akanifungulia mlango. “Shikamoo mzee!” “Marhaba mwanangu,karibu!” “Ahsante,samahani naomba kuuliza,nimemkuta Stella yule…..” akanikatisha “Ni nani wako!” aliuliza yule mzee. “Huwa ananiita mara nyingi kumsomea dua!” “Ahaa,nenda huko nyuma utakuta milango mitatu huo wenye pazia la njano ndio mlango wake” Nikaelekea uani moja kwa moja.Nikakiona chumba alichonielekeza.Nikakiendea huku mapigo ya moyo yakienda kasi.Sijui ni kwa nini lakini kadri nilivyokisogelea kile chumba nilihisi mapigo ya moyo yakiongezeka. Nilipofika mlangoni nikasita kubisha hodi.Nilipoangalia vizuri kumbe kilikuwa chumba na sebule. Nikaendelea kuganda pale mlangoni huku nikisikia muziki wa taarabu ukirindima mle ndani.Kwa mbali niliweza kusikia sauti za watu wanaongea mle ndani. Nikashika kitasa cha ule mlango nikafungua taratibu. Nilikuwa natetemeka sana kwani nilijiuliza iwapo nitaingia kwa mfumo huu na kukutana na stella bila shaka nitapigiwa kelele za mwizi. Nikaupeleka mkono wangu kwenye mfuko suruali ambayo nilikuwa nimevaa,huku ikifichwa vema na kanzu. Ilikuwepo!Ile bastola yangu ambayo niliipata Mbagala. Nikafungua mlango,nikawa natembea kwa kunyata kuelekea kule chumbani. ”Hivi nikimkuta Stella na mumewe nitamueleza nini?” Niliwaza.Nikaufikia mlango wa chumbani,kijasho chembamba kilianza kunitoka. “Tafadhali kuwa mtulivu kama ulivyokuja!” Sauti nene ilinishtua na kukatiza zoezi langu.Nikahisi kitu kigumu chenye ubaridi kikiwa kimegusa kisogoni kwangu. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/“Ujanja wowote utakaojaribu kuufanya nitakulipua!” mapigo yangu ya moyo yalikuwa yanakaribia kuzimika kwa woga niliokuwa nao. Muda ule ule nikapata wazo,iwapo nitaendelea kuwa mwoga basi kifo kilikuwa kinakaribia.Hata hivyo kifo kilikuwa kimekaribia tu! Kama ni kurudi katika mikono ya wale jamaa basi hakukuwa na hukumu nyingine zaidi ya kifo. Nilifikiria kumpiga teke kwa nyuma lakini nikaogopa ile kanzu,ilikuwa haiwezi kutanuka na kutoa teke la haja. Akili ilikuwa inafanya kazi kutafuta namna ya kujiokoa lakini sikuiona.Nikaamua kutulia ili liwalo na liwe. “Hivyo hivyo naomba ujibu maswali yangu!” Akatulia kabla ya kuanza kuuliza. “Wewe ni nani na unatoka wapi?” “Naitwa Athumani Kipande natokea idara ya usalama wa taifa operesheni maalum!” Nilijibu kwa kujiamini “Hapa umefuata nini?” “Nimekuja kumsalimia mpenzi wangu Stella!” “Kwa hiyo unapokuja kumsalimia mpenzi wako huwa unakuja kwa utaratibu wa kunyata tena bila kubisha hodi?!” “Hapana nimesikia sauti ya kiume hivyo nilikuwa nakusudia kufumania!” “Unataka kuniambia humuamini mpenzi wako?” Sikujibu nikakaa kimya “Narudia ina maana hutaki kumuamini mpenzi wako!” “Acha kuniuliza maswali ya kipuuzi unanipotezea muda!” Nilifoka. “Pumbavu,yaani unaona mimi napoteza muda?” “Ndiyo kwa sababu najua wazi kuwa huwezi kunifanya lolote!” “We nyang’au maneno gani unaongea!” “Nina uhakika huwezi kunifanya lolote kwani hata jinsi ulivyoingia tumekuona,na hivi ninavyokuambia yule kiongozi wenu ashakamatwa!” Nilikuwa najaribu bahati yangu kwa kumzubaisha yule jamaa. Kweli nilikuwa nimempatia kwani niliweza kusikia pumzi zake zikipanda na kushuka kwa hofu.Pia nilihisi kuwa amelegeza mkono ambao ameshika ile bastola.Ilikuwa ni fursa ambayo sikutakiwa kuipoteza. Ghafla,niligeuka kwa kasi nikatumia mkono wangu wa kulia kuupiga ngumi mkono uliokamata ile bastola.Akiwa ameduwazwa na kitendo kile cha ghafla nilimsukuma kwa mikono yote miwili akaangukia juu ya meza ndogo iliyokuwa pale sebuleni.Ilikuwa ni meza ya duara yenye mguu mmoja.Nikaishuhudia ile meza ikianguka na kumfanya yule jamaa apige mwereka mkubwa huku akifuatiwa na ile meza kwa juu.Sikuwa na muda zaidi nikaiokota ile bastola yake. Nikafyatua huku nikiwa nimemlenga usoni. Nilishuhudia damu iliyochanganyika na ubongo ikitawanyika sakafuni huku ile bastola ikiwa haijatoa sauti kubwa ya mlipuko. Ilileta kinyaa! Nilishangaa bastola ile kwa nini haikutoa mlio kama nilivyotarajia.Badala yake ikatoka sauti ndogo sana kama kikohozi cha mtoto mchanga.Nikakumbuka kuwa kuna bastola ambazo zina kiwambo cha kuzuia sauti. Kama kulikuwa na mtu kule chumbani basi alishtushwa na kishindo cha mtu kuanguka. “Vipi Steve kuna tatizo?” sauti iliuliza kutoka chumbani. Hakuwahi kupata jibu nilifungua mlango wa chumbani. Alikuwa amenipa mgongo hivyo kazi ilikuwa rahisi nilimtandika risasi mbili za kichwa haraka haraka. Akaruka juu na kutua chini kama gunia la pumba. Alikuwa amekufa! Nilimwona mwanamke ambaye nilihisi kuwa ndiye Stella akiwa mdomo wazi.Alikuwa haamini mambo yaliyokuwa yanatokea. “Usiogope naitwa Kajuna Kazakamba !” Nikatoa baraghashia ambayo nilikuwa nimevaa,akapatwa na mshangao kwani hakutarajia kabisa ugeni huu wa aina yake. Hakuweza kuongea lolote. “Shusha mikono tafadhali kwani uko kwenye mikono salama!” Niliongea kwa sauti ya upole ili kumuondolea hofu. “kuna maiti mbili humu ndani naomba tuondoke haraka kabla mambo hayajaendelea kuharibika!” Simu yake ilikuwa mezani sikuomba nikapiga polisi,112 ni namba ngumu kupatikana lakini siku hiyo haikuwa na usumbufu. Nikatoa taarifa polisi kisha nikamgeukia Stella. “Tafadhali chukua kitu chochote ambacho ni muhimu kwako ujiandae tuondoke!” “Twende wapi?” “Sikiliza we mwanamke itabidi ukae mafichoni kwa muda wa wiki moja la sivyo utakufa.Ni hiari yako ukitaka utaondoka na mimi vinginevyo kwa heri!” Sauti yangu haikuwa na mzaha. Aliniogopa kwani nilikuwa nimebadilika na kuvaa sura ya ukatili. Akachukua begi kubwa la nguo.Sikutaka kumzuia ingawa kwa maficho ya wiki moja hakukuwa na ulazima wa kuchukua begi kubwa kama lile.Katika mawazo yangu nilishapanga ile kazi niimalize ndani ya wiki moja,yaani kama kufa nife kama kupona nipone. “Hapana tukodi tax!” alisema baada ya kuniona nikielekea kituo cha daladala. Alikuwa anatetemeka sana. Ilikuwa ni saa 3.34,wakati tunaelekea kituo cha teksi tukapishana na gari ambalo lilikuwa na askari wenye silaha.Mwanamke alinifuata kwa woga.Hakuwa na imani kuwa yuko kwenye mikono salama au la! Kitendo cha kumuokoa kutoka kwenye mikono ya wale washenzi kidogo kilimpa moyo. “Tandika!” Nilimwambia kwa mkato dereva tax. “Elfu kumi!” Alijibu kwa mkato huku akiwasha gari. Tulikuwa kimya kwenye lile gari huku kila mmoja akijaribu kuchambua hili na lile katika kichwa chake. Hakuna aliyeongea mpaka tulipofika Tandika. Tukatembea hadi kituo cha magari cha Buza kanisani. Huko tukachukua teksi nyingine kwa shilingi elfu tatu hadi Yombo abiola.Kwa kutumia njia zile zile tukafika pale nyumbani kwa Ommy. Nikagonga,Kimya!Mlango haukufunguliwa.Nikagonga mara tatu bado kulikuwa na ukimya ulionitia mashaka. “Mimi Kajuna naomba unifungulie tafadhali!” Nikasikia mlio wa hatua za mtu ambaye alikuwa anakuja mlangoni. Mlango ukafunguliwa.Johari alikuwa amesimama mlangoni huku akionesha wazi hofu kubwa. Kuna kitu nilikisoma kwenye macho ya Johari .Wivu! Sikutegemea kukiona kitu hicho kwenye wakati mgumu kama huo. “Hivi inawezekana kuwa huyu mwanamke ananipenda?” Nilijiuliza huku nikivua ile kanzu. “Johari kutana na Stella yule mwandishi ambaye nilimpigia simu asubuhi!” wakapeana mikono. Niligundua wazi ujio ule ulimkosesha raha Johari . Nikaamua kufanya kitu cha ajabu kidogo ili kutatua tatizo.Nikamshika Johari nikamvutia kwangu kisha nikamkumbatia.Nikampiga busu shavuni kisha nikamtakia usiku mwema. “Unakuja kulala?” Aliniuliza. “Leo utalala na huyu rafiki yako lakini tukimaliza maongezi kwanza!” Nilimjibu baada ya kumuona akiwa na wasiwasi wa kuachwa kwenye mataa. Nilimkazia macho Stella ambaye bila shaka asingeweza kulala bila kuelewa chanzo cha yote yale.Sikumficha kitu nikamsimulia kuanzia mwanzo hadi kufikia pale. Muda wote niliokuwa namsimulia nilimuona akiwa makini,alikuwa ameshangazwa na habari zile za kutisha.Hadi mwisho nilipomsimulia kuhusu nilivyopatwa na wasiwasi kuhusu ile makala yake. Akaniangalia kwa kustaajabu sana!





     “Ulishawahi kupitia mafunzo ya polisi!” Aliniuliza kwa mshangao “Hata mgambo sijawahi kupitia nafikiri nishakueleza nimemaliza kidato cha sita na sikuweza kujiendeleza kwa lolote zaidi ya kuomba vibarua vidogo vidogo kwenye viwanda!” Alizidi kushangaa. “Uliwezaje kutumia silaha?” Aliniuliza.Nikacheka sikuwa na jibu kwa swali hilo kwa sababu sijasomea chuo chochote mafunzo ya kutumia silaha.Pengine ilitokana na uzoefu wa kutumia bastola za watoto. “Unaweza kunieleza ni nini ulitaka kuandika kuhusu mauaji yale?” Nilimuhoji. “Unajua,nilikuwa sifahamu chochote isipokuwa nilikuwa naandika kama mawazo yangu tu,lakini cha ajabu toka asubuhi nimekuwa nikipokea meseji za vitisho!” alitulia kisha akaendelea . “Haya mambo niliyoyasikia ni mazito hivyo sina budi kukushukuru sana kwa msaada wako” Aliongea Stella kwa sauti tulivu. ********* Niliamka saa 12.10. Nikaelekeza macho yangu juu. Nilikuwa katika hatua za mwisho.Hatua ambazo zilikuwa ni karata katika maisha yangu.Ilikuwa lazima nipambane. Nikaamua kuchukua simu ya marehemu Merina.Nikapiga namba ambazo Ommy aliandika kwenye ujumbe wake kuwa ni za Jeromme Mtuvu.Huku nikiwa na wasiwasi nikapiga. “Unaongea na Jerrome Mtuvu,nani mwenzangu!” “Naitwa Kajuna Kazakamba!” “Ni utani?” Aliuliza kwa mshtuko “Ina maana sauti yangu umeisahau?” Nilimtega. “Sauti yako?” “Ndiyo umesahau mara ya mwisho kabla hamjaniteka tena kule polisi si ulinihoji!” Nilisikia upande wa pili mtu akishusha pumzi.Nikasikia simu ikiniashiria kuisha salio,hatimaye ikakata.Baada ya sekunde chache simu ikaanza kuita. “Halloo mbona sikuelewi? Kwanza namba yangu umeipata wapi?” “Hiyo namba nimeipata kwenye barua ambayo nimeachiwa na rafiki yangu Ommy!” ”Mh,naomba kama inawezekana tuonane!” Kwa jinsi alivyokuwa na mshangao nikahisi anaweza kuwa mwingine na si yule mnafiki.Nilishaamua kuonana naye. Nilishaamua liwalo na liwe. “Wapi?” “Njoo sasa hivi maeneo ya mnazi mmoja utanikuta kwenye ofisi za CRDB tawi la Lumumba pale wanapouzia magazeti.” Sikutaka kuchelewa nikaiweka sawa ile bastola yangu niliyoipata Kinondoni.Nikawaita Stella na Johari,nikawaaga. Nikawaambia wazi kuwa huenda ule ukawa mwisho wa maisha yangu.Johari na stella walikuwa wanalia. Johari alionekana kusikia uchungu zaidi,alikuwa ananipenda haikuwa siri. ******** Nilitembea taratibu nikikatiza mitaa mbalimbali ya Kariakoo.Nilipofika mtaa wa Kipata nikaongeza kasi kwani hakukuwa na watu wengi kama mitaa ya Lindi na Gerezani. Nikatokea nyuma ya jengo la CRDB Lumumba.Nikafuata kichochoro ambacho kilikuwa kinatokea mbele ya benki ile. Nilipofika nikawaona watu wengi wakiwa wamezunguka meza ya magazeti iliyopambwa na maandishi makubwa THE CITIZEN AVAILABLE HERE. Ingawa nilikuwa nacheza karata hatari sana kwenye maisha yangu bado sikuwa na hofu.Nilijihisi utulivu kwani nilikuwa tayari kwa lolote.Nilikuwa simjui mtu niliyekubaliana kukutana naye.Nilianza kuingiwa na mashaka kuwa kuna mtego. Nikazungusha macho huku na kule.Hatimaye macho yangu yakatua kwa mtu mmoja ambaye alikuwa amevaa suti ya kijani. Alikuwa anaangaza macho huku na kule huku akijaribu kupiga simu ambayo bila shaka ilikuwa haipatikani kwani nilimuona akikunja uso kwa hasira. “Bila shaka ni yeye!” Niliwaza baada ya kumuona uso wake ukibadilika na kuwa na mikunjo baada ya kushindwa kuipata namba ambayo aliikusudia.Huku mapigo ya moyo yakiongeza kasi yake nilimsogelea. Nikamgusa bega! “Jerry!” “Yaah! Kajuna?” Nikakubali kwa kichwa. Tukapeana mikono, mkono wake ulikuwa mgumu kidogo kiasi kwamba nilisikia maumivu wakati tunasalimiana. “karibu kijana uko very smart!” “Aaah, ahsante!”Nilimjibu huku nikijitazama mavazi yangu na kuushangaa usmart anaouzungumzia. “Simaanishi mavazi kijana,nakusudia utaratibu ulioutumia mpaka tunaonana ni makini na unaokubalika!” Akanipa tena mkono na kuutikisa kwa furaha kisha nikamfuata. Tukaliacha jengo lile la ushirika tukafuata ghorofa moja chakavu ambalo lilikuwa linapakana na jengo lile. Tukaanza kupanda ngazi kuelekea juu.Nilianza kuingiwa na hofu kuwa huenda niko katika mikono ya Bonge kwa mara nyingine. Tulipofika juu tukaelekea upande wa kulia wa korido ile.Upande wa kushoto kulikuwa na madarasa ya wanafunzi waliokuwa wanasoma masomo ya kidato cha nne kwa miaka miwili yaani QT.Upande ule ulikuwa na milango mingi huku kila mlango ukiwa na maandishi yalioutambulisha. Chumba tulichoingia kilikuwa na maandishi MSHAURI NASAHA.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Kilikuwa ni chumba kipana ambacho kilikuwa na vitu vingi sana.Nilishindwa kuelewa chumba cha mshauri nasaha kinakuwaje na vitu vya ajabu namna ile. Upande wa kushoto kulikuwa na kabati kubwa ambalo lilikuwa na vitabu vingi. Upande wa kulia kulikuwa na mlango mdogo ambao ulikuwa unaingia kwenye chumba kingine kidogo. Mezani kulikuwa na vitabu vingi huku nikivutiwa na kile ambacho kilikuwa na jalada jekundu huku kikipambwa na picha ya bastola. Nikaanza kufunua kitabu kile ambacho kiliandikwa kwa lugha ya kiingereza. Nilivutiwa sana na kitabu kile.Lever action pistols ndivyo maandishi ya ukurasa wa kumi wa kitabu kile yalivyoanza. Kulikuwa na picha ya bastola ambayo chini ilikuwa na maandishi yaliyokolezwa kwa wino mweusi Volcanic Pistol .41 cal.Nikatabasamu kwani lilikuwa somo zuri kwangu. Nilisoma kuwa aina hii ya bastola ilikuwa inamilikiwa kwa pamoja na Horace Smith na Daniel B Wesson, hii ilikuwa ni mwaka 1854.Aina hii ya bastola ilitengenezwa Norwich.Baada ya kuanguka wamiliki hawa wawili kiuchumi ikawa chini ya Oliver F Winchester.Alianza kumiliki kampuni inayomiliki silaha hiyo July 1855.Baada ya hapo jina la bastola hiyo likabadilishwa….. Sikuweza kumaliza maelezo kuhusu bastola hiyo kwani Jerry alikuwa amefika kutoka kwenye chumba kile kidogo. “Naitwa Jerrome Mtuvu ukipenda niite Jerry ni afisa usalama wa Taifa kitengo maalum!” Alianza kujitambulisha huku akipanga panga mafaili mbalimbali pale mezani,nikakumbuka hata yule Jerry mnafiki alianza kujitambulisha kama huyu. “Nashukuru sana bwana Jerry kukutana na wewe saa hizi!” Nikatulia kidogo na kumwangalia Jerry ambaye alikuwa ametulia sana pale nilipoanza kuongea. Nikaanza kumsimulia kuanzia mwanzo wa tukio mpaka mwisho. Alikuwa ametulia huku maelezo yale yakiingia moja kwa moja kwenye kifaa maalum ambacho alikuwa anatumia kurekodi mazungumzo yangu. “Umesema muheshimiwa Stefano Kenge pia anahusika! Unaweza kunifafanulia anahusika vipi?” Aliniuliza huku akizidisha utulivu ambao badala ya kunifariji ulionifanya nimuogope. “Ndiyo anahusika kwa asilimia tisini!” “Kama ningekuwa Jaji ungenithibitishia vipi ili niweze kumtia hatiani?” “Ungekuwa Jaji ingekuwa vigumu kidogo lakini kwa kuwa ni wewe nitakueleza vitu vitatu ambavyo vinanifanya niwe na uhakika wa asilimia tisini kuwa anahusika.Moja ni maelezo niliyoyapata kutokana na barua ya Ommy,pili ni ushahidi niliopewa na Johari kuwa muheshimiwa huyo alitakiwa kufanyiwa kafara ambayo ingehusisha kuchinjwa kwake na mwisho ni mimi mwenyewe ambaye nilimshuhudia pale kituoni akiongea na yule Jerrome wa uongo aliyekuja kunihoji hatimaye kunitorosha!” Nikatulia na kumkazia macho Jerry. “Nini kilikutuma kumfuata stella kule Kinondoni?” “Kama nilivyokueleza bwana Jerry watu hawa ni hatari sana kiasi kwamba yeyote anayeonekana kunusa au kutaka kunusa mambo yao basi hukumu yake ni kifo! Hivyo kitendo cha Stella kuandika makala ambayo inakaribia ukweli kilinifanya nitambue wazi kuwa uhai wa Stella uko mashakani” “Uliwezaje kukaa na siri nzito namna hiyo badala ya kuitoa katika vyombo husika?” “Njia zangu zote zilikuwa zimefungwa nilikuwa kama mtumwa niliogopa sana kuhusu ile picha na kubwa zaidi lililonichanaganya ni kuhusika kwa baadhi ya askari kwenye mkasa huu!” Baada ya mahojiano ya hapa na pale nikamuona akibadili mwelekeo wa mazungumzo yetu nilishindwa kuelewa anakusudia nini. “Umeshapata mpenzi baada ya kifo cha Betty!” Swali hilo kidogo lilinishangaza, “sijapata!” Nilimjibu kwa mkato “Ningefurahi sana kama angekuwa Johari !” Nikatabasamu kisha nikashindwa kujizuia nikacheka. “Kwanini awe yeye?” “Kutokana na masimulizi yako inaonesha kuwa umemthamini sana kiasi cha kutumia nguvu kumuokoa basi hata yeye atakuthamini maisha yako yote!” Kwa mara nyingine nikatabasamu lakini sikusema lolote. Nikainamisha kichwa chini huku nikitafakari juu ya kauli ile, alikuwa amenigusa. “Bwana Kajuna nashukuru sana kwa ujio wako na natumai tutashirikiana vema!” Aliongea huku akinitazama kwa upole,kisha akaendelea. “Kwa sasa naomba nikuruhusu uende,kesho naomba tukutane hapa saa 4.00” Alimaliza kisha tukaagana.Kidogo hili lilinishangaza.Niliona swala lile amelifanya kuwa rahisi mno.Afisa wa idara ya usalama tena wakutoka kitengo cha operesheni maalum kwanini asiniwekee utaratibu mzuri wa ulinzi badala yake kirahisi rahisi tu eti ananiambia nenda! Niliondoka pale ofisini nikiwa mnyonge sana,sikutegemea kama swala zito kama lile lingemfanya mtu mwenye wadhifa mzito serikalini aniruhusu hivihivi baada ya kuniuliza maswali ambayo hata polisi wa kawaida wangeuliza. Ghafla,nikiwa nimeliacha kabisa eneo lile nikakiona kitu ambacho kilinishtua sana.Ilikuwa ni maeneo ya gerezani. Sikuamini! Alikuwa ni mmoja kati ya watu niliowaona kule Mbagala.Nilimtazama vizuri nikamkumbuka.Alikuwa yule askari Bandia ambaye alikuja Hospitali akazusha tafrani kubwa baada ya kuua. Nikasimama eneo la wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama wamachinga.Nilitaka kujua yule mtu ataelekea wapi. Muda mfupi baadae akaja mtu mwingine mnene mfupi ambaye alivaa suti nyeusi. Wakapeana mikono kisha wakaondoka eneo lile kuelekea maeneo ya mtaa wa Lindi. Nikaendelea kuwafuata kwa tahadhari kubwa. Baadae wakaingia mtaa wa Kongo. Bado sikusita kuwafuata. Wakaingia kwenye duka moja la madawa na vifaa vya Hospitali. Nikasimama nje takribani dakika ishirini. Walipotoka walikuwa na boksi kubwa ambalo bila shaka lilikuwa na dawa mbalimbali.Wakaondoka na kuelekea maeneo ya Msimbazi. Wakasimama pale klabu ya simba. Nikasogea karibu kiasi cha kuweza kusikia maongezi yao. “Vipi lakini kuna matumaini ya kupona!” Aliuliza yule askari feki kwa sauti ya chini sana. Matumaini ni makubwa mno kwani tumefanikiwa kuondoa ile risasi……….” Sikuweza kusikia maneno ya mwisho kwani gari lilikatisha na kuleta kelele ambazo zilinifanya nishindwe kusikia maneno ya mwisho.Bado magari yaliendelea kukatisha kwa uwingi na kusababisha nikose kusikia maneno yote yaliyoendelea. Dakika chache baadae ikaja gari ambayo niliitambua sana. Ni ile Rav 4 nyekundu ambayo mara nyingi ilikuwa inatumiwa na Bonge. Wale watu wawili wakaingia kwenye ile gari.Sikupata tabu kuifuata ile gari kwani msongamano wa magari ulikuwa mkubwa.Wakaingia barabara ya uhuru. Kutokana na msongamano mkubwa wa magari niliendelea kutembea kwa miguu hadi maeneo ya shule ya uhuru huku lile gari likiwa halijapotea machoni mwangu. Nikafika kwenye kituo cha teksi cha shule ya uhuru. Mmoja wa madereva teksi akanifuata kwa kasi. “Twende bosi wangu!” Alinidaka haraka na kunihimiza niingie kwenye gari lake.Teksi lake halikuwa na ufito wa rangi ya yoyote kama yale mengine ambayo yalikuwa na ufito wa njano. Kutokana na haraka niliyokuwa nayo sikuweza kujiuliza sana. “Wapi bosi!” “Naomba tuifuatilie ile Rav4 nyekundu!” Nilisema huku nikimuonesha kwa kidole ile gari ambayo ilikuwa kwenye foleni. “Poa!” alijibu kwa mkato. Safari yetu ilitufikisha barabara ya Mandela, huku foleni ilikuwa imepungua ingawa hapa na pale tulilazimika kusimama. “Hizi foleni zinakera sana!” Niliongea kwa sauti iliyojaa hasira. “Mbona hata wewe unakera!” Alinijibu dereva kauli ambayo ilinishangaza. “Aaah,acha utani bwana mimi sijawahi kumkera mtu!” Nilimjibu huku nikijifanya kuichukulia kawaida kauli yake. “Si kweli, kero yako ni kubwa kama usingekuwa kero usingefuatilia watu kama hivi unavyofanya kufuatilia mambo yasiyokuhusu!” Safari hii kauli yake ilinitisha zaidi. Kisha akatoa kauli nyingine ambayo ilinitisha zaidi. “Mbona maovu yako hakuna anayefuatilia?” Hapa sikuweza kuficha hasira zangu. “Naomba unishushe hapa!” Nilitamka kwa hasira. “Utashuka tu lakini usisahau hii picha yako!” Akatoa ile picha yangu ya Tabata. Lilikuwa pigo jingine kubwa katika moyo wangu. “Naomba nishuke tafadhali!” Sasa niliongea kwa ukali zaidi. “Hutaki kwenda kumuona majeruhi wako !” Sauti nzito ilitoka nyuma yangu. Sijui nilikosa vipi umakini kiasi cha kushindwa kuwagundua watu wawili ambao walijificha siti za nyuma.Ilikuwa ni uso kwa uso na Martin. Hasira zake hazikuweza kufichika.Nadhani alikuwa anatamani aniue pale pale lakini mazigira yalikuwa hayaruhusu. “Mtoto mdogo umevuruga mambo mengi sana!” Aliongea yule mwingine ambaye alikuwa mgeni machoni kwangu. “Leo utapata malipo kwa kufungua mzigo!” Ailiongea Martin kwa sauti kavu iliyojaa hasira. Bastola mbili zilikuwa zimelenga kichwa changu. Sikuwa na la kufanya zaidi ya kukaa kimya.Nilikuwa nimenasa. Hakuna muujiza ambao ungeniokoa kwenye tukio hilo. Nilikuwa nategemea zaidi muujiza,sikuwa mjuzi wa kupigana kiasi cha kupambana na majitu mawili yaliyoshiba namna ile. Gari ilionyoosha kuelekea Ubungo kupitia barabara ya Mandela. Nilikuwa sielewi tena tunaelekea wapi kwani akili yangu ilikuwa haina nguvu yake ya kawaida.Nilikuwa nusu Mfu. MZIGO umeniponza.Katika nafsi yangu nilimlaumu sana Jerry kwa kutolichukulia ‘sirias’ suala langu. Ghafla,nikahisi kitu kizito kikinigonga kichwani. Nikaanza kujiona kama ninayefunikwa blanketi zito lisilo hata na nafasi ya kutoa hewa.Nikapotea,nikapotea……….Sikumbuki kitu tena baada ya hapo ingawa neno la mwisho nililosikia ni sauti ya Martin aliposema” lazima achinjwe leo akicheleweshwa atazusha balaa lingine kubwa!” Kisha kikafuata kicheko kikubwa ambacho kilikuwa kama radi. Baada ya hapo sikuwa tena katika dunia ya kawaida.



    Nilifumbua macho yangu, nikahisi maumivu makali ya kichwa. Taa yenye mwanga mkali ikanipiga usoni. Bado akili yangu ilikuwa na uwezo wake wa kawaida. Ingawa ilinichukua dakika mbili kuweza kujitambua. Nilikuwa nimelazwa kwenye kitanda kikubwa huku nikiwa nimetundikiwa dripu ya maji. Hakukuwa na mtu kule chumbani. Mandhari ya chumba ilinishangaza. Kilikuwa ni chumba kipana chenye madirisha makubwa. Nilishindwa kubaini hawa watu wana lengo gani. “Kwanini wameniacha hai mpaka saa hizi wakati mimi ni adui yao namba moja!

    Niliendelea kuisanifu mandhari ya chumba kile, haikuwa na kitu cha ajabu zaidi ya vitu vya kawaida ambavyo unaweza kuvikuta kwenye chumba cha kijana yeyote ambaye kayapatia maisha karibuni.

    Wakati nikiendelea kukisanifu chumba kile mlango ukafunguliwa. Maajabu! Msichana mrembo akaingia.

    “Waooo, Umeamka mpenzi!” Aliongea kwa sauti nyororo yenye kuvutia. Lilikuwa ni jambo lingine la ajabu. Akanisogelea na kunibusu shavuni.

    “Vipi unajisikiaje?” Alinisaili.

    “Najisikia vema!” Nilijikakamua kumjibu huku nikificha mshangao wangu. Akanihudumia kama mgonjwa yeyote anavyostahiki kuhudumiwa. Akanionesha upendo wa hali ya juu sana.

    Maigizo mengine?

    “Samahani sister, hivi hapa ni wapi nimefikaje na wewe ni nani?” Uvumilivu ulinisahinda nikalazimika kuuliza. Akacheka kabla ya kujibu. Usihofu Kajuna, mimi nina uwezo wa kujibu swali moja tu, mengine utajibiwa na wahusika!”

    “Kina nani hao wahusika?”

    “Usihofu utawajua tu muda ukifika!”

    “Haya nijibu sasa hilo unaloweza kunijibu!”

    “Naitwa Beatrice Kamugisha ni muuguzi katika hospitali ya Hindu Mandali”

    “Kwa hiyo hapa ni Hindumandal!”

    “hapana!”

    “Ni wapi sasa?” Akatabasamu kabla ya kunijibu.

    “Usiwe na haraka mimi sijaruhusiwa kujibu swali kama hilo!” Alinijibu huku tabasamu lake likiwa halijafutika usoni. Nilishindwa kuelewa kilichokuwa kinaendelea.

    Muda mfupi baadae nikaanza kuhisi usingizi nzito ukininyemelea . Nikajitahidi kupambana na hali ile lakini haikusaidia kitu. Nikalala.

    ***

    Nilipoamka kwa mara nyingine macho yangu yakakutana na sura ya Beatrice ambaye alikaa kando ya kitanda changu. “Amka ule mpenzi!” Aliongea kwa sauti ya kubembeleza.

    Hivi huyu anatania au kuna ukweli….. mpenzi mimi?

    Nilijiuliza huku nikitofautisha kabisa hadhi yangu na yake.

    Ni utani tu! Nilijibu mwenyewe.

    “Kajuna!” Aliita Beatrice kisha akaanza kuongea.

    “Kuna wageni wanahitaji kuonana nawe, wameniambia kama unajisikia vizuri niwaruhusu lakini kama bado hali yako si mzuri basi watakutana nawe siku nyingine” Kwa jinsi nilivyokuwa na udadisi moyoni hata kama hali yangu ingekuwa mbaya vipi bado nilihitaji kuonana na huyo mgeni hata kama atakuwa Bonge na kundi lake.

    “Waruhusu niko tayari!” Nilijibu haraka kwa shauku ya kutaka kuwaona hao wageni.

    Kama ni mshangao basi kwangu ilikuwa zaidi ya mshangao. Nashindwa kueleza kitu kinachozidi mshangao kinaitwaje! Huyu hapa Ommy alikuwa mbele ya macho yangu! Sikutegemea kama nitakuja kumuona tena. Pamoja naye alikuwa Jerry na mzee wa makamo ambaye sura yake ilikuwa ngeni machoni mwangu. “Ommy!” Niliongea kwa mshtuko mkubwa CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kajuna!”Naye alionekana kuwa na mshangao kama wangu.

    “Siamini kama ni wewe kweli!”

    “Ndiyo mimi Kajuna rafiki yangu!” Tulitazamamana dakika kadhaa bila kuongea chochote. Katika nafsi zetu ilipita furaha na faraja ya hali ya juu. Tukapeana mikono ya furaha huku tukiitingisha na kuzikumbuka siku chache zenye matukio mazito tulizokaa kwenye urafiki wetu.

    Jerrome Mtuvu ambaye muda wote alituacha tumalize furaha yetu akasogea pale kitandani. Yule mzee wa makamo alikuwa amekaa kwenye kiti huku akituangalia jinsi tulivyokuwa na furaha.

    “Samahani kwa kukukatishieni furaha yenu ya kukutana!” Aliongea Jerry kwa sauti tulivu kisha akaendelea.

    “Bwana Kajuna naomba utambue uwepo wa mkurugenzi mkuu wa idara usalama wa taifa hapa nchini Dokta Zakaria Mkude, siku tatu mfululizo alikuwa anakuja hapa ili aongee nawe lakini kwa bahati mbaya ulikuwa haujarudiwa na fahamu!” Ina maana niko hapa kwa siku tatu au zaidi! Nilistaajabu.

    “hivyo basi sioni sababu ya kuongea kwa niaba yake wakati mwenyewe akiwa hapa” Bwana Zakaria Mkude akasogezewa kiti karibu na kitanda changu.

    “habari Ndugu Kajuna!” Alinisalimia baada ya kuketi kwenye kiti alichowekewa. “Nzuri shikamoo!”

    “Marhaba, awali ya yote naomba nitoe shukrani kubwa na dhati kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye alitaka kuonana nawe lakini majukumu ya kitaifa yamesababisha akose fursa hiyo adhimu. Pili naomba nikupongeze kwani jina lako limeingia kwenye orodha maalum ya Mashujaa wa nchi hii, hivyo hata kama utakufa leo au kesho basi unastahiki kuzikwa kwa heshima zote za kijeshi, Kimsingi kazi uliyoifanya ni kubwa na unastahili sifa, Umejitoa kwa moyo wako wote kupambana na watu ambao wamekuwa wakiendesha mauaji ambayo yamelitia Doa kubwa Taifa letu. Taifa letu si kisiwa cha amani tena kama kilivyokuwa kikijulikana kutokana ya wenzetu wenye ulemavu wa ngozi. Tena ajabu! Tanzania imekuwa soko zuri kwa watu wa Burundi na Rwanda kuja kufanya biashara hiyo. Tumekuwa na sifa mbaya kiasi cha kuwaambukiza jirani zetu tabia hii ya kishetani. Kwa msaada wako tumeweza kugundua mtandao mkubwa wa wahusika wa biashara hii ambayo ni ya udhalilishaji. Hivi ninavyokueleza yule waziri anaye husika ameshakamatwa baada ya kupata kibali maalum kutoka kwa Rais. Sina mengi ya kuongea nimelazimika kuacha shughuli zangu kutokana na uzito wa kazi ulioifanya hivyo utamaliza shughuli yako kwa kushirikiana nasi bega kwa bega ingawa kimsingi hii kazi ilibidi tuifanye sisi lakini itakuwa ngumu bila msaada wako kwani wewe unafahamu mengi zaidi.” Akatulia na kuniangalia kwa macho yaliyojaa upole. Ingawa alikuwa mzee lakini alikuwa na mwili mkakamavu. Akasimama, akanipa mkono ikiwa ni ishara yakuagana na kutakiana heri.

    ***

    Baada ya kuondoka yule mzee nikamgeukia Jerrome Mtuvu!

    “Hivi hapa ni wapi pia nataka kujua nimefikaje?” Hilo lilikuwa swali ambalo nililirusha moja kwa moja kwa Jerry. Ni kama aliyelitarajia swali hilo. Akakaa pale kwenye kiti ambapo alikuwa amekaa mkuu wake wa kazi.

    “ Ningekuwa mjinga na mtu nisiyeijua kazi yangu kama nisingefuatilia nyendo zako baada ya kutoka pale ofisini. Baada ya kupata simu yako tu, eneo la mnazi mmoja tayari lilikuwa na vijana kumi maalum ambao walikuwa wanafuatilia kuanzia ujaji wako hadi uondokaji wako. Ulipoondokapale ofisini nilikuwa makini kuwasiliana na vijana wangu kwa nyendo zako zote. Nilifanya hivi kwa sababu mbili tofauti moja kanuni hazikutaka nikuamini mapema kiasi kile hivyo niliamua kukufuatilia ili nijue mengi kuhusu wewe kama ni mkweli au ni muhusika halisi wa mauaji. Pili nilifanya hivyo ili kama ulichozungumza ni sahihi basi uwe chini ya uangalizi maalum kwani inaonesha ulikuwa unawindwa kila kona! Ndiyo maana ulipofika mitaa ya Gerezani hukujua kama ulikuwa umeshaingia kwenye mtego wa wale jamaa. Wale waliokuwa mbele yako walijua wazi kuwa uko nyuma yao wakakuchelewesha makusudi huku wakiwasiliana na wenzao wengine kwa meseji bila wewe kutambua. Nikaelezwa yote hayo na vijana wangu. Baada ya kuona hatari imekuwa kubwa kiasi hicho ndipo nikaamua kuingia rasmi. Ulipofika Karume ukatekwa hiyo ikawa fursa nzuri kwetu ya kuweza kukufuatilia. Nikiwa na vijana wangu wenye mafunzo maalum tukakufuatilia hadi ulipoingizwa kwenye nyumba moja kubwa kule kunduchi, Baada ya muda mfupi tukawaona wale watekaji wakiondoka! Tukaiweka chini ya uangalizi mkali ile nyumba ili kuhakikisha hautolewi mle ndani. Baada ya hapo nikapiga simu polisi nyumba ikawekwa chini ya ulinzi wa polisi, wote waliokuwa humo ndani wakakamatwa. Nikakuchukua wewe na kukuleta huku kwa ajili ya matibabu kwa sababu tulikukuta ukiwa umepotelewa na fahamu!” Nikashusha pumzi baada ya kusikia kisa hicho cha kusisimua.

    Kama hao watekaji wa mwanzo waliwahi kuondoka basi Martin atakuwa hajakamatwa! Niliwaza huku nikiwa na wasi wasi. Beatrice akaja pale kitandani akaondoa ile dripu niliyotundikiwa kwani maji yalikuwa yameisha. Kisha akaondoka tena na kutuacha watatu mle chumbani. Nikamgeukia Ommy.

    ” Vipi Ommy nini kimekusibu baada ya kuachana siku ile?”

    “Nafikiri mengi nilikueleza kwenye barua yangu kwa kuchelea wale watu kunigundua nikaamua kuitelekeza nyumba yangu kwa muda kwani kama wale watu wangediriki kunifuatilia vizuri basi wangegundua wapi ninaishi, Nami nikaanza kuwawinda, nilikuwa na shauku kubwa ya kutaka kujua vile viungo vya albino vinatumika kwa kazi ipi! Nikaenda hadi kule Kongowe. Nikapindukia ndani ya lile jengo ambalo ulipeleka ule mzigo. Nilipofika pale watu wote walikuwa ndani. Kwa kuwa ilikuwa ni usiku niliweza kujificha nje karibu na dirisha la chumba ambacho ndani alikuwepo Samson Kipusa au Bonge kwa jina ulilozoea pia nikashtushwa na uwepo wa Mheshimiwa waziri wa Bunge na vikao vya serikali Bwana Stefano Kenge. Kwa kuwa taa ilikuwa inawaka ndani ya chumba kile niliweza kuwachungulia vizuri bila ya wao kuniona kwani taa ya nje ilikuwa haijawashwa. Mjadala wao ulikuwa ni wa kutisha sana kwani kulikuwa na raia wanne wawili kutoka Burundi na wawili wengine walikuwa wanatoka Rwanda. Hawa walikuwa wameleta Viungo kutoka katika nchi zao. Baada ya kujadiliana wakakubaliana walipe shilingi milioni Mia moja kwani walileta viungo vya albino sita. Nilishtuka sana kwani sikutegemea kabisa kama jambo hili linaweza kufanywa na mtu mzito kama yule!”

    “Enhee ikawaje?” Niliuliza huku nikiwa na shauku kubwa ya kusikiliza habari ile ambayo ilikuwa inasisimua sana.

    “Baada ya kukubaliana bei wakawaomba wale wageni watoke kidogo mle chumbani ili waweze kujadili, Mjadala huu ndio ulionifunulia sura halisi ya Mheshimiwa. Ni chui ndani ya ngozi ya kondoo kwani waziri alitoa amri kuwa wale wageni wauwawe na wazikwe mle ndani! Hapo nikakumbuka jinsi ulivyotegewa bomu kwenye lile brifkesi lakini Mungu alikuwa upande wako! Baada ya dakika kama kumi nikaanza kusikia vilio mle ndani kisha kukawa kimya bila shaka wale jamaa walikuwa wameuwawa! Duh, wale jamaa watu hatari sana kuua kwao ni jambo dogo sana. Baada ya hapo nikarudi nyumbani haraka nikaandika ile barua kisha nikapanga kuwa sitarudi nyumbani mpaka nisikie mheshimiwa Stefano Kenge amekamatwa. Kutokana na kuchanganyikiwa na tukio lile nikaamua kwenda ikulu ili niweze kuonana na Raisi nimueleze tatizo hili.

    Kabla sijaonana na rais nikakamatwa na walinzi wa ikulu. Ishu ile ikapewa uzito mkubwa kuliko hali halisi nikapelekwa Idara ya usalama wa Taifa kwenda kuhojiwa huko nikakutana na Jerrome Mtuvu ambaye nilikuwa namfahamu kupitia kwa mdogo wake ambaye niliwahi kufanya naye kazi kambi moja wakati nikiwa mwanajeshi. Yeye ndiye aliyenipa namba ya kaka yake wakati niko jeshini. Ndiyo ile namba niliyokuandikia kwenye barua!” Baada ya kuhojiwa nikapata msaada mkubwa kutoka kwa Jerrome kwani nilifichwa sehemu maalum wakaanza upelelezi wao wa chinichini!” Akatulia na kunikazia macho. Nikashusha pumzi kwa mara nyingine.

    “Kitu kimoja nilitaka kusahau, Mheshimiwa Stefano Kenge anataka kutangaza nia ya kugombea uraisi hivyo anatumia kafara na mazindiko ili aweze kuingia ikulu!” “Unafikiri nini kitatokea iwapo viongozi washirikina wataingia madarakani?” nilimuuliza.

    “Siwezi kujua nini kitatokea, iwapo hata hao ambao tunaamini sio washirikina hatuoni wanachokifanya sijui wakiingia washirikina itakuwaje!”

    “Lakini nasikia waganga wa jadi hupata wateja wengi kipindi ambacho uchaguzi unakuwa umekaribia!”

    “Unamaanisha nini?” Aliniuliza Jerrome ambaye muda mrefu alikuwa kimya. “Inawezekana kuwa viongozi wetu wengi ni washirikina!” Nilimjibu.

    “Usirudie tena hiyo kauli wakikusikia watakujadili bungeni kuwa umewadhalilisha!” Aliongea Ommy na kutufanya mimi na jerry tuangue vicheko.

    “Nafikiri Hali yako ni mzuri Kajuna tutakuacha hapa kwa siku nne ukipumzika na kupata matibabu madogo madogo!” Aliongea Jerry.

    “Lakini bado sijafahamu hapa nilipo ni wapi?”

    “Hapa ni kunduchi na hii ni nyumba maalum ya serikali ambayo hutumika kwa shughuli maalum tu!”

    “Kama shughuli ipi kinyume na hii?”

    “Nitakujibu kwa kifupi na baada ya hapo sitapenda udadisi zaidi kuhusu hii nyumba. Wakati mwingine kuna maraisi ambao hufanya safari za siri ambazo hazijulikani nchini kwao na haziwi wazi hapa nchini huwa wanafikia hapa!” Kweli sikutaka kuuliza tena. Nilielewa kwanini aliniambia nisiendelee kuuliza kuhusu ile nyumba.

    Hatimaye muda wa kuagana nao ukafika, wakaondoka na kuniacha peke yangu. Muda huo niliwaza mambo mengi sana ndipo nikawakumbuka stella na Johari . Sijui kwanini nilisahau kuwazungumzia kwa Jerry. Hata hivyo inaonesha hata Jerry alisahau kuuliza kuhusu yule mwanamke. Kutokana na uwepo wa Stela niliamini wazi kuwa atatoa msada kwa Johari ambaye kisaikolojia alihitaji msaada mkubwa na ukaribu. Hakutakiwa kupata nafasi ya kutosha kukumbuka matukio yale ya kusikitisha. Kama angepata muda wa kutosha kukumbuka tukio lile basi ingeweza kusababisha arudiwe na msimamo wake wa kutaka aachwe kwenye mikono ya wahalifu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati nikiogelea kwenye bahari ile ya mawazo mara, yule nesi akaingia tena. “Karibu mpenzi!” Nilimkaribisha tena kwa namna ya utani ambayo mwenyewe ndiye aliyeianzisha.

    “Hivi ilikuwaje ukapata fursa ya kufanya kazi huku?”

    “Mimi nimfanyakazi wa Hindumandal lakini pia ni mwajiriwa wa Idara ya usalama wa Taifa kitengo cha tiba, pia mimi si nesi kama unavyoniona kwa ishara ya mavazi ni daktari bingwa wa mifupa” Nilitosheka sikuwa na swali lingine



    ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

Blog