Search This Blog

Friday, 20 May 2022

DILI TATA - 5

 







    Simulizi : Dili Tata

    Sehemu Ya Tano (5)



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati bado akiwa anawaza na kuwazua hayo akahisi mkono ukiwa unaingia katika sehemu zake za siri. Akageuka kumungalia Sofi ambaye kwa muda alikuwa amelala

    ‘Vipi mpenzi umeshaamka?’ akamuuliza, tabasamu pana la kinafiki usoni mwake

    ‘Ndio babii. Nimeamshwa na ndoto nzuri niliyokuwa ninaota’ akajibu Sofi akiwa anajihisi raha sana pembeni ya mwanaume K

    ‘Ndoto gani tena hiyo mke wangu mtarajiwa?’

    ‘Nimeota mimi na wewe baada ya kukusanya mahela tumekuwa matajiri tumefunga ndoa na kuzaa watoto mapacha’ akajibu na kujivuta karibu zaidi

    ‘Kweli ee? Ah, mungu ajaalie hivyo mke wangu’ akamjibu na kumpiga busu la shavu

    Kitendo cha kupigwa busu kikamlegeza Sofi akajikuta anaanza kumshikashika Kijo

    ‘Sikia babii.. Itabidi kwanza Chan’duu tuwe naye katika mipango mpaka mwisho ndio ule mpango niliokuambia ninautafakari ndio tutaufanya’

    ‘Sawa babii mi nakusikiliza wewe tu. Kwani hasa Chan’duu ulikuwa umepanga kumfanya nini?’

    ‘Nilikuwa nimepanga nimpe mgao wake na kisha kumueleza ukweli kwamba mimi na wewe tunapendana hivyo achukue hela yake atafute mwanamke mwingine’ akamuambia huku akimpapasa sehemu za mapaja

    ‘Unadhani atakubali?’

    ‘Hawezi kukataa. Hajawahi kushika milioni yule hivyo milioni hamsini tukimpa atatuona kama miungu watu’

    ‘Na kweli babii mimi nakubaliana na wewe unaju..’

    ‘Najua nini! Hebu wasiliana na yule mama mfanyakazi wa mdosi ujaribu kumpekenyua ili tujue je wahindi wanaendeleaje baada ya mume kumkosa mtoto’ akamkatisha na ombi

    ‘Unajua babii hata mimi nilitaka kumpigia lakini nikaona nisifanye hivyo mpaka uniamrishe wewe bwana wangu’ akasema huku akinyanyua simu na kupiga.

    Simu ikaita ikakata. Akapiga tena. Ikaita ikakata. Akapiga tena. Ikapokelewa. Kwanza akaanza kusikia makelele ya watu wanaobwatizana kwa sauti kubwa pembeni ya mama huyo. Aliposikiliza kwa makini akajua kwamba hao watakuwa Ms na Msr Mazarkhan

    Kisha akasikia sauti hizo zikififia ikiwa ni ishara kwamba aliyepokea simu alikuwa anajitenga mbali na watu hao ili aweze kuongea kwa usahihi

    ‘Bi Mai vipi! Kwema?’ Sofi akauliza akimaanisha ni kwema hapo ndani mbona kuna makelele

    ‘Aa mwenzangu hapa hali imechafuka huyu Mazarkhan sijui ana roho gani? Mtu mbahili hata katika uhai wa mwanao’

    ‘Eeh! Kuna nini tena?’ Sofi akauliza akiwa anajua wazi huenda Mazarkhan kakataa tena kutoa hela ya kumlipia mwanawe wa kiume hela ya kwenda kusoma shule nchini marekani akidai hata Uganda anaweza kusoma

    ‘Mh! Huyu mzee hata mrithi wake pia anambania?’ Sofi akawaza

    ‘Yule jamaa mtekaji kapiga tena simu kataka milioni ishirini na tano tu ili amuachie mtoto sasa mama amekwenda benki kuchukua hela bila mumewe kujua hapa alikuwa anasubiri apigiwe simu aelekezwe sehemu ya kwenda kuzipeleka sasa kipindi anapigiwa simu ya kuagizwa sehemu ya kupekeleka hizo hela mumewe kasikia alipouliza mama ndio kamwambia kwamba anapeleka milioni ishirini na tano ili mtoto akombolewe basi baba kaja juu akisema kwanini wapeleke pesa wakati polisi wanalifuatilia suala hili. Hasemi hivyo kwasababu ya mtoto anasema hivyo kwasababu hataki kutoa hela zake’

    ‘Nini?’ Sofi akauliza akiwa ameshituka sana na kukaa vizuri. Kushituka kwa Sofi na kubadilika rangi ya uso kukamshitua pia Kijo naye akakaa kitako kutaka kujua ni kipi kimeshitua Sofi kiasi hicho. Sofi kuuliza nini hakuwa na maana ya kutaka kujua kama kweli Mazarkhan kagoma kutoa hela bali kutaka uhakika kwamba eti mtekaji anataka milioni ishirini na tano

    ‘Ndio hivyo mzee kagoma kutoa hela’

    ‘Aha’ akajibu akiwa anona kama anahisi kizunguzungu ‘sasa hela haipelekwi?’ akamalizia kauli yake kwa swali

    ‘Mama amesema anapeleka na hataki kuende askari hata mmoja na naona kama wameshakubaliana.. Hebu ngoja kidogo’ akakata simu





    Kukatwa kwa simu kulimshtua Sofi kiasi cha kujihisi kama vile ameporomokewa na dari,. Akabaki haoni mbele wala hata hajui alipo. Alikuwa ameshachanganyikiwa. Kitendo cha kuchanganyikiwa kwa Sofi kikamfanya Kj kubaki na maswali yasio na mfano

    ‘Sofi vipi? Akamuuliza akiwa amemkazia macho. Sofi kimya

    ‘Sofi kuna nini?’ akamuuliza kwa nguvu na kumtingisha

    ‘Chan’duu’ akajibu kama vile haoni mbele

    ‘Chan’duu amefanya nini?’

    ‘Ametugeuka’

    ‘Ametugeuka vipi?’

    ‘Ameongea na mama mwenye mtoto anataka milioni ishirini’

    ‘Nini!? Yule Chan’duu anawazimu!? Sasa anataka hela wakati mtoto tuko naye sisi??’

    ‘Hapo ndipo paliponipagawisha’ akajibu Sofi mapigo ya moyo yakidunda kwa kasi ya ajabu

    ‘Anajisumbua tu. Huyo mama naye anataka kulipa fidia mara mbili mbili

    ‘K inamaana hujaona tu?’ Sofi akasema akianza kuona kumbe hata Kijo mwenyewe si mjanja kama alivyodhani

    ‘Sijaona nini sasa? Kama mtoto tunaye sisi’

    ‘Kama tunaye sisi sasa Chan’duu kwa nini adai fidia?’ akauliza akiwa amekaza macho

    ‘Hapo ndipo ninapomuona chizi’CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘K usiwe mjinga. Unadhani Chan’duu akisha chukua milioni ishirini na mtoto hana, atalipa nini sasa?’

    ‘Si itakuwa ameshachukua chake’ Kijo akajibu kiwepesi

    ‘Akishachukua chake?’ Sofi akamuuliza akimuangalia kama vile anamuangalia mtoto mdogo wa darasa la tatu

    ‘Akishachukua ndio nini sasa?’ Kijo akauliza kwa hamaki akihisi anaulizwa maswali ya ajabu

    ‘Wewe humjui Chan’duu. Kwa taarifa yako kila siku ana ndoto za kwenda Brazil, sasa akiipata hii hela itabidi kukimbia mji na kwa vile sisi tumemgeuka basi na yeye atatugeuka kwa kutuchoma. Wewe hujaona tu? Ah! Mimi nilikuona mjanja sana kumbe nawe pia una bahatisha mambo?’ akauliza kwa hasira

    Kj akabaki kuduaa. Kisha akajiona mjinga na mzembe kwa kuona kitu kidogo tu ameshindwa kukigundua mpaka anapewa darasa na mwanamke? Tena mwanamke mwenyewe mshamba tu katika dili? Dah! Huu ni ukweli wa dhahiri kabisa, uko wazi hata mtoto mdogo anaweza kuuona bila shuruti. Ni jambo lililo wazi kuwa hata kama angekuwa yeye pia kama angegeukwa basi angefanya hivyo hivyo. Dawa ya aliyemwaga mbonga ni kumwaga ugali. Hiyo ndio kauli ya mishentown, sasa kwa vile wao wameanza ni lazima Chan’duu angemaliza. Akarudi kukaa kwenye kitanda akiwa amepagawa

    ‘Sasa tunafanyaje?’ akajikuta bado akitaka msaada wa mwanamke

    ‘Unaniuliza mimi wakati wewe ndio planmaster?’ Sofi akajibu akiwa anazidi kumshangaa Kijo

    Hapa mwanaume akajua kwamba amechemka mno na amepagawa, alitakiwa kutoa muongozo na si kutaka msaada

    Wakati akiwa wanajiuliza, kila mtu akiwa amechanganyikiwa kivyake, mara simu ya Sofi ikaita. Akainyanyua kama vile ananyanyua kitu cha kilo mia mbili. Akili yake ikiwa imevinza hata hajui kama anapokea simu..

    Halow!’ kwa sauti ya chini akaita

    ‘Wamekubaliana hivi, kuna kijana ndio kapewa hilo begi la pesa ndio anampelekea huyo mtekaji’ Bi Mai akamjuza

    Sofi akapata nguvu

    Akaiteremsha simu na kuweka sauti ya nje

    ‘Wamekubaliana na huyo mtekaji?’ akauliza kama hajaelewa au hajasikia vizuri

    ‘Ndio’

    ‘Wameelewana vipi?’

    ‘Huyo jamaa amemuambia mama ampe begi lenye hela huyo kijana aende nalo mpaka Mburahati shule akifika atakuta mtu atamkabidhi. Akishafanya hivyo tu basi baada ya siku mbili atampigia simu na kumuelekeza mtu aliye na mwanawe na atampata kwani mtoto amefichwa mbali kidogo lakini yuko mzima kabisaa’ akajibu kisha akaitikia mwito

    ‘Naitwa na mama’ akasema na kukata simu

    Sofi akabaki kuganda tu na simu mkononi. Ni dhahiri kwamba Chan’duu akishakamata hela atakachokifanya ni kumtaarifu mdosi kwamba utekaji huo umefanya na Sofi na ndie mwenye mtoto. Nini mana ya Chan’duu kufanya hivi? Maana yake ni kwamba Chan’duu atakapo kamata hela leo atachukua gari na kukimbilia Kusini. Kesho atakapofika kusini akiwa na uhakika wa kuvuka boda kwenda Sauzi basi ndipo atapiga simu kumwaga mboga akijua wazi kwamba hata akichomwa hatakuwepo nchini

    Kisha ghafla wazo likampata Sofi. Mburahati? Kwanini Mburahati?

    Mburahati kuna rafiki yake wa damu, rafiki pekee wa kweli wa Chan’duu aitwae Mudy. Chan’duu atamtumia Mudy kwenda kuchukua hela na kumsubiri geto kwake na akifika wote wawili watakuwa na safari ya Brazil. Milioni ishirini na tano ni nyingi lakini Mudy alivyokuwa anaelewana na Chan’duu hata iweje hawezi kukimbia na hela hiyo akijua wazi akishaichukua tu watakimbia wote. Kwa vyoyote Chan’duu atakuwa ameshamuambia Mudy kila kitu

    Akageuka kumuangalia Kj aliyekuwa amechanganyikiwa anajiuliza maswali bila majibu

    ‘Najua alipo’

    ‘Nani? Chan’duu?’

    ‘Ndio’

    ‘Kweli?’ akauliza akiwa haamini

    ‘Yuko Mburahati kwa jamaa mmoja anaitwa Mudy’

    ‘Unahakika?’

    ‘Ndio nina hakika asilimia zote. Chan’duu atamtuma Mudy tu kwenda kuchua hiyo hela..’

    ‘Kama Chan’duu atamtuma huyo Mudy basi na yeye ni lazima atakuwepo mahala hapo. Nyanyuka twende’ akasema Kijogobwire huku akinyanyuka na kufuata nguo zake na kuzivaa





    Muda wa kuchukua hela ukafika. Kama mudy alivyoagizwa na rafiki yake ndivyo hivyo alivyofanya. Alifanya mawasiliano kwa ustadi wa hali ya juu akifuata maelekezo ya Chan’duu aliyejifunza kwa kuona kutoka kwa Kijo. Baada ya kuchukua begi taratibu akaanza kupiga hatua kwa umakini kurejea geto ili akapange kilichopo na rafiki yake wa damu

    Ni kweli Chanduu alikuwa mahala hapo kama Kijo alivyodhani. Yeye na Mudy ni marafiki tokea utoto, wanaaminiana kiasi kuna kipindi walikuwa wanashea hadi wanawake. Lakini milioni ishirini na tano hela ambayo Chan’duu hajawahi kuota kuishika katika maisha yake hivyo hawezi kumuamini hata mama yake mzazi achilia mbali rafiki. Wakati Mudy anakwenda sehemu ya tukio Chan’duu naye akachomoka na kumfuata kwa nyuma mpaka mahala hapo na kukaa mbali akiwa anashuhudia mchezo mzima.

    Sasa Mudy tayari ameshakabidhiwa begi lenye mahela na wala hakuna dalili kwamba kuna askari anamfuatilia. Chanduu akachomoka na kumuwahi. Hata Mudy mwenyewe hakuamini alipomuona Chan’duu. Alitabasamu na kukiri kwamba pesa ni mwanaharamu kwani haina urafiki. Wakati alipomkabidhi begi tu ghafla wakakuta kuna taxi imepaki mbele yao. Wakati wakiwa wanajiuliza kama wameingia mtego wa polisi, mara mtu mmoja akachomoka katika taxi hiyo na kumvuta Chan’duu na begi lake ndani ya gari na kisha kuchomoka kwa kasi. wakati Chan’duu akiwa amechanganyikiwa kwa kutokuwa makini kiasi cha kuingia katika mtego, akakutana na sura iliyoiva ya mwanume Kijogobwie

    ‘Unajiona wewe mjanja sio? Sasa leo kiama chako kimefika’ akaambiwa Jasho likaanza kumtoka na utumbo kumnyong’orotaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sofi aliyekuwa ameketi kiti cha mbele hakuwa na uwezo wa kugeuza shingo kumuangalia Chan’duu aliyekuwa anatetemeka kama mtoto wa kike. Aibu na fadhaa vilikuwa vimemkumba Sofi na kujihisi sasa akiwa mhalifu kamili. Ni vipi sasa ameweza kuwa mhuni kiasi hiki? Ghafla tu leo ndio akapata kujua kuwa sasa ameshabadili maisha. Sasa amekuwa jambazi. Si muda mrefu ataanza kuwa nguli wa uhalifu. Watu wawili waliokuwa nyuma pamoja na Kj walikuwa majambazi waliokubuhu. Hili alifahamishwa na K mwenyewe kipindi alipokuwa akiwasiliana na watu hawa kwa ajili ya kuwapa kazi hii iliyoanza kumshinda. Watu hawa, hasa huyu mmoja aliyempinda Chan’duu kwa mbele na kumuweka chini ya miguu yake na mwingine aliyekuwa upande wa pili wa K, walikuwa wakora wazoefu kuanzia miili yao na sura zao na matendo yao

    ‘Vipi Kijo, kambini au Guantanamo?’ Jorg aliyekuwa katika usukani akauliza

    ‘Kambini’ Kj akajibu

    ‘Hapana. Hii shuhuli twende tukaimalize Guantanamo, itatuwepesishia sisi mfungwa kumtia shimoni’ yule jamaa aliyempinda Chan’duu akasema

    ‘Poa’ Kijo akakubali

    Sofi alikuwa hajui Guantanamo ni wapi na mana ya kumtia shimoni mfungwa pia hakuielewa. Lakini laiti kama angejua maana ya lugha hii basi angejirusha nje ya taxi na kukimbilia polisi

    Taxi ikafika Sinza. Ikakunja Sinza makaburini. Na kufika mahala walipokuwa wanakwenda katika nyumba moja iliyokuwa haijamalizika kujengwa. Nyumba hii ya ghorofa moja ilikuwa imekamilika nusu na nusu kuwa kama imesuswa na ilionekana imejengwa muda mrefu na mwenyewe kushindwa kuimalizia na kuiweka kiporo. Ndani yake ilikuwa kuna watu wanaishi lakini watu hawa walikuwa ni majambazi na hii ilikuwa kama maskani yao. Nyumba hii muda huu ilikuwa haina watu, hii ikimaanisha kwamba wenyewe ni watu hawa walioingia sasa hivi

    Nyumba hii iliyokuwa mithili ya godauni ilikuwa chafu na isiyo na hadhi ya kuishi binadamu lakini kulikuwa na chumba chenye kitanda na baadhi ya vitu ikiwa ni ishara kwamba inakaliwa na watu

    Taxi ilipoingia ndani Chan’duu akateremshwa na kupelekwa katika chumba kimoja kilichokuwa na Kiza na joto kali. Akafungwa kamba mikono na miguu na kukalishwa chini katika sakafu

    ‘Ulitaka kunisaliti ee? Unajione wewe mjanja ee? Sasa leo nakupa funzo kwamba usijaribu kumchezea mwanaume Kijogobwire’





    akasema Kijo na kuanza kumpiga mateke kama vile anapiga mpira

    Chan’duu akabaki kuugulia maumivu kwa sauti iliyokuwa haitoki huku kitambaa kilichokuwa mdomoni mwake kikiwa kimejaa mate yaliokuwa yanamtoka pamoja na damu ziliziokuwa zinamvuja mdomoni kutokana na mateke aliyopigwa

    Kitendo cha Kijo kumpiga Chan’duu kama vile anapiga gunia kilimfanya Sofi kuanza kulia na kuomboleza

    ‘Jamani basi. Basi inatosha. K pliiz’ hatimaye akaanza kuomba

    ‘We nyamaza’ Kijo akamuambia kwa ukali

    Sofi akabaki kulia na kujikunyata

    Katika wakati ambao Sofi akiwa anaona Chan’duu amenyong’onyea na amezimia kutokana na kipigo, mara akamuona mmoja kati ya wale jamaa wawili akitoa kamba katika sanduku moja lililokuwemo humo chumbani, kisha akamfuata Chan’duu na kumuingiza nayo ya shingo. Hapa bado pia Sofi alikuwa hajajua kinachoendelea. Kama alisikia kwamba hapa ni Guantanamo basi ameshajua kuwa ni mahala pa mateso lakini sasa alikuwa anatakiwa kujua kile ambacho jamaa walisema kwamba watampeleka shimoni huyu mtu kilimaanisha nini

    Baada ya jamaa kuiingiza kamba hiyo shingoni Kijo akaanza kumsukuma Chan’duu huku akimuambia ‘Amka wewe mpumbavu uone mwisho wako unavyokuwa’

    Alipoona Chan’duu haamki akaenda pembeni palipokuwa na maji na kuyatwaa. Akaja na kummwagia ndoo mzima. Maji haya yakamfanya Chan’duu kupata nguvu kidogo na kuanza kurejewa na fahamu. Wakati akiwa anawaangalia wabaya wake kwa jicho la kujiuliza, Kijo akajua kwamba mtu wake ameshapatwa na fahamu na ni muda wake wa kumuadabisha kama atakavyo. Akaivingirisha kamba vizuri shingoni na upande mmoja akampatia mmoja kati ya wale jamaa wawili, kisha upande mmoja akaushika yeye na kuanza kuuvuta

    Kj alikuwa anamnyonga Chan’duu mchana kweupe. Kitendo hiki kilimfanya Sofi kuanza kutetemeka na kulia huku akiwa haamini anachokiona

    Kj na mwenzake baada ya kuona Chan’duu ameshakata roho wakamuachia

    Kj akamchukua Sofi mzobemzobe na kwenda naye katika chumba ambacho kilikuwa na godoro. Akamuweka hapo na kumsimamia mbele yake

    ‘Acha kelele. We unadhani tungekamatwa ingekuwaje? Yule ni msaliti na wasaliti ndivyo wanavyofanywa’ baada ya kusema maneno hayo akatoka na kuubamiza mlango akimuacha Sofi akilia kwa kwikwi majuto kujiapiza na kujiuliza

    Akiwa sasa ameshamaliza kazi moja kati ya kazi mbili ambazo alikuwa ameshazipanga. Kazi iliyokuwa inafuatia ni kuhakikisha muhindi analipa shilingi milioni mia tatu kamili kama alivyoamua sasa. Hii milioni ishirini na tano sasa itakuwa kama kifuta jasho au kwa lugha nyepesi basi itakuwa ni advansi ya kujitayarisha kuingiza mamilioni hayo ya shilingi

    Sasa kilichopo ni kujipanga kuwadhibiti watu hawa hatari wa kukodi ili huko mbele wasijekuleta tamaa na kumgeuka. Hapa ni kuwaeleza kwamba msaliti huyu begi alilokuja nalo ni la hela kamili ambayo ndio walikuwa wameidai kwa muhindi. Sasa kilichopo ni kuwapa mgao wao wa milioni moja na nusu na kuwadanganya kwamba zilizobaki ni ngawira ya wakuu waliomsaidia katika inshu hii na yeye mwenye mzigo. Labda kikubwa atakachokifanya hapa ni kuwaongeza laki tano ili alitumie dambwe hili katika kumalizia mipango yake

    Akafika alipo Jorg

    ‘Sasa sikia kiongozi.. Nataka ikifika saa tatu usiku uende kambini ukamchukue Yule mtoto umlete hapa. Sawa?’

    Nimekupata kiongozi. Sasa kwa vile kazi yako ni usiku acha mimi muda huu nikapige mishe nyingine’ Jorg akaaga

    Kwa vile hapa hakuwa na kazi nyingine ikabidi amruhusu

    ‘Poa kamanda ukirudi usiku na kunikabidhi mzigo na baaada ya kazi ya kukusanya kilichobaki nitahakikisha unapata mgao wa kununua nyumba’ akamumbia huku moyo ukimuuma kwa nini atoe milioni kumi kumpa mtu huyu, lakini alikuwa hana jinsi huyu ameianza kazi tokea mwanzo hivyo kumletea ujanja itakuwa kujichimbia kaburiCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alipotoka hapo akaingia katika chumba walichokuwa makanda wawili waliokuwa wakivuta bangi

    ‘Sasa makamanda kazi hii imekamilika. Unajua hii kazi kama nilivyowaambia kuwa ni ya wakubwa, hela imeshatoka ninachotaka hapa kwanza usiku mukaitupe maiti katika mtaro mbali kabisa na hapa, pia yule mtoto usiku ataletwa hapa ili wiki ijayo apelekwe kwa mwenyewe’

    ‘Kwanini wiki ijayo wakati mpunga umeshachukua?’ akauliza mmoja katika hali ya wasiwasi

    ‘Unajua mkuu kasema kwamba huyu mateka kila akizidi kukaa hapa ndipo wazazi wake watazidi kutishika hivyo tukimuachia watakaa kimya wakijua kuwa wakileta za kuleta basi itakula kwao’ akadanganya

    ‘Na kweli kwamanda’ yule wa pili akaunga mkono lakini kuunga kwake mkono ilikuwa katika namna ya kutaka mazungumzo haya yakatike tu ili aendelee na starehe yake ya kuvuta

    Sasa mwanaume Kijogobwire alikuwa ameshapanga mambo yake kwa umakini, kilichobaki ni kumaliza muda huu wa mchana na kuingia jioni ili usiku mtoto aletwe hapa. Hapa sasa akaona kuna sababu ya kutoka kidogo ili apate kwenda kutuliza akili yake iliyokuwa imezidiwa na matukio. Kwanza suala la kuua kwake lilikuwa geni lakini sasa anatakiwa kutuliza akili yake kwa ajili ya kulipanga suala la kukamata hela huku wakora hawa hatari wasijue kinachoendelea.

    Atatoka hapa na kwenda Jim kufanya mazoezi. Kisha ataingia toilet na kuoga kwa muda mrefu. Akitoka hapo ataingia mgahawani atajilazimisha kupata mchemsho wa kuku na kisha kushushia na vodka na kuyaweka mawazo yake mbali na matukio haya. Baada ya hapo akili yake itarudi upya. Alishawahi kufanya hivyo mara kadhaa pale anapojihisi fadhaa, na atafanya hivyo leo na kuipoza nafsi kabla ya kurudi akiwa mpya

    Kama alivyopanga ndivyo hivyo hivyo alivyofanya ila tu kuna kitu kimoja alizidisha. Alipokuwa yuko bar akiwa anapata kinywaji mara wazo likamjia baada ya kukutana na dada mmoja aliyewahi kuwa mwanamke wake huko nyuma. Akaona hapa si mbaya akiuchombeza mzigo na kuutangazia dau na kuingia nao chumba cha wageni na kuburudisha roho. Kila alivyofikiri begi la mahela alilolificha katika chumba alicho Sofi hakuwa na wasiwasi akijua kabisa kuwa mwanamke yule hawezi kukimbia nalo huku akiwa na hakika kwamba wakora hawawezi kuingia aliko Sofi na kuondoka na mzigo wa wakubwa kama alivyowatisha. Akaona ya nini kurudi mapema

    Akafanya kama alivyopanga. Baada ya dakika kadhaa tu akajikuta kitandani na mrembo kama alivyotaka

    Alipotoka hapo sasa ikiwa imeshatimu saa mbili kamili, akarudi Guantanamo. Njiani akampigia simu Jorg na kumtaka uchukuaji wa ule mzigo kuufanya mida wa saa tano usiku kwani muda huo umetulia na hakuna mizegwe

    Akarudi geto na kuwakuta jamaa wameagiza bia wanakunywa na moshi wa sigara kama wako kiwandani

    Akaingia ndani na kumkuta Sofi amejikunyata kama vile amefiwa ghafla na wazazi wote wawili katika ajali ya moto na nyumba yao yote kuteketea

    Hapa Kijo akaona kuna kitu anatakiwa kukifanya. Kumuacha Sofi katika hali kama hii kutamletea matatizo makubwa huko mbele. Matatizo atakayoshindwa kuyakabili

    Akamfuata alipo na kumuinamia

    ‘Swety. Unajua wakati mwingine huwa ninafanya vitu mpaka huwa najuta. Kwa kweli kitendo nilichokifanya sio kizuri na nakijutia. Najua kimekuuma sana, so naomba unisamehe babii’ akasema kwa sauti ya chini iliyojaa mazonzi akiwa anaamini kwamba Sofi ataingia katika hadaa hii

    Sofi akamuangalia kwa uso wa hasira zilizowazi wazi

    ‘Unajua umeua?’ akamuuliza akiwa bado haamini alichokiona

    ‘Nimesema najuta na nilifanya kwa kuchanganyikiwa. We unadhani saa hizi tungekuwa wapi kama angefanikiwa mipango yake? Na isitoshe wewe ndio uliniambia lengo lake’ K akajitetea

    Sofi akanyanyua sura na kumuangalia kama ampige kibao lakini akajizuia. Akajiambia kwamba hapa akileta hasira haiwezi katu kukamilika kwa lengo lake alilokuwa amelifikiria kipindi Kijo hayupo. Haiwekani kabisa kuweza kutimiza dhamira yake. Wakati K alioondoka bila kuaga, yeye alibaki akilia mpaka sauti ikakaribia kumkauka. Aliponyamaza akajiuliza binafsi.. Amejiingizaje katika janga hili? Akajiuliza na maswali mengine milioni yaliokuja na majibu kwamba, kilichotokea kimeshatokea katu hakiwezi kurudi nyuma. Sasa afanyeje? Akajiuliza. Jawabu alilolipata ni moja tu. Kwa vile Kijo amejisahau na begi hili la hela kuliacha hapa, basi kikubwa alibebe begi hili na kukimbia. Atakachofanya ni kukimbilia kijijini kwao ikiwa ni kituo cha kwanza kabisa. Hapo atakaa na kusikiliza taarifa za habari na kufuatilia magazeti kuona kisa cha mtoto aliyetekwa kimeishia wapi. Akiona imepita wiki mbili bila taarifa zozote basi hiyo itakuwa ishara kwamba K amefanikiwa kuingiza fedha aliyoitaka na mkasa kumalizika.





     Alijua wazi kwamba akikimbia na hela hii, kikubwa atakachoweza kukifanya Kj ni kudai fedha kwa muhindi haraka sana, kisha si hasha atashukuru kwamba hakuna mtu wa kuwagawa naye tena nusu kwa nusu

    Alipoona wazo hilo ni muafaka akanyanyuka na kwa kunyata akafungua mlango kuchungulia nje. Kitu kilichomkatisha tamaa ni kwamba bado kiza kilikuwa hakijaingia na hiyo inaweza kuwafanya wale wakora wawili kumuona na kufanya afikwe na kile alichokutana nacho bwana wake wa zamani

    Akakaa na kukisubiri kiza huku akiomba kila dua kila anayoijua ili K asirudi mapema na kumfanya suala lake kushindikana

    Ilipofika saa moja na nusu kiza kimeshanza kutanda akaona muda huo ni mufaka kwake. Akalichukua begi na kwa mwendo wa kunyata akaanza kutoka kuelekea mlangoni

    Akavipita vyumba vya awali akinyata na kuziba pumzi huku akikihofia hata kivuli chake

    Alipovipita nyumba vya awali akatokea karibu na getini. Wakati alipokaribia mlangoni katika chumba cha mwisho akasikia sauti kubwa ya mtu kwenda chafya. Akashituka sana akiona sasa amekamatwa, lakini haikuwa hivyo

    Akakipita na chumba hicho na kulifikia geti

    Akafungua komeo la kwanza taratibu akijibana kama vile uhai unataka kumtoka

    Akafungua komeo la kati

    Akafungua na komeo la chini

    Taratibu sana akakizungusha kitasa

    La haulaa

    Akakuta kimefungwa na funguo. Hapo bado kidogo apige kelele. Ikawa haina budi ila kutafuta njia nyingineCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hapa sasa akaona kitu cha msingi ni kuruka ukuta tu. Wakati akiwa anarudi katika chumba cha awali ili atafute namna ya kuruka ukuta mara akasikia sauti ikiuliza ‘Nani?’

    Kikapita kimya kingine kisha sauti ikauliza tena ‘Nani?’

    Akasimama kusikilizia. Akasikia mtu akisimama ili kutoka nje kuchungulia. Akajua kwamba ni mmoja wa wale wakora aliokuwa nao katika nyumba hiyo

    Akatoka mbio na kurudi chumbani kwake na kujiinamia huku analia mpaka Kj aliporudi

    Hapa sasa mbele ya K akaona anatakiwa kutumia hekima ili aangalie nafasi nyingine ya kuitumia

    ‘Sikia babii. Naomba twende bar hapo kati tukapate maji kidogo uondoe mawazo’ K akatoa pendekezo

    Hii kwa Kijo ilikuwa ni kujaribu kumrejesha patna katika hali yake ya kawaida ili waweze kulimaliza suala la ukusanyaji wa pesa kisha hapo kitakachompata patna huyo ni kile kile kilichompata patna maiti. Tofauti yake huyu atakufa taratibu tena kwa kuvizia. Kufa Sofi si kitu sahihi na kwa kweli hata yeye binafsi Kijo alikuwa anajifikiria mara mbili mbili lakini mwanamke huyu kubaki hai ni hatari. Kwanza atataka mgao kamili. Kitu ambacho hakiwezekani katu. Halafu ameshamuona mwanamke huyu tokea pale walipokuwa na marehemu Chan’duu kwamba ana jeuri na ubishi. Si anakumbuka pale alipomwambia Chanduu ‘Kama unataka ninyamaze poa ila katika hilo suala mimi najitoa’ Sasa ni kipi kitamfanya asimtingishie kibiriti litakapotokea suala la kumkanya? Hapana lazima afe

    Wakati akiwaza hayo Sofi akaona hapa amepata upenyo wa kukimbia. Acha suala la kukimbia na hela hapa kilichopo ni kukimbia tu kisha kwenda polisi na kujisalimisha. Kitakachotokea potelea mbali kitokee. Ameshaharibu. Kutengeneza hawezi. Kilichobaki basi na kije tu

    ‘Sawa babii nimekulewa twenzetu lakini mimi sitakunywa si unasikia sauti yangu ilivyo koo limenikauka sana so nitakula kongoro tu’ akasema ili kutilia mkazo suala la kutoka

    ‘Poa nenda kaoge kisha utavaa tishat yangu mimi nitaazima nguo kwa jamaa’

    Akasubiri Sofi anaingia chooni akatoka nje na kwenda kununua kufuli yake mwenyewe ili wakitoka afunge mlango wakora wasije kutimka na begi la manoti kisha ikawa shuhuli nyingine

    Aliporudi ilikuwa bado Sofi yuko chooni akijiswafi. Baada ya muda akatoka na kuingia geto kwenda kuvaa

    …………..

    Wakatoka

    Kwa vile ilikuwa karibu wakaona wakatize mitaa kwa miguu

    Lakini njiani Kijogobwire alikuwa anafanya kila kitu kuhakikisha Sofi hapati upenyo wa kuwa peke yake. Alihakikisha hapati hata nafasi ya kupiga hatua tatu mbele. Ni kama alijua mawazo ya sofi. Kitendo hicho kilimfanya Sofi kuona kwamba suala lake la kukimbia hapa linashindikana na sasa anatakiwa kubuni njia nyingine. Sasa afanyeje?

    Wakafika bar.

    Kijo akaagiza maji na sigara yeye akaagiza kongoro na soda

    Wakati anasubiri chakula na hata kilipoletwa na kuanza kula alikuwa anawaza na kuwazua njia sahihi rahisi na nyepesi kumfanikishia jambo lake la kutoroka. Akaona bado hakuna namna. Kisha kama vile amegutuka akaona njia ipo moja moja tu tena muafaka. Nayo ni kumuua Kijogobwire na kisha kuwavizia watu wale waliokuwa wanalewa wazimike achukue begi na kukimbia mji. Ndio. Hiyo ndio solushen

    Wakati akiwa anawaza hayo hakujua kwamba kumbe kichwani mwa Kj kulikuwa na mawazo hayohayo. Kila K alivyokuwa akimuangalia Sofi alikuwa anapata uhakika kwamba msichana huyu kuna kitu anapanga na kitu hiko si kingine zaidi kama si kukimbia basi kumdhuru. Dhana hii ikamfanya sasa abadili mawazo. Akajiuliza hivi kweli hili suala hawezi kulimaliza bila Sofi. Anaweza. Sasa kama anaweza, ya nini kumsubirisha mtu huyu kwenda alipo mpenzi wake Mr Chan’duu? Hakuna sababu. Kilichopo sasa ni kumuhadaa na kujifanya kumchangamsha, akifika ndani tu atamvizia na kumnyonga. Wazo hili lilikuwa muafaka. Akaona sasa kilichopo hapa ni kurudi Guantanamo na kwenda kutekeleza kitendo

    Akamuita muhudu na kumuagizia bia mbili za takeaway

    Alipomaliza akamuamrisha Sofi waondoke kwenda nyumbani

    Pamoja na kwamba Sofi alikuwa hajamaliza kula lakini hicho ndicho kitu ambacho alikuwa anakihitaji. Hakuna kingine zaidi ya kurudi nyumbani na kwenda kumvizia mtu huyu na kumuua. Lakini pamoja na kuhitaji kurudi Guantanamo kwa udi na uvumba kuna kitu kilikuwa kinamkwaza.

    Ni vipi anaweza kumuu mtu aliyeshababi mara mia kuliko yeye? Huu ni mtihani. Atatumia njia gani? Akajiuliza. Hapo akapata wazo. Kipindi akiwaza hivyo walikuwa wameshakata mitaa miwili na sasa walikuwa mtaa uliokuwa na watu wengi na maduka pia

    ‘Babii naomba hela nikanunue panadol mana kichwa kinaniuma sana’ akaomba

    ‘Twende nikakununulie’ Kj akaweka ngumu

    Suala hili katika hali ya hasira Sofi akaliangulia kicheko

    ‘Najua unadhani kwamba nitakimbia ndio maana kila hatua ninayopiga na wewe uko ubavuni, lakini hapa nitakimbilia wapi? Nikikimbia kisha ukiniitia kelele za mwizi si nitakwisha? Au una lengo la kunifanya kama bwana wangu ulivyomfanya?’ akauliza kwa hasira na sauti ya juu kidogo

    Kitu hiki kilimuudhi Kijo kiasi kama hakujizuia sekunde ya mwisho basi angetokwa na kibao kikali sana. Lakini kilichomzuia ni kule kuona kwamba Sofi ameshakasirika na anaanza kupayuka. Hapa akileta ukali tu ataharibu kila kitu. Akatabasamu

    ‘Mh my, mbona unaniwazi ubaya? Si nimeshakwambia kuwa najuta kilichotokea? Na nitawezaje mimi kukudhuru? Mbona unanionea!’ akauliza kwa sauti ya upole huku moyoni akisema ‘Una muda mchache tu wa kuishi, na wala kifo kipindi kinakuja kutojua kwamba kinakuja’

    Akatoa kiasi cha shilingi elfu tano na kumkabidhi. Hela hii ilikuwa nyingi kwa Sofi na ikampa mawazo mengine

    ‘Nenda kanunue basi twende hom mimi nina hamu na wewe’ akaongea kwa utani

    Sofi wala hakujibu kitu akapiga hatua kuelekea dukani akiifikiria elfu tano iliyoko mkononi mwake

    Wakati akiwa anakaribia katika duka akili yake ilikuwa mbali ikiwaza ni kipi anakwenda kufanya. Hapo akapata wazo kwamba anunue panado zipatazo hamsini kisha wakifika geto amuhadae K kuwa akaoge. Yeye si ana hamu ya kufanya mapenzi? Basi atamuhadaa kwa mabusu na kumuwekea maji ya kuoga kisha atamsubiri atakapokuwa chooni atazisaga panado hizo na kumtilia katika bia zake. Atakapo kunywa sasa, atasubiri afe, atabeba begi na kutoweka.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



     Elfu tano inatosha kabisa kunua panado hizo na usanii alionao ukichanganyisha na mapozi na anavyoyajua mahaba ni la zima K ataingia mkenge wa kwenda chooni na bia atakunywa. Yeye ndio mtoto wa kitanga bwana. Anayajua mahaba na anajua kuyatumia. Pozi za kike alizonazo ni lazima Kj atazimika. Lakini alipolifikiria kwa mapana akaona hili likawa si jambo sahihi. Hivi huo muda wa kununua dawa hamsini anao? Je muuza duka si atamuhoji kama anakwenda kufungua pharmas au anakwenda kujiua? Je K si anaweza kuziona?

    Akaona hilo si jambo muafaka. Lakufanya ni kununua wembe. Atamsubiri atakapokuwa amelala. Atamkata mishipa ya shingo

    Alipofika dukani akatoa hela na kumpa mwenye duka

    ‘Nikupe nini?’ akaulizwa

    ‘Naomba aa nipe sumu ya panya kama ipo’ akajikuta akiropoka bila hata kujua anachoongea

    ‘Ipo. Ya bei gani?’ muuza duka akauliza

    ‘Nipe ya elfu mbili na naomba na panado tatu za Kenya na maji chupa moja kubwa moto’ akajikuta akili yake ikifanya kazi haraka haraka

    ‘Mamdogo hizi dawa za panya za siku hizi unaombwa usiziweke karibu na watoto kwani anaweza kufikiria ni pipi maana kwanza hazina harufu pia zimekaa kama pipi halafu zinafanya kazi fasta’ muuza duka akaonya

    ‘Nashukuru kaka yangu mana zitaniwepesishia kazi yangu. Mana kama zingekuwa zinanuka Panya wangu angegutuka’ akasema kwa utani akimuambia mwenye duka moyoni akijipongeza kwa kuropoka kutaka sumu ya panya badala ya kiwembe au panadol

    Wakati Sofi akiwa dukani Kijogobwire alikuwa yuko bize kwenye simu akiwasiliana na Jorg akimuhimiza kwenda kambini kumchukua mtoto na kumleta Guantanamo muda huo. Wala hakuzingatia ni nini Sofi alinunua na hakuwa na haja ya kujua kwani alijua anamalizia manunuzi yake ya mwisho

    Watu wawili wanaoviziana kuuana wakaanza kujikongoja taratibu kurudi maskani

    Walipofika wakaingia ndani na kuwasalimia makamanda wawili waliokuwa wameshakolea bange na pombe

    Wakapilitiliza hadi geto kwao

    Walipofika cha kwanza Kj aliliangalia begi kama bado liko salama huku akijilaumu kutoka na kuliacha begi humo kwa kutegemea kikufuli

    Walipofika ndani Sofi akawa wa kwanza kusema ‘So babii! Tunaduu au?’ kwa sauti laini huku akimsogelea

    Kama kuna mtu duniani anapenda ngono basi K hana mpinzani. Kule kuguswa tu na kupigwa busu akajikuta akiwa amechanganyikiwa mashetani ya tamaa kumpanda. Akaanza kuvua nguo. Na Sofi naye wala hakumuangusha akaanza kuvua zake. Lakini alipomaliza akamuambia ‘Babii nenda kaoge kwanza mana we hujaoga tokea ulipooga asubuhi’ akashauri kwa sauti laini

    Mshipa wa ngono ulikuwa umeshamshika Kijo na alikuwa hasikii haambiwi hata jambo lake la kummaliza Sofi akalighairisha kwa muda. Bila kulazimishwa akaliafiki wazo hilo. Akatoka na kwenda chooni

    ‘Babii vipi nifungue bia moja nianze kunywa?’ akaomba

    ‘Poa’ akaitikia na kuwahi msalani

    Hiyo ilikuwa nafasi ambayo Sofi alikuwa anaitaka kwa hali zote

    Akatoka kidogo kumchungulia kama kweli jee ameshaingia msalani? Alipoona ndio akazitoa dawa za panya na kuziingiza kwenye pombe. Akaitingisha na kuiweka vizuri. Akakifunga kifungo vizuri na kuiweka pembeni. Akaitoa na chupa ya pili na kuifungua na kuanza kunywa taratibu

    Kj aliporudi tu

    ‘Babii jiweke sawa kwanza ili tukiingia iwe kama siku ile ya kwanza’ akasema Sofi na kumkabidhi chupa ya pombe aliyoichanganya na dawa

    Wakati alipokuwa ameshamkabidhi akageuka na kuivua nguo ya mwisho aliyokuwa nayo kisha naye akachukua chupa yake na kuanza kunywa huku moyo ukimdunda taratibu akiwa haamini kama zoezi lake litafanikiwa kwa rushwa ya ngono tu

    Kijogobwire ni kama vile alikuwa anaona anacheleweshewa muda wa kupata ile kitu roho yake inapenda. Chupa ya pombe akaipeleka mdomoni na kuigida kama vile ana hamu nayo ya karne. Kitendo hicho kilimkosha sana Sofi. Pale K alipoiweka chupa chini akamvamia na kuanza kumtomasa. Kilichoendelea hapo ni mshike mshike uliochukua masaa mawili ya watu kugandana. Wakimaliza na kuanza tena. Halafu tena. Kisha na tena

    Baada ya mizunguko ipatayo minne ya kugandana mwilini na kila mmoja akiwa hana hamu tena ya mwenziwe, Sofi akiwa anasikilizia sumu itafanya kazi muda gani ili apate kutoroka na begi, Kijo yeye alikuwa na mawazo mawili. La kwanza ni muda gani Sofi atalala ili apate kumkaba na kumuua na la pili ni saa ngapi mwanaume Jorg atafika na mtoto ili apate kumuhifadhi awe na hakika na kazi yake. Kitu kimoja ambacho hakukijua na kama angekijua basi muda huu angekuwa ameshabeba begi lake la pesa na kutokomea kizani ni kuwa, Jorg hatafika hapa kwa muda, na atakapofika basi atakuja na maaskari kwa ajili ya kukamatwa kwao. Kitu ambacho Kijo alikuwa hakijui ni kwamba, Jorg alifanikiwa kwenda kambini na kumchua mtoto lakini alipokuwa njiani kumleta hapa Guantanamo saa moja tu iliyopita, alipata ajali ya kuigonga bajaji iliyokuwa na abiria watatu ndani yake. Ajali hiyo haikuwa kubwa lakini mwenye bajaji alikuwa shap sana, akamuwahi Jorg na bahati mbaya kwa Jorg wakatokea askari wa pikipiki na kumkamata. Walipoikagua taxi yake kwa ndani wakakuta kuna mtoto wa kihindi akiwa mchafu na nguo za shule zilizokuwa hazijabadilishwa kama wiki hivi ikawa balaa zito juu yake.

    Sasa hivi Jorg yuko polisi na kashikashi aliyoipata ikizidi kidogo tu basi muda wowote huenda akaropoka na kuwaleta maaskari hapa Guantanamo

    Hilo lilikuwa ghaib, analijua mola na Jorg liliyemtokea, hapa ndani sasa watu wawili hawa walikuwa wakiviziana

    Sofi baada ya kumsikilizia kwa muda mrefu mtu wake na kuona sumu haifanyi kazi kwa kasi aitakayo, akaamua ajifanye kulala ili mtu wake naye alale na sumu impalie akiwa usingizini. Hilo likawa kosa kwani alipojifanya kulala na kukoroma tu, alihisi mtu akimkalia juu ghafla na kuanza kumbakaba kwa nguvu zake zote

    Sofi alikurupuka na kukuruka akitaka kuitoa kabari hiyo lakini wapi jitihada hazikufua dafu

    Juhudi zake zilipokwisha akajikuta akinyoooka taratibu kukubaliana na hali halisi

    Akakata rohoCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Japo kama sofi aliviziwa lakini haikuwa rahisi kama Kijo alivyodhani kwani mwanaume huyu alimaliza kazi hii akiwa mchovu na pumzi imekaba zaidi ya inavyotakiwa. Alipokuwa akipumua mara akijihisi kwamba hapumui kama kawaida au kama vile baada ya kufanya mazoezi. Akajikuta hapa pumzi zinamkaba kwa kasi na mara ghafla akaanza kuona jasho lilimvuja na mara akaanza kutapika matapishi ya damu

    Akaanza kukukuruka na kutaka kupiga kelele au kutafuta msaada lakini mwishowe nguvu zikaanza kumwishia taratibu na hatimaye akakata roho

    ………………….

    Kama Jorg atawaleta maaskari hilo ni suala moja. Kama muhindi atampata mwanawe leo hii hii hilo ni suala jingine. Lakini Dili tata lilikuwa Dili tata kweli na neno Tukigeukana.. Liliishika kwa umauti wa watu watatu waliokuwa katika dili la kumfanya mtu alale masikini na kuamka tajiri



    TAMATI

0 comments:

Post a Comment

Blog