Simulizi : Barua Kutoka Jela
Sehemu Ya Tano (5)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Muongeaji ni Inspekta Jamila, nipe habari.”
Ama kwa hakika kitendo kile hakukitarajia kabisa, akajikuta anamuuliza Jeradi Mwaipopo;
“Umejuaje kama Inspekta Jamila ndiyo unaeongea nae, hali ya kuwa simu niliyoitumia kukupigia ni ya rafiki yako Dokta Masawe?!”
Kwa swali lile alisikia upande wa pili wa simu ile, Jeradi Mwaipopo akicheka sana kisha akajibu kwamba;
“Mimi ni askari Afande, hivyo kutambua jambo hilo na zaidi, ya hilo sio kitu cha kushangaza kabisa!”
Inspekta Jamila alitingisha kichwa juu chini karibu mara tatu!
Akiwafiki maneno yale ya Jeradi Mwaipopo, kisha akarudi katika hali yake ya kawida na kumwambia.
“Hapana JM, ulikuwa Askari hapo mwanzoni, ila sasa ni jambazi hatari sana wewe, na hilo ndilo lililokufanya ufukuzwe kazi katika Jeshi la polisi.”
Jeradi Mwaipopo huku akiendelea kucheka, alijibu kwa kusema.
“Baadhi ya watu wengi sana wanaelewa hivyo, ulivyoelezwa wewe kuhusu mimi, ila ninachokwambia ni kwamba hizo ni taarifa za uzushi mtupu, huku sababu za kweli za kuachishwa kazi kwangu haziwekwi wazi!”
Inspekta Jamila akajilaumu kwa nini asingetumia simu yake kuongea na JM – kwani angeweza kuyarecodi mazungumzo yale, lakini simu ya Marehemu Dokta Masawe haina uwezo wa kurekodi!
Ingawa yale mazungumzo yalikuwa yanamgusa sana, kwani alikuwa anapata maelezo ya kwanini Jeradi Mwaipopo amefukuzwa kazi.
Ingawa Jeradi Mwaipopo anakana tuhuma za kufukuzwa kazi kwa sababu ya uhalifu, lakini picha yake imeonekana katika vipimo vya kitaalamu alivyowekewa machoni marehemu Kiyarwenda Mwemezi, lakini pia aliwajeruhi Askari kwa risasi siku moja nyuma pale Barakuda Bar na leo hii amemuua Dokta Masawe!
“Hapana huyu ni Jambazi anavunga tu, kwani wezi wachache sana hukubali kuwa wameiba!”
Inspekta Jamila baada ya kupita mawazo hayo kichwani mwake, akamtupia swali linguine.
“Kama wewe hukufukuzwa kazi kwa sababu za kujihusisha na uhalifu, lakini upo ushahidi wa kutosha, kuwa wewe ni muhalifu, lakini pia unashirikiana na wahalifu, ambao baadhi yao tumewakamata na wanatuthibitishia kila kitu kuwa wewe ni muhalifu!”
Jeradi Mwaipopo aliacha kucheka, na akasema;CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Acha kutumia simu ya marehemu, kwani sheria haikuruhusu kufanya hivyo, huo pia ni uhalifu!”
Inspekta Jamila alichukia, kwa maneno ya kiburi ya Jeradi Mwaipopo, akamjibu huku akimuuliza swali.
“Kwa taarifa yako, Dokta hukumuua kama ulivyokusudia! Lakini Jeradi kama wewe ni mwanaume kweli, unaejiamini, niambie upo wapi nikufate?”
“Ukiwa wewe ni askari, unatakiwa unitafute unikamate, ili utambue ukweli wa mimi kufukuzwa kwangu kazi, na tumetambua vipi kama wewe ndiyo unayefatilia kesi hii, hata siku yako ya kwanza tu ya kuanza kazi hii, tukakuachia ujumbe kule katika Hospitali ya Taifa ya Rufaa ya Muhimbili!”
Inspekta Jamila alipagawa kweli kweli kwa maelezo yale, akamwambia Jeradi Mwaipopo kwamba.
“Basi Jeradi kwa nini tusipange sehemu tukakutana na tukaongea kwa kirefu kiurafiki?!”
Jeradi Mwaipopo alitungua kicheko kama mwehu vile kisha akamjibu Inspekta Jamila.
“Hata mimi nilipokuwa upande huo, nilikuwa nawalaghai watu hivyo hivyo, na hatimaye niliwatia nguvuni. Sasa kitanda hicho nimeisha kilalia, na nawajua kunguni wake! Ila zingatia kwamba huu ni mtego wa panya Inspekta Jamila wa Ilala Mtaa wa Songea nyumba namb………!”
Simu ile ilikatika na Inspekta Jamila akaingia kiwewe akapiga ngumi katika meza yake!
-
-
Akaipiga tena namba ile ya simu iliyokatika.
Akasikia ujumbe kutoka kwenye simu ile ya Marehemu Dokta Masawe, ikimwambia;
“Salio lako halitoshi kupiga simu hii, tafadhali ongeza pesa katika simu yako kabla hujajaribu kupiga simu nyingine!”
“Shabashi” Inspekta Jamila alisema maneno hayo huku sasa akiwa amesimama na akawa anatembea kwenye ofisi ile toka kwenye kona moja kwenda kwenye kona nyingine, huku akitafakari mazungumzo ya Jeradi Mwaipopo, kwani alimtajia hadi Mtaa anaoishi bila shaka hadi namba ya nyumba alikuwa aitaje kwani kama si kukatika kwa simu ile pengine angesikia namba ya nyumba yake ikitajwa!
Kitu kilichomtia hofu zaidi ni kwamba, watu anaowatafuta wao wanamfahamu vizuri hadi katika nyumba anayoishi, kitu ambacho ni hatari kubwa sana kwa maisha yake kwani angewezwa kuviziwa na kupigwa hata risasi na majambazi wale!
“Ama kweli huu ni mtego wa panya.”
Inspekta Jamila alijikuta akitamka maneno hayo, mara kama mtu aliyegutuka, akakumbuka jambo Fulani, akaenda hadi sehemu alikochomeka simu yake kwenye chaja akaichomoa.
Akaichukua simu ya Marehemu Dokta Masawe, pamoja na simu yake, kwa mwendo wa haraka, akaelekea katika chumba cha mawasiliano ‘Computer Room.’
Akamfuata afande Dihenga na kumpa mkadima mzima.
Vyombo vikawekwa sawa na baada ya kusetiwa mitambo ile, simu ya Jeradi Mwaipopo ikapigwa, na ikasikika sauti katika simu ile;
“Simu unayopiga kwa sasa haipatikani, tafadhali jaribu tena baadae”
“Oh shit” Inspekta Jamila alitamka maneno hayo huku akikunja ngumi katika mikono yake yote miwili kwa hasira.
Walijaribu kuipiga namba ile zaidi ya mara tano, ulipatikana ujumbe ule ule kutoka kwenye simu ile, hii ikimaanisha kwamba simu waliyokuwa wanaipigia imezimwa!
Inspekta Jamila akazichukua simu zile mbili pamoja na chaja yake na kurudi navyo ofisini kwake huku akiwa hoi bin taabani kwani Jeradi Mwaipopo aliiharibu kabisa siku yake kwa maneno aliyomwambia.
Lakini akapiga moyo konde huku akisema kimoyomoyo.
“Vilima Havikutani bali wanadamu wanakutana, hivyo ipo siku nitakutana na Jeradi Mwaipopo uso kwa uso, na mimi mwenyewe nitahakikisha ninamfunga pingu!”
Kichwa cha Inspekta Jamila kilijaa mawazo lukuki, kiasi kwamba akaanza kuhisi uchovu na njaa, huku akili yake ikishindwa kabisa kufanya kazi kwa wakati ule.
Akaangalia saa yake na kuona imetimia saa nane kasorobo.
Robo saa tu ndiyo iliyosalia ili wakutane tena na Afande Kubuta wapate kuendelea na ratiba yao.
Inspekta Jamila alikuwa amechoka sana kiasi hawezi kufanya kazi kwa ufanisi.
Aliiweka simu yake katika chaja huku ikiwa inachajiwa, akampigia simu Dokta Zahala.
“Shoga nakuja nyumbani kwako mchana huu kwa mambo makuu mawili. Jambo la kwanza ni kuja kula chakula cha mchana, na la pili ni kuja kupumzika. Kwani kwako ni mahali salama kwa kazi yangu na maisha yangu kuliko nyumbani kwangu kwa hivi sasa!”.
Dokta Zahala akiwa hakumuelewa vizuri shoga yake, akamuuliza.
“Mbona sikuelewi shoga, yaani leo nyumbani kwangu kuwe pahali salama kwa maisha na kazi yako kuliko nyumbani kwako ki vipi?!”
Inspekta Jamila akamwambia shoga yake
“Punguza Wahka shoga, mimi ninakuja huko huko kwako maswali mengi ya nini?”
Wote wakatungua kicheko kirefu kwani watu wale kila wanapokutana, walikuwa wanapendana kama watoto mapacha.
Baada ya muda Afande Kubuta aliingia ofisini mle, akiwa ameshikilia chupa ya maji safi iliyokuwa shinda.
Akamuona Inspekta Jamila akimaliza kuongea na simu.
Afande Kubuta alistaajabu, kwani kiongozi wake hakuonekana kama ametoka nje kwenda kula. Akamuuliza.
“Vipi kiongozi wangu mbona wewe bado hujaenda kupata chakula hadi muda huu, kumezuka jambo jipya au umeagiza viazi?!”
“Hapana sijala chochote toka wewe uondoke, wala sijaagiza kitu ila kazi zilikuwa zimenibana, sasa kwa kuwa wewe tayari umekwisha pata chakula cha mchana, itakubidi muda huu uende Kijitonyama kwa Bitozi ili ukamchukulie maelezo.
Mimi nakwenda kupata chakula cha mchana nyumbani kwangu, lakini pia ndiyo tutakuwa tumeagana, kwani nikiondoka ofisini hapa sitarajii kurudi tena hadi kesho.
Hivyo asubuhi tutakapokutana kwa majaaliwa ya mungu, tutapeana taarifa kamili na matokeao ya kazi yako huko uendako.”
Afande Kubuta alipatwa na bumbuazi au mzubao kwani yeye alidhani kuwa Inspekta Jamila ndiyo angekwenda kule Kijitonyama lakini pia yeye ndiye aliyesema kwa muda ule wakapate chakula cha mchana.
Sasa iweje tena yeye asiende na kusema kwamba anakwenda kula kwake! Lakini afanye nini na kiongozi wake ndiyo kasema hivyo.
Akageuka na kutoka nje ya ofisi ile na kuelekea katika sehemu ya maegesho ya magari akachukua gari ile yenye namba za kiraia na kufungua mlango na kujipakia mle ndani.
Akawasha gari na kutoka eneo la jengo lile kuelekea Kijitonyama kwa Bwana Bitozi au Predeshee.
Inspekta Jamila akafunga mtoto wake wa meza kwa funguo baada ya kuweka vitu vyake muhimu ndani yake, pia alizima computer na kiyoyozi kilichokuwa kinafanya kazi muda wote.
Kisha akaichukua simu ya Marehemu Dokta Masawe aina ya Siemens MC 60 na simu yake aina ya NOKIA 6230i pamoja na chaja yake, akafunga ofisi na kutoka nje katika maegesho ya magari, akaiendea gari yake na kufungua mlango na kujipakia ndani kisha akawasha gari na kutoka nje ya eneo lile na kuitafuta Wilaya ya Temeke katika maeneo ya Keko Bora nyumbani kwa Dokta Zahala.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
10.
Inspekta Jamila, alishituka kutoka katika usingizi mzito,akawa bado anatafakari katika fikra zake kilichomuamsha muda ule.
Alisikia mlio wa simu, ukihanikiza katika chumba cha wageni alipokuwa amelala, pale kwa shoga yake dokta Zahara. Akatazama saa yake ya mkononi, aliyolala nayo, ilimuonesha kuwa ni saa nane za usiku!
Akanyoosha mkono wake, kivivu akachukua simu yake, akaitazama namba ya mtu aliekuwa akimpigia simu, usiku ule wa manane! Moyo wake ukawa unakwenda mbio kwa furaha, huku akiipokea ile simu na kutamka majina matatu, yalioonekana katika simu ile “SHANY KARAMA RASHIDI” Huku akiitikia kwa madaha “Halow sweety?”
Aliongea kwa mbwembwe nyigi,mizaha, na zihaka, ilitawala mazungumzo yao, huku Bwana Shany aliekuwa nje ya nc
hi kwa mambo yake ya biashara, akimtaka aende kumpokea katika uwanja wa ndege wakimataifa wa mwalimu Nyerere, akamwambia muda atakaotua Tanzania kutoka ughaibuni.
Inspekta Jamila, usingizi ulimpaa akaanza kufikiri mambo mengi kumuhusu Shany, tangu siku ya kwanza walipokutana, hadi kuanzisha mahusiano. Alipokuja kutoka katika mawazo, alisikia majogoo yanawika!
Aliinuka kutoka kitandani, akafanya mazoezi ya viungo kidogo, kisha akaingia bafuni, alipotoka hakujipodoa sana, alitaka kuwahi nyumbani kwake kabla hakujapambazuka, ili kukagua usalama, kisha awahi kazini, kwake kwa utendaji zaidi.
Alipotoka Sebuleni, akamkuta shoga yake Dokta Zahara, ameshaamka muda mrefu, anapata kifungua kinywa.
“Shoga hulali umekuwa kama kolokoloni?”
Inspekta jamila alimtania shoga yake, na Dokta Zahara kwa utani akamjibu.
“Mimi nakulinda wewe, siwezi kulala, kwani wewe ni mtu muhimu sana!”
Wote kwa pamoja, waliangua vicheko huku wakikutanisha, mikono yao hewani (Wakagonga) Baada ya kupata kifungua kinywa, Inspekta jamila, akaagana na Dokta Zahara, akaiendea gari yake, na safari ya nyumbani kwake, ikaanza huku akiwa na shauku, ya kutaka kujua usalama wa nyumbani kwake.
Inspekta Jamila aliendesha gari yake huku akiwa makini, hadi akawa umbali wa alipo na nyumbani kwake, ni takribani nyumba kumi hivi, akaegesha gari yake pembeni, kisha hakushuka ndani ya gari yake, akawa anatazama nyumbani kwake, kama kuna mtu anaetoka au kuingia! Lakini mtaa ule wa Songea pale Ilala, ulikuwa tulivu, na watu wengi walikuwa bado wamelala.
Inspekta jamila, alibakia mle ndani ya gari yake, kwa zaidi ya dakika kumi, lakini hakuambulia kitu cha maana, zaidi ya kumuona mtu mmoja mwembamba mrefu,akiwa katika mavazi machafu na chakavu, akiwa amebeba mfuko aina ya kiroba,kikiwa kichafu, akihangaika eneo lile, kuokota chupa za plastiki, na vyuma chakavu!
Inspekta jamila, alitazama saa yake, na kuona kuwa ilikuwa imeshatimu, saa kumi na mbili na robo, akajisemea kimoyomoyo, “Hawa mateja hawalali?” Kisha baada ya kusema hayo, aliteremka ndani ya gari yake, na kutembea hatua za taratibu, kuelekea nyumbani kwake.
Akiwa yupo karibu na nyumba yake, kwa tofauti ya nyumba mbili, akapishana na Yule muokota chupa. Inspekta Jamila alimtazama Yule bwana,akashangaa kiasi,kwani yeye alishazoea kuwaona vijana walioathirika na madawa ya kulevya, ndiyo, wanaookota chupa za plastiki na vyuma chakavu, lakini huyu jamaa anaepishana nae, hakuonekana sura yake, kama inachembe ya ujana!
Walipopishana, Inspekta Jamila aligeuka kumtizama kwa nyuma Yule bwana, lakini Yule bwana wala hakuwa kabisa na habari na yeye. Inspekta Jamila akafika nyumbani kwake,akawa makini mara dufu, na kila kitu anachokitazama. Akakijaribu kitasa cha mlango wake kama kimefungwa kama alivyo kiacha, naam kitasa kikawa salama! Akatazama katika kipande cha zulia la kufutia miguu pale mlangoni, naam hapo mapigo ya moyo, yakamuenda mbio kama saa mbovu!
Bahasha nyeupe ilikuwa imewekwa pale kwenye futio la miguu, kwa chini. Robo tatu ya bahasha ile ikiwa imefunikwa haionekani na kile kipande cha zulia, na robo ya bahasha ile ikiwa inaonekana dhahiri, shahiri.
Inspekta jamila, aliinama huku akiongeza umakini zaidi, akaiokota bahasha ile.Akatizama huku na huko,asimuone mtu yeyote mahala pale, hata Yule “mteja mtu mzima”hakuonekana eneo lile!
Akatoa fungua za mlango, akafungua akaingia ndani.Alikagua kila kitu muhimu mle ndani kwake,akaviona vimekaa, kama alivyoviweka,hakukuwa na badiliko lolote.
Inspekta Jamila,aliifungua ile bahasha, akakutana na kipande cha karatasi, kilichoandikwa kwa mkono, tena kwa maandishi mekungu, kilichoandikwa “SHANKARA!” Alikisoma tena na tena, lakini hakuelewa maana yake,sasa akawa yupo katika tafakari nzito, akazama katika dimbwi la mawazo, akagutushwa na mlio wa simu yake.
“Halow Dokta?”
Ilikuwa ni simu ya Shoga yake Dokta Zahara.
“Vipi mbona kimya hunambii kama huko ni salama? Kwani roho yangu nimeitundika hapa kama mkungu wa ndizi sina amani?!”
“Mmmmh shoga, sijui niseme salama, au nisemeje, manaake hapa nimepagawa kwelikweli, kifupi nipo salama, ila kuna jambo halipo sawa!”
“Duuuh pole sana shoga, kama huko hakuko sawa beba nguo zako, uje ukae huku, hao wanaharamu wasije kukutoa roho bure!”
“Nikifa kazini,itakuwa heshima kubwa kwangu na familia yangu, ila sitorudi nyuma Dokta, nitapambana hadi hatua ya mwisho, mimi ni askari niliepasi chuoni kwa nadharia na vitendo, sikupita kule kwa njia mkato!”
Inspekta Jamila alijibu majibu ya kishujaa, akakata simu, akabadilisha nguo na kutoka, kuelekea kazini kwake, tayari kwa majukumu, ya siku ile!
Asubuhi ile, bado foleni ilikuwa haijachanganya, hivyo ilimchukua dakika ishirini tu hadi kufika ofisini kwake.
Ilipotimu saa mbili kamili juu ya alama Afande Kubuta nae aliwasili, ofisini kwao, akiwa yupo tayari kwa maelezo ya kazi aliyokuwa ameifatilia.
“Ndiyo Afande, lete taarifa!”
Inspekta Jamila, alianzisha mazungumzo yale, huku akitaka kujua kilichojili.
“Kiongozi kama nilivyowahi kusema, Bitoz alikuwa mpenzi wake Hamida, ila hajui chochote kuhusu kesi hii, tunayoifatilia, kwani nimetumia mbinu, zote za kuhoji, lakini jamaa hakuonyesha maelezo tofauti yenye shaka hata kidogo!”
Inspekta Jamila, alimsikiliza Afande Kubuta kwa umakini, kisha akatingisha kichwa chake kukubaliana, na maelezo yale.
“Sasa leo ni jumaamosi, hivyo andaa jalada la mke wa Dokta Masawe, ili jumatatu apande kizimbani, hatuna sababu ya kukaa nae!”
Inpekta Jamila, baada ya kusema maneno yale, alitoa ule waraka alioukuta nyumbani kwake asubuhi ile, na kumpa Afande Kubuta kisha akamwambia.
“Unaelewa nini juu ya neon hilo?”
“SHANKARA?!”
Alisema Afande kubuta, kwa mfumo wa kuuliza, na kushangaa!
Inspekta Jamila, yeye alikuwa ametulia makini, akimtazama usoni msaidizi wake,katika namna ya kumsoma!
Sasa ikawa zamu ya Afande Kubuta,kuzama katika lindi la mawazo.
“Nini hii?! Na umeipata wapi?” Sasa ikawa zamu ya Afande Kubuta kuuliza.
“Huo waraka, nimeukuta leo mlangoni kwangu! Alieuweka simjui, wala una maana gani vilevile sitambui, ila lazima kuna maana, tena ni kubwa sana!”
Inspekta Jamila, alimueleza msaidizi wake kutokulala kwake ile jana, kwa simu ya Geradi Mwaipopo, hadi asubuhi alipokwenda kukagua nyumba yake, alipoukuta huo waraka, ila hakuthubutu kumweleza mahali, alipolala!
-
-
Askari wale wakapanga na kupangua, hadi saa nane mchana. Walipeana mikakati ya kufanya, ili kushinda kesi ile kwa kishindo.
“Sasa naona leo hapa tulipofika,siyo pabaya sana, itabidi tufunge kazi kwa leo, ila kama ujuavyo, askari muda wote yupo kazini! Hivyo tunaweza kuitana muda wowote ule!” Inpekta Jamila alimwambia msaidizi wake, kasha ule waraka akaufungia katika droo ya meza yake, akaendelea kusema.
“Leo usiku nina mgeni anaingia kutoka ughaibuni, ambae ndiye dakitari wa mwili wangu, nyonda mkalia ini wangu, kipenzi cha roho yangu!” Inspekta Jamila alikuwa akizungumza huku akitabasamu, na kumfanya Afande kubuta nae kuwa katika hali ile ya kutabasamu!
“Haya sasa mie nifanyeje Afande?” Afande Kubuta alisema maneno hayo huku nae akiwa anatabasamu.
“Nataka uniambie duka, wifi yangu anaponunulia Msio, kwani nataka kumsinga Bwana,najua ameyakosa mambo haya muda mrefu”
“Hahaha Afande Msio ndiyo nini? Kwani ndiyo kwanza nakusikia wewe hilo neno!”
“Heee makubwa haya, wewe hujui msio?! Tuseme huyo wifi yangu huko nyumbani kwako, hajawahi kukusinga?!” Inspekta Jamila alimuuliza msaidizi wake, huku akimshangaa!
“Hawa wanawake wenzangu,baadhi yao wamezidi, yaani unakaa na mume au bwana, hujawahi kumsinga hata siku moja, ukamwimbia nyimbo za mahaba, ukamtuliza ndani, hakika unyago ni kitu muhimu sana kwa wanawake!”
“Basi niletee huyo wifi yangu, nikaenae walau siku tatu tu, atabadilika huyo!” Wote wakaangua kicheko kisha wakaagana.
……………
Ilikuwa saa nne za usiku, Inspekta Jamila, alikuwa anakaribia uwanja wa ndege wa kimataifa wa JULIUS KAMBARAGE NYERERE,alipokuwa akikata kona ya kuingia katika uwanja wa ndege, akiiacha ile barabara ya Pugu, mara macho yake yakamvuta kumtiza muokota chupa na vyuma chakavu, aliekuwa amesimama pale kona katika njia ya kutokea uwanjani, akiwa na kiroba na nguo chakavu!
Inpekta Jamila akasimamisha gari ili amtizame sawasawa, akasikia kelele za tairi kutoka nyuma, zilizokuwa zinasuguana kwa breki,iliyokanyagwa ghafla!
Inspekta Jamila, haraka alikanyaga mafuta gari yake, nakuokoa ajali ambayo angeisababisha yeye, kwa kusimama ghaflaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Barabarani.
Ile gari ya nyuma ilitanua kulia, ikasimama sawasawa na gari yake. Dereva wa ile gari alishusha kioo, akatazamana na Inspekta Jamila, huku dereva Yule akiwa amefura kwa hasira, alimuonyesha vidole vya kati vya mikono yake yote miwili, kisha akapandisha kioo akaondoa gari,kuelekea kwenye geti na kuchukua kadi maalum, akaiingiza gari yake katika maegesho akaiegesha na kushuka, akaendelea na hamsini zake!
Inpekta Jamila, pale alipo aliishuhudia ile gari dereva wake aliemtusi,ikiondoka mbele yake, akaiandika namba ya gari ile. Nae akasogeza gari yake hadi pale kwenye lile geti, akachukua kadi nakwenda kuiegesha gari yake, kisha kwa mwendo wa haraka, alitembea ili kumuwahi Yule muokota chupa na vyuma chakavu.
Inspekta Jamila, alitazama eneo lote la pale alipomuona Yule bwana muokota chupa na vyuma chakavu, alipokuwa amesimama awali, lakini hakumuona! Akavuka barabara hadi pale kituo cha basi, chakuendea mjini, pia hakumuona, kichwa chake kikaanza kuchanganyikiwa!
Kinachanganyikiwa kwa sababu, hakuna waokota vyupa na vyuma chakavu, wanapokuwa kazini, wakapanda gari, kwani hivyo vitu wanavyookota watavipataje? Pia hakuna waokota vyupa na vyuma chakavu, wanaofanya kazi zao usiku kama ule! Lakini pia Muokota vyupa na vyuma chakavu huyu, aliemuona muda mfupi uliopita, ndiye aliemuona asubuhi, maeneo ya nyumbani kwake Ilala mtaa wa Songea!
Inspekta Jamila, alirudi uwanja wa ndege ili kuendelea na jambo lililompeleka pale, lakini fikira zake, zikianza kumtilia mashaka Yule bwana.
Alikwenda mpaka katika maegesho lilipokuwa gari lake, akaikagua gari yake, ikawa ipo salama kabisa.
Akaelekea pale wanapokaa watu kuwasubiri abiria, mara wakasikia tangazo kupitia vipaza sauti vilivyokuwa pale uwanjani kuwa, ndege iliyotarajiwa kufika muda ule, imefika salama, na watu wakaanza kujongea, karibu na mlango ule mkuu wa kutokea wageni, ili kuwapokea wageni wao, huku wengine wakiwa na mabango madogomadogo, yaliyoandikwa majina ya wageni wao, ili mgeni iwe rahisi kwake, kumtambua mwenyeji wake, hasa ikiwa hawajawahi kuonana ana kwa ana!
Inspekta Jamila, alikuwa makini na kila aliekuwa akitoka katika mlango ule, na mara, akamuona mtu wake aliekwenda kumpokea, akamkumbatia na kumbusu, kasha akamwambia “Karibu nyumbani mpenzi wangu.”
“Asante nishakaribia mpenzi” Alijibu mgeni Yule,Shani Karama Rashidi.
Inspekta Jamila, alisaidiana mizigo na mpenzi wake, wakaenda kwenye gari yake, akapakia mizigo ndani ya gari yake, akajipakia upande wa dereva, na Shani upande wa abiria, safari ikaanza kuelekea mjini. Baada ya gari ya Inspekta Jamila, kuondoka eneo lile, huku nyuma gari ndogo nyeupe, ilikuwa ikimfatilia kwa mbali!
“Sweety nimekodi hotel,ya Kibodya ile ya mtaa wa Nkruma, ili tupumzike mahala pale!” Inspekta Jamila, alimwambia mpenzi wake, huku akiwa makini katika usukani.
“Alaa kama umeamua hivyo, hakuna tatizo, kwani mfungwa hachagui gereza, nami kwako ni kama mfungwa wa mapenzi kwako!”
Walitabasamu kwa pamoja, huku wakiwa wameshafika katika taa za Tazara. Usiku ule barabara zilikuwa hazina foleni.
Hatimae wakafika Kibodya Hotel,wakateremka na mizigo baadhi, wakaingia hotelini, Inspekta Jamila, alichukua funguo mapokezi, na kwenda hadi katika chumba alichopanga, akafungua mlango huku akitamka “Karibu waukweli, mimi nashuka chini, kumalizia mizigo kwenye gari.” Inspekta Jamila, alimbusu mdomoni mpenzi wake, akashusha ngazi, kuelekea nje ya Hotel ile.
Inpekta Jamila, alifungua mlango wa gari ili atoe mizigo iliyobakia, mara akajihisi hakuwa peke yake mahala pale!
Akageuka nyuma ili ajiridhishe fikira zake, lakini hakuweza kumaliza mzunguko wa shingo yake, kwani kitu chenye ugumu kama wa ubao, kilitua usawa wa kichogoni kwa pigo moja, lililopigwa kiufundi na mpigaji, na Inspekta Jamila, alianguka mle ndani ya gari kama mzigo, akapoteza fahamu.
Inspekta Jamila, alipokuja kutanabahi, alijikuta amefungwa kamba katika kiti cha chuma, akiwa amezingiliswa kamba kutoka mabegani hadi kiunoni, huku mikono yake ikiwa imefungwa kwa nyuma na kamba zile, bila kusahau miguu yake, ambayo pia ilitatalizwa kwa kamba zile za nyloni, huku akiwa amekalishwa katika kiti kile! Ama kwa hakika alikuwa amepatikana khaswa.
“Thatha mkubwa,huyu dem tumalidhe, au tumtie ulemavu wa maisha, kwani huyu mpumbavu thana.”
Inspekta Jamila, aliyasikia mazungumzo yale, ya Yule mtu aliekuwa akizungumza na simu, ili kupata maelekezo, kutoka kwa huyo aliekuwa akizungumza nae. Ila kitu kilichomfanya sasa ainue kichwa chake na kumtizama Yule mtu aliekuwa akizungumza na simu,ni ile lafidhi ya Kithethe!
Alitazamana na mtu Yule, kisha akaona pia na watu wengine wawili, wakiwa mle. Nao pia walikuwa wakimtazama, ingawa wale jamaa, wao walimtazama kwa dharau na kedi ya hali ya juu!
Inspekta Jamila, akiwa pale kitini alipofungwa kamba, aligeuza uso wake, na kutazama kulia na kushoto kwake, hakuona watu wengine zaidi ya hawa watatu, waliokuwa wamesimama mbele yake.
Alikuwa katika chumba kikubwa, ambacho hakikuwa na kitu chochote zaidi ya kile kiti cha chuma, alichofungwa nacho!
“Nimekuelewa bothi, thithi tunamalidha kabitha.” Yule bwana anaezungumza kwa kithethe, alihitimisha mazungumzo yake, akakata simu. Akapiga hatua kubwa mbele, akamnyooshea bastola aliyokuwa ameishika mkono wake wa kulia, huku akitumbukiza simu yake mfukoni kwa mkono wake wa kushoto.
Inspekta Jamila, akawa anaswali kimoyomoyo, kumuomba mungu wake, amnusuru na mkono ule wa mauti, wa madhalimu wale, akawatazama wale jamaa wengine wawili, akawaona wote kwa pamoja, wanampungia mkono wa kwaheri! Aligeuza shingo yake, upande ili asiwaone wale jamaa wanaomdhihaki, macho yake yakatazama upande wa kulia, akauona mlango.
Akiwa katika kuutizama ule mlango,mara akasikia Yule jamaa wa kithethe, akiipandisha risasi kutoka katika megazin yake, na kuipeleka chemba tayari kwa kuiruhusu itoke, ili kufanya kazi aliyoikusudia!
Inspekta Jamila, aliuona ule mlango, kitasa chake, kikiwa kinashuka chini! Akafumba macho huku machozi yakimtiririka mashavuni mwake.
Milio ya risasi, ilisikika ikihanikiza katika chumba kile kwa sekunde kadhaa, kisha ukimya ukatawala mle ndani, huku damu zikisambaa kwa wingi, kiasi khaswa unaweza kusema, kile kilikuwa chumba cha mauti!
Inspekta Jamila, alifumbua macho yake,akamuona mtu aliekuwa amevaa mask katika uso wake, akimfungua kamba ambazo sasa zilikuwa zinamuumiza mwilini mwake.
Akatizama pale chini, akawaona Kithethe akiwa na bastola mkononi, na wenzie wale wawili, wakiwa wamelala chini damu zikiwatoka kwa wingi mwilini mwao, wakiwa wamesambaratisha mikono na miguu, hawana dalili ya uhai!
Baada ya kufunguliwa kamba, Inspekta Jamila akasimama huku akimshukuru mungu, pia akawa anajinyoosha viungo vyake.
Hamadi?! Inspekta Jamila, alipigwa kibao cha kelbu katika shavu lake, akahisi maumivu makubwa!(KIBAO CHA KELBU, NI MKONO UNAOPIGIWA NYUMA YA KIGANJA)
Alipokuja kurudisha uso wake, akamuona yule mtu aliemfungua kamba,ambae ndiye aliyempiga, akiivua ile mask usoni mwake, huku akiwa amempa mgongo Inspekta Jamila,na yule bwana alipogeuka, Inspekta Jamila, akawa anatazamana uso kwa uso na Jeradi Mwaipopo au kifupi JM!
Inspekta Jamila, alitaharuki kupita maelezo, kasha kwa fadhaa akajikuta akitamka “JM?!”
“Yes, my name!” Jeradi Mwaipopo aliitikia kidharau, huku akimtizama usoni bila kupepesa macho! Kisha akaendelea “Bila shaka leo tumekutana, Inspeka Jamila”
-
“Naam hakika,leo tumekutana,tena tukiwa wawili,bila shaka leo,utaweza kunieleza kwa nini upo upande huu!”
Inspekta Jamila,alimwambia Jeradi Mwaipopo,huku akiwa
anachua shavu lake!
“Unajua leo ulikuwa tayari ni marehemu?Je ungewezaje
kujua kwa nini nipo upande huu?!”
JM alimwambia Inspekta Jamila,huku akiwa anamtazama
usoni moja kwa moja!
“Sina ubishi juu ya hilo,kuwa mungu angetaka,leo ningekuwa marehemu,ila naona ameniokoa na kifo kile
cha udhalili,kupitia mikononi mwako JM!”
Inspekta Jamila,alimjibu JM,katika namna ya kuvuta
muda,lakini pia kukusanya nguvu.
“Afande mimi,sijakuokoa na kifo,ila nimetaka mimi,ndiyo
nikuuwe,na siyo hao marehemu wenzako,waliyokutangulia!”
JM,alikuwa akisema maneno hayo huku,kwa mkono ule
uliokuwa umeshika silaha,akiinyooshea miili ya marehemu wale watatu,ambao sasa damu zilizokuwa zikiwamwagika,sasa zilianza kuganda!
Inspekta Jamila,alimtizama JM, usoni mwake, akagundua
kuwa hakika alikuwa hatanii hata kidogo!
“Sasa JM,hata kama utaniuwa mimi,bado na wewe
utakufa vilevile,ama utauwawa!”
Inspekta Jamila,alikuwa akimsemesha JM,ili kupoteza
muda,asaakheri huwenda akapata namna ya kujinusuru,kutoka katika mikono ya mtu mbaya kabisa alieacha zahma kubwa,katika mwenendo wa kesi ile.
“Mimi sitojali,kama nitakufa,ila nakuhakikishia umeingia
kwenye mtego wa panya,na leo umenasa kisawasawa!”
JM muda wote alikuwa akimtazama usoni,Inspekta
Jamila,kumsoma mawazo yake bila shaka.
“Sasa JM,si vibaya ukanieleza walau kwa ufupi,sababu khaswa zilizokupelekea,wewe kugeuka na kuwa upande
mwengine?!”
Inspekta Jamila alisema maneno haya,huku akionesha
utiifu,mkubwa kwa JM aliekuwa ameshikilia silaha ya moto kwa ujasiri mkubwa.
“Afande sina muda wa kupoteza hapa,naona unanikawiza kufanya azma yangu,lakini nitakwambia ili ukawaeleze huko kuzimu!”
JM alisema maneno hayo,kisha akamwemwesa kidogo,akaendelea.
“Kama nilivyokwisha kusema,katika Jeshi la Polisi,kuna baadhi ya viongozi,wameligeuza jeshi hili,kuwa kama mali yao binafsi.
Kwani wapo watu wanalitumikia jeshi,kwa miaka na miaka,lakini hawapandishwi vyeo!
Lakini pia wapo watu wanalipwa mishahara mikubwa kuliko watendaji halisi wa kazi husika!
Hao baadhi ya viongozi,wamekuwa wakijihusisha na
mambo haramu,na mimi nilipokamata,nikaambiwa
naingilia miradi ya watu!
Mwisho nikafanyiwa zengwe,nakusingiziwa kuwa
najihusisha na uhalifu,na nikafukuzwa jeshi,na leo hii,familia yangu nimeirudisha nyumbani Mbeya,ikiwa
hohehahe!”
JM aliposema maneno hayo,huzuni,hasira na dukuduku
lilimjaa moyoni mwake,akajikuta akilia kwa uchungu huku akisema.
“Nachukia kazi ya Polisi,na nawachukia Polisi,kwani hao
ndiyo walionifikisha hapa leo, wao ndiyo waliotoa picha
yangu katika magazeti,nakuniharibia,hadi nimekuwa
siwezi kupata ajira mahala popote ndani ya nchi hii,nikikomeshwa na wakubwa,wanaojali masilahi yao
binafsi,wao na familia zao,wakati wakina JM,wakitaabika kwa kuwa tu,walikuwa wakitekeleza majukumu yao sawasawa!”
Jeradi Mwaipopo alikuwa akitafuna meno yake kwa hasira,na mara akainua mkono wake uliokuwa umeshika silaha,akamuelekezea Inspekta Jamila,ili kutimiza dhamira yake ya kuua!
“No JM. Wewe mtoto wa kiume,hivyo hupaswi kumuua
mwanamke kwa risasi,tumia mikono yako bwana,unakuwa dhaifu mbona?!”
Inpekta Jamila,alikuwa akimpandisha jazba JM,lakini pia akimshusha,ili tu asiweze kuuliwa na risasi.
“Kwa hiyo wewe unataka kupigana na mimi siyo?!”
JM alimuuliza Inspekta Jamila kwa dharau ya hali ya juu!
“Bila shaka JM,kwani mimi sina silaha yoyote mwilini
mwangu,kwa nini wewe utumie silaha?! Kama kweli
unajiamini, na unajiona ni mwanaume hasa, tupa silaha
chini, tupange mtu mbili mimi na wewe!”
Inspekta Jamila,alikuwa akimtia hasira JM,ili ahamaki,na hatimae atupe silaha chini.
Naam bila wasiwasi,JM aliinama na kuiweka silaha yake chini,akawa amempa ubabu Inspekta Jamila,na
aliposimama juu huku akiwa bado yupo ubavu,JM alirusha
teke aina ya YOKO GELI,likatua ubavuni mwa Inspekta Jamila,na kumfanya apepesuke nusura adondoke chini.
(YOKO GELI.NI TEKE LAKUSITUKIZA,LINALOPIGWA UBAVU,ADUI ANAPOKUWA AMEKAA UBAVUNI MWAKO!) Inspekta
Jamila alipata maumivu kwenye mbavu zake,lau kama si kubana pumzi alipopigwa teke lile,bila shaka angevunja mbavu zake.
Baada ya kukaa sawa,akawa anatazamana uso kwa uso na JM.Ispekta Jamila akagundua kuwa mtu anaepambana nae,siyo mtu wa mchezo hata kidogo.
Hivyo alikaa katika mkao wa kupambana na mjuzi mwezie.
JM alipomuona Inspekta Jamila,amekunja ngumi hukuCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
mguu mmoja,akiwa ameutanguliza mbele,alirusha teke lingine,safari hii,akirusha teke aina ya MAWASHI GELI.
(MAWASHI GELI,NI TEKE LINALOPIGWA KUTUMIA FUNIKA,HUKU LIKIZUNGUKA,NA LINAPIGWA USAWA WA SHINGO YA ADUI.)
Inspekta Jamila,aliliona teke lile, hivyo akachanuka
msamba,teke lile likawa linapita juu yake.
Inspekta Jamila,hakufanya ajizi,palepale alipokaa msamba,alipiga ngumi moja maridadi aina ya GEDAN
NZUKI katika korodani za JM,na akatoa mguno mkali kwa
maumivu,lakini pia akiinama na kushikilia korodani zake,huku akirukaruka mwa maumivu(GEDAN NZUKI,NI NGUMI INAYOPIGWA USAWA WA KORODANI NA KITOVU) Inspekta Jamila,alipomuona JM amepoteza kujilinda kwa maumivu aliyompa, aliinuka pale chini haraka,akapeleka ngumi nyingine aina ya SEDAN NZUKI,Jm akapiga yowe kubwa la maumivu,huku sasa mkono mmoja,ukiwa kwenye korodani,na mkono wa pili,akishika kifua chake,usawa wa chembe.(SEDAN NZUKI,NI NGUMI INAYOPIGWA USAWA
WA CHEMBE)Akawa ameuacha uso wake,alioukunja kwa maumivu ukimtazama.
Inspekta Jamila,hakuremba akapeleka ngumi ya tatu,safari hii akipiga ngumi aina ya JODAN NZUKI.
Ikawa imemlewesha JM akawa anayumbayumba.
(JODAN NZUKI, NI NGUMI INAYOPIGWA USAWA WA USO,BAINA YA PUA NA PAJI LA USO)
JM aliyumba hadi akawa karibu na ile silaha,akawa
anainama kwa tabu ili aichukue silaha ile,na Inspekta Jamila,akang’amua alichokuwa anataka kukifanya JM.
Hivyo akapiga pigo moja takatifu,akitumia teke aina ya
JAMPING MAIGELI,teke lile lilimsogeza JM hatua kadhaa
kutoka pale ilipokuwa ile silaha,na damu za pua
zikachukua nafasi yake.
(JAMPING MAIGELI,NI TEKE UNALOPIGA UKIWA UMERUKA HUKU UKIMFATA ADUI,UKIWA UNATAZAMANA NAE USO KWA USO,NA PIGO LAKE HUTUMIKA CHINI YA VIDOLE/UNYAYO.)
Inspekta Jamila alishalichungulia kaburi, hivyo akutaka kufanya maonyesho,alipigana na mtu ambae,muda wowote, anaweza kutoa roho ya mtu!
Mara kikasikika kishindo kikubwa chumbani mle,na
Inspekta Jamila alipotazama kule kilipotokea kishindo kile,alikuwa akitazamaza na Sajenti Kubuta Aliekuwa na silaha mkononi mwake.
Na kabla hajasema kitu akaingia Koplo Magane na
wakaingia askari wengine watatu,wote wakiwa
wamekamata bunduki mikononi mwao aina ya SMG.
“Sajenti KUbuta umechelewa sana bwana,ningekuwa
marehemu sasa hivi,nilikwambia tangu jana ofisini katika mikakati yetu,kuwa uwe ukinifatilia kutokana na kuwindwa kwangu,ila kwa kuwa umefika na nipo salama,basi halijaharibika neno,niambie hapa ni sehemu gani tulipo,kwani mie sijui kabisa nipo wapi!”
“Samahani Afande,kama mikakati ilivyokuwa ikisema,mimi nilikuwa pale uwanja wa ndege,nikakusindikiza hadi pale hotelini,nilipotaka kuondoka nikashuhudia jambo ambalo sikulitarajia.
Yule jamaa wa kithethe alikupiga Karate shingoni,wakakubeba haraka na kukupandisha ndani ya gari yao,mimi ningeweza kupambana nao,ila nilitaka nifike ambapo nilidhani,ndiyo yangekuwa masikani yao,ili tuwatie mbaroni wote,kwa kuwa nilikuwa peke yangu,ilibidi niongeze ngumu kutoka kituoni pale magomeni,kwani hapa tupo Maeneo ya Kawe”
Baada ya kusema maneno yale Sagenti Kubuta alitoa
pingu, ili amfunge JM,ambae sasa alikuwa amelala huku
akitweta kwa maumivu makali.
“No Sagenti Kubuta,huyo nilichukua ahadi kuwa
nitamfunga pingu kwa mikono yangu mwenyewe,hivyo inabidi nitimize ahadi yangu.”
Inspekta Jamila alimfunga pingu JM,akamuendea mzee wa Kithethe, akaichukua simu iliyokuwa mfukoni mwake,akaiangalia simu iliyokuwa ikiwasiliana na bwana Yule,namba ya simu ile iliyokuwa imewasiliana na mzee wa Kithethe, ilimtia fadhaa kubwa sana,ikamtoa machozi,akakata shauri mara moja akiwa na ile simu mkononi mwake
*****Inspekta Jamila,aliingia hotelini kwa nguvu, akakutana uso kwa uso na Mpenzi wake,akiwa amekaa akiegemea mto,huku akiwa amepatwa na mshituko mkubwa!
“Karibu sweety,vipi mbona hivyo?”
Hatimae Shany alifunguka kwa kutoa kauli.
Inspekta Jamila,alimtazama mpenzi wake,kwa jicho la
husda!
“Mimi siyo sweety wako tena kuanzia sasa,wewe ni
mshenzi,na muuaji mkubwa!”
Inspekta Jamila baada ya kusema maneno hayo alikwenda kwa kasi ili amvamie Shany,lakini alipiga hatua mbili tu,hakuweza kuipata hatua ya tatu,Shany aliinua mkono wake na Bastola ikawa inaonekana waziwazi ikimlenga
Inspekta Jamila!
“Hatua moja mbele,nikusaini kifo! Mimi ninakujua kuliko
unavyojijua wewe!”
Shany alisema maneno hayo huku akisimama kutoka
kitandani,na kumkabili Inspekta Jamila.
Huku akiwa amesimama, kwa taharuki,Inspekta Jamila,alisema kwa fadhaa.
“Hata nawe pia?! Mtu niliekuthamini,kukupenda,kukuheshimu na kukupa mapenzi ya dhati,leo umekuwa nyoka wanigeukia?!Kwa lipi lakini baya,nililokutendea?!”
-
“Siku mbili zijazo,nitakuwa katika orodha ya matajiri
wanaotajika duniani,kwani mpango wangu ukishafanikiwa,nitapata pesa nyingi sana,Jamila wewe ni kikwazo kikubwa,katika kufikia malengo yangu,samahani sana,kwani bila ya hivi,siwezi kutimiza malengo yangu!”
Shany alimwambia Inspekta Jamila, akiwa amemuoneshea mtutu wa bunduki,usoni mwake.
Mara baada ya kusema hayo,Inspekta Jamila alilia kwa
huzuni kubwa,na mara Shani akakipeleka kidole husika,katika kiwambo cha kufyatulia risasi,ili amalize kazi yake!
Mara risasi ikalia na Inspekta Jamila,akalala chini!
Alipokuja kuinua uso wake,alimuona Shany anavuja Damu mkononi,huku silaha yake,ikiwa ipo chini!
Kabla hajatahamaki,alimuona mtu akitokea chini ya kitanda na Inspekta Jamila alipomuona mtu Yule,macho yalimtoka pima fadhaa ikamjaa,taharuki na Wahka ukachukua nafasi!
“Naitwa Jongo Janga,ukipenda niite JJ, natoka makao makuu ya usalama wa taifa,kitengo kisichokuwa na mipaka!”
Ilikuwa ni sauti ya ukakamavu,kutoka kwa Yule mtu alietoka uvunguni mwa kitanda kile,ambae Inspekta
Jamila,alimtambua kama muokota chupa za plastiki, na vyuma chakavu!
Alisema maneno yale,na kuonesha kitambulisho chake
juu,katika namna ya kutoa nafasi ya kusomwa!
“Lakini,usalama wa taifa unahusika vipi na kesi hii,lakini pia umeingiaje humu chumbani bila kuonekanwa?!”
Inspekta Jamila,alimuuliza Jongo Janga,huku akiwa
amepatwa na mshangao mkuu!!!
“Bastola ile ya kimada,wa bosi Serikalini,anaeitwa
Hamida,kauwawa Mikocheni!”
Jongo Janga,alikuwa anasoma moja kati ya beti za
BARUA KUTOKA JELA.Kisha akaendelea kusema huku
akimuelekezea mtutu wa Bunduki Shany,aliekuwa
amesimama akishikilia mkono wake uliokuwa unavuja damu!
“Shany Karama Rashidi a.k.a SHANKARA nyoosha mikono
yako juu!”
Inspekta Jamila moyo wake ulipiga sarakasi,kwa mshituko alipolisikia jina lile lililokuwa katika waraka,likihusishwa na aliekuwa mpenzi wake,ama kweli usilolijua,litakusumbua!
Shany alitii amri na kunyoosha mikono juu,Jongo Janga,akapiga hatua kubwa na kuisogeza ile silaha ya Shany,kwa mguu.
“Lakini nataka kujua,wewe umeingiaje humu ndani?!”
Inspekta Jamila,alikuwa na dukuduku la kutaka kujua
namna Jongo Janga,alivyoingia mle ndani.
“Mara baada ya wewe kutekwa,nilikuwa nashuhudia! Na baada ya dakika zisizozidi tatu,Huyu bwana alikwenda nje,ili kumalizia mzigo wake uliokuwa ndani ya gari,kwani
alikuwa akifahamu mtego aliouandaa!nami kwa mwanya huo nikaingia chumbani humu,ingawa alikuwa amefunga na funguo,kwani sisi tunapotaka kuingia mahala popote,huwa tuna uwezo wa kufanya hivyo kwa funguo zetu zenye uwezo wa kufungua mlango na kufuli lolote!”
Jongo Janga,aliondosha shaka ya Inspekta Jamila,na
akatoa pingu,mfukoni mwake,akamrushia Inspekta
Jamila,ili amfunge Shany Karama Rashidi au kwa kifupi Shankara!
Inspekta Jamila,huku akimfunga pingu aliekuwa mpenzi wake,akajisemea moyoni mwake,
“Ama kwa hakika,huu ni mtego wa panya!”
Shany muda wote alikuwa ameinamisha uso wake chini,kwa jinsi alivyoaibika na kufadhaika.
“Shankara,huwezi tena kwa sasa,kulipua chochote ndani
ya nchi hii,waambie hao waliokutuma,serikali ya
Tanzania,ipo makini na ina usalama wa kutosha! Tunazo
taarifa kuwa kesho ilikuwa ulipue bomu,katika benki kuu
ya Tanzania na mitambo yako ambayo ingeingia keshoCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
hapa nchini kwa njia ya Bahari,hivi ninavyoongea na
wewe,tayari tupo nayo katika himaya yetu!”
Jonga Janga,alizizima ndoto za Shany katika moyo wake.
“Yaani wewe Shany,umekuwa na roho ya tamaa namna
hiyo? Unadiriki hata kuuw......!!!
“...Kuuwa huyo ndiyo kazi yake inayompa pesa!Huyu,ndiyo kiongozi wa genge la uhalifu nchini.Amekuwa
akifadhili sana vitendo hivyo,na huyu Shany,ndiye
aliekuwa akifatwa na kina Jeradi Mwaipopo,pale kwa
macheni!”
JJ alimkatisha na kuingilia mazungumzo yale.
Inspekta Jamila,alimchukia Shany,kama mtu ambae,hakuwahi kuwa mpenzi wake!
Kwa mikono yake alimfunga pingu mikononi,akazikaza
pingu zile hadi namba ya mwisho,zikambana Shankara,akalalamika zilegezwe,lakini hakuna mtu,aliemsikiliza!
Shany akiwa mbele ya Inspekta Jamila,huku Jongo Janga,akiwa anapekua mizigo yake,akawashangaza askari wale.
Alizunguka na pigo moja aina ya ORAKEN,likatua katika
shingo ya Inspekta Jamila likampeleka chini kama mzigo, akadondokea kichwa, akanyooka pale chini,akiwa
hatikisiki,yaani alikuwa kama gogo!
Shany haraka akatimua mbio,kuuwahi mlango,lakini
hakufika, Jongo Janga alifyatua risasi mbili,kila moja ikawa imepigwa mguu wake na Shankara akadondoka,huku akipigiza uso wake katika sakafu akatoa yowe kubwa na kutupatupa miguu yake!
(ORAKEN,NI PIGO LINALOPIGWA NA MPIGAJI,AKIWA AMEMPA ADUI MGONGO,HUZUNGUKA NA KUPIGIA NYUMA YA KIGANJA NA LIPIGE SHINGONI KWA ADUI)
Mara Sagenti Kubuta,aliwasili mahala pale, na timu yake,baada ya kumuhifadhi Jambazi,mkorofi Jeradi Mwaipopo katika kituo cha Polisi cha kati.
Na gari nyingine ikiwapeleka wale maiti,katika hospitali
ya taifa ya Muhimbili.
*******
Inspekta Jamila,alipokuja kupata fahamu,alijikuta katika chumba kimoja tulivu,kikiwa na watu watano wakiwa wanamtazama.
Alipotazama vizuri,akaiona sura moja ngeni machoni
mwake, Dokta Zahara akasogea karibu yake, na
kumwambia.
”Pole sana shoga yangu,lakini unaendelea vizuri”
Inspekta Jamila,alitaka kusema jambo,lakini alishindwa,machozi yakawa yanamtiririka,kisha akageuza sura yake,akakutana na Jongo Janga akiwa anamtazama kwa upole.
Inspekta Jamila,alimkazia macho na hatimae
akazungumza katika sauti ya kwikwi.
“Yupo wapi Shankara?!”
Yule mtu aliekuwa mgeni katika macho ya Inspekta Jamila,akasogea karibu na kusema.
“Pumzika Kwanza,ili upate nguvu sawasawa,kwani
ubongo wako,umepata maumivu makubwa,ingeweza
kukulelea Busting chuma ingepasua mishipa ya fahamu.
Hivyo unatakiwa upumzike,ili urudi katika hali yako ya
kawaida!”
Alikuwa ni Dokta Rehema Kanyela,aliekuwa akimtibia kwa karibu,yeye pamoja na Dokta Zahara.
“Inspekta,pumzika umefanya kazi kubwa sana,unahitaji
pongezi kwa kweli.Nimekuja kukuona mara baada ya
kuruhusiwa kutoka kwa madaktari wanaokutibu,ambao tumeona awepo shoga yako,lakini pia yupo mtu wetu hapo ambae ni Dokta na ni Inspekta mwenzio kwa ajili ya
usalama ambae ni Inspekta Rehema Kanyela.Shankara na Jeradi Mwaipopo,wapo chini ya ulinzi mkali,tunaendelea kuwahoji,hivyo tulia,kila kitu kipo sawa umenisoma Inspekta?!”
Ilikuwa ni sauti ya IGP aliemwambia kijana wake
kinachoendelea na kumaliza kwa swali.
“Nimekuelewa Afande,ila kuna kitu kinanichanganya
kidogo ile BARUA KUTOKA JELA, imewapataje watu wa
usalama wa Taifa?”
“Unatakiwa kutii Inspekta,siyo kuuliza tena kumbuka
barua zote zinazotolewa nje kutoka gerezani huwa
zinapitiwa na afisa usalama nae ndiyo anatoa idhini kama
zichapishwe pale gerezani na kutolewa nje au
zikachapishwe nje na kutumwa sehemu husika. Hata Mwaduga Dingo,alipopeleka barua yake ikachapishwe na
kuruhusiwa kutolewa nje,amini ilishapita kwa watu wa
usalama!Hivyo kwa nukta hiyo,sidhani kama utakuwa na mashaka yoyote katika nafsi yako!” IGP alihitimisha
maneno yake,kwa kijana wake,na Inspekta jamila,hakuinua tena mdomo wake,kuuliza au kusema chochote
kile.
Siku tatu baadae Inspekta Jamila,alikuwa katika kikao na IGP,yeye na Sagenti Kubuta, na IGP alikuwa akiongoza kikao kile kama kawaida,akawa anawaeleza vijana wake.
“Inspekta Jamila,kupitia watu wa usalama,tumepata
uthibitisho mkubwa kuwa kwenye gari yako,kulifungwa
kifaa maalum na Shankara,ambacho kila ulipokuwa na
gari ile,ulikuwa unaonekana katika GPS.Na gari hiyo
uliyonunuliwa na Shankara, ilikuwa imewekwa mitambo ile toka Japan,ilipotoka gari ile.”
IGP alikuwa akizungumza huku akiwatazama vijana wake,walivyokuwa wamepigwa na butwaa,kisha akaendelea kutoa habari.
“Hivyo kila ulipokuwa ukizungumza,iwe kwa simu,au na yeyote,kulikuwa na chombo maalum,kilichokuwa kinatoa
taarifa,kila kilipotakiwa kufanya hivyo,kwa mantiki hiyo,mambo yako mengi, yalikuwa yanajulikana na watu wale,katika namna ambayo,ingesumbua kufahamu katika hali
ya kawaida!”
Inspekta Jamila,alikuwa akitingisha kichwa kwa kuelewa taarifa ile nyeti sana.
“Shankara ni wakala wa ugaidi,alipokuwa huko ng’ambo, alipewa mafunzo ya ulipuaji mabomu,na kupitia Interpol,tumeweza kupata taarifa,na usalama wa Taifa, wameshadhibiti kila jambo,vinginevyo Taifa lingepata zahma kubwa sana!”
IGP alihitimisha taarifa yake,na kuwataka vijana wake
kama wana maswali.
“Nimekuelewa Afande,vipi kuhusu Jeradi Mwaipopo,alipohojiwa alikuwa na lipi jipya?!”
Inspekta Jamila,alitaka kufahamu.
“Jeradi Mwaipopo,hakufata taratibu za kazi tangu wakati
yupo kazini,anaposema chochote wakati huu,kinakuwa hakina maana sana!Yeye anazifahamu ngazi husika,kama
alionewa,alipaswa kupanda ngazi za juu ili kutoa taarifa
ifanyiwe kazi,kama alikaa nayo taarifa yake,kwa muda
huu,ninaipokea kama changamoto!”
IGP baada ya kusema hayo, akachukua gilasi ya maji
akanywa,kisha akaendelea.
“JM na Shankara,na mke wa marehemu Dokta Masawe,siyo muda mrefu,watafikishwa mahakamani,mara baada ya Shankara kupata nafuu majeraha ya risasi na Jm kifua
chake kimepata matatizo,nae yupo hospitali,wote wakipata nafuu,watafikishwa katika vyombo vya sheria,ili
wakajibu mashitaka yao!”
IGP alinyamaza kimya ili kutoa nafasi kama kuna swali,alipoona kimya,akaendelea.
“Kuanzia kesho mmepata likizo,ya mwezi mmoja,leo hii
mtapata pesa yenu ya likizo,na kesho nitakuwa na
Mwaduga Dingo,ili nimpe majukumu mapya.”
IGP aliposema maneno yale kabla hajaagana na vijana
wake, kupitia simu yake ya upepo, ilisikika taarifaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
iliyowafanya waume meno kwa ghazabu.Taarifa ile ilisema hivi.
“Jambazi sugu,Jeradi Mwaipopo,ametoroka katika ulinzi wa polisi,pingu alizofungwa,zimekutwa chini ya uvungu wa kitanda,na askari wawili waliokuwa wakimlinda,wamekutwa wamezirai”!
“Kuanzia sasa, kila kitu kimevurugika, Likizo nimeifuta na mtarudi tena kazini, mpaka huyu Jeradi Mwaipopo, tuwe nae mikononi!”
IGP alisema maneno hayo huku akiwa amekasirika vibaya sana.
Na wote askari wale,Inspekta Jamila, na Sajenti Kubuta kwa pamoja wakasema.
“Sawa afande!”
IGP akawataka askari wake aende nao Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ili akajionee mwenyewe, kilichotokea.
Bila kuchelewa, safari ya Hospitali ya Muhimbili ikaanza!
IGP Kupitia kifaa chake cha mawasiliano, akatoa amri kwa wakuu wa polisi wa kanda zote za Dar es salaam, wahakikishe, vituo vya mabasi, uwanja wa ndege, bandari ya kwenda Zanzibar, vyote vinakuwa na ulinzi mara moja, ili kumzuia Jeradi Mwaipopo, asitoroke nje ya Mkoa huu!
Picha za Jeradi Mwaipopo zikasambazwa katika vyombo vya habari, ikiwemo magazeti na Luninga, kuwa anatafutwa na Polisi, na mtu yeyote atakae fanikisha kukamatwa kwake, Donge nono limeandaliwa kwa ajili yake!
IGP, pamoja na vijana wake wakaelekea katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, na wakajionea hali halisi ilivyokuwa!
Askari wawili walikuwa wapo hoi, hawajitambui kwa usingizi! Lakini pia povu jeupe likiwa katika vinywa vyao! Ulimi ukiwa umetoka nje kwa kiasi kikubwa sana!
Walikuwa wakipumua kwa tabu, mithili ya mtu aliekuwa katika ‘Sakalatilmauti’Yaani hatua za mwisho anazozipitia mwanaadam, kabla hajafikwa na umauti.
Pingu zilikuwa chini ya kitanda sakafuni, zikiwa zimefunguliwa!
IGP, alitikisa kichwa kwa masikitiko, nakuwataka askari aliokwenda nao pale hospitali, kuhakikisha kwa gharama yoyote, Jeradi Mwaipopo, anatiwa katika mkono wa sheria, tena haraka iwezekanavyo!
Inspekta Jamila na Sajenti Kubuta, waliitikia “Sawa Afande.” Huku wakisaluti
Inspekta Jamila, alivaa glovu na kuanza kuikagua miili ya askari wale,waliokuwa hawana fahamu.
Akagundua walikuwa hawana simu zao za mikononi, akashangaa!
Akakikagua chumba kizima kwa umakini mkubwa, hatimae macho yake yakakutana na mfuko laini mweusi wa plastiki, uliokuwa pembeni ya chumba kile.
Akauwendea ule mfuko, na alipoufikia akachuchumaa na kuutazama kwa makini. Ule mfuko ulikuwa haukufungwa juu yake, hivyo uliweza kuonesha kitu kilichokuwamo ndani yake!
Inspekta Jamila akiwa pale alipo, aliushuhudia mfuko ule ndani yake, kulikuwa kuna mabaki ya chakula.
Viazi vilivyokaangwa pamoja na mayai, maarufu huitwa chipsi, nyama ya kuku wa kukaanga na mifupa ya kuku iliyokwishaliwa tayari!
Inspekta Jamila, aliuchukua ule mfuko kwa umakini mkubwa, kisha akamgeukia bosi wake na kumwambia. “Afande nahisi hiki chakula watakuwa wamekula askari wetu, na bila shaka kinaweza kikawa ndiyo sababu ya haya matokeo tunayoyaona!” Alisimama kuzungumza Inspekta Jamila, na IGP kwa haraka akadakia.
“Kwa nini unahisi hivyo Inspekta!”
Inspekta jamila huku akiwaoneshea vidole wale askari waliokuwa mahututi, alimjibu kiongozi wake kwa unyenyekevu mkubwa.”Afande, hao askari mikono yao inaonesha walikula chakula hiki na hawakunawa baada ya kula! kwani mafuta yapo katika vidole vya mikono yao na mabaki ya tomato !”
“Inspekta unamaanisha chakula hicho kinaweza kikawa na sumu?!” IGP aliuliza kwa mshangao kisha akaendelea “Itabidi haraka kikapimwe ili tujiridhishe, na kama itathibitika ni kweli, swali hili litahitaji majibu, nani alieiweka sumu hiyo, na atakuwa ametumwa na nani?!”
Tafakari na ukimya ulitanda kwa muda, kisha Inspekta Jamila akasema kumwambia IGP.
“Afande mie naona, hawa askari tufanye kila tuwezalo, ili kuokoa maisha yao, kwani wao pekee kwa sasa ndiyo watakaokuwa na majibu sahihi, ya waliponunua au mtu aliewaletea chakula hiki, au chochote kilichopelekea kikaingia humu ndani chakula hiki!”
Mara moja aliitwa mganga mkuu pale hospitali, na kutakiwa kuzipima zile chipsi zilizosalia kama zipo salama, huku askari wale baada, ya kuwafanyia uchunguzi wa kina askari wenzao, waliokumbwa na masahibu yale, wakakabidhiwa madakitari ili kujaribu kuokoa maisha yao.
Na dakika arubaini baadae, Mganga mkuu aliwapa ripoti ya chakula kile!
“Vipimo vimeonesha kuwa, chakula hiki kimewekwa dawa za usingizi kwa kiasi kikubwa aina ya LAGACTIL, dawa tunazozitumia kuwapa wagonjwa wa akili, ili kupata usingizi! Kama mwendawazimu amezapo dawa hizi hupata usingizi, basi alapo mtu asiekuwa mgonjwa wa fahamu, anaweza kupata madhara makubwa sana katika ubongo wake, kama kulala kwa muda mrefu zaidi, kulewa, kutokwa na ulimi kama mbwa,na hata kufa, ikiwa atakuwa amekula au kulishwa dawa hizo kwa kiasi kikubwa.”
Alihitimisha mganga mkuu taarifa yake kwa askari wale, na wao wakawa wanamaswali mengi yaliokosa majibu sahihi, nani alieweka dawa zile katika chakula kile?! Na je mtandao wa genge la uhalifu lakina JM bado halijamalizika?! Fadhaa, hasira, chuki na sintofahamu, ikawakumba askari wale na kiongozi wao mkuu kabisa!
*******
Jeradi Mwaipopo, akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi wawili, katika chumba maalum pale hospitali ya taifa ya Muhimbili, alikuwa amefungwa pingu za miguu, na pia pingu za mikono! Ingawa katika mikono, alifungwa pingu mkono mmoja, na sehemu nyingine ya pingu ile, ilikuwa imefungwa katika kitanda cha chuma alichokuwa amelazwa.
Jeradi mwaipopo alikuwa katika maumivu makali, lakini akiwa katika fahamu zake kamili!
Alijizoazoa katika kitanda kile na kutaka kukaa kitako,akashindwa. Akawaambia askari wale. “Ndugu zangu nataka kwenda chooni.”
Askari aliekuwa na funguo za pingu, alizofungwa nazo JM, akamsogelea na kumfungua pingu za miguu zenye nyororo ndefu kiasi, kisha akamfungua pingu ya mkononi, ili waende nae chooni.
Jeradi Mwaipopo au kifupi JM, akawatazama askari wale, kisha akawaambia huku akiwatazama usoni moja kwa moja! “Ndugu zangu mnajuwa kuwa mie ni mwenzenu? Mbona mnanifanyia hivi?!”
Askari aliemfungua pingu akamjibu. “JM wewe ulikuwa askari, ila sasa siyo askari, lakini hata kama bado ungalikuwa ni askari, sie tunatekeleza wajibu wetu.”
JM, alitafakari kidogo, kisha akainuka na kuelekea katika choo, huku akifatwa kwa karibu na askari wale.
JM, aliingia chooni akiwa anatembea kwa kuburuza miguu yake, kutokana na pingu alizokuwa amefungwa nazo miguuni mwake muda mrefu, na kukazwa kumpa maumivu.
Alijisaidia haja kubwa na ndogo, huku akiwa akili yake ikifanya kazi kwa haraka na kubawabu hiki na kile, hadi alipomaliza haja zake, akawa amekwisha pata maarifa yakufanya! Akajisafisha na kurudi kitandani kwake, katika mwendo kama ule wa awali. Akakaa kitandani, na kunyoosha mikono yake, ili afungwe pingu kama awali, naam alifanyiwa huduma hiyo, iliyokuwa imemstahili kwa wakati ule, huku askari mwingine akimfunga zile pingu za miguu, JM sasa akiwa amelala chali, akasema kuwaambia askari wale.
“Ngugu zangu, naomba msaada mmoja kwenu, nina ndugu yangu anaishi jirani na hapa, naomba mnifanyie huduma ya simu, kumwambia kama nipo hapa, ili aniletee chakula, lakini pia nitamwambia awawekee vocha simu zenu, tafadhalini sana.”
Wale askari wakatizamana, kisha mmoja akamjibu JM kwa kumwambia. “Huo siyo utaratibu wa kazi yetu JM, wewe upo chini ya ulinzi, hivyo kukuitia watu ni kuhatarisha usalama wako na wetu, hilo halitowezekana, labda isubiri zamu itakayokuja, sie hapana JM!”
JM akiwa ametoa macho kwa jibu lile, akamjibu askari Yule, kwa kumwambia.
“Hiyo ni haki yangu ya msingi askari, sheria inaniruhusu kufanya hivyo! Kisha mie sijahukumiwa bado, bali ninatuhumiwa tu, hivyo nina haki ya msingi kwa mujibu wa sheria, kumbuka mie pia ni askari hivyo ninatambua haki zangu za kimsingi. Pia hiyo zamu ijayo sidhani kama haifanyi kazi kwa mujibu wa sheria. Naomba bwana nisaidie, au kama unataka nikulipe kwa jambo hilo, basi nitajie kima!”
Sasa ikawa zamu ya wale askari kufikiri, huku JM akiombea akubaliwe ili atimize azma yake, aliyoikusudia wakati ule!
“Unataka msaada JM, burebure tu, watu tupo kazini bwana, kama unaweza kutupa elfu hamsini, mie nitakupa simu yangu umpigie huyo jamaa yako, kama huna pesa, basi endelea kuugulia maumivu yako!”
Alisema askari mmoja aliekuwa na funguo za pingu za JM, ambae ndiye aliekuwa kiongozi.
JM,alitabasamu huku akichezesha kichwa chake kushoto kulia, kisha akasema. “Mie kama mnionavyo hapa nilipo, sina pesa hata kidogo, ila huyo ndugu yangu, naweza kuzungumza nae, akawaletea pesa hata elfu hamsini kila mmoja, wachilia mbali wewe kutaka elfu hamsini mgawane, mie natambua kuwa, mbuzi anakula kwa urefu wa kamba yake!”
Naam mjadala ule ukapata muafaka kuwa, JM azungumze na ndugu yake.
Jeradi Mwaipopo, alipewa simu, akabonyeza namba kadhaa kwa ule mkono wake mmoja uliokuwa huru, kwani mkono mmoja wa kulia, ulikuwa umefungwa pingu, pamoja na kitanda! Mkono wa shoto, uliwachwa kusudi, ili aweze kujikuna na kumpa huduma zingine!
JM alizipiga namba zile, na upande wa pili, ikawa inaita simu ile. Ama kweli, penye udhia, penyeza rupia.
“Halow…” JM alisema baada ya kupokelewa ile simu upande wa pili, na kuendelea. “…JM hapa, nipo hospitali ya muhimbili, huku karibu na Moi,nikiwa chini ya ulinzi. Hii simu ya askari nimeiomba hapa ili niwasiliane na wewe uje kunifaa nduguyo, naomba uje na Shilingi laki moja ili niwape viongozi wangu bwana, hawa ni watu muhimu sana kwangu, nakaa nao vizuri tu, kisha niletee……” JM akasimama kuzungumza na simu, akawauliwa wale askari.
“Mtakula nini awaletee, semeheni tu, kwani mchana unaingia!”
Wale askari walitazamana kisha mmoja akatabasamu, akasema .
“Mwambie atuletee chipi yai, na kuku aweke pilipili nyingi.”
JM huku akishusha pumzi ndefu akarejea katika simu na kumwambia mtu aliemuita ndugu yake. “……niletee chipsi mayai, na kuku sahani mbili, weka pilipili nyingi, watengenezee vizuri sana. Mie niletee maziwa fresh yananitosha, ukiniletea na pesa kidogo, utakuwa umenifaa sana!”
Baada ya kusema hayo, JM alikata simu, kisha akaifuta ile namba aliyoipigia, na kuirudisha simu kwa mwenyewe huku akiwa anatabasamu.
Dakika arubaini baadae simu ya Yule askari, iliita na alipoitazama ile namba, ilikuwa ngeni machoni mwake, akaipokea. “Halow, ndiyo hii, ehee, sawa njoo hadi hapa Moi, mie nakufata hapo nje, umevaa nguo rangi gani?, Haya basi sogea nakuja!”
Yule askari alikuwa akizungumza na ndugu wa Mwaipopo, kisha akakata simu na kutoka nje, akimuacha mwenzake akiwa anamdhibiti JM.
Kijana mmoja mrefu wa wastani, mweusi tii, aliekuwa amevalia nguo za kubana mwilini mwake,aliingia katika chumba kile, baada ya dakika zisizozidi saba, akiwa pamoja na askari aliemfata, alikuwa amebeba mfuko laini mweusi wa plastiki, akautoa mfuko wa ndani, na kuwakabidha wale askari. Kisha paketi mbili kubwa za maziwa ya Tanga fresh, akimkabidhi Jeradi Mwaipopo, huku akimwambia. “Pole ndugu yangu, nimekuja kukufaa!”
Aliyasema maneno hayo, huku akiwa amewapa mgongo maaskari wale. JM akamwambia ndugu yake, ”Umeniletea pesa nilizokuambia?!” Yule ndugu yake akajibu kwa vitendo, aliingiza mkono mfukoni, na kutoa burungutu la pesa, akazihesabu shilingi laki mbili, nyingine akazirudisha mfukoni. Akataka kumkabidhi JM, lakini JM akamwambia. “Laki moja wape askari, laki moja nipe mwenyewe. Yule ndugu yake JM, akafanya hivyo.
Wale askari walizipokea zile pesa wakagawana palepale huku wakitabasamu, kisha wakanawa mikono katika bomba lililokuwa chooni mle kwa zamu, wakiwa na pesa mfukoni, wakaanza kula chipsi mayai na kuku, kwa fujo!
Hawakufanikiwa kuzimaliza zile chipsi, walianza kunyong’onyea miili yao, nguvu zikawatupa mkono, wakataka kusema jambo midomo ikawa mizito, mikono yao haikuweza kuhimili uzito hafifu wa chakula walichokuwa nacho mikononi mwao, mifuko ile iliwadondoka! Walipotaka kupiga hatua, miguu yao ikakataa kutii, wakaanguka chini kama mizigo, wakaingia katika usingizi mzito!
Geradi Mwaipopo, akamwambia ndugu yake, “Chukua funguo anazo huyo alielala kushoto kwako.”
Yule bwana hakuchukua funguo peke yake, bali alichukua funguo za pingu, pamoja na pesa zake walizogawana askari wale,na simu zao, kisha akamfungua pingu za miguuni kisha akamfungua pingu ya pili ile iliyofungwa kitandani, ikafunguka na kuningg’inia kipande chake cha pili katika mkono wa kulia wa JM. Nae JM aliimalizia mwenyewe kuifungua,pingu ile akaitupa pingu ile chini ya uvungu wa kitanda!
Yule ndugu yake JM alichukua zile chipsi mayai, akaziweka katika mfuko mmoja, akitaka kuondoka nazo, JM akamwambia. “Wacha kubeba mizigo ya bure!” Na yule bwana akauwacha mfuko ule, ambao sasa ulikuwa katika mfuko mmoja! Akakumbatiana na Jeradi Mwaipopo, kisha wakatoka katika chumba kile, wakatoka katika jengo la hospitali ya taifa ya Muhimbili, na kutokomea kusikojulikana!
*******
Askari waliokuwa wanaingia zamu mchana, kuwatowa wenzao walioingia asubuhi, walipigwa na butwaa ya mwaka, baada yakuwakuta wenzao, wakiwa wamelala chini hawana fahamu, na Jeradi Mwaipopo, akiwa ametoweka! Kupitia simu zao za mikononi, walitoa taarifa kwa mkuu wao wakituo, na mkuu wa kituo alirusha hewani taarifa ile kwa simu ya upepo, ‘Radio call’
na ikasambaa kwa kila radio iliyokuwa wazi katika Jiji la Dar es salaam. Na haikushangaza kuwafikia taarifa ile Inspekta Jamila, na Sajenti Kubuta, wakiwa katika kikao na bosi wao IGP.
11
Inpekta Jamila, akiwa na Sajenti kubuta, baada ya kutoka Hospitali ya taifa ya Muhimbili, alikuwa anawaza mengi, akiwazuwa, hatimae akamwambia Sajenji Kubuta. “Inawezekana huu mtandao wa uhalifu wa kina JM bado upo, tena ni mkubwa sana! Sasa hivi inabidi twende katika mtandao wa simu, ili tukaone na huko kama tunaweza kupata lolote la maana, ingawa mie nahisi, huko kutatufanya tuwe karibu na JM, kwa namna moja au nyingine!”
Aliwasilisha ujumbe wake kwa Sajenti Kubuta, na wakawafikiana lazima wafike huko.
Sajenti Kubuta, akamuuliza kiongozi wake. “Tunakwenda kampuni gani ya simu Afande?!” Inspekta Jamila alimtazama Sajenti Kubuta kwa jicho la udadisi, kisha akampa kikaratasi kidogo kilichokuwa kina namba mbili za mitandao tofauti! Huku namba zile mojawapo ilikuwa imewekewa alama ya nyota mbele yake. Na inspekta Jamila akamwambia Sajenti Kubuta “Tunaanza na kampuni ya simu iliyowekewa alama ya nyota!”
Dakika tano baadae, wakawa barabarani, wakielekea Maeneo ya Moroco katika makutano ya barabara ya Ally Hassan Mwinyi, na Kawawa. Wakaingia kushoto katika jengo moja lililojengwa mithili ya meli, wakaegesha gari yao na kuteremka, wakajichoma ndani ya jengo lile.
Wakiwa ndani ya jengo lile, walifika mapokezi na kujitambulisha mapokezi, kisha wakataka kuonana na meneja wa kampuni ile ya simu, na baada ya mawasiliano haya na yale, wakakaribishwa katika ofisi ya meneja wa kampuni ile ya simu.
“Karibuni ofisini kwetu, niwasaidie nini jamani?” Alisema meneja yule akiwa katika sura ya kutabasamu.
“Asante meneja, kama ulivyotambulishwa na katibu muhutasi, sie ni askari polisi kutoka makao makuu. Tumekuja hapa tunahitaji tupate msaada wako, ili kuweza kufanikisha upelelezi wetu.”
Inspekta Jamila alimwambia yule meneja wa kampuni ya simu, huku akitoa kitambulisho chake na kumuonesha.
“Sawa Inspekta, nikusaidieni nini?”
Aliwajibu meneja yule, baada ya kukitazama kitambulisho kile, huku akiwa katika hali ya utulivu mkubwa.
“Askari mwenzetu, ni mteja wenu, na hivi tuongeavyo, anakaribia kufa kwa hicho alichofanywa, sasa tulitaka kufahamu, na tupate ‘PRINT OUT’ ili tuone simu alizowasiliana nazo leo hadi saa sita mchana!” Inspekta Jamila alihitimisha huku akimtazama moja kwa moja usoni, meneja yule.
“Ahaa hilo halina neno, ila tunautaratibu itabidi muufate, kwani siri ya mteja wetu, hatupaswi kumpa mtu mwingine! Hivyo mtasaini kitabu hapo, na kueleza kuwa, mnataka taarifa zipi na kwa nini, kisha mwanasheria wetu, atasaini na hatimae mtapata hayo mnayoyataka!”
Inspekta Jamila, akafanya kama alivyoelekezwa, na nusu saa baadae, ilichapishwa taarifa ya simu zilizowasiliana na namba ile aliyowapa yeye, ikiwa inasomeka ujumbe, simu zilizobeep, zilizobeepiwa, simu zilizopigwa, na simu zilizo ipigia!
Inspekta Jamila, aliiweka karatasi ile juu ya meza, akiwa anakusudia na Sajenti Kubuta, aione kwa umakini, taarifa ile.
Inspekta Jamila, alitoa kalamu na kuanza kuipitisha juu ya karatasi ile kwa umakini mkubwa sana, mara baada yakuimaliza kuipitia, akapiga mstari katika namba ya mwisho, ambayo ilisomeka simu ya yule askari iliipigia, na simu ile dakika arubaini baadae iliipigia simu ya yule askari!
Inspekta Jamila, alitabasamu, pale alipoiona namba iliyofanya mawasiliano na simu ya yule askari mwenzao, pia ilikuwa ni simu ya kampuni ile waliyokuwa katika ofisi zake!
“Meneja tunashukuru kwa msaada wa kwanza, ila bado tunahitaji msaada wako, tunaomba pia ‘PRINT OUT’ za namba ya mwisho kuwasiliana na simu ya askari mwenzetu, ikibidi ianzwe kuchapwa mawasiliano iliyofanya wiki moja nyuma!” Inspekta Jamila, alimwambia yule meneja, huku akionesha msisitizo!
Yule meneja akafanya kama alivyoelezwa, na dakika tano baadae zikaletwa karatasi zilizokuwa na kila kitu walichokihitaji. Wakaagana na meneja wakiwa wanatabasamu, wakarejea ofisini kwao, wakiwa na matumaini mapya!
Inspekta Jamila, na Sajenti Kubuta, walihamia katika chumba cha compyuta kwa muda, wakiwa na wahka ile mbaya!
Koplo Dihenga, mtaalam wa IT,(Imformation Technology) wa jeshi la polisi, aliwapokea na kuwasikiliza shida yao.
“Koplo, hebu tutafutie picha za mtu huyu, na data zake, kadiri utakavyoweza. ”Inspekta Jamila, alimwambia Koplo Dihenga, huku akimkabidhi karatasi waliyotoka nayo kule katika kampuni ya simu.
Koplo Dihenga, aliekuwa amezungukwa na kompyuta kadhaa! Aliipokea ile karatasi na kuilisha data compyuta iliyokuwa mbele yake, kisha akawa anaisubiri, kompyuta ile ikitafuta mambo iliyotakiwa itoe taarifa zake!
Baada ya dakika takribani tano, kompyuta ile, ilinyambua data zifuatazo! Mwenye namba ya simu, anaeulizwa anaitwa Mwakyembe Anthony. Line ya simu yake, inatumiwa katika simu aina ya Blackbery yenye imei:256436-03-020155-7. Imeongea ikitumia mnara wa kampuni ya simu ya Airtel, uliokuwa upanga mashariki, katika wilaya ya Ilala, mkoa wa Dar es salaa, Tanzania. Simu yake ilikuwa katika mnara wa Muhimbili, saa tano zilizopita! Muda huu namba ya simu hiyo imei,inasomeka katika mnara wa Kongowe ya Mbagala! Ikiwa ipo katika nyumba ya kumi na mbili upande wa kusini, kutoka katika mnara!
Koplo Dihenga, aliiprint taarifa ile, na kumkabidhi Inspekta Jamila.
Inspekta Jamila, akampongeza Koplo Dihenga, na kumwambia. “Hatuna muda wa kupoteza, tunaelekea Kongowe, kadiri simu hiyo itapohama eneo,utatupa taarifa!”
“Timamu Afande” Coplo Dihenga alimwambia Inspekta Jamila, huku akiwa katika ukakamavu, kuonesha heshima kwa mkubwa wake.
Inspekta Jamila, alipanga timu yake, dakika ishirini na tano baadae, gari mbili za kiraia, aina ya TOYOTA NOAH zikiwa na askari nane, wenye silaha za kivita smg, walikuwa wamezipakata katika miguu yao, huku Inspekta Jamila, na Sagenti Kubuta, wakiwa katika gari ndogo Toyota Soluna, ikikamilisha idadi ya gari tatu, zinazoelekea eneo la Kongowe,katika wilaya ya Temeke.
*******
Jeradi Mwaipopo akiwa na mtu aliemwita nduguye, anaeitwa Mwakyembe Anthony, baada ya kutoka katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, wakitumia usafiri wa Mwakyembe, pikipiki aina Boxer kutoka India.Ikiendeshwa na Mwakyembe, walivaa elementi wakawa wanaonekana kama abiria amepanda Bodaboda!
Safari yao, ilielekea Maeneo ya wilaya ya Temeke,katika eneo liitwalo Kongowe, kama unaelekea Mkuranga, nyumbani kwake Mwakyembe.
Walipofika waliingiza pikipiki ndani, wakafunga geti na kukumbatiana upya, kama watu waliokuwa hawajaonana muda mrefu nyuma.
“Asante sana ndugu yangu, kumbe bado unakumbuka maagizo yangu kuwa, nikikwita na kukwambia njoo unifae, namaanisha nini?!”
Jeradi Mwaipopo alimwambia mtu aliependa kumwita ndugu yake, kwa sababu wote walikuwa wanatoka katika mkoa mmoja wa Mbeya.
“Naam nakumbuka sana, kwani natambuwa kama umeshakamatwa, kwani nilikuwa nafatilia kwa karibu sana. Ndiyo maana uliponiambia nije nikufae, upo muhimbili,kisha ukanitaka nije na chakula kwa ajili ya wale askari, nikatambuwa natakiwa nifanye nini! Nilipita duka la dawa pale muhimbili, nikanunua zile ‘Njunja’(LAGACTIL) nikimwambia muuzaji, ndugu yangu anasumbuwa mwenye ugonjwa wa akili akiwa hospitali, na manesi wa pale muhimbili, wamenielekeza nije kununua dawa zao za usingizi hapa! Naomba nisaidie dada yangu. Basi Yule muuzaji wa duka la dawa Muhimu. Alinipa dozi kabisa, nami nikampa elfu ishirini, nikimwambia chenji aendelee nayo! Nikaenda pale karibu na Geti lakuingilia, upande wa kushoto, nikanunua maziwa paketi mbili, nikanunua na chipsi mayai, na kuku, nikasaga zile dawa za wehu za usingizi, nikazinyunyizia katika kile chakula, nikamtafuta Yule askari katika namba yake, akanielekeza ndiyo nikaja kukufaa! Nilidhani wangenambia nionje kile chakula, basi ningeonja kisha ningekunywa yale maziwa pakiti moja kuondosha ile sumu ya zile dawa, nabado balaa lingekuwa upande wao!”
Mwakyembe alihitimisha taarifa yake, kwa JM huku akiwa na wingi wa furaha. “Asante sana ndugu yangu kwa kunifaa, kwani nilikuwa sina mtu mwengine zaidi yako, ambae ni shababi na anaeweza kucheza mchezo ulioufanya leo! Sasa kuanzia sasa, jeshi la polisi litakuwa linakutafuta wewe pamoja na mimi, hivyo umakini unahitajika sana! Nakupongeza kwa kuchukua simu za wale askari, kwani wangebaki nazo, ile simu uliyoipigia namba yako ingebaki, na wangekusumbua, ila kwa kuwa umeichukuwa, umefanya jambo la maana sana!”
JM alimwambia Mwakyembe huku akimtizama kama alikuwa na neno la ziada, alipomuona hakuwa na neno, aliendelea. “Itabidi mie niondoke sasa hivi nielekee nyumbani kwangu Vingunguti, kwani kule ndiyo kuna hazina, na nikiwa kule hujihisi nipo pahala salama zaidi.” Jm alisema maneno yale na kutulia huku akijinyoosha viungo vyake!
*******
“Nipe taarifa tafadhali, amebadilisha eneo?” Inspekta Jamila alikuwa akiwasiliana na Koplo Dihenga kutoka makao makuu.
“Hapana Afande, inaonekana bado yupo hapohapo, kwani Imei inasomeka bado katika mnara huohuo, akiwa katika usawa uleule wa nyumba ya kumi na mbili,upande wa kusini, kutoka katika mnara.” Alijibu Koplo Dihenga, huku akiwa anaangalia katika kompyuta iliyokuwa mbele ya macho yake!
“Sawa Koplo umesomeka, nipo Mbagala Kizuiani nasonga eneo la tukio, tafadhali hakikisha hupotezi lada!” Alihitimisha Inspekta Jamila, kisha akakata simu. Akawa anaangalia mbele huku akiwa kimya na mawazo tele!
Sagenti Kubuta, alikuwa anaendesha gari akiongoza msafara ule, huku akiombea wahusika wanaowafata, wawakute ili wamalizane nao!
Wakiwa njiani eneo la Mbagala rangi tatu, simu ya Inspekta Jamila iliita, nae kwa papara akaitwaa simu yake, nakuitazama namba inayopiga, na hata alipoiona akaipokea simu ile chapu kwa haraka! “Unasomeka nipe taarifa!” Ilikuwa ni simu ya Koplo Dihenga kwa Inspekta Jamila. “Afande simu ya Konstebo Iddy Gebo, imewashwa katika mnara huohuo, ila imetolewa line iliyosajiliwa simu hiyo, na sasa imewekwa line nyingine! Hapa inasoma imei yake katika mnara, umenisoma mpaka hapo?” Alimaliza taarifa yake Koplo Dihenga kwa swali. Na Inspekta Jamila kwa wahaka mkubwa alimjibu.
“Nimekusoma Koplo, hiyo inaonesha mtu mwengine yupo na Mwakyembe, anaweza kuwa ni JM, au Mwakyembe ameamua aitumie pia simu yapili! Endelea kunijuza tafadhali,nakaribia eneo la tukio nipo Tanita mpakani mwa Mbagala na Kongowe!” Alijibu Inspekta Jamila na Koplo Dihenga akakata simu.Dakika kumi baadae, wakawa eneo la Kongowe,wakiikaribia nyumba husika, Inspekta Jamila akampigia Koplo Dihenga, na kumwambia “Nipo eneo la tukio, je kupo vilevile, au kuna badiliko?!” Koplo Dihenga aliangalia komptuta yake akamwambia. “Afande simu ya Constebo Iddy Gebo, imezimwa kama dakika tano hivi, ila simu ya Mwakyembe bado taa ya mnara inasomeka yupo hapohapo!” Alisema Koplo Dihenga na Inspekta Jamila,akamwambia “Labda itakuwa imezimika chaji, ngoja tufanye ambushi tutajuwa hapo hapo ndani, je hapa tumeshahesabu nyumba ya kumi na mbili, kutoka katika mnara wa simu, unaoonekana mbele yetu, kwa upande wa kusini, upo sahihi na data?”
“Hapo sahihi kabisa mkuu, hakuna shaka na data, endelea na kazi mkuu!”
Koplo Dihenga, alimjibu mkubwa wake akiwa anajiamini na majibu yake!
Inspekta Jamila, alikata simu, nakupanga timu yake kuzunguka nyumba ile, kisha yeye akaenda mlangoni nakulijaribu geti la nyumba ile, akaliona limefungwa nganganga! Akamtizama Sajenti Kubuta, kama aliekuwa anataka msaada, Sajenti Kubuta, akamwambia kiongozi wake. “Plani B plus mkuu!”
Na hata alipokwisha kusema maneno yale, Inspekta Jamila akamjibu “Plani B, Sajenti!” Kufumba na kufumbua askari wale waliparamia ukuta wa nyumba ile, huku baadhi ya raia wakishangaa kwa kitendo kile, lakini kwa kuwa wao walikuwa kazini, wala hawakutaka kuwajali, waliendelea na hamsini zao. Askari wanne walikuwa juu ya ukuta, na wanne walibaki chini.Wale askari waliokuwa chini, kila mmoja alikuwa na silaha, aina ya SMG,akiwa ameikamata barabara, akiwa doria katika pembe ya nyumba ile, akihakikisha kwamba hakuna mtu, asiyekuwa wao ataeruka kupitia ukuta wa pembe aliyokuwepo!
Inspekta Jamila, Sajenti Kubuta, na askari wawili, wataalam wa mapambano ya mikono, wote kwa pamoja waliparamia ukuta wa nyumba ile uliokuwa na ruva nyingi, kwa ajili ya kuruhusu hewa kuingiza kwa wingi ndani ya nyumba ile. Kwa ustadi mkubwa waliparamia na kufika juu kabisa ya ukuta ule usiopungua futi nane urefu wake, wakachuchumaa huku mikono yao, ikiwa imezama viunoni mwao, ilipokuja ibuka ilikuwa imekamata silaha ndogo ya Bastola mikononi mwao! Vitendo vyote hivyo vilikuwa vikifanyika kwa pamoja tena bila kelele! Wote wakiwa pale juu ya ukuta na bastola mikononi mwao, waliruka pamoja hadi chini ndani ya uwa wa nyumba ile, wakibimbilika walipofika chini na kulalia tumbo huku silaha zao, zikielekezwa mbele tayari kwa matumizi! Walilala pale chini kwa sekunde kadhaa, walipoona kimya hakuna rabsha yoyote iliyotokea, walitambaa kwa matumbo,na viwiko vya mikono, wakiufata mlango mkubwa wa kuingilia ndani, huku wakichelea kuonekana kama wangelisimama kupitia dirisha lililokuwa pana mbele yao! Na hata walipoufikia mlango, waliukuta mlango ule umefungwa kwa funguo, nyumba ikiwa kimya kabisa!
Sasa wakainuka huku wakijigawa wawili kila pande, waliegemea ukuta, huku silaha zao sasa zikikamatwa kwa mikono miwili, zikiwa zimeelekezwa juu!
Inspekta Jamila, alitoa ishara kwa wenzake, na kitendo bila kuchelewa, Sajenti Kubuta alirudi nyuma, kisha akapiga hatua kubwa na kupitia bega lake, aliukumba ule mlango kwa kishindo kimoja kikubwa, na ule mlango bila khiyana, ukafungukia kwa ndani kwa kasi na kujipigiza ukutani!
Askari wale wote wakalala chini kifudifudi kwa kasi ya ajabu,na kutulia pale chini huku sasa wakiwa wanaitazama korido ikiwa tupu haina mtu! Pia wakijikinga kama adui akiwa na silaha,basi kama angefyatua risasi, risasi ile ingepita juu, na wao wangekuwa salama. Askari wale waliinuka kwa ghafla wawili wakiwa upande wa kulia, na wengine wawili wakiwa upande wa kushoto. Wakatembea na ukuta huku wakiwa makini, safari hii wakiwa katika mwendo wa kunyata, askari mmoja wakila upande wa mbele alikuwa ameielekeza silaha yake mbele, na aliekuwa nyuma yake, aliielekeza silaha yake nyuma! Kifupi ilikuwa kila mmoja alikuwa akimlinda mwenzake, huku wakisonga mbele! Walipofika usawa wa iliyoonekana kama mwanzo wa sebule, walisimama huku wakiegemea ukuta, na Inspekta Jamila kupitia mkono mmoja, alikuwa anatowa ishara, ilihali mkono mwingine, alikuwa amekamata silaha yake sawasawa. Askari wale kila mmoja alitikisa kichwa kuwashiria kuwa ameelewa maelekezo aliyokuwa anayatowa kiongozi wao.Inspekta Jamila na vijana wake, walivamia wakiwa katika mstari mmoja bastola zikilenga mbele, tayari kwa kutumika, naam wakafika katika sebule lakini wasiyaamini macho yao! Wote walipigwa na mzubao wa mwaka, huku wakiongeza umakini mara dufu, walipiga goti, wakawa wanageuka kila upande tayari kwa mashambulizi, lakini bado ulikuwa kama kucheza na kivuli chake mtu, huwa hakina madhara yoyote! Inspekta Jamila huku akiwa ametaharuki kwa hali anayoishuhudia, alitowa ishara ya kusachi vyumbani, katika nyumba ile iliyokuwa mpya kabisa, ikiwa haina samani nyingi ndani yake, pia kulikuwa bado milango ya vyumbani, ilikuwa haijawekwa katika nyumba ile! Hivyo haikuwa shida kufika vyumbani, lakini hadi kinafikiwa chumba cha nne na cha mwisho katika nyumba ile, hakukuwa na majibu yaliyopatikana, yaliyotofautiana na ya vyumba vingine, vilikuwa hakuna mwanaadamu aliekuwa katika vyumba vile, sasa wakiwa wameshusha silaha zao chini, wote walijongea pale sebuleni, wakiwa bado hawaamini kitu wanachokiona kwa macho yao!
Mwakyembe Anthony, alikuwa amelala chali macho yamemtoka pima yakiwa hayaoni yanachotazama! Mwili wake ukiwa na matundu ya risasi usawa wa moyo wake, damu nyingi zilikuwa zimetapakaa sebuleni pale,na zilianza kuganda kuonesha kiasi ya kama dakika kumi na tano hivi, ndiyo roho imeacha mwili wa Mwakyembe Anthony, Lakini Jeradi Mwaipopo, akiwa hajulikani alipo wala hakuwamo katika nyumba ile! simu ya marehemu Mwakyembe, aina ya Blackbery, ilikuwa ipo juu ya stuli ikiwa ipo on! Inspekta Jamila alitikisa kichwa kwa masikitiko, safari hii akimkosa Jeradi Mwaipopo,au JM kwa dakika chache sana!
*******
Jeradi Mwaipopo, alikuwa anajinyoosha viungo vyake,Mwakyembe alitowa simu yake pamoja na simu za wale askari,akawa anazithaminisha, ndipo JM alipoiona ile simu ya Blackbery ya Mwakyembe, na mara moja moyo wake ukapiga paah! Akakumbuka simu hii ndiyo aliyowasiliana na yule askari, akipigiwa na yeye kupiga, JM anatambuwa tangu akiwa askari, madhara ya simu za Blackbery kwani zinaweza kukuonesha kila ulipo, na yeye mwenyewe alishawahi kuwakamata wahalifu waliokuwa wameziiba simu za aina hiyo, kwani hata kama ungebadilisha laini, lakini bado ingeweza kusomwa mahala ulipo, akahisi matatizo mbele yake,yakimjia kwa haraka!
“Akamwambia Mwakyembe, una kitu gani cha kutulinda humu ndani, ikitokezea mahasimu wetu, wakitujia hapa?!” Mwakyembe huku akitabasamu, alimwambia JM. “Ondoa shaka juu ya hilo,hapa nina Bastola inayobeba risasi kumi na nane, tena ikiwa imejaa risasi, lakini kama haitoshi jana tu ndiyo nimepata kiwambo chake cha kuzuia sauti!” Mwakyembe alisema maneno hayo, huku akikigeuza kiti cha kukaa mtu mmoja, aina ya sofa, juu chini na kuibua bastola peke yake ikiwa imevishwa magazini yake, na kiwambo cha kuzuia sauti kikiwa pembeni yake. Akamkabidhi JM kwa maana ya kumuonesha! JM aliipokea ile silaha huku akitabasamu, akakivesha kiwambo cha kuzuia sauti, akapandisha risasi chemba, akiwa kama anaeijaribu ile silaha kama inafanya kazi sawasawa, huku akiwa ameielekeza juu silaha ile, na risasi ikapanda juu, ikisubiri amri ya kutumwa iende wapi, naam JM akiwa anatizamana uso kwa uso na Mwakyembe, aliishusha ile silaha kwa kasi ikamlenga Mwakyembe, usawa wa moyo, na JM huku akifumba macho, aliziruhusu risasi mbili, kutoka katika silaha ile, naam nazo zikajibu kama zilivyotumwa, zikafumua moyo wa Mwakyembe, kila moja ikipiga katika moyo na kufumua nyama kubwa kwa nyuma!Kwa kuwa Mwakyembe alikuwa karibu kama futi tatu kutoka alipokuwa JM, risasi zile zilimrusha nyuma kama mita nzima na kumtupa chali chini kama mzigo alitupa mikono kidogo akatulia tulii kama maji mtungini, akawa amebadilishwa jina na kuwa marehemu Mwakyembe! JM aliibusu ile silaha aliekuwa anaihitaji kuliko kitu chochote kile kwa wakati ule, kisha akafunga usalama wa silaha ile automatic, huku risasi nyingine, ikiwa tayari ipo chemba, ikisubiri safari! Jm aliziendea zile simu zilizokuwa zimewekwa katika stuli na marehemu Mwakyembe, akaichukua simu moja iliyouwa inahadhi na heshima kidogo, mali halali ya Konstebo Iddy Gebo, akatowa line iliyokuwemo mle ndani, akatoa line nyingine ya simu, kutoka katika sehemu ya kuvalia mkanda kwa nje, aliibinjua suruali yake, na sehemu iliyokuwa imekatwa, akasogeza kwa vidole vyake, akatowa line ya kampuni ya simu ya Airtel, na kuipachika katika simu ile akaiwasha, na simu ikakubali kuwaka! Baada ya kujiridhisha kuwa ameshapata simu, silaha kwa ajili ya kujilinda, akaichukua na ile simu ya yule askari mwingine, nokia ya toch, akaziweka mfukoni mwa suruwali yake, mara ile simu aliyoweka line yake, ikatoa mlio wa betri kukosa chaji ya kutosha, na JM akaizima kabisa. Akatoka nje akifunga mlango kwa nje, akaiendea ile pikipiki ya marehemu, akatoka nayo hadi nje, akalifunga lile geti kwa funguo na kuondoka na ufunguo wa nyumba na wa geti, pamoja na ile silaha akatokomea zake, akielekea Vinguguti kwa fida Hussein!
MWISHO WA SEHEMU YA KWANZA!!!
TOA MAONI YAKO!!!!
0 comments:
Post a Comment