Search This Blog

Sunday, 22 May 2022

KIKOMO - 4

 







    Simulizi : Kikomo

    Sehemu Ya Nne (4)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Habari zako dada?"



    "Nzuri" alijibu kwa sauti tamu.



    "Nilikuona leo mchana Mwanza Hoteli kama sikukosea".



    Alishangaa na kunyamaza. Bia yake ilikuwa nusu kwa hiyo nikamwita mwanamke wa baa alete chupa mbili moja yangu na moja ya dada.



    "Mimi hapana, nitaondoka sasa hivi", alijibu huku akiniangalia kwa chati.



    Sikutaka kujirahisi kwa kusisitiza.



    "Oke lete moja. Umefika hapa saa ngapi?"



    "Sasa hivi".



    "Na nini?"



    "Ninaendesha gari".



    Nilipomwangalia vizuri ndipo nikakumbuka kwamba nilimuona Mwanza siku ya ajali ya boti itokayo Ukerewe, ambamo alikuwemo Makungu Majula. Dada huyu ni peke yake aliyepona".



    "Unaelekea wapi?"



    "Nimekuja kumuona rafiki yangu mmoja hapa".



    "Kwani unakaa wapi?"



    "Mwanza".



    "Mimi naitwa Mark, wewe unaitwa nani?"



    "Tausi".



    "Samahani, sijui ndiye wewe uliyepona kwenye ile ajali ya boti iliyokuwa ikitoka Ukerewe kwenda Mwanza, maana sura iliyokuwa kwenye gazeti inafanana sana na yako?"



    Alitabasamu.



    "Ni mimi. Magazeti haya yanaleta shida, kila mtu akiniona anasema msichana huyu ana bahati, watu wote walikufa kapona yeye tu".



    "Hawajui Mungu hapendi kuua viumbe wazuri kama wewe. Ungekufa nani angekuwa anazungumza na mimi sasa?"



    "Samahani naenda Farmera Bar, ndipo rafiki yangu anakonisubiri saa moja na nusu.



    Nilifikiri kidogo kama ningemwacha aende au sivyo.



    "Naweza kwenda nawe? Ningependa kufika huko lakini nitarudi hapa saa mbili.



    NIlilipa pombe tukaongozana nje.



    "Gari hilo hapo."



    Alifungua mlango wa dereva halafu akanifungulia mlango wa mbele wa abiria. Nikaingia ndani kwa chati nikaangalia nyuma hamkuwa na mtu wala kitu chochote. Akatia gari moto tukaondoka na kuingia barabara kuu. Kisha nikasikia sauti kwa nyuma.



    "Kaa hivyo hivyo usijisogeze hata inchi moja, ukijisogeza tu umekufa. Tausi moja kwa moja mpaka ulikoambiwa. Mara hii atarukoma ng'ombe huyu".

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kijasho kilinitoka sikuwa na la kufanya. Nilipotaka kukaa vizuri tu, nikatwangwa na kitu fahamu zikaniruka. Nilisikia kwa mbali watu wakizungumza. Nikajaribu kuinua kichwa lakini sikuweza. Kilikuwa kizito sana.



    "Mmwagie maji apate fahamu. Nataka kuzungumza naye".



    Nilimwagiwa maji ya baridi sana. Haya yalinipa nguvu nikainua kichwa na kufunua macho. Mikono na miguu yangu ilikuwa imefungwa kwenye kitu imara sana. Ndani ya hiki chumba mlikuwa na watu watano. Nilimtambua Pweke mara moja maana nilikuwa nimekwisha kumuona Songwa Club. Tausi alikuwepo pamoja na watu wengine watatu, ambao wote walikuwa wameshika bastola zao tayari tayari. Chumba nilichokuwemo kilikuwa kifinyu sana. Kilikuwa na mlango mdogo wa kuweza kuingia mtu mmoja mmoja. Kilikuwa na madirisha mawili madogo juu kabisa ya dari na hewa ilikuwa ya baridi na safi kwa vile chumba kilikuwa kinatumia mashine ya kufanya hewa iwe baridi.



    "Willy Gamba au Mark Buhulula hujambo?" Pweke alisalimu kwa kebehi.



    "Asante sana Pweke ama nani sijui".



    "Usitake kujua maana hata ukijua ni kazi bure, mwisho wako ni leo".



    "Mwisho wangu unaweza kuwa leo, lakini serikali yangu haina mwisho. Nitakufa leo, kesho atatokea tena mtu mwingine kuliko mimi na ataendelea na pale nilipoishia. Umeua watu wengi mbona bado tunaendelea tukianzia pale walipoishia walipoishia.



    "Sawa, lakini kicho chako kitakuwa tisho kubwa kwa serikali. Itabidi itulie kidogo kabla haijachukua hatua nyingine na wakati huo tutafanya jitihada ya kunyakua kiasi cha kutosha na kutulia".



    "Usijidanganye. Mikifa mimi utakuwa ndiyo umeweka kiberiti kwenye petroli".



    "Umeua watu wangu wengi sana, kwa hivi itabidi upate mateso ya peke yake. Lazima upate uchungu, ujutie nafsi yako - kwanini umekuwa unatufuatafuata. Hii shughuli toka nianze sijatiwa msukosuko kama huu, kwa hivi hasira yangu imepanda mpaka imefurika na lazima ulipe watu wangu wote uliowaua hasa Ole.



    "Na wewe siku ya kukupata utalipa mauaji ya wote uliowaua toka Jack Mbwile mpaka utakayekuwa umemuua wakati huo".



    "Unatania, mambo yangu yameshatengamaa. Baada ya usiku huu wa leo naweza kuondoka na kuishi mahali pengine popote ulimwenguni bila ya taabu. Mali niliyonayo hata wajukuu zangu wanaweza kula bila ya kufanya kazi. Usiku huu wakati wewe umeshaaga dunia sisi tutakuwa tunagawana almasi yenye thamani ambayo serikali itapata pigo kubwa sana, pigo ambalo haitasau, pigo ambalo litafanya hata Kampuni ya Almasi ifungwe. Ni wewe tu ambaye kidogo utuharibie.



    "Saa zimekaribia, fanya twende. Nafikiri wengine watakuwa wameisha wasili", Tausi alisema.



    "Na wewe bibi umejiunga ndani ya kundi hili?" niliuliza.



    "Hujui ni miaka ya wanawake?"



    "Miaka ya wanawake katika kuendeleza nchi au kubomoa?"



    "Wako wengine wanajenga wengine wanabomoa. Mimi ninajenga peke yangu.



    "Lazima ujue kuwa utalipa kifo cha rafiki yangu Makungu Majula pamoja na wananchi wote waliokuwa ndani ya ile boti. ni aibu kuona msichana mzuri kama wewe unashiriki kikamilifu katika uovu na watu washenzi na vichaa kama huyu Pweke na wenzake. Huyu si mtu tena ni mnyama.



    "Nyamaza ng'ombe".



    Pweke aliniwasha kofi la usoni na Tausi akanirukia na kunitia makucha uso mzima na damu ikaanza kububujika.



    "Ukome kama ulivyokopa kunyonya titi la mama yako", Tausi alitukana.



    "Basi na mimi niachie nnimuonyeshe uchungu wa rafiki zangu aliowaua kabla hatujamuua", mmoja wa hao vikaragosi wa Pweke aliomba.



    "Haya chukueni nafasi zenu na kila mtu mmoja amalize uchungu wake. Msimuue kabisa niachieni mimi ndiye nitammalizia".



    Walijiweka sawa na kuanza kunitwanga. Damu ilikuwa inabubujika machoni kutokana na makucha aliyonitia Tausi. Sikuwa naweza hata kuona. Nilikuwa nimefungwa kistadi kiasi cha kwamba nisingeweza kufanya chochote. Nilipigwa makonde ya mashavuni, kifua na tumboni, mwingine aliruka na kunitwanga teke la mbavuni. Hasira zilinipanda kiasi ambacho sijawahi. Niliwachukia kiasi cha ajabu.



    "Mtalipa, hakika mtalipa na mtalipa ghali sana", nilipiga kelele kwa uchungu mwingi.



    "Ha ha ha Willy Gamba mpelelezi mashuhuri analia kama mwanamke. Ha ha ha ha! Niachieni sasa mimi nimmalize", Pweke alisema kwa dharau.



    "Lakini mzee alisema anataka kumuona kabla hatujammaliza kabisa", Tausi alisema.



    "Atafika hapa si muda mrefu lakini hata hivyo alimtaka akiwa amekufa au yu hai kwa hiyo mimi ninakata shauri nipeleke maiti yake."



    "Ngoja kwanza Pweke na mimi nimfaidi kabla hatujammaliza", Taus alisema.



    Tausi alinirukia na kunitia makucha kifuani na tumboni na kuraruaraua shati langu nililokuwa nimevaa. Uchungu niliopata ni Mungu na mimi mwenyewe ndio tunaojua. Nguvu ziliniishia, nilikuwa siwezi hata kusema na nilijua mwisho wangu umefika.  CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Damu zilinitoka kila mahali. Nikaanza kupoteza fahamu. Ghafla taa zikazimika, maana nilikuwa naweza kuona wekundu lakini ghafla kukawa giza. Mashine ya kufanya hewa baridi ikanyamaza. Kufumba na kufumbua nikatumia nguvu zangu zote zilizobaki. nikajitupa upande na kuanguka chini pamoja na kiti nilichokuwa nimefungiwa.



    "Tumeingiliwa. Muue upesi, ng'ombe nyinyi. Hakikisheni mnamuua sitaki kusikia yu hai", nilimsikia Pweke anapiga kelele kwa woga. Nilisikia kwa kutoka juu dirishani risasi zinamiminika halafu nikapoteza fahamu.





    Nilipozinduka nikajikuta kwenye chumba kidogo, nikiwa nimelazwa kitandani na huku nimefungwa bandeji kila mahali nilipokuwa nimeumia na nilipoinua macho karibu yangu alikuwa ameketi msichana mrembo sana huku akitabasamu nikashangaa.



    "Unajisikiaje sasa?" Aliniuliza.



    Nikatabasamu.



    "Mbele ya mtoto mzuri kama wewe nitashindwaje kujisikia vizuri".



    "Watu wa hali yenu ni watu wa ajabu sana".



    "Kwanini?".



    "Hata hushangai umekujaje hapa?".



    "Ili mradi nimetibiwa na msichana mrembo kama wewe, na unaniganga na hakuna watu wenye sura zilizokunjana wakiwa wameshikiria bastola, najua niko kwenye mikono mizuri".



    "Ni kweli".



    Nilijaribu kuinuka.



    "Daktari amesema upumzike kwa muda mpaka upate nguvu".



    "Tayari nina nguvu, sasa ni saa ngapi?"



    "Saa saba unusu usiku".



    Nikatambua kuwa nilikuwa nimezirai kwa muda wa masaa matano hivi na nikataka kujua nini kilikuwa kimenitokea muda wote huo ili niweze kujua nini cha kufanya maana hata hapa nilipokuwa sikujua ni wapi na huyu msichana sikujua ni nani.



    "Wewe ni nani na hapa ni wapi?"



    "Mimi naitwa Amanda Mwakasege, na hapa ni nyumbani kwa rafiki yangu, Songwe Madukani.



    "Nani alinileta hapa?"



    "Mimi na Patrick".



    Moyo wangu ulishtuka kwa jina hilo.



    "Yuko wapi?"



    "Amerudi Maganzo na atarudi wakati wowote".



    "Kwa hiyo nyinyi ndiyo mlioniokoa kutoka mikononi mwa Pweke?"



    Bila shaka".



    Hii ilinishangaza sana.



    "Nafikiri uko tayari kunieleza juu yako mwenyewe na jinsi gani unahusika katika kesi hii, maana wewe hukuajiriwa pamoja na sisi. Vile vile jinsi gani mlijua nilipokuwa na vile mlivyoniokoa".



    "Nitakueleza kwa ufupi ili uweze kujua mpaka sasa pilikapilika yako hii imefikia wapi".



    "Asante, endelea".



    "Mimi naitwa Amanda Mwakasege, kama nilivyokwisha kukueleza. Ni Mwandishi mahsusi wa Meneja wa Kampuni ya Mwadui. Utashangaa nimejiingizaje katika jambo hili au sivyo?".



    "Nina mshangao mkubwa sana, maana ukiwa mwandisi halafu ujiingize kwenye jambo la hatari namna hii haieleweki."



    "Kweli haieleweki. Mimi nilikuwa na mchumba wangu akiitwa Inspekta Joel Zonga, nafikiri uliwahi kumsikia?|



    "Nilikuwa nimesikia habari zake ambazo zilitokana na kifo chake. Alipata ajali ya ndege iliyokuwa mali ya Kampuni Mwadui alipokuwa akisafiri kwenda Mwanza kikazi. Mpaka leo chanzo cha ajali hiyo hakikujulikana maana ndege ilipasuka vibaya mno. Polisi walikisia kuwa mlikuwa na bomu lililotegwa lakini hawakuweza kuendeleza upelelezi wao mbali".



    "Ndivyo ilivyokuwa."

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Pole sana".



    "Siku moja Joel alikuja nyumbani kwangu akiwa na mawazo mengi sana. Nilitengeneza chakula lakini hakuweza kula vizuri. nikajua alikuwa na kitu kilichokuwa kinamsumbua nilimdadisi sana mwishowe akanieleza. Alinieleza ya kwamba alikuwa hapendezewi na jinsi mambo yalivyokuwa yakienda hapo Mwadui na kwamba alikuwa ameamua kufanya uchunguzi madhubuti.



    "Alinieleza kuwa alikuwa amefanya uchunguzi kiasi na kuona ya kwamba kulikuwa na mpango wa hali ya juu sana wa kuiba almasi toka Mwadui! Ila alisema kilichokuwa kinamkera ni kwamba angeweza kuwa hatarini.



    "Alieleza ni nini kilichomfanya afikiri hivyo?"



    "Alikuja kunieleza baadaye. Aliendelea na uchunguzi wake na hatukulizungumzia jambo hili tena. Baada ya miezi miwili hivi siku moja alikuja akiwa na hali isiyo yake ya kawaida. Nilipomuuliza alinieleza ya kwamba mambo aliyokuwa anafikiria ni kweli na sasa alikuwa hatarini.



    Alinieleza kwamba alikuwa amekata shauri kunieleza jinsi mambo yalivyokuwa kusudi ikiwa jambo lolote likimpata siku moja anaweza akaja mtu mwenye kuweza kuendeleza upelelezi huu na habari hizi zingemsaidia sana. Nilimwambia asiseme hivyo, na siku hiyo alilia sana.



    "Alieleza nini?"



    Alinieleza kuwa maafisa wengi wa polisi wa chini wa hapo Mwadui walikuwa wamehongwa na kundi la majambazi ambalo lilikuwa linaendelea na kuendesha wizi wa hali ya juu wa almasi toka Mwadui na ndiyo sababu hali ya uchumi utokanao na machimbo hayo ya almasi ulizidi kwenda chini siku hata siku.



    "Alisema kuwa hili kundi lilikuwa limepachika watu wake kila idara na kila sehemu zinazohusika na almasi. Na hawa watu ndio walikuwa wakitorosha almasi kidogo kidogo na kwa sababu polisi waliokuwa wanahusika wote wamehongwa na walikuwa wanawajua basi ilikuwa rahisi sana kwao kutorosha almasi.



    "Alinieleza kuwa katika miezi hii miwili aliweza kukamata watu kama kumi ana kwa ana na almasi mkononi lakini alipoenda kupiga ripoti kwa maofisa wa juu waliweza kutaka hata kumgeuzia yeye kuwa ndiye mwizi. Hata akanieleza kuwa siku moja wamewahi kuficha almasi nyumbani kwake halafu kukafanywa uchunguzi zikutwe kwake lakini yeye alinong'onezwa kabla na rafiki yake mmoja na walipofika hawakukuta kitu.



    "Kutokana na uchunguzi wake alikuwa amegundua kuwa kwa nje kulikuwa na mtu aitwaye Pweke, ndiye alikuwa mkubwa wa kundi na alikuwa mfanyabiashara wa hapo Maganzo. Kwa ndani mtu aliyekuwa akiongoza kundi Inspekta Mwandamizi Khamis Omari. Huyu Khamis ndiye aliyekuwa anapokea habari na ndiye aliyekuwa kiungo kati ya kundi la nje na la ndani. Vile vile kwa wafanyakazi wa idara zingine".



    "Kwanini hakupeleka habari hizi kwa Mkuu wa Polisi wa Mwadui au Mkuu wa usalama?"



    "Alisema alijaribu kupeleka kwa Mkuu wa Polisi, lakini alipuuzwa na kuelezwa kwamba alikuwa anaanzisha majungu jambo ambalo serikali haipendi hasa jeshini na kwa hivi angeweza kuchukuliwa hatua. Alipoona hivi akaonelea aendelee kufanya uchunguzi wake yeye mwenyewe sasa. Siku aliyokuwa amekuja kwangu na huzuni kunieleza mambo haya ndiyo siku aliyokuwa amekuja kwangu kunieleza kuwa amepata kitisho kutoka kwa mtu aliyekuwa akiitwa Elungata akisema asiingilie mipango yake la sivyo maisha yake yangekuwa mafupi sana".



    Jina la Elungata mara moja nilikumbuka kwani marehamu Matayo Buluba alikuwa ameniletea barua kutoka kwa marehemu Jack Mbwile na hiyo barua ilikuwa na neno moja tu 'Elungata' Sasa nilianza kuona mwanga zaidi.



    "Aliweza kuchunguza na kujua huyu Elungata alikuwa nani?".



    "La hasha. Baada tena siku moja kwenye Mkahawa wa polisi hapo Mwadui alinieleza kuwa alikuwa amegundua tu ya kwamba Pweke siyo mkubwa kabisa wa kundi ila mkubwa alikuwa Elungata, lakini ajabu huyu Elungata hata hakuweza kupata fununu yake".



    Wiki tatu zilizopita akaja siku moja kuniaga kuwa alikuwa anaenda Mwanza kuonana na Mkuu wa Polisi wa Mwanza ampe habari hizi kwa maana sisi tulikuwa tumekata shauri ya kuoana baada ya mwezi mmoja toka siku hiyo kwa hiyo asingekuwa na nafasi ya kuendelea na uchunguzi. Na siku hiyo alipoondoka ndiyo waliyomtega bomu katika ndege. Akafariki".



    Alianza kulia. Nilimvuta na kuanza kumbembeleza.



    "Basi, basi kifo ni mapenzi ya Mungu. Ni jambo la kusikitisha sana lakini kulizuia hatuwezi. Yeye alipangiwa na Mungu mwisho wake uwe huo. Ulikuwa mwisho wa fahari maana alikufa kwa sababu ya kupenda nchi yake na kwa kuitumikia vizuri. Maadui wa maendeleo yetu wamemuua. Kwa hilo linalotupasa mimi na wewe ni kuwafutilia mbali hawa maadui wa nchi yetu".



    "Asante Willy lakini ni vigumu kusahau na vile vile ndiyo sababu nimejitoa mhanga wa kufa na kupona kusudi watu waliomuua mpenzi wangu Joel na wao watiwe nguvuni".



    "Joel alikueleza haya yote kwa sababu alijua atakuwa hatarini na alifanya vizuri. Je umetimiza wajibu wako kwa mzigo aliyekuachia?".



    "Nafikiri leo hii na dakika hii nimetimiza wajibu. Hata hivyo baada ya mazishi na matanga sikukaa bure. Uchungu niliokuwa nao ulifanya nami nianze uchunguzi wangu. Inspekta Mwandamizi Khasimu Omari ambaye ndiye bila shaka aliyepanga kuuawa kwa mpenzi wangu Joel alikuwa akitaka mapenzi nami siku nyingi. Niliporudi tu kazini baada ya matanga alianza kunifuatafuata".



    ..."Alinieleza kuwa ili niweze kusau mapema kifo cha ghafla cha mpenzi wangu ilinibidi nipate mtu wa kunifariji kwa sababu nilikuwa najua habari zake, wazo lilinijia kuwa ningeweza kupata habari za kunisaidia kuchunguza kifo cha mpenzi wangu joel".



    "Kwa hiyo ukamkubali!"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Nilimkubalia kwenye mdomo tu si rohoni".



    "Sawa".



    "Siku moja nilianza kwa kumsifu juu ya vile alivyo tajiri kuliko polisi wengine, jinsi alivyokuwa na akili kuliko polisi wengine na kadhalika. Nilimweleza kuwa ningejua kwamba yeye ana pesa hivyo hata nisingejisumbua kupoteza muda wangu na Joel. Nikamweleza kuwa ni bahati nzuri upande mwingine kwamba Joel amekufa. Hii ilimfurahisha sana akaanza kujitapa akanieleza kuwa yeye alikuwa tajiri sana na utajiri wake usingeweza kupungua kwani alikuwa ameishashika Mwadui nzima mkononi mwake."



    "Siku hiyo nilimfanyia mapenzi ya kila aina mpaka akanieleza juu ya siri zake. Akanieleza baada ya muda si mrefu angeacha kazi na kunioa halafu tungeenda kuishi nchi za nje. Aliniambia ana almasi chungu nzima. Nikamkebehi ya kwamba mbona nasikia kwamba Pweke ana hela kuliko yeye. Akacheka na kusema bila ya yeye Pweke si kitu".



    "Hakugutuka kuwa unamfahamuje Pweke?".



    "Asingeweza, maana Maganzo nzima wanamfahamu Pweke. Ana pesa chungu mbovu. Wakati wote huu nikawa natafuta njia ya kujua mengi lakini sikuweza kuwa na bahati. Waswahili husema mvumilivu hula mbivu, kwa hiyo mimi nikaendelea kumganda nikisubiri bahati yangu huku nikimlaghai kwa mapenzi kwa kweli ya Mungu mengi jana ndiyo siku yenyewe.



    "Jana alikuja nyumbani kwangu huku jasho likimtoka. Nikatengeneza chakula kama kawaida, lakini hakuweza kula na alionekana na wazo linalomsumbua au tuseme mawazo yalikuwa mengi sana. Nilimuuliza nini kilikuwa kinamsumbua. Hakutaka kunieleza. Nikazidi kumbembeleza. Nikambusu, nikamweleza kuwa matatizo yake ni yangu na mimi kwa vile nilikuwa nimekata shauri la kuolewa sikuona kwa nini anifiche jambo lolote hata kama ni kuua mtu.



    "Mwisho akanieleza kuwa mpelelezi mmoja maarufu wa serikali kwa jina la Willy Gamba alikuwa ameanza kuleta matatizo. Nikamwambia mtu mmoja tu si kitu, hatamudu kufanya lolote, kwa hiyo asijali hata kidogo. Basi akafurahi akanishika akanibusu.



    "Akanieleza kwamba ameonelea lazima achukue livu kesho yake maana tungeweza kuondoka ghafla kwa muda. Nilimwambia kwamba isingekuwa taabu. Moyoni nikajua nafsi yangu imefika ya kumtafuta huyu Willy Gamba ili nimweleze yote niyajuayo ili kwamba nitakuwa nimemlipizia kisasi mpenzi wangu Joel."



    "Ama kweli umekuwa kiumbe wa ajabu! Umeweza kufanya yote haya kwa ajili ya mpenzi wako Joel basi".



    "Nakwambia, watu hawajui. mwanamke akipenda kitu huvumilia sana usituone hivi!"



    "Kweli nami nimeona kitu kiitwacho mapenzi ya kweli maana mtu kafa na bado anapendwa tu".



    "Basi leo asubuhi nikaenda ofisini. Nikachukua livu, nikampigia simu sikumpata kwa simu ofisini wala nyumbani. Nikakata shauri kwenda nyumbani kwake sikumkuta lakini mimi nina ufunguo mwingine wa nyumba yake nikaingia ndani, nikaenda chumba cha kulala nikachukua bia, nikajilaza kitandani nikinywa huku mawazo yakinitembeatembea.



    "Mnamo saa sita hivi nikasikia watu wanacheka ukumbini nikasikia mwingine akisema Willy kafa kifo cha kijinga sana cha kugongwa na gari moshi. Khasimu akajibu, ndiyo, sawa hiyo, hakuna hata cha kuuliza. Basi roho yangu ikafa kabisa niliposikia hivyo. Nikajua matumaini yangu yamekwisha".



    "Naona nina maisha marefu," nilisema kwa furaha.



    "kweli una maisha marefu. Khasimu aliponikuta chumbani akaja akanibusu. Nikamuonyesha karatasi zangu za livu. Akaniambia kwamba sasa hamna wasiwasi, tungepanga mambo yetu taratibu. Wakati bado tumekaa, simu ikalia. Alienda kuzungumza na nikasikia akisema, George, basi wamalizie mbali mbali na yeye halafu hana wasiwasi Ole yuko Mwanza, atamaliza tatizo hilo halafu akarudi".



    "Na katika watu wanaovumilia wewe nambari moja!" Nilimpongeza, "Wanawake kwa kawaida wangekuwa wameisha ropoka".



    "Kila nikimfikiria Joel, roho yangu inakuwa jasiri sana. Mnamo saa kumi na moja na nusu hivi simu ikalia. Khassimu alikuwa amelala akaamka na kwenda kuijibu. Nikasikia akisema kwa hasira, nini? Willy yuko hai? Willy au jina lake? Nani, Ole? Ole kafa! lo, mambo yameharibika. Washenzi hao Pweke hakikisha Willy akiingia Maganzo Bar, ndiyo hoteli yake, lazima auawe mara moja. Nani kakupa habari? Basi lazima atafikia Maswa Bar, ndiyo hoteli yake kama atakuwa kaondoka kule saa kumi na moja, saa moja hivi atakuwa Maganzo. Mtume Tausi saa moja pamoja na kundi, yeye ni mbovu sana kwa wanawake. Lazima akimuona tu Tausi hawezi kumwachia. Mpeleke kwenye banda mkiweza kumkamata, mwuweni huko huko. Mimi nitazungumza na mzee najua atakasilika sana. Tuonane kwenye chumba chetu Bantu. Wengine wote watafika saa nne usiku kwaherini!"



    "Kisha akaja akaniambia, mpenzi fungasha nguo zako chache na zangu mimi nitarudi kwenye saa tano au sita hivi nina shughuli.



    "Nikamwambia, hamna taabu. Alipoondoka tu na mimi nikaanza kutafuta njia gani ya kuwahi kufika Maganzo kabla ya saa moja niweze kukupa tahadhari. Nilitafuta gari mpaka kwenye saa moja ndipo nilipopata. Kufika Maganzo na kuingia Maswa Bar saa moja na nusu, na nilipoangaza angaza nikaona hakuna dalili ya mtu kama wewe. Nikajua tayari wamekuwahi. Nikajua wamekupeleka kwenye banda. Na banda mimi nililijua, nilishapelekwa na Khasimu, lakini kukufuata peke yangu ilikuwa haiwezekani. Nikatoka nje ya baa, nikaanza kulia. Bado machozi yananitoka nikaona taksi inasimama na anatoka mtu na mfuko. Moyo ukanieleza ndiye wewe, nikamkimbilia huyu mtu. Bila ya hata kuogopa nikamuuliza kama yeye ni Willy Gamba? Akashituka na kuniuliza, 'kwanini?' Nikamwambia wanakutafuta watakuua. Wanajua utakuja hapa bila ya shaka.



    Alinivuta kando, kisha akanieleza kuwa yeye anaitwa Patrick na ni rafiki yake na Willy Gamba. amekuja kukutana na Willy hapo. Ndipo nikamweleza mipango yao yote. Akafungua mfuko wake, akatoa bastola mbili. Akazijaza risasi akaniambia nimuonyeshe hilo 'banda' lilipo. Basi nikampeleka mpaka kwenye banda. Hii nyumba inayoitwa 'banda' imejengwa mbali kidogo na nyumba zingine. Khasimu alisema hutumika kama kuna sherehe fulani ya vinywaji. Basi nikamleta na kumuonyesha nyumba akanipa mfuko na tukaanza kuinyemelea nyumba akiwa na bastola mbili tayari.



    "Upande wa mlango wa kuingilia, tukamuona mtu na bunduki, Patrick akamnyemelea akampiga konde la shingoni, akazirai bila ya kutoa sauti. Mwingine alikuwa akiangaza upande mwingine, Patrick akamwahi na risasi lakini bunduki haikupiga kelele. Ndipo katika kusikiliza akasikia sauti inatokea kwenye chumba walichokuwa wanakutesa. Alipoangaza akaona dirisha juu kabisa. Akapanda juu kama nyani. Alipofika juu alipiga waya wa umeme na wakati huo huo alikuwa ameishawaona walivyokaa na wewe uliko kwa hiyo ilikuwa rahisi kuwawahi hao wenye silaha. Anasema usingejitupa na kiti wangeweza kukupata na risasi. Wale watatu wenye bastola wote amewaua. Pweke na Tausi wamekimbia. Basi Patrick akaniita, akakufungua, tukakubeba na kukuweka kwenye gari la Tausi. Patric akafungua boneti akaliwashia huko hadi tukafika hapa.



    "Hiki ni chumba cha rafiki yangu, anafanya kazi stesheni ya reli hapa Songwa lakini yuko likizo. Tulienda kumtafuta daktari akaja akakutibu na akasema hukuvunjika chochote ila tu umepoteza damu nyingi. Akaomba upumzike mpaka kesho asubuhi utapata nafuu. Hivi ndivyo ambavyo tumeweza kuonana. Ni hadithi ndefu au sivyo?"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "lO, ama kweli ni ajabu na kweli. Sina budi kukushukuru sana"



    "La hasha! usinishukuru. Nifanyalo ni wajibu wangu ili kulipiza kisasi cha Mpenzi wangu Joel!"



    "Hakukueleza Patric yuko wapi?"



    "Amewafuata Bantu ambako walisema wataonana"



    "Ameenda pekee yake? Watamuua ni watu wabaya sana"



    "Hapana, ameenda na mdogo wa yule daktari maana wao pia wanakisasi na Pweke maana alikataa kufanya mapenzi nao na huyu kijana ni Polisi wa relwe"



    "Bado haitoshi lazima niwafuate"



    "Una silaha? Silaha huna tena bado una maumivu. Wily usiende Patric na huyo kijana Mungu atawasaidia na watamudu"



    "Silaha nitapata usijali lazima niwafuate.



    Nikasikia sauti nje ya mlango wa chumba.



    "Huna haja ya kuwafuata"



    Jasho likatutoka wote.





    Mlango ulifunguliwa wakati mimi nikiwa tayari kwa lolote litakalotokea na kwa mshangao wangu Patrick aliingia ndani. Niliruka hapo nilipokuwa.



    "Patrick!".



    "Willy".



    Tukakumbatiana.



    "Na nyinyi nanyi! Mnapendana hivyo?" Amanda alisema.



    "Usijali," nilimjibu.



    "Yule mdogo wa daktari yuko wapi?" Amanda aliuliza kwa woga.



    "Yupo atakuja," Patrick alijibu.



    "Patrick nipe habari kwa ufupi maana nimekuwa nje ya hii shughuli kwa masaa kwa hiyo niko nyuma sana na habari."



    "Nafikiri Amanda kishakueleza jinsi tulivyokupata."



    "Ndiyo, kanieleza."



    "Huko Dar es Salaam nilipata habari kama saa kumi na moja unusu hivi Chifu alinieleza kwa ufupi juu ya habari zote na maendeleo ya shughuli hii. Mambo mengine yote alimweleza Kamishna Mkuu wa Polisi ashughulikie kama vile kuwatia nguvuni hao majambazi uliokuwa unawakisia. Mimi aliniambia niwe kiwanja cha ndege saa kumi na mbili kamili tayari kwa kuondoka.



    "Wakati nikiwa kiwanja cha ndege nikapata habari toka kwa Chifu kuwa Kamishna Mkuu wa Polisi ndugu Oswald Mengi kapata safari ya ghafla. Maana baada ya kuongea na Chifu alipata habari kuwa mkewe aliyekuwa anasafiri toka Arusha alikuwa amepata ajali kati ya Arusha na Moshi na inasemekana kuwa huenda amekufa kwa jinsi hii ameruhusiwa kwenda kumuona mkewe kwa hiyo sasa mambo yote yako mikononi mwa Chifu na Mkurugenzi wa Upelelezi, Mkuu wa Polisi ameitwa arudi haraka maana jambo hili limefikia hatua ya juu haliwezi kushughulikiwa na maafisa wa chini wa polisi.



    "Baada ya kupata habari hizi nilipanda ndege ya jeshi na mnamo saa moja unusu nilikuwa Maganzo na ndipo nikaonana na Amanda. Mambo mengine yote nafikiri kesha kueleza."



    "Nipe habari za Bantu Bar".



    "Baada ya kukuleta hapa nilionelea niwafuate kwa kufuatana na habari nilizopewa na Amanda. Huyo mdogo wake daktari akasema twende naye nami nikaona bora. Tulipofika hapo tulipeleleza uwezekano wa kuwepo huo mkutano lakini hakukuwa na dalili. Tulingoja sana lakini hatukuonana dalili yoyote. Tukajua kwamba lazima kulikuwa na mabadiliko ya mipango."



    "Mlingoja mpaka saa ngapi?".



    "Mpaka saa tano unusu hivi. Mimi nilionelea nirudi nikamuacha Wilfed Mbogo ambaye ndiye huyo mdogo wake daktari aendelee na uchunguzi na apatapo habari yoyote aje kutueleza kabla sijaja nikaonelea nimpigie simu Chifu, nimweleze tumefikia wapi na mambo yalivyo. Nilipiga nyumbani kwake nikapata habari kuwa amerudi ofisini. Hii ilinishangaza. Nikampigia ofisini.



    "Nilipompata nikamweleza mambo yalivyo mpaka dakika hii. Kisha nikamuuliza kwanini alikuwa ofisini mpaka dakika hiyo. Akanieleza kuwa alikuwa amepata habari zingine za kusikitisha toka Mwadui leo jioni. Habari hizi ni kuwa umetokea wizi wa ajabu, maana almasi zote zilizokuwa tayari kusafirishwa kwenda kwenye masoko yake zimeibiwa!"



    "Zimeibiwa? Saa ngapi?"



    "Anasema ni kati ya saa kumi na saa mbili usiku huu!"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Kwa hiyo inaonekana majambazi hawa wameamua kuchukua kwa mara ya mwisho na kukimbia."



    "Hata mimi nafikiri hivyo hivyo."



    "Nafikiri ndiyo sababu Khasimu alinieleza kwamba nifungashe vitu." Amanda alinieleza.



    "Nadhani walikuwa wamefanya mpango wa kuziiba hizo almas halafu watoroke nchi za nje."



    "Hiyo ni kweli kabisa na vile vile Chifu kanieleza kuwa wale watu uliompigia ripoti watiwe ndani chini ya usalama anashangaa kupata habari kuwa wote hawaonekani na wala haijulikani wako wapi. Mbinu za kila aina zimetumiwa na idara ya upelelezi, Polisi lakini hawaonekani kabisa".



    "Ahaa. Sasa naanza kupata mwanga mkubwa. Hii ina maana kuwa wote wameondoka kuja Maganzo kugawana hizi almasi halafu kila mtu aangalie usalama wake, baada ya kuona karibu watashikwa. Hii ikiwa ni kweli lazima wataonana mahali fulani hapa mjini au wameshaonana au wanaonana saa hizi".



    "Vile vile kumbukeni kuwa Khasimu alisema kwenye simu anamtegemea Mzee leo saa nne." Amanda alitukumbusha.



    "Kwa hiyo hii inazidi kudhihirisha kubuni kwetu. Na kama hata Mzee wao yuko hapa hapa bila ya shaka inabidi tujitoe mhanga na tulikamate hili kundi kabla halijasambaa. Au unasemaje Patrick?"



    "Itabidi tuwe tayari kupambana na Elungata. Maana nahisi huyu Elungata ambaye ni Joel tu aliyewahi kusikia sauti yake, huenda ndiye wanamwita Mzee. Kwa hiyo ndiye kichwa".



    "Bila shaka, lazima tupambane naye. Lililopo sasa ni kufanya mpango wa namna ya kuwasaka watu hawa",



    "Mimi ninavyofikiria, lazima tumkamate Khasimu na Pweke kwanza. Hawa watu wawili ndio watakaotupeleka hata kwenye kichwa".



    "Sawa Patrick, Khasimu alikuwa amemchukua Amanda kati ya saa sita sasa ni saa ngapi?"



    "Saa saba na nusu." Amanda alijibu.



    "Kwa hiyo atakuwa amesharudi nyumbani halafu atakuwa amemkuta Amanda. Hii itamfanya acheleweshe mipango yake kwani hatajua Amanda yuko wapi. Na kwa vile anampenda sana, atajaribu kumtafuta na hii itatupa sisi nafasi ya kuweza kumpata",



    "Milimweleza ndugu Mbogo awe hapa kabla ya saa nane unusu, ikiwa hatakuwa amefika ina maana kuwa jambo fulani limemtokea na itabidi kumfuata kwa hiyo mimi naonelea tujilaze kwa muda huu mchache wa saa moja unaweza kutusaidia kupoteza usingizi mpaka hiyo saa nane unusu"



    "Sawa Patrick nafikiri nyinyi watu wawili mnahitaji sana huo usingizi hasa Amanda ambaye hakuzoea kukaa macho hadi saa hizi".



    "Na wewe pia lazima ukumbuke bado unaumwa kwa hiyo wote hatuna budi kupata usingizi kabla ya mapambano dhidi ya hawa majambazi hayajaanza" Amanda alisema.



    Tulizima taa tukajilaza mimi kichwa kilikuwa bado kinanigonga sana lakini ilinibidi kujitahidi niweze kufanya mapambano ya mwisho kwa hawa majambazo, Mambo haya yalinikera sana kuwa sikuweza kupata usingizi mnamo saa nane na dakika ishirini mlango wa chumba uligongwa, bastola mkononi, Patrick alienda kuufungua.



    "Uko salama", aliuliza huku akiwasha taa.



    "Salama".



    Sisi wote tukaamka na kukaa.



    "Itabidi tuondoke hapa mara moja wanatutafuta", alisema Wilfred Mbogo.



    "Wamejuaje?" Niliuliza.



    "Nitawaeleza njiani watafika hapa wakati wowote". CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Tulichukua vitu vyetu na mara moja tukawa tunaondoka. Patrick alinipa bastola mbili zenye kiwambo cha kunyamazisha sauti.



    "Mimi nafikiri tubane tuwasubiri. Tukiwa na bahati ya kushika mmoja wao anaweza kutupeleka mpaka kwa huyo wanaemuita mzee", nilishauri.



    "Sawa, lakini kama ni hivyo itabidi Amanda atusubiri mahali fulani kwani panaweza kutokea mapigano makubwa sana", Patrick alishauri.



    "Hata kidogo na mimi lazima niwe katika hayo mapambano mpaka nione mwisho wake. Nikifa kwa ajili ya Joel nitakuwa nimekufa kifo cha fahari, Niko nanyi mpaka mwisho mtake msitake".



    "Haya mama ni mapenzi yako", nilimjibu.



    Kabla hata Wilfred hajaanza kutueleza gari likatokea kwa kasi lakini lilikuwa bado mbali kidogo. Nafikiri ni hao, Wilfred alipiga kelele.



    "Wote kwenye majani", niliamrisha.



    Karibu na nyumba kando ya barabara kulikuwa na majani marefu basi tulijificha humo gari lilikuja kasi lilipofika karibu na hiyo nyumba likafunga breki na watu wote watano wakatoka na bastola zikiwa mikononi.



    "Ila Willy na Amanda wanahitajiwa kwanza". Mmoja wao aliwaeleza wenzie.



    Kila mmoja akachukua sehemu yake tayari kwa mashambulizi, watatu walibaki nje wawili wakaingia ndani. Wote tulikuwa tumelala karibu karibu. "Patrick unaweza kufungua buti ya hiyo gari?" Nilimuuliza kwa sauti ya kunong'ona.



    "Naweza bila ya wasiwasi".



    "Mimi nataka niingie kwenye buti ndani nikiwa na bahati wanaweza kunifikisha kwenye watu wenyewe ninaowatafuta".



    "Wazo zuri," alijibu mwenzangu. "Hata tukisema tuwaue hawa tutakuwa hatujafanya lolote. Naona twende wote ndani ya buti la hilo gari,  Amanda na Wilfred watatusubiri kwa Wilfred".



    "Najua mkifanya hivyo safari yenu ni mpaka Shinyanga sasa hivi hakuna muda wa kuelezana niliyosikia. Tuonane Shinyanga Relwe nyumba nambari 13. Mimi na Amanda tutasubiri hapo", Wilfred alitoa rai.



    "Oke vizuri," nilikubali.



    Gari lilikuwa karibu sana na tulipokuwa, "Nendeni mimi nitawalinda ikiwa watawaona," Wilfred alisema.



    Tulinyata na kwa sababu mawazo yao yote yalikuwa ni ndani ya nyumba, tuliweza kuingia ndani ya buti ya kuwashitua. Buti la gari kama alivyosema Patrick lilikuwa kubwa sana, mlikuwa na taili moja na supana. Hewa iliyokuwamo ilikuwa kidogo lakini ingeweza kututosha.



    "Wameisha ondoka ndani ya chumba hamna mtu wala kitu," tulisikia mmoja wao akisema, "Twendeni zetu tukatoe habari mara moja, huenda ana wazo au habari za mahali walipo."



    Waliingia ndani ya gari na safari ikaanza. Walielekea barabara ya Maganzo. Mara kwa mara tulifungua mlango wa buti kuingiza hewa na kuangalia wapi tulipokuwa. Walipofika Maganzo hawakusimama bali waliendelea moja kwa moja kwenye barabara inayoelekea Shinyanga. Kwa vile walikuwa wakienda kasi sana. Patrick na mimi niliweza kunong'onezana juu ya mpango wetu na tulimuomba Mungu atusaidie.



    Kama tulivyokuwa tumebuni gari liliingia Shinyanga mjinina kuelekea barabara iendayo nyumba za watu wa hali ya juu. Kisha gari likasimama na kuzima injini. Mlango wa geti ulifungwa na dereva aliamurishwa kulisogeza mpaka mbele kidogo. Punde milango ikafungunguliwa wakatoka nje.



    ""Twendeni ndani, wanawasubiri kwa hamu sana", kiongozi wao alisema.



    Tuliwangoja waende kwanza. Hatmaye tukainua buti ili kuona kama hakukuwa na mtu. Tulipohakikisha kuwa ni salama, nikashika kifuniko cha buti ili Patrick atoke kwanza kisha nami nikafuata. Bahati mbaya nikagusa debe, likapiga kelele. Mtu wao mmoja aliyekuwa kwenye mlango wa mbele ya hiyo nyumba akaja kuangalia. Sisi tukabana kwenye sehemu ya seng'enge ya ua. Alipokaribia Patrick alikuwa ameshamzunguka. Akamnyemelea, akamkata 'karate' ya shingo na kufa hapo hapo. Hatmaye akanigeukia na kuniamrisha.



    "Nenda sasa, lakini jihadhari sana".



    "Hakuna taabu", nilimpa imani.



    Nilipitia mlango wa mbele, nikaingia ndani. Nilisikia sauti zinatoka kwa mbali kwenye chumba cha ndani. Nilipotaka kuingia mlango ukafunguliwa, nikabana. Akatoka mtu mmoja na bastola mkononi. Kwa vile hamkuwa na taa kwenye ukumbi, hakuniona.Nikamlisha risasi na alipoanguka nikamvuta. Nikamtupa kwenye magunia yaliyokuwa karibu na hapo.



    Nilifungua mlango wa nyumba taratibu.Taa zilikuwa zinawaka lakini hakukuwemo mtu. Nilisikia sauti zikitokea kwenye chumba cha pili yake. Nikazima taa za chumba hiki cha kwanza nikaenda mpaka kwenye mlango wa chumba cha pili. Nikasikia sauti ya kiaskali ikifoka.



    "Kwa nini mlirudi. Nendeni mkawatafute mpaka muwapate. La asivyo msirudi watu kumi na wawili hamuwezi kushindwa na watu wawili"



    "Tutajaribu" Mwingine alijibu.



    "Hakuna kujaribu" CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Nilihisi hiyo sauti ya Khasimu maana ilikuwa ya kiaskari hasa.



    "Khasimu lazima uende nao mumtafute Willy na Umuue pamoja na mwenziwe" sauti hii moja iliamuru.



    "Ndiyo Mzee" Khasimu alijibu kwa sauti ya woga.



    "Twendeni" walijihimiza.



    Mlango wa chumba nilichokuwemo ukafunguliwa



    "Nani alizima taa ?" Khasimu aliuliza.



    "Sijui, huenda Saidi" alijibu mmoja wao.



    "Washa"



    Taa haikuwaka. Nilikuwa nimetoa globu yake. Wakati huo nilikuwa nimebana nyumba ya mlango.



    "Hamna globu"



    "Nini?"



    "Hamna globu"



    "Angalieni huenda Willy tayarai yupo hapa" Khasimu alitahadharisha.



    Kundi lote lilikuwa humo chumbani na wote walikuwa bado hawajaniona. Vilele hawakuwa wanategemea, hivi hawakuwa tayari. Kwa hiyo nikachukua nafasi ya kumjibu.



    "Ndiyo tayari niko hapa Elungata."



    "Nikaachia risasi toka kwenye bastola zangu mbili na kuwaua wote, maana wote walishikwa na bumbuwazi.



    "Njooni,njooni ndani tumeingiliwa. Willy ndani, tumeingiliwa Willy yuko ndani, mkamateni." Sauti ya kutisha ilisikika.



    Nilirukia chumba cha pili. mlikuwa hamna mtu tena kulikuwa na mlango unaoeleka chumba kingine. Nilirudi nyuma bastola ikiwa mkononi. Nikaruka nikaupiga teke na kuingia ndani huku nikiviringika sakafuni. Hamna mtu! Niliposimama tu. Pweke alikuwa tayari amesimama mlangoni na bastola mkononi. Kwa vyovyote vile angeniwahi.



    "Weka bastola chini" alihamru.



    "Mpelee sebule ile. Mikono juu" Nikaweka mikono juu



    "huna ujanja tena!"



    Nilipofika sebuleni nikashangaa kumuona Patrick naye amekamatwa amefungwa kwenye kiti na huku damu zikimtoka hovyo. nikajua kwamba tumekwisha.



    "He, He unashangaa kumuona mwenzio Patrick? Mtanikoma" hiyo sauti ya kutisha ilisema, "Willy Gamba, huu ndiyo mwisho wako. Wengi wamejaribu wameshindwa. Wewe umejaribu sana, na kwa hiyo ninakupongeza."



    "Sina haja ya kupongezwa na wewe".



    "Wewe ulijaribu kuingilia himaya ya Elungata, aliyoijenga kwa miaka mingi. Je, Ungeweza?"



    Nikasikia sauti zinajibu "Asingeweza!" nikajua ya kwamba majambazi wenziwe walikuwa tayari wamewasili na wote walikuwa hapa Khasimu tu ndiye alikuwa amekufa.



    "Leo, Gamba, ni siku ya furaha sana kwangu na vijana wangu. Siku ambayo nimeweza kuichukulia Serikali kiasi cha Almasi inayotoka kwa mwaka mzima. Ni utajiri ulioje! na wakati huo huo Gamba unauawa mbele ya macho yangu nilifikiri kwamba baada ya leo nitaacha shughuli hii. Lakini sasa nitaendelea, maana baada ya kusikia umekufa hakuna hatakayethubutu tena."

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Una kichaa, hujui kuwa wananchi wa nchi hii hawatakata tamaa bali wataendelea kupambana nawe na kundi lako kwa ujasiri na ari zaidi, ili mradi kulinda uchumi wa nchi yao. Hawatakata tamaa kupambana na mtu juha kama wewe. Wengi wataendelea kujitoa mhanga mpaka siku watakayoweza kukuweka mbaroni. Wamenyonywa na wakoloni na sasa wamekataa kuonewa tena. Wakoloni wenyewe wanawaogopa wananchi wa nchi hii. Hawataki kuonewa wala kunyonywa tena sembuse wewe kibaraka chao. La hasha wananchi watakumaliza, na siku hiyo watakugawanya vipande."



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog